Swahili: Unlocked Literal Bible for 1 Mambo ya nyakati, 1 Petro, 1 Samweli, 1 Timotheo, 1 Wafalme, 1 Wakorintho, 1 Wathesalonike, 1 Yohana, 2 Mambo ya nyakati, 2 Petro, 2 Samweli, 2 Timotheo, 2 Wafalme, 2 Wakorintho, 2 Wathesalonike, 2 Yohana, 3 Yohana, Amosi, Danieli, Esther, Ezekieli, Ezra, Filemoni, Habakuki, Hagai, Hesabu, Hosea, Isaya, Job, Joeli, Kumbukumbu la torati, Kutoka, Luke, Malaki, Mambo ya walawi, Maombolezo, Marko, Matendo ya mitume, Mathayo, Mhubiri, Mika, Mwanzo, Nahumu, Nehemiah, Obadia, Proverbs, Psalms, Ruth, Sefania, Tito, Ufunuo, Waamuzi, Waebrania, Waefeso, Wafilipi, Wagalatia, Wakolosai, Waraka wa yakobo, Warumi, Wimbo wa sulemani, Yeremia, Yohana, Yona, Yoshua, Yuda, Zekaria

Formatted for Translators

©2022 Wycliffe Associates
Released under a Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
Bible Text: The English Unlocked Literal Bible (ULB)
©2017 Wycliffe Associates
Available at https://bibleineverylanguage.org/translations
The English Unlocked Literal Bible is based on the unfoldingWord® Literal Text, CC BY-SA 4.0. The original work of the unfoldingWord® Literal Text is available at https://unfoldingword.bible/ult/.
The ULB is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
Notes: English ULB Translation Notes
©2017 Wycliffe Associates
Available at https://bibleineverylanguage.org/translations
The English ULB Translation Notes is based on the unfoldingWord translationNotes, under CC BY-SA 4.0. The original unfoldingWord work is available at https://unfoldingword.bible/utn.
The ULB Notes is licensed under the Creative Commons Attribution-ShareAlike 4.0 International License.
To view a copy of the CC BY-SA 4.0 license visit http://creativecommons.org/licenses/by-sa/4.0/
Below is a human-readable summary of (and not a substitute for) the license.
You are free to:
The licensor cannot revoke these freedoms as long as you follow the license terms.
Under the following conditions:
Notices:
You do not have to comply with the license for elements of the material in the public domain or where your use is permitted by an applicable exception or limitation.
No warranties are given. The license may not give you all of the permissions necessary for your intended use. For example, other rights such as publicity, privacy, or moral rights may limit how you use the material.

Mwanzo

1

1Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na nchi.2Nayo nchi haikuwa na umbo na ilikuwa tupu. Giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi vya maji. Roho wa Mungu alikuwa akielea juu ya uso wa maji.3Mungu akasema, “Na kuwe nuru,” na kulikuwa na nuru.4Mungu akaona nuru kuwa ni njema. Akaigawa nuru na giza.5Mungu akaiita nuru “mchana” na giza akaliita “usiku.” Ikawa jioni na asubuhi, siku ya kwanza.

6Mungu akasema, “Na kuwe na anga kati ya maji, na ligawe maji na maji.”7Mungu akafanya anga na kugawanya maji yaliyo kuwa chini ya anga na maji ambayo yalikuwa juu ya anga. Ikawa hivyo.8Mungu akaita anga “mbingu.” Ikawa jioni na asubuhi siku ya pili.

9Mungu akasema, “Maji yaliyo chini ya mbingu yakusanyike pamoja mahali pamoja, na ardhi kavu ionekane.” Ikawa hivyo.10Mungu aliita ardhi kavu “nchi,” na maji yaliyo kusanyika akayaita “bahari.” Akaona kuwa ni vyema.11Mungu akasema, “Nchi ichipushe mimea: miche itoayo mbegu na miti ya matunda itoayo matunda ambayo mbegu yake imo ndani ya tunda, kila kitu kwa namna yake.” Ikawa hivyo.12Nchi ikatoa mimea, miche itoayo mbegu ya aina yake, na miti itoayo tunda ambalo mbegu yake imo ndani yake, kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.13Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tatu.

14Mungu akasema, “Kuwe na mianga katika anga kutenganisha mchana na usiku. Na ziwe kama ishara, kwa majira, kwa siku na miaka.15Ziwe mianga katika anga ili kutoa mwanga juu ya nchi.” Ikawa hivyo.16Mungu akafanya mianga mikuu miwili, mwanga mkuu zaidi kutawala mchana, na mwanga mdogo kutawala usiku. Akafanya nyota pia.17Mungu akazipanga katika anga kutoa mwanga juu ya nchi,18kutawala mchana na usiku, na kugawanya mwanga kutoka kwenye giza. Mungu akaona kuwa ni vyema.19Ikawa jioni na asubuhi, siku ya nne.20Mungu akasema, “Maji yajae idadi kubwa ya viumbe hai, na ndege waruke juu ya nchi katika anga la mbingu.”21Mungu akaumba viumbe wakubwa wa baharini, pamoja na kila kiumbe hai cha aina yake, viumbe waendao na wanaojaa kila mahali majini, na kila ndege mwenye mabawa kwa aina yake. Mungu akaona kuwa ni vyema.22Mungu akavibariki, akisema, “Zaeni na muongezeke, na mjae majini katika bahari. Ndege waongezeke juu ya nchi.”23Ikawa jioni na asubuhi, siku ya tano.24Mungu akasema, “Nchi na itoe viumbe hai, kila kiumbe kwa aina yake, mnyama wa kufugwa, vitu vitambaavyo, na wanyama wa nchi, kila kitu kwa jinsi yake.” Ikawa hivyo.25Mungu akafanya wanyama wa nchi kwa aina yake, wanyama wa kufugwa kwa aina yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa aina yake. Akaona kuwa ni vyema.

26Mungu akasema, “Na tumfanye mtu katika mfano wetu, wa kufanana na sisi. Wawe na mamlaka juu ya samaki wa bahari, juu ya ndege wa angani, juu ya wanyama wa kufuga, juu ya nchi yote, na juu ya kila kitu kitambaacho kinacho tambaa juu ya nchi.”27Mungu akamuumba mtu kwa mfano wake. Katika mfano wake alimuumba. Mwanaume na mwanamke aliwaumba.28Mungu akawabariki na akawaambia, “Zaeni na kuongezeka. Jazeni nchi, na muitawale. Muwe na mamlaka juu ya samaki wa baharini, juu ya ndege wa angani, na juu ya kila kiumbe hai kiendacho juu ya nchi,”29Mungu akasema, “Tazama, nimewapeni kila mmea uzaao mbegu ambao uko juu ya nchi, na kila mti wenye tunda ambalo lina mbegu ndani yake. Vitakuwa ni chakula kwenu.30Kwa kila mnyama wa nchi, kwa kila ndege wa angani, na kila kitambaacho juu ya nchi, na kila kiumbe ambacho kina pumzi ya uhai nimetoa kila mmea kwa ajili ya chakula.” Ikawa hivyo.31Mungu akaona kila kitu alichokiumba. Tazama, kikawa chema sana. Ikawa jioni na asubuhi siku ya sita.

2

1Kisha mbingu na nchi zilimalizika, na viumbe hai vyote vilivyo jaza mbingu na nchi.2Siku ya saba, Mungu alifikia mwisho wa kazi yake ambayo aliifanya, na kwa hiyo alipumzika siku ya saba kutoka kwenye kazi yake yote.3Mungu akaibarikia siku ya saba na akaitakasa, kwa sababu katika siku hiyo alipumzika kutoka kwenye kazi yake yote ambayo aliifanya katika uumbaji.4Haya yalikuwa ni matukio yahusuyo mbingu na nchi, wakati vilipoumbwa, katika siku ambayo Yahwe Mungu aliumba nchi na mbingu.5Hapakuwa na msitu wa shambani uliokuwa katika nchi, na hapakuwa na mmea wa shambani uliokuwa umechipuka, kwa kuwa Yahwe Mungu alikuwa hajasababisha mvua kunyesha juu ya nchi, na hapakuwa na mtu wa kulima ardhi.6Lakini ukungu uliinuka juu kutoka kwenye nchi na kuutia maji uso wote wa ardhi.7Yahwe Mungu aliumba mtu kutoka mavumbi ya ardhi, na akampulizia puani pumzi ya uhai, na mtu akawa kiumbe hai.8Yahwe Mungu aliotesha bustani upande wa mashariki, katika Edeni, na pale akamuweka mtu ambaye alimuumba.9Kutoka ardhini Yahwe Mungu alifanya kila mti uote ambao unapendeza na ni mzuri kwa chakula. Hii ni pamoja na mti wa uzima ambao ulikuwa katikati ya bustani, na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.

10Mto ukatoka nje ya Edeni kuitia maji bustani. Na kutoka pale ukagawanyika na kuwa mito minne.11Jina la ule wa kwanza ni Pishoni. Huu ni ule ambao unatiririka kupitia nchi yote ya Havila, ambapo kuna dhahabu.12Dhahabu ya inchi ile ni nzuri. Pia kuna bedola na jiwe shohamu.13Jina la mto wa pili ni Gihoni. Huu unatiririka kupitia nchi yote ya kushi.14Jina la mto wa tatu ni Hidekeli, ambao unatiririka mashariki mwa Ashuru. Mto wa nne ni Frati.

15Yahwe Mungu alimtwaa mtu na kumweka ndani ya bustani ya Edeni kuilima na kuitunza.16Yahwe Mungu alimuagiza mtu akisema, “Kutoka kwenye kila mti bustanini waweza kula kwa uhuru.17Lakini kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa kuwa siku utakayo kula kutoka katika mti huo, utakufa hakika.”

18Kisha Yahwe Mungu akasema, “Siyo jambo jema kwamba mtu huyu lazima awe pekeyake. Nitamfanyia msaidizi anaye mfaa.”19Kutoka ardhini Yahwe Mungu akafanya kila mnyama wa kondeni na kila ndege wa angani. Kisha akawaleta kwa mtu huyu aone angewapatia majina gani. Jina ambalo mtu huyu alimwita kila kiumbe hai, hili ndilo lilikuwa jina lake.20Mtu huyu akawapatia majina wanyama wote, ndege wote wa angani, na kila mnyama wa mwitu. Lakini kwa mtu mwenyewe hapakuwa na msaidizi wa kumfaa yeye.21Yahwe Mungu akaleta usingizi mzito kwa mtu huyu, kwa hiyo mtu huyu akalala. Yahwe Mungu akatwaa moja ya mbavu za mtu huyu na akapafunika pale alipo chukua ubavu.22Kwa ubavu ambao Yahwe Mungu alichukua toka kwa mtu huyu, akafanya mwanamke na akamleta kwa mtu huyu.23Mwanaume akasema, “Kwa sasa, huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu. Ataitwa ‘mwanamke,’ kwa sababu ametwaliwa katika mwanaume.”

24Kwa hiyo mwanaume atawaacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake, na watakuwa mwili mmoja.

25Wote wawili walikuwa uchi, mwanaume na mke wake, lakini hawakuona aibu.

3

1Sasa nyoka alikuwa mwerevu kuliko mnyama mwingine yeyote wa kondeni ambaye Yahwe Mungu alikuwa amemuumba. Akamwambia mwanamke, “Je ni kweli Mungu amesema, ‘Msile matunda kutoka kwenye mti wowote bustanini?’”2Mwanamke akamwambia nyoka, “Twaweza kula tunda kutoka kwenye miti ya bustani,3lakini kuhusu tunda la mti ambao uko katikati ya bustani, Mungu alisema, ‘Msile, wala msiuguse, vinginevyo mtakufa.’”4Nyoka akamwambia mwanamke, “Hakika hamtakufa.5Kwa sababu Mungu anajua kwamba siku mkila, macho yenu yatafumbuliwa, na mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.”6Na mwanamke alipoona kuwa mti ni mzuri kwa chakula, na kuwa unapendeza macho, na kwamba mti ulitamanika kwa kumfanya mtu awe mwerevu, alichukua sehemu ya tunda na akala. Na sehemu yake pia akampatia mumewe aliyekuwa naye, naye akala.7Macho ya wote wawili yalifumbuliwa, na wakajua kuwa wako uchi. Wakashona majani ya miti pamoja na wakatengeneza vya kujifunika wao wenyewe.

8Wakasikia sauti ya Yahwe Mungu akitembea bustanini majira ya kupoa kwa jua, kwa hiyo mwanaume na mke wake wakajificha wao wenyewe kwenye miti ya bustani kuepuka uwepo wa Yahwe Mungu.9Yahwe Mungu akamuita mwanaume na kumwambia, “Uko wapi?”10Mwanaume akasema, “Nilikusikia bustanini, na nikaogopa, kwa sababu nilikuwa uchi. Kwa hiyo nikajificha.”11Mungu akasema, “Ni nani alikwambia kuwa ulikuwa uchi? Je umekula kutoka mti ambao nilikuagiza usile matunda yake?”12Mwanaume akasema, “Mwanamke uliyenipa kuwa na mimi, alinipatia tunda kutoka kwenye mti, na nikala.”13Yahwe Mungu akamwambia mwanamke, “Nini hiki ulichofanya?” Mwanamke akasema, “Nyoka alinidanganya, na nikala.”14Yahwe Mungu akamwambia nyoka, “Kwa sababu umefanya jambo hili, umelaaniwa wewe mwenyewe miongoni mwa wanyama wote wa kufugwa na wanyama wote wa mwituni. Itakuwa, kwa tumbo lako utakwenda, na mavumbi utakula kwa siku zote za maisha yako.15Nitaweka uadui kati yako na mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake. Atakujeruhi kichwa chako na utamjeruhi kisigino chake.”16Kwa mwanamke akasema, “Nitaongeza uchungu wakati wa kuzaa watoto; itakuwa katika maumivu utazaa watoto. Tamaa yako itakua kwa mume wako, lakini atakutawala.”17Kwa Adam akasema, “Kwa sababu umesikiliza sauti ya mke wako, na umekula kutoka katika mti, ambao nilikuagiza, nikisema, ‘Usile matunda yake,’ ardhi imelaaniwa kwa sababu yako; kupitia kazi yenye maumivu utakula matunda ya ardhi kwa siku zote za maisha yako.18Ardhi itazaa miiba na mbigili kwa ajili yako, na utakula mimea ya shambani.19Kwa jasho la uso wako utakula mkate, mpaka utakapo irudia ardhi, ambayo kwayo ulitwaliwa. Kwa kuwa wewe ni mavumbi na kwenye mavumbi utarudi.”

20Mwanaume akaita mke wake jina Hawa, kwa sababu alikuwa mama wa wote wenye uhai.21Yahwe Mungu akatengeneza mavazi ya ngozi kwa ajili ya Adam na mke wake na akawavalisha.

22Yahwe Mungu akasema, “Sasa mtu huyu amekuwa kama mmoja wetu, ajuaye mema na mabaya. Kwa hiyo sasa hataruhusiwa kugusa kwa mkono wake, na kuchukua tunda la mti wa uzima, na kula akaishi tena milele.”23Kwa hiyo, Yahwe Mungu akamuondoa kutoka kwenye bustani ya Edeni, kwenda kulima ardhi ambayo kwa hiyo alikuwa ametwaliwa.24Kwa hiyo, Mungu akamfukuza mtu huyu nje ya bustani, na akaweka kerubi mashariki mwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto ulio geuka geuka kila upande, ili kulinda njia ya kwenda kwenye mti wa uzima.

4

1Mwanume akalala na Hawa mke wake. Akabeba mimba na akamzaa Kaini. Akasema, “Nimezaa mwanaume kwa msaada wa Yahwe.”

2Kisha akazaa ndugu yake Habili. Sasa Habili akawa mchungaji, lakini Kaini alilima udongo.3Ikawa kwamba baada ya muda Kaini alileta sehemu ya mazao ya ardhi kama sadaka kwa Yahwe.4Habili pia, alileta sehemu ya wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona. Yahwe akamkubali Habili pamoja na sadaka yake,5lakini Kaini pamoja na sadaka yake, Mungu hakuikubali. Kwa hiyo Kaini alikasirika sana, na uso wake ukakunjamana.6Yahwe akamwambia Kaini, “Kwa nini umekasirika na kwa nini uso wako umekunjamana?7Kama ukifanya vema, je hutapata kibali? Lakini kama hutafanya lilio jema, dhambi iko inakuotea mlangoni na inatamani kukutawala, lakini inakupasa uishinde.”

8Kaini akamwambia Habili ndugu yake. Hata wakati walipokuwa shambani, Kaini aliinuka dhidi ya Habili ndugu yake na akamuua. 1

9Kisha Yahwe akamuuliza Kaini, “Ndugu yako Habili yuko wapi?” Akasema, “Sijui. Je, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?”10Yahwe akasema, “Umefanya nini? Damu ya ndugu yako inaniita mimi kutokea ardhini.11Na sasa umelaaniwa wewe kutoka ardhi, ambayo imefungua kinywa chake kupokea damu ya ndugu yako, kutoka mikononi mwako.12Utakapo ilima ardhi, kuanzia sasa na kuendelea haita kuzalia wewe nguvu yake. Utakuwa mkimbizi na mtu asiye na makao duniani.”13Kaini akamwambia Yahwe, “Adhabu yangu ni kubwa kuliko uwezo wangu wa kustahimili.14Kwa hakika umenifukuza siku hii ya leo kutoka kwenye ardhi hii, na sitaonekana mbele ya uso wako. Nitakuwa mkimbizi na mtu nisiye na makao katika dunia, na yeyote atakaye niona ataniua.”15Yahwe akamwambia, “Ikiwa mtu yeyote atamuua Kaini, kisasi kitakuwa juu yake mara saba.” Kisha Yahwe akaweka alama juu ya Kaini, ili kwamba kama mtu yeyote akimuona, mtu huyo asimshambulie.16Kwa hiyo Kaini akatoka mbele ya uwepo wa Yahwe na akaishi katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni.

17Kaini akamjua mke wake na akapata mimba. Akamzaa Henoko. Akajenga mji na akauita kwa jina la mwanae Henoko.18Kwa Henoko akazaliwa Iradi. Iradi akamzaa Mehuyaeli. Mehuyaeli akamzaa Methushaeli. Methushaeli akamzaa Lameki.19Lameki akajitwalia wake wawili: jina la mmoja alikuwa Ada, na jina la yule mwingine alikuwa Sila.20Ada akamzaa Yabali. Huyu ndiye alikuwa baba yao na wale walioishi hemani ambao wanafuga wanyama.21Ndugu yake aliitwa Yubali. Huyu alikuwa baba yao na wale wapigao kinubi na filimbi.22Sila naye akamzaa Tubal Kaini, mfua vyombo vya shaba na chuma. Dada yake na Tubal Kaini alikuwa Naama.

23Lameki akawaambia wake zake, Ada na Sila, “Sikieni sauti yangu; ninyi wake wa Lameki, sikilizeni nisemacho. Kwa kuwa nimemuua mtu kwa kunijeruhi, kijana kwa kunichubua.24Ikiwa Kaini atalipiwa kisasi mara saba, ndipo Lameki atalipiwa kisasi mara sabini na saba.”

25Adam akamjua mke wake tena, na akazaa mtoto mwanaume. Akamuita jina lake Sethi na akasema, “Mungu amenipatia mtoto mwingine wa kiume kwa nafasi ya Habili, kwa kuwa Kaini alimuuwa.”26Mtoto wa kiume alizaliwa kwa Sethi na akamuita jina lake Enoshi. Wakati huo watu walianza kuliitia jina la Yahwe.


1Katika tafsiri za kale zinasema, Kaini alimwambia Habili ndugu yake, “Twende mashambani.” Na wakati walipokuwa shambani, Kaini alimuinukia Habili ndugu yake na kumuua.

5

1Hii ni orodha ya vizazi vya Adamu. Katika siku ambayo Mungu alimuumba mtu, aliwaumba katika mfano wake mwenyewe.2Mwanaume na mwanamke aliwaumba. Akawabariki na akawaita Adam wakati walipoumbwa.3Wakati Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, akamzaa mwana katika sura yake mwenyewe, kwa mfano wake, na akamuita jina lake Sethi.4Baada ya Adamu kumzaa Sethi, aliishi miaka 800. Akawazaa wana wengi waume na wake.5Adamu akaishi miaka 930 kisha akafariki.6Wakati Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.7Baada ya kumzaa Enoshi, akaishi miaka 807 na akawazaa wana wengi waume na wake.8Sethi akaishi miaka 912 kisha akafariki.9Wakati Enoshi alipokuwa ameishi miaka 90, akamzaa Kenani.10Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815. Akazaa wana wengi wa ume na wake.11Enoshi aliishi miaka 905 na kisha akafariki.12Wakati Kanani alipokuwa ameishi miaka 70, akamzaa Mahalaleli.13Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.14Kenani aliishi miaka 910, na kisha akafariki.15Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka 65, alimzaa Yaredi.16Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830. Akazaa wana wengi wa ume na wake.17Mahalaleli aliishi miaka 895 na kisha akafariki.18Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, alimzaa Henoko.19Baada ya kumzaa Henoko, Yaredi aliishi miaka 800. Akazaa wana wengi waume na wake.20Yaredi aliishi miaka 962 na kisha akafariki.21Henoko alipokuwa ameishi miaka 65, akamzaa Methusela.22Henoko akaenenda na Mungu miaka 300 baada ya kumzaa Methusela. Aliwazaa wana wengi wa ume na wake.23Henoko aliishi miaka 365.24Henoko alienenda na Mungu, na kisha alitoweka, kwa kuwa Mungu alimtwaa.25Wakati Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, alimzaa Lameki.26Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782. Akawazaa wana wengi wa ume na wake.27Methusela aliishi miaka 969. Kisha akafariki.28Wakati Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.29Akamuita jina lake Nuhu, akisema, “Huyu ndiye atatupatia pumziko kutoka katika kazi yetu na kutoka katika kazi ya taabu ya mikono yetu, ambayo lazima tuifanye kwa sababu ya ardhi ambayo Yahwe ameilaani.”30Lameki aliishi miaka 595 baada ya kumzaa baba wa Nuhu. Akazaa wana wengi wa ume na wake.31Lameki aliishi miaka 777. Kisha akafariki.32Baada ya Nuhu kuishi miaka 500, akamzaa Shemu, Hamu, na Yafethi.

6

1Ikawa wakati watu walipoanza kuongezeka juu ya uso wa nchi na wana wa kike wakazaliwa kwao,2wana wa Mungu walipoona kuwa mabinti wa wanadamu ni wenye kuvutia, waliwachukua kuwa wake zao, kila waliye mchagua.3Yahwe akasema, “Roho yangu haitasalia kwa mwanadamu milele, kwa kuwa wao ni nyama. Wataishi miaka 120.”

4Majitu makubwa yalikuwa juu ya uso wa nchi nyakati hizo, na hata baada ya hapo. Hii ilitokea wakati wana wa Mungu walipowao mabinti za wanadamu, na kupata watoto pamoja nao. Hawa walikuwa watu hodari zamani, watu wenye sifa.

5Yahwe akaona kwamba uovu wa watu umezidi katika nchi, na kwamba mawazo ya mioyo yao daima yanaelekea tu katika uovu.6Yahwe akajuta kuwa amemuumba mwanadamu juu ya nchi, na ikamhuzunisha moyo wake.7Kwa hiyo Yahwe akasema, “Nitamfutilia mbali mwanadamu ambaye nimemuumba katika uso wa nchi; mwanadamu na wanyama wakubwa, na vitambaavyo na ndege wa angani, kwa kuwa nimehuzunika kuwa nimeviumba.”

8Lakini Nuhu akapata neema ya upendeleo machoni pa Yahwe.9Kulikuwa na matukio kumhusu Nuhu. Nuhu alikuwa mtu mwenye haki, na asiye na lawama miongoni mwa watu wa kipindi chake. Nuhu alitembea na Mungu.10Nuhu akafanyika baba wa wana watatu wa kiume: Shemu, Hamu na Yafethi.

11Nchi iliharibika mbele za Mungu, na ikajaa ghasia.12Mungu akaiona nchi; tazama, ilikuwa imeharibika, kwa kuwa wote wenye mwili walikuwa wameharibu njia zao juu ya nchi.13Mungu akamwambia Nuhu, “Nimeona kuwa sasa ni wakati wa mwisho kwa wote wenye mwili, kwa kuwa nchi imejaa ghasia kutokana na wao. Hakika, nitawaharibu wao pamoja na nchi.14Tengeneza safina ya mti wa mvinje kwa ajili yako. Tengeneza vyumba katika safina, na vifunike kwa lami ndani na nje.15Hivi ndivyo utakavyofanya: urefu wa safina dhiraa miatatu, upana wake dhiraa hamsini, kwenda juu kwake dhiraa thelathini.16Tengeneza paa la safina, na ulimalize kwa kipimo cha dhiraa kutoka juu ubavuni. Weka mlango katika ubavu wa safina na utengeneze dari ya chini, ya pili na ya tatu.17Sikiliza, nimekaribia kuleta gharika ya maji juu ya nchi, kuharibu wenye mwili wote wakaao ndani ya nchi wenye pumzi ya uhai chini ya mbingu. Kila kitu kilichopo juu ya nchi kitakufa.18Lakini nitalifanya thabiti agano langu na wewe. Utaingia ndani ya safina, wewe, na wana wako wa kiume, na mke wako, pamoja na wake za wanao.19Kwa kila kiumbe hai chenye mwili, viwili vya kila aina utavileta ndani ya safina, ili visalie hai pamoja nawe, vya kike na vya kiume.20Katika ndege kwa jinsi yake, na wanyama wakubwa kwa jinsi yake, kila kitambaacho ardhini kwa jinsi yake, viwili viwili vya kila aina vitakuja kwako ili viwe salama.21Kusanya kila aina ya chakula kinacholiwa kwa ajili yako na ukitunze, ili kwamba viwe chakula chako na chao.”22Kwa hiyo, Nuhu akafanya hivyo kulingana na yote ambayo Mungu alimuagiza, ndivyo alifanya.

7

1Yahwe akamwambia Nuhu, “Njoo, wewe na nyumba yako wote, katika safina, kwa kuwa nimeona kuwa wewe ni mwenye haki mbele yangu katika kizazi hiki.2Kwa kila mnyama aliye safi utakuja nao saba wa kiume na saba wa kike. Na kwa wanyama wasio safi, walete wawili wawili, wa kiume na wa kike.3Pia na kwa ndege wa angani, walete saba wa kiume na saba wa kike, ili kuhifadhi kizazi chao juu ya uso wa nchi yote.4Kwa kuwa ndani ya siku saba nitasababisha mvua kunyesha juu ya nchi muda wa siku arobaini mchana na usiku. Nitaharibu kila kiumbe hai nilichokiumba juu ya uso wa ardhi.”

5Nuhu alifanya yote ambayo Yahwe alimuagiza.6Nuhu alikuwa na umri wa miaka 600 wakati gharika ilipokuja juu ya nchi.7Nuhu, watoto wake wa kiume, mke wake, na wake za watoto wake waliingia katika safina pamoja kwa sababu ya maji ya gharika.8Wanyama ambao ni safi na wanyama ambao si safi, ndege, na kila kitambaacho juu ya ardhi,9wawili wawili, mume na mke wakaja kwa Nuhu na wakaingia katika safina, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza Nuhu.10Ikawa kwamba baada ya siku saba, maji ya gharika yakaja juu ya nchi.11Katika mwaka wa 600 wa maisha yake Nuhu, katika mwezi wa pili, katika siku ya kumi na saba ya mwezi, katika siku iyo hiyo, chemchemi zote za vilindi vikuu zilipasuka na kufunguka, na madirisha ya mbinguni yakafunguka.12Mvua ikaanza kunyesha juu ya nchi kwa siku arobaini mchana na usiku.13Katika siku iyo hiyo Nuhu pamoja na watoto wake, Shem, Ham, na Yafethi na mke wa Nuhu, na wale wake watatu wa wana wa Nuhu pamoja waliingia katika safina.14Waliingia pamoja na kila mnyama wa mwitu kwa jinsi yake, na kila mnyama wa kufugwa kwa jinsi yake, na kila kitambaacho juu ya ardhi kwa jinsi yake, na kila aina ya ndege kwa jinsi yake, kila aina ya kiumbe chenye mabawa.15Viwili viwili katika kila chenye mwili ambacho kilikuwa na pumzi ya uhai kilikuja kwa Nuhu na kuingia katika safina.16Wanyama walioingia ndani walikuwa wa kiume na kike katika wote wenye mwili; wakaingia kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza. Kisha Yahwe akawafungia mlango.

17Kisha gharika ikaja juu ya nchi kwa siku arobaini, na maji yakaongezeka na kuinua safina juu ya nchi.18Maji yakafunika kabisa nchi, na safina ikaelea juu ya uso wa maji.19Maji yakaongezeka zaidi juu ya nchi kiasi kwamba milima yote mirefu ambayo ilikuwa chini ya anga ikafunikwa.20Maji yakaongezeka dhiraa kumi na tano juu ya vilele vya milima.21Vitu vyote vyenye uhai ambavyo vilitembea juu ya nchi vilikufa: ndege, mifugo, wanyama wa mwituni, viumbe hai vyote kwa wingi vilivyoishi juu ya nchi, pamoja na watu.22Viumbe hai vyote ambavyo vilikaa juu ya ardhi, vilivyo pumua pumzi ya uhai kwa njia ya pua, vilikufa.23Hivyo kila kilichokuwa hai ambacho kilikuwa juu ya uso wa nchi kilifutwa, kuanzia watu mpaka wanyama wakubwa, mpaka vitambaavyo, na mpaka ndege wa angani. Vyote viliangamizwa kutoka kwenye nchi. Nuhu tu pamoja na wale waliokuwa naye kwenye safina ndio walisalia.24Maji hayakuzama chini ya nchi kwa muda wa siku 150.

8

1Mungu akamtazama Nuhu, wanyama wote wa mwitu, na wanyama wote wa kufugwa ambao walikuwa pamoja naye kwenye safina. Mungu akafanya upepo uvume juu ya nchi, na maji yakaanza kuzama chini.2Chemichemi za vilindi pamoja na madirisha ya mbingu vikafungwa, na mvua ikakoma kunyesha.3Maji ya gharika yakaanza kuzama kidogo kidogo katika nchi na mwisho wa siku 150 maji yakawa yamezama chini.4Safina ikatulia katika mwezi wa saba, siku ya kumi na saba ya mwezi, juu ya milima ya Ararati.5Maji yakaendelea kuzama chini hadi mwezi wa kumi. Siku ya kwanza ya mwezi, vilele vya milima vikaonekana.6Ikatokea kwamba baada ya siku arobaini Nuhu alifungua dirisha la safina ambayo aliitengeneza.7Akatuma kunguru na akaruka hadi maji yalipo kauka katika nchi.8Kisha akatuma njiwa kuona kama maji yamezama chini kutoka kwenye uso wa nchi,9lakini njiwa hakuona sehemu ya kutua unyayo wake, na akarudi kwake ndani ya safina, kwa kuwa maji yalikuwa bado yamefunika nchi yote. Akanyoosha mkono wake, akamchukua na kumuweka ndani ya safina pamoja naye.10Akasubiri siku saba zingine akatuma tena njiwa kutoka kwenye safina.11Njiwa akarudi kwake jioni. Tazama! Katika mdomo wake kulikuwa na jani bichi la mzeituni lililochumwa. Kwa hiyo Nuhu akatambua kuwa maji yamekwisha zama chini ya nchi.12Akasubiri siku saba zingine na akamtuma njiwa tena. Njiwa hakurudi kwake tena.

13Ikawa kwamba katika mwaka wa 601, katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, maji yalikuwa yamekauka katika nchi. Nuhu akaondoa kifuniko cha safina, akatazama nje, na akaona kwamba, uso wa nchi ulikuwa umekauka.14Katika mwezi wa pili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, nchi ilikuwa imekauka.15Mungu akamwambia Nuhu,16“Toka nje ya safina, wewe, mke wako, wanao wa kiume, na wake wa wanao pamoja nawe.17Wachukuwe utoke nje pamoja nao kila kiumbe hai chenye mwili ambacho kiko nawe - ndege, wanyama wa kufugwa, na kila kitambaacho ambacho hutambaa juu ya nchi - ili kwamba viweze kukua na kuwa na idadi kubwa zaidi ya viumbe hai katika nchi yote, kwa kuzaliana na kuongezeka juu ya nchi.”18Kwa hiyo Nuhu akatoka nje pamoja na watoto wake wa kiume, mke wake, na wake wa wanawe pamoja naye.19Kila kiumbe hai, kila kitambaacho, na kila ndege, na kila kiendacho juu ya nchi, kwa kabila zao, wakaiacha safina.

20Nuhu akajenga madhabahu kwa Yahwe. Akachukua baadhi ya wanyama walio safi na baadhi ya ndege walio safi, na kutoa sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu.21Yahwe akanusa harufu nzuri ya kuridhisha na akasema moyoni mwake, “Sita laani tena ardhi kwa sababu ya mwanadamu, ingawa nia za mioyo yao ni mbaya tokea utoto. Wala sita haribu kila kitu chenye uhai, kama nilivyo fanya.22Wakati nchi isaliapo, majira ya kupanda mbegu na mavuno, baridi na joto, kiangazi na majira ya baridi, mchana na usiku havitakoma.”

9

1Kisha Mungu akambariki Nuhu na wanawe, na kuwaambia, “Zaeni, mkaongezeke, na muijaze nchi.2Hofu na utisho wenu vitakuwa juu ya kila mnyama aliye hai juu ya nchi, juu ya kila ndege wa angani, juu ya kila kitu kiendacho chini juu ya ardhi, na juu ya samaki wote wa baharini. Vimetolewa katika mikono yenu.3Kila kitu kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula kwa ajili yenu. Kama nilivyo wapa mimea, sasa nawapa kila kitu.4Lakini msile nyama pamoja na uhai wake - yaani damu yake - ndani yake.5Lakini kwa ajili ya damu yenu, uhai uliomo katika damu yenu nitataka malipo. Kutoka katika mkono wa kila mnyama nitaitaka. Kutoka katika mkono wa kila mtu, yaani, kutoka katika mkono wa yule ambaye amemuua ndugu yake, nitataka fidia kwa ajili ya uhai wa mtu huyo.6Yeyote amwagaye damu ya mtu, kwa njia ya mtu damu yake itamwagwa, kwa sababu ilikuwa ni katika mfano wa Mungu kwamba Mungu alimuumba mtu.

7Na hivyo nanyi zaeni na kuongezeka, sambaeni katika nchi yote na muongezeke juu yake.”

8Kisha Mungu akazungumza na Nuhu na wanae pamoja naye, akisema,9“Kwa ajili yangu, sikiliza! Ninakwenda kulithibitisha agano langu pamoja nawe na uzao wenu baada yenu,10na kwa kila kiumbe hai kilicho pamoja nawe, pamoja na ndege, mnyama wa kufugwa, na kila kiumbe cha nchi pamoja nawe, kuanzia kwa wote waliotoka kwenye safina, mpaka kwa kila kiumbe hai juu ya nchi.11Kwa sababu hii ninalithibitisha agano langu pamoja nanyi, kwamba hapatatokea kuangamizwa kwa mwenye mwili kwa njia ya maji ya gharika. Tena hapatatokea gharika ya kuangamiza nchi.”

12Mungu akasema, “Na hii ndiyo ishara ya agano ambalo ninafanya kati yangu na ninyi pamoja na kila kiumbe hai kilicho pamoja nanyi, kwa vizazi vyote vya baadaye:13Nimeweka upinde wangu wa mvua katika wingu, na itakuwa ndiyo ishara ya agano kati yangu na nchi.14Hata itakuwa nitakapoleta wingu juu ya nchi na upinde wa mvua ukaonekana katika wingu,15ndipo nitakumbuka agano langu, ambalo ni kati yangu na ninyi na kila kiumbe hai cha wote mwenye mwili. Maji hayatafanyika tena gharika kuharibu wote wenye mwili.16Upinde wa mvua utakuwa katika mawingu na nitauona, ili kukumbuka agano la milele kati ya Mungu na kila kiumbe hai cha wote wenye mwili ambacho kiko juu ya nchi.”

17Kisha Mungu akamwambia Nuhu, “Hii ni ishara ya agano ambalo nimelithibitisha kati yangu na wenye mwili wote ambao wako juu ya nchi.”

18Wana wa Nuhu ambao walitoka katika safina walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi. Na Hamu akamzaa Kanaani.19Watatu hawa walikuwa ndio wana wa Nuhu, na kutokea kwa hawa nchi yote ikajaa watu.

20Nuhu akaanza kuwa mkulima, na akapanda mizabibu.21Akanywa sehemu ya divai na akalewa. Akawa amelala hemeani uchi.22Kisha Hamu, baba yake Kanaani, akaona uchi wa baba yake na akawaambia ndugu zake wawili waliokuwa nje.23Kwa hiyo Shemu na Yafethi wakachukua kanzu wakaitanda juu ya mabega yao, na wakatembea kinyumenyume na wakaufunika uchi wa baba yao. Nyuso zao zikiwa zimegeuka nyuma upande mwingine, kwa hiyo hawakuona uchi wa baba yao.24Nuhu alipozinduka kutoka katika ulevi wake, alijua ni jambo gani mtoto wake mdogo amemfanyia.25Hivyo akasema, “Alaaniwe Kanaani. Na awe mtumishi kwa watumishi wa ndugu zake.”
26Akasema pia, “Yahwe, Mungu wa Shemu, abarikiwe, Kanaani na awe mtumwa wake.
27Mungu na apanue mipaka ya Yafethi, na afanye makazi yake katika hema za Shemu. Kanaani na awe mtumwa wake.”

28Baada ya gharika, Nuhu aliishi miaka 350.29Siku zote za Nuhu zilikuwa ni miaka 950, na kisha akafa.

10

1Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya wana wa Nuhu, ambao ni, Shemu, Hamu, na Yafethi. Wana wa kiume walizaliwa kwao baada ya gharika.2Wana wa Yafethi walikuwa Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Masheki, na Tirasi.3Na wana wa Gomeri walikuwa Ashikenazi, Rifathi na Togama.4Wana wa Yavani walikuwa Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Dodanimu.5Kutoka kwa hawa watu wa pwani waligawanyika na kwenda kwenye ardhi zao, kila mtu na lugha yake, kufuatana na koo zao, kwa mataifa yao.6Wana wa Hamu walikuwa Kushi, Misraimu, Putu, na Kanaani.

7Wana wa Kushi walikuwa Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa Sheba na Dedani.

8Kushi akamzaa Nimrodi, ambaye alikuwa hodari wa kwanza juu ya nchi.9Alikuwa mwindaji mkuu mbele ya Yahwe. Hii ndiyo sababu hunenwa, “Kama Nimrod mwindaji mkuu mbele za Yahwe.”10Miji ya kwanza ya ufalme wake ilikuwa Babeli, Ereku, Akadi na Kalne, katika nchi ya Shinari.11Kutoka katika nchi ile, alienda Ashuru na akajenga Ninawi, Rehoboth- iri na Kala,12na Raseni ambao ulikuwa kati ya Ninawi na Kala. Ulikuwa mji mkubwa.

13Misraimu akazaa Waludi, Waanami, Walehabi, na Wanaftuhi,14Wapathrusi na Wakasluhi (ambao kwao Wafilisti walitokea), na Wakaftori.

15Kanaani akamzaa Sidono, mwanawe wa kwanza, na Hethi,16pia na Myebusi, na Mwamori, Mgirgashi,17Mhivi, Mwarki, Msini,18Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi. Baadaye koo za wakanaani zikasambaa.19Mpaka wa Wakanaani ulianzia Sidoni, katika mwelekeo wa Gerari, hata Gaza, na kama kuelekea Sodoma, Gomora, Adma, na Seboimu hata Lasha.

20Hawa walikuwa wana wa Hamu, kwa koo zao, kwa lugha zao, katika ardhi zao na katika mataifa yao.

21Pia walizaliwa wana kwa Shemu, ndugu yake mkubwa wa Yafethi. Shemu pia alikuwa baba yao na watu wote wa Eberi.22Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Alfaksadi, Ludi, na Aramu.23Wana wa Aramu walikuwa ni Usi, Huli, Getheri, na Mashi.24Arfaksadi akamzaa Sela, na Sela akamzaa Eber.25Eberi akazaa wana wawili wa kiume. Jina la mmoja aliitwa Pelegi, maana katika siku zake nchi iligawanyika. Jina la ndugu yake aliitwa Yoktani.26Yoktani akamzaa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,27Hadoram, Uzali, Dikla,28Obali, Abimaeli, Sheba,29Ofiri, Havila, na Yobabi. Hawa wote walikuwa wana wa Yoktani.30Mpaka wao ulikuwa unaanzia Mesha, hadi Sefari, mlima wa mashariki.31Hawa walikuwa wana wa Shemu, kulingana na koo zao na lugha zao, katika ardhi zao kulingana na mataifa yao.

32Hizi zilikuwa koo za wana wa Nuhu, kulingana na vizazi vyao, kwa mataifa yao. Kutokea kwa hawa mataifa yaligawanyika na kwenda juu ya nchi baada ya gharika.

11

1Sasa nchi yote ilikuwa inatumia lugha moja na ilikua na usemi mmoja.2Ikawa waliposafiri upande wa mashariki, wakaona eneo tambarare katika nchi ya Shinari na wakakaa pale.3Wakasemezana, “Haya njoni, tufanye matofari na tuyachome kikamilifu.” Walikuwa na matofari badala ya mawe na lami kama chokaa.4Wakasema, “Njooni, na tujenge mji sisi wenyewe na mnara ambao kilele chake kitafika angani, na tujifanyie jina. Kama hatutafanya, basi tutatawanyika katika uso wa nchi yote.”

5Kwa hiyo Yahwe akashuka kuona mji na mnara ambao wazao wa Ibrahimu walikuwa wamejenga.6Yahwe akasema, “Tazama, watu hawa ni taifa moja na lugha moja, na wameanza kufanya hivi! Karibuni, halitashindikana jambo watakalo kusudia kulifanya.7Njooni, tushuke na tuvuruge lugha yao pale, ili kwamba wasielewane.”

8Kwa hiyo Yahwe akawatawanya kutoka pale kwenda pande zote za uso wa nchi na wakaacha kujenga mji.9Kwa hiyo, jina lake ukaitwa Babeli, kwa sababu hapo Yahwe alivuruga lugha ya nchi yote na tangu pale Yahwe akawatawanya ng'ambo juu ya uso wa nchi yote.

10Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Shemu. Shemu alikuwa na umri wa 100, na akamzaa Alfaksadi miaka miwili baada ya gharika.11Shemu akaishi miaka 500 baada ya kumzaa Alfaksadi. Pia akazaa wana wengine wa kiume na wa kike.

12Wakati Alfaksadi alipokuwa ameishi miaka 35 akamzaa Shela.13Alfaksadi aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Shela. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

14Wakati Shela alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Eberi.15Shela aliishi miaka 403 baada ya kumzaa Eberi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

16Wakati Eberi alipokuwa ameishi miaka 34, akamzaa Pelegi.17Eberi aliishi miaka 430 baada ya kumzaa Pelegi. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

18Wakati Pelegi alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Reu.19Pelegi aliishi miaka 209 baada ya kumzaa Reu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

20Wakati Reu alipokuwa ameishi miaka 32, alimzaa Serugi.21Reu aliishi miaka 207 baada ya kumzaa Seregu. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

22Wakati Seregu alipokuwa ameishi miaka 30, akamzaa Nahori.23Seregu aliishi miaka 200 baada ya kumzaa Nahori. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

24Wakati Nahori alipokuwa ameishi miaka 29, akamzaa Tera.25Nahori aliishi mika 119 baada ya kumzaa Tera. Akawazaa pia wana wengine wa kiume na wa kike.

26Baada ya Tera kuishi miaka 70, akamzaa Abram, Nahori, na Haran.

27Hivi ndivyo vilikuwa vizazi vya Tera. Tera aliwazaa Abram, Nahori, na Harani, na Harani akamzaa Lutu.28Harani akafa machoni pa baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, katika Ur wa Wakaldayo.29Abram na Nahori wakajitwalia wake. Mke wa Abram aliitwa Sarai na mke wa Nahori aliitwa Milka, binti wa Harani, aliyekuwa baba wa Milka na Iska.30Sasa Sarai alikuwa tasa; hakuwa na mtoto.

31Tera akamtwaa Abram mwanawe, Lutu mwana wa mwanawe Harani, na Sarai mkwewe, mke wa mwanawe Abram, na kwa pamoja wakatoka Ur wa Wakaldayo, kwenda katika nchi ya Kanaani. Lakini walipofika Harani wakakaa pale.32Tera akaishi miaka 205 kisha akafa hapao Harani.

12

1Kisha Yahwe akamwambia Abram, “Nenda utoke katika nchi yako, na toka kwa ndugu zako, na kwa jamaa za baba yako, uende katika nchi nitakayo kuonyesha.2Nitakufanya uwe taifa kubwa, na nitakubariki na kulifanya jina lako kuwa kubwa, na utafanyika baraka.3Nitawabariki wakubarikio, lakini asiye kuheshimu nita mlaani. Kupitia kwako familia zote za nchi zitabarikiwa.”

4Kwa hiyo Abram akaondoka kama vile Yahwe alivyo mwambia kufanya, na Lutu akaenda pamoja naye. Abram alikuwa na miaka 75 wakati alipotoka Harani.5Abram akamchukua Sarai mkewe, Lutu, mtoto wa ndugu yake, na vyote walivyomiliki ambavyo wamevikusanya, na watu ambao wamewapata wakiwa huko Harani. Wakatoka kwenda katika nchi ya Kanaani, wakafika nchi ya Kanaani.6Abram akapitia katikati ya nchi hadi Shekemu, hadi mwaloni wa More. Wakati huo wakanaani waliishi katika nchi hiyo.

7Yahwe akamtokea Abram, na kusema, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Kwa hiyo Abram akamjengea madhabahu, Yahwe ambaye alimtokea.8Kutoka pale akaenda kwenye nchi ya mlima mashariki mwa Betheli, ambapo alipiga hema yake, magaribi kukiwa na Betheli na mashariki kukiwa na mji wa Ai. Akajenga madhabahu ya Yahwe pale na kuliitia jina la Yahwe.9Kisha Abram akaendelea kusafiri, akielekea upande wa Negebu.

10Kulikuwa na njaa katika nchi, kwa hiyo Abram akaenda kukaa Misri, kwa kuwa njaa ilikua kali katika nchi.11Wakati alipokaribia kuingia Misri, akamwambia Sarai mkewe, “Tazama, najua kuwa wewe ni mwanamke mzuri.12Wamisri watakapokuona watasema, huyu ni mke wake, na wataniua mimi, lakini watakuacha wewe hai.13Hivyo wewe sema kuwa ni dada yangu, ili kwamba niwe salama kwa sababu yako, na kumbe maisha yangu yatasalimika kwa sababu yako.”

14Ikawa kwamba Abram alipoingia Misri, Wamisri wakaona kwamba Sarai ni mzuri sana.15Wakuu wa Farao wakamuona, na kumsifia kwa Farao, na huyu mwanamke akachukuliwa kupelekwa nyumbani mwa Farao.16Farao akamtendea kwa wema Abram kwa ajili yake, na akampatia kondoo, maksai, punda waume watumishi wa kiume, watumishi wa kike, punda wake, na ngamia.17Kisha Yahwe akampiga Farao na nyumba yake kwa mapigo makuu kwa sababau ya Sarai, mke wa Abram.18Farao akamwita Abram na kusema, “Nini hiki ambacho umenifanyia? Kwa nini hukuniambia kuwa alikuwa mke wako?19Kwa nini ulisema, ‘Ni dada yangu’; na mimi nikamchukua kuwa mke wangu? Sasa kwa sababu hiyo huyu hapa mke wako. Mchukue na uende zako.”20Kisha Farao akatoa amri kwa watu wake kuhusiana naye, na wakamuondoa, yeye pamoja na mke wake na vyote alivyokuwa navyo.

13

1Kwa hiyo, Abram akaondoka akatoka Misri na akaenda Negebu, yeye, mke wake, na vyote alivyokuwa navyo. Lutu pia akaenda pamoja naye.2Na sasa Abram alikuwa tajiri wa mifugo, fedha na dhahabu.3Aliendelea na safari yake kutoka Negebu hadi Betheli, mahali ambapo hema yake ilikuwa tangu mwanzo, kati ya Betheli na mji wa Ai.4Akaenda mahali ambapo madhabahu ilikuwa imejengwa mwanzoni. Hapa akaliitia jina la Yahwe.5Lutu, aliyekuwa anasafiri na Abram, alikuwa pia na ngo'mbe, makundi ya mifugo, na mahema.6Nchi haikuwatosha wote kukaa pamoja karibu kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana, kiasi kwamba hawakuweza kukaa pamoja.7Pia, kulikuwa na ugomvi kati ya wachunga wanyama wa Abram na wachunga wanyama wa Lutu. Wakanaani pamoja na Waperizi walikuwa wakiishi katika nchi ile wakati huo.8Kwa hiyo Abram akamwambia Lutu, “Pasiwe na ugomvi kati yako na mimi, na kati ya wachunga wanyama wako na wachunga wanyama wangu; licha ya hayo sisi ni familia.9Je nchi hii yote haiko mbele yako? Nenda na ujitenge nami. Ikiwa utakwenda kushoto, mimi nitakwenda kulia, au ikiwa utakwenda kulia, mimi nitakwenda kushoto.”10Kwa hiyo Lutu akatazama, na akaona kuwa nchi yote tambarare ya Yorodani ilikuwa na maji kila mahali hadi Zoari, kama vile bustani ya Yahwe, na kama nchi ya Misri. Hii ilikuwa ni kabla Yahwe hajaiangamiza Sodoma na Gomora.11Kwa hiyo Lutu akajichagulia yeye mwenyewe nchi tambarare ya Yorodani na akasafiri mashariki, na ndugu hawa wakatengana wao kwa wao.12Abram akaishi katika nchi ya Kanaani, na Lutu akaishi katika miji ya tambarare. Akatandaza hema zake hadi Sodoma.13Na sasa watu wa Sodoma walikuwa waovu na wenye dhambi nyingi dhidi ya Yahwe.

14Yahwe akamwambia Abram baada ya Lutu kuondoka kwake, “Angalia kuanzia mahali ulipo simama hadi kaskazini, kusini, mashariki, na magharibi.15Nchi yote hii uionayo, nitakupatia wewe pamoja na uzao wako milele.16Nitawafanya uzao wako kuwa wengi kama mavumbi ya nchi, kiasi kwamba kama kuna mtu anaweza kuhesabu mavumbi ya nchi, ndipo na uzao wako pia utahesabika.17Inuka, tembea katika urefu na upana wa nchi hii, kwa kuwa nitakupatia.”18Kwa hiyo Abram akachukua hema yake, akaja na kukaa katika mwaloni wa Mamre, ambao uko Hebroni, na pale akajenga Madhabahu ya Yahwe.

14

1Ikiwa katika siku za Amrafeli, mfalme wa shinari, Arioko, mfalme wa Elasari, Kedorlaoma, mfalme wa Elam na Tidali, mfalme wa Goimu,2walifanya vita dhidi ya Bera mfalme wa Sodoma, Birsha, mfalme wa Gomora, Shinabu, mfalme wa Adma, Shemeberi, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari).3Hawa wafalme watano wa mwisho waliungana pamoja katika bonde la Sidim (pia likiitwa bahari ya chumvi).4Kwa miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, lakini katika mwaka wa kumi na tatu waliasi.5Kisha katika mwaka wa kumi na nne, Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye walikuja na kuwashambulia Warefai katika Ashteroth Karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, Waemi katika Shawe Kiriathaimu,6na Wahori katika mlima wao wa Seiri, mpaka El Parani iliyo karibu na jangwa.7Kisha wakarudi wakaja En Misifati (Pia ikiitwa Kadeshi), na kuishinda nchi yote ya Waamaleki, na pia Waamori ambao waliishi Hasasoni Tamari.

8Kisha mfalme wa Sodoma, mfalme wa Gomora, mfalme wa Adma, mfalme wa Seboim, na mfalme wa Bela (pia ikiitwa Soari) walikwenda na kuandaa vita9dhidi ya Kadorlaoma, mfalme wa Elam, Tidali mfalme wa Goim, Amrafeli, mfalme wa Shinari, Arioki, mfalme wa Elasari; wafalme wanne dhidi ya wale watano.10Na sasa bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami, na wafalme wa Sodoma na Gomora walipokimbia, wakaanguka pale. Wale waliosalia wakakimbilia milimani.11Kwa hiyo adui akachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, na wakaenda zao.12Walipoondoka, wakamchukua pia Lutu, mtoto wa ndugu yake Abram ambaye aliishi Sodoma, pamoja na mali zake zote.13Mmoja ambaye alitoroka alikuja na kumwambia Abram mwebrania. Alikuwa anaishi katika mialoni ya Mamre, mwamori ambaye alikuwa ni ndugu wa Eshkoli na Aneri ambao walikuwa washirika wa Abram.14Abram aliposikia kuwa maadui wamemteka ndugu yake, akawaongoza wanaume waliofunzwa na kuzaliwa nyumbani mwake 318 na akawaongoza hadi Dani.15Akawagawanya watu wake dhidi yao usiku na kuwavamia, na kuwafukuza mpaka Hoba, ambayo iko kaskazini mwa Dameski.16Kisha akarudisha mali zote, pia akamrudisha ndugu yake Lutu na mali zake, pamoja na wanawake na watu wengine.

17Baada ya Abram kurudi kutoka kumpiga Kadorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka kuonana naye katika bonde la Shawe (pia iliitwa bonde la mfalme).18Melkizedeki, mfalme wa Salem, akaleta mkate na divai. Alikuwa ni kuhani wa Mungu aliye juu sana.19Alimbariki akisema, “Abarikiwe Abram na Mungu aliye juu sana, muumba wa mbingu na nchi.20Abarikiwe Mungu aliye juu sana, ambaye amekupatia adui zako katika mikono yako.” Kisha Abram akampatia sehemu ya kumi ya kila kitu.21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abram, “Nipatie watu, na ujichukulie wewe mwenyewe mali.”22Abram akamwambia mfalme wa Sodoma, “Nimeinua juu mkono wangu kwa Yahwe, Mungu aliye juu sana, muumbaji wa mbingu na nchi,23kwamba sitachukua uzi wala gidamu ya kiatu, au kitu chochote ambacho ni chako, ili kwamba usiseme, ‘Nimemfanya Abram kuwa tajiri.’24Sitachukua chochote isipokuwa kile ambacho vijana wamekula na sehemu za watu waliokwenda nami. Aneri, Eskoli, na Mamre na wachukue sehemu zao.”

15

1Baada ya mambo haya, neno la Yahwe likamjia Abram katika maono, likisema, “Usiogope, Abram! Mimi ni ngao yako na thawabu yako kubwa sana.”2Abram akasema, “Bwana Yahwe, utanipatia nini, kwa kuwa naenda bila mtoto, na mrithi wa nyumba yangu ni Eliezeri wa Dameski?”3Abram akasema, “Kwakuwa hujanipatia uzao, tazama, mwangalizi wa nyumba yangu ndiye mrithi wangu.”4Kisha, tazama, neno la Yahwe likaja kwake, kusema, “Mtu huyu hatakuwa mrithi wako; isipokuwa atakaye toka katika mwili wako ndiye atakuwa mrithi wako.”5Kisha akamtoa nje, na akasema, “Tazama mbinguni, na uzihesabu nyota, ikiwa unaweza kuzihesabu.” Kisha akamwambia, “Hivyo ndivyo uzao wako utakavyokuwa.”6Akamwamini Yahwe, na akamhesabia jambo hili kuwa mwenye haki.7Akamwambia, “Mimi ni Yahwe, niliye kutoa katika Uru ya Wakaldayo, na kukupatia nchi hii kuirithi.”8Akasema, “Bwana Yahwe, nitajuaje kuwa nitairithi?”9Kisha akamwambia, “Nipatie ndama wa umri wa miaka mitatu, mbuzi mke wa umri wa miaka mitatu, na kondoo mume wa umri wa miaka mitatu, na njiwa na mwana njiwa.”10Akamletea hivi vyote, akavipasua katika sehemu mbili, akaweka kila kipande kuelekea mwenzake, ila ndege hakuawapasua.11Wakati ndege walipokuja juu ya mizoga, Abram akawafukuza.12Kisha wakati jua lilipokuwa likizama, Abram akalala usingizi mzito na tazama, hofu ya giza kuu ikamfunika.13Kisha Yahwe akamwambia Abram, “Ujue kwa hakika kwamba uzao wako watakuwa wageni katika nchi ambayo si ya kwao, na watatumikishwa na kuteswa kwa miaka 400.14Nitahukumu taifa ambalo watalitumikia, na baadaye watatoka wakiwa na mali nyingi.15Lakini utakwenda kwa baba zako kwa amani, na utazikwa katika uzee mwema.16Katika kizazi cha nne watakuja tena hapa, kwa sababu uovu wa Waamori haujafikia mwisho wake.”17Jua lilipokuwa limezama na kuwa giza, tazama, chungu cha moshi wenye moto na miali ya mwanga ilipita kati ya vile vipande.18Siku hiyo Yahwe akafanya agano na Abram, akisema, “Ninatoa nchi hii kwa uzao wako, kutoka mto wa Misri hadi kwenye mto mkuu, Frati -19Mkeni, Mkenizi, na Mkadmoni,20Mhiti, Mperizi, Mrefai,21Mwamori, Mkanaani, Mgirgashi, na Myebusi.

16

1Kisha Sarai mke wa Abram, alikuwa hajamzalia mtoto, lakini alikuwa na mtumishi wa kike, Mmisri ambaye jina lake aliitwa Hajiri.2Kwa hiyo Sarai akamwambia Abram, “Tazama, Yahwe hajanifanya mimi kuwa na watoto. Nenda na ulale na mtumishi wangu. Ili kwamba niweze kupata watoto kupitia yeye.” Abram akasikiliza sauti ya Sarai.3Ilikuwa baada ya Abram kuishi miaka kumi katika nchi ya Kanaani ndipo Sarai, mke wa Abram, alimtoa Hajiri yule mmisri mtumishi wake kwa mume wake awe kama mke wake.4Kwa hiyo akawa na mahusiano na Hajiri, na akabeba mimba. Na alipoona kuwa amebeba mimba, akamdharau bibi yake.5Kisha Sarai akamwambia Abram, “Jambo hili baya kwangu ni kwa sababu yako. Nilimtoa mtumishi wangu wa kike katika kumbatio lako. Na alipoona kuwa amebeba mimba, nilidharaulika machoni pake. Na sasa acha Yahwe aamue kati yangu na wewe.”6Lakini Abram akamwambia Sarai, “Tazama, hapa, mtumishi wako yuko katika uwezo wako, fanya unachofikiri ni kizuri sana kwake.” Kwa hiyo Sarai akakabiliana naye kwa ukatili, na akatoroka.7Malaika wa Yahwe akamkuta karibu na chemichemi ya maji katika jangwa, chemichemi iliyo katika njia kuelekea Shuri.8Akasema, “Hajiri, mtumishi wa Sarai, umetoka wapi na unakwenda wapi?” Na akasema, “Ninamtoroka bibi yangu Sarai.”9Malaika wa Yahwe akamwambia, “Rudi kwa bibi yako, na unyenyekee chini ya mamlaka yake.”10Kisha Malaika wa Yahwe akamwambia, “Nitazidisha uzao wako maradufu, kiasi kwamba watakuwa wengi wasioweza kuhesabika.”11Malaika wa Yahwe pia akamwambia, “Tazama, wewe unamimba, na utazaa mtoto wa kiume, na utamwita jina lake Ishmaeli, kwa sababu Yahwe amesikia mateso yako.12Atakuwa punda mwitu wa mtu. Atakuwa adui dhidi ya kila mtu, na kila mtu atakuwa adui yake, na ataishi kando na ndugu zake wote.”13Kisha akamwita jina hili Yahwe aliye zungumza naye, “Wewe ni Mungu unionaye mimi,” kwa kuwa alisema, “Je ninaendelea kweli kuona, hata baada ya kuwa ameniona?”14Kwa hiyo kisima kiliitwa Beer Lahai Roi; Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.

15Hajiri akamzalia Abram mwana wa kiume, na Abram akamwita mwanawe, ambaye Hajiri amemzaa jina, Ishmaeli.16Abram alikuwa na umri wa miaka 86 wakati Hajiri alipomzaa Ishmaeli kwa Abram.

17

1Wakati Abram alipokuwa na umri wa miaka 99, Yahwe alimtokea Abram na akamwambia, “Mimi ni Mungu wa uwezo. Uende mbele yangu, na uwe mkamilifu.2Kisha nitalithibitisha agano langu kati yangu mimi na wewe, na nitakuzidisha sana.”3Abram akainama uso wake hadi chini ardhini na Mungu akazungumza naye, akisema,4“Mimi, tazama, agano langu liko nawe. Utakuwa baba wa mataifa mengi.5Wala jina lako halitakuwa tena Abram, bali jina lako litakuwa Abraham - kwa kuwa ninakuchagua kuwa baba wa mataifa mengi.6Nitakufanya uwe na uzao mwingi zaidi, na nitakufanya mataifa, na wafalme watatoka kwako.7Nitaimarisha agano langu kati yangu mimi na wewe na uzao wako baada yako, katika vizazi vyao vyote kwa agano la milele. Nitakuwa Mungu kwako na kwa wazao wako baada yako.8Nitakupa wewe, na wazao wako baada yako, nchi ambayo ulikuwa unaishi, nchi yote ya Kanaani, kuwa miliki ya milele, na nitakuwa Mungu wao.”

9Kisha Mungu akamwambia Abraham, “Nawe lazima ulishike agano langu, wewe pamoja na uzao wako baada yako kwa vizazi vyao.10Hili ndilo agano langu, ambalo utalishika, kati yangu na wewe na wazao wako baada yako: Kila mwanaume wa kwenu lazima atahiriwe.11Lazima mtatahiriwa katika nyama ya govi la ngozi ya mbele, na hii itakuwa ishara ya agano kati yangu mimi na ninyi.12Kila mwanaume wa kwenu aliye na umri wa siku nane lazima atahiriwe, katika vizazi ya watu wenu. Hii ni pamoja na yule azaliwaye katika nyumba yako na yeye ambaye amenunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni yeyote ambaye si mmoja wa wazao wako.13Mtu ambaye amezaliwa katika nyumba yako na yule aliye nunuliwa kwa fedha yako lazima atahiriwe. Hivyo agano langu litakuwa katika mwili wenu kuwa agano la milele.14Mwanaume yeyote asiye tahiriwa katika mwili govi la ngozi yake ya mbele atatengwa na watu wake. Amevunja agano langu.”

15Mungu akamwambia Abraham, “Kwa habari ya Sarai mkeo, usimuite tena Sarai. Badala yake jina lake litakuwa Sara.16Nitambariki, na nitakupatia mtoto wa kiume kwake. Nitambariki, na atakuwa mama wa mataifa. Wafalme wa watu wa mataifa watapatikana kutokana na yeye.”

17Kisha Abraham akainama uso wake hadi ardhini, na akacheka, akasema moyoni mwake, “Je yawezekana mtoto azaliwe kwa mwanaume ambaye ana umri wa miaka 100? Na je Sara, ambaye ana umri wa miaka 90 anaweza kuzaa mwana?”18Abraham akamwambia Mungu, “Lau Ishmaeli angeweza kuishi kabla yako!”19Mungu akasema, “Hapana, Sarai mkeo atakuzalia mtoto wa kiume na utamwita jina lake Isaka. Nita imarisha agano langu na yeye kama agano la milele pamoja na uzao wake baada yake.20Na kwa habari ya Ishmaeli nimekusikia. Tazama, ninambariki, na nitamfanya kuwa na uzao na kumzidisha maradufu. Atakuwa baba wa viongozi kumi na wawili wa makabila, na nitamfanya kuwa taifa kuu.21Lakini agano langu nitalifanya imara na Isaka, ambaye Sarai atazaa kwako majira haya mwakani.”22Alipokuwa amemaliza kuzungumza naye, Mungu akaondoka kwa Abraham.

23Kisha Abraham akamtwaa Ishmaeli mwanawe, na wote ambao walizaliwa katika nyumba yake, na wote ambao walinunuliwa kwa fedha yake, kila mwanaume miongoni mwa watu wa nyumba ya Abraham, walitahiriwa mwili wa magovi ya ngozi ya mbele katika siku iyo hiyo, kama Mungu alivyo kuwa amesema.24Abraham alikuwa na umri wa miaka 99 alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.25Na Ishmaeli mwanawe alikuwa na umri wa miaka 13 alipotahiriwa katika mwili wa govi la ngozi yake ya mbele.26Siku ile ile ambayo wote wawili Abraham na Ishmael mwanawe walipotahiriwa, ndipo27wanaume wote wa nyumba yake walitahiriwa pia, hawa ni pamoja na wale waliozaliwa katika nyumba ile na wale walionunuliwa kwa fedha kutoka kwa mgeni.

18

1Yahwe alimtokea Abraham katika Mialoni ya Mamre, alipokua ameketi mlangoni pa hema wakati wa jua.2Akatazama juu na, tazama, akaona wanaume watatu wamesimama mbele yake. Alipo waona, alikimbia kupitia mlango wa hema kuwalaki na kuinama chini hadi ardhini.3Akasema, “Bwana, kama nimepata upendeleo machoni pako, nakuomba usinipite na kuniacha mtumishi wako.4Naomba maji kidogo yaletwe, mnawe miguu yenu, na mjipumzishe chini ya mti.5Nami acha nilete chakula kidogo, ili kwamba mjiburudishe wenyewe. Ndipo baadaye mwaweza kwenda zenu, kwa kuwa mmekuja kwa mtumishi wenu.” Nao wakasema, “Fanya kama ulivyo sema.”6Kisha Abraham akaenda upesi hemani kwa Sara, na akasema, “Harakisha, chukua vipimo vitatu vya unga safi, uukande, na fanya mkate.”7Kisha Abraham akakimbia kundini, akachukua ndama wa ng'ombe aliye laini na mzuri, na akampatia mtumishi na kwa haraka akamwandaa.8Akatwaa siagi na maziwa na ndama aliye kwisha andaliwa, na akaweka chakula mbele yao, naye akasimama karibu nao chini ya mti wakati wanakula.9Wakamwambia, “Mke wako Sara yuko wapi?” Akajibu, “Pale hemani.”10Akasema, “Hakika nitarejea kwako majira ya machipuko, na tazama Sara mkeo atakuwa na mtoto wa kiume.” Sara alikuwa akisikiliza mlangoni pa hema iliyokuwa nyuma yake.11Abraham na Sara walikuwa wazee, umri wao ulikuwa umeendelea sana, na Sara alikuwa amepita umri ambao mwanamke anaweza kuzaa watoto.12Kwa hiyo Sara akajicheka mwenyewe, akijisemesha mwenyewe, “Baada ya kuwa nimechakaa na bwana wangu ni mzee, je nitapata furaha hii?”13Yahwe akamwambia Abraham, “Kwa nini Sara amecheka na kusema, ‘Je ni kweli nitazaa mtoto, nikiwa mzee?’14Je kuna jambo lolote gumu sana kwa Yahwe? Itakuwa katika wakati nilioweka mimi majira ya machipuko, nitarejea kwako. Majira haya mwakani, Sara atakuwa na mtoto wa kiume.”15Kisha Sara akakataa na kusema, “Sikucheka,” kwa kuwa aliogopa. Yahwe akasema, “Hapana ulicheka.”

16Kisha wale wanaume walisimama kuondoka na wakatazama chini kuelekea Sodoma. Abraham akafuatana nao kuona njia yao.17Lakini Yahwe akasema, “Je, ni mfiche Abraham kile ninacho kusudia kufanya,18ikiwa kwa hakika Abraham atakuwa mkuu na taifa lenye nguvu, na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa?19Kwa kuwa nimemchagua ili awaelekeze wanawe na nyumba yake baada yake waishike njia ya Yahwe, watende utakatifu na haki, ili kwamba Yahwe ampatie Abraham yale aliyo yasema kwake.”20Kisha Yahwe akasema, “Kwa sababu kilio cha Sodoma na Gomora ni kikuu, na kwa kuwa dhambi yao ni kubwa,21sasa nitashuka pale na kuona kilio kilicho nifikia dhidi yake, ikiwa kweli wamefanya au hawakufanya, nitajua.”22Kwa hiyo wale wanaume wakageuka toka pale, na kuelekea Sodoma, lakini Abraham akabaki amesimama mbele ya Yahwe.23Kisha Abraham alikaribia na kusema, “Je utawafutilia mbali watakatifu pamoja na waovu?24Huenda wakawepo wenye haki hamsini katika mji. Je utawakatilia mbali na usiuache mji kwa ajili ya hao watakatifu hamsini walioko hapo?25Hasha usifanye hivyo, kuwauwa watakatifu pamoja na waovu, ili kwamba watakatifu watendewe sawa na waovu. Hasha! Je muhukumu wa ulimwengu wote hatatenda haki?”26Yahwe akasema, “Katika Sodoma nikipata watakatifu hamsini kwenye mji, nitauacha mji wote kwa ajili ya hao.”27Abraham akajibu na kusema, “Tazama, nimeshika kusema na Bwana wangu, hata kama mimi ni mavumbi na majivu!28Itakuwaje ikiwa kuna watano pungufu katika idadi ya hao watakatifu hamsini? Je utaangamiza mji wote kwa upungufu wa hao watano?” Akasema, “Sitaangamiza, ikiwa nitapata watu arobaini na watano pale.”29Akaongea naye tena, na kusema, “Itakuwaje ikiwa arobaini watapatikana pale?” Akajibu, “Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini.”30Akasema, “Tafadhali usikasirike, Bwana, nikiongea. Pengine thelathini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitafanya, ikiwa nitapata thelathini pale.”31Akasema, “Tazama, nimeshika kusema na Bwana wangu! Pengine ishirini watapatikana pale.” Akajibu, “Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini.”32Akasema, “Tafadhali usikasirike Bwana, na nitasema jambo hili kwa mara ya mwisho. Huenda kumi wakaonekana kule.” Na akasema, “Sitaangamiza kwa ajili ya hao kumi.”33Yahwe akaendelea na njia yake mara tu baada ya kumaliza kuongea na Abraham, na Abraham akarudi nyumbani.

19

1Malaika wawili wakaja Sodoma jioni, wakati ambao Lutu alikuwa amekaa langoni mwa Sodoma. Lutu akawaona, akainuka kuwalaki, na akainama uso wake chini ardhini.2Akasema, “Tafadhali Bwana zangu, nawasihi mgeuke mwende kwenye nyumba ya mtumishi wenu, mlale pale usiku na muoshe miguu yenu. Kisha muamke asubuhi na mapema muondoke.” Nao wakasema, “Hapana, usiku tutalala mjini.”3Lakini akawasihi sana, mwishowe wakaondoka pamoja naye, na wakaingia katika nyumba yake. Akaandaa chakula na kuoka mkate usiotiwa chachu, wakala.4Lakini kabla hawaja lala, wanaume wa mji wa Sodoma, vijana kwa wazee wakaizunguka nyumba, wanaume wote kutoka kila kona ya mji.5Wakamwita Lutu, na kumwambia, “Wale wanaume walioingia kwako usiku wako wapi? Watoe hapa nje waje kwetu, ili tuweze kulala nao.”6Lutu akatoka nje na akafunga mlango.7Akasema, “Nawasihi, ndugu zangu, msitende uovu.8Tazama, nina mabinti wawili ambao hawajawahi kulala na mwanaume yeyote. Nawaomba tafadhali niwalete kwenu, na muwafanyie lolote muonalo kuwa jema machoni penu. Msitende lolote kwa wanaume hawa, kwa kuwa wamekuja chini ya kivuli cha dari yangu.”9Wakasema, “Ondoka hapa!” Wakasema pia, “Huyu alikuja kukaa hapa kama mgeni, na sasa amekuwa mwamuzi! Sasa tutakushugulilia vibaya wewe kuliko wao.” Wakamsonga sana huyo Lutu, na wakakaribia kuvunja mlango.10Lakini wale wanaume wakamkamata Lutu na kumweka ndani na wakafunga mlango.11Kisha wale wageni wa Lutu wakawapiga kwa upofu wale wanaume waliokuwa nje ya nyumba, vijana na wazee kwa pamoja, kiasi kwamba wakachoka wakati wakiutafuta mlango.12Basi wale watu wakamwambia Lutu, “Je una mtu mwingine yeyote hapa? Wakwe zako, wanao na mabinti zako, na yeyote mwingine katika huu mji, ukawatoe hapa.13Kwa kuwa tunakaribia kuiangamiza sehemu hii, kwa sababu mashitaka dhidi yake mbele ya Yahwe yamezidi kiasi kwamba ametutuma kuuangamiza.”14Lutu akatoka na akazungumza na wakwe zake, wanaume ambao walikuwa wamewaposa binti zake, akawambia, “Ondokeni upesi mahali hapa, kwa kuwa Yahwe anakaribia kuuangamiza mji.” Lakini kwa wakwe zake alionekana kuwa anawatania.15Alfajiri, malaika wakamsihi Lutu, wakisema, “Ondoka, mtwae mkeo na binti zako wawili ambao wako hapa, ili kwamba usipotelee katika adhabu ya mji huu.”16Lakini akakawia-kawia. Kwa hiyo watu wale wakamshika mkono wake, na mkono wa mkewe, na mikono ya binti zake wawili, kwa sababu Yahwe alimhurumia. Wakawatoa nje, na kuwaweka nje ya mji.17Wakisha kuwatoa nje mmoja wa wale watu akasema, “Jiponye nafsi yako! Usitazame nyuma, au usikae mahali popote kwenye hili bonde. Toroka uende milimani ili kwamba usije ukatoweshwa mbali.”18Lutu akawambia, “Hapana, tafadhali bwana zangu!19Mtumishi wenu amepata kibali machoni pako, na umenionyesha wema ulio mkuu kwa kuokoa maisha yangu, lakini sitaweza kutorokea milimani, kwa sababu mabaya yataniwahi na nitakufa.20Tazama, ule mji pale uko karibu nijisalimishe pale, na ni mdogo. Tafadhali niacheni nikimbilie pale (Je, siyo mdogo ule?), Na maisha yangu yataokolewa.”21Akamwambia, “Sawa, nimekubali ombi hili pia, kwamba sitaangamiza mji ambao umeutaja.22Harakisha! Toroka uende pale, kwa kuwa sitafanya chochote mpaka ufike pale.” Kwa hiyo mji ule ukaitwa Soari.

23Jua lilikuwa limekwisha chomoza juu ya nchi wakati Lutu alipofika Soari.24Kisha Yahwe akanyesha juu ya Sodoma na Gomora kiberiti na moto toka kwa Yahwe mbinguni.25Akaharibu miji ile, na bonde lote, na vyote vilivyomo katika miji, na mimea iliyo chipua juu ya ardhi.26Lakini mke wa Lutu aliye kuwa nyuma yake, akatazama nyuma, na akawa nguzo ya chumvi.

27Abraham akaamka asubuhi na mapema akaenda mahali alipokuwa amesimama mbele ya Yahwe.28Akatazama chini kuelekea Sodoma na Gomora na kuelekea katika nchi yote bondeni. Akaona na tazama, moshi ulikuwa ukienda juu kutoka chini kama moshi wa tanuru.

29Wakati Mungu alipoharibu miji ya bondeni, Mungu akamkumbuka Abraham. Akamtoa Lutu kutoka katika maangamizi alipoangamiza miji ambayo katika hiyo Lutu aliishi.

30Lakini Lutu akapanda juu kutoka Soari na kwenda kuishi katika milima akiwa pamoja na binti zake wawili, kwa sababu aliogopa kuishi Soari. Kwa hiyo akaishi pangoni, yeye na binti zake wawili.31Yule wa kwanza akamwambia yule mdogo, “Baba yetu ni mzee, na hakuna mwanaume mahali popote wa kulala na sisi kulingana na desturi ya dunia yote.32Njoo na tumnyweshe baba yetu mvinyo na tulale naye ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu.”33Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule. Kisha yule wa kwanza akaingia na akalala na baba yake; Baba yake hakujua ni wakati gani alikuja kulala, wala wakati alipo amka.34Siku iliyo fuata yule wa kwanza akamwambia mdogowake, “Sikiliza, usiku wa jana nililala na baba yangu. Na tumnyweshe mvinyo usiku wa leo pia, na uingie ukalale naye. Ili kwamba tuendeleze uzao wa baba yetu.”35Kwa hiyo wakamnywesha baba yao mvinyo usiku ule pia, na yule mdogo akaenda na akalala naye. Baba yake hakujua ni wakati gani alilala, wala wakati alipoamka.36Basi hao binti wote wawili wa Lutu wakapata mimba kwa baba yao.37Wa kwanza akazaa mwana wa kiume, na akamwita jina lake Moabu. Akawa ndiye baba wa wamoabu hata leo.38Na yule mdogo naye akazaa mwana wa kiume, na akamwita Benami. Huyu ndiye baba wa watu wa Waamoni hata leo.

20

1Abraham akasafiri kutoka pale hadi nchi ya Negebu, na akakaa kati ya Kadeshi na Shuri. Akawa mgeni akiishi Gerari.2Abraham akasema kuhusu mkewe Sara, “Ni dada yangu.” Kwa hiyo Abimeleki mfalme wa Gerari akatuma watu wake kumchukua Sara.3Lakini Mungu akamtokea Abimeleki usiku katika ndoto, akamwambia, “Tazama, wewe ni mfu kutokana na mwanamke uliye mchukua, kwa kuwa ni mke wa mtu.”4Basi Abimeleki alikuwa bado hajamkaribia hivyo akasema, “Bwana, Je utaua hata taifa lenye haki?5Je si yeye mwenyewe aliye niambia, ‘Sara ni dada yangu?’ Hata Sara mwenyewe alisema, ‘Ni kaka yangu.’ Nimefanya hili katika uadilifu wa moyo wangu na katika mikono isiyo na hatia.”6Kisha Mungu akasema naye katika ndoto, “Kweli, ninajua pia kwamba umefanya hili katika uadilifu wa moyo wako, na pia nilikuzuia usitende dhambi dhidi yangu mimi. Ndiyo maana sikuruhusu umshike.7Kwa hiyo, mrudishe huyo mke wa mtu, kwa kuwa ni nabii. Atakuombea, na utaishi. Lakini usipo mrudisha, ujue kwamba wewe pamoja na wote walio wa kwako mtakufa hakika.”8Abimeleki akaamka asubuhi na mapema akawaita watumishi wake wote waje kwake. Akawasimulia mambo haya yote, na watu wale wakaogopa sana.9Kisha Abimeleki akamwita Abraham na kumwambia, “Umetufanyia jambo gani? Ni kwa jinsi gani nimekutenda dhambi kwamba umeniletea mimi na ufalme wangu dhambi hii kubwa? Umenifanyia mimi jambo ambalo halipaswi kufanywa.”10Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini kilikushawishi wewe kutenda jambo hili?”11Abraham akasema, “Ni kwa sababu nilifikiri ‘Hakika hakuna hofu ya Mungu katika sehemu hii, na kwamba wataniua kwa ajili ya mke wangu.’12Licha ya kwamba kweli ni dada yangu, binti wa baba yangu, ingawa si binti wa mama yangu; na ndiye alifanyika kuwa mke wangu.13Wakati Mungu aliponiondoa katika nyumba ya baba yangu na kusafiri kutoka mahali kwenda mahali pengine, nilimwambia mke wangu, kwa kila sehemu tutakayo kwenda, unionyeshe uaminifu wako kama mke wangu: Kila mahali tutakapo kwenda, useme juu yangu kuwa, ‘Ni kaka yangu.’”14Ndipo Abimeleki akatwaa kondoo, maksai, watumwa wa kiume na wa kike akampatia Abraham. Basi Abimeleki akamrudisha Sara, mke wa Abraham.15Abimeleki akasema, “Tazama, nchi yangu i mbele yako. Kaa mahali utakapo pendezewa.”16Na kwa Sara akasema, “Tazama, nimempatia kaka yako vipande elfu vya fedha. Navyo ni kwa ajili ya kufunika kosa lolote dhidi yako machoni pa wote walio pamoja na wewe, na mbele ya kila mtu ambaye umemfanya kuwa na haki.”17Kisha Abraham akaomba kwa Mungu, na Mungu akamponya Abimeleki, mkewe, na watumwa wake wa kike kiasi kwamba wakaweza kupata watoto.18Kwa kuwa Yahwe alikuwa amewafanya wanawake wote wa nyumba ya Abimeleki kuwa tasa kabisa, kwa sababu ya Sara, mke wa Abraham.

21

1Yahwe akamsikiliza Sara kwa umakini kama alivyo kuwa amemwambia, Yahwe akamfanyia Sara kama alivyo kuwa amemwahidi.2Sara akachukua mimba na akamzalia Abraham mtoto wa kiume katika uzee wake, katika muda ule ule ambao Mungu alikuwa amemwambia.3Abraham akamwita jina mwanawe, ambaye alizaliwa kwake, na Sara, Isaka.4Abraham akamtahiri mwanawe Isaka alipofikisha siku nane, kama vile Mungu alivyokuwa amemwagiza.5Abraham alikuwa na umri wa miaka 100 wakati mwanawe Isaka alizaliwa kwake.6Sara akasema, “Mungu amenifanya nicheke; kila mtu atakaye sikia atacheka pamoja na nami.”7Pia akasema, “Nani angesema kwa Abraham kwamba Sara atalea mtoto, na sasa kweli nimemzalia mtoto wakiume katika uzee wake!”

8Mtoto akakua na akaachishwa kunyonya, na Abraham akafanya sherehe kubwa katika siku ambayo Isaka aliachishwa.9Sara akamwona mwana wa Hajiri Mmisri, ambaye alikuwa amezaliwa kwa Abraham, akidhihaki.10Kwa hiyo akamwambia Abraham, “Mfukuze huyu mwanamke huyu mtumwa pamoja na mtoto wake: kwa kuwa mtoto huyu wa mwanamke mtumwa hawezi kuwa mrithi pamoja na mwanangu Isaka.”11Jambo hili likamhuzunisha sana Abraham kwa sababu ya mwanawe.12Lakini Mungu akamwambia Abraham, “Usihuzunike kwa sababu ya kijana huyu, na kwa sababu ya mwanamke huyu mtumwa wako. Sikiliza maneno asemayo Sara juu ya jambo hili, kwa sababu itakuwa kupitia Isaka kwamba uzao wako utaitwa.13Nitamfanya pia mtoto wa mjakazi kuwa taifa, kwa sababu ni uzao wako.”14Abraham akaamka asubuhi na mapema, akachukua mkate na kiriba cha maji, akampatia Hajiri, akaweka juu ya bega lake. Akamtoa kijana akampatia Hajiri na akawaondoa. Hajiri akaondoka akapotea katika jangwa la Beerisheba.

15Maji yalipokwisha kwenye kiriba akamtelekeza kijana katika moja ya vichaka.16Kisha akaondoka, na akakaa umbali kidogo na yule kijana, umbali kama wa kutupa mshale, kwa vile alisema, “Na nisitazame kifo cha mtoto.” Alipokuwa amekaa kumkabili, akapaza sauti yake akalia.17Mungu akasikia kilio cha kijana, na malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, “Nini kinakusumbua? Usiogope, kwa kuwa Mungu amesikia kilio cha kijana mahali alipo.18Inuka msimamishe mtoto, na umtie moyo; kwa kuwa nitamfanya kuwa taifa kubwa.”19Kisha Mungu akayafunua macho ya Hajiri, na tazama, akaona kisima cha maji. Akaenda akajaza kiriba maji, na akampatia kijana akanywa.

20Mungu akawa pamoja na kijana, na akakua. Akaishi jangwani akawa mwindaji.21Akaishi katika jangwa la Parani, na mama yake akampatia mke kutoka Misri.

22Ikawa kwamba katika wakati ule Abimeleki na Fikoli kamanda wa jeshi lake akamwambia Abraham, akisema, “Mungu yuko pamoja na wewe katika yote uyatendayo.23Sasa niapie kwa Mungu kwamba hutanifanyia baya, wala mwanangu, wala uzao wangu. Onyesha kwangu na kwa nchi ambayo umekuwa ukikaa agano lile lile la uaminifu ambalo nimekuonyesha wewe.”24Abraham akasema, “Nina apa.”

25Abraham pia akamlalamikia Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki wamekinyang'anya.26Abimeleki akasema, “Sijui ni nani amefanya jambo hili. Hukuniambia mapema; na sijalisikia ila leo hii.”27Kwa hiyo Abraham akachukua kondoo na ng'ombe maksai akampatia Abimeleki, na wawili hawa wakafanya agano.28Kisha Abraham akatenga wanakondoo wa kike saba peke yao.29Abimeleki akamwambia Abraham, “Nini maana ya hawa wanakondoo wa kike saba ambao umewatenga peke yao?”30Akajibu, “Hawa wanakondoo wa kike saba utawapokea kutoka mkonono mwangu, ili kwamba uwe ushahidi kwangu, kuwa nilichimba kisima hiki.”31Kwa hiyo akaita mahali pale Beersheba, kwa sababu mahali pale wote wawili waliapa kiapo.32Walifanya agano hapo Beerisheba, kisha Abimeleki na Fikoli, amiri wa jeshi, wakarudi katika nchi ya Wafilisti.33Abraham akapanda mti wa mkwaju katika Beerisheba. Na pale akamwabudu Yahwe, Mungu wa milele.34Abraham akasalia kuwa mgeni katika nchi ya Wafilisti kwa siku nyingi.

22

1Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, “Abraham!” Abraham akasema, “Mimi hapa.”2Kisha Mungu akasema, “Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia.”3Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.4Siku ya tatu Abraham akatazama juu na akaona mahali pakiwa mbali.5Abraham akawaambia vijana wake, “Kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu.”6Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja.7Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”8Abraham akasema, “Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu.” Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.9Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.10Abraham akanyoosha mkono wake akachukua kisu ili kumuua mwanawe.11Ndipo malaika wa Yahwe akamwita kutoka mbinguni na kusema, “Abraham, Abraham!” naye akasema, “Mimi hapa.”12Akasema, “Usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru, kwa kuwa sasa najua unamcha Mungu, kwa kuona kuwa hukumzuilia mwanao, mwanao wa pekee, kwa ajili yangu.”

13Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.14Kwa hiyo Abraham akapaita mahali pale, “Yahwe atatoa,” na panaitwa hivyo hata leo. “Juu ya mlima wa Yahwe itatolewa.”

15Malaika wa Yahwe akamwita Abraham kwa mara ya pili kutoka mbinguni16na kusema “Hiki ni kiapo cha Yahwe. Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa kwamba kwa kuwa umefanya jambo hili, na hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,17hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wako watamiliki lango la adui zao.18Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa, kwa sababu umetii sauti yangu.”19Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba.

20Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, “Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori.”21Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu,22Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli.23Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham.24Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka.

23

1Sara akaishi miaka 127. Hii ndiyo ilikuwa ni miaka ya maisha ya Sara.2Sara akafa katika Kiriathi Arba, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani. Abraham akaomboleza na kumlilia Sara.3Kisha Abraham akainuka na kutoka kwa mkewe aliye kufa, akanena na watoto wa kiume wa Hethi, akisema,4“Mimi ni mgeni kati yenu. Tafadhali nipatieni mahali pa kuzikia miongoni mwenu, ili kwamba niweze kuzika wafu wangu.”5Wana wa Hethi wakamjibu Abraham, wakasema,6“Tusikilize, bwana wangu. Wewe ni mwana wa Mungu miongoni mwetu. Zika wafu wako katika makaburi yetu utakayochagua. Hakuna miongoni mwetu atakaye kuzuilia kaburi lake, kwa ajili ya kuzikia wafu wako.”7Abraham akainuka na kusujudu chini kwa watu wa nchi ile, kwa wana wa Hethi.8Akawaambia, akisema, “Ikiwa mmekubali mimi kuzika wafu wangu, ndipo nisikilizeni, msihini Efroni mwana wa Sohari kwa ajili yangu.9Mwambieni aniuzie pango la Makpela, ambalo analimiliki, ambalo liko mwishoni mwa shamba lake. Kwa bei kamili aniuzie waziwazi mbele ya watu kama miliki ya kuzikia.”10Efroni alikuwa ameketi miongoni mwa wana wa Hethi, hivyo Efroni Mhiti akamjibu Abraham alipowasikia wana wa Hethi, wote ambao walikuwa wamekuja langoni mwa mji wake, akasema,11“Hapana, bwana wangu, nisikilize. Ninakupatia shamba na pango ambalo limo ndani yake. Ninakupatia mbele ya wana wa watu wangu. Ninakupatia uzike wafu wako.”12Kisha Abraham akasujudu chini mbele ya watu wa nchi ile.13Akamwambia Efroni watu wa nchi ile wakisikiliza, akasema, “Ikiwa uko radhi, tafadhali nisikilize. Nitalipia shamba. Chukua fedha kwangu, na nitazika wafu wangu pale.”14Efroni akamjibu Abraham, akisema,15“Tafadhali bwana wangu, nisikilize. Kipande cha ardhi kina thamani ya shekeli 400 za fedha, na hiyo ni kitu gani kati yangu mimi na wewe? Wazike wafu wako.”16Abraham akamsikiliza Efroni na akampimia Efroni kiwango cha fedha alizosema mbele ya wana wa Hethi wakisikiliza, shekeli 400 za fedha, kwa mujibu wa viwango vya vipimo vya kibiashara.

17Kwa hiyo shamba la Efroni, lililokuwa katika Makpela, mbele ya Mamre, shamba pamoja na pango lililokuwamo ndani yake na miti yote iliyokuwamo ndani ya shamba na iliyokuwa mpakani ikatolewa18kwa Abraham kwa njia ya manunuzi mbele ya wana wa Hethi, na mbele ya wote waliokuja malangoni pa mji wake.19Baada ya haya, Abraham akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela, lililo mbele ya Mamre, ambayo ni Hebroni, katika nchi ya Kanaani.20Kwa hiyo shamba pamoja na pango likatolewa na wana wa Hethi kwa Abraham kama milki na eneo la kuzikia.

24

1Basi Abraham alikuwa mzee sana na Yahwe akawa amembariki katika mambo yote.2Abraham akamwambia mtumwa wake, ambaye alikuwa mkubwa kuliko wote wa nyumbani mwake na mkuu wa vyote alivyo kuwa navyo. “Weka mkono wako chini ya paja langu3na nitakufanya uape kwa Yahwe, Mungu wa Mbingu na nchi, kwamba hutampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, miongoni mwao wale nikaao kati yao.4Lakini utakwenda kwenye nchi yangu, na kwa ndugu zangu, na kumtafutia mwanangu Isaka mke.”5Yule mtumwa wake akamwambia, “Itakuwaje ikiwa mwanamke hatakuwa tayari kufuatana nami hadi katika nchi hii? Je nitamrudisha mwanao katika nchi ambayo ulitoka?”6Abraham akamwambia, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu kule!7Yahwe, Mungu wa mbingu, ambaye alinitoa mimi kutoka katika nyumba ya baba yangu na kutoka katika nchi ya ndugu zangu, na ambaye aliniahidia kwa kiapo maalumu akisema, ‘Nitawapa uzao wako nchi hii,’ atatuma malaika wake mbele yako, na utapata mke kwa ajili ya mwanangu kutoka huko.8Lakini ikiwa mwanamke hatakuwa tayari, ndipo utakuwa huru katika hiki kiapo changu. Cha muhimu tu ni kwamba usije ukamrudisha mwanangu huko.”9Kwa hiyo mtumwa akaweka mkono wake chini ya paja la Abraham bwana wake, na akaapa kuhusiana na jambo hili.

10Mtumwa akachukua ngamia kumi wa bwana wake na akaondoka. Akachukua pia aina zote za zawadi kutoka kwa bwana wake. Akaondoka na kwenda katika mkoa wa Aramu Naharaimu, mji wa Nahori.11Akawapigisha magoti ngamia nje ya mji karibu na kisima cha maji. Ilikuwa jioni wakati ambao wanawake huenda kuchota maji.12Kisha akasema, “Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, anijalie kufanikiwa leo na aoneshe agano la uaminifu kwa bwana wangu Abraham.13Tazama, nimesimama hapa karibu na chemichemi ya maji na mabinti za watu wa mji wanakuja kuteka maji.14Na itokee hivi kwamba, nikimwambia msichana, ‘Tafadhali tua mtungi wako ili niweze kunywa maji,’ na akiniambia, ‘Kunywa, na kwamba nitawanywesha ngamia wako pia,’ huyo ndiye ambaye umemchagulia mtumwa wako Isaka. Kwa njia hii nitajua kuwa umeonyesha agano la uaminifu kwa bwana wangu.”15Ikawa kwamba hata kabla hajamaliza kuzungumza, tazama, Rebeka akaja akiwa na mtungi wake wa maji begani mwake. Rebeka alizaliwa na Bethueli mwana wa Milka, mke wa Nahori, ndugu yake na Abraham.16Msichana huyu alikuwa mzuri na alikuwa bikira. Hapana mwanaume aliye kuwa amekwisha lala naye. Akashuka kisimani na kuujaza mtungi wake, na kupanda juu.17Kisha mtumwa yule akakimbia kumlaki yule msichana, na kusema, “Tafadhali nipatie maji kidogo ya kunywa kutoka katika mtungi wako.”18Akasema, “Kunywa tafadhali bwana wangu,” na kwa haraka akatua mtungi wake juu ya mkono wake, na akampatia maji ya kunywa.19Alipokuwa amemaliza kumpatia maji, akasema, “Nitachota maji kwa ajili ya ngamia wako pia, mpaka watakapomaliza kunywa.”20Hivyo akaharakisha akamwaga maji yaliyokuwa mtungini kwenye chombo cha kunyweshea mifugo, kisha akakimbia tena kisimani kuchota maji, na kuwanywesha ngamia wake wote.21Yule mtu akamtazama msichana akiwa kimya kuona kama Yahwe amefanikisha njia yake au la.22Ngamia walipomaliza kunywa maji, yule mtu akaleta pete ya pua ya dhahabu yenye uzito wa nusu shekeli, na bangili mbili za dhahabu kwa ajili ya mikono yake zenye uzito wa shekeli kumi,23akamuuliza, “Wewe ni binti wa nani? Niambie tafadhali, Je kuna nafasi nyumbani mwa baba yako kwa ajili yetu kupumzika usiku?”24Akamwambia, “Mimi ni binti wa Bethueli mwana wa Milka, ambaye alimzaa kwa Nahori.”25Akasema pia, “Tunayo malisho tele na chakula, na iko nafasi kwa ajili yako kulala usiku.”26Kisha yule mtu akainama chini na kumwabudu Yahwe.27Akasema, “Abarikiwe Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye hakuacha agano lake la uaminifu na kweli yake mbele ya bwana wangu. Kwa vile Yahwe ameniongoza moja kwa moja kwenye nyumba ya ndugu zake bwana wangu.”28Kisha yule msichana akakimbia na kwenda kuwaeleza watu wa nyumba ya mama yake juu ya mambo yote haya.29Na sasa Rebeka alikuwa na kaka yake, jina lake aliitwa Labani. Labani akakimbia kwa yule mtu aliye kuwa nje barabarani karibu na kisima.30Akisha kuona hereni ya puani pamoja na zile bangili kwenye mikono ya dada yake, na kusikia maneno ya Rebeka dada yake, “Hivi ndivyo yule mtu alivyo niambia,” alikwenda kwa yule mtu, na, tazama, alikuwa amesimama karibu na ngamia pale kisimani.31Labani akasema, “Njoo, wewe uliye barikiwa na Yahwe. Kwa nini umesimama nje? Nimekwisha andaa nyumba, pamoja na mahali kwa ajili ya ngamia.”32Kwa hiyo yule mtu akaingia ndani ya nyumba na akashusha mizigo kutoka kwa wale ngamia. Ngamia wakapatiwa malisho na chakula, na maji yakatolewa kuosha miguu yake pamoja na miguu ya wale watu aliokuwa pamoja nao.33Wakaandaa chakula mbele yake ale, lakini akasema, “Sitakula mpaka niseme kile ninacho paswa kusema.” Kwa hiyo Labani akamwambia, “Sema.”34Akasema, “Mimi ni mtumwa wa Abraham.35Yahwe amembariki sana bwana wangu na amekuwa mtu mkuu. Amempatia mifugo na makundi ya wanyama, fedha, dhahabu, watumwa wa kiume na watumwa wa kike, pamoja na ngamia na punda.36Sara, mke wa bwana wangu, alimzalia mwana bwana wangu alipokuwa mzee, na amempatia mwanawe kila kitu anachomiliki.37Bwana wangu aliniapisha, akisema, ‘Usije ukampatia mwanangu mke kutoka kwa mabinti wa Wakanaani, ambao kwao nimefanya makazi.38Badala yake, lazima uende kwa familia ya baba yangu, na kwa ndugu zangu, na kupata mke kwa ajili ya mwanangu.’39Nikamwambia bwana wangu, ‘Pengine mwanamke huyo asikubali kufuatana nami.’40Lakini akaniambia, ‘Yahwe, ambaye ninakwenda mbele yake, atatuma malaika wake pamoja nawe na atakufanikisha njia yako, kwamba utapata mke kwa ajili ya mwanangu kutoka miongoni mwa ndugu zangu na kutoka katika ukoo wa baba yangu.41Lakini utakuwa huru katika kiapo changu ikiwa utafika kwa ndugu zangu na wasikuruhusu kuja naye. Ndipo utakuwa huru katika kiapo changu.’

42Hivyo nimefika leo kisimani, na nikasema, ‘O Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, tafadhali, ikiwa kweli umekusudia kuifanya safari yangu kuwa yenye kufanikiwa -43tazama niko hapa nimesimama karibu na kisima cha maji - na iwe kwamba binti ajaye kuchota maji, nitakayemwambia, ‘Tafadhali unipatie maji kidogo kutoka kwenye mtungi wako ninywe,’ mwanamke atakaye niambia,44‘Kunywa, na nitakuchotea pia maji kwa ajili ya ngamia wako’ - na awe ndiye ambaye wewe Yahwe, umemchagulia mtoto wa bwana wangu.’45Ikawa hata kabla sijamaliza kuzungumza moyoni mwangu, tazama, Rebeka akaja na mtungi wake juu ya bega lake akashuka chini kisimani akachota maji. Hivyo nikamwambia, ‘Tafadhali nipatie maji ninywe.’46Ndipo kwa haraka alipoushusha mtungi wake begani mwake na akasema, ‘Kunywa, na pia nitawapatia maji ngamia wako.’ Kwa hiyo nikanywa, na akawanywesha ngamia pia.47Nikamuuliza na kusema, ‘Wewe ni binti wa nani?’ Akasema, ‘Binti wa Bethueli, Mwana wa Nahori, ambaye Milka alizaa kwake.’ Kisha nikamwekea pete puani mwake pamoja na bangili mikononi mwake.48Kisha nikainama chini nikamwabudu Yahwe, na kumbariki Yahwe, Mungu wa bwana wangu Abraham, ambaye ameniongoza katika njia sahihi kumpata binti wa ndugu za bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.49Kwa hiyo, ikiwa mko tayari kumfanyia rehema na kweli, niambieni. Lakini kama sivyo, niambieni, ili kwamba niweze kwenda upande wa kulia, au kushoto.”50Ndipo Labani na Bethueli wakajibu na kusema, “Jambo hili limetoka kwa Yahwe; hatuwezi kusema kwako aidha neno baya au zuri.51Tazama, Rebeka yu mbele yako. Mchukue na uende, ili awe mke wa mtoto wa bwana wako, kama Yahwe alivyosema.”

52Mtumwa wa Abraham aliposikia maneno yao, akainama mwenyewe chini ardhini kwa Yahwe.53Mtumwa akaleta vipande vya fedha na vipande vya dhahabu, na nguo, akampatia Rebeka. Akampatia pia kaka yake na mama yake zawadi zenye thamani.54Kisha yeye na watu aliokuwa nao wakala na kunywa. Wakakaa pale mpaka usiku, na walipoamka asubuhi, akasema, “Niruhusuni niende kwa bwana wangu.”55Kaka yake na mama yake wakasema, “Mwache binti abaki nasi kwa siku chache zingine, angalau siku kumi, baada ya hapo anaweza kwenda.”56Lakini akawambia, “Msinizuie, kwa kuwa Yahwe amefanikisha njia yangu. Niruhusuni niende kwa bwana wangu.”57Wakasema, “Tutamwita binti na kumuuliza.”58Kwa hiyo wakamwita Rebeka na kumuuliza, “Je utakwenda na mtu huyu?” Akajibu, “Nitakwenda.”59Kwa hiyo wakampeleka dada yao Rebeka, pamoja na watumishi wake wa kike, kwenda njiani pamoja na mtumishi wa Abraham na watu wake.60Wakambarikia Rebeka, na wakamwambia, “Ndugu yetu, na uwe mama wa maelfu na wa makumi elfu, uzao wako upate kumiliki lango la wale wanao wachukia.”61Kisha Rebeka akasimama, yeye na watumishi wake kwa hesabu ya ngamia, na wakamfuata yule mtu. Hivyo watumishi wakamchukua Rebeka, na wakaenda zao.

62Nyakati hizo Isaka alikuwa anakaa katika Negebu, na alikuwa tu amerejea kutoka Beerlahairoi.63Isaka akaenda kutafakari shambani jioni. Alipotazama akaona, na tazama, kulikuwa na ngamia wakija!64Rebeka akatazama na alipomwona Isaka, akaruka kutoka kwenye ngamia.65Akamwambia mtumwa, “Mtu huyo ni nani anaye tembea shambani akija kutupokea?” Mtumwa akasema, “Ni bwana wangu.” Hivyo Rebeka akachukua shela yake akajifunika.66Mtumwa akamwambia Isaka mambo yote ambayo amefanya.67Kisha Isaka akamleta katika hema ya Sara mama yake na akamchukua Rebeka, na akawa mke wake, na akampenda. Kwa hiyo Isaka akafarijika baada ya kifo cha mama yake.

25

1Abraham akaoa mke mwingine; jina lake aliitwa Ketura.2Akamzalia Zimrani, Jokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua.3Jokshani akamzaa Sheba na Dedani. Wana wa Dedani walikuwa ni Waashuru, Waletushi, na Waleumi.4Wana wa Midiani walikuwa ni Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Hawa wote walikuwa ni wana wa Ketura.

5Abraham akampatia Isaka vitu vyote alivyokuwa navyo.6Ingawaje, wakati alipokua angali akiishi, aliwapatia zawadi wana wa masuria wake na kuwapeleka katika nchi ya mashariki, mbali na Isaka, mwanawe.7Hizi ndizo zilikuwa siku za miaka ya uhai wake Abraham alizoishi, miaka 175.8Abraham akapumua pumzi ya mwisho na akafa katika uzee mwema, mzee aliye shiba siku, na akakusanywa kwa watu wake.9Isaka na Ishmaili, wanae wakamzika katika pango la Makipela, katika shamba la Efron mwana wa Soari Mhiti, pango lililokuwa karibu na Mamre.10Shamba hili Abraham alilinunua kwa watoto wa Hethi. Abraham akazikwa pale pamoja na Sara mkewe.11Baada ya kifo cha Abraham, Mungu akambariki Isaka mwanawe, na Isaka akaishi karibu na Beerlahairoi.

12Na sasa hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, mwana wa Abraham, ambaye Hajiri Mmisri mtumishi wake Sara, alizaa kwa Abraham.13Haya ndiyo yalikuwa majina ya wana wa Ishimaeli, kuanzia mzaliwa wa kwanza: Nebayothi - mzaliwa wa kwanza wa Ishimaeli, Kedari, Abdeeli, Mibsamu,14Mishma, Duma, Masa,15Hadadi, Tema, Yeturi, Nafishi, na Kedema.16Hawa ndio walikuwa wana wa Ishimaeli, na haya ndiyo majina yao, kwa vijiji vyao, na katika vituo vyao; Maseyidi kumi na wawili kufuatana na kabila zao.17Hii ndiyo ilikuwa miaka ya Ishimaeli, miaka 137: akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa pamoja na watu wake.18Walioshi toka Havila mpaka Shuri, ambayo iko karibu na Misri, kuelekea Ashuru. Waliishi kwa uadui kati yao.

19Na hivi ndivyo vizazi vya Isaka, mwana wa Abraham: Abraham alimzaa Isaka.20Isaka alikuwa na umri wa miaka arobaini alipomuoa Rebeka, binti wa Bethueli Mshami wa Padani Aramu, ndugu wa Labani Mshami.21Isaka akamwomba Yahwe kwa ajili ya mke wake kwa sababu alikuwa tasa, na Yahwe akajibu maombi yake, Rebeka mkewe akabeba mimba.22Watoto hawa walipokuwa tumboni mwake wakasumbuka, naye akasema, “Kwa nini jambo hili linatokea kwangu mimi?” Akaenda kumuuliza Yahwe kuhusu jambo hili.23Yahwe akamwambia, “Mataifa mawili yako katika tumbo lako, na mataifa haya mawili yatatengana ndani yako. Taifa moja litakuwa lenye nguvu kuliko lingine, na yule mkubwa atamtumikia mdogo.”

24Ulipo wadia wakati wa kujifungua, tazama, kulikuwa na mapacha ndani ya tumbo lake.25Wa kwanza akatoka akiwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.26Baada ya hapo ndugu yake akatoka. Mkono wake ukiwa umeshika kisigino cha Esau. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati mke wake alipo wazaa hawa watoto.

27Vijana hawa wakakua, Esau akawa mwindaji hodari, mtu wa nyikani; lakini Yakobo alikuwa mtu mkimya, aliye tumia muda wake akiwa katika mahema.28Kisha Isaka akampenda Esau kwa sababu alikula wanyama ambao alikuwa anawinda, lakini Rebeka akampenda Yakobo.

29Yakobo akapika mchuzi. Esau akaja kutoka nyikani, akiwa dhaifu kutokana na njaa.30Esau akamwambia Yakobo, “Nilishe mchuzi mwekundu. Tafadhali, nimechoka!” Na hii ndiyo sababu jina lake aliitwa Edomu.31Yakobo akasema, “Kwanza uniuzie haki yako ya mzaliwa wa kwanza.”32Esau akasema, “Tazama, nakaribia kufa. Ni nini kwangu haki ya mzaliwa wa kwanza?”33Yakobo akasema, “Kwanza uape kwangu mimi.” Kwa hiyo Esau akaapa kiapo na kwa njia hii akawa ameuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa Yakobo.34Yakobo akampatia Esau mkate pamoja na mchuzi wa dengu. Akala na kunywa, kisha akainuka na akaenda zake. Kwa njia hii Esau akawa ameidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza.

26

1Basi njaa ikatokea katika nchi, mbali na njaa ya kwanza iliyotokea siku za Ibrahimu. Isaka akaenda kwa Abimeleki, mfalme wa Wafilisiti huko Gerari.2Basi Yahwe akamtokea na kumwambia, “Usishuke kwenda Misri; kaa katika nchi niliyokuambia.3Kaa katika nchi hii hii niliyokuambia, nami nitakuwa pamoja nawe na kukubariki; kwani kwako wewe na uzao wako, nitawapa nchi hii yote, nami nitatimiza kiapo nilichomwapia Ibrahimu baba yako.4Nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote. Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia yatabarikiwa.5Nitalifanya hili kwa sababu Ibrahimu aliitii sauti yangu na kutunza maelekezo yangu, amri zangu na sheria zangu.”

6Hivyo Isaka akakaa Gerari.

7Watu wa eneo hilo walipomwuliza juu ya mke wake, alisema, “Yeye ni dada yangu.” Aliogopa kusema, “Yeye ni mke wangu,” kwa kuwa alidhani, “Watu wa nchi hii wataniua ili wamchukue Rebeka, kwa kuwa ni mzuri wa uso.”8Baada ya Isaka kuwa amekaa pale kwa muda mrefu, ikatukia kwamba Abimeleki mfalme wa Wafilisiti alichungulia katika dirisha. Tazama, akamwona Isaka akimpapasa Rebeka, mke wake.9Abimeleki akamwita Isaka kwake na kusema, “Tazama, kwa hakika yeye ni mke wako. Kwa nini ulisema, ‘Yeye ni dada yangu?’” Isaka akamwambia, “Kwa sababu nilidhani mtu mmoja aweza kuniua ili amchukue.”10Abimeleki akamwambia, “Ni jambo gani hili ulilotufanyia? Mmojawapo wa watu angeweza bila shaka kulala na mke wako, nawe ungeweza kuleta hatia juu yetu.”11Hivyo Abimeleki akawaonya watu wote na kusema, “Mtu yeyote atakayemgusa mtu huyu au mke wake atauwawa.”

12Isaka akapanda mazao katika nchi hiyo na kuvuna mwaka huo vipimo mia, kwa kuwa Yahwe alimbariki.13Mtu huyo akawa tajiri, naye akaongezeka zaidi hata akawa mkuu sana.14Alikuwa na kondoo na ngombe na familia kubwa. Wafilisiti wakamwonea wivu.15Basi visima vyote watumishi wa baba yake walikuwa wamevichimba katika siku za Ibrahimu baba yake, Wafilisiti wakavikatalia kwa kuvijaza kifusi.16Abimeleki akamwambia Isaka, “Ondoka kati yetu, kwa kuwa wewe una nguvu kuliko sisi.”17Hivyo Isaka akaondoka pale na kukaa katika bonde la Gerari, na kuishi pale.18Kwa mara nyingine tena Isaka akachimba visima vya maji, vilivyokuwa vimechimbwa siku za Ibrahimu baba yake. Wafilisiti walikuwa wamevizuia baada ya kufa kwake Ibrahimu. Isaka akaviita visima kwa majina aliyokuwa ameviita baba yake.19Watumishi wa Isaka walipochimba katika bonde, wakaona kisima cha maji yaliyokuwa yakibubujika.20Wachungaji wa Gerari wakagombana na wachungaji wa Isaka, na kusema, “Haya ni maji yetu.” Hivyo Isaka akakiita kisima hicho Eseki, kwa sababu waligombana naye.21Wakachimba kisima kingine, wakakigombania hicho nacho, hivyo akakiita Sitna.22Akatoka hapo na akachimba kisima kingine, lakini hicho hawakukigombania. Hivyo akakiita Rehobothi, na akasema, “Sasa Yahwe ametufanyia nafasi, na tutafanikiwa katika nchi.”

23Kisha Isaka akaenda Beersheba.24Yahwe akamtokea usiku huo huo na akasema, “Mimi ni Mungu wa Ibrahimu baba yako. Usiogope, kwa maana mimi nipo pamoja nawe na nitakubariki na kuzidisha vizazi vyako, kwa ajili ya mtumishi wangu Ibrahimu.”25Isaka akajenga madhabahu pale na akaliita jina la Yahwe. Akapiga hema yake pale, na watumishi wake wakachimba kisima.

26Kisha Abimeleki akamwendea kutoka Gerari, pamoja na Ahuzathi, rafiki yake, na Fikoli, jemedari wa jeshi.27Isaka akawambia, “Kwa nini mmekuja kwangu, kwani mlinichukia na kunifukuza kwenu.”28Nao wakasema, “Tumeona yakini kwamba Yahwe amekuwa nawe. Hivyo tukaamua kwamba kuwe na kiapo kati yetu, ndiyo, kati yetu nawe. Hivyo na tufanye agano nawe,29kwamba hautatudhuru, kama ambavyo sisi hatukukudhuru, na kama sisi tulivyokutendea vema wewe na tumekuacha uondoke kwa amani. Kwa kweli, Yahwe amekubariki.”30Hivyo Isaka akawaandalia sherehe, na wakala na kunywa.31Wakaamka mapema asubuhi na wakaapiana kiapo. Kisha Isaka akawaruhusu kuondoka, nao wakamwacha katika amani.

32Siku hiyohiyo watumishi wake wakaja na kumwambia juu ya kisima walichokuwa wamekichimba. Wakasema, “Tumeona maji.”33Akakiita kile kisima Shiba, hivyo jina la mji ule ni Beersheba hata leo.

34Esau alipokuwa na umri wa miaka arobaini, akajitwalia mke, Yudithi binti Beeri Mhiti, na Basemathi binti Eloni Mhiti.35Wakamhuzunisha Isaka na Rebeka.

27

1Isaka alipozeeka na macho yake kuwa mazito kiasi cha kutokuona, alimwita Esau, mwanawe mkubwa, na akamwambia, “Mwanangu.” Yeye akasema, “Mimi hapa.”2Akamwambia, “Tazama, mimi nimezeeka. Sijui siku ya kufa kwangu.3Kwa hiyo chukua silaha zako, podo lako na upinde wako, na uende uwandani ukaniwindie mnyama.4Uniandalie chakula kitamu, aina ile niipendayo, uniletee ili nikile na kukubariki kabla sijafa.”5Basi Rebeka akasikia Isaka alipoongea na Esau mwanawe. Esau akaenda uwandani kuwinda mawindo na kuja nayo.6Rebeka akaongea na Yakobo mwanawe na kumwambia, “Tazama, nimemsikia baba yako akiongea na Esau ndugu yako. Akasema,7‘Niletee mnyama na unitengenezee chakula kitamu, ili nikile na kukubariki mbele za Yahwe kabla ya kufa kwangu.’8Kwa hiyo sasa, mwanangu, usikilize sauti yangu kama ninavyokuagiza.9Nenda kundini, na uniletee wanambuzi wawili; nami nitaandaa chakula kitamu kutokana nao kwa ajili ya baba yako, kwa namna aipendayo.10Utakipeleka kwa baba yako, ili kwamba akile, na kukubariki kabla hajafa.”

11Yakobo akamwambia Rebeka mama yake, “Tazama, ndugu yangu Esau ni mtu mwenye manyoya, na mimi ni mtu laini.12Pengine baba yangu atanigusa, nami nitaonekana kama mdanganyifu kwake. Nami nitajiletea laana badala ya baraka.”13Mama yake akamwambia, “Mwanangu, acha laana yoyote iwe juu yangu. Wewe sikiliza sauti yangu, nenda, uniletee.”14Hivyo Yakobo alikwenda na kuchukua wanambuzi na kuwaleta kwa mama yake, na mama yake akaandaa chakula kitamu, kama alichokipenda baba yake.15Rebeka akachukua nguo nzuri za Esau, mwanawe mkubwa, alizokuwa nazo nyumbani mwake, na akamvika Yakobo, mwanawe mdogo.16Akamvalisha ngozi ya mwanambuzi katika mikono yake na katika sehemu laini za shingo yake.17Akaweka katika mikono ya Yakobo kile chakula kitamu na mkate aliokuwa ameuandaa.

18Yakobo akaenda kwa baba yake na kumwambia, “Babangu.” Yeye akasema, “Mimi hapa; U nani wewe, mwanangu?”19Yakobo akamwambia baba yake, “Mimi ni Esau mzaliwa wako wa kwanza; nimefanya kama ulivyoniagiza. Basi kaa na ule sehemu ya mawindo yangu, ili unibariki.”20Isaka akamwambia mwanawe, “Imekuwaje umepata kwa haraka hivyo, mwanangu?” Akasema, “Ni kwa sababu Yahwe Mungu wako ameniletea.”21Isaka akamwambia Yakobo, “Njoo karibu nami, ili nikuguse, mwanangu, ili nijue kama kweli wewe ni mwanangu Esau au hapana.”22Yakobo akamkaribia Isaka baba yake; na Isaka akamgusa na kusema, “Sauti ni sauti ya Yakobo, lakini mikono ni mikono ya Esau.”23Isaka hakumtambua, kwa sababu mikono yake ilikuwa na manyoya, kama mikono ya Esau ndugu yake, hivyo Isaka akambariki.24Akasema, “Wewe kweli ni mwanangu Esau?” Naye akasema, “Ni mimi.”25Isaka akasema, “Kilete chakula kwangu, na nile mawindo yako, ili nikubariki.” Yakobo akakileta chakula kwake. Isaka akala, na Yakobo akamletea mvinyo, akanywa.26Kisha Isaka baba yake akamwambia, “Sogea karibu nami na unibusu, mwanangu.”27Yakobo akasogea na kumbusu, naye akanusa harufu ya nguo zake na kumbariki. Akasema, “Tazama, harufu ya mwanangu ni kama harufu ya shamba alilolibariki Yahwe.28Mungu akupe sehemu ya umande wa mbinguni, sehemu ya unono wa nchi, na wingi wa nafaka na mvinyo mpya.29Watu na wakutumikie na mataifa yainame chini yako. Uwe bwana juu ya ndugu zako, na wana wa mama yako wainame chini yako. Kila anayekulaani na alaaniwe; na kila anayekubariki abarikiwe.”

30Mara Isaka alipomaliza kumbariki Yakobo, na Yakobo ndo ametoka mbele ya Isaka baba yake, Esau ndugu yake akaja kutoka kuwinda.31Yeye pia akaandaa chakula kitamu na kukileta kwa baba yake. Akamwambia baba yake, “Baba, inuka na ule baadhi ya mawindo ya mwanao, ili uweze kunibariki.”32Isaka baba yake akamwambia, “U nani wewe? Akasema, “Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.”33Isaka akatetemeka sana na kusema, “Alikuwa nani aliyewinda mawindo na kuniletea? Nilikula chote kabla haujaja, nami nimembariki. Atabarikiwa, kwa kweli.”34Esau aliposikia maneno ya baba yake, akalia kwa kilio kikubwa na cha uchungu sana, na akamwambia baba yake, “Unibariki nami, mimi pia, babangu.”35Isaka akasema, “Ndugu yako alikuja hapa kwa hila na amechukua baraka yako.”36Esau akasema, “Je hakuitwa Yakobo kwa haki? Kwa maana amenidanganya mara mbili hizi. Alichukua haki ya uzaliwa wangu wa kwanza, na tazama, sasa amechukua baraka yangu.” Na akasema, “Je haukuniachia baraka?”37Isaka akajibu na kumwambia Esau, “Tazama, nimemfanya kuwa bwana wako, na nimempa ndugu zake kuwa watumishi wake. Na nimempa nafaka na divai. Je nikufanyie nini mwanangu?”38Esau akamwambia babaye, “Je hauna hata baraka moja kwa ajili yangu, babangu? Nibariki nami, hata mimi pia, babangu.” Esau akalia kwa sauti.39Isaka baba yake akajibu na kumwambia, “Tazama, mahali unapoishi patakuwa mbali na utajiri wa nchi, mbali na umande juu angani.40Kwa upanga wako utaishi, nawe utamtumikia ndugu yako. Lakini utakapoasi, utaiondoa nira yake shingoni mwako.”

41Esau akamchukia Yakobo kwa sababu ya baraka ambayo baba yake alimpa. Esau akajisemea moyoni, “Siku za maombolezo kwa ajili ya baba yangu zinakaribia; baada ya hapo nitamwua Yakobo ndugu yangu.”42Rebeka akaambiwa maneno ya Esau mwanawe mkubwa. Hivyo akatuma na kumwita Yakobo mwanawe mdogo na kumwambia, “Tazama, Esau ndugu yako anajifariji juu yako kwa kupanga kukuuwa.43Kwa hiyo sasa, mwanangu, unisikie na kukimbilia kwa Labani, ndugu yangu, huko Harani.44Ukae naye kitambo, mpaka hasira ya ndugu yako itakapopungua,45hata hasira ya ndugu yako itakapokuondokea, na kusahau ulivyomtenda. Kisha nitatuma na kukurudisha kutoka pale. Kwa nini niwapoteze ninyi nyote katika siku moja?”

46Rebeka akamwambia Isaka, “Nimechoka na maisha kwa sababu ya hawa binti za Hethi. Ikiwa Yakobo atachukua mmojawapo wa binti wa Hethi kuwa mkewe, kama wanawake hawa, baadhi ya binti za nchi, maisha yatakuwa na maana gani kwangu?”

28

1Isaka akamwita Yakobo, akambariki, na kumwagiza, “Usichukue mwanamke katika wanawake wa Kikanaani.2Inuka, nenda Padani Aramu, katika nyumba ya Bethueli baba wa mama yako, na uchukue mwanamke pale, mmojawapo wa binti za Labani, kaka wa mama yako.3Mungu Mwenyezi na akubariki, akupe uzao na akuzidishe, hata uwe wingi wa watu.4Na akupe baraka ya Ibrahimu, wewe, na uzao wako baada yako, kwamba uweze kumilki nchi ambapo umekuwa ukiishi, ambayo Mungu alimpa Ibrahimu.”5Hivyo Isaka akamwondoa Yakobo. Yakobo akaenda Padani Aramu, kwa Labani mwana wa Bethueli Mwaramu, kaka wa Rebeka, mama yao Yakobo na Esau.

6Basi Esau aliona kwamba Isaka amembariki Yakobo na kumpeleka Padani Aramu, kuchukua mke kutoka pale. Lakini pia akaona kwamba Isaka alikuwa amembariki na kumwagiza, akisema, “Usichukue mke katika wanawake wa Kanaani.”7Esau pia akaona kwamba Yakobo alikuwa amemtii baba yake na mama yake, na alikuwa amekwenda Padan- Aramu.8Esau akaona kwamba wanawake wa Kanaani hawakumpendeza Isaka baba yake.9Hivyo akaenda kwa Ishmaeli, na kuchukua, mbali na wake aliokuwa nao, Mahalathi binti Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, dada wa Nebayothi, kuwa mke wake.

10Yakobo akatoka Beersheba na akaelekea Harani.11Akaja mahali fulani na akakaa pale usiku kucha, kwa kuwa jua lilikuwa limekuchwa. Akachukua mojawapo ya mawe katika eneo hilo, akaliweka chini ya kichwa chake, na akalala usingizi katika eneo hilo.12Akaota na kuona ngazi imewekwa juu ya nchi. Ncha yake ilifika hata mbinguni na malaika wa Mungu walikuwa wakishuka na kupanda juu yake.13Tazama, Yahwe amesimama juu yake na kusema, “Mimi ni Yahwe, Mungu wa Ibrahimu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi uliyolala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.14Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya ardhi, na utaenea mbali kuelekea magharibi, mashariki, kaskazini, na kusini. Kupitia kwako na kupitia uzao wako familia zote za dunia zitabarikiwa.15Tazama, mimi nipo nawe, na nitakulinda kila uendako, Nitakurudisha katika nchi hii tena; kwani sitakuacha. Nitafanya kila nililokuahidi.”

16Yakobo akaamka katika usingizi, na akasema, “Hakika Yahwe yupo mahali hapa, sikujua hili.”17Akaogopa na kusema, “Eneo hili linatisha kama nini! Hili sio kingine zaidi ya nyumba ya Mungu. Hili ni lango la mbinguni.”18Yakobo akaamka mapema asubuhi na akachukua jiwe alilokuwa ameliweka chini ya kichwa chake. Akaliweka kama nguzo na kumimina mafuta juu yake.19Akapaita pale Betheli, lakini jina la kawaida la mji lilikuwa Luzu.

20Yakobo akatoa nadhiri, kusema, “Ikiwa Mungu atakuwa nami na atanilinda katika njia nipitayo, na atanipa mkate wa kula, na mavazi ya kuvaa,21hata nikarudi salama katika nyumba ya baba yangu, ndipo Yahwe atakapokuwa Mungu wangu.22Kisha jiwe hili nililoliweka kama nguzo litakuwa jiwe takatifu. Kutoka katika kila utakachonipa, kwa hakika nitakupa tena sehemu ya kumi.”

29

1Kisha Yakobo akaendelea na safari yake na akafika katika nchi ya watu wa mashariki.2Hata alipotazama, akaona kisima kondeni, na, tazama, makundi matatu ya kondoo yalikuwa yamelala kando yake. Kwani kutoka katika hicho wangeyanywesha makundi, na jiwe juu ya mdomo wa kisima lilikuwa kubwa.3Wakati makundi yote yangekusanyika pale, wachungaji wangevingirisha jiwe kutoka katika mdomo wa kisima na kuwanywesha kondoo, na kisha kurudisha jiwe juu ya mdomo wa kisima, mahali pake.

4Yakobo akawambia, “Ndugu zangu, ninyi mnatokea wapi?” Nao wakasema, “Tunatoka Harani.”5Akawaambia, “Mnamfahamu Labani mwana wa Nahori?” Wakasema, “Tunamfahamu.”6Akawaambia, “Je hajambo?” Wakasema, “Hajambo, na, tazama pale, Raheli binti yake anakuja na kondoo.”7Yakobo akasema, “Tazama, ni mchana. Siyo wakati wa kukusanya kondoo pamoja. Mnapaswa kuwanywesha kondoo na kisha mkaenda na kuwaacha wachunge.”8Wakamwambia, “Hatuwezi kuwanywesha mpaka makundi yote yakusanyike pamoja. Ndipo wanaume watakapovingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na ndipo tutakapowanywesha kondoo.”

9Wakati bado Yakobo anaongea nao, Raheli akaja pamoja na kondoo wa babaye, kwani alikuwa akiwachunga.10Yakobo alipomwona Raheli, binti wa Labani, kaka wa mamaye, na kondoo wa Labani, kaka wa mama yake, Yakobo akaja juu, akalivingirisha jiwe kutoka mlangoni mwa kisima, na akawanywesha kondoo wa Labani, kaka wa mama yake.11Yakobo akambusu Raheli na akalia kwa sauti.12Yakobo akamwambia Raheli kwamba alikuwa ni ndugu wa baba yake, na kwamba alikuwa mwana wa Rebeka. Kisha yeye akakimbia kumwambia baba yake.

13Labani aliposikia habari kuhusu Yakobo mwana wa dada yake, akaenda kukutana naye, akamkumbatia, akambusu, na kumleta nyumbani kwake. Yakobo akamwambia Labani mambo haya yote.14Labani akamwambia, “Kwa hakika wewe ni mfupa wangu na nyama yangu.” Kisha Yakobo akakaa naye kama mwezi mmoja.15Kisha Labani akamwambia Yakobo, “Je unitumikie bure kwa kuwa wewe ni ndugu yangu? Niambie, ujira wako utakuwaje?16Basi Labani alikuwa na binti wawili. Jina la mkubwa lilikuwa ni Lea, na jina la mdogo lilikuwa Raheli.17Macho ya Lea yalikuwa dhaifu, lakini Raheli alikuwa mzuri wa umbo na mwonekano.18Yakobo alimpenda Raheli, hivyo akasema, “Nitakutumikia miaka saba kwa ajili ya Raheli, binti yako mdogo.”19Labani akasema, “Itakuwa vema kukupa wewe, kuliko kumpa mtu mwingine. Kaa nami.”20Hivyo Yakobo akamtumikia kwa miaka saba kwa ajili ya Raheli; nayo ilionekana kwake kama siku chache tu, kwa ajili ya upendo aliokuwa nao kwake.

21Kisha Yakobo akamwambia Labani, “Nipe mke wangu, kwani siku zangu zimetimia - ili kwamba nimwoe!22Hivyo Labani akawaalika watu wa mahali hapo na kuandaa sherehe.23Wakati wa jioni, Labani akamchukua Lea binti yake mkubwa na kumleta kwa Yakobo, aliyelala naye.24Labani akampa mtumishi wake wakike Zilpa kuwa mjakazi wa Lea.

25Ilipofika asubuhi, tazama, kumbe ni Lea! Yakobo akamwambia Labani, “Ni nini hiki ulichonifanyia? Je sikukutumikia kwa ajili ya Raheli? Kwa nini basi umenihadaa?”26Labani akamwambia, “Siyo utamaduni wetu kumtoa binti mdogo kabla ya mzaliwa wa kwanza.27Timiza juma la bibi arusi, na tutakupa yule mwingine pia kwa mbadala wa kunitumikia miaka mingine saba.”

28Yakobo akafanya hivyo, na akatimiza juma la Lea. Kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake.29Lakini pia Labani akampa Raheli binti yake Bilha, kuwa mjakazi wake.30Hivyo Yakobo akalala na Raheli, pia, lakini akampenda Raheli zaidi ya Lea. Hivyo Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka saba mingine.

31Yahwe akaona kwamba Lea hakupendwa, hivyo akalifungua tumbo lake, lakini Raheli hakuwa na mtoto.32Lea akashika mimba na kuzaa mwana, naye akamwita Rubeni. Kwani alisema, “Kwa sababu Yahwe ameliangalia teso langu; bila shaka mme wangu sasa atanipenda.”33Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Kwa sababu Yahwe amesikia kwamba sipendwi, kwa hiyo amenipa mwana mwingine,” na akamwita Simoni.34Kisha akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Wakati huu mme wangu ataungana nami, kwa kuwa nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akaitwa Lawi.35Akashika mimba tena na kuzaa mwana. Akasema, “Wakati huu nitamsifu Yahwe.” Kwa hiyo akamwita jina lake Yuda; kisha akaacha kuzaa watoto.

30

1Raheli alipoona kwamba hamzalii Yakobo watoto, Raheli akamwonea wivu dada yake. Akamwambia Yakobo, “Nipe watoto, sivyo nitakufa.”2Hasira ya Yakobo ikawaka juu ya Raheli. Akasema, “Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia usipate watoto?”3Akasema, “Tazama, kuna mjakazi wangu Bilha. Lala naye, hivyo aweze kuzaa watoto magotini pangu, nami nitapata watoto kwake.”4Hivyo akampa Bilha mjakazi kama mke wake, na Yakobo akalala naye.5Bilha akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana.6Kisha Raheli akasema, “Mungu ameamua kwa faida yangu. Ameyasikiliza maombi yangu na kunipa mwana.” Kwa sababu hiyo akamwita jina lake Dani7Bilha, mjakazi wa Raheli, akashika mimba tena na kumzalia Yakobo mwana wa pili.8Raheli akasema, “Kwa mashindano yenye nguvu nimeshindana na dada yangu na kushinda.” Akamwita jina lake Naftali.

9Lea alipoona kwamba ameacha kuzaa, akamchukua Zilpa, mjakazi wake, na kumpa Yakobo kama mke wake.10Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.11Lea akasema, “Hii ni bahati njema!” Hivyo akamwita jina lake Gadi.12Kisha Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana wa pili.13Lea akasema, “Nina furaha! Kwa maana mabinti wataniita furaha.” Hivyo akamwita jina lake Asheri.

14Siku za mavuno ya ngano Rubeni akaenda shambani na kuona tunguja. Akazileta kwa mama yake. Kisha Raheli akamwambia Lea, “Nipe baadhi ya tunguja za mwanao.”15Lea akamwambia, “Je ni jambo dogo kwako, kumchukua mme wangu? Je na sasa unataka kuchukua tunguja za mwanangu pia?” Raheli akasema, “Kisha atalala nawe leo usiku, kwa kubadilishana na tunguja za mwanao.”

16Jioni Yakobo akaja kutoka uwandani. Lea akaenda kumlaki na kusema, “Leo usiku utalala nami, kwani nimekuajiri kwa tunguja za mwanangu.” Hivyo Yakobo akalala na Lea usiku huo.17Mungu akamsikia Lea, na akashika mimba na kumzalia Yakobo mwana wa tano.18Lea akasema, “Mungu amenipa ujira wangu, kwa sababu nilimpa mme wangu mjakazi wangu.” Akamwita jina lake Isakari.

19Lea akashika mimba tena na kuzaa mwana wa sita kwa Yakobo.20Lea akasema, “Mungu amenipa zawadi njema. Sasa mme wangu ataniheshimu, kwa sababu nimemzalia wana sita.” Akamwita jina lake Zabuloni.

21Baadaye akazaa binti na kumwita jina lake Dina.

22Mungu akamkumbuka Raheli na kumsikiliza. Akampa kushika mimba.23Akashika mimba na kuzaa mwana. Akasema, “Mungu ameiondoa aibu yangu.”24Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Yahwe ameniongeza mwana mwingine.”

25Baada ya Raheli kumzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, “Niache niende, ili kwamba niende nyumbani kwetu na katika nchi yangu.26Nipe wake zangu na watoto wangu niliokutumikia kwa ajili yao, na uniache niondoke, kwani unafahamu nilivyokutumikia.”27Labani akamwambia, “Ikiwa nimepata kibali machoni pako, subiri, kwa sababu nimejifunza kwa kutumia uaguzi kwamba Yahwe amenibariki kwa ajili yako.”28Kisha akasema, “Taja ujira wako, nami nitalipa.”29Yakobo akamwambia, “Unajua nilivyokutumikia, na jinsi ambavyo mifugo wako wamekuwa nami.30Kwani walikuwa wachache kabla sijaja, na wameongezeka kwa wingi. Popote nilipokutumikia Mungu amekubariki. Je ni lini mimi nitaandaa kwa ajili ya nyumba yangu pia?”31Hivyo Labani akasema, “Je nikulipe nini? Yakobo akasema, ‘Usinipe chochote. Ikiwa utafanya jambo hili kwa ajili yangu, nitawalisha tena kondoo wako na kuwatunza.32Niache nipite kati ya kundi lako lote leo, kwa kuondoa kila kondoo mwenye milia na mabaka, na kila kondoo mweusi kati yao, na kati ya wenye mabaka na milia katika mbuzi. Hawa watakuwa ujira wangu.33Uadilifu wangu utashuhudia kwa ajili yangu hapo baadaye, utakapokuja kuangalia ujira wangu. Kila ambaye hana milia na hana madoa miongoni mwa mbuzi, na mweusi kati ya kondoo, ikiwa wataonekana kwangu, watahesabiwa kuwa wameibwa.”

34Labani akasema, “Nakubali. Na iwe kama yalivyo maneno yako.”35Siku hiyo Labani akaondoa mabeberu yaliyokuwa na milia na madoa, na majike ya mbuzi yaliyokuwa na milia na madoa, kila aliyekuwa mweupe, na weusi wote katika mbuzi, akawakabidhi katika mikono ya wanawe.36Pia Labani akaweka safari ya siku tatu kati yake na Yakobo. Hivyo Yakobo akabaki kuchunga wale kondoo wa Labani waliosalia.

37Yakobo akachukua matawi mabichi yaliyokatwa ya mipopla, mlozi na mwaramoni mbichi akatoa maganda ili michilizi myeupe ionekane, na akaifanya sehemu nyeupe ya ndani ya mti iliyokuwa ndani ya fito ionekane.38Kisha akaziweka fito alizokuwa amezibambua mbele ya makundi ya kondoo, mbele ya mabirika yakunyweshea walipokuja kunywa maji. Wakashika mimba walipokuja kunywa maji.39Wanyama wakapandana mbele ya fito; nao wakazaa watoto wenye milia, mabaka na wenye madoa.40Yakobo akawatenga hawa wanakondoo, lakini akawafanya waliosalia kuelekea wanyama wenye milia na kondoo weusi wote katika kundi la Labani. Kisha akayatenga makundi yake mwenyewe pekee na hakuwaweka pamoja na wale wa Labani.41Pindi kondoo wenye nguvu katika kundi walipopandana, Yakobo alilaza fito katika mabirika ya maji mbele ya macho ya kundi, ili kwamba washike mimba kati ya fito.42Lakini wakati waliodhaifu walipokuja, hakuweka fito mbele yao. Hivyo wanyama dhaifu wakawa wa Labani, na wenye nguvu wakawa wa Yakobo.43Mtu huyo akastawi sana. Akawa na kundi kubwa la kondoo, wajakazi na wajoli, ngamia na punda.

31

1Basi Yakobo akasikia maneno ya wana wa Labani, wakisema, “Yakobo amechukuwa yote yaliyokuwa ya baba yetu, na ni kutoka katika mali ya baba yetu amepata utajiri wake.”2Yakobo akaona mwonekano katika uso wa Labani. Akaona kwamba nia yake imebadilika.3Kisha Yahwe akamwambia Yakobo, “Rudi katika nchi ya baba zako na ya ndugu zako, nami nitakuwa nawe.”

4Yakobo akatuma kuwaita Raheli na Lea uwandani katika kundi lake la kondoo5naye akawaambia, “Naona nia ya baba yenu kwangu imebadilika, lakini Mungu wa baba yangu amekuwa nami.6Nanyi mnajua kwamba ni kwa nguvu zangu zote nimemtumikia baba yenu.7Baba yenu amenidanganya na amebadilisha ujira wangu mara kumi, lakini Mungu hakumruhusu kunidhuru.8Ikiwa alisema, ‘Wanyama wenye mabaka watakuwa ujira wako,’ ndipo kondoo wote walipozaa watoto wenye mabaka. Na aliposema, ‘Wenye milia watakuwa ujira wako,’ ndipo kundi lote lilipozaa watoto wenye milia.9Kwa njia hii Mungu amemnyang'anya mifugo baba yenu na kunipa mimi.

10Wakati fulani wa majira ya kupandana, niliona katika ndoto mabeberu yaliyowapanda kundi. Mabeberu yalikuwa ya milia, mabaka na madoa.11Malaika wa Mungu akaniambia katika ndoto, ‘Yakobo.’ Nikasema, ‘Mimi hapa.’12Akasema, ‘Inua macho yako uone mabeberu wanaolipanda kundi. Wana milia, madoa na mabaka, kwani nimeona kila jambo Labani analokutendea.13Mimi ni Mungu wa Betheli, mahali ulipoitia nguzo mafuta, mahali uliponitolea nadhiri. Basi sasa inuka na uondoke katika nchi hii na kurudi katika nchi uliyozaliwa.’”

14Raheli na Lea wakajibu na kumwambia, “Je kuna sehemu yoyote au urithi wetu katika nyumba ya baba yetu?15Je hatutendei kama wageni? Kwa maana ametuuza na kwa ujumla ametapanya pesa zetu.16Mali zote ambazo sasa Mungu amemnyang'anya baba yetu ni zetu na watoto wetu. Sasa basi, lolote Mungu alilokuambia, fanya.”

17Kisha Yakobo akainuka na kuwapandisha wanawe na wakeze kwenye ngamia.18Akawaongoza mifugo wake wote mbele yake, pamoja na mali zake zote, wakiwemo wanyama aliowapata huko Padani Aramu. Kisha akaenda kuelekea kwa Isaka baba yake katika nchi ya Kanaani.

19Labani alipokuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo wake, Raheli akaiba miungu ya nyumba ya baba yake.20Yakobo pia akamdanganya Labani Mwarami, kwa kutomtaarifu kwamba anaondoka.21Hivyo akaondoka na vyote alivyokuwa navyo na kwa haraka akavuka mto, na akaenda kuelekea nchi ya vilima ya Gileadi.

22Siku ya tatu Labani akaambiwa kwamba Yakobo amekimbia.23Hivyo akawachukua ndugu zake pamoja naye na kumfuatia kwa safari ya siku saba. Akampata katika nchi ya vilima ya Gileadi.24Basi Mungu akaja kwa Labani Mwarami katika ndoto usiku na kumwambia, “Ujihadhari kumwambia Yakobo jambo lolote liwe jema au baya.”

25Labani akampata Yakobo. Basi Yakobo alikuwa amepiga hema yake katika nchi ya vilima. Labani pia akapiga kambi pamoja na ndugu zake katika nchi ya kilima ya Gileadi.26Labani akamwambia Yakobo, “Umefanya nini, kwamba umewachukua binti zangu kama mateka wa vita?27Kwa nini umekimbia kwa siri na kunihadaa kwa kutokuniambia? Ningekuruhusu uondoke kwa sherehe na kwa nyimbo, kwa matari na vinubi.28Haukuniacha niwabusu wajukuu wangu na binti zangu kwa kuwaaga. Basi umefanya upumbavu.29Iko katika uwezo wangu kukudhuru, lakini Mungu wa baba yako alisema nami usiku wa leo na kuniambia, ‘Jihadhari usimwambie Yakobo neno la heri wala shari.’30Na sasa, umeondoka kwa sababu umeitamani sana nyumba ya baba yako. Lakini kwa nini umeiba miungu yangu?”

31Yakobo akajibu na kumwambia Labani, “Ni kwa sababu niliogopa na kudhani kuwa ungeninyang'anya binti zako kwa nguvu ndiyo maana nikaondoka kwa siri.32Yeyote aliyeiiba miungu yako hataendelea kuishi. Mbele ya ndugu zetu, onesha chochote kilichochako nilichonacho na uchukue.” Kwa maana Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameviiba.

33Labani akaingia katika hema ya Yakobo, katika hema ya Lea, na katika hema za wale wajakazi wawili, lakini hakuviona. Akatoka katika hema ya Lea na kuingia katika hema ya Raheli.34Basi Raheli alikuwa ameichukua miungu ya nyumbani, na kuiweka katika ngozi ya ngamia, na kukaa juu yake. Labani akatafuta katika hema yote, lakini hakuiona.35Akamwambia baba yake, “Usikasirike, bwana wangu, kwamba siwezi kusimama mbele yako, kwani nipo katika kipindi changu.” Hivyo akatafuta lakini hakuiona miungu ya nyumbani mwake.

36Yakobo akakasirika na kuhojiana na Labani. Akamwambia, “Kosa langu ni nini? Dhambi yangu ni ipi, hata ukanifuatia kwa ukali?37Kwa maana umechunguza mali zangu zote. Umeona nini kati ya kitu chochote cha nyumbani mwako? Viweke hapa mbele ya ndugu zetu, ili waamue kati yetu wawili.

38Kwa miaka ishirini nimekuwa nawe. Kondoo wako na mbuzi wako hawakutoa mimba, wala sikula dume yeyote wa kondoo katika wanyama wako.39Kilichoraruliwa na hayawani sikukuletea. Badala yake, nilichukua upotevu huo, kwamba wameibwa mchana au usiku.40Nilikuwepo wakati wote; mchana joto lilinipata, na baridi wakati wa usiku; na sikupata usingizi.41Miaka hii ishirini nimekuwa katika nyumba yako. Nilikufanyia kazi miaka kumi na nne kwa ajili ya binti zako wawili, na miaka sita kwa ajili ya wanyama wako. Umebadili ujira wangu mara kumi.42Isipokuwa Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu, yule Isaka anaye mhofu, amekuwa nami, bila shaka sasa ungenipeleka mikono mitupu. Mungu ameliona teso langu na jinsi nilivyofanya kazi kwa bidii, na hivyo akakukemea usiku wa leo.”

43Labani akajibu na kumwambia Yakobo, “Mabinti hawa ni mabinti zangu, wajukuu ni wajukuu wangu, na wanyama ni wanyama wangu. Yote uyaonayo ni yangu. Lakini nitafanya nini leo kwa hawa binti zangu, au kwa watoto wao waliowazaa?44Hivyo sasa, na tufanye agano, wewe nami, na liwe shahidi kati yangu nawe.”

45Hivyo Yakobo akachukua jiwe na kuliweka kama nguzo.46Yakobo akawambia ndugu zake, “Kusanyeni mawe.” Hivyo wakachukua mawe na kufanya rundo. Kisha wakala pale kati ya lile rundo.47Labani aliliita Yega Saha Dutha, lakini Yakobo akaiita Galedi.48Labani akasema, “Rundo hili ni shahidi kati yangu nawe leo.” Kwa hiyo jina lake likaitwa Galedi.49Inaitwa pia Mispa, kwa sababu Labani alisema, “Yahwe na atuangalie mimi nawe, tunapokuwa hatuonani.50Ikiwa utawatesa binti zangu, au ikiwa utachukua wanawake wengine mbali na binti zangu, japokuwa hakuna mwingine yupo nasi, tazama, Mungu ni shahidi kati yangu nawe.”

51Labani akamwambia Yakobo, “Tazama rundo hili, na tazama nguzo, nililoliweka kati yako nami.52Rundo hili ni shahidi, na nguzo ni shahidi, kwamba sitapita rundo hili kuja kwako, na kwamba wewe hautapita rundo hili kuja kwangu, kwa madhara.53Mungu wa Ibrahimu, na mungu wa Nahori, miungu ya baba zao, waamue kati yetu.” Yakobo akaapa kwa hofu ya Isaka baba yake.

54Yakobo akatoa sadaka juu ya mlima na akawaita ndugu zake kula chakula. Walikula na kukaa usiku kucha juu ya mlima.55Labani akaamka asubuhi na mapema, akawabusu wajukuu zake na binti zake na kuwabariki. Kisha Labani akaondoka na kurudi kwake.

32

1Yakobo pia akaendelea na safari yake, na malaika wa Mungu wakakutana naye.2Yakobo alipowaona, akasema, “Hii ni kambi ya Mungu,” hivyo akapaita mahali pale Mahanaimu.

3Yakobo akatuma wajumbe mbele yake waende kwa Esau ndugu yake katika nchi ya Seiri, katika eneo la Edomu.4Aliwaagiza, kusema, “Hivi ndivyo mtakavyosema kwa bwana wangu Esau: Hivi ndivyo mtumishi wako Yakobo asemavyo: ‘Nimekuwa nikikaa na Labani, naye amekawilisha kurudi kwangu hata sasa.5Nina ng'ombe, punda, na kondoo, wajori na wajakazi. Nimetuma ujumbe huu kwa bwana wangu, ili kwamba nipate kibali mbele zako.’”

6Wajumbe wakarudi kwa Yakobo na kusema, “Tulikwenda kwa Esau ndugu yako. Anakuja kukulaki, na watu 400 pamoja naye.”

7Ndipo Yakobo alipoogopa sana na kutaabika. Hivyo akagawanya watu aliokuwa nao katika kambi mbili, na kondoo pia, mbuzi na ngamia.8Akasema, “Ikiwa Esau ataishambulia kambi moja, ndipo kambi nyingine itakaposalimika.”9Yakobo akasema, “Mungu wa baba yangu Ibrahimu, na Mungu wa baba yangu Isaka, Yahwe, uliyeniambia, ‘Rudi katika nchi yako na kwa jamaa yako, nami nitakustawisha,’10Mimi sistahili matendo yako yote ya agano la uaminifu na ustahilifu wote uliomfanyia mtumishi wako. Kwa maana nilikuwa na fimbo tu nilipovuka mto huu wa Yordani, na sasa nimekuwa matuo mawili.11Tafadhali niokoe kutoka katika mikono ya ndugu yangu, mikono ya Esau, kwa maana namwogopa, kwamba atakuja na kunishambulia mimi na wamama na watoto.12Lakini ulisema, ‘Hakika nitakufanya ufanikiwe. Nitaufanya uzao wako kuwa kama mchanga wa bahari, ambao hauwezi kuhesabika kwa hesabu yake.’”

13Yakobo akakaa pale usiku huo. Akachukua baadhi ya alivyokuwa navyo kama zawadi kwa Esau, ndugu yake:14Mbuzi majike mia mbili na mabeberu ishirini, kondoo majike mia mbili na madume ya kondoo ishirini,15ngamia wakamwao thelathini na wana wao, ng'ombe madume arobaini na madume kumi ya ng'ombe, punda wa kike ishirini na madume yake ishirini.16Akawaweka katika mikono ya watumishi wake, kila kundi peke yake. Akawaambia watumishi, “Tangulieni mbele yangu na mwache nafasi kati ya makundi ya wanyama.”17Akamwagiza mtumishi wa kwanza, akisema, “Ndugu yangu Esau atakapokutana nawe na kukuuliza, akasema, ‘Ninyi ni wa nani? Mnakwenda wapi? Na wanyama hawa mbele yenu ni wa nani?’18Ndipo umwambie, ‘Ni wa mtumishi wako Yakobo. Ni zawadi wanaopelekwa kwa bwana wangu Esau. Na tazama, yeye pia anakuja nyuma yetu.’”

19Yakobo akatoa maelekezo kwa kundi la pili pia, la tatu, na watu wote walioyafuata makundi ya wanyama. Akasema, “Mseme vilevile kwa Esau mtakapokutana naye.20Mnapaswa pia kusema, ‘Mtumwa wako Yakobo pia anakuja nyuma yetu.’” Kwani alifikiri, “Nitamtuliza Esau kwa zawadi nilizozituma mbele yangu. Kisha baadaye, nitakapomwona, bila shaka atanipokea.”21Hivyo zawadi zikatangulia mbele yake. Yeye mwenyewe akakaa kambini usiku huo.

22Yakobo akaamka wakati wa usiku, na akawachukua wakeze, wajakazi wake na wanawe kumi na wawili. Akawawavusha kijito cha Yaboki.23Kwa njia hii akawapeleka kupitia chemichemi pamoja na mali yake yote.24Yakobo akaachwa peke yake, na mtu akashindana naye mpaka alfajiri.25Mtu yule alipoona kwamba hawezi kumshinda, akalipiga paja lake. Paja la Yakobo likateguka alipokuwa akishindana naye.26Yule mtu akasema, “Niache niende, kwani kunakucha.” Yakobo akasema, “Sitakuacha uende mpaka uwe umenibariki.”27Yule mtu akamwuliza, “Jina lako ni nani?” Yakobo akasema, “Yakobo.” Yule mtu akasema,28“Jina lako halitakuwa Yakobo tena, ila Israeli. Kwa kuwa umeshindana na Mungu na wanadamu na umeshinda.”29Yakobo akamwambia, “Tafadhari niambie jina lako.” Akasema, “Kwa nini kuniuliza jina langu?” Kisha akambariki pale.30Yakobo akapaita mahali pale Penieli kwani alisema, “Nimemwona Mungu uso kwa uso, na maisha yangu yamesalimika.”

31Jua likatoka wakati Yakobo anaipita Penieli. Alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake.32Ndiyo maana wana wa Israeli hawali kano ya paja iliyopo katika nyonga ya paja, kwa sababu yule mtu aliziumiza hizo kano alipotegua paja la Yakobo.

33

1Yakobo akainua macho yake na, tazama, Esau alikuwa anakuja, na alikuwa na watu 400 pamoja naye. Yakobo akawagawanya watoto kati ya Lea, Raheli, na wale wajakazi wawili.2Kisha akawaweka wajakazi na wanao mbele, wakifuatiwa na Lea na watoto wake, Raheli na Yusufu wakafuata mwisho wa wote.3Yeye mwenyewe akatangulia mbele yao. Akasujudu mara saba kuelekea ardhi, hata alipomkaribia ndugu yake.4Esau akakimbia kumlaki, akamkumbatia, akakumbatia shingo yake na kumbusu. Kisha wakalia.5Esau alipoinua macho, aliona wanawake na watoto. Akauliza, “Hawa watu pamoja nawe ni kina nani?” Yakobo akasema, “Ni watoto ambao Mungu amempa mtumishi wako kwa neema.”6Kisha wajakazi wakakaribia pamoja na watoto wao, nao wakasujudia.7Akafuata Lea pia na watoto wake wakaja na kusujudia. Mwisho Yusufu na Raheli wakaja na kusujudia.

8Esau akasema, “Unamaanisha nini kwa makundi haya yote niliyokutana nayo?” Yakobo akasema, “Kutafuta kibali mbele za bwana wangu.”9Esau akasema, “Ninayo ya kutosha, ndugu yangu. Tunza uliyonayo kwa ajili yako mwenyewe.”10Yakobo akasema, “Hapana, tafadhali, ikiwa nimeona kibali mbele zako, basi upokee zawadi yangu kutoka mkononi mwangu, na ni kama kuona uso wa Mungu, na umenipokea.11Tafadhali pokea zawadi yangu uliyoletewa, kwa sababu Mungu amenitendea kwa neema, na kwa sababu ninavyo vya kutosha.” Hivyo Yakobo akamsihi, na Esau akamkubali.

12Kisha Esau akasema, “Haya na tuondoke. Nitakutangulia.”13Yakobo akamwambia, “Bwana wangu anajua kwamba watoto ni wadogo, na kwamba kondoo na ng'ombe wananyonyesha ndama wao. Ikiwa watapelekwa kwa haraka hata siku moja, wanyama wote watakufa.14Tafadhali bwana wangu na amtangulie mtumishi wake. Nitasafiri pole pole, kwa kadili ya mifugo iliyo mbele yangu, na kadili ya watoto, hata nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.”15Esau akasema, “Haya nikuachie baadhi ya watu wangu walio pamoja nami.” Yakobo akasema, “Kwa nini kufanya hivyo? Bwana wangu amekuwa mkarimu kwangu kiasi cha kutosha.”16Hivyo Esau akaanza kurudi Seiri.17Yakobo akasafiri kuelekea Sukothi, akajijengea nyumba, na akafanya mazizi kwa ajili ya mifugo wake. Hivyo jina la eneo linaitwa Sukoti.

18Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, akafika salama katika mji wa Shekemu, uliyo katika nchi ya Kanaani. Akapiga kambi karibu na mji.19Kisha akanunua sehemu ya ardhi alipokuwa ameweka hema yake kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia vya fedha.20Akajenga madhabahu pale na kuiita El Elohe Israeli.

34

1Basi Dina, Binti wa Lea aliyemzalia Yakobo, akaenda kuwaona wasichana wa nchi.2Shekemu mwana wa Hamori Mhivi, mwana mfalme wa nchi, akamwona na akamkamata kwa nguvu na kulala naye.3Akavutiwa na Dina, binti Yakobo. Akampenda msichana na kuongea naye kwa upole.4Shekemu akamwambia Hamori baba yake, kusema, “Nipe msichana huyu kuwa mke wangu.”

5Basi Yakobo akasikia kwamba alikuwa amemchafua Dina binti yake. Wanawe walikuwa pamoja na wanyama uwandani, hivyo Yakobo akawangoja hata walipokuja.

6Hamori baba wa Shekemu akaenda kuongea na Yakobo.7Wana wa Yakobo waliposikia neno hili wakaja kutoka uwandani. Watu hawa walichukizwa sana. Walikasirika sana kwa sababu alikuwa amemwaibisha Israeli kwa kumlazimisha binti wa Yakobo, kwa maana jambo kama hilo halikupasa kutendeka.

8Hamori akaongea nao, akisema, “Shekemu mwanangu anampenda binti yenu. Tafadhali mpeni kuwa mke wake.9Mwoane nasi, tupeni binti zenu, na mjichukulie binti zetu kwa ajili yenu wenyewe.10Mtaishi nasi, na nchi itakuwa wazi kwa ajili yenu kufanya biashara humo, na kupata mali.”

11Shekemu akamwambia baba yake na ndugu zake, “Na nione kibali machoni penu, na chochote mtakachoniambia nitatoa.12Niambieni kiasi kikubwa chochote cha mahari na zawadi kama mtakavyo, nami nitatoa chochote msemacho, lakini mnipe msichana kuwa mke wangu.”

13Wana wa Yakobo wakamjibu Shekemu na Hamori baba yake kwa hila, kwa sababu Shekemu alikuwa amemnajisi Dina dada yao.14Wakawambia, “Hatuwezi kufanya jambo hili, kumpa dada yetu mtu yeyote ambaye hajatairiwa; kwani hiyo ni aibu kwetu.15Kwa sharti hili peke yake tutakubaliana nanyi: iwapo mtatairiwa kama sisi, ikiwa kila mtu mme miongoni mwenu atatairiwa.16Ndipo tutakapowapa binti zetu, nasi tutachukua binti zenu kwetu sisi wenyewe, na tutaishi nanyi na kuwa wamoja.17Lakini kama hamtusikiliza na kutairiwa, ndipo tutakapo mchukua dada yetu na kuondoka.

18Maneno yao yakawafurahisha Hamori na Shekemu mwanaye.19Kijana hakukawia kufanya walichokisema, kwa maana alipendezwa na binti wa Yakobo, na kwa sababu alikuwa mtu aliyeheshimiwa sana katika nyumba ya babaye.20Hamori na Shekemu mwanaye wakaenda katika lango la mji wao na kuongea na watu wa mji, kusema,21“Watu hawa wanaamani nasi, hivyo na waishi katika nchi na kufanya biashara humo kwa maana, kweli, nchi ni kubwa ya kuwatosha. Haya na tuwachukue binti zao kuwa wake, nasi tuwape binti zetu.22Kwa sharti hili pekee watu hawa wanakubali kuishi nasi na kuwa wamoja: ikiwa kila mwanamme miongoni mwetu atatahiriwa, kama wao.23Je wanyama wao na vitu vyao - wanyama wao wote kuwa wetu? Haya na tukubaliane nao, nao wataishi kati yetu.”24Watu wote wa mji wakamsikiliza Hamori na Shekemu, mwanaye. Kila mwanamme akatahiriwa.

25Katika siku ya tatu, walipokuwa katika maumivu bado, wawili wa wana wa Yakobo (Simoni na Lawi, kaka zake Dina), wakachukua kila mmoja upanga wake na kuushambulia mji ambao ulikuwa na uhakika wa ulinzi wake, nao wakawaua wanaume wote.26Wakamwua Hamori na Shekemu kwa makali ya upanga. Wakamchukua Dina kutoka nyumba ya Shekemu na kuondoka.27Wale wana wengine wa Yakobo wakaja kwa maiti na kuuteka nyara mji, kwa sababu watu wale walikuwa wamemnajisi dada yao.28Wakachukua makundi yao ya kondoo, mbuzi, punda, na kila kitu ndani ya mji na viunga vyake29utajiri wote. Watoto na wake zao wote, wakawachukua. Hata wakachukua kila kitu kilichokua katika nyumba.

30Yakobo akawaambia Simoni na Lawi, “Mmeleta shida juu yangu, kunifanya ninuke kwa wenyeji wa nchi, Wakanaani na Waperizi. Mimi nina watu wachache. Ikiwa watajikusanya pamoja kinyume changu na kunishambulia.”31Lakini Simoni na Lawi wakasema, “Je Shekemu alipaswa kumtendea dada yetu kama kahaba?”

35

1Mungu akamwambia Yakobo, “Inuka, panda kwenda Betheli, na ukae pale. Unijengee madhabahu pale, niliyekutokea pale ulipomkimbia Esau kaka yako.”2Kisha Yakobo akawaambia nyumba yake na wote aliokuwa nao, “Wekeni mbali miungu yote ya kigeni iliyo kati yenu, jitakaseni wenyewe, na kubadili mavazi yenu.3Kisha tuondoke na kwenda Betheli. Nitajenga pale madhabahu kwa Mungu, aliyenijibu katika siku ya shida yangu, naye amekuwa pamoja nami kila nilikokwenda.”4Hivyo wakampa Yakobo miungu yote ya kigeni iliyokuwa mikononi mwao, na heleni zilizokuwa katika masikio yao. Yakobo akazifukia chini ya mwaloni uliokuwa karibu na Shekemu.

5Kwa kadiri walivyo safiri, Mungu akaifanya miji yote iliyokuwa karibu nao kuhofu, hivyo watu hao hawakuwafuatia wana wa Yakobo.6Hivyo Yakobo akafika Luzu (ndiyo Betheli), ulioko katika nchi ya Kanaani, yeye na watu wote aliokuwa nao.7Alijenga madhabahu na kuliita eneo hilo El Betheli, kwa sababu Mungu alikuwa amejifunua kwake, alipokuwa akimkimbia ndugu yake.

8Debora, mlezi wa Rebeka, akafa. Akazikwa chini kutoka Betheli chini ya mwaloni, hivyo ikaitwa Aloni Bakuthi.

9Yakobo alipokuja kutoka Padani Aramu, Mungu akamtokea tena na kumbariki.10Mungu akamwambia, “Jina lako ni Yakobo, lakini jina lako halitakuwa Yakobo tena. Jina lako litakuwa Israeli.” Hivyo Mungu akamwita jina lake Israeli.11Mungu akamwambia, “Mimi ni Mungu Mwenyezi, Uwe mwenye kuzaa na kuongezeka. Taifa na wingi wa mataifa watakujia, na wafalme watatoka miongoni mwa uzao wako.12Nchi ambayo nilimpa Ibrahimu na Isaka, nitakupa wewe. Nami nitaupa pia uzao wako baada yako nchi hii.”

13Mungu akapanda kutoka mahali alipoongea naye.14Yakobo akaweka nguzo katika eneo ambalo Mungu alikuwa ameongea naye, nguzo ya jiwe. Akamimina juu yake sadaka ya kinywaji na akamimina mafuta juu yake.15Yakobo akaiita sehemu Mungu aliyoongea naye, Betheli.

16Wakaendelea na safari kutoka Betheli. Walipokuwa kitambo kabla ya kufika Efrathi, Raheli akashikwa na uchungu.17Akawa na uchungu mzito. Alipokuwa katika uchungu mzito zaidi, mkunga akamwambia, “Usiogope, kwani sasa utapata mtoto mwingine wa kiume.”18Hata alipokaribia kufa, kwa pumzi yake ya mwisho akamwita jina lake Benoni, lakini baba yake akamwita jina lake Benjamini.

19Raheli akafa na kuzikwa katika njia iendayo Efrathi (ndio Bethlehemu).20Yakobo akaweka nguzo katika kaburi lake. Ndiyo alama ya kaburi la Raheli hata leo.

21Israeli akaendelea na safari na akaweka hema yake kuvuka mnara wa walinzi wa kondoo.22Yakobo alipokuwa akiishi katika nchi hiyo, Rubeni akalala na Bilha suria wa baba yake, na Israeli akasikia kuhusu hilo. Basi Yakobo alikuwa na wana kumi na wawili.23Wanawe kwa Lea walikuwa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo, na Simoni, Lawi, Yuda, Isakari, na Zabuloni.24Wanawe kwa Raheli walikuwa Yusufu na Benjamini.25Wanawe kwa Bilha, mjakazi wa Raheli walikuwa Dani na Naftali.26Wana wa Zilpa, mjakazi wa Lea, walikuwa Gadi na Asheri. Hawa wote walikuwa wana wa Yakobo waliozaliwa kwake huko Padani Aramu.

27Yakobo akaja kwa Isaka, baba yake, huko Mamre katika Kiriathi Arba (jina sawa na Hebroni), alipoishi Ibrahimu na Isaka.28Isaka akaishi miaka 180.29Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho na akafa, na akakusanywa kwa wahenga wake, na mtu mzee amejaa siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

36

1Hivi ndivyo vizazi vya Esau (aliyeitwa pia Edom).2Esau akachukua wakeze kutoka kwa Wakanaani. Hawa walikuwa wake zake: Ada binti Eloni Mhiti; Oholibama binti Ana, mjukuu wa Zibeoni Mhivi; na3Basemathi, binti Ishmaeli, dada wa Nebayothi.4Ada akamzaa Elifazi kwa Esau, na Basemathi akamzaa Reueli.5Oholibama akamzaa Yeushi, Yalamu, na Kora. Hawa walikuwa wana wa Esau waliozaliwa kwake katika nchi ya Kanaani.

6Esau akawachukua wakeze, wanawe, binti zake, na watu wote wa nyumba yake, mifugo wake - wanyama wake wote, na mali yake yote, aliyokuwa amekusanya katika nchi ya Kanaani, na akaenda katika nchi iliyoko mbali kutoka kwa Yakobo nduguye.7Alifanya hivi kwa sababu mali zao zilikuwa nyingi sana kwa wao kuishi pamoja. Nchi waliyokuwa wamekaa isingeweza kuwafaa kwa mifugo yao.8Hivyo Esau, aliyejulikana pia kama Edomu, akakaa katika nchi ya kilima Seiri.

9Hivi ndivyo vizazi vya Esau, babu wa Waedomu katika nchi ya mlima Seiri.10Haya yalikuwa majina ya wana wa Esau: Elifazi mwana wa Ada, mkewe Esau; Reueli mwana wa Basemathi, mkewe Esau.11Wana wa Elifazi walikuwa Temani, Omari, Zefo, Gatamu, na Kenazi.12Timna, suria wa Elifazi, mwana wa Esau, akamzaa Amaleki. Hawa walikuwa wajukuu wa Ada, mkewe Esau.

13Hawa walikuwa wana wa Reueli: Nahathi, Zera, Shama, na Miza. Hawa walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.

14Hawa walikuwa wana wa Oholibama, mkewe Esau, aliyekuwa binti Ana na mjukuu wa Zibeoni. Alimzalia Esau Yeushi, Yalamu, na Kora.

15Hizi zilikuwa koo kati ya vizazi vya Esau: uzao wa Elifazi, mzaliwa wa kwanza wa Esau: Temani, Omari, Zefo, Kenazi, Kora,16Gatamu, na Amaleki. Hivi vilikuwa vizazi vya koo kutoka kwa Elifazi katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Ada.

17Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli, mwana wa Esau: Nahathi, Zera, Shama, Miza. Hizi zilikuwa koo kutoka kwa Reueli katika nchi ya Edomu. Walikuwa wajukuu wa Basemathi, mkewe Esau.

18Hizi zilikuwa koo za Oholibama, mkewe Esau: Yeushi, Yalamu, Kora. Hizi ni koo zilizotoka kwa Oholibama mkewe Esau, binti Ana.

19Hawa walikuwa wana wa Esau na koo zao.

20Hawa walikuwa wana wa Seiri Mhori, wenyeji wa nchi hiyo: Lotani, Shobali, Zibeoni, Ana,21Dishoni, Ezeri, na Dishani. Hizi zilikuwa koo the Wahori, wenyeji wa Seiri katika nchi ya Edomu.

22Wana wa Lotani walikuwa Hori na Hemani, na Timna alikuwa dada wa Lotani.

23Hawa walikuwa wana wa Shobali: Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu.

24Hawa walikuwa wana wa Zibeoni: Aia na Ana. Huyu ndiye Ana aliyeona chemichemi za moto nyikani, alipokuwa akichunga punda wa Zibeoni babaye.

25Hawa walikuwa watoto wa Ana: Dishoni na Oholibama, binti Ana.

26Hawa walikuwa wana wa Dishoni: Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.

27Hawa walikuwa wana wa Ezeri: Bilhani, Zaavani, na Akani.

28Hawa walikuwa wana wa Dishani: Uzi na Arani.

29Hizi zilikuwa koo za Wahori: Lotani, Shobali, Zibeoni, na Ana,30Dishoni, Ezeri, Dishani: hizi zilikuwa koo za Wahori, kulingana na ukoo ulivyoorodheshwa katika nchi ya Seiri.

31Hawa walikuwa wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kumilika juu ya Waisraeli:32Bela mwana wa Beori, alitawala huko Edomu, na jina la mji wake lilikuwa Dinhaba.

33Bela alipofariki, kisha Yobabu mwana wa Zera kutoka Bozra, akatawala mahali pake.

34Yobabu alipofariki, Hushamu aliyekuwa wa nchi ya Watemani, akatawala mahali pake.

35Hushamu alipofariki, Hadadi mwana wa Bedadi aliyewashinda Wamidiani katika nchi ya Moabu, akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Avithi.

36Hadadi alipofariki, kisha Samla wa Masreka akatawala mahali pake.

37Samla alipofariki, kisha Shauli wa Rehobothi kando ya mto alitawala mahali pake.

38Shauli alipofariki, kisha Baali Hanani mwana wa Akbori akatawala mahali pake.

39Baali Hanani mwana wa Akbori, alipokufa, kisha Hadari akatawala mahali pake. Jina la mji wake lilikuwa Pau. Jina la mkewe lilikuwa Mehetabeli, binti Matredi, mjukuu wa Me Zahabu.

40Haya ndiyo yalikuwa majina ya wakuu wa koo kutoka uzao wa Esau, kwa kufuata koo zao na maeneo yao, kwa majina yao: Timna, Alva, Yethethi,41Oholibama, Ela, Pinoni,42Kenazi, Temani, Mbza,43Magdieli, na Iramu. Hawa walikuwa wakuu wa ukoo wa Edomu, kwa kufuata makao yao katika nchi waliyomiliki. Nao ni Esau, baba wa Waedomu.

37

1Yakobo akaishi katika nchi aliyokaa babaye, katika nchi ya Kanaani.2Haya ndiyo matukio yaliyomhusu Yakobo. Yusufu, aliyekuwa kijana wa miaka kumi na saba, alikuwa akilichunga kundi pamoja na ndugu zake. Alikuwa pamoja na wana wa Bilha na pamoja na wana wa Zilpa, wake wa baba yake. Yusufu akaleta taarifa yao mbaya kwa baba yao.

3Basi Israeli akampenda Yusufu kuliko wanawe wote kwa sababu alikuwa mwana wa uzee wake. Akamshonea vazi zuri.4Ndugu zake wakaona kwamba baba yao alimpenda sana kuliko ndugu zake wote. Wakamchukia na hawakuongea naye vema.

5Yusufu akaota ndoto, na akawambia ndugu zake. Wakamchukia zaidi.6Aliwambia, “Tafadhali sikilizeni ndoto hii niliyoiota.7Tazama, tulikuwa tukifunga miganda ya nafaka shambani na tazama, mganda wangu ukainuka na kusimama wima, na tazama, miganda yenu ikasogea na kuuinamia mganda wangu.”8Ndugu zake wakamwambia, “Je ni kweli utatutawala? Je utatutawala juu yetu?” Hata wakamchukia zaidi kwa ajili ya ndoto zake na maneno yake.

9Akaota ndoto nyingine na kuwasimulia ndugu zake. Alisema, “Tazama, nimeota ndoto nyingine: Jua na mwezi na nyota kumi na moja ziliniinamia.”10Akamwambia baba yake vile vile alivyowambia ndugu zake, na baba yake akamkemea. Akamwambia, “Je umeota ndoto ya namna gani hii? Je mama yako na mimi na ndugu zako kweli tutakuja kukuinamia mpaka chini?”11Ndugu zake wakamwonea wivu, lakini baba yake akaliweka jambo hilo moyoni.

12Ndugu zake wakaenda kulichunga kundi la baba yao huko Shekemu.13Israeli akamwambia Yusufu, “Je ndugu zako hawalichungi kundi huko Shekemu? Njoo, nami nitakutuma kwao.” Yusufu akamwambia, “Nipo tayari.”14Akamwambia, “Basi nenda, uwaone ndugu zako na kundi wanaendeleaje, na uniletee neno.” Hivyo Yakobo akamtuma kutoka katika bonde la Hebroni, na Yusufu akaenda Shekemu.15Mtu mmoja akamwona Yusufu. Tazama, Yusufu alikuwa akizunguka kondeni. Yule mtu akamwuliza, “Unatafuta nini?”16Yusufu akamwambia, “Nawatafuta ndugu zangu. Tafadhali, niambie, wanalichunga wapi kundi.”17Yule mtu akasema, “Waliondoka mahali hapa, kwa maana niliwasikia wakisema, ‘Haya twende Dothani.’” Yusufu akawafuata ndugu zake na kuwaona huko Dothani.18Wakamwona kutokea mbali, na kabla hajawakaribia, wakapanga njama ya kumwua.19Ndugu zake wakaambiana wao kwa wao, “Tazama, mwotaji anakaribia.20Njooni sasa, na tumwue na kumtupa katika mojawapo ya mashimo haya. Nasi tutasema, ‘Mnyama mkali amemrarua.’ Nasi tutaona ndoto zake zitakuwaje.”

21Rubeni alilisikia hilo na kumwokoa kutoka katika mikono yao. Alisema, “Tusiuondoe uhai wake.”22Rubeni aliwaambia, “Msimwage damu. Mtupeni katika shimo hili lililopo nyikani, lakini msiweke mikono yenu juu yake” - ili kwamba aweze kumwokoa katika mikono yao na kumrudisha kwa baba yake.

23Ikawa Yusufu alipowafikia ndugu zake, walimvua vazi lake zuri.24Wakamchukua na kumtupa shimoni. Shimo lilikuwa tupu bila maji.

25Wakakaa chini kula mkate. Walipoinua macho yao na kuangalia, na, tazama, msafara wa Waishmaeli ulikuwa ukija kutoka Gileadi, pamoja na ngamia wao waliochukua viungo, malhamu na manemane. Walikuwa wakisafiri kuvichukua kuelekea Misri.26Yuda akawaambia ndugu zake, “Ni faida gani kama tutamwua ndugu yetu na kufunika damu yake?27Haya, na tumwuze kwa Waishmaeli na wala tusiweke mikono yetu juu yake. Kwani yeye ni ndugu yetu, nyama yetu.” Ndugu zake wakamsikiliza.

28Wafanyabiashara wa Kimidiani wakapita. Ndugu zake wakamwinua na kumtoa Yusufu shimoni. Wakamwuza Yusufu kwa Waishmaeli kwa vipande ishirini vya fedha. Waishmaeli wakamchukua Yusufu mpaka Misri.

29Rubeni akarudi kwenye shimo, na, tazama, Yusufu hakuwemo shimoni. Akararua mavazi yake.30Akarudi kwa ndugu zake na kusema, “Kijana yuko wapi? Na mimi, je niende wapi?”

31Wakachinja mbuzi na kisha wakalichukua vazi la Yusufu na kulichovya katika damu.32Kisha wakalipeleka kwa baba yao na kusema, “Tumeiona hii. Tafadhali angalia kama ni vazi la mwanao au hapana.”33“Yakobo akaitambua na kusema, “Ni nguo ya mwanangu. Mnyama wa mwitu amemrarua. Bila shaka Yusufu ameraruliwa katika vipande.”

34Yakobo akararua mavazi yake na kuvaa mavazi ya magunia katika viuno vyake. Akaomboleza kwa ajili ya mwanawe siku nyingi.35Wanawe na binti zake wote wakainuka na kumfariji, lakini alikataa kufarijiwa. Akasema, “Hakika nitashuka kuzimu nikimwombolezea mwanangu.” Babaye akamlilia.

36Wamidiani wakamwuza huko Misri kwa Potifa, afisa wa Farao, kepteni wa walinzi.

38

1Ikawa wakati ule Yuda akawaacha ndugu zake na kukaa na Mwadulami fulani, jina lake Hira.2Pale akakutana na binti Mkanaani jina lake Shua. Akamwoa na kulala naye.3Akawa mjamzito na kuzaa mwana. Akaitwa Eri.4Akawa mjamzito tena na kuzaa mwana tena. Akamwita jina lake Onani.5Akazaa mwana mwingine akamwita jina lake Shela. Alikuwa huko Kezibu alipomzaa.

6Yuda akaona mke kwa ajili ya Eri, mzaliwa wake wa kwanza. Jina lake Tamari.7Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mwovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua.8Yuda akamwambia Onani, “Lala na mke wa nduguyo. Fanya wajibu wa shemeji kwake, na umwinulie nduguyo mwana.”9Onani alijua kwamba mtoto asingekuwa wake. Pindi alipolala na mke wa kaka yake, alimwaga mbegu juu ya ardhi ili kwamba asimpatie nduguye mtoto.10Alilolifanya lilikuwa ovu mbele za Yahwe. Yahwe akamwua pia.

11Kisha Yuda akamwambia Tamari, mkwewe, “Ukakae mjane katika nyumba ya baba yako hadi Shela, mwanangu, atakapokua.” Kwani aliogopa, “Asije akafa pia, kama nduguze.” Tamari akaondoka na kuishi katika nyumba ya babaye.

12Baada ya muda mrefu, binti Shua, mkewe Yuda, alikufa. Yuda akafarijika na kwenda kwa wakatao kondoo wake manyoya huko Timna, yeye na rafiki yake, Hira Mwadulami.13Tamari akaambiwa, “Tazama, mkweo anakwenda Timna kukata kondoo wake manyoya.”14Akavua mavazi yake ya ujane na akajifunika kwa ushungi. Akakaa katika lango la Enaimu, lililoko kando ya njia iendayo Timna. Kwa maana aliona kwamba Shela amekua lakini hakupewa kuwa mke wake.15Yuda alipomwona alidhani ni kahaba kwa maana alikuwa amefunika uso wake.16Akamwendea kando ya njia na kusema, “Njoo, tafadhali uniruhusu kulala nawe” - kwani hakujua kwamba alikuwa ni mkwewe - naye akasema, “Utanipa nini ili ulale nami?17Akasema, “Nitakuletea mwana mbuzi wa kundi.” Akasema, “Je utanipa rehani hata utakapo leta?”18Akasema, “Nikupe rehani gani?” Naye akasema, “Mhuri wako na mshipi, na fimbo iliyo mkononi mwako.” Akampa na kulala naye. Akawa mjamzito.19Akaamka na kuondoka. Akavua ushungi wake na kuvaa vazi la ujane wake.

20Yuda akatuma mwana mbuzi kutoka kundini kwa mkono wa rafiki yake Mwadulami ili aichukue rehani kutoka katika mkono wa mwanamke, lakini hakumwona.21Kisha Mwadulami akauliza watu wa sehemu hiyo, “Yupo wapi kahaba aliyekuwa Enaimu kando ya njia?” Wakasema, hapajawahi tokea kahaba hapa.”22Akarudi kwa Yuda na kusema, “Sikumwona. Pia watu wa eneo hilo wamesema, ‘Hajawahi kuwapo kahaba hapa.’”23Yuda akasema, “Mwache akae na vitu, tusije tukaaibika. Hakika, nimemletea mwanambuzi, lakini hukumwona.”

24Ikawa baada ya miezi mitatu Yuda akaambiwa, “Tamari mkweo amefanya ukahaba, na kwa hakika, yeye ni mjamzito.” Yuda akasema, “Mleteni hapa ili achomwe.”

25Alipoletwa nje, alipeleka ujumbe kwa mkwewe, “Mimi ni mjamzito kwa mtu mwenye vitu hivi.” Akasema, “Tambua tafadhali, mhuri huu na mshipi na fimbo ni vya nani.”26Yuda akavitambua na kusema, “Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwani sikumpa Shela, mwanangu awe mme wake.” Hakulala naye tena.

27Muda wake wa kujifungua ukafika, tazama, mapacha walikuwa tumboni mwake.28Ikawa alipokuwa akijifungua mmoja akatoa mkono nje, na mkunga akachukua kitambaa cha rangi ya zambarau na kukifunga katika mkono wake na kusema, “Huyu ametoka wa kwanza.”29Ikawa aliporudisha mkono wake, tazama, ndugu yake akatoka kwanza. Mkunga akasema, “Umetokaje” Na akaitwa Peresi.30Kisha ndugu yake akatoka, akiwa na utepe wa zambarau juu ya mkono wake, naye akaitwa Zera.

39

1Yusufu akaletwa Misri. Potifa, aliyekuwa afisa wa Farao mkuu wa walinzi wa Misri, akamnunua kutoka kwa Waishmaeli, waliokuwa wamempeleka pale.2Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na akawa mtu aliyefanikiwa. Aliishi katika nyumba ya Mmisri bwana wake.3Bwana wake akaona kwamba Yahwe alikuwa pamoja naye na kwamba Yahwe alifanikisha kila kitu alichokifanya.4Yusufu akapata kibali mbele zake. Akamtumikia Potifa. Potifa akamfanya msimamizi juu ya nyumba yake, na kila alichokimiliki, akakiweka chini ya uangalizi wake.5Ikawa alipomfanya msimamizi juu ya nyumba yake na juu ya kila kitu alichomiliki, Yahwe akaibariki nyumba ya Mmisri kwa sababu ya Yusufu. Baraka za Yahwe zilikuwa juu ya kila kitu alichokuwa nacho Potifa nyumbani na shambani.6Potifa akaweka kila alichokuwa nacho chini ya uangalizi wa Yusufu. Hakuwa na haja ya kufikiri juu ya lolote isipokuwa chakula alichokula tu. Basi Yusufu alikuwa kijana mzuri na wa kuvutia.7Ikawa baada ya hayo mke wa bwana wake akamtamani Yusufu. Akamwambia, “Lala nami.”8Lakini yeye alikataa na kumwambia mke wa bwana wake, “Tazama, bwana wangu haangalii chochote nikifanyacho nyumbani, na ameweka kila kitu anachokimiliki chini ya uangalizi wangu.9Hakuna mtu aliye mkuu katika nyumba hii kuliko mimi. Hajanizuilia chochote isipokuwa wewe, kwa sababu wewe ni mkewe. Ni kwa namna gani basi naweza kufanya uovu mkuu namna hii na kumtenda dhambi Mungu?”10Akamwambia Yusufu siku baada ya siku, lakini yeye akakataa kulala naye wala kuwa naye.

11Ikawa siku moja aliingia ndani kufanya kazi yake. Hakuna mtu yeyote wa nyumbani aliyekuwepo pale ndani.12Akashika nguo zake na kusema, “Lala nami.” Akaacha nguo zake mikononi mwake, akakimbia, na kutoka nje.13Ikawa, alipoona kwamba ameziacha nguo zake mikononi mwake na kwamba amekimbia nje,14akawaita watu wa nyumbani mwake na kuwaambia, “Tazama, Potifa ameleta Mwebrania huyu kutudhihaki. Aliingia kulala nami, na nikapiga kelele.15Ikawa aliponisikia nikipiga kelele, akaniacha na nguo yake, akakimbia, na kutoka nje.”16Akaweka nguo zake karibu naye hata bwana yake alipokuja nyumbani.17Akamwambia maelelezo haya, “Yule mtumishi Mwebrania uliyemleta kwetu, aliingia kunidhihaki.18Ikawa nilipopiga kelele, akaacha nguo yake kwangu akakimbia nje.”19Ikawa, bwana wake aliposikia maelezo aliyoambiwa na mkewe, “Hivi ndivyo mtumishi wako alivyonitenda,” alikasirika sana.20Bwana wa Yusufu akamchukua na kumweka gerezani, mahali walipowekwa wafungwa wa mfalme. Akawa pale kifungoni.

21Lakini Yahwe alikuwa pamoja na Yusufu na kumwonyesha uaminifu wa agano. Akampa kibali mbele ya mlinzi wa gereza.22Mlinzi wa gereza akawaweka mikononi mwa Yusufu wafungwa wote waliokuwa gerezani. Chochote walichokifanya, kilikuwa chini ya uangalizi wa Yusufu.23Mlinzi wa gereza hakuwa na wasiwasi juu ya chochote kilichokuwa mkononi mwake, kwa sababu Yahwe alikuwa pamoja naye. Yahwe akafanikisha kila alichokifanya.

40

1Ikawa baada ya mambo haya, mnyweshaji wa mfalme wa Misri na mwokaji wa mfalme walimkosea bwana wao, mfalme wa Misri.2Farao akawakasirikia hawa maafisa wawili, mkuu wa wanyweshaji na mkuu wa waokaji.3Akawaweka katika lindo katika nyumba ya kapteni wa walinzi, katika gereza lile Yusufu alimofungwa.4Kapteni wa walinzi akamweka Yusufu kuwa mtumishi wao. Walikaa kifungoni kwa muda fulani.

5Wote wakaota ndoto - mnyweshaji na mwokaji wa mfalme wa Misri waliokuwa wamefungwa gerezani - kila mmoja akaota ndoto usiku huo huo, na kila ndoto ilikuwa na tafsiri yake.

6Yusufu akaja kwao asubuhi na kuwaona. Tazama, walikuwa na huzuni.7Akawauliza maafisa wa Farao waliokuwa pamoja naye kifungoni katika nyumba ya bwana wake, kusema, “Kwa nini leo mnaoneka wenye huzuni?”8Wakamwambia, “Sisi wote tumeota ndoto na hakuna wakuitafsiri.” Yusufu akawaambia, “Je tafsiri haitoki kwa Mungu? Niambieni, tafadhali.”9Mkuu wa wanyweshaji akamwambia Yusufu ndoto yake. Akamwambia, “Katika ndoto yangu, tazama, kulikuwa na mzabibu mbele yangu.10Na kulikuwa na matawi matatu katika mzabibu huo. Ulipochipua, ukachanua maua na kuzaa vichala vya zabibu.11Kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu. Nikachukua zabibu na kuzikamua katika kikombe cha Farao, na kukiweka kikombe katika mkono wa Farao.”12Yusufu akamwambia, “Tafsiri yake ni hii. Yale matawi matatu ni siku tatu.13Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako na kukurudisha katika nafasi yako. Utakiweka kikombe cha Farao katika mkono wake, kama ulivyokuwa ulipokuwa mnyweshaji wake.14Lakini unikumbuke ukifanikiwa, na unionyeshe wema. Unitaje kwa Farao na kuniondoa hapa gerezani.15Maana hakika nilitekwa kutoka katika nchi ya Waebrania. Na hapa sijafanya chochote kinachonipasa niwekwe gerezani.”

16Mkuu wa waokaji alipoona kwamba tafsiri ilikuwa ya kuvutia, akamwambia Yusufu, “Mimi pia niliota ndoto, na tazama, vikapu vitatu vya mikate vilikuwa juu ya kichwa changu.17Katika kikapu cha juu kulikuwa na kila aina za bidhaa ya kuokwa kwa Farao, lakini ndege wakavila ndani ya kikapu juu ya kichwa changu.”18Yusufu akajibu na kusema, “Tafsiri ni hii. Vikapu vitatu ni siku tatu.19Ndani ya siku tatu Farao atakiinua kichwa chako kutoka kwako na atakutundika juu ya mti. Ndege watakula mwili wako.”

20Ikawa siku ya tatu ambayo ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Farao. Akafanya sherehe kwa watumishi wake wote. “Akakiinua juu,” kichwa cha mkuu wa wanyweshaji na kichwa cha mkuu wa waokaji, kati ya watumishi wake.21Akamrudisha mkuu wa wanyweshaji katika majukumu yake, na akakiweka tena kikombe katika mkono wa Farao.22Lakini akamtundika mkuu wa waokaji, kama Yusufu alivyokuwa amewatafsiria.

23Hata hivyo mkuu wa wanyweshaji hakukumbuka kumsaidia Yusufu. Badala yake, alimsahau.

41

1Ikawa mwishoni mwa miaka miwili mizima Farao akaota ndoto.2Tazama, alikuwa amesimama kando ya mto Nile. Tazama, ng'ombe saba wakatoka katika mto Nile, wakupendeza na wanene, na wakajilisha katika nyasi.3Tazama, ng'ombe wengine saba wakatoka katika Nile baada yao, wasiopendeza na wamekondeana. Wakasimama ukingoni mwa mto kando ya wale ng'ombe wengine.4Kisha wale ng'ombe wasiopendeza na waliokonda wakawala wale waliokuwa wanapendeza na walionenepa.

5Kisha Farao akaamka. Kisha akalala na kuota mara ya pili. Tazama, masuke saba ya nafaka yalichipua katika mche mmoja, mema na mazuri.6Tazama, masuke saba, membamba na yaliyokaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.7Masuke membamba yakayameza yale masuke saba mema yote. Farao akaamka, na, tazama, ilikuwa ni ndoto tu.

8Ikawa wakati wa asubuhi roho yake ikafadhaika. Akatuma na kuwaita waganga na wenye hekima wote wa Misri. Farao akawasimulia ndoto zake, lakini hakuna aliyeweza kumtafsiria Farao.

9Kisha mkuu wa wanyweshaji akamwambia Farao, “Leo ninayafikiri makosa yangu.10Farao aliwakasirikia watumishi wake, na kutuweka kifungoni katika nyumba ya kapteni wa walinzi, mkuu wa waokaji na mimi.11Tuliota ndoto usiku huo mmoja, yeye na mimi. Kila mmoja aliota kwa kadiri ya tafsiri yake.12Pamoja nasi kulikuwa na kijana Mwebrania, mtumishi wa kapteni wa walinzi. Tulimwambia na akatutafsiria ndoto zetu. Alitutafsiria kila mmoja wetu kulingana na ndoto yake.13Ikawa kama alivyotutafsiria, ndivyo ilivyokuwa. Farao alinirudisha katika nafasi yangu, lakini akamtundika yule mwingine.”

14Ndipo Farao alipotuma na kumwita Yusufu. Kwa haraka wakamtoa gerezani. Akajinyoa mwenyewe, akabadili mavazi yake, na akaingia kwa Farao.15Farao akamwambia Yusufu, “Nimeota ndoto, lakini hakuna wa kuitafsiri. Lakini nimesikia kuhusu wewe, kwamba unaposikia ndoto unaweza kuitafsiri.”16Yusufu akamjibu Farao, kusema, “Siyo katika mimi. Mungu atamjibu Farao kwa uhakika.”

17Farao akamwambia Yusufu, “Katika ndoto yangu, tazama, nilisimama katika ukingo wa Nile.18Tazama, ng'ombe saba wakatoka ndani ya mto Nile, wanene na wakuvutia, nao wakajilisha katika nyasi.19Tazama, ng'ombe wengine saba wakapanda baada yao, dhaifu, wabaya, na wembaba. Sijawahi kuona wabaya kama hao katika nchi yote ya Misri.20Wale ng'ombe wembamba na wabaya wakawala wale ng'ombe saba na wanene.21Walipokuwa wamemaliza kuwala wote, haikujulikana kama walikuwa wamewala, kwani walibaki wabaya kama mwanzo. Kisha nikaamka.

22Niliona katika ndoto yangu, na tazama, masuke saba yakatoka katika bua moja, jema na limejaa.23Tazama, masuke saba zaidi, yaliyonyauka, membamba na yamekaushwa na upepo wa mashariki, yakachipua baada yake.24Yale masuke membamba yakayameza masuke saba mema. Niliwaambia waganga ndoto hizi, lakini hakuna aliyeweza kunielezea.”

25Yusufu akamwambia Farao, “Ndoto za Farao ni moja. Mungu amemwambia Farao kuhusu jambo analokwenda kulifanya.26Wale ng'ombe saba wema ni miaka saba, na masuke saba mema ni miaka saba. Ndoto ni moja.27Na wale ng'ombe saba wembamba na wabaya waliokuja baadaye ni miaka saba, na pia masuke saba membamba yaliyokaushwa na upepo wa mashariki itakuwa miaka saba ya njaa.28Hilo ni jambo nililomwambia Farao. Mungu amemfunulia Farao jambo analokwenda kulifanya.29Tazama, miaka saba yenye utele mwingi inakuja katika nchi yote ya Misri.30Na miaka saba ya njaa itakuja baada yake, na utele wote katika nchi ya Misri utasahaulika, na njaa itaiharibu nchi.31Utele hautakumbukwa katika nchi kwa sababu ya njaa itakayofuata, kwa kuwa itakuwa kali sana.32Kwamba ndoto ilijirudia kwa Farao sababu ni kwamba jambo hili limeanzishwa na Mungu, na Mungu atalitimiza hivi karibuni.

33Basi Farao atafute mtu mwenye maarifa na busara, na kumweka juu ya nchi ya Misri.34Farao na afanye hivi: achague wasimamizi juu ya nchi. Na wachukue sehemu ya tano ya mazao ya Misri katika miaka saba ya shibe.35Na wakusanye chakula chote cha hii miaka myema ijayo na kuitunza nafaka chini ya mamlaka ya Farao, kwa chakula kutumika katika miji wakihifadhi.36Chakula kitakuwa matumizi ya nchi kwa miaka saba ya njaa itakayokuwa katika nchi ya Misri. Kwa njia hii nchi haitaharibiwa na njaa.”

37Ushauri huu ukawa mwema machoni pa Farao na machoni pa watumishi wake wote.38Farao akawambia watumishi wake, “Je tunaweza kumpata mtu kama huyu, ambaye ndani yake kuna Roho wa Mungu?”

39Hivyo Farao akamwambia Yusufu, “Kwa vile Mungu amekuonyesha yote haya, hakuna mtu mwenye ufahamu na busara kama wewe.40Utakuwa juu ya nyumba yangu, watu wangu watatawaliwa kwa kadiri ya neno lako. Katika kiti cha enzi peke yake mimi nitakuwa mkuu kuliko wewe.”

41Farao akamwambia Yusufu, “Tazama, nimekuweka juu ya nchi yote ya Misri.”42Farao akavua pete yake ya mhuri kutoka katika mkono wake na kuiweka katika mkono wa Yusufu. Akamvika kwa mavazi ya kitani safi, na kuweka mkufu wa dhahabu shingoni mwake.43Akataka apandishwe katika kibandawazi cha pili alichokuwa nacho. Watu wakapiga kelele mbele yake, “Pigeni magoti.” Farao akamweka juu ya nchi yote ya Misri.

44Farao akamwambia Yusufu, “Mimi ni Farao, mbali na wewe, hakuna mtu atakayeinua mkono wake au mguu wake katika nchi ya Misri.”45Farao akamwita Yusufu jina la Zafenathi Panea. Akampa Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa Oni, kuwa mke wake. Yusufu akaenda juu ya nchi yote ya Misri.

46Yusufu alikuwa na umri wa miaka thelathini aliposimama mbele ya Farao, mfalme wa Misri. Yusufu akatoka mbele ya Farao, na kwenda katika nchi yote ya Misri.47Katika miaka saba ya shibe nchi ilipozaa kwa wingi,48akakusanya chakula chote cha miaka saba iliyokuwako katika nchi ya Misri na kukiweka chakula katika miji. Akaweka katika kila mji chakula cha mashamba yaliyokizunguka.49Yusufu akahifadhi nafaka kama mchanga wa bahari, kingi kiasi kwamba akaacha kuhesabu, kwa sababu kilikuwa hakihesabiki.

50Kabla miaka ya njaa kuingia Yusufu akapata wana wawili, ambao Asenathi, binti wa Potifera kuhani wa Oni, alimzalia.51Yusufu akamwita mzaliwa wake wa kwanza Manase, kwani alisema, “Mungu amenisahaulisha shida zangu zote na nyumba yote ya baba yangu.”52Akamwita mwanawe wa pili Efraimu, kwani alisema, Mungu amenipa uzao katika nchi ya mateso yangu.”

53Miaka saba ya shibe iliyokuwa katika nchi ya Misri ikafika mwisho.54Miaka saba ya njaa ikaanza, kama alivyokuwa amesema Yusufu. Kulikuwa na njaa katika nchi zote, lakini katika nchi yote ya Misri kulikuwa na chakula.55Nchi yote ya Misri ilipokuwa na njaa, watu wakapiga kelele kwa Farao kwa ajili ya chakula. Farao akawaambia Wamisri wote, “Nendeni kwa Yusufu na mfanye atakavyosema.”

56Njaa ilikuwa juu ya uso wote wa nchi. Yusufu akafungua ghala zote na kuuza chakula kwa Wamisri. Njaa ilikuwa kali sana katika nchi ya Misri.57Dunia yote ikaja Misri kununua nafaka kutoka kwa Yusufu, kwani njaa ilikuwa kali katika dunia yote.

42

1Basi Yakobo akafahamu kwamba kuna nafaka huko Misri. Akawaambia wanawe, “Kwa nini mnatazamana?”2Akasema, “Tazama, nimesikia kwamba kuna nafaka huko Misri. Shukeni huko mkatununulie chakula ili tuishi wala tusife.”

3Ndugu kumi wa Yusufu wakashuka Misri kununua chakula.4Lakini Benjamini, ndugu wa Yusufu, Yakobo hakumtuma na ndugu zake, kwani alihofu kwamba madhara yaweza kumpata.5Wana wa Israeli wakaja kununua miongoni mwao waliokuja, kwani njaa ilikuwapo katika nchi ya Kanaani.

6Basi Yusufu alikuwa mtawala juu ya nchi. Ndiye aliyekuwa akiwauzia watu wote wa nchi. Ndugu zake Yusufu wakaja na kumwinamia na nyuso zao hata chini.7Yusufu akawaona ndugu zake na kuwatambua, lakini alijibadili kwao na kuongea nao kwa ukali. Akawaambia, “Mmetoka wapi?” Wakasema, “Kutoka nchi ya Kanaani ili kununua chakula.”

8Yusufu akawatambua ndugu zake, lakini wao hawakumtambua.9Yusufu akazikumbuka ndoto alizoziota kuhusu wao. Akawaambia, “Ninyi ni wapelelezi. Mmekuja kuona sehemu za nchi zisizolindwa.”10Wakamwambia, “Hapana, bwana wangu. Watumishi wako wamekuja kununua chakula.11Sisi sote ni wana wa baba mmoja. Ni watu wa kweli. Watumishi wako siyo wapelelezi.”12Akawaambia, “Hapana, mmekuja kuangalia sehemu za nchi zisizolindwa.”13Wakasema, “Sisi watumishi wako tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba mmoja katika nchi ya Kanaani. Tazama, mdogo yupo na baba yetu, na mwingine hayupo hai tena.”

14Yusufu akawaambia, “Ndivyo nilivyowaambia; ninyi ni wapelelezi.15Mtajaribiwa kwa njia hii. Kama aishivyo Farao, hamtaondoka hapa, mdogo wenu asipokuja hapa.16Mtumeni mmoja wenu amlete mdogo wenu. Mtabaki gerezani, hata maneno yenu yatakapothibitishwa, kwamba kuna ukweli ndani yenu.”17Akawaweka kifungoni kwa siku tatu.

18Katika siku ya tatu Yusufu akaongea nao, “Fanyeni hivi nanyi mtaishi, kwani ninamcha Mungu.19Kama ninyi ni watu wa kweli, mmoja wenu atazuiliwa hapa gerezani, lakini ninyi nendeni, chukueni nafaka kwa ajili ya nyumba zenu.20Mleteni mdogo wenu kwangu ili kwamba maneno yenu yathibitishwe nanyi hamtakufa.” Wakafanya hivyo.

21Wakasemezana wao kwa wao, “Kwa kweli tuna hatia juu ya ndugu yetu kwani tuliona taabu ya nafsi yake alipotusihi nasi hatukusikia. Kwa hiyo taabu hii imeturudia.”

22Rubeni akawajibu, “Je sikuwaambia, ‘Msitende dhambi juu ya kijana,’ lakini hamkusikia? Basi, tazama, damu yake inatakiwa juu yetu.”

23Lakini hawakujua kwamba Yusufu anawaelewa, kwani kulikuwa na mkalimani kati yao.24Akatoka kwao na kulia. Akarudi kwao na kuongea nao. Akamchukua Simoni miongoni mwao na kumfunga mbele ya macho yao.

25Kisha Yusufu akaagiza watumishi kujaza mifuko yao kwa nafaka, na kurudisha pesa ya kila mmoja katika gunia lake, nakuwapa mahitaji kwa safari. Wakatendewa hivyo.26Hawa ndugu wakapandisha chakula chao juu ya punda zao na kuondoka pale.

27Mmoja wao alipofungua gunia lake ili kumlisha punda wao katika sehemu waliyokuwa, akaona pesa yake. Tazama, ilikuwa mdomoni mwa gunia lake.28Akawaambia ndugu zake, “Pesa yangu imerudishwa. Tazama, imo katika gunia langu.” Mioyo yao ikazimia na wakageukiana kila mmoja huku wakitetemeka. Wakasema, “Ni nini hiki alichotutendea Mungu?”

29Wakaenda kwa Yakobo, baba yao katika nchi ya Kanaani na kumwambia yote yaliyowapata.30Wakasema, “Yule mtu, bwana wa nchi, aliongea nasi kwa ukali na kutudhania kuwa wapelelezi katika nchi.31Tukamwambia, ‘Tu watu wa kweli sisi. Sisi siyo wapelelezi.32Tupo ndugu kumi na wawili, wana wa baba yetu. Mmoja hayupo hai tena, na mdogo yupo na baba yetu katika nchi ya Kanaani.”33Yule mtu, bwana wa nchi, akatwambia, ‘Kwa hili nitajua kwamba ni watu wa kweli ninyi. Mwacheni mmojawapo wa ndugu zenu, chukueni chakula kwa ajili ya njaa katika nyumba zenu, na mwondoke.34Mleteni mdogo wenu kwangu. Ndipo nitakapojua kwamba ninyi si wapelelezi, lakini ni watu wa kweli. Kisha nitamwachilia ndugu yenu, na mtafanya biashara katika nchi.”

35Ikawa walipoyafungua magunia yao, na tazama, kila mfuko wa fedha wa mmojawao ulikuwa katika gunia lake. Wakati wao na baba yao walipoona mifuko yao ya fedha, wakaogopa.36Yakobo baba yao akawambia, “Mmeniharibia watoto wangu. Yusufu hayupo hai tena, Simoni ameondoka, nanyi mmpeleke Benjamini naye. Mambo haya yote ni kunyume changu.”

37Rubeni akamwambia baba yake, kusema, “Unaweza kuwaua wanangu wawili nisipomrudisha Benjamini kwako. Mweke mikononi mwangu, nami nitamrudisha tena kwako.”38Yakobo akasema, “Mwanangu atashuka pamoja nanyi. Kwani ndugu yake amekufa na yeye peke yake amebaki. Ikiwa madhara yatampata katika njia mnayoiendea, ndipo mtakapozishusha mvi zangu kaburini kwa huzuni.”

43

1Njaa ilikuwa kali katika nchi.2Ikawa walipokuwa wametumia chakula chote walichokitoa Misri, baba yao akawaambia, “Nendeni tena; mtununulie chakula.”3Yuda akamwambia, “Yule mtu alituonya kwa ukali, ‘Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi.’4Ikiwa utamtuma ndugu yetu pamoja nasi, tutashuka na kuwanunulia chakula.5Lakini usipompeleka, hatutashuka. Kwa maana yule mtu alitwambia, ‘Hamtauona uso wangu, ndugu yenu asipokuwa nanyi.’”6Israeli akawaambia, “Kwa nini mlinitendea mimi vibaya hivyo kwa kumwambia mtu huyo kwamba mnaye ndugu mwingine?”7Wakasema, “Yule mtu alituuliza habari zetu na familia yetu kwa kina. Akasema, ‘Je baba yenu bado yuko hai? Je mnaye ndugu mwingine?’ Tukamjibu kulingana na maswali haya. Tungejuaje kwamba angetwambia, ‘Mleteni ndugu yenu?’”

8Yuda akamwambia Israeli baba yake, “Mtume kijana pamoja nami. Tutainuka na kwenda ili kwamba tuishi tusife, wote sisi, wewe, na hata watoto wetu.9Mimi nitakuwa mdhamini wake. Utaniwajibisha mimi. Kama nisipomleta na kumweka mbele yako, basi nibebe lawama daima.10Kwani kama tusingekawia, bila shaka hata sasa tungekuwa tumekwisha rudi mara ya pili.”

11Israeli baba yao akawambia, “Kama ni hivyo, basi fanyeni hivi. Chukueni baadhi ya mazao mazuri ya nchi katika mifuko yenu. Mchukulieni yule mtu zawadi: baadhi ya marhamu, asali, viungo na manemane, jozi na lozi.12Chukueni pesa mara mbili mikononi mwenu. Pesa iliyorudishwa katika magunia yenu, muichukue tena katika mikono yenu. Pengine walikosea.13Mchukueni ndugu yenu pia. Inukeni na mwende tena kwa mtu yule.14Mungu Mwenyezi na awape kuona rehema mbele ya huyo mtu, hivyo kwamba awafungulie ndugu yenu mwingine na Benjamini. Kama nikipotelewa na watoto, nimepotelewa.”

15Watu wale wakachukua zawadi hii, na katika mikono yao wakachukua mara mbili ya kiasi cha pesa, pamoja na Benjamini. Wakaamka na kushuka Misri na kusimama mbele ya Yusufu.16Yusufu alipomwona Benjamini akiwa nao, akamwambia mtunzaji wa nyumba yake, “Walete watu hao ndani ya nyumba, chinja mnyama na umwandae, kwani watu hawa watakula chakula cha mchana pamoja nami.”

17Mtunzaji wa nyumba akafanya kama Yusufu alivyosema. Akawaleta wale watu nyumbani kwa Yusufu.18Wale ndugu wakaogopa kwa vile walivyoletwa katika nyumba ya Yusufu. Wakasema, “Ni kwa sababu ya pesa iliyorudishwa katika magunia yetu mara ya kwanza tulipoletwa ndani, kwamba atafute nafasi kinyume chetu. Kwamba aweze kutukamata na kutuchukua kama watumwa, na kuchukua punda wetu.”

19Wakamsogelea mtunzaji wa nyumba ya Yusufu, nao wakaongea naye mlangoni mwa nyumba,20wakisema, “Bwana wangu, tulikuja mara ya kwanza kununua chakula.21Ikawa, tulipofika katika eneo la kupumzikia, tukafungua magunia yetu, na, tazama, pesa ya kila mtu ilikuwa katika gunia lake, pesa yetu kwa kiasi kamili. Tumeileta katika mikono yetu.22Tumekuja na pesa nyingine pia mikononi mwetu ili kununua chakula. Hatujui aliyeziweka pesa katika magunia yetu.”

23Mtunzaji wa nyumba akasema, “Amani iwe kwenu, msiogope. Mungu wenu na Mungu wa baba yenu ndiye aliyeweka pesa katika magunia yenu. Nilipokea pesa yenu.” Kisha mtunzaji wa nyumba akamleta Simoni kwao.

24Msimamizi wa nyumba akawapeleka watu hao katika nyumba ya Yusufu. Akawapa maji, nao wakaosha miguu yao. Akawalisha punda wao.25Wakaandaa zawadi kwa ajili ya Yusufu aliyekuwa akija mchana, kwani walikuwa wamesikia kwamba watakula pale.

26Yusufu alipokuja nyumbani, wakaleta nyumbani zawadi iliyokuwa mikononi mwao, nao wakainama mbele yake hata chini.27Akawauliza juu ya hali zao na kusema, “Je baba yenu hajambo, yule mzee mliyemnena? Je bado yu hai?”28Wakasema, “Mtumishi wako baba yetu hajambo. Na bado yu hai.” Wakajinyenyekeza na kuinama chini.

29Alipoinua macho yake akamwona Benjamini ndugu yake, mwana wa mamaye, naye akasema, “Je huyu ndiye mdogo wenu mliyemsema?” Na kisha akasema, “Mungu na awe mwenye neema kwako, mwanangu.”30Yusufu akaharakisha kutoka chumbani, kwani aliguswa sana kuhusu nduguye. Akatafuta mahali pa kulia. Akaingia chumbani mwake na kulia umo.31Akaosha uso wake na kutoka nje. Akajizuia mwenyewe, akasema, “karibuni chakula.”

32Watumishi wakamhudumia Yusufu peke yake na wale ndugu peke yao. Wamisri pale wakala pamoja naye peke yao kwa sababu Wamisri hawakuweza kula mkate na Waebrania, kwani hilo ni chukizo kwa Wamisri.33Wale ndugu wakakaa mbele yake, mzaliwa wa kwanza kwa kulingana na haki yake ya uzaliwa, na mdogo kulingana na ujana wake. Wale watu wakashangaa wote.34Yusufu akapeleka sehemu kwao kutoka katika chakula kilichokuwa mbele yake. Lakini sehemu ya Benjamini ilikuwa mara tano zaidi ya kila ndugu zake. Wakanywa na wakamfurahia.

44

1Yusufu akamwamuru msimamizi wa nyumba yake, akisema, “Jaza magunia ya watu hawa kwa chakula, kiasi wawezacho kubeba, na uweke pesa ya kila mtu katika mdomo wa gunia lake.2Uweke kikombe changu, cha fedha, katika mdomo wa gunia la mdogo, na pesa yake ya chakula pia.” Msimamizi akafanya kama Yusufu alivyosema.

3Kukapambazuka asubuhi, na wale watu wakaruhusiwa kuondoka, wao na punda zao.4Walipokuwa wametoka mjini lakini hawajafika mbali, Yusufu akamwambia msimamizi wa nyumba yake, “Inuka, uwafuatie wale watu, na utakapowapata, wambie, ‘Kwa nini mmelipa uovu badala ya mema?5Je hiki sicho kikombe ambacho bwana wangu hukinywea, na kikombe akitumiacho kwa uaguzi? Mmefanya vibaya, kwa jambo hili mlilolifanya.’”

6Msimamizi wa nyumba akawapata na kuwaambia maneno haya.7Wakasema, “Kwa nini bwana wetu anasema maneno kama haya? Na iwe mbali na watumishi wako kwamba wanaweza kufanya jambo hili.8Tazama, pesa tulizozikuta katika midomo ya magunia yetu, tulizileta kwako kutoka katika nchi ya Kanaani. Ni kwa jinsi gani basi tunaweza kuiba katika nyumba ya bwana wako fedha au dhahabu?9Yeyote kitakayeonekana kwake miongoni mwa watumishi wako, atakufa, nasi sote tutakuwa watumwa wa bwana wangu.”

10Msimamizi akasema, “Basi na iwe kwa kadili ya maneno yenu. Yeye ambaye kikombe kitaonekana kwake atakuwa mtumwa wangu, nanyi wengine mtakuwa bila hatia.”

11Kisha kila mtu akaharakisha na kulishusha gunia lake chini. Na kila mtu akalifungua gunia lake.12Msimamizi akatafuta. Akaanza na mkubwa wa wote na kumaliza kwa mdogo wa wote, na kikombe kikaonekana katika gunia la Benjamini.13Wakararua mavazi yao. Kila mtu akapakia juu ya punda wake nao wakarudi mjini.

14Yuda na ndugu zake wakaja katika nyumba ya Yusufu. Bado alikuwepo pale, nao wakainama mbele zake hata chini.15Yusufu akawaambia, “Je ni nini hili mlilolifanya? Je hamjui kwamba mtu kama mimi anafanya uaguzi.”

16Yuda akasema, “Je tunaweza kumwambia nini bwana wangu? Tuseme nini? Au ni jinsi gani twaweza kujithibitisha wenyewe? Mungu ameona uovu wa watumishi wako. Tazama, sisi ni watumwa wa bwana wangu, wote sisi na yule ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake.”17Yusufu akasema, “Na iwe mbali nami kwamba naweza kufanya hivyo. Mtu ambaye kikombe kimeonekana mkononi mwake, huyu ndiye atakuwa mtumwa wangu, lakini ninyi wengine, nendeni kwa amani kwa baba yenu.”

18Ndipo Yuda alipomkaribia na kusema, “Bwana wangu, tafadhali mwache mtumishi wako aseme neno katika masikio ya bwana wangu, na usiziache hasira zako kuwaka dhidi ya mtumishi wako, kwani wewe ni kama Farao.19Bwana wangu aliwauliza watumishi wake, kusema, ‘Je mnaye baba au ndugu?’20Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Tunaye baba, ni mzee, na mwana wa uzee wake, ni mdogo. Na ndugu yake alishakufa, na yeye peke yake ndiye amebaki kwa mama yake, na baba yake anampenda.’21Nawe ukawaambia watumishi wako, ‘Mleteni ili nimwone.’22Nasi tukamwambia bwana wangu, ‘Kijana hawezi kumwacha babaye. Kwani akimwacha babaye baba yake atakufa.’23Na ukawaambia watumishi wako, ‘Mdogo wenu asipokuja pamoja nanyi, hamtauona uso wangu tena.’24Na ikawa tulipokwenda kwa mtumishi wako baba yangu, tulimwambia maneno ya bwana wangu.25Na baba yetu akasema, ‘Nendeni tena, mkatununulie chakula.’26Nasi tukasema, ‘Hatuwezi kushuka. Ikiwa mdogo wetu atakuwa nasi, ndipo tutakaposhuka, kwani hatuwezi kuuona uso wa mtu yule, mdogo wetu asipokuwa pamoja nasi.’27Mtumishi wako baba yetu akatwambia, ‘Mnajua kwamba mke wangu alinizalia wana wawili.28Na mmoja akatoka kwangu nami nikasema, ‘Bila shaka ameraruliwa vipande, na tangu hapo sijamwona.’29Nanyi mkimchukua huyu naye kutoka kwangu mabaya yanaweza kumpata, mtashusha mvi zangu kwa kaburi kwa huzuni.’

30Kwa hiyo, basi, nitakapoenda kwa mtumishi wako baba yangu, na kijana hayupo nasi, kwa kuwa uhai wake umefungamanishwa katika uhai wa kijana,31itakuwa, atakapoona kwamba kijana hayupo nasi atakufa. Na watumishi wako watazishusha mvi za mtumishi wako baba yetu kaburini kwa masikitiko.32Kwani mtumishi wako alikuwa mdhamini wa kijana kwa baba yangu na alisema, ‘Ikiwa sitamleta kwako, ndipo nitakapokuwa mwenye hatia kwa baba yangu daima.’

33Kwa hiyo sasa, tafadhali mwache mtumishi wako akae kama mtumwa kwa bwana wangu badala ya kijana, na umwache kijana aende na ndugu zake.34Kwa maana nitakwenda jinsi gani kwa baba yangu ikiwa kijana hayupo nami? Ninaogopa kuona mabaya yatakayompata baba yangu.”

45

1Ndipo Yusufu hakuweza kujizuia mwenyewe mbele ya watumishi waliosimama kando yake. Akasema kwa sauti, “Kila mtu aondoke.” Hivyo hakuna mtumishi aliyesimama kando yake wakati Yusufu alipojitambulisha kwa ndugu zake.2Akalia kwa sauti, Wamisri wakasikia, na nyumba ya Farao wakasikia kuhusu hilo.3Yusufu akawaambia ndugu zake, “Mimi ni Yusufu. Je baba yangu ni mzima bado?” Ndugu zake hawakuweza kumjibu, kwani walitishwa na uwepo wake.4Kisha Yusufu akawaambia ndugu zake, “Nikaribieni, tafadhali.” Nao wakasogea. Akawaambia, “Mimi ni Yusufu ndugu yenu, mliyemwuza Misri.5Lakini sasa msihuzunike au kukasirika miongoni mwenu kwamba mliniuza huku, kwani Mungu alinituma mbele yenu ili kutunza uhai.6Maana ni miaka miwili njaa imekuwa katika nchi, na bado kuna miaka mitano ambayo hakutakuwa na kulima wala kuvuna.7Mungu alinituma mbele yenu kuwahifadhi kama masalia duniani, na kuwaweka hai kwa ukombozi mkuu.8Hivyo si ninyi mlionipeleka huku bali ni Mungu, na amenifanya baba kwa Farao, bwana wa nyumba yake yote, na mtawala wa nchi yote ya Misri.9Fanyeni haraka mwende kwa baba yangu na mmwambie, ‘Hivi ndivyo asemavyo Yusufu mwanao, “Mungu amenifanya bwana kwa Wamisri wote. Shuka kwangu, usikawie.10Utaishi katika nchi ya Gosheni, nawe utakuwa karibu nami, wewe na watoto wako na watoto wa watoto wako, na kondoo wako na mbuzi wako, na yote uliyonayo.11Nami nitakuhudumia pale, kwa maana bado kuna miaka mitano ya njaa, hivyo usije ukaingia katika uhitaji, wewe, nyumba yako, na yote uliyonayo.”

12Tazama, macho yenu yanaona, na macho ya Benjamini ndugu yangu, kwamba ni kinywa changu kinachoongea nanyi.13Mtamwambia baba yangu juu ya heshima yangu yote huku Misri na yote mliyoyaona. Mtaharakisha na kumleta baba yangu huku.”

14Akaikumbatia shingo ya Benjamini ndugu yake na kulia, na Benjamini akalia shingoni mwake.15Akawabusu ndugu zake wote na kulia kwa ajili yao. Baada ya hayo ndugu zake wakaongea naye.

16Habari ya jambo hili ikasemwa katika nyumba ya Farao: “Ndugu zake Yusufu wamekuja.” Ikampendeza sana Farao na watumishi wake.17Farao akamwambia Yusufu, “Waambie ndugu zako, ‘Fanyeni hivi: Wapakieni wanyama wenu na mwende katika nchi ya Kanaani.18Mchukueni baba yenu na nyumba zenu mnijie. Nami nitawapa mema ya nchi ya Misri, nanyi mtakula unono wa nchi.’19Basi mmeamriwa, ‘Fanyeni hivi, chukueni mikokoteni kutoka Misri kwa ajili ya watoto wenu na kwa ajili ya wake zenu. Mchukueni baba yenu na kuja.20Msijali kuhusu mali zenu, kwani mema yote ya nchi ya Misri ni yenu.’”

21Wana wa Israeli wakafanya hivyo. Yusufu akawapa mikokoteni, kwa kadiri ya agizo la Farao, na akawapa mahitaji ya safari.22Akawapa wote mavazi ya kubadilisha, lakini akampa Benjamini vipande mia tatu vya fedha na mavazi matano ya kubadilisha.23Akampelekea baba yake: punda kumi waliobeba mema ya Misri, punda majike kumi wamebeba nafaka, mikate, na mahitaji mengine kwa baba yake kwa ajili ya safari.24Hivyo akawaruhusu ndugu zake nao wakaondoka. Akawaambia, “Angalieni msije mkagombana njiani.”

25Wakapanda kutoka Misri na kuja katika nchi ya Kanaani, kwa Yakobo baba yao.26Wakamwambia “Yusufu bado yu hai, na ndiye mtawala juu ya nchi yote ya Misri.” Na moyo wake ulishikwa na ushangao, kwani hakuwaamini.27Wakamwambia maneno yote ya Yusufu aliyokuwa amewaambia. Yakobo alipoona mikokoteni Yusufu aliyokuwa amepeleka kuwabeba, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.28Israeli akasema, “Inatosha. Yusufu mwanangu yu hai. Nitakwenda nikamwone kabla sijafa.”

46

1Israeli akasafiri na yote aliyokuwa nayo na akaja Beersheba. Pale akatoa sadaka kwa Mungu wa Isaka baba yake.2Mungu akamwambia Israeli katika ndoto usiku, akisema, “Yakobo, Yakobo.”3Akasema, “Mimi hapa.” Akasema, “Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako. Usiogope kushuka Misri, kwa maana nitakufanya taifa kubwa huko.4Nitakwenda pamoja nawe huko Misri, Nami nitakupandisha huku tena bila shaka. Na Yusufu akayafunika macho yake kwa mikono yake.”

5Yakobo akainuka kutoka Beersheba. Wana wa Israeli wakamsafirisha Yakobo baba yao, watoto wao, na wake wao, katika mikokoteni ambayo Farao alikuwa ameipeleka kuwachukua.6Wakachukua mifugo yao na mali zao walizokuwa wamezipata katika nchi ya Kanaani. Wakaja Misri, Yakobo na uzao wake wote pamoja naye.7Akaja Misri pamoja na wanawe na wana wa wanawe, binti zake na wana wa binti zake, na uzao wake wote.

8Haya ni majina ya watoto wa Israeli waliokuja Misri, Yakobo na wanawe: Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Yakobo;9wana wa Rubeni Hanoki na Palu na Hezroni na Karmi;10wana wa Simoni, Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli, wana wa mwanamke Mkanaani;11wana wa Lawi Gershoni, Kohathi, na Merari.12Wana wa Yuda: Eri, Shela, Peresi, na Zera, (Lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani). Na wana wa Peresi walikuwa Hezroni na Hamuli.13Wana wa Isakari walikuwa Tola, Puva, Lobu, na Shimroni;14Wana wa Zabuloni walikuwa Seredi, Eloni, na Yaleeli15Hawa walikuwa wana wa Lea aliomzalia Yakobo huko Padan aramu, pamoja na na Dina binti yake. Wanawe na binti zake walikuwa thelathini na watatu.16Wana wa Gadi walikuwa sefoni, Hagi, Shuni, Esboni, Eri, Arodi, na Areli.17Wana wa Asheri walikuwa Imna, Ishva, Ishvi, na Beria; na Sera alikuwa dada yao. Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malkieli.18Hawa walikuwa wana wa Zilpa, ambaye Labani alikuwa amempa Lea binti yake. Wana aliomzalia Yakobo wote walikuwa kumi na sita.19Wana wa Raheli mkewe Yakobo walikuwa Yusufu na Benjamini.20Huko Misri Manase na Efraimu walizaliwa kwa Yusufu na Asenathi, binti Potifera kuhani wa Oni.21Wana wa Benjamini walikuwa Bela, Bekeri, Ashbeli, Gera, Naamani, Ehi, Roshi, Mupimu, Hupimu, na Ardi.22Hawa walikuwa wana wa Raheli waliozaliwa kwa Yakobo - jumla yao kumi na wanne.23Mwana wa Dani alikuwa Hushimu.24Wana wa Naftali walikuwa Yaseeli, Guni, Yezeri, na Shilem.25Hawa walikuwa wana Bilha aliomzalia Yakobo, ambaye Labani alimpa Raheli binti yake - wote walikuwa saba.

26Wote waliokwenda na Yakobo, waliokuwa uzao wake, bila kuhesabu wake wa wana wa Yakobo walikuwa sitini na sita.27Pamoja na wana wawili wa Yusufu waliozaliwa kwake huko Misri, watu wa familia yake waliokwenda Misri walikuwa sabini jumla yao.

28Yakobo akamtuma Yuda kuwatangulia mbele kwa Yusufu kuonyesha njia mbele yake kwenda Gosheni, nao wakaja katika eneo la Gosheni.29Yusufu akaandaa kibandawazi chake na akaenda kumlaki baba yake huko Gosheni. Akamwona, akaikumbatia shingo yake, na akalia shingoni mwake kwa kitambo.30Israeli akamwambia Yusufu, “Basi na nife sasa, kwa kuwa nimeuona uso wako, kwamba bado uko hai.”

31Yusufu akawaambia ndugu zake na nyumba ya baba yake, “Nitakwenda na kumwambia Farao, kusema, ‘Ndugu zangu na nyumba ya baba yangu, waliokuwa katika nchi ya Kanaani, wamenijia.32Watu hawa ni wafugaji, kwani wamekuwa watunza wanyama. Wamekuja na makundi yao ya kondoo, na mbuzi, na vyote walivyonavyo.’33Itakuwa, Farao atakapowaita na kuwauliza, ‘Kazi yenu ni ipi?’34mwambieni, ‘Watumishi wako wamekuwa watunza wanyama tangu ujana wetu mpaka sasa, sisi, na baba zetu.’ Fanyeni hivyo ili mweze kuishi katika nchi ya Gosheni, kwani kila mfugaji ni chukizo kwa Wamisri.”

47

1Kisha Yusufu akaingia kwa Farao na kumwambia, “Baba yangu na ndugu zangu, kondoo wao, mbuzi wao, na yote waliyonayo, wamefika kutoka katika nchi ya Kanaani. Tazama, wapo katika nchi ya Gosheni.”2Akawachukua watano katika ndugu zake na kuwatambulisha kwa Farao.3Farao akawaambia ndugu zake, “Kazi yenu ni nini?” Wakamwambia Farao, “Watumishi wako ni wafugaji, kama mababu zetu.”4Kisha wakamwambia Farao, “Tumekuja kukaa kwa muda katika nchi. Hakuna malisho kwa ajili ya makundi ya watumishi wako, kwa maana njaa ni kali sana katika nchi ya Kanaani. Hivyo, tafadhali waache watumishi wako wakae katika nchi ya Gosheni.”

5Kisha Farao akamwambia Yusufu, kusema, “Baba yako na ndugu zako wamekuja kwako.6Nchi ya Misri iko mbele yako. Mkalishe baba yako na ndugu zako katika eneo zuri, nchi ya Gosheni. Ikiwa unafahamu watu wenye uwezo miongoni mwao, uwaweke kuwatunza wanyama wangu.”

7Kisha Yusufu akamwingiza Yakobo baba yake na kumweka mbele ya Farao. Yakobo akambariki Farao.8Farao akamwuliza Yakobo, “Umeishi kwa muda gani?”9Yakobo akamwambia Farao, “Miaka ya safari zangu ni 130. Miaka ya maisha yangu imekuwa mifupi na ya maumivu. Siyo kama miaka ya baba zangu.”10Kisha Yakobo akambariki Farao na kuondoka mbele zake.

11Kisha Yusufu akamweka baba yake na ndugu zake. Akawapa eneo katika nchi ya Misri, sehemu nzuri sana ya nchi, katika eneo la Ramesesi, kama Farao alivyokuwa ameagiza.12Yusufu akamhudumia baba yake kwa chakula, ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake, kulingana na hesabu ya watoto wao.

13Basi hakukuwa na chakula katika nchi yote; kwani njaa ilikuwa kali sana. Nchi ya Misri na nchi ya Kanaani ikaharibika kwa sababu ya njaa.14Yusufu akakusanya pesa yote iliyokuwa katika nchi ya Misri na nchi ya Kanaani, kwa kuwauzia wakaaji wake chakula. Kisha Yusufu akaleta ile pesa katika kasri la Farao.15Pesa yote ya nchi za Misri na Kanaani ilipokwisha, Wamisri wote wakaja kwa Yusufu wakisema, “Tupe chakula! Kwa nini tufe mbele zako kwa maana pesa yetu imekwisha?”16Yusufu akasema, “Ikiwa pesa yenu imekwisha, leteni wanyama wenu nami nitawapa chakula badala ya wanyama wenu.”17Hivyo wakaleta wanyama wao kwa Yusufu. Yusufu akawapa chakula kwa kubadilishana na farasi, kondoo, mbuzi na kwa punda. Akawalisha kwa mkate kwa kubadilisha na wanyama wao mwaka ule.

18Mwaka ule ulipokwisha, wakaja kwake mwaka uliofuata na kumwambia, “Hatutaficha kwa bwana wangu kwamba pesa yetu yote imekwisha, na wanyama ni wa bwana wangu. Hakuna kilichobaki mbele za bwana wangu, isipokuwa miili yetu na nchi yetu.19Kwa nini tufe mbele za macho yake, sisi na nchi yetu? Utununue sisi na nchi yetu badala ya chakula, na sisi na nchi yetu tutakuwa watumishi wa Farao. Tupe mbegu ili kwamba tuishi na tusife, na kwamba nchi isiwe tupu bila watu.

20Hivyo Yusufu akamnunulia Farao nchi yote ya Misri. Kwani kila Mmisri akauza shamba lake, kwa sababu njaa ilikuwa kali sana. Kwa njia hii, nchi ikawa mali ya Farao.21Na watu, akawafanya kuwa watumwa kutoka mpaka mmoja wa Misri hata mkapa mwingine.22Ilikuwa ni nchi ya makuhani pekee ambayo Yusufu hakuinunua, kwa maana makuhani walikuwa wakipewa posho. Walikula katika sehemu aliyowapa Farao. Kwa hiyo hawakuuza nchi yao.

23Kisha Yusufu akawaambia watu, “Tazama, nimewanunua ninyi na nchi yenu leo kwa ajili ya Farao. Basi mbegu hii hapa kwa ajili yenu, nanyi mtapanda katika nchi.24Wakati wa mavuno, mtampa Farao sehemu ya tano, na sehemu nne zitakuwa zenu, kwa mbegu za shamba na kwa chakula cha nyumba zenu na watoto wenu.”25Wakasema, “Umeokoa maisha yetu. Na tupate kibali machoni pako. Tutakuwa watumishi wa Farao.”

26Hivyo Yusufu akaifanya kuwa sheria inayofanya kazi hata leo katika nchi ya Misri, kwamba moja ya tano ni ya Farao. Eneo la makuhani peke yake ndilo halikufanywa kuwa la Farao.

27Hivyo Israeli akaishi katika nchi ya Misri, katika eneo la Gosheni. Watu wake wakapata umiliki pale. Walikuwa wenye kuzaa na kuongezeka sana.

28Yakobo akaishi katika nchi ya Misri miaka kumi na saba, kwa hiyo miaka ya maisha ya Yakobo ilikuwa miaka 147.29Wakati wa kufa kwake Yakobo ulipokaribia, alimwita Yusufu mwanaye na kumwambia, “Ikiwa nimepata kibali mbele zako, weka mkono wako chini ya paja langu, na unitendee kwa uaminifu na kweli. Tafadhali usinizike Misri.30Nitakapolala na baba zangu, utanitoa Misri na kunizika katika eneo la kuzikia la baba zangu.” Yusufu akasema, “Nitafanya kama ulivyosema.”31Israeli akasema, “Niapie,” na Yusufu akamwapia. Kisha Israeli akainama chini mbele ya kitanda chake.

48

1Ikawa baada ya mambo haya, mmojawapo akamwambia Yusufu, “Tazama, baba yako ni mgonjwa.” Hivyo akaondoka pamoja na wanawe wawili, Manase na Efrahimu.2Yakobo alipoambiwa, “Tazama, mwanao Yusufu amekuja kukuona,” Israeli akakusanya nguvu na kukaa juu ya kitanda.3Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu katika nchi ya Kanaani. Akanibariki na4kuniambia, ‘Tazama, nitakupa uzao mwingi, na kukuzidisha. Nitakufanya kuwa kusanyiko la mataifa. Nitakupa nchi hii wewe na uzao wako kuwa milki ya milele.’

5Na sasa wanao wawili, waliozaliwa kwako katika nchi ya Misri kabla sijaja Misri, ni wangu. Efrahimu na Manase watakuwa wangu, kama walivyo Rubeni na Simioni.6Watoto utakaowapata baada ya hapo ni wako; watahesabiwa katika majina ya ndugu zao katika urithi wao.7Lakini kwangu mimi, nilipokuja kutoka Padan, kwa huzuni yangu Raheli alikufa njiani katika nchi ya Kanaani, wakati kungalipo kitambo kwenda Efrathi. Nilimzika pale katika njia iendayo Efrathi” (ndio, Bethlehemu).

8Israeli alipowaona wana wa Yusufu, akasema, “Ni nani hawa?”9Yusufu akamwambia baba yake, “Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa: “Israeli akasema, “Walete kwangu, kwamba niwabariki.”10Basi macho ya Israeli yalikuwa yanashindwa kwa ajili ya umri wake, hivyo hakuweza kuona. Hivyo Yusufu akawasogeza karibu yake, na akawabusu na kuwakumbatia.11Israeli akamwambia Yusufu, “Sikutazamia kuuona uso wako tena, Lakini Mungu ameniruhusu kuwaona hata wanao.”

