1 Nyakati zilizopita Mungu alizungumza na mababu zetu kupitia manabii mara nyingi na kwa njia nyingi. 2 Lakini katika siku hizi tulizonazo, Mungu ameongea nasi kupitia Mwana, ambaye alimweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia yeye pia aliumba ulimwengu. 3 Mwanawe ni nuru ya utukufu wake, tabia pekee ya asili yake, na anayeendeleza vitu vyote kwa neno la nguvu zake. Baada ya kukamilisha utakaso wa dhambi, aliketi chini mkono wa kulia wa enzi huko juu. 4 Amekuwa bora kuliko malaika, kama vile jina alilolirithi lilivyo bora zaidi kuliko jina lao. 5 Kwa maana ni kwa malaika gani aliwahi kusema, "Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako?" Na tena, "Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana kwangu?" 6 Tena, wakati Mungu alipomleta mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, husema, "Malaika wote wa Mungu lazima wamwabudu." 7 Kuhusu malaika asema, "Yeye ambaye hufanya malaika zake kuwa roho, na watumishi wake kuwa ndimi za moto." 8 Lakini kuhusu Mwana husema, "Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele. Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki. 9 Umependa haki na kuchukia uvunjaji wa sheria, kwa hiyo Mungu, Mungu wako, amekupaka mafuta ya furaha kuliko wenzako." 10 Hapo mwanzo, Bwana, uliweka msingi wa dunia. Mbingu ni kazi za mikono yako. 11 Zitatoweka, lakini wewe utaendelea. Zote zitachakaa kama vazi. 12 Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilika kama vazi. Lakini wewe ni yuleyule, na miaka yako haitakoma." 13 Lakini ni kwa malaika yupi Mungu alisema wakati wowote, "Keti mkono wangu wa kulia mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa kiti cha miguu yako"? 14 Je, malaika wote siyo roho zilizotumwa kuwahudumia na kuwatunza wale watakaourithi wokovu?
Sura hii inaonyesha jinsi Yesu ni muhimu kwa sisi kuliko malaika.
Watafsiri wengine wametenga kila mshororo wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 1:5, 7-13, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Mwandishi aliandikia barua hii Wakristo waliokuwa wamekua kama Wayahudi.Hii ndiyo maana barua hii inaitwa "Waebrania".
Mwandishi anatumia maswali ya hadithi kama njia ya kuthibitsha kwamba Yesu ni bora kuliko malaika. Yeye pamoja na wasomaji wake wanafahamu majibu ya maswali na mwandishi anajua kwamba wakati wasomaji wanafikiria juu ya majibu ya maswali, watakuja kufahamu kwamba Mwana wa Mungu ni muhimu kuliko malaika wowote.
Walimu Wayahudi sawa na manabii wa Agano la kale, waliyaweka masomo yao mengi ya muhimu kwa ushairi ili wasikilizaji waelewe na kuyakumbuka.
Hii inaweka msingi wa kitabu chote: Ukuu wa Mwana- Mwana ni mkuu kuliko wote. Kitabu kinaanza na msisitizo kwamba Mwana ni mkuu kuliko manabii na malaika.
Ingawa haijaelezwa mwanzoni mwa kitabu, barua hii iliandikwa kwa Waebrania Wakati (Wayahudi) ambao kimsingi walikuwa wanaelewa maelekezo mengi ya Agano la Kale.
''Mwana" ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
Mwandishi anamwelezea kana kwamba Mwana atarithi utajiri na mali kutoka kwa Baba. AT: " kumilili vitu vyote"
"Ni kupitia yeye pia Mungu aliviumba vitu vyote.
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
"mwanga wa utukufu wake.'Utukufu wa Mungu una muunganiko wa mng'ao sana. Mwandishi anasema Mwana anabeba mng'ao huo na anamwakilisha Mungu kwa ukamilifu.
"sura ya Uungu wa mungu." Hii ina maana sawa na "mng'ao wa utukufu wa Mungu" Mwana anabeba tabia na asili ya Mungu na anawakilisha uungu wote wa Mungu. inaweza kusemwa katika
"neno lake la nguv." Hapa "neno" linamaanisha ujumbe au amri. AT: "amri yake ya nguvu"
Jina dhaniwa"takasa" linaweza kuelezea kama kitenzi: "kufanya safi." AT: "Baada ya kumaliza kutufanya kuwa safi' au baada ya kumaliza kututakasa kutoka katika dhambi zetu"
Mwandishi anaongea juu ya msamaha wa dhambi kana kwamba ulikuwa unamfanya mtu kuwa safi. AT: amefanya uwezekano kwa ajili ya Mungu kusamehe dhambi"
Hapa "mkono wa kulia" linamaanisha sehemu ya utukufu.AT: "aliketi katika sehemu ya utukufu karibu na kwenye enzi"
"Hapa "enzi" linamaanisha Mungu. AT: "Mungu mwenye enzi
Hii ni nukuu ya kinabii (Wewe mwanangu) inatoka katika Zaburi. Nabii Samweli aliandika unabii wa pili (nitakuwa baba kwake). Maneno yote ambaye yanamaanisha Yesu. Neno "Wewe" linamaana ya Yesu, na neno "Mimi" linamaanisha Mungu Baba.
''Mwana amefanyika"
Mwanaidishi anaongea katika swala la kupokea heshima na mamlaka kana kwamba alikuwa akirithi utajiri na mali kutoka kw baba yake.AT: "amepokea."
Swali linasistiza kuwa Mungu hamwita malaika yeyote mwana wake. AT: " kwa sababu Mungu hajawahi kumwabia malaika yeyote 'Wewe ni mwana wangu... mwana kwangu."
"Na tena, hakuwahi kusema kwa malaika yeyote, '...kwangu'?"
Uhusiano maalumu Mungu Baba alionao na Mungu Mwana umeelezwa katika Agno la Kale mamia ya miaka kabla ya Yesu kuzaliwa.
maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kimoja.
Nukuu ya kwanza katika sehemu hii (Malaika wote wa Mungu...) inatoka katika moja ya kitabu alivyoandika Musa. Na nukuu ya pili (Yeye afanyaye ...) inatoka katika kitabu cha Zaburi.
Hii inamanisha Yesu.Mwandishi anamwelezea Yesu kama "mzaliwa wa kwanza" kusisitiza umuhimu na mamlaka juu ya mtu yeyote. Haina maana ya kuwa kulikuwa na wakati fulani ambao Yesu hakuwepo au kwamba Mungu alikuwa na wana kama Yesu. AT: "Mwana wake mheshimiwa, Mwana wake wa pekee.
"Mungu anasema"
Maana inayowezekana: 1) "Mungu amewafanya malaika wae kuwa roho zinazomtumikia kwa nguvu kama miali ya moto." (UDB) au 2)Mungu hufanya upepo na miali ya moto kuwa "watumwa" na watumishi wake. Katika lugha za asili neno "malaika" ni sawa na neno "mtumishi," na neno "roho" ni sawa na "upepo." Kwa maana yoyote ile ujumbe kusudiwa ni kwamba malaika wanamtumika Mwana kwa kuwa ni mkuu,
Nukuu hii ya andiko inatoka katika kitabu cha Zaburi
"Lakini Mungu asema hivi kuhusu Mwana"
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
Kiti cha enzi kinawakilisha utawala. AT: " Wewe ni Mungun na utawala wako utadumu milele"
Fimbo yautawala inamaanisha utawala wa Mwana. AT: "Na utatawala juu ya watu katika ufalme wako kwa haki"
Hapa "mafuta ya furaha" inamaanisha furaha aliyokuwa nayo wakati Mungu alipo muheshimu. AT:"amekuheshimu na amekufanya kuwa na furaha zaidi ya yeyote.
Mwanadishi anaendelea kufanua kwamba Yesu ni mkuu kwa malaika.
Nukuu hii inatoka katika Zaburi.
"Kabla ya kitu chochote hakijakiwapo"
Mwandishi anaongea Mungu kuumba dunia kana kwamba anajenga juu ya msingi. AT: " uliumba dunia"
Hapa "mikono" inamaanisha nguvu na matendo ya Mungu.AT: "uliziumba mbingu"
"Mbingu na nchi zitapotea" au " mbingu na nchi hazitakuwepo tena"
Mwandishi anaongea juu mbingu na nchi kama ilikuwa ni kipande cha vazi ambayo itazeeka na mwishowe na kutofaa.
Mwandishi anaongea kana kwamba mbingu na na nchi ni nguo au aina nyingine ya vazi.
Mwandishi anaongea juu ya mbingu na na nchi kana kwamba ni nguo ambazo zinaweza kubadlishwa
Hii inaweza kusema katika muundo tendaji. AT: "utazibadilisha"
Vipindi vya nyakati vinatumika kuwakilisha Uwepo wa Mungu wa milele.AT: "maisha yako hayatakuwa na mwisho"
Nukuu hii inatoka katika Zaburi nyingine.
Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba Mungu hajawahi kumwambia malaika. AT: '"Lakini Mungu hajamwambia malaika yeeyote wakati wowote"'
Hapa mkono wa kulia unamaanisha sehemu ya heshima. AT: "Kaa karibu yangu katika sehemu ya heshima"
Maadui wa Kristo wanaongelewa kana kwamba watakuwa chombo ambachomfalme anaweka miguu yake, Picha hii inawakilisha kushindwa na aibu kwa maadui wake.
Mwandishi anatumia hili swali kuwakumbusah wasomaji wake kwamba malaika hawana nguvu kama Kristo, lakini wana jukumu tofauti. AT: "malakia wote ni roho ambazo... hurithi wokovu."
Kupokea kile ambacho Mungu amewaahidi waumini imeongelewa kana kwamba wanarithi utajiri na mali kutoka katika mwana familia. AT: "kwa ajili ya wale wote ambao Mungu atawaokoa"
1 Kwa hiyo ni lazima tuweke kipaumbele zaidi kwa yale tuliyosikia, ili kwamba tusije tukatengwa mbali nayo. 2 Kwa maana ikiwa ujumbe uliozungumzwa na malaika ni halali, na kila kosa na uasi hupokea adhabu tu, 3 tutapataje kuepuka kama tusipojali wokovu huu mkuu? —wokuvu ambao kwanza ulitangazwa na Bwana na kuthibitishwa kwetu na wale waliousikia. 4 Mungu pia aliuthibitisha kwa ishara, maajabu, na kwa matendo makuu mbalimbali, na kwa zawadi za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake mwenyewe. 5 Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika. 6 Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, "Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze? 7 mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. "Na umemuweka juu ya kazi ya mikono yako.) 8 Umeweka kila kitu chini ya miguu yake." Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake. 9 Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu. 10 Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake. 11 Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu. 12 Anasema, "Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko." 13 Tena asema, "Nitaamini katika yeye." Na tena, "Tazama, hapa nipo na watoto ambao Mungu amenipa." 14 Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vilevile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni ibilisi. 15 Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa. 16 Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abraham. 17 Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu. 18 Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.
Sura hii inahusu jinsi Yesu ni bora kuliko Musa, Mwisraeli mkuu kuliko wote.
Watafsiri wengine wameweka kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 2:6-8, 12-13, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Huenda mwandishi anatumia neno "ndugu" kuashiria Wakristo waliokua kama Wayahudi.
Hili ni onyo la kwanza kati ya maonyo matano mwandishi anatoa
Hapa "sisi"inamaanisha mwandishi anajijumuisha kwenye kundi lake.
kuamini katika neno la Mungu kidogo huongelewa kana kwamba mtumbwi ulikuwa ukichukuliwa mbali juu ya maji kutoka mahali ulipaswa kuwa. AT: " ili kwamba polepole tusiache kuliamini."
Wayahudi waliamini kuwa Mungu alisema sheria yake kupitia malaika. Hii inaweza kuelezewa katika mfumo tendaji. AT: "Kama ujumbe ambao Mungu aliongea kupitia malaika"
Mwandishi ana hakika kuwa mambo haya ni kweli. AT: "Kwa sababu ujumbe"
"ni sahihi au "kweli"
Neno kosa and uasi husimama kwa ajili ya watu ambao wana hatia kwa ajili ya dhambi hizi. AT: "kila mtu atendaye dhambi atapokea adhabu ya haki"
maneno haya mawili kimsingi yanamaanisha kitu kimoja.
Mwanadishi anatumia swali kusisitiza watu wata pokea adhabu kama watakataa wokovu wa Mungu kupitia Kristo. AT: "hivyo Mungu atatuadhibu kama hatuutilii manani ujumbe wake kuhusu vile Mungu atakavyo tuokoa!"
"kutojali" au "kuona sio muhimu"
Hii inaweza kusemwa katika mtumo tendaji. AT: "Bwana mwenyewe kwanza alitangaza ujumbe vile atakavyo tuokoa"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. " na wale walio siki ujumbe walituthibitishia"
" kama jinsi alivyopenda kufanya"
Mwandishi anawakumbusha Waebrania hawa kwamba siku moja nchi itakuwa chini ya utawala wa Bwana Yesu.
Nukuu hapa inatoka katika kitabu cha Zaburi katika Agano la Kale. Inaendele hadi sehemu inayofuata.
"Kwa kuwa Mungu hakuwaweka malaika kuwa watawala"
"Ulimwengu" hapa unamaanisha kwa watu wanaoishi huko. Na "ujao" unamaanishi huu ni ulimwengu uajao baada ya Yesu atakaporudi. AT: "watu watakaoishi katika ulimwengu wa mpya"
Swali linatumika kusisitiza kuwa wanadamu sio muhimu kwa kumfanya Mungu kuwajal.AT: "Hakuna mwandamu ambaye ni wa Muhimu wa kumfanya Mungu kufikiri kuhusu yeye!"
Kimsingi hii inamaanisha kitu kilekile kinachoelezewa katika swali la kwanza. Swali lisilo hitaji kujibiwa linasisitiza mshangao kwamba wanadamu si wa muhimu kiasi cha kwamba Mungu awajalli.AT: "Hakuna mwanadamu anayesitahili kujaliwa na wewe!"
Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa sio wa muhimu kuliko malaika kana kwamba wanadamuwamesimama katika nafasi amabayo ni ya chini kuliko nafasi ya malaika. AT: "mdogo kuliko malaika."
Maneno haya sio kwa ajili ya mlengwa mmoja bali inajumuisha wanadamu wote, inajumuisha wanaume na wanawake.AT: "amewafanya wanadamu... amewavika...miguu yao... kwao"
zawadi ya utukufu na heshima zinaongelewa kana kwamba ni shada la majani lililowekwa kichwani mwa mshindi wa mchezo. AT:"umewapa utukufu mwing na heshima"
Mwandishi anamuongelea mwanadamu kuwa na utawala juu ya kila kitu kana kwamba wamesimama juu ya kila kitu. AT: "Umewapa kumiliki juu ya vitu vyote"
maneno mawili hasi yanamaanisha kwamba vitu vyote vitawekwa chini ya Kristo. AT: "Mungu alifanya kila kitu kuwa chini yao"
tunafahamu kuwa bado wanadamu hawajawa wamiliki wa kila kitu
Mwanadishi anawakumbusha hawa Webrania waumini kwamba Kristo alipokuaja duniania alifanyika mdogo kuliko malaika alipokuja dunia kuteseka kufa kwa ajili ya msamaha wa dhambi, na kwamba alifanyika kuhani mkuu mwenye huruma.
"twafahamu kuwa kuna mwingine"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji.AT: "ambaye Mungu alimfanya'
Tasifri hii kama ulitafsiri sura ya 2:7
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alimvika'
Uzoefu wa kifo unaongelewa kana kwamba kifo ni chakula kilichoonjwa.AT: "ameonja kifo" au "amekufa"
"Mtu" hapa linamaanisha watu wote. wakijumuishwa wanaume na wanawake. AT: "kwa kuwa kila mtu"
Zawadi ya utukufu hapa inaongelewa kana kwamba ni sehemu ambayo watu wangeweza kuletwa. AT: "awaokoe wana wengi"
Hapa wanamaanishwa waumini wote katika Kristo, ikijumuisha wanaume na wanawake.AT: "waumini wengi"
Mwanadishi anaongea wokovu kana kwamba ni sehemu ambayo Yesu anawaongoza waumini kuelekea katika sehemu hiyo. Hii inamaanisha Yesu ni mtu ambaye alitenda kwanza ili awaokoe wengine. AT:"yeye anayewaokoa watu"
kukua kiroho na kufundishwa kikamilifu kunaongelewa kana kwamba mtu alikuwa akifanywa mtimilifu, pengine mtimilifu katika viungo vya mwili wake.
Nukuu hii ya kinabii inatoka katika Zaburi ya Mfalme Daudi.
yeye anayewafanya wenzake watakatifu" au " "yeye awafanyae wengine kujtenga na dhambi"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji: AT: "wote anao wafanya watakatifu" au" wale anaowasafisha kutoka katika dhambi.
ambaye ni chanzo hicho ni nani inaweza kusemwa kwa ufasaha. AT: "muwe na chanzo, Mungu mwenyewe" au" muwe na yule yule.
