Paulo aliandika Kitabu cha Tito. Hapo awali alijulikana kama Saulo. Alitokea mji wa Tarso. Kabla ya kuwa Mkristo alikuwa Mfarisayo na alikuwa akiwatesa sana Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara nyingi katika himaya nzima ya Warumi akiwahubiria watu kumhusu Yesu
Paulo alimwandikia barua hii Tito, mfanyakazi mwenza aliyekuwa anayaongoza makanisa ya Kisiwa cha Krete.Paulo alimwelekeza jinsi ya kuwachagua viongozi wa kanisa.Paulo pia alifafanua jinsi waumini walipaswa kutendeana.Na akawahimiza wote waishi maisha yanayompendeza Mungu.
Watafsiri wanaweza kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Tito" ama wanaweza kuchagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama, "Barua ya Paulo kwa Tito," ama "Barua kwa Tito."
Kuna mafundisho fulani katika kitabu cha Tito kuhusu iwapo mwanamke ama mwanamume waliopeana talaka wanaweza kutumikia katika nafasi za uongozi kwenye kanisa. Wasomi wanatofautiana kuhusu maana ya mafundisho haya.Mafundisho zaidi kuhusu haya mambo yatakuwa ya muhimu kabla ya kukitafsiri kitabu hiki.
Katika kitabu hiki, neno "mimi" linaashiria Paulo. Mara nyingi neno "wewe" inaashiria mtu moja, ndiye Tito, isipokuwa katika 3:15.
Hili ni tamko la kawaida katika barua hii. Paulo alitaka wasomaji wafikirie jinsi Mungu aliwasamehe kupitia kwa Kristo baada ya hao kumtendea dhambi. Na kwa kuwasamehe aliwaokoa kutoka kuadhibiwa wakati atakapowahukumu watu wote. Tamko sawa na hili katika barua hii ni, "Mungu wetu mkuu na Mkombozi Yesu Kristo."
Paulo anaanzisha barua hii kirasmi katika mistari 1-4. Waandishi walianzisha barua kwa njia hii hapo kale Mashariki ya Karibu.
Katika mistari ya 6-9, Paulo anaorodhesha sifa za mwanaume anayetaka kuwa mzee wa Kanisa. Pauo anapeana orodha sawa katika 1 Timotheo 3.
Kanisa limetumia vyeo tofauti kuashiria viongozi wa kanisa. Baadhi ya vyeo hivi ni: Mwangalizi, mzee, mchungaji na askofu.
ULB hutumia maneno tofauti kuwashiria mahitaji ama mambo ya lazima. Maneno hayo yana matumizi ya viwango tofauti vya misisitizo. Tofauti ndogo ya maana ya hayo maneno inaweza kuwa ngumu kutafsiri. UDB inatafsiri maneno hayo kwa njia ya jumla.
kuimarisha imani ya
"inayofaa katika kumheshimu Mungu"
"Kabla ya kuanza kwa wakati"
"katika wakati unafaa"'
Paulo anaongea juu ya ujumbe wa Mungu kana kwamba ni kitu ambacho chaweza kudhihirishwa dhahiri kwa watu. "Alitangaza neno lake."
"Niliaminiwa kutangaza" au "alinipa wajibu wa kuhubiri"
"Mungu anayetuokoa"
Ingawa Tito hakuwa mwana wa Paulo kimwili, wanashiriki imani moja katika Kristo. Hivyo katika Kristo, Paulo humwona Tito kama mtoto wake. "wewe ni kama mwanangu"
Paulo anaelezea imani ile ile ambayo wote wanayoshiriki katika Kristo. "Mafundisho yale yale ambayo sisi sote tunaamini"
Hii ilikuwa salamu ya kawaida. "Neema,huruma na amani ziwe kwenu" au "mjazwe wema, huruma na amanikwenu."
"Yesu Kristo ambaye ni mwokozi wetu"
"Hii ni sababu"
"Nilikuambia kubaki Krete"
"Ili kwamba ungeamalizia kupanga mambo yaliyohitajika kukamilishwa."
"chagua wazee" au "panga na kudhirisha wazee"
Katika makanisa ya kwanzaya Kikristo ,Wazee wakikristo walipewa uongozi wa kiroho kwa mkutano wa waumini.
Baada ya kuwa amekwisha kumwambia Tito kuwaweka kazini wazee katika kila mji katika kisiwa cha Krete, Paulo anatoa matakwa yanayohitajika kwa wazee.
Kutokulaumiwa ni ilie hali ya kujulikana kuwa mtu huyo hatendi mambo mabaya. "Mzee lazima asiwe na sifa mbaya."
"kuwa mme mwaminifu" Maana zinazokubalika 1) Mme ambaye hatafuti mahusiano na wanawake wengine au 2) asiye na mke wa pila au hawala au suria.
