Swahili: Unlocked Literal Bible for Mathayo

Formatted for Translators

©2022 Wycliffe Associates
Released under a Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
Bible Text: The English Unlocked Literal Bible (ULB)
©2017 Wycliffe Associates
Available at https://bibleineverylanguage.org/translations
The English Unlocked Literal Bible is based on the unfoldingWord® Literal Text, CC BY-SA 4.0. The original work of the unfoldingWord® Literal Text is available at https://unfoldingword.bible/ult/.
The ULB is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
Notes: English ULB Translation Notes
©2017 Wycliffe Associates
Available at https://bibleineverylanguage.org/translations
The English ULB Translation Notes is based on the unfoldingWord translationNotes, under CC BY-SA 4.0. The original unfoldingWord work is available at https://unfoldingword.bible/utn.
The ULB Notes is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
To view a copy of the CC BY-SA 4.0 license visit http://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0/
Below is a human-readable summary of (and not a substitute for) the license.
You are free to:
The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms.
Under the following conditions:
Notices:
You do not have to comply with the license for elements of the material in the public domain or where your use is permitted by an applicable exception or limitation.
No warranties are given. The license may not give you all of the permissions necessary for your intended use. For example, other rights such as publicity, privacy, or moral rights may limit how you use the material.

Utangulizi wa Injili ya Mathayo

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Mathayo

  1. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo na mwanzo wa huduma yake (1:1-4: 25)
  2. Mahubiri ya Yesu mlimani (5:1-7:28)
  3. Yesu anaonyesha ufalme wa Mungu kupitia matendo ya uponyaji (8:1-9:34)
  4. Mafundisho ya Yesu kuhusu utume na ufalme (9:35-10:42)
  5. Mafundisho ya Yesu kuhusu injili ya ufalme wa Mungu. Mwanzo wa upinzani kwa Yesu. (11:1-12: 50)
  6. Mifano ya Yesu kuhusu ufalme wa Mungu (13:1-52)
  7. Upinzani zaidi kwa Yesu na kutokuelewa kuhusu ufalme wa Mungu (13:53-17:57)
  8. Mafundisho ya Yesu kuhusu uhai katika ufalme wa Mungu (18:1-35)
  9. Yesu ahudumu katika Yudea (19:1-22:46)
  10. Mafundisho ya Yesu kuhusu hukumu ya mwisho na wokovu (23:1-25:46)
  11. Kusulubiwa kwa Yesu, kifo chake na ufufuo wake (26:1-28:19)

Je, kitabu cha Mathayo kinahusu nini?

Injili ya Mathayo ni moja ya vitabu vinne katika Agano Jipya ambavyo vinaelezea kuhusu maisha ya Yesu Kristo. Waandishi wa Injili waliandika juu ya mambo mbalimbali yaliyoonyesha kama Yesu alikuwa nani na ni nini alichofanya. Mathayo aliashiria kwamba Yesu alikuwa Masiya, na kama Mungu angeweza kuokoa Israeli kupitia kwake. Mathayo mara nyingi alielezea kwamba Yesu alitimiza unabii wa Agano la Kale kuhusu Masiya. Hii inaweza kuonyesha kwamba alitarajia kuwa wasomaji wake wengi wa kwanza watakuwa Wayahudi.

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kukiita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Injili ya Mathayo," au "Injili kulingana na Mathayo." Au wanaweza kuchagua kichwa ambacho ni wazi, kama vile "Habari Njema ya Yesu ambayo Mathayo aliandika."

Nani aliandika Kitabu cha Mathayo?

Kitabu hakitupi jina la mwandishi. Hata hivyo, tangu nyakati za hapo mwanzo za Kikristo, Wakristo wengi wamefikiri kwamba mwandishi alikuwa Mtume Mathayo.

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, "Ufalme wa mbinguni" ni nini?

Mathayo alizungumza juu ya ufalme wa mbinguni kwa njia ile ile ambayo waandishi wengine wa injili walizungumzia juu ya Ufalme wa Mungu. Ufalme wa mbinguni unawakilisha Mungu akitawala juu ya watu wote na viumbe vyote kila mahali. Wale ambao Mungu anakubali katika ufalme wake watabarikiwa. Wataishi pamoja na Mungu milele.

Je, njia za kufundisha za kufundisha zilikuwa zipi?

Watu walimwona Yesu kama rabi. Rabi ni mwalimu wa sheria ya Mungu. Yesu alifundisha kwa njia iliyokuwa sawa na njia ya walimu wengine wa kidini huko Israeli. Alikuwa na wanafunzi ambao walimfuata kila mahali alipoenda. Wanafunzi hawa waliitwa wanafunzi. Mara nyingi aliwaambia mifano. Mifano ni hadithi zinazofundisha masomo ya maadili. and na )

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Je, vitabu vya kwanza vya Injili ni vipi?

Vitabu vya Mathayo, Marko na Luka huitwa injili za sinoptiki kwa sababu vina vifungu vingi vinavyofanana. Neno "sinoptiki" linamaanisha "kuona kwa pamoja."

Maandiko husemekana kuwa "sawa" wakati ambapo injili mbili au tatu zinafanana au zinakaribia kufanana. Wakati wa kutafsiri vifungu sambamba, wafasiri wanapaswa kutumia maneno sawa na kuyafananisha iwezekanavyo.

Je, kwa nini Yesu anajiita mwenyewe kama "Mwana wa Binadamu"?

Katika Injili, Yesu anajiita mwenyewe "Mwana wa Binadamu." Ni kumbukumbu ya Danieli 7:13-14. Katika kifungu hiki kuna mtu anayeelezewa kuwa "Mwana wa binadamu." Hiyo ina maana kwamba mtu huyo alifanana na mwanadamu. Mungu alitoa mamlaka kwa mwana wa binadamu kutawala mataifa milele. Na watu wote watamwabudu milele.

Wayahudi wa wakati wa Yesu hawakutumia "Mwana wa Binadamu" kama jina la mtu yeyote. Kwa hiyo, Yesu aliitumia kwa ajili yake mwenyewe ili kuwasaidia kuelewa kama yeye alikuwa nani.

Kutafsiri jina "Mwana wa Binadamu" kunaweza kuwa vigumu kwa lugha nyingi. Labda wasomaji hawataelewa tafsiri halisi. Watafsiri pia wanaweza kutumia jina mbadala, kama vile "Yule aliye Mtu." Inaweza pia kusaidia wanapoingiza maelezo ya chini ya tanbihi ili kulielezea.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Mathayo?

Haya ni masuala muhimu zaidi ya maandishi katika Kitabu cha Mathayo:

Watafsiri wanashauriwa kutoingiza vifungu hivi. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha moja au zaidi ya vifungu hivi, watafsiri wanaweza kuvijumuisha. Ikiwa vinajumuishwa, wanapaswa kuviweka ndani ya mabano ya mraba


Mathayo

1

1Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.2Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.3Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.4Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.5Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,6Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.7Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.8Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.9Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.10Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.11Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.

12Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.13Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.14Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.15Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.16Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.

17Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.

18Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.19Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.20Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,” Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.21Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.”22Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,23“Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli”-- maana yake, “Mungu pamoja nasi.”24Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.25Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.


Mathayo 01 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 1:23, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Nasaba

Nasaba ni orodha ambayo hurekodi mababu au wazao wa mtu. Orodha hizo zilikuwa muhimu sana katika kuamua nani aliyekuwa na haki ya kuwa mfalme, kwa sababu mamlaka ya mfalme mara nyingi ilipokelewa au kurithiwa kutoka kwa baba yake. Ilikuwa pia ya kawaida kwa mtu yeyote mashuhuri kuwa na kizazi cha kumbukumbu.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Matumizi ya sauti tulivu

Sauti tulivu hutumiwa kwa makusudi katika sura hii ili kuonyesha kwamba Yesu hakuzaliwa kupitia uhusiano wa ngono. Hapa, sauti tulivu inaashiria Roho Mtakatifu kama aliyetanguliza uja uzito wake Maria alipombeba mtoto Yesu. Kwa kuwa lugha nyingi hazina sauti tulivu, watafsiri wanapaswa kutafuta njia nyingine za kuwasilisha ukweli huo.

Links:


Matthew 1:1

Taarifa kwa ujumla:

Mwandishi anaanza na ukoo wa Yesu ili kuonesha kwamba yeye ni mzaliwa wa mfalme Daudi na wa Ibrahimu.

Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo

Ungeweza kutafsiri hii kama sentenso kamili.

mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu

Kulikuwa na vizazi vingi kati ya Yesu, Daudi, na Ibrahimu. Hapa "mwana" humaanisha "mzaliwa" "mzaliwa wa Daudi, ambaye alikuwa mzaliwa wa Ibrahimu.

mwana wa Daudi

wakati mwingine kirai "mwana wa Daudi" hutumika kama cheo, lakini hapa inaonekana kutumika kutambulisha tu ukoo wa Yesu.

Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka

Kuna njia mbalimbali ungeweza kutafsiri maelezo haya. Kwa namna yoyote unavyo natafsiri hapa, ingekuwa bora zaidi kuyatafsiri kwa namna ilele kwa orodha yote ya mababu wa Yesu. "Ibrahimu akawa baba wa Isaka" au "I brahimu alikuwa na mwana Isaka" au "Ibrahimu alikuwa na mwana aliitwa Isaka."

Peresi na Sera...Hesroni...Ramu

Haya ni majina ya wanaume

Peresi baba... Hesroni baba

"Peresi alikuwa baba... Hesroni alikuwa baba.

Matthew 1:4

Salmoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu

"Salamoni alikuwa baba wa Boazi, na mama wa Boazi alikuwa Rahabu" au "Salmoni na Rahabu walikuwa wazazi wa Boazi.

BOazi baba wa Obedi kwa Ruth

"Boazi alikuwa baba wa Obedi, na mama wa Obedi alikuwa Ruth" au "Boazi na Ruth walikuwa wazazi wa Obedi"

Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.

"Daudi alikuwa baba wa Sulemani, na mama wa Sulemani alikuwa mke wa Uria" au "Daudi na mke wa Uria walikuwa wazazi wa Sulemani"

mke wa Uria

Sulemani alizaliwa baada ya Uria kufa. "mjane wa Uria."

Matthew 1:7

Yoramu baba wa Uzia

Yoramu alikuwa kwa kweli babu ya babu yake na Uzia, hivyo 'baba" linaweza kutafsiriwa kama " babu"

Matthew 1:9

Amoni

Wakati mwingine jina hili limetafsiriwa "Amosi"

Yosia alikuwa baba wa Yekonia

Yosia alikuwa kwa kweli babu yake na Yekonia.

wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli

"wakati walipoamriwa kwa nguvu kuondoka kwenda Babeli" au "wakati Wababeli walipo washinda na kuwahamisha kwenda kuishi Babeli." Kama lugha yako inahitaji kuwataja wazi ambao walienda Babeli, unaweza kusema "Waisraeli" au Waisraeli ambao waliishi Yuda.

Babeli

Hapa humaanisha nchi ya Babeli, sio tu mji wa Babeli.

Matthew 1:12

baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli

Tumia maneno yale yale uliyoyatumia katika Mat.1:9

Shealitieli baba ya Zerubabeli

Shealitieli kwa kweli alikuwa babu yake na Zerubabeli.

Matthew 1:15

Maelezo yanayounganisha

Mwandhishi anahitimisha ukoo wa Yesu, ambayo yalianza katika Mat.1: 1

Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa

Mariamu, ambaye alimzaa Yesu

Aitwaye Kristo

Hii inaweza kuelezwa kwa namna iliyo hai. "watu ambao humwita Kristo."

Kumi na nne

"14"

kuchukuliwa kwenda Babeli

Tumia maneno yale yale uliyotumia katika Mat.1:9.

Matthew 1:18

Taarifa kwa ujumla:Mama yake alikuwa amechumbiwa kuolewa na Yusufu

"Mama yake Mariamu alikuwa mbioni kuolewa na Yusufu" kwa kawaida wazazi walifanya mipango ya ndoa za watoto wao." Wazazi wa Mariamu, mama wa Yesu, walikuwa wamemwahidi kuolewa na Yusufu.

Mama yake Mariamu alikuwa amechumbiwa

Tafsiri kwa namna ambayo huweka wazi kwamba Yesu alikuwa bado hajazaliwa wakati Mariamu alikuwa amechumbiwa na Yusufu. "Mariamu, ambaye angekuwa mama wa Yesu, alikuwa amechumbiwa,"

Kabla hawajapata kuwa pamoja

"kabla hawajaoana." Hii pengine inamaanisha Mariamu na Yusufu kulala pamoja. kabla hawajalala pamoja."

alionekana kuwa mjamzito

Hii inaweza kuelezwa kwa namna iliyo tendaji. "wakatambua kwamba alikuwa mbioni kupata mtoto" au 'ilitokea kuwa alikuwa mjamzito.

kwa Roho Mtakatifu

Uwezo wa Roho Mtakatifu ulikuwa umemwezesha kupata mtoto kabla ya kuwa amelala na mwanamume.

Mumewe Yusufu

Yusufu alikuwa bado hajamwoa Mariamu, lakini wakati mwanamume na mwanamke waliahidi kuoana, Wayahudi waliwahesabu mume na mke ingawa hawakuishi pamoja. "Yusufu, ambaye aliyepaswa kumwpoa Mariamu" au "Yusufu."

alisitisha uchumba kati yake na yeye

kuvunja mipango ya kuoana

Matthew 1:20

Kama alivyofikiri

"Kama Daudi alivyofikiri"

alimtokea katika ndoto

"alikuja kwake wakati Yusufu alikuwa akiota ndoto"

mwana wa Daudi

Hapa "mwana" humaanisha "mzaliwa"

aliyechukuliwa mimba katika tumbo lake amechukliwa mimba kwa Roho Mtakatifu

Hii inaweza kuelezewa kwa namna iliyo tendaji. "Roho Mtakatifu alisababisha Mariamu kuwa mjamzito na kuwa na mtoto huyu."

Naye atamzaa mwana

Kwa sababu Mungu alimtuma malaika, malaika alijua mtoto atakuwa mvulana.

utamwita jina lake

Hii ni amri. "utamwita" au "yakupasa kumpa jina"

kwa kuwa ataokoa

Mtafsiri anaweza kuongeza rejeo inayo sema "Jina 'Yesu' maana yake Bwana huokoa."

watu wake

Hii humaanisha Wayahudi

Matthew 1:22

Taarifa kwa ujumla

Mwandishi amnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba kuzaliwakwa Yesu kulikuwa kwa mujibu wa andiko

Hii yote ilitokea

Malaika hazungumzi tena. Mathayo sasa anaeleza umuhimu wa kile malaika alikisema.

kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii

Hii inaweza kuelezwa kwa namna iliyo tendaji. "kile ambacho Bwana alimwambia nabii Isaya kuandika zamani."

Tazama...Emanueli

Hapa Mathayo anamnukuu nabii Isaya.

Tazama

Neno hili huongeza msisitizo kwa kile kilicho fuata kusemwa. "Tazama" au "Sikia" au "Kuwa makini kwa kile ninachotaka kukuambia"

Emanueli

Hili ni jina la kiume.

maana yake 'Mungu pamoja nasi'

Hii haimo katika kitabu cha Isaya. Mathayo anaeleza maana ya jina "Emanueli." Unaweza kulitafsiri kama sentenso iliyo peke yake. "Jina hili maana yake 'Mungu pamoja nasi.'"

Matthew 1:24

Maelezo yanayo unganisha:

Mwandishi anahitimisha maelezo ya matukio kuelekea kuzaliwa kwa Yesu.

kama malaika wa Bwana alivyoamuru

Malaika alikuwa amemwambia Yusufu kumchukua Mariamu kama mke wake na kumpa mtoto jina Yesu.

akamchukua kama mke wake

"alimwoa Mariamu"

kwa mwana

Hakika ni wazi kuwa Yusufu si baba halisi "kwa mtoto wa kiume" au "kwa mwana wake."

Na alimwita jina lake Yesu

"Yusufu alimwita mtoto Yesu"


Translation Questions

Matthew 1:1

Katika ukoo wa Yesu Kristo, ni mababu wapi wameorodheshwa wa kwanza, kuonesha umuhimu wao?

Mababu wawili walioorodheshwa wa kwanza ni Daudi na Ibrahimu.

Matthew 1:15

Mwishoni mwa orodha ya uzao, mke gani aliyetajwa na kwa nini ametajwa?

Mariam, mke wa Yusufu ametajwa, kwasababu yeye ndiye alimzaa yesu.

Matthew 1:18

Nini kilitokea kwa Mariamu kabla hajawa pamoja na Yusufu?

Mariamu alipata mimba kwa Roho Mtakatifu kabla hajawa pamoja na Yusufu.

Yusufu alikuwa mtu wa namna gani?

Yusufu alikuwa mtu wa haki.

Yusufu aliamua kufanya nini alipogundua kuwa Mariamu alikuwa na mimba?

Yusufu aliamua kuvunja uchumba na Mariamu kwa siri.

Matthew 1:20

Nini kilitokea kwa Yusufu kilichomfanya kubaki mchumba wa Mariamu?

Malaika alimwambia Yusufu katika ndoto kumchukua Mariamu kama mke wake kwa sababu mtoto alichukuliwa mimba kwa Roho Mtakatifu.

Kwa nini Yusufu aliambiwa mtoto amwite jina Yesu?

Yusufu aliambiwa amwite mtoto Yesu kwa sababau atawaokoa watu wake na dhambi zao.

Matthew 1:22

Nini ambacho unabii wa Agano la Kale ulisema kilitimia katika matukio haya?

Unabii wa Agano la Kale ulisema kuwa bikira atazaa mtoto wa kiume, na kwamba watamwita jina lake Emanueli, ambalo maana yake "Mungu pamoja nasi".

Matthew 1:24

Jambo gani ambalo Yusufu alikuwa mwangalifu asilifanye hadi pale Mariamu alipomzaa Yesu?

Yusufu alikuwa mwangalifu kulala na Mariamu hadi pale alipomzaa Yesu.


2

1Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, wataalamu wa nyota kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema,2“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.”

3Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.4Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”5Wakamwabia, “Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii,6Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.”

7Hivyo Herode aliwaita wale watalaamu wa nyota kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana.8Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.”

9Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa.10Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.11Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane.12Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.

13Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, “Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.14Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri.15Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, “Kutoka Misri nimemwita mwanangu.”16Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watalaamu wa nyota, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watalaamu wa nyota.17Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia,
18“Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena.”

19Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema,20“Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa.”21Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.

22Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya23na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.


Mathayo 02 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mstari yote ya mistari ya 6 na18, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Nyota yake"

Huenda labda inaelezea nyota ambayo wasomi waliamini kuwa ishara ya mfalme mpya wa Israeli.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Waakili"

Tafsiri za Kiingereza hutumia maneno mengi tofauti ili kutafsiri maneno haya. Maneno haya ni pamoja na "wanajimu" na "watu wenye hekima." Watu hawa wangeweza kuwa wanasayansi au majusi. Ni bora kutafsiri hii kwa neno la kawaida "waakili," inapowezekana.

Links:


Matthew 2:1

Taarifa kwa ujumla:

Sehsmu mpya ya habari huanza hapa na kuendelea hadi mwisho wa sura. Mwandishi anasimulia kuhusu jaribio la Herode kumwua mfalme mpya wa Wayahudi.

Bthlehemu ya Yuda

"mji wa Bethlehemu katika jimbo la Uyahudi"

katika siku za mfalme Herode

"wakati Herode alipokuwa mfalme huko"

Herode

Hii humaanisha Herode Mkuu.

mamajusi

"watu wenye elimu ya nyota"

kutoka mashariki

"kutoka nchi ya mbali mashariki ya Uyahudi.

Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi?

Watu wale walijua kutokana na elimu ya nyota kwamba yule ambaye atakuja kuwa mfalme alikuwa amekwisha zaliwa. Walikuwa wanajaribu kuchunguza mahali alipokuwa. Mtoto mdogo ambaye atakuja kuwa mfalme wa Wayahudi amezaliwa. Yuko wapi?"

nyota yake

Walikuwa hawasemi kwamba mtoto mdogo alikuwa mmiliki halali wa nyota. "nyota ambayo hutuambia kuhusu yeye" au "nyota ambayo imehusishwa na kuzaliwa kwake.'

mashariki

"ilikuja tokea mashariki" au wakati tulopkuwa katika nchi yetu"

abudu

uwezekano wa maana ni 1) walikusudia kumwabudu mtoto mdogo kama Mungu, au 2) walitka kumpa heshima kama mfalme wa kibinadamu. Kama lugha yako ina neno ambalo huhusisha maana zote mbili, unapaswa kuzingatia kulitumia hapa.

alifadhaika

"alitaabishwa." Herode alitaabishwa kwamba mtoto mdogo huyu atachukua nafasi yake kama mfalme.

Yerusalemu yote

Hapa "Yerusalemu" ina maanisha watu. Pia "yote" humaanisha "wengi." Mathayo anaongeza chumvi kusisitiza watu wangapi walitaabishwa. "watu wengi wa Yerusalemu."

Matthew 2:4

Taarifa kwa ujumla:

Ktoka mstari wa 6, makuhani wakuu na waandishi wa watu wanamnukuu nabii Mika kuonesha kwamba Kristo angezaliwa Bethlehemu.

Katika Bethlehemu ya Yuda

"Katika mji wa Behlehemu katika jimbo la Yuda"

hili ndilo lililoandikwa na nabii

Hili linaweza kuelezwa kwa namna iliyo tendaji. hiki ndicho likchoandikwa na nabii zamani.

Na wewe, Bethlehemu...Israeli

Wanamnukuu nabii Mika.

wewe, Bethlehemu...hu mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda

MIka alikuwa akizungumza na watu wa Bethlehemu kana kwamba walikuwa pamoja naye, lakini hawakuwa naye. Pia "hu mdogo" linaweza kutafsiriwa na kirai chanya. "ninyi watu wa Bethlehemu,...mji wenu ni miongoni mwa miji iliyo muhimu zaidi kuliko yote katika Yuda.

ambaye atawachunga watu wangu Israeli

Mika anamzungumza mtawala huyu mchungaji. Hii inamaanisha ata waongoza na kuwahudumia watu. "ambaye atawaongoza watu wangu Israeli kama mchungaji aongozavyo kondoo wake."

Matthew 2:7

Herode aliwaita mamajusi kwa siri

Hii inamaanisha kwamba Herode alizungumza na mamajusi bila ya watu wengine kujua.

kuwauliza lini hasa nyota ilikuwa imekwisha onekana.

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja. "na akawauliza, lini hasa nyota hii ilionekana?"

nyota ilikuwa imeonekana lini

Hii inadokeza kwamba mamajusi walimwambia nyota ilionekana lini. "wakati gani nyota ilikuwa umeonekana. Mamajusi walimwambia Herode lini wakati nyota ilipoonekana mara ya kwanza."

mtoto mchanga

Inamaanisha Yesu.

nipe neno

"nijulishe" au "niambie"

mwabudu

Tafsiri hii kama ulivyofanya katika Mat 2:1

Matthew 2:9

baada ya

"baada ya mamajusi"

walikuwa wamekwisha iona mashariki

"walikuwa wamekwisha iona ikija kutoka mashariki" au "walikuwa wamekwisha iona katika nchi yao."

ikawatangulia

"iliwaonesha njia" au "iliwaongoza"

ilitulia juu ya

"ilisimama juu"

mahali alipokuwa mtoto

"mahali ambapo mtoto mchanga alikuwapo"

Matthew 2:11

Maelezo yanayounganisha:

Hapa mandhari yanahamia kwenye nyumba mahari Mariamu, Yusufu, na mtoto mchanga Yesu walikuwa wakiishi.

walienda

"Mamajusi walienda"

abudu

Trafsiri neno hili kama ulivyofanya katika Mat.1:1

Hazina zao

"hazina" humaanisha kasha au mifuko waliotumia kubebea hazina. "vyombo ambavyo vilishikilia hazina zao."

Mungu aliwaonya

"Baadaye, Mungu aliwaonya mamajusi." Mungu alijua kwamba Herode alitaka kumdhuru mtoto.

wasirudi kwa Herode

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja. "kusema, 'Msirudi kwa mfalme Herode."

Matthew 2:13

Taarifa za jumla:

Katika mstari wa 15, mwandishi amnukuu nabii Hosea kuonesha kwamba Kristo angekaa Misri.

walikuwa wameondoka

:mamajusi walikuwa wameondoka"

alimtokea yusufu katika ndoto.

"alikuja kwa Yusufu wakati alipokuwa anaota.

Amka, chukua...kimbilia...Baki...wewe

Mungu anazungumza na Yusufu, haya yanapaswa kuwa katika umoja.

hadi nitakapo kuambia

Maana kamili ya maelezo haya yanaweza kufanywa kuwa wazi. "mpaka nitakapo kuambia ni salama kurudi."

Nita kuambia

Hapa "nitakapo kuambia" inamaanisha Mungu. Malaika anazungumza kwa ajili ya Mungu.

Alibaki

Inamaanisha kwamba Yusufu, Mariamu, na Yesu walibaki Misri. "Walibaki"

mpaka kifo cha Herode

Herode hafi mpaka Maelezo haya yanaelezea urefu wa muda wa kukaa Mirsi, na hayasemi kwamba Herode alikufa kwa wakati huu.

Kutoka Misri nitamwita mwanangu

"Nimemwita mwanangu kutoka Misri"

Matthew 2:16

Maelezo yanayounganisha:

Hapa mandhari yahamia kurudi kwa Herode na hueleza alifanya nini baada ya kugundua kuwa mamajusi walikuwa wamemdanganya.

Taarifa kwa ujumla

Matukio haya yalitokea kabla kifo cha Herode, ambayo mwandishi ameyataja katika2:13

amekwisha dhihakiwa na mamajusi

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "mamajusi walikuwa wamemwaibisha kwa kumdanganya."

Alituma na kuwaua watoto wote wa kiume

Herode hakuua watoto yeye mwenyewe. "Alitoa amri ili maaskali wake watoto wote wa kiume" au "Aliwatuma maaskari pale kuwa watoto wote wa kiume.

wenye umri wa miaka miwili na chini yake

"Umri wa miaka 2 na wadogo chini ya umri huo.

kwa mujibu wa wakati

"kutegemeana na wakati"

Matthew 2:17

Taarifa kwa ujumla:

Mwandishi amnukuu nabii Yeremia kuonesha kwamba kifo cha watoto wote wa kiume katika mkoa wa Bethlehemu kilikuwa kwa mujibu wa Maandiko.

Kisha ilitimizwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Hii ilitimizwa" au "matendo ya Herode yalitimiza."

kile kilicho kuwa kimenenwa kwa njia ya nabii Yeremia

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "kile Bwana alikinena hapo zamani kwa njia ya nabii Yeremia"

Sauti ilisikika...hawakuwapo

Mathayo anamnukuu nabii Yeremia.

Sauti ilisikika

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Watu walisikia sauti" au "kulikuwa na sauti kubwa."

Raheli awalilia watoto wake

Raheli aliishi miaka mingi kabla ya wakati huu. Unabii huu huonesha Raheli, ambaye amekufa, akiwalilia wazaliwa wake.

alikataa kufarijiwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "hakuna yeyote angeweza kumfariji"

kwa sababu hawapo tena

kwa sababu watoto walikuwa wametoweka na kamwe hawatarudi." Hapa "hawapo tena" ni njia laini ya kusema wamekufa. "kwa sababu walikuwa wamekufa"

Matthew 2:19

Maelezo yanayounganisha:

Hapa mandhari ya hamia kwenda Misri, mahali Ysufu, Mariamu, na mtoto Yesu wanaishi.

tazama

Hii inaweka alama ya mwanzo wa tukio jingine katika habari ndefu. inaweza kuhusisha watu wengi kuliko matukio yaliyotangulia. Lugha yako inaweza kuwa namna ya kufanya hivi.

wale ambao walitafuta uhai wa mtoto

"wale ambao walikuwa wanamtafuta mtoto ili wamwue"

wale ambao walitafuta

Hii ina maanisha mfalme Herode na washauri wake.

Matthew 2:22

Maelezo yanayounganisha:

Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi ambayo ilianza katika Mat. 2:1. kuhusu jaribio la Herode kumwua mfalme mpya wa Wayahudi.

Lakini aliposikia

"Lakini Yusufu aliposikia"

Arikeleu

Hili ni jina la mwana wa Herode.

aliogopa

"Yusufu aliogopa"

lile lililonenwa na Bwana kwa njia ya nabii

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "lile Bwana alilolinena hapo zamani kwa njia ya manabii"

ataitwa mnazarayo

Hapa "ataitwa" anamaanisha Yesu. Manabii kabla ya wakati wa Yesu wangelimtaja kama Masihi au Kristo. "watu wangesema kuwa Kristo ni Mnazarayo."


Translation Questions

Matthew 2:1

Yesu alizaliwa wapi?

Yesu alizaliwa Bethlehemu ya Uyahudi.

Wenye hekima(mamajusi) kutoka mashariki walimpa cheo gani Yesu?

Wenye hekima(mamajusi) kutoka mashariki walimpa Yesu cheo cha " Mfalme wa Wayahudi"

Wenye hekima(mamajusi) walifahamje kwamba Mfalme wa Wayahudi alikuwa amezaliwa?

Wenye hekima(mamajusi) walikuwa wameona nyota ya Mfalme wa Wayahudi huko mashariki.

Mfalme Herode alikuwa na mwitikio gani juu ya habari kutoka kwa Wenye hekima(mamajusi)?

Mfalme Herode aliposikia habari kutoka kwa Wenye hekima(mamajusi), alifadhaika.

Matthew 2:4

Wakuu wa makuhani na waandishi walifahamuje sehemu ambako Yesu angezaliwa?

Walifahamu juu ya unabii uliosema Kristo angezaliwa katika Bethelehemu.

Wakuu wa makuhani na waandishi walifahamuje sehemu ambako Yesu angezaliwa?

Walifahamu juu ya unabii uliosema Kristo angezaliwa katika Bethelehemu.

Matthew 2:9

Mamajusi waliwezaje kupata mahali penyewe Yesu alipozaliwa?

Nyota kutoka mashariki iliwatangulia hadi ilisimama juu mahali alipozaliwa Yesu.

Matthew 2:11

Yesu alikuwa wa umri gani wakati mamajusi walipo kuja kumwona?

Yesu alikuwa mtoto mdogo wakati mamajusi walipo kuja kumwona.

Mamajusi walitoa zawadi gani kwa Yesu?

Mamajusi walitoa zawadi ya dhahabu, manemane na uvumba kwa Yesu.

Mamajusi walirudi nyumbani kwa njia gani na kwanini walirudi kwa njia hii?

Mamajusi walirudi nyumbani kwa njia nyingine kwa sababu Mungu aliwaonya katika ndoto kwamba wasirudi kwa Herode.

Matthew 2:13

Ni maelekezo gani Yusufu aliyapokea katika ndoto?

Yusufu alielekezwa katika ndoto kumchukua Yesu na Mariamu na kukimbilia Misri, kwa sababu Herode alikuwa anaelekea kujaribu kumuua Yesu.

Ni unabii gani ulitimia baadaye Yesu aliporudi kutoka Misri?

Unabii wa " kutoka Misri nimemwita mwangu" ulitimizwa wakati Yesu aliporudi kutoka Misri?

Matthew 2:16

Herode alifanya nini wakati mamajusi walipoacha kurudi kwake?

Herode aliwaua watoto wote wa kiume katika mkoa wa Bethlehemu waliokuwa wa umri wa miaka miwili au chini yake.

Matthew 2:19

Ni maelekezo gani Yusufu aliyapokea katika ndoto baada ya Herode kufa?

Yusufu alielekezwa katika ndoto kurudi katika nchi ya Israeli.

Ni maelekezo gani Yusufu aliyapokea katika ndoto baada ya Herode kufa?

Yusufu alielekezwa katika ndoto kurudi katika nchi ya Israeli.

Matthew 2:22

Yusufu alifanya makazi wapi ya kuishi pamoja na Mariamu na Yesu?

Yusufu alifanya makazi ya kuishi pamoja na Mariamu na Yesu Nazareti ya Galilaya.

Yusufu alifanya makazi wapi ya kuishi pamoja na Mariamu na Yesu?

Yusufu alifanya makazi ya kuishi pamoja na Mariamu na Yesu Nazareti ya Galilaya.

Ni unabii gani ulitimia wakati Yusufu alipohamia kwenya makazi yao mapya?

Unabii kuwa Kristo ataitwa Mnazorayo ulitimizwa.


3

1Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema,2“Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu.”3Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, “Sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; ‘wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.”’

4Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.5Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake.6Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.

7Lakini alipowaona wengi wa Mafarisayo na Masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, “Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?8Zaeni matunda yaipasayo toba.9Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, ‘Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.’ Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.10Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto.

11Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.12Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.

13Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana.14Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”15Yesu akajibu akasema, “Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Kisha Yohana akamruhusu.

16Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake.17Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa sana naye.”


athayo 03 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya mstari wa 3, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Zaeni matunda yanayostahili toba"

Matunda ni taswira ya kawaida katika maandiko. Inatumika kuelezea matokeo ya tabia nzuri au mbaya. Katika sura hii, matunda mazuri ni matokeo ya kuishi kama Mungu anavyoamuru.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ufalme wa mbinguni umekaribia"

Wataalam wanajadili ikiwa "ufalme wa mbinguni" ulikuwepo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha changamoto katika kutafsiri. Matoleo mengine hutumia maneno "inakaribia" na "yamekaribia."

Links:


Matthew 3:1

Taarifa kwa ujumla:

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi mahali ambapo mwandishi anaisimulia huduma ya Yohana Mbatizaji. Katika mst. 3. mwandishi anamnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa mjumbe aliyechaguliwa na Mungu kuandaa huduma ya Yesu.

Katika siku hizo

Hii ni miaka mingi baada ya Yusufuna familia kuondoka Misri na kwenda Nazareti.Hii pengine karibu na wakati ambao Yesu alianza huduma yake. "Baadaye" au "Miaka kadhaa baadaye."

Tubuni

Hii iko katika wingi. Yohana anazungumza na umati.

ufalme wa mbinguni umekaribia

Kirai "ufalme wa mbinguni" humaanisha Mungu kutawala kama mfalme. Kirai hiki kiko katika kitabu cha Mathayo tu. Kama inawezekana, tumia neno "mbinguni" katika tafsiri yako. "Mungu wetu uliye mbinguni baada ya muda mfupi atajionesha mwenyewe kuwa mfalme."

Kwa kuwa huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema

Hii inaweza kuelezwa katika nmna iliyo tendaji. "Kwa kuwa Isaya nabii alikuwa anamnena Yohana Mbatizaji wakati aliposema."

Sauti ya mtu

Hapa "sauti" humaanisha nafsi yote. "Kuna mtu."

Tengenezeni njia ya Bwana, nyosheni njia yake

"Andaeni njia ya Bwana, nyosheni njia yake." Hii ni sitiari ya ujumbe wa Yohana ambao unawita watu kujiandaa na ujio wa Yesu kwa kufanya toba ya dhambi zao. "Badilika katika maisha yako hivyo utakuwa tayari wakati Bwana ajapo."

Matthew 3:4

Sasa...asali ya nyikani

Neno "sasa" limetumika hapa kuweka alama kutenganisha mtiririko mkuu wa simulizi. Hapa Mathayo ana simulia habari za historia ya nyuma kuhusu Yohana Mbatizaji.

alivaa nguoa za manyoa ya ngamia na mkanda wa ngozi katika kiuno chake.

Vazi hili huashiria kwamba Yohana ni nabii kama manabii wa tangu zamani, hususan nabii Eliya.

Kisha Yerusalemu, Uyahudi yote, na mkoa wote

Hii humaanisha watu kutoka maeneo yale. "Hapa neno "yote" humaanisha "wengi." Mathayo anasisitiza jinsi watu wengi walivyoenda kwa Yohana Mbatizaji.

Walibatizwa naye

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Yohana aliwabatiza."

Wao

Hii inamaanisha watu waliokuja kutoka Yerusalemu, Uyahudi, na mkoa kuzunguka Mto Yordani.

Matthew 3:7

Taarifa kwa ujumla:

Yohana Mbatizaji aanza kuwakemea Mafarisayo na Masadukayo.

Enyi uzao wa nyoka wa sumu

Hii ni sitiari. Nyoka wa sumu ni hatari na wanwaklisha uovu. "Enyi nyoka wa sumu waovu!" au "Mu waovu kama nyoka wa sumu."

nani kawaonya kuikimbia ghadhabu ambayo inakuja

Yohana anatumia swali kuwaonya Mafarisayo na Masadukayo kwa sababu walikuwa wakimwomba kuwabatiza ili kwamba Mungu asiwahukumu, lakini hawakutaka kuacha kufanys dhambi. "hamwezi kuikimbia ghadhabu ya Mungu namna hii" au "msifikiri kwamba mnaweza kuikimbia ghadhabu ya Mungu kwa sababu ya kuwabatiza tu.

Ikimbieni gadhabu inayokuja

Neno "ghadhabu" linatumika kumaanisha adhabu ya Mungu kwa sababu ghadhabu yake hutangulia. "kimbieni kutoka kwenye hukumu ambayo inakuja" au "iepukeni kwa sababu Mungu anaenda kuwaadhibu ninyi."

Zaeni matunda yastahiliyo toba

Kirai "zaeni matunda" ni sitiari inayomaanisha matendo ya mtu. "Acha matendo yenu yaoneshe kwamba mmetubu kweli."

Tunaye Ibrahimu baba yetu

"Ibrahimu ni babu yetu" au "ni wazaliwa wa Ibrahimu." Viongozi wa Kiyahudi walifikiri kwamba Mungu hangewahukumu kwa kuwa ni wazaliwa wa Ibrahimu.

Kwa maana nawambieni

Hii inaongeza msisitizo kwa kile Yohana anchokwenda kukisema

Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.

"Mungu angeweza kufanya wazaliwa wa mwili kutokana hata na mawe haya na kumpa Ibrahimu"

Matthew 3:10

Maelezo yanyounganisha

Yohana Mbatizaji anaendelea kuwakemea Mafarisyo na Masadukayo.

Tayari shoka limekwisha wekwa kwenye shina la miti. Hivyo kila mti usioweza kuzaa matunda mazuri unakatwa na kutupiwa motoni.

Sitiari hii inamaanisha Mungu yuko tayari kuawaadhibu wenye dhambi. Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Mungu ana shoka lake na yuko tayari kukata na kuchoma mti wowote unaozaa matunda mabaya" au "Kama vile mtu atayarishavyo shoka kukata na kuchoma mti ambao huzaa matunda mabaya, Mungu yuko tayari kuwaadhibu ninyi kwa ajili ya dhambi zenu."

kwa ajili ya toba

"kuonesha kwmba umekwisha tubu"

Lakini ajaye nyuma yangu

Yesu ni mtu yule ambaye anakuja nyuma ya Yohana

ni mwenye uwezo kuliko mimi

'ni wa muhimu zaidi kuliko mimi"

Atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto

Sitiari hii hulinganisha ubatizo wa Yohana wa maji kwa ubatizo ujao wa moto. Hii humaanisha ubatizo wa Yohana kiishara huwatakasa watu dhambi zao. Ubatizo kwa Roho Mtakatifu na moto utatakasa dhambi za watu kwa kweli. Kama inawezekana, tumia neno "batiza" katika tafsiri yenu kutunza ulinganishaji wa ubatizo wa Yohana.

Pepeto lake li mkononi mwake kupepeta ngano

Sitiari hii hulinganisha namna Kristo atakavyo watenganisha watu wenye haki na watu wasio haki kwa namna mtu atenganishavyo nafaka ya ngano na makapi. "Kristo ni kama mtu ambaye pepeto lake liko mkononi mwake."

Pepeto lake li mkononi mwake

Hapa "mkononi mwake" humaanisha mtu yuko tayari kutenda. "Kristo ameshikilia pepeto kwa sababu yuko tayari."

pepeto

Hiki ni kifaa kwa ajili ya kurusha juu hewani kutenganisha nafaka za ngano na makapi. Nafaka zenye uzito hurudi na kuanguka chini na makapi yasiyotakiwa hupeperushwa na upepo. Kina fanana na umbo la uma ya nyasi lakini kina meno mapana kimetengenzwa kutokana na mbao.

sakafu yake ya kupuria

"kiwanja chake" au " kiwanja mahali ambapo hutenganisha nafaka na makapi"

kukusanya ngano yake katika ghala...kuchoma makapi kwa moto usioweza kuzimika

Hii ni sitiari inayoonesha jinsi Mungu atakavyowatenganisha watu wenye haki na watu waovu. Wenye haki wataenda mbinguni kama ngano katika ghala ya mkulima, na Mungu atawachoma watu ambao ni kama makapi kwa moto ambao hautazimika.

hautaweza kamwe kuzimika

Hii inweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "kamwe hautazimika."

Matthew 3:13

Maelezo yanayounganisha

Hapa mandhari yahamia kwenda wakati wa baadaye wakati Yohana Mbatizaji ambatiza Yesu.

kubatizwa na Yohana

Hii inaweza kueleza katika namna iliyo tendaji. "hivyo Yohana aliweza kumbatiza."

Nina hitaji kubatizwa wewe, nawe waja kwangu?

Yohana anatumia swali kuonesha kushangazwa kwake na ombi la Yesu. "Wewe ni wa maana zaidi kuliko mimi. Sipaswi kukubatiza wewe. Wewe unapaswa kunibatiza mimi."

kwa ajili yetu

Hapa "sisi" humaanisha Yesu na Yohana.

Matthew 3:16

Maelezo yanayounganisha

Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi kuhusu Yohana Mbatizaji na hueleza kilichotokea baada ya kumbatiza Yesu.

Baada ya kubatizwa

Hii inaweza kueleza katika namna iliyo tendaji. "Baadaya Yohana kumbatiza Yesu"

tazama

Neneo "tazama" hapa hututahadharisha sisi kuwa makini kwa habari ya kushtukiza ambayo inafuata.

mbingu zilifunguka kwake

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Yesu aliona mbingu zimefunguka" au "Mungu alizifungua mbingu kwa Yesu."

kushuka chini kama njiwa

Maana zinaweza kuwa 1) haya ni maelezo dhahiri kwamba Roho alikuwa katika umbo la njiwa au 2) huu ni mfanano ambao hulinganisha Roho kushuka chini kuja juu ya Yesu kwa upole, ndivyo njiwa angefanya.

sauti toka ilitoka mbinguni ikisema

"Yesu alisikia sauti kutoka mbinguni." Hapa "sauti" humaanisha Mungu anazungumza. "Mungu alizungumza kutoka mbinguni."

Mwana

Hiki ni cheo cha maana cha Yesu, Mwana wa Mungu


Translation Questions

Matthew 3:1

Yohana mbatiza alihubiri ujumbe gani nyikani?

Yohana alihubiri "Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu".

Unabii wa Isaya ulisema Yohana mbatizaji angelikuja kufanya?

Unabii ulisema kuwa Yohana Mbatizaji angetayarisha njia ya Bwana.

Matthew 3:4

Watu walifanya nini baada ya kuwa wamebatizwa na Yohana?

Walipokwisha kubatizwa, watu walitubu dhambi zao.

Matthew 3:7

Yohana mbatizaji aliwaambia nini Masadukayo na Mafarisayo?

Yohana mbatizaji aliwaambia Masadukayo na Mafarisayo wazae matunda kulingana na toba.

Yohana mbatizaji aliwaonya Masadukayo na Mafarisayo wasifikiri jambo gani miongoni mwao?

Yohana mbatizaji aliwaonya Masadukayo na Mafarisayo wasifikiri miongoni mwao kuwa wanaye Ibrahimu kama baba yao.

Matthew 3:10

Kwa mujibu wa Yohana, hutokea nini kwa kila mti usiozaa matunda mazuri?

Yohana anasema kwamba kila mti usiozaa matunda mazuri hukutwa na kuanguka chini na kutupwa motoni.

Aliyekuwa anakuja baada ya Yohana angebatiza kwa namna gani?

Aliyekuwa anakuja baada ya Yohana angebatiza kwa Roho Mtakatifu na moto.

Matthew 3:13

Yesu alimwambia nini Yohana kichomshawishi ambatize?

Yesu alimwambia kwamba ilikuwa haki kwa Yohana kumbatiza Yesu ili kutimiza haki yote.

Matthew 3:16

Yesu aliona nini alipotoka majini?

Alipotoka majini, Yesu alimwona Roho wa Mungu akishuka kama njiwa na kuwa juu yake.

Sauti kutoka mbinguni ilisema nini baada ya Yesu kubatizwa?

Sauti kutoka mbinguni ilisema, "huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye".


4

1Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.3Mjaribu akaja na akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate.”4Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.’”5Kisha Ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu,6na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, ‘Ataamuru malaika wake waje wakudake,’ na, ‘watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe.’”7Yesu akamwambia, “Tena imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”

8Kisha, Ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote.9Akamwambia, “Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu.”10Kisha Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’”11Kisha Ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.

12Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya.13Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.14Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya,
15“Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa!
16Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.”

17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”

18Alipokuwa akitembea kandokando ya bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.19Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.”20Mara moja waliziacha nyavu zao na kumfuata.

21Na Yesu alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita,22na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.

23Yesu alikuwa akizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri injili ya ufalme, na akiponya kila aina ya maradhi na magonjwa miongoni mwa watu.24Habari zake zilienea Siria yote, na watu wakawaleta kwake wale wote waliokuwa wakiugua, wakiwa na maradhi mbalimbali na maumivu, waliokuwa na mapepo, na wenye kifafa na waliopooza. Yesu aliwaponya.25Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani.


Mathayo 04 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya mistari ya 6, 10, 15 na 16, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ufalme wa mbinguni umekaribia

Wataalam wanajadili ikiwa "ufalme wa mbinguni" ulikuwepo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha changamoto katika kutafsiri. Matoleo mengine hutumia maneno "inakaribia" na "yamekaribia."

"Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu"

Kwa Kiingereza, msomaji anaweza kuelewa kauli hii katika 4:6 kama inayoonyesha kwamba Shetani hajui kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu. Kwa sababu Shetani anajua kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, haipaswi kutafsiriwa kwa njia hii. Inaweza kutafsiriwa kama "kwa sababu wewe ni Mwana wa Mungu." na )

Links:


Matthew 4:1

Taarifa kwa ujula:

Hapa mwandishi anaanza sehemu mpya ya simulizi ambayo Yesu anatumia siku 40 nyikani, mahali ambapo Shetani anamjaribu. Katika mst. 4, Yesu anamkemea Shetani kwa nukuu kutoka Kumbukumbu la Torati.

Yesu aliongozwa na Roho

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Roho alimwongoza Yesu."

kujaribiwa na Ibilisi

Hiiinaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "hivyo Ibilisi aliweza kumjaribu Yesu."

Ibilisi...Mjaribu

Haya yana maanisha kiumbe yuleyule. unaweza kutumia neno lilelile kutafsiri yote mawili.

alikuwa amefunga ...alikuwa na njaa

Haya yanamaanisha Yesu.

siku arobaini mchana na usiku

"Siku 40 mchana na usiku" Hii ina maanisha vipndi vya saa 24. "siku 40."

Kama wewe ni mwana wa Mungu, amuru

Ina wezekana kuwa na maana 1) hili ni jaribu la kufanya miujiza kwa ajili ya manufaa ya Yesu mwenyewe. "Wewe ni mwana wa Mungu, hivyo amuru." Au 2) "Thibitisha kwamba wewe ni Mwana wa Mungu kwa kuamuru." Ni vizuri kuamini kuwa Shetani alijua kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo muhimu kinacho eleza uhusiano kati ya Yesu na Mungu.

Mwana wa Mungu

Hikini cheo cha maana cha Yesu.

amuru mawe haya kuwa mkate

Ungeweza kutafsiri hii na nukuu ya moja kwa moja. "sema kwa mawe haya, Kuwa mkate."'

mkate

"chakula"

imeandikwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Musa aliandika hivi katika maandiko hapo zamani."

Mtu hataishi kwa mkate tu

Hii inamaanisha kuwa kuna kitu ambacho ni cha muhimu zaidi katika maisha kuliko chakula

bali kwa kila neno ambalo hutoka katika kinywa cha Mungu.

Hapa "neno" na "kinywa" humaanisha kwa kile Mungu anasema.

Matthew 4:5

Taarifa za Jumla:

Katika mstari 6, Shetani ananukuu kutoka Zaburi ili kumjaribu Yesu.

Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini

Inaweza kuwa na maana 1) hili ni jaribu kufanya muujiza kwa ajili ya manufaa ya Yesu mwenyewe. "Kwa kuwa Mwana wa Mungu kwa kweli, unaweza kujitupa chini." Au, 2) hii ni changamoto au shtaka. "Thibitisha kuwa wewe kwakweli ni Mwana wa Mungu kwa kujitupa chini" Ni vizuri kuamini kuwa Shetani alijua kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo cha maana ambacho kinaeleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

jitupe chini

"jiachie mwenyewe hadi chini" au ruka kwenda chini"

kwa maana imeandikwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "kwa maana mwimba zaburi aliandika katika maandiko" au " kwa maana inasema katika maandiko."

Ataagiza malaika wake wakutunze

"Mungu atawaagiza malaika wake wakutunze." Hii inaweza kutafsiriwa na nukuuu ya moja kwa moja. "Mungu atasema kwa malaika wake, Mlindeni."'

Watakuinua juu

"Malaika watakushika

Matthew 4:7

Taarifa kwa ujumla:

Katika mstari wa 7, Yesu amemkemea Shetani na nukuu nyingine kutoka Kumbu kumbu

Tena imeandikwa

Imefahamika kuwa Yesu anamaanisha ana nukuu maandiko tena. Hii inaweza kuelezwa katika namna iliyo tendaji. "Tena, nitawaambia Musa alichoandika katika maandiko."

Usimjaribu

Hapa "usi" inamaanisha yeyote. "Mtu hapaswi kumjaribu" au "Hapana mtu anapaswa kumjaribu."

Tena, Ibilisi

"Baada ya hapo, Ibilisi"

Alimwambia

"Ibilisi alimwambia Yesu"

Vitu vyote hivi nitakupa

"Nitakupa vitu vyote hivi." Mjaribu anasisitiza kuwa atampa "vitu vyote," si tu baadhi yake.

Matthew 4:10

Maelezo yanayounganisha:

Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi kuhusu jinsi Shetani alivyo mjaribu Yesu

Taarifa kwa ujumla

Katika mstari su10, Yesu anamkemea ShetanTi na nukuu nyingine kutoka Kumbukumbu la Torati.

Kwa maana imeandikwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna yamuundo tendaji. "Musa pia aliandika katika maandiko."

Yakupasa

Hapa "yakupasa" inamaanisha yeyote.

Tazama

Neno "tazama" hapa lina tutahadharisha kuwa makini kwenye habari mpya muhimu ambazo zinafuata.

Matthew 4:12

Taarifa kwa ujumla:

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi ambayo katika hiyo mwandishi anaeleza mwanzo wa huduma ya Yesu Galilya. Mistari hii inaeleza jinsi Yesu alivyokuja Galilaya

Sasa

Neno hili lintumika hapa kuweka alama ya kuanzisha mtiririko wa habari kuu wa simulizi. Hapa Mathayo anaanza kutuambia sehemu mpya ya simulizi.

Yohana alikuwa amekamatwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya muundo tendaji. "mfalme alikuwa amemkamata Yohana."

Katika majimbo ya Zabuloni na Naftali

Haya ni majina ya makabila ambayo yaliishi katika maeneo haya kabla ya wageni kudhibiti nchi ya Israeli miaka mingi kabla.

Matthew 4:14

Taarifa kwa ujumla:

Katika mstari wa 15 na 16, mwandishi anamnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba huduma ya Yesu Galilaya ilikuwa ni kutimizwa kwa unabii.

Hii ilitokea

Hii inamaanisha Yesu kwenda kuishi Kaperenaumu.

kilichonenwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya muundo tendaji. "kile Mungu alichonena"

Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali...Galilaya ya Wamataifa.

Majimbo haya yote yanaeleza eneo lilelile. Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi timilifu. "Katika jimbo la Zabuloni na Naftali...katika jimbo hilo huishi Wamataifa wengi."

kuelekea bahari

Hii ni bahari ya Galilaya.

Watu waliokaa katika giza wameona mwanga mkuu

Hapa "giza" humaanisha maisha ya gizani au dhambi ambayo huwatenga watu na Mungu. Na "mwanga" humaanisha ujumbe wa kweli wa Mungu ambao huwaokoa watu kutoka katika dhambi yao. Hii ni taswira ya watu ambao hawa kuwa na tumaini sasa wana tumaini kutoka kwa Mungu.

kwa hao ambao walikaa katika eneo na kivuli cha kifo, juu yao mwanga umewazukia

Kimsingi hii ina maana ileile kama sehemu ya kwanza ya sentensi. Hapa "eneo" na kivuli cha kifo" humaanisha kifo cha kiroho au kutengana na Mungu.

Matthew 4:17

Tubuni, kwa kuwa ufalme wa mbinguni umekaribia

Sentensi "ufalme wa mbinguni" humaanisha utawala ambao Mungu ndiye mfalme. Sentensi hii imetumika katika injili ya Mathayo tu. Kama inawezekana tumia neno "Mbinguni" katika tafsiri yako. "Si muda mrefu Baba yetu aliye mbinguni atajidhirisha kuwa ni mfalme" Angalia jinsi ilivyotafsiriwa katika Mat. 3:1

Matthew 4:18

Taarifa za jumla:

Hii huanza mandhari mpya katika sehemu ya simulizi kuhusu huduma ya Yesu kule Galilaya. Hapa huanza kwa kuwakusanya watu kuwa wanafunzi wake.

Kutupa nyavu baharini

"Kutupa nyavu majini ili kuvua samaki"

Nifuateni

"Yesu anawakaribisha Simoni na Andrea kumfuata, kuishi naye, na kuwa wanafunzi wake. ""Iweni wanafunzi wangu."

Nitawafanya wavuvi wa watu

Hii sitiari humaanisha Simoni na Andrea watawafundisha watu ujumbe wa kweli wa Mungu hivyo wengine pia waanze kumfuata Yesu. "Nitawafundisha kuwaleta watu kwangu kama mlivyo kuwa mnavua samaki"

Matthew 4:21

Sentensi unganishi

Yesu anawaita watu zaidi kuwa wanafunzi wake.

Aliwaita

"Yesu aliwaita Yohana na Yakobo." Kirai hiki pia humaanisha kwamba aliwakaribisha kumfuata, kuishi naye, na kuwa wanafunzi wake.

maramoja

"wakati huo huo"

waliuacha mtumbwi...na walimfuata

Inapaswa kuwa wazi kwamba haya ni mabadiliko ya maisha. Watu hawa hawaendi tena kuwa wavuvi na wanaacha shughuli za familia zao kumfuata Yesu kwa maisha yao waliyo nayo.

Matthew 4:23

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi kuhusu mwanzo wa huduma ya Yesu Galilaya. Mistari hii ni muhtasari wa kile alichofanya na jinsi watu walivyoitikia.

kufundisha katika masinagogi yao

"kufundisha katika masinagogi ya Wagalilaya" au kufundisha katika masinagogi ya watu wale"

kuhubiri injili ya ufalme

Hapa "ufalme" humaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. "kuhubiri habari njema kuhusu jinsi Mungu atakavyojifunua mwenyewe kama mfalme."

"aina zote za maradhi na aina zote za magonjwa"

"kila maradhi na kila ugonjwa." Maneno "maradhi" na :magonjwa" yanakaribia sana lakini yanapaswa kutafsiriwa kama maneno mawili tofauti kama inawezekana. "Maradhi ni kile kinacho sababisha mtu kuwa mgonjwa. "Ugonjwa ni udhifu wa mwili au maumivu ambayo ni matokeo ya kuwa na maradhi.

wale waliopagawa na pepo

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya mfumo tendaji. "walio na pepo" au "wale ambao wanatawaliwa na pepo."

wenye kifafa

"wale waliokuwa na kifafa" au wale walio na maradhi ambayo yalisababisha kuzirai."

waliopooza

"wale ambao hawakuweza kutembea"

Dekapoli

Jina hili humaanisha "Miji Kumi."


Translation Questions

Matthew 4:1

Nani alimwongoza Yesu kwenda nyikani kujaribiwa na mwovu?

Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu kwenda nyikani kujaribiwa na mwovu.

Yesu alifunga kwa muda gani huko nyikani?

Yesu alifunga siku arobaini mchana na usiku huko nyikani.

Jaribu gani la kwanza alilotoa mwovu kwa Yesu?

Mwovu alimjaribu Yesu kugeuza jiwe liwe mkate.

Jibu la Yesu lilikuwaje katika jaribu la kwanza?

Yesu alisema kwamba mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.

Matthew 4:5

Ni jaribu gani la pili ambalo mwovu alilitoa kwa Yesu?

Mwovu alimjaribu Yesu kujitupa mwenyewe chini kutoka kwenye hekalu.

Ni jaribu gani la pili ambalo mwovu alilitoa kwa Yesu?

Mwovu alimjaribu Yesu kujitupa mwenyewe chini kutoka kwenye hekalu.

Matthew 4:7

Jibu la Yesu lilikuwa nini kwa jaribu la pili?

Yesu alisema kwamba usimjaribu Bwana Mungu wako.

Jaribu gani la tatu alilotoa mwovu kwa Yesu?

Mwovu alimjaribu Yesu kumwabudu ili ampe falme zote za ulimwengu.

Matthew 4:10

Jibu la Yesu lilikuwa nini kwa jaribu la tatu?

Yesu alisema kwamba yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake.

Matthew 4:14

Jambo gani lilitizwa Yesu alipokwenda Kaperanaumu ya Galilaya?

Unabii wa Isaya ulitimizwa ambao uliosema kwmba watu wa Galilaya wangeona mwanga mkuu.

Matthew 4:17

Ni ujumbe gani hivyo Yesu alianza kuhubiri?

Yesu alihubiri, "tubuni, kwa kuwa ufalme wa mbinguni umekaribia."

Matthew 4:18

Petro na Andrea waliishi kwa njia gani?

Petro na Andrea walikuwa wavuvi.

Yesu aliwaambia Petro na Andrea atawafanya kuwa nani?

Yesu aliwaambia Petro na Andrea atawafanya kuwa wavuvi wa watu.

Matthew 4:21

Yakobo na Yohana waliishi kwa namna gani?

Yakobo na Yohana walikuwa wavuvi.

Matthew 4:23

Kwa wakati huu Yesu alienda wapi kufundisha?

Yesu alifundisha katika masinagogi ya Galilaya.

Watu gani waliletwa kwa kwa Yesu na Yesu aliwafanyia nini?

Wote waliokuwa wagonjwa na kupagawa na mapepo waliletwa kwa Yesu na Yesu aliwaponya.

Watu wangapi walikuwa wanafuatana na Yesu kwa kipindi hiki?

Umati makubwa ulikuwa ulikuwa ukimfuata Yesu kwa wakati huu.


5

1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,

3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5Heri wenye upole, maana watairithi nchi.
6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.
7Heri wenye rehema maana hao watapata rehema.
8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.
9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.
12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

13Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.14Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.15Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.16Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.

17Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza.18Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.19Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.20Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

21Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, ‘Usiue’ na ‘Yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.’22Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, ‘Wewe ni mtu usiyefaa!’ atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, ‘Wewe mjinga!’ atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.23Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako,24iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.25Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.26Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.

27Mmesikia imenenwa kuwa, ‘Usizini.’28Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.29Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.30Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa Jehanamu.

31Imenenwa pia, ‘Yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.’32Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.

33Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, ‘Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.’34Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu;35wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Yerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.

36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.37Bali maneno yenu yawe, ‘Ndiyo, ndiyo, hapana, hapana.’ Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

38Mmesikia imenenwa kuwa, ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.’39Lakini mimi namwambia, msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.40Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia.41Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.42Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.

43Mmesikia imenenwa, ‘Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.’44Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.46Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?47Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je, watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?48Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Mathayo 05 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Mathayo 5-7, ambayo huitwa "Mahubiri ya Mlimani," ni funzo moja ndefu ya Yesu. Mgawanyiko wa sura husababisha kuchanganyikiwa hapa. Kichwa kinaweza kumsaidia msomaji kuelewa kwamba sura hizi zinaunda sehemu moja au kitengo. Mtafsiri anapaswa kufahamu kuwa kuna swali fulani kuhusu ikiwa mafundisho yanahusu Israeli, kanisa, au ufalme wa Mungu wa baadaye.

5:3-10, inayojulikana kama Heri au Baraka, imewekwa kwa kutumia uingizaji, na kila mstari unaanza na neno "heri." Uingizaji huu unaashiria fomu ya ushairi wa mafundisho haya.

Dhana maalum katika sura hii

"Wanafunzi wake"

Inawezekana kutaja mtu yeyote aliyemfuata Yesu kama mfuasi au mwanafunzi. Yesu aliwachagua wafuasi wake kumi na wawili kuwa watu wake wa ndani, wale wanafunzi kumi na wawili. Baadaye walijulikana kama mitume. Inaweza kuwa na maana kwamba mafundisho haya yalikuwa kwa mitume hao kumi na wawili.

Links:


Matthew 5:1

Sentensi unganishi

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi ambayo Yesu alianza kuwafundisha wanafunzi wake. Sehemu hii huendelea hadi mwisho wa sura ya 7 na mara kwa mara huitwa mahubiri ya Mlimani.

Maelezo ya jumla

Katika msyari wa 3, Yesu anaanza kueleza tabia za watu ambao wamebarikiwa.

Akafunua kinywa chake

"Yesu alianza kunena."

aliwafundisha

Neno "aliwa" humaanisha wanafunzi wake.

maskini katika roho

Hii inamaanisha mtu ambaye ni mnyenyekevu. "wale ambao wanajua wanamhitaji Mungu."

Kwa kuwa uflmeme wa mbinguni ni wao

Hapa "ufalme wa mbinguni" humaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. Kirai hiki kiko katika kitabu cha Mathayo tu. Kama inawezekana weka "mbinguni" katika tafsiri yako. "kwa kuwa Mungu wa mbinguni atakuwa mfalme wao."

wale ambao wana huzunika

Sababu zinazopelekea kuwa wenye huzuni ni 1) hali ya dhambi ya ulimwengu au 2) dhambi zao au 3) kifo cha mtu. Usieleze bayana sababu ya kuhuzunika isipkuwa lugha yako inataka hivyo.

watafarijiwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya mfumo tendaji. "Mungu atawafariji."

Matthew 5:5

wanyenyekevu

"wapole" au "wale ambao hawategemei uwezo wao wenyewe"

watarithi nchi

"Mungu atawapa nchi yote."

wenye njaa na kiu ya haki

Sitiari hii humaanisha mtu anapaswa kwa uhodari kufanya kilicho sahihi. "kutamani kuishi kwa unyofu kama ilivyo kutamani chakula na kinywaji.

watashibishwa

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya mfumo tendaji. "Mungu atawashibisha" au "Mungu atawatosheleza."

walio safi wa moyo

"watu ambao mioyo yao ni safi." Hapa "safi" hurejelea kwa kutamani kwa mtu. wale ambao tu wanataka kumtumikia Mungu."

watamwona Mungu

Hapa "kuona" inamaanistha wataweza kuishi katika uwepo wa Mungu." "Mungu atawaruhusu kuishi naye."

Matthew 5:9

wapatanishi

Hawa ni watu ambao husaidia wengine kuwa na amani na wengine miongoni mwao.

kwa kuwa wataitwa wana wa Mungu

Hii inaweza kuelezwa katika namna ya muundo tendaji. "kwa kuwa Mungu atawaita watoto wake" au "watakuwa watoto wa Mungu.

wana wa Mungu

Ni vizuri kutafsiri "wana" kwa neno lile lile lugha yako kwa kawaida ungelitumia kurujelea kwa mwana au mtoto wa binadamu

wale ambao wameteswa

Hii inaweza kuelezwa katika namna muundo tendaji. "watu wale ambao wengine huwatendea kwa isivyo haki"

kwa ajili ya haki

"kwa sababu wanafanya kile ambacho Mungu hutaka wafanye"

ufalme wa mbinguni ni wao

angalia jinsi ulivyotafsiri katika Mat. 5:1

Matthew 5:11

Sentensi unganishi

Yesu anamaliza kueleza tabia za watu ambao wamebarikiwa.

Mliobarikiwa

Neno "ninyi" ni wingi.

kusema kila aina ya mambo maovu dhidi yenu kwa uongo.

"watasema kila aina ubaya dhidi yenu" au "watasema mambo mabaya juu yenu ambayo si ya kweli"

kwa ajili yangu

"kwa sababu mwanifuata mimi" au "kwa sababu mwaniamini"

Furahini na kushangilia

"Furahini" na "kushangilia" humaanisha karibu kitu kile kile. Yesu alitaka wasikilizaji wake sio tu kufurahi bali hata kufanya zaidi kuliko kufurahi kama inawezekana.

Matthew 5:13

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kufundisha juu ya jinsi wanafunzi wake walivyo kama chumvi na nuru.

Ninyi ni chumvi ya dunia

Inawezekana kumaanisha 1) kama vile chumvi inavyokifanya chakula kuwa kizuri, mwanafunzi wa Yesu yampasa kuwaathiri watu wa ulimwengu ili kwamba wawe wazuri au 2) kama vile chumvi iwezavyo kutumika kwa kutunza chakula, kadhalika wanafunzi wa Yesu wawalinde watu wasiharibike

Matthew 5:15

Pia watu hawawashi taa

"Watu hawawashi taa"

nakuiweka chini ya kikapu

"kuiweka taa chini ya kikapu." Hii ni kusema kuwa ni ujinga kutengeneza nwanga kwa lengo la kuufunika ili watu wasiuone mwanga wa taa.

Nuru yenu na ionekane mbele ya watu

Hii inamaanisha kuwa wanafunzi wa Yesu wanapaswa kuishi maisha ambayo yatawafnya wengine wajifunze kuhusu ukweli wa Mungu. "Maisha yenu yawe kama nuru iangazayo mbele ya watu.

Baba yenu aliye mbinguni

Ni vizuri zaidi ikitafsiriwa "Baba" kwa maana ya maneno sawa na yale yanayotumika kumaanisha baba wa katika mwili huu.

Matthew 5:17

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kwa kufundisha jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya agano la kale

manabii

Hii inamaanisha kile walichoandika manabii katika maandiko.

kweli nawaambieni

"Nawaambia ukweli" Kirai hiki kinaongeza nguvu juu ya kile Yesu atakachosema baadaye.

mpaka mbingu na dunia zote zipite

Hapa "mbingu" na "dunia" humaanisha ulimwengu wote. "Kama vile mbingu zidumuvyo"

hapana yodi moja wala nukta moja

"hapana hata ile herufi ndogo iliyoandikwa au sehemu ndogo ya herufi. Hii ni sitiari inayomaanisha kitu fulani katika maandiko kinachoweza kuonekana kuwa si cha muhimu. "wala sheria zinazoonekana kuwa si za muhimu

kila kitu kitakapokuwa kimetimizwa

Hiki kinaweza kuelezwa kwa kutumia mfumo tendaji. "Mambo yote yametokea" au "Mungu huyafanya mambo yote yatimie".

kila kitu

Kirai cha "kila kitu" kinamaanisha kila kitu kilicho kwenye sheria. "kila kitu kilicho kwenye sheria" au " kila kilichoandikwa kwenye sheria".

Matthew 5:19

yeyote avunjaye

"yeyote asiyetii" au "yeyote apuuziaye"

amri ndogo mojawapo ya amri hizi

"yeyote kati ya amri hizi, hata zile ndogo kabisa"

ataitwa

Hii inaweza kuelezeka kwa muunda tendaji. "Mungu atamwita mtu huyo" au "Mungu atawaita watu hao".

mdogo katika ufalme wa mbinguni

Kirai hiki kimetumika katika injili ya Mathayo tu. Kama inawezekana tumia "mbingu" katika tafsiri yako. "asiye na umuhimu kabisa kwenye ufalme wa Mungu" au "asiye na umuhimu katika utawala wa Mungu wetu wa mbingunij".

azishikaye na kuzifundisha

"anayetii amri zote hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo hivyo"

mkubwa

"wa muhimu zaidi"

Kwa maana nawaambia

Hiki kinaongeza msisitizo kwa kile ambacho Yesu atasema baadaye.

nawa ... yenu ... hamta..

hivi ni viwakilishi vya wingi

haki yenu isipozidi haki ya waandishi n a mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia kataika ufalme wa mbinguni

Hii inaweza kuelezeka kwa muundo hai. "kwamba haki yenu lazima izidi... ili kuingia"

Matthew 5:21

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha jinsi alivyokuja kutimiliza sheria za agano la kale. Hapa anaanza kufundisha juu ya kuua na hasira

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia kikundi cha watu juu ya kile ambacho kinaweza kutokea kwao kama watu binafsi. Neno "mme" katika sentensi "mmesikia" na "nawaambia" ni maneno ya wingi. Ile amri ya "usiue"ni ya umoja, lakini unahitaji kuitafsiri katika wingi.

ilinenwa zamani

Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji. "Mungu alisema na mababu zetu zamani za kale".

auaye yuko katika hatari ya hukumu

Hapa "hukumu" inamaanisha kuwa hakimu ndiye atakayemhukumu mtu kufa. "Hakimu atamhukumu yeyote amuuaye mtu mwingine"

kuua ... auaye

Neno hili linamaanisha kitendo cha mauji ya kudhamiria, na wala siyo kila aina ya mauji

Lakini nawambia

Kiwakilishi "na" kinatia msisitizo. Hii inamaanisha kuwa kile anachosema Yesu kina umuhimu sawa na amri itokayo kwa Mungu. Jaribu kutafsiri hili kataka mazingira yanayonesha msisitizo.

ndugu

Neno hili linamaanisha muumini mwenzetu

atakuwa katika hatari ya hukumu

Inaovyoonekana hapa Yesu hamaanishi hakimu wa kibinadamu bali Mungu anamhukumu mtu mwenye hasira kwa ndugu yake.

mtu usiyefaa ... mjinga

Hii ni mizaha kwa watu wasioweza kufifkiri kwa usahihi. "Mtu asiyefaa" ni sawa na "mtu asiye na akili," ambapo "mjinga" inaongezea wazo la kutokuwa mwaminifu kwa Mungu.

baraza

Yawezekana hili ni baraza dogo, siyo lile kuu.

Matthew 5:23

una

Yesu anawaambia kundi la watu juu ya kile kinachoweza kutokea kwao kibinafsi. matukio yote yanayohusiana na viwakilishi "una" na "yako" yametumika katika hali ya umoja, lakini lugha yako inaweza kukutaka utafsiri katika wingi

unatoa sadaka yako

"kutoa sadaka yako" au "kuleta sadaka yako"

katika madhabahu

Hii inamaanisha kuwa ni madhabahu ya Mungu iliyo hekaluni kule Yerusalemu, " madhabahuni pa Mungu hekaluni".

na unakumbuka kuwa

"na ukumbuke ukiwa umesimama madhabahuni"

ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako

"mtu mwingine ana hasira na wewe kwa sababu ya kile ulichomfanyia"

kapatane kwanza na ndugu yako

Hili linaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "jambo la kwanza ni kutafuta suluhu"

Matthew 5:25

Patana na... wako

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea katika hali ya mtu mmoja. Matukioyote ya viwakilishi vya "uki" na "wako" viko katika umoja, lakini lugha yako inaweza kukutaka uvitafsiri katika wingi.

mshitaki wako

Huyu ni mtu anayemtuhumu mtu kwa kufanya jambo fulani ambalo ni ovu. Anampeleka mtuhumiwa mahakamani ili kumshitaki kwa hakimu.

kukuacha mikononi mwa hakimu

Hapa neno "kukuacha mikononi mwa" inamaanisha kukukabidhi katika udhibiti wa mtu mwingine. "kumwachia hakimu ashughulike na wewe".

hakimu akuache mikononi mwa askari

Hapa neno "kukuacha mikononi mwa" inamaanisha kukukabidhi katika udhibiti wa mtu mwingine. "hakimu atamkabidhi kwa askari"

askari

ni mtu mwenye mamlaka ya kufanya maamuzi ya hakimu.

nawe utatupwa gerezani

Hili linaelezeka katika hali ya muundo tendaji. "na askari anaweza kukutupa gerezani"

amini nawambieni

"Nawaambieni ukweli." Hiki kirai kinaongeza msisitizo kwa kile ambacho Yesu alisema baadaye.

hutawekwa huru

"kutoka gerezani"

Matthew 5:27

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha juu ya jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la Kale. Na hapa anaongelea uzinzi na kutamani mwanamke.

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea katika maisha ya mtu binafsi. Neno "mme..." kutokana na "mmesikia" na "nawaambieni" yametumika katika wingi. Amri ya "Usizini" imetumika katika umoja "usi," lakini unaweza kuitafsiri katika wingi "msi".

imenenwa kuwa

Hii inaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "kuwa Mungu alisema".

fanya (uzinzi)

Hili neno ni kitenzi kikuu cha kufanya jambo fulani

Lakini nawaambieni

Neno "nawa" ni msisitizo. Hii inamaanisha kuwa kile ambacho Yesu anasema kina umhimu sawa na kile kilicho kwenye amri kuu kotoka kwa Mungu. Tafsiri kirai hiki katika namna ambayo inaonesha msisitizo huo. Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:21

yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

Sitiari hii inamaanisha kuwa mwanamume amtamaniye mwanamke anahatia sawa na mwanamume aliyefanya uzinzi halisi.

amtazamaye mwanamke kwa kumtamani

"na kumtamani mwanamke" au "na kutamani kulala naye"

moyoni mwake

Hapa "moyo" inamaanisha fikra za mtu. "akilini mwake" au "Katika fikra zake"

Matthew 5:29

Na kama ... lako

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye kwa mtu binafsi Matukio yote ya viwakilishi vya "ku" na "lako" viko katika umoja, lakini unaweza kuvitafsiri katika wingi.

kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa

Hapa "jicho" linamaanisha kile ambacho mtu hukiona. Na "kujikwaa". Ni sitiari ya "dhambi." "Kama kile ukionacho hukusababisha kujikwaa" au "kama unataka kufanya dhambi kwa sababu ya kile ukionacho"

jicho lako la kulia ... mkono wako wa kuume

Hii inamaanisha jicho au mkono ule wa muhimu zaidi, dhidi ya mkono au jicho la kushoto. Hapa unaweza kutafsri "kulia" kuwa "ndiyo nzuri zaidi" au "kulia pekee."

ling'oe

"litoe kwa nguvu" au "liharibu" kama jicho lako la kulia halijatajwa rasmi, unaweza kuitafsiri hii kama " kuharibu macho yako." kama macho yametajwa, unaweza kuyatafsiri kama "yaharibu"

ling'oe ... likate

Yesu analikuza zaidi jambo hili juu ya jinsi ambavyo mtu anapaswa kuiona jinsi dhambi ilivyo mbaya kulichukulia kwa umakini swala hili.

uutuplie mbali na wewe

"achana nao"

kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike

"upoteze sehemu ya mwili wako"

kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu

Hili linaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "kuliko Mungu kuutupa mwili wako wote jehanamu"

kama mkono wako wa kuume unakusababisha

katika hii lugha ya umbo, mkono unasimama badala ya matendo la mwili wote

Matthew 5:31

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha juu ya jinsi alivyokuja kutimiliza sheria za Agano la kale. Hapa anaanza kwa kufundisha juu ya talaka

Imenenwa pia

Mungu ndiye "alisema." anatumia mfumo tendewa ili kuifanya kuwa laini kuwa si Mungu au neno la Mungu ambalo hakubaliani nalo. Badala yake anasema kuwa talaka inawezekana pale tu sababu ni ya kweli. talaka inaweza isikubalike hata kama mwanamume atatii kuandika hati ya talaka,

amfukuzaye mkewe

hii ni tafisida ya talaka

na ampe

"lazima ampatie"

lakini mimi nawaambia

Kiwakilishi "mimi" ni cha msisitizo. Hiki kinamaanisha kuwa anachosema Yesu kina umuhimu sawa na amri kuu kutoka kwa Mungu. Jaribu kutafsiri kirai hiki katika namna inayoonesha msisitizo. Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:21.

Amfanya kuwa mzinzi

Ni mwanamume anayemtaliki mwanamke bila utaratibu humsababisha kufanya uzinzi" Katika tamadunii nyingi ni kawaida kwake kuolewa tena, lakini kama talaka hiyo haiko sahihi, basi hiyo ndoa ya pili ni batili.

baada ya kupewa talaka

Hii inaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "yeye mwanamke baada ya kutalikiwa na mumewe" au "mwanamke aliyetalikiwa"

Matthew 5:33

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha juu ya jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la kale. Na hapa anaanza kuongelea juu ya kuapa viapo

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha ya mtu binafsi. Kiwakilishi "mme" kutokana na "mmesikia" na "nawaambia" viko kataka wingi. na kiwakilishi cha "msi" katika " msiape" na " ni" katika " pelekeni" navyo pia viko katika wingi

Tena, mme

"Pia, mme" au "huu ni mfano mwingine. wa kiwakilishi "mme."

mmesikis ilinenwa kwamba ... kwa uongo

Yesu anaweka bayana kuwa anakubaliana na Mungu na neno lake. Lakini, anawaambia wasikilizaji wake wasitimie vile amabvyo si vyao il ikuwashawishi watu kuamini maneno yao. "viongozi wenu wa dini wamewaambieni kuwa Mungu alisema ... viapo vya uongo.

Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu

Hi inaweza kumaanisha mambo yafuatayo 1)usiape kwa Mungu kuwa utafanya jambo fulani na usilifanye au 2) Usiape kwa jina la Bwana kuwa unajua kitu fulani kuwa ni kwe ili hali unajua kuwa si kweli.

Lakini nawaambia

Kiwaakilishi "na" ni cha msisitizo. Hii inamaanisha kuwa anachosema Yesu kina umuhimu sawa na kile kilicho kwenye amri kuu kutoka kwa Mungu. Kirai hiki kitafsriwe katika namna inayoonesha msisitizo. Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:21

msiape hata kidogo ... ni mji wa mfalme mkuu

Hapa Yesu anamaanisha kuwa mtu asiape katika jambo lolote. inaonekana kuwa kuna mtu aliyekuwa akifundisha kwamba kuapa haina madhara kama mtu ataapa kwa kitu kingine na asikijali kiapo chake kama hakuapa kwa Mungu. ,kama vile kuapa kwa mbingu, dunia, au Yerusalemu. Yesu anasema hata kiapo cha hivyo ni kibaya kwa sababu vyote ni mali ya Mungu.

msiape hata kidogo

Kama lugha yako ina muundo wa wingi katika agizo inaweza kutumika hapa. "hamtaapa kwa kwa kiapo cha uongo" waruhusu watu watoe viapo lakini wazuieni viapo vya uongo. "msiape hata kidogo" hii inazuia viapo vya uongo.

kwa sababu ni enzi ya Mungu

Hapa neno "enzi" linamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. "linatokana chanzo hiki kwamba Mungu ni mtawala.

maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia miguu yake

Kirai hiki kinamaanisha kuwa dunia ni mali ya Mungu. "ni kama mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia miguu yake"

maana ni mji wa mfalme mkuu

"kwa maana ni mji unaomilikiwa na Mungu

Matthew 5:36

chako ... hu

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. Matukio yote ya viwakilishi hivi viko katika umoja, lakini inakupass kuvitafsiri kama wingi.

kuapa

Hii inamaanisha kuapa. Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:23

Bali maneno yenu yawe 'ndiyo, ndiyo,' au 'hapana. hapana'

kama unamaanisha 'ndiyo.' sema 'ndiyo,' na kama unamaanisha ;hapana,' sema 'hapana,'

Matthew 5:38

sentnsi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la kale. Anaanza kwa kuongelea juu ya kisasi kwa maadui

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha ya mtu kibinafsi. Kiwakilishi cha "mme" katika "mmesikia" na "mimi nawaambia" viko katika wingi. Kirai hiki "mtu akikupiga" kimesemwa katika umoja "akiku...," lakini unaweza kukitafsiri katika wingi "akiwa..."

mmesikia imenenwa kuwa

Yesu anakubaliana na Mungu na neno lake. Lakini hakubaliani na jinsi viongozi wa dini walivyolitumia neno la Mungu. "Viongozi wenu wa dini wamewambieni kuwa Mungu alisema." Tazama ilivyotafsiriwa katika 5:33

jicho kwa jicho na jino kwa jino

Sheria ya Musa ilimruhusu mtu kumwumiza kwa njia ileile kama alivyomwumiza, lakini hakumwumiza zaidiya kiasi kile

Lakini mimi nawaambia

Kiwakilishi cha "mimi" kinaongeza msisitizo. Hii inamaanisha kuwa alichosema Yesu kina umuhimu sawa na ule ulio kwenye amri kuu kuto kwa Mungu. Jaribu kutafsiri kirai hiki katika namna ambayo italeta msisitizo. Tazama ilivyotafsiriwa 5:21.

mtu mwovu

"ni mtu mwovu" au "mtu yeyote aliyewahi kukuumiza"

akikupiga shavu la kulia

Kumpiga mtu upande mmoja wa uso kilikuwa kitendo cha fedheha katika utamaduni wa Yesu. Kama ilivyo katika jicho na mkono, shavu la kulia ni la muhimu, kwa hiyo kukupiga shavu la kulia ilikuwa fedhaha kubwa mno.

akikupiga

"kuzabua," hii inammanisha kupiga kumpiga mtu kofi kwa ubapa wa mkono,

mgeuzie na jingine tena

"mwache akupige na shavu jingine pia"

Matthew 5:40

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha ya watu binafsi. Viwakilishi vyote vya "wewe" na "yako" viko katika umoja kama vile amari za "mwachie," "nenda," "mpatie," na "usimwepuke," lakini waweza kuzitafsiri katika wingi.

kanzu ...joho

Hii "kanzu" ilivaliwa karibu na mwili, kama shati zito au sweta. "kanzu," hili lilikuwa la thamani zaidi kati ya haya mavazi mawili, ilivaliwa juu ya kanzu kwa ajili ya koongeza joto na pia lilitumika usiku kama blanketi.

mwachie na

"mpatie pia huyo mtu"

na yeyote

"na kama mtu," hii inamaanisha kuwa huyu ni askari wa Kirumi.

maili moja

Hizi na sawa na hatua elfu moja ambao ndiyo umbali ambao askari wa kirumi angeweza kumlazimisha kisheria mtu kubeba kitu kwa ajili yake. Kama maili moja haieleweki, basi inaweza kutafsiriwa kama "kilometa moja" au "umbali mrefu."

nenda naye

Hii inamhusu yule akulazimishaye kwenda.

nenda naye maili mbili

"uende ile maili anayokulazimisha kwenda, halafu nenda maili nyingine. kama "maili" haieleweki tumia kilometa mbili" au "mara mbili ya mwendo."

na usimwepuke yeyote

"usikatae kumpatia."hii inaweza kuelezeka kwa kutumia muundo halisi. "na umpatie"

Matthew 5:43

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la Kale. Hapa anaanza kufundisha juu ya kuwapenda maadui.

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kianachoweza kutokea kwao katika maisha yao kibinafsi. "Utampenda ... na kumchukia adui yako" maneno haya yametumika katika hali ya umoja, lakini unaweza kuyatafsiri katika wingi. Matukio mengine ya viwakilishi vya "u" na vile vya amri ya "umpende" na "omba viko katika wingi.

Mmesikia imenenwa

Yesu anakubaliana na Mungu na neno lake. Lakini hakubaliani na jinsi viongozi wa dini wanvyolitumia neno la Mungu. Hili linaweza kuelezeka katika muundo tendaji. "viongozi wenu wa dini wamewaambia kwamba Mungu alisema" Tazama ilivyotafsiriwa 5:33

jirani

Neno "jirani" hapa linamaanisha mtu ndani ya jamii ile ile au watu wa kundi moja ambao mtu hutamani na anapaswa kumtendea kwa upole. Haimaanishi mtu anayeishi karibu. Unaweza kutafsiri katika wingi.

Lakini nawaambia

Kiwakilishi "na.." kinatia msisitizo. Hii inaonesha kuwa kile anachokisema Yesu kina Uzito sawa na kile kilicho kwenye amri kuu ya Mungu.Jaribu kutafsiri kirai hiki kwa kutia msisitizo. Tazama ilivyotafsirwa katika 5:21

muwe watoto wa baba yenu

Ni vizuri kutafsiri "wana" katika lugha ambayo kwa asili hutumika kumaanisha baba wa watoto wa kimwili.

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu

Matthew 5:46

Sentensi unganishi

Yesu anamaliza kufundisha juu ya jinsi alivyokuja kuitimiliza sheria ya Agano la kale. Kipengere hiki kinaanzia 5:17

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao kibinafsi. Matukio yote ya viwakilishi vya "mki.." na "zenu" viko katika wingi. Maswali katika mistari hii ni yale usemaji ambao pengine si lazima kujibiwa

mkiwasalimia

Hili ni neno la jumla kwa ajili ya kuwatamanisha wasikilizaji.

Baba

Hiki ni cheo cha muhimu cha Mungu


Translation Questions

Matthew 5:1

Kwa nini walio masikini wa roho wamebarikiwa?

Walio masikini wa roho wamebarikiwa kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wao.

Kwa nini wanohuzunika sasa wamebarikiwa?

Wale ambao wanahuzunika wamebarikiwa kwa sababu watafarijiwa.

Matthew 5:5

Kwa nini wanyenyekevu wamebarikiwa?

Wanyenyekevu wamebarikiwa kwa sababu watarithi nchi.

kwa nini wenye kiu na njaa ya haki wamebarikiwa?

Wenye kiu na njaa ya haki wamebarikiwa kwa sababu watashibishwa.

Matthew 5:11

Kwa nini wale ambao wanatukanwa na kuteswa kwa ajili ya Yesu wamebarikiwa?

Wale ambao wanatukanwa na kuteswa kwa ajili ya Yesu wamebarikiwa kwa sababu thawabu yao mbinguni ni kubwa.

Matthew 5:15

Nuru ya waumini huangazaje mbele ya watu?

Nuru ya waumini huangaza mbele ya watu kwa kufanya matendo mema.

Matthew 5:17

Yesu alikuja kufanya nini na sheria na manabii wa Agano la Kale?

Yesu alikuja kutimiza sheria na manabii wa Agano la Kale.

Matthew 5:19

Nani ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni?

Wale ambao wazishikao amri na kuzifundisha kwa wengine wataitwa wakubwa katika ufalme wa mbinguni.

Matthew 5:21

Yesu alifundisha kwamba si tu wale ambao wanaua wako katika hatari ya hukumu, bali pia ambao hufanya nini?

Yesu alifundisha kwamba si tu wale ambao wanaua, bali pia wale wanaowachukia ndugu zao wako katika hatari ya hukumu.

Matthew 5:23

Yesu alifundisha tunapaswa kufanya nini kama ndugu yetu ana jambo lolote dhidi yetu?

Yesu alifundisha kwamba tunapaswa kumwendea na kupatanishwa na ndugu yetu kama ana jambo lolote dhidi yetu.

Matthew 5:25

Yesu alifundisha tunapaswa kufanya nini na mshtaki wetu kabla ya kufika mahakamani?

Yesu alifundisha kwamba tunapaswa kukubaliana na mshtaki wetu kabla ya kufika mahakamani.

Matthew 5:27

Yesu alifundisha kwamba haikuwa tu sahihi kuzini, bali pia kufanya nini?

Yesu alifundisha kuwa haikuwa tu sahhi kuzini, bali pia kumtamani mwanamke.

Matthew 5:29

Yesu alisema yatulazimu kufanya nini na kitu chochote ambacho hutusababisha kutenda dhambi?

Yesu alisema kwamba yatulazimu kukiondoa kitu chochote kile kinacho tusababisha kutenda dhambi.

Matthew 5:31

Kwa swala gani Yesu aliruhusu talaka?

Kwa swala la zinaa aliruhusu talaka.

Mume akimwacha mke wake isivyo sitahili na kuolewa tena anamsababisha kuwa?

Mume anamsababisha mke wake kuwa mzinzi kama atamwacha isivyo sitahili na kuolewa tena.

Matthew 5:33

Yesu anasema tunapaswa kufanya nini badala ya kuapa viapo kwa mbingu, kwa nchi, kwa Yerusalemu, au kwa kichwa?

Yesu anasema kwamba badala ya kuapa viapo kwa vitu hivi vyote tunapaswa kusema ndio kuwa ni ndio au hapana kuwa ni hapana.

Matthew 5:36

Badala ya kuapa kwa vitu mbalimbali vya kidunia Yesu anasema maneno yetu yawe ya namna gani?

Yesu anasema badala ya kuapa kwa vitu tunapaswa maneno yetu yawe "Ndiyo, ndiyo" au "Hapana, hapana"

Matthew 5:38

Yesu alifundisha tunapaswa kufanya nini na yule aliye mbaya kwetu?

Yesu alifundisha kwamba hatupaswi kumpinga yule ambaye ni mbaya kwetu.

Matthew 5:43

Yesu alifundisha tunapaswa kufanya nini na maadui wetu na wale ambao wanatutesa?

Yesu alifundisha kwamba tunapaswa kuwapenda na kuwaombea maadui wetu na wale wanao tutesa.

Matthew 5:46

Kwa nini Yesu alisema haitulazimu kuwapenda tu wale ambao wanatupenda sisi, bali pia kuwapenda maadui wetu?

Yesu lisema kwamba kama tunawapenda tu wale ambao wanatupenda sisi, hatupokei thawabu kwa sababu tunafanya tu kile Wamataifa tayari wanafanya.


6

1Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni.2Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.3Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia,4ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.

5Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao.6Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.7Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.8Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.9Hivyo basi omba hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako.
10Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
11Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku.
12Utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu.
13Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.’

14Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi.15Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

16Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.17Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako.18Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.

19Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.20Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.21Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.

22Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru.23Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani!

24Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.

25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?26Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?27Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake?

28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, ‘Je tutakula nini?’ au ‘Je tutakunywa nini?’ au ‘Je tutavaa nguo gani?’32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo.33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.34Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.


Mathayo 06 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Mathayo 6 inaendelea na mafundisho ya Yesu yaliyojulikana kama "Mahubiri ya Mlimani."

Labda mtafsiri atapenda kulitenga sala katika 6:9-11 kwa kutumia uingizaji. Kwa kuwa sura hii hubadilika haraka kutoka kwa mada moja hadi nyingine, inawezekana kutumia mstari wa nafasi kati ya mada tofauti ili kuwasaidia wasomaji kutambua mabadiliko katika mada kwa urahisi zaidi.

Links:


Matthew 6:1

Sentensi unganishi

Yesua anaendelea kufundisha wanafunzi wake katika mafundisho ya mlimani yanayoanzia 5:1.Katika sehemu hii, Yesu anahutubia juu ya "matendo ya haki" ya utoaji sadaka, maombi, na kufunga.

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu kile kinachoweza kutokea kwao baadaye katika maisha yao binafsi. viwakilishi vyote vya "ni" na " yao" viko katika wingi.

mbele ya watu ili kujionyesha

Hii ilimaanisha kuwa wale wanaomuona mtu huyo watamheshimu. Hili linaweza kuelezeka katika mfumo tendaji. "mbele ya watu kwa kusudi la kutazamwa na watu ili wakupe heshima kwa kile ulichofanya."

Kweli nakwambia wewe

"Ninakuambia ukweli." Huu msemo unaongeza na kusisitiza kile ambacho Yesu atakisema baadaye.

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

Usipige panda na kujisifu

Kirai hiki kina maanisha kitendo cha kukusudia kupata usikivu wa watu. "Usijipatie usikivu wa watu kwa lengo binafsi kama mtu anayepiga panda katikati ya watu.

kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile Yesu atakachokisema baadaye.

Matthew 6:3

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwafundisha wanafunzi wake juu ya sadaka

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea kwao baadaye katika maisha binafsi. Viwakilishi vya "wewe" na " ""wako" viko katika wingi.

mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia

Huu ni msemo unaonyesha usiri. Kama vile mikono inavyofanya kazi pamoja na inasemekana "kujua" kila kitu kinachofanywa kwa wakati wote, hivyo hata watu wako wa karibu wasijue unapotoa msaada kwa maskini

sadaka yako itoe kwa siri

Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji "utawapa maskini pasipo watu wengine kujua."

Matthew 6:5

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kufundisha juu ya maombi

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha binafsi.. Viwakilisha vya "una" na "yao" katika mstari wa 5 na 6 viko katika wingi: katika mstari wa 6 viko katika umoja lakini waweza kuvitafsiri katika wingi.

ili kwamba watu wawatazame

Inamaanisha kwamba wale wanaowatazama watawapa heshima. Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji"ili kwamba watu wawatazame wao na kuwapa heshima."

kweli ninawaambia

ukweli ninakuambia." Huu msemo jnaongeza na kusisitiza kile ambacho Yesu atakisema baadaye'

ingia chumbani. Funga mlango

"nenda sehemu ya usiri" au "nenda sehemu ambayo utakuwa peke yako"

Baba aliye sirini

Tafsiri inayowezekana ni 1) hakuna anayeweza kumwona Mungu au 2) Mungu yuko sehemu ya siri pamoja na mtu anayeomba.

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

Baba yako aonaye sirini

Baba yako ataona kile ufanyacho sirini"

kurudia yasiyo na maana

"kurudia maneno yasiyo na maana"

watasikiwa

Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji. "miungu yao ya uongo itawasikiliza"

maneno mengi

sara ndefu" au "maneno mengi"

Matthew 6:8

Maelezo kwa ujumla

Yesu anaongea na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha binfsi. anawaambia kama kundi kwa kutumia wingi kama vile "ombeni hivi." viwakilishi vyote vya "lako" baada ya "baba yetu uliye mbinguni" viko katika umoja.

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

ulitakase jina lako

Hapa "jina" linamaanisha Mungu mwenyewe. "linamfanya kila mmoja kujua yeye ni mtakatifu."

ufalme wako uje

Hapa "ufalme" inamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. AT: "Waweza kutawala juu ya yote na kila kitu kikamilifu"

mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni

Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo hai. AT: "Kila mmoja duniani atii mapenzi yako kama wanavyofanya kila mmoja huko mbinguni."

Matthew 6:11

Maelezo kwa ujumla

Mionekano ya viwakilishi vya "nasi," "utu," "wetu" unaonesha makutano ambao Yesu alikuwa akiwahutubia.

mkate wa kila siku

Hapa "mkate" inamaanisha chakula kwa ujumla,

deni

Deni ni kile ambacho mtu anamdai mwingine. Huu ni msemo wa dhambi.

wadeni

Mdai ni mtu ambaye anadai deni kwa mwingine. Huu ni msemo kwa wenye dhambi.

usitulete katika majaribu

Neno "majaribu" jina la kitenzi, inaweza kuelezwa kama kitenzi. "usituletee kitu chochote cha kutujaribu" au "usituletee kitu cha kutufanya tushawishike na dhambi"

Matthew 6:14

Maelezo kwa ujumla

viwakilishi vyote vya "mta" na "yako" ni vya wingi. hata hivyo, Yesu anawaambia kile kitakachotokea baadaye katika maisha binafsi kama kila mmoja hatasamehe wengine

maovu

"makosa" au "dhambi"

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

Matthew 6:16

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kufundisha juu ya kufunga

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea katika maisha yao binafsi. Viwakilishi vyote vya "una" na "zao" katika mstari wa 17 na 18 viko katika umoja, lakini vinaweza kutafsiriwa katika wingi ili vioane na kile cha "wa" katika mstari wa 16.