"Yesu haoni aibu"
maneno mawili hasi yanamaanisha atawafanya kama ndugu zake. AT: "anafurahishwa kuwaita ndugu"
"Jina" hapa linamaanisha heshima ya mtu na kile walichokifanya. AT: "Nitatangaza kwa ndugu zangu mambo makuu uliyoyafanya"
"wakati waumini wanakuja pamoja kumwabudu Mungu"
Nabii Isaya aliandika nukuu hizi
"Na nabii aliandika andiko katika sura nyingine kuhusu kileKristo achokisema kuhusu Mungu:" (URD)
Hii inaongea wale wanaoamini katika Kristo kana kwamba ni walikuwa watoto wa Mungu.AT: wale walio kama watoto wangu...wale ambaao ni sawa na watoto kwa Mungu"
Fungu hili la maneno limeelezwa na hurejea utumwa kwa hofu ya kifo
maneno "mwili" na "damu" inamaanisha asili ya wanadamu." AT: "wote ni wanadamu"
"Yesu alikuwa mwanadamu kama wao"
kifo hapa kinaweza kuelezewa kama tendo. AT: "kwa kufa"
kifo" hapa kinaweza kuelezewa kama tendo.AT: " alikuwa na kuvungu kuwafanya watu kufa"
Hofu ya kifo inaongelewa kana kwamba ilikuwa utumwa. Kumuondolea mtu hofu inaongelewa kana kwamba ni kumfungua mtu kutoka utumwani.AT: "Hii ilikuwa ili kwamba awafungue watu wote. Kwa sababu tuliishi kama watumwa kwa sababu tulikuwa tukiogopa kufa"
Wana wa Ibrahimu wanaongelewa kana kwamba walikuwa mbegu yake. AT: "wana wa Ibrahimu"
"ilikuwa ni muhimu kwa Yesu"
Neno "ndugu" hapa linamaanisha watu kwa ujumla. AT: "kama wanadamu"
Kifo cha Yesu msalabani kinamaanisha kwamba Mungu anaweza kusamehe dhambi. AT: "ili kwamba afanye uwezekano wa Mungu kusamehe dhambi za watu."
Hii inaweza kusema katika mfumo tendaji. AT: " Shetani akamjaribu"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "ambao shetani anawajaribu"
1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu. 2 Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu. 3 Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe. 4 Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu. 5 Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao. 6 Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini. 7 Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, "Leo, kama utasikia sauti yake, 8 Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani. 9 Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu. 10 Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu. 11 Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu." 12 Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai. 13 Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi. 14 Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho. 15 Kuhusu hili imekwisha kusemwa, "Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi." 16 Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri? 17 Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani? 18 Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye? 19 Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.
Watafsiri wengine wamewaka kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 3:7-11,15, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Huenda mwandishi anatumia neno "ndugu" kuashiria Wakristo waliokua kama Wayahudi.
Mtu anayefanya moyo wake kuwa ngumu ni yule ambaye hatamsikiliza ama kumtii Mungu.
Mwandishi anatumia maswali ya hadithi kama njia ya kuwaonya wasomaji wake. Yeye pamoja na wasomaji wake wanajua majibu ya maswali haya na mwandishi anajua kwamba wakati wasomaji watafikiria juu ya majibu ya haya maswali, watatambua kwamba wanatakikana kumsikiliza Mungu na kumtii.
Hili ni onyo la pili na ni refu na liko katika undani na linajumuisha sura ya 3 na 4. Mwandishi anaanza kwa kwa kuonyesha kwamba Kristo ni bora zaidi ya Musa mtumishi wake.
Neno "ndugu" linamaanisha wakristo wenza, inajumuisha wanaume kwa wanawake. AT: "kaka na dada watakatifu" au "ndugu watakatifu wenzangu"
"Mbinguni" hapa ina mwakilisha Mungu. AT: "Mungu ametuita pamoja"
Neno hili linamaanisha mtu aliyetumwa. Katika kifungu hiki hakimaanishi mtume kati ya wale kumi na wawili. AT: "aliyetumwa"
hii inaweza kusemwa ili kwamba nomino dhaniwa "kutubu" inelezea kama kitenzi "tubu." AT: "ambaye tunayemtubia" au "ambaye katika yeye tunaamini"
Waebrania ambao Mungu amejifunua kana kwamba ilikuwa ni nyumba halisi. AT: "kwa watu wote wa Mungu"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu amemfanya Yesu"
Matendo ya Mungu ya uumbaji wa ulimwengu yanaongelewa kana kwamba amejenga nyumba.
Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. AT: "kila nyumba ina mtu aliyeijenga"
Hili neno linaanzishwa ulinganifu kati ya Musa na Kristo. Hili neno linaweza kuachwa katika tafsiri, kama sio muhimu.
Waebrania ambao Mungu alijifunua mwenyewe wanaongelewa kana kwamba zilikuwa ni nyumba halisi. Tazama vile ulivyo tafasiri kama ulivyofanya 3:1.
Pengine neno hili linamaanisha kwa kazi zote za Musa. AT: "Maisha na kazi za Musa zilielekeza kwenye vitu"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: " Yesu angesema katika siku zijazo"
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
Hii inaongea kuhusu watu wa Mungu kana kwamba zilikuwa nyumba halisi. AT: "ambaye anatawala juu ya watu wa Mungu"
Hii inaongea kwa watu wa Mungu kana kwamba ni nyumba halisi. AT: "Sisi ni watu wa Mungu"
"ujasiri" na "tumaini lenye fahari" ni dhaaniwa na inaweza kusemwa kama vitenzi. AT: "tutaendelea katika ujasiri na furaha na kutumaini Mungu kufanya kile alichoahidi"
Onyo hapa ni ukumbusho kwamba kutokuamini kwa Waisraeli kuliwafanya wote kutoingia katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewahidi. Kutokuamini kwao kulionyeshwa vizuri katika Kutoka 17:1, walipo mlalamikia Musa na kuwa na mashaka juu ya Mungu kama alikuwa pamoja nao.
Nukuu hii inatoka katika Agano la Kale katika Zaburi.
Amri za Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba aliwakuwa amewapa katika sauti ya kusikika. AT: "kama mtasikia Mungu akiongea"
Ugumu wa moyo unaongelewa kana kwamba ni moyo halisi umefanywa kuwa mgumu. AT: "msiwewenye mioyo migumu"
Hapa "uasi" na "kujaribiwa" yanaweza kuelezewa kama vitenzi. AT: "kama vile na mababu zenu walivyo muasi Mungu na kumjaribu jangwani"
Nukuu hii inatoka katika Zaburi.
"zenu" hapa linamaanisha watu wa Israeli
Mungu ndiye anayeongea
"miaka 40"
"Nilikuwa na hasira" au "sikufurahia kabisa"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "mara zote wanaenda katika njia zisizomfurahisha Mungu"
Neno "mioyo" inamaanisha akili au tamaa za
Hii inaongelewa katika hali ya kuyafanya maisha ya mtu kana kwamba ni zilikuwa ni njia. AT: "Hawaelewi jinsi nilivyowataka waishi katika maisha yao"
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu unaongelewa kana kwamba zilikuwa pumziko ambalo angeweza kuwapa, na kama zilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. AT: "Hawataingia kamwe katika sehemu ya pumziko" au "sitawaruhusu kupata baraka zangu za pumziko"
Hili linatulejesha kwa ndugu Wakristo, ikijumuisha jinsia zote mbili za kiume na kike. AT: "kaka na dada" au "waumini wenza"
moyo unaongelewa hapa kana kwamba ni akili ya mtu, sehemu ya utashi ya mtu. AT: "mtu yeyote kati yenu asiache kuamini katika Mungu"
Moyo mtu unaongelewa kana kwamba nimtu mzima, ambaye angeweza kuacha kufuata njia sahihi. AT: "na unaacha kumtii Mungu aishie"
"Mungu wa kweli ambaye kweli anaishi"
"wakati nafasi inapatikana"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "udanganyifu wa dhambi haufanyi moyo mgumu wa mtu yeyote kati yenu"
kutokuwa msikivu kunatazamwa kana kwamba kuwa mgumu au kuwa na moyo mgumu. Ugumu wa moyo ni matokeo ya udanganyifu wa dhambi. Hii inaweza kutiwa neno ili kwamba nomino dhaniwa "udanganyifu" inaelezewa kama kitenzi "danganya." AT: "hakuna mtu miongoni mwenu atanganywa na dhambi na kutokuwa msikivu" au "usitende dhambi, ukijidanganya mwenyewe na kutokuwa msikivu"
Hii inaendelea kutoka Zaburi ile ile ambayo pia ilinukuliwa katika 3:7.
"Tumekuwa" hapa inamaanisha wote, mwandishi na wasomaji,
"kama tukiendelea kutumaini katika yeye kwa ujasiri"
"tangu mwanzo tulipoanza kuamini katika yeye"
Hii ni namna ya kusema kwa upole ikimaanisha mtu anapo kufa.AT: "hadi tunakufa"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "mwandishi aliandika"
Amri ya Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba aliwapa katika hali ya kusikia. AT: "kama utasikia Mungu anaongea." Tazama kama ulivyo tafsiri 3:7.
"Uasi" hapa unaweza kusemwa kama kitenzi. AT: "kama vile mababa zako walivyo muasi Mungu." Tanzama ulivyo tafsiri 3:7.
Neno "wao" linamaanisha kwa kutotii kwa Waisraeli, na "sisi" inamaanisha mwandishi na wasomaji.
Mwandishi anatumia maswali kudundisha wasomaji wake. Maswali haya mawili yanaweza kuunganishwa kama sentensi moja, kama itahitajika. AT: "wale wote waliokuja na Musa kutoka Misri walimsikia Mungu, lakini bado waliasi."
Mwandishi anatumia maswali kuwafundisha wasomaji wake. Maswali haya mawli yanaweza kuunganishwa na kuwa swali moja, kama litahitajika. AT: "Mungu alikuwa na hasira kwa miaka 40 na wale waliotenda dhambi na kuwaacha wafe nyikani."
Amani na ulinzi ambao Mungu vinaomgelewa kana kwamba ni pumziko alilowapa, na kama kwama vilikuwa ni sehemu za kwenda. AT: "hawataingia sehemu ya pumziko" au "hawatapata baraka zake za pumziko"
"kutokuamini" inaweza kusemwa kama kitenzi "tumaini." AT: "kwa sababu hawakuweza kumtumaini"
1 Kwa hiyo, tunapaswa kuwa makini ili kwamba kati yenu asiwepo hata mmoja atakayeonekana kushindwa kufikia ahadi endelevu ya kuingia katika pumzika la Mungu. 2 Kwani tumekuwa na habari njema kuhusu pumziko la Mungu lililotangazwa kwetu kama Waisrael walivyokuwa nayo, lakini ujumbe huo haukuwasaidia wale ambao waliusikia bila kuunganisha imani kwa hilo. 3 Kwa sisi, ambao tumekwisha amini-sisi ndio miongoni tutakaoingia katika lile pumuziko, Kama inavyosema, "Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika pumziko mwangu." Alisema hili, ingawa kazi zote alizotengeneza zilikuwa zimekamilika tangu mwanzo wa ulimwengu. 4 Kwani ameshasema sehemu fulani kuhusu siku ya saba, "Mungu alipumzika siku ya saba katika yote aliyoyafanya." 5 Tena ameshasema, "Hawataingia kwenye pumziko langu." 6 Kwa sababu hiyo, tangu pumziko la Mungu bado ni akiba kwa ajili ya baadhi kuingia, na tangu Waisraeli wengi ambao walisikia habari njema kuhusu pumziko lake hawakuingia kwa sababu ya kutotii, 7 Mungu aliweka tena siku fulani, iitwayo "Leo." Yeye aliiongeza siku hii alipozungumza kupitia Daudi, ambaye alisema kwa muda mrefu baada ya yaliyosemwa kwanza, "Leo kama mtasikia sauti yake, msifanye mioyo yenu kuwa migumu." 8 Kwani kama Yoshua aliwapatia pumziko, Mungu asingelisema juu ya siku nyingine. 9 Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu. 10 Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye. 11 Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya. 12 Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na linaukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika uboho. Na lenye kuweza kufahamu fikira za moyo nia yake. 13 . Hakuna kilichoumbwa kilichojificha katika uso wa Mungu. Badala yake, kila kitu ni dhahiri na wazi kwa macho ya mmoja ambaye ni lazima tutoe hesabu. 14 Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu. 15 Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hana dhambi. 16 Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.
Sura hii inaelezea kwa nini Yesu ni Kuhani Mkuu kuliko wote
Watafsiri wengine wametenga kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 4:3-4,7, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Neno "mapumziko" linaonekana kuashiria vitu viwili katika sura hii. Inaashiria mahali ama wakati Mungu atawaruhusu watu wake kupumzika kutokana na kazi zao (Waebrania 4:3), ama inaashiria kupumzika kwa Mungu siku ya Saba (Waebrania 4:4).
Sura ya 4inaendeleza onyo lililoanza katika sura ya 3:7.Mungu kwa kupitia mwandishi anawapa waumini pumziko ambalo pumziko la Mungu katika uumbaji dunia ni picha.
Ahadi ya Mungu inaongelewa kana kwamba ilikuwa ni zawadi iliyoachwa baada ya Mungu kuwatembelea watu. AT: "mmoja wenu asishindwe kuingia katika pumziko la Mungu , ambalo alituahidi".
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu huongelewa kana kwamba vilikuwa ni pumziko ambalo anaweza kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. AT: "kuingia katika sehemu ya pumziko" au "kupata baraka za pumziko la Mungu.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Kwa kuwa tulisikia habari njema kama walivyosikia"
walivyo hapa linamaanisha mababu/mababa wa Kiebrania ambao walikuwa hai wakati wa Musa.
"Lakini ujumbe ule haukuwafaa wale ambao hawakuungana na watu walio amini na kutii." Mwandishi anaongea kuhusu makundi mawili ya watu, wale waliopokea agano la Mungu kwa imani, na wale walio sikia lakini hawakuamini.
Nukuu ya kwanza hapa (Kama nilivyoapa...) inatoka katika Zaburi, na nukuu ya pili (Mungu akapumzika...) inatoka katika Maandiko ya Musa, na ya tatu (Hawataingia...) inatoka katika Zaburi.
"sisi tulioamini"
Amani na ulinzi alioutoa Mungu vinaongelewa kana kwamba vilikuwa ni pumziko ambazo anaweza kuwapa, na kana kwamba ilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeenda.
"Kama vile Mungu alivyosema"
"Kama nilivyo apa wakati nilipokuwa nimekasirika sana"
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda.
Hii inaweza kuwekwa katika mfumo tendaji. AT: "alimaliza uumbaji" au "alimaliza kazi zake za uumbaji"
Mwandishi anaongelea dunia kana kwamba ni jengo lililowekwa kwenye kwenye msingi.
Hii inasimama kama badala ya "saba"
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji.AT: "Mungu bado anaruhusu baadhi ya watu kuingia katika sehemu yake ya pumziko.
Amri za Mungu kwa Waisraeli zinaongelewa kana kwamba alikuwa amewapa kwa sauti. AT: "kama mtasikia Mungu akiongea"
kutosikia kunaongelewa kana kwamba ni moyo ulikuwa umwefanya kuwa mgumu. AT: "Msiwe wenye mioyo migumu." Tafsiri kama ulivyofanya 3:7.
Mwanadishi anawaonya waumini wasiache kumtii Mungu, bali waiingie katika pumziko ambalo Mungu anawapa. Anawakumbusha kwamba neno la Mungu litawashuhudia na kwamba wanaweza katika maombi kwa ujasiri na kwamba Mungu atawasaidia
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ambayo watu wangeweza kwenda. AT: "kama Yoshua angewaleta Wasraeli kwenye sehemu ambayo Mungu angewapa pumziko"
Amani na ulinzi uliotolewa na Mungu vinaongelwa kana kwamba zilikuwa pumziko la kuwapa, na kana kwamba vilikuwa ni sehemu ya kuingia. AT: "tunapaswa kufanya kila kitu ili tuingie katika mpumziko mahali alipo"
kutokutii kunaongelewa kana kwamba ni mtu mzima ambaye angeweza kuanguka katika ajali.
"Neno la Mungu" hapa linamaanisha kila kitu ambacho Mungu ameongea kwa wanadamu iwe kwa kuongea au kwa kupitia ujumbe ulioandikwa.
Hii inaongelea neno la Mungu kana kwamba linaishi. Inamaanisha wakati Mungu anapoongea ni kuna nguvu na utendaji kazi.
upanga wenye makali. upanga wenye makali kuwili ni rahisi kukata kupitia mwili wa mtu. Neno la Mungu lina nguvu katika kuonyesha kilichomo katika moyo na mawazo ya watu.
Hii inaendelea kuongea kuhusu neno la Mungu kana kwamba ulikuwa ni upanga. Upanga hapa ni mkali sana kiasi kwamba unaweza kukata na kugawa viungo vya mwanadamu ambavyo ni vigumu pengine visivyo wezekana kugawanyika.
Haya ni maneno mawili tofauti lakini sehemu za mwanadamu ambazo hazina mwili. "Nafsi" ndiyo inamfanya mtu kuwa hai na "roho" ni sehemu ya mtu ambayo inamsababisha kuweza kumjua na kumwamini Mungu.
"kiungo" ndicho kinacho shikilia mifupa miwili pamoja. "uboho" ni sehemu ya kati ya mfupa.
