1 Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na ndugu Timotheo kwa Filemoni, mpendwa rafiki yetu na mtenda kazi pamoja nasi, 2 na kwa Afia dada yetu, na kwa Arkipas askari mwenzetu, na kwa kanisa lile linalokutana nyumbani kwako. 3 Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo. 4 Wakati wote namshukuru Mungu. Ninakutaja katika maombi yangu. 5 Nimesikia upendo na imani uliyonayo katika Bwana Yesu na kwa ajili ya waumini wote. 6 Ninaomba kwamba ushirika wa imani yenu iwe na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema lililoko kati yetu katika Kristo. 7 Kwa kuwa nimekuwa na furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa sababu mioyo ya waumini imekuwa ikitulizwa nawe, ndugu. 8 Kwa hiyo, ingawa nina ujasiri wote katika Kristo kukuamuru wewe kufanya kile unachoweza kufanya, 9 lakini kwa sababu ya upendo, badala yake nakusihi - mimi, Paulo niliye mzee, na sasa ni mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu. 10 Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesmo, niliyemzaa katika vifungo vyangu. 11 Kwa kuwa mwanzoni hakukufaa, lakini sasa anakufaa wewe na mimi. 12 Nimemtuma- yeye ambaye ni wa moyo wangu hasa - kurudi kwako. 13 Nataraji angeendelea kubaki pamoja nami, ili anitumikie badala yako, wakati niwako kifungoni kwa ajili ya injili. 14 Lakini sikutaka kufanya jambo lolote bila ruhusa yako. Nilifanya hivi ili kwamba jambo lolote zuri lisifanyike kwa sababu nilikulazimisha, bali kwa sababu ulipenda mwenyewe kulitenda. 15 Labda ni sababu alitengwa nawe kwa muda, ilikuwa hivyo ili uwe pamoja naye milele. 16 Ili kwamba asiwe tena mtumwa, bali bora zaidi ya mtumwa, kama ndugu mpendwa, hasa kwangu, na zaidi sana kwako, katika mwili na katika Bwana. 17 Na hivyo kama wanichukulia mimi mshirika, mpokee kama ambavyo ungenipokea mimi. 18 Lakini kama amekukosea jambo lolote, au unamdai kitu chochote, kidai hicho kutoka kwangu. 19 Mimi Paulo, ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe: mimi nitakulipa. Sisemi kwako kwamba nakudai maisha yako hasa. 20 Naam ndugu, acha nipate furaha ya Bwana toka kwako: uburudishe moyo wangu katika Kristo. 21 Nikiwa na imani kuhusu utii wako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya vile ninavyokuomba. 22 Wakati huo huo andaa chumba cha wageni kwa ajili yangu, kwa kuwa ninatumaini kupitia maombi yako nitakutembelea hivi karibuni. 23 Epafra, mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu anakusalimu, 24 na kama afanyavyo Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi pamoja nami. 25 Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja na roho yako. Amina.
Lugha yako inaweza kuwa na njia maalum kwa mwandishi kujieleza kwa barua. "Sisi, Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo, ndugu yetu, naandika hii barua kwa Filemoni."
"Mtu aliyefungwa kwa kufundisha kuhusu Yesu Kristo."
Hapa hii inamaanisha mkristo mwenzake.
"Aliye, kama sisi, anakazi ya kueneza injili"
Hii inamaanisha "Afia mkristo mwenzetu" au "Afia dada yetu kiroho"
Hili ni jina la mtu
Hapa ni "askari" ni fumbo inayomuelezea mtu anayepambana kwa kueneza injili. "Mwenzetu shujaa kiroho "au pia mpambanaji katika vita vya kiroho pamoja nasi."
"Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo awape neema na amani."Hii ni baraka. Neno "kwenu" ni kwa wengi na inarejea kwa watu wote waliosalimiwa na Paulo katika mstari wa 1 na 2.
Paulo amedhihirisha mara tatu kuwa yeye ni mwandishi wa barua hii. Timotheo alikuwa naye na aliandika maneno aliyoambiwa na Paulo. Paulo aliwasalimia waliokutana kusali katika nyumba ya Filemoni.
Neno "mimi" linamaanisha Paulo. Filemoni ni mtu ambaye aliandikiwa barua hii. Sehemu zote zilizoandikwa "wewe" zinamuelezea Filemoni.
Neno "yetu" inawajumuisha Paulo, Filemoni na waamini wa kanisa waliokuwa wakikutana kwenye nyumba ya Filemoni.
Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu.
Neno "sisi" ni wingi ikimaanisha Paulo, Timotheo na Filemoni.
Hapo na zaidi katika barua hii, neno" wewe" inamtaja Filemoni.
Matokeo ya kujua kilicho chema
"Kwa sababu ya Kristo"
"umewatia moyo waamini" au "umewasaidia waamini"
"marafiki" Paulo anamuita Filemoni rafiki maana wote ni waamini na anasisitiza urafiki wao.