Aidha

"Zaidi ya"

wanakunja sura zao

Wanafiki hawakuosha nyuso zao au kuchana nywele zao. Walifanya hivyo makusudi kuvuta hisia zao ili kwamba watu wawatazame wao na kuwapa heshima kwa sababu ya kufunga.

kweli ninakuambia

"Ukweli ninakuambia." Huu msemo unaongeza na kusisitiza kile ambacho Yesu atakiongea baadaye.

tengeneza kichwa chako

"paka mafuta kwenye nywele zako" au "tengeneza nywele zako" Kutunza kichwa hapa ni hali ya kawaida ya kutunza nywele. Halina uhusiano na "Kristo" ikimaanisha "mpakwa mafuta" Yesu alikuwa anamaanisha kwamba watu wanapaswa kuonekana kawaida haijalishi wamefunga au hawakufunga.

Baba aliye sirini ... yeye anayeona sirini

Tazama unavyotafsiri hii kwenye 6:5

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

aonaye sirini

"Aonaye kile unachokifanya unapokuwa pekee yako" Tazama ilivyotafsriwa katka 6:5

Matthew 6:19

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kufundisha juu ya fedha na mali

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. viwakilishi vya "usi" na "yako" viko katika wingi isipokuwa vile vya mstari wa 21, amabvyo viko katika umoja.

akiba

"utajiri"

ambapo nondo na kutu wanakula

"ambapo nondo na kutu wanashambulia akiba"

nondo

mdudu mdogo, anayeruka na kuharibu nguo

kutu

ni vitu vya rangi ya kahawia vinavyopatikana kwenye chuma

weka akiba yako mbinguni

Huu ni msemo ambao unamaanisha kwamba fanya mambo mazuri hapa duniani ili Mungu akubariki mbinguni.

na moyo wako utakapokuwepo pia.

Hapa "moyo" maana yake ni mawazo ya mtu na mapenzi yake.

Matthew 6:22

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafasi. viwakilishi vya "yako" vimo katika umoja lakini waweza kuvitafsiri katika wingi.

Jicho ni taa ya mwili... hilo giza ni kubwa kiasi gani

Hii inalinganisha macho mazima ambayo yanamwezesha mtu kuona macho mabovu ambayo yanasababisha mtu kuwa kipofu. Huu ni msemo unaomaanisha uzima wa kiroho. Mara nyingi, wayahudi walitumia msemo "macho mabaya" wakimaanisha uovu. Maana yake ni hii ikiwa mtu amejitoa kwa Mungu na kuona vitu vinafanyika kwa njia hiyo wanafanya vizuri. Endapo mtu ana tamaa ya utajiri wa vitu vingine hivyo anafanya uovu.

jicho

Unaweza kutafsiri kwa wingi, "macho"

ikiwa jicho lako ni baya

Hii aimanishi maajabu. Wayahudi mara zote walitumia msemo huu kwa mtu ambaye ni mwovu.

kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumwachaniza mwingine

Yote kwa pamoja kimsingi yana maana moja. Yanasisitiza kwamba mtu hawezi kupenda na kujitoa kwa Mungu na fedha kwa wakati mmoja.

Huwezi kumtumikia Mungu na mali

"Huwezi kumpenda Mungu na fedha kwa wakati mmoja"

Matthew 6:25

Maelezo kwauumla

Hapa viwakilishi vya "ku" na "yako" vyote viko katika wingi

Ninakuambia wewe

Hii inaongeza msisitizo kwa kile atakachosema Yesu baadaye

kwako

Yesu anaongea kwa kikundi cha watu kuhusu kitakachotokea kwao kwa mtu binafsi. Anapotumia "kwako" na "wako" yote ni wingi.

maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?

Yesu anatumia swali kufundisha watu. "uhakika maisha ni zaidi ya kile unachokula, na mwili wako ni zaidi ya kile unachovaa."

ghala

sehemu ya kutunza mazao

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

Je ninyi hamna thamani kuliko wao?

Yesu anatumia swali kufundisha watu. "uhakika ninyi mna thamani zaidi ya ndege."

Matthew 6:27

Maelezo kwa ujumla

Yesu ansema na makutano juu ya kile kinachoweza kutokea kwao katika maisha binafsi.viwakilishi vya "mwenu" na "yake" vimo katika wingi.

Na nani mmoja miongoni mwenu kwa kuwa na wasiwasi anaweza kuongeza siku za kuishi?

Yesu anatumia swali kufundisha watu. Anamaanisha hakuna atakayeishi maisha marefu kwa kuwa na hofu.

inchi moja

"inchi" ni pungufu ya mita. Hapa ni msemo wa kuongeza kiasi cha miaka mingapi ya kuishi mtu.

Na kwa nini mna kuwa na hofu kuhusu mavazi?

Yesu anatumia swali kufundisha watu. AT:"Usiwe na hofu kuhusu nini utavaa."

Fikiria kuhusu

'Zingatia"

maua

aina ya maua ya porini

Ninakuambia wewe

Hii inaongeza msisitizo wa kile ambacho Yesu ataongea baadae

hakuwahi kuvikwa kwa namna hii

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. AT:"hakuvaa nguo nzuri kama haya maua."

Matthew 6:30

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao kibinafsi. viwakilishi vya "ninyi" na "wenye" vimo katika wingi.

anayavalisha majani

Huu ni msemo ukiwa na maana Mungu anayapendezesha maua

majani

Ikiwa lugha yako ina neno linalohisi "majani" na neno ulilotumia kwa "maua" kwa mstari uliopita, unaweza kutumia hapa.

yanatupwa na kuteketea

Wayahudi tena walitumia majani kwa moto na kupikia vyakula vyao. Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. "mtu mmoja alitupa katika moto" au "mtu mmoja alichoma"

ni kwa kiwango gani atawavalisha ninyi ....imani?

Yesu anatumia swali kufundisha watu.AT: yeye hakika atawavisha ninyi...imani."

ninyi wenye imani ndogo

"ninyi ambao mna imani ndogo." Yesu anawatuhumu watu kwa sababu walikuwa na imani ndogo na Mungu.

Hivyo basi

"Kwa sababu ya hayo yote"

Matthew 6:32

Kwa kuwa mataifa wanafuta mambo haya

"kwa mataifa wanajali san juu ya kile watachokula, kunywa na kuvaa"

Baba yenu wa mbinguni anajua mnahitaji hayo

Yesu anamaanisha kwamba Mungu atahakikisha mahitaji ya muhimu mnapata

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

tafuta kwanza ufalme na haki

Hapa "ufalme" inamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. "umaanishe mwenyewe katika kumtumikia Mungu, ambaye ni mfalme wako, na ufanye yaliyo haki."

hayo mengine yote atakupatia wewe

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT: "Mungu atakupatia hayo yote wewe."

Hivyo basi

"Kwa sababu ya hayo yote"

kesho itajua yenyewe

Yesu anafafanua "kesho" kama mtu ambaye anaweza kuhofu. Yesu anamaanisha kwamba mtu anaweza kuhofu endapo siku inayofuata imefika.

kila siku ina tatizo la kujitosheleza yenyewe

"kila siku huwa ina mabaya yake yakujitosheleza" au "Kila siku ina matatizo yake ya kutosha"


Translation Questions

Matthew 6:1

Thawabu yao ni nini wale wanaofanya matendo ya haki ili watazamwe na watu?

Wale wanaofanya matendo ya haki ili watazamwe na watu wanapokea sifa kutoka kwa watu kama thawabu yao.

Matthew 6:3

Tufanye matendo ya haki kwa namna gani ili tupate thawabu toka kwa Baba?

Tuapaswa kufanya matendo yetu ya haki katika faragha.

Matthew 6:5

Thawabu gani wanapata wale wanaoomba kinafiki ili watu wawaone?

Wale wanaoomba kinafiki ili watu wawaone wanapokea thawabu yao kutoka kwa watu.

Wale wanaoomba katika faragha wanapokea thawabu toka kwa nani?

Wale waombao katika faragha wanapokea thawabu kutoka kwa Baba.

Kwa nini Yesu anasema tusiombe kwa kurudia maneno yasiyo na maana?

Yesu anasema tusiombe kwa kurudia maneno yasiyo na maana kwa sababu Baba anajua kitu gani tunahitaji hata kabla hatujamwomba yeye.

Matthew 6:8

Wapi tumwombe Baba ili mapenzi yake yafanyike?

Tumwombe Baba ili mapenzi yake yafanyike hapa duniani kama yanavyofanyika mbinguni.

Matthew 6:14

Kama hatutawasemehe wengine makosa yao, Baba yetu atafanya nini?

Kama hatutawasemehe wengine makosa yao, Baba yetu hatusamehe makosa yetu.

Matthew 6:16

Tufunge kwa njia gani ili tupate thawabu kutoka kwa Baba?

Tunapaswa kufunga bila kuonyesha watu kama tumefunga na ndipo Baba atatupatia thawabu.

Matthew 6:19

Tunapaswa kutunaza wapi hazina zetu na kwa sababu gani?

tunapaswa kutunza hazina zetu mbinguni kwa sababu haziwezi kuharibiwa au kuibiwa.

Nini kitakuwepo mahali pa hazina zetu?

Mioyo yetu itakuwepo mahali zilipo hazina zetu.

Matthew 6:22

Ni mabwana gani wawili tunaopaswa kuchagua mmoja kati yao?

Lazima tuchague kati ya Mungu na utajiri kama mabwana zetu.

Matthew 6:25

Kwa nini tusiwe na hofu kuhusu chakula,vinywaji na mavazi?

Hatupaswi kuwa na hofu kuhusu chakula,vinywaji na mavazi kwa vile Baba anawalinda na kuwatunza ndege, na nasi tuna thamani zaidi kuliko wao.

Matthew 6:27

Yesu anatukumbusha nini amabcho hatuwezi kufanya kwa kuwa na wasiwasi?

Yesu anatukumbusha sisi kwamba hatuwezi kuongeza kipimo kimoja cha maisha ya kuishi kwa kuwa na wasiwasi

Matthew 6:32

Kitu gani tunapaswa kutafuta kwanza na mahitaji yetu yote ya kimwili tutapatiwa?

Ni lazima tutafute kwanza ufalme na haki ya Baba na baada ya hapo mahitajiyetu yote ya mwilini tutapatiwa.


7

1Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.2Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.3Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?4Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?5Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.

6Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.

7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.8Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.

9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake akimwomba kipande cha mkate atampa jiwe?10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?11Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?

12Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.

13Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo.14Njia ni jembamba, njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.

15Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbwa mwitu wakali.16Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti?17Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.18Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.19Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.20Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.

21Si kila mtu aniambiaye mimi, ‘Bwana, Bwana,’ ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22Watu wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?’23Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!’

24Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.26Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.27Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”

28Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake,29kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.


Mathayo 07 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Kwa kuwa sura hii hubadilika haraka kutoka kwa mada moja hadi nyingine, inawezekana kutumia mstari wa nafasi kati ya mada ili kutofautisha kati yao kwa urahisi zaidi.

Dhana maalum katika sura hii

Mathayo 5-7

Mathayo 5-7 kwa pamoja huunda mahubiri au mafundisho ya Yesu. Mgawanyiko wa sura husababisha kuchanganyikiwa hapa.

"Utawajua kwa matunda yao"

Matunda ni taswira ya kawaida katika maandiko. Inatumika kuelezea matokeo ya tabia nzuri au mbaya. Katika sura hii, matunda mazuri ni matokeo ya kuishi kama Mungu anavyoamuru.

Links:


Matthew 7:1

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwafundisha wanafunzi wake katika mahubiri ya mlimani, yanayoanzia 5:1

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea kwao baadaye katika maisha binafsi. viwakilishi vya "nawe" na amri viko katika wingi.

Usihukumu

Inamaanisha hapa kwamba "hukumu" ina maana ya msingi kuwa "kushutumu vibaya" au "kutangaza kosa"AT:"Usishutumu watu vibaya."

nawe usije ukahukumiwa

Hii inaweza kutafsiriwa kwa mfumo hai.AT:"Mungu hawezi kukushutumu wewe vibaya."

Kwa

Uwe na uhakika msomaji anaelewa maelezo ya mstari wa 7:2 uwe na msingi alichokisema Yesu katika wa 7:1

kwa hukumu utakayohukumu, nawe utahukumiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT: "Mungu atakushutumu wewe hivyo hivyo kama

kipimo

Tafsiri inayowezekana ni 1) hii ni kipimo cha hukumu unayopewa au 2) hiki ni kiwango kinachotumika kwa kuhukumu.

utapimiwa hicho hicho

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. "Mungu atatumia kipimo hicho kwako."

Matthew 7:3

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafasi. viwakilishi vya "u" na "yako" vimo katika umoja lakini vinaweza kutafsirika katika wingi.

kwa nini unatazama....Unawezaje kusema

Yesu anatumia maswali yote kufundisha na kutoa changamoto kwa watu. Yeye anataka wao wajiangalie dhambi zao kabla ya kuangalia dhambi za mtu mwingine.

kipande cha mti

ni msemo

kaka

Hii inamaanisha mkristo mwenzako, siyo kaka halisi au jirani

kipande cha mti

Sehemu ya kipande kikubwa cha mti ambacho mtu amekikata chini. Ni kipande cha ubao kwa mbali kikubwa kiualisia kimeingia kwenye jicho la mtu. Huu ni msemo muhimu kwa mtu mwenye makosa

Matthew 7:6

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. viwakilishi vya "u" na "yao" viko katika wingi.

mbwa....nguruwe

Wayahudi waliwachukulia wanyama hawa kuwa wachafu, na Mungu aliwaambia wayahudi wasiwale. Huu ni msemo kwa watu waovu ambao hawathamini vitu vitakatifu. Itakuwa vizuri kutafsiri maneno haya kiualisia.

lulu

Hiki ni sawa na mviringo,jiwe la thamani au glasi. Ni misemo ya elimu ya Mungu au vitu vyenye ubora kiujumla.

wanaweza kuviharibu

"nguruwe wataviharibu"

na tena watageuka na kurarua

"na mbwa watageuka na kurarua"

Matthew 7:7

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. viwakilishi vya "wewe" na "wake" wake katika wingi.

Omba...Tafuta...Bisha

Hii ni misemo ya maombi kwa Mungu. Mfumo wa kitenzi inaonyesha kwamba tuendelee kuomba mpaka yeye ajibu. Ikiwa lugha yako ina mfumo wa kufanya kitu na kurudia rudia tena, unaweza kutumia hapa.

Omba

Hii ina maana ya kuhitaji kitu kutoka kwa Mungu

Nawe utapewa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT:"Mungu atakupa kile unachotaka."

Tafuta

"Tafuta kutoka kwa Mungu kile unachotaka"

Gonga

Kugonga mlango ilikuwa njjia ya upole ya kumwomba mtu aliye ndani ya nyumba au chumba afungue mlango.Ikiwa kugonga mlango si kwa upole kwenye utamaduni wenu, tumia neno ambalo linaelezea kwa upole mtu anapotaka kufunguliwa mlango.

nawe utafunguliwa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. Mungu atakufungulia kwa ajili yako"

au kuna mtu miongoni mwenu ambaye....jiwe?

Yesu anatumia swali kufundisha watu. "Hakuna mtu miongoni mwenu ... jiwe,"

kipande cha mkate

Hii inamaanisha chakula kwa ujumla. "chakula"

jiwe...samaki...nyoka

Haya majina yatafsiriwe kiualisia.

au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?

Yesu anauliza swali jingine kufundisha watu. Inaeleweka kwamba yesu alikuwa anarejea mtu na kijana wake. "Na hakuna mtu miongoni mwenu, ikiwa kijana amemwomba samaki, atampatia nyoka."

Matthew 7:11

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaambia makutano juu ya kile kinachoweza kutokea baadaye katika maisha yao binafsi. Viwakilishi vya "ninyi" na :wenu" ni vya wingi.

ni kwa kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa...... yeye?

Yesu anatumia swali kujibu watu. "ndipo Baba yenu aliye mbinguni hakika atampa....yeye."

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu.

unataka kufanyiwa kitu chochote na watu

kwa njia yeyote lolote unalotaka ufanyiwe na wengine"

kwa kuwa hiyo ni sheria na unabii

Hapa "sheria" na "unabii" kinarejea kile ambacho Musa na manabii walikiandika. kwa kuwa hiki ndicho kile Musa na manabii walifundisha kwenye maandiko."

Matthew 7:13

Maelezo kwa ujumla

unapotafsri, tumia neno sahihi la "pana" na la "pana sana" kama yanavyotofautiana na "embamba" kama inavyowezekana ili kukazia tofauti ya hizo jozi za malango na njia.

Ingia kwa kupitia njia nyembamba...wachache wanaoweza kuiona

Hiki ni kivuli cha mtu anayetembea njiani na kuingia kwenye ufalme kwa kupita lango. Ufalme mmoja ni rahisi kuingia na mwingine si rahisi kuingia. Huu ni msemo unaomaanisha kwamba mtu anapaswa kukubali njia ngumu ya maisha ya kumtii Mungu na kupata uzima wa milele. Ikiwa watachagua njia nyepesi ya maisha ya kutomtii Mungu, wataingia kuzimu.

Ingia kwaa kupitia njia nyembamba

Unatakiwa kuendelea hadi mwisho wa mstari wa 14: "Hivyo basi, ingia kwa kupitia njia nyembamba."

lango.....njia

Tafsiri inayowezekana ni 1) hii inarejea langoi la kuingia katika ufalme na njia inayoongoza kwenye lango. Ikiwa hivyo, unaweza kubadilisha mpangalio kinyume kama walivyofanya UDB au 2) "lango" na "njia" vyote vinarejea lango la ufalme. ikiwa hivyo, una haja ya kubadili mpangilio.

katika uharibifu.... katika uzima

Haya majina ya sifa yanaweza kutafsiriwa kwa vitendo. "katika eneo ambalo utakufa.... katika eneo ambalo utaishi."

Matthew 7:15

Jihadharini na

"jilindeni na"

wanakuja wamevaa ngozi ya kondoo,lakini kweli ni mbwa wakali

Huu msemo una maana manabii wa uongo watajifanya wazuri na kutaka kuwasaidia, lakini kwa ualisia ni waovu na watawadhuru.

Kwa matunda yao utawatambua

Huu msemo unarejea matendo ya mtu. "Kama vile unavyofahamu mti kwa tunda linalotokea, utamtabua nabii wa uongo kwa matendo yao."

Je watu wanaweza kuvuna ....miiba?

Yesu anatumia swali kujibu watu. Watu wangetambua kwamba jibu siyo. "watu hawezi kuvuna...miba."

kila mti mzuri huzaa matunda mazuri

Yesu anaendelea kutumia msemo wa tunda akimaanisha nabii mzuri ambaye anafanya kazi nzuri au maneno mazuri.

mti mbaya huzaa matunda mabaya

Yesu anaendelea kutumia mfano wa matunda kwa kurejea kwa nabii mbaya ambaye anafanya kazi ya uovu.

Matthew 7:18

Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.

Yesu anaendelea kutumia mti wa matunda kama msemo akimaanisha manbii wa uongo. Hapa, yeye anaongelea kile kitakachotokea kwa mti mbaya. Ikimaanisha kwamba kitu hicho kitafanyika kwa manabii wa uongo.

itakatwa chini na kutupwa katika moto

Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo hai. "mtu ataukata chini na kuuchoma."

kwa matunda yao mtawatambua

Neno "yao" inaweza kurejea labda manabii au miti. Huu msemo unamaanisha kwamba matunda ya mti na matendo ya manabii yote yanafunua kuwa yaweza kuwa mabaya au mazuri. Kama ikiwezekana, unaweza kutafsiri ikimaanisha maana moja kati ya hayo'

Matthew 7:21

wataingia katika ufalme wa mbinguni

Hapa "ufalme" inamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. Msemo "ufalme wa mbinguni" umetumika pekee katika kitabu cha mathayo. Ikiwa inawezekana, andika "mbingu" katika tafsiri yako. "wataishi pamoja na Mungu mbinguni pindi atakapojifunua kuwa mfalme."

wale wanaotenda mapenzi ya Baba

"wale wanaotenda kile ambcho Baba yangu anataka"

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

siku hiyo

Yesu alisema "siku hiyo" akijua wasikilizaji walielewa alichomaanisha siku ya hukumu. Unaweza kuhusisha "siku ya hukumu" endapo tu wasikulizaji wako hawatakuelewa vinginevyo.

hatukutoa unabii....kutoa mapepo...tulifanya miujiza mingi?

Watu walitumia maswali kusisitiza kwamba walifanya mambo hayo. "tulitabiri..tulitoa pepo...tulifanya miujiza mingi."

sisi

Hii "sisi" haimuhusishi Yesu.

kwa jina lako

Hapa "jina" maana yake katika nguvu na mamlaka ya Yesu

matendo ya ajabu

"miujiza"

sikuwatambua ninyi

Hii ina maana mtu huyu si wa Yesu."Wewe si mfuasi wangu" au "Sina kitu cha kufanya pamoja nawe"

Matthew 7:24

Hivyo basi

"Kwa sababu hiyo"

maneno yangu

Hapa "maneno" yanarejea kile ambacho Yesu alisema

kama mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba juu ya mwamba

Yesu analinganisha wale wanaotii neno lake na mtu aliyejenga nyumba ambayo haitazulika na kitu.

mwamba

Huu ni mwamba mbaya chini ya mchanga ulio juu na udongo, sio jiwe kubwa au mpaka juu ya ardhi.

ilikuwa imejengwa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "yeye alijenga"

Matthew 7:26

Sentensi unganishi

Huu ndio mwisho wa mahubiri ya Yesu ya mlimani yanayoanzaia 5:1

atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga

Yesu aliendelea kutumia mlinganyo kutoka mstari uliopita. Yeye analinganisha wale ambao hawatii neno lake na mpumbavu aliyejenga nyumba. Mpumbavu pekee aweza kujenga nyumba juu ya mchanga ambapo mvua,mafuriko na upepo vinaweza kuhamisha mchanga.

kuanguka

Tumia neno la ujumla kwa lugha yako ambalo linaelezea kilichotokea wakati nyumba inaanguka chini.

na anguko lake likakamilika

Mvua,mafuriko na upepo hakika yaliangamiza nyumba.

Matthew 7:28

Maelezo kwa ujumla

Mistari hii inafafanua jinsi watu katika makutano walivyoyapokea mafundisho ya Yesu ya mlimani.

ilifika kipindi ambacho

Huu usemi unaonyesha hitimisho la hotuba ya mlimani.

walishangazwa kwa mafundisho yake

iko wazi katika 7:29 kwamba walishangazwa si kwa sababu ya alichofundisha Yesu bali pia jinsi alivyofundisha . "walishangazwa kwa jinsi alivyoweza kufundisha."


Translation Questions

Matthew 7:1

Nini cha lazima cha kufanya kwanza kabla yya kuona vizuri na kuwasaidia ndugu?

Ni lazima kwanza kujihukumu wenyewe na kutoa gogo kwenye macho yako kabla ya kusaidia ndugu zetu.

Matthew 7:3

Tunapaswa kufanya nini kwanza kabla yakutaka kumsaidia ndugu yetu?

Tunapaswa kwanza kujihukumu wenyewe na kuondoa gogo kutoka kwenye macho yetu ndipo tuweze kumsaidia ndugu yetu.

Matthew 7:6

Nini kitatokea endapo utawapa kitu kitakatifu mbwa?

Endapo utawapa kitu kitakatifu mbwa, watakivuruga hicho na tena kukugeukia na kukularua vipande.

Matthew 7:7

Tunapaswa kufanya nini ili tupokee kutoka kwa Baba?

Lazima tuombe, tutafute na kubisha ili kupokea kutoka kwa Baba.

Matthew 7:11

Mungu anawapa nini kwa wale wanaomwomba yeye?

Mungu anawapa vitu wale wanaomwomba.

Sheria na manabii inatufundisha nini juu ya matendo yetu kwa wengine?

Sheria na manabii inatufundisha kuwatendea wengine matendo ambayo nasisi tunapenda watu tutendewe

Matthew 7:13

Njia pana inaongoza kwenda wapi?

Njia pana inaongoza kwenye uharibifu

Matthew 7:15

Tunawezaje kuwatambua manabii wa uongo?

Tunaweza kuwatambua manabii wa uongo kwa matunda ya maisha yao.

Matthew 7:21

Nani ataingia katika ufalme wa mbinguni?

Wale wanaofanya mapenzi ya Baba wataingia katika ufalme wa mbinguni.

Yesu atawaambia nini wengi ambao walitoa utabiri, kufukuza pepo na kufanya miujiza kwa jina la Yesu?

Yesu atawaambia " sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu , ninyi watenda mabaya"!

Matthew 7:24

Nani ni kama mtu mwenye hekima katika mfano waYesu wa nyumba mbili?

Yule anayesikia maneno ya Yesu na kuyatii ni kama mtu mwenye hekima.

Matthew 7:26

Nani ni kama mtu mpumbavu katika mfano wa Yesu wa nyumba mbili?

Yule anayesikia maneno ya Yesu na asiyatii ni kama mtu mpumbavu.

Matthew 7:28

Yesu aliwafundishaje watu ikilinganishwa na waandishi walivyofundisha?

Yesu aliwafundihsa watu kama mtu mwenye mamlaka , si kama waandishi.


8

1Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.2Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, “Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi.”

3Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, “Niko tayari. Uwe msafi.” Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.4Yesu akamwambia, “Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao.”

5Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, jemedari akaja kwake akamuuliza6akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha.”

7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya.”

8Jemedari akajibu na kumwambia, “Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa.9Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu ‘Nenda,’ na huenda, na kwa mwingine ‘Njoo,’ na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ na yeye anafanya hivyo.”

10Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, “Kweli ninawaambia, sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.11Ninawaambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahamu, Isaka, na Yakobo, katika ufalme wa mbinguni.12Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno.”13Yesu akamwambia jemedari, “Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako.” Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.

14Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa.15Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. Kisha akaamka akaanza kumhudumia.

16Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya.17Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, “Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu.”

18Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa bahari ya Galilaya.19Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda.”

20Yesu akamwambia, “Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake.”

21Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.”

22Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao.”

23Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini.24Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala.25Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!”

26Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?” Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu,27wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, “Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?”

28Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.29Tazama, walipaza sauti na kusema, “Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?”30Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa,31pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. “Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe.”

32Yesu akawaambia, “Nendeni!” Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.33Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo.34Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.


Mathayo 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii inaanza sehemu mpya.

Dhana maalum katika sura hii

Miujiza

Miujiza ya Yesu katika sura hii inaonyesha kwamba ana mamlaka juu ya mambo yanayopita udhibiti wa binadamu. Inaonyesha pia kwamba kumwabudu Yesu ni jibu sahihi kwa matendo yake.

Links:


Matthew 8:1

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwanzo wa sehemu mpaya ya simulizi ambalo limebeba simulizi nyingi za uponya wa watu. Wazo hili linaendelea hadi hadi 9:35.

Wakati Yesu alipokuja kushuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.

"Baada ya Yesu kuja kushuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata," Umati yawezekana ulijumuisha watu waliokuwa nae juu mlimani na watu ambao hawakuwahi kuwa nae.

Tazama

Neno "tazama" inatupa dokezo sisi la mtu mwingine katika hadithi. Lugha inaweza kuwa namna ya kufanya hivyo.

mkoma

"mtu ambaye ana ukoma" au "mtu ambaye ana ugonjwa wa ngozi"

kusujudu mbele yake

Hii ni ishara ya unyenyekevu heshima mbele ya Yesu.

Ikiwa unataka

"ikiwa unataka kufanya" au "ikiwa unahitaji" mwenye ukoma alijua yesu ana nguvu za kumponya, lakini hakujua endapo Yesu alitaka kumgusa yeye.

wewe unaweza kunisafisha

Hapa "kusafisha" maana yake kuponywa na ili kuweza kuishi kwenye jamii tena."

mara moja

"sasa hivi"

naye akasafishwa ukoma wake

Matokeo ya Yesu kusema"Uwe mzima" ilikuwa kwamba mtu huyo akaponywa.Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT:"yeye alikuwa mzima" au "ukoma ulimwacha" au "ukoma ulikoma"

Matthew 8:4

yeye

Hii alikuwa anarejea mtu ambaye alimponya

usimwambie mtu yeyote

"usiseme kitu chochote kwa mtu yeyote" au "usimwambie mtu yeyote nimekuponya wewe"

ukajionyeshe kwa makuhani

Sheria ya wayahudi ililazimu kwamba mtu akaonyeshe ngozi aliyoponywa kwa kuhani, ambaye tena angemruhusu yeye au yule kuwa pamoja na watu wengine.

utoe zawadi ambayo Musa aliwaagiza,kwa ajili ya ushuhuda kwao.

Sheria ya Musa ililazimu kwamba yeyote aliyeponywa ukoma atoe sadaka ya shukrani kwa kuhani. Endapo kuhani atakubali zawadi, watu watajua kwamba mtu huyo ameponywa.

kwao

Hii kwa uhakika inaweza kurejea kwa 1) makuhani au 2) wapingaji wa Yesu. Ikiwezekana, tumia kiwakilishi ambacho kitaonyesha kati ya makundi hayo.

Matthew 8:5

Sentensi unganishi

Hapa simulizi hili linabadili mandhari ya muda na eneo na simulizi inakuwa ni ya habari za Yesu akimponya mtu mwingine

akaja kwake na kumwambia yeye

Hapa "yeye" anarejea kwa Yesu.

amepooza

"Asiyeweza kutembea kwa sababu ya ugonjwa"

Yesu akamwambia yeye

"Yesu akamwambia jemedari"

nitakuja na kumponya yeye

"nitakuja nyumbani kwako na kumfanya mtumishi wako apone"

Matthew 8:8

kuingia ndani ya dari langu

Msemo "kuingia ndani ya dari" maana yake "nyumba yangu"

sema neno

Hapa "neno" maana yake sema amri.AT: "toa amri"

ataponywa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT: "atakuja kuwa mzima"

walio chini ya mamlaka

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai.AT:"ambaye yuko chini ya mamlaka ya mwingine"

chini ya mamlaka...... chini yangu

Kuwa "chini" mtu inamaanisha kutokuwa na umuhimu sana na kutii agizo la mtu mwenye umuhimu zaidi.

mwanajeshi

"mtalaamu wa kupigana"

kweli ninawaambia

"Ninawaambia ukweli." Huu usemi unaongeza na kusisitiza kile ambacho yesu atazungumza baadae.

sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu Israel

Wasikilizaji wa Yesu wangefikiri kwamba wayahudi katika Israeli, ambao wanadai kuwa ni watoto wa Mungu, watakuwa na imani kuliko yeyote. Yesu anasema hawako sahihi na kwamba imani ya jemedari ilikuwa kubwa.

Matthew 8:11

wewe

Hapa "wewe" ni wingi na ina maanisha "wale ambao walikuwa wakimfuata yeye"

kutoka mashariki na magharibi

Unapotumia kinyume "mashariki" na "magharibi" ni njia ya kusema "kila mahali," "kutoka kila mahali" au "kutoka mbali kila upande"

wataketi katika meza

watu katika utamaduni walikaa chini pembeni ya meza wakiwa wanakula. Huu msemo unaonyesha kwamba wale walio mezani ni familia na marafiki wa karibu. "ishi kama familia na rafiki."

katika ufalme wa mbinguni

Hapa "ufalme" ina maanisha utawala wa Mungu kama mfalme. Msemo "ufalme wa mbinguni" umetumika katika kitabu cha Mathayo. Ikiwezekana, andika "mbinguni" katika tafsiri yako. "wakati Mungu wetu mbinguni anaonyesha kwamba yeye ni mfalme."

watoto katika ufalme watatupwa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo hai. "Mungu atawatupa watoto katika ufalme."

watoto katika ufalme

Usemi "watoto wa"ina maanisha wale ambao wanamikiwa na kitu fulani, kwa namna hiyo ufame wa Mungu. Kuna kejeli pia hapa kwa sababu "watoto" watatupwa nje wakati wageni watakaribishwa. "wale ambao waliruhusu Mungu awatawale wao."

nje gizani

Haya maelezo yanamaanisha hatua ya mwisho ya milele kwa wale waliomkataa Mungu. "sehemu ya giza mbali kwa Mungu" au "kuzimu"

itendeke hivyo kwako

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. "hivyo nitafanya kwa ajili yako wewe"

mtumishi aliponywa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. "Yesu alimponya mtumishi"

kwa wakati huo

kwa muda ule Yesu alisema yeye atamponya mtumishi."

Matthew 8:14

Sentensi ungsnishi

Hapa simulizi inabadili mandhari ya muda na eneo. simulizi inakuwa ni ya Yesu akimponya mtu mwingine

Yesu alipofika

Hawa wanafunzi yawezekana walikuwa na Yesu, lakini mtazamo wa hadithi Yesu alisema nini na kufanya nini, hivyo watambulishe wanafunzi pekee ikiwa inalazimika kuepusha maana ya uongo.

Mama mkwe wa Petro

Mkwe - "mama wa mke wa Petro"

homa ikamwacha

Ikiwa lugha yako itaelewa msemo kuwa homa inaweza kufikiri na kutenda yenyewe, hii inaweza kutafsiriwa kama "yeye akawa mzima" au "Yesu akamponya yeye:

akaamka

"akaamka toka kitandani"

Matthew 8:16

Sentensi unganishi

Mandhari yanahamia katika muda wa jioni ambapo Simulizi inakuwa ya Yesu kuponya watu zaidi na kufukuza mapepo..

Maelezo ya jumla

Katika mstari wa 17, mwadishi anamnukuu nabii Isaya il ikuonesha kuwa huduma ya Yesu ilikuwa kutimiza unabii.

Na ilipofika jioni

Hii inajulisha kwamba hii ni baada ya Sabato, kwa sababu wayahudi walikuwa hawafanyi kazi au kusafiri siku ya Sabato. Walisubiri muda wa jioni kuleta watu kwa Yesu. Hauhitaji kutaja Sabato isipokuwa unataka kuepuka tafsiri ya uongo

wengi waliotawaliwa na mapepo

Hii inaweza kutafsiriwa kwa mfumo hai.AT:"wengi ambao mapepo yaliwatawala" (UDB) au "wengi ambao walipagawa na mapepo"

Naye akawafukuza roho kwa neno

Hapa "neno" inamaanisha amri. Yeye aliwaamuru pepo kuondoka."

yalitimizwa unabii wa Isaya uliyosema

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo hai. "Yesu alitimiza unabii kwamba nabii Isaya aliongea na watu wa Israeli."

alichukua magonjwa yetu na kubeba malazi yetu

Mathayo anamnukuru nabii Isaya. Hii misemo miwili kiualisi inamaana moja na kusisitiza kwamba yeye aliponya magonjwa yetu yote. "aliponya wale walio wagonjwa na kuwafanya wazima."

Matthew 8:18

Sentensi unganisha

Hapa simulizi linabadilika na kusimulia jinsi Yesu alivyosema juu ya watu waliotaka kumfuata

Kisha

Hili neno limetumika hapa kuonyesha alama ya kikomo cha hadithi. Hapa Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya hadithi.

yeye alitoa maelekezo

"aliwaambia wanafunzi wake"

Ndipo

Hapa inamaanisha baada ya Yesu "kutoa maelekezo" lakini kabla yake kuingia ndani ya boti.

popote

"sehemu yeyote"

Mbwea wana mashimo, na ndege wa angani wana vichari

Hii ina maana hata wanyama wakali wana sehemu ya kupumzika.

mbwea

Mbwea ni wanyama kama mbwa. Wanakula ndege wadogo na wanyama wengine wadogo. Ikiwa mbwea hawajulikani kwenye eneo lako, tumia kwa ujumla mbwa - kama viumbe au mnyama mwingine mkali.

shimo

Mbwea wanatengeneza mashimo ardhini kwa kuishi humo. Tumia neno sahihi kwa eneo ambalo mnyama "mbwea" anaishi.

mwanadamu

Yesu anaongelea kuhusu yeye mwenyewe

hana sehemu ya kulaza kichwa chake

Hii ina maanisha sehemu ya kulala. "hana sehemu yake ya kulala."

Matthew 8:21

niruhusu kwanza niende na kumzika baba yangu

Aieleweki kwamba baba wa mtu alikufa na angemzika mapema, au ikiwa mtu anaataka akae muda mrefu baba yake afe na amzike. Pointi ya muhimu mtu anataka kufanya kitu kingine kwanza kabla ya kumfuata Yesu.

uwaache wafu wazike wafu wenzao

Yesu hana maana halisi kwamba watu wafu watazika wafu wengine. Tafsiri inayowezekanaya "wafu" ni 1) ni msemo kwa wale ambao watakufa punde, au 2) ni msemo kwa wale ambao hawamfuati Yesu na kiroho wamekufa. Pinti ya muhimu ni kwamba wanafunzi wasiruhusu kitu chochote kumchelewesha kumfuata yesu.

Matthew 8:23

Sentensi unganishi

Hapa mandhari yanahamia kwenye simulizi la Yesu akituliza dhoruba wakati yeye na wanafunzi walipokuwa wakivuka bahari ya Galilaya.

alipoingia kwenye boti

"kuingia ndani ya boti"

wanafunzi wake wakamfuata

Jaribu kutumia neno lilelile kwa "wanafunzi" na "kufuata" ambalo umelitumia

Tazama

Hii inaonyesha kuanza kwa kutukio jingine kubwa la hadithi. Lugha yako inaweza ikawa na njia nyingine ya kuonyesha hili.

likatokea wimbi kubwa baharini

"wimbi la nguvu likatokea baharini"

ndipo sasa boti ikazungukwa na mawimbi

Hii inaweza kutafsiriwa kwa mfumo tendaji. "ndipo sasa mawimbi yakafunika boti"

wakamwamsha, wakamwambia,"tuokoe

Maana inayowezekana ni 1) kwanza walimwamsha Yesu na ndipo wakasema, "tuokoe" au 2) walipokuwa wakimwamsha walimwambia "tuokoe"

sisi

ikiwa unataka kutafsiri neno hili kama pamoja au kipekee, ndipo kipekee ni bora. Wanafunzi yawezekana walimaanisha walitaka Yesu awaokoe wanafunzi na yeye mwenyewe kwenye kuzama.

sisi tunaelekea kufa

"sisi tunakwenda kufa"

Matthew 8:26

wao

"kwa wanafunzi"

kwa nini mnaogopa ... imani?

Yesu alikuwa anakemea wanafunzi kwa swali la kejeli. "hampaswi kuogopa...imani" au "hamna sababu ya ninyi kuogopa ....imani."

ninyi wenye imani ndogo

Angalia jinsi unavyotafsiri hii

Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata upepo na bahari vinamtii yeye?

"Hata upepo na bahari vinamtii yeye! Huyu mtu ni wa namna gani?" Hili swali la kejeli linaonyesha kwamba wanafunzi walishangazwa. "huyu mtu niwa tofauti na hatujawahi kumwona! hata upepo na mawimbi vinamtii yeye!"

hata upepo na bahari vinamtii yeye

Kwa watu au wanyama kutii au kutotii haishangazi, lakini kwa upepo na maji inashangaza.Hii kibinadamu inaeleza vitu asili kama viumbe vinaweza kusikia na kuitikia kama watu.

Matthew 8:28

Sentensi unganishi

Hapa mwandishi anaturudisha kwenye wazo kuu la Yesu akiwaponyawatu. Hii inanzisha simulizi la Yesu akiwaponya wanaume wawili waliokuwa na pepo.

upande mwingine

"upande mwingine wa bahari ya galilaya"

nchi ya Gadalene

Gadalene ulitajwa kwa jina la Gadara.

walikuwa wasumbufu, hakuna mpita njia aliyeweza kupita njia ile

Mapepo yaliyowatawala watu hawa wawili yalikuwa hatari kwamba hakuna hata mmoja angeenda kupitia eneo hilo.

Tazama

Hii inaonyesha kuanza kwa kutukio jingine kubwa la hadithi. Inaweza kuhusisha watu tofauti na tukio lililopita, Lugha inaweza kuwa na njia ya kuonyesha hili.

Tuna nini cha kufanya nawe,mwana wa Mungu

Hili swali la kwanza la kejeli ni hostile

Umekuja hapa kututesa sisi kabla ya wakati kufika?

hili swali la pili la kejeli nalo pia ni uhasama na linamaanisha "Haupaswi kutomtii Mungu kwa kutuadhibu sisi kabla ya muda wenyewe ambao Mungu ameupanga ambao atuhukumu sisi"

Matthew 8:30

sasa

hili neno linaonyesha kwamba mwandishi atawaambia wasomaji habari anazotaka kufahamu kabla ya hadithi kuendelea. Nguruwe walikuwa kule kabla ya Yesu kufika.

Ikiwa utatuamuru tutoke

"kwa sababuunakwenda kututoa sisi nje"

sisi

Hii ni pamoja ,ina maanisha nguruwe pekee"

wao

mapepo ndani ya mtu

Mapepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe

"Mapepo wakamwacha mtu na kuwaingia nguruwe"

ndipo

Neno "ndipo" hapa linatoa angalizo kwetu kuwa tayari kwa taarifa za kushangaza zinazokuja.

likashuka chini kutokea mlimani

"kimbia haraka chini kwenye mteremko"

likafia majini

"waliingia kwenye maji na kuzama"

Matthew 8:33

Sentensi unganishi

Hii inahitimisha habari ya Yesu ya kuwaponya wanaume wawili waliokuwa na pepo

kuchunga nguruwe

"kulinda nguruwe"

kilitokea nini kwa mwanaume ambaye ametawaliwa na mapepo

"Yesu alifanya nini kwa mwanaume ambaye alitawaliwa na mapepo"

Ndipo

Hii inaonyesha mwanzo wa tukio jingine kubwa la hadithi. Inaweza kuhusisha watu tofauti na tukio la zamani.Lugha yako inaweza kuwa na njia kwa kuonyesha hili

mji mzima

Hii ina maanisha wengi au idadi ya watu wengi, sio lazima kila mtu.

mji

"jiji na ardhi inayoizunguka"


Translation Questions

Matthew 8:4

Kwa nini Yesu alimwambia aliyeponywa ukoma aende kwa kuhani na kutoa zawadi ambayo Musa aliagiza?

Yesu alimwambia mkoma aliyeponywa kwenda kwa kuhani kwa ushuhuda wao.

Matthew 8:5

Yesu alisema atafanya nini alipoambiwa na Jemedari kuhusu mtumishi wake aliyepooza?

Yesu alisema angeenda kwenye nyumba ya jemedari na kumponya mtumishi wake.

Matthew 8:8

Kwa nini jemedari alisema kwamba Yesu hakuwa na sababu ya kwenda nyumbani kwake?

Jemedari alisema kwamba yeye hanakuwa na thamani kwa Yesu kuingia katika nyumba yake na kwamba Yesu angeweza kusema neno tu na kumponya mtumishi.

Yesu alitoa sifa gani kwa jemedari?

Yesu alisema kwamba hata katika Israeli hajawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama jemedari.

Matthew 8:11

Yesu alisema nani atakuja na kuketi katika meza katika ufalme wa Mbinguni?

Yesu alisema kwamba wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi na kuketi katika meza katika ufalme wa Mungu.

Yesu alisema nani watatupwa katika giza la nje ambapo kuna kilio na kusaga meno?

Yesu alisema kuwa wana wa ufalme wangetupwa katika giza la nje.

Matthew 8:14

Yesu alimponya nani alipoingia katika nyumba ya Petro?

Yesu alimponya mama mkwe wa Petro alipoingia kwenye nyumba ya Petro.

Matthew 8:16

Ni unabii gani kutoka kwa Isaya ulitimia pale Yesu alipowaponya wote waliopagawa na mapepo na wagonjwa?

Unabii wa Isaya,"Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu" ulitimia.

Matthew 8:18

Yesu alisema alikuwa anaishi kwa njia gani pale mwandishi alipomwomba amfuate?

Yesu alisema hakuwa na nyumba ya kudumu.

Matthew 8:21

Kipindi mwanafunzi anaomba kwenda kumzika baba yake kabla ya kumfuata yesu, Yesu alimwambia nini?

Yesu alimwambia mwanafunzi kumfuata yeye na kuacha wafu kuzika wafu wenzao

Matthew 8:23

Yesu alikuwa anafanya nini kwenye mtumbwi yalipotokea dhoruba baharini?

Yesu alikuwa amelala wakati dhiruba kuu inatokea juu ya bahari.

Matthew 8:26

Kipindi wanafunzi wanamwamsha Yesu kwa sababu waliogopa kuangamia, Yesu alisema nini kwao?

Yesu aliwaambia wanafunzi, "Kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo"?

Kwa nini wanafunzi walimshangaa Yesu baada ya kuwa na utulivu?

Wanafunzi walimshangaa Yesu kwa sababu upepo na bahari vilimtii.

Matthew 8:28

Mtu wa aina gani Yesu alikutana naye wakati alipokuja kwenye nchi ya Wagerasi

Yesu alikutana na watu wawili waliopagawa na pepo ambao walikuwa wasumbufu

Pepo walioonge nini kupitia yule mtu kwa Yesu?

Pepo waliongea kuhusu kuja kwa Yesu kuwatesa kabla ya wakati kufika.

Matthew 8:30

Nini kilitokea wakati Yesu alipofukuza pepo?

Wakati Yesu alipowafukuza pepo, waliingia katika kundi la nguruwe na wale nguruwe wakakimbilia majini na kuangamia.

Matthew 8:33

Watu walimsihi Yesu afanye nini walipotoka mjini kuja kuonana naye?

Watu walimsihi Yesu aondoke katika mkoa wao.


9

1Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.2Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. Alipoiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, “Mwanangu, uwe na furaha, dhambi zako zimesamehewa.”

3Tazama, baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, “Huyu mtu anakufuru.”4Yesu akatambua mawazo yao na kusema, “Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?5Kipi kilicho rahisi kusema, ‘Dhambi zako zimesamehewa’ au kusema, ‘Simama na utembee?’6Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi.” Aliyasema haya kwa yule aliyepooza, “Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako.”7Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.8Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.

9Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, “Nifuate mimi.” Naye akasimama na kumfuata.10Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake.

11Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi, “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?”

12Yesu aliposikia hayo, naye alisema, “Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa.13Inawapasa muende mkajifunze maana yake, ‘Ninapenda rehema na siyo dhabihu,’ kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.”

14Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, “Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”

15Yesu akawaambia, “Je, wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.

16Hakuna mtu anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani, kiraka kitaipasua nguo na mpasuko mkubwa utatokea.17Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika chombo cha mvinyo wa zamani, ikiwa watafanya, ngozi itachanika, mvinyo utatoweka na ngozi itaharibika. Badala yake, huweka mvinyo mpya katika ngozi mpya na vyote vitakuwa salama.”

18Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, naye akasema, “Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena.”19Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia.20Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake.

21Kwa kuwa alisema, “Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji.”

22Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. “Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone.” Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji.

23Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.24Naye akasema, “Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala.” Lakini wao walicheka na kumkebehi.25Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka.26Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.

27Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, “Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi.”28Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, “Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?” Nao wakamwambia “Ndiyo, Bwana.”

29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo.”30Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema, “Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili.”31Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.

32Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu.33Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema, “Hii haijawahi kutokea katika Israel.”

34Lakini Mafarisayo walikuwa wakisema, “Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo.”

35Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.36Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.37Naye akawaambia wanafunzi wake. “Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache.38Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake.”


Mathayo 09 Maelezo ya Jumla

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Kuna takwimu nyingi za matamshi katika sura hii. Ilikuwa ni kawaida pia kwa Yesu kutumia mifano ya analojia na sitiari katika mafundisho yake. Jinsi yake ya kufundisha ilikuwa na nia ya kukuza imani ndani yake.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Na", "lakini"

Baadhi ya tafsiri za Kiingereza huanzisha sentensi nyingi katika sura hii na neno "na" au "lakini" ili kuonyesha mfululizo wa matukio katika maelezo. ULB kawaida huondoa maneno haya kwa sababu muktadha wa hadithi yenyewe unaonyesha kuwa matukio hutokea kwa mfululizo. Inakubalika kutumia maneno haya ikiwa yana umuhimu katika tafsiri yako.

Links:


Matthew 9:1

Sentensi unganishi

Mwandishi anarejea kwenye wazo kuu, ambalo linaanzia 8:1, la Yesu akiwaponya watu. Hii inaanzisha habari ya Yesu akimponya mwanamume aliyekuwa amepooza

Yesu akaingia kwenye boti

Wanafunzi yamkini walienda na Yesu'

boti

Yamkini ni boti ile ile

akafika kwenye mji wake

"mji ambao yeye aliishi"

Ndipo

Hii inaonyesha mwanzo wa tukio jingine kubwa la hadithi. Linaweza kuhusisha watu wengine tofauti na tukio lililopita. Lugha yako inaweza kuwa na njia nyingine ya kuonyesha hili.

yao....zao

Hii inaonyesha wale ambao walimleta mgonjwa wa kupooza kwa Yesu. Hii inahusisha mgonjwa aliyepooza mwenyewe.

Mtoto

Huyu mtu hakuwa mtoto halisi wa Yesu. Yesu alikuwa akiongea naye kwa upole. Ikiwa hii inachanganya, inaweza pia kutafsiriwa"Rafiki yangu" au "Kijana" au hata kuondolewa.

Dhambi zako zimesamehewa

"Mungu amesamehe dhambi zako" au "Nimekusamehe dhambi zako"

Matthew 9:3

Tazama

Hii inaonyesha mwanzo wa tukio jingine kubwa la hadithi. Inaweza kutumia watu wengine tofauti na tukio lililopita. Lugha yako inaweza kuwa njia nyingine kufanya hili.

miongoni mwao

Hii inaweza kumaanisha "wao kwa wao,"kwenye mawazo yao, au "kwa kila mmoja," kutumia midomo yao.

anakufuru

Yesu alidai kuweza kufanya vitu ambavyo waandishi wa sheria walifikiri Mungu peke yake angevifanya.

akatambua mawazo yao

Yesu alitambua walichokuwa wakifikiria kwa uwezo wake au kwa sababu aliwaona wakisemezana wao kwa wao.

Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?

Yesu alitumia swali kuwakemea wanasheria.

wewe...yako

Hizi ni wingi

uovu

Huu ni uovu wa kimaadili au ukosefu, sio tu ni kosa kwa uhakika.

kipi ni rahisi......kutembea

Yesu aliuliza swali kukumbusha wanasheria kwamba waliamini mtu amepooza kwa sababu ya dhambi zake na kwamba dhambi zake zimesamehewa, naye angeweza kutembea, ili kwamba alipomponya aliyepooza, wanasheria wajue kwamba yeye anaweza kusamehe dhambi.

kipi kilicho rahisi kusema,dhambi zako zimesamehewa au kusema, simama na utembee?

"kipi ni rahisi kusema,"Dhambi zako zimesamehewa"? au ni rahisi kusema "Simamama na utembee"?

Dhambi zako zimesahewa

Hii inaweza kumaanisha 1)"ninakusamehe dhambi" au 2)"Mungu amesamehe dhambi zako."yako" ni umoja.

mtambue ya kwamba

"Nitawahakikishia ninyi." "ninyi" ni wingi.

yako.....yako

Hizi ni umoja

nenda nyumbani kwako

Yesu hamkatazi mtu kwenda sehemu nyingine. Yeye anampa fursa ya kwenda nyumbani.

Matthew 9:7

Sentensi unganishi

Hii inahitimisha habari ya Yesu ya kumponya mtu aliyepooza. Kisha Yesu akamwita mtoza ushuru kuawa mmoja wa wanafunzi wake.

ambaye amewapa

"kwa sababu amewapa"

mamlaka hayo

mamlaka ya kuthibitisha kusamehe dhambi

Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo

Kirai hiki kinaonyesha mwanzo wa simulizi mpya. Kamalugha yako ina namna ya kufanya hili, unaweza kulitumia mahali hapa.

akaipita kutoka hapo

"alikuwa akiondoka" au "alikuwa akienda"

Mathayo...naye...Yeye

Utamaduni wa kanisa unasema Mathayo ni mwandishi wa hii Injili, lakini andiko halitoi sababu ya kubadilisha kiwakilishi kutoka "naye" na "yeye" kwa "kwangu" na "mimi"

Yeye alisema naye

"Yesu alisema na Mathayo"

naye akamwambia

"Yesu alimwambia Mathayo"

Naye akasimama na kumfuata yeye

"Mathayo alisimama na kumfuata yeye" kama mwanafunzi, siyo tu kujumuika na Yesu kwa kinachofuata kukamilisha.

Matthew 9:10

Maelezo kwa ujumla

Matukio haya yalitokea kwenye nyumba ya Mathayo mtoza ushuru

nyumba

Hii yawezekana ni nyumba ya Mathayo, lakini yawezekana kuwa nyumba ya Yesu(walitumia kula Yesu na wanafunzi wake")Kilitengwa maalum ikiwa kitahitajika kuepusha kuchanganywa.

Ndipo

Hii inaonyesha mwanzo wa tukio jingine katika habari kuu. Inaweza kuhusisha watu tofauti kuliko matukio yale ya kwanza. Lugha yako inaweza kuwa na namna ya kulielezea hili.

Mafarisayo walipoona hayo

"Na mafarisayo walipoona kwamba Yesu alikuwa anakula na watoza ushuru na watu wenye dhambi"

kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na waovu?

Mafarisayo walitumia swali hili kumkosoa Yesu kile alichokuwa akifanya.

Matthew 9:12

Maelezo y a jumla

Matukio haya yanatokea kwenye nyumba ya Mathayo mtoza ushuru.

Na Yesu aliposikia hayo

Hapa "hayo" inarejea swali ambalo mafarisayo waliuliza kuhusu Yesu kula na watoza ushuru na wenye dhambi.

Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa

Yesu anajibu kwa kutumia mithali. Anamaanisha kuwa anakula na watu wa aina hii kwa sababu amekuja kuwaokoa wenye dhambi.

watu walio na afy nzuri

"watu wenye afya"

wale walio wagonjwa

Kirai "wanahitaji mganga" kinaeleweka. "Wagonjwa ndio wanaohitaji mganga"

Inawapasa muende mukajifunze maana yake

Yesu anaelekea kunukuu maandiko. "Inakupasa ujifunze maana ya kile ambacho Mungu alisema katika maandiko"

Inawapasa muende

Kiwakilishi "wa" ni cha wingi kinachomaanisha mafarisayo

Ninapenda rehema na wala siyo dhabihu

Yesu ananukuu kile ambacho nabii Hosea aliandika katika maandiko.. Hapa "Ni" inamaanisha Mungu.

Kwa kuwa nilikuja

Hapa "Ni" inamaanisha Yesu.

haki

Yesu anatumia kejeli. Hadhani kuwa kuna watu wenye haki ambao hawahitaji kutubu. "wale wanaodhani kuwa ni wenye haki"

Matthew 9:14

sentensi unganishi

Wanafunzi wa Yohana mbatizaji walihoji swala la wanafunzi wa Yesu kutokufunga.

msifunge

"endeleeni kula kama kawaida"

Je wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi bwana harusi anapokuwa pamoja nao?

Yesu anatumia swali kuwajibu wanafunzi wa Yohana. Walijua kuwa watu hawaombolezi na kufunga kwenye sherehe ya harusi. Yesu anatumia mithali hii kuonyesha kuwa wanafunzi wake hawaombolezi kwa sababu yeye bado yuko nao.

Lakini siku zinakuja

"lakini muda utafika"

bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao

Hii inaweza kuelezeka katka mfumo tendaji. "Bwana harusi hatakuwa pamoja nao si muda mrefu ujao" au "kuna mmoja atakayemchukua bwana harusi kutoka kwao."

atachukuliwa kutoka kwao

Yamkini Yesu anamaanisha kifo chake, lakini hii isiwekwe wazi kuwa ndichio alichomaanisha. Ili kulinda picha ya harusi, ni vizuri kueleza kuwa bwana harusi ataondoka kitambo.

Matthew 9:16

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kujibu swali ambalo wanafunzi wa Yohana walikuwa wameuliza

Hakuna anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani

Huu msemo una maana kwamba watu wanaojua utamaduni wa zamani pekee hawako tayari kukubali mpya.

vazi

nguo

kipande

"kipande cha nguo mpya" kinatumika kuziba nguo iliyochanika

na mpasuko mkubwa utatokea

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji

Matthew 9:17

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kujibu swali ambalo wanafaunzi wa Yohana walikuwa wameuliza

Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika ngozi ya zamani

Yesu anatumia mithali Nyingine kuwajibu wanafunzi wa Yohana. Hii inamaanisha ni kitu kilekile sawa na mithali ya 9:16

Hakuna watu wanaoweka

"Hakuna hata mmoja anayemwaga" au "Watu hawaweki kamwe"

mvinyo mpya

Huu ni mvinyo ambao haujachacha. Kama mizabibu haijulikani kwenye sehemu yenu, tumia neno la ujumla la tunda."mvinyo wa matunda"

mfuko wa mvinyo mkuukuu

Hii inamaanisha mifuko ya mvinyo ambayo imekuwa ikitumika mara nyingi.

Mfuko wa mvinyo

"mkoba wa mvinyo" au "mkoba wa ngozi". Hii ni mifuko iliyokuwa imetengenezwa kwa ngozi za wanyama.

mvinyo utatoweka na gozi itaharibika

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "Na hii itaharibu mfuko wa mvinyo na mvinyo kumwagika.

ngozi itaharibika

mvinyo mpya unapochacha na kuumuka, ile ngozi huchanika kwa sababu haiwezi tena kutanuka.

ngozi mpya

"mifuko mipya ya mvinyo" au "begi jipya la mvinyo" Hii inamaanisha ngozi ya mvinyo ambayo haijawahi kutumika.

vyote vitakuwa salama

Hili linaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji

Matthew 9:18

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha simulizi ya Yesu kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi baada ya kufa.

mambo hayo

Hii inarejea jibu la Yesu alilowapa wanafunzi wa yohana kuhusu kufunga.

Tazama

Neno "tazama" linatupa dokezo la mtu mwingine mpya katika hadithi. Lugha yako inawezekana ikawa na njia nyingine ya kufanya hivi.

akasujudu kwake

Hii ni njia mtu yeyote kuonyesha heshima katika utamaduni wa kiyahudi.

njoo na uweke mkono wako juu yake, na yeye ataishi tena

Hii inaonyesha kwamba ofisa wa kiyahudi aliamini Yesu ana nguvu ya kurudisha uhai wa binti yake.

wanafunzi wake

wanafunzi wa Yesu

Matthew 9:20

Sentensi unganishi

Hii inafafanua jinsi Yesu alivyomponya mwanamke mwingine wakati akiwa njiani kwenda kwa afisa wa Kiyahudi

Tazama

Neno "tazama" linadokeza juu ya mtu mwingine katika hadithi. Lugha yenu inaweza kuwa na njia nyingine ya kufanya hivi

alikuwa anatokwa damu

"kutokwa damu mfululizo"Yawezekana alikuwa akitokwa damu kwenye tumbo lake ingawa haikuwa kipindi cha kawaida yake. Baadhi ya tamaduni yawezekana wana namna nzuri ya kueleza tatizo hili.

miaka kumi na mbili

"miaka 12"

vazi

"kanzu"

Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji

Alifikiria hivi kabla hajamgusa Yesu. Unaweza kuiweka sentensi hii mwanzoni.

Endapo nitagusa vazi lake

Kwa mjibu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu ya kutokwa na damu hakutakiwa kumgusa yeyote mtu yeyote. Anagusa vazi la Yesu ili nguvu za Yesu zimponye alidhani kuwa Yesu hatagundua kuwa ameguswa

Lakini

"Badala" Kile mwanamke alichotumaini kutokea hakikutokea.

Binti

Mwanamke hakuwa mtoto halisi wa Yesu. Yesu alikuwa akiongea naye kwa upole. Ikiwa hii inachanganya, inaweza kutafsiriwa "kijana wa kike" au hata kutolewa.

imani yako imekufanya upone

"Kwa sababu uliniamini, Nitakuponya"

Muda huo huo mwanamke alipokea uponyaji

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Yesu alimponya hapohapo"

Matthew 9:23

Sentensi unganishi

Hii inarudisha habari ya Yesu kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi

nyumba ya ofisa

Hii ilikuwa nyumba ya kiongozi wa kiyahudi

wapiga tarumbeta na umati wa watu walikuwa wakipiga kelele

Huu ni utamaduni wa kawaida wa kumboleza pale mtu anapokuwa amekufa.

wapiga zumari

"watu ambao wanapiga zumari/filimbi"

Ondoka hapa

Yesu alikuwa akiongea kwa watu wengi, hivyo tumia mfumo wa wingi wa kutoa amri kama lugha yenu inao huo.

binti hajafa, lakini amelala

Yesu anatumia igizo la maneno. Ilikuwa ni kawaida kipindi cha Yesu kusema mtu aliyekufa kuwa "amelala" Lakini hapa binti aliyekufa ataamka, ingawa yeye alikuwa amelala.

Matthew 9:25

Sentensi unganishi

Hii inahitimisha simulizi la Yesu la kumfufua binti wa afisa wa Kiyahudi

Maelezo kwa ujumla

Mstari wa 26 unatoa muhtasari unaofafanua matokeo ya Yesu kumfufua huyu msichana.

Na wale watu walipotolewa nje

"Baada ya yesu kuwatoa watu nje" au "Baada ya familia kuwatoa watu nje"

akaamka

"akaamka kutoka kitandani" Hii ni maana ile ile kama iliyo kwenye 8:14

Habari hii ikaenea mji mzima

Watu wote wa mji ule walisikia kuhusu hilo" au "Watu walioona binti akiwa hai walianza kuwaambia watu wa eneo hilo habari hizi."

Matthew 9:27

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu akiwaponya wanaume wawili waliokuwa vipofu

Alipokuwa akipita Yesu njiani

Yesu alikuwa akiondoka kwenye mji

akipita

"Alikuwa akiondoka" au "alikuwa akienda"

wakamfuata

Hii inamaainisha kuwa walikuwa wakitembea nyuma ya Yesu, siyo lazima kuwa walikuwa wameshakuwa wanafunzi wake.

uturehemu

Inamaanisha kuwa walitaka Yesu awaponye

Mwana wa Daudi

Yesu hakuwa mwana halisi wa Daudi, hivyo inaweza kutafsiriwa kama "Ukoo wa Daudi". Ingawa, "Mwana wa Daudi" pia ni cheo alichopewa Masihi, na wale wanaume yawezekana walikuwa wakimwita Yesu kwa Sifa hii.

Pindi Yesu alipokuwa amefika kwenye nyumba

Hii inaweza kuwa nyumba ya Yesu au nyumba iliyosemwa kwenye 9:10

Ndiyo,Bwana

Jibulote halijatolewa lakini linaeleweka "Ndiyo, Bwana, tunaamini kuwa unaweza kutuponya."

Matthew 9:29

akagusa macho yao na kusema

Haiko wazi kuwa aligusa macho yao wote wakati mmoja au alitumia mkono wake wa kulia kumgusa mmoja na mwingine tena. Mkono wa kushoto kawaida ulitumika kwa makusudi yakutokuwa safi, ni hakika alitumia mkono wa kulia pekee. Pia haiko wazi kwamba aliongea wakati anawagusa au kwanza aliwagusa na ndipo akaongea kwao.

Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo

Hii inaweza kutafsriwa katika mfumo tendaji. "Naitafanya kama ulivyomini" au "kwa sababu unaamini, nitakupaonya"

macho yao yakafumbuka

Hii inamaanisha waliweza kuona. Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Mungu aliponya macho yao" au "wale wanaume wawili vipofu waliweza kuona"

Angalieni mtu yeyote asifahamu jambo hili.

Hapa neno "angalieni" linamaanisha "hakikisha." au "Uwe na Muwe na uhakika hakuna mtu atakaye tafuta juu ya jambo hili" au "Msimwambie mtu yeyeote kuwa nimewaponya"

Lakini

"Badala yake"Wanaume hawakufanya kile ambacho Yesu aliwaambia kufanya.

kutangaza habari

"waliwaambia watu wengi kilichotokea kwao"

Matthew 9:32

Sentensi usganishi

Hii ni habari ya Yesu akiwaponya watu waliokuwa wamepagawa na pepo

tazama

Neno "tazama" linadokeza sisi juu ya mtu mwingine katika simulizi. Lugha yako inaweza ikawa njia nyingine ya kufanya hizi.

mtu mmoja bubu ... akaletwa kwa Yesu.

Hii inaweza kuelezeka kwa muundo tendaji. "mtu mmoja alimleta bubu kwa Yesu... kwa Yesu"

bubu

asiyeweza kuongea

aliyepagawa na pepo

Hii inaweza kueleza katika mfumo tendaji. "ambaye pepo lilikuwa limemumliki" au "amabye pepo lilikuwa linamtawala"

Na pepo walipomtoka

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "Baada ya Yesu kuwa amelitoa pepo" au " Baada ya Yesu kuwa ameliamuru pepo kutoka"

yule bubu aliongea

"Yule bubu akanza kuongea" au "yule aliyekuwa bubu aliongea" au "mtu ambaye alikuwa bubu akaongea" au yule mtu hakuwa bubu tena"

umati ukashangazwa

"Watu walishangazwa"

Hii haijawahi kutokea

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji "Hii haikuwahi kutokea kabla" au "Hakuna hata mmoja aliyewahi kufanya jambo kama hili hapo awali."

anawafukuza pepo

"huwalazimisha pepo kutoka"

huwaondoa

Kiwakilishi "ana" kinamaanisha Yesu

Matthew 9:35

Sentensi unganishi

Mstariwa 35 ni mwisho wa sehemu ya simulizi ambayo imeamnzia katika 8:1 kuhusu huduma ya Yesu ya uponyaji kule Galilaya.

Maelezo kwa ujumla

Mstari wa3 6 unaanzisha sehemu nyingine ya simulizi ambapo Yesu anawafundisha wanafunzi wake na kuwatuma kwenda kuhubiri na kuponya kama alivyokuwa akifanya.

miji yote

Yesu alienda kwa wengi au kwa miji mingi lakini si kwa kila mji. "Katika miji mingi"

miji....vijiji

"vijiji vikubwa...vijiji vidogo" au "miji mikubwa...miji midogo"

injili ya ufalme

Hapa neno "Ufalme" linamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. tazama ilivyotafsiriwa karika 4:23

magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote

"kila magonjwa na kila udhaifu" Neno "magonjwa" na "udhaifu" yanakaribiana kufanana lakini yanapaswa kutafsiliwa tofauti kama inawezekana. "Ugonjwa" unamfanya mtu kuwa dhaifu. "Udhaifu" kukosa nguvu mwili au tokeo linalosababishwa na kuwa na ugonjwa.

Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji

Mfanano huu unamaanisha kuwa hawakuwa na kiongozi wa kuwaangalia. "Watu hawakuwa na kiongozi"

Matthew 9:37

Maelezo kwa ujumla

Yesu anatumia mithali kuwaambia wanafunzi wake juu ya mavuno ili kuona jinsi watavyopokea mahitaji ya makutano yaliyotajwa katika sehemu ambazo tayari zimepita.

Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache

Yesu anatumia mithali kuonyesha jinsi anavyopokea kile anachokiona. Yesu anamaanisha kuwa kuna watu wengi walio tayari kumwani Mungu lakini kuna watu wachache tu wa kuwafundisha ukweli wa Mungu.

mavuno ni mengi

"Kuna mazao mengi yaliyoiva na yako tayari kuvunwa."

wafanya kazi

"watendaji"

mwombeni Bwana wa mavuno

"Mwombeni Bwana, kwa sababu yeye mkuu wa mavuno"


Translation Questions

Matthew 9:3

Kwa nini baadhi ya walimu wa sheria walifikiri kwamba Yesu alimkufuru Mungu?

Baadhi ya walimu wa sheria walifikiri kwamba Yesu alimkufuru Mungu kwa sababu Yesu alimwambia mtu aliyepooza kwamba dhambi zako zimesamehewa.

Kwa nini Yesu alikuwa amemwambia aliyepooza kwamba dhambi zako zimesamehewa badala ya kumwambia simama na utembee?

Yesu alimwambia aliyepooza dhambi zako zimesamehewa ili kuonyesha kuwa anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.

Matthew 9:7

Kwa nini watu walimsifu Mungu walipoona mtu aliyepooza amesamehewa dhambi na kuponywa?

Walishangaa na kumsifu Mungu aliyewapa mamlaka kama hayo kwa watu.

Mathayo alikuwa na kazi gani kabla ya kumfuata Yesu?

Mathayo alikuwa mtoza ushuru kabla ya kumfuata Yesu.

Matthew 9:10

Yesu pamoja na wanafunzi wake walikula na nani?

Yesu na wanafunzi wake walikula pamoja na watoza ushuru na watu wenye dhambi.

Matthew 9:12

Yesu alisema ni akina nani alikuja kuwaita ili watubu?

Yesu alisema alikuja kuwaita mwenye dhambi ili watubu

Matthew 9:14

Yesu alisema ni kwa nini wanafunzi wake walikuwa hawafungi?

Yesu alisema wanafunzi wake walikuwa hawafungi kwa sababu awakuwa bado yupo pamoja nao.

Ni wakati gani Yesu alisema wanafunzi wake wangeweza kufunga?

Yesu alisema wangeweza kufunga wakati atakapokuwa amechukuliwa kutoka kwao.

Matthew 9:20

Mwanamke aliyetokwa na damu kwa wingi alifanya nini na kwa nini?

Mwanamke aliyetokwa na damu kwa wingi aligusa sehemu la nguo ya Yesu akifikiri kwamba endapo atagusa nguo yake tu, atapata uponya na kuwa mzima.

Yesu alisema kitu gani kilimponya mwanamke mwenye kutokwa damu kwa wingi?

Yesu alisema mwanamke mwenye kutokwa damu nyingi alinywa kwa imani yake.

Matthew 9:23

Kwa nini watu walimcheka Yesu alipoingia kwenye nyumba ya afisa wa kiyahudi?

Watu walimcheka Yesu kwa sababu alisema binti alikuwa hajafa bali amelala.

Matthew 9:25

Nini kilitikea baada ya Yesu kumfufua binti?

Habari kuhusu Yesu kumfufua binti zilienea katika mji wote.

Matthew 9:27

Wale vipofu wawili walipiga kelele gani kwa Yesu?

Vipofu wawili waliendelea kupiga kelele, "utuhurumie sisi, mwana wa Daudi

Matthew 9:29

Yesu aliwaponya vipofu wawili kutokana na nini?

Yesu aliwaponya vipofu wawili kutokana na imani yao.

Matthew 9:32

Baada ya Yesu kumponya bubu, Mafarisayo walitoa shutuma gani dhidi yake?

Mafarisayo walimshutumu Yesu kuwa alitoa mapepo kwa nguvu ya mkuu wa mapepo?

Matthew 9:35

Kwa nini Yesu aliuhurumia umati?

Yesu aliwaonea huruma umati kwa sababu kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo, na walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.

Matthew 9:37

Yesu aliwaambia wanafunzi wake ni muhimu waombee nini?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake ni muhimu waombe kwamba Bwana wa mavuno atume wafanyakazi katika mavuno.


10

1Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maradhi na aina zote za magonjwa.2Majina ya mitume kumi na wawili ni haya. La kwanza, Simeoni (ambaye pia anaitwa Petro), na Andrea kaka yake, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake:3Filipo, na Bartelemayo, Thomaso, na Mathayo mtoza ushuru, Yakobo mwana wa Alfayo, na Tadeo,4Simoni mkananayo, na Yuda Iskariote, ambaye alimsaliti.

5Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema, “Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya Wasamaria.6Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel.7Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.9Msichukue dhahabu, almasi au shaba kwenye pochi zenu.10Usichukue mkoba katika safari yenu, au nguo za ziada, viatu au fimbo, kwa kuwa mfanyakazi anastahili chakula chake.11Mji wowote au kijiji mtakachoingia, tafuteni ambaye anastahili na mkae pale mpaka mtakapoondoka.12Mtakapoingia katika nyumba salimieni.13Endapo nyumba inastahili, amani yenu ibaki pale, lakini kama nyumba haistahili, amani yenu iondoke pamoja nanyi.14Na kwa wale wasiowapokea ninyi au kusikiliza maneno yenu, wakati mnaondoka kwenye nyumba au mji huo, kung'uta mavumbi ya nyayo zenu mahali hapo.15Kweli ninawaambia, itakuwa ya kustahimili zaidi miji ya Sodoma na Gomorah siku ya hukumu kuliko mji huo.

16Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.17Muwe waangalifu na watu, watawapeleka kwenye mabaraza, na watawapiga kwenye masinagogi.18Na mtaletwa mbele ya wakuu na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao na kwa mataifa.19Pindi watakapowashutumu, msiwe na wasiwasi jinsi gani au nini cha kuongea, kwa kuwa kitu cha kusema mtapewa kwa wakati huo.20Kwa kuwa sio ninyi mtakaoongea, lakini Roho wa Baba yenu ataongea ndani yenu.21Ndugu atamwinukia ndugu yake kumwua, na baba kwa mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi, na kuwasababishia kifo.22Nanyi mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini yeyote atakayevumilia mpaka mwisho mtu huyo ataokolewa.23Pindi wanapowatesa katika mji huu, kimbilieni mji unaofuata, kwa kweli ninawaambia, hamtakuwa mmekwenda kwenye miji yote ya Israeli kabla ya Mwana wa Adam hajarudi.

24Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya Bwana wake.25Inatosha kwa mwanafunzi kwamba awe kama mwalimu wake, na mtumishi kama Bwana wake. Ikiwa wamemwita Bwana wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi watawakashifu wa nyumba yake!

26Hivyo basi msiwahofu wao, kwa kuwa hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililofichika ambalo halitajulikana.27Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba.28Msiwaogope wale ambao wanaua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho. Badala yake, mwogopeni yule ambaye awezaye kuangamiza mwili na roho kule kuzimu.29Je kasuku wawili hawauzwi kwa senti ndogo? Hata hivyo hakuna anayeweza kuanguka chini bila Baba yenu kufahamu.30Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa.31Msiwe na hofu, kwa kuwa mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi.32Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.33Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

34Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga.35Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.36Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake.37Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili.38Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili.39Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata.

40Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi.41Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki.42Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake.”


Mathayo 10 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Kutumwa kwa wanafunzi kumi na wawili

Sehemu kubwa ya sura hii inazungumza juu ya Yesu kuwatuma wanafunzi kumi na wawili kutoa ujumbe wake kuhusu ufalme wa mbinguni. Walipaswa kufanya huduma yao kwa inchi ya Israeli pekee na wasije wakashiriki habari hii kwa wasio Wayahudi. Maagizo ya Yesu humpa msomaji hisia kwamba hawakupaswa kupoteza wakati wowote. Sauti yake iliashiria kuwa alitaka waharakishe.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Wanafunzi kumi na wawili

Yafuatayo ni orodha ya wanafunzi kumi na wawili: Katika Mathayo: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo, Yohana mwana wa Zebedayo, Filipo, Bartholomayo, Tomasi, Mathayo, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mzeloti na Yuda Iskarioti.

Katika Marko: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana mwana wa Zebedayo (ambaye aliwaita Boanerge, yaani, wana wa ngurumo), Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mzeloti, na Yuda Iskarioti.

Katika Luka: Simoni (Petro), Andrea, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomasi, Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni (aitwaye Mzeloti, Yuda mwana wa Yakobo, na Yuda "Iskarioti.

Inawezekana kuwa Thadayo na Yuda, mwana wa Yakobo, ni majina mawili ya mtu mmoja.

"Ufalme wa mbinguni umekaribia"

Maneno haya yana umuhimu mkubwa wa kitheolojia. Wataalam wanajadili ikiwa "ufalme wa mbinguni" ulikuwepo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha changamoto katika kutafsiri. Matoleo mengine hutumia maneno "inakaribia" na "yamekaribia."

Links:


Matthew 10:1

Sentensi unganishi

Hii inafungua habari ya Yesu akiwatuma wanafunzi wake wakafanye kazi yake.

akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja

"Akawaelezea wanafunzi wake 12"

akawapa mamlaka

Uwe na uhakika kwamba ujumbe unakuwa wazi kuwasilisha kwamba haya mamlaka yalikuwa 1) ni kufukuza roho chafu na 2) kuponya magonjwa na udhaifu

kuwafukuza

"kuwafanya roho wachafu waondoke"

kila aina ya magonjwa na kila aina za udhaifu

"kila ugonjwa na kila udhaifu." Maneno "ugojwa" na "udhaifu" ni kama yanakaribia kufanana lakini yanapaswa kutafsiliwa tofauti kama inawezekana. "Ugonjwa" ni kisababishi cha mtu kuwa dhaifu. "Udhaifu" ni ukosefu wa nguvu mwilini au kisababishi ambacho matokeo yake ni kuwa na ugonjwa.

Matthew 10:2

Maelezo kwa ujumla

Hapa mwanadishi anatoa majina kumi na mbili ya mitume kama taarifa ya itoayo picha ya nyuma.

sasa

Neno hili limetumika hapa kuonesha mwanzo wa simulizi jipya. Hapa Mathayo anaonesha historia ya maisha ya mitume kumi na wawili.

Mitume kumi na wawili

Hili kundi ni sawa na kusema "wanafunzi kumi na wawili" katka 10:1

Kwanza

Hi ya kwanza kwa mpangilio si kwa safu

Mkananayo

Hii inaweza kumaanisha yafuatayo 1) "Mkananayo" hii ni sifa iliyoonesha kuwa alikuwa ni mshirika wa kundi lililotaka kuwaweke huru wayahudi kutoka kwenye utawala wa Warumi. "Mzalendo" au "mmajumui" au 2) Mkereketwa ni neno linalonesha mtu mwenye kutamani kumjengea heshima Muungu. "mwenye uchu"

Mathayo mtoza ushuru

"Mathayo ambaye alikuwa mtoza ushuru"

ambaye atamsaliti yeye

"ambaye atamsaliti Yesu"

Matthew 10:5

Sentensi unganishi

Hapa Yesu anaanza kutoa maelekezo kwa wanafunzi wake juu ya jinsi wanavyopaswa kufanya na wategemee nini wakienda kuhubiri.

Maelezo kwa ujumla

Ijapokuwa mstari wa tano unaanza kwa kusema kuwa alaiwatuma thenashara, Yesualiwapa maelekezo haya kabla ya kuwatuma.

Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma

"Yesu aliwatuma hawa wanaume kumi na wawili" au "Walikuwa ni hawa wanaume kumi na wawili ambao Yesu aliwatuma"

aliwatuma

Yesu aliwatuma kwa kusudi maalumu.

Naye akawaelekeza wao

"Naye aliwaambia kitu gani walipaswa kutenda" au "aliwaamuru wao"

Kondoo aliyepotea wa nyumba ya Israel

Hiki ni kirai kinacholinganisha taifa zima la israel na kondoo ambao wamejitenga kutoka kwa mchungaji

nyumba ya Israel

Haya maelezo yana maanisha taifa la Israel. "watu wa Israel" au "kizazi cha Israel"

Mnapokwenda

Kiwakilishi "mna" ni cha wingi na kinamaanisha mitume kumi na wawili.

Ufalme wa mbinguni umekaribia

Hiki kirai cha "ufalme wa mbinguni", kinapatikana katika injili ya Mathayo tu. Kinamaanisha Mungu ni mfalalme. kama inawezekana tumia neno "mbinguni" katikatafsiri zako. "Mungu wetu wa mbinguni atajidhihirisha mapema kuw a yeyeni mfalme. Tazama ilivyotafsiriwa katika 3:1

Matthew 10:8

Sentensi unganishi

Yesu anaendele kuwaelekeza wanafunzi wake mambo ya kufanya watakapoenda kuhubiri.

mme....zenu

Hivi ni viwakilishi vya wingi vinavyomaanisha mitume kumi na wawili

Mmepokea bure toeni bure

kuna taarifa hapa ambazo hazikuelezwa, lakini inaeleweka . " Nilwasaidia na kuwafundisheni neno la Mungu bure. Kwa hiyo msiwafanye watu wengine wawalipe kwa lengo la kuwasaidia au kuwafundisha ukweli wa Munugu.

dhahabu,fedha au shaba

Hizi ni metali ambazo zilitumika kutengeneza sarafu. Hii orodha ni ya hela, ikiwa metali hazijulikani katika eneo lako, tafasiri orodha kama"hela."

pochi

Hii ina maana "mkanda" au "mkanda wa fedha," lakini kinamaanisha chochote kinachotumika kubebea hela. Mkanda ni kitu kirefu cha kujifunga cha nguo au ngozi kinachopita begani. Kilikuwa ni kipana ambacho kiliweza kukunjwa na kutumiwa kubeba hela

begi la kusafiria

Hii inaweza kuwa begi lolote linalotumika kubeba kitu safarini au begi linalotumiwa na mtu mmoja kukusanya chakula au hela.

nguo ya ziada

Tumia neno hilo hilo ulilotumia kwa "nguo"

mfanyakazi

"mfanyakazi"

chakula chake

Hapa "chakula" Kitu chochote ambacho ni hitaji kwa mtu.

Matthew 10:11

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu nini wanachopaswa kufanya watakapoenda kuhubiri.

mta...yenu

Hivi viwakilishi vinaonyesha mitume kumi na wawili

Kwa kila mji au kijiji mtakachoingia

"Kwa "Kila mji au kijiji" mtakachokwenda" au

Mji..kijiji

"kijiji kikubwa...kijiji kidogo" au "mji mkubwa...mji mdogo." Tazama ilivyotafsriwa katika 9:35.

anayestahili ... asiyestahili

Katika 10:11-13 "anayestahili" inamaanisha mtu aliyetayari kuwakaribisha wanafunzi wa Yesu. Yesu anamlinganisha mtu asiyekuwa tayari kuwakaribisha wanafunzi wake saw namtu asiyestahili

mkae pale mpaka mtakapoondoka

Maana halisi ya sentensi hii inaweza kuwa sahihi kama itasemwa "mkae katika nyumba ya huyo mtu mpaka mtakapoondoka kwenye huo mji au kijiji"

Mtakapoingia katika nyumba,salimuni

Kirai cha "salimieni" inamaanisha isalimuni hiyo nyumba. Salamu ya kawaida kwa nyakati zile ilikuwa "amani iwe katika nyumba hii. "Kaya" inamaanisha watu wanao ishi kwenye hiyo nyumba. mkiwa mnaingia kwenye nyumba, muwasalimu watu wanaoishi ndani yake.

nyumba inastahili

"Nyumba" inamaanisha wale wanaoishi kwenye hiyo nyumba. "watu wanaoishi kwenye nyumba hiyo wakiwakaribisha vizuri" au kaya ile iwakiwakarimu vizuri"

amani yenu ibaki pale

Neno "pale" linamaanisha kaya. Nyumba hapa inamaanisha watu wanaoishi kwenye hiyo nyunba. Amani yenu ibaki pale" au "watu wanaoishi katika nyumba ile wataishi katika amani"

amani yenu

Hii ni amani ambayo mitume wanapaswa kumwomba Mungu awape wanaoishi katika nyumba.

Kama haistahili

Neno "pale" linamaanisha nyumba . "Nyumba" inamaanisha kaya. "ikiwa hawatawakaribisha vizuri" au ikiwa hawatawakarimu"

amani yenu iondoke pamoja nanyi

Yamkini ina maana zifuatazo: 1) Ikiwa nyumba haistahili, ndipo Mungu atazuia amani au baraka katika nyumba hiyo au 2) Ikiwa kaya haistahili, ndipo mitume walipaswa kufanya kitu, kama vile kumwomba Mungu asikubali heshima ya salaam za amani. Ikiwa lugha yako ina maana kama hii ya kurudisha salaam au matokeo, hivyo itumike hapa.

Matthew 10:14

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake cha kufanya watakapoenda kuhubiri

Na kwa wale wasiowapokea au kusikiliza

"Ikiwa hakuna watu watakaowakaribisha au kuwasikia katika mji huo"

ninyi ... yenu

Hivi ni viwakilishi vya wingi ambavyo vinamaanisha mitume kumi na mbili

kusikiliza maneno yenu

Hapa "maneno" inamaanisjha kile ambacho wanafunzi wa Yesu watasema. "kusikiliza ujumbe wenu" au "kusikiliza kile mnachotaka kusema"

mji

Unaweza kutafsiri kama ulivyofanya kwa njia hiyo hiyo

jipanguseni mavumbi ya mguuni

"jipanguseni mavumbi y a miguu yenu mnapoondoka." Hii ni ishara inayoonesha kuwa Mungu amaewakataa watu wa mji au nyumba hiyo.

kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo kwa kile ambacho Yesu atasema baadaye.

itakuwa zaidi ya kuvumilia

"mateso yatakuwa machache"

mji wa Sodoma na Gomora

Hii inamaanisha watu walioishi Sodoma na Gomora."watu ambao waliishi katika miji ya Sodoma na Gomora"

mji huo

Hii inamaanisha watu katika mji ambao hawakutaka kuwapokea mitume au kusikiliza ujumbe wao. "Watu wa mji huo ambao hawakuwapokea"

Matthew 10:16

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake. Hapa anaanza kuwaambia wao kuhusu dhiki ambayo wanatakiwa kuvumilia pindi watapoenda kuhubiri.

Angalia

Neno "Angalia" hapa linaongeza na kusisitiza ambacho kitafuatia. "Tazama"au "Sikiliza" au "Zingatia kile ninachotaka kukuambia"

Ninawatuma

Yesu anawatuma kwa kusudi maalum.

kama kondoo katikati ya mbwa mwitu

Kondoo ni wanyama wasioweza kuijhami ambao mara kwa mara hushambuliwa na mbwa mwitu. Yesu anasema kuwa watu wanaweza kuwaumiza wanafunzi wake. "Kama kondoo katikati ya mbwa mwitu hatari" au "kama kondoo katikati ya watu wenye tabia kama hizo.

muwe na hekima kama nyoka na wapole kama njiwa

Yesu awaambia wanafunzi wake ili wawe na tahadhari na wasiowamiza watu. Kama kuwafananisha wanafunzi na nyoka au na njiwa kunachanganya, basi ni vizuri kutokuutumia huu mlinganyo. "fanya kwa kuelewa na tahadhari, vile vile kwa makini na wema."

Muwe waangalifu na watu watawapeleka

Unaweza kutafsiri kwa kutumia "kwa sababu" ili kuonnesha jinsi hizi sentensi zinavyohusiana. "Muwe waangalifu na watu kwa sababu watawapeleka

Watawapeleka kwenye

"watawasaliti kwa" au "watawakabidhi Kwa" au watawakamata na kuawajaribu"

mabaraza

"mahakama" Hawa ni viongozi wa kidini au wazee ambao kwa pamoja wanalinda amani katika jamii.

watawapiga mijeledi

"kupiga kwa mijeledi"

katikati ya mbwa mwitu

AT:"katikati ya watu ambao ni kama mbwa mwitu wa hatari" au "katikati ya watu ambao watenda kama wanyama wa kutisha" au "katikati ya watu ambao watakuvamia wew"

na mtaletwa

Hii inaweza kuelezeka katika muundo tendaji "watawaleta" au "watawaburuza"

kwa ajili yangu

"kwasababu ninyi ni wangu" au "kwa sababu mnanifuata mimi"

kwao na kwa mataifa

Kiwakilishi "kwao" inamaanisha huenda wakawa "magavana au wafalme" au kwa washitaki wa kiyahudi

Matthew 10:19

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu dhiki wanayotakiwa kuvumilia pindi watapoenda kuhubiri

msi...yenu

kiwakilishi "msi" na "yenu" vinamaanisha mitume kumi na wawili

msiwe na wasiwasi

"msiwe na hofu"

jinsi gani au nini cha kuongea

"jinsi gani ya kuongea au nini cha kusema." Haya mawazo mawili yanaweza kujumuishwa:"Ni nini cha kusema"

kwa kuwa kitu cha kusema mtapewa

Hii inaweza kutafsirika katika mfumo tendaji. "Kwa kuwa Roho mtakatifu atawapa cha kusema"

kwa wakati huo

Hapa wakati" unamaanisha "muda huohuo" au "kwa muda huo"

Pindi watakapowashutumu

Kipindi watu watakapowashitaki kwenye mabaraza.""watu" hapa ni wale wale "watu"

Roho ya Mungu wako

Ikiwa muhimu, inaweza kutafsiliwa kama "Roho ya Mungu baba yako aliye mbinguni" au nyongeza inaweza kuongezwa ili kufafanua kwamba inamaanisha Roho ya Mungu baba na sio roho ya baba wa ulimwengu.

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu.

Ndani yako

"kupitia ninyi"

Matthew 10:21

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu dhiki wanayotikiwa kuvumilia pindi watakapoenda kuhubiri

Ndugu atamwinukia ndugu yake kumwua, na baba kwa mtoto wake

Kirai hiki cha "baba na mtoto wake" kinawza kutafsiriwa kama sentensi timilifumilifu. Ndugu atamwinukia ndugu na kumwua, na baba atamwinukia mtoto wake na kumwua"

kumwinukia

"saliti" au "kumtoa" Tazama ilivyotafsiriwa kwenye 10:6

kifo

Nomino dhania "kifo" inaweza kutafsiriwa uthabiti, kwa uwazi zaidi. "mahakamani il mamlaka iweze kuwahumu

kumwinukia dhidi ya

"kupigana dhidi" au "kwenda kinyume dhidi ya"

na kusababisha kuingia katika kifo

Hii inaweza kutafsiriwa katika mfumo tendaji. "na kuwaweka katika kifo" au "na wenye mamlaka kuwaweka katika kifo"

Nanyi mtachukiwa na kila mtu

Hii inaweza kutafsirika katika muundo tendaji. "Kila mtu atawachukia" au "Watu wote watawachukia ninyi"

nanyi

Hiki ni kiwakilishi cha wingi kichonamaanisha mitume kumi na mbili.

kwa sababu ya jina langu

Hapa "jina" inamaanisha ukamilfu wa nafsi "kwa sababu yangu" au "kwa sababu mlinitumaini mimi"

yeyote atakayevumilia

" atakayebaki kuwa mwaminif."u

mtu huyo ataokolewa

"yeyote atakayekuwa mwaminifu"

mji huu

Neno "hapa" halina maana ya mji maalumu. "mji mmoja"

kimbilieni mji unaofuata

"mwende mji unaofuata"

Kwa kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile ambacho Yesu atasema baadaye.

Mwana wa Adamu

Yesu anaongea juu yake mwenyewe

amekuja

"amewasili"

Matthew 10:24

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu dhiki wanayotakiwa kuvumilia wakati watakapoenda kuhubiri.

Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya bwana wake

Yesu anatumia mithali kuwafundisha wanafunzi wake ukweli wa jumla. Yesu anasisitiza kwamba wanafunzi wake wasitegeme watu kuwatendea vizuri kuliko walivyomtendea Yesu.

Mwanafunzi si mkuu kuliko mwanafunzi wake

"Mwanafunzi daima si wa mhimu kuliko mwalimu wake". Mwalimu daima ni wa mhimu kuliko mwanafunzi wake.

wala mtumwa aliye juu ya bwana wake

"na mtumwa daima si wa mhimu kuliko bwana wake" au "na bwana daima ni wa muhimu kuliko mtumwa wake"

Inatosha kwa mwanfunzi kwamba awe kama mwalimu wake

"Mwanafunzi atalizika pale atakapokuwa kama mwalimu wake"

awe kama mwalimu wake

Kama inawezekana, unaweza kueleza dhahIri jinsi mwanafunzi anavyofanyika kuwa kama mwalimu, "Ajue kma mwalimu anavyojua"

na mtumwa kama bwana wake

Kama inawezekana uieleze dhahiri jinsi mtumwa anvyoweza kuwa kama bwana ." "na mtumishi atarizika pale tu atakapokuwa na umuhimu kama Bwana wake"

Ikiwa wamwita bwana ... wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi kwa wale wa nyumba yake

Kwa mara nyingine Yesu anasisitiza kuwa kama watu walimtenda vibaya, hivyo wanafunzi wategemee kufanyiwa hivyo au zaidi.'

ni kwa kiasi gani watawakashifu watu wa nyumba yake

" majina yale wanayotumia kuwaita watu wa nyumba yake hakika yatakuwa mabaya zaidi" au "kwa hakika wataita watu wa nyumba yake majina mabaya zaidi"

Ikiwa wamemwita

"kwa watu wamemwita"

Bwana wa nyumba

Yesu anatumia hiii kama msemo kwa ajili yake

Belzabuli

Hili jina linaweza 1) likaelezwa moja kwa moja kama "Belzabuli" au "2) Kutafsiri kama asili yake, kumaanisha "shetani"

wa nyumba yake

Hii ni sitiari kwa maana ya wanafunzi wa Yesu

Matthew 10:26

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu dhiki wanayopaswa kuivumilia wakati watakapoenda kuhubiri.

msiwahofu wao

Hapa "wao" inamaanisha watu wanaowatenda vibaya wafuasi wa Yesu

hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililojifichwa ambalo halitajulikana

Hizi sentensi zote mbili zinamaanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa Mungu atayafichua mabo yote. Hii inaweza kutafasiriwa katika mafumo tendaji. "Mungu atafunua mambo ambayo watu wanayaficha."

Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba

Sentensi zote hizi mbili zinamanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa wanafunzi wanapaswa kumwambia kila mmoja kile anachowaambia wanafunzi sirini. "Waambie watu mchana kile ninachokuambia gizani, na tangazeni mkiwa juu ya nyumba kile mnchosikia kwenye masikio yenu"

Kile ninachokuambia gizani

Hapa "giza" linamaanisha "sirini" Ninachowaambia kisirisiri" au "mambo ninayowaambia peke yenu"

kile ninachokisema nuruni

Hapa neno :nuruni" linamaanisha "kwa uwazi. "Semeni kwa uwazi" au "semeni katika umma"

Kile mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu

Hii ni namna ya kusema kunakomaanisha kunong'ona. "Kile ninachowanong'onezea"

mkitangaze mkiwa juu ya nyumba

mapaa ya nyumba wakati wa Yesu yalikuwa ya bapa, hata watu wali mbali wangeweza kumsikia mtu anapokuwa anaongea kwa sauti ya juu. Hapa mapaa ya nyumba yanamaanisha mahali popote ambapo watu wanaweza kusikia. "Ongea kwa sauti katika eneo la umma ili watu wote wasikie"

Matthew 10:28

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake juu ya dhiki amabyo wanapaswa kuivumilia wakati watakapoenda kuhubiri

Melezo kwa ujumla

Hapa Yesu pia anaanza kutoa sababa kwa nini wanafunzi wake hawapaswi kuiogopa dhiki ambayo itawapata.