12Yusufu akawaondoa kati ya magoti ya Israeli, na kisha akainama na uso wake juu ya nchi.13Yusufu akawachukua wote wawili, Efrahimu katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli, na Manase katika mkono wake wa kulia kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, na akawasongeza kwake.14Israeli akainua mkono wake wa kulia na kuuweka juu ya kichwa cha Efrahimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto juu ya kichwa cha Manase. Akaipishanisha mikono yake, kwani Manase ndiye alikuwa mzaliwa wa kwanza.15Israeli akambariki Yusufu, akisema, “Mungu ambaye mbele zake baba zangu Ibrahimu na Isaka walitembea, Mungu aliyenilinda hata leo,16malaika walionilinda na madhara yote, awabariki vijana hawa. Jina langu na litajwe kwao, na majina ya baba zangu Ibrahimu na Isaka. Na wawe makutano ya watu juu ya nchi.”

17Yusufu alipoona baba yake ameweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efrahimu, haikumpendeza. Akauchukua mkono wa baba yake auweke katika kichwa cha Manase.18Yusufu akamwambia baba yake, “Sivyo babangu; kwani huyu ndiye mzaliwa wa kwanza. Uweke mkono wako juu ya kichwa chake.”19Baba yake akakataa na kusema, “Ninafahamu, mwanangu, nafahamu. Yeye naye atakuwa watu, naye pia atakuwa mkuu. Lakini mdogo wake atakuwa mkuu kuliko yeye, na uzao wake utakuwa wingi wa mataifa.”20Israeli akawabariki siku hiyo kwa maneno haya, “Watu wa Israeli watatamka baraka kwa majina yenu wakisema, ‘Mungu na akufanye kama Efrahimu na kama Manase.’” Kwa njia hii, Israeli akamweka Efrahimu mbele ya Manase.

21Israeli akamwambia Yusufu, “Tazama, ninakaribia kufa, lakini Mungu atakuwa nanyi, na atawarudisha katika nchi ya baba zenu.22Kwako wewe, kwa kuwa uko juu ya ndugu zako, ninakupa mtelemko wa mlima niliouchukuwa kutoka kwa Waamori kwa upanga wangu na upinde wangu.”

49

1Kisha Yakobo akawaita wana wake, na kusema: “Jikusanyeni pamoja, ili niwaambie yatakayowapata nyakati zijazo.2Kusanyikeni ninyi wenyewe na msikilize, enyi wana wa Yakobo. Msikilizeni Israeli, baba yenu.

3Reubeni, wewe ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu zangu, na mwanzo wa uwezo wangu, aliyesalia katika heshima na nguvu.4Asiyezuilika kama maji yarukayo, hautakuwa na umaharufu, kwa sababu ulikwenda juu ya kitanda cha baba yako. Hata ukakitia unajisi; ulikipanda kwa kuvizia.

5Simoni na Lawi ni ndugu. Panga zao ni silaha za vurugu.6Ee nafsi yangu, usiingie barazani pao; usiingie katika mikutano yao, kwani moyo wangu unaheshima kubwa kwa ajili yao. Kwani katika hasira yao waliua watu. Iliwapendeza kuwakata visigino ng'ombe.

7Hasira yao na ilaaniwe, kwani ilikuwa kali - na ukali wao, kwani ulikuwa ni katili. Nitawagawa katika Yakobo na kuwatawanya katika Israeli.

8Yuda, ndugu zako watakusifu. Mkono wako utakuwa shingoni mwa adui zako. Wana wa baba yako watainama mbele zako.

9Yuda ni mwana simba. Mwanangu, umetoka katika mawindo yako. Alisimama chini, alijikunyata kama simba, kama simba jike. Je ninani atakayejaribu kumwamsha?

10Fimbo haitaondoka katika Yuda, wala fimbo ya utawala kutoka katika miguu yake, hata atakapo kuja Shilo. Mataifa yatamtii.

11Kumfunga punda wake kwenye mzabibu, na mwanapunda wake katika mzabibu mzuri, amefua mavazi yake katika divai, na kanzu yake katika damu ya vichala vya mzabibu.12Macho yake yatakuwa mekundu kama mvinyo, na meno yake meupe kama maziwa.

13Zabuloni atakaa katika fukwe ya bahari. Atakuwa bandari kwa ajili ya meli, na mpaka wake utakuwa hata Sidoni.

14Isakari ni punda mwenye nguvu, ajilazaye kati ya kondoo.15Anaona mahali pazuri pa kupumzikia na nchi ya kupendeza. Atainamisha bega lake kwa mzigo na kuwa mtumishi wake.

16Dani atawaamua watu wake kama mojawapo ya makabila ya Israeli.17Dani atakuwa nyoka kando ya njia, nyoka mwenye sumu aumaye visigino vya farasi katika njia, hivyo aongozaye farasi huanguka nyuma.

18Ninaungoja wokovu wako, Yahwe.

19Gadi - wapanda farasi watamshambulia, lakini yeye atawapiga katika visigino vyao.

20Vyakula vya Asheri vitakuwa vingi, naye ataandaa vyakula vya kifalme.

21Naftali ni dubu jike asiyefungwa; atakuwa na watoto wa dubu walio wazuri.

22Yusufu ni tawi lizaalo, tawi lizaalo karibu na kijito, ambaye matawi yake yako juu wa ukuta.23Mpiga mishale atamshambulia na kumrushia na kumsumbua.24Lakini upinde wake utakuwa imara, na mikono yake itakuwa hodari kwa sababu ya mikono ya Mwenye nguvu wa Yakobo, kwa ajili ya jina la Mchungaji, Mwamba wa Israeli.

25Mungu wa baba yako atakusaidia na Mungu Mwenye enzi atakubariki kwa baraka ya mbinguni juu, baraka za vilindi vilivyo chini, na baraka za maziwa na mimba.

26Baraka za baba yako ni kuu kuliko baraka za milima ya zamani au vitu vilivyotamaniwa vya milima ya kale. Na viwe katika kichwa cha Yusufu, hata juu ya taji ya kifalme kichwani pa ndugu zake.

27Benjamini ni mbwamwitu mwenye njaa. Wakati wa asubuhi atararua mawindo, na jioni atagawa mateka.”

28Haya ni makabila kumi na mawili ya Israeli. Hiki ndicho baba yao alichowambia alipowabariki. Aliwabariki kila mmoja kwa baraka iliyomstahili.

29Kisha akawaelekeza na kuwaambia, “Ninakaribia kwenda kwa watu wangu. Mnizike pamoja na babu zangu katika pango lililoko katika shamba la Efroni Mhiti,30katika pango lililo katika shamba la Makpela, karibu na Mamre katika nchi ya Kanaani, shamba Ibrahimu alilolinunua kwa Efron Mhiti kwa ajili ya eneo la kuzikia.31Pale walimzika Ibrahimu na Sara mkewe; pale wakamzika Isaka na Rebeka mkewe; na pale nikamzika Lea.32Shamba na pango lililomo lilinunuliwa kutoka kwa watu wa Hethi.”

33Yakobo alipomaliza maagizo hayo kwa wanawe, akaiweka miguu yake kitandani, akakata roho, akawaendea watu wake.

50

1Yusufu akahuzunika sana hata akauangukia uso wa baba yake, akamlilia, na kumbusu.2Yusufu akawaagiza watumishi wake matabibu kumtia dawa babaye. Hivyo matabibu wakampaka dawa Israeli.3Wakatimiza siku arobaini, kwani huo ndio uliokuwa muda kamili wa kutia dawa. Wamisri wakamlilia kwa siku sabini.4Siku za maombolezo zilipotimia, Yusufu akaongea na watumishi wa baraza la kifalme wa Farao kusema, “Ikiwa nimepata kibali machoni penu, tafadhalini ongeeni na Farao, kusema,5‘Baba yangu aliniapisha, kusema, “Tazama, ninakaribia kufa. Unizike katika kaburi nililolichimba kwa ajili yangu mwenyewe katika nchi ya Kanaani. Ndipo utakaponizika.” Basi sasa niruhusu niende nimzike baba yangu, na kisha nitarudi.”

6Farao akajibu, “Nenda na umzike baba yako, kama alivyokuapisha.”7Yusufu akaenda kumzika baba yake. Maofisa wa Farao wote wakaenda pamoja naye - washauri wa nyumba yake, maofisa waandamizi wote wa nchi ya Misri,8pamoja na nyumba yote ya Yusufu na ndugu zake, na nyumba yote ya baba yake. Lakini watoto wao, kondoo wao na makundi ya mbuzi wao yaliachwa katika nchi ya Gosheni.9Vibandawazi na wapanda farasi pia walikwenda pamoja naye. Lilikuwa kundi kubwa sana la watu.

10Hata walipokuja katika sakafu ya kupuria ya Atadi upande mwingine wa Yordani, wakaomboleza kwa majonzi ya huzuni kubwa. Yusufu akafanya maombolezo ya siku saba kwa ajili ya babaye pale.11Wenyeji wa nchi, Wakanaani, walipoona maombolezo katika sakafu ya Atadi, wakasema, “Hili ni tukio la kuhuzunisha sana kwa Wamisri.” Ndiyo maana eneo hilo likaitwa Abeli Mizraimu, lililoko mbele ya Yordani.

12Hivyo wanawe wakamfanyia Yakobo kama alivyokuwa amewaagiza.13Wana wake wakampeleka katika nchi ya Kanaani na wakamzika katika pango katika shamba la Makpela, karibu na Mamre. Ibrahimu alikuwa amelinunua pango pamoja na shamba kwa ajili ya eneo la kuzikia. Alikuwa amelinunua kutoka kwa Efroni Mhiti.

14Baada ya kuwa amemzika babaye, Yusufu akarudi Misri, yeye, pamoja na ndugu zake, na wote waliokuwa wamemsindikiza ili kumzika babaye.

15Nduguze Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, “Itakuwaje ikiwa Yusufu atatukasirikia na akataka kutulipa kikamilifu kwa ajili ya uovu tuliomtenda?”16Hivyo wakamwagiza Yusufu, kusema, “Baba yako alitoa maelekezo kabla hajafa, kusema,17‘Mwambieni hivi Yusufu, “Tafadhali samehe makosa ya ndugu zako na dhambi yao uovu waliokutenda.” Basi wasamehe watumishi wa Mungu wa baba yako.” Yusufu akalia walipomwambia.18Ndugu zake pia wakaenda na kuinamisha nyuso zao mbele zake. Wakasema, “Tazama, sisi ni watumishi wako.”19Lakini Yusufu akawajibu, “Msiogope, Je mimi ni badala ya Mungu?20Lakini kwenu, mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, kuhifadhi maisha ya watu wengi, kama mwonavyo leo.21Hivyo basi msiogope. Nitawahudumia ninyi na watoto wenu wadogo.” Kwa njia hii aliwatia moyo na kuongea na mioyo yao kwa upole.

22Yusufu akakaa Misri, pamoja na familia ya baba yake. Akaishi miaka 110.23Yusufu akawaona wana wa Efraimu hata kizazi cha tatu. Pia aliwaona wana wa Makiri mwana wa Manase, waliowekwa katika magoti ya Yusufu.24Yusufu akawambia ndugu zake, “Ninakaribia kufa; lakini kwa hakika Mungu atawajilia na kuwaongoza kutoka katika nchi hii na kuwapeleka katika nchi aliyoapa kumpa Ibrahimu, kwa Isaka na kwa Yakobo.”25Kisha Yusufu akawaapisha watu wa Israeli kwa kiapo. Akasema, “Bila shaka Mungu atawajilia. Wakati huo mtachukua mifupa yangu kutoka hapa.”

26Hivyo Yusufu akafa, mwenye miaka 110. Wakampaka dawa na akawekwa katika jeneza huko Misri.

Kutoka

1

1Haya ndiyo majina ya wana wa Israeli walioakuja Misri pamoja na Yakobo, kila moja na familia yake:2Rubeni, Simioni, Lawi, na Yuda,3Isakari, Zebuluni, na Benjamini,4Dani, Naftali, Gadi, na Asheri.5Jumla ya watu wa ukoo wa Yakobo walikuwa sabini. Yusufu alikuwa Misri tayari.

6Ndipo Yusufu, pamoja na kaka zake wote, na kizazi chote wakafa.7Waisraeli walifanikiwa sana, wakaongezeka sana idadi yao, na wakawa na nguvu maana nchi ilijazwa nao.8Wakati huu sasa mfalme mpya asiyemjua Yusufu aliinuka katika Misri.9Akawaambia watu wake, “Tazama, hawa Waisraeli ni wengi na wenye nguvu kuliko sisi.10Njooni na tukae nao kwa akili, ama sivyo wataendelea kuongezeka na kama vita vikalipuka, wataungana na adui zetu, watapigana nasi, na kisha wataondoka.”

11Hivyo wakawawekea walinzi ambao waliwatesa kwa kuwafanyisha kazi ngumu. Waisraeli walijenga maghala ya miji kwa ajili ya Farao: Pishoni na Ramsei.12Lakini kadiri Wamisri walivyowatesa, ndivyo Waisraeli waliendelea kuongezeka na kusambaa. Hivyo Wamisri wakaanza kuwaogopa Waisraeli.13Wamisri waliwafanya Waisraeli wafanye kazi kwa nguvu nyingi.14Waliyafanya maisha yao kuwa machungu kwa kuwafanyisha kazi ngumu kwa vinu na matofali na kwa kila aina ya kazi za shambani. Kazi zao zote zilikuwa ngumu.

15Kisha mfalme wa Misri akawaambia wakunga wa Kiebrania; mmoja wao aliitwa jina lake Shifra, na mwingine aliitwa Puha.16Akasema, “Wakati mnapowasaidia wanawake wa Kiebrania wanapojifungua, chunguzeni wanapozaa. Ikiwa ni mtoto wa kiume, basi muueni; bali ikiwa ni mtoto wa kike, basi mwacheni aishi.”17Lakini wale Wakunga walimwogopa Mungu na hawakufanya kama mfalme wa Misri alivyowaagiza; badala yake waliwaacha watoto wa kiume waishi.18Mfalme wa Misri akawaita Wakunga na kuwaambia, “Kwanini mmefanya haya, na kuwaacha watoto wa kiume wakaishi?”19Wale Wakunga wakamjibu Farao, “Hawa wanawake wa Kiebrania siyo kama wanawake wa Kimisri. Hawa wana nguvu na jasiri sana maana wao humaliza kuzaa kabla hata mkunga hajafika.”

20Mungu aliwalinda hawa Wakunga. Watu waliongezeka kwa idadi na kuwa na nguvu sana.21Kwa sababu wale Wakunga walimwogopa Mungu, aliwapa familia.

22Farao akawaagiza watu wote, “Lazima mtupe kila mtoto wa kiume anayezaliwa katika mto, lakini kila mtoto wa kike wamwache aishi.”

2

1Sasa mwanamme wa kabila la Lawi alimuoa mwanamke Mlawi.2Yule mwanamke akapata mimba na kuzaa mtoto wa kiume. Alipoona kuwa alikuwa mtoto mwenye afya, alimficha kwa miezi mitatu.3Lakini alipokuwa hawezi kuendelea kumficha tena, alichukua kikapu cha manyasi akakipaka sifa na lami. Akamtia mtoto ndani yake na kukiweka juu ya maji katika majani kando ya mto.4Dada yake akasimama kwa mbali ili ajue yatakayompata.

5Binti Farao akashuka kuoga mtoni wakati vijakazi wake wakitembea kando ya mto. Naye akaona kile kikapu katika majani na akamtuma kijakazi wake kwenda kukileta.6Alipokifungua, aliomwona mtoto. Tazama, mtoto alikuwa analia. Alimhurumia na kusema, “Bila shaka huyu ni mmoja wapo wa watoto wa Waebrania.”

7Basi dada wa yule mtoto akamwambia binti Farao, “Je naweza kwenda kukutafutia mwanamke wa Kiebrania aje akulelee mtoto kwa ajili yako?”8Binti Farao akamwambia, “Nenda.” Hivyo yule binti akaenda na kumwita mama yake yule mtoto.9Binti Farao akamwambia mama yake yule mtoto, “Mchukue mtoto huyu ukaninyonyeshee, nami nitakupa malipo.” Hivyo yule mwanamke akamchukua mtoto na kumnyonyesha.10Mtoto alipokuwa mkubwa, akamleta kwa binti Farao, na akawa mtoto wake. Akamwita jina lake Musa akisema, “Kwa sababu nilimtoa katika maji.”

11Musa alipokuwa mtu mzima, alienda kwa watu wake na kuona kazi ngumu walizokuwa wanafanya. Alimuona Mmisri akimpiga Mwebrania, mmoja wa watu wa jamii yake.12Aliangalia huku na kule, na alipoona ya kuwa hakuna mtu, alimuua yule mmisri na kuuficha mwili wake katika mchanga.

13Alienda tena siku iliyofuata, na tazama, Waebrania wawili walikuwa wanapigana. Alimwambia yule aliyekuwa na makosa, “Kwa nini unampigia mwenzako?”14Lakini yule mtu alisema, “Ni nani aliyekuweka wewe kuwa kiongozi na mwamuzi juu yetu? Unataka kuniua na mimi kama ulivyomuua yule mmisri?” Ndipo Musa akaogopa na kusema, “Hakika niliyoyafanya yamejulikana.”

15Farao aliposikia habari hizi, alijaribu kumuua Musa. Lakini Musa alikimbia na kwenda kuishi katika nchi ya Wamidiani. Kule alikaa chini kando ya mto.16Wakati huo kuhani wa Midiani alikuwa na mabinti saba. Walikuja mtoni kuchota maji na kujaza vyombo vyao ili wawanyweshe mifugo ya baba yao.17Wachungaji walikuja na kutaka kuwafukuza, lakini Musa alienda kuwasaidia. Kisha akawanywesha mifugo wao.18Wale mabinti walipoenda kwa Reueli baba yao, aliwauliza, “Kwa nini mmerudi nyumbani mapema hivi leo?”19Wakamwambia, “Mmisri mmoja alituokoa dhidi ya wachungaji. Pia alichota maji na kuwanywesha mifugo wetu.”

20Kisha akawauliza binti zake, “Yu wapi sasa? Kwa nini mlimwacha? Mwiteni ili apate kula chakula pamoja nasi.”21Musa akakubali kukaa na yule mtu ambaye pia alimpa binti yake Zipora ili amuoe.22Alizaa mtoto wa kiume, na Musa akamwita jina lake Geshomu; akisema; “Nimekuwa mkazi katika nchi ya ugeni.”

23Muda mrefu baadaye, mfalme wa Misri akafa. Waisraeli walilalamika kwa sababu ya kazi za utumwa. Walilia kutafuta msaada, na maombi yao yakamfikia Mungu kwa sababu ya mateso yao.24Mungu aliposikia malalamiko yao, Mungu alikumbuka agano lake na Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.25Mungu aliwaona Waisraeli na akaielewa hali yao.

3

1Wakati huu Musa aliendelea kuchunga mifugo ya Yethro baba mkwe wake, kuhani wa Midiani. Musa aliliongoza kundi la mifugo kuelekea upande wa mbali wa jangwa mpaka kufika Horebu, mlima wa Mungu.2Akiwa pale malaika wa Yahweh akamtokea kama mwali wa moto katika kichaka. Musa aliangalia, na tazama, kichaka kiliwaka moto lakini hakikuteketea.3Musa akasema, “Nitageuka ili nione kitu hiki cha ajabu, kwa nini kichaka hakiteketei.”

4Yahweh alipoona ya kuwa amegeuka upande ili aone, Mungu alimwita kutoka katika kile kichaka na kusema, “Musa, Musa.” Musa akasema, “Mimi hapa.”5Mungu akasema, “Usinikaribie! Vua viatu katika miguu yako, kwa kuwa mahali uliposimama ni mahali palipowekwa wakfu kwa ajili yangu.”6Aliongeza kusema, “Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.” Kisha Musa akaufunika uso wake, kwa kuwa aliogopa kumwangalia Mungu.

7Yahweh akasema, “Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri. Nimesikia kelele zao kwa sababu ya mabwana wao, kwa kuwa nayajua mateso yao.8Nimekuja chini kuwaokoa dhidi ya mamlaka ya Wamisri na kuwatoa katika nchi ile na kuwaleta katika nchi nzuri, pana, nchi ijaayo maziwa na asali; kwenye ukanda wa Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.9Sasa kilio cha watu wa Israeli kimenifikia mimi. Zaidi sana, Mimi nimeyaona mateso ambayo Wamisri wanawatesa.10Sasa basi, nitakutuma wewe kwa Farao ili upate kuwatoa watu wangu, wana wa Israeli, kutoka katika nchi ya Misri.”

11Lakini Musa akamwambia Mungu, “Mimi ni nani hata niende kwa Farao na kuwatoa Waisraeli kutoka Misri?”12Mungu akamjibu, “Hakika nitakuwa pamoja nawe. Hii itakuwa ishara kwako ya kuwa nimekutuma. Utakapokuwa umewatoa watu kutoka Misri, mtaniabudu mimi katika mlima huu.”

13Musa akamwambia Mungu, “Nikienda kwa Waisraeli na kuwaambia, ‘Mungu wa baba zenu amenituma mimi kwenu,’ na kisha wakiniuliza, ‘jina lake nani?’ nitawaambia nini?”14Mungu akamwambia Musa, “MIMI NIPO AMBAYE NIPO.” Mungu akasema, “Ni lazima uwaambie Waisraeli, “MIMI NIPO amenituma kwenu.”

15Pia Mungu akamwambia Musa, “Lazima uwaambie Waisraeli, ‘Yahweh, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amenituma mimi kwenu. Hili ndio jina langu milele, na hivi ndivyo nitakavyokumbukwa na vizazi vyote.’16Nenda ukawakusanye wazee wa Israeli pamoja. Waambie, ‘Yahweh, Mungu wa baba zenu, Mungu wa Abrahamu, wa Isaka na Yakobo, amenitokea mimi na kusema, “Hakika nimewatazama na nimeona yale mliyotendewa huko Misri.17Nimeahidi kuwatoa ninyi katika mateso ya Misri na kuwaleta katika nchi ya Wakanaani, Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi. Nchi ijaayo maziwa na asali.”18Watakusikiliza. Wewe pamoja na wazee wa Israeli itawapasa kwenda kwa mfalme wa Misri, na imewapasa kumwambia, ‘Yahweh, Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Hivyo tuache sisi twende safari ya siku tatu katika jangwa ili tupate kutoa sadaka kwa Yahweh Mungu wetu.’19Lakini nafahamu ya kuwa mfalme wa Misri hatawaacha ninyi mwende, isipokuwa kwa kulazimishwa.20Nitainua mkono wangu na kuwapiga Wamisri kwa miujiza yote nitakayoifanya kati yao. Baada ya hayo, atawaacha mwende.21Nitawapa watu hawa kufadhiliwa kutoka kwa Wamisri ili muondokapo msiende mikono mitupu.22Kila mwanamke ataomba kwa jirani yake Mmisri na kwa kila mwanamke akaaye kwenye nyumba ya jirani yake, vyombo vya fedha na vya dhahabu na nguo. Nanyi mtawavika watoto wenu wa kiume na binti zenu. Kwa njia hii mtawateka nyara Wamisri.”

4

1Musa akajibu, “Lakini itakuwaje wasiponiamini mimi au wasiponisikiliza na kusema, ‘Yahweh hajakutokea wewe?”2Yahweh akamwambia, “Hicho ni nini mkononi mwako?” Musa akasema, “Ni fimbo.”3Yahweh akasema, “Itupe chini.” Musa akaitupa chini ile fimbo, nayo ikageuka na kuwa nyoka. Musa akarudi nyuma.4Yahweh akamwambia Musa, “Mchukue kwa kumshikia mkia wake.” Hivyo alimchukua yule nyoka. Mara ikageuka na kuwa fimbo mkononi mwake tena.

5“Hii ni ili wapate kuamini ya kuwa Yahweh, Mungu wa baba zao, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo amekutokea wewe.”

6Yahweh pia alimwambia, “Sasa ingiza mkono wako ndani ya vazi lako.” Hivyo Musa akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake. Na alipoutoa nje, tazama, mkono wake ulikuwa na ukoma, mweupe kama theluji.7Yahweh akasema, “Ingiza mkono wako ndani ya vazi lako tena.” Hivyo akaingiza mkono wake ndani ya vazi lake, na alipoutoa nje aliona ukiwa mzima tena kama ulivyo mwili wake wote.8Yahweh akasema, “Kama hawatakuamini wewe - kama hawatazingatia ishara yangu ya kwanza ya nguvu zangu au kuziamini, basi wataamini ishara ya pili.9Na ikiwa hawataamini hata ishara hizi zote mbili za nguvu zangu, au wasipokusikiliza wewe, basi chota maji kutoka katika mto na uyamwage katika nchi kavu. Maji utakayoyamwaga yatakuwa damu katika nchi kavu.”

10Ndipo Musa akamwambia Yahweh, “Bwana, mimi si mzuri wa kuongea, si hapo kwanza au hata baada ya kuwa umeongea na mtumishi wako. Mimi ni mdhaifu wa kuongea na nina kigugumizi.”11Yahweh akamwambia, “Ni nani anayeumba mdomo wa mwanadamu? Ni nani amfanyaye mwanadamu kuwa bubu au aone au kipofu? Je si mimi Yahweh?12Sasa nenda, nami nitauongoza mdomo wako na nitakufundisha cha kusema.”13Lakini Musa akasema, “Bwana, tafadhali mtume mtu mwingine, yeyote unayependa kumtuma.”

14Kisha Yahweh akamkasirikia Musa. Akasema, “Vipi kuhusu Haruni kaka yako yule Mlawi? Najua ya kuwa anaweza kuongea vizuri. Hata hivyo, anakuja kukutana na wewe, na atakapokuona moyo wake utajawa na furaha.15Wewe utaongea naye na utaweka maneno ya kusema kinywani mwake. Nami nitakiongoza kinywa chako na kinywa chake pia, nami nitaonyesha ninyi nyote yawapasayo kutenda.16Yeye ataongea na watu kwa niaba yako. Yeye atakuwa msemaji wako, na wewe utakuwa kama Mungu kwake.17Utachukua hii fimbo pamoja nawe mkononi mwako. Kwa fimbo hii utafanya ishara.”

18Hivyo Musa alirudi kwa Yethro - baba mkwe wake na kumwambia, “Niruhusu nipate kurudi kwa ndugu zangu walioko Misri ili niweze kuona kama bado wako hai.” Yethro akamwabia Musa, “Nenda kwa amani.”

19Yahweh akamwambia Musa kule Midiani, “Nenda, rudi Misri, kwa kuwa watu wote waliotaka kukuua wameshakufa.”20Musa akamchukua mke wake na watoto wake wa kiume na kuwapandisha kwenye punda. Akarudi mpaka nchi ya Misri, naye alichukua fimbo ya Mungu pamoja naye mkononi mwake.

21Yahweh akamwambia Musa, “Utakaporudi Misri, jitahidi kufanya ishara zote nilizokupa kufanya mbele ya Farao. Lakini nitaufanya moyo wake kuwa mgumu, naye hawatawaacha watu waende.22Lazima umwambie Farao, ‘Hivi ndivyo asemavyo Yahweh: Israeli ni mtoto wangu, mzaliwa wa kwanza wangu,23nami nakuamuru, “Mwache mwanangu aende ili apate kuniabudu mimi.” Lakini kwa kuwa umekataa kumwachia, hakika nitamuua mtoto wako wa kiume, mzaliwa wa kwanza wako.”’

24Sasa wakiwa njiani, wakati wa usiku walipopumzika, Yahweh alikutana na Musa na kutaka kumuua.25Kisha Zipora akachukua kisu kikali na kukata govi la mtoto wake wa kiume na kuligusisha miguuni pake. Kisha akasema, “Hakika wewe ni bwana harusi wangu kwa njia ya damu.”26Hivyo Yahweh akamwachia. Akasema, “Wewe ni bwana harusi wa damu” kwa sababu ya kutahiriwa.

27Yahweh akamwambia Haruni, “Nenda nyikani ukutane na Musa.” Haruni akaenda na kukutana naye katika mlima wa Mungu, na kumbusu.28Musa akwambia Haruni maneno yote ya Yahweh ambayo alimtuma kusema na kwa habari za ishara zote za nguvu za Yahwe ambazo alimwagiza kutenda.

29Kisha Musa na Haruni wakaenda na kuwakusanya wazee wote wa Israeli.30Haruni akawaambia maneno yote ambayo Yahweh alimwambia Musa. Pia alionesha ishara na miujiza ya nguvu za Yahweh mbele ya watu.31Watu waliamini. Waliposikia ya kuwa Yahweh aliwaona Waisraeli na ya kwamba aliyaona mateso yao, waliinamisha vichwa vyao na kumwabudu.

5

1Baada ya mambo haya kutokea, Musa na Haruni walienda kwa Farao na kumwambia, “Hivi ndivyo Yahweh, Mungu wa Israeli anasema: ‘Waache watu wangu waende, ili wapate kunifanyia karamu jangwani.’”2Farao akasema, “Yahweh ni nani? Kwa nini mimi nisikilize sauti yake na kuwaacha Israeli waende? Mimi simjui Yahweh; na la zaidi, sitawaacha Israeli waende.”3Wakasema, “Mungu wa Waebrania amekutana nasi. Tuache twende safari jangwani kwa siku tatu ili tutoe sadaka kwa Yahweh Mungu wetu ili asituadhibu kwa mapigo au kwa upanga.”4Lakini mfalme wa Misri aliwaambia, “Musa na Haruni, kwa nini mnawatoa watu kazini mwao? Nendeni kazini kwenu.”5Pia alisema, “Sasa kuna Waebrania wengi nchini mwetu, na ninyi mnawafanya waache kazi zao.”

6Siku ile ile, Farao alitoa amri kwa wasimamizi na wanyapara wa wale watu. Akasema,7“Tofauti na ilivyokuwa mwanzo, “Tofauti ni ilivyokuwa awali, msiwapatie tena watu majani ya kutengenezea tofali. Waacheni wao waende kujitafutia majani wenyewe.8Ingawa wanapaswa kuleta hesabu sawa ya matofali watakayotengeneza kama ilivyokuwa awali. Msipokee pungufu, kwasababu wao ni wavivu. Ndiyo maana wanapiga kelele na kusema, ‘turuhusu tuende tukamtolee sadaka Mungu wetu.’9Waongezeeni kazi wanaume ili wasipate tena muda wa kusikiliza maneno ya upotosha.”

10Kwa hiyo viongozi wa watu na waangalizi wao waliwajulisha watu. Walisema, “Hivi ndivyo farao amesema: ‘Sitawapeni tena malighafi.11Nyinyi wenyewe mtaenda kutafuta majani popote mtakapopata, lakini kazi zenu hazitapunguzwa.12Basi watu hao wakatawanyika katika nchi yote ya Misri ili wapate kukusanya matakataka badala ya majani.13Wasimamizi wao wakawahimiza na kusema, “Malizeni kazi zenu, sawa na wakati ule majani yalipokuwapo.”14Wanyapara wa Farao wakawapiga wasimamizi wa Waisraeli, watu walewale ambao waliwaweka kuwa wasimamizi wa watumishi. Wale Wanyapara wakakazana kuwauliza, “Kwanini hamjatimiza idadi ya matofali inayotakiwa kwenu, siku ya jana na hata leo kama ambavyo mlifanya siku za nyuma?”

15Basi Wanyapara wa wana wa Israeli wakamwendea Farao na kumlilia. Walisema, “Kwanini unawatendea watumishi wako hivi?16Sisi watumishi wako hatupewi majani tena, lakini bado wanatuambia sisi, “Tengenezeni tofali!’ Sisi watumwa wako tunapigwa sasa, lakini kosa hilo ni la watu wako.”17Lakini Farao akasema, “Ninyi ni wavivu! Wavivu ninyi! Ninyi mwasema, ‘Turuhusu twende kumtolea Yahweh sadaka.’18Sasa rudini kazini. Hamtapewa majani tena, lakini mnapaswa kutengeneza idadi ile ile ya matofali.”

19Wanyapara wa wana wa Israeli wakagundua ya kuwa walikuwa kwenye shida kubwa mara walipoambiwa, “Hamtapunguza kamwe idadi ya matofali mnayotengeneza kila siku.”20Wakakutana na Musa na Haruni, waliokuwa wamesimama nje ya Ikulu wakati wanatoka kwa Farao.21Wakawaambia Musa na Haruni, “Yahweh awatazame ninyi na kuwaadhibu, kwa sababu mmetufanya sisi kuonekana wabaya mbele ya Farao na watumishi wake. Mmetia upanga mikononi mwao ili watuue.”

22Musa akarudi kwa BWANA na kumwambia, “Bwana, kwanini umewatenda mabaya watu hawa? Kwanini kunituma mimi kwanza?23Tangu nilipokuja kwa Farao kusema naye kwa jina lako, amewatenda mabaya watu hawa, wala hujawaokoa watu wako hata kidogo.”

6

1Kisha Yahweh akasema na Musa, “Sasa utaona nitakacho fanya kwa Farao. Utaona hili, kwa kuwa ata waacha waenda kwa mkono wangu hodari. Kwasababu ya mkono wangu hodari, atawaondoa nje ya nchi.”

2Mungu akasema na Musa na kumwambia, “Mimi ni Yahweh.3Nilimtokea Ibrahimu, Isaka, na Yakobo kama Mungu mwenye nguvu; lakini kwa jina langu, Yahweh, sikujuliikana kwao.4Pia niliimarisha agano langu na wao, ilikuwapatia nchi ya Kanani, nchi walioishi kama sio raia, nchi walio tanga tanga.5Zaidi ya yote, nimesikia kilio cha Waisraeli ambao wa Misri wamewafanya watumwa, na nimekumbuka agano langu.6Kisha basi, sema kwa Waisraeli, ‘Mimi ni Yahweh. Nitawatoa kwenye utumwa chini ya wa Misri, na kuwaweka huru na nguvu zao. Nitawaokoa kwa kudhihirisha nguvu zangu, na kwa matendo ya ajabu ya hukumu.7Nitawaleta kwangu kama watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu. Mtajua kuwa mimi ndiye Yahweh Mungu wenu, aliye watoa kwenye utumwa chini ya wa Misri.8Nitawaleta kwenye nchi niliyomuahidi kumpa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Nitawapa kama mali yenu. Mimi ni Yahweh.

9Musa alipowaambia haya Waisraeli, hawakumsikiliza kwasababu ya mateso magumu ya utumwa wao.

10Hivyo Yahweh akazungumza na Musa na kumwambia,11“Nenda umwambie Farao, mfalme wa Misri, awaache watu wa Israeli waondoke kwenye nchi yake.”12Musa akamwambia Yahweh, “Kama Waisraeli hawajanisikiliza mimi, kwa nini Farao anisikillize mimi, ili hali mimi sio mzuri wakuzungumza?”13Yahweh akasema na Musa na Haruni. Akawapa amri ya Waisraeli na Farao, mfalme wa Misri, awatoe Waisraeli kutoka nchi ya Misri.

14Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao: wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli, walikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Rubeni.

15Wana wa Simeoni walikuwa Yemueli, Yamini, Ohadi, Yakini, Zohari, na Shauli - mwana wa mwanamke wa Kanani. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Simeoni.

16Hapa yameorodheshwa majina ya wana wa Lawi, pamoja na uzo wao. Walikuwa ni Gerishoni, Kohathi, na Merari. Lawi aliishi mpaka alipo kuwa na miaka 137.

17Wana wa Gerishoni walikuwa Libni na Shimei.

18Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na uzieli. Kohathi aliishi hadi miaka 133.

19Wana wa Merari walikuwa Mahli na Mushi. Hawa walikuja kuwa mababu wa ukoo wa Walawi, pamoja na uzao wao.

20Amramu alimuoa Yokebedi, dada yake baba yake. Alimzalia Haruni na Musa. Amramu aliishi miaka 137 na akafa.

21Wana wa Izhari walikuwa Kora, Nefegi, na Zikri.

22Wana wa Uzieli walikuwa Mishaeli, Elizafani na Sithri.

23Haruni alimuoa Elisheba, binti wa Aminadabu, dada wa Nashoni. Alimzaa Nadabu na Abihu, Eleazari na Ithamari.

24Wana wa Kora walikuwa Asiri, Elikana na Abiasa. Hawa walikuwa mababu wa ukoo wa Wakora.

25Eleazari, mwana wa Haruni, alimuoa mmoja wa mabinti Wa Putieli. Alimzalia Fineazi. Hawa walikuwa vichwa wa nyumba za baba yao miongoni mwa Walawi, pamoja na uzao wao.26Hawa wanaume wawili walikuwa Musa na Haruni ambao Yahweh alisema, “Waleteni Waisraeli kutoka nchi ya Misri, kwa makundi ya wanaume wapiganaji.”27Haruni na Musa wakazungumza na Farao, mfalme wa Misri, awaruhusu Waisraeli watoke Misri. Hawa walikuwa Musa na Haruni wale wale.28Pale Yahweh alipo zungumza na Musa katika nchi ya Misri,29alimwambia, “Mimi ni Yahweh. Sema kwa Farao, mfalme wa MIsri, kila kitu nitacho kwambia.”30Lakini Musa alimwambia Yahweh, “Mimi sio mzuri wa kuongea, hivyo kwanini Farao anisikilize mimi?”

7

1Yahweh akasema na Musa, “Ona, nimekufanya kama mungu kwa Farao. Haruni kaka yako atakuwa nabii wako.2Utasema kila kitu nitakacho kuamuru kusema. Haruni kaka yako atasema na Farao ili awaachie watu wa Israeli watoke kwenye nchi yake.3Lakini nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, na nitaonyesha ishara nyingi za nguvu zangu, maajabu mengi, katika nchi ya Misri.4Lakini Farao hatakusikiliza, kwa hiyo nitaweka mkono wangu juu ya Misri na kutoa makundi yangu ya wanaume wapiganaji, watu wangu, wazao wa Israeli, watoke nchi ya Misri kwa matendo makubwa ya hukumu.5Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitakapo nyoosha mkono wangu kwa Misri na kuwatoa Waisraeli kutoka miongoni mwao.”

6Musa na Haruni wakafanya hivyo; walifanya kama Yahweh alivyo waamuru.7Musa alikuwa na miaka themanini, na Haruni miaka themanini na tatu walipo ongea na Farao.

8Yahweh akamwambia Musa na Haruni,9“Wakati Farao atakapo waambia, ‘Fanya muujiza,’ utamwambia Haruni, ‘Chukua gongo lako na ulirushe chini mbele ya Farao, ili ligeuke nyoka.”10Kisha Musa na Haruni wakaenda kwa Farao, na wakafanya kama Yahweh alivyo waamuru. Haruni akarusha chini gongo lake mbele ya Farao na watumishi wake, na likageuka nyoka.11Kisha naye Farao akawaita wazee wenye hekima na wachawi. Wakafanya jambo hilo hilo kwa uchawi wao.12Kila mtu akarusha chini gongo lake, na magongo yakawa nyoka. Lakini gongo la Haruni lilimeza nyoka zao.13Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, na hakusikiliza, kama Yahweh alivyo tabiri.

14Yahweh akasema na Musa, “Moyo wa Farao ni mgumu, na anakataa kuacha watu waende.15Nenda kwa Farao asubui anapoenda kwenye maji. Simama kwenye chanzo cha mto kukutana naye, na uchukuwe mkononi mwako gongo ambalo liligeuka nyoka.16Mwambie, ‘Yahweh, Mungu wa Waebrania, amenituma kwako, “Acha watu wangu waende, iliwaniabudu nyikani. Mpaka sasa haujanisikiliza.”17Yahweh anasema hili: “Kwa hili utajua kuwa mimi ni Yahweh. Ninaenda kupiga maji ya mto wa Misri kwa gongo langu lililo mikononi mwangu, na mto utageuzwa kuwa damu.18Samaki walio kwenye mto watakufa, na mto utanuka. Wa Misri Hawataweza kunywa maji yalio kwenye mto.”

19Kisha Yahweh akasema na Musa, “Mwambie Haruni, ‘Chukua gongo lako na unyooshe mkono kwenye maji ya Misri, na juu ya mito yake, mifereji, visima, na madimbwi yote, ili maji yao yawe damu. Fanya hivi ili kuwe na damu nchi nzima ya Misri, hadi kwenye vyombo vyote vya mbao na mawe.”

20Musa na Haruni walifanya kama Yahweh alivyo waamuru. Haruni alinyanyua gongo na kupiga maji ya mto, machoni pa Farao na watumishi wake. Maji yote kwenye mto yaligeuka damu.21Samaki kwenye mito wakafa, na mto ukaanza kunuka. Wamisri hawakuweza kunywa maji kwenye mto, na damu ilikuwa kila mahali katika nchi ya Misri.22Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao. Kwa hiyo moyo wa Farao ukawa mgumu, na akakataa kuwasikiliza Musa na Haruni, kama Yahweh alivyo sema itatokea.23Kisha Farao akarudi na kwenda nyumbani kwake. Wala hakutilia maanani hili.24Wamisri wote walichimba pembeni ya mto kwa ajili ya maji ya kunywa, lakini hawakuweza kunywa maji ya mto.

25Siku saba zilipita baada ya Yahweh kushambulia mto.

8

1Kisha Yahweh akazungumza na Musa, “Nenda kwa Farao na umwambie, ‘Yahweh anasema hivi: Acha watu wangu waende ili wakaniabudu.2Ukikataa kuwaruhusu waende, nitaidhuru nchi yako yote kwa vyura.3Mito itajawa na vyura. Watatoka na kuingia nyumbani kwako, chumbani kwako, na kitandani kwako. Wataenda nyumbani mwa watumishi wako. Wataenda kwa watu wako, kwenye majiko yako, na vyombo vya kukandia mkate.4Vyura watakushambulia wewe, watu wako, na watumishi wako wote.”

5Yahweh akamwambia Musa, “Mwambie Haruni, ‘Nyoosha mkono wako na gongo lako kwenye mito, mifereji, na kwenye mabwawa, na uwatoe vyura juu ya nchi ya Misri.”’6Haruni akanyoosha mkono juu ya maji ya Misri, na vyura wakatoka na kujaza nchi ya Misri.7Lakini wachawi walifanya vivyo hivyo na uchawi wao: waliwatoa vyura juu ya nchi ya Misri.8Kisha Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Muombeni Yahweh ili awaondoe vyura kwangu na kwa watu wangu. Kisha nitawaacha watu waende, ili wamtolee dhabihu.”9Musa akamwambia Farao, “Unaweza chukua fursa ya kuniambia lini nikuombee wewe, watumishi wako, na watu wako, ili vyura waondolewe kwako na nyumbani kwako na wabaki tu kwenye mito.”10Farao akasema, “Kesho.” Musa akasema, “Acha iwe kama ulivyo sema, ili kwamba ujue hakuna Mungu mwengine kama Yahweh, Mungu wetu.11Vyura wataondoka kutoka kwako, nyumbani mwako, kwa watumishi wako, na kwa watu wako. Watabaki tu kwenye mito.”

12Musa na Haruni wakaondoka kwa Farao. Kisha Musa akamlilia Yahweh kuhusu hao vyura alio waleta kwa Farao.13Yahweh akafanya kama Musa alivyo omba: Vyura wakafa kwenye nyumba, nyuani, na mashambani.14Watu wakawakusanya kwa mafungu, na nchi ikanuka.15Lakini Farao alipoona kuna afadhali, aliufanya moyo wake kuwa mgumu na hakumsikiliza Musa na Haruni, kama Yahwe alivyosema.

16Yahweh akamwambia Musa, “Mwambie Haruni, ‘Nyoosha gongo lako na upige udongo chini, ili kuwe chawa katika nchi yote ya Misri”17Wakanya hivyo: Haruni akanyoosha mkono wake na gongo lake. Akaupiga udongo wa ardhi. Chawa wakaja juu ya watu na wanyama. Udongo wote kwenye ardhi ukawa chawa katika nchi ya Misri.18Wachawi walijaribu kufanya chawa kwa uganga wao lakini hawakuweza. Palikuwa na chawa kwa watu na kwa wanyama.19Kisha wachawi wakamwambia Farao, “Hiki ni kidole cha Mungu.” Lakini moyo wa Farao ulikuwa Mgumu, hivyo akakataa kuwasikiliza. Ilikuwa kama Yahwe alivyo sema Farao atafanya.

20Yahweh akamwambia Musa, “Inuka asubui mapema na usimame mbele ya Farao anapoenda mtoni. Umwambie, ‘Yahweh anasema hivi: “Acha watu wangu waende wakaniabudu mimi.21Lakini usipo acha watu wangu waende nitatuma kundi la nzi kwako, watumishi wako, na watu wako, na kwenye nyumba zenu. Nyumba za wa Misri zitajawa na makundi ya nzi, na ata ardhi wanayo simama itajawa na nzi.22Lakini katika siku hiyo nitaitendea nchi ya Gosheni tofauti, nchi ambayo watu wangu wanaishi, ili kwamba kusiwe na makundi ya nzi huko. Hili litatokea ili kwamba mjue mimi ni Yahweh katika hii nchi.23Nitaweka utofauti kati ya watu wangu na watu wako. Hii ishara ya nguvu zangu itatokea kesho.”

24Yahwe akafanya hivyo, na kundi kubwa la nzi likaja nyumbani mwa Farao na nyumbani mwa watumishi wake. Katika nchi yote ya Misri, nchi iliharibiwa na makundi ya nzi25Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Nendeni, mtolee Mungu wenu dhabihu kwenye nchi yetu.”26Musa akasema, “Sio vyema sisi kufanya hivyo, kwa kuwa dhabihu tunazo mtolea Yahweh Mungu wetu zinachukiza kwa Wamisri. Kama tutatoa dhabihu mbele ya macho yao zilizo chukizo kwa Wamisri, hawata tupiga mawe?27Hapana, ni safari ya siku tatu kwenda nyikani ambayo lazima tuende, ili kiutoa dhabihu kwa Yahweh Mungu wetu, kama anavyo tuamuru.”28Farao akasema, “Nitakuruhusu kwenda kumtolea dhabihu Yahweh Mungu wenu nyikani. Ila usiende mbali sana. Niombee.”29Musa akasema, “Wakati tu nitakapoenda kutoka kwako, nitamuomba Yahweh ili makundi ya nzi yatoke kwako, wewe Farao, na watumishi wako na watu kesho. Lakini usifanye udhalimu tena kwa kutowaacha watu wetu waende kumtolea dhabihu Yahweh.”

30Musa akaenda nje kutoka kwa Farao na kumuomba Yahweh.31Yahweh akafanya kama Musa alivyo muomba: alitoa makundi ya nzi kutoka kwa Farao, watumishi wake, na watu wake. Hakuna ata mmoja aliye baki.32Lakini Farao aliufanya moyo wake mgumu tena, na hakuwaacha watu waende.

9

1Kisha Yahweh akamwambia Musa, Nenda kwa Farao na umwambie, ‘Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: “Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.”2Lakini ukikataa kuwaruhusu waende, kama utaendelea kuwabakisha nyuma,3basi mkono wa Yahweh utakuwa kinyume dhidi ya mifugo yako shambani na kwa farasi, punda, ngamia, ng'ombe na kondoo, naitasababisha ugonjwa mbaya sana.4Yahweh atatendea tofauti mifugo ya Israeli na mifugo ya Misri: Haukuna mnyama wa Waisraeli ataye kufa.5Yahweh ametenga muda; amesema, “Ni kesho ambapo nitafanya ilitukio katika nchi.”

6Yahweh akafanya hivi siku iliyofuata: mifugo yote ya Misri ikafa. Lakini hamna mnyama wa Waisraeli aliye kufa, hamna mnyama ata mmoja.7Farao akafanya utafiti, na tazama, hakuna mnyama ata mmoja aliye kufa. Lakini moyo wake ulikuwa mjeuri, hivyo hakuwaacha watu waende.

8Kisha Yahweh akawambia Musa na Haruni, “Chukua majivu na uyajaze mkononi kutoka kwenye tanuru. Wewe, Musa, lazima uyarushe juu wakati Farao akitazama.9Yatakuwa vumbi safi nchi nzima ya Misri. Yatasababisha majipu na mafua kulipuka kwa watu na wanyama katika nchi yote ya Misri.”10Hivyo Musa na Haruni wakachukuwa majivu kutoka kwenye tanuru na kusimama mbele ya Farao. Kisha Musa akarusha majivu juu. Majivu yakasababisha majipu na mafua kutokea kwa watu na wanyama.11Waganga hawakuweza kumzuia Musa kwa sababu ya majipu, kwa sababu majipu yalikuwa kwao na kwa Wamisri wote.12Yahweh akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, Farao hakuwasikiliza Musa na Haruni. Hili ndilo Yahweh alilo mwambia Musa Farao atakalo fanya.

13Kisha Yahweh akamwambia Musa, Amka asubuhi mapema, simama mbele ya Farao, na umwambie, ‘Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: Acha watu wangu waende ili wakaniabudu mimi.14Kwa muda huu nitatuma mapigo kwako wewe, kwa watumishi wako na watu wako. Nitafanya hivi ili ujue hakuna kama mimi kwenye dunia yote.15Mpaka sasa ningeweza kuunyosha mkono wangu na kukushambulia wewe na watu wako kwa ugonjwa, na ungeondolewa kwenye nchi.16Lakini ni kwa sababu hii nimekuruhusu uishi: ili kukuonyesha nguvu zangu, ili kwamba jina langu litangazwe dunia nzima.17Bado unajiinua dhidi ya watu wangu kwa kuwaacha wasiende.18Sikiliza! Kesho muda kama huu nita leta mvua ya mawe ya barafu kubwa, kama ambayo haijawai kuonekana Misri toka ilipo anza hadi sasa.19Kisha sasa, tuma wanaume na ukusanye mifugo yako na vitu vyote ulivyo navyo mashambani sehemu salama. Kila mtu na mnyama aliyeko shambani na hajaletwa nyumbani - mawe ya barafu yatawashukia, na watakufa.”

20Kisha hao watumishi wa Farao walio amini ujumbe wa Yahweh wakaharakisha kuleta watumwa na mifugo yao ndani ya nyumba zao.21Lakini hao ambao hawakuchukuwa ujumbe wa Yahweh maanani waliacha watumwa wao na mifugo shambani.22Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu ili kuwe na mawe ya barafu katika nchi yote ya Misri, kwa watu, kwa wanyama, na kwenye mimea yote shambani na nchi nzima ya Misri.”23Musa akanyoosha mkono na gongo lake kuelekea mbiguni, na Yahweh akatuma mngurumo, mawe ya barafu, na radi kwenye nchi. Pia alinyesha mvua kwenye nchi ya Misri.24Hivyo kulikuwa na radi iliyo changanyika na mawe ya barafu, ilikuwa hatari sana, kuliko yeyote iliyowahi kutokea kwenye nchi ya Misri tangu iwe taifa.25Katika nchi yote ya Misri, barafu ya mawe ilipiga kila kitu kwenye shamba, watu na wanyama. Ilipiga kila mmea shambani na kuvunja kila mti.26Isipo kuwa tu nchi ya Gosheni, walipoishi Waisraeli, hapakuwa na mawe ya barafu.

27Kisha Farao akatuma wanaume wakawaite Musa na Haruni. Akawaambia, “Nimetenda dhambi wakati huu. Yahweh ni mwenye haki, na mimi na watu wangu ni waovu.28Muombe Yahweh, kwa sababu radi na barafu ya mawe imezidi. Nitawaacha muende, na hamtabaki tena hapa.”

29Musa akamwambia, “Nitakapo ondoka tu kwenye mji, nitaitanua mikono yangu kwa Yahweh. Mngurumo utaacha, na hakutakuwa na barafu ya mawe tena. Kwa hili utajua kuwa nchi ni ya Yahweh.30Lakini kwa wewe na watu wako, najua bado hamu mheshimu Yahweh Mungu.”

31Sasa kitani na shayiri ziliharibiwa, kwa kuwa shayiri ilikuwa katika kukomaa, na kitani ilikuwa imestawi.32Lakini ngano na kusemethu hazikupigwa mana zinachelewa kukua.

33Musa alipo muacha Farao na mji, alitanua mikono yake kwa Yahweh; mngurumo na barafu ya mawe ikasimama, na mvua haikunyesha tena.34Farao alipoona mvua, barafu ya mawe, na mngurumo umekatika, akatenda dhambi na kufanya moyo wake kuwa mgumu, pamoja na watumishi wake.35Moyo wa Farao ulikuwa mgumu, hakuacha watu wa Israeli waende. Hivi ndivyo Yahweh alimwambia Musa Farao atafanya.

10

1Yahweh akamwambia Musa, “Nenda kwa Farao, kwa kuwa nimeufanya moyo wake kuwa mgumu na moyo wa watumishi wake. Nimefanya hivi kuonyesha hizi ishara za nguvu zangu miongoni mwao.2Pia nimefanya hivi ili muwaambie watoto wenu na wajukuu wenu vitu nilivyo fanya, jinsi nilivyo itendea Misri kwa ukali, na jinsi nilivyo onyesha aina tofauti za ishara za nguvu zangu miongoni mwao. Kwa hili mtajua kuwa mimi ni Yahweh.”

3Hivyo Musa na Haruni wakaenda kwa Farao na kumwambia, “Yahweh, Mungu wa Waebrania, anasema hivi: ‘Kwa muda gani utaendelea kukataa kujinyenyekesha mbele zangu? Acha watu wangu waende ili wakaniabudu.4Lakini ukikataa kuwaruhusu watu wangu kwenda, sikiliza, kesho nitaleta nzige kwenye nchi yako.5Watafunika ardhi ya juu ili kwamba mtu asiweze kuona udongo. Watakula mabaki yote yalio salia kwenye mvua ya barafu ya mawe. Pia watakula kila mti unaokua shambani.6Watajaza nyumba zenu, zote za watumishi wenu, na zote za Wamisri wote - jambo ambalo baba zenu wala mababu zenu hawakuwai kuona, jambo ambalo halikuwai shuhudiwa toka walipo kuwa duniani hadi leo.” Kisha Musa akaondoka na kutoka kwa Farao.

7Watumishi wa Farao wakamwambia, “Mpaka lini huyu mwanaume ata kuwa msumbufu kwetu? Acha Waisraeli waende wakamuabudu Yahweh Mungu wao. Bado haujatambua kuwa Misri imeharibiwa?”8Musa na Haruni wakaletwa tena kwa Farao, ambaye aliwaambia, “Nendeni mkamuabudu Yahweh Mungu wenu. Lakini watu gani wataenda?”9Musa akasema, “Tutaondoka na wadogo wetu na wakubwa wetu, pamoja na wana wetu na mabinti zetu. Tutaondoka na ng'ombe na kondoo zetu, maana lazima tufanye siku kuu ya Yahweh.”

10Farao akawaambia, “Yahweh kwa kweli awe nanyi, kama nitawaacha muende na wadogo zenu waende. Angalia, una uovu kwenye nia.11Hapana! Nenda, wanaume tu miongoni mwenu, na mmuabudu Yahweh, kwa kuwa hilo ndilo mnalo litaka.” Kisha Musa na Haruni wakaondolewa uweponi mwa Farao.

12Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kwenye nchi ya Misri palipo na nzige, ili washambulie nchi ya Misri na kula kila mmea, kila kitu mvua ya mawe iliyo acha.”

13Musa akanyoosha na gongo lake juu ya nchi ya Misri, na Yahweh akaleta upepo wa mashariki juu ya nchi mchana wote na usiku mzima. Palipo kuwa asubui, upepo wa mashariki ulileta nzige.14Nzige wakaenda nchi yote ya Misri na kuharibu sehemu zote. Hapajawai kuwa na kundi kama hilo la nzige juu ya nchi, hakuna tena kama hilo litawai kutokea.15Walifunika ardhi yote ya juu ikawa giza. Walikula kila mmea na kila tunda la miti ambayo barafu ya mawe ilibakisha. Kila eneo la nchi ya Misri, hakuna mmea wa kijani ulibaki, wala mti au mmea wa shambani.

16Kisha Farao akawaita Musa na Haruni na kuwaambia, “Nimefanya dhambi dhidi ya Yahweh na dhidi yako.17Kisha sasa, nisamehe dhambi yangu wakati huu, na uombe kwa Yahweh Mungu wako aondoe hiki kifo kwangu.”

18Musa akaondoka kwa Farao na kumuomba Yahweh.19Yahweh akaleta upepo mkali wa magharibi ulio wachukuwa wale nzige na kuwapeleka Bahari ya Shamu; hakuna nzige ata mmoja aliye baki eneo la Misri.

20Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, na Farao hakuacha Waisraeli waende.

21Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono wako kuelekea mbingu, ili kuwe na giza nchi yote ya Misri, giza linalo weza kuhisiwa.”22Musa akanyoosha mkono wake kuelekea mbingu, na kulikuwa na giza nene nchi yote ya Misri kwa siku tatu.23Hakuna aliye muona mwingine; hakuna aliyetoka nyumbani mwake kwa siku tatu. Walakini, Waisraeli wote walikuwa na taa katika sehemu walizo ishi.

24Farao alimuita Musa na kusema, “Nenda umuabudu Yahweh. Hata familia zenu za weza kwenda nanyi, lakini ng'ombe zenu na kondoo zenu zitabaki.”25Lakini Musa akasema, “Lazima utupe wanyama kwa ajili ya dhabihu na sadaka za kuteketeza ili tuwatoe dhabihu kwa Yahweh Mungu wetu.26Mifugo yetu lazima iende na sisi; hata mmoja hawezi kubaki, lazima tuwapeleke wakamuabudu Yahweh Mungu wetu. Kwa kuwa hatujui tutakacho muabudu nacho Yahweh mpaka tufike pale.

27Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, na hakuwaacha waende.28Farao alimwambia Musa, “Toka kwangu! Kuwa muangalifu na jambo moja, kwamba usinione tena, kwa kuwa siku utakapo uona uso wangu, utakufa.”29Musa akasema, “Wewe mwenyewe umesema. Sitauona uso wako tena.”

11

1Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Bado kuna pigo moja nitakalo lileta kwa Farao na Misri. Baada ya hilo, atakuacha uondoke hapa. Atakapo kuachia uende, hata kuondoa kabisa.2Waelekeze watu kwamba kila mwanaume na mwanamke amuulizie jirani yake vitu vya fedha na vitu vya dhahabu.”3Sasa Yahweh aliwafanya Wamisri kuwa na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Aidha, Musa alikuwa wakuvutia sana machoni pa watumishi wa Farao na watu wa Misri.

4Musa akasema, “Yahweh asema hivi: ‘Wakati wa usiku wa manane nitaenda Misri yote.5Wazaliwa wa kwanza wote wa nchi ya Misri watakufa, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, anaye keti kiti chake cha enzi, mpaka mzaliwa wa kwanza wa misichana mtumwa anaye saga mbegu, na kwa wazaliwa wa kwanza wa mifugo.6Kisha kutakuwa na kilio kikubwa nchi yote ya Misri, kama ambacho hakijawai wala hakitatokea tena.7Lakini hata mbwa hata bweka kwa watu wa Israeli, dhidi ya mtu au mnyama. Kwa hili utajua kuwa nina watendea Wamisri na Waisraeli tofauti.8Watumishi wote hawa wako, Farao, watakuja chini yangu na kunisujudu mimi. Watasema, ‘Nenda, wewe na watu wote wanao kufuata!’ Baada ya hapo nitaondoka.” Kisha akaondoka mbele ya Farao kwa hasira kubwa.

9Yahweh akamwambia Musa, Farao hatakusikiliza. Hii ni ili nifanye mambo ya ajabu katika nchi ya Misri.”

10Musa na Haruni wakafanya mambo haya ya kushangaza mbele za Farao. Lakini Yahweh aliufanya moyo wa Farao kwa mgumu, na Farao hakuwaacha watu wa Israeli kuondoka katika nchi yake.

12

1Yahweh akasema na Musa na Haruni katika nchi ya Misri. Alisema,2“Kwako wewe, mwezi huu utakuwa mwanzo wa miezi, mwezi wa kwanza wa mwaka kwako.3Liambie kusanyiko la Israeli, ‘Siku ya kumi mwezi huu kila mtu lazima achukue mwana kondoo au mbuzi mdogo wa kwake, kila familia ifanye hivi, mwana kondoo kwa kila nyumba.4Kama hiyo nyumba ni ndogo sana kwa mwana kondoo, mwanaume na jirani yake wachukue mwana kondoo au nyama ya mbuzi mdogo ambayo itatosha watu. Lazima iwe yatosha kwa kila mtu kula, kwaiyo lazima wachukue nyama ya kutosha kulisha wote.5Mwana kondoo wako au mbuzi wako mdogo lazima asiwe na upungufu, dume mwenye mwaka mmoja. Unaweza kuchukua mmoja wa kondoo au mbuzi.6Lazima umtunze mpaka siku ya kumi na nne ya huo mwezi. Kisha kusanyiko lote la Israeli lazima liwaue hawa wanyama jioni.7Lazima uchukue baadhi ya damu na uweke kwenye sehemu mbili za mihimo ya milango na juu ya fremu za milango ambapo utalia hizo nyama.8Lazima ule hizo nyama usiku, baada ya kuchoma kwenye moto. Kula na mkate ulio andaliwa kwa hamira, pamoja na mimea michungu.9Usiile mbichi au imechemshwa kwenye maji. Badala yake, choma kwenye moto na kichwa chake, miguu na sehemu za ndani.10Usiache ata kidogo kubaki mpaka asubui. Lazima uchome chochote kilicho baki asubui.11Hivi ndivyo wa paswa kula: ukiwa umefunga mkanda wako, umevaa viatu vyako, na gongo lako mkononi mwako. Lazima ule kwa haraka. Ni Pasaka ya Yahweh.12Yahweh anasema hili: Nitaenda katika nchi ya Misri usiku na kushambulia wazaliwa wote wa kwanza wa wanadamu na wanyama katika nchi ya Misri. Nitaleta pigo kwa miungu yote ya Misri. Mimi ni Yahweh.13Damu itakuwa ishara kwenye nyumba zenu ya kuja kwangu. Nitakapoona damu, nitapita nitakapo shambulia nchi ya Misri. Hili pigo halitawajia na kuwaharibu.

14Hii siku itakuwa kumbukumbu kwenu, ambayo lazima muadhimishe kama sherehe ya Yahweh. Itakuwa sheria kwenu pia, kwenye vizazi vyote vya watu wenu, ambayo mwapaswa kuadhimisha leo.15Utakula mkate bila hamira wakati wa siku saba. Siku ya kwanza utaondoa hamira kwenye nyumba zenu. Yeyote atakaye kula mkate uliyotiwa chachu kwanzia siku ya kwanza mpaka siku ya saba, huyo mtu lazima akatwe kutoka Israeli.16Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko lililo tengwa kwa ajili yangu, na siku ya saba kutakuwa na kusanyiko kama hilo. Hakuna kazi itakayo fanywa hizi siku, zaidi ya kupika kila mmoja ale. Hiyo ndio kazi pekee itakayofanywa na wewe.

17Lazima uadhimishe hii Sherehe ya Mkate Usiotiwa Chachu kwa sababu ni siku hii ambayo nitawaleta watu wako, kwa makundi yaliyo na silaha, kutoka nchi ya Misri. Lazima uadhimishe hii siku kwa vizazi vyote vya watu wako. Hii itakuwa sheria kwako.18Lazima ule mkate usiotiwa chachu kuanzia jioni ya siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza wa mwaka, mpaka jioni ya siku ya ishirini na moja ya mwezi.19Wakati wa hizi siku, nyumbani mwenu kusipatikane na hamira. Yeyote atakaye kula mkate ulio andaliwa na hamira lazima akatwe kutoka jamii ya Israeli, huyo mtu awe ni mgeni au mtu aliye zaliwa nchini mwenu.20Hautakula chochote kilicho andaliwa na hamira. Popote utakapo ishi, lazima ule mkate usio na hamira.”

21Kisha Musa akawaita viongozi wote wa Israeli na kuwaambia, “Nendeni na mchague mwanakondoo au mbuzi watakao tosha kulisha familia zenu na muue mwanakondoo wa pasaka.22Kisha chukua jani la hisopu na uchovye kwenye damu itakayo kuwa kwenye beseni. Paka damu iliyo kwenye beseni juu ya fremu ya mlango na kwenye mihimo miwili ya mlango. Hakuna ata mmoja atakayetoka nje ya mlango wake mpaka asubuhi23Kwa kuwa Yahweh atapita kushambulia Wamisri. Atakapoona damu juu ya fremu ya mlango na kwenye miimo miwili ya mlango, atapita mlango wako na hata ruhusu mharibifu kuja nyumbani kwenu kuwashambulia.24Lazima uadhimishe hili tukio. Hili litakuwa daima sheria kwako na kwa uzao wenu.25Utakapoingia nchi Yahweh atakayokupa, kama alivyo ahidi kufanya, lazima uadhimishe hili tendo la ibada.26Watoto wako watakapo kuuliza, ‘Hili tendo la ibada lina maana gani?’27kisha lazima useme, ‘Ni sadaka ya Pasaka ya Yahweh, kwa sababu Yahweh kapita nyumba za Waisraeli Misri alipo washambulia Wamisri. Aliweka nyumba zetu huru.”’ Kisha watu wakamsujudia Yahweh.28Waisraeli wakaenda na kufanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Haruni.

29Ikawa usiku wa manane, Yahwe akawashambulia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, kuanzia mzaliwa wa kwanza wa Farao, aliyeketi kiti chake cha enzi, mzaliwa wa kwanza wa mtu aliye gerezani na wazaliwa wote wa kwanza wa mifugo.30Farao akaamka usiku - yeye, watumishi wake, na Wamisri. Palikuwa na kelele za maombolezo Misri, kwa kuwa hakukuwa na nyumba ambayo hamna mtu hakufa.

31Farao akamuita Musa na Haruni usiku na kusema, “Inuka, tokeni miongoni mwa watu wangu, nyie pamoja na Waisraeli. Nenda, mmuabudu Yahweh, kama mlivyo sema mnataka kufanya.32Chukuweni ng'ombe zenu na kondoo zenu, kama mlivyo sema, na muende, na pia mnibariki.”

33Wamisri walikuwa na haraka ya kuwaondoa nchini, kwa kuwa walisema, “Sisi ni watu tuliokufa.”34Watu wakachukua ngano yao pasipo kuongeza hamira yeyote. Bakuli zao zakukandia ngano zilifungiwa kwenye nguo zao na kwenye mabega yao.35Watu Waisraeli walifanya kama Musa alivyo waambia. Waliwaomba Wamisri vitu vya fedha, vitu vya dhahabu, na nguo.36Yahweh aliwafanya Wamisri na shauku ya kuwapendeza Waisraeli. Hivyo Wamisri waliwapa chochote walicho waomba. Katika hili, Waisraeli waliwachukulia vingi Wamisri.

37Waisraeli wakasafiri kutoka Ramesi kwenda Sakothi. Walikuwa na idadi ya wanaume 600,000 kwa miguu, kuongezea kwa wanawake na watoto.38Mchanganyiko wa kundi la wasio Waisraeli pia walienda nao, pamoja na ng'ombe na kondoo, idadi kumbwa ya mifugo.39Walioka mikate na unga wa ngano wenye hamira waliotoa Misri. Ulikuwa hauna hamira kwasababu waliondolewa Misri na hawakuweza chelewa kuandaa chakula.

40Waisraeli waliishi Misri kwa miaka 430.41Baada ya miaka 430, siku hiyo hiyo, majeshi yote ya Yahweh yalio jiami waliondoka kutoka nchi ya Misri.42Huu ulikuwa usiku wakuwa macho, ili Yahwe awatoe kutoka nchi ya Misri. Huu ulikuwa usiku wa Yahweh wa kuadhimishwa na Waisraeli wote na watu wa vizazi vyao vyote.

43Yahweh akamwambia Musa na Haruni, “Hii ni sheria ya Pasaka: hakuna mgeni anaye ruhusiwa kuila.44Walakini, kila mtumwa wa Misraeli, aliye nunuliwa kwa pesa, anaeza kula baada ya kutahiriwa.45Wageni na watumishi waajiriwa hawapaswi kula chakula chochote.46Chakula chapaswa kuliwa ndani ya nyumba moja. Hauruhusiwi kubeba nyama yeyote nje ya nyumba, na hauruhusiwi kuvunja mfupa wowote.47Jamii zote za Israeli za paswa kuadhimisha sherehe.48Kama mgeni anaishi na wewe na anataka kuadhimisha Pasaka kwa Yahweh, ndugu zake wote wa kiume wapaswa kutahiriwa. Kisha anaeza kuja na kuadhimisha. Atakuwa kama watu waliozaliwa kwenye nchi. Walakini, hakuna mtu asiye tahiriwa anaruhusiwa kula chakula chochote.49Sheria hii itahusika kwa mzaliwa wa asili na mgeni anayeishi miongoni mwenu.”

50Waisraeli wote walifanya kama Yahweh alivyo waamuru Musa na Haruni.51Ikaja kuwa siku hiyo Yahweh akawaleta Israeli kutoka nchi ya Misri kwa makundi yalio jiami.

13

1Yahweh akasema na Musa na kumwambia,2“Nitengee wazaliwa wote wa kwanza, kila mzaliwa wa kwanza wa Waisraeli, watu na wanyama. Mzaliwa wa kwanza ni wangu.”

3Musa akawambia watu, “Kumbukeni hii siku, siku mliotoka Misri, kutoka nyumba ya utumwa, kwa mkono hodari wa Yahweh amewatoa kutoka hii sehemu. Hakuna mkate wa hamira waruhusiwa kuliwa.4Mnatoka Misri hii siku, mwezi wa Abibu.5Yahweh atakapo waleta nchi ya Wakanani, Wahiti, Waamori, Wahivi, na Wayebusi, nchi aliyo waapia mababu zenu kuwapa, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali - kisha wapaswa kuadhimisha hili tendo la ibada kila mwezi.6Kwa siku saba utakula mkate bila hamira; siku ya saba kutakuwa na maakuli ya kumuadhimisha Yahweh.7Mkate usio na hamira wapaswa kuliwa kwa siku saba zote; hakuna mkate ulio na hamira wapaswa kuliwa miongoni mwenu. Hakuna hamira yapaswa kuonekana kwenye mipaka yenu.8Hiyo siku utasema kwa watoto wako, ‘Hii ni kwa sababu ya kile Yahweh alichofanya kwangu nilipotoka Misri.’9Hii itakuwa kumbukumbu mkononi mwako, na kumbukumbu kwenye paji la uso wako. Hii ni ili sheria ya Yahweh iwe kinywani mwako, maana kwa mkono hodari Yahweh amewatoa kutoka Misri.10Kisha basi wapaswa kushika hii sheria kwa wakati uliyo kusudiwa kutoka mwaka hadi mwaka.

11Yahweh atakapo waleta kwenye nchi ya Wakanani, kama alivyo apa kwenu na kwa mababu zenu kufanya, na atakapo wapa nchi ninyi,12lazima umtengee mzaliwa wa kwanza mtoto na uzao wa kwanza wa wanyama wenu. Wakiume watakuwa wa Yahweh.13Kila mzaliwa wa kwanza wa punda lazima umnunue tena na mwanakondoo. Kama hautamnunua tena, lazima uivunje shingo yake. Lakini kila mzaliwa wa kwanza wakiume miongoni mwenu - lazima umnunue tena.14Mwanae atakapo kuuliza baadae, ‘Hii ina maana gani?’ kisha utamwambia, ‘Ni kwa mkono hodari Yahweh katutoa Misri, kutoka nyumba ya utumwa.15Farao alipokataa kwa ujeuri kutuachia twende, Yahweh aliwaua wazaliwa wa kwanza wa nchi ya Misri, wazaliwa wa kwanza wa watu na wa wanyama. Ndio sababu ninatoa dhabihu kwa Yahweh kwa kila mzaliwa wa kwanza wa kila mnyama, na pia sababu ninanunua wazaliwa wa kwanza wa wanangu tena.’16Hii itakuwa kumbukumbu mikononi mwako na kumbukumbu kwenye paji lako la uso, kwa kuwa ni kwa mkono hodari Yahweh alitutoa kutoka Misri.”

17Farao alipo waachia watu waende, Mungu akuwaongoza kwa njia ya Wafilisti, japo hiyo njia ilikuwa karibu. Kwa kuwa Mungu alisema, “Labda watu watabadili nia zao watakapoona vita na watarudi Misri.”18Hivyo Mungu akawaongoza watu kuzunguka nyikani kupita Bahari ya Shamu. Waisraeli waliondoka kutoka nchi ya Misri wakiwa wamejiami kwa pambano.

19Musa akachukuwa mifupa ya Yusufu pamoja naye, kwa kuwa Yusufu aliwaapisha Waisraeli na kusema, “Mungu atawaokoa, na muibebe mifupa yangu na nyie.”

20Waisraeli walisafiri kutoka Sakothi na kuweka kambi Ethamu pembezoni mwa nyikani.21Yahweh alitangulia mbele yao mchana kama nguzo ya wingu kuwaongoza njiani. Usiku alienda kama nguzo ya moto kuwapa mwanga. Kwa namna hii waliweza kusafiri mchana na usiku.22Yahweh hakuchukuwa kutoka kwa watu nguzo ya wingu mchana wala nguzo ya moto usiku.

14

1Yahweh akasema na Musa na kumwambia,2“Waambie Waisraeli wageuke na kuweka kambi mbele ya Pi Hahirothi, katikati ya Migdoli na bahari, mbele ya Baali Zefoni. Wapaswa kuweka kambi pembeni ya Pi Hahirothi.3Farao atasema kuhusu Waisraeli, ‘Wanahangaika kwenye nchi. Nyikani imewafunika.’4Nitaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, na yeye atawakimbiza. Nitapata utukufu kwa sababu ya Farao na jeshi lake lote. Wamisri watajua mimi ni Yahweh.” Kisha Waisraeli wakaweka kambi kama walivyo elekezwa.

5Mfalme wa Misri alipo ambiwa Waisraeli wametoroka, nia ya Farao na watumishi wake ikageuka dhidi ya watu. Wakasema, “Tumefanya nini kwa kuwaacha Waisraeli waende huru na wasitutumikie?”6Kisha Farao akachukua magari yake ya farasi na jeshi lake.7Alichukua magari ya farasi mia sita imara na magari yote ya farasi ya Misri, pamoja na maafisa wa hayo magari.8Yahweh akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, na mfalme akawafukuzia Waisraeli. Sasa Waisraeli waliondoka kwa shangwe.9Lakini Wamisri wali wafukuzia, pamoja na farasi na magari ya farasi, wapanda farasi, na jeshi lake. Walikuta Waisraeli wameeka kambi pembezoni mwa bahari kati ya Pi Hahirothi na Baali Zefoni.

10Farao alipo karibia, Waisraeli walitazama juu na kushangaa. Wamisri walikuwa wakija kwao, na waliogopa. Waisraeli walimlilia Yahweh.11Walimwambia Musa, “Ni kwasababu hakukuwa na makaburi Misri, hadi umetuleta tufe huku nyikani? Kwa nini umetutendea hivi, kwa kututoa Misri?12Hili si ndilo tulilo kwambia Misri? Tulikwambia, ‘Utuache, ili tuwafanyie Wamisri kazi.’ Ingekuwa bora kwetu sisi kuwafanyia kazi kuliko kufa nyikani.”

13Musa akawaambia watu, “Msiogope. Simameni imara na muone wokovu Yahweh atakao uleta kwenu leo. Kwa maana hamtawaona tena Wamisri mnaowaona leo.14Yahweh atawapigania, na ninyi mtasimama imara.”

15Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Kwa nini wewe, Musa, unaendelea kuniita mimi? Waambie Waisraeli waendelee mbele.16Nyanyua gongo lako juu, nyoosha mkono wako kuelekea baharini na uigawanye sehemu mbili, ili watu wa Israeli wapite baharini kwenye nchi kavu.17Jitahadharishe kuwa nitafanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu ili wawafuate. Nitapata utukufu kwasababu ya Farao na jeshi lake lote, magari yake ya farasi, na wapanda farasi.18Kisha Wamisri watajua kuwa mimi ni Yahweh nitakapo pata utukufu kwa sababu ya Farao, magari yake na farasi, na wapanda farasi wake.”

19Malaika wa Mungu, aliyeenda mbele ya Waisraeli, alihama na kwenda nyuma yao. Nguzo ya wingu ili sogea mbele yao na kwenda kusimama nyuma yao.20Wingu lilikuja katikati ya kambi ya Misri na kambi ya Israeli. Lilikuwa wingu jeusi kwa Wamisri, lakini liliangaza usiku kwa ajili ya Waisraeli, hivyo upande mmoja haukuweza kuja karibu na ya mwingine usiku wote.

21Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari. Yahweh akasogeza bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku huo wote na kufanya bahari nchi kavu. Kwa namna hii maji yaligawanyika.22Waisraeli walienda katikati ya bahari kwa nchi kavu. Maji yaliunda ukuta mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto.23Wamisri wakawafukuzia. Waliwafuata hadi katikati ya bahari - farasi wote wa Farao, magari ya farasi, na wapanda farasi.24Lakini masaa ya mapema ya asubui, Yahweh alitazama chini jeshi la Wamisri kupitia nguzo ya moto na wingu. Alisababisha hofu miongoni mwa Wamisri.25Magari yao ya farasi yalikuwa yana kwama matairi, na wapanda farasi waliendesha kwa ugumu. Hivyo Wamisri walisema, “Acha tuwakimbie Waisraeli, kwa kuwa Yahweh anawapigania dhidi yetu.”

26Yahweh akamwambia Musa, “Nyoosha mkono kuelekea bahari ili maji yawarudie Wamisri, magari yao ya farasi, na wapanda farasi wao.”27Hivyo Musa akanyoosha mkono wake kuelekea bahari, na ikarudi kwenye hali yake ya kawaida kulipo pambazuka. Wamisri walikimbilia ndani ya bahari, na Yahweh akawaingiza Wamisri kati kati yake.28Maji yakarudi na kufunika magari ya farasi ya Farao, wapanda farasi, na jeshi lake lote lililofwata magari ya farasi kwenye bahari. Hakuna aliyepona.29Walakini, Waisraeli walitembea kwenye nchi kavu katikati ya bahari. Maji yalikuwa ukuta kwa mkono wa kulia na mkono wa kushoto.

30Hivyo Yahweh akaokoa Israeli kutoka kwa mkono wa Wamisri, na Israeli ikaona maiti za Wamisri ufuoni.31Israeli ilipoona nguvu kubwa Yahweh aliyoitumia dhidi ya Wamisri, watu walimsifu Yahweh, na kumwamini Yahweh na mtumishi wake Musa.

15

1Kisha Musa na watu wa Israeli wakaimba huu nyimbo kwa Yahweh. Waliimba, “Nitaimba kwa Yahweh, kwa kuwa ameshinda kwa utukufu; farasi na dereva wake amewatupa kwenye bahari.

2Yahweh ni uweza wangu na nyimbo zangu, na amekuwa wokovu wangu. Huyu ni Mungu wangu, na nitamsifu, Mungu wa baba yangu, nitamtukuza.
3Yahweh ni shujaa; Yahweh ni jina lake.
4Ametupa magari ya farasi. Ya Farao na jeshi lake kwenye bahari. Maafisa wa Farao hodari walizama kwenye Bahari ya Shamu.
5Kina kiliwafunika; walienda kwenye kina kama jiwe.
6Mkono wako wa kulia, Yahweh, una nguvu ya utukufu; mkono wako, Yahweh, umewavunja adui.
7Kwa utukufu mkubwa umewapindua walioinuka dhidi yako. Umetuma gadhabu; imewateketeza kama karatasi.
8Kwa pumzi ya pua yako maji yaliojaa; maji yanayotembea yalisimama wima na kujaa juu; maji yalikuwa manene ndani ya kilindi cha bahari.
9Adui alisema, ‘Nitakimbiza, nitapita, nitagawa nitakacho chukua; tamanio langu litatimizwa kwao; nitavuta upanga wangu; mkono wangu utawaharibu wao.’
10Lakini ulipuliza kwa upepo wako, na bahari ikawafunika wao; walizama kama chuma nzito kwenye maji mengi.
11Ni nani kama wewe, Yahweh, miongoni mwa miungu? Nani kama wewe, mtakatifu wa utukufu, katika sifa umetukuzwa, anayefanya miujiza?
12Ulinyoosha mkono wako wa kulia, na dunia ikawameza.
13Katika uaminifu wa agano lako umewaongoza watu ulio waokoa. Katika uweza wako, umewaongoza katika sehemu takatifu unayo ishi.
14Watu watasikia, na watatetemeka; hofu itawakumba wakazi wa Filistia.
15Kisha wazee wa Edomu wataogopa; wanajeshi wa Moabu watetemeka; wakazi wote wa Kanani watayeyuka.
16Mshituko na hofu vitawaangukia. Kwa sababu ya nguvu ya mkono wako, watakuwa kimya kama jiwe hadi watu wako watakapo pita, Yahweh - hadi watu uliowaokoa watakapo pita.
17Utawaleta na kuwapanda kwenye mlima wa urithi wako, sehemu, Yahweh, ulio jenga ya kuishi, sehemu takatifu, Bwana wetu, mikono yako iliyojenga.
18Yahweh atatawala milele na milele.”

19Kwa kuwa farasi wa Farao walienda na magari ya farasi na wapanda farasi kwenye bahari. Yahweh alileta maji ya bahari juu yao. Lakini Waisraeli walienda juu ya nchi kavu katikati ya bahari.20Miriamu nabii wa kike, dada wa Haruni, akanyanyua tari, na wanawake wote wakatoka na matari, wakicheza naye.21Miriamu akawaimbia: “Muimbieni Yahweh, kwa kuwa ameshinda kwa utukufu. Farasi na mpanda farasi amewatupa baharini.

22Kisha Musa akaongoza Israeli mbele kupita Bahari ya Shamu. Walienda nyikani ya Shuri. Walisafiri kwa siku tatu nyikani pasipo kuona maji yeyote.23Kisha wakaja Mara, lakini hawakunywa maji ya huko kwa sababu yalikuwa machungu. Hivyo wakaita hiyo sehemu Mara.24Hivyo watu wakamlalamikia Musa na kusema, “Nini tunaweza kunywa?”25Musa akamlilia Yahweh, na kumuonyesha mti. Musa akautupa kwenye maji, na maji yakawa matamu kunywa. Ndio pale Yahweh alipowapa sheria kali, na ndio pale alipowajaribu.26Alisema, “Kama utasikiliza sauti ya Yahweh Mungu wako kwa umakini, na kufanya yaliyo sahihi machoni pake, na kama utatega sikio kwa amri zake na kutii sheria zake zote - sitawaletea ninyi magonjwa yale niliyowaletea Wamisri, kwa kuwa mimi ni Yahweh ninaye kuponya.”

27Kisha watu wakaja Elimu, palipo kuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mtende. Waliweka kambi hapo pembeni mwa maji.

16

1Watu wakaendelea na safari kutoka Elimu, na jamii yote ya Waisraeli ikaja nyikani mwa Sinu, iliopo katikati ya Elimu na Sinai, siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili walipotoka Misri.2Jamii yote ya Waisraeli wali walalamikia Musa na Haruni nyikani.3Waisraeli waliwaambia, “Kama tu tungekufa kwa mkono wa Yahweh nchi ya Misri tulipokuwa tumeketi kwenye vyombo vya nyama na tulikuwa tunakula mkate kwa tele. Maana umetuleta nyikani uue jamii zetu zote kwa njaa.”

4Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Nitakunyeshea mvua ya mikate. Watu wataenda na kukusanya kiasi cha siku kila siku ili niwajaribu kama wataendelea kushika sheria yangu au hapana.5Itakuja kuwa siku ya sita, kwamba watakusanya mara mbili zaidi ya wanavyokusanya, na watapika wanacholeta.”

6Kisha Musa na Haruni wakawaambia watu wote wa Israeli, “Jioni mtajua kuwa ni Yahweh aliyewaleta kutoka nchi ya Misri.7Asubui utaona utukufu wa Yahweh, kwa maana anasikia mna mlalamikia. Sisi ni nani hadi mtulalamikie?”8Musa pia akasema, “Utajua hili pale Yahweh atakapo kupa nyama jioni na mkate asubui kwa utele - kwa kuwa amesikia malalamishi mnayotamka dhidi yake. Nani ni Haruni na mimi? Malalamishi yenu sio dhidi yetu; ni dhidi ya Yahweh.”

9Musa akamwambia Haruni, “Sema kwa jamii yote ya watu wa Israeli, ‘Njoo karibu na Yahweh, kwa kuwa amesikia malalamishi yenu.’

10Ikawa, Haruni aliposema na jamii yote ya watu wa Israeli, wakaangalia kuelekea nyikani, na, tazama, utukufu wa Yahweh ukatokea kwenye wingu.11Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,12“Nimesikia malalamishi ya watu wa Israeli. Sema nao na useme, ‘Jioni utakula nyama, na asubui utashiba mkate. Kisha utajua mimi ni Yahweh Mungu wako.’”

13Ikaja kuwa kwamba jioni kware wakaja juu na kufunika kambi. Asubui umande ulitanda kambini.14Umande ulipo kwisha, pale juu ya ardhi ya nyikani kulikuwa na kama barafu iliyoganda kwenye ardhi.15Watu wa Israeli walipooona, walisema mmoja kwa mwenzake, “Hii ni nini?” Hawakujua ilikuwa ni nini. Musa akawaambia, “Ni mkate Yahweh aliyowapa mle.16Hii ni amri Yahweh aliyotoa: ‘Lazima mkusanye, kila mmoja wenu, kiasi unachoitaji kula, lita mbili kwa kila mtu. Hivi ndivyo utakavyo kusanya: kila mtu akusanye chakula cha kutosha kwa kila mtu anayeishi hemani mwako.’

17Watu wa Israeli wakafanya hivyo. Baadhi, wakakusanya zaidi, baadhi wakakusanya kidogo.18Walipopima kwa kipimo cha lita, hao walio kusanya zaidi. Hawakuwa na kilicho salia, na hao walio kusanya kidogo hawakuwa na upungufu. Kila mmoja alikusanya cha kutosha kukidhi maitaji yake.

19Kisha Musa akawaambia, “Hakuna hata mmoja kubaki hadi asubui.”20Walakini, hawakumsikiliza Musa. Baadhi yao waliacha baadhi hadi asubui, lakini ilizalisha wadudu na kuwa batili. Kisha Musa akawa na hasira juu yao.

21Walikusanya asubui kwa asubui. Kila mtu alikusanya cha kutosha kula kwa hiyo siku. Jua lilipokuwa kali, iliyayuka.

22Siku ya sita walikusanya mikate mara mbili zaidi, lita mbili kwa kila mtu. Viongozi wote wa jamii walikuja na kumwambia hili kwa Musa.23Aliwaambia, “Hili ndilo Yahweh alililolisema: ‘Kesho ni mapumziko ya kujiliwaza, sabato takatifu kwa utukufu wa Yahweh. Oka kile unataka kuoka, na chemsha kile unataka kuchemsha. Vyote vitakavyobaki, jihifadhie hadi asubui.”

24Hivyo wakaweka pembeni hadi asubui, kama Musa alivyowaelekeza. Haikuharibika, wala haikuwa na mdudu yeyote.25Musa alisema, “Kula hicho chakula leo, kwa kuwa leo ni siku iliyotengwa ya kumtukuza Yahweh. Leo hamtaikuta mashambani.26Mtaikusanya ndani ya siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato. Siku ya Sabato hakutakuwa na manna.”27Ilikuja kuwa siku ya saba ambapo baadhi ya watu walienda kukusanya manna, lakini hawakukuta28Kisha Yahweh akamwambia Musa, Kwa muda gani utaendelea kukataa kushika amri zangu na sheria zangu?29Tazama, Yahweh amekupa Sabato. Hivyo siku ya sita anakupa mkate wa siku mbili. Kila mmoja wenu lazima akae kwenye sehemu yake; hakuna hata mmoja wa kutoka sehemu yake siku ya saba.”30Hivyo watu watapumzika siku ya saba.

31Watu wa Israeli walikiita chakula kile “manna.” Ilikuwa ni nyeupe kama mbegu ya mgiligani, na ladha yake kama maandazi yaliyopikwa na asali.32Musa akasema, “Hili ndilo Yahweh alilo amuru: ‘Acha lita mbili ya manna ihifadhiwe kwa ajili ya vizazi vya watu wako ili kwamba uzao wako uone mkate niliyokulisha nyikani, baada ya kukutoa kutoka nchi ya Misri.33Musa akamwambia Haruni, “Chukua jagi na uweke lita mbili za manna ndani yake. Hifadhi kwa Yahweh idumu vizazi vyote vya watu.”34Kama Yahweh alivyomuamuru Musa, Haruni akahifadhi pembeni mwa mawe yaliyokuwa na amri za agano.35Watu wa Israeli walikula manna miaka arobaini mpaka walipokuja nchi yenye watu. Walikula mpaka walipofika kwenye mipaka ya nchi ya Kanani.36Lita mbili ni makumi ya efa.

17

1Jamii yote ya Israeli ili safiri kutoka nyikani ya Sini, wakifuata maelekezo ya Yahweh. Walieka kambi Refidimu, lakini hapakuwa na maji ya watu kunywa.2Hivyo watu wakamlaumu Musa kwa hali yao na kusema, “Tupe maji ya kunywa.” Musa akasema, “Kwanini mnagombana na mimi? Kwanini mnajaribu Yahweh?”3Watu walikuwa na kiu sana, na wakamlalamikia Musa. Wakasema, “Kwa nini umetutoa Misri? Ili utuue sisi na watoto wetu na mifugo yetu kwa kiu?”

4Kisha Musa akamlilia Yahweh, “Nini nimefanya kwa hawa watu? Wako tayari ata kunipiga mawe.”5Yahweh akamwambia Musa, “Nenda mbele yao, na uchukue baadhi ya wazee wa Israeli. Chukua gongo ulilopiga nalo mto, na uende.6Nitasimama mbele yako pale kwenye mwamba wa Horebu, na utaupiga mwamba. Maji yatatoka ya watu kunywa.” Kisha Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.7Aliita ile sehemu Massa na Meriba kwa sababu ya malalamishi ya Waisraeli, na kwa sababu walimjaribu Bwana kwa kusema, “Je Yahweh yupo miongoni mwetu au hapana?”

8Kisha jeshi la watu wa Ameleki wakaja na kushambulia Israeli huko Refidimu.9Hivyo Musa akamwambia Yoshua, “Chagau wanaume kadha na uende nje. Pigana na Ameleki. Kesho nitasimama juu ya kilima na gongo la Mungu mkononi mwangu.”10Hivyo Yoshua akapigana na Ameleki kama Musa alivyo elekeza, wakati Musa, Haruni, na Huri walienda juu ya kilima.11Wakati Musa alipokuwa ameshikilia mikono yake juu, Israeli ilikuwa yashinda; alipoacha mikono yake ipumzike, Ameleki alianza kushinda12Mikono ya Musa yalipokuwa mizito, Haruni na Huri walichukua jiwe na kuweka chini yake alikalie. Muda huo huo, Haruni na Huri walinyanyua mikono yake juu, mtu mmoja upande mmoja, na mtu mmoja upande mwingine. Hivyo mikono ya Musa ilishikiliwa tuli mpaka jua lilipozama.13Hivyo Yoshua akawashinda watu wa Ameleki kwa upanga.14Yahweh akamwambia Musa, “Andika haya kwenye kitabu na umsomee Yoshua, kwa sababu nitaondoa kumbukumbu ya Ameleki kutoka chini ya mbingu.”15Kisha Musa akajenga madhabahu na kuiita “Yahweh ni bendera yangu.”16Alisema, “Kwa kuwa mkono ulinyanyuliwa juu kuelekea kiti cha enzi cha Yahweh - kwamba Yahweh atafanya vita na Ameleki vizazi na vizazi.”

18

1Yethro, kuhani wa Midiani, baba mkwe wake Musa, alisikia yote Mungu aliyofanya kwa Musa na kwa Israeli watu wake. Alisikia Yahweh ametoa Israeli kutoka Misri.2Yethro, baba mkwe wake Musa, akamchukua Zipora, mke wa Musa, baada ya kumpeleka nyumbani,3na wanawake wawili; jina mmoja lilikuwa Gershomu, kwa kuwa Musa alisema, “Nimekuwa mgeni katika nchi ya kigeni.”4Jina la mwingine lilikuwa Eliezeri, kwa kuwa Musa alisema, “Mungu wa babu yangu alikuwa msaada wangu. Aliniokoa na mkono wa Farao.”

5Yethro, baba mkwe wake Musa, alikuja na watoto wake Musa na mke wake Musa nyikani alipoweka kambi katika mlima wa Mungu.6Alimwambia Musa, “Mimi, baba mkwe wako Yethro, ninakuja kwako na mke wako na wanao wawili.”7Musa alitoka kwenda kukutana na baba mkwe wake, akamwinamia, na kumbusu. Wakajuliana hali na wakaingia ndani ya hema.8Musa akamwambia baba mkwe wake yale yote Yahweh aliyoyafanya kwa Farao na Wamisri kwa ajili ya Waisraeli, magumu yote yaliyowatokea njiani na jinsi Yahweh alivyowaokoa.9Yethro akafurahia yale mema yote Yahweh aliyowatendea Israeli, kwa hilo amewaokoa na mkono wa Wamisri.10Yethro akasema, “Yahweh atukuzwe, kwa kuwa amekuokoa na mkono wa Wamisri na mkono wa Farao na kuwatoa watu kwenye mkono wa Wamisri.11Sasa najua Yahweh ni mkuu kuliko miungu yote, kwa sababu Wamisri walipowatendea Waisraeli kwa kiburi, Mungu aliwaokoa watu wake.”12Yethro, baba mkwe wake Musa, akaleta sadaka ya kuteketeza na dhabihu kwa Mungu. Haruni na wazee wote wa Israeli wakaja kula chakula mbele za Yahweh na baba mkwe wake Musa.

13Siku iliyofuata Musa aliketi kuwahukumu watu. Watu walisimama kumzunguka Musa kwanzia asubuhi hadi jioni.14Baba mkwe wake Musa alipoona yale yote aliyoyafanya kwa watu, alisema, “Ni nini unachofanya na watu? Kwa nini unaketi pekeyako na watu wote wamesimama kukuzunguka asubuhi hadi jioni?”15Musa akamwambia baba mkwe wake, “Watu wanakuja kuniuliza mwongozo wa Mungu.16Wanapokuwa na malumbano, wanakuja kwangu. Ninaamua kati ya mtu mmoja na mwingine, na nina wafundisha maagizo na sheria.”17Baba mkwe wake Musa alimwambia, “Unachofanya sicho kizuri sana.18Hakika utajichosha, wewe na watu waliyopo na wewe. Huu mzigo ni mzito sana kwako. Hauwezi kufanya pekyako.19Nisikilize. Nitakupa ushauri, na Mungu atakuwa na wewe, kwa sababu wewe nimwakilishi wa watu kwa Mungu, na unaleta malumbano yao kwake.20Lazima uwafundishe maagizo yake na sheria. Lazima uwafundishe njia yakutembea na kazi ya kufanya.21Mbali zaidi, lazima uchague wanaume wenye uwezo kutoka watu wote, wanaume wanao mheshimu Mungu, wanaume wa kweli wanao chukia mapato ya ufisadi. Lazima uwaweke juu ya watu, kuwa viongozi wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.22Watawa hukumu watu na kesi za kawaida, lakini kesi ngumu wataleta kwako. Kwa kesi ndogo, wanaweza kuhukumu wenyewe. Kwa hivyo itakuwa rahisi kwako, na watabeba mzigo na wewe.23Ukifanya hivi, na kama Mungu akikuamuru kufanya hali kadhalika, basi utaweza kuvumilia, na watu wote watarudi nyumbani wameridhika.”

24Hivyo Musa akasikiliza maneno ya baba mkwe wake na akafanya yale yote aliyoyasema.25Musa alichagua wanaume wenye uwezo kutoka Israeli na kuwafanya vichwa juu ya watu, viongozi wahusika wa maelfu, mamia, hamsini, na makumi.26Waliwahukumu watu katika hali za kawaida. Kesi ngumu walimletea Musa, lakini wao wenyewe walihukumu kesi ndogo.27Kisha Musa akamwacha baba mkwe wake kuondoka, na Yethro akarudi kwenye nchi yake.

19

1Katika mwezi wa tatu baada ya watu wa Israeli kutoka Misri, siku hiyo, walikwenda nyikani ya Sinai.2Walipoondoka Refidimu na kuja nyikani ya Sinai, waliweka kambi mbele ya mlima.3Musa akaenda juu kwa Mungu. Yahweh alimuita kutoka mlimani na kusema, “Lazima uiambie nyumba ya Yakobo, watu wa Israeli:4Uliona nilichofanya kwa Wamisri, jinsi nilivyokubeba kwa mabawa ya tai na kukuleta kwangu.5Kisha sasa, ukinisikiliza kwa kutii sauti yangu na kushika agano langu, kisha utakuwa mali yangu ya pekee miongoni mwa watu wote, kwa kuwa dunia yote ni yangu.6Utakuwa ufalme wa kikuhani na taifa takatifu langu. Haya ni maneno wapaswa kuwaambia Waisraeli.

7Hivyo Musa akaja na kuwaita wazee wa watu. Aliweka mbele yao maneno yote haya Yahweh aliyomuamuru.8Watu wote walijibu pamoja na kusema, “Tutafanya yote Yahweh aliyotuambia.” Kisha musa akaja kutoa taarifa ya maneno ya watu kwa Yahweh.

9Yahweh akamwambia Musa, “Nitakuja kwako kwa wingu nene ili watu wasikie ninaposema na wewe na wakuamini milele.” Kisha Musa kamwambia Yahweh maneno ya watu.10Yahweh akamwambia Musa, “Nenda kwa watu. Leo na kesho lazima uwatenge, na kuwafanya waoshe mavazi yao.11Kuwa tayari kwa siku ya tatu, kwa kuwa siku ya tatu Yahweh atashuka chini ya Mlima Sayuni.12Lazima uweke mipaka kote kuzunguka mlima kwa ajili ya watu. Uwaambie, ‘Kuweni waangalifu msiende juu ya mlima au kushika mipaka yake. Yeyote atakayeshika mlima atauawa.’13Hakuna mkono wa mtu yeyote kumshika mtu huyu. Badala yake, lazima apigwe mawe au kuchomwa mshale. Iwe ni mtu au mnyama, lazima auawe. Tarumbeta itakapopigwa muda mrefu, wanaweza kuja chini ya mguu wa mlima.”

14Kisha Musa akashuka mlimani kwenda kwa watu. Aliwatenga watu kwa ajili ya Yahweh na wakaosha mavazi yao.15Aliwaambia watu, “Kuweni tayari siku ya tatu; msiwakaribie wake zenu.”

16Siku ya tatu, ilipofika asubui, kulikuwa na ngurumo na radi na wingu nene kwenye mlima, na sauti kubwa ya tarumbeta. Watu wote kambini waliogopa.17Musa akaleta watu kutoka kambini kukutana na Mungu, na wakasimama miguuni mwa mlima.18Mlima Sinai ulijwa kabisa na moshi kwa sababu Yahweh alishuka na moto na moshi. Moshi ulipanda juu kama moshi wa tanuru, na mlima wote ulitikisika kwa vurugu.19Sauti ya tarumbeta ilipoongezeka na zaidi, Musa akazungumza, na Mungu kamjibu kwa sauti.20Yahweh akashuka chini ya Mlima Sinai, juu ya mlima, na akamuita Musa kuja juu. Kisha Musa akapanda juu.21Yahweh akamwambia Musa, “Shuka chini na uwaonye watu wasipite kuniangalia, au wengi wao wataangamia.22Acha pia makuhani wanaokuja karibu yangu waijitenge - wajiandae kwa ujio - ili nisiwashambulie.”

23Musa akamwambia Yahweh, “Watu hawawezi kuja juu ya mlima, kwa kuwa umetuamuru: ‘weka mipaka kuzunguka mlima na uutenge kwa ajili ya Yahweh.”24Yahweh akamwambia, Nenda, shuka chini ya mlima, na umlete Haruni na wewe, lakini usiache makuhani na watu kupita vizuizi na kuja kwangu, au nitawashambulia.”25Hivyo Musa akaenda chini kwa watu na kusema nao.

20

1Mungu alisema maneno yote haya:2Ndimi Bwana Mungu wenu, niliyewatoa katika ardhi ya Misri, nje ya nyumba ya utumwa.3Msiwe na miungu mingine ila mimi tu.4Msijitengenezee sanamu za kuchonga kufananisha na kitu chochote kilichopo juu ya mbingu, chini ya ardhi, au ndani ya maji.5Msipende kuabudu sanamu, mimi Yahweh Mungu wenu, ni Mungu mwenye wivu. Nitaadhibu uovu wa mababu kwa kuleta adhabu juu ya kizazi, cha tatu hadi kizazi cha nne kwa wale wanaonichukia.6Ila nitaweka agano la uaminifu kwa maelfu watakao nipenda na kushika amri zangu.

7Usilitaje bure jina la Yahweh Mungu wako, sitkuwa na hatia kwa yeyote atakayetaja jina langu bure.

8Ikumbuke siku ya Sabato, na kunitengea.9Lazima ufanye kazi zako zote kwa siku sita.10Ila siku ya saba ni Sabato kwa ajili ya Yahweh Mungu wako. Siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, au mwana wako, au binti yako, au mtumishi wako wakiume, au mtumishi wako mwanamke, au ng'ombe wako, au mgeni aliye ndani ya malango yako.11Kwa siku sita Yahweh aliumba mbingu na nchi, bahari, na vitu vyote vilivyomo, na siku ya saba alipumzika. Kwa hiyo Yahweh aliibariki siku ya Sabato na kuitenga.

12Waheshimu baba na mama yako, ili uweze kuishi miaka mingi duniani Yahweh Mungu wako ametoa.

13Usiue.

14Usifanye uasherati (usizini).

15Usiibe kwa mtu yoyote.

16Usishuhudie uongo dhidi ya jirani yako.

17Usitamani nyumba ya jirani yako; usitamani mke wa jirani yako, wala mtumishi wake wakiume, mtumishi wake mwanamke, ng'ombe wake, punda wake, au chochote cha jirani yako.

18Watu wote waliona radi na umeme, na kusikia sauti ya mbiu, na mlima ukitoa moshi. Watu walipoona hivyo, walitetemeka na kusimama mbali.19Wakamwambia Musa, ongea na sisi, na tutakusikiliza; lakini usiruhusu Mungu kuongea nasi, ama tutakufa.20Musa akawaambia watu, “msiogope, Mungu alikuja kuwajaribu ili heshima yake iwe ndani yenu, kwa hiyo msitende dhambi.”

21Hivyo watu walisimama mbali, na Musa alikaribia giza nene Mungu alipokuwa.

22Yahweh alimwambia Musa, “Ni lazima uwaambie hili Waisraeli: ‘Wewe mwenyewe umeona niliongea na wewe kutoka mbinguni.23Misjitengenezee miungu mingine pamoja nami, miungu ya fedha au miungu ya dhahabu.24Tengenezeni madhabahu ya udongo kwa ajili yangu, na lazima mtoe sadaka ya kuteketeza, sadaka ya ushirika, kondoo, na ng'ombe. Kila sehemu nitakapotaka jina langu liheshimiwe, nitakuja kwenu na kuwabariki.25Kama mtatengeneza madhabahu ya mawe, msijenge na mawe yaliyokatika, na kama mtatumia vyombo vyenu juu yake, mtaweka unajisi.26Msije juu ya madhabahu yangu kwa hatua zenu; hii ni ili msionyeshe sehemu zenu za siri.”

21

1Sasa hizi ni amri utakazoweka kabla yao:2‘kama mtanunua mtumishi wa kiebrania, atawatumikia kwa miaka sita, na mwaka wa saba ataachiliwa huru bila kulipwa chochote.3Kama alikuja mwenyewe, ataenda huru kwa ridhaa yake;4kama bwana wake atampa mke na kumzalia mwana na binti, mke pamoja na watoto wake watabaki mali ya bwana wake, na ataenda zake huru.5Lakini kama mtumishi atasema waziwazi, “Nampenda bwana wangu, mke wangu, na watoto; sitaenda nje,”6“kisha bwana wake atapaswa kumleta kwa Mungu. Bwana wake atapaswa kumleta katika mlango au katika muhimili wa mlango, na bwana wake atatoboa sikio lake kwa sindano. Kisha mtumishi wake atamtumikia kwa maisha yake yote.

7Kama mwanaume ata muuza binti wake kama mtumishi wa kike, ataweza kwenda huru kama watumishi wa kiume wanavyoenda.8Kama hamridhishi bwana wake, aliyemtenga kwa ajili yake, kisha lazima amnunue tena. Hana ruhusa ya kumuuza kwa watu wengine wa kigeni. Hana ruhusa hiyo, sababu amemtendea kwa hila.9Ikiwa bwana wake atamposa awe mke wa mwanawe, atamtendea kama desturi zipasavyo sawa na binti zake.10Ikiwa atajitwalia mke mwingine, asimpunguzie huyo chakula chake, nguo na haki zake za unyumba.11Lakini asipofanyiwa mambo haya matatu, basi anaweza kwenda bure pasipo kutolewa mali.

12Mtu au yeyote ampigaye mtu hata akafa, inampasa mtu huyo auawe pia.13Lakini kama hakumvizia, ila kwa bahati mbaya, basi nitamfanyia mahali pa kukimbilia.14Lakini mtu akimwendea mwenzake kwa kujikinai, kusudi apate kumwua kwa hila; huyo utamwondoa hata kama ni madhabahuni pangu, ili auawe.

15Yeyote atakayempiga baba au mama yake lazima auawe.

16Yeyote atakayemteka mtu na kumuuza, au mtu amekutwa kama mali yake, huyo mtekaji lazima auawe.

17Yeyote atakayemlaani baba au mama yake lazima auawe.

18Kama wanaume watapigana na mmoja akimpiga mwengine kwa jiwe au ngumi, na huyo mtu asife, lakini alazwe kitandani;19kisha akapona na anaweza kutembea kwa gongo lake, yeye aliyempiga lazima alipe muda aliyempotezea; na lazima alipematibabu yake yote. Lakini huyo mtu hana hatia ya mauaji.

20Kama mwanaume akimpiga mtumishi wake wa kiume au wa kike kwa gongo, na kama mtumishi huyo akifa kwa madhara ya pigo, kisha huyo mtu lazima aadhibiwe.21Walakini, mtumishi huyo akiishi siku moja au mbili, bwana aruhusiwi kuadhibiwa, kwa kuwa atateseka kupoteza mtumishi huyo.

22Kama wanaume wakipigana pamoja na wakamuumiza wanamke mwenye mimba na kuiharibu, lakini hakuna majeraha mengine kwake, kisha huyo mwanaume mwenye hatia lazima alipe kama mme wa mwanamke anavyotaka kwake, na kulipa kama hakimu anavyokusudia.23Lakini kama kuna majeraha makubwa, lazima utoe uhai kwa uhai, jicho kwa jicho,24jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,25kuchoma kwa kuchoma, jeraha kwa jeraha, au mkwaruzo kwa mkwaruzo.26Kama mwanaume akipiga jicho la mtumishi wake kiume au mtumishi wake wa kike na kuliharibu, kisha lazima amuache mtumishi aende pasipo fidia ya jicho.27Kama akitoa jino la mtumishi wake wa kiume au mtumishi wake wa kike, lazima amuache mtumishi kwenda huru kama fidia ya jino.

28Kama ng'ombe akimpiga mwanaume au mwanamke akafa, ng'ombe lazima apigwe mawe, na nyama yake hairuhusiwi kuliwa; lakini mmiliki wa ng'ombe lazima awe huru kwa hatia.29Lakini kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake alionywa lakini hakumzuia, na ng'ombe ameua mwanaume au mwanamke, huyo ng'ombe lazima apigwe mawe, na mmiliki wake lazima auawe pia.30Kama malipo ya uhai yanahitajika, lazima alipe chochote anachotakiwa kulipa.31Kama ng'ombe amempiga mwana wa mwanaume au binti wake, mmiliki wa ng'ombe anapaswa kufanya kama masharti yanavyomlazimu.32Kama ng'ombe akimpiga mtumishi wa kiume au wakike, mmiliki wa ngombe lazima alipe shekeli thelathini za fedha, na ng'ombe lazima apigwe mawe.

33Kama mwanaume akifungua shimo, au kama mwanume akichimba shimo na asifunike, na ng'ombe au punda akaanguka ndani,34mmiliki wa shimo lazima alipe madhara. Lazima atoe hela kwa mmiliki wa mnyama aliyekufa, na mnyama aliyekufa atakuwa wake.35Kama ng'ombe wa mwanaume akimuumiza ng'ombe wa mwanume mwengine hadi kufa, kisha lazima wamuuze ng'ombe aliyehai na kugawana gharama, na pia lazima wagawane ng'ombe aliyekufa.36Lakini kama ilijulikana kama ng'ombe alikuwa na tabia ya kupiga hapo awali, na mmiliki wake hakumfunga ndani, hakika lazima alipe ng'ombe kwa ng'ombe, na mnyama aliyekufa atakuwa wake.

22

1Kama mwanaume akiiba ng'ombe au kondoo, na kumuua au kumuuza, lazima alipe ng'ombe watano au ng'ombe mmoja, na kondoo wanne kwa mmoja.

2Kama mwizi akikutwa anavunja ndani, na kama akipigwa na kufa, hakutakuwa na hatia ya mauaji hayatakuwa juu ya mtu yeyote.3Lakini kama jua limechomoza kabla ya yeye kuvunja ndani, hatia ya mauaji itakuwa juu ya aliyemuua. Mwizi lazima alipe alichoiba. Kama hana chochote, kisha lazima auzwe kwa wizi wake.4Kama mnyama amekutwa hai eneo lake, kama ni ng'ombe, punda, au kondoo, lazima alipe mara mbili.

5Kama mwanaume akiwapeleka malishoni mifugo yake au shamba la mizabibu na akawaachia wanyama wake, na kama wanakula shambani mwa mwanaume mwengine, lazima afanye malipo bora kutoka shambani mwake na shamba lake la mizabibu.

6Kama moto ukitokea na kusambaa kwenye miba hadi mbegu, au mimea, au shamba kuteketezwa, yeye aliyeanzisha moto lazima afanye malipo.

7Kama mwanaume akitoa pesa au mali kwa jirani yake amtunzie, na kama itaibiwa nyumbani mwa huyo mwanaume, kama mwizi akipatikana, huyo mwizi lazima alipe mara mbili.8Lakini kama mwizi asipopatikana, kisha mmiliki wa nyumba atakuja mbele za waamuzi kuona kama ameweka mkono wake kwenye mali za jirani yake.

9Kwa kila lumbano kuhusu jambo, kama ni ng'ombe, punda, kondoo, nguo, au chochote kilichopotea mtu anachosema, “Hiki ni changu,” malalamiko ya pande zote lazima zije kwa waamuzi. Mwanaume ambaye waamuzi wanamkuta na hatia atalipa mara mbili kwa jirani yake.

10Kama mwanaume akimpa jirani yake punda, ng'ombe, kondoo, au mnyama yeyote kumuhifadhi, na kama akifa au kuumia au akibebwa pasipo mtu kumuona,11kiapo kwa Yahweh lazima wafanye wote wawili, kama ndio au hapana mtu ameweka mkono wake kwenye mali ya jirani yake. Mmiliki lazima akubali hili, na mwengine hatafanya malipo.12Lakini kama iliibwa kwake, mwengine lazima afanye malipo kwa mmiliki kwa ajili yake.13Kama mnyama alikatwa vipande, acha mwanaume mwengine alete huyo mnyama kama ushahidi. Hatalipa kwa ajili ya vile vipande.

14Kama mwanaume akiazima mnyama kutoka kwa jirani yake na mnyama akajeruhiwa au akafa pasipo mmiliki kuwa naye, mwanaume mwengine lazima afanye malipo.15Lakini kama mmiliki alikuwa naye, mwanaume mwengine haitaji kulipa; kama mnyama aliazimwa, atalipwa kwa gharama ya kuazima.

16Kama mwanaume akimtongoza bikra ambaye hana mchumba, na kama akilala naye, lazima amfanye kuwa mke wake kwa kulipa gharama za bibi arusi zinazostahili.17Kama baba yake akikataa kabisa kumpatia, lazima alipe hela inayolingana na gharama za bibi arusi bikira.

18Hautamwacha mchawi kuishi.

19Yeyote atakaye lala na mnyama lazima auawe.

20Yeyote atakaye toa dhabihu kwa mungu mwengine isipokuwa Yahweh lazima auawe.

21Hauta mkosea mgeni au kumnyanyasa, kwa kuwa ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri.

22Hauruhusiwi kumtendea vibaya mjane au mtoto asiyekuwa na baba.23Ukiwadhuru hata kidogo, na kama wakiniita mimi, hakika nitasikia sauti yao.24Hasira yangu itawaka, na nitakuua kwa upanga; wake zenu watakuwa wajane, na watoto wenu pasipo baba.

25Ukiazima hela kwa watu wangu walio maskini, haupaswi kuwa kama anayekopesha hela kwake au kutoza faida.26Ukichukua vazi la jirani yako kwa deni, lazima umrudishie kabla jua kuzama,27kwa kuwa hilo ndilo funiko lake, ni vazi la mwili wake. Nini tena ambacho anaweza kulalia? Atakapo niita mimi, nitasikia, kwa kuwa mimi ni mwenye huruma.

28Usinikufuru mimi, Mungu, wala kumtukana mtawala wa watu wako.

29Usizuie sadaka kutoka kwenye mavuno yako au kwenye hifadhi ya mvinyo wako. Lazima unipe mzaliwa wa kwanza wa wana wako.

30Lazima ufanye hivyo hivyo kwa ng'ombe na kondoo wako. Kwa siku saba lazima wabaki na mama zao, lakini siku ya nane lazima unipe mimi.

31Mtakuwa watu waliotengwa kwa ajili yangu. Hivyo hamtakula nyama iliyo uliwa na wanyama porini. Badala yake, uwatupie mbwa.

23

1Haupaswi kutoa taarifa ya uongo kuhusu yeyote. Usijiunge na mwanaume mwovu kuwa shahidi wa uongo.

2Haupaswi kufuata umati kufanya uovu, wala kutoa ushahidi ukiwa na umati ili kupotosha haki.3Haupaswi kumpendelea mwanaume maskini kwenye kesi yake.

4Ukikutana na ng'ombe wa adui wako au punda wake amepotea, lazima umrudishie.5Ukiona punda wa yule anayekuchukia ameanguka chini na mzigo wake, hautamuacha huyo mtu. Lazima umsaidie na punda wake

6Haupaswi kupotosha haki kama yapaswa kwenda kwa watu maskini katika kesi ya mwanaume maskini.

7Usijiunge na wengine kufanya shutuma za uongo, na usiue asiye na hatia wala mwenye haki, kwa kuwa sitamuacha mwovu.

8Usiwahi chukua rushwa, kwa kuwa rushwa inawapofusha wanaoona, na kupotosha maneno ya wakweli.

9Haupaswi kumnyanyasa mgeni, kwa kuwa wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri.

10Kwa miaka sita utapanda mbegu kwenye nchi yako na kukusanya mazao yake.11Lakini katika mwezi wa saba utaacha hakujalimwa, ili kwamba maskini miongoni mwenu wale. Wanacho acha, wanyama wa porini watakula. Utafanya hivyo na mashamba yenu ya mizabibu na ya mizaituni.

12Wakati wa siku sita utafanya kazi, lakini siku ya saba utapumzika. Fanya hivi ili ng'ombe na punda wako wapumzike, na ili wana wa watumwa wako wa kike na wageni wapumzike na kupata hafweni.

13Kuwa makini kwa kila kitu nilichokwambia. Usitaje majina ya miungu mingine, wala kuruhusu majina yao kusikika kutoka mdomoni mwako.

14Lazima usafiri kusherehekea mara tatu kwa ajili yangu kila mwaka.15Lazima uadhimishe sherehe ya Mkate usiotiwa Chachu. Kama nilivyokuamuru, utakula mkate usiotiwa chachu kwa siku saba. Wakati huo, utajitokeza kwangu mwezi wa Abibu, uliowekwa kwa ajili ya kusudi hili. Ni kwa mwezi huu uliyotoka Misri. Lakini usijitokeze kwangu mikono mitupu.16Lazima uadhimishe Sherehe ya Mavuno, matunda ya kwanza ya kazi yako ulipopanda mbegu shambani. Pia lazima uadhimishe Sherehe ya Ukusanyaji wa mwisho wa mwaka, unapokusanya mazao yako kutoka shambani.17Wanaume wote wako lazima wajitokeze kwa Bwana Yahweh mara tatu kila mwaka.

18Haupaswi kutoa damu iliyotolewa dhabihu kwangu na mkate uliyotiwa hamira. Mafuta kutoka kwa dhabihu za sherehe zangu hayapaswi kubaki usiku wote mpaka asubui.

19Lazima ulete matunda ya kwanza bora kutoka shambani mwako ndani ya nyumba yangu, nyumba ya Yahweh Mungu wako. Haupaswi kumchemsha mbuzi mtoto akiwa bado ananyonya.

20Ninaenda kumleta malaika mbele yako kukuongoza njiani, na kukuleta sehemu niliyoandaa.21Kuwa makini naye na kumtii.22Usimkasirishe, kwa kuwa hatasamehe makosa yako. Jina langu liko kwake. Kama hakika ukimtii sauti yake na kufanya kila ninachokuambia, kisha nitakuwa adui kwa adui zako na mpinzani kwa wapinzani wako.23Malaika wangu ataenda mbele zako na kukuleta kwa Waamori, Wahiti, Waperizi, Wakanani, Wahivi, na Wayebusi. Nitawaharibu.24Haupaswi kuinamia miungu yao, kuabudu, au kufanya wanavyofanya. Badala yake, lazima uwapindue kabisa na kuvunja nguzo zao za mawe vipande vipande.

25Lazima umuabudu Yahweh Mungu wako, na atabariki mkate wako na maji. Nitaondoa magonjwa miongoni mwenu.26Hakuna mwanamke atakayekuwa tasa au mimba kuharibika katika nchi yako. Nitawapa maisha marefu.

27Nitatuma hofu yangu kwao ambao mnaenda. Nitaua wote mnaokutana nao. Nitafanya maadui zenu wawaogope kwa kugeuza migongo yao kwenu.28Nitatuma mavu kwenu watakao fukuza Wahivi, Wakanani, na Wahiti mbele zenu.29Sitawaondoa kwenu kwa mwaka mmoja, au nchi itakuwa imetelekezwa, na wanyama wa porini watakuwa wengi kwenu.30Badala yake, nitawafukuza kidogo kidogo kutoka kwenu mpaka utakapokuwa umestawi na kurithi nchi.31Nitatengeneza mipaka yako kutoka Bahari ya Shamu hadi Bahari ya Wafilisti, na kutoka nyikani hadi Mto Frati. Nitakupa ushindi juu ya wakazi wote wa nchi. Utawaondoa kutoka kwako mwenyewe.32Haupaswi kufanya agano na wao au na miungu yao.33Hawapaswi kuishi nchini mwako, au watakufanya ufanye dhambi dhidi yangu. Ukiabudu miungu yao, hakika watakuwa mtego kwako.’

24

1Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Njoo juu kwangu -wewe, Haruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli, na kuniabudu kwa mbali.2Musa pekeake anawezakuja karibu yangu. Wengine hawapaswi kuja karibu, wala watu kuja juu na yeye.”

3Musa akaenda juu na kuwaambia watu maneno yote ya Yahweh na amri zake. Watu wote wakajibu kwa sauti moja na kusema, “Tutafanya maneno yote Yahweh aliyo tuamuru.”4Kisha Musa akaandika chini maneno yote ya Yahweh. Asubuhi na mapema, Musa akajenga madhabahu chini ya mguu wa mlima na kupanga nguzo kumi na mbili za mawe, ili mawe yawakilishe makabila kumi na mbili ya Israeli.5Aliwatuma vijana Wakiisraeli kutoa sadaka ya kuteketeza na kutoa dhabihu za ng'ombe za sadaka ya ushirika kwa Yahweh.6Musa allichukua nusu ya damu na kuweka kwenye mabeseni; alinyunyuzia nusu ingine kwenye madhabahu.7Alichukuwa kitabu cha agano na kuwasomea kwa nguvu watu. Walisema, “Tutafanya yote Yahweh aliyosema. Tutakuwa watiifu.”

8Kisha Musa akachukua damu na kunyunyiza kwa watu. Alisema, “Hii ni damu ya agano Yahweh alilolifanya nanyi kwa kuwapa hii ahadi kwa maneno yote haya.”

9Kisha Musa, Haruni, Nadabu, Abihu, na wazee sabini wa Israeli wakaenda juu ya mlima.10Walimwona Mungu wa Israeli.11Chini ya miguu yake kulikuwa na sakafu iliyojengwa kwa jiwe la yakuti samawati, safi kama mbingu yenyewe. Mungu hakugusa na mkono kwa hasira viongozi wa Israeli walimwona Mungu, na wakanywa na kula.

12Yahweh akamwambia Musa, “Njoo juu kwangu mlimani na ubaki pale. Nitakupa sahani za mawe na sheria na amri nilizoziandika, ili uwafundishe.”13Hivyo Musa akaenda na msaidizi wake Yoshua na kwenda juu mlima wa Mungu.14Musa akawaambia wazee, “Baki hapa na mtusubiri hadi tutakapo warudia. Haruni na Huri wapo nanyi. Kama kuna mtu mwenye malalamiko, acha awaende.”15Hivyo Musa akaenda juu ya mlima, na wingu likafunika.16Utukufu wa Yahweh ukabaki juu ya Mlima wa Sinai, na wingu likafunika kwa siku sita. Siku ya saba ata Musa kutoka ndani ya wingu.17Utukufu wa Yahweh ulikuwa kama moto ulao juu ya mlima kwenye macho ya Waisraeli.18Musa akaingia kwenye wingu na kwenda juu ya mlima. Alikuwa mlimani siku arobaini na usiku arobaini.

25

1Yahweh akamwambia Musa,2“Waambie Waisraeli wanitolee sadaka kila mtu nawe utapokea kutoka kwa mtu yeyote atakayetoa kwa moyo mkunjufu. Lazima upokee hizi sadaka kwa ajili yangu.3Hizi ndio sadaka utakazopokea kwao; dhahabu, fedha na shaba,4Samawati, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani safi, na manyoya ya mbuzi;5Na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo, miti ya mjohoro,6Mafuta ya ile taa, na viungo vya manukato kwa yale mafuta ya kupaka na kwa ule uvumba wenye harufu nzuri;7mawe ya shohamu na mawe mengine ya kutiwa kwa ile naivera na kwa kile kifuko cha kifuani.8Waache wanifanyie patakatifu ili nipate kukaa kati yao.9Lazima ufanye sawa na haya yote nikuonyeshayo, mfano wa maskani, na vifaa vyake, ndivyo utakavyovifanya.

10Wanapaswa wafanye sanduku la mti wa mjohoro. Urefu wake na uwe dhiraa mbili na nusu; na upana wake moja na nusu, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.11Lazima ulifunike ndani kwa dhahabu safi, na utie na ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.12Nawe utayeyusha katika viduara vinne vya dhahabu, na kuviweka katika miguu yake minne; viduara viwili upande mmoja, na viduara viwili upande wake wa pili.13Nawe lazima ufanya miti mirefu ya mshita na kuifunika dhahabu.14Nawe lazima uweka hiyo miti katika vile viduara vilivyo katika pande mbili za sanduku ili kulichukua hilo sanduku.15Hiyo miti itakaa katika vile viduara vya sanduku; haitaondolewa.16Kisha weka ndani ya sanduku hizo amri nitakazokupa.

17Nawe lazima utengeneze kifuniko cha dhahabu safi. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili na nusu, na upana wake dhiraa moja na nusu.18Nawe fanya makerubi mawili ya dhahabu katika hiyo miisho miwili ya kiti cha rehema.19Weka kerubi moja mwisho mmoja wa kiti cha rehema, na kerubi la pili mwisho wa pili. Lazima hao makerubi wawe kitu kimoja na kiti cha rehema.20Na hao makerubi watainua mabawa yao juu, na kukifunika hicho kiti cha rehema kwa mabawa yao. Nyuso zao makerubi zitaelekeana na zitaelekea kiti cha rehema.21Lazima uweke kiti cha rehema juu ya hilo sanduku, kisha uweke hizo amri nitakazokupa ndani ya sanduku.22Nami nitaonana nawe hapo katika sanduku. Nitazungumza nawe pale nilipo juu ya kiti cha rehema. Itakuwa katikati ya hao makerubi wawili waliyo juu ya sanduku la ushuhuda nitakapozungumza na wewe katika mambo yote nitakayokuagiza kwa ajili ya wana wa Israeli.

23Nawe fanya meza ya mti wa mshiti. Urefu wake utakuwa dhiraa mbili, na upana wake dhiraa moja, na kwenda juu kwake dhiraa moja na nusu.24Uifunike dhahabu safi na kuifanyia ukingo wa dhahabu wa kuizunguka pande zote.25Lazima ufanyie fremu ya kuizunguka pande zote, upana wake utakuwa nyanda nne, ukingo wa dhahabu wa kuuzunguka fremu pande zote.26Uifanyie viduara vinne vya dhahabu na kuvitia vile viduara katika pembe zake nne, katika miguu yake minne ilipokuwa.27Vile viduara na viwe karibu na ile fremu ili viwe mahali pa kutilia ile miti, ya kuichukulia meza.28Fanya ile miti ya mti wa mshita, na kuifunika dhahabu, kwamba ile meza ichukuliwe kwayo.29Nawe fanya sahani zake, na miiko yake, na makopo yake, na vikombe vyake vya kumiminia. Vifanye vyote vya dhahabu safi.30Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.

31Nawe fanya kinara cha taa cha dhahabu safi; hicho kinara na kifanywe cha kazi ya kufua, kitako chake, na mti wake, vikombe vyake, na matovu yake, na maua yake, vyote vitakuwa vya kitu kimoja nacho.32Nacho kitakuwa na matawi sita yenye kutoka ubavuni mwake - matawi matatu ya kinara upande wake mmoja, na matawi matatu ya kinara upande wake wa pili.33Tawi la kwanza lazima liwe na vikombe vitatu vilivyotengenezwa mfano wa maua ya mlozi katika tawi moja, tovu na ua na vikombe vitatu vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi katika tawi la pili, tovu na ua. Vivyo hivyo hayo matawi yote sita yatokayo katika kile kinara.34Katika hicho kinara, lazima kuwe na vikombe vinne vilivyofanywa mfano wa maua ya mlozi, matovu yake, na maua yake.35Lazima kuwe na tovu chini ya matawi - mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, na tovu chini ya matawi mawili la kitu kimoja nacho, kwa hayo matawi sita yatokayo katika kile kinara.36Matovu yake na matawi yake yatakuwa ya kitu kimoja nacho, kiwe chote, pia kazi moja ya kufua, ya dhahabu safi.37Lazima nawe uzifanye hivyo vinara saba na taa zake saba, nao wataziwasha hizo taa zake, zitoe nuru mbele yake.38Na makoleo yake, na visahani vyake, vyote vitakuwa vya dhahabu safi.39Tumia talanta moja ya dhahabu safi, pamoja na vyombo hivi vyote.40Nawe angalia ya kwamba uvifanye kama mfano wake, uliooneshwa mlimani.

26

1Lazima ufanye hiyo maskani iwe na mapazia kumi ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi. Kazi ya fundi stadi.2Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa ishirini na nane, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Mapazia yote yatakuwa ya kipimo kimoja.3Mapazia matano yataungwa pamoja, na mapazia matano mengine yataungwa pamoja.4Lazima ufanye tanzi za rangi ya samawati upande wa mwisho wa pazia moja katika ule upindo wa fungu lake. Vivyo hivyo utafanya upande wa mwisho wa ile pazia iliyokatika fungu la pili.5Fanya matanzi hamsini katika pazia moja, na matanzi hamsini katika upande wa mwisho wa ile pazia iliyokatika kuungana kwa pili.6Fanya hivi, ili hizo tanzi zielekeana. Kisha ufanye vifungo hamsini vya dhahabu, na kuunganisha hayo mapazia pamoja kwa vile vifungo na hiyo maskani itakuwa ni moja.

7Lazima ufanye mapazia ya nywele za mbuzi yawe hema juu ya maskani. Lazima ufanye mapazia kumi na moja.8Urefu wa kila pazia utakuwa dhiraa thelathini, na upana wa kila pazia utakuwa dhiraa nne. Hayo mapazia kumi na moja yatakuwa ya kipimo kimoja.9Lazima utaunganisha mapazia matano mbali, na mapazia sita mbali, na lile pazia la sita utalikunja hapo upande wa mbele wa ile hema.10Ufanye tanzi hamsini upande wa mwisho wa pazia lile lililo la mwisho katika hayo yaliyounganishwa pamoja, na tanzi hamsini upande wa mwisho wa lile pazia lililo nje katika hayo ya pili yaliyounganishwa pamoja.11Kisha ufanye vifungo hamsini vya shaba, na kuvitia vile vifungo katika zile tanzi, na kuiunganya ile hema pamoja, ili iwe hema moja.12Kipande kile kilichosalia, kile kiangukacho, cha yale mapazia ya hema, itaanguka huko upande wa nyuma wa maskani.13Lazima kuwe na dhiraa moja upande mmoja, na ile dhiraa moja upande wa pili - ya urefu wa mapazia ya hema uliosalia, zitaanguka katika ubavu wa maskani upande huu na upande huu, ili kuifunika.14Nawe fanya kifuniko cha ile hema, cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na juu yake kifuniko cha ngozi za pomboo.

15Nawe lazima ufanye hizo fremu za maskani za mti wa mjohoro.16Kila fremu itakuwa na urefu wa dhiraa kumi, na upana wake kila ubao utakuwa dhiraa moja na nusu.17Kila fremu itakuwa na ndimi mbili, zenye kuunganishwa huu na huu. Ndivyo utakavyozifanya mbao zote za maskani.18Kisha ufanye zile mbao za maskani, mbao ishirini kwa upande wa kusini kuelekea kusini.19Lazima nawe ufanye vitako arubaini vya fedha chini ya zile fremu ishirini. Vitako viwili chini ya fremu moja, kupokea zile ndimi zake mbili, na vitako viwili chini ya fremu nyingine kupokea zile ndimi zake mbili.20Kwa upande wa pili wa maskani, upande wa kaskazini, mbao ishirini21na vitako vyake vya fedha arubaini. Lazima kuwe na vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya fremu nyingine.22Ufanye fremu sita kwa ajili ya upande wa nyuma wa maskani kuelekea magharibi.23Tena ufanye fremu mbili kwa ajili ya hizo pembe za maskani zilizo upande wa nyuma.24Hizi fremu zitakuwa zimetengana upande wa chini, lakini zimeshikana kwa juu ya duara moja.25Fremu zitakuwa ni nane, na vitako vyake vya fedha. Vitako kumi na sita, vitako viwili chini ya fremu moja, na vitako viwili chini ya ubao wa pili.

26Lazima ufanye mataruma ya mti wa mshita- mataruma matano kwa ajili ya mbao za upande mmoja wa maskani,27na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa pili wa maskani, na mataruma matano kwa ajili ya fremu za upande wa maskani ulio nyuma kuelekea magharibi.28Na hilo taruma la katikati lililo katikati ya zile fremu, litapenya toka mwisho huu hata mwisho huu.29Lazima uzifunuke hizo fremu kwa dhahabu. Nawe lazima ufanye maduara yake ya dhahabu, kuwa kama vishikizo, na hayo mataruma utayafunika dhahabu.30Nawe utaisimamisha hiyo maskani sawasawa na mfano wake ulioonyeshwa mlimani.

31Nawe fanya pazia la nyuzi za rangi ya samawati, zambarau na nyekundu, na nguo za kitani nzuri zenye kusokotwa, litafumwa na kutiwa makerubi, kazi ya fundi stadi.32Kisha litungike katika nguzo nne za mti wa mshita zilizofunikwa dhahabu, vifungo vyake vitakuwa vya dhahabu, katika vitako vya fedha vinne.33Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda. Lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.34Nawe lazima utaweka kiti cha rehema juu ya lile sanduku la ushuhuda ndani ya mahali pale patakatifu sana. Na ile meza utaiweka nje ya pazia.35Lazima uweke kinara cha taa kuikabili ile meza upande wa maskani wa kuelekea kusini. Ile meza utaiweka upande wa kaskazini.36Kisha utafanya kisitiri kwa mlango wa hema, cha nyuzi za rangi ya samawati, zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji wa taraza.37Nawe fanya nguzo tano za mti wa mshita kwa kile kisitiri, na kuzifunika dhahabu; kulabu zake zitakuwa za dhahabu. Nawe utasubu vitako vya shaba vitano kwa ajili yake.

27

1Nawe fanya madhabahu ya mti wa mshita, urefu wake utakuwa ni dhiraa tano na upana wake dhiraa tano. Hiyo madhabahu itakuwa mraba na kwenda juu kwake kutakuwa dhiraa tatu.2Nawe fanya pembe nne kama mfano wa pembe za ng'ombe. Hizo pembe zitakuwa za kitu kimoja na madhabahu, nawe utayafunika kwa shaba.3Lazima vyombo vyake vya kuyaondoa majivu yake utavifanya, na majembe yake, na mabakuli yake, na uma zake, na meko yake. Vyombo vyake vyote utavifanya vya shaba.4Nawe uifanyie hiyo madhabahu wavu wa shaba. Kisha utie pete nne za shaba katika hizo pembe nne za ule wavu.5Nawe lazima uweke huo wavu chini ya kizingo kiizungukacho madhabahu upande wa chini.6Nawe fanya miti kwa ajili ya madhabahu, miti ya mshita, na kuifunika shaba.7Na hiyo miti itatiwa katika viduara, na ile miti itakuwa katika pande mbili za madhabahu, wakati wa kuichukua.8Uifanye ya mbao, yenye mvungu ndani yake kama ulivyoonyeshwa mlimani.

9Nawe ufanye ua wa maskani. Upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja.10Na nguzo zake zitakuwa nguzo ishirini, na vitako vyake ishirini, vitako vyake vitakuwa vya shaba kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.11Ni vivyo hivyo upande wa kaskazini, urefu wake hiyo chandarua utakuwa ni dhiraa mia moja, na nguzo zake ishirini, na vitako vyake ishirini vitakuwa vya shaba, kulabu za zile nguzo na vitanzi vyake vitakuwa vya fedha.12Na upande wa magharibi, upana wa ua kutakuwa na chandarua ya dhiraa hamsini; nguzo zake kumi, na vitako vyake kumi.13Na upana wa ule ua upande wa mashariki kuelekea mashariki utakuwa ni dhiraa hamsini.14Chandarua upande mmoja wa lango itakuwa dhiraa kumi na tano upana wake. Lazima nguzo zake zitakuwa tatu na vitako vyake vitatu.15Upande wa pili ni vivyo hivyo chandarua ya dhiraa kumi na tano; nguzo zake tatu, na vitako vyake vitatu.16Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya samawati, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.17Nguzo zote za ule ua ziuzungukao pande zote zitakuwa na vitanzi vya fedha; kulabu zake za fedha, na vitako vyake vya shaba.18Urefu wa huo ua utakuwa dhiraa mia moja, na upana wake utakuwa dhiraa hamsini kotekote, na kwenda juu kwake dhiraa tano; yawe ya nguo ya kitani nzuri, na vitako vyake vitakuwa vya shaba.19Vyombo vyote vya maskani vitumiwavyo katika utumishi wake wote, na vigingi vyake vyote, na vigingi vyote vya ule ua, vitakuwa vya shaba.

20Waamuru wana wa Israeli wakuletee mafuta ya zeituni safi ya kupondwa kwa ajili ya nuru, ili kufanya ile taa kuwaka daima.21Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeneza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

28

1Umuite Haruni kaka yako na wana wake - Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari - miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.2Nawe utamfanyia Haruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri.3Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Haruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.4Na mavazi watakayoyafanya ni kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo, na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguye, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.5Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawati, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu.

6Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawati, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi.7Lazima itakuwa na vipande viwili vya mabegani, vilivyoungana kwenye ncha zake mbili; ili ipate kuunganishwa.8Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile vya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawati, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.9Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;10Majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao.11Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri uchorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.12Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabega vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli. Naye Haruni atayachukua majina yao mbele za Yahweh juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.13Nawe fanya vijalizo viwili vya dhahabu14na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo.

15Nawe lazima utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera. Fanya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawati, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.16Kitakuwa mraba, tena cha kukunjwa; urefu wake utakuwa shibiri moja, na upana wake shibiri moja.17Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza.18Na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawati, na almasi.19Na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto.20Na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi. Vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.21Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao. Mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.22Nawe lazima utie katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa, ya dhahabu safi.23Nawe utie maduara mawili ya dhahabu katika kile kifuko cha kifuani, na kuzitia hizo pete mbili katika ncha mbili za kifuko cha kifuani.24Nawe utie hiyo mikufu miwili ya dhahabu iliyosokotwa katika zile pete mbili zilizo katika ncha za kifuko cha kifuani.25Na ncha zile nyingine za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa utazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera upande wa mbele.26Nawe utafanya viduara viwili vya dhahabu, uzitie katika hizo ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake.27Nawe lazima ufanye viduara viwili vya dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.28Nao watakikaza kile kileso kwa vile viduara vyake kwenye viduara za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawati, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera.29Na Haruni atakapo yachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake kwa kufanya maamuzi, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele ya Yahweh daima.30Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Haruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Yahweh na Haruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Yahweh daima.

31Nawe fanya hiyo joho ya naivera ya rangi ya samawati yote.32Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, ili lisipasuke.33Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote.34Kengele ya dhahabu na komamanga, kengele ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote.35Nayo itakuwa juu ya Haruni akitumika; na sauti ya hizo kengele zitasikika hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Yahweh na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.

36Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, “Mtakatifu kwa Yahweh.”37Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya samawati, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba.38Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Yahweh.

39Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wa kazi ya mwenye kutia taraza.

40Kisha utafanya kanzu kwa ajili ya wana wa Haruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.41Nawe mvike huyo nduguye Haruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.42Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani.43Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.

29

1Sasa Hivi ndivyo wapaswa kufanya kuwatenga ili wanitumikie kama makuhani. Chukua mtoto wa ng'ombe dume na kondoo bila lawama,2mkate bila hamira, na keki bila hamira iliyo changanywa na mafuta. Pia chukua maandazi bila hamira yaliopakwa mafuta. Fanya maandazi kwa unga mzuri wa ngano.3Lazima uweke kwenye ndoo moja, leta kwenye ndoo, na kuleta pamoja na ng'ombe dume na wana kondoo wawili.4Lazima nawe umlete Haruni na wana wake wawili katika lango la kuingilia hema la kukutania. Lazima uwasafishe Haruni na wana wake kwenye maji.5Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho ya naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.6Nawe mvike kile kilemba kichwani, na ile taji takatifu utaitia katika kile kilemba.7Ndipo utakapotwaa hayo mafuta ya kutiwa, na kummiminia kichwani mwake, na kumtia mafuta.8Kisha walete hao wanawe na kuwavika kanzu.9Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia. Nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele. Nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.

10Kisha utamleta huyo ng'ombe mbele ya hema ya kukutania; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo ng'ombe.11Kisha utamchinja huyo ng'ombe mbele ya Yahweh penye hema ya kukutania. BWANA,12Kisha twaa baadhi ya damu ya ng'ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.13Kisha chukua mafuta yote yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo juu yake, uyateketeze yote juu ya madhabahu.14Lakini nyama yake huyo ng'ombe, na ngozi yake, na mavi yake, utayachoma kwa moto nje ya marango; ni sadaka kwa ajili ya dhambi.

15Pia mtwae kondoo mume mmoja; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo mume.16Kisha utamchinja huyo kondoo mume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kando-kando.17Kisha utamkata-kata kondoo vipande vyake, na kuyaosha matumbo yake na miguu yake, na kuiweka pamoja na vipande vyake na kichwa chake,18Nawe mteketeze kondoo mzima juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Yahweh; ni harufu nzuri, sadaka iliyosongezwa kwa Yahweh kwa njia ya moto.

19Kisha mtwae huyo kondoo mwingine; na Haruni na wanawe wataweka mikono yao juu ya kichwa chake huyo kondoo.20Kisha utamchinja kondoo, na kuitwaa damu yake, na kuitia katika ncha ya sikio la Haruni la upande wa kuume, na katika ncha za masikio ya kuume ya wanawe, na katika vyanda vya gumba vya mikono yao ya kuume, na katika vidole vikuu vya miguu yao ya kuume, na kuinyunyiza hiyo damu katika madhabahu kuizunguka kando-kando.21Kisha twaa katika hiyo damu iliyo juu ya madhabahu, na katika hayo mafuta ya kutiwa, na kumnyunyizia Haruni, juu ya mavazi yake, na wanawe, na mavazi yao pia, pamoja naye; naye atatakaswa, na mavazi yake, na wanawe, na mavazi ya wanawe, pamoja naye.

22Tena yatwae mafuta ya huyo kondoo mume, na mkia wake wa mafuta, na mafuta yafunikayo matumbo, na kitambi kilicho katika ini, na figo mbili, na mafuta yaliyo katika hizo figo, na paja la kuume; kwani ni kondoo ambaye ni wa kuwekwa kwa kazi takatifu.23Utwae na mkate mmoja wa unga, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na kaki moja katika kile kikapu cha mikate isiyotiwa chachu, kilichowekwa mbele ya Yahweh.24Nawe utavitia hivi vyote katika mikono ya Haruni, na katika mikono ya wanawe; nawe utavitikisa-tikisa viwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh.25Kisha uvitwae vile vitu mikononi mwao, na kuviteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa, viwe harufu nzuri mbele yangu; ni sadaka iliyotengenezwa kwangu kwa njia ya moto.26Kisha twaa kidari cha huyo kondoo wa kuwekwa kwake Haruni kwa kazi takatifu, na kukitikisa-tikisa kiwe sadaka ya kutikiswa mbele za Yahwe nacho kitakuwa ni sehemu yako.27Nawe kitakase kile kidari cha ile sadaka ya kutikiswa, na lile paja la sadaka ya kuinuliwa, lililotikiswa, na lililoinuliwa juu, vya yule kondoo wa kuwekwa kwa kazi takatifu, huyo aliyekuwa kwa ajili ya Haruni na wanawe.28Navyo vitakuwa vya Haruni na wanawe posho ya lazima sikuzote itokayo kwa hao wana wa Israeli; kwa kuwa ni sadaka ya kuinuliwa; itokayo kwa hao wana wa Israeli katika dhabihu zao za sadaka za amani, ni sadaka yao ya kuinuliwa kwa ajili ya Yahweh.

29Na hayo mavazi matakatifu ya Haruni yatakuwa ya wanawe baada yake, wayavae watakapotiwa mafuta, na watakapowekwa kwa kazi takatifu.30Huyo mwanawe atakayekuwa kuhani badala yake atayavaa muda wa siku saba, hapo atakapoingia ndani ya hiyo hema ya kukutania, ili atumike ndani ya mahali patakatifu.

31Nawe twaa huyo kondoo mume aliyekuwa wa kuwekwa kwa kazi takatifu, na kuichemusha nyama yake katika mahali patakatifu.32Na Haruni na wanawe wataila ile nyama ya kondoo, na mikate iliyo katika kile kikapu, hapo mbele ya mlango wa hema ya kukutania.33Nao watakula vile vitu ambavyo upatanisho ulifanywa kwa hivyo, ili kuwaweka kwa kazi takatifu na kuwatakasa; lakini mgeni asivile, maana, ni vitu vitakatifu.34Na kwamba kitu chochote cha ile nyama, iliyokwa ajili ya kuweka kwa kazi takatifu, au chochote cha hiyo mikate, kikisalia hata asubuhi, ndipo utavichoma kwa moto hivyo vilivyosalia; havitaliwa, maana, ni vitu vitakatifu

35Ni hivyo utakavyowatendea Haruni na wanawe kama nilivyo kuagiza. Utawaweka kwa kazi takatifu siku saba.36Kila siku utamtoa ng'ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya upatanisho; nawe utaisafisha hiyo madhabahu, hapo utakapofanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu; nawe utaitia mafuta, ili kuitakasa.37Utafanya upatanisho kwa ajili ya hiyo madhabahu muda wa siku saba, na kuitakasa; ndipo madhabahu itakapokuwa takatifu sana; kila kitu kiigusacho madhabahu kitakuwa kitakatifu.

38Lazima utoe kwenye madhabahu wana-kondoo wa mwaka mmoja wawili siku baada ya siku39daima. Mwana-kondoo mmoja utamchinja asubuhi; na mwana-kondoo wa pili utamchinja jioni40Pamoja na mwana-kondoo mmoja utatoa vibaba vitatu vya unga mzuri uliochanganyika na mafuta yenye kupondwa, kiasi cha kibaba na robo kibaba; na divai kiasi cha kibaba na robo kibaba, iwe sadaka ya kinywaji.41Na huyo mwana- kondoo wa pili utamchinja wakati wa jioni. Nawe utamfanyia vivyo kama ile sadaka ya unga ya asubuhi, na kama ile sadaka yake ya kinywaji. Hii itatoa harufu nzuri, ni dhabihu ya kusongezwa kwangu kwa njia ya moto.42Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya Yahweh, hapo nitakapokutana nanyi, ili niseme na wewe hapo.43Nami nitakutana na wana wa Israeli hapo; na hiyo hema itafanywa takatifu na utukufu wangu. Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu.44Pia Haruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.45Na mimi nitakaa kati ya wana wa Israeli, nami nitakuwa Mungu wao.46Nao watanijua kuwa mimi ndimi Yahweh, Mungu wao, niliyewaleta watoke katika nchi ya Misri, nipate kukaa kati yao. Ni mimi Yahweh, Mungu wao.

30

1Nawe fanya madhabahu ya kufukizia uvumba; utaifanyiza kwa mti wa mshita.2Urefu wake utakuwa dhiraa moja, na upana wake dhiraa moja; itakuwa mraba; na kwenda juu kwake dhiraa mbili; pembe zake zitakuwa za kitu kimoja nayo.3Nawe utaifunikiza dhahabu safi juu yake - na mbavu zake kando kando, na pembe zake. Nawe utaifanyia ukingo wa dhahabu kuizunguka.4Kisha utaifanyia pete mbili za dhahabu, chini ya ukingo wake katika mbavu zake mbili, katika pande zake mbili utazifanya; nazo zitakuwa mahali pa kuitia miti ya kuichukulia madhabahu.5Na ile miti utaifanya kwa mti wa mshita, na kuifunikiza dhahabu safi.6Nawe utaitia mbele ya lile pazia lililo karibu na sanduku la ushuhuda mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya ushuhuda, hapo nitakapokutana nawe.7Na Haruni atafukiza uvumba wa manukato juu yake; kila siku asubuhi. Atakapozitengeneza zile taa, ataufukiza,8Na Haruni atakapoziwasha zile taa wakati wa jioni, ataufukiza, uwe uvumba wa daima mbele za Yahweh katika vizazi vyenu vyote.9Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji10Naye Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka. Kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote. Ni takatifu sana kwa Yahweh.”

11BWANA akanena na Musa,12“Utakapowahesabu wana wa Israeli, kama itakavyotokea hesabu yao, ndipo watakapo mpa BWANA kila mtu ukombozi kwa ajili ya roho yake, hapo utakapowahesabu; ili kwamba yasiwe maradhi kati yao, hapo utakapowahesabu.13Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini). Nusu shekeli kwa sadaka ya Yahweh.14Kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa tangu huyo ambaye umri wake ni miaka ishirini, au zaidi, atatoa hiyo sadaka kwangu.15Watu watakapo leta hii sadaka kwangu kufanya upatananisho, matajiri hawataleta zaidi, wala maskini hawataleta kilichopungua katika hiyo nusu shekeli.16Nawe utapokea hizo fedha za upatanisho mikononi mwa hao wana wa Israeli, na kuziweka kwa ajili ya utumishi wa hema ya kukutania. Ili kwamba ziwe ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli mbele yangu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya roho zenu.

17Yahweh akamwambia Musa,18“Fanya na birika la shaba, na tako lake la shaba, ili kuogea; nawe utaliweka kati ya hema ya kukutania na madhabahu, nawe utalitia maji.19Na Haruni na wanawe wataosha mikono yao na miguu yao humo.20Hapo waingiapo ndani ya hema ya kukutania au waendepo karibu na madhabahu kunitumikia kwa kuchoma sadaka, watajiosha majini, ili wasife.21Basi wataosha mikono yao na miguu yao ili kwamba wasife; na neno hili litakuwa amri kwao milele, kwake yeye na kwa wazao wake katika vizazi vyao vyote.

22Kisha Yahweh akasema na Musa,23“Jitwalie manukato yaliyo bora, manemane mbichi shekeli mia tano, na mdalasini wenye harufu nzuri 250, na kane shekeli 25024na kida shekeli mia tano, kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu, na mafuta ya zeituni kiasi cha vibaba vitano.25Nawe utayafanya mafuta ya kutiwa matakatifu, marhamu iliyochanganywa kwa kazi ya ustadi ya mtengenezaji manukato; yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa.26Nawe utaipaka hema ya kukutania kwa mafuta hayo, na hilo sanduku la ushuhuda,27Na hiyo meza, na vyombo vyake vyote, na kinara cha taa, na vyombo vyake,28na madhabahu ya kufukizia uvumba, na madhabahu ya kuteketezea sadaka, pamoja na vyombo vyake vyote, na birika, na tako lake.29Nawe utavitakasa vitu hivyo, ili viwe vitakatifu sana; tena kila kivigusacho vyombo vile kitakuwa kitakatifu.30Nawe utawatia mafuta Haruni na wanawe, na kuwatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.31Nawe utanena na wana wa Israeli na kuwaambia, Haya yatakuwa ni mafuta matakatifu ya kutiwa kwa ajili yangu mimi katika vizazi vyenu vyote.32Hayatamiminwa katika kiwiliwili cha binadamu, wala msifanye mengine mfano wa haya kama yalivyoungwa kwa viungo vyake; ni matakatifu, na kwenu ninyi yatakuwa matakatifu.33Mtu awaye yote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu awaye yote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.’”

34Yahweh akamwambia Musa, “Jitwalie manukato mazuri, yaani, natafi, na shekelethi, na kelbena; viungo vya manukato vizuri pamoja na ubani safi; vitu hivyo vyote na viwe vya kipimo kimoja.35Nawe utafanya uvumba wa vitu hivyo, manukato ya kazi ya ustadi wa mtengenazaji manukato, yatakuwa yamekolea, safi, matakatifu.36Nawe baadhi yake utayaponda sana, na kuyaweka mbele ya ushuhuda ndani ya hema ya kukutania, hapo nitakapokutana nawe; nayo yatakuwa kwenu matakatifu sana.37Na uvumba utakaofanya, hamtajifanyia uvumba wenye viungo sawasawa na uvumba huo; utakuwa kwenu mtakatifu kwa ajili yangu.38Mtu yeyote atakayefanya mfano wa huo, ili kuunusa, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.

31

1Yahweh akasema na Musa,2“Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila la Yuda3Nami nimemjaza Bezaleli na roho wa Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,4ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,5Na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.6Tena, nimemchagua, awe pamoja naye Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani. Nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza. Hii ni,7Hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;8Na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote,9Na madhabahu ya kufukizia uvumba; na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake.10Pia mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani.11Pia mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawa sawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

12Akasema na Musa,13“Waambie wana wa Israeli, ‘Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.14Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika, atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.15Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku ya Sabato, hakika, atauawa.16Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato. Kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.17Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Yahweh alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

18Hapo Mungu alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa mkono wake.

32

1Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, “Njoo, katufanyizie sanamu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.”2Hivyo Haruni akawaambia, “Zitoeni pete za dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, na wana wenu, na binti zenu, mkaniletee.”3Watu wote wakavua pete za dhahabu zilizo katika masikio yao, na wakamletea Haruni.4Akapokea mikononi mwao akaitengeneza kwa patasi, akaifanya iwe sanamu ya ndama kwa kuiyeyusha. Nao wakasema, “Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.”

5Naye Haruni alipoona jambo hili, akajenga madhabahu mbele yake; Haruni akatangaza akasema,6“Kesho itakuwa sikukuu kwa Yahweh.” Wakaondoka asubuhi na mapema, wakatoa dhabihu, wakaleta sadaka za amani, watu wakaketi kula na kunywa, wakaanza kucheza.

7Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Shuka upesi, kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao.8Wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha wakaiabudu na kuitolea dhabihu. Wakasema, ‘Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokutoa katika nchi ya Misri.

9Kisha Yahweh akamwambia Musa, “Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo ngumu.10Basi sasa usinizuie. Ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize. Nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.”

11Musa akamsihi sana Yahweh Mungu wake, na kusema, “Yahweh, kwa nini hasira zako kuwaka juu ya watu wako uliowaleta kutoka nchi ya Misri kwa uweza mkuu, na kwa mkono wenye nguvu?12Kwa nini Wamisri kusema, ‘Amewatoa kwa kuwatenda uovu, ili apate kuwaua milimani, na kuwaondoa watoke juu ya uso wa nchi?’ Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu huu ulio nao juu ya watu wako.13Mkumbuke Ibrahimu, na Isaka, na Israeli, watumishi wako, ambao uliwaapia kwa nafsi yako, na kuwaambia, ‘Nitazidisha kizazi chenu mfano wa nyota za mbinguni; tena nchi hii yote niliyoinena nitakipa kizazi chenu nao watairithi milele.’

14Na Yahweh akaughairi ule uovu aliosema ya kwamba atawatenda watu wake.

15Kisha Musa akageuka akashuka katika mlima, na zile mbao mbili za mawe mikononi mwake. Mbao zilizoandikwa pande zote mbili, upande huu na upande huu ziliandikwa.16Na zile mbao zilikuwa kazi ya Mungu nayo maandiko yalikuwa maandiko ya Mungu, yaliyochorwa katika zile mbao.

17Na Yoshua aliposikia kelele za watu walipokuwa wakipiga kelele, akamwambia Musa, “Kuna kelele ya vita kambini.18“Lakini Musa akasema, “Hiyo si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushinda vitani, wala si sauti ya watu wapigao kelele kwa sababu ya kushindwa; bali kelele za watu waimbao ndizo ninazozisikia mimi.”

19Hata alipokaribia kambini akaiona ile ndama, na watu wakicheza. Hasira ya Musa ikawaka. Akazitupa zile mbao mikononi mwake, akazivunja chini ya mlima.20Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji. Akawanywesha wana wa Israeli.21Musa akamwambia Haruni, “Watu hawa wamekufanyanini hata ukaleta dhambi hii kuu juu yao?22Haruni akasema, “Hasira yako isiwake, bwana wangu. Wewe unawajua watu hawa, ya kuwa wamejielekeza kwa mabaya.23Maana waliniambia, ‘Katufanyie miungu, itakayokwenda mbele yetu. Kwa maana mtu huyo Musa, aliyetutoa katika nchi ya Misri, hatujui yaliyompata.’24Nikawaambia, ‘Mtu yeyote aliye na dhahabu na aivue; basi wakanipa, nami nikaitupa ndani ya moto, akatoka ndama huyu.”

25Basi Musa alipoona ya kuwa watu hawa wameasi (maana Haruni amewaacha waasi, ili wawe dhihaka kati ya adui zao)26Ndipo Musa akasimama katika mlango wa marago, akasema, “Mtu awaye yote aliye upande wa Yahweh na aje kwangu.” Wana wa Lawi wote wakamkusanyikia.27Akawaambia, Yahweh, Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Kila mtu na ajifunge upanga wake pajani mwake, akapite huko na huko toka mlango hata mlango kati ya marago, mkamchinje kila mtu ndugu yake, na kila mtu mwenziwe na kila mtu jirani yake.’28Na hao wana wa Lawi wakafanya kama vile alivyosema Musa, wakaanguka siku ile kama watu elfu tatu.29Musa akasema, Jiwekeni wakfu kwa Yahweh leo, kila mtu juu ya mwanawe na juu ya ndugu yake; ili Yahweh awape baraka leo.”

30Hata asubuhi yake Musa akawaambia watu, “Mmetenda dhambi kuu. Sasa nitakwenda juu kwa Yahweh. Labda nitafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi yenu.”31Musa akarejea kwa Yahweh akasema,” Oh! Watu hawa wametenda dhambi kuu wamejifanyia miungu ya dhahabu.32Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi yao – na kama sivyo, unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichoandika.”33Yahweh akamwambia Musa, “Mtu ye yote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.34Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake. Tazama, malaika wangu atakutangulia. Lakini pamoja na hayo siku nitakayowajilia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.”

35Kisha Yahweh akawapiga hao watu, kwa sababu ile ndama, ambayo Haruni aliifanya.

33

1Yahweh akasema na Musa, “Nenda kutoka hapa, wewe na watu ulio watoa kutoka nchi ya Misri. Nenda kwenye nchi nilio fanya nadhiri na Ibrahimu, Isaka, Yakobo, nilipo sema, ‘Nitakupa wewe na uzao wako.’2Nitatuma malaika mbele yako, na kuwaondoa Wakanani, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.3Nenda kwenye hiyo nchi, inayotiririka kwa maziwa na asali, lakini sitaenda nawe, kwa sababu ninyi ni watu wajehuri. Ninaweza kuwaharibu njiani.”

4Watu waliposikia haya maneno ya kushtua, walilia, na hakuna aliyevaa mikufu.5Yahweh alisema kwa Musa, “Waambie Waisraeli, ‘Ninyi ni watu wakorofi. Kama ningeenda miongoni mwenu ata kwa muda kidogo, nigewaharibu ninyi. Hivyo sasa, toa mikufu yenu ili niamue nini cha kufanya kwenu.”’6Hivyo Waisraeli hawakuvaa mikufu kutoka Mlima Horebu na kwendelea.

7Musa akachukua hema na kukita nje ya kambi, umbali kidogo na kambini. Aliita hema ya kukutania. Kila mtu aliyemuuliza Yahweh kitu chochote alienda kwenye hema ya kukutania, nje ya kambi.8Kisha Musa alipoenda kwenye hema, watu wote walisimama kando ya hema yao na kumuangalia Musa hadi alipoingia ndani.9Wakati wowote Musa alipoingia hemani, nguzo ya wingu ilishuka chini na kusimama nje ya lango la hema, na Yahweh alizungumza na Musa.10Wakati wowote watu walipoona nguzo ya wingu imesimama langoni mwa hema, waliamka na kuabudu, kila lango mwa hema yake.11Yahweh alizungumza na Musa uso kwa uso, kama mtu anapo zungumza na rafiki yake. Kisha Musa alirudi kambini, lakini mtumishi wake Yoshua mwana wa Nuni, kijana, alibaki hemani.

12Musa alisema na Yahweh, “Ona, umekuwa ukisema na mimi, ‘Chukua watu hawa safarini,’ lakini haujaniambia nani utamtuma na mimi. Umesema, ‘Nina kujua kwa jina, na umepata upendeleo kwangu.’13Kama nimepata upendeleo machoni pako, nionyeshe njia zako ili nikujue na kuendelea kupata upendeleo machoni pako. Kumbuka ili taifa ni watu wako.”14Yahweh akajibu, “Uwepo wangu utaenda nawe, na nitakupa pumziko.”15Musa akasema, “Kama uwepo wako hautaenda nasi, usitutoe hapa.16Au je, itajulikanaje nimepata upendeleo machoni pako, mimi na watu wako? Haitakuwa tu kama ukienda nasi mimi na watu wako tutakuwa na utofauti na watu wengine wote waliopo katika uso wa dunia?”17Yahweh akamwambia Musa, “Nitafanya pia hichi kitu ulicho niomba, kwa kuwa umepata upendeleo machoni mwangu, na nina kujua kwa jina lako.”

18Musa akasema, Tafadhali nionyeshe utukufu wako.”19Yahweh akasema, “Nitafanya wema wangu wote ujulikane kwako, na nitatangaza jina langu ‘Yahweh’ kwako. Nitakuwa na neema kwake nitakaye kuwa na neema, na nitaonyesha rehema kwake nitakaye onyesha rehema.”20Lakini Yahweh akasema, “Hautaona uso wangu, kwa kuwa hakuna aonaye uso wangu na kuiishi.”21Yahweh akasema, “Ona, hapa kuna sehemu yangu; utasimama kwenye huu mwamba.22Wakati utukufu wangu unapita, nitakuweka kwenye shimo kubwa la mwamba na kukufunika kwa mkono wangu mpaka nitakapo pita.23Kisha nitaondoa mkono wangu, na utaona mgongo wangu, ila uso wangu hautaonekana.”

34

1Yahweh akamwabia Musa, “Kata mbao mbili za mawe kama zile za awali. Nitaandika kwenye hizi mbao za mawe maneno yaliyokuwa kwenye mbao za mawe za mwanzo, mbao za mawe ulizo zivunja.2Kuwa tayari asubuhi na uje Mlimani Sinai, na uje mbele zangu juu ya mlima.3Hakuna atakaye kuja nawe. Usiruhusu mtu yeyote aonekane popote kwenye mlima. Hakuna kundi la mifugo wanao ruhusiwa hata kula mbele ya mlima.”4Hivyo Musa akakata mbao mbili za mawe kama za mwanzo, na akaamka asubuhi mapema na kwenda juu ya Mlima Sinai, kama Yahweh alivyomuelekeza. Musa alibeba mbao za mawe mikononi mwake.5Yahweh akaja chini katika wingu na akasimama mbele za Musa, na akatamka jina “Yahweh”6Yahweh akapita kwake na kukiri, “Yahweh, Yahweh, Mungu ni wa rehema na wa neema, sio mwepesi wa hasira, na anadumu katika uwaminifu wa agano na uadilifu,7ukishika uaminifu wa agano kwa vizazi maelfu, ukisamehe maasi, makosa, na dhambi. Lakini hamsafishi mwenye hatia. Ataleta adhabu ya dhambi za baba kwa watoto wao na watoto wa watoto wao, kwa kizazi cha tatu na hadi cha nne.”

8Musa haraka akainamisha kichwa chake kwenye ardhi na kuabudu.9Kisha akasema, “Kama sasa nimepata upendeleo machoni pako, Bwana wangu, tafadhali nenda pamoja nasi, kwa kuwa hawa watu ni wakorofi. Samehe maasi yetu na dhambi zetu, na utuchukue kama urithi wako.”

10Yahweh akasema, “Ona, ninakaribia kufanya agano. Mbele za watu wako, nitafanya maajabu ambayo hayajawahi kufanywa duniani kote wala kwenye taifa lote. Watu wote miongoni mwako wataona matendo yangu, kwa kuwa ni kitu cha hofu ninacho fanya kwako.11Tii amri zangu leo. Ninawaondoa mbele yako Waamori, Wakanani, Wahivi, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.12Kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi unayo kwenda, au wata kuwa mtego kwako.13Badala yake, lazima uvunje madhabahu zao, ponda nguzo zao za mawe, na kukata nguzo zao za Ashera.14Kwa kuwa wewe haupaswi kumuabudu mungu mwingine, maana Yahweh ambaye jina lake ni wivu, ni Mungu mwenye wivu.15Hivyo kuwa mwangalifu usifanye agano na wakazi wa nchi, kwa kuwa wanajifanyia ukahaba kwa miungu yao, na wanatoa dhabihu kwa miungu yao. Kisha mmoja wao atakukaribisha na wewe utakula baadhi ya dhabihu zake,16Na kisha utachukua baadhi ya mabinti zake kwa wanao, na mabinti wake watafanya ukahaba kwa miungu yao, na watafanya wanaokufanya ukahaba kwa miungu yao.

17Usifanye Miungu ya chuma ya kuyayusha.

18Lazima ushike Sherehe ya Mkate Usiotiwa chachu. Kama nilivyokuamuru, lazima ule mkate usio na hamira kwa siku saba kwa muda uliotengwa wa mwezi wa Abibu, maana nikatika mwezi wa Abibu ulitoka Misri.

19Wazaliwa wote ni wangu, hata mzaliwa wa kwanza wa kiume wa mifugo, yote ya ng'ombe na kondoo.20Lazima umnunue tena mzaliwa kwanza wa punda kwa kondoo, lakini usipo mnunua tena, kisha uivunje shingo yake. Lazima ununue tena wazaliwa wa kwanza wote wa wanao. Hakuna hata mmoja atakayekuja kwangu mikono mitupu.

21Utafanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba utapumzika. Hata wakati wa kilimo na wa mavuno, lazima upumzike.

22Lazima uadhimishe Sherehe ya Majuma kwa mazao ya kwanza ya mavuno ya ngano, na lazima uadhimishe Sherehe ya Makusanyo ya mwisho wa mwaka.

23Mara tatu kwa mwaka wanaume wenu wote watajitokeza kwa Bwana Yahweh, Mungu wa Israeli.24Kwa kuwa nitaondoa mataifa mbele yenu na kutanua mipaka. Hakuna atakayetamani kuwa na ardhi yenu kama yao utakapotoka mbele za Yahweh mara tatu kwa mwaka.

25Hautatoa damu ya dhabihu yangu na hamira yeyote, wala nyama yeyote kutoka dhabihu za Sherehe ya Pasaka kubaki hadi asubui.

26Lazima ulete matunda ya kwanza yalio bora kutoka nyumbani kwako. Usimchemshe mbuzi mtoto katika maziwa ya mama yake.”

27Yahweh akamwabia Musa, “Andika chini haya maneno, kwa kuwa nimejiahidi haya maneno niliyoyasema, na nimefanya agano kwako na Israeli.”

28Musa alikuwa huko na Yahweh kwa siku arobaini na usiku; hakula chakula chochote wala kunywa maji yeyote. Aliandika katika mbao maneno ya agano, Amri kumi.

29Musa aliposhuka chini ya Mlima Sinai na mbao mbili za agano za ushuhuda mikononi mwake, hakujua kuwa ngozi ya uso wake ilikuwa ina'ngaa akizungumza na Mungu.30Wakati Haruni na Waisraeli walipo muona Musa, ngozi ya uso yake ilikuwa inang'aa, na waliogopa kuja karibu naye.31Lakini Musa aliwaita, na Haruni na viongozi wa jamii wakaja kwake. Kisha Musa akasema nao.32Baada ya haya, watu wote wa Israeli wakaja kwa Musa, na akawambia amri zote Yahweh alizompa katika Mlima Sinai.33Musa alipomaliza kuzungumza nao, alifunika uso wake kwa kitambaa.34Wakati Musa alipoenda mbele za Yahweh kusema naye, aliondoa kitambaa, hadi alipotoka. Alipotoka, aliwaambia Waisraeli alichoamriwa kusema.35Waisraeli walipomuona Musa ana'ngaa uso, alirudisha kitambaa tena usoni mpaka alipokuwa anaenda kuongea na Yahweh.

35

1Musa akawakusanya jamii yote ya Waisraeli na kuwaambia, “Haya ndio mambo Yahweh aliyowaamuru mfanye.2Kwa siku sita kazi ya weza fanywa, lakini kwako, siku ya saba lazima iwe siku takatifu, siku ya Sabato ya mapumziko, takatifu kwa Yahweh. Yeyote atakaye fanya kazi hiyo siku lazima auawe.3Haupaswi kuwasha moto kwenye nyumba zenu siku ya Sabato.”

4Musa akasema na jamii yote ya Waisraeli, kwa kusema, “Hiki ndicho kitu Yahweh alichoamuru.5Chukua sadaka kwa ajili ya Yahweh, wote wenye moyo mkunjufu. Leta sadaka kwa Yahweh - dhahabu, fedha, shaba,6buluu, zambarau, sufu nyekundu na kitambaa kizuri; nywele za mbuzi;7ngozi za kondoo zilizotiwa rangi nyekundu na ngozi za pomboo; na mbao za mshita;8mafuta ya taa kwa pahali patakatifu, viungo vya manukato kwa hayo mafuta ya kutiwa,9kwa uvumba mzuri na vito vya shohamu na vito vya kutiwa kwa hiyo naivera, na kwa hicho kifuko cha kifuani.

10Kila mwanaume mwenye ustadi kati yenu aje na afanye kila kitu ambacho Yahweh aliyaamuru --11hema la kuabudia, na kifuniko chake, na vifungo vyake, na mbao zake, nguzo, na sakafu;12pia sanduku na nguzo zake, kiti cha rehema, na pazia la kusitiri.13Walileta meza na miguu yake, vyombo vyake vyote, na mkate wa wonyesho;14kinara cha taa, vyombo vyake, taa, na mafuta ya zile taa;15ile madhabahu ya uvumba na nguzo zake, mafuta ya upako na uvumba ulitiwa manukato; kishikizo cha mwingilio wa hema ya kuabudia;16madhabahu ya sadaka ya kuteketeza na kitunzi cha shaba na nguzo na vyombo; na ile beseni kubwa na sakafu yake.17Walileta vishikizo kwa ajili ya nyuani na nguzo zake na sakafu yake, na pazia kwa ajili ya mwingilio wa nyauni;18na ile misumari ya hema la kuabudia na nyuani, pamoja na kamba zake.19Walileta mavazi yaliyofumwa kutumikia sehemu takatifu, mavazi takatifu ya Haruni kuhani na wanawe, kwa wao kutumika kama makuhani.”

20Kisha makabila yote ya Israeli yakaondoka na kwenda kutoka uweponi mwa Musa.21Kila mtu moyo wake ulimchochea na aliyeandaliwa na roho yake alikuja na kuleta sadaka kwa Yahweh kwa matengenezo ya hema ya kuabudia, kwa vitu vyote kwajili ya huduma ndani yake, na kwa vazi takatifu.22Walikuja, wote wanaume kwa wanawake, wote waliokuwa na moyo wa utayari. Walileta madini, hereni, pete, na vitu vya thamani, vitu vyote tofauti vyenye madini ya dhahabu. Waliwasilisha sadaka za dhahabu kama sadaka ya kupunga kwa Yahweh.23Kila mmoja alikuwa na sufu ya samawati, zambarau, au nyekundu, nguo nzuri, singa za mbuzi, ngozi za kondoo zilizobadili kuwa nyekundu, na ngozi ya pomboo walivileta.24Kila mmoja alitengeneza sadaka ya fedha au shaba walizileta kama sadaka kwa Yahweh, na kila mmoja aliyekuwa na mti wa mshita kwa matumizi ya kazi aliuleta.25Kila mwanamke mwenye ustadi walisokota sufu kwa mikono yao na walileta sufu walizosokota za samawati, zambarau, au sufu nyekundu, au nguo nzuri.26Wanawake wote wenye mioyo iliyochochewa na walio na ustadi walisokota singa za mbuzi.27Viongozi walileta mawe ya shohamu na mawe mengine kwa ajili ya kuwekwa kwenye hiyo naivera na hicho kifuko cha kifuani;28walileta viungo na mafuta kwa ajili ya taa, kwa mafuta ya upako, na kwa uvumba wa manukato.29Waisraeli walileta sadaka ya hiyari kwa Yahweh; kila mwanaume na mwanamke ambao mioyo yao ilikuwa tayari walileta vifaa kwa ajili ya kazi zote ambazo Yahweh aliamuru kupitia Musa zifanyike.

30Musa alisema kwa waisraeli, “Tazama, Yahwe ameita kwa jina juu ya Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huri, kutoka kabila la Yuda.31Aliijaza Bezaleli kwa Roho yake, kumpa hekima, kuwelewa, na maarifa, kwa aina zote za ujenzi,32kufanya sanaa za ubunifu na kufanya kazi za dhahabu, na shaba;33pia kukata na kupanga mawe na mbao zilizochongwa- kufanya kazi za aina zote kwa ubunifu na ujenzi.34Aliiweka kufundisha ndani ya moyo wake, yeye pamoja na Oholiabu mwana wa Ahisamaki, kutoka kabila la Dani.35Aliwajaza kwa ustadi wa kufanya kazi za aina zote, kufanya kazi ya kama kuchora mawe, kama mwerevu, kama mtia taraza katika nyuzi za rangu ya samawati, zambarau, na nyekundu na nguo nzuri, na kama washonaji. Walikuwa wachonga mawe wa kazi zote, na walikuwa wabunifu wa sanaa.

36

1Hivyo Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Yahweh aliyempa ustadi na uwezo kujua jinsi ya kufanya kazi katika ujenzi wa sehemu takatifu wafanye kazi kadiri ya yote Yahwhe aliyoamuru.”

2Musa akamwita Bezaleli, Oholiabu, na kila mtu mwenye ujuzi ambaye Yahweh alimpa, na ambaye moyoni mwake ulichochewa kuja na kufanya kazi.3Walipokea kutoka kwa Musa sadaka zote ambazo Waisraeli walizo leta kwa ujenzi ya sehemu takatifu. Watu walikuwa bado wanaleta sadaka za hiari kila asubui kwa Musa.4Hivyo watu wote walikuwa na ujuzi walikuwa wakifanya kazi sehemu takatifu walikuja kutoka kwenye kazi walikuwa wakifanya.5Wachonga mawe walimwambia Musa, “Watu wanaleta zaidi sana ya yanayohitajika kufanya kazi Yahweh aliyotuamuru.”6Hivyo Musa akaamuru mtu yeyote asilete tena kwa ujenzi wa sehemu takatifu. Kisha watu wakaacha kuleta hivi vitu.7Walikuwa na zaidi ya vitu vya ujenzi.

8Hivyo wachonga mawe miongoni mwao wakajenga lile hema la kuabudia kwa mapazia kumi yaliyojengwa kitamba kizuri na samawati, zambarau, na sufu nyekundu kwa aina ya kerubi. Hii ni kazi ya Bezaleli, mjenzi mwenye ujuzi sana.9Urefu wa kila pazia ulikuwa mikono ishirini na nane, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa vyote hivyo vilikuwa na kipimo kimoja.10Bezaleli akaunganisha vitambaa vitano pamoja, na vile vitambaa vingine vitano akaviunganisha pamoja.11Kisha akafanya vitanzi vya uzi wa samawati kwenye upindo wa kitambaa kilicho mahali pa kuungania. Akafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa cha inje kabisa kilicho mahali pale pengine pa kuungania.12Akafanya vitanzi hamsini kwenye kitambaa kimoja, akafanya vitanzi hamsini kwenye mwisho wa kitambaa kilichokuwa mahali pale pengine pa kuungania, vitanzi hivyo vikiwa vinaelekeana.13Mwishowe akafanya kulabu hamsini za dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa kulabu hizo, hivi kwamba hiyo ikawa maskani moja.14Bezaleli akafanya vitambaa vya mahema vya manyoya ya mbuzi kwa ajili ya hema lililo juu ya maskani. Vitambaa kumi na moja ndivyo alivyofanyiza.15Urefu wa kila kitambaa ulikuwa mikono thelathini, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa hivyo kumi na moja vilikuwa na kipimo kimoja.16Kisha akaunganisha vitambaa vitano pamoja na vile vitambaa vingine sita pamoja.17Kisha akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pa kuungania, naye akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kile kitambaa kingine kilichoungana nacho.18Bezaleli akafanya kulabu hamsini za shaba kwa ajili ya kuliunganisha hilo hema pamoja liwe kipande kimoja.19Naye akafanya kifuniko cha hema kutokana na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko kutokana na ngozi za sili, upande wa juu.20Bezaleli akafanya viunzi vya mbao vya hema ya kukutania, kutokana na mbao za mshita.21Urefu wa kiunzi ulikuwa mikono kumi, nao upana wa kila kiunzi ulikuwa mkono mmoja na nusu.22Kila kiunzi kilikuwa na ndimi mbili zilizounganishwa. Hivyo ndivyo alivyofanya viunzi vyote vya maskani.23Basi akafanya viunzi vya maskani, viunzi ishirini kwa ajili ya upande kuelekea kusini.24Bezaleli akafanya vikalio arobaini vya fedha viwe chini ya vile viunzi ishirini, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja pamoja na ndimi zake mbili na vikalio vingine viwili chini ya kiunzi kingine pamoja na ndimi zake mbili.25Na kwa ajili ya ule upande mwingine wa maskani, upande wa kaskazini, akafanya viunzi ishirini26na vikalio vyake arobaini vya fedha. Vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kiunzi kingine27Na kwa ajili ya zile pande za nyuma za maskani kuelekea magharibi, akafanya viunzi sita.28Naye akafanya viunzi viwili vya pembeni ya maskani kwenye pande zake mbili za nyuma29Hizi zilikuwa pacha upande wa chini, lakini juu ya kila moja kwenye pete ya kwanza. Hivyo ndivyo alivyoifanya yote miwili, ile miimo ya pembeni.30Basi vikajumlika kuwa viunzi vinane na vikalio vyake kumi na sita vya fedha, vikalio viwili kando ya vikalio viwili chini ya kila kiunzi.31Bezaleli akafanya miti ya mshita, mitano kwa ajili ya viunzi vya upande mmoja wa maskani,32na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande ule mwingine wa maskani na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya maskani kwa ajili ya zile pande mbili za nyuma za magharibi.33Kisha akafanya mti wa katikati upitie katikati ya vile viunzi toka mwisho mmoja mpaka ule mwingine.34Naye akavifunika vile viunzi kwa dhahabu, akazifanya pete zake za dhahabu ziwe vitegemezo kwa ajili ya ile miti, akaifunika ile miti kwa dhahabu.

35Bezaleli akafanya pazia, la uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa cha rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kalitia makerubi kwa kazi ya mjenzi.36Kisha akalifanyia nguzo nne za mshita na kuzifunika kwa dhahabu, vibanio vyake vikiwa vya dhahabu, na kutengeneza vikalio vinne vya fedha kwa ajili yake.37Naye akafanya kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema kutokana na uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kazi ya mfumaji.38Pia akafanya na nguzo zake tano na vibanio vyake. Naye akavifunika vilele vyake na viungo vyake kwa dhahabu, lakini vile vikalio vyake vitano vilikuwa vya shaba.

37

1Bezaleli akafanya Sanduku la mbao za mshita. Mikono miwili na nusu urefu wake, na mkono mmoja na nusu upana wake, na mkono mmoja na nusu kimo chake.2Kisha akalifunika kwa dhahabu safi ndani na nje na kulifanyia ukingo wa dhahabu kulizunguka pande zote.3Kisha akalitengenezea pete nne za dhahabu, za juu ya miguu yake minne, pete mbili upande wake mmoja na pete mbili upande wake mwingine4Kisha akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.5Halafu akaitia miti hiyo kwenye zile pete zilizo pande za Sanduku ili kulibeba Sanduku.6Naye akafanya kifuniko cha dhahabu safi. Mikono miwili na nusu urefu wake, na mkono mmoja na nusu upana wake.7Bezaleli akafanya makerubi wawili wa dhahabu. Kwa kazi ya kufua akawafanya kwenye miisho yote miwili ya kifuniko.8Kerubi mmoja kwenye mwisho ule, na yule kerubi mwingine kwenye mwisho huu. Aliwafanya makerubi juu ya kifuniko kwenye miisho yote miwili.9Nao wakawa makerubi wanaonyoosha mabawa yao mawili kuelekea juu, wakisitiri kifuniko kwa mabawa yao, nazo nyuso zao zilikuwa zikielekeana. Nyuso za makerubi hao zilielekea kifuniko hicho.

10Bezaleli akafanya meza ya mbao za mshita. Mikono miwili urefu wake, na mkono mmoja upana wake, na mkono mmoja na nusu kimo chake.11Halafu akaifunika kwa dhahabu safi na kufanya ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.12Kisha akafanya mzingo wa upana wa kiganja kuizunguka na kufanya ukingo wa dhahabu kwa ajili ya mzingo wake kuizunguka pande zote.13Tena, akatengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili yake na kuziweka pete hizo kwenye zile pembe nne zilizokuwa kwa ajili ya ile miguu minne.14Pete hizo zilikuwa karibu na ule mzingo, ili kutegemeza ile miti ya kuibeba meza hiyo.15Halafu akafanya ile miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu ili kuibeba ile meza.16Baada ya hilo akafanya kutokana na dhahabu safi vile vyombo vilivyo juu ya meza, sahani zake na vikombe vyake na mabakuli yake na mitungi yake iliyotumiwa kumimina matoleo ya kinywaji.17Kisha akafanya kinara cha taa cha dhahabu safi. Kwa kazi ya kufua akakifanya kinara cha taa. Pande zake na matawi yake, vikombe vyake, mafundo yake na maua yake vikatokea kwake.18Na matawi sita yalikuwa yakitoka kwenye pande zake, matawi matatu ya kinara cha taa kutoka kwenye upande wake mmoja na matawi mengine matatu ya kinara cha taa kutoka kwenye ule upande wake mwingine.19Vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kikundi kimoja cha matawi, vifundo na maua yakifuatana; na vikombe vitatu vyenye umbo la maua ya mlozi vilikuwa kwenye kile kikundi kingine cha matawi, vifundo na maua yakifuatana. Hivyo ndivyo ilivyokuwa kwa yale matawi sita yaliyokuwa yakitoka katika kile kinara cha taa.20Na kwenye kile kinara cha taa kulikuwa na vikombe vinne vyenye umbo la maua ya mlozi, vifundo vyake na maua yake yakifuatana.21Na kile kifundo chini ya matawi mawili kilitoka kwake, na kifundo kilicho chini ya yale matawi mengine mawili kilitoka kwake, na kifundo kingine kilicho chini ya matawi mengine mawili zaidi kilitoka kwake, kwa ajili ya matawi sita yanayotoka katika kinara.22Vifundo vyake na matawi yake vilitoka kwake, vyote vilikuwa kitu kimoja cha kazi ya kufua, cha dhahabu safi.23Kisha akafanya taa zake saba na mikasi ya tambi zake na vyetezo vyake kutokana na dhahabu safi.24Alikifanya kwa talanta ya dhahabu safi, hicho pamoja na vyombo vyake vyote.

25Sasa akafanya madhabahu ya uvumba, kutokana na mbao za mshita. Mkono mmoja urefu wake na mkono mmoja upana wake, ikiwa mraba, na mikono miwili kimo chake. Pembe zake zilitoka kwake.26Kisha akaifunika kwa dhahabu safi, upande wake wa juu na pande zake za kando kuizunguka na pembe zake, naye akafanya ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote.27Naye akaifanyia pete mbili za dhahabu chini ya ukingo wake kwenye pande zake mbili, kwenye pande zake mbili zinazoelekeana, za kutegemeza ile miti ya kuibeba.28Kisha akafanya ile miti ya mshita na kuifunika kwa dhahabu.29Tena akafanya yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba safi uliotiwa manukato, + kazi ya mtengenezaji wa marhamu.

38

1Naye akafanya madhabahu ya matoleo ya kuteketezwa kwa mbao za mshita. Mikono mitano urefu wake, na mikono mitano upana wake, ilikuwa mraba, na mikono mitatu kimo chake.2Halafu akafanya pembe zake kwenye zile ncha zake nne. Pembe zake zilitoka kwake. Kisha akaifunika kwa shaba.3Baada ya hilo akavifanya vyombo vyote vya madhabahu, yale makopo na zile sepetu na yale mabakuli, zile nyuma na vile vyetezo. Vyombo vyake vyote alivifanya kwa shaba.4Tena akaifanyia madhabahu kiunzi cha fito, mtandao wa shaba, chini ya ukingo wake, chini kuelekea katikati yake.5Halafu akatengeneza pete nne kwenye ile miisho minne karibu na kile kiunzi cha shaba, ili kuitegemeza ile miti.6Bezaleli akafanya miti ya mshita na kuifunika kwa shaba.7Kisha akaitia ile miti kwenye zile pete zilizo pande za madhabahu ili kuibeba. Akaifanya kuwa sanduku la mbao lenye uwazi.

8Kisha akafanya beseni ya shaba na kinara chake cha shaba. Kwa kutumia vioo vya watumishi wanawake ambao walifanya utumishi uliopangwa kwenye mwingilio wa hema la mkutano.

9Naye akafanya ule ua. Upande unaokabili Negebu, kuelekea kusini, mapazia ya ua yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa, kwa mikono mia moja.10Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha11Pia, kwa ajili ya upande wa kaskazini kulikuwa na mikono mia. Nguzo zake ishirini na vikalio vyake ishirini vilikuwa vya shaba. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.12Lakini kwa ajili ya upande wa magharibi mapazia yalikuwa mikono hamsini. Nguzo zake zilikuwa kumi na vikalio vyake kumi. Misumari ya nguzo na viungo vyake vilikuwa vya fedha.13Na kwa ajili ya upande wa mashariki kulikuwa na mikono hamsini.14Mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano kwa upande mmoja. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.15Na kwa ajili ya upande ule mwingine, huu na ule, wa lango la ua, mapazia yalikuwa mikono kumi na mitano. Nguzo zake zilikuwa tatu na vikalio vyake vitatu.16Mapazia yote ya ua kuzunguka pande zote yalikuwa ya kitani bora kilichosokotwa.17Navyo vikalio vya nguzo vilikuwa vya shaba. Vibanio vya vikalio na viungo vyake vilikuwa vya fedha navyo vilifunikwa kwa shaba sehemu ya juu, na kulikuwa na viungo vya shaba kwa ajili ya nguzo zote za ua.18Nacho kisitiri cha lango la ua kilikuwa na mikono ishirini urefu. Cha uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kocho laini na kitani bora kilichosokotwa, na urefu wake ulikuwa mikono ishirini, nacho kimo kotekote kilikuwa mikono mitano sawa sawa na mapazia ya ua.19Na nguzo zake nne na vikalio vyake vinne vilikuwa vya shaba. Misumari yake ilikuwa ya fedha na utando wa vichwa vyake na viungo vyake ulikuwa wa fedha.20Na misumari yote ya hema kwa ajili ya maskani na kwa ajili ya ua kuzunguka pande zote ilikuwa ya shaba

21Hivi ndivyo vitu vilivyohesabiwa vya maskani, pa Ushuhuda, vilivyohesabiwa kwa amri ya Musa, kuwa utumishi wa Walawi chini ya uongozi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani.22Naye Bezaleli mwana wa Uri mwana wa Huru wa kabila la Yuda alifanya yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.23Na pamoja naye alikuwa Oholiabu mwana wa Ahisamaki wa kabila la Dani, fundi na mtarizi na mfumaji wa uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora.24Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya kazi katika kazi yote ya mahali patakatifu ikawa jumla ya dhahabu ya toleo la kutikisa, talanta ishirini na tisa na shekeli 730 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu.25Nayo fedha ya wale walioandikishwa kati ya kusanyiko ilikuwa talanta mia moja na shekeli 1,775 kulingana na shekeli ya mahali patakatifu,26Ile nusu shekeli kwa ajili ya mtu mmoja ilikuwa nusu shekeli kulingana na shekeli ya mahali patakatifu. Kwa kila mtu aliyekuwa akipita kuingia upande wa wale waliokuwa wameandikishwa kuanzia miaka ishirini na zaidi, jumla ya watu 603,550.27Na talanta mia moja za fedha zilitumiwa kutengeneza vikalio vya mahali patakatifu na vikalio vya lile pazia. Vikalio mia moja vilitoshana na talanta mia moja, talanta moja kwa kikalio kimoja.28Na kutokana na zile shekeli 1,775 alitengeneza vibanio vya nguzo na kuvifunika sehemu yake ya juu na kuviunganisha pamoja.29Nayo shaba ya toleo la kutikisa ilikuwa talanta sabini na shekeli 2,400.30Naye akaitumia kufanya vile vikalio vya mwingilio wa hema la mkutano na ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, na vyombo vyote vya madhabahu,31Na vile vikalio vya ua kuzunguka pande zote, na vile vikalio vya lango la ua, na misumari yote ya maskani na misumari+ yote ya ua kuzunguka pande zote.

39

1Na kutokana na ule uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili wakafanya mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika mahali patakatifu. Basi wakafanya yale mavazi matakatifu yaliyokuwa kwa ajili ya Haruni, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.2Basi akaifanya ile naivera ya dhahabu, uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.3Kisha wakafua mabamba ya dhahabu yawe mabamba membamba, naye akakata nyuzi za kufuma pamoja na ule uzi wa samawati na ile sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kile kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kile kitani bora, kama kazi ya mjenzi.4Wakaifanyia vipande vya begani vilivyounganishwa. Iliunganishwa kwenye miisho yake miwili.5Nao mshipi, uliokuwa juu yake ili kuifunga, ulikuwa wa kitambaa kile kile kulingana na ufundi wake, wa dhahabu, uzi wa samawati, na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.6Kisha wakafanya mawe ya shohamu yaliyopangwa kwenye mapambo ya dhahabu, yaliyochongwa kwa michoro ya muhuri kulingana na majina ya wana wa Israeli.7Bezaleli akayaweka kwenye vile vipande vya begani vya naivera yawe mawe ya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli, kama vile Yehova alivyokuwa amemwamuru Musa8Kisha akafanya kile kifuko cha kifuani kwa ufundi wa mjenzi, kama ule ufundi wa naivera, kutokana na dhahabu, uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa.9Kilikuwa mraba kilipokunjwa. Walikifanya kile kifuko cha kifuani, kinapokunjwa, shubiri moja urefu wake na shubiri moja upana wake.10Kisha wakakijaza kwa mistari minne ya mawe. Mstari wa zabarijadi, topazi na zumaridi ulikuwa mstari wa kwanza.11Nao mstari wa pili ulikuwa feruzi, yakuti na yaspi.12Nao mstari wa tatu ulikuwa jiwe la leshemi, akiki na amethisti.13Nao mstari wa nne ulikuwa krisolito na shohamu na yashefi. Yaliwekwa katika mapambo ya dhahabu katika mahali pake.14Na mawe hayo yalikuwa kulingana na majina ya wana wa Israeli. Yalikuwa kumi na mawili kulingana na majina yao, kwa michongo ya muhuri, kila moja kulingana na jina lake kwa ajili ya yale makabila kumi na mawili.15Nao wakafanya juu ya kile kifuko cha kifuani minyororo yenye mashada, msokoto wa kamba, wa dhahabu safi.16Kisha wakafanya mapambo mawili ya dhahabu na pete mbili za dhahabu na kuziweka hizo pete mbili kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani.17Baada ya hilo wakapitisha zile kamba mbili za dhahabu kwenye zile pete mbili zilizo kwenye miisho ya kile kifuko cha kifuani.18Nao wakapitisha ile miisho miwili ya zile kamba mbili kwenye yale mapambo mawili. Halafu wakaiweka juu ya vile vipande vya begani vya naivera, mbele yake.19Kisha wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka kwenye ile miisho miwili ya kile kifuko cha kifuani kwenye upindo wake ulio upande unaoelekea ile efodi upande wa ndani.20Halafu wakafanya pete mbili za dhahabu na kuziweka juu ya vile vipande viwili vya begani vya efodi upande wake wa chini, sehemu yake ya mbele, karibu na mahali pake pa kuungania, juu ya ule mshipi wa naivera.21Mwishowe wakakifunga kile kifuko cha kifuani kwa pete zake kwenye zile pete za efodi kwa uzi wa samawati, ili kipate kuwa juu ya mshipi wa efodi na kile kifuko cha kifuani kisiondoke juu ya efodi, kama vile Yahwe alivyokuwa amemwamuru Musa.

22Bezaleli akafanya lile koti la naivera, lote la uzi wa zambarau, kazi ya mshonaji.23Na sehemu wazi ya hilo koti ilikuwa katikati yake, kama sehemu wazi ya vazi la chuma. Sehemu hiyo iliyo wazi ilikuwa na ukingo kuizunguka pande zote ili isiraruke.24Halafu wakafanya kwenye upindo wa hilo koti makomamanga ya uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, vilivyosokotwa pamoja.25Wakafanya kengele za dhahabu safi na kuziweka kengele hizo katikati ya makomamanga kwenye upindo wa lile koti kuzunguka pande zote, katikati ya makomamanga;26kengele na komamanga, kengele na komamanga kwenye upindo wa hilo koti kuzunguka pande zote, kwa ajili ya kuhudumu, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.

27Kisha wakafanya zile kamba za kitani bora, kwa ajili ya Haruni na wanawe.28Na kile kilemba cha kitani bora na yale mavalio ya kichwani ya mapambo ya kitani bora na zile suruali za kitani bora kilichosokotwa,29Na ule ukumbuu wa kitani bora kilichosokotwa na uzi wa samawati na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili, kazi ya mfumaji, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.30Mwishowe wakafanya lile bamba linalong’aa, ishara takatifu ya wakfu, kutokana na dhahabu safi na kuandika juu yake maandishi kwa mchongo wa muhuri: “Utakatifu kwa Yahweh.”31Kisha wakalitia uzi wa samawati ili waliweke juu ya kile kilemba upande wa juu. Kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.

32Basi kazi ya ile maskani ya hema la mkutano ikafikia mwisho wake. Kwa maana wana wa Israeli waliendelea kufanya kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa.33Nao wakaileta maskani kwa Musa, lile hema pamoja na vyombo vyake vyote, kulabu zake, viunzi vyake vya mbao, miti yake na nguzo zake na vikalio vyake,34na kifuniko chake cha ngozi za kondoo-dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko chake cha ngozi za sili na pazia la kisitiri,35na sanduku la ushuhuda na miti yake na kifuniko.36Wakaleta meza, vyombo vyake vyote, na ule mkate wa wonyesho,37Kile kinara cha taa cha dhahabu safi, taa zake, ule mstari wa taa, na vyombo vyake vyote na yale mafuta ya kuangazia taa,38Na madhabahu ya dhahabu na yale mafuta yanayotumiwa kutia mafuta na ule uvumba uliotiwa manukato na kile kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema,39Ile madhabahu ya shaba na kile kiunzi chake cha shaba, miti yake na vyombo vyake vyote, ile beseni na kinara chake,40Wakaleta mapazia ya ua, nguzo zake na vikalio vyake na kile kisitiri, kwa ajili ya lango la ua, kamba zake za hema na misumari yake ya hema na vyombo vyote kwa ajili ya utumishi wa maskani, kwa ajili ya hema ya kukutania.41Wakaleta yale mavazi yaliyofumwa kwa ajili ya kuhudumu katika patakatifu, yale mavazi matakatifu kwa ajili ya Haruni kuhani na mavazi ya wanawe ya kutumikia wakiwa makuhani.42Kulingana na yote ambayo Yahweh alikuwa amemwamuru Musa, hivyo ndivyo wana wa Israeli walivyoufanya utumishi wote.43Naye Musa akaiona ile kazi yote, na, tazama, walikuwa wameifanya kama vile Yahweh alivyokuwa ameamuru. Hivyo ndivyo walivyokuwa wamefanya. Basi Musa akawabariki.

40

1Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,2“Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka lazima wewe uandae hema la kukutania.3Utaweka sanduku la ushuhuda ndani yake, na utaziba sanduku kwa pazia.4Utaleta ndani meza na kuandaa kwa mpangilio vitu vyake. Kisha utaleta kinara cha taa na kuandaa taa.5Nawe utaweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na utaweka pazia katika mwingilio wa hema la kukutania.6Utaweka madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa mbele ya mwingilio wa hema ya kukutania.7Utaweka ile saani kubwa katikati ya hema la kukutania na madhabahu na utaweka maji ndani yake.8Uandae nyuani inayoizunguka, na utundike pazia katika mwingilio wa nyuani.9Lazima uchukuwe mafuta ya upako na upake hema la kukutania na kila kitu kilichopo ndani yake. Lazima uitenge na samani zake kwangu; kisha itakuwa takatifu.10Lazima upake mafuta madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake. Lazima utenge madhabhu kwa ajili yangu na itakuwa takatifu kwangu.11Upake mafuta beseni la shaba na sakafu yake na uitenge kwa ajili yangu.12Umlete Haruni na wanawe kwa mwingilio wa hema la kukutania na uwaoshe wote kwa maji.13Utamfunika Haruni kwa mavazi yaliyotengwa kwa ajili yangu, mpake mafuta na umtenge ili anitumikie kama kuhani.14Utawaleta wana wake na kuwafunika kwa nguo nzito.15Utawapaka mafuta kama ulivyompaka baba yao ili wanitumikie kama makuhani. Upako wao utawafanya makuhani wa kudumu vizazi vyote vya watu wao.”

16Hivi ndivyo Musa alivyosema; alifuata yote Yahweh aliyomuamuru. Alifanya vitu vyote hivi.17Hivyo hema la kukutania liliandaliwa siku ya kwanza ya mwezi wa mwaka wa pili.18Musa aliandaa hema la kukutania, akaweka sakafu zake sehemu yake, akaandaa fremu zake, akashikisha chuma zake, na akaandaa minara na nguzo zake.19Alitandaza mfuniko juu ya hema la kukutania na kuweka hema juu yake, kama Yahweh alivyoamuru.20Alichukua amri za agano na kuweka kwenye sanduku. Pia aliweka nguzo kwenye sanduku na kuweka mfuniko wa kiti cha rehema.21Aliichukua sanduku na kuweka ndani ya hema la kukutania. Aliandaa pazia ili lizibe sanduku la ushuhuda, kama Yahweh alivyo muamuru.22Aliweka meza kwenye hema la kukutania, kwa upande wa kaskazini mwa hema la kukutania, nje ya pazia.23Aliweka mkate kwa mpangilio katika meza ya Yahweh, kama Yahweh alivyoamuru.24Aliweka kinara cha taa kwenye hema la kukutania, upande wa pili wa meza, kusini mwa hema la kukutania.25Aliwasha taa mbele za Yahweh, kama Yahweh alivyo muamuru.26Aliweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba ndani ya hema la kukutania mbele ya pazia.27Alichoma uvumba wa manukato hapo, kama Yahweh alivyo muamuru.28Alitundika pazia katika hema ya kukutania.29Aliweka madhabahu ya sadaka ya kuteketeza katika hema ya kukutania. Aliitolea sadaka yakuteketeza na sadaka ya unga, kama Yahweh alivyomuamuru.30Aliweka beseni katikati ya hema ya kukutania na madhabahu, na maji ya kuoshea.31Musa, Haruni, na wanawe waliosha mikono yao na miguu kwenye beseni32muda wowote walipoenda kwenye hema ya kukutania na muda wowote walipoenda kwenye madhabahu. Walijisafisha, kama Yahweh alivyomuamuru Musa.33Musa alianda nyuani nyuma ya hema ya kukutania na madhabahu. Aliandaa pazia katika mwingilio wa nyuani. Katika hili, Musa alimaliza kazi.

34Kisha wingu likafunika hema ya kukutania, na utukufu wa Yahweh ukafunika hema ya kukutania.35Musa hakuweza kuingia hema ya kukutania kwa sababu wingu lilikuwa juu yake, na kwa sababu utukufu wa Yahweh ulijaza hema ya kukutania.36Muda wowote wingu lilipochukuliwa juu kutoka hema ya kukutania, watu wa Israeli waliendelea na safari yao.37Lakini kama wingu halikunyanyuka juu kutoka hema ya kukutania, kisha basi watu hawakusafiri. Walibaki hadi siku liliponyanyuliwa juu.38Kwa kuwa wingu la Yahweh lilikuwa juu ya hema ya kukutania mchana, na moto wake ulikuwa juu yake usiku, wazi kwa watu wote wa Israeli kipindi chote cha safari yao.

Mambo ya walawi

1

1Mungu alimwita Musa na alisema naye kutoka kweye hema la kukutania, akasema,2“Sema na wana wa Israeli na uwaambie, ‘Mwanaume yeyote miongoni mwenu akileta sadaka kwa Bwana, aleta kama matoleo katika wanyama wako, iwapo mifugo au katika kundi.”

3Kama matoleo yake ni ya sadaka ya kuteketezwa kutoka katika kundi, atatoa dume asiyekuwa na kasoro. Atamtoa katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania, ili iwe imekubaliwa mbele za Bwana.4Ataweka mikono yake kichwani pa sadaka ya kuteketezwa, na ndipo itakuwa imekubaliwa badala yake kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe.5Ndipo atapaswa kuchinja ng'ombe mbele ya Bwana. Watoto wa Haruni, makuhani wataleta damu na kuinyunyizia katika madhabahu iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema la kukutania.6Ndipo ataichuna sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande.7Kisha wana wa Haruni kuhani wataweka moto katika madhabahu na kuweka kuni ili kuchochea moto.8Wana wa Haruni, makuhani wataweka vipande, kichwa na mafuta, watazipanga juu ya kuni zilizoko juu ya moto ulio madhabahuni.9Lakini matumbo yake na miguu lazima ataiosha kwa maji. Kisha kuhani atateketeza kila kitu kilicho juu ya madhabahu kama sadaka ya kuteketeza. Italeta harufu nzuri sana kwangu; itakuwa sadaka iliyotolewa kwa moto kwa ajili yangu.

10Kama sadaka kwa ajili ya sadaka ya kuteketeza kutoka kundi, kondoo au mbuzi, lazima atoe dume asiye na kasoro.11Lazima atamchinja juu ya madhabahu yaliyo katika upande wa kaskazini mbele ya Bwana. Wana wa Haruni makuhani, watanyunyiza damu kila upande wa madhabahu.12Kisha ataikata katika vipande, pamoja na kichwa na mafuta yake, kuhani atavipanga juu ya kuni zilizo katika moto ulio madhabahuni,13lakini matumbo yake na miguu yake lazima ioshwe kwa maji. Kisha kuhani atatoa yote na kuiteketeza juu ya madhabahu. Ni sadaka ya kuteketezwa, italeta harufu nzuri kwa ajili ya Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.

14Kama sadaka yake kwa Bwana itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa ni ndege, ndipo ataleta kama sadaka yake pengine ni hua au kinda wa njiwa.15Kuhani ataileta madhabahuni, atamnyonga kichwa chake, na kuiteketeza juu ya madhabahu. Kisha damu yake itachuruzishwa juu ya pande za madhabahu.16Kisha atakiondoa kibofu chake pamoja na uchafu wake, na kukiweka upande wa mashariki mwa madhabahu, katika sehemu ya majivu.17Kisha atapasua mabawa yake, lakini hatagawanya katika vipande viwili. Kisha Kuhani atamteketeza katika madhabahu, juu ya kuni amabazo ziko juu ya moto. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa, na italeta harufu nzuri sana kwa Bwana; itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.

2

1Yeyote akitoa sadaka ya nafaka kwa Bwana, sadaka yake lazima iwe unga safi, na atamwaga mafuta juu yake na kuweka ubani juu yake.2Atachukua sadaka kwa wana wa Haruni, makuhani na pale kuhani atachukua konzi moja ya unga safi pamoja na mafuta na ubani. Kisha kuhani atateketeza hiyo sadaka juu ya madhabahu kuwa shukrani kwa uzuri wa Bwana. Italeta harufu nzuri sana kwa Bwana, itakuwa sadaka ya Bwana iliyotolewa kwa moto.3Unga wowote uliobaki utakuwa ni wa Haruni na watoto wake. Ni takatifu sana kwa Bwana iliyotolewa sadaka kwa Bwana kwa moto.

4Kisha utakapotoa sadaka ya unga bila chachu iliyookwa kweye kiokeo, itakuwa mkate laini wa unga safi uliochanganywa na mafuta, au mkate mgumu usiokuwa na chachu, ambao umesambazwa na mafuta.5Kama matoleo yako ya nafaka yameokwa na kikaango cha chuma ni lazima iwe unga safi bila chachu uliochanganywa na mafuta.6Utagawanya katika vipande na kumwaga mafuta juu yake. Hii ni sadaka ya nafaka.7Kama sadaka yako ya nafaka imepikwa katika kikaango, ni lazima iwe imetengenezwa kwa unga safi na mafuta.8Utaleta matoleo ya nafaka yaliyotengenezwa kwa vitu hivi kwa Bwana, utaleta kwa kuhani, ambaye ataleta mbele ya madhabahu.9Ndipo kuhani atachukua baadhi ya sadaka ya nafaka ya shukrani ya Bwana, ataiteketeza katika madhabahu. Itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa moto, italeta harufu nzuri kwa Bwana.10Itakayobaki sadaka ya nafaka itakuwa ya Haruni na wanawe. Itakuwa takatifu kamili ya Bwana kutoka matoleo kwa Bwana yatolewayo kwa moto.

11Sadaka ya nafaka itolewayo kwa Bwana isiwe na chachu, hautateketeza chachu wala asali kama matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana.12Utayatoa kwa Bwana kama mazao ya kwanza, lakini hayatatumika kama matoleo ya harufu nzuri ya moto juu ya madhabahu.13Utaweka chumvi katika kila matoleo yako ya nafaka. Usipungukie chumvi ya agano la Bwana katika matoleo yako ya unga. Matoleo yako yote hayatapungukiwa na chumvi.

14Kama ukitoa matoleo ya nafaka ya mazao ya kwanza kwa Bwana, utatoa nafaka mbichi yaliyookwa kwa moto, na yaliyopondwa.15Lazima utaweka mafuta na ubani juu yake. Haya ni matoleo ya nafaka.16Kuhani atatoa sehemu ya nafaka iliyopondwa na mafuta na ubani, kama sadaka ya shukrani itolewayo kwa uzuri wa Bwana. Hii ni sadaka ya Bwana inayotolewa kwa moto.

3

1Kama mtu atatoa dhabihu ambayo ni matoleo ya amani ya mnyama kutoka katika kundi, dume au jike, lazima atatoa mnyama asiye na kasoro mbele ya Bwana.2Ataweka mikono yake juu ya sadaka yake na atamchinja mbele ya mlango wa hema ya kukutania. Kisha wana wa Haruni makuhani watanyunyizia damu yake katika pande za madhabahu.3Mtu akitoa dhabihu ya amani itolewayo kwa moto kwa ajili ya Bwana. Mafuta yanayofunika au yanayoungana na hizo sehemu za ndani,4figo mbili na mafuta yaliyofunika kiunoni na yanayozunguka ini, pamoja na figo atayatoa pamoja.5Wana wa Haruni watayachoma hayo katika madhabahu pamoja na sadaka ya kuteketezwa, juu ya kuni zilizo kwenye moto. Zitaleta harufu nzuri mbele ya Bwana; itakuwa sadaka itolewayo kwake kwa moto.

6Kama dhabihu ya amani ya mtu itolewayo kwa Bwana ni kutoka katika mifugo ni mbuzi au kondoo ni dume au jike, atatoa dhabihu isiyo na kasoro.7Kama atatoa mwanakondoo kwa ajili ya dhabihu yake, atamtoa mbele za Bwana.8Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha dhabihu yake na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande za madhabahu.9Mtu akitoa sadaka ya dhabihu ya amani kama sadaka ya kusogezwa kwa moto kwa Bwana. Mafuta, mafuta ya mkia yatakatwa hapo karibu na mfupa wa kiuno, na mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yaliyo katika matumbo,10na figo zote mbili na mafuta yanayofunika yaliyo karibu na kiuno kitambi kilicho karibu na ini na figo ataziondoa zote.11Na kuhani atayateketeza yote kwa moto katika madhabahu kama sadaka ya chakula isogezwayo kwa moto kwa Bwana.

12Kama matoleo ya mtu ni mbuzi, ndipo ataitoa mbele ya Bwana.13Ataweka mikono yake juu ya kichwa cha mbuzi na atamchinja mbele ya hema ya kukutania. Ndipo wana wa Haruni watanyunyizia damu pande zote za madhabahu.14Mtu akitoa dhabihu kwa Bwana kwa njia ya moto. Ataondoa mafuta yanayozunguka matumbo, na mafuta yote yanayozunguka matumbo.15Ataondoa pia figo mbili na mafuta yanayozunguka, ambayo yanazunguka kiuno na kitambi cha maini pamoja na figo.16Kuhani atateketeza yote juu ya madhabahu kama matoleo ya chakula yatolewayo kwa moto, ni sadaka ya kuleta harufu nzuri sana. Mafuta yote ni ya Bwana.

17Itakuwa ni amri ya kudumu kwa kizazi cha watu katika maeneo yote mtakapotengeneza makazi, kwamba hamtakula mafuta au damu.”’

4

1Bwana alisema na Musa na kumwambia,2“Waambie wana wa Israeli ‘Mtu yeyote akifanya dhambi bila kukusudia, kufanya chochote ambacho Bwana ameagiza kutofanya, na kama akifanya chochote kilichozuiliwa, yafuatayo lazima yatatendeka.

3Kama ni kuhani mkuu aliyetenda dhambi na kuleta hatia kwa watu, atatoa dume asiyekuwa na kasoro kwa Bwana kwa ajili ya dhambi aliyotenda kama sadaka ya dhambi.4Ataleta dume mbele ya mlango wa hema ya kukutania mbele ya Bwana, ataweka mikono juu ya dume, na atamchinja huyo dume mbele za Bwana.5Kuhani aliyewekewa mafuta atachukua damu ya dume na kuileta mbele ya hema ya kukutania.6Kuhani atazamisha kidole chake katika damu na kuinyunyiza mara saba mbele za Bwana, mbele ya pazia la mahali pa takatifu.7Na kuhani ataweka kiasi cha damu ya huyo dume juu ya pembe za madhabahu ya kuvukizia uvumba mbele za Bwana, katika hema ya kukutania na ataimwaga yote iliyobaki chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mahali pa kuinglia katika hema ya kukutania.8Atakata mafuta yote ya dume wa sadaka ya dhambi, mafuta yanayofunika matumbo na mafuta yote yaliyo katika matumbo,9figo mbili na mafuta yaliyopo pamoja nazo, yaliyo karibu na kiuno na kitambi cha maini pamoja na hizo figo.10Ataondoa zote vile vile kama yanavyoondolewa katika dume wa sadaka ya dhabihu ya amani. Kuhani atatekeza sehemu hizo katika madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.11Ngozi ya dume na mabaki yoyote ya nyama, pamoja na kichwa chake, miguu yake, matumbo yake na mavi yake,12mabaki yote ya dume atayachukua nje ya mji mahali palipo safi, mahali wanapomwaga majivu; watateketeza sehemu zote juu ya kuni. Watateketeza sehemu zote mahali wanapomwaga majivu.

13Kama mkutano wote wa wana wa Israeli wakitenda dhambi bila kukusudia, na mkutano hawatakumbuka kwamba wametenda dhambi, na kufanya vile Bwana aliagiza wasifanye na wakajisikia hatia.14Na dhambi waliyofanya ikajulikana, mkutano watatoa ng'ombe dume mchanga kuwa sadaka ya dhambi watamleta mbele ya hema ya kukutania.15Wazee wa mkutano wataweka mikono yao juu ya kichwa cha ng'ombe mbele za Bwana, na ng'ombe atachinjwa mbele za Bwana.16Kuhani aliyetiwa mafuta ataleta damu ya ng'ombe katika hema ya kukutania,17kuhani atachovya kidole chake katika damu na kuinyunyizia mara saba mbele za Bwana mbele ya pazia.18Ataweka kiasi cha damu katika pembe za madhabahu mbele za Bwana iliyo katika hema ya kukutania na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo katika mlango wa kuingilia katika hema ya kukutania.19Atakata mafuta yote na kuyatekeza katika madhabahu.20Hivyo ndivyo atakavyomfanya huyo ng'ombe, kama alivyomfanya ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia vivyo hivyo huyu ng'ombe, kuhani atawafanyia upatanisho watu nao watasamehewa.21Atamchukua huyo ng'ombe nje ya mji na kumteketeza kama alivyomteketeza ng'ombe wa kwanza. Hii ni sadaka ya dhambi kwa ajili ya mkutano.

22Mtawala akitenda dhambi bila kukusudia kufanya moja ya yale Bwana Mungu wake ameagiza kutotenda, na anajisikia hatia23na kama dhambi yake aliyotenda anaifahamu, ataleta dhabihu yake mbuzi wa kiume asiye na kasoro.24Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha mbuzi na kumchinja mahali ambapo huchinja sadaka ya kuteketezwa mbele za Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.25Kuhani atachukua damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuiweka juu ya pembe za madhabahu kwa dhabihu ya kuteketezwa, na atamwaga damu chini ya madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa.26Atateketeza mafuta yote katika madhabahu, kama vile mafuta ya dhabihu ya sadaka ya amani, Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtawala kulingana na dhambi yake, na mtawala atakuwa amesamehewa.

27Kama yeyote wa watu wa kawaida akitenda dhambi bila kukusudia, kufanya vitu ambavyo Bwana ameagiza kutokufanywa na kama ana hatia,28ndipo dhambi yake aliyoitenda ikajulikana kwake, ndipo ataleta mbuzi wa kike asiyekuwa na kasoro awe dhabihu kwa ajili ya dhambi zake alizotenda.29Ataweka mikono yake juu ya sadaka ya dhambi na kuchinja sadaka ya dhambi mahali pa sadaka ya kuteketezwa.30Kuhani atachukua kiasi cha damu kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu ya dhabihu ya kuteketezwa. Damu yote iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu.31Atayaondoa mafuta yote, kama alivyoondoa mafuta katika dhabihu ya amani. Kuhani ataiteketeza katika madhabahu ili kuwa harufu nzuri kwa Bwana. Kuhani atafanya upatanisho kwa mtu, na atasamehewa.

32Kama mtu ataleta mwanakondoo kama dhabihu yake kwa sadaka ya dhambi, ataleta jike asiye na kasoro.33Ataweka mikono kichwani mwa sadaka ya dhambi na atamchinja kuwa sadaka ya dhambi mahali wanapochinjwa sadaka ya kuteketezwa.34Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi kwa kidole chake na kuweka katika pembe za madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, na ataimwaga damu yote chini ya madhabahu.35Ataondoa mafuta yote, kama akatavyo mafuta ya mwanakondoo dhabihu ya sadaka ya amani na kuhani ataiteketeza juu ya madhabahu juu ya sadaka ya Bwana itolewayo kwa moto. Kuhani ataleta upatanisho kwa dhambi aliyoifanya, naye atasamehewa.

5

1Kama mtu atatenda dhambi kwa sababu hakusema ukweli wakati alipotakiwa kutoa ushahidi fulani kuhusu kile alichotakiwa, ameona au kufahamu habari zake, yeye anastahili adhabu.

2Au mtu akigusa kitu chochote ambacho Mungu amekitaja kuwa ni najisi hata kama ni mzoga wa wanyama wa porini au ni mzoga wa wanyama wa kufugwa au wataambaao hata kama mtu huyo hakukusudia kumgusa, yeye ni najisi na mwenye hatia.

3Au amegusa kitu chochote kilicho kichafu, kwa vyovyote kama hakujua, ndipo atakuwa na hatia akijua vile.

4Au kama yeyote akiapa bila kufikiri kwa midomo yake kufanya ubaya, au kufanya vyema kwa vyovyote vile mtu ameapa kwa haraka atakapotambua atakuwa na hatia kwa vitu hivyo.

5Mtu yeyote akiwa na hatia kwa vitu hivi, lazima akiri kwa dhambi yoyote aliyotenda.6Ndipo atakapoleta sadaka yake ya hatia mbele za Bwana kwa dhambi aliyokwisha tenda. Ataleta kondoo jike au mbuzi kutoka katika kundi lake kuwa matoleo ya dhambi, kuhani atafanya upatanisho kuhusu dhambi yake.

7Kama hata weza kununua mwana kondoo ataleta kama sadaka ya hatia, hua wawili au makinda mawili ya njiwa kwa Bwana, mmoja kwa sadaka ya dhambi na mwingine ni sadaka ya kutekeketezwa.8Atawaleta kwa kuhani, wa kwanza atatoa kwa ajili ya sadaka ya dhambi. Atamvunja shingo yake lakini ataacha kichwa chake kinaning'inia wala hataiondoa kabisa shingo yake katika mwili.9Ndipo atanyunyizia damu yake katika sehemu za madhabahu, na damu inayobaki ataimwaga chini ya madhabahu. Hii ni dhabihu ya dhambi.10Ndipo atatoa ndege wa pili kama sadaka ya kuteketezwa kama ilivyoelekezwa, na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya dhambi alizokwisha kufanya, na huyo mtu atakuwa amesamehewa.

11Lakini kama hataweza kununua hua wawili au makinda ya njiwa mawili, ndipo ataleta kama dhabihu ya dhambi zake sehemu ya kumi ya unga laini kama sadaka ya dhambi. Asiweke mafuta wala ubani juu yake, kwa kuwa ni sadaka ya dhambi.12Atauleta kwa kuhani, na kuhani atachukua konzi moja ya unga kama ukumbusho wa wema wa Bwana na atauweka juu ya madhabahu na kuteketeza juu ya sadaka za kuteketezwa kwa moto kwa ajili ya Bwana. Hii ni sadaka ya dhambi.13Kuhani atafanya upatanisho kwa dhambi yoyote aliyofanya mtu yeyote, mtu huyo atasamehewa. Na sadaka inayobaki itakuwa ya kuhani, kama ilivyo sadaka ya nafaka.’”

14Bwana akamwambia Musa, akasema,15“Kama mtu akikiuka amri na kufanya dhambi kinyume na mambo matakatifu ya Bwana, lakini akifanya bila kukusudia ataleta sadaka ya hatia kwa Bwana. Sadaka hii itakuwa ni kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi; thamani yake halisi kifedha kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, kama sadaka ya hatia.16Lazima atalipa kwa Bwana kwa kile alichokosa kulingana na kitakatifu, na ataongezea moja ya tano na kumpa kuhani. Ndipo kuhani ataweka upatanisho kwa ajili yake pamoja na kondoo wa sadaka ya hatia, na mtu atakuwa amesamehewa.

17Kama mtu akitenda dhambi kwa kufanya kile ambacho Bwana aliagiza kisifanyike, hata kama hakujua, atakuwa na hatia na ataibeba hatia yake.18Lazima ataleta kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi, anayestahili thamani ya fedha, kama sadaka ya hatia kwa kuhani. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kulingana na dhambi aliyotenda, ambayo hakujua atakuwa amesamehewa.19Ni sadaka ya hatia, na amekuwa na hatia mbele za Bwana.”

6

1Bwana alisema na Musa kumwambia,2“Kama mtu akifanya dhambi na kuvunja amri kinyume na Bwana, kama kujihusisha na uongo dhidi ya jirani yake kuhusu kitu fulani cha kutokuwa mwaminifu, au kama akidanganya au kuiba au amemdhulumu jirani.3Au akiokota kitu fulani ambacho jirani yake amepoteza na kusema uongo kuhusu hicho, na kuapa kwa uongo au kwa mambo kama haya ambayo watu wanaweza kutenda dhambi.4Ndipo itakuwa hivi, kama ametenda dhambi na hatia, kwamba lazima akirudishe kwa vyovyote alichoiba au kudanganya au amedhulumu au kitu kilichopotea naye kukiokota.5Au kama amedanganya kwa jambo lolote, lazima atakirudisha kamili na kuongezea sehemu ya tano kwa kumlipa anayedai, kwa siku ile anayopatikana na hatia.6Ataleta sadka ya hatia kwa Bwana: kondoo dume asiye na kasoro kutoka katika kundi lake kulingana na thamani yake, kama sadaka ya hatia kwa kuhani.7Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele ya Bwana, atakuwa amesamehewa kulingana na chochote kilicho mfanya kuwa na hatia.”

8Ndipo Bwana alisema na Musa kumwambia,9“Mwagize Haruni na wanawe, kusema, ‘hii ni sheria ya sadaka ya kuteketezwa: Sadaka ya kuteketezwa lazima iwe juu ya makaa ya madhabahu usiku wote hata asubuhi, na moto wa madhabahu utaendelea kuwaka.10Kuhani atavaa nguo zake za kitani na atavaa nguo za kitani ndani yake. Atatoa majivu yaliyobaki baada ya moto kutekeza sadaka ya kuteketezwa juu ya madhabahu, na ataweka majivu pembeni mwa madhabahu.11Atavua mavazi haya na kuvaa mavazi mengine ili kuchukua majivu nje ya kambi na kupeleka mahali palipo safi.12Moto katika madhabahu utaendelea kuwaka. Usizimike, na kuhani ataongeza kuni kila asubuhi. Atapanga juu yake sadaka ya kuteketezwa kama inavyotakiwa, na atateketeza juu yake mafuta ya sadaka ya amani.13Moto lazima utaendelea kuwaka katika madhabahu, kamwe usizimike.

14Hii ni sheria ya sadaka ya nafaka. Wana wa Haruni watatoa mbele ya Bwana katika madhabahu.15Kuhani atachukua konzi ya unga laini wa sadaka ya nafaka na mafuta na ubani ambao uko juu ya sadaka ya nafaka, atateketeza juu ya madhabahu kuleta harufu nzuri ya shukrani ya kumpendeza Bwana.16Haruni na wanawe watakula sadaka inayobaki, italiwa bila kutiwa chachu mahali patakatifu. Watakula katika ua ya hema ya kukutania.17Haitaokwa pamoja na chachu. Nimewapa kama sehemu ya sadaka yangu itolewayo kwa moto, ni takatifu sana, kama sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.18Kwa nyakati zote zijazo kupitia watu wa kizazi chako, mwanaume yeyote mzaliwa kutoka kwa Haruni aweza kula ni sehemu yake, ichukuliwayo katika sadaka ya Bwana kwa moto. Yeyote anayeigusa atakuwa mtakatifu.”

19Bwana aliongea tena na Musa kumwambia,20“Hii ni sadaka ya Haruni na wanawe ambayo watatoa kwa Bwana katika siku ambayo kila mwana atawekwa wakfu: sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kama kawaida sadaka ya nafaka nusu yake asubuhi na nusu yake jioni.21Itatengenezwa na mafuta katika kikaango, utaileta ikiwa imeandaliwa imeokwa katika vipande utatoa sadaka ya nafaka ili kuleta harufu nzuri kwa Bwana.22Mwana wa Kuhani Mkuu atakayekuwa Kuhani Mkuu mpya kutoka miongoni mwa wanawe ataitoa. Kama amri ya milele, yote itateketezwa kwa Bwana.23Kila sadaka ya nafaka ya kuhani itatekezwa yote. Haitaliwa kamwe.”

24Bwana alisema tena na Musa, kumwambia,25“Sema na Haruni na watoto wake kwamba, ‘Hii ni sheria ya sadaka ya dhambi: Sadaka ya dhambi lazima kuchinjwa mahali pa sadaka ya kuteketezwa, itachinjwa mbele ya Bwana. Ni takatifu sana.26Kuhani atakayeitoa kwa ajili ya dhambi ndiye atakayeila. Italiwa mahali patakatifu katika ua wa hema ya kukutania.27Yeyote atakayeigusa nyama yake atakuwa ni mtakatifu na kama damu itadondokea mavazi yatafuliwa mahali palipodondokewa, mahali patakatifu.28Lakini chungu kikipikiwa kitavunjwa, kama imepikiwa katika chombo cha shaba, lazima kitasuguliwa na kusafishwa kwa maji.29Mwanaume yeyote miongoni mwa makuhani anaweza kula nyama hiyo kwa sababu ni takatifu sana.30Na hakuna sadaka ya dhambi italiwa ambayo damu yake imeletwa katika hema ya kukutania kufanya upatanisho katika mahali patakatifu. Ni lazima iteketezwe.

7

1Hii ndiyo sheria ya sadaka ya hatia. Kwa sababu hiyo ni sadaka takatifu sana.2Ni lazima waichinje sadaka ya hatia mahali panapostali kuchinjwa, na ni lazima watainyunyiza damu yake pande zote za madhabahu.3Mafuta yote yaliyomo ndani yake yataondolewa: mafuta ya mkiani, mafuta yaliyo sehamu za ndani,4zile figo mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake, yaliyo karibu na kiuno, na yanayofunika ini—nyama hii yote lazima iondolewe pamoja na hizo figo.5Kuhani ataviteketeza vipande hivi juu ya madhabahu viwe dhabihu iliyofanywa kwa Yahwe kwa moto. Hii ni sadaka ya hatia6Kila mwanaume miongoni mwa familia ya kuhani anaweza kula sehemu ya sadaka hii. Lakini ni lazima iliwe ndani ya mahali patakatifu kwa sababu ni takatifu sana.

7Nayo sadaka ya dhambi ni kama ilivyo sadaka ya hatia. Ni sheria ile ile hutumika kwa zote mbili. Zote ni mali ya kuhani azitumiaye kufanya upatanisho.8Kuhani atoaye sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya mtu yeyote anaweza kuchukua ngozi ya sadaka hiyo kwa ajili yake mwenyewe.9Kila sadaka ya nafaka inayo okwa mekoni, na kila sadaka kama hiyo ipikwayo kaangoni au kwenye sufuria itakuwa ya kuhani aitoaye.10Kila sadaka ya nafaka, ama iwe unga mkavu au uliochanganywa na mafuta ya zeitu itakuwa ya ukoo wa Haruni kwa usawa.

11Hii ndiyo sheria ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo watu watazitoa kwa Yahwe.

12Iwapo mtu yeyote anaitoa ili kuonyesha shukrani kwa Yahwe, basi ataitoa pamoja na dhabihu ya mikate iliyotengenezwa bila hamira, bali kwa mafuta ya zeituni yaliyochanganywa na unga lakini bila hamira, na maandazi yaliyotengenezwa bila hamira, bali yaliyopakwa mafuta juu yake, na mikate miembamba iliyofanywa kwa unga laini uliochanganywa na mafuta.13Kwa kusudi la kutoa shukrani, pia anapaswa kutoa pamoja na sadaka yake ya amani, vipande vya mikate iliyotiwa hamira.14Ni lazima atatoa moja kila aina ya sadaka hizi kama sadaka iliyoletwa kwa Yahwe. Nayo itakuwa ya makuhani wanaonyunyizia damu ya sadaka ya amani kwenye madhabahu.15Mtu anayeleta sadaka ya amani kwa kusudi la kutoa shukrani ni lazima ataila nyama ya sadaka yake siku ya kutoa dhabihu. Hatakiwi kusaza chochote kilicho cha sadaka hiyo hata asubuhi ya pili.

16Lakini iwapo dhabihu ya matoleo yake kusudi lake ni nadhiri, au kwa kusudi la sadaka ya hiari, nyama yake italiwa siku iyo hiyo aitoapo dhabihu yake, lakini chochote kinachosalia cha sadaka hiyo kinaweza kuliwa siku inayofuata.17Hata hivyo, nyama yoyote ya dhabihu inayobaki siku ya tatu ni lazima ichomwe moto.18Iwapo kipande chochote cha nyama hiyo ya dhabihu kinachobaki kinaliwa katika siku ya tatu, hakitakubalika, wala hakitatolewa kwa aliyeitoa. Kitakuwa ni kitu cha kuchukiza, na mtu akilaye atabeba hatia ya dhambi yake mwenyewe.

19Nyama yoyote inayogusa kitu kilicho najisi haitaliwa. Ni lazima ichomwe moto. Na kwa ajili ya nyama inayobaki, yeyote aliye safi anaweza kuila.20Hata hivyo, mtu najisi anayekula nyama kutoka kwenye dhabihu ya matoleo ya amani ambayo ni ya Yahwe yapasa mtu huyu akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.21Iwapo mtu yeyote anagusa kitu chochote kilicho najisi—iwe ni unajisi wa binadamu, au wa mnyama aliye najisi, au wa kitu fulani kilicho najisi na chenye kuchukiza, na kisha akala baadhi ya nyama ya dhabihu ya sadaka ya amani iliyotolewa kwa Yahwe, lazima mtu huyo akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.

22Kisha Yahwe akazungumza na Musa, akisema,23“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, ‘hamruhusiwi kula mafuta ya fahali au kondoo au mbuzi.24Mafuta ya mnyama yoyote afaye peke yake bila ya kuwa dhabihu, au mafuta ya mnyama yeyote aliyeraruliwa na wanyama pori, yanaweza kutumika kwa makusudi mengine, lakini hakika hamtayala.25Yeyote atakayekula mafuta ya mnyama ambayo watu wanaweza kuyatoa kuwa dhabihu ya iliyofanywa kwa Yahwe kwa moto, mtu huyo lazima atakatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.26Hamtakula damu yoyote katika moja wapo ya nyumba zenu, ama iwe kutoka kwa ndege au mnyama.27Yeyote alaye damu yoyote, mtu huyo lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.’”