Imaana zinazokubalika ni 1)watoto wanaomwaminiYesu au 2)watoto ambao ni waaminifu
"waasi" au "ambao hawafuati maagizo"
Paulo anaongelea juu ya wazee kana kwamba walikuwa vichwa vya familia, wakuu wa nyumba ya Mungu"
"asiwe mtu mwenye kutumia kileo" au "asiwe mnywaji" au "asiwe mlevi sana wa pombe"
"Asiwe mtu wa fujo"au "asiwe anapenda kupigana na kugombana"
Paulo anabadili hoja kutoka mada inayohusu mambo yasimpasa mzee kwenda kwa mambo anayopaswa kufanya
"kukumbatia mambo mazuri na tabia nzuri"
Paulo anazungumzia hali ya kujitoa katika imani ya Kikristo kama kushikilia imani katika mikono. "kujitoa kwa " au " kuwa na ufahamu mzuri wa.."
Lazima afundishe iliyo kweli kuhusu Mungu na mambo mengine ya kiroho.
Kwa sababu ya wale wanaopinga neno la Mungu, Paulo anampa Tito sababu za kufundisha Neno la Mungu na kumwonya kuhusu waalimu wa uongo.
Hawa ni watu waasi waliokuwa wakiupinga ujumbe wa injili ya Paulo.
inarejea wakristo wa Kiyahudi walikuwa wakifundisha kwamba ili kumfuata Kristo, mtu lazima atahiriwe.
'Maneno yao hayana faida yoyote"
"Ni lazima kuwazuia wasieneze mafundisho yao" au "Ni lazima kuwakataza kwa ushawishi wa maneno yao"
Vitu ambavyo si sahihi kuvifundisha kuhusu Kristo na sheria.
"Hii inarejela faida ambayo watu wanapata kwa kufanya mambo yasiyo na heshima.
"huharibu imani za familia yote"
"Mmoja wa Wakrete" au mtu fulani kutoka kwa watu wa Krete
Maana zinazokubalika ni 1) nabii au 2) "mshairi au mwana falsafa au 3) mwalimu
"Wakrete hudanganya kila wakati" Maneno haya yametiwa chumvi kuonesha tabia wa Wakrete ya kudanganya.
Msemo huu unawalinganish Wakrete na hayawani au wanyama hatari.
Ni msemo unaoonesha watu wasiopenda kufanya kazi yoyote lakini wanakula sana.
kwa hiyo waambie kwa ujasiri kwamba hawako sahihi (wamekosea)"
"Watakuwa na imani imara" au " kwamba imani yao itakuwa ya kweli"
Paulo anaendelea na maagizo yake kwa kumwelekeza Tito kile anachotakiwa kufundisha
Hii inaonyesha kwa mafundisho ya uongo ya Wayahudi
Paulo anaongelea ukweli kana kwamba ni kitu kilicho katika mwendo ambacho chaweza kurudishwa nyuma. "Kukataa ukweli"
Kila kitu ni safi kwa yule aliye safi ndani yake. " kila kitu anachofanya kitakuwa safi"
kwa wale walimpokea Mungu
Paulo anaongelea watu wenye dhambi kana kwamba ni wachafu kimwili. "Yeyote aliiye najisi kimaadili na ambaye haamini hawezi kuwa safi."
"matendo yao yanaonesha kuwa hawamjui"
mbaya, ya kutia kinyaa au isiyofaa
"hakuna mtu yeyote anayewatarajia kufanya kitu chochote kizuri"
Wasomi wanatofautiana kuhusu jinsi ya kuielewa aya hii katika muktadha wake wa kihistoria na kitamaduni. Wasomi wengine wanaamini kwamba wanaume na wanawake wako sawa kwa maswala yote. Wengine wanaamini Mungu aliwaumba wanaume na wanawake kutumikia majukumu ya kipekee katika kanisa na ndoa.Watafsiri wawe makini wasiathiriwe na jinsi wanavyoelewa swala hili wakati wa kutafsiri aya hii.
Katika sura hii, Paulo haandiki iwapo utumwa ni mzuri ama mbaya. Paulo anafundisha kwamba watumwa wawafanyie mabwana wao kazi kwa uaminifu. Anawafundisha waumini wote kumcha Mungu na kuishi vyema katika kila hali.
Paulo anaendelea kumweleza Tito sababu za yeye kuhubiri Neno la Mungu, na jinsi ambavyo wazee, akina mama wazee, vijana, na watumwa au watumishi wanapaswa kuishi kama waamini.