Hii inaongea neno la Mungu kana kwamba ni mtu ambaye angewezakujua kitu.
Hii inaongea kuhusu moyo kana kwamba ni sehemu ya kati ya mawaazo na hisia za mwanadamu.
Hili linaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. AT: "hakuna kitu kilichoumbwa na Mungu kinaweza kujificha mbele zake"
Hii inaongelea kila kitu kana kwamba ni mtu amesimama wazi au boksi lililo wazi.
Kimsingi maneno haya mawilii yanamaanisha kitu kimoja na kusisitiza kwamba hakuna kitu chochote kilichojificha mbele za Mungu.
Mungu anaongelwa kana mwamba ana macho ya nyama. AT" Mungu atatuhukumu kulingana na vile tulivyoishi"
"aliyeingia mahali alipo Mungu"
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
imani na tumaini vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo mtu angeweza kuvikumbatia.
Maneno haya yakukanusha yanalenga kuonyesha kwamba Yesu ni mwenye huruma kwa watu . AT: " tunaye kuhani mkuu anayeweza kutuhurumia...Kweli tunaye"
"kiti cha enzi cha Mungu, pale palipo na neema" au "pale Mungu, ambaye ni neema, ameketi katika kiti chake cha enzi"
Hii inaweza kusemwa katikamfumo tendaji. AT: "yeye ambaye amevumilia majaribu katika kila hali tunayoipitia" au "ambaye movu amekuwa akimjaribu katika kila njia anavyotujaribu"
"hakutenda dhambi"
"kwemye kiti cha enzi cha Mungu palipo na neema." "kiti cha enzi" hapa kina maanisha utawala wa Mungu kama mfalme.
"rehema" na "neema" hapa vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kupewa au kupatikana.
1 Kwani kila kuhani mkuu, aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa watu, amechaguliwa kusimama badala yao katika vitu vinavyohusiana na Mungu, ili aweze kutoa kwa pamoja zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi. 2 Anaweza kujishughulisha kwa upole na wajinga na wabishi kwa kuwa yeye mwenyewe pia amezungukwa na udhaifu. 3 Kwa sababu ya hili, ana wajibu wa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake kama afanyavyo kwa dhambi za watu. 4 Na hakuna mtu achukuaye heshima hii kwa ajili yake mwenyewe, lakini badala yake, lazima aitwe na Mungu, kama alivyokuwa Haruni. 5 Hata Kristo hakujipa heshimu mwenyewe kwa kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Badala yake, Mungu alisema kwake, " Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako." 6 Ni kama asemavyo pia sehemu nyingine, " Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki." 7 Wakati wa kipindi chake katika mwili, aliomba na kuombea, alimwomba Mungu kwa machozi, kwa yeye awezaye kumwokoa kutoka kwenye kifo. Kwa sababu ya unyenyekevu wake kwa Mungu, alisikiwa. 8 Ijapokuwa alikua mwana, alijifunza kutii kwa mambo yaliyomtesa. 9 Alikamilishwa na kwa njia hii alifanyika kwa kila mtu amwaminiye kuwa sababu ya wokovu wa milele, 10 kwa kutengwa na Mungu kama kuhani Mkuu baada ya zamu ya Melkizedeki. 11 Tuna mengi ya kusema kuhusu Yesu, lakini ni vigumu kuwaelezea kwa kuwa ninyi ni wavivu wa kusikia. 12 Ijapokuwa kwa kipindi hiki mlipaswa kuwa walimu, bado kuna umuhimu wa mtu kuwafundisha mafundisho ya awali ya kanuni za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa na si chakula kigumu. 13 Kwa kuwa yeyote anywaye maziwa tu hana uzoefu katika ujumbe wa haki, kwa kuwa bado ni mtoto. 14 Kwa upande mwingine, chakula kigumu ni cha watu wazima, wale ambao kwa sababu ya uzoefu wao katika kutofautisha haki na ubaya wamefundishwa kutambua jema na ovu.
Sura hii inaendeleza mafundisho ya sura iliyopita.
Watafsiri wengine wametenga kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 5:5-6.
Ni kuhani mkuu tu angetoa dhabihu ili Mungu asamehe dhambi na kwa hivyo lazima Yesu alikuwa kuhani Mkuu. Sheria ya Musa iliamuru kwamba kuhani mkuu atoke kwa kabila la Walawi lakini Yesu alitoka kabila la Yuda.Mungu alimfanya kuhani kama Melikizedeki aliyeishi nyakati za Abarahamu kabla ya kuwepo kabila la Walawi.
Mwandishi anazungumzia Wakristo ambao wako tu na uwezo wa kuelewa vitu rahisi kumhusu Yesu kana kwamba walikuwa watoto wachanga wanaokunywa tu maziwa na hawawezi kulaa chakula kigumu.
Mwandishi anafafanua dhambi za makuhani wa Agano la Kale, na kisha anaonyesha kuwa Kristo anao ukuhani bora, na hautokani na ukuhani wa haruni, bali unaotokana na ule waMelkizedeki.
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: "ambaye Mungu anachagua kutoka miongoni mwa watu"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu huachangua/ huteuwa"
"kuwawakilisha watu"
"wale walio wajinga waovu"
watu ambao wanaishi katika njia za dhambi"
udhaifu wa kuhani mkuu unaongelewa kana kwamba ni nguvu zilizo mzunguka
hapa inamaanisha hamu ya kutenda dhambi.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. "Mungu pia anamhitaji"
Nukuu hii inatoka katika Zaburi katika Agano la Kale
Heshima inaongelewa kana kwamba ni kitu ambacho Mungu kukichukua katika mkono wake.
heshima au sifa na heshima ambazo watu walimpa kuhani mkuu husimama kwa ajili ya majukumu yake
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alimwita kama alivyomwita Haruni"
"Mungu alisema kwake"
kimsingi neno hili linamaanisha kitu kimoja. Tazama ulivyotafsiri 1:4.
Unabi huu unatoka katika Zabur ya Daudi.
kwa yule ambaye Mungu anaongea naye inaweza kusemwa wazi. AT: "pia anamwambia Kristo"
"katika sehemu nyingine katika maandiko"
Hii inamaana kuwa Kristo kama kuhani ana vitu vinavyofananana Melkizedeki kama kuhani.
Neno siku/ kipindi zinasimama badala ya kipindi cha muda. Na "mwili" unasimama badala ya maisha ya Yesu duniani, AT: "wakati aliposhi duniani"
Kimsingi maneno haya yanamaanisha kitu kimoja
Kifo kinaongelewa kana kwamba ilikuwa ni sehemu kKristo angezuiliwa kutoingia, au kana kwamba ni sehemu ambayo angeokolewa.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alimsikia"
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
mateso kana kwamba ni vitu.
Katika mst wa11 mwandishi anaanza onyo lake la tatu. Anawaonya hawa wauminikuwa bado ni wachanga wa kiroho na kuwatia moyo kujjifunza neno la Mungu ili kwamba waweze kutambua jema na baya.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alifanya mkamilifu"
hapa inamaanisha kuweza kufanywa mtu mzima kiroho, kuwa tayari kumtii Mungu katika nyanja zote za maisha.
Nomino dhaaniwa "wokovu" inaweza kusemwa kama kitenzi. AT: "hivyo anawaokoa wale wote wanaomtii na kuwafanya waishi milele"
Hii inaweza kusems katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alimtenga" au "Mungu alimteua"
hii inamaanisha kwamba Kristo kama kuhani ana vitu vinavyofanana na Melkizedeki kama kuhani.
Ingawa mwandishi anatumia neno la wingi lakini inaweza kuwa anamaanisha yeye mwenyewe.
uwezo wa kuelewa na kutii kunaongelewa kana kwamba ulikuwa ni uwezo wa kusikia. Na uwezo wa kusikia kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni chuma cha kilichohabika katika matumizi.
kanuni hapa zinamaanisha maelekezo au viwango vya kufanya maamuzi. AT:"msingi wa ukweli"
mafundisho kuhusu Mungu ambayo ni rahisi kuelewa yanaongelewa ni maziwa, chakula pekee ambacho watoto wachanga wanaweza kula. AT: "mmekuwa watoto na mnaweza kunywa maziwa pekee"
mafundisho ambayo ni magumu kuelwa yanaongelewa kana kwamba kilikuwa ni chakula kigumu, kifaacho kwa watu wazima.
anywaye linasimama ka kunywa.
hii inaongelea waumni ambao wanaweza kuelewa mafundisho rahisi ya injili kana kwamba walikuwa watoto halisi.
watu walifundishwa kuelwa jambo wanaelezewa kana kwamba ni uwezo wa kuelewa umefundishwa.
1 Kwa hiyo, tukiacha tulichojifunza kwanza kuhusu ujumbe wa Kristo, twapaswa kuwa na juhudi kuelekea kwenye ukomavu, tusiweke tena misingi ya toba kutoka katika kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu, 2 wala misingi ya mafundisho ya ubatizo, na kuwawekea mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. 3 Na tutafanya hivi ikiwa Mungu ataruhusu. 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa wale ambao waliipata nuru awali, ambao walionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu, 5 na ambao walionja uzuri wa neno la Mungu na kwa nguvu za wakati ujao, 6 na kisha wakaanguka - haiwezekani kuwarejesha tena katika toba. Hii ni kwa sababu wamemsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, wakimfanya kuwa chombo cha dhihaka hadharani. 7 Kwa kuwa ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake, na ikatoa mazao muhimu kwa hao waliofanya kazi katika ardhi, hupokea baraka kutoka kwa Mungu. 8 Lakini ikiwa huzaa miiba na magugu, haina tena thamani na ipo katika hatari ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuteketezwa. 9 Ijapokuwa tunazungumza hivi, rafiki wapenzi, tunashawishiwa na mambo mazuri yawahusuyo ninyi na mambo yahusuyo wokovu. 10 Kwa kuwa Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na kwa upendo mliouonesha kwa ajili ya jina lake, katika hili mliwatumikia waamini na bado mngali mnawatumikia. 11 Na tunatamani sana kwamba kila mmoja wenu aweze kuonesha bidii ile ile mpaka mwisho kwa uhakika wa ujasiri. 12 Hatutaki muwe wavivu, lakini muwe wafuasi wa wale warithio ahadi kwa sababu ya imani na uvumilivu. 13 Kwa maana Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa nafsi yake, kwa kuwa asingeliapa kwa mwingine yeyote aliye mkubwa kuliko yeye. 14 Alisema, "Hakika nitakubariki, na nitauongeza uzao wako zaidi." 15 Kwa njia hii, Abrahamu alipokea kile alichoahidiwa baada ya kusubiria kwa uvumilivu. 16 Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, na kwao ukomo wa mashindano yote ni kiapo kwa kuyathibitisha. 17 Wakati Mungu alipoamua kuonesha kwa uwazi zaidi kwa warithi wa ahadi kusudi lake zuri lisilobadilika, alilithibitisha kwa kiapo. 18 Alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tulioikimbilia hifadhi tupate kutiwa moyo kushikilia kwa nguvu tumaini lililowekwa mbele yetu. 19 Tunao ujasiri huu kama nanga imara na ya kutegemea ya roho zetu, ujasiri ambao unaingia sehemu ya ndani nyuma ya pazia. 20 Yesu aliingia sehemu ile kama mtangulizi wetu, akisha kufanyika kuhani mkuu hata milele baada ya utaratibu wa Melkizedeki.
Katika agano Mungu alifanya na Abrahamu, Mungu aliahidi kuwafanya uzao wake kuwa taifa kubwa. Aliahidi pia kuwakinga uzao wa Abrahamu na kuwapa ardhi yao.
mwandishi anendele na kile Waebrania waumini walipaswa kufanya ili wawe wakristo wakomavu. Anawakumbusha mafundisho ya msingi.
Hii inaongelea kuhusu mafundisho ya msingi kana kwamba yalikuwa ni mwanzo wa safari na mafundisho makomavu kana kwamba ni mwisho wa safari.
Mafundisho ya msingi yanaongelewa kana kwamba yalikuwa ni jengo ambalo mjenzi alianza kwa kuweka msingi. AT: "tusirudie mafundisho ya awali... ya imani katika Mungu"
matendo ya dhambi yanaongelwa kana kwamba yalitoka katika ulimwengu wa wafu.
Mafundisho ya msingi yanaongelea kana kwamba yalikuwa ni jengo ambalo mjenzi wake alianza kwa kuweka msingi. AT: "wala mafundisho ya msingi... uzima wa milele"
Huduma hii iliwekwa kwa kumtenga mtu kwa huduma au nafasi maalum.
uelewa unaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kupatiwa nuru. AT: "wale ambao awali walielewa ujumbe kuhusu Kristo"
kuonja wokovu kunaongelewa kana kwamba ni kuoonja chakula. AT: walionja nguvu ya Mungu ya kuokoa"
Roho Mtakatifu ambaye anakuja kwa waumini, anaongelewa kana kwamba ni chombo ambacho watu wangeweza kushiriki. AT: "waliopoke Roho Mtakatifu"
Kujifunza neno la Mungu kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kuonja chakula. AT: "waliojifunza neno zuri la Mungu"
Hii inamaanisha nguvuza Mungu wakati ufalme wake utakapo kuwa umetimilka duniani kote. kwa mantiki hii "nguvu" ina maanishaMungu mwenyewe, ambaye anamiliki nguvu zote.
kupoteza uaminifu kwa Mungu kunaongelewa kana kwamba anguko la kimwili.AT: "walioacha kuamini katika Mungu"
"Haiwezekani kuwarejesha tena kwenye toba"
watu wanapoondoka kwa Mungu ni kana kwamba wanamsulubisha tena Yesu.
Hiki ni cheo muhimu ambacho kinaelezea uhusiano kwa Mungu.
ardhi inufaikayo na mvua nyingi inaongelewa kana kwamba ni mtu aliyekunywa maji mengi ya mvua.
Ardhi izaayo mazao inaongelewa kana kwamba iliwazalia.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kwa wale kwa ajili yao mtu aliandaa ardhi"
Mvua naa mazao vinaonekana kama ushahidi kama Mungu amemsaidia mkulima. Ardhi inaongelewa kana kwamba ni mtu ambaye angeweza kupokea baraka za Mungu.
Hii inaongelea "laana" kana kwamba ni ilikuwa ni sehemu ambayo mtu angeweza kukaribia. AT: "iko katika hatari ya Mungu kuilaani.
Mungu atasababisha kila kitu katika shamba hilo kuteketea.
ingawa mwandishi anatumia nomino ya wingi "Tuna" mara nyingi anamaanisha yeye mwenyewe.
Hii inamaana kuwa wanafanya vizuri kuliko wale walio mkataa Mungu, wasiomtii yeye, na hawawezi tena kutubu ili kwamba awasamene.
Nomino dhaaniwa "wokovu" inaweza kuwekwa kama kitenzi.
Maneno haya yanamaanisha kuwa Mungu katika haki yake atakumbuka mambo mazuri ambayo watu wake wameyafanya.
"Jina" lake lina maanisha Mungu
Ingawa mwandishi anatumia wingi lakini anamaanisha yeye mwenyewe.
uangalifu, kazi ngumu
AT: "mpaka mwisho wa maisha yako"
"ili kuwa na uhakika timilifu kuwa mtapokea kile ambacho Mungu amewaahidi ninyi"
"muigaji" ni mtu ambaye ana nakili tabia ya mtu mwingine.
kupokea kile ambacho Mungu alichowaahidi waumini kinaongelewa kana kwamba ilikuwa wanarithi kitu na utajiri kutoka kwa mwanafamilia. AT: " pokea kileambacho Mungu amewaahidi"
Mungu akasema
Neno "ongeza" hapa linasimama kwa uzao. AT: "Nitakupa uzao mwingi'
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: " Kile ambacho Mungu alimuahidi"
kwa watu ambao Mungu amewawekea ahadi wanaongelewa kana kwamba walikuwa warithi kitu na utajiri kutoka kwa mwanafamilia. AT: "kwa wote ambao wangepokea kile alichoahidi"
"kwamba kusudi lake halitabadilika kamwe" au "kwamba mara zote atafanya kile alichosema atafanya"
Hii ina maana ahadi ya Mungu na kiapo cha Mungu. Wala hivi haviwezi kubadilika.
Vikanushi hivi viwili vinaweza kumaanisha kwamba Mungu atasema kweli kuhusu hali hii. AT:"ambayo mara zote Mungu husema kweli"
Waumini, ambao wanatumaini katika Mungu kwa yeye kuwalinda, wanaongelewa kana kwamba walikuwa wanakimbilia kwenye sehemu salama. AT: ""sisi, ambao tuliomtumaini yeye"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kile ambacho Mungu ameweka mbele zetu"
Baada ya kumaliza onyo lake la tatu na maneno ya kuwatia moyo waumini, mwandishi wa Waebrania anaendeleza ulinganifu wake wa Yesu kama kuhani dhidi ya kuhani Melikizedeki.
Kama vile nanga inanyoshikilia mtumwi kutoenda sehemu nyingine ndani ya maji, Yesu anatuweka sisi sehemu salama katika uwepo wa Mungu.
Ujasiri unaongelewa kana kwamba ni mtu ambaye angeweza kwenda katika mahali patakatifu pa patakatifu pa hekalu.