28Kwa hiyo Yahwe akazungumza na Musa na akasema,29“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Yeye atoaye dhabidhu ya sadaka ya amani kwa Yahwe lazima alete sehemu ya dhabihu yake kwa Yahwe.30Mikono yake mwenyewe lazima iilete hiyo sadaka ifanywayo kwa Yahweh kwa moto. Naye atayaleta hayo mafuta pamoja na kidari, ili kwamba kidari kiweze kutikiswa kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahwe.31Kuhani atayachoma mafuta hayo juu ya madhabahu, lakini kile kidari kitakuwa mali ya Haruni na uzao wake.32Ni lazima utatoa paja la kulia kwa kuhani kama sadaka iliyotokana na dhabihu ya sadaka yako ya amani.33Yule kuhani, mmoja wa wazao wa Haruni, atoaye damu na mafuta ya sadaka ya amani—ni lazima atapata paja la kulia kama mgao wake wa sadaka.34Kwa kuwa nimetwaa kidari, na paja la sadaka ya kutikiswa kutoka kwa watu wa Israeli uwe mchango wao, na amepewa Haruni kuhani na wanawe kuwa mgao wao wa kawaida.

35Huu ndiyo mgao wa Haruni na uzao wake utokanao na matoleo yaliyofanywa kwa Yahwe kwa moto, siku ile Musa alipowaweka wakfu ili kumtumikia Yahwe katika kazi ya kuhani.36Huu ndio mgao ambao Yahwe aliamru waweze kupewa kutoka kwa watu wa Israeli, katika siku hiyo aliyowatia mafuta ya upako wawe makuhani. Nao utakuwa mgao wao wa kila siku katika vizazi vyote.

37Hii ndiyo sheria ya sadaka ya kuteketezwa, ya sadaka ya nafaka, ya sadaka ya dhambi, ya sadaka ya hatia, ya sadaka ya kuweka wakfu, na ya dhabihu, ya sadaka za amani,38ni sheria ambazo Yahwe alizitoa kwa Musa kwenye Mlima Sinai siku aliyo waamru watu wa Israeli kutoa dhabihu zao kwa Yahweh katika jangwa la Sinai.’”

8

1Yahwe akazungumza na Musa, akisema,2“Walete Haruni na wanawe pamoja naye, mavazi na mafuta ya upako, fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, kondoo dume wawili, na kikapu cha mkate usio na hamira.3Ita kusanyiko lote kwenye ingilio la hema la kukutania.”4Kwa hiyo Musa akafanya kama Yahwe alivyo mwamuru, nalo kusanyiko lilikuja pamoja mbele ya ingilio la hema la kukutania. Kisha Musa akaliambia kusanyiko,

5“Hivi ndivyo alivyotuamuru Yahwe tutende.”6Musa akamleta Haruni na wanawe na kuwaosha kwa maji.7Akamvika Haruni kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini na kumfunga ukumbuu kiunoni mwake, akamvika joho la nje lenye mikono mirefu na kumvika kile kizibao chenye vipande viwili tumboni na mgongoni na kukifunga kuzunguka kiunoni mwake kwa mshipi uliosokotwa kwa ustadi na kukikaza mwilini mwake.8Kisha Musa akaweka kifuko kifuani mwa Haruni, na ndani ya kifuko hicho akaweka Urimu na Thumimu.9Na kisha akamfunga kilemba kichwani, na juu ya kilemba kwa mbele, akaweka bamba la dhahabu; liwe taji takatifu, kama Yahwe alivyo mwamuru yeye.

10Musa akayatwaa hayo mafuta ya upako, akalipaka lile hema la kukutania na kila kitu kilichokuwamo ndani yake na kuvitenga kwa ajili ya Yahweh.11Akayanyunyiza hayo mafuta juu ya madhabahu mara saba, na kisha akaipaka mafuta hiyo madhabahu na vyombo vyake vyote, na sinia la kunawia na kitako chake ili kuvitenga wa ajili ya Yahwe.12Akamimina sehemu ya mafuta ya upako juu ya kichwa cha Haruni na kisha akampaka mafuta ili kumtenga.13Musa akawaleta wana wa Haruni na kuwavika kila mmoja kanzu ya ndani yenye urefu wa kufika magotini. Kila mmoja wao akamfunga kwa ukumbuu kiunoni mwake na kuwafunga vitambaa vya kitani kichwani pao, kama vile Yahweh alivyokuwa amemwamuru Musa.

14Musa akamleta huyo fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha fahali ambaye wamemlete kwa ajili ya sadaka ya dhambi.15Musa akamchinja, na kisha akachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuiweka juu ya mpembe za madhabahu, akaitakasa hiyo madhabahu, na kuitenga kwa Mungu, ambapo kwa kufanya hivyo, aliisababisha madhabahu kuwa sehemu ya kufaa kwa kufanyia upatanisho.16Akachukua mafuta yote yaliyokuwa sehemu za ndani, kile kiwambo cha ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake, Musa akaichoma hiyo nyama yote juu ya madhabahu.17Lakini yule fahali, ngozi yake, nyama yake na kinyesi chake, akavichoma nje ya kambi, kama vile Yahwe alivyokuwa amemwamru yeye.

18Musa akamleta yule kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha huyo kondoo.19Musa akamchinja kondoo na kuinyunyizia damu yake kila upande wa madhabahu.20Naye akamkatakata kondoo vipande vipande na akakiteketeza kichwa chake pamoja na vile vipande na mafuta.21Akaziosha kwa maji zile sehemu za ndani pamoja na miguu na akamteketeza kondoo mzima juu ya madhabahu. Ilikuwa ni dhabihu ya kuteketezwa na ilitoa harufu ya kupendeza, sadaka iliyofanywa kwa Yahweh kwa moto kama vile Yahwe alivyokuwa amemwamuru Musa.

22Kisha Musa akamleta yule kondoo dume mwingine, kondoo wa kuwekwa wakfu, naye Haruni na wanawe wakaweka mikono yao juu ya kichwa cha kondoo.23Haruni akamchinja, naye Musa akachukua sehemu ya damu na kuiweka kwenye ncha ya sikio la Haruni la kulia, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye kidole kikubwa cha mguu wake wa kulia.24Akawaleta wana wa Haruni, naye akaweka sehemu ya damu ya kondoo yule kwenye ncha ya sikio lao la kulia, kwenye dole gumba lao cha mkono wa kulia na kwenye kidole chao kikubwa cha mguu wa kulia. Kisha Musa akainyunyiza damu ya huyo kila upande wa madhabahu25Naye akayatwaa yale mafuta, mafuta ya mkia, mafuta iliyokuwa sehemu za ndani, na mafuta yafunikayo ini, zile figo mbili pamoja na mafuta yake na paja la kulia.26Akachukua mkate mmoja kutoka kwenye kikapu cha mikate isiyo na hamira ambayo ilikuwa mbele za Yahweh, akatwaa mkate moja usio na hamira, na mkate mmoja ulioandaliwa kwa mafuta, na mkate mwembamba wa kaki na akaiweka juu ya mafuta na juu ya paja la kulia la kondoo.27Akaiweka yote mikononi mwa Haruni na katika mikono ya wanawe na kuitikisa mbele za Yahwe kuwa sadaka ya kutikiswa.28Kisha Musa akaichukua mikate hiyo kutoka mikononi mwao na kuiteketeza juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa. Zilikuwa ni sadaka ya kuwekwa wakfu na ilitoa harufu ya kupendeza. Ilikuwa sadaka iliyofanywa kwa Yahwe kwa moto.29Musa akakichukua kidari na kukitikisa kuwa sadaka ya kutikiswa kwa Yahwe. Ilikuwa ni mgao wa Musa wa kondoo wa kuwekewa mikono kwa makuhani, Kama vile Yahwe alivyokuwa amemwamuru yeye.

30Musa akatwaa sehemu ya mafuta ya upako na damu iliyokuwa juu ya madhabahu; naye akayanyunyiza haya juu ya nguo za Haruni, juu ya nguo zake mwenyewe na juu ya nguo za wana wa Haruni waliokua pamoja naye. Kwa njia hii alimtenga Haruni na nguo zake, na wanawe na nguo zao kwa ajili ya Yahwe.

31Kwa hiyo Musa akawambia Haruni na wanawe, “Ipikeni nyama mbele ya ingilio la hema la kukutania, na hapo mtaila pamoja na mkate ulio kwenye kikapu cha kuwekwa wakfu, kama ilivyo amriwa, kusema, ‘Haruni na wanawe wataila.’32Masalio yoyote ya nyama na mikate utayateketeza kwa moto.33Na hamtatoka kwenye ingilio la hema la kukutania kwa muda wa siku saba, hata zitakapotimia siku za kuwekwa mikono kwenu. Kwa kuwa kwa muda wa siku saba, Yahwe atawaweka wakfu.34Kilichotendeka siku hii— Yahwe ndiye amekiamuru kitendeke ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.35Mtakaa kwenye ingilio la hema la kukutania mchana na usiku siku saba, nanyi ishikeni amri ya Yahwe ili msije mkafa, kwa sababu hivi ndivyo ilivyoamriwa.

36Kwa hiyo Haruni na wanawe wakafanya mambo yote ambayo Yahwe alikuwa amewaamru kwa kinywa cha Musa.

9

1Katika siku ya nane, Musa akawaita Haruni na wanawe pamoja na wazee wa Israeli.2Akamwambia Haruni, “Twaa ndama dume kutoka kundini kwa ajili ya sadaka ya dhambi zako, na kondoo dume kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, wote wawili wasiwe na dosari, na uwatoe mbele za Yahwe.3Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Twaeni beberu kwa ajili ya sadaka ya dhambi na ndama na mwana-kondoo, hawa wawili wawe na umri wa mwaka mmoja na bila dosari, ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa;4pia twaeni fahali na kondoo dume kwa sadaka za amani ili kuwatoa mbele za Yahwe, na sadaka za nafaka iliyochanganywa na mafuta, kwa sababu leo Yahwe atajidhihirisha kwenu.

5Kwa hiyo wakaleta kwenye hema la kukutania vyote ambavyo Musa aliagiza, nalo kusanyiko lote la Israeli likakaribia na kusimama mbele za Yahwe.6Kisha Musa akasema, “Hivi ndivyo Yahwe amewaamuru nyinyi mfanye, ili kwamba utukufu wake uweze kuonekana kwenu.

7“Musa akamwambia Haruni, “Njoo karibu na Madhabahu na utoe sadaka yako ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, na kufanya upatanisho kwa ajili ya watu ili kufanya upatanisho kwa ajili yao kama vile ambavyo Yahwe amekwisha amuru.”

8Kwa hiyo Haruni akaikaribia madhabahu na akamchinja yule ndama kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo ilikuwa kwa ajili yake mwenyewe.9Nao wana wa Haruni wakamletea hiyo damu, naye akakichofya kidole chake kwenye damu na kuiweka kwenye pembe za madhabahu, kisha akaimwaga damu chini ya kitako cha madhabahu.10Hata hivyo, aliyateketeza hayo mafuta, figo, na mafuta yanayofunika ini juu ya madhabahu kuwa sadaka ya dhambi, kama vile Yahwe alivyokuwa amemwamuru Musa.11Na akaiteketeza hiyo nyama pamoja na ngozi nje ya kambi

12Haruni akaichinja sadaka ya kuteketezwa, nao wanawe wakampa hiyo damu, ambayo alinyunyuzia pande zote za madhabahu.13Kisha wakampa ile sadaka ya kuteketezwa, kipande kwa kipande, pamoja na kichwa, naye akaviteketeza juu ya madhabahu.14Akaziosha sehemu za ndani pamoja na miguu na kuziteketeza juu ya dhabihu ya kuteketezwa juu ya Madhabahu.

15Haruni akaleta dhabihu ya watu— mbuzi, kisha akamtoa kuwa dhabihu kwa ajili ya dhambi yao naye akamchinja, akaitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi, kama alivyofanya kwa yule mbuzi wa kwanza.

16Akaileta sadaka ya kuteketezwa na kuitoa kama Yahwe alivyokuwa ameamuru.17Akaileta sadaka ya nafaka; akakijaza kiganja chake nafaka na kuiteketeza juu ya madhabahu, pamoja na sadaka ya asubuhi ya kuteketezwa.

18Pia akamchinja fahali na yule kondoo dume, dhabihu kwa ajili ya sadaka ya amani, ambayo ilikuwa kwa ajili ya watu. Nao wana wa Haruni wakampa damu, ambayo alinyunyizia kila upande wa madhabahu.19Hata hivyo, waliyakata mafuta ya fahali na ya yule kondoo dume, mafuta ya kwenye mkia, mafuta yafunikayo sehemu za ndani, figo, na yale mafuta yaliyofunika mapafu.20Wakazichukua hizi sehemu zilizokatwa wakaziweka juu ya vidari, na kisha Haruni akateketeza mafuta juu ya madhabahu.21Naye Haruni akavitikisa vidari na paja la kulia kuwa sadaka ya kutikiswa mbele za Yahweh, kama vile Musa alivyokuwa ameamuru,

22Kisha Haruni akainua juu mikono yake mbele ya watu na kuwabariki, kisha akashuka chini kutoka mahali alipokuwa akitoa hiyo sadaka ya dhambi, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya amani.

23Musa na Haruni wakaingia ndani ya hema la kukutania, kisha wakatoka nje tena na kuwabariki watu, na utukufu wa Yahwe ukaonekana kwa watu wote.24Moto ukashuka kutoka kwa Yahwe na ukairamba sadaka ya kuteketezwa na mafuta yaliyokuwa juu ya madhabahu. Watu walipoona jambo hili, wakapiga kelele na kulala chini.

10

1Nadabu na Abihu, wana wa Haruni, wakachukua kila mtu kifukizo chake, akaweka moto ndani yake, na kisha uvumba. Kisha wakatoa moto usiokubalika mbele za Yahwe, moto ambao hawakuwa wameamuriwa wao kuutoa.2Kwa hiyo moto ukashuka chini mbele za Yahwe na kuwala, nao wakafa mbele za Yahwe.3Kisha Musa akamwambia Haruni, Hivi ndiyo Yahwe alivyokuwa akizunguzia aliposema, ‘Nitaufunua utakatifu wangu kwa wale wajao mbele zangu. Nami nitatukuzwa mbele za watu wote.’” Naye Haruni hakusema neno lolote.

4Musa akamwita Mishaeli na Elzafani, wana wa Uzieli mjomba wa Haruni, naye akamwambia, “Njoo huku na uwatoe ndugu zako nje ya kambi watoke mbele ya hema.”5Hivyo wakakaribia na kuwachukua wangali wamevaa kanzu zao za kikuhani, nao wakawapeleka nje ya kambi, kama Musa alivyokuwa ameelekeza. Kisha Musa akamwambia Haruni na wanawe wengine wawili, Eliezari na Ithamari,

6“Msiache wazi nywele za vichwa vyenu, wala msirarue nguo zenu, ili kwamba msije mkafa, na kwamba Yahwe asilikasirikie kusanyiko zima. Lakini waacheni jamaa zenu, nyumba yote ya Israeli waweze kufanya ibada za maombolezo kwa ajili ya hao ambao Yahwe amewaangamiza kwa moto.7Msiende nje kutoka kwenye ingilio la hema la kukutania, ama sivyo mtakufa, kwa kuwa mafuta ya Yahwe ya upako yako juu yenu.” Kwa hiyo wakatenda sawasawa na maelekezo ya Musa.

8Mungu akazungumza na Haruni, akisema,9“Msinywe mvinyo wala kinywaji kikali, wewe, au wanao wanaobaki pamoja nawe, ili kwamba mtakapoingia kwenye hema ya kukutania msije mkafa. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu,10ili kupambanua kati ya mambo matakatifu na mambo ya kawaida, na kati ya najisi na safi,11ili kwamba mweze kuwafundisha watu wa Israeli amri zote ambazo Yahwe ameziamru kwa kinywa cha Musa.

12Musa akazungumza na Haruni na wanawe wawili waliosalia; Eliazari na Ithamari, Twaeni sadaka ya nafaka inayobaki kutokana na sadaka ifanywayo kwa Yahwe kwa moto, nanyi ileni kando ya madhabahu bila hamira, kwa kuwa ni takatifu sana.13Lazima mtaila mahali patakatifu kwa sababu huo ni mgao wako wewe na mgao wa wanao wa matoleo yaliyofanywa kwa Yahwe kwa moto, kwa kuwa hivi ndivyo limeamuriwa niwaambie.14Kile kidari kitikiswacho na lile paja ambalo hutolewa kwa Yahwe, yapasa mzile mahali palipo safi panapokubalika kwa Mungu. Wewe mwenyewe, wanao na binti zako walio pamoja nawe mtakula sehemu hizo, kwa kuwa zimetolewa kuwa mgao wako na mgao wa wanao kutokana na dhabihu ya sadaka ya ushirika wa watu wa Israeli.15Lile paja lililotolewa na kidari kilichotikiswa, ni lazima ziletwe pamoja na sadaka ya mafuta iliyofanywa kwa moto, ili kutikiswa mbele za Yahweh. Nazo zitakuwa zako wewe na wanao kuwa mgao wenu daima, kama Yahwe alivyoamru.

16Kisha Musa akauliza kuhusu yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, naye akagundua kwamba alikuwa ameteketezwa kwa moto. Kwa hiyo akawakasirikia Eliazari na Ithamari, wana wa Haruni waliosalia; akawaambia,17“Kwa nini hamjaila sadaka ya dhambi katika eneo la hema, kwa kuwa ni takatifu sana, na kwa kuwa Yahwe ameshaitoa kwenu ili kuchukua uovu wa kusanyiko, ili kufanya upatanisho kwa aijli yao mbele zake?18Tazama, damu yake haikuletwa ndani ya hema, kwa hiyo iliwapasa kwa hakika kuwa mekwisha ila kwenye eneo la hema, kama nilivyoagiza?

19Kisha Haruni akamjibu Musa, “Tazama, leo walitoa sadaka yao ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa mbele za Yahwe, na jambo hili vile vile limetendeka kwangu leo. Ikiwa nimeshakula sadaka ya dhambi leo, Je! Isingekuwa imeshapendeza mbele za Yahwe?”20Naye Musa aliposikia hivyo, akaridhika.

11

1Yahwe akazungumza na Musa na Haruni, akasema,2“Zungumzeni na watu wa Israeli muwaambie, ‘Hivi ndivyo viumbe vyenye uhai ambavyo mwaweza kula miongoni mwa wanyama walioko juu ya nchi.3Mnaweza kula mnyama yeyote aliye na kwato zenye kugawanyika na ambaye pia hucheua.

4Hata hivyo, kuna baadhi ya wanyama ambao ama hawacheui au hawana kwato zilizogawanyika, nanyi msiwale hao, wanyama kama ngamia, kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika. Kwa hiyo ngamia ni najisi kwenu.5Pimbi pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyo pia ni najisi kwenu.6Na sungura pia: kwa sababu yeye hucheua lakini hana kwato zilizogawanyika mara mbili, huyu naye ni najisi kwenu.7Na nguruwe pia: ingawaje yeye anazo kwato zilizogawanyika lakini hacheui, kwa hiyo yeye ni najisi kwenu.8Msile aina yoyote ya nyama yao, wala msiiguse mizoga yao. Hao ni najisi kwenu.

9Nao wanyama waishio majini mnaoweza kuwala na wale wote walio na mapezi na magamba, iwe waliomo baharini au mitoni.10Lakini viumbe wote hai wasio na mapezi na magamba waliomo baharini au mitoni, pamoja na wale waendao majini na viumbe hai waliomo majini —watakuwa chukizo kwenu.11Kwa kuwa watakuwa chukizo, msile nyama yao, pia mizoga yao sharti itakuwa chukizo.12Chochote kisichokuwa na mapezi au magamba kilichomo majini ni lazima kiwe chukizo kwenu.

13Nao ndege mtakaowachukia na msiopaswa kuwala ni hawa wafuatao: tai, furukombe, kipungu,14mwewe mwekundu, aina yoyote ya kipanga,15kila aina ya kunguru,16kiruka-njia, kipasua sanda, Shakwe, na aina yoyote ya mwewe.17Ni lazima pia bundi mdogo na bundi mkubwa muwaone kuwa chukizo, mnandi,18bundi mweupe na mwari,19korongo na aina zote za koikoi, huduhudi na popo pia.

20Wadudu wote wenye mabawa wanatembea kwa miguu minne kwenu ni machukizo.21Lakini mnaweza kula wadudu wenye mabawa wanaotembea kwa miguu minne ya kurukia ardhini yenye vifundo.22Na manaweza kula aina zote za nzige, senene, parare, au panzi.23Lakini wadudu wote warukao wenye miguu minne ni chukizo kwenu.

24Nanyi mtakuwa najisi hata jioni kutokana na wanyama hawa endapo mtagusa mizogo yao.25Na yeyote atakayeokota mojawapo wa mizoga yao ni lazima atazifua nguo zake naye atakuwa najisi hata jioni.

26Mnyama yeyote ambaye anazo kwato zilioachana ambazo hazikugawanyika kabisa au hacheui huyo ni najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa najisi.27Mnyama yeyote anayetembea kwa vitanga vyake miongoni mwa wanyama waendao kwa miguu yote minne ni najisi kwenu. Yeyote agusaye mzoga kama huo atakuwa najisi hata jioni.28Na yeyote aokotaye mzoga kama huo ni lazima atazifua nguo zake na kuwa najisi hata jioni. Wanyama hawa watakuwa najisi kwenu.

29Kuhusiana na wanyama watambaao juu ya ardhi, hawa ndiyo walio najisi kwenu: kicheche, panya, aina zote za mijusi mikubwa, guruguru,30kenge, mijusi ya ukutani, goromoe, na kinyonga.31Wanyama hawa wote ambao hutambaa, hawa ndiyo watakua najisi kwenu. Yeyote awagusaye atakuwa najisi hata jioni.32Na iwapo mmoja wao anakufa na kuanguka juu ya chombo, chombo hicho kitakuwa najisi, ama kiwe kimetengenezwa kwa mbao, nguo, ngozi, au gunia. Kiwe chombo cha namna gani na kiwe kwa matumizi gani, ni lazima kitalowekwa katika maji nacho kitakuwa najisi hata jioni. Kisha kitakuwa safi.33Kwa hiyo kila chungu ambacho mnyama najisi atakiangukia juu yake au ndani yake, chochote kilichomo kwenye chungu hicho kitakuwa najisi, na ni lazima mtakivunja chungu hicho.34Vyakula vyote ambavyo ni safi na vilivyokusudiwa kuliwa, lakini vikaingiwa na maji kutoka kwenye chungu najisi kilichoanguka, nacho kitakuwa najisi.35Na kitu chochote kinachoweza kunywewa kutoka kwenye chungu kama hicho kitakuwa najisi. Kila kitu kitakachoangukiwa juu yake na kipande cha mzoga wa mnyama najisi nacho kitakuwa najisi, ama liwe ni jiko au vyungu vya kupikia. Ni najisi na ni lazima kiwe najisi kwenu.36Chemichemi au kisima cha maji ya kunywa yanapokusanyika patabaki kuwa safi, iwapo kiumbe najisi kama hicho kitaangukia humo. Lakini ikiwa yeyote anaugusa mzoga wa mnyama aliye najisi uliomo ndani ya maji, yeye atakuwa najisi.37Iwapo sehemu yoyote ya mzoga wa mnyama aliye najisi inaangukia juu ya mbegu zozote zilizo kwa ajili ya kupanda. Mbegu hizo zitakuwa bado zingali safi.38Lakini kama maji yanawekwa juu ya mbegu, na kama sehemu ya mzoga unaangukia juu yake, nazo zitakuwa najisi kwenu.

39Iwapo mnyama yeyote awezaye kuliwa anakufa, naye yeyote amgusaye atakuwa najisi hata jioni.40Na yeyote alaye chochote cha mzoga huo atalazimika kufua nguo zake naye atakuwa najisi hata jioni. Na yeyote aokotaye mzoga kama huo atafua nguo zake na kuwa najisi hata jioni.

41Kila mnyama atambaaye juu ya ardhi atakuwa chukizo; hatakuwa wa kuliwa.42Chochote kitambaacho kwa kujivuta juu ya tumbo lake, na chochote kitembeacho kwa miguu yake yote minne, au chochote kilicho na miguu mingi—wanyama wote ambao hutambaa juu ya nchi, hawa msiwale, kwa sababu watakuwa machukizo.43Msijinajisi wenyewe kwa kiumbe chochote najisi kitaambacho; msijinajisi wenyewe kwavyo, ili kwamba msije mkachafuliwa navyo.44Kwa kuwa Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu. Nanyi lazima muwe watakatifu, kwa hiyo na iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu. Haiwapasi kujichafua kwa aina yoyote ya kiendacho juu ya nchi.45Kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh, aliyewaleta ninyi kutoka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Kwa hiyo lazima muwe watakatifu, kwa kuwa Mimi ni mtakatifu.

46Hii ndiyo sheria kuhusu wanyama, ndege, kila kiumbe hai kiendacho majini, na ya kila kiumbe kitambaacho juu ya nchi,47kwa ajili ya kile kinachopaswa kutofautishwa kati ya kilicho najisi na kilicho safi, na kati ya vitu vilivyokufa na vilivyo hai ambavyo vyaweza kuliwa na vitu vyenye uhai visivyoweza kuliwa.”

12

1Yahwe akamwambia Musa,2“zungumza na watu wa Israeli, uwaambie, ‘endapo mwanamke anakuwa mjamzito na kujifungua mtoto wa kiume, naye atakuwa najisi kwa muda wa siku saba, ni kama tu vile anavyokuwa najisi katika siku za kipindi chake kwa mwezi.3Katika siku ya nane nyama ya govi la mtoto mvulana itatahiriwa.4Kisha utakaso wa mama wa kutokwa damu yake utaendelea kwa muda wa siku tatu. Haimpasi kugusa kitu chochote kilicho kitakatifu au kukaribia eneo la hema mpaka zitakapomalizika siku za kutakaswa kwake.5Lakini kama atajifungua mtoto wa kike, naye atakuwa najisi kwa muda wa majuma mawili, kama alivyo wakati wa kipindi chake. Kisha utakaso wa mama utaendelea kwa siku sitini na sita.

6Siku za kutakaswa kwake zitakapoisha, kwa ajili ya mwana au binti, atalazimika kuleta kwa kuhani mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na kinda la njiwa au huwa kuwa sadaka ya dhambi, mbele ya ingilio la hema la kukutania,7Kisha atawatoa mbele za Yahwe na kufanya sadaka ya upatanisho kwa ajili yake, naye atatakaswa kutokana kutiririka kwa damu yake. Hii ndiyo sheria kuhusu mwanamke ajifunguaye mtoto wa kiume au wa kike.8Na kama hana uwezo wa kutoa mwana-kondoo, naye ataleta makinda mawili wa njiwa ua hua, mmoja kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na mwingine kuwa sadaka ya dhambi, naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake; naye atakuwa safi.”

13

1Yahwe akazungumza na Musa na Haruni, akasema,2Mtu yeyote anayeonekana na uvimbe au upele au doa ling'aalo juu ya ngozi ya mwili wake, na likawa limeambukizwa ugonjwa wa ngozi mwilini mwake, ni lazima aletwe kwa Haruni kuhani mkuu au kwa mmoja wa wanawe makuhani.3Naye kuhani atachunguza ugonjwa huo kwenye ngozi ya mwili wake. Iwapo malaika zilizopo eneo lenye ugonjwa zimegeuka kuwa nyeupe, na iwapo ugonjwa umejitokeza juu ya ngozi, huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Baada ya kuhani kumchunguza, atamtangaza kuwa ni najisi.4Iwapo lile doa ling'aalo katika ngozi yake ni jeupe, na kuonekana kwake halikwenda chini zaidi ya ngozi, na iwapo malaika za eneo lenye ugonjwa hazijabadilika kuwa nyeupe, naye kuhani atamtenga mgonjwa kwa siku saba.5Katika siku ya saba, huyo kuhani itambidi kumchunguza tena ili kuona kama katika maamuzi yake huo ugonjwa siyo mbaya, na kama haujaenea kwenye ngozi. Iwapo haujaenea, basi, kuhani atamtenga kwa siku saba zaidi.6Naye kuhani atamchunga tena katika siku ya saba ili kuona kama ugonjwa umepona na haujasambaa zaidi kwenye ngozi. Kama haujasambaa, basi, kuhani atamtangaza kuwa yeye ni safi. Ni upele tu. Naye atafua nguo zake, na kisha yeye yu safi.7Lakini endapo ule upele utakuwa umeshasambaa kwenye ngozi baada ya kuwa amejionyesha kwa kuhani kwa ajili kusafishwa kwake, itambidi kujionyesha tena kwa kuhani.8Naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo upele umesambaa zaidi ndani ya ngozi. Na endapo utakuwa umesambaa, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.

9Iwapo ugonjwa wa ngozi wa kuambukiza umo kwa mtu fulani, naye mtu huyo yapasa aletwe kwa kuhani.10Kuhani atamchunguza ili kuona kama kuna uvimbe mweupe katika ngozi yake, endapo malaika zitakuwa zimebadilika kuwa nyeupe, au kumekuwa na nyama mbichi kwenye uvimbe.11Kama ipo, basi, huo ni ugonjwa sugu wa ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Hatamtenga kwa kuwa yeye tayari ni najisi.

12Iwapo huo ugonjwa unajitokeza na kupanuka zaidi kwenye ngozi, na kuifunika ngozi ya mtu kwa ugonjwa tangu kichwani pake hata miguuni, maadamu anajitokeza kwa kuhani,13naye kuhani atamchunguza ili kuona kama huo ugonjwa umeshaenea mwili wake wote. Ikiwa imetokea hivyo, kuhani atamtangaza mtu huyo aliye na ugonjwa kuwa ni safi. Ikiwa amebadilika kuwa mweupe, huyo ni safi.14Lakini ikiwa nyama mbichi imeonekana juu yake, atakuwa najisi.15Kuhani ataiangalia hiyo nyama mbichi na kumtangaza kuwa najisi kwa sababu hiyo nyama mbichi ni najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.16Lakini endapo hiyo nyama mbichi inageuka kuwa nyeupe tena, naye huyo mtu hana budi kwenda kwa kuhani.17Kuhani atamchunguza ili kuona kama hiyo nyama imebadilika kuwa nyeupe. Kama imekuwa hivyo naye kuhani atatangaza kwamba mtu huyo kuwa ni msafi.

18Mtu anapokuwa na jipu juu ya ngozi yake na limeshapona,19na mahali pa jipu pamekuwa na uvimbe au doa lenye kung'aa, wekundu unaochanganyikana na weupe, yapasa kuonyeshwa kwa kuhani.20Naye kuhani atalichunguza ili kuona kama linaonekana limekwenda chini ya ngozi, na kama hizo malaika zimebadilika kuwa nyeupe, kama ni hivyo, kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza, endapo utakuwa umezalishwa mahali lilipokuwa jipu hilo.21Lakini endapo kuhani atakuwa amelichunguza na haoni malaika nyeupe ndani yake, na kwamba haliko chini ya ngozi bali limefifia, kisha kuhani atamtenga kwa siku saba.22Kama linaenea kwa kupanuka kwenye ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.23Lakini kama hilo doa lenye kung'ara linabaki mahali pake na halijasambaa, basi hilo ni kovu la jipu, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.

24Ngozi inapougua na nyama mbichi inapokuwa na wekundu uliochanganyika na weupe au doa jeupe,25kisha kuhani ataichunguza kuona kama malaika zilizoko kwenye doa hilo zimebadilika na kuwa nyeupe, na kama limeonekana kwenda chini zaidi ya ngozi, kama limekuwa hivyo, basi huo ni ugonjwa wa kuambukiza. Umejitokeza kwenye jeraha la moto, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugonjwa wa kuambukiza.26Lakini endapo kuhani analichunguza na anaona kwamba hakuna malaika nyeupe kwenye doa, na kwamba halikuenda chini ya ngozi bali linafifia, basi, kuhani atamtenga mtu huyo kwa siku saba.27Kisha yapasa kuhani kumchunguza tena katika siku ya saba. Iwapo litakuwa limesambaa kwa upana kwenye ngozi, naye kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni ugojwa wa kuambukiza.28Iwapo hilo doa litasalia mahali pake na halitakuwa limesambaa kwenye ngozi bali limefifia, ni uvimbe tu kutokana na kuungua moto, naye kuhani atamtangaza kuwa safi, kwa kuwa siyo zaidi ya jeraha la kuungua.

29Iwapo mwanaume au mwanamke ana ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni pake,30kisha kuhani atamchunguza mtu huyo kwa ajili ya ugonjwa wa kuambukiza ili kuona kama unakwenda ndani zaidi ya ngozi, na kama kuna nywele za manjano, nyembamba ndani yake. Endapo zinaonekana, kisha kuhani atamtangaza kuwa najisi. Huo ni mwasho, ugonjwa wa kuambukiza kichwani au kidevuni.31Iwapo kuhani anachunguza ugonjwa wa mwasho na anagundua kuwa hauko chini ya ngozi, na kama hakuna nywele nyeusi ndani yake, kisha kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.32Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena huo ugonjwa ili kuona kama umesambaa. Endapo hakuna malaika za manjano, na iwapo ugonjwa uko kwenye ngozi tu,33Basi, yampasa mtu huyo kunyolewa. Lakini sehemu yenye ugonjwa haitanyolewa, naye kuhani atamtenga mtu huyo mwenye ugonjwa wa mwasho kwa siku saba.34Katika siku ya saba kuhani atauchunguza tena ugonjwa ili kuona kama umemuacha kusambaa ndani ya ngozi. Iwapo unaonekana kuwa haukwenda chini zaidi ya ngozi, kisha kuhani atamtangaza kuwa safi. Mtu huyo yapasa kufua nguo zake, na kisha atakuwa safi.35Lakini ikiwa ugonjwa wa mwasho umeenea kwa sehemu kubwa kwenye ngozi baada ya kuhani kutangaza kuwa alikuwa safi,36naye kuhani itabidi amchunguze tena. Iwapo ugonjwa utakuwa umesambaa katika ngozi, kuhani hahitajiki kutafuta nywele za manjano. Mtu huyo ni najisi.37Lakini iwapo katika mtazamo wa kuhani inaonekana kuwa huo ugonjwa wa mwasho umekoma kusambaa, basi huo ugonjwa umekwisha pona. Yeye ni safi, naye kuhani atamtangaza kuwa safi.

38Iwapo mwanaume au mwanamke ana madoa juu ya ngozi,39kisha kuhani atamchunguza mtu huyo ili kuona kama hayo madoa ni meupe kwa kufiifia, ambalo ni kovu tu lililojitokeza kwenye ngozi. Yeye yu safi.

40Iwapo nywele za mtu zimenyonyoka kichwani, yeye ni kipara lakini yu safi.41Na iwapo nywele zake zimenyonyoka upande wa mbele wa kichwa chake, na iwapo paji lake la uso lina kipara, yeye yu safi42Lakini endapo kuna kidonda chenye wekundu uliochanganyika na weupe, juu ya kipara chake au paji lake la uso, huo ni ugonjwa wa kuambukiza uliojitokeza.43Naye kuhani atamchunguza ili kuona iwapo uvimbe wa eneo linaugua juu ya upara wake au paji lake la uso lina wekundu uliochanganyika na weupe, kama kuonekana kwa ugonjwa wa kuambukiza kwenye ngozi.44Ikionekana hivyo, basi huyo ana ugonjwa wa kuambukiza naye ni najisi. Hakika kuhani atamtangaza kuwa najisi kwa sababu ya ugonjwa wake kichwani pake.

45Mtu aliye na ugojwa wa kuambukiza atavaa nguo zilizochanika, ni lazima nywele zake ziachwe wazi, na yampasa kufunika uso wake mpaka puani na kupiga kelele, ‘Najisi, najisi.’46Naye atakuwa najisi siku zote za ugonjwa wake wa kuambukiza. Kwa sababu anao ugonjwa unaosambaa, yapasa kuishi peke yake nje ya kambi.

47Kuna wakati fulani vazi la mtu hupata ukungu juu yake. Laweza kuwa vazi, ama la sufu au kitani,48au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi.49Iwapo sehemu iliyochafuliwa ina rangi ya kijani au nyekundu katika vazi, ngozi, kifaa kilichosukwa au kufumwa, basi huo ni ukungu unasambaa, ni lazima uonyeshwe kwa kuhani.50Yapasa kuhani akichunguze hicho kifaa kwa ajili ya ukungu; ni lazima akitenge kitu chochote kilicho na ukungu kwa siku saba.51Naye akauchunguza tena huo ukungu katika siku ya saba. Endapo utakuwa umesambaa katika kifaa hicho, basi ni wazi kwamba huo ni ukungu wenye kuangamiza, na hicho kifaa ni najisi.52Na mwenye kukimiliki atalazimika kukichoma na kukiteketeza kabisa hicho kifaa kilicho onekana na ukungu ndani yake, haijalishi kiwe ni kifaa cha aina gani, kwani huo ukungu unaweza kusababisha ugonjwa.

53Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa na kuona kwamba ukungu haujaenea kwenye vazi au chombo kilichosukwa au kusokotwa kutokana na sufu, kitani au ngozi,54basi atawaagiza wakisafishe hicho kifaa kilichopatikana na ukungu, naye yampasa kukitenga kwa siku saba zaidi.55Kisha kuhani atakichunguza tena hicho kifaa chenye ukungu baada ya kuwa kimesafishwa. Kama ukungu haukubadilika rangi yake, hata kama haukusambaa, kifaa hicho ni najisi. Yapasa kichomwe, haijalishi ni wapi ukungu huo utakuwa umekichafua.56Iwapo kuhani anakichunguza hicho kifaa, na kama ukungu umefifia baada ya kuwa umeoshwa, basi atakirarua kile kipande kilichochaufuliwa kutoka kwenye vazi au kutoka kwenye ngozi, au kutoka kwenye chombo kilichosukwa au kusokotwa.57Ikiwa ukungu unazidi kuonekana katika vazi, ama katika chombo kilichosukwa au kufumwa, au katika kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi, basi, ukungu utakuwa unasambaa. Kifaa chochote kilicho na ukungu ni lazima kichomwe.58Vazi au kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au ngozi au kitu chochote kilichotengenezwa kwa ngozi—iwapo unakisafisha kifaa nao ukungu ukawa umetoka, nacho kifaa lazima kisafishwe mara ya pili, kisha kitakuwa safi.

59Hii ndiyo sheria ihusuyo ukungu katika vazi la sufu au kitani, au kwenye kitu chochote kilichosukwa au kufumwa kutokana na sufu, au kitani, au kitu chochote kilichotengenewa kwa ngozi, ili kwamba muweze kuvitangaza kuwa safi au najisi.

14

1Yahwe alizungumza na Musa, akisema,2“Hii itakuwa sheria kwa ajili ya mtu aliyekufa kwenye siku ya utakaso. Lazima aletwe kwa kuhani.3Kuhani atakwenda nje ya kambi kumchunguza mtu kuona kama madhara ya ugonjwa wa ngozi yameponywa.4Ndipo kuhani ataamuru kwamba mtu mwenye kutakaswa lazima achukue ndege safi wawili, waliohai, mti wa mwerezi, kitani nyekundu na hisopo.5Kuhani atamwamuru kuua moja ya hao ndege juu ya maji safi yaliyo kwenye chungu cha udongo.6Ndipo kuhani atamchukua ndege aliyehai na mti wa mwerezi, na kitani nyekundu na hisopo, na vyote hivi, pamoja na ndege aliye hai atavichovya kwenye damu ya ndege aliyechinjiwa kwenye maji safi.7Ndipo kuhani atanyunyiza maji haya mara saba juu ya mtu anayetakaswa katika ugonjwa, na ndipo kuhani atamtangaza kuwa msafi. Ndipo kuhani atamwachia ndege aliyehai katika eneo wazi.

8Mtu aliyetakaswa atafua nguo zake, atanyoa nywele zake zote, ataoga kwa maji, na ndipo atakuwa safi. Baada ya hayo lazima aje kwenye kambi, lakini ataishi nje ya hema lake kwa siku saba.9Katika siku ya saba lazima anyoe nywele za kichwa chake, na lazima pia anyoe ndevu zake na nyusi. Lazima anyoe nywele zake zote, na lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji; ndipo atakuwa safi.

10Katika siku ya nane lazima achukue dume wa wana kondoo wawili wasio na lawama, mwana kondoo jike wa mwaka mmoja asiye na lawama, na tatu ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa mafuta kama sadaka ya nafaka, na kipimo kimoja cha mafuta.11Kuhani ambaye amemtakasa mtu atamsimamisha mtu ambaye aliyemtakasa, pamoja na vile vitu, mbele ya Yahwe mahali pa kuingilia kwenye hema ya mkutano.

12Kuhani atachukua mmoja wa wanakondoo dume na kumtoa kama sadaka ya hatia, pamoja na kipimo cha mafuta; atavitikisa kwa sadaka ya kutikiswa mbele ya Yahwe.13Lazima aue mwana kondoo dume mahali ambapo wanapochinjia sadaka ya dhambi na sadaka ya kuteketezwa, katika eneo la hema, sababu sadaka ya dhambi ni ya kuhani, kama afanyavyo sadaka ya hatia, kwa sababu ni takatifu zaidi.14Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu yule wa kutakaswa, katika dole gumba la kulia, katika dole la mguu wa kulia.15Ndipo kuhani atachukua mafuta kutoka chombo na kuyamimina katika kiganja cha mkono wake wa kushoto, na kuzamisha kidole chake katika mafuta hayo yaliyo kwenye mkono wa kushoto,16na kunyunyiza baadhi ya mafuta kwa kidole mara saba mbele za Yahwe.17Kuhani ataweka mafuta yaliyobaki kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la kulia la mtu wa kutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wa kulia, na katika dole kubwa la mguu wa kulia. Lazima aweke mafuta haya juu ya damu kutoka kwenye sadaka ya hatia.18Kama kwa mafuta yaliyosalia kwamba katika mkono wa kuhani, atayaweka juu ya kichwa cha mtu ambaye atakaswaye, na kuhani atafanya utakaso kwa ajili yake mbele za Yahwe.

19Ndipo kuhani atatoa sadaka ya dhambi na kufanya upatanisho kwa ajili yake atakaswaye kwa sababu ya kutokuwa safi kwake, na baadaye ataua sadaka ya kuchomwa.20Ndipo kuhani atatoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka juu ya madhabahu. Kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya mtu huyo, na ndipo atakuwa safi.

21Kwa namna hiyo, kama mtu ni maskini na hawezi kumudu matoleo haya, ndipo anaweza kuchukua kondoo mmoja dume kama sadaka ya hatia ya kutikiswa, kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe, na moja ya kumi ya efa ya unga safi uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka, na chombo cha mafuta,22pamoja na njiwa wawili au kinda mbili za njiwa, ambao anaweza kupata; ndege mmoja atakuwa sadaka ya dhambi na mwingine sadaka ya kuteketezwa.

23Katika siku ya nane lazima awalete kwa kuhani kwa ajili ya utakaso, pakuingilia katika hema ya mkutano, mbele ya Yahwe.24Kuhani atachukua mwana kondoo kwa ajili ya sadaka, na atachukua pamoja na kiasi cha mafuta ya mzeituni, na ataviinua juu kama anaviwasilisha kwa Yahwe.25Atamuua mwana kondoo kwa ajili ya sadaka ya hatia, na atachukua baadhi ya ya damu ya sadaka ya hatia na kuiweka juu ya ncha ya sikio la kulia la yule wakutakaswa, juu ya dole gumba la mkono wake wa kulia, na kwenye dole kubwa la mguu, wa kulia.26Ndipo kuhani atamimina baadhi ya mafuta katika kiganja cha mkono wake wa kushoto,27na atanyunyiza kwa kidole chake cha kulia baadhi ya mafuta ambayo yako kwenye mkono wa kushoto mara saba mbele za Yahwe.28Ndipo kuhani ataweka kiasi cha mafuta ambayo yako kwenye mkono wake kwenye ncha ya sikio la yule mtu wa kutakaswa, katika dole gumba lake la mkono wa kulia, na dole kubwa la mguu wa kulia, maeneo yale yale ambayo kaweka damu ya sadaka ya hatia.29Ataweka mafuta yaliyobaki yaliyo mkononi mwake juu ya yule wakutakaswa, kufanya upatanisho kwa ajili yake mbele za Yahwe.30Lazima atoe sadaka ya njiwa au makinda ya njiwa, yale ambayo mtu ameweza kupata -31moja kama ya sadaka ya dhambi na nyingine kama sadaka ya kuteketezwa, pamoja na sadaka ya nafaka. Ndipo kuhani atafanya upatanisho kwa ajili ya yule ambaye atatakaswa mbele za Yahwe.

32Hii ni sheria kwa ajili ya mtu kwake kuna athari za ugonjwa wa ngozi, ambaye hawezi kumudu kiwango cha sadaka kwa ajili ya utakaso wake.”

33Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,34“Wakati mtakuja katika nchi ya Kanaani ambayo nimewapa kama miliki, na kama naweka ukungu unaenea ndani ya nyumba katika nchi ya miliki yenu,35ndipo yeye ambaye anamiliki nyumba ile lazima aje na kumwambia kuhani. Lazima aseme ‘Inaonekana kwangu kuna kitu fulani kama ukungu ndani ya nyumba yangu.’36Ndipo kuhani ataamuru kwamba watoe vitu vyote ndani kabla hajaenda ndani kuona uthibitisho wa ukungu, kiasi kwamba hakuna ndani ya nyumba kitakachofanywa najisi. Baadaye kuhani lazima aende ndani kuona humo ndani.37Yeye lazima achunguze ukungu kuona kama umo katika kuta za nyumba, na kuona ikiwa kunaonekana ukijani au wekundu katika bonde za mwonekano wa kuta.38Kama nyumba inao ukungu, ndipo kuhani atatoka nje ya nyumba na kufunga mlango wa nyumba kwa siku saba.39Ndipo kuhani atarudi tena katika siku ya saba na kuichunguza kuona kama ukungu umeenea katika kuta za nyumba.40Kama hivyo, ndipo kuhani ataamuru kwamba wayaondoe mawe ambayo ukungu umepatikana na yatupwe katika sehemu najisi nje ya mji.41Yeye atataka kuta zote za ndani ya nyumba zikwanguliwe, na lazima achukue vitu vilivyo chafuliwa na hivyo vilivyo kwanguliwa nje ya mji na kuvitupa kwenye eneo lisilosafi.42Lazima wayachukue mawe mengine na kuyaweka katika sehemu ya mawe yaliyoondolewa, na lazima watumie udongo mpya kupigia lipu nyumba.

43Kama ukungu unakuja tena na unaingia katika nyumba ambayo mawe yameondolewa na kuta zimekwanguliwa na kupigwa lipu upya,44Ndipo kuhani lazima aje aingie ndani na kuchunguza nyumba kuona kama ukungu umeenea ndani ya nyumba. Kama hivyo, huo ni ukungu mbaya, na nyumba ni najisi.45Nyumba hiyo lazima iangushwe chini. Hayo mawe, mbao, na lipu yote ndani ya nyumba lazima vibebwe kupelekwa nje ya mji kwenye sehemu najisi.

46Kwa nyongeza, yeyote anaenda ndani ya nyumba wakati imefungwa atakuwa najisi mpaka jioni.47Na yeyote aliyelala ndani ya nyumba lazima afue nguo zake, na yeyote aliyekula ndani ya nyumba lazima afue nguo zake.

48Kama kuhani ataingia kuichunguza kuona ikiwa ukungu umeenea katika nyumba baada ya nyumba kupigwa lipu, ndipo, kama ukungu umetoweka, ataitangaza nyumba hiyo kuwa ni safi.49Ndipo kuhani lazima achukue ndege wawili kuitakasa nyumba, na mti wa mwelezi, na sufu nyekundu, na hisopo.50Atamuua ndege mmoja wapo katika maji masafi kwenye dumu la udongo.51Atachukua mti wa mwerezi, hisopo, sufu nyekundu na ndege aliyehai, na kuvichovya kwenye damu ya ndege aliyekufa, kwenye maji safi, na kunyunyizia nyumba mara saba.52Ataitakasa nyumba kwa damu ya ndege na maji safi, pamoja na ndege aliyehai, mti wa mwerezi, hisopo, na sufu nyekundu. Lakini atamwachia ndege aliye hai aende nje ya mji mashambani.53Kwa njia hii lazima afanye upatanisho kwa ajili ya nyumba, na itakuwa safi.

54Hii ni sheria kwa aina zote za athari ya ugonjwa wa ngozi na vitu vyote vinavyosababisha ugonjwa kama huo, na kwa ajili ya kuwashwa,55na kwa ukungu kwenye mavazi na nyumba,56kwa ajili ya uvimbe, kwa ajili ya vipele, madoa,57kutambua wakati wowote tatizo hili ni najisi au lini limetakaswa. Hii ni sheria kwa ajili ya athari za ugonjwa wa ukungu.

15

1Yahwe alizungumza na Musa na Haruni, akisema,2“Waambie watu wa Israeli, na sema kwao, ‘Wakati mtu yeyote kisonono kimemwathiri mwili wake unatoa ugiligili, anakuwa najisi.3Unajisi wake unatokana na athari ya kisonono. Iwe mwili wake unatoa ugiligili au umekoma, huo ni unajisi.”

4Kitanda chochote anachokilalia kitakuwa najisi, na kila kitu ambacho anakaa juu yake kitakuwa najisi.5Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na awe amenajisika mpaka jioni.6Yeyote anayekaa katika kitu chochote ambacho mtu ambaye ameathiriwa na kisonono alikaa, mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.

7Na yeyote anayegusa mwili wa ambaye ameathirika na kisonono lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na awe najisi hadi jioni.

8Kama mtu ambaye anaona majimaji kama hayo kwa mtu fulani ambaye ametakasika, ndipo mtu huyo lazima afue nguo zake na aoge kwenye maji, na atakuwa najisi hata jioni.

9Tandiko lolote ambalo ambaye anamajimaji ya kisonono atalikalia litakuwa najisi.10Yeyote anayegusa kitu chochote kilichokuwa chini ya mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni, na yeyote anayebeba vitu hivyo lazima afue nguo zake na aoge katika maji; atanajisika mpaka jioni.11Ambaye ana majimaji kama hayo akimgusa kabla ya kuosha kwa maji safi mikono yake, mtu aliyeguswa lazima afue nguo zake na aoge katika maji, na atakuwa najisi mpaka jioni.

12Chungu chochote cha udongo ambacho ambaye anamajimaji kama hayo akigusa lazima kivunjwe, na kila chombo cha mti lazima kioshwe na maji safi.

13Wakati mwenye kisonono anapotakaswa katika kisonono chake, ndipo lazima ahesabu kwa ajili yake siku saba kwa ajili ya kutakasika kwake; ndipo afue nguo na aoshe mwili wake kwenye maji yatiririkayo. Ndipo atakuwa safi.14Katika siku ya nane lazima achukue njiwa wawili au kinda mbili za njiwa na aje mbele za Yahwe pakuingilia kwenye hema ya mkutano; pale lazima atoe hao ndege kwa kuhani.15Lazima kuhani awatoe, moja kama sadaka ya dhambi na nyingine kama ya kuteketezwa, na kuhani lazima afanye upatanisho kwa ajili yake mbele za Yahwe kwa ajili ya kisonono chake.

16Kama mtu yeyote ametokwa na shahawa, ndipo lazima aoge mwili wake wote katika maji; atanajisika mpaka jioni.17Kila vazi au ngozi ambayo juu yake kuna shahawa lazima paoshwe kwa maji; itakuwa najisi mpaka jioni.18Na kama mwanamke na mwanaume watalala pamoja na kunakutokwa kwa shahawa kwenda kwa mwanamke, lazima wote wawili waoge katika maji; watakuwa najisi mpaka jioni.

19Mwanamke anapokuwa kwenye hedhi, ataendelea kunajisika kwa siku saba, na yeyote anayemgusa atakuwa najisi mpaka jioni.20Chochote anacholalia juu yake wakati wa hedhi kitakuwa najisi; kila kitu ambacho anakalia kitakuwa pia najisi.21Yeyote anayegusa kitanda chake lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.22Yeyote anayegusa chochote ambacho amekikalia lazima afue nguo zake na aoge kwa maji; mtu huyo anakuwa najisi mpaka jioni.23Iwe juu ya kitanda au kitu chochote juu ya popote atakapokaa, kama akikigusa, mtu huyo atakuwa najisi mpaka jioni.

24Kama mwanaume yeyote akilala naye, na unajisi wa mwanamke ukamgusa, atakuwa amejinajisi siku saba. Kila kitanda ambacho anakilalia mwanaume huyo kitanajisika.

25Kama mwanamke ametokwa damu kwa siku nyingi ambayo siyo kipindi cha hedhi yake, au ikitoka zaidi ya kipindi chake cha hedhi, wakati wote wa siku za kunajisika, atakuwa kama alikuwa kwenye siku zake za hedhi. Yeye ni najisi.26Kila kitanda anachokilalia wakati wote wa kutokwa damu itakuwa kwake sawa tu kama kitanda anacholalia wakati wa hedhi, na kila kitu ambacho anakalia kitakuwa najisi, kama tu unajisi wa hedhi yake.27Na yeyote anayegusa kitu kati ya vitu hivyo atakuwa najisi; lazima yeye afue nguo zake na aoge mwenyewe kwenye maji, na atakuwa amenajisika mpaka jioni.

28Lakini kama mwanamke ametakasika katika kutokwa na damu, ndipo atahesabu kwa ajili yake siku saba, baada ya hizo atakuwa safi.29Katika siku ya nane atachukua kwake njiwa wawili au kinda wawili wa njiwa na atawaleta kwa kuhani pakuingilia hema ya mkutano.30Huyo kuhani atatoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa, na atafanya upatanisho kwa ajili ya huyo mbele ya Yahwe kwa ajili unajisi wa mwanamke atokwaye damu.

31Hivi ndivyo lazima uwatenge watu wa Israeli katika unajisi wao, hivyo hawatakufa tokana na unajisi wao, kwa kuchafua hema langu, ambapo naishi kati yao.

32Huu ndio utaratibu kwa kila ambaye ana kisonono, kwa ajili kila mwanaume ambaye shahawa yake inatoka na inamfanya kuwa najisi,33kwa ajili ya mwanamke ambaye yuko katika kipindi cha hedhi, kwa ajili ya yeyote aliye na kisonono, awe mwanaume au mwanamke, na kwa ajili ya yeyote anayelala na mwanamke najisi.

16

1Yahwe alizungumza na Musa - hii ni baada vifo vya wana wawili wa Haruni, walipomkaribia Yahwe na ndipo wakafa.2Yahwe alimwambia Musa, “Ongea na Haruni kaka yako na umwambie hapana kuja tu wakati wowote katika patakatifu pa patakatifu ndani ya pazia, mbele ya kifuniko cha upatanisho kilicho juu ya sanduku. Akifanya hivyo, anakufa, kwa sababu naonekana katika wingu juu ya kifuniko cha upatanisho.

3Hivi ndivyo jinsi Haruni lazima aje katika patakatifu pa patakatifu. Yeye lazima aingie pamoja na ndama kama sadaka ya dhambi, na kondoo dume kama sadaka ya dhambi.4Ni lazima avae kanzu ya kitatani, na lazima avae ndani yake nguo ya kitani, na lazima avae mshipi wa kitani na kilemba cha kitani. Haya ni mavazi matakatifu. Lazima aoge mwili wake katika maji na avae mavazi haya.5Lazima achukue kwenye umati wa watu wa Israeli mbuzi wawili waume kama sadaka ya dhambi na kondoo dume moja ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa.

6Ndipo Haruni lazima alete ng'ombe kama sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwa ajili yake mwenyewe, kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na familia yake.7Ndipo lazima achukue mbuzi wawili na kuwaweka mbele ya Yahwe katika mlango wa kuingilia kwenye hema ya mkutano.8Ndipo Haruni lazima apige kura kwa ajili ya mbuzi hao wawili, kura moja kwa ajili ya Yahwe, na kura nyingine kwa ajili ya msingiziwa.9Ndipo Haruni lazima awasilishe mbuzi ambaye kura imeangukia kwa Yahwe, na kumtoa mbuzi huyo kama sadaka ya dhambi.10Lakini mbuzi ambaye kura ya usingiziwa imemwangukia lazima aletwe kwa Yahwe akiwa hai, kufanya upatanisho kwa kumwachia aende porini kama, mbuzi msingiziwa.

11Pia Haruni lazima alete ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya dhambi, ambayo itakuwa kwa ajili yake mwenyewe, lazima afanye upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na familia yake, hivyo lazima yeye amuue huyo ng'ombe kama sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe.12Haruni lazima achukue chetezo iliyojaa mkaa wa moto kutoka kwenye madhabahu mbele ya Yahwe, na mikono imejaa ubani mzuri, na kuleta vitu hivi ndani ya pazia.13Hapo lazima aweke ubani juu ya moto mbele za Yahwe ili kwamba wingu kutoka kwenye ubani liweze kufunika kifuniko cha agano la imani ya upatanisho. Yeye afanye hivyo ili kwamba asife.14Ndipo lazima achukue kiasi cha damu ya ng'ombe na kuinyunyiza kwa kidole chake mbele ya kifuniko cha upatanisho. Lazima anyunyize kiasi cha damu kwa kidole chake mara saba mbele ya kifuniko cha upatanisho.

15Ndipo lazima aue mbuzi kwa ajili ya sadaka ya dhambi ambayo ni kwa ajili ya watu na kuileta damu yake ndani kwenye pazi. Hapo lazima aifanyie damu kama alivyo fanya kwenye damu ya fahali: lazima ainyunyize juu ya kifuniko cha upatanisho na mbele ya kifunuko cha upatanisho.16Yeye lazima afanye upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu kwa sababu ya matendo ya unajisi ya watu wa Israeli, na kwa sababu ya uasi na dhambi zao zote. Yeye pia lazima afanye haya kwa ajili ya hema ya mkutano, ambapo Yahwe anaishi kati yao, katika uwepo wa matendo yao ya unajisi.17Hakuna mtu anayetakiwa kuwepo katika hema ya mkutano wakati Haruni anaingia kufanya upatanisho katika mahali patakatifu pa patakatifu, na mpaka atoke nje na amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya familia yake, na kwa ajili ya umati wa Israeli.

18Yeye lazima aende nje kwenye madhabahu hapo mbele za Yahwe na kufanya upatanisho kwa ajili ya hiyo, na lazima achukue kiasi cha damu ya mbuzi na kuiweka juu ya pembe za madhabahu yote kuzunguka.19Anatakiwa anyunyize kiasi cha damu juu yake kwa kidole chake mara saba kuitakasa na kuitenga maalum kwa Yahwe, mbali kutoka matendo ya unajisi wa watu wa Israeli.

20Atakapo maliza kupatanisha kwa ajili ya mahali patakatifu sana, hema la mkutano, na madhabahu, lazima amlete mbuzi aliyehai.21Haruni lazima aweke mikono yake yote juu ya kichwa cha mbuzi huyu aliyehai na akiri juu yake maovu yote ya watu wa Israeli, uasi wao wote, dhambi zao zote. Ndipo lazima aweke dhambi hizo juu ya kichwa cha mbuzi na amwachie katika uangalizi wa mtu aliye tayari kumwongoza mbuzi huyo porini.22Mbuzi lazima abebe juu yake mwenyewe uovu wote kwenda mahali pakiwa. Kule msituni, huyo mtu amwache mbuzi aende huru.

23Ndipo Haruni anapaswa kwenda tena humo kwenye hema ya mkutano na kuvua mavazi ya kitani ambayo amayavaa kabla hajaenda mahali patakatifu sana, na anatakiwa kuyaacha mavazi hayo pale.24Anapaswa aoshe mwili wake kwa maji mahali patakatifu, na avae nguo zake za kawaida; pia lazima atoke nje kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya wale watu, na kwa njia hii anafanya upatanisho kwa ajili yake mwenyewe na kwa ajili ya watu.25Lazima yeye achome mafuta ya sadaka ya dhambi juu ya madhabahu.

26Huyu mtu anayemwacha mbuzi msingiziwa aende huru anafua nguo zake na kuosha mwili wake katika maji; baada ya hayo, anaweza kurudi tena kambini.27Yule fahali kwa ajili ya sadaka ya dhambi na mbuzi kwa ajili ya sadaka za dhambi, ambaye damu yake ililetwa kufanya upatanisho katika mahali patakatifu, lazima ipelekwe nje ya kambi. Kule lazima wachome, ngozi zao, nyama yao na kinyesi chao.28Huyu anayechoma sehemu hizo lazima afue nguo zake na aoge mwili wake katika maji; baada ya hapo, anaweza kurudi tena kwenye kambi.

29Hii itakuwa sharti kwa ajili yenu kwamba katika mwezi wa saba, kwenye siku ya kumi ya mwezi, mtanyenyekea wenyewe na msifanye kazi, iwe mwenyeji wa kuzaliwa au mgeni anayeishi kati yenu.30Hii ni kwa sababu katika siku hii ya upatanisho utafanywa kwa ajili yenu, kuwatakasa ninyi kutoka dhambi zenu zote ili muwe safi mbele za Yahwe.31Hii ni maalum kwa Sabato ya kupumzika kwa ajili yenu, na lazima mnyenyekee wenyewe na msifanye kazi. Hili litakuwa sharti kati yenu.32Kuhani mkuu, ambaye atapakwa mafuta na kuwekwa wakfu kuwa kuhani mkuu katika nafasi ya baba yake, lazima afanye upatanisho huu na kuvaa mavazi ya kitani, hayo ni mavazi matakatifu.33Lazima afanye upatanisho kwa ajili ya mahali patakatifu sana; lazima afanye upatanisho kwa ajili ya hema ya mkutano na madhabahu, na lazima afanye upatanisho kwa ajili ya makuhani na kwa ajili ya kusanyiko la watu.34Hii daima itakuwa sharti kwa ajili yako, kufanya upatanisho kwa ajili ya watu wa Israeli kwa sababu ya dhambi zao zote, mara moja kwa kila mwaka.” Na ilikuwa ikifanyika kama Yahwe alivyo mwamuru Musa.

17

1Yahwe akamwambia Musa,2“Zungumza na Haruni na wanawe, na watu wote wa Israeli. Waambie mambo ambayo ameamru Yahwe:3Mtu yeyote wa Israeli anayeua fahali au mwana —kondoo au mbuzi kambini, au amuuaye nje ya kambi, ili kumtoa dhabihu—4kama hamleti katika ingilio la hema la kukutania ili kumtoa dhabihu kwa Yahwe mbele za hema lake la kukutania, mtu huyo ana hatia ya damu iliyomwagika. Amemwaga damu, na mtu huyo ni sharti akatiliwe mbali kutoka miongoni mwa watu wake.5Kusudi la amri hii ni kwamba watu wa Israeli wataleta dhabihu zao kwa Yahwe kwenye ingilio la hema la kukutania, watazileta kwa kuhani ziweze kutolewa kuwa matoleo ya shukrani kwa Yahweh, badala ya kutoa dhabihu hadharani katika shamba.6Kuhani atainyunyiza damu juu ya madhabahu ya Yahwe kwenye ingilio la hema la kukutania; atayachoma mafuta yake ili kutoa harufu ya kupendeza mbele za Yahwe.7Ni lazima watu wasitoe tena dhabihu zao kwa sanamu za mbuzi, ambazo kwazo hutenda kama makahaba. Hili litakuwa agizo la kudumu kwa ajili yao katika vizazi vya watu wao vyote.

8Ni lazima uwaambie, ‘Mtu yeyote wa Israeli, au Mgeni yeyote aishiye miongoni mwao, atowaye dhabihu9na asiilete kwenye ingilio la hema la kukutania ili kuitoa kwa Yahweh, mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali kutoka kwa watu wake.’

10Na Mtu yeyote wa Israeli, au yeyote wa Wageni anayeishi miongoni mwao, ambaye hunywa damu; nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.11Kwa kuwa uhai wa mnyama yeyote umo katika damu yake. Nimeitoa damu yake kwenu kufanya upatanisho juu ya madhabahu kwa ajili ya uhai wenu, kwa sababu ni damu ndiyo ifanyayo upatanisho, kwa kuwa ni damu ipatanishayo kwa ajili ya uhai12Kwa hiyo Niliwaambia Watu wa Israeli kwamba hayupo miongoni mwenu impasaye kula damu, wala yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu atakaye kula damu.

13Na yeyote miongoni mwa watu wa Israeli, au yeyote wa Wageni aishiye miongoni mwenu ni lazima aimwage damu ya mnyama na kuifukia hiyo damu kwa mavumbi.14Kwa kuwa uhai wa kila kiumbe umo katika damu yake. Ni kwa sababu hii niliwaambia watu wa Israeli, ni lazima msile damu ya kiumbe cho chote, kwa kuwa maisha ya kila kiumbe chenye uhai ni damu yake. Yeyote ailaye ni lazima akatiliwe mbali.

15Mtu yeyote alaye mnyama aliye kufa au ambaye ameraruliwa na wanyama pori, ama yule mtu ni mwenyeji wa kuzaliwa au ni mgeni aishiye miongoni mwenu, ni lazima atazifua nguo zake na kujiosha katika maji, naye atakuwa najisi hata jioni. Kisha atakuwa safi.16Lakini kama hazifui nguo zake au kuosha mwili wake, ni lazima aichukue hatia yake.”

18

1Yahwe akazungumza na Musa, akisema,2“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.3Msitende mambo ambayo watu wa Misri huyatenda, mahali mlikokuwa mkiishi awali. Na ni lazima msitende mambo yale wanayoyatenda watu wa Kanaani, nchi ambayo ninawapeleka nyinyi. Msifuate desturi zao.4Sheria zangu ndizo mtakazozitenda, na amri zangu ndizo mtakazozishika, kwa sababu Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.5Kwa hiyo ni lazima mzitunze hukumu zangu na sheria zangu. Ikiwa mtu amezitii, ataishi kwa sababu ya hizo. Mimi Ndimi Yahwe.

6Pasiwepo kwenu atakayelala na yeyote aliye na uhusiano wa karibu naye. Mimi ndimi Yahweh.

7Usimfedheheshe baba yako kwa kulala na mama yako. Yeye ni mama yako! Haikupasi kumfedhehesha yeye.

8Usilale na yeyote wa wake za baba yako; Usimfedheheshe namna hiyo baba yako.

9Usilale na yeyote aliye mmoja miongoni mwa dada zako, ama ni binti ya baba yako au ni binti ya mama yako, ama aliyelelewa nyumbani mwenu au mbali nawe. Usilale na dada zako.

10Usilale na binti ya mwanao, au binti ya binti yako. Hiyo ingekuwa aibu yako mwenyewe.

11Usilale na binti ya mke wa baba yako, aliyezaliwa kwa baba yako, yeye ni dada yako, na usilale naye.

12Usilale na dada ya baba yako. Yeye ni ndugu wa karibu kwa baba yako.

13Usilale na dada ya mama yako. Yeye ni ndugu wa mama yako.

14Usimfedheheshe ndugu wa baba yako kwa kulala na mke wake. Usimkaribie kwa kusudi hilo; yeye ni shangazi yako.

15Usilale na binti- mkwe wako, Yeye ni mke wa mwanao; usilale naye.

16Usilale na mke wa kaka yako; usije ukamfedhesha yeye katika njia hii.

17Usilale na mwanamke kisha na binti yake, au binti wa mwanawe au binti wa binti yake. Hao ni ndugu zake wa karibu, na kulala nao lingekuwa ni uovu.

18Usimwoe dada ya mke wako kuwa mke wako wa pili na kulala naye wakati bado mke wako wa kwanza angali hai.

19Usilale na mwanamke wakati wake wa hedhi.

20Yeye ni najisi kwa wakati huo. Usilale na mke wa jirani yako na kujichafua mwenyewe kwake katika njia hii.

21Msiwatoe watoto wenu ili kuwapitisha kwenye moto, ili kwamba muwatoe sadaka kwa Moleki, kwa sababu msije mkalinajisi jina la Mungu wenu. Mimi ndimi Yahwe.

22Usilale na mwanaume mwingine kama ulalavyo na mwanamke. Jambo hili lingekuwa uovu.

23Usilale na myama yeyote na kujitia unajisi kwake. Haimpasi mwanamke kufikiria kulala na mnyama yeyote. Huo ungekuwa upotovu.

24Msijichafue wenyewe katika njia hizi, kwa kuwa katika njia hizi mataifa yamechafuliwa, mataifa ambayo Nitayafukuza yatoke kwa ajili yenu.25Ni kwa sababu nchi imenajisiwa, hivyo niliiadhibu dhambi yao, nayo nchi ikawatapika wakazi wake26Kwa hiyo, yawapasa kuzishika amri zangu na maagizo yangu, na msifanye aina yoyote ya mambo haya ya machukizo, wala Mwisraeli mzaliwa au Mgeni aishie miongoni mwenu.27Kwa kuwa ni uovu huu ambao watu wametenda, wale ambao waliishi hapa kabla yenu, na sasa nchi imenajisiwa.28Kwa hiyo, muwe waangalifu ili kwamba nchi isiwatapike nyinyi baada ya kuwa mmeinajisi, kama ilivyowatapika wale watu waliokuwako kabla yenu.

29Yeyote anayefanya mambo haya ya kuchukiza, watu wafanyao mambo hayo ya kuchukiza lazima watakatiliwa mbali kutoka miongoni mwa watu wao.30Kwa hiyo inawapasa kuzishika amri zangu na wasitende mojawapo ya desturi hizi zenye kuchukiza ambazo zilitendwa hapo kabla yenu, ili msijinajisi wenyewe kwa hizo. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.

19

1Yahwe akazungumza na Musa, akisema.2Zungumza na kusanyiko lote la watu wa Israeli na uwaambie, ‘Ni lazima muwe watakatifu, kwa kuwa mimi Yahwe Mungu wenu ni mtakatifu.

3Kila mtu amstahi mama yake na baba yake. Na ni lazima muzishike Sabato zangu. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.

4Msizigeukie sanamu zisizo na thamani, wala kujitengenezea wenyewe miungu kutokana na chuma. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.

5Unapotoa dhabihu za sadaka ya ushirika kwa Yahweh, utatoa ili kupata kibali.6Ni sharti iliwe siku hiyo hiyo uliyoitoa, au siku inayofuata.7Kama kinabaki kitu cho chote hata siku ya tatu ni lazima kiteketezwe kwa moto. Kama kitaliwa katika siku ya tatu kitakuwa najisi. Hakitakubalika,8lakini kila akilaye ni lazima atachukua hatia yake kwa sababu amekivunjia heshima kilicho kitakatifu kwa Yahwe. Mtu huyo ni lazima akatiliwe mbali na watu wake.

9Unapovuna mavuno ya ardhi yako, usivune hata pembezo mwa shamba lako kabisa, wala hutakusanya mabaki ya mavuno yako yote.10Usikusanye kila zabibu kutoka katika mizabibu yako, wala usiziokote dhabibu zilizoanguka chini katika shamba la mizabibu. Ni lazima uziache kwa ajili ya masikini na kwa ajili ya wageni. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.

11Usiibe. Usiseme uongo. Msidanganyane.

12Usiape kwa jina langu kwa uongo na kulinajisi jina la Mungu wako. Mimi ndimi Yahwe.

13Usimgandamize jirani yako wala kumwibia. Usishikilie malipo ya kibarua usiku kucha hata asubuhi.

14Usimlaani kiziwi au kuweka kikwazo mbele ya kipofu. Badala yake, yakupasa umwogope Mungu wako. Mimi ndimi Yahwe.

15Usisababishe hukumu ikawa ya uongo. Usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni masikini na usionyeshe upendeleo kwa mtu fulani eti kwa kuwa tu yeye ni mtu muhimu. Badala yake, amua juu ya jirani yako kwa haki.

16Usiende huku na huko ukisema habari za uchochezi miongoni mwa watu wako, bali tafuta kuyalinda maisha ya jirani yako. Mimi ndimi Yahweh.

17Usimchukie ndugu yako moyoni mwako. Mkemee jirani yako kwa heshima ili kwamba usishiriki katika dhambi kwa sababu yake.

18Usijilipizie kisasi au kuwa na chuki yoyote dhidi ya mtu yeyote wa watu wako, lakini badala yake mpende jirani yako kama unavyojipenda wewe mwenyewe. Mimi ndimi Yahweh.

19Shika amri zangu. Usiwazalishe wanyama wako kwa kutumia wanyama wa aina nyingine tofauti. Usichanganye aina mbili tofauti za mbegu unapopanda shamba lako. Usivae vazi lililofumwa kwa kutumia nyuzi za rangi mbili tofauti zilizochanganywa pamoja.

20Yeyote anayelala na msichana mtumwa aliyeposwa na mume mwingine, lakini ambaye hajakombolewa au hajaachwa huru, lazima waadhibiwe. Hawatauawa kwa sababu yule msichana hakuwa huru.21Ni lazima mtu huyo alete sadaka yake ya hatia kwenye ingilio la hema la kukutania—kondoo dume iwe sadaka ya hatia.22Kisha kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa huyo kondoo dume mbele za Yahweh kutokana na dhambi aliyoitenda. Nayo dhambi iliyotendwa itasamehewa.

23Mtakapoingia katika nchi na kupanda aina zote za miti kwa chakula, kisha mtayahesabu matunda yatakayozaliwa kuwa yamekatazwa kuliwa. Tunda litakatazwa kwako kwa miaka mitatu. Halitaliwa.24Lakini katika mwaka wa nne matunda yote yatakuwa matakatiifu, matoleo ya sifa kwa Yahweh.25Katika mwaka wa tano unaweza kula tunda, ambalo umelisubiri ili kwamba mti uweze kuzaa zaidi. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.

26Usile nyama yoyote ambayo damu ingalimo ndani yake. Usiulize kwa roho juu ya wakati ujao,

27Usitafute kuwadhibiti wengine kwa njia ya nguvu za kichawi. Msifuate tabia za kipagani kama vile kunyoa denge au kunyoa pembe za ndevu zenu.

28Usiukate mwili wako kwa ajili ya wafu au kuchanja chale juu ya mwili wako. Mimi ndimi Yahwe.

29Usimwaibishe binti yako kwa kumfanya kahaba, la sivyo taifa litaangukia kwenye ukahaba na nchi itajawa na uovu.

30Utazitunza Sabato zangu na kupaheshimu mahali patakatifu pa hema langu la kukutania. Mimi ndimi Yahwe.

31Msiwageukie wale wanaoongea na wafu au roho wachafu. Msiwatafute, la sivyo watawanajisi ninyi, Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.

32Ni lazima usimame mbele za mtu mwenye mvi na uheshimu uwepo wa mzee. Yakupasa umwogope Mungu wako. Mimi ndimi Yahwe.

33Mgeni anapoishi miongoni mwenu katika nchi yenu, usimtendee lolote lililobaya.34Mgeni anayeishi pamoja nanyi ni lazima awe kama mwenyeji Mwisraeli mzaliwa anayeishi kwenu, na sharti umpende kama unavyojipenda wewe mwenyewe, ni kwa sababu wewe ulikuwa mgeni katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wako.

35Unapopima urefu, uzito, au wingi usitumie vipimo vya udanganyifu.36Tumia mizani iliyo halali, mawe ya kupimia uzito yaliyo halali, efa halali, hini iliyo halali. Mimi ndimi Yahwe Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya utumwa ya Misri.

37Utayatii maagizo yangu na sheria zangu zote na kuzitenda. Mimi ndimi Yahwe.

20

1Yahwe akazungumza na Musa, akasema,2“Waambie watu wa Waisraeli, ‘Mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe.3Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu.4Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake,5Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki.

6Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.

7Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.8Mtazitunza amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Yahwe anayewatenga ninyi muwe watakatifu.

9Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa.

10Mwanaume yeyote afanyaye uzinzi na mke wa mwanaume mwingine, yaani, yeyote anayezini na mke wa jirani yake—yule mwanaume mzinzi na mwanamke mzinzi ni lazima wote wawili wauawe.

11Mwanaume yeyote anayelala na mke wa baba yake ili kukutana naye kimwili amemfedhehesha baba yake mwenye. Wote wawili; mwana huyo na mke huyo wa baba yake kwa hakika watauawa. Wanahatia na wanastahili kufa.

12Kama mwanaume atalala na mke wa mwanawe, wote wawili; mwanaume huyo na mke huyo wa mwanawe hakika watauawa. Wametenda upotovu. Wana hatia na wanastahili kufa.

13Kama mwanaume analala na mwanaume mwingine kama alalavyo na mwanamke, wote wawili watakuwa wamefanya jambo lililo ovu. Hakika watauawa. Wana hatia na wanastahili kufa.

14Ikiwa mwanaume atamwoa mwanamke na pia akamwoa mama wa mwanamke huyo, huu ni uovu. Ni lazima wachomwe kwa moto, wote wawili, mwanaume huyo na mwanamke huyo, ili kwamba hapatakuwepo na uovu miongoni mwenu.

15Ikiwa mwanaume analala na mnyama, hakika atauawa, ni lazima mumuue na mnyama huyo pia.

16Ikiwa mwanamke anamkaribia mnyama ili kulala naye, ni lazima mmuue mwanamke huyo pamoja na huyo mnyama. Kwa hakika ni lazima wauawe. Wana hatia na wanastahili kufa.

17Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake.

18Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lazima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao.

19Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe.

20Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.

21Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote ambayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.

22Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.23Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao.24Nami nikawaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo maziwa na asali. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine.

25Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanyama najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi.26Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahwe, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu.

27Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.

21

1Yahwe akamwambia Musa, “Zungumza na makuhani, wana wa Haruni, nawe waambie, ‘Hakuna hata mmoja miongoni mwenu atakayejitia unajisi kwa wale wanaokufa miongoni mwa watu wake,2isipokuwa yule aliye ndugu wa karibu—mama yake, baba yake, mwanawe, bintiye, nduguye,3Au dada yake bikira anayemtegemea, kwa kuwa hana mume—kwake huyo anaweza kujitia unajisi.4Lakini hatajitia unajisi na kujichafua kwa ajili ya jamaa wengine.

5Makuhani hawatanyoa vichwa vyao wala kunyoa pembeni mwa ndevu zao, wala hawatachanja chale miili yao.6Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala hawataliaibisha jina la Mungu wao, kwa sababu makuhani hutoa sadaka ya Yahwe ya chakula, mkate wa Mungu wao. Kwa hiyo makuhani lazima wawe watakatifu.

7Hawataoa mwanamke aliye kahaba na aliyetiwa unajisi, na hawataoa mwanamke aliyetalikiwa kutoka kwa mume wake kwa sababu wametengwa kwa ajili ya Mungu wao.8Utamtenga kwa sababu yeye ndiye anayetoa mkate kwa Mungu wako. Ni lazima awe mtakatifu, kwa sababu—Mimi, Yahwe ndimi niwatakasaye nyinyi—pia Mimi mwenyewe ni mtakatifu.

9Binti yeyote wa kuhani anayejitia unajisi kwa kujifanya kahaba anajifedhehesha mwenyewe. Ni lazima ateketezwe kwa moto.

10Mtu ambaye ni kuhani mkuu miongoni mwa nduguze, ambaye mafuta ya upako yamekwisha kumiminwa kichwani pake, na ambaye amekwisha kuwekwa wakfu ili kuvaa mavazi maalum ya kuhani mkuu, kamwe hataziacha wazi nywele zake wala hatazirarua nguo zake.11Hataingia kamwe mahali popote ambapo kuna maiti na kujitia unajisi, hata kama ni maiti ya baba yake au ya mama yake.12Kuhani mkuu hataondoka eneo takatifu la hema la kukutania au kupatia unajisi patakatifu pa Mungu wake, kwa sababu amewekwa wakfu kuwa kuhani mkuu kwa kutiwa mafuta ya upako ya Mungu wake. Mimi ndimi Yahwe.

13Kuhani mkuu nilazima aoe bikira kuwa mke wake.14Hataoa mjane, mwanamke mtalaka au mwanamke aliye kahaba. Anaweza kuoa mwanamke bikira kutoka kwa watu wake,15kwa hiyo asiwatie unajisi watoto wake miongoni mwa watu wake. Kwa kuwa Mimi Yahwe, ndimi ninayemfanya yeye mtakatifu.”

16Yahwe akamwambia Musa, akasema,17Zungumza na Haruni na umwambie, ‘mtu yeyote wa ukoo wako katika vizazi vyako vyote mwenye kasoro mwilini mwake, asisogee kutoa chakula kwa Mungu wake.18Mtu yeyote mwenye kasoro mwilini mwake asimkaribie Yahwe,19Mtu kama vile: kipofu au mtu asiyeweza kutembea, mtu aliyeharibiwa uso au kupungukiwa na viungo mwilini, mtu aliye na mguu au mkono wenye ulemavu,20Mtu mwenye kibiongo mgongoni mwake au aliye na kimo kidogo au wembamba usio wa kawaida, au mtu mwenye kasoro machoni mwake, au mwenye ugonjwa, kidonda, upele, au yule ambaye korodani zake zimeharibiwa.21Hakutakuwa na mtu miongoni mwa ukoo wa Haruni kuhani mkuu mwenye kasoro mwilini atakayekaribia kutoa matoleo yatakayoteketezwa kwa moto kwa ajili ya Yahwe. Mtu kama huyo mwenye kasoro mwilini hatakaribia ili kutoa mkate wa Mungu wake.22Anaweza kula chakula cha Mungu wake, ama iwe baadhi ya vile vilivyo vitakatifu sana au vile vitakatifu.23Hata hivyo, hataingia ndani ya pazia wala kuisogelea madhabahu, kwa sababu ana kasoro mwilini mwake, ili kwamba asipanajisi mahali patakatifu pangu, kwa kuwa Mimi ndimi Yahwe anayewafanya watakatifu.”

24Kwa hiyo Musa akamwambia maneno haya Haruni, wanawe, na watu wote wa Israeli.

22

1Yahwe akazungumza na Musa, kusema,2“Ongea na Haruni na wanawe, waambie wajiepushe na vitu vitakatifu vya watu wa Israeli wanavyovitenga kwangu. Wasilinajisi jina langu. Mimi ndimi Yahwe.

3Waambie, ‘Ikiwa mmoja wa wazao wenu katika vizazi vyenu vyote anakaribia vitu vitakatiifu vile ambavyo watu wa Israeli wamevitenga kwa Yahwe, wakati akiwa najisi, sharti mtu huyo akatiliwe mbali atoke mbele zangu. Mimi ndimi Yahwe.

4Hatakuwapo yeyote wa uzao wa Haruni aliye na ungonjwa wa ngozi wa kuambukiza, au maambukizi yatirirkayo kutoka mwilini mwake, atakayekula sehemu yoyote ya dhabihu itolewayo kwa Yahwe mpaka atakapotakasika. Yeyote agusaye kitu chochote kilichonajisi kwa njia ya kugusa maiti, au kwa kumgusa mtu yeyote aliyetokwa na shahawa,5au yeyote agusaye mnyama atakayemtia unajisi, au mtu yeyote atakayemfanya najisi, kwa hiyo unajisi wowote unaweza kuwa—6kuhani yeyote agusaye kitu chochote kisichosafi atakuwa najisi hata jioni. Hatakula chochote cha vitu vitakatifu, isipokuwa ameuosha mwili wake katika maji.7Jua linapotua, ndipo atakuwa safi. Baada ya machweo anaweza kula kutoka katika vitu vitakatifu, kwa sababu hivyo ni vyakula vyake.8Asile mzoga wowote uliookotwa au mnyama aliyeraruliwa na wanyama pori, ambaye kwake atajitia unajisi. Mimi ndimi Yahwe.

9Ni lazima makuhani wafuate maagizo yangu, ama sivyo watakuwa na hatia ya dhambi na wangeweza kufa kwa kunitia unajisi. Mimi ndimi Yahwe ninayewafanya wao watakatifu.

10Hakuna mtu kutoka nje ya familia ya kuhani, wakiwemo wageni wa kuhani au watumwa wake wa kuajiriwa, atakayeweza kula kitu chochote kilicho kitakatifu.11Lakini kama huyo kuhani amenunua mtumwa kwa fedha yake mwenyewe, mtumwa huyo anaweza kula kutoka katika vitu vilivyotengwa kwa Yahwe. Na watu wa familia ya kuhani na watumwa waliozaliwa nyumbani mwake, pia wanaweza kula pamoja naye kutoka katika vitu hivyo.12Ikiwa binti wa kuhani ameolewa na mtu asiye kuhani, hataweza kula chochote cha mchango wa matoleo matakatifu.13Lakini ikiwa huyo binti wa kuhani ni mjane au ametalikiwa, na ikiwa hana mtoto, na anarudi kuishi nyumbani kwa baba yake kama alivyokuwa wakati wa ujana wake, anaweza kula kutoka katika chakula cha baba yake. Lakini hakuna yeyote asiye wa familia ya kikuhani atakayeruhusiwa kula kutoka katika chakula cha kuhani.

14Kama mtu anakula chakula kitakatifu bila ya kukijua, naye atamlipa kuhani kwa ajili ya hicho; itampasa kuongeza moja ya tano juu yake na kukirejesha kwa kuhani.15Haiwapasi watu wa Israeli kutoheshimu vitu vitakatifu ambavyo vimeinuliwa juu na kuletwa kwa Yahwe,16Kisha wakajisababishia wenyewe kuchukua dhambi ambayo ingewafanya kuwa na hatia ya kula chakula kitakatifu, kwa kuwa mimi ndimi Yahwe awafanyaye wao watakatifu.”

17Yahwe akazungumza na Musa, akasema,18“Sema na Haruni na wanawe, na kwa watu wa Israeli wote. Waambie, Mwisraeli yeyote, au Mgeni anayeishi katika Israeli, waletapo dhabihu—iwe ni kutimiza kiapo, au iwe ni sadaka ya hiari, au wanaleta kwa Yahweh sadaka ya kuteketezwa kwa moto,19Ikiwa wanataka ikubalike, ni lazima watoe mnyama dume asiye na dosari, kutoka kwenye kundi la ng'ombe, kondoo au mbuzi20Lakini hamtatoa chochote kilicho na dosari. Sitakipokea kwa niaba yenu.21Yeyote atoae dhabihu ya sadaka ya ushirika kutoka katika kundi la ng'ombe au la kondoo kwa Yahwe ili kutimiza kiapo, au kama sadaka ya hiari, ili ikubalike, ni lazima isiwe na kilema. Ni lazima pasiweko na kasoro katika mnyama.22Msitoe kabisa wanyama walio vipofu, walio jeruhiwa, wala walio na kilema, wenye upele, vidonda vitokavyo usaha, wala wenye vigaga. Msiwatoe hawa kuwa dhabihu ya kuteketezwa kwa moto iliyotolewa kwa Yahwe juu ya madhabahu.23Unaweza kumleta makisai au mwana-kondoo mlemavu au aliyedumaa kuwa sadaka ya hiari, lakini sadaka kama hiyo kwa ajili kutimiza kiapo, haitapokelewa.24Usitoe kwa Yahwe mnyama yeyote aliyetiwa jeraha, kupondwa, au kukatwa korodani zake.25Usifanye haya katika nchi yako. Usilete mkate wa Mungu wako kutoka mkononi mwa mgeni. Hao wanyama wenye vilema na dosari ndani yao, hawatapokelewa kabisa kwa ajili yako.

26Yahwe akamwambia Musa na akasema,27“Wakati ndama, mwana—kondo au mwana—mbuzi azaliwapo, sharti abaki na mama yake kwa muda wa siku saba. Ndipo kuanzia siku ya nane na kuendelea, anaweza kupokelewa kuwa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahwe.28Usimchinje ng'ombe jike pamoja na ndama wake au mbuzi jike pamoja na kitoto chake kwa siku moja.

29Utoapo sadaka ya shukrani kwa Yahwe utaitoa kwa njia iliyokubalika.30Ni lazima iliwe siku iyo hiyo inayotolewa. Hutakiwi kubakiza chochote hata asubuhi. Mimi ndimi Yahwe.

31Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Yahwe.32Msiliabishe jina langu takatifu. Ni lazima nitambuliwe kuwa ni mtakatifu na watu wa Israeli. Mimi ndimi Yahwe niwafanyaye ninyi watakatifu,33ambaye amewaleta kutoka katika nchi ya Misri ili niwe Mungu wenu: Mimi ndimi Yahwe.”

23

1Yahwe akamwambia Musa:2“Zungumza na watu wa Israeli, na uwaambie, ‘Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahwe, ambazo ni lazima mzitangaze kuwa makusanyiko matakatifu, ni sikukuu zangu za mara kwa mara.

3Mnaweza kufanya kazi kwa siku sita, lakini siku ya saba ni Sabato ya kupumzika kabisa. Usifanye kazi kwa sababu ni Sabato kwa ajili ya Yahwe mahali pote mnapoishi.

4Hizi ndizo sikukuu za Yahwe zilizoamriwa, Makusanyiko matakatifu mtakayoyatangaza kwa nyakati zilioamriwa:5Katika mwenzi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi kwenye mwanga hafifu wa machweo ya jua, ni Pasaka ya Yahwe.6Siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu ya mikate isiotiwa hamira kwa ajili ya Yahwe. Kwa muda wa siku saba mtakula mikate isiotiwa hamira.7Siku ya kwanza ni lazima mjitenge kwa pamoja, hamtafanya kazi ya kawaida.8Kwa siku saba mtamletea Yahwe matoleo ya chakula. Siku ya saba ni ya kusanyiko takatifu lililotengwa kwa ajili ya Yahwe, nanyi katika siku hiyo hamtafanya kazi yoyote ya kawaida.”

9Yahwe akamwambia Musa, akisema,10“Sema na watu wa Israeli uwaambie, ‘mtakapofika kwenye nchi nitakayowapa nyinyi, na mtakapovuna mazao yake, nanyi yawapasa kumletea kuhani fungu la masuke ya nafaka ya matunda yake ya kwanza.11Naye ataliinua hilo fungu la masuke ya nafaka mbele za Yahwe na kulileta kwake, kwa kuwa litakubalika kwa niaba yenu. Nalo litaletwa siku baada ya Sabato ili kwamba kuhani ataliinua na kulileta kwangu.12Siku ile mtakapoliinua lile fungu la masuke ya nafaka na kulileta kwangu, itawabidi kutoa mwana—kondoo dume wa mwaka mmoja na asiye na dosari awe sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe.13Matoleo ya nafaka yatakuwa sehemu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta, uwe matoleo yaliyofanywa kwa moto kwa Yahwe, ili kutoa harufu nzuri ya kupendeza, pamoja na hiyo kutakuwa na matoleo ya kinywaji ya divai, moja ya nne ya hini.14Hamtakula mkate, wala nafaka iliyokaangwa au nafaka mpya hata siku ile mliyoleta matoleo haya kwa Mungu wenu. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu, popote pale mnapoishi.

15Tangu siku iliyofuata baada ya Sabato—hiyo ilikuwa siku mlipolileta lile fungu la nafaka la matoleo ya kutikiswa—hesabuni majuma saba kamili.16Mtahesabu siku hamsini, ambazo zingekuwa siku baada ya Sabato ya saba. Kisha mtaleta matoleo ya nafaka mpya kwa Yahwe.17Mtaleta kutoka nyumbani mwenu mikate miwili iliyotengenezwa kutokana na mbili za kumi za efa. Ni lazima ifanywe kwa unga laini na uliochanganywa na hamira; zitakuwa matoleo ya kutikiswa ya malimbuko ya kwanza kwa Yahwe.18Mtaileta hiyo mikate pamoja na wana—kondoo saba wa mwaka mmoja na wasiokuwa na dosari, fahali mmoja mchanga na dume wa kondoo wawili. Watakuwa matoleo ya kuteketezwa kwa moto kwa Yahwe, pamoja na matoleo yao ya nafaka na matoleo ya kinywaji, matoleo yaliyofanywa kwa moto na kutoa harufu nzuri ya kupendeza kwa Yahwe.19Ni lazima mtoe mbuzi dume mmoja kwa ajili ya matoleo ya dhambi, na wana—kondoo dume wawili wa mwaka mmoja kwa ajili ya dhabihu, wawe matoleo ya ushirika.20Ni lazima kuhani azitikise pamoja na mkate wa malimbuko ya kwanza mbele za Yahwe na kuzileta kwake kuwa matoleo pamoja na kondoo dume wawili. Watakuwa sadaka takatifu kwa Yahwe kwa ajili ya kuhani.21Mtatoa tangazo siku iyo hiyo. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na hamtafanya kazi za kawaida. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vya watu wenu mahali pote mnapoishi.

22Mtakapovuna mazao ya nchi yenu, Msivune kabisa kabisa pembeni mwa mashamba yenu, wala msivune mazazo ya mavuno yenu. Inawapasa kuyaacha kwa ajili ya masikini na mgeni. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.”

23Yahwe akazungumza na Musa, akisema,24“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza itakuwa siku ya pumziko makini kwa ajili yenu, kumbukumbu pamoja na kupigwa kwa tarumbeta na kusanyiko takatifu,25Hamtafanya kazi ya kawaida, na ni lazima mtoe dhabihu inayofanywa kwa moto kwa Yahwe.”

26Kisha Yahwe akamwambia Musa, akisema,27“Sasa, siku ya kumi ya mwezi huu wa saba, ni Siku ya Upatanisho. Kutakuwa na kusanyiko takatifu, na ni lazima mjinyenyekeze na kuleta kwa Yahwe matoleo kwa moto.28Hamtafanya kazi katika siku hiyo kwa sababu ni Siku ya Upatanisho, ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu mbele za Yahwe Mungu wenu.29Yeyote asiyejinyenyekeza siku hiyo lazima akatiliwe mbali na watu wake.30Yeye afanyaye kazi yoyote katika siku hiyo, Mimi, Yahwe, nitamwangamiza atoke miongoni mwa watu wake.31Msifanye kazi ya aina yoyote katika siku hiyo. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali pote mnapoishi.32Siku hii itakuwa Sabato ya pumziko lenye utulivu, na ni lazima siku ya tisa ya mwezi mjinyenyekeze katika majira ya jioni. Tangu jioni hata jioni mtaishika Sabato yenu.”

33Yahwe akazungumza na Musa, akisema,34“Zungumza na watu Israeli, uwaambie ‘Katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba kutakuwa na Sikukuu ya vibanda kwa Yahwe. Nayo itadumu siku saba.35Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu. Hamtafanya kazi ya kawaida.36Kwa muda wa siku saba mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahwe. Siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu, nanyi mtatoa dhabihu iliyofanywa kwa moto kwa Yahwe. Hili ni kusanyiko lenye utulivu, nanyi msifanye kazi yoyote ya kawaida.

37Hizi ndizo sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahwe, ambazo mnapaswa kuzitangaza kuwa ni makusanyiko matakatifu ya kutoa dhabihu kwa moto kwa Yahwe, matoleo ya kuteketezwa na matoleo ya nafaka, dhabihu na matoleo ya vinywaji, kila moja kwa siku yake.38Sikukuu hizi zitakuwa nyongeza kwa Sabato za Yahwe na zawadi zenu, viapo vyenu vyote, na sadaka zenu zote za hiari mzitoazo kwa Yahwe.

39Kuhusu Sikukuu ya vibanda, siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakapokuwa mmeyakusanya ndani matunda ya nchi, ni lazima muitunze sikukuu hii ya Yahwe kwa muda wa siku saba. Siku ya kwanza itakuwa ya pumziko lenye utulivu, na siku ya nane pia itakuwa ya pumziko lenye utulivu.40Siku ya kwanza mtachuma tunda lililobora kutoka kwenye miti, mtakata makuti ya mtende, na matawi ya miti minene yenye majani mengi, na majani ya mierebi kutoka chemichemi za maji, nanyi mtashangilia mbele za Yahwe Mungu wenu kwa siku saba.41Kwa muda wa siku saba kila mwaka, mtaisherehekea sikukuu hii kwa Yahwe. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu mahali potepote mtakapoishi. Mtaisherehekea sikukuu hii katika mwezi wa saba.42Mtaishi kwenye vibanda vidogo vidogo kwa siku saba. Waisraeli wenyeji wa kuzaliwa wote itawapasa kuishi katika vibanda vidogo vidogo kwa siku saba,43ili kwamba wazao wenu, kizazi baada ya kizazi, waweze kujifunza nilivyowafanya wana wa Israeli kuishi kwenye vibanda kama hivi nilipowaongoza kutoka katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.’”

44Katika njia hii Musa akazitangaza kwa watu wa Israeli sikukuu zilizoamriwa kwa ajili ya Yahwe.

24

1Yahwe akamwambia Musa, akisema,2“Waamuru watu wa Israeli wakuletee mafuta halisi yaliyokamliwa kutokana na mizeituni ili yatumike kwenye taa, ili kwamba taa ziweze kuwaka daima na kuleta mwanga.3Nje ya pazia lililoko mbele ya sanduku la maamzi ndani ya hema la kukutania, Haruni ataiwasha daima taa mbele za Yahwe, tangu asubuhi hata jioni. Hii itakuwa amri ya kudumu katika vizazi vyote vya watu wenu.4Kuhani mkuu atazifanya taa ziwake daima mbele za Yahwe, taa hizo zilizo kwenye kinara cha dhahabu safi.

5Yawapasa kuchukua unga laini na kuoka kwa huo mikate kumi na miwili. Ni lazima kuwe na mbili za kumi za efa za unga katika kila mkate.6Kisha mtaipanga juu ya meza ya dhahabu safi mbele za Yahwe katika safu mbili, mikate sita katika kila safu,7Mtaweka uvumba safi kando ya kila safu ya mikata kuwa sadaka ya kuwakilisha. Uvumba huo utachomwa kwa moto kwa ajili ya Yahwe.8Kila siku ya Sabato kuhani mkuu sharti aipange kwa utaratibu hiyo mikate mbele za Yahwe kwa niaba ya watu wa Israeli, iwe ishara ya agano la milele.9Sadaka hii itakuwa kwa ajili ya Haruni na wanawe, na ni lazima waile mahali palipo patakatifu, kwa kuwa ni sehemu ya matoleo kwa Yahwe yaliyofanywa kwa moto.”

10Sasa ilitokea kwamba mwana wa mwanamke Mwisraeli, ambaye baba yake alikuwa Mmisri, alikwenda miongoni mwa watu wa Israeli. Huyu mwana wa mwanamke Mwisraeli akagombana na mwanaume Mwisraeli kambini.11Mwana wa mwanamke Mwisraeli akalikufuru jina la Yahwe na kumlaani Mungu, kwa hiyo watu wakamleta kwa Musa. Jina la mama yake aliitwa Shelomithi, binti wa Dibri, kutoka kabila la Dani.12Wakamweka kizuizini mpaka Yahweh mwenyewe atakapotangaza mapenzi yake kwao.

13Kisha Yahwe akamwambia Musa,14“Mchukue nje ya kambi huyo aliyemlaani Mungu. Wale wote waliomskia wataweka mikono yao juu ya kichwa chake, na kisha kusanyiko lote watamponda kwa mawe.15Ni lazima uwaeleze watu wa Israeli na kusema, ‘Yeyote anayemlaani Mungu wake imempasa kubeba hatia yake mwenyewe.16Yeye anayelikufuru jina la Yahwe kwa hakika ni lazima auawe. Hakika, kusanyiko lote litampiga mawe, ama awe mgeni au Mwisraeli mwenyeji mzaliwa. Ikiwa yeyote analikufuru jina la Yahwe, ni lazima auawe.

17Naye amuuaye mtu mwingine ni lazima kwa hakika auwe.18Yeye anayemuua mnyama wa mwingine sharti amfidie, uhai kwa uhai.19Iwapo mtu anamjeruhi jirani yake, ni lazima atendewe vivyo hivyo alivyomtendea jirani yake:20Mvunjiko kwa mvunjiko, jicho kwa jicho, jino kwa jino. Kama amesababisha jeraha kwa mtu, ndivyo ipasavyo kutendwa kwake.21Yeyote auaye mnyama ni lazima amfidie, na yeyote auaye mtu ni lazima auawe.22Ni lazima muwe na sheria moja kwa wote, mgeni na Mwisraeli mwenyeji mzaliwa, kwa kuwa Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.”

23Kwa hiyo Musa akazungumza na watu wa Israeli, nao watu wakamleta mwanaume huyo nje ya kambi, yule ambaye alikuwa amemlaani Yahwe. Wakampiga kwa mawe. Watu waisraeli wakaitekeleza amri ya Yahwe aliyoitoa kupitia Musa.

25

1Yahwe akazungumza na Musa kwenye Mlima wa Sinai, akisema,2“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, “Mtakapoingia katika nchi ambayo ninawapa, kisha hiyo nchi lazima ifanywe iwe ya kuishika Sabato kwa ajili ya Yahwe.3Ni lazima mtapanda mazao yenu kwa miaka sita, na kwa miaka sita mtaikatia matawi mizabibu yenu na kukusanya mazao yake.4Lakini katika mwaka wa saba, Sabato ya pumziko la utulivu kwa nchi itashikwa, ni Sabato kwa Yahwe. Hamtapanda mashamba yenu wala kuikatia mizabibu yenu matawi yake.5Hamtasimamia mavuno yoyote ya mazao ya mizabibu iliyojiotesha yenyewe katika mashamba yenu ya mizabibu isiyokatiwa matawi. Huu utakuwa mwaka wa pumziko lenye utulivu kwa ardhi.6Chochote ardhi isiyofanyiwa kazi itakachotoa wakati wa Sabato ndicho kitakuwa chakula chako. Wewe mwenyewe, watumwa wako wa kiume na wa kike, watumishi wako wa kuajiriwa na wageni wanaoishi pamoja nawe mnaweza kujikusanyia chakula.7Na wanyama wako wa kufugwa na wanyama pori waweze kula chochote ardhi itoacho.

8Ni lazima kwenu kuhesabu Sabato saba za miaka, yaani, saba mara miaka saba, ikifanya jumla ya miaka arobaini na tisa.9Kisha mtapiga sauti ya tarumbeta kila mahali katika siku ya kumi ya mwezi wa saba. Katika Siku ya Upatanisho ni lazima mtapiga tarumbeta katika nchi yenu yote.10Nanyi mtautenga mwaka wa hamsini kwa ajili ya Yahwe na mtatangaza uhuru katika nchi yote kwa wakazi wote. Kutakuwa na Yubile kwa ajili yenu, ambayo kwayo mali na watumwa ni lazima warejeshwe kwa familia zao.11Mwaka wa saba kutakuwa na Yubile kwenu. Hamtapanda wala kusimamia mavuno ya kijiotesha yenyewe, na kukusanya kichipukacho kwenye mizabibu isiyokatiwa matawi.12Kwa sababu hiyo ni Yubile takatifu kwenu. Nanyi mtakula mazao yanayokua yenyewe kutoka mashambani.

13Ni lazima muwarejeshe kila mmoja kwenye miliki yake katika mwaka huu wa Yubile.

14Iwapo utauza ardhi yoyote ya jirani yako au kununua ardhi yake, ni sharti msipunjane au kutendeana kwa hila.15Iwapo unanunua ardhi kutoka kwa jirani yako, zingatia idadi ya miaka na mazao ambayo yaweza kuvunwa mpaka mwaka wa Yubile nyingine. Jirani yako anayeuza ardhi ni lazima aihesabu miaka hiyo pia.16Miaka inapoongezeka mpaka Yubile nyingine, ataongeza thamani ya ardhi, na miaka inapokuwa michache kufikia Yubile nyingine atashusha thamani, kwa sababu idadi ya mavuno inahusiana na idadi ya miaka kabla ya Yubile nyingine.17Msipunjane au kutendeana kwa hila, badala yake, yawapasa kumheshimu Yahwe Mungu wenu.

18Kwa hiyo basi, ni lazima muyatii maagizo, kuzitunza sheria zangu na kuzitekeleza. Nanyi mtaishi katika nchi katika usalama.19Nayo nchi itawapa mavuno yake, nanyi mtakula matunda yenu na mtaishi humo salama.20Labda mtasema, Tutakula nini katika mwaka wa saba? Tazama, hatuwezi kupanda wala kukusanya mazao yetu.”21Nitaiamru baraka yangu ije juu yenu katika mwaka wa sita, nayo itatoa mavuno ya kutosha kwa miaka mitatu.22Mtapanda katika mwaka wa nane na mtaendelea kula mazao ya miaka iliyopita na kutoka kwenye ghala la chakula. Mpaka mavuno ya mwaka wa tisa yatakapofika, mtaweza kula kutoka kwenye riziki iliyohifadhiwa katika miaka iliyopita

23Ardhi haitauzwa kwa mmiliki mpya wa kudumu, kwa sababu ardhi ni mali yangu. Ninyi nyote mu wageni na wakazi wa muda juu ya ardhi yangu.24Ni lazima muitunze haki ya ukombozi kwa ajili ya ardhi yote mtakayoimiliki; itawapasa kuruhusu ardhi inunuliwe tena na familia ambayo wewe uliinunua hiyo ardhi kutoka kwao.

25Iwapo Mwisraeli mwenzako anakuwa masikini na kwa sababu hiyo anauza baadhi ya miliki yake, kisha jamaa yake wa karibu anaweza kuja na kuikomboa hiyo miliki ambayo jamaa yake kaiuza kwako.26Iwapo mtu hana jamaa wa kuikomboa mali yake, lakini ikiwa kafanikiwa na anao uwezo wa kuikomboa,27kisha atahesabu miaka tangu ardhi hiyo ilipouzwa na kurejesha kwa mtu aliyemuuzia fedha iliyosalia. Naye anaweza kuirejesha kwenye miliki yake mwenyewe.28Lakini ikiwa hawezi kuirejesha kwake ardhi aliyoiuza, nayo hiyo ardhi aliyoiuza itabaki katika umiliki wa yule aliyeinunua mpaka mwaka wa Yubile. Kwenye mwaka wa Yubile, ardhi itarejeshwa kwa mtu aliyeiuza, naye mmiliki wa asili atarejea kwenye mali yake.

29Ikiwa mtu anauza nyumba iliyo kwenye mji uliozungushiwa ukuta, naye anaweza kuinunua tena ndani ya mwaka baada ya kuuzwa. Kwa kuwa, kwa mwaka mzima atakuwa na haki ya ukombozi.30Kama nyumba hiyo haitakombolewa kabla ya mwaka mzima, ndipo hiyo nyumba iliyoko kwenye mji uliozungushiwa ukuta itakuwa mali ya kudumu ya yule aliyeinunua, katika vizazi vyote vya uzao wake. Nyumba hiyo haitakuwa ya kurejeshwa katika mwaka wa Yubile.31Lakini nyumba za vijijini zisizokuwa na ukuta kuzizunguka, zitahesabiwa kuwa shamba la nchi. Zaweza kukombolewa, na ni lazima zirejeshwe katika mwaka wa Yubile.

32Hata hivyo, nyumba zinazomilikiwa na makuhani katika miji yao zaweza kukombelewa wakati wowote.33Iwapo mmoja wa makuhani haikomboi nyumba iliyouzwa, kisha nyumba hiyo iliyouzwa katika miji iliomo, ni lazima irejeshwe katika mwaka wa Yubile, kwa kuwa nyumba za miji ya makuhani ni mali yao miongoni mwa watu wa Israeli.34Lakini yale mashamba yanayozunguka miji yao, hayataweza kuuzwa kwa sababu, hiyo ni mali ya kudumu ya Makuhani.

35Ikiwa mwananchi mwenzako anakuwa masikini, kiasi kwamba hawezi kujihudumia, nawe utalazimika kumsaidia kama vile ungemsaidia mgeni au mwingine yeyote kutoka nje aishie miongoni mwenu.36Usimtoze riba au kujaribu kunufaika kutoka kwake katika njia yoyote, bali mheshimu Mungu wako ili kwamba ndugu yako aendelee kuishi nawe.37Hutampa mkopo wa fedha na kumtoza riba, wala hutamuuzia chakula chako ili kupata faida.38Mimi ndimi Yahwe Mungu wako, aliye kuleta wewe kutoka nchi ya Misri, ili kwamba Nikupe nchi ya Kanaani, na kwamba niwe Mungu wako.

39Iwapo mwananchi mwenzako atakuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwako, hutamfanyisha kazi kama mtumwa.40Mtendee kama mtumishi wa kuajiriwa. Ni lazima awe kama yule ahudumuye nawe kwa muda mpaka mwaka wa Yubile.41Kisha ataondoka kwako, yeye mwenyewe na watoto wake pamoja naye, na atarejea kwenye familia yake mwenyewe na kwenye miliki ya babaye.42Kwa sababu wao ni watumishi wangu niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri. Hawatauzwa kama watumwa.43Usitawale juu yao kwa ukatili, bali yakupasa kumheshimu Mungu wako.

44Kwa upande wa watumwa wako wakiume na watumwa wako wa kike, unaweza kuwapata kutoka kwa mataifa yanayokuzunguka, waweza kununua watumwa kutoka kwao.45Unaweza pia kununua watumwa kutoka kwa wageni wanaoishi miongoni mwenu, yaani, kutoka familia zao waliopamoja nawe, wale watoto waliozaliwa katika nchi yako. Wanaweza kuwa mali yako.46Unaweza kuzalisha watumwa hao kama urithi kwa watoto wako baada yako, ili kuwamiliki kama mali. Kutoka kwao waweza kununua watumwa daima, lakini hamtaweza kutawala kwa ukali juu ya ndugu zenu walio miongoni mwa watu wa Israeli.

47Iwapo mgeni anayeishi nawe kwa muda anakuwa tajiri, na ikiwa mmoja wa Waisraeli amekuwa masikini na kujiuza mwenyewe kwa familia ya mgeni, au kwa mtu fulani katika familia,48baada ya Mwisraeli mwenzako kuwa amenunuliwa. Anaweza kurejeshwa kwa malipo. Iwapo anaweza kurejeshwa. Mtu fulani katika familia yake anaweza kumkomboa.49Anaweza kuwa mjomba wake, au mjomba wa mwanawe, anayemkomboa yeye, au yeyote aliye ndugu yake wa karibu kutoka kwa ukoo wake. Au, iwapo ni mwenye mafanikio, anaweza kujikomboa mwenyewe.50Ni lazima apatane na mtu aliyemnunua, itawapasa kuhesabu miaka tangu mwaka aliojiuza kwa mnunuzi wake mpaka mwaka wa Yubile. Ile thamani ya ukombozi wake ihesabiwe kulingana na kiwango cha mshahara anaolipwa mtumishi aliyeajiriwa, kwa idadi ya miaka ambayo angeweza kuendelea kufanya kazi kwa yule aliyemnunua.51Endapo kutakuwa kungali na miaka mingi iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atalazimika kulipa fungu kubwa la fedha kwa ajili ya ukombozi ambao ni wingi wa idadi ya miaka hiyo.52Iwapo kuna miaka michache tu iliyobaki mpaka mwaka wa Yubile, atapatana na aliyemnunua ili kuipitia idadi ya miaka iliyobaki mpaka Yubile, naye atalazimika kulipia ukombozi wake kulingana na idadi ya miaka.53Naye atatendewa kama mtu aliyeajiriwa mwaka kwa mwaka. Utahakikisha kwamba hatendewi kwa ukali.

54Iwapo hakukombolewa katika njia hizi, basi atatumika mpaka mwaka wa Yubile, yeye pamoja na watoto wake.55Kwangu mimi watu wa Israeli ni watumishi. Wao ni watumishi wangu ambao Niliwatoa katika nchi ya Misri. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.

26

1Msijitengenezee sanamu, wala msisimamishe kinyago cha kuchonga au nguzo ya jiwe ya kuabudia, na msisimamisha sura ya jiwe la kuchonga katika nchi yenu mtakayo iinamia, kwa kuwa Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu.

2Ni lazima muitunze Sabato Yangu na kupaheshimu patakatifu pangu. Mimi ndimi Yahwe.

3Iwapo mtatembea katika sheria zangu na kuzishika amri zangu na kuzitii,4Nami nitawapa ninyi mvua katika majira yake; nayo nchi itatoa mazao yake, na miti ya shambani itatoa matunda yake.5Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupanda mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.

6Nitawapa amani; mtalala bila ya kitu chochote kuwatia hofu. Nitawaondolea mbali wanyama waliohatari katika nchi, na upanga hautapita katika nchi yenu.7Mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga.8Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi; adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.

9Nitawatazama kwa upendeleo na kuwafanya nyinyi mzae na kuwazidisha nyinyi.10Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.11Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami sitachukizwa nanyi.12Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.13Mimi ndimi Yahwe Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.

14Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,15Na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—16—Kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.17Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.

18Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.19Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.20Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.

21Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.22Nitatuma wanyama wa pori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya muwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.

23Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,24ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.25Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.26Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa

27Endapo hamtanisikiliza licha ya mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,28kisha nami nitaenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.29Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.30Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.31Nitaigeuza miji yenu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.32Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.33Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.34Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za adui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.35Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.

36Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo, mtayaogopeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na mwenye kuwafukuza.37Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya adui zenu.38Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.39Wale watakoasalia miongoni mwenu watapotelea katika dhambi zao, huko kwenye nchi za adui zenu, na kwa sababu ya dhambi zao, na za baba zao, watapotelea mbali pia.

40Lakini kama watakiri dhambi zao na dhambi ya baba zao, na usaliti wao ambao kwao hawakuwa waaminifu kwangu, pia na mwenendo wao dhidi yangu—41ambao ulinisababisha kuwa kinyume nao, na kuwaleta katika nchi ya adui zao—iwapo mioyo yao isiyotahiriwa itanynyekezwa,42na iwapo wataikubali adhabu kwa ajili ya dhambi zao, nami nitalikumbuka agano langu na Yakobo, agano langu na Isaka, agano langu na Abrahamu; Pia, nitaikumbuka nchi.43Nchi itakayotelekezwa na wao, hivyo itapendezwa na Sabato zake inapobaki imetelekezwa na wao. Itawapasa kulipa hatia kwa dhambi zao kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walioyakataa maagizo yangu na kuzichukia sheria zangu.44Lakini pamoja na haya yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, Mimi sitawakataa wao, wala sitawachukia ili kuwaangamiza kabisa na kulifutilia mbali agano langu nililoagana nao, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wao.45Bali kwa ajili yao, nitalikumbuka agano langu na baba zao, niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri machoni pa mataifa, ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Yahwe.”

46Hizi ndizo amri, hukumu, na sheria ambazo Yahwe alifanya baina yake na watu wa Israeli kwenye Mlima Sinai kwa kupitia Musa.

27

1Yahwe akazungumza na Musa na akasema,2“Zungumza na watu wa Israeli na uwaambie, ‘Iwapo mtu yeyote anatoa kiapo maalum cha kuwa mnathiri kwa Yahwe, tumieni tathmini zifuatazo:3Viwango vyenu vya thamani kwa mwanaume aliye na umri kati ya miaka ishirini na miaka sitini yaweza kuwa shekeli hamsini za fedha, kulingana na vipimo vya shekeli ya mahali pa patakatifu.

4Kwa mwanamke wa umri uleule viwango vyenu vya thamani yapasa viwe shekeli thelathini vya fedha.
5Tangu wenye umri wa miaka mitano mpaka wa miaka ishirini, viwango vyenu vya thamani kwa mwananume vitakuwa shekeli ishirini za fedha, na kwa mwanamke ni shekeli kumi za fedha,
6Kwa wenye umri wa tangu mwezi mmoja mpaka miaka mitano viwango vyenu vya thamani kwa mawanaume vitakuwa shekeli tano za fedha na kwa mwanamke shekeli tatu za fedha.
7Tangu wenye umri wa miaka sitini na zaidi kwa mwanaume viwango vyenu vya thamani vitakuwa shekeli kumi na tano, na kwa mwanamke ni shekeli kumi.

8Lakini kama mtu atoaye kiapo cha mnadhiri hawezi kulipa kiwango hicho cha thamani, kisha huyo mtu anayetolewa lazima atapelekwa kwa kuhani, naye kuhani atamthamanisha huyo atolewaye kwa kiasi anachoweza kutoa yule anayetoa kiapo cha mnadhiri.

9Iwapo mtu anataka kutoa sadaka ya mnyama kwa Yahwe, na iwapo Yahwe ataikubali, kisha huyo mnyama atatengwa kwake.10Mtu huyo hataruhusiwa kumtoa madhabahuni au kumbadilisha huyo mnyama, mzuri kwa mbaya au mbaya kwa mzuri. Endapo atatoa mnyama badala ya mwingine, kisha wanyama hao wawili; yule anayetolewa na yule anayebadilishwa wanakuwa watakatifu.11Hata hivyo, iwapo kile mtu ameshaapa kumtolea Yahwe kwa uhalisia siyo kisafi, kwa hiyo, Yahwe hatakikubali, naye huyo mtu atalazimika kumleta huyo mnyama kwa kuhani.12Kuhani atamthamanisha, kwa thamani ya soko la mnyama. Thamani yoyote kuhani atakayoiweka juu ya mnyama, hiyo ndiyo itakuwa thamani yake.13Na kama mmiliki anapenda kumkomboa, kisha tano ya thamani yake itaongezwa kwenye gharama yake ya ukombozi.

14Mtu aitengapo nyumba yake iwe zawadi takatifu kwa Yahwe, kisha kuhani ataweka thamani yake ama iwe ni nzuri au mbaya. Thamani yoyote itakayowekwa na kuhani juu yake, ndiyo itakuwa thamani yake.15Lakini kama mmiliki wake anayeitenga nyumba yake anapenda kuikomboa, atalazimika kuongeza sehemu ya tano ya thamani yake kwenye gharama ya ukombozi wake, nayo nyumba itakuwa yake.

16Iwapo mtu anatenga sehemu ya ardhi yake mwenye, kisha tathmini yake itakuwa katika uwiano kwa kiwango cha kiasi cha mbegu inayotakiwa kuipanda katika ardhi hiyo—homeri moja ya mbegu za shairi ambayo itathamanishwa kwa shekeli hamsini za fedha.17Na kama analitenga shamba lake katika mwaka wa Yubile, hata thamani yake ya awali itabaki kuwa ileile.18Lakini endapo atalitenga shamba hilo baada ya mwaka wa Yubile, kisha kuhani atalazimika kukokotoa thamani yake kwa idadi ya miaka inayobaki mpaka mwaka wa Yubile, na thamani yake lazima ishushwe.19Iwapo mtu anayelitenga shamba lake anapenda kulikomboa, naye atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani, nalo shamba litakuwa lake tena.20Iwapo halikomboi shamba, au iwapo ameshaliuza shamba kwa mtu mwingine, haliwezi kukombolewa tena.21Badala yake, shamba hilo litakapoachwa huru katika mwaka wa Yubile, litakuwa zawadi takatifu kwa Yahwe, kama lilivyo shamba lililotolewa kabisa kwa Yahwe. Nalo litakuwa mali ya kuhani.

22Iwapo mtu anatenga shamba alilolinunua, lakini hilo shamba siyo sehemu ya ardhi ya familia yake,23kuhani atafanya tathmini yake mpaka mwaka wa Yubile, na mtu huyo lazima atalipa thamani yake katika siku hiyo kuwa zawadi takatifu kwa Yahwe.24Katika mwaka wa Yubile, shamba litarejeshwa kwa mtu yule ambaye lilikuwa limenunuliwa, kwa mmiliki wa ardhi.25Tathmini yote lazima ifanywe kwa uzani wa shekeli ya mahali patakatifu. Gera ishirini kwa shekeli moja.

26Asiwepo mtu atakayetenga mzaliwa wa kwanza miongoni mwa wanyama, kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza wa wanyama tayari ni mali ya Yahwe; iwe ni makisai au kondoo, ni wa Yahwe.27Na kama ni mnyama aliye najisi, kisha mmiliki wake anaweza kumnunua tena sawa sawa na thamani yake, na sehemu ya tano lazima itaongezwa kwenye thamani hiyo. Na kama mnyama hakombolewi, naye atauzwa kwa thamani iliyowekwa.

28Hakutakuwa na kitu ambacho mtu anakitoa kwa Yahwe, kutoka katika vyote alivyo navyo, iwe ni mwanadamu au mnyama, au ardhi ya familia yake, ambacho chaweza kuuzwa au kukombolewa. Kila kitu kitolewacho ni kitakatifu sana kwa Yahwe.

29Hakuna fidia inayoweza kulipwa kwa ajili ya mtu aliyetolewa ili kuangamizwa. Mtu huyo sharti auawe

30Zaka yote iliyo ya ardhini, iwe nafaka ichipukayo juu ya ardhi au tunda kutoka kwenye miti, ni mali ya Yahwe. Ni takatifu kwa Yahwe.31Iwapo mtu anakomboa chochote cha zaka yake, atalazimika kuongeza sehemu ya tano kwenye thamani yake.32Na kwa kila mnyama wa kumi wa kundi la ng'ombe au la kondoo, yeyote anayepita chini ya fimbo ya mchungaji, atatengwa kwa ajili ya Yahwe.33Mchungaji hatatafuta wanyama waliobora au wabaya kabisa, na haruhusiwi kubadili mnyama mmoja kwa mnyama mwingine. Iwapo anambadilisha kwa namna yoyote ile, kisha wote wawili yule wa kwanza na huyo aliyebadiliwa watakuwa watakatifu. Mnyama huyo atolewaye hawezi kukombolewa.’”

34Hizi ndizo amri ambazo Yahwe alimpa Musa kwenye mlima Sinai kwa ajili ya watu wa Israeli.

Hesabu

1

1Mungu alimwambia Musa katika hema ya kukutania walipokuwa katika jangwa la Sinai. Hii ilitokea katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili miaka miwili baadaya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Mungu alisema,2‘fanya sensa ya wanaume wote wa Israeli kutoka kila ukoo, katika familia za baba zao. Wahesabu kwa majina, wahesabu kila mume, kila mwanamume3kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi. Uwahesabu wote wanaoweza kupigana kama askari wa Israeli. Wewe na Haruni mtaandika idadi ya wanaume katika makundi ya majeshi yao.4Kila mwanaume kwa kila kabila, kichwa cha ukoo, lazima atumike na wewe kama kiongozi wa kabila.

5Haya ndiyo majina ya viongozi ambao watapigana pamoja na wewe: Kutoka kabila la Reubeni, Elizuri mwana wa Shedeuri;
6kutoka kabila la Simeoni, Shelumiel mwana wa Zurishadai7Kutoka kabila la Yuda, Nashoni mwana wa Aminadabu;8Kutoka kabila la Isakari, Nethaneli mwana wa Zuari;9kutoka kabila Zebuluni, Eliabu mwana wa Heloni10kutoka kabila la Efraimu mwana wa Yusufu, Elishama mwana wa Ammihudi; kutoka kabila la Manase, Gamaliel mwana wa Pedazuri;11kutoka kabila la Benjamini mwana wa Yusufu, Abidani mwana wa Gidion;
12Kutoka kabila la Dan, Ahizeri mwana wa Amishadai;
13kutoka kabila la Asheri, Pagieli mwana wa Okirani;14kutoka kabila la Gadi, Eliasafu mwana wa Deuli;15na kutoka kabila la Naftali, Ahira mwana wa Enani.”

16Hawa ndio wanaume waliochaguliwa kutoka kwa watu. Waliongoza kabila za mababu zao. Walikuwa viongozi wa koo katika Israel.

17Musa na Haruni wakawachukua wale wanaume, waliokuwa wameandikwa kwa majina,18na pamoja na wanaume hao waliwakusanya wanaume wote katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Kisha kila mwanaume wa miaka ishirini na zaidi alitambua babu zake. Alitakiwa kutaja koo na famila kutoka katika ukoo.19Kisha Musa akaandika hesabu yao huko katika nyika ya Sinai, Kama Mungu alivyokuwa amemwamuru kufanya.
20Kutoka uzao wa Reubeni, mtoto wa kwanza wa Israel, yalihesabiwa majina yote ya kila mwanamume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka hesabu ya ukoo na familia.
21Waliwahesabu wanaume 46,000 kutoka ukoo wa Reubeni.
22Kutoka uzao wa Simeoni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini na zaidi au wenye uwezo wa kwenda vitani, kutokana na hesabu ya ukoo na familia.
23Walihesabu wanaume 59,300 kutoka kabila la Simeoni.
24Kutoka uzao wa Gadi yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
25Walihesabu wanaume 45,650 kutoka kabila la Gadi.
26Kutoka uzao wa Yuda yalihesabiwa majina yote ya wanaume wenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
27Walihesabiwa wanaume 74,000 kutoka kabila la Yuda.
28Kutoka uzao wa Isakari yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
29Walihesabiwa wanaume 54,000 kutoka kabila la Isakari.
30Kutoka uzao wa Zabuloni yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
31Walihesabiwa wanume 57,400 kutoka kabila la Zabuloni.
32Kutoka uzao wa Efraimu mwana wa Yusufu yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na wenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
33Walihesabiwa wanaume 40,500 kutoka kabila la Efraimu.
34Kutoka uzao wa Manase mwana wa Yusufu yaliheabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
35Walihesabiwa wanaume 32,000 kutoka kabila la Manase.
36Kutoka uzao wa Benjamini yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
37Walihesabiwa wanaume 35,000 kutoka kabila la Benjamini.
38Kutoka uzao wa Dani yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, Kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
39Walihesabiwa wanaume 62,000 kutoka kabila la Dani.
40Kutoka uzao wa Asheri yalihesabiwa majina yote ya kila mwanume mwenye umri wa miaka ishirini au zadi na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu y a ukoo na familia.
41Walihesabiwa wanaume 41,500 kutoka ukoo wa Asheri.
42Kutoka ukoo wa Naftali yalihesabiwa majina yote ya kila mwanaume mwenye umri wa miaka ishirini au zaidi, na mwenye uwezo wa kwenda vitani, kutoka kwenye hesabu ya ukoo na familia.
43Walihesabiwa wanaume 53,400 kutoka kabila la Naftali.

44Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote hawa, pamoja na wale wanaume kumi na wawili waliokuwa wakiongoza yale makabila kumi na mawili ya Israeli.45Kwa hiyo wanaume wote wa Israeli wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, wote wenye uwezo wa kwenda vitani, walihesabiwa kutoka kwenye familia zao.46Walihesabu wanaume 603,550.

47Lakini wanaume toka uzao wa Lawi hawakuhesabiwa,48Kwa sababu BWANA alimwambia Musa,49“usiwahesabu wale wa kabila la Lawi wala kuwajumuisha kwenye jumla ya watu wa Israeli.50Badala yake, waagize Walawi kuliangalia hema la amri za agano, na kuangalia mapambo ya hema na vyote vilivyomo. Walawi watalazimika kulibeba hema na lazima wayabebe mapambo ya hema. Lazima waliangalie hema na kuyatengeneza mazingira yake. Wataiangalia masikani na kuzitengeneza kambi zinazolizunguka.51Kila hema litakapotakiwa kuhamishiwa eneo lingine, Walawi ndio watakaolipeleka pale. Na kila hema litakapotakiwa kusimamishwa, Walawi ndio watakao lisimamisha. Na mgeni yeyote atakayelisogelea hema lazima auawe.52Wakati watu wa Israeli watakaposimamisha hema zao, kila mwanaume lazima awe karibu na bango la jeshi lake.53Hata hivyo Walawi lazima waweke hema zao kuizunguka hiyo masikani ya amri za agano ili kwamba hasira yangu isije ikawaka juu ya wana wa Israeli. Walawi lazima wailinde hiyo masikani ya amri za agano.”

54Wana wa Israeli walifanya haya yote. Walifanya yote ambayo BWANA aliagiza kupitia Musa.

2

1BWANA akasema na Musa na Haruni tena. Akamwambia,2Kila mtu atapanga kulingana na mahali pake, pamoja na mabango ya baba zao. Watapanga kuzunguka hema ya kukutania kila upande.3Wale watakaopanga mashariki mwa hema ya kukutania, mahali ambapo jua huonekana wakati wa kuchomoza, ni makambi ya Yuda nao watakuwa katika kundi lao. Nashoni mwana wa Aminadabu ni kiongozi wa watu wa Yuda.4Idadi ya watu wa Yuda ni 74,600.5Kabila la Isakari litapanga mbele ya Yuda. Nethaneli mwana wa Zuari ataliongoza jeshi la Isakari.6Idadi ya kikosi chake ni wanaume 54,000.7Kabila la Zabuloni litapanga mbele ya Isakari. Eliabu mwana wa Heloni ndiye atakaye liongoza jeshi la Zabuloni.8Idadi ya kikosi chake ni 57,400.

9Idadi yote ya kambi ya Yuda ni 186,400. Watakuwa wa kwanza kuondoka.10Upande wa kusini kutakuwa na kambi ya Reubeni katika kundi lao. Kiongozi wa kundi la Reubeni ni Elizuri mwana wa Shedeuri.11Idadi ya kikosi chake ni 46,500.12Simeoni atapanga mbele ya Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Zurishadai.13Waliohesabiwa kwenye kikosi chake ni 59,300.14Kabila la Gadi litafuatia. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deuli.15Idadi ya kikosi chake ni 45,650.

16Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Reubeni, kulingana na kikosi chake, ni 151,450. Watakuwa wa pili kuondoka.

17Kifuatacho, ni hema la kukutania kuondoka kambini pamoja na Walawi likiwa katikati ya kambi zote. Lazima waondoke hapo kambini kwa mpangilio huo kama walivyoingia kwenye kambi. Kila mwanaume lazima awe mahali pake kwa kufuata bango lake.18Migawanyiko ya kambi y Efraimu kufuata mahali pake. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.19Hesabu ya kikosi hiki ni 40,500.20Baada ya hao lilifuata kabila la Manase. Kiongozi wa Manase ni Gamaliel mwana wa Pedazuri.21Hesabu ya kikosi hiki ni 32,200.22Kabila litakalofuata ni la Benjamini. Kiongozi wa Benjamini ni Abidani mwana wa Gidioni.23Hesabu ya kikosi hiki ni 35,000

24Wote waliohesabiwa katika kambi ya Efraimu ni 108,100. Watakuwa wa tatu kuondoka.25Upande wa kaskazini kutakuwa na kambi ya kikosi cha Dani. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.26Hesabu ya kikosi hiki ni 62,700.27Watu wa kabila ya Asheri watapanga mbele ya Dani. Kiongozi wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okirani.28Hesabu ya Kikosi hiki ni 41,500.29Kabila la Naftali ndilo litakalofuatia. Kiongozi wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.30Hesabu ya kikosi hiki ni 53,400.

31Wote waliohesabiwa kwenye kambi ya Dani ni 157,600. Hawa watakuwa wa mwisho kuondoka kambini, wakifuata bango lao.

32Hawa ndio Waisraeli, waliohesabiwa kufuata familia zao. Wote waliohesabiwa kwenye kambi zao, kwa kufuata vikosi vyao ni 603,550.33Lakini Musa na Haruni hawakujumuisha Walawi kwenye Hesabu ya Waisrael. Ilikuwa kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa.

34Watu wa Israeli walifanya yote ambayo BWANA alimwagiza Musa. Walipanga kwa kufuata mabango yao. Walisafiri kutoka kambini kwa kufuata jamaa zao, kwa mpangilio wa familia za koo zao.

3

1Sasa hii ndiyo historia ya uzao wa Haruni na Musa wakati BWANA aliposema na Musa kwenye mlima Sinai.

2Majina ya watoto wa Haruni walikuwa Nadabu ambaye ndiyo mtoto wa kwanza, na Abihu, na Eliezeri, na Ithamari.3Haya ndiyo majina ya wana wa Haruni, makuhani waliokuwa wamepakwa mafuta na kuwekwa wakfu kutumika kama makuhani.4Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya BWANA walipomtolea moto usiokubalika walipokuwa katika nyika ya Sinai. Nadabu na Abihu hawakuwa na watoto, kwa hiyo Eliazari na Ithamari walitumika kama makuhani pamoja na baba yao.

5BWANA alinena na Musa, akamwambia,6“Walete kabila ya Lawi na uwaweke kwa Haruni kuhani ili wamsaidie7Nao lazima wafanye majukumu badala ya Haruni na jumuiya yote mbele ya hema ya kukutania. Lazima watumike hemani.8Watayatunza mapambo ya hema ya kukutania, na watawatumikia makabila ya Israeli kwa huduma ya hemani.9Uwaweke Walawi kwa Haruni na watoto wake. Nimewatoa kikamilifu ili wamsaidie kuwatumikia watu wa Israel.10Umchague Haruni na watoto wake kuwa makuhani, lakini mgeni yeyote atakayekaribia lazima auawe.”

11BWANA alinena na Musa. Akamwambia,12“Tazama, nimewachagua Walawi katika watu wa Israeli. Nimefanya hivyo badala ya kuchukua mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wana wa Israeli. Hawa Walawi ni wangu.13Na hata wazaliwa wa kwanza ni mali yangu. Katika siku ambayo niliwavamia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, Niliwatenga wazaliwa wa kwanza wa Israeli kwa ajili yangu, watu na wanyama pia. Ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.”

14BWANA alinena na Musa katika nyika ya Sinai. Akasema,15“Wahesabu uzao wa Lawi katika kila familia, katika nyumba za koo zao. Hesabu kila mume kuanzia mwezi mmoja au zaidi.”16Musa aliwahesabu, kufuata maelekezo ya BWANA, kama alivyoamriwa kufanya.
17Majina ya watoto wa Lawi yalikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
18Ukoo uliotokana na watoto wa Gerishoni walikuwa ni Libni na Shimei.
19Ukoo uliotokana na watoto Kohathi walikuwa ni Amramu na, Izihari, Hebroni, na Uzieli.
20Ukoo uliotokana na watoto wa Merari walikuwa ni Mahili na Mushi. Hizi ndizo koo za Walawi, zilizoorodheshwa ukoo kwa ukoo.

21Koo za Walibini na Washimei zilitokana na Wagerishoni. Hizi ndizo koo za Wagerishoni.22Wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa na kufikia idadi ya 7,500.23Koo za Wagerishoni watapanga upande wa magharibi wa hema.24Eliasafu mwana wa Laeli ataongoza koo za uzao wa Wagerishoni.25Familia ya Gerishoni watalilinda hema la kukutania pamoja na hiyo masikani. Watalilinda hema, kifuniko chake, na lile pazia la lango la hema ya kukutania.26Wataulinda ua, lile pazia kwenye lango--ua unaozunguka mahali patakatifu na madhabahu. Watazilinda kamba za hema ya kukutania na vyote vilivyomo.

27Koo zifuatazo zinatokana na Kohathi: ukoo wa Waamrami, ukoo wa Waizihari ukoo wa Wahebroni, na ukoo wa Wauzieli. Koo hizi zinatokana na Wakohathi.28Wanaume 8,600 wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa ili kulinda vitu vya BWANA.29Familia ya uzao wa Kohathi watapanga upande wa kusini wa Hema.30Elizafani mwana wa Uzieli ndiye atakayeongoza ukoo wa Wakohathi.31Watalilinda sanduku, meza, vikalishio vya taa, madhabahu, vitu vitakatifu ambvyo hutumika katika huduma yao, pazia, na kazi zote zinazoambatana na hema.

32Eliazari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza wanaume wanaowaongoza Walawi. Atawasimamia wanaume wanaongoza eneo takatifu.

33Koo mbili zimetoka kwa Merari: Ukoo wa Mahili na ukoo wa Mushi. Koo hizi zimetokana na Merari,34Wanaume 6,200 wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi walihesabiwa.35Zurieli mwana wa Abihaili ataongoza ukoo wa Merari. Hawa watapanga upande wa kaskazini mwa hema.36Uzao wa Merari utatunza mbao za hema, mataruma, nguzo, makalishio, viifaa vya ujenzi na vitu vyote vinavyohusika,37na nguzo za ua zinazozunguka hema, makalishio, vigingi na kamba zake.

38Musa na Haruni na watoto wake watapanga upande wa mashariki wa masikani, mbele ya hema ya kukutania kuelekea mawio ya jua. Wao wataajibika na majukumu ya mahali patakatifu na majukumu ya wana wa Israeli. Mgeni atakayekaribia mahali patakatifu auawe.

39Musa na Haruni wakawahesabu wanaume wote wa ukoo wa Walawi walikuwa na umri wa mwezi mmoja na zaidi, kama vile BWANA alivyokuwa ameagiza. Walihesabu wanaume ishirini na mbili elfu.

40BWANA alisema na Musa, “Wahesabu wanaume wote ambao ni wazaliwa wa kwanza wa Israeli ambao wana umri wa mwezi mmoja na zaidi. Orodhesha majina yao.41Unitwalie walawi kwa ajili yangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Israeli, Mimi ndimi BWANA. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa uzao wa Israeli,”

42Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli kama BWANA alivyomwagiza kufanya.43Aliwahesabu wazaliwa wote wa kwanza kwa majina, wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi. Alihesabu wanaume 22,273.

44Tena BWANA alinena na Musa. Akasema,45“Watwae Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa wana wa Israeli. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wanyama wa Waisreli wengine. Walawi ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.46Unikusanyie shekeli tano za wokovu kwa kila hao 273 za hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli za hao wanaozidi idadi ya Walawi.47Utazitumia hizo shekeli tano kwa kipimo cha mahali patakatifu. Shekeli moja ni sawa na gera ishirini.48Utawalipa hizo shekeli za wokovu kwa Haruni na wanawe.”

49Kwa hiyo Musa akakusanya shakeli za wokovu kutoka kwa wale waliozidi idadi ya wale walio okolewa na Walawi.50Musa akakusanya zile fedha kutoka kwa hao wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli. Alikusanya jumla ya shekeli 1,365, zenye kipimo sawa na mahali patakatifu. Musa akamlipa Haruni na wanawe hizo shekeli za wokovu.51Musa akafanya kila kitu alichoagizwa na neno la BWANA kama BWANA alivyomwagiza.

4

1BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,2Fanya sensa ya uzao wa waume wa Kohathi kutoka kwa Walawi, kwa kufuata jamaa na familia za ukoo.3Uwahesabu wanaume ambao wana umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Hawa wataungana na kundi linalotumika kutoa huduma kwenye hema ya kukutania.

4Uzao wa Kohathi watalinda vile vitu vitakatifu zaidi vilivyohifadhiwa kwa ajili yangu katika hema ya kukutania.5Wakati kambi inapojiandaa kusonga mbele, Haruni na wanawe lazima waende hemani, kulishusha pazia linalotenganisha mahali patakatifu na kulifunika sanduku la ushuhuda kwa pazia hilo. Watalifunika hilo sanduku kwa ngozi za pomboo.6Watatandika juu yake nguo za rangi ya samawi. Watachomeka hiyo miti ya kubebea.

7Watatandika nguo ya rangi ya samawi kwenye meza ya mikate ya wonyesho. Juu yake wataweka sahani, vijiko, mabakuli na vikombe vya kumiminia. Mikate itakuwepo daima mezani.8Wataifunika na nguo ya rangi nyekundu na ngozi za pomboo. Na kuweka miti ya kubebea.

9Watachukua nguo ya rangi ya samawi na kukifunika kinara, pamoja na taa zake, na koleo zake, na sahani zake na vikombe vyake vya kuwekea mafuta ya taa.10Wataweka kinara na vifaa vyake vikiwa vimefunikwa kwa ngozi ya pomboo, na wataweka kwenye miti ya kukibebea.

11Watafunika kwa nguo ya samawi katika madhabau ya dhahabu. Wataifunika na ngozi za pomboo, na kuweka ile miti ya kubebea.

12Watavichukua vyombo vyote vya kazi takatifu na kuvizonga kwenye hiyo nguo ya rangi ya samawi. Watavifunika na ngozi za pomboo na kuviweka hivyo vyombo kwenye miti ya kubebea.

13Watayaondoa majivu kwenye madhabahu na kutandika nguo ya rangi ya zambarau juu yake.14Wataviweka kwenye miti ya kubebea vyombo vyote wanavyovitumia kwa kazi ya madhabahuni. Vyombo hivi ni vyetezo, majembe, mabakuli na vitu vingine vya madhabahuni. Watayafunika madhabahu na ngozi za pomboo na kuweka ile miti ya kubebea.

15Wakati Haruni na wanawe walipokuwa wamekamilisha kupafunika mahali patakatifu na vyombo vyote, na kambi itakapoanza kuendelea mbele, ndipo wana wa Kohathi watakapokuja kubeba vitu vya mahali patakatifu. Kama watagusa vyombo vitakatifu, lazima watakufa. Hii ni kazi ya wana wa uzao wa Kohathi, kubeba mapambo ya hema ya kukutania.

16Eliazari mwana wa Haruni kuhani atalinda na kusimamia mafuta ya taa, ubani mzuri, sadaka za mara kwa mara na mafuta ya upako. Atasimamia ulinzi wa hema lote na vyote vilivyomo, mahali patakatifu na vyombo vyake.”

17BWANA akanena na Musa na Haruni. Akasema,18Usiruhusu kabila la Wakohathi kuondolewa kati ya Walawi.19Walinde waishi ili wasije wakafa, kwa kufanya hivi. Wanapokuwa wanasogelea20wasije wakaingia ndani ili kuona eneo takatifu hata kwa kitambo, vinginevyo watakufa. Bali Haruni na wanawe wanaweza kuingia, ndipo Haruni na Wanawe watakapowapangia Wakohathi kazi maalumu ya kufanya, kwa kila mmoja.”

21BWANA akanena na Musa tena, Akasema, “Fanya sensa kwa wana Gerishoni pia, kwa kufuata familia za mababu zao, koo zao.22Uwahesabu wale wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini.23Uwahesabu wote ili waje kuungana na wale wanaotumika katika hema ya kukutania.

24Hii ndiyo itakuwa kazi ya koo za Gerishoni, wanapotumikia na wanachobeba.25Watabeba pazia la masikani, hema la kukutania, na vifunikio vyake, vifuniko vya ngozi ya pomboo ambavyo viko juu yake, na pazia kwenye lango la hema ya kukutania.26Watabeba pazia la ua, pazia la kwenye mlango wa ua, ambao uko karibu na maskani karibu na madhabahu, kamba zake na vifaa vyote vya utumishi wake. Chochote kinachotakiwa kufanywa kutokana na vitu hivi, wao ndio watakaofanya.27Haruni na wanawe ndio watakaongoza utumishi wa uzao wa Wagerishoni, kwa vitu vyote vile vya kusafirisha, na katika utumishi wao wote. Lazima uwagawie majukumu yao yote.28Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa wana wa Wagerishoni katika hema ya kukutania. Ithamari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza katika utumishi.

29Utawahesabu uzao wa Merari kwa koo zao, na uwapange katika familia za mabau zao,30kuanzia wenye umri wa miaka thelatini hadi miaka hamsini. Umuhesabu kila atakayeungana na kundi lenye utumishi katika hema ya kukutania.31Huu ndio wajibu na kazi yao katika utumishi wao kwenye hema ya kukutania. Watazilinda mbao za maskani, mataluma yake, nguzo na makalishio yake,32pamoja na nguzo za ua zinazozunguka masikani, makalishio yake, vigingi na kamba zake, na vifaa vingine vya ujenzi. Waorodheshe kwa majina na majukumu yao.33Huu ndio utumishi wa koo za uzao wa Merari, ambao wanatakiwa kufanya katika hema ya kukutania, chini ya uongozi wa Ithmari mwana wa Haruni kuhani.”

34Musa na Haruni na viongozi wa watu waliwahesabu wana wa uzao wa Wakohathi kwa kufuata koo za familia za mababu zao.35Waliwahesabu wale wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Walimhesabu kila mmoja aliyepaswa kuungana na kundi linalotoa huduma ya utumishi kwenye hema ya kukutania.36Waliwahesabu wanaume 2,750 kwa kufuata koo zao.37Musa na Haruni waliwahesabu wanaume wote kutoka koo na familia za Wakohathi ambao hutumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi kwa kumtii BWANA aliyewaagiza kupitia kwa Musa.

38Uzao wa Gerishoni walihesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao,39kuanzia umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kwa kila mmoja aliyetakiwa kuungana na watu wanaotoa huduma kwenye hema ya kukutania.40Wanaume wote waliohesabiwa kufuata koo na familia za mababu zao walikuwa 2,630.41Musa na Haruni walizihesabu koo za uzao wa Gerishoni ambao watatumika kwenye hema ya kukutania. Walifanya hivi ili kutii kile ambacho BWANA aliwaamuru kufanya kuptia kwa Musa.

42Uzao wa Merari walihesabiwa kwa koo kupitia familia za mababu zao,43kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini, kila anayepaswa kuungana na watu wanaotumika kwenye hema ya kukutania.44Wanaume wote waliohesabiwa kupitia koo za familia za mababu zao walikuwa 3 200.45Musa na Haruni waliwahesabu wanaume hawa, uzao wa Merari. Kwa kufanya hivi walitii amri ya BWANA aliyowaaagiza kufanya kupitia kwa Musa.

46Kwa hiyo Musa na Haruni na viongozi wa Israeli waliwahesabu Walawi wote kwa kufuata koo na familia za mababu zao47kuanzia wenye umri wa miaka thelathini hadi miaka hamsini. Walimhesabu kila aliyepaswa kufanya kazi kwenye masikani, na kila aliyepaswa kubeba na kulinda vitu vya kwenye hema ya kukutania.48Waliwahesabu wanaume 8,580.49Kwa agizo la BWANA, Musa alimhesabu kila mwanaume na kutunza kumbukumbu ya kazi ambayo kila mmoja anaweza kufanya. Kwa hivyo, walitii kile ambacho BWANA alikuwa amewaagiza kufanya kupitia kwa Musa.

5

1BWANA alinena na Musa. Akasema,2“Waamuru wana wa Israeli wawatoe watu wote wenye magonjwa ya ngozi yanayoambukiza, na kila mwenye vidonda vinavyotoa harufu, na ambaye amenajisika kwa kugusa maiti.3Awe mume au mke, atolewe kambini. Ili wasije wakaitia unajisi kambi, kwa sababu Mimi huishi ndani yake,”4Watu wa Israeli walifanya hivyo. Waliwatoa kambini, Kama BWANA alivyomwagiza Musa. Watu wa Israeli walimtii BWANA.

5Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,6“Nena na wana wa Israeli. Mtu mume na mtu mke akifanya dhambi yeyote ambayo watu hufanyiana wao kwa wao, na mtu huyo akamwasi BWANA, mtu huyo atakuwa na hatia.7Ndipo huyo mtu ataungama hiyo dhambi aliyoifanya. Mtu huyo atarudisha malipo ya hatia yake na kuongeza kwenye malipo hayo sehemu ya tano zaidi. Atamlipa huyo aliyemtendea makosa8Lakini kama huyo mtu huyu aliyetendewa kosa hana ndugu wa kupokea hayo malipo, basi atalipa hayo malipo ya hatia kwangu kupitia kuhani pamoja na kondoo dume kwa ajili ya sadaka yake mwenyewe.9Kila sadaka ya wana wa Israeli, vitu ambavyo vimetengwa na vikaletwa kwa kuhani na watu wa Israeli, vitakuwa vyake.10Sadaka ya kila mtu itakuwa ya kuhani; kama mtu yeyote atatoa kitu chochote kwa kuhani, kitakuwa chake.”

11Tena BWANA akanena na Musa. Akasema,12“Nena na wana wa Israeli. Uwaambie, ‘kama mke wa mtu ataasi na kufanya dhambi dhidi ya mume wake.13Halafu mtu mwingine akalala naye. Kwa sababu, hiyo atakuwa amenajisika. Na hata kama mume wake hakuona na hajui, hata kama hakuna mtu aliyemkamata akiwa katika tendo na hakuna mtu wa kushuhudia dhidi yake; hata hivyo ile roho ya wivu itaendelea kumjulisha yule mume kuwa mke wake amenajisika.14Ingawa, roho ya wivu inaweza kumdanganya yule mwanaume wakati mke wake hajanajisika.15Kwa mazingira hayo, yule mwanaume anapaswa kumpeleka mke wake kwa kuhani. Yule mwanaume anapaswa kutoa sadaka ya divai kwa ajili yake. Atapaswa kuleta sehemu ya kumi ya efa ya unga wa shayiri. Asitie mafuta juu yake wala asitie ubani juu yake maana ni sadaka ya unga ya wivu, ni sadaka ya unga ya ukumbusho wa uovu.

16Ndipo kuhani atasogeza karibu na kumweka mbele ya BWANA.17Kuhani atachukua kikombe cha maji matakatifu na atachukua mavumbi kutoka kwenye masikani. Ataweka yale mavumbi kwenye maji.18Kisha kuhani atamweka huyo mwanamke mbele za BWANA na atazifungua nywele kichwani kwa huyo mwanamke. Atamwekea mikononi mwake hiyo sadaka ya unga kwa ajili ya ukumbusho, ambayo ni sadaka ya unga kwa ajili ya wivu.19Kuhani atashikilia mikononi mwake maji machungu yanayoweza kuleta laana. Kuhani atamweka huyo mwanamke chini ya kiapo na kumwambia. ‘Kama haujafanya uzinzi na mwanaume mwingine, na kama hajakengeuka na kufanya uovu, basi utakuwa huru na maji haya yanayoweza kuleta laana.20Lakini kama wewe, mwanamke uliye chini ya mume wako, umekengeuka, na kama umenajisika, na kama mwanaume mwingine amelala nawe,21ndipo, (kuhani atamtaka huyo mwanamke aape kiapo kinachoweza kuleta laana kwake, na kwamba ataendelea kumwambia yule mwanamke) ‘BWANA atakufanya wewe kuwa laana itakayoonyeshwa kuwa hivyo kwa watu wako. Hii itatokea pale BWANA atakapoyafanya mapaja yako kuoza na tumbo lako kuvimba.22Haya maji ambayo huleta laana yataingia tumboni mwako na kulifanya tumbo lako kuvimba na mapaja yako kuoza,’ mwanamke alitakiwa kujibu, ‘Ndiyo, hayo yanipate kama mimi ni mwenye hatia.’

23Naye kuhani ataziandika laana hizi kwenye kitabu, na kisha kuzifuta laana zilizoandikwa kwa maji ya uchungu.24Naye kuhani atamwelekeza yule mwanamke kunywa yale maji machungu yaletayo laana. Yale maji yaletayo laana yataingia na kuwa machungu.25Kuhani ataitwaa ile sadaka ya unga ya wivu mikononi mwa yule mwanamke. Atailekeza ile sadaka ya unga mbele ya BWANA na kuileta madhabahuni.26Kuhani atachukua konzi ya sadaka ya unga mkononi mwake kama sadaka ya kuwakilisha, na kuiteketeza madhabahuni. Ndipo atakapompatia mwanamke yale maji machungu ili ayanywe.27Wakati wa kumpa yale maji ili anywe, kama amenajisika kwa sababu alifanya uovu dhidi ya mume wake, ndipo yale maji yaletayo laana yatamwingia na kuwa machungu. Tumbo lake litavimba na paja lake litaoza. Yule mwanamke atalaaniwa kati ya watu wake.28Lakini kama yule mwanamke hajanajisika na kama ni msafi, basi atakuwa huru. Tena ataweza kubeba uja uzito.

29Hii ndiyo sheria ya wivu. Ni sheria ya mwanamke anaye mgeuka mumewe na kunajisika.30Ni sheria ya mwanaume mwenye roho ya wivu kwa mkewe. Atamleta mwanamke mbele ya BWANA, na kuhani atamfanyia huyo mwanamke kila kitu ambacho sheria ya wivu inamtaka kufanya.31Yule mwanaume atakuwa hana hatia kwa kumleta mke wake kwa kuhani. Na yule mwanamke atauchukua uovu wake.”

6

1BWANA alinena na Musa. Akamwambia,2‘Nena na wana wa Israeli, uwaambie, ‘Kama mume au mke ataweka nadhiri kwa BWANA kwa kiapo maalumu cha mnadhiri, ndipo atajiepusha na divai na vileo. Hatakunywa siki itokanayo na divai.3Asinywe kileo kitokanacho na siki au kilevi. Asinywe maji ya divai yeyote au kula zabibu mbichi wala zilizokauka.4Katika siku zote ambazo amejitenga kwa ajili yangu, asile chochote kinachotokana na zabibu, wala kitu chochote kitokanacho na makokwa hadi maganda.

5Wakati wote wa nadhiri yake, wembe usiipite kichwani mwake mpaka siku zake za nadhiri kwa BWANA zitimilike. Lazima ajitenge kwa BWANA. Ataziacha nywele zake zikue kichwani mwake.6Wakati wote wa kujidhiri kwake kwa BWANA, asiikaribie maiti.7Asijinajisi kwa namna yeyote hata kama atakufa baba yake, mama, dada, au ndugu yake. Hii ni kwa sababu amejitenga kwa ajili ya Mungu, kama ambavyo kila mmoja anavyoweza kumuona kwa urefu wa nywele zake.8Wakati wote wa kujidhiri kwake atakuwa mtakatifu, alijitunza kwa ajili ya BWANA.

9Ikitokea mtu amekufa ghafla pembeni yake na kukitia unajisi kichwa chake kitakatifu, ndipo atakaponyoa kichwa chake katika siku ya kujitakasa --Siku ya saba atanyoa kichwa chake.10Siku ya nane atamletea kuhani njiwa wawili au makinda mawili ya njiwa kwenye lango la hema ya kukutania.11Naye kuhani atamtoa ndege mmoja kama sadaka ya dhambi na mwingine kama sadaka ya kuteketezwa. Hawa watafanyika sadaka ya upatanisho kwake kwa sababu atakuwa ametenda dhambi ya kuwa karibu na mfu. Atatakasika kichwa chake siku hiyo.12Atajitenga kwa BWANA tena katika siku hizo za utakaso. Ataleta kondoo mume mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya hatia. Zile siku zake kabla ya kunajisika hazitahesabiwa, kwa sababu kujiweka wakfu kwake kulinajisika.

13Hii ndiyo sheria ya mnadhiri wakati wa muda wa kujidhiri unapokuwa umetimia. Ataletwa kwenye mlango wa hema ya kukutania.14Ataleta sadaka yake kwa BWANA. Atatoa mwanakondoo mume wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya kuteketezwa. Ataleta kondoo mke wa mwaka mmoja asiye na hila kama sadaka ya dhambi. Ataleta kondoo mume asiye na hila kama sadaka ya amani.

15Ataleta kikapu cha mikate iliyotengenezwa bila amira, mikate ya unga mwembamba iliyokandwa kwa mafuta, mikate ya kaki isiyo na amira iliyopakwa mafuta, pamoja na sadaka za unga na sadaka za vinywaji

16Kuhani atawaleta mbele za BWANA. Atazitoa hizo sadaka zake za dhambi na kuteketezwa.17Na kikapu cha mikate isiyowekwa amira, atamtoa yule kondoo mume kama sadaka ya amani kwa BWANA. Pia kuhani atatoa hiyo sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji.

18Mnadhiri atanyoa nywele zake kama ishara ya kujitenga kwa ajili ya Mungu kwenye mlango wa hema ya kukutania. Atazitoa nywele zake kichwani kwake na kuzichoma kwa moto ulio chini ya sadaka ya amani.

19Kuhani atachukua bega la kondoo mume lililotokoswa, na mkate usiotiwa amira toka kikapuni, na mkate mmoja wa kaki usiotiwa amira. Atauweka kwenye mikono ya Mnadhiri baada ya kuwa amenyoa nywele kwa ishara ya kujidhiri.20Kisha kuhani atavitikisa kuwa sadaka kwa BWANA, sehemu takatifu kwa kuhani, pamoja na kidari cha kutikiswa na paja lililotolewa kwa kuhani. Baadaye, Mnadhiri anaweza kunywa divai.

21Hii ndiyo sheria ya Mnadhiri anayeapia sadaka yake kwa BWANA kwa ajili ya kujidhiri kwake. Chochote atakachotoa, lazima afanye kama alivyoapa, kuilinda ahadi yake kama ilivyoaniswa katika sheria ya Mnadhiri.

22Tena BWANA akanena na Musa, akasema,23“nena na Haruni na wanawe. Uwaambie, ‘mtawabariki wana wa Israeli kwa njia hii. Mtawaambia,
24BWANA na awabariki na kuwatunza.
25BWANA na awaangazie nuru ya uso wake na awe mwenye neema kwenu.
26BWANA na awatazame kwa neema na awape amani.’”

27Ni kwa jinsi hii kwamba wanaweza kuwapa jina langu wana wa Israeli.”

7

1Siku ambayo Musa alikamilsha masikani, alitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA, pamoja na mapambo yake. Aliifanyia hivyo madhabahu na vyombo vyake. Aliitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA.2Siku hiyo, viongozi wa Israeli na wale vichwa vya familia za mababu walitoa sadaka. Hawa wanaume walikuwa viongozi wa makabila. Walisaidia kuhesabu watu kwenye ile sensa.3Walileta sadaka zao kwa BWANA. Walileta magari sita yaliyofunikwa na mafahari kumi na mbili. Walileta gari moja kwa kila viongozi wawili, kila kiongozi alileta fahari moja. Walileta vitu hivi mbele ya masikani.

4Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,5“Uzipokee hizo sadaka kutoka kwao na uzitumie kwa matumizi ya kazi ya hema ya kukutania. Uwape hizo sadaka Walawi, kwa kila mmoja kadri ya uhitaji wa kazi yake.”

6Musa akayatwaa yale magari na mafahari. Na kuwapatia Walawi.7Aliwapa magari mawili na mafahari wanne wale wa uzao wa Gerishoni, kwa sababu ndivyo kazi yao ilivyohitaji.8Aliwapatia uzao wa Merari magari manne na mafahari nane, chini ya uangalizi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Alifanya hivi kwa sababu ya uhitaji wa kazi yao.9Lakini wale wa uzao wa Kohathi hakuwapa chochote kwa sababu wao waliangalia vitu vitakatifu ambavyo vilipaswa vibebwe mabegani mwao, siyo kwa magari.

10Viongozi walitoa bidhaa zao zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo.11BWANA akasema na Musa, “kila kiongozi atatoa sadaka kwa siku yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.”12Katika siku ya kwanza, Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda, alitoa sadaka yake.13Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.14Pia alimpa unga wa dhahabu kiasi cha bakuli moja chenye uzani wa shekeli kumi kilichojaa ubani15Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.16Alitoa beberu kama sadaka ya hatia.17Alitoa makisai mbili, kondoo waume watano, beberu watano na wanakondoo dume watano wenye umri wa mwaka mmoja, kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.

18Siku ya pili, Nethanel mwana wa Zuari, kiongozi wa Isakari, alitoa sadaka yake.19Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga.20Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, iliyojaa ubani.21Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo mmoja dume.22Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.23Alitoa makisai wawili, Kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Zuari.24Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa uzao wa Zabuloni alitoa sadaka yake.25Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimeja unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.26Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.27Alitoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja.28Alitoa beberu mmoja kama sadaka ya dhambi.29Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja. Kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana Heloni.30Siku ya nne, Elizuri mwana wa shedeuri, kiongozi wa uzao wa Reubeni, alitoa sadaka yake.31Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.32Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilicho jaa ubani.33Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, mwanakondoo dume mmoja mchanga wa mwaka mmoja.34Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.35Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Elizuri mwana wa Shedeuri.36Siku ya tano, Shelumieli mwana wa Zurishadai, kiongozi wa uzao wa Simeoni, alitoa sadaka yake.37Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.38Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, uliojaa ubani.39Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, dume la kondoo, na dume la mwanakondoo la mwaka mmoja.40Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.41Alitoa maksai wawili, dume wawili wa kondoo, beberu watano, na dume watano wa wanakondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Shelumei mwana wa Zurishadai.42Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake.43Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga.44Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.45Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari changa, kondoo ndume mmoja, na dume la mwanakondoo mmoja wa mwaka mmoja.46Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.47Alitoa makisai wawili, dume watano wa kondoo, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.48Siku ya saba, Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa uzao wa Efraimu, alitoa sadaka yake.49Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.50Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu, kilichojaa ubani51Alitoa sadaka ya kuteketezwa, fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.52Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.53Alitoa maksai wawili, kondoo ndume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Elishama mwana wa Amidu.54Siku ya nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake.55Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.56Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.57Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.58Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.59Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamaliel mwana wa Pedazuri.60Siku ya tisa, Abidani mwana wa Gidioni, kiongozi wa uzao wa Benjamini, alitoa sadaka yake.61Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.62Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.63Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.64Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.65Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gidioni.66Siku ya kumi, Ahizeri mwana wa Amishadai kiongozi wa Dani alitoa sadaka yake.67Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.68Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.69Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.70Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.71Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja, kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahizeri mwana wa Amishadai.72Siku ya kumi na moja. Pagieli mwana wa Okrani kiongozi wa uzao wa Asheri alitoa sadaka yake.73Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.74Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.75Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga. Dume la kondoo moja, dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.76Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.77Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.78Siku ya kumi na mbili. Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa uzao wa Naftali, alitoa sadaka yake.79Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.80Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilicho jaa ubani.81Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na mwanakondoo dume moja wa mwaka mmoja.82Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.83Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahra mwana wa Enani.

84Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na mbili vya dhahabu.85Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ya fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedha vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2,400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu.86Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120.87Waliwatenga wanyama wote kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, fahari kumi na wawili, kondoo dume kumi na wawili, na wanakondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja mmoja. Walitoa sadaka yao ya unga. Walitoa beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi.88Kutokana na ng'ombe zao, walitoa fahari ishirini na nne, kondoo dume sitini beberu sitini, na wanakondoo dume sitini wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa kwa ajili ya kuiweka wakfu ile madhabahu baada ya kumiminiwa mafuta.

89Musa alipoingia kwenye hema ya kukutania kusema na BWANA, ndipo alipoisikia sauti yake ikisema naye. BWANA alinena naye kutoka juu ya kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, kutoka katikati ya makerubi. Alinena naye.

8

1BWANA akanena na Musa, akamwambia,2“Sema na Haruni umwambie, ‘zile taa saba lazima zimulike mbele ya kinara utakapoziwasha,”

3Haroni alifanya haya. Aliziwasha zile taa juu ya kinara ili ziangaze mbele yake kama BWANA alivyomwagiza Musa.4Kinara kilitengenezwa kwa njia hii kama BWANA alivyomwelekeza Musa muundo wake. Kiitakaiwa kutengenezwa kwa dhahabu kuanzia kwenye kitako chake hadi juu, ndivyo kilivyotakiwa kutengenezwa kwa dhahabu kwa maua hadi juu.

5Tena, BWANA akanena na Musa, akasema,6‘“Uwatwae Walawi kati ya wana wa Israeli na uwatakase.”7Uwafanyie hivi ili kuwatakasa: Uwanyunyizie maji ya utakaso juu yao. Hakikisha wamenyoa miili yao yote, wafue nguo zao, na kwa njia hii wajitakase wenyewe.8Kisha wachukue fahari mchanga na sadaka ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta. Halafu wachukue fahari mchanga kwa ajili ya sadaka ya dhambi.9Uwalete Walawi mbele ya hema ya kukutania, na uwakusanye jamii yote ya wana wa Israeli.10Uwalete Walawi mbele ya Bwana, wana wa Israeli wataweka mikono yao juu ya Walawi.11Haruni atawatoa Walawi mbele yangu, kuwa sadaka ya kutikiswa. Atafanya hivi ili kwamba Walawi wanitumikie.

12Walawi wataweka mikono yao juu ya hao fahari. Mtatoa fahari mmoja kuwa sadaka ya dhambi na fahari mwingine kuwa sadaka ya kuteketezwa kwangu, ili kuwa upatanisho kwa Walawi.13Walete Walawi mbele ya Haruni na mbele ya wana wake, uwainue kuwa sadaka ya kutikiswa kwa ajili yangu.14Kwa njia hii, utawatenganisha Walawi toka wana wa Israeli. Walawi watakuwa wangu.

15Baadaye, Walawi wataingia ndani ya hema ya kukutania. Utawatakasa. Utawatoa kuwa sadaka ya kutikiswa16Fanya hivi kwa sababu wao ni wangu wote kutoka kwa wana wa Israeli. Watachukua nafasi ya kila mzaliwa wa kwanza afunguaye tumbo, mzaliwa wa kwanza wa uzao wa Israeli. Nimewachukua Walawi kwa ajili yangu.17Wazaliwa wa kwanza wote kutoka kwa wana wa Israeli ni wangu, watu wote pamoja na wanyama pia. Siku ile nilipowachukua wazaliwa wa kwanza katika nchi ya Misri, Niliwatenga kwa ajili yangu18Nimewachukua Walawi kutoka kwa wana wa Israeli badala ya wazaliwa wa kwanza.19Nimewatoa Walawi kuwa zawadi kwa Haruni na wana wake. Nimewachukua kutoka kwa wana wa Isreali ili kuwatumikia wana wa Israeli katika hema ya kukutania. Nimewatoa ili kuwa upatanisho kwa watu ili kwamba wasipatwe na mapigo wakati wanapokaribia kwenye eneo takatifu.

20Musa, Haruni na jamii ya Waisraeli wote waliwafanyia Walawi hivi. Walifanya kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru Musa kuhusu Walawi. Wana wa Israeli wakafanya haya pamoja nao.21Walawi wakajitakasa wenyewe na kufua mavazi yao, Na Haruni akawatoa kama sadaka ya kutikiswa kwa BWANA na akafanya upatanisho kwao ili kuwatakasa.22Baada ya hayo, Walawi waliingia ndani kufanya utumishi wao katika hema ya kukutania mbele ya Haruni na mbele ya wanawe. Kama BWANA alivyokuwa amemwagiza Musa juu ya Walawi. Waliwahudumia Walawi wote kwa jinsi hii.

23BWANA akanena na Musa tena, Akasema,24“Haya yote ni kwa ajili ya Walawi ambao wana umri wa miaka ishirini na mitano na zaidi. Wataungana na wale wanaohudumia hekaluni.25Wataacha kutoa huduma hii watakapokuwa na umri wa miaka hamsini. Katika umri huu hawatakiwi kuendelea na huduma tena.26Wanaweza kuwasaidia ndugu zao wanaoendelea kufanya kazi ndani ya hema ya kukutania, lakini hawatakiwi kufanya kazi tena. Utawaelekeza Walawi kuyafahamu haya yote.”

9

1BWANA akanena na Musa katika jangwa la Sinai, mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili baada ya kutoka katika nchi ya Misri. Akasema,2“Wana wa Israeli wataikumbuka Pasaka katika wakati wake kila mwaka.3Siku ya kumi na nne ya mwezi huu, muda wa jioni, utaikumbuka Pasaka kila mwaka kwa muda uliopangwa. Lazima uikumbuke, fuata taratibu zake zote na utii sheria zake zote zinazohusiana na tukio hilo.

4Kwa hiyo, Musa akawaambia wana wa Isareli kuwa wataishika sikukuu ya Pasaka.5Kwa hiyo wakaishika siku ya Pasaka katika mwezi wa kwanza, wakati wa jioni wa siku ya kumi na nne ya mwezi katika jangwa la Sinai. Wana wa Israeli walitii kila kitu ambacho BWANA alimwamuru Musa kukifanya.

6Kulikuwa na watu fulani walionajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Hawakuweza kuishika Pasaka siku hiyo. Kwa hiyo walikwenda kwa Musa na Haruni siku hiyo hiyo.7Wakamwambia Musa, “Sisi tumenajisika kwa sababu ya maiti ya mtu. Kwa nini basi unatutaka tuendelee kutoa sadaka kwa BWANA kwa wakati wa mwaka uliopangwa kwa wana wa Israeli?”

8Naye Musa akawaambia, “Subirini nimsikilize BWANA ataniambia nini juu Yenu.”

9BWANA akanena na Musa, akamwambia,10“Nena na wana wa Israeli, uwaambie, ‘kama mmoja wenu au mwana wa uzao wenu amenajisika kwa sababu ya maiti, au ana safari ndefu, bado anaweza kuishika Pasaka ya BWANA.11Wataishika Pasaka siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili wakati wa jioni. Wataila kwa mikate isiyotiwa chachu na mboga chungu.12Wasiiache mpaka jioni, au kuvunja mifupa yake. Watafuata taratibu zote za Pasaka.13Lakini mtu yeyote asiye najisi na hayuko safarini, na akashindwa kuishika Pasaka, huyo mtu lazima aondolewe kati ya watu wake kwa sababu hakutoa sadaka ambayo BWANA huitaka kwa wakati wa mwaka uliopangwa. Huyo mtu lazima aibebe dhambi yake.

14Kama mtu mgeni anayeishi kati yenu na akaishika, Pasaka kwa heshima ya BWANA, ataishika na kufanya amri zote, na kutii taratibu zake. Utakuwa na sheria hizo hizo kwa wageni na kwa wote waliaozaliwa katika nchi.

15Na siku hiyo ambayo masikani iliposimamishwa, wingu lilifunika masikani, ile hema ya amri ya agano. Ilipokuwa jioni, wingu lilkuwa juu ya masikani. Lilionekana kama moto mpaka asubuhi.16Liliendelea hivyo hivyo. Lile wingu lilifunika masikani na kuonekana kama moto wakati wa usiku.17Na kila wingu lilipochukuliwa kutoka kwenye hema, wana wa Isareli waliendelea na safari yao. Na kila wingu liliposimama, watu waliweka kambi.18Wana wa Israeli walisafiri kwa amri ya BWANA, na kwa amri yake waliweka kambi. Wakati wingu liliposimama juu ya masikani, nao walikaa kwenye kambi zao.19Na wingu lilipobaki kwenye masikani kwa siku nyingi, wana wa Israeli walitakiwa kutii maelekezo ya BWANA na kusitisha safari yao.20Wakati mwingine wingu lilibaki kwa siku chache tu kwenye masikani. Kwa mazingira kama hayo walilazimika kutii amri ya BWANA - waliweka kambi na kisha kuendelea na safari tena kwa amri yake.21Wakati mwingine wingu lilikuwepo kambini kuanzia jioni mpaka asubuhi. Na wingu liliponyanyuliwa asubuhi, walisafiri. Kama liliendelea kwa mchana wote na kwa usiku wote, ni pale tu wingu liliponyanyuliwa ndipo walipoendelea na safari.22Hata kama wingu lilibaki kwenye masikani kwa siku mbili, kwa mwezi mmoja, au kwa mwaka mmoja, ili mradi tu limebaki pale, wana wa Israeli walibaki kwenye kambi zao na kusitisha safari. Lakini pale wingu liliponyanyuliwa, walianza safari yao.23Walifanya kambi kwa amri ya BWANA, na walisafiri kwa amri yake. Walitii amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa.

10

1BWANA alinena na Musa, akasema,2“Tengeneza tarumbeta mbili za fedha. Uzitengeneze kwa kufua hizo fedha. Utazitumia hizo tarumbeta kwa kuwaita watu waje pamoja na kwa kuwaita watu wote wakati wa kuondoka kwenye kambi zao.3Makuhani watapiga tarumbeta kwa ajili ya kuwaita watu wote mbele yako kwenye lango la hema ya kukutania.4Kama makuhani watapiga tarumbeta moja tu, basi viongozi, wakuu wa koo za Israeli watakutana kwako.5Utakapopiga tarumbeta ya sauti kuu, ile kambi ya upande wa mashariki itaanza kusafiri.6Nawe utakapopiga tarumbeta kwa sauti kuu mara ya pili, ile kambi ya upande wa kusini wataanza kusafiri. Watapiga tarumbeta kwa sauti kuu ili kuanza safari yao.7Watu wote watakapokutana pamoja, piga hizo tarumbeta lakini si kwa sauti kuu.

8Wana wa Haruni, makuhani, watapiga hizo tarumbeta. Huu ndio utakaokuwa utaratibu wa watu wako kwa vizazi vyote.9Nanyi mtakapoenda vitani katika ardhi yenu dhidi ya maadui wenu wanaowakandamiza, ndipo mtakapotoa ishara ya sauti ya tarumbeta. Mimi, BWANA Mungu wako nitawaita kuwakumbuka na kuwaokoa kutoka kwa maadui wenu.10Pia, wakati wa kusherehekea, sikukuu zenu za kawaida na katika miandamo ya miezi, mtapiga tarumbeta zenu kwa heshima ya sadaka zenu za kuteketezwa na kwa sadaka zenu za amani. Huu utakuwa ukumbusho wenu kwangu, Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.”

11Katika siku ya ishirini, mwezi wa pili, mwaka wa pili, Lile wingu liliinuliwa toka masikani ya amri za maagano.12Wana wa Israeli wakaendelea na safari yao toka jangwa la Sinai. Lile wingu likasimama kwenye jangwa la Parani.13Walifanya safari yao ya kwanza, kufuatia amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa.

14Kambi ya mahali pa uzao wa Yuda iliondoka ya kwanza, wakiondoa majeshi yao binafsi. Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyeongoza jeshi la Yuda.15Nethaneli mwana wa Zuari aliongoza jeshi la kabila la uzao wa Isakari.16Eliabu mwana wa Heloni aliongoza jeshi la kabila la Zabuloni.17Uzao wa Gerishoni na Merari, ambao walitunza masikani, na kuanza kusafiri.

18Baadaye Walifuata jeshi la mahali pa kambi ya Reubeni walianza safari yao. Elizuri mwana wa Shedeuri alliongoza jeshi la Reubebni.19Shelumieli mwana wa Zurishadai aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Simeoni.20Eliasafu mwana Deuli aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Gadi.21Kabila la Kohathi nalo lilianza safari. Wao walibeba vyombo vya mahali patakatifu. Wengine waliisimamisha masikani kabla ya Wakohathi kufika kambi inayofuata.

22Majeshi ya kabila la uzao wa Efraimu ndio waliofuata. Elishama mwana wa Amihudi ndiye aliyeongoza jeshi la Efraimu.23Gamalieli mwana wa Pedazuri aliongoza jeshi la uzao wa Manase.24Abidani mwana wa Gidioni aliongoza jeshi la uzao wa kabila la Benjamini.

25Lile jeshi lililoweka kambi mahali pa bango la uzao wa Dani lilikuwa la mwisho kuondoka. Ahizeri mwana wa Amishadai ndiye aliyeongoza jeshi la Dani.26Pagieli mwana wa Okirani aliongoza jeshi la wana wa uzao wa Asheri.27Ahira mwana wa Enani aliongoza jeshi la uzao wa kabila ya Naftali.28Hivi ndivyo majeshi ya wana wa Israeli yalivyo safiri.

29Musa alinena na Hobibu mwana wa Reueli wa kabila la Midiani. Reueli alikuwa baba mke wa Musa. Musa akanena na Hobibu akasema, “Tunasafiri kuelekea mahali ambapo BWANA ametuahidi. BWANA alisema kuwa, “Nitawapeni ninyi hilo eneo, ‘Njooni pamoja nasi na tutawatendea mema. BWANA ameahidi kuwafanyia mema Waisraeli.”

30Lakini Hobibu akamwambia Musa, “Sitaambatana nanyi.”

31Naye Musa akamjibu, “Tafadhali msituache. Mnajua jinsi ilivyo kuweka kambi jangwani. Tunaomba mtujali.32Kama mtaambatana nasi tutawatendea mema sawa na jinsi BWANA anavyotutendea.”

33Walisafiri kutoka mlima wa BWANA kwa siku tatu. Sanduku la agano la BWANA liliwatangulia kwa siku tatu ili kupata mahali pa kupumzika.34Wingu la BWANA lilikuwa juu yao muda wote wa mchana walipokuwa safarini.

35Kila hilo sanduku liliposafiri kwenda mbele, Musa alisema, “Inuka BWANA, Uwatawanye maadui wako. Uwafanye wale wanaokuchukia kukukimbia.”

36Na kila lile sanduku liliposimama, Musa alisema, “BWANA uwarudie, hawa Waisraeli makumi elfu.”

11

1Sasa watu wakanung'unika juu ya matatizo yao wakati BWANA alipokuwa akiwasikiliza. BWANA akawasikia watu naye akakasirika. Moto kutoka kwa BWANA ukashuka na ukawaka kati yao na kuteketeza baadhi ya kambi kwenye pembe zake.2Ndipo watu wakamwita Musa kwa nguvu, Naye Musa akamwomba BWANA, na ule moto ukazimika.3Mahali pale paliitwa Tabera, kwa sababu moto wa BWANA uliwaka kati yao.

4Baadhi ya wageni wakaanza kuweka kambi zao pamoja na wana wa Israeli. Walitaka kula chakula kizuri. Kisha wana wa Israeli walipoanza kulia wakisema, “Ni nani atakayetupatia nyama za kula?5Tunakumbuka samaki tulizokula bure kule Misri, yale matango, na matikiti maji, na mboga na vitunguu na vitunguu saumu.6Na sasa hatuna hamu ya kula, kwa sababu tunaona mana tu.

7Mana ilifanana na punje ya mtama. Ilionekana kama bedola.8Watu wakazunguka kisha wakakusanyika. Wakaisaga, wakaitwanga kwa vinu, wakaitokosa nyunguni, na kuitengeneza mikate. Ladha yake ilikuwa kama mafuta mapya ya mizeituni.9Na umande ulipoanguka kambini usiku ule, na mana ilianguka pia.

10Musa akawasikia watu wakilia katika familia zao, na kila mtu alikuwa kwenye lango la hema yake. BWANA alikasirika sana, na mbele ya macho ya Musa malalamiko yao yalikuwa mabaya.11Musa akasema na BWANA, “Kwa nini umemtendea mtumishi wako vibaya namna hiyo? Kwa nini hujapendezwa na mimi? Unanifanya kubeba mizigo ya hawa watu.12Je, mimi ndiye niliyewatungia mimba hawa watu? Mimi ndiye niliyewazaa kiasi kwamba unaniambia, “Wabebe kwa ukaribu vifuani mwako kama baba abebavyo mtoto wake? Je, nitawabeba mpaka kwenye nchi ambayo uliwaahidi mababu zao kuwapa?13Naweza kupata wapi nyama za kuwapa watu wote hawa? Wanalia mbele zangu na wanasema, ‘Tupe nyama tule.’14Mimi peke yangu siwezi kuwabeba watu wote hawa. Ni wengi sana kwangu.15Kwa vile unanitendea hivi, basi uniue, na kama wewe ni mpole kwangu, basi niondolee mzigo huu.”

16BWANA akamwambia Musa, “Niletee wazee sabini miongoni mwa Waisraeli. Hakikisha ni wazee na viongozi wa watu. Uwalete kwenye hema ya kukutania wasimame pamoja na wewe.17Nami nitashuka niseme nawe mahali pale. Nitatoa sehemu ya roho iliyo ndani yako na kuwapatia wao. Nao watabeba mzigo wa watu pamoja nawe. Na hautaubeba peke yako.

18Waambie watu, ‘Jitakaseni ninyi wenyewe, kwa kuwa kesho mtakula nyama, kwa kuwa mmelia na BWANA amesikia, “Mlipokuwa mkisema kuwa nani atakayetupa nyama tule? Kule Misri tulikula chakula kizuri!” Kwa hiyo BWANA atawapeni nyama, nanyi mtakula nyama.19Hamtakula nyama kwa siku moja tu, au siku mbili, au siku tano, au siku kumi, au siku ishirini,20Lakini mtakula nyama kwa mwezi mmoja mpaka zitakapowatokea puani. Mpaka mtazikina kwa sababu mmemkataa BWANA ambaye yuko kati yenu. Mmelia mbele yake. Mmesema, “Kwa nini tulitoka Misri?”’”

21Kisha Musa akasema, “Mimi nina watu 600,000, na wewe umesema, “Nitawapa nyama mle kwa mwezi mmoja,’22Je, tutayachinja haya makundi ya ng'ombe na kondoo ili kuwatosheleza?”23BWANA akasema na Musa, “Je mkono wangu ni mfupi? Sasa utaona kama maneno yangu ni ya kweli ama sivyo.

24Musa alitoka nje kwenda kuwaambia watu maneno ya BWANA. Aliwakusanya wazee sabini wa watu na kuwaweka kuizunguka hema.

25BWANA akashuka chini katika wingu akaongea na Musa. BWANA akachukua sehemu ya roho iliyokuwa kwa Musa na kuiweka kwa wale wazee sabini. Roho alipowashukia, wakaanza kutoa unabii, lakini ilitokea kwenye tukio hilo tu na haikujirudia tena.

26Watu wawili waitwao Elidadi na Medadi walibaki kambini. Lakini Roho aliwashukia pia. Majina yao yalikuwa yameandikwa kwenye orodha lakini walikuwa hawajaenda hemani. Hata hivyo nao walitoa unabii wakiwa kambini.27Kijana mmoja huko kambini alikimbia akaenda kumwambia Musa, “Elidadi na Medadi wanatoa unabii kambini.”

28Joshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Musa, ambaye ni miongoni mwa wale aliowachagua akamwambia Musa, “Bwana wangu Musa, wazuie.”

29Musa akamwambia, “una wivu kwa niaba yangu? Natamani kama watu wote wa BWANA wangekuwa manabii na kwamba angeweka Roho yake juu yao wote!”30Kisha Musa na wale wazee wakarudi kambini.

31Kisha upepo ukavuma kutoka kwa BWANA ukaja na kware kutokea baharini. Wakaanguka karibu na kambi, kiasi cha umbali wa safari ya siku moja upande huu na umbali wa siku moja upande mwingine. Wale kware wakaizunguka kambi kiasi cha mita moja toka uso wa dunia.32Watu wakawakusanya hao kware kwa bidii mchana huo wote na usiku huo wote, na mchana wote uliofuatia. Hakuna aliyekusanya pungufu ya mita mbili za ujazo. Wakawaanika kweye ardhi yote hapo kambini.33Wakati ile nyama ikiwa bado iko kwenye meno yao, wakiwa bado wanatafuna, BWANA akawakasirikia. Akawapiga watu wale kwa ugonjwa mkubwa sana.34Mahali pale pakaiitwa Kibroti Hataava, kwa sababu pale walizika watu waliotamani nyama.

35Kutoka Kibroti Hataava watu wakasafiri hadi Hazeroti, ambapo walipumzika.

12

1Kisha Miriamu na Haruni wakasema kinyume na Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi ambaye alikuwa amemwoa.2Walisema, “Hivi BWANA amesema na Musa tu? Ni kweli hajawahi kusema nasi pia?” Sasa BWANA akasikia kile walichokuwa wanaongea. Sasa

3Musa alikuwa mtu mpole sana, mpole kuliko mtu yeyote duniani.

4Wakati huo, BWANA akanena na Musa, Haruni na Miriamu: “Tokeni nje ninyi watatu kwenye hema ya kukutania.” Kwa hivyo wale watatu wakatoka nje.5Kisha BWANA akashuka katika nguzo ya wingu. Akasimama kwenye lango la hema na akamwita Haruni na Miriamu. Wote wakaja mbele.6BWANA akasema, “Sasa sikilizeni maneno yangu, Nabii wangu anapokuwa nanyi, Mimi nitajifunua kwake kwa maono na kusema naye katika ndoto.
7Lakini si hivyo kwa mtumishi wangu Musa. Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
8Mimi huongea na Musa moja kwa moja, si kwa maono wala mafumbo. Yeye huniona umbo langu. Kwa hiyo, kwa nini hamuogopi kumnenea kinyume, mtumishi wangu Musa?”

9Hasira ya BWANA ikawawakia, kisha akawaacha.

10Lile wingu likainuka juu ya hema, Miriamu akapata ukoma ghafla - akawa mweupe kama theluji. Naye Haruni alipogeuka kumwona Miriamu, akamwona amepata ukoma.11Haruni akamwambia Musa, “Bwana wangu, usituadhibu kwa uovu wetu huu. Tumenena katika upumbuvu, na tumetenda dhambi.12Tafadhali nakuomba usimwache akawa kama mtoto mchanga aliyekufa ambaye nusu ya nyama yake imeoza tangu kuzaliwa”

13Kwa hivyo Musa akamwomba BWANA, akasema, “Mungu ninakusihi umponye tafadhali.”

14BWANA akamwambia Musa, “kama baba yake angemtemea mate usoni angepata aibu kwa muda wa siku saba. Umfungie nje ya kambi kwa muda wa siku saba Kisha umrejeshe ndani tena.”15Kwa hivyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba. Watu hawakusafiri mpaka aliporudi kambini.

16Kisha watu wakasafiri kutoka Hazeroti na kuweka kambi kwenye jangwa la Parani.

13

1Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia, “Tuma watu waende kuipeleleza nchi ya Kanani, ambayo nimewapa wana wa Israeli.2Tuma mwanaume mmoja kutoka kila jamaa ya kabila. Kila mwanaume awe kiongozi katika kabila lake.”

3Musa akawatuma kutoka jangwa la Parani, ili watii amri ya BWANA. Watu wote hao walikuwa viongozi wa watu wa Israeli.4Majina yao yalikuwa haya yafuatayo: kutoka kabila la Reubeni, Shamua mwana wa Zakuri;
5Kutoka kabila la Simeoni, Shafati mwana wa Hori;
6Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune;
7Kutoka kabila la Isakari, Igali mwana wa Yusufu,
8Kutoka kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Nuni;
9Kutoka kabila la Benjamini, Paliti mwana wa Rafu;
10kutoka kabila ya Zabuloni, Gadieli mwana wa Sodi;
11kutoka kabila la Yusufu (hiyo inamaanisha kutoka kabila la Manase), Gadi mwana wa Susi;
12kutoka kabila la Dani, Amieli mwana wa Gemalili;
13Kutoka kabila Asheri, Setu mwana wa Mikaili;
14Kutoka kabila la Naftali, Nabi mwana wa Vofisi;
15Kutoka kabila la Gadi, Geuli mwana wa Machi.
16Haya ndiyo majina ya wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuipeleleza ile nchi. Musa akamwita Hoshea mwana wa Nuni kwa jina la Joshua.

17Musa akawatuma kwenda kuipeleleza ile nchi ya Kanani. Naye akawaambia, “Mkaanzie Negebu hadi mahali pa milima.18Kaipelelezeni nchi kujua ni nchi ya namna gani. Wachunguzeni watu wake, kama ni watu wenye nguvu au dhaifu, kama ni wachache au ni wengi.19Chunguzeni nchi hiyo wanayoishi ni nchi ya namna gani. Ni nzuri au mbaya? Miji yao ikoje? Je iko kama kambi au ni miji yenye ngome?20Chunguzeni ni nchi ya namna gani, kama ni njema kwa mazao au la kama kuna miti au hapana. Muwe hodari mkalete sampuli za mazao ya nchi,” Sasa ni muda wa msimu wa malimbuko ya mizabibu.

21Kwa hivyo wale wanaume wakaenda kuipeleleza ile nchi kutoka jangwa la Sini mpaka Rehobi, karibu na Lebo Hamati.22Walienda kutoka Negebu nao wakafika Hebroni. Ahimani, Sheshai, na Talmai, Uzao wa Anaki nao walikuweko, Sasa Hebroni ilikuwa imejengwa miaka saba iliyokuwa imepita kabla ya Zoani wa Misri.23Nao walipofika katika bonde la Eshikoli, walikata tawi la mizabibu lenye kishada cha zabibu. Na makundi mawili ya wapelelezi wakakibeba kwenye mti. Pia wakaleta makomamanga na mtini.24Mahali pale paliitwa Eshikoli, kwa sababu ya kishada cha mizabibu ambacho wana wa Israeli walikata kule.25Baada ya siku arobaini, wakarudi kutoka kuipeleleza nchi.

26Wakaja kwa Musa, Haruni na kwa watu wote wa Israeli katika jangwa la Parani, kule Kadeshi. Wakaleta taarifa kwao na kwa Waisraeli wote, na kuwaonyesha matunda ya nchi ile.27Wakamwambia Musa, “Tulifika katika ile nchi uliyotutuma. Kwa hakika ni nchi ya kutiririka maziwa na asali. Na baadhi ya matunda yake ni haya hapa.28Hata hivyo, watu wanaoishi huko ni wenye nguvu. Miji yao ni mikubwa tena ina maboma. Pia tuliwaona wana wa Anaki huko.29Waamaleki wanaishi Negebu. Wahiti, Wayebusi, na Waamori nao wanaishi katika milima ya hiyo nchi. Wakanaani wanaishi kando ya bahari na mto Yordani.”

30Kisha Kalebu akawatuliza watu waliokuwa mbele ya Musa, akasema, “Twendeni tukaiteke nyara hiyo nchi, kwa kuwa tuna uhakika wa kuikamata.”

31Lakini wale watu waliokuwa wameenda naye walisema, “Hatutaweza kuwashinda hao watu kwa kuwa wao ni hodari kuliko sisi.”32Kwa hiyo wakasambaza taarifa za kukatisha tamaa kwa wana wa Israeli juu ya nchi ile waliyoipeleleza. Walisema, “Ile nchi tuliyoiona ni nchi inayowala watu wake. Watu wote tuliowaona ni watu warefu.33Kule tuliiona majitu, wana wa uzao wa Anaki, ambao ni uzao wa majitu. Sisi tulionekana kama panzi machoni mwao tulipojilinganisha nao, hivyo ndivyo tulivyoonekana machoni mwao pia.”

14

1Usiku huo watu wote walilia kwa sauti.2Watu wote wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haroni. Watu wote wakawaambia, “Ni bora kama tungelifia katika nchi ya Misri, au katika hili!3Kwa nini BWANA alituleta katika nchi hii ili tufe kwa upanga? Wake zetu na watoto wetu watakuwa watumwa wao. Je, si bora kwetu kurudi Misri?”4Wakasemezana wao kwa wao, “Na tuchague kiongozi mwingine, turudi Misri.”

5Ndipo Musa na Haruni wakalala kifudifudi mbele ya kundi lote la wana wa Israeli.6Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune, ambao walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wametumwa kwenda kuipeleleza nchi wakachana mavazi yao.7Wakawaambia watu wote wa Israeli. Walisema, “Ile nchi tuliyopita katikati yake ni nchi nzuri sana.8Kama BWANA amependezwa nasi, basi atatuingiza katika nchi hii na kutupatia. Ile nchi inatiririka maziwa na asali.9Lakini msimwasi BWANA, na msiwahofie hao wakazi wa nchi hiyo. Tutawateketeza kwa urahisi kama kula chakula. Ulinzi wao utaondolewa kutoka kwao, kwa sababu BWANA yuko pamoja nasi. Msiwahofie.”

10Lakini watu wote walitishia kuwapiga kwa mawe mpaka wafe. Kisha utukufu wa BWANA ukaonekana kwenye hema ya kukutania kwa watu wote wa Israeli.11BWANA akamwambia Musa, “watu hawa watanidharau hadi lini? Wataendelea kutoniamini mpaka lini? Licha ya kuwa nimefanya ishara kwa nguvu zangu kati yao?12Nitawapiga kwa mapigo, na kuwaondolea urithi, na kufanya taifa kubwa kutoka kwenye ukoo wako ambao utakuwa mkubwa na wenye nguvu kuliko wao.

13Musa akamwambia BWANA, “Kama utafanya hivi, Na Wamisiri wakisikia habari hizi, na kwa sababu uliwaokoa kutoka kwao kwa nguvu zako.14Basi watawaambia wakazi wa nchi hii. Wamesikia ya kuwa wewe BWANA u kati ya watu hawa, kwa sababu uso wako waonekana. Wingu lako husimama juu ya watu wetu. Wewe huwatangulia katika nguzo ya wingu wakati wa mchana na katika nguzo ya moto wakati wa usiku.15Sasa kama utawaua hawa watu kama mtu mmoja, basi mataifa ambao wamesikia sifa zako watasema,16“Kwa Sababu BWANA hana uwezo wa kuwapeleka watu hawa katika nchi ambayo aliwaapia kuwapa, ndiyo maana amewaua katika jangwa hili.

17Sasa, nakusihi, utumie uweza wako. Kwa kuwa umesema kuwa,18‘BWANA si mwepesi wa hasira na ni mwingi wa uaminifu katika agano. Yeye husamehe uovu na uasi. Kwa vyo vyote vile atafutilia hatia atakapoleta hukumu ya dhambi za mababu juu ya wazaowao, kwa kizazi cha tatu na cha nne.’19Ninakusihi uwasameha watu hawa dhambi zao kwa sababu ya ukuu wa uaminifu wa agano lako, kama vile ambavyo umekuwa ukiwasamehe watu hawa tokea wakati wakiwa Misri mpaka sasa.”

20BWANA akasema, Nimewasamehe kama ulivyoomba,21bali kama Niishivyo, na kama vile dunia yote itakavyojazwa na utukufu wangu,22Watu wote walioona utukufu wangu na ishara za nguvu zangu nilizotenda kule Misri na kule jangwani - Lakini bado wamenijaribu mara kumi sasa na hawakuisikiliza sauti yangu.23Kwa hiyo nasema kwamba hakika hawataiona nchi ile ambayo niliwaahdi kuwapa mababu zao. Hakuna hata mmoja wao ambao wamenidharau watakaoiona,24isipokuwa mtumishi wangu Kalebu, kwa sababu alikuwa na roho nyingine. Yeye amenifuata kwa ukamilifu; Yeye nitampeleka katika nchi hiyo ambayo alienda kuipeleleza. Wazao wake wataimilki.25(Sasa Waamaleki na Wakanani waliishi katika bonde.) Kesho mtageuka na kwenda katika jangwa kwa njia ya bahari ya Shamu.”

26BWANA akanena na Musa na Haruni, akasema,27“Nitaivumilia jamii ya watu hawa waovu ambao wananinung'unikia mpaka lini? Nimeyasikia malalamiko ya wana wa Israeli dhidi yangu.28Waambie, ‘Kama niishivyo,’ asema BWANA, ‘Kama vile mlivyosema katika masikio yake, nitawafanyia jambo hili:29Maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili, ninyi nyote mliolalamika dhidi yangu, ninyi mliohesabiwa kwenye ile sensa, idadi yote ya watu kuanzia umri wa mika ishirini na kuendelea.30Kwa hakika hamtaingia kwenye ile nchi ambayo niliahidi kuwapa kuwa makazi yenu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.31Bali watoto wenu ambao mlisema kuwa watakuwa watumwa, wao ndio nitakaowapeleka katika nchi hiyo. Wao wataifurahia nchi ambayo ninyi mmeikataa!32Lakini ninyi, maiti zenu zitaanguka katika jangwa hili.33Watoto wenu watakuwa wachungaji katika jangwa hili kwa muda wa miaka arobaini. Lazima watabeba madhara ya matendo yenu ya kutokuamini mpaka mwisho wa maiti ya mwisho jangwani.34Kama vile ilivyo hesabu ya siku ambayo mliipeleleza nchi--siku arobaini, vivyo hivyo mtabeba madhara ya dhambi zenu kwa muda wa miaka arobaini--mwaka mmoja kwa kila siku moja, na mtajua kuwa ni sawa na kuwa adui yangu.35Mimi BWANA nimesema. Hakika nitafanya hivi kwa kizazi hiki chote kiovu ambacho kimekusanyika kinyume na Mimi. Wao watakatwa kabisa, na watafia hapa.’”

36Kwa hiyo wale wanaume ambao Musa aliwatuma kwenda kuingalia ile nchi wote walikufa kwa tauni mbele ya BWANA.37Hawa ni wale ambao waliorudi na kutoa taarifa mbaya juu ya nchi. Hii iliwafanya watu wote wamlalamikie Musa.38Kati ya watu wale waliokuwa wameenda kuiangalia nchi ile, ni Joshua mwana wa Nuni na Kalebu mwana wa Yefune tu ndio waliobaki hai.

39Musa alipowataarifu mambo haya watu wote wa Israeli waliomboleza sana.40Waliamka asubuhi na mapema wakaenda juu ya mlima na kisha wakasema, “Tazama, tuko hapa, na tutaenda mahali pale ambapo BWANA ametuahidi, kwa kuwa tumetenda dhambi.”

41Lakini Musa akasema, “Kwa nini sasa mnapinga amri ya BWANA? Hamtafanikiwa.42Msiende, kwa sababu BWANA hayuko pamoja nanyi kuwalinda dhidi ya maadui zenu.43Waamaleki na Wakanaani wako kule, na mtakufa kwa upanga kwa sababu mliumtegea mgongo BWANA na hamkumfuata. Kwa hivyo hatakuwa pamoja nanyi.

44Lakini walithubutu kukwea mlimani; lakini si Musa wala Sanduku la agano la BWANA walio ondoka kambini.45Kisha Waamaleki walikuja chini, pia wale Wakanaani walioshi kwenye hiyo milima. Wakawavamia Waisreli wakawapiga na kuwaangusha mpaka Horima.

15

1Kisha BWANA akanena na Musa, akasema,2“Sema na wana wa Israeli uwaambie, ‘Mtakapoingia katika nchi ambayo mtaishi, ambayo BWANA atawapa,3mtatakiwa kuandaa sadaka kwa moto kwa BWANA, sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kukamilisha kiapo au sadaka ya hiari, au sadaka katika sikukuu zenu, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA ya ng'ombe au ya kondoo.4Utamtolea BWANA sadaka ya kuteketezwa pamoja na sehemu ya kumi ya efa ya sadaka ya unga mwembamba uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta.5Na tena mtatoa pamoja na sadaka ya kuteketezwa, au kwa sadaka ya divai robo ya hini ya sadaka ya vinywaji kwa kila mwanakondoo.

6Kama unatoa sadaka ya kondoo dume, utaandaa sadaka ya unga ya sehemu za kumi mbili za efa ya unga mwembamba uliochanganywa na sehemu ya tatu ya hini ya divai.7Kwa sadaka ya kinywaji, mtatoa sehemu ya tatu ya hini ya divai ambayo itatoa harufu nzuri kwa BWANA.

8Utakapoandaa fahari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya kutimiza kiapo, au sadaka ya amani kwa BWANA,9Ndipo utakapotoa sadaka ya fahari pamoja na sadaka ya unga ya sehemu za kumi tatu za unga mwembamba uliochanganywa na nusu ya hini ya mafuta.10Mtatoa sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai, sadaka iloyotengenezwa kwa moto ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.11Itafanyika hivi kwa kila fahari, kwa kila kondoo dume, na kila mwanakondoo dume au mbuzi mchanga.12Kila sadaka utakayoindaa na kuitoa itafanyika kama ilivyoanishwa hapa.

13Wazawa wote wa Israeli watafanya mambo haya kwa utaratibu huu, yeyote atakayeleta sadaka iliyotengenezwa kwa moto, ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA.14Na kama kuna mgeni anayeishi kati yenu, au yeyote atakayeishi na watu wa vizazi vyenu vyote, lazima atengeneze sadaka iliotengenezwa kwa moto, ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Atafanya kama mnavyofanya.15Kutakuwa na sheria hiyo hiyo kwa watu wote na kwa mgeni anayeishi kati yenu, sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Ninyi mlivyo, ndivyo atakavyokuwa mgeni aliyeishi kati yenu. Atafanya kama mnavyofanya mbele ya BWANA.16Sheria na amri hiyo hiyo ndiyo itakayotumika kwa mgeni anayeishi kati yenu.”

17Tena BWANA akanena na Musa, akasema,18“Nena na wana wa Israeli uwaambie, ‘mtakapofika katika nchi ninayowapeleka,19Mtakapokula chakula kinachozalishwa katika nchi hiyo, mtatoa sadaka ya kunipendeza mimi.20Kutoka kwenye mikate yenu ya kwanza mtatoa mkate wa kuinuliwa kama sadaka iliyoinuliwa kutoka mahali pa kupuria nafaka. Mtainua kwa jinsi hii.21Watu wa uzao wako wote watanitolea sadaka ya kuinuliwa kutoka kwenye unga wenu wa kwanza.

22Wakati mwingine mtafanya dhambi pasipo kukusudia, Kama hamtatii amri zote hizi ambazo nimemwambia Musa23-kila kitu ambacho nimewaamuru kupitia Musa kuanzia siku ambayo nilianza kuwaamuru na kuendelea kwa watu wote wa uzao wako.24Kwa swala la dhambi isiyokusudiwa ambayo watu wote hawaijui, basi watu wote watatoa fahari mchanga sadaka ya kuteketezwa ili kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Pamoja na haya yote, lazima itengenezwe sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji, kama ilivyoagaizwa katika amri, na beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.25Kuhani atafanya sadaka ya upatanisho kwa watu wote wa Israeli. Watasemehewa kwa sababu dhambi haikukusudiwa. Wametoa sadaka yao, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili yangu. Wameleta sadaka yao kwangu iliyotengenezwa kwa moto. Wameleta sadaka yao ya uovu mbele yangu kwa ajili ya kosa lao.26Ndipo watu wote wa Israeli watasamehewa, pia wageni wote wanaoishi kati yao, kwa sababu watu wote walitenda dhambi pasipo kukusudia.

27Kama mtu atatenda dhambi bila kukusudia, atatoa mbuzi jike wa umri wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya dhambi.28Naye kuhani atafanya upatanisho kwa BWANA kwa ajili ya mtu yule aliyefanya dhambi pasipo kukusudia. Yule mtu atasamehewa baada ya upatanisho kufanyika.29Mtakuwa na sheria hiyo hiyo kwa mtu yeyote anayefanya dhambi hiyo pasipo kukusudia, sheria hiyohiyo hata kwa mzawa wa Israeli na kwa wageni wanaoishi kati yao.

30Lakini mtu afanyaye chochote kwa Kukusudia, awe mzawa au mgeni, ananifukuru mimi. Huyo mtu ataondolewa kati ya watu wake.31Kwa sababu atakuwa amedharau neno langu na amevunja neno na amri yangu, mtu huyo ataondolewa kabisa. Dhambi yake itakuwa juu yake.’”

32Wakati wana wa Israeli walipokuwa katika jangwa, wakamuona mwanaume akikusanya kuni siku ya Sabato.33Wale waliomwona wakamleta kwa Musa, Haruni na kwa watu wote.34Wakamweka kifungoni kwa sababu ilikuwa haijaamuliwa atakachotendewa.35Kisha BWANA akanena na Musa, “Yule mwanaume lazima auawe. Watu wote lazima wampige kwa mawe nje ya kambi.”36Kwa hiyo watu wote wakamtoa nje ya kambi nao wakampiga kwa mawe mpaka akafa kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.

37BWANA akanena na Musa tena, akasema,38“Waambie wana wa Israeli na uwaamuru wajifanyie vishada wavining'inize katika mapindo ya mavazi yao, wavining'ineze katika ncha zote kwa nyuzi za rangi ya samawati. Watu wote watafanya hivi kwa watu wote wa kizazi chote.39Huu utakuwa ukumbusho maalumu kwenu, kila mtakapovitazama, mtakumbuka amri zangu, na kuzishika ili kwamba msije mkatangatanga katika mioyo na macho yenu na kuwa waasherati wa hayo.40Fanyeni hivi ili kwamba mweze kukumbuka na kutii amri zangu zote, na ili kwamba mpate kuwa watakatifu, waliotunzwa kwa ajili yangu, Mungu wenu.41Mimi ndimi BWANA Mungu wenu niliyekutoa toka nchi ya Misri, ili niwe Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.”

16

1Sasa Kora mwana wa Izihari mwana wa Kohathi mwana wa Lawi, pamoja na Dathani na Abiramu mwana wa Eliabu, na Oni mwana wa Peleti, wa uzao wa Reubeni, waliwakusanya wanaume kadhaa.2Wakamwinukia Musa, pamoja na wanaume fulani kutoka wana wa Israeli, viongozi wa watu wapatao mia mbili na hamsini waliokuwa wakifahamika katika ile jamii.3Walikusanyika pamoja kumpinga Musa na Haruni. Wakawaambia, “Ninyi sasa mnatumia mamlaka zaidi ya uwezo wenu! Watu wote wamejitenga, kila mmoja wao, na BWANA yuko pamoja nao. Kwa nini mnajiinua sana juu ya watu wengine wa BWANA?”

4Musa alipoyasikia hayo, akalala kifudifudi.5Akamwambia Kora na wote aliokuwa nao, “Asubuhi BWANA atafanya ijulikane ni nani walio wake na nani aliyetengwa kwa ajili yake. Atamleta huyo mtu karibu na yeye. Yule anayemchagua atamleta karibu naye.6Fanya hivi, wewe Kora na kundi lako.7Kesho mchukue vyetezo na muweke moto na ubani ndani yake mbele ya BWANA. Yule ambaye BWANA amemchagua, atamtenga kwa BWANA. Sasa imetosha ninyi watu wa uzao wa Lawi,”

8Tena Musa akamwambia Kora, “Sasa mnisikilize, ninyi watu wa uzao wa Lawi:9Je ni jambo dogo kwenu kwamba Mungu wa mbinguni amewatenga ninyi kutoka kwa watu wa Israeli, ili awalete ninyi karibu na yeye, ili mfanye kazi katika masikani ya BWANA na kusimama mbele ya watu ili muwatumikie?10Amewasongeza karibu, na ndugu zako, wa uzao wa Lawi pamoja nanyi, na sasa mnataka na ukuhani pia!11Hiyo ndiyo sababu wewe na kundi lako mmekusanyika pamoja kinyume na BWANA. Kwa nini mnalalamika juu ya Haruni, ambaye anamtii BWANA?”

12Kisha Musa akamwita Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, lakini wakasema, “hatutakuja.13Kwani jambo dogo kwamba umetuleta mpaka kwenye nchi inayotiririka maziwa na asali, ili kutuua katika jangwa hili? Sasa unataka kujifanya kuwa mtawala wetu!14Na kwa nyongeza, haujatuingiza kwenye nchi ya kutiririka maziwa na asali, au kutupa urithi wa mashamba na mashamba ya mizabibu. Sasa unataka kutupofusha na ahadi hewa? Hatutakuja kwako.”

15Musa alikasirika sana na akamwambia BWANA, “husipokee sadaka zao. Sijachukua punda mmoja kutoka kwao, na sijamdhuru hata mmoja wao.”

16Kisha Musa akamwambia Kora, “Kesho wewe na kundi lako mtaenda mbele za BWANA-wewe na wao na Haruni.17Kila mmoja wenu atatwaa chetezo na kuweka ubani ndani yake. Ndipo kila mtu atamletea BWANA chetezo chake, vyetezo mia mbili na hamsini. Wewe na Haruni, pia, kila mmoja ataleta chetezo chake.

18Kwa hivyo kila mtu alitwaa chetezo chake, akaweka moto ndani yake, akaweka na ubani ndani yake, na kusimama mbele ya lango la hema ya kukutania pamoja na Musa na Haruni.19Kora naye akawakusanya watu wote waliokuwa kinyume na Musa na Haruni hapo kwenye lango la hema ya kukutania, na kisha utukufu wa BWANA ukaonekana kwa watu wote.20Ndipo BWANA aliposema na Musa na Haruni:21“Tokeni ninyi kutoka kwa hawa watu ili nipate kuwaangamiza haraka.”

22Musa na Haruni wakalala kifudifudi na kusema, “Mungu, Mungu wa wote wenye mwili, kama mtu akitenda dhambi, ni lazima uwe na hasira na watu wote?”

23BWANA akanena na Musa, akamwambia,24“Sema na watu wote, uwaaambie, ‘Tokeni kwenye hema ya Kora, Dathani, na Abiramu.’”

25Kisha Musa akaamuka akaenda kwa Dathani na Kwa Abiramu; viongozi wa Israeli wakamfuata.26Akaongea na watu wote akasema, “Sasa jitengeni na hema ya hawa watu waovu na msiguse kitu chochote kilicho chao, vinginevyo mtaangamizwa na dhambi zao.”27Kwa hiyo watu wote toka pande zote za hema ya Kora, Dathani na Abiramu wakaondoka. Dathani na Abiramu wakatoka nje wakasimama kwenye lango la hema zao, wakiwa na wake wao, wana, na watoto wao.

28Kisha Musa akasema, “Kwa hili sasa mtatambua kuwa BWANA amenituma kufanya kazi hizi zote, kwa kuwa sijazifanya kwa uwezo wangu.29Kama hawa watu watakufa kifo cha kawaida ambacho humpata kila mmoja, basi BWANA hakunituma.30Lakini kama BWANA aumbaye malango ya ardhi ambayo huwameza kama mdomo mkubwa, pamoja na familia zao, na kama wataingia ndani ya shimo wakiwa hai, ndipo mtakapojua kuwa wamemdharau BWANA,”

31Mara ghafla Musa alipomaliza kusema maneno haya, ardhi ya pale walipokuwa ikafunguka.32Dunia ikafungua kinywa chake na kuwameza, familia zao na watu wote wa Kora, pamoja na mali zao zote.33Wao na kila mmoja kwenye familia zao wakaingia ndani shimoni wakiwa hai. Dunia ikawafunika, na kwa njia hii wakapotea kutoka miongoni mwa ile jamii.34Nao Israeli wote waliokuwa karibu nao wakakimbia kwa sababu ya vilio vyao. Walisema kwa mshangao, “Nchi isije kutumeza na sisi!”

35Kisha moto ukashuka toka kwa BWANA na kuwaangamiza wale wanaume 250 waliokuwa wametoa ubani.

36Tena BWANA akanena na Musa, akasema,37“Mwambie Eliazari mwana wa Haruni yule kuhani achukue vile vyetezo kutoka ule moto, kwa kuwa vile vyetezo vimetengwa kwa ajili yangu. Na aumwage ule moto mbali.38Vitwae vile vyetezo vya wale waliopoteza maisha yao kwa sababu ya dhambi zao. Na vifanyike kuwa mbao za kufuliwa ili viwe vifuniko vya madhabahu. Kwa kuwa wale watu walivitoa kwangu, kwa hivyo ni vitakatifu. Vitakuwa ishara ya uwepo wangu kwa wana wa Israeli.”

39Naye Eleazari yule kuhani akavichukua vile vyetezo vya shaba ambavyo vilikuwa vimetumiwa na wale watu walioungua, na vikafuliwa kuwa vifuniko vya madhabahu,40ili kuwa ukumbusho kwa wana wa Israeli, ili kwamba asije akatokea mtu toka nje ya uzao wa Haruni akaja kutoa ubani kwa BWANA, ili wasije kuwa kama Kora na kundi lake-- kama vile BWANA alivyoamuru kupitia kinywa cha Musa.

41Lakini siku iliyofuata asubuhi watu wa Israeli wakamlalamikia Musa na Haruni. Nao walisema, “Umeua watu wa BWANA.”

42Kisha ikatokea, wakati watu walipokuwa wamekusanyika kinyume na Musa na Haruni, wakatazama kuielekea hema ya kukutania, na tazama lile wingu lilikuwa likiifunika. Utukufu wa BWANA ukaonekana,43Musa na Haruni wakaja mbele ya hema ya kukutania.44Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,45“Toka kati ya watu hawa ili niwaangamize haraka.” Musa na Haruni wakalala chini kifudifudi.

46Musa akamwambia Haruni, uchukue chetezo, na utie ndani moto kutoka madhabahuni, tia na uvumba ndani yake, upeleke haraka kwa watu, na ukafanye upatanisho kwao, kwa sababu hasira hii inatoka kwa BWANA. Tauni imeanza.”47Kwa hiyo Haruni akafanya kama alivyoelekezwa na Musa. Akakimbia kati ya watu. Na Tauni ilikuwa imeanza kuenea kati ya watu, kwa hiyo akaweka ndani yake uvumba na akafanya upatanisho wa watu.48Haruni akasimama kati kati ya zile maiti na watu walio hai; na kwa njia hii ile tauni ikazuiwa.49Idadi ya wale waliokuwa wamekufa kwa tauni walikuwa 14,000, nje na wale waliokufa kutokana na swala la Kora.50Haruni akarudi kwa Musa kwenye lango la hema ya kukutania, na ile tauni ikakoma.

17

1BWANA akanena na Musa, akasema,2“Waambie wana wa Israeli wakuletee fimbo za kutembelea moja kwa kila jamaa, fimbo kumi na mbili. Uandika jina la kila mmoja kwenye hizo fimbo.3Utaandika jina la Haruni kwenye jina la Lawi. Kutakuwa na fimbo moja kwa kila kiongozi kutoka kwenye kabila la mababu zake.4Utaziweka hizo fimbo kwenye hema ya kukutania mbele ya amri za agano, ambapo Mimi hukutana na wewe. Itakuwa hivi,5fimbo ya mtu yule ninayemchagua itachipua. Nitazuia watu wa Israeli walalamikao, ambao wanaongea kinyume na wewe.”

6Kwa hivyo Musa akawaambia wana wa Israeli. Viongozi wote wa kabila wakampatia fimbo, fimbo moja kutoka kwa kila kiongozi, aliyechaguliwa kutoka kwenye kila kabila ya babu zao, jumla yake fimbo kumi na mbili. Fimbo ya Haruni ilikuwa miongoni mwa fimbo hizo.7Ndipo Musa alipoziweka zile fimbo mbele ya BWANA katika hema ya amri ya agano.

8Siku iliyofuata Musa aliingia kwenye hema ya amri ya agano, na tazama, fimbo ya Haruni kwa ajili ya Kabila la Lawi ilikuwa imetoa machipukizi. Machipukizi yalikuwa hadi kuchanua maua na kuzaa malozi mabivu!9Musa akazitoa fimbo zote kutoka kwa BWANA kwa watu wote wa Israeli, na kila mtu akachukua fimbo yake.

10BWANA akamwambia Musa, “Iweke fimbo ya Haruni mbele ya amri za agano. Iweke iwe ishara ya hatia mbele ya watu waliopinga ili ukomeshe malalamiko dhidi yangu, bila hivyo watakufa.”11Musa akafanya kama BWANA alivyoagiza.

12Wana wa Israeli wakanena na Musa wakisema, “tutakufa hapa! Wote tutaangamia!13Kila mmoja anayekuja hapa, anayekaribia masikani ya BWANA, atakufa. Je, ni lazima wote tuangamie?”

18

1BWANA akamwambia Haruni, “Wewe, wana wako, na uzao wa baba yako mtawajibika kwa dhambi zote zilizotendwa mahali patakatifu. Lakini wewe na wana wako pekee mtawajibika kwa uovu uliofanywa na yeyote mahali pa patakatifu.2Na ndugu zako nao wa kabila ya Lawi, kabila la ukoo wako, utawaleta pamoja na wewe ili kwamba waweze kuungana na wewe ili wakusaidie wakati wewe na wanao mnapokuwa mnatumikia mbele ya hema ya amri ya agano.3Watakutumikia wewe na hema yote. Hata hivyo, wasisonge karibu na chochote ndani ya mahali pa patakatifu au kwa kitu chochote kilichounganishwa na madhabahu, la sivyo, wewe na wao mtakufa.4Wataungana na wewe na kuitunza hema ya kukutania, kwa kazi zote zinazohusiana na hema. Mtu mgeni asikukaribie.

5Wewe utawajibika kwa ajili ya mahali papatakatifu na kwa ajili ya madhabahu ili kwamba hasira yangu isiwajilie watu wa Israeli tena.6Tazama, Mimi mwenyewe nimewachagua ndugu zako wa kabila ya Walawi kutoka mioingoni mwa uzao wa Israeli. Wao ni zawadi kwako. Walitolewa kwangu ili waifanye kazi inayohusiana na hema ya kukutania.7Lakini ni wewe pekee yako na wanao ndio mnaoruhusiwa kufanya kazi ya ukuhani kuhusiana na kila kitu kilichounganishwa na madhabahu na kitu chochote ndani ya lile pazia. Wewe mwenyewe lazima ukamilishe majukumu hayo. Mimi ninakupa ukuhani kama zawadi. Mgeni yeyote anayekaribia atauawa.”

8Kisha BWANA akamwambia Haruni, “Tazama, Nimekupa majukumu ya kusimamia sadaka za kuinuliwa kwangu, na sadaka zengine takatifu ambazo wana wa Israeli wanatoa kwangu. Nimekupa sadaka hizi wewe na wana wako kuwa haki yako milele.9Hivi ni vitu vitakatifu sana, ambavyo visiteketezwe kwa moto: kutoka kwenye sadaka zao-kila sadaka ya unga, kila sadaka ya dhambi, na kila sadaka ya hatia- ni vitu vitakatifu sana kwa ajili yako na wana wako.10Sadaka hizi ni takatifu sana; kila mume lazima aile, kwa kuwa ni vitakatifu kwako.

11Hizi ni sadaka ambazo zitakuwa zako: Sadaka zao, sadaka zote za kuinuliwa za wana wa Israeli. Nimekupa wewe, wana wako na binti zako kuwa gawio lako la milele. Kila mmoja ambaye ni msafi katika familia yako anaweza kula sadaka zozote katika hizi.

12Mafuta yote mazuri, ile divai nzuri yote mpya na unga, malimbuko ambyo watu hutoa kwangu- vitu hivi vyote nimekupa wewe.13Mavuno ya kwanza yaliyoiva yaliyo katika ardhi yao ambayo wanaleta kwangu, yatakuwa yako. Kila mtu aliye msafi kwenye famila yako anaweza kula vitu hivi.

14Kila kitu kilichotolewa wakfu katika Israeli kitakuwa chako.15Kila kitu kinachofungua tumbo, kila limbuko ambalo watu hutoa kwa BWANA, vyote vya watu na wanyama, vitakuwa vyako. Hata hivyo, watu lazima wawakomboe wazaliwa wa kwanza wa kiume, na watawakomboa wazaliwa wa kwanza wa wanyama wasio safi.16Wale ambao wanahitaji kukombolewa na watu watakombolewa wakiwa na umri wa mwezi mmoja. Ndipo watu watawakomboa kwa bei ya shekeli tano, kwa kiwango cha shekeli za mahali patakatifu, ambacho ni sawa na gera ishirini.

17Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi-msiwakomboe hawa wanyama, wametengwa kwa ajili yangu. Utanyunyizia damu yake madhabahuni na kuteketeza mafuta yao kama sadaka ya moto, ambayo ni harufu nzuri ya kumpendeza BWANA.18Nyama yao itakuwa yako. Kama kidali cha kuinuliwa na paja la kulia, nyama yao itakuwa yako.19Sadaka yote takatifu ambayo watu wa Israeli wanaitoa kwa BWANA, nimekupa wewe, na wana wako na binti zako walio pamoja nawe. Kama gawio la kudumu. Hili ni agano la milele la chumvi, agano linalofunga milele, mbele za BWANA kwako wewe na uzao wako walio pamoja na wewe.”

20BWANA akasema na Haruni, Hautakuwa na urithi katika ardhi ya watu, wala hautakuwa na gawio miongoni mwa watu. Mimi ndimi gawio lenu na urithi wenu miongoni mwa watu wa Israeli.

21Tazama, Nimewapatia uzao wa Lawi, zaka zote za Israeli kuwa urithi wao kwa sababu ya huduma wanayotoa katika hema ya kukutania.22Kuanzia sasa, watu wa Israeli wasisonge karibu na hema ya kukutania, la sivyo, watawajibika kwa dhambi hii na kufa.23Walawi wafanya kazi inayohusiana na hema ya kukutania. Watawajibika kwa dhambi inayohusiana na hema. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wote wa uzao wako. Na miongoni mwa watu wa Israeli hawa hawatakuwa na urithi.24Kwa kuwa zaka za wana wa Israeli, wanazotoa kama mchango kwangu -ndivyo hivyo ambavyo nimewapa Walawi kuwa urithi wao. Hiyo ndiyo sababu ya kuwaambia, Kuwa hawatakuwa na urithi kati ya watu wa Israeli.

25BWANA akanena na Musa, akamwambia,26“Inakupasa ukaseme na Walawi uwaambie, ‘Mnapopokea zaka toka kwa watu ambayo BWANA amewapa kutoka kwao kuwa urithi, ndipo na nyie mtakapotoa sehemu ya kumi ya zaka hizo.27Zaka yenu itahesabika kama moja ya mapato ya sakafu ya kupuria nafaka ya mazao yenu au mazao ya vinu vya kukamulia zabibu.28Kwa hivyo na nyinyi lazima mtoe mchango wenu kwa BWANA kutokana na zaka mnazopata kutoka kwa watu wa Israeli. Kutokana na hizo mtatoa matoleo yenu kwa Haruni yule kuhani.29Kwa kila sadaka mnayopata, mtatoa matoleo yenu kwa BWANA. Mtafanya hivi kutokana na vitu vizuri na vitakatifu sana ambavyo mmepewa.

30Kwa hivyo utawaambia, ‘Mnapotoa hayo matoleo mazuri, ndipo itahesabika kwa Walawi kuwa ni mazao yao kutoka kwenye sakafu za kupuria na vinu vyao vya kukamulia.31Ndipo matakapokula nafaka zote zinazobaki mahali popote, nyinyi na familia zenu kwa sababu ndiyo malipo yenu ya kazi kwenye hema ya kukutania.32Hamtakuwa na hatia yeyote kwa kuvila na kuvinywa, kama mtatoa kwa BWANA matoleo yenu mazuri mliyopokea. Lakini msizinajisi sadaka takatifu za wana wa Israeli, la sivyo mtakufa.”

19

1BWANA akanena na Musa na Haruni, Akasema,2“Hii ni amri, ni sheria ninayokuamuru: Waambie wana waIsraeli wakuletee ng'ombe mke mwekundu asiyekuwa na kipaku wala waa, ambaye hajawahi kubeba nira.3Mpatie Eliazari kuhani huyo ng'ombe jike. Naye atamtoa nje ya kambi, na mtu mmoja amchinje mbele yake.4Kisha Eliazari kuhani atachukua sehemu ya damu yake kwa kidole chake na kuinyunyiza mara saba akielekea sehemu ya mbele ya ile hema ya kukutania.5Na kuhani mwingine atamchoma huyo ng'ombe mbele ya macho yake. Ataichoma ngozi yake, nyama yake, na damu yake pamoja na mavi yake,6Yule kuhani atachukua mti wa mwerezi, na hisopo na sufu na kivitupa katikati ya huyo ng'ombe anayechomwa.

7Kisha atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Ndipo atakuja kambini, ambapo atabaki najisi mpaka jioni ya siku hiyo.8Yule aliyemchoma huyo ng'ombe mke atafua nguo zake kwa maji na kuoga majini. Naye atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile.

9Baadaye mtu aliyesafi atayakusanya hayo majivu ya ng'ombe huyo na kuyaweka nje ya kambi kwenye eneo safi. Majivu haya yatatunzwa kwa ajili ya jamii ya watu wa Israeli. Watayachanganya majivu na maji kwa ajili ya utakaso wa dhambi, kwa kuwa majivu yalitokana na sadaka ya dhambi.10Yule aliyeyakusanya majivu ya ng'ombe huyo lazima afue mavazi yake. Atabaki najisi mpaka jioni ya siku ile. Hii itakuwa sheria ya kudumu kwa watu wa Israeli na kwa wageni wanaoishi nao.

11Yeyote atakayegusa maiti ya mtu atakuwa najisi kwa siku saba.12Mtu wa jinsi hiyo atajitakasa mwenyewe siku ya tatu na siku ya saba. Ndipo atakapokuwa safi. Lakini kama hatajitakasa mwenyewe katika siku ya tatu, basi hatakuwa safi siku ya saba.13Yeyote atakayegusa mtu aliyekufa, maiti ya mtu aliyekufa na hajajitakasa - mtu huyu anainajisi masikani ya BWANA. Mtu huyo ataondolewa kuwa miongoni mwa Waisraeli kwa sababu maji ya farakano hayakunyunyiziwa kwake. Atabaki najisi; na unajisi wake utabaki kwake.

14Hii ndiyo sheria ya mtu anayefia hemani. Kila mtu aingiaye hemani na kila mtu ambaye tayari yumo hemani atakuwa najisi kwa siku saba.15Kila chombo ambacho hakina kifuniko kinanajisika.16Vivyo hivyo, kwa mtu aliye nje ya hema ambaye atamgusa mtu aliyeuawa kwa upanga, au mzoga wowote, au mfupa wa mtu, au kaburi--mtu huyo atakuwa najisi kwa siku saba.

17Fanyeni hivi kwa mtu najisi: twaeni majivu ya sadaka ya dhambi ya kuteketezwa na myachanganye kwenye chombo chenye maji ya mto.18Ndipo mtu aliye safi atachukua hisopo, na kutia katika hayo maji, na kunyunyizia juu ya hema, na katika vyombo vyote vilivyo hemani, na kwa watu waliokuwepo, na kwa yule aliyegusa ule mfupa, mtu aliyeuawa, maiti, au kaburi.19Katika siku ya tatu na siku ya saba, yule mtu aliye msafi atamnyunyizia yule mtu asiyekuwa safi. Katika siku ya saba mtu najisi atajitakasa mwenyewe. Atazifua nguo zake na kuoga kwenye maji. Jioni yake atakuwa safi.

20Lakini yule atakayebaki najisi, anayekataa kujitakasa mwenyewe -- huyo mtu ataondolewa kutoka kwenye jamii, kwa sababu amepanajisi patakatifu pa BWANA. Hajanyunyiziwa maji ya utakaso; atabaki najisi.21Hii itakuwa sheria ya kudumu kuhusiana na hali ya hivi. Yule mtu anayenyunyizia maji ya farakano atafua mavazi yake. Yule atakayeyagusa maji ya farakano atakuwa najisi mpaka jioni.

22Chochote kile ambacho kitaguswa na mtu najisi kitakuwa najisi. Na mtu atakayekigusa naye atakuwa najisi mpaka jioni.

20

1Kwa hivyo wana wa Israeli, na jamii yote ya watu, wakaenda katika jangwa la Sini katika mwezi wa kwanza; wakakaa Kadeshi. Hapo ndipo Miriamu alipofia na kuzikwa.

2Huko hapakuwa na maji kwa ajili ya watu, kwa hiyo wakakusanyika kinyume na Musa na Haruni huko.3Watu wakamlalamikia Musa. Wakasema, “Ilikuwa ni bora kama tungelikufa wakati Waisraeli wenzetu walipokufa mbele za BWANA.4Kwa nini umewaleta watu wa BWANA kufia katika jangwa hili, sisi na wanyama wetu?5Kwa nini ulitutoa Misri na kutuleta katika eneo hili baya? Hapa hakuna nafaka, wala mitini, wala mizabibu, wala makomamanga. Na hakuna maji ya kunywa.”

6Basi Musa na Haruni wakatoweka mbele ya mkutano huo. Wakaenda kwenye hema ya kukutania wakalala kifudifudi. Ndipo pale utukufu wa Busara wa BWANA ukaonekana kwao.7BWANA akanena na Musa, akamwambia,8“Chukua fimbo yako na uwakusanye watu, wewe na Haruni ndugu yako. Uambie huu mwamba mbele ya macho yao, na uamuru utoe maji. Nawe utawapa maji kutoka kwenye huu mwamba, nawe utawapa maji ya kunywa hao watu na wanyama wao.”

9Musa akachukua hiyo fimbo mbele ya BWANA, kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.10Kisha Musa na Haroni wakawakusanya watu pamoja mbele ya ule mwamba. Ndipo Musa akawaambia, “Sasa sikilizeni, enyi wapinzani. Lazima tuwape maji kutoka kwenye huu mwamba?”11Ndipo Musa akanyosha mkono wake na kuupiga ule mwamba mara mbili kwa fimbo yake, na maji mengi yakatoka. Wale watu wakanywa pamoja na wanyama wao.

12Kisha BWANA akamwambia Musa na Haruni, “Kwa kuwa hamkuniheshimu mimi na kuniamini mbele ya watu wa Israeli, hamtawaingiza hawa watu katika nchi niliyowaahidi.

13Mahali hapa paliitwa maji ya Meriba kwa sababu wana wa Israeli walitofautiana na BWANA pale, na akajionyesha kwao kuwa mtakatifu.

14Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi kwa mfalme wa Edom: Ndugu yako Israeli anasema hivi: “Wewe unajua magumu yote ambayo yametupata.15Na unajua kuwa babu zetu walienda Misri na waliishi Misri kwa muda mrefu. Wamisri walitutendea vibaya pamoja na babu zetu.16Tulipomlilia BWANA, akatusikia na kututumia malaika ambaye alitutoa toka Misri. Tazama, sasa tuko Kadeshi, mji unaopakana na nchi yako.17Tunakuomba uturuhusu kupita katika nchi yako. Hatutapita mashambani wala kwenye mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita kwenye njia kuu ya mfalme. Hatutageuka upande wa kulia wala upande wa kushoto mpaka tutakapopita mpaka wako.”

18Lakini mfalme wa Edomu akamjibu, “Msipite hapa. Kama mtafanya hivyo, Nitakuja na upanga kukuvamia.”

19Ndipo wana wa Israeli wakamwambia, “tutapitia njia kuu. Kama sisi au wanyama wetu watakunywa maji yako, basi tutalipa. Tunaomba uturuhusu tupite tukitembea kwa miguu yetu, bila kufanya jambo lolote lile.”

20Lakini mfalme wa Edomu akajibu, “Usipite hapa.” Kwa hivyo nfalme wa Edomu akawa kinyume cha Israeli kwa mkono wenye nguvu pamoja na jeshi kubwa sana.

21Mfalme wa Edomu akawazuia wana wa Israeli kupita kwenye mipaka yake. Kwa sababu ya hili, Israeli akageuka kuiacha nchi ya Edomu.