Paulo anatofautisha "Lakini wewe Tito, kinyume na walimu wa uongo"
"mafundisho ya kweli" au "na mafundisho sahihi"
"akili tengefu" au " "inayojijithibiti binafsi"
"inayojithibiti binafsi" au "inayotawala tamaa"
"yenye afya"
"yenye afya katika imani" au "sahihi katika imani zao"
"na upendo wenye afya"
"imara" au "ya kudumu" au "isiyochoka"
"kwa njia iyo hiyo." "Kama unavyowaelekeza wazee, waelekeze akina mama pia."
"wanapawa kudhihirisha wao wenyewe kuwa" au "Lazima uishi kama..."
Neno hili linarejelea watu wale wanaowasema vibaya wenzao kwa mambo ya kweli au ya uongo.
Mtu ambaye anatabia ya kuhitaji kunywa pombe mara kwa mara hupenda kunywa pombe nyingi. Paulo anaongelea juu ya watu waliokubuu au kuzoelea ulevi kiasi cha kuwaita watumwa. "watumwa wa pombe"
kuwa na mawazo sahihi au kufikiri vizuri
Tito alitakiwa kuwafundisha wasichana kama alivyokuwa akiwafundisha wazee.
Jioneshe wewe mwenyewe kuwa
kielelezo cha mtu yule anayefanya mambo sahihi na yenye kufaa.
Paulo anaongelea juu ya mahubiri na mafundisho ya Tito kana kwamba ni mtu mwenye afya katika mwili wake.
Hii inawakilisha hali ya kufikirika ya kwamba mtu yeyote atakayempinga Tito ataaibishwa kwa kufanya hivyo. Ilikuwa haizungumzii hali halisi iliyokuwepo dhahiri. Huenda lugha yako yaweza kkuwa na njia fulani ya kuelezea jambo hili.
"mabwana zao wenyewe"
"katika kila hali" au "mara zote"
"kuwafanya mabwana zao wafurahi" au "kuwaridhisha mabwana zao"
kuwaibia vitu vidogo mabwana zao
"kudhihirisha kuwa wanaaminika kwa mabwana zao"
"katika kila jambo wanalolifanya"
Paulo anazungumzia mafundisho ya kikristo kana kwamba ni kitu ambacho chaweza kupambwa. "Yafanyeni mafundisho yetu ili yawavutie watu wengine"
"Mungu wetu anayetuokoa"
Paulo anamtia moyo Tito kuutarajia ujio wa Yesu na kukumbuka mamlaka yake kupitia kwa Yesu.
Paulo anaiongelea neema ya Mungu kama ni Mtu anayeenda kwa watu wengine na kuwafundisha jinsi ya kuishi maisha matakatifu.
Inatufundisha tusimwasi Mungu
"Hizi ni tamaa kali kwa ajili ya vitu vya dunia hii" au "tamaa kwa ajili anasa"
"wakati bado tunaishi katika dunia hii" au " "muda huu"
"Tunasubiri kupokea"
Paulo anamaanisha kwamba Mungu atakuja kwetu ambaye ndani yake tumeweka tumaini letu .
Paulo anaongelea juu ya utukufu wa Mungu kumaanisha kwamba Mungu mwenyewe atajidhihirisha.
"kujitoa mwenyewe afe kwa ajili yetu."
Paulo anamzungumzia Yesu aliyetukomboa kana kwamba anawaweka huru watumwa kutoka katika mikono ya mabwana zao waovu.
Ni kundi la watu anaowawekezea hazina
"kuwa na tamaa au hamu kubwa ya ajabu"
"Fundisha mambo haya na uwatie moyo wasikilizaji ili wayafanye mambo haya."
Maelezo haya yanaweza kuwekwa wazi kama: " Wakemea au wasahihishe kwa mamlaka yote watu wale ambao hawayafanyi mambo haya"
"Usimruhusu mtu yeyote ku..."
Neno hili linnaweza kuwekwa wazi kumaanisha: " Kataa kusikiliza maneno yako" au "kukataa kukuheshimu"
Paulo anampa Tito maelekezo ya kibinafsi katika sura hii.
Mstari wa 15 unamalizia barua hii kirasmi. Hii ni njia ya kawaida ya kumaliza barua siku za kale katika Mashariki ya Karibu.
Orodha ya ukoo no orodha inayorekodi mababu wa mtu. Wayahudi walitumia ordha za ukoo kumchagua mtu aliyestahili kuwa mfalme. Walifanya hivi kwa vile mwana wa kiume wa mfalme angekuwa mfalme. Zilionyesha pia ni kabila na familia gani walitokea. Kwa mfano makuhani walitoka katika kabila la Walawi na kwa familia ya Aruni.
Paulo anaendelea kumpa Tito maelekezo juu ya namna ya kufundisha wazee na watu chini ya uangalizi wake huko Krete.
"Kuwaambia watu wetu tena kile ambacho tayari wanakijua" au "Kuendelea kuwakumbusha"
"fanyeni kama watawala wa kisiasa na wenye mamlaka ya kiserikali wasemavyo kwa kuwatii"
Maneno haya yana maana zinazofanana na yametumika pamoja kumuhusisha kila mmoja ambaye anashikilia mamlaka katika serikari.