Inawezekana inamaanisha "mamlaka kwa sababu ya Kristo" au " kutiwa moyo kwa sababu ya Kristo."
Inawezekana inamaanisha ni 1) "kwa sababu 1 ninajua unawapenda watu wa Mungu,"2) "kwa sababu unanipenda mimi" au 3) "kwa sababu ninakupenda."
Paulo anaanza kutoa sababu ya kuandika barua yake.
"kijana wangu Onesmo." Paulo analinganisha uhusiano wake wa karibu na Onesmo sawa na ule uhusiano walionao baba na mwanawe. Kiuhalisia Onesmo sio kijana wa Paulo, lakini alipata maisha ya kiroho wakati Paulo alipomfundisha kuhusu Yesu, na Paulo alimpenda. "Mwanangu mpendwa Onesmo" au "Onesmo mwanangu wa kiroho."
Hili ni jina la mtu
Jinsi Onesmo alivyokuwa kama kijana kwa Paulo alimfanya kuwa muwazi. Niliyemfanya mwanangu wa kiroho wakati nilipomfundisha kuhusu Kristo na kuzaliwa mara ya pili." "amekuwa mwanangu"
"katika minyororo. "Wafungwa mara nyingi kwa minyororo. Paulo alikuwa kifungoni wakati akimfundisha Timotheo, na aliendelea kuwa kifungoni hata wakati alipoandika barua hii. Wakati akiwa kifungoni."
Paulo pengine ameandika barua kabla ya kumtuma Onesmo.
Hapa neno "moyo" ilitumika kwa mtu anayependwa sana. Paulo alisema hivi kuhusu Oesmo. "Ambaye nampenda daima."
"kwamba, tangu wewe usipokuwepo hapa, yeye ananguvu kunisaidia. Inaweza kutafsiriwa pia kama ni sentensi tofauti: Yeye angenisaidia mimi badala yako."
"wakati nilipokuwa nimefungwa" au "kwa sababu nipo kifungoni."
kwa sababu ya kuhubiri injili
Onesmo alikuwa mtumwa na Filemoni aliyemuibia kila kitu na kukimbia.
"Lakini sikutakutaka kumweka yeye hapa bila idhini yako" au "Lakini nilitaka awe pamoja nami kama wewe umekubali"
hivyo kila jambo jema utakalofanya, si kwa sababu nakulazimisha."
"kwa sababu uliwa huru kuchagua kufanya jambo lililo jema"
Hii yaweza kutafsiriwa hivi "Labda ni sababu ya Mungu kumpeleka Onesmo awe mbali nawe."
"kwa muda huu"
"ana thamani zaidi ya mtumwa"
"ndugu mpendwa" au "ndugu wa thamani katika Kristo"
"anamaanisha zaidi sana kwako"
uhusiano wa kibinadamu unaweza kuonekana wazi: "kwa sababu yeye ni mtumwa wenu" "kama mtu" au "uhusiano wa kibinadamu."
"na kama ndugu katika Bwana" au na kwa sababu yeye ni mali ya Bwana."
"kama wewe unanidhania mimi mtenda kazi wa Kristo"
"malipo yatatoka kwangu" au "sema kwamba mimi ni mmoja wa unaowadai."
Paulo niliyeandika hivyo, kwamba Filemoni ujue kwamba ni maneno ya kweli; Paulo kweli angemlipa. "Mimi, Paulo, ninaandika hivi mwenyewe."
"Sikuhitaji kukukumbusha wewe" "wewe unajua"
"wewe unanidai maisha yako" Paulo anamwambia Filemoni asiseme kuwa anawadai Onesmo au Paulo maisha yake kwa sababu Paulo anamdai zaidi Filemoni. "Ninakudai zaidi maana nimeyaokoa maisha yako"
Paulo alitaka Onesmo angefanya kwa uaminifu: furahisha moyo wangu kwa kumkubali Onesmo. "uufanye moyo wangu ufurahi" au "unifurahishe" au "unifariji."
"Kwa sababu nina hakika kwamba utafanya kile nilichosema"
"Pia"
andaa chumba hapo kwako iwe tayari kwa ajili yangu. Paulo alimwambia Filemoni afanye hivyo.
"Wale walioniweka gerezani wataniachia huru hivyo ntakuja kwako"
Paulo anamalizia barua yake kwa kuwabariki Filemoni na waamini wote waliokuwa wakikusanyika kusali katika nyumba ya Filemoni.
Maneno "wewe, ninyi" yanawaelezea Filemoni na waamini waliokutana nyumbani.
Huyu alikuwa mwaminu na mfungwa pamoja na Paulo.
"ambaye yupo gerezani pamoja na mimi kwa sababu ya Yesu Kristo"
Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi wenzangu nawasalimu.
Haya ni majina ya watu.
"wafanyakazi wenzangu" au "wote wanaofanya kazi na mimi"
Neno "yako" inawaelezea Filemoni na wote waliokutana nyumbani. "roho yako" inawakilisha watu wenyewe. "Bwana wetu Yesu Kristo awe mwema kwenu"