Hii ilikuwa ni sehemu ya ndani ya hekalu.Ilidhaniwa kuwa ndiyo sehemu Mungu alikuwa akikaa miongoni mwa watu wake. Katika sura hii sehemu hii inasimama kama mbingu na chumba cha kiti cha enzi cha Mungu.
Ukweli kwamba Yesu alikufa na kufufuka, na kwamba sasa yuko na Mungu Baba, inaonyesha kwamba sisi tunaoamini katika yeye tutapata mambo yaleyale.Yesu anaoglewa hapa kana kwamba ni mtu ambaye anakimbia mbele yetu na kwamba tunamfuata.
Hii ina maana kuwa Kristo kama kuhani ana vigezi sawa na vya kuhani Melikizedeki,
1 Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki. 2 Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake "Melkizedeki " maana yake" mfalme wa haki" na pia "mflame wa Salemu" ambayo ni "mfalme wa amani." 3 Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu. 4 Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani. 5 Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Wairaeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu. 6 Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi. 7 Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa. 8 Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi. 9 Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alilipa moja ya kumi kwa Abrahamu, 10 kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu. 11 Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni? 12 Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika. 13 Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni. 14 Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani. 15 Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki. 16 Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika. 17 Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: "Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki." 18 Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai. 19 Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu. 20 Na Ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote. 21 Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, "Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.' wewe ni kuhani milele." 22 Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora. 23 Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine. 24 Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki. 25 Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao. 26 Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu. 27 Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe. 28 Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele.
Watafsiri wengine wametenga kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 7:17,21, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Ni kuhani mkuu tu angetoa dhabihu ili Mungu asamehe dhambi na kwa hivyo lazima Yesu alikuwa kuhani Mkuu. Sheria ya Musa iliamuru kwamba kuhani mkuu atoke kwa kabila la Walawi lakini Yesu alitoka kabila la Yuda.Mungu alimfanya kuhani kama Melikizedeki aliyeishi dhabihui za Abarahamu kabla ya kuwepo kabila la Walawi.
Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaendeleza ulinganifu wake juu ya Yesu kama kuhani na kuhani Melikizedeki.
Hili ni jina la mji.
Hii ina maanisha wakati Abrahamu na watu wake walipoenda na kuyashinda majeshi ya wafalme wanneili kumwokoa benamu yake, Lutu, na familia yake.
"Ilikuwa kwa Melikizedeki"
"mfalme wa haki... mfalme wa amani"
Inawezekana kufikiri kutoka katika ukurasa huu kwamba Melikizedeki hakuzaliwa wala hakufa. Ingawa, ni kama inamaanisha mwandishi anamaanisha kwamba Maandiko hayaarifu chochote kuhusu wazazi wa Melkizedeki, kuzaliwa, au kifo.
Mwandishi anasema kwamba ukuhani wa Melikizedeki ni bora kuliko wa ukuhani wa haruni na anakumbusha kuwa ukuhani wa Haruni haukukamilisha chochote.
'Melikizedeki alikuwa"
maneno haya yametumika kulinganishwa vitu viwili. Lugha yako inaweza kuwa na namna ya msisitizo kwamba mwandishi anaweka ulinganifu. Au unaweza kutumia "kwa upande mwingine"
Mwandishi anasema hili kwa sababu sio wana wote wa Lawi walikuwa makuhani.
"kutoka kwa watu wa Israeli"
Neno ndugu hapa linamaanisha kuwa wote wanahusiana kupitia kwa Abrahamu.
Hii ni namna nyigine ya kusema walikuwa wana wa Abrahamu.
"ambao hawakuwa wana wa Lawi"
Mambo ambayo Mungu aliahidi kufanya kwa ajili ya Abrahamu yanaongelewa kana kwamba vilikuwa ni vitu ambavyo angeweza kumiliki.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji: AT: "Mtu wa muhimu humbariki mtu asiye wa muhimu kama yeye"
Maneno haya hutumika katika kulinganisha ukuhani wa Lawi na ukuhani wa Melikizedeki. Lugha yako unaweza kuwa kunaweza kuwa na namna ya kusisitiza kwamba mwandishi anafanya ulinganifu.
haijaandikwa katika maandiko kwamba kwamba Melikizedeki anakufa. Mwandishi wa kitabu cha Waebrania anaandika kukosekana kwa taarifa ya kifo cha Melikizedeki kana kwamba bado anaendelea kuishi. Hii inaweza kuelezewa katika muundo tendaji. AT: "andiko linaonyesha kuwa anaendele kuishi:
kwa kuwa Lawi alikuwa hajazaliwa bado, mwandishi kana kwamba bado alikuwa katika mwili wa Abrahamu. Kwa jinsi hii mwandishi anatia hoja kuwa Lawi alilipa zaka kwa Melikizedeki kupitia Abrahamu.
Hii haimanishi "kwa wakati huu," imetumika kuvuta usikivu kwa kipengele muhimu kinachofuata.
Swali hili linasisitiza kwamba haikutegemewa kwamba kuhani angeweza kuja kwa mfano wa Melikizedeki.
"kuja" au "kutokeza"
Hii ina maana kuwa Kristo kama kuhani ana sifa zifananazo na kuhani Melikizedeki.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "na sio kuwa kwa jinsi ya Haruni" au "ambaye ni kuhani sio kwa mfano wa Haruni"
Hii inaweza kutamkwa katika mfumo tendaji. AT: " kwa kuwa Mungu alipobdilishwa ukuhani, pia alipaswa kubadlisha sheria"
Hii ina maanisha Yesu.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "ambaye ninaongea kuhusu yeye
Hii haimanishi "wakati huu," lakini linatumika kuvuta usikivu kwa ajili ya kipengele muhimu kinachofuata.
Haya maneno "Bwana wetu" linamaanisha Yesu.
"kutoka katika kabila la Yuda"
Nukuu hii inatoka katika Zaburi ya mfalme Daudi
" tunaweza kuelewa hata zaidi." "tuna" inamaanisha mwandishi na watu anaowaandikia.
"kama kuhani mwingine atakuja"
Hii ina maana kwamba kristo ana sifa sawa na kuhani Melikizedeki.
wazo la huzao wa mtu linaongelewa kana kwamba ilikuwa inashughulika na mwili wa mtu.
Neno " alifanyika kuhani" linaeleweka. AT: "lakini alikuwa kuhani kwa msingi wa nguvu ya maisha ambayo hayatakoma"
Hii inaongelewa kana kwamba andiko ni mtu ambaye angeweza kushuhudia kuhusu kitu.
Hii ina maanisha kwamba Kristo kama kuhani ana sifa sawa na za kuhani Melikizedeki.
Mungu aliifanya amri yake ya kwanza kutofaa"
sheria inaongelewa kana kwamba alikuwa ni mtu ambaye angeweza mutenda.
"Mungu ametupa hoja bora ya kuwa na ujasiri"
Ujasiri kwa wakati ujao unaongelewa kana kwamba ni kitu ambacho kutia hicho mtu lazima amkaribie Mungu.
Kumwabudu Mungu na kuwa na upendeleo wake vinaongelewa kana kwamba ni tendo la kumkaribia yeye.
Nukuu hii inatoka katika Zaburiya Daudi kama mstari wa 17
Tendo la kula kiapo linaongelewa bila kusema ni nani aliyekula hicho kiapo. Japo kuwa alikuwa Mungu.
hii inawea kusemwa katika mfumo tendaji. AT:"kwa sababu Mungu aliapa kwake kwa kusema"
Mwandishi anawahakikishia aumini hawa wa Kiyahudi kwamba Kristo na ukuhani ulio bora kwa sababu anaishi milele na makuhani wote waliotoka kwa Haruni walikufa.
"uhakika" au "ukweli"
maneno haya yametumika kulinganisha mambo mawili. Lungha yako inaweza kuwa na msisitizo kwamba mwandishi anafanya ulinganifu.
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: '"mwishowe wanakufa na hawawezi kuendelea"
kazi ya kikuhani inaongelewa kana kwamba ni chombo ambach Yesu alikimiliki. AT: "yeye ni kuhani asiye badilika"
unaweza kufafanunua "neno "Kwa hiyo" linachomaanisha. AT: " Kwa sababu Kristo ni kuhani wetu mkuu anayeishi milele"
"wale wanaokuja kwa Mungu kwa sababu ya kile Yesu alichofanya"
"na Mungu amemuinua juu kupita mbingu." Mwandishi anaongelea kumiliki heshima zaidi na nguvu zaidi ya mtu yeyote kana kwamba ni nafasi ambayo ni zidi ya vitu vyote. AT: "na Mungu amempaheshima na nguvu kuliko mtu yeyote"
Maneno "Yeye" na "mwenyewe" yanaamaniisha Kristo. Neno "yake" linamaanisha makuhani wakuu wa duniani.
Neno sheria hapa ni neno linalosimama kwa niaba ya Mungu, ambaye alianzisha sheria. Waisraeli waliteuwa makuhani wao kwa mjibu wa sheria.
wanaume waliokuwa dhaifu kiroho" au "wanaume ambao ni wadhaifu kw dhambi"
"baada ya kuwapa sheria, Mungu aliapa kwa kiapo na kumteua Mwanawe"
neno "kiapo" limepewa nafsi na linaelezewa kana kwamba ni mtu ambaye aliongea.
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
"aliyekamilishwa kumtii Mungu na kuwa mkomavu"
1 Sasa jambo ambalo tunasema ni hili: tunaye kuhani mkuu aliyekaa chini katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi Mbinguni. 2 Yeye ni mtumishi katika mahali patakatifu, hema la kweli ambalo Bwana ameliweka, siyo mtu yeyote wa kufa. 3 Kwa maana kila kuhani mkuu huwekwa kutoa zawadi na dhabihu; kwa hiyo ni muhimu kuwa na kitu cha kutoa. 4 Sasa kama Kristo alikuwa juu ya nchi, yeye asingekuwa kuhani zaidi ya hapo. Kwa kuwa walikuwa tayari wale waliotoa vipawa kulingana na sheria. 5 Walihudumu kitu ambacho kilikuwa nakala na kivuli cha vitu vya mbinguni, sawa kama Musa alipoonywa na Mungu wakati alipotaka kujenga hema. "Ona," Mungu akasema, "kwamba tengeneza kila kitu kulingana na muundo ulioonyeshwa juu ya mlima". 6 Lakini sasa Kristo amepokea huduma bora zaidi kwa sababu yeye pia ni mpatanishi wa agano zuri, ambalo limekwisha kuimarishwa kwa ahadi nzuri. 7 Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili. 8 Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, "Tazama, siku zinakuja, 'asema Bwana, 'wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda. 9 Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,' asema Bwana. 10 Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,' asema Bwana. 'nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 11 Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, "Mjue Bwana," hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao. 12 Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena." 13 Kwa kusema "Mpya," amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.
Mwandishi anamalizia kwa kufafanua jinsi gani na ni kwa nini Yesu ndiye kuhani mkuu muhumu. Halafu anaanza kuzungumzia jinsi agano jipya ni bora kuliko agano Mungu alifanya na Musa.
Watafsiri wengine wametenga kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 8:8-12, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Mwandishi anaelezea jinsi Yesu ameanzisha agano jipya ambalo ni bora kuliko agano Mungu alianzisha na wana wa Israeli.
Baadaa ya mwandishi kuonyesha ukuhani wa Kristo ulivyo bora kuliko ukuhani wa duniani, anaonyesha kuwa ukuhani wa duniani ulikuwa ni mfano wa mambo ya mbinguni. Kristo ana huduma iliyo bora, au agano lililobora.
Hii haimaanishi ni "wakati huu," lakini neno hili limetumika kuvuta usikivu kwa kipengele muhimu kinachofuata.
Ingawa mwandishi anatumia wingi "tuna" kimsingi anaongea yeye mwenyewe.AT: "Ninasema" au "ninaandika"
Neno "mkono wa kuume" linamaanisha sehemu ya heshima. AT: "aliketi katika sehemu ya heshima"
Neno "Ukuu" linamaanisha Mungu, na kiti chan enzi linamaanisha utawala wa Mungu kama mtawala,
watu walijenga hema za dunianikwa kutumia ngozi za wanyama zilizofungwa katika nguzo za mbao, na zikawekwa kwa namna ya hema. Hema ya kweli hapa inamaanisha hema ya mbinguni ambayo Mungu ameitengeneza.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji.AT: "kwa kuwa Mungu huteua kila kuhani'
hII haimaanishi "wakati huu," lakini imetumika ili kuvuta usikivu kwenye kipengele muhimu kinachofuata.
"kama Mungu anavyotaka katika sheria"
Haya maneno yana kimsingi yana maana moja ili kusisitiza kwamba hema ilikuwa ni sura halisi ya hema ya mbinguni.
Mwandishi anaongea hekalu la duniani, ambalo ni nakala ya hekalu la mbinguni, kana kwamba ilikuwa ni kivuli.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. "kama vile Mungu alivyomwonya Musa wakati Musa alipokuwa"
Musa hakujenga hema yeye mwenyewe. Aliwaamuru watu kuijenga. AT: "alitaka kuwaawamuru watu kuijenga hema"
unaweza kutoa nukuu. AT: "Mungu akasema, 'tazama kwamba wewe... mlima""
"Hakikisha"
"kwa muundo"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Ile niliyokuonyesha"
Mlima inanaanisha mlima Sinai.
Sehemu hii inaanza kwa kuonyesha kwamba agano jipya ni bora kuliko agano la kale la Israeli na Yuda.
"Mungu amempa Kristo"
"huduma iliyo bora zaidi, kama Kristo alivyo mpatanishi wa agano bora"
Hii ina maanisha kuwa Kristo alisababisha agano bora kuendelea kati ya Mungu na wanadamu.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: ''ni agano hili ambalo Mungu alilifanya kulingana na ahadi zilizo bora" au "Mungu aliahidi vitu bora wakati alipofanya agano hili"
Haya maneno "kwanza" na "pili" ni namba za kawaida. AT:" agano la zamani ... agano jipya"
"ingekuwa kamilifu"
Ktika nukuu hii nabii Yeremia alikuwa amesema agano jipya ambalo Mungu angefanya
"na watu wa Israeli"
"Tazama" au "Sikiliza" au "Kuwa na tahadhari kwa lile ninalotaka kuwaambia."
Ziku zijazo zinaongelewa kana kwamba zinatembea kumkabiri mzungumzaji. AT:"ktakuwa na wakati"
Watu wa Israeli na watu wa Yuda wanaongelewa kana kwamba wao ni nyumba. AT:"watu wa Isareli na watu wa Yuda"
Picha inawakilisha upendo mkuu wa Mungu na kujali kwake.
Kutii agano la Mungu kunaongelewa kana kwamba mtu alipaswa kuendelea katika hilo. AT: "hawakutii agano langu"
Nukuu hii inatoka kwa nabii Yeremia.
Watu wa Israeli wanaongelewa kana kwamba walikuwa ni nyumba.
"baada ya wakati huo"
Sheria za Mungu zinaongelewa kana kwamba ni vyombo ambavyo vingeweza kuwekwa mahali fulani. Uwezo wa watu kufikiri kunaongelewa kana kwamba ni sehemu.AT: "Nitawawezesha kuelewa sheria zangu"
Mioyo ya watu ilifikiriwa kuwa kituo cha uaminifu kwa Mungu, na imeongelewa kana kwamba ni ukurasa ambao ungeweza kuandikwa.
"Nitakuwa Mungu wanae mwabudu"
"watakuwa watu ambao ninawajali"
Hii inaendeleza nukuu kutoka kwa nabii Yeremia.
Nukuu hii ya moja kwa moja inaweza kuengelewa kana kwamba ni nukuu isiyo ya moja kwa moja. AT: "Hawatahitaji kuwafundisha jirani zao au ndugu za kunijua"
Haya maneno mawili yanalenga Waisraeli wenzao.
Neno "kujua" hapa linasimama kwa maana ya kutambua.
Hili linasimama kwa ajili ya watu waliofanya matendo haya yasiyo ya haki.