22Kwa hiyo watu wakasafiri kutoka Kadeshi. Wana wa Israeli, watu wote, wakafika Mlima Hori.23BWANA akanena na Musa na Haruni hapo kwenye Mlima Hori, kwenye mpaka wa Edomu. Akasema,24“Sasa ni wakati wa Haruni kukusanyika na watu wake, hataingia katika nchi ile niliyowaahidi wana wa Israeli. Hii ni kwa sababu ninyi wawili hamkuitii sauti yangu pale kwenye maji ya Meriba.25Mchukue Haruni na Eliazari mwanaye, na uwalete juu ya Mlima Hori.26Umvalishe Haruni yale mavazi ya kikuhani na umvalishe Eliazari mwanaye. Haruni atakufa na kulazwa pamoja na watu wake.”

27Musa akafanya kama BWANA alivyo mwamuru. Wakaenda juu y a Mlima Hori na watu wote wakiona.28Musa akamvalisha Haruni yale mavazi ya kikuhani na kumvalisha Mwanaye Eliazari. Haruni akafa pale juu ya Mlima Hori. Kisha Musa na Eliazari wakashuka.29Watu walipoona kuwa Haruni amekufa, taifa lote wakamlilia Haruni kwa siku arobaini.

21

1Aradi mfalme wa Wakanaani, aliyekuwa akiishi Negebu, aliposikia kuwa Israeli ilikuwa ikisafiri kwa kupitia barabara kuelekea Atharimu, akapigana dhidi ya Israeli na kujitwalia baadhi ya mateka.2Israeli akaapa mbele za BWANA akasema, “Kama utatupa ushindi dhidi ya hawa watu, ndipo tutakapoiangamiza kabisa miji yao,”3BWANA akaisikia sauti ya Israeli na kuwapa ushindi dhidi ya Wakanaani. Wakawaangamiza kabisa pamoja na miji yao. Mahali pale paliitwa Horima.

4Wakasafiri kutoka Mlima Hori kwa barabara kuelekea bahari ya shamu wakiizunguka nchi ya Edomu. Watu walikufa moyo kwa njia hiyo.5Watu wakamnung'unikia Mungu na Musa: “Kwa nini umetutoa Misiri ili tufe katika jangwa hili? Hapa hakuna mikate, wala maji, na chakula hiki dhaifu kimetukinai.”

6Basi Mungu akatuma nyoka wa sumu kati yao. Wale nyoka wakawauma wale watu; watu wengi walikufa.7Watu wakaenda kwa Musa wakamwambia, “Tumetenda dhambi kwa sababu tumemnung'unikia Mungu na wewe. Mwombe Mungu atuondolee hawa nyoka.” Kwa hiyo Musa akawaombea watu.

8BWANA akamwambia Musa, “Tengeneza nyoka na umweke kwenye nguzo. Na itakuwa kila anayeumwa, akimwangalia huyo nyoka atapona,”9Kwa hivyo Musa akatengeneza nyoka wa shaba naye akamweka juu ya nguzo. Na kila mtu alipoumwa na nyoka na kumwangalia huyo nyoka alipona.

10Kisha watu wa Israeli wakasafiri na kisha kuweka kambi Obothi.11Kisha wakasafiri kutoka pale na kuweka kambi Iye Abarimu katika jangwa linalokabili Moabu kuelekea upande wa mashariki.12Kutoka pale wakasafiri na kuweka kambi katika bonde la Zeredi.13Kutoka pale walisafiri na kuweka kambi kwenye upande mwingine wa mto Amoni, ambao ukubwa wake unaanzia kwenye mpaka wa Waamori. Mto wa Amoni ndio unaootengeneza mpaka wa Moabu, kati ya Moabu na Waamori.14Ndiyo maana imeandikwa katika gombo la Kitabu cha BWANA, “Wahebu katika Sufa, na bonde la Amoni,
15mtelemko wa bonde linaloelekea katika mji wa Ari na kuelekea kwenye mpaka wa Moabu,”
16Kutoka pale wakasafiri mpaka Beeri, hapo ndipo palipo na kisima ambacho Bwana alimwambia Musa, “Wakusanye watu kwa ajili yangu ili uwape maji,”17Ndipo Israeli waipoimba wimbo huu: “enyi visima, yajazeni maji. Imbeni juu ya kisima hiki.
18Kisima ambacho viongozi wetu walichimba, kisima ambacho wenye hekima walichimba kwa fimbo ya kifalme na kwa fimbo ya kutembelea.” Kisha kutoka jangwani walitembea mpaka Matanaha.
19Kutoka Matanaha walisafiri mpaka Nathalieli, na kutoka Nathalieli mpaka Bamothi,20na kutoka Bamothi hadi kwenye bonde la Moabu. Hapo ndipo kilele cha Mlima Piska kinapoonekana jangwani.

21Kisha Israeli akatuma wajumbe kwa Sihoni mfalme wa Waamori akisema,22Tunaomba tupite katika nchi yako. Hatutapita katika shamba au kwenye shamba la mizabibu. Hatutakunywa maji ya visima vyako. Tutapita katika njia kuu ya mfalme mpaka tutakapopita mpaka wako.”

23Lakini mfalme Sihoni hakumruhusu Israeli kupita kwenye mpaka wao. Badala yake, Sihoni akakusanya jeshi lake lote na kumvamia Israeli huko jangwani. Akaja kwa Jahazi, ambapo alipigana dhidi ya Israeli.24Israeli akalivamia jeshi la Sihoni na nchi ya upanga na kuchukua nchi yao kutoka Amoni mpaka mto Jabboki, hadi kufikia nchi ya watu wa Amoni. Sasa mpaka wa watu wa Amoni ulikuwa umefungwa.25Israeli akachukua miji yote ya Waamori na akaishi ndani yake, pamoja na Heshiboni na vijiji vyake wote.26Heshiboni ulikuwa mji wa Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye hapo awali alipigana dhidi ya mfalme wa kwanza wa Moabu. Sihoni alikuwa ameteka ardhi yake yote toka mipaka yake mpaka mto wa Amoni.

27Hiyo ndiyo sababu wale ambao huongea kwa Mitahali husema, “Njoni Heshboni. Mji wa Sihoni ujengwe na kuimarishwa tena.
28Moto uliwaka toka Heshiboni, moto kutoka mji wa Sihoni ambao uliiteketeza Ari ya Moabu, na wenyeji wa miji ya juu ya Amoni.
29Ole wako, Moabu! Umepotea, enyi watu wa Chemoshi. Amewafanya watu wake kuwa wakimbizi na binti zake kuwa wafungwa wa Sihoni mfalme wa Waamori.
30Lakini tumempiga Sihoni. Tumeiangamiza Heshibon mpaka Diboni. Tumewaharibu wote mpaka Nofa, ambayo inafika mpaka Madeba.”

31Kwa hiyo Israeli akaanza kuishi katika nchi ya Waamori,

32Kisha Musa akatuma watu kwenda kuingalia Yaziri. Waliviteka vijiji vyake na kuwafukuza Waamori waliokuwa wakiishi humo.33Kisha wakageuka na kuelekea njia inayoelekea Bashani. Ogu mfalme wa Bashani akatofautiana nao, yeye na Jeshi lake lote, ili apigane nao kule Ederei.

34Kisha BWANA akasema na Musa, “Msimwogope, kwa sababu nimewapeni ushindi dhidi yake, Jeshi lake lote na nchi yake. Mfanyeni kama mlivyomfanya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akiishi Heshiboni.”

35Kwa hivyo wakamuua, na wanawe, na jeshi lake lote, mpaka wote wakaishi na hakubaki hata mmoja aliyekuwa hai. Kisha wakaichukua nchi yake.

22

1Watu wa Israeli wakasafiri mpaka wakaweka kambi kwenye uwanda wa Moabu karibu na Yeriko, kwenye upande mwingine wa mto Yorodani kutoka mji ule.

2Balaki mwana wa Zippori aliona yote ambayo Israeli aliwafanyia Waamori. Moabu aliogopa sana hao watu kwa sababu walikuwa wengi sana,3na Moabu aliwaogopa wana wa Israeli.

4Mfalme wa Moabu akawaambia wazee wa Midiani, “Huu umati utakula kila kitu tulicho nacho kama vile maksai hula nyasi za kondeni.” Sasa Balaki mwana wa Zippori alikuwa mfalme wa Moabu.5Akatuma wajumbe kwenda kwa Balamu mwana wa Beori, kule Petho ambayo iko karibu na mto Frati, katika nchi ya taifa lake na watu wake. Akamwita na kumwambia, “Tazama, Kuna taifa ambalo wamekuja hapa tokea Misiri. Wanafunika uso wa dunia na sasa wananifuatia mimi.6Tafadhali naomba uje unilaanie hili taifa, kwa sababu wana nguvu kuniliko. Labda nitaweza kuwavamia na kuwafukuza watoke katika nchi yangu. Najua kuwa yeyote unayembariki hubarikiwa na yeyote unayemlaani atalaaniwa.”

7Kwa hiyo wazee wa Moabu na wale wa Midiani wakaondoka, pamoja nao wakachukua malipo ya uganga. Wakafika kwa Balaamu wakamwambia maneno ya Balaki.

8Balaamu akawaambia, “Bakini hapa usiku wa leo. Kesho nitawaletea atakachoniambia BWANA.” Kwa hiyo wale viongozi wa Moabu wakabaki na Balaamu kwa usiku huo.9Mungu akaja kwa Balaamu na kumwambia, “Ni akina nani hawa waliokuja kwako?”

10Balaamu akamjibu Mungu, “Balaki mwana wa Zippori, Mfalme wa Moabu amewatuma kwangu. Alisema,11‘Tazama hawa watu waliotoka Misri wanafunika uso wa nchi yangu. Sasa naomba uje unilaanie hawa watu. Labada nitaweza kuwashinda na kuwafukuza.’”

12Mungu akamjibu Balaamu, “Usiambatane na hao wanaume. Na usiwalaani hawa wana wa Israeli kwa sababu wamebarikiwa.”

13Balaamu akaamka asubuhi na kuwaambia wale viongozi wa Balaki, “Rudini nchini kwenu kwa sababu BWANA amenikataza kuambatana nanyi.”

14Kwa hivyo wale viongozi wa Moabu wakaondoka na kurudi kwa Balaki. Wakamwambia, “Balaamu amekataa kuambatana nasi.

15Balaki akatuma viongozi wengine waliokuwa wanaheshimiwa zaidi kuliko kundi lile la awali.16Wakaja kwa Balaamu na kumwambia, “Balaki mwana wa Zippori anasema hivi, ‘Tafadhali hebu kitu chochote kisikuzuie kuja kwangu,17kwa sababu nitakulipa malipo mazuri sana na kukupa heshima kubwa, nami nitakufanyia chochote utakachoniambia. Tafadhali sana uje unilaanie hawa watu.’”

18Balaamu akawajibu watu wa Balaki akawaambia, “Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitaweza kufanya dhidi ya maneno ya BWANA, Mungu wangu na kufanya pungufu au zaidi ya kile anachoniambia.19Sasa basi, tafadhali subirini hapa usiku wa leo pia, ili kwamba nipate kujifunza kitu zaidi ambacho BWANA ananiambia.”

20BWANA akaja kwa Balaamu usiku ule na kumwambia, “kwa kuwa hawa watu wamekuja kukuita, inuka uende nao. Lakini utafanya tu kile nitakachokuambia kufanya.”

21Balaamu akainuka asubuhi, akatandika punda wake, akaenda pamoja na viongozi wa Moabu.22Lakini kwa sababu alienda, hasira za Mungu zikawaka. Malaika wa BWANA akasimama barabarani kama adui wa Balaamu, aliyekuwa akimpanda yule punda. Watumishi wawili wa Balaamu walikuwa pamoja naye.23Yule punda alimwona yule malaika wa BWANA akiwa amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Yule punda akageuka na kwenda shambani. Balaamu akampiga yule punda ili arudi barabarani.24Sasa malaika wa BWANA akasimama kwenye njia nyembamba katikati ya mashamba ya mizabibu, na kushoto kwake kulikuwa na ukuta.25Yule punda akamwona yule malaika wa BWANA tena. Akasogea zaidi ukutani na kuubana mguu wa Balaamu ukutani. Balaamu akampiga tena yule punda.

26Yule malaika wa BWANA akasogea mbele zaidi kwenye eneo jingine jembamba zaidi ambalo haikuwezekana kugeuka upande mwingine.27Yule Punda akamwona tena yule malaika wa BWANA, akalala chini na Balaamu. Hasira za Balaamu zikawaka, akampiga yule punda kwa fimbo yake.28Kisha BWANA akafungua kinywa cha punda na akaongea. Akamwambia Balaamu, “Nimekukosea nini kiasi kwamba umenipiga mara tatu?”

29Balaamu akamjibu yule punda, “Ni kwa sababu umenitendea ujinga. Natamani kama ningekuwa na upanga mkononi mwangu, kama ningekuua nao, sasa hivi ningekuwa nimekuua.”

30Yule punda akamwambia Balaamu, “Je, mimi si punda wako ambaye umenipanda maishani mwako mwote mpaka hivi sasa? Je, nimewahi kuwa na tabia ya kukufanyia hivi hapo awali?” Balaamu akasema “hapana.”

31Basi BWANA akafungua macho ya Balaamu, na akamwona malaika wa BWANA amesimama barabarani akiwa na upanga mkononi mwake. Balaamu akainamisha kichwa chake chini.

32Yule malaika wa BWANA akamwambia, “Kwa nini umempiga punda wako mara tatu? Tazama, Nimekuja kama adui yako kwa sababu matendo yako kwangu yamekuwa maovu.33Yule punda aliniona na akageuka kutoka kwangu mara tatu. Kama asingekuwa amegeuka kutoka kwangu, hakika ningekuwa nimekua na yeye kumwacha hai.

34Balaamu akamwambia malaika wa BWANA, nimetenda dhambi. Sikujua kuwa ulisimama kinyume na mimi barabarani. Kwa hivyo sasa, kama haikupendezi, Nitageuka.”

35Lakini yule malaika wa BWANA akamwambia Balaamu, “endelea na wale watu. Lakini utasema maneno nitakayokwambia tu.” Kwa hivyo Balaamu akaendelea na wale vioingozi wa Balaki.

36Balaki aliposikia kuwa Balaamu alikuwa amekuja, alienda kukutana naye kule mjini Moabu pale Amoni, huko mpakani.37Balaki akamwambia Balaamu, “Je, mimi sikutuma watu kukuita? Basi kwa nini hukuja kwangu? Je, mimi sina uwezo wa kukufanya uheshimike?”

38Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Tazama, mimi nimekuja kwako. Je mimi sina mamlaka ya kusema chochote? Mimi ninaweza kusema maneno ambayo Mungu ameweka kinywani mwangu.”

39Balaamu akaenda na Balaki, na Wakafika Kiriathi Huzothi.40Kisha Balaki akatoa sadaka ya makisai na kondoo na kumpatia Balaamu baadhi ya hiyo nyama na wale viongozi waliokuwa pamoja naye.41Kesho yake asubuhi, Balaki akampeleka Balaamu mpaka juu mahali pa Baali. Kule juu Balaamu aliweza kuona sehemu tu ya kambi za Waisraeli.

23

1Balaamu akamwabia Balaki, “Jenga madhabahu saba kwa ajili yangu na uandae mafahari saba na kondoo dume saba.”2Kwa hiyo Balaki akafanya kama Balaamu alivyoomba. Kisha Balaki na Balaamu wakatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume mmoja kwa kila madhabahu.

3Ndipo Balaamu alipomwamwambia Balaki, “Simama kwenye sadaka yako ya kuteketezwa na mimi nitaenda. Labda BWANA atakuja kukutana na mimi. Chochote atakachoniambia nitakuambia.” Kwa hiyo akaenda juu ya mlima usiokuwa na miti.4Wakati bado akiwa juu ya mlima. Mungu akakutana naye, na Balaamu akamwambia, “Nimejenga madhabahu saba, na nimetoa sadaka ya fahari na kondoo dume kwa kila madhabahu.”

5BWANA akaweka ujumbe kwenye kinywa cha Baalamu akasema, “Rudi kwa Balaki ukamwambie.”

6Kwa hivyo Balaamu akarudi kwa Balaki aliyekuwa amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na viongozi wote wa Moabu walikuwa pamoja naye.7Ndipo Balaamu alipoanza kunena unabii wake akisema, “Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka katika milima ya mashariki, ‘Njoo, nilaanie Yakobo kwa ajili yangu,’ alisema, ‘Njoo umtie unajisi Israeli,’
8Nawezaje kuwalaani wale ambao Mungu hajawalaani? Nawezaje kuwapinga wale ambao Mungu hawapingi?
9Kwa kuwa kutoka juu ya miamba Ninamwona; kutoka kwenye milima ninamtazama. Kuna watu wanaoishi pekee yao na hawajioni wenyewe kama ni taifa la kawaida.
10Nani awezaye kuyahesabu mavumbi ya Yakobo au kuhesabu hata robo ya Israeli? Naomba nife kifo cha mtu mwenye haki, na mwisho wa maisha yangu uwe kama wake!”

11Balaki akamwambia Balaamu, “Umenifanyia nini? Nilikuleta ili uwalaani maadui wangu, lakini ona, umewabariki,”

12Balaamu akajibu akasema, “Kwa nini nisiwe mwangalifu kusema kile ambacho BWANA anaweka kinywani mwangu?”

13Basi Balaki akamwambia, “Hebu uje nami kwenye eneo jingine ili uwaone. Utakaowaona ni wale wa karibu tu, huwezi kuwaona wote. Huko sasa unaweza kunilaania hawa watu.”14Kwa hivyo akampeleka Balaamu kwenye shamba la Zofimu, lililo juu ya Mlima Pisiga, na kule akajenga madhabau zingine saba. Akatoa sadaka ya fahari mmoja na kondoo dume kwa kila madhabahu.

15Kisha Balaamu akamwambia Balaki, “Simama hapa karibu na sadaka zako, wakati mimi naenda kukutana na BWANA kule.”

16Kwa hivyo BWANA akakutana na Balaamu na kumuwekea ujumbe kinywani mwake. Alimwambia, “Rudi kwa Balaki ukamwambie huu ujumbe toka kwangu.”

17Balaamu akamrudia, na tazama, alikuwa amesimama karibu na sadaka zake za kuteketezwa, na viongozi wa Moabu walikuwa pamoja naye. Balaki akamwuliza, “BWANA amekwambiaje?”

18Balaamu akaanza kutoa unabii. Akasema, “Inuka, Balaki na usikilize. Nisikilize mimi wewe mwana wa Zippori.
19Mungu siyo mtu, kwamba umdanganye, au mwanadamu awezaye kubadili mawazo. Je, alishawahi kuahidi kitu pasipo kukitekeleza? Je, alishawahi kusema kuwa atafanya kitu bila kufanya kama alivyosema?
20Tazama, Mimi nimeamriwa kuwabariki. Mungu ametoa baraka, nami siwezi kuibadilisha.
21Hajawahi kuona magumu katika Yakobo au tabu katika Israeli. BWANA Mungu wao yuko pamoja nao, na kelele za wafalme wao ziko pamoja nao.
22Mungu aliwatoa Misri kwa nguvu kama za nyati.
23Hakuna uganga utakaofanikiwa dhidi ya Yakobo, na hakuna uchawi utakaomuumiza Israeli. Badala yake, itasemwa juu ya Yakobo na Israeli, ‘Tazama kile ambacho Mungu amefanya!’
24Tazama, watu wanainuka kama simba jike, kama vile simba ainukavyo na kuvamia. Halali chini mpaka ale windo lake na kunywa damu ya windo lake,”

25Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Kamwe usiwalaani wala kuwabariki.”

26Lakini Balaamu akamjibu Balaki, “Sijakuambia kuwa nitasema yote ambayo BWANA ananiambia kusema?

27Balaki akamwambia Balaamu, “Njoo sasa, Nami nitakupeleka mahali pengine. Labda kule itampendeza Mungu kunilaania hawa watu.”28Kwa hiyo Balaki akampeleka Balaamu juu ya Mlima Peori, ambao unalitazama chini lile jangwa,

29Balaamu akamwambia Balaki, “Nijengee madhabahu saba hapa na uniandalie mafahari saba na kondoo dume saba.30“Kwa hivyo Balaki akafanya kama alivyoambiwa; akatoa sadaka ya fahari na kondoo mume kwenye kila madhabahu.

24

1Balaamu alipoona kuwa ilimpendeza BWANA kubariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, kwa kutumia uganga, badala yake akatazama jangwani.2Akayainua macho yake na kumwona Israeli akiwa kwenye kambi, kila mmoja kwa kabila yake, na Roho wa Mungu akamjia.3Akapokea huu unabii na kusema, “Balaamu mwana wa Beori anataka kusema, yeye ambaye macho yake yemefunuliwa sana.

4Huongea na kusikia maneno ya Mungu. Huona maono toka kwa Mwenyezi, ambaye mbele zake humwinamia na macho yake yakiwa yamefumbuliwa.
5Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli!
6Wamesambaa kama bonde, kama bustani zilizo pembezoni mwa mto, Kama miti ya mishubiri iliyopandwa na BWANA, ni kama mfano wa mielezi pembezoni mwa maji.
7Maji yanatiririka katika ndoo zao, na mbegu zao zimemwagiwa maji vizuri. Mfalme wao atakuwa juu ya Agagi, na ufalme wao utaheshimiwa.
8Mungu anamtoa Misri, na nguvu kama za nyati. Atawameza mataifa wanaopigana nao. Ataivunja mifupa yao katika vipande vipande. Atawapiga kwa mishale yake.
9Ananyatia kama simba mume, na kama simba jike. Ni nani atakayejaribu kumsumbua? Kila mmoja anayembariki na abarikiwe; na kila mmoja anayemlaani na alaaniwe.”

10Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, “Nilikuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu.11Kwa hivyo ondoka uende nyumbani uniache sasa hivi. Nilisema ningekupa zawadi kubwa sana, lakini BWANA amekuzuilia kupata zawadi.”

12Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia,13‘Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,’ Je, sikuwaambia haya?14Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo.”

15Balaamu alianza unabii huu. Akisema, “Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake.
16Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa.
17Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbo ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi
18Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa miliki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake.
19Kutoka kwa Yakobo atatoka mfalme ambaye utawala wake naye atawaangamiza waliosalia katika mji.”

20Kisha Balaamu akamtazama Amaleki na akaanza kutoa unabii wake. Alisema, “Amaleki alikuwa mkuu katika mataifa, lakini mwisho wake utakuwa uharibifu.”

21Kisha Balaamu akawatazama Wakeni na akaanza kutoa unabii wake. Akasema, “Mahali unapoishi pana usalama, na viiota vyake viko kwenye miamba.
22Lakini pamoja na hayo, Kaini ataharibiwa na Ashuru atakapowachukua mateka.”

23Kisha Balaamu akaanza unabii wake wa mwisho. Akasema, “Ole wake, nani atakayesalia Mungu atakapoyafanya haya?
24Merikebu zitakuja toka pwani ya Kittimu; Zitaivamia Ashuru na kuiharibu Eberi, lakini wao pia wataishia kwenye uharibifu.” Kisha Balaamu akainuka na kuondoka. Akarudi nyumbani kwake, na Balaki naye akaondoka.

25Ndipo Balaamu akaamka akaenda. Akarudi kwa boma lake, na Balaki naye akaondoka.

25

1Israeli akakaa Shitimu, na wanaume wakaanza kufanya ukahaba na wanawake wa Moabu,2kwa kuwa Wamoabu waliwakaribishsa kutoa sadaka kwa miungu wao. Kwa hivyo watu wakala na kuisujudia miungu wa wa Moabu.3Watu wa Israeli wakaungana kumwabudu Baali wa Peori, na hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli.

4BWANA akamwambia Musa, “Waue viongozi wote wa watu na uwanyonge mbele yangu ili waonekane wakati wa mchana, ili kwamba hasira yangu kali iondoke kwa Israeli.”

5Kwa hivyo Musa akawaambia viongozi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awanyonge watu wake ambao wameshiriki kumwabudu Baali wa Peori.”

6Kisha mtu mmoja wa Israeli akaleta mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa familia yake. Hili lilitokea mbele ya macho ya Musa na watu wa Israeli, wakati walipokuwa wakilia mbele ya lango la hema ya kukutania.7Finehasi mwana wa Eliazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona hivyo, akainuka kutoka jamii ya watu akachukua mkuki mkononi mwake.8Akamfuata yule mwanaume Muisraeli hemani na kuwachoma kwa mkuki wote wawili kwenye miili yao, wote yule Muisraeli na yule mwanamke. Kwa hiyo ile tauni ambayo Mungu alikuwa ameituma kwa watu wa Israeli ikakoma.9Idadi ya wale waliokufa kwa tauni walikuwa elfu ishirini na nne.

10BWANA akanena na Musa, akasema,11“Finehasi mwana wa Eliazari mwana wa Haruni kuhani amaigeuza hasira yangu isiwe kwa wana wa Israeli kwa sababu alikuwa na wivu kati yao juu ya wivu wangu. Kwa hivyo sijawaangamiza watu wa Israeli kwa hasira yangu.12Kwa hiyo waambie, ‘BWANA anasema, “Tazama, Ninampa Finehasi agano la amani.13Kwake na kwa wana wake baada yake, litakuwa agano la kudumu la ukuhani kwa sababu alikuwa na wivu juu yangu, Mungu wake. Amewapatanisha wana wa Israeli.

14Sasa yule Muisraeli aliyeuwawa pamoja na Yule mwanamke Mmidiani alikuwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa familia ya uzao wa Simeoni.15Jina la yule Mmidiani aliyeuwawa lilikuwa Cozibi binti wa Zuri, ambaye alikuwa mkuu wa familia wa kabila huko Midiani.

16Kwa hiyo BWANA akanena na Musa na kusema,17“Watendee Wamidiani kama maadui na uwaangamize, kwa kuwa waliwatendea kama maadui18kwa kuwadanganya. Waliwaongoza katika uovu kwa swala la Peori na kwa swala la dada yao Cozibi, binti wa kiongozi wa Wamidiani, ambaye aliuawa siku ile ya tauni kwa swala la Peori.”

26

1Ilitokea baada ya tauni ambayo BWANA alimwambia Musa na Eliazari mwana wa Haruni kuhani, alisema,2Wahesabu watu wote wa Israeli, kuanzia miaka ishirini na zaidi, kwa jamaa ya familia zao wote ambao wanaweza kwenda kwenye vita kwa ajili ya Israeli.”3Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakawaambia katika uwanda wa Moabu karibu na Yordani kule Yeriko na kusema,4Wahesabuni watu, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi kama BWANA alivyomwamuru Musa na watu wa Israeli walitoka katika nchi ya Misri.”5Reubeni ndiye aliyekuwa wa kwanza, Kutoka kwa mwana wake Hanoki ulitokea ukoo wa Wahanoki. Kutoka kwa Palu ulitokea ukoo wa Wapalu.6Kutoka Hezroni. Ulitokea ukoo wa Wahezroni. Kutoka kwa Kami ulitokea ukoo wa Wakami.7Hizi ndizo zilikuwa koo za uzao wa Reubeni, ambazo idadi yao ilikuwa wanaume 43,730.8Eliabu alikuwa mwana wa Palu.9Wana wa Eliabu walikuwa ni Nemueli, Dathani. Na Abiramu. Hawa ni walewale Dathani na Abiramu waliomfuata Kora waliompinga Musa na Haruni na kumpinga BWANA.

10Pale ambapo dunia ilifungua kinywa na kuwameza pamoja na Kora wakati ambapo wafuasi wa Kora walikufa. Wakati ule, moto uliteketeza wanaume 250, ambao walikuwa ishara ya onyo.11Lakini uzao wa Kora haukufa.12Ukoo wa uzao wa Simeoni walikuwa hawa wafuatao: Kutoka kwa Nemueli, ukoo wa Wanemueli, kwa Jamini, ukoo wa Wajamini, kwa Jakini, ukoo wa Wajakini,13kwa Zera, ukoo wa Wazera, kwa Shauli, ukoo wa Washauli.14Hizi ndizo koo za uzao wa Simeoni, idadi yao ilikuwa wanaume 22,200.15Koo za uzao wa Gadi zilikuwa hizi: Kwa Zefoni, Ukoo wa Wazefoni, kwa Hagi, ukoo wa Wahagi, kwa Shuni, ukoo wa Washuni,16kwa Ozini, ukoo wa Waozini, kwa Eri, ukoo wa Waeri,17kwa Arodi, ukoo wa Waarodi, kwa Areli, ukoo wa Waareli.18Hizi ndizo koo za uzao wa Gadi, idadi yao walikuwa wanaume 40,500.19Wana wa Yuda walikwa Er na Onani, lakini hawa walifia katika nchi ya Kanaani.20Koo zingine za uzao wa Yuda zilikuwa hizi: Kwa Shela, ukoo wa Washela, kwa Perezi, ukoo wa Waperezi, na kwa Zera, ukoo wa Wazera.21Uzao wa Perezi walikuwa hawa: Kwa Hezroni, ukoo wa Wahezroni, kwa Hamuli, ukoo wa Wahamuli.22Hizi ndizo zilizokuwa koo za Yuda, idadi yao ilikuwa wanaume 76,500.23Koo za uzao wa Isakari zilikuwa hizi: Kwa Tola, ukoo wa Watola, kwa Puva, ukoo wa Wapuva,24kwa Jashubu, ukoo wa Wajashubu, kwa Shimroni, ukoo wa Washimroni.25Hizi ndizo zilikuwa koo za Isakari, Idadi yao ilikuwa wanaume 64,300.26Koo za uzao wa Zabuloni zilikuwa hizi: Kwa Seredi, ukoo wa Waseredi, kwa Eloni, ukoo wa Waeloni, kwa Jahaleeli, ukoo wa Wajahaleeli.27Hizi ndizo zilikuwa koo za Zabuloni, idadi yao ilikuwa wanaume 60,500.28Koo za uzao wa Ysufu zilikuwa Manase na Efraimu.29Huu ndio uliokuwa uzao wa Manase: Kwa Machiri, ukoo wa Wamachiri (Machiri ndiye aliyekuwa baba wa Giliedi), kwa Giliedi, ukoo wa Wagiliedi.30Wazo wa Giliedi walikuwa hawa wafuatao: Kwa Lezeri, ukoo wa Walezeri, kwa Helweki, ukoo wa Waheleki, kwa Asrieli,31ukoo wa Asrieli wa Waasrieli, kwa Shekemu, ukoo wa Washekemu,32kwa Shemida, ukoo wa Washemida, kwa Hefa, ukoo wa Wahefa.33Zelofehadi mwana wa Hefa hakuwa na watoto wa kiume bali alikuwa na mabinti. Majina ya binti zake yalikuwa Mahilahi, Noha, Hoglaha, Milika, na Tiriza.34Hizi ndizo koo za Manase, idadi yao ilikuwa wanaume 52,700.35Koo za wana wa uzao wa Efraimu zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuthelaha, ukoo wa Washutheleha, kwa Becheri, ukoo wa Wabecheri, kwa Tahana, ukoo wa Watahana.36Uzao wa Shuthelaha walikuwa, kwa Erani, ukoo wa Waerani.37Hizi ndizo koo za uzao wa Efraimu, idadi yao ilikuwa wanaume 32,500. Huu ndio uzao wa Yusufu, uliohesabiwa toka kila koo zao.38Koo za uzao wa Benjamini zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Bela ukoo wa Wabela, kwa Ashibeli, ukoo wa Washibeli, kwa Ahiramu, ukoo wa Wahiramu,39kwa Shefufamu, ukoo wa Washefumamu, kwa Hufamu, ukoo wa Wahufamu.40Wana wa Bela walikuwa ni Ardi na Naamani. Kutoka kwa Ardi ulijitokeza ukoo wa Waardi, na kutoka kwa Naamani ukajaitokeza ukoo wa Wanaamani.41Hizi ndizo koo za uzao wa Benjamini. Idadai yao ilikuwa wanaume 45,600.42Kooo za uzao wa Dani zilikuwa hizi zifuatazo: Kwa Shuhamu, ukoo wa Washuhamu. Hizi ndizo koo za uzao wa Dani.43Idadi ya koo zote za Washuhamu ilikuwa wanaume 64,400.44Koo za uzao wa Asheri zilikuwa zifuatazo: Kwa Imna, ukoo wa Waimna, kwa Ishvi, ukoo wa Waishivi, kwa Beria, ukoo wa Waberia.45Uzao wa Beria walikuwa hawa: Kwa Heberi, ukoo wa Waheberi, kwa Malikieli, ukoo wa Wamalikieli.46Jina la binti wa Asheri lilikuwa Sera.47Hizi ndizo koo za uzao wa Asheri, idadi yao ilikuwa wanaume 53,400.48Koo za uzao wa Naftali zilikuwa zifuatazo: Kwa Jahazeeli, ukoo wa Wajahazeel, kwa Guni, ukoo wa Waguni,49kwa Jezeri, ukoo wa Wajezeri, kwa Shilemu, ukoo wa Washilemu.50Hizi ndizo zilizokuwa koo za uzao wa Naftali, idadi yao walikuwa wanaume 45,000.51Hii ndiyo iliyokuwa jumla kuu ya wanaume wa Israeli: 601,730.

52BWANA akanena na Musa akamwambia,53Ile ardhi itagawanywa kati ya wanaume hawa kama urithi wao kwa kufuata idadi ya majina yao.54Kwa zile koo kubwa utawagawia urithi mkubwa, na kwa koo ndogo ndogo utawagawia urithi kidogo. Kwa kila familia utawapa urithi kufuata idadi ya wanaume waliohesabiwa.55Lakini ardhi itagawiwa kwa kupigiwa kura. Watairithi nchi kama itakavyogawiwa kwa kufuata koo za mababu.56Urithi huu utagawiwa kufuata koo kubwa na ndogo, watagawiwa kwa kufuata kura zitakavyokuwa.

57Koo za Walawi, zilizohesabiwa kwa kufuata ukoo kwa ukoo, walikuwa hivi: Kwa Gerishoni, ukoo wa Wagerishoni, kwa Kohathi, ukoo wa Wakohathi, kwa Merari, ukoo wa Wamerari.58Koo za walawi zilikuwa hzi: ukoo wa Walibni, Ukoo wa Wahebroni, ukoo wa Wamahali, ukoo wa Wamushi, na ukoo wa Wakora. Kohathi alikuwa wa uzao wa Amramu.59Jina la mke wa Amramu lilikuwa Jokibed, wa ukoo wa Lawi, aliyekuwa amezaliwa kwa Walawi kule Misri. Alimzalia Amramu watoto wao, ambao walikuwa ni Haroni, Musa, na Miriamu dada yao.60Kwa Haruni alizaliwa Nadabu na Abihu, Eliazari na Ithamari.61Nadabu na Abihu walikufa walipotoa sadaka kwa BWANA sadaka ya moto isiyokubalika.

62Waume waliohesabiwa mionigoni mwao walikuwa elfu ishirini na tatu, hawa ni wale wa umri wa mwezi mmoja na zaidi. Lakini hawakuhesabiwa kati ya wazawa wa Israeli kwa sababu hawakupewa urithi miongoni mwa wana wa Israeli.

63Hawa ndio wale walihesabiwa na Musa na Eliazari kuhani. Waliwahesabu watu wa Israeli katika uwanda wa Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko.64Lakini miongoni mwa hawa hapakuwa na mwanamume aliyehasabiwa na Musa na Haruni kuhani wakati wana wa uzao wa Israeli walipohesabiwa katika jangwa la Sinai.65Kwa BWANA alikuwa amesema kuwa kwa hakika watu hao wote wangefia jangwani. Hapakuwa na mtu aliyebaki miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune na Joshua mwana wa Nuni.

27

1Kisah wakaja kwa Musa binti wa Zelofehadi mwana wa Hefa mwana wa Gilied mwana wa Machiri mwana wa Manase, wa ukoo wa Manase mwana wa Yusufu. Hawa ndio waliokuwa binti zake: Mahala, Noha, Hogla, Milika, na Tiriza.2Walisimama mbele ya Musa, Eliazari kuhani, kwa. Viongozi, na mbele ya watu wote langoni mwa hema ya kukutania. Walisema,3“Baba yetu alifia jangwani. Hakuwa mmoja wa wale waliompinga BWANA katika lile kundi la Kora. Alikufa kwa dhambi zake, na hakuwa na watoto wa kiume.4Kwa nini jina la baba yetu liondolewe miongoni mwa ukoo wa jamaa zake kwa sababu ya kukosa wana? Tupeni ardhi miongoni mwa ndugu wa baba zetu.”

5Kwa hiyo Musa alileta shauri hilo mbele za BWANA.6BWANA akanena na Musa akamwambia, “Binti wa7Zelofehadi wanasema kitu sahihi. Lazima uwaptie ardhi kama urithi miongoni mwa ndugu wa baba zao, na uhakikishe kuwa urithi wa baba zao wanapata.

8Utawaambia wana wa Israeli na kusema, ‘Kama mtu anakufa na hana mtoto wa kiume, basi utaufanya urithi wake wapewe binti zake.9Kama hana binti, basi urithi wake atapewa kaka zake.10Kama hana kaka zake basi huo urithi watapewa ndugu wa baba yake.11Kama baba yake hana ndugu, basi huo urithi atapewa ndugu yake wa karibu katika ukoo, na utauchukua kuwa wake. Hii itakuwa sheria iliyoanzishwa kwa amri kwa ajili ya watu wa Israeli kama BWANA akivyoniamuru.”

12BWANA alimwambia Musa, “Nenda juu ya mlima Abaraimu na uitazama nchi ambayo nimewapa wana wa Israeli.13Baada ya kuwa umeiona, pia lazima ufe, kama Haruni kaka yako.14Hii itatokea kwa sababu ulipinga amri yangu katika jangwa la Sini. Pale ambapo maji yalitoka kwenye mwamba, katika hasira yako ulishindwa kuniheshimu mimi kama mtakatifu mbele ya macho ya watu wote.” Haya ni yale maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.

15Ndipo Musa akamwambia BWANA akisema,16“Wewe, BWANA, Mungu wa wote wenye mwili, uchague mtu awe juu ya watu,17mtu ambaye atatoka na kuingia kuja kwao na kuwatoa kisha kuwarudisha, ili kwamba watu wako wasije kuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.”

18BWANA akanena na Musa, “Mchukue Joshua mwana wa Nuni, mtu ambaye Roho yangu hukaa, na umwekee mikono yako juu yake.19Umweke mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya watu wote, na umwamuru kuwaongoza mbele ya macho yao.20Utaweka baadhi ya mamlaka yako kwake, ili kwamba watu wote wa Israeli wamtii.21Ataenda mbele ya Eliazari kuhani ili kutafuta mapenzi yangu kwake kwa ajili ya maamuzi ya kura. Yeye ndiye atakayetoa amri ili watu waweze kutoka na kuingia, yeye pamoja na watu wa Israeli, ambao ni watu wote.”

22Kwa hiyo Musa akafanya kama alivyoagizwa na BWANA. Alimchukua Joshua na kumweka mbele ya Eliazari kuhani na mbele ya jamii yote.23Akaweka mikono yake juu yake na kumwamuru aongoze, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.

28

1BWANA akanena na Musa akamwambia,2“Waamuru wana wa Isrseli uwaambie, ‘Mtanitolea sadaka kwa wakati uliopangwa, chakula cha sadaka yangu kilichotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa ajili yangu.3Pia uwaambie, ‘Hii ni sadaka iliyotengenezwa kwa moto ambayo mtaitoa kwa BWANA- mwanakondoo dume wa mwaka mmoja asiyekuwa na waa, wawili kila siku kuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku.4Mwanakondoo mmoja atatolewa sadaka asubuhi, na mwingine atatolewa sadaka jioni.5Mtatoa sadaka ya sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga, uliochanganywa na robo ya hini ya mafuta yaliyokamuliwa.6Hii ni sadaka ya ya kuteketezwa ya kila siku iliyoamriwa mlima Sinai ili kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajili ya BWANA.7Pamoja na robo ya hini ya sadaka ya kinywaji kwa mmoja wa hao wanakondoo. Utaimimina mahali patakatifu hiyo sadaka ya kinywaji kwa BWANA.8Yule mwanakondoo mwingine utamtoa sadaka jioni pamoja na sadaka ya unga kama yule wa asubuhi alivyotolewa. Pia utatoa tena sadaka ya kinywaji pamoja naye, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA.

9Katika siku ya Sabato utatoa wanakondoo dume wawili, wa umri wa mwaka mmoja kila mmoja wasiokuwa na dosari, na sehemu ya kumi mbili ya efa ya unga mwembamba kwa sadaka ya unga, uliochanganywa na mafuta, pamoja na sadaka ya kinywaji.10Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa kwa kila siku ya Sabato, kama nyongeza ya ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya kinywaji.

11Kila mwanzo wa mwezi, mtatoa sadaka za kuteketezwa kwa BWANA. Utatoa sadaka ya fahari wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na wanakondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari.12Pia mtatoa sehemu ya kumi tatu ya efa ya unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari, na sehemu za kumi mbili za unga mwembamba kuwa sadaka ya unga uliochanganywa na mafuta kwa yule kondoo mume mmoja.13Pia mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga kwa kila mwanakondoo. Hii itakuwa sadaka ya kuteketezwa, ya kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa ajilI ya BWANA.14Sadaka ya kinywaji ya watu itakuwa nusu ya hini ya divai ya yule fahari, sehemu ya tatu ya hini ya kondoo dume, na robo ya hini ya mwanakondoo. Hii ndiyo itakuwa sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi kwa miezi yote ya mwaka.15Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kwa BWANA. Hii itakuwa nyongeza kwa ile sadaka ya kila siku pamoja na ile sadaka ya vinywaji.

16Katika siku kumi na nne, ya mwezi wa kwanza itakuwa Pasaka ya BWANA.17Katika sku ya kumi na tano ya mwezi huu kutakuwa na sikukuu. Mtakula mikate isiyo na chachu kwa siku saba.18Katika siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA. Katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku19Hata hivyo, mtatoa sadaka iliyotengenezwa kwa moto, sadaka ya kuteketezwa kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari wawili, kondoo dume mmoja, na kondoo dume saba wa umri wa mwaka mmoja wakamilifu.20Pamoja na yule fahari, mtatoa sadaka sehemu za tatu efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, pamoja na yule kondoo mume sehemu za pili za kumi.21Kwa kila wale wanakondoo saba, mtatoa sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta,22na beberu mmoja kuwa sdaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.23Mtatoa hivi vitu kama sadaka ya nyongeza katika ile sadaka ya kila siku inayotakiwa kila asubuhi.24Kama ilivyofafanuliwa hapa, mtatoa sadaka hizi kila siku, kwa zile siku saba za Pasaka, kile chakula cha sadaka kilichotengenezwa kwa moto kuwa harufu nzuri kwa BWANA. Hiki kitatolewa kuwa sadaka ya nyongeza ya ile sadaka ya kuteketezwa na pamoja na ile sadaka ya vinywaji.25Siku ya saba mtakuwa na kusanyiko takatifu ili kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye zile kazi zenu za kila siku.

26Pia katika siku ya malimbuko, mtakapokuwa mnatoa sadaka ya unga mpya katika sikukuu zenu za Majuma, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumheshimu BWANA, na katika siku hiyo msifanye kazi zenu za kila siku.27Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari wawili wachanga, kondoo mume mmoja, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja.28Pamoja na hiyo mtatoa sadaka ya unga: unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa za unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila fahari na sehemu kumi mbili za yule kondoo mume.29Toeni sehemu ya kumi ya efa ya unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa kila wale wanakondoo saba,30na beberu mmoja ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.31Mtakapotoa hao wanyama wasio na dosari, pamoja na sadaka zake za vinywaji, hii itakuwa sadaka ya nyongeza katika zile sadaka za kila siku na pamoja na zile sadaka za unga.’”

29

1Katika siku ya kwanza, ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Katika siku hiyo hamtafanya kazi zenu za kila siku. Itakuwa siku ya kupiga matarumbeta.

2Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ya kufanya harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja na wanakondoo dume saba wa mwaka mmoja, kila mmoja mkamilifu.3Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya huyo fahari, sehemu mbili za kumi kwa ajili ya huyo kondoo mume,4na sehemu ya kumi ya kila hao wanakondoo waume saba.5Na mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi ili kufanya upatanisho kwa ajili yenu.6Toeni hizo sadaka katika mwezi wa saba kama nyongeza ya sadaka mtakazotoa kila mwanzo wa kila mwezi: pamoja na sadaka maalumu za kuteketezwa na sadaka za unga. Hizi zitakuwa nyongeza za sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji. Utakapokuwa ukiendelea na sadaka hizi, utakuwa ukitii kile kilichoamriwa kutoa harufu nzuri, sadaka iliyotengenezwa kwa moto kwa BWANA.

7Siku ya kumi ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu la kumwabudu BWANA. Mtajinyenyekeza na hamtafanya kazi.8Mtatoa sadaka ya kuteketezwa ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja mchanga ili kutoa harufu nzuri, kondoo mmoja mume, na wanakondoo saba waume wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.9Pamoja na sadaka hizo utatoa sadaka ya unga, unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa ajili ya fahari, sehemu mbili za kumi za kondoo dume mmoja,10na sehemu ya kumi ya efa moja kwa kila mwanakondoo wale saba.11Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya upatanisho. Hii itakuwa sadaka ya nyongeza ya upatanisho, ya sadaka ya kila siku ya kuteketezwa, pamoja na sadaka za unga, na sadaka zake za vinywaji.

12Siku ya kumi na tano ya mwezi wa saba, mtakuwa na kusanyiko takatifu lakumwabudu BWANA. Siku hiyo hamtafanya kazi za kila siku, na mtazitunza hizo sikukuu kwa muda wa siku saba kwa ajili ya BWANA.13Mtatoa sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ilikutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa mafahari wachanga kumi na tatu, kondoo waume wawili, na wanakondoo waume kumi na nne wa mwaka mmoja. Wote wakamilifu.14Pamoja na hao mtatoa sadaka ya unga, unga mwembaba uliochanganywa na mafuta, sehemu tatu za kumi za efa kwa kila fahari katika hao kumi na tatu, sehemu mbili za kumi kwa kila hao kondoo dume wawili,15na sehemu ya kumi ya efa ya hao wanakondoo kumi na nne.16Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi katika nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa, sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka za vinywaji.

17Siku ya pili ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi na mbili, kondoo dume wawili na wanakondoo dume kumi na mbili wa umri wa mwaka mmoja, wote wakamilifu.18Pamoja nao mtatoa sadaka ya unga, na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na kwa ajili ya wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilvyoamriwa.19Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kila siku, sadaka yake ya unga, na sadaka zake za vinywaji.

20Siku ya tatu ya kusanyiko, mtatoa sadaka mafahari kumi na moja, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.21Pamoja na hizo sadaka mtatoa sadaka ya unga na sdaka ya vinywaji kwa wale mafahari, kwa wale kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, utoe sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.22Mtatoa sadaka beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya zile sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.

23Siku ya nne ya kusanyiko, mtatoa mafahari kumi, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.24Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sdaka za vinywaji kwa wale mafahari, na kwa wale kondoo dume na kwa wale wanakodoo, mtatoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.25Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kuwa nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji

26Siku ya tano ya kusanyiko, mtatoa mafahari tisa, kondoo dume wawili, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.27Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, kondoo dume, na wale wanakondoo, mkitoa sdaka nyingi kama ilivyoamriwa.28Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kuteketezwa za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka za vinywaji.

29Siku ya sita ya kusanyiko, mtatoa mafahari wanane, kondoo dume wawili, na wanakondoo kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.30Pamoja na sadaka hizo mtatoa sadaka za unga nasadaka za vinywaji kwa wale mafahari, kondoo wa dume na wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.31Mtatoa beberu kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku za kuteketezwa, zadaka za unga, na sadaka za vinywaji.

32Siku ya saba ya kusanyiko, mtatoa mafahari saba, kondoo dume saba, na wanakondoo dume kumi na nne wa mwaka mmoja, wakamilifu.33Pamoja nao mtataengeneza sadaka ya unga na sadaka ya vinywaji kwa ajili ya wale mafahari, na kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkitoa sadaka nyingi kama ilivyoamriwa.34Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, na sadaka yake ya unga, na sadaka yake ya vinywaji.

35Siku ya nane mtakuwa na kusanyiko lingine makini. Hamtafanya kazi zenu za kila siku.36Mtafanya sadaka za kuteketezwa, sadaka iliyotengenezwa kwa moto ili kutoa harufu nzuri kwa BWANA. Mtatoa fahari mmoja, kondoo mmoja dume, na wanakondoo saba dume wa umri wa mwaka mmoja, wakamilifu.37Mtatoa sadaka zake za unga na sadaka zake za vinywaji kwa ajili ya yule fahari, kondoo dume, na kwa wale wanakondoo, mkifanya sadaka nyingi kadri ilivyoamriwa.38Mtatoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi kama nyongeza ya sadaka za kila siku, na sadaka zake za unga, na sadaka zake za vinywaji.

39Hivi ndivyo utakavyotoa sadaka kwa BWANA katika sikukuu zenu za kila mwaka. Hivi vitakuwa nyongeza ya viapo vyenu na sadaka zenu za hiari. Mtavitoa hivi kama sadaka zenu za kuteketezwa, sadaka za unga, sadaka za vinywaji, na sadaka za amani.”

40Musa aliwaambia wana wa Israeli kila kitu ambacho BWANA alikuwa amemwamuru kusema.

30

1Musa aliwambia viongozi wote wa makabila ya watu wa Israeli. “Hiki ndicho ambacho BWANA ameamuru.

2Mtu yeyote atakayefanya nadhiri kwa BWANA, au kuapa kwa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa ahadi, asivunje neno lake. Atafanya sawa na ahadi yake imtokayo kinywani mwake.

3Na kama binti anaishi katika nyumba ya baba yake na atafanya nadhiri kwa BWANA na kuifunga nafsi yake kwa kiapo,4na kama baba yake atasikia hiyo nadhiri na ahadi ambayo ametumia kuifunga nafsi yake, naye asiseme kitu kumzuia, ndipo nadhiri zake zitakuwa na nguvu. Kila ahadi ambayo ameitumia kuifunga nafsi yake itabaki kuwa na nguvu.5Lakini kama baba yake atasikia nadhiri yake na ahadi zake, na kama hatasema chochote kwake, ndipo nadhiri zake zote na ahadi alizofanya zitakapokuwa na nguvu.

6Hata hivyo, kama baba yake atasikia nadhri zake zote alizofanya na ahadi zake makini ambazo ametumia kufunga nafsi yake, na kama atazitengua ndani ya siku hiyo, ndipo hizo nadhiri hazitakuwa na nguvu. BWANA atamsamehe kwa kuwa baba yake amemzuia.7Kama ataolewa angali katika hivyo viapo, au kama atafanya ahadi za bila kufikiri ambazo atajifunga nazo, hivyo vifungo vitakuwa na nguvu.8Lakini kama mume wake atamzuia siku hiyo hiyo ambayo atamskia akiapa, basi atabatilisha hicho kiapo alichokifanya, kwa maneno yake ya midomo yake bila kufikiri ambayo kwayo amefunga nafsi yake. BWANA atamsamehe.

9Lakini kwa mjane au kwa mwanamke aliyetalikiwa, kila kitu amabacho atakisema kufunga nafsi yake lazima kitabaki na nguvu kinyume na yeye.

10Na kama mwanamke atafanya kiapo katika nyumba ya mume wake au akijifunga mwenyewe kwa kiapo,11na mume wake akakisikia hicho kiapo na hakusema chochote kwake na hakumpinga, basi viapo vyake vitasimama na vifungo alivyovifanaya vitabaki na nguvu.12Lakini kama mume wake atamzuilia katika siku hiyo ambayo atavisikia, basi chochote ambacho kitatoka katika kinywa chake kuhusu viapo vyake au ahadi zake havitabaki kuwa na nguvu. Mume wake atkuwa amevibatilisha. BWANA atamfungua.13Kila kiapo ambacho mwanamke anakifanya ambacho kinamfunga ili kujikana kinaweza kuthibitika au kubatilishwa na mume wake.14Lakini kama hatasema chochote kwake siku baada ya siku, basi atathibitisha nadhiri zake na ahadi zake zinazomfunga ambazo amefanya. Atakuwa amezithibitisha kwa sababu hakusema chochote wakati alipozisikia.15Na kama mume wake atajariibu kubatilisha kiapo cha mke wake baada ya kuzisikia kwa muda mrefu, basi ataajibika kwa dhambi zake.”

16Hizi ndizo amri ambazo Mungu alimwamuru Musa kuzitangaza - amri ambazo ziko kati ya mume na mke wake na kati ya baba na binti yake wakati akiwa katika ujana wake katika familia ya baba yake.

31

1BWANA alinena na Musa na kumwambia,2“Uwalipizie kisasi Wamidiani kwa kile walichowafanyia Waisraeli. Baada ya kufanya hivyo utakufa na kukusanyika na watu wako.”

3Kwa hiyo Musa akawaambia watu. Akasema, “Andaeni baadhi ya majeshi yenu kwa ajili ya vita ili kwamba wakawapige Wamidiani na kubeba kiapo cha BWANA.4Kwa kila kabila la Israeli watatuma askari elfu moja kwa ajili ya vita.”5Kwa hiyo kati ya wanaume maelfu elfu wa Israeli, wanaume elfu moja walitolewa kwa ajili ya vita, jumla ya wanaume elfu kumi na mbili.6Kisha Musa akawatuma kwenda vitani, elfu moja toka kila kabila pamoja na Finehasi mwana wa Eliazari kuhani, wakiwa na vitu kutoka mahali patakatifu wakiwa na matarumbeta kwa ajili ya ishara za sauti.

7Wakapigana na Wamidiani, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Wakawaua kila mwanaume.8Wakawaua wafalme wamidiani pamoja na wengine waliowaua ni: Evi, Rekimu, Zuri, Huri, na Reba, hawa walaikuwa ndio waflme watano wa Midiani. Pia walimwua Balaamu mwana wa Beori, kwa upanga.9Jeshi la Israeli likawachukua mateka wanawake wa Midiani, watoto wao, mifugo yao yote, kondoo wao na bidhaa zao zote. Walivichukua hivi kama mateka.10Waliichoma moto miji yao yote walimoishi na kambi zao zote.11Walichukua vitu vyote na wafungwa, watu na wanyama.12Wakawaleta mateka, nyara, na wakakamata vitu wakavileta kwa Musa, na Eliazari kuhani, na kwa jamii ya watu wa Israeli. Wakavileta hivi vitu kambini katika uwanda wa Moabu, kule Yorodani karibu na Yeriko.13Musa, Eliazari kuhani, pamoja na viongozi wa watu wakaenda kukutana nao nje ya kambi.

14Lakini Musa alikuwa na hasira dhidi ya viongozi wa jeshi, Wale majemedari wa maelfu na maakida wa mamia, waliotoka kupigana.15Musa akawaambia, “Je, mmewaacha wanawake wote kuishi?16Tazama, wanawake hawa ndio waliosababisha watatu wa Israeli, kupitia ushauri wa Balaamu, kufanya dhambi dhidi ya BWANA huko Peori, wakati ile tauni iliposambaa kwa watu wa Mungu.17Sasa basi, ueni kila mwanaume kuanzia wadogo, na ueni kila mwanamke aliyelala na mwanamume.18Lakini chukueni wale mabinti wadogo ambao hawajalala na mwanamume.

19Mtaweka kambi nje na kambi za Israeli kwa muda wa siku saba. Ninyi wote ambao mmeua watu au ambao mmegusa maiti yeyote mtajitakasa wenyewe katika siku ya tatu na katika siku ya saba - ninyi na mateka wenu.20Na mtayatakasa mavazi yenu yote, na kila kitu kilichotengenezwa kwa ngozi za wanyama, na manyoya ya mbuzi, na kila kitu kilichotengenezwa kwa mbao.”

21Eliazarai kuahani akawaambia wale wanajeshi waliokuwa wameenda vitani, “Hii ni amri ya sheria ambayo BWANA alimpa Musa:22Zile dhahabu, fedha, vyuma, bati, risasi,23na kila kitu knaweza kuhhimili moto, mtakiweka katka moto, navyo vitakuwa safi. Nakisha mtavitakasa vitu hivyo na maji ya farakano. Na vitu vyote ambavyo haviwezi kupita katika moto, mtavitakasa kwa maji hayo.24Na mtazifua nguao zenu katika siku ya saba, ndipo mtakapokuwa safi. Baada ya hapo mnaweza kurudi kwenye kambi za Israeli.”

25Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,26“Vihesabu vitu vyote vilivyochukuliwa nyara, wote watu na wanyama. Wewe, Eliazari kuhani, na viongozi wa watu kufuata koo27watavigawa hivi vitu katika mkundi mawili. Mvigawe kwa wanajeshi walioenda kupigana na kwa watu wote.28Kisha toza kodi ambayo itatolewa kwangu kutoka kwa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani. Hii kodi itakuwa moja kati ya mia tano, katika watu, ng'ombe, punda, kondoo, au mbuzi.29Uichukue hii kodi kutoka katika nusu yao na umpe Eliazari kuhani kwa ajili ya sadaka itakayotolewa kwangu.30Pia kutoka katika nusu ya watu wa Israeli, utachukua moja kati ya hamsini -kutoka vitu, ng'ombe, punda, na mbuzi. Uvitoe hivi kwa Walawi wanaotumika katika masikani yangu.”31Kwa hiyo Musa na Eliazari kuhani wakafanya kama BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa.

32Sasa zile nyara zilizokuwa zimebaki ambazo wanajeshi walikuwa wameteka zilikuwa kondoo 675,000,33makisai elfu sabini na mbili,34punda elfu sitini na moja,35Na wanawake elfu thelathini na mbili ambao walikuwa hawajalala na mwanaume yeyote.

36Ile hesabu ya nusu iliyokuwa imetunzwa kwa ajili ya wanajeshi ilikuwa kondoo 337,000.37Ile sehemu ya BWANA ya kondoo ilikuwa kondoo 675.38Makisai walikuwa elfu thelathini na sita ambayo kodi ya BWANA ilikuwa sabini na mbili.39Punda walikuwa 30,500 ambao sehemu ya BWANA ilikuwa sitini na moja.40Watu walikuwa wanawake elfu kumi na sita ambao kodi ya BWANA ilikuwa thelathini na mbili.

41Musa alichukuaaliichukua ile kodi ambayo ilitakiwa kuwekwa sadaka kwa BWANA. Akampatia Eliazari kuhani, kama BWANA alivyo mwamuru Musa.

42Ile nusu ya watu wa Israeli ambayo Musa alikuwa ameichukua toka kwa wanawjeshi waliokuwa wameenda vitani -43ile nusu y a watu ilikuwa kondoo 337,500,44maksai elfu thelathini na sita,45punda 30,500,46na wanawake elfu kumi na sita.47Kutoka kwenye nusu ya watu wa Israeli, Musa alichukua moja katika hamsini, wote watu na wanyama. Aliwapa Walawi ambao huitumikia masikani ya BWANA, kama BWANA alivyokuwa amemwamuru kufanya.

48Kisha wale maakida wa jeshi, makamanda wa elfu na makapteni wa mamia, wakaja kwa Musa.49Wakamwambia, “watumishi wako wamewahesabu wanajeshi ambao wako chini yetu, hakuna hata mmoja wao aliyekosa.50Tumemletea BWANA sadaka, ambayo kila mmoja amepata, vitu vya dhahabu, metali, timbi, pete za mhuri, vipini na vikuku, ili kujifanyia upatanisho kwa BWANA.”

51Musa na Eliazari kuhani wakapokea kutoka kwao dhahabu na vitu vyote vilivyotengenezwa kwa ufundi.52Vitu vyote vya sadaka ya dhahabu ambavyo walimpa BWANA- sadaka toka kwa makamanda wa maelfu na kutoka kwa makepteni wa mamia - vilikuwa na uzito wa shekeli 16,750.53Kila mwanajeshi alikuwa ameteka nyara ya kila mtu kwa ajili yake.54Musa na Eliazari kuhani wakazichukua zile dhahabu toka kwa makamanda wa maelfu na makepteni wa mamia. Wakavipeleka kwenye hema ya kukutania kama ukumbusho wa watu wa Israeli kwa BWANA.

32

1Sasa wana wa uzao wa Reubeni na wa Gadi walikuwa na idadi kubwa ya wanyama. Waliona ardhi ya Jazeri na Gileadi, kua ni ardhi nzuri kwa mifugo.2Kwa hivyo wana wa Gadi na wa Reubeni wakaja kumwambia Musa, na Eliazari kuhani, na viongozi wa watu. Wakasema,3“Hii ndiyo orodha ya maeneo ambayo tumeyatembelea: Diboni, Jazeri, Nimraha, Heshibonni, Ellealehi, Sebamu, Nebo, na Beoni.4Haya ni maeneo ambayo BWANA aliyachukua mbele ya watu wa Israeli, na maeneo mazuri kwa ajili ya mifugo. Sisi watumishi wako tuna mifugo mingi sana.5Wakasema kuwa, “Kama tutapata kibali mbele ya macho yako, tunaomba ardhi hii tupewe, sisi watumishi wako, kuwa urithi. Usituvushe ng'ambo ya Yorodani.”

6Musa akawajibu wale wana wa auzao wa Gadi na Reubeni, “Je, mngependa ndugu zenu waende vitani wakati ninyi mkikaa hapa?7Kwa nini kuwafunja moyo watu wa Israeli wasivuke kwenda kwenye nchi ambayo BWANA amewapa?8Baba zenu walifanya hivyo nilipowatuma kutoka Kadeshi Banea kwenda kuipeleleza ile nchi.9Walienda mpaka kwenye bonde la Esko waliona ile ardhi kisha wakawafunja mioyo watu wa Israeli kwa hiyo wakagoma kuingia kwenye nchi ambayo BWANA alikuwa amewapa.10Siku hiyo hasira ya BWANA iliwaka. Akaapa akisema,11‘Kwa hakika hakuna mtu aliyetoka Misri, kuanzia wa umri wa miaka ishirini na zaidi ambaye ataiona nchi ambayo niliwaapia Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwa sababu hawakunifuata mimi kwa ukamilifu, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni.12Ni Kalebu na Joshua tu ndio walionifuata kwa ukamilifu.’13Kwa hivyo hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israei. Akawafanya wazunguke zunguke jangwani kwa miaka arobaini mpaka kile kizazi kilichofanya maovu mbele za macho yake kilipoteketea.14Tazama, mmetokea katika nafasi za baba zenu, kama watu wengine wenye dhambi zaidi, ili kuongeza hasira ya BWANA kwa Israeli.15Kama hamtamfuata, ataiacha Israeli jangwani na mtakuwa mmewateketeza watu hawa wote.

16Kwa hiyo wakaja karibu na Musa wakamwambia, “Turuhusu tujenge hapa uzio kwa ajili ya ng'ombe zetu na miji hapa kwa ajili ya familia zetu.17Hata hivyo, sisi wenyewe tutajipanga kijeshi kwenda na jeshi la Israeli mpaka tumewaongoza kupata maeneo yao. Lakini familia zetu zitakuwa kwenye miji ya maboma kwa sababu ya watu wengine ambao bado wanaishi katika nchi hii.18Hatutarudi kwenye familia zetu mpaka kila mmoja wa watu wa Israeli apate urithi wake.19Sisi hatutachukua urithi wa ardhi pamoja nao kule ng'ambo ya Yorodani, kwa sababu urithi wetu uko hapa upande wa mashariki mwa Yorodani.”

20Kwa hivyo Musa akawajibu, “Kama mtafanya mnachokisema, kama mtajipanga wenyewe mbele za BWANA kwenda vitani,21basi kila mmoja wa wanajeshi wenu lazima avuke Yorodani mbele za BWANA, mpaka atakapowafukuza maadui zake kutoka mbele zake22na nchi itawaliwe na Israeli mbele zake. Kisha mtaweza kurudi. Hamtakuwa na hatia mbele za BWANA na mbele ya Israeli. Hii nchi itakuwa miliki yenu mbele za BWANA.

23Bali kama hamtafanya hivyo, tazama, mtakuwa mmefanya dhambi mbele ya BWANA. Muwe na hakika kuwa dhambi yenu itaonekana24wazi. Jengeni miji kwa ajili ya familia zenu na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; kisha fanyeni kile mlichokisema.”

25Wale wana wa Gadi na Reubeni wakamwambia Musa, wakisema, “Watumishi wako wtafanya kama vile wewe, bwana wetu, unavyotuamuru.26Watoto wetu, wake zetu, makundi yetu, na wanyama wetu wote watakaa huko kwenye miji ya Gileadi.27Hata hivyo, sisi watumishi wako, tutavuka kwenda ng'ambo mbele za BWANA kupigana, kila mtu ambaye yuko tayari kwa vita, kama vile wewe, bwana wetu, unavyosema.”

28Kwa hiyo Musa akawapa maelekezo yaliyowahusu kwa Eliazari kuhani, kwa Joshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa koo kufuata jamaa zao katika makabila ya wana wa Israeli.29Musa akawaambia, “Kama uzao wa Reubeni na Gadi watavuka ng'ambo ya Yorodani pamoja nanyi, kila mwanaume anayetakiwa kuwa vitani mbele za BWANA, na kama nchi mtaitawala mbele zenu, ndipo mtakapowapa eneo la Gileadi kuwa miliki yao.30Lakini kama hawatavuka pamoja nanyi wakiwa na silaha zao, basi mtawapa urithi wao katika nchi ya Kanaani.”

31Kwa hiyo wana wa uzao wa Gadi na wa Reubeni wakamjibu wakisema, Kama vile BWANA alivyosema nasi, sisi watumwa wako, hiki ndicho tutakachokifanya.32Tutavuka tukiwa na silaha zetu mbele za BWANA kuingia katika nchi ya Kanaani, lakini urithi wetu utabaki upande huu wa Yordani.”

33Kwa hiyo uzao wa Gadi na Reubeni, na pia nusu ya kabila la Manase mwana wa Yusufu, Musa akawapa ufalme wa Sihoni, mfalme wa Waamori, na wa Ogi, mfalme wa Bashani, Aliwapa hiyo nchi, na kuwagawia miji yake yote pamoja na mipaka yake, miji yote ya nchi inayowazunguka.

34Wale wa uzao wa Gadi wakaijenga Diboni,35Atarothi, Aroeri, Atrothi, Jazeri, Jogbehaha, Bethi Nimraha,36na Bethi Harani kuwa miji iliyo na maboma na mazizi ya kondoo wao.

37Wale wa uzao wa Reubeni wakaijenga Heshiboni. Elealehi, Kiriathaimu,38Nebo, Baali Meoni - baadaye waliyabadili majina yao, na Sibimaha.

39Wale wa uzao wa Machiri mwana wa Manase walienda Gileadi na kuutwaa kutoka kwa Waamori waliokuwa wakiishi humo.40Kisha Musa akaitoa Gileadi kwa Machiri mwana wa Manase, na watu wake wakaishi humo.41Jairi mwana wa Manase alienda kuiteka miji yake na kuiita Havothi Jairi.42Nobaha alienda kutheka Kenathi na vijiji vyake, na akauita kwa jina lake Nobaha.

33

1Hizi ndizo safari za wana wa Israeli hapo walipotoka katika nchi ya Misri pamoja na makundi yao ya kijeshi chini ya uongozi wa Musa na Haruni.2Musa aliandika maeneo yote tangu walipoondoka mpaka walipofika, kama alivyoamuriwa na BWANA. Hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa kwa kila walipotoka.3Mwezi wa kwanza walisafiri kutoka Ramesi, waliondoka siku ya kumi na tano. Asubuhi siku iliyofuata baada ya Pasaka, Wana wa Israeli waliondoka wazi wazi, mbele ya machoya Wamisri wote.4Hii ilitokea wakati Wamisiri walipokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza, ambao BWANA alikuwa amewaua miongoni mwao, kwa kuwa pia alikuwa ameiadhibu miungu yao.5Wana wa Israeli walisafiri kutoka Ramesi na kuweka kambi6Sukothi. Walisafiri toka Sukothi na kuweka kambi Ethamu, mwisho wa nyika.7Wakasafiri kutoka Ethamu wakarudi mpaka Pi-Hahirothi, ambayo inaikabili Baali Zephoni, ambapo waliweka kambi kuikabili Migidoli8Kisha wakasafiri toka mkabala wa Pi- Hairothi na kupita katikati ya bahari kuelekea nyikani. Wakasafiri safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu na kuweka kambi Mara.9Wakasafiri kutoka Mara kufika Elimu. Pale Elimu kulikuwa na chemichemi kumi na mbili za maji na miti sabini ya mitende. Hapo ndipo walipoweka kambi.10Walisafiri kutoka Elimu na kuweka kambi karibu na Bahari ya Shamu.11Walisafiri kutoka Bahari ya Shamu na kuweka kambi katika nyika ya Sini.12Walisafiri kutoka nyika ya Sini na kuweka kambi Dofka.13Wakasafiri kutoka Dofka na kuweka kambi Alushi.14Wakasafiri kutoka Alushi na kuweka kambi Refidimu, ambapo watu walikosa maji ya kunywa.15Walisafiri kutoka Refidimu na kuweka kambi kwenye nyika ya Sinai.16Walisafiri kutoka nyika ya Sinai na kuweka kambi Kibrothi Hataava.17Walisafiri kutoka Kibrothi Hataava na kuweka kambi Hazerothi.18Walisafiri kutoka Hazerothi na kuweka kambi Rithima.19Walisafiri kutoka Rithima na kuweka kambi Rimoni Perezi.20Walisafiri kutoka Rimoni Perezi na kuweka kambi Libna.21Walisafiri kutoka Libna na kuweka kambi Risa.22Walisafiri kutoka Risa na kuweka kambi Kehelatha.23Walisafiri kutoka Kehelatha na kuweka kambi kwenye Mlima Sheferi.24Walisafiri kutoka Mlima Sheferi na kuweka kambi Harada.25Walisafiri kutoka Harada na kuweka kambi Makelothi.26Walisafiri kutoka Makelothi na kuweka kambi Tahathi.27Walisafiri kutoka Ttahalathi na kuweka kambi Tera.28Walisafiri kutokaTera na kuweka kambi Mithika.29Walisafiri kutoka Mithika na kuweka kambi Hashimona.30Walisafiri kutoka Hashimona na kuweka kambi Moserothi.31Walisafiri kutoka Moserothi na kuweka kambi Bene Jaakani.32Walisafiri kutoka Bene Jaakani na kuweka kambi Hori Hagidigadi.33Walisafiri kutoka Hori Hagidigadi na kuweka kambi Jotibatha.34Walisafiri kutoka Jotibatha na kuweka kambi Abrona.35Walisafiri kutoka Abrona na kuweka kambi Ezioni Geberi.36Walisafiri toka Ezioini Geberi na kuweka kambi katika nyika ya Sini kule Kadeshi.37Walisafiri kutoka Kadeshi na kuweka kambi Mlima Hori, Pembezoni mwa nchi ya Edomu.38Hapo ndipo Haruni kuhani alipoenda kwenye Mlima Hori kwa amri ya BWANA na kufa kule mwaka wa arobaini bada ya Wisraeli kutoka katika nchi ya Misri, katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano.39Haruni alikuwa na umri wa mika 123 alipokufa pale juu ya Mlima Hori.40Wakanaani, mfalme wa Aradi, ambao waliishi kusini mwa nyika katika nchi ya Kanaani, walisikia juu ya ujio wa wana wa Israeli.41Walisafiri kutoka Mlima Hori n a kuweka kambi Zalimona.42Walisafiri kutoka Zalimona na kuweka kambi Punoni.43Walisafiri kutoka Punoni na kuweka kambi Obothi.44Walisafiri kutoka Obothi na kuweka kambi Abarimu, katika mpaka wa Moabu.45Walisafiri kutoka Abarimu na kuweka kambi Diboni Gadi.46Walisafiri kutoka Diboni Gadi na kuweka kambi Alimoni Diblathaimu.47Walisafiri kutoka Alimoni Diblathaimu na kuweka kambi kwenye milima ya Abarimu mkabala na Nebo.48Walisafiri kutoka mlima wa Abarimuna kuweka kambi kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani huko Yeriko.49Waliweka kambi karibu na Yorodani, kutoka Bethi Jeshimothi mpaka Abeli Shitimu katika nyanda za Moabu.

50Hapo BWANA alinenana na Musa katika nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,51“Nena na wana wa Israeli uwaambie. ‘Mtakapovuka mto Yorodani kuingia Kanaani,52ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote mbele yenu. Mtaziharibu sanamu zote za kuchongwa. Mtaziharibu sanamu zao za kusubu na kuharibu mahali pao pote palipoinuka.53Mtachukua hiyo ardhi iwe mali yenu na muishi ndani yake, kwa sababu nimewapeni hiyo nchi iwe mali yenu.

54Mtairithi hiyo nchi kwa kupiga kura, kwa kufuata kila ukoo. Kwa zile koo kubwa kubwa mtawapa sehemu kubwa ya ardhi, na kwa zile koo ndogo ndogo mtawapa sehemu ndogo ya ardhi. Kura itakapoanguka kwenye kila ukoo, hiyo ardhi itakuwa mali yake. Mtairithi ardhi kufuata ukoo wa kabila la jamaa zenu.55Lakini kama hamtawafukuza wenyeji wa nchi hiyo watoke mbele yenu, ndipo wale watu mtakaowaruhusu wakae nanyi watakapokuwa kama sindano machoni mwenu na miiba katika mbavu zenu. Watayafanya maisha yenu yawe magumu katika nchi mnayoishi.56Ndipo itakapotokea kuwa kile ambacho Mimi ninakusudia kufanya kwa wale watu, Nitawafanyia pia ninyi.’”

34

1BWANA akanena na Musa akasema,2“Waamuru watu wa Israeli na uwaambie, ‘Mtakapoingia katika nchi ya Kanaani, nchi ambayo itakuwa mali yenu, nchi ya Kanaani na mipaka yake, mpaka wenu wa kusini utaendelea kutoka nyika ya Sini hadi mpaka wa Edomu.3Mwisho wa mpaka wa kusini utakuwa mwisho wa bahari ya chumvi kuelekea mashariki.

4Mpaka wenu utageukia kusini kutoka mlima kuelekea Akrabimu na kupitia nyika ya Sini. Na kutokea huko utaelelkea kusini mwa Kadeshi Barinea na kuelekea Hazari Adari mpaka Azimoni.5Kutoka huko, mpaka utageuka kutoka Azimoni kuelekea kijito cha Misri na kukifuata mpaka baharini.

6Mpaka wa Magharibi utakuwa pwani ya bahari kuu. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa wa Magharibi.

7Mpaka wenu wa kaskazini utaanzia kwenye bahari kuu hadi Mlima Hori,8kisha kutoka Mlima Hori hadi Lebo Hamathi, kisha Zedadi.9Mpaka utaendelea hadi Zifroni na kuishia Hazari Enani. Huu ndio utakuwa mpaka wenu wa kaskazini.

10Kisha mtaweka alama za mpaka wenu wa mashariki ambao utaanzia Hazari Enani kuelekea kusini Shefamu.11Kisha mpaka wa kusini utaendelea kutoka Shefamu hadi Ribla, upande wa masharikia mwa Aini. Mpaka utaedelea upande huo wa mashariki hadi upande wa mashariki wa bahari ya Kinerethi.12Kisha mpaka utaendelea kuelekea kusini hadi mto Yordani na hadi bahari ya chumvi. Hii ndiyo itakuwa nchi yenu, kwa kuifuata mipaka yake yote inayozunguka.’”

13Kisha Musa akawaamuru watu wa Israeli akasema, “Hii ndiyo nchi ambayo mtaipokea kwa kura, ambayo BWANA ameamuru kuwapa yale makabila tisa na nusu.14Kabila ya uzao wa Reubeni, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na uzao wa kabila la Gadi, kwa kufuata jinsi walivyopewa urithi kwa jamaa ya kabila yao, na nusu ya Manase wamepata ardhi yao.15Wale makabila mawili na nusu wameshapata mgao wao ng'ambo ya mto Yordani upande wa mashariki, kuelekea kule linakotokea jua.”

16BWANA akanena na Musa akasema,
17“Haya ndiyo majina ya watu watakaoigawa ardhi kwa ajili ya urithi wao: Eliazari kuhani na Joshua mwana wa Nuni.
18Mtachagua kiongozi mmoja toka kila kabila ili kuigawa ardhi kwa koo zao.19Haya ndiyo majina ya wanaume: Kutoka kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.
20Kutoka kwenye kabila la uzao wa Simeoni, Shemueli mwana wa Amihudi.
21Kutoka kabila la Benjamini, Elidadi mwana wa Kisloni.
22Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Dani, Buki mwana wa Jogili.
23Kiongozi kutoka uzao wa Yusufu, kwenye kabila la Manase, Hannieli mwana wa Efodi.
24Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Efraimu, Kemueli mwana wa Shiftani.
25Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Zabuloni, Elizafani mwana wa Parinaki.
26Kiongozi kutoka kwenye kabila la uzao wa Isakari, Palitieli mwana wa Azzani.
27Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Asheri, Ahihudi mwana wa Shelomi.
28Kiongozi kutoka kabila la uzao wa Naftali, Pedaheli mwana wa Amihudi.”

29BWANA aliwaamuru wanaume hawa kuigawa nchi ya Kanaani na kuwapa kila kabla sehemu yao.

35

1BWANA akanena na Musa kwenye nyanda za Moabu karibu na Yorodani kule Yeriko akasema,2“Waamuru watu wa Israeli kutoa sehemu ya urithi wa ardhi yao kwa Walawi. Watawapa miji ya kuishi ndani yake na eneo la malisho kuzunguka miji hiyo.3Walawi watakuwa na miji hiyo ya kuishi. Eneo la malisho litakuwa kwa ajili ya ng'ombe zao, kondoo zao, na wanyama wao wote.

4Hayo malisho yatakayozunguka miji hiyo ambayo mtawapa Walawi yataanzia kwenye maboma kwa ukubwa wa “mita 457” kila upande.5Utapima dhiraa elfu mbili kutoka nje ya mji kuelekea mashariki, na dhiraa elfu mbili kuelekea kusini, na dhiraa elfu mbili kuelekea upande wa magharibi, na dhiraa elfu mbilii kuelekea upandewa kaskazini. Haya yatakuwa maeneo ya malisho yao. Miji itakuwa katikati.

6Katika hiyo miji sita mtakayowapatia Walawi, itatumika kama miji ya ukimbizi. Mtatoa maeneo haya ili kama mtu ameua mtu apate mahali pa kukimbilia. Pia mtatoa miji mingine arobaini na mbli.7Jumla ya miji ambyo mtawapa Walawi itakuwa arobaini na nane. Mtawapa hiyo miji pamoja na maeneo yao ya malisho.8Zile kabila kubwa za watu wa Israeli, kabila ambalo lina ardhi zaidi, watatoa ardhi zaidi. Makabila madogo madogo watatoa miji michache. Kila kabila lazima watoe kwa ajili ya Walawi kwa kufuata mgawo waliopata.”

9Kisha BWANA akanena na Musa akamwambia,10“Sema na wana wa Israeli na uwaambie, ‘Mtakapovuka Yordani kuingia Kanaani,11Kisha mchague miji itakayotumika kama miji ya ukimbizi kwa, ajili yenu, mahali ambapo mtu aliyeua mtu pasipo kukusudia anaweza kukimbilia.12Hii miji itakuwa kwenu miji ya ukimbizi kwa mtu anayetaka kulipa kisasi. Ili kwamba mtuhumiwa asije akauawa bila kwanza kusikilizwa na jamii.13Mtachagua miji sita kuwa miji ya ukimbizi.14Mtatoa miji mitatu kule ng'ambo ya Yorodani na miji mitatu huko Kanaani. Itakuwa miji ya ukimbizi.15Kwa ajili ya watu wa Israeli, wageni, kwa yeyote anayeishi kati yenu, hii miji sita itatumika kama miji ya ukimbizi kwa mtu yeyote atakayeua mtu bila kukusudia anaweza kukimbila.

16Lakini kama mtuhumiwa amempiga mtu na chombo cha chuma, na huyo mtu akafa, basi kwa hakika yule mtuhumiwa ni muuaji. Kwa hivyo anatakiwa kuuawa.17Kama yule mtuhumiwa amempiga mtu kwa jiwe mkononi mwake ambalo linaweza kumwua mtu, na kama yule mtu atakufa, basi hakika huyo mtuhumiwa ni muwaji. Kwa hakika anatakiwa kuuawa.18Kama mtuhumiwa amempiga mtu kwa silaha ya mti ambayo inaweza kuua mtu na kama huyo mtu atakufa, basi kwa hakika huyo mtuhumiwa ni muwaji. Kwa hakika huyo anataikwa kuuawa.19Mwenye kulipa kisasi cha damu ndiye atakayemua muaji. Atakapokutana naye, anaweza kumua.20Lakini kama yule mtuhumiwa atamshinda mtu yeyote yule anayemchukia au kama atamtupia kitu, wakati akimvizia, kiasi kwamba huyo mtu akafa,21Au kama atampiga ngumi kwa chuki na mtu huyo akafa, ndipo yule mtuhumiwa aliyempiga hakika atauawa. Yeye ni muaji. Yule mlipa kisasi cha damu anaweza kumua muuaji pale atakapokutana naye.

22Lakini kama mtuhumiwa atampiga mtu ghafla bila kuwa na chuki hapo awali, au kama atamtupia kitu ambacho kitampiga mtu bila kumvizia23Au kama atatupa jiwe amabalo linaweza kumua mtu bila kumwona, basi huyo mtu hakua adui yake, hakukusudia kumwumiza huyo mtu. Basi hiki ndicho kitachofanywa kama mtu huyo atakufa.24Kwa tatizo la jinsi hiyo, Watu wataamua kati ya mlipa kisasi na mtuhumiwa kwa kufuata taratibu zifuatazo.25Watu watamwokoa mtuhumiwa kutoka kwenye nguvu za mlipa kisasi cha damu. Watu watamrudisha mtuhumiwa katika mji wa ukimbizi ambao hapo awali alikimbilia. Ataishi pale mpaka yule kuhani anayetumikia atakapokufa, ambaye alipakwa mafuta matakatifu.

26Lakini kama yule mtuhumiwa muda fulani ataenda nje ya mipaka ya mji a ukimbizi ambao alikimbilia,27na kama yule mlipa kisasi cha damu atamwona nje ya mipaka ya mji wake wa ukimbizi, kama atamuwa huyo mtuhumiwa, mlipa kisasi cha damu hatakuwa na hatia ya mauaji hayo.28Hii ni kwa sababu yule mtuhumiwa alitakiwa kubaki katika mji wake wa ukimbizi mpaka kuhani mkuu atakapokufa. Baada ya kifo cha kuhani mkuu, yule mtuhumiwa atarejea kwenye nchi yake ambako kuna mali yake.

29Hizi amri zitakuwa maagizo kwenu kwa kizazi chote mahali kote mnakoishi.

30Yeyote amwuaye mtu, muwaji lazima atauawa, kama neno la ushahidi litakavyotolewa. Lakini ushahidi wa mtu mmoja unaweza usitoshe kusababisha mtu kuuawa.

31Pia, msipokee fidia kwa ajili ya uhai wa muwaji ambaye ana hatia ya mauti. Kwa hakika lazima auawe.

32Na msipokee fidia ya mtu aliyekimbilia kwenye miji ya ukimbizi. Msimruhusu kwa namna yeyote kurudi kwenye mali zake mpaka pale kuhani mkuu atakapokufa.

33Msiiharibu nchi mnayokaa kwa namna hii, kwa kuwa damu ya muwaji huharibu nchi. Hakuna sadaka ya upatanisho inayoweza kufanywa kwa nchi pale damu inapomwagika juu yake, isipokuwa kwa damu ya mtu aliyeimwaga.34Kwa hiyo msiinajisi nchi mnayoishi kwa sababu Mimi ninaishi ndani yake. Mimi BWANA huishi kati ya watu wa Israeli.”’

36

1Kisha wale viongozi wa nyumba za mababu wa ukoo wa Gileadi mwana wa Machiri (ambaye alikuwa mwana wa Manase), ambao walikuwa wa ukoo wa uzao wa Yusufu, walikuja wakasema mbele za Musa na mbele za vionigozi wa familia za mababa wa watu wa Israeli.2Wakasema, “BWANA alikuamuru, wewe bwana wetu, kutupa mgao wa ardhi kwa kura kwa wana wa Israeli. Uliamuriwa na BWANA kutoa mgao wa Zerofehadi kaka yetu kwa binti zake.3Lakini hawa binti wameolewa na wanaume toka kabila zingine za wana wa Israeli, basi mgao wao wa ardhi utaondolewa kutoka kwenye mgao wa mababu zao. Utaongezwa kwenye mgao wa makabila ambayo wao wanaungana nao. Kwa sababu hiyo, Utaondolewa kwenye mgao uliopangwa kwenye urithi wetu.4Kwa sababu hiyo, wakati wa mwaka wa yubilee ya wana wa Israeli utakapofika, mgao wao utaunganishwa na kabila ile waliyoungana nao. Kwa sababu hii mgao wao utaondolewa kwenye mgao wa mababu zetu.”

5Basi Musa akawapa amri wana wa Israeli, kwa neno la BWANA. Akasema, “Kile wanachosema watu wa kabila la Yusufu kiko sahihi.6Hiki ndicho BWANA anaagiza kuhusu mabinti wa Zelofehadi. Anasema, ‘Acha waolewa na wale ambao wao wanaofikiri ni vizuri zaidi, lakini lazima waolewe ndani ya kabila ya baba yao.’7Hakuna mgao wa watu utakaobadilika kutoka kabila moja kwenda jingine. Kila mtu wa Israeli ataendelea na mgao wa kabila ya baba yake.8Kila mwanamke wa watu wa Israeli aliye na mgao kwenye kabila lake lazima aolewe na mtu wa ukoo unaotoka kwenye kabila la baba yake. Hii itafanyika hivyo ili kila mtu wa wana wa Israeli aweze kuwa na urithi kutoka kwa mababu zake.9Hakuna mgao utakaobadilika kutoka kabila lingine kwenda kabila lingine. Kila mtu wa kabila za watu wa Israeli atalinda urithi wake.”

10Kwa hivyo wale binti wa Zelofehadi walifanya kama vile BWANA alivyokuwa amemwamuru Musa. Mahila, Tiriza, Hogila, Milika, na Noha, binti za11Zelofehadi, waliolewa na wana wa uzao wa Manase.12Waliolewa katika koo za uzao wa Manase mwana wa Yusufu. Kwa sababu hii, urithi wao ulibaki kwenye kabila la ukoo ambalo baba yao alikuwa anatoka.

13Hizi ndizo amri na maagizo ambayo BWANA aliyatoa kupitia Musa kwa wana wa Israeli katika nyanda za Moabu karibu na Yordani huko Yeriko.

Kumbukumbu la torati

1

1Haya ni maneno ambayo Musa aliyasema kwa Israeli wote ng'ambo ya jangwa la Yordani, katika tambarare ya mto wa Yordani juu ya Suph, katikati mwa Paran, Topheli, Laban, Hazeroth, na Di Zahab.2Ni safari ya siku kumi na moja toka Horabu kupitia njia ya mlima wa Seir kwenda Kadeshi Barnea.

3Ilitokea kwenye mwaka wa arobaini, mwezi wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, Musa alizungumza kwa watu wa Israeli, kuwaambia yote yale Yahwe aliyomwamuru kuhusu wao.4Hii ilikuwa baada ya Yahwe kumvamia Sihoni mfalme wa Amoria, ambaye aliishi huko Heshboni, na Ogi mfalme wa Bashani, ambaye aliishi huko Ashtarothi ya Edrei.

5Ng'ambo ya Yordani, katika nchi ya Moabu, Musa alianza kutangaza maelekezo haya, akisema,

6“Yahwe Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, akisema, ‘Umeishi vya kutosha katika milima ya nchi hii.7Geuka na uanze safari yako, na uende kwenye nchi ya milima ya Waamori, na kwenye maeneo yote karibu na tambarare ya mto Yordani, katika nchi ya milima, na nyanda za chini, huko Negebu na pwani - nchi ya Wakanani na huko Lebanoni mbali ya mto mkuu wa Euphratesi.8Tazama, nimetenga nchi kwa ajili yako, nenda ndani na umiliki nchi ambayo Yahwe aliapa kwa baba zako, Ibrahimu, Isaka na Yakobo, kuwapa na uzao wao baada yao.’”

9Nilisema nanyi kwa wakati huo, nikisema, “Siwezi kuwabeba mimi peke yangu.10Yahwe Mungu wenu amewazidisha, na tazama, leo mmekuwa umati wa nyota za angani.11Yahwe aweza, Mungu wa baba zenu, kuwafanya ninyi mara elfu moja zaidi ya mlivyo, na kuwabariki, kama alivyoahidi!12Lakini inawezekanaje mimi peke yangu kubeba shehena zenu, mizigo yenu, na migogoro yenu?13Chukueni wanaume wa hekima, wanaume wanao elewa, na wanaume walio na sifa nzuri toka kila kabila, nitawafanya kuwa vichwa juu yenu.”

14Mlinijibu na kusema, “Jambo ulilolisema ni zuri kwetu kufanya.”

15Kwa hiyo nilichukua vichwa vya makabila yenu, wanaume wa hekima, na wanaume wenye sifa nzuri, na nikawafanya kuwa vichwa juu yenu, jemedari kwa elfu, jemedari kwa hamsini, jemedari kwa kumi, na maakida, kabila kwa kabila.16Niliwaamuru waamuzi wenu kwa wakati huo, kusema, “Sikiliza mabishano kati ya ndugu zenu, na muhukumu kwa haki kati ya ndugu na ndugu zenu, na wageni walio pamoja nanyi.17Hamtaonyesha upendeleo kwa yeyote katika mgogoro, mtasikia madogo na makubwa pia. Hamtaogopa uso wa mtu, kwa kuwa hukumu ni ya Mungu. Migogoro iliyo migumu kwenu, mtaniletea mimi, na mimi nitaisikiliza.”18Niliwaamuru kwa wakati huo mambo yote mtakayofanya.

19Tulisafiri toka Horebu na kwenda kupitia jangwa lile kubwa lote na lenye kutisha lile mliloliona, katika njia yetu kuelekea nchi ya milima ya Waamori, kama Yahwe Mungu wetu alivyotuamuru sisi, na tukaja Kadeshi ya Barnea.20Niliwaambia, “Mmekuja kwenye nchi ya milima ya Waamori, ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi.21Tazama, Yahwe Mungu wenu amekwisha weka nchi mbele yenu; nenda, muimiliki, kama Yahwe, Mungu wa baba zenu, amekwisha zungumza nanyi, msiogope wala kukata tamaa.”

22Kila moja wenu alikuja kwangu na kusema, “Basi tutume watu mbele yetu, ili kwamba waweze kupeleleza nchi kwa ajili yetu, na kutuletea sisi neno kuhusiana na njia ya wapi tuvamie, na kuhusiana na miji tutakayoingia.”

23Shauri hilo lilinibariki mimi, nilichukua watu kumi na wawili kutoka kwenu, mtu moja kwa kila kabila.24Waligeuka na kwenda juu ya nchi ya milima, kufika kwenye bonde la Eshkoli na kufanya upepelezi wa kina.25Walichukua baadhi ya mazao ya ardhi mikononi mwao na kuleta kwetu. Pia walileta neno na kusema, “Ni nchi nzuri ambayo Yahweh Mungu wetu anatupa sisi.”

26Bado mlikataa kushambulia, lakini mliasi dhidi ya amri ya Yahwe Mungu wenu.27Mlilalamika katika mahema yenu na kusema, “Ni kwa sababu Yahwe alituchukia sisi kwa kuwa ametutoa katika nchi ya Misri, kutuweka katika mikono ya Waamori kutuangamiza.28Tuende wapi sasa? Ndugu zetu wamefanya mioyo yetu kuyeyuka, kusema, ‘Hao watu ni wakubwa na warefu zaidi yetu, miji yao ni mikubwa na imeimarishwa kwenda mbinguni; zaidi ya yote, tumewaona wana wa Anaki huko.’”

29Kisha nikasema nao, “Msitishwe wala msiwaogope.30Yahwe Mungu wenu, ambaye aenda mbele yenu, atawapigania, kama yote aliyofanya kwa ajili yenu huko Misri mbele ya macho yenu,31na pia katika jangwa, ambapo mmekwisha muona Yahwe Mungu wenu jinsi alivyowabeba, kama mtu abebavyo mtoto wake, kote mlikoenda mpaka kufika hapa.”

32Bado licha ya neno hili hamkumuamini Yahwe Mungu wenu,33aliyeenda mbele yenu kwenye njia kutafuta eneo kwa ajili yenu kuweka kambi, katika moto usiku, na katika wingu, mchana.

34Yahwe alisikia sauti ya maneno yenu na alikasirika; aliapa na kusema,35“Hakika hakuna mmoja ya hawa watu wa kizazi hiki kiovu wataona nchi nzuri ambayo niliapa kuwapa babu zao,36kasoro Kalebu mwana wa Jephuneeh; yeye ataiona. Nitampa nchi ambayo amekwisha kuikanyanga, na watoto wake, kwa sababu alimfuata Yahwe kwa ukamilifu.”

37Pia Yahweh alinikasirikia mimi kwa sababu yenu, kusema, “Wewe pia hautaingia huko,38Yoshua mwana wa Nuni, ambaye amesimama mbele yako, yeye ataingia, mtie moyo, kwani yeye atawaongoza Israeli kuimiliki.

39Zaidi ya yote, watoto wenu wadogo, ambao mlisema watakuwa waathirika, ambao leo hawana elimu ya uzuri au ubaya- wataenda ndani huko. Wao nitawapa nchi hiyo, na wataimiliki.40Lakini ninyi, geukeni na muanze safari kwenda jangwani kwa kufuata njia ya bahari ya mianzi.”

41Kisha mlinijibu na kusema kwangu, “Tumetenda dhambi dhidi ya Yahwe, tutaenda juu na kupigana, tutafuata yote ambayo Yahwe Mungu wetu ametuamuru sisi kufanya.” Kila mtu miongoni mwenu aliweka silaha za vita, na mlikuwa tayari kuvamia nchi ya milima.

42Yahwe alisema nami, “Waambie, msivamie na kupigana, kwa kuwa sitakuwa pamoja nanyi, na mtashindwa na adui zenu.”

43Nilizungumza nanyi kwa njia hii, lakini hamkunisikiliza. Mliasi dhidi ya amri ya Yahwe, mlikuwa wenye kiburi na mlivamia nchi ya milima.44Lakini Waamori, ambao waliishi katika nchi hiyo ya milima, walitoka dhidi yenu na kuwafukuza kama nyuki, na kuwapiga chini huko Seir, mbali kama Hormah.45Mlirudi na kulia mbele ya Yahwe; lakini Yahwe hakusikiliza sauti zenu, wala hakuwa makini kwenu.46Kwa hivyo mlibaki Kadeshi siku nyingi, siku zote mlibaki huko.

2

1Kisha tuligeuka na kuanza safari kuelekea jangwani kwa njia ya Bahari ya Mianzi, kama Yahwe alivyosema nami. Tulienda kuzunguka mlima wa Seir kwa siku nyingi.

2Yahwe alizungumza nami, kusema,3“Mmeuzunguka mlima huu kwa muda mrefu; geukeni kaskazini.4Waamuru watu kwa kusema, ‘Mtapita kupitia mpaka wa ndugu zenu, wazao wa Esau, ambao wanaishi Seir; watawaogopa ninyi. Kwa hivyo muwe makini5msipigane nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote yao, hapana, hakuna hata vya kutosheleza unyao wa mguu kukanyaga, kwa kuwa nimekwisha mpa Esau Mlima wa Seiri kama miliki.6Mtanunua chakula kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kula, pia mtanunua maji kutoka kwao kwa pesa, ili kwamba muweze kunywa. Kwa kuwa

7Yahwe Mungu wenu amewabariki katika kazi za mikono yenu, amejua kutembea kwenu kupitia jangwa hili kuu. Kwa hii miaka arobaini Yahwe Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamjapungukiwa chochote.’”

8Basi tulipita karibu na ndugu zetu, wa wazao wa Esau, ambao wanaishi Seiri, mbali na barabara la Arabah, kutoka Elathi, na kutoka Ezioni Geberi. Na tuligeuka na kupita karibu na jangwa la Moabu.

9Yahweh aliniambia mimi, “Usiwasumbue Moabu, na usipigane nao katika vita. Kwa kuwa sitakupa nchi yake kwa miliki yako, kwa sababu nimewapa Ari wazao wa Lutu, kuwa miliki yao.”

10(Hapo awali waliishi Waemi, watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Waanaki;11hawa pia wanafikiriwa kuwa Rephaimu, kama Waanaki, lakini Wamoabi huwaita Waemi.12Wahori pia waliishi hapo awali Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafuata. Waliwaharibu kutoka mbele yao na kuishi katika eneo lao, kama Israeli ilivyofanya kwa nchi ya umiliki wake ambayo Yahwe aliwapa.)

13“Sasa inuka na uende kwenye kijito cha Zeredi.” Kwa hivyo tulienda kwenye kijito cha Zeredi.14Sasa tangu siku ambapo tulikuja kutoka Kadesh Barnea mpaka tukavuka kijito cha Zeredi, ilikuwa miaka thelathini na nane. Ilikuwa kwa wakati huo kizazi chote cha watu waliofaa kupigana walikuwa wamekwisha ondoka kwa watu, kama Yahwe alivyokuwa ameapa kwao.15Zaidi ya yote, mkono wa Yahwe ulikuwa kinyume na kizazi hicho ili kuweza kuwaangamiza kutoka kwa watu mpaka walipoondoka.

16Basi ilitokea, wakati watu wote waliofaa kwa kupigana walikuwa wamekufa, na kutoweka miongoni mwa watu,17kwamba Yahwe alizungumza nami, kusema,18“Leo mtavuka Ari, mpaka wa Moabu.19Wakati mtakapofika karibu na mkabala wa watu wa Ammoni, msiwasumbue au kupigana nao, kwa kuwa sitawapa nchi yoyote ya watu wa Ammoni kama miliki, kwa sababu nimekwisha wapa wazao wa Lutu kama miliki.”

20(Hiyo tena ilifikiriwa kuwa nchi ya Rephaimu. Warephaimu waliishi hapo awali-lakini Waamori wanawaita Zamzummim,21watu kama wakuu, wengi, na warefu kama Waanaki. Lakini Yahwe aliwaharibu mbele ya Waamoni, waliwafuata na kuishi katika maeneo yao.22Yahwe huyu pia alifanya watu wa Esau ambao wanaishi Seiri, wakati alipowaangamiza Wahori kutoka mbele yao, na wazao wa Esau waliwafuata na waliishi katika maeneo yao mpaka leo.23Na Waavi, walioishi katika vijiji vya mbali ya Gaza, Wakaftori, ambao wanatokana na Kaftori, waliwaangamiza na kuishi katika maeneo yao.)

24“Sasa inuka, nenda njia yako na uvuke bonde la Arnoni, tazama, nimekupa mkononi mwako Sihoni ya Waamori, mfalme wa Heshboni, na nchi yake. Anza kuimiliki na pigana naye katika vita.25Leo nitaanza kuweka woga na hofu yenu kwa watu ambao wako chini ya anga lote. Watasikia habari kuhusu ninyi na watatetemeka na kuwa na shida kwa sababu yenu.”

26Nilituma wajumbe toka jangwa la Kedemothi kuelekea Sihoni, mfalme wa Heshbon, pamoja na maneno ya amani, kusema,27“Hebu nipite katika nchi yako; nitapita kwenye barabara kuu, sitageuka mkono wa kulia wala kushoto.28Mtaniuzia mimi chakula kwa pesa, ili kwamba niweze kula, nipe maji kwa pesa, ili kwamba niweze kunywa, peke niruhusu kupitia kwa miguu yangu,29kama wazao wa Esau wanaoishi Seiri, na Moabu wanaoishi Ari, walifanya kwangu, mpaka nivuke Yordani ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wetu anatupa sisi.”30Lakini Sihon, mfalme wa Heshbon, asingeturuhusu kupitia kwake; kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ameifanya ngumu akili yake na kufanya moyo wake kuwa ukaidi, ili kwamba aweze kumshinda kwa nguvu zake, ambayo amekwisha kufanya leo.

31Yahwe alisema kwangu, “Tazama, nimeanza kumtia Sihoni na nchi yake mbele yako; kuanza kuimiliki, ili kusudi muweze kumiliki nchi yake.”

32Kisha Sihon alikuja dhidi yetu, yeye na watu wote wake, kupigana huko Jahazi.33Yahwe Mungu wetu alimtoa kwetu na tulimshinda, tulimpiga mpaka kufa, watoto wake, na watu wake wote.34Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo na kuharibu kabisa kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo; hatukuacha aliyenusurika.35Ng'ombe peke tulichukua kama mateka kwa ajili yetu, sambamba na mateka ya miji tuliochukua.36Kutoka Aroeri, ambayo iko kwenye ukingo wa bonde la Arnoni, na kutoka kwenye mji ambao uko bondeni, yote kwa njia ya kuelekea Galeadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kwetu. Yahwe Mungu wetu alitupa ushindi dhidi ya maadui zetu mbele yetu.37Ilikuwa nchi ya wazao wa Ammoni peke yake ambayo hamkuingia, sambamba na sehemu zote za mto Jabboki, na miji ya nchi ya milima- popote pale Yahwe Mungu wetu ametukataza sisi kwenda.

3

1Kisha tuligeuka na kwenda njia ya juu Bashani. Ogi, mfalme wa Bashani, alikuja na kutuvamia, yeye na watu wake wote, kupigana huko Edrei.2Yahwe aliniambia mimi, “Usimuogope; kwa kuwa nimekupa ushindi dhidi yake na nimewaweka watu wake wote na nchi yake chini ya utawala wako. Utamfanya kama ulivyomfanya Sihoni, mfalme waamori, aliyeishi Heshbon.”

3Kwa hiyo Yahwe Mungu wetu pia alitupa ushindi dhidi ya Ogi mfalme wa Bashani, na watu wake wote waliwekwa chini ya utawala wetu. Na tulimpiga mpaka kufa na hakuna yoyote wa watu wake walibaki.4Tulichukua miji yake yote kwa wakati huo; hapakuwa na mji hata mmoja ambao hatukuchukua kutoka kwao: miji sitini - mikoa ya Argobi yote, ufalme wa Ogi Bashani.5Hii ilikuwa miji iliyoimarishwa na kuta ndefu malango, na vizuizi, hii ilikuwa licha ya vijiji vingi sana vilivyokuwa havina kuta.6Tuliviangamiza kabisa, kama tulivyofanya kwa Sihoni mfalme wa Heshbon, kabisa tuliangamiza kila mji- wanaume na wanawake na watoto wadogo.7Lakini ng'ombe wote na mateka ya miji, ilichukuliwa kama mateka wetu.

8Kwa wakati huo tulichukua nchi kutoka kwenye mikono ya wafalme wawili waamori, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kutoka kwenye bonde la Arnoni kwenda mlima wa Hermoni,9(Mlima wa Hermoni, Wasidonia huita Sirioni, na waamori huita Senir10na miji yote ya tambarare, yote Gileadi, na yote Bashani kupita njia yote ya Salekah na Edrei, miji ya ufalme wa Ogi huko Bashani.11(Kwa mabaki ya Refaimu, mfalme Ogi pekee wa Bashani alikuwa amebaki. Tazama! Kitanda chake kilikuwa cha chuma. Hakuna huko Rabbah, ambako wazao wa Ammoni waliishi? Ilikuwa dhiraa tisa urefu na dhiraa nne upana, hiyo njia walitumia watu kupima.)

12Hili eneo ambalo tulichukua kumiliki kwa wakati huo-kutoka Aroer, kwamba ni kwa bonde la Arnon, na nusu ya nchi ya mlima wa Gileadi, na miji yake niliwapa Wareubeni na Wagadi.13Waliobaki wa Gileadi na Bashani yote, ufalme wa Ogi, niliwapa nusu kabila la Manasseh: kwa wote wa Argob, na Bashani yote. (Eneo hilo linaitwa nchi ya Refaim.)14Jair, mzao wa Manasseh, alichukuwa mkoa wote wa Argob, kuelekea mpaka wa Geshunites na wa Maacathites. Aliita mkoa hata Bashani kwa jina lake, Havvothi Jair, hadi leo.)

15Nilimpa Gileadi kwa Machir.16Na Wareubeni na kwa Wagadi, nilitoa eneo kutoka kwa Gileadi kuelekea bonde la Arnon- katikati mwa bonde ni mpaka wa eneo- na kuelekea mto wa Jabbok, ambao umepakana na wazao wa Ammoni.17Moja ya mipaka mingine pia ni tambarare ya bonde la mto wa Yordani, kutoka Kinnerethi kuelekea bahari ya Arabah (ambayo ni bahari ya chumvi) kuelekea miteremko wa mlima wa Pisgah mashariki.

18Nikawaamuru ninyi kwa wakati huo, kusema, “Yahwe Mungu wako amekupa nchi hii kuimiliki, wewe, wanaume wote wa vita, watapita wakiwa na silaha mbele ya ndugu zako, watu wa Israeli.19Lakini wake zenu, watoto wenu, na ng'ombe zenu (najua ya kuwa una ng'ombe wengi) watabaki katika miji yenu niliyowapa,20mpaka Yahwe awape pumziko ndugu zenu, kama alivyo kwenu, mpaka wamiliki pia nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ng'ambo ya pili Yordani, kisha mtageuka, kila mtu wenu, kwa mali zenu ambazo nimekwishawapa.”

21Nilimwamuru Yoshua kwa wakati huo, kusema, “Macho yenu yameona yote yale Yahwe Mungu wenu amefanya kwa hawa wafalme wawili; Yahwe atafanya hivyo kwa falme zote kote mtakakoenda.22Hamtawaogopa, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye atakao wapigania.”

23Nilimsihi Yahwe kwa wakati huo, kusema,24“O Bwana Yahwe, umeanza kumuonyesha mtumwa wako ukuu wako na mkono wako wa hodari; kwa kuwa nani mungu aliyeko huko mbinguni au duniani ambaye anaweza kufanya kazi zilezile kama ulivyofanya, na matendo yaleyale makuu?25Hebu niende juu, Ninakuomba, na nione nchi nzuri ambayo ng'ambo ya pili ya Yordani, ile nchi nzuri ya mlima, na pia Lebanoni.”

26Lakini Yahwe alikuwa amenikasirikia mimi kwa sababu yenu, hamkunisikiliza mimi. Yahwe alisema kwangu, “Hebu hii iwe ya kutosha kwako - usizungumze zaidi tena kwangu kuhusu jambo hili.27Nenda juu ya kilele cha Pisgah na uinue macho yako magharibi, kaskazini, kusini na mashariki; tazama kwa macho yako kwa kuwa hautaenda zaidi ya Yordani.28Badala yake, mwelekeze Yoshua na kumtia moyo na kumuimarisha, kwa kuwa ataenda zaidi mbele ya watu, na atawasababisha kuirithi nchi ambayo mtaiona.”

29Kwa hiyo tulibaki katika bonde mkabala mwa Beth Peori.

4

1Sasa, Israeli, sikiliza sheria na amri ambayo niko karibu kukufundisha, kuzifanya, ili kwamba uweze kuishi na kuingia ndani na kumiliki nchi ambayo Yahwe, Mungu wa baba zako, anakupa.2Hautaongeza maneno ambayo nakuamuru, wala hautayapunguza, ili kwamba uweze kushika amri ya Yahwe Mungu wako ambazo naenda kukuamuru.

3Macho yako yamekwisha ona nini Yahwe alifanya kwa sababu ya Baal Peori, kwa kuwa watu wote waliomfuata Baali Peor, i Yahwe Mungu wenu amekwisha kuwaangamiza kutoka miongoni mwenu.4Lakini walioambatana na Yahwe Mungu wenu wako hai leo, kila moja wenu.

5Tazama, nimewafundisha sheria na amri, kama Yahwe Mungu wangu alivyoniamuru mimi, ila kwamba mfanye hivyo katikati mwa nchi ambayo mnaiendea ili kusudi muimiliki.6Kwa hiyo zishikeni mkazifanye, kwa kuwa hii ni hekima yenu na ufahamu wenu mbele ya macho ya watu watakaosikia amri hizi zote na kusema, “Hakika taifa hili kubwa lina watu wa hekima na ufahamu.”7Kuna taifa gani jingine la vile liko hapo lina mungu karibu nao, kama Yahwe Mungu wetu tunapomwita wakati wowote?8Kuna taifa kubwa gani jingine liko hapo ambalo lina sheria na amri ili kwamba haki pamoja na sheria ambayo ninaweka mbele yenu leo?

9Zingatia peke na kuwa makini kujilinda, ili usisahau mambo ambayo macho yako yameona, ili kwamba yasiuache moyo wako kwa siku zote za maisha yako. Badala yake, yafanye yajulikane kwa watoto wako na wajukuu wako.10Kuhusu siku ile uliosimama mbele ya Yahwe Mungu wako katika Horebu, wakati Yahwe alisema nami, “Nikusanyie watu, na nitawafanya wasikie maneno yangu, ili kwamba waweze kujifunza kuniogopa mimi siku zote ambazo wanazoishi duniani, na kwamba waweze kuwafundisha watoto wao.”11Mlikuja karibu na kusimama katika wayo wa mlima. Mlima uliwaka moto kwenye moyo wa mbinguni, pamoja na giza, mawingu na giza jembamba.12Yahwe alizungumza katikati ya moto, ulisikia suati pamoja na maneno yake, lakini hakuona umbo, ila ulisikia sauti pekee.13Alitangaza kwenu agano lake ambalo aliwaamuru ninyi kulifanya, amri kumi. Aliziandika kwenye vibao viwili vya mawe.14Yahwe aliniamuru mimi kwa wakati huo kuwafundisha sheria na amri, ili kwamba muweze kuzifanya katika nchi mnayovuka kwenda kuimiliki.

15Basi iweni waangalifu ninyi wenyewe - kwa kuwa mliona hakuna namna ya umbo siku hiyo ambapo Yahweh alizungumza nanyi huko Horebu kutoka katikati mwa moto,16ili kwamba usiharibike na kuchonga umbo katika sura ya kiumbe chochote, umbo la mwanaume au mtu wa kike,17au sura ya mnyama aliye katika nchi, au sura ya ndege yoyote wa mabawa arukae katika anga, au18sura ya kitu chochote kitambaacho katika ardhi, au sura ya samaki yoyote katika maji chini ya ardhi.19Hautainua macho yako juu mbinguni na kutazama jua, mwezi, au nyota - jeshi lote la mbinguni- ukusogezwa na kuviabudu na kuvisujudia- vile vyote ambavyo Yahwe Mungu wenu amewapa hira watu wote walio chini ya anga lote.20Lakini Yahwe amewatoa ninyi na kuwaleta nje ya tanuru la chuma, nje ya Misri, kuwa kwake watu wa urithi wake, kama mlivyo leo.

21Yahwe alinikasirikia mimi kwa sababu yenu; aliapa kwamba nisiende ng'ambo ya Yordani, na kwamba nisiende kwenye nchi nzuri, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa ninyi kama urithi.22Badala yake, ninapaswa kufa katika nchi hii, sipaswi kwenda ng'ambo ya Yordani, lakini mtaenda ng'ambo na kuimiliki nchi nzuri.23Zingatia ninyi wenyewe, ili kwamba msisahau agano la Yahwe Mungu wenu, alilolifanya pamoja nanyi, na kujichongea mfano wa sanamu katika umbo la kitu chochote ambacho Yahwe Mungu wenu amewakataza kufanya.24Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni moto ulao, Mungu wa wivu.

25Wakati mnapozaa watoto na wana watoto, na wakati mtakapo kuwa katika nchi kwa muda mrefu, na kama mtaharibikiwa ninyi na kuchonga umbo la umbo lolote, na kufanya uovu machoni pa Yahwe Mungu wenu, kumchochea katika hasira,26nitaita nchi na mbingu kushuhudia dhidi yenu leo kwa kuwa mapema kabisa mtaangamia kutoka katika nchi ambayo mnaiendea huko ng'ambo ya Yordani kuimiliki, hamtazidisha siku zenu ndani yake, lakini mtaangamizwa kabisa.27Yahwe atawatawanyisha ninyi miongoni mwa watu, na mtabaki wachache ki-idadi miongoni mwa mataifa, ambapo Yahwe atawaongoza mbali.28Huko mtatumikia miungu mingine, kazi ya mikono ya watu, mbao na mawe, ambayo wala haioni, kusikia, wala kunusa.29Lakini kuanzia hapo mtamtafuta Yahwe Mungu wenu, na mtampata, wakati mtakapomtafuta kwa moyo wenu wote na roho zenu zote.30Wakati mnakuwa katika dhiki, na wakati haya yote yatakuwa yamekuja kwenu, katika siku za baadaye mtamrudia Yahwe Mungu wenu na kusikia sauti yake.31Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ni Mungu wa rehema; hatawaangusha wala kuwaangamiza ninyi, wala kusahau agano la baba zenu ambalo aliapa kwao.

32Kwa ajili ya kuuliza sasa kuhusu siku zilizopita ambazo zilikuwa mbele yenu: tangu siku ile ambayo Mungu alimuumba mtu katika nchi, kutoka pande moja ya mbingu hadi nyingine, uliza kama kumekuwepo chochote kama hiki kikubwa, au chochote kama hicho imewahi kusikiwa?33Ilishawahi kutokea watu kusikia sauti ya Mungu kuongea katikati ya moto, kama mlivyosikia, na kuishi?34Au Mungu ameshawahi kujaribu kwenda na kujichukulia kwa ajili yake taifa kutoka miongoni mwa taifa, kwa majaribu, ishara na maajabu na kwa vita, na mkono wa nguvu, na mkono ulionyoshwa, na magaidi wakuu, vile vyovyote ambavyo Yahwe Mungu wenu alifanya kwa ajili yenu Misri mbele ya macho yenu?

35Kwenu haya yalionyeshwa, ili muweze kujua kuwa Yahwe ni Mungu, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.36Toka mbinguni alifanya msikie sauti yake, ili kwamba aweze kuwaelekeza, juu ya nchi aliwafanya muone moto wake mkuu, mlisikia maneno yake toka katikati ya moto.37Kwa sababu aliwapenda baba zenu, alichagua wazao wao baada yao, na kuwatoa ninyi Misri kwa uwepo wake, kwa nguvu yake kubwa,38ili kusudi awatoe kutoka mbele ya mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi, kuwaleta ndani, kuwapa ninyi nchi yao kama urithi, hivi leo.

39Tambua hivi leo, weka kwenye moyo wako, Yahwe ni Mungu juu ya mbingu na chini ya dunia, hakuna mwingine yeyote.40Mtazishika sheria zake na amri zake ambazo nawaamuru leo, ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu na watoto wenu baada yenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu amewapa milele.

41Kisha Musa alichagua miji mitatu mashariki mwa Yordani,42ili kwamba yoyote aweze kukimbia kati ya moja yao kama imemuua mtu mwingine kwa ajili, pasipo kuwa adui hapo awali. Kwa kukimbilia kwenye moja ya miji hii, atakuwa amenusurika.43Walikuwa: Bezeri katika jangwa, nchi tambarare, kwa Wareubeni; Ramothi huko Gileadi, kwa Wagadi; na Golani huko Bashani, kwa Wamanase.

44Hii ni sheria ambayo Musa aliweka mbele ya watu wa Israeli;45hizi ni amri za agano, sheria, na amri zingine alizungumza na watu wa Israeli wakati walipotoka Misri,46nao walikuwa mashariki mwa Yordani, katika bonde la Beth Peori, katika nchi ya Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyewahi kuishi Heshbon, ambaye Musa na watu wa Israeli waliwahi kumshinda wakati walipotoka Misri.47Walichukua nchi yake kama urithi, na nchi ya Ogi mfalme wa Bashani- hawa, wafalme wawili wa Waamori, waliokuwa ng'ambo ya pili ya Yordani kuelekea Mashariki.48Himaya hii ilienda kutoka Aroer, katika ukingo wa bonde la Arnoni, kwa mlima wa Sioni (mlima Hermoni),49na ilijumuisha tambarare zote za bonde la mto Yordani, Mashariki mwa ng'ambo ya pili ya Yordani, kuelekea bahari ya Arabah, kuelekea miteremko ya mlima Pisgah.

5

1Musa aliwaita Israeli yote na akasema nao, “Sikiliza, Israeli, kwa amri na sheria ambazo nitasema katika masikio yenu leo, muweze kujifunza na kuzishika.2Yahwe Mungu wetu alifanya agano nasi huko Horebu.3Yahwe hakufanya agano hili pamoja na mababu zetu, lakini na sisi, sisi wote tu hai hapa leo.4Yahwe alizungumza nanyi uso kwa uso kwenye mlima toka katikati mwa moto5(Nilisimama kati ya Yahwe nanyi kwa wakati huo, kuwafunulia ninyi neno lake, kwa kuwa mlikuwa mmeogopa kwa sababu ya moto, na hamkwenda juu ya mlima), Yahwe alisema,6‘Mimi ni Yahweh Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa.

7Hautakuwa na miungu mingine mbele yangu.
8Hautajifanyia mwenyewe sanamu ya kuchonga wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini ya dunia, au kilicho chini ya maji.
9Hautavisujudia au kuvitumikia, kwa kuwa Mimi, Yahwe Mungu wako, ni Mungu wa wivu. Nawaadhibu uovu wa mababu kwa kuleta adhabu juu ya watoto, kwa kizazi cha tatu na cha nne cha wale wanichukiao,
10na kuonyesha agano la uaminifu kwa maelfu, kwa wale wanaonipenda na kushika amri zangu.
11Hautalichukua jina la Yahwe Mungu wako bure, kwa kuwa Yahwe atamshikilia kuwa ana hatia yeye alichukuae jina bure.
12Zingatia siku ya Sabato kwa kuiweka takatifu, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru.
13Kwa siku sita utafanya kazi zako zote,14lakini siku ya saba ni Sabato kwa Yahwe Mungu wako. Kwa siku hiyo hautafanya kazi yoyote- si wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mjakazi wako wa kiume, wala maksai wako, wala punda wako, wala mifugo wako, wala mgeni yeyote aliye katika malango yako. Hii ni kwamba mjakazi wako wa kiume na mjakazi wako wa kike wapate kumpuzika pamoja na wewe.15Utakumbuka katika akili yako kwamba ulikua mtumwa katika nchi ya Misri, na Yahwe Mungu wako alikutoa kutoka huko kwa mkono wa uweza na mkono ulionyoshwa. Kwa hivyo Yahwe Mungu wako amekuamuru kuitunza siku ya Sabato.
16Mheshimu baba yako na mama yako, kama Yahwe Mungu wako alivyokuamuru kufanya, ili kwamba uweze kuishi muda mrefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako amekupa, ili kwamba siku zako zipate kuwa nyingi kwako.
17Hautaua,
18hautazini,19hautaiba,20hautashuhudia uongo dhidi ya ndugu yako.
21Hautamtamani mke wa jirani yako, hautatamani nyumba ya jirani yako, shamba lake, au mjakazi wake wa kiume, au mjakazi wake wa kike, maksai au punda wako, au chochote ambacho ni mali ya jirani yako.’”

22Haya maneno Yahwe alisema kwa sauti kubwa kwa kusanyiko lenyu lote kwenye mlima toka katikati mwa moto, mawingu, giza zito, hakuongeza maneno yoyote zaidi. Na aliandika chini kwenye mbao mbili za mawe na akanipa mimi.

23Mlipokaribia, mlisikia sauti toka katikati mwa giza, wakati mlima unawaka moto, kuwa mlikuja karibu nami, wazee wenu wote, na wakuu wa makabila yenu.24Mlisema, “Tazama, Yahwe Mungu wetu ametuonyesha utukufu wake na ukuu wake, na tumeisikia sauti yake toka katikati mwa moto. Tumeona leo kwamba wakati Mungu azungumza na watu, wanaweza kuishi.25Lakini kwanini tufe? Kwa kuwa moto huu mkuu utatutosheleza sisi; kama tutasikia sauti ya Yahwe Mungu wetu tena, tutakufa.26Kwa kuwa badala yetu kuna miongoni mwetu wa mwili ambao wamesikia sauti ya Mungu aliye hai akizungumza toka katikati mwa moto na kuishi, kama tulivyofanya?27Kwenu ninyi, mnapaswa kwenda na kusikiliza kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema; rudia kwetu kila kitu ambacho Yahwe Mungu wetu asema kwenu; tutamsikiliza na kumtii.”

28Yahweh alisikia maneno yenu pindi mlipozungumza nami. Alisema na mimi, “Nimekwisha sikia maneno ya watu hawa, kile wanasema kwako. Kile walichosema kilikuwa kizuri.29Oh, kulikuwa na moyo wa namba hiyo ndani yao, kwamba wataniheshimu na daima kushika amri zangu zote, ili iweze kuwa vizuri kwao na pamoja na watoto wao milele!

30Nenda useme nao, ‘Rudini kwenye mahema.’31Lakini kwenu, simama karibu nami, na nitakuambia amri zote, sheria, na maagizo ambayo utawafundisha, ili kwamba waweze kuyashika katika nchi ambayo nitawapa kumiliki.

32Mtashika, kwa hiyo, kile Yahwe Mungu wenu amewaamuru; hamtageukia mkono wa kulia au kushoto.33Mtatembea katika njia zote ambazo Yahwe Mungu wenu, amewaamuru ili kusudi muweze kuishi, na ili kwamba iwe vizuri kwenu, na kwamba muweze kuongeza siku zenu katika nchi ambayo mtaimiliki.”

6

1Sasa haya ni maagizo, amri, na sheria ambazo Yahwe Mungu wetu ameniamuru mimi kuwafundisha ninyi, ili kwamba muweze kuzishika katika nchi ambayo mnaenda ng'ambo ya pili ya Yordani kumiliki,2ili kwamba mpate kumheshimu Yahwe wenu, ili muzishike amri zake zote na maagizo ninayowaamuru-ninyi, wana wenu na wana wa wana wenu, siku zenu zote za maisha, ili kwamba siku zenu ziongezeke.3Kwa hiyo sikilizeni, Israeli, na kuzishika ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu, ili kusudi muweze kuzidi mno kwenye nchi itiririkayo maziwa na asali, kama Yahwe Mungu wa baba zenu, amewaahidi atafanya.

4Sikiliza, Israel: Yahwe Mungu wetu ni mmoja.5Mtampenda Yahwe Mungu wenu kwa moyo wenu wote, kwa roho zenu zote, na kwa akili zenu zote.6Maneno ninayowaamuru ninyi leo yatakuwa katika moyo wenu;7na mtayafundisha kwa bidii kwa watoto wenu, mtayazungumza wakati mkaapo katika nyumba zenu, wakati mlalapo, na wakati mwinukapo.8Mtazifunga kama ishara juu ya mikono yenu, nayo yatakuwa utepe kati ya macho yenu.9Mtaziandika kwenye miimo ya milango ya nyumba yenu na kwenye malango.

10Wakati Yahwe Mungu wenu atawaleta kwenye nchi ambayo aliaapa kwa baba zenu, Ibrahimu, Isaka, na Yakobo, kwamba angewapa, pamoja na miji mikubwa na mizuri ambayo hamkuijenga,11na nyumba zilizojaa kila aina ya vitu vizuri ambavyo hamkuvifanya, visima ambavyo hamkuvichimba, mashamba na miti ya mizeituni ambayo hamkuipanda, mtakula na kutosheka-12basi iweni makini ili kwamba msije kumsahau Yahwe, aliyewaleta toka nchi ya Misri, toka nyumba ya utumwa.

13Mtamheshimu Yahwe Mungu wenu, yeye mtamwabudu, na mtaapa kwa jina lake.14Hamtawaendea miungu mingine, miungu ya watu wanaowazunguka wote-15kwa kuwa Yahwe Mungu wenu katikati yenu ni Mungu wa wivu- kama mtafanya, hasira ya Yahwe Mungu wenu itawasha dhidi yenu na atawaangamiza kutoka kwenye uso wa dunia.16Hamtamjaribu Yahwe Mungu wenu kama mlivyomjaribu huko Massah.17Kwa bidii mtayashika maagizo ya Yahwe Mungu wenu, maagizo yake makini, na amri ambazo amewaamuru.18Mtafanya kile kilicho sahihi na kizuri katika macho ya Yahwe, kwamba iwe vizuri kwenu, na kwamba muweze kuingia na kumiliki nchi nzuri ambayo Yahwe aliaapa kwa baba zenu,19kuwaondoa maadui zenu wote mbele zenu, kama Yahwe alivyosema.

20Wakati mwana wako auliza kwa wakati unaokuja, kusema, “Ni zipi amri za agano, sheria, na amri zingine ambazo Yahwe Mungu wetu alituamuru?”21Basi utasema kwa mwana wako, tulikuwa watumwa wa Farao huko Misri, Yahwe alitutoa Misri kwa mkono wa uweza,22na alionyesha ishara na maajabu, makuu na makali, Misri kwa Farao, na kwa nyumba yake yote, mbele ya macho yenu,23na alitutoa kutoka huko, ili kwamba atulete ndani, kutupa nchi ambayo aliaapa kwa baba zetu.24Yahwe alituamuru daima kuzishika amri hizi, kumuogopa Yahwe Mungu wetu kwa uzuri wetu, ili kwamba atuweke hai, kama tulivyo leo.25Kama tutashika maagizo haya yote mbele ya Yahwe Mungu wetu kama alivyotuamuru, hii itakuwa haki yetu.

7

1Wakati Yahwe Mungu wenu atatuleta katika nchi ambayo mnaenda kuimiliki na kuwaondoa mataifa mengi mbele zenu- Mhiti, Mgirgashi na Mwamori, na Mkanaani, na Mperizi, Mhivi, Myebusi- mataifa saba makubwa na yenye nguvu kuliko wewe.2Na wakati Yahwe Mungu wenu atawapa ninyi ushindi juu yao pindi mnakutana nao katika vita, mtawashambulia, basi mnapaswa kuwateketeza kabisa. Hamtafanya agano nao, wala kuonyesha huruma kwao.3Wala hamtapanga ndoa zozote pamoja nao, hamtawatoa binti zenu kwa vijana wao, na hamtawachukua binti zao kwa vijana wenu.4Kwa kuwa watawabadilisha vijana wenu kutonifuata mimi, ili kwamba waweze kuabudu miungu yao. Kwa hiyo hasira ya Yahwe itawashwa dhidi yenu na atawaangamiza haraka.5Hivi ndivyo mtakavyo washughulikia nao; mtavunja madhabahu zao, vunja nguzo zao za mawe katika vipande, kata chini ncha za Asherahi, na kuzichoma sanamu za kutupwa.6Kwa kuwa wewe ni taifa uliyetengwa kwa Yahwe Mungu wako. Amekuchagua wewe kuwa watu kwa ajili yake kumiliki, zaidi ya watu wengine wote ambao wako katika uso wa dunia.

7Yahwe hakuweka upendo wake juu yenu au kuwachagua kwa sababu mlikuwa zaidi katika idadi kuliko watu wowote, kwa kuwa mlikuwa wachache kuliko watu wote-8Lakini kwa sababu anawapenda ninyi, anataka kushika kiapo alichoapa kwa baba zenu. Huyu ni Yahwe aliyewatoa kwa mkono wa uweza na kuwakomboa kutoka nyumba ya utumwa, kutoka mkono wa Farao, mfalme wa Misri.9Kwa hiyo tambua ya kuwa Yahwe Mungu wako-ni Mungu, Mungu mwaminifu, anayetunza maagano na uaminifu kwa vizazi elfu kwa wale wanaompenda na kuyashika maagizo yake,10lakini huwalipa wale wanaomchukia kwa sura zao, kuwaangamiza, hatakuwa na huruma kwa yeyote anayemchukia; atamlipa kwa uso wake.11Kwa hiyo utashika maagizo, amri, na sheria ninazokuamuru leo, ili kwamba uzifanye.12Kama mtasikiliza maagizo haya, kuyashika na kuyafanya, itakuwa Yahwe Mungu wenu atawashika pamoja na agano na uaminifu ambao aliapa kwa baba zenu.13Atawapenda, atawabariki, na kuwazidisha, pia atabariki tunda la miili yenu na tunda la ardhi yenu, nafaka zenu, divai mpya, mafuta yenu, atazidisha mifugo na kundi lako la mifugo michanga, katika nchi ambayo aliapa kwa baba zenu kuwapa.14Mtabarikiwa zaidi kuliko watu wengine wote; hapatakuwa na mwanaume asiyekuwa na mtoto au mwanamke tasa miongoni mwenu au miongoni mwa mifugo.15Yahwe atawaondolea magonjwa yote; hakuna magonjwa mabaya ya Misri ambayo mnayajua yatawekwa juu yenu, lakini atayaweka kwa wote wanaowachukia ninyi.16Mtayaondoa makundi ya watu wote ambayo Yahwe Mungu wenu awapa ushindi, na jicho lenu halitawaonea huruma. Na hamtaabudu miungu yao, kwa kuwa huo utakuwa mtego kwenu.

17Kama mtasema kwenye mioyo, “Haya mataifa ni mengi zaidi kuliko sisi; tutawezaje kuwafukuza?”18Msiwaogope; mtakumbuka akilini kile Yahwe Mungu wenu alifanya kwa Farao na Misri yote?19Mateso makuu ambayo macho yenu yaliona, ishara, maajabu, mkono wa uweza, mkono ulionyoshwa ambao Yahwe Mungu wenu alivyowatoa. Yahwe Mungu wenu atafanya kile kile kwa watu wote ambao mnawaogopa.20Zaidi ya yote, Yahwe Mungu wenu atatuma nyigu miongoni mwao, mpaka wale waliobaki na wale wanaojificha wenyewe mbele yenu waangamizwe mbele ya uwepo wenu.21Hamtatishikeni nao, kwa kuwa Yahwe Mungu wenu yuko miongoni mwenu, Mungu mkuu na wa kuogofya.22Yahwe Mungu wenu atayaondoa mataifa mbele zenu kidogo kidogo. Hamtayashinda yote kwa wakati mmoja, au wanyama wa mwitu watakuwa wengi karibu nanyi.23Lakini Yahwe Mungu wenu atawapa ninyi ushindi dhidi yao wakati mkutanapo vitani; atawachanganya kwa kiasi kikubwa mpaka wameangamizwa.24Atawaweka wafalme wao chini ya utawala wenu, na mtafanya jina lao kuangamia toka chini ya mbingu. Hakuna atakayeweza kusimama mbele yenu, mpaka muwaangamize.25Utazichoma sanamu za kuchonga za miungu yao- usitamani madini ya fedha au dhahabu yanayofunika na kuichukua kwa ajili yenu, kwa sababu mkifanya, mtanaswa nayo-kwa kuwa ni chukizo kwa Yahwe Mungu wenu.26Hamtaleta chukizo lolote ndani ya nyumba zenu na kuanza kuiabudu. Mtachukizwa kabisa na kuchukia kwa kuwa imetengwa kwa ajili ya uharibifu.

8

1Mnapaswa kuyashika maagizo yote ninayowapa leo, ili kwamba mweze kuishi na kuongezeka, na kuingia na kuimiliki nchi ambayo Yahwe aliaapa kwa baba zenu.2Mtakumbuka akilini njia zote ambazo Yahwe Mungu amewaongoza miaka hii arobaini kwenye jangwa, ili kwamba apate kuwanyenyekeza, ili kwamba awajaribu kujua nini kilikuwa ndani ya mioyo yenu, kama mungeweza kuyashika maagizo yake au hapana.3Aliwanyenyekeza, na kuwafanya kuwa na njaa, na kuwalisha mana, ambayo hamkuijua na ambayo baba zenu hawakuijua. Alifanya hivyo kuwafanya nyie kujua si kwa mkate tu watu wanaishi, badala ni kwa chochote hutoka kwenye kinywa cha Yahwe kwamba watu wanaishi.4Mavazi yenu hayakuchanika na kudondoka, na miguu yenu haikuvimba kipindi cha miaka hiyo arobaini.5Mtatafakari katika mioyo yenu kuhusu, namna, kama mtu anavyo mwadibisha kijana wake, hivyo Yahwe Mungu wenu anawaadibisha ninyi.

6Mtayashika maagizo ya Yahwe Mungu wenu, ili kwamba mweze kutembea katika njia zake na kumheshimu.7Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu anawaleta katika nchi nzuri, nchi ya vijito vya maji, visima na chemchemi, vitiririkavyo kwenda kwenye mabonde na miongoni mwa milima,8nchi ya ngano na shayiri, mizabibu, mtini, na komamanga; nchi mizeituni na asali.9Ni nchi ambayo mtakula mkate bila kupungukiwa, na ambapo mtaenda bila chochote; nchi ambayo mawe yametenganishwa kwa chuma, na kutokana na milima, mtaweza kuchimba shaba.10Mtakula na kushiba, na mtambariki Yahwe Mungu wenu kwa nchi nzuri ambayo amewapa.

11Iweni makini kwamba msimsahau Yahwe Mungu wenu, na kwamba msipuuzie maagizo yake, hukumu zake, na sheria zake ambazo ninakuamuru leo,12vinginevyo unapokula na ukashiba, na wakati unajenga nyumba nzuri na kuishi ndani zao.13Na muwe makini wakati makundi yenu na mifugo yenu ikiongezeka, na wakati wa fedha zenu na dhahabu zenu zikiongezeka, na vyote mlivyonavyo kuongezeka,14basi kwamba mioyo yenu iliniuliza juu ya kumsahau Yahwe Mungu wenu-aliyewaleta kutoka nchi ya Misri, toka nyumba ya utumwa.15Usimsahau yeye aliyewaongoza kupitia jangwa kuu na la kutisha, ambako ndani yake kulikuwa na nyoka wa moto na nge, na pitia nchi yenye kiu ambako hapakuwa na maji, ambaye yeye alileta maji toka kwenye mwamba wa jiwe.16Ambaye aliwalisha kwenye jangwa kwa mana ambayo mababu zenu hawakuijua, ili kwamba awajaribu, kufanya uzuri kwenu mwishoni-17lakini mnaweza kusema mioyoni mwenu, “Nguvu yangu na mkono wangu wa uweza umepata utajiri huu wote.”18Lakini mtamkumbuka akilini Yahwe Mungu wenu, kwa kuwa ni yeye awapae ninyi nguvu ya kupata utajiri, ili kwamba aweze kuanzisha agano lake aliloapa kwa baba zenu, kama ilivyo leo.

19Itakuwa kwamba, kama mtamsahau Yahwe Mungu wenu na kuwaendea miungu mingine, kuiabudu, na kuiheshimu, nashuhudia kinyume dhidi yenu leo kwamba mtateketea.20Kama mataifa ambayo Yahwe anatengeneza kuyaangamiza mbele yenu, hivyo mtaangamia, kwa sababu hamkusikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu.

9

1Sikiliza, Israeli; umekaribia kuvuka ng'ambo ya pili ya Yordani leo, kuyafukuza mataifa yenye nguvu na ushujaa kuliko ninyi, na miji ambayo ni mikuu na yenye boma iliyoenda juu,2watu wakuu na warefu, wana wa Anaki, ambaye mnamjua, na yule mliomsikia watu wakisema, “Nani atasimama mbele ya wana wa Anaki?”3Kwa hiyo tambua leo kwamba, Yahwe Mungu wenu ni yeye ambaye huenda mbele yenu kama moto uwalao; atawaharibu na kuwaangamiza mbele yenu, kwa hivyo mtawaondosha na kuwafanya kupotea kwa haraka, kama Yahwe alivyosema kwenu.

4Msiseme kwenye mioyo yenu, baada ya Yahwe Mungu wenu kuwatupilia toka mbele yenu, “Ilikuwa kwa sababu ya haki yangu kwamba Yahwe amenileta mimi kuimiliki nchi hii,” kwa kuwa ilikuwa kwa sababu ya maovu ya mataifa haya kwamba Yahwe anawaondoa mbele yenu.5Si kwa sababu ya uadilifu wenu au unyofu wa mioyo yenu ambayo mnaenda kuingia kumiliki nchi yao, lakini ni kwa sababu ya maovu ya mataifa haya ambayo Mungu anawaondoa mbele zenu, na kusudi alifanye kuwa kweli neno ambalo aliapa kwa mababu zenu, Ibrahimu, Isaka na Yakabo.6Kwa hiyo tambua, kwamba Yahwe Mungu wenu awape ninyi nchi hii nzuri kuimiliki kwa sababu ya uadilifu wenu, ni kwa kuwa ninyi ni watu wakaidi.

7Kumbuka na msisahau jinsi mlivyomchochea Yahwe Mungu wenu katika hasira huko jangwani; kutoka siku hiyo ambayo mliacha nchi ya Misri mpaka mlipokuja kwenye eneo hili, mmekuwa waasi dhidi ya Yahwe.8Pia huko Horebu mlimchochea Yahwe katika hasira, na Yahwe alikasirika vya kutosha kwenu kuwaangamiza.9Wakati nilipoenda juu ya mlima kupokea mbao za mawe, mbao za agano ambalo Yahwe alifanya nanyi, Nilibaki kwenye mlima kwa siku arobaini na usiku arobaini; Wala sikula mkate wala kunywa maji.10Yahwe alinipa mbao mbili za mawe zilizoandikwa kwa kidole chake; juu yake kuliandikwa kila kitu kama tu maneno yote ambayo Yahwe alitangaza kwenu juu ya mlima toka katikati mwa moto siku hiyo ya kusanyiko.

11Ilitokea mwishoni mwa siku hizo arobaini na usiku arobaini ya kwamba Yahwe alinipa mimi mbao mbili za mawe, mbao za agano.12Yahwe alisema nami, “Inuka, nenda chini haraka kutokea hapa, kwa kuwa watu wako, ambao uliwaleta toka Misri, wamekuwa wafisadi wenyewe. Kwa haraka wamegeuka toka kwenye njia ambayo niliwaamuru. Wamejifanyia wenyewe umbo la kutupwa.”

13Zaidi ya hayo, Yahwe alizungumza na mimi na kusema, “Nimewaona watu hawa; ni watu wakaidi.14Acha mimi peke yangu, ili kwamba niweze kuwaangamiza na kulifuta jina lao kutoka chini ya mbingu, na nitawafanya ninyi taifa lenye nguvu na kuu kuliko wao.”

15Kwa hivyo niligeuka nyuma na kushuka chini ya mlima, na mlima ulikuwa ukiwaka moto. Mbao mbili za agano zilikuwa kwenye mikono yangu.16Nilitazama, na tazama, mlikuwa mmefanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wenu. Mmejitengenezea wenyewe ndama. Kwa haraka mmegeuka toka njia ambayo Yahwe alikuwa amewaamuru.17Nilizichukua mbao mbili na kuzitupa toka mikononi mwangu. Nilizivunja mbele ya macho yenu.

18Tena nililala kifudifudi mbele ya Yahwe kwa siku arobaini na usiku arobaini; wala sikula mkate wala kunywa maji, kwa sababu dhambi zenu zote ambazo mlikuwa mmefanya, kwa kufanya hivyo ambavyo ilikuwa ni mbaya machoni pa Yahwe, ili kwamba kumchochea yeye katika hasira.19Kwa kuwa nilikuwa nimeogopa hasira na gadhabu kali ambayo Yahwe alikuwa amekasirika vya kutosha dhidi yenu kuwaangamiza. Lakini Yahwe alinisikiliza mimi kwa wakati huo pia.20Yahwe alikuwa na hasira nyingi na Haruni kwa kusudi la kumuangamiza; pia niliomba kwa ajili ya Haruni kwa wakati huohuo.21Nilichukua dhambi zenu, ndama mliyekuwa mmetengeza, na kumchoma, kumpiga, kumweka chini kuwa mdogo, mpaka ilipokuwa laini kama vumbi. Nilirusha vumbi lake katika mkondo ambao ulitiririka chini kutoka mlimani.

22Huko Taberah, Massah, na huko Kibrothi Hattaavah, mlimchochea Yahwe kwenye adhabu.

23Wakati Yahwe aliwatoa kutoka Kadeshi ya Barnea na kusema, “Nenda juu na umiliki nchi ambayo nimekupa,” ndipo mliasi dhidi ya agizo la Yahwe Mungu wenu, na hamkumwamini na kumsikiliza sauti yake.24Mmekuwa waasi dhidi ya Yahwe toka siku ile nilipowajua.

25Kwa hiyo nililala kifudifudi mbele ya Yahwe siku zile arobaini na usiku arobaini, kwa sababu alikuwa amesema kwamba angewaangamiza.26Niliomba kwa Yahwe na kusema, “Oh Bwana Yahwe, usiwaangamize watu wako au warithi wako ambao uliwaokoa kwa ukuu wako, ambapo uliwatoa toka Misri kwa mkono wa uweza.27Akilini waite watumishi wenu Ibrahimu, Isaka, na Yakobo; msiangalie ukaidi wa watu hawa, wala maovu yao, dhambi zao,28ili kwamba nchi ambayo ulitutoa iseme, ‘Kwa sababu Yahwe hakuweza kuwaleta katika nchi aliyowaahadia, na kwa sababu aliwachukia, amewaleta nje kuwaua katika jangwa.’29Bado ni watu wa kwenu na urithi wenu, ambao uliwatoa kwa nguvu zako kuu na kwa kuonyesha mamlaka yako.”

10

1Kwa wakati ule Yahwe aliniambia, “Chonga mbao mbili za mawe kama zile za kwanza, na njoo kwangu huku juu ya mlima, na utengeneze sanduku la mbao.2Nitaandika kwenye mbao maneno ambayo yalikuwa kwenye mbao za kwanza ulizozivunja, na utaziweka ndani ya sanduku.”

3Basi nilitengeneza sanduku la mbao za mikaratusi, na nikachonga mbao mbili za mawe kama zile za kwanza, na nikaenda juu ya mlima, nikiwa na mbao mbili mkononi mwangu.4Aliandika kwenye mbao, kama maandishi ya kwanza, amri kumi ambazo Yahwe amesema nanyi kwenye mlima kutoka katikati mwa moto katika siku ya kusanyiko; ndipo Yahwe alinipa.5Niligeuka na kushuka chini kutoka mlimani, na kuweka mbao ndani ya sanduku nililokuwa nimetengeneza; hapo zilikaa, kama Yahwe alivyoniamuru.

6(Watu wa Israeli walisafiri kutoka Beerothi ya Bene Jaakan kwenda Moserathi. Huko Aroni alikufa, na huko alizikwa; Eleazar, mwana wake, alitumika katika ofisi ya ukuhani kwenye nafasi yake.7Kutokea huko, walisafiri kwenda Gudgodah, na kutoka Gudgodah kwenda Jotbathah, nchi yenye mikondo ya maji.8Kwa wakati huo, Yahwe alichagua kabila la Lawi kubeba sanduku la agano la Yahwe, kusimama mbele ya Yahwe kumtumikia na kubariki watu kwa jina lake, kama ilivyo leo.9Kwa hivyo Lawi hawana sehemu wala urithi wa nchi pamoja na ndugu zake; Yahwe ni urithi wao, kama Yahwe Mungu wenu alizungumza naye).

10Nilibaki kwenye mlima kama ilivyokuwa mara ya kwanza, siku arobaini na usiku arobaini. Yahwe alinisikiliza wakati huo pia; Yahwe hakutaka kuwaangamiza.11Yahwe alisema nami, “Inuka, nenda mbele ya watu uwaongoze katika safari yao; wataingia na kumiliki nchi ambayo niliapa kwa mababu zao kuwapa.”

12Sasa, Israeli, Yahwe Mungu wenu ataka nini kwenu, isipokuwa hofu ya Yahwe Mungu wenu, kutembea katika njia zake zote, kumpenda yeye, na kumwabudu Yahwe Mungu wenu kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.13Kuzishika amri za Yahwe, na maagizo ambayo ninawaamuru ninyi leo kwa ajili ya uzuri wenu?

14Tazama, kuwa Yahwe Mungu wenu mbingu ni zake na mbingu za mbingu, dunia, vyote vilivyomo.15Yahwe pekee alichukua furaha kwa baba zenu ili kwamba awapende, na aliwachagua ninyi, wazao wao, baada yao, zaidi kuliko ya watu wengine wowote, kama afanyavyo leo.16Kwa hivyo basi tahiri govi la mioyo yenu, na msiwe wakaidi tena.17Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu, ni Mungu wa miungu na Bwana wa bwana, Mungu mkuu, mwenye nguvu na wakutisha, ambaye hapendelei yeyote na hapokei rushwa-18Hutekeleza haki kwa yatima na wajane, na huonyesha upendo kwa mgeni kwa kumpa chakula na mavazi.19Kwa hivyo basi mpende mgeni; kwa kuwa mlikuwa wageni kutoka nchi ya Misri.20Mtamcha Yahwe Mungu wenu yeye mtamwabudu. Mtashikamana kwake, na kwa jina lake mtaapa.21Yeye ni sifa yenu, ni Mungu wenu, ambaye amefanya kwa ajili yenu haya mambo makuu na kutisha, ambayo macho yenu yameyaona.22Baba zako walienda Misri kama watu sabini; sasa Yahwe Mungu wako amekufanya wewe kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

11

1Kwa hivyo mtampenda Yahwe Mungu wenu na daima mtashika maelekezo yake, maagizo yake, sheria zake, na amri zake.2Kumbuka kwamba siongei kwa watoto wako, ambao hawajajua wala kuona hukumu ya Yahwe Mungu wako, ukuu wake, mkono wake wa uweza, mkono wake ulionyoshwa,3Ishara na matendo ambayo alifanya katikati ya Misri kwa Farao, mfalme wa Misri, na nchi yake yote.4Wala hawakuona kile alichofanya kwa jeshi la Misri, kwa farasi wao, au magari yao; namna alivyoyafanya maji ya bahari ya shamu kuwalemea kwa sababu ya kuwafuatilia, na namna Yahwe alivyowaangamiza mpaka leo,5au nini alifanya kwenu kwenye jangwa mpaka mlikuja eneo hili.6Hawajaona nini Yahwe alichofanya kwa Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; namna dunia ilifungua kinywa chake na kuwameza, nyumba zao, mahema yao, na kila kitu hai kilichowafuata, katikati mwa Israeli yote.7Lakini macho yenu yameona kazi yote kuu ya Yahwe aliyoifanya.

8Kwa hivyo shikeni amri zote ambazo ninawaamuru leo, kwamba mweze kuwa imara, na kuingia na kuimiliki nchi, ambayo unaenda zaidi kuimiliki;9na kwamba uweze kuongeza siku zako katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa baba zako kuwapa na uzao wao, nchi itiririkayo maziwa na asali.10Kwa kuwa nchi, ambayo unaingia kumiliki, siyo kama nchi ya Misri, ambako mlitoka, ambako mlipanda mbegu na kumwagilizia kwa miguu yenu, kama bustani ya mitishamba;11Lakini nchi, ambayo unaenda kuimiliki, ni nchi ya milima na mabonde, na kunywa maji ya mvua mbinguni,12nchi ambayo Yahwe Mungu wenu awajali; macho ya Yahwe Mungu wenu daima yako juu yake, kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka mwisho wa mwaka.

13Itatokea, kama mtazisikiliza kwa bidii amri zangu ambazo ninawaamuru leo kumpenda Yahwe Mungu wenu, na kumtumikia kwa moyo wenu wote na roho zenu zote,14kwamba nitawapa mvua nchi yenu kwa majira yake, mvua za awali na mvua za badaye, ili kwamba muweze kukusanya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, na mafuta yenu.15Nitawapa nyasi kwenye mashamba yenu kwa ajili ya mifugo yenu, na mtakula na kushiba.

16Uwe makini mwenyewe, ili kwamba moyo wako usidanganyike, na kugeuka na kuabudu miungu mingine, na kuisujudia;17ili kwamba hasira ya Yahwe isiwashwe dhidi yenu, na ili kwamba asifunge mbingu, kwamba pasiwe na mvua, na nchi haitavuna matunda, na ili kwamba mpotee kwa haraka kutoka nchi nzuri ambayo Yahwe anawapa.18Kwa hiyo yaweke haya maneno ndani ya moyo wako na roho; yafunge kama ishara kwenye mkono wako, na yawe utepe katikati ya macho yako.19Utayafundisha kwa watoto na kuongea juu yake wakati uketipo ndani ya nyumba yako, wakati utembeapo barabarani, wakati ulalapo, na wakati uinukapo.20Utayaandika kwenye miimo ya milango ya nyumba zenu na kwenye malango yenu,21kwamba siku zenu na siku za watoto wenu ziweze kuongezeka katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa mababu zenu kuwapa, maadamu mbingu ziko juu ya ardhi.

22Kama mtayashika kwa bidii maagizo haya yote ambayo ninawaamuru ninyi, ili kwamba myafanye, mpende Yahwe Mungu wenu, tembea katika njia zake zote, na kushikamana naye,23basi Yahwe atawaondosha mataifa haya yote kutoka mbele yenu, na mtayafukuza mataifa makubwa na yenye nguvu kuliko ninyi.24Kila eneo ambalo unyao wa miguu utatembea litakuwa lenu; kutoka jangwani hadi Lebanoni, toka mto wa Euphratesi, hadi magharibi mwa bahari itakuwa mpaka wenu.25Hakuna mtu ataweza kusimama mbele yenu; Yahwe Mungu wenu ataweka hofu yenu na ugaidi wenu juu ya nchi yote mnayotembea juu yake kama alivyosema na ninyi.

26Tazama, naweka mbele yenu baraka na laana;27baraka, kama mtasikiliza amri za Yahwe ambazo ninakuamuru leo,28na laana, kama hamtasikiliza amri za Yahwe Mungu wenu, lakini mkaicha njia ninayokuamuru leo, kuendea miungu mingine ambayo hamjaijua.29Itakuwa wakati Yahwe Mungu wenu anawaleta ninyi katika nchi ambayo mnaenda kumiliki, kwamba mtaweka baraka juu ya mlima Gerizimu na laana juu ya mlima Ebali.30Hawako ng'ambo ya pili zaidi ya Yordani, magharibi mwa barabara ya magharibi, katika nchi ya Wakanani wanaoishi Arabah, juu dhidi ya Gilgali, kando ya mialo ya Moreh?31Kwa maana mtavuka ng'ambo ya pili ya Yordani kuingia kumiliki nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, na mtamiliki na kuishi ndani yake.32Mtashika sheria zote na amri ninazoweka mbele yenu leo.

12

1Hizi ni amri na sheria ambazo mtazishika katika nchi ambayo, Yahwe Mungu wa baba zenu, amewapa kumiliki, siku zote mtakazoishi kwenye ardhi.2Hakika mtaharibu maeneo yote ambapo mataifa mtakayofukuza miungu yao walioabudu, kwenye milima mirefu, kwenye vilima, na chini ya kila mti wa kijani.3Na mtayavunja madhabahu yao, mtaharibu kwa vipandevipande nguzo zao za mawe, na kuchoma ncha za Asherahi, mtazikata sanaa za kuchongwa za miungu yao na kuangamiza jina lao nje ya eneo hilo.

4Hamtamwabudu Yahwe Mungu wenu kama hivyo.5Lakini kwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kutoka makabila yenu kuweka jina lake, hapo patakuwa ni eneo analoishi na huko ndiko mtaenda.6Ni huko ndiko mtaleta sadaka ya kutekeketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, na sadaka zinazotolewa kwa mkono wenu, sadaka zenu za viapo, sadaka za utayari na mzao wa kwanza wa mifugo na wanyama.7Ni huko mtakula mbele za Yahwe Mungu wenu na kufurahi kuhusu kila kitu ambacho mmeweka mkono, nyie na jamaa zenu, ambapo Yahwe Mungu wenu amewabariki.

8Hamtafanya mambo yote ambayo tunafanya hapa leo; sasa kila moja anafanya chochote kile kizuri machoni pake,9kwa kuwa bado hamjapumzika, kwa urithi ambao Yahwe Mungu wenu anawapa.10Lakini wakati mnaenda ng'ambo ya pili ya Yordani na kuishi ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anasababisha ninyi kurithi, na wakati awapa pumziko kutoka kwa maadui zenu wanaowazunguka karibu, ili kusudi muishi kwa usalama,11kisha itakuwa eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kusababisha jina lake kuishi, huko mtaleta yote ninayowaamuru; sadaka za kuteketezwa, dhabihu zenu, zaka zenu, sadaka zilizotolewa kwa mkono wenu, na sadaka za chaguo lenu kwa ajili ya nadhiri mtakazotoa kwa Yahwe.12Mtafurahi mbele za Yahwe Mungu wenu-nyie, na watoto wenu, binti zenu, wajakazi wa kiume, wajakazi wa kike, na Walawi walio ndani ya lango lenu, kwa sababu hana sehemu au urithi miongoni mwenu.13Uwe makini mwenyewe kwamba usitoe sadaka zako za kuteketezwa kila eneo unaloona;14lakini ni katika eneo hilo ambalo Yahwe atawachagua miongoni moja kati ya makabila yenu ambalo litatoa sadaka ya kuteketezwa, na huko mtafanya kila kitu ninachokuamuru.

15Hata hivyo, mtaweza kuua na kula wanyama ndani ya malango yenu, kama mnavyotaka, kupokea baraka ya Yahwe Mungu wenu kwa ajili ya yote amewapa; na watu wasio wasafi na wasafi wote wanaweza kula, wanyama kama vile paa na kulungu.16Lakini hamtakula damu, mtaimwaga kwenye ardhi kama maji.17Msile ndani ya malango kutoka kwenye zaka ya nafaka zenu, mvinyo wenu mpya, mafuta yenu au mzao wa kwanza wa mifugo au wanyama; na msile nyama yoyote mnayoitoa dhabihu pamoja na viapo vyovyote vyenu mnafanya, wala sadaka yenu ya utayari, wala sadaka mnayotoa kwa mkono wenu.18Badala yake, mtakula mbele ya Yahwe Mungu wenu katika eneo ambalo Yahwe Mungu atachagua- nyie, mtoto wenu, binti yenu, mjakazi wa kiume, mjakazi wa kike, na Mlawi aliye malangoni mwenu; mtafurahi mbele ya Yahwe Mungu wenu kuhusu kila kitu ambacho mnaweka mkono wenu.19Muwe makini wenyewe ili kwamba msimwache Mlawi maadamu mnaishi kwenye nchi yenu.

20Wakati Yahwe Mungu wenu atapanua mipaka yenu, kama alivyowaahidi, na kusema, “Nitakula nyama,” kwa sababu ya tamaa zenu mnakula nyama, mnaweza kula nyama, kama tamaa za roho zenu.21Kama eneo ambalo Yahwe Mungu wenu achagua kuliweka jina lake ni mbali kutoka kwenu, basi mtaua baadhi ya mifugo yenu na wanyama wenu ambao Yahwe amewapa, kama nilivyowaamuru: hivyo mnaweza kula ndani ya malango yenu, kama tamaa za roho zenu.22Kama paa na Kulungu wanaliwa, hivyo mtakula watu wasio safi na wasafi wanaweze kula kadhalika.23Lakini muwe na uhakika kwamba hamtumii damu, kwa kuwa damu ni uhai, hamtakula uhai pamoja na nyama.24Hamtakula, mtaimwaga nje kwenye ardhi kama maji.25Hamtakula, ili kwamba iweze kuwa vizuri kwenu, na watoto wenu baada yenu, wakati mtafanya kile kilicho sahihi machoni pa Yahwe.

26Lakini mambo ambayo ni ya Yahwe ambayo mnayo na sadaka za viapo vyenu-mtachukua hizi na kwenda eneo ambalo Yahwe atachagua.27Hapo mtatoa sadaka ya kuteketezwa, nyama na damu, kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, damu ya dhabihu zenu itamwagwa nje kwenye madhabahu ya Yahwe Mungu wenu, na mtakula nyama.28Mchunguze na msikilize haya maneno yote ambayo - ninawaamuru, ili iwe uzuri kwenu na watoto wenu baada yenu milele, wakati mnafanya kile kilicho kizuri na sawa machoni pa Yahwe Mungu wenu.

29Wakati Yahwe Mungu wenu anapunguza mataifa kutoka kwenu, wakati mnaingia kuwafukuza, na mnawafukuza na kuishi katika nchi yao,30muwe makini wenyewe ili kwamba msinaswe kwa kuwafuata, baada ya kuangamizwa kutoka kwenu kunaswa katika kuchunguza miungu yao, katika kuuliza, “Kwa namna gani haya mataifa yanaabudu muingu yao? Nitafanya vivyo hivyo.”31Hautafanya hivyo katika kumuabudu Yahwe Mungu wako, kwa kuwa kila kitu ambacho ni chukizo kwa Yahwe, mambo ambayo anayachukia- wamefanya haya na miungu yao, hata mnateketeza vijana wao na binti zao kwenye moto kwa ajili ya miungu yao.

32Chochote ninakuamuru, chunguza. Usiongeze juu yake au kupunguza.

13

1Kama miongoni mwenu ainuka nabii au muota ndoto,2na kama anawapa ishara au maajabu, na kama ishara au maajabu yanatokea, kama alivyozungumza kwenu na kusema, “Ebu tuifuate miungu mingine, ambayo hatuijui, na tuiabudu.”3Usisikilize maneno ya nabii huyo, au kwa huyo muota ndoto, kwa kuwa Yahwe Mungu wako anakujaribu kujua kama unampenda Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na roho yako yote.4Mtatembea kulingana na Yahwe Mungu wenu, mheshimu, mzishike amri zake, na mtii sauti yake, na mtamwabudu na kushikamana naye.

5Nabii huyo au muota ndoto atauwawa, kwa sababu amezungumza uasi dhidi ya Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwaleta toka nchi ya Misri, na aliyewakomboa kutoka nyumba ya utumwa. Hivyo nabii anataka kuwaondoa katika njia ambayo Yahwe Mungu wenu aliwaamuru kutembea. Kwa hiyo weka mbali maouvu kutoka kwenu.6Tuseme kwamba ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa karibu nawe, au rafiki yako ambaye ni kama roho yako, kukushawishi kwa siri na kusema, “Acha tuende na tukaabudu miungu mingine ambayo hatujazijua, wala wewe wala mababu zako-7Miungu yeyote ya watu ambayo imewazunguka, karibu nanyi au mbali kutoka mwisho wa dunia kwenda mwisho mwingine wa dunia.”8Usimkubali au kumsikiliza. Wala macho yako yasione huruma, wala hautamuacha akiba au kumficha.9Badala yake, utamuacha hakika; mkono wako utakuwa wa kwanza kumuua, na badae mkono wa watu wote.10Mtamponda kwa mawe mpaka kufa, kwa sababu amejaribu kuwaondoa kutoka kwa Yahwe Mungu wenu, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri, nje ya nyumba ya utumwa.11Israel yote itasikia na kuogopa, na haitaendelea kufanya aina ya uovu miongoni mwenu.

12Kama utasikia yeyote anasema kuhusu moja ya miji yenu, kwamba Yahwe Mungu wenu anawapa kuishi ndani yake.13Baadhi ya wenzenu waovu wamewaacha miongoni mwenu na kuacha kwa mbali wakazi wa miji yao na kusema, “Acha tuende na kuabudu miungu mingine ambayo hamjaijua.”14Basi utaichunguza uthibitisho, kufanya utafiti na kuipeleleza kwa kina. Wakati unagundua kwamba ni kweli na hakuna shaka kwamba chukizo hilo lililofanyika miongoni mwenu, kisha utachukua hatua.15Utawashambulia hakika wenyeji wa mji huo kwa makali ya upanga. Utaangamiza kabisa na watu wote walio ndani yake, pamoja na mifugo yake, pamoja na makali ya upanga.16Utakusanya nyara zote kutoka katikati mwa mitaa yake na utaunguza mji, pamoja na nyara zake zote - kwa kuwa Yahwe Mungu wako. Mji utakuwa mchungu wa uharibifu milele; haupaswi kujengwa tena.17Hakuna hata kimoja kati ya vitu hivyo vimewekwa wakfu kwa ajili ya kuangamizwa vinapaswa kugadamana kwenye mkono wako. Hii inapaswa kuwa kesi, ili kwamba Yahwe atageuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, kumuonyesha rehema, kuwa na huruma kwako, na kukufanya wewe kuongezeka katika idadi, kama alivyoapa kwa baba zako.18Atafanya hivi kwa sababu unasikiliza sauti ya Yahwe Mungu wako, kuzishika amri zake ambazo ninakuamuru leo, kufanya kile kilicho sahihi mbele ya macho ya Yahwe Mungu wako.

14

1Ninyi ni watu wa Yahwe Mungu wenu. Msijikate wenyewe, wala kunyoa sehemu za nyuso zenu kwa ajili ya wafu.2Kwa kuwa mu taifa lilowekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wenu, na Yahwe amewachagua kuwa watu kwa ajili ya urithi wake, zaidi kuliko watu wote walio juu ya uso wa dunia.

3Hampaswi kula kitu chochote kilicho chukizo.4Hawa ni wanyama ambao mnaweza kula: ng'ombe, kondoo, mbuzi,5kulungu, paa, kulungu wa kiume, mbuzi wa mwituni, paa mweupe na pofu na kondoo wa mlimani.6Mnaweza kula wanyama wowote ambao wamegawanyika kwato, ambaye ana kwato zilizogawanyika mara mbili, na utafuna macheuo.7Hata hivyo, hampaswi kula baadhi ya wanyama ambao utafuna macheuo au ambao wana kwato zilizogawanyika mara mbili: ngamia, sungura, pomono, kwa sababu watafuna macheuo lakini hawajagawanyika kwato, ni najisi kwenu.8Nguruwe ni najisi kwenu pia kwa sababu amegawanyika kwato lakini hatafuni macheuo; ni najisi kwenu. Msile nyama ya nguruwe, na msiguse mizoga yao.9Haya yaliyo ndani ya maji mnaweza kula: chochote kilicho na mapesi na magamba;10lakini chochote kisichokuwa na mapesi na magamba msile; ni najisi kwenu.

11Ndege wote safi mnaweza kula.12Lakini hawa ni ndege ambao hampaswi kula: tai, tumbusi, kipungu,13mwewe mwekundu na mweusi, aina yoyote ya kipanga.14Hampaswi kula aina yoyote ya kunguru,15na mbuni na mwewe wa usiku, ndege wa baharini, aina yoyote ya mwewe,16bundi mdogo, bundi mkubwa, na bundi mweupe,17Mwari, nyamafu ya tai, mnandio.18Hampaswi kula korongo, aina yoyote ya kongoti, hudihudi, na popo.

19Wote wenye mabawa; vitu vya utando ni najisi kwenu; havipaswi kuliwa.20Mnaweza kula vitu vyote virukavyo.

21Hampaswi kula chochote kinachokufa chenyewe; mnaweza kumpa mgeni ambaye yuko katika mji wenu, kwamba anaweza kula au mnaweza kuuza kwa mgeni. Kwa kuwa mu taifa lililowekwa wakfu kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu. Hampaswi kumchemusha mbuzi kijana katika maziwa ya mama yake.

22Hakika mnapaswa kutoa fungu la kumi la mavuno ya mbegu zenu zote, ambazo huja kutoka kwenye shamba kila mwaka.23Mnapaswa kula mbele ya Yahwe Mungu wenu, katika eneo ambalo atachagua kama patakatifu pake, fungu la kumi la nafaka zenu, za mvinyo mpya, na mafuta yenu, na mzaliwa wa kwanza wa wanyama na mifugo, kwamba mnaweza kujifunza daima kumheshimu Yahwe Mungu wenu.24Kama safari ni ndefu kwenu na kwamba hamwezi kuibeba, kwa sababu eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake ni mbali kwenu, basi, wakati Yahwe Mngu anawabariki,25mtabadilisha sadaka katika pesa. Fungeni pesa kwenye mkono, na nendeni kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua.26Huko mtatumia pesa kwa chochote mnatamani kwa ng'ombe au kondoo, au kwa mvinyo, au kwa kinywaji imara, au kwa chochote mnatamani; mtakula hapo mbele ya Yahwe Mungu wenu, na mtafurahi, nyie na nyumba zenu.27Mlawi ambaye yuko malangoni mwenu- msimsahau, kwa kuwa hana sehemu wala urithi pamoja nanyi.

28Mwisho mwa kila miaka mitatu mtawasilisha mafungu yote ya kumi ya mazao kwa mwaka huo huo, na mtatunza katika malango yenu;29na Mlawi, kwa sababu hana sehemu wala urithi pamoja nanyi, na mgeni, na yatima, na wajane walio ndani ya malango yenu, watakuja na kula na kurithika. Fanya hivyo kwa Yahwe Mungu wenu aweze kuwabariki katika kazi zote za mikono yenuo mnazofanya.

15

1Kila mwisho wa kila miaka saba, mnapaswa kufuta madeni.2Hii ni tabia ya ukombozi. Kila mkopeshaji atafuta kile alichompa jirani yake, hata dai kutoka kwa jirani yake au ndugu yake kwa sababu ufutaji wa madeni wa Yahwe umetangazwa.3Kutoka kwa mgeni mnaweza kudai; lakini kwa chochote chenu kilicho na ndugu yenu mnapaswa mkitoe.4Hata hivyo, pasiwepo maskini miongoni mwenu (kwa kuwa Yahwe kwa hakika atawabariki kwenye nchi ambayo anawapa kama urithi kumiliki)5kama peke yenu mnasikiliza kwa bidii sauti ya Yahwe Mungu wenu, kuzishika amri zote ambazo anawaamuru leo.6Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu atawabariki, kama alivyowaahidia; mtakopesha mataifa mengi, lakini hamtaazima; mtaongoza juu ya mataifa mengi, lakini hayatawaongoza ninyi.

7Kama kuna mtu maskini miongoni mwenu, moja wa ndugu zenu, ndani ya malango yenu yoyote kwenye nchi yenu ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, msifanye migumu mioyo yenu wala kufunga mkono wenu toka kwa ndugu yenu,8Lakini mnapaswa hakika kufungua mkono wenu kwake na hakika mkopeshe yeye vya kutosha hitaji lake.9Muwe makini kutokuwa na wazo ovu au potovu katika moyo wenu, kusema, “Mwaka wa saba, mwaka wa ukombozi u karibu;” ili kwamba msiwe wachoyo kuhusiana na ndugu zenu maskini na haumpi chochote; anaweza kumlilia Yahwe kuhusu nyie, na itakuwa dhambi yenu.10Mnapaswa kwa hakika mmpe, na moyo wenu hampaswi kuhuzunika wakati mnampa, kwa sababu kurudishiwa kwa Yahwe huyu Mungu wenu atawabariki katika kazi zenu zote na katika chochote mnaweka mkono wenu.11Kwa kuwa maskini kamwe hatakoma kuishi katika nchi, kwa hiyo nakuamuru wewe na kusema, “Unapaswa kwa hakika ufungue mkono wako kwa ndugu yako, kwa mhitaji wako, na kwa maskini wako katika nchi yako.”

12Kama ndugu yako, ni mwebrania wa kiume au mwebrania wa kike, ameuzwa kwako na anakutumikia kwa miaka saba, basi katika mwaka wa saba unapaswa umwache aende zake huru.13Unapomwacha aende zake huru, usimwache aende mkono mtupu.14Unapaswa kwa ukarimu utoe kwake kutoka mifugo yako, kutoka pura iliyo chini, na kinu chako cha mvinyo. Kama Yahwe Mungu wako alivyokubariki, unapaswa umpe yeye.15Unapaswa kukumbuka kwamba ulikuwa mtumwa kwenye nchi ya Misri, na kwamba Yahwe Mungu wako alikukomboa; kwa hiyo ninakuamuru leo kufanya hivi.

16Itakuwa kwamba kama atasema kwako, “Sitaenda mbali yako;” kwa sababu anakupenda na nyumba yako, na kwa sababu ni mzuri kwako,17basi unapaswa kuchukua uma na msukumo kupitia sikio lake kwenye mlango, na atakuwa mtumwa wako milele. Na pia kwa mtumwa wako wa kike utafanya vilevile.

18Isionekane kuwa vigumu kwako kumwachia aende zake huru, kwa sababu amekutumikia kwa miaka sita na amekupa mara mbili udhamani wa mtu aliyeajiriwa. Yahwe Mungu wako atakubariki katika yote unayofanya.

19Wazao wote wa kwanza wa kiume katika wanyama na mifugo wako unapaswa uwatenge kwa Yahwe Mungu wako. Hautafanya kazi na mzao wa kwanza wa wanyama wako wala kumnyoa mzao wa kwanza wa mfugo wako.20Unapaswa umle mzaliwa wa kwanza mbele ya Yahwe Mungu wako kila mwaka katika eneo ambalo Yahwe atachagua, wewe na nyumba yako.21Kama ina kasoro yoyote- kwa mfano, kama ni kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote- haupaswi kumtoa dhabihu kwa Yahwe Mungu wako.22Utamla ndani ya malango yako; mtu asiye najisi na aliye najisi ni sawa unapaswa kula, kama ungekula paa au kulungu.23Pekee haupaswi kunywa damu yake; unapaswa kuimwanga damu yake juu ya ardhi kama maji.

16

1Angalia mwezi wa Abibu, na uishike pasaka ya Yahwe Mungu wako, kwa kuwa katika mwezi wa Abibu Yahwe Mungu wako alikuleta toka Misri usiku.2Utamtolea dhabibu ya pasaka Yahwe Mungu wako na baadhi ya mifugo na wanyama kwenye eneo ambalo Yahwe atachagua kama patakatifu pake.3Hautakula mkate wa chachu pamoja nayo, siku saba utakula mkate usio na chachu, mkate wa mateso; kwa kuwa mlitoka katika nchi ya Misri kwa haraka. Fanya haya katika siku zako zote za maisha yako ili uweze kukumbuka akilini siku mliotoka nchi ya Misri.4Hakuna chachu inapaswa kuonekana miongoni mwenu ndani ya mipaka yenu wakati wa siku saba; wala nyama yoyote mnayotoa dhabihu jioni kwa siku ya kwanza inabaki mpaka asubuhi.

5Msitoe dhabihu ya pasaka kati ya malango yenu ya ndani ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa.6Badala yake, toa dhabihu katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua kama patakatifu pake. Hapo mtatoa dhabihu ya pasaka jioni wakati jua linazama, kwa wakati huo wa mwaka mlitoka Misri.7Mtapaswa kuichoma na kuila katika eneo ambalo Yahwe Mungu wenu atachagua; asubuhi mtageuka na kwenda kwenye mahema yenu.8Kwa siku sita mtakula mkate usiotia chachu; katika siku ya saba kutakuwa na kusanyiko makini kwa ajili ya Yahwe Mungu wenu; katika siku hiyo hamtafanya kazi.

9Mtahesabu wiki saba kwa ajili yenu; tangu wakati mlipoanza kuweka mundu kwenye nafaka iliyosimama mtapaswa kuanza kuhesabu wiki saba.10Mtapaswa kushika wiki za sherehe ya Yahwe Mungu wenu pamoja na mchango wa sadaka ya utayari kutoka mkono wako ambayo utatoa, kulingana na Yahwe alivyokubariki.11Utafurahi mbele ya Yahwe Mungu wako- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi aliye katika malango yako, na mgeni, yatima, na mjane alio miongoni mwenu, katika eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kwa ajili ya patakatifu pake.

12Utakumbuka akilini kwamba ulikuwa mtumwa Misri; unapaswa kuangalia na kuzishika amri hizi.

13Unapaswa kushika sherehe za vibanda kwa siku saba baada ya kuwa mmekusanya mavuno toka kwenye sakafu ya mapura na kutoka kwenye kinu chako cha divai.14Utafurahi wakati wa sherehe- wewe, kijana wako, binti wako, mjakazi wako wa kiume, mjakazi wako wa kike, Mlawi, na mgeni, na yatima na mjane walio ndani ya malango yako.15Kwa siku saba, unapaswa kuangalia sherehe ya Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo Yahwe atachagua, kwa sababu Yahwe Mungu wako atakubariki katika mavuno yako yote na kazi ya mikono yako yote, na unapaswa kuwa na furaha kabisa.

16Mara tatu kwa mwaka, wanaume wako wote wanapaswa kuonekana mbele za Yahwe Mungu wako katika eneo ambalo atachagua: katika sherehe ya mkate usiotiwa chachu, katika sherehe za wiki, na sherehe ya vibanda; na hawataonekana mbele za Yahwe mikono mitupu;17badala yake, kila mtu atatoa kama awezavyo, kwamba mtajua baraka kwamba Yahwe Mungu wako amekupa.

18Unapaswa kufanya waamuzi na maakida ndani ya malango yako ambayo Yahwe Mungu wako anakupa; watachukuliwa toka kila kabila, and watahukumu watu kwa hukumu ya haki.19Haupaswi kuiondoa haki kwa nguvu; haupaswi kuonyesha upendeleo wala kuchukua rushwa, kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya hekima na kupotosha maneno ya haki.20Unapaswa kufuata haki, baada ya haki peke yake, ili kwamba uishi na kurithi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa.

21Haupaswi kujitengenezea Asherahi, aina yoyote ya mti, kando ya madhabahu ya Yahwe Mungu wako ambayo utakayojitengenezea.22Wala usijitengenezee jiwe takatifu la nguzo, ambalo Yahwe Mungu wako anachukia.

17

1Haupaswi kumtolea dhabihu Yahwe Mungu wako ng'ombe au kondoo aliye na kasoro au kitu chochote kibaya, kwa kuwa hiyo itakuwa chukizo kwa Yahwe Mungu wako.

2Kama kunapatikana miongoni mwenu, ndani ya malango ya mji wowote ambao Yahwe Mungu wenu anawapatia, mwanaume yoyote au mwanamke ambaye anafanya uovu mbele ya Yahwe Mungu wenu kuiharibu agano lake -3yoyote ambaye ameenda na kuabudu miungu mingine na kuisujudia, wala jua, mwezi, au kati ya jeshi la mbinguni- hakuna chochote nimekuamuru,4na kama ungeambiwa kuhusu hiki, au kama una mifugo- basi unapaswa kufanya uchunguzi wa makini. Kama ni kweli na hakika kwamba chukizo kama hilo limefanyika Israeli-5-basi utamleta huyo mwanaume au mwanamke, aliyefanya uovu huu, katika malango ya mji, kwamba mwanaume kabisa au mwanamke, na umpende huyo mtu mpaka kufa.6Kwa kinywa cha mashahidi wawili, au mashahidi watatu, itakuwa yeye anayepaswa kuuwawa; lakini kwa kinywa cha shahidi mmoja peke hatauwawa.7Mkono wa mashahidi unapaswa kuwa wa kwanza kumuuwa, na badae mkono wa watu wote; na mtamuondoa muovu miongoni mwenu.

8Kama jambo linatokea ambalo ni gumu kwenu kufanya maamuzi- pengine swali la mauaji au kifo cha ajali, haki ya mtu mmoja na haki ya mtu mwingine, au swali moja la aina ya kuzulu kufanyika, au aina nyingine ya jambo-mambo ya utata ndani ya malango yenu, basi utapaswa kwenda kwenye eneo ambalo Yahwe Mungu wako atachagua kama patakatifu pake.9Utapaswa kwenda kwa makuhani, wazao wa Lawi, na kwa mwamuzi atakayetumika kwa wakati huo; mtatafuta ushauri wao, na watawapa ninyi maamuzi.10Mnapaswa kufuata sheria mliyopewa, katika eneo Yahwe atachagua kama patakatifu pake. Mtakuwa makini kufanya kila kitu ambacho wanawaelekeza kufanya.11Fuata sheria wanayo wafundisha, na kufanya kulingana na maamuzi wanawapa. Msigeuke kutoka kwa kile wanawambia, kwa kulia au kushoto.12Yeyote anayefanya kwa kiburi, kwa kutomsikiliza kuhani anayesimama kutumika mbele ya Yahwe Mungu wako, au kwa kutomsikiliza mwamuzi- huyu mtu atakufa; mtaweka mbali uovu kutoka Israeli.13Watu wote wanapaswa kusikia na kuogopa, na kutofanya kwa kiburi tena.

14Wakati mlipokuja kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu anawapa, na wakati mnamiliki na kuanza kuishi ndani yake, na halafu unasema, “Nitajiwekea mfalme juu yangu, kama mataifa yote yanayonizunguka mimi,”15basi unapaswa kwa hakika kujiwekea mfalme juu yako mtu yeyote ambaye Yahwe atachagua. Unapaswa kujiweka kama mfalme juu yako mtu yeyote kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Haupaswi kuweka mgeni, ambaye si ndugu yenu, juu yenu.16Lakini hapaswi kuzidisha farasi kwa ajili yake, wala kusababisha watu kurudi Misri ili kwamba aweze kuzidisha farasi, kwa kuwa Yahwe alikwisha sema kwako, “Unapaswa kuanzia sasa usirudi njia hiyo tena.”17Na hapaswi kuzidisha wake kwa ajili yake, ili kwamba moyo wake usigeuke kotoka kwa Yahwe; wala hapaswi sana kuzidisha fedha au dhaha.

18Wakati aketipo kwenye kiti cha enzi cha ufalme wake, anapaswa kuandika kwenye kitabu kwa ajili yake, nakala ya sheria hii, kutoka kwenye sheria ambayo iko mbele ya makuhani, ambao ni Walawi.19Kitabu kinapaswa kuwa na yeye, na anapaswa kusoma ndani yake kwa siku zake zote, ili kwamba aweze kujifunza kumheshimu Yahwe Mungu wako, ili kwamba ashike maneno yote ya sheria hii na amri hizi, kuzishika.20Anapaswa kufanya hivi ili kwamba moyo wake usiinuliwe zaidi ya ndugu zake, na ili kwamba asigeuke mbali na amri, kwa mkono wake wakulia, au kwa kushoto kwa kusudi kwamba, aweze kuzidisha siku zake katika ufalme wake, yeye na watoto wake, miongoni mwa Israel.

18

1Makuhani, ambao ni Walawi, na makabila yote ya Lawi, hayatakuwa na mgao wala urithi pamoja na Israel; wanapaswa kula dhabihu ya Yahwe iliyotengenezwa kwa moto kama urithi wao.2Hawatakuwa na urithi miongoni mwa ndugu zao; Yahwe ni urithi wao, kama alivyosema nao.

3Hii ni sababu ya makuhani kutoka kwa watu, kutoka kwa wale wanaotoa dhabihu, kama itakuwa ng'ombe au kondoo: wanapaswa kutoa kwa kuhani bega, mashavu mawili, na sehemu za ndani.4Mazao ya kwanza ya nafaka zako, mvinyo wako mpya, na mafuta yako, na manyoya ya kwanza ya kondoo zako, unapaswa umpe.5Kwa kuwa Yahwe Mungu wako amemchagua kutoka kwenye makabila yote yako kusimama kutumika kwa jina la Yahwe, yeye na wana wake milele.

6Kama Mlawi anatoka kati ya miji yenu nje ya Israel yote kutoka ambapo anaishi, na utamani kwa moyo wake wote kuja katika eneo Yahwe atachagua,7basi anapaswa kutumika kwa jina la Yahwe Mungu wake kama ndugu zake wote Walawi wanafanya, wanaosimama mbele ya Yahwe.8Wanapaswa kuwa na mgao wa kufanana wa kula, badala ya kile kinachokuja kutokana na mauzo ya urithi wa familia yake.

9Wakati mmekuja katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa, mnapaswa kujifunza kuangalia machukizo ya mataifa.10Pasipatikane miongoni mwenu mmoja anayemweka kijana wake au binti yake kwenye moto, yeyote anatumia uganga, yeyote anatabiri, au mchawi, mchawi yeyote,11yeyote aongeae na wafu, au yeyote aongeae na roho.12Kwa yeyote afanyae mambo haya ni chukizo kwa Yahwe; ni kwa sababu ya machukizo haya ambayo Yahwe Mungu wenu anawaondosha mbele zenu.13Mnapaswa kuwa wakamilifu mbele ya Yahwe Mungu wenu.

14Kwa mataifa haya ambayo mtayafukuza kusikiliza wale wafanyao uchawi na uganga; lakini kwenu, Yahwe Mungu wenu amewakataza ninyi kufanya hivyo.15Yahwe Mungu wenu atainua kwa ajili yenu nabii kutoka miongoni mwenu, mmoja wa ndugu zenu, kama mimi. Mnapaswa kumsikiliza.16Hiki ndicho mlichouliza kutoka kwa Yahwe Mungu wenu huko Horebu katika siku ya kusanyiko, kusema, “Acha tusisikie tena sauti ya Yahwe Mungu wetu, wala kuona moto mkuu tena, wala tutakufa.”

17Yahwe alisema nami, “Kile walichosema ni kizuri.18Nitamwinua nabii kwa ajili yao kutoka miongoni mwa ndugu zao, kama wewe. Nitaweka maneno yangu katika kinywa chake, na ataongea nao yote niliyo waamuru.19Itakuwa kama yeyote hatasikia maneno yangu ambayo anazungumza kwa jina langu, nitalitaka kwake.20Lakini nabii ambaye anazungumza neno kwa kiburi kwa jina langu, neno ambalo sijamuamuru kusema, au ambaye anayezungumza kwa jina la miungu mingine, huyo nabii atakufa.”

21Hivyo ndivyo unapaswa kusema katika mioyo yenu: “Tutagunduaje kuwa ujumbe ambao Yahwe hajazungumza?”22Mtagundua ujumbe ambao Yahwe amezungumza pindi nabii azungumzapo kwa jina la Yahwe. Kama hiyo haitokei wala kufanyika, basi hicho ni kile ambacho Yahwe hajazungumza na nabii amezungumza kwa kiburi, na hampaswi kumuogopa.

19

1Wakati Yahwe Mungu wenu anayafutilia mbali mataifa, yale ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa nchi yao, na wakati mnakuja kwao na kuishi katika miji yao na nyumba,2mnapaswa kuchagua miji mitatu kwa ajili yenu katikati mwa nchi yenu ambayo Yahwe Mungu anawapa kuimiliki.3Mnapaswa kujenga barabara na kugawa mipaka ya nchi yenu katika maeneo matatu, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anafanya kuimiliki, ili kwamba kila mmoja anayeua mtu mwingine apate kukimbia hapo.

4Hii ni sheria kwa ajili ya mtu anayeua mwingine na anayekimbilia huko kuishi: yeyote auae jirani yake bila kujua, na hapo awali hakumchukia-5kama wakati mtu aingiapo katika msitu pamoja na jirani yake kukata kuni, na mkono anapozungusha shoka, na kichwa uteleza kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake mpaka akafa- basi mtu huyu anapaswa kukimbilia katika moja ya miji hii na kuishi.6Vinginevyo damu ya mlipiza kisasi atamfuata yeye aliyetoa uhai, na kwa hasira kali anampita kwa sababu ilikuwa safari ndefu. Na anampiga na kumuua, ijapokuwa mtu huyo akustahili kufa; na hata akustahili adhabu ya kifo kwa sababu hakumchukia jirani yake kabla hili halijatokea.7Basi sasa ninakuamuru kuchagua miji mitatu kwa ajili yako.

8Kama Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyoapa kwa mababu zenu kufanya, na kuwapa nchi yote ambayo amewaahidia kuwapa mababu zenu;9kama mnazishika amri hizi zote kuzifanya, ambazo ninakuamuru leo- amri za kumpenda Yahwe Mungu wenu na daima kutembea katika njia zake, basi mnapaswa kuongeza miji mitatu zaidi kwa ajili yenu, isipokuwa ile mitatu.10Fanya hivi ili kwamba damu isiyo na hatia isimwagwe katikati ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kwa ajili ya urithi, ili kwamba pasiwepo hatia ya damu kwenu.

11Lakini kama yeyote anamchukia jirani yake, uongo unamsubiri, uinuka dhidi yake, na majeraha ya kufa kwake ili kwamba anakufa, na kama basi anakimbia katika moja ya miji hii-12basi wazee wa mji wake wanapaswa kumtoa na kumrudisha toka huko, na kumkabidhi katika mkono wa ndugu mhusika, ili kwamba amuue.13Jicho lako halipaswi kumuonea huruma; badala yake; unapaswa kuondoa hatia ya damu kutoka Israel, ili kwamba iwe vizuri kwako.

14Haupaswi kuondoa alama ya jirani yako ambayo wameweka katika eneo muda mrefu, katika urithi wako ambao utarithi, katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa kumiliki.

15Shahidi moja pekee hapaswi kuinuka dhidi ya mtu kwa ajili ya uovu wowote, au kwa ajili ya dhambi yoyote, katika jambo lolote ambalo amefanya dhambi; kwa kinywa cha mashahidi wawili, au kwa kinywa cha mashahidi watatu, kunapaswa jambo lolote lidhibitishwe.

16Kama ushuhuda wa mtu asiye na haki anainua dhidi ya mtu yeyote kushuhudia dhidi yake kwa mambo mabaya.17Basi watu wote wawili, mmoja kati ya yule utata upo, anapaswa kusimama mbele ya Yahwe, mbele ya makuhani na waamuzi ambao wanatumika siku hizo.18Waamuzi wanapaswa kuchunguza kwa uangalifu; ona, kama ushahidi ni ushahidi wa uongo na umeshuhudiwa kwa uongo dhidi ya ndugu yake,19basi unapaswa kufanya kwake, kama alivyokusudia kufanya kwa ndugu yake, na utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.20Basi wale wanaobaki watasikia na kuogopa, na kuanzia hapo na kuendelea hawatafanya tena aina ya ouvu miongoni mwao.21Macho yako hayapaswi kuona huruma; maisha yatalipa kwa maisha, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

20

1Pindi utokapo kwenda vitani kupigana dhidi ya adui zako, na kuona farasi, magari, na watu wengi zaidi kuliko wewe, haupaswi kuwaogopa; kwa kuwa Yahwe Mungu wako yu pamoja nawe, yeye aliyekuleta kutoka nchi ya Misri.2Wakati unakaribia kuingia kwenye vita, kuhani anapaswa kuwasongelea watu nakuwaambia,3“Sikilizeni, Israel, mnaenda kupigana dhidi ya maadui zenu. Msidhofishe mioyo yenu. Msiohofu au kutetemeka. Msiwaogope.4Kwa kuwa Yahwe Mungu wenu ndiye aendaye pamoja nanyi kupigana kwa ajili yenu dhidi ya maadui zenu na kuwaokoa.”

5Maakida wanapaswa kuzungumza na watu na kusema, “Ni mtu yupi aliyejenga nyumba mpya na hajaiweka wakfu? Acha aende na arudi nyumbani kwake, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine aiweke wakfu.6Kuna yeyote ambaye amepanda mzabibu na hajafurahia matunda yake? Acha aende nyumbani, ili kwamba asife vitani na mtu mwingine afurahie matunda yake.7Ni mtu yupi aliyeposa kuoa mwanamke lakini bado hajamuoa? Acha aende nyumbani ili kwamba asife vitani na mume mwingine amuoa.”

8Maakida wanapaswa kuzungumza zaidi kwa watu na kusema, “Ni mwanaume gani aliye hapa ambaye ni mwenye hofu au mnyonge? Acha aende na arudi nyumbani kwake, ili kwamba moyo wa ndugu yake usiyeyuke kama moyo wake.”9Wakati maakida wamemaliza kuzungumza na watu, wanapaswa kuwateua majemedari juu yao.

10Wakati mtokapo kuteka mji, wafanye watu hao toleo la amani.11Kama watapokea amani na kufungua malango yao kwenu, watu wote wanaopatikana ndani yake wanapaswa kulazimishwa kuwafanyia kazi na wanapaswa kuwatumikia.12Lakini kama haitengenezi amani kwenu, lakani badala yake inatengeneza vita dhidi yenu, basi mnapaswa kumruhusu,13na wakati Yahwe Mungu wenu anawapa ushindi na kuwaweka chini ya utawala wenu, mnapaswa kuua kila mtu katika mji.14Lakini wanawake, wadogo, ng'ombe, na kila kitu kilicho ndani ya mji, na nyara zake zote, utavichukua kama mateka yako. Nawe utawamaliza mateka wa maadui zako, ambao Yahwe Mungu amekupa.15Unapaswa kuifanyia hivyo kuelekea miji yote ambayo iko mbali nawe, miji ambayo siyo miji ya mataifa yafuatayo.

16Katika miji ya watu hawa ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kama urithi, mnapaswa kutunza chochote kilicho na uhai.17Badala yake, mnapaswa kabisa kuagamiza: Hittite, na Amorite, Wakanani, Waperezi, Hivite, na Wayebusi, kama Yahwe Mungu wenu alivyowaamuru.18Fanya hivi ili kwamba wasiwafundishe kufanya katika njia za machukizo, kama walivyofanya kwa miungu yao. Kama mtafanya, mtafanya dhambi dhidi ya Yahwe Mungu wenu.

19Wakati mtakapouzingira mji kwa muda mrefu, huku mkipigana dhidi yake kuuteka, hampaswi kuharibu miti yake kwa kushika shoka dhidi yake. Kwa kuwa utaweza kula matunda yake, kwa hivyo usiukate. Kwa maana mti wa kondeni mtu ambaye atauzingira?20Ila miti ambayo unaijua sio miti ya chakula, unaweza kuharibu na kuikatia chini; utajenga maburuji dhidi ya mji unaofanya vita nawe, mpaka uanguke.

21

1Iwapo mtu amekutwa kauwawa ndani ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapatia kumiliki, kalala shambani, na haijulikani aliyemshambulia;2basi wazee wenu pamoja na waamuzi wenu wanapaswa kutoka nje, na kupima katika miji ambayo inamzunguka yule aliyeuawa.3Kisha wazee wa mji ulio karibu na mwili wa marehemu wanapaswa kuchukua mtamba kutoka kwenye kundi la mifugo, ambaye hajawahi kutumikishwa, wala kubebeshwa nira.4Kisha wanapaswa kumuongoza mtamba huyo mpaka chini ya bonde litiririkalo maji, bonde ambalo halijawahi kulimwa wala kupandwa, na mle bondeni wanapaswa kuvunja shingo ya mtamba huyo.5Makuhani, uzao wa Lawi, wanapaswa kuja mbele, kwa maana Yahwe Mungu wako amewachagua wamtumikie yeye na kutoa baraka katika jina la Yahwe na kuamua kila mtafaruku na ugomvi kwa neno lao.6Wazee wote wa mji ulio karibu na mtu aliyeuawa wanapaswa kunawa mikono yao juu ya mtamba aliyevunjwa shingo bondeni;7na wanapaswa kutoa suhuluisho juu ya jambo hilo na kusema, “Mikono yetu haijamwaga damu hii, wala macho yetu hayajaona suala hili.8Tusamehe watu wako Israeli, Yahwe, ambao umewakomboa, na usiweke hatia juu ya umwagaji damu usio na kosa miongoni mwa watu wako Israeli.” Kisha umwagaji damu utasamehewa kwao.9Kwa njia hii utaweka mbali umwagaji damu usio na hatia miongoni mwenu, mtakapofanya yaliyo mema machoni pa YAHWE.

10Utakapokwenda kupigana vita dhidi ya maadui zako na Yahwe Mungu wako atakapokupa ushindi na kuwaweka chini ya mamlaka yako, na ukawachukua mbali kuwa mateka,11kama kati ya mateka ukamwona mwanamke mzuri, nawe ukamtamani na kutaka kujitwalia awe mke wako,12basi utamleta nyumbani kwako; atanyoa nywele zake na kukata kucha zake.13Kisha atazivua nguo alizokuwa amezivaa wakati alipochukuliwa mateka na atabaki nyumbani kwako na kuwaomboleza baba yake na mama yake kwa mwezi mzima. Baada ya hapo unaweza kulala naye na kuwa mume wake, naye atakuwa mke wako.14Lakini usipofurahishwa naye, basi unatakiwa kumruhusu aondoke apendaye yeye. Lakini haupaswi kamwe kumuuza kwa fedha, pia haupaswi kumfanya kama mtumwa, kwa sababu umemdhalilisha.

15Iwapo mwanamume ana wake wawili na mmoja wao ampenda na mwingine kumchukia, na wote wamekwisha mzalia watoto –wote mwanamke mpendwa na mwanamke achukiwae –16basi katika siku ambayo mwanamume atakapowarithisha mali zake wanawe, hapaswi kumfanya mwana wa mke ampendaye kuwa mzawa wa kwanza kabla ya mwana wa mke amchukiaye, ambaye ndiye mwana wa kwanza.17Badala yake, anapaswa kumtambua mwana wa kwanza, mwana wa mke asiyempenda, kwa kumpatia mara mbili ya mali zake; kwa maana huyo mwana ni mwanzo wa nguvu zake; haki za mzawa wa kwanza ni zake.

18Iwapo mwanamume ana mwana mkaidi na muasi ambaye hatatii sauti ya baba yake au sauti ya mama yake, ambaye, hata baada ya kurekebishwa, hatawasikia;19basi baba yake na mama yake wanapaswa kumshika na kumleta mbele ya wazee wa mji na kwenye malango ya mji.20Wanapaswa kuwaambia wazee wa mji, “Huyu mwanetu ni mkaidi na muasi; hataki kusikia sauti zetu; ni mwasherati na pia ni mlevi.”21Kisha wanaume wote wa mji wanapaswa kumpiga kwa mawe hadi kufa; nanyi mtaondoa uovu miongoni mwenu. Israeli yote itasikia juu ya hili na kuogopa.

22Iwapo mwanamume kafanya dhambi inayostahili kifo na kisha akauwawa, kwa kunyongwa juu ya mti,23basi mwili wake haupaswi kubaki usiku kucha juu ya mti. Badala yake, unapaswa kuhakikisha unamzika siku hiyo; kwa maana yeyote anyongwaye amekwisha laaniwa na Mungu. Tii amri hii ili kwamba usitie najisi nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia kama urithi.

22

1Hautakiwi kumtazama ng'ombe au kondoo wa Muisraeli mwenzako akikosea njia na ukajificha kwao; hakika unapaswa kuwarejesha kwake.2Iwapo Muisraeli mwenzako hayupo karibu nawe, au kama haumfahamu, basi unapaswa kumleta mnyama huyo nyumbani kwako, na lazima uwe naye mpaka pale mwenyewe atakapomtafuta, na kisha lazima umrejeshee mwenyewe.3Unapaswa kufanya vivyo hivyo kwa punda wake; unapaswa kufanya vivyo hivyo na vazi lake; unapaswa kufanya vivyo hivyo kwa kila kitu alichopoteza Muisraeli mwenzako, kitu chochote alichopoteza na ukakipata; hautakiwi kujificha.

4Haupaswi kumwona punda wa Muisraeli mwenzako au ng'ombe wake kaanguka chini barabarani na kujificha dhidi yao; hakika unapaswa kumsaidia kumwinua tena.

5Mwanamke hatakiwi kuvaa kinachokusudiwa kwa mwanamume, vilevile mwanamume hapaswi kuvaa mavazi ya mwanamke; kwa maana yeyote afanyaye vitu hivi ni chukizo kwa Yahwe Mungu wako.

6Iwapo kiota cha ndege kikaonekana barabarani mbele yako, kwenye mti wowote au juu ya ardhi, kikiwa na makinda ya ndege au mayai ndani mwake, na mama yao akiwa juu yao au juu ya mayai, haupaswi kumchukua mama pamoja na makinda au mayai yake.7Hakika unapaswa kumuacha mama aende zake, ila makinda yake unaweza kuyachukua. Tii amri hii ili uenende vyema, na siku zako ziweze kurefushwa.

8Ujengapo nyumba mpya, basi unapaswa kujenga kitalu kwa ajili ya paa yako ili usilete damu juu ya nyumba yako mtu akianguka kutoka pale.

9Haupaswi kupanda shamba lako la mizabibu kwa mbegu mbili, ili kwamba mavuno yote yasichukuliwe na sehemu takatifu, mbegu uliyoipanda pamoja na matunda ya mzabibu.

10Haupaswi kulimia ng'ombe na punda kwa pamoja.

11Haupaswi kuvaa kitambaa kilichotengenezwa kwa sufu na kitani kwa pamoja.

12Unapaswa kutengeneza pindo katika pembe nne za nguo unayoivaa.

13Iwapo mwanamume kachukua mke, kisha kalala naye, na baadae kumchukia,14na kisha kumtuhumu kwa vitu vya aibu na kumharibia sifa yake kwa kusema, “Nilimchukua huyu mwanamke, lakini nilipomkaribia sikukuta ushahidi waubikra kwake.”15Kisha baba na mama mzazi wa binti wanatakiwa kupeleka ushahidi wa ubikra wake kwa wazee mlangoni mwa mji.16Baba wa binti anapaswa kuwaambia wazee, “Nilimpatia binti yangu kwa mwanamume huyu awe mkewe, naye anamchukia.17Tazama, amemtuhumu na vitu vya aibu na kusema, ‘Sikukuta ushahidi wa ubikra kwa binti yako.’ Lakini ushahidi huu hapa wa ubikra wa binti yangu.” Kisha watatandaza shuka mbele ya wazee wa mji.18Wazee wa mji wanapaswa kumchukua mwanaume huyo na kumuadhibu;19nao wanapaswa kumtoza faini ya shekeli mia moja ya fedha, na kumpatia baba wa binti, kwa sababu mwanaume kasababisha sifa mbaya kwa bikra wa Israeli. Binti huyu anapaswa kuwa mke wake; mwanaume huyu hatakiwi kumfukuza katika siku zake zote.

20Ila kama jambo hili ni la kweli, kwamba ushahidi wa bikra ya binti haukupatikana,21basi wanapaswa kumpeleka binti mlangoni kwa baba yake, na kisha wanaume wa mji wake wanatakiwa kumpiga kwa mawe hadi afe, kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli, kwa kutenda kama kahaba chini ya nyumba ya baba yake, nanyi mtakuwa mmeondoa uovu miongoni mwenu.

22Iwapo mwanaume kakutwa analala na mwanamke ambaye ni mke wa mtu, basi wote wanapaswa kufa, mwanaume aliyelala na mwanamke pamoja na mwanamke mwenyewe; nanyi mtakuwa mmeondoa uovu miongoni mwenu.

23Iwapo kuna msichana bikra, ambaye amechumbiwa na mwanaume, kisha mwanaume mwingine kamkuta mjini na kulala naye,24wachukueni wote wawili malangoni mwa mji, na kuwapiga mawe. Unapaswa kumpiga msichana mawe, kwa sababu hakupaza sauti kuomba msaada, ingawa alikuwa ndani ya mji. Unapaswa kumpiga mwanaume mawe, kwa sababu amemwingilia mke wa jirani yake; nanyi mtakuwa mmeondoa uovu miongoni mwenu

25Lakini kama mwanaume amemkuta msichana aliyechumbiwa shambani, na kama akamkamata na kulala naye, basi mwanaume pekee aliyelala naye ndiye lazima afe.26Lakini kwake msichana, msifanye chochote; hakuna dhambi inayostahili kifo kwake msichana. Kwa maana suala hili ni kama mwanaume amshambuliapo jirani yake na kumuua.27Kwa maana alimkuta shambani; msichana huyu aliyechumbiwa alipaza sauti, lakini hapakuwa na mtu wa kumuokoa.

28Iwapo mwanaume amemkuta msichana ambaye ni bikra lakini hajachumbiwa, na kama akamkamata na kulala naye, na kama wakagundulika,29basi mwanaume aliyelala naye lazima atoe shekeli hamsini za fedha kwa baba wa msichana, naye lazima awe mke wake, kwa sababu amemdhalilisha. Hatakiwi kumfukuza katika siku zake zote.

30Mwanamume hapaswi kumchukua mke wa baba yake kama wake; hatakiwi kuchukua haki za ndoa za baba yake.

23

1Mwanaume aliyejeruhiwa kwa kupondwa au kukatwa, haruhusiwi kuingia katika kusanyiko la Yahwe.

2Mwana haramu haruhusiwi kuwa miongoni mwa kusanyiko la Yahwe; kutoka hadi kizazi cha kumi cha uzao wake, hakuna kati yao anatakiwa kuwa kwenye kusanyiko la Yahwe.

3Muamori au Mmoabu haruhusiwi kuwa miongoni mwa kusanyiko la Yahwe; kutoka hadi kizazi cha kumi cha uzao wake, hakuna kati yao anatakiwa kuwa kwenye kusanyiko la Yahwe.4Hii ni kwa sababu hawakukutana nanyi kwa mkate na maji barabarani mlipokuwa mmetoka nje ya Misri, na kwa sababu walimkodisha Balaamu mwana wa Beoro kutoka Pethoro kule Aramu Naharaimu, awalaani.5Lakini Yahwe Mungu wako hakumsikiliza Balaamu; badala yake, Yahwe Mungu wako aligeuza laana kuwa baraka kwenu, kwa sababu Yahwe Mungu wako aliwapenda.6Hamtakiwi kutafuta amani au mafanikio yao, katika siku zenu zote.

7Hutakiwi kumchukia Muedomi, kwa maana ni kaka yako; hutakiwi kumchukia Mmisri, kwa maana ulikuwa mgeni katika nchi yake.8Wazawa wa kizazi cha tatu wanaozaliwa kwao wanaweza kuwa katika kusanyiko la Yahwe.

9Utakapotembea kijeshi dhidi ya maadui zako, basi unapaswa kujitenga na kila aina ya uovu.10Iwapo miongoni mwenu kuna mwanaume ambaye sio msafi kwa sababu ya jambo lililofanyika kwake usiku, basi anatakiwa atoke nje ya kambi ya jeshi; hatakiwi kurudi kambini.11Jioni ikifika, anatakiwa ajiogeshe kwa maji; na jua likizama atarudi ndani kambini.

12Pia unatakiwa kuwa na eneo nje ya kambi ambayo utakwenda;13na utakuwa na kitu katika zana zako cha kuchimbia; utakapochuchumaa kujisaidia, unapaswa kuchimbia nacho na kisha kurudishia udongo na kufunika kile kilichotoka kwako.14Kwa maana Yahwe Mungu wako anatembea miongoni mwa kambi yenu kuwapa ushindi na kuwapa maadui zenu mkononi mwenu. Kwa hiyo kambi yenu lazima iwe takatifu, ili kwamba asione kitu chochote kichafu miongoni mwenu na kuwaacha.

15Hutakiwi kumrudishia bwana mtumwa aliyetoroka kwake.16Mruhusu aishi pamoja nawe, katika mji wowote atakaochagua. Usimuonee.

17Hapatakiwi kuwa na kahaba wa kidhehebu miongoni mwa mabinti wa Israeli, na wala hapatakiwi kuwa na kahaba wa kidhehebu miongoni mwa wana wa kiume wa Israeli.18Hautakiwi kuleta mshahara wa kahaba au mshahara wa mbwa katika nyumba ya Yahwe Mungu wako kwa kiapo chochote; kwa maana vyote hivi na machukizo mbele ya Yahwe Mungu wako.

19Hutakiwi kumkopesha Muisraeli mwenzako kwa riba – riba ya fedha, riba ya chakula, au riba ya kitu chochote kinachokopeshwa kwa riba.20Kwa mgeni unaweza kukopesha kwa riba; lakini kwa Muisraeli mwenzako haupaswi kukopesha kwa riba, ili kwamba Yahwe Mungu wako aweze kukubariki katika kila jambo uwekalo mkono wako, katika nchi ambayo mnaenda kumiliki.

21Unapofanya kiapo kwa Yahwe Mungu wako, haupaswi kukawia kuikamilsha, kwa maana Yahwe Mungu wako hakika atadai kiapo hicho; itakuwa dhambi kwako usipokamilisha.22Lakini iwapo utajizuia kutoa kiapo, haitakuwa dhambi kwako.23Kile ambacho kimetoka kinywani mwako unapaswa kukifuata na kukitekeleza; kulingana na kiapo ulichotamka kwa Yahwe Mungu wako, chochote ulichotamka kwa hiari kwa kinywa chako.

24Utakapokwenda katika shamba la mizabibu la jirani yako, unatakiwa kula mizabibu idadi yoyote unayotaka, lakini hautakiwi kuhifadhi yoyote katika kikapu chako.25Utakapokwenda katika shamba la zao lililoiva la jirani yako, unaweza kuvuna kichwa cha mavuno kwa mkono wako, lakini haupaswi kutumia mundu kuvuna zao lililoiva la jirani yako.

24

1Mwanaume akimchukua mke na kumuoa, na mke asipokubalika machoni pa mumewe kwa sababu kagundua jambo ambalo si jema kwake, basi anatakiwa amwandikie talaka, aiweke mkononi mwake, na kumfukuza nyumbani kwake.2Akishaondoka nyumbani kwake, anaweza kwenda na kuwa mke wa mwanaume mwingine.3Iwapo mume wa pili akamchukia na kumwandikia talaka, akaiweka mkononi mwake, na kumfukuza nyumbani kwake; au huyu mume wa pili akafariki, mwanaume aliyemchukua kuwa mke wake –4basi mume wa awali, yule aliyemfukuza mara ya kwanza, haruhusiwi kumchukua tena awe mke wake, baada ya yeye kuwa mchafu, kwa maana hiyo itakuwa ni chukizo kwa Yahwe. Hautakiwi kusababisha nchi iwe na hatia, nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia kama urithi.

5Mwanaume atakapochukua mke mpya, hatakwenda vitani na jeshi, na wala hataamrishwa kwenda kwenye shughuli yoyote ya kulazimishwa; atakuwa huru kuwa nyumbani kwa mwaka mzima na atamfurahisha mke wake aliyemchukua.

6Mwanaume yeyote hatachukua kinu wala jiwe la kinu kama dhamana, kwa maana hivyo itakuwa kuchukua Maisha ya mtu kama dhamana.

7Iwapo mwanaume kakutwa kamteka mmoja wa kaka zake miongoni mwa watu wa Israeli, na kumtendea kama mtumwa na kisha kumuuza, huyo mwizi lazima afe; na utakuwa umeondoa uovu miongoni mwenu.

8Kuwa mwangalifu kuhusu kiini chochote cha ukoma, ili kwamba uwe makini katika kuchunguza na kufuata kila agizo linalopewa kwako ambalo makuhani, Walawi, wanakufundisha; kama nilivyowaamuru, ili utekeleze.9Kumbukeni nini Yahwe Mungu wako alichomfanya Miriam ulipokuwa ukitoka Misri.

10Utoapo mkopo wa aina yoyote kwa jirani yako, hautakiwi kwenda ndani ya nyumba yake kutafuta dhamana yake.11Utasimama nje, na mwanamume aliyekopa kwako ataleta dhamana yake nje kwako.12Iwapo ni mtu maskini, hautakiwi kulala na dhamana yake ikiwa mikononi mwako.13Hakika unapaswa kumrejeshea dhamana yake kabla jua halijazama, ili aweze kulala ndani ya vazi lake na akubariki; itakuwa utakatifu kwako mbele za Yahwe Mungu wako.

14Hautakiwi kumuonea mtumishi wa kuajiriwa ambaye ni maskini na mhitaji, hata kama ni jamaa wa Israeli, au ni kati ya wageni mbao wamo katika nchi ndani ya malango ya mji wako;15Kila siku unapaswa kumlipa mshahara wake; jua halipaswi kuzama kabla ya suala hili kutatuliwa, kwa maana ni maskini na anautegemea. Fanya hivi ili asilie dhidi yako kwa Yahwe, na kwamba isiwe ikawa dhambi ambayo umeitenda.

16Wazazi hawapaswi kuuwawa kwa niaba ya watoto wao, na wala watoto hawapaswi kuuawa kwa niaba ya wazazi wao. Badala yake, kila mtu anapaswa kuuwawa kwa dhambi yake mwenyewe.

17Haupaswi kutumia nguvu kuchukua haki inayomhusu mgeni au yatima, wala kuchukua vazi la mjane kama dhamana.18Badala yake, unapaswa ukumbuke ya kwamba ulikuwa mtumwa Misri, na kwamba Yahwe Mungu wako alikukomboa kutoka kule. Kwa hiyo ninakuagiza kutii amri hii.

19Utakapovuna zao lako shambani mwako, na ukasahau kipande cha mbegu shambani, haupaswi kurudi na kukichukua; kinapaswa kuwa cha mgeni, cha yatima, au cha mjane, ili Yahwe Mungu wako akubariki katika kazi ya mikono yako.20Utakapotikisa mti wako wa mzeituni, haupaswi kupanda juu ya matawi tena; itakuwa kwa ajili ya mgeni, kwa yatima na kwa mjane.21Utakapokusanya mizabibu shambani mwako, haupaswi kukusanya masazo yake tena. Kinachobaki kitakuwa cha mgeni, cha yatima na cha mjane.22Unatakiwa ukumbuke kuwa ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri; kwa hiyo nakuagiza kutii amri hii.

25

1Iwapo kutakuwa na malumbano kati ya wanaume na wakaenda mahakamani, na waamuzi wakawahukumu, basi watamwachilia mtakatifu na kumhukumu muovu.2Iwapo mwanaume mwenye hatia anastahili kupigwa, basi muamuzi atamfanya alale chini na kupigwa mbele zake kwa idadi iliyoamriwa kulingana na kosa lake.3Muamuzi anaweza kumpatia mapigo arobaini, lakini hapaswi kuvuka idadi hiyo; kwa maana akivuka idadi hiyo na kumpiga kwa mapigo mengi zaidi, basi Muisraeli mwenzako atakuwa kaaibishwa mbele ya macho yenu.

4Haupaswi kumfunga punda wako pua na mdomo anapokuwa akilima shamba lako.

5Iwapo kaka wanaishi pamoja na mmoja wao akafariki bila kuwa na mwana, basi mke wa marehemu hatakiwi kuolewa na mtu nje ya familia. Badala yake, kaka yake mumewe anapaswa kulala naye na kumchukua kuwa mke wake na kutekeleza wajibu wa kaka wa mume kwake.6Hii ni kwamba mtoto wa kwanza atakayezaliwa arithi chini ya jina la kaka yake mwanamume aliyefariki, ili jina lake lisiangamie ndani ya Israeli.

7Lakini kama mwanamume hataki kumchukua mke wa kaka yake awe wake, basi mke wa kaka yake anapaswa kwenda malangoni mpaka kwa wazee na kusema, “Kaka wa mume wangu amekataa kuwajibika kwa niaba ya jina la kaka yake humu Israeli; hataki kufanya wajibu wa kaka wa mume kwangu.”8Kisha wazee wa mji wake wanapaswa kumuita na kuzungumza naye. Lakini tuseme atasisitiza na kusema, “Sitaki kumchukua.”9Basi mke wa kaka yake anatakiwa kuja kwake mbele ya wazee, kumvua ndara zake miguuni mwake, na kumtemea usoni. Anapaswa kumjibu na kusema, “Hivi ndivyo kinachofanyika kwa mwanaume asiyetaka kujenga nyumba ya kaka yake.”10Jina lake Israeli litaitwa, “Nyumba ya mtu aliyevuliwa ndara zake.”

11Iwapo wanaume wamepigana wao kwa wao, na mke wa mmoja wao kaja kumkomboa mumewe dhidi ya yule aliyempiga, naye akanyosha mkono wake na kumshika sehemu za siri,12basi unapaswa kuukata mkono wake; jicho lako halipaswi kuwa na huruma.

13Haupaswi kuwa na mizani ya uzito tofauti katika mfuko wako, mkubwa na mdogo.14Hautakiwi kuwa na vipimo tofauti ndani ya nyumba yako, vikubwa na vidogo.15Unatakiwa kuwa na uzito kamili na wa haki; unatakiwa kuwa na vipimo kamili na vya haki, ili siku zako ziwe ndefu katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia.16Kwa maana wote wanaofanya vitu hivi, wote wanaovunja haki, ni chukizo kwa Yahwe Mungu wako.

17Kumbuka ni jambo gani Amaleki alilofanya kwako barabarani ulipokuwa ukitoka Misri,18jinsi alivyokutana na wewe barabarani na kuwashambulia kati yenu kwa nyuma, wale waliokuwa wamelegea nyuma, mlipokuwa dhaifu na kuchoka, hakumheshimu Mungu.19Kwa hiyo, Yahwe Mungu wako atakapowapa pumziko kutoka kwa maadui zako kila sehemu, katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anawapatia kumiliki kama urithi, hautakiwi kusahau kuwa unapaswa kufuta kumbukumbu ya Waamaleki chini ya mbingu.

26

1Utakapofika katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia kama urithi, na utakapoimiliki na kuishi ndani yake,2basi unatakiwa kuchukua baadhi ya mavuno yote ya kwanza ya ardhi uliyoyaleta kutoka katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupatia. Unatakiwa kuyaweka ndani ya kikapu na kuelekea katika eneo ambalo Yahwe Mungu wako atapachagua kama mahali patakatifu.3Unatakiwa kwenda kwa kuhani ambaye atakuwa akihudumu katika siku hizo na kumwambia, “Siku ya leo ninakiri kwa Yahwe Mungu wako ya kuwa nimekuja katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa mababu zetu kutupatia.”4Kuhani anatakiwa kuchukua kikapu mkononi mwako na kukiweka madhabahuni ya Yahwe Mungu wako.5Unapaswa kusema mbele ya Yahwe Mungu wako, “Babu yangu alikuwa Mwaremi mzururaji. Alikwenda chini hadi Misri na kukaa kule, na idadi ya watu wake ilikuwa chache. Kule akawa taifa kubwa, lenye nguvu na idadi kubwa.6Wamisri walitutendea vibaya na kututesa. Walitulazimisha kufanya kazi za watumwa.7Tulimlilia Yahwe, Mungu wa baba zetu, naye akasikia sauti yetu na kuona mateso yetu, kazi zetu na mateso yetu.8Yahwe alituondoa Misri kwa mkono wake mkuu, kwa mkono wake ulionyoshwa, kwa hofu kuu, kwa ishara na miujiza;9na ametuleta katika sehemu hii na kutupatia nchi hii, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali.10Tazama sasa, nimeleta mavuno ya kwanza kutoka katika nchi ambayo wewe, Yahwe, umenipatia.” Unapaswa kuweka chini mbele ya Yahwe Mungu wako na kuabudu mbele zake;11na unapaswa kufurahia katika mema yote ambayo Yahwe Mungu wako amekufanyia, kwa ajili na nyumba yako – wewe, na Mlawi, na mgeni aliye miongoni mwako.

12Utakapomaliza kutoa zaka yote ya mavuno katika mwaka wa tatu, yaani, mwaka wa kutoa zaka, basi unapaswa kuwapatia Mlawi, kwa mgeni, kwa yatima, na kwa mjane, ili kwamba waweze kula ndani ya malango yenu ya mji na kujazilishwa.13Unatakiwa kusema mbele ya Yahwe Mungu wako, “Nimetoa kutoka nyumbani mwangu vitu ambavyo ni mali ya Yahwe, na kumpatia Mlawi, mgeni, yatima, na mjane, kulingana na amri zote ulizonipatia. Sijavunja amri yako yoyote, wala sijazisahau.14Sijala kati yao wakati wa maombolezo yangu, wala sijaziweka mahali pengine nilipokuwa mchafu, wala sijazitoa kati yao kwa heshima ya wafu. Nimesikiliza sauti ya Yahwe Mungu wangu; Nimetii kila kitu ulichoniamuru kukifanya.15Tazama chini kutoka mahali patakatifu unapoishi, kutoka mbinguni, na ubariki watu wako Israeli, na nchi uliyotupatia, kama ulivyoapa kwa mababu zetu, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali.”

16Leo Yahwe Mungu wako anakuaamuru kuzitii sheria na amri hizi; basi utazishikilia na kuzitenda kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote.17Umetamka leo ya kuwa Yahwe ni Mungu wako, na kwamba utatembea katika njia zake na kushikilia sheria zake, maagizo yake na amri zake, na kwamba utaisikiliza sauti yake.18Leo Yahwe ametamka ya kwamba mu watu ambao ni mali yake, kama alivyoahidi kwenu, na kwamba mnapaswa kushikilia amri zake zote.19Na atawaweka juu zaidi ya mataifa mengine aliyoyaumba nanyi mtapokea sifa, umaarufu na heshima. Mtakuwa watu waliowekwa kando kwa Yahwe Mungu wenu, kama alivyosema.

27

1Musa na wazee wa Israeli waliwaamuru watu na kusema, “Zishikeni amri zote ninazowaamuru leo.2Katika siku mtakapopita juu ya Yordani kwenye nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapatia, mnapaswa kutengeneza mawe kiasi makubwa na kuyachapa kwa lipu.3Mnatakiwa kuyaandika juu yake maneno yote ya sheria hii pale mtakapovuka; ili muweze kwenda katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapatia, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali, kama Yahwe, Mungu wa mababu zenu, alivyowaahidi.4Mtakapovuka juu ya Yordani, yapange haya mawe ninayowaamuru leo, juu ya mlima wa Ebali, na myapige kwa lipu.5Hapo mnapaswa kujenga dhabahu kwa Yahwe Mungu wako, dhabahu la mawe; lakini hautakiwi kuinua chombo cha chuma kujenga mawe.6Unatakiwa kujenga dhabahu ya Yahwe Mungu wako kwa mawe yasiyokuwa na kazi; unatakiwa kutoa dhabihu ya kuteketeza juu yake kwa Yahwe Mungu wako,7na utatoa sadaka ya pamoja na utakula pale; utafurahia mbele ya Yahwe Mungu wako.8Utaandika juu ya mawe maneno yote ya sheria hii kwa wazi.”

9Musa na makuhani, Walawi, waliongea na Waisraeli wote na kusema, “Nyamazeni na sikilizeni Israel: Leo mmekuwa watu wa Yahwe Mungu wenu.10Mnapaswa basi kutii sauti ya Yahwe Mungu wenu na kutii amri na sheria zake ambazo ninawaamuru leo.”

11Musa aliwaamuru watu siku hiyo hiyo na kusema,12“Makabila haya yanapaswa kusimama katika mlima Gerizimu kuwabariki watu baada ya nyinyi kuvuka Yordani; Simeoni, Lawi, Judah, Isakari, Yusufu na Benyamini.13Haya ni makabila ambayo lazima yasimame juu ya mlima Ebali kutamka laana: Rubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dan na Naftali.

14Walawi watajibu na kusema kwa wanamume wote wa Israeli kwa sauti kubwa:
15‘Alaaniwe mwanamume atakayechonga sanamu au kinyago, chukizo kwa Yahwe, kazi ya mikono ya fundi, ambayo ataifanya sirini.’ Kisha watu wote wanapaswa kujibu na kusema, ‘Amina.’
16‘Alaaniwe mwanamume atakayemuaibisha baba yake au mama yake.’ Kisha watu wote waseme, ‘Amina.’
17‘Alaaniwe mwanamume anayetoa alama ya ardhi.’ Kisha watu wote na waseme, ‘Amina.’
18‘Alaaniwe mwanamume asababishae kipofu kutoka nje ya barabara.’ Kisha watu wote waseme, ‘Amina.’
19‘Alaaniwe mwanamume atumiaye nguvu kupokonya haki inayomstahili mgeni, yatima, au mjane.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
20‘Alaaniwe mwanamume atakayelala na mke wa baba yake, kwa sababu atakuwa amechukua haki za baba yake.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
21‘Alaaniwe mwanamume atakayelala na aina yoyote ya mnyama.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
22‘Alaaniwe mwanamume atakayelala na dada yake, binti wa baba yake, au binti wa mama yake.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
23‘Alaaniwe mwanamume atakayelala na mama mkwe.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
24‘Alaaniwe mwanamume atakayemuua jirani yake kwa siri.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
25‘Alaaniwe mwanamume apokeaye rushwa kumuua mtu asiye na hatia.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’
26‘Alaaniwe mwanamume asiyethibitisha maneno ya sheria hii, ili kwamba ayatii.’ Kisha watu wote lazima waseme, ‘Amina.’”

28

1Utakaposikiliza kwa makini sauti ya Yahwe Mungu wako ili kwamba ushikilie amri zake zote ambazo nakuamuru leo, Yahwe Mungu wako atakuweka juu ya mataifa yote ya ulimwengu.2Baraka hizi zote zitakuja kwako na kukupita, kama utasikiliza sauti ya Yahwe Mungu wako.3Utabarikiwa ndani ya mji, na utabarikiwa shambani.4Matunda ya mwili wako yatabarikiwa, na matunda ya ardhi yako, na matunda ya wanyama wako, ongezeko la ng'ombe wako, na wachanga wa mifugo wako.5Kitabarikiwa kikapu chako na chombo cha kukandia.6Utabarikiwa utakaporudi ndani, na utabarikiwa utakapotoka nje.7Yahwe atasababisha maadui zako wanaoinuka dhidi yako kupigwa chini mbele yako; watajitokeza dhidi yako kwa njia moja lakini watakimbia mbele zako kwa njia saba.8Yahwe ataamuru baraka kuja kwako katika maghala yako na katika kila unapoweka mkono wako; atakubariki katika nchi anayokupatia.

9Yahwe atawaimarisha kama watu waliotengwa kwa ajili yake, kama alivyoapa kwenu, iwapo mtashikilia amri za Yahwe Mungu wenu, na kutembea katika njia zake.

10Watu wote wa ulimwengu wataona ya kwamba mmeitwa kwa jina la Yahwe, nao watawaogopa.

11Yahwe atakufanya kuwa na mafanikio sana katika matunda ya mwili wako, katika matunda ya ng'ombe zako, katika matunda ya ardhi yako, katika nchi aliyoapa kwa mababu zako kuwapatia.

12Yahwe atafungua kwako ghala lake la mbingu kuruhusu mvua juu ya ardhi katika muda sahihi, na kubariki kazi zote za mikono yako; utakopesha kwa mataifa mengi, lakini wewe hautakopa.

13Yahwe atakufanya kuwa kichwa, na sio mkia; utakuwa juu tu, na hautakuwa chini, iwapo utaisikiliza amri za Yahwe Mungu wako ambazo ninakuamuru leo, ili kuzishikilia na kuzitenda,14na usipogeuka kinyume na maneno yoyote ninayokuamuru leo, kulia kwako wala kushoto kwako, na kufuata miungu mingine na kuwatumikia.

15Lakini usiposikiliza sauti ya Yahwe Mungu wako, na kushikilia amri zake zote na sheria zake ninazokuamuru leo, basi laana hizi zote zitakuja kwako kukupata.16Utalaaniwa utakapokuwa mjini, na utalaaniwa utakapokuwa shambani.17Kitalaaniwa kikapu chako na chombo chako cha kukandia.18Litalaaniwa tunda la mwili wako, tunda la ardhi yako, ongezeko la ng'ombe wako, na wachanga wa mifugo.19Utalaaniwa utakaporudi, na utalaaniwa utokapo.

20Yahwe atatuma laana juu yako, kuchanganyikiwa, na shutuma katika kila jambo uwekalo mikono yako, hadi utakapoangamizwa, na hadi utakapotoweka haraka kwa sababu ya matendo yako maovu ambayo utakuwa umenitelekeza mimi.21Yahwe atafanya pigo likung'ang'anie mpaka kukuangamiza kutoka katika nchi utakayoenda kumiliki.22Yahwe atakushambulia kwa magonjwa ya kuambukiza, kwa homa, kwa uvimbe, na kwa kiangazi na jua kali, na kwa upepo mkali na ukungu. Hivi vitakufukuza hadi uangamie.23Mbingu zilizo juu ya vichwa vyenu zitakuwa shaba, na ardhi chini yenu itakuwa chuma.24Yahwe atafanya mvua ya ardhi yako kuwa unga na vumbi, kutoka mbinguni vitashuka kwako, hadi utakapoangamizwa.25Yahwe atakusababishia upigwe mbele ya maadui zako; utawafuata kwa njia moja dhidi yao lakini utakimbia mbele zao kwa njia saba. Utapelekwa huku na kule miongoni mwa falme za nchi.26Mzoga wako utakuwa chakula kwa ndege wote wa angani na kwa wanyama wa ulimwengu; hakutakuwa na mtu wa kuwatisha.27Yahwe atawashambulia na majipu ya Misri na vidonda, kiseyeye na mwasho ambazo hautapona.28Yahwe atakushambulia kwa ukichaa, kwa upofu, pamoja na kuchanganyikiwa kwa akili.29Utapapasa papasa mchana kama kipofu apapasavyo usiku, na hautafanikiwa katika njia zako; daima utakandamizwa na kuporwa, na hakutakuwa na mtu wa kukuokoa.30Utamchumbia mwanamke, lakini mwanamume mwingine atamkamata na kumbaka. Utajenga nyumba lakini hautaishi ndani mwake; utapanda shamba la mizabibu lakini hautafurahia matunda yake.31Ng'ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, lakini hautakula nyama yake; punda wako atachukuliwa kwa nguvu mbele yako na hatarejeshwa kwako. Kondoo wako watapewa maadui zako, na hautakuwa na mtu wa kukusaidia.32Watoto wa kiume na mabinti zako watapewa kwa watu wengine; macho yako yatawatafuta siku nzima, lakini yatashindwa kwa shauku juu yao. Hakutakuwa na nguvu mikononi mwako.33Mavuno ya ardhi yako na ya kazi yako yote – taifa usilolijua litayatafuna; daima utaonewa na kugandamizwa,34ili upatwe na wazimu kwa yale utakayoona yakitendeka.35Yahwe atakushambulia kwenye magoti na miguu kwa majibu makali ambayo hutaweza kupona, kutoka chini ya miguu yako mpaka juu ya kichwa chako.36Yahwe atawachukua pamoja na mfalme ambaye mtakuwa mmemuweka juu yenu kwa taifa ambalo hamjalijua, wala nyie au mababu zenu; kule mtaabudu miungu mingine ya mbao na mawe.37Nawe utakuwa chanzo cha kitisho, mithali, na uvumi, miongoni mwa watu wote ambako Yahwe atakupeleka.38Utaweka mbegu nyingi shambani, lakini utakusanya mbegu chache, kwa maana nzige itaziangamiza.39Utapanda mashamba ya mizabibu na kuyapalilia, lakini hautakunywa divai yoyote, wala hautakusanya matunda yoyote, kwa maana funza watayala.40Utakuwa na miti ya mizeituni katika eneo lako, lakini hautajipaka mafuta yoyote juu yako, kwa maana mti wako wa mzeituni utaangusha matunda yake.41Utakuwa na wana wa kiume na mabinti, lakini hawatabaki kuwa wako, kwani watachukuliwa mateka.42Miti yako yote na matunda ya ardhi yako – nzige watajitwalia.43Mgeni aliye miongoni mwako atainuka juu zaidi yako juu na juu; wewe mwenyewe utashuka chini na chini.44Atakukopesha, lakini hautamkopesha; atakuwa kichwa, nawe utakuwa mkia.

45Laana hizi zote zitakujia juu yako na kukuandama na kukupata hadi utakapoangamizwa. Hii itatokea kwa sababu haukuisikia sauti ya Yahwe Mungu wako, ili kushikilia amri na maagizo yake aliyokuamuru.

46Laana hizi zitakuwa juu yako kama ishara na miujiza, na juu ya uzao wako milele.

47Kwa sababu hukumuabudu Yahwe Mungu wako kwa shangwe na furaha moyoni mwako ulipokuwa na mafanikio,48kwa hiyo utatumikia maadui ambao Yahwe atatuma dhidi yako; utawatumikia katika njaa, katika kiu, katika uchi, na katika umaskini. Ataweka mzigo wa chuma juu ya shingo yako hadi akuangamize.

49Yahwe ataleta taifa dhidi yako kutoka mbali, kutoka mwisho wa ulimwengu, kama tai arukaye kwa mhanga wake, taifa ambalo lugha yake hauelewi;50taifa lenye sura katili ambalo haliheshimu wazee na halionyeshi fadhila kwa wadogo.51Watakula wachanga wa ng'ombe wako na matunda ya ardhi yako hadi utakapoangamizwa. Hawatawaachia nafaka, divai mpya, au mafuta, wachanga wa ng'ombe au mifugo yako, hadi watakaposababisha kutoweka kwako.52Watawazingira katika malango ya miji yenu, hadi kuta zenu ndefu na imara zitakaposhuka chini ardhini, kuta ambazo mliziamini. Watawazingira ndani ya malango ya miji yenu kotekote katika nchi ambayo Yahwe Mungu wenu amewapatia.

53Utakula tunda la mwili wako mwenyewe, nyama ya watoto wa kiume na binti zako, ambao Yahwe Mungu wako aliwapatia, katika uvamizi na katika dhiki ambayo adui zako wataweka juu yako.54Mwanamume laini na mlegevu miongoni mwenu – atakuwa na wivu kwa kaka yake na kwa mkewe, na kwa watoto wowote waliosalia.55Kwa hiyo hatawapatia kati yao nyama ya watoto wake ambayo ataenda kuila, kwa sababu hatabakiwa na chochote katika uvamizi na dhiki ambayo adui yako ataiweka juu yako ndani ya malango yote ya mji wako.56Mwanamke laini na mlegevu miongoni mwenu, ambaye hatadiriki kuweka tako la mguu wake ardhini kwa sababu ya ulaini na maringo yake – atakuwa na wivu kwa mume kipenzi wake mwenyewe, kwa mtoto wake wa kiume, na kwa binti yake,57na kwa mtoto wake mchanga atakayetoka katikati ya miguu yake, na kwa watoto atakayewazaa. Atawala kwa siri kwa kukosa kitu kingine, katika uvamizi na dhiki ambayo adui yako ataweka juu yako ndani ya malango ya mji wako.