"muwe rayari kufanya mema wakati wote palipo na fursa"
"ongea mabaya juu ya"
Paulo anawasihi waumini kufanya mambo kama vile watu wengine wanavyopendelea kufanya, ilimradi tu matakwa yao na matendo yao yasiwe ya dhambi. "
"kwa sababu"
"zamani" au "kwa wakati fulani" au "awali"
"ujinga" au "kutokuwa na hekima"
Paulo anaongelea juu ya tamaa za dhambi kana kwamba ni watu wanaotupotosha kutoka katika njia ya kweli "tumepotoshwa"
Paulo anazizungumzia tamaa zetu mbaya za mwanzo na kuzifananisha na mabwana zetu waliotutumikisha.
"tamaa" au "hamu"
"uovu na "wivu " ni maneno haya yako sawa kimaana, yaote yanamaanisha "dhambi." "Siku zote tulifanya mambo maovu na kutaka vitu vya watu wengine."
"tuliwafanya au tuliwasababisha wengine watuchukie"
Paulo anaongelea juu ya wema wa Mungu na Upendo wake kana kwamba walikuwa ni watu waliojitokeza mbele yetu.
"Kwasababu alikuw na rehema juu yetu"
Paulo anazungumzia juu ya msamaha wa Mungu kwa wenye dhambi kwa kuufananisha na kitendo cha kuosha mwili wa mtu. Lakini pia, anaongelea juu ya wenye dhambi kuwa wasikivu mbele za Mungu kama wamezaliwa upya tena.
"kwa wingi" au "ukarimu"
imekuwa kawaida kwa Waandishi wa Agano lake kumwongelea Roho Mtakatifu kama kimiminika ambacho humwagwa. "alitupa Roho Mtakatifu kwa ukarimu"
"Yesu alipotuokoa sisi"
"Mungu ametutangaza kuwa hatuna dhambi" "Tayari tumefanywa wenye haki na Mungu"
Watu walioahidiwa na Mungu waongelewa kama warithi wa mali na utajiri kutoka kwa mwana familia.
Hii inarejea kwenye maelezo kuhusu Mungu kutupa Roho Mtakatifu kupitia Yesu katika 3:6.
"kutafuta na kufanya matendo au kazi njema"
Paulo anaongelea kuhusu matendo meme kana kwamba ni vitu ambavyo Mungu aliweza kuviweka mbele ya watu. "ambayo Mungu aliyaandaa kwa ajili yao kuyafanya"
Paulo anaelezea kile Tito anapaswa kuepuka na kuwashughulikia wale ambao wanasababisha ubishi miongoni mwa waumini.
"lakini wewe, Tito,"
"mabishano kuhusu mambo yasiyo ya muhimu"
mambo yanayohusu habari za uhusiano wa kifamilia au ukoo
"kugombana"
"sheria za Musa"
"kujitenga" au "kutoingiliana na" au "msikae na" au "kuepuka"
"baada ya kumuonya mtu huyo mara moja au mara mbili"
"mtu kama huyo"
Paulo anamzungumzia mtu yule anayefanya makosa kana kwamba anaiacha njia ambayo amekuwa akiiendea.
"analeta hukumu juu yake mwenyewe"
Paulo anafunga barua akimwambia Tito cha kufanya baada ya kuchagua viongozi katika Krete na kwa kumpa salamu kutoka kwa wale aliokuwa pamoja nao.
"Baada ya kumtuma"
Haya ni majina ya wanaume
"fanya haraka na uje" au "njoo haraka"
"kukaa wakati wa majira ya baridi"
"Harakisha" au "Usichelewe kutuma"
"na pia umtume Apolo"
Paulo anafafanua kwanini ni muhimu wa kuwatoa akina Zena na Apolo.
Paulo alikuwa anawarejelea waumini wa Krete.
"washughulike kufanya"
Haya ni mahitaji ya ambayo yalikuwa hayakupangwa na ya haraka ambayo yalikuwa hayajulikani hapo awali.
Paulo anaongelea watu ambao hufanya matendo mazuri kama mimea inayozaa matunda ya kula. "ili waweze kuzaa matunda" au "ili maisha yao yawe na maana."
Paulo anahitimisha barua yake kwa Tito.
"Watu wote"
Maana zinazokubalika hapa ni 1) Waumini wanaotupenda au 2) Waumini wanaotupenda kwasababu tunashiriki imani moja.
Hii ilikuwa ni salamu ya kawaida ya kikristo. "Neema ya Mungu na iwe pamoja nanyi" au "Ninamwomba Mungu awe mwenye neema kwenu ninyi nyote."