Neno "kumbuka" linamaanisha "sitafikiri kuhusu dhambi hizo"
"limekaribia kabisa kutoweka" au "litatoweka hivi karibuni"
1 Sasa hata agano la kwanza lilikuwa na sehemu ya ibada hapa duniani na taratibu za ibada. 2 Kwani katika hema kulikuwa na chumba kimeandaliwa, chumba cha nje, paliitwa mahali patakatifu. Katika eneo hili palikuwa na kinara cha taa, meza na mikate ya wonyesho. 3 Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi. 4 Mlikuwemo madhabahu ya dhahabu kwa kuvukizia uvumba. Pia mlikuwemo sanduku la agano, ambalo lilikuwa limejengwa kwa dhahabu tupu. Ndani yake kulikuwa na bakuli la dhahabu lenye manna, fimbo ya Haruni iliyoota majani, na zile mbao za mawe za agano. 5 Juu ya sanduku la agano maumbo ya maserafi wa utukufu wafunika mabawa yao mbele ya kiti cha upatanisho, ambacho kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa kina. 6 Baada ya vitu hivi kuwa vimekwisha andaliwa, Makuhani kawaida huingia chumba cha nje cha hema kutoa huduma zao. 7 Lakini kuhani mkuu huingia kile chumba cha pili pekee mara moja kila mwaka, na pasipo kuacha kutoa dhabihu kwa ajili yake binafsi, na kwa dhambi za watu walizozitenda pasipo kukusudia. 8 Roho Mtakatifu anashuhudia kwamba, njia ya mahali patakatifu zaidi bado haijafunuliwa kwa vile ile hema la kwanza bado linasimama. 9 Hili ni kielelezo cha muda huu wa sasa. Vyote zawadi na dhabihu ambavyo vinatolewa sasa haviwezi kukamilisha dhamiri ya anayeabudu. 10 Ni vyakula na vinywaji pekee vimeunganishwa katika namna ya taratibu za ibada ya kujiosha. Vyote hivi vilikuwa taratibu za kimwili vilivyokuwa vimeandaliwa hadi ije amri mpya itakayowekwa mahali pake. 11 Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa. 12 Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele. 13 Kama kwa damu ya mbuzi na mafahari na kunyunyiziwa kwa majivu ya ndama katika hao wasiosafi walitengwa kwa Mungu na kufanya miili yao safi, 14 Je si zaidi sana damu ya Kristo ambaye kupitia Roho wa milele alijitoa mwenyewe bila mawaa kwa Mungu, kuosha dhamiri zetu kutoka matendo mafu kumtumikia Mungu aliye hai? 15 Kwa sababu hiyo, Kristo ni mjumbe wa agano jipya. Hii ndiyo sababu mauti imewaacha huru wote walio wa agano la kwanza kutoka katika hatia ya dhambi zao, ili kwamba wote walioitwa na Mungu waweze kupokea ahadi ya urithi wao wa milele. 16 Kama kuna agano linadumu, ni lazima kuthibitishwa kwa kifo cha mtu yule aliyelifanya. 17 Kwani agano linakuwa na nguvu mahali kunatokea mauti, kwa sababu hakuna nguvu wakati mwenye kulifanya akiwa anaishi. 18 Hivyo hata si lile agano la kwanza lilikuwa limewekwa pasipo damu. 19 Wakati Musa alipokuwa ametoa kila agizo la sheria kwa watu wote, alichukua damu ya ng'ombe na mbuzi, pamoja na maji, kitambaa chekundu, na hisopo, na kuwanyunyizia gombo lenyewe na watu wote. 20 Kisha alisema, "Hii ni damu ya agano ambayo Mungu amewapa amri kwenu". 21 Katika hali ileile, aliinyunyiza damu juu ya hema na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa huduma ya ukuhani. 22 Na kulingana na sheria, karibu kila kitu kinatakaswa kwa damu. Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha. 23 Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba nakala za vitu vya mbinguni sharti visafishwe kwa hii dhabihu ya wanyama. Hata hivyo, vitu vya mbinguni vyenyewe vilipaswa kusafishwa kwa dhabihu iliyo bora zaidi. 24 Kwani Kristo hakuingia mahali patakatifu sana palipofanywa na mikono, ambayo ni nakala ya kitu halisi. Badala yake aliingia mbingu yenyewe, mahali ambapo sasa yuko mbele za uso wa Mungu kwa ajili yetu. 25 Hakuingia kule kwa ajili ya kujitoa sadaka kwa ajili yake mara kwa mara, kama afanyavyo kuhani mkuu, ambaye huingia mahali patakatifu zaidi mwaka baada ya mwaka pamoja na damu ya mwingine, 26 kama hiyo ilikuwa kweli, basi ingekuwa lazima kwake kuteswa mara nyingi zaidi tangu mwanzo wa ulimwengu. Lakini sasa ni mara moja hadi mwisho wa miaka aliyojifunua kuiondoa dhambi kwa dhabihu yake mwenyewe. 27 Kama ilivyo kwa kila mtu kufa mara moja, na baada ya hiyo huja hukumu, 28 ndivyo hivyo Kristo naye ambaye alitolewa mara moja kuziondoa dhambi za wengi, atatokea mara ya pili, si kwa kusudi la kushughulikia dhambi, bali kwa ukombozi kwa wale wamgojeao kwa saburi.
Sura hii inaonyesha jinsi Yesu ni bora kuliko hekalu na sheria na masharti yake. Sura hii itakuwa ngumu kuelewa iwapo vitabo vitanu vya kwanza vya Agano la Kale havijatafsiriwa.
Agano la urithi ni hati ya kisheria ambayo huelezea kile ambacho kitafanyikia mali ya mtu baada ya kifo chake.
Katika Agano la kale, Mungu alikuwa ameamuru Waisraeli kutoa dhabihu ili dhambi zao zisamehewe. Kabla hawajatoa dhabihu hizi, walipaswa kuwaua wanyama na siyo kutoa tu miili ya wanyama hao lakini pia damu zao. Kutoa damu ni tamathali ya kumuua binadamu ama mnyama.Mungu alipeana uhai na damu yake kama dhabihu/kafara alipowaruhusu watu kumuua.Mwandishi wa Waebrania anasema kwamba hii dhabihu ni bora kuliko dhabihu ya agano la kale.
Yesu atarudi kumaliza kazi aliyoianzisha wakati alipokufa ili Mungu angewasamehe watu dhambi zao. Atamalizia kuwaokoa watu wanaomngojea.
Hii inaashiria agano ambalo Mungu alifanya na Musa. Hata hivyo, kabla hajafanya agano hili, Mungu alikuwa amefanya agano na Abrahamu. Lakini hili lilikuwa ni agano la kwanza ambalo Mungu alifanya na watu wa Israeli. Unaweza amua kutafsiri "agano la kwanza" kama "agano la awali."
Mwandishi anawaweka wazi hawa waumini wa Kiyahudi kwamba sheria na hema ya agano la kale vilikuwa ni picha ya agano bora na jipya.
Hii inaonyesha sehemu mpya ya fundisho.
Tafsiri hii kama ulivyotafsiri sura ya 8:6
"ilikuwa na maelekezo ya ndani" au "ilikuwa na miongozo"
mwandishi anaendeleza mazungumzo kutoka sura ya 8:6
Hema ilijengwa na kuwa tayari kwa matumizi
Vyombo hivi vyote vinafuatwa neno la linaloonyesha upekee wa vyombo. Kwa sababu mwandishi anadhani kwamba wasomaji wake tayari wanafahamu kuhusu vitu vyombo hivi.
mkate wa wonyesho mbele za Mungu au mkate ambao makuhani waliuwakilisha kwa Mungu.
pazia la kwanza kulikuwa na ukuta wa nje wa hema, hivyo pazia la pili lilikuwa ni pazia la pili kati ya mahali patakatifu na mahali patakatifu pa patakatifu.
Hii ni nambaya kawaida ya namba mbili
"Ndani ya sanduku la agano"
Hii ina maanisha wakati Mungu alipoonyesha kwa watu wa Israeli kwamba alikuwa amemchagua Haruni kama kuhani kwa kuichipusha maua fimbo ya Haruni.
"kuwa na maua" au "kuchipua" au "ilikuwa na kuendelea"
"Mbao" ni vipande bapa vya mawe vilivyokuwa na maandishi juu yake. Hizi zinamaanisha mbao za mawe ambazo ziliandkwa amri kumi.
wakati Waisraeli walipokuwa wakitengeneza sanduku la agano, Mungu aliwaamuru Waisraeli kuchonga makerubi wawili wanatazamana pamoja na mbao zao zigusa juu ya kifuniko upatanisho cha sanduku la agano. Hapa vinaongelewa kana kwamba kama vinaweka kivuri kwenye sanduku la agano.
Ingawa mwandishi anatumia kiwakilishi cha wingi "tuna" kimsingi anasema kwa nafsi yake mwenyewe.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji.AT: "Baada ya makuhani kuandaa vitu hivi"
Hii inaweza kusemwa katika muundo tendewa. AT: "na mara zote alileta damu"
Hii ni damu ya dume na mbuzi ambazo kuhani mkuu alipaswa kudhabihu siku ya upatanisho.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mungu alikuwa bado hajaifunua njia ya sehemu takatifu zaidi"
Maana zinazowezekana: 1) chumba cha ndani cha hema duniani au 2) Uwepo wa Mungu mbinguni.
Maana zinazowezekana: 1) "chumba cha nje cha hema bado kinasimama" au 2) "hema ya duniani na taratibu za dhabihu zilikuwa zikiendelea."
"Hii ilikuwa ni "picha" au "Hii ilikuwa ni alama"
"kwa sasa"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. "ambayo sasa makuhani wanatoa"
Mwandishi anaongelea dhamiri ya mtu kana kwamba ni kilikuwa ni chombo ambacho kilikuwa kikifanywa bora zaidi. Dhamiri ya mtu ni ni ujuzi wa kujua baya na jema. Pia ni uelewa wake kama amekosa au amefanya jema. Na kama akifahamu kwamba ametenda baya tunasema anajisikia hatia.
Mwili hapa unamaanisha mwili wa binadamu." AT: "taratibu za mwili"
"desturi za maisha ya kimwili"
"Mungu aliandaa taratibu zote hizi kwa ajili ya mwili"
Hii inawezakusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Kwamba Mungu alitoa hadi alipoumba mpangilio mpya"
"agano jipya"
Baada ya kufafanua huduma ya hema la agano chini ya sheria ya Mungu, mwandishi anaweka bayana kwamba huduma ya Kristo chini ya agano jipya ni bora pia kwa sababu imefunikwa kwa damu yake. Ni bora pia kwa sababu Kristo ameingia hekalu la kweli, ambalo ni uwepo wa Mungu mbinguni, badala ya ya kuingia, kama makuhani wakuu, ndani ya hema ya duniani, ambayo kimsingi ilikuwa ni nakala isiyo timilifu.
Hii haimaanishi vitu vinavyoshikika. Inamaanishavitu vizuri ambavyo Mungu ameahidi katika agano lake jipya.
Hii inamaanisha hema la mbingunini muhimu zaidi na timilifu zaidi ya hema ya duniani.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "ambayo haikufanywa kwa mikono ya binadamu"
"Mikono" inamanisha mtu.
Uwepo wa Mungumbinguni unaongelewa kana kwamba kana kwamba ilikuwa sehemu takatifu zaidi, chumbacha ndani cha hekalu.
Kuhani angemimina kiasi kidogo cha majivu kwa watu wasiosafi.
Mwandishi anatumia nukuu kusisitiza kwamba dhabihu ya Kristo ilikuwa na nguvu. AT: Hivyo hakika damu ya Kristo itatusafisha nafsi zetu hata zaidi kutoka katika kazi/ matendo mafu na kumtumikia Mungu aliye hai! Kwa sababu, kupitia kwa kupitia Roho wa milele, alijitoa mwenyewe pasipo hatia kwa Mungu.
"damu" ya Yesu inasimama kwa kifo chake.
"Dhamiri" hapa inamaanisha mtu kujisikia hatia. Kwa sababu Yesu alijidhabihu yeye mwenyewe, waumini hawapaswi tena kujisikia hatia kwa ajili ya dhambi zao walizozifanya kwa sababu amewasamehe.
Hii ni dhambi ndogo au kosa la kimaadili hapa linaongelewa kana kwamba lilikuwa dogo,doa lisilo la kawaida kuharibu juu ya mwili wa Kristo.
"kusafisha" linasimama kwa tendo la nafsi zetu kupokea msamaha wa kutokuwa na hatia kwa ajili ya dhambi tulizozitenda
wale ambao Mungu amewateua au kuchaguliwa na kuwa watoto wake
matendo mafu yanaongelewa kana kwamba yalikuwa yakitoka katika ulimwengu wa wafu.
"kama matokeo" au "kwa sababu hii"
Hii inamaanisha Kristo alisababisha agano jipya kati ya Mungu na wanadamu kuwepo.
tafsiri hii kama ulivyotafsiri 8:6
Hii inaweza kuelezwa katika mfumo tendaji. AT: "wale ambao Mungu aliowachagua kuwa wana wake"
upokeaji wa kile ambacho Mungu alikuwa amewaahidi waumini kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kurithi kitu na mali kutoka katika mwanafamilia.
hati ya kisheria ambayo inamtaja mtu ambaye angepokea zile mali wakati mwenye mali akifa.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "mtu ni lazima ahakikishe kwamba mtu aliweka wosia amekufa"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Hivyo Mungu alianzisha hata lile agano la kwanza kwa damu"
Tafsiri hii kama ulivyotafsiri 8:6
kifo cha wanyama waliotolewa dhabihu kunaongelewa kana kwamba hakukuwa na kitu kingine isipokuwa damu.
Kuhani alichovyawa hissopo katika damu na maji na kisha alikitikisa kijiti cha hissopo na kudondosha damu na maji juu ya magombo na watu.Kunyunyiza damu lilikuwa ni tendo la ishara lililofanywa na makuhani ambalo kwa hilo walipata faida ya agano kwa watu na vyombo. Na hapa upokelewaji wa gombo na watu vinafanywa upya.
mmea uliotumika katika ibada ya kunyunyiza
"Damu" hapa linamaanisha kifo cha wanyama waliotolewa dhabihu ili kuftimiza matakwa ya agano.
"Musa alinyunyuzia"
Kunyunyuzia kulikuwa ni tendo la ishara ambalo lilifanywa na makuhani ambalo kwa hilo walipata faida ya agano kwa watu na kwa viyombo.
huu ni mkebe au chombo ambacho unaweza kubeba vyombo. Hii inamaanisha vyombo au kitu. AT: " vyombo vyote vilivyotumika katika huduma"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Makuhani walivitumia katika kazi zao"
kufanya kitu kipokelewe na Mungu kunafanywa kana kwamba kitu hicho kilikuwa kinatakaswa. Wazo hili linaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Makuhani hutumia damu kusafisha karibia ila kitu"
Hapa damu ya mnyama inaongelewa kuhusu kifo cha mnyama.
Hapa "kumwaga damu" kunamaanisha kwa kitu kufa kama dhabihu kwa Mungu. mambo haya hasi yanaweza kumaanisha msamaha wote unapatikana kwa njia ya kumwaga damu.
"msamaha wa dahmbi ya watu"
Mwandishi anasisitiza kwamba Kristo (sasa yuko mbinguni anatuombea) alipaswa kufa mara moja tu kwa ajili ya dhambi na kwamba atarudi duniani mara ya pili.
"Makuhani wanapaswa kutumia dhabihu hii ya wanyama kusafisha nakala za vitu vya mbinguni"
Ile ni bora zaidi ya dahabihu zilizotumika kusafisha nakala za duniani. Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kama kwa vitu vya mbinguni vyenyewe, Mungu alipaswa kuvisafisha kwa dhabihu iliyo bora"
"Mikono" hapa inamaanisha mwanadamu. AT: "ambayo wanadamu walitengeneza na"
"sehemu ya kweli na takatifu ya patakatifu pa patakatifu"
" Hakuingia mbinguni"
"kila mwaka" au "mwaka baada ya mwa
Hii inamaanisha na damu ya mnyama wa kafara, na sio kwa damu yake mwenyewe.
"Kama alipaswa kutoa mara nyingi"
Uumbaji wa dunia unaongelewa kana kwamba ni jengo na msingi wake ulikuwa sehemu ya kwanza kujengwa. AT: "tangu Mungu alipoanza kuiumba dunia"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Mung amemfunua"
Hii inaongea kuhusu dhambi kana kwamba kilikuwa ni chombo ambach mtu angeweza kukiondoa. AT: "kumsababisha Mungu kusamehe dhambi kwa kujidhabihu mwenyewe"
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "Pia Kristo, ambaye "aliyejitoa mwenyewe"
Tendo la kutufanya wasio na hatia badala ya kuwa na hatia kwa ajili ya dhambi zetu kunaongelewa kana kwamba dhambi zetu zilikuwa vyombo ambavyo vinashikika ambavyo Kristo aliweza kuzibeba.
dhambi inamaanishahatia ambayo watu waliyonayo mbele za Mungukwa sababu ya dhambi walizotenda.
1 Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka. 2 Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi. 3 Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka. 4 Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi. 5 Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, "Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu. 6 Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi. 7 Kisha nilisema, "Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo". 8 Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: "Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake" dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria. 9 Kisha alisema, "Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako". Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili. 10 Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote. 11 Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi. 12 Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu, 13 akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake. 14 Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu. 15 Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema, 16 "Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao". 17 Kisha alisema, "Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu". 18 Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi. 19 Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu. 20 Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia. 21 Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu, 22 na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi. 23 Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu. 24 Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema. 25 Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia. 26 Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena. 27 Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu. 28 Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu. 29 kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahiri kilammoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema? 30 Kwakuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, "Kisasi ni changu, nitalipa". Na tena, "Bwana atawahukumu watu wake". 31 Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai! 32 Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali. 33 Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo. 34 Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele. 35 Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu. 36 Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake. 37 Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia. 38 Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye." 39 Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.
Katika hii sura, mwandishi anamalizia kwa kufafanua jinsi sadaka ya Yesu ni bora kuliko sadaka zilizotolewa hekaluni.