58Iwapo hautashika maneno yote ya sheria yaliyoandikwa katika kitabu hiki, ili kuheshimu jina hili tukufu na la kutisha, Yahwe Mungu wako,59basi Yahwe atafanya mapigo yako kuwa ya kutisha, na yale ya wazao wako; yatakuwa mapigo makuu, ya muda mrefu, na magonjwa makali, ya muda mrefu.60Ataleta juu yako mara nyingine magonjwa yote ya Misri ambayo ulikuwa unayaogopa; yatakung'ang'ania.61Pia kila gonjwa na pigo ambalo halijaandikwa katika kitabu cha sheria hii, hayo pia Yahwe atayaleta juu yako hadi utakapoangamizwa.62Utabaki wachache kwa idadi, ingawa ulikuwa kama nyota wa mbinguni kwa idadi, kwa sababu haukuisikiliza sauti ya Yawhe Mungu wako.63Kama vile hapo awali Yawhe alivyofurahia juu yako na kutenda mema, na kuwazidisha, basi atafurahia juu yako kwa kufanya upotee na kwa kukuangamiza. Utang'olewa katika nchi utakayoenda kuimiliki.

64Yahwe atakusambaza miongoni mwa watu wote kutoka mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine wa dunia; huko utaabudu miungu mingine ambayo hujawajua, wewe wala mababu zako, miungu ya mbao na jiwe.65Miongoni mwa mataifa haya hautapata utulivu, na hakutakuwa na pumziko chini ya miguu yako; badala yake, Yahwe atakupatia huko moyo wa kutetemeka, macho yanayofeli na nafsi inayoomboleza.66Maisha yako yataning’inia kwa mashaka mbele yako; utaogopa kila usiku na mchana na hutakuwa na uhakika kabisa maishani mwako.67Asubuhi utasema, “Natamani ingekuwa jioni!” na jioni utasema, “Natamani ingekuwa asubuhi!” kwa sababu ya hofu mioyoni mwenu na vitu ambavyo macho yako italazimu kuona.68Yahwe atakuleta Misri mara nyingine kwa meli, kwa njia ambayo nilikuambia, “Hutaiona Misri tena.” Kule utajitoa kuuzwa kwa maadui zako kama watumwa wa kiume na kike, lakini hakutakuwa na mtu wa kuwanunua.

29

1Haya ni maneno ambayo Yahwe alimuamuru Musa kuwaambia watu wa Israeli katika nchi ya Moabu, maneno ambayo yaliongezwa katika agano alilolifanya pamoja nao kule Horebu.

2Musa aliwaita Waisraeli wote na kuwaambia, “Mmeona kila kitu ambacho Yahwe alifanya mbele ya macho yenu katika nchi ya Misri kwa Farao, kwa watumishi wake wote, na kwa nchi yake yote –3mateso makubwa ambayo macho yenu yaliona, ishara, pamoja na ile miujiza mikubwa.4Lakini mpaka leo Yahwe hajawapatia moyo wa kufahamu, macho ya kuona, au masikio ya kusikia.5Nimewaongoza kwa miaka arobaini jangwani; mavazi yenu hayakuchakaa juu yenu, na ndala zenu hazikuchakaa miguuni mwenu.6Hamkula mkate wowote, na wala hamkunywa divai yoyote au kinywaji chochote chenye ulevi, ili kwamba muweze kujua kuwa mimi ni Yahwe Mungu wenu.

7Mlipokuja mahali hapa, Sihoni, mfalme wa Heshboni, na Ogu, mfalme wa Bashani, walikuja dhidi yetu kutupiga, na tukawapiga.8Tulichukua ardhi yao na kuwapa kama urithi Wareubeni, kwa Wagadi, na kwa nusu ya kabila ya Manase.

9Kwa hiyo shikilia maneno ya agano hili na kuyatenda, ili ufanikiwe katika kila kitu ufanyacho.10Nyie wote, mnasimama leo, mbele ya Yahwe Mungu wenu; machifu wenu, makabila yenu, wazee wenu, na maafisa wenu – wanaume wote wa Israeli,11watoto wenu, wake zenu, na wageni ambao wamo miongoni wa kambi yenu, kutoka kwa yule anayekata mbao zenu mpaka kwa yule atekaye maji.12Mpo hapa ili kwamba muingie katika agano la Yahwe Mungu wenu na katika kiapo ambacho Yahwe Mungu wako anafanya na wewe leo,13ili kwamba awafanye leo kuwa watu wake, na kwamba aweze kuwa Mungu kwa ajili yako, kama alivyonena kwako, na kama alivyoapa kwa mababu zako, kwa Abrahamu, kwa Isaka na kwa Yakobo.14Kwa maana ninafanya agano hili na kiapo hiki sio na wewe tu –15pamoja kila mtu aliyesimama hapa pamoja nasi leo mbele ya Yahwe Mungu wetu – bali na wale ambao hawapo pamoja nasi leo pia.

16Unajua jinsi tulivyoishi katika nchi ya Misri, na jinsi tulivyopenya miongoni mwa mataifa ambao uliwapita.17Mmeona sanamu zao zinazokera zilizotengenezwa kwa mbao na mawe, fedha na dhahabu, ambazo zilikuwa miongoni mwenu.18Hakikisha hakuna kati yenu mwanamume, mwanamke, ukoo, au kabila ambaye moyo wake unamuacha Yahwe Mungu wetu leo, ili kwenda na kuabudu miungu ya mataifa hayo. Hakikisha hakuna kati yenu mzizi utakaozaa nyongo na pakanga.

19Wakati mtu huyo anaposikia maneno ya laana hii, atajifariji moyoni mwake na kusema, ‘Nitakuwa na amani, ingawa natembea katika ukaidi wa moyo wangu.’ Hii itaangamiza ubichi pamoja na ukavu.20Yahwe hatamsamehe, lakini badala yake, hasira ya Yahwe na wivu wake utambanika mtu huyo, na laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki vitakuwa juu yake, na Yahwe ataliondoa jina lake kutoka mbinguni.21Yahwe atamuweka kando kwa ajili ya maafa kutoka katika makabila yote ya Israeli, kwa kuzingatia laana zote za agano ambazo zimeandikwa katika kitabu hiki cha sheria.

22Kizazi kifuatacho, watoto wako watakaoinuka baada yako, na mgeni atakayekuja kutoka nchi ya mbali, watazungumza watakapoona mapigo juu ya nchi hii na magonjwa ambayo Yahwe ameyafanya yawe –23na watakapoona kuwa nchi yote imekuwa salfa na chumvi ichomayo, ambapo hakuna kitu kipandwacho au kuzaa matunda, ambapo hapaoti mmea wowote, kama anguko la Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, ambayo Yahwe aliangamiza katika ghadhabu na hasira yake –24watasema kwa pamoja na mataifa mengine, ‘Kwa nini Yahwe amefanya hili katika nchi hii? Joto ya hasira hii kali inamaanisha nini?’

25Kisha watu watasema, ‘Ni kwa sababu walitelekeza agano la Yahwe, Mungu wa mababu zao, alilofanya nao alipowatoa kutoka Misri,26na kwa sababu waliondoka na kutumikia miungu mingine na kuzisujudu, miungu ambayo hawakujiua na ambayo hakuwapatia.27Kwa hiyo hasira ya Yahwe imewaka dhidi ya nchi hii, ili kuleta juu yake laana zote zilizoandikwa katika kitabu hiki.28Yahwe amewang'oa kutoka nchini kwao kwa hasira, kwa ghadhanu, na kwa ghadhabu kali, na kuwatupa katika nchi nyingine, leo.’

29Mambo ya siri ni ya Yahwe Mungu wetu pekee; lakini mambo yaliyofichuliwa ni ya kwetu milele pamoja na wazawa wetu, ili tufanye maneno yote ya sheria hii.

30

1Vitu hivi vitakavyokuja juu yako, baraka na laana nilizoziweka mbele yako, na utakapozirejea akilini miongoni mwa mataifa mengine ambapo Yahwe Mungu wako kawapeleka,2na utakapomrudia Yahwe Mungu wako na kutii sauti yake, na kufuata yote ambayo nayokuamuru leo – wewe na watoto wako – kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote,3kisha Yahwe Mungu wako atageuza kutekwa kwako na kukuhurumia; atawarudisha na kuwakusanya kutoka kwa watu wote ambapo Yahwe Mungu wako aliwatawanya.4Iwapo yeyote ya watu walio uhamishoni wapo katika sehemu za mbali sana chini ya mbingu, kutoka huko Yahwe Mungu wako atawakusanya, na kutoka huko atawarejesha.5Yahwe Mungu wako atawaleta katika nchi ambayo mababu zenu walimiliki, nanyi mtaimiliki tena; atawatendea mema na kuwazidisha zaidi ya alivyofanya kwa mababu zenu.6Yahwe Mungu wako atatahiri moyo wako na moyo wa uzao wako, ili umpende Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote, ili kwamba uweze kuishi.7Yahwe Mungu wako ataweka laana hizi zote kwa maadui zako na kwa wote wakuchukiayo, wale waliokutesa.8Utarudi na kutii sauti ya Yahwe, nawe utatenda amri zake zote ambazo ninakuamuru leo.9Yahwe Mungu wako atakufanikisha katika kazi yote ya mkono wako, katika matunda ya mwili wako, katika matunda ya mifugo yako, na katika matunda ya nchi yako, kwa mafanikio; kwa maana Yahwe atafurahia tena mafanikio yako, kama alivyofurahia kwa baba zako.10Atafanya hivi iwapo utatii sauti ya Yahwe Mungu wako, ili kuzishika amri zake na kanuni zake zilizoandikwa katika kitabu hiki cha sheria, iwapo utamgeukia Yahwe Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa nafsi yako yote.

11Kwa maana amri hii nayokuamuru leo sio ngumu sana, wala haipo nje ya uwezo wako kufikia.12Haipo mbinguni, ili usije ukasema, ‘Nani atayekwenda kwa ajili yetu mbinguni na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kutekeleza?’13Wala haipo ng'ambo ya bahari, ili usije ukasema, ‘Nani atakwenda ng'ambo ya pili ya bahari kwa ajili yetu na kutuletea kwetu na kutufanya tuisikie, ili tuweze kuifanya?’14Lakini neno lipo karibu sana kwako, katika kinywa chako na moyo wako, ili uweze kutekeleza.

15Tazama, leo nimeweka mbele yako uzima na wema, mauti na uovu.16Iwapo utatii maagizo ya Yahwe Mungu wako, ambayo ninakuamuru leo kumpenda Yahwe Mungu wako, kutembea katika njia zake, na kushikilia amri zake, kanuni zake, na sheria zake, utaishi na kuongezeka, na Yahwe Mungu wako atakubariki katika nchi ambayo unaingia kumiliki.

17Lakini moyo wako ukigeuka, na usisikilize na badala yake unavutwa na kusujudia miungu mingine na kuwaabudu,18basi leo nakutangazia kwako ya kwamba hakika utaangamia; siku zako hazitaongezeka katika nchi unayoipita juu ya Yordani kuingia na kumiliki.

19Naziita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yako ya kuwa nimeweka mbele yako uzima na mauti, baraka na laana; kwa hiyo chagua uzima ili kwamba uweze kuishi, wewe na uzao wako.20Fanya hivi ili umpende Yahwe Mungu wako, kutii sauti yake, na kung'ang'ania kwake. Kwa maana yeye ni uzima wako na urefu wa siku zako; fanya hivi ili kwamba uweze kuishi katika nchi ambayo Yahwe aliapa kwa mababu zako, kwa Abrahamu, kwa Isaka, na kwa Yakobo, kuwapatia.”

31

1Musa alikwenda na kuzungumza maneno haya kwa Israeli yote.2Alisema kwao, “Kwa sasa nina umri wa miaka 120; Siwezi kutoka na kuingia tena; Yahwe ameniambia, ‘Hautavuka Yordani hii.’3Yahwe Mungu wako, atakutangulia mbele yako; ataangamiza mataifa haya mbele yako, nawe utawanyanganya. Yoshua atakwenda kabla yako, kama Yahwe alivyonena.4Yahwe atawafanya kwao kama alivyofanya kwa Sihoni na kwa Ogu, wafalme wa Waamori, na kwa nchi yao, aliyoiangamiza.5Yahwe atakupatia ushindi juu yao utakapokutana nao vitani, nawe utafanya kwao yote nitakayokuamuru.6Uwe hodari na mwenye ujasiri mwema, usiogope, na usiwaogope; kwa maana Yahwe Mungu wako, ni yeye aendaye kabla yako; hatakuangusha wala kukuacha.”

7Musa akamwita Yoshua na akamwambia machoni pa Israeli yote, “Uwe hodari na mwenye ujasiri mwema, kwa kuwa utaondoka na hawa watu katika nchi ambayo Yahwe ameapa kwa mababu zao kuwapatia; utafanya wairithi.8Yahwe, yeye ndiye atakwenda kabla yako; atakuwa pamoja nawe; hatakuangusha wala hatakutelekeza; usiogope, usivunjike moyo.”

9Musa aliandika sheria hii na kuwapatia makuhani, wana wa Walawi, ambao walibeba sanduku la agano la Yahwe; pia aligawa nakala zake kwa wazee wote wa Israeli.10Musa aliwaamuru na kusema, “Katika kila mwisho wa miaka saba, kwa muda uliowekwa wa kudumu kwa ajili ya kufuta madeni, katika Sikukuu ya Vibanda,11ambapo Israeli yote imekuja kujitokeza mbele ya Yahwe Mungu wako katika mahali atakayochagua kuwa patakatifu pake, utasoma sheria hii mbele ya Israeli yote wakisikia.12Kusanya watu, wanaume, wanawake, na wadogo, na mgeni wako aliye miongoni mwa malango yako, ili waweze kusikia na kujifunza, na ili kwamba wamheshimu Yahwe Mungu wako na kushika maneno yote ya sheria hii.13Fanya hivi ili kwamba watoto wao, ambao hawajajua, waweze kusikia na kujifunza kumheshimu Yahwe Mungu wako, maadamu unaishi katika nchi ambayo utaenda juu ya Yordani kuimiliki.”

14Yahwe alimwambia Musa, “Tazama, siku inakuja ambayo lazima utakufa; muite Yoshua na mjidhihirishe katika hema la makutano, ili kwamba niweze kuwapatia amri.” Musa an Yoshua waliondoka na kujidhihirisha katika hema la makutano.

15Yahwe alijifunua kwenye hema kwa nguzo ya wingu; nguzo ya wingu ilisimama juu ya mlango wa hema.16Yahwe alimwambia Musa, “Tazama, utalala na baba zako; watu hawa watainuka na kujifanya kama kahaba na kwenda kwa miungu ya ajabu ambayo imo miongoni mwao katika nchi wanapokwenda. Wataniacha na kuvunja agano langu ambalo nimefanya nao.17Basi, katika siku hiyo, hasira yangu itawaka dhidi yao nami nitawaacha. Nitaficha uso wangu kutoka kwao, nao watamezwa. Maafa na taabu nyingi yatawakumba ili waseme katika siku hiyo, ‘Maafa haya hayajaja kwetu kwa sababu Mungu hayupo kati yetu?’18Hakika nitaficha uso wangu kutoka kwao katika siku hiyo kwa sababu ya uovu wote ambao watakuwa wametenda, kwa sababu wamegeukia miungu mingine.

19Basi sasa andika wimbo huu kwa ajili yenu na wafundishe watu wa Israeli. Uweke vinywani mwao, ili kwamba wimbo huu uweze kuwa shahidi kwangu dhidi ya watu wa Israeli.20Kwa maana nitakapowaleta katika nchi ambayo niliapa kwa mababu zao, nchi inayotiririka kwa maziwa na asali, na watakapokula na kuridhika na kunenepa, ndipo watageukia miungu mingine nao watawatumikia na kunidharau na watavunja agano langu.21Maovu na taabu nyingi zitakapokuja juu ya watu hawa, huu wimbo utashuhudia mbele yao (kwa maana hautasahaulika vinywani mwa uzao wao). Kwa maana najua mipango wanayotengeneza leo, hata kabla sijawaleta katika nchi niliyowaahidi.”22Kwa hiyo Musa aliandika huu wimbo siku hiyo hiyo na kuwafundisha watu wa Israeli.

23Yahwe alimpa Yoshua mwana wa Nuni amri na kusema, “Uwe hodari na mwenye ujasiri mwema; kwa maana utawaleta watu wa Israeli katika nchi niliyoapa kwao, nami nitakuwa pamoja nawe.”

24Ikatokea kwamba Musa alipomaliza kuandika maneno ya sheria hii katika kitabu,25aliwaamuru Walawi waliobeba sanduku la agano la Yahwe, na kusema,26“Chukua kitabu hiki cha sheria na kiweke pembeni mwa sanduku la agano la Yahwe Mungu wenu, ili kiweze kuwa pale kama ushahidi dhidi yenu.27Maana nafahamu uasi wenu na shingo zenu ngumu; tazama, maadamu nipo hai pamoja nanyi hata leo, mmekuwa waasi dhidi ya Yahwe; itakuaje baada ya mimi kufa?28Nikusanyieni wazee wote wa makabila yenu, na maafisa wenu, ili nizungumze maneno haya masikioni mwao na kuziita mbingu na nchi kushuhudia dhidi yao.29Kwa maana najua baada ya kifo changu mtajiharibu kabisa na kugeuka kuiacha njia niliyowaamuru; maafa yatawakumba katika siku zijazo. Haya yatatokea kwa sababu mtafanya yaliyo maovu machoni pa Yahwe, ili kumchokoza katika hasira kwa mikono ya kazi yenu.”

30Musa alinena masikioni mwa kusanyiko lote la Israeli maneno yote ya wimbo huu hadi yalipokamilika.

32

1Tega sikio, enyi mbingu, na niruhusu kuzungumza.

2Acha dunia isikie maneno ya kinywa changu. Acha mafundisho yangu yamwagike chini kama mvua, acha usemi wangu udondoke kama umande, kama mvua tulivu juu ya majani laini, na kama mvua za manyunyu juu ya mimea.
3Kwa maana nitatangaza jina la Yahwe, na kumpatia ukuu Mungu wetu.
4Mwamba, kazi yake ni kamili; kwa maana njia zake ni za haki. Yeye ni Mungu mwaminifu, hana udhalimu. Yeye ni wa haki na mwadilifu.
5Wamefanya yaliyo maovu dhidi yake. Wao sio watoto wake. Ni aibu kwao. Wao ni kizazi kiovu na kilichopindika.
6Je! Unamzawadia Yahwe kwa njia hii, enyi watu wapumbavu na msiojitambua? Je! Yeye si baba yenu, yule ambaye aliwaumba? Aliwaumba na kuwaimarisha.
7Kumbukeni siku zile za zamani, tafakari juu ya miaka mingi ya nyuma. Muulize baba yako naye atakuonyesha, wazee wako nao watakuambia.
8Pale ambapo Aliye Juu alipowapatia mataifa urithi wao – alipowagawa wanadamu wote, na kuweka mipaka ya watu, na alipoimarisha idadi ya miungu yao.
9Kwa maana fungu la Yahwe ni watu wake; Yakobo ni mgao wa urithi wake.
10Alimpata katika nchi ya jangwa, na katika jangwa kame na livumalo upepo; alimkinga na kumtunza, alimlinda kama mboni ya jicho lake.
11Kama tai akichungaye kiota chake na kupiga piga mabawa juu ya makinda yake, Yahwe alitandaza mabawa yake na kuwachukua, na kuwabeba kwenye mapapatio yake.
12Yahwe pekee alimuongoza, hapakuwa na mungu mgeni pamoja naye.
13Alimfanya aendeshe katika maeneo ya juu ya nchi, na alimlisha matunda ya mbugani; alimrutubisha kwa asali kutoka kwenye jiwe, na mafuta kutoka kwenye mwamba mgumu sana.
14Alikula siagi kutoka katika kundi na kunywa maziwa kutoka katika kundi la mifugo, pamoja na mafuta ya wanakondoo, kondoo dume wa Bashani na mbuzi, pamoja na ngano safi kabisa – nawe ulikunywa divai itokayo povu iliyotengenezwa kwa juisi ya mizabibu.
15Lakini Yeshuruni akakua kwa unene na kupiga mateke – ulikua kwa unene, ulikua mnene sana, na ulikuwa umekula ujazo wako – alimuacha Mungu aliyemuumba, na kukataa Mwamba wa wokovu wake.
16Walimfanya Yahwe apatwe wivu kwa miungu yao ya ajabu; kwa maudhi yao walimkasirisha.
17Walitoa dhabihu kwa mapepo, ambayo sio Mungu – miungu ambayo hawajaijua, miungu ambayo imejitokeza hivi karibuni, miungu ambayo mababu zenu hawakuogopa.
18Umetelekeza Mwamba, ambao ulikuwa baba yako, na ukasahau Mungu aliyekuzaa.
19Yahwe aliliona hili na kuwakataa, kwa sababu watoto wake wa kiume na mabinti zake walimchokoza.
20“Nitaficha uso wangu kwao”, alisema, “Nami nitaona mwisho wao utakuaje; maana wao ni kizazi kaidi, watoto ambao sio waaminifu.
21Wamenifanya kuwa na wivu kwa kile ambacho sio mungu na kunikasirisha kwa mambo yao yasiyo na maana. Nitawafanya waone wivu kwa wale ambao sio taifa; nitawakasirisha kwa taifa pumbavu.
22Kwa maana moto kuwashwa kwa hasira yangu na inawaka hadi chini mwa Sheoli; inameza ulimwengu na mavuno yake; inawasha moto misingi ya milima.
23Nitarundia maafa juu yao; nitafyatua mishale yangu yote kwao;
24Watapotea kwa njaa na kumezwa kwa joto liwakalo na uharibifu mchungu; nitatuma kwao meno ya wanyama wa mwituni, pamoja na sumu ya vitu vitambaao mavumbini.
25Nje, panga litawatwaa, na ndani ya vyumba hofu kuu itafanya hivyo. Wote mwanamume kijana na bikra nitawaangamiza, mchanga anyonyaye, na mwanaume mwenye mvi.
26Nilisema nitawasambaza mbali, kwamba nitafanya kumbukumbu yao kukoma miongoni mwa wanadamu.
27Isingekuwa kwamba naogopa uchokozi wa adui, na kwamba adui zake wangehukumu kimakosa, na kwamba wangesema, ‘Mkono wetu umeinuliwa,’ ningefanya haya yote.
28Kwa maana Israeli ni taifa linalopungukiwa na hekima, na hakuna ufahamu ndani mwao.
29Ah laiti wangekuwa na hekima, wangeelewa hili, na kuzingatia ujio wa hatima yao!
30Inawezekanaje mmoja kufukuza maelfu, na wawili kuweka makumi elfu mbioni, isipokuwa Mwamba wao hajawauza, na Yahwe hajawaachilia kwao?
31Kwa maana mwamba wa maadui zetu si kama Mwamba wetu, kama vile maadui zetu wanavyokiri.
32Kwa maana mzabibu wao unatoka kwenye mzabibu wa Sodoma, na kwenye mashamba ya Gomorra; na zabibu zake ni zabibu za sumu; vishada vyao ni vichungu.
33Mvinyo yao ni sumu ya nyoka na sumu katili ya nyoka.
34Huu mpango haujafichwa kwangu kwa siri, na kufungwa kabisa katika hazina zangu?
35Kisasi ni changu kutoa, na fidia, katika muda mguu wao utakapotereza; kwa maana siku ya maafa kwao ipo karibu, na vitu vitakavyokuja juu yao vitaharakisha kutendeka.”
36Kwa maana Yahwe atatoa haki kwa watu wake, na atawahurumia watumishi wake. Atahakikisha kuwa nguvu yao imetoweka, na hakuna atakayesalia, iwe watumwa au watu huru.
37Kisha atasema, “Wako wapi miungu yao, mwamba ambao wamekimbilia? –
38Miungu iliyokula sadaka zao nene na kunywa mvinyo wa sadaka zao za kinywaji? Na wainuke na kukusaidia; na wawe ulinzi kwako.
39Tazama sasa mimi, hata mimi, ni Mungu, na kwamba hakuna mungu tofauti yangu; ninaua, na ninaleta uhai; ninajeruhi, na ninaponya, na hakuna mtu atakayekuokoa kutoka kwa uwezo wangu.
40Kwa maana ninainua mikono yangu mbinguni na kusema, ‘Niishivyo milele, nitatenda.
41Nitakapong'oa panga langu lingaaro, na mkono wangu utakapoanza kuleta haki, nitalipiza kisasi juu ya maadui zangu, na kuwalipa wale wote wanichukiao.
42Nitafanya mishale yangu kulewa na damu, na panga langu litameza nyama kwa damu ya waliouawa na mateka, na kutoka kwa vichwa vya viongozi wa adui.’”
43Furahi, enyi mataifa, na watu wa Mungu, kwa maana atalipiza kisasi damu ya watumishi wake; atalipiza kisasi juu ya maadui zake, naye atafanya upatanisho kwa ajili ya nchi yake, kwa watu wake.

44Musa alikuja na kunena maneno yote ya wimbo huu masikioni mwa watu, yeye na Yoshua mwana wa Nuni.45Kisha Musa alimaliza kunena maneno haya yote kwa Israeli yote.46Aliwaambia, “Imarisheni akili yenu kwa haya maneno ambayo nimewashuhudia kwenu leo, ili kwamba muwaamuru watoto wenu kuyashika, maneno yote ya sheria hii.47Kwa maana hili si jambo dogo kwako, kwa sababu ni uzima wako, na kupitia jambo hili utarefusha siku zako katika nchi ambayo unakwenda juu ya Yordani kumiliki.”

48Yahwe alizungumza na Musa katika siku hiyo hiyo na kusema,49“Nenda katika usawa huu wa milima wa Abarimu, juu ya mlima wa Nebo, ambao upo katika nchi ya Moabu, mkabala na Yeriko. Utatazama nchi ya Kanani, ambayo ninawapatia watu wa Israeli kama miliki yao.50Utakufa katika mlima utakaopanda, na utakusanywa kwa watu wako, kama Haruni Muisraeli mwenzako alivyokufa juu ya mlima wa Hori na kukusanywa kwa watu wake. Hii51itatendeka kwa sababu haukuwa mwaminifu kwangu miongoni mwa watu wa Israeli katika maji ya Meriba kule Kadeshi, katika jangwa la Zini; kwa sababu haukunitendea utukufu na heshima miongoni mwa watu wa Israeli.52Kwa maana utaona nchi mbele yako, lakini hautakwenda kule, katika nchi ninayowapatia watu wa Israeli.”

33

1Hii ni baraka ambayo Musa mtu wa Mungu aliwabariki watu wa Israeli kabla ya kifo chake.2Alisema: Yahwe alikuja kutoka Sinai na akainuka kutoka Seiri juu yao. Aling'ara kutoka mlima wa Paramu, na akaja na elfu kumi ya watakatifu. Katika mkono wake wa kuume radi zilimulika.

3Kweli, anawapenda watu; watakatifu wake wote wapo mikononi mwako, na walimsujudu mguuni mwake; walipokea maneno yako.
4Musa alituamuru sheria, urithi kwa kusanyiko la Yakobo.
5Kisha pakawa na mfalme Yeshurumu, pale ambapo wakuu wa watu walipokusanyika, makabila yote ya Israeli pamoja.

6“Acha Rubeni aishi na asife, lakini wanaume wake wawe wachache.”

7Hii ni baraka ya Yuda. Musa akasema: “Sikiliza sauti ya Yuda, Yahwe, na umlete kwa watu wake tena. Mpiganie; kuwa msaada dhidi ya maadui wake.”

8Kuhusu Lawi, Musa akasema: “Thumimu yako na Urimu yako ni ya mtakatifu wako, yule uliyemjaribu kule Masa, ambaye ulishindana naye katika maji ya Meriba.
9Mtu aliyesema juu ya baba na mama yake, ‘Sijawaona.’ Wala hakuwatambua kaka zake, wala hakuzingatia juu ya watoto wake wenyewe. Kwa maana alilinda neno lako na kushika agano lako.
10Anafundisha Yakobo maagizo yako na Israeli sheria yako. Ataweka ubani mbele yako na sadaka kamili ya kuteketezwa juu ya dhabahu lako.
11Bariki mali zake, Yahwe, na kubali kazi ya mikono yake. Vunja viuno vya wale wanaoinuka dhidi yake, na wale watu wanaomchukia, ili wasiinuke tena.”

12Kuhusu Benyamini, Musa akasema: “Yule anayependwa na Yahwe anaishi kwa usalama kando yake; Yahwe anamkinga siku nzima, naye huishi katikati ya mikono ya Yahwe.”

13Kuhusu Yusufu, Musa akasema: “Nchi yake na ibarikiwe na Yahwe na vitu vya thamani vya mbinguni, na umande, na kina kilalacho chini.
14Nchi yake na ibarikiwe na vitu vya thamani mavuno ya jua, na vitu vya thamani mazao ya miezi,
15kwa vitu vizuri vya milima ya zamani, na kwa vitu vya thamani vya milima ya milele.
16Nchi yake ibarikiwe na vitu vya thamani vya ardhi na wingi wake, na kwa mapenzi mema ya yule aliyekuwa kichakani. Baraka na ifike juu ya kichwa cha Yusufu, na juu ya kichwa cha yule aliyekuwa mwana wa mfalme kwa kaka zake.
17Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, katika utukufu wake, na pembe zake ni pembe za ng'ombe mwitu. Kwa hawa atawasukuma watu, wote, hadi mwisho wa ulimwengu. Hawa ni maelfu makumi ya Efraimu; hawa ni maelfu wa Manase.”

18Kuhusu Zabuloni, Musa alisema: “Furahi, Zabuloni, katika kutoka kwako, na wewe, Isakari, katika hema zako.
19Watawaita watu hadi milimani. Huko watatoa sadaka za utakatifu. Maana watanyonya wingi wa bahari, na mchanga wa ufukweni.”

20Kuhusu Gadi, Musa alisema: “Abarikiwe yule amkuzaye Gadi. Ataishi pale kama simba jike, naye atanyakua mkono au kichwa.
21Alitoa sehemu nzuri kwake mwenyewe, maana kulikuwa na fungu la ardhi la kiongozi lililohifadhiwa. Alikuja na vichwa vya watu. Alitekeleza haki ya Yahwe na maagizo yake pamoja na Israeli.”

22Kuhusu Dani, Musa alisema: “Dani ni mwana wa simba arukaye kutoka Bashani.”

23Kuhusu Naftali, Musa alisema: “Naftali, aliyeridhika na fadhila, na kujaa kwa baraka za Yahwe, miliki nchi iliyopo magharibi na kusini.”

24Kuhusu Asheri, Musa alisema: “Abarakiwe Asheri Zaidi ya watoto wengine wa kiume; naye akubalike kwa kaka zake, na achovye mguu wake ndani ya mafuta ya zeituni.
25Vyuma vya mji wako na viwe chuma na shaba; kama vile siku zako zitakavyokuwa, ndivyo usalama wako utakavyokuwa.
26Hakuna aliye kama Mungu, Yeshurumu – aliyekamili, anayeendesha katika mbingu kukusaidia, na katika utukufu wake juu ya mawingu.
27Mungu wa milele ni kimbilio, na chini yake kuna mikono ya milele. Husukuma adui mbele yako, naye alisema, ‘Angamiza!’
28Israeli waliishi katika usalama. Wana wa Yakobo walikuwa salama katika nchi ya nafaka na divai mpya; hakika, mbingu na idondoshe umande juu yake.
29Baraka zako ni nyingi, Israeli! Nani kama wewe, watu waliokombolewa na Yahwe, ngao ya msaada wako, na upanga wa utukufu wako? Maadui zako watakuja kwako kwa kutetemeka; utakanyanga sehemu zao zilizoinuka.”

34

1Musa aliondoka kutoka nyanda za Moabu mpaka mlima wa Nebo, hadi kilele cha Pisga, kilicho mkabala na Yericho. Huko Yahwe alimwonyesha nchi yote ya Gileadi kutoka umbali wa Dani,2na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda, mpaka bahari ya magharibi,3na Negevi, na uwanda wa bonde la Yericho, mji wa mitende, mpaka umbali wa Soari.4Yahwe alimwambia, “Hii ni nchi niliyoapa kwa Abrahamu, kwa Isaka, na kwa Yakobo, na kusema, ‘Nitawapatia uzao wako.’ Nimekuruhusu uitazame kwa macho yako, lakini hautakwenda kule.”

5Basi Musa mtumishi wa Yahwe, alikufa pale katika nchi ya Moabu, kama neno la Yahwe lilivyoahidi.6Yahwe alimzika katika bonde katika nchi ya Moabu mkabala na Beth-peori, lakini hakuna ajuaye kaburi lake lilipo hadi leo hii.7Musa alikuwa na umri wa miaka mia moja na ishirini alipokufa; macho yake hayakufifia, wala nguvu asili zake hazikupungua.8Watu wa Israeli walimuomboleza Musa katika nyanda za Moabu kwa siku thelathini, hapo ndipo siku za maombolezo ya Musa zilipotimia.

9Yoshua mwana wa Nuni alikuwa amejawa na roho ya hekima, kwa maana Musa alimwekea mkono juu yake. Watu wa Israeli walimsikiliza na kufanya yale ambayo Yahwe alimuamuru Musa.

10Tangu hapo hakujatokea nabii katika Israeli kama Musa, ambaye Yahwe alimjua uso kwa uso.11Hakujawahi kuwa na nabii yeyote kama yeye kwa ishara na miujiza ambayo Yahwe alimtuma kufanya katika nchi ya Misri, kwa Farao, na kwa watumishi wake, na kwa nchi yake yote.12Hakujawahi kuwa na nabii yeyote kama yeye kwa mambo yote makubwa, ya kutisha ambayo Musa aliyafanya machoni pa Israeli yote.

Yoshua

1

1Ikawa baada ya kifo cha Musa, mtumishi wa Yahweh, Yahweh alimwambia Yoshua, mwana wa Nuni, msaidizi mkuu wa Musa, kusema,2“Musa, mtumishi wangu amekufa. Sasa basi inuka, vuka mto huu wa Yordani, wewe na watu hawa wote, kuingia katika nchi ambayo ninawapa - watu waisraeli.3Nimewapa ninyi kila sehemu ambapo nyayo za miguu yenu itakanyaga. Nimewapa ninyi, kama nilivyomwahidi Musa.4Kuanzia jangwani la Lebanoni, hadi mto mkubwa wa Frati, nchi yote ya Wahiti, na hata Bahari kuu, ambako jua huzama, itakuwa nchi yenu.5Hakuna mtu au yeyote atakayeweza kusimama kinyume chako siku zote za maisha yako. Nitakuwa pamoja nawe kama nilivyokuwa na Musa. Sitakupungukia wala kukuacha.

6Uwe hodari na jasiri. Wewe utawafanya watu hawa wairithi nchi ambayo niliwaahidi baba zao kuwa ningewapa.7Uwe hodari na jasiri sana. Uwe makini kutii sheria zote ambazo Musa mtumishi wangu alikuagiza. Usikengeuke upande wa kulia au wa kushoto, ili uweze kufanikiwa kila mahali utakapoenda.8Siku zote uongee juu ya kitabu hiki cha sheria. Utakitafakari mchana na usiku ili kwamba uweze kutii yote yaliyoandikwa humo. Kisha utastawi na kufanikiwa.9Je si mimi niliyekuagiza? Uwe hodari na jasiri! Usiogope. Usivunjike moyo. Yahweh Mungu wako yuko pamoja nawe kila uendeko.

10Kisha Yoshua akawaagiza viongozi wa watu,11“Nendeni katika kambi na waagizeni watu, ‘Andaeni chakula kwa ajili yenu. Baada ya siku tatu mtavuka mto huu wa Yordani na kuingia ndani na kuimiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi ili kuimiliki.”

12Yoshua akawaambia Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase,13“Kumbukeni maneno ambayo Musa, mtumishi wa Yahweh, aliwaaagiza aliposema, ‘Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi pumziko, naye awapeni ninyi nchi hii.’14Wake zenu, na watoto wenu na mifugo yenu itakaa katika nchi ambayo Musa aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani. Lakini watu wenu wa vita wataenda pamoja na ndugu zao na kuwasaidia.15Mpaka hapo Yahweh atakapowapa ndugu zenu pumziko kama alivyowapa ninyi. Na wao pia watamiliki nchi ambayo Yahweh Mungu wenu awapeni ninyi. Kisha mtarudi katika nchi yenu na kuimiliki, nchi ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa ninyi ng'ambo ya Yordani, mahali pa mapambazuko ya jua.”

16Nao wakamjibu Yoshua, na kusema, “Mambo yote uliyotuagiza tutayafanya, na kila mahali utakapotutuma tutaenda.17Tutakutii kama tulivyomtii Musa. Yahweh Mungu wako na awe pamoja nawe tu kama aliyokuwa pamoja na Musa.18Yeyote anayeasi maagizo yako na kutotii maneno yako atauawa. Uwe hodari na jasiri tu.

2

1Kisha Yoshua mwana wa Nuni aliwatuma watu wawili kwa siri kama wapelelezi kutoka Shitimu. Akisema, “Nendeni mkaiangalie nchi, hasa Yeriko.” Walienda na wakafika katika nyumba ya kahaba ambaye jina lake ni Rahabu, na wakalala hapo.2Mfalme wa Yeriko aliambiwa, “Tazama watu wa Israeli wamekuja kuipeleleza nchi.”3Mfalme akatuma neno kwa Rahabu kusema, “Watoe watu waliokuja kwako ambao wameingia nyumbani mwako, kwa kuwa wamekuja kuipeleleza nchi yote.”4Lakini mwanamke alikuwa amekwisha kuwachukua wale watu wawili na kuwaficha. Na akasema, “Ndiyo, watu walikuja kwangu, lakini sikujua walikotoka.5Ilipokuwa jioni wakati wa kufungwa kwa lango la mji, waliondoka. Sijui mahali walikoelekea. Mnaweza kuwakamata kama mtawafuata upesi.6Lakini yeye aliwapandisha juu darini na kuwaficha kwa mabua ya kitani ambayo alikuwa ameyalaza darini.7Hivyo, watu waliwafuatilia njiani iliyoelekea katika vivuko vya Yordani. Na milango ilifungwa mara tu baada ya wale watu waliofuata kutoka nje.

8Wale wanaume walikuwa hawajalala usiku, wakati alipowaendea kule darini.9Akawaambia, “Ninajua kwamba Yahweh amewapa ninyi nchi na kwamba hofu juu yenu imetuingia. Watu wote wanaoishi katika nchi watayeyuka mbele yenu.10Tumesikia jinsi ambavyo Yahweh alivyokausha maji ya Bahari ya Mianzi kwa ajili yenu wakati mkitoka Misri. Na tumesikia mlichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori walioko upande mwingine wa Yordani - Sihoni na Ogu - ambao mmewaangamiza kabisa.11Mara tu tuliposikia, mioyo yetu iliyeyuka na hapakuwa na ujasiri wowote uliosalia kwa mtu yeyote - kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ni Mungu aliye juu mbinguni na chini duniani.12Sasa basi, tafadhali mniapie kwa Yahweh kwamba kama nilivyokuwa mwema kwenu, nanyi pia mtaitendea mema nyumba ya baba yangu. Nipeeni ishara ya uhakika13kwamba mtanihifadhi maisha ya baba, mama, kaka, dada zangu na familia zao, na kwamba mtatuokoa kutoka katika kifo.14Wanaume wakamjibu, “maisha yetu kwa ajili ya yenu, hata kifo! Kama hamtasema habari zetu, na Yahweh akisha kutupa nchi hii, tutakuwa wenye huruma na waaminifu kwenu.”15Hivyo aliwashusha chini kwa kupitia dirishani kwa kutumia kamba. Nyumba ambayo alikuwa anaishi ilijengwa katika ukuta wa mji.16Akawaambia, “Nendeni milimani la sivyo watu waliowafuata watawaona. Jificheni huko kwa siku tatu mpaka watu waliowafuata watakaporudi. Kisha nendeni zenu.”17Wanaume wakamwambia, “Hatutakuwa tumefungwa na ahadi ulizotufanya tuape mbele zako, kama hautalifanya hili.18Tutakapokuja katika nchi, ni lazima uifunge kamba hii nyekundu katika dirisha ulilotushushia chini, na utawakusanya katika nyumba baba yako, mama yako, kaka zako na wote wa nyumba ya baba yako.19Na yeyote aendaye mtaani nje ya milango ya nyumba yako, damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao na hatutakuwa na hatia yoyote. Lakini kama mkono utanyoshwa juu ya mtu yeyote aliye pamoja nawe katika nyumba, damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu.20Na ikiwa utaongea juu ya suala letu, tutakuwa huru dhidi ya kiapo ulichotuapisha.21Rahabu akawajibu, “Yote mliyosema na yatimie.” Akawatoa mbali na wakaondoka. Kisha akaifunga kamba nyekundu katika dirisha.22Wakaondoka na kwenda juu milimani na walikaa huko kwa siku tatu hadi pale wale waliowafuata waliporudi. Wale waliowafuata walitafuta njiani pote bila kuwaona.23Wale watu wawili walirudi na kuvuka mto na wakafika kwa Yoshua mwana wa Nuni, na walimwambia kila kitu kilichotokea kwao.24Nao wakasema kwa Joshua, “kwa kweli Yahweh ametupa nchi hii. Wenyeji wote wa nchi wanayeyuka kwasababu yetu.

3

1Yoshua aliamka asubuhi na mapema, nao walisafiri kutoka Shitimu. Walifika Yordani, yeye na watu wote wa Israeli, na wakapiga kambi hapo kabla hawajavuka ng'ambo.2Baada ya siku tatu, maafisa walienda katika kambi, wakawaagiza watu,3“Mtakapoona sanduku la agano la Yahweh Mungu wenu, na makuhani kutoka miongoni mwa Walawi wamelibeba, ni lazima muondoke sehemu hii na kulifuata.4Lazima kuwe na umbali wa dhiraa elfu moja kati yenu na sanduku. Msilisogelee karibu, ili muweze kuiona njia ya kupitia, kwakuwa hamjawahi kupita njia hii kabla.

5Yoshua akawaambia watu, “Jitakaseni ninyi wenyewe keso, kwa kuwa Yahweh atafanya maajabu miongoni mwenu.”

6Kisha Yoshua akawaambia makuhani, “Chukueni sanduku la agano, na kulipitisha mbele za watu.” Hivyo, wakalichukua sanduku la agano na wakaenda mbele za watu.

7Yahweh akamwambia Yoshua, “Siku hii nitakufanya kuwa mtu mkubwa katika macho ya Waisraeli wote. Watajua kuwa kama nilivyokuwa na Musa ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe.8Utawaamuru makuhani ambao hulibeba sanduku la agano, ‘Mtakapofika katika ukingo wa maji ya Yordani, ni lazima msimame katika Mto Yordani.’9Kisha Yoshua akawaambia watu wa Israeli, “Njooni hapa na msikilize maneno ya Yahweh Mungu wenu.10Kwa hili mtajua kwamba Mungu aliye hai yuko miongoni mwenu na kwamba atawaondosha mbele yenu Wakanaani, Wahiti, Wahivi, Waperizi, Wagrigashi, Waamori na Wayebusi.11Tazama! Sanduku la agano la Bwana wa nchi yote litavuka mbele yenu katika Yordani.12Sasa chagueni wanaume kumi na wawili kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja katika kila kabila.13Wakati nyayo za miguu ya makuhani walichukualo sanduku la Yahweh, Bwana wa nchi yote, zitakapogusa maji ya Yordani, maji ya Yordani yatatindika, na hata maji yatiririkayo kutoka juu yatakoma kutiririka nayo yatasimama kama chuguu.

14Hivyo wakati watu walipotoka ili kuvuka Yordani, makuhani waliobeba sanduku la agano waende mbele ya watu.15Mara tu wale walichukuao sanduku wakiisha kufika Yordani, na miguu ya watu wale waliobeba sanduku itakapotiwa katika ukingo wa maji (maana sasa Yordani hujaa hadi katika kingo zake zote katika kipindi chote cha mavuno),16Maji yote yaliyotiririka kutoka juu yalisimama katika chuguu kimoja. Maji yakakoma kutiririka kutoka katika umbali mrefu. Maji yaliacha kutiririka kutoka Adam, mji ulio karibu na Zarethani, hadi bahari ya Negevu, Bahari ya Chumvi. Na watu walivuka ng'ambo karibu na Yeriko.17Makuhani waliolibeba sanduku la agano la Yahweh walisimama katika nchi kavu katikati ya Yordani mpaka watu wote wa Israeli walipokwisha kuvuka katika nchi kavu.

4

1Watu wote walipokwisha kuvuka Yordani, Yahweh akamwambia Yoshua,2“Chagueni wenyewe watu waume kumi na wawili, mmoja katika kila kabila.3Wape agizo hilo: ‘Chukueni mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani mahali wanaposimama makuhani katika nchi kavu, na wayalete na kuyaweka chini katika sehemu ambapo mtalala usiku wa leo.

4Kisha Yoshua akawaita wanaume kumi na wawili ambao aliwachagua kutoka katika makabila ya Israeli, mmoja kutoka kila kabila.5Yoshua akawaambia, “Nendeni mbele za sanduku la Yahweh Mungu wenu katikati ya Yordani. Kila mmoja wenu achukue jiwe moja mabegani mwake, kulingana na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli.6Hii itakuwa ni ishara miongoni mwenu kwa ajili yenu wakati watoto wenu watakapowauliza katika siku zijazo, ‘Nini maana ya mawe haya kwenu?’7Ndipo mtakapowaambia, ‘Maji ya Yordani yalitengwa mbele ya sanduku la Yahweh. Lililpopitishwa katika Yordani, maji ya Yordani yalisimamishwa. Hivyo, mawe haya yatakuwa kumbukumbu kwa watu wa Israeli milele.’”

8Watu waisraeli walifanya kama Yoshua alivyowaagiza, na walichukua mawe kumi na mbili kutoka katikati ya Yordani, kama Yahweh alivyomwambia Yoshua, walipangwa sawa sawa na hesabu ya makabila ya watu wa Israeli. Waliyachukua mawe mpaka mahali walipolala na wakayaweka chini huko.9Kisha Yoshua akayapanga mawe kumi na mbili katikati ya Yordani, katika sehemu ambapo ilisimama miguu ya makuhani waliolichukua sanduku la agano. Na kumbukumbu hiyo ipo hadi leo.

10Makuhani waliolichukua sanduku walisimama katikati ya Yordani mpaka pale kila kitu ambacho Yahweh alimwamuru Yoshua kuwaambia watu kilipokamilika, sawa sawa na yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua. Watu walifanya haraka na wakavuka.11Wakati watu wote walipokwisha kuvuka, sanduku la Yahweh pamoja na makuhani walivuka mbele za watu.12Kabila la Rubeni, kabila la Gadi, na nusu ya kabila la Manase walipita kama jeshi mbele ya watu wa Israeli, kama ambavyo Musa alivyowaambia.13Yapata watu elfu arobaini walioandaliwa kwa vita walipita mbele za Yahweh, kwa ajili ya vita katika uwanda wa Yeriko.14Katika siku hiyo Yahweh alimfanya Yoshua kuwa mkuu katika macho ya watu wote wa Israeli. Walimheshimu - kama walivyomheshimu Musa - siku zake zote.15Kisha Yahweh akamwambia Yoshua,16“Waamuru makuhani wanaolibeba sanduku la ushuhuda watoke katika Yordani.”17Hivyo Yoshua akawaamuru makuhani, “pandeni mtoke Yordani.”18Wakati makuhani wenye kulibeba sanduku la agano la Yahweh walitoka katikati ya Yordani, na nyayo za miguu yao ilikuwa imeinuliwa katika nchi kavu, kisha maji ya Yordani yalirudi katika sehemu zake na kujaa hadi katika kingo zake kama ilivyokuwa siku nne zilizopita.

19Katika siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, watu walikwea kutoka Yordani. Wakakaa huko Gilgali, mashariki mwa Yeriko.20Mawe kumi na mawili ambayo yalichukuliwa katika Yordani, Yoshua aliyasimamisha hapo Gilgali.21Aliwaambia watu wa Israeli, “Wakati watoto wenu watakapowauliza baba zao katika wakati ujao, ‘Mawe haya ni ya nini?’22Waambieni watoto wenu, ‘Hapa ndipo Waisraeli walivuka Yordani katika nchi kavu.23Yahweh Mungu wenu aliyakausha maji ya Yordani, mpaka hapo Yahweh Mungu wako aliyoyafanya katika bahari ya mianzi, ambayo aliikausha kwa ajili yetu ili tupite juu yake,24Ili kwamba watu wote wa nchi wajue kwamba mkono wa Yahweh ni wa nguvu, na kwamba mtamweshimu Yahweh Mungu wenu milele.”

5

1Mara tu waliposikia wafalme wa Waamori walio upande wa magharibi wa Yordani, na wafalme wote wa Wakanaani waliokuwa katika pwani ya Ziwa kuu, waliposikia ya kwamba Yahweh alikuwa ameyakausha maji ya Yordani mpaka pale waisraeli wote walipomaliza kuvuka, mioyo yao ikayeyuka, na hapakuwa na moyo wowote ndani yao kwa sababu ya watu wa Israeli.

2Kwa wakati huo Yahweh alimwambia Yoshua, “Tengenezeni visu vya mawe na mara moja muwatahiri wanaume wote wa Israeli.”3Kisha Yoshua alijifanyia visu vya mawe na akawatahiri wanaume wote wa Gibea Haaraloti.4Na hii ndio sababu ya Yoshua kuwatahiri; wanaume wote waliotoka Misri, pamoja na wanaume wa vita walikuwa wamekwisha kufa njiani katika nyikani, baada ya kukwea kutoka Misri.5Ingawa wanaume wote waliotoka Misri walikuwa wametahiriwa, bado hapakuwa na kijana yeyote aliyekuwa ametahiriwa kati ya vijana wote waliozaliwa nyikani katika njia ya kutoka Misri.6Kwasababu watu wa Israeli walitembea nyikani miaka arobaini, mpaka watu wa vita, yaani wanaume wote waliotoka Misri walikufa, kwasababu hawakuitii sauti ya Yahweh. Yahweh aliwaapia kwamba hawataruhusu kuiona nchi ambayo aliwaapia baba zao kwamba angetupatia sisi, nchi inayotiririka maziwa na asali.7Na badala yao, Yahweh aliwainua watoto wao kuchukua nafasi zao ambao Yoshua aliwatahiri, kwasababu walikuwa bado hajatahiriwa njiani.8Walipokwisha kutahiriwa wote, walibaki mahali walipokuwa katika kambi mpaka walipopona.9Na Yahweh akasema na Yoshua, “Siku hii nimeiondoa kwenu aibu ya Misri.” Hivyo, mahali pale paliitwa Gilgali hadi leo.

10Watu wa Israeli walipiga kambi hapo Gilgali. Waliitunza Pasaka katika siku ya kumi na nne ya mwezi, wakati wa jioni, katika uwanda wa Yeriko.11Na siku iliyofuata baada ya Pasaka, walikula sehemu ya mazao ya nchi, mikate isiyotiwa chachu na nafaka iliyokaangwa katika siku hiyo hiyo.12Mana zilikoma siku ile walipokula mazao ya nchi. Hapakuwa tena na mana kwa watu wa Israeli, bali walikula mazao ya nchi ya Kanaani mwaka huo.

13Wakati Yoshua alipokaribia Yeriko, aliinua macho na kuangalia, na tazama, mtu alikuwa amesimama mbele yake, alikuwa amechomoa upanga wake na ulikuwa mkononi mwake. Yoshua alimwendea na kumwambia, “Je uko kwa ajili yetu au kwa ajli ya maadui zetu?”14Akajibu, la hasha. Maana mimi ni amiri wa jeshi la Yahweh. Sasa nimekuja. Kisha Yoshua akainamisha uso wake juu ya nchi akaabudu na akamwambia, “Bwana wangu anasema nini kwa mtumwa wake?”15Amiri wa jeshi la Yahweh akamwambia Yoshua, “Vua viatu vyako miguuni mwako, kwa sababu sehemu uliyosimama ni takatifu.” Na Yoshua akafanya hivyo.

6

1Basi, milango yote ya Yeriko ilikuwa imefungwa kwa sababu ya jeshi la Israeli. Hapakuwa na mtu wa kutoka nje au kuingia ndani.2Yahweh akamwambia Yoshua, “Tazama, nimeweka Yeriko katika mkono wako, mfalme wake pamoja na wanajeshi wake waliofunzwa.3Ni lazima kutembea kwa kuuzunguka mji, wanaume wote wa vita wauzunguke mji mara moja. Ni lazima mfanye hivi kwa siku sita.4Makuhani saba lazima wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku. Na katika siku ya saba, ni lazima mtembee kwa kuuzunguka mji mara saba, na makuhani lazima wapulize tarumbeta.5Kisha watapuliza pembe za kondoo waume kwa nguvu kuu, na mtakaposikia sauti za tarumbeta watu wote na wapige kelele kwa mshindo kuu, na ukuta wa mji utaanguka chini pale pale. Wanajeshi ni lazime washambulie, kila mmoja aende mbele moja kwa moja.

6Ndipo Yoshua mwana wa Nuni, aliwaita makuhani na kuwaambia, “Lichukueni sanduku la agano, na waacheni makuhani saba wabebe tarumbeta za pembe za kondoo waume mbele ya sanduku la Yahweh.”7Yoshua aliwaambia watu, “Nendeni na mkatembee kuuzunguka mji, na watu wa vita wataenda mbele ya sanduku la Yahweh.”

8Makuhani saba walibeba tarumbeta saba za pembe za kondoo mbele ya Yahweh kama Yoshua alivyowaambia watu. Na walivyokuwa akiendelea mbele, walipuliza tarumbeta.9Sanduku la Yahweh liliwafuata kwa nyuma yao. Watu wa vita walitembea mbele ya makuhani, na walipuliza tarumbeta zao, lakini walinzi wa nyuma walilifuata sanduku kwa nyuma, na makuhani waliendelea kupuliza tarumbeta zao.10Lakini Yoshua aliwaagiza watu, akisema, “Msipige kelele. Sauti yoyote isitoke vinywani mwenu mpaka siku nitakayowaambia kupiga kelele. Ndipo hapo mtakapopiga kelele.”11Hivyo, alisababisha sanduku la Yahweh kuuzunguka mji mara moja kwa siku hiyo. Kisha wakaingia katika kambi yao, wakakaa usiku ule katika kambi.

12Basi Yoshua aliamka asubuhi na mapema, na makuhani wakalichukua sanduku la Yahweh.13Makuhani saba waliobeba tarumbeta saba za pembe za kondoo waume walikuwa mbele ya sanduku la Yahweh wakitembea kwa ushupavu, huku wakipuliza tarumbeta. Wanajeshi wenye silaha walikuwa wakitembea mbele yao, lakini walinzi wa nyuma walitembea nyuma ya sanduku la Yahweh, huku tarumbeta ziliendelea kupigwa.14Walitembea kuuzunguka mji mara moja katika siku ya pili na kisha wakarudi kambini. Walifanya hivi kwa siku sita.

15Ilikuwa ni katika siku ya saba ambayo waliamka mapema katika mapambazuko, na walitembea kuuzunguka mji kwa namna ile kama ilivyokuwa kawaida yao, katika siku hii walifanya mara saba.16Ilikuwa ni katika siku ya saba ambapo makuhani walipiga tarumbeta, na ya kwamba Yoshua aliwaagiza watu, “Pigeni kelele! Kwa kuwa Yahwe amewapa ninyi mji.17Mji pamoja na vitu vyote ndani yake vitatengwa kwa Yahweh kwa ajili ya uharibifu. Ni Rahabu yule kahaba pekee ataishi - yeye pamoja wote waliokuwa pamoja naye katika nyumba- kwa sababu aliwaficha watu tuliowatuma.18Lakini kwenu, iweni waangalifu juu ya kuchukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu, ili baada ya kuvitia alama kwa ajili ya kuharibiwa, msichukue hata kimoja wapo. Na kama mtafanya hivi, mtaifanya kambi ya Waisraeli iharibiwe na mtaleta matatizo katika kambi.19Fedha zote, dhahabu na vitu vilivyotengenezwa kwa shaba na chuma vilitengwa kwa ajli ya Yahweh.”

20Hivyo, watu wakapiga kelele, na wakatoa sauti kwa kupuliza tarumbeta. Ilikuwa watu waliposikia sauti za tarumbeta, walipiga kelele kwa sauti kuu, na ukuta ulianguka chini kabisa na kwamba watu waliuingia mji, kila mmoja alisonga mbele moja kwa moja. Na waliuteka mji.21Waliteketeza kabisa kila kitu kilichokuwa katika mji kwa makali ya upanga - wanaume kwa wanawake, wadogo kwa wakubwa, ng'ombe, kondoo na punda.

22Kisha Yoshua akawaambia wale watu wawili walioipeleleza nchi, “Nendeni katika nyumba ya kahaba, mtoeni mwanamke na wote walio pamoja naye, kama mlivyomwaapia.”23Basi, vijana wale walioipeleleza nchi waliingia ndani na kumtoa Rahabu nje. Walimtoa nje baba yake, mama, kaka, na ndugu wote waliokuwa pamoja naye. Waliwaleta katika sehemu ya nje ya kambi ya Waisraeli.24Na ndipo waliuteketeza mji na kila kitu ndani yake. Isipokuwa fedha, dhahabu na vyombo vya fedha na chuma viliwekwa kwa hazina ya nyumba ya Yahweh.25Bali Yoshua alimruhusu Rahabu kahaba, nyumba ya baba yake, na wote waliokuwa pamoja naye waishi. Mpaka leo hivi anaishi Israeli kwa sababu aliwaficha watu waliotumwa na Yoshua kuipeleleza Yeriko.

26Kisha katika kipindi hicho, Yoshua aliwaamuru kwa kiapo na kusema, “Alaaniwe machoni pa Yahweh mtu yule anayeujenga mji huu, Yeriko. Ataujenga msingi kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza, na kwa gharama ya mzaliwa wake wa pili atapachika milango yake.”

27Basi Yahweh alikuwa pamoja na Yoshua, na umaarufu wake ulienea katika nchi yote.

7

1Lakini watu wa Israeli hawakutenda katika uaminifu kuhusiana na vitu vilivyotengwa kwa ajili ya uharibifu. Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka katika kabila la Yuda, alivitwaa baadhi ya vitu hivyo vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya uharibifu, na hasira ya Yahweh iliwaka juu ya watu wa Israeli.

2Yoshua alituma watu kutoka Yeriko kwenda Ai, mji uliokuwa karibu na Bethi Aveni, mashariki mwa Betheli. Aliwaambia, “Nendeni na mkaipeleleza nchi.” Wale watu walikwea na kuipeleleza Ai.

3Waliporudi kwa Yoshua, walimwambia, “Usitume watu wote kwenda Ai. Tuma tu watu elfu mbili au elfu tatu waende kuiteka Ai. Usiwafanye watu wateseke katika vita, kwani ni watu wachache.”4Hivyo ni watu wapatao elfu tatu tu kutoka katika jeshi ndio walioenda, lakini watu hawa waliwakimbia watu wa Ai.5Watu wa Ai waliwaua watu wapatao thelathini na sita, waliwafuata katika lango la mji hadi katika machimbo ya mawe, na waliwauwa walipokuwa wakishuka katika kilima. Na mioyo ya watu ilijawa hofu na ujasiri wao ukawatoka.

6Basi Yoshua alizirarua nguo zake. Yeye pamoja na wazee wa Israeli waliweka mavumbi juu ya vichwa vyao na wakainamisha vichwa vyao hadi katika nchi mbele ya sanduku la Yahweh, na walibaki pale mpaka jioni.7Kisha Yoshua akasema, “Oo, Yahweh Bwana, kwa nini umewavusha watu hawa ng'ambo ya Yordani? Kutuweka katika mikono ya Waamori ili kutuangamiza? Ikiwa kama tulifanya maamuzi tofauti na tungekaa katika upande mwingine wa Yordani!8Bwana, niseme nini, baada ya Israeli kuwatega migongo maadui zao?9Kwa kuwa Wakaanani na wenyeji wote wa nchi watakaposikia, watatuzunguka na kuwafanya watu wa nchi kulisahau jina letu. Na utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?

10Yahweh akamwambia Yoshua, “Inuka! Kwanini umelala kifudifudi?11Israeli imetenda dhambi. Wamevunja agano langu nililowaagiza. Wameiba baadhi ya vitu vilivyokuwa vimetengwa. Wameiba na kisha pia wakaficha dhambi yao kwa kuweka vitu vile walivyochukua miongoni mwa mali zao wenyewe.12Na matokeo yake ni kwamba watu wa Israeli hawataweza kusimama mbele za maadui zao. Walitega migongo yao kwa maadui zao kwa sababu wao wenyewe wametengwa kwa ajili ya uharibifu. Sitakuwa pamoja nanyi tena mpaka pale mtakapoteketeza vitu vile vilivyotakiwa kuharibiwa, lakini sasa bado viko miongoni mwenu.

13Inuka! Waweke watu wakfu kwangu, na uwaambie, ‘Jiwekeeni wakfu ninyi wenyewe kesho. Kwa kuwa, Yahweh, Mungu wa Israeli asema hivi, “Kuna vitu vilitengwa ili kuteketezwa ambavyo bado viko miongoni mwenu, Israeli. Hamtaweza kusimama mbele ya maadui zenu mpaka pale mtakapoviondoa miongoni mwenu vitu vyote ambavyo vilitengwa kwa ajili ya kuteketezwa.”

14Asubuhi, mtajisogeza wenyewe kwa makabila. Kabila lile ambalo Yahweh atalichagua litasogea karibu kwa koo zake. Ukoo ule ambao Yahweh atauchagua lazima usogee karibu na nyumba. Nyumba ambayo Yahweh ataichagua lazima isogee karibu na mtu mmoja mmoja.15Itakuwa hivi mtu yule atakayechaguliwa na aliye na vitu hivyo vilivyotengwa kwa ajili ya kuharibiwa, atachomwa moto, yeye na kila kitu alichonacho, kwa sababu amelivunja agano la Yahweh na kwa sababu amefanya jambo la aibu katika Israeli.’”

16Basi, Yoshua aliamka asubuhi na mapema na aliwaleta Israeli karibu, kabila kwa kabila, na kabila la Yuda lilichaguliwa.17Yoshua akazisogeza koo za Yuda karibu, na ukoo wa Zera ulichaguliwa. Akausogeza karibu ukoo wa Zera mtu na mtu, na Zabdi alichaguliwa.18Akaisogeza karibu nyumba ya Zabdi mtu na mtu, na Akani mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, kutoka kabila la Yuda, alichaguliwa.

19Kisha Yoshua akamwambia Akani, “Mwanangu, niambie ukweli mbele za Yahweh, Mungu wa Israel, na ufanye ukiri wako kwake. Tafadhali niambie kile ulichofanya. Usinifiche.”

20Akani akamjibu Yoshua, “Kwa kweli nimetenda dhambi mbele Yahweh, Mungu wa Israeli.21Nilichofanya ni hiki: Nilipoona miongoni mwa nyara mkoti mzuri kutoka Babeli, shekeli mia mbili za fedha, na kipande cha dhahabu chenye uzito wa shekeli hamsini, nilivitamani na nikavichukua. Vimefichwa chini ardhini katikati ya hema langu, na fedha iko chini yake.”

22Yoshua akatuma wajumbe waliokimbia mpaka kwenye hema mahali palipokuwa na vile vitu. Walipoangalia, waliviona vimefichwa katika hema lake, na fedha chini yake.23Walivichukua vitu hivyo kutoka katikati ya hema na kuvileta kwa Yoshua na watu wote wa Israeli. Walivimwaga mbele za Yahweh.

24Kisha Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walimchukua Akani mwana wa Zera, na fedha, na koti, na kipande cha dhahabu, wana na binti zake, ng'ombe zake, punda zake, kondoo zake, hema lake, na kila kitu alichokuwa nacho, na wakavileta hata bonde la Akori.25Kisha Yoshua akasema, “Kwa nini umetusumbua? Leo Yahweh atakutesa na wewe.” Waisraeli wote wakampiga kwa mawe. Na wakawachoma wote kwa moto, na wakawapiga mawe.

26Kisha wakaweka juu yake kichuguu kikubwa cha mawe ambayo yapo hata leo. Yahweh akaachilia mbali hasira yake. Hivyo basi, jina la mahali hapo likawa Akori hata leo.

8

1Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope; usikate tamaa. Wachukue watu wote wa vita waende pamoja nawe. Pandeni kwenda Ai, Tazama nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai, watu wake, mji wake na nchi yake.2Mtafanya hivyo pia huko Ai na mfalme wake kama mlivyofanya kwa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mtachukua nyara na mifugo kwa ajili yenu. Pangeni mashambulizi ya uviziaji nyuma ya mji.”

3Basi Yoshua aliinuka na akawachukua kwenda Ai watu wote wa vita. Kisha Yoshua akachagua watu elfu thelathini - wenye nguvu na ujasiri - na aliwatuma waende wakati wa usiku.4Aliwaamuru, “Tazama, mtalala katika hali ya mashambulizi ya uviziaji dhidi ya mji, kwa nyuma yake. Usiende mbali sana na mji, lakini ninyi nyote muwe tayari.5Mimi pamoja na watu wote walio pamoja nami tutaukaribia mji. Na wakati watakapokuja kutushambulia sisi, tutawakimbia kama tulivyofanya hapo mwanzo.6Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, “Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.’ Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali.7Kisha mtapanda kutoka sehemu mliyojificha, na mtauteka mji. Yahweh Mungu wenu atawapa mkononi mwenu.8Tazama nimewaamuru, mtakapouteka mji, mtauchoma moto. Mtayafanya haya wakati mtakapotii agizo lililotolewa katika neno la Yahweh.”

9Yoshua akawatuma, na wakaenda sehemu ya uviziajia, na wakajificha kati ya Betheli na Ai sehemu ya magharibi ya Ai. Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku ule.

10Yoshua aliamka asubuhi na mapema na akawaandaa tayari wanajeshi wake, Yoshua na wazee wa Israeli walishambulia watu wa Ai.11Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda na kuukaribia mji. Walisogea karibu na mji na wakapiga kambi sehemu ya kasikazini mwa Ai. Kulikuwa na bonde kati yao na Ai.12Alichukua watu wapatao elfu tano hivi na akawaweka katika hali ya kuvizia katika upande wa magharibi mwa mji kati ya Betheli na Ai.13Waliwapanga wanajeshi wote, jeshi kuu katika upande wa kaskazini mwa mji, na walinzi wa nyuma upande wa magharibi mwa mji. Yoshua alilala bondeni usiku ule.

14Na alipoona hilo mfalme wa Ai, yeye pamoja na jeshi lake, waliamka asubuhi na mapema na walitoka kwa haraka kwenda kuwashambulia Israeli katika eneo linalokabili bonde la Mto Yordani. Hakujua kuwa kulikuwa na shambulizi la kuvizia lilikuwa linasubiria kushambulia kutokea kwa nyuma ya mji.15Yoshua na Waisraeli wote walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu, na wakakimbia kuelekea nyikani.16Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja waende mbele yao, na walienda mbele ya Yoshua na kwa jinsi hiyo walivutwa mbali na mji.17Hapakuwa na mtu mme aliyesalia Ai na Betheli ambaye alikuwa hajaenda nje kuwafuatilia waisraeli. Na walipokuwa wanawafuatilia Waisraeli, Wakatoka na waliuacha mji wazi.

18Yahweh akamwambia Yoshua, “Nyosha mkuki huo ulio mkononi mwako kuelekea Ai, kwa kuwa nitaitia Ai mikononi mwako.” Yoshua akaunyosha mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea mji.19Wanajeshi waliojificha katika hali ya kuvizia walitoka upesi katika eneo lao mara tu alipounyosha mkono wake. Walikimbia mbio na kuuingia mji na kuuteka. Na kwa haraka wakauchoma moto mji.

20Watu wa Ai waligeuka na kuangalia nyuma. Waliona moshi kutoka katika mji ukipanda kwenda angani, na hawakuweza kutoroka kwa njia hii au ile. Kwa kuwa wanajeshi wa Israelei waliokuwa wamekimbia katika nyika, sasa walirudi kuwakabili wale waliokuwa wanawafuata.21Na wakati Yoshua na Israeli wote walipoona kuwa wale watu wa kuvizia wameuteka mji kwa ule moshi uliokuwa ukipanda, waligeuka nyuma na kuwaua watu wa Ai.22Na wanajeshi wengine wa Israeli, wale waliokuwa wameingia ndani ya mji, walitoka nje ili kuwashambulia. Hivyo, watu wa Ai walikamatwa katikati ya majeshi ya Israeli, baadhi katika upande huu na wengine katika upande ule.23Lakini walimhifadhi mfalme wa Ai, ambaye walimteka akiwa hai, na kisha wakamleta kwa Yoshua.

24Ilikuwa baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuwaua wenyeji wote wa Ai katika uwanda kariibu na nyika mahali walipowafuata, na baada ya wao wote, hata yule wa mwisho, walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga, Waisraeli wote walirudi Ai. Waliuteka mji kwa ncha ya upanga.25Wale wote walikufa siku hiyo walikuwa watu elfu kumi na mbili elfu, wanaume na wanawake, wote watu wa Ai.26Yoshua hakuukunja mkono wake ambao alikuwa ameunyosha huku akishikilia mkuki wake, mpaka pale alipowateketeza kabisa watu wote wa Ai.27Waisraeli walichukua tu wanyama na nyara kutoka katika mji kwa ajili yao wenyewe, kama Yahweh alivyokuwa amemwagiza Yoshua.

28Yoshua aliichoma Ai na kuigeuza kuwa kichuguu cha mapango. Ni mahali palipoachwa ukiwa hata leo.29Alimtundika mfalme wa Ai juu ya mti mpaka jioni. Na jua lilipokuwa linaenda kuzama, Yoshua aliwaagiza na wakautoa mwili wa mfalme wakaushusha chini ya mti na kuutupa mbele ya malango ya mji. Huko wakaweka kichuguu kikubwa cha mawe juu yake. Kichuguu hicho kimebaki huko hata leo.

30Kisha Yoshua akajenga madhabahu kwa Yahweh, Mungu wa Israeli katika Mlima wa Ebali,31kama vile Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza watu wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa: “Madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna mtu yeyote aliyetumia zana ya chuma.” Na allimtolea Yahweh sadaka ya kuteketezwa juu yake na wakatoa sadaka ya amani.32Na huko aliandika juu ya mawe nakala ya sheria za Musa mbele ya watu wa Israeli.33Waisraeli wote, wazee wao, maafisa, na waamuzi wao walisimama katika sehemu mbili za sanduku mbele ya makuhani na Walawi ambao hulibeba sanduku la Agano la Yahweh - wageni pamoja na wazalia, nusu yao walisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu walisimama mbele ya Mlima Ebali. Waliwabariki watu wa Israeli kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza hapo mwanzo.

34Baada ya hayo, Yoshua alisoma maneno yote ya sheria, baraka na laana, kama zilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.35Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.

9

1Kisha wafalme wote walioishi ng'ambo ya mto Yordani katika nchi ya milima, na katika nchi za chini katika pwani za Bahari Kuu mbele ya Lebanoni - Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi na Wayebusi -2hawa waliungana pamoja chini ya amri moja kupigana vita dhidi ya Yoshua na Israeli.

3Waliposikia wenyeji wa Gibeoni juu ya mambo aliyoyafanya Yoshua katika Yeriko na Ai,4walipanga mpango wa udanganyifu. Walienda kama wajumbe. Walichukua magunia yaliyochakaa na kuyaweka juu ya punda. Walichukua pia viriba vilivyochakaa na kuchanika chanika na vilivyozibwa zibwa.5Walivaa miguuni mwao viatu vikuukuu na kutoboka toboka, na walivaa nguo kuukuu, zilichanika chanika. Na mikate yote katika chombo ilikuwa mikavu na yenye uvundo.6Kisha wakamwendea Yoshua katika kambi huko Giligali na wakamwambia yeye pamoja wa watu wa Israeli wakisema,

7“Tumesafiri kutoka nchi ya mbali, basi fanyeni agano nasi.” Watu wa Israeli wakawaamba Wahivi, “Huenda mnaishi karibu nasi. Twawezeje kufanya agano nanyi?”

8Wakamwambia Yoshua, “Sisi ni watumishi wako.” Yoshua akawauliza, “Ninyi ni akina nani? Mnatokea wapi?

9Wakamwambia, “Watumishi wako wamekuja hapa kutokea nchi ya mbali, kwa sababu ya jina la Yahweh Mungu wako. Tumesikia habari kumhusu na kuhusu kila kitu alichokifanya Misri -10Na kila kitu alichokifanya kwa wafalme wawili wa Waamori katika upande mwingine wa Yordani - kwa mfalme Sihoni wa Heshiboni, na kwa Ogu wa Bashani aliyekuwa katika Ashitarothi.11Wazee wetu na wenyeji wote wa nchi yetu walituambia,” Chukueni chakula mikononi mwenu kwa ajili ya safari. Nendeni mkakutane nao, na kisha muwambie, “Sisi ni watumishi wenu. Fanyeni agano pamoja nasi.”12Huu ni mkate wetu, ulikuwa wa moto tulipouchukua kutoka katika nyumba zetu katika siku ile tulipotoka kuja kwenu. Lakini sasa, tazama, imekuwa kavu na yenye ukungu.13Viriba hivi vilikuwa vipya tulipovijaza, na tazama, sasa vinavuja. Nguo zetu na viatu vyetu vimechakaa na kuwa vikuukuu kwa sababu ya safari ndefu.”

14Kwa hiyo, Waisraeli wakatwaa sehemu ya vyakula vyao, lakini walifanya hivyo bila ya kumwuliza Yahweh ili awaongoze.15Yoshua akafanya amani pamoja nao na kufanya agano pamoja nao ili waishi. Viongozi wa watu nao pia wakawaapia.

16Siku tatu baada ya Waisraeli kufanya agano pamoja nao, waligundua kuwa walikuwa ni majirani zao na ya kwamba waliishi karibu nao.17Kisha watu wa Israeli walisafiri na kufika katika miji yao katika siku ya tatu. Miji yao ilikuwa Gibeoni, Kefira, Beerothi, na Kiriathi Yearimu.18Watu wa Israeli wakushambulia kwasababu viongozi wao walikuwa wamewaapia mbele za Yahweh, Mungu wa Israeli. Waisraeli wote walikuwa wananung'unika kinyume na viongozi wao.19Lakini viongozi wote waliawaambia watu wote wa Israeli, “Tumeapa kwa Yahweh, Mungu wa Israeli kwa ajili yao, na sasa hatuwezi kuwadhuru.20Hiki ndicho tutakachowafanyia: Tutawaacha waishi ili tuepuke ghadhabu ambayo yaweza kuja juu yetu kwasababu ya kiapo tulichowaapia.”21Viongozi wakawaambia watu, “Waacheni waishi.” Hivyo Wagibeoni wakawa wakata kuni na wachota maji wa Waisraeli wote, kama vile viongozi walivyosema juu yao.

22Yoshua aliwaita na kuwaambia, “Kwa nini mlitudanya wakati mliposema, “Tuko mbali sana nanyi’ wakati mnaishi hapa hapa miongoni mwetu?23Na kwa sababu hii, mmelaaniwa na baadhi yenu mtakuwa watumwa siku zote, wenye kukata kuni na kuchota maji kwa ajli ya nyumba ya Mungu wangu.”

24Walimjibu Yoshua na kusema, “Ni kwa sababu watumishi wako waliambiwa kwamba Yahweh Mungu wenu alimwagiza Musa mtumishi wake kuwapa ninyi nchi yote, na kuwaangamiza wenyeji wote wa nchi mbele yenu - hivyo tuliogopa kwasababu yenu kwa ajili ya maisha yetu. Ndio maana tulifanya jambo hili.25Tazama sasa, mnatumiliki chini ya utawala wenu. Chochote kilichochema na haki kwenu kutufanyia, fanyeni.”

26Basi Yoshua aliwafanyia hivi: aliwaondoa katika mamlaka ya watu wa Israeli, na Waisraeli hawakuwaua.27Siku hiyo Yoshua aliwafanya Wagibeoni kuwa wakata kuni na wachotaji wa maji kwa jamii, na kwa madhabahu ya Yahweh hadi leo katika sehemu ambayo Yahweh huichagua.

10

1Ikawa Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alisikia kuwa Yoshua ameiteka Ai na ameiteketeza kabisa, kama alivyokwisha kufaya huko Yeriko na mfalme wake. Na alisikia jinsi ambavyo watu wa Gibeoni walivyofanya amani na watu wa Israeli na walikuwa wanaishi miongoni mwao.2Watu wa Yerusalemu waliogopa sana kwa sababu Gibeoni ulikuwa mji mkubwa, kama mmoja wa miji ya kifalme. Ilikuwa kubwa kuliko Ai, na watu wake wote walikuwa ni mashujaa wenye nguvu.3Hivyo Adonizedeki, mfalme wa Yerusalemu, alituma ujumbe kwa Hohamu, mfalme wa Hebroni, na kwa Piramu, mfalme wa Yarimuthi, na kwa Yafia, mfalme wa Lakishi, na kwa Debiri, mfalme wa Eguloni:4“Njooni kwangu na mnisaidie. Tuishambulie Gibeoni kwa sababu wamefanya amani na Yoshua pamoja na watu wa Israeli.

5Wafalme watano wa Waamori; mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarimuthi, mfalme wa Lakishi, na mfalme wa Eguloni walikwea, wao pamoja na majeshi yao yote. Walipanga sehemu yao kinyume na Wagibeoni na waliwashambulia.

6Watu wa Gibeoni walituma ujumbe kwa Yoshua na kwa jeshi huko Giligali. Walisema, “Upesi! Msiutoe mkono wenu kutoka kwa watumishi wenu. Mje haraka na mtuokoe. Mtusaide, maana wafalme wote wa Waamori wanaoishi katika nchi ya milima wamekusanyika kwa pamoja ili watushambulie.

7“Yoshua alipanda kutoka Giligali, yeye na watu wote wa vita pamoja naye, na watu wote wapiganaji.8Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiwaogope. Nimewatia wote katika mkono wako. Hakuna hata mmoja wao atakayeweza kuzuia mashambulizi yako.”

9Baada ya kutembea usiku kucha kutoka Giligali, ghafla Yoshua aliwafikilia.10Na Yahweh aliwachanganya maadui mbele za Israeli - ambao waliwaua mauaji makubwa mno huko Gibeoni, na wale waliowafuata njiani iendayo Bethi Horoni, nao waliuwaua katika njia iendayo Azeka na Makeda.11Na walipokuwa wakikimbia mbio kutoka kwa Waisraeli, chini ya mlima kutoka Bethi Horoni, Yahweh alitupa mawe makubwa kutoka mbinguni juu yao wote katika njia iendayo Azeka, nao wakafa. Watu waliouawa kwa mawe walikuwa ni wengi zaidi kuliko wale waliouawa kwa upanga wa watu wa Israeli.

12Kisha Yoshua akamwambia Yahweh katika siku ambayo Yahweh aliwapa watu wa Israeli ushindi dhidi ya Waamori. Hiki ndicho Yoshua alichosema kwa Yahweh mbele ya Israeli. “Jua lisimame katika Gibeoni, na mwezi, usimame katika bonde la Aijaloni.”

13Jua lilisimama, na mwezi ukaacha kwenda mpaka taifa lilipolipiza kisasi dhidi ya maadui zao. Je hili halikuandikwa katika Kitabu cha Yashari? Jua lilikaa katikati ya anga; halilkuzama kwa siku nzima hivi.

14Haijawahi kutokea siku nyingine kama hiyo kabla au baada yake, wakati Yahweh alipotii sauti ya mtu. Kwa kuwa Yahweh alikuwa akifanya vita badala ya Israeli.

15Yoshua na Israeli yote pamoja naye walirudi kambini huko Giligali.

16Basi wale wafalme watano walikuwa wametoroka na kujificha wao wenyewe katika pango huko Makeda.17Taarifa zilimfikia Yoshua kusema, “Wafalme watano wamepatikana wamejificha katika pango huko Makeda!”18Yoshua akasema, “Viringisheni mawe makubwa katika mlango wa pango na muweke wanajeshi hapo ili kuwalinda.19Msibaki na kukaa nyie wenyewe. Bali wafuatilieni maadui zenu na kuwashumbulia kutokea kwa nyuma. Msiwaruhusu kuingia katika miji yao, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu amewatia katika mkono wenu.”

20Yoshua na wana Waisraeli walikuwa wamemaliza kuwaua kwa mauaji makubwa sana, mpaka pale walipokuwa wameteketezwa kabisa; watu wachache tu walipona waliotoroka walifika miji ya ngome.21Kisha jeshi lote lilirudi kwa Yoshua likiwa na amani katika kambi huko Makeda, Na hakuna hata mmoja aliyethubutu kusema hata neno moja kinyume na watu wa Israeli.

22Kisha Yoshua akasema, “Fungueni mlango wa pango, watoeni nje na waleteni kwangu hawa wafalme watano.”23Walifanya kama Yoshua alivyosema. Waliwaleta wafalme watano kutoka katika pango - mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Hebroni, mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi na mfalme wa Egloni.24Na walipowaleta wafalme kwa Yoshua, alimwita kila mtu wa Israeli, na aliwaambia maakida wa wanajeshi waliokuwa wameenda vitani pamoja naye “Kanyageni miguu yenu juu ya shingo zao.” Basi walikuja na kukanyaga miguu yao juu ya shingo zao.25Kisha akawaambia, ‘Msiogope wala kufadhaika. Uwe na moyo mkuu na jasiri. Na hiki ndicho Mungu atakachokifanya kwa maadui wenu wote ambao mtapigana nao.’26Kisha Yoshua akawashambulia na kuwaua wafalme. Aliwatundika wote watano juu ya miti. Waliwatundika juu ya miti hata jioni.27Ilipokuwa jioni, Yoshua alitoa maagizo, nao waliwashusha chini ya miti na kisha wakawatupa katika pango ambalo walikuwa wamejificha wao wenyewe. Waliweka mawe makubwa juu ya mlango wa pango. Mawe hayo yapo pale hadi leo hii.

28Na kwa namna hii, katika siku hiyo Yoshua aliuteka mji wa Makeda na aliwaua watu wote huko kwa upanga, pamoja na mfalme wake. Aliwateketeza wote kabisa pamoja na kila kiumbe hai kilichokuwa huko. Hakuna hata mmoja aliyesalia. Alichomfanyia mfalme wa Makeda ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.

29Yoshua na Israeli wote waliipita Makeda na kufika Libna. Na huko waliingia katika vita dhidi ya Libna.30Yahweh pia aliitia katika mkono wa Israeli pamoja na mfalme wake. Yoshua alishambulia kila kiumbe hai ndani yake kwa upanga. Hakuacha hai hata mtu mmoja. Alichomfanyia mfalme ni sawa sawa na kile alichokuwa amemfanyia mfalme wa Yeriko.

31Baadaye Yoshua na Israeli wote pamoja naye walipanda kutoka Libna na kwenda Lakishi. Alipiga kambi karibu yake na wakafanya vita dhidi yake.32Yahweh aliitia Lakishi katika mkono wa Israeli. Yoshua aliiteka katika siku ya pili. Alishambulia kwa upanga kilia kiumbe hai kilichokuwa ndani yake, kama vile aliyokuwa amefanya huko Libna.33Kisha Horamu, mfalme wa Gezeri alikwea ili kuisaida Lakishi. Yoshua alimshambulia yeye na jeshi lake mpaka pale ambapo hapakuwa na mtu hata mmoja aliyesalia.

34Baada ya hapo, Yoshua na Israeli wote walitoka Lakishi na kwenda Egloni. Walipiga kambi karibu yake na kisha wakafanya vita dhidi yake,35na siku hiyo hiyo wakaiteka. Waliupiga kwa upanga na waliteketeza kila mtu ndani yake kama vile Yoshua alivyofanya huko Lakishi.

36Kisha Joshua na Israeli wote wakatoka Egloni na kwenda Hebroni. Wakapigana vita dhidi yake.37Waliuteka mji na kuwaua kwa upanga watu wote ndani yake pamoja na mfalme wake, kujumuisha na vijiji vyote vilivyoizunguka. Waliteketeza kabisa kila kiumbe hai ndani yake, hawakuacha hata mtu mmoja aliyesalia, ni sawa sawa na vile Yoshua alivyoitenda Egloni. Aliiteketeza kabisa, na kila kiumbe hai ndani yake.

38Baada ya hapo, Yoshua alirudi pamoja na jeshi lote la Israeli pamoja naye, wakasafiri kwenda Debiri na kupigana vita dhidi yake.39Aliuteka mji na mfalme wake, pamoja na vijiji vyake vya jirani. Waliwaua wote kwa upanga na waliteketeza kila kiumbe hai ndani yake. Joshua hakuacha hata mmoja hai, kama alivyokuwa amefanya kwa Hebroni na mfalme wake, na kama alivyokuwa amefanya kwa Libna na mfalme wake.

40Yoshua aliishinda nchi yote, nchi ya milima, Negevu, nchi, nchi ya tambarare na nchi ya miteremko. Hakuna hata mfalme moja aliyebaki hai kati ya wafalme wake wote. Kwa kweli aliteketeza kila kiumbe hai, kama ambavyo Yahweh, Mungu wa Israeli alivyomwaagiza.41Yoshua aliwaua kwa upanga kutoka Kadeshi Barnea hadi Gaza, na nchi yote ya Gosheni hata Gibeoni.42Yoshua aliwateka wafalme wote hawa na nchi zao kwa wakati mmoja, kwa sababu Yahweh, Mungu wa Israeli, alipigana kwa ajili ya Israeli.

43Baada ya hayo Yoshua na Waisraeli wote pamoja naye, walirudi katika kambi huko Gilgali.

11

1Basi ikawa aliposikia haya, Yabini, mfalme wa Hazori, alituma ujumbe kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme Shimroni, na kwa mfalme wa Akshafu.2Alituma pia ujumbe kwa wafalme walikuwa katika mlima wa kaskazini mwa nchi, katika bonde la Mto Yordani kusini mwa Kinerethi, katika nchi za tambarare, na katika nchi za milima ya Dori kuelekea magharibi.3Pia, alituma ujumbe kwa Wakanaani walioko mashariki na magharibi, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wayebusi katika nchi za milima, na Wahivi karibu na Mlima Hermoni katika nchi ya Mizipa.4Maadui zao wote walitoka pamoja nao, wanajeshi wengi sana, hesabu yao ilikuwa kama mchanga wa pwani. Walikuwa na farasi wengi sana na magari.5Wafalme wote hawa walikutana katika muda waliokuwa wameupanga, na walipiga kambi katika maji ya Meromu ili kupigana vita na Israeli.

6Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope mbele zao, kwa kuwa muda kama huu kesho ninawatia hao kwa Waisraeli wakiwa wafu. Utaivunja vunja miguu ya farasi zao, na utayachoma moto magari yao.”

7Yoshua na watu wote wa vita walitoka na mara wakafika katika maji ya Meromu, na wakawashambulia maadui.8Yahweh akawatia maadui katika mkono wa Israeli, na waliwapiga kwa upanga na wakawafuata mpaka Sidoni, Misrefothi - Maimu, na katika bonde la Mizipa upande wa mashariki. Waliwaua wote hakuna hata mmoja aliyeachwa hai.9Yoshua aliwatendea kama vile Yahweh alivyomwambia. Alivunja miguu ya farasi na magari aliyachoma moto.

10Kwa wakati huo, Yoshua alirudi na akauteka mji wa Hazori. Alimuua mfalme wake kwa upanga (Hazori ulikuwa ni kichwa cha falme hizi zote).11Waliwapiga kwa upanga kila kiumbe chenye uhai kilichokuwa huko, na alivitenga ili viteketezwe, hivyo hapakuwa na kiumbe hai kilichoachwa hai. Na kisha aliuchoma moto Hazori.

12Yoshua aliiteka miji yote ya wafalme hawa. Aliwateka pia wafalme wake wote na akawapiga wote kwa upanga. Aliwateketeza kabisa kwa upanga, kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyoagiza.13Waisraeli hawakuchoma moto mji wowote miongoni mwa miji iliyojengwa juu ya vilima vya vifusi vya udongo, isipokuwa Hazori, ndio mji pekee ambao Yoshua aliuchoma kwa moto.14Jeshi la Israeli lilichukua nyara kutoka katika miji pamoja na mifugo kwa ajili yao wenyewe. Waliua kila mtu kwa upanga hadi pale walipokufa wote. Hakuna kiumbe hai kilichoachwa hai.15Kama vile Yahweh alivyomwagiza mtumishi wake Musa, na kwa namna hiyo hiyo, Musa alivyomwagiza Yoshua. Na katika mambo yote ambayo Yahweh alimwamuru Musa kuyafanya, Yoshua hakuacha kufanya hata jambo moja.

16Yoshua alitwaa nchi hiyo yote, nchi ya milima, Negevu yote, nchi yote ya Gosheni, nchi ya vilima vidogo, bonde la Mto Yordani, nchi ya milima ya Israeli, na nchi tambarare.17Kutoka Mlima Halaki karibu na Edomu, kuelekea kasikazini hadi Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni chini ya Mlima Hermoni, aliwateka wafalme wake wote na kuwaua.18Yoshua alipigana vita na wafalme wote kwa muda mrefu.19Hakuna hata mji mmoja uliofanya amani na jeshi la Israeli isipokuwa Wahivi walioishi Gibeoni. Israeli ilitwaa miji yote iliyosalia katika vita.20Kwa kuwa alikuwa ni Yahweh ambaye alikuwa ameifanya kuwa migumu mioyo yao ili wapande na kupigana vita dhidi ya Israeli, ili kwamba aweze kuwaangamiza kabisa, na kutowaonesha huruma, kama alivyomwaagiza Musa.

21Kisha Yoshua akaja kwa wakati ule na aliiangamiza Anakimu. Aliyafanya haya katika nchi ya milima, huko Hebroni, Debiri, Anabu, na katika nchi yote ya Yuda, na katika nchi yote ya milima ya Israeli. Yoshua aliwaangamiza kabisa pamoja na miji yao.22Hakuna hata mmoja wa watu wa Anakimu aliyeachwa katika nchi ya Israeli, isipokuwa huko Gaza, Gathi na Ashidodi.23Hivyo Yoshua aliiteka nchi yote, kama vile Yahweh alivyomwambia Musa. Yoshua aliwapa Israeli kama urithi, kila kabila lilipewa sehemu yake. Kisha nchi ikapumzika bila vita.

12

1Basi hawa ndio wafalme wa nchi, ambao watu wa Israeli walishinda. Waisraeli walichukua miliki ya nchi katika upande wa mashariki mwa Yordani sehemu ambako jua huchomoza, kutoka bonde la Mto Arnoni hadi Mlima Hermoni, na nchi yote ya Araba kuelekea kusini.2Sihoni, mfalme wa Waamori, aliishi katika Heshiboni. Alitawala kutoka Aroeri, ambayo iko juu ya bonde la Arnoni kutoka katikati ya bonde, na nusu ya Geleadi kushuka mpaka Mto Yaboki katika mpaka wa Waamori.3Sihoni pia alitawala juu ya Araba mpaka Bahari ya Kinerethi, kwenda mashariki, kuelekea Bahari ya Araba (Bahari ya Chumvi) upande wa mashariki, hadi huko Bethi Yeshimothi na upande wa kusini, kuelekea chini ya miteremko wa Mlima Pisiga.4Ogu, mfalme wa Bashani, mmoja kati ya mabaki ya Rephaimu, aliyeishi huko Shatarothi na Edrei.5Alitawala juu ya Mlima Hermoni, Saleka, na Bahani yote, hadi mpaka wa watu wa Geshuri na Wamakathi, na nusu ya Gleadi, hadi kufika mpaka wa Sihohi, mfalme wa Heshboni.

6Musa mtumishi wa Yahweh, na watu wa Israeli walikuwa wamewashinda, na Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa nchi kama mali ya Wareubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase.

7Hawa ndio wafalme wa nchi ambayo Yoshua na watu wa Israeli waliwashinda katika upande wa magharibi mwa mto Yordani, kutoka Baali Gadi katika bonde karibu na Lebanoni hadi Mlima Halaki karibu na Edom. Yoshua aliyapa nchi makabila ya Israeli ili yaimiliki.8Aliwapa nchi ya milima, tambarare, Araba, sehemu za milima, nyika na Negevu, nchi ya Wahiti, Waamori, Wakanaani, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi.9Wafalme hawa walikuwa ni mfalme wa Yeriko, mfalme wa Ai iliyo karibu na Betheli,10mfalme wa Yerusalemu, mfalme wa Enaimu,11mfalme wa Yarmuthi, mfalme wa Lakishi,12mfalme wa Egloni, mfalme wa Gezeri,13mfalme wa Debiri, mfalme wa Gederi,14mfalme wa Horima, mfalme wa Aradi,15mfalme wa Libna, mfalme wa Adula,16mfalme wa Makeda, mfalme wa Betheli,17mfalme wa Tapua, mfalme wa Heferi,18mfalme wa Afeki, mfalme wa Lasharoni,19mfalme wa Madoni, mfalme wa Hazori,20mfalme wa Shimroni - Meroni, mfalme wa Akshafu.21Mfalme wa Taanaki, mfalme wa Megido,22mfalme wa Kedeshi, mfalme wa Jokineamu katika Karmeli,23mfalme wa Dori katika Nafutali Dori, mfalme Goyimu katika Giligali, na24mfalme Tiriza. Hesabu ya wafalme ilikuwa ni thelathini na moja kwa ujumla wake.

13

1Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, “Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka.2Nchi iliyosalia ndio hii: mikoa yote ya Wafilisti, na mikoa ile ya Wageshuri,3(tangu Shihori, iliyoko mashariki mwa Misri, na upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Ekroni, inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani; wafalme watano wa Wafilisti, wale wafalme wa Gaza, Ashidodi, Ashikeloni, Gathi na Ekroni - miliki ya Waavi.4Katika upande wa kusini, kulisalia nchi yote ya Wakanaani, na Meara ambayo ni miliki ya Wasidoni, hadi Afeki, hata mpaka wa Waamori;5Nchi ya Wagebali, Lebanoni kuelekea upande wa mapambazuko ya jua, kutoka Baali- Gadi chini ya Mlima Hermoni mpaka Lebo Hamathi.

6Pia, wenyeji wote wa nchi ya milima kutoka Lebanoni hadi Misrefothi - Maimu, pamoja na watu wa Sidoni. Nitawafukuza mbele ya jeshi la Israeli. Uwe na uhakika wa kuwapa Waisraeli nchi kama urithi, kama nilivyokuagiza.7Igawanye nchi hii kama urithi kwa makabila tisa na kwa nusu ya kabila la Manase.8Pamoja na nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi wamekwisha kupokea urithi wao ambao Musa aliwapa katika upande wa mashariki wa Yordani,9Kutoka Aroeri, iliyo katika ukingo wa bonde la mto Arnoni (kujumuisha na mji ambao uko katikati ya bonde), kwa nyanda zote za Medeba hadi Diboni;10miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori,11Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka;12Ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali.13Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo.

14Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa.

15Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo.16Milki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba.17Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamothi Baali, na Bethi Baalimeoni,18na Yahazi, na Kedemothi, na Mefathi,19na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde.20Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi,21miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi.22Pia, watu wa Israeli walimuua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua.23Mpaka wa kabila la Rubeni ni Mto Yordani; huu ndio mpaka wao. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Rubeni, uliotolewa kwa kila ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.

24Hiki ndicho Musa alilipa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:25Himaya yao ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni, hadi Aroeri, iliyo mashariki mwa Raba,26kutoka Heshiboni hadi Ramathi - Mizipe na Betonimu, kutoka Mahanaimu mpaka himaya ya Debiri.27Katika bonde, Musa aliwapa Bethi -Haramu, Bethi - Nimra, Sukothi, na Zafoni, ufalme uliobakia wa Sihoni mfalme wa Heshiboni, pamoja na Yordani kama mpaka, katika sehemu za chini za mwisho wa Bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki ng'ambo ya Yordani.28Huu ni urithi wa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.

29Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase. Urithi uligawiwa kwa nusu ya kabila la watu wa Manase kutokana na kabila zao.30Miliki yao ilikuwa kutoka Mahanaimu, Bashani yote, ufalme wote wa mfalme Ogu wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;31nusu ya Gileadi, na Ashitarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Miji hii iligawanywa kwa ukoo wa Makiri mwana wa Manase -nusu ya watu wa Makiri, walipewa kwa kila familia zao.

32Huu ndio urithi ambao Musa aliowagawia katika nyanda za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko.33Musa hakulipa urithi kabila la Lawi. Kwa kuwa Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao, kama vile alivyowaambia.

14

1Maeneo haya ya nchi ambayo watu wa Israeli waliyapokea kama urithi wao katika nchi ya Kanaani. Urithi huu uligawanywa kwao na Eliazeri kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya mababu wa familia zao kati ya watu wa Israeli.2Urithi wao ulichaguliwa kwa kupiga kura kwa makabila tisa na nusu, kama vile Yahweh alivyoagiza kwa mkono wa Musa.3Kwa kuwa Musa alikuwa amewapa urithi makabila mawili na nusu ng'ambo ya Yordani, lakini Walawi hawakupewa urithi wowote.4Kabila la Yusufu kwa uhalisia yalikuwa makabila mawili, Manase na Efraimu. Na hakuna sehemu yoyote ya urithi waliyopewa Walawi katika nchi, lakini walipewa miji ya kuishi ndani yake pamoja na sehemu ya malisho ya mifugo yao na kwa ajili ya riziki zao.5Watu wa Israeli walifanya hivyo kama vile Yahweh alivyomwagiza Musa, basi waliiganywa nchi.

6Kisha kabila la Yuda lilikuja kwa Yoshua huko Giligali. Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi, akamwambia, “Unajua kile Yahweh alichomwambia Musa mtu wa Mungu juu yako na mimi huko Barnea.7Nilikuwa na umri wa miaka arobani wakati Musa mtumishi wa Yahweh aliponituma kutoka Kadeshi Barnea kuipeleleza nchi. Nilimletea taarifa tena kama nilivyotakiwa kufanya katika moyo wangu.8Lakini ndugu zangu walioenda pamoja nami waliifanya mioyo ya watu iyeyuke kwa woga. Lakini mimi nilimfuata Yahweh kabisa.9Musa aliapa katika siku hiyo akisema, “Hakika nchi ambayo miguu yako imetembea juu yake itakuwa urithi wako na kwa watoto wako milele, kwasababu umemfuata kabisa Yahweh Mungu wangu.

10Tazama! Sasa, Yahweh amenihifadhi hai kwa miaka hii arobaini na tano, kama alivyosema - tangu kipindi kile Yahweh alivyomwambia Musa neno hili, wakati huo Waisraeli walikuwa wakitembea jangwani. Tazama! Sasa katika siku hii ya leo nina miaka themanini na mitano.11Bado hata siku hii ya leo nina nguvu kama nilivyokuwa katika siku ile ambayo Musa alinituma. Nguvu zangu za sasa ni sawa na nguvu zangu za kipindi kile, kwa ajili ya vita na kwa kwenda na kwa kuja.12Sasa basi, nipe nchi hii ya milima, ambayo Yahweh aliniahidi katika siku hiyo. Kwa kuwa ulisikia katika siku hiyo kuwa Wanakimu walikuwa huko katika miji yenye ngome. Itakuwa kwamba Yahweh atakuwa pamoja nami na ya kwamba nitawafukuzia mbali, kama vile Yahweh alivyosema.”

13Kisha Yoshua alimbariki Kalebu mwana wa Yefune na alimpa Hebroni kama urithi wake.14Hivyo Hebroni ikawa urithi wa Kalebu mwana wa Yefune Mkenizi hata leo, kwasababu alimfuata kabisa Yahweh, Mungu wa Israeli.15Basi, jina la Hebroni hapo mwanzo lilikuwa ni Kiriathi Arba (Arba ambaye alikuwa ni mtu mkuu miongoni mwa Wanakim). Kisha nchi ikawa na raha bila vita.

15

1Ugawanaji wa nchi kwa kabila la watu wa Yuda, walipewa kwa kufuatana na koo zao, kutoka upande wa kusini hadi mpaka wa Edomu, pamoja na nyika ya Sini iliyokuwa mbali sana kuelekea kusini.2Mpaka wao wa upande wa kusini ulianzia mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ghuba iliyokabili upande wa kusini.3Mpaka wao mwingine ulielekea upande wa kusini wa mlima wa Akrabimu na kupita kuelekea Sini, na kupanda upande wa Kadeshi Barnea, karibu na Hezroni, hadi Addari mahali ambapo ulipinda kuelekea Karika.4Ulipita katika Azimoni, kuelekea kijito cha Misri, na mwisho ulikuwa katika bahari. Huu ulikuwa ni mpaka wa kusini.5Mpaka wa mashariki ulikuwa ni Bahari ya Chumvi, katika mdomo wa Yordani. Mpaka wa upande wa kasikazini ulianzia katika ghuba ya bahari katika mdomo wa Yordani.6Ulielekea mpaka Bethi Hogla na ulipita kaskazini mwa Bethi Araba. Kisha ulipanda hata Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.7Basi mpaka ule ulienda hadi Debiri kutoka katika bonde la Akori, kuelekea upande wa kasikazini, kuendelea hadi Giligali, ambayo iko mkabala na mlima Adumimu, iliyo upande wa kusini wa bonde. Kisha mpaka uliendelea hata katika chemichemi za En Shemeshi na kufika En Rogeli.8Kisha mpaka ulishuka hadi bonde la Beni Hinomu kuelekea upande wa kusini wa mji wa Wayebusi (ambao ni Yerusalemu). Kisha ulipanda hata katika mlima ulio juu ya bonde la Hinomu, katika upande wa magharibi, ulio mwishoni mwa bonde la Refaimu katika upande wa kaskazini.9Kisha mpaka ulitanuka kutoka katika kilele cha milima hata chemichemi ya Nefutoa, na ulipanda kutoka hapo kuelekea miji ya Mlima Efroni. Kisha mpaka ulipiga kona kuelekea Baala (ambao ndio Kiriathi Yearimu).10Baadaye mpaka ulizunguka kuelekea magharibi mwa Baala kukabili Mlima Seiri, na kupita kufuata upande wa Mlima wa Yearimu katika upande wa kasikazini (ambao ndio Kesaloni), ulienda chini hadi Bethi Shemeshi na kuvuka hata ng'ambo ya Timna.11Mpaka uliendelea karibu na mlima wa kaskazini mwa mlima wa Ekroni, na kisha ukakata kona kuzunguka Shikeroni na kupita kuelekea sambamba na Mlima Baala, kutoka hapo uliendelea hadi Yabneeli. Mpaka ule ulikomea katika bahari.12Mpaka wa magharibi ulikuwa Bahari Kuu na katika ukanda wa pwani yake. Huu ndio mpaka uliozunguka kabila la Yuda, ukoo kwa ukoo.

13Katika kulitunza agizo la Yahweh kwa Yoshua, Yoshua alimpa Kalebu mwana wa Yefune mgao wa nchi ya. Miongoni mwa kabila la Yuda, alimgawia nchi Kiriathi Arba, ambayo ndio Hebroni (Arba alikuwa ni baba wa Anaki).14Kalebu aliwafukuzia mbali wana watatu wa Anaki: Sheshai, Ahimani na Talmai, wazawa wa Anaki.15Alipanda kutoka pale kinyume cha wenyeji wa Debiri (Debiri hapo mwanzo iliitwa Kiriathi Seferi).16Kalebu akasema, “Mtu atakayeishambulia Kiriathi Seferi na kuiteka, nitampa binti yangu, Akisa, awe mke wake.17Wakati huo Othinieli mwana wa Kenazi, kaka yake Kalebu, aliuteka mji, na Kalebu alimpatia Akisa, binti yake awe mke wake.

18Mara baada ya hayo, Akisa alienda kwa Othinieli na alimsihi amwombe baba yake shamba. Na mara aliposhuka kutoka katika punda wake, Kalebu alimwambia Akisa, “Unataka nini?”

19Akisa akamjibu, “Nifanyie neema. Kwa kuwa umeshanipa nchi ya Negebu, nipe pia baadhi ya chemichemi za maji.” Na Kalebu alimpa chemichemi ya juu na chemichemi ya chini.

20Huu ulikuwa ndio urithi wa kabila la Yuda, waliopewa kufuatana na ukoo wao.21Miji iliyo mali ya kabila la Yuda katika upande wa kusini, kuelekea mpaka wa Edomu, ilikuwa ni Kabzeeli, Eda, Yaguri,22Kina, Dimona, Adada,23Kadeshi, Hazor, Ithinani,24Zifu, Telemu, Bealothi.25Hazori Hadata, Keriothi Hezroni (mji huu ulijulikana kama Hazori),26Amamu, shema, Molada,27Hazari Gada, Heshimoni, Bethi Peleti,28Hazari Shuali, Beerisheba, Biziothia.29Baala, Limu, Ezemu,30Eltoladi, Kesili, Horma,31Ziklagi, Madimana, Sansana,32Lebaothi, Shilihimu, Aini, na Rimoni. Miji hii ilikuwa ishirini na tisa kwa ujumla, kujumlisha na vijiji vyake.33Katika nchi iliyo chini ya mlima upande wa magharibi, kulikuwa na miji ya Eshtaoli, Zora, Ashina,34Zanaoa, Eni Ganimu, Tapua, Enamu,35Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka,36Shaaraimu, Adithaimu, na Gedera (ambayo ndio Gederothaimu). Hesabu ya miji hii ilikuwa ni kumi na nne, pamoja na vijiji vyao.37Zena, Hadasha, Migidagadi,38Dileani, Mizipa, Yokitheeli,39Lakishi, Bozikathi, Egloni.40Kaboni, Lahmamu, Kitilishi,41Gederothi, Bethi Dagoni, Naama, Makeda. Hesabu ya miji hii ilikuwa kumi na sita, kujumlisha na vijiji vyao.42Libna, Etheri, Ashani,43Ifuta, Ashina, Nezibu,44Keila, Akizibu, na Maresha. Hii ilikuwa ni miji tisa, kujumlisha na vijiji vyao.45Ekroni, pamoja na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka;46kutoka Ekroni kuelekea Bahari Kuu, makazi yote ambayo yalikuwa karibu na Ashidodi, pamoja na vijiji vyake.

47Ashidodi, na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; Gaza na miji na vijiji vyake vinavyoizunguka; hata kufika kijito cha Misri, na kuelekea Bahari Kuu pamoja na ukanda wake wa pwani.48Katika nchi ya milima, kuna miji ya Shamiri, Yatiri, Soko,49Dana, Kiriathi Sana (ambayo ndio Debiri),50Anabu, Eshitemo, Animu,51Gosheni, Holoni, na Gilo. Hii ilikuwa ni miji kumi na moja, kujumuisha na vijiji vyake.52Arabu, Duma, Ehani,53Yanimu, Bethi Tapua, Afeka,54Humta, Kiriathi Arba (ambayo ndio Hebroni), na Ziori. Hii ilikuwa miji tisa, pamoja na vijiji vyake.55Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta,56Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa,57Kaini, Gibea, na Timna. Hii ilikuwa ni miji kumi, kujumuisha na vijiji vyake.58Halhuli, Bethi Zuri, Gedori,59Maarathi, Bethi Anothi, na Elitekoni. Hii ilikuwa miji sita, pamoja na vijiji vyake.60Kiriathi Baali (ambayo ndio Kiriathi Yearimu), na Raba. Hii ilikuwa ni miji miwili, pamoja na vijiji vyake.61Katika nyika, kulikuwa na miji ya Bethi Araba, Midini, Sekaka,62Nibushani, mji wa chumvi, na Eni Gedi. Hii ilikuwa miji, pamoja na vijiji vyao.

63Lakini kwa Wayebusi, wenyeji wa Yerusalemu, kabila la Yuda halikuweza kuwafukuza, na hivyo, Wayebusi wanaishi pamoja na kabila la Yuda hadi leo hii.

16

1Nchi waliyopewa kabila la Yusufu ilianzia katika Yordani huko Yeriko, mashariki mwa chemichemi za Yeriko, kupitia nyikani, kupanda kutoka Yeriko kupitia nchi ya milima ya Betheli.2Kisha uliendelea kutoka Betheli hadi Luzi na kupita hata Atarothi, iliyo miliki ya Waarkiti.3Kisha ilishuka chini upande wa magharibi kuelekea himaya ya Wayafuleti, hadi kufika miliki ya Loweri Bethi Horoni, na kisha iliendelea hadi Gezeri; na ilikomea katika bahari.4Ilikuwa ni kwa njia hii makabila ya Yusufu, yaani Manase na Efraimu yalipata urithi wao.5Eneo la kabila la Efraimu ambalo lilikuwa limegawanya kwa koo zao lilikuwa kama ifuatavyo: mpaka wa urithi wao katika upande wa mashariki ulikuwa Atarothi Addari uliopanda kuelekea Bethi Horoni ya juu,6Na kutoka pale uliendelea hadi katika bahari. Kutoka Mikimethathi katika upande wa Kasikazini ulipinda upande wa mashariki kuelkea Taanathi Shilo na kupita ng'ambo yake katika upande wa mashariki kukabili Yanoa.7Kisha ulishuka kutoka Yanoa hadi Atarothi na hata Naara, na kisha ukafika Yeriko, na kuishia katika Yordani.8Kutoka Tapua, mpaka uliendelea katika upande wa magharibi hata kijito cha Kana na ulikomea katika bahari. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Efraimu, uliogawanywa katika koo zao,9pamoja na miji yao iliyochaguliwa kwa ajili ya kabila la Efraimu iliyokuwa ndani ya urithi wa kabila la Manase - miji yote pamoja na vijiji vyao.10Lakini hawakuwafukuza Wakanaani walioishi katika Gezeri, hivyo basi Wakanaani wanaishi ndani ya Efraimu hadi leo, lakini watu hawa walifanywa kuwa watumwa.

17

1Na huu ndio mgao wa nchi kwa ajili ya kabila la Manase (aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Yusufu), ambayo ilikuwa kwa ajili ya Makiri, mzaliwa wa kwanza wa Manase, ambaye alikuwa ni baba wa Gilieadi. Watoto wa Makiri walipewa nchi ya Gileadi na Bashani, kwa sababu Makiri alikuwa ni mtu wa vita.2Nchi iliyobaki iligawiwa kwa kabila la Manase, walipewa kwa koo zao, ambazo ni Abi Ezeri, Heleki, Asrieli, Shekemu, Heferi, na Shemida. Hawa walikuwa ni watoto wa kiume wa Manase mwana wa Yusufu, waliwakilishwa na koo zao.

3Basi Zelofe hadi mwana wa Heferi mwana wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase hakuwa na watoto wa kiume, bali alikuwa na watoto wa kike tu. Na majina ya binti zake yalikuwa Mahila, Noa, Hogla, Milka na Tirsa.4Walimwendea Eliazeri kuhani, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi na wakasema, “Yahweh alimwagiza Musa atupatie urithi wetu pamoja na kaka zetu.” Hivyo, kwa kuzingatia agizo la Yahweh, aliwapa wanawake hao urithi miongoni mwa ndugu za baba yao.5Manase alipewa sehemu kumi za nchi katika Gileadi na Bashani, ambayo iko upande mwingine wa Yordani,6kwa sababu ya binti za Manase walipokea urithi pamona na watoto wake wa kiume. Nchi ya Gileadi iligawanywa kwa kabila la Manase lililosalia.7Eneo la Manase lilianzia Asheri hadi Mikimethathi, ambayo iko mashariki mwa Shekemu. Kisha mpaka ulienda upande wa kusini kwa wale walioishi karibu na chemichemi ya Tapua.8(Nchi ya Tapua ilikuwa ni miliki ya Manase, lakini mji wa Tapua katika mpaka wa Manase ilikuwa ni mali ya kabila la Efraimu.)9Kisha mpaka ulishuka kuelekea kijito cha Kana. Miji hii kusini mwa kijito miongoni mwa miji ya Manase ilikuwa ni mali ya Efraimu. Mpaka wa Manase ulikuwa upande wa kaskazini wa kijito, na ulikomea katika10Bahari na nchi iliyokuwa upande wa kusini ilikuwa ni ya Efraimu, na nchi iliyo upande wa Kaskazini ilikuwa ni ya Manase; bahari ilikuwa ndio mpaka. Kwa upande wa kaskazini ulifika hata Asheri, na upande wa mashariki, Isakari11Pia katika Isakari na katika Asheri, Manase alimiliki Bethi Shani na vijiji vyake, Ibleamu na vijiji vyake, wenyeji wa Dori na vijiji vyake, wenyeji wa Endori na vijiji vyake, wenyeji wa Taanaki na vijiji vyake, na wenyeji wa Megido na vijiji vyake (na mji wa tatu ni Nafethi).12Lakini kabila la Manase halikuweza kuimiliki miji hiyo, kwa kuwa Wakanaani waliendelea kuishi katika nchi hii.13Hata wakati watu wa Israeli walipopata nguvu zaidi, hawakuwafukuza mbali kabisa Wakanaani, bali waliwafanya kuwa watumwa.

14Kisha wazawa wa Yusufu wakamwambia Yoshua, wakisema, “Kwa nini umetupa mgao mmoja wa nchi na sehemu moja kwa ajili ya urithi, kwa kuwa tuko wengi, na kwa muda wote Yahweh umetubaliriki?

15Yoshua akawaambia, “Kama ninyi ni watu wengi katika hesabu, pandeni ninyi wenyewe katika msitu na kuisafisha nchi kwa ajili yenu wenyewe katika nchi ya Waperezi na ya Refaimu. Fanyeni hivi kwa kuwa nchi ya milima ya Efraimu ni ndogo kwenu.”

16Wazawa wa Yusufu wakasema, “Nchi ya milima haitutoshi. Lakini Wakanaani wote wanaoishi katika bonde wana magari ya chuma, wote walio katika Bethi Shani na vijiji vyake, na wale walio katika bonde la Yezreeli.”

17Kisha Yoshua akawaambia nyumba ya Yusufu, ambao ni Efraimu na Manase, “Ninyi ni watu mlio wengi katika hesabu, na mna nguvu kubwa. Hamtakiwi kuwa na sehemu moja ya nchi mliogawiwa.18Nchi ya milima itakuwa yenu pia. Ingawa ni msitu, mtaufyeka na kuimiliki hata mipaka yake ya mbali. Mtawafukuzia mbali Wakanaani, ingawa wanayo magari ya chuma na ingawa pia wanazo nguvu.”

18

1Kisha kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika pamoja hapo Shilo. Walilijenga hema la kukutania hapo na waliishinda nchi mbele yao.2Kulikuwa na makabila saba miongoni mwa watu wa Israeli ambayo yalikuwa bado hayajapewa urithi wao.3Yoshua aliwaambia watu wa Israeli, “Je mtaacha mpaka lini katika kuingia nchi ambayo Yahweh, Mungu wa baba zenu, amewapeni ninyi?

4Chagueni ninyi wenyewe watu watatu kutoka katika kila kabila, na nitawatuma. Wataenda na kuipeleleza nchi juu na chini. Wataandika maelezo pamoja na maelekezo kuhusu urithi wao, na kisha watarudi kwangu.5Wataigawanya nchi katika sehemu saba. Yuda itasalia katika eneo lao upande wa kusini, na nyumba ya Yusufu itaendelea katika himaya yao katika upande wa kaskazini.6Mtaigawanya nchi katika sehemu saba na kisha mtaniletea maelezo hayo hapa kwangu. Nami nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh Mungu wetu.7Walawi hana sehemu miongoni mwenu, kwa kuwa ukuhani wa Yahweh ni urithi wao. Makabila ya Gadi, Rubeni na nusu ya kabila la Manase wameshapokea urithi wao ng'ambo ya Yordani. Huu ni urithi ambao Musa mtumishi wa Yahweh aliwapa wao.

8Hivyo, watu waliinuka na wakaenda. Yoshua akawaamuru wale walioenda kuandika maelezo ya nchi, akisema, “Pandeni juu na mshuke chini katika nchi na andikeni maelezo kuhusu nchi na kisha mrejee kwangu. Nitapiga kura kwa ajili yenu hapa mbele za Yahweh huko Shilo.9Watu walienda na walitembea juu na chini katika nchi na wakaandika maelezo kuihusu nchi hiyo juu ya gombo kwa miji yake katika sehemu saba, kwa kutaja miji, kila mmoja katika sehemu moja. Kisha wakarudi kwa Yoshua katika kambi huko Shilo.10Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao huko Shilo mbele za Yahweh. Na hapo Yoshua akaigawa nchi kwa watu wa Israeli, kila kabila lilipewa sehemu ya nchi.11Katika kabila la Benyamini, ugawanaji wa nchi ulifanyika kwa kupewa kwa koo zao. Eneo la nchi waliyopewa lilikuwa kati ya wazawa wa Yuda na wazawa wa Yusufu.12Katika upande wa kusini, mpaka wao ulianzia katika Yordani. Mpaka ulipanda hata sehemu ya juu kaskazini mwa Yeriko, na kisha ukapita katikati ya nchi ya milima upande wa magharibi. Huko ukafika hadi nyika ya Bethi Aveni.13Kutoka hapo mpaka ulipita upande wa kusini katika mwelekeo wa Luzi (sehemu ile ile inayoitwa Betheli). Kisha mpaka ukashuka chini hata Atarothi Addari, karibu na mlima uliolekea kusini mwa Bethi Horoni.14Kisha mpaka ukaendelea upande mwingine: katika upande wa magharibi uligeukia upande wa kusini, ulienda mbele kuukabili mlima ulio ng'ambo ya Bethi Horoni. Mpaka huu ulikomea huko Kiriathi Baali (ambao ndio Kiriathi Yearimu), mji ambao ulikuwa ni wa kabila la Yuda. Na huu ndio ulikuwa ni mpaka katika upande wa magharibi.15Katika upande wa kusini, mpaka ulianzia nje tu ya Kiriathi Yearimu. Mpaka uliendelea kutoka Efroni hata chemichemi ya maji ya Neftoa.16Kisha mpaka ulishuka chini hadi mpaka wa mlima ambao ulikuwa mkabala ya bonde la Beni Hinomu, ambalo lililokuwa katika upande wa kaskazini mwishoni mwa bonde la Refaimu. Kisha ulishuka chini kuelekea bonde la Hinomu, sehemu ya kusini mwa mteremko wa Wayebusi, na uliendelea kushuka chini hadi Eni Rogeli.17Ulizunguka upande wa kaskazini, kuelekea mwelekeo wa Eni Shemeshi, na kutoka hapa ulienda hadi Gelilothi, ambao ulikuwa mkabala na mwinuko wa Adumimu. Kisha ulishuka chini kuelekea Jiwe la Bohani mwana wa Rubeni.18Ulipita kuelekea upande wa kaskazini wa bega la Bethi Araba na chini kuelekea Araba.19Mpaka ulipita hadi upande wa bega la kaskazini la Bethi Hogla. Mpaka ulikome katika ghuba ya kaskazini mwa Bahari ya Chumvi, katika upande wa kusini mwishoni mwa Yordani. Huu ulikuwa ni mpaka wa upande wa kusini.20Yordani ulikuwa mpaka wake katika upande wa mashariki. Na huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Benyamini, na walipewa kwa kila ukoo wao, mpaka baada ya mpaka, kwa kuizunguka nchi yote.21Kwa hiyo sasa miji ya kabila la Benyamini kufuatana na koo zao ilikuwa ni Yeriko,22Bethi Hogla, Emeki Kezizi, Bethi Araba, Zemaraimu, Betheli,23Avimu, Para, Ofra,24Kefari Amoni, Ofini, a Geba. Ilikuwa ni miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.25Kulikuwa pia na miji ya Gibeoni, Rama, Beerothi,26Mizpe, Kefira, Moza,27Rekemu, Iripeeli, Tarala,28Zela, Haelefu, Yebusi (ambao ndio Yerusalemu), Gibea, na Kiriathi. Kulikuwa na miji kumi na nne, pamoja na vijiji vyake. Huu ulikuwa ni urithi wa Benyamini kufuatana na koo zao.

19

1Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.2Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,3Hazari Shuali, Bala, Ezemu,4Elitoladi, Bethuli na Horma.5Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,6Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile7Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.8Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.9Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwa sababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.10Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.11Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.12Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.13Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.14Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Efta Eli.15Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.16Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.17Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.18Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,19Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.20Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,21Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.22Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.23Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.24Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.25Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,26Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.27Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la iftaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.28Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.29Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,30Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.31Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.32Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.33Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.34Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.35Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinerethi,36Adama, Rama, Hazori,37Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.38Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.39Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.40Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.41Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,42Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.43Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,44Eliteke, Gibethoni, Baalathi,45Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,46Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.

47Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.48Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.

49Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.50Kwa amri ya YahweH walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.

51Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele ya Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.

20

1Baada ya hayo, Yahweh akamwambia Yoshua,2“Waambie watu wa Israeli, na kusema, ‘Chagueni miji ya makimbilio ambayo niliwaambia kupitia kwa Musa.3Fanyeni hivi ili mtu akiua mtu bila kukusudia aweze kwenda huko. Miji hii itakuwa ni sehemu ya kukimbilia kutoka kwa mtu yeyote yule anayetaka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu aliyeuliwa.

4Atakimbilia kwa mji mmoja miongoni mwa miji hiyo na atasimama mlangoni mwa lango la mji, na ataeleza kesi yake kwa wazee wa mji ule. Kisha watamwingiza ndani ya mji na watampatia sehemu yake ya kuishi miongoni mwao.5Na kama mtu akija akataka kulipiza kisasi kwa damu ya mtu yule ambaye aliuliwa, ndipo watu wa mji hawatatakiwa kumtoa kwa wenye mamlaka mtu huyo aliyeua. Hawaruhusiwi kufanya hivyo kwasababu alimuua jirani bila kukusudia na hakuwa na chuki naye hapo awali.6Ni lazima akae katika mji ule mpaka pale atakapokuwa amesimama mbele ya kusanyiko kwa ajili ya kuhukumiwa, hadi pale atakapokufa mtu yule anayetumika katika nafasi ya kuhani mkuu katka siku hizo. Na kisha mtu yule aliyeua bila kukusudia aweza kurudi nyumbani kwake, katika mji ule ulikotoka.

7Kwa hiyo, Waisraeli wakaichagua Kedeshi iliyoko Galilaya katika nchi ya milima ya Nafutali, Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na Kiriathi Arba (ambayo ndio Herbroni) katika nchi ya milima ya Yuda.8Katika ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko, walichagua mji wa Bezeri huko nyikani katika nyanda za kabila la Rubeni; na Ramothi Gileadi kutoka kabila la Gadi; na Golani katika Bashani, kutoka katika kabila la Manase.9Hii ni miji iliyochaguliwa kwa ajili ya watu wote wa Israeli na kwa ajili ya wageni wanaoishi miongoni mwao, ili kwamba mtu yeyote amuuaye mtu bila kukusudia aweza kukimbilia huko kwa ajili ya kupata usalama. Mtu huyu hatakufa kwa mkono wa mtu yule anayetaka kulipiza kisasi cha damu iliyomwagwa, mpaka hapo kwanza mtuhumiwa atakaposimama mbele ya kusanyiko la watu.

21

1Kisha wakuu wa koo za Walawi walimwendea Eliazari kuhani, na kwa Yoshua mwana wa Nuni, na kwa viongozi wa familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli.2Waliwaambia, “Yahweh aliwaamuru ninyi kwa mkono wa Musa kwamba mtupatieni miji ya kuishi yenye maeneo kwa ajili ya kuchungia ya mifugo.” Waliyasema haya huko Shilo katika nchi ya Kanaani.3Hivyo, kwa agizo la Yahweh, watu wa Israeli waliwapa Walawi kutoka katika urithi wa wao miji ifuatayo pamoja na maeneo yao ya kuchungia.

4Upigaji wa kura kwa ajili ya koo za Wakohathi ulileta matokeo haya: makuhani ambao ni wazawa wa Haruni ambao walitokana na Walawi, walipokea miji kumi na mitatu waliopewa kutoka kwa kabila la Yuda, kutoka kabila la Simoni, na kutoka kabila la Benyamini.5Koo zilizobaki za Wakohathi walipokea kwa kupiga kura kwa miji kumi kutoka katika kabila za Efraimu, Dani, na kutoka kwa nusu ya kabila la Manase.

6Na watu wazawa wa Gershoni walipewa miji kumi na mitatu kwa kupigiwa kura kutoka kwa koo za kabila la Isakari, Asheri, Nafutali, na nusu ya kabila la Manase katika Bashani.

7Watu waliokuwa wazawa wa Merari walipokea miji kumi na miwili kutoka katika makabila ya Rubeni, Gadi na Zabuloni.

8Basi, watu wa Israeli waliwapa Walawi miji hii pamoja na maeneo yao ya kuchungia, kwa kupiga kura, kama vile Yahweh alivyokuwa ameagiza kwa mkono wa Musa.9Kutoka kwa makabila la Yuda na Simoni, waliwapa nchi katika miji ifuatayo iliyo orodheshwa kwa majina.10Miji hii walipewa wazawa wa Haruni, ambao walikuwa miongoni mwa koo za Wakohathi, ambao walitoka katika kabila la Lawi. Kwa kuwa upigaji wa kura ya kwanza uliwaangukiwa wao.11Waisraeli waliwapatia Kiriathi Arba (Arba alikuwa ni baba wa Anaki), eneo hilo liliitwa pia Hebroni, katika nchi ya milima ya Yuda, pamoja na maeneo ya kulishia mifugo yaliyouzunguka mji.12Lakini mashamba ya mji na vijiji vyake vilikuwa tayari ameshapewa Kalebu mwana Yefune, kama mali yake.13Na kwa wana wa Haruni kuhani, waliwapa Hebroni pamoja na eneo lake la kulishia mifugo ambao ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia na Libna pamoja na maeneo ya kulishia mifugo.14Na Yatiri pamoja na maeno yake ya kuchungia, na Eshitemoa pamoja na maeneo yake ya malisho.15Lakini pia waliwapa Holoni pamoja na maeneo yake ya malisho, Debiri pamoja na maeneo yake ya malisho,16Aini pampoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Shemeshi pamoja na maeneo yake ya malisho. Ilikuwa ni miji kumi na tisa ambayo walipewa kutoka katika makabila haya mawili.17Kutoka katika kabila la Benyamini walipewa Gibea pamoja na maeneo yake ya malisho, na Geba pamoja na maeneo yake ya malisho,18na Anathothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na amoni pamoja na vitongoji vyake vinne.19Miji waliyopewa makuhani, wana wa Haruni, ilikuwa ni miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumlisha na maeneo yake ya malisho.20Na kwa ajili ya sehemu ya familia ya Kohathi iliyosalia, wale Walawi walio wa familia ya Kohathi, walipewa miji kutoka katika kabila la Efraimu kwa kupiga kura.21Walipewa Shekemu pamoja na maeneo yake ya malisho katika nchi ya milima ya Efraimu - mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu bila kukusudia, na Gezeri pamoja na maeneo yake ya malisho,22na Kibzaimu pamoja na maeneo yake ya malisho, na Bethi Horoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa miji minne kwa ujumla wake.23Kutoka katika kabila la Dani, ukoo wa Kohathi ulipewa Elteke pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gibethoni pamoja na maeneo yake ya malisho, na24Aijaloni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Gathrimoni pamoja na maeneo yake ya malisho, ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake.25Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, ukoo wa Kohathi walipewa miji miwili - Taanaki pamoja na maeneo yake ya malisho na Gathirimoni pamoja na maeneo yake ya malisho.26Kulikuwa na miji kumi kwa ujumla wake kwa ajili ya koo zilizosalia za Wakohathi, pamoja na maeneo yao ya malisho.27Kutoka katika nusu ya kabila la Manase, jamaa za Gershoni, ambazo hizi zilikuwa ni koo zingine za Walawi, zilipewa Golani katika Bashani pamoja na maeneo yao ya malisho, ni mji wa makimbilio kwa ajili ya mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia, sambamba na Beeshitera pamoja na maeneo yake ya malisho - ilikuwa miji miwili kwa ujumla.28Koo za Gershoni zilipewa pia miji minne kutoka kwa kabila la Isakari - Kishoni sambamba na maeneo yake ya malisho, Daberathi pamoja na maeneo yake ya malisho,29Yarmuthi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Enganimu pamoja na maeneo yake ya malisho.30Kutoka katika kabila la Asheri, walipewa miji minne kwa ujumla - Mishali pamoja na maeneo yake ya malisho, Abdoni pamoja na maeneo yake ya malisho,31Helikathi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Rehobu pamoja na maeneo yake ya malisho.32Kutoka kwa kabila la Nafutali, nasaba za Gershoni walipewa miji mitatu kwa ujumla - Kedeshi katika Galilaya pamoja na maeneo yake ya malisho, ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu yeyote aliyeua mtu bila kukusudia; na Hamothidori pamoja na maeneo yake ya malisho, na Kartani pamoja na maeneo yake ya malisho.33Kulikuwa na miji kumi na mitatu kwa ujumla, kujumuisha na maeneo yake ya malisho, kwa ajili ya koo za Gershoni.34Na kwa Walawi waliosalia, koo za Merari waliokuwa wamepewa kutoka katika kabila la Zabuloni: Yokneamu pamoa na maeneo yake ya marisho, Karta pamoja na maeneo yake ya malisho,35Dimna pamoja na maeneo yake ya malisho, na Nahalali pamoja na maeneo yake ya malisho- ilikuwa ni miji minne kwa ujumla.36Kwa mbari za Merari walipewa miji minne kutoka katika kabila la Rubeni: Bezeri pamoja na maeneo yake ya malisho, Yahazi pamoja na maene yake ya malisho,37na Kedemothi pamoja na maeneo yake ya malisho, na Mefaathi pamoja na maeneo yake ya malisho.38Kutoka katika kabila la Gadi walipewa miji ya Ramothi katika Gileadi pamoja na sehemu zake za malisho - huu ulikuwa ni mji wa makimbilio kwa mtu aliyeua mtu mwenzake bila kukusudia - na Mahanaimu pamoja na sehemu zake za malisho.39Koo za Merari zilipewa pia Heshiboni pamoja na maeneo yake ya malisho, na Yazeri pamoja na malisho yake.40Hii ilikuwa ni miji minne kwa ujumla wake. Hii yote ilikuwa ni miji ya koo kadhaa za Merari, ambao walitoka katika kabila la Lawi, miji kumi na miwili walipewa wao kwa kupiga kura.

41Miji waliyopewa Walawi kutoka katikati ya nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli ilikuwa miji arobaini na nane, kujumuisha na sehemu za malisho yao.42Miji hii kila mmoja ulikuwa na maeneo yake ya malisho kwa kuuzunguka mji. Miji hii yote ilikuwa hivyo.

43Basi Yahweh aliwapa Israeli nchi yote ambayo aliwaapia baba zao kuwa atawapa. Waisraeli waliimiliki nchi na wakakaa humo.44Kisha Yahweh akawapa pumziko kwa kila upande, kama tu alivyowaahidia baba zao. Hakuna hata adui mmoja atakayeweza kuwashinda. Yawheh aliwatia maadui wao wote mikononi mwao.45Hakuna hata kitu kimoja miongoni kwa ahadi nzuri ambazo Yahweh alizisema kwa nyumba ya Israeli ambazo hazikutimia. Ahadi zote zilitimia.

22

1Kwa wakati huo, Yoshua aliwaita Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase.2Aliwaambia, “Mmefanya kila kitu ambacho Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi. Mmeitii sauti yangu katika yote niliyowaagiza.3Bado hamjawaacha ndugu zenu hawa kwa siku zote hizi, mpaka siku hii ya leo. Na mmetimiza wajibu unaotakiwa na amri za Yahweh Mungu wenu.4Sasa Yahweh Mungu wenu amewapa pumziko ndugu zenu, kama alivyowaahidi. Hivyo basi, rudini na mwende katika hema zenu katika nchi mnayoimiliki, ambayo Musa mtumishi wa Yahweh aliwapeni katika upande mwingine wa Yordani.5Lakini zingatieni kuzishika amri na sheria ambazo Musa mtumishi wa Yahweh aliwaagiza ninyi, kumpenda Yahweh Mungu wenu, kutembea katika njia zake, kuzitunza amri zake, na kuambatana naye na kumwabudu yeye kwa moyo wenu wote na kwa roho zenu zote.

6Basi Yoshua akawabariki na kisha akawaacha waende zao, nao wakarudi katika hema zao.7Na kwa nusu ya kabila la Manase, Musa alikuwa amewapa urithi katika Bashani, lakini kwa nusu ya kabila hilo, Yoshua aliwapa urithi karibu na ndugu zao katika nchi magharibi mwa Yordani. Yoshua aliwaaga waende katika hema zao; aliwabarikia,8na kisha akawaambia, “Rudini katika hema zenu mkiwa na pesa nyingi, na mkiwa na mifugo mingi, pamoja na na fedha, na dhahabu, na shaba na chuma, na nguo nyingi. Gawaneni na ndugu zenu nyara mlizochukua kutoka kwa maadui zenu.

9Hivyo, wazawa wa Rubeni, wazawa wa Gadi na nusu ya kabila la Manase walirudi nyumbani, waliwaacha watu wa Isaeli hapo Shilo, ambayo imo ndani ya nchi ya Kanaani. Waliondoka wakaenda katika mkoa wa Gileadi, katika nchi yao, ambayo wao wenyewe waliimiliki, katika utiifu wa amri za Yahweh, kwa mkono wa Musa.

10Nao walipofika hapo Yordani iliyo katika nchi ya Kanaani, Warubeni na Wagadi na nusu ya kabila la Manase walijenga madhabahu karibu na Yordani, madhabahu kubwa na iliyotokeza na mashuhuri.11Watu wa Israeli walisikia habari hizo na wakaseama, “Tazama! Watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wamejenga madhabahu mbele ya nchi ya Kanaani, huko Gelilothi, katika mkoa karibu na Yordani, katika upande ambao ni miliki ya watu wa Israeli.”12Wakati watu wa Israeli waliposikia hivyo, kusanyiko lote la watu wa Israeli walikusanyika kwa pamoja huko Shilo ili wapande kupigana vita nao.

13Kisha watu wa Israeli walituma wajumbe kwa Warubeni, Wagadi na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi. Walimtuma pia Finehasi mwana wa Eliezari, kuhani,14na viongozi kumi pamoja naye, mmoja kutoka katika familia za mababa wa Israeli, na kila mmoja wao alikuwa ni kiongozi wa ukoo miongoni mwa watu wa Israeli.

15Walienda kwa watu wa Rubeni, Gadi, na nusu ya kabila la Manase, katika nchi ya Gileadi, na wakawaambia:16“Kusanyiko lote la Yahweh linasema kuwa, ‘Ni jambo gani hili lisilo la uaminifu ambalo mmelitenda kinyume na Mungu wa Israeli, kwa kugeuka badala ya kumfuata Yahweh siku hii na kujijengea wenyewe madhabahu katika uasi kinyume na Yahweh katika siku hii?17Je dhambi zetu huko Peori hazikututosha? Bado hata sasa hatujajitakasa wenyewe kwa dhambi hiyo. Kwa ajili ya dhambi ile lilikuja pigo kwa kusanyiko lote la Yahweh.18Je, nanyi leo pia mwageuka na kuacha kumfuata Yahweh? Kama mtaasi kinyume na Yahweh leo, kesho atakuwa na hasira na kusanyiko lote la Israeli.

19Na kama nchi ambayo mnaimiliki imetiwa unajisi, basi mwaweza kuvuka katika nchi ambayo Sanduku la Yahweh lasimama na mjichukulie kwa ajili yenu umiliki miongoni mwetu. Hamtakiwi kuasi kinyume na Yahweh tu, wala kuasi kinyume chetu kwa kujenga madhabahu kwa ajili yenu wenyewe badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu.20Je hakuwa Akani mwana wa Zera aliyeivunja imani kwa vitu vile ambavyo vilikuwa vimetunzwa kwa ajili ya Mungu? Na je ghadhabu ya Mungu haikushuka kwa watu wote wa Israeli? Mtu yule hakuangamia peke yake kwa uovu wake.

21Kisha makabila ya Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase wakawajibu wazee wa koo za Israeli:22“Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yahweh, Mungu Mwenye nguvu! Yeye anajua, na Israeli naijua yenyewe! Kama ilikuwa ni katika uasi au katika kuvunja imani kinyume na Yahweh, msituache hai katika siku hii ya leo,23kwa ajili ya kujenga madhabahu ili tugeuka na kuacha kumfuata Yahweh. Kama tumejenga madhabahu hii ili kutoa juu yake sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya nafaka, au sadaka ya amani, basi Yahweh na atuadhibu.

24La hasha, tulifanya hivyo kwa sababu ya hofu kwamba katika siku zijazo watoto wenu wanaweza kuwaambia watoto wetu, ‘Mna nini ninyi na Yahweh, Mungu wa Israeli?25Kwa kuwa Yahweh ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi. Ninyi watu wa Rubeni na watu wa Gadi, hamna kitu chochote na Yahweh.’ Na kwa hali hiyo, watoto wenu wanaweza kuwafanya watoto wetu waache kumwabudu Yahweh.

26Basi tukasema, ‘Hebu na tujenge sasa madhabahu, si kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa wala si kwa sadaka yoyote ile,27ila iwe ni ushahidi kati yetu na ninyi, na kati ya kizazi chetu baada yetu, kwamba tutafanya ibada ya Yahweh mbele yake, pamoja na sadaka zetu za kuteketezwa na dhabihu zetu na sadaka zetu za amani, ili kwamba watoto wenu wasiweze kuwaambia watoto wetu katika siku zijazo kuwa, “Hamna sehemu katika Yahweh.”’

28Hivyo tukasema, ‘kama hili litasemwa kwa kwetu au kwa watoto wetu katika siku zijazo, tutasema, “Tazama! Huu ni mfano wa madhabahu ya Yahweh, ambayo mababu zetu waliifanya, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala si kwa dhabihu, bali kwa ajili ya ushahidi kati yetu ninyi.”29Na iwe mbali nasi kwamba tunataka kugeuka kinyume na Yahweh, na kuacha kumfuata yeye kwa kujenga madhabahu kwa ajili sadaka ya kuteketezwa, na kwa sadaka ya nafaka, au kwa dhabihu, badala ya madhabahu ya Yahweh Mungu wetu ambayo iko mbele ya hema la kukutania.’

30Finehasi kuhani na viongozi wa watu, ambao ni wakuu wa koo za Waisraeli ambao walikuwa pamoja naye, waliposikia maneno amabayo watu wa Rubeni, Gadi na nusu ya kabila la Manase, kwamba yalikuwa ni mazuri machoni pao.31Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani aliwaambia watu wa Rubeni, Gadi na Manase, “Leo tumejua kwamba Yahweh yuko miongoni mwetu, kwa kuwa hamjatenda uvunjaji wa imani kinyume naye. Sasa, mmewaokoa watu wa Israeli kutoka katika mkono wa Yahweh.”

32Kisha Finehasi mwana wa Eliazeri kuhani, na viongozi walirudi kutoka kwa Warubeni na Wagadi, kutoka katika nchi ya Gileadi, na kurudi katika nchi ya Kanaani, kwa watu wa Israeli, na waliwaletea taarifa.33Taarifa yao ilikuwa nzuri katika macho ya watu wa Israeli. Watu wa Israeli walimbarikia Mungu na hawakuendelea kusema tena juu ya kuinua vita dhidi ya Warubeni na Wagadi, ili kuiharibu nchi ambayo walikuwa wanaishi.

34Warubeni na Wagadi waliita ile madhabahu “Ushahidi,” kwa kuwa walisema, “Ni ushahidi miongoni mwetu kuwa Yahweh ni Mungu.”

23

1Na baada ya siku nyingi, kipindi ambacho Yahweh alikuwa ameipa Israeli pumziko kutoka maadui zao waliowazunguka,

2Yoshua alikuwa mzee sana. Yoshua aliwaita Waisraeli wote, na wazee wao, na viongozi, na waamuzi, na kwa maafisa, na kisha akawaambia, “Mimi nimezeeka sana.3Mmeshaona kila kitu ambacho Yahweh Mungu wenu ameshafanya kwa mataifa haya yote kwa ajili yenu, kwa kuwa ni Yahweh Mungu wenu ambaye amewapigania ninyi.4Tazama! Nimeshawakabidhi kwenu mataifa yaliyosalia ili kuyateka kwa ajili ya kupata urithi ya makabila yenu, sambasamba na mataifa yote ambayo tayari nimeshayaangamiza, tangu Yordani hadi Bahari kuu katika upande wa magharibi.5Yahweh Mungu wenu atayaondoa. Atayafukuzia mbali kutoka kwenu. Ataiteka nchi yao, nanyi mtaimiliki nchi yao, kama vile Yahweh Mungu wenu alivyowaahidi ninyi.

6Hivyo, iweni jasiri, ili kwamba mtunze na kuyafanya yale yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa, msikengeuke upande wa kulia wala upande wa kushoto,7Basi msichanganyikane na mataifa haya ambayo yamesalia miongoni mwenu, wala msiyataje majina ya miungu yao, wala msiape kwao, wala msiiabudu, wala msiipigie magoti.8Badala yake, mnatakiwa kumshika sana Yahweh Mungu wenu kama vile mlivyofanya siku hii ya leo.

9Kwa kuwa Yahweh ameyafukuzia mbali mbele yenu mataifa makubwa yenye nguvu. Hakuna hata mmoja aliyeweza kusimama mbele yenu hata siku hii ya leo.10Mtu yeyote mmoja wa kwenu atawafanya watu elfu wakimbie mbali, kwa kuwa Yahweh Mungu wenu, ndiye anayepigania ninyi, kama vile alivyowaahidi.11Zingatieni kwa uangalifu ili mmpende Yahweh Mungu wenu.

12Lakini kama mkiegeuka na kushikamana na watu walioathiriwa na mataifa haya waliobaki miongoni mwenu, au kuoana nao, au kama mkishirikiana pamoja nao, na wao pamoja nanyi,13Jueni kwa hakika kwamba Yahweh Mungu wenu hatayafukuzia mbali mataifa haya yatoke kati yenu. Badala yake, watakuwa kitanzi na mtego kwenu, viboko migongoni mwenu na miiba machoni mwenu, mpaka pale mtakapoangamia katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.

14Na sasa ninaenda katika njia ya dunia yote, na mnajua kwa moyo na roho zenu zote kwamba hakuna hata neno moja ambalo halijatimia kati ya mambo yote mazuri ambayo Yahweh Mungu wenu aliyaahidi juu yenu. Vitu hivi vyote vimetokea kwa ajili yenu. Hakuna hata moja lililoshindikana.15Lakini kama kila neno ambalo Yahweh Mungu wenu alilowaahidi limekwisha kutimia, hivyo Yahweh atawaletea juu yenu mabaya yote mpaka pale atakapokuwa amewaangamiza katika nchi hii nzuri ambayo Yahweh Mungu wenu amewapeni ninyi.16Atafanya hivi kama mtalivunja agano la Yahweh Mungu wenu, ambalo aliwaagizeni kulitunza. Kama mtaenda na kuiabudu miungu mingine na kuiinamia, ndipo hasira ya Yahweh itawaka kinyume nanyi, na ninyi mtaangamia upesi katika nchi nzuri ambayo amekwisha kuwapeni ninyi.”

24

1Kisha Yoshua aliyakusanya pamoja makabila yote ya Israeli huko Shekemu na aliwaita wazee wa Israeli, viongozi, waamuzi na maafisa wao, nao wakajihudhurisha mbele za Mungu.2Yoshua akawaambia watu wote, “Hiki ndicho Yahweh, Mungu wa Israeli anachokisema, ‘Mababu zenu kwa miaka mingi iliyopita waliishi ng'ambo ya mto Frati - Tera, baba wa Ibrahimu na baba wa Nahori - nao waliabudu miungu mingine.3Lakini nilimchukua baba yenu kutoka ng'ambo ya Frati na nikamwongoza mpaka katika nchi ya Kanaani, na nilimpa watoto wengi kupitia kwa Isaka mwanaye.4Na Isaka nikampa Yakobo na Esau. Nilimpa Esau nchi ya milima ya Seiri ili aimiliki, lakini Yakobo na watoto wake walishuka kwenda Misri.

5Nilimtuma Musa na Haruni, na niliwapiga Wamisri kwa mapigo. Baada ya hapo, niliwatoa ninyi.6Niliwatoa baba zenu nje ya nchi ya Misri, nanyi mkafika hata katika bahari. Wamisri waliwafuata kwa magari na wapanda farasi hata katika bahari ya matete.7Na baba zenu walipomwita Yahweh aliweka giza kati yenu na Wamisri. Aliileta bahari ije juu yao na kuwafunika. Mliona yale niliyoyafanya huko Misri. Kisha mliishi jangwaani kwa muda mrefu.

8Niliwaleta katika nchi ya Waamori, ambao waliishi katika upande mwingine mwa Yordani. Walipigana nanyi, nami niliwatia katika mkono wenu. Mliimiliki nchi yao, nami niliwaangamiza mbele yenu.9Kisha Balaki mwana wa Zipori, mfalme wa Moabu, aliinuka na kuishambulia Israeli. Alimwita na kumtuma Baalamu mwana wa Beori, ili kuwalaani ninyi.10Lakini sikumsikiliza Balaamu. Kwa hakika, aliwabarikia ninyi. Basi, niliwaokoa na mkono wake.

11Mlivuka Yordani na mkafika Yeriko. Viongozi wa Yeriko waliinuka wapigane nanyi, pamoja na Waamori, Waperizi, Wakanaani, Wahiti, Wagirgashi, Wahivi na Wayebusi. Niliwapa ninyi ushindi dhidi yao na niliwaweka chini ya mamlaka yenu.12Nilituma manyingu mbele yenu, ambayo yaliwafukuzia mbali na wafalme wawili wa Waamori watoke mbele yenu. Haikutokea kwa sababu ya upanga wenu wala kwa upinde wenu.13Niliwapeni ninyi nchi ambayo hamkuifanyia kazi na miji ambayo hamkuijenga, na sasa mnaishi ndani yake. Mnakula matunda ya mizabibu na na mashamba ya mizeituni ambayo hamkuyapanda.’

14Basi sasa mcheni Yahweh na kumwabudu yeye kwa uadilifu na uaminifu wote; jitengeni na miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati na katika Misri, na mkamwabudu Yahweh.15Na kama inaonekana kuwa ni vibaya machoni penu kumwabudu Yahweh, chagueni ninyi katika siku hii ya leo ni nani mtakayemtumikia, kama ni miungu ambayo baba zenu waliiabudu ng'ambo ya Frati, au miungu ya Waamori, ambao ninyi mnakaa ndani ya nchi yao. Lakini kwangu mimi na nyumba yangu, tutumwabudu Yahweh.”

16Watu walijibu na kusema, “Hatutaweza kumwacha Yahweh na kuitumikia miungu mingine,17kwa kuwa ni Yahweh Mungu wetu ambaye alitutoa sisi na baba zetu kutoka katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa, na ambaye alifanya hizo ishara kubwa mbele yetu, na ambaye alituhifadhi sisi katika njia zote ambazo sisi tuliziendea, na miongoni mwa mataifa yote ambayo tulipita kati kati yake,18Na Yahweh aliwaondoa mbele yetu watu wote, na Waamori walioishi katika nchi hii. Hivyo, tutamwabudu Yahweh pia, kwa kuwa ni Mungu wetu”

19Lakini Yoshua akawaambia watu, “Hamwezi kumtumikia Yahweh, kwa kuwa ni Mungu mtakatifu; ni Mungu mwenye wivu; hatawasamehe makosa na dhambi zenu.20Kama mtamwacha Yahweh na kuabudu miungu wa kigeni, basi atageuka na kuwaharibu. Atawaangamizeni baada ya kuwa amewatendea mema.”21Lakini watu walimwambia Yoshua, “Hapana, tutamwabudu Yahweh.”

22Kisha Yoshua akawaambia watu, “Ninyi ni mashahidi dhidi yenu wenyewe kuwa mmemchagua Yahweh ninyi wenyewe, ili mmwabudu yeye.” Watu walijibu, “Sisi ni mashahidi.”23“Sasa wekeni mbali miungu ya kigeni iliyoko kwenu, na geuzeni mioyo yenu mmwelekee Yahweh, Mungu wa Israeli.”24Watu wakamwambia Yoshua, “Tutamwabudu Yahweh Mungu wetu. Tutaisikiliza sauti yake.

25Yoshua alifanya agano na watu siku hiyo. Aliziweka maagizo na sheria huko Shekemu.26Yoshua aliyaandika maneno haya katika kitabu cha sheria za Mungu. Alichukua jiwe kubwa na kulisimamisha hapo chini ya mti wa mwaloni uliokuwa karibu na mahali patakatifu pa Yahweh.27Yoshua akawaambia watu, “Tazama, jiwe hili litakuwa ushuhuda dhidi yenu. Limeyasikia maneno yote ambayo Yahweh alitwambia. Hivyo, litakuwa ni shahidi dhidi yenu, hamtakiwi kumkana Mungu wenu.”28Basi Yoshua aliwaacha watu waende zao, kila mmoja alienda kwenye urithi wake.

29Baada ya mambo haya, Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Yahweh, alikufa akiwa na miaka 110.30Walimzika katika mpaka wa urithi wake mwenyewe huko Timnathi Sera, ambayo iko kwenye nchi ya milima ya Efraimu, upande wa Mlima Gaashi.31Israeli ilimwabudu Yahweh siku zote za maisha ya Yoshua, na siku zote za wazee ambao walidumu pamoja na Yoshua, wale ambao waliona kila kitu ambacho Yahweh alikuwa ameifanyia Israeli.32Mifupa ya Yusufu ambayo watu wa Israeli waliileta kutoka Misri, waliizika huko shekemu, katika sehemu ya nchi ambayo Yakobo alikuwa ameinunua kutoka kwa wana wa Hamori, baba wa Shekemu. Aliinunua kwa vipande mia moja vya fedha, na ulikuwa urithi kwa wazawa wa Yusufu.33Eliazeri mwana wa Haruni alikufa pia. Walimzika huko Gibea, katika mji ambao alikuwa amepewa Finehasi mwanaye, na ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu.

Waamuzi

1

1Baada ya kifo cha Yoshua, wana wa Israeli walimuuliza Yahweh wakisema, “Ni nani atawashambulia kwanza Wakanaani kwa ajili yetu, ili kupigana nao?”

2Yahweh akasema, “Yuda atawashambulia. Tazama, nimewapa kumiliki nchi hii.”

3Watu wa Yuda wakawaambia wana wa Simeoni, ndugu zao, “Njoo pamoja nasi katika eneo letu ambalo tumepewa ili kwa pamoja tupigane na Wakanaani. Na sisi pia tutakwenda nanyi katika eneo mlilopewa.” Basi kabila la Simeoni wakaenda pamoja nao.

4Watu wa Yuda wakashinda, na Bwana akawapa ushindi juu ya Wakanaani na Waperizi. Wakawaua watu elfu kumi huko Bezeki.5Wakamkuta Adoni Bezeki huko Bezeki, nao wakapigana naye na kuwashinda Wakanaani na Waperizi.6Lakini Adoni Bezeki akamkimbilia, wakamfuata na kumshika, nao wakavikata vidole gumba na vidole vyake vikubwa.

7Adoni Bezek akasema, “Wafalme sabini, ambao na vidole gumba vyao na vidole vikubwa vilivyokatwa, walikusanya chakula chao chini ya meza yangu. Kama nilivyofanya, hata hivyo Mungu amefanya kwangu.” Wakamleta Yerusalemu, naye akafa huko.

8Watu wa Yuda wakapigana dhidi ya jiji la Yerusalemu na kulichukua. Walishambulia kwa makali ya upanga na wakauwasha mji kwa moto.

9Baada ya hayo, watu wa Yuda walikwenda kupigana na Wakanaani waliokaa mlimani, Negebu, na magharibi mwa milima.10Yuda akaenda dhidi ya Wakanaani waliokaa Hebroni (jina la Hebroni hapo awali ilikuwa Kiriath-arba), nao wakamshinda Sheshai, Ahimani na Talmai.

11Kutoka huko watu wa Yuda walipigana na wenyeji wa Debiri (jina la Debiri hapo awali ilikuwa Kiriath-seferi).12Kalebu akasema, “Yeyote atakayeivamia Kiriath-seferi na kuichukua, nitampa Aksa, binti yangu, awe mkewe.”13Othnieli, mwana wa Kenazi, ndugu mdogo wa Kalebu, akaiteka Debiri, naye Kalebu akampa Aksa, binti yake, awe mkewe.

14Ndipo Aksa alifika kwa Othnieli, naye akamsihi amuombe baba yake ampe shamba. Alipokuwa akishuka katika punda wake, Kalebu akamwuliza, “Nikufanyie nini?”

15Akamwambia, “Nibariki. Kwa kuwa umenipa nchi ya Negebu, nipe pia chemchemi za maji.” Kwa hiyo Kalebu akampa chemchemi za juu na chemchemi za chini.

16Kizazi cha Mkeeni shemeji yake na Musa, walikwenda kutoka mji wa Mitende pamoja na watu wa Yuda, mpaka jangwa la Yuda, kuishi na watu wa Yuda karibu na Arad iliyoko upande wa kusini.

17Nao watu wa Yuda wakaenda pamoja na wana wa Simeoni ndugu zao, wakawaangamiza Wakanaani waliokaa Zefathi, wakaiharibu kabisa. Mji uliitwa Horma.18Watu wa Yuda pia waliiteka Gaza na nchi iliyoizunguka, Ashkeloni na nchi iliyoizunguka, na Ekron na nchi iliyoizunguka.19Yahweh alikuwa pamoja na watu wa Yuda na wakaimiliki nchi ya milima, lakini hawakuweza kuwatoa wenyeji wa kwenye bonde kwa sababu walikuwa na magari ya chuma.

20Hebroni alipewa Kalebu (kama Musa alivyosema), naye akawafukuza kutoka huko wana watatu wa Anaki.21Lakini wana wa Benyamini hawakuwafukuza Wayebusi waliokaa Yerusalemu. Basi Wayebusi wakakaa na watu wa Benyamini huko Yerusalemu hata leo.

22Nyumba ya Yusufu ilijiandaa kuishambulia Betheli, na Yahweh alikuwa pamoja nao.23Walipeleka watu kuipeleleza Betheli (jina la mji huo hapo kwanza uliitwa Luzu).24Wapelelezi waliona mtu akitoka nje ya jiji, wakamwambia, “Tafadhali tuonyeshe jinsi ya kuingia ndani ya mji, na tutakutendea mema.”25Aliwaonyesha njia ya kuingia kwenye mji. Waliuteka mji kwa makali ya upanga, lakini wakamuacha mtu huyo na ndugu zake wote waondoke.26Na mtu huyo akaenda nchi ya Wahiti, akajenga mji, akauita Luzu, ambalo jina lake hata leo.

27Watu wa Manase hawakuwafukuza watu waliokuwa katika miji ya Bethsheani na vijiji vyake, au Taanaki na vijiji vyake, au wale waliokaa Dori na vijiji vyake, wala wale waliokaa Ibleamu na vijiji vyake, wala walioshi Megido na vijiji vyake, kwa sababu Wakanaani walikuwa wameamua kuishi katika nchi hiyo.28Israeli ipokuwa na nguvu, waliwalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu, lakini hawakuwafukuza kabisa.29Efraimu hakuwafukuza Wakanaani waliokaa Gezeri; kwa hiyo Wakanaani wakakaa kati yao.30Zebuloni hakuwafukuza watu wa Kitroni, wala watu waliokuwa Nahaloli; na Wakanaani wakaendelea kuishi pamoja nao; lakini Zabuloni akawalazimisha Wakanaani wawatumikie kwa kazi ngumu.31Asheri hakuwafukuza watu wanaoishi Aka, au watu wanaoishi Sidoni, au wale wanaoishi Alabu, Akzib, Helba, Afeka, au Rehobu.32Kwa hiyo kabila ya Asheri iliishi kati ya Wakanaani (waliokaa katika nchi hiyo), kwa sababu hawakuwafukuza.33Na kabila la Naftali halikuwafukuza watu waliokuwa wakiishi Bethshemeshi, wala waliokuwa wakiishi Bethanathi. Kwa hiyo kabila la Naftali liliishi kati ya Wakanaani (watu waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo). Hata hivyo, wenyeji wa Bethshemeshi na Bethanathi walilazimishwa kufanya kazi ngumu kwa Naphthali.34Waamori waliwalazimisha kabila la Dani kuishi katika nchi ya kilima, hawakuwaruhusu kuja bondeni.35Basi Waamori waliishi katika mlima wa Heresi, huko Aiyaloni, na Shaalbimu, lakini nguvu za kijeshi za nyumba ya Yusufu ziliwashinda, nao wakalazimishwa kuwatumikia kwa kazi ngumu.36Mpaka wa Waamori ulikuwa kutoka kilima cha Akrabimu huko Sela hadi nchi ya vilima.

2

1Malaika wa Bwana akatoka Gilgali, akaenda Bokimu, akasema, “Nimekuleta kutoka Misri, na nimekuleta katika nchi niliyoapa kuwapa baba zako.2Nikasema, ‘Sitalivunja kamwe agano langu na wewe. Usifanye agano na wale wanaoishi katika nchi hii. Ziangushe madhabahu zao. Lakini hukusikiliza sauti yangu. Je! Ni nini hiki ulichokifanya?’3Basi sasa nasema, ‘Sitawafukuza Wakanaani mbele yenu, nao watakuwa miiba kwenu, na miungu yao itakuwa mtego kwa ajili yenu.’”

4Malaika wa Bwana alipowaambia maneno hayo kwa watu wote wa Israeli, watu wakapiga kelele na kulia.5Waliita mahali hapo Bokimu. Hapo wakatoa dhabihu kwa Bwana.

6Yoshua alipowaruhusu watu waende zao, wana wa Israeli kila mmoja akaenda mahali alipopewa, wakiwa na umiliki wa ardhi yao.7Watu walimtumikia Bwana wakati wa maisha ya Yoshua na wazee walioendelea baada yake, ni wale waliokuwa wameona matendo yote makuu ya Bwana aliyoyafanya kwa Israeli.

8Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, alikufa akiwa na umri wa miaka 110.9Wakamzika ndani ya mpaka wa nchi aliyopewa huko Timnath Heresi, katika mlima wa Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaash.

10Kizazi hicho chote kilikusanyika kwa baba zao. Kizazi kingine kilichofuata baada yao ambao hakikumjua Bwana au kile alichokifanya kwa Israeli.11Watu wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.12Wakaondoka kwa Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa kutoka Misri. Wakaifuata miungu mingine, miungu ya watu waliokuwa karibu nao, nao wakaisujudia. Wakamkasirisha BWANA kwa sababu13waliondoka kwa Bwana na kumwabudu Baal na Maashtoreti.14Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao. Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao.15Israeli walipokwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda, kama alivyowaapia. Na walikuwa katika shida kali.

16Ndipo Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa katika mikono ya wale waliokuwa wakiiba mali zao.17Hata hivyo hawakuwasikiliza waamuzi wao. Hawakuwa waaminifu kwa Bwana na wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao-wale waliotii amri za Bwana-lakini wao wenyewe hawakufanya hivyo.18Bwana aliinua waamuzi kwa ajili yao, Bwana akawasaidia waamuzi na kuwakomboa kutoka kwa mikono ya adui zao siku zote muamuzi aliishi. Bwana aliwahurumia walipougua kwa sababu ya wale waliowadhulumu na kuwasumbua.19Lakini mwamuzi alipokufa, waligeuka na kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko baba zao walivyofanya. Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.

20Hasira ya Bwana iliwaka juu ya Israeli; akasema, “Kwa sababu taifa hili limevunja masharti ya agano langu ambalo nililiweka kwa ajili ya baba zao-kwa sababu hawakuisikiliza sauti yangu.21Tangu sasa sitaliondoa mbele yao taifa lolote aliloliacha Yoshua baada ya kufa.22Nitafanya hivi ili kuwajaribu Israeli, ikiwa watafuata njia ya Bwana au sivyo, kama vile baba zao walivyoifuata.”23Ndiyo sababu Bwana aliwaacha mataifa hayo, wala hakuwafukuza haraka na kuwatia mikononi mwa Yoshua.

3

1Sasa Bwana aliyaacha mataifa haya yaijaribu Israeli, yaani kila mtu katika Israeli ambaye hakushiriki vita yoyote huko Kanaani.2(Alifanya hivyo ili kuwafundisha vita kizazi kipya cha Waisraeli ambao hawakujua kabla).3Haya ndio mataifa: wafalme watano kutoka kwa Wafilisti, Wakanaani wote, Wasidoni, na Wahivi waliokaa milima ya Lebanoni, kutoka Mlima Baali Hermoni hadi Hamathi.4Mataifa haya yaliachwa kama njia ambayo Bwana angeijaribu Israeli, kuthibitisha kama watazitii amri alizowapa babu zao kupitia Musa.5Basi wana wa Israeli wakakaa kati ya Wakanaani, na Wahiti, na Waamori, na Waperizi, na Wahivi, na Wayebusi.6Waliwachukua binti zao kuwa wake zao, nao wakawapa wana wao binti zao, nao wakaitumikia miungu yao.

7Wana wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wakamsahau Bwana, Mungu wao. Waliabudu Baali na Asherah.8Basi, hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawauza mkononi mwa Kushan-rishathaimu mfalme wa Aram Naharaimu. Watu wa Israeli walitumikia Kushan Rishathaimu kwa miaka nane.9Watu wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamuinua mtu atakayewasaidia wana wa Israeli, na mtu atakayewaokoa: Othnieli mwana wa Kenazi (ndugu mdogo wa Kalebu).10Roho wa Bwana akamtia nguvu, naye akahukumu Israeli na akatoka kwenda vitani. Bwana akampa kuishinda Kush-rishataimu mfalme wa Aramu. Mkono wa Othnieli alishinda Kushan Rishathaimu.11Nchi ilikuwa na amani kwa miaka arobaini. Ndipo Otinieli mwana wa Kenazi akafa.

12Baada ya hayo, Waisraeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; Bwana akampa Egloni mfalme wa Moabu nguvu, kuwashinda Waisraeli.13Eglon alijiunga na wana wa Amoni na Waamaleki wakaenda na kuwashinda Israeli, na walichukua mji wa Mitende.14Watu wa Israeli walimtumikia Eglon mfalme wa Moabu kwa miaka kumi na nane.

15Wana wa Israeli walipomwomba Bwana, Bwana akamwinua mtu aliyewasaidia, Ehudi mwana wa Gera, Mbenjamini, mtu shoto. Wana wa Israeli wakamtuma kwa Egloni, mfalme wa Moabu, kwa malipo yao ya kodi.16Ehudi akajifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wa dhiraa moja; aliufunga chini ya nguo zake juu ya mguu wake wa kulia.17Akampa Egloni Mfalme wa Moabu malipo ya kodi. (Egloni alikuwa mtu mnene sana.)18Baada ya Ehudi kulipa malipo ya kodi, aliondoka na wale waliokuwa wameibeba.19Hata hivyo Ehudi mwenyewe, alipofikia mahali ambapo sanamu za kuchonga zilitengenezwa karibu na Gilgali, akageuka na kurudi, akasema, “Nina ujumbe wa siri kwako, mfalme wangu.” Eglon akasema, “Nyamazeni kimya!” Kwa hiyo wote waliomtumikia wakatoka kwenye chumba.

20Ehudi akaja kwake. Mfalme alikuwa amekaa peke yake katika chumba cha juu cha baridi. Ehudi akasema, “Nina ujumbe kutoka kwa Mungu kwa ajili yako.” Mfalme akasimama kutoka katika kiti chake.21Ehudi akanyoosha mkono wake wa kushoto na akachukua upanga kutoka mguu wake wa kulia, na akautia ndani ya mwili wa mfalme.22Na kipini cha upanga kikaingia ndani yake baada ya upanga, nao ukatokea nyuma yake, na mafuta yakashikamana juu ya upanga, kwa kuwa Ehudi hakuutoa upanga nje ya mwili wake.23Kisha Ehudi akatoka kwenye ukumbi na akafunga milango ya chumba cha juu nyuma yake na akamfungia.

24Baada ya Ehudi kuondoka, watumishi wa mfalme wakaja; wakaona milango ya chumba cha juu imefungwa, kwa hiyo wakafikiri, “Hakika atakuwa anajitoa mwenyewe katika hali ya baridi ya chumba cha juu.”25Walizidi kuwa na wasiwasi hata walipoanza kuhisi kuwa walikuwa wakipuuza wajibu wao wakati mfalme bado hakufungua milango ya chumba cha juu. Kwa hiyo walichukua ufunguo wakaifungua, tazama bwana wao, ameanguka chini, amekufa.

26Wakati watumishi wakisubiri, wakijiuliza nini wanapaswa kufanya, Ehudi alikimbia na kupita mahali ambako kulikuwa na sanamu za kuchonga, na hivyo akakimbia kwenda Seira.27Alipofika, alipiga tarumbeta katika nchi ya mlima wa Efraimu. Kisha wana wa Israeli wakashuka pamoja naye kutoka milimani, naye akawaongoza.

28Akawaambia, “Nifuate, kwa kuwa Bwana atawashinda adui zenu, Wamoabu.” Wakamfuata, wakakamata vivuko vya Bonde la Yordani, toka kwa Wamoabi, wala hawakuruhusu mtu yeyote kuvuka mto.29Wakati huo waliwaua watu 10,000 wa Moabu, na wote walikuwa watu wenye nguvu na wenye uwezo. Hakuna aliyekimbia.30Kwa hiyo siku hiyo Moabu ilishindwa na nguvu ya Israeli. Na nchi ilikuwa na amani kwa miaka themanini.

31Baada ya Ehudi, mwamuzi aliyefuata alikuwa Shamgari mwana wa Anathi ambaye aliwaua Wafilisti 600 kwa konzo la ng'ombe. Pia aliwaokoa Israeli kutoka kwenye hatari.

4

1Baada ya Ehudi kufa, watu wa Israeli walifanya tena yaliyo mabaya machoni pa Bwana.2Bwana akawatia mkononi mwa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori. Kamanda wa jeshi lake aitwaye Sisera, naye aliishi Harosheti ya Mataifa.3Wana wa Israeli wakamwomba Bwana awasaidie, kwa sababu Sisera alikuwa na magari ya chuma 900 na akawashinda wana wa Israeli kwa nguvu kwa miaka ishirini.

4Basi Debora, nabii wa kike (mke wa Lapidothi), alikuwa mwamuzi anayeongoza katika Israeli wakati huo.5Naye aliketi chini ya mtende wa Debora kati ya Rama na Betheli katika nchi ya mlima wa Efraimu, na watu wa Israeli walimwendea ili kutatua migogoro yao.6Akamtuma Baraka mwana wa Abinoamu kutoka Kedeshi huko Naftali. Akamwambia, “Bwana, Mungu wa Israeli, anakuamuru, ‘Nenda katika mlima wa Tabori, uende pamoja nawe watu 10,000 kutoka Naftali na Zabuloni.7Nitamfukuza Sisera, jemadari wa jeshi la Yabini, akutane nawe karibu na mto Kishoni, pamoja na magari yake na jeshi lake, na nitakupa ushindi juu yake.’”

8Baraka akamwambia, “Ikiwa utakwenda nami, nitakwenda, lakini ikiwa huendi pamoja nami, sitaenda.”

9Alisema, “Nitakwenda nawe. Hata hivyo, njia unayoienda haitakupa heshima wewe, kwa kuwa Bwana atamuuza Sisera mkononi mwa mwanamke.” Ndipo Debora akainuka, akaenda pamoja na Baraka Kedeshi.10Baraki akawaita wana wa Zebuloni na Naftali kusanyika Kedeshi. Watu 10,000 walimfuata, na Debora akaenda pamoja naye.

11Heberi (Mkeni) alijitenganisha na Wakeni - walikuwa wazao wa Hobabu (mkwe wa Musa) - na akaweka hema yake mwaloni uliopo huko Saanaimu karibu na Kedesh.

12Walipomwambia Sisera kwamba Baraka, mwana wa Abinoamu, alikuwa amekwenda mlima wa Tabori,13Sisera akayaita magari yake yote, magari ya farasi mia tisa, na askari wote waliokuwa pamoja naye, kutoka Haroshethi ya Mataifa mpaka Mto Kishoni.

14Debora akamwambia Baraka, “Nenda! Kwa maana hii ndiyo siku ambayo Bwana amekupa ushindi juu ya Sisera. Je! Si Bwana anayekuongoza?” Basi Baraka akashuka kutoka mlima wa Tabori na watu 10,000 wakamfuata.15Bwana alifanya jeshi la Sisera kuchanganyikiwa, magari yake yote, na jeshi lake lote. Watu wa Baraka waliwashinda na Sisera akaanguka kutoka kwenye gari lake na kukimbia kwa miguu.16Lakini Baraka akayafuata magari na jeshi mpaka Haroshethi ya Mataifa, na jeshi lote la Sisera likauawa kwa upanga, wala hakuna mtu aliyeokoka.

17Lakini Sisera akakimbia kwa miguu mpaka hema ya Yaeli, mkewe Heberi Mkeni; kwa sababu kulikuwa na amani kati ya Yabini mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi Mkeni.

18Jaeli akatoka kumlaki Sisera, akamwambia, “Karibu, bwana wangu; karibu kwangu, wala usiogope.” Basi akakaribia kwake, akaingia hemani kwake, naye akamvika bushuti.

19Akamwambia, “Tafadhali nipe maji kidogo ninywe, kwa maana nina kiu.” Alifungua mfuko wa ngozi ya maziwa akampa anywe, kisha akamfunika tena.

20Akamwambia, “Simama mlangoni pa hema. Ikiwa mtu atakuja na kukuuliza, ‘Je, kuna mtu hapa?’, Sema ‘Hapana.’”

21Kisha Jaeli (mke wa Heberi) akachukua kigingi cha hema na nyundo mkononi mwake akamwendea kwa siri, kwa sababu alikuwa amelala usingizi mzito, naye akakitia kigingi cha hema upande wa kichwa chake akamchoma na kikapenya kushuka chini. Hivyo akafa.

22Baraka alipokuwa akimfuata Sisera, Yaeli alitoka kukutana naye akamwambia, “Njoo, nitakuonyesha mtu unayemtafuta.” Basi akaingia pamoja naye, tazama Sisera amekufa, na kigingi cha hema kando ya kichwa chake.

23Basi siku hiyo Mungu alimshinda Yabin, mfalme wa Kanaani, mbele ya watu wa Israeli.24Uwezo wa watu wa Israeli ulikua na nguvu zaidi dhidi ya Jabin mfalme wa Kanaani, hata walipomwangamiza.

5

1Siku hiyo Debora na Baraka, mwana wa Abinoamu waliimba wimbo huu:

2“Viongozi wanapoongoza mbele ya Israeli, watu wanapojitolea kupigana vita, tunamsifu Bwana!
3Sikiliza, ninyi wafalme! Sikiliza kwa makini, ninyi viongozi! Mimi nitamwimbia Bwana; Nami nitamsifu Bwana, Mungu wa Israeli.
4Ee Bwana, wakati ulipotoka Seiri, ulipokwenda kutoka Edomu, nchi ilitetemeka, na mbingu pia ilitetemeka; pia mawingu yalitoa maji.
5Milima ikatoka mbele ya uso wa Bwana; hata Mlima Sinai ukatetemeka mbele ya uso wa Bwana, Mungu wa Israeli.
6Katika siku za Shamgari (mwana wa Anathi), katika siku za Yaeli, barabara kuu ziliachwa, na wale ambao walitembea tu walitumia njia za upepo.
7Kulikuwa na mashujaa wachache huko Israeli, mpaka mimi, Debora, nilipochukua amri- mama alichukua amri katika Israeli!
8Walichagua miungu wapya, kulikuwa na vita katika malango ya mji lakini bado hapakuwa na ngao au mikuki iliyoonekana kati ya watu 40,000 nchini Israeli.
9Moyo wangu unawaendea wakuu wa Israeli, pamoja na watu ambao walijitolea -tunambariki Bwana kwa ajili yao!
10Fikiria juu ya hili- ninyi ambao hupanda punda weupe mmeketi kwenye mazulia, nanyi mnaotembea njiani.
11Sikiliza sauti za wale wanaoimba kwenye maeneo ya kutekea maji. Huko wanasema tena juu ya matendo ya haki ya Bwana, na matendo ya haki ya wapiganaji wake katika Israeli. Ndipo watu wa Bwana wakashuka kwenye malango ya mji.
12Amka, amka, Debora! Amka, amka, imba wimbo! Simama, Baraka, na uwakamate wafungwa wako, wewe mwana wa Abinoamu.
13Wale waliokoka wakaja chini kwa watu wenye nguvu; watu wa Bwana walikuja kwangu pamoja na mashujaa.
14Walikuja kutoka Efraimu, ambao mizizi yao iko katika Amaleki; watu wa Benyamini walikufuata. Wakuu wa Makiri walitoka, na kutoka Zebuloni wale wanaobeba fimbo ya jemedari.
15Na wakuu wangu katika Isakari walikuwa pamoja na Debora; na Isakari alikuwa na Baraka waliingia bondeni kwa kasi chini ya amri yake. Miongoni mwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
16Kwa nini uliketi katikati ya moto, ukisikiliza wachungaji wakipiga filimbi yao kwa makundi yao? Na kwa jamaa za Reubeni kulikuwa na utafutaji mkubwa wa moyo.
17Gileadi alikaa upande wa pili wa Yordani; na Dani, kwa nini alizunguka juu ya meli? Asheri alibakia pwani na akaishi karibu na bandari zake.
18Zabuloni lilikuwa kabila ambalo lingeweza kuhatarisha maisha yao mpaka kufikia kifo, Naftali, pia, katika uwanja wa vita.
19Wafalme walikuja, wakapigana; wafalme wa Kanaani wakapigana huko Taanaki karibu na maji ya Megido. Lakini hawakuondoa fedha kama nyara.
20Nyota zilipigana kutoka mbinguni, kutoka katika njia zao za mbinguni zilipigana na Sisera.
21Mto Kishoni uliwaondoa, mto ule wa kale, Mto Kishoni. Endelea mbele nafsi yangu, jipe nguvu!
22Kisha sauti za hofu za farasi-kupiga mbio, kupigana kwa watu wake wenye nguvu.
23‘Ilaani Merozi’ asema malaika wa Bwana. ‘Hakika walaani wenyeji wake kwa sababu hawakuja kumsaidia Bwana, kumsaidia Bwana katika vita dhidi ya mashujaa wenye nguvu.’
24Yaeli amebarikiwa zaidi kuliko wanawake wengine wote, Yaeli (mke wa Heberi Mkeni), amebarikiwa zaidi kuliko wanawake wote wanaoishi katika hema.
25Mtu yule aliomba maji, naye akampa maziwa; akamletea siagi katika sahani inayofaa kwa wakuu.
26Aliweka mkono wake kwenye kigingi cha hema, na mkono wake wa kulia katika nyundo ya mfanyakazi; kwa nyundo akampiga Sisera, alimpiga kichwani kwake. Aliligawanya fuvu lake vipande vipande wakati alipompiga pembeni ya kichwa chake.
27Akaanguka katikati ya miguu yake, akaanguka akalala pale. Kati ya miguu yake akaanguka. Mahali alipoanguka ni pale ambapo aliuawa kwa ukatili.
28Aliangalia dirishani - mama yake Sisera aliangalia kupitia kamba na akasema kwa huzuni, ‘Kwa nini gari lake limechelewa kuja? Kwa nini viboko vya farasi vinavyovuta magari yake vimechelewa?’
29Wafalme wake wenye hekima walijibu, na yeye mwenyewe akajibu jibu lile
30‘Je, hawakupata na kugawanya nyara? Tumbo, matumbo mawili kwa kila mtu; nyara ya kitambaa kilichofunikwa kwa Sisera, nyara ya kitambaa kilichofunikwa, nguo mbili za rangi iliyofunikwa kwa misumari ya wale waliopora?
31Naam, adui zako wote wataangamia, Ee Bwana! Lakini marafiki zako watakuwa kama jua wakati linapoongezeka kwa uwezo wake. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini.”

6

1Wana wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; naye akawatia mikononi mwa Midiani kwa miaka saba.2Uwezo wa Midiani uliwanyanyasa Israeli. Kwa sababu ya Midiani, watu wa Israeli walitengeneza makao wenyewe kutoka kwenye mabwawa katika milima, mapango, na ngome.3Kisha ikawa kwamba wakati wowote Waisraeli walipopanda mazao yao, Wamidiani na Waamaleki na watu kutoka mashariki waliwavamia Waisraeli.4Waliweza kutengeneza jeshi lao juu ya ardhi na kuharibu mazao, mpaka njia ya Gaza. Hawakuacha chakula huko Israeli, wala kondoo wala ng'ombe wala punda.5Kila wakati wao na mifugo yao na mahema walipokuja, walikuja kama kundi la nzige, na haikuwezekana kuhesabu watu au ngamia zao. Walivamia ardhi ili kuiharibu.6Midiani iliwadhoofisha Waisraeli sana mpaka watu wa Israeli wakamwita Bwana.

7Watu wa Israeli walipomwomba Bwana kwa sababu ya Midiani,8Bwana alimtuma nabii kwa wana wa Israeli. Nabii akawaambia, “Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Nimekuleta kutoka Misri; nilikutoa nje ya nyumba ya utumwa.9Naliwaokoa kutoka kwenye mikono ya Wamisri, na kutoka kwenye mkono wa wote waliokuwa wakiwanyanyasa. Niliwafukuza mbele yenu, na nimewapa nchi yao.10Niliwaambia, Mimi ndimi Bwana, Mungu wenu; Nimewaamuru msiabudu miungu ya Waamori, ambao mnaishi katika nchi yao. Lakini hamkuitii sauti yangu.’”

11Basi malaika wa Bwana akaja na kukaa chini ya mwaloni huko Ofra, uliokuwa wa Yoashi (Mwabiyezeri), wakati Gedioni, mwana wa Yoashi, akipepeta ngano katika sakafu, katika kikapu cha divai-kuificha toka kwa Wamidiani.12Malaika wa Bwana akamtokea, akamwambia, “Bwana yu pamoja nawe, mpiganaji mwenye nguvu!”

13Gideoni akamwambia, “Oo, bwana wangu, ikiwa Bwana yu pamoja nasi, kwa nini basi yote haya yanatupata? Je, yako wapi matendo yake yote mazuri ambayo baba zetu walituambia, waliposema, ‘Je! Si Bwana aliyetukomboa kutoka Misri?’ Lakini sasa Bwana ametuacha na kututia mikononi mwa Midiani.”

14Bwana akamtazama na kusema, “Nenda katika nguvu uliyo nayo tayari. Uiokoe Israeli kutoka mkononi wa Midiani. Je, sikukutuma?”

15Gideoni akamwambia, “Tafadhali, Bwana, nawezaje kuwaokoa Israeli? Angalia, familia yangu ni dhaifu zaidi katika Manase, na mimi si muhimu katika nyumba ya baba yangu.”

16Bwana akamwambia, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utalishinda jeshi lote la Midiani kama mtu mmoja.”

17Gideoni akamwambia, “Ikiwa unapendezwa na mimi, nipe basi ishara kwamba wewe ndio umenena nami.18Tafadhali, usiondoke hapa, mpaka nitakapokuja kwako na kuleta zawadi yangu na kuiweka mbele yako.” Bwana akasema, “Nitasubiri mpaka utakaporudi.”

19Gideoni akaenda, akaandaa mwana mbuzi, na efa moja ya unga akafanya mikate isiyotiwa chachu. Akaiweka nyama hiyo katika kikapu, na akaweka mchuzi ndani ya sufuria na kuviletea chini ya mti wa mwaloni, akavitoa.

20Malaika wa Mungu akamwambia, “Chukua nyama na mikate isiyotiwa chachu, ukaweke juu ya mwamba huu, ukamwage mchuzi juu yake.” Gideoni akafanya hivyo.21Kisha malaika wa Bwana akashika ncha ya fimbo mkononi mwake. Kwa hiyo akagusa nyama na mikate isiyotiwa chachu; moto ukatoka nje ya mwamba, ukateketeza nyama na mikate isiyotiwa chachu. Kisha malaika wa Bwana akaenda, na Gideoni hakuweza kumwona tena.22Gideoni alielewa kuwa yule alikuwa malaika wa Bwana. Gideoni akasema, “Ewe Bwana MUNGU! Kwa maana nimemwona malaika wa Bwana uso kwa uso!”

23Bwana akamwambia, “Amani iwe kwako! Usiogope, huwezi kufa.”

24Basi Gideoni akamjengea Bwana madhabahu huko. Aliiita, “Bwana ni Amani.” Hadi leo bado iko katika Ofra ya jamaa ya Waabiezeri.

25Usiku huo, Bwana akamwambia, “Twaa ng'ombe wa baba yako, na ng'ombe wa pili wa umri wa miaka saba, ukaondoe madhabahu ya Baali, ambayo ni ya baba yako, na kukata Ashera iliyo karibu nayo.26Jenga madhabahu kwa Bwana, Mungu wako juu ya mahali pa kukimbilia, na kuijenga njia sahihi. Toa ng'ombe ya pili kama sadaka ya kuteketezwa, ukitumia kuni kutoka Ashera uliyoikata.”

27Gideoni akachukua watumishi wake kumi na kufanya kama Bwana alivyomwambia. Lakini kwa sababu aliogopa sana watu wa nyumba ya baba yake na watu wa mji hakufanya hivyo wakati wa mchana, alifanya hivyo usiku.

28Asubuhi wakati watu wa mji walipoamka, madhabahu ya Baali imebomolewa, na Ashera iliyokuwa karibu nayo imekatwa, na ng'ombe wa pili ametolewa sadaka kwenye madhabahu iliyojengwa.

29Watu wa mji wakaambiana, “Ni nani aliyefanya jambo hili?” Walipokuwa wakiongea na wengine na kutafuta majibu, wakasema, “Gedioni mwana wa Yoashi amefanya jambo hili.”

30Ndipo watu wa mji wakamwambia Yoashi, “Mtoe mtoto wako ili afe, kwa sababu ameibomoa madhabahu ya Baali, na kwa sababu ameikata Ashera karibu nayo.”

31Yoashi akawaambia wote waliompinga, “Je, ninyi mtamsihi Baali? Je, mtamuokoa? Mtu yeyote atakayemtetea, basi atauawa asubuhi hii. Ikiwa Baali ni mungu, basi atajitetea mwenyewe wakati mtu anaibomoa madhabahu yake.”32Kwa hiyo siku hiyo wakamwita Gideoni “Yerubaali,” kwa sababu alisema, “Baali ajijitetee dhidi yake,” kwa sababu Gideoni alivunja madhabahu ya Baali.

33Basi Wamidiani wote, Waamaleki, na watu wa mashariki walikusanyika pamoja. Wakavuka Yordani na wakapanga katika bonde la Yezreeli.34Lakini Roho wa Bwana akaja juu ya Gideoni. Gideoni akapiga tarumbeta, akawaita jamaa ya Abiezeri, ili wapate kumfuata.35Aliwatuma wajumbe wote katika Manase, na wao pia, waliitwa nje kumfuata. Naye akatuma wajumbe kwa Asheri, na Zabuloni, na Naftali; nao wakaenda kumlaki.

36Gideoni akamwambia Mungu, “Ikiwa ungependa kunitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema,37tazameni, ninaweka ngozi ya samazi kwenye sakafu. Ikiwa kuna umande tu juu ya ngozi, na ni kavu duniani, basi nitajua kwamba utanitumia kuokoa Israeli, kama ulivyosema.”38Hivi ndivyo ilivyotokea-Gideoni aliamka mapama asubuhi, akaikamua ngozi hiyo, na akatoa umande kwenye ngozi, wa kutosha kujaza bakuli kwa maji.

39Gideoni akamwambia Mungu, “Usinikasirikie, nitasema tena kwa mara nyingine. Tafadhali niruhusu nijaribu tena kwa kutumia ngozi. Wakati huu uifanye kavu, na iwe na umande juu ya ardhi yote kuzunguka.”40Mungu alifanya kile alichoomba usiku huo. Ngozi ilikuwa kavu, na kulikuwa na umande katika ardhi yote iliyozunguka.

7

1Ndipo Yerubaali (yaani Gideoni) akainuka mapema, na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaweka kambi kando ya chemchemi ya Harodi. Kambi ya Midiani ilikuwa kaskazini mwao katika bonde karibu na kilima cha More.2Bwana akamwambia Gideoni, “Kuna askari wengi sana kwa mimi kukupa ushindi juu ya Wamidiani, ili Waisraeli wasijisifu juu yangu, wakisema, ‘Nguvu zetu zimetuokoa.’3Basi, tangaza masikioni mwa watu, ukisema, ‘Yeyote anayeogopa, anayetetemeka, arudi na atoke katika mlima Gileadi.’” Basi, watu 22,000 wakaondoka, na 10,000 wakabaki.

4Bwana akamwambia Gideoni, “Watu bado ni wengi sana. Wapeleke chini kwenye maji, na nitafanya idadi yao iwe ndogo kwa ajili yako. Kama nikisema, ‘Huyu atakwenda pamoja nawe,’ atakwenda pamoja nawe; lakini kama nikisema, ‘Huyu hawezi kwenda pamoja nawe,’ hatakwenda.”

5Gideoni akawapeleka watu kwenye maji; Bwana akamwambia, “Ondoa kila mtu atakayelamba maji, kama mbwa alambavyo, kutoka kwa wale wanaopiga magoti na kunywa.”6Wanaume 300 walilamba. Wengine wote walipiga magoti kunywa maji.

7Bwana akamwambia Gideoni, “Chukua watu hawa 300 waliokwisha kulamba maji, nitakuokoa na kukupa ushindi juu ya Wamidiani. Acha kila mtu arudi mahali pake.”8Kwa hiyo wale waliochaguliwa walichukua vifaa vyao na tarumbeta zao. Gideoni akawarudisha watu wote wa Israeli, kila mtu kwenda kwenye hema yake, lakini akawaweka watu 300. Basi kambi ya Midiani ilikuwa chini yake katika bonde.9Usiku huo huo Bwana akamwambia, “Simama! Kavamie kambi, kwa maana nitakupa ushindi juu yake.10Lakini ikiwa unaogopa kushuka, shuka kwenye kambi pamoja na Pura mtumishi wako,11na usikilize kile wanachosema, na ujasiri wako utaimarishwa kushambulia kambi.” Basi Gideoni akaenda pamoja na Pura mtumishi wake, mpaka chini kwa walinzi wa kambi.12Wamidiani, Waamaleki, na watu wote wa mashariki walikaa karibu na bonde, wengi kama nzige. Ngamia zao walikuwa kama mchanga katika bahari.

13Gideoni alipofika huko, mtu alikuwa akimwambia mwenzake ndoto. Mtu huyo akasema, “Angalia! Niliota ndoto, na nikaona mkate wa shayiri umeanguka ndani ya kambi ya Midiani. Ukaja hemani, na kuipiga kwa nguvu sana hata ikaanguka chini ikapinduka na kulala chini.”

14Mtu mwingine akasema, “Hii si kitu kingine isipokuwa upanga wa Gideoni (mwana wa Yoashi), Mwisraeli. Mungu amempa ushindi juu ya Midiani na jeshi lake lote.”

15Gideoni aliposikia habari ya ile ndoto na tafsiri yake, akainama chini na kuabudu. Alirudi kwenye kambi ya Israeli na kusema, “Simameni! Bwana ametupa ushindi juu ya jeshi la Midiani.”16Akawagawa watu 300 katika makundi matatu, na akawapa tarumbeta zote na mitungi tupu, na taa ndani ya kila mtungi.

17Akawaambia, “Niangalieni mimi na kufanya yale ninayoyafanya. Tazama! Ninapofika kwenye mwisho wa kambi, ni lazima mfanye kile ninachofanya.18Nitakapopiga tarumbeta, mimi na wote mlio pamoja nami, basi mtapiga tarumbeta zenu katika kila upande wa kambi nzima na kupiga kelele, kwa Bwana na Gideoni!”

19Basi Gideoni na watu mia moja waliokuwa pamoja naye walifika mwisho wa kambi, hapo mwanzoni mwa saa ya kati. Wakati Wamidiani walikuwa wakibadilisha walinzi, walipiga tarumbeta na kuvunja mitungi iliyokuwa mikononi mwao.20Vikosi vitatu vilipiga tarumbeta na kuvunja mitungi. Walikuwa na taa katika mikono yao ya kushoto na tarumbeta katika mikono yao ya kulia ili kuwapiga. Walipiga kelele, “Upanga wa Bwana na wa Gideoni.”21Kila mtu alisimama mahali pake kando ya kambi na jeshi la Midiani likakimbia. Walipiga kelele na kukimbia.

22Walipopiga tarumbeta 300, Bwana akaweka upanga wa kila mtu wa Midiani dhidi ya wenzake na dhidi ya jeshi lake lote. Jeshi likakimbia mpaka Bethshita kuelekea Serera, mpaka, mpaka wa Abel Mehola, karibu na Tabathi.23Watu wa Israeli kutoka Naftali, Asheri, na Manase wote waliitwa nje, nao wakawafuata Midiani.24Gideoni akatuma wajumbe katika nchi zote za mlima wa Efraimu, akisema, “Nenda chini dhidi ya Midiani na umiliki Mto Yordani mpaka Bethbara, ukawazuie.” Basi wanaume wote wa Efraimu walikusanyika pamoja na kuimiliki maji, mpaka Bethbara na Mto Yordani.25Wakawatwaa wakuu wawili wa Midiani, Orebu na Zeebu. Wakamuua Orebu kwenye mwamba wa Orebu, nao wakamuua Zeebu katika shinikizo la divai la Zeebu. Wakawafuata Wamidiani, wakamletea Gideoni vichwa vya Orebu na Zeebu, ng'ambo ya pili ya Yordani.

8

1Watu wa Efraimu wakamwambia Gideoni, “Ni nini hiki umetutenda? Haukutuita wakati ulipokwenda kupigana na Midiani.” Wakamwambia kwa nguvu.

2Akawaambia, “Nimefanya nini sasa kulinganisha na mlichofanya ninyi? Je! Mavuno ya zabibu za Efraimu si bora zaidi kuliko mavuno ya zabibu ya Abiezeri?3Mungu amewapa ushindi juu ya wakuu wa Midiani-Orebu na Zeeb! Mimi nimefanya nini ukilinganisha na ninyi?” Hasira yao ikashuka chini aliposema hili.

4Gideoni alikuja Yordani na akavuka juu yake, yeye na watu 300 waliokuwa pamoja naye. Walikuwa wamechoka, lakini bado waliendelea kufuatilia.5Akawaambia watu wa Sukothi, “Tafadhali wape mikate kwa watu wanaonifuata, kwa kuwa wamechoka, nami niwafuatilie Zeba na Salmuna, wafalme wa Midiani.”

6Na wakuu wakasema, “Je, mikono ya Zeba na Salmuna sasa ipo mikononi mwako? Kwa nini tulipe jeshi lako mikate?”

7Gideoni akasema, “Bwana akitupa ushindi juu ya Zeba na Salmunna, nitainyunyiza ngozi yenu kwa miiba ya jangwani na michongoma.”

8Akatoka huko, akaenda Penieli, akawaambia watu maneno hayo hayo; lakini watu wa Penieli wakamjibu kama watu wa Sukothi walivyojibu.9Akawaambia pia watu wa Penieli, akasema, “Nitakapokuja kwa amani, nitauangusha mnara huu.”

10Sasa Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao, karibu na watu 15,000 wote waliosalia nje ya jeshi lote la watu wa Mashariki, kwa kuwa walianguka watu 120,000 waliofundishwa kupigana na upanga.11Gideoni akapanda barabara iliyochukuliwa na wakaazi wa hema, Noba na Yogbena. Akalishinda jeshi la adui, kwa sababu hawakuwa wanatarajia shambulio.12Zeba na Salmuna walikimbia, na Gideoni alipowafuata, akawatwaa wafalme wawili wa Midiani-Zeba na Salmunna- na kulifanya jeshi lote kuwa na hofu.

13Gideoni, mwana wa Yoashi, alirudi kutoka kwenye vita kwenda kupitia Heresi.14Akamkimbilia kijana mmoja wa watu wa Sukothi na kutafuta ushauri kutoka kwake. Kijana huyo alimwelezea viongozi wa Sukothi na wazee wake, watu sabini na saba.15Gideoni akaja kwa watu wa Sukothi, akasema, “Tazameni Zeba na Salmuna, ambao mlinidhihaki kwa ajili yao, mkasema, ‘Je! Mmemshinda Zeba na Salmuna? Hatujui kwamba tunapaswa kulipa jeshi lako mkate.’”16Gideoni akawachukua wazee wa mji, naye akawaadhibu watu wa Sukothi kwa miiba ya jangwa na michongoma.17Akaangusha mnara wa Penieli na kuwaua watu wa mji huo.

18Gideoni akamwambia Zeba na Salmuna, “Ni watu wa aina gani mliwaua Tabori?” Wakajibu, “Kama wewe ulivyo, ndivyo walivyokuwa. Kila mmoja wao alionekana kama mwana wa mfalme.”

19Gideoni akasema, ‘Wao walikuwa ndugu zangu, wana wa mama yangu. Kama Bwana aishivyo, kama mngewaacha hai, nisingewauwa.”20Akamwambia Yetheri (mzaliwa wake wa kwanza), “Simama uwaue!” Lakini kijana huyo hakutoa upanga wake kwa kuwa aliogopa, kwa sababu alikuwa bado kijana mdogo.

21Ndipo Zeba na Salmuna wakasema, simama mwenyewe, utuue! Kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Gideoni akasimama na kumwua Zeba na Salmuna. Pia aliondoa mapambo yaliyokuwa juu ya shingo za ngamia zao.

22Ndipo wana wa Israeli wakamwambia Gideoni, “Ututawale, wewe, mtoto wako, na mjukuu wako; kwa sababu umetuokoa mikononi mwa Midiani.”

23Gideoni akawaambia, “Mimi sitatawala juu yenu, wala mtoto wangu hatatawala juu yenu. Bwana atatawala juu yenu.”24Gideoni akawaambia, “Nina haja yangu niitakayo kwenu kwamba kila mmoja wenu atanipe pete kutoka kwenye nyara zake.” (Wamidiani walikuwa na pete za dhahabu kwa sababu walikuwa Waishmaeli.)

25Wakamjibu, “Tunafurahi kukupa.” Wakatandika vazi na kila mtu akatupa pete kutoka kwenye nyara zake.26Uzito wa pete za dhahabu alizoomba zilikuwa shekeli 1,700 za dhahabu. Nyara hizi zilikuwa ni pamoja na mapambo ya makoja, vidani, nguo ya rangi ya zambarau waliyovaa na wafalme wa Midiani, na zaidi ya minyororo iliyokuwa karibu na shingo za ngamia zao.27Gideoni akafanya efodi kutoka katika pete na kuiweka katika mji wake, huko Ofra, na Israeli wote wakaiandama kwa ukahaba na kuabudu. Ilikuwa mtego kwa Gideoni na kwa wale walio nyumbani kwake.

28Kwa hiyo Midiani ilishindwa mbele ya watu wa Israeli na hawakuinua vichwa vyao tena. Na nchi ikawa na amani kwa miaka arobaini siku za Gideoni.

29Yerubaali, mwana wa Yoashi, akaenda akakaa nyumbani kwake.30Gideoni alikuwa na wana sabini, waliokuwa uzao wake, kwa kuwa alikuwa na wake wengi.31Mwanamke wake, aliyekuwa Shekemu, akamzaa pia mwana, na Gideoni akampa jina lake Abimeleki.32Gideoni, mwana wa Yoashi, akafa katika uzee mzuri, akazikwa huko Ofra katika kaburi la baba yake Yoashi, wa jamaa ya Abiyezeri.

33Ikawa, Gideoni alipokufa, watu wa Israeli wakageuka tena na kujifanyia ukahaba wenyewe kwa kuabudu Mabaali. Walimfanya Baali Berith kuwa mungu wao.34Watu wa Israeli hawakukumbuka kumtukuza Bwana, Mungu wao, aliyewaokoa kutoka kwa mikono ya adui zao kila upande.35Hawakuweka ahadi zao kwa nyumba ya Yerubaali (yaani Gideoni), kwa ajili ya mema yote aliyoyafanya katika Israeli.

9

1Abimeleki, mwana wa Yerubaali, akaenda kwa jamaa za mama yake huko Shekemu, akawaambia, na jamaa yote ya mama yake,2“Tafadhali semeni haya, ili wakuu wote wa Shekemu wasikie. Ni kipi bora kwako, Je, wana sabini wote wa Yerubali kutawala juu yenu, au kwamba moja tu atawale juu yenu? Kumbuka kwamba mimi ni mfupa na nyama yenu.”

3Ndugu za mama yake waliongea kwa niaba yake kwa viongozi wa Shekemu, nao wakakubali kumfuata Abimeleki, wakasema, Yeye ndiye ndugu yetu.4Wakampa vipande sabini vya fedha katika nyumba ya Baali Berith; Abimeleki akazitumia kwa kuajiri watu wasio na sheria na waliokuwa wajinga, waliomfuata.5Abimeleki akaenda nyumbani kwa baba yake huko Ofra; na juu ya jiwe moja akawaua ndugu zake sabini, wana wa Yerubaali. Yotamu ndiye aliyebaki, mwana mdogo kabisa wa Yerubaali, kwa kuwa alijificha.6Wakuu wote wa Shekemu na Beth Milo wakaungana, wakaenda kumfanya Abimeleki mfalme, karibu na mwaloni karibu na nguzo iliyoko Shekemu.

7Yotamu alipoambiwa juu ya jambo hilo, akaenda, akasimama juu ya mlima Gerizimu. Alipiga kelele akawaambia, “Sikilizeni, enyi viongozi wa Shekemu, ili Mungu awasikilize.8Siku moja miti ilikwenda kumtia mafuta mfalme juu yao. Wakauambia mzeituni, ‘Tawala juu yetu!’

9Lakini mti wa mizeituni ukawaambia, ‘Je! Nitaacha mafuta yangu, ambayo hutumiwa kuheshimu miungu na wanadamu, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?’

10Miti hiyo ikamwambia mtini, ‘Njoo utawale juu yetu.’

11Lakini mtini ukawaambia, ‘Je, nitaacha utamu wangu na matunda yangu mazuri, ili nipate kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?’

12Miti hiyo ikamwambia mzabibu, ‘Njoo utawale juu yetu.’

13Mzabibu ukawaambia, ‘Je, nitaacha divai yangu mpya, ambayo hufurahisha miungu na wanadamu, na kurudi na kuvuka juu ya miti mingine?

14Kisha miti yote ikamwambia mti wa miiba, ‘Njoo utawale juu yetu.’

15Mti wa miiba ikaiambia miti, ‘Ikiwa mnataka kunipaka mafuta niwe mfalme juu yenu, njooni na mpate usalama chini ya kivuli changu. Ikiwa sivyo, basi moto lazima uondoke kwenye mti wa miiba na uiteketeze mierezi ya Lebanoni.’

16Basi, ikiwa mmefanya kweli na uaminifu, mlimfanya Abimeleki mfalme, na ikiwa mmefanya vizuri juu ya Yerubaali na nyumba yake, na ikiwa mmemuadhibu kama anavyostahili,17- na kufikiri kwamba baba yangu alipigana kwa ajili yenu, akahatarisha maisha yake, na akawaokoa kutoka kwenye mkono wa Midiani -18lakini leo mmeamka juu ya nyumba ya baba yangu na kuwaua watoto wake, watu sabini, juu ya jiwe moja. Na mmemfanya Abimeleki, mwana wa mtumishi wake, awe mfalme juu ya wakuu wa Shekemu, kwa sababu yeye ni ndugu yenu.19Ikiwa mlifanya kwa uaminifu na uelekevu pamoja na Yerubaal na nyumba yake, basi mnapaswa kufurahi katika Abimeleki, naye apate kufurahi ndani yenu.20Lakini ikiwa sio, moto utoke kwa Abimeleki, ukawaangamize watu wa Shekemu na Beth Milo. Basi moto utoke kwa watu wa Shekemu na Beth Milo, ili kumteketeza Abimeleki.”

21Yothamu akakimbia, naye akaenda Beeri. Aliishi huko kwa sababu ilikuwa mbali na Abimeleki, kaka yake.

22Abimeleki akatawala juu ya Israeli kwa miaka mitatu.23Mungu alituma roho mbaya kati ya Abimeleki na viongozi wa Shekemu. Viongozi wa Shekemu walisaliti uaminifu waliokuwa nao kwa Abimeleki.24Mungu alifanya hivyo ili uhalifu uliofanywa kwa wana sabini wa Yerubaali uweze kulipizwa kisasi, na Abimeleki ndugu yao atawajibishwa kwa kuwaua, na watu wa Shekemu watawajibishwa kwa sababu walimsaidia kuua ndugu zake.25Basi wakuu wa Shekemu wakawaweka wanaume wakimsubiri juu ya vilima ili wamwangamize, nao wakawaibia wote waliokuwa wamepita katika barabara hiyo. Hii iliripotiwa kwa Abimeleki.

26Gaali mwana wa Ebedi akenda pamoja na ndugu zake, wakavuka Shekemu. Viongozi wa Shekemu walimwamini.27Wakaenda shambani wakakusanya zabibu kutoka kwa mizabibu, nao wakazikanyaga. Walifanya sherehe katika nyumba ya mungu wao, walikula na kunywa, kumlaani Abimeleki.28Gaali mwana wa Ebedi, akasema, “Abimeleki ni nani, na Shekemu ni nani, hata tumtumikie? Je, si mwana wa Yerubaali? Na Zebuli si afisa wake? Watumikieni watu wa Hamori, baba yake Shekemu! Kwa nini tunapaswa kumtumikia?29Laiti watu hawa wangelikuwa chini ya amri yangu! Kisha ningemuondoa Abimeleki. Ningemwambia Abimeleki, ‘Liondoe nje jeshi lako lote.’”

30Zebul, mkuu wa mji, aliposikia maneno ya Gaali, mwana wa Ebedi, hasira yake ikawaka.31Akatuma wajumbe kwa Abimeleki ili wapate kudanganya, akisema, “Tazama, Gaali mwana wa Ebedi na ndugu zake wanafika Shekemu; nao wanauchochea mji dhidi yako.32Sasa, amka wakati wa usiku, wewe na askari pamoja nawe, na uandae uvamizi katika mashamba.33Kisha asubuhi, jua litakapokwisha, inuka mapema na uangamize mji. Na yeye na watu waliokuwa pamoja naye watakapokuja juu yenu, fanyeni chochote mnachoweza.”

34Basi Abimeleki akainuka usiku, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye, wakaandaa uvamizi dhidi ya Shekemu, wakagawanyika vitengo vinne.35Gaali mwana wa Ebedi akatoka, akasimama penye mlango wa mji. Abimeleki na watu waliokuwa pamoja naye wakatoka mahali pa kuficha.

36Gaali alipowaona hao watu, akamwambia Zebuli, “Tazama, watu wanatoka kwenye vilima!” Zebuli akamwambia, “Wewe unaona vivuli juu ya vilima kama vile watu.”37Gaali akaongea tena na kusema, “Angalia, watu wanashuka katikati ya nchi, na kitengo kimoja kinakuja kwa njia ya mwaloni wa Maenenimu.”

38Ndipo Zebuli akamwambia, “Je, maneno yako ya kiburi yako wapi sasa, wewe uliyesema, ‘Abimeleki ni nani, ili tumtumikie?’ Je, hao sio watu ambao uliwadharau? Toka sasa na pigana nao.”

39Gaali akatoka na alikuwa akiwaongoza watu wa Shekemu, naye alipigana na Abimeleki.40Abimeleki akamfukuza, na Gaali akakimbia mbele yake. Na wengi wakaanguka na majeraha ya mauti mbele ya mingilio ya lango la mji.41Abimeleki alikaa Aruma. Zebul akawalazimisha Gaal na ndugu zake watoke Shekemu.

42Siku ya pili watu wa Shekemu wakatoka shambani, na habari hii ikamfikia Abimeleki.43Aliwachukua watu wake, akawagawanya katika vitengo vitatu, na wakaandaa uvamizi mashambani. Aliangalia na kuona watu wakitoka mjini. Akawakamata na kuwaua.44Abimeleki na vitengo vilivyokuwa pamoja naye vilishambulia na kuzuia maingilio ya lango la mji. Vitengo vingine viwili vilishambulia wote waliokuwa katika shamba na wakawaua.45Abimeleki alipigana na huo mji siku nzima. Aliteka mji huo, na kuwaua watu waliokuwa ndani yake. Akabomoa kuta za mji na kueneza chumvi juu yake.

46Wakati wakuu wote wa mnara wa Shekemu waliposikia hayo, waliingia katika ngome ya nyumba ya El Berithi.47Abimeleki aliambiwa kuwa viongozi wote walikuwa wamekusanyika pamoja kwenye mnara wa Shekemu.48Abimeleki akaenda mpaka mlima wa Salmoni, yeye na watu wote waliokuwa pamoja naye. Abimeleki akachukua shoka na kukata matawi. Akaweka juu ya bega lake na kuwaagiza watu waliokuwa pamoja naye, “Mlichoona nimekifanya fanyeni kama nilivyofanya.”49Basi kila mmoja akakata matawi, wakamfuata Abimeleki. Wakayafungia juu ya ukuta wa mnara, nao wakawasha moto, hata watu wote wa mnara wa Shekemu wakafa, wanaume na wanawake elfu.

50Abimeleki akaenda Tebezi, naye akapiga kambi dhidi ya Thebezi, akautwaa.51Lakini kulikuwa na mnara wenye nguvu katika mji, wanaume na wanawake wote na viongozi wote wa mji walikimbilia na kujifungia wenyewe. Kisha wakaenda juu ya paa la mnara.52Abimeleki alikwenda kwenye mnara na kupigana nao, naye akaenda karibu na mlango wa mnara ili kuuchoma.53Lakini mwanamke akatupa jiwe la juu, juu ya kichwa cha Abimeleki likavunja fuvu lake.

54Kisha akamwita yule kijana aliyekuwa anamchukulia silaha zake, akamwambia, “Chukua upanga wako ukaniue, kwa hiyo hakuna mtu atakayesema juu yangu, ‘Mwanamke alimwua.’” Basi kijana wake akamchoma naye akafa.55Watu wa Israeli walipoona kwamba Abimeleki amekufa, wakaenda nyumbani.

56Basi Mungu akalipiza kisasi cha uovu wa Abimeleki alichomfanyia baba yake kwa kuua ndugu zake sabini.57Mungu akafanya uovu wote wa watu wa Shekemu ugeuke juu ya vichwa vyao wenyewe, na juu yao ilikuja laana ya Yothamu mwana wa Yerubaali.

10

1Baada ya Abimeleki, Tola, mwana wa Pua, mwana wa Dodo, mtu wa Isakari, aliyekaa Shamiri, katika mlima wa Efraimu, akaondoka ili kuwaokoa Israeli.2Akawa mwamuzi wa Israeli miaka ishirini na mitatu. Alikufa na kuzikwa Shamiri.

3Alifuatiwa na Yairi Mgileadi. Akawa mwamuzi wa Israeli miaka ishirini na miwili.4Alikuwa na wana thelathini waliokuwa wakipanda kwenye punda thelathini, na walikuwa na miji thelathini, ambayo inaitwa Hawoth Yairi hata leo, iliyo katika nchi ya Gileadi.5Yairi alikufa na kuzikwa Kamoni.

6Watu wa Israeli waliendelea kutenda maovu mbele za Bwana, wakaabudu Mabaali, Maashtoreti, miungu ya Aramu, miungu ya Sidoni, miungu ya Moabu, miungu ya wana wa Amoni, na miungu ya Wafilisti. Wakamsahau Bwana na hawakamsujudia tena.7Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawauza mikononi mwa Wafilisti na katika mikono ya wana wa Amoni.8Wakawaangamiza na kuwadhulumu watu wa Israeli mwaka huo, na kwa muda wa miaka kumi na nane waliwafukuza watu wote wa Israeli waliokuwa ng'ambo ya Yordani katika nchi ya Waamori, iliyoko Gileadi.9Nao wana wa Amoni wakavuka Yordani, wakapigana na Yuda, na Benyamini, na nyumba ya Efraimu; Israeli akasumbuliwa sana.10Ndipo wana wa Israeli wakamwita Bwana, wakisema, “Tumekukosea, kwa sababu tumemwacha Mungu wetu, tukaabudu Mabaali.”

11Bwana akawaambia wana wa Israeli, “Je, sikuwatoa ninyi kutoka kwa Wamisri, na Waamori, na Waamoni, na Wafilisti,12na pia kwa Wasidoni? Waamaleki na Wamaoni walipowakandamiza; mliniita, nami nikawaokoa kutoka katika nguvu zao.13Lakini ninyi mliniacha tena na kuabudu miungu mingine. Kwa hiyo, sitawaokoa tena.14Nendeni mkaiite miungu mnayoiabudu. Ili iwaokoe wakati wa shida.

15Wana wa Israeli wakamwambia Bwana, Tumefanya dhambi. Tufanyie chochote kinachoonekana kuwa kizuri kwako. Tafadhali, tuokoe leo.16Wakaiacha miungu ya kigeni waliyokuwa nayo, nao wakamwabudu Bwana. Naye akawa na subira juu ya taabu ya Israeli.

17Ndipo Waamoni wakakusanyika, wakaweka kambi Gileadi. Waisraeli walikutana na kuweka kambi yao huko Mispa.18Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana, “Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Yeye atakuwa kiongozi juu ya wote wanaoishi Gileadi.”

11

1Yeftha Mgileadi alikuwa shujaa mwenye nguvu, lakini alikuwa mwana wa kahaba. Gileadi alikuwa baba yake.2Mke wa Gileadi pia alizaa wanawe wengine. Wana wa mkewe walipokua, walimlazimisha Yeftha aondoke nyumbani na kumwambia, “Huwezi kurithi chochote kutoka katika familia yetu. Wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.”3Basi Yeftha akaondoka toka kwa ndugu zake, akaishi katika nchi ya Tobu. Watu wasiokuwa na sheria waliungana na Yeftha na wakaja na kwenda pamoja naye.

4Siku kadhaa baadaye, wana wa Amoni walipigana na Israeli.5Wana wa Amoni walipopigana na Israeli, wazee wa Gileadi wakaenda kumleta Yeftha kutoka nchi ya Tobu.6Wakamwambia Yeftha, “Njoo uwe kiongozi wetu ili tupigane na wana wa Amoni.”

7Yefta akawaambia viongozi wa Gileadi, “Mlinichukia na kunilazimisha kuondoka nyumbani kwa baba yangu. Kwa nini mnakuja kwangu sasa munapokuwa na shida?”

8Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, “Ndiyo sababu tunakugeukia sasa; njoo pamoja nasi pigana na watu wa Amoni, na wewe utakuwa kiongozi juu ya wote wanaoishi Gileadi.

9Yeftha akawaambia wazee wa Gileadi, “Ikiwa mnanirejesha nyumbani tena ili kupigana na wana wa Amoni, na kama Bwana atatupa ushindi juu yao, nitakuwa kiongozi wenu.”

10Wazee wa Gileadi wakamwambia Yeftha, “Bwana awe shahidi kati yetu ikiwa hatutafanya kama tunavyosema!”11Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, nao watu wakamfanya awe msimamizi na mkuu juu yao. Alipokuwa mbele ya Bwana huko Mispa, Yeftha akarudia ahadi zote alizozifanya.

12Ndipo Yeftha akatuma wajumbe kwa mfalme wa wana wa Amoni, akisema, “Ni nini mgogoro huu kati yetu? Kwa nini umekuja kwa nguvu kuchukua ardhi yetu?”

13Mfalme wa wana wa Amoni akawajibu wajumbe wa Yeftha, “Kwa sababu Israeli walipopanda kutoka Misri, walichukua nchi yangu toka Arnoni hata Yaboki, mpaka Yordani. Sasa rudisha ardhi hizo kwa amani.”

14Yeftha akatuma tena wajumbe kwa mfalme wa wana wa Amoni,15akasema, “Yeftha asema hivi, Israeli hawakuchukua nchi ya Moabu na nchi ya wana wa Amoni;16lakini walitoka Misri, na Israeli wakaenda kupitia jangwa hadi Bahari ya Shamu na Kadeshi.17Israeli walipotuma wajumbe kwa mfalme wa Edomu, wakisema, ‘Tafadhali tunaomba ruhusa tupite katika nchi yako,’ mfalme wa Edomu hakuwasikiliza. Wakawatuma wajumbe kwa mfalme wa Moabu, lakini akakataa. Basi Israeli wakakaa Kadeshi.18Kisha wakapitia jangwani, wakaondoka katika nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu; wakavuka upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, wakapanga ng'ambo ya Arnoni. Lakini hawakuingia mpaka wa Moabu, maana Arnoni ilikuwa mpaka wa Moabu.

19Israeli wakatuma wajumbe kwa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala huko Heshboni; Israeli akamwambia, ‘Tafadhali, tunaomba tupite katika nchi yako hata mahali petu.’20Lakini Sihoni hakumwamini Israeli apite katika eneo lake. Basi Sihoni akakusanya jeshi lake lote, akalipeleka Yahasa, na huko akapigana na Israeli.21Bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mkononi mwa Israeli, nao wakawashinda. Basi Israeli wakachukua nchi yote ya Waamori waliokaa katika nchi hiyo.22Wachukua kila kitu ndani ya wilaya ya Waamori, kutoka Arnoni hadi Yaboki, na kutoka jangwani hadi Yordani.

23Basi, Bwana, Mungu wa Israeli, amewafukuza Waamori mbele ya watu wake Israeli, na sasa mnataka kuimiliki nchi yao?24Je, huwezi kuchukua nchi ambayo Kemoshi, mungu wako, anakupa? Kwa hiyo nchi yoyote Bwana, Mungu wetu, ametupa, tutachukua.25Sasa wewe ni bora zaidi kuliko Balaki, mwana wa Sipori, mfalme wa Moabu? Je, alidai kuwa na hoja na Israeli? Je, yeye amewahi kupigana vita dhidi yao?26Wakati Israeli walipoishia miaka 300 huko Heshboni na vijiji vyake, na Aroeri na vijiji vyake, na katika miji yote iliyo karibu na Arnoni, kwa nini hamkuwachukua tena wakati huo?27Sijawafanyia vibaya, lakini mnanifanyia vibaya kwa kunishambulia. Bwana, mwamuzi, ataamua leo kati ya wana wa Israeli na wana wa Amoni.”28Lakini mfalme wa wana wa Amoni akakataa onyo alilotumiwa na Yeftha.

29Basi, Roho wa Bwana akamjia Yeftha, akapita Gileadi na Manase, akapitia Mispa ya Gileadi, na kutoka Mispa ya Gileadi akapita kwa wana wa Amoni.30Yeftha akaahidi kwa Bwana, akasema, “Ikiwa utanipa ushindi juu ya wana wa Amoni,31chochote kinachotoka mlangoni mwa nyumba yangu kunijia mimi nitakaporudi kwa amani kutoka kwa wana wa Amoni kitakuwa cha Bwana; nami nitatoa hiyo sadaka ya kuteketezwa.”

32Basi Yeftha akapita kwa wana wa Amoni ili kupigana nao, naye Bwana akampa ushindi.33Akawashinda na kusababisha mauaji makubwa kutoka Aroeri hadi miji ishirini na miwili-na Abeli Keramimu. Basi wana wa Amoni waliwekwa chini ya uangalizi wa watu wa Israeli.

34Yeftha alifika nyumbani kwake huko Mizpa, na binti yake akatoka kumlaki na ngoma na kucheza. Alikuwa mtoto wake pekee, na badala yake hakuwa na mwana wa kiume wala binti.35Mara tu alipomwona, alirarua nguo zake akasema, “Loo! Binti yangu! Umenivunja kwa huzuni, na umekuwa mtu anayenisababishia maumivu yangu! Kwa maana nimeapa kwa Bwana, wala siwezi kurudisha ahadi yangu.”

36Akamwambia, “Baba yangu, umeweka ahadi kwa Bwana, unifanyie kila kitu ulichoahidi; kwa kuwa Bwana amekulipia kisasi juu ya adui zako, wana wa Amoni.”37Akamwambia baba yake, “Hebu ahadi hii ihifadhiwe kwa ajili yangu. Niache kwa miezi miwili, nipate kuondoka na kwenda kwenye vilima na kuomboleza juu ya ubikira wangu, mimi na wenzangu.”

38Akasema, “Nenda.” Alimtuma kwa muda wa miezi miwili. Akamwondoa, yeye na wenzake, nao wakauomboleza ubikira wake katika milimani.39Mwishoni mwa miezi miwili alirudi kwa baba yake, ambaye alifanya kulingana na ahadi aliyoifanya. Sasa alikuwa hajalala na mwanaume, na ikawa desturi katika Israeli40kwamba binti za Israeli kila mwaka, kwa siku nne, waweze kurejea hadithi ya binti ya Yeftha Mgileadi.

12

1Watu wa Efraimu walitoka pamoja; nao wakapitia Zafoni, wakamwambia Yeftha, “Kwa nini umetangulia kupigana na wana wa Amoni, wala hukutuita twende pamoja nawe? Tutachoma nyumba yako.”

2Yeftha akawaambia, “Mimi na watu wangu tulikuwa katika vita kubwa na wana wa Amoni. Nilipokuita, hukuniokoa kutoka kwao.3Nilipoona ya kuwa hamkuniokoa, nikaweka uhai wangu na nguvu yangu mwenyewe, na kupita kipita ili kupigana na wana wa Amoni, na Bwana alinipa ushindi. Kwa nini mmekuja kupigana nami leo?”

4Yeftha akawakusanya watu wote wa Gileadi na akapigana na Efraimu. Watu wa Gileadi waliwaangamiza wana wa Efraimu kwa sababu walisema, “Ninyi Wagileadi ni wakimbizi katika Efraimu-katika Efraimu na Manase.”5Wagileadi waliteketeza ngome za Yordani zinazoelekea Efraimu. Ikiwa yeyote kati ya waliopona wa Efraimu akisema, “Nipe ruhusa niende juu ya mto;” watu wa Gileadi wakamwambia, “Je, wewe ni Mwefraimu?” Ikiwa akasema, “Hapana,”6basi watamwambia, “Sema Shiboleth.” Na kama akisema ‘Sibboleth’ (kwa maana hakuweza kutamka neno hilo kwa usahihi), Wagileadi watamkamata na kumwua kwenye mabwawa ya Yordani. Waefraimu 42,000 waliuawa wakati huo.7Yeftha alikuwa mwamuzi juu ya Israeli kwa miaka sita. Ndipo Yeftha Mgileadi akafa, akazikwa katika moja ya miji ya Gileadi.

8Baada yake, Ibzani wa Bethlehemu akawa mwamuzi juu ya Israeli.9Alikuwa na wana thelathini. Aliwapeleka binti thelathini katika ndoa, naye akaleta binti thelathini kutoka nje kwa ajili ya wanawe. Alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka saba.10Ibzani alikufa na kuzikwa huko Bethlehemu.

11Baada yake, Eloni wa Zabuloni akawa mwamuzi juu ya Israeli. Akawaamua Israeli kwa miaka kumi.12Eloni wa Zabuloni akafa, akazikwa huko Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni.

13Baada ya huyo, Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akawa mwamuzi juu ya Israeli.14Alikuwa na wana arobaini na wajukuu thelathini. Walikuwa wakipanda punda sabini, naye akawaamua Israeli kwa miaka nane.15Abdoni mwana wa Hileli, Mpirathoni, akafa, akazikwa huko Pirathoni katika nchi ya Efraimu, katika kilima cha Waamaleki.

13

1Watu wa Israeli wakafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, naye akawatia mikononi mwa Wafilisti kwa miaka arobaini.

2Kulikuwa na mtu kutoka Sora, wa jamaa ya Wadani, jina lake Manoa. Mke wake hakuweza kupata mimba na hivyo hakuzaa.3Malaika wa Bwana akamtokea yule mwanamke akamwambia, “Tazame sasa, umeshindwa kupata mimba, wala hujazaa, lakini utakuwa na mimba na utazaa mtoto.4Sasa kuwa makini usinywe divai au kileo, wala usile kitu chochote kilicho najisi.5Angalia, utakuwa na mjamzito na kuzaliwa mtoto mwanaume. Hakuna wembe itakayotumiwa juu ya kichwa chake, kwa kuwa mtoto atakuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni, naye ataanza kuwaokoa Israeli kutoka mkono wa Wafilisti.”

6Kisha mwanamke akaenda kumwambia mumewe, “Mtu wa Mungu alikuja kwangu, na kuonekana kwake kulikuwa kama malaika wa Mungu, wa kutisha sana. Sikumwuliza ametokea wapi, na hakuniambia jina lake.7Akaniambia, ‘Tazama! Utakuwa mjamzito, na utazaa mtoto. Basi usinywe divai au kileo, wala usile chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi, kwa kuwa mtoto huyo atakuwa Mnaziri kwa Mungu tangu alipokuwa tumboni mwako mpaka siku ya kufa kwake.’”

8Ndipo Manoa akamwomba Bwana, akasema, “Ee Bwana, tafadhali mruhusu mtu wa Mungu uliyemtuma arudi kwetu ili atufundishe kile tutakachotendea kwa mtoto atakayezaliwa hivi karibuni.”

9Mungu akajibu sala ya Manoa, na malaika wa Mungu akamwendea mwanamke tena akiwa ameketi shambani. Lakini Manoa mumewe hakuwa pamoja naye.10Basi mwanamke akakimbia haraka akamwambia mumewe, “Tazama! Yule mtu ameonekana kwangu-aliyekuja kwangu siku ile!”

11Manoa akasimama na kumfuata mkewe. Alipofika kwa mtu huyo, akasema, “Je, wewe ndiwe mtu aliyezungumza na mke wangu?” Mtu huyo akasema, “Ni mimi.”

12Manoa akasema, “Sasa maneno yako yatimike. Je! Kuna maagizo gani kwa ajili ya mtoto, na kazi yake itakuwa nini?”

13Malaika wa Bwana akamwambia Manoa, “Lazima mkeo afanye kila kitu nilichomwambia.14Asile kitu chochote kinachotokana na mizabibu, wala usimruhusu kunywa divai au kileo; usimruhusu ale chakula chochote ambacho sheria inasema kuwa si safi. Anapaswa kutii kila kitu nilichoamuru afanye.”

15Manoa akamwambia malaika wa Bwana, “Tafadhali keti kwa muda, utupe wakati wa kuandaa mbuzi kwa ajili yako.”

16Malaika wa Bwana akamwambia Manoa, “Hata kama nitakaa, sitakula chakula chako. Lakini ukitayarisha sadaka ya kuteketezwa, toa kwa Bwana.” (Manoa hakujua kwamba alikuwa malaika wa Bwana.)

17Manoa akamwambia malaika wa Bwana, “Jina lako ni nani, ili tukuheshimu wakati maneno yako yatakapotimia?”

18Malaika wa Bwana akamwambia, “Mbona unauliza jina langu? Ni ajabu!”19Manoa akamchukua huyo mbuzi pamoja na sadaka ya nafaka, akatoa sadaka juu ya mwamba kwa Bwana. Alifanya jambo la ajabu wakati Manoa na mke wake walikuwa wakiangalia.20Wakati huo moto ukatoka juu ya madhabahu kwenda mbinguni, malaika wa Bwana akapanda katika moto wa madhabahu. Manoa na mkewe waliona jambo hilo wakainamisha vichwa vyao chini.21Malaika wa Bwana hakuonekana tena kwa Manoa au mkewe. Manoa akajua kwamba yule ndiye malaika wa Bwana.

22Manoa akamwambia mkewe, “Hakika tutakufa, kwa sababu tumemwona Mungu!”

23Lakini mkewe akamwambia, “Ikiwa Bwana alitaka kutuua, asingepokea sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya nafaka tuliyompa. Asingetuonesha mambo haya yote, wala wakati huu asingeweza kuturuhusu tusikie mambo hayo.”

24Baadaye mwanamke akamzaa mtoto, akamwita jina lake Samsoni. Mtoto alikua na Bwana akambariki.25Roho wa Bwana akaanza kumchochea Mahane Dani, kati ya Sora na Eshtaoli.

14

1Samsoni akashuka kwenda Timna, na huko akaona mwanamke, mmoja wapo wa binti za Wafilisti. Aliporudi, akamwambia baba yake na mama yake,2“Nimemwona mwanamke huko Timna, mmoja wapo wa binti za Wafilisti. Sasa mkanichukulie awe mke wangu.”

3Baba yake na mama yake wakamwambia, “Je, hakuna mwanamke kati ya binti za ndugu zako, au kati ya watu wetu wote? Je! Utachukua mke kutoka kwa Wafilisti wasiotahiriwa?” Samsoni akamwambia baba yake, “Nichukulie kwa ajili yangu, kwa maana wakati nilipomwangalia, alinipendeza.”4Lakini baba yake na mama yake hawakujua kwamba suala hili lilikuja kutoka kwa Bwana, kwa maana alitaka kutengeneza mgogoro na Wafilisti (kwa wakati huo Wafilisti walikuwa wakitawala Israeli).5Basi Samsoni akaenda Timna pamoja na baba yake na mama yake; nao wakafika kwenye mashamba ya mizabibu ya Timna. Na, tazama, kuna simba mdogo alikuja na alikuwa akiunguruma.6Roho wa Bwana ghafla akaja juu yake, naye akamrarua simba kwa urahisi kama ambavyo angeweza kumrarua mbuzi mdogo, naye hakuwa na kitu mkononi mwake. Lakini hakuwaambia baba au mama yake kile alichofanya.7Alikwenda na kuzungumza na mwanamke, na alipomtazama, alimpendeza Samsoni.

8Siku chache baadaye aliporudi kumwoa, akageuka na kutafuta mzoga wa simba. Na, tazama, kulikuwa na kundi la nyuki na asali katika kile kilichobaki katika mwili wa simba.9Akaweka asali mikononi mwake na akaenda, akala huku akienda. Alipokuja kwa baba yake na mama yake, akawapa, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa amechukua asali nje ya kile kilichobaki kwenye mwili wa simba.

10Baba yake Samsoni akaenda chini alipokuwa mwanamke, na Samsoni akafanya sikukuu huko, kwa maana hii ilikuwa desturi ya vijana.11Mara tu ndugu zake walipomwona, walimletea rafiki zao thelathini kuwa pamoja naye.

12Samsoni akawaambia, “Hebu nawaambieni kitendawili. Ikiwa mmoja wenu anaweza kuipata na kuniambia jibu wakati wa siku saba za sikukuu, nitatoa nguo za kitani thelathini na seti ya nguo thelathini.13Lakini ikiwa hamuwezi kuniambia jibu, basi mtanipa nguo za kitani thelathini na seti za nguo thelathini.” Wakamwambia, “Utuambie kitendawili chako, ili tukisikie.”

14Akawaambia, “Kati ya mtu aliyekula alikuwa kitu cha kula; nje ya nguvu ilikuwa kitu tamu.” Lakini wageni wake hawakuweza kupata jibu katika siku tatu.

15Siku ya nne wakamwambia mkewe Samsoni, “Mdanganye mume wako ili atuambie jibu la kitendawili, au tutakuchoma moto wewe na nyumba ya baba yako. Je, umetualika hapa ili kutufanya maskini?”

16Mke wa Samsoni alianza kulia mbele yake; Akasema, “Yote unayoyafanya ni kunichukia! Hunipendi. Umesema kitendawili kwa baadhi ya watu wangu, lakini hujawaambia jibu.” Samsoni akamwambia, “Angalia hapa, kama sijawaambia baba yangu au mama yangu, nikuambie wewe?”17Alilia kwa siku saba ambazo sikukuu yao iliendelea. Siku ya saba alimwambia jibu kwa sababu alimlazimisha sana. Akawaambia jibu jamaa zake.