Msiwaogope wale wanaoua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho

Hii haina maana ya kutenganisha kati ya watu wanaoweza kuua mwili na wale wanaoweza kuua roho. Hakuna mtu anayeweza kuua roho. "Msiwaogope watu. Wanaweza kuua mwili, lakini hawawezi kuua roho"

Kuua mwili

Hii inamaanisha kusababisha mauti ya mwili. Ikiwa maneno haya ni magumu, yanaweza kutafsiriwa kama "kukua wewe" au "Kuua watu wengine."

mwili

Sehemu ya mtu inayoweza kuguswa, tofauti na roho au nafsi isiyoweza kuguswa.

kuua roho

kudhuru watu baada ya kufa

roho

sehemu ya mwanadamu ambayo haiwezi kuguswa na ambayo inaishi baada ya kifo cha mwili

mwogopeni yule anayeweza

unaweza kuongeza "kwa sababu" ili kufafanua kwa nini watu wamwogope Mungu. "Mwogopeni Mungu kwa sababu yeye anaweza"

Je, mashomoro wawili hawauzwi kwa senti ndogo

Yesu anaieleza mithali hii kwa njia ya swali kuwafundisha wanafunzi wake. "Fikiria kuhusu mashomoro . Wana thamani ndogo sana kiasi kwamba unaweza kuwanunua wawili kwa salafu kidogo.

Mashomoro

Hawa ni ndege wadogo, wanaokula mbegu. "ndege wadogowadogo"

sarafu ndogo

Hii mara nyingi inatafsiriwa kama sarafu yenye thamani ndogo kabisa katika nchi. inamaanisha sarafu ya shaba thamani yake ni sawa na sehemu ya kumi na sita ya malaipo ya kibarua. "kiasi kidogo cha fedha"

hakuna anayeweza kuanguka chini bila baba yenu kufahamu

Haya maelezo yanaweza kutafsiriwa kataika mfumo tendaji. "Baba yenu anafahamu hata shomoro mmoja akifa na kuanguka chini"

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu

Hata idadi ya nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa

Hii inaweza kuelezeka katika mfumo tendaji. "Mungu anajua hata kiasi cha nywele kichwani pako"

zimehesabiwa

"zimehesabiwa"

Mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi

"Mungu anawathamini kuliko mashomoro wengi"

Matthew 10:32

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu sababu kuhofia dhiki ambayo itawapata

yeyote atakayenikiri mbele za mtu

"yeyote atakayewaambia wengine huyo ni mwanafunzi wangu" au "Yeyote anayekubali mbele za wengine kwamba yeye ni mwamanifu wangu"

nami pia nitamkiri mbele ya baba yangu aliye mbinguni

Unaweza kuifafanua hiyo ili ieleweke wazi. "nami nitamkiri mbele za Mungu wangu aliye mbinguni kwamba hawa watu ni wangu"

Babab yangu aliye mbinguni

"Baba wa mbinguni"

Baba

Hii ni sifa muhimu ya Mungu"

yeyote atakayenikana mbele za mtu

"yeyote atakayenikana mbele za watu" au "yeye atakayenikataa mbele za watu" au "yeyote atakayekataa kunitambua mimi kwa wengine kuwa yeye ni mwanafunzi wangu"

Nami nitamkana mbele ya Babayangu wa mbinguni

Unaweza kulifafanua kwa uwazi unaoweza kueleweka. "Nitamkana mbele ya Baba aliye mbinguni kuwa huyu ni wangu"

Matthew 10:34

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu sababu kutohofia dhiki ambayo itawapata.

Msifikiri

"Msidhani" au "msilazimike kufikiri"

duniani

Hii inamaanisha watu wanaoishi duniani. "kwa watu wa duniani" au "kwa watu"

upanga

Hii inamaanisha mgawanyiko, mapigano, na mauji kati ya watu

weka

"kugeuka" au "kugawanya" au "kutenganisha"

mtu dhidi ya baba yake

"mwana dhidi ya baba yake"

Adui wa mtu

"Adui wa mtu" au "Adui mbaya wa mtu"

wale wa nyumbani mwake

"watu wa familia yake"

Matthew 10:37

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu sababu kutohofia dhiki itakayowapata.

Yeye ambaye ....hanistahili

Hapa "ana" anamaanisha mtu yeyote kwa ujumla. "Wale ambao ... hawastahili" au "Kama uta... haustahili"

anampenda

Neno la "upendo" hapa linamaanisha upendo wa ndugu" au "upendo kutoka kwa rafiki." "KuMjali" au "aliyejitoa kwa" mwenye kupenda"

anayestahili

"anafaa kuwa wangu" au "anastahili kuwa mwanafunzi wangu"

beba msalaba na kunifuata

"bebea msalaba wake na kunifuata" Huu ni mfano wa kuwa tayari kufa. Kubeba msalalba inamaanisha utayari wa kuteseka na kufa. "lazima anitii kiasi cha kukubali kuteseka na kufa"

beba

"chukua" au "beba na kunyanyua"

Yeye atakayetafuta...atayapoteza...yeye atakayeyapoteza...atayapata

Yesu anatumia mithali kuwafundisha wanafunzi wake. Haya yatafsiriwa kwa maneno machache kwa kadri iwezekanavyo. "Wale wanaotafuta... watayapoteza ... wale wanaoyapoteza ... watayapata" au "wakaoyapata ... uta watakaopoteza ... watapata" au "ikiwa utayapata ... utakosa ... ikiwa utayakosa...utayapata."

atayapata

Hii ni sitiari ya "kutunza" au "kuhifadhi"" jaribu kuhifadhi" au "jaribu kutunza"

atayapoteza

Hii haina maana kwamba mtu atakufa. Ni sitiari " inayomaanisha kuwa mtu hatakuwa na maisha mazuri ya kiroho na Mungu. "Hatakuwa na maisha ya kweli"

anayepoteza maisha yake

Hii haimanishi kufa. Ni sitiari Inayomaanisha mtu kumtii Yesu ni muhimu zaidi kuliko maisha yake. "ambaye anayejikana"

kwa ajili yangu

"kwa sababu ananitumaini mimi" au "kwa ajili yangu" au "kwa sababu yangu" Hili ni wazo lile lile kama "kwa ajili yangu" katika 10:6

yeye ambaye hatabeba ...hana

Tafsiri nyingine:"Wale ambao hawatabeba....sio" au "ikiwa hautabeba...wewe sio" au "endapo utakapobeba ... wewe sio

atayapata

Huu msemo maana yake "atapata maisha ya kweli"

Matthew 10:40

Sentensi unganishi.

Yesu anaendelea kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu kutohofia dhiki itakayowakabili.

Yeye atakaye

Neno "yeye" linamaanisha mtu yeyote. "yeyote" au "yeyote ambaye" au " ambaye"

atakayewakaribisha

Inamaanisha kumkaribisha mtu kama mgeni

Wa

Kiwakilishi "wa" kinamaanisha mitume kumi na wawili ambao Yesu anawaaambia.

ananikaribisha mimi

Yesu anamaanisha ni sawa na kumkaribisha yeye. "ni kama ananikaribisha mimi" au "ni kama vile alikuwa ananikaribisha mimi"

kumkaribisha yeye aliyenituma

Hii inamaanisha wakati mtu anamkaribisha Yesu ni sawa na kumkaribisha Mungu. "ni kama vile kumkaribisha Mungu aliyenituma"

Kwa sababu ni nabii

Hapa kiwakilishi cha "ni" kinamaanisha mtu anayekaribishwa.

thawabu ya nabii

Hii inamaanisha zawadi ambayo Mungu anampa nabii. wala siyo zawadi ambayo nabii anampatia mtu mwingine.

mtu wa haki

Hapa "wa" haimaanishi mtu anayekaribisha. Inamaaanisha mtu anayekaribishwa.

thawabu ya mtu wa haki

Hii inamaanisha zawadi ambayo Mungu humpa mtu wa haki, siyo zawadi ambayo mtu wa haki humpatia mtu mwingine.

Matthew 10:42

Sentensi unganishi

Yesu anamalizia kuwaelekeza wanafunzi wake kuhusu kitu cha kufanya na nini watarajie watakapoenda kuhubiri.

yeyote atakayempatia

"yeyote ambaye atampatia."

mmoja wa wadogo hawa

"mmoja wa hawa wanyenyekevu" au "hawa wasio wa muhimu," Kirai "mmoja wa" mmoja kati ya wanafunzi waYesu.

kweli ninwaambia

"Ninawambia ukweli." Kirai hiki kinongeza msisitizo wa kile Yesu atakachokisema baadaye.

hawezi... kukosa thawabu yake

Kiwakiloishi "ha" na "yake" kinamaanisha mtu yule anayetoa.

yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake

"kwamba mtu hakika atapokea thawabu yake"

hawezi kukosa kwa njia yeyote

"Mungu hatamkana." "kukanwa" Hii haimanishi kutoweka kwa mali. Hii inaweza kuelezeka kwa mfumo tendaji. "Kwa hakika Mungu atampatia"


Translation Questions

Matthew 10:1

Mamlaka gani Yesu aliwapa wanafunzi wake kumi na wawili?

Yesu aliwapa wanafunzi wake kumi na wawili mamlaka ya kutoa pepo wachafu, na kuponya magonjwa ya kila namna.

Matthew 10:2

Ni jina gani la mwanafunzi ambaye angemsaliti Yesu?

Jina la mwanafunzi ambaye angemsaliti Yesu alikuwa Yuda Iskariote.

Matthew 10:5

Yesu aliwatuma wapi wanafunzi wake kwa wakati huu?

Yesu aliwatuma wanafunzi wake kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli tu.

Matthew 10:8

Wanafunzi walipaswa kubeba pesa yoyote au mavazi ya ziada?

Hapana, wanafunzi hawakupaswa kubeba pesa yoyote au mavazi ya ziada.

Matthew 10:11

Wanafunzi wa Yesu walipaswa kukaa wapi walipokwenda kijiji kwa kijiji?

Wanafunzi walipasa kutafuta mtu ambaye ni anayestahili katika kijiji na kukaa mpaka walipoondoka.

Matthew 10:14

Kutakuwa na hukumu gani katika miji ambayo haikuwakaribisha wanafunzi au kuwasikiliza maneno yao?

Hukumu katika miji ambayo haikuwapokea wanafunzi au kusikiliza maneno yao itakuwa mbaya zaidi kuliko hukumu ya Sodoma na Gomora.

Matthew 10:16

Yesu alisema watu wangeliwatendea nini wanafunzi?

Yesu alisema watu wangewapeleka wanafunzi kwenye mabaraza, watawapiga na kuwapeleka mbele ya wakuu na wafalme.

Matthew 10:19

Nani ataongea ndani ya wanafunzi watakapokuwa wamekamatwa?

Roho wa Baba ataongea ndani ya wanafunzi watakapokuwa wamekamatwa

Matthew 10:21

Yesu alisema ni kina nani hatimaye wataokolewa?

Yesu alisema wataokolewa wale watakaovumilia hadi mwisho.

Matthew 10:24

Kwa namna gani wale waliomchukia Yesu wangewatendea wanafunzi wa Yesu?

Wale waliomchukia Yesu pia wangewachukia wanafunzi wake.

Matthew 10:28

Je ni nani Yesu alisema tusiwaogope?

Tusiwaogope wale wauao mwili lakini hawawezi kuua roho.

Je ni nani Yesu alisema tumwogope?

Tunapaswa kumwogopa yeye awezaye kuangamiza mwili na roho katika jehanamu

Matthew 10:32

Je Yesu atafanya nini kwa kila mtu anaye mkiri mbele za watu?

Yesu atamkiri yeye mbele za Baba yake wa mbinguni

Je Yesu atafanya nini kwa kila mtu anaye mkana mbele za watu?

Yesu pia atamkana mtu huyo mbele Baba wa mbinguni

Matthew 10:34

Ni migawanyiko ya aina gani Yesu alisema alikuja kuileta?

Yesu alisema kwamba alikuja kuleta mgawanyiko hata ndani ya familia.

Matthew 10:37

Mtu anayepoteza maisha yake kwa ajili ya Yesu atapata nini?

Mtu anayepoteza maisha yake kwa ajili ya Yesu atayapata maisha yake.

Matthew 10:42

Nini atakachopokea yule anaye toa hata kikombe cha maji baridi kwa mwanafunzi asiye na umuhimu ?

Mtu ambaye humpatia hata kikombe cha maji baridi kwa mwanafunzi asiye na umuhimu atapokea zawadi yake.


11

1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka pale kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2Na Yohana akiwa gerezani aliposikia habari juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,3na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”

4Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamwambie Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.5Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, viziwi wanasikia tena, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.6Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.

7Wakati watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, “Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa, matete likitikiswa na upepo?8Lakini nini mlikwenda kuona huko, mtu aliyevaa mavazi mororo? Hakika, wale wavaao mavazi mororo hukaa katika nyumba za wafalme.9Lakini mliondoka kuona nini - Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.10Huyu ndiye aliyeandikiwa, ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.’

11Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.12Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.13Kwa kuwa manabii na sheria, walikuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.14Na kama mko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.15Aliye na masikio ya kusikia na asikie.

16Nikifananishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana17na kusema, ‘Tuliwapigia filimbi na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.’18Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, ‘Ana pepo.’19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema, ‘Angalia, ni mtu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!’ Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.”

20Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu,21Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yaliyofanyika kwenu yangefanyika Tiro na Sidoni, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.22Lakini nawaambia itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili siku ya hukumu kuliko ninyi.23Wewe, Kapernaumu, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana, utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo.24Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.

25Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyaweka wazi kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.26Baba, kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.

27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.28Njooni kwangu, ninyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu.30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”


Mathayo 11 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri huingiza kidogo mistari ya nukuu kutoka kwa Agano la Kale. ULB inafanya hivyo kwa mistari ya nukuu zilizotajwa katika 11:10.

Wasomi wengine wanaamini kwamba Mathayo 11:20 huanzisha hatua mpya katika huduma ya Kristo kwa sababu ya kukataliwa kwake na Israeli.

Dhana maalum katika sura hii

Ufunuo uliofichwa

Baada ya Mathayo 11:20, Yesu anaanza kufunua habari kumhusu yeye mwenyewe na kuhusu mipango ya Mungu Baba, huku akificha habari hii kwa wale wanaomkataa. (Angalia: Mathayo 11:25)

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ufalme wa mbinguni umekaribia"

Maneno haya yana umuhimu mkubwa wa kitheolojia. Wataalam wanajadili ikiwa "ufalme wa mbinguni" ulikuwepo wakati huu au bado unakuja. Tafsiri za Kiingereza mara nyingi hutumia maneno "karibu," lakini hii inaweza kusababisha changamoto katika kutafsiri. Matoleo mengine hutumia maneno "inakaribia" na "yamekaribia."

Links:


Matthew 11:1

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya wa simulizi amabapo mwandishi anaonesha jinsi ambavyo Yesu aliwaijibu wanafunzi wa Yohana Mbatizaji.

Ikawa baada ya

Hiki kirai kinaibadilisha kutoka habari ya mafundisho ya Yesu kwenda kile kilichotokea baadaye. "Kisha" au "baadaye"

Kuwaelekeza

"kufundisha" au "kuamurisha".

wanafunzi wake kumi na mbili.

Hii inawahusu wale mitume kumi na wawili waliochaguliwa na Yesu.

katika miji yao

Kimilikishi "yao" kinamaanisha Wayahudi wote kwa ujumla

Sasa

Neno hili limetumika hapa kuonesha mwanzo katika habari kuu. Mathayo anaanza kusimulia habari mpaya

Na Yohana akiwa gerezani aliposikia juu ya

"Wakati Yohana, akiwa gerezani aliposikia juu ya" au "Yohana alipoambiwa na mtu, wakati akiwa gerezani kuhusu, "Ingawa Mathayo hajawaambia wasomaji kwamba mfalme Herode alikuwa amemfunga gerezani Yohana mbatizaji, wasomaji wa kwanza wangekuwa wanaielewa habari na maana yake. Mathayo atatoa habari za Yohana mbatizaji baadaye, kwa hiyo yawezekana si vizuri kufafanua zaidi hapa.

alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake.

Yohana Mbatizaji aliwatuma wanafunzi wake ujumbe kumpelekea Yesu.

na wakamuuliza

kiwakilishi "mu'' kinamrejea Yesu.

Wewe ni yule ajaye

"Wewe ndiye yule amabye tunamtarajia kuja." Hii ni namna nyingine ya kumaanisha Masihi au Kristo.

au kuna mwiingine tunayepaswa kumtazamia

''Tunapaswa kumtazamia mwingine." kiwakilishi "tu" kinarejerea ,wayahudi wote, siyo wanafunzi wa Yohana pekee.

Matthew 11:4

mkamtaarifu Yohana

"mwambieni Yohana''

wakoma wanatakaswa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Ninawaponya wenye ukoma"

Watu waliokufa wanafufuliwa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. " Ninawafanya wale waliokufa kuwa hai tena

Watu wahitaji wanahubiriwa habari njema

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji "Ninawaambia wahitaji"

yule asiyeona shaka juu yangu

Hapa neno "shaka" ni nahau inayomaanisha kupoteza imani. "mtu asiyeachca kuamini kwa sababu ya kile ninachofanya" au "mtu asiyeona mashaka kwa sababu yangu"

Matthew 11:7

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kusema na makutano kuhusu Yohana mbatizaji.

Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa tete likitikiswa na upepo?

Yesu alitumia swali ili kuwafanya watu wafikiri kuhusu Yohana kuwa ni mtu wa aina gani." Kwa hakika hamkuenda jangwani kuona tete ... upepo.

tete likitikiswa na upepo

Hii inaweza kumaanisha 1) majani halisi ya mto Yorodani au 2) Yesu anatumia sitiari kumaanisha aina ya mtu. "mtu anayebadili fikra zake ni kama tete linalopeperushwa na upepo.

likitikiswa na upepo

Hii inaweza kutafsirwa katika mfumo tendaji. "yumbishwa na upepo" au "peperushwa na upepo"

Lakini ni nini mlikwenda kuona _ mtu aliyevaa mavazi?

Yesu anatumia swali ili kuwafanya watu wafikiri juu ya Yohana kuwa ni mtu wa aina gani. Kwa kweli hamkwenda jangwani ili kuona mtu ... aliyevaa?

aliyevaa mavazi mororo

"kuvaa mavazi yenye gharama kubwa." Watu majiri walivaa mavazi ya aina hii.

Hakika

Hili neno, linaongezea msisitizo kwa kile kinachofuata. "kwa kweli"

nyumba za wafalme

"ikulu za wafalme"

Matthew 11:9

Sentesi unganishi:

Yesu aliendelea kuongea na umati kuhusu Yohana Mbatizaji.

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 10, Yesu anamnukuru nabii Malaki kuonyesha kuwa maisha na huduma ya Yohana imetimiza unabii.

Lakini mliondoka kuona nini--nabii?

Yesu anatumia swali ili kuwafikirisha watu juu ya Yohana mbatizaji kuwa ni mtu wa aina gani. "Lakinini kweli kwamba mlienda jajngwani kumuona nabii"

Lakini mlienda nje kuona nini--nabii? Ndiyo, nawaambia nyinyi.

Kiwakilishi cha wingi ''nyinyi'' inarejelea kwa katika hali zote.

ni zaidi ya nabii

Hii inaweza kutafsirika kama sentensi timilifu. "Siyo nabii wa kawaida" au ''siyo mtu wa kawaida'' au ''ni wa muhimu kuliko nabii wa kawaida''

huyu ndiye aliye andikiwa

Hii inaweza kutafsirika katik mfumo tendaji. "Hiki ndicho nabii Malaki aliandika zamamni za kale kuhusu Yohana mbatizaji"

namtuma mjumbe wangu

Kiwakilishi ''na'' na ''wangu'' kinamrejea Mungu. Malaki ananukuu ambacho Mungu alisema.

mbele ya uso wako

Kiwakilishi "wako" ni cha umoja kwa sababu Mungu alikuwa anasema juu ya Masihi katika nukuu.vPia "uso" inamaanisha nafsi timilifu, "mbele yako" au "kutangulia"

ataandaa njia yako

Hii ni sitiari inayomaanisha kuwa mjumbe atawaandaa watu kupokea ujumbe wa Masihi.

Matthew 11:11

Sentensi Unganishi:

Yesu aliendelea kuwaambia makutano juu ya Yohana Mbatizaji

Mimi nawaambia ukweli

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye.

kati ya waliozaliwa na wanwake

Hii ni namna ya inayomaanisha watu wote. "kati ya watu wote waliopata kuishi"

Hakuna aliye mkuu kuliko Yohana mbatizaji

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. ''Yohana Mbatizaji ni mkuu zaidi" au " Yohana mbatizaji ni wa muhimu zaidi".

aliyemdogo katika ufalme wa mbinguni

Ha " ufalme wa mbinguni" unamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. Kirai "ufalme wa mbinguni" kimetumika katika injili ya Mathayo tu. Kama inawezekana jaribu kutumia "mbinguni" unapotafsiri. "aliye mdogo kabisa katika utawala wa Mungu wetu mbinguni"

ni mkuu kuliko yeye

'' wa muhimu kuliko Yohana''

Tokea siku za Yohana Mbatizajihadi leo

''Tokea muda ambao Yohana alianza kuhubiri ujumbe''

ufalme wa mbinguni ni wa nguvu, na wenye nguvu huuchukua kwa nguvu

Kuna maana nyingi zinzazoweza kumaanisha katika mstari huu. 1) Watu wengine huutumia ufalme wa Mungu kwa malengo yao binafsi. na kwamba wako tayari kutumia nguvu dhidi ya watu wengine ili kutimiza hitaji hili. 2)Tafsiri zingine zingine zinatumia maana sahihi kwamba wito wa kuingia katika ufalme wa mbinguni kimekuwa ni kitu cha muhimu, kwamba watu lazima wapokee kwa kuzingatia kabisa. ili kuupokea wito na kuzuia majaribu ya kufanya uovu. 3 )Watu wenye nguvu wanawadhuru watu wa Mungu na kujaribu kumzuia Mungu asitawale.

Matthew 11:13

Sentensi unganishi

Yesu aliendelea kuongea na umati juu ya Yohana Mbatizaji.

kwa kuwa manabii na sheria, imekuwa ikitabiri mpka kwa Yohana

Hapa neno " manabii na sheria"linamaanisha kile ambacho manabii na Musa waliandika katika maandiko. "Kwa kuwa haya ndiyo mambo ambayo manabii na Musa walitabiri katika maandiko mpaka wakati wa Yohana mbatizaji

na kama mko

Kiwakilishi ''mko''kinarejelea watu katika umati.

huyu ni Eliya, yule ajaye

''Hii inarejelea kwa Yohana Mbatizaji. Hii haimaanishi Yohana Mbatizaji ni sawa na Eliya. Yesu anamaanisha Yohana mbatizaji anatimiza unabii juu ya "Eliya ajaye" au "Eliya anayefuata". "Wakati nabii Malaki aliposema kuwa Eliya atarudi, alikuwa akiongea juu ya Yohana mbatizaji"

Aliye na masiko ya kusikia

Hii ni namna ya kumwambia kila anayesikilza. ''Kila anayenisikiliza''

na asike

Hapa ''asikie" inamaanisha kuwa msikivu. " lazima awe mwangalifu kwa kile nisemacho''

Matthew 11:16

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuongea na makutano juu ya Yohana Mbatizaji.

Nikilinganishe na nini

Yesu anaitumia swali kutoa mlinganisho kati ya watu wa nyakati zile na kile amabacho watoto wanaweza kusema katika eneo la soko. "Hivi ndivyo kizazi hiki kilivyo"

kizazi hiki

''watu wanaoishi sasa'' au ''watu hawa'' au ''ninyi watu wa kizazi hiki''

Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni ... na hamkulia

Yesu anatumia mfano kuwaelezea watu waliokuwa hai kipindi hicho. Anawalinganisha na kikundi cha watoto wanaojaribu kuwavuta watoto wengine ili wacheze nao. Lakini haijarishi aina ya mbinu yeyote wanayotumia, wale watoto wengine hawataungana nao. Yesu anamaanisha kuwa haijalishi kama Mungu alimtuma mtu kama Yohana mbatizaji, anaishi nyikani na kufunga, au mtu kama Yesu, ambaye anasherehekea na wenye dhambi bila kufunga. Watu, hususani Mafarisayo na viongozi wa dini, bado wanabaki wasumbufu na wanakataa kuupokea ukweli wa Mungu

maeneo ya soko

eneo kubwa, la wazi ambapo watu walikuja kuuza na kununu bidhaa zao.

tuliwapigia zomari

''tu'' inarejelea watoto waliokuwa wamekaa katika maeneo ya soko. ''wa'' ni wingi na inarejelea lile kundi lingine la watoto

na hamukucheza

''lakini hamukucheza ule muziki mzuri''

tuliomboleza

Hii inamaanisha waliimba nyimbo za huzuni kama vile wanawake wafanyavyo kwenye mazishi.

na hamukulia

''lakini hamukulia pamoja nasi''

Matthew 11:18

Sentensi unganishi:

Yesu anahitimisha kuongea na makutano kuhusu Yohana Mbatizaji.

bila kula mkate au kunywa mvinyo

Hapa "mkate" unamaanisha chakula. Haimanishi kuwa Yohana alikuwa hali chakula. Inamaanisha kuwa alikuwa anafunga mara kwa mara na alipofungua hakula vizuri, chakula cha gharama. "Mfungo endelevu na kutokunywa pombe" au "kutokula chakula kizuri na kutokunywa divai"

walisema, 'ana pepo.'

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya mojakwa moja. ''wanasema kwamba ana pepo'' au ''walimtuhumu kuwa na pepo.''

wanasema

Matukio yote ya "wali" yanamaanisha watu wa kizazi kile, na zaidi sana mafarisayo na viongozi wa dini.

Mwana wa Adamu

Yesu anamaanisha yeye mwenyewe. " Mimi mwana wa Adamu"

alikuja akila nakunywa

Hiki ni kinyume cha tabia ya Yohana. Hii ni zaidi ya kula kiasi cha kawaida cha chakula na kinywaji. Inamaanisha Yesu alisherehekea na kufurahia chakula na kinywaji kizuri kama vile watu wengine walivyofanya.

wakasema, anagalia, ni mtu mlaji

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu ya moja kwa moja. "wanasema kuwa ni mlaji" "wanamtuhumu kuwa anakula sana" Kama ulitafasiri "Mwana wa mtu" kama "Mimi, Mwana wa mtu," Ile nukuu ya moja kwa moja inaweza kutafsiriwa kama "wanasema kwamba mimi ni mlaji"

mlevi

"mlevi" au "hunywa pombe nyingi daima."

Lakini hekima huthibitishwa kwa mataendo yake

Hii ni mithali ambayo Yesu anaitumia katika mazingira haya, kwa sababu watu waliomkataa yeye na Yohana walikuwa hawapati hekima. Yesu na Yohana mbatizaji ni watu wa hekima, na ,matokeo ya matendo yao yanathibitisha.

Hekima huthibitiswa kwa matendo yake

Hapa "hekima" imefafanuliwa kama mwanamke aliyethibitishwa kuwa ni mwema kwa matendo yake. Yesu anamaanisha kuwa matokeo ya matendo ya mtu huthibitisha kuwa ni mwenye hekima. "Hii inawza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Matokeo ya matendo ya mtu humthibitisha kuwa ni mwenye hekima"

hekima inaonekana

Haya maelezo, Yesu anafafanua hekima kama vile ilikuwa ni mwanamke, haitumiki hapa kwa namna kwamba hekima inatoa haki mbele ya Mungu ila kwamba hekima inaonekana haki.

Matthew 11:20

Maelezo kwa ujumla:

Yesu alianza kuwakemea watu wa miji ambayo alianza kufanya miujiza.

kukemea miji

Hapa "miji" inamaanisha watu walioishi kwenye hiyo miji. "alikemea watu wa miji hiyo"

miji

''miji''

ambamo baadhi ya matendo yake makuu yalitendekea

Hii inaweza kutafsiriwa kwa mfumo tendaji ''ambamo baadhi ya matendo yake makuu yalitendekea''

Matendo makuu

" matendo makubwa" au " kazi za nguvu ya Mungu" au "miujiza"

Ole kwako, Kolazini! Ole kwako, Bethsaiida!

Yesu anaongea kiasi kwamba watu wa miji ya Kolazini na Bethsaida walikuwa pale wakimsikiliza, lakini hawakuwa wao.

kwa sababu hawakutubu

Kiwakilishi ''hawa'' inarejelea kwa watu wa miji ile ambayo haikutubu.

Kama matendo makuu yangetendeka ... kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu

Yesu anafafanua kwa kubuni kuwa kama yangekuwa yametokea huko nyuma, lakini haikotokea

Kama matendo makuu yangetokea Tiro na Sidoni yale yaliyotendeka kwako

Hii inaweza kutafsiriwa kwa mfumo tendaji. "Kama ningefanya matendo makubwa katika watu wa Tiro na Sidoni ambayo nimeyafanya kwenu"

Yale yaliyotendeka kwako ... kwako

Kiwakilishi cha "kwako" ni cha wingi na kinamaanisha Korazini na Bethisaida. Kama tafsiri hii si kawaida ya lugha yako, utumie neno lenye maana mbili likimaanisha miji miwili au kiwakilishi cha wingi cha "ninyi" kwa kumaanisha watu wa miji ile.

Wangekuwa wametubu zamani

Kiwakilishi "wa"kinarejelea watu wa Tiro na Sidoni.

wangetubu

"inaonesha walihuzunishwa na dhambi zao"

Itakuwa uvumilivu kwa Tiro na Sidonisiku ya hukumu kuliko kwako

Hapa " Tiro na Sidoni'' zinamaanisha watu wanoishi kwenye hiyo miji. "Mungu ataonyesha huruma zaidi kwa watu wa Tiro na Sidoni katika siku ya hukumu kuliko ninyi" au "Mungu atawapa adhabu kalizadi katika siku ya hukumu kuliko watu wa Tiro na Sidoni"

kuliko kwako

maelezo kusudiwa yangewekwa wazi. "kuliko kwako, kwas sabasbu haukutubu na kuniamini, ingawa ulioniona nikifanya miujiza"

Matthew 11:23

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kukemea miji ambayo miujiza yake ilitendeka karibuni.

Wewe, Kapernaum

Yesu sasa anaongea na watu wa mji wa Kapernaum kama vile walikuwa wanamsikiliza, lakini walikuwa hawasikilizi. Kiwakilishi ''wewe'' ni cha umoja kinarejelea Kapernaum kwa mistari yote miwili.

wewe

Matukio yote ya kiwakilishi cha "wewe" yakao katika umoja. Kama kinatumika kila mahali kuonyesha watu wa mji, basi kiwakilishi cha wewe kitafsiriwe katika wingi wake

Kapernaum...Sodoma

Majina ya miji hii yametumika kumaanisha watu waliokuwa wanaishi Kapernaum na Sodoma.

unadhani utainuliwa hadi mbinguni?

"unadhani utainuliwa hadi mbinguni ?" Yesu anatumia balagha kuwakemea watu wa Kapernaum kwa majivuno yao. "inaweza pia kutumika kwa mfumo tendaji. "huwezi kujiinua mwenyewe hadi mbinguni" au "sifa za watu wengine haziwezi kukuinua hadi mbinguni kama unavyodhani atafanya"

utashuswa hadi chini kuzimu

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji ''Mungu atakupeleka hadi kuzimu.''

Kama katika Sodoma ... ingekuwepe hadi leo

Yesu anatumia mazingira ya kubuni ambayo yangetokea katika siku zilizopita, lakini haikutokea.

matendo makuu

''''matendo makuu'' au ''kazi ya nguvu za Mungu'' au "miujiza"

ingekuwepo hadi leo

Kiwakilishi ''inge'' kinarejelea kwa mji wa Sodoma

nasema kwako

Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoa kusimama katika siku ya hukumu kuliko wewe

Hapa "nchi ya Sodoma" inamaansha watu walioishi kule. ''Mungu ataonyesha rehema kwa watu wa Sodoma katika siku ya hukumu kuliko kwako'' au Mungu atawapa adhabu kali zaidi katika siku ya hukumu kuliko watu wa Sodoma.''

kuliko wewe

Taarifa zilizofumbwa ziwekwe wazi. "kwa sababu haukutubu na kuniamini, ingawa uliniona nikifanya miujiza"

Matthew 11:25

Maelezo kwa ujumla:

katika mstari wa 25 na 26, Yesu anomba kwa baba yake aliye mbinguni wakati akiwa bado katika uwepo wa makutano. Katika mstari wa 27, anaanza kusema na watu tena.

Baba

Hi ni sifa muhimu ya Mungu

Bwana wa mbingu na nchi

"Bwana anayetawala mbingu na nchi" Kirai cha mbingu na nchi ni cha mlinganyo wa jumla amabcho kinaonesha watu wote na vitu vyote duniani. ''Bwana atawalaye ulimwenguni kote"

uliwaficha mambo haya ... na kuyafunua

Haiko wazi ina maanisha nini kwa ''mambo haya.'' Kama lugha yako inahitaji kuweka maana halisi, tafsiri nzuri ni hii ''umeuficha ukweli huu na kuwafunulia"

umewaficha mambo haya

''umewaficha mambo haya '' au ''haujafanya mambo haya kueleweka kwao.'' Hili tendo ni kinyume cha ''kufunuliwa.''

wenye hekima na ufahamu

Hizi nomino sifa zinzweza kutafasiriwa kama visifa ''kutokawatu wenye hekima na ufahamu.''

na kuyafunua

"kuyafanya yafahamike." kiwakilisha "ya" kinamaanisha "mambo haya" viko mwanzoni katika mstari huu.

kwa wasio na elimu,

"kwa wajinga"

kama watoto wadogo

Yesu anamlinganisha mtu asiye na elimu na mtoto mdogo. Yesu anasisitiza kwamba wengi wa wale wanaomwamini ni watu wasio na elimu au wanaojidhania kuwa si wenye elimu

kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako

kupendeza machoni pako - Hi kirai "machoni pako" ni sentensi mbadala ionyeshayo jinsi mtu apendavyo kitu kuwa ni cha muhimu. "kwa vile ilikupendeza kuwa ni vizuri kufanya hivi"

Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa baba yangu

Hii inaweza kutafasiriwa kwa muundo tendaji: ''Baba yangu amekabidhi mambo yote kwangu'' au ''Baba yangu ameweka kila kitu kwangu."

Mambo yote

Maana kusudiwa ni 1)Mungu Baba amefunua kila kitu kuhusu yeye na ufalme wake kwa Yesu. aua 2) Mungu ametoa mamlaka yote kwa Yesu

Baba yangu

Hii ni sifa muhimu ya Mungu amabyo inaonyesha uhusiano kati ya Yesu na Mongu

hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba

''Ni Baba pekee amjuaye Mwana.''

hakuna ajuaye

Nyakati zote Yesu hutumia kirai hiki, neno "ajuaye" linamaanisha zaidi ya kumjua mtu. Linamaanisha kumjua mtu kwa undani kwa sababu wanauhusiano maalumu

Mwana pekee

Yesu alikuwa anajirejelea yeye mwenyewe binafsi katika nafsi ya tatu.

mwana

Hii ni sifa ya muhimu ya Yesu mwana wa Mungu

hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba

''Ni Mwana pekee amjuye Baba''

hakuna amjuaye Baba isipokuwa mwana pekee

"ni mwana pekeeamjuaye Baba

na yeyote ambaye Mwana ana hamu kumfunulia

"na watu wale ambao mwana anapenda kuwafunulia jinsi Mungu alivyo"

Matthew 11:28

Sentensi unganishi

Yesu anamalizia kuongea na makutano.

ninyi nyote

Viwakilishi vyote vya "niniyi" ni vya wingi

mnaolemewa na mzigo mizito

Yesu anaongea kwa watu kama na wanyama, amabao bwana zao wamewabebesha mizigo migongoni mwao. Hii ni sitiari kwa ajili ya Sheria na kanuni ambaazo viongozi wa Kiyahudi waliwabebesha watu ili kuzitii. "msumbukao na sheria ambazo mmebeshwa na viongozi wa dini"

Nitawapumzisha

''Nitawaruhusu nyinyi kupumzika kazi na mizigo''

Mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo

Hapa neno"mpole" na "mnyenyekevu wa moyo" ki msingi yanamaanisha kitu kilekile. Yesu anayaunganisha kuongeza msisitizo kuwa atawajali kwa upole zaidi kuliko vioingozi wa . dini. "mimi ni mpole na mnyenyekevu" au "mimi ni mpole sana"

Jitieni nira yangu

Yesu anaendelea kutumia sitiari. Yesu anawakaribisha watu kuwa wanafunziwake na kumfuata"

mtapata pumziko la nafsi zenu

Hapa "nafsi" inamaanisha mtu kamili. "mtapumzikia ninyi wenyewe" au "mtaweza kupumzika"

kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi

Virai vyote hivi vinamaanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa ni rahisi kumtii yeye kuliko sheria za Wayahudi. "kile nitakacho wabebesha kitakuwa ni chepesi"

Mzigo wangu ni mwepesi

Neno "mwepesi" hapa ni kinyume cha kizito, siyo kinyume cha giza.


Translation Questions

Matthew 11:1

Yesu alikamilisha jambo gani kabla ya kuondoka kwenda kufundisha na kuhubiri kwenye miji?

Kabla ya kuondoka Yesu akamilisha kuwapa maelekezo wanafunzi wake kumi na wawili.

Yohana Mbatizaji alituma ujumbe gani kwa Yesu?

Yohana Mbatizaji alituma ujumbe, "Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?"

Matthew 11:4

Yesu alisema kitu gani kilikuwa kinatokea kama ushahidi kwa yule ajaye?

Yesu alisema wagonjwa walikuwa wanaponywa, wafu wanafufufliwa, na wahitaji kuhubiriwa habari njema.

Yesu aliahidi nini kwa kwa wale wasiojikwaa dhidi yake?

Yesu aliahidi baraka kwa wale wasiojikwaa dhidi yake.

Matthew 11:9

Yesu alisema Yohana Mbatizaji alikuwa na wajibu gani katika maisha yake?

Yesu alisema Yohana Mbatizaji alikuwa ni mjumbe aliyetabiliwa ambaye angeandaa njia kabla ya kuja yule ajaye.

Matthew 11:13

Yesu alisema Yohana Mbatizaji alikuwa ni nani?

Yesu alisema kuwa Yohana Mbatizaji alikuwa Eliya.

Matthew 11:18

Watu wa kizazi kile walisema nini kuhusu Yohana Mbatizaji aliyekuja hali mkate wala kunywa divai?

Watu wa kizazi kile walisema Yohana alikuwa na pepo

Watu wa kizazi kile walisema nini kuhusu Yesu aliyekuja akila na kunywa?

KWatu wa kizazi kile walisema mrafi na mlevi, na rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi.

Matthew 11:20

Yesu alitamka ninki kuhusu miji ambayo alifanya matendo makuu lakini bado walikuwa hawajatubu?

Yesu aliikemea miji ile ambayo alifanya matendo makuu lakini walikuwa bado hawajatubu.

Matthew 11:25

Yesu alimtukuza Baba kwa kumficha nani ufalme wa mbinguni?

Yesu alimtukuza Baba kwa kuwaficha wenye hekima na akili habari za ufalme wa mbinguni.

Yesu alimtukuza Baba kwa kumfunulia nani ufalme wa mbinguni?

Yesu alimtukuza Baba kwa kuwafunua habari za ufalme wa mbinguni wasio na elimu, na ambao wapo kama watoto wadogo

Yesu alisema ni nani anayemjua Baba?

Yesu alisema yeye ndiye anayemjua Baba na yeyote ambaye anapenda kumfunulia.

Matthew 11:28

Yesu aliahidi pumziko kwa nani?

Yesua aliahidi pumziko kwa wote wanaosumbuka na wenye mizigo mizito.


12

1Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.2Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda yasiyo ruhusiwa siku ya Sabato.”

3Lakini Yesu akawaambia, “Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao?4Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa makuhani?5Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato makuhani ndani ya hekalu huiharibu Sabato, lakini hawana hatia?6Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa.7Kama mngelifahamu hii ina maanisha nini, ‘Nataka rehema na siyo dhabihu,’ msingaliwahukumu wasio na hatia.8Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

9Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao.10Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi.

11Yesu akawaambia, “Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?12Je, ni kipi chenye thamani zaidi, kwani mtu si zaidi ya kondoo? Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”13Kisha Yesu akamwambia yule mtu,” Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.14Lakini Mafarisayo wakatoka nje na wakapanga jinsi ya kumwangamiza, walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua.

15Yesu alipojua hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaponya wote.16Aliwaagiza wasije wakamfanya ajulikane kwa wengine.17Kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema,
18“Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa mataifa.
19Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani.
20Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda.
21Na mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake.”

22Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona.23Umati wote walishangaa na kusema, “Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?”

24Lakini wakati Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, “Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo.”

25Lakini Yesu alijua fikra zao na kuwaambia, “Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama.26Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe.27Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu watatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu.28Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu.

29Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndipo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba.

30Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya.

31Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.32Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, huyo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao.

33Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake.34Enyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa husema kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni.35Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu.36Nasema kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.37Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.”

38Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema, “Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako.”

39Lakini Yesu alijibu na kusema, “Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.40Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.41Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu huyu mkuu kuliko Yona yuko hapa.42Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu huyu mkuu kuliko Selemani yupo hapa.

43Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni44Kisha husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.’ Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari.45Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu.”

46Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.47Mtu mmoja akamwambia, “Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe.”

48Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?”49Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, “Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!50Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu.”


Mathayo12 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea huingiza kidogo mistari ya nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 12: 18-21, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Sabato

Kutii Sabato ni sehemu muhimu katika sura hii. Hata hivyo, Yesu anafafanua kati ya kufuata Sabato jinsi Mungu alivyoamuru na kufuata sheria ambazo Mafarisayo waliziunda kuhusu Sabato.

"Kukufuru Roho"

Kuna utata mkubwa juu ya kutambua vizuri dhambi hii maalum. Hata hivyo, inaonekana kuwa inahusisha kumtukana Roho Mtakatifu na kazi yake. Kwa kuwa sehemu ya kazi yake ni kuwashawishi watu kuwa wao ni wenye dhambi na kwamba wanahitaji msamaha wa Mungu, yeyote ambaye alikejeli ukweli huu hangetaka kuja kwake Mungu kwa toba. Kwa sababu hii, hangeweza kusamehewa.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kaka na Dada

Sura hii inaanzisha dhana ya kaka na dada "wa kiroho". Maandiko hutumia maneno haya kwa kutaja uhusiano kati ya Waisraeli. Hapa, wale wanaomfuata Yesu sasa wanajulikana kama kaka na dada. na )

Links:


Matthew 12:1

Maelezo kwa ujumla:

Huu ni mwanzo wa sehemu mpya ya simulizi ambapo mwandishi anazungumza juu ya kukua kwa upinzani kwa huduma ya Yesu. Hapa, Mafarisaya wanawakosoa wanafunzi wa Yesu kwa kuvuna nafaka ya ngano siku ya sabato.

Wakati huo

Hii inaonyesha mwanzo mpya wa simulizi. "Baadaye kidogo"

shamba la nafaka

sehemu ya kupanda nafaka. Kama ngano haifahamiki na "nafaka" ni neno la jumla sana, basi waweza kutumia "shamba" la mazao ambayo wanatengeneza mikate."

kuvunja masuke ya nafaka na kuyala...wanajunja sheria ya sabato

Kuvuna nafaka kwenye mashamba ya wengine na kula haikuchukuliwa kuwa ni kuiba. Swali lilikuwa kama mwingine angeweza kufanya shughuli hii kisheria katika siku ya sabato.

kuyavunja masuke na kuyala

"kuchukua baadhi ya ngano na kula" au "kuchukua baadhiya mbegu za ngano na kula"

masuke ya nafaka

Hii ni shsemu ya juu ya mmea wa ngano ambayo ni aina ya jani kubwa. Hushikilia nafaka iliyokomaa au mbegu za mmea.

Mafarisayo

Hiihaimanisha mafarisayo wote. "baadhi tu ya mafarisayo"

Tazama

"angalia." Mafarisayo hutumia neno hili kupata usikifu wa kile wanafunzi wa Yesu walichokuwa wakifanya.

Matthew 12:3

Sentensi unganishi

Yesu anajibu ukosoaji wa mafarisayo

akawaambia

Mafarisayo

Hamjasoma ... nao

Yesu anatumia swali kujibu ukosoaji wa mafarisayo. Yesu anawapa changamoto ili kufikiri juu ya maana ya andiko ambalo walisoma. "Najua mmesoma juu yaa...nao"

nyumba ya Mungu

Wakati wa Daudi bado hapakuwa na hekalu. "hema" au " mahali pa kumwabudia Mungu"

mkate wa wonyesho

Huu ni mkate uliotakaswa ambao makuhani walipeleka mbele za Mungu hemani. "Mikate ambayo makuhani walipeleka mbele za Mungu

wale aliokuwa pamoja nao

"watu waliokuwa pamoja na Daudi"

ila halali kwa makuhani

"ni makuhani tu walioruhusiwa kuula."

Matthew 12:5

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuwaitikia Mafarisayo.

bado hamjasoma katika sheria ... lakini hawana hatia

Yesu antumia swali kijbu hoja za mafarisayo. Yesu anawataka wafikirie maana yakile walichosoma katika maandiko. "And, na mmesoma katika sheria za Musa... lakini hawana hatia.

huinajisi Sabato

"kufanya katika sabato ambayo wangefanya katika siku nyingine."

hawana hatia

" Mungu hatawaadhibu" au "Mungu hatawaonea hatia"

nasema kwenu

Hiki kinaongeza msisitizo kwa kile alichosema baadaye.

aliye mkuu kuliko hekalu

" aliye wa muhimu zaidi kuliko hekalu." Yesu alikuwa anarejelea kwake yeye mwenyewe kama mmoja aliye mkuu.

Matthew 12:7

Sentensi unganishi:

Yesu anaendelea kuwajibu Mafarisayo

Maelezo kwa ujumla:

Katika mstari 7, Yesu anamnukuu nabii Hosea kuwakemea Mafarisayo.

Kama mngalijua hii inamaanisha nini, nataka rehema na siyo dhabihu; msingaliwahukumu wasio na hatia

Hapa Yesu ananukuu andiko. "Nabii Hosea aliandika juu ya haya tangu zamani. "Natakarehema na siyo dhabihu. 'Kama mngalielewa hii ilimaanisha nini, msingaliwalaumu wasio na hatia'

Nataka rehema na sio dhabihu

Katika sheria za Musa, Mungu aliwaagiza Waisraeli kutoa sadaka. Hii inamaanisha kuwa Mungu huichukulia rehema kuwa muhimu kuliko sadaka.

hii inamaanisha nini

"nini Mungu amesema katika maandiko"

Nataka

Kiwakilishi "Na" kinamrejelea Mungu.

wasio na hatia

Hii inaweza kutafsiriwa katika muundo tendaji. "Wale wasiokuwa na hatia"

Mwana wa Adamu

Yesu anamaanisha yeye mwenyewe

ndiye Bwana wa Sabato

"anaitawala Sabato" au "anatengeneza sheria juu ya nini watu wanaweza kufanya siku ya Sabato"

Matthew 12:9

Maelezo kwa ujumla

Hapa mandhari yanahamia kwenye kitu kingine mahali ambapo mafarisayo wanamkosoa Yesu kwa kumponya mtu siku ya Sabato.

Kisha Yesu akaondoka pale

"Yesu akaondoka kwenye lile shamba la ngano" au "Kisha Yesu akaondoka"

Sinagogi lao

"singogi" Hapa "lao" inamaanisha Wayahudi kwa ujumla na wala si Mafarisayo tu, kutokana na kipengere kilichopita.

Tazama

Neno " tazama" linatuelekeza kwa mtu mwingine katka simulizi. Lugha yako inaweza kuwa na njia ya kulifanya hili.

mtu aliyepooza mkon

"mtu alikuwa namkono uliopooza" au "mtu mwenye ulemavu wa mkono"

Mafarisayo wakamuuliza Yesu wakisema . J"e, ni halali kumponya mtu siku ya Sabato? Ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi

"Mafarisayo walitaka kumshitaki Yesu kwa kutenda dhambi, kwa hiyo walimuuliza, 'Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?"

Je, ni halali kuponya siku yaSabato?

Kwa mjibu wa sharia za Musa, Yawezekana mtu kumponya mtu mwingine siku ya Sabato?"

ili waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi

Si tu walitaka kumshitaki Yesu mbele za watu, Mafarisayo walitaka Yesu atoa jibu linalopingana na sheria ili waweze kumpeleka kwa hakimu iwamshitaki kwa kuvunja sheria.

Matthew 12:11

Sentensi ungsnishi

Yesu anjibu hoja za Mafarisayo

Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja ... hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?

Yesu antumia swali kuwajibu Mafarisayo. Anawapa changamoto ya kufikiri juu ya aina gani ya kazi wanayoweza kuifanya siku ya sabato. "Kila mmoja wenu, kama una kondoo mmoja ... angemshika na kumtoa kwa nguvu

Je, ni kipi chenye thamani, zaidi kwani, si zaidi ya kondoo?

Kirai "kipi chenye thamani zaidi" kinaongeza msisitizo kwenye sentensi. " ni wazi mtu ni wa thamani zaidi ya kondoo!" au "Jaribu kufiri vile mtu alivyo wa muhimu kuliko kondoo"

ni halali kutenda mema siku ya Sabato

"Wale wanofanya mema siku ya Sabato wantii sheria"

Matthew 12:13

Kisha Yesu akamwambia yule mtu nyosha mkono wako

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu isiyo ya moja kwa moja, "Kisha Yesu akamwamuru yule mtu kunyosha mkono wake"

yule mtu

"yule mtu mwenye mkono uliopoza au " yule mtu mwenye ulemavu wa mkono"

Nyosha mkono wako

"Utoe mkono wako" au "utanue mkon wako"

Akaunyosha

"Yule mtu akaunyosha"

ukapata afyfa

Hii inaweza kutafsiriwa katika muundo tendaji. "ule mkono ukawa na afya tena" au "ukawa salama tena"

kupanga kinyume chake

"wakapanga kinyume chake"

Matthew 12:15

Maelezo kwa ujumla

Simulizi hii inaeleza jinsi matendo ya Yesu yalivyotimiza moja kati ya unabii wa Isaya

Yesu alivyoelewa hili

"Yesu alikuwa anatambua kile Mafarisayo walichokuwa wakipanga

aliondoka hapo

"alitoka" au "aliondoka"

wasije wakamfanya afahamike kwa wengine

wasimwambie mtu yeyote kuhusu yeye"

kwamba itimie ile kweli

Hii inaweza kutafsriwa kama sentensi mpya. "Hii ilitimiza kile"

iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Kile Mungu alichokuwa amesema zamani kupitia Isaya akaisema..

Matthew 12:18

Sentensi unganishi

Hapa Mthayo anamnukuu nabii Isaya kuonesha kuwa huduma ya Yesu ilitimiza unabii

Tazama

"Angalia." Mungu alitumia neno hili kumleta mtu mwingine

mpe ...Nita

Viwakilishi vyote vinamrejelea Mungu. Isaya ananukuu kile ambacho Mungu alimwambia

katika yeye nafsi yangu imependezwa

Hapa "nafsi" inamanisha nafasi kamil. "na nimependezwa naye"

na atatangaza

"na mtumishi wangu atatangaza"

atatangaza hukumu

Hapa "hukumu" haimaanishi "adhabu" inamaanisha mtumishi atawambia mtaifa Mungu ni mwenye haki, na atawaokoa

Matthew 12:19

Sentensi unganishi

Mathayo anaendelea kumnukuu Isaya

wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani

hapa "sauti" inamaanisha nafsi kamili "na hataongea kwa sauti"

yake ... hata

Viwakilishivyote hivi vinamaanisha mtumishi wa Mungualiyechaguliwa

mitaani

Hii ni nahau inayomaanisha "umma."katika miji"

hatalivunja tet liliochubuliwa .. hatazima utambi wowote unatoa moshi

Senttensi hizi zote zinamaanisha kitu kilekile. Ni sitiari zinazosisitiza kuwa mtumishi wa Mungu atakuwa mnyenyekevu na mpole. Vyote "tete lililochubuliwa na utambi utoa moshi" vinawakilisha watu dhaifu na wenye kudhuru.

hatalivunja

"hataliweka nje"

utambi utoa moto

Hii inamaanisha utambi ambao moto umezima lakini bado unatoa moshi

moshi, mpaka

Hii inaweza kutafsiriwa kwa sentensi mpya; "moshi Hiki ndicho atachofanya"

Mpaka atakapoleta hukumu ikashinda

"mpaka atakapofaulu kuleta haki na wokovu kwa watu. Maana ya nomino dhania "hukumu" inaweza kutafsiriwa kama "haki" au "okoa". "watuwajue kuwa mimi ni wa haki na nitawaokoa"

katika jina lake

Hapa "jina" linamaanisha nafsi kamili

Matthew 12:22

Maelezo kwa ujumla

Hapa mandhari yanabadilika na kuongelea wakati mwingine wakati Mafarisyao walipomshitaki Yesu kwa kumponyamtu kwa nguvu za shetani.

Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele za Yesu

Hiiinaweza kutafsiriwa katikamfumo tendaji. "Mtu mmoja alimleta kwa Yesu mtu aliyekuwa kipofu na bubu kwa sababu pepo lilikuwa likimtawala"

Mtu kipofu na bubu

"mtu asiyeweza kuona na hawezi kuongea"

Makutano wote walishsangaa

"Watu wote waliomwona Yesu akimponya yule mtu walishangaa"

Mwana wa Daudi

Hi ni sifa ya Masihi au Kristo

Mwana wa

Hapa hii inamaanisha "kizazi cha"

Matthew 12:24

Maelezo kwa ujumla

Katika mastari wa 25, Yesu anaanza kuwajibu mashataka ya Mafarisayo kwamba amemponya mtu kwa nguvu za shatani

muujiza huu

Hii inamaanisha muujiza wa kumponya yule kipofu, bubu na alaiyepagawa na pepo.

Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake isipokuwa isipokuwa nguvu za Belzebuli,

Hii inaweza kuelezwa katika muundo chanya. "Huyu mtu anaweza kufukuza pepo kwa sababu ni mtumishi wa Belzabul"

Huyu mtu

Mafarisayo waliepuka kumwita Yesu kwa jina ili kuonesha kuwa hawamkubali.

mkuu wa pepo

"mfalme wa pepo"

kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba iliyogawanyika haitasimama

Yesu anatumia mithali kuwajibu Mafarisayo. Sentenzi hizi mbili zinmaanishakitu kilekile. Zinasisitiza kuwa haimanishi chochote kwa Belzabul kutumia nguvu zake kuwapinga pepo wengine.

Kila ufalme uliogawanyika huharibika

Hpa "ufalme" unamaanisha wale wanaoishi kwenye huo ufalme. Hii inaweza kutafsiriwa katika mfumo tendaji. "Ufalme hautadumu wakati wake wanapigana wao kwa wao"

kila mji au nyumba iliyogawanyika haitasimama

Hapa"mji" unamaanisha watu wanaoishi humo na. "nyumba" inamaanisha familia. "inaharibu mji au familia watu wanapopigana wao kwa wao

Matthew 12:26

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kujibu hoja za mafarisayo za kwamba alimponya mtu kwa nguvu za shetani

ikiwa shetani atamwondoa shetani mwenzake

Matumizi ya pili ya shetani yanamaanisha pepo wanaomtumikia shetani. "Kama shetani atafanya kazi kinyume na pepo zake"

Shetani ... Beelzabul

Majina yote yanamaanisha nafsi moja

ufalme wake utasimama?

Yesu anatumia swali kwapa changamoto Mafarisayo. "Ufalme wa shetani hauwezi kusimama" au "ufalme wa shatani hautadumu"

wafuasi wenu huwatoa kwa njia ya nani

Yesu anatumia swali lingine kuwapa changamoto Mfarisayo. "kisha lazima useme wafuasi wenu pia huwatoa pepo kwa nguvu za beelzabul. Lakini mnajua kuwa hii siyo kweli"

kwa ajili hii watakuwa mahakimu wenu

"Kwa sababu wafuasi wenu huwatoa pepo kwa nguvu za Mungu, wanahakikisha kuwa mmekosea."

Matthew 12:28

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwajibu Mafarisayo

Na kama natoa

Hapa "kama" haimaanishi kuwa Yesuanahoji jinsi anavyowatoa pepo. Hapa Yesu anatumia neno kuleta sentensi ya kweli. "Lakimi kwa sababu nina"

basu ufalme wa Mungu umekuja kwenu

"Basi ufalme wa mbinguni umefika kwenu." Hapa "ufalme" utawala wa Mungu kama mfalme. "Hii inamaanisha Mungu anaanzisha ufame kwenu"

umekuja kwenu

Hapa "kwenu" ni wingi na inamaanisha watu wa Israel,

na mtu awezaje kuingia ndani ya nyumba ... atakapoiba mali yake

Yesu anatumia mfanokuendelea na majibu yake kwa Mafarisayo. Yesu anamaanisha anaweza kuwatoa pepo kwa sababu ana nguvu kuliko shetani.

Awezaje mtu kuingi ... asipomfunga mwenye nguvu kwanza?

Yesu anatuumia swali kuwafundisha Mafarisauo na makutano. "Hakuna awezaye kuingia ..bila kumfunga mwenye nguvu kwanza"

Ndipo atakapoiba

"Ndipo atakapoiba" au "Ndipo atakapoweza kuiba"

yeyote asiyekuwa pamoja nami

"ambaye hashirikiani nami" au "amabye hafanyi kazi p amoja nami"

yuko kinyume changu

"ananipinga mimi" au "hufanya kazi kinyume na mimi"

Huyo asiyekusanya nami hutapanya

Yesu anatumia kirai amabcho kinamunesha mtu amabye aidha anakusanya kundi la wanyama kwa mchungaji au anayewatapanya totka kwa mchungaji.

Matthew 12:31

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwajibu Mafarisayo

nasema kwenu

Hii inaongeza msisitizo wakile Yesu alichosema baadaye

sema kwenu

Hapa "kwenj" ni wingi. Yesu anaongea moja kwa moja na Mafarisayo, lakini pia anwafundisha makutano

kila dhambi na kufuruwatu watasamehewa

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Mungu atasamahe kila dhambi ambayo watu wanafanya na kila jambo ovu wanlosema

ila kumkufuru Roho Mtakatifu watu hawatasamehewa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "Mungu hatamsamehe mtu yule amabye anasema mabo maovu dhidi ya Roho Mtakatifu.

Na yeyotte asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu

Hapa "neno" linamaanisha kile amabcho mtu husema, "N kama mtu atasema chchote kibaya kuhusu Mwana wa Adamu"

Mwana wa Adamu

Yesu anaongea juu yake mwenyewe

hilo atasamahewa

Hili linaweza kuelezwa katikamfumo tendaji. "Mungu atamsamehe mtu kwa ajiloi yahilo"

huyo hatasamehewa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "Mungu hatamsamehe mtu huyo"

katika ulimwengu huu, na wala ule ujao

Hapa " ulimwengu huu" na " ule ujao" inamaanisha maisha haya ya leo na maisha yajayo. " katika maisha haya au yajayo" au "sasa au baadaye"

Matthew 12:33

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwajibu Mafarisayo

Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake kuwa zuri, au uharibu mti na tunda lake

maana yake ni 1) kama utafanya mti kuwa mziri na mtunda yake yatakuwa mazuri na kama ukiuharibu mti na matunda yake yatakuwa mabaya" au 2) "Kama ukiufanya mti kuwa mzuri na mataunda yake yatakuwa mazuri kwa sababu matunda yake ni mazuri na kama ukiyafanya matunda kuwa mabaya yatakuwa kwa sababu matunda yake ni mabaya." Hii ni mithali watu walipaswa kuutumia ukweli kwa jinsi wawezavyo kujua kama mtu ni mbaya au mzuri.

mazuri ... mabaya

"eneye afya ... iliyougua"

mti hutambulika kwa tunda lake

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Watu hujua kama mti n mbaya aua mzuri kwa kutazama matunda yake"

ninyi kizazi cha nyoka

Hapa "kizazi" inamaanisha "kuwa na tabia za." Kipiribao ni aina ya nyoka wenye sumu ambao ni hatarina wanawakilisha uovu"

niny ...nyie

Hivi ni viwakilishi vya wingi na vinamaanisha Mafarisayo

mwawezaje kusema mambo mazuri

Yesu anatumia swali kuwakemea Mafarisayo. "huwezi kusema mambo mazuri "Unaweza kusema mambo maovu tu"

kwa kuwa kinywa hunena kutoka katika akiba ya yaliyo moyoni

Hapa "akiba ya moyoni" inamaanisha mawazo ya mtu katika akil iyake. "Kinywa" kinawakilishsa mtu. "Kile ambacho mtu husema katikakinywa chake kinafunua jinsi alivyo katika akili yake"

Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoa wema, na mtu mwovu katika akiba ya uovuwake hutoa kilicho kovu.

Yesu anaongea juu ya "moyo" kama vile kontena lilivyo amablo mtu anaweza kulijaza kwa mambo mazuri au maovu. Hii ni sitiari inayoonesha kile mtu anachosema kinafunua jinsi mtu alivyo.

Matthew 12:36

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha majibu yake hoja za Mafarisayo za kwamba alimponya mtu kwa nguvu za shetani.

Nawaambia

Msisitizo wa kileYesu alichosema baadaye

Watu atatoa hesabu ya kila neno

"Mungu atawauliza watu kuhusu" au "atu watajieleza mbele za Mungu"

Kila neno lililo la maana walilosema

Hapa "neno" inamaanisha kitu ambacho mtu husema. "kila jambo lenye kudhuru watakolokuwa wamesema"

utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa

Hii inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Mungu atakuhesabia haki ... Mungu atakuhukumu"

Matthew 12:38

Sentensi unganishi

Maongezi katika mistari hii yananza mara baada tu ya Yesu kujibu hoja za Mafarisayo kwamba alimponya mtu kwa nguvu za shetani

Maelezo kwa ujumla

Katikamstari wa 39, Yesu anaanza kuwakemea waandishi na Mafarisayo

tungependa

"taka"

kuona ishara totka kwako

Unaweza kuiweka wazi kwa nini wanataka kuona ishara "kuona ishara toka kwako ili kuhakikisha kuwa kile unachosema ni kweli.

kizazi kiovu na cha zinaa kinatafua ishara ... itakayotolewa kwao

Yesu anasema na kizazi kilichokuwepo. "ninyi ni waovu na kizazi cha zinaa wanaotafuta ishara toka kwangu ... itakayotolewa kwao

kizazi cha zinaa

Hapa "zinaa" ni sitiari ya watu wasio waaminifu kwa Mungu.

kinatafuta ishara

Ombi hili linamkasirisha Yesu kwa sababu ya mashaka na tabia ya viongozi wa dini juu ya Yesu. Alikuwa amefanya miujiza mingi, lakini bado walikuwa hawamwamini

hakuna ishara itakayotolewa

Hii inaweza kuelezwa katika mmundo tendaji. "Mungu hatawapa ishara"

isipokuwa ile ishara ya nabii Yona

"isipokuwa ishara ileile amabyo Mungu alimpa nabii Yona"

siku tatu mchan nausiku

Hapa "usiku" na "mchana" inamaanisha kipindi cha saa 24 kamili. "siku tatu kamili"

Mwana wa Adamu

Yesu anaongea juu ya yeye mwenyewe

ndani y a moyo wa nchi

Hii inammanisha ndani ya kaburi halisi

Matthew 12:41

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwakemea waandishi na Mafarisayo

Watu wa ninawi

"Raia wa Ninawi"

watasimama mbele ya watu pamoja na kizazi cha watu hawa

"watasimama siku ya hukumu na kuwahukumu kizazi hiki"

Kizazi cha watu hawa

Yesu anamaanisha watu walioishikipindi hiki

watakihukumu

Atakuwa Mungu atayekihukumu kizazi cha watu wa Yesu

na tazama

"na angalia" Hii inatia msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

mtu fulani mkuu

"mtu wa muhimu sana"

kulikoYona yuko hapa

Unaweza kifanya maana ya sentensi ya Yesu iliyofumbwa kuwa wazi. "kuliko Yona yuko hapa, Lakini bado hamjatubu, hii ndiyo sababu Mungu atawahukumu.

Matthew 12:42

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwakemea waandishi na Mafarisayo

Malkia wa kusini

Hii inamaanisha Malkia wa sheba. Sheba ni nchi iliyo kusini mwa Israeli

atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki

"atasimama siku ya hukumu na kuwahukumu watu wa kizazi hiki, Tazama ilivyotafsiriwa katika 12:41

kizazi hiki

Hii inamaanisha watu walioishi wakati Yesu alipokuwa akihubiri

na kukihukumu

Ni Mungu atakayekihukumu kizazi chxa Yesu. "Na Mungu atawasiliza raiawa Ninawi na kukihukumu kizazi hiki "

alikuja toka miishio ya dunia

Hapa "miishio ya dunia" ni nahau inayomaanisha "mbali." Alikuja tokea mbali"

Alikuja

Sentensi hii inaeleza kwa nini Malkia wa kusini atakihukumu kizazi cha Yesu, "allikuja kwa hilo"

na Tazama

"na anagalia" Hii inaongeza msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

mtu fulani mkuu

"mtu wa muhimu sana"

fulani

Yesu anaongea juu yake

Kuliko Selemani Yuko hapa

Unaweza kuiweka maana ya sentensi ya Yesu iliyofumbwa kuwa wazi. "Kuliko Selemani yuko hapa, lakini hausikilizi. Hiyo ndiyo sababu ya Mungu kuwahukumu"

Matthew 12:43

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwakemea waandishi na Mafarisyao.

Wakati pepo machafu ... kwa kizazi hiki kibovu

Yesu anatumia mfano kuwaonya watu hatari ya kutokuamini

"mahali pasipo na maji

"eneo kavu"au "mahali ambapo watu hawaishi"

lakini hapaoni

Hapa "ni" inamaanisha kupumzika

Kisha husema, 'nitarudi kwenye nyumba yangu niloyotoka

Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi na wala si nukuu "kwa hiyo yule roho mchafu huamua kurudi kwenye nyumba yake ambayo alitoka"

kwenye nyumba yangu niliyotoka

Hii ni sitiari ya ya mtu ambaye pepo lilitoka. "pale nilikotoka

arudipo akikuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari

Hii inaweza kutafsiriwa katika muunda tendaji. "yule roho mchafu akikuta ile nyumba iko safi na imewekwa kila kitu katika mahali pake",

Hivi ndivyo itavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu

Hii inamaanisha kama watu wa kizazi cha Yesu hawatamwamini na kuwa wanfunzi wake, watakuwa katika hali mbaya kuliko walivyokuwa mwanzoni

Matthew 12:46

Maelezo kwa ujumla

Kufika kwa Mama wa Yesu na ndugu zake inakuwa fursa Kwa Yesu kueleza juu ya familia yake ya kiroho

tazama

neno "tazama" lintatuandaakwa ajili ya watu wapya katika simulizi. Lugha yako yaweza kuwa na namna mpya ya kueleza hili

mama yake

Huyu ni Mariamu, Mam wa Yesu wa mwili.

wakitafuta kuongea

"wakitaka kuongea"

mtu mmoja akamwambia, "tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe",

Hii inaweza kutafsiriwa kama nukuu isiyo ya moja kwa moja. "mtu mmoja alaimwambia Yesu kuwa mama yake na ndugu zake walikuwa nje na walitaka kuongea naye"

Matthew 12:48

Sentensi unganishi

Huu ni mwisho wa sehemu ya simulizi lililoanzia 12:1 amabapomwadishi ameeleza juu ya kukua kwa upinzani katika huduma ya Yesu

aliyemjulisha

ukweli wa ujumbe ambao yule mtu aliomwambia Yesu unaeleweka na haukurudiwa. "aliyemwambia Yesu kuwa mama yake na ndugu zake walitka kuongea naye"

mamayangu ni nani? na ndugu zangu nu akina nani?

Yesu antumia swali hili kuwafundisha watu. "nitwaambia kweli mamayangu na ndugu zangu ni nani"

Tazama

"anagalia" Hii inatia msisitizo wa kile ambacho Yesu alisema baadaye"

hawa ni mama na ndugu zangu

Hii ni sitiari inayoonesha kuwa wanafunzi wa Yesu ni wake katika familia ya kiroho. Hii ni ya muhimu kuliko kuwa kwenye familia ya kimwili.

yeyote

"mtu yeyote"

baba

Hii ni sifa muhimu ya Yesu

huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu

Hii ni sitiari inayomaanisha kuwa wale amabo wanamtii Mungu wanakuwa kwenye familia ya Yesu kiroho. Hii ni muhmu zaidi ya kuwa kwenye familia ya kimwili


Translation Questions

Matthew 12:1

Wanafunzi wa Yesu walikuwa wanafanya nini walipolalamikiwa na mafarisayo?

Mafarisayo walilalamika kuwa wanafunzi wa Yesu walikuwa wakivunja na suke ya ngano na kula, jambo ambalo Mafarisayo waliamini halikuwa halali kufanyika siku ya sabato.

Matthew 12:5

Yesu alisema ni nani alikuwa mkuu kuliko hekalu?

Yesu alisema alikuwa mkuu kuliko hekalu.

Matthew 12:7

Yesu mwana wa Adamu anamamlaka gani?

Yesu, mwana wa Adamu ni Bwana wa sabato

Matthew 12:9

Mafarisayo walimuuliza swali gani Yesu ndani ya sinagogi mbele ya mtu ya mwenye mkono uliopooza?

Mafarisayo walimuuliza Yesu "Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?"

Matthew 12:11

Yesu alisema ilikuwa halali kufanya nini siku ya sabato?

Yesu alisema likuwa ni halali kutenda mema siku ya Sabato.

Matthew 12:13

Mafarisayo walipoona Yesu amemponya mwenye mkono uliopooza walifanya nini?

Mafarisayo walitoka nje na na kupanga njama dhidi yake na kutafuta jinsi ya kumwangamiza.

Matthew 12:18

Katika unabii wa Isaya kuhusu Yesu, nani angesikia hukumu ya Mungu na kuwa na matumaini kwa Yesu?

Watu wa mataifa wangesikia hukumu ya Mungu na kumtumaini Yesu.

Matthew 12:19

Katika unabii wa Isaya kuhusu Yesu, jambo gani Yesu asingelifanya?

Yesu hatalia kwa nguvu, hatavunja tete lilichubuka, au kuuzima utambi unaotoa moshi.

Matthew 12:26

Yesu alisema nini juu ya tuhuma kwamba alitoa mapepo kwa nguvu ya Belizabuli?

Yesu alisema kuwa kama shetani anampinga Shetani, basi je ufalme wa Shatani utasimama?

Matthew 12:28

Yesu alisema jambo gani lilikuwa likitokea kama alikuwa anatoa pepo kwa Roho wa Mungu?

Yesu alisema kwamba ufalme wa Mungu umekuja juu yao kama alikuwa anatoa mapepo kwa Roho wa Mungu.

Matthew 12:31

Yesu alisema ni dhambi gani haina hatasamehewa?

Yesu alisema kufuru dhidi ya Roho haitasamehewa.

Matthew 12:33

Mtu hujulikana kwa namna gani?

Mtu hujulikana kwa matunda yake.

Matthew 12:36

Yesu alisema kwa jambo gani Mafarisayo wangepata hukumu na haki?

Yesu alisema kuwa Mafarisayo wangepata hukumu na haki kwa maneno yao.

Matthew 12:38

Yesu alisema ni ishara gani angetoa katika kizazi chache?

Yesu alisema katika kizazi chake angetoa ishara ya Yona, kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.

Matthew 12:41

Yesu alisema ni nani alikuwa mkuu kuliko Yona?

Yesu alisema Yeye alikuwa mkuu kuliko Yona.

Kwa nini watu wa Ninawi watawahukumu wa kizazi cha Yesu?

Watu wa Ninawi watakihukumu kizazi cha Yesu kwa sababu walisikia ujumbe wa Mungu kwa Yona lakini kizazi cha Yesu hakikusikiliza ujumbe wa Mwana wa Adamu ambaye ni mkuu kuliko Yona.

Matthew 12:42

Yesu alisema ni nani alikuwa mkuu kuliko Selemani?

Yesu alisema kuwa Yeye alikuwa mkuu kuliko Sulemani.

Matthew 12:43

Kizazi cha Yesu kitamwacha na kufanana na mtu mwenye pepo mchafu kwa namna gani?

Kizazi cha Yesu kitamwacha na kufanana na mtu mwenye roho mchafu kwa sababu roho mchafu hurudi na roho wachafu wengine saba na hali mwisho ya mtu huwa mbaya zaidi kuliko ya kwanza.

Matthew 12:48

Yesu alisema ni nani walikuwa ndugu zake na mama yake?

Yesu alisema wale wanaofanya mapenzi ya Baba ni ndugu zake na ni mama yake.


13

1Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.2Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama pembeni ya bahari.3Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano. Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda.4Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.5Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.6Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.7Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini.9Aliye na masikio na asikie.

10Wanafunzi walikuja na kumwambia Yesu, “Kwa nini unazungumza na umati kwa mifano?”

11Yesu alijibu kusema, “Mmepewa upendeleo wa kujua siri za ufalme wa mbinguni, bali kwao hawajapewa.12Lakini yeyote aliyenacho, kwake yeye ataongezewa zaidi, na atapata faida kubwa. Ila asiye nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa.13Hivyo naongea nao kwa mifano kwa sababu ingawa wanaona, wasione kweli. Na ingawa wanasikia wasisikie wala kujua.14Unabii wa Isaya umetimia kwao, ule usemao, ‘Msikiapo msikie, lakini kwa namna yoyote hamtaelewa; wakati mwonapo mwaweza kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue.

15Na mioyo ya watu hawa imekuwa giza, ni vigumu kusikia, na wamefumba macho yao, ili wasiweze kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao, au kufahamu kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena, na ningewaponya.’

16Bali macho yenu yamebarikiwa, kwa kuwa yanaona, na masikio yenu kwa kuwa yanasikia.17Hakika nawaambia manabii wengi na watu wenye haki walikuwa na hamu ya kuyaona mambo yale myaonayo, na hawakuweza kuyaona. Walitamani kusikia mambo yale mnayosikia, hawakuyasikia.

18Sasa sikilizeni mfano wa mpanzi.19Wakati wowote asikiapo neno la ufalme na asilielewe, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kuwekwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.20Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.21Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.22Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.23Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.”

24Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, “Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake.25Lakini watu walipolala, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake.26Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia.27Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, ‘Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu?’

28Akawaambia, ‘Adui ametenda hili.’ Watumishi walimwambia, ‘Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?’

29Mwenye shamba akasema, ‘Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano.30Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, ‘Kwanza yang'oeni magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.’”

31Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake.32Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”

33Akawaambia mfano mwingine tena. “Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke.”

34Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao.35Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, “Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu.”

36Kisha Yesu aliwaacha umati na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.”

37Yesu alijibu na kusema, “Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.38Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni Ibilisi.39Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.40Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu.41Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi.42Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.43Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na asikie.

44Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba.

45Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani.46Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.

47Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina.48Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali.49Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki.50Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno.

51Mmefahamu mambo yote haya?” Wanafunzi walimjibu, “Ndiyo.”

52Kisha Yesu akawaambia, “Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

53IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo.54Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, “Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?55Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda?56Na dada zake tunao hapa kwetu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?”

57Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, “Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao.”58Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.


Mathayo13 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka mbele kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari ya 13:14-15, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Sura hii inaanza sehemu mpya. Ina baadhi ya mifano ya Yesu kuhusu ufalme wa mbinguni.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Mfano ni hadithi fupi inayotumika kuonyesha mfano wa maadili au wa kidini. Katika sura hii, mifano, yanatangaza ukweli kuhusu ufalme wa mbinguni kwa wale ambao wana imani katika Yesu. Pia yanaficha ukweli huo huo kutoka kwa wale wanaomkataa Yesu (Mathayo 13:11-13). Kawaida mifano hii huchukua fomu ya hadithi.

Nahau

Katika sura hii, Yesu anazungumzia macho kuona na masikio kusikia. Anatumia takwimu hizi za matamshi ili kuwahimiza wasikilizaji wake kuelewa masomo ya mifano hiyo.

Links:


Matthew 13:1

maelezo ya jumla

Huu nimwanzo wa simulizi jipaya amabapo Yesu anaanza kufundisha makutano, kwa kutumia mifano juu ya ufalme wa mbinguni

katika siku hiyo

Tukio hili liltokea siku hiyohiyo sawa na yale yaliyo kwenye sura iliyopita.

alikaa kando ya bahari

ilimaanisha kuwa alikaa chini kuwafundishsa watu.

aliondoka nyumbani

Haijatajwa kuwa ilikuwa nyumba ya nani ambayo Yesu alikuwa akiishi

aliingia nadni ya mtumbwi

Inamaanisha kuwa Yesu aliingia kwenye mtumbwi kwa sababu ingemfanya iwe rahisi kuwafundisha watu.

mtumbwi

Huu yawezekana mtumbwi wa wazi, uliotengenezwa kwa miti wa kuvulia samaki wenye tanga.

Matthew 13:3

Sentensi unganishi

Yesu anafafanua juu ya ufalme wa mbinguni kwa kutumia mfano wa mpanzi

Yesu alisema maneno mengi kwa mfano

"Yesu aliwaambia maneno mengi kwa mifano"

nao

"kwa wale watu kwenye mkutano"

Tazama

"angalia" au "sikiliza." neno hili linavuta usukivu wa kile Yesu anachotaka kusema baadaye. "uwe tayari kusikiliza jambo amablo nataka kuwaambia"

mpanzi alienda kupanda

"mpanzi alienda kumwaga mbegu shambani"

alipokuwa akipanda

"mpanzi alipokuwa akiendelea kumwaga mbegu"

kandoya njia

Hii inamanisha "njiani wanapopita" peembeni mwa shamba. araidhi ya pale ni ngumu kwa sababu ya watu kuikanyaga.

wakazidonoa

"wakazila mbegu zote"

juu ya mwamba

Hii ni eneo lililojaa miamba na sehemu nyembamba ya udongo ulio juu ya miamba

Ghafla zilichipuka

"zile mbegu zilimea na kukua"

zilichomwa

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "jua lilichoma ile mimea na ikaungua"

Matthew 13:7

Sentensi unganishi

Yesu anamaliza mfano wa mpanzi

zilianguka katai ya miti ya miiba

"zilianguka mahali ambapo miiba na mimea hukua"

ikaisonga

"ikaisinga ile mimea mipya" tumia neno lako magugu kuzuia mimea mingine kukua vizuri.

kuzaa mbegu

"kuzaa mazao" au "kuzalisha mbegu zaidi" au kutoa matunda"

zingine maramiamoja zadi, zingine sitini, na zingine thelathini

unaweza kuiweka vizuri zaidi katika maana inayoeleweka

mia moja ... sitini ... thelathini

"100 ... 60 ... 30"

aliye na masikio

Hii ni njia inayomaaisha kwa kila anayesikiliza. "Kila anayenisikilza." Tazamaulivyotafsiri katika 11:13

asikie

Hapa "kusikia" inamaanisha kuwa msikivu. "lazima awe makini na kile ninachokisema"

Matthew 13:10

Maelezo kwa ujumla

Yesu anawaeleza wanafunzi wake kwa nini anafundisha kwa kutumia mifano

kwao

Hapa"kwao" inamaanisha wanafunzi wa Yesu

mmepewa upendeleo wa kufahamu siri za ufalme wa mbinguni bali kwao hawajapewa

Hii inaweza kutafasiriwa kwa kutumia muundo tendaji na kutumia taarifa zinazotolewa. " Mungu amewapa fursa ya kuelewa siri za ufalme wa mbinguni" lakini Mungu hajawapa siri hizi watu hawa" au " Mungu amewafnya ninyi kuzielwa siri za ufalme wa mbinguni lakini hajawafanya hawa tayri kuzielewa"

mme

ni kiwakilishi cha wingi kinacho maanisha wanafunzi wa Yesu

siri za ufalme wa mbinguni

Hapa"ufalme" inamaanisha utawala wa Mungu. Kirai"udalme wa mbinguni" kinaonekena kwenye kitabucha mathayo tu. Kama inawezekana jaribu kuiweka katika tafsiri y ako. "siri kuhusu Mungu wetu na utawala wake"

yeyote aliye nacho

"yeyote aliye na ufahamu" au "yeyote anayepokea kile nanachofundisha"

ataongezewa zadi

Hiiinaweza kutafsiriwa katika muundo tendaji. "Mungu atampatia ufahamu zaidi"

ila asiye nacho

"asiye na ufahamu" au " asiyepokea hiki ninachofudisha"

hata kile alicho nacho atanyang'anywa

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Mungu atakichukua hata kile alicho nacho"

Matthew 13:13

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwafundisha wanafunzi wake kwa nini anafundisha kwa kutumia mifano

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 14 Yesu anamnukuu nabii Isaya ku onyesha kuwa kushindwa kwa watu kuelewa mafundisho ya Yesu ni kutimilika kwa unabii

kwao ... hamta

Viwakilishi vyote vya "kwao" na "hamta" vinamaanisha watu katika kumati.

na ingawawanasikia wasisikie wala kufahamu....

Huu ni mwanzo wa nukuu kutoka kwa nabii Isaya kuhusu watu wasioamini wakatiwa Isaya. Yesu anatumia nukuu hii kuwa kuwaeleza watu waliokuwa wanamsikiliza. Hii ni semi misambamba inayosisitiza kwamba watu walikataakumwani Yesu.

ingawa wanaona, wasione kweli

Matumizi ya pili ya "kuona" hapa yanamaanisha kuelewa.

Ingawa wanasikia wasisike wala kufahamu

Inaweza kuwekwa wazi kwa kile watu wanachosikia. "Ingawa wanasikia kile ninachosema, hawaelewi kile ninachomaanisha.

kwao unabii wa Isaya umetimia ule usemao

Hii inaweza kuelzwa katika mfumo tendaji. "wanatimiza kile Mungu alisema zamani kuptia nabii Isaya"

Msikiapo msikie, lakini kwa namna yeyote hamtaelewa, wakati mwonapo muweze kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue

Huu ni mwanzo wa nukuu kutoka kwa nabii Isaya kwa watu wasioamini wakati wa Isaya. Yesu anatumia nukuu hii kuwaeleza watu waliokuwa wanamsikiliza. Hii ni misemo sambamba inayosisitiza kuwa watu walikataa kuuelewa ukweli wa Mungu.

msikiapo msikie lakini kwa namna yeyeote msiweze kuelewa.

"mtaskia vitu lakini hamtavielewa" unaweza kuviweka wazi kile amabcho watu watasikia. "Mtasikia kile Mungu asemacho kupitia nabii lakini hamtaelewa maana halisi"

wakati mwonapo muweze kuona lakini kwa namna yeyote msiweze kuelewa

Unaweza kuweka wazi kile ambacho watu wataona. "mtaona kile amabcho Mungu anafanya kupitia nabii, lakini hamtaelewa"

Matthew 13:15

Sentens iunganishi

Yesu anamaliza kumnukuu Isaya

Na mioyo ya watu hawa ... ningewaponya

Ktika 13:15 Mungu anawaeleza watu wa Israwli kana kwamba ni wenya ugonjwa wa mwili ambao unawafanya wasiweze kuelewa, kuona na kusikia Mungu anawataka waje kwake ili awaponye.

Mioyo ya watu hawa imekuwa giza

Mioyo inamaanisha akili. "mioyo yao imekuwa migumu kujifunza"

ni vigumu kusika

wao si viziwa wa masikioya mwili 'vigumu kusikia"wanakataa kusika na kujifunza ukweli wa Mungu

wamefumba macho yao

hawajafumba macho yao ya mwaili. hii inamaanisha hawataki kuelewa.

ili wasiweze kuona kwa macho yao au kusikia kwa masikkio yao auakuelewa kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena.

"ili kwamba wasiweze kuona kwa macho yao, kusikia kwa masiko yao, au kuelewa kwa mioyo yao amabyo matokeo yake ni kumrudia Mungu.

wangenigeukia

"kugeukia kwangu tena" au "kutubu"

ningewaponya

"mimi ningewaponya" Hii inamaanisha Mungu angewaponya kiroho kwa kuwasamehe makosa yao na kuwapokea tena kama awatu wake.

Matthew 13:16

Sentensi unganishi

Yesu anamaliza kuongea na wanafyunzi wake kwa nini anaongea nao kwa mifano

Bali macho yenu yameberikiwa kwa kuwa yanaona, na masikio yenu, kwa kuwa yanasikia

Sentensi zote zina maanisha kitu kilekile. Yesu anasisitiza kuwa wamempendeza kwa sababu wameamini kile ambacho Yesu amesema na wamefanya.

Bali macho yenuyamebarikiwa kwa kuwa yanaona

macho yanamaanisha nafsi kamili. mmebarikiwa kwa sababu machoyenu yanaweza kuona

Yenu .. wewe

viwakilishi hivi ni vya wingi

na masikio yenu, kwa vile yanaona

masikio yanmaanisha nafsi kamili

hakika nawambia

"nawambia ukweli" hii inaongeza msisitizo kwa kile anlichosema Yesu baadaye.

mamabo mnayoyaona

Unaweza kuyaweka wazi yale waliyoyaona "Yle mambo uliyoyaona mimi nikfanya

mambo uliyoyasikia

mambo uliyosikia mimi nikisema

Matthew 13:18

sentensi unganishi

Yesu anaanza kufafanua kwa wanafunzi wake ule mfano wa mpanzi unaoanzi 13:3

neno la ufalme

neno linamaanisha ujumbe "ufalme" unamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme

mwovu huja nakukinyakua kilichokwisha kupandwa mioyoni mwenu

Yesu anaongea juu ya shaetani anayewafanya kusahau kile walichosikia kama ndege anavyozidonoa mbegu zilizoanguka chini.

mwovu

shetani

kukinyakua

kukichukua kitu kwa mtu aliyesahihi

kilichokwishapandwa ndani ya moyo wake

ujume ule Mungu aliopanda nadani ya moyo wake.

ndani ya moyo ake

moyo unamanisha akili ya msikilizaji

hii ni mbegu iliyopandwa kando ya njia

tafsiri kama ilivyo 13:3

Matthew 13:20

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kwaeleza wanafunzi wake mfano wa mpanzi

yeye aliyepandwa katika miamba

"kilichopandwa" kinamaanisha mbegu iliyoanguka kwenye miamba.

Kilichopandwa kwenye miamba ni

miamba ambapo mbegu zilianguka inmaanisha udongo uliokuwa juu ya miamba ambapo mbegu zilianguka

yule asikiaye neno

katika mfano, mbegu zinamaanisha neno

neno

ujumbe wa Muungu

hulipokea kwa furaha

kulipokea neno kwa furaha

ila hana mizizi ndani yake hiyo huvumilia kwa kitambo kifupi.

mizizi inamaanisha kile kinachomfanya mtu aendelee kuamini ujumbe wa Mungu

hujikwaa ghafla

kujikwaa humaanisha kuacha kuamini ujumbe wa Mungu

Matthew 13:22

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwawleza wanafunziwake kuhusu mfano wa mpanzi

aliyepandwa

hii ni mbegu iliyopandwa au iliyoanguka

iliyopandwa kati ya miiba

ardhi ilyo na miiba amabapo mbegu ilipandwa

huyu ni yule

inamaanisha mtu

neno

inaanisha ujumbe wa Mungu

masumbuko ya ulimwengu na udanganyifu wa utajiri hulisonga lile nenoi

Yesu anaongelea masumbufu ya ulimwengu na udanganyifu wa utajiri hugeuza nia ya mtu na kushindwa kutii neno la Mungu kama vile magugu yanavyoweza kuuelemea mmea na kushindwa kukua.

masumbko ya ulimwengu

"mamabo ya dunia ambayo huwafanyawatu wawe na mashaka

udanganyifu wa utajiri

Yesu anautumia utajiri kama mtu adanganyaye watu. Hii inamaanisha kuwa watu hudhani kuwa na pesa nyingi huwafanya kuwa na furaha, lakini si kweli.

lisije likazaa matunda

kutokuzaa matunda

aliyepandwa kwenye udongo mzuri

kwenye udongo mzuri ambapo mbegu zilipandwa

azaaye matunda na kuendela kuzaa

Hapa mtu amefananishwa na mti uzaao. "Kama mti wenye afya uzaoa matunda, ambaye ni mzalishaji.

kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelatiini

watu wengine huzalisha 100 mara, wengine 60 na wengine 30.

Matthew 13:24

Sentensi unganishi

Hapa Yesu anaelezea juu ya uafalme wa mbinguni kwa kutumia mfanao wa shamba lilikuwa na ngano na magugu vikikuwa pamoja

Ufalme wa mbinguni umefananishwa

tafasiri islinganishe ufame wa mbinguni na mtu, bali ufalme wa mbinguni kama ulivyoelezwa kwenye mfano.

ufalme wa mbinguni umefananishwana mtu

"Wakti Mungu wa mbinguni atakapojionesha kama mfalme"

ufalme wa mbinguni umefananishwa n

wakati Mungu wetu wa mbinguni atakapojidhirisha kama mfalme, itkuwa kama

mbegu nzuri

"mbegu nzuru ya chakula" au "nafaka nzuri"

adaui ake akaja

"adaui wake akaja shambani"

magugu

magugu huonekena kama mimea ya chakula yanapokuwa hayajakomaa. laini mbegu zake huwa nasumu" au "mbegu mbaya" au mbegu za magugu"

baadaye ngano ilipoota

"badaye mbegu za ngano zilipoota" au "wakati mimea ilipochipua"

ilipotoa mazao

"ilipotoa nafaka" au "ilipotoa mbegu za ngano"

ndipo magugu yalitokea pia

"watu waliweza kuyaona magugu shambani pia"

Matthew 13:27

Sentensi ungsnishi

Yesu anaendelea kueleza mfano wa magaugu na ngano kukua kwa pamoja katika shamba

mwenye shamba

huyu ndiye aliyepanda mbegu nzuri shambani

Haukupanda mbegunzuri katika shamba lako?

ulipanda mbegu nzuri katika shamba

je, haukupanda

tulipanda

akawaambia

"mwenye shamba akawaambia watumishi"

kwa hiyo unatutaka

kiwakilishi "tu" kinamaanisha watumishi

Matthew 13:29

Sentensi unganishi

Yesu anahitimishas mfano wa magugu yalyokua pamaoja na ngano shambani

Mwenye shamba akasema

"Mwenye shamba akasema kwa watumishi"

nitasema kwa wavunaji, 'kwanza yang'oeni magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu,"

"Nitawaambia wavunaji kwanza kuyakusanya magugu na kuyafunga matita matita na kuyachoma, kisha kusanyeni ngano katika ghala langu"

ghala

Jengo la shambani ambalo lilitumika kwa kukusanyia nafaka.

Matthew 13:31

Esntensi ungsnishi

Yesu anaufafanua ufalme wa mbinguni kwa kutumia mfano wa mbegu ambayo hukua na kuwa mti mkubwa

Ufalme wa mbinguni unafanana n a

"Wakati Mungu wetu wa mbinguni atakapojidhihirisha kama mfalme kuwa mfalme, itakuwa kama", Tazama 13:24.

mbegu ya haradari

ni mbegu ndogo sana ambayo huweza kukua na kuwa mti mkubwa

Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote

Mbegu za haradari zilikuwa mbegu ndogo zadi ambazo zilifahamika kwa wasikilizaji wa kwanza

Lakini imeapo

"Lakini mmea unapokuwa"

huwa kubwa kuliko

ni mkubwa kuliko

huwa mti

Mmea wa haradli hukua kiasi cha mita 2 had 4 za urefu

ndege awa angani

"ndege"

Matthew 13:33

Sentensi unganishi

Yesu anaelezea ufalme wa mbinguni kwa kutumia mfano wa chahu na jinsi inavyoweza kuufanya udongo

Ufalme wa mbinguni ni kama chachu

Ufalme si kama chachu, lakini kusambaa kwa ufalme ni kama kusambaa kwa chachu

ufalme wa mbinguni ni kama

ufalme wa mbinguni una, maanisha utawala wa Mungu kama mfalme..Kirai "ufalme wa mbinguni" kimetumika katika Mthayo tu. Mungu wetuwa mbinguni atakapojidhihirisha kama mfalme itakuwa kama"

vipimo vitatu kwa unga

"kipimo kikubwa cha unga" au tumia kipimo kinachotumika katika utamaduni wako cha kuonesha kipimo kikubwa cha unga.

mpaka viumuke

Maana kusudiwa hpa ni kwamba, chachu na vile vipimo vitatu vya unga vilitengenezwa kwa ajiliya kuumulia.