Watafsiri wengine wametenga kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 10:5-7,:15-17, 37-38, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Kuishi kitakatifu ni muhimu kwa Wakristo. Mungu atawajibisha watu jinsi walivyoishi maisha yao ya Kikristo. Ingawa hakutakuwa na hukumu ya milele kwa Wakristo, matendo yasiyo pendeza Mungu yatakuwa na matokeo. Zaidi ya hayo maisha ya uaminifu yatatuzwa. , and and )
Dhabihu zenyewe hazikuwa na nguvu za kuokoa. Zilifanikiwa kwa sababu zilikuwa dhihirisho la imani ambayo ilitokana na aliyekuwa anatoa hiyo Dhabihu. ilikuwa ni sadaka ya Yesu inayofanya sadaka hizi "kuondoa dhambi". Kulingana na hayo, Mungu hataki sadaka iltolewao bila imani. and )
Haiko wazi iwapo huu unabii ulikuwa unatimizwa wakati mwandishi huyu alikuwa anaandika ama iwapo ungetimizwa baadaye. Mtafsiri aepuke kusema wakati muda wa agano hili inaanza. and )
Mwandishi anaonyesha udhaifu wa sheria na dhabihu zake, kwa nini Mungu aliwapa sheria, na utimilifu wa ukuhani mpya na dhabihu ya Kristo.
Hii inaongewa kuhusu sheria kana kwamba kilikuwa ni kivuli. Mwandishi anaongea kwamba sheria haikuwa vitu vizuri ambavyo Mungu alikuwa ameviahidi. Ni sehemu ndogo tu ya mambo mazuri ambayo Mungu alipaswa kuyafanya.
" sio vitu halisi vyenyewe"
"kila mwaka"
Mwandishi antaumia swali kuelezea kwamba dhabihu zilikuwa na nguvu ya ukomo. "wangekuwa wameacha kudhabihu dhabihu"
"sitisha"
"kwa hali hiyo"
Dhambi za watu zinaongelewa kana kwamba ziklikuwa zikioshwa ana kwa ana. AT: " Kama Mungu alikuwa tayari amekwisha samehewa dhambi zao"
"wangeweza kufahamu kuwa hawana hatia ya dhambi tena."
Dhambi zinaongelewa kana kwamba zikuwa vyombo ambavyo damu ya wanyama ingeweza kuziondoa. AT: "Kwa sababu haiwezekani kabisa Mungu kusamehe dhambi kwa kwa sababu ya damu ya mafahar na mbuzi.
"Damu" hapa inamaanisha kwa wanyama hawa waliokuwa wanakufa kwa kama dhabihu kwa Mungu.
Maneno ya Kristo alipokuwa duniani yalikuwa yamesemwa katika nukuu hii kutoka Zaburi ya Daudi.
"Wewe" hapa ni nafsi ya umoja na inamaanisha Mungu.
"kufanya tayari"
"Nilisema" inamaanisha Kristo
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: " kama manabii walivyoandika katika gombo kuhusu mimi"
Hii inamaanisha maandiko au maandiko matakatifu.
pamoja na kwamba anabadilisha maneno polepole, mwandishi anarudia nukuu hii kufoka Zaburi ya Daudi kusisitiza.
Tafsiri maneno haya kama ulivyotafsiri 10:5
"ambayo makuhani hutoa"
"Tazama" au "sikiliza"
Jina la tendo dhaaniwa "taratibu"/ tendo hapa inamaanisha njia ya kudhabihu kwa ajili ya dhambi.Kusitisha kufanya kunaongelewa kana kwamba kilikuwa ni chombo ambacho kingeweza kuondolewa.
Maneno "kwanza" na "pili" ni namba za kawaida.AT: "taratibu za zamani ...taratibu mpya"
Kuanzisha njia ya pili ya kudhabihu inaongelewa kana kwamba kuanzisha utaratibu AT: "ill kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi kwa mara nyingine"
"Mungu ametutakasa" au "Mungu ametuweka kwake kwa ajili yake"
"Mungu alitaka Kristo kujitoa mwenyewe dhabihu na kwamba dhabihu ilishatutenga sisi kwa Mungu"
"wakati Yesu Kristo alipotoa mwili wake kama dhambihu" au "kwa sababu Yesu Kristo aliudhabihu mwili wake"
Haya maneno yanatumika kulinganisha vitu viwili . Lugha yako inaweza kuwa na njia ya kusisitiza kwamba mwandishi anaweka ulinganifu. Au unaweza kutumia "Lakini."
"siku hadi siku" au "kila siku"
Hii inaongelea. dhambi kana kwamba ni chombo ambacho mtu anaweza kukiondoa. AT: "haiwezi kumfanya Mungu asamehe dhambi"
kuteswa kwa maadui wa Kristo kunaongelewa kana kwamba ni sehemu iliyotengenezwa kwa ajili yake kupumzishia migu yake. AT: "hadi Mungu atakapowaseta maadui wa Kristo na kuwa kana kiti cha miguu yake"
"wale ambao Mungu amewatenga kwa ajili yake mwenyewe"
Hii ni nukuu kutoka kwa nabii Yeremia katika Agano la Kale.
"amoja na watu wangu"
"wakati wa agano la kwanza na watu wangu ulipokwisha"
Mioyo ya watu na akili vinaongelewa kana kwamba sheria ya Mungu ingeweza kuwekwa au kuandikwa juu yake. AT: "Nitawasababisha kuzielewa shria zangu na nitawasababisha kuzitii sheria zangu"
Hii inaendeleza nukuu ya nabii Yeremia katika Agano la Kale
Hii ni sehemu ya pili ya ushuhuda wa Roho Mtakatifu (tazama 10:15). Kisha asema, "Sitazikumbuka dhambi zao na makosa yao."
"Sitazikumbuka dhambi zao"au "sitafikiri tena kuhusu dhambi zao"
Hii haimaanishi "wakati huu," lakini imetumika kuvuta usikivu kwa kipengele kinachofuata.
"wakati Mungu aliposamehe mambo haya"
"watu wao hawahitajiki kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi"
Baada ya kuweka wazi kwamba kuna dhabihu moja kwa ajili ya dhambi, mwandishi anaendelea na picha ya patakatifu pa patakatifu katika hekalu, mahali ambapo kuhani mkuu aliweza kuingia kila mwaka na damu ya dhabihu
Hii inamaanisha kwa waumini wote katika Kristo awe mwanaume au mwanamke. "dada" au "waumini"
Hii inamaanisha uwepo wa Mungu, sio mahali patakatifu zaidi katika hema ya zamani.
"Damu ya Yesu" inamanisha kwa kifo cha Yesu.
pengine inamaana 1) Njia hii mpya kwa Mungu kwamba Yesu ametoa matokeo ndani ya waumini kuishi milele au 2) Yesu yu hai, na na ni njia ambayo waumini wanaingia kuingia katika uwepo wa Mungu.
neno mwili hapa inasimama kama kwa mwili wa Yesu, na mwili wake unasimama kwa kifo chake the kujidhabihu. AT: "kwa jinsi ya mwili wake"
Hii ni lazima itafsiriwe katika namna kuweka wazi kwamba Yesu ni "kuhani Mkuu."
"Msimamizi wa nyumba"
"watu wote wa Mungu"
Kumkaribia hapa inasimama kwa kumwabudu Mungu, kama kuhani alipaswa kwenda juu ya mimbali ili kudhabihu wanyama kwa Mungu.
"mioyo ambayo Mungu ameinyunyizia kwa damu ya Yesu na kuifanya safi"
"kana kwamba alifanya mioyo yetu safi kwa damu yake"
"kazi ya kuweka vitu kuwa safi"
"kana kwamba alikuwa ameosha miili yetu kwa maji halisi"
Kama mtafasirianaelewa kwamba sentensi hii yanamaanishaubatizo wa Kikristo, hivyo maji ni maji halisi na sio mfano. Lakini kama maji yanachukuliwa kama maji, hivyo "halisi" inasimama kwa niaba ya usafi wa kiroho ambao ubatizo unaosemwa hapa umetimiliza. "Kuoshwa" kunasimama kama waumini kuwa kupokelewa na Mungu.
"endelea kuwaambia watu kwamba tuna ujasiri kwa sababu tunaamini kuwa Mungu atatenda kile alichoahidi kutenda"
pasipokuwa na kuwa na hakika" au "pasipokuwa na shaka"
"tusiache kujumuika pamoja kwa ajili ya ibada"
"Kama mnavyofahamu kuwa Kristo atakuja hivi karibuni"
Mwandishi anatoa onyo la nne.
"kwa kukusudia"
Ujuzi wa kweli kunaongelewa kana kwamba ni chombo ambacho kinaweza kumpa mtu mmoja hadi mwingine. AT: "baaba ya kuwa tumejifunza kweli"
"hakuna awezaye kutoa dhabihu ambayo Mungu atatusamehe dhambi zetu"
Ukweli kuhusu Mungu.
Hakuna mtu yeyote awezaye kutoa dhabihu mpya kwa sababu dhabihu ya Kristo ndiyo pekee inayofanya kazi.
"dhabihu kwa ajili ya dhambi" inasimama kama njia tendaji ya kudhabihu wanyama ili kuondoa dhambi"
ya hukumu ya Mungu. ambayo, Mungu atahukumu.
Ukali wa Mungu unaongelwa kana ni moto ambao ungechoma maadui wake.
Imepewa maana ya kwambahii inamaanisha "angalau wawili au watatu"
Mwandishi anasisitiza ukuu wa adhabu kwa wale wote wanaomkataa Kristo.
Kutokumjali Kristo na kumtukana kunaongelewa kana kwamba mtu anakanyaga.
Hii inaonyesha jinsi mtu alivyokanyaga Mwana wa Mungu. Kwa kuihesbu damu ya agano kama sio takatifu"
Hili ni jina muhimu la cheo cha Yesu
"damu" hapa inasimama kama kifo cha Kristo, ambacho kwa hicho Mungu alianzisha agano jipya.
"damu ambayo Mungu alimtakasa kwa hiyo"
"Roho wa Mungu anayetoa neema"
Neno "tuna" linamaanisha kwa mwandishi na waumini wote. Nukuu hizi mbili zinatoka kwenye sheria ambayo Musa alitoa katika Agano la Kale.
kisasi kinaongelewa kana kwambani chombo ambacho kinatoka kwa Mungu, ambaye alikuwa na haki ya kufanya na kama alivyotaka na kile alichomiliki. Mungu anayo haki kulipa kisasi juuya maadui zake.
Ulipaji wa Mungu wa kisasi kunaongelewa kana kwamba ni kumlipa mtu ujira umfaao
kupokea adhabu ya Mungu kunaongelewa kana kwamba mtu anaangukia katika mikono ya Mungu. Mikono" hapa inamaanisha uwezo wa Mungu wa kuhukumu.
"wakati uliopita"
kujifunza kweli kunaongelewa kana kwamba Mungu aliwasha taa juu ya mtu. AT: "baada ya kujifunza ukweli kuhusu Kristo"
"ni jinsi gani umevumilia mateso mengi"
"Watu waliwadhihaki kwa matukano na mateso ya wazi wazi"
watu waliwaasi ninyi na kukutukana wazi
"mlijiuna na wale"
Baraka za Munguza milele zinaongelewa kana kwamba ni mali
katika 10:37 ni nukuu kutoka kwa nabii Isaya katika Agano la Kale.
"Kukataa ahadi kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kutupa kitu kisicho na thamani au kisicho na maana.
" kama Mungu alivyosema katika maandiko, kwa kila kitambo kidogo"
"mapema mno"
katika 10:38 mwandishi ananukuu kutoka kwa nabii Habakuki, ambayo moja kwa moja inafuata nukuu kutoka kwa nabii Isaya 10:37.
Haya maneno yanamaanisha kwa watu wa Mungu wowote.AT: "watu wangu waaminifu ...kama mmoja wao akigeuka...kwa mtu huyo" au " watu wangu waaminifu... kama wakigeuka ... nao"
kukosa ujasiri na imani kunaongelewa kana kwamba ilikuwa nikugeuka kutoka kufuata njia.
kukosa ujasiri na imani kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kugeuka kutoka katika kufuata njia.
kuishi milele na Mungu kunaongelewa kana kwamba ilikuwa ni kutunza roho ya mtu, Na roho hapa inamaanisha mtu mzima mzima.
1 Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana. 2 Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao. 3 Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana. 4 Ilikuwa kwa sababu ya imani kwamba Habili alimtolea Mungu sadaka ya kufaa kuliko alivyofanya Kaini. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisifiwa kuwa mwenye haki. Mungu alimsifu kwa sababu ya zawadi alizoleta. Kwa sababu hiyo, Habili bado ananena, ingawa amekufa. 5 Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. "Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua" kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu. 6 Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao. 7 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Nuhu, akiwa ameonywa na Mungu kuhusiana na mambo ambayo hayakuwa yameonekana, kwa heshima ya ki Mungu alitengeneza safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Kwa kufanya hivi, aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ambayo huja kupitia imani. 8 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, alipoitwa alitii na kwenda mahali ambapo alipaswa kupokea kama urithi. Alitoka bila kujua mahali gani alikuwa anakwenda. 9 Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishi katika nchi ya ahadi kama mgeni. Aliishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi wenzake wa ahadi ile ile. 10 Hii ni kwa sababu alitarajia kuupata mji ambao mwenye kuubuni na mjenzi wake angelikuwa ni Mungu. 11 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, na Sara mwenyewe, walipokea nguvu ya kutunga mimba ingawa walikuwa wazee sana, kwa kuwa walimuona Mungu kuwa mwaminifu, ambaye aliwaahidia mtoto wa kiume. 12 Kwa hiyo pia kutoka kwa mtu huyu mmoja ambaye alikuwa amekaribia kufa wakazaliwa watoto wasiohesabika. Walikuwa wengi kama nyota za angani na wengi kama mbegu za mchanga katika ufukwe wa bahari. 13 Hawa wote walikufa katika imani pasipo kupokea ahadi. Isipokuwa, wakiwa wameziona na kuzikaribisha kwa mbali, walikiri kwamba walikuwa wageni na wapitaji juu ya nchi. 14 Kwa wale wasemao mambo kama haya wanaweka bayana kuwa wanatafuta nchi yao wenyewe. 15 Kwa kweli, kama wangekuwa wakiifikiria nchi ambayo kwayo walitoka, wangelikuwa na nafasi ya kurejea. 16 Lakini kama ilivyo, wanatamani nchi iliyo bora, ambayo, ni ya kimbingu. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa ametayarisha mji kwa ajili yao. 17 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu baada ya kujaribiwa, alimtoa Isaka. Ndiyo, yeye ambaye alipokea kwa furaha ahadi, alimtoa mwanawe wa pekee, 18 ambaye juu yake ilinenwa, "Kutoka kwa Isaka uzao wako utaitwa." 19 IbrahImU alijua kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua Isaka kutoka katika wafu, na kwa kuzungumza kwa lugha ya maumbo, alimpokea. 20 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Isaka alimbariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yajayo. 21 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yakobo alipokuwa katika hali ya kufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yusufu. Yakobo akaabudu, akiegemea juu ya fimbo yake. 22 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Yusufu wakati wake wa mwisho ulipokaribia, alinena juu ya kutoka kwa wana wa Israel Misri na akawaagiza kuchukua pamoja nao mifupa yake. 23 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipozaliwa, alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake kwa sababu walimuona kuwa ni mtoto mchanga aliyekuwa mzuri, na hawakutishwa na amri ya mfalme. 24 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa, alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mtoto wa binti Farao. 25 Badala yake, alichagua kushiriki mateso pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia anasa za dhambi kwa kitambo. 26 Alifikiri aibu ya kumfuata Kristo kuwa ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri kwa kuwa alikaza macho yake katika zawadi ya wakati wake ujao. 27 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Musa alitoka Misri. Hakuhofia hasira ya Mfalme, kwa kuwa alivumilia kwa kutazama kwa asiyeonekana. 28 Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishika pasaka na kunyunyiza damu, ili kwamba mharibu wa mzaliwa wa kwanza asiweze kuwagusa wazaliwa wa kwanza wa kiume wa waisrael. 29 Ilikuwa ni kwa imani kwamba walipita katika bahari ya shamu kama katika nchi kavu. Wakati wamisri walipojaribu kupita, walimezwa. 30 Ilikuwa ni kwa imani kwamba ukuta wa Yeriko ulianguka chini, baada ya kuuzunguka kwa siku saba. 31 Ilikuwa ni kwa imani kwamba Rahabu yule kahaba hakuangamia pamoja na wale ambao hawakuwa watiifu, kwa sababu alikuwa amewapokea wapelelezi na kuwahifadhi salama. 32 Na niseme nini zaidi? Maana muda hautoshi kusimulia ya Gideoni, Barak, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samwel na za manabii, 33 ambao kupitia imani walizishinda falme, walitenda haki, na wakapokea ahadi. Walizuia vinywa vya simba, 34 walizima nguvu za moto, walikwepa ncha ya upanga, waliponywa kutoka katika magonjwa, walikuwa mashujaa vitani, na walisababisha majeshi wageni kukimbia. 35 Wanawake walipokea wafu wao kwa njia ya ufufuo. Wengine waliteswa, bila kukubali kuachwa huru ili kwamba waweze kupata uzoefu wa ufufuo ulio bora zaidi. 36 Wengine waliteswa kwa dhihaka na kwa vichapo, naam, hata kwa vifungo na kwa kutiwa gerezani. 37 Walipondwa mawe. Walikatwa vipande kwa misumeno. Waliuawa kwa upanga. Walikwenda kwa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi walikuwa wahitaji, wakiendelea katika maumivu na wakitendewa mabaya 38 (ambayo ulimwengu haukustahili kuwa nao), wakitangatanga nyikani, milimani, katika mapango na katika mashimo ya ardhini. 39 Ingawa watu wote hawa walikubaliwa na Mungu kwa sababu ya imani yao, hawakupokea alichoahidi. 40 Mungu alitangulia kutupatia kitu kilichobora, ili kwamba bila sisi wasingeweza kukamilishwa.