18Na watu wa mji wakamwambia, siku ya saba kabla ya jua kuzama, “Ni nini kilicho bora zaidi kuliko asali? Ni kitu gani chenye nguvu kuliko simba?” Samsoni akawaambia, “Ikiwa hamkulima na ng'ombe wangu, hamngepata jibu la kitendawili changu.”

19Kisha Roho wa Bwana akaja kwa Samsoni kwa nguvu. Samsoni akashuka kwenda Ashkeloni na kuuwa watu thelathini kati ya watu hao. Akachukua mateka yao, na akawapa seti ya nguo kwa wale waliomjibu kitendawili chake. Alikasirika akaenda nyumbani kwa baba yake.20Na mke wake akachukuliwa na rafiki yake wa karibu.

15

1Baada ya siku kadhaa, wakati wa mavuno ya ngano, Samsoni akachukua mbuzi mdogo akaenda kumtembelea mkewe. Akajiambia mwenyewe, “Nitaenda kwenye chumba cha mke wangu.” Lakini baba yake hakumruhusu aingie.

2Baba yake akasema, “Nilidhani umemchukia, hivyo nikampatia rafiki yako. Dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye, mchukue badala yake.”

3Samsoni akawaambia, “Wakati huu sitakuwa na hatia juu ya Wafilisti wakati nikiwaumiza.”4Samsoni akaenda na kukamata mbweha 300 akawafunga pamoja kila jozi, mkia hadi mkia. Kisha akachukua taa na kuzifunga katikati ya kila mkia.5Alipokwisha kuviwasha moto vienge, akawaachia mbweha katika nafaka za Wafilisti zilizosimama, nao wakawasha moto nafaka zote zilizopandwa, na nafaka iliyosimama shambani, pamoja na mashamba ya mizabibu na mizeituni.

6Wafilisti waliuliza, “Ni nani aliyefanya hili?” Wakaambiwa, “Samsoni, mkwe wa Mtimna alifanya hivyo kwa sababu Mtimna alimchukua mke wa Samsoni akampa rafiki yake. “Basi Wafilisti wakamwendea wakamchoma kwa moto yeye na baba yake.

7Samsoni akawaambia, “Ikiwa ndivyo mnavyofanya, nitalipiza kisasi juu yenu, na baada ya hayo, nitaacha.”8Kisha akawakata vipande vipande, paja na mguu, kwa kuwauwa sana. Kisha akashuka chini akaishi katika pango katika mwamba wa Etamu.

9Ndipo Wafilisti wakaja, wakajitahidi kupigana vita huko Yuda, wakaanzisha jeshi lao huko Lehi.10Watu wa Yuda wakasema, “Kwa nini mmekuja kutupiga?” Wakasema, “Tunashambulia ili tuweze kumkamata Samsoni, na tumtendee kama alivyotutendea.”

11Kisha watu 3,000 wa Yuda wakashuka hata kwenye pango la Etamu, wakamwambia Samsoni, “Je, hujui kwamba Wafilisti hutawala juu yetu? Je! Umetutendea nini?” Samsoni akawaambia, “Kwa kadili walivyonitendea mimi, vivyo hivyo nimewatendea wao.”

12Wakamwambia Samsoni, “Tumeshuka kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba hamtaniua ninyi wenyewe.”

13Wakamwambia, “La, tutakufunga tu kwa kamba na kukupeleka kwao. Tunakuahidi sisi hatutakuua.” Kisha wakamfunga na kamba mbili mpya na kumleta kutoka kwenye mwamba.14Alipofika Lehi, Wafilisti walipiga kelele walipokutana naye. Kisha Roho wa Bwana akaja juu yake kwa nguvu. Kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitambaa cha kuteketezwa, na zikaanguka mikononi mwake.15Samsoni alipata mfupa mbichi wa taya ya punda, naye akaichukua na kuua watu elfu kwa mfupa huo.16Samsoni akasema, “Kwa taya ya punda, chungu juu ya chungu, na njaa ya punda nimewaua watu elfu.”17Samsoni alipomaliza kuzungumza, akatupa taya, na akaita mahali pale Ramath Lehi.

18Samsoni alikuwa na kiu sana akamwita Bwana na kusema, “Umempa mtumishi wako ushindi mkubwa. Lakini sasa nitakufa kwa kiu na kuanguka mikononi mwa wale wasiootahiriwa?”19Na Mungu akapafungua mahali pa shimo palipo katika Lehi, na maji yakatoka. Alipokunywa, nguvu zake zikarejea na akahuishwa. Kwa hiyo aliita jina la mahali hapo Enhakore, na ni huko Lehi hadi leo.

20Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli katika siku za Wafilisti kwa miaka ishirini.

16

1Samsoni alikwenda Gaza na akamwona kahaba huko, naye akalala pamoja naye.2Watu wa Gaza wakaambiwa, “Samsoni amekuja hapa.” Watu wa Gaza wakazunguka mahali hapo kwa siri, wakamngoja usiku wote katika lango la mji. Walikaa kimya usiku wote. Wakisema, “Hebu tusubiri mpaka mchana, na kisha tumwuue.”

3Samsoni akalala kitandani mpaka usiku wa manane. Usiku wa manane akaamka na akashika lango la mji na miimo yake miwili. Akavivuta kutoka nje, komeo na vyote, akaviweka kwenye mabega yake, akavichukua hadi juu ya kilima, mbele ya Hebroni.

4Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke aliyeishi katika bonde la Soreki. Jina lake alikuwa Delila.5Wale wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, “Mdanganye Samsoni ili uone mahali zilipo nguvu zake kuu, na kwa namna gani tunaweza kumshinda, ili tumfunge na kumtesa. Fanya hili, na kila mmoja wetu atakupa vipande elfu moja na mia moja vya fedha.”

6Ndipo Delila akamwambia Samsoni, “Tafadhali, niambie ni kwa jinsi gani wewe ni mwenye nguvu sana, na kwa namna gani mtu anaweza kukufunga, ili aweze kukudhibiti?”

7Samsoni akamwambia, “Ikiwa watanifunga na kamba saba safi ambazo hazijakauka, nitakuwa dhaifu na kuwa kama mtu mwingine yeyote.”

8Basi wakuu wa Wafilisti wakamletea Delila kamba saba ambazo hazijakauka, naye akamfunga Samsoni.9Sasa alikuwa na watu waliojificha kwa siri, walikaa katika chumba chake cha ndani. Akamwambia, “Wafilisti wako juu yako, Samsoni!” Lakini akazikata kamba kama uzi wakati unapogusa moto. Na hawakujifunza siri ya nguvu zake.

10Ndipo Delila akamwambia Samsoni, “Ndivyo ulivyonidanganya mimi na kuniambia uongo. Tafadhali, niambie kwa namna gani unaweza kufungwa.”

11Akamwambia, “Ikiwa watanifunga na kamba mpya ambayo haijawahi kutumika kwa kazi, nitakuwa dhaifu na kama mtu mwingine yeyote.”

12Basi Delila alichukua kamba mpya akamfunga pamoja naye, akamwambia, “Wafilisti wako juu yako Samsoni!” Watu waliokuwa wakisubiri walikuwa ndani ya chumba cha ndani. Lakini Samsoni akaondoa kamba kutoka mikono yake kama kilikuwa kipande cha uzi.

13Delila akamwambia Samsoni, “Mpaka sasa umenidanganya na kuniambia uongo. Niambie kwa namna gani unaweza kufungwa.” Samsoni akamwambia, ‘Ikiwa utavifuma vifungo saba vya nywele zangu na kuvifunga kwenye kitambaa, kisha kufunga kwenye msumari, nitakuwa kama mtu mwingine yeyote.”14Alipokuwa amelala, Dalila akavifuma vifungo saba vya nywele zake akavifunga ndani ya kitambaa na kuzifunga kwenye msumari, akamwambia, “Wafilisti wako juu yako, Samsoni!” Aliamka kutoka usingizini akang'oa kitambaa na pini zilizokuwa zimefungwa.

15Akamwambia, “Wawezaje kusema unanipenda, wakati hushiriki siri zako na mimi? Umenidhihaki mara tatu hizi na hukuniambia ni kwa jinsi gani unazo nguvu nyingi.”16Kila siku alisisitiza kwa bidii na maneno yake, naye akamkemea sana kiasi kwamba alitamani kufa.

17Basi Samsoni alimwambia kila kitu, akamwambia, “Wembe haujawahi kukata nywele juu ya kichwa changu, kwa maana nimekuwa Mnaziri kwa Mungu kutoka tumboni mwa mama yangu. Ikiwa kichwa changu kitanyolewa, basi nguvu zangu zitaniacha, nami nitakuwa dhaifu na kuwa kama kila mtu mwingine.”

18Delila alipoona kwamba amemwambia ukweli juu ya kila kitu, akawatuma na kuwaita watawala wa Wafilisti, akisema, “Njooni tena, kwa maana ameniambia kila kitu. “Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakaleta fedha mkononi mwao.19Alimfanya alale katika magoti yake. Alimwita mtu avinyoe vifungo saba vya kichwa chake, naye akaanza kumshinda, kwa maana nguvu zake zilikuwa zimemwacha.

20Alisema, “Wafilisti wako juu yako, Samsoni!” Aliamka nje ya usingizi wake akasema, “Nitatoka nje kama nyakati nyingine na kujiweka huru.” Lakini hakujua kwamba Bwana amemwacha.

21Wafilisti walimkamata na kumng'oa macho. Wakampeleka Gaza na kumfunga kwa shaba. Alikuwa akisaga ngano katika gerezani.22Lakini nywele juu ya kichwa chake zilianza kukua tena baada ya kunyolewa.

23Watawala wa Wafilisti walikusanyika ili kutoa dhabihu kubwa kwa Dagoni mungu wao, na kufurahi. Walisema, “Mungu wetu amemshinda Samsoni, adui yetu, na kumtia katika ufahamu wetu.”

24Watu walipomwona, walimsifu mungu wao, kwa sababu walisema, “Mungu wetu ameshinda adui yetu na kutupa sisi - mharibifu wa nchi yetu, ambaye aliwaua wengi wetu.”

25Walipokuwa wakisherehekea, wakasema, “Mwite Samsoni, aje kutufurahisha.” Walimwita Samsoni nje ya jela na akawafanya wacheke. Walimsimamisha katikati ya nguzo.26Samsoni akamwambia yule kijana ambaye alikuwa ameshika mkono wake, “Niruhusu nishike nguzo zilizoshikilia nyumba hii, ili nipate kuegemea.”27Sasa nyumba ilikuwa imejaa wanaume na wanawake. Watawala wote wa Wafilisti walikuwa huko. Juu ya paa kulikuwa na wanaume na wanawake 3,000 ambao walikuwa wakiangalia wakati Samsoni alipokuwa akiwafurahisha.28Samsoni akamwita Bwana, akasema, “Bwana MUNGU, nipe nia! Tafadhali niimarishe mara moja tu, Mungu, ili nipate kulipiza kisasi kwa Wafilisti kwa kuchukua macho yangu mawili.”29Samsoni aliweka nguzo mbili katikati ambazo zinashikilia nyumba hiyo, naye akaegemea juu yake, nguzo moja kwa mkono wake wa kuume, na mwingine kwa kushoto kwake.30Samsoni akasema, “Na nife pamoja na Wafilisti!” Alipanda kwa nguvu zake na jengo likaanguka juu ya watawala na juu ya watu wote waliokuwa ndani yake. Hivyo waliouawa wakati alikufa walikuwa zaidi ya wale waliouawa wakati wa maisha yake.

31Kisha ndugu zake na nyumba yote ya baba yake wakashuka. Wakamchukua, wakamrudisha na kumzika kati ya Sora na Eshtaoli katika mahali pa kuzikwa Manoa, baba yake. Samsoni alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka ishirini.

17

1Kulikuwa na mtu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na jina lake ni Mika.2Akamwambia mama yake, “Vipande 1,100 vya fedha ambazo zilichukuliwa kutoka kwako, ambazo ulizungumza kwa kiapo, na kuniambia- ‘Tazama hapa!’ Ninazo fedha pamoja nami. Nimeziiba.” Mama yake akasema, “Na Bwana atakubariki, mwanangu!”

3Alirejesha vipande 1,100 vya fedha kwa mama yake na mama yake akasema, “Nimeweka fedha hii kwa Bwana, kwa ajili ya mwanangu kuifanya na kuchonga takwimu za chuma.

4Kwa hiyo sasa, ninarejesha.” Alipokuwa amrudishia mama yake fedha, mama yake alichukua vipande 200 vya fedha na akampa mfanyakazi wa chuma ambaye alivifanya kuwa sanamu na kuchonga takwimu za chuma, na wakawekwa ndani ya nyumba ya Mika.

5Mtu huyo Mika alikuwa na nyumba ya sanamu, naye akafanya efodi na nyumba ya miungu, naye akaajiri mmoja wa wanawe awe mkuhani wake.6Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli, na kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake.

7Kisha kulikuwa na kijana mmoja wa Bethlehemu huko Yuda, wa jamaa ya Yuda, ambaye alikuwa Mlawi. Alikaa huko ili kutimiza majukumu yake.8Mtu huyo aliondoka Bethlehemu huko Yuda kwenda kutafuta mahali pa kuishi. Alipokuwa akienda, afika nyumbani kwa Mika katika nchi ya mlima wa Efraimu.

9Mika akamwambia, “Unatoka wapi?” Huyo mtu akamwambia, “Mimi ni Mlawi wa Bethlehemu huko Yuda, ninakwenda kutafuta mahali nipate kuishi.”10Mika akamwambia, “Kaa pamoja nami, uwe baba yangu na kuhani wangu. Nitakupa vipande kumi vya fedha kwa mwaka, suti ya nguo, na chakula chako.” Basi Mlawi akaingia nyumbani mwake.11Mlawi alikuwa na furaha ya kuishi na mtu huyo, na huyo kijana kwa Mika akawa kama mmoja wa wanawe.12Mika akamtenga Mlawi kwa ajili ya kazi takatifu, na huyo kijana akawa kuhani wake, naye alikuwa katika nyumba ya Mika.13Ndipo Mika akasema, “Sasa najua ya kuwa Bwana atanifanyia mema, kwa kuwa Mlawi huyu amekuwa kuhani wangu.”

18

1Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli. Kabila la Wadani lilikuwa linatafuta makazi ya kuishi, kwa maana mpaka siku hiyo hawakupokea urithi wowote kutoka miongoni mwa makabila ya Israeli.2Watu wa Dani walituma watu watano kutoka kwa idadi yote ya kabila lao, wanaume wenye ujasiri kutoka Sora na kutoka Eshtaoi, ili kukagua ardhi kwa miguu, na kuiangalia. Wakawaambia, “Nendeni mkaangalie nchi.” Wakafika nchi ya mlima wa Efraimu, kwa nyumba ya Mika wakalala huko.3Walipokuwa karibu na nyumba ya Mika, walitambua maneno ya Mlawi. Basi wakasimama na kumwuliza, “Nani alikuleta hapa? Unafanya nini hapa? Kwa nini uko hapa?”

4Akawaambia, “Hivi ndivyo Mika amefanya kwa ajili yangu. Yeye aliniajiri mimi kuwa kuhani wake.”

5Wakamwambia, “Tafadhali tafuta ushauri kwa Mungu, ili tuweze kujua kama safari tunayoendea itafanikiwa.”

6Kuhani huyo akawaambia, “Nenda kwa amani. Bwana atakuongoza katika njia unayoiendea.”

7Kisha wale watu watano wakaondoka na wakafika Laishia, na waliona watu waliokuwa pale waliishi salama- vivyo hivyo Wasidoni waliishi bila kusumbuliwa na kwa usalama. Hapakuwa na mtu aliyewashinda katika nchi hiyo, au aliyewasumbua kwa namna yoyote. Waliishi mbali na Wasidoni, na hawakuwa na ushirikiano na mtu yeyote.

8Walirudi kwa kabila lao huko Zora na Eshtaol. Ndugu zao waliwauliza, “Mna habari gani?”

9Wakasema, “Njoo! Hebu tuwashambulie! Tumeona ardhi na ni nzuri sana. Je hamfanyi kitu? Msiwe wavivu kushambulia na kuchukua ardhi.10Mnapoenda, mtakuta watu wanaofikiri wapo salama, na nchi ni pana! Mungu amewapa ninyi-mahali ambako hapajapungukiwa kitu chochote duniani.”

11Watu 600 wa kabila la Dani, wenye silaha za vita, waliondoka kutoka Sora na Eshtaoli.12Wakasafiri, wakapanga Kiriath-yearimu, huko Yuda. Ndio maana watu walipaita mahali pale Mahane Dani hata leo; ni magharibi ya Kiriath yearimu.13Wakaondoka huko na kwenda nchi ya mlima wa Efraimu, wakafika nyumbani kwa Mika.

14Kisha watu watano waliokuwa wamekwenda kutazama nchi ya Laisha waliwaambia jamaa zao, “Je, mnajua kwamba katika nyumba hizi kuna efodi, miungu ya kaya, sanamu zilizochongwa, na sanamu za chuma? Amua sasa utakachofanya.”15Basi wakarudi huko, wakafika nyumbani mwa Mlawi, nyumbani mwa Mika; wakamsalimu.16Wana wa Dani 600, wenye silaha za vita, walisimama kwenye maingilio ya lango.17Wale watu watano waliokuwa wamekwenda kutembelea nchi walikwenda huko na wakachukua sanamu zilizochongwa, efodi, na miungu ya nyumba, na sanamu ya chuma, wakati kuhani alipokuwa amesimama kwenye maingilio ya lango na wanaume 600 wenye silaha za vita.

18Walipokuwa wakiingia nyumbani kwa Mika na kuchukua sanamu zilizochongwa, efodi, miungu ya nyumba, na sanamu za chuma, kuhani akasema, “Mnafanya nini?”

19Wakamwambia, “Tulia! Weka mkono wako kwenye kinywa chako na uje nasi, na uwe kwetu baba na kuhani. Je, ni bora kuwa wewe kuhani kwa ajili ya nyumba ya mtu mmoja, au kuhani kwa kabila na jamaa katika Israeli?”20Moyo wa kuhani ulifurahi. Akachukua efodi, miungu ya nyumba, na sanamu ya kuchongwa, akaenda pamoja na hao watu.21Basi wakageuka wakaenda. Wameweka watoto wadogo mbele yao wenyewe, pamoja na ng'ombe na mali zao.

22Walipokuwa umbali mzuri kutoka kwa nyumba ya Mika, watu waliokuwa ndani ya nyumba iliyo karibu na nyumba ya Mika waliitwa, nao wakawafikia Wadani.23Waliwapigia kelele Wadani, nao wakageuka, wakamwambia Mika, “Kwa nini mmekuja pamoja?”

24Akasema, “Ninyi mmeiba miungu niliyoifanya, mmemchukua kuhani wangu, na mnaondoka. Je, nina nini tena? Unawezaje kuniuliza, ‘Ni nini kinachokusumbua?’”

25Watu wa Dani wakamwambia, “Usiruhusu tusikie chochote unachosema, au baadhi ya watu wenye hasira sana watawapiga, wewe na familia yako mtauawa.”26Ndipo watu wa Dani wakaenda zao. Mika alipoona kwamba walikuwa na nguvu sana juu yake, akageuka na kurudi nyumbani kwake.

27Watu wa Dani walichukua kile alichokifanya Mika, pamoja na kuhani wake, na wakafika Laisha, kwa watu waliokuwa hawasumbuliwi na wenye usalama na salama wakawaua kwa upanga na kuuchoma mji huo.28Hapakuwa na mtu wa kuwaokoa kwa sababu palikuwa na umbali mrefu kutoka Sidoni, na hawakuwa na uhusiano na mtu yeyote. Palikuwa katika bonde lililo karibu na Beth Rehobu. Wadani wakaujenga mji na kuishi huko.29Wakauita jina lake Dani, jina la baba zao Dani, ambaye alikuwa mmoja wa wana wa Israeli. Lakini jina la mji hapo mwanzo ulikuwa Laisha.30Watu wa Dani walijenga sanamu za kuchonga wenyewe. Naye Yonathani, mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa makuhani wa kabila la Wadani mpaka siku ya uhamisho wa nchi.31Basi wakaiabudu sanamu ya kuchonga ya Mika aliyoifanya wakati wa nyumba ya Mungu huko Shilo.

19

1Katika siku hizo, wakati hakuna mfalme katika Israeli, kulikuwa na mtu, Mlawi, aliyekuwa akiishi kwa muda kidogo katika eneo la mbali zaidi ya nchi ya Efraimu. Alijichukulia mwanamke, masuria kutoka Bethlehemu huko Yuda.2Lakini mkewe hakuwa mwaminifu kwake; akaondoka na kurudi nyumbani kwa baba yake huko Bethlehemu ya Yuda. Alikaa huko kwa muda wa miezi minne.3Kisha mumewe akaondoka na kumfuata ili kumshawishi arudi. Mtumishi wake alikuwa pamoja naye, na punda wawili. Akamleta nyumbani kwa baba yake. Baba wa msichana alipomwona, alifurahi.4Baba mkwe wake, baba wa msichana, alimshawishi kukaa siku tatu. Walikula na kunywa, na walikaa usiku huko.

5Siku ya nne waliamka mapema na alijiandaa kuondoka, lakini baba wa msichana akamwambia mkwewe, “Jipe nguvu na mkate kidogo, kisha unaweza kwenda.”6Basi hao wawili wakaketi kula na kunywa pamoja. Kisha baba ya msichana akasema, “Tafadhali uwe tayari kukaa usiku huu na kuwa na wakati mzuri.”7Mlawi alipoinuka ili aondoke, baba wa mwanamke huyo alimwomba akae, hivyo alibadili mpango wake na akalala usiku tena.8Siku ya tano aliamka mapema kuondoka, lakini baba wa msichana akasema, “Jitie nguvu mwenyewe, na kusubiri mpaka alasiri.” Kwa hiyo hao wawili wakala chakula.

9Mlawi na suria wake na mtumishi wake wakainuka ili kuondoka, baba mkwe wake, baba wa msichana akamwambia, “Angalia, sasa mchana unaelekea jioni. Tafadhali kaa usiku mwingine, na uwe na wakati mzuri. Unaweza kuamka kesho mapema na kurudi nyumbani.”10Lakini Mlawi hakuwa tayari kukaa usiku. Aliamka na kuondoka. Akaenda kuelekea Yebusi (hiyo ni Yerusalemu). Alikuwa na pande mbili za punda-na masuria wake walikuwa pamoja naye.

11Walipokuwa karibu na Yebusi, siku hiyo ilikuwa imeenda mno, na mtumishi akamwambia bwana wake, “Haya, tupate kwenda kwa mji wa Wayebusi, tukakae ndani yake usiku huu.”

12Bwana wake akamwambia, “Hatuwezi kwenda katika mji wa wageni ambao si wa wana wa Israeli.” Tutakwenda Gibea.13Mlawi akamwambia yule kijana, “Njoo, twende sehemu moja wapo, na tukae usiku huko Gibea au Rama.”14Basi, wakaenda, na jua likachwea wakiwa karibu na Gibea, katika eneo la Benyamini.15Wakageuka huko ili waweze kukaa usiku huko Gibea. Naye akaingia na kukaa katika njia kuu ya jiji, maana hakuna mtu aliyewaingiza nyumbani kwake usiku.

16Lakini mtu mzee alikuwa akija kutoka kazini kwake katika shamba jioni hiyo. Alikuwa kutoka mlima wa Efraimu, naye alikuwa akikaa kwa muda huko Gibea. Lakini watu wanaoishi mahali hapo walikuwa Wabenyamini.17Aliinua macho na kumwona msafiri katika njia kuu ya mji. Huyo mzee akasema, “Unakwenda wapi? Unatoka wapi?”

18Mlawi akamwambia, “Tunaenda kutoka Bethelehemu ya Yuda mpaka sehemu ya mbali zaidi ya nchi ya kilima ya Efraimu, ambako mimi hutoka. Nilikwenda Bethlehemu huko Yuda, nami naenda nyumbani mwa Bwana; lakini hakuna mtu atakayenichukua nyumbani kwake.19Tuna nyasi za kulisha punda zetu, na kuna mkate na divai kwa ajili yangu na mtumishi wako mwanamke hapa, na kwa kijana huyu pamoja na watumishi wako. Hatujapungukiwa chochote.”

20Huyo mzee akawasalimu, “Amani iwe na wewe! Nitakupatia mahitaji yako yote. Usikae usiku tu katika njia kuu.”21Basi huyo mtu akamleta Mlawi nyumbani kwake, akawalisha punda. Wakaosha miguu yao na kula na kunywa.

22Walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, watu wengine wa mji, watu wasiokuwa na maana, walizunguka nyumba, wakipiga mlango. Wakamwambia yule mzee, mwenye nyumba, wakisema, “Mtoe mtu aliyeingia nyumbani kwako, ili tuweze kuzini naye.”

23Yule mtu, mwenye nyumba, akawajia, akawaambia, “Hapana, ndugu zangu, tafadhali msifanye jambo baya! Kwa kuwa mtu huyu ni mgeni nyumbani kwangu, musifanye jambo hili baya!24Angalia, binti yangu bikira na masuria wake hawa hapa. Ngoja niwalete sasa. Wapuuze na kufanya nao chochote mnachopenda. Lakini msifanyie jambo hili mbaya kwa mtu huyu!”

25Lakini watu hawakumsikiliza, kwa hiyo huyo mwanamume akamshika yule mwanamke, akamleta nje. Walimkamata, wakambaka, na kumtendea uovu usiku mzima, na asubuhi wakamruhusu aende.26Asubuhi mwanamke alikuja akaanguka chini ya mlango wa nyumba ya mtu ambapo bwana wake alikuwa, na yeye akalala pale mpaka kulipokucha.

27Bwana wake akaondoka asubuhi na kufungua milango ya nyumba, akatoka kwenda njiani. Aliweza kumwona mwanamke wake amelala pale mlangoni, mikono yake ikiwa juu ya kizingiti.28Mlawi akamwambia, “Simama twende.” Lakini hakujibiwa. Alimuweka juu ya punda, na huyo mtu akaondoka nyumbani.

29Mlawi alipofika nyumbani kwake, akachukua kisu, naye akamshika suria wake, akamkataa, mguu kwa mguu, akafanya vipande kumi na viwili, akapeleka vipande kila mahali katika Israeli.30Wote waliona hili wakasema, “Kitu hicho hakijawahi kufanyika au kuonekana tangu siku ambayo watu wa Israeli walikuja kutoka nchi ya Misri mpaka leo. Fikiria juu ya hili! Tupe ushauri! Tuambie nini cha kufanya!”

20

1Ndipo watu wote wa Israeli wakatoka kama mtu mmoja, toka Dani mpaka Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi; nao wakakusanyika mbele za Bwana huko Mispa.2Viongozi wa watu wote, wa kabila zote za Israeli, wakachukua nafasi zao kwenye kusanyiko la watu wa Mungu-watu 400,000 waendao kwa miguu, ambao walikuwa tayari kupigana na upanga.3Basi wana wa Benyamini walisikia kwamba watu wa Israeli walikuwa wamepanda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, “Tuambieni ni kwa namna gani huu uovu umefanyika.”4Mlawi, mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu, “Nilikuja Gibea katika nchi ya Benyamini, mimi na suria wangu, ili tulale.5Wakati wa usiku, viongozi wa Gibea walinishambulia, wakizunguka nyumba na wakakusudia kuniua. Walimkamata na kumbaka suria wangu, naye akafa.6Nilimchukua suria wangu na kumkata mwili wake vipande vipande, na kuweka katika kila nchi ya urithi wa Israeli, kwa sababu wamefanya uovu huo na upumbavu katika Israeli.7Sasa, ninyi Waisraeli wote, toeni maneno na ushauri wenu hapa.”

8Watu wote wakaondoka pamoja kama mtu mmoja, wakasema, “Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake, wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake.9Lakini sasa hivi ndivyo tutakavyoifanyia Gibea tutaishambulia kama kura inavyotuongoza.10Tutachukua watu kumi katika mia moja katika makabila yote ya Israeli, na mia moja katika elfu, na elfu moja katika elfu kumi, kuwapa chakula kwa ajili ya watu hawa, ili waweze kufika Gibea katika Benyamini, watawaadhibu kwa uovu wao waliofanya katika Israeli.”11Basi askari wote wa Israeli wakakusanyika juu ya mji, kama mtu mmoja.

12Makabila ya Israeli waliwatuma watu kwa kabila lote la Benyamini, wakisema, “Uovu huu uliofanywa kati yenu ni nini?13Kwa hiyo, tupeni watu hao waovu wa Gibea, tupate kuwaua, na hivyo tutaondoa kabisa uovu huu kutoka kwa Israeli.” Lakini Wabenyamini hawakusikiliza sauti ya ndugu zao, watu wa Israeli,14Ndipo wana wa Benyamini wakakusanyika kutoka mijini kwenda Gibea, wakajiandaa kupigana na wana wa Israeli.15Watu wa Benyamini wakakusanya kutoka miji yao ili kupigana siku ile, askari 26,000 waliopangwa kupigana na upanga. Walakini, kuna watu 700 waliochaguliwa kutoka kwa wenyeji wa Gibea.16Miongoni mwa askari wote hawa walikuwa watu 700 waliochaguliwa ambao walikuwa wenye shoto. Kila mmoja wao angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose.

17Watu wa Israeli, bila kuhesabu namba kutoka kwa Benyamini, walikuwa na watu 400,000 waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga. Wote hawa walikuwa watu wa vita.

18Watu wa Israeli waliondoka, wakaenda Betheli, wakaomba ushauri kutoka kwa Mungu. Wakauliza, “Ni nani kwanza atakayewaangamiza watu wa Benyamini kwa ajili yetu?” Bwana akasema, “Yuda atashambulia kwanza.”

19Watu wa Israeli waliamka asubuhi na wakahamisha kambi yao karibu na Gibea.20Watu wa Israeli walikwenda kupigana na Benyamini. Wakaweka nafasi zao za vita dhidi yao huko Gibea.21Watu wa Benyamini wakatoka Gibea, nao wakawaua watu 22,000 wa jeshi la Israeli siku ile.22Wana wa Israeli walijitia nguvu wenyewe, na wakaunda mstari wa vita mahali pale walipokwisha kuchukua nafasi siku ya kwanza.23Na wana wa Israeli wakaenda, wakalia mbele za Bwana hata jioni. Walitaka mwongozo kutoka kwa Bwana “Je, tunapaswa kwenda tena kupigana na ndugu zetu, watu wa Benyamini?” Naye Bwana akasema, “Wapigeni!”24Basi watu wa Israeli wakapigana na askari wa Benyamini siku ya pili.25Siku ya pili, Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea, nao wakawaua watu wa Israeli 18,000. Wote walikuwa watu ambao walijifunza kupigana na upanga.

26Basi askari wote wa Israeli na watu wote wakaenda Betheli, wakalia, wakakaa mbele za Bwana; nao wakafunga siku hiyo hata jioni, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.27Wana wa Israeli wakamwomba Bwana, - kwa sababu ya sanduku la agano la Mungu lilikuwapo siku hizo;28na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, aliyekuwa akihudumia mbele ya sanduku siku hizo. “Je twende vitani tena dhidi ya watu wa Benyamini, ndugu zetu, au tuache?” Bwana akasema, “Wapigeni, kwa maana kesho nitawasaidia kuwashinda.”29Basi Israeli akaweka watu mahali pa siri karibu na Gibea.30Watu wa Israeli wakapigana na wana wa Benyamini kwa siku ya tatu, nao wakajenga vita vyao juu ya Gibea, kama walivyotangulia.31Watu wa Benyamini wakaenda kupigana na watu, nao wakachukuliwa mbali na mji. Walianza kuua baadhi ya watu. Kulikuwa na watu thelathini wa Israeli ambao walikufa katika mashamba na barabara. Njia moja ilienda Betheli, na nyingine ikaenda Gibea.

32Ndipo wana wa Benyamini wakasema, “Wameshindwa na wanatukimbia, kama hapo awali.” Lakini askari wa Israeli wakasema, “Hebu tukimbie na kuwavuta mbali na mji hadi barabarani.”

33Watu wote wa Israeli waliondoka kutoka mahali pao na wakajipanga kwa vita huko Baal-Tamari. Basi askari wa Israeli waliokuwa wakijificha mahali pa siri walikimbia kutoka Maare-Geba.34Wakatoka juu ya Gibea watu kumi elfu waliochaguliwa kutoka Israeli yote, na vita vilikuwa kali, lakini Wabenjamini hawakujua kwamba msiba ulikuwa karibu nao.35Bwana akamshinda Benyamini mbele ya Israeli. Siku hiyo, askari wa Israeli waliwauawa watu wa Benyamini 25,100. Wote hawa waliokufa walikuwa wale waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga.36Basi askari wa Benyamini waliona wameshindwa. Wana wa Israeli walikuwa wametoa ardhi kwa Benyamini, kwa kuwa walikuwa wakihesabu watu waliowaweka katika nafasi zilizofichwa nje ya Gibea.37Ndipo watu waliokuwa wameficha wakainuka na haraka na wakamkimbia Gibea. Nao wakauawa kila mtu aliyeishi mjini kwa upanga wao.38Ishara iliyopangwa kati ya askari wa Israeli na watu waliojificha kwa siri itakuwa wingu kubwa la moshi litatokea nje ya mji.

39Ishara ilipokuja askari wa Israeli wakageuka kutoka kwenye vita. Basi Benyamini wakaanza kushambulia na wakawaua watu wa Israeli thelathini, wakasema, “Hakika wanapigwa mbele yetu, kama katika vita vya kwanza.”40Lakini wakati nguzo ya moshi ilipoanza kuinuka nje ya mji, Wabenjamini waligeuka na kuona moshi ukitanda mbinguni kutoka mji mzima.41Ndipo watu wa Israeli wakawageuka. Wana wa Benyamini waliogopa, kwa sababu waliona kwamba maafa yaliwajia.42Basi wakakimbia kutoka kwa wana wa Israeli, kuelekea njia ya jangwani. Lakini vita viliwapata. Askari wa Israeli walitoka mijini na wakawaua pale waliposimama.43Waliwazungukia wana wa Benjamini na wakawafuata. Nao wakawakanyaga huko Noha, wakawaua mpaka upande wa mashariki wa Gibea.44Kutoka kabila la Benyamini, watu 18,000 walikufa, wote walikuwa wanaume waliojulikana katika vita.45Wakageuka na kukimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Waisraeli waliuawa zaidi ya elfu tano kati yao barabarani. Waliendelea kuwafuata, wakifuata kwa njia kuu kwenda Gidomu, na huko waliuawa elfu mbili zaidi.

46Askari wote wa Benyamini walioshuka siku hiyo walikuwa watu ishirini na tano waliokuwa wamejifunza kupigana kwa upanga; wote walikuwa wanajulikana katika vita.47Lakini watu mia sita wakageuka na kukimbilia jangwani, kuelekea mwamba wa Rimoni. Wakakaa katika mwamba wa Rimoni kwa muda wa miezi minne.48Askari wa Israeli waliwarudia watu wa Benyamini na wakawashinda na kuwaua-mji mzima, ng'ombe, na kila kitu walichopata. Pia walichoma moto kila mji katika njia yao.

21

1Sasa watu wa Israeli walikuwa wameahidi huko Mispa, “Hakuna hata mmoja wetu atakayempa binti yake kuolewa na Mbenyamini.”2Ndipo watu wakaenda Betheli, wakakaa huko mbele ya Mungu hata jioni; wakalia kwa sauti kubwa.3Walipiga kelele, “Kwa nini, Bwana, Mungu wa Israeli, amefanya jambo hili kwa Waisraeli, kwamba moja ya makabila yetu linapotea leo?”

4Siku iliyofuata watu waliamka mapema na wakajenga madhabahu huko na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.

5Watu wa Israeli wakasema, “Ni nani kati ya kabila zote za Israeli hawakuja katika mkutano wa Bwana?” Kwa kuwa walikuwa wamefanya ahadi muhimu juu ya mtu yeyote ambaye hakuja kwa Bwana huko Mispa. Wakasema, “Hakika yeye atauawa.”

6Watu wa Israeli walikuwa na huruma kwa ndugu yao Benyamini. Wakasema, “Leo hii kabila moja limekatiliwa mbali kutoka Israeli.7Ni nani atakayewapa wale walioachwa wake, kwa kuwa tumeahidi kwa Bwana kwamba hatuwezi kuwaruhusu yeyote kati yao aoe binti zetu?”8Wakasema, “Ni nani kati ya kabila za Israeli hawakuja kwa Bwana huko Mispa? Ilionekana kuwa hakuna mtu aliyekuja kwenye mkusanyiko kutoka Jabeshi-Gileadi.9Kwa maana watu walipokuwa wamepangwa kwa utaratibu, tazama, hakuna hata mmoja wa wenyeji wa Yabeshi Gileadi.

10Mkutano huo uliwatuma watu kumi na wawili wa watu wao wenye ujasiri kwa maagizo ya kwenda Yabeshi-gileadi na kuwaangamiza, na kuwaua, hata wanawake na watoto.11“Fanya hivi unapaswa kuua kila mume na kila mwanamke aliyelala na mwanaume.”12Watu wale walikuta watu kati ya hao waliokaa Yabeshi-gileadi, wanawake 400 ambao hawakulala na mwanaume, wakawapeleka kwenye kambi huko Shilo, huko Kanaani.

13Mkutano wote ukatuma ujumbe na kuwaambia watu wa Benyamini waliokuwa kwenye mwamba wa Rimoni kwamba walikuwa wanawapa amani.14Wabenyamini walirudi wakati huo na walipewa wanawake wa Yabeshi Gileadi, lakini hapakuwa na wanawake wa kutosha kwa wote.

15Watu waliomboleza kwa kile kilichotokea Benyamini, kwa kuwa Bwana alifanya mgawanyiko kati ya makabila ya Israeli.16Kisha wakuu wa mkutano wakasema, “Tutafanyaje ili Wabenyamini wapate wake, kwa kuwa wanawake wa Benyamini wameuwawa?”17Wakasema, “Lazima kuwe na urithi kwa Wabenyamini waliosalia, ili kabila lisiharibiwe kutoka Israeli.18Hatuwezi kuwapa wake kutoka kwa binti zetu, kwa kuwa wana wa Israeli walikuwa wametoa ahadi, ‘Na alaaniwe mtu atakayempa Benyamini mke.’”19Wakasema, “Mnajua kuwa kuna sikukuu kwa Bwana kila mwaka huko Shilo (ambayo ni kaskazini ya Betheli, mashariki ya barabara inayopanda kutoka Betheli hadi Shekemu, na kusini mwa Lebona).”

20Wakawaagiza wana wa Benyamini, wakisema, “Nendeni, mjifiche kwa siri, na kusubiri katika mashamba ya mizabibu.21Tazama wakati ambapo wasichana kutoka Shilo watatoka kucheza, Tokeni nje ya mizabibu na kila mmoja wenu anapaswa kunyakua mke kutoka kwa wasichana wa Shilo, kisha kurudi kwenye nchi ya Benyamini.22Wakati baba zao au ndugu zao watakapokuja kutupinga, tutawaambia, ‘Tupeni neema! Waache wabaki kwa sababu hatukupata wake kwa kila mtu wakati wa vita. Na ninyi hamna hatia juu ya ahadi, kwa sababu hamkuwapa wao binti zenu.’”

23Watu wa Benyamini walifanya hivyo. Walichukua idadi ya wake waliowahitaji kutoka kwa wasichana waliokuwa wakicheza, nao wakawachukua ili wawe wake zao. Wakaenda na kurudi mahali pa urithi wao; wakajenga tena miji, na wakaishi ndani yao.

24Kisha watu wa Israeli wakatoka mahali hapo na kwenda nyumbani, kila mmoja kwa kabila lake na ukoo, na kila mmoja kwa urithi wake mwenyewe.

25Siku hizo hapakuwa na mfalme huko Israeli. Kila mtu alifanya yaliyo sawa machoni pake mwenyewe.

Ruth

1

1Ilitokea katika siku za utawala wa majaji kuwa kulikuwa na njaa katika nchi, na mtu mmoja wa Bethelehemu ya Yuda alikwenda katika nchi ya Moabu pamoja na mke wake na watoto wake wawili wa kiume.2Jina la mtu huyo lilikuwa Elimeleki, na jina la mke wake lilikuwa Naomi. Majina ya watoto wake wawili wa kiume waliitwa Mahiloni na Kileoni, ambao walikuwa Waefraimu wa Bethelehemu ya Yuda. Waliwasili katika nchi ya Moabu na kuishi hapo.

3Ndipo Elimeleki, mume wa Naomi, alikufa, na Naomi aliachwa na watoto wake wa kiume wawili.4Watoto hawa walioa wanawake wa Moabu; jina la mmoja lilikuwa Oripa, na jina la mwingine lilikuwa Ruth. Waliishi huko kwa takribani miaka kumi.5Kisha wote Mahiloni na Kileoni walikufa, na kumuacha Naomi bila mme wake na bila watoto wake wawili.

6Ndipo Naomi aliamua kuondoka Moabu pamoja na wake wa watoto wake na kurudi Yuda kwa sababu alikuwa amesikia katika mkoa wa Moabu kuwa Yahweh amewasaidia watu wake katika uhitaji na amewapa chakula.7Hivyo aliondoka sehemu aliyokuwa pamoja na wake wa watoto wake wawili, waliteremka njia kurudi kwenye nchi ya Yuda.8Naomi aliwaambia wake wa watoto wake, “Nendeni, mrudi, kila mmoja wenu, kwenye nyumba ya mama yake. Na Mungu aonyeshe wema juu yenu, kama mlivyo onyesha wema kwao waliokufa na kwangu.9Mungu awajalie ninyi kupata pumziko, kila mmoja wenu katika nyumba ya mme mwingine.” Kisha akawabusu, na wakapaza sauti zao na kulia.10Wakamwambia, “Hapana! Tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako.”

11Lakini Naomi alisema, “Rudini, wanangu! Kwa nini mtakwenda na mimi? Kwani bado nina watoto katika tumbo langu kwa ajili yenu, ili kwamba waje wawe waume zenu?12Rudini, wanangu, nendeni katika njia zenu wenyewe, kwa kuwa mimi ni mzee sana kuwa na mme. Kama nikisema, ‘Natumaini nipate mume usiku huu,’ na kisha kuzaa watoto wakiume, kwa hiyo mnaweza kusubiri mpaka wakue?13Mtasubiri na msiolewe sasa? Hapana, wanangu! Ina nihuzunisha zaidi, kuliko inavyo wahuzunisha ninyi, kwa sababu mkono wa Yahweh umeenda kinyume na mimi.”

14Ndipo wake wa watoto wake wakapaza sauti zao na kulia tena. Oripa alimuaga kwa kumbusu, lakini Ruth aliendelea kubaki naye.15Naomi alisema, “sikiliza, mwenzako amerudi kwa watu wake na miungu yake. Rudi pamoja naye.”16Lakini Ruth alisema, “Usiniache niondoke mbali nawe, kwa kuwa uendako, nitakwenda, utakapoishi, nitaishi; watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu.17Mahali utakapofia, nitafia hapo, na hapo nitazikwa. Yahweh aniwezeshe, na hata zaidi, ikiwa kuna chochote isipokuwa kifo kamwe hakiwezi kututenganisha.18Naomi alipoona kuwa Ruth alikuwa ameamua kwenda naye, aliacha kubishana naye.

19Hivyo wote wawili walisafiri mpaka walipofika mjini Bethelehemu. Kwa hiyo walipofika Bethlehemu, mji wote uliwafurahia, wanawake walisema, “Huyu ni Naomi?”20Lakini aliwaambia, “Msiniite Naomi. Niiteni Mchungu, kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitenda mambo machungu sana.21Nilikwenda nikiwa nimejaa, lakini Yahweh kanirudisha nyumbani nikiwa sina wote. Hivyo kwa nini mnaniita Naomi, wakati mnaona Yahweh amenihukumu, kuwa Mwenyezi Mungu amenitaabisha?”

22Kwa hivyo Naomi na Ruth Mmoabu, mke wa mtoto wake, walirudi kutoka nchi ya Moabu. Walirudi Bethelehemu mwazo wa mavuno ya shairi.

2

1Basi Elimeleki mme wa Naomi, alikuwa na jamaa aitwaye Boazi, aliye kuwa tajiri, na mtu maarufu.

2Ruth, Mmoabu, alimwambia Naomi, “Ngoja niende nikakusanye mabaki ya chakula katika shamba. Nitamfuata yeyote ambaye nitapata kibali machoni pake.” Hivyo Naomi akamwambia, “Nenda, mwanangu.”3Ruth alienda kuvuna kwenye shamba akiwafuata kwa nyuma wavunaji. Na kumbe ile sehemu ya shamba ilikuwa ni mali ya Boazi, aliyekuwa na mahusiano na Elimeleki.

4Tazama, Boazi alikuja kutoka Bethelehemu na kuwaambia wavunaji, “Yahweh awe nanyi.” Wakamjibu, “Yahweh akubariki.”

5Ndipo Boazi akamwambia mtumishi wake aliyekuwa akiwasimamia wavunaji, “Vipi bwana, huyu msichana ni wa nani?”6Mtumishi - msimamizi wa wavunaji alijibu na kusema, “Ni msichana Mmoabu aliyerudi na Naomi kutoka nchi ya Moabu.7Aliniambia, ‘Tafadhali niruhusu kuvuna na kukusanya mabaki ya wavunaji.’ Hivyo alikuja na ameendelea kuvuna toka asubuhi mpaka sasa, isipokuwa amepumzika kidogo katika nyumba.”

8Kisha Boazi akamwambia Ruth, “Unanisikiliza, mwanangu? Usiende kuvuna kwenye shamba lingine; usiondoke shambani kwangu. Badala yake, baki hapa na wasichana wangu wa kazi.9Yaelekeze tu macho yako kwenye shamba ambalo wanaume wanavuna na ufuatie nyuma ya wanawake wengine. Je, sikuwaelekeza wanaume wasikuguse? Na upatapo kiu, unaweza kwenda kunywa maji kwenye mtungi ambao wanaume wamejaza.”

10Ndipo akapiga magoti mbele ya Boazi, na kugusisha kichwa chake chini. Akamwambia, “Kwa nini nimepata kibali machoni pako, hata unijali mimi mgeni?”11Boazi akajibu na kumwabia, “Nimekwisha ambiwa, yote uliyo yafanya tangu mme wako afariki. Umewaacha baba yako, mama, na nchi uliyozaliwa kumfuata mama mkwe wako na kuja kwa watu usiowajua.12Yahweh akulipe kwa matendo yako. Yahweh akulipe kwa wingi, Mungu wa Israeli, ambaye chini ya mbawa zake umepata kimbilio.”

13Ruth akasema, “Nipate kibali machoni pako, bwana wangu, kwa kuwa umenifariji, na umeongea wema kwangu, ingawa mimi sio mmoja wa watumishi wako wa kike.”

14Wakati wa chakula Boazi alimwambia Ruth, “Njoo hapa, ule baadhi ya mikate, na uchovye kipande katika divai.” Alikaa kando ya wavunaji, na Boazi akampatia kiasi cha nafaka zilizo kaangwa. Ruth alikula mpaka alipotosheka na kusaza.15Alipoinuka kwenda kuvuna, Boazi aliamuru vijana wake, akisema, “Mwacheni avune hata katika masuke, na msimwambie lolote baya.16Na pia muachie baadhi ya masuke katika vifurushi kwa ajili yake, na muyaache ili ayavune. Msimkemee.”

17Kwa hiyo alivuna mpaka jioni. Kisha akatenganisha nafaka na majani ambayo amevuna, nazo nafaka zilikuwa kama efa moja ya shairi.18Akazibeba na kwenda katika mji. Ndipo mama mkwe wake aliona kile alichokivuna. Ruth pia alimletea mama mkwe wake nafaka zilizo kaangwa alizobakisha kwenye chakula chake19Mama mkwe wake akamwambia, “Umevunia wapi leo? Ulienda kufanyia wapi kazi? Abarikiwe mtu aliye kusaidia.” Ndipo Ruth akamwambia mama mkwe wake kuhusu mtu aliye miliki shamba alilokuwa akifanya kazi. Alimwambia, “Jina la mtu ambaye alimiliki shamba nililokuwa nikifanya kazi ni Boazi.”20Naomi akamwambia Ruth, “Abarikiwe na Yahweh, ambaye hakuondoa uaminifu wake kwa walio hai na wafu.” Naomi akamwambia, “Huyo mtu ni jamaa wa karibu nasi, ni jamaa yetu mkombozi.”

21Ruth Mmoabu akamwambia, “Ni kweli, aliniambia, ‘Ukae karibu na vijana wangu wa kiume mpaka watakapo maliza mavuno yangu yote.’

22Naomi akamwambia Ruth mke wa mtoto wake wa kiume, “Ni vizuri, mwanangu, kuwa uende pamoja na wasichana wake wa kazi, ili kwamba usije pata madhara yoyote katika shamba lolote.”

23Kwa hiyo alikaa karibu na wafanyakazi wa kike ili avune mpaka mwisho wa mavuno ya shayiri na mavuno ya ngano. Na alikuwa akiishi pamoja na mama mkwe wake.

3

1Naomi, mama mkwe wake, alimwambia, “Mwanangu, hainilazimu kutafuta mahali pa wewe kupumzika, ili kwamba mambo yako yaende vizuri?2Naye Boazi, mtu ambaye umekuwa pamoja na wasichana wake wa kazi, yeye si jamaa yetu? Tazama, jioni hii atakuwa akikung'uta shairi katika sakafu ya kupuria.3Kwa hiyo, oga, jipake mafuta, uvae nguo zako nzuri, na ushuke kwenda kwenye sakafu ya kupuria. Lakini usijulikane kwa mtu huyu mpaka atakapo maliza kula na kunywa.4Na uhakikishe kuwa, atakapo lala chini, ukumbuke mahali alipo lala ili kwamba baadaye uende kwake, ufunue miguu yake, na ulale hapo. Kisha atakuambia cha kufanya.”

5Ruth alimwambia Naomi, “Nitafanya kila kitu ulicho sema.”6Alishuka kwenda kwenye sakafu ya kupuria, na alifuata maelekezo aliyopewa na mama mkwe wake.

7Boazi alipomaliza kula na kunywa na moyo wake ulikuwa na furaha, alienda kulala chini mwisho wa sehemu ya kuhifadhia nafaka. Kisha Ruth akaenda taratibu, akaaifunua miguu ya Boazi, na kulala hapo chini.8Panapo usiku wa manane Boazi alishtuka. Akajigeuza, na hapo mwanamke alikuwa amelala katika miguu yake!9Akamwambia, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Ni mimi Ruth, mtumishi wako wa kike. Nifunike shuka lako mimi mtumishi wako wa kike, kwa kuwa wewe ni jamaa wa karibu.”

10Boazi akamwambia, “Mwanangu, Yahweh akubariki. Umeonyesha wema mwishoni kuliko mwazoni, kwa sababu hukwenda kwa wanaume vijana, awe tajiri au masikini.11Na sasa, mwanangu, usiogope! Nitakufanyia yote unayosema, kwa sababu mji wa watu wangu wote wanajua kuwa wewe ni mwanamke unayestahili.12Nikweli kuwa mimi ni jamaa wa karibu; hata hivyo, kuna jamaa wa karibu kuliko mimi.13Baki hapa usiku huu, na asubuhi, ikiwa atafanya jukumu lake la jamaa wa karibu, vizuri, muache afanye jukumu lake la kindugu. Lakini kama hata fanya jukumu la kindugu kwako, ndipo mimi nitafanya, kama Yahweh aishivyo. Lala mpaka asubuhi.”

14Kwa hiyo Ruth alilala kwenye miguu ya Boazi hadi asubuhi. Lakini aliamka mapema kabla ya yeyote kuweza kumtambua mtu mwingine. Kwa kuwa alikwisha mwambia, “Isijulikane kuwa mwanamke alikuja kwenye sakafu ya kupuria.”15Kisha Boazi akamwambia, lete mtandio wako na uushikilie.” Alipo fanya hivyo, alipima vipimo vikubwa sita vya shairi katika mtandio na kuweka mzigo juu ya Ruth. Kisha Boazi akaenda mjini.

16Ruth aliporudi kwa mama mkwe wake, alisema, “Ulifanyaje, mwanangu?” Ndipo Ruth akamwambia mambo yote aliyotendewa na mtu huyo.17Alimwambia, “Hivi vipimo sita vya shairi ni vile alivyonipa yeye, kwa kuwa alisema, ‘Usiende mikono mitupu kwa mama mkwe wako.’”18Kisha Naomi akasema, “Baki hapa, mwanangu, mpaka utakapojua yatakavyo kuwa, kwa kuwa Boazi hata pumzika mpaka atakapolimaliza jambo hili leo.”

4

1Ndipo Boazi akaenda kwenye lango la Bethelehemu na kukaa chini. Muda mfupi tu akaja ndugu wa karibu ambaye Boazi alimuongelea. Boazi akamwambia, “Rafiki yangu, njoo hapa na uketi. Kisha mtu huyo akaja na kuketi.2Ndipo Boazi akakusanya viongozi kumi wa mji na kusema, “Ketini hapa.” Hivyo wakaketi.3Boazi alimwambia yule jamaa wa karibu, “Naomi aliyerudi kutoka mji wa Moabu, anauza sehemu ya ardhi ambayo ilikuwa ni miliki ya kaka yetu Elimeleki.4Nilifikiria kukujulisha na kukwambia, ‘Inunue mbele ya hawa waliokaa hapa, na mbele ya viongozi wa watu wangu.’ Ikiwa utapenda kuikomboa, ikomboe. Lakini ikiwa hauhitaji kuikomboa, uniambie, ili nijue, kwa kuwa hakuna mwingine wa kuikomboa isipokuwa wewe, na mimi ni mdogo wako.” Ndipo huyo mtu mwingine akasema, “Nitaikomboa.”5Kisha Boazi akasema, “Ile siku utakayonunua shamba kutoka mkononi mwa Naomi, yakupasa pia kumchukua Ruth Mmoabu, mjane wa mtoto wa Elimeleki, ili kuliinua jina la marehemu kama urithi wake.”6Ndipo yule jamaa wa karibu akasema, “Mimi siwezi kuikomboa ardhi kwa ajili yangu bila kuleta athari kwenye urithi wangu binafsi. Nakupa wewe haki ya kuikomboa kwa ajili yako mwenyewe, kwa kuwa mimi sitoweza.”

7Hii ilikuwa ni desturi ya zamani ya Israeli kuhusu ukombozi na kubadilishana mazuri. Kuthibitisha mambo haya yote, mtu huyu alivua kiatu chake na kumpatia jirani yake; hii ilikuwa ni namna ya kufanya makubaliano ya kisheria katika Israeli.8Kwa hiyo huyu jamaa wa karibu akamwambia Boazi, “Inunue mwenyewe.” Kisha akavua kiatu chake.

9Ndipo Boazi akawaambia viongozi na watu wote, “Ninyi ni mashaidi kuwa nimenunua kila kilichokuwa cha Elimeleki na kila kilichokuwa na Kileoni na Mahilon kutoka kwenye mikono ya Naomi.10Zaidi ya hayo kumhusu Ruth Mmoabu, mke wa Mahlon: nimempa kibali cha kuwa mke wangu, ili kuendeleza jina na urithi wa marehumu, ili kwamba jina lake lisipotee kati ya ndugu zake na lango la watu wake. Ninyi ni mashahidi leo.”

11Watu wote na viongozi waliokuwa katika lango, walisema, “Tu mashahidi. Yahweh amfanye mwanamke huyu ambaye amekuja nyumbani kwako kama Raheli na Leya, ambao wawili hawa wameijenga nyumba ya Israeli. Na ubarikiwe katika Efrata na kuwa mashuhuri katika Bethelehem.12Na nyumba yako kama nyumba ya Peresi, ambaye Tamari alimzalia yuda, kupitia uzao ambao Yahweh atakupatia pamoja na msichana huyu.”

13Hivyo Boazi alimchukua Ruth, na akawa mke wake. Boazi alilala naye, na Yahweh alimruhusu kupata mimba, na alizaa mtoto wa kiume.14Mwanamke huyu akamwambia Naomi, “Yahweh abarikiwe, ambaye hajakuacha bila ndugu wa karibu, yaani mtoto huyu. Jina lake na liwe maarufu katika Israeli.15Na awe kwako mrejeshaji wa maisha na mwenye lishe uzeeni mwako, kwa kuwa mtoto wako mkwe, ambaye anakupenda, ambaye ni bora kwako kuliko watoto wa kiume saba, amemzaa.

16Kisha naomi akamchukua mtoto, akamlaza kifuani pake, na kumhudumia.17Na majirani wa yule mwanamke, wakampa jina, wakisema, “Mtoto amezaliwa kwa Naomi.” Wakamwita Obedi. Ambaye alikuja kuwa baba yake na Jese, ambaye alikuja kuwa baba yake na Daudi.

18Hiki kilikuwa ni kizazi cha Peresi: Peresi alimzaa Hesroni,19Hesroni akamzaa Ramu, Ramu akamzaa Aminadabu,20Aminadabu akamzaa Nashoni, Nashoni akamzaa Salmoni,21Salmoni akamzaa Boazi, Boazi akamzaa Obedi,22Obedi akamzaa Yese, na Yese akamzaa Daudi.

1 Samweli

1

1Palikuwa na mtu mmoja wa Rama Msufi, wa nchi ya milima ya Efraimu; jina lake aliitwa Elikana mwana Yerohamu mwana Elihu mwana wa Tohu mwana wa Sufu, Mwefraimu.2Mtu huyo alioa wanawake wawili, jina la mke wa kwanza aliitwa Hana, na yule wa pili aliitwa Penina, Penina alizaa watoto, lakini Hana hakuzaa.

3Kila mwaka, mtu huyu aliondoka mjini kwake kwenda kuabudu na kutoa dhabihu kwa BWANA wa majeshi huko Shilo. Wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwepo huko Shilo.4Kila mwaka zamu ya Elikana ya kutoa dhabihu ilipofika, alikuwa daima akimpa sehemu ya nyama Penina mkewe, watoto wake wote wa kiume na wa kike.5Lakini kwa mgawo wa Hana daima alimpa mara mbili zaidi, kwa sababu alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.6Hasimu wake alimchokoza sana ili kumkasirisha, kwa sababu BWANA alikuwa amelifunga tumbo lake.7Hivyo kila mwaka, alipokuwa akienda katika nyumba ya BWANA pamoja na familia yake, hasimu wake alizidi kumchokoza. Hatimaye alikuwa mtu wa kulia kila wakati na hakula kitu chochote.8Elikana mmewe kila wakati alimuuliza, “Hana, kwa nini unalia? Kwa nini huli chakula? Kwa nini una huzuni moyoni mwako? Mimi si bora kwako kuliko wana kumi?”

9Wakati fulani, walipokuwa wamemaliza kula na kunywa huko Shilo, Hana alinyanyuka. Wakati huo Eli, kuhani alikuwa amekaa juu ya kiti chake mlangoni kuelekea nyumba ya BWANA.10Hana alijawa na uchungu sana; akamwomba BWANA na akalia mno.11Aliweka nadhiri na kusema, “BWANA wa majeshi, kama utalitazama teso la mjakazi wako na kunikumbuka, na usipomsahau mjakazi wako, na kumpatia mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa huyo mtoto kwa BWANA siku zote za maisha yake, na wembe hautapita juu ya kichwa chake kamwe.”

12Hana akiendelea kuomba mbele za BWANA, Eli alikitazama kinywa chake.13Hana aliongea moyoni mwake. Midomo yake ilitikisika, lakini sauti yake haikusikika. Hivyo Eli alimdhania kuwa amelewa.14Eli akamwambia, “Utakuwa mlevi mpaka lini? Weka mbali divai yako.”

15Hana akajibu, “Sivyo bwana wangu, mimi ni mwanamke mwenye roho ya huzuni. Sijanywa divai wala kinywaji chochote cha kulevya, bali nimekuwa nikiimimina nafsi yangu mbele za BWANA.16Usimchukulie mjakazi wako kama mwanamke duni; nimekuwa nikiongea kutokana na maumivu na masikitiko yangu.”

17Kisha Eli alimjibu na kusema, “Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akupatie kile ulichomuomba.”

18Hana akasema, “Na mjakazi wako apate kibali machoni pako.” Ndipo huyo mwanamke alienda zake na kula chakula na hakuhuzunika tena.

19Waliamka asubuhi na mapema wakaenda wakamtukuza BWANA, na baadaye walirudi nyumbani kwao Rama. Elikana alilala na mke wake Hana, na BWANA akamkumbuka.20Baada ya muda fulani, Hana alibeba mimba na akazaa mtoto wa kiume. Akamwita jina lake Samweli, akasema, “Kwa sababu huyu nilimuomba kutoka kwa BWANA.”

21Mara nyingine, Elikana na nyumba yake, walipanda kwenda kumtolea BWANA dhabihu ya Mwaka na kuondoa nadhiri yake.22Lakini Hana hakwenda huko; alikuwa amekwisha mwambia mmewe, “Sitaenda huko hadi mtoto aache kunyonya; ndipo nitamleta, ili ahudhurie mbele za BWANA na akae huko daima.”

23Mme wake Hana, Elikana, akamwambia, “Fanya yale yakupendezayo. Ngojea hadi utakapokuwa umemwachisha kunyonya; BWANA aweze peke yake kuthibitisha neno lake.” Hivyo yule mwanamke alibaki akimnyonyesha mtoto wake mpaka pale alipomwachisha kunyonya.

24Alipokuwa amemwachisha kunyonya, alimbeba, akimchukua pamoja ng'ombe dume wa miaka mitatu, unga kama kilo thelathini na chupa ya mvinyo, akampeleka katika nyumba ya BWANA huko Shilo. Na mtoto huyo alikuwa bado mdogo.25Walimchinja yule ng'ombe, na wakamkabidhi mtoto kwa Eli.26Akasema, “Ee bwana wangu! Kama uishivyo, bwana wangu, mimi ndiye yule mwanamke niliyesimama hapa karibu nawe nikimwomba BWANA.27Niliomba kwa ajili ya mtoto huyu na BWANA akawa amenijibu ombi la dua yangu nililomwomba.28Nami nimemtoa kwa BWANA; kwa maisha yake yote, nimempa BWANA.” Ndipo Elikana na familia yake wakamtukuza BWANA huko Shilo.

2

1Hana aliomba akasema, “Moyo wangu wamtukuza BWANA. Pembe yangu imejulikana katika BWANA. Kinywa changu hujisifu dhidi ya maadui zangu, kwa kuwa naufurahia wokovu wako.

2Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA, kwa kuwa hakuna mwingine zaidi yako; hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3Msijivune sana hivyo kwa kiburi; vinywa vyenu visitoke majivuno. Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa; yeye huyapima matendo kwa mizani.
4Pinde za mashujaa zimevunjika, bali wale wanaojikwaa hujivika nguvu kama mshipi.
5Wale walio na shibe ya kutosha wamejikodisha ili wapate chakula; wale waliokuwa na njaa hawana njaa tena. Hata yule aliye kuwa tasa amezaa watoto saba, bali mwanamke mwenye watoto wengi amekua dhaifu.
6BWANA huua na huuisha. Hushusha kuzimu na huleta tena juu.
7BWANA humfanya maskini, na yeye ndiye humtajirisha mtu. Yeye hushusha chini, lakini pia huleta juu.
8Yeye humwinua juu maskini toka mavumbini: Huwainua wahitaji toka jalalani na kuwaketisha pamoja na wakuu na kuwarithisha kiti cha enzi cha utukufu. Kwa kuwa nguzo za dunia ni za BWANA na ameukalisha ulimwengu juu yake.
9Yeye atazilinda nyayo za watu wake waaminifu, bali waovu watanyamazishwa gizani, kwa maana hakuna atayeshinda kwa nguvu zake.
10Wale wampingao BWANA watavunjwa vipande vipande; atawapiga radi kutokea mbinguni. BWANA atahukumu miisho ya dunia; atampa nguvu mfalme wake na kuinua pembe ya mtiwa mafuta wake.”

11Ndipo Elikana akaenda Rama, nyumbani kwake. Na yule mtoto akamtumikia BWANA machoni pa Eli, kuhani.

12Basi, watoto wa Eli walikuwa wakorofi. Wao hawakumheshimu BWANA.13Desturi ya makuhani na watu ilikuwa kwamba endapo mtu yeyote ametoa dhabihu, mtumishi wa kuhani angekuja akiwa na uma wa meno matatu mkononi mwake, nyama ilipokuwa inachemka.14Naye angeutia uma huo sufuriani, au birikani au chomboni au chunguni; nyama yote ambayo ingeinuliwa na uma huo ingetwaliwa na kuhani mwenyewe. Ndivyo walivyofanya huko Shilo kwa Waisraeli wote waliokwenda huko.15Tena, kabla ya kuteketeza mafuta, mtumishi wa kuhani alikuja, na kumwambia aliyekuwa akitoa dhabihu, “Tenga nyama ya kuchoma kwa ajili ya kuhani; kwa sababu hataikubali ile ya kuchemsha kutoka kwako, bali tu ile mbichi.”

16Ikiwa mtu atamwambia, “Wachome mafuta kwanza, na kisha uchukue kiasi utakacho.” Ndipo angesema, “Hapana, utanipatia sasa hivi; la sivyo; nitaichukua kwa lazima.”

17Dhambi ya vijana hawa ilikuwa mbaya sana mbele za BWANA, kwa sababu waliidharau dhabihu ya BWANA.

18Lakini Samweli alimtumikia BWANA akiwa mdogo akivaa nguo ya naivera ya kitani.19Kila mwaka mama yake alimtengenezea kanzu dogo na kumletea, wakati wakija na mmewe kutoa dhabihu ya kila mwaka.20Eli aliwabariki Elikana na mke wake na kusema, “BWANA akupatie watoto zaidi kwa mwanamke huyu kwa sababu ya ahadi yake aliyoitoa kwa BWANA.” Baadaye walirudi nyumbani kwao.21BWANA alimsaidia tena Hana, akawa amebeba mimba nyingine. Akazaa watoto watatu wa kiume na wa kike wawili. Wakati huo huo mtoto Samweli akakua akiwa mbele za BWANA.

22Basi Eli alikuwa mzee sana, akayasikia yote ambayo watoto wake walikuwa wakiwafanyia Waisraeli wote, na jinsi walivyotembea na mwanamke aliyekuwa akitumika katika lango la hema ya kukutania.23Akawaambia, “Kwa nini mnafanya mambo hayo? Kwa maana nasikia matendo yenu maovu kutoka kwa watu hawa wote.”24Sivyo hivyo, watoto wangu, maana hii ninayoisikia siyo taarifa njema. Mnawakosesha watu wa BWANA.25“Kama mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; Lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea mtu huyo?” Lakini hawakuitii sauti ya baba yao, sababu BWANA alinuia kuwaua.

26Yule mtoto Samweli aliongezeka umri, na kupata kibali kwa BWANA na kwa watu pia.27Kisha mtu wa Mungu akamwendea Eli na kumwambia, “BWANA asema, ‘Je, sikujifunua mwenyewe kwa nyumba ya baba zako, walipokuwa Misri utumwani nyumbani mwa Farao?28Mimi nilimchagua yeye kutoka makabila yote ya Israeli awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu, na kufukiza uvumba, na kuvaa kanzu ya naivera mbele yangu. Niliwapa nyumba ya baba zako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto.29Kwanini basi, unaidharau dhabihu yangu na sadaka ambazo ninazitaka mahali ninapoishi? Kwanini unawaheshimu watoto wako kuliko mimi, kwa kujinenepesha ninyi wenyewe kwa uzuri wa kila sadaka ya watu wangu Israeli?’

30Maana, BWANA, Mungu wa Isareli, asema, ‘Niliahidi kwamba nyumba yako, na nyumba ya baba yako, yawapasa kwenda mbele zangu milele,’ lakini sasa BWANA asema. ‘Mambo haya yapishe mbali nami nisifanye hivi, maana nitawaheshimu wanaoniheshimu, bali wanaonidharau mimi hawatakuwa na thamani.31Tazama, siku zinakuja nitakapoondoa nguvu zako na nguvu za nyumba za baba yako, ili kwamba pasije kuwepo mtu mzee katika nyumba yako.32Nawe utalitazama hangaiko katika makao yangu. Ingawa Israeli watapewa jambo jema, hapatakuwapo tena mtu yeyote mzee katika nyumba yako.33Yeyote miongoni mwenu nisiye mwondoa kutoka madhabahuni pangu, nitasababisha macho yenu yakose kuona, na nitasababisha huzuni maishani mwenu. Wanaume wote waliozaliwa katika familia yako watakufa.34Hii ndiyo itakuwa ishara kwako ambayo itakayowajia watoto wako wa kiume wawili, juu ya Hofni na Finehasi: Wote wawili watakufa siku moja.

35Nami nitamwinua juu kuhani wangu mwaminifu atakaye fanya kile kilichomo moyoni mwangu na nafsini mwangu. Nami nitamjengea nyumba imara; naye atakwenda mbele ya mfalme wangu mbarikiwa milele.36Kila mmoja aliyebakia nyumbani mwako atakuja na kusujudu mbele ya mtu huyo, akiomba kipande cha fedha na mkate mmoja, naye atasema, ‘Tafadhali uniajiri katika moja ya nafasi za kuhani ili niweze kula kipande cha mkate.’”

3

1Yule mtoto Samweli alimtumikia BWANA chini ya uangalizi wa Eli. Neno la BWANA halikupatikana kwa wingi siku hizo; hapakuwa na maono ya mara kwa mara ya kinabii.

2Wakati huo, nguvu ya macho ya Eli ilikuwa imefifia kiasi cha kutoweza kuona vizuri, na alikuwa amelala kitandani mwake.3Ile taa ya BWANA bado ilikuwa bado inawaka, na Samweli alikuwa amelala katika nyumba ya BWANA, palipokuwa na sanduku la Mungu.4BWANA akamwita Samweli, naye akaitika, “Niko hapa.”

5Samweli alimwedea Eli na kusema, “Niko hapa, sababu uliniita.” Eli akasema, “Sikukuita; kalale tena.” Hivyo Samweli akarudi na kulala.

6BWANA akamwita tena, “Samweli.” Samweli aliamka tena na kwenda kwa Eli na kusema, “Niko hapa, sababu umeniita.” Eli akajibu, “Sijakuita, mwanangu; kalale tu tena.”

7Basi Samweli bado hakuwa na uzoefu kuhusu Bwana, wala hakuwahi kupata ujumbe wowote kutoka kwa BWANA ukifunuliwa kwake.

8BWANA akamwita tena Samweli kwa mara ya tatu. Samweli alinyanyuka tena na kwenda kwa Eli na kusema, “Niko hapa, sababu uliniita,” Ndipo Eli alitambua kwamba BWANA alimwita kijana.9Kisha Eli akamwambia Samweli, “Nenda ukalale tena; ikiwa atakuita tena, sharti useme, ‘Sema, BWANA, maana mtumwa wako anasikiliza.”’ Hivyo Samweli akaenda na kulala mahali pake tena.10BWANA alikuja na kusimama; akaita vilevile kama vile mwanzoni, “Samweli, Samweli.” Ndipo Samweli akasema, “Nena, kwa sababu mtumwa wako anasikiliza.”

11BWANA akasema na Samweli, “Tazama, niko tayari kufanya jambo katika Israeli ambalo masikio ya kila mmoja akisikia atashtuka.12Siku hiyo nitatimiza kila kitu nilichokisema dhidi ya Eli kuhusu nyumba yake, kutoka mwanzo hadi mwisho.13Nimemwambia kwamba niko tayari kuhukumu nyumba yake mara moja kwa ile dhambi aliyoifahamu, kwa sababu watoto wake walijiletea laana juu yao wenyewe na hakuwazuia.14Hii ndiyo sababu nimeapa kwa nyumba ya Eli, kwamba dhambi za nyumba yake hazitasamehewa kwa dhabihu au kwa sadaka kamwe.”

15Samweli akalala hadi asubuhi; baadaye alifungua milango ya nyumba ya BWANA. Lakini Samweli aliogopa kumwambia Eli kuhusu maono hayo.16Kisha Eli akamwita Samweli na kusema, “Samweli, mwanangu.” Samweli akasema, “Niko hapa.”

17Akamuuliza, “Ni neno gani alilokusemesha? Tafadhali usinifiche jambo hilo. Mungu akutendee hivyo na kukuzidishia, endapo utanificha kitu chochote kati ya yote ambayo amesema nawe.”

18Samweli akamweleza kila kitu; hakumficha jambo lolote. Eli akasema, “Ni BWANA. Na afanye linaloonekana jema kwake.”

19Samweli akakua, na BWANA alikuwa pamoja naye na hakuacha kutimiza maneno yake ya unabii.20Israeli yote tokea Dani hadi Beersheba walijua kwamba Samweli aliteuliwa kuwa nabii wa BWANA.21Naye BWANA alionekana tena huko Shilo, maana alijifunua mwenyewe kwa Samweli huko Shilo kwa neno lake.

4

1Neno la Samweli likawafikia Israeli wote. Basi Israeli wakatoka kupigana dhidi ya Wafilisti. Nao wakaweka kambi hapo Ebenezeri, na Wafilisti waliweka kambi yao huko Afeki.2Nao Wafilisti walijipanga kwa ajili ya vita dhidi ya Waisraeli. Vita ilipopamba moto, Israeli ilishindwa na Wafilisti, wakauawa watu wapatao 4,000 kwenye uwanja wa vita.3Watu walipokuja kambini, wazee wa Israeli walisema, “Kwa nini BWANA ametushinda leo mbele ya Wafilisti? Hebu tulilete hapa sanduku la ushuhuda wa BWANA kutoka Shilo, ili kwamba liwe hapa pamoja nasi, ili litufanye tuwe salama kutokana na nguvu za maadui zetu.”

4Hivyo waliwatuma watu huko Shilo; kutokea huko walilibeba sanduku la ushuhuda wa BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi. Hofni na Finehasi, watoto wawili wa Eli, walikuwapo pamoja na lile sanduku la ushuhuda wa Mungu.

5Sanduku la ushuhuda wa BWANA lilipofika kambini, watu wote wa Israeli walipiga kelele kwa sauti kuu yenye furaha, na nchi ikavuma.6Wafilisti waliposikia kelele za furaha, wakasema, “Sauti hii kubwa ya furaha katika kambi ya Waebrania inamaanisha nini?” Baadaye walitambua kwamba sanduku la BWANA limefika kambini.7Wafilisti waliogopa sana; wakasema “Mungu ameingia kambini.” Wakasema, “Ole wetu! Hakuna kitu kama hiki kilichotokea hapo awali!8Ole wetu! Ni nani atatulinda dhidi ya nguvu za miungu wenye uwezo? Hawa ndio miungu waliowashambulia Wamisri kwa aina tofauti za mapigo mengi jangwani.9Enyi Wafilisti, iweni hodari, na fanyeni kiume, msije mkawa watumwa wa Waebrania, kama walivyokuwa watumwa wenu. Fanyeni kiume, na piganeni nao.”

10Wafilisti walipigana, na Waisraeli wakashindwa. Kila mtu alikimbilia hemani kwake, na mauaji yalikuwa makubwa sana; maana askari wa Israeli 30,000 waendao kwa miguu vitani, walianguka.11Lile sanduku la Mungu lilichukuliwa, na watoto wa Eli, Hofni na Finehasi waliuawa.

12Mtu mmoja wa Benjamini alikimbia kutoka uwanja wa vita akaja Shilo siku iyo hiyo, aliwasili na mavazi yake yamechanika na matope kichwani pake.13Alipofika, Eli alikuwa amekaa kitini pake karibu na barabara akitazama kwa sababu moyo wake ulitetemeka kwa ajili ya sanduku la Mungu. Mtu yule alipoingia mjini na kutoa taarifa, mji wote ulilia.

14Eli aliposikia kelele ya kilio kile, alisema, “Kilio hicho kina maana gani?” Kwa haraka mtu yule alikuja na kumweleza Eli.

15Basi Eli alikuwa na umri wa miaka tisini na nane; macho yake yamepofuka, na hakuweza kuona.16Yule mtu akamwambia Eli, “Mimi ndiye nimechomoka kutoka vitani. Nimetoroka kutoka kwenye mapigano leo.” Eli akasema, “Mambo yalienda namna gani, mwanangu?”

17Yule mtu aliyeleta hizo habari alijibu na kusema, “Israeli wamewakimbia Wafilisti. Pia watu wengi wameuwawa. Watoto wako, Hofni na Finehasi, wamekufa, na sanduku la Mungu limechukuliwa.”

18Alipotamka sanduku la Mungu, Eli alianguka chali kutoka kwenye kiti chake karibu na mlango akavunjika shingo lake, na kufariki, kwa sababu alikuwa mzee tena mzito. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli kwa miaka arobaini.

19Basi mkwewe, mke wa Finihasi, alikuwa mjamzito akikaribia kujifungua. Aliposikia habari kwamba sanduku la Mungu limetekwa nyara na kwamba baba mkwe na mme wake wamefariki, alichuchumaa chini akajifungua, lakini uchungu wa kuzaa ulimzidi nguvu.20Alipokaribia kufariki, wanawake waliokuwa wakimhudumia walisema, “Usiogope, maana umejifungua mtoto wa kiume.” Lakini hakuwajibu lolote au kuzingatia alichoambiwa.

21Akamwita mtoto Ikabodi, akisema, “Utukufu umetoweka Israeli!” Kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyara, na kwa sababu ya vifo vya baba mkwe na mme wake.22Na alisema, “Utukufu umetoweka kutoka Israeli, kwa sababu sanduku la Mungu limetekwa nyara.”

5

1Basi Wafilisti wakawa wamelitwaa sanduku la Mungu, wakalileta kutoka Ebenezeri hadi Ashdodi.2Wafilisti walilichukua sanduku la Mungu, wakalileta ndani ya nyumba ya Dagoni, na wakalikalisha pembeni mwa Dagoni.3Watu wa Ashdodi walipoamka mapema siku ya pili, tazama, Dagoni ilianguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Hivyo waliichukua Dagoni na kuisimamisha tena katika sehemu yake.4Lakini walipoamka mapema kesho yake, tazama, Dagoni alikuwa ameanguka chini kifudifudi mbele ya sanduku la BWANA. Kichwa cha Dagoni na vitanga vyake viwili vilikatika na kulala mlangoni. Kiwiliwili cha Dagoni ndicho kilibaki tu.5Na hii ndiyo sababu, makuhani wa Dagoni na yeyote aingiaye ndani ya nyumba ya Dagoni, hata leo, hawezi kukanyaga mlango wa Dagoni katika Ashdodi.

6Mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi. Aliwaangamiza akawatesa kwa majipu, Ashdodi na wilaya zake kwa pamoja.7Watu wa Ashdodi walipotambua kilichokuwa kinatokea, walisema, “Sanduku la Mungu wa Israeli lisikae kwetu, kwa sababu mkono wake ni mzito juu yetu na juu ya mungu wetu Dagoni.”8Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, “Tufanye nini na sanduku la Mungu wa Israeli?” Wakawajibu, “Sanduku la Mungu wa Israeli lihamishwe na kupelekwa Gathi.” Basi wakalihamisha hilo sanduku la Mungu wa Israeli hadi huko Gathi.9Lakini baada ya kulipeleka huko, mkono wa BWANA ulikuwa juu ya mji huo, ukasababisha machafuko makubwa. Akawatesa watu wa mji huo, wakubwa kwa wadogo; na majipu yakaota juu ya miili yao.10Basi, wakalipeleka sanduku la Mungu hadi Ekroni. Lakini mara tu sanduku la Mungu lilipoingia Ekroni, watu wa Ekroni walipiga kelele wakisema, “Wametuletea sanduku la Mungu wa Israeli kutuua sisi na watu wetu.”11Basi wakawatuma watu wawakusanye pamoja viongozi wote wa Wafilisti; wakawambia, “Lipelekeni mbali sanduku la Mungu wa Israeli, na lirudishwe katika makao yake, ili lisije kutuua sisi na watu wetu.” Kwa maana kulikuwa na hofu ya kutisha mjini kote; Mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.12Watu ambao hawakufa waliteswa na majipu, na kilio cha mji kilipanda hadi mbinguni.

6

1Basi sanduku la BWANA lilikaa katika nchi ya Wafilisti kwa miezi saba.2Ndipo Wafilisti wakawaita makuhani na waganga; wakawaambia, “Tulifanyie nini sanduku la BWANA? Twambieni jinsi ambavyo tunapaswa kulirudisha sanduku katika nchi yake.”

3Makuhani na waganga wakasema, “Kama mtalirudisha sanduku la Mungu wa Israeli, msilipeleke bila zawadi; kwa namna yoyote ile mpelekeeni sadakaa ya hatia. Hapo ndipo mtapona, na mtajua ni kwanini mkono wake hadi sasa haujaondoka juu yenu.”

4Ndipo wakawauliza, “Sadaka ya hatia itakuwa nini kwamba tunampelekea?” Wakawajibu, “Majipu matano ya dhahabu na panya watano wa dhahabu, Idadi hiyo ya watano ni sawa na idadi ya viongozi wa Wafilisti. Kwa sababu tauni ya aina moja iliwashambulia ninyi na viongozi wenu.5Kwa hiyo, ni lazima mtengeneze mifano ya majipu yenu, na mifano ya panya wenu wanaoharibu nchi, na mpeni utukufu Mungu wa Israeli. Labda ataondoa mkono wake kutoka juu yenu, kutoka juu ya miungu yenu, na kutoka juu ya nchi yenu.6Kwa nini mfanye mioyo yenu kuwa migumu, kama vile Wamisri na Farao walifanya mioyo yao kuwa migumu? Hicho ni kipindi ambacho Mungu wa Israeli aliwashughulikia vikali; Je, Wamisri hawakuwaachilia watu, na wakaondoka?

7Basi sasa, andaeni mkokoteni mpya pamoja na ng'ombe wawili wake wanaonyonyesha, ambao hawajawahi kufungwa nira. Wafungeni ng'ombe hao kwenye mkokoteni, lakini warudisheni wale ndama wao nyumbani.8Kisha lichukueni sanduku la BWANA na kuliweka ndani ya mkokoteni. Wekeni ndani ya kasha yale maumbo ya dhahabu mnayompelekea ambayo ni sadaka ya hatia kando yake. Mlitume mbali liende zake.9Kisha muwe makini; kama litapanda kwenda kwa njia hadi nchini mwake hadi Beth Shemeshi, basi mjue kuwa BWANA ndiye aliyetenda pigo hili kubwa. Lakini kama halitakwenda, ndipo tutajua kwamba siyo mkono wake uliotupatia mateso; badala yake tutajua kuwa yaliyotupata ilikuwa ni kwa bahati mbaya tu.

10Watu hao wakafanya kama walivyoambiwa, walichukuwa ng'ombe wawili wanaonyonyesha, wakawafunga kwenye mkokoteni, na kuwabakiza ndama wao nyumbani.11Wakaliweka sanduku la BWANA juu ya mkokoteni, pamoja na lile kasha lililobeba panya wa dhahabu na yale maumbo ya majipu yao.12Hao ng'ombe waliondoka moja kwa moja kuelekea Beth Shemeshi. Walikwenda kwa kuifuata njia moja kuu, wakiteremka walipokuwa wakienda, na hawakugeuka upande wa kushoto au kulia. Viongozi wa Wafilisti walifuata kwa nyuma hadi mpaka wa Beth Shemeshi.

13Nao watu wa Beth Shemeshi walikuwa wakivuna ngano yao katika bonde. Waliponyanyua macho yao juu na kuliona sanduku, wakafurahi.14Huo mkokoteni ulifikia ndani ya shamba la Yoshua wa Beth Shemeshi na ukasimama hapo. Kulikuapo jiwe kubwa mahali hapo, wakatayarisha kuni kutokana na mkokoteni huo, na wakawatoa ng'ombe hao kama sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya BWANA.15Walawi waliliteremsha sanduku la BWANA chini pamoja na kasha lake lililoyatunza yale maumbo ya dhahabu, wakaweka vitu hivyo juu ya hilo jiwe kubwa. Watu wa Beth Shemeshi walitoa sadaka za kuteketezwa na kutoa dhabihu kwa BWANA siku iyo hiyo.16Hao viongozi watano wa Wafilisti walipoona hayo, walirejea Ekroni siku iyo hiyo.

17Haya ndiyo majipu ya dhahabu ambayo Wafilisti walirudisha kama sadaka ya hatia kwa BWANA: moja kwa ajili ya Ashdodi, moja kwa Gaza, moja kwa Ashkeloni, moja kwa Gathi, na moja kwa Ekroni.18Idadi ya wale panya wa dhahabu ilikuwa sawa na ile ya idadi ya miji yote ya Wafilisti inayomilikiwa na viongozi watano, kwa miji iliyojengewa maboma na vijiji vya mashambani. Lile jiwe kubwa, ambalo kando yake waliweka sanduku la BWANA, lipo kama ushuhuda hadi leo katika shamba la Yoshua Mbeth- Shemeshi.

19BWANA akawashambulia baadhi ya watu wa Bethi Shemeshi kwa sababu walichungulia ndani ya sanduku lake. Aliwaua watu sabini. Watu wakaomboleza, kwa sababu BWANA aliwapa watu pigo kubwa mno.20Watu wa Bethi Shemeshi wakasema, “Je, ni nani awezaye kusimama mbele ya BWANA, huyu Mungu mtakatifu? Na ni kwa nani ambako sanduku litaenda likitoka hapa.”

21Wakawatuma wajumbe kwenda kwa wenyeji wa Kiriath Yearimu, wakisema, “Wafilisti wamelirudisha sanduku la BWANA; teremkeni na mkalipeleke kwenu.”

7

1Watu wa Kiriath Yearimu walikuja, wakalichukua sanduku la BWANA, wakalileta ndani ya nyumba ya Abinadabu mlimani iliyokuwa kilimani. Wakamteua Eleazari, mwanawe, kulitunza sanduku la BWANA.

2Tangu siku ambayo sanduku lilikaa huko Kiiriath Yearimu, ulipita muda mrefu, miaka ishirini. Nyumba yote ya Israeli iliomboleza na ikaazimu kumrudia BWANA.

3Samweli akawaambia watu wote wa Israeli, “Kama mtamrudia BWANA kwa moyo wenu wote, mkaiondoe miungu migeni na Ashtorethi kutoka katikati yenu, igeuzeni mioyo yenu kwa BWANA, na mwabuduni yeye peke yake, ndipo atawaokoa kutoka mkono wa Wafilisti.”4Ndipo watu wa Israeli wakamuondoa Baali na Ashtorethi, na wakamwabudu BWANA peke yake.

5Ndipo Samweli akasema, “Waleteni pamoja Israeli wote huko Mispa, nami nitamwomba BWANA kwa ajili yenu.”6Wakakusanyika Mispa, wakateka maji na kuyamwaga chini mbele za BWANA. Siku hiyo walifunga na kusema, “Tumemfanyia BWANA dhambi.” Hapo Mispa ndipo Samweli aliwaamua na kuwaongoza watu wa Israeli.

7Basi Wafilisti waliposikia kwamba Waisraeli wamekusanyika hapo Mispa, viongozi wa Wafilisti waliwashambulia Israeli. Waisraeli waliposikia hivyo, waliwaogopa Wafilisti.8Ndipo Waisraeli wakamwambia Samweli, “Usiache kumwomba BWANA Mungu wetu kwa ajili yetu, ili atuokoe kutoka mkono wa Wafilisti.”9Samweli alimchukua kondoo mchanga nakumtoa sadaka ya kuteketezwa kikamilifu kwa BWANA. Ndipo Samweli akamlilia BWANA kwa ajili ya Israeli, na BWANA akamjibu.

10Hata Samweli alipokuwa akitoa sadaka ya kuteketezwa, Wafilisti wakasogea karibu kuwashambulia Israeli; lakini BWANA alipiga kwa nguromo ya sauti kubwa siku hiyo dhidi ya Wafilisti na kuwatia kiwewe, na wakashindwa mbele ya Israeli.11Waisraeli wakaondoka Mispa, wakawafuatia Wafilisti na kuwaua hadi kufika chini ya Beth kari.

12Kisha Samweli akachukua jiwe akalisimamisha kati ya Mispa na Sheni. Akaliita hilo jiwe Ebeneza, akisema, “Hata sasa BWANA ametusaidia.”13Kwa hiyo, Wafilisti walishindwa na hawakuingia katika mipaka ya Israeli. Mkono wa BWANA ulikuwa dhidi ya Wafilisti siku zote za Samweli.

14Miji ambayo Wafilisti waliokuwa wamewapokonya Waisraeli ilirudishwa, kutokea Ekroni hadi Gathi; Israeli ikarudisha tena sehemu za nchi zake kutoka kwa Wafilisti. Ndipo ikawa amani kati ya Israeli na Waamori.

15Samweli akawa mwamuzi wa Israeli siku zote za maisha yake.16Kila mwaka alienda kwa kuzunguka Betheli, Gilgali, na huko Mispa. Na akawa mwamuzi wa Israeli sehemu hizo zote.17Kisha angerudi Rama, kwa sababu mji wake ulikuwa huko; na huko pia aliwaamua Waisiraeli. Hata huko Rama, pia alimjengea BWANA madhabahu.

8

1Samweli alipozeeka, aliwaweka watoto wake wawe waamuzi juu ya Israeli.2Mtoto wake wa kwanza aliitwa Yoeli, na mtoto wake wa pili aliitwa Abiya. Hawa walikuwa waamuzi katika Beersheba.3Watoto wake hawakuenenda katika njia za baba yao, bali walipiga mbio kutafuta mapato ya udhalimu. Walipokea rushwa na kupotosha hukumu.

4Ndipo wazee wote wa Israeli walikutana pamoja na kumwendea Samweli huko Rama.5Wakamwambia, “Angalia, wewe umekuwa mzee, na watoto wako hawaenendi katika njia zako. Tuchagulie mfalme wakutuamua kama yalivyo mataifa yote.”

6Lakini haikumpendeza Sameli waliposema, “Utupatie mfalme wa kutuamua.” Hivyo akamwomba BWANA.7Na BWANA akamwambia Samweli, “Sikiliza sauti ya watu kwa kila jambo wanalokwambia; kwa sababu hawajakukataa wewe, bali wamenikataa mimi nisiwe mfalme wao.8Sasa wanafanya kama vile walivyotenda tangu siku ile nilipowatoa huko Misri, kwa kuniacha, na kuwatumikia miungu mingine, na ndivyo hivyo pia wanakufanyia na wewe.9Basi sasa uwasikilize; lakini uwaonye sawasawa na uwafahamishe tabia ya mfalme atakaye waongoza.”

10Kwa hiyo Samweli akawaambia watu waliokuwa wakiomba mfalme maneno yote ya BWANA.11Akasema, “Hizi ndizo zitakazo kuwa amri za mfalme atakaye watawala. Atawachukua watoto wenu wa kiume na kuwaweka juu ya magari ya vita na kuwa wapanda farasi wake, na kukimbia mbele ya magari yake.12Atawaweka ma- kapteni wake juu ya maelfu ya askari, na ma-kapteni juu ya askari hamsini. Wengine atawafanya wakulima wamashamba yake, wengine wavunaji wa mazao yake, wengine watatengeneza silaha zake na za magari yake.13Naye atawachukua binti zenu kuwa watengeneza manukato, wapishi, na waoka mikate.14Atachukua mashamba yenu mazuri, mashamba ya mizabibu, na yale ya mizeituni na kuwapa watumishi wake.15Atachukua moja ya kumi ya nafaka zenu na mizabibu na kuwapa maofisa na watumishi wake.16Atawachukua watumwa wenu na wajakazi wenu na vijana wenu waliowazuri na punda wenu; atawatumikisha wote kwa ajili yake.17Atawatoza moja ya kumi ya mifugo yenu, na mtakuwa watumwa wake.18Ndipo mtalia siku ile kwa sababu ya mfalme wenu mliyemchagua kwa ajili yenu; lakini siku ile BWANA hatawajibu.”

19Lakini watu walikataa kumsikiliza Samweli; wakasema, “Hapana! Lazima awepo mfalme juu yetu.20Ili tuweze kuwa kama mataifa mengine yote, na hivyo mfalme wetu aweze kutuamua na atoke mbele yetu na atupiganie vita vyetu.”

21Naye Samweli aliposikia maneno yote ya watu, akayarudia katika masiko ya BWANA.22BWANA akamwambia Samweli, “Sikiliza sauti yao na uwafanyie mfalme.” Hivyo Samweli akawaambia watu wa Israeli, “Kila mtu na arudi mjini kwake.”

9

1Basi kulikuwa na mtu mmoja kutoka Benyaminijina lake aliitwa Kishi mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa mwenye nguvu.2Huyu alikuwa na mtoto wa kiume aliyeitwa Sauli, kijana mzuri wa uso. Hapakuwapo mwanaume mzuri wa uso kuliko huyu miongoni mwa watu wote wa Israeli. Kutoka mabegani kwenda juu alikuwa mrefu kuliko watu wengine.

3Na punda wa Kishi, baba yake na Sauli walipotea. Hivyo Kishi akamwambia Sauli mwanawe, “Mchukue mmoja wa watumishi; uamke uende kuwatafuta punda,”4Sauli akapita katika nchi ya vilima ya Efraimu na akaenda akapita katika nchi ya Shalisha, lakini hawakuwaona. Kisha walipita katika nchi ya Shaalimu, lakini hawakuwa huko. Baadaye alipita katika nchi ya Wabenyamini, lakini hawakuwaona wale punda.

5Na walipofika nchi ya Sufu, Sauli alimwambia mtumishi wake aliyekuwa naye, “Njoo na turudi, pengine baba aweza kuacha kufikiri habari za punda na kuanza kutuhofia sisi.”

6Lakini mtumishi akamwmbia, “Sikiliza, yupo mtu wa Mungu katika mji huu. Naye ni mtu wa kuheshimiwa sana; kila asemalo huwa kweli. Hebu twende huko; labda anaweza kutuambia tupitie wapi katika safari yetu.”

7Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, “Lakini kama tukienda kwake, twaweza kumpelekea nini? Maana hata mkate katika mfuko wetu umekwisha, na hakuna zawadi ya kumpelekea mtumishi wa Mungu. Tuna kitu gani?”

8Huyo mtumishi akamjibu Sauli na kusema, “Hapa, ninayo robo ya shekeli ya fedha ambayo nitampa mtumishi wa Mungu, atuambie ni njia ipi yatupasa tuiendee.”9(Zamani katika Israeli, mtu alipotaka kujua neno kuhusu mapenzi ya Mungu, alisema, “Njoo, haya twende kwa mwonaji.” Kwa maana nabii wa leo, zamani aliitwa Mwonaji).10Ndipo Sauli akamwambia mtumishi wake, “Umesema vyema. Haya, njoo twende.” Basi wakaenda katika mji ambao mtu wa Mungu alikuwamo.11Walipopanda mlima kuelekea mjini, walikutana na wasichana wakienda kuteka maji; Sauli na mtumishi wake wakawauliza, “Mwonaji hupo hapa?”12Nao wakawajibu, na kusema, “Yupo; tazameni, yuko mbele yenu. Harakisheni, kwa maana anakuja mjini leo, sababu leo watu wanatoa dhabihu zao mahali pa juu.13Mara tu mtakapoingia mjini mtamuona, kabla hajapanda mahali pa juu kula chakula. Watu hawatakula hata atakapokuja, kwa sababu ndiye ataibariki dhabihu; na baadaye wale ambao wamealikwa hula. Basi pandeni, mtamuona sasa hivi.”

14Kwa hiyo walikwea kwenda mjini. Walipokuwa wakiingia mjini, walimuona Samweli akija mbele yao, akipanda kwenda mahali pa juu.

15Siku moja kabla Sauli hajafika, BWANA alikuwa amemfunulia Samweli:16“Kesho wakati kama huu nitakutumia mtu kutoka nchi ya Benyamini, nawe utamtia mafuta awe mfalme juu ya watu wangu Israeli. Atawaokoa watu wangu kutoka mkono wa Wafilisti. Kwa kuwa nimewaonea huruma watu wangu na kilio cha kutaka msaada kimenifikia.”

17Samweli alipomuona Sauli, BWANA akamwambia, “Huyu ndiye mtu niliyekwambia habari zake! Yeye ndiye atakayewatawala watu wangu.”

18Ndipo Sauli akaja karibu na Samweli katika lango na kusema, “Niambie nyumba ya Mwonaji iko wapi?

19Samweli akamjibu Sauli akisema, “Mimi ndiye mwonaji. Tangulia mbele hadi mahali pa juu, nami nitakueleza kila kitu kilichomoyoni mwako.20Kama punda wenu waliopotea siku tatu zilizopita, msihofu kuhusu hao punda, kwa kuwa wamekwishapatikana. Na yote yaliyotamanika kwa ajili ya Israeli yanamwangukia nani? Siyo kwako na nyumba ya baba yako yote?”

21Sauli akamjibu na kusema, “Siyo mimi Mbenyamini, kutoka kabila lililo dogo sana kwa makabila ya Israeli? Siyo ukoo wangu ulio mdogo sana kwa kabila la Benyamini? Kwa nini basi unaniambia kwa namna hii?”

22Hivyo Samweli akamchukua Sauli na mtumishi wake, akawaingiza ukumbini, akawakalisha mahali pa heshima pa wale walioalikwa, idadi yao takribani watu thelathini.23Samweli akamwambia mpishi, “Lete sehemu niliyokupatia, sehemu ambayo nilikwambia hivi, “Itenge.”’

24Basi mpishi alichukua paja lililokuwa limeinuliwa katika dhabihu na kile kilichokuwa pamoja nalo, akaitenga mbele ya Sauli. Kisha Samweli akasema, “Angalia kile kilichokuwa kimetunzwa kwa ajili yako! Kula, kwa sababu kilitunzwa hadi wakati maalum ufike kwa ajili yako. Na kwa sasa waweza kusema, ‘Nimewaalika watu.”’ Kwa hiyo Sauli alikula pamoja na Samweli siku hiyo.

25Walipokuwa wamekwisha shuka chini kutoka sehemu ya juu na kuingia mjini, Samweli akazungumza na Sauli darini.

26Na kulipopambazuka, Samweli alimwita Sauli darini na kusema, “Amka, kusudi nikusindikize uende zako,” Hivyo Sauli aliamka, na wote wawili, yeye na Samweli walitoka kwenda mtaani.

27Walipokuwa wakienda nje ya viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, “Mwambie mtumishi wako atanguliye mbele yetu (na alitangulia mbele), Lakini wewe sharti usubiri kidogo, nipate kukuambia ujumbe wa Mungu.”

10

1Ndipo Samweli akachukua chupa ya mafuta, akayamimina juu ya kichwa cha Sauli, na akambusu. Akasema, “Je, Mungu hajakutia mafuta uwe mtawala juu ya urithi wake?2Utakapoondoka kwangu leo, utakutana na wanaume wawili karibu na kaburi la Raheli, katika nchi ya Benjamini hapo Selsa. Watu hao watakuambia, ‘Wale punda mliokuwa mkiwatafuta wamepatikana. Sasa, Baba yako ameacha kuwafikiria punda, na ana hofu juu yenu, anasema, ‘Nitafanya nini kuhusu mwanangu?’

3Kisha utakwenda mbele kutoka hapo, na utafika katika mwaloni wa Tabori. Utakutana na watu watatu hapo wakienda kwa Mungu huko Betheli, mmoja akibeba wana-mbuzi watatu, mwingine akibeba mikate mitatu, na mwingine akibeba kiriba cha divai.4Watakusalimu na watakupatia mikate miwili, nawe utaipokea mikononi mwao.

5Baada ya hayo, utafika katika mlima wa Mungu, mahali ilipo ngome ya Wafilisti. Utakapofika mjini, utakutana na kundi la manabii wakiteremka chini kutoka mahali pa juu wakiwa na kinanda, tari, kinubi na filimbi mbele yao; na watakuwa wakitabiri.6Roho wa BWANA utakujaza, nawe utatabiri pamoja nao, na utabadilishwa na kuwa mtu tofauti.7Basi, ishara hizi zikikufikia, fanya lolote ambalo mikono yako itaona ifanye, kwa sababu Mungu yu pamoja nawe.

8Nenda ushuke mbele yangu hadi Gilgali. Kisha nitakufuata huko nitoe dhabihu za kuteketezwa na kutoa dhabihu za amani. Nisubiri kwa muda wa siku saba hadi nije kwako na nikuonyeshe unachopaswa kufanya.”

9Sauli alipogeuka amuache Samweli, Mungu akampa moyo mwingine. Ndipo ishara zote hizi zikatimia siku hiyo.10Walipofika mlimani, kundi la manabii lilikutana naye, na Roho wa Mungu ukamjilia kwa nguvu ili atabiri pamoja nao.11Kila mtu aliyemfahamu kabla hajamwona akitabiri pamoja na manabii, watu waliambiana wao kwa wao, “Kitu gani kimempata mtoto wa Kishi? Hivi Sauli ni mmoja wa manabii siku hizi?”

12Mtu mmoja kutoka eneo hilo akajibu, “Na ni nani baba yao?” Kwa sababu ya jambo hili, ukawapo msemo, “Hivi Sauli naye ni mmoja wa manabii?”13Alipomaliza kutabiri, akafika mahali pa juu.

14Ndipo baba yake mdogo na akamuuliza Sauli na mtumishi wake, “Mlienda wapi?” Naye akamjibu, “Kuwatafuta punda; tulipoona kwamba hatuwezi kuwapata, tukaenda kwa Samweli.”

15Baba yake mdogo akasema, “Tafadhali niambie kile alichosema kwako Samweli,”

16Sauli akamjibu baba yake mdogo, “Alituambia waziwazi kwamba punda wamepatikana.” Lakini kuhusu swala la ufalme alilosema Samweli hakumwambia.

17Basi Samweli aliwaita watu pamoja huko Mispa.18Akawaambia watu wa Israeli, “Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli asemavyo: ‘Niliwatoa Israeli kutoka Misri, na niliwaokoa kutoka nchi ya Wamisri, na kutoka mkono wa falme zote zilizowaonea.’19Lakini leo mmemkataa Mungu wenu, awaokoaye kutoka kwenye majanga na mahangaiko; na mmemwambia, ‘Tuwekee mfalme juu yetu.’ Sasa jihudhurisheni wenyewe mbele za BWANA kwa kabila na jamaa zenu.”

20Kisha Samweli akawaleta kabila zote za Isareli karibu, na kulichagua kabila la Benjamini.21Akawasogeza karibu kabila la Benjamini kwa kufuata jamaa zao; na jamaa ya Wamatri ikachaguliwa; na Sauli mwana wa Kishi akachaguliwa. Lakini walipokwenda kumtafuta, hakuweza kuonekana.22Kisha watu walitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, “Bado yupo mtu mwingine ajaye?” BWANA akajibu, “Yeye mwenyewe kajificha kwenye mizigo.”

23Wakaenda mbio na kumleta Sauli kutoka humo. Aliposimama kati yao, alikuwa mrefu kuliko watu wote kuanzia mabega yake kwenda juu.24Kisha Samweli akawaambia watu, “Je, mnamuona mtu ambaye BWANA amemchagua? Hakuna mtu kama yeye kati ya watu wote.” Watu wote wakapiga Kelele, “Mfalme na aishi”

25Ndipo Samweli akawaambia watu desturi na sheria za ufalme, akaziandika katika kitabu, na kuziweke mbele za BWANA. Baadaye Samweli akawaruhusu watu waondoke kila mtu aende nyumbani kwake.

26Sauli pia alienda nyumbani kwake huko Gibea, akiwa na baadhi ya watu wenye nguvu, wenye mioyo iliyoguswa na Mungu.27Lakini baadhi ya watu wasiofaa walisema, “Huyu mtu atatuokoaje?” Watu hawa walimdharau Sauli na hawakumletea zawadi zozote. Lakini Sauli alinyamaza kimya.

11

1Ndipo Nahashi Mwamoni akaenda na kupiga kambi kuzunguka Yabeshi Gileadi. Watu wote wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, “Fanya mkataba nasi, na tutakutumikia,”

2Nahashi Mwamoni akawajibu, “Kwa sharti hili nitafanya mkataba na ninyi, kwamba wote niwang'oe macho ya kulia, na kwa kitendo hiki kilete fedheha katika Israeli yote.”

3Basi wazee wa Yabeshi wakamjibu, “Tuache kwa siku saba, ili tuwatume wajumbe katika nchi yote ya Israeli. Ndiposa, kama hakuna mtu wa kutuokoa, tutasalimu amri kwako.”

4Nao wajumbe wakafika Gibea, alipoishi Sauli, na wakawaeleza watu kile kilichotokea. Watu wote wakalia kwa sauti kuu.5Na Sauli alikuwa akiwafuata nyuma ng'ombe kutoka shambani. Sauli akauliza, “Watu wamepatwa na nini hadi wanalia?” Ndipo wakamueleza Sauli kile ambacho watu wa Yabeshi walikisema.

6Sauli aliposikia kile walichosema, Roho wa Mungu ukamjia kwa nguvu, na akakasirika.7Akashika nira ya ng'ombe, akawakata hao ng'ombe vipande vipande, na akavituma hivyo vipande katika nchi yote ya Israeli kwa kuwatumia wajumbe, akasema, “Yeyote asiyejitokeza akimfuata Sauli na Samweli, hivi ndivyo ng'ombe wake watakavyofanywa.” Na hofu ya BWANA ikawaingia watu, na wakajitokeza wote kwa pamoja.8Alipowahesabu hapo Beseki, watu wa Israeli walikuwa 300,000, na watu wa Yuda 30,000.

9Wakawaambia wale wajumbe waliotumwa, “Mtawaambia watu wa Yabeshi Gileadi, ‘Kesho, wakati wa jua kali, mtaokolewa.”’ Basi wale wajumbe wakaenda na kuwaambia watu wa Yabeshi, na watu wakafurahi.10Ndipo watu wa Yabeshi wakamwambia Nahashi, “Kesho tutasalimu amri kwako, na utaweza kutufanyia chochote unachoona kinakupendeza.”

11Siku iliyofuata Sauli akawapanga watu katika vikosi vitatu. Wakafika katikati ya Kambi wakati wa asubuhi, wakawashambulia na kuwashinda Waamoni ilipofika mchana. Waliosalimika nao walitawanyika, kiasi kwamba hata watu wawili hawakuachwa pamoja.

12Ndipo watu wakamwambia Samweli, “Wako wapi waliosema, ‘Hivi kweli Sauli atatutawala?’ Walete watu hao, ili tuwauwe.”

13Lakini Sauli akasema, “Hakuna atakayeuwawa siku ya leo, kwa sababu leo BWANA ameokoa Isreli.”

14Kisha Samweli akawaambia watu, “Njoni, twendeni Gilgali na tuimarishe ufalme tena huko.”15Hivyo watu wote wakaenda Gilgali na wakamfanya Sauli kuwa mfalme mbele za BWANA huko Gilgali. Na huko walitoa sadaka za amani mbele za BWANA, na watu wote wa Israeli wakafurahi sana.

12

1Samweli akasema na Israeli wote, “Nimesikia kila kitu mlichoniambia, na nimemuweka mfalme juu yenu.2Basi, yupo hapa mfalme anakwenda mbele yenu, mimi nimezeeka nakujaa mvi; na watoto wangu wako pamoja nanyi. Nimekuwa kiongozi wenu tangu ujana wangu hadi leo.3Mimi niko hapa, nishuhudieni mbele za BWANA na mbele za mtiwa mafuta wake. Nimechukua ng'ombe wa nani? Nimechukua punda wa nani? Ni nani nimemdhulumu? Nimemuonea nani? Nimepokea rushwa kutoka mikono ya nani inipofushe macho yangu? Nishuhudieni, nami nitawarudishia.”

4Nao wakasema, “Haujatudanganya, kutuonea, au kuiba chochote kutoka mkono wa mtu yeyote.”

5Akawaambia, “BWANA ni shahidi juu yenu, na masihi wake leo ni shahidi, kwamba hamkuona kitu mkononi mwangu.” Na wao wakajibu, “BWANA ni shahidi.”

6Samweli akawaambia watu, “BWANA ndiye aliyemteua Musa na Haruni, na ndiye aliyewatoa baba zenu kutoka nchi ya Misri.7Basi sasa, jihudhurisheni, ili niweze kutoa utetezi juu yenu kwa BWANA kuhusu matendo yote ya haki ya BWANA, ambayo aliwafanyia ninyi na baba zenu.

8Yakobo alipokuwa amefika Misri, na babu zenu walimlilia BWANA. BWANA alimtuma Musa na Haruni, waliowaongoza babu zenu kutoka Misri na wakaja kukaa sehemu hii.

9Lakini walimsahau BWANA Mungu wao; akawauza katika mkono wa Sisera, jemedari wa majeshi ya Hazori, katika mkono wa Wafilisti, na katika mkono wa mfalme wa Moabu; hawa wote walipigana na babu zenu.10Wakamlilia BWANA wakisema, ‘Tumefanya dhambi, kwa sababu tumemuacha BWANA na tumewatumikia Mabaali na Mashtorethi. Lakini sasa tuokoe kutoka mikono ya maadui zetu, na tutakutumikia.’11Hivyo BWANA akawatuma Yerubu Baali, Bedani, Yefta na Samweli, na akawapa ushindi dhidi ya maadui zenu wote waliowazunguka, na kwamba mliishi kwa amani.

12Mlipoona kwamba Nahashi mfalme wa watu wa Amoni amekuja dhidi yenu, mkaniambia, ‘Hapana! Badala yake, mfalme awepo atawale juu yetu’- ingawa BWANA, Mungu wenu, alikuwa mfalme wenu.13Sasa yupo hapa mfalme ambaye mmemchagua, mliyemuomba na ambaye BWANA amemteua awe mfalme juu yenu.14Ikiwa mnamhofu BWANA, mtumikieni, muitii sauti yake, msiiasi amri ya BWANA, basi wote wawili ninyi na mfalme anayewatawala mtakuwa wafuasi wa BWANA Mungu wenu.15Kama hamtaitii sauti ya BWANA, mkaasi amri za BWANA, ndipo mkono wa BWANA utakuwa juu yenu, kama ulivyokuwa juu ya babu zenu.

16Hata sasa muwepo kabisa na muone jambo kubwa ambalo BWANA atalifanya mbele ya macho yenu.17Je, leo si mavuno ya ngano? Nitamuomba BWANA, naye ataleta ngurumo na mvua. Ndipo mtajua na kuona kwamba uovu wenu ni mwingi, mlioufanya machoni pa BWANA, kujiombea mfalme wenu ninyi wenyewe.”

18Hivyo Samweli akamwomba BWANA; na siku iyo hiyo BWANA akatuma ngurumo na mvua. Ndipo watu wote wakamuogopa sana BWANA pamoja na Samweli.

19Kisha watu wote wakamwambia Samweli, “Waombee watumishi wako kwa BWANA Mungu wako, ili tusife. Kwa maana tumeongeza uovu huu juu ya dhambi zetu tulipojiombea mfalme sisi wenyewe.”

20Samweli akawajibu, “Msiogope. Mmefanya uovu wote huu, lakini msigeukie mbali na BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa moyo wenu wote.21Wala msigeuke na kufuata mambo matupu yasiyo na faida au kuwaokoa, kwa sababu ni ubatili.22Kwa ajili ya jina lake kuu, BWANA hatawakataa watu wake, kwa sababu imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu kwa ajili yake.23Kwangu mimi, iwe mbali nami kumtenda BWANA dhambi kwa kuacha kuwaombea ninyi. Badala yake, nitawafundisha njia iliyo njema na sahihi.24Mcheni BWANA tu na mtumikieni yeye katika kweli kwa moyo wenu wote. Tafakarini mambo makuu aliyowatendeeni.25Lakini kama mtadumu kufanya uovu, ninyi wote na mfalme wenu mtaangamizwa.”

13

1Sauli alikuwa na umri wa miaka [thelathini] alipoanza kutawala; alipokuwa ametawala Israeli kwa miaka [arobaini],2aliwachagua wanaume 3,000 wa Israeli. Elfu mbili walikuwa pamoja naye huko Mikmashi na katika nchi ya milima ya Betheli, wakati huo wale elfu moja walikuwa pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini. Askari waliobaki aliwarudisha nyumbani, kila mtu hemani kwake.

3Yonathani akaishinda ngome ya jeshi la Wafilisti iliyokuwa Gibea na Wafilisti wakasikia habari hiyo. Baadaye Sauli alipiga tarumbeta katika nchi yote, akisema, “Sikieni enyi Waebrania.”4Waisraeli wote wakasikia kwamba Sauli ameipiga ngome ya Wafilisti, na pia kwamba Israeli imekuwa uvundo kwa Wafilisti. Ndipo askari wakaitwa kwa pamoja kuungana na Sauli huko Gilgali.

5Wafilisti walijikusanya pamoja kupigana dhidi ya Waisraeli: magari 3,000, watu 6,000 wakuendesha magari, na majeshi mengi kama mchanga ufukoni mwa bahari. Wakapanda na kupiga kambi huko Mikimashi, mashariki mwa Beth aveni.6Watu wa Israeli walipoona kuwa wapo katika matatizo -kwa maana watu walikata tamaa, wakajificha kwenye mapango, kwenye vichaka, kwenye miamba, kwenye visima na katika mashimo.7Baadhi ya Waebrania walipanda kwenda Yordani katika nchi ya Gadi na Gileadi. Lakini Sauli alibaki Gilgali, na watu waliomfuata wakitetemeka.8Alisubiri kwa siku saba, muda uliopangwa na Samweli. Lakini Samweli hakufika huko Gilgali, na watu wakatawanyika mbali na Sauli.9Sauli akasema, “Nileteeni sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani.” Kisha akatoa sadaka ya kuteketezwa.10Mara tu alipomaliza kutoa sadaka ya kuteketezwa Samweli akawasili. Sauli akatoka nje wakutane na kumsalimia.

11Basi Samweli akasema, “Umefanya nini?” Sauli akajibu, “Nilipoona kwamba watu wananiacha, na kwamba umechelewa hukufika kwa muda uliopangwa, na kwamba Wafilisti wamekwisha jikusanya huko Mikmashi,12nikasema, ‘Sasa Wafilisti watashuka dhidi yangu huko Gilgali, na sijaomba kibali cha BWANA.’ Kwa hiyo nikajilazimisha mwenyewe kutoa sadaka ya kuteketezwa.”

13Ndipo Samweli akamwambia Sauli, “Umetenda mambo ya kipumbavu. Hukuheshimu amri ya BWANA Mungu wako aliyokupatia. Kwa maana BWANA angeutengeneza utawala wako juu ya Israeli milele.14Lakini sasa utawala wako hautaendelea. BWANA ametafuta mtu anayekubaliwa na moyo wake, kwa sababu wewe hukutii alichokuamuru.”

15Ndipo Samweli akasimama akapanda kutoka Gilgali hadi Gibea ya Benyamini. Basi Sauli akawahesabu watu waliokuwapo pamoja naye, idadi yao ilikuwa kama watu 600.

16Sauli, mtoto wake Yonathani, na watu waliokuwa pamoja nao, wakabaki Geba ya Benyamimni. Lakini Wafilisti wakapiga kambi huko Mikmashi.17Wateka nyara makundi matatu wakaja kutoka kambi ya Wafilisti. Kundi moja likapinda kuelekea Ofra, hadi nchi ya Shuali.18Kundi jingine likageuka kuelekea Beth-horoni, na kundi jingine likaelekea katika mpaka kulikabili bonde la Seboimu kuelekea jangwani.

19Hakuna hata mhunzi aliyeonekana katika nchi yote ya Israeli, kwa sababu Wafilisti walisema, “Waebrania wasije wakajitengenezea mapanga au mikuki.”20Lakini Waisraeli wote huwa wakiteremka kwa Wafilisti, kila mtu kunoa jembe lake, sululu yake, shoka lake na mundu wake.21Gharama za kunoa ncha za majembe, sululu, mashoka na kunyoosha michokoo ilikuwa theluthi moja ya shekeli.

22Hivyo siku ya vita, hakukuwa na mapanga au mikuki iliyoonekana katika mikono yoyote ya askari waliokuwa na Sauli na Yonathani; Ni Sauli na mtoto wake tu ndio walikuwa nazo.

23Vikosi vya Wafilisti wakatokeza katika kivuko cha Mikmashi.

14

1Siku moja, Yonathani mwana wa Sauli alimwambia mbeba silaha wake aliye mdogo, “Njoo, hebu twende hadi upande mwingine kwenye ngome ya Wafilisti.” Lakini hakumjulisha baba yake.

2Sauli alikuwa akikaa nje ya mji wa Gibea chini ya mti wa mkomamanga ulio katika Migroni. Takribani watu 600 walikuwa pamoja naye,3akiwemo Ahiya mwana wa Ahitubu (nduguye Ikabodi) mwana wa Finehasi, mwana wa Eli, kuhani wa BWANA huko Shilo, aliyevaa naivera. Watu hao hawakujua kwamba Yonathani ameondoka.

4Katikati ya vichochoro, ambavyo Yonathani alinuia kuvipita hadi ngome ya Wafilisti, kulikuwa na mwamba wenye mteremko mkali upande mmoja, na mteremko mkali upande mwingine. Jabali moja liliitwa Bosesi, na jingine liliitwa Sene.5Lile jabali lenye mteremko mkali zaidi liliinuka upande wa kaskazini mbele ya Mikmashi, na jingine upande wa kusini mbele ya Geba.

6Yonathani akamwambia kijana mbeba silaha, “Njoo, na tuvuke hadi ngome ya hawa wasiotahiriwa. Pengine BWANA atatenda kwa niaba yetu, kwa maana hakuna kitu kiwezacho kumzuia BWANA asiokoe kwa wengi au kwa watu wachache.”

7Mbeba silaha wake akajibu, “Fanya kila kitu kilicho ndani ya moyo wako. Songa mbele, tazama, niko pamoja nawe, nitatii maagizo yako yote.”

8Ndipo Yonathani akasema, “Tutavuka twende kwa watu hao, na tutajionesha wenyewe kwao.9Kama watatuambia, ‘Subirini hapo hadi tutakapokuja kwenu’ - basi tutabaki katika sehemu yetu na hatutavuka kwenda kwao.10Lakini kama watajibu, ‘Njooni kwetu,’ ndipo tutavuka; kwa sababu BWANA amewaweka mkononi mwetu. Hii ndiyo itakuwa ishara yetu.”

11Kwa hiyo wote wawili wakajidhihirisha mbele ya ngome ya Wafilisti. Wafilisti wakasema, “Angalia, Waebrania wanakuja kutokea kwenye mashimo walimojificha.”12Ndipo watu wa ile ngome wakamwita Yonathani na mbeba silaha wake, wakisema, “Njooni huku kwetu, tutawaonesha jambo fulani.” Na Yonathani akamwambia mbeba silaha wake; “Nifuate nyuma yangu, kwa sababu BWANA amewaweka katika mkono wa Israeli.”13Yonathani alipanda juu kwa mikono na miguu yake, na mbeba silaha akimfuata nyuma yake. Wafilisti waliuwawa mbele ya Yonathani, na mbeba silaha wake akiwaua baadhi nyuma yake.14Hilo shambulio la kwanza walilofanya Yonathani na mbeba silaha wake, waliua watu wapatao ishirini katika urefu wa nusu handaki kwenye eka moja ya ardhi.

15Kukawa na hofu kubwa katika kambi, uwandani, na katika watu. Hata ngome ya jeshi na watekaji nyara nao wakawa na hofu kubwa.

16Ndipo walinzi wa Sauli huko Gibea ya Benyamini wakaona kundi la askari wa Wafilisti likitawanyika, wakienda kule na huku.17Kisha Sauli akawaambia watu aliokuwa nao, “Mjihesabu ili muone nani hayupo hapa.” Walipokuwa wamehesabu, wakagundua kuwa Yonathani na mbebaji wa silaha zake hawapo.

18Sauli akamwambia Ahiya, “Lete hapa sanduku la Mungu”- kwa maana wakati huo ilikuwa na wana wa Israeli.19Wakati Sauli akiongea na kuhani, kelele na ghasia kubwa iliendelea na kuongezeka katika kambi ya Wafilisti. Ndipo sauli akamwambia kuhani, “Acha kazi unayofanya.”

20Sauli na watu wote aliokuwa nao wakajipanga na kwenda kwenye mapigano. Upanga wa kila Mfilisti ulikwa juu ya Mfilisti mwenzake, na kulikuwa na ghasia kubwa.21Basi Waebrania ambao mwanzoni walijiunga na Wafilisti, na kwenda kwenye kambi yao, wao pia waliungana na Waisraeli waliokuwa pamoja na Sauli na Yonathani.22Waisraeli wote waliokuwa wamejificha katika milima karibu na Efraimu waliposikia kwamba Wafilisti wamekimbia, nao pia wakawafuata Wafilisti na kuwafukuza kwenye hiyo vita.23Hivyo siku hiyo BWANA aliwaokoa Israeli, na mapigano yalivuka kupitiliza Beth aveni.

24Siku hiyo watu wa Israeli walifadhaika kwa sababu Sauli aliwaweka watu chini ya kiapo akasema, “Na alaaniwe mtu atakaye kula chakula kabla ya jioni na kabla sijalipiza kisasi kwa maadui zangu.” Hivyo hakuna hata mmoja kati ya watu wote aliyeonja chakula.

25Ndipo watu wote wakaingia msituni na kuona asali ikiwa juu ya ardhi.26Watu walipoingia humo msituni, asali ilitiririka, lakini hakuna aliyeweka mkono wake kinywani kwa maana watu waliogopa kiapo.27Lakini Yonathani alikuwa hajasikia kwamba baba yake amewaagiza watu kwa kiapo. Akanyoosha ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwake na kuichovya kwenye sega la asali. Kisha akanyoosha mkono wake hadi kinywani mwake, na macho yake yakaangaziwa.

28Ndipo mmoja wa watu hao, akamwambia, “Baba yako aliwaagiza watu kwa mkazo na kwa kiapo, kwa kusema, ‘Alaaniwe mtu atakaye kula chakula kwa siku ya leo,’ ingawa watu wamedhoofika kwa ajili ya njaa.”29Baadaye Yonathani alisema, “Baba yangu amefanya matatizo katika nchi. Angalia jinsi macho yangu yalivyotiwa nuru kwa sababu nilionja asali hii kidogo.30Je, siyo vivuri sana kama leo watu wangekula bila kizuizi nyara walizopata kutoka kwa maadui zao? Kwa sababu sasa mauaji hayakuwa makubwa katikati ya Wafilisti.”

31Siku hiyo waliwashambulia Wafilisti kutoka Mikmashi hadi Aiyaloni. Na watu walikuwa wamechoka sana.32Hivyo watu wakazivamia nyara na kuchukua kondoo, ng'ombe na ndama na kuwachinja hapo chini. Watu walikula nyama zao pamoja na damu.33Kisha wakamwambia Sauli, “Tazama, watu wanamtenda BWANA dhambi kwa kula pamoja na damu.” Sauli akasema, “Mmetenda isivyo haki. Sasa, viringisheni jiwe kubwa kwangu.” Sauli akasema,

34“Nendeni kati ya watu, na muwaambie, ‘Kila mtu alete ng'ombe na kondoo wake, wawachinje hapa, na kuwala. Msimtende BWANA dhambi kwa kula na damu.”’ Kwa hiyo watu wote wakaleta kila mtu na ng'ombe wake usiku huo na kuwachinja mahali hapo.35Sauli akamjengea BWANA madhabahu, ambayo ilikuwa ya kwanza kwake kumjengea BWANA.

36Ndipo Sauli akasema, “Haya tuwafukuze Wafilisti usiku na kuwateka nyara hadi asubuhi; tusimwache hata mtu mmoja akiwa hai.” Nao wakamjibu, “Fanya unaloona linakupendeza.” Lakini kuhani akasema, “Hebu na tumkaribie Mungu mahali hapa.”37Sauli alitaka kumuuliza Mungu maswali zaidi, “Je, inanipasa kuwafukuza Wafilisti? Je, utawaweka katika mkono wa Israeli?” Lakini siku hiyo BWANA hakumjibu kitu.

38Ndipo Sauli akasema, “Njooni hapa, viongozi wote wa watu; mjue na kuona jinsi dhambi hii ilivyotokea leo.39Kwa maana, kama BWANA aishivyo, aliyewaokoa Israeli, hata kama angekuwa mwanangu Yonathani, atapaswa kufa.” Lakini hakuna hata mtu mmoja miongoni mwa watu aliye mjibu neno.40Basi akawaambia Waisraeli wote, “Simameni upande mmoja, na mimi na Yonathani tutasimama upande mwingine.” Kisha watu wakamwambia Sauli, “Fanya lile unaloona jema kwako.”41Kwa hiyo, Sauli akamwambia BWANA, Mungu wa Israeli, “ikiwa hii dhambi ni mimi nimeifanya au Yonathani mwanangu basi, BWANA, Mungu wa Israeli tuonyeshe Urimu. Lakini kama hii dhambi imefanywa na watu wako Israeli tuonyeshe Thumimu.” Yonathani na Sauli wakatwaliwa, lakini watu walinusurika kuchaguliwa.42Basi Sauli akasema, “Tupa mawe ya bahati nasibu tuone kati yangu na mwanangu Yonathani.” Ndipo Yonathani akatwaliwa.

43Kisha Sauli akamwambia Yonathani, “Niambie umefanya nini.” Yonathani akamwambia baba yake, “Nilionja asali kidogo kwa kutumia ncha ya fimbo iliyokuwa mkononi mwangu. Niko hapa: Nitakufa.”44Sauli akasema, “Mungu afanye hivyo na kuzidi hata kwangu, kama Yonathani hautakufa.”

45Basi watu wakamuuliza Sauli, “Je, inampasa Yonathani afe, ni nani aliyetekeleza ushindi huu mkubwa kwa ajili ya Israeli? Mbali na hayo! Kama BWANA aishivyo, hata unywele mmoja wa kichwa chake hautaanguka chini, kwa maana leo amefanya kazi pamoja na Mungu.” Hivyo hao watu walimuokoa Yonathani ili asife.46Basi Sauli akasita kuwafuatia Wafilisti, nao wakarudi katika makao yao.

47Sauli alipoanza kutawala juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote kila upande. Alipigana dhidi ya Moabu, dhidi ya watu wa Amoni, Edomu, wafalme wa Zoba, na Wafilisti. Popote alipogeukia aliwapiga kwa adhabu adui zake.48Alitenda kwa ushujaa mkubwa na kuwashinda Waamaleki. Aliwaokoa Israeli kutoka mikono ya watu ambao waliwateka nyara.

49Basi wana wa Sauli walikuwa ni hawa Yonathani, Ishvi, na Malkishua. Na majina ya binti zake wawili yalikuwa ni haya, Merabu mzaliwa wa kwanza, na mdogo aliitwa Mikali.50Jina la mke wa Sauli aliitwa Ahinoamu; naye alikuwa binti Ahimaasi. Na jina la Jemedari wa jeshi lake aliitwa Abneri mwana wa Neri, baba mdogo wa Sauli.51Kishi alikuwa baba yake Sauli; na Neri alikuwa baba yake na Abneri, wote walikuwa wana wa Abieli.

52Kulikuwa na mapigano makali dhidi ya Wafilisti katika siku zote za Sauli. Naye alipomwona mtu yeyote mwenye nguvu, au mtu yeyote jasiri, alimshikamanisha na yeye mwenyewe.

15

1Samweli akamwambia Sauli, “BWANA alinituma nikutie mafuta uwe mfalme wa watu wake Israeli. Basi sikiliza maneno ya BWANA.2Hivi ndivyo BWANA wa majeshi asemavyo, ‘Nilichunguza jinsi Amaleki alivyomfanyia Israeli kwa kuwapinga njiani, walipopanda kutoka Misri.3Sasa nenda umshambulie Amaleki na ukaangamize kabisa vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache, ua wote mwanamme na mwanamke, mtoto na mtoto mchanga, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.”’

4Sauli akawaita watu na kuwahesabu katika mji wa Telemu: watu 200,000 waendao kwa miguu, na watu 10,000 kutoka Yuda.5Kisha Sauli akaja hadi mji wa Amaleki akangoja huko bondeni.6Ndipo Sauli akawaambia Wakeni, “Nendeni, muondoke, mkajitenge na Waamaleki, nisije kuwaangamiza pamoja nao. Kwa maana ulionyesha wema kwa watu wote wa Israeli, walipotoka Misri.” Kwa hiyo Wakeni wakajitenga na Waamaleki.

7Kisha Sauli akawashambulia Waamaleki, kutoka Havila hadi kufika Shuri, ulio mashariki mwa Misri.8Basi akamchukua Agagi mfalme wa Waamaleki akiwa hai; aliwaangamiza kabisa watu wote kwa ncha ya upanga.9Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi akiwa hai, pamoja na kondoo wazuri, ng'ombe, ndama wanono, na wanakondoo. Kila kitu kilichokuwa kizuri, hawakukiangamiza. Bali waliangamiza kabisa chochote kilichodharaulika na kisicho na thamani.

10Baadaye neno la BWANA likamjia Samweli, kusema,11“Inanihuzunisha kwamba nimemchagua Sauli awe mfalme, kwa maana aligeuka nyuma asinifuate na hakutekeleza maagizo yangu.” Samweli alikasirika; akamlilia BWANA usiku kucha.

12Samweli aliamka mapema akutane na Sauli wakati wa asubuhi. Samweli aliambiwa, “Sauli alifika Karmeli na amejijengea ukumbusho kwa ajili yake, kisha aligeuka na kuendelea chini hadi Gilgali.” Ndipo

13Samweli akamwendea Sauli, na Sauli akamwambia, “Umebarikiwa na BWANA! Nami nimetekeleza amri ya BWANA.”

14Samweli akasema, “Hicho kilio cha kondoo ni cha nini basi masikioni mwangu, na hiyo milio ya ng'ombe ninayosikia?

15Sauli akamjibu, “Wao wamewaleta kutoka kwa Waamaleki. Kwa sababu watu waliwaacha hai kondoo wazuri na ng'ombe, kwa ajili ya sadaka kwa BWANA Mungu wako. Zilizobaki tuliziangamiza kabisa.”

16Ndipo Samweli akamwambia Sauli, “Subiri nitakuambia kile ambacho BWANA amekisema kwangu usiku.” Sauli akamwambia, “Sema!”17Samweli akasema, “Ingawa wewe ni mdogo machoni pako mwenyewe, je, hukufanywa mkuu wa kabila za Israeli? Na BWANA akakutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli;18BWANA alikutuma katika safari yako akisema, ‘Nenda na uangamize kabisa wenye dhambi, Waamaleki, na upigane dhidi yao hadi wameangamizwa.’19Kwa nini basi haukuitii sauti ya BWANA, bali badala yake ulishikilia nyara na ukafanya uovu machoni pa BWANA?”

20Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Kweli kabisa niliitii sauti ya BWANA, Na nimeifuata njia ambayo BWANA alinituma. Nimemteka Agagi, mfalme wa Waamaleki, na kuwaangamiza kabisa Waamaleki.21Lakini watu walichukua baadhi ya nyara-kondoo na ng'ombe, na vitu vizuri vilivyokusudiwa kuangamizwa, ili wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.”

22Samweli akajibu, “Je, BWANA hufurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu kama ilivyo kuitii sauti yake? Kutii ni bora kuliko dhabihu, na kusikia ni bora kuliko mafuta ya beberu.
23Kwa maana uasi ni sawa na dhambi ya uchawi, na ukaidi ni sawa na uovu na udhalimu. Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA, naye pia amekukataa usiwe mfalme.”

24Ndipo Sauli akamwambia Samweli, “Nimetenda dhambi; kwa maana nimevunja amri ya BWANA na maneno yako, kwa sababu niliwaogopa watu na kuitii sauti yao.25Sasa, tafadhali nisamehe dhambi yangu, na urudi nami ili nipate kumwabudu BWANA.”

26Samweli akamwambia Sauli, “Sitarudi pamoja na wewe; kwa sababu umekataa neno la BWANA, naye BWANA amekukataa usiwe mfalme juu ya Israeli.”

27Samweli alipogeuka kuondoka, Sauli akashika pindo la kanzu lake, na likararuka.28Samweli akamwambia, “BWANA ameurarua ufalme wa Israeli kutoka kwako leo na amempa ufalme huo jirani yako, aliye bora kuliko wewe.29Pia, yeye aliye Uwezo wa Israeli hatasema uongo wala kubadili nia yake; kwa sababu si mwanadamu, kwamba abadili nia yake.”

30Kisha Sauli akasema, “Nimetenda dhambi. Lakini tafadhali nipe heshima wakati huu mbele ya wakuu wa watu wangu na mbele ya Israeli. Urudi tena pamoja nami, kusudi niweze kumwabudu BWANA, Mungu wako.”31Hivyo Samweli akamrudia tena Sauli, na Sauli akamwabudu BWANA.

32Kisha Samweli akasema, “Mlete hapa kwangu Agagi mfalme wa Waamaleki.” Agagi akafika kwake akiwa amefungwa minyororo na kusema, “Hakika uchungu wa kifo umepita.”

33Naye Samweli akamjibu, “Jinsi upanga wako ulivyofanya wanawake wapoteze watoto, vivyo hivyo mama yako naye hatakuwa na mtoto miongoni mwa wanawake.” Kisha Samweli akamkata Agagi vipande vipande mbele za BWANA huko Gilgali.

34Samweli akaenda Rama, na Sauli akapanda kwenda nyumbani kwake Gibea ya Sauli.35Samweli hakumuona tena Sauli hadi siku ya kifo chake, lakini alimwombolezea Sauli. Na BWANA alijuta kwa kumfanya Sauli awe mfalme juu ya Israeli.

16

1BWANA akamwambia Samweli, “Utamlilia Sauli kwa muda gani, ikiwa nimemkataa asiwe mfalme juu ya Israeli? Ijaze pembe yako mafuta na uende. Nitakutuma kwa Yese akaaye Bethlehemu, maana nimejichagulia mfalme katika wanawe.

2Samweli akasema, “Jinsi gani nitaenda? Kama Sauli akisikia jambo hili, ataniua.” BWANA akasema, “Chukua mtamba na useme, ‘Nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA.’

3Umwite Yese aje kwenye dhabihu, nami nitakuonyesha kile utakachofanya. Utamtia mafuta kwa ajili yangu yule nitakaye kuambia.”

4Samweli akafanya kama BWANA alivyosema na akaenda Bethlehemu. Wazee wa mji walikuwa wakitetemeka walipokuja kuonana naye na wakasema, “Je, umekuja kwa amani?”

5Naye akasema, “Kwa amani; nimekuja kutoa dhabihu kwa BWANA. Jitoeni wenyewe kwa BWANA kwa ajili ya dhabihu na muandamane nami.” Na akamweka wakfu Yese na watoto wake kwa BWANA, na baadaye aliwaita wote kwenye dhabihu.

6Walipofika, akamwangalia Eliabu na akajisemea mwenyewe kwamba mtiwa mafuta wa BWANA hakika amesimama mbele yake.

7Lakini BWANA akamwambia Samweli, “Usimwangalie sura yake ya nje, au kimo cha umbo lake; kwa sababu nimemkataa. Maana BWANA haangalii kama mtu aangaliavyo; mtu hutazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.”

8Kisha Yese akamwita Abinadabu akamwambia apite mbele ya Samweli. Na Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua.”9Kisha Yese akmwambia Shama apite karibu. Na Samweli akasema, “Hata huyu BWANA hakumchagua.”10Yese akawaleta watoto wake saba wakapita mbele ya Samweli. Na Samweli akamwambia Yese, “Hakuna hata mmoja aliyechaguliwa na BWANA kati ya hawa.”11Kisha Samweli akamwambia Yese, “Je, watoto wako wote wako hapa?” Naye akajibu, “Yupo mdogo kabisa lakini anachunga kondoo.” Samweli akamwambia Yese, “Tuma watu wakamwite; maana hatutakaa chini hadi atakapofika hapa.”

12Yese akawatuma watu wakamleta. Naye kijana huyu alikuwa mwekundu na mwenye macho mazuri na mwenye muonekano mzuri. BWANA akasema, “Amka, umtie mafuta; maana huyu ndiye.”

13Ndipo Samweli akachukua pembe yenye mafuta na kumtia mafuta katikati ya kaka zake. Roho wa BWANA akamjilia Daudi kwa nguvu tangu siku hiyo na kuendelea. Kisha Samweli akanyanyuka na kwenda Rama.

14Basi Roho wa BWANA akamuacha Sauli, badala yake roho ya ubaya kutoka kwa BWANA ikamsumbua.

15Watumishi wa Sauli wakamwambia, “Tazama, roho ya ubaya kutoka kwa Mungu inakusumbua.16Haya bwana wetu hebu sasa amuru watumishi wako walio mbele yako wamtafute mtu mwenye ujuzi wa kupiga kinubi. Basi ikiwa roho wa ubaya kutoka kwa Mungu yuko juu yako, atakipiga kinubi nawe utajisikia vizuri.”

17Sauli akawaambia watumishi wake, “Mnitafutie mtu anayeweza kupiga vizuri na mmlete kwangu.”

18Ndipo kijana mmoja kati yao akajibu, na kusema, “Nimemuona mtoto wa Yese Mbethelehemu, aliye mjuzi katika kupiga, ni mwenye nguvu, mtu jasiri, mtu wa vita, mwenye busara aongeapo, mtu mzuri kwa uso; na BWANA yuko pamoja naye.”

19Hivyo Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, na kusema, “Nitumie mtoto wako Daudi, anayewatunza kondoo.”20Yese akamchukua punda aliyebeba mikate, na kiriba cha divai, na mwana-mbuzi, na akamtuma kwa Sauli pamoja na vitu hivyo.

21Ndipo Daudi akafika kwa Sauli na kuanza kazi yake. Sauli alimpenda sana Daudi, na akawa mbeba silaha wake.22Sauli akawatuma wajumbe kwa Yese, akisema, “Mruhusu Daudi awe mbele yangu, maana amepata kibali machoni pangu.”

23Wakati wowote roho ya usumbufu kutoka kwa Mungu ikiwapo juu ya Sauli, Daudi alichukuwa kinubi na kukipiga. Hivyo Sauli angeburudishwa na kupona, na huyo roho wa usumbufu angemtoka.

17

1Basi Wafilisti walikusanya majeshi yao kwa ajili ya vita. Walikusanyika huko Soko, iliyoko Yuda. Nao wakapiga kambi kati ya Soko na Aseka katika Efesdamimu.2Sauli na watu wa Israeli walijikusanya na kuweka kambi katika bonde la Ela, na wakapanga vita kukutana na Wafilisti.3Wafilisti walisimama juu ya mlima upande mmoja, na Israeli nao walisimama juu ya mlima upande mwingine wakitenganishwa na bonde kati yao.

4Mtu mmoja mwenye nguvu akatoka katika kambi ya Wafilisti, mtu huyo aliitwa Goliathi wa Gathi, kimo chake mikono sita na shubiri moja.5Alikuwa na chepeo ya shaba kichwani mwake, na alivaa dirii ya chuma. Hiyo dirii ilikuwa na uzito wa shekeli elfu hamsini za shaba.6Alikuwa na mabamba ya shaba kwenye miguu yake na mkuki wa shaba katikati ya mabega yake.7Ule mpini wa mkuki wake ulikuwa mkubwa, wenye kamba iliyo na kitanzi kwa ajili ya kuutupia kama kamba ya sindano ya mfumaji. Kichwa cha mkuki wake kilikuwa na uzito wa shekeli mia sita za chuma. Aliyembebea ngao alitembea mbele yake.

8Alisimama akayapigia kelele majeshi ya Israeli, “Kwa nini mmekuja na mmejipanga kwa ajili ya vita? Mimi si Mfilisti, na ninyi si watumishi wa Sauli? Chagueni mtu kutoka kwenu ateremke na kuja kwangu.9Kama anaweza kupigana nami na kuniua, hapo ndipo tutakuwa watumwa wenu. Lakini kama nitamshinda na kumuua, basi mtakuwa watumwa wetu na kututumikia.”10Mfilisti huyo akasema tena, “Leo ninayapa changamoto majeshi ya Israeli. Mnipe mtu ili tuweze kupigana naye.”11Sauli na Israeli wote waliposikia alichosema Mfilisti huyo, walikata tamaa na kuogopa sana.

12Basi Daudi alikuwa mwana wa Mwefraimu wa Bethelehemu ya Yuda, aliyeitwa Yese. Naye alikuwa na watoto wanane wa kiume. Yese alikuwa mtu mzee katika siku za Sauli, mwenye umri mkubwa kati ya watu.13Watoto watatu wakubwa wa Yese walimfuata Sauli vitani. Majina ya watoto wake watatu waliokwenda vitani yalikuwa ni Eliabu mzaliwa wa kwanza, aliyemfuata Abinadabu, na watatu aliitwa Shama.14Daudi ndiye aliyekuwa mdogo kabisa. Hao wakubwa watatu walimfuata Sauli.15Basi Daudi alikwenda na kurudi akipita kati ya majeshi ya Sauli akiwa na kondoo za baba yake huko Bethelehemu, ili kuwachunga.

16Kwa muda wa siku arobaini yule Mfilisti mwenye nguvu alikuwa akijitokeza asubuhi na jioni kwa ajili ya vita.

17Kisha Yese akamwambia mwanawe Daudi, “Wapelekee kaka zako efa ya bisi na hii mikate kumi, na uzipeleke upesi kule kambini kwa ajili ya kaka zako.18Pia peleka hizi jibini kumi kwa jemedari wa kikosi chao cha elfu. Ukawaangalie wako na hali gani kisha uniletee habari kuhusu wanavyoendelea vizuri.

19Kaka zako wako pamoja na Sauli na watu wote wa Israeli katika bonde la Ela, wanapigana na Wafilisti.”20Daudi aliamka asubuhi na mapema na kuliacha kundi chini ya uangalizi wa mchungaji. Akachukua vile vitu na kuondoka, kama Yese alivyomwamuru. Akafika kambini wakati jeshi linaondoka kwenda uwanja wa vita wakipiga kelele za vita.21Nao Israeli na Wafilisti walijipanga kivita, jeshi dhidi ya jeshi.22Daudi aliviacha vitu vyake kwa mtunza mahitaji, akalikimbilia jeshi, na kuwasalimia kaka zake.23Alipoongea nao, yule mtu mwenye nguvu, Mfilisti wa Gathi, jina lake Goliathi, akajitokeza kutoka majeshi ya Wafilisti, naye akasema maneno yaleyale kama hapo mwanzo. Naye Daudi akayasikia.24Watu wote wa Israeli walipomwona Goliathi, walimkimbia na waliogopa sana.25Watu wa Israeli wakasema, “Umemuona mtu huyu aliyejitokeza? Amekuja kuipa changamoto Israeli. Basi mfalme atampa mali nyingi mtu atakayemuua, atamuozesha binti yake, na familia ya baba yake haitalipa kodi katika Israeli.”

26Daudi akawauliza watu waliosimama karibu naye, “Atafanyiwa nini mtu ambaye atamuua Mfilisti huyu na kuiondolea Israeli fedheha? Ni nani Mfilisti huyu asiyetahiriwa ayatukanaye majeshi ya Mungu aliye hai?”

27Ndipo watu wakarudia kile walichokuwa wamesema na kumwambia, “Ndivyo iitakavyofanyika kwa mtu atakayemuua.”

28Kaka yake mkubwa Eliabu, alisikia wakati akisema na watu. Hasira ya Eliabu ikawaka moto dhidi ya Daudi, naye akamuuliza, “Kwa nini umekuja hapa? Wale kondoo wachache umewaacha na nani huko nyikani? Nakijua kiburi chako, na utundu wa moyo wako; maana umekuja hapa ili uweze kuona mapigano.”

29Naye Daudi akamjibu, “Nimefanya nini sasa? Mimi si niliuliza swali tu?30Akamgeukia mtu mwingine na kumwacha huyo, na kusema vivyo hivyo. Nao watu wakajibu vilevile kama mwanzo.31Maneno aliyosema Daudi yaliposikika, askari waliyasema tena kwa Sauli, naye akawatuma kwa Daudi.

32Kisha Daudi akamwambia Sauli, “Pasiwepo moyo wa mtu utakayezimia kwa sababu ya Mfilisti huyo; Mtumishi wako atakwenda kupigana na Mfilisti huyu.”

33Sauli akamwambia Daudi, “Huwezi kumpinga Mfilisti ama kupigana naye; wewe ni kijana tu, na yeye amekuwa mtu wa vita tangu ujana wake.”

34Lakini Daudi akamwambia Sauli, “Mtumishi wako alikuwa akichunga kondoo za baba yake. Mara simba au dubu alikuja akamchukua mwana kondoo kutoka kundini,35Nilimfukuza na kumshambulia na kumpokonya kutoka kinywani mwake. Na aliponirukia, nilimshika ndevu zake, nilimpiga, na kumuua.36Mtumishi wako amekwisha kumuua simba na dubu. Huyu Mfilisti asiyetahiriwa atakuwa kama mmoja wa wanyama hao, kwa kuwa ameyadharau majeshi ya Mungu aliye hai.”37Daudi akasema, “BWANA aliyeniokoa kutoka makucha ya simba na makucha ya dubu. Ataniokoa kutoka mkono wa Mfilisti huyu.” Kisha Sauli akamwambia Daudi, “Nenda, BWANA awe pamoja nawe.”

38Sauli akamvika Daudi vazi lake la vita. Akamvika chepeo ya shaba kichwani pake, na akamvika koti la chuma.39Daudi akaufunga upanga wake juu ya vazi la Sauli. Lakini hakuweza kutembea, kwa sababu hakupata mafunzo kwa mavazi hayo. Ndipo Daudi akamwambia Sauli, “Siwezi kwenda kupigana nikiwa na haya, maana sikupata mafunzo kwa haya.” Kwa hiyo Daudi akayavua.

40Akachukua fimbo mkononi mwake na akachagua mawe matano laini kutoka katika kijito; akayaweka kwenye mfuko wake wa kichungaji. Kombeo lake lilikuwa mkononi akawa anamsogelea yule Mfilisti.

41Yule Mfilisti akaja na kumsogelea Daudi, mbeba ngao yake akiwa mbele yake.42Mfilisti alipotazama kila upande na kumuona Daudi, akamdharau, maana alikuwa kijana tu, mwekundu, na umbo la kupendeza.43Ndipo Mfilisti akamuuliza Daudi, “Je, mimi ni mbwa, hata ukanijia na fimbo? Naye Mfilisti kwa miungu yake akamlaani Daudi.44Huyo Mfilisti akamwambia Daudi, “Njoo kwangu, na nyama yako nitawatupia ndege wa angani na wanyama wa mwituni.”

45Daudi akamjibu Mfilisti, “Unanijia kwa upanga, kwa mkuki na mkuki mdogo. Bali mimi ninakujia kwa jina la BWANA wa majeshi, Mungu wa Majeshi ya Israeli, uliyemdharau.46Leo BWANA atanipa ushindi dhidi yako, na nitakuua na kukiondoa kichwa chako kwenye kiwiliwili. Leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa mwituni walioko duniani mizoga ya jeshi la Wafilisti, ili dunia yote ijue kwamba yupo Mungu katika Israeli,47na kusanyiko hili lote lijue kwamba BWANA hatoi ushindi kwa upanga wala kwa mkuki. Kwa kuwa vita ni vya BWANA, na atawaweka katika mkono wetu.”

48Mfilisti aliponyanyuka na kukaribia akutane na Daudi, ndipo Daudi akakimbia kwa haraka kuelekea jeshi la adui ili akutane naye.49Daudi aliweka mkono wake mfukoni, akachukua jiwe kutoka humo, akalitupa kwa kombeo, na likampiga Mfilisti kwenye paji la uso, akaanguka chini kifudifudi.

50Daudi alimshinda Mfilisti kwa kombeo na kwa jiwe moja. Alimpiga huyo Mfilisti na kumuua. Mkononi mwa Daudi hakukuwa na upanga.51Ndipo Daudi akakimbia akasimama juu ya Mfilisti na kutwaa upanga wake, akauchomoa kutoka alani, akamuua, na kukata kichwa chake kwa upanga huo.52Ndipo watu wa Israeli na wale wa Yuda wakaamka kwa kelele, na kuwafukuza Wafilisti kuvuka bonde na malango ya Ekroni. Na maiti za Wafilisti walilala katika njia iendayo Shaaraimu, na njia yote kuelekea Gathi na Ekroni.53Watu wa Israeli wakarejea kutoka kuwafukuza Wafilisti, na wakateka nyara kambi yao.54Daudi akachukua kichwa cha Mfilisti na kukipeleka Yerusalemu, lakini akaliweka vazi la vita katika hema lake.

55Sauli alipomuona Daudi akienda kukabiliana na yule Mfilisti, akamwambia Abneri, jemedari wa jeshi, “Abneri, kijana huyu ni mtoto wa nani?” Abneri akasema, “Kama uishivyo, mfalme, mimi sijui.”

56Naye mfalme akasema, “Waulize wanaoweza kufahamu, mvulana huyu ni kijana wa nani.”

57Daudi aliporudi kutoka kumuua yule Mfilisti, Abneri alimchukuwa, na kumleta mbele ya Sauli akiwa na kichwa cha Mfilisti mkononi mwake.

58Sauli akamuuliza, “Kijana, wewe ni mtoto wa nani?” Na Daudi akamjibu, “Mimi ni mtoto wa mtumishi wako Yese Mbethlehemu.”

18

1Daudi alipokuwa amemaliza kuongea na Sauli, roho ya Yonathani ilishikana na roho ya Daudi, na Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.2Sauli akamweka kazini Daudi siku hiyo, hakumwacha arudi nyumbani kwa baba yake.3Kisha Yonathani na Daudi wakafanya makubaliano ya urafiki kwa sababu Yonathani alimpenda kama roho yake mwenyewe.4Yonathani akavua kanzu aliyokuwa amevaa na kumpa Daudi, akampa na vazi lake la kivita, pamoja na upanga, upinde, na mshipi.

5Daudi alikwenda popote ambapo Sauli alimtuma, naye alifanikiwa. Sauli akamteua Daudi awe mkuu wa wapiganaji. Jambo hili lilipendeza machoni pa watu na katika macho ya watumishi wa Sauli.

6Wakati wanarudi nyumbani kutoka kuwapiga Wafilisti, wanawake walitoka miji yote ya Israeli, wakiimba na kucheza, ili kukutana na mfalme Sauli, wakiwa na matowazi, wenye furaha, na wakiwa na ala za muziki.7Hao wanawake waliimba kwa kupokezana huku wakicheza; wakiimba: “Sauli ameua maelfu yake, na Daudi ameua makumi elfu yake.”

8Sauli alikasirika sana, na wimbo huu haukumpendeza. Naye akasema, “Wamemsifia Daudi juu ya makumi elfu, lakini wamenisifia melfu tu mimi! Atapata kitu gani zaidi isipokuwa ufalme?9Kuanzia siku hiyo na kuendelea, Sauli alimuangalia Daudi kwa mashaka.

10Kesho yake yule roho ya ubaya kutoka kwa Mungu ikamwingia Sauli kwa nguvu, naye akatabiri nyumbani mwake. Hivyo Daudi akapiga kifaa chake, kama alivyofanya kila siku. Sauli alikuwa na mkuki wake mkononi.11Sauli akatupa mkuki wake, kwani alifikiri, “Nitampigilia ukutani.” Lakini Daudi mara mbili aliepa uwepo wa Sauli.

12Sauli alimwogopa Daudi, kwa sababu BWANA alikuwa pamoja naye, lakini hakuwa na Sauli tena.13Hivyo Sauli alimuondoa Daudi mbele yake na akamteua kuwa kamanda wa kikosi cha askari elfu moja. Kwa namna hii Daudi alitoka na kuingia mbele ya watu.14Daudi alikuwa akistawi kwa mambo yake yote, maana BWANA alikuwa pamoja naye.15Sauli alipoona kwamba Daudi anastawi, alimwogopa.16Lakini Israeli yote na Yuda walimpenda Daudi, maana alitoka na kuingia mbele yao.

17Kisha Sauli akamwambia Daudi, “Huyu hapa ni binti yangu mkubwa Merabu. Nitakupatia awe mke wako. Ila tu uwe jasiri kwa ajili yangu na upigane vita vya BWANA.” Maana Sauli alifikiri, “Usije mkono wangu ukawa juu yake, ila acha mkono wa Wafilisti uwe juu yake.”

18Daudi akamwambia Sauli, “Mimi ni nani, na maisha yangu yana nini, au hata maisha ya familia ya baba yangu katika Israeli, kiasi cha kuwa mkwe wa mfalme?”19Lakini wakati ambao Merabu, binti Sauli, ilipasa kuwa ameolewa na Daudi, aliozwa kwa Adrieli Mmeholathi.

20Lakini Mikali, binti Sauli, alimpenda Daudi. Na watu walimwambia Sauli, na jambo hilo likampendeza.21Ndipo Sauli akafikiri, “Nitampatia huyu awe mke wake, ili uwe mtego kwake, na hivyo mkono wa Wafilisti uwe juu yake.” Kwa hiyo Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, “Wewe utakuwa mkwe wangu.”

22Sauli akawaamuru watumishi wake, “Ongeeni na Daudi kwa njia ya siri, na mseme, ‘Tazama, mfalme anakufurahia, na watumishi wake wote wanakupenda. Sasa basi, uwe mkwe wa mfalme.’”

23Hivyo watumishi wa Sauli wakayasema maneno haya kwa Daudi. Na Daudi akasema, “Kwenu ninyi mnaona ni jambo dogo kuwa mkwe wa mfalme, mimi ni maskini, na heshima yangu ni ndogo.”

24Watumishi wa Sauli wakarudisha kwake taarifa ya maneno ambayo Daudi aliyasema.25Na Sauli akasema, “Hivi ndivyo mtakavyo mwambia Daudi, ‘Mfalme haitaji mahari yoyote, isipokuwa govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi kwa adui wa mfalme.”’ Basi Sauli alifikiri atamwangusha Daudi kwa mkono wa Wafilisti.

26Watumishi wake walipomwambia maneno haya, yakamvutia Daudi awe mkwe wa mfalme.27Kabla siku hizo hazijapita, Daudi aliondoka na watu wake na kuwaua Wafilisti mia mbili. Daudi akazileta govi zao, na kumkabidhi mfalme kulingana na idadi yake, ili aweze kufanyika mkwe wa mfalme. Kwa hiyo Sauli akamwoza Mikali, binti yake, awe mkewe.

28Basi Sauli aliona na kufahamu kwamba BWANA alikuwa pamoja na Daudi. Mikali, binti Sauli, akampenda Daudi.29Sauli akazidi kumwogopa Daudi. Sauli akawa adui wa Daudi daima.

30Ndipo wakuu wa Wafilisti wakajitokeza kwa ajili ya vita, na mara zote walipojitokeza Daudi alifanikiwa zaidi kuliko watumishi wote wa Sauli, hivyo jina lake likapata heshima kubwa.

19

1Sauli akamwambia Yonathani mwanawe na watumishi wake wote kwamba wanapaswa kumuua Daudi. Lakini Yonathani, mwana wa Sauli, alitamani sana akae na Daudi.2Hivyo Yonathani akamwambia Daudi, “Baba yangu Sauli anatafuta kukuua. Kwa hiyo uwe macho wakati wa asubuhi na jifiche mahali pa siri.3Nami nitatoka nje na kusimama kando ya baba yangu huko shambani uliko wewe, na nitazungumza na baba yangu kuhusu wewe. Kama nikijua jambo lolote nitakuambia.”

4Yonathani alimsifia Daudi mbele ya Sauli baba yake akisema, “Mfalme asije akafanya dhambi dhidi ya mtumishi wake Daudi. Maana yeye hajakutenda dhambi, mambo aliyofanya yamekusaidia sana.5Maana alijitoa maisha yake na kumuua yule Mfilisti, naye BWANA akawaletea Waisraeli wote wokovu mkuu. Tena uliuona na kufurahi. Kwa nini utende dhambi juu ya damu isiyo na hatia kwa kumuua Daudi bila sababu?”

6Sauli alimsikiliza Yonathani. Sauli akaapa, “Kama BWANA aishivyo, yeye hatauawa.”

7Ndipo Yonathani akamwita Daudi na kumwambia mambo hayo yote. Na Yonathani akamleta Daudi kwa Sauli, naye Daudi akawa mbele zake kama zamani.

8Baadaye kukawa na vita tena. Daudi akatoka na kupigana na Wafilisti na kuwashinda kwa mauaji makubwa mno. Nao wakakimbia mbele yake.

9Yule roho wa ubaya kutoka kwa BWANA ikamjia Sauli alipokuwa ameketi nyumbani mwake na mkuki mkononi mwake, na Daudi akiwa anapiga chombo chake.10Sauli alijaribu kumpigilia Daudi ukutani kwa mkuki wake, lakini akaponyoka kutoka machoni pake, na kwamba Sauli akashindilia mkuki ndani ya ukuta. Daudi alikimbia na kutoroka usiku huo.

11Bado Sauli aliwatuma wajumbe nyumbani kwa Daudi wamvizie kusudi aweze kumuua asubuhi. Mkewe Daudi, Mikali, akamwambia, “Usipoyaokoa maisha yako usiku huu, kesho utauwawa.”12Hivyo Mikali akamteremsha Daudi kupita dirishani. Naye akaenda, akakimbia na kutoroka.13Mikali alichukua kinyago na kukilaza juu ya kitanda. Kisha akaweka mto wa singa za mbuzi kichwani pake, na akakifunika na nguo.

14Sauli alipowatuma wajumbe kumchukua Daudi, mkewe akasema, “Daudi ni mgonjwa.”

15Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumtazama; akisema, “Mleteni kwangu akiwa kitandani, ili nimuue.”16Wale wajumbe walipoingia ndani, tazama, kile kinyago kilikuwa kitandani pamoja na mto wa singa za mbuzi kichwani.

17Sauli akamuuliza Mikali, “Kwa nini umenidanganya na kumwachilia adui yangu aende, na tena ametoroka?” Mikali akamjibu Sauli, “Aliniambia, ‘Acha niende. Kwa nini nikuuwe?”’

18Basi Daudi akakimbia na kutoroka, na akaenda kwa Samweli huko Rama na kumweleza yote ambayo Sauli amemtendea. Ndipo yeye na Samweli wakaenda na kukaa Nayothi.19Naye Sauli akaambiwa kwamba, “Tazama, Daudi yuko huko Nayothi iliyoko Rama.”20Kisha Sauli akawatuma wajumbe kumkamata Daudi. Nao walipowaona kundi la manabii wakitabiri, na Samweli akisimama kama kiongozi wao, Roho wa Mungu akawaingia wale wajumbe wa Sauli, nao pia wakatabiri.21Sauli alipoambiwa hivyo, akawatuma wajumbe wengine, nao pia wakatabiri. Basi Sauli aliwatuma tena wajumbe kwa mara ya tatu, na hao pia wakatabiri.22Kisha naye akaenda Rama na kufika katika kisima kirefu kilichoko huko Seku. Akauliza, “Samweli na Daudi wako wapi?” Mtu mmoja akasema, “Angalia, Wako Nayothi huko Rama.”23Hivyo Sauli akaenda Nayothi huko Rama. Ndipo Roho wa Mungu pia akaja juu yake, naye alipokuwa akienda alitabiri, hadi alipofika Nayothi huko Rama.24Na yeye pia, alirarua mavazi yake, naye pia akatabiri mbele ya Samweli siku hiyo akilala uchi mchana kutwa na usiku kucha. Kwa sababu ya jambo hili, watu husema, “Je, Sauli pia ni miongoni mwa manabii?”

20

1Kisha Daudi akakimbia kutoka Nayothi huko Rama akaenda na kumwambia Yonathani, “Nimefanya nini? Uovu wangu ni upi? Dhambi yangu ni ipi kwa baba yako, inayofanya atafute kuutoa uhai wangu.”

2Yonathani akamwambia Daudi, “La hasha; hautakufa. Baba yangu hafanyi jambo kubwa wala dogo bila kunijulisha. Kwa nini inamlazimu baba yangu anifiche jambo hili? La, siyo hivyo?”

3Bado Daudi aliapa tena na akasema, “Baba yako anajua wazi kwamba nimepata kibali machoni pako. Pengine anasema, ‘Asije Yonathani akajua jambo hili, labda atahuzunika.’ Lakini kweli kama BWANA aishivyo, kama wewe uishivyo, kuna hatua moja tu kati yangu na mauti.”

4Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Lolote utakalosema, nitakufanyia.”

5Daudi akamwambia Yonathani, “Kesho ni siku ya mwezi mpya, na inanibidi kukaa na kula pamoja na mfalme. Lakini acha niende, ili niweze kujificha katika shamba hadi siku ya tatu jioni.6Baba yako akinikosa kabisa, ndipo utasema, ‘Daudi aliniomba kwa msisitizo ruhusa aondoke kwenda mjini kwake Bethlehemu; kwa sababu huko ni kipindi cha utoaji wa dhabihu ya mwaka kwa familia yao yote.’7Kama atasema kuwa ni vyema, ‘basi mtumishi wako atakuwa na amani. Lakini kama atakasirika sana, ndipo utajua kwamba ameamua kunitendea uovu.8Kwa hiyo, umtendee wema mtumishi wako. Kwa maana umemweka mtumishi katika agano la BWANA pamoja na wewe. Lakini kama kuna dhambi ndani yangu, wewe mwenyewe uniue; maana kwa nini basi unipeleke kwa baba yako?”

9Yonathani akasema, “La hasha! Ikiwa ninajua kwamba baba ameamua baya likupate, siwezi kukuambia?”

10Ndipo Daudi akamwambia Yonathani, “Ni nani ataniambia ikiwa imetokea, baba yako akakujibu kwa ukali?”11Yonathani akamwambia Daudi, “Njoo, hebu twende huko shambani.” Ndipo wote wakaondoka kwenda shambani.

12Yonathani akamwambia Daudi, “Na BWANA, Mungu wa Israeli, awe shahidi. Kesho muda kama huu, nitakuwa nimemuuliza baba yangu, au siku ya tatu, tazama, ikiwa kutakuwa na jambo zuri upande wa Daudi; je, nisikutumie taarifa na kulidhihirisha kwako?13Na kama ikimpendeza baba yangu akufanyie madhara, Basi BWANA ayafanye hayo kwa Yonathani na kuzidi ikiwa sitakujulisha jambo na kukupeleka mbali, ili kwamba uende kwa amani. Na BWANA awe pamoja nawe, kama alivyokuwa na baba yangu.14Kama bado nikiwa hai, hautanionyesha uaminifu wa agano la BWANA, kwamba siwezi kufa?15Na usivunje kabisa uaminifu wako wa agano kati yako na nyumba yangu, hata wakati BWANA atakapowaodoa kila mmoja wa adui za Daudi kutoka uso wa dunia.”

16Basi Yonathani akafanya agano na nyumba ya Daudi na kusema, “Naye BWANA atawaondoa maadui wa Daudi.”17Yonathani akamtaka Daudi aape tena kwa sababu ya upendo aliokuwa nao juu yake, kwa sababu alimpenda kama alivyopenda roho yake mwenyewe.

18Kisha Yonathani akamwambia Daudi, “Kesho ni siku ya mwezi mpya. Hautakuwapo, kwa sababu kiti chako kitakuwa wazi.19Utakapokuwa umekaa huko siku tatu, uende upesi hadi mahala ulipojificha mara ya kwanza, wakati shughuli ikifanyika, na ukae karibu na jiwe Ezeli.20Nitatupa mishale mitatu pembeni mwa jiwe, kama vile ninalenga kitu fulani.21Kisha nitamtuma kijana wangu na kumwambia, ‘Nenda utafute hiyo mishale.’ Kama nitamwambia kijana hivi, ‘Tazama, mishale iko upande huu wa kwako; kaichukue,” ndipo uje; maana hapo kutakuwa na usalama kwako na siyo madhara, kama BWANA aishivyo.22“Lakini kama nikimwambia kijana hivi, ‘Tazama, mishale iko mbele yako,’ ndipo utakapokwenda zako, maana BWANA ametaka uende zako.23Kulingana na makubaliano ambayo mimi na wewe tumeongea, angalia, BWANA yupo kati yangu na wewe milele.’”

24Kwa hiyo Daudi akajificha mle shambani. Pindi mwezi ulipoandama, mfalme aliketi chini ale chakula.25Mfalme alikaa juu ya kiti chake, kama kawaida kwenye kiti karibu na ukuta. Yonathani alisimama wima, na Abneri alikaa ubavuni mwa Sauli. Lakini nafasi ya Daudi ilikuwa wazi.26Hata hivyo Sauli hakusema kitu siku hiyo, kwa sababu alifikiri, “Kuna jambo limempata Daudi. Hayuko safi; hakika hayuko safi.”27Lakini siku ya pili, siku moja baada ya mwandamo wa mwezi, bado nafasi ya Daudi ilikuwa tupu. Ndipo Sauli akamuuliza Yonathani mwanaye, “Kwa nini mwana wa Yese hakuja kwenye chakula, jana na hata leo?”

28Yonathani akamjibu Sauli, “Daudi aliomba kwangu ruhusa kwa dhati ili aende Bethlehemu.29Alisema, ‘Tafadhali niruhusu niende. Maana familia yetu wanayo dhabihu huko mjini, na kaka yangu ameniagiza niwe huko. Basi kama nimepata kibali machoni pako, tafadhali niruhusu niende nikawaone kaka zangu.’ Hakuja kwenye meza ya mfalme kwa sababu hii.”

30Ndipo hasira ya Sauli iliwaka juu ya Yonathani, na akamwambia, “Wee mwana wa mwanamke mkaidi na muasi! Wadhani kwamba sijui kuwa umemchagua mwana wa Yese kwa ajili ya aibu yako, na kwa aibu ya uchi wa mama yako?31Kwa kuwa mwana wa Yese anaishi duniani, siyo wewe wala ufalme wako utakaoimarika. Sasa basi, tuma watu wamlete kwangu, kwa sababu inampasa kufa.”

32Yonathani akamjibu Sauli baba yake, “Kwa sababu gani inampasa kuuwawa? Amefanya nini?”33Ndipo Sauli akamtupia mkuki apate kumuua. Kwa hiyo Yonatani akatambua kwamba baba yake alinuia kumuua Daudi.

34Yonathani alitoka mezani akiwa na hasira kali bila kula chakula siku ya pili ya mwezi, kwa sababu alimhuzunikia Daudi, na kwa sababu baba yake amemwaibisha.

35Ikawa asubuhi, Yonathani akaenda huko shambani kama walivyoahidiana na Daudi, akiwa pamoja na kijana wake.36Akamwambia yule kijana wake, “Kimbia utafute ile mishale niliyoitupa.” Na kijana alikimbia, akatupa mshale mwingine mbele yake.37Kijana alipofika katika eneo ambapo mshale ulitua, ule alioutuma Yonathani, akamwita tena kijana, na kusema, “Huo mshale hauko mbele yako?”38Kisha Yonathani akamwita yule kijana, “Upesi, harakisha, usikawie!” Hivyo kijana wa Yonathani akaikusanya mishale na kurudi kwa bwana wake.39Lakini huyo kijana hakujua lolote. Ni Yonathani na Daudi tu ndio walijua habari yenyewe.40Yonathani akampa kijana wake silaha na kumwambia, “Nenda, uzipeleke mjini.”

41Punde tu kijana alipoondoka, Daudi akasimama kutokea upande wa kusini, akiwa amelala kifudifudi, akainama mara tatu. Walibusiana wao kwa wao na wote wakalia kwa pamoja, Daudi akilia zaidi.

42Yonathani akamwambia Daudi, “Nenda kwa amani, kwa sababu wote tumeapa kwa jina la BWANA na tulisema, ‘BWANA awe kati yangu na wewe, na awe kati ya uzao wangu na uzao wako, milele.’” Kisha Daudi alisimama na akaondoka, na Yonathani akarudi mjini.

21

1Kisha Daudi akafika Nobu kumuona Ahimeleki kuhani. Ahimeleki akaja akutane na Daudi huku akitetemeka na kumwambia, “Kwa nini uko peke yako huna mtu wa kuambatana na wewe?”

2Daudi akamjibu Ahimeleki kuhani, “Mfalme amenituma kwa jambo maalum na ameniambia hivi, ‘Asiwepo hata mtu mmoja anayejua chochote kuhusu shughuli niliyokutuma, na kile nilichokuagiza.’ Nimewaelekeza vijana kwenda sehemu fulani.3Sasa basi chakula gani kinapatikana hapa? Nipatie mikate mitano, au chochote kilichopo hapa.”

4Huyo Kuhani alimjibu Daudi na kusema, “Hakuna mkate wa kawaida mkononi, lakini ipo mikate takatifu- kama vijana hawajatembea na wanawake.”

5Daudi akamjibu kuhani, “Hakika hatujatembea na wanawake kwa siku hizi tatu. Nilipoanza safari, miili ya vijana iliwekwa wakfu kwa BWANA, ingawa ilikuwa safari ya kawaida. Je, si zaidi sana leo miili yao ikawekwa wakfu kwa BWANA.”6Hivyo kuhani akampa mikate iliyokuwa imewekwa wakfu kwa BWANA. Maana haikuwepo mikate mingine hapo, isipokuwa tu ile ya wonyesho, ambayo iliondolewa kutoka kwa BWANA, ili sehemu yake iwekwe mikate ya moto, inapokuwa imeondolewa.

7Basi siku hiyo mmoja wa watumishi wa Sauli alikuwapo mahali hapo, ameshilkiliwa mbele za BWANA. Jina la mtu huyo aliitwa Doegi Mwedomu, mkuu wa wachungaji wa Sauli.

8Daudi akamwambia Ahimeleki, “Je, hakuna hata mkuki wowote au upanga? Maana mimi sikubeba upanga wangu wala silaha zangu, maana ile shughuli ya mfalme ilikuwa ya muhimu.”

9Kuhani akasema, “Ule upanga wa Mfilisti Goliathi, uliyemuua katika bonde la Ela, uko hapa umefunikwa katika nguo nyuma ya naivera. Kama unataka kuuchukua huo, uchukue, maana hakuna silaha nyingine hapa.” Daudi akasema, “Hakuna silaha nyingine kama hiyo, nipatie hiyo.”10Daudi aliamka na kukimbia mbali na Sauli na akaenda kwa Akishi, mfalme wa Gathi.11Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, “Huyu siye Daudi mfalme wa nchi hii? Je, wanawake hawakupokezana wakiimba na kucheza, ‘Sauli ameua maelfu yake, na Daudi makumi elfu yake?”’

12Daudi akayaweka maneno hayo moyoni mwake na akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi.13Daudi akabadili mwenendo wake mbele yao na akajifanya kuwa mwendawazimu machoni pao; akachora-chora alama kwenye vizingiti vya milango huku akitiririsha mate yake chini ya ndevu zake.

14Ndipo Akishi akawaambia watumishi wake, “Tazameni, mnaona mtu huyu ana wazimu.15Kwa nini mmemleta kwangu? Je, mimi nina haja ya watu wazimu, kumbe mmemleta mtu huyu ili anifanyie hayo mbele yangu? Hivi kweli huyu ataingia nyumbani mwangu?

22

1Basi Daudi aliondoka hapo na akatoroka kwenda kwenye pango la Adulamu. Kaka zake na wote wa nyumba ya baba yake waliposikia hayo, wakateremka kumwendea huko.2Kila mmoja aliyekuwa na mahangaiko, kila mmoja aliyekuwa na deni, na kila mmoja ambaye hakuwa na furaha moyoni-wote walijikusanya kwake, na Daudi akawa jemedari wao. Kulikuwa na wanaume wapatao 400 waliokuwa pamoja naye.

3Kisha Daudi alitoka huko akaenda Mispa huko Moabu. Akamwambia mfalme wa Moabu, “Tafadhali waruhusu baba na mama yangu wakae kwako hadi hapo nitakapojua kitu gani ambacho Mungu atafanya kwa ajili yangu.”4Basi akawaacha kwa Mfalme wa Moabu. Baba na mama yake wakakaa na mfalme kwa muda wote ambao Daudi alikuwa kwenye ngome yake.

5Kisha nabii Gadi akamwambia Daudi, “Usikae tena katika ngome yako. Ondoka na uende katika nchi ya Yuda.” Kwa hiyo Daudi akatoka hapo na akaenda katika msitu wa Harethi.

6Sauli akasikia kwamba Daudi amepatikana, akiwa pamoja na watu aliokuwa nao. Wakati huo Sauli alikuwa akikaa Gibea chini ya mti wa mkwaju huko Rama, akiwa na mkuki wake mkononi mwake, na watumishi wake wote walikuwa wamesimama wamemzunguka.7Sauli akawaambia watumishi wake, “Sasa sikilizeni, watu wa Benyamini! Je, mwana wa Yese atawapa mashamba na mashamba ya mizabibu? Je, atawafanya nyote kuwa majemedari wa maelfu na majemedari wa mamia,8hata ninyi nyote mnapanga njama dhidi yangu? Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anafanya agano na mwana wa Yese. Hakuna hata mmoja wenu anayenionea huruma. Hakuna hata mmoja wenu anayenijulisha kwamba mwanangu anamchochea mtumishi wangu Daudi awe kinyume changu. Leo amejificha na ananisubiri ili anishambulie.”

9Kisha Doegi Mwedomu, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akajibu, “Nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki mwana wa Ahitubu.10Alimwomba BWANA ili apate kumsaidia, na alimpatia mahitaji na upanga wa Goliathi, Mfilisti.”

11Kisha Mfalme akamtuma mtu amwite kuhani Ahimeleki mwana wa Ahitubu na watu wote wa nyumba ya baba yake, makuhani waliokuwa huko Nobu. Wote walifika mbele ya mfalme.12Sauli akasema, “Sasa sikiliza, mwana wa Ahitubu,” Naye akajibu, “Niko hapa, bwana wangu.”13Sauli akamwambia, “Kwa nini unapanga njama dhidi yangu, wewe pamoja na mwana wa Yese, kwa kumpatia mikate, na upanga, na umemwomba Mungu kusudi amsaidie Daudi, kusudi aniasi mimi, na kujificha sehemu ya siri, kama alivyofanya leo?”

14Ndipo Ahimeleki akamjibu mfalme na kusema, “Je, ni nani miongoni mwa watumishi wako wote aliyemwaminifu kama Daudi, ni nani mkwe wa mfalme na yuko juu ya walinzi wako, na mwenye heshima nyumbani mwako?15Je, leo ni mara ya kwanza kwangu kumuomba Mungu apate kumsaidia? Hapana! Mfalme usinilaumu mimi mtumishi wako kwa jambo lolote wala jamaa zangu wote. Maana mimi mtumishi wako sijui lolote kuhusu jambo hili zima.”

16Mfalme akamjibu, “Hakika utakufa, Ahimeleki, wewe na jamaa yote ya nyumba ya baba yako.”

17Mfalme akamwambia mlinzi aliyesimama karibu naye, “Geuka na uwauwe makuhani wa BWANA. Kwa sababu wanamuunga mkono Daudi, na sababu walijua kwamba alikimbia, lakini hawakunijulisha.” Lakini watumishi wa mfalme hawakunyoosha mkono wao kuwaua makuhani wa BWANA.

18Ndipo mfalme akamwambia Doegi, “Geuka na uwauwe makuhani.” Hivyo Doegi Mwedomu akageuka na kuwapiga makuhani; akawaua watu themanini na watano waliovaa naivera ya kitani siku hiyo.19Kwa ncha ya upanga, aliupiga Nobu, mji wa makuhani, akiwaua wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao, ng'ombe na punda na kondoo. Wote aliwaua kwa ncha ya upanga.

20Lakini mmoja wa wana wa Ahimeleki mwana wa Ahitubu, aliyeitwa Abiathari, aliponyoka na kukimbilia kwa Daudi.21Abiathari akamwambia Daudi kwamba Sauli amewaua manabii wa BWANA.22Daudi akamwambia Abiathari, “Nilifahamu kuwa siku hiyo, Doegi Mwedomu alikuwa mahali pale, kwamba hakika angemwambia Sauli. Nina wajibika kwa kifo cha kila mtu katika familia ya baba yako!23Kaa pamoja nami na usiogope. Maana mtu anayetafuta roho yako anatafuta pia roho yangu. Utakuwa salama ukiwa pamoja nami.”

23

1Wakamwambia Daudi, “Tazama, Wafilisti wanapigana vita juu ya Keila na wanapora nafaka inayopurwa sakafuni.”2Hivyo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, na akamuuliza, “Je, niondoke niwapige hawa Wafilisti?” BWANA akamwambia Daudi, “Nenda ukawapige Wafilisti na kuokoa Keila.”3Daudi akaambiwa na watu wake, “Angalia, hapa Yuda tunaogopa. Je, si zaidi sana kama tutaenda Keila kupambana na majeshi ya Wafilisti?”

4Ndipo Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya msaada, bado tena, BWANA akamjibu, “Amka, uteremke hadi Keila. Maana nitakupatia ushindi dhidi ya Wafilisti.”5Daudi na watu wake wakaenda Keila na kupigana na Wafilisti. Wakahamisha ng'ombe wao na kuwapiga kwa mauaji makubwa mno. Hivyo Daudi akawaokoa wenyeji wa Keila.

6Abiathari mwana wa Ahimeleki alipokuwa amekimbilia kwa Daudi huko Keila, alibeba naivera mkononi mwake.

7Sauli aliambiwa kwamba Daudi amekwenda Keila. Sauli akasema, “Mungu amemweka mkononi mwangu. Bila shaka amefungiwa ndani kwa sababu ameingia katika mji ulio na malango na makomeo.”

8Sauli akayaita majeshi yake yote kwa ajili ya vita, waende hadi Keila, wamteke Daudi na watu wake.

9Daudi alijua kwamba Sauli alikuwa anapanga njama za kumdhuru yeye. Ndipo akamwambia kuhani Abiathari kuhani, “Ulete hapa naivera.”10Kisha Daudi akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, mtumishi wako hakika amesikia kwamba Sauli anatafuta namna ya kuja Keila, ili auteketeze mji kwa ajili yangu.11Je, watu wa Keila watanisalimisha mkononi mwake? Je, Sauli atashuka hadi huko, kama mtumishi wako alivyosikia? BWANA, Mungu wa Israeli, nakusihi, tafadhali mwambie mtumishi wako.” BWANA akasema, “Atakuja huko.”12Kisha Daudi akauliza, “Je, watu wa Keila watanisalimisha mimi na watu wangu katika mkono wa Sauli?” BWANA akasema, “Watakusalimisha.”13Kisha Daudi na watu wake, waliokuwa kama 600, walitoka na kwenda mbali na Keila, na wakazunguka kila sehemu. Kisha Sauli akaambiwa kwamba Daudi ametoroka kutoka Keila, hivyo akasitisha kumfuatia.

14Daudi alikaa ngomeni katika jangwa, kwenye nchi ya milima katika jangwa la Zifu. Kila siku Sauli alimtafuta, lakini Mungu hakumweka mkononi mwake.

15Daudi aliona kwamba Sauli amejitokeza kuangamiza maisha yake; basi Daudi alikuwa katika jangwa la Zifu huko Horeshi.16Kisha Yonathani, mwana wa Sauli, akaamka akaenda kwa Daudi huko Horeshi, naye akamtia moyo amtumainie Mungu.17Akamwambia, “Usiogope. Kwa maana mkono wa baba yangu Sauli hautakupata. Utakuwa mfalme juu ya Israeli, na mimi nitakuwa msaidizi wako. Baba yangu Sauli pia anajua hivyo.”18Basi wote wawili wakafanya agano mbele za BWANA. Kisha Daudi alibaki Horeshi, na Yonathani akaenda nyumbani.

19Ndipo Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea wakisema, “Je, Daudi hakujificha kati yetu kwenye ngome huko Horeshi, juu ya mlima wa Hakila, ulioko kusini mwa Yeshimoni?20Basi uje, mfalme! Kulingana na matakwa yako, uje! Kazi yetu itakuwa kumtia katika mkono wa mfalme.”

21Sauli akasema, “Mbarikiwe na BWANA. Kwa sababu mmenihurumia.22Nendeni, mhakikishe sawasawa. Tafuteni na kujua maficho yake yako wapi na ni nani amemwona huko. Nimeambiwa kwamba yeye ni mjanja sana.23Kwa hiyo chunguzeni, mjue sehemu zote anakojificha. Baadaye rudini kwangu mkiwa na taarifa kamili, na kisha nitaongozana nanyi. Ikiwa yupo katika nchi, nitamtafuta kutoka miongoni mwa elfu zote za Yuda.”

24Ndipo wakaamka na kwenda hadi Zifu mbele ya Sauli. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa katika jangwa la Maoni, huko Araba upande wa kusini mwa Yeshimoni.25Sauli na watu wake wakaenda kumtafuta Daudi. Na Daudi akaambiwa habari hiyo, hivyo akateremka hadi kwenye mlima wa miamba na akakaa katika jangwa la Maoni. Sauli aliposikia hivyo, akamfukuza Daudi katika Jangwa la Maoni.

26Sauli akaenda akawa upande mmoja wa mlima, na Daudi na watu wake walikuwa wakienda upande mwingine wa mlima. Daudi kwa haraka akatoweka akae mbali na Sauli. Kwa sababu Sauli na watu wake walikuwa wakimzunguka Daudi na watu wake wawakamate,27mjumbe mmoja akaja kwa Sauli na kusema, “Njoo, harakisha maana Wafilisti wamepanga uvamizi juu ya nchi.”28Kwa hiyo Sauli akarudi asimfuatie Daudi na akaenda kupambana na Wafilisti. Kwa hiyo sehemu ile iliitwa Mwamba wa Maficho.29Daudi akapanda kutoka huko na kukaa katika ngome ya Engedi.

24

1Sauli aliporudi kuwafukuza Wafilisti, akaambiwa kwamba, “Daudi yuko katika jangwa la Engedi.”2Ndipo Sauli akachukua watu 3,000 waliochaguliwa kutoka Israeli yote, wakaenda kumtafuta Daudi na watu wake katika miamba ya Mbuzi Mwitu.

3Akafika penye mazizi ya kondoo kando ya njia, mahali palipokuwa na pango. Sauli akaingia ndani yake ili kuifunika miguu. Wakati huo Daudi na watu wake walikuwa wamekaa mbali zaidi ndani ya pango lilelile.4Watu wake Daudi wakamwambia, “Hii ndiyo siku ambayo BWANA aliisema akikuambia, ‘Nitamweka adui wako mkononi mwako, ili umtendee kama unavyotaka.”’ Kisha Daudi akainuka na kumnyemelea kwa mbele kimya kimya na kulikata pindo la kanzu ya Sauli.5Baadaye moyo wa Daudi ukamchoma kwa sababu alilikata pindo la kanzu ya Sauli.6Akawaambia watu wake, “BWANA apishe mbali, nisimtendee jambo hili bwana wangu, Mtiwa mafuta wa BWANA, kwa kunyoosha mkono wangu juu yake, maana yeye ni masihi wa BWANA.”7Hivyo Daudi akawakemea watu wake kwa maneno haya, na kuwazuia wasimpige Sauli. Sauli akasimama, akatoka pangoni, na kwenda zake.

8Baadaye tena, Daudi akasimama juu, akatoka pangoni, na kumwita Sauli: “Bwana wangu mfalme.” Sauli alipotazama nyuma, Daudi akasujudu hadi chini na kuonyesha heshima.9Daudi akamwambia Sauli, “Kwa nini unawasikiliza watu ambao wanasema, ‘Angalia, Daudi anatafuta kukudhuru?’10Leo macho yako yameona jinsi BWANA alivyokuweka mkononi mwangu tulipokuwa ndani ya pango. Wengine waliniambia nikuuwe, lakini nilikuacha hai. Nikasema, ‘Sitanyoosha mkono wangu juu ya bwana wangu; kwa kuwa ni masihi wa BWANA.’11Tazama, baba yangu, angalia pindo la kanzu yako mkononi mwangu. Kwa maana kama nilikata pindo la kanzu yako na sikukuua, basi ujue na uone kwamba sina uovu au kosa katika mkono wangu, na sijafanya dhambi juu yako, ingawa unawinda kuutoa uhai wangu.12BWANA aamue kati yangu na wewe, na BWANA anilipizie kisasi juu yako, lakini mkono wangu kamwe hautakuwa juu yako.13Kama mithali ya wazee isemavyo, ‘Katika waovu hutoka uovu.’ Lakini mkono wangu hautakuwa juu yako.

14Mfalme wa Israeli ametoka kumuandama nani? Unamsaka nani? Unasaka mzoga wa mbwa! Unasaka kiroboto!15BWANA na awe mwamuzi na atoe hukumu kati yangu na wewe, na akaione, na akatetee sababu yangu na aniruhusu kuepuka mkono wako.”

16Daudi alipomaliza kuongea maneno haya kwa Sauli, Sauli akasema, “Hii ni sauti yako, mwanangu Daudi?” Sauli alipaza sauti yake akalia.17Akamwambia Daudi, “Wewe ni mwenye haki kuliko mimi. Kwa sababu umenilipa mazuri, wakati mimi nimekulipa maovu.18Leo umetangaza jinsi ulivyonitendea mazuri, kwa sababu hukuniua wakati BWANA aliponiweka katika rehema yako.19Kwa kuwa mtu akimpata adui yake, atamwacha aende zake salama? Na BWANA akuzawadie mema kwa kile ulichonifanyia leo.20Basi, najua kwa hakika kwamba utakuwa mfalme na kwamba ufalme wa Israeli utaimarika katika mkono wako.21Niapie kwa BWANA kwamba baada yangu hautawakatilia mbali uzao wangu, na kwamba hautaliharibu jina langu katika nyumba ya baba yangu.”

22Hivyo Daudi akamwapia Sauli kiapo. Kisha Sauli akaenda nyumbani, lakini Daudi na watu wake wakapanda kwenda ngomeni.

25

1Basi Samweli akafariki. Waisraeli wote wakakusanyika pamoja na kumwomboleza, na wakamzika nyumbani kwake huko Rama. Kisha Daudi akainuka na akashuka hadi jangwa la Parani.2Kulikuwa na mtu mmoja huko Maoni, na mali zake zilikuwa huko Karmali. Mtu huyo alikuwa tajiri sana. Alikuwa na kondoo elfu tatu na mbuzi elfu moja. Naye alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake huko Karmeli.3Na mtu huyo aliitwa Nabali, na jina la mke wake aliitwa Abigaili. Mwanamke huyo alikuwa mwenye busara na mzuri kwa sura. Lakini mwanaume alikuwa mkaidi na mwovu katika mambo yake. Alikuwa wa uzao wa nyumba ya Kalebu.

4Daudi akasikia akiwa jangwani kwamba Nabali alikuwa akiwakata manyoya kondoo wake.5Hivyo Daudi aliwatuma kwake vijana kumi. Akawaambia wale vijana, “Pandeni kwenda Karmeli, mwendeeni Nabali, na mkamsalimie kwa jina langu.6Mtamwambia, ‘Uishi katika baraka, uwe na amani na nyumba yako iwe na amani, na wote ulionao wawe na amani.

7Nasikia kwamba unao wakata manyoya. Wachungaji wako walikuwa pamoja nasi, na hatukuwafanyia ubaya, na muda wote wakiwa Karmeli hawakupotelewa kitu chochote.8Waulize vijana wako, nao watakuambia. Basi vijana wangu wapate kibali machoni pako, maana tumefika siku ya sherehe. Tafadhali utoe chochote ulicho nacho mkononi kwa watumishi wako na kwa Daudi mwanao.’”

9Vijana wa Daudi walipofika, walimwambia Nabali yote haya kwa niaba ya Daudi na kisha wakasubiri.10Nabali akawajibu watumishi wa Daudi, “Daudi ni nani? Na ni nani mwana wa Yese? Siku hizi wapo watumishi wengi wanaotoroka bwana zao.11Je, nichukue mkate wangu na maji yangu na nyama yangu ambayo nimewachinjia wakata manyoya wangu, na niwape watu wanaotoka nisikokujua?”

12Hivyo vijana wa Daudi waligeuka na kurudi, nakumwambia kila kitu kilichosemwa.13Daudi akawaambia watu wake, “Kila mtu ajifunge upanga wake.” Kila mtu akajifunga upanga wake. Daudi naye pia akajifunga upanga wake. Yapata kama watu mia nne wakafuatana na Daudi, na wengine mia mbili walibaki kulinda mizigo yao.

14Lakini kijana mmojawapo alimwambia Abigaili, mke wa Nabali akasema, “Daudi aliwatuma wajumbe kutoka jangwani waje wamsalimu bwana wetu, na yeye akawatukana.15Bado watu hawa walitutendea mema. Hatukudhurika na hatukupoteza chochote wakati wote tulipotembea nao tulipokuwa mbugani.16Walikuwa ukuta wetu usiku na mchana, wakati wote tulikuwa pamoja nao tukichunga kondoo.17Kwa hiyo tambua hili na zingatia utafanya nini, maana ubaya unamvizia bwana wetu, na utakuwa juu ya nyumba yake yote. Yeye ni mtu asiyefaa na hakuna awezaye kushauriana naye.”

18Ndipo Abigaili akaharakisha na akachukua mikate mia mbili, chupa mbili za divai, kondoo watano waliokwisha andaliwa, vipimo vitano vya bisi, vishada mia moja vya zabibu, na mikate mia mbili ya tini na akavipakia juu ya punda.19Akawaambia vijana wake, “Tangulieni mbele yangu, nami nitakuja nyuma yenu.” Lakini hakumwambia mmewe Nabali.

20Alipokuwa akienda juu ya punda wake na kuteremka penye kificho cha mlima, Daudi na watu wake walishuka chini wakimwelekea Abigaili, naye akakutana nao.21Basi Daudi alikuwa amesema, “Hakika nimelinda bure vyote alivyonavyo mtu huyu huko nyikani, na vyote alivyonavyo hakuna kilichopotea, pamoja na hayo amenilipa mabaya badala ya mema.22Mungu naye awatendee hivyo adui za Daudi, pia iwe zaidi, iwapo nitamwacha hata mtu mmoja wa kwake akiwa hai ifikapo kesho asubuhi.

23Abigaili alipomwona Daudi, aliharakisha na kushuka chini ya punda wake, akalala kifudifudi na kujiinamisha hadi chini.24Akamwangukia miguuni pake na kusema, “Juu yangu tu, bwana wangu, na uwe uovu. Tafadhali acha mjakazi wako aseme nawe, tena uyasikilize maneno ya mjakazi wako.25Nakusihi bwana wangu usimjali mtu huyu asiyefaa, Nabali, kwa maana kama jina lake lilivyo, ndivyo alivyo. Jina lake ni Nabali, na upumbavu uko pamoja naye. Lakini mimi mjakazi wako sikuwaona vijana wa bwana wangu, uliowatuma.26Sasa basi, bwana wangu, kama BWANA aishivyo, na kama unavyoishi, kwa kuwa BWANA amekuondoa kutoka kumwaga damu, na kuacha kulipiza kisasi kwa mkono mwenyewe, basi adui zako, na wale ambao wanatafuta kumfanyia uovu bwana wangu, wawe kama Nabali27Na sasa zawadi hii ambayo mjakazi wako ameileta kwa bwana wangu, na wapewe vijana ambao wanamfuata bwana wangu.28Tafadhali ulisamehe kosa la mjakazi wako, maana BWANA hakika atamfanyia bwana wangu nyumba imara, kwa sababu bwana wangu anapigana vita vya BWANA; na uovu hautaonekana ndani yako maadamu unaishi.29Na ingawa watu wangeinuka na kukuandama ili wakuue, bado uhai wa bwana wangu utafungwa katika furushi la walio hai na BWANA Mungu wako; na atayatupa maisha ya adui zako mbali, kama vile kutoka katika mfuko wa kombeo.30Na itakuwa, BWANA atakapokuwa amemtimizia bwana wangu mambo yote mazuri ambayo amekuahidi, na alivyokufanya kiongozi juu ya Israeli,31jambo hili halitakuwa huzuni kwako, wala chukizo moyoni kwa bwana wangu, kwa sababu hukumwaga damu bila sababu, na hujajilipizia kisasi. Na BWANA akikuletea mafanikio, umkumbuke mjakazi wako.”

32Ndipo Daudi akamwambia Abigaili, “BWANA, Mungu wa Israeli, abarikiwe, aliyekutuma uonane na mimi leo.33Na hekima yako ibarikiwe, nawe umebarikiwa, kwa sababu leo umenizuia nisiwe na hatia ya kumwaga damu, na kutojilipizia kisasi kwa mkono wangu mwenyewe.34Kwa kweli, kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye amenizuia nisikuumize, kama usinge harakisha kuja ukutane nami, kwa hakika kesho asubuhi asinge salia hata mtoto mmoja wa kiume kwa Nabali.”

35Kwa hiyo Daudi akavipokea kutoka mkononi mwake vile alivyokuwa amemletea; akamwambia, “Nenda kwa amani hadi nyumbani kwako; tazama, nimeisikiliza sauti yako na nimekubali.”

36Abigaili akarudi kwa Nabali; tazama, alikuwa akifanya sherehe katika mji wake, kama sherehe ya mfalme; na moyo wa Nabali ulifurahi ndani yake, kwa sababu alikuwa amelewa sana. Kwa hiyo hakumwambia chochote kabisa hadi kulipopambazuka37Ikawa asubuhi, divai ilipokuwa imemtoka Nabali, basi mkewe akamwambia mambo hayo; moyo wake ukafa ndani yake, na akawa kama jiwe.38Ikawa baada ya siku kumi BWANA alimpiga Nabali naye akafa.

39Naye Daudi aliposikia kwamba Nabali amekufa, akasema, “BWANA abarikiwe, aliyenichukulia hatua ya shutuma yangu kutoka mkono wa Nabali, na kumzuia mtumishi wake asifanye maovu. Na amemrudishia Nabali tendo la uovu juu ya kichwa chake mwenyewe.” Ndipo Daudi akawatuma watu wakaongee na Abigaili, ili amchukue awe mke wake.40Watumishi wake Daudi walipofika kwa Abigaili huko Karmeli, wakaongea naye na kusema, “Daudi ametutuma kwako tukuchukue hadi kwake uwe mke wake.”41Abigaili aliinuka, akainamisha uso chini, na akasema, “Tazama, mjakazi wako ni mtumwa aoshaye miguu ya watumishi wa bwana wangu.”42Akaharakisha na kuamka, akapanda punda akiwa na vijakazi wake watano waliofuatana naye; akawafuata wajumbe wa Daudi, na akawa mke wake.43Daudi pia alimchukua Ahinoamu wa Yezreeli akamwoa; wote wawili wakawa wake zake.44Wakati huo Sauli alikuwa amempa Palti, mwana wa Laishi mtu wa Galimu, Mikali, binti yake, aliyekuwa mke wa Daudi.

26

1Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea na kusema, “Je, Daudi hakujificha katika vilima vya Hakila, ambavyo viko mbele ya jangwa?”

2Kisha Sauli akaamka na kwenda chini ya jangwa la Zifu, akiwa na watu 3,000 waliochaguliwa katika Israeli, wamtafute Daudi katika jangwa la Zifu.3Sauli akaweka kambi kwenye kilima cha Hakila, kilicho mbele ya jangwa, kando ya barabara. Lakini Daudi alikuwa akikaa nyikani, na akaona kwamba Sauli alikuwa anamfuatia huko jangwani.4Hivyo Daudi akawatuma wapelelezi na akafahamu kwamba hakika Sauli alikuwa amekuja.

5Daudi akaamka na kwenda hadi mahali ambapo Sauli alipiga kambi; akaona mahali alipolala Sauli, na Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi lake; Sauli alilala katikati ya kambi, na watu walipiga kambi kumzunguka, na wote wamesinzia.

6Ndipo Daudi akamwambia Ahimeleki Mhiti, na Abishai mwana wa Seruya, ndugu yake Yoabu, “Ni nani atakwenda nami kambini kwa Sauli? Abishai akasema, “Mimi nitashuka pamoja nawe.”7Hivyo Daudi na Abishai wakaliendea jeshi usiku. Na Sauli alikuwapo akisinzia ndani ya kambi, mkuki wake umechomekwa chini pembeni mwa kichwa chake. Abneri na Askari wake wamelala kwa kumzunguka.

8Kisha Abishai akamwambia Daudi, “Leo Mungu amemweka adui yako mkononi mwako. Basi tafadhali acha nimchome mkuki nimtoboe hadi chini kwa pigo moja. Sitampiga mara mbili.”

9Daudi akamwambia Abishai, “Usimwangamize; kwa maana nani awezaye kunyoosha mkono wake dhidi ya mtiwa mafuta wa BWANA na asiwe na hatia?”10Daudi akasema, “Kama BWANA aishivyo, BWANA atamuua, au siku ya kufa kwake itakuja, au atakwenda katika vita na ataangamia.11BWANA apishe mbali nisinyooshe mkono wangu dhidi ya mtiwa mafuta wake; lakini sasa, nakusihi chukua mkuki uliokichwani pake na jagi la maji, tuondoke.”

12Hivyo Daudi akachukua mkuki na jagi la maji kutoka kichwani pa Sauli, wakatoweka. Hakuna mtu aliyewaona au kufahamu habari hii, wala hakuna aliyetoka usingizini, maana wote walisinzia, kwa sababu usingizi mzito kutoka kwa BWANA uliwaangukia.

13Kisha Daudi akaenda upande mwingine na akasimama juu ya mlima mbali sana; ukiwepo umbali mkubwa katikati yao.

14Daudi akawapigia kelele watu hao na Abneri mwana wa Neri; akisema, “Hujibu neno, Abneri?” Ndipo Abneri akajibu na kusema, “Wewe ni nani unayempigia mfalme kelele?”15Daudi akamwambia Abneri, “Wewe siye mtu jasiri? Ni nani yuko kama wewe katika Israeli? Kwa nini basi hukukaa macho kumlinda bwana wako mfalme? Kwa maana mtu fulani aliingia kumuua mfalme, bwana wako.16Jambo hili ulilolifanya siyo zuri. Kama BWANA aishivyo, unapaswa kufa kwa sababu hukumlinda bwana wako, mtiwa mafuta wa BWANA. Na sasa tazama ulipo mkuki wa mfalme, na jagi la maji lililokuwa kichwani pake.”

17Sauli aliitambua sauti ya Daudi akasema, “Hiyo ni sauti yako, Daudi mwanangu?” Daudi akasema, “Ni sauti yangu, mfalme, bwana wangu.”

18Daudi akasema, “Kwa nini bwana wangu anamwandama mtumishi wake? Nimefanya nini? Mkononi mwangu kuna uovu gani?19Kwa hiyo sasa, nakusihi, bwana wangu mfalme asikilize maneno ya mtumishi wake. Kama ni BWANA ndiye amekuchochea dhidi yangu, na aikubali sadaka; lakini kama ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA, maana leo wamenifukuza, nisishikamane na urithi wa BWANA; wameniambia, ‘Nenda ukaabudu miungu mingine.’20Kwa hiyo, sasa, usiiachilie damu yangu ianguke ardhini mbali na uwepo wa BWANA; kwa kuwa mfalme wa Israeli ametoka nje kutafuta kiroboto, kama vile mtu awindavyo kware milimani.”

21Kisha Sauli akasema, “Nimefanya dhambi. Rudi, Mwanangu, Daudi; maana sitakudhuru tena, kwa sababu leo maisha yangu yalikuwa yenye thamani machoni pako. Tazama, nimetenda upumbavu na nimekosa sana.”

22Daudi akajibu na akasema, “Tazama, mkuki wako uko hapa, mfalme! Mruhusu kijana mmojawapo aje auchukue na aulete kwako.23Na BWANA amlipe kila mtu kwa ajili ya uadilifu wake na kwa uaminifu wake; kwa sababu leo BWANA alikuweka mkononi mwangu, lakini nisinge mpiga mtiwa mafuta wake.24Na tazama, kama maisha yako leo yalivyokuwa ya thamani machoni pangu, vivyo hivyo maisha yangu yathaminiwe sana machoni pa BWANA, na aweze kuniokoa katika shida zote.”

25Ndipo Sauli akamwambia Daudi, “Na ubarikiwe, mwanangu Daudi, ili uweze kutenda mambo makuu, na hakika uweze kufanikiwa.” Ndipo Daudi akaenda zake, na Sauli akarudi kwake.

27

1Daudi alisema moyoni mwake, “Basi, siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jambo zuri kwangu kuliko kutoroka hadi nchi ya Wafilisti; Sauli atakata tamaa asinitafute tena ndani ya mipaka yote ya Israeli; kwa njia hii nitaponyoka kutoka mkono wake.”

2Daudi akaondoka na kuvuka, akiwa pamoja na watu mia sita hadi kwa Akishi mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.3Daudi akaishi na Akishi huko Gathi pamoja na watu wake, na kila mtu na familia yake, na Daudi akiwa na wake zake wawili, Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili Mkarmeli aliyekuwa mke wa Nabali.4Sauli akaambiwa kuwa Daudi amekimbilia Gathi, hivyo hakumtafuta tena.

5Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, wanipatie mahali katika mojawapo ya miji ya nchi, ili nikae huko: kwa nini mtumishi wako akae pamoja na wewe katika mji wa kifalme?”

6Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi Ziklagi; ndiyo sababu mji wa Ziklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hadi leo.

7Idadi ya siku ambazo Daudi aliishi katika nchi ya Wafilisti ulikuwa mwaka mmoja na miezi minne.8Daudi na watu wake walizipiga sehemu mbalimbali, wakiteka nyara Wageshuri, Wagirizi, na Waamaleki; kwa maana mataifa hayo ndio walikuwa wakaaji wa nchi, kwa uelekeo wa kwenda Shuri hadi kufika nchi ya Misri. Walikuwa wamekaa katika nchi hiyo toka nyakati za zamani.9Daudi aliipiga nchi na hakumwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai; akatwaa kondoo, ng'ombe, punda, ngamia, na nguo; kisha alirudi na kufika tena kwa Akishi.

10Akishi alipomuuliza, “Je, leo umefanya mashambulizi dhidi ya nani?” Daudi angesema, “Nimefanya dhidi ya kusini mwa Yuda,” au “dhidi ya kusini mwa Wayerameeli,” au “dhidi ya kusini mwa Wakeni.”11Daudi asingemwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai awalete hadi Gathi, akisema, “ili wasije kututeta, ‘Daudi amefanya hivi na vile.”’ Hivi ndivyo alivyofanya kwa kipindi chote alichokaa katika nchi ya Wafilisti.12Akishi alimwamini Daudi, akisema, “Amesababisha watu wake Israeli wamchukie kabisa; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu milele.”

28

1Ikawa katika siku hizo Wafilisti walikusanya majeshi yao pamoja kwa ajili ya vita, wapigane na Israeli. Akishi akamwambia Daudi, “Ujue kwa hakika kwamba utakwenda nami ndani ya jeshi, wewe na watu wako.”

2Naye Daudi akamwambia Akishi, “Sasa utajua kile ambacho mtumishi wako anaweza kufanya.” Akishi akamwambia Daudi, “Basi sasa, nitakufanya uwe mlinzi wangu binafsi daima.”

3Samweli alikuwa amefariki; Waisraeli wote walimwomboleza na kumzika huko Rama, katika mji wake mwenyewe. Wakati huo Sauli alikuwa amewafukuza kutoka nchini wote walioongea na wafu au pepo.

4Wafilisti walijikusanya wao wenyewe wakaja na kuweka kambi huko Shunemu; na Sauli akawakusanya Israeli wote pamoja, na wakaweka kambi yao huko Gilboa.5Sauli alipoona jeshi la Wafilisti, aliogopa na moyo wake ukatetemeka sana.6Sauli alipomuomba BWANA kwa ajili ya msaada, BWANA hakumjibu - si kwa ndoto wala kwa Urimu, wala kwa manabii.7Ndipo Sauli akawaambia watumishi wake, “Mnitafutie mwanamke ambaye anaweza kuongea na wafu, ili ni mwendee na kutafuta msaada wake.” Watumishi wake wakamwambia, “Tazama, yupo mwanamke huko Endori awezaye kuongea na wafu.”

8Basi Sauli akajigeuza, akavaa nguo nyingine tofauti, akaondoka yeye pamoja na watu wawili; wakamwendea yule mwanamke wakati wa usiku. Akasema, “Nitabirie, nakuomba, kwa kuongea na wafu, na uniinulie yule nitakayekutajia.”

9Yule mwanamke akamwambia, “Tazama, unajua alichofanya Sauli, jinsi alivyowafukuza kutoka katika nchi wanaoongea na wafu au mizimu. Basi kwa nini mnatega mtego kwa ajili ya uhai wangu, ili kuniua?”

10Sauli akamwapia kwa BWANA na kusema, “Kama BWANA aishivyo, hakuna adhabu utakayopata kutokana na jambo hili.”

11Kisha yule mwanamke akasema, “Je, nikuinulie nani?” Sauli akasema, “Niinulie Samweli.”

12Yule mwanamke alipomwona Samweli, akalia kwa sauti kuu na kusema na Sauli, akisema, “Kwa nini umenidanganya? Maana wewe ni Sauli.”

13Mfalme akamwambia, “Usiogope. Unaona kitu gani?” Yule mwanamke akamwambia Sauli, “Naona mungu akitoka katika nchi.” Akamuuliza mwanamke,14“Je, anafanana na nani?” Mwanamke akajibu, “Mtu mzee anazuka; naye amevaa kanzu.” Sauli akafahamu kuwa huyo ni Samweli, naye Sauli akainamisha uso wake hadi chini akionyesha heshima.15Samweli akamwambia Sauli, “Kwa nini umenisumbua na kuniinua juu?” Sauli akajibu, “Nimetaabika sana, maana Wafilisti wamepanga vita dhidi yangu, na Mungu ameniacha na hanipi majibu tena, si kwa manabii, wala kwa ndoto. Kwa hiyo nimekuita, ili unijulishe kile nitakachofanya.”16Samweli akasema, “Kwa kuwa BWANA amekuacha, basi unaniuliza nini, naye amekuwa adui yako?17BWANA amekutendea kile alichosema kuwa angekifanya. BWANA amerarua ufalme kutoka mkononi mwako na amempa ufalme mtu mwingine - amempa Daudi.18Kwa sababu hukuitii sauti ya BWANA na hukutekeleza hasira yake kali juu ya Amaleki, kwa hiyo leo naye amefanya hili kwako.19Zaidi ya hayo, BWANA atamweka Israeli pamoja na wewe katika mkono wa Wafilisti. Kesho wewe na wanao mtakuwa pamoja nami. BWANA pia ataliweka jeshi la Israeli katika mkono wa Wafilisti.”

20Ndipo ghafla Sauli alianguka chini kifudifudi na aliogopa kwa sababu ya yale maneno ya Samweli. Aliishiwa nguvu mwilini mwake, kwa kuwa siku hiyo alikuwa hajala chakula, hata kwa usiku huo wote.

21Ndipo yule mwanamke akaja kwa Sauli na akaona kwamba Sauli amepata shida, naye akamwambia, “Tazama, mjakazi wako ameisikiliza sauti yako; Nimeyaweka maisha yangu mkononi mwangu na nimeyasikiliza maneno uliyoniambia.22Hivyo basi, nakusihi, sikiliza pia sauti ya mjakazi wako, na uniruhusu nilete chakula kidogo mbele yako. Ule ili upate nguvu za kwenda kule uendako.”

23Lakini Sauli alikataa na kusema, “Sitakula.” Lakini watumishi wake, pamoja na yule mwanamke, wakamlazimisha hatimaye alisikiliza sauti zao. Hivyo aliinuka kutoka chini na kukaa kitandani.

24Yule mwanamke alikuwa na ndama mnono hapo nyumbani; akafanya haraka na kumchinja; akachukua unga, akaukanda, na akatengeneza mikate isiyotiwa chachu kwa unga huo.25Akaileta mbele ya Sauli na watumishi wake, nao wakala. Baaadaye waliinuka na kuondoka usiku huo.

29

1Basi Wafilisti walikusanya pamoja majeshi yao yote huko Afeki; Waisraeli wakapiga kambi karibu na chemichemi iliyoko Yezreeli.2Nao wakuu wa Wafilisti wakapitwa na mamia kwa maelfu; Daudi na watu wake wakapita wakiwa wa mwisho pamoja na Akishi.3Kisha wakuu wa Wafilisti wakasema, “Hawa Waebrania wanafanya nini hapa?” Akishi akawaambia wakuu wengine wa Wafilisti, “Huyu si Daudi, mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amekaa nami kwa siku hizi, au kwa miaka hii, nami nimeona hana kosa tangu aje kwangu hadi leo?”4Lakini wale wakuu wa Wafilisti walimkasirikia Akishi; wakamwabia, Mfukuze mtu huyo, aende kwake kule ulikompatia; usimruhusu aende nasi vitani, ili asiwe adui yetu katika vita. Kwa jinsi gani mtu huyu angeweza kufanya amani na bwana wake? Siyo kwa gharama ya vichwa vya watu wetu?5Je, huyu siye Daudi ambaye walimuimba kwa kupokezana na kucheza, wakisema: ‘Sauli ameua maelfu yake, Na Daudi makumi elfu yake?”’

6Ndipo Akishi alimwita Daudi na kumwambia, “Kama BWANA aishivyo, umekuwa mwema, na kutoka kwako na kuingia kwako pamoja nami katika jeshi ni kwema kama nionavyo mimi; maana sijaona kosa kwako tangu siku unakuja kwangu hadi siku hii ya leo. Hata hivyo, wakuu hawakupendi.7Basi sasa rudi na uende kwa amani, ili usiwakwaze wakuu wa Wafilisti.”

8Daudi akamwambia Akishi, “Lakini nimefanya nini? Kitu gani umekiona kwa mtumishi wako kwa muda ambao nimekuwa mbele yako hadi leo, kiasi kwamba nisiende kupigana na adui za bwana wangu mfalme?”

9Akishi akajibu na kumwambia Daudi, “Najua kwamba hauna lawama mbele zangu kama alivyo malaika wa Mungu; hata hivyo, wale wakuu wa Wafilisti wamesema, kamwe hatapanda pamoja nasi hadi vitani.10Basi sasa amka asubuhi na mapema na watumishi wa bwana wako waliokuja pamoja nawe; mara tu muamkapo asubuhi na mapema na kupata mwanga, ondokeni.”

11Hivyo Daudi aliamka mapema, yeye pamoja na watu wake, waondoke asubuhi, warudi kule katika nchi ya Wafilisti. Lakini Wafilisti walipanda kwenda Yezreeli.

30

1Ikawa, Daudi na watu wake walipokuwa wamefika Ziklagi siku ya tatu, Waamaleki walifanya mashambulizi katika Negevu na Ziklagi. Waliupiga Ziklagi, wakauchoma moto mji,2na kuwachukua mateka wanawake na kila mmoja aliyekuwa ndani yake, mkubwa kwa mdogo. Wao hawakuua hata mmoja, lakini waliwachukua watu na kuondoka nao.

3Daudi na watu wake walipofika kwenye mji, ulikuwa umechomwa moto - na wake zao, watoto wao wakiume na wakike walichukuliwa mateka.4Ndipo Daudi na watu aliokuwa nao wakapaza sauti zao na kulia hadi walipokuwa hawana nguvu zaidi za kulia.5Wake wawili wa Daudi walichukuliwa mateka, yaani Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili aliyekuwa mke wa Nabali Mkarmeli.6Daudi aliguswa sana, maana watu walikuwa wanaongea kuhusu kumpiga mawe, kwa sababu roho za watu wote walihuzunika, kila mtu kwa ajili ya mtoto wake wakiume na wakike, lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.

7Daudi akamwambia Abiathari, kuhani, mwana wa Ahimeleki, “Tafadhali, niletee hapa ile naivera.” Abiathari akaileta hiyo naivera kwa Daudi.8Daudi akamwomba BWANA kwa ajili ya mwongozo, akisema, “Je, kama nikiliandama jeshi hili, nitalipata?” BWANA akamjibu, “Wafuate, maana kweli utawapata, na kwa hakika utarudisha kila kitu.”9Kwa hiyo Daudi akaenda, yeye na wale watu 600 waliokuwa pamoja naye; nao wakafika katika kijito cha Bethori, mahali walipokaa wale walioachwa nyuma.10Lakini Daudi aliendelea kuwafuata, yeye na watu 400; maana wale 200 walibaki nyuma, wakiwa wamechoka kiasi cha kutoweza kuvuka kijito cha Besori.

11Nao walimkuta Mmisri shambani na wakamleta kwa Daudi; wakampatia mkate, na akala; wakampa maji ya kunywa;12kisha walimpa kipande cha keki ya tini na vishada viwili vya zabibu. Alipomaliza kula, akapata nguvu tena, kwa kuwa alikuwa hajala mkate wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.

13Ndipo Daudi akamuuliza, “Wewe ni mtu wa nani? Je, unatoka wapi?” Naye akajibu, “Mimi ni kijana wa Misri, mtumishi wa Mwamaleki mmoja; bwana wangu aliniacha, kwa sababu siku tatu zilizopita nilikuwa mgonjwa.14Tulifanya mashambulizi dhidi ya Negevu ya Wakereth, na iliyochini ya Yuda, na ile Negevu ya Kalebu, na kuichoma moto Ziklagi.”

15Daudi akamwambia, “Je, utanipeleka hadi kwa jeshi lililofanya mashabulizi?” Huyo Mmisri akasema, “Uniapie kwa Mungu kwamba hautaniua au kunisaliti na kuniweka katika mikono ya bwana wangu, nami nitakupeleka liliko hilo jeshi.”16Yule Mmisri alipompeleka huko Daudi, hao wateka nyara walikuwa wametawanyika kila sehemu, wakila na kunywa, na wakicheza, kwa sababu ya nyara zote walizokuwa wamezitwaa kutoka nchi ya Wafilisti na kutoka nchi ya Yuda.17Daudi akawashambulia tangu jua lilipozama hadi jioni ya siku ya pili. Hakuna mtu aliyeponyoka isipokuwa vijana 400, waliopanda ngamia na kukimbia.18Daudi akarudisha vyote ambavyo Waamaleki walikuwa wamevichukua; na Daudi akawaokoa wake zake wawili.19Hakuna kilichopotea, si kidogo wala kikubwa, si watoto wa kiume wala wa kike, si mali iliyotekwa, wala chochote ambacho wavamizi walikichukua kwa ajili yao. Daudi akawa amerejesha kila kitu.20Akachukua makundi yote ya kondoo na ng'ombe, ambayo watu waliyatanguliza mbele ya ng'ombe wengine. Wakisema, “Hizi ni nyara za Daudi.”

21Daudi akafika kwa wale watu mia mbili waliokuwa wamechoka kufuatana naye, wale walioachwa wakae katika kijito cha Besori. Watu hawa wakajitokeza kumlaki na watu waliokuwa naye.

22Ndipo watu wote waovu na wasiofaa miongoni mwa waliokwenda na Daudi wakasema, “Kwa sababu watu hawa hawakwenda nasi, hatutawapa chochote kutoka katika nyara tulizorudisha. Isipokuwa kila mtu aweza kuchukuwa mke na watoto wake, wawatoe na kwenda zao.”

23Ndipo Daudi akasema, “Ndugu zangu, msifanye hivyo, kwa vitu ambavyo BWANA ametupatia. Ametuhifadhi na kuwaweka mkononi mwetu wavamizi waliotuinukia.24Ni nani atawasikiliza kuhusu jambo hili? Kwa maana mgawo ni kwa yeyote aendae vitani, basi pia mgawo ni kwa yeyote aliyelinda mizigo; Nao watapata tena kilicho sawa.”25Ilikuwa hivyo tangu siku hiyo hadi leo, maana Daudi aliamua iwe sheria na amri kwa Israeli.

26Daudi alipofika Ziklagi, alituma sehemu ya nyara kwa wazee wa Yuda, kwa rafiki zake, akisema, “Tazama, hii ni zawadi yenu kutokana na nyara za adui wa BWANA.”

27Zawadi zilienda kwa wazee waliokuwa Bethueli, na kwa hao waliokuwa Ramothi iliyoko kusini, na kwa hao waliokuwa Yatiri,28na kwa hao waliokuwa Aroeri, na kwa hao waliokuwa Sifmothi, na kwa hao waliokuwa Eshtemoa29Pia kwa wazee waliokuwa Rakali, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wayerameeli, na kwa hao waliokuwa katika miji ya Wakeni,30na kwa hao waliokuwa Horma, na kwa hao waliokuwa Borashani, na kwa hao waliokuwa Athaki,31na kwa hao waliokuwa Hebroni, na kwa sehemu zote ambazo Daudi mwenyewe na watu wake walizoea kwenda.

31

1Basi Wafilisti wakapigana dhidi ya Waisraeli. Waisraeli wakakimbia mbele ya Wafilisti na wakaanguka chini wakafa katika mlima wa Gilboa.2Wafilisti wakamwandama Sauli na wanawe kwa karibu. Wakawaua wanawe Yonathani, Abinadabu, and Malkishua.3Vita vikamlemea Sauli, na wapiga upinde wakampata. Akapata maumivu makali kwa sababu yao.

4Kisha Sauli akamwambia mbeba silaha wake, “Chomoa upanga wako unichome nao. Vinginevyo, hawa wasiotahiriwa watakuja na kuninyanyasa.” Lakini mbeba silaha wake hakukubali, kwa kuwa aliogopa sana. Hivyo Sauli alichukua upanga wake mwenyewe na kuuangukia.5Yule mbeba silaha akaona kwamba Sauli amekufa, yeye naye vivyo hivyo akauangukia upanga wake akafa pamoja naye.6Kwa hiyo Sauli alikufa, wanawe watatu, na mbeba silaha wake - watu hawa wote walikufa pamoja siku iyo hiyo.

7Watu wa Israeli waliokuwa upande mwingine wa bonde, na hao waliokuwa ng'ambo ya Yordani, walipoona kwamba Waisraeli wamekimbia, na kwamba Sauli na wanawe wamekufa, waliiacha miji yao na kukimbia, nao Wafilisti wakaja na kukaa humo.

8IKawa katika siku iliyofuata, Wafilisti wakafika kuchukua nyara za waliokufa, ndipo wakamuona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.9Nao wakakata kichwa chake na kuondoa silaha zake, na wakawatuma wajumbe kwenda pande zote katika nchi ya Wafilisti kutangaza habari hizo katika mahekalu yao ya sanamu na kwa watu.10Wakaziweka silaha zake katika hekalu la Ashtorethi, nao wakakitundika kiwiliwili chake kwenye ukuta wa mji wa Bethi Shani.

11Na wenyeji wa Yabeshi Gileadi waliposikia kile Wafilisti walichomfanyia Sauli,12wapiganaji wote wakainuka na kwenda usiku wote na wakauondoa mwili wa Sauli na miili ya wanawe kutoka ukuta wa Bethi Shani. Nao wakaenda Yabeshi na wakaichoma moto hiyo miili huko.13Kisha wakachukua mifupa yao na kuizika chini ya mti wa mkwaju huko Yabeshi, na wakafunga siku saba.

2 Samweli

1

1Baada ya kifo cha Sauli, Daudi alirudi kutoka kuwashambulia Waamaleki na akakaa Siklagi kwa siku mbili.2Siku ya tatu, mtu mmoja alikuja kutoka kambi ya Sauli nguo zake zikiwa zimeraruliwa na akiwa na vumbi juu ya kichwa chake. Alipofika kwa Daudi akaanguka chini na akamsujudia.

3Daudi akamuuliza, “Unatoka wapi?” Yeye akajibu, “Nimeponyoka kutoka kambi ya Israeli.”

4Daudi akamwambia, “Tafadhali nieleze jinsi mambo yalivyokuwa.” Akajibu, “Watu walikimbia kutoka vitani. Wengi wameanguka, na wengi wao wameuawa. Sauli na Yonathani mwanawe pia wameuawa.”

5Daudi akamwuliza kijana, “Unajuaje kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wameuawa?”

6Yule kijana akajibu, “Kwa bahati nilikuwa juu ya Mlima Gilboa, na pale alikuwepo Sauli ameegemea mkuki wake, na magari ya farasi na waongozaji walikuwa karibu kumkamata.7Sauli alipogeuka aliniona na akaniita. Nikajibu, ‘Mimi hapa.’

8Akaniuliza, ‘Wewe ni nani?’ Nikamjibu, ‘Mimi ni Mwamaleki,’

9Akaniambia, Tafadhali simama juu yangu uniue, kwa kuwa shida kubwa imenipata, lakini uhai ungalimo ndani yangu.’

10Hivyo nilisimama juu yake nikamuua, kwa maana nilijua kwamba asingeweza kuishi baada ya kuwa ameanguka. Ndipo nikachukua taji iliyokuwa juu ya kichwa chake na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, na nimevileta hapa kwako, bwana wangu.”

11Kisha Daudi akararua mavazi yake, na watu wote waliokuwa pamoja naye wakafanya vilevile.12Walilia, wakaomboleza na kufunga mpaka jioni kwa ajili ya Sauli, Yonathani mwanawe, watu wa Yahwe, na kwa ajili ya nyumba ya Israeli kwa maana wameanguka kwa upanga.

13Daudi akamwambia yule kijana, “Unatokea wapi?” Akajibu, “Mimi ni kijana wa mgeni Mwamaleki.”

14Daudi akamwambia, “Kwa nini haukuogopa kumuua mfalme, mtiwa mafuta wa Yahwe kwa mkono wako?”15Daudi akamwita mmojawapo wa vijana na akamwambia, “Nenda ukamuue.” Hivyo kijana huyo akaenda na kumpiga hata chini, Mwamaleki akafa.16Ndipo Daudi akamwambia Mwamaleki aliyekufa, “Damu yako iwe juu ya kichwa chako kwa kuwa kinywa chako kimeshuhudia dhidi yako kusema, ‘Nimemuua mfalme mtiwa mafuta wa Yahwe.’”

17Ndipo Daudi akaimba wimbo wa maombolezo juu ya Sauli na Yonathani mwanawe.18Akawaamuru watu kuufundisha wimbo wa Upinde kwa wana wa Yuda, ambao umeandikwa katika Kitabu cha Yashari.
19“Utukufu wako, Israel, umeondolewa, umeondolewa juu ya mahali pako pa juu! Jinsi mwenye nguvu alivyoanguka!
20Msiiseme katika Gathi, msiitangaze katika mitaa ya Ashikeloni, ili binti za wafilisti wasifurahi, ili binti za wasiotailiwa wasisherehekee.
21Enyi Milima ya Gilboa, kusiwe na umande au mvua juu yenu, wala mashamba yasitoe nafaka kwa ajili ya sadaka, kwa maana hapo ngao ya mwenye nguvu imeharibiwa. Ngao ya Sauli haikupakwa mafuta.
22Kutoka katika damu ya waliouawa, kutoka katika miili ya wenye nguvu, upinde wa Yonathani haukurudi nyuma, na upanga wa Sauli haukurudi patupu.
23Sauli na Yonathani walikuwa wakipendwa na walikuwa wenye neema maishani, hata wakati wa mauti yao walikuwa pamoja. Walikuwa na kasi kuliko tai, walikuwa na nguvu kuliko simba.
24Enyi binti wa Israeli lieni juu ya Sauli, aliyewavika mavazi ya thamani pamoja na vito vya thamani, na aliyetia mapambo ya dhahabu katika mavazi yenu.
25Jinsi wenye nguvu walivyoanguka vitani! Yonathani ameuawa juu ya mahali pako pa juu.
26Nimesikitishwa sana kwa ajili yako, Yonathani ndugu yangu. Ulikuwa mpendwa wangu sana. Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, ukipita upendo wa wanawake.
27Jinsi wenye nguvu walivyoanguka na silaha za vita zimeteketea!”

2

1Ikawa baada ya haya Daudi akamuuliza Yahwe, “Je naweza kuupandia mmojawapo wa miji ya Yuda?” Yahweh akamjibu, “Panda.” Daudi akauliza, “Niuendee mji upi? Yahwe akajibu, “Hebroni”

2Hivyo Daudi akakwea pamoja na wake zake wawili, Ahinoamu wa Yezreeli, na Abigaili wa Karmeli, mjane wa Nabali.3Daudi akawaleta watu waliokuwa pamoja naye, na kila mmoja akaleta familia yake katika mji wa Hebroni walipoanza kuishi.4Kisha watu wa Yuda wakaja na kumtia Daudi mafuta kuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda. Wakamwambia Daudi, “Watu wa Yabeshi Gileadi wamemzika Sauli.”5Hivyo Daudi akatuma wajumbe kwa watu wa Yabeshi Gileadi akawaambia, “Mbarikiwe na Yahwe, kwa kuwa mmeonyesha utiifu huu kwa bwana wenu Sauli mliyemzika.6Sasa Yahwe awadhihirishie utiifu na uaminifu wa kiagano. Nami pia nitawaonyesha wema kwa sababu ya yale mliyoyafanya.7Sasa basi, mikono yenu itiwe nguvu; mwe jasiri kwa maana Sauli bwana wenu amekufa, na nyumba yote ya Yuda imenitia mafuta niwe mfalme wao.”

8Lakini Abneri mwana wa Neri, mkuu wa jeshi la Sauli, akamchukuwa Ishboshethi mwana wa Sauli akamleta Mahanaimu.9Akamfanya Ishboshethi mfalme juu ya Gileadi, Asheri, Yezreeli, Efraimu, Benjamini na juu ya Israeli yote.

10Ishiboshethi mwana wa Sauli alikuwa na umri wa miaka arobaini alipoanza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka miwili. Lakini nyumba ya Yuda ikaambatana na Daudi.11Muda ambao Daudi alikuwa mfalme juu ya nyumba ya Yuda huko Hebroni ni miaka saba na miezi sita.

12Abneri mwana wa Neri na watumishi wa Ishboshethi mwana wa Sauli walitoka Mahanaimu kwenda Gibeoni.13Yoabu mwana wa Seruya na watumishi wa Daudi wakatoka na kukutana nao katika bwawa la Gibeoni. Wakakaa pale, kundi moja upande huu wa bwawa na kundi lingine upande wa pili.

14Abneri akamwambia Yoabu, “Haya, vijana na wainuke na kushindana mbele yetu.” Yoabu akajibu, “Haya na wainuke.”

15Ndipo vijana walipoinuka na kukutana, kumi na wawili kwa ajili ya Banjamini na Ishboshethi mwana wa Sauli, na kumi na wawili kutoka kwa watumishi wa Daudi.16Kila mtu akakamata kichwa cha adui yake na kupiga upanga wake katika ubavu wa adui yake, wakaanguka chini pamoja. Kwa hiyo mahali pale pakaitwa kwa Kiebrania, “Helkath-Hasurimu,” yaani “konde la upanga,” lililopo Gibeoni.

17Vita vikawa vikali sana siku ile na Abneri na watu wa Israeli wakashindwa mbele ya watumishi wa Daudi.

18Wana watatu wa Seruya walikuwepo pale: Yoabu, Abishai na Asaheli.19Asaheli alikuwa mwepesi miguuni kama paa. Akamfuatilia Abneri kwa karibu bila kugeuka upande wowote.20Abneri akaangalia nyuma yake na kusema, “Ni wewe Asaheli?” Akajibu, “Ni mimi.”

21Abneri akamwambia, “Geuka upande wako wa kulia au kushoto umshike mmojawapo wa vijana na kuchukua silaha yake.” Lakini Asaheli hakugeuka.

22Ndipo Abneri alipomwambia tena Asaheli, “Simama usinifuate. Kwa nini nikupige hata chini? Nitautazamaje uso wa Yoabu ndugu yako?”

23Lakini Asaheli hakukubali kugeuka; na hivyo Abneri akamchoma kwa nchi ya mkuki wake, hata ukatokea upande wa pili. Asaheli akaanguka chini akafa. Hata ikawa kila mmoja aliyefika mahali pale Asaheli alipoanguka na kufa, alisimama hapo hapo.

24Lakini Yoabu na Abishai wakamfuatilia Abneri. Wakati jua linazama walikuwa wamefika mlima wa Amma, uliopo karibu na Gia katika njia ielekeayo nyika ya Gibeoni.25Wabenjamini wakajikusanya nyuma ya Abneri na kusimama juu ya kilima.