Matthew 13:34

Maelezo kwa umumla

Mwandishi anannukuu toka Zaburi kuonesha kuwa mafundisho ya Yesu kwa mfano ni kwa ajili kutimiza unabii

Hayo yote Yesu aliyasema kwa mifano, Na pasipo mifano hakusema chochote kwao

Sentensi zote zina maana moja. Zimeunganishwa kusisitiza kwamba Yesu alifundisha makutano kwa kutumia mifano.

hayo yote

Hii inamaanisha kuwa kile alichofundisha Yesu kinaanzia 13"1

Pasipo mifano hakusema chochote kwao

""hakufundisha chochote isipokuwa kwa mifano"

kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema

alaikifanya kiwe kweli kile alichokuwa amemwambia mmoja wa manabii kukiandika hapo zamani

aliposema

nabii aliposema

nitafumbua kinywa chcangu

Hii ni nahau inayomaanisha kuwa nitasema "nitasema"

yaliyokuwa yamefichwa

mambo ambayo Mungu ameyaficha

tangu misingi ya ulimwengu

"tangu kuanza kwa ulimwengu" au tangu Mungu aumbe ulimwengu"

Matthew 13:36

Sentensi ungnishi

Mandhari yanahamia kwenye nyumba amabyo Yesu na wanafunzi wake walikuwa wanaishi. Yesu anaanza kuwafundiasha mfano wa shamba ambalo lilikuwa na magugu na ngano alilokuwa amewaambia mwanzoni katika 13:24.

kwenda nyumbani

"aliingia ndani" au "aliingia kwenye nyumba ile aliyokuwa anaishi"

apandae

"mpamzi"

Mwana wa Adamu

Yesu anamaanisha yeye mwenyewe

wana wa ufalme

Hapa "wana wa" inamaanisha kuwa mali ya au kuwa na tabia zilezile alizo nazo.

wa ufalme

Mungu ni mfalme

wana wa yule mwovu

watu ambao ni mali ya yule mwovu

adui aliyezipanda

"adui aliyepanda magugu"

mwisho wa ulimwengu

"mwisho wa nyakati

Matthew 13:40

Sentensi unganishi

Yesu anamaliza kuwaeleza wanafunzi wake mfano wa shamba lenye magugu na ngano

Kama vile magugu yanavyokusanywa nakuchomwa moto

Kwa hiyo, kama watu wayakusanyavyo magugu na kuyachoma moto"

mwisho wa ulimwengu

mwisho wa nyakati

Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake

Yesu anamaanisha yeye mwenyewe

wale watendao maasi

"wale wasio na sheria" au "watu waovu"

tanuru la moto

moto wa kuzimu

kulia nakusaga meno

Hii inamaanisha huzuni kubwa na mateso

watakapong'aa kama jua

watakuwa rahisi kuwaona kama jua

Baba

hiki ni cheo muhimu cha Mungu

yeye aliye na masikio

kila anayenisikiliza

Matthew 13:44

Sentensi unganishi

Yesu anaelezea juu y a ufalme wa Mungu kwa kutumia mifano miwili ya watu waliouza mali zao kwa kununua kitu cha thamani zaidi

Maelezo kwa ujumla

Katika mifano hii Yesu anatumia milinganyo miwili kuwafundisha wanfanzi wake kuhusu mfano wa ufalme wa mbinguni

Ufalme wa mbinguni ni kama

Tazama ilivyotafsiriwa katika 13:24

kama hazina iliyofichwa shambani

hazina ambayo mtu alificha shambani

hazina

kkitu cha thamani sana au vitu vilivyokusanywa

kuficha

alifunika kwa juu

aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kulinunua shamba lile

Maana yake nin kwamba yule mtu ananunua lile shamba ili ili achukue ile hazina iliyofichwa

ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu ya thamani

maana yake ni kwamba yule mtu alikuwa anatafuta ile luu ya thamani ili aweze kuinunua

mfanya biashara

mchuuzaji au mtu anayeshughulika kuuza vitu vya jumla ambaye mara kwa mara hupata wateaja tokea mbali

lulu ya tahmani

"lulu" ni kitu lain, kigumu, kinachong'aa, cheupe au shanga yenye mng'ao inayopatikana kwenye viumbe wenye asili ya konokono baharini. Lulu ina bei y a juu sana na hutengenezwa vitu vya thamani kama pete.

Matthew 13:47

Sentensi unganishi

Yesu anaelezea ufalme wa mbinguni kwa kutumia mfano wa mvuvi anayetumia nyavu kubwa kukamata samaki

Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu

ufalme sikama nyavu, lakini ufalme hukokota watu wa kila aina kamavile nyavu zikokotavyo aina zote za samaki

ufalme wa mbinguni ni kama

tazama katika 13:24

ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari

kama nyavu ambayo wavuvi hutupa ndani ya bahari

iliyotupwa ndani ya bahari

"iliyotupwa baharini"

hukusanya viumbe wa kila aina

"ilikamata viumbe wa kila aina

walivuta ufukweni

"walivuta ule wavu mpaka ufukweni"

vitu vyema

"vile vizuri"

visivyo na thamani

"samaki wabaya" au "samaki wasiofaa"

vilitupwa mbali

"havikutunzwa"

Matthew 13:49

Sentensi unganishi

Yesu anaeleza mfano wa mvuvi aliyetumia wavu mkubwa kukamata samaki

mwisho wa dunia

"mwisho wa nyakati"

watakuja

"kuja" au "kwenda" au "kuja toka mbinguni"

watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki

watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki"

na kuwatupa

"malaika watawatupa watu waovu"

tanuru ya moto

tazama 13:40

maombolezo na kusaga meno

Tazama 8:11

Matthew 13:51

Sentensi unganishi

Yesu anaeleza ufalme wa mbinguni kwa kueleza mfano wa mtu anayewatawala watumishi wa nyumbani.Huu ni mwisho wa habari ya Yesu kuwafundisha watu kuhusu ufalme wa mbinguni kwa kutumia mifano

Mmefahamu mambo yote haya? wanafunzi walimjibu, "Ndiyo"

Yesu aliwaulizakamawalikuwa wameelewa yote haya, na walisema kwamba walielwa

amakuwa mwanafunzi wa ufalme wa mbingun

amaejifunza ukweli kuhusu Mungu wetu wa mbinguni ambaye ni mfalme.

unafananan na mwenye nyumba ataoaye katika hazina yake vitu vipya.

Yesu anafundisha mfano mwingine. Anawafananisha waandishi, ambao wanalyafahamu maandiko vizuri ambayo Musa na manabii waliandika, na ambao pia sasa wanayapokea mafundisho ya Yesu na kuyalinganisha namwenye nyumba anayetumia vitu hazina ya zamani na mpaya.

hazina

Hazina ni kitu cha thamani. Hapa panafananishwa na mahali ambapo vitu huhifadhiwa. "chumba cha kutunzia".

Ikawa Yesu alipomaliza

Kirai hiki kinatuhamishaia simulizi yetu ya mafundisho ya Yesu kwenda kile kilichotokea baadaye.

Matthew 13:54

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwanzo wa habari mpya inyotupeleka hadi 17:26, ambapo mwandishi anaeleza juu ya mwendelezo wa upinzani katika huduma ya Yesu kuhusu ufalme wa mbinguni. Hapa watu wa nyumbani kwao Yesu wanamkataa..

"mji wa nyumbani kwao

" Huu ni mji wa Nazarethi ambapo Yesu alikulia

katika masinagogi yao

kiwakilishi "yao" kinamaanisha watu wa eneo hilo

walishangaa

"walishangaa

Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza

"Yawezekananje mtu wa kawaida kama huyu kuwa na mwenye hekima na kufanya miujiza mikubwa.

Mtu hyu siyo mwana wa seremala ...ameyapata wapi haya yote.

Makutano wanatumia maswali haya, kuonyesha mshangao wao kuwa mtu wa kawaida kutoka mji wao anafanya mambo haya yote. Mtu wa kawaida hawezi kuyafanaya haya yote.

Matthew 13:57

Aliwachukiza

watu walimkataa Yesu

Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao

nabii hupokea heshima kila mahli

nchini yao

"mji wa kwao"

kwao

"nyumbani kwao"

Na hakuweza kufanya miujiza mingi

"Yesu hakuweza kufanya miujiza nyumbani kwao"


Translation Questions

Matthew 13:3

Katika mfano wa Yesu wa mpanzi, kilitokea nini kwenye mbegu zilizoanguka kando ya njia?

Mbegu zilizoanguka kando ya njia zililiwa na ndege.

Katika mfano wa Yesu wa mpanzi, kilitokea nini kwenye mbegu zilizoanguka juu ya mwamba?

Mbegu zilizoanguka juu ya mwamba ghafla zilichipuka lakini zilichomwa na jua na zilikauka.

Matthew 13:7

Katika mfano wa Yesu wa mpanzi, kilitokea nini kwenye mbegu zilizoanguka katika miti yenye miiba?

wenye mbegu zilizoanguka katika miti yenye miiba zilisongwa na miti yenye miiba.

Katika mfano wa Yesu wa mpanzi, kilitokea nini kwenye mbegu zilizoanguka katika udongo mzuri?

Mbegu zilizoanguka katika udongo mzuri zilizaa, zingine mar mia, zingine mara sitini na zingine thelathini.

Matthew 13:13

Unabii wa Isaya ulisema watu wangesikia lakini wasiweze kufanya nini?

Unabii wa Isaya ulisema watu wangesikia lakini wasiweze kuelewa na wangeona lakini wasiweze kutambua.

Matthew 13:15

Watu waliomsikia Yesu bila kumwelewa walikuwa na tatizo gani?

Watu waliomsikia Yesu wasiweze kumwelewa walikuwa na mioyo yenge giza na wagumu kusikia na walifumba macho yao.

Matthew 13:18

Katika mfano wa mpanzi ni aina gani ya mtu ambaye ni kama mbegu iliyopandwa kando ya njia?

Mbegu iliyopandwa kando ya njia ni yule ambaye husikia neno la ufalme lakini na halielewi, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kupandwa ndani ya moyo wake.

Matthew 13:20

Katika mfano wa mpanzi ni aina gani ya mtu ambaye ni kama mbegu iliyopandwa kwenye ardhi yenye mwamba?

Mbegu iliyopandwa kwenye ardhi yenye mwamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha, lakini hujikwaa ghafla wakati mateso yanapotokea.

Matthew 13:22

Katika mfano wa mpanzi ni aina gani ya mtu ambaye ni kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba?

Mbegu iliyopandwa kwenye miiba ni yule mtu anayesikia neno la Mungu, lakini masumbufu ya dunia na udanganyifu wa utajiri hulisonga neno.

Katika mfano wa mpanzi ni aina gani ya mtu ambaye ni kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri?

Mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri ni yule mtu anayesikia neno la Mungu na kulielewa na kisha huzaa matunda.

Matthew 13:27

Katika mfano wa magugu ni nani aliyepanda magugu shambani?

Adui alipanda magugu katika shamba.

Matthew 13:29

Mwenye shamba aliwapa maelekezo gani watumishi juu ya ngano na magugu?

Mwenye shamba aliwaambia watumishi kuviacha vyote vikue pamoja hadi wakati wa mavuno, kisha kuyakusanya magugu na kuyachaoma na ngano kuikusanya kwenye ghala.

Matthew 13:31

Katika mfano wa Yesu juu ya mbegu ya haradari, nini kilitokea kwenye mbegu ndogo ya haradari?

Mbegu ya haradari ilistawi kuwa mti mkubwa kuliko mimea ya bustani hivyo ndege hujenga viota vyao katika matawi yake.

Matthew 13:33

Yesu alisema ni kwa jinsi gani ufalme wa mbinguni ni kama hamira?

Yesu alisema kuwa ufalme wa mbinguni ulikuwa kama hamira iliyochanganywa kwa vipimo vitatu vya unga hadi ilipoumuka.

Matthew 13:36

Katika mfano wa magugu, ni nani alipanda mbegu njema, shamba ni nini, mbegu njema ni nini, na ni nani aliyepanda magugu?

Aliyepanda mbegu ni mwana wa Adamu, shamba ni ulimwengu, mbegu njema ni wana wa ufalme, magugu ni wana wa yule mwovu, na aliyepanda magugu ni mwovu.

Katika mfano wa magugu wavunaji ni nani na mavuno yanawakilisha nini?

Wavunaji ni malaika, na mavuno ni mwisho wa ulimwengu.

Matthew 13:40

Mwisho wa dunia kitatokea kitu gani kwa watenda maasi?

Katika mwisho wa dunia wale wanaofanya maovu watatupwa katika tanuru ya moto.

Mwisho wa dunia kitatokea kitu gani kwa watenda haki?

Katika mwisho wa dunia watendao haki watang'aa kama jua.

Matthew 13:44

Katika mfano wa Yesu yule mtu alifanya nini ili kupata hazina kwenye shamba ambacho kinawakisha ufalme wa mbinguni?

Mtu aliyepata hazina aliuza kila kitu alichakuwa nacho na kununua lile shamba.

Katika mfano wa Yesu yule mtu alifanya nini ili kupata lulu ya thamani kuu inawakilisha ufalme wa mbinguni?

Mtu yule aliyepata lulu ya thamani kuu aliuza kila kitu alichokuwa nacho na kuinunua.

Matthew 13:47

Namna gani mfano wa nyavu ya kuvulia samaki unafanaishwa na tukio la mwisho wa dunia?

Kama vile vitu vitu vibaya vilivyotengenishwa na vitu vizuri kutoka kwenye nyavu na vibaya vikatupwa, mwisho wa dunia watu waovu watatenganishwa kutoka miongoni mwa wenye haki na kutupwa katika tanuru ya moto.

Matthew 13:54

Watu wa mkoa wa Yesu waliuliza swali gani waliposikia habari za mafundisho ya Yesu?

Watu waliuliza, "Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?

Matthew 13:57

Yesu alisema kitu gani huwa kinatokea kwa nabii katika nchi yake?

Yesu aliisema nabii hapati heshima katika nchi yake.

Nini kilitokea katika mkoa wa Yesu kwa sababu watu hawakuamini?

Kwa sababu watu hawakuamini, Yesu hakufanya miujiza mingi katika mko wake.


14

1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu.2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.”

3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.”5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.

6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.7Katika kujibu aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.”9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.13Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.14Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao.

15Jioni ilifika, wanafunzi wakaja kwake na kusema, “Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao.

16Lakini Yesu akawaambia, “Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula”

17Wakamwambia, “Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu.”

18Yesu akasema, “Ileteni kwangu.”19Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini kwenye nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati.20Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili.21Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.

22Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.23Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.24Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mbisho.25Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.26Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, “Ni mzuka,” na kupaza sauti katika hali ya uoga.27Yesu akawaambia mara moja, akisema, “Jipeni moyo! Ni mimi! Msiogope.”

28Petro alimjibu kwa kusema, “Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.”

29Yesu akasema, “Njoo.” Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.30Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, “Bwana, niokoe!”

31Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?”32Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulitulia kuvuma.

33Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, “Kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”

34Na walipokwisha kuvuka, walifika katika nchi ya Genesareti.35Na watu katika eneo lile walipomtambua Yesu, walituma ujumbe kila sehemu za kando, na kuleta kila aliyekuwa mgonjwa.

36Walimsihi kwamba waweze kugusa pindo la vazi lake, na wengi walioligusa waliponywa.


Mathayo14 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

14:3-12 inataja matukio yaliyotokea hapo awali. Kwa hiyo, kuna mkatizo katika utaratibu wa matukio wa hadithi. Kusudi la mkatizo huu ni ufafanuzi; mtafsiri ataona umuhimu wa kuashiria mkatizo huu.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Kinaya

Herode aliamini kwamba kuvunja kiapo kulikuwa na aibu, hivyo aliamuru kuuawa kwa Yohana Mbatizaji. Hata hivyo, mauaji ambayo aliwajibika ilikuwa mbaya zaidi. Hii ni kinaya.

Links:


Matthew 14:1

Maelezo kwa ujumla

Mistari hii inaeleza jinsi Herode alivyopokea aliposikia habari za Yesu. Tukio hili linfuatia baada ya tukio linalofuata katika simulizi

Kwa wakati huo

"Katika siku hizo" au "wakati Yesu akiendelea na huduma huko Galilaya"

alaisikia habari juuya Yesu

alaisikia juu ya uvumi wa Yesu

Akawaambia

"Herode alisema"

amaefufuka ktoka wafu

amerudi kuishi

kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake

Baadhi ya Wayahudi waliamini kuwa kama mtu atarudikutoka wafu anaweza kuwa nanguvu za kufanya mambo makubwa.

Matthew 14:3

Sentensi unganishi

Hapa mwandishi anaanza kueleza jinsi Herode alivyomnyonga Yohana mbatizaji. Matukio haya yanaanza kuonekana kabal y a matukio yaliyo kwenye mistari iliyopita

Maelezo kwa ujumla

Mwandishi anaeleza upya habari ya kifo cha Yohana mbatizaji ili kuonesha kwa nini Herode aliitikia kwa jinsi alivyofanya aliposikia habari za Yesu

Kwa kuwa Herode .... kuwa mke wako

Kama inahitajika unaweza kurudia mpangilio wa tukio kama ulivyo 9:3 -4.

Herode alikuwa amemkamata Yohana na kumfunga, na kumtupa gerezani

Inasemekana kuwa Herode alifanya mabo haya kwa sababu aliwaamuru wengine kufanya kwa ajili yake.

mke wa Filipo

Filipo ni jina la kakawa Herode

Kwa kuwa Yohana alimwambia kuwa si halali kumchukua yeye kuwa mke wako

Kwa kuwa Yohana alikuwa amemwambia kuwa siahali kwake kumchukua kama mke wake"

kwa kuwa Yohana alimwambia

"Kwa kuwa Yohana aliendelea kumwambia Herode"

si halali

Filipo bado alikuwa hai wakati Herode anamwoa Herodia

aliogopa

Herode aliogopa

walimwona

"walimwona Yohana

Matthew 14:6

katkati ya watu

katikati ya wageni waliokuwa wamehudhuria ile sherehe ya kuzaliwa

Matthew 14:8

Baada ya kushauriwa na mama yake

baada ya mama yake kumpa maelekezo

kumwelekeza

"kumfundisha" au "kumwambia"

alisema

"binti wa Herodia alaisema kwa Herode"

kombe

sahani kubwa sana

mfalme alikuwa na sikitiko

ombilake lilimfanya mfalme asikitike

mfalme

"mfalme Herode"

aliamuru kwamba inapaswa ifanyike

"aliwaamuru watu wake wafanye alichosema"

Matthew 14:10

Sentensi unganishi

Hii inakamilisha habari ya Herode alivyomuua Yohana mbatizaji

kichwa chake kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti

mtu mmoja akaleta kichwa chake kwenye sinia akpeewa yule binti

sinia

sahani kubwa sana

binti

binti ambaye hajaolewa

wanafunzi wake

wanafunzi wa Yohana

mwili

maiti

walienda kumwambia Yesu

wanafunzi wa Yohana walienda kumwambia Yesu kile kilichotokea kwa Yohana mbatizaji

Matthew 14:13

Sentensi unganishi

Mistari hii inaeleza jinsi Yesu alivyopokea taarifa za kuuawa kwa Yohana mbatizaji.

Maelezo kwa ujumla

Mistari hii inatoa historia yaju ya muujiza ambao Yesu anataka kuufanya wa kulisha watu elfu tano.

Naye

Neno hili limetumika hapa kama mwanzo wa habari mpya. Hapa Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya habari hii.

ulipofahamu

" walposika kilichoteka kwa Yohana au waliposikia habari za Yohana

akajitenga

"aliondoka" au "alaienda mbali n a kundi

kutoka mahali pale

"kutoka eneo hilo"

wakati umati ulipofahamu

"wakati umati waliposikia kule Yesu alikokuwa ameenda

umati

"makutano ya watu" aua "kundi kubwa la watu"

kwa miguu

Hii inamaanisha kuwa wale watu walikuwa wkitembea

kisha Yesualikuja mbele zao akauona umati

Yesu alipokuja karibu na ufukwe akauona umati wa watu

Matthew 14:15

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu akiwalisha watu elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili

wanafunzi wakaja kwake

"wanafunzi wa Yesu wakaja kwake"

Matthew 14:16

hawana haja

"watu hawana haja"

wapeni ninyi

neno "ninyi" ni la wingi linalomaanisha wanafunzi

wakamwambia

"wanafunzi wakamwambia Yesu

mikate mitano

mkate ni bonge lenye sura kama donge lililookwa

"ileteni kwangu"

"leteni mkate na samaki kwangu

Matthew 14:19

Sentensi unganishi

Hii inahitimisha habari ya Yesu ya kuwalisha watu elfu tano

kukaa chini

kaeni

akachukua

akabeba mikononi mwake

kumega mikate

kuivunja mikate

mikate

mikate mizima

akatazama juu

maana zaweza kuwa 1) alipokuwa akitazama juu 2) baada ya kutazama juu

wakala wote na kushiba

walishiba hadi walipokuwa hawana njaa

walikusanya

wanafunzi walikusanya aua waaaaatu walikusanya

vikapu kumi na mbili

vikapu 12 vilivyojaa

waliokula

waliokula mikate na samaki

elfu tano

wanaume 5,000

Matthew 14:22

Sentensi unganishi

Mistari ifuatayo inaelaza matukio yaliyotokea baada ya Yesu kuwalisha watu elfu tano

Maelezo kwa ujumla

Mistari hii inatoa historia juu ya muujiza amabo Yesu anataka kuuonesha juu ya kutumbea juu ya maji

Mara moja

"Punde tu baada ya Yesu kuwalisha watu wote"

ilipokuwa jioni

"baadaye jioni" au "giza lilipoingia"

bahari ikiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi

"na wanafunzi hahawezi kuiongoza mashua kwa sababu ya mawimbi makubwa"

kwani upepo ulikuwa wa mbisho

kwani upepo ulivuma kinyume nao

Matthew 14:25

zamu ya nne

zamu ya inne ilikuwa kati ya saa 9 za usiku mpaka machweo

akaitembea juu ya bahari

akaitembea juu ya maji

walihofu

"waliogopa sana

Ni mzuka

Roho ile iliyotengana na mwili wa mtu baada ya kifo

Matthew 14:28

Petro alimjibu

Petro alimjibuYesu

Lakini Petro alipoona mawimbi

Hapa "kuona mawimbki" maana yake ni kwamba ni kwamba alitambua kuwa kulikuwa na upepo

Matthew 14:31

wewe mwenye imani ndogo

"wewe uliye na imani ndogo kiasi hicho

kwa nini ulikuwa na mashaka

Haukupaswa kuwa na mashaka

Mwana wa Mungu

Hii ni sifa ya muhimu ya Yesu inayoonesha mahusiano kati yake na Mungu

Matthew 14:34

Sentensi unganishi

Mistari hii inaeelza kile kilichotokea baada ya Yesu kutembea juu ya maji. Mistari hii inatoa muhtasari wa jinsi watu walivyokuwa wakiitikia kwenye huduma ya Yesu

Na walipokwisha kuvuka

Wakati Yesu na wanafunzi walipokuwa wamevuka bahari

Genesareti

Huu ni mji mdogo ulioko Kaskazini Magharibi mwa mji wa bahari ya Galilaya

walituma ujumbe

"wanaume wa eneohilo waltuma ujumbe

walmsihi

waagonjwa walimsihi

Pindo la vazi lake

"chini yavazi" au "ncha ya vazi"

vazi

"joho" au "kile alichokuwa amevaa"

waliponywa

wakawa salama


Translation Questions

Matthew 14:1

Herode alifikiri Yesu kuwa ni nani?

Herode alifikiri kuwa Yesu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu.

Matthew 14:3

Herode alikuwa anafanya kosa gani ambalo lilimfanya Yohana mbatizaji amkemee?

Herodealikuwa amemwoa mke wa ndugu yake

Kwa nini Herode hakumwuaYohana Mbatizaji mara moja?

Herode hakumwua Yohana mbatizaji mara moja kwa sababu aliwahofia watu ambao walimtambua Yohana kuwa ni nabii

Matthew 14:6

Herode alifanya nini baada ya Herodia kucheza katika siku ya kuzaliwa kwake?

Herode aliahidi kwa kiapo kumpa Herodia chochote ambacho angeomba.

Matthew 14:8

Binti wa Herodia aliomba kitu gani?

Binti wa Herodia aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji kiletwe kwenye sahani

Kwa nini Herode alimpatia binti wa Herodia kama ombi lake lilivyokuwa?

Herode alimpatia Binti wa Herodia kwa sababu ya kiapo chake na kwa sababu ya watu waaliokuwapo kwenya sherehe hiyo.

Matthew 14:13

Yesu alifanya nini alipoona umati mkubwa ukimfuata?

Yesu aliwahurumia na kuwaponya wagonjwa wao.

Matthew 14:16

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wafanye nini kwa umati?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwapa umati chakula.

Matthew 14:19

Yesu alifanya nini kwa mikate mitano na samaki wawili alipoletewa na wanafunzi?

Yesu alitazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate na akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa umati.

Watu wangapi walikula na chakula kiasi gani kilibaki?

Waliokula walikuwa wanaume elfu tano bila ya kuwahesabu wanawake na watoto, na vilibaki vikapu kumi na mbili.

Matthew 14:22

Yesu alifanya nini baada ya kuwatawanya makutano?

Yesu alipanda yeye mwenyewe mlimani kuomba.

Kilikuwa kinatokea nini kwa wanafunzi walipokuwa katikati ya bahari?

Ile mashua ya wanafunzi ilikuwa ikiyumbayumba kwa sababu y a upepo na mawimbi.

Matthew 14:25

Yesu alikwenda kwa wanafunzi wake kwa namna gani?

Yesu alikwenda kwa wanafunzi kwa kutembea juu ya maji.

Wanafunzi walipomwona Yesu aliwaambia nini?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wajipe moyo na wasiogope.

Matthew 14:28

Yesu alimwambia Petro aje na afanye nini?

Yesu alimwambia Petro aje na atembee juu ya maji.

Kwa nini Petro alianza kuzama ndani ya maji?

Petro alianza kuzama ndani ya maji alipoogopa.

Matthew 14:31

Nini kilitokea wakati Yesu na Petro walipoingia kwenye mashua?

Wakati Yesu na Petro walipoingia kwenye mashua upepo ulikoma kuvuma.

Wanafuzi wakifanya nini walipoona jambo hili?

Wanafunzi walipoona jambo hili walimwabudu Yesu na kusema kweli alikuwa ni Mwana wa Mungu.

Matthew 14:34

Watu walifanya nini wakati Yesu na wanafunzi walipokwenda upande mwingine wa bahari?

Wakati Yesu na wanafunzi walipokwenda upande mwingine wa bahari, watu walimletea Yesu wagonjwa wote.


15

1Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,2“Kwa nini wanafunzi wanayaharibu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.”

3Yesu akawajibu na kusema, “Nanyi, kwa nini mnaiharibu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?4Kwa kuwa Mungu alisema, ‘Mheshimu baba yako na mama yako;’ na ‘Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.’

5Lakini ninyi husema, ‘Kila amwambiaye baba yake na mama yake, ‘Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kwa Mungu,”6Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitoa neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.7Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,8‘Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.9Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”’

10Ndipo akawaita umati na kuwaambia, “Sikilizeni na muelewe.11Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.”

12Ndipo wanafunzi wakamfuata na kusema na Yesu, “Je! Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?”13Yesu aliwajibu na kusema, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.14Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni.”

15Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Tuelezee mfano huu kwetu.”

16Yesu akajibu, “Nanyi pia bado hamuelewi?17Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?18Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.19Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.20Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi.”

21Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.22Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.”

23Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsisitiza, wakisema, “Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.”

24Yesu aliwajibu na kusema, “Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”

25Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, “Bwana nisaidie.”

26Alimjibu na kusema, “Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

27Akasema, “Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao.”

28Ndipo Yesu akajibu na akisema, “Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo.” Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.

29Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko.30Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya.31Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.

32Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, “Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani.”

33Wanafunzi wake wakamwambia, “Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkubwa hivi?”34Yesu akawaambia, “Mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba, na samaki wadogo wachache.”

35Yesu akawaamuru umati uketi chini.36Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.37Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.38Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.

39Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.


Mathayo15 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka mbele kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 15: 8-9, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

"Desturi"

"Desturi za wazee," yaani, sheria zilizotamkwa, ni dhana muhimu katika sura hii. Hizi ndizo sheria ambazo viongozi wa kidini kati ya Wayahudi walikuza ili kuhakikisha kwamba Sheria ya Musa ilipata utii. Hata hivyo, sheria hizi mara nyingi zilikuwa muhimu zaidi katika vitendo kuliko Sheria ya Musa yenyewe. Yesu aliwakemea viongozi wa kidini kwa hili, na kwa sababu hiyo wao wakawa na hasira.

Wayahudi na Wayunani

Imani ya mwanamke Mkanaani kwake Yesu ulikuwa tofauti sana na kutomkubali kwa viongozi wa Kiyahudi. Tofauti hii ilichangia kukemewa vikali kwa viongozi hao.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kondoo

Watu mara nyingi huashiriwa kama kondoo katika maandiko. Katika sura hii, taswira ya kondoo inaonyesha kuwa Wayahudi walikuwa wamepotea kiroho bila ya kuwa na kiongozi mwafaka wa kuwaongoza.

Links:


Matthew 15:1

Maelezo kw ujumla

Hapa Yesu anajibu hoja za Wayahudi

kwa nini wanafunzi wanayahalifu mapokeo ya wazee?

wanafunzi wako hawaziheshimu taratibu amabzo mababu zetu walitupa

Mapokeo ya wazee

Hizi si sawa na sheria za Musa. haya ni mafundisho na tafsiri za sheria zilizotolewa na viongozi wa dini baada ya Musa

hawanawi mikono y ao

kunawa huku siyo tu kwa kusafisha mikono. Hii inamaanisha kunawa kwa desturi kutokana na taratibu za wazee. Hawaoshi mikono yao vizuri

Nanyi kwa nini mnaihalfu sheri ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu

Nami n aona kwamba mnakataa kuzitii sheria za Mungu ili tu mweze kufuata kile ambacho mababu zenu waliwafundisha

Matthew 15:4

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kwajibu Mafarisayo

Maelezo kwa ujumla

Katika mstariwa 4, Yesu ananukuu m ara mbili kutoka kitabu cha kutoka ili kuonyesha jinsi Mungu anavyotegemea watu kuwatendea wazazi wao

hakika atakufa

watu watamuua

Lakini ninyio husema, 'kila amwambiaye baba yake na mama yake ... mtu huyo hana haja ya kumheshimu baba yake

Lakini mnafundisha kuwa mtu hahitajio kuwaheshimu wazazi wake kwa kuwapa kitu ambacho kingeweza kuwasaidia kama mtu atawaambia wazazi wake hivyo tayari ameto zawadi kwa Mungu

hana haja ya kumheshimu baba yake

inamaanisha kuwa baba yake ni mzazi wake. Hii inamaanisha kuwa viongozi wa dini waliwafundisha kuwa mtu hana haja ya kumheshimu mzazi wake kwa kumsaidia.

mmelitangua neno la Mungu kwa ajiliya mapkeo yanu

Mmezifanya desturi zenu kuwa za muhimu kulikko neno la Mungu

Matthew 15:7

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha majibu yake kwa Mafarisayo

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 8 na 9Yesu anamnukuu nabii Isaya kwa kuwakemea Mafarisayo na waandishi

ni vyema kama Isaya alivyotabiri juu yenu

Isaya alisema ukweli katika unabii wake juu ayenu

alaposema

aliposema kile ambacho Mungu alisema

watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao

Watu hawa wanasema kweli kwangu

kwangu

viwakilishi vya "kwang"u vinaanisha Mungu

lakini mioyo yaoiko mbali na mimi

watu hawjajitoa kwa ukweli kwa Mungu

wananiabudu bure

"Ibaada zao hazina maana kwangu" au "wanaigiza kuniabudu mimi"

maagizo ya wanadanu

"shseria ambazo watu hutengeneza

Matthew 15:10

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuwafundisha makutano na wanafunzi wake juu ya kile kinachomtia mtu unajisi na kwa nini mMafarisayo na waandishi walikuwa wamekosea kumkosoa Yesu

Sikilizeni na mfahamu

Sikilizeni kwa makini kile ninachosema ili muelewe maana yake.

Kiingiacho mdomono ... kitokacho kinywani

Yesu anatofautisha kile ambacho mtu hula na kile asemacho. Yesu anamaanisha kuwa Mungu hujali zaidikile ambacho mtu husema kuliko kile ambacho hula

Matthew 15:12

Mafaaarisayo walipolisikia lile neno walikwazika

Usemi huu uliwafanya Mafarisayo wachukie

Kila mmea ambao baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa

Hiki ni kirai kinachomaanisha kuwa Mafarisayo si watu wa Mungu, kwa hiyo Mungu atawatoa

Baba yangu wa mbinguni

Hiki ni cheo cha Yesu kinachoonesha uhusiano kati yake na Mungu

watang'olewa

Baba yangu atawang'oa

waacheni pekee

neno pekee linamaanisha Mafrarisayo

mtu kipofu ... wataanguka shimoni

Inamaanisha kuwa Mafarisayo hawajui amari za Mungu au jinsi ya kumpendeza Mungu Kwa hiyo, hawawezi kuwafundisha wengine jinsi ya kumpendeza Mungu

Matthew 15:15

Sentensi unganishi

Yesu anaeleza mfano amabao amefundisha katika 15:12

kwetu

kwetu wanafunzi

bado hamuelewi

Yesu mfano kuwakemea wanafunzi kwa kutokuelewa mfano. Pia kwakilisha cha "hamu" kimesisitizwa. Yesu hawezi kuwaamini wanafunzi wake kwa kutokuelewa. Nimekatishwa tamaa na ninyi wanafunzi wangu kwa kuwa hamjaelewa kile ninachofundisha.

Nanyi hamuoni kuwa kile kiendacho ... na kwenda chooni

Yesu anatumia swli kuwakemea wanafunzi kwa kutokuelewa mfano. "hakika mnaelewa ... kwenda chooni"

kiendacho mdomoni

hupitia mdomoni

chooni

Hii ni tafsida kwa eneo ambalo watu huzika uchafu wa mwili

Matthew 15:18

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kufundisha mfano aliofundisha katika 15:12

vyote vitokavyo mdomoni

Hii inamaanisha kile ambacho mtu husema

katika moyo

Hapa "moyo" inamaanisha akili za mtu au ndani ya mtu.

uuaji

kuua mtu asiye na kosa

ushuhuda wa uongo

Kusema kitu juu ya mtu mwingine ambacho ni cha kuumiza na si cha kweli

bila kunawa mikono

Hii inamaansha mtu ambaye hajaosha mikono kwa desturi za wazee

Matthew 15:21

Maelezo kwa ujumla

Hii inaazisha habari y aYesu kumponya binti wa mwanamke Mkananayo

Yesu akatoka

Inamaanisha kuwa wanafunzi waliondoka na Yesu

Tazama, akaja mwanmke Mkanani

Kulikuwa na mwanamke Mkanaani aliyekuja kwa Yesu

Akaja mwanamke Mkanaani kutoka pande hizo

"mwanamke kutoka kundi la watu aliyeitw Mkaanani anayeishi katika eneo hilo.

Nihurumie

Kirai hiki kinamaanisha kuwa alikuwa akimuomba Yesu amponye binti yake.

Mwana wa Daudi

Yesu hakuwa Mwana wa Daudi kimwili, hii inaweza kutafsiriwa kama "wa kizazi cha Daudi"

binti yangu anateswa sana na pepo

Pepo linamtesa sana binti yangu

lakini Yesu hakumjibu neno

Hapa "neno" linamaanisha kile mtu asemacho

Matthew 15:24

Sikutumwa kwa mtu yeyote

Mungu hakunituma kwa yeyote

isipokuwa kwa kondoo waliopotea

Tazama 10:5

alaikuja

mwanamke Mkanaani alikuja

akainama

Hii inaonesha kuwa yule mwanake alikuwa akinyeynyekeza mbele za Yesu

Siyo vyema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa

Yesu anamjibu mwanamke kwa kutumia mithali. Maana yake ni kwamba siyo sawa kuchukua kitu cha Wayahudi n a kuwapa watu wasio kuwa Wayahudi.

mkate wa watoto

mkate unamaanisha chakula kwa ujumla

mbwa wadogo

Wayahudi waliona mbwa kuwa ni wanyama najisi. hapa wanamanisha kama sura ya watu wasio Wayahudi

Matthew 15:27

hata hivyo mbwa waadogo hula chkula ... mezani mwa bwana zao

Yule Mwanamke akamjibu Yesu kwa kutumia mazingira yale yale aliyetumia Yesu kwenye mithali. Alimaanisha kuwa wasiokuwa Wayahudi waliweza kupata kiasi kidogo cha kile walichopata Wayahudi amabcho walikuwa wanatupa.

mbwa wadogo

tazama 15"24

na ifanyike kwako kama ulivyotaka

Nitafanya

binti yake alikuwa ameponywa

Yesu alimponya yule binti

wakati huo

ghafla

Matthew 15:29

Maelezo kwa ujumla

Mstari huu unatoa histora ya muujiza amba Yesu anataka kuufanya wakulisha watu elfu nne

viwete, vipofu, bubu vilema na wengine wengi

wale wasioweza kutembea, wale wasioona, wasiongea, na wale ambao miguu yao na mkono haifanyi kazi

waliwaweka katika miguu ya Yesu

waliwaweka katika mbele ya ya Yesu

vilema wakifanywa wazima

vilema wakaw salama

vilema... viwete ... vipofu

watu viwete ... watu vilema ... watu vipofu.

Matthew 15:32

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu akiwalisha watu elfu nne

wasije wakazimia njiani

"kwa sababu wanaweza kuzimia njiani

ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati huu mkubwa?

hakuna mahali pa karibu tunapoweza kupata mikate ya kutosha huu umati mkubwa

saba na samaki wadogo

mikate saba na samaki wachache wadogo

uketi chini

kaeni mkao wa kula

Matthew 15:36

alitwaa

Yesu alibeba mkononi mwake

akaimega i

akaigawa mikate

na kuwapa

akawapa mikate na samaki

wakakusanya

wanafunzi walikusanya au watu walikusanya

wotewaliokula

watu waliokula

wanaume elfu nne

wanaume 4,000

kwenda sehemu

lile eneo

Magadani

Hili eneo wakati mwingine huitwa Magdala


Translation Questions

Matthew 15:4

Je, Yesu alitoa mfano gani wa jinsi Mafarisayo walivyolifanya neno la Mungu kuwa halina thamani mbele ya mapokeo yao ?

Mafarisayo waliwazuia watoto kuwasaidia wazazi wao kwa kuchukua fedha kuwa "ni zawadi kutoka kwa Mungu"

Je, Yesu alitumia mfano gani unoonesha kuwa Mafarisayo walilifanya neno la Mungu kuwa si kitu mbele ya mapokeo yao.

Mafarisayo waliwazuia watoto kuwasaidia wazazi wao kwa kuchukua pesa na kuzifanya kuwa ni "zawadi toka kwa Mungu"

Matthew 15:7

Je, Isaya alitoa unabii gani juu ya midomo na mioyo ya mafalisayo

Isaya alitabiri kuwa mafarisyo watmheshimu Mungu kwa midomo yao, bali mioyo yao itakuwa mbali na Mungu

Je, Isaya alitabiri nini juu ya midomo ya Mfaisayo na mioyo yao?

Isaya alitabiri kuwa Mafarisayo watamuheshimu Mungu kwa midomo y ao, lakini mioyo yao itakuwa mbali.

Badala ya kufundisha neno la Mungu, Mafarisayo walifundisha nini badala yake kuwa ndiyo mafundisho

Mafarisayo walifundisha maagizo ya wanadamu kuwa ndiyo mafundisho

Matthew 15:10

Je, Yesu alisema ni kitu gani ambacho hakimtii mtu unajisi?

Yesu alisema kuwa kiingiacho mdomoni hakimtii mtu unajisi

Je, Yesu alisema ni kitu gani ambacho humtia mtu unajisi?

Yesu alisema kile kitokachokinywani, ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.

Matthew 15:12

Je, Yesu aliwaitaje Mafarisyo, na alisema kitatokea nini kwao?

Yesu aliwaita Mafarisayo kuwa ni viongozi vipofu, na kwamba alisema kuwa watatumbukia shimoni.

Matthew 15:18

Nivitu gani vikaavyo moyoniambavyo humtia mtu unajisi?

Kutoka moyoni hukaa mawazo machafu, uuaji, uasherati, tamaa mbaya, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi

Matthew 15:21

Je, Yesu alifanya nini kwanza wakati yule mwanamke Mkananayo alipomwaomba Yesu msaada?

Yesu hakumjibu neno lolte

Matthew 15:24

Je, maelezo ya Yesu yalikuwaje juu ya kutokumsaidia yule mwanamke Mkanani?

Yesu alieleza kuwa Yeye alikua ametumwa kwa kondoo wa nyumba Israeli waliokuwa waliopotea.

Matthew 15:27

Yle mwanamke Mkananayo aliponyinyekeza, Yesu alimwabia nini na kumfanyia nini?

Yesu alisema kuwa yule mwanamke ana imani kubwa.

Matthew 15:29

Je, Yesu aliwanyia nini wale makutano waliokuja kwake kule galilaya?

Yesu aliwaponya mabubu, viwete, vilema, na vipofu

Yesua aliwafanyia nini wale makutano waliokuja kwake kule Galilaya?

Yesu aliwaponya mabubu, viwete, vilema, na vipofu

Matthew 15:32

Wale wanafunzi walikuwa na mikate mingapi na samaki wangapi ya kuwalisha makutano?

Wanafunzi walikuwa na mikate saba na samaki wadogo wachache?

Matthew 15:36

Yesu alifanya nini kwa ile mikate na samaki?

Yesu aliichukua ile mikate na samaki halafu akashukuru, akaivunja ile mikate na akawapa wanafunzi.

Ni kiasi gani cha chakula kilibaki baada ya wote kula?

Kulikuwa na vikapu saba vilivyojaa vilibaki baada ya kila mmoja kula.

Ni watu wangapi waliokula na kutosheka kutokana na ile mikate na wale samaki?

Wanaume elfu nne, pamoja na wanawake na watoto walikula na walitosheka.


16

1Mafarisayo na Masadukayo walimjia na kumjaribu Yesu awaonyeshe ishara inayotoka angani.

2Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kuwa “Ikiwa ni jioni mnasema kuwa hali ya hewa ni nzuri, kwa kuwa anga ni jekundu.3Na asubuhi mnasema ‘Hali ya hewa leo si nzuri kwa kuwa anga ni jekundu na mawingu yameifunika anga yote.’ Mnajua kufafanua mwonekano wa anga, lakini hamwezi kufafanua ishara za nyakati.4Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakuna ishara yoyote kitakachopewa, isipokuwa ile ya Yona.” Kisha Yesu akawaacha na akaenda zake.

5Wanafunzi wakaja upande wa pili, lakini walikuwa wamesahau kuchukua mikate.6Yesu akawaambia “Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”

7Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. “Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.”

8Yesu alitambua hilo na kusema, “Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate?9Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya?10Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlichukua?11Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”12Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

13Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, “Watu wanasema kuwa Mwana wa Adamu ni nani?”

14Wakasema, “Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii.”

15Akawaambia, “Ninyi mwasema mimi ni nani?”

16Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.”

17Yesu akamjibu na kumwambia, “Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.18Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda.19Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni.”20Kisha Yesu akawaamuru wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye alikuwa ni Kristo.

21Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.22Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, na kusema, “Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako.”

23Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu Shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu.”

24Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kama mtu yeyote akitaka kunifuata mimi, ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.25Kwa kuwa anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na kwa yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.26Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?27Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika wake. Naye atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.28Kweli nawaambieni kuna baadhi yenu mliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.”


Mathayo16 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mkate

Mkate ni picha maalum katika 16:5-12. Yesu alitumia mjadala wa wanafunzi wake kuhusu mkate ili kuwaonya dhidi ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo. Aliyazungumzia mafundisho haya kana kwamba yalikuwa chachu, kiungo ambacho husababisha mkate kuinuka kabla ya kuokwa.

Wakati huo huo, kutajwa kwa mkate katika sura hii ni maana ya kuwakumbusha wasomaji kwamba Yesu alilisha watu elfu tano na mkate (tazama: Mathayo 14:13-21) na pia watu elfu nne (tazama: Mathayo 15:29-39 ). Maana ni kwamba Yesu hutoa mkate mzuri (mafundishoa), lakini Mafarisayo na Masadukayo hawafanyi hivyo.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Mathayo 16:21 huunda mkatizo katika maelezo haya. Katika hatua hii, Mathayo anatoa maoni kuhusu matendo ya Yesu ambayo yataendelea katika siku zijazo. Ni muhimu kwa mtafsiri kuashiria wazi wazi kwamba maoni haya ni kuhusu siku zijazo, yaliyoingizwa katika maelezo.

Paradox

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Kitendawili kiko katika sura hii: "Yeyote anayetaka kuokoa maisha yake ataipoteza, na yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu ataipata." (Mathayo 16: 24-28).

Links:


Matthew 16:1

Maelezo ya jumla

Hii inaanzisha mapambano kati y a Mafarisayo na Masadukayo

kumjaribu

walimkosoa au walitaka kukamata

ilipokuwa jioni

ni wakati wa siku ambapo juu huzama

hali nzuri ya hewa

hali nzuri, shwali na ya kuvutia

anga jekundu

Wayahudi walijua kuwa, kama anaga litabarika na kuwa jekundu ilikuwa dalili ya kuwa siku inayofuat itakuwa nzuri

Matthew 16:3

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwajibu Mafarisayo na Masadukayo

asubuhi

jua linapochomoza

hali ya hewa mbaya

hali ya mawingu na ya kimbunga

jekundu na mawingu

jekundu na zito

Mnajua kutambua mwonekano wa anaga

mwajua namna ya kutazama na kutambua aina ya hali ya hewa mtakayokuwa nanyo

lakini hamuwezi kutambua ishara za nyakati

lakini hamwezi kutambua kile kinachotokea sasa na kujua maana yake

kizazi kiovu na cha uzinzi

watu amabao si waaminifu kwa Mungu

kinatafuta ishara

tazama 12:38

lakini hakuna ishara yeyote

Mungu hatawapeni ishara

isipokuwa ishara ya Yona

tazama 12:38

Matthew 16:5

Sentensi unganishi

Mandhari yanabadilika nakuto eleka wakati wa mbale. Yesu anatumia nafasi ya kuwaonya wanafunzi juu ya Mafarisayo na Masadukayo

upande wa pili

upande wa pili wa ziwa au upande wa pili wa bahari ya Galilaya

chachu ya Mafarisayo na Masadukayo

Hapa chachu inamaanisha mawazo macahfu na mafundisho yasiyo sahihi ya Mafarisayo Tazama 16:12.

Wakahojiana miongoni mwao

wakajadiliana

eneyi wenye imani ndogo

Ninyi mlio na imani ndogo Tazama 6:30

kwa nini mnawaza... hamkuchukua mikate

Ninasikitika kuwa mnadhani kuwa mlisahau kuchukua mikate kwa sabasbu nimeongea juu ya chahu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Matthew 16:9

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaonya wanafunzi juu ya Mafarisayo na Masadukayo

Je, bado hamtambui na kukumbuka au ... mlivyokusanya

Kwa hakika mnakumbuka ... mlivyokusanya

elfu tano ... elfunne

"5,000 ... 4,000"

au mikate saba ... mlichukua?

kwa hakika mnakumbuka ... mlivyokusanya!

Matthew 16:11

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaonya wanafunzi wake juu ya Mafarisayo na Masadukayo

Imekuwaje hata hamuelewii kuwa sizungumzi nanyi kuhusu mikate?

"Inatakiwa muelewe kwamba siongei kumaanisha mikate kweli."

chachu ya Mafarisayo n a Masadukayo

tazama 16:12

wao...wao

"wanafunzi"

Matthew 16:13

Sentensi unganishi

Yesu anawauliza wanafunzi kama wanaelewa kuwa yeye ni nani

Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?

"Lakini ni ninyi ninaowauliza:mnasema kuwa mimi ni nani?"

wakati

Neno hili limetumika kuonesha mwanzo wa habari kuu au kumtambulisha mtu mwingine, Mathayo anaanza kueleza habari mpya.

Mwana wa Adamu

Yesu anamaanisha yeye mwenyewe

Mungu aliye hai

Hapa neno "hai" linalinganisha Mungu wa Israeli na Miungu wengine wa uongo na masananu ambayo watu waliabudu. Mungu aliye ndiye Mungu pekee mwenye nguvu za kutenda.

Matthew 16:17

Simoni Bar Yona

"Simoni, mwana wa Yona"

damu na nyama havikukufunulia hilo

damu na nyama inamaanisha binadamu

hili kwako

neno "hili" inamaanisha jibu la Petro kwamba Yesu ni Kristo mwana wa Mungu aliye juu

Baba yangu aliye mbinguni

Hicho ni cheo cha muhimu kwa Mungu ambacho kinaelezea uhusiano kati ya Mungu na Yesu

Nami pia ninakwambia

hii inaongeza msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

wewe ni Petro

jina Petro linamaanisha "mwamba"

juu y a mwamba huu nitalijenga kanisa

hii inamaanisha kuwa Petro atakuwa kiongozi wa jamii ya watu wanomwamini Yesu

Milango ya kuzimu haitalishinda

Maana zinazowezekana:1)"nguvu za kifo hazitaliweza kanaisa au 2) Kanaisa langu zitaivunja nguvu ya kifo kama jeshi liingiavyo katika mji

Matthew 16:19

nitkupa wewe

neno wewe linamaanisha Petro

Funguo za ufalme wa mbinguni

Hapa "funguo" zinamaanisha Yesu akimpatia Petro mamlaka. Hii haimaanishi kuwa Petroni mmliki wa ufalme, lakini ana mamlaka ya kuamu nani ataiingia katika ufalme wa Mungu

ufalme wa mbinguni

Ufalme wa mbinguni limetumika katika Mathayo tu. tumia "mbingu"

fungwa duniani...funguliwa mbinguni

kuwatangazia watu kusamehewa au kuhukumiwa kama ilivyofanyika mbinguni

funguo

kitu kinachotumika kufungua na kufunga milango

chochote utakachokifunga mbinguni ...kifungua duniani kimefungiliwa duniani

Mungu wa mbinguni ataruhusu maombi ya Petro kuruhusu au kufunga duniani

itafunga ... itafunguliwa

Mungu atafunga .. Mungu atafungua

Matthew 16:21

Sentensi unganishi

Yesu antabiri kifochake na anaanza kuwambia wanafunzi wake gharama za kumfuata.

kuanzia muda huo

Baada ya Yesu kuwaamuru wanafunzi wake kutokumwambia yeyote kuwa yeye ni Kristo, alianza kushirikisha kile kitakachotokea Yerusakamu

Kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi

Hapa "mikono " inamaanisha mamlaka. Ambapo wazee, makuhani na waandishi watamsababishia maumivu

kuuawa

watamuua

jambo hilina liwe mbali n a wewe

"hapana" au "halitatokea" au "Mungu alizuie"

kufufuka siku ya tatu

"siku ya tatu, Mungu atamfanya aishi tena"

rudi nyuma yangu shetani wewe ni kizuizi

Yesu anamaanisha kuwa Petro anafanya kazi kama shatani kwa sababu Petro anajaribu kumzuia Yesu kukamilisha kile ambacho Mungu amemtuma Yesu. "Rudi nyuma yangu kwa sababu unafanya kama shetani! wewe ni kikwazo kwangu.

Matthew 16:24

nifuate

"uwe mwanafunzi wangu" au "uwe mmoja wa wanafunzi wangu"

auchukue msalaba wake na anifuate

msalaba unawakilisha mateso na kifo. lazima anitii hata kiasi cha kufa"

, na kunifuata

"na kunitii"

Kwa yeyote atakaye

"Kwa yeyote anayetaka"

atayapoteza

Hii haimanishi kuwa yule mtu lazima afe. inamaanisha kumwamini Yesu kuwa jambo la muhimu kuliko maisha yake.

kwa ajili yangu

"kwa sababu ananiamini mimi" au " kwa sababu yangu"

atayaokoa

atapata maisha ya kweli

Ni faida gani atakayopata mtu ... akapoteza maisha yake

Haimpi mtu faida ...maisha yake

akaipata dunia yote

hakuna kitu cha thamani duniani kuliko kuishi na Mungu. " kama akipata kila kitu ulimwenguni"

lakini akapoteza maisha yake

"lakini akapoteza maisha yake"

ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake

"Hakuna kitu ambacho mtu atatoa ili kurudisha uhai wake"

Matthew 16:27

Mwana wa Adamu...baba yake

Yesu alikuwa anajirejelea yeye mwenyewe katika nafsi ya tatu kama "Mwana wa mtu"

katika utukufu wa baba yake

"kupata utukufu sawa na Baba yake"

na malaika wake

"na malaika watakuwa pamoja naye" au "na malaika wa Baba watakuwa pamoja na mimi"

baba yake

Hicho ni cheo kikubwa kwa Mungu ambacho kinaelezea uhusiano wa Mungu na Mwana wa mtu, Yesu

kweli nawambia

"Nawaambieni ukweli"

wewe

kiwakilishi cha wingi kinachomaanisha wanafunzi wa Yesu.

hawataonja kifo

"kuonja" inamaanisha kupitia kifo" au "hawatapitia kifo" aua "hawatakufa"

Mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake

"Ufalme" inamaanisha Mwana Adamu akitawala kama mfalme" aua "mpaka watakapomwona wa Adamu akija kutawala kama mfalme"

mpaka watakapomwaona

Yesu bado anaongelea wanafunzi. "mpaka mtakapomwona"


Translation Questions

Matthew 16:1

Mafarisayo na Masukayo walitaka kuona nini kwa Yesu?

Walitaka awaonyeshe Ishara

Matthew 16:3

Yesu alisema angewapatia nini Mafarisayo na Masdukayo?

Yesu alisema angewapatia Mafarisayo na Masadukayo ishara ya Yona.

Matthew 16:5

Je, Yesu aliwaambia wanafunzi wajitaharishe na nini?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wajitahadharishe na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.

Matthew 16:11

Yesu alikuwa anaongelea nini wakati alipokuwa akiwaambia wnafunzi wajitahadharishe nacho?

Yesu alikuwa akiwaambia juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo

Matthew 16:13

Ni swali gani ambalo Yesu aliwauliza wanafunzi wake wakati walipokuwa wakitoka Kaisaria ya Filipi?

Watu wanasema kuwa Mwana wa Adamu ni nani?

Je, watu wengine walidhani kuwa Yesu alikuwa nani?

Watu wengine walidhani kuwa Yesu alikuwaYohana Mbatizaji

Ni jibu gani ambalo Petro alimjibu Yesu kkwa swali lake?

Jibu la Petro lilikuwa hivi, "Wewe ni Kristo, mwana wa Mungu aliye hai".

Matthew 16:17

Petro alijuwaje jibu la swali la Yesu?

Alifunuliwa na Baba wa mbiguni

Matthew 16:19

Ni mamlaka gani ambayo Yesu alimpa Petro hapa duniani?

Alipewa mamlaka ya kufunga chochote duniani, na kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote atachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni.

Matthew 16:21

katika kipindi hiki, ni kitu gani Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kwa uwazi?

Ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.

Je, Yesu alimwambia niniPetro wakati Petro alipopinga kile ambacho Yesu alikuwa akieleza kuwa kitampata?

Yesu alimwambia Petro, "Rudi nyuma yangu shetani"

Matthew 16:24

Ni jambo gani ambalo kila mmoja anayetaka kumfuata Yesu ni lazima alifanye?

Ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na amfuate Yesu.

Yesu alisema kitu gani ambacho hakimpi faida mwanadamu?

Yesu alisema kuwa haimpii faida mwanadamu kuupata ulimwengu wote.

Matthew 16:27

Yesu alisema Mwana wa Adamu atakuja kwa namna gani?

Yesu alisema kuwa Mwana Adamu atakuja katika utukufu wa baba yake na malaika wake.

Mwana wa Adamu atamlipaje kila mtu atakapokuja?

Mwana wa Adamu atamlipa kila mtu kutokana na matendo yake atakapokuja

Yesu alisema ni nani atakayemwona mwana wa Adamu akija katika ufalme wake?

Yesu alisema kuwa baadhi yao waliokuwa wamesimama naye watamwona mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


17

1Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.2Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.3Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.4Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya.”

5Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni.”6Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.

7Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, “Inukeni wala msiogope.”8Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.

9Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, “Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu.”

10Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “Ni kwa nini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?”

11Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.12Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.”13Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.

14Walipofika katika umati, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.”

17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.”18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.

19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwa nini hatukuweza kumfukuza?”

20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.211

22Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.23Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka.” Wanafunzi walihuzunika sana.

24Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?”25Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “Unafikiria nini Simoni? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawala au kutoka kwa wageni?

26Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.


1Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 “Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga” hayaonekani katika nakala bora za kale.

Mathayo17 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Eliya

Nabii Malaki alitabiri kwamba siku moja Eliya atarudi kabla Masihi hajaja. Yesu anaelezea kwamba Yohana Mbatizaji alitimiza unabii huu kwa kumtumikia Mungu kwa namna ile ile kama Eliya. na )

"Yeye (Yesu) alibadilishwa"

Utukufu wa Mungu unaonekana kama mwanga mkubwa, katika maandiko. Utukufu wa Mungu daima humhofisha mtu anayeuona. Tukio hilo, lililoko katika sura hii, linaitwa "kubadilika," ambako Yesu anabadilika ili aonyeshe utukufu wake wa uungu. na )

Links:


Matthew 17:1

Maelezo kwa ujumla

Hii inazisha habariya Yesu kubadilika sura

Petro, na Yakobo, na Yohana kaka yake

"Petro, Yakobo, na kaka yake Yakobo Yohana"

Alibadilishwa

"Mungu amembadilisha kabisa Yesu

mavazi

"nguo"

Uso wake ukang'aa kama jua ...kung'aa kama nuru

Hii ni milinganyo inayosisitiza jinsi Yesu alivyong'aa.

Matthew 17:3

Tazama

Neno hili linatutayarisha kuwa tayari kwa taarifa za kushangaza zinazofuata.

kwao

kwa wanafunzi waliokuwa na Yesu amabao ni Petro, Yakobo na Yohana

akajibu na kusema

"sema." Petro hajibu swali.

pamoja naye

"pamoja na Yesu"

ni vizuri kwetu kuwa hapa

Maana zinazowezekana: 1)"ni vizuri kwamba sisi wanafunzi tuko hapa pamoja nawe, Musa, na Eliya au 2)"ni vizuri kuwa wewe, Musa, Eliya, na sisi wanafunzi wote tuko hapa pamoja"

mahala pa kujihifadhi

Maana zinazowezekana: 1)mahali pa watu kuja kuabudia au 2)mahali pa muda pa watu kulala.

Matthew 17:5

Tazama

Hii hutahadharisha msomaji kuwa makini na maelezo ya kushangaza yanayofuata

likawatia kivuli

"lilikuaj juu yao"

ikatokea sauti toka kwenye wingu

"Sauti inamaanisha Mungu aliogea" aua "Mungu aliongea noa kutoka kwenye wingu"

waanafunzi waliposikia

"wanafunzi walimsikia Mungu akiongea"

Walianguka kifulifuli

Wanafunzi waliinama kwa nyuso zao kugusa chini ardhini.

Matthew 17:9

Sentensi unganishi

Tukio lifuatalo lilitokea mara tu baada ya wale wanafunzi watatu kushuhudia Yesu akibadilishwa

Na walipokuwa

Na Yesu na wanafunzi wake

mwana wa Adamu

yeye anajinenea mwenyewe

kwa nini wandishai husema kuwa Eliya atakuja kwanza?

Wanafunzi wanazingatia mafundisho ya kwamba Eliya atarudi kwanza kwa wana wa Israel kabla ya Masihi kurudi

Matthew 17:11

Kurudisha vitu vyote

"kuweka vitu katika mpangilio au utaratibu" au " waandae watu tayari kwa ajili kumpokea Masihi"

Lakini nawaambieni

huu ni msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

hawa .... yake

Maana zinazowezekana: 1) viongozi wa wayahudi au 2) wayahudi wote

Mwan wa Adamu atakavyoteswa

Hapa "mikono" inamaanisha nguvu. "watamfanya mwana wa Adamu kuteseka"

Mwana wa Adamu

Yesu anajineneea mwenyewe.

Matthew 17:14

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu akimponya kijana aliyekuwa na roho mchafu.Tukio hili limetokea baada ya Yesu na wanafunzi wake kushuka kutoka mlimani.

umhrumie mwanangu

inamanisha kuwa yule mtu alimtaka Yesu amponye mwanae. "umhurumie mwangu na umponye"

amaekuwa na kifafa

Hii inamaanisha kuwa wakati mwingine hupoteza fahamu

Matthew 17:17

kisichoamini na kilichoharibika

"Kizazi hiki hakimwani Mungu na hakijiui kitu kibaya na kizuri.

nitakaa pamoja nanyi mpaka lini, nitavumiliana nanyi mpaka lini?

nimechoka kukaa pamojana nyi, nichoshwa na kutokuamni kwenu

kijana aliponywa

kijana akawa mzima

tangu saa ile

mara moja

Matthew 17:19

Sisi

waongeaji na si wasikilizaji

Kwa nini tusingeweza kuifukuza?

"Kwa nini tusimfanye pepo amtoke kijana?"

Hakuna kitakachowezekana kwenu kukifanya

"Mtaweza kufanya kitu chochote

kweli nawaambieni

"nawambia ukweli"

kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu haradali

Yesu analinganisha ukubwa wa mbegu ya haradari na kiasi cha imani kinachotakiwa ili kufanya miujiza. inahitajika imani ndogo tu ili kufanya miujiza.

hakutakuwa na kitu chochotte cha kushindikan kwenu

mtaweza kufanya kila kitu

Matthew 17:22

Sentensi unganishi

Yesu anatabiri kifo chake na ufufuo

wamekaa

"wanafunzi na Yesu wamekaa"

Mwan wa Adamu Watamuua

"mmoja atamuua Mwana wa Adamu"

Mwana wa Adamu ...mwa ...watu

inamaanisha yeye yenyewe

Atafufuka

"Mungu atamfufua" au" ataishi tena"

atatiwa

atatolewa

mikononi mwa watu

mikononi inamaanisha mamlaka ya kutwala. "katika utawala wa watu

siku ya tatu

siku ya tau

atafufuka

Mungu atamfufua

Matthew 17:24

Sentensi unganishi

Yesu anamfundisha Petro juu ya kulipa ada ya hekalu

wakati wao

wakati yesu na wanafunzi wake

kodi ya nusu shekeli

kodi juu ya wanaume wote wa kiyahudi ambayo ilitolewa ili kuwezesha kazi za hekaluni

nyumba

mahali Yesu alipokaa

Unafifkiri nini Simoni? wafalme wa dunia ...kutoka kwa wageni?

Yesu anauliza swali hili kumfundisha Simoni asitafute taarifa kutoka kwake. "Sikiliza Simoni, tunafahamu kuwawafalme wa dunia hukusanya kodi kutoka kwa wageni na wala si kwa raia wake.

wafalme wa dunia

viongozi kwa ujumla

Raia

watu chini ya kiongozi au mfalme

wanaotawaliwa

watu walio chini ya mfalme

Matthew 17:26

Sentensi unganishi

Yesu anaendela kumfundisha Petro juu ya kulipa kodi

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwisho wa habariinayoanzi 13:54 amabpo mwandishi amaeelza juu ya upinzani wa wa huduma ya Yesu kuhusu ufalme wa mbinguni

Petro aliposema kutoka kwa wageni

wakati Petro aliposema "ndiyo. hiyo ni sawa ,wafalme hukusanya kodi kutoka kwa wageni"

kutoka kwa wageni

Nyakati hizi za leo. wafalme wanatoza kodi toka kwa raia wake, lakini katika nyakati za zamani wafalme walitoza kodi toka kwa watu waliokuwa wamewashinda na si raia wao.

watawaliwa

Watu chini ya kiongozi au mfalme.

lakini tusije tukawafanya watoza ushuru kutenda dhambi

lakini tusiwafanye watoza ushuru kutenda kuwa na hasira

tupa ndoano

wavuvi hufunga ndoano mwisho wa uzi, na kisha huitupa majini ili kukamata samaki

mdomo wake

"mdomo wa samaki"

shsekeli

sarafu iliyotosha malipo ya kibarau kwa siku moja

chukua

chukua shekeli

kwangu na wewe

wewe inamaanisha Petro. Kila mwanamume alipaswa kulipa shekeli moja. kwa hiyo Shekel moja iliweza kutosha kwa kodi ya Peteo na Yesu


Translation Questions

Matthew 17:1

Ni akina nani walioienda na Yesu juu ya mlima mrefu?

Petro, na Yakobo na Yohana kaka yake.

Kilitokea kitu gani katika muonekano wa Yesu kule mlimani?

Yesu alibalishwasura kiasI kwamba sura yake iling'aa kama jua, na mavazi yake yaling'aa kama nuru.

Matthew 17:3

Ni akina nani waliomtokea Yesu na kuongea naye?

Akawatokea Musa na Eliya wakaongea naye

Je, Petro alisema wafanye nini?

Yesu alisema wajenge vibanda vitatu kwa ajili ya wale wanaume watatu.

Matthew 17:5

Sauti iliyosikika kutoka katika wingu ilisema nini?

Huyu ni mwanangu mpedwa, niliyependezwa naye.

Matthew 17:9

Yesu aliwaagiza nini wanafunzi wake walipokuwa wakishuka chini ya mlima?

Wasitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.

Matthew 17:11

Yesu alisema nini juu ya mafundisho ya waandishi kuwa Eliya atakuja kwanza?

Yesu akawajibu na kusema, Eliya atakuja kweli na atarudisha vitu vyote.

Yesu alisema Yohana Mbatizaji ndiye aliyekuwa Eliya ambaye tayari alikuwa amekwisha kuja, na kile alichofanyiwa.

Yesu alisema kuwa Yohana Mbatizaji ndiye aliyekuwa Eliya ambaye tayari alikuwa amekwisha kuja, na walimfanyia kile walichotaka kumfanyia.

Yesu alisema kuwa Eliya alikuwa amekwisha kuja alikuwa nani, na kile alichofanyiwa?

Yesu alisema Yohana Mbatizaji alikuwa Eliya ambaye tayari alikuwa amekwisha kuja, na walimfanyia chochote walichotaka kumfanyia.

Matthew 17:14

Ni kitu gani wanafunzi walikuwa wakikiweza kukifanya kwa mvulana aliyekuwa na kifafa?

Walikuwa wakiweza kumponya kijana mwenye kifafa.

Wanafunzi wa Yesu waliweza kufanya nini kwa yule mgonjwa wa kifafa?

Wanafunzi hawakuwa na uwezo wa kumponya yule mgonjwa wa kifafa.

Matthew 17:17

Yesu alifanya nini kwa yule mgonjwa kifafa?

Yesu alilikemea lile pepo, na yule kijana alipona tangu saa ile

Matthew 17:19

Kwa nini wale wanafunzi hawakuweza kumponya yule kijana?

Yesu alisema kuwa ni kwa sababu ya imani yao ndogo kwa hiyo wasingeweza kumponya yule kijana mwenye kifafa.

Matthew 17:22

Yesu aliwaambia nini wanafunzi wake kilichowafanya wawe na huzuni?

Kuwa Mwana wa Mtu atatiwa mikononi mwa watu, watamwua, na siku ya tatu atafufuka.

Yesu aliwaambia kitu gani wanafunzi wake kilichowafanya kuwa na huzuni?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa atatiwa mikononi watu ambao watamwua, na kwamba siku ya tatu atafufuliwa.

Matthew 17:26

Yesu na Petro walilipaje ile kodiya nusu shekeli?

alimwambia Petro kwenda baharini, akatupe ndoano na kuchuku yule samaki wa kwanza, naye atakuwa na shekeli mdomoni mwake kwa ajili ya kodi.


18

1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?”

2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao,3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi.

6Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari.7Ole kwa dunia kwa sababu ya wakati wa kukwazwa! Kwa kuwa haina budi kwa nyakati hizo kuja, lakini ole kwake kwa mtu yule nyakati hizo zitakuja kwa ajili yake!8Kama mkono wako au mguu wako ukikusababishia kukwazika, ukate na uutupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe kuingia kwenye uzima ukiwa bila mkono au kilema, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote au miguu yote.9Kama jicho lako likikukwaza, uling`oe na ulitupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe uingie kwenye uzima na jicho moja, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na macho yote.

10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.11112Mnafikiri nini? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je hatawaacha tisini na tisa mlimani na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea?13Na akisha kumpata, kweli nawaambieni, anamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.14Vivyo hivyo, siyo mapenzi ya Baba yenu wa mbinguni kuwa mmoja wa wadogo hawa aangamie.

15Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako.16Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa.17Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.18Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. Na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa.19Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya.20Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.

21Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?”

22Yesu akamwambia, “Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba.23Kwa sababu hiyo ufalme wa mbinguni ni sawa na mfalme fulani aliyetaka kusahihisha hesabu kutoka kwa watumwa wake.24Alipoanza kusahihisha hesabu, mtumwa moja akaletwa kwake ambaye alikuwa anamdai talanta elfu kumi.25Kwa kuwa hakuwa na njia ya kulipa, bwana wake aliagiza auzwe, mke wake pamoja na watoto wake na kila kitu alichokuwa nacho, na malipo yafanyike.26Hivyo mtumwa alianguka, akapiga magoti mbele yake, akisema, ‘Bwana, uwe na uvumilivu pamoja nami, na nitakulipa kila kitu.’27Hivyo bwana wa yule mtumwa, kwa kuwa alisukumwa sana na huruma, alimwachilia na kumsamehe deni hilo28Lakini mtumwa yule alitoka na kumpata mmoja kati ya watumwa wenzake, aliyekuwa anamdai denari mia. Alimvuta, akamkaba kooni, na kumwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai.’

29Lakini yule mtumwa mwenzake alianguka na kumsihi sana, akisema, ‘Uwe na uvumilivu nami, na nitakulipa.’30Lakini mtumwa yule wa kwanza alikataa. Badala yake, alienda na kumtupa gerezani, mpaka atakapo mlipa kile anachomdai.31Na walipoona watumwa wenzake kile kilichotokea. Walisikitishwa sana. Walikuja na kumwambia bwana wao kila kitu kilichotokea.

32Ndipo yule bwana wa mtumwa yule alimwita, na kumwambia, ‘Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni langu lote kwa sababu ulinisihi sana.33Je! Haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio, kama mimi nilivyokuhurumia wewe?34Bwana wake alikasirika na kumkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa kiasi chote alichokuwa anadaiwa.35Hivyo ndivyo Baba yangu wa Mbinguni atakavyowafanyia, kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwenu.”


1Zingatia: Maneno yanayoonekana kama ya msitari wa 11, “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichokuwa kimepotea” hayakuonekana katika nakala bora za kale.

Mathayo18 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Je, unapaswa kufanya nini "ndugu yako akikukosea"?

Katika sura hii, Yesu anafundisha kwamba ni muhimu kwa wafuasi wake kuacha ugomvi kati yao wenyewe. Anafundisha kwamba kikundi cha waumini lazima kiwe tayari kuwezesha hii kufanyika kwa njia "inayomheshimu Mungu.

Kanisa lina jukuma pia wa kuwahimiza waumini kutubu ikiwa wanafanya dhambi. na )

Links:


Matthew 18:1

Maelezo kwa ujumla

Hii ni mwanzo wa habari mpya inayoanzia 18:34, mahali Yesu anapofundisha juu ya maisha katika uflme wa mbinguni. Hapa Yesu anatumia mtoto mdogo kufundisha wanafunzi wake.

nanai mkuu

Nani ambaye ni wa muhimu zaidi"au "nani kati yetu atakuwa wa muhimu zaid

katika ufalme wa mbinguni

wakati Mungu wetu wa mbinguni atakapoanzisha utawala wake duniani

Kweli nawaambia

"nawambia ukweli" au hii inaongeza msisitizo kwa kile Yesu alichosema baadaye

msipotubu na kuwa ... hamtaweza kuingia

lazima mbadilike .. ili kuingia"

kuwa kama watoto

lazima wawe wanyeyenyekevu kama watoto.

kuingia katika ufalme wa mbinguni

Mungu kutawala kama mfalme

Matthew 18:4

Sentensi unganishi

Yesu anawafundisha wanafunzi wake kwamba wanahitaji kuwa wanyeyekevu kama watoto ili kuwa watu wa muhimu kwenye ufakme wa mbingini

ni mkuu

ni wa muhimu zaidi aua atakuwa ni wa muhimu

katika ufame wa mbinguni

katika ufalme wa mbinguni

kwa jina langu

kwa sababu yangu

anipokea mimi

ni kama ananipokea mimi

Jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake,na kuzamishwa kilindini mwa bahari.

"kama wangemwekea jiwe la kusagia shingoni mwake na kumtupa kilindini mwa bahari"

Jiwe la kusagia

Jiwe kubwa, zito iliyotengenezwa kama duara inayotumika kusagia nafaka kuwa unga .

Matthew 18:7

Sentensi unganishi

Yesu anaendela kutumia watoto wadogo kuwafundisha wanafunzi wake na kuwaonya dhidi ya madhara makubwa ya kuwaangusha watoto

kwa dunia

dunia inamaanisha watu

kwa sababu ya wakati wa kukwazwa

kwa sababu ya mambo yanyowafanya watu kukwazwa

Mkono wako

Yesu anaongea na wanafunzi wake kama ni mtu mmoja.

kwa nyakati hizo huja

kwamba mambo hayo huja yanayowafanya watu kufanya dhambi

kwake kwa mtu yule nyakati hizo

mtu yeyote anayewafnya wengine kufanya dhambi

kama mkon wako ... utupe mbali

Yesu anamaanisha kuwa mtu lazima afanye kila linalolazimika ili kukitoa katika maisha kile kinachomfanya mtu kufanya dhambi

wako ... uki

Yesu anaongea kwa watu wote kwa ujumla

kwenye uzima

uzima wa milele

kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote aua miguu yote

kuliko kuwa na mikono miwil na miguu miwili wakati Mungu anakutupa kwenye moto wa milele.

Matthew 18:9

Ng'oa na tupa

Fungu hili linaonesha ukweli wa kutokuamini na ulazima wa kuizuia kwa gharama yoyote

Ingia uzimani

"Ingia katika uzima wa milele"

Matthew 18:10

Tazameni

Muwe waangalifu

musiwadharau hawa wadogo

"Msidhani kuwa hawa wadogo hawana umuhimu". onyesheni heshima kwa hawa wadogo

kwa maana nawaambia

hii inatia msisitizo kwa kile Yesu alichosema baadaye

mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa baba yangu aliye mbinguni

Yesu anammanisha kuwa malaika wa mbinguni humwambia Mungu juu ya wadogo hawa

Muda wote tazama uso wa

"wapo karibu muda wote"

siku zote wakiutazama uso wa baba yangu

kila mara wako karibu na baba yangu"

baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu kinachonesha uhsiano kati ya Yesu na Mungu

Matthew 18:12

Sentensi unganishi

Yesu anaendele kuwatumia watoto wadogo kuwafundisha wanafunzi kueleza ulinzi wa Mungu kwa watu

Unawaza nini?

"Fikiri watu wanavyofanya,"

wewe ... yako

viwakilishi vya wingi

ikiwa mtu ...wasiopotea

Yesu anatumia mfano kuwafundisha wanafunzi

kondoo mia moja ...tisini n a tisa

100 ...99

hatawaacha ...aliyepotea

Yesu anatumia swali kuwafundisha wanafunzi

kweli nawaambia

nawaambia ukweli

Siyo matakwa ya baba yenu wa mbinguni kuwa moja wa wadogo hao apotee

"Baba yenu mbinguni anataka wadogo wote hao waishi"

Matthew 18:15

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuwafundisha wanafunzi wake juuy msamaha

ndugu yao

waumini wenzake

utampata ndugu yako

"mtafanya mahusiano yenu mazuri tena na ndugu yako"

kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili ...kila neno linaweza kuthibitishwa

"mdomo" na "maneno" inamaanisha kile amabcho mtu anasema " ili kwamba wawili au watatu wanaweza kuthibitisha kile unachosema juu ya mwamini mwenzako"

Kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitika

Yesu anatumia moja katai ya sheria ambazo Musa alaiwapati watu

Matthew 18:17

akipuuza kuwasikiliza

kama huyo nndugu akipuuza kuwasiliza mashahidiuliokuja nao

kanisani

kwa waumini wote

Mwacheni awe kwenu kama mtu wa mataifa na mkusanya ushuru

"Mchukulie kama utakavyomchukulia mtu wa mataifa au "mtoza ushuru. Maana yake ni kwamba wamwondoe kati ya jamii ya waumini.

Matthew 18:18

mta

viwakilishi vyote hivi viko katka wingi

Funga...fungwa...fungua...funguliwa

tazama 16:19

Itafungwa...itafunguliwa

"Mungu atafunga...Mungu atafungua."

nawaambieni

Msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

Baba yangu

Hicho ni cheo cha muhimu kwa Mungu kinachoonesha uhusiano wa Mungu na Yesu.

kama wawili wenu

anagalau wawili

wawili au watatu

"wawili au zaidi" au "angalau wawili"

Wamekusanyika

"kutana"

waki ... wao

inamaanisha "wawili wenu"

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu kinachoonesha uhusiano kati ya Mungu na Yesu

Matthew 18:21

Mara saba

"mara 7"

Sabini mara saba

Maana zenye kufaa: 1) "70 mara 7". au 2) "mara 77." kama kutumia namba kutachanganya,unaweza kusema, "mara nyingi kuliko utakavyohesabu"

Matthew 18:23

Sentensi unganishi

Yesu anatumia mfano kufundisha juuya msamaha na mapatano

Ufalme wa mbinguni unafanana

Hii inatoa utangulizi wa mfano. Tazama 13:24

Kusahihisha hesabu na mtumwa wake

"ili awalipe watumwa wake kile walichostahili"

Mtumishi mmoja akaletwa

"mtu fulani akamleta mmoja wa watumishi wa wafalme"

Talanta elfu kumi

"Talanta 10,000" au " fedha nyingi zaidi kuliko mtumishi alizoweza kulipa

Mkuu wake aliamuru auzwe,...na malipo kufanyika

"mfalme aliwaamuru watumishi wake kumuuza huyo mtu...na kulipa deni kwa fedha ya mauzo"

Matthew 18:26

alianguka, akapiga magoti chini

Hii inammanisha kuwa yule mtumwa aliongea na yule mfalme katika hali ua unnyenyekevu mkubwa.

mbele yake

"mbele ya mfalme"

alaisukumwa sana na huruma

"alimhurumia yulemtumwa"

alimwachilia

alimwacha aende"

Matthew 18:28

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaambia mfano wanafunzi wake

Dinari mia moja

"dinari 100" au "malipo ya kibarua ya siku miamoja"

alimvuta, akamkaba kooni

"yulemtumwa wa kwanza alimkaba mtumwa mwenzake

alimkaba

kumung'ang'nia " au "kamata kwa nguvu"

alianguka

Tazama 18:26

Matthew 18:30

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaambia mfano wanafunzi wake

alienda na kumtupa gerezani

"yule mtumwa wa kwanza alienda na kumtupa gerezani mtumwa mwenzake"

"watumwa menzake"

"watumwa wengine"

walimwambia bwana wao

"walimwambia mfalme"

Matthew 18:32

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwambia mfano wanafunzi wake

Kisha bwana wa mtumishi yule akamwita

"Kisha mfalme akamwita mtumwa wa kwanza"

ulinisihi

"uliniomba

Je, haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio?

Mfalme anatuma swalikumkalipia mtumwa wa kwanza. "ulitakiwa ... wewe"

Matthew 18:34

Sentensi unganishi

Yesu anamalizia mfano wake juu ya msamaha na upatanishi

Maelezo kwa ujumla

Huuni mwaisho wa shsemu y a simulizi iliyoanzia 18:1 mahali ambapo Yesu anafundisha juu ya maisha katika ufalme wa mbinguni.

Bwana wake

"Mfalme"

kumkabidhi kwa

"alimtoa kwa" inawezekena kuwa mfalme mwenyewe hakumkabidhi yule mtumwa wa kwanza kwa watesaji," "Aliwaagiza watumwa wake wamkabidhi"

kwa watesaji

"kwa wale ambao wangemtesa"

alichokuwa anadaiwa

Hii inaweza kutafasiriwa kwa mafumo tendaji. Kile ambacho mfalme alimdai yule mtumwa wa kwanza"

baba yangu wa mbinguni

Hiki ni cheo muhimu kwa Mungu kinachoonesha uhusiano kati ya Mungu ya Yesu.

mmoja wenu ... kwenu

Viwakilishi vyote hivi viko katika wingi. Yesu anaongea na wanafunzi wake, lakini mfanohuu unafundisha ukweli ambao unaweza kutumiwa na waamini wote

ndugu yake

"ndugu yake"

moyoni mwenu

Hii ni nahau. "kwa ukweli" au "kwa ukamilifu"


Translation Questions

Matthew 18:1

Yesu alisema kitu gani ambacho ni lazima tukifanye ili kuingia mbinguni?

Yesu alisema lazima tutubu na kuwa kama watoto wadogo.

Matthew 18:4

Yesu alisema mkuu katika ufalme wa mbinguni ni nani?

Yeye ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.

kInatokea nini kwa mtu yule anayemkosesha mtoto mdogo amwaminiye Yesu kufanya dhambi?

Yeyote anayemkosesha mtoto mdogo amwaminiye Yesu kufanya dhami, ni vizuri mtu huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingono mwake na kutupwa baharini.

Matthew 18:7

Je, Yesu alisema tufanye nini juu ya kitu kile kinachokwaza?

Yesu alisema lazima tukitupe kila kitu ambacho kinatukwaza.

Matthew 18:10

kwa nini Yesu alisema tusiwadharau walio wadogo?

Kwa maana huko mbinguni malaika wao huutazama uso wa Baba siku zote.

Matthew 18:12

Ni kwa namna gani mtu amtafutaye kondoo aliyepotea ni kama Baba wa mbinguni?

Ni kwa sababu si mapenzi ya Baba kwamba mmoja wa wadogo hawa kupotea

Ni kwa nanmna gani mtu amtafutaye kondoo aliyepotea ni kama Baba wa mbinguni?

Ni kwa sababu kuwa si mapenzi ya Baba kwamba mmoja wa wadogo hawa kupotea

Matthew 18:15

kama ndugu yako akikukosea, ni kitu gani cha kwanza unatakiwa kufanya?

Nenda ukwamwonyeshe kosa lililopo kati yako na yeye mwenyewe.

Kama ndugu yako hakusikilizi, ni kitu gani cha pili unachotakiwa kufanya?

Kitu cha pili, ni kumchukua mtu mmoja au wawili kwa ajili ya ushahidi.

Matthew 18:17

Kama ndugu yako bado hakusikilizi, ni jambo gani la tatu unalotakiwa kufanya?

Kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo. kwenu kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.

Kama akipuuza kukusikiliza ni nini unachotakiwa kufanya?

Mwisho, kama hatalisikiliza kanisa, anataikwa umchukulie kama mtu wa mataifa au mtoza ushuru.

Matthew 18:18

Yesu anaahidi kitu gani kitataokea pale ambapo wawili au watatu wamekusanyika kwa jina lake

Yesu anaahidi kuwepo pamoja nao wawili au watatu waliokusanyika kwa jina lake.

Matthew 18:21

Yesu alisema tunatakiwa tuwasamehe ndugu zetu mara ngapi?

Yesu alisema hata saba mara sabini.

Yesu alisema tunatakiwa tuwasamamehe ndugu zetu mara ngapi?

Yesu alisema tunatakiwa kuwasamehe saba mara sabini.

Matthew 18:23

Je, yule mtumishi alikuwa anadaiwa nini na bwana wake, alichotakiwa kulipa?

Yule mtumwa alikuwa anadaiwa talanta kumi, ambazo hakuweza kuzilipa.

Je, yule mtumishi alikuwa anadaiwa nini na bwana wake, alichotakiwa kulipa?

Yule mtumwa alikuwa anadaiwa talanta kumi, ambazo hakuweza kuzilipa.

Matthew 18:26

Kwa nini Yule Bwana alimsamehe mtumishi wake?

Yule Bwana alimhurumia mtumwa wake na kumsamehe deni lake

Matthew 18:30

Je mtumwa alifanya nini kwa mtumwa mwenzie aliyekuwa anamdai dinari mia moja?

Alienda akamtupa gerezani mpaka atakapomlipa kile anachomdai.

Matthew 18:32

Yuele Bwana alimwambia nini yule mtumishi ambacho alichopaswa kumnyia mtumishi mwenzake?

Yule Bwana alimwambia yule mtumishi kuwa alipaswa kumhurumia mtumishi mwenzake.

Matthew 18:34

Bwana wao alifanya nini kwa mtumwa?

Alimkasirikia na akamkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa yote aliyokuwa anadaiwa.

Je, Yesu alisema Baba atafanya nini, kama hatutawasamehe ndugu zetu kutoka moyoni?

Yesu alisema kuwa Baba atatufanya kama yule Bwana alivyomfanyia mtumishi wake kama hatutawasamehe ndugu zetu kutoka mioyoni mwetu.


19

1Ilitokea wakati Yesu alipomaliza maneno hayo, akaondoka Galilaya, na akaenda mpakani mwa Yudea mbele ya mto Jordani.2Umati mkubwa ukamfuata, na akawaponya huko.

3Mafarisayo wakamjia, wakamjaribu, wakamwambia, “Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?”

4Yesu akajibu na kusema, “Hamkusoma, kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke?5Na tena akasema, ‘Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’6Hivyo siyo wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, kile alichokiunganisha Mungu, mtu yeyote asikitenganishe.”

7Wakamwambia, “Sasa kwa nini Musa alituamuru kutoa hati ya talaka na kumwacha?”

8Akawaambia, “Kwa ugumu wenu wa mioyo Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.9Nawaambieni, kwamba yeyote atakayemwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, na akamwoa mwingine, amezini. Na mwanaume atakayemwoa mke aliyeachwa amezini.”

10Wanafunzi wakamwambia Yesu, “Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa.”

11Lakini Yesu akawaambia, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea.12Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vile vile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee.”

13Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea.14Bali Yesu akasema, “Waruhusu watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.15Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.

16Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, “Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?”

17Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu.”

18Yule mtu akamwuliza, “Ni sheria zipi?” Yesu akasema, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,19waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.”

20Mtu yule akamwambia, “Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini?

21“Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.”22Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa amemiliki mali nyingi.

23Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni, ni vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.24Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”

25Wanafunzi waliposikia hivyo, wakashangaa sana na kusema, “Ni yupi basi atakayeokoka?”

26Yesu akawatazama na kusema, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.”

27Kisha Petro akamjibu na kumwambia, “Tazama, tumeacha vyote na kukufuata wewe. Ni kitu gani tutakachopata?”

28Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, yeye aliyenifuata mimi, katika uzao mpya wakati Mwana wa Adam atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake, ninyi pia mtaketi juu ya viti kumi na viwili vya enzi, kuwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.29Kila mmoja wenu aliyeacha nyumba, kaka, dada, baba, mama, watoto, au shamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele.

30Lakini wengi walio wa kwanza sasa, watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.


Mathayo19 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mafundisho ya Yesu kuhusu talaka

Katika sura hii, Yesu anafundisha kuhusu talaka. Ilikuwa jibu la changamoto lililotolewa na Mafarisayo. Mafundisho yake Yesu yanategemea nia ya awali ya Mungu katika kuunda ndoa. Yesu anaonyesha makosa ambayo viongozi wa dini walifanya katika desturi zao kuhusu ndoa.

Links:


Matthew 19:1

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwanzo wa simulizi jipyaamabalo linanaishia 22:45, ambayo inaonesha Yesu akihudumia huko Yudea

Maelezo kwa ujumla

Mistari hii inatoa historia ya jinsi Yesu alivyokuja Yudea

Ilitokea wakati

Habari inaeleza jinsi Yesu alivyositisha mafundisho yake kwenda tukio lililofuata

Alipomaliza maneno hayo

kile Yesu alichofundisha kuanzi 18:1

akaondoka

"alitembea kutoka" au "akatoka"

Matthew 19:3

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kufundisha juu ya ndoa na talaka

wakamjia

"walikuja kwa Yesu

wakaimjaribi wakisema

kujaribu limetumika kwa maana hasi. "wakamkosoa kwa kumuuliza" au "walitaka kumkamata kwa kumuuliza"

Hamkusoma kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwauumba mume na mke?

Yesu anatumia swali kuwajibu Mafarisayo. "Kwa hakika mmesoma kwamba mwanzo Mungu aliwaumba watu,aliwaumba"mume na mke

Matthew 19:5

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 5, Yesu ananukuu kutoka Mwanzo kuonesha kuwa Mume na mke hawatakiwi kuachana

Na yeyealiyewaumba pia alisema, 'kwa sababu hii ...mwili mmoja?

Huu ni mwandelezo wa swali ambal oYesu alilitumia kuwaliza Mafarisayo katika 19:3. Hii nukuu ya moja kwa moja inaweza kuelezwa kama nukuu isyo ya moja kwa moja. Kwa hakika mnajua kuwa Mungu alisema kuwa kwa sababu hii...mwili mmoja.

kwa sababu hii

sababu ya mwanamume kumwacha baba na mama ni kwamba Mungu alimuumba mwanamke kuwa msaidizi wa mwanamume

Ungana na mke wake

"Kaa na mke wake"

Na wale wawili watakuwa mwili mmoja

"watakuwa kama mwili mmoja"

Hivyo si wawili tena, bali mwili mmoja

Kwahiyo mwanamume na mwanake siwawil tena bali mwili mmoja"

Matthew 19:7

Wakamwambia

"Mafarisayo walimwambia Yesu"

Tuamuru

"Amuru sisi Wayahudi"

Hati ya talaka

Waraka unaohalalisha kisheria mwisho wa ndoa

kwa sabau ya ugumu wa mioyo yenu

kwa sababu ninyi ni wasumbufu

kwa ugumu ... aliwaruhusu ....wake zenu

wewe na yenu ziko katika wingi. Yesu anaongea na Mafarisayo, lakini Musa aliwapa shaeria hii miaka mingi iliyopita kwa mababu zao. amri ya Musa ilitumika kwa Wayahudi wote.

tangu mwanzo

"Wakati Mungu alipomuumba mume mke hakupanga waachane"

nawaambieni

anaongeza msisitizo

na kumwoa mwingine

na kumwoa mwanamke mwingine

Na mwanaume anayemwoa mwanamke ambaye ameachwa amefanya uzinzi

Maandishi mengi ya mwanzo hayajumuishi maneno haya.

Matthew 19:10

walioruhusiwa

wale ambao Mungu amewaruhusu au ambao Mungu huwaruhusu

kwa kuwa wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama

kwa kuwa kuna wanaume waliozaliwa kuwa matowashi

Matowashi waliojifanya matowashi

kuna matowashi waliofanywa kuwa matowashi

kuna matowashi waliojifanya kuwa matowashi

inawweza kumaanisha 1)wanaume waliojifanya wenyewe kwa kutoa sehehmu zao za siri 2) wanaume waliochagua kutokuoana ni wasafi katika swala la zinaa.

kwa ajili ya ufalme wa mbinguni

ualame wa mbinguni inamaanisha Mungu kutawala kama mfalme

Pokea mafundisho haya...pokea

Anayeweza kupokea mafundisho haya na ayapokee."

Matthew 19:13

Sentensi unganishi

Yesu anawapokea na kuwabariki wat.oto wadogo

Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo

watu baadhi wakaleta watoto wadogo kwa Yesu

Kibali

"Ruhusu"

Msiwazuie kuja kwangu

Msiwazuie kwa kuja kwangu

Kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama hao

Mungu kuwa mfalme kwa watu anaowatawla

ni wa watu kama hao

ni wa watu kama watoto

Matthew 19:16

Sentensi unganishi

Yesu anaongelea habariya mtu tajiri na jinsi iwezavyo kumgharimuamafuatapo Yesu

Tazama

Mwandishi anamweka mtu mpya kwenye habari.Lugha yako inaweza kuwa na njia nyingine ya kufanya hivyo.

Kitu kizuri

kitu kinachompendeza Mungu

kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri

usiniulize juu ya kitu kilicho kizuri

kuna mmoja tu aliye mwema

"Mungu pekee ndiye mwema aliyekamilka"

kuingia uzimani

"ikupokea uzima wa milele"

Matthew 19:18

mpende jirani yako

Wayahudi waliamni kuwa majirani zao ni wayahudi tu. Yesu alipanua maana ya jirani il kujuisha watu wote.

Matthew 19:20

kama ukitaka

"kama unataka"

uwape masikini

kwa wale amabao ni masikini

utakuwa na hazina mbinguni

Mungu atakuzawadia mbinguni

Matthew 19:23

Sentensi unganishi

Yesuanawaeleza wanafunziwake zawadi ya kutokutafuta mali ya hapa duniani na uhusianao wa kumfuata yeye.

kweli nawaambia

nawaambia ukeli. huunimsisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

kuingia katika ufalme wa mbinguni

kumpokea Mungu wa mbinguni kama mfalme wetu.

ni rahisi ... ufalme wa mbinguni

Yesu anatumia mbalagha kusisitiza kuwa ni vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Tundu la sindano

Tobo katika mwisho wa sindano kwa kupitishia uzi

Matthew 19:25

Wakashangaa sana

"wanafunzi wameshtushwa au kushangazwa." walishangazwa kwa sababu waliamini kuwa na utajiri ilikuwa ishara ya kukubarika kwa Mungu

Ni nani basi atakayeokoka?

Kwa hiyo hakuna ambayae Mungu atamwokoa" au "hakuna ambaye atapokea uzima wa milele

Tumeacha kila kitu

"tumeacha utajiri wetu wote" au "tumeacha miliki yetu yote"

Hivyo tutapata nini?

"Kitu gani kizuri Mungu atakachotupa?"

Matthew 19:28

kweli nawaambia

msisistizo wa kile kinachofuatia

kaika uzao mpya

"wakatimpya" inamaanisha wakatiMungu akirudisha kila ktu" au "wakati ule ambao Mungu atafanya kila kitu kuwa kipya.

Mwana wa Adamu

Yesuanaonge juuyake mwenyewe

atakapoketikatika kiti cha enzi

Kukaa katika enzi kunamaanisha kutawala kama mfalme. enzi yake kuwa tukufu minawakilisha "utawala wake kuwa wa utukufu" au "kutawala kwa utukufu kama mfalme"

mtaketi juu ya viti kumi na viwili vya enzi

Hapa "enzi" inamaanisha kutawala kama mfalme. Wanafunzi hawatakuwa sawa na Yesu ambaye pia yuko kwenye enzi.. Watapokeamamlaka kutoka kwake."kukaa kama kwenye enzi 12"

makabila kumi na mawili ya Israel

Hapa "makabila" inamaanisha wtu kutoka kabila hizo

Matthew 19:29

kwa ajili ya jina langu

hapa "jina" linamaanisha nafasi nzima. "kwa sababu yangu" au " kwa sababu ananiamini mimi"

atapata mara mia

Kupokea kutoka kwa Mungu mara 100 na vitu vingine vizuri kama walivyoacha

kuurithi uzima wa milelel

Hii ni nahau inayomaanisha "Mungu atawabariki na uzima wa milele" au "Mungu atawafanya kuishi milele

Lakini wengi walio wa kwanza sasa, watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwawa kwanza.

Yesu analinganisha kizazi hiki na kile kijacho. Wale ambao ni wa muhimu sasa Mungu atawafanya kuwa si wa muhimu atakapoanzisha utawala wake hapa duniani. Wale wanaoonekana si wa muhimu leo Mungu atawafanya kuwa wa muhimu atakapoanzisha utawala wake.


Translation Questions

Matthew 19:3

Ni swali gani Mafarisayo walimwuuliza Yesu ili kumjaribu?

Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?

Yesu alisema ukweli ulikuwaje tokea mwanzo?

Yesu alisema kuwa tokea mwanzo wa kuumbwa, Mungu aliwaumba mume na mke.

Matthew 19:5

Kwa kuwa Mungu aliwaumba mtu mume na mke, Yesu alisema mume anatakiwa afanye nini?

Yesu alisema kuwa mume atawaacha babana mama yake na kushikamana na mke wake.

Je, Yesu alisema kuwa huwa kinatokea nini pale mume anaposhikaman na mke wake?

Yesu alisema kuwa, mume anaposhikamana na mke wake wale wawili huwa mwili mmoja.

Je, Yesu alisema mwanmume asifanye nini juu ya kile alichokiunganisha Mungu?