Mwandishi anaanza sura hii kwa kuelezea nini maana ya imani. Baadaye anapeana mifano mingi ya watu waliokuwa na imani na jinsi walivyoishi.
Katika maagano yote mapya na ya zamani, Mungu alihitaji imani. Watu wengine wa imani walifanya miujiza na walikuwa wenye nguvu sana. Watu wengine wa imani waliteseka sana.
Mwandishi anaongea vitu vtatu kuhusu imani katika maelekezo haya mafupi.
Neno hili limetumika hapa kufanya kupumzika katika fundisho lake kuu. Hapa mwandishi anaanza kufafanua maana ya "imani."
"imani ni msingi alionao mtu katika tegemeo"
Hapa jambo hili hurejea katika ahadi za Mungu, hususani uhakika walionao waamini wote wa Yesu kuwa kunawakati watakuwa na Mungu mbinguni milele.
"yale ambayohatujayaona" au "ambayo hayajaonekana"
"Kwa sababu kulikuwa na matukio ya hakika ambayo yalikuwa hayajatokea"
"Mungu aliwathibisha mababu zetu kwa sababu ya imani yao"
"Mungu aliimba dunia kwa kuiamuru iwepo"
"Mungu hakuumba tunavyoviona kutokana na vitu vinavyoonekana"
kisha mwandishi anatoa mifano mara nyingi kutoka Agano la Kale ya watu walioishi ka imani ingawa hawakupokea kile ambacho alikuwa amekiahidi wakati walipoishi duniani.
'Mungu alishuhudia kwamba Habili alikuwa mwenye haki"
Yale aliyofanya Abel yanaendelea kutufundisha
Mungu alimshuhudia kuwa mwenye haki"
Kwa imani Enoko hakufa kwa sababu Mungu alimchukua.
Kufa.
"Kabla Mungu hajamchukua juu"
sasa pasipo imani
Pasipo imani haiwezekani kumpendeza yeye
yeyote ajaye kwa Mungu
anayetaka kumwabudu Mungu na kuwa sehemu ya watu wake kunaongelewa kana kwamba ni kuja kwa Mungu. "mtu yeyote anayehitaji kuwa sehemu ya Mungu"
"huwapatia wale"
Kujifunza kuhusu Mungu na kufanya juhudi kumtii kunaongelewa kana kwamba mtu anamtafuta mtu mwingine.
"Kwa sababu Mungu alimwambia yeye"
"kuhusu vitu ambavyo hapana hakuna hata mmoja amewahi kuviona kabla" au " kuhusu matukio ambayo hayajatokea bado"
Watu wanaoishi duniani wakati huo
Nuhu anaongelewa kana kwamba alikuwa akirithi mali ana utajiri kutoka kwa mwana familia. "alipokea kutoka kwa Mungu mwenye haki"
"kwamba Mungu huwapa wale walio na imani katika yeye"
"pindi Mungu alipomwita"
"Aliacha nyummba yake kwenda kwenye sehemu"
"Nchi ambayo Mungu alimuahidia.
"aliishi kama mgeni katika nchi ambayo Mungu alikuwa amemuahidi."
"warith pamoja." Hii inaongea kuhusu Abrahamu, Isaka, na Yakobo kana kwamba walikuwa warithi ambao wangepokea urithi kutoka kwa baba yao.
Mungu anaongelewa kana kwamba ni mbunifu na mjenzi.
Mtu ambaye anaunda majengo.
mtu anayebuni majengo
"Uwezo wa kuwa baba"
"walimwamini Mungu, ambaye alikuwa amewaahidi vitu kuwa mwaninifu"
"mzee sana kupata" au "mzee sana"
Hii ilimuhusu Abrahamu kuwa na wana uzao mwingi sana.
"ambayo mengi sana kuhesabu"
"pasipo kupokea ahadiambazo Mungu alikuwa ameawaahidi
"baada ya kujifunza kile Mungu atakachofanya wakati ujao"
walitambua" au walipokea"
"wageni" na "wapitaji" kimsingi yanamaanisha kitu kimoja. Hii inasisitiza kwamba nchi haikuwa nyumbani kwao kweli. Walikuwa wakisubiri kwa ajili ya nyumbani kwao kweli ambapo Mungu ametengeneza kwa ajili yao.
"Nchi ambayo wanatokea"
"nchi ya kimbingu" au "nchi mbinguni"
"Mungu anafurahi kuitwa Mungu wao" au "Mungu anajivuna kuwa Mungu wao"
"pindi Mungu alipomjaribu"
"kwake ambaye Mungu alisema"
"Ni katika uzao wa Isaka amabao Mungu atafikiri uzao wako.
namna ya kuongea." Hii ina maana kwamba mwandishi anachosema kisichukuliwe kama tukio ambalo linatokea kimwili. Mungu hakumleta Isaka kutoka kwa wafu.Lakini Abrahamu alikuwa anataka kumdhabihu Isaka wakati Mungu alipomzuia, ilikuwa kana kwamba Mungu alikmrudisha kutoka kwa wafu.
"Abraham alimpokea Isaka tena
"ilikuwa kutoka kwa wafu
"Abrahamu alimpokea Isaka"
"Yakobo alimwabudu Mungu"
"alipokuwa amekaribia kufa"
"aliongea wakati wana wa Israeli wangeondoka Misri"
"wana wa Israeli" au " uzao wa Israeli"
Yusufu alikufa akiwa Misri. Aliwataka waru wake kuchukua mifupa yake wakati wataondoka Misri ili kwamba waizike mifuka katika nchi ambayo Mungu alikuwa amewaahidi.
"Wazazi wa Musa walimfika kwa miezi mitatu baada ya kuzaliwa."
"Akawa mtu mzima
"aliwazuia watu kumuita"
"udhoefu wa watu kutokumuheshimu kwa sababu alifanya kile ambacho Kristo angetaka"
"Kufanya kile alichojua kuwa kitampatia zawadi huko mbinguni."
kumtii Kristo kunaongelewa kana kwamba walikuwa wakimfuata katika njia.
Kufanya kile alichokifahamu kungemwezesha kupata taji mbinguni"
Musa anaongelewa kana kwamba alimwona Mungu, ambaye haonekani.
"yeye ambaye hakuna mtu anaweza kumwona"
Hii inamaanisha amri ya Mungu kwa Waisraeli kuchinja mwana kondoo na kusambaza juu ya kila muimo wa kila nyumba mahali ambapo waliishi Hii ingezuia muharibifu kutowaaribu wazaliwa wao wa kwanza.
"usidhuru" au " usiue"
"wao" ya kwanza ina maanisha Waisraeli, na "wao" ya pili inamaanisha Wamisri na "wao" ya tatu inamaanisha kuta za Yeriko.
Waisraeli walipita kupitia Bahari ya Shamu'
"Maji yaliwameza Wamisri"
"Wamisri walizama ndani ya maji"
"Waisrael walitembea kwa kuzunguka kuta kwa siku saba"
"Aliwaficha wapelelezi ili wawe salama
mwandishi anaendelea kuongelea kwa kile ambacho Mungu angefanya kwa mababu wa Israeli.
Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba kuna mifani mingi ambayo aliyoinukuu.
"Sita kuwa na muda wa kutosha"
Jina la mtu.
"ilikuwa ni kwa ajili ya imani wale wanaume kama hivi"
"waliwashinda watu wa falme ngeni"
Iliyoshinda
Njia ambazo watu wa Israeli waliokoka kutoka kifo. "Simba hawakuwala... moto haukuwaunguza." Upanga haukuwaua."
"walipokea uponyaji kutoka kwa Mungu"
"wakawa hodari katika vita na wakashinda"
"Wanawake walipokea wafu waliokuwa wamekufa wakati Mungu alipowafufua"
Wengine waliteseka wakati wengine wanadhihakiwa... na wakachapwa wengine walikufa kwa sababu ya kutupiwa mawe... wengine walikufa walipokatwa na misumeno... watu waliwaua
Maana zinazo dhaaniwa 1) hawa watu watapata maisha bora mbinguni au 2)Watu hawa watapata ufufuo ulio bora zaidi ya wale wasio na imani.
watu waliwatukana na kuwapiga wengine... watu waliwaponda mawe.
Mungu aliwajaribu wengine kwa kuwaruhusu adui zao kuwa tukana na kuwachapa na hata kuwaweka vifungo"
"wakiva tu ngozi za kondoo na mbuzi"
"hawakuwa na kitu" au " walikuwa masikini sana"
"watu wa dunia hii haikuwastahili"
"na wengine waliishi katika mapango na mashimo ya ardhi"
"Mungu aliheshimu hawa kwa sababuya imani yao, lakini wenyewe hawakupokea kile ambacho Mungu alikuwa amekiahidi"
"kile ambacho Mungu alikuwa amewaahidi."
" ili kwamba Mungu angetukamikamilisha sisi na wao pamoja"
1 Kwahiyo, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa la mashaidi, na tutupe kila kitu kinacho tulemea pamoja na dhambi ambayo inatuzingira kwa urahisi. Tupige mbio kwa saburi katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu. 2 Tuyaelekeze macho yetu kwa Yesu, aliye mwanzilishi na mwenye kutimiliza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahmili msalaba, akiidharau aibu yake, na akakaa chini mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu. 3 Maana mtafakarini yeye aliye stahimili maneno ya chuki kutoka kwa wenye dhambi, dhidi yake mwenyewe ili kwamba msije mkachoka au kuzimia mioyo yenu. 4 Hamjataabika au kuteseka mkishindana na dhambi kiasi cha kuishiwa damu. 5 Tena mmesahau kule kutiwa moyo ambako kunawaelekeza kama watoto wa kiume: "Mwanangu, usiyachukuwe kwa wepesi marudia ya Bwana, wala usikate tamaa unapo rekebishwa na yeye." 6 Kwa kuwa Bwana humrudi yeyote ambaye anampenda, na humwadhibu kila mwana ambaye humpokea. 7 Stahimili majaribu kama kurudiwa. Mungu hushughulika nanyi kama anavyoshughulika na watoto, maana ni mtoto yupi ambaye baba yake hawezi kumrudi? 8 Lakini kama hakuna kurudiwa, ambako sisi sote tunashiriki, basi ninyi ni haramu na si watoto wake. 9 Zaidi ya yote, tulikuwa na baba zetu kidunia wa kuturudi, na tuliwaheshimu. Je haitupasi hata zaidi kumtii Baba wa kiroho na kuishi? 10 Kwa hakika baba zetu walituadhibu kwa miaka michache kama ilivyoonekana sawa kwao, lakini Mungu hutuadhibu kwa faida yetu ili tushiriki utakatifu wake. 11 Hakuna adhabu inayofurahisha kwa wakati huo. Huwa na maumivu. Hata hivyo, baadaye huzaa tunda la amani ya utauwa kwa wale waliofundishwa nayo. 12 Kwa hiyo inueni mikono yenu iliyolegea na kufanya magoti yenu yaliyo dhaifu kuwa yenye nguvu tena; 13 nyosheni mapito ya nyayo zenu, ili kwamba yeyote aliye mlemavu hataongozwa upotevuni lakini apate kuponywa. 14 Tafuteni amani na watu wote, na pia utakatifu ambao bila huo hakuna atakayemwona Bwana. 15 Muwe waangalifu ili kwamba asiwepo atakayetengwa mbali na neema ya Mungu, na kwamba lisije shina la uchungu litakalochipuka na kusababisha shida na kukengeusha wengi. 16 Angalieni kuwa hakuna zinaa au mtu asiye mtauwa kama vile Esau, ambaye kwa sababu ya mlo mmoja aliuza haki yake ya kuzaliwa. 17 Kwa kuwa mnajua kwamba baadaye, alipotamani kurithi baraka, alikataliwa, kwa sababu hakupata fursa ya kutubu pamoja na baba yake, hata ingawa alitafuta sana kwa machozi. 18 Kwa kuwa hamkuja katika mlima ambao unaweza kuguswa, Mlima unaowaka moto, giza, kukatisha tamaa na dhoruba. 19 Hamkuja kwa sauti za tarumbeta, au kwa maneno yatokanayo na sauti ambayo ilisababisha kila wasikiao wasiombe neno lolote kusemwa kwao. 20 Kwa kuwa hawakuweza kuvumilia kile kilichoamuliwa: "Ikiwa hata mnyama agusaye mlima, lazima apigwe kwa mawe." 21 Ya kutisha zaidi aliyoyaona Musa alisema, "Nimeogopa sana kiasi cha kutetemeka". 22 Badala yake, mmekuja mlima Sayuni na katika mji wa Mungu aliye hai, Yerualem ya mbinguni, na kwa malaika elfu kumi wanaosherehekea. 23 Mmekuja katika kusanyiko la wazaliwa wa kwanza wote waliosajiliwa mbinguni, kwa Mungu hakimu wa wote, na kwa roho za watakatifu ambao wamekamilishwa. 24 Mmekuja kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa ambayo hunena mema zaidi kuliko damu ya Habili. 25 Angalia kuwa usije ukamkataa mmoja ambaye anenaye. Kwa kuwa kama hawakuepuka walipomkataa mmoja aliye waonya duniani, kwa hakika hatutaepuka ikiwa tutageuka mbali kutoka kwa yule atuonyaye kutoka mbinguni. 26 Kwa wakati huo sauti yake ilitikisa dunia. Lakini sasa ameahidi na kunena, "Bado mara nyingine tena sitatikisa dunia pekee, bali mbingu pia." 27 Maneno haya, "Mara moja tena," inaonesha kutoweshwa kwa vitu vile vitetemeshwavyo, hivi ni, vitu vile ambavyo vimeumbwa, ili kwamba vile vitu visivyotetemeshwa vibakie. 28 Kwa hiyo, tupokee ufalme ambao hautetemeshwi, tufurahi katika hali ya kumwabudu Mungu kwa kukubali pamoja na kunyenyekea katika kicho, 29 kwa maana Mungu wetu ni moto ulao.
Baada ya kuwafundisha watu umuhimu wa adhabu, mwandishi anaanza mfuatano ya mahubiri. .
Watafsiri wengine wameweka kila msitari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 12:5-6, ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Mungu anataka watu wake kutenda yaliyo mema.Wakifanya kile hakipendi, anatakikana kuwarekebisha ama kuwadhibu. Yeye hufanya hivi jinsi baba wa duniani huwarekebisha na kuwadhibu watoto wao wanaowapenda.
Kwa sababu ya idadi kubwa ya waumini wa Agano la Kale, mwandishi anaongelea maisha ya imani ambayo waamini wanapswa kuishi na Yesu kama kielezo chao.
inamaanisha mwandishi na wasomaji wake. Neno nyie linamaanisha wasomaji.
" kundi kubwa la mashahidi linatuzunguka sisi" au "Kundi kubwa la mashahidi linasimama kama mfano kwetu."
"Mashahidi" hapa inamaanisha waumini wa Agano la Kale katika sura ya 11 walioishi kabla ya shindano la imani ambayo waumini wanashindana sasa hivi.
"mzito" hapana "dhambi inayozonga kwa urahisi" vinaongelewa kana kwamba mtu angeweza kuziondoa na kuzitua chini.
"muumbaji na mkamilishaji." Hii inamaanisha kwamba Yesu ni chanzo imani ya waumini.Ndiye ambaye waumini wanamtumaini, na atahakikisha waumini wanafikia lengo lao.
Furaha ungetoka kwa Yesu kunaongelewa kana kwamba Mungu Baba aliyoiwekambele yake kufikia lengo.
Hii inamaanisha hakujali kuhusu aibu ya ya kufa msalabani.
"Mkono wa kuume" hapa unamaanisha sehemu ya heshima.
"enzi" inamaanisha utawala wa Mungu kama mfalme.
"mioyo" inamaanisha mawazo ya mtu na hisia.
"Umeshindana na dhambi, lakini wengine wamefanya hivyo kiasi cha kupoteza damu
Neno "dhambi" linamaanisha matendo, mawazo, na maneno ambayo yako kinyume na mapenzi na sheria za Mungu. Dhambi pia inaweza kumaanisha kutokufanya kitu ambacho Mungu anahitaji sisi tufanye.
Neno "damu" linamaanisha kimiminikka chekundu ambacho kinatoka kwa mtu katika ngozi ya mtu wakati anapoumia au kidonda. Damu huleta virubtubisho vya uzima katika mwili wa mtu. Damu pia inamaanisha uzima na inapomwagika inaonyesha kifo. watu walipotengeneza dhabihu, waliua mnyama na kumwaga damu yake juu ya madhabahu. Na hii iliwakilisha dhabihu ya uhai wa wanyama kulipa kwa ajili ya dhambi za watu.