26Kisha Abneri akamwita Yoabu na kusema, “Je! Ni lazima upanga uendelee kurarua daima? Je, haujui kwamba mwisho wake utakuwa mchungu? Hata lini ndipo uwaambie watu wako waache kuwafuatia ndugu zao?”

27Yoabu akajibu, “Kama Mungu aishivyo, usingesema hivyo, askari wangu wangewafuatia ndugu zao hata asubuhi!”

28Ndipo Yoabu akapiga tarumbeta, na watu wake wote wakasimama na hawakuendelea kuwafuata Israeli tena wala hawakupigana tena.

29Abneri na watu wake wakasafiri usiku wote kupitia Araba. Wakavuka Yordani, wakatembea asubuhi yote iliyofuata, na hata wakafika Mahanaimu.

30Yoabu akarudi kutoka katika kumfuatia Abneri. Akawakusanya watu wake wote, ambopo Asahali na askari wengine kumi na tisa wa Daudi walipungua.31Lakini watu wa Daudi walikuwa wameua watu 360 wa Benjamini na Abneri.32Kisha wakamchukua Asahali na kumzika katika kaburi la baba yake, lililokuwapo Bethlehemu. Yoabu na watu wake wakasafiri usiku wote, kukacha wakati wanafika Hebroni.

3

1Kulikuwa na vita ya mda mrefu kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi. Daudi akaendelea kupata nguvu zaidi, lakini nyumba ya Sauli iliendelea kudhoofika na kudhoofika.

2Wana wakazaliwa kwa Daudi huko Hebroni. Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu wa Yezreeli.
3Mwanawe wa pili, Kileabu, alizaliwa kwa Abigaili, mjane wa Nabali wa Karmeli. Wa tatu, Absalomu, alikuwa mwana wa Maaka, binti Talmai, mfalme wa Geshuri.
4Mwana wa nne wa Daudi, Adoniya, alikuwa mwana wa Hagithi. Mwanawe wa tano alikuwa Shefatia mwana wa Abitali,
5na wa sita, Ithreamu, alikuwa mwana wa Egla mkewe Daudi. Hawa wote walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni.

6Ikawa wakati wa vita kati ya nyumba ya Sauli na nyumba ya Daudi Abneri akajifanya mwenye nguvu katika nyumba ya Sauli.7Sauli alikuwa na suria jina lake Rispa, binti Aiya. Ishboshethi akamuuliza Abneri, “Kwa nini umeingia kwa suria ya baba yangu?”

8Hata ikawa Abneri akakasirika sana kutokana na maneno ya Ishboshethi naye akasema, “Je mimi ni kichwa cha mbwa wa Yuda? Ninaonyesha uaminifu kwa nyumba ya Sauli, baba yako, kwa jamaa yake, na rafiki zake, kwa kutokukuweka katika mkono wa Daudi. Na bado leo unanishtaki kwa uovu kuhusu huyu mwanamke.9Mungu na anifanyie hivyo, Abneri, na kuzidi, ikiwa sitafanya kwa Daudi kama Yahwe alivyomwapia,10kuuhamisha ufalme kutoka nyumba ya Sauli na kukisimamisha kiti cha enzi cha Daudi juu ya Israeli na juu ya Yuda, kutoka Dani hadi Beersheba.”11Ishboshethi hakuweza kumjibu Abneri neno tena, kwani alimuogopa.

12Kisha Abneri akatuma wajumbe kwa Daudi kusema, “Nchi hii ni ya nani? Fanya agano nami, nawe utaona kwamba mkono wangu uko nawe, kuiIeta Israeli yote kwako.”13Daudi akajibu, “Vema, nitafanya agano nawe. Lakini neno moja ninalolitaka kutoka kwako ni kwamba hautauona uso wangu usipomleta kwanza Mikali, binti Sauli, unapokuja kuonana nami.”14Kisha Daudi akatuma wajumbe kwa Ishboshethi, mwana wa Sauli, kusema, “Nipe Mikali, mke wangu niliyetoa kwa ajili yake govi mia moja za Wafilisti.”

15Hivyo Ishboshethi akatuma kwa Mikali na kumchukua kutoka kwa mme wake, Paltieli mwana wa Laishi.16Mme wake akafuatana naye, huku akilia, akaendelea hadi Bahurimu. Kisha Abneri akamwambia, “Basi sasa rudi nyumbani.” Hivyo akarudi.

17Abneri akaongea na wazee wa Israeli kusema, “Zamani mlitaka Daudi awe mfalme wenu.18Basi sasa fanyeni hivyo. Kwa maana Yahwe alisema kuhusu Daudi kusema, “Kwa mkono wa Daudi mtumishi wangu nitawaokoa watu wangu Israeli kutoka katika mkono wa Wafilisti na kutoka katika mkono wa adui zao wote.”19Pia Abneri akasema na watu wa Benjamini ana kwa ana. Kisha Abneri akaenda kuongea na Daudi huko Hebroni akaeleza kila jambo ambalo Israeli na nyumba yote ya Benjamini walitamani kulitimiza.

20Wakati Abneri na watu ishirini kati ya watu wake walifika Hebroni kumuona Daudi, Daudi akaandaa sherehe kwa ajili yao.21Abneri akamueleza Daudi, “Nitainuka na kukukusanyia Israeli wote, bwana wangu mfalme, ili kwamba wafanye agano nawe, kwamba utawale juu ya yote unayotaka.” Hivyo Daudi akamruhusu Abneri kuondoka, Abneri akaondoka kwa amani.

22Kisha askari wa Daudi na Yoabu wakarudi kutoka katika kuteka nyara na wakaja na nyara nyingi. Lakini Abneri hakuwepo Hebroni pamoja na Daudi. Daudi alikuwa amemruhusu kuondoka, na alikuwa ameondoka kwa amani.23Wakati Yoabu na Jeshi lote walipofika, Yoabu aliambiwa, “Abneri mwana wa Neri alikuja kwa mfalme, na mfalme amemruhusu kuondoka, naye Abneri ameondoka kwa amani.”

24Kisha Yoabu akaja kwa mfalme na kusema, “Umefanya nini? Tazama, Abneri alikuja kwako! Kwa nini umemruhusu kuondoka, naye ameenda?25Haujui kwamba Abneri mwana wa Neri alikuja kukudanganya na kupeleleza hali yako na kuangalia kila unalofanya?”

26Yoabu alipoondoka kwa Daudi, alituma wajumbe kumfuatia Abneri, nao wakamrudisha kutoka katika kisima cha Sira, lakini Daudi hakulijua hili.27Abneri aliporudi Hebroni, Yoabu alimchukua kando kati ya lango ili aongee naye faraghani. Hapohapo Yoabu alimchoma tumboni na kumuua. Hivyo, akalipa kisasi cha damu ya Asaheli nduguye.

28Daudi alipolisikia jambo hili akasema, “Mimi na ufalme wangu hatuna hatia mbele za Yahwe daima, kuhusiana na damu ya Abneri mwana wa Neri.29Hatia ya damu ya Abneri na iwe juu ya Yoabu na nyumba yote ya baba yake. Na asikosekane katika familia ya Yoabu mtu mwenye vidonda, au mwenye ukoma, au kilema atembeaye kwa fimbo au aliyeuawa kwa upanga au mwenye kukosa chakula.”

30Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamuua Abneri, kwa sababu alimuua Asaheli ndugu yao vitani huko Gibeoni.

31Daudi akamwambia Yoabu na wote waliokuwa pamoja naye, “Rarueni mavazi yenu, jivikeni nguo za magunia, na muomboleze mbele ya mwili wa Abneri.” Na mfalme Daudi akaufuata mwili wa Abneri wakati wa mazishi.32Wakamzika Abneri huko Hebroni. Mfalme akalia kwa sauti katika kaburi la Abneri, na watu wote pia wakalia.

33Mfalme akamwomboleza Abneri naye akaimba, “Je ilipasa Abneri afe kama afavyo mpumbavu?
34Mikono yako haikufungwa. Miguu yako haikuwa imefungwa minyororo. Kama mtu aangukavyo mbele ya wana wa uovu, ndivyo ulivyoanguka.” Watu wote wakamlilia zaidi.

35Watu wote wakaja kumtaka Daudi ale wakati kungali mchana, lakini Daudi akaapa, “Mungu na anifanyie hivyo, na kuzidi, ikiwa nitaonja mkate au chochote kabla jua halijazama.”36Watu wote wakaiona huzuni ya Daudi, na ikawapendeza, hivyo kila alichokifanya mfalme kikawapendeza.

37Hivyo watu wote na Israeli yote wakatambua siku hiyo kwamba haikuwa nia ya mfalme Abneri mwana wa Neri afe.38Mfalme akawaambia watumishi wake, “Je hamjui kuwa mtu mkuu ameanguka leo hii katika Israeli?39Nami leo nimedhoofika, japokuwa nimetiwa mafuta kuwa mfalme. Watu hawa, wana wa Seruya ni hatari sana kwangu. Yahwe na amrudishie muovu kwa kumlipa kwa ajili ya uovu wake kama anavyostahili.”

4

1Ikawa Ishboshethi, mwana wa Sauli, aliposikia kwamba Abneri amekufa huko Hebroni, mikono yake ikadhoofika, na Israeli yote ikataabika.2Basi mwana wa Sauli alikuwa na watu wawili waliokuwa wakuu wa vikosi vya askari. Mmoja wao alikuwa Baana na mwingine alikuwa Rekabu, wana wa Rimoni Mbeerothi wa wana wa Benjamini (kwa maana Berothi ilihesabiwa kuwa sehemu ya Benjamini,3na Waberothi walikimbilia Gitaimu na wamekuwa wakiishi pale hadi sasa).

4Basi Yonathani, mwana wa Sauli, alikuwa na mwana mlemavu wa miguu. Alikuwa na umri wa miaka mitano habari kuhusu Sauli na Yonathani ilipofika Yezreeli. Yaya wake akamchukua ili akimbie. Lakini wakati anakimbia, mwana wa Yonathani alianguka na akawa kilema. Jina lake aliitwa Mefiboshethi.

5Hivyo wana wa Rimoni Mbeerothi, Rekabu na Baana, wakasafiri mchana wakati wa jua kali mpaka nyumbani mwa Ishbothethi, yeye alikuwa amepumzika mchana.6Mwanamke aliyekuwa akililinda lango alisinzia wakati akipepeta ngano, Rekabu na Baana waliingia ndani polepole na wakampita.

7Hivyo walipoingia ndani ya nyumba, walimpiga na kumuua wakati amelala chumbani mwake. Kisha wakakata kichwa chake na wakaondoka nacho, wakasafiri njiani usiku kucha mpaka Araba.8Wakaleta kichwa cha Ishboshethi kwa Daudi huko Hebroni, nao wakamwambia mfalme, “Tazama, hiki ni kichwa cha Ishboshethi mwana wa Sauli, adui yako, aliyekuwa akiutafuta uhai wako. Leo Yahwe amemlipia kisasi bwana wetu mfalme dhidi ya Sauli na uzao wake.”

9Daudi akawajibu Rekabu na Baana nduguye, wana wa Rimoni Mbeerothi, akawambia, “Kama Yahwe aishivyo, aliyeuokoa uhai wangu na kila shida,10mtu mmoja aliponiambia, ‘Tazama, Sauli amekufa,’ akifikiri alileta habari njema, nilimkamata na kumuua huko Siklagi. Huo ndio ujira niliompa kwa habari yake.11Namna gani, watu waovu wamemuua mwenye haki kitandani mwake ndani ya nyumba, Je, nisiitake damu yake kutoka katika mikono yenu, na kuwaondoa duniani?”

12Kisha Daudi akawaagiza vijana, nao wakawaua wakakata mikono na miguu yao na kuwatundika kando ya bwawa huko Hebroni. Lakini wakakichukua kichwa cha Ishboshethi na kukizika katika kaburi la Abneri katika Hebroni.

5

1Kisha kabila zote za Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni nao wakasema, “Tazama, sisi ni nyama na mifupa yako.2Kipindi kilichopita, Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliyeliongoza jeshi la Waisraeli. Yahwe akakwambia, ‘Utawachunga watu wangu Israeli, na utakuwa mtawala juu ya Israeli.’”

3Hivyo wazee wote wa Israeli wakaja kwa mfalme huko Hebroni na mfalme Daudi akafanya nao agano mbele ya Yahweh. Wakamtawaza Daudi kuwa mfalme wa Israeli.4Daudi alikuwa na umri wa miaka thelathini alipoanza kutawala, naye akatawala miaka arobaini.5Alitawala juu ya Yuda miaka saba na miezi sita huko Hebroni, na huko Yerusalemu akatawala miaka thelathini na mitatu juu ya Israeli yote na Yuda.

6Mfalme na watu wake wakaenda Yerusalemu kupigana na Wayebusi, waliokuwa wenyeji wa nchi. Wakamwambia Daudi, “Hautaweza kuja hapa kwani hata vipofu na vilema waweza kukuzuia kuingia. Daudi hawezi kuja hapa.”7Lakini, Daudi akaiteka ngome ya Sayuni, ambayo sasa ni mji wa Daudi.8Wakati huo Daudi akasema, “Waliowashambulia wayebusi watapaswa kupita katika mfereji wa maji ili wawafikie vilema na vipofu ambao ni adui wa Daudi.” Hii ndiyo maana watu husema, “Vipofu na vilema wasiingie katika kasri.”

9Hivyo Daudi akaishi ngomeni naye akaiita mji wa Daudi. Akaizungushia ukuta, kuanzia barazani kuelekea ndani.10Daudi akawa na nguvu sana kwa maana Yahwe, Mungu wa utukufu, alikuwa pamoja naye.

11Kisha Hiramu mfalme wa Tiro akatuma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, mafundi seremala na wajenzi. Wakamjengea Daudi nyumba.12Daudi akatambua kuwa Yahwe alikuwa amemuweka ili awe mfalme juu ya Israeli, na kwamba alikuwa ameutukuza ufalme wake kwa ajili ya Israeli watu wake.

13Baada ya Daudi kuondoka Hebroni na kwenda Yerusalemu, akajitwalia wake na masuria wengi huko Yerusalemu, na wana na binti wengi walizaliwa kwake.14Haya ndiyo majina ya wanawe waliozaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, Selemani,15Ibhari, Elishua, Nefegi, Yafia,16Elishama, Eliada na Elifeleti.

17Basi wafilisti waliposikia kwamba Daudi ametiwa mafuta kuwa mfalme juu ya Israeli, wakaenda wote kumtafuta. Daudi aliposikia hilo akashuka ngomeni.18Basi Wafilisti walikuwa wamekuja na kuenea katika bonde la Mrefai.19Kisha Daudi akaomba msaada kutoka kwa Yahwe. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Je utanipa ushindi juu yao?” Yahwe akamwambia Daudi, “Washambulie, kwa hakika nitakupa ushindi juu ya Wafilisti.”

20Hivyo Daudi akawashambulia huko Baali Perasimu, naye akawashinda. Akasema, Yahwe amewafurikia adui zangu mbele yangu kama mafuriko ya maji. Kwa hiyo jina la mahali pale likawa Baali Perasimu.21Wafilisti wakaacha vinyago vyao pale, na Daudi na watu wake wakaviondoa.

22Kisha Wafilisti wakaja kwa mara nyingine tena na kujieneza zaidi katika bonde la Mrefai.23Hivyo Daudi akatafuta msaada tena kutoka kwa Yahweh, naye Yahweh akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini uwazunguke kwa nyuma na uwaendee kupitia miti ya miforosadi.24Wakati utakaposikia sauti za mwendo katika upepo uvumao juu ya miti ya miforosadi, hapo ushambulie kwa nguvu. Fanya hivi kwa kuwa Yahwe atatangulia mbele yako kulishambulia jeshi la Wafilisti.”25Hivyo Daudi akafanya kama Yahwe alivyomuamuru. Akawauwa wafilisti njiani mwote toka Geba hadi Gezeri.

6

1Basi kwa mara nyingine Daudi akawakusanya wateule wa Israeli, 30,000.2Daudi akainuka na akaenda na watu wake wote waliokuwa pamoja naye kutoka Baala mji ulioko Yuda ili alilete sanduku la Mungu, liitwalo kwa jina la Yahwe wa majeshi, akaaye juu ya makerubi.3Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyokuwa juu ya kilima. Uza na Ahio, wanawe, wakauongoza mkokoteni.4Wakautoa mkokoteni na sanduku la Mungu juu yake nyumbani mwa Abinadabu juu ya kilima. Ahio alikuwa ametangulia mbele ya sanduku.5Kisha Daudi na nyumba yote ya Israeli wakaanza kucheza mbele ya Yahwe, wakishangilia kwa vyombo vya mziki, vinubi, vinanda, matari, kayamba na matowazi.

6Hata walipofika katika shinikizo la Nasoni, wale ng'ombe wakakwama, Uza akanyosha mkono wake na kulikumbatia sanduku la Mungu, naye akalishikilia.7Kisha hasira ya Yahweh ikawaka dhidi ya Uza. Mungu akampiga kwa ajili ya dhambi yake. Uza akafa pale pale kando ya sandaku la Mungu.

8Daudi akakasirika kwa kuwa Yahwe alimpiga Uza, naye akapaita mahali pale Peresi Uza. Eneo hilo linaitwa Peresi Uza hata leo.

9Daudi akamuogopa Yahweh siku hiyo. Akasema, “Sanduku la Yahwe lawezaje kuja kwangu?”10Hivyo Daudi hakuwa tayari tena kulichukua sanduku la Yahwe katika mji wa Daudi. Badala yake, akaliweka kando katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.11Sanduku la Yahwe likakaa katika nyumba ya Obedi Edomu Mgiti kwa miezi mitatu. Kwa hiyo Yahwe akambariki yeye na nyumba yake yote.

12Kisha mfalme Daudi akaambiwa, “Yahwe ameibariki nyumba ya Obedi Edomu na kila kitu alichonacho kwa sababu ya sanduku la Mungu.” Hivyo Daudi akaenda na kulipandisha sanduku la Mungu kutoka katika nyumba ya Obedi Edomu hadi mji wa Daudi kwa furaha.13Ikawa waliolibeba sanduku la Yahwe walipochukua hatua sita, akatoa sadaka ng'ombe na ndama aliyenona.14Daudi akacheza mbele ya Yahwe kwa nguvu zake zote; alikuwa amevaa naivera ya kitani pekee.15Hivyo Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalipandisha sanduku la Yahwe kwa vifijo na sauti za tarumbeta.

16Hata ikawa sanduku la Yahwe lilipofika mjini mwa Daudi, Mikali, binti Sauli, alichungulia dirishani. Akamuona mfalme Daudi akiruka na kucheza mbele ya Yahwe. Akamdharau moyoni mwake.

17Wakaliingiza sanduku la Yahwe na kuliweka mahali pake, katikati ya hema ambayo Daudi alikuwa ameliwekea. Kisha Daudi akatoa sadaka ya kuteketezwa na matoleo ya amani mbele za Yahwe.18Ikawa Daudi alipomaliza kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, akawabariki watu kwa jina la Yahwe wa majeshi.19Kisha akawagawia watu wote, umati wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kipande cha mkate, nyama na keki ya zabibu. Kisha watu wote wakaondoka; kila mmoja akarudi kwake.

20Kisha Daudi akarudi ili aibariki familia yake. Mikali, binti Sauli, akatoka ili akutane na Daudi naye akasema, “Jinsi gani mtukufu mfalme wa Israeli alivyokuwa leo, aliyejiacha uchi mbele ya macho ya vijakazi miongoni mwa watumishi wake, kama mmoja wa wapumbavu ambaye bila aibu hujifunua yeye mwenyewe!”

21Daudi akamjibu Mikali, “Nilifanya hivyo mbele ya Yahwe, aliyenichagua juu ya baba yako na juu ya familia yake yote, aliyeniweka kuwa kiongozi juu ya watu wa Yahwe, juu ya Israeli. Mbele ya Yahwe nitafurahi!22Nitakuwa nisiye na heshima hata zaidi ya hapa, na nitajishusha mbele za macho yangu mwenyewe. Lakini kwa hawa vijakazi uliowasema, nitaheshimiwa.”

23Hivyo Mikali, binti Sauli, hakuwa na watoto hata alipokufa.

7

1Ikawa mfalme alipokuwa amekwisha kukaa katika nyumba yake, na baada ya Yahwe kuwa amemstarehesha kutokana na adui zake wote waliomzunguka,2mfalme akamwambia nabii Nathani, “Tazama, mimi ninaishi katika nyumba ya mierezi, lakini sanduku la Mungu lipo hemani.”

3Basi Nathani akamwambia mfalme, “Nenda, fanya lililo moyoni mwako, kwa maana Yahwe yupo nawe.”

4Lakini usiku uleule neno la Yahwe lilimjia Nathani kusema,5“Nenda na umwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: Je utanijengea nyumba ya kuishi?”6Kwa maana sijawai kuishi katika nyumba tangu siku ile nilipowaleta wana wa Israeli kutoka Misri hata leo; badala yake nimekuwa nikitembea katika hema, hema la kukutania.7Mahali pote ambapo nimekuwa nikihama miongoni mwa wana wote wa Israeli, Je niliwahi kusema lolote na viongozi wa Israeli niliowaweka kuwachunga watu wangu Israeli, kusema, ‘Kwa nini hamjanijengea nyumba ya mierezi?’8Sasa basi, mwambie Daudi, mtumishi wangu, Hiki ndicho asemacho Yahwe wa majeshi: ‘Nilikutwaa kutoka machungani, kutoka katika kuwafuata kondoo, ili uwe mtawala juu ya watu wangu Israeli.9Nimekuwa pamoja nawe popote ulipokwenda na nimewakatilia mbali adui zako wote mbele yako. Na nitakutengenezea jina kubwa, kama jina la mojawapo ya wakuu walio juu ya nchi.10Nitatenga mahali kwa ajili ya watu wangu Israeli nami nitawapanda pale, ili kwamba waweze kuishi mahali pao wenyewe na wasisumbuliwe tena. Waovu hawatawatesa tena, kama walivyofanya mwanzo.11Kama walivyofanya tangu siku ile nilipoamuru waamuzi juu ya watu wangu Israeli. Nami nitakustarehesha kutokana na adui zako wote. Zaidi ya hayo, Mimi, Yahwe, nakutamkia kwamba nitakutengenezea nyumba.12Siku zako zitakapokwisha na ukalala pamoja na baba zako, nitainua mzao baada yako, atokaye katika mwili wako mwenyewe, nitauimarisha ufalme wake.13Naye atajenga nyumba kwa jina langu, nami nitakiimarisha kiti chake cha enzi daima.14Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwanangu. Atakapotenda dhambi, nitamwadhibu kwa fimbo ya wanadamu na kwa mapigo ya wana wa watu.15Lakini uaminifu wa agano langu hautamwondokea, kama nilivyouondoa kutoka kwa Sauli, niliyemwondoa mbele yako.16Nyumba yako na ufalme wako utathibitishwa mbele yako daima. Kiti chako cha enzi kitakuwa imara daima.’”

17Nathani akamwambia Daudi na kumtaarifu maneno haya yote, na akamwambia kuhusu ono lote.

18Kisha mfalme Daudi akaingia ndani na kuketi mbele ya Yahwe; akasema, “Mimi ni nani, Yahwe Mungu, na familia yangu ni nini hata umenileta hapa nilipo?19Na hili lilikuwa jambo dogo mbele yako, Bwana Yahwe. Hata ukasema kuhusu familia ya mtumishi wako wakati mkuu ujao, nawe umenionyesha vizazi vijavyo, Bwana Yahwe!20Mimi Daudi, niseme nini zaidi kwako? Umemjua mtumishi wako, Bwana Yahwe.21Kwa ajili ya neno lako, na kwa ajili ya kutimiza kusudi lako mwenyewe, umefanya jambo kubwa namna hii na kulidhihirisha kwa mtumishi wako.22Kwa hiyo wewe ni mkuu, Bwana Yahwe. Kwa maana hakuna mwingine aliye kama wewe, na hakuna Mungu mwingine badala yako, kama jinsi ambayo tumesikia kwa masikio yetu wenyewe.23Kwani kuna taifa lipi lililo kama watu wako Israeli, taifa moja juu ya nchi ambalo wewe, Mungu, ulikwenda na kuwakomboa kwa ajili yako wewe mwenyewe? Ulifanya hivi ili kwamba wawe watu kwa ajili yako mwenyewe, kujifanyia jina kwa ajili yako mwenyewe, na kufanya matendo makuu na ya kuogofya kwa ajili ya nchi yako. Uliyaondoa mataifa na miungu yao kutoka mbele ya watu wako, uliowakomboa kutoka Misri.24Umeiimarisha Israel kama watu wako daima, na wewe, Yahwe, kuwa Mungu wao.25Basi sasa, Yahwe Mungu, ahadi uliyofanya kuhusu mtumishi wako na familia yake iwe imara daima. Ufanye kama ulivyo sema.26Na jina lako liwe kuu daima, ili watu waseme, ‘Yahwe wa majeshi ni Mungu wa Israeli,’ wakati nyumba yangu, Daudi, mtumishi wako itakapokaa imara mbele zako daima.27Kwa maana wewe, Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, umedhihirisha kwa mtumishi wako kwamba utamjengea nyumba. Ndiyo maana mimi, mtumishi wako, nimepata ujasiri kuomba kwako.28Sasa, Bwana Yahwe, wewe ni Mungu, na maneno yako ni amini, na umefanya ahadi hii njema kwa mtumishi wako.29Sasa basi, na ikupendeze kuibariki nyumba ya mtumishi wako, ili iendelee mbele yako daima. Kwa maana wewe, Bwana Yahwe, umeyasema mambo haya, na kwa ahadi yako nyumba ya mtumishi wako itabarikiwa daima.

8

1Ikawa baada ya haya Daudi aliwashambulia Wafilisti na kuwashinda. Hivyo Daudi akaichukua Gathi na vijiji vyake kutoka katika mamlaka ya wafilisti.

2Kisha akaishinda Moabu na akawapima watu wake kwa mstari kwa kuwafanya walale chini juu ya ardhi. Alipima mistari miwili ya kuua, na mstari mmoja kamili kuwahifadhi hai. Hivyo Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakaanza kumlipa kodi.

3Kisha Daudi akamshinda Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, Hadadezeri aliposafiri kuurudisha ufalme wake katika mto Frati.4Daudi aliteka magari 1,700 ya farasi na askari 20,000 waendao kwa miguu. Daudi akawakata miguu farasi wa magari, lakini akahifadhi wakutosha magari mia moja.

5Wakati Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadeziri mfalme wa Soba, Daudi akaua katika Washami watu 22,000.6Daudi akaweka ngome huko Shamu ya Dameski, na Washami wakawa watumishi wake na wakaleta kodi. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alikokwenda.

7Daudi akachukua ngao za dhahabu walizokuwa nazo watumishi wa Hadadezeri naye akazileta Yerusalemu.8Mfalme Daudi akachukua shaba nyingi kutoka Beta na Berosai, miji ya Hadadezeri.

9Wakati Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia kwamba Daudi amelishinda jeshi lote la Hadadezeri,10Tou akamtuma Hadoramu mwanawe kwa mfalme Daudi kumpa salamu na kumbariki, kwa kuwa Daudi alikuwa amepigana na Hadadezeri na kumshinda, maana Hadadezeri alikuwa amepiga vita dhidi ya Tou. Hadoramu akaja pamoja na vitu vya fedha, dhahabu, na shaba.

11Mfalme Daudi akaviweka wakfu vitu hivi kwa ajili ya Yahwe, pamoja na fedha na dhahabu kutoka katika mataifa yote aliyokuwa ameyashinda-12kutoka Shamu, Moabu, Waamoni, Wafilisti, Waamaleki, pamoja na nyara zote alizoziteka kutoka kwa Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba.

13Jina la Daudi likajulikana sana alipowashinda washami katika bonde la Chumvi, pamoja na watu wao wapatao 18,000.

14Akaweka ngome katika Edomu yote, na Waedomu wote wakawa watumishi wake. Yahwe akampa Daudi ushindi kila alipokwenda.

15Daudi akatawala juu ya Israeli yote, naye akatenda kwa haki na usawa kwa watu wote.16Yoabu mwana wa Seruya alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mwenye kuandika taarifa.17Sadoki mwana wa Ahitubu na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Seraya alikuwa mwandishi.18Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa washauri wa mfalme.

9

1Kisha Daudi akasema, “Je, kuna yeyote aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumuonyesha wema kwa ajili ya Yonathani?”

2Alikuwepo mtumishi katika familia ya Sauli jina lake Siba, akaitwa kwa Daudi. Mfalme akamuuliza, “Je wewe ndiye Siba?” Akajibu, “Mimi ni mtumishi wako, ndiye.”

3Hivyo mfalme akasema, “Je hakuna aliyesalia wa familia ya Sauli ambaye naweza kumuonyesha wema wa Mungu?” Siba akamjibu mfalme, “Yonathani ana mwana, ambaye ni mlemavu wa miguu.”

4Mfalme akamwambia, “Yupo wapi?” Siba akamjibu mfalme, “Tazama, yupo katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.”

5Ndipo mfalme Daudi akatuma watu na kumtoa katika nyumba ya Makiri mwana wa Amieli huko Lo Debari.

6Hivyo Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, akaja kwa Daudi naye akainama uso wake hadi katika sakafu kwa kumheshimu Daudi. Daudi akasema, “Mefiboshethi.” Naye akajibu, “Angalia, mimi ni mtumishi wako!”

7Daudi akamwambia, “Usiogope, maana hakika nitakufadhili kwa ajili ya Yonathani baba yako, nami nitakurudishia ardhi yote ya Sauli babu yako, nawe utakula katika meza yangu daima.”

8Mefiboshethi akainama na kusema, “Mtumishi wako ni nani, hata ukamwangalia kwa fadhili mbwa mfu kama nilivyo?”

9Kisha mfalme akamwita Siba, mtumishi wa Sauli, na kumwambia, “Yote yaliyo ya Sauli na familia yake nimempa mjukuu wa bwana wako.10Wewe, wanao, na watumishi wako mtalima mashamba kwa ajili yake nanyi mtavuna mazao ili kwamba mjukuu wa bwana wako apate chakula. Kwa maana Mefiboshethi, mjukuu wa bwana wako, atakula katika meza yangu daima.” Basi Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumishi ishirini.

11Kisha Siba akamwambia mfalme, “Mtumishi wako atafanya yote ambayo bwana wangu mfalme amemwamuru mtumishi wake.” Mfalme akaongeza kusema, “Kwa Mefiboshethi yeye atakula katika meza yangu, kama mmojawapo ya wana wa mfalme.”

12Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo jina lake Mika. Na wote waliokuwa wanaishi katika nyumba ya Siba walikuwa watumishi wa Mefiboshethi.13Hivyo Mefiboshethi akaishi Yerusalemu, naye akala chakula cha daima katika meza ya mfalme, japokuwa alikuwa mlemavu wa miguu yote.

10

1Ikawa baadaye, mfalme wa watu wa Amoni akafa, na Hanuni mwanaye akawa mfalme mahali pake.2Daudi akasema, “Nitamtendea wema Hanuni mwana wa Nahashi, kwa kuwa baba yake alinitendea wema.” Hivyo Daudi akatuma watumishi wake kumfariji Hanuni kwa habari ya baba yake. Watumishi wake wakaingia katika nchi ya watu wa Amoni.3Lakini viongozi wa watu wa Amoni wakamwambia Hanuni bwana wao, “Je, unadhani kwa hakika Daudi anamheshimu baba yako hata ametuma watu kukutia moyo? Daudi hajawatuma watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, kuupeleleza, ili kuuangamiza?4Hivyo Hanuni akawachukua watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia mavazi yao hadi kwenye matako, naye akawaacha waende zao.

5Daudi alipoelezwa kuhusu hili, akatuma watu kwenda kuwalaki, kwa kuwa walikuwa wamefedheheshwa sana. Mfalme akawaambia, “Kaeni Yeriko mpaka ndevu zenu zitakapoota, ndipo mrudi.”

6Watu wa Amoni walipoona kwamba wamenuka kwa Daudi, wakatuma wajumbe na kuwaajiri Washami wa Bethi Rehobu na Soba, askari 20,000 waendao kwa mguu, na mfalme wa Maaka pamoja na watu 1,000, na watu wa Tobu 12,000.

7Daudi aliposikia, akamtuma Yoabu na jeshi lote la askari.8Waamoni wakatoka na wakafanya mistari ya vita katika maingilio ya lango la mji wao, wakati Washami wa Soba na wale wa Rehobu, na watu wa Tobu na Maaka, wakasimama peke yao uwandani.

9Yoabu alipoona mistari ya vita ikimkabili pote mbele na nyuma, alichagua baadhi ya waisraeli wajuao kupigana vizuri na akawapanga dhidi ya Washami.10Na sehemu iliyosalia ya jeshi, akawaweka chini ya Abishai nduguye, naye akawaweka katika mistari ya vita dhidi ya jeshi la Amoni.11Yoabu akasema, “Ikiwa Washami watakuwa na nguvu zaidi juu yangu, kisha wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini ikiwa jeshi la Amoni litakuwa na nguvu zaidi juu yako, nitakuja kukuokoa.12Iweni na nguvu, nasi tujionyeshe kuwa wenye nguvu kwa ajili ya watu wetu na miji ya Mungu wetu, kwa maana Yahwe atatenda yapendezayo kwa ajili ya kusudi lake.

13Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasonga mbele katika vita dhidi ya Washami, waliolazimika kukimbia mbele ya jeshi la Israeli.14Jeshi la Amoni lilipoona kwamba Washami wamekimbia, nao pia wakakimbia kutoka kwa Abishai wakarudi ndani ya mji. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na akarejea Yerusalemu.

15Washami walipoona kwamba wameshindwa na Israeli, walijikusanya pamoja tena.16Kisha Hadareza akatuma kuleta vikosi vya Washami ng'ambo ya Mto Frati. Wakaja Helamu pamoja na Shobaki, mkuu wa jeshi la Hadareza juu yao.

17Daudi alipoambiwa, aliwakusanya Israeli wote pamoja, akavuka Yordani, na akafika Helamu. Washami wakajipanga katika mistari ya vita dhidi ya Daudi na wakapigana naye.18Washami wakakimbia mbele ya Israeli. Daudi akaua askari mia saba wa magari na askari wa farasi elfu arobaini. Shobaki mkuu wa jeshi lao alijeruhiwa na akafa huko.19Wafalme wote waliokuwa watumishi wa Hadareza walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Israeli na wakawa watumishi wao. Hivyo washami wakaogopa kuwasaidia watu wa Amoni tena.

11

1Ikawa wakati wa majira ya kipupwe, wakati ambapo kwa kawaida wafalme huenda vitani, Daudi akamtuma Yoabu, mtumishi wake, na jeshi lote la Israeli. Wakaliaribu jeshi la Amoni na kuuhusuru Raba. Lakini Daudi akakaa Yerusalemu.

2Hivyo ikawa siku moja wakati wa jioni Daudi akaamka kutoka kitandani na akatembea katika dari la kasri. Akiwa pale akamwona mwanamke aliyekuwa akioga, mwanamke yule alikuwa mzuri sana wa kupendeza macho.3Hivyo Daudi akatuma na kuuliza watu waliomfahamu yule mwanamke. Mtu mmoja akasema, “Je huyu siye Bathsheba, binti Eliamu, naye si mke wa Uria mhiti?

4Daudi akatuma wajumbe nao wakamchukua; akaja kwake, na akalala naye (kwani ndio alikuwa amejitakasa kutoka uchafu wake). Kisha akarudi nyumbani kwake.5Mwanamke akawa mjamzito, naye akatuma na kumwambia Daudi; akasema, “Mimi ni mjamzito.”

6Kisha Daudi akatuma watu kwa Yoabu kusema, “Umtume kwangu Uria mhiti.” Hivyo Yoabu akamtuma Uria kwa Daudi.7Uria alipofika, Daudi akamuuliza hali ya Yoabu. Jinsi jeshi lilivyokuwa likiendelea, na jinsi vita vilivyokuwa vinaendelea.8Daudi akamwambia Uria, “Shuka nyumbani kwako, unawe miguu yako.” Hivyo Uria akaondoka katika kasri la mfalme, mfalme akamtumia zawadi kwa Uria alipoondoka.9Lakini Uria akalala pamoja na watumishi wa bwana wake katika lango la kasri, wala hakushuka nyumbani kwake.

10Daudi alipoambiwa, “Uria hakushuka nyumbani kwake,” akamwambia Uria, “Je haukutoka safarini? Kwa nini haukushuka nyumbani kwako?”

11Uria akamjibu Daudi, “Sanduku, na Israeli na Yuda wamo kwenye mahema, na Yoabu na watumishi wa bwana wangu wamepiga hema uwandani. Jinsi gani basi mimi naweza kwenda nyumbani kwangu kula kunywa na kulala na mke wangu? Kwa hakika kama uishivyo, sitafanya hivyo.”

12Hivyo Daudi akamwambia Uria, “Ukae leo pia, kesho nitakuacha uende.” Kwa hiyo uria akakaa Yerusalemu siku hiyo na iliyofuata.13Daudi alipomwita, alikula na kunywa pamoja naye, Daudi akamfanya alewe. Wakati wa jioni Uria akaenda kulala kitandani pake pamoja na watumishi wa bwana wake; hakushuka nyumbani kwake.

14Hivyo asubuhi Daudi akamwandikia Yoabu barua, naye akaituma kwa mkono wa Uria.15Ndani ya barua Daudi aliandika hivi, “Muweke Uria mbele ya vita vikali sana, na kisha, mmwache, ili apigwe na afe.”

16Hivyo Yoabu alipoona mji ukizingirwa, alimuweka Uria katika sehemu aliyojua askari adui wenye nguvu wangekuwa wakipigana.17Wakati watu wa mji walipotoka na kupigana dhidi ya jeshi la Yoabu, baadhi ya askari wa Daudi wakaanguka, na Uria Mhiti pia akauwawa.

18Wakati Yoabu alipotuma neno kwa mfalme kuhusu hali ya vita,19alimwagiza mjumbe, kusema, “Utakapomaliza kumwambia mfalme kuhusu hali ya vita,20yawezekana mfalme akakasirika, naye akakwambia, ‘Kwa nini mlipigana na mji kwa karibu hivyo, hamkujua kwamba wangeweza kushambulia kutokea ukutani?21Ni nani aliyemuua Abimeleki mwana wa Yerubeshethi? Siye mwanamke aliyerusha jiwe la kusagia juu yake kutoka ukutani, hata akafa huko Thebesi? Kwanini basi mliukaribia ukuta jinsi hiyo?’ Nawe umjibu, ‘Uria mtumishi wako amekufa pia.’”

22Hivyo mjumbe akaondoka na kwenda kwa Daudi akamwambia kila jambo ambalo Yoabu alimtuma kusema.23Na mjumbe akamwambia Daudi, “Mwanzoni adui walikuwa na nguvu kuliko sisi; walitukabili uwandani, lakini tukawarudisha nyuma kwenye maingilio ya lango.24Na wapiga mishale wao wakawarushia watumishi wako kutoka ukutani, na baadhi ya watumishi wa mfalme wameuawa, na mtumishi wako Uria mhiti pia ameuawa.”

25Kisha Daudi akamwambia mjumbe, “Mwambie hivi Yoabu, ‘Usiruhusu jambo hili likuhuzunishe, kwa maana upanga huangamiza huyu kama uangamizavyo na mwingine. Vifanye vita vyako kuwa vyenye nguvu zaidi dhidi ya mji, na uuteke.’ Mtie moyo Yoabu.”

26Hivyo mke Uria aliposikia kwamba mme wake amekufa, akaomboleza sana kwa ajili yake.27Huzuni yake ilipoisha, Daudi akatuma na kumchukua kwake katika kasri lake, naye akawa mkewe na akamzalia mwana. Lakini alichokifanya Daudi hakikumpendeza Yahwe.

12

1Kisha Yahwe akamtuma Nathani kwa Daudi. Akaja kwake na kusema, “Kulikuwa na watu wawili katika mji. Mmoja alikuwa tajiri na mwingine alikuwa maskini.2Yule tajiri alikuwa na kundi la ng'ombe na kondoo wengi sana,3lakini maskini hakuwa na chochote isipokuwa mwanakondoo, aliyekuwa amemnunua na kumlisha na kumlea. Akakua pamoja naye na pamoja na watoto wake. Yule mwanakondoo hata alikula naye na kunywa kutoka katika kikombe chake, naye akalala katika mikono yake na alikuwa kama binti kwake.

4Siku moja mgeni akaja kwa tajiri, lakini tajiri hakuwa tayari kuchukua mnyama kutoka katika kundi lake la ng'ombe au kundi la kondoo ili kumuandalia chakula. Badala yake alichukua mwanakondoo wa maskini na akampika kwa ajili ya mgeni wake.”

5Hasira ya Daudi ikawaka dhidi ya tajiri yule, naye akamwambia Nathani kwa hasira, “Kama Yahwe aishivyo, mtu aliyelitenda jambo hili anastahili kufa.6Ni lazima alipe mwanakondoo mara nne zaidi kwa ajili ya kile alichokifanya, na kwa sababu hakuwa na huruma kwa mtu maskini.”

7Ndipo Nathani akamwambia Daudi, “Wewe ndiye yule mtu! Yahweh, Mungu wa Israeli, asema, ‘Nilikutia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli, na nilikuokoa kutoka katika mkono wa Sauli.8Nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake zake mikononi mwako. Nilikupa pia nyumba ya Israeli na Yuda. Na ikiwa hayo yalikuwa kidogo zaidi kwako, ningeweza kukuongezea mengine zaidi.9Hivyo basi kwa nini umedharau maagizo ya Yahwe, hata ukafanya yaliyo maovu mbele zake? Umeua Uria Mhiti kwa upanga na umechukua mkewe kuwa mke wako. Uliua kwa upanga wa jeshi la Amoni.10Hivyo basi upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa kuwa umenidharau na umemchukua mke wa Uria mhiti kuwa mke wako.’11Yahwe asema, ‘Tazama, nitaleta maafa dhidi yako kutoka katika nyumba yako mwenyewe. Nitachukua wake zako, mbele ya macho yako na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako wakati wa mchana.12Kwa maana wewe ulitenda dhambi hii sirini, lakini mimi nitatenda jambo hili wakati wa mchana mbele za Israeli wote.’”

13Ndipo Daudi alipomwambia Nathani, “Nimemtenda dhambi Yahwe.” Nathani akamjibu Daudi, “Yahwe naye ameiachilia dhambi yako. Hautauliwa.14Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umemdharau Yahwe, mtoto aliyezaliwa kwako hakika atakufa.”

15Kisha Nathani akaondoka na kwenda kwake. Yahwe akampiga mtoto ambaye mke wa Uria alimzaa kwa Daudi, naye akaugua sana.16Kisha Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya kijana. Daudi akafunga naye akaingia ndani na kulala usiku wote juu ya sakafu.17Wazee wa nyumba yake wakainuka na kusimama kando yake, ili wamwinue kutoka sakafuni. Lakini hakuinuka, na hakula pamoja nao.

18Ikawa siku ya saba mtoto akafa. Watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia kwamba mtoto amekufa, kwa maana walisema, “Tazama, wakati mtoto alipokuwa hai tuliongea naye, lakini hakuisikiliza sauti yetu. Atakuwaje ikiwa tutamwambia kwamba kijana amekufa?!”

19Daudi alipoona kwamba watumishi wake walikuwa wakinong'onezana, Akatambua kwamba mtoto amekufa. Akawauliza, “Je mtoto amekufa?” Wakajibu, “Amekufa.”

20Kisha Daudi akainuka kutoka sakafuni naye akaoga, akajipaka mafuta, na kubadili mavazi yake. Akaenda katika hema la kukutania na akaabudu pale, kisha akarudi katika kasri lake. Akataka chakula kiletwe, wakamwandalia, naye akala.

21Ndipo watumishi wake walipomwambia, “Kwa nini umefanya jambo hili? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto wakati alipokuwa hai, lakini mtoto alipokufa, ukainuka na kula.”

22Daudi akajibu, “Wakati mtoto alipokuwa hai nilifunga na kulia. Nilisema, “Ni nani ajuaye kwamba Yahwe angeweza kunihurumia mtoto akaishi au sivyo?23Lakini sasa amekufa, hivyo nifungie nini? Je naweza kumrudisha tena? Nitakwenda kwake, lakini yeye hawezi kunirudia.”

24Daudi akamfariji Bethsheba mkewe, akaingia kwake, na akalala naye. Baadaye akazaa mtoto wa kiume, naye akaitwa Selemani. Yahwe akampenda25naye akatuma neno kupitia nabii Nathani kumwita Yedidia, kwa sababu Yahwe alimpenda.

26Basi Yoabu akapigana na Raba, mji wa kifalme wa watu wa Amoni, naye akaiteka ngome yake.27Hivyo Yoabu akatuma wajumbe kwa Daudi na kusema, “Nimepigana na Raba, nami nimeshikilia sehemu inayosambaza maji ya mji.28Kwa hiyo sasa likusanye jeshi lililosalia uhuzingire mji na kuuteka, kwa maana ikiwa nitauteka, utaitwa kwa jina langu.”

29Hivyo Daudi akalikusanya jeshi lote na kwenda Raba; akapigana nao na kuuteka.30Daudi akachukua taji ya dhahabu kutoka katika kichwa cha mfalme wao iliyokuwa na uzito wa talanta, na ilikuwa na jiwe la thamani ndani yake. Taji ikawekwa juu ya kichwa cha Daudi. Kisha akachukua nyara za mji kwa wingi.31Akawatoa watu waliokuwa mjini naye akawalazimisha kufanya kazi kwa misumeno, sululu na shoka; lakini pia akawalazimisha kutengeneza matofali. Daudi akailazimisha miji yote ya watu wa Amoni kufanya kazi hiyo. Kisha Daudi na jeshi lote wakarudi Yerusalemu.

13

1Ikawa baada ya hayo kwamba Amnoni mwana wa Daudi, akamtamani sana Tamari dada yake wa kambo aliyekuwa mzuri, alikuwa tumbo moja na Absalomu, mwana mwingine wa Daudi.2Amnoni akasononeka sana kiasi cha kuugua kwa ajili ya Tamari dada yake. Tamari alikuwa bikra, na hivyo ilionekana haiwezekani Amnoni kufanya neno lolote kwake.

3Lakini Amnoni alikuwa na rafiki jina lake Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi.

4Yehonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. Akamwambia Amnoni, “Kwa nini, mwana wa mfalme, unadhoofika kila siku? Kwa nini huniambii?” Ndipo Amnoni akamjibu, “Nampenda Tamari, dada yake Absalomu ndugu yangu.”

5Ndipo Yehonadabu akamwambia, “Lala kitandani mwako na ujifanye kuwa mgonjwa. Wakati baba yako atakapo kuja kukuona, mwambie, ‘Tafadhali mtume dada yangu Tamari aandae chakula mbele yangu, ili kwamba nikione na kula kutoka mkononi mwake?’”

6Hivyo Amnoni akalala na kujifanya kuwa mgonjwa. Mfalme alipokuja kumwona, Amnoni akamwambia mfalme, “Tafadhari mtume Tamari dada yangu aandae chakula kwa ajili ya ugonjwa wangu mbele yangu ili kwamba nikile kutoka mkononi mwake.”

7Ndipo Daudi katika kasri lake akatuma neno kwa Tamari, kusema, “Nenda katika nyumba ya nduguyo Amnoni na umwandalie chakula.”8Hivyo Tamari akaenda katika nyumba ya Amnoni nduguye alipokuwa amelala. Akachukua donge na kulifinyanga na kuandaa mkate mbele zake, kisha akauoka.9Akachukua kikaangio na kumpa mkate, lakini akakataa kula. Kisha Amnoni akawaambia waliokuwepo, “Kila mtu na aondoke mbali nami.” Hivyo kila mmoja akaondoka.

10Amnoni akamwambia Tamari, “Lete chakula chumbani kwangu nikile katika mkono wako.” Tamari akachukua mkate aliokuwa ameuandaa, na kuuleta katika chumba cha Amnoni kaka yake.11Alipoleta chakula kwake, Amnoni akamshikilia na kumwambia, “Njoo, ulale nami, dada yangu.”

12Yeye akamjibu, “Hapana, kaka yangu, usinilazimishe, kwani hakuna jambo kama hili linapaswa kufanyika katika Israeli. Usifanye jambo la aibu kiasi hiki!13Nitakwenda wapi ili nijiepushe na aibu ambayo jambo hili litaileta juu ya maisha yangu? Na tendo hili litakuonyesha kuwa mpumbavu usiye na aibu katika Israeli yote. Tafadhali, ninakuomba uongee na mfalme. Yeye atakuruhusu unioe.”14Lakini Amnoni hakuweza kumsikiliza. Kwa kuwa alikuwa zaidi akamkamata na akalala naye.

15Kisha Amnoni akamchukia Tamari kwa chuki kuu. Akamchukia zaidi ya jinsi alivyokuwa amemtamani. Amnoni akamwambia, “Inuka na uondoke.”

16Lakini yeye akamjibu, “Hapana! Kwa maana uovu wa kunifanya niondoke ni mmbaya zaidi ya kile ulichonitenda!” Lakini Amnoni hakumsikiliza.

17Badala yake, akamwita mtumishi wake na akasema, “Mwondoe mwanamke huyu mbele yangu, na uufunge mlango nyuma yake.”18Hivyo mtumishi wake akamtoa na kufunga mlango. Tamari alikuwa amevaa vazi lililopambwa kwa uzuri kwani ndivyo binti za wafalme waliobikra walikuwa wakivaa.19Tamari akaweka majivu juu ya kichwa chake na akairarua vazi lake lililopambwa kwa uzuri. Akaweka mikono kichwani mwake na akaenda zake huku akilia kwa sauti.

20Absalomu, kaka yake, akamwambia, “Amnoni, kaka yako, amekuwa nawe? Lakini sasa nyamaza, dada yangu. Yeye ni kaka yako. Usiliweke hili moyoni.” Hivyo Tamari akakaa peke yake katika nyumba ya Absalomu kaka yake.

21Mfalme Daudi aliposikia haya yote, alikasirika sana.22Absalomu hakusema chochote kwa Amnoni, kwa maana Absalomu alimchukia kwa kile alichokifanya, kumdhalilisha Tamari, dada yake.

23Ikawa baada ya miaka miwili mizima Absalomu akawa na wakatao kondoo manyoya wakifanya kazi huko Baali Hazori, ulioko karibu na Efraim, naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme kufika huko.24Absalomu akamwendea mfalme na kusema, “Tazama sasa, mtumishi wako anao wakatao kondoo manyoya. Tafadhali, naomba mfalme na watumishi wake waende nami, mtumishi wako.”

25Mfalme akamjibu Absalomu, “Hapana mwanangu, tusiende sisi sote kwani tutakuwa mzigo kwako.” Absalomu akamsihi mfalme, lakini yeye asikubali kwenda, ila alimbariki Absalomu.

26Kisha Absalomu akasema, “Kama sivyo, basi tafadhali mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi.” Mfalme akamuliza, “Kwa nini Amnoni aende nanyi?”

27Absalomu akamsihi Daudi, hivyo akamruhusu Amnoni na wana wengine wa mfalme kwenda naye.

28Absalomu akawaamuru watumishi wake kusema, “Sikilizeni kwa makini. Amnoni atakapokuwa amelewa mvinyo, na nitakapowaambia, ‘Mpigeni Amnoni,’ msiogope muueni. Je, siyo mimi niliyewaamuru? Muwe jasiri na hodari.”29Hivyo watumishi wa Absalomu wakamtendea Amnoni kama walivyoamriwa. Kisha wana wote wa mfalme wakainuka na kila mmoja akapanda nyumbu wake akakimbia.

30Hata ikawa wakati wakiwa njiani habari zikafika kwa Daudi kusema, “Absalomu ameua wana wote wa mfalme na hakuna hata mmoja aliyesalia.”31Kisha mfalme akainuka na kurarua mavazi yake na kujilaza juu ya sakafu; watumishi wake wote wakasimama karibu naye mavazi yao yameraruriwa.

32Yehonadabu mwana wa Shama, nduguye Daudi, akajibu na kusema, “Bwana wangu asidhani kuwa vijana wote ambao ni wana wa mfalme wameuawa, kwa maana ni Amnoni pekee ndiye aliyeuawa. Absalomu alilipanga jambo hili tangu siku ile Amnoni alivyomdhulumu Tamari, dada yake.33Kwa hiyo basi, bwana wangu mfalme asiiweke taarifa hii moyoni, kudhani kwamba wana wote wa mfalme wameuawa, kwani aliyeuawa ni Amnoni peke yake.”

34Absalomu akakimbia. Mtumishi aliyekuwa akiangalia akainua macho yake na kuona watu wengi wakija njiani kando ya kilima upande wake wa magharibi.35Kisha Yehonadabu akamwambia mfalme, “Tazama, wana wa mfalme wanakuja, kama mtumishi wako alivyosema.”

36Ikawa mara alipomaliza kusema wana wa mfalme wakafika, wakainua sauti zao na kulia. Na mfalme pamoja na watumishi wake wote pia wakalia kwa uchungu.

37Lakini Absalomu akakimbia na kwenda kwa Talmai mwana wa Amihudi, mfalme wa Geshuri. Mfalme akaomboleza kila siku kwa ajili ya mwanaye.38Hivyo Absalomu akakimbia na kwenda Geshuri na akakaa huko kwa miaka mitatu.39Moyo wa mfalme Daudi ukatamani kwenda kumwona Absalomu, kwa maana alikuwa amefarijika kwa habari ya kifo cha Amnoni.

14

1Yoabu mwana wa Seruya akatambua kwamba moyo wa mfalme ulitamani kumwona Absalomu.2Hivyo Yoabu akatuma neno huko Tekoa kumleta kwake mwanamke mwerevu. Akamwambia, “Tafadhali, vaa mavazi ya uombolezaji ujifanye kuwa mwombolezaji. Usijipake mafuta, lakini uwe kama mwanamke ambaye ameomboleza kwa muda mrefu kwa ajili yake aliyekufa.3Kisha ingia kwa mfalme na umwambie maneno nitakayokueleza.” Hivyo Yoabu akamwambia maneno ambayo angeyasema kwa mfalme.

4Wakati mwanamke kutoka Tekoa alipoongea na mfalme, aliinamisha uso wake chini na kusema,

5“Mfalme, nisaidie.” Mfalme akamwambia, “Shida yako ni nini?” Akajibu, Ukweli ni kwamba mimi ni mjane, mme wangu alikufa.6Mimi, mtumishi wako, nilikuwa na wana wawili, wakagombana shambani, na hakukuwa na wa kuwaachanisha. Mmoja wao akampiga mwenziwe na kumwua.7Na sasa ukoo wote umeinuka juu ya mtumishi wako, wanasema, ‘Mtoe aliyempiga nduguye, ili tumuue kulipa uhai wa nduguye aliyeuawa.’ Na hivyo watamwangamiza mrithi. Hivyo watalizima kaa liwakalo nililobakisha, hata kumwondolea mme wangu jina na uzao juu ya uso wa nchi.”

8Hivyo mfalme akamwambia mwanamke, “Nenda nyumbani kwako, nami nitaagiza jambo la kukufanyia.”

9Mwanamke kutoka Tekoa akamjibu mfalme, “Bwana wangu mfalme, hatia na iwe juu yangu na juu ya familia ya baba yangu. Mfalme na kiti chake cha enzi hawana hatia.”

10Mfalme akasema, “Yeyote atakayekwambia neno umlete kwangu, naye hatakugusa tena.”

11Kisha mwanamke akasema, “Tafadhali mfalme amkumbuke Yahwe Mungu wake, ili kwamba mlipa kisasi cha damu asiharibu zaidi, ili kwamba wasimwangamize mwanangu.” Mfalme akajibu, “Kama Mungu aishivyo, hakuna hata unywele mmoja wa mwanao utaanguka chini.”12Kisha mwanamke akasema, “Tafadhali acha mtumishi wako anene neno moja zaidi kwa bwana wangu mfalme.” Akasema, “Sema.”

13Hivyo mwanamke akasema, “Kwa nini basi umetenda kwa hila dhidi ya watu wa Mungu? Maana kwa kusema hivi, mfalme ni kama mtu mwenye hatia, kwa kuwa mfalme hajamrudisha tena mwanaye aliyeondoka.14Kwa maana sisi sote tutakufa, kwa kuwa tu kama maji yamwagwayo juu ya ardhi na kwamba hayawezi kukusanywa tena. Lakini Mungu hatachukua uhai; badala yake, utafuta njia kwa walio mbali kurejeshwa.

15Sasa basi, nimesema jambo hili kwa bwana wangu mfalme, kwa sababu watu wamenitisha. Hivyo mtumishi wako akajinenea nafsini mwake, ‘Sasa nitaongea na mfalme. Huenda mfalme akampa mtumishi wake haja yake.16Kwa maana mfalme atanisikiliza, ili kwamba kumtoa mtumishi wake katika mikono ya mtu ambaye angeniangamiza mimi na mwanangu pamoja, tutoke katika urithi wa Mungu.

17Kisha mtumishi wako akaomba, ‘Yahwe, tafadhali ruhusu neno la bwana wangu mfalme linipe msaada, kwa maana bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu kwa kutofautisha wema na ubaya.’ Yahwe, Mungu na awe pamoja nawe.”

18Ndipo mfalme akajibu na kumwambia yule mwanamke, “Tafadhali usinifiche neno lolote nikuulizalo.” Mwanamke akajibu, “Basi bwana wangu mfalme na aseme sasa.”

19Mfalme akasema, “Je siyo mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu na kusema, “Kama uishivyo bwana wangu mfalme, hakuna awezaye kuelekea mkono wa kulia wala wa kushoto kwa yale bwana wangu mfalme aliyosema. Ni mtumishi wako Yoabu aliyeniambia na kuniagiza kusema kile mtumishi wako alichokisema.20Mtumishi wako Yoabu amefanya hivi ili kubadilisha hali ya kile kinachotendeka. Bwana wangu ni mwenye akili kama hekima ya malaika wa Mungu, ajuaye yote yatendekayo ndani ya nchi.”

21Hivyo mfalme akamwambia Yoabu, “Tazama, nitatenda jambo hili. Nenda na umrudishe huyo kijana Absalomu.”

22Hivyo Yoabu akainamisha uso wake chini juu ya ardhi katika heshima na shukrani kwa mfalme. Yoabu akasema, “Mtumishi wako amejua kwamba amepata neema mbele zako, bwana wangu, mfalme, kwa vile mfalme amempa mtumishi wake haja ya moyo wake.” Ycv

23Hivyo Yoabu akainuka na kwenda Geshuri, akamrejesha Absalomu Yerusalemu tena.24Mfalme akasema, “Na arudi nyumbani kwake, lakini hasinione uso wangu.” Hivyo Absalomu akarudi katika nyumba yake mwenyewe, na hakuweza kuuona uso wa mfalme.

25Hakukuwa na mtu katika Israeli aliyesifiwa kwa urembo wake kama Absalomu. Kutoka katika wayo wa mguu wake hadi katika utosi wake hakuwa na waa lolote.26Alipokata nywele za kichwa chake mwishoni mwa kila mwaka, kwa sababu zilikuwa nzito juu yake, alipima nywele zake zaidi ya shekeli mia mbili, kwa kiwango cha kipimo cha mfalme.27Kwake Absalomu walizaliwa wana watatu na binti mmoja, jina lake Tamari. Alikuwa mwanamke mzuri.

28Absalomu akaishi Yerusalem miaka miwili pasipo kuona uso wa mfalme.29Kisha Absalomu akatuma neno kwa Yoabu ili ampeleke kwa mfalme, lakini Yoabu hakuenda kwake. Hivyo Absalomu akatuma neno mara ya pili, lakini Yoabu hakuja bado.

30Hivyo Absalomu akawaambia watumishi wake, “Tazameni, shamba la Yoabu lipo karibu na langu, naye ana shayiri kule. Nendeni mkalichome moto.” Hivyo watumishi wa Absalomu wakalichoma moto lile shamba.

31Kisha Yoabu akainuka na kwenda nyumbani kwa Absalomu akamwambia, “Kwa nini watumishi wako wamelichoma moto shamba langu?”32Absalomu akamjibu Yoabu, “Tazama nilituma neno kwako kusema, ‘Njoo ili nikutume kwa mfalme kusema, kwa nini nilikuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningesalia huko. Kwa hivyo sasa niache niuone uso wa mfalme na kama nina hatia basi na aniue.”33Hivyo Yoabu akaenda kwa mfalme na kumwambia. Mfalme alipomwita, Absalomu alikuja kwa mfalme na akainama hadi ardhini mbele ya mfalme na mfalme akambusu Absalomu.

15

1Ikawa baada ya haya Absalomu akaandaa gari la farasi na farasi kwa ajili yake pamoja na watu hamsini wa kwenda mbele zake.2Absalomu alikuwa akiamka mapema na kusimama kando ya njia iliyoelekea katika lango la mji. Mtu yeyote aliyekuwa na shauri la kuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu, Absalomu alimwita na kumuuliza, “Unatoka mji upi?” Na mtu yule hujibu, Mtumishi wako anatoka mojawapo ya kabila za Israeli.”3Hivyo Absalomu angemwambia, “Tazama, shitaka lako ni jema na la haki, lakini hakuna aliyepewa mamlaka na mfalme kusikiliza shitaka lako.”4Tena Absalomu huongeza, “Natamani kwamba ningefanywa mwamuzi ndani ya nchi ili kwamba kila mtu aliye na shitaka angeweza kuja kwangu nami ningempa haki.”

5Hivyo ikawa kila mtu aliyekuja kumheshimu Absalomu yeye angenyosha mkono na kumshika na kumbusu.6Absalomu alifanya hivi kwa Israeli wote waliokuja kwa mfalme kwa ajili ya hukumu. Hivyo Absalomu akaipotosha mioyo ya watu wa Israeli.

7Ikawa mwishoni mwa miaka minne Absalomu akamwambia mfalme, “Tafadhali niruhusu niende ili nitimize nadhili niliyoiweka kwa Yahwe huko Hebroni.8Kwa maana mtumishi wako aliweka nadhili alipokuwako Geshuri katika Shamu akisema, ‘Ikiwa Yahwe kweli atanirejesha Yerusalemu, ndipo nitamwabudu yeye.”

9Hivyo mfalme akamwambia, “Nenda kwa amani.” Absalomu akainuka na kwenda Hebroni.

10Kisha Absalomu akatuma wapelelezi katika jamaa zote za Israeli, kusema, “Mara msikiapo sauti ya tarumbeta semeni, ‘Absalomu anatawala katika Hebroni.”11Watu mia mbili waliokuwa wamealikwa kutoka Yerusalemu wakaenda na Absalomu. Wakaenda katika ujinga wao bila kujua Absalomu alichokipanga.12Wakati Absalomu akitoa dhabihu, alituma watu kwa Ahithofeli katika mji wake huko Gilo. Yeye alikuwa mshauri wa Daudi. Fitina za Absalomu zikawa na nguvu kwa kuwa watu waliomfuata waliendelea kuongezeka.

13Mjumbe akaja kwa Daudi na kusema, “Mioyo ya watu wa Israeli inaambatana na Absalomu.”

14Hivyo Daudi akawaambia watumishi wake waliokuwa pamoja naye huko Yerusalemu, “Haya na tuinuke na kukimbia kwani hakuna hata mmoja atakayeokoka kwa Absalomu. Jiandaeni kuondoka mara moja asije akatupata mara hata akasababisha madhara juu yetu na kuushambulia mji kwa makali ya upanga.”

15Watumishi wa mfalme wakamwambia, “Tazama, watumishi wako wapo tiyari kufanya lolote bwana wetu mfalme atakaloamua.

16Mfalme akaondoka na familia yake yote pamoja naye, lakini mfalme akawaacha wanawake kumi waliokuwa masuria wa mfalme ili walitunze kasri.17Baada ya mfalme kwenda na watu wote pamoja naye, wakasimama katika nyumba ya mwisho.18Watumishi wako wote wakaenda pamoja naye na mbele yake wakaenda Wakerethi na Wapelethi, na Wagiti 600 wote waliokuwa wamemfuata kutoka Gathi.

19Kisha mfalme akamwambia Itai Mgiti, “Kwa nini wewe pia uende nasi? Rudi na ukae na mfalme Absalomu kwa kuwa wewe ni mgeni tena mfungwa. Rudi mahali pako mwenyewe.20Kwani ni jana tu umeondoka, kwa nini nikufanye uzunguke nasi popote? Hata sijui niendako. Hivyo rudi pamoja na wenzako. Utiifu na uaminifu viambatane nawe.”

21Lakini Itai akamjibu mfalme na kusema, “Kama Yahwe aishivyo na kama bwana wangu mfalme aishivyo, kwa hakika mahali popote bwana wangu mfalme aendako, mtumishi wako pia ndipo atakapokwenda, kwamba ni maisha au kifo.”

22Hivyo Daudi akamwambia Itai, haya tangulia uende pamoja nasi.” Hivyo Itai Mgiti akaenda pamoja na mfalme, pamoja na watu wake wote na familia zao zote.

23Nchi yote ikalia kwa sauti kama watu walivyokuwa wakivuka Bonde la Kidroni, na pia mfalme naye akivuka. Watu wote wakasafiri kuelekea nyikani.

24Walikuwepo pia Sadoki pamoja na Walawi wote wamebeba sanduku la Mungu la agano. Wakaliweka sanduku la Mungu chini na kisha Abiathari akaungana nao. Wakasubiri mpaka watu wote wakapita kutoka mjini.

25Mfalme akamwambia Sadoki, “Ulirudishe sanduku la Mungu mjini. Ikiwa nitaona neema machoni pa Yahwe atanirudisha na kunionyesha tena sanduku na mahali likaapo.26Lakini ikiwa atasema, ‘Sipendezwi nawe,’ tazama mimi nipo hapa, na anitendee yaliyo mema machoni pake.”

27Pia mfalme akamwambia Sadoki kuhani, “Je wewe siyo mwonaji? Rudi mjini kwa amani na wanao wawili, Ahimaazi mwanao na Yonathani mwana wa Abiathari.28Tazama nitasubiri katika vivuko vya nyikani mpaka nitakapo pata neno kutoka kwenu kunipasha habari.”29Hivyo Sadoki na Abiathari wakalirudisha sanduku la Mungu Yerusalemu nao wakakaa humo.

30Lakini Daudi akaenda bila viatu huku akilia hata Mlima wa Mizeituni, naye alikuwa amefunika kichwa chake. Kila mtu miongoni mwao waliokuwa pamoja naye akafunika kichwa chake, nao wakaenda huku wakilia.31Mtu mmoja akamwambia Daudi akisema, “Ahithofeli ni miongoni mwa wafitini walio pamoja na Absalomu.” Hivyo Daudi akaomba, “Ee Yahwe, tafadhali badili ushauri wa Ahithofeli kuwa upumbavu.”

32Ikawa Daudi alipofika juu njiani mahala Mungu alipokuwa akiabudiwa, Hushai Mwarki akaja kumlaki vazi lake likiwa limeraruliwa na mavumbi kichwani pake.33Daudi akamwambia, “Ikiwa utaenda nami utakuwa mzigo kwangu.34Lakini ukirudi mjini na kumwambia Absalomu, ‘Nitakuwa mtumishi wa mfalme kama nilivyokuwa mtumishi wa baba yako, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako,’ ndipo utayageuza mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu.35Je haunao pamoja nawe Sadoki na Abiathari makuhani? Hivyo chochote ukisikiacho katika kasri, uwaambie Sadoki na Abiathari makuhani.36Tazama wanao pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani mwana wa Abiathari. Mniletee habari juu ya kila mnachokisikia.”

37Hivyo Hushai, rafiki wa Daudi, akaja mjini wakati Absalomu anafika na kuingia Yerusalemu.

16

1Daudi alipokuwa amekwenda kitambo juu ya kilele cha kilima, Siba mtumishi wa Mefiboshethi akaja kumlaki akiwa na punda wawili waliokuwa wamebeba vipande mia mbili vya mikate, vishada mia moja vya mizeituni, vishada mia moja vya tini na mfuko wa ngozi uliojaa mvinyo.

2Mfalme akamuuliza Siba, “Kwa nini umeleta hivi vitu?” Siba akajibu, “Punda ni kwa ajili ya familia yako kupanda, mikate na matunda ni kwa ajili ya matumizi ya askari wako, na mvinyo ni kwa ajili ya kunywa kwa yeyote atakayezimia nyikani.”

3Mfalme akauliza, “Na mjukuu wa bwana wako yuko wapi?” Siba akamjibu mfalme, “Tazama, yeye amesalia Yerusalemu kwa maana alisema, ‘Leo nyumba ya Israeli itanirudishia ufalme wa baba yangu.”

4Kisha mfalme akamwambia Siba, “Tazama, yote yaliyomilikiwa na Mefiboshethi sasa yatakuwa yako.” Siba akajibu, “Nainama kwa unyenyekevu kwako bwana wangu mfalme. Na nipate kibali mbele zako.”

5Mfalme Daudi alipokaribia Bahurimu, akaja mtu kutoka katika ukoo wa Sauli, jina lake Shimei mwana wa Gera. Kadiri alivyokuwa akitembea alikuwa akilaani.6Akamrushia Daudi mawe na maofisa wa mfalme, bila kujali jeshi na walinzi wa mfalme waliokuwa kulia na kushoto mwa mfalme.7Shimei akalaani, “Nenda zako, toka hapa, mwovu wewe, mtu wa damu!8Yahwe amelipa yote kwa ajili ya damu ya familia ya Sauli, ambaye unatawala badala yake. Yahwe ameweka ufalme katika mkono wa Absalomu mwanao. Na sasa umeangamia kwa kuwa wewe ni mtu wa damu.”

9Ndipo Abishai mwana wa Seruya, akamwambia mfalme, “Kwa nini mbwa mfu anamlaani bwana wangu mfalme? Tafadhali niache niende nikamwondolee kichwa chake.”

10Lakini mfalme akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya? Pengine ananilaani kwa kuwa Yahwe amemwambia, ‘Mlaani Daudi.’ Nani sasa awezaye kumwambia, ‘Kwa nini unamlaani mfalme.”

11Hivyo Daudi akamwambia Abishai na watumishi wake wote, “Tazameni, mwanangu aliyezaliwa kutoka katika mwili wangu anatafuta uhai wangu. “Si zaidi sana mbenjamini huyu akatamani anguko langu? Mwacheni alaani, kwa maana Yahwe amemwamuru kufanya hivyo.12Huenda Yahwe akaangalia taabu iliyonijia, na kunirudishia mema kwa jinsi nilivyolaaniwa leo.”13Hivyo Daudi na watu wake wakaendelea njiani wakati Shimei kando yake ubavuni mwa mlima, aliendelea kulaani na kumrushia mavumbi na mawe huku akienda.14Kisha mfalme na watu wake wote wakachoka, na akapumzika wakati wa usiku walipopumzika wote.

15Absalomu na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye wakaja Yerusalemu na Ahithofeli alikuwa pamoja naye.16Ikawa Hushai Mwarki, rafiki yake Daudi, akaja kwa Absalomu, naye akamwambia Absalomu, “Mfalme aishi daima! Mfalme aishi daima.”

17Absalomu akamwambia Hushai, “Je huu ndio utiifu wako kwa rafiki yako? Kwa nini haukwenda pamoja naye?”

18Hushai akamwambia Absalomu, “Hapana! Badala yake, yule ambaye Yahwe, watu hawa na watu wote wa Israeli wamemchagua huyo ndiye nitakaye kuwa upande wake na ndiye nitakaye kaa naye.19Kwani ni nani ninayepaswa kumtumikia? Je sipaswi kutumika mbele za mwana wake? Kama nilivyotumika mbele za baba yako ndivyo nitakavyofanya mbele zako”

20Kisha Absalomu akamwambia Ahithofeli, “Tupe shauri lako kuhusu tunachopaswa kufanya.”

21Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Nenda kwa masuria wa baba yako aliowaacha kutunza kasri, na Waisraeli wote watasikia kwamba umekuwa chukizo kwa baba yako. Kisha mikono ya wote walio pamoja nawe itatiwa nguvu.”22Hivyo wakasimamisha hema kwa ajili ya Absalomu juu ya kasiri na, Absalomu akalala na masuria wa baba yake mbele za Israeli wote.

23Nyakati hizo ushauri aliokuwa akitoa Ahithofeli ulikuwa ni kama mtu anavyosikia kutoka katika kinywa cha Mungu mwenyewe. Hivyo ndivyo jinsi ushauri wa Ahithofeli ulivyoonekana kwa Daudi na Absalomu.

17

1Kisha Ahithofeli akamwambia Absalomu, “Niruhusu sasa nichague watu 12,000 nami nitaondoka na kumfuatia Daudi usiku huu.2Nitampata kwa ghafla wakati amechoka na dhaifu nami nitamstukiza kwa hofu. Watu waliopamoja naye watakimbia nami nitamshambulia mfalme peke yake.3Nitawarejesha watu wote kwako kama bibi harusi ajavyo kwa bwana wake, na watu wote watakuwa katika amani chini yako.”4Alichokisema Ahithofeli kikampendeza mfalme na wazee wote wa Israeli.

5Kisha Absalomu akasema, “Sasa mwiteni pia Hushai Mwarki ili tusikie yeye pia anavyosema.”6Hushai alipofika kwa Absalomu, Absalomu akamweleza kile ambacho Ahithofeli alikuwa amesema na kisha akamwuliza Hushai, “Je tufanye alivyosema Ahithofeli? Ikiwa hapana, tueleze kile unachoshauri.”

7Hivyo Hushai akamwambia Absalomu, “Ushauri aliotoa Ahithofeli siyo mzuri kwa wakati huu.”8Hushai akaongeza, “Unamjua baba yako na kwamba watu wake ni mashujaa na kwa sasa wanauchungu, ni kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake mwituni. Baba yako ni mtu wa vita; hatalala na jeshi usiku huu.9Tazama, kwa wakati huu pengine amejificha katika shimo fulani au mahali pengine. Itakuwa kwamba baadhi ya watu wako watakapokuwa wameuawa mwanzoni mwa shambulio hata kila mtu atakayesikia atasema, mauaji yamefanyika kwa askari wanaomfuata Absalomu.’10Kisha hata askari jasiri zaidi ambao moyo wao ni kama moyo wa simba, wataogopa kwa kuwa Israeli yote inajua kwamba baba yako ni mtu mwenye nguvu na kwamba watu alionao ni wenye nguvu sana.

11Hivyo ninashauri kwamba Israeli wote wakutanike kwako pamoja kutoka Dani hadi Beersheba, wengi kama mchanga ufuoni mwa bahari na kwamba wewe mwenyewe uende vitani.12Kisha tutampata popote atakapokuwa nasi tutamfunika kama umande uangukavyo juu ya nchi. Hatutamwachia hata mmoja aliye hai kati ya watu wake wala yeye mwenyewe.13Ikiwa ataingia ndani ya mji kisha Israeli wote tutaleta kamba juu ya mji huo na kuukokotea mtoni, hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia.”

14Kisha Absalomu na watu wa Israeli wakasema, “Shauri la Hushai Mwarki ni jema kuliko lile la Ahithofeli. Yahwe aliwafanya wakatae shauri jema la Ahithofeli ili kumwangamiza Absalomu.

15Kisha Hushai akawaambia Sadoki na Abiathari makuhani, “Ahithofeli alimshauri Absalomu na wazee wa Israeli hivi na hivi, lakini mimi nimeshauri vinginevyo.16Sasa basi, nendeni haraka na mmpashe habari Daudi kusema, ‘Usipige kambi usiku huu katika vivuko vya Araba, lakini kwa namna yoyote vukeni, tofauti na hapo mfalme atamezwa pamoja na watu wote walio pamoja naye.”

17Yonathani na Ahimaasi walikuwako katika chemichemi za En Rogeli. Hivyo kijakazi mmoja alikuwa akienda na kuwapasha habari waliyopaswa kuifahamu, ili kwamba wasihatarishe maisha yao kwa kuonekana wakiingia mjini. Ujumbe ulipofika ndipo walikuwa wanaenda kumpasha habari mfalme Daudi.18Lakini kijana mmoja akawaona wakati huo na akamwambia Absalomu. Hivyo Yonathani na Ahimaasi wakaenda kwa haraka na wakaingia katika nyumba ya mtu mmoja huko Bahurimu, aliyekuwa na kisima uani mwake, wakashuka humo.19Mke wa mtu huyo akachukua kifuniko na kukikufunika kwenye mlango wa kisima kisha akaanika nafaka juu yake, hivyo hakuna aliyejua kwamba Yonathani na Ahimaasi walikuwa kisimani.

20Watu wa Absalomu wakaja kwa mwanamke na kumuuliza, “Ahimaasi na Yonathani wako wapi?” Mwanamke akawaambia, “Wamevuka mto.” Hivyo baada ya kuwatafuta bila kuwaona, wakarejea Yerusalemu.21Ikawa baada yao kuondoka Yonathani na Ahimaasi wakatoka ndani ya kisima. Wakaenda kumtaarifu mfalme Daudi; wakamwambia, “Inuka na uvuke maji haraka kwa maana Ahithofeli ametoa mashauri haya na haya juu yako.”22Kisha Daudi akainuka pamoja na watu wote waliokuwa pamoja naye, nao wakauvuka Yordani. Hata ilipofika alfajiri hakuna hata mmoja aliyesalia kwa kutouvuka Yordani.

23Ikawa Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, akapanda punda wake na kuondoka. Akaenda nyumbani katika mji wake mwenyewe, akaweka mambo yake katika utaratibu na kisha akajinyonga. Kwa hiyo akafa na kuzikwa katika kaburi la baba yake.

24Ndipo Daudi akaja Mahanaimu. Lakini Absalomu yeye akavuka Yordani yeye pamoja na watu wote wa Israeli waliokuwa pamoja naye.25Absalomu alikuwa amemweka Amasa juu ya jeshi badala ya Yoabu. Naye huyo Amasa alikuwa mwana wa Yetheri Mwishmaeli, aliyekuwa ameenda kwa Abigaili, aliyekuwa binti wa Nahashi na dada wa Seruya, mamaye Yoabu.26Kisha Israeli na Absalomu wakapiga kambi katika nchi ya Gileadi.

27Ikawa wakati Daudi alipokuwa amekuja Mahanaimu, huyo Shobi mwana wa Nahashi kutoka Raba ya Waamoni na Makiri mwana wa Amieli wa kutoka Lo Debari, na Berzilai Mgileadi wa Rogelimu,28wakaleta magodoro na blanketi, mabakuri na vyungu, na ngano, unga wa shayiri, nafaka zilizokaangwa, maharage, dengu,29asali, siagi, kondoo na samli, ili kwamba Daudi na watu waliokuwa pamoja naye waweze kula. Kwani walisema, “Watu wana njaa, wamechoka na wana kiu huko nyikani.”

18

1Daudi akawahesabu askari waliokuwa pamoja naye na akaweka akida wa elfu na akida wa mia juu yao.2Kisha Daudi akalipeleka jeshi, theluthi moja chini ya Yoabu, theluthi nyingine chini ya Abishai mwana wa Seruya, ndugu wa Yoabu, na theluthi nyingine tena chini ya Itai Mgiti. Mfalme akaliambia jeshi, “Kwa hakika mimi mwenyewe pia nitakwenda pamoja nanyi.

3Lakini watu wakasema, “Wewe usiende vitani, kwani ikiwa tutakimbia hawatatujali sisi, ama nusu yetu wakifa hawatajali. Lakini wewe ni zaidi ya elfu kumi yetu sisi! Kwa hiyo ni afadhali zaidi ukitusaidia ukiwa mjini.”

4Hivyo mfalme akawajibu, “Nitafanya lolote lionekanalo jema machoni penu.” Mfalme akasimama kati ya lango la mji wakati jeshi lilipoondoka katika mamia na katika maelfu.

5Mfalme akawaagiza Yoabu, Abishai, na Itai akisema, “Mmtendee huyo kijana, Absalomu, kwa upole kwa ajili yangu.” Watu wote wakasikia jinsi mfalme alivyowaagiza maakida kuhusu Absalomu.

6Hivyo jeshi likaenda nyikani dhidi ya Israeli; vita ikaenea katika msitu wa Efraimu.7Jeshi la Israeli likashindwa mbele ya askari wa Daudi; kulikuwa na machinjo makuu kwa watu 20,000 siku hiyo.8Vita ikaenea katika eneo lote na watu wengi wakaangamizwa na msitu kuliko upanga.

9Ikatukia kwamba Absalomu akakutana na askari wa Daudi. Absalomu alikuwa amepanda juu ya nyumbu wake na nyumbu akapita chini ya matawi manene ya mti wa mwaloni, na kichwa chake kikanaswa katika matawi ya mti. Akaachwa akining'inia kati ya nchi na anga wakati nyumbu alipoendelea mbele.

10Mtu mmoja akaona lililotukia na akamwambia Yoabu, “Tazama, nilimuona Absalomu akining'inia katika mwaloni!”

11Yoabu akamwambia aliyemwambia kuhusu Absalomu, “Tazama! Ulimuona! Kwa nini haukumpiga hata chini. Ningekupa shekeli kumi za fedha na mkanda.”

12Yule mtu akamjibu Yoabu, “Hata kama ningepewa shekeli elfu za fedha hata hivyo nisingeinua mkono wangu juu ya mwana wa mfalme, kwa maana sisi sote tulimsikia mfalme akiwaagiza wewe, Abishai na Itai akisema, mtu asimguse huyo kijana Absalomu.’13Ikiwa ningehatarisha maisha yangu kwa uongo (na hakuna jambo linalofichika kwa mfalme), ungejitenga nami.”

14Ndipo Yoabu akasema, “Sitakusubiri.” Kisha akachukua mishale mitatu mkononi mwake na akairusha katika moyo wa Absalomu wakati yu ngali hai na amening'inia katika mwaloni.15Kisha vijana kumi waliochukua silaha za Yoabu wakamzunguka Absalomu, wakampiga na kumuua.

16Kisha Yoabu akapiga tarumbeta na jeshi likarudi kutoka kuwafuatia Israeli, hivyo Yoabu akalirudisha jeshi.17Wakamchukua Absalomu na kumtupa katika shimo kubwa msituni; wakauzika mwili wake chini ya rundo kubwa la mawe, wakati Israeli wote walikimbia kila mtu hemani mwake.

18Wakati Absalomu alipokuwa yungali hai alijijengea nguzo kubwa ya jiwe katika Bonde la Mfalme, kwani alisema, “Sina mwana wa kuchukua kumbukumbu ya jina langu.” Akaiita nguzo kwa jina lake, hivyo inaitwa Mnara wa Absalomu hata leo.

19Kisha Ahimaasi mwana wa Sadoki akasema, “Niruhusu niende kwa mfalme na habari njema, jinsi Yahwe alivyomuokoa kutoka mkono wa adui zake.”

20Yoabu akamjibu, “Wewe hautakuwa mchukua habari leo; utafanya hivyo siku nyingine. Leo hautachukua habari yoyote kwa maana mwana wa mfalme ameuawa.”

21Ndipo Yoabu akamwambia Mkushi, “Nenda umwambia mfalme ulichokiona.” Mkushi akamuinamia Yoabu, na kisha akakimbia.

22Kisha tena, Ahimaasi mwana wa Sadoki akamwambia Yoabu, “Pamoja na yote yanayoweza kutokea, tafadhali niruhusu nami pia niende nimfuate Mkushi.” Yoabu akajibu, “Mwanangu kwa nini unataka kwenda, hautapata thawabu yoyote kwa ajili ya habari hii?”

23“Vyovyote itakavyokuwa niache niende,” Ahimaasi alijibu. Hivyo Yoabu akamjibu, “Nenda.” Ndipo Ahimaasi akakimbia kwa njia ya tambarare na akampita Mkushi.

24Basi Daudi alikuwa amekaa kati ya lango la ndani na lango la nje. Na mlinzi alikuwa juu ya lango ukutani naye akainua macho yake. Alipokuwa akiangalia, akamwona mtu anakaribia huku akikimbia peke yake.25Mlinzi akaita kwa sauti na kumwambia mfalme. Ndipo mfalme akasema, “Ikiwa yupo peke yake ana habari katika kinywa chake.” Mkimbiaji akasogea na kuukaribia mji.

26Kisha mlinzi akaona mtu mwingine aliyekuwa anakimbia, naye akamwambia bawabu; kusema, “Tazama, kuna mtu mwingine anakimbia peke yake.” Mfalme akasema, “Yeye pia analeta habari.”

27Ndipo mlinzi akasema, Nadhani kukimbia kwake mtu aliye mbele ni kama kukimbia kwake Ahimaasi mwana wa Sadoki.” Mfalme akasema, “Yeye ni mtu mwema naye anakuja na habari njema.”

28Ndipo Ahimaasi akaita na kumwambia mfalme, “Yote ni mema.” Kisha akainama yeye mwenyewe uso wake chini mbele ya mfalme na kusema, Atukuzwe Yahwe Mungu wako, aliyewatoa watu walioinua mkono wao kinyume cha bwana wangu mfalme.”

29Hivyo mfalme akauliza, “Je huyo kijana Absalomu hajambo?” Ahimaasi akajibu, “Wakati Yoabu ananituma kwako mfalme, mimi mtumishi wa mfalme, niliona fujo kubwa sana lakini sikutambua ilihusu nini.”

30Mfalme akamwambia, “Geuka usimame kando.” Hivyo Ahimaasi akageuka na kusimama.

31Mara Mkushi akafika na kusema, “Kuna habari njema kwa bwana wangu mfalme kwa kuwa leo Yahwe amekulipia kisasi kwa wale wote walioinuka kinyume chako.”

32Ndipo mfalme akamuuliza, “Je, huyo kijana Absalomu ni mzima?” Mkushi akajibu, “Adui wa bwana wangu mfalme na wote wainukao kukudhuru na wawe kama huyo kijana.”

33Ndipo mfalme alipohuzunishwa sana, naye akaenda chumbani juu ya lango na kulia. Kadili alivyokwenda aliomboleza, “Mwanangu Absalomu, mwanangu, mwanangu Absalomu! Afadhali ningekufa badala yako, Absalomu, mwanangu, mwanangu!”

19

1Yoabu akaambiwa, “Tazama, mfalme analia na kumuomboleza Absalomu.”2Hivyo siku ile ushindi uligeuzwa kuwa maombolezo kwa jeshi lote, kwa maana jeshi likasikia ikisemwa siku hiyo, “Mfalme anaomboleza kwa ajili ya mwanaye.”3Siku ile askari waliingia mjini kwa kunyemelea kimyakimya kama watu waonao haya baada ya kukimbia vitani.4Mfalme akafunika uso wake na kulia kwa sauti, “Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwangangu!”

5Ndipo Yoabu akaingia ndani kwa mfalme na kumwambia, “Leo umeziaibisha nyuso za askari wako, waliookoa maisha yako leo, maisha ya wanao na binti zako, maisha ya wake zako na maisha ya masuria wako,6kwa maana wawapenda wakuchukiao na kuwachukia wakupendao. Kwa kuwa leo umeonyesha kwamba maakida na askari si chochote kwako. Natambua sasa kwamba kama Absalomu angesalia na sisi sote tungekufa hilo lingekufurahisha.7Sasa basi, inuka na uende kuongea na askari wako kwa upole, kwani nakuapia kwa Yahwe, ikiwa hutakwenda hakuna mtu hata mmoja atakayesalia nawe usiku huu. Na hii itakuwa vibaya sana kwako kuliko madhara yoyote yaliyowai kukupata tangu ujana wako.”

8Hivyo mfalme akainuka na kuketi kati ya lango la mji, watu wote wakaambiwa, “Tazama, mfalme ameketi kati ya lango.” Ndipo watu wote wakaja mbele za mfalme. Walakini, Israeli walikuwa wamekimbia kila mtu hemani mwake.

9Watu wote wakahojiana wao kwa wao katika jamaa zote za Israeli wakisema, “Mfalme alituokoa na mkono wa adui zetu. Alitukomboa na mkono wa Wafilisti lakini sasa ameikimbia nchi mbele ya Absalomu.10Na Absalomu tuliyemtia mafuta juu yetu amekufa vitani. Hivyo kwa nini hatuongei juu ya kumrudisha mfalme tena?”

11Mfalme Daudi akatuma kwa Sadoki na kwa Abiathari makuhani akisema, “Ongeeni na wazee wa Yuda mkisema, Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme kwenye kasri lake tena, kwa vile usemi wa Israeli wote unamtaka mfalme arudi katika kasri lake?12Ninyi ni ndugu zangu, mwili na mifupa yangu. Kwa nini basi mmekuwa wa mwisho kumrudisha mfalme?”13Na mwambieni Amasa, “Je wewe si mwili na mfupa wangu? Mungu anifanyie hivyo na kuzidi pia ikiwa hautakuwa jemedari wa jeshi langu tangu sasa na baadaye mahali pa Yoabu.

14Naye akaishinda mioyo ya watu wote wa Yuda kama mtu mmoja. Wakatuma kwa mfalme wakisema, “Rudi sasa na watu wako wote.”15Hivyo mfalme akarudi naye akaja Yordani. Na watu wa Yuda wakaja Gilgali kwenda kumlaki mfalme ili kumvusha mfalme juu ya Yordani.

16Shimei mwana wa Gera, Mbenjamini, kutoka Bahurimu, akaharakisha kushuka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki mfalme Daudi.17Kulikuwa na watu 1,000 kutoka Benjamini waliokuwa pamoja naye, na Siba mtumishi wa Sauli na wanawe kumi na watano na watumishi wake ishirini walikuwa pamoja naye. Wakavuka Yordani mbele za mfalme.18Wakavuka ili kuivusha familia ya mfalme na kumfanyia lolote aliloona jema. Shimei mwana wa Gera akainama chini mbele za mfalme mara alipoanza kuuvuka Yordani.

19Shimei akamwambia mfalme, “Bwana wangu asinione mwenye hatia au kuyaweka moyoni ambayo mtumishi wake alifanya kwa ukaidi siku bwana wangu mfalme alipoondoka Yerusalemu. Tafadhali, mfalme na asiyaweke moyoni.20Kwa maana mtumishi wako anatambua kwamba amekosa. Tazama, ndiyo maana nimekuja leo wa kwanza katika nyumba ya Yusufu ili kumlaki bwana wangu mfalme.”

21Lakini Abishai mwana wa Seruya akajibu na kusema, “Je Shimei asife kwa hili kwa vile alivyomlaani mtiwa mafuta wa Yahweh?”

22Ndipo Daudi akasema, “Nifanye nini nanyi enyi wana wa Seruya, hata leo mkawa adui zangu? Je mtu yeyote atauawa leo katika Israeli? Kwani sijui kama leo mimi ni mfalme juu ya Israeli?23Hivyo mfalme akamwambia Shimei, “Hautakufa.” Mfalme akamuahidi kwa kiapo.

24Kisha Mefiboshethi mwana wa Sauli akashuka ili kumlaki mfalme. Hakuwa ameivalisha miguu yake wala kunyoa ndevu zake wala kufua nguo zake tangu siku mfalme alipoondoka hata siku aliporudi kwa amani.25Na hivyo alipotoka Yerusalemu ili kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, “Mefiboshethi kwa nini haukwenda pamoja nami?”

26Akajibu, “Bwana wangu mfalme mtumishi wangu alinidanganya, kwani nilisema, nitapanda juu ya punda ili niende na mfalme, kwa kuwa mtumishi wako ni mlemavu.’27Mtumishi wangu Siba amenisemea uongo, mtumishi wako, kwa bwana wangu mfalme. Lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu. Kwa hiyo fanya lililojema machoni pako.28Kwa maana nyumba yote ya baba yangu walikuwa maiti mbele ya bwana wangu mfalme, lakini ukamuweka mtumishi wako miongoni mwao walao mezani pako. Kwa hiyo nililiye haki gani zaidi kwa mfalme?”

29“Kisha mfalme akamwambia, “Kwa nini kueleza yote zaidi? Nimekwisha amua kwamba wewe na Siba mtagawana mashamba.”

30Ndipo Mefiboshethi akamjibu mfalme, “Sawa, acha achukue yote kwa vile bwana wangu mfalme amerudi salama nyumbani kwake.”

31Kisha Berzilai Mgileadi akashuka kutoka Rogelimu ili avuke Yordani pamoja na mfalme, naye akamsaidia mfalme kuuvuka Yordani.32Basi Berzilai alikuwa mzee sana mwenye umri wa miaka themanini. Alikuwa amemsaidia mfalme kwa mahitaji alipokuwako Mahanaimu kwani alikuwa na mali nyingi.33Mfalme akamwambia Berzilai, njoo pamoja nami, nami nitakupa riziki ukae nami huko Yerusalemu.”

34Berzilai akamjibu mfalme, “Kwani kuna siku ngapi zilizosalia maishani mwangu, hata niende na mfalme huko Yerusalemu?35Nina umri wa miaka themanini. Je, naweza kutofautisha mema na mabaya? Je, mtumishi wako anaweza kuonja anachokula au kunywa? Je, naweza kusikia sauti zaidi za wanaume na wanawake waimbao? Kwa nini basi mtumishi wako awe mzigo kwa bwana wangu mfalme?36Mtumishi wako angependa tu kuvuka Yordani pamoja na mfalme. Kwa nini mfalme anilipe kwa thawabu kama hiyo?37Tafadhali mruhusu mtumishi wako arudi nyumbani, ili kwamba nife katika mji wangu katika kaburi la baba na mama yangu. Lakini tazama, huyu hapa mtumishi wako Kimhamu. Haya yeye na avuke na bwana wangu mfalme na umfanyie lolote lipendezalo kwako.”

38Mfalme akajibu, “Kimhamu atakwenda pamoja nami, nami nitamtendea kila lionekanalo jema kwako, na lolote unalotamani kutoka kwangu nitakutendea.”

39Kisha watu wote wakavuka Yordani, mfalme naye akavuka, kisha mfalme akambusu Berzilai na kumbariki. Kisha Berzilai akarudi nyumbani kwake.

40Hivyo mfalme akavuka kuelekea Gilgali, na Kimhamu akavuka pamoja naye. Jeshi la Yuda lote na nusu ya jeshi la Israeli likamleta mfalme.

41Mara watu wa Israeli wote wakaanza kuja kwa mfalme na kumwambia, “Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda, wamemuiba na kumleta mfalme na familia yake juu ya Yordani na watu wote wa Daudi pamoja naye?”

42Hivyo watu wa Yuda wakawajibu watu wa Israeli, “Ni kwa kuwa mfalme anahusiana nasi kwa karibu zaidi. Kwa nini basi mkasirike juu ya hili? Je sisi tumekula chochote ambacho mfalme amekitoa? Je ametupa zawadi yoyote?”

43Watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, “Sisi tuna kabila kumi zaidi kwa mfalme hivyo tuna sehemu kubwa zaidi kwa Daudi kuliko ninyi. Kwa nini basi mlitudharau? Je hatukuwa wa kwanza kupendekeza kumrudisha mfalme wetu?” Lakini maneno ya watu wa Yuda hata yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli.

20

1Ikatukia pia kuwa katika eneo lilelile kulikuwa mtu asiye na thamani jina lake Sheba mwana wa Bikri Mbenjamini. Akapiga tarumbeta na kusema, “Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya kila mtu na aende hemani mwake, Israeli!”

2Hivyo watu wote wa Israeli wakamuacha Daudi na kumfuata Sheba mwana wa Bikri. Lakini watu wa Yuda wakamfuata mfalme wao kwa karibu sana, kutoka Yordani njia yote hadi Yerusalemu.

3Daudi alipofika katika kasri lake huko Yerusalemu, akawachukua masuria aliokuwa amewaacha kulitunza kasri, na akawaweka katika nyumba chini ya uangalizi. Aliwaandalia mahitaji yao lakini hakuenda kwao tena. Hivyo walikuwa wametengwa hadi siku ya kufa kwao, waliishi kama wajane.

4Kisha mfalme akamwambia Amasa, “Uwaite watu wa Yuda ndani ya siku hizi tatu; wewe pia uwepo hapa.”5Hivyo Amasa akaenda kuwaalika watu wote wa Yuda kwa pamoja, lakini akatumia muda mrefu kuliko mfalme alivyokuwa amemuamuru.

6Hivyo Daudi akamwambia Abishai, “Sasa Sheba mwana wa Bikri atatufanyia madhara zaidi ya Absalomu. Chukua watumishi wa bwana wako, askari wangu, na umfuatie asije akaingia katika mji wenye ngome na kututoroka.”7Ndipo watu wa Yoabu wakamfuatia, pamoja na Wakerethi na Wapelethi na mashujaa wote. Wakatoka Yerusalemu ili kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.

8Walipokuwa katika jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Yoabu alikuwa amevaa silaha ya vita aliyokuwa ameivaa, alikuwa pia na upanga uliokuwa umefungwa na mkanda katika kiuno chake. Kadili alivyoendelea mbele upanga ukaanguka.

9Hivyo Yoabu akamwambia Amasa, “Haujambo binamu yangu?” Kwa utaratibu Yoabu akakishika kidevu cha Amasa kwa mkono wake wa kulia ili ambusu.10Amasa hakutambua kwamba kulikuwa na jambia katika mkono wa kushoto wa Yoabu. Yoabu akamchoma Amasa tumboni na matumbo yake yakamwagika chini. Wala Yoabu hakumpiga tena, na Amasa akafa. Hivyo Yoabu na Abishai nduguye wakamfuatia Sheba mwana wa Bikri.

11Kisha mmoja wa watu wa Yoabu akasimama kando ya Amasa naye akasema, “Aliye upande wa Yoabu na aliyeupande wa Daudi na amfuate Yoabu.”12Amasa akawa anagalagala katika damu yake katikati ya njia. Mtu yule alipoona kwamba watu wote wamesimama, akambeba Amasa na kumuweka shambani kando ya njia. Akatupa vazi juu yake kwa maana aliona kila mmoja aliyekuja alisimama pale.13Baada ya Amasa kuondolewa njiani watu wote wakamfuata Yoabu katika kumfuatia Sheba mwana wa Bikri.

14Sheba akazipita kabila zote za Israeli mpaka Abeli wa Beth Maaka, na katika nchi yote ya Berite ambao pia walijikusanya pamoja pia na kumfuatia Sheba.15Walimpata na kumzingira huko Abeli wa Bethi Maaka. Wakajenga buruji ya kuhusuru mji nyuma ya ukuta. Jeshi lote lililokuwa pamoja na Yoabu likaugongagonga ukuta ili uanguke.16Ndipo mwanamke mwerevu akapiga kelele kutoka ndani ya mji, “Sikiliza, Yoabu, tafadhali sikiliza! Sogea karibu nami ili niongee nawe.”17Hivyo Yoabu akakaribia, mwanamke akamwambia, “Je wewe ni Yoabu? Akajibu, “Ni mimi.” Mwanamke akamwambia, “Sikiliza maneno ya mtumishi wako.” Akajibu, “Nasikiliza.”18Ndipo aliposema, “Hapo zamani ilisemwa, ‘Bila shaka tafuteni ushauri huko Abeli, na kwamba ushauri huo utamaliza maneno.’19Sisi ni mji ulio miongoni mwa miji yenye nguvu na aminifu sana katika Israeli. Mnataka kuharibu mji ambao ni mama katika Israeli. Kwa nini unataka kuumeza urithi wa Yahwe?”

20Ndipo Yoabu alipojibu na kusema, “Iwe mbali, iwe mbali nami, hata nikameze au kuharibu.21Hiyo si kweli. Lakini mtu kutoka katika nchi ya milima ya Efraimu, aitwaye Sheba mwana wa Bikri, ameinua mkono wake kinyume cha mfalme, kinyume cha Daudi. Mtoeni yeye nami nitauacha mji.” Mwanamke akamwambia Yoabu, “Utarushiwa kichwa chake kutoka juu ya ukuta.”

22Kisha mwanamke akawaendea watu wote wa mji kwa hekima yake. Wakakiondoa kichwa cha Sheba mwana wa Bikri na kumrushia Yoabu. Ndipo alipopiga tarumbeta na watu wa Yoabu wakauacha mji, kila mtu hemani mwake. Na Yoabu akarejea Yerusalemu kwa mfalme.

23Yoabu alikuwa juu ya jeshi lote la Israeli na Benaya mwana wa Yehoiada alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi.24Adoramu alikuwa juu ya watu waliofanya kazi ya kulazimishwa na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mkumbushaji.25Sheva alikuwa mwandishi, na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani.26Ira MYairi alikuwa kuhani wa Daudi.

21

1Kulikuwa na njaa kwa miaka mitatu katika siku za utawala wa Daudi, na Daudi akautafuta uso wa Yahwe. Hivyo Yahwe akasema, “Njaa hii ni kwa sababu ya mauaji ya Sauli na familia yake, kwa kuwa aliwauwa Wagibeoni.”

2Basi Wagibeoni hawakuwa uzao wa Israeli; walikuwa ni masalia ya Waamori. Watu wa Israeli walikuwa wameapa kutowauwa, lakini Sauli alitaka kuwaangamiza wote kwa husuda kwa ajili ya watu wa Israeli na Yuda.3Ndipo Daudi alipowaita pamoja Wagibeoni na kuwaambia, “Niwafanyie nini kwa ajili ya upatanisho? Ili kwamba mweze kuwabariki watu wa Yahwe wanaorithi wema na ahadi zake?”

4Wagibeoni wakamjibu, “Hili siyo jambo la fedha wala dhahabu kati yetu na Sauli au familia yake. Na siyo hitaji letu kumuua mtu yeyote katika Israeli.” Daudi akasema, “Mnasema nini ili niwafanyie nyinyi?”5Wakamjibu mfalme, “Mtu aliyetaka kutuuwa aliyepanga kinyume chetu, ili kutuangamiza na kukosa eneo katika mipaka ya Israeli -6haya na tupewe watu saba kutoka katika uzao wake, nasi tutawatundika mbele ya Yahwe katika Gibea ya Sauli, palipochaguliwa na Yahwe.” Mfalme akasema, “Nitawapen. I”7Lakini mfalme akamuifadhi Mefiboshethi mwana wa Yonathani mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Yahwe kati ya Daudi na Yonathani mwana wa Sauli.8Mfalme akawachukua wana wawili wa Rispa binti Ayia aliomzalia Sauli, hawa wana wawili waliitwa Armoni na Mefiboshethi; na pia Daudi akawachukua wana watano wa Mikali binti Sauli, aliomzalia Adrieli mwana wa Berzilai Mmeholathi.9Akawaweka katika mikono ya Wagibeoni. Nao wakawatundika juu ya mlima mbele za Bwana, na wote saba wakafa pamoja. Waliuawa katika kipindi cha mavuno, katika siku ya kwanza mwanzoni mwa mavuno ya shayiri.

10Kisha Rispa, binti Aiya, akachukua nguo ya gunia na akajitanda mwenyewe juu ya mlima kando ya miili ya waliokufa tangu mwanzo wa mavuno mpaka wakati mvua ilipoanza kunyesha. Hakuruhusu ndege wa angani kutua juu ya miili mchana wala hayawani wa mwituni wakati wa usiku.11Daudi akaambiwa alichokifanya Rispa, binti Aiya, suria wa Sauli.12Hivyo Daudi akaenda na kuchukua mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe kutoka kwa watu wa Yabeshi Gileadi, waliokuwa wameiiba kutoka katika eneo la jumuiya la Beth Shani, Wafilisti walipokuwa wamewatundika baada ya Wafilisti kumuua Sauli katika Gilboa.13Daudi akaiondoa pale mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe, na wakakusanya pia mifupa ya wale watu saba waliotundikwa.

14Wakaizika mifupa ya Sauli na Yonathani mwanawe huko Zela katika nchi ya Benjamini, katika kaburi la Kishi babaye. Wakafanya kila alichoagiza mfalme. Ndipo Mungu akajibu maombi yao kwa ajili ya nchi.

15Kisha Wafilisti wakaenda tena katika vita na Israeli. Hivyo Daudi na jeshi lake wakashuka na kupigana na Wafilisti. Akiwa vitani Daudi akachoshwa na vita.16Ishbibenobu, wa uzao wa Warefai, ambaye mkuki wake wa shaba ulikuwa na uzito wa shekeli 300 na alikuwa na upanga mpya, alitaka kumuua Daudi.17Lakini Abishai mwana wa Seruya akamuokoa Daudi, akampiga Mfilisti na kumuua. Ndipo watu wa Daudi wakamuapia, kusema, “Hautakwenda vitani pamoja nasi tena usije ukaizima taa ya Israeli.”

18Ikawa baadaye kuwa na vita tena kati ya Wafilisti huko Gobu, wakati Sibekai Mhushathi alipomuua Safu, aliyekuwa miongoni mwa uzao wa Warefai.

19Ikawa tena katika vita na Wafilisti huko Gobu, huyo Elhanani mwana wa Jari Mbethlehemu akamuua Goliathi Mgiti, ambaye fumo la mkuki wake lilikuwa kama mti wa mfumaji.

20Ikawa katika vita nyingine huko Gathi kulikuwa na mtu mrefu sana mwenye vidole sita katika kila mkono na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne. Yeye naye alikuwa wa uzao wa Warefai.21Alipowatukana Israeli, Yonathani mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamuua.

22Hawa walikuwa wa uzao wa Warefai wa Gathi, waliuawa kwa mkono wa Daudi na kwa mkono wa askari wake.

22

1Daudi akamuimbia Yahwe maneno ya wimbo huu siku ile Yahwe alipomuokoa katika mkono wa adui zake wote na katika mkono wa Sauli.2Akaomba hivi, “Yahwe ni mwamba wangu, ngome yangu, aliyeniokoa.

3Mungu ni mwamba wangu. Yeye ni kimbilio langu. Ngao yangu, pembe ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu, aniokoaye na mabaya yote.
4Nitamuita Yahwe, astahiliye kutukuzwa, nami nitaokolewa kutoka kwa adui zangu.
5Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maji ya uharibifu yakanishinda.
6Vifungo vya kuzimu vilinizunguka; kamba za mauti zikaninasa.
7Katika shida yangu nilimwita Yahwe; nilimwita Mungu wangu; akaisikia sauti yangu katika hekalu lake, na kilio changu cha msaada kikafika masikioni mwake.
8Ndipo nchi ilipotikisika na kutetemeka. Misingi ya mbingu ikatetemeka na kutikiswa, kwa kuwa Mungu alikasirika.
9Moshi ukatoka katika pua yake, na miale ya moto ikatoka katika kinywa chake. Makaa yakawashwa nayo.
10Alizifungua mbingu akashuka, na giza totoro lilikuwa chini ya miguu yake.
11Alipanda juu ya kerubi na kuruka. Alionekana katika mawingu ya upepo.
12Naye akalifanya giza kuwa hema kumzunguka, akakusanya mawingu makubwa ya mvua angani.
13Makaa ya moto yalidondoka mbele zake kutoka katika radi.
14Yahwe alishuka kutoka katika mbingu. Aliye juu alipiga kelele.
15Alipiga mishale na kuwatawanya adui zake--miale ya radi na kuwatupa katika kuchanganyikiwa.
16Kisha njia za bahari zikaonekana; misingi ya dunia ikawa wazi katika kukanywa na Yahweh, katika sauti za pumzi ya pua zake.
17Kutoka juu alifika chini; akanishikilia! Aliniondoa katika vilindi vya maji.
18Aliniokoa kutoka kwa adui zangu wenye nguvu, kwao walionichukia, kwa maana walikuwa na nguvu sana kwangu.
19Walikuja kinyume changu siku ya shida yangu, lakini Yahwe alikuwa msaada wangu.
20Pia aliniweka mahali panapo nafasi. Aliniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
21Yahwe amenituza kwa kipimo cha haki yangu; amenirejesha kwa kiwango cha usafi wa mikono yangu.
22Kwa maana nimezishika njia za Yahwe na sijafanya uovu kwa kugeuka kutoka kwa Mungu.
23Kwa kuwa maagizo yake yote ya haki yamekuwa mbele yangu; kwa kuwa sheria zake, sikujiepusha nazo.
24Nimekuwa bila hatia mbele zake pia, na nimejiepusha na dhambi.
25Kwa hiyo Yahwe amenirejesha kwa kiasi cha uadilifu wangu, kwa kipimo cha usafi wangu mbele zake.
26Kwa mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu; kwake asiye na hatia; unajionyesha kuwa hauna hatia.
27Kwa usafi unajionyesha kuwa msafi, lakini kwa wakaidi unajionyesha kuwa mkaidi.
28Unaokoa walioteswa, lakini macho yako ni kinyume cha wenye kiburi, na unawashusha chini.
29Kwa maana wewe ni taa yangu, Yahwe. Yahwe huangaza katika giza langu.
30Kwa ajili yako ninaweza kukimbia juu ya jeshi; kwa msaada wa Mungu wangu naweza kuruka juu ya ukuta.
31Maana njia za Mungu ni kamilifu. Neno la Yahwe ni safi. Yeye ni ngao yao wanaomkimbilia.
32Maana ni nani aliye Mungu isipokuwa Yahwe? Na ni nani aliyemwamba isipokuwa Mungu?
33Mungu ni kimbilio langu, na umuongoza katika njia yake mtu asiye na hatia.
34Huifanya myepesi miguu yangu kama kurungu na kuniweka katika vilima virefu.
35Huifundisha mikono yangu kwa vita, na viganja vyangu kupinda upinde wa shaba.
36Umenipa ngao ya wokovu wako, na upendeleo wako umenifanya mkuu.
37Umeitengenezea miguu yangu nafasi chini yangu, hivyo miguu yangu haijateleza.
38Niliwafuatia adui zangu na kuwaangamiza. Sikurudi nyuma hadi walipoangamizwa.
39Niliwararua na kuwapiga; hawawezi kuinuka. Wameanguka chini ya miguu yangu.
40Ulinifunga mshipi wa nguvu kwa vita; unawaweka chini yangu wanaoinuka kinyume changu.
41Ulinipa migongo ya shingo za adui zangu; niliwaangamiza kabisa wale wanaonichukia.
42Walilia kwa msaada, lakini hakuna aliyewaokoa; walimlilia Yahwe, lakini hakuwajibu.
43Niliwaponda katika vipande kama mavumbi juu ya ardhi, niliwakanyaga kama matope mitaani.
44Umeniokoa pia kutoka katika mashutumu ya watu wangu. Umeniweka kama kichwa cha mataifa. Watu nisiowajua wananitumikia.
45Wageni walishurutishwa kuniinamia. Mara waliposikia kuhusu mimi, walinitii.
46Wageni walikuja wakitetemeka kutoka katika ngome zao.
47Yahwe anaishi! Mwamba wangu atukuzwe. Mungu na ainuliwe, mwamba wa wokovu wangu.
48Huyu ndiye Mungu anilipiaye kisasi, awawekaye watu chini yangu.
49Uniweka huru mbali na adui zangu. Hakika, uliniinua juu yao walioinuka kinyume changu. Uliniokoa kutoka kwa watu wenye ghasia.
50Kwa hiyo nitakushukuru, Yahwe, kati ya mataifa; nitaliimbia sifa jina lako.
51Mungu hutoa ushindi mkuu kwa mfalme wake, na huonyesha uaminifu wake wa kiagano kwa mtiwa mafuta wake, kwa Daudi na uzao wake daima.”

23

1Haya ni maneno ya mwisho ya Daudi-Daudi mwana wa Yese, mtu aliyeheshimiwa sana, aliyetiwa mafuta na Mungu wa Yakobo, mwandishi mzuri wa zaburi wa Israeli.

2“Roho ya Yahwe alisema nami, na neno lake lilikuwa ulimini mwangu.
3Mungu wa Israeli alinena, Mwamba wa Israeli aliniambia, “Atawalaye kwa haki juu yangu, atawalaye katika hofu ya Mungu.
4Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua linapochomoza, asubuhi isiyo na mawingu, wakati mche mwororo unapochipua kutoka ardhini kupitia mwangaza wa mng'ao wa jua baada ya mvua.
5Hakika, je familia yangu haiko hivi mbele za Mungu? Je hajafanya nami agano la milele, taratibu la uhakika kwa kila njia? Je yeye haongezi wokovu wangu na kutimiza kila hitaji langu?
6Lakini yasiyofaa yote yatakuwa kama miiba na kutupwa mbali, kwa maana haiwezekani kukusanywa kwa mikono.
7Ayagusaye ni lazima atumie chombo cha chuma au fumo la mkuki. Ni lazima yachomwe mahali yalipo.

8Haya ni majina ya askari wa Daudi: Yashobeamu Mhakmoni alikuwa kiongozi wa mashujaa. Aliua watu 800 wakati mmoja.

9Baada yake alikuwa Elieza mwana wa Dodo, mwana wa mwahohi, mmoja wa mashujaa watatu wa Daudi. Alikuwepo walipowashinda Wafilisti waliokuwa wamekusanyika kwa vita, na wakati watu wa Israeli walipokuwa wamekimbia.10Elieza akasimama na kuwapiga Wafilisti mpaka mkono wake ukachoka, mpaka mkono wake ukang'ang'ania mpini wa upanga wake. Siku hiyo Yahwe akatoa ushindi mkuu. Jeshi likarejea kwa ajili ya kuteka tu nyara za waliouawa na Elieza.

11Baada yake alikuwa Shama mwana wa Agee, Mharari. Wafilisti wakajikusanya pamoja palipokuwa na shamba la dengu, na jeshi likawakimbia.12Lakini Shama akasimama katikati ya shamba na kulitetea. Aliwauwa Wafilisti, na Yahwe akaleta ushindi mkuu.

13Watatu kati ya askari thelathini walishuka kwa Daudi nyakati za mavuno, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti lilikuwa limepiga kambi katika bonde la Mrefai.14Wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, wakati Wafilisti walikuwa imara Bethlehemu.15Daudi alitamani maji na akasema, “Kama ingekuwa mtu mmoja angenipa maji ya kunywa kutoka kisima kilichopo Bethlehemu, kisima kilichopo langoni!”16Hivyo mashujaa hawa watatu wakapita kati ya jeshi la Wafilisti na kuchota maji katika kisima cha Bethlehemu, kilichopo langoni. Wakachukua maji na kuyaleta kwa Daudi, lakini yeye akakataa kuyanywa. Badala yake akayamwaga mbele za Yahwe.17Kisha akasema, “Iwe mbali nami, Yahwe, kwamba niyanywe haya. Je, ninywe damu ya watu waliohatarisha maisha yao?” Hivyo akakataa kuyanywa. Haya ni mambo yaliyofanywa na mashujaa watatu.

18Abishai, nduguye Yoabu na mwana wa Seruya, alikuwa akida wa watatu. Alipigana kwa mkuki wake na watu mia tatu na akawauwa wote. Mara kwa mara alitajwa kati ya mashujaa watatu.19Je, hakuwa maarufu kuliko wale watatu? Alifanywa akida wao. Lakini, umaarufu wake haukulingana na umaarufu wa wale mashujaa watatu.

20Benaya kutoka Kabseeli mwana wa Yehoyada; alikuwa mtu hodari aliyefanya matendo makuu. Aliwauwa wana wawili wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka shimoni na kuuwa simba wakati wa theruji.21Na alimuua Mmisri aliyekuwa mtu mnene sana. Mmisri alikuwa na mkuki mkononi, lakini Benaya alipigana naye kwa fimbo tu. Aliuchukua mkuki mkononi mwa Mmisri na kisha kumuua nao.22Benaya mwana wa Yehoyada alifanya matendo haya, naye alitajwa kati ya mashujaa watatu.23Alikuwa na heshima kuliko mashujaa thelathini kwa ujumla wao, lakini hakuwa na heshima kama wale mashujaa watatu. Hata hivyo Daudi alimuweka kuwa mlinzi wake.
24Wafuatao ni wale watu thelathini: Asaheli nduguye Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo kutoka Bethlehemu,
25Shama Mharodi, Elika Mharodi,26Helesi Mpeloni, Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi,27Abi Ezeri Mwanathothi, Mebunai Mhushathi,28Salmoni Mhahoi, Maharai Mnetofathi;29Helebu mwana wa Baana, Mnetofathi, Itai mwana wa Rabai kutoka Gibea ya Wabenjamini,30Benaya Mpirathoni, Hidai wa mabonde ya Gaashi.31Abieliboni Mwarbathi, Azmawethi Mbarhumi,32Eliaba Mshalboni, wana wa Yasheni, Yonathani mwana wa Shama Mharari;33Ahiamu mwana wa Sharari Mharari,34Elifeleti mwana wa Ahasbai Mmaakathi, Eliamu mwana wa Ahithofeli Mgiloni,35Hezro Mkarmeli, Parai Mwarbi,36Igali mwana wa Nathani kutoka Soba, Bani kutoka kabila la Gadi,37Zeleki Mwamoni, Naharai Mbeerothi, mbeba silaha wa Yoabu mwana wa Seruya,38Ira Mwithri, Garebu Mwithri,39Uria Mhiti - jumla yao wote thelathini na saba.

24

1Kisha hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Israeli, naye akamchochea Daudi kinyume chao kusema, “Nenda, ukawahesabu Israeli na Yuda.”

2Mfalme akamwambia Yoabu, jemedari wa jeshi, aliyekuwa pamoja naye, “Nenda upite katika kabila zote za Israeli, toka Dani mpaka Beersheba, uwahesabu watu wote, ili niweze kujua idadi kamili ya watu wanaofaa kwa vita.”

3Yoabu akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na aizidishe hesabu ya watu mara mia, na macho ya bwana wangu mfalme yaone ikifanyika. Lakini kwa nini bwana wangu mfalme analitaka jambo hili?”

4Walakini neno la mfalme lilikuwa la mwisho dhidi ya Yoabu na dhidhi ya majemedari wa jeshi. Hivyo Yoabu na majemedari wakatoka mbele ya mfalme kuwahesabu watu wa Israeli.

5Wakavuka Yordani na kupiga kambi karibu na Aroeri, kusini mwa mji bondeni. Kisha wakasafiri kupitia Gadi mpaka Yazeri.6Wakaja Gileadi na nchi ya Tahtimu Hodshi, kisha Dani, Jaani na karibu kuelekea Sidoni.7Wakafika ngome ya Tiro na miji yote ya Wahivi na Wakanaani. Kisha wakaenda Negebu katika Yuda huko Beersheba.

8Walipokuwa wamepita katika nchi yote, wakarejea Yerusalemu mwishoni mwa miezi tisa na siku ishirini.

9Ndipo Yoabu alipotoa taarifa ya hesabu kamili kwa mfalme kuhusu watu wawezao kupigana vita. Katika Israeli kulikuwa na watu 800,000 jasiri wawezao kutoa upanga, na wale wa Yuda walikuwa watu 500,000.

10Ndipo moyo wa Daudi ukamsumbua baada ya kuwahesabu watu. Hivyo akamwambia Yahwe, “Kwa kufanya hivi nimetenda dhambi sana. Sasa, Yahwe, uiondoe hatia ya mtumishi wako, kwani nimetenda kwa upumbavu.”

11Daudi alipoinuka asubuhi, neno la Yahwe likamjia nabii Gadi, mwonaji wa Daudi, ikisema,12Nenda umwambie Daudi; “Hivi ndivyo asemavyo Yahwe: ‘Ninakupa mambo matatu. Uchague mojawapo.’

13Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kumwambia, “Je miaka mitatu ya njaa ije katika nchi yako? Au miezi mitatu ukimbie kutoka kwa adui zako huku wakikufuatia? Au kuwe na tauni ya siku tatu katika nchi yako? Amua sasa jibu gani nimrudishie aliyenituma.”

14Ndipo Daudi akamwambia Gadi, “Nipo katika shida kubwa. Haya na tuanguke katika mikono ya Yahwe kuliko kuanguka katika mikono ya mwanadamu, kwani matendo yake ya rehema ni makuu sana.”

15Hivyo akatuma tauni juu ya Israeli kuanzia asubuhi kwa muda ulioamliwa, na watu 75,000 kutoka Dani mpaka Beersheba wakafa.16Malaika aliponyosha mkono wake kuelekea Yerusalemu ili kuuharibu, Yahwe akabadili nia yake kuhusu madhara, na akamwambia malaika aliyekuwa tiyari kuwaangamiza watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako sasa.” Wakati huo malaika wa Yahwe alikuwa amesimama katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.

17Daudi alipomwona malaika aliyekuwa amewapiga watu, akamwambia Yahwe akisema, “Nimetenda dhambi, na nimetenda kwa upumbavu. Lakini kondoo hawa, wamefanya nini? Tafadhali, mkono wako na uniadhibu mimi na familia ya baba yangu!”

18Kisha Gadi akaja siku hiyo kwa Daudi na kumwambia, “Kwea na ujenge madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika kiwanja cha kupuria cha Arauna Myebusi.”19Hivyo Daudi akakwea kama Gadi alivyomuelekeza kufanya, kama Yahwe alivyokuwa ameagiza.20Arauna akatazama na kumuona mfalme na watumishi wake wakikaribia. Ndipo Arauna akaondoka na kumsujudia mfalme uso wake mpaka juu ya ardhi.

21Kisha Arauna akasema, “Kwa nini bwana wangu mfalme amekuja kwangu, mtumishi wake?” Daudi akajibu, “Kununua uwanja wako wa kupuria, ili nimjengee Yahwe madhabahu, ili kwamba tauni iondolewe kwa watu.”

22Arauna akamwambia Daudi, “Chukua liwe lako, bwana wangu mfalme. Ulifanyie lolote lililojema machoni pako. Tazama, ng'ombe kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa na miganda ya kupuria na nira kwa kuni.23Haya Yote bwana wangu mfalme, mimi Arauna nakupa.” Kisha akamwambia mfalme, “Yahwe Mungu wako na awe nawe.”

24Mfalme akamwambia Arauna, “Hapana, nahimiza kukinunua kwa thamani yake. Sitatoa kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe chochote ambacho hakijanigharimu kitu.” Hivyo Daudi akakinunua kiwanja cha kupuria na ng'ombe kwa shekeli hamsini za fedha.

25Daudi akajenga madhabahu kwa Yahwe pale na kutoa juu yake sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani. Hivyo wakamsihi Yahwe kwa niaba ya nchi, hivyo akaizuia tauni katika Israeli yote.

1 Wafalme

1

1Mfalme Daudi alipokuwa mzee sana, walimfunika kwa nguo, lakini hakupata joto.2Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, “Na tutafute msichana bikira kwa ajili ya mfalme Bwana wetu, ili amtumikie na kumtunza. Naye atalala kwenye mikono yake ili Bwana mfalme wetu apate joto.”

3Kwa hiyo wakatafuta msichana mrembo katika mipaka yote ya Israeli. Wakampata Abishagi Mshunami wakamuleta kwa mfalme.4Yule msichana alikuwa mrembo sana. Naye akamtumikia mfalme na kumtunza, Lakini mfalme hakumjua.

5Wakati huo, Adoniya mwana wa Hagithi alijiinua akisema, “Nitakuwa mfalme.” Kwa hiyo akajiandalia magari na wapanda farasi hamsini ili wapige mbio mbele yake.6Baba yake alikuwa hajawahi kumsumbua kwa kusema, “Kwa nini umefanya hili na lile?” Adonia alikuwa mwanamume mzuri sana aliyezaliwa baada ya Absalomu.

7Akashauriana na Yoabu mwana wa Seruya na Abiathari kuhani. Wakamfuata Adonia wakamsaidia.8Lakini Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, nabii Nathani, Shimei, Rei, na watu mashujaa wa Daudi hawakumfuata Adoniya.

9Adoniya akataoa dhabihu za Kondoo, na ndama walionona kwenye jiwe la Sohelethi, ambalo liko karibu na Eni Rogeli. Akawakaribisha ndugu zake wote, watoto wa mfalme, wanaume wote wa Yuda, na watumishi wa mfalme.10Lakini hakumkaribisha nabii Nathan, Benaya, wanaume mashujaa, au ndugu yake Sulemani.

11Kisha Nathani akamwambia Bethsheba mama wa Sulemani, akisema, “Je, haujasikia kuwa Adonia mwana wa Hagathi amekuwa mfalme, na Daudi Bwana wetu halijui hilo?12Kwa hiyo sasa nakupa ushauri, ili kwamba uweze kuokoa maisha yako na maisha ya mwanao Sulemani.13Nenda kwa mfalme Daudi; ukamwambie, ‘Bwana wangu mfalme, Je, haukumwapia mtumishi wako, ukisema, ‘Hakika Sulemani mwanao atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?’ Kwa nini basi Adonia anatawala?’14Wakati ukiwa pale ukiongea na mfalme, Nitaingia baada yako na kuthibitisha hayo.”

15Kwa hiyo Bathsheba akaingia chumbani kwa mfalme. Wakati huo mfalme alikuwa mzee sana, na Abishagi Mshunami alikuwa akimtunza mfalme.16Bathsheba akainama kifudifudi mbele ya mfalme. Na kisha mfalme akasema, “Una haja gani?”

17Naye akamwambia, “Bwana wangu, ulimwapia mtumishi wako kwa jina la Bwana, Mungu wako, ukisema, ‘Hakika Sulemani mwanao atatawala, baada yangu, naye ataketi kwenye kiti changu cha enzi.’18Sasa, tazama, Adonia ni mfalme, na Bwana wangu mfalme hajui jambo hili.19Ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, Abiathari kuhani, na Yoabu jemedari wa jeshi, lakini hajamkaribisha Sulemani mtumishi wako.20Mfalme Bwana wangu, macho yote ya Israeli yako kwako, yakisubiri usemi wako juu ya nani atakayeti kwenye kiti cha enzi baada yako, Bwana wangu.21Vinginevyo itatokea, wakati Bwana wangu atakapolala na baba zake, kwamba mimi na mwanangu Sulemani tutahesabiwa wahaini.”

22Wakati alipokuwa akiendelea na mfalme, nabii Nathani aliingia.23Watumshi wakamwambia mfalme, “Nabii Nathani yuko hapa,” Naye alipoingia mbele ya mfalme, akalala kifudifudi mbele ya mfalme na uso wake ukielekea chini.

24Nathani akamwambia, “Mfalme Bwana wangu, Je, umesema, ‘Adonia atatawala baada yangu, na ataketi kwenye kiti changu cha enzi?’25Kwani leo ameshuka na ametoa dhabihu ya makisai, ndama walionona, na kondoo wengi, na amewakaribisha wana wote wa mfalme, jemedari wa jeshi, na Abiathari kuhani. Nao wanakula na kunywa mbele zake, na kusema, ‘Mfalme Adonia na aishi milele!’26Lakini mimi, mtumishi wako, Sadoki kuhani, Benaya mwana wa Yehoyada, na mtumishi wako Sulemani, hajatukaribisha.27Je, Bwana wangu mfalme amefanya haya pasipo kutuambia sisi, watumishi wako, ni nani atakayeketi kwenye kiti cha enzi baada yake?”

28Ndipo mfalme Daudi alipojibu na kusema, “Mwiteni Bathsheba arudi.” Naye akaja akasimama mbele ya mfalme.

29Mfalme akafanya kiapo akasema, “Kama BWANA aishivyo, ambaye ameniokoa toka tabu zote,30kama nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikisema, ‘Sulemani mwanao atatawala baada yangu, naye ndiye atakayeketi kwenye kiti changu cha enzi, mahali pangu,’ nitafanya hivi leo.”31Kisha Bathsheba akalala kifudifudi na sura yake ikielekea chini mbele ya mfalme akasema, “Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele!”

32Mfalme Daudi akasema, “Niitieni Sadoki kuhani, nabii Nathani na Benaya mwana wa Yehoyada.” Nao wakaja mbele ya mfalme.33Mfalme akawaambia, “Uwachukue watumishi wangu, wana wako, na umfanye Sulemani mwanangu apande juu ya nyumbu wangu mimi na mkamteremshe mpaka chini Gihoni.34Na Sadoki kuhani na nabii Nathani wamtawaze awe mfalme wa Israeli na tarumbeta zipigwe, ‘Mfalme Sulemani na uishi milele!’35Kisha njoni mkiwa nyuma yake, naye atakuja na kukaa kwenye kiti changu cha enzi; kwani yeye ndiye atakayekuwa mfalme mahali pangu. Nimemchagua yeye kuwa mtawala wa Israeli na Yuda.”

36Benaya mwana wa Yehoyada akamjibu mfalme, akasema, “Na iwe hivyo! Na BWANA, Mungu wa mfalme Bwana wangu, alithibitishe hilo.37Kama vile BWANA alivyokuwa na mfalme Bwana wangu na awe na Sulemani hivyo hivyo, na kuifanya enzi yake kuwa kubwa kuliko zaidi ya enzi ya Bwana wangu Daudi.”

38Kwa hiyo Sadoki kuhani, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi na Wapelethi wakamfanya Sulemani akapanda juu ya nyumbu wa mfalme Daudi; wakamleta Gihoni.39Naye Sadoki kuhani akachukua pembe lenye mafuta hemani akamtia mafuta Sulemani kisha wakapiga tarumbeta, na watu wote wakasema, “Mfalme Sulemani na aishi milele!”40Kisha watu wote wakamfuata, na watu wakapiga zomari wakafurahi furaha kubwa mno, kiasi kwamba dunia ikatetemeka kwa sauti zao.

41Kisha Adonia na wageni wake waliokuwa pamoja naye wakasikia hayo walipomaliza kula. Yoabu alipozisikia sauti za panda, akasema, “Kwa nini jiji liko katika hali ya taharuki?”

42Wakati alipokuwa akiongea, Yonatahani mwana wa Abiathari kuhani alifika. Adonia akamwambia, “Karibu, kwa kuwa wewe wastahili kutuletea habari.”

43Naye Yonathani akamjibu Adonia, “Mfalme Bwana wetu Daudi amemfanya Sulemani kuwa mfalme.44Na mfalme amemtuma pamoja naye Sadoki, nabii Nathani, Benaya mwana wa Yehoyada, na Wakerethi pamoja na Wapelethi. Wamempandisha Sulemani juu ya nyumbu wa mfalme.45Sadoki kuhani na nabii Nathani wamemtawaza kuwa mfalme kule Gihoni, na wametokea huko wakifurahi, ndiyo maana jiji liko katika taharuki. Na hizi ndizo sauti ulizosikia.46Pia, Sulemani ameketi kwenye kiti cha enzi cha ufalme.47Zaidi ya yote, watumishi wa mfalme walikuja kumbariki mfalme Bwana wetu Daudi, wakisema, “Mungu wako na alifanye jina la Sulemani kuwa zuri kuliko jina lako, na kuifanya enzi yako kuwa kubwa kuliko yako.” Na mfalme akasujudu mwenyewe kitandani.48Mfalme pia alisema, “Abarikiwe BWANA, Mungu wa Israeli, ambaye amempa mtu kuketi kwenye enzi yangu siku hii ya leo, na kwamba macho yangu yamejionea hilo.”

49Ndipo wageni wote wa Adonia walipoogopa sana. Wakasimama na kila mtu akaenda njia yake.50Pia Adonia alimwogopa Sulemani na akasimama, na akaondoka, akachukua pembe la madhabahuni.51Kisha Sulemani akaambiwa hilo, wakasema, “Tazama, Adonia amemwogopa mfalme Sulemani, kwa kuwa ameshikilia pembe la madhabahuni, akisema, ‘Mfalme Sulemani na aniapie kwanza kuwa hatamwua mtumishi wake kwa upanga.’”

52Sulemani akasema, “Kama atajionyesha kuwa ni mtu wa kweli, hakuna hata unywele mmoja utakaoanguka duniani, bali kama uovu utaonekana kwake, atakufa.”53Kwa hiyo mfalme Sulemani akatuma watu, waliomleta Adonia kutoka madhabahuni. Naye akaja akapiga magoti kwa Sulemani, na Sulemani akamwambia, “Nenda nyumbani kwako.”

2

1Daudi alipokaribia kufa, alimwamuru Sulemani mwanae, akisema,

2“Mimi sasa ninaiendea njia ya dunia yote. Kwa hiyo, uwe imara, na ujionyeshe mwenyewe kama mwanamume. Uzilinde amri za BWANA, Mungu wako ukitembea katika njia zake, utii maaagizo yake, amri zake,3maamuzi yake, na maagizo ya maagano yake, uwe mwangalifu kufanya yale yaliyoandikwa katika sheria za Musa, ili ufanikiwe katika yote utakayoyafanya, popote kule utakakokuwa,4na BWANA atayatimiza maneno yake aliyosema kuhusu mimi, aliposema, ‘Kama wanao watajilinda katika tabia zao, wakatembea mbele yangu kwa uaminifu kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote, hawatakoma kuwa na mtu aliyeketi katika kiti cha enzi cha Israeli.’

5Wewe pia wajua kile Yoabu mwana wa Seruya alichonifanyia, na kile alichowafanyia majemedari wa majeshi ya Israeli, kwa Abina mwana wa Neri, na kwa Amasa mwana wa Yetheri, ambaye alimwua. Alimwaga damu vitani wakati wa amani na kuiweka ile damu kwenye mshipi uliokuwa kiunoni mwake na kwenye vile viatu miguuni mwake.6Mshughulikie Yoabu kwa hekima ambayo umejifunza, lakini usiache mvi zake ziingie kaburini kwa amani.

7Hata hivyo, uonyeshe utu kwa wana wa Barizilai Mgileadi, na uwaache wawe miongoni mwa wale wanaokula mezani kwako, kwa kuwa walikuja kwangu wakati nilipomkimbia ndugu yangu Absalomu.

8Tazama, Shimei mwana wa Gera yuko pamoja na wewe, Wabenjamini wa Bahurimu, walionilaani kwa laana ya fujo siku niliyoenda kwa Mahanaimu. Shimei alishuka kuja kuniona pale Yorodani, na nikamwapia kwa BWANA, nikisema, ‘Sitawaua kwa upanga,’9Kwa hiyo sasa usimwache aiepuke adhabu, Wewe ni mwenye hekima, na utajua jinsi itakavyokupasa kumtendea. Utakileta hicho kichwa chenye mvi chini kaburini.”

10Ndipo Daudi alipolala na mababu zake na alizikwa kwenye mji wa Daudi.11Siku ambazo Daudi alitawala Israeli zilikuwa ni miaka arobaini. Alikuwa ametawala kwa miaka saba kule Hebroni na kwa miaka thelethini na tatu kule Yerusalemu.12Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha baba yake Daudi, na utawala wake ulikuwa imara.

13Kisha Adoniya mwana wa Hagathi alikuja kwa Bathsheba mama wa Sulemani. Naye akamwuliza, “Je, unakuja kwa amani?” Naye akajibu, “Kwa amani.”

14Kisha akasema, “Nina jambo la kukuambia.” Naye akajibu, “Sema.”

15Adoniya akasema, “Unajua kuwa ufalme ulikuwa wangu, na kwamba Israeli yote ilikuwa inanitegemea mimi kuwa mfalme. Hata hivyo, ufalme umegeuzwa na umekuwa wa ndugu yangu, kwani ulikuwa wake toka kwa BWANA.16Sasa nina ombi moja kwako, usinikatalie.” Bathsheba akamwambia, “Sema.”

17Naye akamwambia, “Tafadhali mwambie mfalme Sulemani, kwa kuwa hatakukatalia, ili kwamba anipatie Abishagi Mshunami awe mke wangu.”

18Bathisheba akamwambia, “Vyema sana, nitamwambia mfalme.”

19Kwa hiyo Bathsheba akaenda kumwambia mfalme Sulemani kwa niaba ya Adoniya. Mfalme akainuka kumlaki na akapiga magoti mbele yake. Kisha akakaa kwenye kiti chake cha enzi na kulikuwa na kiti kingine cha enzi kilicholetwa kwa ajili ya mama wa mfalme. Naye akakaa mkono wa kuume wa mfalme.

20Ndipo alipomwambia, “Napenda kukuomba ombi moja dogo. Usinikalie.” Mfalme, akamjibu, “Mama omba kwa kuwa sitakukatalia.”

21Naye akamwambia, “Naomba Abishagi Mshunami apewe Adoniya ndugu yako awe mke wake.”

22Mfalme Sulemani akamjibu mama yake, “Kwa nini unamwombea Adonia huyo Abishagi Mshunami? Kwa nini usimwombee ufalme pia, kwa kuwa ni ndugu yangu mkubwa? Au kwa Abiathari kuhani, au Yoabu mwana wa Seruya?”

23Kisha mfalme Sulemani akaapa kwa BWANA, akisema, “Mungu wangu na anifanyie hivyo, na zaidi pia, kama Adonia hajayasema haya kinyume na maisha yake.24Sasa basi kama BWANA aishivyo, ambaye ndiye alinifanya mimi kuwepo na kunipa kiti cha enzi cha Daudi baba yangu, na ambaye amenifanyia nyumba kwa ahadi yake, hakika Adoniya lazima auawe leo.”25Kwa hiyo mfalme Sulemani akamtuma Benaya mwana wa Yehoyada naye akamkuta Adoniya na kumwua.

26Kisha akamwambia Abiathari kuhani, “Nenda kwa Anathothi, kwenye mashamba yako. Unastahili kufa, lakini sitakuua sasa hivi, kwa sababu ulilibeba sanduku la BWANA mbele ya Daudi baba yangu na kujitaabisha kwa namna mbalimbali kama baba yangu alivyopata taabu.”27Kwa hiyo Sulemani akamfukuza Abiathari asiwe kuhani wa BWANA, ili kwamba atimilize maneno ya BWANA, aliyokuwa amesema juu ya nyumba ya Eli.

28Habari hizo zikamfikia Yoabu, Kwani Yoabu alimuunga mkono Adonia, ingawa hakumuunga mkono Absalomu. Kwa hiyo Yoabu akakimbilia kwenye hema ya BWANA karibu na madhabahu na akabeba pembe za madhabahu.29Sulemani alipoambiwa kuwa Yoabu amekimbilia kwenye hema ya BWANA na sasa alikuwa karibu na madhabahu. Ndipo Sulemani alipomtuma Benaya mwana wa Yehoyada, akisema, “Nenda, ukamwue.”

30Kwa hiyo Benaya akaenda kwenye hema ya BWANA na kumwambia, “Mfalme anasema utoke hemani.” Yoabu akamjibu, “Hapana. Nitafia hapa.” Kwa hiyo Benaya akarudi kwa mfalme, akasema, “Yoabu amesema atafia kwenye madhabahu.”

31Naye mfalme akamwambia, “Kafanye kama alivyosema. Muue na ukamzike, ili kwamba uitoe kwangu na kwenye nyumba ya baba yangu damu ambayo Yoabu alimwaga bila sababu.32BWANA na amrudishie damu yake kichwani kwake, kwa sababu aliwaua wanaume wawili wasio na hatia na wema kuliko yeye na akawaua kwa upanga, Abineri mwana wa Neri, Jemedari wa Jeshi la Israeli, na Amasa mwana wa Jetheri, jemedari wa jeshi la Yuda, bila baba yangu Daudi kujua.33Kwa hiyo damu yao na imrudie Yoabu kichwani pake na kwenye vichwa vya uzao wake milele na milele. Lakini kwa Daudi na uzao wake, na nyumba yake, na kwenye kiti chake cha enzi, kuwe na amani ya kudumu kutoka kwa BWANA.”

34Kisha Benaya mwana wa Yehoyada akaenda akamvamia Yoabu na kumwua. Alizikwa kwenye nyumba yake kule jangwani.35Mfalme akamwinua Benaya mwana wa Yehoyada kuwa juu ya jeshi badala yake, na akamweka Sadoki kuhani kwenye nafasi ya Abiatahari.

36Kisha Mfalme akatuma watu kumwita Shimei, na akamwambia, “Kajijengee nyumba kwa ajili yako kule Yerusalemu na uishi huko, na usitoke nje ya huo mji na kwenda mahali pengine.37Kwa kuwa siku utakayoenda mahali pengine, na kupita bonde la Kidroni, ujue kwa hakika kuwa utakufa. Damu yako itakuwa juu ya kichwa chako.”

38Kwa hiyo Shimei akamwambia mfalme, “Unachosema ni chema. Kama vile mfalme bwana wangu alivyosema, ndivyo ambavyo mtumishi wako atakavyofanya.” Kwa hiyo Shimei akaishi Yerusalemu kwa miaka mingi.

39Lakini mwishoni mwa mwaka wa tatu, watumishi wawili wa Shimei wakakimbilia kwa Akishi mwana wa Maaka, mfalme wa Gathi. Kwa hiyo wakamwambia Shimei, wakisema, “Tazama, watumishi wako wameenda Gathi.”40Kisha Shimei akainuka, akapanda punda wake akaenda kwa Akishi huko Gathi kuwatafuta watumishi wake. Akaenda na akawaleta watumishi wake toka Gathi.

41Sulemani alipoambiwa kuwa Shimei alikuwa ametoka Yerusalemu kwenda Gathi na amerudi,42mfalme akatuma wito kwa Shimei na kumwambia, “Je, sikukuapisha kwa BWANA na kushuhudia kwako, nikisema, ‘Tambua kuwa siku utakayotoka kwenda nje na kwenda mahali popote, hakika utakufa?’ Na ukaniambia kuwa unachosema ni chema.43Kwa nini basi umeshindwa kulinda kiapo chako kwa BWANA na amri niliyokupa?”

44Pia mfalme akamwambia Shimei, “Unajua katika moyo wako maovu yote uliyofanya kwa baba yangu Daudi. Kwa hiyo BWANA atakurudishia maovu yako kichwani pako.45Lakini Sulemani atabarikiwa na enzi ya Daudi itaimarika mbele ya BWANA milele.”

46Kwa hiyo mfalme akamwamuru Benaya mwana wa Yehoyada kwenda kumwua Shimei. Kwa hiyo ule utawala ulikuwa mwema kwa mkono wa Sulemani.

3

1Sulemani akawa na ushirikiano wa kindoa na Farao mfalme wa Misri. Alimwoa binti wa Farao na kumleta katika mji wa Daudi mpaka alipomaliza kujenga nyumba yake, nyumba ya BWANA, na ukuta wa Yerusalemu.2Watu walikuwa wakitoa sadaka kwenye maeneo ya juu, kwa sababu hapakuwa bado na nyumba iliyokuwa imejengwa kwa jina la BWANA.3Sulemani alionyesha upendo wake kwa BWANA kwa kutembea katika maagizo ya Daudi baba yake, isipokuwa tu alitoa dhabihu na kuchoma uvumba mahali pa juu.

4Mfalme akaenda Gibioni kutoa sadaka kule, kwa kuwa hilo ndilo lilikuwa eneo kuu la juu. Sulemani akatoa sadaka maelfu katika madhabahu hiyo.5BWANA akaonekana kwa Sulemani huko Gibioni katika ndoto ya usiku; akasema, “Omba! Unataka nikupe nini?”

6Kwa hiyo Sulemani akasema, “Umeonyesha uaminifu wa agano mkuu kwa mtumishi wako Daudi, baba yangu, kwa sababu alitembea mbele yako kwa ukweli na uaminifu, katika haki ya moyo na katika unyofu wa moyo. Umetunza kwa ajili yake hili agano kuu kwa uaminifu na umempa mwana wake kuketi kwenye kiti chake cha enzi leo.

7Na sasa, BWANA, Mungu wangu, umemfanya mtumishi wako kuwa mfalme katika nafasi ya Daudi baba yangu, japo mimi ni mtoto mdogo. Sijui namna ya kuiingia na kutoka.8Mtumishi wako yuko katikati ya watu wako uliowachagua, kundi kubwa, watu wengi wasiohesabika.9Kwa hiyo umpe mtumishi wako moyo wa uelewa wa kuwahukumu watu wako. Kwani ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?”

10Ombi hili la Sulemani likampendeza Bwana.11Kwa hiyo Mungu akamwambia. “Kwa sababu umeomba jambo hili na haujajiombea maisha marefu au utajiri au uhai wa maadui wako, lakini umeomba ufahamu wa kutambua hukumu ya haki,12tazama sasa nitafanya yote uliyoniomba wakati uliponipa ombi lako. Ninakupa moyo wa hekima na ufahamu, kwa kuwa hapajawahi kuwa na mtu wa kuwa kama wewe kabla yako, na hakuna wa kuwa kama wewe atakayeinuka baada yako.13Pia ninakupa hata ambayo hujaomba, vyote heshima na utajiri, ili kwamba pasije pakawa na mfalme wa kuwa kama wewe katika siku zako zote.14Kama utatembea katika njia zangu na kuyatunza maagizo yangu, kama alivyofanya baba yako Daudi, ndipo nitakapoziongeza siku zako.”

15Kisha Sulemani alipoamka, na tazama, ilikuwa ndoto. Akaja Yerusalemu na akasimama mbele ya sanduku na agano la Bwana. Akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, na akawafanyia sherehe watumishi wake wote.

16Kisha wanawake wawili waliokuwa makahaba wakaja mbele ya mfalme wakasimama mbele yake.17Mwanamke mmoja akasema, “Aa, bwana wangu, mwanamke huyu na mimi tunaishi katika nyumba moja, Nilizaa mtoto tukiwa pamoja na yeye katika nyumba yetu.18Ikatokea siku ya tatu baada ya kujifungua na yeye akajifungua. Tulikuwa sisi tu. Hapakuwepo na mtu mwingine yeyote katika nyumba yetu, ila sisi tu wawili katika hiyo nyumba.

19Kisha mtoto wa mwanamke huyu akafa wakati wa usiku, kwa sababu alimlalia.20Kwa hiyo akaamka wakati huo wa usiku wa manane akamchukua mwanangu toka pembeni yangu, wakati mimi mtumishi wako nilipokuwa usingizini, na akamlaza kwenye kifua chake, na akamlaza mtoto wake aliyekufa juu ya kifua changu.21Asubuhi nilipoamka ili kumhudumia mwanangu, nikaona kuwa alikuwa amekufa. Lakini nilipomwangalia kwa makini wakati huo wa asubuhi, nikagundua kuwa hakuwa yule mwanangu niliyezaa,”

22Yule mwanamke mwingine akasema, “Hapana, huyu aliye hai ndiye wangu, na yule aliyekufa ndiye wako.” Yule mwanamke wa kwanza akasema, “Hapana, yule mtoto aliyekufa ndiye mwanao, na huyu aliye hai ndiye wangu.” Hivi ndivyo walivyoongea mbele ya mfalme.

23Kisha mfalme akasema, “Mmoja wenu anasema, ‘Huyu aliye hai ni wangu, na kumbe mwanao ndiye aliye kufa,’ na mwingine naye anasema, ‘Hapana, mwanao ni yule aliyekufa, na mwanangu ni huyu aliye hai.’”24Mfalme akasema, “Nileteeni upanga.” Kwa hiyo wakaleta upanga kwa mfalme.25Kisha mfalme akasema, “Mgawe mtoto aliye hai katika vipande viwili, na huyu mwanamke apewe nusu na yule mwingine naye apewe nusu.”

26Yule mwanamke mwenye mtoto aliyekuwa hai akamwambia mfalme, kwa kuwa moyo wake ulikuwa na huruma sana kwa mwanae, akasema, “Aa, bwana wangu, mpatie huyu mtoto aliye hai, na usimwue kamwe.” Lakini yule mwanamke mwingine akasema, “Hatakuwa wangu wala wako. Mgawe.”

27Ndipo mfalme aliposema, “Mpe yule mwanamke wa kwanza mtoto aliye hai, na kamwe usimwue. Yeye ndiye mama wa mtoto huyu.”

28Israeli wote waliposikia hukumu ambayo mfalme ametoa, walimwogopa mfalme, kwa sababu waliona kuwa hekima ya Mungu ilikuwa ndani yake kwa ajili ya kutoa kuhukumu.

4

1Mfalme Sulemani alikuwa mfalme wa Israeli.2Hawa ndio waliokuwa wakuu wake: Azaria mwana wa Sadoki alikuwa kuhani.

3Elihorefu na Ahiya mwana wa Shisha, walikuwa makatibu. Yehoshafati mwana wa Ahilui alikuwa mwandishi.
4Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa mkuu wa jeshi. Sadoki na Abiatahari walikuwa makuhani.
5Azaria mwana wa Natahani ndiye aliyekuwa juu ya hawa maakida. Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani na rafiki wa mfalme.
6Ahishari alikuwa mkuu wa nyumba. Adoniramu mwana wa Abda alikuwa mkuu wa watenda kazi.

7Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli yote, ambao walitoa chakula kwa mfalme na watu wake wote. Kila mtu alikuwa na zamu ya kuhudumia kwa mwezi mmoja katika mwaka.8Majina yao yalikuwa ndiyo haya: mwana wa Huri, kutoka milima ya Efraimu;
9mwana wa Dekeri wa Makazi, Shaalibimu, Bethi Shemeshi, na Elonbethi Hanaan;
10mwana wa Hesed, wa Arubothi (kutoka kwake alipatikana Sokohi na nchi yote ya Hefa);
11Mwana wa Abinadabu, wa wilaya yote ya Dori (alikuwa na Tafathi binti wa mfalme ambaye alikuwa mke wake);
12Baana mwana wa Ahiludi, wa Taanaki na Megido, na Beth Shani iliyo upande mwingine wa Zarethani chini ya Yezreel, Kutoka Bethi Shani mpaka Abeli Mehola iliyo upande mwingine wa Jokimeamu;
13mwana wa Geberi, wa Ramothi Gileadi (kutoka kwake tunapata miji ya Yairi mwana wa Manase, ambayo iko Gileadi, na mkoa wa Arigobu ulikuwa wake, ambao uko Bashani, miji sitini yenye maboma na yenye nguzo za malango ya shaba);
14Ahinadabu mwana wa Ido, wa Mahanaimu;
15Ahimaasi, wa Naftali (ambaye pia alimwoa Basemathi binti wa Sulemani kuwa mke wake);
16Baana mwana wa Hushai, ya Asherina Bealothi;
17Yehoshafati mwana wa Paruha, kwa Isakari;
18Shimei mwana wa Ela, wa Benjamini;
19na Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, ambayo ni nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori na Ogi mfalme wa Bashani, na yeye ndiye akida pekee aliyekuwa katika nchi hiyo.

20Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa baharini, nao walikuwa wakila na kunywa na kufurahi.21Sulemani alitawala utawala wote kutoka mtoni hadi kwenye nchi ya Wafilisti na hadi kwenye mpaka wa Misri. Wote walileta kodi na walimtumikia Sulemani katika siku za maisha yake yote.

22Vyakula vya Sulemani kwa siku moja yalikuwa ni Kori thelathini za unga mzuri na kori unga wa ngano,23makisai kumi walionona, na fahari ishirini wa malisho, na kondoo mia moja, nje ya ayala, paa, na kulungu na kuku walionona.24Kwa kuwa utawala wake ulikuwa zaidi ya nchi yote upande huu wa mto, kutoka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa mto, naye alikuwa na amani pande zote.25Yuda na Israeli waliishi kwa usalama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, kutoka Dani mpaka Beerisheba, siku zote za Sulemani.

26Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi 40,000 kwa ajili ya magari yake, na wapanda farasi 12,000.

27Na maakida walileta chakula kwa Sulemani na kwa wale walioketi kwenye meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake. Walihakikisha hakuna kinachopungua.28Na pia walileta kwenye eneo husika shayiri na majani kwa ajili ya wale farasi wa magari na kwa wale farasi wa mbio kila mmoja alileta kadri alivyoweza.

29Mungu alimpa Sulemani hekima kubwa, ufahamu, na upana wa uelewa kama mchanga wa baharini.30Hekima ya Sulemani ilizidi hekima ya watu wote wa mashariki na hekima yote ya Misri.31Alikuwa na hekima kuliko wanaume wote, kuliko Ethani Muezrahi, Hemani, Kaliko, na Darda, wana wa Maholi na habari zake zikaenea hadi kwenye mataifa yote yaliyomzunguka.32Aliongea mithali 3,000 na idadi ya nyimbo zake zilikuwa 1,005.33Aliifafanua mimea, kuanzia mierezi iliyoko Lebanoni hadi Hisopo imeao ukutani. Aliwafafanua wanyama, ndege, vitu vitambaavyo na samaki. Watu walikuja kutoka mataifa yote kuisikia hekima ya Sulemani.34Watu walikuja kutoka falme zote za duniani waliosikia juu ya hekima yake.

5

1Hiramu mfalme wa Tiro aliwatuma watumishi wake kwa Sulemani kwa kuwa alisikia kuwa walikuwa wamemtawaza kuwa mfalme mahali pa baba yake, kwani Hiramu alimpenda Daudi.2Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, akisema,3“Unajua kuwa Daudi baba yangu hakujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wake kwa sababu ya vile vita vilivyomzunguka, kwa kuwa wakati wa uhai wake BWANA alikuwa akiweka maadui wake chini ya nyayo za miguu yake.4Lakini sasa BWANA amenipa mimi pumziko toka pande zote. Hakuna maadui wala majanga.5Kwa hiyo ninakusudia kujenga hekalu kwa jina la BWANA, Mungu wangu, kama BWANA alivyosema kwa Daudi baba yangu, akisema, ‘Mwanao ambaye nitamweka kwenye kiti chako cha enzi mahali pako, ndiye atakayenijengea hekalu kwa jina langu.’6Kwa hiyo sasa amuru wakate mierezi kutoka Lebanoni kwa ajili yangu. Watumishi wangu wataungana na watumishi wako, nami nitakulipa kwa ajili ya watumishi wako ili kwamba upate malipo mazuri kwa kila kitu utakachokubali kukifanya. Kwa kuwa unajua kuwa hakuna mtu mioingoni mwetu anayejua kukata miti kama Wasidoni.”

7Hiramu aliposikia maneno ya Sulemani, akafurahi sana akasema, “BWANA na abarikiwe leo, ambaye amempa Daudi mwana wa hekima juu ya kundi hili kubwa.”

8Hiramu akatuma neno kwa Sulemani, akisema, “Nimeupata ujumbe ule ulionitumia. Nitatoa miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo unahitaji.9Watumishi wangu wataileta miti kutoka Lebanoni hadi baharini, nami nitaiendesha baharini mpaka mahali utakaponielekeza. Nitaigawa pale, nawe utaichukua. Utafanya kile ninachohitaji kwa kuwapa chakula watumishi wangu.”

10Kwa hiyo Hiramu akampa Sulemani miti yote ya mierezi na miti ya miberoshi ambayo alihitaji.11Sulemani akampa Hiramu kori ishirini elfu za ngano kwa ajili ya chakula cha watumishi wake na kori ishirini za mafuta safi. Sulemani akavitoa hivi kwa Hiramu mwaka baada ya mwaka.12BWANA akampa Sulemani hekima, kama alivyokuwa amemwahidi. Kulikuwa na amani kati ya Hiramu na Sulemani na wote wawili wakafanya agano.

13Mfalme Sulemani akaandaa wafanya kazi kutoka Israeli yote. Idadi ya watenda kazi walioandaliwa ilikuwa wanaume 30,000.14Aliwatuma kwenda Lebanoni, aliwatuma kwa zamu ya watu 10,000 kila mwezi. Kwa mwezi mmoja walienda Lebanoni na miezi miwili walikaa nyumbani. Adoniramu ndiye aliyekuwa msimamizi wa watenda kazi.15Sulemani alikuwa na watu 70,000 waliokuwa wabeba mizigo na watu 80,000 wa kukata mawe milimani.16Zaidi ya hao, walikuwepo maakida 3,300 ambao pia waliokuwa wakiisimamia hiyo kazi.17Kwa amri ya mfalme walileta mawe makubwa ya thamani kwa ajili ya kulaza kwenye msingi wa hekalu.18Kwa hiyo wajenzi wa Sulemani na wajenzi wa Hiramu na Wagebaliti walifanya kazi ya kukata na kuandaa mbao kwa ajili ya ujenzi wa hekalu.

6

1Kwa hiyo Sulemani akaanza kulijenga hekalu. Hii ilikuwa mwaka wa 480 baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, katika mwaka wa nne wa utawala wa Sulemani huko Israeli, katika mwezi wa Ziv, ambao ndio mwezi wa pili.

2Hekalu ambalo mfalme Sulemani alimjengea BWANA lilikuwa na urefu wa mita 27, na upana wa mita 9, na kimo cha mita 13.5.3Na ukumbi uliokuwa mbele ya hekalu ulikuwa na urefu wa mita 9 na upana wa mita 4.5 sawa na upana wa sehemu kuu ya hekalu.4Lile hekalu alilitengenezea madirisha ambayo fremu zake kwa nje yalifanya yaonekane membamba kuliko ile sehemu ya ndani.5Na ukuta wa nyumba aliuzungushia vyumba kuzunguka pande zake, kushikamana na vyumba vya nje na vya ndani ya hekalu. Akajenga vyumba katika pande zote.6Kile chumba cha chini kilikuwa na upana wa mita 2.3, kile cha kati kilikuwa na upana wa mita 2.8, na kile cha tatu kilikuwa na upana wa mita 3.2. Upande wa nje akaupunguza ukuta wa nyumba pande zote, ili boriti zisishikamane ukutani mwa nyumba.

7Hekalu lilijengwa kwa mawe yaliyokuwa yamechongwa chimboni. Hakuna nyundo, wala shoka au chombo chochote cha chuma kilisikika wakati hekalu lilipokuwa likijengwa.

8Upande wa kusini wa hekalu kulikuwa na lango la chini, ambalo mtu hupanda kwa madaraja mpaka juu kwenye chumba cha kati, na kutoka chumba cha kati hadi chumba cha tatu.9Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza, akalifunika hekalu kwa boriti na mbao za mwerezi.10Akajenga vyumba vya pembeni mwa hekalu, kila upande mita 2.3 kwenda juu. Navyo vikaunganishwa na hekalu kwa mbao za mierezi.

11Neno la BWANA likamjia Sulemani, likisema,12“Kuhusu hili hekalu ambalo unajenga, kama utatembea katika maagizo yangu na kuhukumu kwa haki, na kutunza amri zangu na kuishi kwa hizo, ndipo nitakapozithibitisha ahadi zangu na wewe ambazo niliziahidi kwa baba yako Daudi.13Nitaishi kati ya watu wa Israeli nami sitawatupa.”

14Kwa hiyo Sulemani akalijenga hekalu mpaka akalimaliza.15Kisha akajenga kuta za ndani za hekalu kwa mbao za mwerezi. Kuanzia sakafu ya hekalu hadi boriti za juu, kwa ndani akazifunika kwa miti, na akaifunika sakafu kwa mbao za miberoshi.16Alijenga mita 9 ndani ya hekalu kwa mbao za miberoshi kutoka sakafuni hadi juu. Hiki ni chumba cha ndani, cha patakatifu sana.17Ule ukumbi mkuu, ulikuwa mahali pakatifu amabao ulikuwa mbele ya patakatifu sana, ulikuwa wa mita 18. Hapo kulikwa na mbao za mwerezi ndani ya hekalu, zilizokuwa zimechongwa kwa sura ya vibuyu na maua yaliyochanua.18Zote zilikuwa za mierezi kwa ndani. Hapakuonekana chochote ndani kilichokuwa kimetengenezwa kwa mawe.

19Sulemani alitengeneza kile chumba cha ndani kwa lengo la kuweka sanduku la agano la BWANA.20Kile chumba cha ndani kilikuwa na upana wa mita 9, na kimo cha mita 9. Sulemani alizifunika kuta kwa dhabahu na madhabahu aliifunika kwa mbao za mierezi.21Sulemani alifunika ndani ya hekalu kwa dhahabu safi na akaweka mikufu ya dhahabu iliyopita mbele ya chumba cha ndani, na kulifunika eneo la mbele kwa dhabahu.22Akalisakafia kwa dhahabu eneo lote la ndani mpaka akamaliza hekalu lote. Pia akalisakafia kwa dhahabu madhahabu yote ya chumba cha ndani.

23Sulemani akatengeneza makerubi mawili kwa mbao za mizeituni, kila moja lilikuwa na kimo cha mita 4.5 kwa ajili ya chumba cha ndani.24Bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mita 2.3. Kwa hiyo kutoka ncha ya bawa moja hadi ncha ya bawa lingine kulikuwa na umbali wa mita 4.5. Yule25kerubi mwingine naye alikuwa na bawa lenye kipimo cha mita 4.5 Makerubi hawa walikuwa wanafanana kwa umbo na kwa vipimo.26Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mita 4.5 na yule wa pili alikuwa hivyo hivyo.27Sulemani aliwaweka hao kerubi kwenye chumba cha patakatifu sana. Bawa moja la kerubi lilikuwa limeenea kiasi kwamba bawa moja liligusa ukuta huu na bawa la yule wa pili nalo liligusa ukuta wa upande mwingine. Hayo mabawa yalikuwa yanakutana katikati ya chumba cha patakatifu sana.28Sulemani aliwafunika hao kerubi kwa dhahabu.

29Akazinakshi kuta zote kwa sura za makerubi, miti ya mitende, na maua yaliyochanua, kwa vyumba vya nje na vya ndani.30Sulemani akalisakafia hekalu kwa dhahabu, kwa vyumba vyote vya ndani na vya nje.

31Sulemani akatengeneza milango ya mbao za mizeituni kwenye lango la kuingia ndani. Aliweka vizingiti na miimo kwenye pande tano.32Kwa hiyo akatengeneza na milango miwili ya mizeituni, na akainakshi kwa makerubi, na mitende, na maua yaliyochanua. Akasakafia kwa dhahabu na akatandaza dhahabu kwenye makerubi na kwenye mitende.33Kwa njia hii, akalitengenezea hekalu miimo miwili ya mbao za mizeituni yenye pande nne34na milango miwili ya mbao za mierezi. Zile mbao mbili za mlango mmoja zilikuwa zikijikunja na mbao mbili za mlango wa pili nazo zilikuwa zikijikunja pia.35Akazinakshi kwa makerubi, mitende, na maua yaliyochanua, na pia akazisakafia kwa dhahabu juu ya zile nakshi.

36Akalijenga Korido la ndani kwa safu tatu za mawe ya kuchongwa na safu moja ya mhimili wa mierezi.

37Msingi wa hekalu ulijengwa katika mwaka wa nne, wa mwezi wa Ziv.38Mwaka wa kumi na moja mwezi wa Buli, ambao ndio mwezi wa nane, sehemu zote za hekalu zilimalizika na sharti zake zote. Sulemani alilijenga hekalu kwa miaka saba.

7

1Ilimchukua Sulemani miaka kumi na tatu kujenga ikulu yake.2Aliijenga ikulu iliyoitwa mwitu wa Lebanoni. Urefu wake ulikuwa mita 46, na upana wake ulikuwa mita 23, na kimo chake kilikuwa mita 14. Nayo ilikuwa na safu nne ya nguzo za mierezi na mithili ya mwerezi juu ya nguzo.3Paa la ikulu lilikuwa la mwerezi ambalo lilikaa juu ya mihimili. Mihimili hiyo ilikuwa imeshikiliwa na nguzo. Kulikuwa na mihimili arobaini na tano, ambayo ilikuwa katika safu kumi na tano.4Nayo mihimili ilikuwa safu tatu, na kila dirisha lilikabili dirisha lingine katika madaraja matatu.5Milango yote na miimo ilitengenezwa kwa mraba, na madirisha yalikuwa yakikabiliana katika madaraja matatu.

6Akatengeneza baraza lenye urefu wa mita 23 na upana wa mita 14. Mbele yake kulikuwa na ukumbi ulioezekwa.

7Sulemani akajenga baraza yenye kiti cha enzi ambacho alitolea hukumu ya haki. Nayo ilikuwa imeezekwa kwa mwerezi kutoka sakafu moja hadi nyingine.

8Nyumba ya Sulemani ambayo alikusudia kuishi, katika behewa nyingine ndani ya sehemu ya chini ya ikulu, ilitengenezwa kwa kazi hiyo hiyo. Pia alimjengea binti wa Farao nyumba kama hii, ambaye alikuwa mke wake

9Majengo haya yalipambwa kwa vitu vya thamani, mawe ya thamani, yaliyochongwa na kukatwa kwa msumeno kufuata vipimo sahihi na kulainishwa pande zote. Mawe ya namna hii ndiyo yale yaliyotumika kuanzia kwenye msingi hadi juu, pia na nje hadi kwenye baraza.10Msingi ulijengwa kwa mawe makubwa sana na ya thamani yenye urefu wa mita 3.7 na mengine mita 4.8.11Kwa juu ilipambwa kwa, mawe ya thamani yaliyochongwa sawa sawa kwa msumeno na kwa mihimili ya mierezi.12Na behewa kubwa iliyokuwa ikizunguka ikulu ilikuwa na safu tatu za mawe yaliyokatwa na safu moja ya mihimili ya mierezi kama ilivyo kwenye baraza la ndani la hekalu la BWANA na ule ukumbi wa hekalu.

13Mfalme Sulemani alituma watu kumleta Huramu kutoka Tiro.14Huramu alikuwa mwana wa mjane wa kabila ya Naftali; baba yake alikuwa mtu wa Tiro, mfua shaba. Huramu alikuwa mwingi wa hekima na ufahamu na stadi za kufanya kazi kubwa za shaba. Aliletwa kwa mfalme ili kufanya kazi zilizohusiana na shaba kwa mfalme.

15Huramu alizilemba zile nguzo mbili za shaba, kila moja ilikuwa na kimo cha mita 8.3 na mzingo wa mita 5.5.16Akatengeneza taji mbili za shaba za kuwekwa juu ya zile nguzo. Kimo cha kila taji ilikuwa mita 2.3.17Kulikuwa na nyavu za kuwa kama kazi ya kusuka, na masongo ya mikufu, kwa ajili ya kuvipamba vile vichwa vya nguzo, nayo yalikuwa saba kwa kila kichwa.18Kwa hiyo Huramu akafanya safu mbili za komamanga kuzunguka vile vichwa vya nguzo ili kuvipamba vile vichwa.19Zile taji kwenye vile vichwa vya nguzo za ukumbi zilikuwa zimepambwa kwa maua, yenye vimo vya mita 1.8.20Hizo taji kwenye hizo nguzo mbili kwenye vichwa vyake, karibu yake kulikuwa na makomamanga 200 yote yakiwa kwenye safu.21Alisimamisha nguzo kwenye ukumbi wa hekalu; Ile nguzo ya kuume akaipa jina la Yakini; na ile ya kushoto akaipa jina la Boazi.22Na juu ya zile nguzo kulikuwa na mapambo kama maua. Hivyo ndivyo zile nguzo zilivyotengenezwa.

23Tena akafanya bahari ya kusubu, yenye mita 2.3 kutoka ukingo hadi ukingo, kimo chake kilikuwa mita 4.6, mzingo wake ulikuwa mita 13.7.24Na chini ya ile bahari kulikuwa na vibuyu vilivyoizunguka, vilikuwa vibuyu kumi na nane katika kila mita, vilivyowekwa katika kila hicho kipande wakati bahari inapokuwa kalibu.

25Bahari ikakaa juu ya makisai kumi na mbili; tatu zilitazama kaskazini, tatu zikitazama magharibi, tatu zikitazama kusini na tatu zikitazama kaskazini. Ile bahari iliwekwa juu yao, na pande zao zote za nyuma zilikuwa ndani.26Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi huingia bathi 2,000 za maji.

27Huramu akatengeneza makalio kumi ya shaba. Kila kalio lilikuwa na urefu wa mita 18, upana wa mita 1.8, na kimo cha mita 1.3.28Hivi ndivyo kazi za makalio zilivyofanywa. Yalikuwa na papi ambazo zilikaa kati kati ya vipandio,29na juu ya papi na vipandio kulikuwa na simba, makisai, na makerubi. Chini na juu ya simba kulikuwa na masongo ya kazi ya kufuliwa.30Kila kalio lilikuwa na magurudumu ya shaba na vipini, na pande zake nne na miguu yake minne ilikuwa na mataruma chini ya birika. Chini ya birika yalikuweko mataruma ya kusubu yenye masongo katika kila upande.31Na kinywa chake kilikuwa cha kuviringana, chenye upana wa sentimita arobaini na sita, na ile taji ilikuwa na sentimita ishirini na tatu. Na kinywa chake kilikuwa na nakshi, na papi zake zilikuwa za mraba, na wala sio za mviringo.32Yale magurudumu mawili yalikuwa chini ya papi, na mikono ya magurudumu yalikuwa ndani ya makalio. Kimo cha yale magurudumu kilikuwa sentimeta 69.33Yale magurudumu yalikuwa kama ya gari. Mikono yake, na maduara, matindi yake, na vipande vya ndani vyote vilikuwa vya kusubu.

34Kulikuwa na mataruma manne katika pande zake nne za makalio, yaliyokuwa yameshikamanishwa na kalio lenyewe.35Juu ya makalio kulikuwa na duara yenye kina cha sentimita ishirini na tatu, na juu ya makalio mashikio yake na papi zake zikiwa zimeshikamanishwa.36Juu ya mabamba na papi zake Huramu akachora makerubi, simba, na mitende ambayo ilifunika nafasi ya juu, nayo ilikuwa imezungukwa na masongo.37Alitengeneza makalio kumi kwa jinsi hii. Yote yalikuwa yametengenezwa kwa kufanana, na yalikuwa ya vipimo sawa, na sura inayofanana.

38Huramu akatengeneza birika kumi za shaba. Birika moja liliweza kubeba bathi arobaini za maji. Kila birika lilikuwa mita 1.8 toka birika moja hadi jingine na kulikuwa na birika moja katika kila kalio kati ya yale kumi.39Alitengeneza makalio tano upande wa kusini unaoelekea upande wa hekalu. Akatengeneza bahari katika upande wa mashariki, ukielekea upande wa kusini wa hekalu.40Huramu akatengeneza birika na koleo na besini la kunyunyizia, Kisha akamaliza kazi yote aliyofanya kwa mfalme Sulemani katika hekalu la BWANA:
41Zile nguzo mbili, na lile besini likawa kama taji ambalo lilikuwa juu ya zile nguzo, na nyavu mbili za mapambo za kufunika zile besini mbili za kuwa kama taji zilizokuwa juu ya nguzo.
42Kisha akatengeneza makomamanga 400 kwa ajili ya zile nyavu mbili za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila kazi ya nyavu kwa ajili ya kufunikia zile besini mbili kama taji iliyo juu ya nguzo,
43yale makalio kumi, na birika kumi kwenye makalio.
44Akatengeneza bahari na makisai kumi chini yake;45na masufuria, koleo, birika na vyombo vingine vyote. Huramu akivitengeneza kwa shaba iliyosuguliwa, kwa ajili ya mfalme Sulemani, na kwa ajili ya hekalu la BWANA.

46Mfalme alivisubu katika uwanda wa Yorodani, katika udongo mfinyanzi kati ya Sukoti na Zarethani.

47Sulemani hakuvipima vyombo vyote kwa sababu vilikuwa vingi mno kuvipima, na kwa sababu uzito wa shaba ulikuwa hauwezi kupimwa.

48Sulemani akatengeneza mapambo yote yaliyokuwa kwenye hekalu la BWANA kwa kutumia dhahabu: Ile madhabahu ya dhahabu na ile meza ambayo iliwekwa mikate ya wonyesho.
49Vile vinara vya dhahabu, ambavyo vitano vilikuwa upande wa kulia na vitano mkono wa kushoto, mbele ya chumba cha ndani, vilikuwa vya dhahabu safi, na maua, na taa na koleo zilikuwa za dhahabu.
50Vile vikombe, na makasi, mabakuri, na vijiko, na vyetezo vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa dhahabu safi. Na bawaba za dhahabu za milango ya ndani, ambazo ndio mahali patakatifu sana, na milango ya ukumbi mkubwa, vyote vilitengenezwa kwa dhahabu.

51Kwa njia hii, kazi yote ambayo mfalme Sulemani alifanya kwa ajili ya hekalu ilimalizika. Kwa Sulemani akaviingiza ndani yake vitu vile vilivyokuwa vimewekwa wakfu na Daudi, baba yake, na fedha na dhahabu, na mapambo, na vile vya ndani ya hazina ya BWANA.

8

1Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wote wa makabila, na viongozi wa familia za wana wa Israeli, mbele yake kule Yerusalemu, ili waliingize ndani lile sanduku la agano la BWANA kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.2Wanaume wote wa Israeli walikusanyika mbele ya mfalme Sulemani kwenye sherehe, katika mwezi wa Ethanim, ambao ndio mwezi wa saba.

3Wazee wote wa Israeli walikuja, na makuhani wakalibeba lile sanduku.4Wakalileta lile sanduku la BWANA, lile hema la kukutania na mapambo yote matakatifu ambayo yalikuwa kwenye hema. Makuhani na Walawi wakavileta vitu hivi.5Mfame Sulemani na mkutano wote wa Israeli wakaja pamoja mbele ya sanduku, wakatoa sadaka za kondoo na makisai ambazo hazikuweza kuhesabika.

6Makuhani wakaliingiza ndani lile sanduku la agano la BWANA na wakaliweka mahali pake, ndani ya chumba cha ndani, patakatifu sana, chini ya yale mabawa ya makerubi.7Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao hadi mahali pa sanduku la agano, na walifunika sanduku na miti yake kwani ilitumika kulibeba.8Ile miti ilikuwa mirefu sana kiasi kwamba miishio yake ilionekana tokea kwenye eneo takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini haikuweza kuonekana kutokea nje. Miti hiyo iko mpaka leo.9Ndani ya sanduku hapakuwemo na kitu chochote isipokuwa vile vidonge vya mawe ambavyo Musa aliviweka alipokuwa mlima Horebu, wakati BWANA alipofanya agano na watu wa Israeli walipotoka kwenye nchi ya Misri.

10Ilitokea kwamba wakati makuhani walipotoka mahali patakatifu, lile wingu lilifunika hekalu la BWANA.11Makuhani hawakuweza kusimama kwa ajili ya kutumika kwa sababu utukufu wa BWANA ulifunika hekalu.

12Kisha Sulemani akasema, “BWANA amesema kuwa anaweza kuishi hata kwenye giza nene.
13Lakini nimekujengea makao ya kujivunia, mahali pako pa kuishi milele.”

14Kisha mfalme akageuka na kuwabariki mkusanyiko wa watu wa Israeli, wakati huo mkusanyiko wa Waisraeli walikuwa wamesimama.15Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, asifiwe, ambaye alisema na baba yangu Daudi, na ametimiza kwa mikono yake, akisema,16‘Tangu siku ile niliyowatoa watu wangu Israeli kutoka Misri, sikuchagua mji wowote toka kwa makabila yote ya Israeli ambako ningeijenga nyumba, kwa ajili ya jina langu kuwemo humo. Hata hivyo, nilimchagua Daudi kuwatawala watu wangu Israeli.

17Sasa ilikuwa kwenye moyo wa Daudi baba yangu kujenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.18Lakini BWANA alimwambia baba yangu Daudi, ‘Ilikuwa ndani ya moyo wako kunijengea nyumba kwa jina langu, ulifanya vyema kwa hilo kuwa ndani ya moyo wako.19Ingawa hutanijengea nyumba; badala yake mwanao, mmoja wa wanao atakayezaliwa toka viunoni mwako, atanijengea nyumba kwa jina langu,’

20BWANA amelibeba lile neno alilokuwa amesema, kwa kuwa nimeinuka mahali pa baba yangu Daudi, na nimeketi kwenye kiti cha enzi cha Israeli, kama BWANA alivyoahidi. Nimeijenga nyumba kwa jina la BWANA, Mungu wa Israeli.21Nimetengeneza mahali kwa ajili ya sanduku ndani yake, ambamo ndani yake kuna agano la BWANA, ambalo alifanya na baba zetu alipowatoa toka nchi ya Misri.”

22Sulemani alisimama mbele ya madhabahu ya BWANA, mbele ya mkusanyiko wote wa Waisraeli, naye akanyosha mikono yake kuelekea mbinguni.23Akasema, “BWANA, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe juu mbinguni au chini duniani, ambaye hutunza agano lake kwa uaminifu kwa watumishi wako ambao hutembea mbele yako kwa mioyo yao yote;24wewe ambaye umetunza ahadi yako na mtumishi wako Daudi baba yangu ile uliyomwahidi. Naam, ulisema kwa kinywa chako na sasa umeitimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.25Sasa basi, BWANA, Mungu wa Israeli, timiza kile ulichomwahidi mtumishi wako Daudi baba yangu, pale uliposema, ‘Hautashindwa kunipa mtu mbele ya macho yangu ambaye ataketi katika kiti cha enzi cha Israeli, kama tu uzao wako watakuwa waangalifu kutembea mbele yangu, kama vile wewe ulivyotembea mbele yangu.’26Sasa basi, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ile ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, itimie.27Je, ni kweli kwamba Mungu ataishi duniani? Tazama, ulimwengu wote na mbingu hazikutoshi sembuse nyumba hii niliyoijenga!28Kwa hiyo Mungu naomba uyajali maombi haya ya mtumishi wako na maombi yake, BWANA, Mungu wangu; sikiliza kilio na maombi ambayo mtumishi wako anakuomba leo.29Naomba ulitazame hekalu hili mchana na usiku, mahali ambapo ulisema, ‘Jina langu na uwepo wangu utakuwa’ ili niweze kuwa nasikiliza maombi ambayo mtumishi wako ataomba mahali hapa.30Kwa hiyo sikia maombi ya mtumishi wako na ya watu wako Israeli tunapokuwa tunaomba mahali hapa. Ndiyo, sikia kutokea mahali ambapo unaishi, kutoka katika mbingu za mbingu; na unaposikia tafadhali samehe.31Kama mtu atamtendea uovu jirani yake na anapewa sharti la kiapo, na kama atakuja na kuapa mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,32basi usikie kutoka mbinguni ukatende na kuwahukumu watumishi wako, ukamhukumu mwovu, ili kumletea tabia zake kichwani mwake, na kumtunza mwenye haki kuwa hana hatia, na kumpa thawabu yake ya haki.33Watu wako Israeli watakapopigwa na adui kwa sababu ya kutenda dhambi dhidi yako, na kama watakurudia, na kulikiri jina lako, na kukusihi, na kuomba msamaha kwako katika hekalu hili,34tafadhali nakuomba usikie kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi ambayo uliwapa mababu zao.35Kama mbingu zitafungwa na mvua hazinyeshi kwa sababu watu wamekutenda dhambi wewe na kama wataomba mahali hapa, na kulikiri jina lako, na kugeuka toka dhambi zao na kama umewapiga,36basi sikia tokea mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na za watu wako Israeli, utakapowafundisha njia njema inayowapasa; basi uinyeshee mvua nchi yako, ambayo uliwapa watu wako kuwa urithi.37Na kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna magonjwa, au ukungu, nzige au funza; au kama adui atavamia malango ya mji katika nchi yao, kama kuna tauni au magonjwa yeyote,38na kama kuna mtu au watu wa Israeli wataomba kila mmoja akaijua hiyo tauni katika moyo wake wakati akinyosha mikono yake katika hekalu hili.39Basi usikie kutoka mbinguni, mahali unapoishi, utende na kusamehe, na umpe kila mtu thawabu anayostahili kwa kile anachofanya; wewe unajua moyo wake, kwa sababu ni wewe pekee yako ujuaye mioyo ya watu.40Fanya hivi ili kwamba wawe na hofu kwako katika siku zote za maisha yao wanayoishi katika nchi uliyowapa mababu zetu.41Na nyongeza yake, kuhusiana na mgeni ambaye si mtu wako wa Israeli: atakapokuja kutokea nchi ya mbali kwa sababu ya jina lako -42kwa sababu watasikia jina lako lilivyo kuu, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulioinuliwa, atakapokuja na kuomba mahali hapa pa hekalu,43tafadhali usikie kutokea katika mbingu, mahali unapoishi, na umfanyie huyo mgeni akuombacho. Fanya hivi ili makundi ya watu wote duniani wakujue jina lako na kukuhofia, kama wanavyofanya watu Israeli. Fanya hivyo ili wajue kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.44Na kama watu wako wataenda vitani dhidi ya adui, kwa njia yeyote unayoweza kuwatuma, na kama watakuomba wewe, BWANA, kuelekea mji huu uliouchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.45Basi sikia tokea mbinguni maombi yao, dua zao, na uwasaidie wanachohitaji.46Na kama watafanya dhambi dhidi yako, kwa kuwa hakuna hata mtu mmoja asiyefanya dhambi, na kama una hasira dhidi yao na kuwapeleka kwa maadui, ili kwamba maadui wawachukue mateka katika nchi yao, mbali au karibu.47Na kama watatambua kuwa wako katika nchi ya utumwa, na kama watatubu na kuomba neema kwako kutokea katika nchi ya watekaji. Na kama watasema, ‘Tumetenda kwa ukaidi na tumefanya dhambi. Tumetenda kwa uovu.’48Na kama watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa roho zao zote katika nchi ya maadui ambao wanawakamata, na kama watakuomba wewe kuelekea nchi yao, ambayo uliwapa mababu zao, na kuelekea katika mji uliouchagua, nakuelekea katika nyumba ambayo nimeijenga kwa jina lako.49Basi usikie maombi yao, na dua zao tokea mbinguni, mahali unapoishi, na ukaitetee haki yao.50Wasamehe watu wako waliotenda dhambi dhidi yako, na dhambi zao zote ambazo kwazo wamekukosea wewe dhidi ya amri zako. Uwahurumie mbele ya maadui zao ambao waliwachukua mateka, ili kwamba maadui zao pia wawahurumie watu wako.51Hawa ni watu wako uliowachagua, ambao uliwaokoa toka nchi ya Misri kama kwamba walikuwa katikati ya tanuru ambamo vyuma huyeyushwa.52Naomba kwamba macho yako yatazame dua za mtumishi wako na kwa dua za watu wako Israeli, ili uwasikie kila wanapokulilia.53Kwa kuwa uliwatenga toka kwa watu wengine wa duniani ili wawe wako nakupokea ahadi zako, kama vile ulivyomwambia Musa mtumishi wako, wakati ulipowatoa baba zetu toka Misri, BWANA.”

54Kwa hiyo ilitokea wakati Sulemani alipomaliza kuomba maombi haya na dua zake kwa BWANA, aliamka toka madhabahu ya BWANA, pale alipokuwa amepiga magoti na mikono yake ikiwa imenyoshwa kuelekea mbinguni.55Alisimama na kuubariki mkutano wote wa Israeli kwa sauti kuu. Alisema,56“Asifiwe BWANA, aliyewapatia pumziko watu hawa Israeli, akitunza ahadi zake zote. Hakuna hata moja ambayo haijatekelezwa katika ahadi njema za BWANA ambazo aliahidi akiwa na Musa mtumishi wake.57BWANA, Mungu wetu awe pamoja nasi, kama alivyokuwa pamoja na mababu zetu. Asituache wala kututelekeza,58kwamba aunganishe mioyo yetu na yeye, ili tuishi katika njia zake na kuzishika amri zake na taratibu zake na maagizo yake, ambayo aliwaagiza baba zetu.59Na maeneo haya ambayo nimesema, ambayo nimesihi mbele ya BWANA, yawe karibu na BWANA, Mungu wetu usiku na mchana, ili kwamba awasadie katika haki za mtumishi wake na haki za watu wake Israeli, kama watakavyoomba kila siku;60kwamba watu wote duniani wajue kwamba BWANA, ndiye Mungu, na hakuna Mungu mwingine!61Kwa hiyo ifanyeni mioyo yenu iwe ya haki mbele ya BWANA. Mungu wetu, ili tutembee katika maagizo na kuzishika amri zake, kama ilivyo leo.”

62Kwa hiyo mfalme na watu wote pamoja naye wakatoa sadaka kwa BWANA.63Sulemani akatoa sadaka ya amani, ambayo aliifanya kwa BWANA: Nayo ilikuwa makisai 22,000, na kondoo 120,000. Kwa hiyo mfalme na watu wa Israeli wakaiweka wakfu nyumba ya BWANA.

64Siku hiyo mfalme aliweka wakfu behewa ya katikati mbele ya hekalu la BWANA, kwa kuwa pale ndipo alipotoa sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga, na sadaka za mafuta ya amani, kwa sababu ile madhabahu ya shaba iliyokuwa mbele ya BWANA ilikuwa ndogo sana kwa sadaka za kuteketezwa, sadaka za unga, na mafuta ya sadaka za amani.

65Kwa hiyo Sulemani akafanya sherehe wakati huo, Nayo Israeli yote pamoja naye, mkutano mkubwa, kutoka Lebo Hamathi hadi kijito cha Misri, wakaja mbele ya BWANA, Mungu wetu kwa muda wa siku saba na pia kwa siku saba zingine, ambayo jumla yake ni siku kumi na nne.66Na ilipofika siku ya nane aliwatawanya watu, nao wakambariki mfalme kisha wakaenda nyumbani kwao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa wema wote ambao BWANA alimwonyesha Daudi, mtumishi wake, na kwa watu wake, Israeli.

9

1Sulemani alipomaliza kulijenga hekalu la BWANA, na ikulu ya mfalme, na baada ya kukamilisha vyote alivyokusudia kufanya,2BWANA alionekana kwa Sulemani kwa mara ya pili, kama alivyoonekana kwake kule Gibeoni.3Na BWANA akamwambia, “Nimeyasikia maombi yako na dua zako ambazo umeniomba. Nimeitakasa nyumba hii ambayo umeijenga, kwa ajili yangu, ili niweke jina langu humo milele. Macho yangu na moyo wangu yatakuwa humo kwa nyakati zote.4Lakini pia na wewe, kama utatembea mbele zangu kama Daudi baba yako alivyotembea kwa haki na unyofu katika moyo wako, ukitii yote niliyokuamuru na kuyashika maagizo na sheria zangu,5ndipo nitakapoimarisha kiti cha enzi kwa Israeli milele, kama nilivyomwahidi baba yako Daudi, nikisema, uzao wako hautaondoka katika kiti cha enzi cha Israeli.6Lakini kama utageuka, wewe au watoto wako, na kutozishika amri zangu na maagizo yangu ambayo nimeyaweka mbele zako, na kama utaenda kuabudu miungu mingine na kuisujudia,7basi nitaikatilia mbali Israeli kutoka katika ardhi niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli itakuwa mfano wa kukejeliwa na kitu cha kutusiwa katika mataifa yote.8Ijapokuwa hekalu hili limetukuka sasa, kila mtu atakayepita pembeni yake atasituka na kuzoomea. Watajiuliza, ‘Kwa nini BWANA amefanya hili katika nchi hii na kwa nyumba hii?’9Na wengine watajibu, ‘Ni kwa sababu walimwacha BWANA, Mungu wao, ambaye aliwaleta mababu zao toka Misri, na sasa wamegeukia miungu mingine ambayo wameiinamia na kuisujudu. Hiyo ndiyo sababu BWANA amewaletea majanga haya yote.’”

10Ilitokea mwishoni mwa miaka ishirini, Sulemani alikuwa amemaliza kuyajenga majengo yote mawili, hekalu la BWANA na ikulu ya mfalme.11Basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mbao za mierezi na miboreshi, pamoja na dhahabu; vitu vyote ambavyo Sulemani alitamani. Kwa hiyo mfalme Sulemani akampatia Hiramu miji ishirini huko Galilaya.12Hiramu akaja kutoka Tiro kuiona ile miji ambayo Sulemani alikuwa amempatia, lakini hakupendezwa nayo.13Kwa hiyo Hiramu akasema, “Ndugu yangu, ni miji gani hii uliyonipatia?” Hiramu akaiita nchi ya Kabuli mpaka leo.14Hiramu alikuwa amemtumia mfalme tani nne za dhahabu.

15Vifuatavyo ndivyo vigezo ambavyo mfalme Sulemani aliweka: ili kulijenga hekalu la BWANA na ikulu yake, kuijenga Milo na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, Megido, na Gezari.16Farao mfalme wa Misri alikuwa ameenda kuitwaa Gezeri, akaichoma moto, na kuwaua Wakanaani katika mji. Kisha Farao akampatia binti yake ule mji, mke wa Sulemani kuwa zawadi ya arusi.17Kwa hiyo Sulemani akaijenga Gezeri na Bethi Horoni ya Loweri,18Baalathi na Tamari jangwani katika nchi ya Yuda,19na miji yote ya hazina yote iliyokuwa yake, na miji ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na hata kama alipenda kuijenga kwa ajili ya fahari yake kule Yerusalemu, Lebanoni, na katika nchi yote kwenye utawala wake.

20Na kwa watu wote waliokuwa wamesalia wa Waamori, Wahiti, Waperezi, Wahivi, na Yebu, ambao hawakuwa Waisraeli,21na uzao wao waliokuwa wamesalia baada yao katika nchi, ambao Waisraeli hawakuweza kuwaangamiza kabisa, Sulemani akawafanya kuwa vibarua, ambao wako hata leo.22Hata hivyo, Sulemani hakuwafanya kuwa shokoa watu wa Israeli. Badala yake, walifanyika kuwa wanajeshi wake na watumishi wake, maakida wake, na wakuu wake, na majemedari wake na wapanda farasi wake.23Hawa ndio waliokuwa maakida wakuu waliokuwa wakiwasimamia kazi za Sulemani, watu 550, walikuwa wasimamizi wa watu waliokuwa wakifanya kazi.

24Binti wa Farao alihama kutoka mji wa Daudi kwenda kwenye ile nyumba ambayo Sulemani alimjengea. Baadaye, Sulemani akaijenga Milo.

25Mara tatu kwa kila mwaka Sulemani alitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani katika madhabahu ambayo alimjengea BWANA, akifukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwa mbele ya BWANA. Kwa hiyo akalimalizia hekalu na sasa alikuwa akilitumia.

26Tena Sulemani alitengeneza merikebu kule Ezioni Geberi, ambayo iko karibu na Elathi katika ufukwe wa bahari ya shamu, katika nchi ya Edomu.27Hiramu alituma watumishi kwenye merikebu ya Sulemani, wanamaji wanaoijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani.28Walikwenda kwa Ofri pamoja na watumishi wa Sulemani. Kutoka huko walileta takribani tani 14.5 za dhahabu kwa Sulemani.

10

1Malkia wa Sheba aliposikia uvumi wa Sulemani kuhusu jina la BWANA, alikuja kumjaribu kwa maswali magumu.2Alikuja Yerusalemu na msafara mrefu, pamoja na ngamia waliokuwa wamebeba mizigo ya manukato, dhahabu nyingi, na mawe mengi ya thamani, akamwambia Sulemani yote yaliyokuwa moyoni mwake.3Sulemani akajibu maswali yake yote. Hapakuwepo na swali ambalo aliulizwa na mfalme akashindwa kujibu.4Malkia wa Sheba alipoona hekima yote ya Sulemani, na ikulu aliyokuwa amejenga,5chakula cha mezani kwake, kuketi kwa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na kuvaa kwao, pia wanyweshaji wake, na jinsi alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya BWANA, roho yake ilizimia.

6Akamwambia mfalme, “Ni kweli, ile taarifa ambayo nimeisikia nchini kwangu juu ya maneno yako na hekima yako.7Sikuamini kile nilichosikia hadi nilipofika hapa, na sasa macho yangu yamejionea. Hata nusu ya hekima na utajiri wako! Umezidi uvumi ambao nilikuwa nimesikia.8Tazama jinsi walivyobarikiwa wake zako, na jinsi walivyobarikwa watumishi wako ambao daima husimama mbele yako, kwa sababu wanasikia hekima zako.9BWANA, Mungu wako asifiwe, ambaye amependezwa na wewe, ambaye alikuweka kwenye kiti cha enzi cha Israeli. Kwa sababu BWANA aliipenda Israeli milele, na sasa amekufanya wewe kuwa mfalme, ili kwamba utoe hukumu ya kweli na ya haki.

10Basi Malkia alimpatia mfalme zaidi ya kilo 4,500 za dhahabu na kiasi kikubwa cha mawe ya thamani. Hapakuwahi kutokea kiasi kikubwa cha viungo kama hiki ambacho Malkia wa Sheba alitoa kwa mfalme Sulemani kuwahi kutolewa tena.

11Ile merikebu ya Hiramu, ambayo ilileta dhahabu kutoka Ofri, pia ilileta Kutoka Ofri kiasi kikubwa cha miti ya msandali na vito vya thamani.12Mfalme alitengeneza nguzo za hekalu kwa ajili ya hekalu la BWANA na kwa nyumba ya mfalme, na vinubi na vinanda kwa hao waimbaji. Haijatokea kiasi cha miti ya misandali kama hicho ambacho kimewahi kutokea hadi leo.

13Mfame Sulemani alimpatia Malkia wa Sheba kila kitu ambacho alihitaji, na kila kitu alichoomba, na zaidi ya yote Sulemani alimpatia kwa ukarimu wake vitu vya kifalme. Kisha akarudi kwake na watumishi wake.

14Kiasi cha dhahabu ambazo zililetwa kwa Sulemani kwa mwaka mmoja kilikuwa takribani kilo 23,000 za dhahabu,15zaidi ya dhahabu ambazo wafanya biashara na wachuuzi walileta. Wafalme wote wa Uarabuni na maliwali wa nchi pia walileta dhahabu na fedha kwa Sulemani.

16Mfalme Sulemani alitengeneza ngao 200 za dhahabu iliyofuliwa, shekeli 600 za dhahabu zilichukuliwa pamoja na ngao.17Pia alitengeneza ngao 300 za dhahabu iliyofuliwa. Mane tatu za dhahabu ziliambatana pamoja na ngao moja moja; mfalme aliviweka katika ikulu ya mwitu ya Lebanoni.

18Kisha mfalme akafanya kiti kikubwa cha enzi kwa pembe na akakisakafia kwa dhahabu laini.19Hicho kiti kilikuwa na ngazi sita, na kitako chake kilikuwa cha mviringo. Na kilikuwa kimezungushiwa kwa mikono pande zake zote. Na simba wawili walisimama pembeni mwa ile mikono.20Kulikuwa na simba kumi na wawili waliokuwa wamesimama kwenye ile ngazi. Moja katika kila upande wa ngazi hizo. Hapakuwepo na kiti kama hicho katika ufalme mwingine.21Vikombe vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu. Na vikombe vyote vya kunywea vya ikulu ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu safi. Hapakuwepo na kikombe cha fedha, kwa sababu fedha haikuwa na thamani katika siku za Sulemani.22Mfalme alikuwa na merikebu za kusafiri pamoja na merikebu za Hiramu. Mara moja kila mwaka merikebu zilileta dhahabu, fedha, na pembe za ndovu, pamoja na nyani na tumbili.

23Kwa hiyo mfalme Sulemani aliwazidi wafalme wote ulimwenguni katika utajiri na hekima.24Dunia yote ilitafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameweka katika moyo wake.25Na wote waliomtembelea walilipa kodi, vyombo vya fedha na vya dhahabu, na nguo na manukato na silaha na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.

26Sulemani alikusanya pamoja magari na wapanda farasi. Alikuwa na magari 1,400, na wapanda farasi 12,000 ambao alikuwa amewaweka kwenye miji ya magari pamoja naye Yerusalemu.27Mfalme alikuwa na fedha kule Yerusalemu, pamoja na mawe ardhini. Alitengeneza miti ya mierezi kuwa mingi kama mikuyu iliyo katika nyanda za chini.28Sulemani alimiliki farasi waliokuwa wamenunuliwa kutoka Misri na Kilikia. Wachuuzi wa mfalme waliwanunua kwa makundi, kila kundi kwa bei yake.29Magari yalinunuliwa kutoka Misri kwa shekeli mia sita za fedha kila moja, na farasi kwa shekeli mia hamsini kila moja. Vitu vingi katika hivi baadaye viliuzwa kwa wafalme wote wa Wahiti na Aramu.

11

1Basi mfalme Sulemani aliwapenda wanawake wengi wa kigeni, binti wa Farao na wanawake wa Wamoabu, Waamori, Waedomu, Wasidoni, na Wahiti. Haya na2mataifa ambayo BWANA alikuwa amewaambia Waisraeli kwamba, “Msiwaoe, wala binti zenu kuolewa nao, kwani kwa hakika wataigeuza mioyo yenu ili mfuate miungu yao.” Lakini Sulemani aliwapenda wanawake hao.3Sulemani alikuwa na wanawake halali 700 na masuria 300. Wake zake waliugeuza moyo wake.4Kwa kuwa Sulemani alipozeeka, wake zake waliugeuza moyo wake kwa miungu mingine; hakuutoa moyo wake wote kwa BWANA, Mungu wake, kama ulivyokuwa moyo wa Daudi baba yake.5Kwani Sulemani alimfuata Ashtoreth, mungu mke wa Wasidoni, na alimfuata Milkom, ambayo ni sanamu chukizo ya Waamori.6Sulemani akafanya maovu mbele ya BWANA; hakumfuata BWANA kwa moyo wake wote, kama alivyofanya Daudi baba yake.

7Kisha Sulemani akajenga mahali pa juu pa Kemoshi, ambayo ni sanamu chukizo ya Wamoabu, mashariki mwa Yerusalemu juu ya kilima, na vivyo hivyo na Moleki, Sanamu chukizo ya Waamoni.8Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa kigeni, ambao walifukiza uvumba na kutoa sadaka kwa miungu yao.

9BWANA alichukizwa na Sulemani, kwa sababu moyo wake ulikuwa umemwacha Mungu wa Israeli, ingawa alikuwa amejionyesha kwake mara mbili10na kumwamuru juu ya mambo haya, kwamba asiwaendee miungu wengine. Bali Sulemani hakutii kile ambacho BWANA alikuwa amemwamuru.11Kwa hiyo BWANA akamwambia Sulemani, “Kwa kuwa umeyafanya haya haukulishika agano langu na maagizo ambayo nilikuamuru, basi nitaugawa ufalme kutoka kwako na kuwapatia watumishi wako.12Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, sitalifanya hilo wakati wa uhai wako, bali nitaugawa wakati ukiwa chini ya mwanao.13Bado sitaugawanya ufalme wote; Nitampa mwanao kabila moja kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu, ambayo nimeichagua.”

14Kisha BWANA akamwinulia uadui Sulemani, Hadadi Mwedomu. Alikuwa anatoka kwenye familia ya mfalme wa Edomu.15Daudi alipokuwa Edomu, Yoabu mkuu wa jeshi alikuwa ameenda kuzika mfu, kila mtu aliyekuwa ameuawa kule Edomu.16Yoabu na Israeli yote walibaki huko kwa miezi sita mpaka alipokuwa amewaua wanaume wote wa Edomu.17Lakini Hadadi alichukuliwa na Waedomu wengine na watumishi wa baba yake hadi Misri, kuanzia Hadadi alipokuwa mtoto mdogo.18Waliondoka Midiani wakaja Parani, ambapo walichukuliwa na wanaume mpaka Misri, kwa Farao wa Misri, ambaye alimpa nyumba na ardhi yenye chakula.19Hadadi alipata neema kubwa machoni pa Farao, kwa hiyo Farao akampatia mke, umbu wa mke wake mwenyewe, Umbu la Tapenesi aliyekuwa Malkia.

20Naye huyo Umbu la Tapenesi alimzalia Hadadi mwana, wakamwita jina lake Genubathi. Tapenesi akamlea katika ikulu ya Farao. Kwa hiyo Genubathi alikulia kwenye ikulu ya Farao pamoja na watoto wa Farao.

21Naye alipokuwa huko Misri, Hadadi alisikia kuwa Daudi alishalala na mababu zake na kwamba Yoabu mkuu wa majeshi alishakufa, Hadadi akamwambia Farao, “Acha niondoke nirudi nchini kwangu.”

22Lakini Farao alimwambia, “Umepungukiwa nini kwangu, kwamba sasa unatafuta kurudi nchini kwako?” Naye Hadadi akamjibu, “Hapana kitu lakini tafadhali niache niende.”

23Pia Mungu akamwinulia Sulemani adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyekuwa amemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba.24Rezoni alijikusanyia wanaume naye akawa mkuu wa jeshi dogo, Daudi alilowapiga wanaume wa Soba. Wale wanume Rezoni walienda Dameski kuishi huko, na Rezoni aliitawala Dameski.25Yeye akawa adui wa Israeli katika siku zote za mfalme Sulemani, zaidi ya madhara ambayo Hadadi alisababisha. Rezoni akawachukia Israeli na akawa juu ya Shamu.

26Kisha Yeroboamu mwana wa Nebati, mwefraimu wa Sereda, akida wa Sulemani, ambaye jina la mama yake lilikuwa Serua, mjane, pia akainua mkono wake dhidi ya mfalme.

27Kisa cha kuinua mkono wake kinyume cha mfalme ilikuwa ni mfalme Sulemani kujenga Milo na kufunga mahali palipo bomoka katika mji wa Daudi baba yake.28Yeroboamu alikuwa mtu hodari na shujaa. Sulemani akaona kuwa huyo kijana alikuwa na bidii, kwa hiyo akampa kuwa na mamlaka juu ya wafanyakazi katika nyumba ya Yusufu.

29Wakati huo, Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya Mshilo akamkuta barabarani. Sasa Ahiya alikuwa amevaa vazi jipya na kwamba hawa wawili walikuwa pekee yao kondeni.30Kisha Ahiya akalishika lile vazi jipya ambalo alikuwa nalo na akalichana katika vipande kumi na viwili.31Akamwambia Yeroboamu. “Chukua vipande kumi, kwani BWANA, Mungu wa Israeli, anasema, ‘Tazama, Nitaugawa ufalme toka katika mkono wa Sulemani nami nitakupa makabila kumi.32(Lakini Sulemani atabaki na kabila moja, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi na kwa ajili ya mji wangu Yerusalemu mji ambao nimeuchagua toka kwenye kabila zote za Israeli),33kwa kuwa ameniacha na kumwabudu Ashtorethi mungu mke wa Wasidoni, Kemoshi Mungu wa Wamoabu, na Milikomu mungu wa watu wa Amoni. Wameziacha njia zangu, hawakufanya kilicho chema katika macho yangu, wala hawa kuzishika amri na maagizo yangu, kama alivyofanya Daudi baba yake.

34Hata hivyo sitauchukua ufalme wote toka kwenye mkono wa Sulemani. Badala yake, nimemfanya kuwa mtawala katika siku zake zote za uhai wake, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu ambaye nilimchagua, mtu ambaye alizishika amri na maagizo yangu.35Bali nitauchukua ufalme ukiwa chini ya mkono wa mwanae na nitakupa wewe, makabila kumi.36Nitampa kabila moja mwana wa Sulemani ili kwamba Daudi mtumishi wangu atabaki kuwa nuru mbele yangu huko Yerusalemu, mji ambao nimeuchagua ili niweke jina langu.37Nami nitakuchukua, nawe utatawala ili kutimiza haja yako, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli.38Kama utasikiliza yote ninayokuagiza, na kama utatembea katika njia zangu na kufanya kinachopendeza mbele ya macho yangu, ukayashika maagizo na amri zangu, kama Daudi mtumishi wangu alivyofanya, ndipo nitakapokuwa na wewe na nitakujengea nyumba ya uhakika, kama niliyomjengea Daudi, nami nitakupa Israeli.39Nitawaadhibu uzao wa Daudi, lakini si milele.”

40Kwa hiyo Sulemani akajaribu kumwua Yeroboamu. Lakini Yeroboamu akaamka na kukimbilia Misri, Kwa Shishaki mfalme wa Misri, naye akabaki Misri mpaka Sulemani alipokufa.

41Na kwa mambo mengine yanayomhusu Sulemani, yote ambayo alifanya na hekima zake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya Sulemani?42Sulemani alitawala Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.43Naye akalala na mababu zake na alizikwa katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu mwanae akawa mfalme mahali pake.

12

1Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa kuwa Israeli yote walikuwa wameenda Shekemu kumfanya awe mfalme.2Ikatokea kuwa Yeroboamu mwana wa Nebati akayasikia haya (Kwa kuwa alikuwa bado yuko Misri, ambako alikuwa amekimbilia kumkwepa mfalme Sulemani), Kwani Yeroboamu alikuwa anaishi Misri.3Kwa hiyo wakatuma watu kumwita, na Yeroboamu pamoja na mkutano wote wa Israeli wakaja wakamwambia Rehoboamu,4Baba yako aliifanya nira yetu kuwa nzito. Sasa ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa nyepesi kuliko nira ngumu ambayo baba yako alituwekea, nasi tutakutumikia.”

5Naye Rehoboamu akawaambia, “Ondokeni kwa siku tatu, kisha nirudieni.” Kwa hiyo watu wakaondoka.

6Mfalme Rehoboamu akatafuta ushauri kwa wazee waliokuwa wamesimama mbele ya Sulemani baba yake wakati wa uhai wake, naye akasema, “Mnanishauri niwajibuje hawa watu?”

7Nao wakamwambia, “Kama wewe utakuwa mtumishi wa hawa watu na akawatumikia, na akawapa majibu ya maneno mema, ndipo watakapokuwa watumishi wako daima.”

8Lakini Rehoboamu akapuuzia ushauri aliopewa na wazee na akaenda kuomba ushauri kwa vijana ambao alikua pamoja nao wakasimama mbele yake.9Akawaambia, “Mnanipa ushauri gani ili niweze kuwajibu hawa watu waliosema nami kwamba, ‘Ifanye nyepesi nira ambayo baba yako alituwekea’”

10Wale vijana waliokua pamoja na Rehoboamu wakamjibu, wakisema, “Waambie hawa watu kuwa baba yako Sulemani aliifanya nira yenu kuwa nzito lakini ninyi wenyewe mnaweza kuifanya rahisi. Uwaambie hivi, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.11Kwa hiyo sasa, ingawa baba yangu aliwatwika kongwa zito, Mimi nitaiongeza kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, Lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.’”

12Kwa hiyo siku ya tatu Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu, kama mfalme alivyokuwa amewaelekeza aliposema, “Mrudi kwangu siku ya tatu.”13Naye mfalme akawaambia wale watu kwa ukali na akapuuzia ushauri wa wale wazee ule waliokuwa wamempatia.14Akawaambia akifuata ushauri wa wale vijana; akasema, “Baba yangu aliwatwika kongwa zito, lakini mimi nitaongeze kongwa lenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, mimi nitawaadhibu kwa nge.”15Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza wale watu, kwa kuwa ilikuwa zamu ya tukio lililoletwa na BWANA, ili kwamba aweze kulitimiza neno lake ambalo alikuwa amelisema kupitia Ahiya.

16Israeli yote ilipoona kuwa mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu wakimwambia, “Je, tuna sehemu gani kwa Daudi? Hatuna urithi kwa mwana wa Yese! Nenda kwenye hema zako, ewe Israeli. Sasa tazama kwenye nyumba yako, Daudi.” Kwa hiyo Israeli akarudi kwenye hema zake.17Lakini kwa watu wa Israeli waliokuwa wakiishi kwenye miji ya Yuda, Rehoboamu akawa mfalme juu yao.

18Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, lakini Waisraeli wote wakampiga kwa mawe wakamwua kwa mawe. Mfalme Rehoboamu akakimbia haraka kwa gari lake kwenda Yerusalemu.19Kwa hiyo Israeli wakawa wapinzani dhidi ya nyumba ya Daudi mpaka leo.

20Ndipo Israeli yote waliposikia kuwa Yeroboamu alikuwa amerudi, walimwita kwenye kusanyiko lao wakamweka kuwa mfalme wa Israeli. Hapakuwepo na mtu aliyeifuata familia ya Daudi, isipokuwa tu kabila la Yuda.

21Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akawakusanya wote wa nyumba ya Yuda na kabila la Benjamini; walichaguliwa wanaume wanajeshi 180,000 ili wapigane na nyumba ya Israeli, kwa lengo la kurudisha ufalme kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani.

22Lakini neno la Mungu likamjia Shemaya, mtu wa Mungu; likisema,23“Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na kwa nyumba yote ya Yuda na Benjamini, na kwa watu wote; uwaambie,24“BWANA asema hivi, ‘Usipigane wala kuwavamia ndugu zako watu wa Israeli. Kila mtu lazima arudi nyumbani kwake, kwa kuwa jambo hili nimelisababisha mimi.’” Kwa hiyo wakalisikiliza neno la BWANA na wakarudi nyumbani kwa njia zao na wakalitii neno lake.

25Kisha Yeroboamu akaijenga Shekemu katika nchi ya milima ya Efraimu, na akaishi huko. Akatoka huko na kuijenga Penueli.

26Yeroboamu akafikiri moyoni mwake, “Sasa ufalme utarudi kwenye nyumba ya Daudi.27Kama hawa watu wataenda kutoa sadaka kwenye hekalu la BWANA kule Yerusalemu, basi mioyo ya hawa watu itarudi tena kwa bwana wao, kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda. Wataniua na kurudi kwa Rehoboamu mfalme wa Yuda.”

28Kwa hiyo mfalme Yeroboamu akatafuta ushauri na akafanya ndama wawili wa dhahabu; akawaambia watu, “Ni vigumu sana kwenu kwenda Yerusalemu. Tazameni, hawa ndiyo miungu yenu, Ee Israeli, iliyowatoa toka nchi ya Misri.”29Akamweka mmoja Betheli na mwingine Dani.30Kwa hiyo jambo hili likawa dhambi. Watu wakaenda kwa huyo na wengine kwa hawa, mpaka huko Dani.

31Yeroboamu akajenga nyumba mahali pa juu na kufanya makuhani kutoka kwa watu wote, ambao hawakuwa wana wa Lawi.32Yeroboamu akafanya sikukuu katika mwezi wa nane, katika siku ya kumi na tano ya mwezi, kama sikukuu ambayo iko Yuda, na akaenda juu kwenye madhabahu. Akafanya hivyo kule Betheli, akawatolea sadaka wale ndama aliokuwa amewatengeneza, na akaweka kuhani huko Betheli mahali pa juu alipokuwa amepatengeneza.33Yeroboamu akapanda kwenda kwenye madhabahu ambayo aliitengeneza kule Betheli katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, ndio mwezi aliokuwa amefikiri katika akili yake; akafanya sikukuu kwa watu wa Israeli n a akaenda madhabahuni kufukiza uvumba.

13

1Mtu wa Mungu alikuja tokea Yuda kwa neno la BWANA kule Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa amesimama karibu na madhabahu ili kufukiza uvumba.2Akalia kinyume na zile madhabahu kwa neno la BWANA: “Ee madhabahu, madhabahu, hivi ndivyo asemavyo BWANA, ‘Tazama, mwana aitwaye Yosia atazaliwa katika familia ya Daudi, na juu yenu atawachinja makuhani ambao sasa wanafukiza uvumba mahali hapa pa juu kwa ajili yako. Juu yako watachoma mifupa ya watu.’”3Kisha mtu wa Mungu akatoa ishara siku hiyohiyo, akisema, “Hii ndiyo ishara ya kwamba BWANA amesema: ‘Tazama, madhabahu zitavunjika, na majivu yaliyo juu yatamwagika.”

4Naye mfalme aliposikia kile mtu wa Mungu alichosema, kwamba amelia kinyume cha zile madhabahu kule Betheli, Yeroboamu akanyosha mkono wake kutoka madhabahuni, akisema, “Mkamateni.” Ndipo ule mkono aliokuwa ameunyosha dhidi ya mtu wa Mungu ukakauka, kiasi kwamba hakuweza kuurudisha mwenyewe.5Na ile madhabahu ikavunjika vipande vipande, na yale majivu yakamwagika kutoka madhabahuni, kama ilivyokuwa imefafanuliwa kuwa ndiyo ishara ya kwamba mtu wa Mungu alikuwa amepewa kwa neno la BWANA.

6Mfalme Yeroboamu akajibu akimwambia mtu wa Mungu, “Msihi BWANA, Mungu wako akupe neema ili uniombee, ili kwamba mkono wangu urejee kwangu tena.” Kwa hiyo mtu wa Mungu akamwomba BWANA, na mkono wa mfalme ukarejea katika hali yake tena, na ukawa kama ulivyokuwa mwanzoni.

7Yule mfalme akamwambia mtu wa Mungu, “Twende nyumbani kwangu upate chakula, nami nitakupa zawadi.”

8Yule mtu wa Mungu akamwambia mfalme, “Hata kama utanipa nusu ya miliki yako, sitaende na wewe, wala sitakula au kunywa maji mahali hapa,9kwa sababu BWANA ameniamuru kwa neno lake, ‘Hutakula mkate wala kunywa maji, wala kurudi kwa njia ulioijia.’”10Kwa hiyo mtu wa Mungu akaondoka na hakurudi nyumbani kwa njia aliyokuja nayo huko Betheli.

11Sasa kulikuwa na nabii mwingine mzee aliyekuwa akiishi Betheli, na mmoja wa wana wake akaja kumwambia mambo yote ambayo mtu wa Mungu amefanya siku hiyo kule Betheli. Wana wake wakamwambia pia maneno ambayo Yule mtu wa Mungu alimwambia mfalme.12Baba yao akawaambia, “Alienda kwa njia gani?” Wale wanawe walikuwa wamemwona yule mtu wa Mungu kutoka Yuda njia aliyotumia kurudi.13Kwa hiyo akawaambia wanawe, “Nitandikeni punda.” Kwa hiyo wakamtandikia punda naye akampanda.14Yule nabii mzee akamfuata yule mtu wa Mungu na akamkuta amekaa chini ya mti wa mwaloni; akamwambia, “Je, wewe ndiye mtu wa Mungu aliyetoka Yuda?” Naye akamjibu, “Mimi ndiye.”

15Kisha yule nabii mzee akamwambia, “Twende nyumbani kwangu ukale chakula.”

16Yule mtu wa Mungu akamjibu, “Siwezi kurudi na wewe wala kuingia ndani na wewe, tena sitakula chakula wala kunywa maji pamoja na wewe mahali hapa,17kwa sababu niliamuriwa hivyo kwa neno la BWANA, ‘Hautakula chakula wala kunywa maji kule, wala kurudi kwa njia utakayokuja nayo.’”

18Kwa hiyo yule nabii mzee akamwambia, “Mimi pia ni nabii kama ulivyo, na malaika amesema na mimi neno la BWANA, akisema, ‘Mrudishe aje na wewe katika nyumba yako, ili aweze kula chakula na kunywa maji.’” Lakini alikuwa anamdanganya mtu wa Mungu.19Kwa hiyo yule mtu wa Mungu akarudi pamoja na yule nabii mzee na akala chakula nyumbani kwake na akanywa maji.

20Walipokuwa wamekaa mezani, neno la BWANA likamjia yule nabii aliyemrudisha,21naye akalia kwa mtu wa Mungu aliyetoka Yuda, akisema “BWANA anasema, ‘Kwa kuwa umeshindwa kutii neno la BWANA na umeshindwa kuishika amri ya BWANA ambayo Mungu wako alikupa,22bali umerudi na umekula chakula na kunywa maji mahali ambapo BWANA alikwambia usile chakula wala kunywa maji, basi mwili wako hautazikwa kwenye makaburi ya baba zako.’”

23Baada ya kula chakula na kunywa maji, yule nabii akatandika punda wa mtu wa Mungu, yule mtu aliyerudi naye.24Baada ya mtu wa Mungu kuondoka, akakutana na simba njiani na kumwua barabarani, na mwili wake uliachwa barabarani. Na yule punda akasimama pembeni yake, na yule simba naye akasimama pembeni ya ule mwili.25Watu walipopita na kuuona ule mwili umeachwa barabarani, na yule simba akisimama karibu na ule mwili, walikuja wakaeleza habari hiyo mjini kule ambako yule nabii mzee aliishi.

26Yule nabii aliyemrudisha toka njiani aliposikia, akasema, “Yeye mtu wa Mungu ndiye aliyeshindwa kutii neno la BWANA. Kwa hiyo BWANA alimtoa kwa simba, ambaye amemrarua katika vipande vipande na kumwua, kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limemwonya.”

27Kwa hiyo yule nabii mzee akawaamnbia wanawe, akisema, “Tandikeni punda wangu,” nao wakamtandikia.28Akaenda akaukuta mwili umeachwa barabarani, punda na simba wamesimama pembeni ya ule mwili. Yule simba hakuula ule mwili, wala hakumshambulia yule punda.29Yule nabii akauchukua ule mwili wa mtu wa Mungu, akaulaza juu ya punda, na akaurudisha. Akaja kwenye mji wake kuomboleza na kuuzika.30Akaulaza mwili kwenye kaburi lake, nao wakamwombolezea, wakisema, “Aa! Ndugu yangu!”

31Kisha baada ya kumzika, yule nabii mzee akawaambia wanawe, akasema, “Nitakapokufa, mtanizika kwenye kaburi ambalo tumemzika mtu wa Mungu. Mtalaza mifupa yangu pembeni mwa mifupa yake.32Kwa kuwa ule ujumbe uliosemwa na BWANA, dhidi ya madhabahu kule Betheli na dhidi ya nyumba zote za mahali pa juu katika mji wa Samaria, hakika yatatokea.”

33Baada ya haya Yeroboamu hakuuacha uovu wake, aliendelea kuchagua makuhani wa kawaida kwa ajili ya mahali pa juu kutoka kwa watu wa kila aina. Yeyote ambaye angeweza kutumika alimtakasa kuwa kuhani.34Jambo hili likawa dhambi kwenye familia ya Yeroboamu na kusababisha familia yake kuangamizwa na kuondolewa kabisa katika uso wa dunia.

14

1Wakati huo Abiya mwana wa Yeroboamu akawa mgonjwa sana.2Yeroboamu akamwambia mke wake, “Amka ujibadilishe, ili wasikutambue kuwa wewe ndiye mke wangu, na uende Shilo, kwa sababu nabii Ahiya yuko huko, yeye ndiye aliyeninenea mimi kuwa nitakuwa mfalme juu ya watu hawa.3Uchukue mikate kumi, na kaki na mtungi wa asali, na uende kwa Ahiya. Naye atakuambia kitakachotokea kwa mtoto.”4Mke wa Yeroboamu akafanya hivyo; akaenda Shilo mpaka kwenye nyumba ya Ahiya. Wakati huo Ahiya alikuwa hawezi kuona, kwa kuwa macho yake yalikuwa yameishiwa nguvu kwa sababu ya umri wake.

5BWANA akamwambia Ahiya, “Tazama mke wa Ahiya anakuja kutafuta kutaka ushauri toka kwako kuhusiana na mwanae, kwa kuwa ni mgonjwa. Mwambie hivi na hivi, kwa sababu atakapofika atajifanya kuwa ni mwanamke mwingine.”6Naye Ahiya aliposikia sauti za miguu yake alipokuwa akiukaribia mlango, akasema, “Karibu, mke wa Yeroboamu. Kwa nini unajifanya kuwa mtu mwingine? Nimetumwa kwako nikiwa na habari mbaya.7Nenda ukamwambia Yeroboamu kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, anasema, ‘Nilikuinua kutoka kati ya watu na kukufanya uwe kiongozi wa watu wangu Israeli.8Niliugawa ufalme kutoka kwa Daudi na kukupa wewe, lakini bado hutaki kuwa kama mtumishi wangu Daudi, ambaye alizishika amri zangu na kunifuata kwa moyo wake wote, na kufanya kilichokuwa sawa mbele ya macho yangu.9Badala yake, umefanya maovu, zaidi ya wote waliokutangulia. Umetengeneza miungu mingine, na umetengeneza sanamu za kuyeyushwa ili kunikasirisha na kunitupa nyuma yako.

10Kwa hiyo, tazama, nitaleta majanga kwenye familia yako; Nitawatupilia mbali watoto wako wote wa kiume katika Israeli, kama ni mtumwa au ni huru, na nitaiondoa familia yako, kama mtu anayechoma mavi mpaka yaishe.11Yeyote ambaye ni mwanafamilia yako atakayefia mjini ataliwa na mbwa, na yeyote atakayefia shambani ataliwa na ndege wa angani, kwa kuwa Mimi BWANA, nimesema.’

12Kwa hiyo inuka wewe mke wa Yeroboamu, na uende nyumbani kwako; na mguu wako utakapokanyaga mjini, yule mtoto wa Abiya atakufa.13Na Israeli yote itamwombolezea na kumzika. Ni yeye pekee katika familia ya Abiya atakayepeleka makaburini, kwa sababu ni yeye pekee yake kutoka kwenye nyumba ya Abiya, ambaye BWANA, Mungu wa Israeli alimwona kuwa ni mwema.

14Pia BWANA atainua mfalme katika Israeli ambaye ataifutilia mbali familia ya Yeroboamu katika siku hiyo. Leo ndiyo siku hiyo, sasa hivi.15Kwa kuwa BWANA ataishambulia Israeli kama vile majani yanavyotikiswa majini, na ataing'oa Israeli katika nchi hii njema ambayo aliwapa mababu. Atawatawanya hata ng'ambo ya Mto Frati, kwa sababu wamefanya nguzo za Ashera kumkasirisha BWANA.16Ataiacha Israeli kwa sababu ya dhambi ya Yeroboamu, dhambi ambazo ametenda, na kwa hizo ameifanya Israeli kufanya dhambi.”

17Kwa hiyo mke wa Yeroboamu akainuka na akaondoka na akaenda mpaka Tirza. Naye alipofika kizingitini kwa nyumba yake, yule mtoto akafa.18Israeli wote wakamzika na kumwombolezea, kama vile alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA ambalo amelisema kupitia mtumishi wake nabii Ahiya.

19Na kwa mambo mengine yanayomhusu Yeroboamu, jinsi alivyopigana vita na jinsi alivyotawala, tazama yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.20Yeroboamu alitawala kwa miaka ishirini na mbili naye akalala na babu zake, na Nadabu mwanawe akawa mfalme mahali pake.

21Sasa Rehoboamu mwana wa Sulemani alikuwa mtawala wa Yuda. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipokuwa mfalme, na akatawala kwa miaka kumi na saba kule Yerusalemu, mji ambao BWANA alikuwa ameuchagua kati ya makabila yote ya Israeli ili aweke jina lake kule. Jina la mama yake alikuwa Naama Mwamori.

22Yuda ikafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA; wakamtia wivu kwa makosa yao, zaidi ya yote ambayo baba zao walikuwa wamefanya.23Kwa kuwa walijijengea wenyewe mahali pa juu, nguzo za mawe, na nguzo za Ashera katika kila mahali pa juu na katika kila mti wenye majani mabichi.24Pia kulikuwepo na ukahaba wa kipagani katika nchi. Walifanya machukizo yaleyale kama wa mataifa yale ambayo BWANA alikuwa amewafukuza kutoka kwa watu wa Israeli.

25Ilitokea wakati wa mwaka wa tano wa mfalme Rehoboamu wakati Shishaki akiwa mfalme wa Misri, akaja kinyume na Yerusalemu.26Akaichukua hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya BWANA, na ile hazina iliyokuwa kwenye nyumba ya Mfalme. Akachukua kila kitu; Pia alizichukua zile ngao za dhahabu ambazo Sulemani alikuwa ametengeneza.27Mfalme Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba mahali pake na akazikabidhi kwa wakuu wa walinzi, ambao walilinda malango ya kuingia kwa mfalme.28Na ikawa kila mfalme alipoingia kwenye nyumba ya BWANA, wale walinzi walizibeba na baadaye walizirudisha katika chumba cha walinzi.

29Lakini katika mambo mengine kuhusiana na Rehoboamu, na yote yale aliyofanya je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?30Kulikuwa na mapigano yasiyokoma kati ya nyumba ya Rehoboamu na nyumba ya Yeroboamu.31Kwa hiyo Rehoboamu akalala na mababu zake naye akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi Jina la mama yake alikuwa Naama Mwamori. Abiya mwanawe akawa mfalme mahali pake.

15

1Katika mwaka wa kumi na tano wa mfame Yeroboamu mwana wa Nebati, Abiya alianza kutawala juu yaYuda.2Alitawala kwa miaka mitatu kule Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Maaka. Alikuwa binti wa Absalomu.

3Naye alitembea katika dhambi zote ambazo baba yake alizifanya kabla yake; moyo wake haukuwa mkamilifu kwa BWANA, Mungu wake kama moyo wa Daudi, babu yake ulivyokuwa.4Hata hivyo, kwa ajili ya Daudi, BWANA, Mungu wake alimpa taa Yerusalemu kwa kumwinua mwanae baada yake ili kuiimarisha Yerusalemu.5Mungu alifanya haya kwa sababu Daudi alifanya yaliyo mema machoni pake; wakati wote wa uhai wake, hakugeuka wala hakukosa katika yote aliyomwamuru, isipokuwa tu swala la Uria Mhiti.

6Sasa kulikuwa na vita kati ya Rehoboamu na Jeroboamu katika siku zote za maisha ya Abiya.7Kwa mambo mengine ya Abiya, yote aliyofanya, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Sasa kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.8Abiya akalala na mababu zake, nao wakamzika katika mji wa Daudi. Asa mwanae akawa mfalme mahali pake.

9Katika mwaka wa ishirini wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Asa akaanza kutawala Yuda.10Alitawala kwa miaka arobaini na moja kule Yerusalemu. Bibi yake alikuwa Maaka, binti wa Absalomu.

11Asa akafanya yaliyo mema machoni mwa BWANA, kama alivyofanya Daudi, babu yake.12Yeye aliwafukuza kutoka katika nchi wale makahaba wa kipagani na akaziondoa sanamu zote ambazo babu zake walikuwa wametengeneza.13Pia alimwondoa bibi yake asiwe Malkia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza kwa Ashera. Asa aliikata sanamu ya kuchukiza na kuiteketeza katika Bonde la Kidroni.14Lakini pale mahali pa juu hapakuchukuliwa. Hata hivyo. Moyo wa Asa ulikuwa mkamilifu mbele ya BWANA katika siku zake zote.15Alivirerejesha katika nyumba ya BWANA vitu vile vilivyokuwa vimetengwa kwa ajili ya BWANA, na vile vitu vyake vilivyokuwa vimetengenezwa kwa fedha, na dhahabu na vyombo.

16Basi kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli, kwa miaka yao yote.17Baasha mfalme wa Israeli, akaivamia na kuijenga Rama, kiasi kwamba hakumruhusu yeyote kuondoka au kuingia katika nchi ya Asa mfalme wa Yuda.

18Kisha Asa akazichukua zile fedha na dhahabu zilizokuwa zimebaki kwenye hazina kwenye nyumba ya BWANA, na katika hazina ya ikulu ya mfalme, kaziweka katika mikono ya watumishi wake na kuzituma kwa Beni Hadadi mwana wa Tabrimoni mwana wa Hezioni, mfalme wa Shamu ambaye alikuwa akishi Dameski. Akamwambia,19“Naomba tufanye patano kati yangu na wewe, kama ilivyokuwa kati ya baba yangu na baba yako. Tazama, nimekutumia zawadi ya fedha na dhahabu. Ili uvunje agano lako na Baasha mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”20Beni Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma wakuu wa majeshi yake, nao wakaishambulia miji ya Israeli. Wakaishambulia Ijoni, Dani, Abeliya Bethi Maaka, na Kinerothi yote, pamoja na nchi yote ya Naftali.21Ikawa Baasha aliposikia haya, akaacha kuijenga Rama akarudi Tirza.22Kisha mfalme Asa akaitangazia Yuda yote. Hakuna aliyeachwa. Wakayabeba mawe na miti ya Rama ambayo Baasha alikuwa akijengea mji. Kisha mfalme Asa akavitumia hivyo vitu kuijenga Geba ya Benjamini na Mispa.

23Mambo mengine yanayohusu utawala wa Asa, uwezo wake wote, yote aliyofanya, na miji aliyoijenga, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda? Lakini wakati wa uzee wake alipata ugonjwa wa miguu.24Kisha Asa akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi baba yake. Yehoshafati mwanae akawa mfalme mahali pake.

25Nadabu mwana wa Yeroboamu alianza kutawala huko Israeli wakati wa mwaka wa pili wa Asa mfalme wa Yuda; Aliitawala Israeli kwa miaka miwili.26Akafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA naye akatembea katika njia ya baba yake, na katika dhambi yake, aliisababisha Israeli kufanya dhambi.

27Baasha mwana wa Ahiya, wa familia ya Isakari, akafanya hila dhidi ya Nadabu; Baasha akamwua huko Gibethoni, ambao ulikuwa mji wa Wafilisti, kwa kuwa Nadabu na Israeli walikuwa wakiuhusuru Gibethoni.28Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha alimwua Nadabu naye akawa mfalme mahali pake.

29Mara tu baada ya kuwa mfalme, Baasha aliwaua watu wote wa familia ya Yeroboamu. Hakumwacha hata mmoja wa uzao wa Yeroboamu awe hai; Kwa njia hii akawa ameuharibu ukoo wote wa kifalme, kama vile BWANA alivyokuwa amesema kupitia mtumishi wake Ahiya Mshilo,30kwa sababu ya dhambi za Yeroboamu ambazo alifanya na akaisababishia Israeli kufanya dhambi, kwa kuwa alimkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli.

31Mambo mengine yanayomhusu Nadabu, na yote aliyofanya, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?32Kisha kulikuwa na vita kati ya Asa na Baasha mfalme wa Israeli katika siku zao zote.