Yesu alisema kuwa alichokiunganisha Mungu mtu asikitenganishe.

Matthew 19:7

Yesu alitoa sababu gani ya Musa kuruhusu talaka?

Ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao

Yesu alitoa sababu gani ya Musa kuruhusa=u talaka?

Ni kwa sababu y a ugumu wa mioyo yao

Yesu alisema ni mtu gani anayefanya uzinzi?

Yesu alisemayeyote amwachaye mke wake isipokuwa kwa uzinzi, na kuoa mwanake mwingine huyo afanya uzinzi, na kwamba mwanamumeanyeoa mwanamke aliyeachwa afanya uzinzi.

Matthew 19:10

Yesu alisema ni nani awezaye kuwa towashi?

Ni kwa wale walioruhusiwa na Mungu kuipokea hali hiyo.

Yesu alisema ni nani awezaye kuwa towashi?

Ni kwa wale walioruhusiwa na Munga kuipokea hali hiyo.

Matthew 19:13

Wanafunzi walifanya nini walipowaona watoto wadogo wameletwa kwa Yesu?

Wanafunzi wake waliwakemea

Yesu alisema nini alipowaona watoto wadogo

Yesu aliseamawaacheni watoto wadogo waje, kwa kuwa ufalme wa mbinguni ni wa watoto kama hawa.

Matthew 19:16

Yesu alimwambia kijana afanye nini ili kuuingia katika uzima wa milele?

Alimwambia ashike sheria za Mungu

Yesu alimwambia kijana anapaswa kufanya nini ili kuingia kwenye uzima wa milele?

Yesu alimwambia yule kijana kuzishika amri ili kuingia kwenye uzima wa milele

Matthew 19:20

Baadaya kijana kusema kuwa anazishika amri, Yesu alimwambia nini?

Nenda ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni.

Baada ya lkijana kusema anazishika amri, Yesu alimwambia nini?

Nenda ukauze ulivyo navyo, na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni

Mwitikio a yule kijana ulikuwaje kwa amri ya Yesu ya kuuza vyote alivyokuwa navyo?

Yule kijana aliondoka akiwa amehuzunika sana kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Matthew 19:23

Yesu alisema nini juu ya matajiri kuuingia ufalme wa Mbinguni?

Ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.

Matthew 19:25

Je, Yesu alisemaje juu ya uwezekano wa mtu tajiri kuurithi ufalme wa mbinguni?

Yesu alisema kuwa kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.

Matthew 19:28

Yesu aliwaahidi nini wanafunzi wake waliokuwa wakimfuata?

Katika uzao mpya wakati Mwana wa Adamu atakapoketi katika kiti cha enzi, wanafunzi nao wataketi naye wakiyahukumu makabila kumi na mbili ya Israel.

Matthew 19:29

Je, Yesu alisemaje juu ya wale ambao ni wa kwanza kwa sasa na wale ambao ni wa mwisho sasa?

Yesu alisema kwamba ambao ni wa kwanza sasa watakuwa wa mwisho na wale ambao ni wa mwisho sasa watakuwa wa kwanza.


20

1Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu.2Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.3Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.4Akawaambia, ‘Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.’ Hivyo wakaenda kufanya kazi.5Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo.6Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, ‘kwa nini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?

7Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, ‘Nanyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.’

8Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, ‘Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.’9Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.10Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu.11Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba.

12Wakasema, ‘Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.’

13Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, ‘Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! Hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja?14Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe.

15Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?16Hivyo wa mwisho atakuwa wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho”

17Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,18“Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo19na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulubisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.”

20Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake.21Yesu akamwambia, “Unataka nini?” Akamwambia, “Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.”

22Lakini Yesu akajibu na kusema, “Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?” Wakamwambia, “Tunaweza.”

23Akawaambia, “Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu.”

24Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.25Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, “Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao.26Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.27Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.28Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi.”

29Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.30Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”31Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”

32Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”33Wakamwambia, “Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe.”34Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.


athayo 20 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Mfano wa mwenye shamba na shamba lake la mizabibu

Yesu anatumia mfano huu (Mathayo 20:1-16) ili kuwafundisha wanafunzi wake kwamba kanuni za Mungu kuhusu kile kilicho sawa ni tofauti na kanuni za binadamu.

Links:


Matthew 20:1

Sentensi unganishi

Yesu anaelzea mfano wa mtu mmoja aliyekuwa anamiliki shamba anayeajiri wafanya kazi, ili kufafanua jinsi atakavyowalipa watu wa ualme wake.

Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana

Tazama 13:24

Baada ya kukubaliana

"baada ya mmiliki wa shamba kukubaliana"

Dinari moja

"malipo ya kibarau ya siku moja"

aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu

aliwatuma kwenda kufanya kazi katika shamba lake

Matthew 20:3

Sentensi unganishi

Yesu anaendela kuelza mfano

Alienda tena

"Mmiliki wa shamba alienda tena"

baada ya masaa matatu

saa ya tatu ni sawa na saa tatu asubuhi

wamesimama bila kazi katika eneo la soko

"Wamesisma eneo la soko pasipo kufanya kazi yeyote"

eneo la soko

Hili ni eneokubwa la wazi ambapowatu huuza na kununua chakula na bidhaa zingine.

Matthew 20:5

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kusimulia mfano

akaenda tena

"Mmiliki wa shamba akaenda tena"

saa ya sita

saa ya sita ni sawa na sasa sita mchana. saa ya tisa ni sawa na saa tisa mchana

alifanya hivyo hivyo

Hii inamaanisha yule mmilikiwashamba alienda sokono kuaajiri atu wengine

saa ya kumi n a moja

Hii ni sawa na saa kumi na moja mchana

bila kazi

"bila kufanya chochote" au "bila kuwa na kazi yote"

Matthew 20:8

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano

kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza

Waweza kuzi kuyafanya maelezo h aya yaeleweke kwa uwazi. "Kwa kuanza na wafanyakazi niliowaajiri mwishoni, kisha lipa wafanyakazi niliowaajiri kwanza"

walioajiriwa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "wale aliowaajiri mwenye shamba"

Dinari moja

"malipo kibarua ya siku moja"

Matthew 20:11

Sentensi ungsnishi

Yesu anaendelea kueleza mfano

Baada ya kupokea

"pindi wafanyakazi waliofanya kazi kwa muda mrefu walipopokea"

Mmiliki wa shamba

"mmiliki shamba" au "mwenye mizabibu"

umewalinganisha na sisi

"umewalipa kiasi kilekile cha fedha sawa na ulivyotulipa"

Sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto

Kirai "tumebeba mzigo kwa siku nzima" ni nahau inayomaanisha kuwa "sisi ambao tumefanya kazi kwa siku nzima tukiungua na joto la jua"

Matthew 20:13

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano

Mmoja wao

"mmoja wa wafanyakazi waliofanyakazi kwa muda mrefu

Rafiki

Tumia neno ambalo mtu moja angelitumia kumtambulisha mtu mwingine ambaye anamkemea kwa upole

Je, hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja

Mmilki wa shamba anatumia swali kumkemea mfanykazi aliyekuwa akilalamika. "tumeshakubaliana kuwa nitakulipa dinari moja"

Dinari moja

"malipo ya kibarua ya siku moja"

Matthew 20:15

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha mfano wake juu ya mmiliki wa shamba aliyeajili wafanya kazi

Je! si haki kwangu kufanya kile ninachotaka juu ya mali zangu?

Yule mmiliki wa shamba anatumia swali kuwanyamazi wafanyakazi waliokuwa wakilalamika. "Ninaweza kufanya chochote ninachotakajuuya mali yangu"

Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?

Yule mmiliki wa shanba anaatumia swali kuwanyamazisha wale wafanyakazi waliokuwa wakilalamika. "Msiwe na wivu kwa sababu ya ukarimu wangu kwa watu wengine

Au mnaona wivu kwa sababu ya ukarimu wangu?

Yule mmiliki w a shamba anatumia swali kuwanyamazisha wafanyakazi waliokuwa wakilalamika. "Msione wivu kwa sababu ya ukarimu kwa watu wengine"

wa mwisho atakuwa wa kwanza na kwanza atakuwa wa mwisho.

Tazama 19:29

Hivyo wa mwisho atakuwa wa kwanza

Yesu anasema kwa kuhitimisha kwa mfano huu. "Ndipo Yesu aliposema. 'wa mwisho atakuwa wa kwanza'"

Matthew 20:17

Sentensi unganishi

Yesu anatabiri juu ya kifo na ufufuo wake kwa mara ya tatu wakati akisafiri na wanafunzi wake

alipokuwa akipanda kwenda Yerusalemu

Yesu alikuwa juu ya mlima kwa hiyo watu walipanda kwenda pale.

Tazama tunaelekea

Yesu anatumia neno "tazama" ili kuwajengea usikivu wanafunzi wake juu kile anachotaka kuwaambia.

tunaelekea

Kiwakilishi "tu" kinamaanisha Yesu na wanafunzi wake.

Mwana wa Adamu atatiwa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji "mtu fulani atamtoa Mwana wa Adamu"

mwana wa Adamu ... watamhumkumu ... ata

Yesu anaongea juu yake akitumia nafsi ya tatu. Kama inawezekana unaweza kutafsiri hii kwa kutumia nafsi ya kwanza

Watamtoa.. ili kumdhihaki

Makuhani wakuu na waandishi watamhukumu na kumtoa kwa watu wa mataifa, na watu wa mataifa watamdhihaki.

kumchapa

"kumchapa" au "kumpiga kwa mijeredi"

siku ya tatu

siku ya 3

atafufuka

Hi inaweza kuelezwa kwa mfumo tendaji. "Mungu atamfufua"

Matthew 20:20

Sentensi ungsnishi

Akijibu swali ambalo Yesu aliulizwa na mama wa wale wanafunzi wawili, Yesu anafundisha wanafunzi wake juu ya mamlaka na kuwatumikia wengine katika ufalme wa mbinguni

Wana wa Zebedayo

Hii inamaanisha Yakobo na Yohana

mkono wako wa kulia ... mkono wako wa kushoto

Maana yake ni uwezo wa kuwa na nguvu, mamlaka, na heshima.

katika ufalme wako

Hapa "ufalme inamaanisha utawala wa Yesu kama mfalme. "utakapokuwa mfalme"

Matthew 20:22

Haujui

Hapa "ham" iko katika wingi na inamaanisha mama na watoto

Je! unaweza

Hapa "mna" ni wingi, lakini Yesu anasema na wale wana wawili.

kukinywea kikombe ambacho nitakinywea

Hii ni nahau inayomaanisha kupita katika mateso. "kupitia mateso ambayo punde nitayapitia"

wakamwambia

"wale wana wa Zebebdayo walimwambia" au "Yakobo na Yohana walisema"

kikombe changu hakika mtakinywea

Hii ni nahau kupitia dhiki. "kwa hakika mtateseka kama nitakavyoteseka

mkono wa kulia ... mkono wa kushoto

tazama 20:20

ni kwale ambao imekwisha kuandaliwa na baba yangu

Hii inaweza kuelezwa katika muundo tendaji. "Baba yangu amekwisha kuyaandaa hayo maeneo, na atawapatia wale anaowachagua.

Baba yangu

Hiki ni cheo muhimu kwa ajili ya Mungu kinachoonesha mahusiano kati ya Yesu na Mungu.

waliposikia hivyo

"Waliposikia ambacho Yakobo na Yohana walimwuliza Yesu"

walihuzunishwa sana na wale ndugu wawili

Kama inawezekana unaweza kukiweka wazi kilichowahuzunisha wale wanafunzi kumi. "Walikasirishwa sana na wale ndugu wawili kwa sababu kilammoja wao alitaka kuketi kwenye upande wa heshima karibu na Yesu.

Matthew 20:25

Sentensi unganishi

Yesu anamalizia kufundisha juu ya mamlaka na kuwatumikia wengine

aliwaita

"aliwaita wale thenashara"

watawala wa wa mataifa huwatiisha,

watawala wa mataifa hulazimisha watu wa mataifa kufanya kile watawala wanataka.

watawala wa mataifa

"watawala wa watu wa mataifa"

huwatiisha

"huwatawalawatu"

yeyote atakayetaka

"yeyote atakaye" au "yeyote atamaniye"

kuwa wa kwanza

"kuwa wa muhimu"

Mwana wa Adamu ... maisha yake

Yesu anaonge juu yake mwenyewe kwa kutumia nafsi ya tatu. kama inawezekana unaweza kuitafsiri hii katika nafsi ya kwanza.

hakuja kutumikiwa

Hii inaweza kutafsiriwa katika mfumo tendaji. "Hakuja ili kwamba watu wengine wamtumikie" au "sikuja ili kwamba watu wengine wanitumikie"

bali kutumika

"bali kuwatumikia watu wengiine"

na kutoa uhai wake

Hii ni nahau. "kufa"

kuwa ukombozi kwa wengi

Neno "ukombozi" htumika kwa maana ya kuwafanya wengine kuwa huru kutoka gerezani au utumwani. Hii ni sitiari ya Yesu kuwaokoa watu kutoka kwenye hukumu ya adhbu ya Mungu kwa ajili y a dhanbi zao

kwa wengi

"kwa ajili ya watu wengi"

Matthew 20:29

Sentensi unganishi

Hii inaanza na habari ya Yesu akiwaponya vipofu wawili

Wakati wakitoka

Hii inaongelea wanafunzi na Yesu

ulimfuata

"ulimfuata Yesu"

vipofu wawili wameketi

Wakati mwingine jambo hili limetafsiriwa kama "Tazama kulikuwa na wanaume wawili weameketi." Mwandishi anatambulisha watu wawili kwenye hii habari. Lugha yako inaweza kuwa na namna ya kulifanya jambo hili.

waliposikia

"wale vipofu wawili waliposikia"

na waliona

wakati mwingine hutafsiriwa , "Tazama" Mwandishi anamwambia msomaji kuwa makini kwa maelezo ya kushangaza yanayofuata. Lugha yako inaweza ikawa na njia fulani ya kufanya hivi.

Alikuwa akipita

Alikuwa akitembea kati yao

Mwana wa Daudi

Yesu hakuwa mwana halisi wa Daudi, Kwa hiyoinaweza kutafsiriwa kama "kizazi cha mfalme wa Daudi." Hata hivyo "mwana wa Daudi " ni cheo cha Masihi, na huenda wale wanaume walikuwa wakimwita Yesu kwa cheo hiki.

Matthew 20:32

Aliwaita

Aliwaita vipofu

je! mnatamani?

"je! mnataka"

kwamba macho yetu yafumbuliwe

Kirai cha "macho yetu yafumbuliwe" ni nahau inayomaanisha kuweza kuona tena. "tunataka utufanye kuona" au "tunataka uwezo wa kuona"

akiwa amevutwa na huruma

"kuwa na hurma" au "kusukumwa na huruma kwa ajili yao"


Translation Questions

Matthew 20:1

Ni kiwango gani cha malipo, mwenye shamba alikubali kuwalipa wale aliokuwa amewaajiri asubuhi na mapema?

Dinari moja kwa kutwa

Ni kiwango gani cha malipo, mwenye shamba alikubali kuwalipa wale aliokuwa amewaajiri asubuhi na mapema?

Dinari moja kwa kutwa

Matthew 20:3

Ni kiasi gani mwenye shamba alisema atawalipa wale aliowaajiri mara ya tatu?

Atawalipa chochote kilicho halali

Matthew 20:8

Ni kiasi gani walicholipwa wale wafanya kazi walioajiriwa saa kumi na moja?

Dinari moja

Matthew 20:11

Ni malalamiko gani waliyokuwa nayo wafanyakazi walioajiriwa asubuhi na mapema?

Walilalamika kuwa wao walikuwa wamefanya kazi kwa siku nzima, lakini wamepokea kiasi sawa na wale waliofanya kazi kwa saa moja.

Ni malalamiko gani waliokuwa nayo wafanyakazi walioajiriwa asubuhi namapema?

Walilalamika kuwa wao walikuwa wamefanya kazi kwa siku nzima, Lakini wa,epokes kiasi sawa na wale waliofanya kazi kwa saa moja.

Matthew 20:13

Mwenye shamba alijibuje kwa malalamiko ya wafanyakazi?

Mwenye shamba aliwaambia kuwa hajawakosea chochote wafanyakazi na amewalipa kile walichostahili.

Mwenye shamba alijibuje malalmiko ya wawafanyakazi?

Mwenye shamba aliwaambia kuwa hajawakosea chochote wafanya kazi na amewalipa kile waliochostahili.

Matthew 20:17

Ni tukio gani Yesu aliwaambia wanafunzi wake mapema walipokuwa wakienda Yerusalemu?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa atatolewa kwa makuhani wakuu na waandishi, na kuhukumiwa kifo, atasulibiwa, na siku ya tatu atafufuka.

Ni tukio gani amabloYesu aliwaambia wanafunzi wake mapema walipokuwa wakienda Yerusalemu

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kuwa atatolewa kwa makuhani wakuu na waandishi, na kuhukumiwa kifo, atasulibiwa na siku ya tatu atafufuka.

Matthew 20:20

Ni ombi gani alilokuwa nalo mama wa watoto wa Zebedayo?

Alimtaka Yesu aamuru kuwa watoto wake wawili wakae, mmoja mkono wake wa kushoto na mmoja mkono wake wa kuume.

Ni ombi gani alilokuwa nalo mama wa watoto wa Zebedayo?

Alimtaka Yesu aamuru kuwa watoto wake wawili wakae mmoja mkono wake wa kushoto na mmoja mko wake wa kuume

Matthew 20:22

Je, Yesu alisema ni nani mwenye kuamua nani akae mkono wake wa kushoto na nani akae mkono wake wa kuume kataka ufalme wake?

Yesu alisema kuwa Baba ameyaandaa maeneo hayo kwa ajili y a wale aliowachagua.

Matthew 20:25

Yesu alisemaje juu ya yule anayetaka kuwa mkuu kati ya wanafunzi wake

Yesu aliseam kuwa anayetaka kuwa mkuu lazima awe mtumwa.

Kwa nini Yesu alisema kuwa alikuja?

Yesu alisema kuwa alikuja kutumika na kuyatoa maisha yake kuwa ukombozi kwa wengi.

Matthew 20:29

Je, wale vipofu wawili waliokuwa wakikaa kando ya nija walifanya nini?

Wale vipofu wawili walipiga kelele, "Bwana, Mwana wa Daudi, uturehemu."

Matthew 20:32

Je, kwa nini Yesu aliwapnya wale vipofu wawili?

Yesu aliwaponya wale vipofu wawili kwa sababu aliwaonea huruma.


21

1Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethania, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,2akiwaambia, “Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. Wafungueni na kuwaleta kwangu.3Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, ‘Bwana anawahitaji,’ na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao.”

4Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,5‘Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme.’

6Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.7Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.8Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.9Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema, “Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!”

10Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, “Huyu ni nani?

11“Umati ulijibu, “Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya.”

12Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. Akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.13Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi,’ lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi.”

14Kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.

15Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi,” walishikwa na hasira.

16Wakamwambia, “Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?” Yesu akawaambia, “Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, ‘Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?”

17Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.

18Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.19Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka.

20Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?”

21Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ‘Uchukuliwe na ukatupwe baharini,’ na itafanyika.22Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”

23Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, “Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

24Yesu akajibu na kuwaambia, “Nami tena nitawauliza swali moja. Kama mkiniambia, nami vile vile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.25Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wenyewe, wakisema, “Tukisema, ulitoka mbinguni, atatuambia, ‘Kwa nini hamkumwamini?’26Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii.”27Kisha wakamjibu Yesu na kusema, “Hatujui” Akawaambia pia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.

28Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu29leo.’ ‘Mwana akajibu na kusema, ‘sitakwenda.’ Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda.

30Na mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kile kile. Mwana huyu akajibu na kusema, ‘Nitakwenda, bwana.’ Lakini hakwenda.31Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, “Mwana wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia.32Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.

33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye eneo kubwa la ardhi. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamulia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.34Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.35Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.36Kwa mara nyingine, mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vile vile.37Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’

38Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambiana, ‘Huyu ni mrithi. Njooni tumuue na tumiliki urithi.’39Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.40Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?”

41Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.”

42Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?’

43Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.44Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga.”

45Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.46Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.


Mathayo 21 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri hupendelea kuweka kando kidogo nukuu za Agano la Kale. ULB na tafsiri nyingine nyingi za Kiingereza huingiza mistari yote ya 21:5,16 na 42, ambayo ni nukuu kutoka Agano la Kale.

Dhana maalum katika sura hii

Hosana

Hili ndilo neno ambalo watu walisema wakipiga kelele walipomkaribisha Yesu huko Yerusalemu. Ilikuwa ni tamko la sifa, ingawa pia ilikuwa neno la Kiebrania linalomaanisha, "Tuokoe!"

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ufalme wa Mungu utaondolewa kutoka kwenu"

Wasomi wametofautiana kuhusu maana ya maneno haya. Swali muhimu ni hili: Je, tukio hili itakuwa la kudumu au la muda? Ikiwezekana, uziache wezekano zote mbili kuwa wazi katika tafsiri yako.

Links:


Matthew 21:1

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu akiingia Yerusalemu. Yesu anawapa maalekezo ya kile wanachopaswa kufanya.

Bethfage

Hikini kijiji kilichoko karibu na Yerusalemu

mwanapunda amefungwa

"mwanapunda ambaye amefungwa na mtu"

amefungwa pale

"amefungwa kwenye nguzo" au "amefungwa kwenye mti.

Matthew 21:4

Taarifa kwa ujumla

Hapa mwandishi anamnukuu nabii Zecharia kuonesha kuwa Yesu anataimiza unabii kwa kumpanda mwanapunda kuelekea Yerusalemu.

Sasa

Hili neno limetumika hapa kuonesha mwanzo wa habari mpya. Hapa Mathayo anafafanua jinsi matendo ya Yesu yanatimiza maandiko

Jambo hili lilitokea lile lililonenwa ili kupitia kwa nabii litimizwe

Jambo hili linaweza kutafsiriwa katika mfumo tendaji. "Hili lilitokea ili Yesu atimize kile alichosema Mungu kupitia manabii tangu zamani za kale"

kupitia kwa nabii

"kupitia kwa nabii Zekaria"

Binti wa sayuni

Binti wa mji inamaanisha watu wa ule mji. "watu wa mji ule" au"watu waishio Sayuni"

Sayuni

Hili ni jina jingiine la Yerusalemu

Mwanapunda mme, mwanapunda mchanga

Neno mwanapunda na mwanapunda mchanga inamaanisha mnyama yuleyule, haimaanishi wanyama wawili tofauti

mwanapunda

dume changa la punda

Matthew 21:6

Mavazi

Makutano wakatandaka mavazi yao chini, na wengine wakakata matawi ya miti wakayatandika barabarani

Matthew 21:9

Hosana

Neno la Kiebrania linalomaanisha "Tuokoe" lakini pia linaweza kumaanisha "Kumsifu Mungu!"

Mwana wa Daudi

Yesu hakuwa mwana halisi wa Daudi, kwa hiyo hii inaweza kutafsiriwa kama "kizazi cha mfalme Daudi. Lakini pia, "Mwana wa Daudi" ni cheo cha Masihi, Huenda makutano walikuwa wakimwita Yesu kwa cheo hiki.

kwa jina la Bwana

Hapa "kwa jina la Bwana" inamaanisha "kwa nguvu ya Bwana" au "kama mwakilish wa Bwana"

Hosana juu zaidi

Neno "juu zaidi" linamaanisha Mungu atawalaye kutoka juu mbinguni. "Mungu asifiwe, ambaye yuko juu mbinguni" au "Sifa kwake Mungu"

Mji mzima ulitaharuki

Neno "mji" linamaanisha wakazi wa mji huo. "Watu wengi mjini kote walitaharuki"

Matthew 21:12

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu alipoingia Hekaluni

Maelezo kwa ujumla

Katika msari wa 13, Yesu anamnukuu nabii Isaya kuwakememea wachuuzina wabadilishaji wa fedha.

Yesu akaingia hekaluni

Yesu hakuliingia lile hekalu halisi. Aliingia kwenye lile korido la hekalu

waliokuwa wakinunua na kuuza

Wachhuzi waliokuwa wakiuza wanyama na bidhaa ziingine ambavyo wasafiri walinunua ili wapate sadaka halisi ya kutoa hekeluni.

Akawaambia

"Yesu aliwaambia wale waliokuwa wanabadilisha fedha na kununua na kuuza vitu"

Imeandkikwa

Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. "Nabii aliandika zamani za kale" au "Mungu alishasema tangu zamani

Nyunba yangu itaitwa

"Nyumba yangu itaitwa"

Nyumba yangu

Kiwakilishi "yangu" kinamaanisha Mungu "Nyumba" inamaanisha hekalu

nyumba ya maombi

"mahali ambapo watu wataomba

Pango la wanyang'anyi

Yesu anatumia sitiari kuwakemea watu wanouza na kununua bidhaa hekaluni. "Kama mahali ambapo wanyang'nyi hujificha"

vipofu na vilema

wale waliokuwa vipofu na vilema"

mlemavu

kuwa na mguu ulioumia ambao unaosababisha kutembea kwa tabu"

Matthew 21:15

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 16,Yesu anatumia nukuu toka Zaburi kuthibitisha jinsi watu walivyokuwa wamemwitikia

maajabu aliyoyataenda

"vitu vya kushangaza" au "miujiza." Hii inamaanisha Yesu alivyowaponya vipofu na vilema kati ka 21:12

Hosana

Tazama 21:9

Mwana wa Daudi

Tazama 21:9

walishikwa na hasira

Inamaanisha kuwa walishikwa na hasira kwa sababu hawakuamini kuwa Yesu ndiyo Kristo na hawakutaka watu wamsifu. "Walikasirika sana kwa sababu watu walikuwa wanamsifu"

umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?

Wakuu wa Makuhani na waandishi wanauliza swali hili kumkemea Yesu kwa sababu wanamchukia, "Usiwaruhusu watu kusema mambo haya juu yako"

Lakini hamjawahi kusoma ... sifakamili?

Yesu anauliza swali hili kuwakumbusha wakuu wa makuhani na waandishi kile walichosoma kwenye maandiko. "Naam, nawasikia, lakini inawapasa mkumbuke mlichokisoma katika maandiko ... sifa"

Lakini hamkusoma...sifu'?

"Ndiyo nimewasikia lakini mnatakiwa kukumbuka mlichokisoma katika maandiko matakatifu...sifu'."

kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga mnayo sifa kamili

Kirai hiki "kutoka kwenye midomo" kinamaanisha kuongea. "uliwafanya watoto na watoto wachanga kusema sifa kamili"

Yesu akawaacha

"Yesu aliwaacha makuhani wakuu na waandishi"

Matthew 21:18

Sentensi unganishi

Yesu anatumia mtini kuwafundisha wanafunzi juu ya imani na maombi

Sasa

Hili neno limetumika kuonesha mwanzo wa habari mpya. Mathayo anaeleza kuwa Yesu alikuwa na njaa na ndiyo sababu anasimama kwenye ule mtini.

ukanyauka

"ukafa"

Matthew 21:20

Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?

Wanafunzi wanatumia swali kuonesha mshangao wao. "Tumeduwaa kuona kuwa ule mtiini umenyauka haraka!"

kweli nawaambieni.

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaonggeza msisitizo wa kile Yesu anachosema baadaye.

kama mkiwa na imani na bila wasiwasi

kama mtaamini kwa ukweli

kunyauka

"kukauka na kufa"

mtauambia hata huo mlima, 'uchukuliwe na kutupwa baharini;

mtaweza kuumbia mlima huu kuondoka na kutupwa baharini"

itafanyika

itatokea

Matthew 21:23

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya viongozi wa dini wakimhoji Yesu

alipofika hekaluni

Inamaanisha kuwa Yesu hakuingia hekaluni ndani. Aliingia kwenye korido la hekalu

mambo haya

Hii inamaanisha mafundisho na uponyaji wa Yesu mle hekaluni. Pia inaweza kumaanisha tukio lililofanyika siku moja kabla la Yesu kuwafukuza wanunuzi na wachuuzi.

Matthew 21:25

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwajibu viongozi wa dini

ulitoka wapi

"alipata mamlaka toka wapi?"

tukisema, ulitoka mbinguni; atatuambia, kwa nini hamkumwamini?

"kama tukisema kuwa tunaamini kuwa Yohana alipokea mamlaka toka mbinguni, Yesu atatuuliza kuwa kwa nini hatukumwamini Yohana"

Toka mbinguni

"mbinguni" inamaanisha Mungu."Kutoka kwa Mungu mbinguni"

Kwa nini hamkumwamini?

Basi mngekuwa mmemwamini Yohana Mbatizaji"

lakini tukisema, 'ulitoka kwa watu'

"lakini kama tukisema kuwa tunaamini kuwa Yohana alipokea mamlaka kutoka kwa watu"

tunawaogopa watu

tunaogopa kile makutano watakachotufikiria au kile watakachotufanyia"

Wote wanamwona Yohana kama nabii

"Wanaamini kuwaYohana ni nabii"

Matthew 21:28

Sentensi unganishi

Yesu anatumia mfano wa wana wawili kuwakemea viongozi wa dini na kufafanua kutokuamini kwao

Lakini mnafikiri nini?

Yesu anatumia swali ili kuwafanya viongozi wa dini wafikirie zaidi juu ya mfano aliotaka kuwaambia. "Niambieni mnafikiri nini juu ya kile ninachotaka kuwaambia"

akabadilisha mawazo yake

Hii inamlenga yule mwana akifikiri kana kwamba alikuwa na fikra zaidi ili achague

Matthew 21:31

Wakasema

"Makuhani wakuu na wazee walisema"

Yesu akawaambia

Yesu aliwaambia wakuu wa makuhani na wazee"

Kweli nawaambieni

"Nawaambia ukweli." Kirai hiki kinaongeza msisitizo wa kile ambacho Yesu atasema baadaye

Wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla Yenu kuingia

Neno "ufalme wa Mungu" linamaanisha utawala wa Mungu kama Mfalme. "Mungu atakaposimamisha utawalawake duniani, atawabariki watoza ushuru na makahaba kwa kuwatawala kabla ya kufanya hivyo kwenu"

kabla yenu kuingia

Yaweza 1)Yesu atawapokea watoza ushuru na makahaba kabla ya kuwapokea viongozi wa dini 2) Mungu atawapokea watoza ushuru na makahaba badala ya kuwapokea viongozi wa dini wa Kiyahudi

Yohana alikuja kwenu

Kiwakilishi cha "ninyi" ni cha wingi na kinamaanisha watu wote wa Israel na wala si viongozi wadini tu. "Yohana alikuja kwa watu wa Israel"

kwa njia iliyo nyoofu

Hii ni nahau inayomaanisha kuwa Yohana aliwaonesha watu njia sahihi ya maisha. "na aliwaambia njia sahihi ambayo Mungu anataka ninyi muishi"

hamkumwamini

kiwakilishi cha"hamku.." ni cha wingi. nacho kinamaanisha viongoziwa dini.

Matthew 21:33

Sentensi unganishi

Kuwakemea viongoziwa dini na kufafanua kutokuamini kwao, Yesu anaeleza mfano wa watumishi wapinzani.

Mtu mwenye eneo kubwa la aridhi

"mtu anayemiliki sehemu ya mali"

uzio

"ukuta" au "kizuizi"

akachimba shinikizo

"alichimba shimo la kukamulia zabibu"

akalikodisha kwa watunza zabibu

"kuwaweka wakulima wa mizabibu kuwa wasimamizi wa shamba la mizabibu" Mwenye shamba bado ni mmliki wa shamba.

Wakulima wa mizabibu

watu waliojua jinsi ya kutunza mizabibu na divai

Matthew 21:35

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuelezea mfano

Watumishi wake

Watumwa wa "Mtu mwenye shamba kubwa"

Matthew 21:38

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuelezea mfano.

Matthew 21:40

Sasa

Neno "sasa" halimaanisha "wakati huu," bali limetumika kuvuta usikivu kwa ajili ya fundisho linalofuata.

Wakamwambia

"Watu wakamwambia Yesu"

Matthew 21:42

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuelezea mafano wa watumishi wapinazani

Maelezo kwa ujumla

Yesu anamnukuu nabii Isaya kuonesha kwamba Mungu atamheshimu yule ambaye viongozi wa dini wanamkataa.

Yesu akawaambia

Tazama 21:40

Hamkusomakatika maandiko ... machoni'?

"Fikiria juu ya kile ambacho mmesoma ... macho"

Jiwe waliliolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni

Yesu ananukuu kutoka Zaburi. Hii ni sitiari inamaanisha viongozi wa dini, kama wajenzi, watamkataa Yesu, lakini Mungu atamfanya kuwa wa muhinmu katika ufalme wake, kama jiwe kuu la pembeni katika ujenzi.

limekuwa jiwe kuu la pembeni

"limekuwa jiwe kuu la pembeni"

Hili lilitoka kwa Bwana

"Bwana ndiye aliyefanya haya mabadiliko

inashangaza machoni petu

Kirai cha "machoni petu" kinamaanisha kuona. "ni maajabu kuona"

Matthew 21:43

Nawaambieni

Hii inaongeza msisitizo juu ya kile ambacho Yesu anasema baadaye

wa..

Kiwakilishi cha wa... ni cha wingi. Yesu alikuwa anaongea na viongozi wa dini na Wayahudi pia katika ujumla wao.

Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake

Neno "ufalme wa Mungu" inamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme. "Mungu atawakataa, Wayahudi, na atakuwa mfalme wa watu toka mataifa mengine watakaozaa matunda"

linalojali matunda yake

Hii ni nahau inayomaanisha utii. "wale wanaotii amri za Mungu"

Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande.

Neno "jiwe hili" nijiwe sawa na lile la 21:42. Hii ni sitiari inayomaanisha kuwa Kristo atamharibu mtu yeyote anayempinga. "Jiwe litamvunjavunja yeyote anayeanguka juu yake"

Kwa yeyeote litayemwangukia litamsaga

Hiki ni krai kinachoonesha kuwa Kristo ndiye atakuwa hakimu wa mwisho na atamharibu kila mtu atakayempinga.

Matthew 21:45

Sentensi unganishi

Viongozi wa dini wanamwinukia Yesu juu ya mfano ambao Yesu alifundisha

Mifano yake

Mifano ya Yesu


Translation Questions

Matthew 21:1

Je, Yesu alisema wanafunzi wake wawili wataona nini kwenye kile kijiji kinachowakabili?

Yesu aliseama watamwona punda amefunwa, na mwanapunda pamoja naye.

Matthew 21:4

Nabii alikuwa ametabiri nini juu ya hili tukio?

Nabii alitabri kuwa mfalme anawaijieni, akiwa amempanda punda na mwanapunda.

Nabii alikuwa ametabiri nini juu ya hili tukio?

Nabii alikuwa ametabiri kuwa Mfalme anawaijieni, akiwa amempanda punda na mwanapunda.

Matthew 21:6

Je, makutano walifanya nini njiani wakati wanaingia Yerusalemu?

Makutano walitandika mavazi yao juu yake na waliweka matawi ya miti njiani

Matthew 21:9

Umati ulikuwa ukisema nini wakati Yesu alikuwa akiingia Yerusalemu?

walisema Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu!!

Matthew 21:12

Yesu alifanya nini alipoingia katika hekalu la Mungu huko Yerusalemu?

Aliwavurumisha nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilisha fedha na viti vya wauza njiwa.

Matthew 21:15

Wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipopinga kile watoto walichokuwa wakipiga kelele juu ya Yesu, Yesu aliwaambia nini?

Yesu aliwaambia, "Ndiyo!" Hajasoma ilivyoaandikwa kuwa katika midomo ya watoto kuna sifa kamili?

Matthew 21:18

Yesu alifanya nini kwa mtini na ni kwa nini?

Aliulaani mtini, ukakauka, kwasababu haukuwa na matunda.

Matthew 21:20

Yesu aliwafundisha nini wanafunzi wake kuhusu maombi kupitia kukauka kwa mtini?

Kweli nawaambieni kama mkiwa na imanin na hamna wasiwasi yoyote, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtasema hata kwa huo mlima, uchukuliwe na utupwe bahrini, na itafanyika hivyo.

Matthew 21:23

Wakati Yesu alipokuwa akifundisha, wakuu wa makuhani na wazee walimuuliza juu ya nini?

walimuuliza juu ya mamlaka gani alikuwa anayafanya hayo?

Matthew 21:25

Ni swali gani Yesu aliwauliza wakuu wa makuhani na wazee?

Ubatizo wa Yohana ulitoka wapi? mbinguni au kwa wanadamu?

Matthew 21:28

Katika mfano wa Yesu wa wana wawili, Yule mtoto wa kwanza alifanya nini alipoambiwa kufanya kazi kwenya shamba la mizabibu?

Yule wa kwanza alisema hataweza kufka, lakini baadaye akaenda.

Katika mfano wa Yesuwa wan wawili, Yule mtoto wa kwanza alifanya nini alipoambiwa kufanya kwenye shamba la mizabiu?

Yule mtoto wa kwanza alisema hataenda lakini baadaye akaenda

Yule mtoto wa pili alifanya nini alipoambiwa kwenda kufanya kazi kwenye shamba la mizabibu?

Yule mtoto wa pili alisema atakwenda, halafu hakwenda.

Matthew 21:31

Ni mtoto yupi aliyefanya mapenzi ya Mungu?

Mtoto wa kwanza

Kwanini Yesu alisema kuwa watoza ushuru na makahaba watauingia ufalme wa Mungu kabla ya makuhani wakuu na waandishi?

Ni kwasababu watoza ushuru na makahaba walimwamini Yohana, lakini Wakuu wa Makuhani na waandishi hawakumwamini Yohana.

Matthew 21:35

wakulima wa mizabibu walifanya nini kwa watumishi ambao mwenye shamba alikuwa amewatuma?

Waliwachukua wake, wakawapiga, na kuwaua.

Matthew 21:38

Wakukima wa mizabibu walimfanya nini yule mtu aliyetumwa na mwenye shamba kwa mara ya mwisho?

Wakulima wa mizabibu walimwua mtoto wa mwenye shamba.

Wakulima wa mizabibu walimfanya nini yule mtu aliyetumwa kwa maraa ya mwisho na mwenye shamba?

wakulima wa mizabibu walimwua mtoto wa mwenye shamba.

Matthew 21:40

Watu walisema nini alichotakiwa kufanya mmliki wa shamba?

Watu walisema kuwa mmiliki anapaswa kuwaangamiza wale wakulima wa kwanza wa mizabibu na kulipangasha shamba kwa wakulima wengine

Watu walisema nin alichotakiwa kufanya mmiliki wa shamba?

Watu walisema kuwa mmiliki anapaswa kuwaangamiza wale wakulima wa kwanza wa mizabibu na kulipangasha shamba kwa wakulima wengine

Matthew 21:42

katika maandiko ambayo Yesu aliyanukuuu, ni nini kilitokea kwa jiwe lililokataliwa na waashi?

Jiwe lililokataliwa na waashi limekuwa jiwe kuu la pembeni/msingi

Matthew 21:43

kwa kuzingatia maandiko ambayo Yesu aliyanukuu, Yesu alisema kutatokea nini?

Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwa wakuu wa Makuhani na Mafarisayo na wapea taifa linalojali matunda yake.

Matthew 21:45

Kwa nini Wkuu wa makuhani na Mfarisayo hawakumnyoshea mikono Yesu mapema?

Waliwaogopa makutano, kwa sababu makutano walimwona Yesu kuwa ni nabii.


22

1Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,2“Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.3Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.4Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, ‘Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari. Njoni katika sherehe ya harusi.”5Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.6Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadhalilisha na kuwaua.7Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.8Kisha aliwaambia watumishi wake, ‘Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.9Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.’10Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.11Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!12Mfalme alimwuliza, ‘Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?’ Na mtu huyo hakujibu chochote.13Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.14Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.’”

15Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.16Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.17Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?”

18Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?19Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari.20Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?”

21Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”22Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.

23Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,24wakisema, “Mwalimu, Musa alisema, ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.25Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.26Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.27Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.28Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa.”

29Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.30Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.31Lakini kuhusu ufufuo wa walio kufa, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,32“Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa waliokufa, bali ni Mungu wa walio hai.”

33Wakati umati waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.

34Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.35Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.36“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?”

37Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.38Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.39Na ya pili inafanana na hiyo. Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.40Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”

41Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.42Akisema, “Je, mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.”

43Yesu akawajibu, “Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,44‘Bwana alimwambia Bwana wangu, ‘Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako.”45Kama Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ jinsi gani atakuwa mtoto wake?”46Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.


Mathayo 22 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Some translations set poetry farther to the right than the rest of the text to show that it is poetry. The ULB does this with the poetry in verse 44, which is from the Old Testament.

Dhana maalum katika sura hii

Wedding Feast

In the parable of the wedding feast (Matthew 22:1-14), Jesus taught that when God offers to save a person, that person needs to accept the offer. Jesus spoke of life with God as a feast that a king prepares for his son, who has just gotten married. In addition, Jesus emphasized that not everyone whom God invites will properly prepare themselves to come to the feast. God will throw these people out from the feast.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Maana iliyodokezwa

Kama waandishi wengine wa Injili, Mathayo anadhani kwamba wasomaji wake wataelewa hali nyingi ambazo anawasilisha, kwa hiyo hatoi maelezo mengi. Anasema, kwa mfano, katika Mathayo 22:15-22, kwamba Wafarisayo walijaribu kumdanganya Yesu ili aseme mambo mabaya, lakini anadhani kwamba wasomaji wataelewa kwa nini swali lao kwa Yesu lilikuwa la hatari kujibu (Mathayo 22:16) ). Walitarajia kwamba Yesu katika jibu lake angewakasirisha Wayahudi au mamlaka ya Kirumi.

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Katika sura hii, Yesu ananukuu Zaburi ambapo Daudi anamwita mwanawe "bwana," yaani, mkuu. Wayahudi daima walitarajia kwamba mababu wangekuwa wakubwa kuliko wazao wao. Katika kifungu hiki, Yesu anajaribu kuwaongoza wasikilizaji hatua kwa hatua kuelewa ukweli kwamba Masihi mwenyewe atakuwa Mungu, na kwamba yeye, Yesu, kwa hakika ndiye Masihi. (Mathayo 22:43-44)

Links:


Matthew 22:1

Sentensi unganishi

Kuwakemea viongozi wa dini na kuonesha kutokuamini kwao, Yesuanafundisha mfano wa sherehe ya harusi

nao

"watu"

Ufalme wa mbinguni unafanana na.

Tazama 13:24

Wale wote waliokuwa wamealikwa.

"Watu ambao mfalme alikuwa amewaalika."

Matthew 22:4

Sentensi unganishi

Yesuanaendelea kuelezea mfano

watumishi wengine, akisema waambieni wote walioalikwa

akawaamuru, watumishi wawaambie wale aliowaalika.

Angalieni

"Angalia" au "Sikiliza" au "Kuwa msikivu kwa kile ninachotaka kukuambia."

Fahali na ndama wangu wameuawa

Inamaanisha kuwa wale wanyama wameshapikwa na wako tayari kwa kuliwa. "Watumishi wangu wamechinja na wamewapika mafahali na ndama wangu wanono"

Mafahali na ndama wangu wanono

"Mafahali wangu na ndama wangu walio wazuri kwa kula"

Matthew 22:5

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuelezea mfano

Hawakuzingatia kwa dhati.

"Lakini wale wageni walioalikwa na mfalme walipuuzia"

akawaua wale wauaji

Inamaanisha kuwa, askari wa mafalme waliawaua wale wauaji.

Matthew 22:8

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuelezea mfano

walioalikwa

"Wale ambao nimewaalika"

Makutano ya njia kuu.

"Mahali ambapo barabara hukutana." mfalme anawatuma watumishi kwenye maeneo ambayo wana uhakika mkubwa wa kupata watu.

wema na wabaya

"watu wabaya na watu wema"

Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa watu

"kwa hivyo wageni waliujaza ukumbi wa harusi"

ukumbi

chumba kikubwa

Matthew 22:11

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuelezea mfano

ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?

"haujavaa vazi rasmi kwa ajili ya harusi. haupaswi kuwa hapa"

mtu huyo hakujibu kitu chochote

"yule mtu alikuwa kimya"

Matthew 22:13

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha mfano wa harusi

mfungeni mtu huyu mikono na miguu

"mfungeni kiasi kwamba hawezi kusogeza mikono na miguu"

nje katika giza kuu

Tazama 8:11

kilio na kusaga meno

Tazama 8:11

Kwa kuwa watu wengi wanaitwa lakini wateule ni wachahe

"Kwa kuwa Mungu huwakaribisha watu wengi, lakini huchagua wachache"

kwa

Neno hili linamaaisha mpito. Yesu anamaliza mfano na sasa ataeleza maana ya mfano

Matthew 22:15

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya viongozi wa dini wakipanga jinsi ya kumkamata Yesu kwa kutumia maswali mengi magumu. Hapa Mafarisayo wanamuuliza Yesu juu ya kulipa kodi kwa Kaisari.

Jinsi ya kumkamta Yesu katika maneno yake mwenyewe.

"Jinsi ambavyo wangeweza kumsababisha Yesu kukosea katika kauli ili wamkamate"

wanafaunzi wao ... Maherode

Wanafunzi wa Mafarisayo walikubaliana na swala kulipa kodi kwa mamlaka za Kiyahudi. Maherode walikubaliana na swala la kulipa kodi kwa mamlaka za Kirumi. kwa maana hiyo, Mafarisayo waliamini kuwa kwa vyote ambavyo Yesu angejibu; angelikosea moja ya makundi hayo.

Maherode

Hawa walikuwa wafuasi na maofisa wa Herode mfalme wa Wayahudi. Alikuwa rafiki wa mamlaka za Kirumi.

Hauoneshi upendeleo kwa watu.

"Huoneshi heshima ya kipekee kwa baadhi ya watu" au " haujali tu watu maarufu zaidi."

Kulipa kodi kwa kaisari

Watu hawakulipa kodi moja kwa moja kwa Kaisari lakini kwa mmoja wa maofisa wake. "Kulipa kodi ambayo Kaisari alilitaka"

Matthew 22:18

Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?

"msinijaribu mimi enyi wanafiki" au "Najua kuwa ninyi wanafiki mnajaribu kunijaribu!"

Dinari.

Sarafu ya kirumi yenye thamani ya ujira wa siku.

Matthew 22:20

wa

kiwakilishi "wa" kinamaanisha Maherode na wanafunzi wa Mafarisayo.

Sura na jina hili ni vya nani

Niambieni sura na jina mnavyoviona kwenye hii sarafu ni vya nani?

vya Kaisari.

"Sarafu hii ina sura na jina la Kaisari"

vitu ambavyo ni vya Kaisari

"Vitu ambavyo ni mali ya Kaisari"

Vitu ambavyo ni vya Mungu.

"Vitu ambavyo ni mali ya Mungu."

Matthew 22:23

Sentensi unganishi

Masadukayo wanajaribu kumkamata Yesu kwa kumtega kwa swali gumu kuhusu ndoa na ufufuo wa wafu.

Mwalimu, Musa alisema, 'ikiwa mtu amekufa.

Walikuwa wakimuuliza kuhusu alichoandika Musa katika Maandiko. "Musa alisema kwamba ikiwa mtu amekufa."

Ndugu yake...mke wake...ndugu yake.

Kimilikishi "yake" inamaanisha yule mfu

Matthew 22:25

Sentensi unganishi

Mafarisayo wanaendelea kumwuliza Yesu swali

wa kwanza ... wa pili ... wa saba

namba za mpangiliio

Baada ya wote.

"Baada ya kila ndugu kuwa amemuoa" au " Baada ya kila ndugu kuwa amefariki."

baada ya kufanya hivyo wote

"baada ya kila ndugu kufa"

sasa

Hapa Masadukayo wanabadilisha habari ya ndugu yule wa saba na kuuliza swali halisi

Matthew 22:29

Mnakosea

"Mnakosea juu ya ufufuo"

Nguvu za Mungu.

"Kile ambacho Mungu anaweza kufanya."

katika ufufuo

"wakati wafu watapofufuka"

hawaoi

"watu hawataoa"

wala kuolewa

"wala watu hawataruhusu watoto wao kuolewa"

Matthew 22:31

Sentensi unganishi

Katika 22:32, Yesu ananukuu kutoka kitabu cha Kutoka ili kuhakikisha kuwa watu wataishi tena baada ya kifo

Hamjasoma kile ambacho ...Yakobo?'

"Najua mmekwisha soma, Lakini inaonekana hamkuelewa ambacho...Yakobo.'

Kile kilichosemwa kwenu na.

"Kile alichowaambia Mungu"

Mungu, anasema, Mimi ni...Yakobo?'

"Mungu alimwambia Musa kwamba Yeye, Mungu, ni Mungu wa Abramu,Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo."

"Si Mungu wa wafu balini Mungu wawalio hai

wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai"

Matthew 22:34

Sentensi unganishi

Farisayo mwanasheria alimtega Yesu kwa swali kwa kumwuliza swali gumu juu ya amri kuu

Mwanasheria.

Farisayo ambaye alikuwa na ujuzi maalum katika kuelewa sheria ya Musa.

Matthew 22:37

Maelezo kwa ujumla

Yesu ananukuu ile amri kuu kutoka Kumbukumbu la torati

kwa moyo wako wote, na kwa akili zako zote. na kwa roho yako yote.

Virai vyote vitatu vinamaanisha kitu kilekile. Vinamaanisha kuwa mtu lazima ampende Mungu kwa pendo la ndani na kwa kujito kwa ukweli.

.kuu na ya kwanza

Neno "kuu" na ya "kwanza" yanamaanisha kitu kilekile. vinasisitiza kuwa hii ni amri ya muhimu

Matthew 22:39

Maelezo kwa ujumla

Yesu ananukuu mstari toka Walawi kama amri kuu ya pili

Na ya pili inafana na hiyo

Yaweza kumaanisha 1) "kuna amri ya pili ambayo inafuatia kwa umuhimu" au 2) "kuna amri ya pili ambayo nayo ni ya muhimu." Kwa namna yeyote ile, Yesu anamaanisha kuwa amri hizi zote ni za muhimu kuliko amri zingine zote.

Na amri ya pili

Ya pili ni katika kupangilia

inafanana

Tazama 2:37

jiraniyako

Neno "jirani" inamaana zaidi ya mtu aliye karibu na wewe. inamaanisha kuwa mtu lazima awapende watu wote

Sheria zote na Manabii hutegemea hutegemea amri hizi mbili

Neno "sheria zote na manabii" limzznisha maandiko yote. "Kila kitu ambacho Musa na Manabii waliandika katika maandiko zinategemea amri hizi zote mbili"

Matthew 22:41

Sentensi unganishi

Yesu anawauliza Mafarisayo swali gumu ili kuzuia mpango wao wa kumkamata.

Sasa

Neno hili limetumika ili kuonesha mwanzo wa habari mpya. Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi wakati Yesu alipowauliza viongozi wa dini swali.

Mwana ... mwana wa Daudi

vyote hivi "mwana" vinamaanisha "kizazi"

Matthew 22:43

Maelezo kwa ujumla

Yesu ananukuu toka Zaburi kuonesha kuwa Kristo ni zaidi ya "mwana wa Daudi"

Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana

"Yesu anatumia swali kuwafanya viongozi wa dini kufikiri kwa undani zaidi juu ya Zaburi anyotaka kuinukuu "Niambieni kwa nini Daudi katika Roho anamwita Bwana"

Daudi katika Roho

"Daudi ambaye anavuviwa na Roho. "Hii inamaanisha kuwa Roho Mtakatifu anamwezesha Daudi kusema.

anamwita

Hapa "mwi" inasimama badala ya Kristo, ambaye pia ni kizazi cha Daudi.

Bwana alimwambia

Neno "Bwana" inamaanisha Mungu Baba

Katika mkono wangu wa kuume,

Kiwakilishi "wangu" kinamaanisha Mungu Baba. "Mkono wa kuume" huwa inatumika kuonesha sehemu ya heshima

Hadi nitakapowaweka maadui zako wawekwe chini ya miguu yako

Hii ni nahau. "hadi nitakapowashinda adui zako" au hadi nitakapowafanya maadui zako kukuinamia"

Matthew 22:45

Sentewnsi unganishi

Huu nu mwisho wa jitihada za viongozi wa dini kutaka kumkamata Yesu kwa maswali mengi

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwisho wa sehemu ya habari hii inayoanzia 19:1, ambayo inaelezea habari za Yesu akihudumia Yuda

Kama Daudi anamwita Kristo "Bwana," kwa namna gani awe mtoto wa Daudi?

"Daudi anamwita Yeye Bwana, kwa hiyo Kristo lazima awe zaidi kuliko mzao wa Daudi."

Kama Daudi tena anamwita Kristo.

Daudi amemrejea Yesu kama "Bwana" kwa sababu Yesu hakuwa tu mzao wa Daudi, lakini pia alikuwa bora kuliko Daudi.

kumjibu neno

"Neno" inamaanisha kile amabacho watu husema. "kumjibu yeye chochote" au " kumjibu"

maswali zaidi

Inamaanisha kuwa hakuna aliyemuuliza maswali ya jinsi hiyo ambayo yalikusudiwa kuwaYesu angeyajibu kimakosa ili viongozi wa dini wamkamate


Translation Questions

Matthew 22:5

Je wale waliokuwa wamealikwa kwenye harausi ya mwana wa mfalme walifanya nini walipoletewa mialiko na watumishi wa mfalme?

Baadhi yao hawakuizingatia ile mialiko na kuendelea na shughuli zao, na wengine waliwanyoshea mikono wale watumishi wa mfalme na kuwaua.

Je, wale waliokuwa wamealikwa kwenye harusi ya mwana wa mfalme walifanya nini walipoletewa mialiko na watumishi wa mfalme?

Baadhiyao hawakuzingatia hiyo mialiko na kuendelea na shughuli zao, na wengine waliwanyoshea mikono hao watumishi wa mfalme na kuwaua.

Mfalme alifanya nini kwa wale waliokuwa wa kwanza kukaribishwa kwenye hiyo Harusi?

Mfalme alituma jeshi, na kuwaua wale wauuaji, na kuichoma miji yao

Matthew 22:8

Je, ni watu gani basi ambao mfalme aliwakaribisha kwenye hiyo harusi?

Basi, malme alikarisha watu wengi kadri watumishi wake walivyoweza kuwapata. wote wema na wabaya.

Je, ni watu gani basi ambao mfalme aliwajkaribisha kwenye hiyo harusi?

Basi, mfalme aliwakaribisha watu wengi kadri watumishi wake walivyoweza kuwapata. Wote wema na wabaya.

Matthew 22:13

Mfalme alimfanyia nini mtu yule aliyekuja katika sherehe bila vazi la harusi?

Mfalme aliamuru afungwe na atupwe nje kwenye giza.

Matthew 22:15

Mafarisayo walijaribu kumfanyia nini Yesu?

Mafarisayo walijaribu kumnasa Yesu katika mazungumzo yake.

Ni swali gani ambalo wanafunzi wa Mfarisayo walimwuliza Yesu?

Walimwuliza Yesu kama ilikuwa halali kulpa kodi kwa Kaisari.

Matthew 22:20

Yesu alilijibuje swali la wanafunzi wa Mfarisayo?

Yesu aliseam kumpa Kaosari kilicho chake, na kumpa Mungu kilicho cha Mungu.

Matthew 22:23

Je, Masadukayo walikuwa na imani ya gani kuhusu ufufuo wa wafu?

Masadukayo waliamini kwamba hakutakuwaepo na ufufuo wa wafu.

Matthew 22:25

Katika habari ya Masadukayo, yule mwanamke alikuwa na waume wangapi?

Yule mwanamke alikuwa na waume saba

Katika habari ya Masadukayo, yule mwanamke alikuwa na waume wangapi?

Yule mwanamke alikuwa na waume saba

Matthew 22:29

Je, Yesu alisema vitu gani viwili ambavyo Masadukayo hawakuvifahamu?

Yesu alisema kwamba Mafarisayo hawakujua Maandiko Matakatifu wala nguvu za Mungu.

Je, Yesu alisemaje juu ya kuoa na kuolewa katika ufufuo?

Yesu alisema katika ufufuo hakuna kuolewa wala kuoa

Matthew 22:31

Je, Yesu aliyatumiaje aandiko kuonesha kuwa kutakuwa na ufufuo?

Yesu alinukuu maandiko ambayo Mungu anasema kuwa yeye ni Mungu wa Ibrahimu, wa Isaka, na Mungu wa Yakobo - Mungu wa walio hai.

Matthew 22:34

Ni swali gani ambalo farisayo mwansheria alimwuliza Yesu?

Yule mwanasheria alimwuliza Yesu kuwa sheria iliyo kuu ni ipi?

Matthew 22:37

Je, Yesu alisema amri kuu na ya kwanza ni ipi?

Yesu alisema lazima, kumpenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote na kwa akili zako zote, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako, hizo ndizo amri kuu mbili.

Je, Yesu alisema amri kuu na ya kwanza katika amri ni ipi?

Yesu alisema lazima, umpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote, na kumpenda jirani yako kama nafsi yako, hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.

Matthew 22:39

Je Yesu alisema amri ya pili ni ipi?

Yesu alisema kumpenda jirani yako kama nafsi yako, hiyo ndiyo amri ya pili.

Matthew 22:41

Je, Yesu aliwauliza swali gani wale Mafarisayo?

Yesu aliwauliza kuwa, Kristo ni mwana wa nani?

Wale Mafarisayo walimjibuje Yesu?

Mafarisayo walimjibu Yesu kuwa Kristo alikuwa Mwana wa Daudi.

Matthew 22:45

Swali lipi la pili ambalo baadaye Yesu aliwauliza Mafarisayo?

Baadaye Yesu aliwauliza jinsi gani Daudi angeweza kumwita mwana wake, Kristo, Bwana,

Mafarisayo walimjibuje Yesu?

Mafarisayo hawakuweza kumjibu Yesu neno lolote.


23

1Baadaye aliongea na umati na wanafunzi wake. Akasema,2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa ‘Walimu’ na watu.8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.10Wala msije kuitwa ‘walimu,’ kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.

13Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.141

15Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ng'ambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo.

16Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, ‘Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.’17Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?18Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.19Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?20Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.21Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.22Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.

23Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.24Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!

25Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.26Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.

27Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya waliokufa na kila kitu kilicho kichafu.28Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.

29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.30Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.31Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.32Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.33Enyi nyoka, wana wa majoka, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu?34Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.35Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.36Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.

37Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! Mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini haukukubali!38Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.39Nami nakuambia, kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.”’


1Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 ‘Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane.’

Mathayo 23 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

Wanafiki

Unafiki wa Wafarisayo ni neno kuu katika sura hii. Yesu anazungumzia kwa kina kuhusu unafiki huu. Wafarisayo waliunda sheria ambayo hakuna mtu angeweza kutii, na kisha wakawashawishi watu kwamba walikuwa na hatia kwa sababu ya kutotii sheria. Pia, sheria za Wafarisayo ziliwapa sababu za kutotii amri za asili za Mungu za Sheria ya Musa.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kutusi

Katika tamaduni nyingi, ni makosa kuwaalumu watu. Maneno mengi katika sura hii yaliyowalenga Wafarisayo yanaweza kuchukuliwa kama matusi. Wanaitwa "wanafiki," "viongozi vipofu," "wajinga," na "nyoka." Yesu anatumia maneno haya kuelezea na kuhukumu tabia zao.

Kitendawili

Kitendawili ni taarifa inayoonekana kuwa ya ajabu, ambayo ni kana kwamba inajikana yenyewe, lakini kwa hakika sio ya ajabu. Kwa mfano, "aliye mkuu kati yenu atakuwa mtumishi wenu" (Mathayo 23:11-12).

Links:


Matthew 23:1

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwamnzowa habari mpya inyoenedelea hadi 25:44, amabpo Yesu anafundisha juu ya wokovu na hukumu ya mwisho. Anaanza kuwaonya watu juu ya Mafarisayo na waandishi

Wanakalia kiti cha Musa.

Kiti kinamaanisha mamlaka ya kutawala na kuhukumu. "Wanayo mamlaka kama aliyokuwanayo Musa." au "wanayo mamlaka ya kusema maana ya sheria Musa."

Chochote.

"Yoyote" au "kila kitu."

Matthew 23:4

Wanafunga mizigo mizito ambayo ni migumu kubeba, na kisha kuwabebesha watumabegani

"Wanawawekea ninyi kanuni nyingi ambazo ni ngumu kufuata."

Wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba

"Wao hawatatoa msaada hata msasada kidogo"

Matendo yao yote huyafanya ili watazamwe na watu

wanafanya mataendo yao kwa kusuadi la kutazamwa na watu

Kwa sababu wao hupanua masanduku yao, na huongeza ukubwa wa mapindo wa mavazi yao

Hivi vyote ni vitu ambavyo Mafarisayo huvifanya ili waonekane kuwa wanamtii Mungu kuliko watu wengine

Masanduku

Haya ni makasha madogo ya ngozi yenye karatasi za maandiko

hongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao

Mafarisayo huweka mapindo marefu chini ya kanzu zao kuonesha uchaji wao kwa Mungu.

Matthew 23:6

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuongea na makutano kuhusu Mafarisayo

maeaneo ya kifahari ... viti vya heshima

Maeneo yaote haya na yale amabayo watu muhimu hukaa

maeneo ya sokoni

Maeneo makubwa ya wazi amabyo watu huuza na kununua bidhaa

na kuitwa 'Rabi' na watu

"ili watu wawaite rabi"

Matthew 23:8

Lakini ninyi hampaswi kuitwa

"Msimruhusu mtu yeyote awaite"

ninyi

viwakilishi vyote vya "ninyi" viko katka wingi na vinamaanisha wafauasi wote wa Yesu

wote ni ndugu

Neno "ndugu" linamaanisha "waumini wenzenu"

msimwite mtu yeyeote hapa duniani kuwa baba

"msiseme kwamba mtu yeyote hapa duniani ni baba yenu"

kwa kuwa mnaye baba mmoja tu

"baba" ni cheo muhimu cha Mungu

walla msije mkaitwa

"pia msimruhusu mtu kuwaita"

Kwa kuwa mnaye mwalimu mmoja tu, yaani Kristo

Wakati Yesu aliposema "Kristo" alikuwa anasema juu yake mwenyewe katika nafsi ya tatu. AT: "Mimi, Kristo ndiye mwalimu wenu pekee."

Matthew 23:11

Bali aliye mkubwa miongoni mwenu

"mtu maarufu miongono mwenu"

miongoni mwenu

kiwakilishi "mwenu" ni cha wingi na kinamaanisha wafuasi wa Yesu

Yeyote ajiinuaye

"ajifanyaye mwenyewe kuwa maarufu."

atashushwa

"Mungu atamshusha

atainuliwa

Mungu atamuheshimu

Matthew 23:13

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuwakemea viongozi wa dini kwa sababu ya unafiki wao

Lakini ole wenu

tazama 11:20

Mnawaffungia watuufalme wa mbinguni

"Mnawazuia watu kumpokea Mungu wetu wa mbinguni kuwa mfalme wao"

Hamwezi kuingia

"Hamumruhusu Mungu kuwa mfalme wenu"

na hamuwaruhusu wanaoingiakufanya hivyo

"wala hamuwarusu wale wanaotaka kumpokea Mungu kuwa mfalme wao kufanya hivyo"

mnavuka ng'ambo ya bahari

"mnasafiri umbali mrefu"

kumfanya mtu mmoja aamini

"kumfanya mtu mmoja aamini dini yenu"

mwana wa jehanamu

"Mtu ambaye mahali pake ni kuzimu." au mtu ambaye hanabudi kwenda kuzimu."

mnawameza wajane wajane.

"Kuiba kila kitu kutoka kwa wanawake wasio na wanaume wa kuwalinda."

Matthew 23:16

Viongozi vipofu...wapumbavu.

Tazama 15:12

kwa hekalu, si kitu

"kwa hekalu hawezi kulinda kiapo chake

Amefungwa na kiapo chake.

"Lazima atende kile alichoahidi kufanya."

Kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhabu, au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu ya Mungu?

Hekalu amablo limetumika kuweka wakfu dhahabu kwa Mungu ni la muhimu kuliko dhahabu ile"

Hekalu amabalo limeweka wakfu dhahabu

"Hekalu ambalo hutengeneza dhahabu ni mali ya Mungu pekee"

Matthew 23:18

Na

"na ninyi pia husema"

si kitu

"hakuna haja ya kulinda kiapo chake"

sadaka

ni mnyama au nafaka ambayo mtu anaweza kuileta kwa Bwana na kuiweka madhabahuni

amefungwa na kiapo chake

"lazima afanye kile alichoahidi kufanya"

Watu vipofu.

Viongozi wa Kiyahudi walikuwa vipofu kiroho. Ingawa walijidhania kuwa walimu, hawakuwaeza kuuelewa ukweli wa Mungu

Kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka, au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?

"Madhabahu ambayo huzifanya sadaka kuwa takatifu ni kuu kuliko sadaka

"madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka"

madhabahu ambayo huziweka sadaka kuwa rasmi kwa Mungu"

Matthew 23:20

na kwa vitu vyote vilivyo juu yake

"kwa vitu vyote ambvyo sadaka zote huwekwa juu yake"

na kwa yeye akaaye ndani yake ... na kwa yeye aketiye juu yake

virai vyote hivi vinamaanisha Mungu Baba.

Matthew 23:23

Ole wenu.

Tazama 11:20.

Bizali, Mnanaa, na Mchicha.

Majani na mbegu zinazotumika kuungia chakula.

kuacha mengine bila kutekeleza

"hamkutii

mambo mazito

"mambo y a muhimu zaidi"

lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya

"mnapaswa kuwa mmeziheshimu hizi sheria za muhimu"

na siyo kuyaacha mengine bila kuyatekeleza

"wakati pia mnatii zile sheria ndogondogo"

Ninyi viongozi vipofu.

Tazama 15:12

Ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia.

Kuwa mwaangalifu kufuatilia sheria zenye uzito kidogo na kupuuzia sheria zenye uzito mkubwa, hiyo ni upumbavu sawa na kuwa mwangalifu kwa kutokumeza mnyama mdogo aliye najisi, bali unakula nyama ya mnyama mkubwa sana aliye najisi pengine kwa makusudi au kwa kutokujuwa. AT: "Wewe ni mpumbavu kama mtu ambaye anachuja mdudu aliyeangukia ndani ya kinywaji chake lakini akimeza ngamia."

Kuchuja mdudu.

Kujucha kwa kutumia ktambaa ili kuondoa mdudu katika kinywaji

Mdudu.

Mdudu mdogo arukae.

Matthew 23:25

Ole wenu.

Tazama 11:20

Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe a nje ya sahani... kutokuwa na kiasi

"Waandishi" na "Mafarisayo" kwa wengine wanaonekana "safi kwa nje, lakini ndani ni wachafu

Kwa ndani wamejaa dhuluma and kutokuwa na kiasi.

"Wanachukua vitu vya watu kwa ubinafsi

Ewe Mfarisayo kipofu.

Mafarisayo walikuwa vipofu kiroho. Ingawa wao wenyewe walijidhania kuwa walimu. hawakuwa na uwezo wa kuelewa ukweli wa Mungu

Safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili nje pia pawe safi.

Hii ni sitiari inayomaanisha kuwa kama wangekuwa safi mioyoni mwao, basi matokeo yake wangekuwa safi kwa nje pia

Matthew 23:27

kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa... kichafu

hii ni kejeli inayoonesha kuwa Mafarisayo na waandishi wanaonekana kuwa safi nje, lakini ndani ni wachafu

makaburi yaliyopakwaa chokaa

"makaburi ambayo mtu ameyapaka chokaa" Wayahudi walipakaa makaburi kwa chokaa ili kuepusha kuyagusa. Kugusa kaburi ilihesabiwa kuwa ni unajisi.

Matthew 23:29

ya wenye haki

"ya watu wenye haki"

siku za baba zetu

"wakati wa mababu zetu"

tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao

"tusingekuwa tumeshirikiana nao"

kumwaga damu

Damu inamaanisha uhai. kumwaga damu inamaanisha kuua. "kuua" au "mauaji"

watoto wa hao

"watoto inamaanisha uzao"

Matthew 23:32

Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.

"Ninyi mna kamilisha dhambi ambazo babu zenu walizianzisha,"

Enyi nyoka, enyi wana wa vipiribao.

"Ninyi ni waovu na hatari kama nyoka wenye sumu."

wana wa vipiribao

tazama 3:7

Jinsi gani mtaepuka hukumu ya jehanamu?

"Hakuna njia mnayoweza kutumia kuepuka hukumu ya jehanamu!"

Matthew 23:34

nawatuma

"nitawatuma." Hapa "ni" inamaanisha Yesu.

juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani

"Mungu atawahukumu kwa mauaji ya watu wenye haki"

kuanzia damu ... kwa damu

"kutoka mauji hadi ... mauaji"

Kutoka...Abeli...to...Zekaria.

Abeli alikuwa mhanga wa kwanza katika mauaji, na Zakaria huenda akafikiriwa kuwa wa mwisho kuuwawa na Wayahudi hekaluni.Watu hawawaili wanawakilisha mauaji ya watu wote wenye haki

Zakaria.

Siyo baba yake na Yohana Mbatizaji.

mliyemuua

Yesu hamaanisha watu wale aliokuwa akisema nao kuwa ndio waliomua Zekaria. Anamaanisha kuwa mababu zao ndio waliomuua.

Kweli nawaambieni

"Nawaambia ukweli." Hii inaongeza msisitizo wa kile Yesu atakachosema baadye.

Matthew 23:37

Sentensi unganishi

Yesu anaomboleza juuya watu wa Yerusalemu kwa sababu wanamkataa kila aliyetumwa na Mungu kwao

Yerusalemu, Yerusalemu.

Yesu anazungumza na watu wa Yerusalemu kana kwamba wao wenyewe ndio walikuwa mji.

ambao wanatumwa kwako

wale ambao Mungu huwatuma kwako

Watoto wenu.

"watu wako" au 'kizazi chako"

kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake

Huu ni usemi unaosisitiza upendowa Yesu kwa watu n a jinsi alivyotaka kuwajali.

Nyumba yako imeachwa ukiwa.

"Mungu ataiacha nyumba yako, na itabaki tupu."

Nyumba yako.

Maana yake ni : (1). Mji wa Yerusalemu au (2). Hekalu.

Nami nakuambia

Huu ni msisitizo wa kile Yesualichosema baadaye

Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana

Tazama 21:9


Translation Questions

Matthew 23:1

Kwa kuwa Mafarisayo walikaa kwenye kiti cha Musa, Yesu aliwaambiaje watu juu ya mafundisho yao?

Yesu aliwaambia watu kufanya na kuyasikiliza mafundisho ya Mafarisayo waliyofundisho toka kwenye kiti cha Musa.

Kwa kuwa Mafarisayo walikaa kwenye kti cha Musa, Yesu aliwaambiaje watu juu ya mafundisho yao?

Yesu aliwaaambia watu kufanya na kuyasikiliza mafundisho ya Mafarisayo waliyofundisha toka kwenye kti cha Musa.

Kwa nini Yesu alisema kwamba watu wasiyafuate matendo ya waandishi na Mafarisayo?

Yesu alisema wasiyafuate matendo yao kwa sababu walikuwa wakisema vitu ambavyo wao wenyewe hawavifanyi.

Matthew 23:4

Je, Mafarisayo na waandishi walifanya matendo yao kwa lengo gani?

Walifanya matendo yao kusudi watazamwe na watu.

Matthew 23:8

Je, Yesu alimsema nani aliye Baba yetu na mwalimu wetu pekee?

Yesu alisema kwamba, Baba yetu aliye mmoja ni Yeye Mwenyewe aliye mbinguni, na mwalimu wetu pekee ni Kristo.

Je, Yesu alimsema ni nani aliye baba yetu na mwalimu wetu pekee?

Yesu alisema kwamba, Baba yetu aliye mmoja ni yeye mwenyewe aliye mbinguni, na mwalimu wetu pekee ni Kristo.

Matthew 23:11

Je, Mungu atamfanya nini mtu yule ajikwezaye, na mtu yule ajinyenyekezaye mwenyewe?

Mungu atamshusha mtu yule ajikwezaye mwenyewe na kumwinua mtu yule ajishushaye.

Matthew 23:13

Je, ni jina gani ambalo Yesu mara kwa mara aliwaita waandishi na Mafarisayo lililoeleza tabia yao?

Mara kwa mara Yesu aliwaita waandishi na Mafarisayo wanafiki.

Waandishi na Mafarisayo walipopata mfuasi mpya, alikuwa mwana wa nani?

Mafarisayo na waandishi walipopata mfuasi mpya alikuwa mwana wa kuzimu mara mbili.

Je, ni jina gani ambalo Yesu aliwaita mara kwa mara waandishi na Mafarisayo lilieleza tabia yao?

Mara kwa mara Yesu aliwaita waandishi na Mafarisayo wanafiki

Matthew 23:16

Juu ya kufungwa na viapo, je, Yesu alisema nini kuhusu mafundisho ya waandishi na Mafarisayo?

Yesu alisema kwamba waandishi na Mafarisayo walikuwa viongozi vipofu na vipofu wapumbavu.

Juuya kufungwa na viapo, Yesu alisema nini kuhusu mafundisho ya waandishi na Mafarisayo?

Yesu alisema kwamba waandishi na Mafarisayo walikuwa viongozi vipofu na vipofu wapumbavu.

Matthew 23:23

Japokuwa walilipa zaka zao za mnanaa, bizali na mchicha, waandishi na Mafarisayo walishindwa kufanya nini?

Waandishi na Mafarisayo walishindwa kufanya mambo makubwa ya sheria haki, rehema, na imani.

Matthew 23:25

Je, waandishi na Mafarisayo walishindwa kusafisha nini?

Waandishi na Mafarisayo walishindwa kusafisha ndani ya kikombe chao, ili upande wa nje pia uwe safi.

Je, waandishi na Mafarisayo walishindwa kusafisha nini?

Waandishi na Mafarisayo walishiindwa kusafisha ndani ya kikombe chao, ili upande wa nje pia uwe safi.

Matthew 23:27

Mafarisayo na waandishi walikuwa wamejaa nini ndani?

Waandishi na Mfarisayo ndani yao walikuwa wamejaa majivuno, udhalimu, unafiki na uovu.

Matthew 23:29

Mababa wa Mafarisayo na wa Waandishi waliwafnyia nini manabii?

Waliwaua manabii

Je, wazazi wa waandishi na Mafarisayo waliwafanyia nini manabii wa Mungu?

Wazazi wa waandishi na Mafarisayo waliwaua manabii wa Mungu.

Matthew 23:32

Ni hukumu gani ambayo waandishi na Mafarisayo wataipata?

Hukumu ya Jehanamu

Matthew 23:34

Je, Yesu alisema waandishi na Mafarisayo wangefanya nini juu manabii, watu wenye hekima na waandishi ambao angewatuma Yeye?

Yesu alisema watawaua na kuwasulibisha baadhi yao, kuwapiga baadhi yao, na wengine kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.

Kama matokeo ya tabia yao, Mafarisayo na Waandishi watapata hatia gani?

Hatia ya kumwagika kwa damu ya wenye haki katika duniani itakuja juu ya waandishi na Mafarisayo.

Ni kwa kizazi gani ambacho Yesu alisema kuwa haya yote yangetokea?

Yesu alisema kuwa haya yote yatatokea kwenye kizazi hiki.

Matthew 23:37

Yesu alikuwa na haja gani kwa ajili ya watoto wa Yerusalemu, na kwa nini haikutimizwa?

Yesu alitamani kuwakusanya watoto wa Yerusalemu pamoja, lakini hawakukubali.

Ni kwa namna gani nyumba za Yerusalemu zitabaki ukiwa?

Nyumba za Yerusalemu zitabaki ukiwa.


24

1Yesu alitoka hekaluni na kwenda zake. Wanafunzi wake walimwendea na kumuonesha majengo ya hekalu.2Lakini aliwajibu na kusema, “Je, hamuyaoni mambo haya yote? Kweli nawaambia, hakuna jiwe litalobaki juu ya lingine bila kubomolewa.”

3Na alipokaa katika lima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, “Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?”

4Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha.5Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, ‘Mimi ndiye Kristo,’ na watawapotosha wengi.6Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado.7Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali.8Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua.

9Ndipo watawatoa kwa ajili ya mateso na kuwaua. Mtachukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.10Ndipo wengi watajikwaa na kusalitiana na watachukiana wenyewe kwa wenyewe.11Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.12Kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapungua.13Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa.14Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote. Na ndipo ule mwisho utafika.

15Kwa hiyo, mtakapoona chukizo la uharibifu, lililosemwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),16ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani.17Na yule aliyeko juu ya paa la nyumba asiweze kuteremka chini kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya nyumba yake,18naye aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.19Lakini ole wao ambao wana mtoto na wale ambao wananyonyesha katika siku hizo!20Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.21Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi sasa, na wala haitakuwapo tena.22Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka. Lakini kwa sababu ya wateule, siku hizo zitafupishwa.

23Kisha ikiwa mtu yeyote atawaambia ‘Tazama, Kristo yuko hapa! Au, ‘Kristo yuko kule’ msiamini maneno hayo.24Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo watakuja na kuonesha ishara kubwa na maajabu, kwa kusudi la kupotosha, kama ingewezekana hata na wateule.25Tazameni, nimewatahadharisha kabla ya mambo hayo kutokea.26Kwa hiyo, ikiwa watawaambia, “Kristo yuko jangwani,’ msiende huko jangwani. Au, ‘Tazameni, yuko ndani ya nyumba,’ msiamini maneno hayo.27Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.28Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.

29Lakini mara baada ya dhiki kuu ya siku zile, Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbinguni zitatikisika.30Ndipo ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na makabila yote ya dunia wataomboleza. Watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu ya angani kwa nguvu na utukufu mkuu.31Atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine.

32Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.33Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango.34Kweli nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

36Lakini kuhusu siku ile na saa hakuna mtu ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, bali Baba peke yake.37Kama vile ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.38Kwa kuwa katika siku hizo kabla ya gharika watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa hadi siku ile ambayo Nuhu aliingia katika safina,39na hawakujua kitu chochote hadi gharika ilipokuja na kuwasomba wote - ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.40Ndipo watu wawili watakuwa shambani- mmoja atachukuliwa, na mmoja ataachwa nyuma.41Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja - mmoja atachukuliwa, na mmoja atabaki.42Kwa hiyo, kuweni macho kwa sababu hamjui ni siku gani ambayo atakuja Bwana wenu.43Lakini mjue kwamba, ikiwa bwana mwenye nyumba angejua ni saa ipi ambayo mwizi angekuja, angekesha na asingeruhusu nyumba yake kuvamiwa.44Kwa hiyo, pia mnapaswa kuwa tayari, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika saa msiyoitarajia.

45Hivyo ni nani aliye mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake amempa madaraka juu ya walio katika nyumba yake, ili awape chakula kwa wakati unaofaa?46Amebarikiwa mtumishi huyo, ambaye bwana wake atamkuta akifanya hivyo wakati ajapo.47Kweli nawaambia kwamba bwana atamweka juu ya kila kitu kilicho chake.48Lakini kama mtumwa mwovu akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu amekawia,’49na akaanza kuwapiga watumishi wake, na akala na kulewa vileo,50Bwana wa mtumwa huyo atakuja katika siku ambayo haitarajii, na katika saa ambayo haijui.51Bwana wake atamkata vipande viwili na kumweka katika nafasi moja sawa na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.


Mathayo 24 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Katika sura hii, Yesu anaanza kutabiri kuhusu wakati ujao kutoka wakati huo hadi atakaporudi kama mfalme wa ulimwengu.

Dhana maalum katika sura hii

"Mwisho wa ulimwengu"

Katika sura hii, Yesu anatoa jibu kwa wanafunzi wake wakati wanauliza jinsi watakavyojua wakati atakapokuja tena.

Mfano wa Nuhu

Katika wakati wa Nuhu, Mungu alituma gharika kuu kuwaadhibu watu kwa dhambi zao. Aliwaonya mara nyingi kuhusu kuja kwa mafuriko hayo, lakini kwa hakika yalianza ghafla. Katika sura hii, Yesu analinganisha mafuriko hayo na siku za mwisho.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

"Ruhusu"

ULB hutumia neno hili kuanzisha amri kadhaa za Yesu, kama "wacha wale walio Yudea wakimbilie milimani" (24:16), "yule aliye juu ya nyumba asije akashuka kuchukua chochote kutoka kwa nyumba yake "(24:17), na" aliye mashambani asirudi kuchukua nguo yake "(24:18). Kuna njia nyingi za kuunda amri. Watafsiri wanapaswa kuchagua njia za asili zaidi katika lugha zao wenyewe.

Links:


Matthew 24:1

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kueleza matukio amabayo yatakuja tokea kabla hajarudi mara ya pili

alitoka hekaluni

Inaonesha kuwa Yesu hakuwa ndani ya hekalu. alikuwa kwenye korido la hekalu.

Je, hamyaoni mambo haya yote?

"Ngoja niwaambie kitu fulani kuhusu majengo haya yote."

kweli nawambia

"Nawaambia ukweli." huu ni msisitizo wa kile alichosema Yesu badaye

Hakuna jiwe litakalobaki juu ya jiwe lingine ambalo halitabomolewa

"wakati maaskari walio adui watakapokuja, watabomoa kila jiwe juu ya majengo haya"

Matthew 24:3

kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu

Neno "kuja kwako" linamaanisha wakati Yesu atakapokuja katika nguvu, kuanzisha utawala wa Mungu duniani na kukifikisha kizazi hiki mwisho wake.

Mwe waangalifu asije mtu akawapotosha.

"Mwe waangalifu kwamba msiamini yeyote ambaye atawaongopea kuhusu mambo haya."

wengi watakuja kwa jina langu

Neno "jina" linamaanisha "katika mamlaka" au " kama mwakilishi" wa mwingine. "Wengi watadai kuwa wamekuja kama wawakilishi wangu" au "wengi watasema kuwa wanaongea kwa niaba yangu"

Matthew 24:6

Angalieni msiwe na wasiwasi.

"Msije mkaruhusu mambo haya kuwapa wasiwasi."

kwa kuwa taifa litainuka juu ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme

Hii inamaanisha kitu kilekile. na msisitizo wake ni kwamba kutakuwa na mapigano kila mahali

ni mwanzo tu wa uchungu

Hii inamaanisha maumivu mwanamke huyapata wakati anapotaka kujifungua mtoto. Sitiari hii inamaanisha kuwa haya matetemeko, njaa na vita ni mwanzo tu wa matukio yatakayotuongoza kuelekea mwisho wa dunia

Matthew 24:9

Watawatoa kwa ajili ya mataeso na kuwaua

"watuwatawatoa kwa mamlaka amaboa watawatesa na kisha kuwaua"

mtatchukiwa na mataifa yote

"watu kutoka kilataifa watawachukia"

kwa sababu ya ina langu

"kwa sababu mnaniamini "

watatokea

"watakuja"

Matthew 24:12

uovu utaongezeka

"watu watafanya dhambi zaidi na zaidi"

Upendo wa wengi utapoa.

Maana ya karibu: 1."watu wengi hawatawapenda wenzao." au 2."watu wengi hawatampenda Mungu."

atakayevumilia

"yeyote atayebaki na uvumilivu"

mpaka mwisho

haieleweki kama "mwisho" inamaanisha mtu anapokufa, au wakati dhiki itakapokoma, au mwisho wa nyakati wakati Mungu atakapojionesha kuwa mfalme. jambo l a kuzingatia hapa ni uvumilivu usiokoma

ataokolewa

"Mungu atamwokoa mtu huyo"

Hii injili ya ufalme itahubiriwa

"Watu watahubiri ujumbe juu ya utawala wa Mungu"

Mataifa yote.

"Watu wote katika sehemu zote."

na ndipo ule mwisho

"mwisho wa ulimwengu" aua "mwisho wa nyakati"

Matthew 24:15

chukizo la uharibifu

"mtu wa aibu atakayevinajisi vitu vya Mungu"

Lililosemwa na nabii Danieli.

"Kuhusu ambacho nabii Danieli aliandika."

asomaye na afahamu

Haya maneno hayakusemwa na Yesu. Matahayo aliongezea haya ili kupata usikivu

Na yule aliyeko juu ya paa

mapaa wakati wa Yesu yalikuwa tambarare, kiasi kwamba watu wangeweza kusimama

Matthew 24:19

Wao ambao wana mtoto.

"wanawake wenye mimba"

katika siku hizo

"wakati huo"

kukimbia kwenu kusiwe

"kwamba msikimbie"

Wakati wa baridi.

"Majira ya baridi."

kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka

"kama Mungu hatazifupisha siku zadhiki watu wote wangekufa"

Wenye mwili

Watu.

siku hizo zitafupishwa

"Mungu atazifupisha siku za dhiki"

Matthew 24:23

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwaambia wanafunzi wake

Msiamini maneno hayo

"Msiamini mambo ya uongo wanayowaambia."

kwa kusudi la kuwapotosha

"ili kuwafanya watu wasitii"

kupotosha, kama ingeliwezekana hata na wateule

"kupotosha, kama ingeliwezekana, watawafanya hata na wateule kutotii"

Matthew 24:26

ikiwa watawambia, 'Kristo yuko jangwani,' msiende huko jangwani. Au 'Tazameni, 'yuko ndani ya nyumba,'

"au, kama mtu atawambia kuwa Kristo yumo ndani ya nyumba"

ndani ya nyumba

"ndani ya chumba cha siri"

kama vile radi inavyomulika ... ndivyo itavyokuwa kuja

Hiiinamaanisha mwana wa mtu atakuja kwa kasi sana na itakuwa rahisi kumwona

Kama vile radi inavyomulika...ndivyo itakavyokuwa kuja.

Atakuja kwa kasi na itakuwa rahisi kuonekana.

mwana wa Adamu

Yesu anaongea juu yake katika nafsi ya tatu

Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.

Maana ya karibu ni: (1). Mwana wa Adamu atakapokuja, kila mtu atamuona na kujua kwamba amekuja; (2). Popote walipo watu aliokufa kiroho, manabii wa uongo watakuwepo huko kuwaambia uongo.

tai

Ndege ambao wanakula mizoga au wanyama wanaokaribia kukata roho.

Matthew 24:29

Lakini mara

"wakati huo"

dhiki y a siku hizo

"wakati huo wa dhiki"

Jua litatiwa giza.

"Mungu atalifanya jua liwe giza."

Nguvu za mbinguni zitatikisika.

" Mungu atatikisa vitu katika mbingu na juu ya anga."

Matthew 24:30

Mwana wa Adamu ... mwo ... wake

Yesu anaongea juu yake katika nafsi ya tatu.

makabila yote

watu wa makabila yote

atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta

"wakati tarumbeta itakapolia atawatuma malaika wake"

Watakusanya.

"Malaika wake watakusanya."

Wateule wake.

Watu ambao Mwana wa Adamu amewachagua.

kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho wa mmoja wa mbingu hadi mwingine

kutoka kila upande

Matthew 24:32

amekaribia

"wakati wangu wa kuja umekaribia"

Karibu na malango.

karibu na malango

Matthew 24:34

kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli" huu ni msisitizo wa kile kinachosemwa baadaye

Kizazi hiki hakitapita.

"Watu wanaoishi kipindi hiki hawatafariki wote."

Hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.

"Mpaka Mungu asababishe mambo haya yote yatimie."

Mbingu na nchi zitapita.

"Mbingu na nchi hazitaendelea kuwapo."

maneno yangu hayatapita kamwe

"kile ninachosema daima kitabaki kuwa ukweli"

Matthew 24:36

siku ile na saa

hapa "siku" na "saa" vinamaanisha muda halisi ambao mwana wa Adamu atarudi

Wala Mwana.

"Hakuna hata mwana"

mwana

Hiki ni cheo muhimu cha Yesu, Mwana wa Mungu

Baba

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu

Matthew 24:37

Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.

"Siku ambayo Mwana wa Adamu atakuja tena itakuwa kama ilivyokuwa siku za Nuhu,"

Mwana wa Adamu

Yesu anaongea juu yake akaitumia nafsi ya tatu

katika safina na hawakujua kitu

"katika safina. Na watu hawakuju kuwa kuna kitu kilikuwa kinaenda kutokea"

ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu

"Hivyo ndivyo itakavyokuwa wakati wa kuja kwa Mwana wa Adamu"

Matthew 24:40

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuwaambia wanfunzi wake kuwa tayari kwa ajili ya kurudi kwake

Ndipo.

Wakati Mwana wa Adamu ajapo.

Mmoja atachukulia, na mmoja ataachwa nyuma.

Maana za karibu: 1. Mungu atamchukuwa mmoja kwenda mbinguni na ataacha mmoja duniani kwa ajili ya adhabu, au 2. Malaika watamchukua mmoja kwa ajili ya adhabu na kumuacha mwingine kwa ajili ya baraka.

Kinu.

Chombo cha kusagia.

Kwa hiyo.

"Kwa sababu ya kile nilicho waambia."

Kuweni macho.

Kaa tayari.

Matthew 24:43

ikiwa bwana mwenye nyumba ... nyumba yake kuvamiwa

Yesu anaatumia mfano wa bwana na mtumwa kufafanua kuwa wansfunzi wake wanatakiwa kujiandaa kwa ajili ya kurudi kwa Yesu

Mwizi.

Yesu anasema atakuja wakati ambao watu hawamtarajii, siyo kwamba atakuja kuiba.

Angekuwa amelinda.

"Angelinda nyumba yake" kuisalimisha.

Na asingeruhusu nyumba yake ivamiwe.

"Asingeruhusu mtu yeyote kuingia ndani ya nyumba yake aibe vitu."

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia nafasi ya tatu kujisemea yeye

Matthew 24:45

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea na mithali yake ya bwana na mtumwa kufafanua kuwa wanafunzi wake wanapaswa kujiandaa kwa ajili y a kurudi kwa Yesu.

Hivyo ni nani mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake...wakati?

"Hivyo ni nani mwaminifu, mtumwa mwenye akili? Ndiye yule ambaye bwana wake...wakati."

Awape chakula chao

"Awape watu chakula chao katika mji wa bwana wake"

Kweli nawambia

"Nawaambieni ukweli" Hii inaongeza msisitizo wa kile ambacho Yesu atakuja kusema baadaye.

Matthew 24:48

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha mithali yake ya bwana na mtumwa ...

Anasema moyoni mwake.

"Anafikiri akilini mwake."

Bwana wangu amekawia

Bwana wangu hafanyi haraka kuja

katika siku ambayo hatarjii, na katika saa ambayo haijui

Virai hivi vyote vinamaanisha kitu kilekile. vinasisitiza kuwa bwana atakuja wakati ambao mtumwa wake hamtarajii kuja.

Kumweka katika nafasi au kumhesabu kama.

"Kumtendea"

kumweka katika nafasi

"kumtendea"

atamkata vipande

kumfanya mtu aumie sana

kilio na kusaga meno

Tazama 8:11


Translation Questions

Matthew 24:1

Je, Yesu alitabiri nini juu ya hekalu huko Yerusalemu?

Yesu alitabiri kuwa haltabakijiwe juu ya jiwe ambalo halitabomolewa.

Matthew 24:3

Baada ya kusikia unabii kuhusu Hekalu, wanafunzi walimuuliza nini Bwana Yesu?

Wanafunzi walimuuliza ni lini mambo haya yangetokea, na ni nini dalili za kuja kwake na mwisho wa ulimwengu?

Ni aina gani ya watu ambao Yesu alisema kuwa watawapotosha wengi?

Yesu alisema kuwa wengi watakuja wakisema wao ni makristo, watawapotosha wengi.

Matthew 24:6

Ni matukio gani ambayo yesu alisema yatakuwa mwanzo wa utungu?

Yesu alisema kwamba vita, njaa, na matetemeko yatakuwa mwanzo wa utungu.

Ni matukio gani ambayo Yesu alisema kuwa yatakuwa mwanzo wa utungu?

Yesu alisema kuwa vita njaa, na matetemeko yatakuwa mwanzo wa utungu

Matthew 24:9

Yesu alisema kungetokea nini kati ya wanafunzi katika majira hayo?

Yesu alisema kwamba wanafunzi watapata mateso ya dhiki kuu, baadhi watajikwaa na kusalitiana, na mioyo ya watu wengi itapoa.

Yesu alisema kungetokea nini kati ya wanafunzi katika majira hayo?

Yesu alisema kuwa wanafunzi wangepata mateso ya dhiki kuu, baadhi watajikwaa na kusalitiana,na mioyo ya watu wengi itapoa

Matthew 24:12

Yesu alisema ni nani atakaye okoka?

Yesu alisema kwamba atakayevumilia mpaka mwisho ndiyo atakayeokoka?

Kitatokea ni juu ya injili kabla ya mwisho kufika?

Injil ya ufalme itahubiriwa duniani kote kabla mwisho kuja.

Matthew 24:15

Yesu alisema waumini wanapaswa kufanya nini watakapoona chukizo la uharibifu limesimama mahali patakatifu? (24:15)

Yesu alisema waumini watakimibilia milimani.

Yesu alisema waumini wanapaswa kufanya niiwatapoona chukizo la uharibifu limesimama mahali patakatifu?

Yesu alisema waumini watakimblia milimani.

Matthew 24:19

Ile dhiki itakuwa kubwa kiasi gani siku zile?

Katika siku zile, ile dhiki itakuwa kubwa sana kuliko ambavyo ilishawahi kutokea tangu kuumbwa kwa dunia.

Matthew 24:23

Ni kwa jinsi gani makristo wa uongo na manabii wa uongo watawapotosha watu?

Makristo wa uongo na manabii wa uongo watawapotosha watu kwa kufanya ishara na maajabu.

Matthew 24:26

Kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwaje?

Kuja kwa Mwana wa Adamu kutakuwa kama radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi.

Matthew 24:29

Kitu gani kitalitokea jua, mwezi, na nyota baada dhiki kuu ya siku hizo?

Jua na mwezi vitatiwa giza, na nyota zitaanguka kutoka mbinguni.

Matthew 24:30

Je, makabila yote duniani yatafanya nini watakapomwona Mwana wa Adamu akija katka nguvu na utukufu mkuu?

Makabila ya duniani watapigapiga vifua vyao.

Ni sauti gani itakayosikika Mwana wa Adamu atakapotuma malaika wake kuwakusanya wateule?

Sauti kuu ya tarumbeta itasikika malaika watakapowakusanya wataeule.

Matthew 24:34

Yesu alisema kitu gani hakitapita hadi mambo haya yote yatimie?

Yesu alisema kwamba kizazi hiki hakitapita mpaka mambo haya yote yatimie.

Yesu alisema kitu gani kitapita, na kitu gani hakitapita kamwe?

Yesu alisema kuwa mbingu na dunia zitapita, lakini neno lake halitapita kamwe.

Matthew 24:36

Ni nani ajuae wakati gani mambo haya yatatokea?

Ni Baba peke yake ajuae lini matukio haya yatatokea.

Matthew 24:37

Jinsi gani kuja kwa Mwana wa Adamu kuna fanana na siku za Nuhu kabla ya Gharika?