Maneno kutia moyo na utiaji moyo inamaanisha kusema na kufanya vitu vinavyosababisha mtu kupata faraja, tumaini, ujasiri na moyo.
Neno "kuelekeza" na "elekezo" yanamaanisha kutoa maalekezo ya moja kwa moja kuhusu nini kifanyike.
Neno "mwana" linamaanisha mvulama au mwanaume katika uhusiano na wazazi wake.Inaweza pia kumaanisha uzao wa mtu mme au kwa mtu mwana aliye asiliwa.
Neno "Bwana" linamaanisha kwa mtu ambaye anaumiliki au uwezo juu ya watu. Inapotumika kwa herufi kubwa ni cheo kinachomaanisha Mungu.
Neno "adhibu" linamaanisha kufundiisha watu kutii maelekezo au kanuni kwa tabia njema.
kumpenda mtu mwingine in kumjali mtu huyo na na kufanya vitu vitakavyo mnufaisha. Kuna maana tofauti za upendo katika baadhi ya lugha inaweza konyeshwa kwa kutumia maneno tofauti: 1 Upendo utokao kwa Mungu kuna lengamazuri juu ya wengine hata kama kama haimnufaishi. Aina hii ya upendo unajali wengine bila kujali wanafanya nini. Mungu mwenyewe ni upendo na chanzo cha upendo wa kweli.
Neno adhibu maana ni kusababisha mtu kuteseka kwa sababu ya kukosea kwake.
"Elewa nyakati wa mateso Mungu hutufundisha nidhamu"
Hii inalinganisha unidhamishaji kwa Mungu kwa watu wake kama baba anavyo wanidhamisha watoto.
Hiii ina jumuisha wamaume na wanawake, AT: "watoto... mtoto"
Mwandishi anatumia swali kuelewesha kwamba ni kawaida kwa kila baba mzuri kuwarudi watoto wake.
"Hivyo kama haujapata kurudiwa na Mungu kama anavyowarudi wana wake wote"
wale ambao Mungu hawarudi kunaongelewa kana kwamba ni wana ambao wamezaliwa na mwanamke na mwanaume ambao hawajaoana.
Neno "mwili" hapa linamaanisha mwanadamu.
wanao turudi
Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba wangeweza kumtii Mungu Baba,
"ili kwamba tuishi"
"Baba yetu wa kiroho" au Baba yetu wa mbinguni"
"ili kwamba tuwe watakatifu kama Mungu alivyo mtakatifu"
"Tunda" hapa ni alama na inaongelewa kana kwamba ni mtu aliye katika amani na ambaye alileta amani kwa wengine.
Utauwa, ni hali ya mtu anaye mtii Mungu, inaongelewa kana kwamba ni tunda linakuwa juu ya mti. Mwandishi hapa anasema kwamba utauwa unaongezeka kama matokeo ya kurudiwa.
"wale walio fundishwa kwa kurudiwa." Ambao Mungu amewafundisha kwa kuwarudi."
Katika namna hii mwandishi anaongea kuhusu kuishi kama wakristo na kuwasaidia wengine.
Kuishi kama kumuheshimu na kumtukuza Mungu kunaongelewa kana kwamba ni kufuata njia iliyonyooka.
katika mfano huu wa kukimbia mashindanoni, "dahaifu" inawakilisha mtu mwingine katika shindano aliyeumia na anataka kuandoka katika shindano.Hili "geuka" linawakilisha wakristo wenyewe.
"badala yake aimalike" au "badala yake Mungu atamponya"
Esau, ambaye amesema katika maandishi ya Musa, inamaanisha kwa mwana wa kwanza wa Isaka na ndugu yake Yakobo.
" jaribu kuishi na kila mtu"
"na pia fanya bidii kuwa mtakatifu, kwa sababu ni watakatifu pekee ndio watakaomwona Mungu"
"pia tafuta utakatifu"
"hakuna mtu anapokea neema ya Mungu na kisha akaiachia" au " hakuna anaikataa neema baada ya kwanza kuamini katika yeye"
kwamba hakuna yeyote anayekuwa kama mzizi mchungu, ambao unaweza kukua na kusababisha matatizo uharibifu kwa watu wengi"
"baba yake, Isaka, alikataa kumbariki"
"kwa sababu haikuwa inawezekana kwa baba yake, Isaka, kubadilisha uamuzi wake"
Hapa aliyetafuta ni Esau
Mwandishi anakinzanisha katika waumini wakati wa Musa walipaswa kufanya chini ya sheria na kile ambacho waumini wa sasa wanapaswa kusihi baada ya kuja kwa Yesu chini ya agano jipya.
Maneno haya "ninyi" "Nyie" inamaanisha waumini wa Kiebrania ambao mwandishi anawaandikia. Neno "wale" linamaanisha watu wa Israeli baada ya Musa kuwaongoza kutoka Misri. Nukuu ya kwanza inatoka katika maandishi ya Musa. Mungu anafunua katika ukurasa huu katika Waebrania kwamba Musa alisema alitetemeka alipoona mlima.
kwa kuwa hamjafikia, kama watu wa Israeli walivyokuja, mlimani ambao unaweza kuguswa"
Hii inamaanisha waumini katika Kristo hawajafikia mlima kama Mlima Sinai ambao mtu anaweza kugusa au kuona.
"Hamjafikia mahali ambapo palipo na mlio mkubwa wa tarumbeta"
"sauti" inamaanisha mtu anaye ongea. pale ambapo Mungu anaongea kwa namna ya kwamba wale waliosikia walimtaka asiongee neno jingine kwao"
'kile ambacho Mungu aliamuru"
"ni lazima uiponde"
Abeli alikuwa mwana wa mwanamme na mwanamke wa kwanza, Adamu na Eva. Pia Kaini mwana wao alimuua Habili.
Mwandishi anaongea Mlima Sayuni, hekalu la mlima Yerusalem kana kwamba lenyewe ilikuwa mbingu, nyumbani kwa Mungu.
Wamewasili
"Idadi isiyohesabika ya malaika"
Hii inaongea waumini katika Kristo kana kwamba ni wana ambao ni wazaliwa wa kwanza. Hii inasisitiza sehemu yao maalumu na faida kama watu wa Mungu.
"ambao majina yao yameandikwa mbinguni
Hii inamaana Yesu alisababisha agano jipya kuwepo kati ya Mungu na wanadamu
"ambao Mungu amewafanya wakamilifu"
"Damu ya Yesu iliyonyunyizwa ambayo inamaana kubwa zaidi kuliko damu ya Habili, ambaye aliuawa na Kaini"
damu hapa inasimama kwa kifo cha Yesu, kama damu ya Habili inavyoisimama kwa kifo chake.
Baada ya kulinganisha uzoefu wa Waisraeli katika Mlima Sinai na uzoefu wa waumini baada ya Kristo kufa, mwandishi anawakumbusha waumini kwamba wana Mungu yuleyule anayewaonya leo. Hili ni onyo la tanzo kwa waumini.
Hii nukuu inatoka kwa nabii Hagai katika Agano la Kale.
"msikilizeni anaye ongea.
"kama watu wa Israeli hakuepuka hukumu"
Pengine 1) Musa aliye waonya duniani." au) Mungu aliyewaonya katika Mlima Sinai"
Kutmtii Mungu kunaongelewa kana kwamba mtu alikuwa akigeuka na kutoka kwake. "kama tusipomtii yeye anayeonya"
"Mungu alipoongea mlio wa sauti yake ilisababisha ardhi kutikisika"
tumia neno ambalo tetemeko la ardhi inafanya katika kuitetemesha adrhi.
Nukuu hii hapa kutoka kwa nabii Hagai inarudiwa kutoka mstari wa mwanzo.
'Mungu ataondoa vitu vyote vinavyotetemeshwa"
Tumia neno kwa tetemeko la ardhi linachofanya katika kutembea kwenye ardhi.
"kwamba amekwisha umba."
'vitu ambavyo havitetemeki"
"kwa sababu tunapokea ufalme au " kwa "sababu Mungu anatufanya sisi kuwa wanafamilia wa ufalme wake"
"tumshukuru Mungu"
"kunyenyekea" na "kicho" yana maanshabiliana maana na inasisitiza ukuu wa unyenyekevu kwa sababu ya Mungu"
Mungu anaongelewa kana kwamba ni moto ambao unaweza kuchoma kitu chochote.
1 Basi upendo wa ndugu na uendelee. 2 Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua. 3 Kumbuka wote waliomo gerezani, kana kwamba mulikuwa nao kule pamoja nao, na kama miili yenu ilitendewa kama wao. 4 Basi ndoa na iheshimiwe na wote na basi kitanda cha ndoa kifanywe kuwa safi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi. 5 Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, "Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi." 6 Basi tulidhikeni ili tusema kwa ujasiri, "Bawa ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?" 7 Wafikirieni wale walio waongoza, wale waliongea neno la Mungu kwenu, na kumbukeni matokeo ya mienendo yao; igeni imani zao. 8 Yesu Kristo ni yeye jana, leo, na ata milele. 9 Usije ukaongozwa na mafundisho mbalimbali ya kigeni kwani ni vizuri kwamba moyo ujengwe kwa neema, na siyo kwa sheria kuhusu chakula hayo hayatawasaidia wale wanaoishi kwa hayo. 10 Tunayo madhabau ambayo wale wanaotumika ndani ya hekalu hawana haki ya kula. 11 Kwa kuwa damu za wanyama, zilizotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi, ililetwa na kuhani mkuu ndani ya sehemu takatifu, lakini miili yao ilichomwa nje ya kambi. 12 Kwa hiyo Yesu naye aliteseka nje ya lango la mji, hili kwamba kuweka wakfu watu kwa Mungu kupitia damu yake. 13 Na kwa hiyo twendeni kwake nje ya kambi, tukizibeba fadheha zake. 14 Kwani hatuna makao ya kudumu katika mji huu. Badala yake tutafute mji ambao unakuja. 15 Kupitia Yesu mnapaswa mara kwa mara kujitoa sadaka ya kumtukuza Mungu, kumsifu kwamba tunda la midomo yetu likili jina lake. 16 Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni kwa sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana. 17 Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia. 18 Tuombeni, kwani tuna uhakikwa kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote. 19 Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni. 20 Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele, 21 Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina. 22 Sasa ninakutia moyo, ndugu, kuchukualiana na neno la kutia moyo ambalo kwa ufupi nililiandika kwenu. 23 Fahamu kwamba ndugu yetu Timotheo ameshaachiwa huru, ambaye pamoja naye nitawaona kama atakuja hivi karibuni. 24 Salimia viongozi wako wote na waumini wote. Wale wanaotoka Italia wanakusalimia. 25 Na neema iwe nanyi nyote.
Mwandishi anamalizia orodha ya mashauri aliyoyaanza katika sura ya 12. Halafu anawauliza wasomaji wake kumuombea anapomalizia barua hii.
Watafsiri wengine wametenga kila mistari wa ushairi kulia kuliko maandishi mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB inafanya hivi na ushairi katika 13:6 ambayo ni maneno kutoka Agano la Kale.
Mungu anataka watu wake wakaribishe watu wengine kuja kwa nyumba zao kula chakula na hata kulala. Watu wake wanastahili wafanye hivi hata kama hafahamu vizuri watu wanaowaalika. Katika Agano la Kale, Abrahamu na binamu yake Lutu walionyesha ukarimu kwa watu ambao hawakuwafahamu. Abrahamu aliandaa chakula cha bei na Lutu akawakaribisha kulala kwake.Walikuja kufahamu baadaye kwamba watu hao walikua malaika.
katika kufunga sehemu hii, mwandishi anatoa maelekezo ya moja kwa moja kwa waumini namna wanapaswa kuishi.
"Endeleeni kuonyesha upendo wenu kwa waumini wengine kama mfanyavyo kwa mwana familia"
"hakikisha unakumbuka"
"kuwaribisha wageni na kuwaonyesha wema"
"kana kwamba mlikuwa gerezani pamoja nao"
"wanaume na wanawake walio na kuolewa waliolewa ni lazima waheshimiane.
Hii inawatia moyo waumini kufikiri kuhusu mateso ya watu wengine kama ambaavyo wangeweza kufikiri juu ya mateso yao.
Hii inamaanisha tendo la ndoa kana kwamba n kitanda cha watu walioana. AT: "wanaume na wanawakewaheshimu mahusiano ya ndoa yao na sio kwenda na watu wengine"
"Msipende pesa"
"Toshekeni"
Hii nukuu inatoka katika Zaburi ndani ya Agano la Kale.
Mwandishi anatumia swali kusisitiza kwamba haogopi watu kwa sababu Mungu anamsaidia.
"matoke ya
Tumaini katika Mungu na njia ya uzima iliyoongozwa na viongozi hawa inaongelewa kama "imani ya kweli'
"Jana" hapa ina maana muda wote uliopita.
Sehemu hii inamaanisha dhabihu ya wanyama walio wafanya waumini katika Mungu katika kipindi cha Agano Kale, ambayo inafunika dhambi zao kwa muda hadi kifo cha Yesu kilipokuja.
usisawichiwe kwa mafundisho mbalimbali kunaongelewa kana kwamba mtu alikuwa amechukuliwa kwa lazima.
"moyo" unasimama kwa ujasiri wa mtu, upendo, na ushupavu.
"tunapata nguvu pale tunapofikilia jinsi Mungu ambavyo amekuwa mwema kwetu, lakini hatuwi na nguvu kwa kutii sheria za kuhusiana na chakula"
Vyakula hapa vinasimama kuhusu sheria za chakula.
Kuishi kunaongelewa kana kwamba ni kutembea.
madhabahu inasimama kwa sehemu ya ibada. Pia inasimama kwa ajili ya wanyama ambao makuhani katika dhabihu za agano la kale, ambavyo walichukua nyama kwa ajili yao na familia.
kuhani mkuu analeta ndani ya sehemu takatifu damu ya wanyama ambao makuhani waliwachinja kwa ajili ya dhambi.
"wakati makuhani wanapochoma miili ya wanyama"
"mbali na mahali ambapo watu waliishi"
Kuna ulinganifu kati ya dhabihu ya Yesu na dhabihu za hekalu ya Agano la Kale.
" Kwa njia hiyohiyo" au "Kwa sababu miili ya kujitoa iliunguzwa nje ya kambi"
"Nje ya mji."
Kumtii Yesu kunaongelewa kana kwamba ni mtu alipaswa kuacha kambi kwenda nje Yesu alipo.
kutokuwa na huruma kunaongelewa kana kwamba in chombo ambacho kinapaswa kubebwa katika mikono ya mtu au juu ya mgongo wa mtu.
Sifa inaongelewa kana kwamba ni dhabihu ya wanyama au uvumba.
sifa inaongelewa kana kwamba ni tunda, na "midomo" inaongelewa kana kwamba ni miti inayozaa matunda. Kwa nyongeza "midomo" inawakilisha watu wakimsifu Mungu.
Jina la mtu linamwakilisha mtu.
"mara zote tukumbuke kufanya mema na kusaidia wengine"
Kufanya wema na kuwasaidia kunaongelewa kana kwamba ni dhabihu juu ya mimbari.
roho za waumini,ambayo ni mwenendo wa maisha ya kiroho, yanaongelewa kana kwamba ni vyombo au wanyamaambao waangaliz wangeweza kutazama.
"huzunu" inasimama kama msiba au huzuni.
Mwandishi anafunga kwa baraka na salaamu
"Tuombeeni"hapa anamanisha mwandishi na wenzake.
njema/ safi hapa inamaanisha hatuna hatia.
Hii inaweza kusemwa katika mfumo tendaji. AT: "kwamba Mungu akipenda nitaondoa mambo yanayonizuia kuja kwenu"
Hii ni sehemu ya mpya ya barua. Mwandishi hapa anamsifu Mungu na anatoa maombi ya mwisho kwa wasomaji wake.
Kristo katika jukumu lake la kiongozi na mlinzi wa wale wanaoaminikatika yeye kunaongelewa kana kwamba ni mchungaji wa kondoo.
"Damu" hapa linasimama kwa kifo cha Yesu, ambacho ni msing kwa agano ambalo litakalodumu milele kati ya Mungu na waumini katika Kristo.
"kuwakamilisha" hapa inamaanisha kuwafanya "kuweza" au "kuwafundisha"
Neno hili "yetu" inamaanisha kwa mwandishi na wasomaji wake.
ambaye watu wote watamsifu milele
Hii inaonyesha sehemu mpya ya barua. Hapa mwandishi anatoa maoni yake ya mwisho kwa wale anaowaandikia.
Hii inamaanisha waumini wote anaowandikia wanume au wanawake.
"kwa uvumilivu fikirini juu ya nilichokiandika kuwatieni moyo.
"Neno" hapa linasimama kwa niaba ya ujumbe.
"hayuko tena gerezani"
Maana zinazodhaaniwa ni 1) mwandishi hayuko Italia, lakini kuna kundi la waumini waliotoka Italia walio pamoja naye au 2) mwandishi yuo Italia anapoandika barua hii.
Hili ni jina la sehemu wakati huo. Rumi ilikuwa mji mkuu wa Italia.