Watu watakuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, bila kujua hukumu itawajilia kuwaangamiza.

Jinsi gani kuja kwa mwana wa Adamu kunafanana na siku za Nuhu kabla ya Gahrika?

Watu watkuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa, bila kujua hukumu itawajilia kuwaangamiza.

Matthew 24:40

Ni tabia gani ambayo Yesu alisema waumini wake lazima waendelee kuwa nayo juu ya ujio wake, na kwa nini?

Yesu alisema kuwa waumini wake lazima wawe tayari, kwa sababu hawajui ni siku gani Bwana atakapokuja.

Matthew 24:45

Kitu gani mtumwa mwaminifu na mwenye busara alifanya kipindi bwana wake alipokuwa ameondoka?

Mtumwa mwaminifu na mwenye busara alitunza mali yote ya bwana wake wakati bwana wake alipokuwa amesafiri.

Kitugani mtumwa mwaminifu na mwenye busara alifanya kipindi bwana wake alipokuwa ameondoka?

Mtumwa mwaminifu na mwenye busara alitunza mali yote ya bwana wake wakati bwana wake aliokuwa amesafiri

Kitu gani bwana wake atafanya kwa mtumwa mwaminifu na mwenye busara wakati bwana wake atakaporudi?

Takapokuja, bwana wake atamweka mtumwa mwaminnifu na mwenye busara juu ya kila kitu anachokimiliki.

Matthew 24:48

Je, yule mtumwa mwovu alifanya nini wakati bwana wake alipokuwa amesafiri?

Mtumwa mwovu aliwapiga wafanyakazi wake na akala na kunywa pamoja na walevi wakati bwana hajarudi.

Je, yule mtumwa mwovu alifanya nini wakati bwana wake alipokuwa amesafiri?

Mtumwa mwovu aliwapiga wafnyakazi wake na akala na kunywa pamoja na walevi wakati bwana hajarudi.

Bwana atamfanya nini yule mtumwa mwovu atakaporudi?

Bwana atakaporudi, atamkata yule mtumwa mwovu katika vipande viwili na kumpeleka mahali ambapo kutakuwa na kilo na kusaga meno.


25

1Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi.2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu.3Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote.4Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.5Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala.

6Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, ‘Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.’7Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao.

8Wale wapumbavu waliwaambia wale werevu, ‘Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.’9Lakini wale werevu waliwajibu na kuwaambia, ‘Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.’10Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa.

11Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, ‘Bwana, bwana, tufungulie.’12Lakini alijibu na kusema, ‘Kweli nawaambia, Mimi siwajui.’

13Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.

14Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake.15Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake.16Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.17Vile vile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili.18Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.

19Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao.20Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, ‘Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.’

21Bwana wake akamwambia, ‘Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.’

22Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, ‘Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,’

23Bwana wake akamwambia, ‘Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.’

24Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, ‘Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia.25Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.’

26Lakini bwana wake alijibu na kusema, ‘Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.27Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.28Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi.29Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa.30Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

31Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu.32Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi.33Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto.

34Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, ‘Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.35Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;36Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.’

37Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, ‘Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji?38Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo?39Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia?

40Na mfalme atawajibu na kuwaambia, ‘Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’

41Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake,42kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji;43Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.’

44Ndipo wao pia watamjibu na kusema, ‘Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia?

45Kisha atawajibu na kusema, ‘Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.’

46Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele.”


Mathayo 25 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Sura hii inaendeleza mafundisho ya sura ya awali.

Dhana maalum katika sura hii

Mfano wa bikira kumi

Miongoni mwa Wayahudi, wakati ndoa ilipangwa, kulikuwa na muda kabla ya harusi. Mwisho wa muda huo, kijana huyo angeenda nyumbani kwa bibi arusi, ambako alikuwa anamngojea. Sherehe ya harusi basi ingefanyika. Kwa furaha kubwa wangeweza kusafiri hadi nyumba ya bwana harusi, ambako kungekuwa na sikukuu.

Yesu anatumia desturi hii kwa kuwaambia mfano wa bikira kumi (Mathayo 25:1-13).

Links:


Matthew 25:1

Sentensi unganishi

Yesu anaongea mfano wa wanawali wenyebusara na wale wanawali wajinga kufundisha kuwa wanafunzi wake wanapaswa kujiandaa kwa ajili y a kurudi kwa Yesu

ufslme wa mbinguni utafananishwa na

Tazama 13:24

Lamps.

Hizi ziliweza kuwa, 1.taa zenyewe au mienge iliyotengenezwa kwa kuwekewa kitambaa kuzunguka mwisho wa mti na hulowanishwa na mafuta.

Watano kati yao.

Watano kati ya wanawali.

Hawakuchukua mafuta yoyote.

"Waliyokuwa nayo ni yale tu yaliyokuwa katika taa zao."

Matthew 25:5

Sasa

Neno linaloonesha kuanzisha habari mpya. Yesu anaanza kueleza sehemu ya habari hii.

bwana harusi amechelewa

"wakati bwana harusi alipochukua muda mrefu kuwasili"

Wote walianza kusinzia.

Wanawali wote kumi walianza kusinzia.

kulikuwa na yowe

"mtu mmoja alianza kupiga kelele"

Matthew 25:7

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano

Kutayarisha taa zao.

"Wakarekebisha taa zao ili ziwake kwa mng'ao."

Wapumbavu walisema na welevu.

"Wanawali wapumbavu walisema na wanawali welevu."

Taa zetu zinazimika

"Moto katika taa zetu unaelekea kuzima."

Matthew 25:10

Sentensi ungsnishi

Yesu anahitimisha mfano wa wanawali kumi

wakati wameenda huko

"Wanawali wapumbavu waliondoka."

kununua

"kununua mafuta zaidi"

Wale ambao walikuwa tayari.

Wanawali waliokuwa na mafuta ya ziada.

Mlango ulifungwa.

"watumishi walifunga mlango."

Tufungulie.

"Fungua mlango kwa ajili yetu ili tuingie ndani"

kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli" Hiiinatia msisitizo wa kile Yesu alichosema baadaye

"Siwatambui ninyi."

"Si watambui ninyi ni akina nani" au 'si wajui ninyi ni akina nani."

kwa kuwa hamjui siku wala saa

"Hamjui muda halisi ambao Mwana wa Adamu atakuja"

Matthew 25:14

Sentensi unganishi

Yesu anaeleza mfano wa mtumishi mwaminifu na asiye mwaminifu ili kuwafundisha wanafunzi wake kubaki waaminifu wakati yeye hatakuwepo na wawe tayari kwa ajili ya kurudi kwa Yesu.

Ni sawa na.

"Ufalme wa mbinguni ni unafanana na."

Alipotaka kuondoka

"Alipokuwa tayari kuondoka" au mara alipotaka kuondoka."

Aliwakabidhi utajiri wake.

"Akawapa usimamizi wa mali yake." au "akawapa usimamizi wa utajiri wake."

Utajiri wake.

"Mali yake."

Talanta tano.

"Talanta moja" ilikuwa na thamani ya mishahara wa miaka ishirini. Epuka kutafsiri jambo hili katika pesa za siku hizi. Mfano huo unalinganisha uwiano wa kiasi cha tano, cha mbili na kiasi cha moja sawia na kiasi kikubwa cha utajiri uliotumika. "mifuko mitano ya dhahabu."

kulingana nauwezo wake

"kulingana na uwezo wa kila mtumishi wa kusimsmia mali"

Na kuzalisha talanta zingine tano.

"Kutokana na uwekezaji wake, alipata faida ya talanta zingine tano."

na kuzalisha talanta zingine tano

"kutokana na uwekezaji wake, akazalisha talanta zingine tano"

Matthew 25:17

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea mafano wa watumishi na talanta

Alizalisha zingine mbili.

"Alipata faida ya talanta zingine mbili.'

Matthew 25:19

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano wa watumishi na talanta

na baada ya muda

Kirai hiki kimetumika kuonesha mwanzo wa habari mpya. Yesu anaanza kueleza sehemu mpya ya simulizi.

Nimepata talanta tano zaidi

"Nimepata faida ya talanta tano zaidi."

Talanta

Mali yenye thamani kubwa. talanta moja ilikuwa sawa na mishahara ya miaka ishirini.Tazama tafsiri katika. 25:14--15.

Hongera.

"Umefanya kazi vizuri." au "Umefanya vema." Katika utamaduni wako pengine mnao usemi ambao mkuu (mtu mwenye mamlaka) angetumia kuthibitisha kile ambacho mtumishi wake (au yeyote chini yake) amekitekeleza.

Ingia katika furaha ya Bwana wako

"Njoo ufurahie na mimi"

Matthew 25:22

Sentensi unganishi

Yesu anaendelelea kueleza mfano wa watumishi na talanta

Nimepata faida ya talanta zingine mbili

"Nimepata fada ya talanta mbili zaidi"

Umefanya vema

umefanya vema.

Ingia katika furaha ya bwana wako

Tazama 25:19

Matthew 25:24

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano wa watumishi na talanta

Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahli ambapo hukupanda.

Maelezo haya mawili yanamaanisha kitu kilekile. Mtumwa anamlaumu bwana kwa kukusanya mazao ambayo siyo yake. "Unakusanya mazao ya bustani kutoka katika bustani ambazo huna haki ya kukusanya mazao hayo."

Kupanda

Siku hizo walizoea kutupa kiasi kidogo cha mbegu pande zote badala ya kupanda katika mistari.

Tazama, unapata ile ile ya kwako.

"Angalia, hii n"diyo yako"

Matthew 25:26

Sentensi unganishi

Yesu anaenedelea kueleza mfano wa watumishi na talanta.

Wewe mtumwa mwovu na mzembe.

"wewe ni mtumwa mwovu ambaye hutaki kufanya kazi."

Ninachuma mahali ambapo sikupanda na kuvuna mahali ambapo sikusiha.

Tazama 25:24

Kupokea tena ile yangu.

"Kupokea tena fedha yangu mwenyewe"

Faida.

Malipo yanayotolewa na benki kutokana na matumizi yasiyo ya kudumu ya pesa ya bwana.

Matthew 25:28

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kueleza mfano wa watumishi na talanta

mnyang'anyeni hiyo talanta

Bwana anawaambia wale watumishi wengine

talanta

Tazama 25:14

aliye na

"anayetumia vizuri alicho nacho"

ataongezewa zaidi

"Mungu atampa zaidi"

hata kwa kuzidishiwa

"hata zaidi"

kwa yeyote asiye na kitu

"Kwa yeyeote asiyetumia vizuri hicho alicho nacho.

Ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno

"Mahali ambapo watu watalia na kusaga meno yao."

"nacho atanyang'anywa"

nitakiondoa

mtupeni nje gizani huyo mtumishi asiyefaa, ambako kutakuwa na kilion a kusaga meno

"nje gizani ambako kuna kilio na kusaga meno"

Matthew 25:31

Sentensi unganishi

Yesu anaanza kuwaambia wanafunzi wake jinsi atakavyowahukumu watu atakaporudi wakatiwa mwisho

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia nafsi ya tatu kuongea juu yake mwenyewe

Mataifa yote yatakusanyika mbele zake.

"Atayakusanya mataifa yote mbele zake."

Mbele zake.

"Mbele za uso wake."

Mataifa yote.

"Watu wote kutoka kila nchi."

kama vile mchungaji anavyotenganisha kondoo na mbuzi

Yesuanatumia msemo kuonesha jinsi atakavyowatenganisha watu

atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wake wa kushoto

atawaweka watu wenye haki upande wake wa kuume na atawaweka wenye dhambi upande wake wa kushoto

Matthew 25:34

Mfalme... mkono wake wa kulia

"Mimi mfalme, ... mkono wangu wa kulia"

Mfalme...mkono wake wa kulia

Yesu alijisema yeye mwenyewe katka nafsi ya tatu. AT: "Mimi, Mfalme...mkono wangu wa kulia."

Njoni, ninyi mliobarikiwa na Baba yangu.

"Njoni, ninyi ambao baba yangu amewabariki."

Baba yangu

Hili ni jina mashuhuri la Mungu linaloonesha uhusiano kati ya Mungu na Yesu

Urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu.

"Urithini ufalme ambao Mungu ameufanya tayari kwa ajili yenu."

urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajiloi yenu

"pokeeni baraka za utawala wa Mungu ambazo Mungu alipanga kuwapeni"

tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu

"Tangu hapo alipouumba ulimwengu"

Matthew 25:37

wenye haki

watu wenye haki

au kiu ... au uchi

"au ni lini tulipokuwa ukiwa na kiuau nilini tulipokuona u uchi"

Mfalme.

Hiki ni cheo kingine cha Mwana wa Mungu

na kuwaambia

"Akasema na wale walio mkono wa kulia."

Kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli, "Huu ni msisitizo wa kile ambacho Yesu alikuja kusema baadaye"

kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo

"mmoja wa wasio wa muhimu"

Ndugu zangu

"kaka zangu na dada" au "hawa ambao ni kama kaka zangu na dada zangu

mlinitendea mimi

"Ninajali kwamba mlifanya hivyo kwa ajili yangu."

Matthew 25:41

Ndipo atawaambia

"Ndipo mfalme atawaambia"

Mlio laaniwa.

"enyi watu ambao Mungu amewalaani."

Moto wa milele ambao umeandaliwa.

"Moto wa milele ambao Mungu ameandaa."

Malaika wake.

Wasaidizi wake.

Uchi lakini hamkunivika.

"Nilikuwa uchi lakini hamkunipa nguo."

Mgonjwa na niko kifungoni.

"Nilikuwa mgonjwa na nilikuwa kifungoni."

nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni

"nilikuwa mgonjwa na nilikuwa gerezani"

Matthew 25:44

Sentensi unganishi

Yesu anahitimisha kuwaambia wanafunzi wake jinsi atakavyowahukumu watu atakapokuja mara ya pili

Maelezokwa ujumla

Huu ni mwisho wa sehemu ya habari inayoanzaia 23:1, mahali ambapo Yesu anafundisha juu ya wokovu na hukumu ya mwisho.

Wao pia watamjibu.

"Hao walioko kushoto pia watamjibu"

Mmoja wa wadogo hawa.

"Kwa yeyote kati ya watu wangu walio wadogo."

Hamkunitendea mimi.

"Nina jali kuwa hamkufanya kwa aajili yangu" au "Mimi ndiye hasa yule ambaye hamkumsaidia"

Hawa watakwenda katika adhabu ya milele

"Mfalme atawapeleka hawa kwenye eneo amablo watapata adhabu ambayo haitakoma"

Wenye haki kwenda katika uzima wa milele.

"Watu wenye haki wataenda katika uzima wa milele."

bali wenye haki katika uzima wa milele

"lakini mfalme atawapeleka hawa mahali ambapo wataishi milele pamoja na Mungu"

wenye haki

"watu wenye haki"


Translation Questions

Matthew 25:1

Je, wale wanawali wapumbuvu hawakufanya nini walipoenda kumwona bwana harusi?

Wale wanawali wapumbavu walipochukua taa zao hawakuchukua mafuta.

Je, wale wanawali wenye busara walifanya nini walipoenda kumpokea bwana harusi?

Wale wanawali wenye busara walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.

Matthew 25:5

Bwana arusi alifika saa ngapi, na je, huu ndio muda uliotarajiwa?

Bwana arusi alifika usiku wa manane, baada ya muda uliotarajiwa.

Bwana Harusi alifika saa ngapi, na je huu ndio muda uliotarajiwa?

Bwana Harusi alifika usiku wa manane, baada ya muda uliotarajiwa.

Matthew 25:10

Kitu gani kiliwatokea wale wanawali welevu alipokuja bwana arusi?

Wanawali welevu walienda pamoja na bwana arusi katika sherehe ya harusi.

Kilitokea kitu gani kwa wale wanawali wapumbavu bwana harusi alipokuja?

Wale wanawali wapumbavu walienda kununua mafuta, na walipokuja ule mlango wa kuingia kwenye sherehe ulikuwa umefungwa.

Kilitokea kitu gani kwa wanawali wapumavu bwana harusi alipokuja?

Wale wanawali wapumbavu walienda kunua mafuta, na walipokuja ule mlango wa kuingia kwenye sherehe ulikuwa umefungwa.

Je, Yesu alisema alitaka waumini wajifunze nini kutokana na mfano wa wanawali?

Yesu alisema kuwa waumii wanapaswa kuwa tayari kwa kuwa hawajui siku wala saa.

Matthew 25:14

Je, yule watumishi wenye talanta tano, na mwenye talanta mbili walizifanyia nini zile talanta wakati bwana wao alipokuwa safarini?

Yule mtumishi mwenye talanta tano alizalisha talanta zingine tano na yule mwenye talanta mbili alizalisha zingine mbili.

Matthew 25:17

Yule mtumwa, mwenye taranta moja na alifanya nini ile talanta wakati bwana wake alipokuwa safarini?

Yule mwenye moja alichimba shimo na kuifukia ile talanta ya bwana wake .

Matthew 25:19

Huyu bwana alikaa muda gani akiwa huko safarini.

Huyo bwana alikaa huko safarini kwa muda mrefu.

Huyo bwana aliporudi, alifanya nini kwa mtumwa aliyekuwa amepewa talanta tano na yule aliye kuwa amepewa talanta mbili?

Yule bwana alisema, "hongera, watumwa wazuri na waamiinifu" na aliwaweka kuwa wasimamizi wa mambo mengi.

Huyo bwana aliporudi, alifanya nini kwa mtumwa aliyekuwa amepewa talanta tano na yule aliye kuwa amepewa talanta mbili?

Yule bwana alisema, "hongera, watumwa wazuri na waamiinifu" na aliwaweka kuwa wasimamizi wa mambo mengi.

Matthew 25:26

Yule bwana aliporudi alimfanya nini yule mtumwa aliyekuwa amepewa talanta moja

Tule bwana alisema, "wewe mtumwa mwovu na mzembe," alimnyanga'nya ile talanta moja, na kumtupa katika giza la nje.

Matthew 25:31

Mwana wa Adamu atafanya nini atakapokuja na kukaa juu ya kiti chake cha utukufu?

Mwana Adamu atayakusanya mataifa yote na atawatenganisha watu kundi moja kutoka kundi jingine.

Mwana wa Adamu atafanya nini atakapokuja na kukaa juu ya kiti chake cha utukufu?

Mwana Adamu atayakusanya mataifa yote na atawatenganisha watu kundi moja kutoka kundi jingine.

Matthew 25:34

Wale watakaokuwa upande wa kulia wa Mfalme watapokea nini?

Wale wa upande wa kulia wa Mfalme kupokea ufalme ulioandaliwa kwa ajili yao tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.

Matthew 25:41

Wale watakaokuwa upande wa kushoto wa Mfalme watapokea nini?

Wale wa upande kushoto wa Mfalme watapokea moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake.

Je, walewa upande wa kushoto kwa mfalme hawakufanya nini maishani mwao?

Wale wa upande wa kushoto wa mfalme hawakuwapa chakula wenye njaa, wala kinywaji wenye kiu, hawakuwakaribisha wageni, hawakuwapa nguo walio uchi, hawakuwajali wagonjwa, wala kuwatembelea wafungwa.

Je, walewa upande wa kushoto kwa mfalme hawakufanya nini maishani mwao?

Wale wa upande wa kushoto wa mfalme hawakuwapa chakula wenye njaa, wala kinywaji wenye kiu, hawakuwakaribisha wageni, hawakuwapa nguo walio uchi, hawakuwajali wagonjwa, wala kuwatembelea wafungwa.


26

1Wakati Yesu alipomaliza kusema maneno yote hayo, aliwaambia wanafunzi wake,2“Mnajua kwamba baada ya siku mbili kutakuwa na sikukuu ya pasaka, na mwana wa Adamu atatolewa ili asulibiwe.”

3Baadaye wakuu wa makuhani na wazee wa watu walikutana pamoja katika makao ya Kuhani Mkuu, aliye kuwa anaitwa Kayafa.4Kwa pamoja walipanga njama ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.5Kwa kuwa walisema, “Isifanyike wakati wa sikukuu, kusudi isije ikazuka ghasia miongoni mwa watu.”

6Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,7alipokuwa amejinyoosha mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa amebeba mkebe wa alabasta iliyokuwa na mafuta yenye thamani kubwa, na aliyamimina juu ya kichwa chake.8Lakini wanafunzi wake walipoona jambo hilo, walichukia na kusema, “Nini sababu ya hasara hii?9Haya yangeweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa na kupewa maskini.”

10Lakini Yesu, akiwa anajua hili, akawaambia, “Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Kwa kuwa amefanya kitu kizuri kwangu.11Masikini mnao siku zote, lakini hamtakuwa pamoja nami daima.12Kwa sababu alipomimina mafuta haya juu ya mwili wangu, alifanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.13Kweli nawaambieni, popote Injili hii itakapohubiriwa katika ulimwengu mzima, kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka.”

14Ndipo mmoja wa wale Kumi na wawili, aliyeitwa Yuda Iskariote, alienda kwa wakuu wa makuhani15na kusema, “Mtanipatia nini nikimsaliti?” Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.16Tangu muda huo alitafuta nafasi ya kumsaliti.

17Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, “Wapi unataka tukuandalie ule chakula cha Pasaka?”

18Akawaambia, “Nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni, Mwalimu anasema, ‘Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’”19Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza, na waliandaa chakula cha Pasaka.

20Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi kumi na wawili.21Walipokuwa wanakula chakula, alisema, “Kweli nawaambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”

22Walihuzunika sana, na kila mmoja alianza kumuuliza, “Je, hakika siyo mimi, Bwana?”

23Akawajibu, “Yule ambaye anachovya mkono wake pamoja nami katika bakuli ndiye atakaye nisaliti.24Mwana wa Adamu ataondoka, kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu ambaye atamsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama asingezaliwa.”25Yuda, ambaye angemsaliti alisema, “Je, ni mimi Rabi?” Yesu akamwambia, “Umesema jambo hilo wewe mwenyewe.”

26Walipokuwa wakila chakula, Yesu aliutwaa mkate, akaubariki, na kuumega. Akawapa wanafunzi wake akisema, “Chukueni, mle. Huu ni mwili wangu.”27Akatwaa kikombe na kushukuru, akawapa na kusema, “Kunyweni wote katika hiki.28Kwa kuwa hii ni damu ya agano langu, inayomwagwa kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.29Lakini nawaambieni, sitakunywa tena matunda ya mzabibu huu, hadi siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

30Walipokuwa wamemaliza kuimba wimbo, walitoka kwenda Mlima wa Mizeituni.

31Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu ninyi nyote mtajikwaa kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika.32Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

33Lakini Petro alimwambia, “Hata kama wote watakukataa kwa sababu ya mambo yatakayokupata, mimi sitakukataa.”

34Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”

35Petro akamwambia, “Hata kama ingenipasa kufa na wewe, sitakukana.” Na wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.

36Baadaye Yesu alienda nao mahali panapoitwa Gethsemane na aliwaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati nikienda huko na kuomba.”37Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo na akaanza kuhuzunika na kusononeka.38Kisha akawaambia, “Roho yangu ina huzuni kubwa sana, hata kiasi cha kufa. Bakini hapa na mkeshe pamoja nami.”39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, na kuomba. Akasema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniepuke. Isiwe kama ninavyotaka mimi, bali kama utakavyo wewe.”40Akawaendea wanafunzi na akawakuta wamelala usingizi, na akamwambia Petro, “Kwa nini hamkuweza kukesha nami kwa saa moja?41Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”

42Akaenda zake mara ya pili na kuomba, akasema, “Baba yangu, kama jambo hili haliwezi kuepukika na ni lazima nikinywee kikombe hiki, mapenzi yako yatimizwe.”

43Akarudi tena na kuwakuta wamelala usingizi, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito.44Kisha akawaacha tena akaenda zake. Akaomba mara ya tatu akisema maneno yaleyale.45Baadaye Yesu aliwaendea wanafunzi wake na kuwaambia, “Bado mmelala tu na kujipumzisha? Tazameni, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.46Amkeni, tuondoke. Tazama, yule anaye nisaliti amekaribia.”

47Wakati alipokuwa bado anaongea, Yuda mmoja wa wale kumi na wawili, akafika. Kundi kubwa lilifika pamoja naye likitokea kwa wakuu wa Makuhani na wazee wa watu. Walikuja na mapanga na marungu.48Tena mtu aliyekusudia kumsaliti Yesu alikuwa amewapa ishara, akisema, “Yule nitakayembusu, ndiye yeye. Mkamateni.”49Mara hiyo alikuja kwa Yesu na kusema, “Salamu, Mwalimu!” Na akambusu.

50Yesu akamwambia, “Rafiki, lifanye lile ambalo limekuleta.” Ndipo wakaja, na kumnyoshea mikono Yesu, na kumkamata.51Tazama, mtu mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu, alinyosha mkono wake, akachomoa upanga wake, na akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, na kumkata sikio lake.52Ndipo Yesu akamwambia, rudisha upanga wako pale ulipoutoa, kwa kuwa wote watumiao upanga wataangamizwa kwa upanga.53Mnadhani kuwa siwezi kumwita Baba yangu, naye akanitumia makundi ya majeshi zaidi ya kumi na mawili ya malaika?54Lakini basi jinsi gani maandiko yangeweza kutimizwa, hivi ndivyo inapasa kutokea?”

55Wakati huo Yesu akauambia umati, “Je! Mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi? Kila siku nilikaa hekaluni nikifundisha, na hamkunishika!56Lakini yote haya yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie.” Ndipo wanafunzi wake wakamwacha na kukimbia.

57Wale waliomkamata Yesu walimpeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, mahali ambapo waandishi na wazee walikuwa wamekusanyika pamoja.58Lakini Petro alimfuata nyuma kwa mbali hadi katika ukumbi wa Kuhani Mkuu. Aliingia ndani na kukaa pamoja na walinzi aone kitakachotokea.

59Basi wakuu wa makuhani na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu, kusudi wapate kumuua.60Ingawa walijitokeza mashahidi wengi, lakini hawakupata sababu yoyote. Baadaye mashahidi wawili walijitokeza mbele61na kusema, “Mtu huyu alisema, “Naweza kulivunja hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.”

62Kuhani Mkuu alisimama na kumwuliza, “Hauwezi kujibu? Hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?”63Lakini Yesu alikaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, “Kama Mungu aishivyo, nakuamuru utwambie, kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu.”

64Yesu akamjibu, “Wewe mwenyewe umesema jambo hilo. Lakini nakuambia, toka sasa na kuendelea utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wenye nguvu, na akija katika mawingu ya mbinguni.”

65Ndipo Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Je, twahitaji tena ushahidi wa nini? Angalia, tayari mmesikia akikufuru.66Je! Mnawaza nini? Wakajibu na kusema, “Anastahili kifo.”67Kisha walimtemea mate usoni na kumpiga ngumi, na kumchapa makofi kwa mikono yao,68na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo. Ni nani amekuchapa?”

69Wakati huo Petro alikuwa amekaa nje katika ukumbi, na mtumishi wa kike alimwendea na kusema, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

70Lakini alikana mbele yao wote, akisema, “Sijui kitu unachosema.”

71Alipoenda nje ya lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona na kuwaambia waliokuwepo hapo, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.”

72Akakana tena kwa kiapo, “Mimi simjui mtu huyu.”

73Muda mfupi baadaye, wale waliokuwa wamesimama karibu, walimwendea na kusema na Petro, “Kwa hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa kuwa hata lafudhi yako inaonesha.”

74Ndipo alianza kulaani na kuapa, “Mimi simfahamu mtu huyu,” na mara hiyo jogoo akawika.

75Petro alikumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.”


Mathayo 26 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Baadhi ya tafsiri zinaingiza nukuu kutoka kwa Agano la Kale. ULB inafanya hivyo kwa mistari iliyonukuliwa katika 26:31.

Dhana maalum katika sura hii

Kondoo

Hii ni taswira ya kawaida inayotumiwa katika Maandiko ya kutaja watu wa Israeli. Lakini, katika Mathayo 26:31, "kondoo" inawakilisha wanafunzi wa Yesu, ambao walikimbia wakati alikamatwa.

Pasaka

Kifo cha Yesu kilitokea kwa uhusiano na Sikukuu ya Pasaka kwa sababu yeye ndiye timizo la mwanakondoo wa Pasika. Ni kifo chake cha dhabihu ambacho kinatuokoa kutokana na hukumu ya Mungu.

Kula mwili na damu

Sherehe hii, ambayo mara nyingi huitwa "Meza ya Bwana," "Ekaristi", au "Ushirika Mtakatifu," hufanyika katika karibu makanisa yote hadi siku hii kwa ukumbusho wa dhabihu ya Kristo kwa ajili ya dhambi za binadamu. Hufanyika kwa kutii maagizo ya Yesu kwa wanafunzi wake katika Mathayo 26:26-28.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Aibu na woga

Kote katika sura hii, matendo ya viongozi wa Kiyahudi ni ya aibu na ya woga. Waliwaogopa watu waliopaswa kuwaongoza. Matendo yao ya aibu na ya uoga yanaweza kuwa vigumu kueleza katika kutafsiri.

Yuda kumbusu Yesu

Yuda amenakiliwa katika Mathayo 26:49 kumbusu Yesu ili kutoa ishara kwa askari ili kumtambua yule watakaomkamata. Miongoni mwa Wayahudi, kubusu ilikuwa njia ya kawaida ya kumsalimu mtu. Walikuwa na busu za aina mbalimbali kati ya watu wa tabaka mbalimbali. Kwa kuwa Yesu alikuwa mwalimu wa Yuda, labda alibusu mkono wake kama ishara ya heshima na utii.

"Haribu hekalu la Mungu"

Katika Mathayo 26:61, watu wawili wanamshtaki Yesu kwa kutaka hekalu la Yerusalemu liangamizwe ili aweze kulijenga kwa "siku tatu." Labda walikuwa wakimshtaki Yesu kwa kutukana hekalu na kwa hiyo, kwa njia nyingine, kumtukana Mungu. Mathayo hana rekodi ya Yesu akitamka haya, lakini maneno haya yapo katika Yohana 2:19.

Maneno "katika siku tatu" yanapaswa kueleweka kwa njia ya Kiyahudi kama "ndani ya siku tatu," wala sio "baada ya siku tatu."

Links:


Matthew 26:1

Maelezo kwa ujumla

Huu ni mwanzo wa sehehmu mpya wa simulizi amablao linaelezea kusulibiwa kwa Yesu, kufa na kufufuka. Hapa anawaeleza wanafunzi wake jinsi atakavyoteseka

Wakati Yesu alipomaliza

"kisha " au"baadaye"

Maneno haya yote.

Tazama 24:3

Mwana wa Adamu atatolewa ili asulibiwe.

"Baadhi ya watu watamtoa Mwana wa Adamu kwa watu wengine ambao watamsulibisha."

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia nafsi ya tatu kuongea juu yake

Matthew 26:3

Sentensi unganishi

Mstari huu unatoa historia ya mpango wa viongozi wa Wayahudi wa kumkamata na kumwua Yesu

walikutana pamoja

"walikutana"

Kwa siri.

"Bila kujulikana kwa wengi"

Siyo wakati wa sikukuu.

"Tusimuue Yesu wakati wa sikukuu"

Sikukuu.

Sikukuu ya kila mwaka ya Pasaka.

Matthew 26:6

Sentensi unganishi

Hii inaanza na habari ya mwanamke akimwaga manukato ya gharama kabla ya kifo cha Yesu

Wakati

Hil ni neno linalotumika kuazisha habari mpya. Mathayo anaanza kuelezea habari mpya

Simoni mkoma

Inamaanisha kuwa huyu ndiye mtu ambaye Yesu alimponya kwa ukoma

Alipokuw amejinyoosha.

"Yesu alikuwa amekaa upande wake". Unaweza kutumia neno la lugha yako kwa mkao wa watu ambavyo huwa wakati wa kula.

Mwanamke alimwendea.

Mwanamke alikuja kwa Yesu.

Mkebe wa alabasta.

chombo ambacho hugharimu sana kwa kukinunua kilicho tengenezwa na jiwe laini.

Mafuta

Mafuta ambayo yana harufu nzuri.

aliyamimina juu ya kichwa chake

Yule mwanamke alifanya hivi kuonesha heshima kwa Yesu

Ni nini sababu ya hasara hii.

"Mwanamke huyu amefanya jambo baya kwa kuharibu mafuta haya"

Haya yangeweza kuuzwa kwa thamani kubwa na kupew masikini

"angweza kuyauza kwa thamani kubwa ya pesa na kuitoa ile pesa

kupewa masikini

"kwa watu masikini"

Matthew 26:10

Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu?

"Hamkupaswa kumsumbua mwnamke huyu"

kwa nini mna

viwakilishi vyote vya "mna" viko katika wingi

masikini

"watu masikini"

Matthew 26:12

mafuta

Tazama 26:6

kweli nawaambia

"nawambia ukweli" huu ni msisitizo wa kile kilichofuata

popote injili hii itakapohubiriwa

"popote pale watu watakapohubiri injili hii"

kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka

"watakumbuka kile ambacho mwanamke huyu amefanya na wataambiwa wengine juu yake"

Matthew 26:14

Sentensi unganishi

Yuda Iskaariote anakubali kuwasaidia viongozi wa Wayahudi kumkamata na kumwua Yesu

Nikimsaliti

"kuwasaidia kumkamata Yesu."

Vipande therathini vya fedha.

Kwa kuwa maneno haya ni sawa na yale ya unabii katika Agano la Kale, endeleza muundo huu badala ya kuugeuza katika pesa ya leo.

Kumsaliti kwao.

"Kuwasaidia wakuu wa makuhani kumkamata Yesu."

vipande thelathini

"vipande 30"

Matthew 26:17

Sentensi unganishi

Hii inaazisha hanari y a Yesu akisherehekea Pasaka pamoja na wanafunzi wake

Sasa

Hili ni neno amablo limetumika kuonesha mwazo wa habari mpya. Matahyo anaanza kueleza sehemu mpya ya habari

Alisema , "nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni , 'Mwalimu anasema," Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako."''

"Aliwaambia wanafunzi wake kuingia mjini kwa mtu fulani na kumwambia kwamba Mwalimu anamwambia, 'Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu nyumbani mwako.'" au "Aliwaambia wanafunzi wake kwenda mjini kwa mtu fulani na kumweleza mtu huyo kwamba Mwalimu anasema muda wake umekaribia na atatimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wake katika nyumba ya mtu huyo."

Muda wangu.

Maana yake yaweza kuwa: 1) " Muda ambao niliwahi kuwajulisha" au 2 "Muda ambao Mungu amepanga kwa ajili yangu."

Umekaribia.

Maana yake yaweza kuwa: 1) "uko karibu" au 2) "Umefika."

Timiza Pasaka.

"Kula chakula cha Pasaka" au "sherekea sikukuu ya Pasaka kwa kula chakula maalum."

Matthew 26:20

Aliketi chini apate kula.

Tumia neno kwa mkao ambao watu katika utamaduni wako daima hukaa wakati wa kula.

kweli nawaambia

"Nawaambia ukweli." Huu ni msisitizo wa kile kilichofuata

Hakika siyo mimi, Bwana?

"Nina hakika mimi siye, Je, ni mimi?"

Matthew 26:23

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia nafsi ya tatu kuongea juu y ake mwenyewe

ataondoka

"akufa"

kama ilivyoandikwa

"kama vile manabii walivyoandika juu yake katika maandiko"

Mtu yule ambaye kwake Mwana wa Adamu asalitiwa.

"Mtu ambaye amsaliti Mwana wa Adamu."

Je, ni mimi Tabi?

"Rabi, kwa hakika si mimi nitakayekusaliti"

Umesema jambo hilo wewe mwenyewe

"wewe ndiye unayesema"

Matthew 26:26

Sentensi unganishi

Yesu anakula chakula na wanafunzi kwa kusherehekea Pasaka na wanafunzi wake

Alichukua... alibariki.

Tazama 14:19

Matthew 26:27

kutwaa au chukua.

Tazama14:19

kikombe

Kikombe kinamaanisha kikombe kikiwa na divai ndani yake

kunyweni

"kunywa divai kutoka kikombe hiki"

kwa kuwa hii ni damu yangu

"kwa kuwa hii divai ni damu yangu"

Damu ya agano.

"Damu ambayo huonesha kwamba agano linafanya kazi" au "damu ambayo hufanya agano liwezekane.

Inamwagwa.

"Inamwagwa kwa ajili ya kifo" au "hivi punde itachuruzika kutoka mwilini mwangu." au "itachuruzika kutoka katika majeraha yangu nitakapo kufa."

matunda ya mzabibu.

"mvinyo"

Lakini nawaambia

Hii inaongeza msisitzo

katika Ufalme wa Baba yangu.

Baba atakapoanzisha ufalme wake duniani "hapa"

wa baba yangu

Hiki ni cheo muhimu cha Mungu kinachoonesha uhusiano muhimu kati ya Mungu na Yesu.

Matthew 26:30

Sentensi unganishi

Yesu anaendelea kuwafundisha wanafunzi wake wakati wakielekea mlima wa Mizeituni

Maelezo kwa ujumla

Katika mstari wa 31, Yesu anamnukuu Nabii Zekaria kuonesha kuwa ili kutimiza unabii, wanaaafunzi wake wataondoka.

Wimbo.

Wimbo wa sifa kwa Mungu.

kujikwaa

"mtaniacha"

Kukataa.

"Kuniacha."

kwa kuwa imeandikwa

Kwa kuwa nabii zekaria aliandika tangu awali katika maandiko"

Nitampiga

kiwakilishi "ni" kinamaanisha Mungu. Inamaanisha kuwa Mungu atasababisha au kuruhusu watu kumwumiza na kumwua Yesu

mchungaji ... na kondoo wa kundi

Yesu na wanafunziwake

Kondoo wa kundi watatawanyika

"Watawatawanya kondoo wote wa kundi"

Baada ya kufufuka kwangu

"Baada ya Mungu kunifufua"

Matthew 26:33

Kukataa.

Tazama 26:30

kweli nakuambia

"Ninakuambia ukweli" Hiiinaongeza msisitizo wa kile kilichofuata baadaye

Kabla jogoo hajawika.

"Kabla jua halijachomoza."

Jogoo.

Ndege ambaye huwika kwa sauti kubwa karibu na majira ya jua kuchomoza.

Kuwika.

Sauti ambayo jogoo hufanya anapowika.

utanikana mara tatu

"utasema mara tatu kuwa wewe si mfuasi wangu"

Matthew 26:36

Sentensi unganishi

Hii inaazisha habariy a Yesu akiomba Gethsemane

na akaanza kuhuzuniaka

"na akawa na huzuni sana"

Roho yangu inahuzuni kubwa sana

Hapa roho inamaanisha nafsi nzima ya mtu. "Nina huzuni sana"

kiasi cha kufa

"Najihisi kama nataka kufa"

Matthew 26:39

Alianguka kifudifudi.

Kwa makusudi kuweka uso chini ili upate kuomba.

Baba yangu.

Hili ni jina maarufu la Mungu ambalo huonesha uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

KIkombe hiki kiniepuke.

Usemi huu, "kikombe hiki" huashiria mateso ambayo Yesu atapitia.

Hata hivyo, siyo kama nipendavyo, bali kama utakavyo.

Hii inaweza kuelezwa kama sentensi iliyo kamilika. "Lakini usifanye kile nitakacho bali kile utakacho."

akamwambia Petro, kwa nini hamkukesha

Yesu anamwambia Petro, kiwakilishai cha "hamku" ni cha wingi kinamaanisha Petro, Yakobo na Yohana.

kwa nini hamkuweza kukesha nami hata kwa saa moja?

"Ninasikitaka kuwa hamkuweza kukesha nami hata kwa saa moja"

msiingie katika majaribuni

"mtu yeyote asiwajaribu mtende dhambi"

Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu

Roho inamaanishahamu ya nafsi. Na "mwili" inamaanisha mwanadamu kamili. Yesu anamaanisha wanaweza kuwa na hamu ya kufanya mapenzi ya Mungu, Lakini kama wanadamu ni wadhaifu na wanaweza kushindwa

Matthew 26:42

Akaenda zake.

"Yesu alienda zake."

mara ya pili ... mara ya tatu

mpangilio kwa nafasi za namba

Nisipokinywea.

"Isipokuwa kukinywea kikombe hiki cha mateso."

Baba yangu.

Hili ni jina mashuhuri la Mungu ambalo hueleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

Macho yao yalikuwa mazito.

"Walikuwa wakisinzia- sinzia sana."

hili haliwezi kuepukika

"lazima nikinywee"

kama jambo hili

J"ambo hili" inamaanisha kikombe na kile kilichomo.

na ni lazima nikinywee

"lazima nikinywee" lazima nikinywee kikombe cha mateso"

mapenzi yako yatimizwe

"kile utakacho kifanyike"

macho yako yalikuwa mazito

"walikuwa na usingizi mzito"

Matthew 26:45

Bado mmelala tu na kijipumzisha

Ninasikitika kwamba bado mmelala na kupumzika"

Saa imekaribia.

"Muda umefika."

na Mwana wa Adamu anasalitiwa

"kuna mmoja wenu anamsaliti mwana wa Aadamu"

Mikono ya wenye dhambi.

Neno "mikono" linamaanisha mamlaka ya kutawala. "Watu wenye dhambi."

Tazameni

"Zingatia kile ambacho nataka kuwaambia."

Matthew 26:47

Sentensi unganishi

Hii inaazisha habari ya Yuda wakati alipomsaliti Yesu na viongozi wa dini wakamkamata

Wakati alipokuwa bado akiongea.

"Wakati Yesu alipokuwa bado akiongea."

marungu

vipande vikubwa vya miti vya kupigia watu

Sasa ... mkamateni

Neno "sasa" linaonesha kuanza kwa habari mpya. Mathayo anaeleza jinsi Yuda atakavyotoa ishara atakayotoa kwa nia ya kumsaliti.

Akisema, "Yule nitakaye mbusu, ndiye yeye. Mkamateni."

"Akasema kwamba yule aliye mbusu ndiye waliyepaswa kumkamata."

Huyo nitakaye mbusu.

"Yule nitakaye mbusu" au "Mtu ambaye nita mbusu."

Busu.

Namna ya heshima ya kumsalimia mwalimu wa mtu mwingine.

Matthew 26:49

alikuja kwaYesu.

"Yuda alimtokea Yesu."

Alimbusu.

"Akakutana naye kwa kumbusu."

ndipo wakaja

"Kiwakilishi "waka.." kinamaanisha wale watu waliokuja na Yuda wakiwaa na marungu na mapanga pamoja na viongozi wa dini

Wakamnyooshea Yesu mikono.

Wakamkamata Yesu"

Matthew 26:51

Tazama.

Neno "tazama" linatuvuta usikivu kwa ajili ya taarifa ya kugusa inayofuatia.

alichomoa upanga

"aliyechukua upanga ili aue wengine"

wataangamizwa kwa upanga

"watakufa kwa njia ya upanga" au "mtu atawaua kwa upanga"

Mnadhani kuwa siwezi kumwita Baba, na angenitumia zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?

"Mlipaswa kujua kwamba ningeweza kumwita Baba yangu, na angenitumia majeshi zaidi ya kumi na mawili ya malaika."

mnadhani

hapa "mna" neno la umoja linlomaanisha yule mtu aliye na upanaga.

Baba yangu.

Hili ni jina mashuhuri la Mungu ambalo hueleza uhusiano kati ya Mungu na Yesu.

Majeshi ya malaika zaidi ya kumi na mawili.

Neno "jeshi" ni neno la kijeshi linalojumuisha wanajeshi 6,000. Yesu anamaanisha kuwa Mungu angeweza kutuma malaika wa kutosha kuwazuia wale waliokuwa wanamkamata. Zaidi ya makundi 12 ya malaika.

lakini bai jinsi gani maandiko yangeweza kutimizwa, hivi ndivyo ilipswa kutoka

"Lakini kama nkifanya hivyo, nisingeweza kutimiza,kile Mungu alichosema kwenye maandiko kitokee"

Matthew 26:55

Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi?

"Mnajua kwamba mimi siyo mnyang'anyi, hivyo ni makosa yenu kuniijia mkiwa na mapanga na marungu.

Marungu.

Vipande vikubwa vya miti migumu kwa ajili ya kupigia watu.hekaluni

hekaluni

Inaoneshakuwa Yesu hakuwa hekaluni. alikuwa kwenye korido la hekalu

ili maandiko ya manabii yatimie

"napenda kutimiza kile ambacho manabii waliandika kwenye maandiko"

Kumuacha.

Kujitenga naye au walijitenga naye.

Matthew 26:57

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya majaribu ya Yesu kwenye baraza la viongozi wa dini ya Wayahudi

Petro alimfuata

"Petro alimfuata Yesu

Ukumbi wa Kuhani Mkuu.

Sehemu ya uwazi karibu na nyumba ya Kuhani Mkuu.

Aliingia ndani

"Petro aliingia ndani"

Matthew 26:59

Sasa

Hili neno linaonesha kuazisha habari mpya kwenye simulizi. Matahyo anaanza kueleza habari mpya ya simulizi

kusudi wapate

kiwakilisi "wa" kinamaanisha wale wakuu wa Makuhani na wale wajumbe wa baraza.

Wawili walitokeza mbele.

"Wanaume wawili walikuja mbele" au "mashahidi wawili walitokeza mbele."

Walisema, "Mtu huyu alisema, 'Ninaweza kuliharibu hekalu la Mungu na kulijenga upya kwa siku tatu.'"

"Walishuhudia kwamba walimsikia Yesu akisema angeweza kuvunja hekalu la Mungu na kulijenga upya kwa muda wa siku tatu."

Mtu huyu alisema.

"Mtu huyu Yesu alisema."

Matthew 26:62

hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?

"unajibu nini juu ya ushuhuda huu dhidi yako?"

Mwana wa Mungu.

Hili ni jina mashuhuri ambalo hueleza uhusiano kati ya Kristo na Mungu.

Mungu aishivyo

Tazama 16:13

Umesema jambo hilo wewe mwenyewe.

Yesu anathibitisha kwamba yeye "ndiye Kristo, Mwana wa Mungu. "Kama ulivyosema, Mimi ndiye" au "Umekubaliana na ukweli huo"

Lakini nakuambia, tangu sasa na kuendelea

Neno "wewe" ni la wingi. Yesu anamwambia kuhani mkuu na kwa wengine waliokuwapo hapo.

Tangu sasa na kuendelea mtamwona Mwana wa Adamu.

Maana zinaweza kuwa: 1) Watamuona Mwana wa Adamu baadaye kwa wakati ujao au 2) kwa "sasa" Yesu anamaanisha wakati wa kifo chake, kule kurudi kwake kutoka kwa wafu, na kupaa kwake kwenda mbinguni.

Mwana wa Adamu

Yesu anatumia nafsi ya tatu kuongea juu yake

Upande wa mkono wa kulia wenye nguvu.

"Upande wa mkono wa kulia wa Mungu mwenyezi"

Akija katika mawingu ya mbinguni.

"Akisafiri kuja duniani katika mawingu ya mbinguni."

Matthew 26:65

Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake.

Kuchana mavazi ilikuwa ni ishara ya huzuni na hasira.

amekufuru

kwa kufuru hii, inamaanisha kuwa Yesu alikuwa akidai kuwa yeye ni sawa na Mungu

Je, twahitaji tena ushahidi?

"hatuhitaji kusikia ushahidi mwingine"

Tayari mmesikia

kiwakilishi cha "mme" kikokatika wingi kinamaanisha wajumbe wa baraza.

Matthew 26:67

Kisha wali

Maana yaweza kuwa: "Kisha baadhi ya watu" au "Kisha askari"

Walimtemea usoni.

Hili ni tendo la kufedhehesha.

Tutabirie.

Hapa "tutabirie" humaanisha, "tuambie kwa kutumia uwezo wa Mungu." Haimaanishi, "tuambie kitu gani kitatokea kwa wakati ujao."

Wewe Kristo

Wale waliokuwa wakimpiga Yesu. Walimwita kwa kumdhihaki

Matthew 26:69

Sentensi unganishi

Hii ni habri ya Petro akimkana mara tatu kuwa anamjua Yesu, kama vile Yesu alivypkuwa amaesema kuwa atafanya.

Maelezo kwa ujumla

Matukio haya yanatokea sambamba na majaribu ya Yesu kwa viongozi wa dini

Wakati huo

Hili neno linaonesha kuanza kwa habari nyingine. Mathayo anaanza kuwaambia sehemu ya habari.

Sijui kile unachosema.

Petro aliweza kufahamu alichosema mjakazi. Alitumia maneno haya kukana kwamba alikuwa pamoja na Yesu.

Matthew 26:71

Alipo...

"Petro alipo..."

Lango.

Uwazi katika ukuta kwenye ukumbi.

Akakana tena kwa kiapo, "mimi sim"jui mtu huyu

"akakana tena na kusema, 'Naapa simjui mtu huyu'"

Matthew 26:73

Mmoja wao.

"Mmoja wa hao waliokuwa pamoja na Yesu."

Kwa kuwa rafudhi yako huonesha.

"Tunaweza kukuambia kwamba unatoka Galilaya kwa sababu unaongea kama Mgalilaya."

kulaani.

"Kujitakia laana iwe juu yake mwenyewe."

jogoo akawika

Tazama 26:33

Petro alikumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, "kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu."

Ptro alikumbuka kuwa Yesu alikuwa amemwambia kuwa kabla jogoo hajawika atakuwa amemkana mara tatu"


Translation Questions

Matthew 26:1

Ni sikukuu gani ya Wayahudi ambayo yesu alisema ingetokea baada ya siku mbili.

Yesu alisema Pasaka ilikuwa inawadia baada ya siku mbili.

Matthew 26:3

Wale wakuu wa Makuhani na wazee walikuwa wanapanga njama gani katika makao makuu ya kuhani mkuu?

Walikuwa wanapanga kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.

Wale wakuu wa makuhani na wazee walikuwa wanaogopa nini?

Walikuwa wanaogopa kumwua Yesu wakati wa Pasaka kwa hofu ya watu wasije kuzua ghasia.

Matthew 26:6

Mwanamke alipomimina mafuta yenye thamani juu ya kichwa cha Yesu mwitikio wa wanafunzi wake ulikuwaje?

Wanafunzi walikasirika na walitaka kujua kwa nini mafuta yasingeuzwa na pesa zake wakapewa maskini.

Mwanamke alipomimina mafuta yenye thamani juu ya kichwa cha Yesu mwitikio wa wanafunzi wake ulikuwaje?

Wanafunzi walikasirika na walitaka kujua kwa nini mafuta yasingeuzwa na pesa zake wakapewa maskini.

Matthew 26:12

Yesu alisema sababu gani ilimfanya mwanamke amimine mafuta juu yake?

Yesu alisema mwanamke alimimina mafuta juu yake kwa ajili ya maziko yake.

Matthew 26:14

Yuda Iskariote alilipwa nini ili kumkabidhi Yesu katika mikono ya wakuu wa makuhani?

Yuda alilipwa vipande thelathini vya fedha ili kumkabidhi Yesu katika mikono ya wakuu wa makuhani.

Yuda Iskariote alilipwa nini ili kumkabidhi Yesu katika mikono ya wakuu wa makuhani?

Yuda alilipwa vipande thelathini vya fedha ili kumkabidhi Yesu katika mikono ya wakuu wa makuhani.

Matthew 26:20

Yesu alisema nini kwenye chakula cha jionni juu mwanafunzi wake mmoja?

Yesu alisema kuwa mmoja wa wanafunzi wake angemsaliti.

Matthew 26:23

Yesu alisemaje juu ya maisha ya baadaye ya yule ambaye atamsaliti?

Yesu alisema kuwa ingekuwaafadhali kwa mtu atakayemasaliti kama asingezaliwa.

Je, Yesu alimjibuje Yuda alipomwuliza kuwa kama ni yeye ambaye atamsaliti.?

Yesu alisema "wewe wasema"

Matthew 26:26

Yesu alisema nini alipochukua mkate, akaubariki,akauvunja, na kuwapa wanafunzi?

Yesu alisema, "Twaeni, mle. Huu ni mwili wangu."

Matthew 26:27

Yesu alisema nini juu ya kikombe na kisha kuwapa wanafunzi?

Yesu alisema kuwa kile kikombe ni damu yake ya agano ambayo inamwagwa kwa ajili ya wengi kwamsamaha wa dhambi.

Matthew 26:30

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wote kuwa wangefanya nini usiku ule katika Mlima wa Mizeituni?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kwamba wote wangetawanyika usiku ule kwa sababu yake.

Yesu aliwaambia wanafunzi wake wote kuwa wangefanya nini usiku ule katika Mlima wa Mizeituni?

Yesu aliwote wangetawanyika usiku ule kwa sababu yake.waambia wanafunzi wake kwamba

Matthew 26:33

Petro alisema asingemuacha kamwe, je, Yesu alimwambia angefanya nini usiku ule?

Yesu alisema kwamba Petro angemkana Yesu usiku ule mara tatu kabla jogoo hajawika.

Petro alisema asingemuacha kamwe, je, Yesu alimwambia angefanya nini usiku ule?

Yesu alisema kwamba Petro angemkana Yesu usiku ule mara tatu kabla jogoo hajawika.

Matthew 26:36

Yesua limwambia nini Petro na wale wawili wa Zebedayo wakati anaomba?

Yesu aliwaambia kaeni hapa na kukusha naye.

Yesua limwambia nini Petro na wale wawili wa Zebedayo wakati anaomba?

Yesu aliwaambia kaeni hapa na kukusha naye.

Matthew 26:39

Ni ombi gani alilofanya Yesu kwa Baba katika sala yake?

Yesu aliomba kwamba, kama ingewezekana kikombe hiki kimwepuke.

Yesu aliporudi toka kwenye maombi aliwakuta wanafunzi wanafanya nini?

Wanafunzi walikuwa wamesinzia Yesu aliporudi toka kwenye maombi

Matthew 26:42

Yesu aliomba nini kitimia, ambacho si kwa mapenzi yake?

Yesu aliomba kwamba mapenzi ya Baba yatimie, kuliko mapenzi yake mwenyewe.

Ni mara ngapi Yesu aliwaacha wanafunzi wake akaenda kuomba?

Yesu aliwaacha wanafunzi wake mara tatu naye akaenda kuomba

Ni mara ngapi Yesu aliwaacha wanafunzi wake akaenda kuomba?

Yesu aliwaacha wanafunzi wake mara tatu naye akaenda kuomba

Matthew 26:45

Wanafunzi walikuwa wakifanya nini wakati Yesu akirudi kutoka maombini?

Wanafunzi walikuwa wamesinzia wakati Yesu akirudi kutoka maombini.

Matthew 26:47

Yuda aliwapa kikosi ishara gani ya kumtambua Yesu kuwa ndiye wa kukamatwa?

Yuda alimbusu kama ishara kwa kikosi kwamba Yesu ndiye wa kukamatwa.

Yuda aliwapa kikosi ishara gani ya kumtambua Yesu kuwa ndiye wa kukamatwa?

Yuda alimbusu kama ishara kwa kikosi kwamba Yesu ndiye wa kukamatwa.

Matthew 26:51

Je, mmoja wa wanafunziwa wa Yesu alifanya nini Yesu alipokamatwa?

Mmoja wa wanafunzi wa Yesu alichomoa upanga wake na kumkata sikio mtumishi wa Kuhani Mkuu.

Yesu aliseam angefanya nini kama angetaka kujihami?

Mmoja wa wanafunzi wa Yesu alifuta upanga wake na kumkata sikio mtumishi wa kuhani mkuu.

Yesu alisema kitu gani kilichokuwa kinatimilika kutokana na matukio hayo?

Yesu alisema kuwa maandiko yalikuwa yanatimizwa kwa matukio hayo

Matthew 26:55

Je, wanafunzi wote walifanya nini?

Wanafunzi wote walimwacha na kukimbia

Matthew 26:59

Kwa sababu gani wakuu wa makuhani na baraza zima walitafuta ili kumuua Yesu?

Walikuwa wakitafuta ushahidi wa uongo dhidi ya yake ili kumuua Yesu.

Matthew 26:62

Ni amri gani ambayo kuhani mkuu alimwamuru Yesu kama Mungu aishivyo?

Kuhani mkuu alimwamuru Yesu asema kama yeye ndiye Kristo, Mwana wa Mungu

Yesu alimjibuje kuhani mkuu kwa amri yake?

Yesu alisema "wewe wasema"

Yesu alisema nini ambacho kuhan mkuui atakiona?

Yesu alimwambia kuhani mkuu atamwona Mwana wa Adamu amekaa mkono wa kuume wa mamlaka, na akija katika mawingu ya mbinguni.

Matthew 26:65

Ni mashitaka gani ambayo Kuhani Mkuu aliyafanya dhidi ya Yesu?

Kuhani Mkuu alimshitaki Yesu kwa kosa la kukufuru.

Matthew 26:67

Walimfanyia nini Yesu baada ya kuwa wamemkamta?

Walimtemea Yesu usoni, wakampiga, na kumchapa makofi kwa mikono yao.

Matthew 26:73

Petro alijibu mara tatu jibu gani kwa swali amabalo mtu alimwuliza kama na yeye alikuwa na Yesu?

Petro alijibu kuwa hakumfahamu Yesu

Kilitokea nini baada ya Petro kujibu ile mara ya tutu?

Baada tu ya Petro kujibu mara ya tatu, jogoo aliwika.

Petro alijibu mara tatu jibu gani kwa swali amabalo mtu alimwuliza kama na yeye alikuwa na Yesu?

Petro alijibu kuwa hakumfahamu Yesu

Je, Petro alikumbuka nini baada ya jibu lake la tatu?

Petro alikumbuka kuwa Yesu alikuwa amesema kuwa, kabala jogoo hajawika atakuwa amemkana mara tatu..


27

1Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.2Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.

3Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,4na akasema, “Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini wakajibu, “Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe.”5Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.

6Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, “Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu.”7Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.8Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, “Shamba la damu” hadi leo hii.

9Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, “Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,10na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza.”

11Sasa Yesu alisimama mbele ya Liwali, na Liwali akamwuliza, “Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu alimjibu, “Wewe wasema hivyo.”

12Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.

13Kisha Pilato akamwambia, “Hujayasikia haya mashitaka yote dhidi yako?”14Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo Liwali alijawa na mshangao.

15Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya Liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.16Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.

17Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, “Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?” Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?”18Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.

19Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”

20Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.21Liwali aliwauliza, “Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?” Walisema, “Baraba.”

22Pilato akawaambia, “Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?” Wote wakajibu, “Msulibishe”23Naye akasema, “Kwa nini, ni kosa gani ametenda?” Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, “Msulibishe.”

24Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, “Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe.”

25Watu wote wakasema, “Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu.”26Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.

27Kisha askari wa Liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakakusanyishwa.28Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.29Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeli, wakisema, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi?”30Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.31Wakati walipokuwa wakimkejeli, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.

32Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.33Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, ‘Eneo la fuvu la Kichwa.’34Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.35Wakati walipokuwa wamemsulubisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.36Na waliketi na kumwangalia.37Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, “Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi.”38Wanyang'anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.39Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao40na kusema, “Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!”

41Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,42“Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.43Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’”44Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulubiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.

45Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.46Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”47Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.”48Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.

49Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”50Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.51Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.52Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.53Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.

54Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

55Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.56Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo

57Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.58Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.59Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na sanda ya sufi safi,60na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.61Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.

62Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.63Wakamwambia, “Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, ‘Baada ya siku tatu atafufuka tena.’64Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu.’ Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”

65Pilato akawaambia, “Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo.”66Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.


Mathayo 27 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Walimpeleka kwa gavana Pilato"

Wayahudi walikuwa chini ya utawala wa Ufalme wa Kirumi, na Warumi hawakuwaruhusu watoe uhai wa mhalifu yeyote bila kupata ruhusa kwanza. Kwa hivyo viongozi wa Kiyahudi walimuomba Pontio Pilato athibitishe hukumu yao juu ya Yesu. Pilato alijaribu kuepuka kuthibitisha uamuzi wao. Alijaribu kuwafanya viongozi wa Kiyahudi kuchagua kati ya kumkomboa Yesu au mfungwa mbaya sana aliyeitwa Baraba.

Kaburi

Kaburi ambamo Yesu alizikwa (tazama: Mathayo 27:59-60) ilikuwa ni aina ya kaburi ambamo Wayahudi tajiri walizikwa. Ilikuwa na chumba halisi ambacho kilichombwa kwenye mwamba, ambapo miili ilikuwa imefungwa na kuwekwa kwenye miamba ilivyokuwa kwenye kuta. Baadaye, wakati miili imeharibika na kubakia mifupa iliyo wazi, mifupa hiyo ilikusanywa na kuingizwa kwenye mitungi maalum inayoitwa mabasi. Makaburi hayo yalifungwa na mwamba mmoja mkubwa wa kutosha kuufunga mlango. Mwamba huu ulikuwa umevingirwa au kuwekwa mahali pa mlango mwa kaburi.

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

"Shikamoo, Mfalme wa Wayahudi!"

Kifungu hiki, kinachopatikana katika Mathayo 27:29, ni mfano wa kinaya. Katika takwimu hii ya matamshi, kitu kinasemwa ili kuashiria kitu kingine, mara nyingi maana yake ikiwa ni kinyume. Tamko "Shikamoo" ilikuwa salamu iliyotumiwa na watu nyakati maalum, mara nyingi mbele ya wafalme na malkia. Hata hivyo, askari waliomdhihaki Yesu hawakutaka kumheshimu.

Links:


Matthew 27:1

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha kujariwa kwa Yesu mbele ya Pilato

Muda wa asubuhi

neno linamaanisha kuazisha habari mpyakataika simulizi. Matahyo anaanza kueleza habari mpya katika sehemu hii

walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua

Viongozi wa Wayahudi walikuwa wakipanga jinsi ya kuwashawishi viongozi wa Rumi jinsi ya kumuua Yesu

walimwongoza

"walimkabidhi" au "walimpeleka"

Matthew 27:3

Sentensi unganishi

Mwanadishi amekoma kueleza habari ya kuhojiwa kwa Yesu na anaeleza jinsi Yuda alivyojiua

Maelezo kwa ujumla

Tukio hili limeanza baada ya Yesu kuhojiwa mbele ya baraza la viongozi wa Wayahudi, lakinni hatujui kama hii ilitokea baada au kabla ya mahojiano ya Yesu kwa Pilato

Kisha wakati Yuda

Kama lugha yako ina namna ya kuonesha habari mpya inapoanza, unaweza kuitumia hapa.

Yesu amaekwisha kuhukumiwa

"Viongozi wa Wayahudi wameshamhukumu Yesu"

vipande thelathini vya fedha

Tazam 26:14

damu isiyo na hatia

"mtu ambaye hakustahili kufa"

inatuhusu nini?

"hilo siyo tatizo letu" au "hilo ni tatizo lako"

alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu"

Hii inamaanisha 1) alivitupa vile vipande vya fedha akiwa kwenye korido la hekalu, au 2) alikuwa amesimama kwenye korido la hekalu na akavitupa vile vipande vya fedha hekaluni.

Matthew 27:6

si halali kuiweka fedha hii

"Sheria zetu hazituruhusu kuiweka hii"

Kuiweka hii

"kuiweka fedha hii"

hazina

ahaili ni eneo ambalo waliweka ile fedha waliyotumia kwa mahitaji ya hekaluni nakwa makuhani.

gharama ya damu

Hii ni nahau inayomaanisha pesa i;iyotumika kumlipa mtu aliyeua mtu. "Pesa iliyolipwa kwa ajili ya kuuawa kwa mtu"

shamba la mfinyanzi

Hili n ishamba ambalo lilikuwa limenunuliwa kwa ajili ya kuwazikia wageni waliofia Yerusalemu

hilo shamba limekuwa likiitwa

"watu huliita shamba hilo"

hadi leo hii

Hadi wakati ambao Mathayo alikuwa anaandika kitabu hiki.

Matthew 27:9

Maelezo kwa ujumla

Mwandishi ananukuu toka maandiko ya Agano Jipya kuonesha kuwa kujinyonga kwa Yuda kulikuwa kutimiza unabii

Kisha lile neno lililokuwa limenwa na nabii Yeremia litimie

"Hili liltimiza unabii ambao nabii Yeremia alisema"

gharama iliyopngwa na watu wa Israel

"Gharama ambayo watu wa Isrel walimpngia"

watu wa Israel

Hii inamaanisha baadhi ya watu wa Isrel waliolipa ili Yesu auawe. "baadhi ya watu wa Israel" au "viongozi wa Israel"

alivyokuwa amenielekeza

kiwakilishi "ni" kinamaanisha Yeremia

Matthew 27:11

Senteni unganishi

Ni habari inayoanzi 27:1

Sasa

Kama lugha yako ina maneno yanyotumika kuendeleza mazungumzo baada ya pumziko la hadithi kubwa, waweza kuyatumia hapa

liwali

"Pilato"

wewe wasema hivyo

Hii ni nahau ambayo Yesu anatumia kumaanisha "ndiyo" lenye lengo lakumaanisha kutoweka wazi alichokuwa anasema "wewe ndiye unayesema" au "unaonesha kukiri"

wakati aliposhitakiwa na wakuu wa Makuhani na wazee

"Lakini wakati wakuu wa makuhani na wazee walipomshitaki"

Hyasikii mashaitaka yote dhidi yako?

Pilatoanauliza swali kwa sababu anashangazwa na ukimya wa Yewsu. "Ninashangazwa kwamba huwajibu hawa watu wanokushitaki kwa kutenda mabaya"

neno moja, hivyo liwali alijawa na mshangao

"neno moja; hii ilimshangaza sana liwali"

Matthew 27:15

Sasa

Hili ni neno linalotumika kuosha mwanzo wa habari kuu ili kwamba mwandishi aweze kutoa taarifa za kumsaidia msomaji kinachotokea kuanzia 27:17

Sikukuu

Hii ni sikuu ya kusherehekea Pasaka

mfungw mmoja anayechaguliwa na umati

"mfungwa ambaye umati utamchagua"

walikuwa na mfungwa sugu

"kulikuwa na funwa sugu"

sugu

anayejulikan vizuri kwa kutenda makosa makubwa

Matthew 27:17

walipokiuwa wamekusanyika

"umati ulikuwa umekusanyika"

Yesu anayeitwa Kristo

ambaye watu baadhi humwita Kristo

wamekwisha kumkamata Yesu

viongozi wa Wayahudi walikuwa wamemleta Yesu kwake. "walifanya haya ili kwamba Pilato amhukumu Yesu.

alipokuwa akiketi

"Pilato alopokuwa ameketi"

alipokuwa akiketi kwenye kti chake cha hukumu"

"Kuketi kwenye kiti cha hakimu." Hapa ndipo hakimu huketi anapokuwa akifanya maamuzi.

alimtumia neno

"neno" inamaanisha ujumbe. "alituma ujumbe"

leo nimeteswa mno

"Nimeteseka san leo"

Matthew 27:20

Ndipo ... Yesu auawe

Neno "ndipo" limetumika kumaanisha mwanzo wa habari. Yesu anaeleza kwa nini umati ulimchagua Baraba.

Yesu auawe

Askari wa Rumi wamuue Yesu"

aliwauliza

"aliuliza umati"

anayeitwa Kristo

"ambaye watu baadhi humwita Kristo"

Matthew 27:23

ametenda

"ambalo Yesu ametenda"

walipaza sauti

"walipiga kelele"

akanawa mikono yake mbele ya umati

Pilato alifanya hivi kama ishara ya kuwa yeye hawajibiki kwa kifo cha Yesu

damu

"damu" inamaanisha damu ya mtu "kifo"

yaangalieni haya wenyewe

"huu ni wajibu wenu"

Matthew 27:25

Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu

damu inamaanisha kifo cha mtu. Kirqai cha "iwe juu yetu na watoto wetu" ni nahau inayomaanisha kuwa wanakubali kuajibika kwa kile kinachotokea. "Ndiyo! Sisi na wa watoto wetu tutaajibika kwa kifo cha Yesu"

alimpiga mijeredi

Maaskari wa Pilato walimpiga mijeredi Yesu.

kupiga mijeredi

kumpiga mtu kwa kutumia mjeredi

Kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa

"na Pilato akaamuru Yesu asulibiwe"

Matthew 27:27

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya kusulibiwa kwa Yesu

kundi kubwa la maaskari

"kikosi cha maaskari

wakamvua

"kumvulisha nguo"

nyekundu

"nyekundu yenye mng'ao

taji ya miiba

"taji iliyotengenezwa kwa matawi ya miiba" au "taji ilitengenezwa ka matawi yalyo na miiba"

mwanzi katika mkono wake wa kuume

Walimpa Yesu ashikilie fimbo kuonesha kuwa wafalme hushilia fimboya enzi. walifanya hivi kumkejeli.

salalmu mfalme wa Wayahudi

walisema hivi kumkejeliYesu. walikuwa wakimwita Yesu "mfalme, wa Wayahudi," lakini kwa hakika hawakuamini kuwa Yesu alikuwa mfalme. Lakini walichokuwa wakisema kilikuwa kweli.

Matthew 27:30

walimtemea mate

"maaskari walimtemea Yesu"

Matthew 27:32

Walipotoka nje

Hii inamaanisha Yesu na maaskari walitoka nje ya mji, "walipokuwa wakitoka nje ya Yerusalaem"

walimwonamtu

"maaskari walimwona mtu"

ambaye walimulazimisha kwenda nao ili apate kubeba msalaba wake

"amabye maaskari walimlazimisha kwenda naye ili kwamba abebe msalaba wa Yesu"

mahali paitwapo fuvu la kichwa

"eneo ambalo watu waliliita Golgotha"

Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo.

"walimpa siki, ambayo walikuwa wameichanganya na nyongo"

siki

kinwaji kichungu cha njano ambacho miili hukitumia kwa mmeng'enyo wa chakula

Matthew 27:35

mavazi

Hili ni vazi ambalo Yesu alikuwa akilivaa

Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake

"mashitaka" inamaanisha waliandika ili kuonesha sababu za kumsulibisha Yesu

Matthew 27:38

wanyang'anyi wawili walisulibishwa pamoja naye

Maskari walimsulibishaYesu pamoja na wanyanga'nyi wawili

wakitikisa vichwa vyao

walifanya hivi kumcheka Yesu

Kama nia mwana wa Mungu shuka chini

Kama wewe ni mwana wa Mungu thibitisha kwa "kushuka msalabani"

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo cha muhimu amabcho kinaonesha uhusiano kati ya Kristo na Mwanawa Mungu

Matthew 27:41

Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe

Maana yake yaweza kuwa 1) viongozi wa Wayahudi hawakuamini kuwa Yesu aliwaokoa wengine au kwamba anaweza kujiokoa wenyewe au 2) waliamini kuwa Yesu aliwaokoa wengine na sasa wanamcheka kwa sababu sasa hawezi kujiokoa mwenyewe

yeye ni mfalme

Viongozi wanamkejeli Yesu. Wanamwita "Mfalme wa Israel," Lakini kwa uhalisia hawaamini kuwa yeye ni Mfalme. "Anasema kuwa yeye ni mfalme wa Israel"

Matthew 27:43

Sentensi unganishi

Viongozi wa Wayahudi wanaendelea kumkejeli Yesu

Kwa sababu alisema, 'Mimi ni Mwana wa Mungu.'

"Kwa sababu Yesu alisema kuwa yeye ni Mwana wa Mungu"

Mwana wa Mungu

Hiki ni cheo cha maalumu cha Yesu ambacho kinaelezea uhusiano na Mungu

Na wale wanyang.nyi waliokuwa wamesulibiwa pamoja naye

"Na wale wanyanga'nyi ambao maaskari waliwasulibisha pamoja na Yesu"

Matthew 27:45

Sasa

Neno hili limetumika kuonesha kuanza kwa habari nyingine. Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya habari

kutoka saa ya sita ... hadi saa tisa

Kuanzia mnamo adhuhuri ... kwa muda wa saa tatu" au "kuazia mnamo muda wa saa sita mchana ... hadi mnamo muda wa saa tisa mchana"

kulikuwa na giza katika nchi yote

Neno "giza" ni nomino. "ilikuwa giza nchi yote"

Yesu akalia

"Yesu akaita" au "Yesu alipiga kelele"

Eloi. Eloi. lamathabakithani

Haya ndiyo maneno amabyo Yesu aliita kwa sauti kuu katika lugha ya.ke

Matthew 27:48

mmoja wao

inaweza kumaanisha 1)mmoja wa maaskari au 2) mmoja wale waliokuwa wamesimama karibu wakitazama

sifingo

Huyu ni mnyama wa majini ambaye anapokuwa amevuliwa lile ganda lake liliweza kutumika kwa kuwekea vitu kama maji na kinywaji ambacho kinaweza kusukumwa nje.

na kumpa

"akampa Yeu

akaitoa nafsi yake

"akafa akiitoa roho yake kwa Mungu" au "akapumua pumzi ya mwisho"

Matthew 27:51

Sentensi unganishi

Hii inaanza na matukio ambayo yalitokea baada ya Yesu kufa

Tazama

Neno "tazama" linatutaka kuwa makini kwa taarifa za kushangaza zinazofuata.

pazia la hekalu lilipasuka

"lile pazia la hekaluni lilipasuka katika sehamu mbili" au "Mungu alilifanya pazia la hekalu ligawanyike mara mbili"

Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.

"Mungu alifunua makaburi na kuifufua miili ya watu wengi wa Mungu waliokuwa wamekufa"

wamelala usingizi

Hii ni tafsida yenye maana ya kufa "waliokuwa wamekufa"

Makaburiyalifunuka ... na walionekana kwa wengi

Mpangilio wa matukio haya hauko wazi sana. Baada ya tetemeko la ardhi wakati Yesu alipokufa na makaburi kufunuka 1)Watu watakatifu walikuwa hai tena, kisha baada ya Yesu kufufuka, watakatifu wakauingi mji wa Yerusalemu na watu wengi waliwaona, au 2)Yesu alifufuka, kisha watakatifu nao wakafufuka na kuuingia mji ambapo watu wengi waliwaona.

Matthew 27:54

Basi

Hili neno limetumika kuonesha mwanzo wa habari mpya. Mathayo anaaza kueleza sehemu nyingine ya habari

na wale ambao walikuwa wakimtazama

"na wale maaskari waliokuwa wakimtazama Yesu"

Mwana waMungu

Hiki ni cheo maalumucha Yesu kinachoonesh uhusiano na Mungu

mama wa watoto wa Zebedayo

"Mama wa Yohana na Yakobo" au "mke wa Zebedayo"

Matthew 27:57

Sentensi unganishi

Hii inaanza na habari ya kuzikwa Kwa Yessu

Arimathayo

Hili jina la mji ulioko Israel

Pilato aliagiza apate kupewa

"Pilato aliwaagiza maaskari kumpa Yusufu mwili wa Yesu"

Matthew 27:59

sufi safi

Nguo laini ya thamani

aliliokuwa amelichonga mwambani

Inamaanisha kuwa Yusufu aliajiri watu ambao waliochonga hilo akaburi

akavingirisha jiwe kubwa

Yawekana Yusufu alikuwa na watu wengine pale waliomsaidia kulivingirisha lile jiwe

kuelekea kaburi

"karibu na kaburi"

Matthew 27:62

maandalio

Hii ni siku ambayyo watu waliandaa mabo yao kwa sababu ya sabato

walikusanyika pamoja kwaPilato

"walikutana na Pilato"

yule mdanganyifu alipokuwa hai

"wakati mdanganyifuYesu alipokuwa hai"

alisema, 'baada ya siku tatu atafufuka tena.'

"alisema kwamba baada ya siku tatu atafufuka tena"

agiza kwamba kaburi lilindwe salama

"waagize maaskari wako kulilinda kaburi"

siku ya tatu

siku ya 3

kumuiba

"kuiba mwili wake"

na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.'

"na kuwaambia watu kwamba amefufuka kutoka wafu"

Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko wa kwanza

"kama watawadanganya watu kwa kusema hivyo, itakuwa vibaya kuliko alivyowadanganya watu kwa kusema kuwa yeye ni Kristo"

Matthew 27:65

walinzi

kwa Warumi Ilimaanisha maaskari wanne hadi kumi na sita

jiwe liligongwa muhuri

Inaweza kumaanisha 1) waliweka kamba karibu na jiwe na kuliunganishana kuta za lile jiwe katika pande zote za lango la kaburi au 2) waliweka mihuri katkati ya jiwe na kuta

na kuweka walinzi

"kuwaambia walinzi wasimame mahali ambapo wataweza kuwazuia watu ambao watadirika kufanya chochote kaburini.


Translation Questions

Matthew 27:1

Je, asubuhi wakuu wa makuhani na wazee walimpeleka wapi Yesu?

Asubuhi walimpeleka Yesu kwa Liwali Pilato

Matthew 27:3

Je, Yuda alifanya nini alipoona kuwa Yesu amehukumiwa?

Yesu alikiri kuisaliti damu isiyo hatia, akazirudisha zile fedha, akatoka nje, akajinyonga.

Je, Yuda alifanya nini alipoona kuwa Yesu amehukumiwa?

Yesu alikiri kuisaliti damu isiyo hatia, akazirudisha zile fedha, akatoka nje, akajinyonga.

Matthew 27:6

Je, wakuu wa makuhani walifanya nini na vile viapende thelathini vya fedha?

Walinunua shamba la mfinyanzi kwa ajili ya maziko ya wageni.

Je, wakuu wa makuhani walifanya nini na vile viapende thelathini vya fedha?

Walinunua shamba la mfinyanzi kwa ajili ya maziko ya wageni

Matthew 27:9

Ni unabii gani ambao unatimiza matukio haya?

Matukio haya yanatimiza unabii wa Yeremia.

Ni unabii gani ambao unatimiza matukio haya?

Matukio haya yanatimiza unabii wa Yeremia.

Matthew 27:11

Ni swali gani ambalo Pilato alimwuliza Yesu, na jibu la Yesu lilikuwaje?

Pilato alimwuliza Yesu kama yeye alikuwa ni maflme wa Wayahudi, na Yesu alimjibu, "wewe wasema".

Yesu alijibu nini kwa mashitaka yote ya wazee na wakuu wa Makuhani?

Yesu hakujibu hata neno moja.

Yesu alijibu nini kwa mashitaka yote ya wazee na wakuu wa Makuhani?

Yesu hakujibu hata neno moja.

Matthew 27:15

Je, Pilato alitamani kufanya nini kwa Yesu, kwa mjibu wa tamaduni za Wayahudi?

Pilato alitamani kumwachia huru Yesu. kwa mjibu watamaduni za Wayahudi.

Je, Pilato alitamani kufanya nini kwa Yesu, kwa mjibu wa tamaduni za Wayahudi?

Pilato alitamani kumwachia huru Yesu. kwa mjibu watamaduni za Wayahudi.

Matthew 27:17

Ni ujumbe gani ambao mke wa Pilato alimtumia mume wake alipokuwa ameketi kwenye kiti chake cha hukumu?

Alimwambia Pilato kuwa asimfanyechochote huyo mtu asiyekuwa na hatia.

Matthew 27:20

Kwa nini Baraba aliachiwa huru na wala siyo Yesu kwa mjibu wa tamaduni za siku kuu?

Wkuu wa makuhani nawazee waliwashawishi makutano wamwombe baraba afunguliwe badala ya Yesu.

Je, makutanao walipiga kelele wakiomba Yesu afanywe nini?

Makutano walipiga kelele wakiomba Yesu asulibiwe.

Matthew 27:23

Pilato alipoona makutano wameanza kupiga kelele alifanya nini?

Pilato alinawa mikona yake, alikuwa hana hatia kwa damu ya mtu asiyekuwa na hatia, na kisha akamtoa Yesu kwa makutano.

Matthew 27:25

Je, watu walisemaje Pilato alipomtoa Yesu kwao?

Watu waalisema hivi, "damu yake na iwe juu yetu na watoto wetu".

Matthew 27:27

Je, wale maaskari wa Liwali walimwekea nini Yesu?

Wale maaskari walimvalisha kanzu ya rangi nyekundu, na taji ya miiba kichwani mwake.

Je, wale maaskari wa Liwali walimwekea nini Yesu?

Wale maaskari walimvalisha kanzu ya rangi nyekundu, na taji ya miiba kichwani mwake.

Matthew 27:32

Simoni wa Krene alilazimishwa kufanya nini?

Simon alilazimishwa kubeba msalaba wa Yesu.

Walimpeleka wapi Yesu kwa ajili ya kumsulubisha?

Walimpeleka Golgotha, maana yake "fuvu la kichwa".

Matthew 27:35

Je, wale maaskari walifanya nii baada ya kumsulibisha Yesu?

Maaskari walipiga kura ili kugawana mavazi yake na waliketi na kumwangalia".

Je, wale maaskari walifanya nii baada ya kumsulibisha Yesu?

Maaskari walipiga kura ili kugawana mavazi yake na waliketi na kumwangalia".

Waliweka maandisjhi gani juu ya kichwa cha Yesu?

Waliandika, "HUYU NDIYE YESU MFALME WA WAYAHUDI".

Matthew 27:38

Ni nani ambao walisulibishwa pamoja na Yesu"

Wanyang'anyi wawili walisulibuwa pamoja na Yesu, mmoja upande wa kushoto na mwingine upande wa kulia.

Matthew 27:41

Je, watu, wakuu wa makuhani, wazee, na waandishi walimtaka Yesu kufanya nini?

Wote walimtaka Yesu ajiokoe nakushuka msalabani?

Matthew 27:45

Kilitokea nini kuanzia saa sita mpaka saa tisa?

Giza lilikuja juuya dunia kuanzia saa sita mpaka saa tisa.

Yesu aliliaje ilipofika saa tisa?

"Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?"

Matthew 27:48

Kilitokea nini baad ya Yesu kulia tena kwasauti kuu?

Yesu aliitoa nafsi yake.

Matthew 27:51

Kilitokea nini hekaluni Yesu alipokufa?

Lile pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutoka juu hadi chini baada ya Yesu kufa.

Kilitokea nini makaburini Yesu alipokufa?

Watakatifu wengi aliokuwa wamelala usingizi walifufuka nao wakawatokea wengi baada ya Yesu kufa.

Kilitokea nini makaburini Yesu alipokufa?

Watakatifu wengi aliokuwa wamelala usingizi walifufuka nao wakawatokea wengi baada ya Yesu kufa.

Matthew 27:54

Baada ya kushuhudia matukio haya yote, yule akida alitoa ushuhuda gani?

Yule akida alishuhudia kuwa, "Hakika huyu alikuwa mwana wa Mungu".

Matthew 27:57

Baada ya kuwa amesulibishwa kilitokea nini kwenye mwili wa Yesu?

Mwanafunzi tajiri wa Yesu, Yusufu, alimwomba Yesu mwili wa Yesu, aliufunga sanda ya sufi, na kuulaza kwenye kaburi lake jipya.

Baada ya kuwa amesulibishwa kilitokea nini kwenye mwili wa Yesu?

Mwanafunzi tajirialimwomba Yesu mwili wa Yesu, aliuzonga kwenye sanda ya kitani, na kuulaza kwenye kaburi lake jipya. wa Yesu, Yusufu,

Matthew 27:59

Kiliwekwa nini kwenye mlango wa kaburi ambaplo Yesu alikuwa amelazwa?

Jiwe kubwa liliwekwa kwenye mlango wa lile kaburi ambamo mwili wa Yesu ulikuwa umelazwa.

Matthew 27:62

Kwsa nini wakuu wamakuhani na Mafarisayo waliktana na Pilato siku iliyofuata?

Wakuuwa makuhani na Mafarisayo walitaka kuhakikisha kuwa kaburi la Yesu liko salama ili mtu asije akauiba mwili wa Yesu.

Kwsa nini wakuu wamakuhani na Mafarisayo waliktana na Pilato siku iliyofuata?

Wakuuwa makuhani na Mafarisayo walitaka kuhakikisha kuwa kaburi la Yesu liko salama ili mtu asije akauiba mwili wa Yesu.

Matthew 27:65

Je, ni kitu gani ambacho Pilato aliwaruhusu kuweka kaburini?

Pilato aliwaruhusu waweke mhuri kaburini na kulilinda.

Je, ni kitu gani ambacho Pilato aliwaruhusu kuweka kaburini?

Pilato aliwaruhusu waweke mhuri kaburini na kulilinda.


28

1Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi.2Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.3Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.4Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.

5Yule malaika akawafafanulia wale wanawake akisema, “Msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulubiwa.6Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala.

7Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, ‘Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.’ Tazama mimi nimewaambia.”

8Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.9Tazama Yesu akakutana nao na kusema, “Salamu.” Wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu.10Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.”

11Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea.12Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari13na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, ‘Wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.’14Kama taarifa hii itamfikia Liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote.”15Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.

16Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza.17Nao walipomwona, walimwabudu. Lakini baadhi yao waliona shaka.18Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni.19Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.20Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaagiza, na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.


Mathayo 28 Maelezo ya Jumla

Dhana maalum katika sura hii

"Wafanye wanafunzi"

Aya mbili za mwisho (Mathayo 28:19-20) zinajulikana kama "Tume Kubwa" kwa sababu zina amri muhimu sana iliyotolewa kwa Wakristo wote. Wakristo wanapaswa "wafanye wanafunzi" kwa kwenda kwa watu, kuwapa injili na kuwafundisha kuishi kama Wakristo.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Malaika wa Bwana

Mathayo, Marko, Luka, na Yohana wote waliandika juu ya malaika waliovalia nguo nyeupe wakiwa pamoja na wanawake kwa kaburi la Yesu. Waandishi wawili kati yao waliwaita wanaume, lakini ni kwa sababu tu malaika walikuwa katika hali ya kibinadamu. Waandishi wawili waliandika kuhusu malaika wawili, lakini waandishi wengine wawili waliandika juu ya moja tu. Ni bora kutafsiri kila moja ya vifungu hivi kama inavyoonekana katika ULB bila kujaribu kufanya vifungu vyote kufanana. (Angalia: Mathayo 28:1-2, Marko 16: 5 na Luka 24: 4 na Yohana 20:12)

Links:


Matthew 28:1

Sentensi ungsnishi

Hii ni habari ya ufufuo wa Yesu kutoka wafu

Baadye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma

Baada ya Sabato kuisha, jua lilipokuwa likichomoza Jumapili asubuhi"

Baadaye

Hili ni nenolinaloonesha kuanza kwa habari mpya. Mathayo anaanza kueleza sehemu mpya ya habari hii

Mariamu mwingine

Huyu ni Mariamu mama wa Yakobo na Yusufu Tazma (27:54)

Tazama

Neno "tazama" linatutahadharisha kuwa tayari kwa ajili ya taarifa kushanagaza ambazo zinafuata. Lugha yako inaweza kuwa namna ya kulisema hili.

kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sabau malaika wa Bwana alishuka ... na kulivingirisha jiwe

Yaweza kumaanisha yafatayo 1) tetemeko lilitokea kwa sababu alishuka na kulivingirisha lile jiwe au 2) matukio yote haya yalitokea kwa wakati mmoja.

tetemeko

kutetemeka ghafla kwa ardhi

Matthew 28:3

Sura yake

"Sura ya malaika"

ilikuwa kama ya umeme

"ilikuwa inang'aa kama ya umeme"

mavazi yake yalikuwameupe kama theluji

"mavazi yake yalikuwa meupe sana kama theluji"

na kuwa kama wafu

Huu ni msemo unaomaanisha kuwa wale maaskari walianguka chini na hawakuweza hata kutikisika. "na walianguka chini na kulala pale kama watu waliokufa"

Matthew 28:5

wale wanawake

"Mariamu Magadalena na yule Mariamu mwingine"

aliyesulibiwa

"yule ambaye watu na maaskari walimsulibisha" au "yula ambaye walimsulibisha"

amefufuka toka wafu

kirai cha "toka wafu" kinamaanisha eneo ambalo roho za wale waliokufa huenda. 'Lakini amefufuka"

mkawaambie wanfunzi wake, 'amefufuka toka wafu. Tazama amewatangulia Galilaya ambako mtamkuta"

waambieni wanafunzi wake kuwa amefufuka wafu na kwamba Yesu amewatangulia kwenda Galilaya ambako mtamwona"

amewatangulia ... mtamwona

kiwakilishi cha "mta" ni cha wingi. kinamaanisha wale wanawake na wanafunzi

nimewaambia

kiwakilishi "wa" ni cha wingi. kinamaanisha wale wanawake

Matthew 28:8

Wale wanawake

"Mariamu Magedalena na Mariamu yule mwingine"

Tazama

neno "Tazama" linatuandaa kusikiliza taarifa zinazofuata. Lugha yako yaweza kuwa namfumo wa kulisema hili.

Salamu

Hii ni salamu ya kawaida

na kushika miguu yake

"walipiga magoti na kugusa miguu yake"

ndugu zangu

Hii inamaanisha wanafunzi wa Yesu.

Matthew 28:11

Sentensi unganishi

Hii inaanza kwa habari ya mwitikio wa viongozi wa dini waliposikia habari ya kufufuka kwa Yesu

Sasa

Hili neno linaonesha mwanzo wa habari kuu. Mathayo anaanza kusimuliasehemu ya habari

wale wanawake

Inamaanisha Mariamu Magadelena na yula Mariamu mwingine

Tazama

Hii inaonesha mwanzo wa tukio lingine katika habari kuu. Inaweza kujumuisha watu tofauti katika matukio yalitangulia. Lugha yako inaweza kuwa na namna ya kulifanya hilo.

kujadili jambo hilo pamoja nao

"walipanga mpango wao wenyewe." Makuhani na wazee waliamua kuwapa zile fedha wale maaskari

Waambieni wengine kuwa, 'wanafunzi wa Yesu walikuja ... wakati tulipokuwa tumelala,'

Wambieni wengine kuwa wanafunzi wa Yesu waikuja ... wakati mlipokuwa mmelala"

Matthew 28:14

Kamataarifa hii itmfikia liwali

"Kama liwali atasikia haya kuwa mlikuwa mmesinzia wakati wanafunzi wa Yesu walipouchukua mwili"

Liwali

"Pilato"

Tutamshawishi na kuwaaondoleeni ninyi mashaka

"msihuzunike. tutongea naye ili asiwaadhibu"

na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa

"walifanya kile ambacho makuhani waliwaambia kufanya"

Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo

"Wayahudi wengi waliisikia habari hii na wanaeendelea kuwaambia wengine hadi leo"

hadi leo

Hii inamaanisha wakati Mathayo alipokuwa akiandika kitabu.

Matthew 28:16

Sentensi unganishi

Hii inaanzisha habari ya Yesu kukutana na wanafunzi wake

walimwabudu, lakini wengine waliona shaka

Maana zake zaweza kuwa 1) wote walimwabudu Yesu ingawa baadhi yao waliona shaka au) Baadhi yao walimwabudu Yesu, lakini wengine hawakumwabudu kwa sababu waliona shaka

lakini baadhi yao waliona shaka

"Wengine wlions shaka kuwa ni kweli yeye ndiye aliyekuwa Yesu na kwamba amefufuka

Matthew 28:18

Nimepewa mamlaka yote

"Baba yangu amaenipa mamlaka yote"

dunuani na mbinguni

"Mbingini" na "duniani"zimetumika pamoja kumaanisha kila kitu na kila mmoja duniani na mbinguni.

mataifa yote

Hapa "mataifa" inamaanisha watu. "kwa watu wote kwa kila taifa"

kwa jina

Hapa "jina" linamaanisha mamlaka. 'kwa mamlaka"

Baba ... Mwana

hIvi ni vyeo maalumu vinavyoonesha uhusiano wa Yesu na Mungu.

Matthew 28:20

"Na azama

"Sikilizeni" au "iweni tayari"

mpaka mwisho wa dunia

"mpaka mwisho wa nyakati" au "mpaka mwisho wa ulimwengu"


Translation Questions

Matthew 28:1

Ni siku gani na wakati gani ambapo Mariam Magadalena na yule Mariamu wa pilli walipoende kwenye kabiri la Yesu?

Jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya Juma, walienda kwenye kaburi la Yesu.

Lile jiwe lilivingirishwaje kutoka kwenye kaburi la Yesu?

Malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe.

Matthew 28:3

Je, wale walinzi walifanya nii walipomwona malaika?

Wale walinzi waloishikwa na hofu wakawa kama wafu walipomwona malaika.

Matthew 28:5

Yule malaika aliwaambia nini wale wanawake wawili juu ya Yesu?

Malaika alisema kuwa Yesu alikuwa amefufuka naye alikuwa anawatangulia kwenda Galilaya

Yule malaika aliwaambia nini wale wanawake wawili juu ya Yesu?

Malaika alisema kuwa Yesu alikuwa amefufuka naye alikuwa anawatangulia kwenda Galilaya

Matthew 28:8

Kiliwatokea nini wale wanawake wawili walipokuwa njiani kwenda kuwaambia wanafunzi?

Wale wanawake walikutana na Yesu na kumshikilia miguu yake na kisha kumwabudu.

Kiliwatokea nini wale wanawake wawili walipokuwa njiani kwenda kuwaambia wanafunzi?

Wale wanawake walikutana na Yesu na kumshikilia miguu yake na kisha kumwabudu.

Matthew 28:11

Wakati wale walizi walipowaambia wale wakuu Makuhani kilichokuwa kimetokea pale kaburini, wale wakuu wa Makuhani walifanya nini?

Wakuu wa Makuhani waliwalipa wale askari kiasi kikubwa cha pesa na kuwaambia waseme kuwa wanafunzi wa Yesu waliuiba mwili wa Yesu

Wakati wale walizi walipowaambia wale wakuu Makuhani kilichokuwa kimetokea pale kaburini, wale wakuu wa Makuhani walifanya nini?

Wakuu wa Makuhani waliwalipa wale askari kiasi kikubwa cha pesa na kuwaambia waseme kuwa wanafunzi wa Yesu waliuiba mwili wa Yesu

Matthew 28:16

Je, wanafunzi walifanya nii walipomwona Yesu kule Galilaya?

Wale wanafunzi walimwabudu Yesu, japo wengine waliona shaka.

Matthew 28:18

Ni mamlaka gsni ambayo Yesu alisema kuwa alikuwa amepewa?

Yesu alisema kuwa alikuwa amepewa mamlka yote yaliyo mbinguni na duniani.

Je,Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kufanya nini?

Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kwenda na kuwafanya watu kuwa wanafunzi wake na kuwabatiza.

Ni katika jina gani ambalo Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kubatiza?

Yesu aliwaambia wanafunzi wake kubatiza katika jina la Baba na la mwana na la Roho mtakatifu.

Matthew 28:20

Je, Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kufundisha nini?

Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kuwafundisha mataifa kutii mambo yote aliyoamuru.

Je, Yesu aliwapa ahadi gani ya mwisho wanafunzi.

Yesu aliahidi kuwa nao mpaka mwisho wa Ulimwengu


Translation Words

Abiya

Ufafanuzi

Abiya ni jina la watu mbalimbali katika agano la kale. Wafuatao ni watu hao:

Abiya

Ufafanuzi

Abiya lilikuwa jina la Mfalme wa Yuda aliyetawala tangu 915-913 BC. Alikuwa mtoto wa mfalme Rehoboamu. Walikuwepo watu wengine walioitwa Abiya katika agano la kale. Watoto wa Samweli Abiya na Yoeli walikuwa viongozi wa wana wa Israeli huko Belisheba. Kwa kuwa Abiya na kaka yake hawakuwa waaminifu watu walimuomba Samweli ateue mfalme mwingine wa kuwaongoza. Abiya mwingine ni yule aliyekuwa kwenye hekalu la kinabii wakati wa mfalme Daudi. Abiya lilikuwa jina la mtoto wa mfalme Yeroboamu. Abiya pia lilikuwa jina la kuhani mkuu aliyerudi na Zerubabeli Yerusalemu toka utumwani Babiloni.

Abrahamu, Abramu

Ufafanuzi

Abramu alikuwa Mkalidayo toka mji wa Urialiyechaguliwa na Mungu kuwa baba wa Waisraeli. Mungu alibadilisha jina lake na kuwa "Abrahamu."

Adamu

Ufafanuzi

Adamu alikuwa binadamu wa kwanza aliyeumbwa na Mungu. Yeye na mke wake Hawa walitengenezwa kwa mfano wa Mungu.

Adui

Ufafanuzi

"Adui" ni mtu au kundi lililo kinyume na mtu au kitu fulani.

Ahazi

Ufafanuzi

Ahazi alikuwa mfalme muovu aliyetawala ufalme wa Yuda toka 732-716 BC. Hii ilikuwa yapata miaka 140 kabla ya wakati ambao wana wa Israeli na Yuda walichukuliwa mateka Babiloni.

Amina, kweli

Ufafanuzi

Neno "Amina" hutumika kusisitiza au kuweka mkazo jambo ambalo mtu amesema. Mara nyingi hutumika mwisho wa sala. Mara nyingine hutafsiriwa kama "kweli."

Amoni, Waamoni wanaume, Waamoni wanawake.

Ufafanuzi

"Waamoni" lilikuwa kundi la watu walioishi Kaanani. Walikuwa uzao wa Benyamini, aliyekuwa mtoto wa Lutu.

Andrea

Ufafanuzi

Andrea alikuwa mmoja kati ya wanafunzi kumi na wawili aliowachangua Yesu kuwa karibu naye ambao baadaye waliitwa Mitume.

Angalia, Mlinzi

Ufafanuzi

"Angalia" inamaanisha kuwa kutazama kitu kwa ukaribu na kwa makini. "Mlinzi" ni mtu ambaye kazi yake ni kuulinda mji kwa kuangalia kwa makini vyote vinavyomzunguka kama kuna hatari yoyote kwa watu wa mji ule.

Asa

Ufafanuzi

Asa alikuwa mfalme aliyetawana ufalme wa Yuda kwa miaka arobaini. toka 913-873 BC.

Babeli

Ufafanuzi

Babeli ulikuwa mji mkuu katika eneo lililoitwa Shinari kusini mwa Mesopotamia. Shinari ulikuja baadaye kuitwa Babiloni.

Bahari ya Galilaya, Bahari ya Shinerethi, Ziwa la Genezareti, Bahari ya Tiberia

Ufafanuzi

"Bahari ya Galilaya" ni jina la ziwa mashariki mwa Israeli. Katika Agano la Kale liliitwa "Bahari ya Shinerethi."

Baraba

Ufafanuzi

Baraba alikuwa mfungwa huko Yerusalemu wakati Yesu anakamatwa.

Boazi

Ufafanuzi

Boazi alikuwa mwisraeli aliyekuwa amemwoa Ruthi, babu wa mfalme Daudi, na babu wa Yesu Kristo.

Bwana

Ufafanuzi

Neno "Bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine. Inapokuwa na herufi kubwa, ni jina linalomaanisha Mungu. (Noti hata hivyo inapotumika kama njia ya kumtambua mtu mwanzo mwa sentesi inaweza kuwa na herufi kubwa na kuwa na maana ya "mkuu.")

Katika Agano la Kale, msemo huu pia unatumika maneno kama, "Bwana Mungu Mkuu" au "Bwana Yahwe" au "Yahwe Bwana wetu." Katika Agano Jipya, mitume walitumia neno hili katika misemo kama, "Bwana Yesu" na "Bwana Yesu Kristo," illiyoonyesha kuwa Yesu ni Mungu. Neno "Bwana" katika Agano Jipya pia linatumika peke yake kama njia ya moja kwa moja ya kumtambua Mungu, hasa katika nukuu za kutoka Agano la Kale. Kwa mfano, maandishi ya Agano la Kale ya, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Yahwe" na Agano Jipya lina, "Amebarikiwa ajaye kwa jina la Bwana." Katika ULB na UDB, jina "Bwana" linatumika tu kutafsiri maneno halisi ya Kihebrania na Kigriki yanayomaanisha "Bwana." Halitumiki kama tafsiri ya jina la Mungu (Yahwe), kama inavyofanywa na tafsiri zingine.

Bwana harusi

Ufafanuzi

Bwana harusi ni mtu anayemwoa bibi arusi katika sherehe ya harusi.

Dani

Ufafanuzi

Dani alikuwa mwana wa tano wa Yakobo na alikuwa mmoja wa makabila kumi na mawili ya Israeli. Eneo lililokaliwa na kabila la Dani sehemu ya kaskazini ya Kaanani pia lilipatiwa jina hili.

Katika kipindi cha Abrahamu, kulikuwa na mji ulioitwa Dani uliokuwa magharibi mwa Yerusalemu.

Miaka ya baadaye, katika kipindi ambapo taifa la Israeli lilipoingia katika nchi ya ahadi, mji tofauti ulioitwa Dani ulikuwa kama maili 60 kaskazini mwa Yerusalemu.

Msemo "Wadani" una maana ya vizazi vya Dani, ambao pia ni wanajumuiya wa ukoo wake.

Danieli

Ufafanuzi

Danieli alikuwa nabii wa Kiisraeli ambaye alikuwa kijana mdogo aliyechukuliwa mateka na mfalme wa Babeli Nebukadreza mnamo wa 600 KK.

Huu ulikuwa wakati ambapo Waisraeli wengine wengi kutoka Yuda walishikwa mateka huko Babeli kwa miaka 70.

Danieli alipewa jina la Kibabeli la Belteshaza.

Danieli alikuwa kijana aliyeheshimika na mwenye haki aliyemtii Mungu.

Mungu alimwezesha Danieli kutafsiri ndoto kadhaa au maono kwa wafalme wa Babeli.

Kwa sababu ya uwezo huu na kwa sababu ya hulka yake ya heshima, Danieli alipewa nafasi ya juu ya uongozi katika ufalme wa Kibabeli.

Miaka mingi baadaye, maadui wa Danieli walimdanganya mfalme wa Babeli Dario kutunga sheria inayokataza kumwabudu mtu yeyote isipokuwa mfalme. Danieli aliendelea kuomba kwa Mungu, kwa hiyo alikamatwa na kutupwa katika tundu la simba. Lakini Mungu alimkomboa na hakudhuriwa kabisa.

Daudi

Ufafanuzi

Daudi alikuwa mfalme wa pili wa Israeli na alimpenda na kumtumikia Mungu. Alikuwa mwandishi mkuu wa kitabu cha Zaburi.

Daudi alipokuwa mvulana mdogo akichunga kondoo wa familia yake, Mungu alimchagua kuwa mfalme afuataye wa Israeli.

Daudi alikuwa mpiganaji hodari na aliongoza jeshi la Israeli katika vita dhidi ya maadui zake. Kumshinda kwake Goliati na Wafilisti kunajulikana sana.

Mfalme Sauli alijaribu kumuua Daudi, lakini Mungu alimlinda, na kumfanya awe mfalme baada ya kifo cha Sauli.

Daudi alitenda dhambi mbaya sana, lakini alitubu na Mungu alimsamehe.

Yesu, Masihi, anaitwa "Mwana wa Daudi" kwa sababu ni uzao wa Mfalme Daudi.

Eliakimu

Ufafanuzi

Eliakimu lilikuwa jina la wanamume wawili katika Agano la Kale.

Mwanamume mmoja aliyeitwa Eliakimu alikuwa msimamizi wa kasri chini ya Mfalme Hezekia.

Mwanamume mwingine aliyeitwa Eliakimu alikuwa mwana wa Mfalme Yosia. Alifanywa mfalme wa Yuda na farao wa Misri, Necho.

Necho alibadili jina la Eliakimu kuwa Yehoyakimu.

Eliya

Ufafanuzi

Eliya alikuwa mmoja wa manabii muhimu sana wa Yahwe. Eliya alitabiri katika wakati wa tawala za wafalme kadhaa wa Israeli au Yuda, akiwemo Mfalme Ahabu.

Mungu alifanya miujiza mingi kupitia Eliya, ikiwemo kumfufua mvulana mfu kurudi katika uhai.

Eliya alimkaripia Mfalme Ahabu kwa kuabudu mungu wa uongo Baali.

Aliwapa changamoto manabii wa Baali katika mtihani ambao ulithibitisha ya kwamba Yahwe ni Mungu mmoja wa kweli.

Katika mwisho wa maisha ya Eliya, Mungu alimchukua kimuujiza juu mbinguni angali bado yu hai.

Miaka mia moja baadaye, Eliya, pamoja na Musa, walijitokeza na Yesu juu ya mlima na waliongea pamoja juu ya kurudi, kuteseka na kufa kwa Yesu Yerusalemu.

Filipi

Ufafanuzi

Filipi ulikuwa mji muhimu na koloni la Rumi lililokuwa Makedonia kaskazini mwa Ugiriki ya kale.

Filipo, mwinjilisti

Ufafanuzi

Katika kanisa la kwanza huko Yerusalemu Filipo alikuwa mmoja wa viongozi saba waliochaguliwa ili kuwajali masikini, Wakristo wenye uhitaji hasa wajane.

Filipo, mtume

Ufafanuzi

Mtume Filipo alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu alikuwa anatoka mji wa Bethsaida.

Galilaya, Mgalilaya

Ufafanuzi

Galilaya ni eneo la kaskazini ya Israeli, kaskazini ya Samaria. "Mgalilaya" alikuwa mtu ambaye aliishi Galilaya.

Galilaya, Samaria, na Yudea ilikuwa miji mitatu ya msingi ya Israeli wakati wa Agano Jipya.

Galilaya imepakana upande wa mashariki na ziwa kubwa liitwalo "Ziwa la Galilaya".

Yesu alikua na kuishi katika mji wa Nazareti Galilaya.

Miujiza mingi na mafundisho ya Yesu yalifanyika katika eneo la Galilaya.

Gethsemane

Ufafanuzi

Gethsemane ilikuwa bustani ya mizeituni mashariki mwa Yerusalemu mbali ya bonde la Kidroni karibu na Mlima wa Mizeutuni.

Bustani ya Gethsemane ilikuwa sehemu ambapo Yesu na wafuasi wake walienda kuwa wenyewe na kupumzika, mbali na mikusanyiko.

Ilikuwa Gethsemane ambapo Yesu aliomba kwa huzuni kubwa, kabla ya kukamatwa pale na viongozi wa Kiyahudi.

Gomora

Ufafanuzi

Gomora ilikuwa mji katika bonde lenye rutuba, karibu na Sodoma ambapo mpwa wa Abrahamu Lutu alichagua kuishi.

Mahali haswa pa Gomora na Sodoma hapajulikani, lakina kuna viashiria ya kwamba inaweza kuwa mahali moja kwa moja kusini mwa Bahari ya Chumvi, karibu na Bonde la Sidimu.

Kulikuwa na wafalme wengi vitani katika eneo ambapo Sodoma na Gomora na ilikuwepo.

Familia ya Lutu ilipokamtwa katika ugomvi kati ya Sodoma na miji mingine, Abrahamu na wanamume wake waliwakomboa.

Sio muda baada ya hapo, Sodoma na Gomora ziliteketezwa na Mungu kwa sababu ya uovu wa watu walioishi pale.

Habili

Ufafanuzi

Habili alikuwa mtoto wa Adamu na Hawa. Alikuwa ndogo wake na Kaini. Habili alikuwa mfugaji. Habili alitoa sadaka ya baadhi ya mifugo yake kwa Mungu. Mungu alipendezwa na sadaka ya Habili.
Mtoto wa kwanza wa Adamu na Hawa, Kaini alimuua Habili.

Hamu

Ufafanuzi

Hamu ni mtoto wa pili kati ya wana watatu wa Nuhu. katika gharika kuu la kidunia ambalo liliigharikisha dunia yote, Hamu na ndugu zake pamoja na wake zao walikuwa pamoja na baba yao, Nuhu katika safina. Baada ya gharika, kulikuwa na tukio la Hamu kutomweshimu baba yake, Nuhu. Na matokeo yake, Nuhu alimlaani mtoto wa Hamu alilyeitwa Kanaani pamoja na uzao wake wote, ambao baadaye walijulikana kama Wakanaani.

Hawa

Ufafanuzi

Hili lilikuwa jina la mwanamke wa kwanza. Jina lake linamaanisha "uhai" au "kuishi".

Mungu alimuumba Hawa kutoka kwa ubavu ambao aliuchukua kutoka kwa Adamu.

Hawa aliumbwa kuwa "msaidizi" wa Adamu. Alikuja kando ya Adamu kumsaidia katika kazi ambayo Mungu aliwapa kufanya.

Hawa alijaribiwa na Shetani (kwa mfano wa nyoka) na alikuwa wa kwanza kufanya dhambi kwa kula tunda ambalo Mungu aliwaambia kutokula.

Herodia

Ufafanuzi

Herodia alikuwa ni mke wa Herode Antipa huko Uyahudi kipindi cha Yohana Mbatizaji. Herodia alikuwa mke halali wa kaka yake na Antipa, aliyeitwa Philipo, lakini baadaye aliolewa na Herodi Antipa kinyume na sheria. Yohana mbatizaji aliwakemea Herode na Herodia kwa sababu ya ndoa yao haramu. Na kwasababu hiyo, Yohana alifungwa gerezani na baadaye aliuawa kwa kukatwa kichwa.

Hezekia

Ufafanuzi

Hezekia alikuwa ni mfalme wa 13 wa ufalme wa Yuda. Alikuwa ni mfalme aliyemtumaini Mungu na kumtii. Tofauti na baba yake, Ahazi aliyekuwa mfalme mwovu, Mfalme Hezekia alikuwa ni mfalme mzuri aliyeharibu maeneo yote ya ibada ya miungu katika Yuda. Wakati Hezekia alipougua na alipokuwa karibu kufa, alimwomba Mungu sana ili alinde na kuhifadhi maisha yake. Mungu alimponya na alimruhusu kuishi miaka 15 zaidi. Mungu alifanya muujiza kwa Hezekia kwa kurudisha muda nyuma. Mungu alijibu maombi ya Hezekia kwa kuwaokoa watu wake kutoka mikononi mwa Mfalme Senakaribu wa Siria, aliyekuwa akiwashambulia.

Imeandikwa

Ufafanuzi

maneno haya "Kama ilivyoandikwa" au "kilichoandikwa" yametokea mara nyingi katika agano jipya na yameelezea amri au unabii ulioandikwa katika maandiko ya Kiebrania.

Isaka

Ufafanuzi

Isaka alikuwa mwana pekee wa Abrahamu na Sara. Mungu aliwaahidi kuwapa mwana wa kiume ingiwa walikuwa wazee sana.

Jina "Isaka" linamaanisha "kicheko." Mungu alipomuambia Abrahamu kuwa Sara atazaa mwana wa kiume, Abrahamu alicheka kwa sababu wote walikuwa wazee sana. Baada ya muda, Sara pia alicheka aliposikia taarifa hii. Lakini Mungu alitimiza ahadi yake na Isaka alizaliwa kwa Abrahamu na sara katika uzee wao. Mungu alimuambia Abrahamu kuwa agano alilofanya na Abrahamu itakuwa pia ya Isaka na vizazi vyake milele. Wakati Isaka alikuwa kijana, Mungu aliijaribu imani ya Abrahamu kwa kumuamuru kumtoa isaka kama sadaka. Mwana wa Isaka, Yakobo, alikuwa na wana kumi na mbili ambao uzao wao baadaye ukawa makabila kumi na mbili ya taifa la Israeli.

Isaya

Ufafanuzi

Isaya alikuwa nabii wa Mungu aliyetabiri wakati wa utawala wa wafalme wanne wa Yuda: Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia.

Aliishi Yerusalemu wakati Waashuri walipokuwa wakivamia mji, wakati wa utawala wa Hezekia. Kitabu cha Agano la Kale cha Isaya ni moja ya vitabu vikuu vya Biblia. Isaya aliandika unabii mwingi ulitokea wakati wa uhai wake. Isaya anajulikana zaidi kwa unabii alioandika kumhusu Masihi uliotimia miaka 700 baadaye wakati Yesu alipoishi duniani. Yesu na wanafunzi wake walinukuu utabiri wa Isaya kuwafundisha watu kuhusu Masihi.

Israeli, Waisraeli, taifa la Israeli

Ufafanuzi

Neno "Israeli" ni jina ambalo Mungu alimpa Yakobo. Linamaanisha, "anashindana na Mungu."

Uzao wa Yakobo walijulikana kama "watu wa Israeli," "taifa la Israeli" au "Waisraeli." Mungu aliunda agano lake na watu wa Israeli. Walikuwa watu wake aliowachagua. Taifa la Israeli liliundwa na makabila kumi na mbili. Mara baada ya mfalme Sulemani kufa, Israeli iligawanyika katika falme mbili: ufalme wa kusini, uliitwa "Yuda" na ufalme wa kaskazini, uliitwa "Israeli."

Jehanamu, ziwa la moto

Ufafanuzi

Jehanamu ni sehemu ya mwisho iliyo na maumivu na mateso yasiyokoma, mahali ambapo Mungu atamhukumu kila mmoja anayemwasi Yeye na kuukataa mpango wake wa kuwaokoa kupitia kwa sadaka ya Yesu. Pia inarejelewa kama 'ziwa la moto. Jehanamu au Kuzimu kunatajwa kama sehemu ya moto na mateso makali. Shetani na roho chafu zinazomfuata zitatupwa katika Jehanamu kwa ajli ya hukumu ya milele. Watu wasioamini sadaka ya Yesu kwa ajili ya ondoleo la dhambi zao, na wasiomtumaini Yeye, watahukumiwa Jehanamu milele

Mapendekezo ya tafsiri Maneno haya yanapaswa kutafsiriwa tofauti tofuauti kwasababu yanatokea tofauti katika muktadaha tofauti. Katika baadhi ya lugha haziwezi kutumia neno 'ziwa' kwa sababu kwao ziwa ni 'maji' Neno Jehanamu laweza kutafsiriwa kama 'sehemu ya mateso au sehemu yenye giza na maumivu' Maneno 'ziwa la moto' yanaweza pia kutafsiriwa kama 'bahari ya moto' au 'moto mkubwa.'

Kaisari

Ufafanuzi

Neno "Kaisari" lilikuwa jina au jina la heshima lililotumika kwa watawala wengi wa Dola ya Rumi. Katika Biblia, hili neno linahusisha kwa tawala tatu tofauti tofauti.

Katika majina kama Kaisari Agustino au Tiberia Kaisari, "Kaisari" inaweza kutamkwa karibia na vile lugha ya taifa inavolitamka.

Kaisaria, Kaisaria Filipi

Ufafanuzi

Kaisaria ulikuwa mji wa muhimu katika pwani ya Bahari ya Meditrania, kama 39 kilomita kusini mwa Mlima Karmeli Kaisaria Filipi ulikuwa mji unaoonyesha kusinimagharibi sehemu ya Israeli, karibu na Mlima Herimoni.

Kichwa

Ufafanuzi

Katika Biblia neno 'kichwa' lilmetumika kama tamathali ya semi likiwa lina maana nyingi: Mara nyingi neno hili limetumika kurejelea hali ya kuwa na mamlaka juu ya watu , kwa mfano, "mmenifanya kichwa cha mataifa" Sentensi hiyo yaweza kutafsiriwa kuwa "mmenifanya kuwa mtawala" au "mmenipa mamlaka juu ya..." Yesu anaitwa 'kichwa cha kanisa.' Kama ambavyo kichwa cha mtu huongoza viungo vingine vya mwili, hivyo na Yesu huongoza na huelekeza viungo vingine vya mwili wake, yaani kanisa. Agano la Jipya linatufundisha kuwa mme ni "kichwa'' au mwenye mamlaka kwa mkewe. Amepewa wajibu wa kumwongoza na kumwelekeza mkewe na familia. Maneno yanayosema "wembe hautagusa kich chake" maana yake ni kwamba" hatakata au hatanyoa nywele zake. Neno 'kichwa' laweza pia kurejelea mwanzo au asili ya kitu fulani, mfano 'kichwa cha mtaa" Maneno kama "kichwa cha nafaka" hurejelea sehemu ya juu ya ngano au mche wa shayiri ambao una mbegu ndani yake. Mfano mwingine wa 'kichwa' ni pale unapotumika kuwakilisha mtu mzima. Mfano, 'kichwa cheupe' humrejelea mtu mzee au tunaposema ' kicha cha Yusufu, tunamaanisha Yusufu mwenyewe. Msemo unaosema 'acha damu yao iwe juu ya kichwa chake' humaanisha kuwa mtu yule anawajibika kwa vifo vyao na atapokea adhabu/hukumu yake.

Mapendekezo ya tafsiri Neno 'kichwa' laweza kutafsiriwa kama 'mamlaka' au 'mtu anayeongoza na kuelekeza' au 'mtu anayewajibika kwa..' kwa kutegemea na muktadha wenyewe. Maneno kama ' kichwa cha' hurejelea mtu mwenyewe mzima, na hivyo maneno hayo yaweza kutafsiriwa kwa kutumia jina la mtu husika. kwa mfano ''kichwa cha Yusufu'' ina maana ya 'Yusufu' Maelezo kama ' itakuwa juu ya kichwa chake' yanaweza kutafsiriwa kama " itakuwa juu yake'' au 'ataadhibiw'a kwa ajili ya' au 'atawajibika kwa ajili ya... Kwa kutegemea na muktadha wenyewe, maana zingine za neno kichwa zaweza kuwa "mwanzo' au "asili'' au ''chanzo'' au "mtawala" au ''juu ya''

Krene

Ufafanuzi

Krene ulikuwa mji wa Kigiriki kaskazini mwa pwani ya Afrika kwa upande wa bahari ya Mediteraniani, moja kwa moja kusini mwa kisiwa cha Krene.

Kristo, Masihi

Ufafanuzi

Masihi na Kristo inamaana ya mpakwa mafuta na inamuelezea Yesu mwana wa Mungu.

Kuhani, ukuhani

Ufafanuzi

Katika Biblia Kuhani alikuwa mtu aliyechaguliwa kutoa sadaka ya kuteketezwa kwa Mungu kwa niaba ya watu wa Mungu. Ukuhani lilikuwa jina au masharti ya kuwa kuhani.

Maji

Ufafanuzi

Pamoja na maana yake ya kawaida maji yaweza kuwelezea vyanzo vya maji kama vile bahari, mto au ziwa.

Malaika, Malaika mkuu

Ufafanuzi

Malaika ni kiumbe chenye roho na chenye nguvu kilichoumbwa na Mungu. Malaika wanamtumikia Mungu kwa kufanya yale wanayoagizwa kuyafanya na Mungu. Malaika mkuu ni malaika anayewaongoza malaika wengine.

Malkia

Ufafanuzi

Malkia ni kiongozi mwanamke wa nchi fulani au mke wa mfalme.

Manase

Ufafanuzi

Hawa walikuw wanaume watano kwa jina Manase katika Agano la Kale:

Mariamu, mama yake Yesu

Ufafanuzi

Mariamu alikuwa mwanamke mdogo aliye ishi katika mji wa Nazarethi aliye poswa kuolewa na Yusufu. Mungu alimchagua Mariamu kuwa mama wa Yesu Mesia, Mwana wa Mungu.

Mariamu Magdalena

Ufafanuzi

Mariamu Magdalena alikuwa miongoni mwa wanawake waliyo muamini Yesu na kumfuata katika huduma yake. Alijulikana kama kama Yesu aliye mponya kutoka kwa mapepo saba waliyo mtawala.

Mataifa

Ufafanuzi

Msemo "mataifa" una maana ya mtu yeyote ambaye sio Myahudi. Watu wa mataifa ni watu ambao sio uzao wa Yakobo.

Katika Biblia, msemo "kutotahiriwa" pia hutumika kitamathali kumaanisha watu wa Mataifa kwa sababu wengi wao hawakutahiri watoto wao wa kiume kama Waisraeli walivyofanya.

Kwa sababu Mungu aliwachagua Wayahudi kuwa watu maalumu, walifikiria juu ya watu wa mataifa kama watu wa nje ambao wasingeweza kuwa watu wa Mungu.

Wayahudi pia waliitwa "Waisraeli" au "Waebrania" katika vipindi tofauti vya historia. Waliwajua wengine wote kama "watu wa Mataifa".

Watu wa mataifa pia inaweza kutafsiriwa kama "asiye Myahudi" au "asiye Muisraeli" (Agano la Kale).

Kitamaduni, Wayahudi hawakula na watu wa mataifa au kujihusishanao, ambapo mara ya kwanza ilisababisha matatizo miongoni mwa kanisa la kwanza.

Mathayo, Lawi

Ufafanuzi

Mathayo alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliyo wachagua kuwa mitume wake. Alijulikana kama pia kama Lawi, mwana wa Alfayo.

Mfalme wa Wayahudi

Ufafanuzi

Usemi, "Mfalme wa Wayahudi" ni jina linalomaanisha Yesu, Masihi.

Mara ya kwanza Biblia inaandika hili jina wakati linapotumika na wanaume wenye hekima waliosafiri kwenda Bethlehemu wakimtafuta mtoto aliye "Mfalme wa Wayahudi." Malaika alimfunulia Mariamu kuwa mwanaye, mzawa wa mfalme Daudi, atakuwa mfalme ambaye ufalme wake utadumu milele. Kabla Yesu hajasulibishwa, askari Wakirumi walimdhihaki Yesu kwa kumuita "Mfalme wa Wayahudi." JIna hili liliandikwa pia katika kipande cha mbao na kupigwa msumari juu ya msalaba wa Yesu. Yesu kweli ni Mfalme wa Wayahudi na mfalme wa viumbe vyote.

Mimi, Yahwe

Ufafanuzi

Mara nyingi katika Agano la Kale, wakati Mungu akijizungumzia, hutumia jina lake badala ya nomino kiwakilishi.

Kwa mfano, badala ya kusema, "Niheshimu mimi," husema "Mheshimu Yahwe." Kuiweka wazi kuwa ni Mungu anayejizungumzia, ULB kawaida hutafsiri hii kwa kuongezea nomino kiwakilishi kama, "Niheshimu mimi, Yahwe" au "Mimi, Yahwe ninasema." Kwa kuongeza nomino kiwakilishi "mimi", ULB inaashiria kwa msomaji kuwa Mungu ndiye anayezungumza.

Misri, Mmisri

Ufafanuzi

Misri ni nchi katika sehemu ya kaskazini ya Afrika, kusini mashariki mwa nchi ya Kaanani. Mmisri ni mtu ambaye anatoka katika nchi ya Misri.

Katika miaka ya zamani, Misri ilikuwa nchi yenye nguvu na utajiri.

Misri ya zamani iligawanyika katika sehemu mbili, Misri ya Chini (sehemu ya kaskazini ambapo mto hutiririka chini kuelekea baharini) na Misri ya Juu (sehemu ya kusini). Katika Agano la Kale, sehemu hizi zinajulikana kama "Misri" na "Pathrosi" katika lugha ya maandishi asili.

Wakati mwingine ambapo kuna chakula kichache Kaanani, wakuu wa koo walisafiri kwenda Misri kununua chakula kwa ajili ya familia zao.

Kwa miaka mia moja hivi, Waisraeli walikuwa watumwa Misri.

Yusufu na Mariamu walishuka chini Misri na mtoto mdogo Yesu kutoroka kwa Herode Mkuu.

Mkuu, Binti wa Mfalme

Ufafanuzi

Mkuu ni mtoto wa kiume wa mfalme. Binti wa mfalme ni mtoto wa kike wa mfalme.

Mkuu

Ufafanuzi

"Mkuu" ni kiongozi wa muhimu na mwenye nguvu sana katika kundi fulani.

Mlima wa Mizeituni

Ufafanuzi

Mlima wa Mizeituni ni mlima au kilima kikubwa karibu na mashariki mwa mji wa Yerusalemu. Una mita787 kwenda juu.

Mnafiki, unafiki

Ufafanuzi

Neno 'mnafiki' humrejelea mtu ambaye hufanya mambo ili aonekane mwema, ingawa kwa siri hufanya mambo maovu. Neno 'unafiki' hurejelea tabia ambayo huwahadaa watu kwa kufikiri kuwa mtu huyo ni mwenye haki. Wanafiki wanapenda kuonekana wakiwa wanafanya mambo mazuri, hivyo watu hufikiri kuwa ni watu wazuri. Mara kwa mara watu wanafiki huwakosoa watu wengine kwa kufanya mambo yale yale ya dhambi ambayo wao wenyewe huyafanya. Yesu aliwaita Mafarisayo kuwa ni wanafiki kwasababu walifanya matendo ya kidini kama vile kuvaa aina fulani ya nguo na kula chakula fulani, lakini hawakuwa wema na wenye haki kwa watu. Mtu mnafiki huweka wazi makosa ya watu wengine, lakini yeye mwenyewe hakubali makosa yake.

Mapendekezo ya tafsiri Baadhi ya lugha huwa na maneno kama "sura mbili" ambayo hutumika kumrejelea mnafiki au matendo ya mnafiki. Namna nyingine ya kutafsiri neno mnafiki ni "mdanganyifu, mtu anayejifanya, mwongo,"

Mungu

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "Mungu" una maana ya kiumbe wa milele ambaye aliumba ulimwengu bila chochote. Mungu alikuwepo kama Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Jina binafsi la Mungu ni "Yahwe".

Mungu mara zote alikuwepo; alikuwepo kabla ya kitu chochote kuwepo, na ataendelea kuwepo milele.

Yeye ni Mungu mmoja wa kweli na ana mamlaka juu ya kila kitu ulimwenguni.

Mungu ana haki timilifu, hekima isiyo na mwisho, mtakatifu, bila dhambi, wa haki, wa rehema, na upendo.

Ni Mungu wa kutunza agano, ambaye hutimiza ahadi zake daima.

Watu waliumvwa kumwabudu Mungu na ni yeye pekee wanaopaswa kumwabudu.

Mungu alifunua jina lake kama "Yahwe" ambayo ina maana ya "yeye ni" au "Mimi ni" au "Yule anayekuwepo daima".

Biblia pia hufundisha kuhusu "miungu" wa uongo ambao ni sanamu wasioishi ambao watu huabudu kwa makosa.

Musa

Ufafanuzi

Musa alikuwa nabii na kiongozi wa watu wa Israeli kwa miaka 40.

Mwana wa Adamu, mwana wa adamu

Ufafanuzi

Jina, "Mwana wa Adamu" lilitumika na Yesu akijieleza. Mara nyingi alitumia hili jina badala ya kusema "mimi."

Mwana wa Mungu, Mwana

Ufafanuzi

Neno "Mwana wa Mungu la husu Yesu, Neno la Mungu aliye kuja duniani kama binadamu. Anajulikana kama "Mwana."

Nabii, unabii, mwonaji, nabii mwanamke.

Ufafanuzi

"Nabii ni mtu anayesema ujumbe wa Mungu kwa watu. Mwanamke anayefanya hivi anaitwa "nabii mwanamke."

Naftali

Ufafanuzi

Naftali alikuwa mwana wa sita wa Yakobo. Uzao wake uliunda kabila la Naftali, ambalo lilikuwa moja ya kabila la Israeli.

Ninawi, Mninwai

Ufafanuzi

Ninawi ilikuwa mji mkuu wa Asyria. Mninawi alikuwa mtu aliye ishi Ninawi.

Nuhu

Ufafanuzi

Nuhu alikuwa mwanaume aliye ishi miaka 4,000 iliyo pita, kipindi ambacho Mungu alipotuma garika duniani kuharibu watu waovu. Mungu alimwambia Nuhu ajenge meli kubwa ambayo yeye na familia yake waliweza kuishi wakati mafuriko yalipo funika dunia.

Nyumba

Ufafanuzi

Istilahi 'nyumba' hutumika kama tamathali ya semi (mfano) katika Biblia. Mara nyingine hutumika kumaanisha 'kaya' kurejelea watu wanaoishi pamoja katika nyumba. Mara zote neno 'nyumba' humaanisha wazao au watoto au ndugu wengine. Mfano, nyumba ya Daudi huwa na maana ya uzao wa Daudi. Maneno kama 'nyumba ya Mungu' au 'nyumba ya Yahweh' huwa na maana ya hekalu au hema la kukutania au sehemu Mungu alipo. Katika Waebrania 3, "Nyumba ya Mungu" ni sitiari ikimaanisha Watu wa Mungu. Kifungu cha maneno ' nyumba ya Israeli" kwa ujumla huwa na maana ya taifa laote la Israeli au hasa hasa kwa makabila ya ufalme wa Kasikazini wa Israeli.

Mapendekezo ya tafsiri kwa kutegemeana na muktadha, neno, nyumba linaweza kuwa na maana ya 'kaya' ' watu, familia, uzao, hekalu au sehemu ya kukaa.'' "Nyumba ya Daudi' in maana ya ''ukoo wa Daudi, familia ya Daudi au uzao wa Daudi. "Nyumba ya Israeli' ina maana ya watu wa Israeli au wazao wa Israeli au waisraeli. 'Nyumba ya Yahweh' ina maana ya hekalu au sehemu ya kumwabudia Mungu.

Pasaka

Ufafanuzi

"Pasaka " ni jina la sherehe ya kidini ambayo Wayahudi walisherehekea kila mwaka kukumbuka mi kwa namna gani Mungu aliwaokoa mababu zao Waisraeli toka utumwani Misri.

Pazia

Ufafanuzi

Katika Biblia pazia ni kitu kinene, chenye nyenzo nzito kinachotumika kutengenezea maskani na hekalu.

Petro, Simoni Petro, Kefa

Ufafanuzi

Petro alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa kiongozi wa muhimu katika kanisa la kwanza.

Pilato

Ufafanuzi

Pilato alikuwa kiongozi wa serikali ya Rumi katika Yudea aliyumuhukumu Yesu kifo.

Rabi, Raboni

Ufafanuzi

Rabi ina maana ya bwana wangu au mwalimu wangu.

Rahabu

Ufafanuzi

Rahabu alikuwa mwanamke aliyeishi Yeriko Waisraeli walipovamia mji. Alikuwa kahaba.

Raheli

Ufafanuzi

Raheli alikuwa mmoja wa wake wa Yakobo. Yeye na dada yake Lea walikuwa watoto wa mjomba wake Yakobo.

Rama

Ufafanuzi

Rama ulikuwa mji wa zamani wa Israeli uliokuwa kilometa 8 toka Yerusalemu. Ulikuwa mji ambao Benyamini aliishi.

Rehoboamu

Ufafanuzi

Rehoboamu alikuwa mmoja wa wana wa mfalme Sulemani na alikuja kuwa mfalme baada ya Sulemani kufa.

Roho Mtakatifu, Roho wa Mungu, Roho wa Bwana.

Ufafanuzi

Maneno haya yote humrejelea Roho Mtakatifu ambaye ni Mungu. Mungu mmoja na wa kweli aishiye milele katika nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu mara zingine hutajwa kama 'Roho' na 'Roho ya Yahweh' au 'Roho wa ukweli' Roho Mtakatifu ni mtakatifu kwa sababu yeye ni Mungu. Yeye yuko kamili na mwadilifu katika kila jambo alifanyalo. Roho Mtakatifu alishiriki kikamilifu katika uumbaji wa ulimwengu pamoja na Baba na Mwana. Wakati Mwana wa Mungu, Yesu aliporudi mbinguni, Mungu alimtuma Roho Mtakatifu kwa watu ili awaongoze, kuwafundisha, kuwafariji na kuwawezesha kufunya mapenzi ya Mungu. Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu na pia anawaongoza wale wanaomwamini Yesu.

Mapendekezo ya tafsiri Neno hili laweza kutafsiriwa tu kwa kutumia maneno yenye kumaanisha 'roho' na 'mtakatifu' Lakini maneno mengine ambayo yaweza kutumika ni kama 'Roho Safi' au 'Roho aliye Mtakatifu' au 'Mungu Roho.'

Rudi

Ufafanuzi

Neno "rudi" linamaanisha kurudi au kurudisha kitu.

Sabato

Ufafanuzi

Neno "Sabato" la husu siku ya saba ya wiki, ambayo Mungu aliwaamuru Waisraeli waitenge kama siku ya kupumzika na kutofanya kazi.

Sauti

Ufafanuzi

Sauti hutumika kumaanisha kuongea au kuwasiliana kitu au jambo.

Sayuni, Mlima Sayuni

Ufafanuzi

Hapo awali, neno "Sayuni" au "Mlima Sayuni" lilimaanisha ngome ambayo Mfalme Daudi aliiteka kutoka kwa Wayebusi. Majina haya yakawa njia nyingine ya kuitaja Yerusalemu.

Shetani, ibilisi, yule muovu

Ufafanuzi

Ibilisi ni roho hai Mungu aliyo umba, lakini aliasi dhidi ya Mungu na kuwa adui wa Mungu. Ibilisi anaitwa "Shetani" na "yule muovu."

Sidoni, Wasidoni

Ufafanuzi

Sidoni alikuwa mwana wa kwanza wa Kanani. Pia kuna mji wa Kikanani unao itwa Sidoni, labda uliitwa baada ya mwana wa Kanani.

Simeoni

Ufafanuzi

Katika Biblia, kuna wanaume kadhaa wenye jina Simeoni.

Simoni

Ufafanuzi

Simoni alikuwa mmoja wa wanafunzi kumi na mbili wa Yesu.

Sodoma

Ufafanuzi

Sodoma ulikuwa mji kusini mwa kanani ambapo mpwa wa Ibrahimu Lutu aliishi na mke na watoto wake.

Sulemani

Ufafanuzi

Sulemani alikuwa mmoja wa wana wa Mfalme Daudi. Mama yake alikuwa ni Bathsheba.

Tamari

Ufafanuzi

Tamari ni jina la wanawake kadhaa katika Agano la Kale. Ni jina la miji ya maeno kadhaa katika Agano la Kale.

Thomaso

Ufafanuzi

Thomaso alikuwa mmoja wa wanaume kumi na mbili Yesu aliye wachagua kuwa wanafunzi na baadae, mitume. Alijulikana kama "Didimasi" yenye maana ya "pacha."

Ufalme

Ufafanuzi

Neno ufalme linawaelezea watu au vitu ambavyo vinahusiana na mfalme au malkia.

Uri

Ufafanuzi

Uri ulikuwa mji muhimu pembeni mwa Mto Frati katika mji wa zamani wa Kalidea, ambao ulikuwa sehemu ya Mesopotamia. Hili eneo lilikuwa ambapo sasa ni Iraqi.

Uria

Ufafanuzi

Uria alikuwa mwanaume mwenye haki na mmoja wanajeshi hodari wa Mfalme Daudi. Utajwa kama "Uria Mhiti"

Uyahudi, dini ya Kiyahudi

Ufafanuzi

Neno "Uyahudi" inamaanisha dini inayofuatwa na Wayahudi. Inajulikana piakama "dini ya Kiyahudi."

Katika Agano la Kale, neno "dini ya Kiyahudi" inatumika wakati katika Agano Jipya neno "Uyahudi" ndio linatumika. Uyahudi inajumuisha sheria zote za na maelekezo ya Agano la Kale ambayo Mungu aliwapa Wasiraeli kutii. Inajumuisha pia desturi na tamaduni zilizoongezwa katika dini ya Kiyahudi kadri muda ulivyoenda. Wakati wakutafsiri, usemi "dini ya Kiyahudi" au "dini ya Wayahudi" zinaweza kutumika katika Agano la Kale au Jipya. Lakini, neno "Uyahudi" linapaswa kutumika tu kwenye Agano Jipya, kwa sababu neno hilo halikuwepo kabla ya wakati huo

Uzia, Azaria

Ufafanuzi

Uzia alikuwa mfalme wa Yuda akiwa ni umri wa miaka 16 na akatawala miaka 52, ambao ulikuwa utawala mrefu. Uzia alijulikana kama "Azaria."

Watoto, mtoto

Ufafanuzi

Katika Biblia mtoto limetumika kwa namna ya jumla kuelezea mtu ambaye ni mdogo kwa umri. Watoto ni wingi wa neno mtoto.

Yakobo, Israeli

Ufafanuzi

Yakobo alikuwa pacha mdogo aliyekuwa mwana wa Isaka na Rebeka.

Jina la Yakobo linamaanisha "anakamata kisigino" ambao ni usemi unaomaanisha, "hudanganya." Wakati yakobo alipozaliwa, alikuwa akishilia kisigino cha pacha wake Esau. Miaka mingi baadaye, Mungu alibalisha jina la Yakobo kuwa "Israeli," inayomaanisha, "anashindana na Mungu." Yakobo alikuwa mjanja na muongo. Alipata njia ya kupata baraka za mwana wa kwanza na kurithi haki kutoka kwa kaka yake, Esau. Esau alikasirika na kupanga kumuua, kwa hiyo Yakobo akaondoka nchini mwake. Lakini baada ya miaka Yakobo alirudi na wake zake na watoto katika nchi ya Kanaani ambamo Esau alikuwa akiishi, na familia zao ziliishi kwa amani zikiwa jirani. Yakobo alikuwa na wana kumi na mbili. Uzao wao ukawa makabila kumi na mbili ya Israeli. Mwanaume tofauti aitwaye Yakobo ameorodheshwa kama baba wa Yusufu katika ukoo wa Mathayo.

Yehoshafati

Ufafanuzi

Yehoshafati ni jina la angalua watu wawili katika Agano la Kale.

Mtu anayejulikana vizuri zaidi kwa hili jina ni Mfalme Yehoshafati ambaye alikuwa mfalme wa nne kutawala ufalme wa Yuda. Alirejesha amani kati ya Yuda na Israeli, na kuangamiza madhabahu ya miungu wa uongo. Yehoshafati mwingine alikuwa "mtunza kumbukumbu" wa Daudi na Sulemani. Kazi yake ilikuwa pamoja na kuandika nyaraka kwa ajili ya mfalme kusaini na kurekodi historia ya matukio muhumi yaliyotokea katika ufalme.

Yeremia

Ufafanuzi

Yeremia alikuwa nabii wa Mungu katika ufalme wa yuda. Kitabu cha Agano la Kale cha Yeremia kina unabii wake.

Kama manabii wengi, Yeremia mara nyingi ilimbidi kuwaonya watu wa Israeli kuwa Mungu atawaadabisha kwa dhambi zao. Yeremia alitabiri kuwa Wababeli wataiteka Yerusalemu, jambo lililowafanya baadhi ya watu wa Yuda kukasirika. Kwa hiyo walimuweka katika kisima kilichokauka na kumuacha humo kufa. Lakini mfalme wa Yuda aliwaamuru watumishi wake kumuokoa Yeremia kutoka katika kisima. Yeremia aliandika kuwa alitamani macho yake yawe "chemchemi ya machozi," kuonesha masikitiko yake makali kuhusu uasi na mateso ya watu wake.

Yeriko

Ufafanuzi

Yeriko ulikuwa mji wenye nguvu katika nchi ya Kanaani. Ulikuwa magharabi mwa mto wa Yordani na kaskazini mwa Bahari ya Chumvi.

Kama Wakanaani wote, watu wa Yeriko waliabudu miungu ya uongo. Yeriko ulikuwa mji wa kwanza katika nchi ya Kanaani ambao Mungu aliwaambia Waisraeli kuuteka. Wakati Yoshua alipowaongoza Waisraeli dhidi ya Yeriko, Mungu alifanya muujiza mkubwa kuwasaidia kuushinda huo mji.

Yerusalemu

Ufafanuzi

Yerusalemu mwanzoni ulikuwa mji wa zamani wa Kikanaani ambao baadaye ulikuwa mji muhimu zaidi katika Israeli. Inapatikana karibu kilomita 34 magharibi mwa Bahari ya Chumvi na kaskazini mwa Bethlehemu. Bado ni mji mkuu wa Israeli ya leo.

Jina "Yerusalemu" imetajwa kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Yoshua. Majina mengine ya mji huu katika Agano la Kale ni pamoja na "Salemu", "mji wa Yebusi," na "Sayuni." "Yerusalemu" na "Salemu" zote zina msingi wa "amani" katika maana. Yerusalemu mwanzoni ilikuwa ngome ya Yebusi iitwayo "Sayuni" amabyo mfalme Daudi aliikamata na kuifanya kuwa mji wake mkuu. Mwana wa Daudi Sulemani alijenga hekalu la kwanza Yerusalemu, katika mlima Moria, ambao ulikuwa mlima ambao Abrahamu alimtoa Isaka kama sadaka kwa Mungu. Hekalu lilirudiwa kujengwa hapo baada ya kutetezwa na Wababeli. Kwa sababu hekalu lilikuwa Yerusalemu, sherehe kuu za Kiyahudi ziliadhimishwa huko. Watu kawaida husema kwenda "juu" Yerusalemu kwa sababu palikuwa mlimani.

Yese

Ufafanuzi

Yese Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi, na mjukuu wa Ruthu na Boazi.

Yesu, Yesu Kristo, Kristo Yesu

Ufafanuzi

Yesu ni mwana wa Mungu. Jina "Yesu" linamaanisha, "Yahwe anaokoa." Neno "Kristo" ni jina linalomaanisha "mtiwa mafuta" na ni jina jingine la Masihi.

Majina mawili mara nyingi yanaunganishwa kama "Yesu Kristo" au "Kristo Yesu." Majina haya yanasisitiza kuwa mwana wa Mungu ndiye Masihi aliyekuja kuwaokoa watu kutoadhibiwa milele kwa dhambi zao. Katika njia za kimiujiza, Roho Mtakatifu alisababisha mwana wa milele wa Mungu kuzaliwa kama binadamu. Wazazi wake wa duniani waliambiwa na malaika kumuita "Yesu" kwa sababu alikusudiwa kuwaokoa watu kutoka katika dhambi zao. Yesu alifanya miujiza mingi iliyoonesha kuwa yeye ni Mungu na ni Kristo, au Masihi.

Yona

Ufafanuzi

Yona alikuwa nabii wa Kihebrania katika Agano la Kale.

Kitabu cha Yona kinaelezea hadithi ya wakati Mungu alipomtuma Yona kuhubiri kwa watu wa Ninawi. Yona alikataa kwenda Ninawi na badala yake akapanda katika meli iliyokuwa inaelekea mji mwingine. Mungu alisababisha dhoruba kali kuilemea meli. Watu waliukuwa wakidafiri katika meli walipogundua kuwa Yona hakuwaanamtii Mungu, walimtupa katika bahari na dhoruba ikakoma. Yona alimezwa na samaki mkubwa na akawa tumboni mwake kwa siku tatu, mchana na usiku. Baada ya hayo, Yona alienda Ninawi na kuwahubiri watu wa huko, na wakaziacha dhambi zao.

Yoramu

Ufafanuzi

Yoramu mwana wa Ahabu alikuwa mfalme Israeli. Wakati mwingine anajulikana kama "Yehoramu."

Mfalme Yoramu wa Israeli alitawala wakati mmoja kama Yehoramu wa Yuda. Yoramu alikuwa mfalme muovu aliyeabudu miungu ya uongo na kusababisha watu wa Israeli kutenda dhambi. Mfalme Yoramu wa Israeli pia alitawala wakati wa nabii Eliya na Obadia. Mwanamme mwingine aitwaye Yoramu alikua mwana wa mfalme wa Hamathi wakati Daudi ni mfalme.

Yosia

Ufafanuzi

Yosia alikuwa mfalme mcha Mungu aliyetawala juu ya ufalme wa Yuda kwa miaka thelathini na moja. Aliwaongoza watu wa Yuda kutubu na kumuabudu Yahwe.

Baada ya baba yake mfalme Amoni kuuwawa, Yosia akawa mfalme juu ya Yuda akiwa na miaka minane. Katika mwaka wa kumi na nane wa utawala wake, mfalme Yosia alimuamuru kuhani mkuu Hilkia kulijenga tena hekalu la Mungu. Wakati hili likifanyika, vitabu vya Sheria vilipatikana. Vitabu vya Sheria viliposomwa kwa Yosia, alisikitishwa na jinsi watu wake walivyokuwa hawamtii Mungu. Aliamuru kwamba sehemu zote za kuabudia sanamu ziteketezwe na makuhani wa miungu wa uongo wauwawe. Pia aliwaamuru watu kuanza kuadhimisha sherehe ya Pasaka tena.

Yothamu

Ufafanuzi

Katika Agano la Kale kuna wanaume watatu wenye jina Yothamu.

Mwanaume mmoja aitwaye Yothamu alikuwa mwana wa mwisho wa Gideoni. Yothamu alisaidia kumshinda kaka yake mkubwa Abimeleki, ambaye aliwauwa ndugu zake wengine wote. Mwanamme mwingine aitwaye Yothamu alikuwa mfalme juu ya Yuda kwa miaka kumi na sita baada ya kifo cha baba yake Uzia (Azaria). Kama baba yake, Yothamu alimtii Mungu na likuwa mfalme mzuri. Lakini hakuondoa sehemu za kuabudia sanamu na hii ilisababisha watu wa Yuda baadaye kumgeuka Mungu tena.

Yuda

Ufafanuzi

Yuda alikuwa mmoja wa wana wakubwa wa Yakobo. Mama yake alikuwa Lea. Uzao wake uliitwa "kabila la Yuda."

Alikuwa ni Yuda aliyewaambia ndugu zake kumuuza mdogo wao Yusufu kama mtumwa badala ya kumuuacha afe katika shimo. Mfalme Daudi na wafalme wote baada yake walikuwa uzao wa Yuda. Yesu pia alikuwa uzao wa Yuda. Utawala wa Sulemani ulipoisha na taifa la Israeli kugawanyika, ufalme wa Yuda ulikuwa wa sehemu ya kusini mwa nchi. Katika kitabu cha Agano Jipya cha Ufunuo, Yesu anaitwa "Simba wa Yuda." Maneno "Yahudi" na mji wa "Yuda" yametoka katika jina "Yuda."

Yuda, ufalme wa Yuda

Ufafanuzi

Kabila la Yuda lilikuwa kubwa zaidi kati ya makabila kumi na mbili ya Israeli. Ufalme wa Yuda uliundwa na makanila ya Yuda na Benyamini.

Baada ya mfalme Sulemani kufa, taifa la Israeli liligawanyika katika falme mbili: Israeli na Yuda. Ufalme wa Yuda ulikuwa ufalme wa kusini, uliokuwa magharabi mwa Bahari ya Chumvi. Mji mkuu wa ufalme wa Yuda ulikuwa Yerusalemu. Wafalme wanane wa Yuda walimtii Yahwe na kuwaongoza watu kumwabudu yeye. Wafalme wengine wa Yuda walikuwa waovu na kuwaongoza watu kuabudu sanamu. Zaidi ya miaka 120 baada ya Ashuru kuishinda Israeli (ufalme wa kaskazini), Yuda ilitekwa na taifa la Babeli. Wababeli waliangamiza mji na hekalu, na kuwachukua watu wengi wa Yuda kwenda Babeli kama watekwa.

Yuda

Ufafanuzi

Neno "Yuda" linamaanisha sehemu katika nchi ya Israeli ya zamani. Wakati mwingine linatumika katika maana finyu na wakati mwingine katika maana pana.

Wakati mwingine"Yuda" inatumika katika maana finyu kumaanisha jimbo lililo sehemu ya kusini ya Israeli ya zamani magharibi tu mwa Bahari iliyo Kufa. Wakati mwingine "Yuda" inamaana pana na inamaanisha majimbo yote ya Israeli ya zamani, ikiwemo Galilaya, Samaria, Perea, Edomu na Yuda. Maana pana ya Yuda (mfano. Luka 1:5) inaweza kutafsiriwa kama "nchi ya Yuda" na katika maana finyu (mfano Luka 1:39) inaweza kutafsiriwa kama "jimbo la Yuda" kwa sababu hii ndio sehemu ya nchi ya Israeli ya zamani ambapo kabila la Yuda ya lilikuwepo.

Yuda Iskariote

Ufafanuzi

Yuda Iskariote alikuwa mmoja wa mitume wa Yesu. Alikuwa ndiye aliyemsaliti Yesu kwa viongozi wa Kiyahudi.

Jina "Iskariote" inaweza kumaanisha "kutoka Keriothi", labada kuashiria kuwa Yuda alikulia katika huo mji. Yuda Iskariote alitunza fedha ya mitume na mara kwa mara aliiba kutumia kwa ajili yake. Yuda alimsaliti Yesu kwa kuwaambia viongozi wa dini mahali alipo Yesu ili wamkamate. Baada ya viongozi wa dini kumhukumu Yesu kifo, Yuda alijuta kuwa alimsaliti Yesu kwa hiyo akarudisha fedha ya usaliti kwa viongozi wa Kiyahudi na kisha kujiua. Mtume mwingine pia aliitwa Yuda na alikuwa mmoja wandugu wa Yesu. Kuna wanaume wengi waitwao Yuda katika Biblia, kama vile ndugu yake Yesu na mtume mwingine.

Zabuloni

Ufafanuzi

Zabuloni alikuwa mwana wa mwisho wa Yakobo na Lea na ni jina la mojawapo wa makabila kumi na mbili ya Israeli

Zakaria

Ufafanuzi

Zakaria alikuwa nabii aliyetabiri wakati wa utawala wa Mfalme Dario I wa Uajemi. Kitabu cha Zakari katika Agano la Kale kina unabii wake, ambacho kinawasihi mateka waliorudi kulijenga tena hekalu.

Zebedayo

Ufafanuzi

Zebedayo alikuwa mvuvi kutoka Galilaya anayejulikana kwa sababu ya wanawe, Yakobo na Yohana, waliokuwa wanafunzi wa Yesu. Hawa wamekuwa wakitajwa katika Agano Jipya kama "wana wa Zebedayo."

Zerubabeli

Ufafanuzi

Zerubabeli lilikuwa jina la Waisraeli wawili katika Agano la Kale.

agizo

Ufafanuzi

Agizo ni sharti au sheria ya hadhara inayo toa amri au maelekezo ya watu kufuata. Hili neno lina maana sawa na "kisimika"

aibisha, ya kuaibisha

Ufafanuzi

Msemo wa "aibisha" una maana ya kufanya kitu ambacho si cha heshima kwa mtu. Hii inaweza pia kumsababishia mtu huyo aibu au fedheha.

Msemo "ya kuaibisha" inaelezea tendo ambalo ni la aibu au litasababisha mtu kupungukiwa na sifa.

Mara nyingine "kuabisha" inatumika kumaanisha vyombo ambavyo havina kazi kwa jambo lolote muhimu.

Watoto wanaamuriwa kuwaheshimu na kuwatii wazazi wao. Pale ambapo watoto hawatii, wanakuwa hawaheshimu wazazi wao. Wanawafanya wazazi wao kwa njia ambayo haiwapi heshima kwao.

Waisraeli walipunguza sifa kwa Yahwe walipoabudu miungu ya uongo na kutenda mwenendo muovu.

Wayahudi hawakumheshimu Yesu kwa kusema ya kwamba alikuwa amepagawa na pepo.

Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kutenda bila heshima.

Nomino ya "kutoheshimu" inaweza kutafsiriwa kama "kutoheshimu" au "kupotea kwa sifa".

Kutegemea na muktadha, "ya kuaibisha" inaweza kutafsiriwa kama "siyo na heshima" au "ya aibu" au "haifai" au "haina thamani".

aina

Ufafanuzi

Neno "aina" linamaanisha makundi ya vitu vilivyoungana kwa kugawana tabia.

Katika Biblia, usemi huu unatumika bayana kumaanisha aina tofauti za mimea na wanyama ambao Mungu alivyotengeza alipoumba ulimwengu. Mara nyingi kuna tofauti nyingi za spishi katika kila "aina." Kwa mfano, farasi, punda milia, na punda zote ni sehemu ya "aina" moja lakini ni spishi tofauti. Kitu kikuu kinachotofautisha kila "aina" kama kundi tofauti ni kwamba kila mmoja wa hilo kundi anaweza kuzaa zaidi wa "aina" hiyo. Viumbe wa aina tofauti hawawezi kufanya hivyo pamoja.

amri, kuamuru

Ufafanuzi

Kuamuru ni kutoa amri kwa mtu afanye jambo fulani. Amri ni jambo ambalo mtu ameamriwa afanye.

amri

Ufafanuzi

Amri ni sheria maalumu iliyo andikwa inayo toa muongozo watu kuishi.

amri

Ufafanuzi

Amri ni tamko au sheria ambayo inatolewa kwa umma kwa watu wote.

Sheria za Mungu pia zinajulikana kama makataa, maagizo au amri.

Kama sheria na amri, makataa lazima yanapaswa kufuatwa.

Mfano wa makataa ya mtawala wa kibinadamu ulikuwa ni tangazo la Kaisari Augusto ya kwamba kila mmoja aliyeishi katika milki ya Roma alipaswa kurudi nyumbani kwake ili ahesabiwe katika sensa.

Kutoa amri juu ya jambo ina maana ya kutoa amri ambayo ilikuwa lazima kuitii. Hii inaweza kutafsiriwa kama, "kuamuru" au "kuamrisha" au "kutaka rasmi" au "kuweka sheria kwa umma".

Jambo linalofanywa kuwa "amri" kufanyika ina maana ya kwamba "lazima ifanyike" au "imeamuliwa na haitabadilishwa" au "kutamkwa kwa uhakika ya kuwa itafanyika"

bahari, Bahari Kuu, bahari ya magharibi, Bahari ya Medeterenia

Ufafanuzi

Katika Biblia, "Bahari Kuu" au " bahari ya magharibi" inaelezea ile ambayo sasa ujulikana "Bahari ya Medeterenia," ambayo ilikuwa ni eneo la maji lilokulikana na watu wa Biblia.

baya, ovu, uovu

Ufafanuzi

Msemo "baya" na "uovu" yote ina maana ya chochote ambacho kinapingana na tabia takatifu na mapenzi ya Mungu.

Wakati "ubaya" unaweza kuelezea tabia ya mtu, "ovu" unaweza kumaanisha zaidi ya tabia ya mtu. Hata hivyo, misemo yote inafanana maana.

Msemo "uovu" una maana ya hali ambayo watu hufanya maovu.

Matokeo ya uovu yanaonywesha kwa uwazi kwa jinsi watu wanavyotenda vibaya wengine kwa kuwaua, kuiba, kusengenya au kuwa katili na kutokuwa mwema.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, misemo "uovu" na "ovu" inaweza kutafsiriwa kama "ubaya" au "dhambi" au "kinyume na maadili".

Njia zingine za kutafsiri hii zinaweza kujumuisha "isiyo nzuri" au "sio takatifu" au "sio adilifu".

Hakikisha maneno au misemo ambayo inatumika kutafsiri misemo hii kutosha muktadha ambayo ni kawaida katika lugha husika.

bwana, mkuu

Ufafanuzi

Neno "bwana" linamaanisha mtu anayemiliki na mwenye mamlaka juu ya watu wengine.

Neno hili wakati mwingine linatafsiriwa kama "mkuu" wakati wakumuita Yesu au wakati wakumaanisha mtu anayemiliki watumwa.

chafu

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "chafu" utumika kama fumbo kueleza vitu ambavyo Mungu alitangaza sio sahihi kwa watu wake kugusa,kula, au kutoa dhabihu.

chukiza, chukia

Ufafanuzi

Msemo "chukiza" unaelezea jambo ambalo linapaswa kutopendwa na kukataliwa. "Kuchukia" kitu ina maan ya kutokipenda kabisa.

Mara nyingi Biblia huzungumzia kuhusu kuchukia uovu. Hii ina maana kuchukia uovu na kuukataa.

Mungu alitumia neno "chukiza" kuelezea matendo maovu ya wale waliomwabudu miungu ya uongo.

Waisraeli waliamriwa "kuchukia" matendo ya dhambi, na kinyume na maadili ambayo baadhi ya makundi ya watu majirani waliyafanya.

Mungu aliyataja matendo yote ya uasherati kuwa "chukizo".

Uaguzi, uchawi, na sadaka za mtoto yote yalikuwa "chukizo" kwa Mungu.

Msemo "chukizo" unaweza kutafsiriwa kama "uovu mbaya" au "inayochukiza" au "inayostahili kukataliwa".

Inapotumika na kiumbe takatifu "chukizo kwa" waovu, hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukuliwa kutotamanika kwa" au "kutokuwa na ladha" au "kukataliwa na"

Mungu aliwaambia Waisraeli "kuchukia" aina kadhaa ya wanyama ambao Mungu alitamka kuwa "wachafu" na kutofaa kwa chakula. Hii inaweza kutafsiriwa kama "kuchukia kwa uzito" au "kukataa" au "kuchukua kama kutokubalika".

dada

Ufafanuzi

Dada ni mtu wa jinsi ya kike anaye shiriki wastani wa mzazi mmoja na mtu mwingine.

damu

Ufafanuzi

Neno "damu" linamaanisha kimiminika chekundu kinachotoka katika ngozi ya mtu panapokuwa na jeraha au kidonda. Damu inaleta viini lishe vya uhai katika mwili wote wa mtu.

Maoni ya Kutafasiri

desturi

Ufafanuzi

Neno "desturi" la eleza tamaduni na mapokeo yaliyo tunzwa kwa muda na yanayo pokelewa na vizazi vijavyo.

dhabihu, sadaka

Ufafanuzi

Katika Biblia, maneno "dhabihu" na "sadaka" ya husu zawadi maalumu anazopewa Mungu kama kitendo cha kumuabudu. Watu pia walitoa sadaka kwa miungu ya uongo.

dhahabu

Ufafanuzi

Dhahabu ni chuma cha manjano, cha ubora wa juu sana kinachotumika kutengeneza vito na vyombo vya dini. Ilikuwa chuma ya thamani zaidi katika kipindi cha zamani.

Katika kipindi cha Biblia, aina nyingi tofauti ya vyombo vilitengezwa kwa dhahabu ngumu au kufunikwa na safu nyembamba ya dhahabu.

Vyombo hivi vilijumuisha heleni na vito vingine, sanamu, madhabahu, na vyombo vingine vilivyotumika katika tabenakulo au hekalu, kama vile sanduku la agano.

Katika Agano la Kale, dhahabu ilitumika kama njia ya kubadilishana katika kununua na kuuza. Ilipimwa juu ya mizani kupata thamani yake.

Baadaye, dhahabu na vyuma vingine kama vile fedha vilitumika kutengeneza sarafu kutumiwa kununua na kuuza.

Pale inapomaanisha kitu ambacho sio dhahabu ngumu, lakini ina safu nyembamba tu ya dhahabu, msemo "ya dhahabu" au "kufunikwa kwa dhahabu" inaweza kutumika.

Mara nyingi chombo kinaelezewa kama "rangi ya dhahabu" ambayo ina maana ina rangi ya njano ya dhahabu, lakini haijatengenezwa kwa dhahabu.

dhalimu, kwa dhalimu, udhalimu

Ufafanuzi

Maneno "dhalimu" na "kwa dhalimu" yanaeleza kutendea watu pasipo haki, na mara nyingi, namna ya kudhuru.

dhambi,yenye dhambi, mwenye dhambi, kufanya dhambi

Ufafanuzi

Neno "dhambi" la husu matendo, mawazo, na maneno yaliyo kinyume dhidi ya mapenzi ya Mungu na Sheria. Dhambi yaweza maanisha kutofanya kitu Mungu alicho tuambia tufanye.

dhihaki

Ufafanuzi

Neno kudhihaki ni kumtania mtu, kwa namna mbaya.

dhiki

Ufafanuzi

Neno "dhiki" la husu kipindi cha ugumu, mateso, na msongo wa mawazo.

dunia, kidunia

Ufafanuzi

Msemo "dunia" una maana ya dunia ambayo wanadamu wanaishi, pamoja na kila aina ya viumbe hai.

"Dunia" pia inaweza kumaanisha ardhi au udongo ambayo hufunika nchi.

Msemo huu mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha watu wanaoishi juu ya dunia.

Misemo, "acha dunia iwe na furaha" na "Atahukumu dunia" ni mifano ya matumizi ya tamathali ya msemo huu.

Msemo "kidunia" mara kwa mara humaanisha vitu vya kimwili kinyume na vitu vya kiroho.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao lugha ya taifa hutumia kumaanisha sayari ya dunia ambayo tunaishi.

Kulingana na muktadha, "dunia" pia inaweza kutafsiriwa kama, "ulimwengu" au "ardhi" au "udongo".

Unapotumika kitamathali, "dunia" inaweza kutafsiriwa kama, "watu wa dunia" au "watu wanaoishi juu ya dunia" au "kila kitu juu ya dunia".

Njia za kutafsiri "kidunia" zinaweza kujumuisha, "kimwili" au "vitu vya dunia hii" au "vinavyoonekana".

elekeza, maelekezo

Ufafanuzi

Usemi "elekeza" na "maelekezo" yanamaanisha kutoka uongozo bayana ya nini cha kufanya.

"Kutoa maelekezo" inamaanisha kumuambia mtu bayana kitu anachotakiwa kufanya. Yesu alipowapa wanafunzi wake mikate na samaki kuwapa watu, aliwapa maelekezo bayana ya jinsi ya kuifanya. Kulingana na mazingira, neno "elekeza" inaweza kutafsiriwa kama "kumuambia" au "kuongoza" au "kufundisha" au "kutoa maelekezo kwa." Neno "maelekezo" inaweza kutafsiriwa kama "uongozo" au"ufafanuzi" au "kitu alichokuambia kufanya." Mungu akikupa maelekezo, huu usemi wakati mwingine unatafsiriwa kama "kuamuru" au "kuamrisha."

erevu

Ufafanuzi

Neno "erevu" la elezea mtu enye akili na mahiri, hususani katika mambo ya utendaji.

fahamu, ufahamu

Ufafanuzi

Neno "fahamu" lina maana ya kusikia ua kupokea taarifa na kuelewa ina maana gani.

fedha

Ufafanuzi

Fedha ya ng'aa, ni ya chuma ya kijivu inayo tumika kufanya sarafu, mikufu, vyombo, na mapambo.

filimbi, zumari

Ufafanuzi

Katika kipindi cha Biblia, zumari ilikuwa vyombo vya muziki iliyotengenezwa kwa mfupa au mbao na mashimo inayoruhusu sauti kutoka nje. Filimbi ilikuwa aina ya zumari.

Zumari nyingi ilikuwa na matete yaliyotengenezwa kutoka kwa nyasi nene ambayo hutikisika pale hewa inapopulizwa kwake.

Zumari bila matete mara kwa mara ilijulikana kama "filimbi".

Mfugaji alicheza filimbi kutuliza mifugo yao ya kondoo.

Zumari na filimbi ilitumika kucheza muziki wa huzuni na furaha.

fundisha, kufundisha, mwalimu, fundishwa

Ufafanuzi

Haya maneno "fundisha" na "kufundisha" yanaeleza kuambia watu wengine taarifa wasiyo ijua kabla. Mara nyingi maelezo utolewa rasmi au kwa utaratibu.

funga

Ufafanuzi

Neno "funga" linamaanisha kukaza kitu kwa usalama. Kitu kilichofungwa au kuunganishwa pamoja kinaitwa "muungano". Neno "kufunga" ni sehemu ya neno hili katika wakati uliopita.

Maoni ya Tafasiri

Neno "funga" laweza pia kutafasiriwa kama "kaza" au "zungushia"

funga

Ufafanuzi

Msemo "kufunga" una maana ya kuacha kula chakula kwa kipindi fulani, kama vile siku moja au zaidi. Mara nyingi inajumulisha kutokunywa.

Kufunga kunaweza kusaidia watu kumlenga Mungu na kuomba bila kutolewa mawazo kwa kuandaa chakula na kula.

Yesu aliwalaani viongozi wa dini wa Kiyahudi kwa kufunga kwa sababu ambazo sio sahihi. Walifunga ili kwamba wengine wafikiri kuwa wao ni watakatifu.

Mara nyingi watu walifunga kwa sababu walikuwa na huzuni sana au majonzi juu ya jambo.

Kitenzi cha "kufunga" kinaweza kutafsiriwa kama "kujizuia kula" au "kutokula".

Nomino ya "funga" inaweza kutafsiriwa kama "muda wa kutokula" au "muda wa kujizuia na chakula"

funga

Ufafanuzi

Msemo "funga" una maana ya kufunga kitu kuzunguka kitu kingine. Mara kwa mara humaanisha kutumia mkanda kuzunguka kiuno kuweka kanzu au gwanda mahali pake.

Msemo wa kibliblia unaojulikana, "funga kiuno" una maana ya kuchomekea chini ya vazi ndani ya mkanda kuruhusu mtu kusogea kwa uhuru zaidi, mara nyingi kufanya kazi.

Msemo una maana ya kujiweka tayari kufanya kazi au kujiandaa kufanya kitu kigumu.

Msemo "funga kiuno" unaweza kutafsiriwa kutumia msemo katika lugha husika yenye maana moja. Au inaweza kutafsiriwa bila tamathali kama "jiandae kwa ajili ya tukio" au "jiandae"

Msemo "kufngwa na" inaweza kutafsiriwa kama "kuzungushwa na" au "kufungwa na".

furaha, mwenye furaha

Ufafanuzi

Furaha ni hisia ya kupendezwa au kuridhika inayotoka kwa Mungu. Maana inayokaribiana, "mwenye furaha" inaelezea mtu anayejisikia vizuri sana na mwenye furaha nyingi.

Mtu anasikia furaha anapokua anahisi kuwa anachopitia ni chema sana. Mungu ndiye anayegawa furaha ya kweli kwa watu. Kuwa na furaha hakutegemei hali nzuri. Mungu anaweza kuwapa watu furaha hata kama vitu vigumu kabisa vinatokea katika maisha yao. Sehemu zingine zinaelezwa kama za furaha, kama nyumba na miji. Hii inamaanisha kuwa watu waiishio humo ni wenye furaha.

fuvu

Ufafanuzi

Neno "fuvu" la eleza kichwa cha mifupa kisicho na nyama cha mtu au mnyama

geuka, geuka kando, geuka nyuma

Ufafanuzi

"Kugeuka" kuna maana ya kubadili mwelekeo wa mwili au kusababisha kitu kingine kubadilisha muelekeo.

ghadhabu, hasira

Ufafanuzi

Ghadabu ni hasira kali ambayo mara nyingine hudumu kwa mda mrefu. Hii maranyingi huelezea hukumu ya Mungu ya haki na adhabu ya watu walioasi dhidi yake.

habari njema, injili

Ufafanuzi

Msemo "injili" una maana ya "habari njema" na una maana ya ujumbe au tangazo ambalo linawaambia watu jambo ambalo lina manufaa kwako na kuwapa furaha.

Katika Biblia, msemo huu humaanisha ujumbe kuhusu wokovu wa Mungu kwa watu kupitia sadaka ya Yesu msalabani.

Katika Biblia nyingi za Kiingereza, "habari njema" mara nyingi hutafsiriwa kama "injili" na pia hutumika katika misemo kama vile "injili ya Yesu Kristo" au "injili ya Mungu" na "injili ya ufalme".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia tofauti za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "jumbe mzuri" au "tangazo zuri" au "ujumbe wa Mungu wa wokovu" au "mambo mazuri Mungu anayofundisha kuhusu Yesu".

Kulingana na muktadha, njia za kutafsiri msemo "habari njema ya" inaweza kujumuisha "ujumbe/havbari njema" au "ujumbe mzuri kutoka" au "mambo mazuri Mungu husema juu ya" au "kile Mungu anasema kuhusu jinsi anavyookoa watu".

haki, adilifu

Ufafanuzi

Maneno haya yanamaanisha kuwatendea watu vyema kulingana na sheria za Mungu. Sheria za binadamu zinazo onesha kiwango cha Mungu cha tabia sawa kwa watu wengine.

Kuwa wa "haki" ni kutenda ya haki na mema kwa mtu mwingine. Pia inaashiria uaminifu na msimamo kufanya kilicho adilifu machoni pa Mungu. Kutenda kwa "haki" inamaanisha kuwatendea watu kwa njia iliyo sawa, nzuri na ya kufaa kulingana na sheria za Mungu. Kupokea "haki" inamaanisha kutendewa vyema chini ya sheria, aidha kulindwa kwa sheria au kuadhibiwa kwa kuvunja sheria. Wakati mwingine neno "haki" lina maana pana ya "utakatifu"au "kufuata sheria za Mungu."

hakimu

Ufafanuzi

Hakimu ni mtu anayeamua nini kiko sawa au la ukiwepo ugomvi kati ya watu, mara nyingi katika mambo yanayofungamana na sheria.

Katika Biblia, Mungu mara nyingi anatajwa kama hakimu kwa sababu yeye ndiye hakimu aliye kamili anayefanya maamuzi ya mwisho kuhusu nini kiko sawa au kisicho sawa. Baada ya watu wa Israeli kuingia nchi ya Kanaani na kabla hawajawa na wafalme wa kuwatawala, Mungu aliwapa viongozi waitwao "waamuzi" kuwaongoza nyakati za shida. Mara nyingi waamuzi hao walikuwa viongozi wa kijeshi waliowaokoa Waisraeli kwa kuwaangamiza maadui zao. Neno "hakimu" linaweza pia kuitwa "muamuzi" au "kiongozi" au "mkombozi" au "gavana," kutegemea na mazingira.

halali, ipasavyo, kinyume na sheria

Ufafanuzi

Msemo "halali" unamaanisha kitu kinachoruhusiwa kufanywa kulingana na sheria au mahitaji mengine. Kinyume cha hiki ni "kinyume na sheria" inyomaanisha "sio halali."

Katika Biblia, kama kitu kinasemwa kuwa "halali" inamaanisha inaruhusiwa na sheria ya kimaadili ya Mungu, au kwa sheria ya Musa au sheria zingine za Kiyahudi. Kitu ambacho "sio halali" "hakiruhusiwi" na sheria hizo. Kufanya kitu "ipasavyo" inamaanisha kuifanya "sawa" au "katika njia sahihi." Mambo mengi Wayahudi waliyoona ni halali au sio halali hayakuwa kwenye makubaliano na sheria za Mungu kuhusu kuwapenda wengine. Kulinga na mazingira, njia za kuafsiri "halali" ni pamoja na, "kuruhusu" au "kulingana na sheria ya Mungu" au "kufuatana na sheria zetu" au "sawa" au inafaa." Msemo "Je ni halali" inaweza pia kutafsiriwa kama "Je, sheria zetu zinaruhusu" au "Hilo ni jambo ambalo sheria zetu zinaruhusu?"

hati

Ufafanuzi

Zamani za kale, hati ilikuwa aina ya kitabu kilicho tengenezwa kwa karatasi ndefu ya mafunjo au ngozi.

hatia, mwenye hatia

Ufafanuzi

Msemo "hatia" una maana ya ukweli wa kufanya dhambi au kutenda kosa.

Kuwa na "hatia" ina maana ya kuwa umefanya kitu kiouvu kimaadili, yaani, kutomtii Mungu.

Kinyume cha "mwenye hatia" ni "asiye na hatia".

Mapendekezo ya Tafsiri

Baadhi ya lugha zinaweza kutafsiri "hatia" kama "uzito wa dhambi" au "hesabu ya dhambi".

Njia za kutafsiri "kuwa na hatia" inaweza kujumuisha neno au msemo ambayo ina maana ya "kuwa katika kosa" au "kuwa umefanya jambo ovu kimaadili" au "kuwa umefanya dhambi".

haya, aibu

Ufafanuzi

Neno "haya" la husu hali ya maumivu ya kuumizwa kihisia kwa kuaibishwa kwasababu ya kitu cha fedheha ambacho yeye au mtu mwingine amefanya.

hekalu

Ufafanuzi

Hekalu lilikuwa ni jengo lililo zungukwa na kuta za nyuani ambapo Waisraeli walikuja kuombaa na kutoa dhabihu kwa Mungu. Lilikuwa Mlima Moria katika mji wa Yerusalemu.

hema

Ufafanuzi

Hema ni hifadhi linalo hama lililo tengenezwa na uzi uliyo zungushiwa kwenye nguzo pamoja.

heshima, kuheshimu

Ufafanuzi

Istilahi 'heshima' na 'kuheshimu' hurejelea kitendo cha kumpa mtu heshima au kumstahi mtu. Heshima mara kwa mara hutolewa kwa mtu mwenye hadhi ya juu na umuhimu wa juu kama vile mfalme au Mungu. Mungu pia huwaagiza Wakristo wote kuwaheshimu watu wengine, lakini si kutafuta heshima zao wenyewe. Watoto wameagizwa kuwatii wazazi wao na kuwatii. Maneno kama 'heshima' na 'utukufu' ni maneno yanayoenda kwa pamoja hasa yanapomrejelea Yesu. Heshima kwa Mungu inajumuisha kumshukuru na kumsifu Mungu, na kuonesha heshima kwa kumtii Mungu na kuishi katika njia inayoonesha kuwa Mungu ni Mkuu.

Mapendekezo Njia nyingine za kutafsiri neno 'heshima' linajumuisha 'staha' Neno 'kuheshimu' laweza kutafsiriwa kama 'kuonesha heshima maalumu kwa au kuonesha mtu thamani ya juu.

hukumu

Ufafanuzi

Neno "hukumu" mara nyingi humaanisha kufanya maamuzi kama jambo liko sawa kimaadili au kama haliko sawa.

"Hukumu ya Mungu" mara nyingi humaanisha uamuzi wake kulaani kitu au mtu muovu. Hukumu ya Mungu mara nyingi huhusisha kuwaadhibu watu kwa dhambi zao. Neno "hukumu" inaweza pia kumaanisha "kulaani." Mungu anawaagiza watu wake kutowahukumu wengine kwa naamna hii. Maana nyingine ni "uamuzi kati ya" au "kuhukumu kati ya", yaani kuchagua ni mtu gani yuko sahihi katika ugomvi kati yao. Katika mazingira mengine, "hukumu" za Mungu ni yale aliyeamua ni mema na yenye haki. Zinafanana na amri, sheria na maagizo yake. "Hukumu" inaweza kumaanisha uwezo wa busara wa kufanya maamuzi. Mtu anayekosa "hukumu" hana hekima kufanya maamuzi ya busara.

huru, uhuru

Ufafanuzi

Msemo "huru" au "uhuru" una maana ya kutokuwa katika utumwa au aina yoyote ya kifungo.

Msemo "kumweka mtu huru" au "kumweka huru mtu" ina maana ya kutoa njia kwa mtu ili asiwe katika utumwa au kifungo.

Katika Biblia, misemo hii mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha jinsi gani muamini katika Yesu hayupo chini ya nguvu ya dhambi.

Kuwa "huru" au "uhuru" inaweza kumaanisha kutohitajika kutii Sheria ya Musa, lakini badala yake kuwa huru kuishi kwa mafunzo na uongozi wa Roho Mtakatifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "huru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kutofungwa" au "kutokuwa katika utumwa" au "kutokuwa katika kifungo".

Msemo "ukuru" unaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana, "hali ya kuwa huru" au "hali ya kutokuwa mtumwa" au "kutofungwa".

Msemo "kuweka huru" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa huru" au "kukomboa mtu kutoka utumwani" au "kumwachia kutoka kifungoni".

Mtu ambaye "amewekwa huru" atakauwa "ameachiliwa" au "kutolewa kutoka" katika kifungo au utumwa.

iga, mwigaji

Ufafanuzi

Maneno "iga" na "mwigaji" yanamaanisha kumuiga mtu mwingine na kuigiza sawa na mtu huyu afanyavyo.

Wakristo wanafundishwa kumuiga Yesu Kristo kwa kumtii Mungu na kuwapenda wengine, kama Yesu alivyofanya. Mtume Paulo aliliambia kanisa la awali kumuiga yeye, kama yeye alivyomuiga Yesu.

imani, aminifu,

Ufafanuzi

Neno "imani" la eleza kuamini kwamba kitu au mtu ni wa kweli au tegemeo. Mtu "mwaminifu" na weza kuwa tegemevu kufanya kitu na kusema kilicho sawa na kweli.

imani

Ufafanuzi

Kwa ujumla, msemo "imani" una maana ya imani, au matumaini ndani ya mtu au jambo.

"Kuwa na imani" na mtu ni kuamini ya kwamba kile anachosema na kufanya ni kweli na kuaminika.

"Kuwa na imani na Yesu" ina maana ya kuamini mafundisho yote ya Mungu kuhusu Yesu. Ina maana haswa ya kwamba watu wanamuamini Yesu na sadaka yake kuwasafisha kutoka kwa dhambi zao na kuwakomboa kutoka na adhabu wanayostahili kwa sababu ya dhambi yao.

Imani ya kweli kwa Yesu itamsababisha mtu kuzaa matunda mazuri ya kiroho au tabia kwa sababu ya Roho Mtakatifu anayeishi ndani yake.

Mara kwa mara "imani" kwa ujumla ina maana ya mafundisho yote kuhusu Yesu, yaani kama msemo, "ukweli wa imani".

Katika muktadha kama wa "tunza imani" au "telekeza imani", msemo "imani" una maana ya hali ya kuamini mafundisho yote kuhusu Yesu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika baadhi ya muktadha, "imani" inaweza kutafsiriwa kama "imani" au "hatia" au "kujiamini" au "kuamini".

Kwa baadhi ya lugha misemo hii inaweza kutafsiriwa kutumia aina za kitenzi cha "imani".

inua, inuka

Ufafanuzi

Inua, inua juu inamaana ya kuinua kitu juu au kukuweka juu.

ishara, kithibitisho, ukumbusho

Ufafanuzi

Ishara ni kitu, tukio, au kitendo kinacho wasilisha maana maalumu.

jangwa, njika

Ufafanuzi

jangwa, au nyika, ni sehemu iliyokauka, isiyokuwa na mazao ambayo mimea na miti michache inaweza kuota pale.

Jangwa ni eneo la ardhi lenye tabia ya nchi ya ukavu na mimea na wanyama wachache.

Kwa sababu ya mazingira magumu, watu wachache sana wanaweza kuishi katika jangwa, kwa hiyo pia inajulikana kama "nyika".

"Nyika" inaleta maana ya sehemu iliyojitenga, ya kipekee mbali na watu.

Neno hili pia linaweza kutafsiriwa kama "sehemu ya jangwa" au "sehemu iliyojitenga" au "sehemu isiyokaliwa".

jasiri, ujasiri, ushujaa

Ufafanuzi

Maneno yote haya yanamaanisha kuwa na ujasiri na ushujaa kwa kuongea ukweli kuhusu jambo halali hata kama ni vigumu na hatari.

jikwaa

Ufafanuzi

Neno "jikwaa" lina maana ya "karibu kuanguka" wakati wakutembea au kukimbia. Kujikwaa juu ya kitu.

jina

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "jina" linatumika kwa mifano kadhaa.

jirani

Ufafanuzi

Neno "jirani" mara kwa mara la mueleza mtu anaye ishi karibu. Pia yaweza kueleza kwa ujumla mtu anaye ishi katika jamii moja au kundi la watu.

jitu

Ufafanuzi

Jitu mara nyingi ilimaanisha mtu ambaye alikuwa na ukubwa usio wa kawaida wa urefu na nguvu.

Goliati, mwanajeshi wa Kifilisti aliyepigana na Daudi, aliitwa Daudi kwa sababu alikuwa mrefu sana, mkubwa, na mtu mwenye nguvu.

Wapelelezi wa Israeli waliotafiti nchi ya Kaanani walisema ya kwamba watu wanaoishi pale walikuwa kama majitu.

jiwe, kupiga jiwe

Ufafanuzi

Jiwe ni mwamba mdogo. Neno "kupiga jiwe" la husu kurusha mawe na majabali makubwa kwa mtu kuweza kumuua.

joho

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "joho" uleza vazi lililo valiwa chini ya ngozi, chini nguo nyingine.

juma

Ufafanuzi

Neno "juma" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha kuishia siku saba.

juu, juu sana

Ufafanuzi

Maneno " juu" na " juu sana" ni misemo inayo maanisha, "mbinguni."

kabila

Ufafanuzi

Kabila ni kundi la watu waliyo toka kwa babu mmoja.

kaburi

Ufafanuzi

Neno "kaburi" ni sehemu watu wanapo weka mwili wa mtu aliye kufa.

kama, mfano

Ufafanuzi

Misemo "kama" na "mfano" inamaanisha kitu kuwa sawa au kufanana na kitu kingine.

Neno "kama" pia inatumika katika mithali zinazoitwa "mfanano" ambapo kitu kinalinganishwa na kitu kingine, kawaida huonyesha tabia zinazolingana. Kwa mfano, "nguo zake zinang'aa kama jua" na "sauti ilivuma kama ngurumo." "Kuwa kama" au "kusikika kama" au "kuonekana kama" kitu au mtu inamaana kuwa na sifa zinazofanana na kitu anacholinganishwa nacho au mtu anayelingishwa naye. Watu waliumbwa katika "mfano" wa Mungu. Inamaanisha wana sifa au tabia ambazo ni "kama" au "zizafanana" na sifa ambazo Mungu anazo, kama uwezo wakufikiri, kuhisi na kuwasiliana. Kuwa na "mfano" wa kitu au mtu inamaana kuwa na tabia zinazofanana na hicho kitu au mtu.

kamata

Ufafanuzi

Neno "kamata" la maanisha kuchukuwa au kumteka mtu au kitu kwa nguvu. Inaweza maanisha ya kumzidi nguvu au kumtawala mtu.

kanyaga

Ufafanuzi

"Kanyaga" ina maana ya kukanyaga kitu na kukisaga kwa mguu. Neno pia utumika kimfano katika Biblia kumaanisha "haribu" au "shinda" au "aibisha."

kazi, vitendo, matendo

Ufafanuzi

Katika Biblia maneno kazi, vitendo, matendo ni vitu ambavyo Mungu au watu hufanya.

kazi, mfanyakazi

Ufafanuzi

Neno "kazi" linamaanisha kufanya kazi ngumu ya aina yoyote.

Kwa ujumla, kazi ni shughuli inayotumia nguvu, mara nyingi inaashiria kuwa shughuli ni ngumu. Mfanyakazi ni mtu afanyae aina yoyote ya kazi.

kiapo, kuapa,

Ufafanuzi

Katika Biblia, kiapo ni ahadi rasmi ya kufanya kitu. Mtu anaye kiapo anapswa kutimiza hiyo ahadi. Kiapo kinahusu kuwa mwaminifu na wa kweli.

kiasi

Ufafanuzi

Kiasi ni uwezo wa kutawala tabia ya mtu ili kuepusha kutenda dhambi.

kifo, kufa, mfu

Ufafanuzi

Msemo huu unatumika kumaanisha vyote kifo cha kimwili na kiroho. Kimwili, ina maana ya mwili wa kihalisia wa mtu kukoma kuishi. Kiroho, ina maana ya wenye dhambi kutengwa na Mungu mtakatifu kwa sababu ya dhambi yao.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kutafsiri msemo huu, ni vyema kutumia neno la kila siku au usemi ambao una maana ya kifo katika lugha husika.

Katika baadhi ya lugha, "kufa" inaweza kuelezwa kama "kutokuishi". Msemo "kufa" unaweza kutafsiriwa kama "kutokuwa hai" au "kutokuwa na uhai wowote" au "kutokuishi".

Lugha nyingi zinatumia msemo wa tamathali kuelezea kifo, kama "kuondoka" kwa Kiingereza. Ila katika Biblia ni bora kutumia msemo wa moja kwa moja kwa ajili ya kifo ambao unatumika kila siku katika lugha.

Katika Biblia, uhai na kifo wa kimwili mara kwa mara hulinganishwa na uhai na kifo cha kiroho. Ni muhimu katika tafsiri kutumia neno moja au msemo kwa ajili kifo cha kimwili na kifo cha kiroho.

Katika baadhi ya lugha inaweza kuwa wazi zaidi kusema, "kifo cha kiroho" ambapo muktadha unahitaji maana hiyo. Watafsiri wengine wanaweza kuhisi ni bora kusema, "kifo cha kimwili" katika muktadha ambapo unalinganishwa na kifo cha kiroho.

Msemo wa "wafu" ni kivumishi chenye maana ya watu waliokufa. Baadhi ya lugha zitatafsiri hili kama, "watu waliokufa" au "watu ambao wamekufa"

kikapu

Ufafanuzi

Neno "kikapu" linamaanisha chombo kilichotengenezwa kwa kusukwa.

kiti cha enzi

Ufafanuzi

Kiti cha enzi ni kiti ambacho mfalme ana keti kuamua mambo muhimu na kusikiliza maombi ya watu wake.

kizazi

Ufafanuzi

Msemo "kizazi" una maana ya kundi la watu ambao wote wamezaliwa katika kipindi cha kufanana.

Kizazi pia kinaweza kumaanisha kipindi cha muda. Katika kipindi cha Biblia, kizazi kilichukuliwa kuwa kama miaka 40.

Wazazi na watoto waoo wanatoka katika vizazi viwili tofauti.

Katika Biblia, msemo "kizazi" pia hutumika kitamathali kumaanisha kwa ujumla watu ambao huwa na tabia za kufanana.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo " kizazi hiki" au "watu wa kizazi hiki" unaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa" au "nyie watu".

"Kizazi hiki kiovu" inaweza kutafsiriwa kama "watu hawa waovu wanaoishi sasa".

Msemo "kutoka kizazi hadi kizazi" au "kutoka kizazi kimoja hadi kingine" inaweza kutafsiriwa kama "watu wanaoishi sasa, pamoja na watoto na wajukuu wao" au "watu katika kipini chote" au "watu wa kipindi hili na vipindi vya baadaye" au "watu wote na uzao wao".

"Kizazi kinachokuja kitamtumikia; watawaambia kizazi kifuatacho juu ya Yahwe" inaweza kutafsiriwa kama "Watu wengi hapo baadaye watamtumikia Yahwe na kuwaambia watoto na wajukuu wao juu yangu".

kondoo, kondoo dume, kondoo jike

Ufafanuzi

"kondoo" ni mnyama wa saizi ya kati wa miguu minne mwenye manyoya mwili mzima.

kubeba

Ufafanuzi

Neno "kubeba" linamaanisha "kubeba" kitu fulani. Lakini pia kuna kuna matumizi ya tamathari mbalimbali ya neno hili.

kufuru

Ufafanuzi

Neno la "kufuru" lina maana ya kuharibu au kuchafua sehemu takatifu au kitu katika namna ambayo haikubaliki kutumika katika kuabudu.

Mara kwa mara kukufuru kitu inahusisha kuonyesha okosefu mkubwa wa keshima kwake.

Kwa mfano, wafalme wa kipagani walikufuru vyombo maalumu kutoka hekalu la Mungu kwa kuvitumia kwa ajili ya sherehe katika kasri zao.

Mifupa kutoka watu waliokufa ilitumika na maadui kukufuru madhabahu katika hekalu la Mungu.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kutokuwa mtakatifu" au "kumvunjia heshima kwa kufanya asiwe mtakatifu" au "kukufuru kwa kuvunja heshima" au "kusababisha kutokuwa msafi".

kuhani mkuu

Ufafanuzi

Neno 'kuhani mkuu' hurejelea kuhani maalumu aliyekuwa ameteuliwa kutumika kwa mwaka mmoja kama kiongozi wa makuhani wote wa Wayahudi. Kuhani mkuu alikuwa na majukuu mahususi. Alikuwa ni mtu pekee aliyeruhusiwa kuingia mahali patakatifu sana katika hekalu ili kutoa sadaka maalumu mara moja kwa mwaka. Waisraeli walikuwa na makuhani wengi sana, lakini walikuwa na kuhani mkuu mmoja kwa muda fulani. Kipindi alichokamatwa Yesu, Kayafa alikuwa kuhani mkuu. Anasi, Baba mkwe wa Kayafa anatajwa mara kadhaa kwasababu alikuwa kuhani mkuu hapo awali, huenda alikuwa bado na mamlaka na nguvu fulani juu ya watu.

Mapendekezo ya tafsiri 'Kuhani mkuu" tunaweza kutafsiri kama "kuhani wa daraja la juu"

kujua, ufahamu, kufanya kujulikana

Ufafanuzi

"Kujua" inamaanisha kuelewa kitu au kuwa na ufahamu wa jambo. Usemi "kufanya kujulikana" ni usemi unaomaanisha kutoa taarifa.

Neno "ufahamu" linamaanisha taarifa ambazo watu wanajua. Inaweza kuwa kujua vitu katika dunia ya kimwili na kiroho. "Kujua kuhusu" Mungu inamaanisha kuelewa mambo kumhusu kwa sababu ya yale aliyotufunulia. "Kumjua" Mungu inamaanisha kuwa na uhusiano naye. Hii inamaanisha pia kuwajua watu wake. Kujua mapenzi ya Mungu inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale aliyetoagiza, au kuelewa ni nini anataka mtu afanye. "Kujua Sheria" inamaanisha kuwa na ufahamu wa yale Mungu aliyoagiza au kuelewa yale Mungu aliyoagiza katika sheria alizompa Musa. Wakati mwingine "ufahamu" unatumika kama neno lingine la "hekima," linalojumuisha kuishi katika njia inayompendeza Mungu. "Ufahamu wa Mungu" wakati mwingine unatumika kama njia nyingine ya kusema hofu ya Yahwe.

kukesha

Ufafanuzi

Katika nyakati za Biblia, "kukesha" ulikuwa wakati wa usiku ambao katika huo mlinzi au mwangalizi wa mji alikuwa kazini akiangalia hatari yoyote kutoka kwa maadui.

kulala na, kuwa na mahusiano na, fanya mapenzi

Ufafanuzi

Katika Biblia, haya maneno ni tafsida yanayo eleza kufanya ngono.

kulewa, mlevi

Ufafanuzi

Msemo "kulewa" ina maana ya kuleweshwa kutokana na kunywa kileo.

"Mlevi" ni mtu ambaye hulewa mara kwa mara. Mtu wa aina hii anajulikana kama "mlevi".

Biblia inawaambia waumini kutolewa na vilevi, lakini kutawaliwa na Roho Mtakatifu wa Mungu.

Biblia inafundisha ya kwamba ulevi sio busara na inamshawishi mtu kutenda dhambi kwa njia zingine.

Njia zingine za kutafsiri "kulewa" zinaweza kujumuisha "levya" au "kulewa" au "kupata kilevi kingi sana" au "kushiba kwa kinywaji chachu"

kumwaga damu

Ufafanuzi

Neno "kumwaga damu" linamaanisha kifo cha mwanadamu kwa sababu ya mauaji, vita, au sababu nyingine ya kikatiri.

Maoni ya Kutafasiri

kundi, mifugo

Ufafanuzi

Katika Biblia "kundi" ina maana ya kundi la kondoo na mbuzi na "mifugo" ina maana ya kikundi cha ng'ombe, maksai, au nguruwe.

Lugha tofauti zinaweza kuwa na njia tofauti za kutaja makundi ya wanyama au ndege.

Kwa mfano, katika Kiingereza msemo "kundi" unaweza pia kutumika kwa ajili ya kondoo au mbuzi, lakini katika maandishi ya Biblia haitumiki kwa njia hii.

Msemo "kundi" katika Kiingereza pia hutumika kwa ajili ya kundi la ndege, lakini unaweza kutumika kwa ajili ya nguruwe, maksai au ng'ombe.

Fikiria ni misemo gani inatumika katika lugha yako kumaanisha makundi tofauti ya wanyama.

Kwa mistari ambayo ina maana ya "makundi au mifugo" inaweza kuwa bora kuongeza "ya kondoo" au "ya ng'ombe" kwa mfano, kama lugha haina maneno tofauti kumaanisha aina tofauti za makundi ya wanyama.

kuomba

Ufafanuzi

Neno "kuomba" lamaanisha kumwomba mtu kitu fulani kwa umuhimu. Mara kwa mara inamaanisha kuomba pesa, lakini pia limetumika kuonesha kuombeleza jambo fulani.

kura, kupiga kura

Ufafanuzi

"Kura" ni kitu kilichowekwa alama kinachochaguliwa miongoni mwa vitu vya kufanana kama naamna ya kuamua jambo. "Kupiga kura" inamaanisha kurusha vitu vilivyo wekwa alama kwenye sakafu au ardhi yoyote.

Mara nyingi kura yalikuwa mawe madogo yenye alama au vipande vidogo vilivyovunjika vya udongo. Tamaduni zingine zinafanya "bahati nasibu" au "kuvuta" kura kwa kutumia majani makavu. Mtu anayashikilia majani makavu ili asiwepo wakuona yana urefu gani. Kila mtu anavuta jani na yule atakayepata jani kavu refu zaidi (au fupi) ndiye atakayekuwa amechaguliwa. Zoezi la kupiga kura lilitumika na Waisraeli kujua ni nini Mungu aliwataka wafanye. Kama nyakati za Zekaria na Elisabeti, ilitumika pia kuchagua ni kuhani yupi atatenda jukumu bayana hekaluni katika muda maalumu. Askari walio msulubisha Yesu walipiga kura kuamua ni nani atakaa na joho la Yesu. Usemi "kupiga kura" inawezakutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu" au "kurusha kura". Kulinga na mazingira, neno "kura" inaweza pia kutafsiriwa kama "jiwe lenye alama" au "kipande cha udongo" au "kijiti" au "kipande cha jani." Kama maamuzi yakifanyika "kwa kura" hii inaweza kutafsiriwa kama "kufanya bahati nasibu (au kurusha) ya kura."

kusaliti

Ufafanuzi

Neno "kusaliti" lamaanisha tendo la kumdanganya na kumdhuru mwingine. "Msaliti" ni mtu amsalitiye rafiki yake mwenye kumwamini.

Maoni ya Tafasiri

kusanya, kukusanya

Ufafanuzi

Msemo "kusanya" una maana ya kupita katika shamba au shamba la matunda kuokota nafaka yoyote au tunda ambao wavunaji wameacha nyuma.

Mungu aliwaambia Waisraeli kuruhusu wajane, watu maskini, na wageni kukusanya mabaki ya nafaka ili kwamba wapate chakula kwa ajili yao.

Mara nyingine mmiliki wa shamba angeruhusu wakusanyaji kwenda moja kwa moja nyuma ya wavunaji kukusanya, ambayo iliwawezesha wao kukusanya nafaka zaidi.

Mfano wa wazi ni jinsi hii ilivyofanya kazi katika simulizi ya Ruhtu, ambaye aliruhusiwa kwa ukarimu kukusanya miongoni mwa wavunaji katika mashamba ya ndugu wa Boazi.

kuza

Ufafanuzi

Neno "kuza" lina maana ya kufanya kitu au mtu mkubwa au kuvuta umakini kwa ukuu wa mtu.

kuzika, zika

Ufafanuzi

Neno "zika" kwa kawaida linamaanisha kuweka kaburini mwili wa mtu aliyekufa. Neno "kuzika" ni kitendo cha kuzika kitu au linaweza kutumika kueleza sehemu itumikayo kuzikia.

kuzimu

Ufafanuzi

katika Biblia kuna maneno mawili yametumika, neno la Kiebrania 'sheol' na neno la Kigriki 'hades.' Maneno haya yametumika katika Biblia kumaanisha kifo na sehemu ambako roho za watu waliokufa huenda. katika Kiebrania neno 'sheol' limetumika katika Agano la Kale kurejelea sehemu ya watu waliokufa au sehemu ya kifo. katika agano jipya, neno la Kigriki 'hades" limetumika kumaanisha sehemu ya roho za watu waliomwasi Mungu. Roho hizi hurejelewa kama zinaenda "chini." Wakati mwingine linaweza kutofautishwa na 'kwenda juu' mbinguni mahali ambako roho za watu za watu wanaomwamini Yesu zinaishi.

Mapendekezo ya tafsiri Katika Agano la Kale neno "sheol" linaweza kutafsiriwa kama " sehemu ya wafu" au "sehemu kwa ajli ya roho za wafu" Baadhi ya tafsiri hufasiri neno hili kama "shimo" au "kifo" kwa kutegemea na muktadha. Neno "hades" limetumika sana katika Agano Jipya ambalo laweza kutafsiriwa kama "sehemu kwa ajili ya roho za wafu za watu wasioamini" au " sehemu ya mateso na adhabu ya kwa roho za wafu wasioamini." Baadhi ya tafsiri hutunza neno ''sheol" au ''Hades'' kwa kutumia herufi ambazo zinakubaliana katika mfumo wa sauti wa lugha husika. kwa kiswahili twaweza kusema 'sheoli" na 'hadesi'

kweli, ukweli, kuwa kweli

Ufafanuzi

Maneno "kweli" na "ukweli" yana eleza mambo ambyo ni halisi, matukio yaliyo tukia, na maneno yaliyo semwa.

la kumi, zaka

Ufafanuzi

Maneno "la kumi" na "zaka" yanaeleza "asilimia ya kumi" au "moja-kati-ya -sehemu- ya-kumi" ya pesa, mazao, mifugo, au mali za mtu anazo mpa Mungu.

lala, kulala, aliye lala

Ufafanuzi

Haya maneno yana maana ya kimafumbo kuhusu kifo.

lango, nguzo ya lango

Ufafanuzi

"Lango" ni kizuizi chenye bawaba katika njia ya kufikia ya uzio au ukuta ambao huzunguka nyumba au mji. "Nguzo ya lango" ina maana ya nguzo ya chuma au mbao ambayo inaweza kusogezwa katika sehemu kufunga lango.

Lango la mji linaweza kufunguliwa kuruhusu watu, wanyama, na mizigo kusafiri ndani na nje ya mji.

Kulinda mji, kuta zake na malango ilikuwa nene na imara. Malango yalifungwa na kukazwa na nguzo ya chuma au mbao kuzuia wanajeshi wa maadui kuingia mji.

Lango la mji mara kwa mara ilikuwa kiini cha habari na katikati ya jamii ya kijiji. Pia ilikuwa mahali ambapo mihamala ya kibiashara hufanyika na hukumu kufanyika, kwa sababu kuta za mji zilikuwa na unene wa kutosha kuwa na njia ambayo ilitoa kivuli cha baridi kutoka kwa jua kali. Raia walifurahia kukaa chini ya kivui na kufanya biashara zao na pia kuhumu masuala ya kisheria.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, njia zingine za kutafsiri "lango" inaweza kuwa "mlango" au "uwazi wa ukuta" au "kizuizi" au "njia ya kuingia".

Msemo "nguzo za lango" unaweza kutafsiriwa kama "komeo za lango" au "mihimili ya mbao ya kufunga lango" au "chuma cha kufunga lango"

mafuriko

Ufafanuzi

Msemo "mafuriko" ina maana ya kiasi kikubwa cha maji ambacho kinafunika juu ya nchi.

Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha kiasi kikubwa cha kitu, haswa kitu ambacho hutokea ghafla.

Katika kipindi cha Nuhu, watu walikuwa waovu hadi Mungu akasababisha mafuriko duniani kote kuwa juu ya uso wote wa dunia, hata kufunika juu za milima. Kila mtu ambaye hakuwa katika mtumbwi pamoja na Nuhu alizama. Mafuriko yote mengine hufunika eneo dogo la nchi.

Msemo huu pia unaweza kuwa tendo kama, "nchi ilifurika na maji ya mto".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri maana halisi ya "mafuriko" inaweza kujumuisha, "maji yanayomwagikia" au "kiasi kikubwa cha maji"

Mlinganisho wa kitamathali, "kama mafuriko" unaweza kukaa na msemo halisi, au msemo mbadala unaweza kutumika ambao una maana ya kitu ambacho kina hali ya kutiririka kwake, kama vile mto.

Kwa msemo "kama mafuriko ya maji" pale ambapo maji yametajwa tayari, neno "mafuriko" linaweza kutafsiriwa kama "kiasi kikubwa sana" au "yanayomwagikia".

Msemo huu unaweza kutumika kama sitiari kama, "usiruhusu mafuriko kunizoa juu yangu", ambayo ina maana ya "usiruhusu maafa haya makubwa kutokea kwangu" au "usiniache niteketezwe kwa maafa" au "usiache hasira yako initeketeze".

mafuta

Ufafanuzi

Mafuta ni maji mazito yanayo chukuliwa kutoka kwenye mimea au matunda. Katika Biblia, mafuta yalito kwenye mizeituni.

maisha, uhai, kuishi, kuwa hai

Ufafanuzi

Maneno haya yote yanamaanisha kuwa hai kimwili, sio kufa. Yanatumika pia kimafumbo kumaanisha kuwa hai kiroho. Yanayofuata yanaelezea nini kinamaanishwa na "maisha ya kimwili" na "maisha ya kiroho."

Kulingana na mazingira, "maisha" inaweza kuetafsiriwa kama "kuwepo" au "mtu" au "roho" au "kuwa" au "kupitia." Neno "uhai" inaweza kutafsiriwa kama "kuishi" au "kukaa" au "kuwepo." Msemo "mwisho wa maisha yake" inaweza kutafsiriwa kama, "alipoacha kuishi." Msemo "alinusuru maisha yao" unaweza kutafisiri kama, "aliwaruhusu waishi" au "hakuwaua." Msemo "walihatarisha maisha yao" unaweza kutafsiriwa kama, "walijiweka hatarini" au "walifanya kitu ambacho kingiweza kuwaua." Bibilia inapozungumzia kuwa hai kiroho, "maisha" yanaweza kutafsiriwa kama "maisha ya kiroho" au "maisha ya milele," kulingana na mazingira. Wazo la "maisha ya kiroho" linaweza pia kutafsiriwa kama, "Mungu kutufanya kuwa hai katika roho zetu" au "maisha mapya kwa Roho wa Mungu" au "kufanywa hai ndani yetu." Kulingana na mazingira, msemo "toa maisha" unaweza kutafsiriwa kama, "kusababisha kuishi" au "kutoa uzima wa milele" au "kusababisha kuishi milele."

majivu, vumbi

Ufafanuzi

Majivu ni vumbi la kijivu linalobaki baada ya kuni kuungua. Hutumika pia kama lugha ya picha kuonesha kitu kisicho na thamani.

makapi

Ufafanuzi

Makapi ni ganda kavu linalolinda mbegu ya nafaka. Makapi sio mazuri kwa chakula hivyo watu hutenganisha na mbegu na kuyatupa.

manemane

Ufafanuzi

Manemane ni mafuta au manukato yanayo tengenezwa kwa majani ya manemane yanayo ota Africa na Asia.

mbegu, manii

Ufafanuzi

Mbegu ni sehemu ya mmea unao oteshwa kwenye ardhi kuzalisha aina moja zaidi ya mmea huo. Pia ina maana kadha ya mafumbo.

mbingu, anga, mbinguni

Ufafanuzi

Neno linalotafsiriwa kama "mbingu" hurejelea mahali anapoishi Mungu. Neno hilo hilo laweza kumaanisha " anga" kwa kutegemea na muktadha. Neno 'mbingu' hurejelea kila kitu tunachokiona juu mawinguni kama vile jua, mwezi, na nyota. Inaweza pia kujumuisha vitu vingine vya anga la mbali kama vile sayari, vitu ambavyo hatuwezi kuviona tukiwa hapa duniani. Neno "anga' hurejelea anga la bluu lililo juu ya dunia ambalo lina mawingu na hewa tunayopumua. Mara kwa mara, jua na mwezi husemwa kuwa ziko 'juu angani. Neno 'mbingu' laweza kumaanisha 'anga' au sehemu ambako Mungu anaishi' hii hutegemea na muktadha mbalimbali. Wakati neno 'mbingu' linapotumika kama tamathali ya semi, humrejelea Mungu mwenyewe. Kwa mfano, Mathayo anapoandika juu ya 'ufalme wa mbinguni' anarejelea ufalme wa Mungu.

Mapendekezo ya tafsiri Wakati neno 'mbingu' linapotumika kimfano laweza kutafsiriwa kama 'Mungu" Maneno 'mbingu' au " vitu vya kimbingu' yaweza kutafsiriwa kama 'jua, mwezi na nyota. Kirai "nyota za mbinguni" chaweza kutafsiriwa kama " nyota za angani."

mbuzi, mwanakibuzi

Ufafanuzi

Mbuzi ni mnyama wa ukubwa wa kati, mwenye miguu minne ambaye analingana na kondoo na hukuzwa kimsingi kwa ajili ya maziwa yake na nyama. Mtoto wa mbuzi huitwa "mwanakibuzi".

Kama kondoo, mbuzi walikuwa wanyama muhimu wa sadaka, haswa wakati wa Pasaka.

Ingawa mbuzi na kondoo wanaweza kufanana, kuna namna ambavyo wako tofauti.

Mbuzi wanya manyoya ya kukwaruza; kondoo wana sufu.

Mkia wa mbuzi husimama juu; mkia wa kondoo huning'inia chini.

Kondoo mara kwa mara hupenda kukaa katika kundi lake, lakini mbuzi wanajitegemea zaidi na kutembea mbali na kundi lao.

Katika kipindi cha Biblia, mbuzi walikuwa chanzo kikuu cha maziwa Israeli.

Ngozi ya mbuzi ilitumika kwa ajili ya kufunika mahema na kutengeza mifuko ya kubeba divai.

Pote katika Agano la Kale na Jipya, mbuzi alitumika kama ishara ya ukosefu wa utakatifu wa watu, labda kwa sababu ya mazoea yao ya kutangatanga mbali na yule aliyekuwa akiwatunza.

Waisraeli pia walitumia mbuzi kama mfano wa mtu mwenye dhambi. Mbuzi mmoja anapotolewa sadaka, kuhani huweka mikono yake juu ya mbuzi wa pili aliye hai na kumwachilia jangwani kama alama ya mnyama kubeba dhambi ya watu.

mbwa mwitu

Ufafanuzi

Mbwa mwitu ni mnyama mkali, anayekula nyama na anafanana na mbwa.

mchungaji, kuchunga

Ufafanuzi

Mchungaji ni mtu anaye linda kondoo. Kitenzi "kuchunga" ina maana ya kulinda kondoo na kuwapa chakula na maji.

meza

Ufafanuzi

Msemo wa "meza" una maana ya kula au kutumia kwa hali ya fujo.

Kutumia neno hili kwa hisi ya tamathali, Paulo anatahadharisha waumini kutojimeza wao kwa wao, akimaanisha kutojishambulia au kuangamizana wao kwa wao kwa maneno au matendo (Wagalitia 5:15).

Pia katika hisi ya tamathali, msemo "kumeza" mara kwa mara hutumika kwa maana ya "kuangamiza kabisa" kama kuzungumzia juu ya mataifa kumeza mengine au moto kumeza majengo na watu.

Msemo huu pia unaweza kutafsiriwa kama "kumeza kabisa" au "kuangamiza kabisa".

mfalme

Ufafanuzi

Neno "mfalme" linamaanisha mwanamme ambaye ni mtawala mkuu wa mji, jimbo, au nchi.

Mfalme kawaida huchaguliwa kutawala kwa sababu ya uhsiano wake kifamilia na wafalme wa nyuma. Mfalme anapokufa, kawaida mwana wake mkubwa ndiye anayekuwa mfalme mpya. Katika nyakati za zamani, mfalme alikuwa na mamlaka yote juu ya watu katika ufalme wake. Neno "mfalme" halitumiki sana kwa mtu asiye mfalme wa kweli, kama "mfalme Herode" katika Agano Jipya. Katika Biblia, Mungu anajulikana kama mfalme anaye tawala juu ya watu wake. "Ufalme wa Mungu" unamaanisha utawala wa Mungu juu ya watu wake. Yesu aliitwa "Mfalme wa Wayahudi," "mfalme wa Israeli," na "mfalme wa wafalme." Yesu atakaporudi, atatawala kama mfalme wa dunia. Neno hili linaweza kutafsiriwa kama, "mkuu" au "kiongozi kamili" au "mtawala mwenye nguvu." Usemi "mfalme wa wafalme" unaweza kutasiriwa kama "mfalme anayetawala juu ya wafalme wengine wote" au "kiongozi mkuu aliye na mamlaka juu ya viongozi wengine wote."

mgeni, ugeni, mgeni

Ufafanuzi

Msemo, "mgeni" una maana ya mtu anayeishi katika nchi ambayo sio yake.

Katika Agano la Kale, msemo huu haswa humaanisha mtu yeyote ambaye alikuja kutoka kwa kundi tofauti la watu na watu ambao anaishi miongoni mwao.

Mgeni pia ni mtu ambaye lugha yake na utamaduni ni tofauti na ya kwako.

Kwa mfano, Naomi na familia yake alipohama kwenda Moabu, walikuwa wageni kule. Naomi na mkwe wake Ruthu walipohamia Israeli baadaye, Ruthu aliitwa "mgeni" kule kwa saba hakuwa wa Israeli kiasili.

Mtume Paulo aliwaambia Waefeso ya kuwa kabla hawajamjua Kristo, walikuwa "wageni" kwa agano la Mungu.

Mara nyingi, "mgeni" hutafsiriwa kama "mgeni" mtu ambaye hajulikani au hajazoeleka.

milele

Ufafanuzi

Msemo huu "milele" una maana ya kitu ambacho kitaendelea kuwepo au kutadumu daima.

Msemo "milele" una maana ya hali ya kutokuwa na mwanzo au mwisho. Pia inaweza kumaanisha maisha ambayo hayana mwisho.

Baada ya maisha haya ya sasa ya duniani, binadamu wataishi milele aidha mbinguni na Mungu au jehanamu kutengana na Mungu.

Misemo "maisha ya milele" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha kuishi milele pamoja na Mungu mbinguni.

Msemo "milele na milele" ina wazo la muda ambao hauna mwisho na huelezea nini milele au maisha ya milele yakoje.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia zingine za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kutokuwa na mwisho" au "kuendelea siku zote".

Msemo "maisha ya milele" unaweza kutafsiriwa kama "maisha ambayo hayana mwisho" au "maisha ambayo yanaendelea bila kikomo" au "kufufua miili yetu kuishi milele".

Kulingana na muktadha, njia tofauti za kutafsiri "milele" zinaweza kujumuisha "kuwepo nje ya muda" au "maisha yasiyo na mwisho" au "maisha mbinguni".

Pia fikiria namna neno hili linatafsiriwa katika Biblia katika lugha ya taifa.

milele

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "milele" una maana ya muda usiofika mwisho. Mara kwa mara hutumika kitamathali kumaanisha, "muda mrefu sana".

Msemo "milele na milele" unasisitiza ya kwamba jambo litakuwepo milele.

Msemo "milele na milele" ni njia ya kuelezea maisha ya milele yakoje. Pia una wazo la muda ambao hauishi.

Mungu alisema ya kwamba ufalme wa Daudi utakuwepo "milele". Hii inamaanisha ukweli ya kwamba uzao wa Daudi Yesu atatawala kama mfalme milele.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mara zote" au "kutokuwa na mwisho". Msemo, "utadumu milele" unaweza kutafsiriwa kama "kuwepo mara zote" au "hautakoma" au "utaendelea mara zote". Msemo wa kishindo, "milele na milele" unaweza kutafsiriwa kama "kwa mara zote na zote" au "kutomalizika" au "ambayo haifiki mwisho". Ufalme wa Daudi kudumu milele unaweza kutafsiriwa kama, "uzao wa Daudi atatawala milele" au "uzao wangu ataendelea kutawala".

mjumbe

Ufafanuzi

Neno, "mjumbe" la husu mtu anaye pewa ujumbe kuwa ambia wengine.

mkono, mkono wa kuume,

Ufafanuzi

Neno 'mkono' limetumika katika Biblia kama lugha ya picha kwa njia mbalimbali Kuweka kitu katika mikono ya mtu fulani inamaana ya kukabidhi kitu hicho. Neno 'mkono' limetumika kurejelea uweza au nguvu ya Mungu na matendo yake. kwa mfano, Mungu anaposema "je si mkono wangu uliyoyafanya haya?" Neno "kabidhi" hurejelea maana ya kuweka kitu katika mkono au utawala wa mtu fulani. Kuweka mikono juu ya mtu fulani mara nyingi huambatana na utoaji wa baraka kwa mtu huyo. Pia kitendo cha 'kuweka mikono" juu ya mtu kinamaanisha kumweka mtu huyo wakfu kwa ajili ya kazi ya Mungu au kwa ajili ya kumwombea mtu huyo uponyaji. Baadhi ya lugha za picha za neno mkono ni: Kunyosha mkono juu ya mtu maana yake ni kumdhuru. ''kumwokoa kutoka katika mkono wa..." ni kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. matumizi mengine ya mkono ni kama: "kunyosha mkono" ina maana ya 'kudhuru' au kuumiza" "kumwokoa mtu mikononi mwa" ina maana ya kumzuia mtu ili asimdhuru mtu mwingine. "kuwa karibu na mkono " kuwa 'karibu' "kuwa mkono wa kuume" humaanisha kuwa 'nafasi'' au ''sehemu ya'' au "upande wa kulia" Maelezo yanayosema "kwa mkono wa'' au ''kupitia mkono'' ina maana kuwa kitendo kimefanya na mtu huyo. kwa mfano, "kwa mkono wa Bwana'' ina maana kuwa Bwana ndiye amefanya tendo hilo. Wakati Paulo anasema " imeandikwa kwa mkono wangu" ina maana kuwa sehemu hii ya barua iliandikwa kwa mkono wake kabisa, badala tu kusema na mtu mwingine akayaandika.

Mapendekezo ya tafsiri. Maelezo haya na tamathali hizi za semi zaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha zingine za picha ambazo zina maana sawa. Au maana inaweza kutafsiriwa kwa kutumia lugha ya moja kwa moja.

moto

Ufafanuzi

Moto ni joto, mwanga na miale ambayo hutokana pale kitu kinapochomwa.

Kuchoma mbao kwa moto hugeuza mbao kuwa majivu.

Msemo "moto" pia hutumika kitamathali, mara kwa mara kumaanisha hukumu au utakaso.

Hukumu ya mwisho ya wasioamini ipo katika moto wa jehanamu.

Moto hutumika kusafisha dhahabu na vyuma vingine. Katika Biblia, hatua hii hutumika kuelezea jinsi Mungu husafisha watu kupitia mambo magumu ambayo hutokea katika maisha yao.

Msemo "kuwabatiza kwa moto" unaweza kutafsiriwa kama "kukusababisha upitie mateso ili kwamba yakusafishe"

mpendwa

Ufafanuzi

Neno "mpendwa" ni kifungu cha kitabia kinachomweleza mtu anayependa na mwingine.

Maoni ya Ufasiri

mpumbavu, upumbavu, upuuzi

Ufafanuzi

Msemo "mpumbavu" una maana ya mtu ambaye mara kwa mara hutengeneza uchaguzi mbaya, haswa kuchagua kutokutii. Msemo "upumbavu" unaelezea mtu au tabia ambayo siyo ya hekima.

Katika Biblia, msemo "mpumbavu" mara kwa mara una maana ya mtu ambaye haamini au kumtii Mungu. Mara nyingi hii hutofautishwa na mtu mwenye hekima, ambaye humwamini Mungu na kumtii.

Katika Zaburi, Daudi anaelezea mtu mpumbavu kama mtu ambaye hamwamini Mungu, ambaye hupuuza ushahidi wote wa Mungu na uumbaji wake.

Kitabu cha Agano la Kale cha Mithali pia hutoa maelezo mengi ya mpumbavu ni nani, mtu mpumbavu yukoje.

Msemo "upuuzi" una maana ya tendo ambao sio la hekima kwa sababu ni kinyume na mapenzi ya Mungu. Mara nyingi "upuuzi" pia hujumuisha maana ya kitu ambacho ni cha kudharaulika au hatari.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "mpumbavu" unaweza kutafsiriwa kama "mtu mpumbavu" au "mtu asiye na hekima" au "mtu asiyejitambua" au "mtu asiyemcha Mungu"

Njia za kutafsiri "mpumbavu" zinawvza kujumuisha "upungufu wa uelewa" au "kutokuwa na hekima" au "kutojitambua".

msimamizi

Ufafanuzi

Neno "msimamizi" la husu mtu aliye mwangalizi wa kazi na maendeleo ya watu wengine.

msingi, kuanzishwa

Ufafanuzi

Kitenzi cha "kuanzishwa" ina maana ya kujengwa juu ya au kutokana na kitu. Msingi ni sehemu ya chini ambapo kitu kunajengwa.

Msingi wa nyumba or jengo lazima uwe na nguvu na kutegemewa ili kuimarisha umbo lote.

Msemo "msingi" unawvza kumaanisha mwanzo wa jambo au muda ambao kitu kiliumbwa.

Kwa kitenzi cha kitamathali, waumini katika Kristo wanalinganishwa na jengo ambalo limejengwa juu ya mafunzo ya mitume na manabii, na Kristo mwenyewe kuwa jiwe la pembeni la jengo.

"Jiwe la msingi" lilikuwa jiwe ambalo lililazwa kama sehemu ya msingi. Mawe haya yalijaribiwa kuhakikisha yalikuwa na nguvu ya kutosha kuimarisha jengo kamili.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "kabla ya msingi wa dunia" inaweza kutafsiriwa kama "kabla ya uumbaji wa ulimwengu" au "kabla ya muda ambapo dunia ilianza kuwepo".

Msemo "kujengwa juu ya" inaweza kutafsiriwa kama "kujengwa kwa imara juu ya" au "kujengwa kwa imara kwa".

Kulingana na muktadha, "msingi" inaweza kutafsiriwa kama "msingi imara" au "uimara wa kudumu" au "mwanzo" au "uumbaji"

mtakatifu

Ufafanuzi

Neno "mtakatifu'' ni jina ambalo katika Biblia mara zote humrejelea Mungu. Katika Agano la kale, jina hili mara kwa mara lilitokea katika kirai ''mtakatifu wa Israeli" Katika Agano Jipya, jina mtakatifu lilitumika kumrejelea Yesu Mara nyingine katika Biblia, neno mtakatifu hutumika kumrejelea malaika.

mtini

Ufafanuzi

Tini ni tunda dogo, laini, tamu ambalo huota juu ya miti. Linapoiva, tunda hili linaweza kuwa na rangi nyingi, ikiwemo kahawia, njano na zambarau.

Mitini inaweza kuota kuwa urefu wa mita 6 na matawi yao makubwa hutoa kivuli kizuri. Tunda hili lina urefu wa sentimita 3-5.

Adamu na Hawa walitumia majani ya mtini kutengeneza mavazi kwa ajili yao baada ya kutenda dhambi.

Mitini inaweza kuliwa mibichi, ikiwa imepikwa, au kukaushwa. Watu pia walikata katika vipande vidogo vidogo na kuzikandamiza kuwa keki kuliwa baadaye.

Katika kipindi cha Biblia, mitini ilikuwa muhimu kama chanzo cha chakula na kipato.

Uwepo wa mitini inayozaa mara kwa mara hutajwa katika Biblia kama ishara ya mafanikio.

Mara kadhaa Yesu alitumia mitini kama mfano wa kufundisha wanafunzi wake kweli za kiroho.

mtumishi, mtumwa, utumwa

Ufafanuzi

Neno "mtumishi" la weza pia maanisha "mtumwa" na kumueleza mtu anaye mfanyia mtu mwingine kazi, iwe kwa uwamuzi au kwa lazima. Muktadha wa maneno yaliyo zunguka yanaweka dhahiri kuwa kama mtumishi au mtumwa ndiye anaye tajwa.

muda

Ufafanuzi

Katika Biblia neno "muda" utumika sana kama fumbo kueleza wakati maalumu au kipindi cha muda fulani matukio yametokea. Lina maana sawa na "umri" au "wakati."

muujiza, ajabu, ishara

Ufafanuzi

"Muujiza" ni kitu kinacho shangaza ambacho hakiwezekani pasipo Mungu kusababisha kitokee.

mwalimu,Mwalimu

Ufafanuzi

Mwalimu ni mtu anaye toa taarifa mpya. Waalimu wanasaidiana kupata na kutumia maarifa na ujuzi.

mwamini

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "mwamini" larejerea mtu anayeamini na kumtegemea Yesu Kristo kama Mwokozi.

Maoni ya Kutafasiri.

mwaminifu, uaminifu

Ufafanuzi

Kuwa "mwaminifu" kwa Mungu ina maana kuwa na desturi ya kuishi kulingana na mafunzo ya Mungu. Ina maana ya kuwa mwaminifu kwake na kumuamini. Hali ya kuwa mwaminifu ni "uaminifu".

Mtu ambaye ni mwaminifu anaweza kuaminiwa kuweza kushika ahadi zake na kutimiza majukumu yake daima kwa watu wengine.

Mtu mwaminifu huvumilia katika kutenda kazi, hata pale ambapo ni ndefu au ngumu.

Uaminifu kwa Mungu ni matendo ya daima ya kutenda ambacho Mungu anatutaka kufanya.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha nyingi, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kama "uaminifu" au "kujitolea" au "kutegemea".

Katika muktadha zingine, "mwaminifu" inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuendelea kuamini" au "kuvumilia katika kuamini na kumtii Mungu".

Njia ambazo "uaminifu" inaweza kutafsiriwa inaweza kumaanisha "kuvumilia katika kuamini" au "uaminifu" au "kuamini na kumtii Mungu".

mwana, mwana wa

Ufafanuzi

Neno "mwana" la husu mvulana au mwanaume na wazazi wake. La weza eleza mzao wa kiume wa mwanaume au mwana aliye pangwa.

mwandishi, mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi

Ufafanuzi

Waandishi walikuwa wasimamizi waliyo wajibika katika kuandika au kunakili nyaraka muhimu za serikali au za kidini kwa mkono. Jina lingine la mwandishi wa Kiyahudi ni "mtaalamu katika sheria ya Kiyahudi."

mwenzi

Ufafanuzi

Mwenzi ni mtu anayekwenda na mtu mwingine au mwenye ushirika na mtu mwingine kwa mfano urafiki au ndoa.

mwezi

Ufafanuzi

Neno "mwezi" linataja kipindi cha kuishia karibia majuma manne. Idadi ya majuma katika kila mwezi yalitofautiana kulingana na matumizi ya kalenda iliyotumika kwamba ilikumia jua au mwezi.

mwiba, mbaruti

Ufafanuzi

Vicha vya miba na mbaruti ni majani matawi yaliyo chongoka au maua. Haya majani haya zalishi matunda au chochote kinacho tumika.

mwili

Ufafanuzi

Neno "mwili" kwa kawaida linamaanisha mwili wa binadamu au mnyama. Nene hili hutumika pia kitamathari kurejerea kitu au jumla ya kundi lenye wajumbe.

Maoni ya Tafasiri

mwili

Ufafanuzi

Katika Biblia, msemo "mwili" una maana ya tishu laini ya mwili wa mwanadamu au mnyama.

Biblia pia hutumia msemo "mwili" kitamathali kumaanisha wanadamu wote au viumbe wote.

Katika Agano Jipya, msemo "mwili" unatumika kumaanisha asili ya dhambi ya wanadamu. Hii hutumika mara kwa mara kinyume na asili yao ya kiroho.

Msemo, "mwili na damu yake" ina maana ya mtu ambaye anahusiana kibiolojia na mtu mwingine, kama vile mzazi, ndugu, mtoto au mjukuu.

Msemo "mwili na damu" pia unaweza kumaanisha mababu au vizazi vya mtu.

Msemo "mwili mmoja" una maana ya muungano wa kimwili wa mwanamume na mwanamke katika ndoa.

Mapendekezo ya Tafsiri

Katika muktadha wa mwili wa mnyama, "mwili" unaweza kutafsiriwa kama "mwili" au "ngozi" au "nyama".

Inapotumika kumaanisha viumbe wote hai, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "viumbe hai" au "kila kitu chenye uhai".

Inapomaanisha kwa jumla watu wote, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "watu" au "binadamu" au "kila mtu anayeishi".

Msemo "mwili na damu" unaweza kutafsiriwa kama "jamaa" au "familia" au "ndugu wa karibu" au "ukoo wa familia". Kunaweza kuwa na muktadha ambapo inaweza kutafsiriwa kama "mababu" au "vizazi".

Baadhi ya lugha zinaweza kuwa na msemo ambao unafanana na "mwili na damu".

Msemo "kuwa mwili mmoja" unaweza kutafsiriwa kama "kuungana kimapenzi" au "kuwa kama mwili mmoja" au "kuwa kama mtu mmoja kimwili na roho". Tafsiri ya msemo huu unaweza kuangaliwa kuhakikisha inakubalika katika lugha na utamaduni wako.

mwizi, wezi, jambazi

Ufafanuzi

Haya maneno "mwizi" na "wezi" yanaeleza kwa jumla watu wanao iba pesa au mali kwa wengine. Neno "jambazi" mara nyingi la eleza mwizi anaye dhuru kimwili au kutishia watu anao waibia.

mzigo

Ufafanuzi

Mzigo ni kitu kizito. Kwa uhalisia inamaanisha uzito wa kitu ambacho mnyama wa kazi angeweza kubeba. Neno "mzigo" pia linamaana kadhaa za kimafumbo:

nabii wa uongo

Ufafanuzi

Nabii wa uongo ni mtu ambaye hudai kimakosa ya kwamba ujumbe wake unatoka kwa Mungu.

Tabiri za manabii wa uongo mara kwa mara hazitimiliki. Yaani, haziji kuwa kweli.

Manabii wa uongo hufundisha ujumbe ambao kwa juu juu au kwa ukamili hupingana na kile ambacho Biblia husema.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "mtu ambaye hudai kwa uongo ya kuwa ni msemaji wa Mungu" au "mtu ambaye hudai kimakosa kuzungumza maneno ya Mungu".

Agano Jipya hufundisha ya kwamba kipindi cha mwisho kutakuwa na manabii wengi wa uongo ambao watajaribu kudanganya watu kufikiri ya kwamba wanatoka kwa Mungu.

nafsi

Ufafanuzi

Nafsi ni sehemu ya ndani, isiyo onekana ya mtu. Ya husu sehemu isiyo ya kimwili ya mtu.

najisi, kunajisiwa

Ufafanuzi

Msemo wa "najisi" na "kunajisiwa" ina maana ya kuchafuliwa au uchafu. Kitu kinaweza kunajisiwa kihalisia, kimaadili au kwa kaida za dini.

Mungu aliwaonya Waisraeli wasijinajisi kwa kula au kugusa vitu ambavyo vimewekwa wakfu kuwa "chafu" au "kiovu".

Baadhi ya vitu kama maiti na magonjwa ya kuambukiza vilitamkwa na Mungu kuwa vichafu na vinaweza kunajisi mtu iwapo atavigusa.

Mungu aliwaamuru Waisraeli kuacha uasherati. Hivi vingewatia unajisi na kuwafanya kutokubalika kwa Mungu.

Pia kulikuwa na aina kadhaa ya hatua za kimwili ambazo zilimnajisi mtu kwa muda mfupi hadi atakapokuwa safi kwa kaida za dini tena.

Katika Agano Jipya, Yesu alifundisha ya kwamba mawazo ya dhambi na matendo ndiyo haswa yanayomnajisi mtu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa "najisi" unaweza kutafsiriwa kama "kusababisha kuwa chafu" au "kusababisha kuwa muovu" au "kusababisha kutokubalika kwa kaida za dini".

"Kunajisiwa" kunaweza kutafsiriwa kama "kuwa mchafu" au "kusababisha kutokubalika kimaadili"

ndoto

Ufafanuzi

Ndoto ni kitu ambacho watu huna au kupitia akilini mwao wanapokuwa wamelala.

Ndoto mara kwa mara huonekana kama zinatokea kihalisia, lakini haziko hivyo.

Mara nyingine Mungu husababisha watu kuota juu ya kitu ili waweze kujifunza kutoka na hicho kitu. Pia anaweza kuzungumza moja kwa moja na watu ndani ya ndoto zao.

Katika Biblia, Mungu alitoa ndoto maalumu kwa baadhi ya watu kuwapa ujumbe, mara nyingi kuhusu jambo ambalo lingetoke hapo baadaye.

Ndoto ni tofauti na maono. Ndoto hutokea wakati mtu amelala, lakini maono mara kwa mara hutokea wakati mtu yupo macho.

ndugu

Ufafanuzi

Neno "ndugu" kwa kawaida linamaanisha ndugu wa kiume ambaye wanaunganishwa angalau na mzazi mmoja.

Maoni ya Kutafasiri

ngao

Ufafanuzi

Ngao ni chombo kinacho shikiliwa na mwanajeshi katika pambano kuweza kujilinda hasiumizwe na silaha za maadui.

nia

Ufafanuzi

Neno "nia" la husu sehemu ya mtu inayo fikiri na kufanya maamuzi.

njaa

Ufafanuzi

Msemo "njaa" una maana ya upungufu mkubwa sana wa chakula katika nchi au eneo lote, mara nyingi kutokana na kutokuwa na mvua ya kutosha.

Mazao ya chakula yanawvza kushindwa kutokana na sababu za asili kama vile ukosefu wa mvua, magonjwa ya mazao, au wadudu.

Upungufu wa chakula pia unaweza kusababishwa na watu, kama vile adui kuangamiza mazao.

Katika Biblia, Mungu mara nyingi huleta njaa kama njia ya kuadhibu mataifa wanapotenda dhambi dhidi yake.

Katika Amosi 8:11 msemo "njaa" unatumika kitamathali kumaanisha kipindi ambapo Mungu aliadhibu watu wake kwa kutozungumza nao. Hii naweza kutafsiriwa kwa neno moja kwa ajili ya "njaa" kwa lugha yako, au kwa msemo kama wa "upungufu mkubwa".

njiwa, ninga

Ufafanuzi

Njiwa na ninga ni aina mbili ya ndege wadogo wa kijivu na kahawia ambao wanafanana. Njiwa mara nyingi hufikiriwa kuwa na rangi iliyo nyepesi, karibu na nyeupe.

Baadhi ya lugha zina majina mawili tofauti kwa ajili yao, wakati wengine wanatumia jina moja kwa wote wawili.

Njiwa na ninga walitumiwa katika sadaka kwa Mungu, hasa kwa watu ambao hawakuweza kununua wanyama wakubwa.

Njiwa mara nyingine huashiria usafi, sio na hatia, au amani.

Kama njiwa au ninga hawajulikani katika lugha ambayo tafsiri inafanywa, msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "ndege mdogo, wa kijivu na kahawia anayeitwa njiwa".

Kama njiwa na ninga wote wanawekwa katika mstari mmoja, ni vyema kutumia maneno mawili tofauti kwa ndege hawa, ikiwezekana.

nuru

Ufafanuzi

Kuna matumizi kadhaa ya kimafumbo ya neno "nuru" katika Biblia. Mara nyingi inatumika kama sitiari ya haki, utakatifu, na ukweli.

Yesu alisema, "Mimi ni nuru ya ulimwengu" kumaanisha kuwa analeta ujumbe wa kweli wa Mungu duniani na kuwaokoa watu kutoka kwenye giza la dhambi zao. Wakristo wanaamriwa "kutembea nuruni," ambayo inamaanisha wanatakiwa kuishi jinsi Mungu anavyotaka waishi na kuacha kutenda maovu. Mtume Paulo alisema kuwa "Mungu ni nuru," na hakuna giza ndani yake. Nuru na giza ni tofauti kabisa. Giza ni ukosefu wa nuru. Yesu alisema kuwa yeye "ni nuru ya ulimwengu" na kwamba wafuasi wake wanapaswa kung'aa kama nuru duniani, kwa kuishi kwa naamna inayoonesha ukubwa wa Mungu. "Kutembea nuruni" inaonesha kuishi njia inayompendeza Mungu, kufanya yaliyo mema na sawa. Kutembea gizani inaonesha kuishi kwa kuasi dhidi ya Mungu, kufanya mambo maovu.

nyoka

Ufafanuzi

Neno "nyoka" la husu

nzige

Ufafanuzi

Neno "nzige" linamaanisha aina kubwa ya panzi anayepaa ambaye wakati mwingine hupaa katika makundi makubwa ambayo huleta madhara makubwa, wakila mboga zote njiani.

Nzige na panzi wengine ni wakubwa, wenye mabawa yaliyo wima na miguu ya nyuma mirefu inayowapa uwezo wa kuruka mbali. Katika Agano la Kale, makundi ya nzige yanazungumziwa kimafumbo kama alama au picha ya uharibifu mkubwa utakaokuja kama matokeo ya kutokutii kwa Israeli. Mungu alituma nzige kama moja ya mapigo kumi dhidi ya Wamisri. Agano Jipya linasema kuwa nzige walikuwa chanzo kikubwa cha chakula cha Yohana mbatizaji alipokuwa akiishi jangwani.

okoa, salama

Ufafanuzi

Neno "okoa" la husu kumzuia mtu kutopitia kitu kibaya au cha hatari. Kuwa "salama" ya maanisha kulindwa na hatari au majanga.

omboleza, maombolezo

Ufafanuzi

usemi "omboleza" na "maombolezo" yanamaanisha hisia kali ya kulia, majonzi au huzuni.

Wakati mwingine hii ni pamoja na kujuta kwa kina kwa ajili ya dhambi, au huruma kwa watu waliopitia maafa. Maombolezo yanaweza kujumuisha kulia, kutoa machozi au kulia kwa sauti.

panda, mpandaji, mmea

Ufafanuzi

"kupanda" ina maana kuweka mbegu kwenye ardhi ilikuweza kuotesha mimea. "Mpandaji" ni mtu anaye mpanda au kupanda mbegu.

punda, nyumbu

Ufafanuzi

Punda ni mnyama wa kazi mwenye miguu minne, anayefanana na farasi, lakini mdogo kidogo na mwenye masikio marefu zaidi.

Nyumbu ni uzao tasa atokanaye na punda dume na farasi jike.

Nyumbu ni wanyama wenye nguvu sana na kwa hiyo ni wanyama wa kazi wenye thamani sana.

Punda na nyumbu wote wanatumika kubeba mizigo na watu wanaposafiri.

Katika kipindi cha Biblia, wafalme huendesha punda katika wakati wa amani, kuliko farasi, ambaye alitumika katika kipindi cha vita.

Yesu aliendesha kuingia Yerusalemu juu ya punda mdogo wiki moja kabla hajasulubiwa kule.

rehema

Ufafanuzi

Neno "rehema" lina husu kusaidia mtu waliyo na shida, hususani wanapo kuwa chini au hali ngumu.

rithi, urithi, mrithi

Ufafanuzi

Maneno "rithi" na "urithi" zinamaanisha kupokea kitu cha dhamani kutoka kwa mzazi au mtu mwingine kwa sababu ya uhusiano maalumu na huyo mtu. "Mrithi" ni mtu ambaye anapokea urithi.

Urithi wa halisia ambao unapokelewa unaweza kuwa fedha, ardhi, au aina zingine za mali. Urithi wa kiroho ni vyote ambavyo Mungu huwapa watu wanaomuamini Yesu, zikiwemo baraka za maisha ya sasa pamoja na maisha ya milele pamoja naye. Biblia pia inawaiita watu wa Mungu urithi wake, kinachomaanisha kuwa ni wake, ni mali yake ya dhamani. Mungu alimuahidi Abrahamu na uzao wake kuwa watarithi nchi ya Kanaani, kwamba itakuwa yao milele. Kuna maana ya kitamathali na kiroho ya jinsi watu walio wa Mungu wanasemwa "kurithi nchi." Hii inamaanisha kuwa watafanikiwa na kubarikiwa na Mungu kwa mambo ya kimwili na kiroho. Katika Agano Jipya, Mungu anaahidi kuwa wale wanaomuamini Yesu "watarithi wokovu" na "kurithi uzima wa milele." Pia inaelezwa kama, "kurithi ufalme wa Mungu." Huu ni urithi wa milele unaodumu milele. Kuna maana zingine za kitamathali za haya maneno: Biblia inasema kuwa watu wenye hekima "watarithi utukufu" na watakatifu "watarithi vitu vizuri." "Kurithi ahadi" inamaanisha kupokea vitu vizuri ambavyo Mungu ameahidi kuwapa watu wake. Msemo huu pia unatumika kwa njia ya uhasi kumaanisha watu wapumbavu au wasiotii ambao "wanarithi upepo" au "kurithi upumbavu." Hii inamaanisha wanapokea matokeo ya matendo yao ya dhambi, ikiwemo adhabu na maisha yasiyo na maana.

roho, kiroho

Ufafanuzi

Neno "roho" la eleza sehemu isiyo ya kimwili ya watu isiyo onekana. Mtu anapo kufa, roho yake inaacha mwili wake. "Roho" inaweza eleza tabia au hali ya kihisia ya mtu.

saa

Ufafanuzi

Neno "saa" linatumika mara kwa mara katika Biblia kuonesha muda wa siku jambo fulani lilipotendeka. Pia linatumia tamathari kumaanisha "wakati" au "kitambo"

safi, kusafisha

Ufafanuzi

Kuwa "safi" inamaana kutokuwa na mapungufu au kutochanganya kitu ndani ya kitu ambacho hakitakiwi kuchanganywa. Kukisafisha kitu ni kitendo cha kukisafisha na kuondoa chochote kinachoweza kuchafua.

samehe, kusamehe

Ufafanuzi

Kumsamehe mtu ina maana ya kutokaa na kinyongo dhidi ya mtu ambaye alifanya jambo la kuumiza. "Kusamehe" ni tendo la kumsamehe mtu.

Kumsamehe mtu mara nyingi humaanisha kutomuadhibu mtu huyo kwa jambo ambalo amekosa.

Msemo huu unaweza kutumika kitamathali kumaanisha, "katisha" kama msemo "kusamehe deni".

Watu wanapokiri dhambi zao, Mungu huwasamehe kutokana na sadaka ya kifo cha Yesu msalabani.

Yesu aliwafundisha wanafunzi wake kusamehe wengine kama jinsi alivyowasamehe wao.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "samehe" inaweza kutafsiriwa kama "omba radhi" au "katisha" au "achilia" au "kutoshikilia dhidi ya"

shaba

Ufafanuzi

Neno "shaba" linamaanisha aina ya madini yatengenezwayo kwa kuyeyusha kwa pamoja metali, shaba nyekundu na bati. Ina rangi nyeusi inayoelekea njano, nyekundu kiasi.

shahidi, Shahidi

Ufafanuzi

Shahidi ni mtu ambaye amepata uzoefu binafsi wa kitu kilichotokea. Maranyingi shahidi ni mtu anayetoa ushahidi wa jambo analijua kuwa ni kweli. Shahidi pia aneweza kuwa mtu aliyekuwepo pale na kuona kilichotokea.

shahidi wa uongo, shahidi aliyepotoka, ushuhuda wa uongo, taarifa ya uongo

Ufafanuzi

Misemo ya "shahidi wa uongo" na "shahidi aliyepotoka" ina maana ya mtu anayesema vitu vya uongo juu ya mtu au tukio, mara kwa mara katika mahala rasmi kama mahakamani.

"Ushuhuda wa uongo" au "taarifa ya uongo" ni uongo halisia ambao unaambiwa.

"kutoa ushahidi wa uongo" ina maana ya kudanganya au kutoa taarifa ya uongo kuhusu jambo.

Biblia hutoa habari kadhaa ambapo mashahidi wa uongo waliajiriwa kudanganya kuhusu mtu ili kumfanya mtu huyo kuadhibiwa au kuuwawa.

Mapendekezo ya Tafsiri

"Kuwa shahidi wa uongo" au "kutoa ushahidi wa uongo" unaweza kutafsiriwa kama "kushuhudia uongo" au "kutoa taarifa ya uongo juu ya mtu" au "kuzungumza uongo dhidi ya mtu" au "uongo".

Pale ambapo "shahidi wa uongo" ina maana ya mtu, inaweza kutafsiriwa kama "mtu anayedanganya" au "mtu anayeshuhudia uongo" au "mtu anayesema mambo ambayo siyo ya kweli".

shawishi, ushawishi

Ufafanuzi

Msemo "shawishi" una maana ya kumsihi mtu kwa nguvu na kumbembeleza mtu kufanya kilicho sahihi. Aini hii ya kusihi inaitwa "kushawishi".

Kusudi la kushawishi ni kusihi watu wengine kuepukana na dhambi na kufuata mapenzi ya Mungu.

Agano Jipya hufundisha Wakristo kujishawishi baina yao kwa upendo, sio kwa ukali au ghafula.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "kushawishi" pia inaweza kutafsiriwa kama "kubembeleza kwa nguvu" au "kusihi" au "kushauri".

Hakikisha tafsiri ya msemo huu hainyoeshi ya kuwa anayeshawishi ana hasira. Msemo unatakiwa kuonyesha nguvu na uzito, lakini usionyeshe kauli ya ukali.

Katika muktadha nyingi, msemo "shawishi" unatakiwa kutafsiriwa tofauti na "kutia moyo" ambayo ina maana ya kutia msukumo, aminisha, au kufariji mtu.

Mara kwa mara msemo huu pia unatafsiriwa tofauti na "onya" ambayo ina maana ya kuonya au kusahisha mtu kwa tabia yake mbaya.

sheria, sheria ya Musa, sheria ya Mungu, sheria ya Yahwe

Ufafanuzi

Misemo hii yote inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu alimpa Musa kwa ajili ya Waisraeli kutii. Misemo "sheria" na "sheria ya Mungu" zinatumika pia kwa ujumla kumaanisha kila kitu Mungu anachotaka watu wake kutii.

Kulingana na mazingira, "sheria" inaweza kumaanisha: Amri kumi ambazo Mungu aliandika katika jiwe kwa ajili ya Waisraeli. sheria zote alizopewa Musa vitabu vitano vya kwanza vya Agano la Kale. Agano lote la Kale (pia inajulikana kama "maandiko" katika Agano Jipya). maelekezo yote ya Mungu na mapenzi yake. Usemi "sheria na manabii" inatumika katika Agano Jipya kumaanisha maandiko ya Kihebrania (au "Agano la Kale").

sheria, kanuni

Ufafanuzi

"Sheria" ni amri ambayo kawaida huandikwa chini na kushurutishwa na mtu aliye madarakani. "Kanuni" ni uongozo kwa ajili ya kufanya maamuzi na tabia.

Zote "sheria" na "kanuni" zinaweza kumaanisha amri au imani inayoongoza tabia ya mtu. Maana hii ya "sheria" ni tofauti kwa maana ya kutoka "sheria ya Musa" ambapo inamaanisha amri na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli. Wakati sheria ya ujumla inapotajwa,"sheria" inaweza kutafsiriwa kama "kanuni" au "amri ya jumla."

sifa, mashuhuri

Ufafanuzi

Sifa ni kitendo cha kujulikana na kuwa na sifa.

siku

Ufafanuzi

Neno "siku" kwa kawaida lamaanisha kipindi cha masaa 24 kuanzia kuzama kwa jua. Linatumika pia kitamathari.

siku ya hukumu

Ufafanuzi

Usemi "siku ya hukumu" inamaanisha siku ya usoni ambapo Mungu atamhukumu kila mtu.

Mungu amemfanya Mwanaye, Yesu Kristo, kuhukumu watu wote. Katika siku ya hukumu, Kristo atawahukumu watu kulingana na asili yake ya haki.

sikukuu

Ufafanuzi

Kwa ujumla, sikukuu ni sherehe iliyofanyika na jamii ya watu.

Neno kwa ajili ya "sikukuu" katika Agano la Kale lina maana ya "muda ulioteuliwa".

Sikukuu zinazosherehekewa na Waisraeli zilikuwa nyakati maalumu zilizoteuliwa au nyakati ambazo Mungu aliwaamuru wao kuzifuata.

Katika baadhi ya tafasiri za Kiingereza, neno "sikukuu" linatumika badala ya karamu kwa sababu sherehe zilijumuisha mlo mkubwa wa pamoja.

Kulikuwa na karamu kadhaa ambazo Waisraeli walisherehekea kila mwaka: Pasaka Sikukuu ya Mkate Usiotiwa Chachu Mavuno ya Kwanza Sikukuu ya Wiki (Pentakuki) Sikukuu ya Tarumbeta Sikukuu ya Kulipia Kosa Sikukuu ya Vibanda Kusudi la sikukuu hizi ilikuwa kumshukuru Mungu na kukumbuka mambo ya ajabu aliyofanya kuwaokoa, kuwalinda na kuwapa watu wake.

sinagogi

Ufafanuzi

Sinagogi ni jengo la watu wa Kiyahudi wanapo kutania pamoja kumuabudu Mungu.

sio na hatia

Ufafanuzi

Usemi "sio na hatia" unamaanisha kutokuwa na hatia la uhalifu au makosa mengine. Inaweza pia kumaanisha kwa ujumla watu ambayo hawahusiki na matendo maovu.

Mtu anayetuhumiwa kwa kufanya kitu kibaya hana hatia kama hataambatanishwa na hilo kosa. Wakati mwingine usemi "sio na hatia" unatumika kumaanisha watu ambao hawajafanya kosa kustahili ubaya wanaoupata, kama jeshi la adui kushambulia "watu wasio na hatia."

siri, ukweli uliyo fichika

Ufafanuzi

Katika Biblia, neno "siri" la husu kitu kisicho julikana au kigumu kuelewa ambacho Mungu sasa anaelezea.

stahili, yenye thamani ya, wasiofaa, isiyo na maana

Ufafanuzi

"Stahili" linaelezea mtu au kitu kinachofaa kupewa heshima. "Kustahilisha" inamaana ya kuwa na thamani au muhimu. "isiyo na maana" inamaanisha isiyo na thamani.

taa

Ufafanuzi

Neno "taa" kawaida inamaanisha kitu kinachotoa mwanga. Taa zilizotumika nyakati za Biblia kawaida zilikuwa taa za mafuta. Aina ya taa iliyotumika katika Biblia ni chombo na sehemu ya kuwekea mafuta, yanayotoa mwanga inapowashwa.

Kawaida taa za mafuta zilitengenezwa kwa chombo cha kawaida cha udongo kilichojaa mafuta ya mzeituni, na utambi ukiwekwa kwenye mafuta ili uwake. Kwa baadhi ya taa, chombo lilikuwa na umbo la yai, na sehemu moja ikiwa imefinywa karibu kuushikilia utambi. Taa ya mafuta iliweza kubebwa au kuwekwa katika kinara ili mwanga wake ujaze chumba au nyumba. Katika maandiko, taa zinatumika kwa njia kadhaa kimithali kama ishara ya mwanaga na uhai.

tafuta

Ufafanuzi

Neno "tafuta" la maanisha kutafuta kitu au mtu. Inaweza kuwa na maana ya "jaribu kwa bidii" au "tia juhudi" kufanya kitu.

tai

Ufafanuzi

Tai ni ndege mbua mkubwa sana, mwenye nguvu ambaye hula wanyama wadogo kama vile samaki, panya, nyoka na kuku.

Biblia hulinganisha kasi na nguvu ya jeshi kwa jinsi tai hupaa chini kukamata nyama yake kwa kasi na ghafla.

Isaya anasema ya kwamba wale wanaomtumaini Bwana watapaa juu kama tai afanyavyo. Hii ni lugha ya tamathali inayotumika kuelezea uhuru na nguvu ambao unakuja kutokana na kumuamini na kumtii Mungu.

Katika kitabu cha Danieli, urefu wa nywele za Mfalme Nebukadreza zililinganishwa na urefu wa manyoya ya tai, ambayo yanaweza kuwa zaidi ya sentimita 50.

takatifu

Ufafanuzi

Msemo "takatifu" una maana ya kitu chochote kinachomhusu Mungu.

Baadhi ya njia ambazo msemo huu unatumika ni, "mamlaka takatifu", "hukumu takatifu", "asili takatifu", "nguvu takatifu", na "utukufu mtakatifu".

Katika sehemu moja ndani ya Biblia, msemo "takatifu" unatumika kuelezea jambo juu ya uungu wa uongo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri msemo wa "takatifu" zinaweza kujumuisha "ya Mungu" au "kutoka kwa Mungu" au "fungamana na Mungu" au "huonyesha ni ya Mungu".

Kwa mfano, "mamlaka takatifu" inaweza kutafsiriwa kama "mamlaka ya Mungu" au "mamlaka ambayo yanatoka kwa Mungu".

Msemo wa "utukutufu takatifu" unaweza kutafsiriwa kama "utukufu wa Mungu" au "utukufu ambao Mungu ame" au "utukufu unatoka kwa Mungu".

Baadhi ya tafsiri zinapendelea kutumia neno tofauti wanapofafanua jambo ambalo linafungamana na mungu wa uongo.

takatifu, utakatifu

Ufafanuzi

Maneno 'takatifu' na 'utakatifu' hurejelea tabia ya Mungu ambayo imetengwa na kutofautishwa na kila kitu ambacho ni chenye dhambi na kisicho kamili. Mungu pekee ndiye mtakatifu kweli. Hufawafanya watu na vitu kuwa vitakatifu. Mtu aliye mtakatifu ni mali ya Mungu na ametengwa maalumu kwa kusudi la kumtumika Mungu na kumpa utukufu Yeye. Na kitu ambacho Mungu amekitangaza kuwa ni kitakatifu ni kile ambacho Mungu amekitenga kwa ajili ya utukufu wake na matumizi yake, kwa mfano madhabahu ambayo makusudi yake ni kumtolea Mungu sadaka. Kwa kuwa Mungu ni mtakatifu, hakuna mtu awezaye kumkaribia Mungu isipokuwa awe ameruhusiwa na Yeye kufanya hivyo, hii ni kwasababu wao ni watu tu, wenye dhambi na wasiokamili. katika Agano la Kale, Mungu alitenga makuhani kama watakatifu kwa huduma maalumu kwake. Walitakiwa kutakaswa kwa sherehe maalumu ili waweze kumkaribia Mungu. Mungu pia aliweza kutenga sehemu na vitu maalumu kuwa vitakatifu vilivyo mali yake au kupitia kwa vitu hivyo aweze kujifunua mwenyewe, vitu hivi ni kama hekalu.

Mapendekezo ya tafsiri Njia za kutafsiri neno 'takatifu' zinaweza kuwa ' kutengwa kwa ajili ya Mungu,' au "kuwa mali ya Mungu" au "hali ya kutokuwa na dhambi" au "kuwa safi." kufanya kitu/kuwa kuwa mtakatifu ina maana ya "kutakasa'' au ''kutenga''

takatifu

Ufafanuzi

Neno "takatifu" la elezea kitu kinacho husu kumuabudu Mungu au wapagani wanao abudu miungu ya uongo.

tambua, tambuzi

Ufafanuzi

Msemo "tambua" una maana ya kuweza kuelewa jambo, haswa kuweza kujua kama jambo ni sahihi au baya.

Msemo wa "tambuzi" una maana ya kuelewa na kuamua kwa hekima kuhusu jambo fulani.

Ina maana kuwa na hekima na maamuzi mazuri.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "tambua" inaweza pia kutafsiriwa kama "kuelewa" au "kujua tofauti kati ya" au "kutofautisha mema na mabaya" au "kuhukumu sahihi kuhusu" au "kuelewa mema kwa mabaya".

"Tambuzi" inaweza kutafsiriwa kama, "uelewa" au "uwezo wa kuchambua mema na mabaya"

tamka, tamko

Ufafanuzi

Msemo wa "tamka" au "tamko" una maana ya kutoa kauli maalumu kwa umma, mara nyingi kusisitiza jambo.

"Tamko" halisisitizi umuhimu tu wa kile kinachotamkwa, lakini inavuta nadhari kwa yule anayetoa tamko hilo.

Kwa mfano, katika Agano la Kale, ujumbe kutoka kwa Mungu mara nyingi hutanguliwa na "tamko la Yahwe" au "hivi ndivyo Yahwe asemavyo". Msemo huu unasisitiza ya kwamba ni Yahwe mwenyewe anayesema hivi. Ukweli ya kwamba ujumbe unatoka kwa Yahwe unaonyesha jinsi ujumbe ulivyo na umuhimu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "tamka" inaweza pia kutafsiriwa kama "tangaza" au "eneza wazi" au "sema kwa nguvu" au "tamka kwa kishindo".

Msemo "tamko" unaweza kutafsiriwa kama, "kauli" au "tangazo".

Msemo, "hili ni tamko la Yahwe" linaweza kutafsiriwa kama, "hivi ndivyo Yahwe anavyotamka" au "hivi ndivyo Yahwe anavyosema".

tarumbeta

Ufafanuzi

Neno "tarumbeta" la eleza chombo cha kutoa mziki au kuita watu pamoka kwa mkutano au kikao.

tawanya, mtawanyiko

Ufafanuzi

Msemo "tawanya" na "mtawanyiko" ina maana ya kutawanya watu au vitu katika pande nyingi tofauti.

Katika Agano la Kale, Mungu anazungumza kuhusu "kutawanya" watu, kusababisha wao wajitenge na kuishi katika maeneo tofauti kati yao. Alifanya hivi kuwaadhibu kwa dhambi yao. Huenda kutawanyika ingeweza kuwasaidia kutubu na kuanza kumwabudu Mungu tena.

Msemo "mtawanyiko" unatumika katika Agano Jipya kumaanisha Wakristo ambao walitakiwa kuacha nyumba zao na kuhamia katika mahali tofauti nyingi kutoroka mateso.

Msemo "tawanyiko" unaweza kutafsiriwa kama "waumini katika maeneo mengi tofauti" au "watu waliohama kuishi katika mataifa tofauti".

Msemo "tawanya" unaweza kutafsiriwa kama "kutuma mbali katika maeneo mengi tofauti" au "kusambaza ng'ambo" au "kusababisha kuhamisha mbali kuishi katika nchi tofauti"

teketeza, uharibifu

Ufafanuzi

Msemo wa "kuteketezwa" au "uharibifu" ina maana ya kufanya mali ya mtu au ardhi kuharibika au kuangamizwa. Pia mara kwa mara hujumuisha kuangamiza au kukamata watu waishio katika ardhi hiyo.

Hii ina maana ya maangamizi kamili na makali sana.

Kwa mfano, mji wa Sodoma uliteketezwa na Mungu kama adhabu kwa dhambi za watu walioishi pale.

Msemo "uharibifu" unaweza kujumuisha kusababisha majonzi ya hisia yatokanayo na hiyo adhabu au uharibifu.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "teketeza" unaweza kutafsiriwa kama "kuangamiza kabisa" au "kuharibu kabisa".

Kulingana na muktadha, "uharibifu" inaweza kutafsiriwa kama "maangamizi kamili" au "uharibifu kamili" au "majonzi ya juu sana" au "balaa".

teseka, kuteseka

Ufafanuzi

Maneno "teseka" na "kuteseka" yanaeleza kupitia kitu kisicho pendeza, kama ugonjwa, maumivu, au magumu.

tetemeka

Ufafanuzi

Neno "tetemeka" lina maana ya kutikisika kwa hofu au msongamano wa mawazo.

theluji

Ufafanuzi

Neno "theluji" ya husu chembe nyeupe za maji yaliyo ganda yanayo anguka kutoka mawinguni sehemu ambazo hali ya hewa ni ya baridi.

thibitisha, uthibitisho

Ufafanuzi

Thibitisha au uthibitisho ni kuwa na hakika kuwa jambo fulani ni la kweli au kuaminika.

tii, mtiifu, utiifu

Ufafanuzi

Neno "tii" lina maana ya kufanya unachopaswa au kuamriwa. Neno "mtiifu" la eleza tabia ya mtu anaye tii. Wakati mwengine amri ni kuhusu kutofanya kitu, "usiibe"

timiza

Ufafanuzi

Msemo "timiza" una maana ya kukamilisha au fanikisha jambo ambalo lilitarajiwa.

Pale ambapo unabii unatimizwa, ina maana ya kwamba Mungu alisababisha itokee kile kilichotabiriwa katika unabii.

Kama mtu anatimiza ahadi au kiapo, ina maana ya kwamba anafanya kile alichoahidi kufanya.

Kutimiza jukumu ina maana kufanya kazi ambayo ulipangiwa au unapaswa kufanya.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "timiza" unaweza kutafsiriwa kama "fanikisha" au "kamilisha" au "kusababisha kutokea" au "kutii" au "kutenda".

Msemo "imetimizwa" inaweza kutafsiriwa kama "imekuwa kweli" au "imetokea".

Njia za kutafsiri "timiza" kama vile "timiza huduma yako" inaweza kujumuisha, "maliza" au "fanya" au "mazoezi" au "tumikia watu wengine kama vile Mungu amekuita kufanya"

towashi

Ufafanuzi

Mara kwa mara, "towashi" ina maana ya mwanamume ambaye amehanithishwa. Msemo baadaye ukawa msemo wa jumla kumaanisha afisa yeyote wa serikali, hata wale ambao hawana ulemavu huu.

Yesu alisema ya kwamba baadhi ya towashi walizaliwa vile, yawezekana kwa sababu ya uharibifu ya viuongo vya siri au kwa sababu ya kutokuwa kutekeleza jukumu la kuingiliana. Wengine huchagua kuishi kama towashi kwa maisha ya mseja.

Katika nyakati za kale, matowashi mara nyingi walikuwa watumishi wa wafalme ambao waliwekwa kama walinzi katika maeneo ya wanawake.

Baadhi ya matowashi walikuwa maafisa muhimu wa serikali, kama vile towashi wa Ethiopia ambaye alikutana na mtume Filipo katika jangwa.

tukuza, kutukuza

Ufafanuzi

Kutukuza ni kusifu kwa juu sana na kumheshimu mtu. Inaweza kumaanisha kumweka mtu katika nafasi ya juu.

Katika Biblia, msemo "tukuza" unatumika sana kwa ajili ya kumtukuza Mungu.

Mtu anapojitukuza mwenyewe, ina maana anawaza juu yake mwenyewe kwa hali ya kujiinua au namna ya kiburi.

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri "tukuza" zinaweza kujumuisha "kusifu kwa juu" au "kuheshimu sana" au "sifu sana" au "kuzungumza kwa juu sana"

Katika baadhi ya muktadha, inaweza kutafsiriwa kwa neno au msemo ambao una maana ya "kuweka nafasi ya juu zaidi" au "kutoa heshima zaidi" au "kuzungumza kuhusu kwa kiburi".

"Usijitukuze mwenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Usijiwazie kuwa juu sana" au "Usijidai juu yako mwenyewe".

"Wale wanaojiinua wenyewe" inaweza kutafsiriwa kama "Wale ambao hufikiri kwa kiburi kuhusu wao wenyewe" au "Wale wanaojidai juu yao wenyewe"

tukuza

Ufafanuzi

Msemo "tukuza" ina maana ya kuonyesha au kunena jinsi gani kitu au mtu ni mkubwa au muhimu. Ina maana ya "kutoa utukufu".

Watu wanaweza kumtukuza Mungu kwa kunena juu ya mambo mazuri aliyoyafanya.

Wanaweza kumtukuza Mungu kwa kuishi kwa njia ambayo inampa heshima na kuonyesha jinsi alivyo mkuu na wa ajabu.

Biblia inaposema ya kwamba Mungu hujitukuza mwenyewe, ina maana anajifunua kwa watu ukubwa wake wa ajabu, mara kwa mara kupitia miujiza.

Mungu Baba atamtukuza Mungu Mwana kwa kudhihirisha kwa watu ukamilifu wa Mwana, ufaharu na ukuu.

Kila mtu anayemwamini Kristo atatukuzwa na yeye. Wanapofufuliwa katika uzima, watabadilishwa kuakisi utukufu wake na kuonyesha neema yake kwa uumbaji wote.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo huu unaweza kutafsiriwa kama "kutoa utukufu kwa" au "kuleta utukufu kwa" au "kusababisha kuonekana kubwa".

Msemo "mtukuza Mungu" unaweza kutafsiriwa kama "kumsifu Mungu" au "kuzungumza juu ya ukuu wa Mungu" au "kuonyesha jinsi Mungu alivyo mkuu" au "kumheshimu Mungu"

tuma, kutuma nje, kutumwa

Ufafanuzi

"Kutuma" ni kusababisha mtu au kitu kwenda sehemu. "Kutuma nje" mtu ni kumwambia huyu mtu kwenda na kufanya japo au shughuli.

tunda, kuzaa

Ufafanuzi

Msemo "tunda" lina maana ya sehemu ya mmea ambao inaweza kuliwa. Kitu ambacho "kinazaa" kina matunda mengi. Misemo hii pia hutumika kitamathali katika Biblia.

Biblia mara kwa mara hutumia "tunda" kumaanisha matendo na mawazo ya mtu. Kama vile tunda juu ya mti linavyoonyesha ni aina gani ya mti, vile vile maneno na matendo ya mtu hudhihirisha silika yake ikoje.

Mtu anaweza kuzaa matunda ya kiroho mazuri au mabaya, lakini msemo "kuzaa" mara kwa mara una maana chanya ya kuzaa matunda mema.

Msemo "kuzaa" pia hutumika kitamathali kumaanisha "mafanikio". Hii mara kwa mara humaanisha kuwa na watoto na uzao mwingi, pamoja na kuwa na chakula kingi na utajiri mwingine.

Kwa ujumla, msemo "tunda la" una maana ya kitu chochote ambacho hutoka kwa au ambacho huzalishwa na kitu kingine. Kwa mfano, "tunda la hekima" lina maana ya mambo mazuri ambayo hutokana na kuwa na hekima.

Msemo "tunda la roho" una maana kijumla ya kila kitu ambacho nchi huzaa kwa ajili ya watu kula. Hii inajumlisha sio matunda pekee kama mizabibu au tende, lakini pia mboga, karanga na nafaka.

Msemo wa tamathali "tunda la Roho" una maana ya sifa nzuri ambazo Roho Mtakatifu hutoa katika maisha ya watu ambao humtii yeye.

Msemo "tunda la tumbo" una maana ya "kile ambacho tumbo huzaa" yaani, watotot.

ua, mahakama

Ufafanuzi

"Ua" ni eneo ambalo liko wazi juu na limezungukwa na ukuta. Neno "mahakama" linamaanisha sehemu ambayo hakimu huamua mambo ya sheria na jinai.

ufalme

Ufafanuzi

Ufalme ni kundi la watu linalotawalwana mfalme. Linamaanisha pia dola au sehemu za kisiasa ambalo mfalme au kiongozi mwingine ana madaraka na mamlaka.

Ufalme unaweza kuwa na ukubwa wowote kijiografia. Mfalme anaweza kutawala taifa au nchi au mji mmoja tu. Neno "ufalme" linaweza pia kumaanisha utawala wa kiroho au madaraka, kama usemi "ufalme wa Mungu." Mungu ni mtawala wa viumbe vyote, lakini usemi "ufalme wa Mungu" kwa mahsusi linamaanisha utawala juu ya watu waliomwamini Yesu na walionyenyekea kwa utawala wake. Biblia pia inazungumzia kuhusu Shetani kuwa na "ufalme" anao tawala kwa muda juu ya vitu vingi duniani. Ufalme wake ni uovu na unajulikana kama wa "giza."

ufalme wa Mungu, ufalme wa mbinguni

Ufafanuzi

Usemi wa "ufalme wa Mungu" na "ufalme wa mbinguni" zote zinamaanisha utawala wa Mungu na madaraka yake juu ya watu wake na viumbe vyote.

Wayahudi mara nyingi hutumia neno "mbingu" kumaanisha Mungu, ili kuepuka kutaja jina lake moja kwa moja. Katika kitabu cha Agano Jipya alichoandika Mathayo, aliuita ufalme wa Mungu kama "ufalme wa mbinguni," inawezekana kwa sababu alikuwa akiwaandikia zaidi Wayahudi. Ufalme wa Mungu unamaanisha Mungu kuwatawala watu kiroho pamoja na kuwatawala katika dunia ya kimwili. Manabii wa Agano la Kale walisema kuwa Mungu atamtuma Masihi kutawala kwa haki. Yesu, mwana wa Mungu, ndiye Masihi atakaye tawala juu ya watu wa Mungu milele.

ujasiri, jasiri

Ufafanuzi

Ujasiri ni kitendo cha kukabiliana au kufanya jambo gumu au la hatari.

ukoma, mkoma

Ufafanuzi

Neno "ukoma" linatumika katika Biblia kumaanisha aina kadhaaza magonjwa ya ngozi. "Mkoma" ni mtu mwenye ukoma. Neno "ukoma" pia linaweza kutumika kuelezea mtu au sehemu ya mwili iliyoadhirika na ukoma.

Aina flani za ukoma zinasababisha ngozi kupoteza rangi na mabaka meupe, kama Miriamu na Naamani walivyokuwa na ukoma. Katika nyakati za sasa, ukoma mara nyingi husababisha mikono, miguu, na sehemu zingine za mwili kuharibika. Kulingana na maelekezo ambayo Mungu aliwapa Waisraeli, mtu akiwa na ukoma, alionekana "mchafu" na ilimbidi kukaa mbali na watu wengine ili asiwaambukize na ugonjwa. Mkoma kawaida angasema "mchafu" ili wengine waonywe wasije karibu yake. Yesu aliponya wakoma wengi, pamoja na aina zingine za magonjwa.

umbo, sanamu ya kuchonga, umbo la kuchonga, umbo la chuma

Ufafanuzi

Maneno haya yote yanatumika kumaanisha sanamu ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kuabudu miungu ya uongo. Katika mazingira ya kuabudu sanamu, neno "sanamu" ni njia fupi ya kusema "sanamu ya kuchonga."

"Sanamu ya kuchonga" au "umbo la kuchonga" ni kitu cha mbao kilichofanywa kuonekana kama mnyama, mtu, au kitu. "Umbo la chuma" ni kitu au sanamu iliyoundwa kwa kuyeyusha chuma na kuimwaga katika umbo tupu ambalo lina umbo la kitu, mnyama, au mtu. Vitu hivi vya mbao na chuma vilitumika katika kuabudu miungu ya uongo. Neno "umbo" wakati wa kuzungumzia sanamu inamaanisha kati ya sanamu ya mbao au ya chuma.

uongo, ukaidi, kuipotosha

Ufafanuzi

Neno "kilichopotoka" linatumika kumuelezea mtu au tendo fulani ambalo linapotosha kimaadili. Neno "ukaidi" linamaana ya tabia ya kikaidi". Kupotosha kitu inamaana ya kugeuza jambo toka kwenye usahihi wake au uzuri wake.

uovu

Ufafanuzi

Neno "uovu" ni neno ambalo liko karibu kwa maana na neno "dhambi," lakini inaweza kumaanisha zaidi matendo ya ufahamu mabaya au uovu mkubwa.

Neno "uovu" ina maana halisi ya kupindisha au kupotosha (sheria). Inamaanisha udhalimu mkubwa. Uovu unaweza kuelezwa kama matendo ya kudhuru ya makusudi dhidi ya watu wengine. Maana zingine za uovu ni pamoja na "ukaidi" na "kunyima," ambayo yote ni maneno yanayoeleza hali za dhambi mbaya.

upanga

Ufafanuzi

Upanga ni silaha ya chuma nyembamba inayo tumika kukata au kuchoma. Ina mshikio na nch ndefu.

upendo

Ufafanuzi

Kumpenda mtu mwingine ni kumjali huyo mtu na kufanya vitu vitakavyo msaidia. Kuna maana tofauti za "upendo" ambazo lugha zingine zinawezakueleza kwa kutumia maneno tofauti:

  1. Aina ya upendo utokao kwa Mungu unalenga kwa ajili ya mema ya wengine, hata kama hayamnufaishi mtu anayependa. Aina hii ya upendo inawajali watu bila kujali wanachokifanya. Mungu mwenyewe ni upendo na ndiye chanzo cha upendo wa kweli.

Yesu alionesha aina hii ya upendo kwa kujitolea maisha yake kama sadak ili kutuokoa kutoka kwenye dhambi na mauti. Aliwafundisha pia wafuasi wake kuwapenda wengine kwa kujitolea. Watu wanapowapenda wengine na aina hii ya upendo, inahusisha matendo yanayoonesha kuwa mtu anafikiria yale yatakomsaidia mtu mwingine kufanikiwa. Aina hii ya upendo inahusisha zaidi kusamehe wengine. Katika ULB, neno "upendo" linamaanisha aina hiiya upendo wa kujitoa, isipokuwa noti ya tafsiri iashirie maana tofauti.

  1. Neno jingine katika Agano Jipya linamaanisha upendo wa kindugu au upendo kwa ajili ya rafiki au mwana familia.

Neno hili linamaanisha upendo wa asili wa binadamu kati ya marafiki na ndugu. Inawezekana kutumika katika mazingira kama, "Wanapenda kukaa kwenye viti muhimu katika sherehe." Hii inamaanisha "wanatamani sana" kufanya hivyo.

  1. Neno "upendo" linaweza pia kumaanisha upendo wa kimapenzi kati ya mwanamme na mwanamke.
  2. Katika hali ya kimithali, "Yakobo nimempenda, lakini Esau nimemchukia", neno "mpenda" linamaanisha Mungu kumchagua Yakobo kuwa katika mahusiano ya maagano na yeye. Hii inaweza pia kutafsiriwa kama "kuchaguliwa." Ingawa Esau alibarikiwa pia na Mungu, hakupewa heshima ya kuwa katika maagano. Neno "kuchukia" linatumika kimithali hapa kumaanisha "kukataliwa" au "kutokuchaguliwa."

upole

Ufafanuzi

Neno "upole" la elezea mtu aliye mtaratibu, mnyenyekevu, na aliye tayari kuteseka dhuluma. Upole ni uwezo wa kuwa mtaratibu ata kama ukali au nguvu inaonekana ni sahihi.

ushauri, mshauri

Ufafanuzi

Ushauri inamaana ya kumsaidia mtu kuamua kwa busara juu ya jambo fulani. Mshauri mwenye busara ni mtu anayetoa ushauri ambao utamsaidia mtu kuamua kwa usahihi.

ushuhuda, shuhudia

Ufafanuzi

Maneno, "ushuhuda" na "shuhudia" yanaeleza kutamka tamko kuhusu kitu ambacho mtu anajua kuwa ni kweli.

ushuru

Ufafanuzi

Neno "ushuru" la husu zawadi kutoka kwa mtawala mmoja kwenda kwa mwingine, kwa kusudi la ulinzi na mausiano mema kati ya mataifa yao.

ushuru

Ufafanuzi

Ushuru ni pesa au bidha watu wanazo lipa kwa serikali iliyo na mamlaka juu yao.

uso

Ufafanuzi

Neno "uso" lina maana ya sehemu ya mbele ya kichwa cha mtu. Msemo huu pia una maana kadhaa za tamathali.

Msemo wa "uso wako" mara kwa mara ni njia ya tamathali ya kusema "wewe". Vivyo hivyo, msemo "uso wangu" mara kwa mara una maana ya "Mimi".

Katika hali ya kimwili, "kumkabili" mtu au kitu ina maana ya kutazama upande wa huyo mtu au kitu.

"Kukabiliana" ina maana ya "kutazamana"

Kuwa "uso kwa uso" ina maana ya kwamba watu wawili wanatazamana katika umbali wa karibu.

Yesu "alipoweka uso wake kuelekea Yerusalemu" ina maana ya kwamba aliamua kwa dhati kwenda.

"Kuweka uso dhidi ya" watu au mji ina maana kuamua kwa nguvu: kutoimarisha tena, au kumkataa mtu au mji huo.

Msemo "uso wa nchi" una maana ya sehemu ya juu ya dunia na mara kwa mara ni kumbukumbu ya jumla ya dunia nzima. Kwa mfano, "njaa inayofunika uso wa dunia" ina maana ya njaa inayosambaa ambayo hugusa watu wengi wanaoishi juu ya nchi.

Msemo wa tamathali, "usifiche uso wako kwa watu wako" una maana "usiwakatae watu wako" au "usiwaache watu wako" au "usiache kuwatunza watu wako".

Mapendekezo ya Tafsiri

Ikiwezekana, ni bora kubaki na msemo au kutumia msemo katika lugha hii ambayo ina maana ya kufanana.

Msemo "kukabili" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka upande wa" au "kutazama moja kwa moja" au "kuangalia uso wa".

Msemo "uso kwa uso" unaweza kutafsiriwa kama "karibu kabisa" au "mbele ya" au "katika uwepo wa".

Kulingana na muktadha, msemo "mbele ya uso wake" unaweza kutafsiriwa kama "kabla yake" au "mbele yake" au "katika uwepo wake".

Msemo "weka uso wake kuelekea" unaweza kutafsiriwa kama "kuanza kusafiri kuelekea" au "aliamua akilini mwake kuondoka".

Msemo "kuficha uso wake kutoka kwa" unaweza kutafsiriwa kama "kugeuka kutoka kwa" au "kuacha kusaidia au kulinda" au "kukataa".

"Kuweka uso wake dhidi ya" mji au watu inaweza kutafsiri kama "kutazama kwa hasira na kushutumu" au "kukataa kukubali" au "kuamua kukataa" au "kulaumu na kukataa" au "kutoa kuhukumu".

Msemo "tamka mbele ya uso wao" inaweza kutafsiriwa kama "sema kwao moja kwa moja".

Msemo " katika uso wa nchi" inaweza kutafsiriwa kama "katika nchi yote" au "juu ya dunia nzima" au "kuishi katika dunia".

utukufu, fahari

Ufafanuzi

Kwa ujumla, msemo "utukufu" una maana ya heshima, fahari, na ukuu wa hali ya juu sana. Kitu chochote ambacho kina utukufu kinasemekana kuwa na "fahari".

Mara nyingi, "utukufu" ina maana ya kitu chenye thamani kubwa na umuhimu. Katika muktadha zingine inawasilisha ufahari, mwanga, au hukumu.

Kwa mfano, msemo "utukufu wa wafugaji" una maana ya malisho yaliyostawi sana ambapo kondoo wao walikuwa na nyasi nyingi za kula.

Utukufu haswa hutumika kumfafanua Mungu, ambay ana ufahari zaidi ya yeyote au chochote katika ulimwengu. Kila kitu katika tabia yake huonyesha utukufu na ufahari wake.

Msemo "kutukuzwa na" una maana ya kujidai juu ya au kujivunia na kitu.

utukufu

Ufafanuzi

Neno "utukufu" la eleza uzuri wa ajabu na umaridadi ambao una ambatana na utajiri na muonekano wa kuvutia.

uvumba

Ufafanuzi

Neno "uvumba" linamaanisha mchanganyiko wa vikolezo vyenye manukato mazuri vinavyochomwa kutoa moshi wenye harufu nzuri.

Mungu aliwaambia Waisraeli kuchoma uvumba kama sadaka kwake. Huu uvumba ulitakiwa kutengenezwa kwa kuchanganya kiwango sawa cha vikolezo maalumu vitano kama Mungu alivyoagiza. Huu ulikuwa uvumba mtakatifu, kwa hiyo hawakutakiwa kuutumia kwa kitu kingine chochote. "Madhabahu ya kufukuzia uvumba" ilikuwa madhabahu maalumu ya kuchomea uvumba. Uvumba ulitolewa angalau mara nne kwa siku, kwa kila saa ya maombi. Ilitolewa pia kila wakati sadaka ya kuteketeza ilipotolewa. Kuchomwa kwa uvumba kunaashiria maombi na kuabudu vinaponyanyuka juu kwa Mungu kutoka kwa watu wake. Njia zingine za kutafsiri "uvumba" zinaweza kuwa, "vikolezo vya manukato mazuri" au "mimea yenye harufu nzuri."

uwezo

Ufafanuzi

Neno "uwezo" la husu kuwa na nguvu nyingi.

uwezo

Ufafanuzi

Neno "uwezo" la husu hali ya kuwa na nguvu kimwili, kihisia, au kiroho.

uzao, kutokana na

Ufafanuzi

"Uzao" ni mtu ambaye ni ndugu wa damu moja kwa moja wa mtu mwingine nyuma kabisa katika historia.

Kwa mfano, Abrahamu alikuwa uzao wa Nuhu. Uzao wa mtu ni watoto wake, wajukuu, na watukuu, na kuendelea. Vizazi vya Yakobo vilikuwa makabila kumi na mawili ya Israeli.

msemo "kutokana na" ni njia nyingine ya kusema "uzao wa" kama vile "Abrahamu alitokana na Nuhu". Hii inaweza kutafsiriwa kama "kutokana na uzao wa"

vumilia, uvumilivu

Ufafanuzi

Msemo "vumilia" una maana ya kudumu muda mrefu au kustahamili jambo gumu kwa uvumilivu.

Pia ina maana ya kusimama imara wakati wa mitihani kuwepo, bila kukata tamaa.

Msemo "uvumilivu" unaweza kumaanisha "subira", "ustahamilivu katika majaribu" au "kustahamili pale unapoteswa".

Faraja kwa Wakristo "kuvumilia mpaka mwisho" ni kuwaambia wamtii Yesu, hata kama hili litasababisha wao kuteseka.

"Kuvumilia mateso" pia inaweza kumaanisha "kupitia mateso".

Mapendekezo ya Tafsiri

Njia za kutafsiri msemo "vumilia" zinaweza kujumuisha "stahamili" au "kuendelea kuamini" au "kuendelea kufanya kile Mungu anachotaka ufanye" au "simama imara".

Katika baadhi ya muktadha, "kuvumilia" kunaweza kutafsiriwa kama, "kupitia jaribu" au "kupitia".

Kwa maana ya kudumu muda mrefu, msemo "vumilia" unaweza kutafsiriwa kama "kudumu" au "kuendelea". Msemo, "hatavumilia" unaweza kutafsiriwa kama, "hatadumu" au "hataendele kuishi".

Njia za kutafsiri "uvumilivu" unaweza kujumuisha "ustahamilivu" au "kuendelea kuamini" au "kubaki mwaminifu".

wana wa Mungu

Ufafanuzi

Jina, "wana wa Mungu" ni msemo wa mfano wenye maana kadhaa.

watakatifu

Ufafanuzi

Neno "watakatifu" lina maana ya halisi ya "waliyo wasafi" na kueleza waamini wa Yesu.

watoza ushuru

Ufafanuzi

"Mtoza ushuru" alikuwa mfanya kazi wa serikali ambaye kazi yake ilikuwa kupokea pesa watu waliyo paswa kulipa serikali ushuru.

wavuvi

Ufafanuzi

Wavuvi ni wanamume ambao hukamata samaki kutoka majini kama njia ya kupata pesa. Katika Agano Jipya, wavuvi walitumia mitego mikubwa kukamata samaki. Msemo "wavuvi" ni jina lingine la mvuvi.

Petro na mitume wengine walifanya kazi kabla ya kuitwa na Yesu.

Kwa kuwa nchi ya Israeli ilikuwa karibu na maji, Biblia ina kumbukumbu nyingi ya samaki na wavuvi.

Msemo huu unaweza kutafsiriwa na msemo kama "wanamume wanaokamata samaki" au "wanamume wanaopata pesa kwa kukamata samaki"

weka wakfu, kuwekwa wakfu kwa

Ufafanuzi

Kuweka wakfu ni kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu au shughuli.

Daudi aliweka wakfu dhahabu na fedha zake kwa Bwana.

Mara kwa mara, neno "kujitolea" lina maana ya tukio rasmi au sherehe ya kuweka kando kitu kwa ajili ya kusudi maalumu.

Kuweka wakfu kwa madhabahu ilijumuisha kutoa sadaka kwa Mungu.

Nehemia aliwaongoza Waisraeli katika kuweka wakfu kwa kuta za Yerusalemu zilizotengenezwa kwa ahadi mpya ya kumtumikia Yahwe pekee kwa vyombo vya muziki na kuimba.

Msemo wa "kuweka wakfu" unaweza kutafsiriwa kama "kutenga kusudi maalumu" au "kabidhi kitu kutumika kwa kazi maalumu" au "kabidhi mtu kutenda tendo maalumu".

wema, uzuri

Ufafanuzi

Neno "uzuri" una maana nyingi kutegemea na muktadha. Lugha nyingi hutumia maneno tofauti kutafsiri maana hizi tofauti.

Kwa ujumla, kitu ni kizuri kama kinalingana na tabia ya Mungu, kusudi na mapenzi.

Kitu ambacho ni "kizuri" kinaweza kufurahisha, bora, msaada, kinachofaa, chenye manufaa, au sahihi kimaadili.

Ardhi ambayo ni "nzuri" inaweza kuitwa "yenye rutuba" au "yenye kuzaa".

Zao "zuri" linaweza kuwa zao "la wingi".

Mtu anaweza kuwa "mzuri" katika kile afanyacho kama ana ujuzi katika kazi yao, yaani "mkulima mzuri".

Katika Biblia, maana ya jumla ya "nzuri" mara nyingi hutofautishwa na "uovu".

Msemo "wema" mara nyingi humaanisha kuwa mzuri kimaadili kwa kutoa mambo mazuri na yenye manufaa. Inaweza kumaanisha utimilifu wake wa kimaadili.

woga, hofu, hofu ya Yahwe

Ufafanuzi

Msemo "woga" au "hofu" ina maana ya hisia zisizo nzuri mtu huwa nazo ambapo kuna tishio la kudhuriwa kwake au kwa wengine.

Msemo "hofu" unaweza kumaanisha heshima kubwa na hofu mtu huwa nayo kwa mamlaka.

Msemo "hofu ya Yahwe" na misemo ya kufanana "hofu ya Mungu" an "hofu ya Bwana" ina maana ya kumheshimu sana Mungu na konyesha heshima kwa kumtii yeye. Hofu hii inahamasishwa kwa kujua ya kwamba Mungu ni mtakatifu na anachukia dhambi.

Biblia inafundisha ya kwamba mtu anayemwogopa Yahwe atakuwa na hekima.

Mapendekezo ya Tafsiri

Kulingana na muktadha, "kuwa na hofu" kunaweza kutafsiriwa kama "kuogopa" au "kuheshimu sana" au "kuhofu" au " kuwa na hofu ya"

Msemo "woga" inaweza kutafsiriwa kama "kuogopa".

Sentensi, "Hofu ya Mungu ilianguka juu yao wote" inaweza kutafsiriwa kama, "Ghafla wote wakapatwa na hofu kuu na heshima kwa Mungu" au "Mara ghafla wote wakahisi kushangazwa sana na kumhofu Mungu sana" au "Wakati huo huo, wote wakapatwa na hofu ya Mungu"

woga, kutishwa

Ufafanuzi

Istilahi ' hofu' hurejelea hisia kali za woga or kitisho. Mtu aliye na hofu huwa ameogopa. woga ni hali kali na kubwa zaidi ya hofu, zaidi ya hofu ya kawaida. Mara kwa mara mtu anapokuwa ametishwa huwa ameshitushwa na ameshangazwa sana.

woga, kuogopesha

Ufafanuzi

Neno "woga" uelezea hisia ya hofu kuu. "Kuogopesha" mtu ina maana ya kusababisha huyo mtu kujisikia wasi wasi sana.

zawadi

Ufafanuzi

Msemo "zawadi" una maana ya kitu chochote ambacho hupewa au kutolvwa kwa mtu. Zawadi inatolewa bila matarajio ya kurudishiwa kitu chochote.

Pesa, chakula, mavazi, au vitu vingine zitolewazo kwa watu maskini zinaitwa "zawadi".

Katika Biblia, sadaka itolewayo kwa Mungu pia hujulikana kama zawadi.

Zawadi ya wokovu ni kitu ambacho Mungu anatupatia kupitia imani kwa Yesu.

Katika Agano Jipya, msemo "zawadi" pia hutumika kumaanisha uwezo maalumu wa kiroho ambao Mungu hutoa kwa Wakristo wote kutumikia watu wengine.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo wa jumla wa "zawadi" unaweza kutafsiriwa na neno au msemo ambao una maana ya "kitu ambacho kinatolewa".

Katika muktadha wa mtu kuwa na zawadi au uwezo maalumu ambao unatoka kwa Mungu, msemo "zawadi kutoka kwa Roho" unaweza kutafsiriwa kama "uwezo wa kiroho" au "uwezo maalumu kutoka kwa Roho Mtakatifu" au "kipaji maalumu cha kiroho ambacho Mungu ametoa"

zinaa

Ufafanuzi

Msemo "zinaa" una maana ya tendo la ngono ambalo hufanyika nje ya mahusiano ya ndoa ya mwanamume na mwanamke. Hii ni kinyume na mpango wa Mungu.

Msemo huu unaweza kumaanisha tendo lolote la kingono ambalo ni kinyume na mapenzi ya Mungu, ikiwemo matendo ya usenge na ponografia.

Aina moja ya zinaa ni uzinzi, ambayo ni tendo la ngono haswa kati ya mtu aliyeoa na mtu ambaye sio mke au mume wake.

Aina nyingine ya zinaa ni "ukahaba" ambayo uhusisha kulipwa kufanya ngono na mtu.

Msemo huu pia hutumika kitamathali kumaanisha ukosefu wa uaminifu wa Israeli kwa Mungu walipoabudu miungu ya uongo.

Mapendekezo ya Tafsiri

Msemo "zinaa" unaweza kutafsiriwa kama "uzinzi" ikiwa maana sahihi ya msemo inaeleweka.

Njia zingine za kutafsiri msemo huu zinaweza kujumuisha "matendo mabaya ya ngono" au "ngono nje ya ndoa".

Msemo huu unaweza kutafsiriwa katika njia nyingine kutoka kwa neno "uzinzi".

Tafsiri ya matumizi ya tamathali ya msemo huu unatakiwa kukaa na maana halisi ikiwezekana kwa kuwa kuna ulinganisho wa kufanana katika Biblia kati ya kutokuwa mwaminifu kwa Mungu na kutokuwa mwaminifu katika mahusiano ya kimapenzi.