33Katika mwaka wa tatu wa Asa mfalme wa Yuda, Baasha mwana wa Ahiya alianza kuitawala Israeli yote huko Tirza naye alitawala kwa miaka ishirini na nne.34Naye akafanya yaliyo mabaya katika macho ya BWANA na akatembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi yake ambayo kwa hiyo aliifanya Israeli kufanya dhambi.

16

1Neno la BWANA lilimjia Yehu mwana wa Hanani kinyume cha Baasha, likisema,2“Ingawa nilikuinua kutoka kwenye mavumbi na kukufanya kuwa kiongozi wa watu wangu Israeli, lakini umetembea katika njia za Yeroboamu na umewafanya watu wangu Israeli kufanya dhambi, ili kunikasirisha dhidi ya dhambi zao.3Tazama, nitamfagia kabisa Baasha na familia yake na nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati.4Mbwa watamla yeyote ambaye anatoka kwa Baasha wanaofia mjini, na ndege wa angani watamla yeyote anayaefia shambani.”

5Lakini kwa mambo mengine yanayohusiana na Baasha, aliyofanya, na uwezo wake, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?6Baasha akalala na mababu zake na akazikwa Tirza, na Ela mwanae akawa mfalme mahali pake.

7Kwa kupitia nabii Yehu mwana wa Hanani neno la BWANA likaja kinyume na Baasha na familia yake, wote kwa sababu ya maovu yote aliyofanya machoni pa BWANA, akamghadhabisha kwa kazi ya mikono yake, kama familia ya Yeroboamu, na kwa sababu alikuwa ameiua familia yote ya Yeroboamu.

8Katika mwaka wa kumi na sita wa Asa mfalme wa Yuda, Ela mwana wa Baasha akaanza kutawala juu ya Israeli kule Tirza; akatawala kwa miaka miwili.

9Mtumishi wake Zimri, mkuu wa nusu ya magari yake akatengeneza hila dhidi yake. Wakati huo Ela alikuwa Tirza, akinywa na kulewa kwenye nyumba ya Arza, ambaye alikuwa mkuu wa watumishi wa nyumbani huko Tirza.10Zimri akaiingia ndani, akamshambulia na kumwua, katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, naye akawa mfalme mahali pake.

11Zimri alipoaanza kutawala, mara tu baada ya kukaa kwenye kiti cha enzi, akawaua wanafamilia wote wa Baasha. Hakumwacha mtoto hata mmoja wa kiume, hakuna hata wa ndugu yake wala wa rafiki zake.12Kwa hiyo Zimri aliiangamiza familia yote ya Baasha, kama alivyokuwa ameambiwa kwa neno la BWANA, ambalo lilinenwa kinyume na Baasha na nabii Yehu,13kwa dhambi zote za Baasha na za Ela mwanae ambazo walizifanya, ambazo kwazo waliisababisha Israeli kufanya dhambi, kiasi cha kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, kuzikasilikia sanamu zao.

14Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ela, yote ambayo alifanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

15Katika mwaka wa ishirini na saba wa Asa mfalme wa Yuda, Zimri alitawala kwa siku saba tu kule Tirza. Jeshi likafanya kambi kule Gibethoni, ambao ni mji wa Wafilisti.16Lile jeshi lililokuwa limeweka kambi kule lilisikika likisema, “Zimri amepanga njama na amemwua mfalme.” Kwa hiyo siku hiyo hapo kambini, Israeli yote ikamtangaza Omri, mkuu wa jeshi, kuwa mfalme wa Israeli.17Omri akapanda kutoka Gibethoni na Israeli yote pamoja naye, nao wakauhusuru Tirza.18Kwa hiyo Zimri alipoona kuwa mji umetekwa, akaingia kwenye ngome na akaivamia ikulu ya mfalme na kulichoma moto jengo lote pamoja na yeye; kwa hiyo akafa kwa moto.19Hii ilikuwa ni kwa sababu ya dhambi alizofanya kwa kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, kwa kutembea katika njia ya Yeroboamu na katika dhambi ambazo alifanya, kiasi cha kuifanya Israeli wafanye dhambi.

20Pia kwa mambo mengine yanayomhusu Zimri, na fitina yake aliyofanya, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

21Sasa watu wa Israeli walikuwa wamegawanyika katika makundi mawili. Nusu ya watu walimfuata Tibni mwana wa Ginathi, wakamfanya kuwa mfalme, na Nusu walimfuata Omri.22Lakini watu waliomfuata Omri walikuwa na nguvu kuliko wale waliomfuata Tibni mwana wa Ginathi. Kwa hiyo Tibni akafa, na Omri akawa mfalme.

23Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na moja wa Asa mfalme wa Yuda, naye akatawala miaka kumi na miwili. Alitawala akiwa Tirza kwa miaka sita.24Akakinunua kilima cha Samaria kutoka kwa Shemeri kwa kilo sitini na nane za fedha. Akajenga mji juu ya mlima na ule mji akauita Samaria, kwa sababu ya jina la Shemeri, mmiliki wa awali wa kile kilima.

25Omri akafanya maovu mbele ya BWANA na akafanya yaliyo maovu zaidi kuliko wale waliokuwa kabla yake.26Kwa kuwa alitembea katika njia zote za Yeroboamu mwana wa Nebati na katika dhambi zake ambazo kwa hizo aliwaongoza Waisraeli kufanya dhambi, ili kumkasirisha BWANA, Mungu wa Israeli, ili kuwa na hasira juu ya sanamu zao za ubatili.

27Kwa mambo mengine yanayomhusu Omri ambayo alifanya, na nguvu zake alizoonyesha, je, hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?28Kwa hiyo Omri akalala na mababu zake na akazikwa Samaria na Ahabu mwanae akawa mfalme mahali pake.

29Katika mwaka wa thelathini na nane wa Asa mfalme wa Yuda, Ahabu mwana wa Omri akaanza kutawala juu ya Israeli. Ahabu mwana wa Omri akatawala Israeli kule Samaria kwa miaka ishirini na mbili.30Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo maovu mbele ya BWANA, zaidi ya wote waliokuwa kabla yake.31Ikawa kidogo tu Ahabu ayaendee makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa hiyo akamwoa Yezebeli binti wa Ethibaali, mfalme wa Wasidoni; akaenda akamwabudu baali na akamsujudia.32Akamjengea madhabahu Baali, ambayo alikuwa ameijenga kule Samaria.33Ahabu akatengeneza Ashera. Ahabu akafanya maovu zaidi kumghadhabisha BWANA, Mungu wa Isareli, akamkasirisha kuliko wafalme wote wa Israeli waliokuwa kabla yake.

34Katika siku zake Hieli Mbetheli aliijenga tena Yeriko. Akaijenga misingi ya mji kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, naye akayajenga malango ya mji kwa kufiwa na mwanae mdogo Segebu, na walifanya hivi kwa sababu walitii neno la BWANA, ambalo alikuwa amelinena kwa kinywa cha Joshua mwana wa Nuni.

17

1Eliya Mtishibi, kutoka Tishibi ya Gileadi, akamwambia Ahabu, “Kama BWANA, Mungu wa Israeli aishivyo, ambaye ninasimama, hakutakuwa na umande wala mvua isiipokuwa kwa neno langu.”

2Kisha neno la BWANA, likamjia Eliya, likisema,3“Ondoka hapa uende mashariki; ukajifiche karibu na kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yorodani.4Nawe utakunywa maji ya kijito, na nimewaamuru kunguru kukulisha mahali hapo.”

5Kwa hiyo Eliya akaenda kama neno la BWANA lilivyomwamuru. Akaenda kuishi karibu na kijito cha Kerithi, mashariki mwa Yorodani.6Nao kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, naye akanywa maji ya kijito kile.

7Lakini baada ya muda kile kijito kikakauka kwa sababu hapakuwepo na mvua katika nchi.8Neno la BWANA likamjia, likisema,9“Inuka, uende Sarepta, ambao ni mji wa Sidoni, na ukaishi huko. Tazama nimemwamuru mjane kukulisha.”10Kwa hiyo akainuka na akaenda Sarepta, na alipofika kwenye lango la mji, kulikuwa na mjane akiokota kuni. Kwa hiyo akamwita na akamwambia, “Tafadhali niletee maji kidogo kwenye jagi ninywe.”11Naye alipokuwa akienda kuleta maji alimwita, akamwambia, “Tafadhali uniletee na kipande cha mkate mkononi.”

12Naye akamjibu, “Kama BWANA Mungu wako aishivyo, sina mkate wowote, bali konzi moja ya unga katika chombo na mafuta kidogo kwenye chupa. Tazama, ninaokota kuni mbili ili niende kupika kwa ajili yangu na mwanangu, ili tule, na tusubiri kufa.”

13Eliya akamwambia, “Usiogope. Nenda ukafanye kama usemavyo. Lakini nitengenezee kwanza mimi na uniletee. Ndipo baadaye ujitenegenezee wewe na mwanao.14Kwa kuwa BWANA, Mungu wa Israeli anasema ‘Lile pipa la unga halitaisha, wala ile chupa ya mafuta kukoma kutoa mafuta, mpaka siku ile BWANA atakapotuma mvua duniani.”

15Kwa hiyo yule mjane akafanya kama Eliya alivyomwelekeza, yeye, na Eliya, na mwanae wakala kwa siku nyingi.16Lile pipa la Unga halikuisha, wala ile chupa ya mafuta haikukoma kutoa mafuta, kama vile neno la BWANA lilivyosema, kupitia kinywa cha Eliya.

17Baada ya hayo mambo, yule mwana wa yule mwanamke, yule mwanamke mwenye nyumba, aliugua. Ugonjwa wake ukazidi hata akaishiwa pumzi kabisa.18Kwa hiyo mama yake akamwambia Eliya, “Je, una nini nami, ewe mtu wa Mungu? Je, umekuja kwangu ili kunikumbusha dhambi zangu na kumwua mwanangu?”

19Naye Eliya akamjibu, “Nipe hapa mwanao.” Akambeba mtoto mikononi mwake na akampeleka mpaka chumbani alimokuwa akikaa, akamlaza yule mtoto kitandani pake mwenyewe.20Akamlilia BWANA akisema, “BWANA Mungu wangu, kwa nini umeleta majanga kwa mjane ambaye mimi ninakaa, kwa kumwua mwanae?”21Kisha Eliya akajinyosha mwenyewe juu ya mtoto mara tatu; akamlilia BWANA akisema, “BWANA Mungu wangu, Ninakuomba, tafadhali uhai wa mtoto huyu umrudie.”

22BWANA akaisikiliza sauti ya Eliya; uhai wa mtoto ukamrudia, na akawa hai.23Eliya akamchukua mtoto na akamtoa toka chumbani kwake akamleta kwenye ile nyumba; akampatia mama yake yule mtoto na akasema, “Tazama, mwanao yuko hai.”

24Yule mwanamke akamwambia Eliya, “Sasa natambua kuwa wewe ni mtu wa Mungu, na kwamba neno la BWANA kinywani mwako ni la kweli.”

18

1Kwa hiyo baada ya siku nyingi neno la BWANA likamjia Eliya, katika mwaka wa tatu wa ukame, likisema, “Nenda ukajionyeshe mwenyewe kwa Ahabu nami nitainyeshea ardhi mvua.”2Eliya akaenda kujionyesha mwenyewe kwa Ahabu; sasa njaa ilikuwa kali sana kule Samaria.3Ahabu akamwita Obadia, aliyekuwa mkuu wa ikulu. Obadia alimheshimu sana BWANA,4kwa kuwa wakati Yezebeli alipokuwa akiwaua manabii wa BWANA, Obadia alichukua manabii mia akawaficha katika makundi ya hamsini hamsini katika pango na akawalisha kwa mikate na maji.

5Ahabu akamwambia Obadia, “Pita katika nchi yote na katika chemichemi zote za maji na vijito. Yamkini tunaweza kupata maji na nyasi ili tuwaokoa hawa farasi na nyumbu, ili tusiwakose wanyama wote.”6Kwa hiyo wakaigawa nchi kati yao ili wapite kati yake wakitafuta maji. Ahabu akaenda njia yake mwenyewe na Obadia naye akaenda njia yake.

7Wakati Obadia akiwa njiani, akakutana na Eliya pasipo kutegemea. Obadia akamtambua na akalala kifudifudi chini. Akamwambia, “Ndiye wewe, bwana wangu Eliya?”

8Naye Eliya akamjibu, Ni mimi. Nenda umwambie bwana wako, ‘Tazama, Eliya yuko hapa.’”

9Obadia akamjibu. “Nimekoseaje, kwamba umtoe mtumishi wako katika mkono wa Ahabu ili aniue?10Kama BWANA Mungu wako aishivyo, hakuna taifa wala ufalme ambapo bwana wangu hajatuma watu kukutafuta. Kila taifa au ufalme unaposema, ‘Eliya hayuko hapa,’ Ahabu hufanya waape ni kweli hawajakuona.11Na sasa wewe unasema, ‘Nenda, ukamwambie bwana wako kwamba Eliya yuko hapa.’12Mara tu baada ya kukuacha Roho wa BWANA atakuchukua na kukupeleka mahali ambapo sitapajua. Kisha nikienda na kumwambia Ahabu, na asipokuona, ataniua. Bado, mimi, mtumishi wako, nimekuwa nikimwabudu BWANA kutoka ujana wangu.13Je, haujaambiwa, bwana wangu, nilichokifanya wakati Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, jinsi nilivyowaficha wale manabii mia moja wa BWANA katika makundi ya hamsini kwenye pango na kuwalisha kwa mikate na maji?14Na sasa unasema, ‘Nenda umwambie bwana wako kwamba Eliya yuko hapa,’ kwa hiyo ataniua.”

15Ndipo Eliya alipomjibu, “Kama vile BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye mimi ninasimama, Kwa hakika nitajionyesha kwa Ahabu leo.”

16Kwa hiyo Obadia akaenda kukutana na Ahabu, nakumwambia kile Eliya alichokuwa amemwambia. Ndipo mfalme alipoenda kukutana na Eliya.17Ahabu alipomwona Eliya, akamwambia, “Je, ni wewe? Wewe mtabishaji wa Israeli!”

18Eliya akamwambia, “Mimi sijaitabisha Israeli, Lakini wewe na familia ya baba yako ndio watabishaji kwa kuziacha amri za BWANA na kufuata sanamu za Baali.19Kwa hiyo sasa, Tuma neno na unikusanyie Israeli yote katika mlima Karmeli, pamoja na manabii mia nne na hamsini wa Baali na wale manabii mia nne wa Ashera wanaokula kwenye meza ya Yezebeli.”

20Kwa hiyo Ahabu akatuma neno kwa watu wote wa Israeli na akawakusanya manabii wote kwenye mlima Karmeli.21Eliya akaja karibu na watu wote akasema, “Mtaendelea kubadilisha mawazo yenu mpaka lini? Kama BWANA ni Mungu, mfuateni yeye, Lakini kama Baali ni Mungu, basi mfuateni yeye,” Lakini watu hawakumjibu neno.

22Kisha Eliya akawaambia wale watu, “Mimi, pekee yangu, ndiye niliyebaki kuwa nabii wa BWANA, lakini manabii wa Baali wako mia nne na hamsini.23Hebu tutoleeni ng'ombe wawili. Nao wajichagulie ng'ombe mmoja na wamchinje na kumkatakata katika vipnde, na wamweke kwenye kuni, na wasitie moto chini yake. Nami nitamwandaa yule wa pili na kumweke juu ya kuni nami sitatia moto chini yake.24Kisha mtaliita jina la mungu wenu, nami nitaliita jina la BWANA, na Mungu atakayejibu kwa moto, huyo ndiye Mungu.” Watu wote wakajibu na kusema, “Hilo ni jambo jema.”

25Kwa Eliya akawaambia manabii wa Baali, “Chagueni ng'ombe mmoja kwa ajili yenu na mwe wa kwanza kumwandaa, kwa kuwa ninyi ni wengi, Kisha liiteni jina la mungu wenu, lakini msiwashe moto.”26Nao wakamchukua yule ng'ombe waliokuwa wamepewa na wakamwandaa, na ndipo walipoliita jina la Baali kuanzia asubuhi hadi adhuhuri, wakisema, “Baali, tusikie.” Lakini hapakuwepo na Sauti, na wala hakuna aliyejibu. Wakachezacheza kuizunguka madhabahu waliyotengeneza.

27Ilipofika adhuhuri Eliya akawakejeli akisema, “Mwiteni kwa nguvu! Huyo ni mungu! Labda anawaza kitu, au amepumzika, au yuko safarini, au pengine amelala sharti aamshwe.”28Kwa hiyo wakamwita kwa nguvu, wakajikatakata kama kawaida yao ilivyokuwa, kwa upanga na nyembe, mpaka damu ikawachuruzika.29Ikawa wakati wa adhuhuri ulipopita, na bado walikuwa wakiendelea kutabiri mpaka wakati wa jioni wa kutoa dhabihu, lakini hapakuwepo na sauti wala mtu wa kuwajibu; wala hapakuwepo na yeyote wa kujibu wala wa kuangalia.

30Kisha Eliya akawaambia watu wote, “Nisogeleeni,” na watu wote wakamsogelea. Naye akatengeneza ile madhabahu ya BWANA ambayo ilikuwa imeharibika.31Eliya akachukua mawe kumi na mawili, kila jiwe moja liliwakilisha kabila moja la wana wa Yakobo, ni kupitia Yakobo kwamba neno la BWANA lilikuja, likisema, “Jina lako litakuwa Israel.”32Kwa kutumia hayo mawe aliijenga ile madhabahu kwa jina la BWANA na akachimba mfereji kuizunguka ile madhabahu kubwa kiasi cha kubeba pipa kumi na tano za maji.33Kisha akaweka kuni kwa ajili ya moto na akamkatakata yule ng'ombe katika vipande vipande na akaweka vile vipande juu ya kuni. Na akasema, “Vijazeni maji hivyo vyombo na yamwageni kwenye hiyo sadaka ya kueketezwa na juu ya hizo kuni.”

34Akasema tena fanyeni hivyo mara ya pili,” nao wakafanya kwa mara ya pili. Kisha akasema, “Fanyeni mara ya tatu,” nao wakafanya kwa mara ya tatu.

35Maji yakaizunguka ile madhabahu na kuujaza ule mfereji.

36Ikawa wakati wa kutoa dhabihu ya jioni, nabii Eliya akasogea na akasema, “BWANA, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Israeli, na ijulikane leo kwamba wewe ndiye Mungu wa Israeli, na kwamba mimi ni mtumishi wako, na kwamba nimeyafanya mambo haya yote kwa jina lako.37Nisikie, BWANA, nisikie, ili hawa watu wajue kuwa wewe, BWANA, ndiye Mungu, na kwamba umeirudisha mioyo yao kwako tena.”

38Ndipo moto wa BWANA ukashuka ukairamba ile sadaka, pamoja na zile kuni, mawe na mavumbi, na kuyaramba yale maji yaliyokuwa kwenye ule mfereji.

39Watu wote walipoona haya, wakalala kifudifudi chini wakasema, “BWANA, ndiye Mungu! BWANA ndiye Mungu!

40Kwa hiyo Eliya akawaambia, “Wakamateni manabii wa Baali. Msimwache hata mmoja wao atoroke.” Kwa hiyo wakawakamata, na Eliya akawaleta manabii wa Baali chini kwenye kijito cha Kishoni na akawaua huko.

41Eliya akamwambia Ahabu, “Inuka, ule na kunywa, kwa kuwa kuna sauti ya mvua kubwa.”42Kwa hiyo Ahabu akaenda akala na kunywa. Kisha Eliya akaenda juu ya mlima Karmeli, akasujudu chini na akaweka uso wake katikati ya magoti.

43Akamwambia mtumishi wake, “Nenda sasa, utazame upande wa bahari.” Mtumishi wake akaenda na akasema, “Hakuna kitu,” Eliya akamwambia, “Nenda tena, mpaka mara saba.”44Ile mara ya saba mtumishi wake akasema, “Tazama, kuna wingu linapanda kutoka baharini, ni dogo kama mkono wa mtu.” Eliya akamjibu, Nenda ukamwambie Ahabu, ‘Andaa gari lako na ushuke kabla mvua haijakuzuia.’”45Ikatokea baada ya muda mfupi mbingu zikawa nyeusi kwa mawingu na upepo, na kulikuwa na mvua kubwa. Ahabu akapanda gari akaenda zake Yezreeli,46lakini mkono wa BWANA ulikuwa juu ya Eliya. Akalikaza vazi lake kwa mshipi wake na akakimbia mbele ya Ahabu kwenye lango la Yezreeli.

19

1Ahabu akamwambia Yezebeli mambo yote ambayo Eliya amefanya na jinsi alivyowaua manabii wote kwa upanga.2Ndipo Yezebeli alipotuma mjumbe kwa Eliya, akisema, “Miungu wanifanye hivyo na mimi, na zaidi yake, kama kesho muda kama huu sitayafanya maisha yako kuwa kama mmoja wa hao manabii waliokufa.”

3Eliya aliposikia hayo, akaiinuka na akakimbia kwa ajili ya kuokoa maisha yake akaja mpaka Beerisheba, ambao ni mji wa Yuda, na kamwacha mtumishi wake huko.4Lakini yeye mwenyewe akaenda mwendo wa siku moja huko jangwani, akaja akakaa chini ya mti wa mretemu. Akajiombea mwenyewe kufa, akasema, “Sasa yatosha, BWANA, ichukue roho yangu, kwa kuwa mimi si mzuri kuliko mababu zangu waliokufa.”

5Kwa hiyo akalala chini ya mretemu. Ghafula malaika akamgusa na akamwambia, “Inuka ule.”

6Eliya akatazama, karibu na kichwa chake kulikuwa na mkate uliokuwa umeokwa kwa mkaa na gudulia la maji. Kwa hiyo akala na kunywa na kulala tena.

7Malaika wa BWANA akaja tena mara ya pili akamgusa na kumwambia, “Inuka ule, kwa sababu safari bado ndefu kwako.”8Kwa hiyo akainuka na kula na kunywa, naye akasafiri kwa nguvu ya chakula hicho kwa siku arobaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.9Akaingia kwenye pango akakaa humo. Kisha neno la BWANA likamjia likimwambia, “Unafanya nini hapa, Eliya?”10Eliya akajibu, “Nimeona wivu mwingi kwa BWANA, Mungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wameziharibu madhabahu zako, na wamewaua manabii wako kwa upanga. Sasa ni mimi, pekee yangu, nimebaki na wanataka kuichukua roho yangu.

11BWANA akamwambia, “Nenda nje ukasimame kwenye mlima mbele yangu.” Kisha BWANA akapita, na upepo mkali ukaupiga mlima ukavunja miamba katika vipande vipande mbele ya BWANA, lakini BWANA hakuwemo kwenye huo mlima. Kisha baada ya upepo, tetemeko likaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye hilo tetemeko.

12Kisha baada ya tetemeko, moto ukaja, lakini BWANA hakuwemo kwenye moto. Ndipo baada ya moto, sauti ya upole ikaja.13Naye Eliya alipoisikia sauti, akafunika uso wake kwa vazi lake, akatoka nje, akasimama kwenye lango la hilo pango. Na sauti ikaja kwake ikisema, “Unafanya nini hapa?”

14Eliya akajibu, “Nimeona wivu sana kwa ajili ya BWANA, Mungu wa majeshi, kwa kuwa watu wa Israeli wameliacha agano lako, wamezihariibu madhabahu zako, na wamewaua manabii kwa upanga. Sasa, ni mimi pekee yangu, nimebaki na wanajaribu kuichukua roho yangu.”

15Kisha BWANA akamwambia, “Nenda, rudi kwa njia yako kwenye jangwa la Dameski, na utakapofika utamtia mafuta Hazaeli awe Mfalme wa Shamu,16na utamtia mafuta Yehu mwana wa Nimshi kuwa mfalme wa Israeli, na utamtia mafuta Elisha mwana wa Shafeti wa Abeli Mehola kuwa nabii mahali pako.17Itakuwa hivi Yehu atamwua kila mmoja atakayejaribu kutoroka upanga wa Hazaeli, na kwamba Elisha atamwua kila atakayejaribu kukwepa upanga wa Yehu.18Lakini nitawaacha watu 7,000 katika Israeli kwa ajili yangu, ambao magoti yao hayajawahi kupigwa kwa Baali, na ambao midomo yao haijambusu.”

19Kwa hiyo Eliya akaondoka mahali pale na akamkuta Elisha mwana wa Shafati, akilima na jozi za makisai kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa akilima na ile jozi ya kumi na mbili. Eliya akaenda mpaka kwa Elisha akamtupia vazi lake juu yake.20Elisha naye akawaacha wale makisai akamkimbilia Eliya; akamwambia, “Tafadhali naomba nikambusu baba yangu na mama yangu kisha nitakufuata.” Naye Eliya akamwambia, “Rudi, lakini fikiria juu ya kile nilichokufanyia.”21Kwa hiyo Elisha akarudi toka kwa Eliya na akachukua ile jozi ya makisai, akawaua wale wanyama, na akapika ile nyama kwa kuni za ile nira. Kisha akawapa watu wakala. Kisha akaamka, akamfuata Eliya akamtumikia.

20

1Beni Hadadi mfalme wa Shamu akakusanya jeshi lake lote pamoja. Kulikuwa na wafalme thelathini na mbili wasaidizi pamoja naye, na magari na farasi. Akapanda, akaihusuru Samaria na kupigana nayo.2Akatuma wajumbe katika mji kwa Ahabu mfalme wa Israeli, akamwambia, “Beni Hadadi anasema hivi:3Fedha zako na dhahabu zako ni zangu. Pia wake zako na watoto, wale wazuri, sasa ni wangu.”

4Mfalme wa Israeli akajibu akasema, “Na iwe kama unavyosema, bwana wangu, mfalme. Mimi pamoja na vile nilivyo navyo ni mali yako.”

5Wale wajumbe wakaja tena wakasema, “Beni Hadadi anasema hivi, ‘Nilituma neno kwako nikisema kwamba lazima ukabidhi kwangu fedha zako, dhahabu zako, wake zako na watoto wako.6Lakini kesho nitatuma watumishi wangu kwako wakati kama huu, nao wataichunguza nyumba yako na nyumba za watumishi wako. Nao watatia mikononi mwao na kukichukua kila wakipendacho machoni mwao.’”

7Ndipo mfalme wa Israeli akawaita wazee wote wa nchi pamoja akawaambia, “Hebu angalieni jinsi huyu mtu anavyotafuta matatizo. Amenitumia ujumbe kwamba anataka kuchukua wake zangu, watoto wangu, fedha na dhahabu zangu, nami sijamkatalia.”

8Wazee wote na watu wote wakamwambia Ahabu, “Usimsikilize wala kukubaliana na matakwa yake.”

9Ahabu akawaambia wajumbe wa Beni Hadadi, “Mwambieni bwana wangu mfalme kwamba, ‘Ninakubaliana na kila kitu ambacho kwanza uliwatuma watumishi wako kufanya kwangu, lakini sikubaliani na matakwa yako haya ya pili.’” Wale watumishi wa Beni Hadadi wakaondoka wakampelekea mrejesho Beni Hadadi.

10Naye Beni Hadadi akatuma tena majibu yake kwa Ahabu, akasema, “Basi miungu inifanyie hivyo na zaidi, kama hata mavumbi ya Samaria yatawatosheleza watu wote wanaonifuata kuchukua kila mmoja angalau konzi mkononi mwake.”

11Naye mfalme wa Israeli akamjibu akisema, “Mwambieni Beni Hadadi, ‘Hakuna abebaye silaha yake, atakayejivuna kama wakati wa kuishusha.”’

12Beni Hadadi aliusikia ujumbe huu wakati alipokuwa akinywa, yeye na wafalme walikuwa pamoja naye waliokuwa kwenye mahema yao. Beni Hadadi akayaamuru majeshi yake, “Jipangeni katika sehemu zenu kwa ajili ya vita.” Kwa hiyo wakajiandaa kivita ili kuuvamia mji.

13Tazama, nabii akaja kwa Ahabu mfalme wa Israeli akasema, “BWANA asema, ‘Je umeliona hili jeshi kubwa? Tazama, nitaliweka katika mkono wako leo, nawe utatambua kuwa mimi ni BWANA.’”

14Naye Ahabu akajibu, “kwa nani? BWANA akamjibu akasema, “kwa kuwatumia vijana wanaotumikia maliwali wa wilaya.” Kisha Ahabu akasema, “Ni nani atakayepewa hiyo vita?’ BWANA akamwambia, “Wewe.”

15Ndipo Ahabu alipowataarifu wale vijana wanaowatumikia maliwali wa wilaya. Idadi yao ilikuwa mia mbili therathini na mbili. Baada yao aliwahesabu wanajeshi wote, jeshi lote la Israeli; idadi yao ilikuwa elfu saba.16Nao wakatoka wakati wa adhuhuri. Naye Beni Hadadi alikuwa akinywa na kulewa hemani mwake, yeye na wale wafalme wadogo thelathini na mbili waliokuwa wakimsaidia.17Wale maakida vijana waliokuwa wakiwasaidia maliwali wa wilaya walitangulia kwanza. Kisha Beni Hadadi alitaarifiwa na wanaskauti aliokuwa amewatuma kwamba, “kuna watu wanakuja kutoka Samaria.”

18Beni Hadadi akasema, “Wawe wamekuja kwa amani au kwa vita, wakamateni wakiwa hai.”

19Kwa hiyo wale vijana wanaowatumikia maliwali wa wilaya wakaenda mjini na jeshi likawafuata kwa nyuma.20Kila mmoja akaua adui wake na wale washami wakakimbia. Israeli ikawashinda. Beni Hadadi mfalme wa Shamu akatoroka kwa farasi pamoja na wapanda farasi.21Kisha mfalme wa Israeli akaenda akawashambulia farasi na magari, na kuwaua washami kwa mauaji makubwa.

22Yule nabii akaja kwa mfalme wa Israeli akamwambia, “Nenda, ukajiimarishe mwenyewe, uelewa na kupanga kile unachofanya, kwa sababu mwakani mfalme wa Shamu atapanda dhidi yako tena.”

23Wale watumishi wa mfalme wa Shamu wakamwambia, “Mungu wao ni mungu wa milimani. Hiyo ndiyo sababu walikuwa na nguvu kuliko tulivyokuwa. Lakini sasa hebu tupigane nao katika nchi tambarare, na kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko wao.24Na ufanye hivi waondoe wafalme; mwondoe kila mmoja mahali pake ukaweke majemedari mahali pao.25Kisha ujihesabie jeshi kama lile jeshi ulilopoteza, farasi kwa farasi na gari kwa gari, nasi tutapigana nao katika nchi tambarare, Kwa hakika tutakuwa na nguvu kuliko walivyo.” Kwa hiyo Beni Hadadi akausikiliza ushauri huo naye akafanya kama alivyoshauriwa.26Baada ya mwanzo wa mwaka mpya, Beni Hadadi akawahesabu Washami na akapanda Afeki kupigana na Israeli.27Watu wa Israeli walikuwa amehesabiwa na walikuwa wamejipanga kupigana nao. Watu wa Israeli wakafanya kambi mbele yao kama makundi mawili madogo ya mbuzi, lakini Washami wakaujaza upande wa nchi.

28Ndipo mtu wa Mungu akaja karibu akaongea mfalme wa Israeli akamwambia, “BWANA anasema: ‘Kwa kuwa Washami wamesema kuwa BWANA ni mungu wa milima, na wala si mungu wa mabondeni, nitaliweka hili jeshi kubwa mkononi mwako, nawe utajua kuwa mimi ni BWANA.’”

29Kwa hiyo majeshi yakaweka kambi yakikabiliana kwa muda wa siku saba. Kisha siku ya saba vita vikaanza. Watu wa Israeli wakawaua Washami 100,000 wanajeshi wa ardhini kwa siku moja.30Waliobaki wakakimbilia Afeki, mjini, na ule ukuta ukaanguka juu ya watu ishirini na saba elfu waliobaki. Naye Beni Hadadi akakimbilia mjini. Akaingia kwenye chumba cha ndani.31Wale watumishi wa Beni Hadadi wakamwambia, “Tazama sasa, tumesikia kwamba wale wafalme wa nyumba ya Israeli ni wenye rehema. Tafadhali hebu tuvaeni magunia viunoni mwetu na kamba vichwani mwetu, na twendeni kwa mfalme wa Israeli. Labda atakuokoa roho yako.”

32Kwa hiyo wakavaa magunia viunoni mwao na kujifunga kamba vichwani mwao na kisha wakaenda kwa mfalme wa Israeli wakamwambia, “Mtumishi wako Beni Hadadi, anasema, ‘Tafadhali niachie uhai wangu.” Ahabu akawaambia, “Je, bado yuko hai? Yeye ni ndugu yangu.”

33Sasa wale watu walikuwa wakisikiliza ishara yeyote kutoka kwa Ahabu, kwa hiyo wakamjibu haraka, “Ndiyo ndugu yako Beni Hadadi bado yuko hai.” Ahabu akawaambia, “Nendeni mkamlete.” Ndipo Beni Hadadi alipokuja kwake, na Ahabu akamwacha aje kwenye gari lake.

34Beni Hadadi akamwambia Ahabu, “Nitakurudishia miji yako ambayo baba yangu alichukua toka kwa baba yako, na unaweza kutengeneza masoko kwa ajili yako Dameski, kama baba yangu alivyofanya kule Samaria.” Ahabu akajibu, “Nitakuacha uende kwa agano hili.” Kwa hiyo Ahabu akafanya agano naye kisha akamwacha aende.

35Mtu mmoja, mmoja wana wa wana wa manabii, akamwambia mmoja wa wale manabii wenzake kwa neno la BWANA, “Tafadhali nipige.” Lakini yule mtu akakataa kumpiga.

36Kisha yule nabii akamwambia nabii mwenzake, “Kwa sababu umekataa kutii sauti ya BWANA, mara tu utakaponiacha, simba atakuua.” Na mara tu baada ya yule mtu kumwacha, simba akamkuta na kumwua.

37Kisha yule nabii akamkuta mtu mwingine akamwambia, “Tafadhali nipige.” Yule mtu akampiga na kumwumiza.38Kisha yule nabii akaondoka akaenda kumsubiri yule mfalme barabarani; naye alikuwa amejibadilisha kwa kilemba machoni pake.39Ikawa mfalme alipokuwa akipita, Yule nabii akamwita mfalme na kumwambia, “Mtumishi wako alienda katikati ya pigano, na askari akasimama akamleta adui kwangu akasema, ‘Mwangalie mtu huyu. Na ikiwa kwa vyovyote atatoroka, basi maisha yako yatatolewa kwa ajili ya maisha yake vinginevyo utalipa kilo thelathini za fedha.40Lakini kwa kuwa mtumishi wako alikuwa na mambo mengi akienda huku na kule, yule askari adui akatoroka.” Basi mfalme wa Israeli akamwambia, “Hivyo ndivyo itakavyokuwa hukumu yako umejihukumu mwenyewe.”

41Ndipo yule nabii alipoondoa haraka kile kilemba machoni pake, na mfalme wa Israeli alipotambua kuwa huyo alikuwa mmoja wa manabii.42Yule nabii akamwambia mfalme, “BWANA anasema, ‘Kwa sababu umemwachia aende mtu yule niliyekuwa nimemhukumu kifo, maisha yako yatachukua nafasi ya maisha yake.’”43Kwa hiyo mfalme wa Israeli akaenda nyumbani kwake akiwa na moyo mzito na mwenye hasira, akafika Samaria.

21

1Basi ikawa baada ya hayo, Nabothi Myezreeli alikuwa na shamba la mizabibu kule Yezreeli, karibu na ikulu ya Ahabu, mfalme wa Samaria.2Ahabu akamwambia Nabothi, akisema, “Nipe shamba lako, ili nilifanye kuwa bustani ya mboga, kwa sababu iko karibu na nyumba yangu. Badala yake nitakupa shamba zuri la mizabibu, au, kama ukipenda nitakulipa thamani yake kwa fedha.”

3Nabothi akamjibu Ahabu, “BWANA na alizuie hilo nisije nikatoa urithi wa mababu zangu kwako.”

4Ahabu akaingia kwenye ikulu yake akiwa mchovu na mwenye hasira kwa sababu ya jibu ambalo Nabothi Myezreeli alimpa aliposema, “Sitakupa urithi wa mababu zangu.” Akalala kitandani kwake, akiwa amegeuza uso wake upande ule, na akagoma kula chakula chochote.

5Yezebeli mke wake akaiingia kwake, akamwambia “Kwa nini moyo wako una huzuni, kiasi kwamba hutaki kula?”

6Naye akamjibu, “Niliongea na Nabothi Myezreeli nikamwambia, ‘Nipe shamba lako nami nitakupa pesa, au kama inakupendeza, nitakupa shamba jingine ili liwe lako.’ Naye akanijibu, ‘Sitakupa shamba langu.’”

7Naye Yezebeli mkewe akamjibu, “Je, wewe si mtawala wa ufalme wa Israeli? Inuka ule; na moyo wako uwe na amani. Nitalichukua hilo shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli kwa ajili yako.

8Kwa hiyo Yezebeli akaandika barua kwa jina la Ahabu, akaitia muhuri wake, akazituma kwa wazee na kwa watu tajiri alioketi nao kwenye vikao, na ambao pia waliishi karibu na Nabothi.9Katika ile barua aliyoandika, ilisema hivi, “Pigeni mbiu ya kufunga mkamkalishe Nabothi juu mbele ya watu.10Pia mwaweke watu wawili wasiokuwa waaminifu pamoja naye na wale watu watoe ushahidi kinyume naye, waseme, ‘Ulimlaani Mungu na mfalme.” Halafu mchukueni nje mkampige kwa mawe mpaka afe.

11Kwa hiyo watu wa mji wake, wazee na watu tajiri waishio kwenye huo mji, wakafanya kama Yezebeli alivyowaeleza, kama ilivyoandikwa kwenye zile barua ambazo alikuwa amewatumia.12Wakapiga mbiu ya kufunga wakamkalisha Nabothi juu mbele ya watu.13Na wale watu wawili wasiokuwa waaminifu wakaja wakakaa mbele ya Nabothi; nao wakatoa ushuhuda wao dhidi ya Nabothi kuwa amemlaani Mungu na mfalme.” Kisha wakamchukua nje ya mji wakampiga kwa mawe mpaka akafa.14Kisha wazee wakatuma neno kwa Yezebeli, wakisema, “Nabothi ameshapigwa mawe na amekufa.”

15Naye Yezebeli aliposikia kuwa Nabothi ameshapigwa mawe na alikuwa amekufa, akamwambia Ahabu, “Inuka na ukamiliki shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli, ambalo alikataa kukuuzia, kwa sababu Nabothi hayuko hai, bali amekufa.”16Ahabu aliposikia kuwa Nabothi amekufa, akainuka ili aende kwenye lile shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli na kulimiliki.

17Ndipo neno la BWANA likamjia Eliya Mtishibi, likisema,18“Inuka uende ukakutane na Ahabu mfalme wa Israeli, ambaye anaishi Samaria. Yumo kwenye shamba la Nabothi, ambako ameenda kuchukua umiliki wa shamba hilo.19Ukaongee naye umwambie kwamba BWANA anasema, ‘Je, umeua na kujimilikisha?’ na utamwambia kwamba BWANA anasema, ‘Mahali pale ambapo mbwa wameramba damu ya Nabothi, ndipo mbwa watakaporamba damu yako, ndiyo, damu yako.’”

20Ahabu akamwambia Eliya, “Je, umenipatia, adui yangu?” Eliya akamjibu, “Nimekupata wewe kwa sababu, umejiuza mwenyewe kufanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA.

21BWANA anakwambia hivi: ‘Tazama, Nitaleta janga kwako na litakuangamiza kabisa na kufutilia mbali kila mtoto mume na mtumwa na mtu huru katika Israeli.22Nitaifanya familia yako kama familia ya Yeroboamu mwana wa Nebati, na kama familia ya Baasha mwana wa Ahiya, kwa sababu umenighadhabisha na umewasababisha Israeli kufanya dhambi.

23Pia BWANA ameongea kuhusu Yezebeli, amesema, “Mbwa watamla Yezebeli pembeni mwa ukuta wa Yezreeli.’24Yeyote ambaye ni mtu wa familia ya Ahabu ambaye atafia mjini mbwa watamla. Na yeyote ambaye atafia shambani ataliwa na ndege wa angani.”

25Hapakuwepo na mtu kama Ahabu, ambaye alijiuza mwenyewe kufanya maovu mbele ya macho ya BWANA, ambaye mke wake Yezebeli alimchochea kufanya dhambi.26Ahabu alifanya matendo yachukizayo kwa ajili ya sanamu alizofanya, kama vile yale yote ambayo Waamori walifanya, BWANA akawafukuza mbele ya watu wa Israeli.

27Ahabu aliposikia maneno haya, Akachana mavazi yake na akavaa magunia kwenye mwili wake na akafunga, na akalala kwenye magunia na akahuzunika sana.

28Kisha neno la BWANA likamjia Eliya Mtishibi likisema,29“Je, unamwona jinsi Ahabu anavyojinyenyekeza mbele yangu? Kwa sababu anajinyeyenyekeza mwenyewe mbele yangu, sitaleta lile janga katika siku zake; Ni katika siku za mwanae, nitakapolileta hilo janga katika familia yake.”

22

1Miaka mitatu ilipita bila kuwepo na vita kati ya Washami na Waisraeli.2Ikawa katika mwaka wa tatu, Yehoshafati mfalme wa Israeli akashuka kwa mfalme wa Isreli.3Mfalme wa Israeli alikuwa amewaambia watumishi wake, “Je, mnajua kuwa Ramothi Gileadi ni yetu, ila hatufanyi chochote kuitwaa kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Shamu?”4Kwa hiyo akamwambia Yehoshafati, “Je, utakwenda na mimi katika vita huko Ramothi Gileadi?” Yehoshafati akamjibu mfalme wa Israeli, “Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, na farasi wangu ni kama farasi wako.”5Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, “Tafadhali tafuta mwongozo kutoka neno la BWANA juu ya kile unachopaswa kufanya kwanza.”6Ndipo mfalme wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, walikuwa wanaume 4,000 akawaambia, “Je, niende Ramothi Gileadi kupigana, au nisiende?” Nao wakamwambia, “Ivamie, kwa kuwa Bwana ataitoa katika mkono wa mfalme.”

7Lakini Yehoshafati akasema, “Je, hapa hayupo nabii mwingine wa BWANA ambaye tunaweza kupata ushauri?”

8Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Bado kuna mtu mmoja ambaye tunaweza kupata ushauri toka kwa BWANA ili kusaidia, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu huwa hanitabirii mazuri yanayonihusu, ila hunitabiria matatizo tu.” Lakini Yehoshafati akasema, “Mfalme na asiseme hivyo,”

9Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na akamwamuru, “Kamlete Mikaya mwana wa Imla, sasa hivi.”

10Wakati huo Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wameketi kila mmoja kwenye kiti cha enzi, wamevaa mavazi yao, katika eneo la wazi kwenye lango la kuingilia Samaria, na manabii walikuwa wakiwatabiria.11Sedekia mwana wa Kenaana akajitengenezea pembe za chuma akasema, “BWANA asema hivi: ‘Kwa hili utawasukuma Washami mpaka watakapoisha.’”

12Na manabii wengine wote wakasema hivyo, wakisema, “Ishambulie Ramothi Gileadi na ushinde, kwa kuwa BWANA ameiweka kwenye mkono wa mfalme.”

13Yule mjumbe aliyeenda kumwita Mikaya akamwambia, akisema, “Tazama sasa, maneno ya manabii kwa kinywa kimoja wanatabiri mambo mema kwa mfalme. Tafadhali maneno yako yawe kama yao ukaseme mambo mazuri.”

14Mikaya akajibu, “Kama BWANA aishivyo, kile BWANA atakachosema kwangu ndicho nitakachosema.’”

15Naye alipokuja kwa mfalme, mfalme akamwambia, “Mikaya, je twende Ramothi Gileadi kupigana, au tusiende?” Mikaya akamjibu, “Ivamie na ushinde. BWANA ataitoa kwenye mkono wa mfalme.”16Kisha mfalme akamwambia. “Je, nikutake mara ngapi ili kuniapia ukweli kwa jina la BWANA?”

17Mikaya akasema, “Ninaiona Israeli yote imesambaa kwenye milima, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji, na BWANA amesema, ‘Hawa hawana mchungaji. Kila mtu na arudi nyumbani kwake kwa amani.’”

18Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Je sikukwambia kuwa huwa hanitabirii mambo mema yanayonihusu, ila majanga tu?”

19Kisha Mikaya akasema, “Kwa hiyo sikiliza neno la BWANA: Nimemwona BWANA akiwa ameketi kwenye kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamesimama karibu yake upande wake wa kulia na upande wake wa kushoto.20BWANA akasema, ‘Ni nani atakayemdanganya Ahabu, ili kwamba apande akafie Ramothi Gileadi? Na mtu mmoja akajibu kwa njia hii, na mwingine akajibu kwa njia ile.21Ndipo pepo moja akajitokeza, akasimama mbele ya BWANA, akasema, ‘Mimi nitamdanganya.’ BWANA akmwuliza, ‘Kwa jinsi gani?’

22Yule pepo akamjibu, ‘Nitakwenda na kuwa roho idanganyayo katika vinywa vya manabii wake,’ BWANA akamjibu, ‘Utaweza kumdanganya, na utafanikiwa. Nenda sasa ukafanye hivyo.’23Tazama sasa, BWANA ameweka roho idanganyayo kwenye vinywa vya hawa manabii wako, na BWANA ametangaza janga kwako.”

24Kisha Sedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga Mikaya shavuni, akasema, “Je, yule roho wa Bwana alitokaje kwangu ili aseme na wewe?”

25Mikaya akasema, “Tazama, utatambua hilo katika siku hiyo, utakapokimbilia katika chumba cha ndani kujificha.”

26Mfalme wa Israeli akamwambia mtumishi wake, “Mkamate Mikaya umpeleke kwa Amoni, liwali wa mji, na kwa mwanangu, Yoashi.27Mwambie, ‘mfalme anasema mweke huyo gerezani na awe anampa mkate kidogo na maji kidogo, mpaka nitakaporudi salama.’”

28Naye Mikaya akasema, “Kama utarudi salama basi BWANA hajasema kupitia kinywa changu.” Na akaongeza, “Sikilizeni hili, ninyi watu.”

29Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati mfalme wa Yuda, wamepanda Ramothi Gileadi.30Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe niende vitani, lakini wewe uvae vazi lako la kifalme.” Kwa hiyo mfalme wa Israeli akajibadilisha na akaenda vitani.

31Naye mfalme wa Shamu alikuwa amewaamuru majemedari thelathini na mbili wa magari yake, akisema, “Msimwangamize askari wa muhimu au ambaye si wa muhimu, badala yake mshambulieni mfalme wa Israeli tu.”32Ikawa wakati majemedari wa magari walipomwona Yehoshafati wakasema, “Hakika huyu ndiye mfalme wa Israeli.” Wakageuka ili kumshambulia, kwa hiyo Yehoshafati akapiga kelele.33Ikawa majemedari wa magari walipoona kuwa yeye hakuwa mfalme wa Israeli, wakamwacha.

34Lakini mtu mmoja akavuta upinde wake kwa kubahatisha na akampiga mfalme wa Israeli katikati ya mwunganiko wa mavazi yake ya chuma. Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Geuza unirudishe kutoka vitani, kwa kuwa nimeumizwa sana.”35Vita ikawa mbaya sana siku hiyo na mfalme akalazwa garini mwake akiwakabili Washami. Akafa jioni hiyo. Damu ilimwagika kutoka kwenye jeraha lake ndani ya gari.36Ikawa wakati wa kuzama jua, kilio kikatawala kwa jeshi lote, wakisema, “Kila mtu arudi kwenye mji wake; na kila mtu arudi kwenye mkoa wake!”

37Kwa hiyo mfalme Ahabu akafa na akaletwa Samaria, wakamzika huko Samaria.38Wakaliosha lile gari kwenye birika la Samaria, na mbwa wakaramba damu yake (hapa ni mahali ambapo makahaba waliogea), kama vile neno la BWANA lilivyokuwa limesema.

39Kwa mambo mengine yanayohusiana na Ahabu, yote ambayo alifanya, ile nyumba ya pembe aliyojenga, na miji yote aliyojenga, je, hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?40Kwa hiyo Ahabu akalala pamoja na mababu zake, na Ahazia mwanae akawa mfalme mahali pake.

41Kisha Yehoshafati mwana wa Asa alianza kutawala juu ya Yuda katika mwaka wa nne wa Ahabu mfalme wa Israeli.42Yehoshafati alikuwa na umri wa miaka thelathini na tano alipoanza kutawala, na akatawala Yerusalemu kwa miaka ishirini na mitano. Mama yake alikuwa Azuba, binti wa Shilhi.43Akatembea katika njia za Asa, baba yake, hakuziacha; akafanya yaliyokuwa mema mbele ya macho ya BWANA. Lakini bado mahali pa juu palikuwa hapajabomolewa. Watu walikuwa bado wanaendelea kutoa dhabihu na kufukiza uvumba mahali pa juu.44Yehoshafati akafanya amani na mfalme wa Israeli.

45Kwa mambo mengine kuhusiana na Yehoshafati, na nguvu zake alizoonyesha, na jinsi alivyopigana vita, je, hayajaandikwa katika kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli?46Aliwaondoa kutoka katka nchi wale makahaba wa kipagani waliokuwa wamebaki katika siku za baba yake Asa.

47Hapakuwepo mfalme katika Edomu isipokuwa kaimu mtawala.

48Yehoshafati alijenga merikebu ziende Tarshishi na Ofri kuleta dhahabu, lakini hazikusafiri kwa sababu zile merikebu zilivunjika kule Esioni Geberi. Kisha49Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, “Naomba watumishi wangu waende pamoja na watumishi wako merikebuni.” Lakini Yehoshafati hakuruhusu hilo.

50Yehoshafati akalala na mababu zake na akazikwa pamoja nao katika mji wa Daudi, babu yake; Yoramu mwanawe akawa mfalme mahali pake.

51Ahazia mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli ya Samaria katika mwaka wa kumi na saba wa mfalme Yehoshafati mfalme wa Yuda, na akatawala kwa miaka miwili juu ya Israeli.52Naye akafanya yaliyo maovu mbele ya macho ya BWANA akatembea katika njia za baba yake, katika njia za mama yake na katika njia za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwazo aliifanya Israeli kufanya dhambi.53Alimtumikia Baali na kumwabudu na kwa hiyo akamghadhabisha BWANA, Mungu wa Israeli, katika hasira, kama vile baba yake alivyofanya.

2 Wafalme

1

1Moabu aliasi dhidi ya Israeli baada ya kifo cha Ahabu.2Baada hapo Ahazia akaanguka chini ya dirisha zinazokinzana kwenye chumba chake juu katika Samaria, na alikuwa amejeruhiwa. Kwa hiyo alituma wajumbe na kuwaambia, “Nendeni, muulizeni Baal Zebubu, mungu wa Ekroni, kama nitapona hili jeraha.”

3Lakini malaika wa Yahwe wakamwambia Eliya Mtishbi, “Inuka, nenda ukaonane na wajumbe wa mfalme wa Samaria, na uwaulize, ‘Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israel hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-Zebebu, mungu wa Ekroni?’4Kwa hiyo Yahwe anasema, ‘Hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ambacho ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika.’” Baada ya hapo Eliya akaondoka.

5Wakati wale wajumbe waliporudi kwa Ahazia, akawaambia, “Kwa nini mmerudi?”

6Wakamwambia, “Mtu amekuja kuonana na sisi ambaye ametuambia, ‘Rudini kwa mfalme ambaye aliyewatuma, na mkamwambie, Yahwe amesema hivi: ‘Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli mpaka mmewatuma watu kwenda kumuuliza kwa Baal Zabubu, mungu wa Ekron? Kwa hiyo hutashuka kutoka kitanda ulichokipanda; badala yake, utakufa hakika.’”

7Ahazia akawaambia wajumbe wake, “‘Alikuwa mtu wa aina gani, yule ambaye alikuja kuonana nanyi na akasema haya maneno kwenu?”

8Wakamjibu, “Alikuwa amevaa kanzu yenye manyoya na alikuwa na mkanda wa ngozi kiunoni kwake.” Hivyo mfalme akajibu, “Yule alikuwa Eliya Mtishbi.”

9Ndipo mfalme akatuma mkuu wa askari hamsini kwa Eliya. Akaenda mpaka kwa Eliya ambapo alipokuwa amekaa juu ya mlima. Mkuu wa askari akamwambia Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme amesema, ‘Shuka chini.’”

10Eliya akajibu na kusema; “Kama mimi ni mtu wa Mungu, moto na ushuke chini kutoka mbinguni na ukuteketeze wewe na watu wako hamsini.” Kisha moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.

11Tena Mfalme Ahazia akamtuma mkuu mwingine pamoja na maaskari wengine hamsini. Huyu mkuu pia akasema kwa Eliya, “Wewe, mtu wa Mungu, mfalme anasema, ‘Teremka chini haraka.’”

12Eliya akajibu na kuwaambia, “Kama mimi ni mtu wa Mungu, ngoja moto ushuke kutoka mbinguni na ukuteketeze wewe na watu wako hamsini.” Moto wa Mungu ukashuka chini tena kutoka mbinguni na kumla yeye na watu wake hamsini.

13Bado tena mfalme alituma kundi la tatu la wapiganaji hamsini. Huyu mkuu akaenda, akaanguka mbele ya miguu ya Eliya, na kumsihi na kumwambia, “Wewe, mtu wa Mungu, nakuomba, acha uzima wangu na uzima wa hawa watumishi wako hamsini uwe na thamani machoni kwako.14Ndipo, moto ukashuka chini kutoka mbinguni na kuwala wale wakuu wawili wa kwanza pamoja na watu wao, bali sasa acha uzima wangu uwe na thamani machoni kwako.”

15Malaika wa Yahwe akamwambia Eliya, “Nenda chini pamoja naye. Usimwogope.” Hivyo Eliya akainuka na kwenda chini pamoja naye kwenda kwa mfalme.

16Baadaye Eliya akamwambia Ahazia, “Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, ‘Umewatuma wajumbe kuzungumza pamoja na Baal-Zebubu, mungu wa Ekron. Je ni kwa sababu hakuna Mungu katika Israeli ambaye unayeweza kumuuliza habari? Kwa hiyo sasa, hutaweza kushuka chini kutoka kwenye kitanda ulichokipanda; utakufa hakika.’”17Hivyo Mfalme Ahazia alikufa kulingana na neno la Yahwe ambalo Eliya alilisema. Yoramu alianza kutawala katika eneo lake, katika mwaka wa pili Yoramu mwana wa Yohoshafati mfalme wa Yuda, kwa sababu Ahazia hakuwa na mtoto.

18Na mambo mengine yanayomhusu Ahazia, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

2

1Ulipofika, wakati BWANA alipopenda kumpandisha Eliya kwenda mbinguni kwa upepo wa kisulisuli, Eliya aliondoka pamoja na Elisha kutoka Gilgali.2Eliya akamwambia Elisha, “Kaa hapa, tafadhali, kwa sababu BWANA amenituma niende mpaka Betheli.” Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakashuka chini kuelekea Betheli.3Wana wa manabii ambao walikuwa Betheli walikuja kwa Elisha na kumwambia, “Je unajua kwamba BWANA atamwondoa bwana wako kuanzia leo?” Elisha akajibu, “Ndiyo, nalijua hilo, ila msizungumze kuhusu hilo.”4Eliya akamwambia, “Elisha, subiri hapa, tafadhali, kwa kuwa BWANA amenituma niende Yeriko.” Kisha Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wakaenda Yeriko.

5Kisha wana wa manabii ambao walikuwa Yeriko wakaja kwa Elisha na kumwambia, “Je unajua kwamba BWANA atamwondoa bwana wako kutoka kwako leo?” Elisha akajibu, “Ndiyo, nalijua hilo, lakini msilizungumzie hilo.”

6Kisha Eliya akamwambia, “Kaa hapa, tafadhali, kwa kuwa BWANA amenituma kwenda Yeriko.” Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo wawili wakaenda mbele.7Baadaye watu hamsini wa watoto wa wale manabii wakasimama kuwakabili kwa mbali kidogo wale wawili wakasimama karibu na Yordani.8Eliya akachukua vazi lake, akaliviringisha, na kuyapiga maji kwa kutumia lile vazi. Ule mto ukagawanyika katika sehemu mbili hivyo basi wawili hao wakatembea hadi nchi kavu.

9Ilitokea, walipokwisha kuvuka, kwamba Eliya akamwambia Elisha, “Niambie unachotaka nifanye kwako kabla sijaondolewa kutoka kwako.” Elisha akajibu, “Naomba sehemu kubwa ya roho yako ije kwangu.”

10Eliya akajibu, “Umeomba jambo gumu. Hata hivyo, kama ukiniona wakati nitakapoondolewa kutoka kwako, hii itatokea kwako, lakini kama sivyo, haitatokea.”

11Ikawa walipokuwa bado wakienda mbele na kuzungumza, gari la kukokotwa na farasi lenye moto na farasi wa moto ikatokea, ambapo iliwatenga kutoka kila mmoja, na Eliya akaenda juu kwa upepo wa kisulisuli kwenda mbinguni.12Elisha akaiona akalia kwa sauti, “Baba yangu, baba yangu, gari la kukokotwa na farasi la Israeli na waendesha farasi!” Hakumwona Eliya tena, na akashikilia nguo zake mwenyewe na kugawanya kwenye vipande viwili.13Akachukua vazi la Eliya lililokuwa limemwangukia, na kurudi kusimama kwenye ukingo wa Yordani.14Akayapiga maji pamoja na lile vazi la Eliya alilokuwa ameliangusha na kusema, “BWANA uko wapi, Mungu wa Eliya?” Wakati alipoyapiga yale maji, yaligawanyika katika pande mbili na Elisha akavuka.

15Wakati hao wana wa manabii ambao walitoka Yeriko walipomuona akikatiza kwao, wakasema, “Roho ya Eliya imepumzika kwa Elisha!” Hivyo wakaja kuonana naye, na wakasujudu ardhini mbele yake.16Wakamwambia, “Ona sasa, miongoni mwa watumishi wako kuna watu hamsini hodari. Tunakuomba waache waende, na kumtafuta bwana wako, endapo huyo Roho wa BWANA alipomchukua juu na kumtupa juu ya mlima mmoja au kwenye bonde moja.” Elisha akajibu, “Hapana, msiwatume.”

17Lakini walimsihi Elisha hadi akaona aibu, akasema, “Watume.” Ndipo wakawatuma watu hamsini, na wakatafuta kwa muda wa siku tatu, lakini hawakumpata.18Wakarudi kwa Elisha, wakati alipokuwa bado yuko Yeriko, na akasema, “Je sikusema, ‘msiende?’”

19Watu wa mjini wakamwambia Elisha, “Ona, tunakuomba, hali ya mjini hapa ni pazuri, kama bwana wangu awezavyo kuona, lakini maji ni mabaya na hiyo nchi huzaa mapooza.”

20Elisha akajibu, “Nileteeni chombo kipya na muweke chumvi ndani ya hicho chombo,” hivyo wakamletea.

21Elisha akaenda hadi kwenye chemichemi za maji na kutupia chumvi ndani; halafu akasema, “BWANA asema hivi, ‘Nimeyaponya haya maji. Kuanzia muda huu, hakutakuwa na kifo au nchi isiyozaa matunda.’”22Hivyo hayo maji yakapona hata leo, kwa lile neno ambalo Elisha aliongea.

23Ndipo Elisha akapanda kutoka pale mpaka Betheli. Naye lipokuwa akienda hadi kwenye barabara, wakatokea vijana nje ya mji na kumtania, wakamwambia, “Paa juu, wewe mwenye kipara! Paa juu, wewe mwenye kipara!”24Elisha alipotazama nyuma yake na kuwaona; akawalaani kwa jina la BWANA, na dubu wa kike wawili wakatokea kichakani na kuwararua vijana arobaini na mbili.25Ndipo Elisha alipoondoka pale na kuelekea Mlima Karmeli, na kutoka huko alirudi samaria.

3

1Basi katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshefati mfalme wa Yuda, Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu yata Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na miwili.2Alifanya yaliyo maovo machoni pa BWANA, lakini si kama baba yake na mama yake; kwa kuwa aliiondoa ile nguzo ya mungu wa Baali ambayo baba yake aliitengeneza.3Hata hivyo alishikilia dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi; wala hakuziacha mbali nao.

4Basi Mesha mfalme wa Moabu alifuga kondoo. Alikuwa akimpatia mfalme wa Israeli kondoo 100,000 na manyoya ya kondoo dume 100,000.5Ila baada ya Ahabu kufa, yule mfalme wa Moabu aliasi dhidi ya mfalme wa Israeli.6Hivyo Mfalme Yoramu akaondoka Samaria katika muda huo kuwahamasisha Waisraeli wote kwa ajili ya vita.7Akatuma mjumbe kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akisema, “Mfalme wa Moabu ameasi dhidi yangu. Je mtakwenda pamoja nami kupigana dhidi ya Moabu?” Yehoshafati akajibu, “Nitaenda. Mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi wangu ni kama farasi wako.”

8Ndipo akasema, “Tutawashambulia kwa njia gani?” Yehoshafati akajibu, “Kwa njia ya jangwa la Edemu.”

9Hivyo huyo mfalme wa Israeli, Yuda, na Edomu wakazunguka kwa muda wa siku saba. Hapakuwa na maji kwa ajili ya jeshi lao, wala kwa farasi au wanyama.

10Basi mfalme wa Israeli akasema, “Hii ni nini? Yahwe amewaita wafalme watatu ili kutekwa mikononi mwa Moabu?”

11Lakini Yehoshafati akasema, “Je hakuna nabii wa BWANA, ambaye tunaweza kufanya shauri kuhusu BWANA kupitia yeye?” Mtumishi mmoja wa wafalme wa Israeli akajibu na kusema, “Elisha mwana wa Shafati yuko hapa, ambaye alikuwa akimimina maji kwenye mikono ya Eliya.”

12Yehoshafati akasema, “Neno la Yahwe liko pamoja naye.” Hivyo mfalme wa Israeli, Yehoshafati, na mfalme wa Edomu wakashuka chini kwenda kwake.13Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Nifanye nini kwa ajili yako? Nenda kwa manabii wa baba na mama yako.” Ndipo mfalme wa Israeli akamwambia, “Hapana, kwa sababu BWANA amewaita hawa wafalme watatu pamoja ili kuruhusu jeshi la Moabu liwateke.”

14Elisha akajibu, “Kama BWANA wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, hakika kama nisingemheshimu uwepo wa Yehoshafati mfalme wa Yuda, nisingevuta usikivu kwako, au hata kukutazama.15Lakini sasa niletee mpiga kinanda.” Ndipo alipokuja mpiga kinanda alipocheza, mkono wa BWANA ukaja juu ya Elisha.16Akasema, “BWANA asema hivi, ‘Fanya hili bonde la mto mkavu lijae mahandaki.’17Kwa kuwa BWANA asema hivi, ‘Hutaona upepo, wala hamtaona mvua, bali hili bonde la mto litajaa maji, na mtakunywa, ninyi na mifugo yenu na wanyama wenu wote.’18Jambo hili ni jepesi machoni pa BWANA. Pia atawapa ushindi juu ya hao Wamoabu.19Mtaiteka kila ngome ya mji na kila mji mzuri, kukata kila mti mzuri, kusimamisha chemichemi zote za maji, na kuharibu kila sehemu nzuri ya nchi na miamba.”

20Hivyo asubuhi karibia na muda wa kutoa sadaka ya kuteketeza, yakaja maji kutoka uelekeo wa Edomu; nchi ikajaa maji.

21Ndipo wakati Wamoabu wote waliposikia kwamba wafalme wamekuja kupigana dhidi yao, walikusanyika pamoja, wote waliotakiwa kubeba silaha, na wakasimama mpakani.22Walitembea asubuhi na mapema na jua likang'aa kwenye maji. Wakati Wamoabu walipoyaona yale maji yaliyowaelekea, yanaonekana mekundu kama damu.23Wakatamka kwa hasira, “Hii ni damu! Yamkini hao wafalme wameharibiwa, na wameuana wao kwa wao! Sasa basi, Moabu, ngoja tuende tukawateke nyara!”

24Wakati walipokuja kwenye kambi ya Israeli, Waisraeli wakawashtukiza na kuwashambulia Wamoabi, ambao walikimbia mbele yao. Hilo jeshi la Israeli waliwakimbiza hao Wamoabu hadi kwao wakiwaua.25Waliiharibu miji, na kila aina ya amani ya nchi kila mtu alirusha jiwe mpaka ulipojaa. Walizuia kila chemichemi ya maji na kukata chini miti mizuri yote. Kir-haresethi tu ndiyo ilichwa na mawe yake. Lakini hao maaskari wakawashambulia na makombeo wakiwazunguka na kuishambulia.26Ndipo Mfalme Mesha wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa, alichukua watu hodari wa upanga 700 pamoja naye kwenda kwa mfalme wa Edomu, lakini walishindwa.27Ndipo akamchukua mtoto wake wa kwanza, ambaye angetawala baada ya yeye, na akamuudhi kwa kumtoa kama sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Hivyo, kulikuwa na hasira kubwa dhidi ya Israeli, na hao Waisraeli, na Jeshi la Israeli likamuacha mfalme Mesha na kurudi kwenye nchi yao.

4

1Ndipo mke wa mmoja wa watoto wa manabii alipokuja kwa Elisha akilia, akisema, “Mtumishi wako mume wangu amekufa, na unajua kwamba mtumishi wako alikuwa anamcha BWANA. Basi aliyemdai amekuja kuwachukua watoto wangu wawili kwenda kuwa watumwa.”

2Hivyo Elisha akamwambia, “Nikusaidie nini? Niambie una nini kwenye nyumba yako?” Akamwambia “Mtumishi wako hana kitu kwenye nyumba, isipokuwa chupa ya mafuta.”

3Kisha Elisha akasema, “Nenda kaazime vyombo kwa majirani zako, vyombo vitupu. Azima vyombo vingi uwezavyo.4Kisha lazima uende ndani na kujifungia mlango wewe na watoto wako, na kumiminia mafuta vyombo vyote; vile vilivyojaa ukavitenge.”

5Basi akamuacha Elisha na kujifungia mlango yeye na watoto wake. Wakavileta vile vyombo kwake, na akivijaza kwa mafuta.6Ikawa vyombo vilipojaa, akamwambia mtoto wake, “Niletee chombo kingine.” Ila akamwambia, “Hakuna vyombo vingine.” Kisha mafuta yakakoma kutoka.

7Ndipo akaja na kumwambia mtu wa Mungu. Akasema, “Nenda kauze mafuta; lipa deni lako, na yatakayobaki waachie watoto wako.”

8Siku moja Elisha alitembea Shunemu ambapo mwanamke Mwenye cheo aliishi; alimsihi ale chakula pamoja naye. Ikawa alipopita mara nyingi, angeweza kusimama pale na kula.9Huyo mwanamke akamwambia mme wake, “Ona, sasa nadhani kwamba huyu ni mtu mtakatifu wa Mungu ambaye hupita siku zote.10Ngoja tutengeneze chumba kidogo kwenye paa kwa ajili ya Elisha, na tuweke kitanda juu ya hicho chumba, meza, na taa. Kisha atakapokuwa anakuja kwetu, atakuwa anakaa hapo.”

11Ikawa siku moja akaja tena kwamba Elisha akasimama pale, akakaa kwenye hicho chumba na kupumzika hapo.12Elisha akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Mwite huyu Mshunami.” Wakati alipomuita, alisimama mbele yake.13Elisha akamwambia, “Mwambie, ‘Umetusumbukia kwa kutujali. Nini kifanyike kwa ajili yako? Tunaweza kukuombea kwa mfalme au kamanda wa jeshi?’” Akajibu, “Ninaishi miongoni mwa watu wangu.”

14Kisha Elisha akajibu, “Tumfanyie nini kwa ajili yake, sasa?” Gehazi akajibu, “Kweli hana mtoto, na mume wake ni mzee.”

15Hivyo Elisha akajibu, “Mwite.” Wakati alipomuita, akasimama kwenye mlango.16Elisha akasema, “Katika kipindi kama hiki mwakani, katika kipindi cha mwaka mmoja, utakuwa ukimkumbatia mtoto.” Akasema “Hapana, bwana wangu na mtu wa Mungu, usidanganye kwa mtumishi wako.”

17Lakini yule mwanamke akabeba mimba na kujifungua mtoto wa kiume kipindi hicho hicho katika mwaka uliofuata, kama Elisha alivyokuwa amemwambia.

18Wakati mtoto alipokuwa mkubwa, akaenda kwa baba yake siku moja, ambaye alikuwa na watu wanaovuna.19Akamwambia baba yake, “Kichwa changu, kichwa changu.” Baba yake akamwambia mtumishi wake, “Mbebe mpeleke kwa mama yake.”20Wakati mtumishi alipombeba kumrudisha kwa mama yake, yule mtoto alikaa kwenye magoti yake hadi mchana na baada ya hapo mtoto alikufa.21Hivyo yule mwanamke akambeba na kumlaza kwenye kile kitanda cha mtu wa Mungu, akafunga mlango, na kutoka nje.

22Akamwita mume wake, na kusema, “Tafadhali nitumie mmoja wa watumishi wako na moja ya punda wako ili niweze kuwahi kwa mtu wa Mungu ili niweze kurudi.”

23Mume wake akasema, “Kwa nini unataka kwenda kwake leo? Sio mwezi mpya wala Sabato.” Alijibu, “Itakuwa sawa.”

24Ndipo akatandika kwenye punda na kumwambia mtumishi wake, “Mwendeshe haraka; usinipunguzie mwendo hadi nitakapokwambia ufanye hivyo.”25Hivyo alienda na kuja na mtu wa Mungu katika mlima Karmeli. Basi wakati mtu wa Mungu alipomuona kwa mbali, akamwambia Gehazi mtumishi wake, “Tazama, mwanamke Mshunami anakuja.26Tafadhali mkimbilie na umwambie, ‘Hamjambo kwako pamoja na mume wako na mtoto wako?’” Akajibu, “Hawajambo.”

27Baada ya kufika kwa huyo mtu wa Mungu katika mlima, alimkumbatia miguu yake. Gehazi akaja karibu ili kumuondoa lakini mtu wa Mungu akasema, “Muache, kwa kuwa amefadhaika sana. Na BWANA amenificha tatizo lake kwangu, na hajaniambia kitu.”

28Ndipo akasema, “Nilikuuliza mtoto wako, bwana wangu? Sikusema, ‘Usinifiche?’”

29Ndipo Elisha akamwambia Gehazi, “Vaa kwa ajili ya safari na uchukue fimbo yangu mkononi mwako. Nenda kwake. Kama ukimkuta mtu yeyote, usimsalimie, na kama mtu yeyote akikusalimia, usimjibu. Laza fimbo yangu kwenye uso wa mtoto.

30Lakini mama yake na huyo mtoto akasema, “Kama BWANA aishivyo, na kama uishivyo, sitakuacha.” Hivyo Elisha akainuka na kumfuata.

31Gehazi akawatangulia na kulaza ile fimbo kwenye uso wa yule mtoto, lakini yule mtoto hakuongea wala kusikia. Hivyo baada ya hapo Gehazi akarudi kuonana na Elisha na kumwambia akisema, “Mtoto hakuamka.”32Ndipo Elisha alipofika kwenye ile nyumba, yule mtoto alikuwa amekufa na alikuwa bado yupo kwenye kitanda.33Hivyo Elisha aliingia ndani na kufunga mlango yeye mwenyewe na yule mtoto na kuomba kwa BWANA.34Alipanda juu na kulala juu ya yule mtoto; aliweka mdomo wake kwenye mdomo wake, macho yake kwenye macho yake, na mikono yake kwenye mikono yake. Akajinyoosha yeye mwenyewe kwa yule kijana, na mwili wa yule mtoto ukaanza kupata joto.35Baada ya hapo Elisha aliinuka na kuanza kutembea kuzunguka kile chumba na kurudi tena juu na kujinyoosha mwenyewe kwa yule kijana. Yule kijana alipiga chafya mara saba na kisha akafungua macho yake!

36Hivyo Elisha akamwita Gehazi na kumwambia, “Mwite yule Mshunami!” Hivyo akamwita, na wakati alipofika kwenye kile chumba, Elisha akasema, “Mchukue mtoto wako.”37Kisha akainamisha uso wake chini kwenye miguu yake na kusujudu, na kisha kumchukua mtoto wake na kuondoka.

38Kisha Elisha akarudi tena Gilgali. Kulikuwa na njaa katika nchi, na wana wa manabii walikuwa wamekaa mbele yake. Akamwambia mtumishi wake, “Weka sufuria kubwa kwenye moto na pika kwa ajili ya watoto wa manabii.”

39Mmoja wao akaenda kwenye shamba kukusanya mboga mboga. Alikuta matango ya porini na kukusanya ya kutosha hadi alipojaza kwenye nguo yake. Walizikata na kuziweka kwenye sufuria, lakini hakujua zilikuwa za aina gani.40Basi, wakawapakulia na kusambaziwa kwa watu kwa ajili ya kula. Baadaye, kadiri walivyokuwa wakiendelea kula, walipiga kelele na kusema, “Mtu wa Mungu, kuna kifo kwenye sufuria!” Hivyo wasingeweza kula tena.41Lakini Elisha akasema, “Lete unga.” Alitupia kwenye sufuria na kusema, “Pakua kwa watu kwa ajili ya kula, kwa hiyo wanaweza kula.” Kisha hapakuwa kitu chochote kibaya kwenye ile sufuria.

42Akaja mtu kutoka Baal Shalisha kwa mtu wa Mungu na kumletea chakula cha kwanza cha mavuno yake mikate Ishirini ya shayiri, na masuke mabichi kwenye gunia. Akasema, “Wape haya watu ili waweze kula.”43Mtumishi wake akasema, “Je, niandae hii mbele ya watu mia moja?” Lakini Elisha akasema, “Wapeni hawa watu, ili waweze kula, kwa sababu BWANA anasema, ‘Watakula na kingine kitabaki.”’44Basi mtumishi wake akawaandalia mbele yao; wakala, na kuacha kingine kimebaki, kama neno la BWANA lilivyokuwa limesema.

5

1Basi Naamani, kamanda wa jeshi la mfalme wa Shamu, alikuwa mtu mkubwa na mtu mwenye kuheshimiwa mbele ya bwana wake, kwa ajili yake BWANA aliwapa ushindi Washami. Pia alikuwa hodari, mtu shujaa, lakini alikuwa ana ukoma.

2Washami walikuwa wametoka kuongoza kikosi na kumchukua kijana mdogo wa kike kutoka nchi ya Israeli. Akamuhudumia mke wa Naamani.3Yule binti akamwambia bibi yake, “Natamani kwamba bwana wangu angelikuwa pamoja na nabii ambaye yupo Samaria! Halafu angelimponya bwana wangu ukoma wake.

4Hivyo Naamani akaingia na kumwambia mfalme kile ambacho yule binti kutoka nchi ya Israeli alichokuwa amekisema.5Kisha mfalme wa Shamu akasema, “Nenda sasa, na nitatuma barua kwa mfalme wa Israeli.” Naamani akaondoka na kuchukua talanta zake kumi za fedha, vipande elfu sita vya dhahabu, na nguo kumi za kubadilisha.6Pia alichukua barua ya kumpelekea mfalme wa Israeli inayosema, “Sasa wakati hii barua itakapoletwa kwako, utaona kwamba nimemtuma mtumishi wangu Naamani kwako, hivyo basi utamponya ukoma wake.”

7Wakati mfalme wa Israeli alipoisoma ile barua, alichana mavazi yake na kusema, “Je mimi ni Mungu, niue na nirudishe uhai, kwamba huyu mtu anataka nimponye mtu ukoma wake? Inaonekana anatafuta vita na mimi.”

8Ikawa wakati Elisha mtu wa Mungu aliposikia kwamba mfalme wa Israeli alichana nguo zake, akatuma neno kwa mfalme akisema, “Kwa nini umechana nguo zako? Muache aje kwangu sasa, na atajua kwamba kuna nabii katika Israeli.”9Basi Naamani akaja na farasi wake na magari yake ya kukokotwa na farasi na kusimama kwenye mlango wa nyumba ya Elisha.10Elisha akamtumia mjumbe, akisema, “Nenda na ukazame mwenyewe katika Yordani mara saba, na ngozi ya mwili wako itajirudi; utakuwa msafi.”

11Lakini Naamani alikasirika na kuondoka na kusema, “Tazama, nilidhani bila shaka angekuja kwangu na kusimama na kuliita jina la BWANA Mungu wake, na kupitisha mkono wake kwenye sehemu ya ugonjwa na kuponya ukoma wangu.12Je sio Abana na Faepari, mito ya Damaskasi, bora kuliko maji yote ya Israeli? Je siwezi kuoga ndani yao na kuwa safi?” Hivyo akageuka na kwenda kwa hasira.

13Ndipo watumishi wa Naamani wakaja karibu na kumwambia, “Baba yangu, kama yule nabii angekuambia kufanya kitu kigumu, usingelifanya? Je si zaidi basi, atakapokwambia rahisi, ‘Zama mwenyewe na uwe safi?’”14Ndipo akashuka chini na kuzama mwenyewe mara saba kwenye mto Yordani, akitii maelekezo ya mtu wa Mungu. Nyama ya mwili wake ikarudi tena kama nyama ya mwili wa mtoto mdogo, na alikuwa amepona.

15Naamani akarudi kwa yule mtu wa Mungu, yeye na watu wake wengine, na kuja na kusimama mbele yake. Akasema, “Tazama, sasa najua kwamba hakuna Mungu katika Dunia nzima isipokuwa katika Israeli. Kwa hiyo basi, chukua zawadi kutoka kwa mtumishi wako tafadhali.”

16Lakini Elisha akajibu, “Kama BWANA aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sitapokea chochote.” Naamani akamsihi Elisha apokee zawadi, lakini alikataa.

17Hivyo Naamani akasema, “Kama sivyo, nakuomba acha apewe mtumishi wako pale mzigo wa baghala mbili za udongo, kwa kuwa kuanzia sasa, mtumishi wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa mungu yeyote isipokuwa BWANA.18Katika jambo hili moja BWANA anaweza kumsamehe mtumishi wako, hii ni, wakati mfalme wangu atakapoenda kwenye nyumba ya Rimoni kuabudu pale, na kujifunza kwenye mikono yangu na kumuinamia mwenyewe kwenye nyumba ya Rimoni, BWANA aweze kumsamehe mtumishi wako katika hili jambo.”

19Elisha akamwambia, “Nenda kwa amani.” Hivyo Naamani akaondoka.

20Alikuwa amesafiri lakini umbali mfupi, wakati Gehazi mtumishi wa Elisha mtumishi wa Mungu alisema mwenyewe, “Tazama, bwana wangu amemuachilia huyu Naamani Mshami kwa kuacha kupokea zawadi kutoka kwenye mikono yake ambazo alizileta. Kama BWANA aishivyo, nitakimbia nikimfuata na kupokea kitu kutoka kwake.”

21Hivyo Gehazi akamfuata Naamani. Wakati Naamani alipomuona mtu mmoja anakimbia akimfuata, aliruka chini kutoka kwenye gari lake kuonana naye na kusema, “Je kila kitu kiko sawa?”

22Gehazi akasema, “kila kitu kiko sawa. Bwana wangu amenituma, akisema, ‘Tazama, sasa wamekuja kwangu kutoka nchi ya mlima ya Efraimu vijana wawili wa watoto wa manabii. Tafadhali, wapatie talanta ya fedha na nguo mbili za kubadilisha.’”

23Naamani akajibu, “Ninafuraha kubwa kukupatia talanta mbili.” Naamani akamsihi Gehazi na kumpa talanta mbili za fedha kwenye mifuko miwili ya kubebea, pamoja na nguo mbili za kubadilisha, na kutandaza kwa wafanyakazi wake wawili, ambao walikuwa wamebebea ile mifuko miwili ya fedha mbele ya Gehazi.24Wakati Gehazi alipokuja kwenye ule mlima, alichukua ile mifuko ya fedha kutoka kwenye mikono yao na kuificha kwenye nyumba; akawatuma wale watu, na wakaondoka.25Wakati Gehazi alipoingia na kusimama mbele ya bwana wake, Elisha akamwambia, “Umetokea wapi, Gehazi?” Akajibu, “Mtumishi wako hakwenda mahali.”

26Elisha akamwambia Gehazi, “Je roho yangu haikuwa na wewe wakati yule mtu alipoyarudisha magari yake ya farasi ili kukutana na wewe? Je huu ni muda wa kupokea pesa na nguo, mashamba ya mzaituni na mizabibu, na kondoo na Ng'ombe, na watumishi wakiume na watumishi wakike?27Basi ukoma wa Naamani utakuwa kwenye uzao wako daima.” Basi Gehazi akatoka kwenye uwepo wake, mwenye ukoma kama theluji.

6

1Wana wa manabii wakamwambia Elisha, “Sehemu ambayo tunayoishi na wewe ni ndogo sana kwa ajili ya wote.2Tafadhali, tuache tuende Yordani, na umwache kila mtu akate mti hapo ambako tunaweza kuishi.” Elisha akajibu, “Unaweza kwenda mbele.”

3Mmoja wao akasema, “Nenda na watumishi wako tafadhali.” Elisha akajibu, “Nitaenda.”

4Kwa hiyo akaenda pamoja nao, na wakati walipokuja Yordani, wakaanza kukata miti.

5Lakini mmoja wao alipokuwa akikata, kichwa cha shoka kikaangukia kwenye maji; akalia kwa sauti na kusema, “La hasha, bwana wangu, kilikuwa kimeazimwa!”

6Basi mtu wa Mungu akasema, “kiliangukia wapi?” Yule mtu akamwonyesha Elisha ile sehemu. Akakata kijiti, akarusha kwenye maji, na kufanya chuma kuelea.7Elisha akasema, “Kichukue.” Basi yule mtu akafikisha mkono wake na kukinyakua.

8Basi mfalme wa Shamu alikuwa akipigana vita dhidi ya Israel. Akafanya shauri na watumishi wake, akisema, “kambi yangu itakuwa sehemu fulani na fulani.”

9Basi huyo mtu wa Mungu akapeleka habari kwa mfalme wa Israeli, akisema, “Kuwa makini usipite ile sehemu, kwa kuwa ndipo Washamu wanakoshukia hapo.”10Mfalme wa Israeli akatuma mjumbe kwenda pale sehemu ambayo mtu wa Mungu alipaongelea na kumtahadharisha. Zaidi ya mara moja au mbili, wakati mfalme alipoenda pale, alikuwa kwenye ulinzi wake.

11Huyo mfalme wa Shamu alikasirishwa kuhusu haya maonyo, na akawaita watumishi wake na kuwaambia, “Je hamtaniambia ni nani miongoni mwetu aliye upande wa Israeli?”

12Hivyo mmoja wa watumishi wake akasema, “Hapana, bwana wangu, mfalme, kwa ajili ya Elisha yule nabii katika Israeli humwambia yule mfalme wa Israeli maneno ambayo uyaongeayo kwenye kitanda chako cha kulala.”

13Yule mfalme akajibu, “Nenda na uone Elisha alipo hivyo naweza kutuma watu na kumkamata.” Akaambiwa, “Tazama yuko Dothani.”14Kwa hiyo yule mfalme akatuma farasi kwenda Donathi, magari ya farasi, na jeshi kubwa. Wakaja usiku na kuzunguka ule mji.

15Wakati yule mtumishi wa mtu wa Mungu alipoamka mapema na kutoka nje, kumbe, jeshi kubwa pamoja na farasi na magari ya farasi yameuzunguka mji. Mtumishi wake akamwabia, “Kumbe, bwana wangu! Tutafanya nini?”

16Elisha akajibu, “Usiogope, wale walio na sisi ni zaidi kuliko wale walio nao.”

17Elisha akajibu na kusema, “BWANA, nakuomba kwamba utamfungua macho yake ili kwamba aweze kuona.” Ndipo BWANA alipofungua macho ya mtumishi, na akaona. Kumbe, ule mlima ulikuwa umejaa farasi na magari ya farasi ya moto yamemzunguka Elisha!

18Wakati hao Washami walipomshukia chini, Elisha aliomba kwa BWANA na kusema, “Uwapige hawa watu kwa upofu, nakuomba.” Hivyo BWANA akawafanya vipofu, kama Elisha alivyoomba.

19Kisha Elisha akawaambia Washami, “Hii njia sio, pia mji huu sio. Nifuateni mimi, na nitawaleta kwa yule mtu ambaye mnayemtafuta.” Ndipo akawaongoza kwenda Samaria.

20Hata walipokwisha kufika Samaria, Elisha akasema, “BWANA, fungua macho ya hawa watu ili waweze kuona.” BWANA akawafungua macho yao na wakaona, na kumbe, walikuwa katikati ya mji wa Samaria.

21Yule mfalme wa Israeli akamwambia Elisha, wakati alipowaona, “Baba yangu, niwaue? Niwaue?”

22Elisha akajibu, “Usiwaue. Ungeweza kuwaua wale ambao uliokuwa umewachukua mateka kwa upanga na upinde wako? Weka mkate na maji mbele yao, ili kwamba waweze kula na kunywa, na kwenda kwa bwana wao.”23Ndipo mfalme akaandaa chakula kingi kwa ajili yao, na wakati walipokula na kunywa, akawapeleka mbali, na walirudi kwa bwana wao. Lile kundi la jeshi la Washami halikurudi kwa muda mrefu katika nchi ya Israeli.

24Baadaye baada ya huyu Ben Hadadi mfalme wa Shamu kukusanya majeshi yake yote na kuiteka Samaria na kuizingira.25Hivyo kulikuwa na njaa kubwa katika Samaria. Kumbe, wakauzingira hadi kichwa cha punda kilipouzwa kwa vipande themanini vya fedha, na sehemu ya nne ya sehemu ya kibaba cha kinyesi cha njiwa kwa vipande vitano vya fedha.

26Wakati mfalme wa Israeli alipokuwa akipita karibu na ukuta, mwanamke mmoja akamlilia akisema, “Nisaidie, bwana wangu, mfalme.”

27Akasema, “Kama BWANA hawezi kukusaidia, je nitakusaidiaje? Je kuna kitu chochote kinakuja kutoka sehemu ya kupuria nafaka au shinikizoni?”28Mfalme akaendelea, “Nini kinakusumbua?” Akajibu, “Huyu mwanamke ameniambia, ‘Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla leo, na tutamla wa kwangu kesho.’”

29Hivyo tulimchemsha mtoto wangu na kumla, na siku ya pili yake nikamwambia, “Mtoe mtoto wako ili tuweze kumla, lakini alikuwa amemficha mtoto wake.”

30Basi mfalme aliposikia yale maneno ya yule mwanamke, akayachana mavazi yake (sasa alikuwa akitembelea kwenye ukuta), na watu wakatazama na kuona kwamba alikuwa amevaa nguo ya gunia31Kisha akasema, “Mungu afanye hivyo kwangu, na zaidi pia, kama kichwa cha Elisha mwana wa Shafati kitabaki juu yake leo.”

32Basi Elisha alikuwa ameketi kwenye nyumba yake, na wazee walikuwa wamekaa pamoja naye. Yule mfalme akamtuma mtu wa mbele yake, lakini wakati mjumbe alipokuja kwa Elisha, akawaambia wazee, “Ona jinsi huyu mwana wa muuaji alivyotumwa kuchukua kichwa changu? Tazama, wakati yule mjumbe atakapokuja, funga mlango, na uushikilie huo mlango funga dhidi yake asiingie. Je sio sauti ya bwana wake nyuma mguuni pake?”33Wakati alipokuwa bado akiongea pamoja nao, kumbe, yule mjumbe alishuka kwake. Mfalme akasema, “Kumbe, masumbuko haya yatoka kwa BWANA. Kwa nini nimsubiri BWANA tena?”

7

1Elisha akasema, “Sikiliza neno la BWANA. Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: ‘Kesho muda kama huu kipimo cha unga mzuri kitauzwa kwa shekeli, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli, kwenye lango la Samaria.’”

2Basi yule mkuu ambaye alikuwa akitegemea mkono wake akamjibu mtu wa Mungu, na kusema, “Ona, hata kama BWANA ataweka madirisha mbinguni, je jambo hili linawezekana?” Elisha akajibu, “Ona, utaona ikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hilo.”

3Basi, kulikuwa na watu wanne wenye ukoma upande wa nje wa lango la mji. Wakaambizana kila mmoja, “Kwa nini tukae hapa hadi hapo tutakapokufa?4Kama tukisema kwamba tutaenda kwenye ule mji, maana mjini kuna njaa, na tutakufa hapo. Lakini kama tukiendelea kukaa hapa, bado tutakufa. Sawa, njooni, twendeni kwenye lile jeshi la Washami. Kama wakitupa uhai, tutakuwa hai, na kama wakituua, tutakufa tu.”5Hivyo wakaamka asubuhi kabla giza halijaisha kwenda kwenye kambi ya Washami; Wakati walipofika sehemu ya mwanzo wa kambi, hapakuwa na mtu hapo.

6Kwa kuwa Bwana alikuwa amelifanya jeshi la Washami kusikia sauti ya magari ya farasi, na sauti za farasi, sauti za jeshi jingine kubwa, ndipo wakaambizana kila mmoja wao, “Yule mfalme wa Israeli amekodisha wafalme wa Wahiti na Wamisri waje wapigane dhidi yetu.”7Hivyo wale maaskari wakaondoka kungali giza; waliacha mahema yao, punda zao, na kambi kama ilivyokuwa, na kukimbia kwa ajili ya maisha yao.

8Wakati wale watu wenye ukoma walipokuja sehemu ya mwisho wa kambi, wakaenda kwenye hema moja na kula na kunywa, na kubeba fedha na dhahabu na nguo, na kwenda na kuzificha. Wakarudi na kuingia kwenye hema nyingine na kubeba kutoka pale pia, na kwenda kuvificha.

9Basi, wakaambizana kila mmoja, “Hatufanyi sahihi. Siku hii ni siku ya habari njema, lakini tunanyamaza kimya kuhusu hili. Kama tukisubiri mpaka kutakapopambazuka, adhabu itakuwa juu yetu. Basi, njooni, twendeni na kuwaambia nyumba ya mfalme.”

10Kwa hiyo wakaenda na kuwaita mabawabu wa mji. Wakawaambia, wakisema, “Tumeenda kambi ya Washami, lakini hapakuwa na mtu pale, hakuna sauti ya mtu yeyote, lakini kulikuwa na farasi wamefungwa, na punda wamefungwa, na zile hema kama zilivyokuwa.”11Ndipo mabawabu wakatoa habari, ndipo wakaambiwa ndani ya nyumba ya mfalme.

12Basi yule mfalme akainuka usiku nakusema kwa watumishi wake, “Nitawaambia sasa kile ambacho Washami walichotufanyia. Wanajua kwamba tuna njaa, hivyo wameondoka kwenye kambi kwenda kujificha kwenye mashamba. Wanasema, ‘Wakati watakapotoka mjini, tutawakamata wakiwa hai, na kuingia mjini.”

13Mmoja wa wale watumishi wa mfalme akajibu na kusema, “Nakuomba, ngoja baadhi ya watu wachukue farasi watano wale waliosalia, ambao wamebaki kwenye mji. Wako kama mkutano wote wa Israeli waliobaki wengi wamekufa; ngoja tuwatume na tuone.”

14Hivyo wakachukua magari mawili ya farasi pamoja na farasi, na mfalme akawatuma baada ya jeshi la Washami, akisema, “Enendeni mkaone.”15Wakawafuata kwenda Yordani, na barabara zote zilikuwa zimejaa na vifaa ambavyo Washami walivitupa wapate kukimbia haraka. Kwa hiyo wale wajumbe wakarudi na kumwambia mfalme.16Wale watu wakatoka nje na wakaziteka nyara zile kambi za Washami. Hivyo kipimo cha unga mzuri uliuzwa kwa shekeli moja, na vipimo viwili vya shayiri kwa shekeli moja, kama vile ambavyo neno la BWANA lilivyosema.

17Naye mfalme alimwagiza yule akida ambaye alitegemea mkono wake kuwa mkuu wa lango, na watu wakamkanyaga chini langoni. Alikufa kama mtu wa Mungu alivyosema, ambaye ameongea wakati yule mfalme alipomshukia.18Basi ikatokea kama yule mtu wa Mungu alivyosema kwa mfalme akisema, “Muda kama huu kwenye lango la Samaria, vipimo viwili vya shayiri vitapatikana kwa shekeli, na kipimo cha unga mzuri kwa shekeli.”

19Yule akida alimjibu yule mtu wa Mungu na kusema, “Tazama, hata kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je hiki kitu kingeweza kutokea.” Elisha akasema, “Tazama, utaona kikitokea kwa macho yako mwenyewe, lakini hutakula chochote katika hicho.”20Hivyo ndivyo haswa kilichompata, kwa kuwa watu wakamkanyaga kwenye lango, na kufa.

8

1Basi, Elisha alikuwa amemwambia yule mwanamke ambaye alimfufulia mtoto wake. Akamwambia, “Inuka na uende pamoja na nyumba yako, na uishi popote uwezapo katika nchi nyingine, kwa sababu BWANA ameiita njaa ambayo itakuja katika hii nchi kwa miaka saba.”2Basi yule mwanamke akainuka na akatii lile neno la mtumishi wa Mungu. Akaenda na nyumba yake na kuishi kwenye nchi ya Wafilisti miaka saba.

3Ikafika kama mwishoni mwa miaka saba yule mwanamke akarudi kutoka kwenye ile nchi ya Wafilisti, na kwenda kwa mfalme kumuomba nyumba yake na kwa ajili ya nchi yake.4Basi mfalme alikuwa anaongea na Gehazi yule mtumishi wa Mungu, akisema, “Tafadhali niambie yale mambo makubwa ambayo Elisha ameyafanya.”5Basi alipokuwa akimwambia yule mfalme jinsi gani Elisha alivyomfufua yule mtoto aliyekufa, huyo mwanamke ambaye mtoto wake aliyekuwa amefufuliwa akaja kumuomba yule mfalme kwa ajili ya nyumba yake na nchi yake. Gehazi akasema, “Bwana wangu, mfalme, huyu ndiye yule mwanamke, na huyu ndiye mtoto wake, ambaye Elisha amemfufua.”

6Wakati yule mfalme alipomuuliza yule mwanamke kuhusu mtoto wake, alimwelezea yule mfalme. Ndipo mfalme akamwagizia akida, akisema, “Mrudishie vyote vilivyokuwa vyake na mavuno yake yote ya mashamba tangu siku alipoondoka hadi sasa.”

7Elisha akaja Dameski ambako Ben Hadadi yule mfalme wa Shamu alikuwa anaumwa. Yule mfalme aliambiwa, “Yule mtu wa Mungu amekuja hapa.”8Mfalme akamwambia Hazaeli, “Chukua zawadi kwenye mkono wako na uende ukakutane na mtu wa Mungu, na ukazungumze na BWANA kupitia yeye, ukisema, “Je nitapona huu ugonjwa wangu?”

9Basi Hazaeli akaenda kuonana naye na kuchukua zawadi zake za kila kitu kizuri cha Dameski, akabeba ngamia arobaini. Hivyo Hazaeli akaja na kusimama mbele ya Elisha na kusema, “Mtoto wako Ben Hadadi mfalme wa Shamu amenituma kwako, kusema, “Je nitapona huu ugonjwa?”

10Elisha akamwambia, “Nenda, kwa Ben Hadadi, ‘ukamwambie Utapona hakika,’ lakini BWANA amenionyesha kwamba atakufa hakika.”11Basi Elisha akamkazia macho Hazaeli hadi alipojisikia aibu, na yule mtu wa Mungu akalia machozi.

12Hazaeli akauliza, kwa nini unalia, bwana wangu?” Akajibu, “Kwa sababu najua uovu ambao utakaoufanya kwa watu wa Israeli. Utazichoma moto ngome zao kwa moto, na utawaua vijana wao kwa upanga, kuwaseta vipande vipande watoto wao wachanga, na kuwapasua mimba zao wanawake wenye mimba.”

13Hazaeli akajibu, Ni nani mtumwa wako, ambaye atafanya jambo hili kubwa? Yeye ni mbwa tu.” Elisha akajibu, “BWANA amenionyesha kwamba utakuwa mfalme juu ya Shamu.”

14Ndipo Hazaeli akamwacha Elisha na kuja kwa bwana wake, ambaye alimwambia, “Je Elisha alikwambiaje?” Akajibu, “Ameniambia kwamba utapona bila shaka.”15Basi siku ya pili yake Hazaeli akachukua tandiko la kitandai na kulichovya kwenye maji, na kulitandaza kwenye uso wa Ben Hadadi hivyo akafa. Basi Hazaeli akawa mfalme katika sehemu yake.

16Katika mwaka wa kumi na tano wa Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Yehoramu akaanza kutawala. Alikuwa mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda. Alianza wakati Yehoshafati alikuwa mfalme wa Yuda.17Yoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka minane katika Yerusalemu.18Yoramu akatembea kwenye njia ya huyo mfalme wa Israeli, kama walivyokuwa wakifanya kwenye nyumba ya Ahabu; kwa kuwa alikuwa na binti wa Ahabu kama mke wake, na alifanya uovu machoni pa BWANA.19Walakini, kwa sababu ya mtumishi wake Daudi, BWANA hakutaka kuiharibu Yuda, tangu alipomwambia kwamba atampatia wazao.

20Katika siku za Yoramu, Edomu akaasi kutoka chini ya mkono wa Yuda, na wakamfanya mfalme juu yao wenyewe.21Basi Yoramu akaenda na makamanda wa jeshi na magari ya farasi yote. Ilitokea kwamba akaamka usiku na kushambulia na kuwazunguka Waedomu, waliokuwa wamemzunguka na wale makamanda wa jeshi la magari ya farasi. Ndipo wanajeshi wa Yehoramu wakakimbilia majumbani kwao.22Hivyo Edomu aliasi dhidi ya utawala wa Yuda katika siku hizi. Libna pia aliasi katika kipindi hicho hicho.

23Kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoramu, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?24Yehoramu akafa na kuzikwa pamoja na baba zake, na akalala pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Ndipo Ahazi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

25Katika mwaka wa kumi na mbili wa Yehoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.26Ahazi alikuwa ana umri wa miaka ishirini na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Athalia; alikuwa mtoto wa Omri, mfalme wa Israeli.27Ahazia alitembelea katika nyumba ya Ahabu; alifanya yale yaliyo maovu katika uso wa BWANA, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa kuwa Ahazia alikuwa mkwe kwenye nyumba ya Ahabu.

28Ahazia akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Shamu, katika Ramoth Geleadi. Washami wakamjeruhi Yoramu.29Mfalme Yoramu akarudi ili auguzwe huko Yezreeli kwenye yale majeraha ambayo Washami walimpatia huko Rama. Wakati alipopigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Hivyo Ahazi mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akashuka kwa Yezreeli kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.

9

1Nabii Elisha akamwita mmoja wa watoto wa manabii na kumwambia, “Vaa kwa safari, halafu chukua hii chupa ndogo ya mafuta kwenye mikono yako na uende Ramoth Geliadi.2Wakati utakapofika, mtafute Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi, na uende ukaingie na kumfanya ainuke kutoka miongoni mwa rafiki zake, na ukampeleke katika chumba cha ndani.3Kisha chukua ile chupa ya mafuta na imiminie kwenye kichwa chake na kusema, ‘BWANA anasema hivi: “Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya Israeli. “Halafu fungua mlango, na kukimbia; usichelewe.”

4Basi yule kijana, yule nabii kijana, akaenda Ramoth Geliadi.5Wakati alipofika, kumbe, wale majemedari wa lile jeshi walikuwa wamekaa. Hivyo yule nabii kijana akasema, “Nimekuja mara moja na neno kwako, jemedari.” Yehu akajibu, “kwa yupi katika sisi?” Yule nabii kijana akajibu, “Kwako ee Jemedari.”

6Basi Yehu akainuka na kwenda kwenye nyumba, na yule nabii akammiminia mafuta kwenye kichwa chake na kumwambia Yehu, “BWANA, Mungu wa Israeli, anasema hivi: ‘Nimekumiminia mafuta uwe mfalme juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli.7Wewe lazima uiue familia ya Ahabu bwana wako, ili niweze kulipiza kisasi cha damu ya watumishi wangu manabii, na damu ya watumishi wote wa BWANA, ambao waliokuwa wameuawa kwa mkono wa Yezebeli.8Kwa kuwa nyumba yote ya Ahabu itaangamia, na nitamkatilia mbali kila mtoto wa kiume wa Ahabu, yeyote awe mtumwa au mtu huru.9Nitaifanya nyumba ya Ahabu kama nyumba ya Yerobohamu mwana wa Nebati na kama nyumba ya Baasha mwana wa Ahiya.10Mbwa watamla Yezebeli katika Yezreeli, na hakutakuwa na mtu wa kumzika.” Kisha nabii akafungua mlango na kukimbia.11Kisha Yehu akatoka kwenda kwa watumishi wa bwana wake, na mmoja akamwambia, “Je kila kitu kiko sawa? Kwa nini huyu mwenda wazimu amekuja kwako?” Yehu akawajibu, “Mnamjua huyo mtu na mambo asemayo.”

12Wakasema, “Huo ni uongo. Tuambie.” Yehu akajibu, “Alisema hivi na vile juu yangu, na pia akasema, ‘hivi ndivyo BWANA asemavyo: Nimekumiminia mafuta kama mfalme juu ya Israeli.’”

13Kisha kila mmoja wao akachukua vazi haraka na kuweka chini ya Yehu juu ya madaraja. Wakapiga baragumu na kusema, “Yehu ni mfalme.”

14Katika njia hii Yehu mwana wa Yehoshafati mwana wa Nimshi akafanya njama juu ya Yoramu. Basi Yoramu alikuwa akiilinda Ramothi Gileadi, yeye na Israeli yote, kwa sababu ya Hazaeli mfalme wa Shamu,15lakini mfalme Yoramu alikuwa amesharudi kwa Yezreeli ili kuponywa yale majeraha aliyokuwa ameyapata na Washami, wakati akiwa anapigana dhidi ya Hazaeli mfalme wa Shamu. Yehu akawaambia watumishi wa Yoramu, “kama hili ndilo wazo lako, kisha usimwache mtu aondoke na kwenda nje ya mji, ili aende kupeleka habari hii Yezreeli.”16Basi Yehu akaendesha gari la farasi mpaka Yezreeli; kwa kuwa Yoramu alikuwa amelala huko. Basi Ahazi mfalme wa Yuda alikuwa ameshuka chini kuonana na Yoramu.

17Mlinzi alikuwa amesimama juu ya mnara katika Yezreeli, akaliona lile kundi la Yehu alipokuwa akija kwa mbali kidogo; akasema, “Naona kundi la watu wanakuja.” Yoramu akasema, “Chukua mwendesha farasi, na umtume akakutane nao; mwambie aseme, ‘Je mnakuja kwa amani?’”

18Hivyo mwendesha farasi akatoka kumlaki; akasema, “Mfalme asema hivi: ‘Je mnakuja kwa amani?’” Basi Yehu akasema, “Wewe una nini na amani? Geuka na unifuate nyuma.” Kisha yule mlinzi akamwambia mfalme, Yule mjumbe ameshaonana nao, lakini anarudi.”

19Kisha akapeleka mpanda farasi wa pili, ambaye alikuja kwao na kusema, “Mfalme asema hivi: ‘Je mnakuja na amani?”’ Yehu akajibu, “Wewe una nini na amani? Geuka na kunifuata nyuma.

20Tena yule mlinzi akatoa taarifa, “Amekwisha kuonana nao, lakini hatorudi. Kwa kuwa hilo gari la farasi limekuwa likiendeshwa ndivyo ambavyo Yehu mwana wa Nimshi aendeshavyo; anaendesha kwa kasi.”

21Hivyo Yoramu akasema, “Andaa gari langu la farasi liwe tayari.” Wakaandaa gari lake la farasi, na Yoramu mfalme wa Israeli na Ahazi mfalme wa Yuda akaendesha, kila mmoja kwenye gari lake la farasi, kumlaki Yehu. Wakamkuta kwenye mali ya Nabothi Myezreeli.22Wakati Yoramu alipomuona Yehu, alisema, “Je unakuja katika hali ya amani, Yehu?” Akajibu, “Amani gani hapo, wakati uzinzi wa ukahaba hufanywa na uchawi wa mama yako Yezebeli umejaa tele?”

23Basi Yoramu akarudisha magari yake ya farasi na kukimbia na kumwambia Ahazia, “Kuna uhaini, Ahazia.

24Ndipo Yehu akauvuta upinde wake kwa nguvu zake zote na kumpiga Yoramu kati ya mabega yake; mshale ukaenda kwenye moyo wake, akaanguka chini kwenye gari lake la farasi.25Ndipo Yehu akamwambia Bidkari Jemedari wake, “Mchukue na mtupie kwenye shamba la Nabothi Myezreeni. Fikiria kuhusu vile ambavyo wewe na mimi tulivyoendesha pamoja baada ya Ahabu baba yake, BWANA aliuweka juu unabii dhidi yake:26Jana niliona damu ya Nabothi na damu ya watoto wake asema BWANA na nitahakikisha unalipia hili shamba asema BWANA. Sasa basi, mchukue na mtupe kwenye hili shamba, sawa sawa na neno la BWANA.”

27Wakati Ahazi yule mfalme wa Yuda alipoliona hili, akakimbia kwa njia ya Bethi Hagani. Lakini Yehu akamfuata, na kusema, “Muulie humo kwenye gari la farasi,” na wakampiga mahali pa kupandia Guri, karibu na Ebleamu. Ahazi akakimbilia Megido na kufia pale.28Watumishi wake wakaubeba mwili wake kwa magari ya farasi kwenda Yerusalemu na kumzika kwenye kaburi lake pamoja na baba zake katika mji wa Daudi.29Basi ilikuwa mwaka wa kumi na moja wa Yoramu mwana wa Ahabu huyo Ahazia akaanza kutawala juu ya Yuda.

30Wakati Yehu alipokuja kwa Yezebeli, Yezebeli akasikia juu ya hilo, akapaka wanja kwenye macho yake, akatengeneza nywele zake vizuri, na kuchungulia kwenye dirisha.31Kadiri Yehu alipokuwa akiingia kwenye lango, akamwambia, “Je unakuja kwa amani, wewe Zimri, muuaji wa bwana wako?”

32Yehu akatazama juu ya dirisha na kusema, “Ni nani yuko upande wangu? Nani?” Matowashi wawili au watatu wakachungulia nje.33Basi Yehu akasema, “Mtupeni chini.” Hivyo wakamtupa Yezebeli chini, na damu yake ikamwagika kwenye ukuta na farasi, na Yehu akamkanyaga kanyaga chini ya miguu.34Basi Yehu akaingia hiyo sehemu, akala na kunywa. Kisha akasema, “Mtazameni sasa huyu mwanamke aliyelaaniwa na kumzika, kwa kuwa ni binti wa mfalme.”35Wakaenda kumzika, lakini hawakumkuta ila fuvu, miguu, na viganja vya mikono yake.36Basi wakarudi na kumwambia Yehu. Akasema, “Hili ndilo neno la BWANA ambalo ameliongea kupitia Eliya Mtishbi, likisema, ‘Katika nchi Yezreeli mbwa ataula mwili wa Yezebeli,37na mwili wa Yezebeli utakuwa kama kinyesi juu ya uso wa mashamba katika nchi ya Yezreeli, kwa hiyo basi hakuna atakayeweza kusema, ‘Huyu ni Yezebeli.’”

10

1Basi Ahabu alikuwa na watoto sabini katika Samaria. Yehu akaandika barua na kuzituma kwenda Samaria, kwa watawala wa Yezreeli, pamoja na wazee na walinzi wa wana wa Ahabu akisema,2Hivyo basi, haraka iwezekanavyo barua hii ikufikiapo “Wana wa bwana wako pamoja nawe, kwa kuwa mna magari na farasi na mji wenye boma na silaha.3Mchagueni aliye bora na anayestahili miongoni mwa mtoto wa bwana wenu na kumuweka kwenye kiti cha kifalme cha baba yake, na kupigania ufalme wa bwana wenu.”

4Lakini waliogopa na kusema miongoni mwao, “Tazama, wafalme wawili hawatasimama mbele ya Yehu. Hivyo tutasimamaje?”

5Kisha yule mtu ambaye alikuwa kiongozi kwenye nyumba ya mfalme, na wale waliowalea watoto, wakatuma ujumbe kwa Yehu, kusema, “Sisi ni watumishi wako. Tutafanya chochote utakacho tuamuru. Hatutamfanya mtu yeyote kuwa mfalme. Fanya lile lililo jema machoni pako.”

6Kisha Yehu akaandika barua mara ya pili, akisema, “Kama mko upande wangu, na kama mtasikiliza sauti yangu, mtachukua vichwa vya watu wa wana wa mabwana wenu, na mje kwangu Yezreeli kesho muda kama huu.” Ndipo wana wa wafalme, sabini kwa hesabu, waliokuwa watu muhimu huko mjini, ambao walikuwa waliowalea.7Hivyo barua ilipokuja kwao, waliwachukua wana wa wafalme na kisha kuwaua, watu sabini, wakaweka vichwa vyao kwenye vikapu, na kuvituma kwa Yehu katika Yezreeli.8Mjumbe mmoja akaja kwa Yehu, akisema, “Wamevileta vile vichwa vya watoto wa wafalme.” Hivyo akasema, viwekeni kwenye mafungu mawili kwenye lango hadi asubuhi.”

9Asubuhi Yehu akatoka nje na kusimama, na kusema kwa watu wote, “Ninyi hamna hatia. Tazameni, nimefanya fitina dhidi ya bwana wangu na kumuua, lakini ni nani aliyewaua hawa wote?10Sasa hakika tafakarini kwamba hakuna sehemu ya neno la BWANA, lile alilonena BWANA kuhusu familia ya Ahabu, itaanguka kwenye udongo, kwa kuwa BWANA amefanya kile alichokisema kupitia mtumishi wake Eliya.”11Basi Yehu akawaua wote waliokuwa wamebakia wa familia ya Ahabu katika Yezreeli, na watu wake muhimu wote, marafiki zake wa karibu, na makuhani wake, hakuna hata mmoja wao alisalia.

12Kisha Yehu akainuka na kuondoka; akaenda Samaria. Kadri alivyokuwa akikaribia Bethi Ekedi ya wachungaji,13akamlaki na ndugu wa Ahazia mfalme wa Yuda. Yehu akawaambia, “Ninyi ni akina nani?” Wakajibu, “Sisi ni ndugu zake na Ahazia, na tunashuka chini kuwasalimia watoto wa mfalme na watoto wa Malkia Yezebeli.”

14Yehu akawaambia watu wake mwenyewe, “Wachukue wakiwa hai.” Hivyo wakawachukua wakiwa hai na kuwaua kwenye kisima cha Bethi Ekedi, watu wote arobaini na mbili. Hakumwacha hata mmoja wao akiwa hai.

15Baada ya Yehu kuondoka huko, akakutana na Yehonadabu mwana wa Rekabu anakuja kukutana naye. Yehu akamsalimia na kisha akamwambia, “Je moyo wako uko na mimi, kama moyo wangu ulivyo pamoja na wako?” Yehonadabu akajibu, Ndio.” Yehu akasema, “kama ni ndio, nipatie mkono wako.” Kisha Yehonadabu akampatia mkono wake, na Yehu akampandisha Yehonadabu juu kwenye magari ya farasi pamoja naye.16Yehu akasema, “Fuatana pamoja nami na uone wivu wangu kwa BWANA.” Hivyo alikuwa na Yehonadabu akiendesha gari la farasi.

17Wakati alipokuja Samaria, Yehu akawaua wote waliobakia kutoka uzao wa Ahabu katika Samaria, hata akawaangamiza ukoo wa kifalme wa Ahabu, kama walivyokuwa wameambiwa kabla ya neno la Yahwe, ambalo aliloambiwa Eliya.

18Kisha Yehu akawakusanya watu wote akawaambia, “Ahabu alimtumikia Baali kidogo, lakini Yehu atamtumikia sana.19Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote. Asikosekane mtu hata mmoja, kwa kuwa nina dhabihu kubwa nataka kutoa kwa Baali. Yeyote atakayeshindwa kuja hataishi.” Lakini Yehu alifanya haya kwa udanganyifu, kwa dhamira ya kuwaua wanaomwabudu Baali.

20Yehu akasema, “Tengeni muda tuwe na mkutano kwa ajili ya Baali.” Hivyo wakalitangaza.21Kisha Yehu akatuma Israeli yote na wamwabuduo Baali waje, hivyo basi hakuna mtu hata mmoja ambaye aliacha kuja. Walikuja kwenye hekalu la Baali, na ilijaa kutoka mwanzo hadi mwisho.22Yehu akamwambia yule mtu aliyekuwa anatunza kabati la nguo za makuhani, “Uwatolee mavazi wote wamwabuduo Baali.” Basi yule mtu akawatolea nguo.

23Basi Yehu akaingia pamoja na Yohonadabu mwana wa Rekabu kwenye nyumba ya Baali, na kisha akawaambia wanaomwabudu Baali, “Tafuteni na muhahakishe kwamba hakuna mtu hapa pamoja na ninyi walio watumishi wa BWANA, lakini wamwabuduo Baali peke yao.”24Kisha wakaenda kutoa dhabihu na sadaka ya kuteketeza. Basi Yehu alichagua watu themanini ambao walikuwa wamesimama nje, na aliwaambia, Kama mtu yeyote miongoni mwa hawa watu ambao nimewaleta kwenye mikono yenu atoroke, yeyote atakayemwacha huyo mtu atoroke, maisha yake yatachukuliwa kwa ajili ya yule aliyeokoka.”

25Hivyo kisha baada ya muda mfupi Yehu alipomaliza kutoa sadaka ya kutekezwa, akamwambia mlinzi na majemedari, “Ingieni na muwaue. Msimwache mtu yeyote atoke.” Basi waliwaua kwa makali ya upanga, na mlinzi na majemedari wakawatupa nje na kwenda kwenye chumba cha ndani cha nyumba ya Baali.26Wakazitoa nguzo za mawe ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Baali, na kisha kuzichoma.27Kisha wakazivunja zile nguzo za Baali, na kuiharibu nyumba ya Baali na kuifanya choo, ambacho kipo hadi leo.

28Hivi ndivyo ambavyo Yehu alivyomharibu muabudu Baali kutoka Israeli.29Lakini Yehu hakuacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo ilifanya Israeli kutenda dhambi ambayo ni kumwabudu ndama wa dhahabu katika Betheli na Dani.

30Hivyo BWANA akamwambia Yehu, “Kwa kuwa umefanya vema kwa kufanya yaliyo sahihi kwenye macho yangu, na kuitendea nyumba ya Ahabu kulingana na yote yaliyokuwa kwenye moyo wangu, uzao wako utakaa kwenye kiti cha Israeli hadi kizazi cha nne.”31Lakini Yehu hakujali kutembea kwenye sheria ya BWANA, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote. Hakugeuka kutoka kwenye dhambi za Yeroboamu, ambayo iliwafanya Israeli kutende dhambi.

32Siku zile BWANA akaanza kupunguza mikoa ya Israeli, na Hazaeli kuwashinda Waisraeli mipakani mwa Israeli,33kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri, alipo karibu na bonde la Arnoni, kupita Geleadi hadi Bashani.

34Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Yehu, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?

35Yehu akalala na wazee wake, na walimzika katika Samaria. Kisha Yehoahazi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.36Muda ambao Yehu alitawala juu ya Israeli katika Samaria ulikuwa miaka ishirini na nane.

11

1Basi Athalia, mama yake na Ahazia, alipoona kwamba mtoto wake amekufa, aliinuka na kuwaua watoto wote wa kifalme.2Lakini Yehosheba, binti wa mfalme Yehoramu na dada wa Ahazia, akamchukua Yoashi mwana wa Ahazia, na kumficha mbali mwa miongoni mwa watoto wa mfalme waliokuwa wameuawa, wakati wote pamoja na mlezi wake; akawaweka kwenye chumba cha kulala. Wakamficha kutoka Athalia kwa hiyo hakuuawa.3Alikuwa amoja na Yehosheba, wamejificha kwenye nyumba ya BWANA, kwa muda wa miaka sita, wakati Athalia alipotawala juu ya nchi.

4Katika mwaka wa saba, Yehoyada alituma ujumbe na kuleta makamanda wamaamiri jeshi mamia wa Wakari na wa walinzi, na kuwaleta kwake mwenyewe, ndani ya nyumba ya BWANA. Akafanya agano pamoja nao, na kuwaapisha kiapo katika nyumba ya BWANA. Kisha akawaonyesha mtoto wa mfalme.5Akawaamuru, akisema, “Hivi ndivyo mnavyotakiwa kufanya. Theluthi yenu mtakaokuja kwenye Sabato mtakuwa mkiiangalia nyumba ya mfalme,6na theluthi mtakuwa langoni mwa Suri, na theluthi langoni nyuma ya walinzi.”7Makundi mengine mawili ambayo hayatumikii Sabato, Mtayalinda juu ya nyumba ya BWANA kwa ajili ya mfalme.8Ni lazima mumzunguke mfalme, kila mmoja na silaha zake kwenye mkono wake. Yeyote aingiaye ndani ya safu, auwawe. Lazima mkae pamoja na mfalme kila atokapo na kila aingiapo.

9Hivyo mamia ya makamanda wamaamri jeshi wakatii kila kitu Yehoyada kuhani alichokiamuru. Kila mmoja akachukua watu wake, wale ambao walitakiwa kuja kutumika siku ya hiyo Sabato, na wale ambao wataacha kuitumika kwenye hiyo Sabato; ndipo wakaja kwa Yehoyada kuhani.10Kisha Yehoyada yule kuhani akawapa mikuki na ngao mamia wa makamanda wamaamri jeshi ambayo ilikuwa mali ya mfalme Daudi ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya BWANA.11Basi walinzi wakasimama, kila mtu na silaha kwenye mkono wake, kutoka upande wa kuume wa hekalu, kwenda upande wa kushoto, karibu na madhabahu ya hekelu, wakimzunguka mfalme.

12Kisha Yehoyada akamleta nje mtoto wa mfalme Yoashi, na kumvalisha taji la kifalme, na kumpa ushuhuda. Kisha wakamfanya mfalme na kummiminia mafuta. Wakapiga makofi wakisema, “Mfalme na aishi!”

13Wakati Athalia aliposikia sauti za walinzi na za watu, alikuja kwa wale watu kwenye nyumba ya BWANA14Akatazama, na, kisha, yule mfalme alikuwa amesimama kwenye nguzo, kama ilivyokuwa desturi, na wakuu na wapiga baragumu walikuwa karibu na mfalme. Watu wote wa nchi hiyo walikuwa wakifurahi na kupiga matarumbeta. Kisha Athalia akachana mavazi yake kwa hasira na kupiga kelele, “Uhaini! Uhaini!”15Ndipo Yehoyada yule kuhani akawaagiza makamanda wa jeshi wa mamia ambao waliokuwa juu ya jeshi, akisema, “Mtoeni kwenye safu.” Atakayemfuata, muueni kwa upanga.” Kwa kuwa kuhani alisema, “Msimwache auawe kwenye nyumba ya BWANA.”16Hivyo wakamtwaa kadiri walivyokuwa wakiikaribia hiyo sehemu iliyokuwa na farasi wakaingia chini, na akauawa huko.

17Kisha Yehoyada akafanya agano kati ya BWANA na mfalme na watu, ambao wangekuwa watu wa BWANA, na pia kati ya mfalme na watu.18Basi watu wote wa nchi wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. Wakaangusha madhabahu ya Baali na sanamu zake wakazivunja vipande vipande, na kumuua Matani, mfalme wa Baali, mbele ya haya madhabahu. Kisha Yehoyada kuhani akawachagua walinzi juu ya hekalu la BWANA.19Yehoyada akawachukua makamanda wa jeshi wa mamia, Wakari, walinzi, na watu wote wa nchi, na kwa pamoja wakamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya BWANA na wakaenda kwenye nyumba ya mfalme, wakaingia kwa njia ya lango la walinzi. Yoashi akachukua nafasi yake kwenye kiti cha enzi cha mfalme.20Hivyo watu wote wa nchi wakamsifu, na nchi ilikuwa kimya baada ya Athalia kuuawa kwa upanga kwenye nyumba ya mfalme.

21Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba tangu alipoanza kutawala.

12

1Katika mwaka wa saba wa Yehu, utawala wa Yoashi ulianza; alitawala kwa muda wa miaka arobaini huko Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Sibia, wa Beersheba.2Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote, kwa sababu Yehoyada kuhani alimfundisha.3Lakini sehemu ya juu haikuchukuliwa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kuchoma ubani kwenye sehemu za juu.

4Yoashi akamwambia kuhani, “Pesa zote zilizokuja kama sadaka takatifu kwenye nyumba ya BWANA, pesa za matumizi, pesa ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na pesa yote aonayo moyoni mwake kuileta kwenye nyumba ya BWANA5makuhani watapokea pesa kutoka miongoni mwa mmoja wa watunza pesa na kutengeneza kila sehemu itakayoonekana imeharibika kwenye hekalu.”

6Lakini kama mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani hawakuwa wameandaa kitu chochote kwenye hekalu.7Mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani na kuhani mwingine; akawaambia, “Kwa nini hamjaandaa kitu chochote kwenye hekalu? Sasa msichukue tena pesa kutoka kwa walipa kodi wenu, lakini chukueni kile kilichokuwa kikikusanywa kwa ajili ya matengenezo ya hekalu na uwapatie wale wanaoweza kufanya matengenezo.8Hivyo makuhani wakakubaliana wasichukue pesa tena kutoka kwa watu na wasitengeneze wenyewe.

9Badala yake, Yehoyada yule kuhani akachukua kasha, akatoboa tundu kwenye kifuniko chake, na kuliweka karibu na madhabahu, upande wa kulia kama mtu anaingia kwenye madhabahu ya BWANA. Makuhani ambao walikuwa wakilinda mlango wa hekalu wakatumbukiza pesa zote ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya BWANA10Ikawa walipoona kwamba kulikuwa na pesa za kutosha kwenye kasha, mwandishi wa mfalme na kuhani mkuu wakaja na kuweka pesa kwenye mifuko na kisha kuhesabu, pesa ikaonekana kwenye nyumba ya BWANA.11Wakawapa pesa ambayo ilikuwa imepimwa kwenye mikono ya watu ambao waliokuwa wanatunza nyumba ya BWANA. Wakawalipa mafundi seremala na wajenzi ambao walikuwa wemefanya kazi kwenye nyumba ya BWANA,12na waashi na wakata mawe, kwa ajili ya kununua mbao na kukata mawe kwa ajili ya kutengenezea nyumba ya BWANA, na yote iliyokuwa inahitajika kulipwa kwa ajili ya kuitengeneza.13Lakini ile pesa iliyokuwa imeletwa kwenye nyumba ya BWANA haikulipwa kwa ajili ya vikombe vya fedha, mabeseni, au dhahabu au fedha yoyote ya vyombo.

14Waliwapa hizi fedha wale ambao waliokuwa wamefanya kazi ya kutengeneza nyumba ya BWANA.15Pia, hakukuhitajika zile pesa zilipwe kwa ajili ya matengenezo ili kuwajibika kwa kuwa watu walizipokea nakuzilipa kwa watenda kazi, kwa sababu hawa watu walikuwa waadilifu.16Lakini pesa kwa ajili ya matoleo ya hatia na pesa kwa ajili ya matoleo ya dhambi hazikuwa zimeletwa kwenye hekalu la BWANA, kwa sababu zilikuwa mali ya makuhani.

17Kisha Hazaeli mfalme wa Shamu akashambulia na kupigana dhidi ya Gathi, na kuichukua.18Ndipo Hazaeli akageuka kuishambulia Yerusalemu. Yoashi mfalme wa Yuda akavichukua vitu vyote ambavyo Yehoshefati na Yehoramu na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, na kuviweka wakfu, na vile alivyokuwa ameviweka wakfu, na dhahabu zote zilizokuwa zimeonekana kwenye ghala la nyumba ya BWANA na la mfalme akawatuma kwenda kwa Ahazi mfalme wa Shamu. Kisha Hazaeli akaenda zake kutoka Yerusamu.

19Kama mambo mengine yanayomuhusu Yoashi, yote aliyoyafanya, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?20Watumishi wake wakainuka na kupanga pamoja; wakamteka Yoashi katika Bethi Milo, kwenye njia ya kushukia kwa Sila.21Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakamshambulia na akafa. Wakamzika Yoashi pamoja na mababu zake katika mji wa Daudi, na Amazia, mtoto wake, akawa mfalme kwenye sehemu yake.

13

1Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Yoashi mwana wa Ahazia mfalme wa Yuda, Yehoazi mwana wa Yehu alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na saba.2Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe na kufuata dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambaye alisababisha Israeli kuasi; na Yehoazi hakurudi kutoka kwao.3Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, na akaendelea kuwakabidhi kwenye mikono ya Hazaeli mfalme wa Shamu na kwenye mikono ya Ben Hadadi mwana wa Hazaeli.

4Hivyo Yehoazi akamsihi Yahwe, na Yahwe akamsikiliza kwa sababu aliona mateso ya Israeli, vile mfalme wa Shamu alivyokuwa akiwatesa.5Basi BWANA akawapa Israeli ulinzi, na wakakimbia kutoka kwenye mikono ya Washami, na watu wa Israeli wakaanza kuishi kwenye nyumba zao kama walivyokuwa kabla.6Hata hivyo, hawakuziacha dhambi za nyumba ya Yeroboamu, ambaye alisababisha Israeli kuasi, na wakaendelea katika hayo; na huyo Ashera akabaki hivyo katika Samaria.

7Washami wakamuacha Yehoazi pamoja na waendesha farasi hamsini tu, magari ya farasi kumi, na watembea kwa miguu 10,000, kwa ajili ya mfalme wa Shamu alikuwa ameiharibu na kuwafanya kama makapi yaliyopurwa.

8Kama mambo mengine yanayomuhusu Yehoazi, na yote aliyoyafanya na nguvu zake, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?9Basi Yehoyazi akalala na mababu zake, na wakamzika katika samaria. Yohoashi mwanaye akawa mfalme katika sehemu yake.

10Katika mwaka wa thelathini na saba wa Yoashi mfalme wa Yuda, utawala wa Yehoashi mwana wa Yehoazi ulianza juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka kumi na sita.11Akafanya yaliyo maovu kwenye uso wa Yahwe. Hakuacha nyuma dhambi zozote za Yeroboamu mwana wa Nebati, kwa kuwa aliwafanya Israeli kuasi, lakini alitembea pamoja nao.

12Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoashi, na yote aliyoyafanya, na shujaa wake ambaye aliyepigana dhidi ya Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?13Yehoashi akalala na mababu zake, na Yeroboamu akakalia kiti chake cha enzi cha kifalme. Yehoashi akazikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli.

14Basi Elisha akaugua ugonjwa ambao hatimaye ulimuua, hivyo Yehoashi yule mfalme wa Israeli akashuka chini kwake na kumlilia juu yake. Akasema, “Baba yangu, baba yangu, haya magari ya farasi ya Israeli na hawa waendesha farasi wanakuchukua!”

15Elisha akamwambia, “Chukua upinde na mishale,” basi Yoashi akachukua upinde na mishale.16Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, “Weka mkono wako kwenye upinde,” basi akaweka mkono wake kwenye huo. Kisha Elisha akalaza mikono yake kwenye mikono ya mfalme.

17Elisha akasema, “Fungua dirisha upande wa mashariki,” basi akalifungua. Kisha Elisha akasema, “Funga,” na akafunga. Elisha akasema, “Huu ndiyo mshale wa ushindi wa Yahwe, huu mshale wa ushindi juu ya Shamu, kwa kuwa utawapiga Washami katika Afeki hadi utakapowaangamiza.”

18Kisha Elisha akasema, “Chukua mishale,” basi Yoashi akaichukua. Akamwambia mfalme wa Israeli, “Piga chini pamoja nao,” na akapiga chini mara tatu, kisha akaacha.19Lakini mtu wa Mungu alikuwa na hasira naye na akasema, “Ungelipiga chini mara tano au mara sita. Ndipo ungeipiga Shamu hadi kuiangamiza, lakini sasa utaipiga Shamu mara tatu tu.”

20Kisha Elisha akafa, na wakamzika. Sasa vikundi vya Wamoabi wakaingia kwenye nchi mwanzoni mwa mwaka.21Ikawa walipokuwa wakimzika huyo mtu, wakaona kundi la Wamoabi, hivyo wakautupia ule mwili kwenye kaburi la Elisha. Mara yule mtu alipoigusa mifupa ya Elisha, alifufuka na kusimama kwa miguu yake.

22Hazaeli mfalme wa Shamu akawatesa Israeli siku zote za Yehoazi.23Lakini Yahwe aliwahurumia Israeli, na alikuwa na huruma juu yao na kushughulika kwa ajili yao, kwa sababu ya agano lake na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo. Hivyo Yahwe hakuwaangamiza, na bado hakuwatupa kutoka kwenye uwepo wake.

24Hazaeli mfalme wa Shamu akafa, na Ben Hadadi mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.25Yehoashi mwana wa Yehoazi akairudisha kutoka kwa Ben Hadadi mwana wa Hazaeli miji ambayo aliichukua kutoka Yehoazi baba yake kwa vita. Yehoashi akamshambulia mara tatu, na akaipata miji ya Israeli.

14

1Katika mwaka wa pili wa Yehoashi mwana wa Yehoazi, mfalme wa Israeli, Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, alianza kutawala.2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu.3Mama yake alikuwa anaitwa Yehoyadani, wa Yerusalemu. Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa macho ya BWANA, sio kama baba yake Daudi. Alifanya kila kitu ambacho Yoashi, baba yake, alichokuwa amekifanya.4Lakini sehemu ya juu haikuondolewa. Watu wakaendelea kutoa dhabihu na kufukiza ubani katika sehemu mahala pa juu.

5Ikawa mara utawala wake ulipokuwa imara, aliwaua watumishi ambao waliokuwa wamemuua baba yake, mfalme.6Ila hakuwaweka watoto wa wale wauaji kwenye kifo; isipokuwa, alifanya kutokana na kile kilichokuwa kimeandikwa kwenye sheria, kwenye kitabu cha Musa, kama BWANA alivyokuwa ameamuru, akisema, “Wababa wasife kwa ajili ya watoto wao, wala watoto wasife kwa ajili ya makosa ya wazazi wao. Isipokuwa, kila mtu atakufa kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”

7Aliua maaskari 10,000 wa Edomi kwenye bonde la chumvi; pia alimchukua Sela kwenye vita na kuiita Yoktheeli, ndivyo paitwavyo hadi leo.

8Kisha Amazia akatuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu mfalme wa Israeli, akisema, “Njoo, tuonane kila mmoja macho kwa macho kwenye mashinadano.”

9Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akawatuma wajumbe kurudi kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, “Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma kwa mwerezi katika Lebanoni, kusema, ‘Mpatie mwanangu binti yako amuoe; lakini hayawani aliyekuwako Lebanoni akaukanyaga chini ule mbaruti.10Umempiga sana Edomu, na moyo wako umekuinua. Jisifu katika ushindi wako, lakini kaa nyumbani, kwa nini unataka kujisababishia matatizo na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?”

11Lakini Amazia hakutaka kusikia. Hivyo Yehoashi mfalme wa Israeli akakwea yeye na Amazia mfalme wa Yuda wakakutana uso kwa uso huko Beth Shemeshi, ambayo ilikuwa ya Yuda.12Yuda walishindwa mbele ya Israeli, na kila mtu akakimbia nyumbani.13Yehoashi mfalme wa Israeli, akamchukua Amazia, mfalme wa Yuda mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, huko Beth Shemeshi. Akaja Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kutoka lango la Efraimu mpaka kwenye pembe ya lango, urefu wa mbali wa dhiraa mia nne.14Akachukua dhahabu na fedha zote, na vitu vyote ambavyo vilipatikana katika nyumba ya BWANA, na vitu vya thamani kwenye nyumba ya mfalme, pamoja na mateka pia, na kurudi samaria.

15Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yehoashi, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, na jinsi alivyopigana na Amazia mfalme wa Yuda, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Israeli?16Kisha Yehoashi akalala na wazee wake na ailizikwa katika Samaria pamoja na wafalme wa Israeli, na Yeroboamu, mwanaye, akawa mfalme katika eneo lake.

17Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, akaishi miaka kumi na tano baada ya Yehoashi mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.18Kama ilivyo kwa mambo mengine yanayomhusu Amazia, je hayakuandikwa kwenye kitabu cha matukio ya mfalme wa Yuda?

19Wakafanya njama dhidi ya Amazia katika Yerusalimu, akakimbilia Lakishi. Akakimbia hadi Lakishi, lakini wakawatuma watu kumfuata hadi Lakishi na kumuua huko.20Wakamrudisha kwa farasi, na alizikwa pamoja na wazee wake katika mji wa Saudi.

21Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na minne, na walimfanya kuwa mfalme katika nyumba ya kifalme wa baba yake Uzaria.22Alikuwa Uzia ambaye alijenga Elathi na kuirudisha kwa Yuda, baada ya mfalme Uzaria akalala pamoja na mababu zake.

23Katika mwaka wa kumi na tano wa Amazia mwana wa Yoashi mfalme wa Yuda, Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli alianza kutawala katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka arobaini na moja.24Akafanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA. Hakuziacha dhambi zake za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye aliisababisha Israeli kuasi.25Akairudisha mipaka ya Israeli kutoka Lebo Hamathi mpaka kwenye Bahari ya Araba, kufuata amri ya neno la BWANA, Mungu wa Israeli, ambalo aliongea kupitia mtumishi wake Yona mwana wa Amitai, yule nabii, ambaye alitokea Gathi Heferi.

26Kwa kuwa BWANA aliyaona mateso ya Israeli, ambayo yalikuwa makali kwa kila mmoja, wote mtumwa na asiyemtumwa, na kwamba hapakuwa na ulinzi kwa ajili ya Israeli.27Basi BWANA akasema kwamba hataweza kulifuta jina la Israeli chini ya mbingu; badala yake, aliwaokoa kwa mkono wa Yeroboamu mwana wa Yehoashi.

28Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Yeroboamu, yote aliyoyafanya, ushujaa wake, jinsi alivyo pigana vita na kuipata tena Dameski na Hamathi, ambayo ilikuwa ya Yuda, kwa Israeli, je hayakuandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?29Yeroboamu akalala na mababu zake, pamoja na mfalme wa Israeli, na Zekaria mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

15

1Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli, Azaria mwana wa Amazia mfalme wa Yuda akaanza kutawala.2Azaria alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka hamsini na mbili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yekolia, na alikuwa anatokea Yerusalemu.3Alifanya yaliyo mema machoni pa BWANA, kama baba yake Amazia alivyofanya.4Lakini, mahali pa juu hapakuwa pameondolewa. Watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza ubani katika mahala pa juu.

5BWANA akampiga mfalme hivyo basi akawa na ukoma mpaka siku ya kifo chake na alikaa kwenye nyumba ya pekee. Yothamu, mtoto wa mfalme, alikuwa juu ya watu na kuwaongoza watu wa nchi.

6Kama kwa mambo mengine yanayomhusu Azaria, yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?7Hivyo Azaria alilala pamoja na babu zake katika mji wa Daudi. Yothamu, mtoto wake, akawa mfalme katika mahala pake.

8Katika mwaka wa thelathini na nane mwaka wa Azaria mfalme wa Yuda, Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita.9Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA, kama baba zake waliyoyafanya. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kuasi

10Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya njama dhidi ya Zekaria, akamshambulia katika Ibleamu, na kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahala pake.11Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Zekaria, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.12Hili ndilo lililokuwa neno la BWANA ambalo aliongea na Yehu, kusema, “Kizazi chako kitakaa katika kiti cha Israeli mpaka kizazi cha nne.” Hiyo ikatokea.

13Shalumu mwana wa Yabeshi akaanza kutawala katika mwaka wa thelathini na tisa wa Azaria mfalme wa Yuda, na kutawala kwa mwezi mmoja tu katika Samaria.14Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza kwenda Samaria. Akamshambulia Shalumu mwana wa Yabeshi hapo, katika Samria. Akamuua na kuwa mfalme katika mahali pake.

15Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Shalumu na njama aliyoifanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Israeli.

16Ndipo Menahemu akamshambulia Tifsa na wote waliokuwa pale, na mipaka yote kuzunguka Tizra, kwa sababu hawakufungua kwenye mji. Hivyo akaushambulia, na akawapasua wanawake wajawazito wote katika hicho kijiji.

17Katika mwaka wa thelathini na tisa wa Ahazia mfalme wa Yuda, Menahemu mwana wa Gadi akaanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi katika Samaria.18Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA. Katika maisha yake yote, hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti, ambaye alifanya Israeli kufanya dhambi.

19Kisha Pulu mfalme wa Ashuru akaja kinyume cha nchi, na Menahemu akampatia Pulu talanta 1,000 za fedha, hivyo msaada wa Pulu ungeweza kuwa na yeye kuimarisha utawala wa Israeli katika nchi yake.20Menahemu akatoza hii pesa kutoka Israeli kwa kumtaka kila mtu tajiri alipe shekeli hamsini za fedha kwake kumpatia mfalme wa Ashuru. Hivyo mfalme wa Ashuru akarudi na hakukaa pale katika ile nchi.

21Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Menahemu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli?22Hivyo Menahemu akalala pamoja na babu zake, na Pekahia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.

23Katika mwaka wa hamsini wa Azaria mfalme wa Yuda, Pekahia mwana wa Menahemu akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala kwa muda wa miaka miwili.24Alifanya yaliyo maovu usoni pa BWANA. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambazo kwa hizo alisababisha Israeli kufanya dhambi.25Pekahia alikuwa na afisa aliyekuwa anaitwa Peka mwana wa Remalia, ambaye alifanya njama dhidi yake. Pamoja na watu hamsini wa Gileadi, Peka akamuua Pekahia pamoja na Argobu na Arie katika Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme. Peka akamuua, alipomuua Pekahia akawa mfalme katika mahala pake.

26Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Pekahia, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.

27Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Azia mfalme wa Yuda, Peka mwana wa Remalia akaanza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; alitawala miaka Ishirini.28Alifanya yaliyo maovu usoni mwa Yahwe. Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabati, ambaye alisababisha Israeli kufanya dhambi.

29Katika siku za Peka mfalme wa Israeli, Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru akaja na kuichukua Iyoni, Abel Beth Maaka, Yanoa, Kadeshi, Hazori, Gileadi, na nchi yote ya Naftali. Akawachukua hao watu hadi Ashuru.

30Hivyo Hoshea mwana wa Ela akafanya njama dhidi ya Peka mwana wa Remalia. Akaishambulia na kisha kumuua. Kisha akawa mfalme katika mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia.

31Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Peka, yote aliyoyafanya, yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Israeli.

32Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, Yothamu mwana wa Azaria, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.33Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalimu. Mama yake alikuwa anaitwa Yerusha; alikuwa binti ya Sadoki.34Yothamu alifanya yaliyo sahihi usoni pa Yahwe. Alifuata mfano wa yote baba yake Azaria aliyofanya.35Ila, mahali pa juu hapakuchukuliwa. Watu walikuwa wakitoa sadaka na kufukiza ubani katika mahali pa juu. Yothamu akajenga lango la juu la nyumba ya Yahwe.

36Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yothamu, na yote aliyoyafanya, je yameandikwa katika kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?37Katika zamani hizo BWANA akaanza kumtuma dhidi ya Yuda Rezini mfalme wa Sahmu, na Peka mwana wa Remalia.38Yothamu akalala pamoja na babu zake na akazikwa pamoja na babu zake katika mji wa Daudi, babu yake. Kisha Ahazi, mtoto wake, akawa mfalme katika mahali pake.

16

1Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Remalia, Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda, akaanza kutawala.2Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala, na alitawala kwa muda wa miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Alifanya yasiyo haki usoni mwa BWANA Mungu wake, kama Daudi baba yake.3Badala yake, akatembea katika njia ya wafalme wa Israeli; hasa, akamuweka mwanaye kwenye moto kama sadaka ya kuteketeza, kufuatana na machukizo ya mataifa, ambayo BWANA aliwafukuza wana wa Israeli.4Akatoa sadaka na kuchoma ubani mahali pa juu, juu ya milima, na chini ya kila mti mbichi.

5Kisha Riseni, mfalme wa Shamu na Peka mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakaja mpaka Yerusalemu kuteka. Wakamzunguka Ahazi, lakini hawakuweza kumshinda.6Katika kipindi hicho, Resini mfalme wa Shamu akawarudishia Elathi kwa Shamu na kuwapeleka watu wa Yuda nje ya Elathi. Kisha Washami wakaja kwa Elathi ambapo waliishi hadi leo.

7Hivyo Ahazi akatuma wajumbe kwenda kwa Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru, akisema, “Mimi ni mtumishi wako na mwanao. Panda juu na uniokoe kutoka kwenye mikononi ya mfalme wa Shamu na kutoka kwenye mkono wa mfalme wa Israeli, ambao wameniteka.”8Hivyo Ahazi akachukua fedha na dhahabu iliyokuwa imepatikana katika nyumba ya BWANA na mingoni mwa waweka hazina wa nyumba ya mfalme na kuituma kama zawadi kwa mfalme wa Ashuru.9Kisha mfalme wa Ashuru akamsikiliza, na mfalme wa Ashuru akaenda juu dhidi ya Dameski, akaishinda na kuwabeba watu wake kama wafungwa hadi Kiri. Akamuua Resini pia yule mfalme wa Shamu.

10Mfalme Ahazi akaenda Dameski kuonana na Tiglath Pileseri mfalme wa Ashuru. Akaiona madhabahu huko Dameski. Akampelekea Uria kuhani mfano wa ile madhabahu na mpangilio wake na mchoro kwa ustadi wote ulikuwa umehitajika.11Hivyo Uria yule kuhani akajenga madhabahu kuwa kama mipango ambayo Mfalme Ahazi atakaporudi kutoka Dameski. Akaimaliza kabla mfalme Ahazi hajarudi kutoka Dameski.12Kisha mfalme akaja kutoka Dameski akaiona ile madhabahu; mfalme akaikaribia ile madhabahu na kutoa sadaka juu yake.13Akatengeneza sadaka yake ya kuteketezwa na sadaka yake ya nafaka, na kunyunyiza damu ya washirika wake sadaka juu ya madhabahu.14Madhabahu ya shaba ambayo ilikuwa mbele ya Yahwe akaileta kutoka mbele ya hekalu, kutoka kati ya madhabahu yake na hekalu la Yahwe na kuiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake.

15Kisha mfalme Ahazi akamwamuru Uria kuhani, akisema, “Juu ya madhabahu kubwa teketeza sadaka ya kutekezwa ya asubuhi na sadaka ya kuteketezwa ya nafaka ya jioni, pamoja na sadaka ya watu wote wa nchi, na matoleo ya sadaka ya mazao na sadaka zao za kinywaji. Nyunyiza juu ya hiyo damu yote ya sadaka ya kuteketeza, na damu yote ya kuteketeza. Lakini ile madhabahu ya shaba itakuwa kwa ajili yangu ili niulize ushauri.”16Uria kuhani akafanya kile ambacho Ahazi aliamuru.

17Kisha mfalme Ahazi akaondoa jopo na mabeseni vitako vinavyobebeka; pia akachukua bahari kutoka juu ya ng'ombe wa shaba ambayo ilikuwa chini ya hiyo na kuiweka juu ya sakafu ya mawe.18Aliondoa njia iliyokuwa kwa ajili ya kuingia kwenye Sabato ambayo walikuwa wamejenga kwenye hekalu, wote pamoja na mahali pa kuingilia mfalme kwenye hekalu la BWANA, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru.

19Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Ahazi na yale aliyoyafanya, je yameandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?20Ahazi alilala pamoja na baba zake na kuzikwa pamoja na baba zake katika mji wa Daudi. Hezekia mtoto wake akawa mfalme katika mahala pake.

17

1Katika mwaka wa kumi na moja wa Ahazi mfalme Yuda, utawala wa Hoshea mwana wa Ela ulianza. Alitawala katika Samaria juu ya Israeli kwa muda wa miaka minane.2Alifanya yaliyo maovu usoni pa BWANA, ila sio kama wafalme wa Israeli ambao ulikuwa kabla yake.

3Shalmanesa mfalme wa Ashuru akamshambulia, na Hoshea akawa mtumishi na kumletea kodi.4Kisha mfalme wa Ashuru akaona kwamba Hoshea alikuwa na njama dhidi yake, kwa kuwa Hoshea aliwatuma wajumbe kwa So mfalme wa Misri; pia, hakumpatia kodi mfalme wa Ashuru, kama alivyofanya mwaka hadi mwaka.5Basi mfalme wa Ashuru akamfunga akamtia kifungoni. Kisha mfalme wa Ashuru akaishambulia nchi yote, akaishambulia Samaria na kuizunguka kwa miaka mitatu.6Katika mwaka wa tisa wa Hoshea, mfalme wa Ashuru akaichukua Samaria na akawapeleka Israeli hadi Ashuru. Akawaweka kwenye Hala, kwenye Habori Mto wa Gozani, na katika mji wa Wamedi.

7Utekwaji huu ulitokea kwa sababu wana wa Israeli walifanya dhambi dhidi ya BWANA Mungu wao, ambaye aliwaleta kutoka nchi ya Misri, kutoka chini ya mkono wa Farao mfalme wa Misri. Watu walikuwa wakiabudu miungu mingine8na kutembea katika matendo ya wamataifa ambao BWANA aliwafukuza mbele ya watu wa Israeli, na katika matendo ya wafalme wa Israeli ambayo waliyokuwa wameyafanya.9Wana wa Israeli wakafanya kwa siri mambo mabaya dhidi ya BWANA Mungu wao. Wakajijengea mahala pa juu katika miji yao yote, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye boma.10Pia wakasimamisha nguzo za mawe na Ashera juu ya kila mlima chini ya kila mti mbichi.11Huko wakafukiza ubani katika mahali pa juu pote, kama mataifa walivyokuwa wamefanya, ambao Yahwe aliwafukuza mbele yao. Waisraeli wakafanya mambo maovu ili kuchochea hasira ya BWANA,12wakaabudu sanamu, ambazo BWANA alizokuwa amewaambia, “Msifanye jambo hili.”13Bado BWANA aliwashuhudia Israeli na Yuda kwa kila nabii na kila muonaji, kusema, “Geukeni kutoka njia zenu mbaya na kuzishika amri zangu na hukumu zangu, na kuwa makini kufuata ile sheria yote niliyowaamuru baba zenu, na ambayo niliwapelekea kwa watumishi wangu manabii.”

14Lakini hawakuweza kusikia; badala yake walikuwa wakaidi kama baba zao ambao hawakumwamini BWANA Mungu wao.15Walizikataa sheria zake na lile agano ambalo alilifanya pamoja na babu zao, na hilo agano wakakubaliana wapewe. Wakafuata mambo yao yasiyofaa na wakawa hawafai. Wakawafuata mataifa ya kipagani ambayo yaliwazunguka, ambao BWANA alikuwa amewaamuru wasiige.

16Wakazipuuza amri zote za BWANA Mungu wao. Wakatengeneza sanamu za kusubu za ndama wawili kuziabudu. Wakatengeza nguzo ya Ashera, na wakaziabudu nyota zote za mbinguni na Baali.17Wakawatupia watoto wao wakike kwa wakiume kwenye moto, wakapiga ramli na uchawi, wakajiuza wenyewe kufanya yale ambayo yalikuwa maovu usoni pa BWANA, na kuichochea hasira yake.

18Kwa hiyo BWANA alikuwa na hasira na Israeli na kuwaondoa usoni mwake. Hakubakia mtu hata mmoja isipokuwa kabila la Yuda peke yake.19Hata watu wa Yuda hawakushika amri za BWANA Mungu wao, lakini badala yake walifuata mambo hayo hayo ya kipagani ambayo Israeli walifuata.20Hivyo BWANA akawakataa vizazi vyote vya Israeli; akawatesa na kuwatia kwenye mkono wa wale wenye kuwateka nyara, hadi atakapokuwa amewatupa usoni mwake.

21Akawatoa Israeli kutoka kwenye mstari wa kifalme wa Daudi, na wakamfanya Yeroboamu mwana wa Nebati mfalme. Yeroboamu akawapeleka Israeli mbali kutoka kumfuata BWANA na kuwafanya wafanye dhambi kubwa.22Wana wa Israeli wakafuata dhambi zote za Yeroboamu na hawakujiepusha nazo,23basi BWANA akawaondoa Israeli kutoka usoni pake, kama alivyokuwa amesema kupitia watumishi wake wote manabii kwamba angeweza kufanya. Hivyo Israeli walichukuliwa kutoka nchi yao kwenda Ashuru, na iko hivyo hata leo.

24Mfalme wa Ashuru akawaleta watu kutoka Babeli na kutoka Kutha, na kutoka Ava, na kutoka Hamathi na Sefarvaimu, na kuwaweka katika mji wa Samaria na kuishi katika huo mji wake.25Ikatokea wakati walipoanza kuishi huko hawakumcha BWANA. Hivyo BWANA akatuma simba miongoni mwao ambao waliwaua baadhi yao.26Basi wakaongea na mfalme wa Ashuru, wakisema, “Wale mataifa uliowahamisha na kuwaweka kwenye miji ya Samaria hawayajui mambo wanayotakiwa kuyafanya kutokana na mungu wa nchi. Hivyo alikuwa amewatuma simba kwenda kwao, na, tazama, wale simba walikuwa wakiwaua watu huko kwa sababu hawakufahamu yale mambo waliyokuwa wanatakiwa kuyafanya kwa mungu wa nchi.”

27Kisha mfalme wa Ashuru akatoa amri, akisema, “Mchukueni mmoja wa makuhani hapo ambaye mmemleta kutoka huko, na mumwache aende na kuishi huko, na mumwache awafundishe mambo yanayotakiwa kwa mungu wa nchi.”28Hivyo mmoja wa makuhani ambaye walimchukua kutoka Samaria akaja na kuishi katika Betheli; akawafundisha jinsi wanavyotakiwa kumcha MUNGU.

29Watu wa kila kabila wakajifanyia miungu yao wenyewe, na kuiweka mahala pa juu ambapo Wasamaria walifanya kila kabila katika mji ambako walipoishi.30Watu wa Babeli wakatengeneza Sakoth Benithi; watu wa Sakoth wakatengeneza Nergali; watu wa Hamathi wakatengeza Ashima;31Waavi wakatengeneza Nibhazi na Tartaki. Nao Wasefarvi wakachoma watoto wao kwenye moto kwa Adrameleki na Anameleki, wale miungu wa Sefarvaimu.32Pia wakamcha BWANA, na kuwateua kutoka miongoni mwao makuhani wa mahali pa juu, ambao waliteketeza kwa ajili yao kwenye hekaluni mahali pa juu.

33Wakamcha BWANA na pia kuabudu miungu yao wenyewe, sawa sawa na tamaduni za mataifa kutoka miongoni mwao waliokuwa wamewachukua.34Hadi siku hii ya leo wameshikilia tamaduni zao za zamani. Wala hawamwogopi BWANA, wala hawazifuati sheria zake, torati, au amri ambazo BWANA aliwapa watu wa Yakobo ambaye alimwita jina Israeli35pamoja na ambao BWANA alifanya agano nao na kuwaamuru, “Msiiche miungu mingine, wala kuisujudia, wala kuiabudu, wala kuitolea sadaka.36Lakini BWANA, ambaye aliwatoa kutoka nchi ya Misri kwa nguvu kubwa na mkono ulionyooshwa, yeye ndiye mnayetakiwa kumwabudu, yeye ndiye mnayetakiwa kumsujudia, na yeye ndiye mnayetakiwa kumtolea sadaka.37Na sheria na hukumu, na torati na amri ambazo alizoziandika kwa ajili yenu, mtazishika milele. Hivyo msiiche miungu mingine,38na agano ambalo nimelifanya pamoja nanyi, hamtalisahau; wala kuicha miungu mingine.39Lakini BWANA Mungu wenu, ndiye ambaye mtakayemcha. Atawalinda mbali na nguvu ya maadui zenu,”

40Hawakusikia, kwa sababu waliendelea kufanya yale waliyokuwa wameyafanya nyuma.41Hivyo haya mataifa wakamcha wakamcha BWANA na pia wakaabudu sanamu zao za kuchonga, na watoto wao wakafanya hivyo na watoto wao, Wakaendelea kufanya yale ambayo baba zao waliyoyafanya, hata leo.

18

1Ikawa katika mwaka wa tatu wa Hoshea mwana wa Ela, mfalme wa Israeli, Hezekia mwana wa Ahazi, mfalme wa Yuda akaanza kutawala.2Alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake alikuwa anaitwa Abija; alikuwa binti wa Zekaria.3Alifanya yaliyo mema usoni pa BWANA, kufuata mfano wa yote ambayo Daudi, babu yake, aliyoyafanya.4Alipaondoa mahali pa juu, akaiharibu nguzo ya jiwe, akaikata hiyo nguzo ya Ashera. Akavunja vipande vipande ile nyoka ambayo Musa aliyokuwa ameifanya, kwa sababu siku zile wana wa Israeli walikuwa wakichoma ubani katika hiyo; ilikuwa inaitwa “Nehushtani.”

5Hezekia alimwamini BWANA, Mungu wa Israeli, hivyo basi baada ya yeye hapakuwa kama yeye miongoni mwa wafalme wote wa Yuda, wala miongoni mwa wafalme ambao walikuwa kabla yake.6Aliambatana na BWANA. Hakuacha kumfuata lakini alizifuata amri zake, ambazo BWANA alimwamuru Musa.7Hivyo BWANA alikuwa na Hezekia, kila alipokwenda alifanikiwa. Akaasi dhidi ya mfalme wa Ashuru na hakumtumikia.8Akawashambulia Wafilisti hadi Gaza na mipaka inayoizunguka, kutoka mnara wa walinzi hadi mji wenye ngome.

9Katika mwaka wa nne wa Mfalme Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa saba wa Hoshea mwana wa Ela mfalme wa Israeli, Shalmanesa mfalme wa Ashuru akapanda hadi Samaria na kuizunguka.10Mwishoni mwa miaka mitatu wakaichukua, katika mwaka wa sita wa Hezekia, ambao ulikuwa mwaka wa tisa wa Hoshea mfalme wa Israeli; hivi ndivyo Samaria ilivyotekwa.11Basi mfalme wa Ashuru akawachukua Israeli kwenda Ashuru na kuwaweka kwenye Hala, na katika mto Habori katika Gozani, na katika mji wa Wamedi.12Alifanya hivi kwa sababu hawakutii sauti ya BWANA Mungu wao, lakini walikiuka makubaliano ya agano lake, yote yale ambayo Musa yule mtumishi wa BWANA aliwaamuru. Walikataa kuyasikiliza au kuyafanya.

13Kisha katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senakerebu mfalme wa Ashuru akaishambulia miji yote yenye boma na kuwateka mateka.14Basi Hezekia mfalme wa Yuda akatuma neno kwenda kwa mfalme wa Yuda akatuma neno kwa mfalme wa Ashuru, ambaye alikuwa Lakishi, akisema, “Nimekuudhi. Nichukue. Popote utakaponiweka nitavumulia.” Mfalme wa Ashuru akamtaka Hezekia mfalme wa Yuda kulipa talanta mia tatu za fedha na talanta thelathini za dhahabu.

15Hivyo Hezekia akampatia fedha zote ambazo zilikuwa zimepatikana kwenye nyumba ya BWANA na kwenye hazina ya nyumba ya mfalme.

16Kisha Hezekia akaikata ile dhahabu kutoka kwenye milango ya hekalu la BWANA na kutoka juu ya nguzo; akampatia dhahabu mfalme wa Ashuru.17Lakini mfalme wa Ashuru akalihamasisha jeshi lake kubwa, akawatuma Tartani na Rabsarisi na amiri jeshi mkuu kutoka Lakishi kwenda kwa Hezekia huko Yerusalemu. Wakasafiri hadi kwenye mabarabara na kufika nje ya Yerusalemu. Wakakaribia karibu na mfereji wa birika la juu, kwenye barabara kuu ya shamba la dobi, na kusimama hapo.18Wakati walipokuwa wamemwita Mfalme Hezekia, Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa kiongozi wa nyumba ya mfalme na Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, anayeandika kumbukumbu, wakatoka nje kwenda kuwalaki.

19Basi yule amiri jeshi mkuu akawaambia wamwambie Hezekia kile alichosema mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru, amesema: “Nini chanzo cha ujasiri wako?20Unaongea maneno yasiyo na maana, kusema lipo neno na nguvu ya vita. Sasa unamtumainia nani? Nani anakupa ujasiri wa kuasi dhidi yangu?21Tazama, unatumainia kutembelea fimbo ya mwanzi huu uliopondeka wa Misri, lakini kama mtu akiutegemea, utamchapa kwenye mkono wake na kuutoboa. Hivyo ndivyo alivyo Farao mfalme wa Misri kwa mtu yeyote ambaye anayemtumainia.”22Lakini kama ukiniambia, “Tunamwamini BWANA Mungu wetu;” je si yeye ambaye mahali pa juu na madhabahu Hezekia amezichukua, na kumwambia Yuda na kwa Yerusalemu, ‘Lazima uabudu mbele ya hii madhabahu katika Yerusalemu?’

23Basi kwa hiyo, nataka kukufanyia ahadi nzuri kutoka kwa bwana wangu mfalme wa Ashuru. Nitakupatia farasi 2,000, kama unaweza kuwatafuta wa kuwaendesha kwa ajili yao.24Wawezaje kumpinga hata akida mmoja wa watumishi walio wadogo? Mmeweka tumaini lenu katika Misri kwa magari ya farasi na waendesha farasi!25Je nimesafiri kwenda huko juu bila BWANA kupapigania hapa mahali na kupaharibu? BWANA ameniambia, ‘Ishambulie hii nchi na uiharibu.”’

26Kisha Elikana mwana wa Hilkia, na Shebna, na Joa wakamwambia amiri jeshi mkuu, “Tafadhali ongea na watumishi wako katika lugha ya Kiaramu, kwa kuwa tunaielewa. Usiongee nasi katika lugha ya Yuda katika masikio ya watu ambao wako ukutani.”

27Lakini yule amiri jeshi mkuu akawaambia, “Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako niyaseme maneno haya? Je hajanituma kwa hawa watu ambao wameketi kwenye ukuta, ambao watakula kinyesi chao na kunywa mkojo wao wenyewe?”

28Kisha yule amiri jeshi mkuu akasimama na akapiga kelele kubwa kwa lugha ya Kiyahudi, akisema, “Sikilizeni neno la mfalme mkuu, mfalme wa Ashuru.29Mfalme asema, ‘Msimwache Hezekia akawadanganya, kwa kuwa hataweza kuwaokoa kwenye nguvu yangu.’30Msimwache Hezekia akawatumainisha katika BWANA, akisema, ‘BWANA atatuokoa hakika, na huu mji hautawekwa kwenye mkono wa mfalme wa Ashuru.’

31Msimsikilize Hezekia, kwa kuwa hivi ndivyo mfalme wa Ashuru asemavyo: ‘Fanyeni amani pamoja nami na njooni kwangu. Kisha kila mmoja wenu atakula kutoka kwenye mzabibu wake mwenyewe na kutoka kwenye mtini wake mwenyewe, na kunywa kutoka kwenye maji kwenye maji ya birika lake mwenyewe.32Mtafanya hivyo hadi nitakapokuja na kuwachukua kwenda kwenye nchi kama nchi yenu, nchi ya nafaka na divai, nchi ya mkate na mashamba ya mizabibu, nchi ya miti ya mizaituni na asali, ili muweze kuishi na sio kufa. Msimsikilize Hezekia wakati atakapojaribu kuwashawishi, akisema, ‘BWANA atatuokoa.’33Je miungu yeyote ya watu inaweza kuwaokoa kutoka kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru?34Iko wapi miungu ya Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu, Hena, na Iva? Je imeiokoa Samaria kutoka mkono wangu?35Miongoni mwa miungu yote ya nchi, je kuna mungu ambaye ameiokoa nchi yake kutoka kwenye nguvu yangu? Inawezekanaje BWANA akaiokoa Yerusalemu kutoka kwenye uwezo wangu?”

36Lakini watu wakabaki kimya na hawakujibu, kwa kuwa mfalme alikuwa ameamuru, “Msimjibu.”

37Kisha Eliakimu mwana wa Hilkia, ambaye alikuwa juu ya nyumba ya mfalme; Shebna yule mwandishi; na Joa mwana wa Asafu, mtunza kumbukumbu, akaja kwa Hezekia pamoja na nguo zao zilizoraruliwa, na kumpatia taarifa ya maneno ya yule amiri mkuu.

19

1Ikawa kuhusu kwamba wakati Mfalme Hezekia aliposikia taarifa zao, akararua mavazi yake, akavaa nguo za magunia, na kwenda kwenye nyumba ya BWANA.2Akamtuma Elkana, ambaye alikua msimamizi wa nyumba ya mfalme, na Shebna yule mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walikuwa wamefunikwa na nguo za magunia, kwenda kwa Isaya mwana wa Amozi, yule nabii.3Wakamwambia, Hezekia wakisema, “Siku hii ni siku ya mateso, shutuma, na fedheha, kwa kuwa wakati umewadia watoto kuzaliwa, lakini hakuna nguvu ili wazaliwe.4Inaweza kuwa BWANA Mungu wako atasikia maneno yote ya amiri jeshi mkuu, ambaye mfalme wa Ashuru bwana wake amemtuma kumdhihaki Mungu aliye hai, naye atayakemea yale maneno ambayo BWANA Mungu wako aliyasikia. Sasa inua maombi yako juu kwa ajili ya mabaki yaliyo bakia hapo.”’

5Hivyo watumishi wa mfalme Hezekia wakaja kwa Isaya,6na Isaya akawaambia, “Mwambieni bwana wenu: ‘BWANA asema hivi, ‘Usiyaogope maneno ambayo uliyoyasikia, pamoja na kwamba watumishi wa mfalme wa Ashuru wamenitukana.7Tazama, nitaweka roho ndani yake, na yamkini atasikia taarifa na kurudi kwenye nchi yake mwenyewe. Nitamfanya aanguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.’”

8Kisha amiri jeshi mkuu akarudi na kumkuta mfalme wa Ashuru akipigana dhidi ya Libna, kwa kuwa alisikia kwamba mfalme alikuwa ameenda kutoka Lakishi.

9Kisha Senakeribu akasikia kwamba Tirhaka mfalme wa Kushi na Misri alihamasisha kupigana dhidi yake, hivyo akatuma wajumbe tena kwa Hezekia pamoja na ujumbe:10“Mwambieni Hezekia mfalme wa Yuda, ‘Asikudanganye Mungu wako unayemwamini, kusema, ‘Yerusalemu haitawekwa kwenye mikono ya mfalme wa Ashuru.’11Tazama, umesikia kwamba wafalme wa Ashuru wamemaliza nchi zote kwa kuziharibu kabisa. Kwa hiyo je utaokoka?12Je wale miungu wa mataifa wamewaokoa, mataifa ambao baba zangu waliyaharibu: Gozani, Harani, Resefu, na watu wa Edeni katika Telasari?13Je yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaimu, wa Hena, na Iva?’”

14Hezekia akapokea hii barua kutoka wale wajumbe na kuisoma. Kisha akapanda hata kwenye nyumba ya BWANA na kuukunjua mbele yake.15Kisha Hezekia akaomba mbele ya BWANA na kusema, “BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, uketiye juu ya makerubi, wewe ni Mungu wa pekee juu ya tawala zote za dunia. Uliyeziumba mbingu na nchi.16Tega sikio lako, BWANA, na usikie. Fungua macho yako, BWANA, na tazama, na sikia maneno ya Senakeribu, ambayo ameyatuma kumdhihaki Mungu aliye hai.

17Ni kweli BWANA, wafalme wa Ashuru wameyaharibu mataifa na nchi zao.18Wameiweka miungu yao kwenye moto, kwa kuwa hawakuwa miungu lakini ilikuwa kazi ya mikono ya watu, ilikuwa miti na mawe. Hivyo Waashuru wamewaharibu.19Basi sasa, BWANA Mungu wetu, tuokoe, nakusihi, kutoka kwenye nguvu zake, ili kwamba mamlaka zote za dunia zipate kujua ya kwamba wewe, BWANA, ndiye Mungu wa pekee.”

20Kisha Isaya mwana wa Amozi akatuma ujumbe kwa Hezekia, akisema, “BWANA, Mungu wa Israeli asema, ‘Kwa sababu umeomba kwangu kuhusiana na Senakeribu mfalme wa Ashuru, nimekusikia.’21Hili ndilo neno ambalo BWANA ameliongea kuhusu yeye: ‘Bikira binti Sayuni amekudharau na kukucheka kwa dharau. Binti wa Yerusalemu akatikisa kichwa juu yako.
22Je ni nani uliyemchokoza na kumtukana? Dhidi ya nani umeinua sauti yako na kuinua macho yako katika majivuno? Juu ya Mtakatifu wa Israeli!
23Kupitia wajumbe wako wamemdharau Bwana, na kusema, ‘Pamoja na wingi wa magari yangu ya farasi nimeenda juu ya vilele ya milima, hata juu ya kilele cha Lebanoni. Nitaikata mierezi mirefu na kuchagua miti ya mivinje huko. Nitaingia sehemu za makazi yake yaliyo mbali, msitu wake uzaao sana.
24Nimechimba visima na kunywa maji mageni. Nimekausha mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yangu.’
25Je hukusikia jinsi nilivyoagiza tangu zamani, na kuyafanya tangu siku za zamani? Sasa ninalileta kupita. Uko hapa kupunguza miji isiyoingilika kwenye rundo la maangamizi.
26Makazi yao, ya nguvu kidogo, imevunjwa vunjwa na aibu. Wamekuwa mimea katika shamba, majani ya kijani, majani juu kwenye dari au kwenye shamba, lililochomwa kabla halijakua.
27Lakini najua kuketi kwako chini, na kutoka kwako, kuingia kwako dhidi yangu.
28Kwa sababu kiburi chako kimeyafikia masikio yangu, nitaweka kulabu yangu kwenye pua yako, na hatamu yangu kwenye mdomo wako; nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.”
29Hii ndiyo itakuwa ishara kwako: Mwaka huu mtakula vitu viotavyo porini, na katika mwaka wa pili vile vikuavyo katika huo. Lakini katika mwaka wa tatu ni lazima mpande na kuvuna, kupanda mashamba ya mizabibu na kula matunda yake.
30Mabaki ya nyumba ya Yuda ambayo yataokoka yatachukua tena mizizi na kuzaa matunda.
31Kwa kuwa mabaki yatatoka Yerusalemu, kutoka Mlima Sayuni wenye kuokoka utakuja. Wivu wa BWANA wa majeshi utafanya hivyo.
32Kwa hiyo BWANA asema hivi kuhusu mfalme wa Ashuru: “Hatakuja kwenye huu mji wala kupiga mshale hapa. Wala hatakuja mbele yake na ngao au kujenga boma dhidi yake.
33Njia ile ile aliyoijia ndiyo njia atakayoondokea; hatoingia mji huu hivi ndivyo asemavyo BWANA.”
34Kwa maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa ajili yangu mwenyewe na kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu.”’

35Ikawa kuhusu usiku huo ambao malaika wa BWANA alitoka na kuvamia kambi ya Waashuru, akawaua maaskari mia themanini na tano elfu. Kisha watu wakaamka asubuhi na mapema, miili ya watu waliokuwa wamekufa ilikuwa imelala kila mahali.36Hivyo Senakeribu mfalme wa Ashuru akaondoka Israeli na kwenda nyumbani na kuishi katika Ninawi.

37Baadaye, alipokuwa akiabudu kwenye nyumba ya Nisroki mungu wake, watoto wake Adramaleki na Shareza wakamuua kwa upanga. Kisha wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Kisha Esarhodani mwanaye akawa mfalme katika mahali pake.

20

1Katika siku hizo Hezekia aliugua akawa kwenye hatari ya kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, akaja, na kumwambia, “BWANA asema, ‘Weka nyumba yako kwenye mpangilio; kwa kuwa utakufa, na hutapona.’”

2Kisha Ahazi akageuza uso wake kwenye ukuta na kumuomba BWANA, akisema,3“Tafadhali, BWANA, ukumbuke jinsi nilivyo mwaminifu kutembea mbele yako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya yaliyo mazuri usoni kwako.” Kisha Hezekia akalia kwa sauti.

4Kabla ya Isaya hajatoka nje kwenye mji wa kati, neno la BWANA likamjia, kusema,5“Rudi, na umwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, ‘Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Daudi babu yako, asemavyo: ‘Nimesikia maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Nitakuponya katika siku ya tatu, na utapanda juu kwenye nyumba ya BWANA.6Nitakuongeza miaka kumi na tano ya maisha yako, na nitakulinda na huu mji kwa ajili yangu na kwa ajili ya mtumishi wangu.’”

7Hivyo Isaya akasema, “Chukueni mkate wa tini.” Walifanya hivyo na kuweka kwenye jipu lake, na akapona.

8Hezekia akamwambia Isaya, “Je kutakuwa na alama gani ambayo BWANA ataniponya, na kwamba nitapanda juu hadi kwenye hekalu la BWANA katika siku ya tatu?”

9Isaya akajibu, “Hii ndiyo itakuwa ishara kwako kutoka kwa BWANA kwamba BWANA atafanya kitu amacho alichokisema. Je kivuli kitaenda mbele hatua saba, au kurudi nyuma hatua saba?”

10Hezekia akajibu, “Ni kitu chepesi kwa kivuli kwenda mbele hatua kumi. Hapana, hicho kivuli kirudi nyuma hatua kumi.”

11Hivyo Isaya nabii akamlilia BWANA, na akaleta kivuli hatua kumi nyuma, kutoka pale ambapo zilikuwa zimevuka kwenye ngazi za Ahazi.

12Katika kipindi hicho Merodak Baladani mfalme wa Babeli alituma barua na zawadi kwa Hezekia, kwa kuwa alisikia kwamba Hezekia alikuwa anaumwa.13Hezekia akasikiliza hizo barua, na kisha kuwaonyesha wajumbe sehemu zote na sehemu zake za thamani, fedha, dhahabu, manukato na marhamu na nyumba yenye ghala la silaha zake, na yote yaliyokutwa kwenye ghala za nyumba zake. Hapakuwa na kitu kwenye nyumba, wala kwenye ufalme wake wote, ambao Hezekia hakuwaonyesha.

14Kisha Isaya akaja kwa Hezekia na kumuuliza, “Hawa watu walikuwa wanakwambiaje? Wanatokea wapi?” Hezekia akasema, “Wamekuja kutoka nchi ya mbali ya Babeli.

15Isaya akauliza, “Wameona nini kwenye nyumba yako?” Hezekia akajibu, “Wameona kila kitu kwenye nyumba yangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.”

16Basi Isaya akamwambia Hezekia, “Sikiliza neno la BWANA:17‘Tazama siku zinakuja wakati kila kitu kwenye nyumba yako ya kifalme, vitu ambavyo baba zako walivitunza huko hadi leo, vitabebwa kwenda Babeli. Hakuna kitakachobakia, asema BWANA.18Watoto waliozaliwa na wewe, ambao umewazaa wewe mwenyewe watawachukua mbali, na watakuwa matowashi kwenye nyumba ya kifalme ya mfalme wa Babeli.’”

19Hezekia akamwambia Isaya, “Neno la BWANA uliloliongea ni jema.” Kwa kuwa alifikiri, Je sivyo ikiwapo amani na kweli katika siku zangu?”

20Kama kwa mambo mengine yanamuhusu Hezekia, na ushujaa wake wote, na jinsi alivyotengeza bwawa la maji na mfereji, na kuleta maji kwenye mji-hayakuandikwa kwenye kitabu cha ya matukio ya wafalme wa Yuda?21Hezekia akalala na baba zake, na Manase mwanae akawa mfalme katika sehemu yake.

21

1Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hefziba.2Alifanya maovu usoni kwa BWANA, kama machukizo ya mataifa ambayo BWANA aliyafukuza nje mbele ya wana wa Israeli.3Kwa kupajenga tena mahala pa juu ambapo Hezekia baba yake alipaharibu, na akajenga madhabahu kwa ajili ya Baali, akafanya Ashera, kama Ahabu mfalme wa Israeli alivyofanya, akasujudu kwa nyota zote za mbinguni na kuwaabudu wao.4Manase akajenga madhabahu za kipagani kwenye nyumba ya BWANA, ingawaje BWANA aliamuru, “Jina langu litakuwa Yerusalemu daima.”5Akajenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya BWANA.6Akamuweka mtoto wake wa kiume kwenye moto; akatazama bao, akafanya ushirikina na kujishuhulisha pamoja na wale ambao wenye pepo wa utambuzi na wale wachawi. Akafanya maovu mengi usoni mwa BWANA na kuchochea hasira kwa Mungu.

7Sanamu ya kuchongwa ya Ashera ambayo aliitengeneza, akaiweka kwenye nyumba ya BWANA. Nyumba hii ndiyo ambayo BWANA alimwambia Daudi na Sulemani mwanawe; akisema: “Ni nyumba hii na katika Yerusalemu, ambayo nimeichagua kutoka makabila yote ya Israeli, ambako nitaliweka jina langu milele.8Sitafanya miguu ya Israeli kushindwa tena nje ya nchi ambayo niliwapa babu zao, kama tu watakuwa makini kutii yale yote niliyowaamuru, na kufuata sheria zote ambazo mtumishi wangu Musa aliwaamuru.”9Lakini watu hawakusikia, na Manase akawaongoza kufanya maovu zaidi kuliko yale ya mataifa ambayo BWANA aliyaharibu mbele ya watu wa Israeli.

10Basi BWANA akaongea na watumishi wake manabii, akisema,11“Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya haya machukizo, na kutenda maovu zaidi kuliko yote waliyoyatenda Waamori ambao walikuwa mbele yake walikubali, na pia aliwafanya Yuda kuasi kwa sanamu zake,12kwa hiyo BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi: ‘Tazama, nakaribia kuleta uovu juu ya Yerusalemu na Yuda ambayo kila mtu asikiapo kuhusu hilo, masikio yake yote yatawasha.13Nitanyoosha juu ya Yerusalemu kipimo kilichotumika dhidi ya Samaria, na kuangusha mstari utakaotumika dhidi ya nyumba ya Ahabu; Nitaifuta Yerusalemu safi, kama kufuta sahani, kuifuta na kuifunika juu chini.14Nitawatupa masalia ya urithi wangu na kuwaweka mikononi mwa maadui zao. Watakuwa nyara na mateka kwa maadui zao wote,15kwa sababu wamefanya yaliyo maovu usoni kwangu, na kunichochea hasira, tangu siku babu zao walipotoka Misri, hadi leo.’”

16Aidha, Manase akazimwaga damu nyingi za wasio na hatia, hadi alipoijaza Yerusalemu kutoka upande huu kwenda mwingine kwa kifo. Hii ilikuwa ni kuongeza kwenye dhambi ambayo aliifanya Yuda kuasi, wakati walipofanya uovu mbele za BWANA.

17Kama kwa mambo mengine yamhusuyo Manase, yote aliyoyafanya, na dhambi ambayo aliyoifanya, je haya hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio cha wafalme wa Yuda?18Manase akalala pamoja na baba zake na alizikwa kwenye bustani ya nyumba yake, katika bustani ya Uza. Amoni mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.

19Amoni alikuwa na miaka Ishirini na mbili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Meshlemethi; alikuwa binti wa Haruzi wa Yotba.20Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA, kama manase baba yake alivyofanya.21Amoni alifuata njia zote ambazo baba yake alizotembelea na kuabudu sanamu ambazo baba yake aliziabudu, na kuzisujudia.22Akajitenga na BWANA Mungu wa baba zake, na hakutembea katika njia ya BWANA.23Watumishi wa Amoni wakafanya njama dhidi yake na kumuua mfalme kwenye nyumba yake mwenyewe.

24Lakini watu wa nchi wakawaua watu wote waliofanya njama dhidi ya mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia mtoto wake kuwa mfalme katika sehemu yake.

25Kama ilivyo kwa mambo mengine yamhusuyo Amoni yale aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?26Watu wakamzika kwenye kaburi lake katika bustani ya Uza, na Yosia mwanawe akawa mfalme katika sehemu yake.

22

1Yosia alikuwa na umri wa miaka minane wakati alipoanza kutawala; alitawala kwa mda wa miaka thelathini na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Yedida (Alikuwa binti wa Adaye wa Bozkathi).2Alifanya yale yaliyo mema usoni mwa BWANA. Alitembea kwenye njia zote za Daudi baba yake, na hakugeuka wala upande wa kulia au kushoto.

3Ikawa kwamba katika mwaka wa kumi na nane mfalme Yosia, akamtuma Shafani mwana wa Azalia mwana wa Meshulamu, mwandishi, kwenye nyumba ya BWANA, akisema,4“Panda juu kwa Hilkia yule kuhani mkuu na mwambie ahesabu pesa ambazo zilizokuwa zimeletwa kwenye nyumba ya BWANA, ambazo walinzi wa hekalu wamezikusanya kutoka kwa watu.5Zigawanywe kwenye mikono ya wafanyakazi ambao ni wasimamizi wa nyumba ya BWANA, na waache wawapatie wafanya kazi ambao wako kwenye nyumba ya BWANA, ili waweze kutengeneza pale palipoharibika.6Wapewe pesa maseremala, wajenzi, na waashi, na pia kununua mbao na kukata jiwe kukarabati nyumba ya BWANA.”7Lakini zile pesa hazikutakiwa kuhesabiwa wakati walipokuwa wanapewa, kwa sababu waliimudu ile kazi kwa uaminifu.

8Hilkia kuhani mkuu akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya BWANA.” Basi Hilkia akampatia kile kitabu Shafani, na kukisoma.9Shafani akaenda na kuchukua kile kitabu kwa mfalme, na pia kumjulisha, akisema, “Watumishi wako wamezitumia zile pesa ambazo zilizokuwa zimepatikana kwenye hekalu na zimegawiwa kwenye mikono ya wafanya kazi ambao husimamia kuangalia nyumba ya BWANA.”10Kisha Shafani yule mwandishi akamwambia mfalme, “Hilkia yule kuhani amenipatia kitabu.” Kisha Shafani akakisoma mbele ya mfalme.

11Ikawa kwamba wakati mfalme aliposikia maneno ya sheria, alichana nguo zake.12Kisha mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani, Ahikamu mwana wa Shafani, Akbori mwana wa Mikaya, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake mwenyewe, akisema,13Nenda na ukaongee pamoja na BWANA kwa ajili yangu, na kwa ajili ya watu na kwa Yuda yote, kwa sababu ya maneno ya hiki kitabu ambacho kilichopatikana. Kwa hasira kubwa ya BWANA ambayo ametukasirikia dhidi yetu kwa sababu baba zetu hawakusikiliza maneno ya hiki kitabu hivyo kama kutii yote ambayo yalikuwa yameandikwa kuhusiana na sisi.

14Basi Hilkia yule kuhani, Ahikamu, Akbori, Shafani, na Asaya wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tikva mwana wa Harhasi, mtunza kabati la nguo (aliishi katika Yerusalemu katika mtaa wa pili), na wakaongea pamoja naye.

15Akawaambia, “Hivi ndivyo BWANA, Mungu wa Israeli, asemavyo: ‘Mwambie huyu mtu aliyekutuma kwangu,16hivi ndivyo BWANA asemavyo: ‘Tazama, nitaleta janga kwenye hii sehemu na juu ya wakaao hapa, kulingana na kila kitu kilichoandikwa kwenye kitabu ambacho mfalme wa Yuda alichokisoma.17Kwa sababu wamenitelekeza na kufukiza ubani kwa miungu mingine, hivyo basi wanaweza kunichochea hasira pamoja na matendo yote waliyoyafanya, kwa hiyo hasira yangu ilikuwa inawaka dhidi ya hii sehemu, na haitazimika.”’18Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliye watuma kuuliza mapenzi ya BWANA, hivi ndivyo mtakavyo mwambia: “BWANA, Mungu wa Israeli asema hivi: Kuhusu yale maneno uliyoyasikia,19kwa sababu moyo wako ulikuwa mlaini, na kwa sababu umejinyenyekesha mwenyewe mbele za BWANA, wakati uliposikia nilichokisema dhidi ya hii sehemu na wenyeji wake, kwamba wanaweza kuwa wakiwa na laana, na kwa sababu ulizozirarua nguo zako na kulia mbele yangu, Nami pia nimekusikia hivi ndivyo BWANA asemavyo.20Tazama, nitakukusanya na baba zako, nawe utawekwa kaburini kwako kwa amani. Macho yako hayataona maafa yote ambayo nitayaleta kwenye hii sehemu.’” Hivyo watu wakachukua ujumbe huu kuurudisha kwa mfalme.

23

1Hivyo mfalme akawatuma wajumbe waliokuwa wamemzunguka wazee wote wa Yuda na wa Yerusalemu.2Kisha mfalme akapanda hadi kwenye nyumba ya BWANA, na watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu pamoja naye, na makuhani, manabii, na watu wote, kuanzia mdogo hadi mkubwa. Kisha akasoma masikioni kwao maneno yote ya kitabu cha agano ambalo lililokuwa limepatikana kwenye nyumba ya BWANA.3Mfalme akasimama karibu na nguzo na kufanya agano mbele ya Yahwe, kutembea pamoja na Yahwe na kukumbuka maagizo yake, kanuni zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na kwa roho yake yote, kuthibitisha maneno ya hili agano ambalo lililokuwa limeandikwa kwenye hiki kitabu. Hivyo watu wote wakakubaliana kusimama kwenye agano

4Mfalme akamwamuru Hilkia yule kuhani mkuu, makuhani chini yake, na walinzi wa lango watoe kwenye hekalu vyombo vilivyokuwa vimetengenezwa kwa ajili ya Baali na Ashera, na kwa ajili ya nyota zote za mbinguni. Akavichoma moto Yerusalimu kwenye mashamba ya bonde la Kidroni na kubeba majivu yake kwenda Betheli.5Akawaondoa makuhani waliokuwa wanaabudu miungu ambao wafalme wa Yuda waliwachagua ili kwa ajili ya kufukiza ubani katika mahali pa juu kwenye miji ya Yuda na sehemu zinazoizunguka Yerusalemu wale waliokuwa wanachoma ubani kwa Baali, kwa jua na kwa mwezi, kwa sayari, na kwa nyota zote za mbinguni.6Akaiondoa Ashera kutoka kwenye hekalu la BWANA, nje ya Yerusalemu hata bonde la Kidroni na kuichoma hapo. Akaipiga kwenye mavumbi na kuyatupa yale mavumbi kwenye makaburi ya watu wa kawaida.7Akavisafisha vyumba vya makahaba ambao walikuwa kwenye hekalu la BWANA, ambako wanawake waliposhonea nguo kwa ajili ya Ashera.

8Yosia akawaleta makuhani wote nje ya miji ya Yuda na kupanajisi mahali pa juu ambako makuhani walipokuwa wakichomea ubani, kutoka Geba hata Bersheba. Akapaharibu mahala pa juu kwenye malango ambayo yaliyokuwa ya kuingilia kwenda kwenye lango la Yoshua (liwali wa mji), upande wa kushoto wa lango la mji.9Ingawa makuhani wa mahali pa juu hawakuruhusiwa kuhudumu kwenye madhabahu ya BWANA katika Yerusalemu, wakala mikate isiyotiwa chachu miongoni mwa ndugu zao.

10Yosia akainajisi Tofethi, ambayo ipo kwenye bonde la Ben Hinomu, ili kwamba mtu yeyote asimuweke mtoto wake wa kiume au binti yake kwenye moto kama sadaka kwa Moleki.11Akawachukua farasi ambao wafalme wa Yuda waliokuwa wametolewa kwa ajili ya jua. Walikuwa kwenye eneo la lango la kuingilia kwenye hekalu la BWANA, karibu na chumba cha Nathani Meleki, msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. Yosia akayachoma yale magari ya farasi ya jua.

12Yosia mfalme akayaharibu madhabahu yaliyokuwa kwenye dari ya juu ya chumba cha Ahazi, ambacho wafalme wa Yuda walikitengeneza, na madhabahu ambayo Manase aliyatengeneza kwenye behewa mbili za nyumba ya BWANA. Yosia akazivunga vipande vipande na kuvitupa kwenye bonde la Kidroni.13Mfalme akapaangamiza mahali pa juu magharibi mwa Yerusalemu, kusini mwa mlima wa uharibifu ambapo Sulemani mfalme wa Israeli alipajenga kwa ajili ya Ashtorithi, chukizo la Wamoabu; sanamu za karaha za Wasidoni; kwa Kemoshi, sanamu za karaha wa Moabu; na kwa Moleki, sanamu wa karaha wa watu wa Amoni.14Akazivunja nguzo za jiwe kuwa vipande vipande na kuziangusha chini nguzo za Ashera na kuzijaza zile sehemu kwa mifupa ya watu.

15Yosia pia akaiteketeza kabisa madhabahu iliyokuwa Betheli na mahali pa juu ambako Yeroboamu mwana wa Nebati (ambaye aliwafanya Waisraeli kuasi) aliijenga. Pia aliichoma moto ile madhabahu na mahali pa juu na kupapiga hadi pakawa vumbi. Pia akaichoma moto nguzo ya Ashera.16Yosia alipotazama kwenye lile eneo, akagundua kwamba yale makaburi yalikuwa juu ya mlima. Akawatuma watu kuichukua mifupa kutoka kwenye yale makaburi; kisha akaichoma kwenye madhabahu, akainajisi. Hii ilitokana na neno la BWANA ambalo mtu wa Mungu alilonena, yule mtu alikuwa amenena haya mambo kabla.

17Kisha akasema, “Ni ukumbusho wa nani ule ninao uona?” Mtu wa ule mji akamwambia, “Lile ni kaburi la mtu wa Mungu ambaye alikuja kutoka Yuda na kutabiri kuhusu haya mambo ambayo umeyafanya dhidi ya madhabahu ya Betheli.”

18Hivyo Yosia akasema, “Mwacheni. Mtu asihamishe mifupa yake.” Hivyo wakaacha mifupa yake, pamoja na mifupa ya nabii ambaye alikuja kutoka Samaria.

19Kisha Yosia akahamisha nyumba zote za mahali pa juu ambazo zilikuwa katika mji wa Samaria, ambazo wafalme wa Israeli walizokuwa wamezitengeneza, na ambazo zilizokuwa zimemgadhabisha BWANA.20Aliwafanyia kile ambacho kilikuwa kimefanyika katika Betheli. Aliwachinja makuhani wote wa mahali pa juu ya madhabahu na aliichoma mifupa ya watu juu yao. Kisha akarudi Yerusalemu.

21Kisha mfalme akawaamuru watu wote, akisema, “Itunzeni Pasaka ya BWANA Mungu wenu, kama ilivyoandikwa kwenye hiki kitabu cha agano.”22Hiyo Pasaka haijawahi kufanyika tangu siku za waamuzi ambao waliiongoza Israeli, wala katika siku zote za wafalme wa Israeli au Yuda.23Lakini katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yosia Pasaka ya BWANA ilisheherekewa katika Yerusalemu.

24Yosia pia akawafukuza wale ambao waliokuwa wameongea na wafu au na roho. Pia aliifukuza miungu ya sanamu, na vitu vyote ambavyo ni chukizo vilivyokuwa vinaonekana katika nchi ya Yuda na katika Yerusalemu, hivyo kwa kuthibitisha yale maneno ya sheria ambayo iliyokuwa imeandikwa kwenye kitabu cha Hilkia yule kuhani aliyekuwa amepatikana kwenye nyumba ya BWANA.25Kabla ya Yosia, hapakuwa na mfalme kama yeye, aliyekuwa amemwelekea BWANA kwa moyo wake wote, roho yake yote, na nguvu zake zote, ambaye alifuata sheria zote za Musa. Hapakuwa na mfalme kama Yosia aliyeinuka baada ya yeye.

26Walakini, BWANA hakugeuka kutoka kwenye ukali wa hasira yake, ambayo ilikuwa dhidi ya Yuda kwa waabudu wapagani wote pamoja ambao Manase aliokuwa amemgadhibisha.27Hivyo BWANA akasema, “Pia nitaiondoa Yuda usoni kwangu, kama nilivyoiondoa Israeli, na nitautupilia mbali huu mji ambao nilio uchagua, Yerusalemu, na ile nyumba ambayo niliyokuwa nimesema, ‘Jina langu litakuwa humo.”’

28Kama kwa mambo mengine yanayo mhusu Yosia, kila kitu alichofanya, je vimeandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?

29Katika siku zake, Farao Neko, mfalme wa Misri, alienda kupigana dhidi ya mfalme wa Ashuru huko mto Frati. Mfalme Yosia akaenda kuonana na Neco katika mapigano, na Neko akamuua huko Megido.30Watumishi wa Yosia wakambeba kwenye gari la farasi akiwa amekufa kutoka Migido, kumleta Yerusalemu, na kumzika katika kaburi lake mwenyewe. Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoahazi mwana wa Yosia, wakamtia mafuta, na kumfanya kuwa mfalme katika mahali pake.

31Yehoahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na tatu alipoanza kutawala, na alitawala miezi mitatu katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia wa Libana.32Yehoahazi alifanya yaliyo maovu usoni kwa Yahwe, kama kila kitu ambacho babu zake walichokifanya.33Farao Neko akamfunga gerezani huko Ribla katika nchi ya Hamathi, hivyo asiweze kutawala katika Yerusalemu. Kisha Neko akaitoza Yuda talanta mia moja za fedha na talanta moja ya dhahabu.34Farao Neko akamfanya Eliakimu mwana wa Yosia mfalme katika mahali pa Yosia baba yake, na kubadilisha jina lake kuwa Yehoyakimu. Lakini akamchukua mfalme Yehoahazi kwenda Misri, na Yehoahazi akafia huko.

35Yehoyakimu akalipa fedha na dhahabu kwa Farao. Ili akutane na amri ya Farao, Yehoyakimu akaitoza nchi na kulazimisha kila mtu miongoni mwa watu wa nchi wamlipe fedha na dhahabu kulingana na makadirio yao.

36Yehoyakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa akiitwa Zebida; alikuwa binti wa Pedaia wa Ruma.37Yehoyakimu akafanya yale yaliyo maovu usoni kwa BWANA, kama waliyoyafanya babu zake.

24

1Katika siku za Yehoyakimu, Nebukadreza mfalme wa Babeli akaiteka Yuda; Yehoyakimu akawa mtumishi kwa muda wa miaka mitatu. Kisha Yehoyakimu akarudi na kuasi dhidi ya Nebukadreza.2BWANA akatuma vikosi vya Wakaldayo dhidi ya Yehoyakimu, Washami, Wamoabu, na Waamoni; akawatuma dhidi ya Yuda kuiharibu. Hii ilikuwa ni kuthibitisha pamoja na neno la BWANA ambalo aliloliongea kupitia watumishi wake manabii.3Ilikuwa baada ya muda mfupi kwenye kinywa cha BWANA kwamba hili likaja juu ya Yuda, kuwaondoa usoni mwa uso wake, kwa sababu ya dhambi za Manase, yote aliyoyafanya,4na pia kwa sababu ya damu isiyokuwa na hatia aliyoimwaga, kwa kuijaza Yerusalemu kwa damu isiyokuwa na hatia. BWANA hakuwa tayari kusamehe hilo.

5Kama kwa mambo mengine yanayomuhusu Yehoyakimu, na yote aliyoyafanya, je hayajaandikwa kwenye kitabu cha matukio ya wafalme wa Yuda?6Yehoyakimu akalala pamoja na wazee wake, na Yekonia mtoto wake akawa mfalme katika sehemu yake.

7Mfalme wa Misri hakushambulia tena nje ya nchi yake, kwa sababu mfalme wa Babeli alikuwa amezishinda nchi zote ambazo zilikuwa zikitawaliwa na mfalme wa Misri, kutoka kwenye kijito cha Misri mpaka Mto wa Frati.

8Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na nane alipoanza kutawala; alitawala Yerusalemu miezi mitatu. Mama yake alikuwa anaitwa Nehushta; alikuwa binti wa Elnathani wa Yerusalemu.9Alifanya yaliyo maovu usoni mwa BWANA; alifanya yale yote ambayo baba yake aliyafanya.

10Katika kipindi hicho jeshi la Nebukadreza mfalme wa Babeli liliishambulia Yerusalemu na kuuzunguka mji.11Nebukadreza mfalme wa Babeli akaja kwenye mji wakati maaskari wake walipokuwa wameuzunguka,12na Yekonia mfalme wa Yuda akatoka nje kwenda kwa mfalme wa Babeli, yeye, mama yake, watumishi wake, watoto wake, na maafisa wake. Mfalme wa Babeli akamteka katika mwaka wa nane wa utawala wake.13Nebukadreza akachukua kutoka pale vitu vyote vya thamani katika nyumba ya BWANA, na walio katika nyumba ya kifalme. Akavikata vipande vipande vitu vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani mfalme wa Israeli alivitengeneza katika hekalu la BWANA, kama alivyokuwa amesema ingetokea.14Akawachukua wote utumwani Yerusalemu, viongozi wote, na wapiganaji wote, mateka elfu kumi, na mafundi wote, na wafua vyuma. Hakuna aliyekuwa amesalia isipokuwa watu masikini katika nchi.

15Nebukadreza akamchukua Yekonia utumwani Babeli, pia na mama yake na mfalme, wake, maafisa, na wakuu wa nchi. Akawachukua kwenda utumwani kutoka Yerusalemu mpaka Babeli.16Wapiganaji wote, 7,000 kwa hesabu, na mafundi 1,000 na wafua vyuma, wote wanaostahili kumpiga mfalme wa Babeli aliwaleta hawa watu kwenye utumwa Babeli.17Mfalme wa Babeli akamfanya Matania, kaka yake na baba yake na Yehokimu, mfalme katika sehemu yake, na kubadilisha jina lake kuwa Sedekia.

18Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja wakati alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Mama yake alikuwa anaitwa Hamutali; alikuwa binti wa Yeremia kutoka Libna.19Alifanya yaliyo maovu machoni mwa BWANA; aliyafanya yale yote ambayo Yehokimu aliyoyafanya.20Kupitia hasira ya BWANA, haya matukio yote yalitokea Yerusalemu na Yuda, hadi alipowaondoa kwenye uso wake. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.

25

1Ilitokea kwamba katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya huo mwezi, Nebukadreza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote kwa ajili ya kupigana dhidi ya Yerusalemu. Akaweka kambi kuelekeana nayo, na wakajenga ukuta kuizunguka.2Hivyo mji huo ulizungukwa mpaka miaka kumi na moja ya utawala wa Sedekia.3Katika siku ya tisa ya mwezi wa nne wa huo mwaka, njaa ilikuwa kali sana kwenye huo mji kwamba hapakuwa na chakula kwa ajili ya watu wa nchi.4Wakati huo ule mji ulikuwa umebomoka ndani, na wapiganaji wote wakakimbia usiku kwa njia ya lango kati ya kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme, ingawa Wakaldayo walikuwa wote wameuzunguka mji. Mfalme akaenda kuelekea upande wa Araba.5Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuata mfalme Sedekia na kumchukua katika tambarare ya bonde la Mto Yoradani karibu na Yeriko. Jeshi lake lote lilitawanyika wakamwacha.6Wakamkamata mfalme na kumleta mpaka kwa mfalme wa Babeli huko Ribla, ambapo walipitisha hukumu juu yake.7Wakawachinja watoto wake mbele ya macho yake. Kisha wakamtoa macho Sedekia, wakamfunga pingu, na kumpeleka hadi Babeli.

8Basi katika mwezi wa tano, katika siku ya saba ya mwezi, ambapo ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa Nebukadreza mfalme wa Babeli, Nebuzaradani, mtumishi wa mfalme wa Babeli na amri jeshi wa walinzi wake, wakaja hadi Yerusalemu.9Akaichoma moto nyumba ya BWANA, nyumba ya mfalme, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo la muhimu katika mji akayachoma,10kuta zote zilizoizunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli ambao walikuwa chini ya amri jeshi wa walinzi wakaziharibu.11Basi watu waliokuwa wamebaki ambao walikuwa wameondoka katika mji, wale waliokuwa wameasi kwa mfalme wa Babeli, na mabaki ya watu Nebuzadani, amiri jeshi wa mlinzi, wakachukuliwa kwenda utumwani.12Lakini amiri jeshi wa mlinzi aliwaacha baadhi ya maskini wa nchi ili wafanye kazi kwenye shamba la mizabibu na kulima.

13Na zile nguzo za shaba ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, na misimamio na bahari ya chuma ambayo ilikuwa kwenye nyumba ya Yahwe, Wakaldayo wakazivunja vipande vipande na kubeba shaba kuirudisha Babeli.14Masufuria, mabeleshi, makasi, vijiko, na vyombo vyote vya shaba ambavyo kuhani alivyokuwa amevitunza kwenye hekalu- Wakaldayo wakavichukua vyote.15Masufuria ya kuhamisha majivu na mabakuli ambayo yalikuwa yametengenezwa kwa dhahabu, na yale yaliyotengenezwa kwa fedha, yule nahodha wa mlinzi wa mfalme akavichukua pia.

16Zile nguzo mbili, ile bahari, na vile vitako ambavyo Sulemani alivitengeneza kwa ajili ya nyumba ya Yahwe shaba ya vyombo hivyo vyote haikuwa na uzani.17Urefu wa ile nguzo ya kwanza ulikuwa ridhaa kumi na nane, na kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Na urefu wa kichwa ulikuwa ridhaa tatu, pamoja na mapambo ya wavu na makomamanga yote yakizunguka kwenye hicho kichwa, vyote vilikuwa vimetengenezwa kwa shaba. Na ile nguzo nyingine ilikuwa vivyo hivyo kama ile ya kwanza pamoja na wavu wake.

18Yule amiri jeshi wa mlinzi akamchukua Seraya kuhani mkuu, pamoja za Sefania, yule kuhani wa pili, na walinzi watatu wa kwenye lango.19Kutoka mjini akamchukua mlinzi, afisa mmoja ambaye aliyekuwa msimamizi wa maaskari, na watu watano ambao walikuwa wakimshauri mfalme, ambao walikuwa bado katika mji. Pia alimchukua mfungwa wa afisa jeshi la mfalme, kwa ajili ya kuandika watu kwenye jeshi, pamoja na watu sitini muhimu kutoka hiyo nchi ambao walikuwa katika mji.20Kisha Nebuzaradani, amiri wa mlinzi, akawachukua na kuwapeleka kwa mfalme Babeli huko Ribla.21Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaiacha nchi yake kwenda utumwani.

22Na wale watu waliokuwa wamebakia katika nchi ya Yuda, wale ambao Nebukadreza mfalme wa Babeli aliwaacha, akamuweka Gedalia mwana wa Ahikamu, mwana wa Shafani, msimamizi wao.23Kisha wakati maamiri wote wa majeshi, wao na watu wao, waliposikia kwamba mfalme wa Babeli amemfanya Gedalia kuwa liwali, wakaenda kwa Gedalia huko Mispa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana wa Nethania, Yohanani mwana wa Karea, Seraya mwana wa Tanhumethi Mnetofa, na Yezania mwana wa Mmaaka wao na watu wao.

24Gedalia akafanya kiapo kwa watu wake na kuwaambia, “Msiwaogope Wakaldayo. Muishi katika nchi na kumtumikia mfalme wa Babeli, na itakuwa vema kwenu.”

25Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, kutoka familia ya kifalme, wakaja na watu kumi na kumshambulia Gedalia. Gedalia akafa, pamoja na watu wa Yuda na Wababeli ambao walikuwa pamoja nae huko Mizpa.26Kisha wale watu wote, kutoka chini kwenda juu, na maamiri wa jeshi, wakainuka na kwenda Misri, kwa sababu walikuwa wanawaogopa Wababeli.

27Ilitokea baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa utumwa wa Yekonia mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na saba ya mwezi, Evil-merodaki mfalme wa Babeli akamtoa Yekonia mfalme wa Yuda kutoka gerezani. Hii ilitokea katika mwaka ambao Evil-Merodaki alipoanza kutawala.28Akaongea naye kwa ukarimu na kumpatia kiti kizuri zaidi kuliko kile cha wafalme wengine ambao walikuwa pamoja naye Babeli.29Evil-Merodaki akamvua Yekonia nguo za gerezani,30na Yekinia akala siku zote kwenye meza ya mfalme katika maisha yake yote yaliyokuwa yamebakia.

1 Mambo ya nyakati

1

1Adamu, Sethi, Enoshi,2Kenani, Mahalaleli, Yaredi,3Henoko, Methusela, Lameki.4Wana wa Nuhu walikuwa ni Shemu, Hamu, na Yafethi.

5Wana wa Yafethi walikuwa ni Gomeri, Magogu, Madai, Yavani, Tubali, Mesheki, na Tirasi.
6Wana wa Gomeri walikuwa Ashkenazi, Rifathi na Togama.
7Wana wa Yavani walikuwa ni Elisha, Tarshishi, Kitimu, na Warodani.
8Wana wa Hamu walikuwa ni Kushi, Misri, Putu, na Kanaani.
9Wana wa Kushi walikuwa ni Seba, Havila, Sabta, Raama, na Sabteka. Wana wa Raama walikuwa ni Sheba na Dedani.
10Kushi akawa baba wa Nimrodi, aliyekuwa shujaa wa Kwanza katika dunia.
11Misri akawa babu wa Waludi, Waanami, Walehabi, Wanaftuhi,
12Wapathrusi, Wakasluhi (Wafilisti walipotoka), na Wakaftori.
13Kanaani akawa baba wa Sidoni, mwanae wa kwanza, na wa Hethi.
14Pia akawa babu wa Myebusi, Mwamori, Mgirgashi,15Mhivi, Mwarki, Msini,16Mwarvadi, Msemari, na Mhamathi.
17Wana wa Shemu walikuwa Elamu, Ashuru, Arfaksadi, Ludi, Aramu, Usi, Huli, Getheri, na Mesheki
18Arfaksadi akawa baba wa Sala, na Sala akawa baba wa Eberi.
19Eberi alikuwa na wana wawili wa kiume. Jina la wa kwanza lilikuwa Pelegi, kwa kuwa katika siku zake dunia ilikuwa imegawanyika. Jina la kaka yake lilikuwa Yoktani.
20Yoktani akawa baba wa Almodadi, Shelefu, Hasarmawethi, Yera,
21Hadoramu, Uzali, Dikla,22Obali, Abimaeli, Sheba,23Ofiri, Havila, na Yobabu; wote hawa walikuwa uzao wa Yoktani.
24Shemu, Arfaksadi, Shela,
25Eberi, Pelegi, Reu,26Serugi, Nahori, Tera,27Abramu, aliye kuwa Ibrahimu.
28Wana wa Ibrahimu walikuwa Isaka na Ishmaeli.
29Hawa ndio wanao: mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli alikuwa ni Nebayothi, kisha Kedari, Abdeeli, Mibsamu,
30Mishma, Duma, Masa, Hadadi, Tema,31Yeturi, Nafishi, na Kedem. Hawa ndio wana wa Ishamaeli.
32Wana wa Ketura, suria wa Ibrahimu, walikuwa Zimrani, Yokshani, Medani, Midiani, Ishbaki, na Shua. Wana wa Yokshani walikuwa Sheba na Dedani.
33Wana wa Midiani walikuwa Efa, Eferi, Hanoki, Abida, na Eldaa. Wote hawa walikuwa uzaowa Ketura.
34Ibrahimu akawa baba wa Isaka. Wana wa Isaka walikuwa Esau na Israeli.
35Wana wa Esau walikuwa ni Elifazi, Reueli, Yeushi, Yalamu, na Kora.
36Wana wa Elifazi walikuwa ni Temani, Omari, Sefo, Gatamu, Kenazi, Timna, na Amaleki.
37Wana wa Reueli walikuwa ni Nahathi, Zera, Shama, na Miza.
38Wana wa Seiri walikuwa ni Lotani, Shobali, Sebioni, Ana, Dishoni, Eseri, na Dishani.
39Wana wa Lotani walikuwa ni Hori na Hemamu, na Timna alikuwa dada yake Lotani.
40Wana wa Shobali walikuwa ni Alvani, Manahathi, Ebali, Shefo, na Onamu. Wana wa Sebeoni walikuwa ni Aya na Ana.
41Mwana wa Ana alikuwa ni Dishoni. Wana wa Dishoni walikuwa Hemdani, Eshbani, Ithrani, na Kerani.
42Wana wa Eseri walikuwa Bilhani, Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani walikuwa Usi na Arani.

43Hawa ndio wafalme walio tawala katika nchi ya Edomu kabla ya mfalme yeyote kuwatawala Waisraeli: Bela mwana wa Beori; na jina la mji wake ulikuwa Dinhaba.
44Bela alipo kufa, Yohabu mwana wa Zera wa Bosra akatawala badala yake.
45Yohabu alipo kufa, Hushamu wa nchi ya Watemani akatawala badala yake.
46Hushamu alipo kufa, Hadadi mwana wa Bedadi, aliye washinda Wamidiani katika uwanja wa Moabu, akatawa badala yake. Jina la mji wake ulikuwa Avithi.
47Hadadi alipo kufa, Samla wa Masreka akatawala badala yake.
48Samla alipo kufa, Shauli wa Rehobothi Hanahari akatawala badala yake.
49Shauli alipo kufa, Baal-Hanani mwana wa Akbori akatawala badala yake.
50Baal-Hanani mwana wa Akbori alipo kufa, Hadari akatawala badala yake. Jina la mji wake ni Pau. Jina la mke wake lilikuwa ni Mehetabeli binti wa Matredi binti wa Mezahabu.
51Hadadi akafa. Waku wa Edomu walikuwa Timna, Alva, Yethethi,52Oholibama, Ela, Pinoni,53Kenazi, Temani, Mibsari,54Magdieli, na Iramu. Hawa ndio walikuwa wakuu wa Edomu.

2

1Hawa ndio wana wa Israeli: Reubeni, Simioni, Lawi, Yuda, Isakari, Zebuloni,2Dani, Yusufu, Benyamini, Naftali, Gadi, na Asheri.

3Wana wa Yuda walikuwa Eri, Onani, na Shela, ambao walizaliwa na binti wa Shua, Wakanaani. Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa muovu katika macho ya Yahweh, na Yahweh akamuua
4Tamari, binti-mkwe wake, alimzalia Peresi na Zera. Yuda alikuwa na wana wa kiume wa tano.
5Wana wa Peresi walikuwa Hesroni na Hamuli.
6Wana wa Zera walikuwa Zimri, Ethani, Hemani, Kalikoli na Darda, wote kwa jumla ni watano.
7Mwana wa Karmi alikuwa ni Akani, aliye leta taabu katika Israeli alipo iba kile kilicho hifadhiwa kwa ajili ya Mungu.
8Mwana wa Ethani alikuwa Azaria.
9Wana wa Hezroni walikuwa ni Yerameeli, Ramu, na Kalebu.
10Ramu akawa baba wa Aminadabu, na Aminadabu akawa baba wa Nashoni, kiongozi miongoni wa uzao wa Yuda.
11Nashoni akawa baba wa Salmoni, na Salmon akawa baba wa Boazi.
12Boazi akawa baba wa Obedi, na Obedi akawa baba wa Yese.
13Yese akawa baba wa mzaliwa wake wa kwanza Eliabu, wa pili Abinadabu, wa tatu Shimia.
14Nethaneli wa nne, Radai wa tano.15Ozemu wa sita, na Daudi wa saba.
16Dada zao walikuwa Seruya na Abigaili. Wana wa Seruya walikuwa Abishai, Yoabu, na Asaheli, jumla watatu.
17Abigali akamzaa Amasa, ambaye baba yake alikuwa Yetheri Mwishmaeli.
18Kalebu mwana wa Hesroni akawa baba wa watoto wa Azubu mkewe, na Yeriothi. Wanawe walikuwa Yesheri, Shobabu, na Ardoni.
19Azuba akafa, na Kalebu akamuoa Efrathi, aliye mzalia Huri.20Huri akawa baba wa Uri, na Uri akawa baba wa Besaleli.
21Baadae Hesroni (alipo kuwa na miaka sitini) akamuoa binti wa Makiri, baba wa Gileadi. Akamzalia Segubu.
22Segubu akawa baba wa Yairi, aliye miliki miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi na Kenathi, pamoja na miji sitini iliyo zunguka. Hawa wakazi wote walikuwa ni uzao wa Makiri, baba wa Gileadi.
24Baada ya kifo cha Hesroni, Kalebu akalala na Efrata, mke wa baba yake Hesroni. Akamzalia Ashuri, baba wa Tekoa.
25Wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa ni Ramu mzaliwa wa kwanza, Buna, Oreni, Ozemu, na Ahiya.
26Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake lilikuwa Atara. Yeye alikuwa mama wa Onamu.
27Wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, Yamini, na Ekeri.
28Wana wa Onamu walikuwa ni Shamai na Yada. Wana wa Shamai walikuwa ni Nadabu na Abishuri.
29Jina la mke wa Abishuri lilikuwa Abihaili, na akamzalia Abani na Molidi.
30Wana wa Nadabu walikuwa Seledi na Apaimu, lakini Seledi alikufa pasipo watoto.
31Mwana wa Apaimu alikuwa Ishi. Mwana wa Ishi alikuwa Sheshani. Mwana wa Sheshani alikuwa Alai.32Wana wa Yada, kaka yake Shamai, walikuwa Yetheri na Yonathani. Yetheri alikufa pasipo mtoto.
33Wana wa Yonathani walikuwa Pelethi na Zaza. Hawa ndio uzao wa Yerameeli.
34Sasa Sheshani hakuwa na watoto wa kiume, bali wa kike pekee. Sheshani alikuwa na mtumishi, wa Kimisri, ambaye jina lake lilikuwa Yariha.
35Sheshani alimkabidhi binti yake kwa Yariha mtumishi wake kama mke wake. Akamzalia Atai.
36Atai akawa baba wa Nathani, na Nathani akawa baba wa Zabadi.
37Zabadi akawa baba wa Efalali, na Efalal akawa baba wa Obedi.
38Obedi akawa baba wa Yehu, na Yehu akawa baba wa Azaria.
39Azaria akawa baba wa Helesi, na Helesi akawa baba wa Eleasa.
40Eleasa akawa baba wa Sismai, na Sismai akawa baba wa Shalumu.
41Shalumu akawa baba wa Yekamia, na Yekamia akawa baba wa Elishama.
42Wana wa Kalebu, kaka yake Yerameeli, walikuwa ni Mesha mzaliwa wake wa kwanza, aliye kuwa baba wa Zifu. Mwanae wa pili, Maresha, allikuwa baba wa Hebroni.
43Wana wa Hebroni walikuwa Kora, Tapua, Rekemu, na Shema.44Shema akawa baba wa Rahamu, baba wa Yorkeamu. Rekemu akawa baba wa Shamai.
45Mwana wa Shamai alikuwa Maoni, na Maoni alikuwa baba wa Bethsuri.
46Efa, suria wa Kalebu, alimzaa Harani, Mosa, na Gazezi. Harani akawa baba wa Gazezi.
47Wana wa Yadai walikuwa Regemu, Yothamu, Geshani, Peleti, Efa, na Shaafa.
48Maaka, suria wa Kalebu, alimza Sheberi na Tirhana.
49Pia akamza Shaafu baba wa Madmana, Sheva baba wa Makbena na baba wa Gibea. Binti wa Kalebu alikuwa Aksa. Hawa walikuwa uzao wa Kalebu.
50Hawa walikuwa wana wa Huri, mzaliwa wake wa kwanza kwa Efratha: Shobali baba wa Kiriath-Yearimu.
51Salma babake Bethlehemu, na Harefu babake Beth- Gaderi.
52Shobali baba wa Kiriath Yearimu alikuwa na uzao: Haroe, nusu ya Wamenuthite,
53na ukoo wa Kiriath-Yearimu: Waithri, Waputhi, Washumathi, na Wamishrai. Wasorathi na Waeshtaoli walitoka huku.
54Ukoo wa Salma ulikuwa kama ufatao: Bethlehemu, Wanetofathi, Atroth-Beth-Yoabu, na nusu ya Wamanahathi Wazori,
55na ukoo wa waandishi walioishi Yabesi: Watirathi, Washimeathi, na Wasukathi. Hawa walikuwa Wakeni walio toka kwa Hamathi, baba wa nyumba ya Warekabu.

3

1Sasa hawa ndio wana wa Daudi waliozaliwa kwake huko Hebroni: mzaliwa wa kwanza alikuwa Amnoni, kwa Ahinoamu kutoka Yezreeli; wa pili alikuwa Danieli, kwa Abigaili kutoka Karmeli;2watatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa ni Maaka, binti wa Talmai mfalme wa Geshuri. Wanne alikuwa ni Adoniya mwana wa Hagithi;3watano alikuwa ni Shefatia kwa Abitali, wasita alikuwa ni Ithraeamu kwa Egla mkewe.

4Hawa sita walizaliwa kwa Daudi huko Hebroni, alipo tawala miaka saba na miezi sita. Kisha akatawala miaka thelathini na mitatu huko Yerusalemu.
5Hawa wana wa nne, kwa Bathishiba binti wa Amieli, walizaliwa kwake huko Yerusalemu: Shamua, Shobabu, Nathani, na Sulemani.
6Wana tisa wengine wa Daudi walikuwa ni: Ibhari, Elishua, Elipeleti,
7Noga, Nefegi, Yafia,8Elishama, Eliada na Elifeleti.
9Hawa walikuwa wana wa Daudi, pasipo kuwehesababu wana wa masuria wake. Tamari alikuwa dada yao.
10Mwana wa Sulemani alikuwa ni Rehoboamu. Mwana wa Rehoboamu alikuwa Abiya. Mwana wa Abiya alikuwa Asa. Mwana wa Asa alikuwa Yehoshafati.
11Mwana wa Yehoshafati alikuwa Yoramu. Mwana wa Yehoramu alikuwa Ahazia. Mwana wa Ahazia alikuwa Yoashi.
12Mwana wa Yoashi alikuwa Amazia. Mwana wa Amazia alikuwa Azaria. Mwana wa Azaria alikuwa Yothamu.
13Mwana wa Yothamu alikuwa Ahazi. Mwana wa Ahazi alikuwa Hezekia. Mwana wa Hezekia alikuwa Manase.
14Mwana wa Manase alikuwa Amoni. Mwana wa Amoni alikuwa Yosia.
15Wana wa Yosia aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza ni Yohana, wapili Yehoyakimu, mwanae watatu Sedekia, na mwanae wanne Shalumu.
16Wana wa Yehoyakimu walikuwa Yehoyakini na Sedekia.
17Wana wa Yehoyakini, mateka, walikuwa Shealtieli,
18Malkiramu, Pedaya, Shenezari, Yekamia, Hoshama, na Nedabia.
19Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Wana wa Zerubabeli walikuwa Meshulamu na Hanania; Shelomithi alikuwa dada yao.
20Wanawe wengine watano walikuwa Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia, na Yushabu Hesedi.
21Wana wa Hanania walikuwa Pelatia na Yeshaya. Mwanawe alikuwa Refaya, na uzao wake zaidi walikuwa ni Arnani, Obadia, na Shekania.
22Wana wa Shekania walikuwa Shemaya na wanawe: Hatushi, Igali, Baria, Nearia, na Shafati.
23Wana watatu wa Nearia walikuwa Elioenai, Hizekia, na Azrikamu.
24Wana saba wa Elioenai walikuwa Hodavia, Eliashibu, Pelaya, Akubu, Yohana, Delaya, na Anani.

4

1Uzao wa Yuda ulikuwa Peresi, Hesroni, Karmi, Huri, na Shobali.

2Reaya, mwana wa Shobali alikuwa baba waYahathi. Yahathi alikuwa baba wa Ahumai na Lahadi. Hawa walikuwawa koo za Wasorathi.
3Hawa walikuwa wana wa Etamu: Yezreeli, Ishma, na Idbashi. Dada yao alikuwa Haselelponi.
4Penueli alikuwa mwanzilish wa Gedori. Ezeri alikuwa mwanzilishi wa Husha. Hawa walikuwa uzao wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, na muanzilishi wa Bethelehemu.
5Ashuri baba wa Tekoa alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.
6Naara alimzalia Ahuzamu, Heferi, Temeni na Ahashtari. Hawa walikua wana wa Naara.
7Wana wa Hela walikua Serethi, Sohari, Ethnani,
8na Kozi, aliyekua baba wa Anubu na Hasobeba, na koo zilizotoka kwa Aharheli mwana wa Harumu.

9Yabesi aliheshimika zaidi ya kaka zake. Mama yake alimuita Yabesi. Alisema, “Kwa sababu nimemzaa katika uchungu10Yabesi akamuita Mungu wa Israeli na kusema, “Laiti ungenibanibariki kweli, upanue eneo langu, na mkono wako ukuwe jpamoja nami. Ukifanya hivi utaniepusha na madhara, ili kwamba niwe huru na huzuni!” Kwa hivyo Mungu akamjalia maombi yake.
11Kelubu kaka wa Shuha akawa baba wa Mehiri, aliyekuwa baba wa Eshtoni.
12Eshtoni akawa baba wa Beth-Rafa, Pasea, na Tehina, ambaye alianzisha mji wa Iri Nahashi. Hawa ni wanaume walioishi Reka.
13Wana wa Kenazi walikua Othinieli na Seraia. Wana wa Othinieli walikuwa Hathathi na Meonothai.
14Meonothai akawa baba wa Ofara, na Seraia akawa baba wa Yohabu, mwanzilishi wa Ge Harashimu, ambao watu wake walikua wahunzi.15Wana wa Kalebu mwana wa Yefune walikua Iru, Ela na Namu. Mwana wa Ela alikua Kenazi.
16Wana wa Yehaleli walikua Zifi, Zifa, Tiriya, na Azareli.
17Wana wa Ezra walikua Yetheri, Meredi, Eferi, na Yaloni.
18Mke wake Meredi wa Kimisri alishika mimba na kuwazaa Miriamu, Shamai, na Ishiba, aliyekua baba wa Eshitemoa. Hawa walikua wana wa Bithia, binti wa Farao, ambaye Meredi alimuoa. Mke wa Kiyahudi wa Meredi alimzaa Yeredi ambaye alikua baba wa Gedore; Heberi, aliyekua baba wa Soko; na Yekuthieli aliyekua baba wa Zanoa.
19Kati ya wana wawili wa mke wa Hodia, dadake Nahamu, mmoja wao akawa baba wa Keila Mgarimi. Mwingine alikua Eshitemoa Mmakathi
20Wana wa Shimoni walikua Amnoni, Rina, Beni Hanani, na Tiloni. Uzao wa Ishi walikua Zohethi na Beni-Zohethi.
21Uzao wa Shela mwana wa Yuda, ulikua ni Eri baba wa Leka, Laada baba wa Maresha na koo za wafanyakazi wa kushona kule Beth Ashbea,
22Yoakimu, wanaume wa Kozeba, na Yoashi na Sarafi, aliyekuwa na mamlaka huko Moabu na Yashubi Lehemu. Maelezo haya yametoka kwenye nakala za zamani.)23Hawa walikuwa ni wafinyanzi walioishi Netaimu na Gedera na kufanya kazi kwaMfalme.
24Uzao wa Simeoni ulikua Nemueli, Yamini, Yaribu, Zera, na Shauli.
25Shalumu alikua mwana wa Shauli, Mibisamu alikua mwana wa Shalumu, na Mishima alikua mwana wa Mibisamu.
26Ukoo wa Mishima ulikua Hamueli mwana wake, Zakuri mjukuu wake, na Shimei kitukuu chake.

27Shimei alikua na wana kumi na sita na mabinti sita. Kaka zake hawakuwa na watoto wengi, Kwa hiyo koo zao hazikuongezeka sana kwa kama watu wa Yuda walivyoongezeka.28Waliishi Beasheba, Molada, na Hazari Shuali.29Pia waliishi Bilha, Ezemu, Toladi,30Bethueli, Horma, Zikilagi,31Bethi Markabothi, Hazari Susimi, Bethi Biri, na Shaaraimu. Hii ilikua miji yao mpaka wakati wa utawala wa Daudi.32Vijiji vyao vitano vilikua Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani,33pamoja na vijiji vya kando mpaka Balith Haya yalikua makazi yao, na walitunza kumbukumbu za uzao wao.

34Viongozi wa ukoo walikua Meshobabu, Yamileki, Yoshahi mwana wa Amazia,35Yoeli, Yehu mwana wa Yoshibia mwana wa Seraia mwana wa Asieli,36Elioenai, Yaakoba, Yeshohaia, Asaia, Adieli, Yesimieli, Benaia,37na Ziza mwana wa Shifi mwana wa Aloni mwana wa Yedaia mwana wa Shimiri mwana wa Shemaia.38Hawa walio orodheshwa kwa majina walikua viongozi wa koo zao, na koo zao ziliongezeka sana.39Walienda karibu na Gedori, upande wa mashariki wa bonde, kutafuta malisho ya mifugo yao.40Walipata malisho mengi na mazuri. Nchi ilikua tambarare, tulivu na ya amani. Wahamu waliishi hapo awali.41Hao walio orodheshwa hapo kwa majina walikuja katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda, na wakashambulia makazi ya Wahamu na Wameuni, ambao pia walikua hapo. Waliwaangamiza kabisa na kuishi hapo sababu walipata malisho kwa ajili ya mifugo yao.

42Wanaume mia tano wa kabila la Simeoni walienda katika mlima Seiri, pamoja na Pelatia, Nearia, Refaia, na Uzieli, wana wa Ishi, kama kiongozi wao.43Waliwashinda wakimbizi wa Waamaleki waliobakia, na wakaishi hapo hadi siku hii.

5

1Wana wa Rubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli - sasa Rubeni alikuwa mzaliwa wa kwanza wa Israeli, lakini haki yake ya mzaliwa wa kwanza ilipewa kwa wana wa Yusufu mwana wa Israeli kwa sababu Rubeni alinajisi kochi la baba yake. Kwa hivyo hajaandikwa katika nasaba kuwa ana haki ya mzaliwa wa kwanza.2Yuda ndiye alikuwa na nguvu kati ya ndugu zake, na kiongozi angetoka kwake. Lakini haki ya mzaliwa wa kwanza ilikuwa ya Yusufu -3wana wa Rubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli alikuwa Hanoki, Palu, Hezroni, na Karmi.

4Uzao wa Yoeli ulikuwa huu: Mwana wa Yoeli alikuwa Shemaia. Mwana wa Shemaia alikuwa Gogi. Mwana wa Gogi alikuwa Shimei.
5Mwana wa Shimei alikuwa Mika. Mwana wa Mika alikuwa Reaia. Mwana wa Reaia alikuwa Baali.6Mwana wa Baali alikuwa Bera, ambaye Tiligathi Pileseri alimpeleka matekani kule Assiria. Bera alikuwa kiongozi katika kabila la Rubeni.
7Ndugu zake kwa na koo zao, walioandikishwa katika nasaba kwa vizazi vyao: Yeieli kiongozi, Zekaria,
8na Bela mwana wa Azazi mwana wa Shema mwana wa Yoeli. Waliishi Aroeri, kwa umbali wa Nebo na Baali Meoni,9na kuelekea mashariki hadi mwanzo wa jangwa linaloendelea hadi Mto Efarati, kwa sababu mifugo yao ilikuwa imeongezeka katika nchi ya Gileadi.
10Katika siku za Sauli, kabila la Rubeni lilishambulia Wahagiri na kuwashindaWakaishi ndani ya hema za Wahagiri katika nchi yote mashariki mwa Gileadi.
11Watu wa kabila la Gadi waliishi karibu nao, katika nchi ya Basha Saleka.
12Yoeli alikuwa kiongozi wao, Shafamu alikuwa wa pili na Yanai na Shafati walikuwa wa Bashani.
13Ndugu zao, kwa koo zao, walikuwa Mikaeli, Meshulamu, Sheba, Yorai, Yakani, Sia na Eberi - jumla saba wote.
14Hawa watu walio tajwa hapo juu ni uzao wa Abihaili, na Abihaili alikuwa mwana wa Huri. Huri alikuwa mwana wa Yaroa. Yaroa alikuwa mwana wa Gileadi. Gileadi alikuwa mwana wa Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Yeshishai. Yeshishai alikuwa mwana wa Yado. Yado alikuwa mwana wa Buzi.
15Ahi mwana wa Abidieli mwana wa Guni, alikuwa kichwa cha ukoo wao.
16Waliishi Gileadi, Bashani, katika miji yake, na katika nchi zote za malisho ya Sharoni kwa umbali wa mipaka yake.
17Hawa wote waliorodheshwa katika nakaka za uzao katika siku za Yothamu mfalme wa Yuda na Yeroboamu mfalme wa Israeli.

18Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase walikuwa na wana jeshi 44,760 walio fuzu kwa vita, walio beba ngao na upanga, na waliovuta upinde, ambao wangewezakwenda vitani.19Waliwashambulia Wahagiri, Yeturi, Nafishi, na Nodabu.20Walipokea msaada wa kiungu dhidi yao. Katika hili Wahagiri na wote walio kuwa nao walishindwa. Hii ni kwa sababu Waisraeli walipaza sauti katika vita, na yeye akawajibu, kwa sababu waliweka tumaini lao kwake.21Walikamata wanya wao, pamoja na ngamia elfu hamsini, kondoo 250,000, punda elfu mbili, na wanaume 100,000.22Kwa sababu Mungu aliwapigania, waliua maadui wengi. Waliishi katika nchi yao mpaka nyakati za kuwekwa utumwani.

23Wana wa nusu ya kabila la Manase waliishi katika nchi ya Bashani kwa umbali wa Bali Hermoni na Seniri (hiyo ni, Mlima Hermoni).

24Hawa walikuwa viongozi wa koo zao: Eferi, Ishi, Elieli, Azrieli, Yeremia, Hodavia, na Yahdieli. Walikuwa mashujaa hodari, wanaume mashuhuri, viongozi wa familia zao.25Lakini walikuwa sio waaminifu kwa Mungu wa babu zao. Walifanya uzinzi na miungu ya watu wa hiyo nchi, ambao Mungu aliwaangamiza mbele yao.26Mungu wa Israeli akamchochea Puli mfalme wa Assiria (ambaye pia uitwa Tiligathi Pileseri, mfalme wa Assiria). Aliwapeleka matekani Warubeni, Wagadi, na nusu ya kabila la Manase. Aliwaleta kwa Hala, Habori, Hara, na kwenye mto wa Gozani, ambapo wapo hadi leo.

6

1Wana wa Levi walikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.

2Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
3Wana wa Amramu walikuwa Aruni, Musa, Miriamu. Wana wa Aruni walikuwa Nadabu, Abihu, Eleazari, na Ithamari.
4Eleazari akawa baba wa Finehasi, na Finehasi akawa baba wa Abishua.
5Abishua akawa baba wa Buki, na Buki akawa baba wa Uzi.
6Uzi akawa baba wa Zerahia, na Zerahia akawa baba wa Meraioti.
7Meraioti akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
8Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Ahimazi.
9Ahimazi akawa baba wa Azaria, na Azaria akawa baba wa Yohanani.
10Yohanani akawa baba wa Azaria, aliye hudumu katika hekalu alilo lijenga Sulemani ndaniya Yerusalemu.
11Azaria akawa baba wa Amaria, na Amaria akawa baba wa Ahitubi.
12Ahitubi akawa baba wa Zadoki, na Zadoki akawa baba wa Shalumu.
13Shalumu akawa baba wa Hilikia, na Hilikia akawa baba wa Azaria.
14Azaria akawa baba Seraia, na Seraia akawa baba wa Yehozadaki.
15Yehozadaki akaenda matekani Yahweh alipo wapeleka utumwani Yuda na Yerusalemu kwa mkono wa Nebukadneza.
16Wana wa Levi walikuwa Gerishomu, Kohathi, na Merari.
17Wana wa Gerishomu walikuwa Libini na Shimei.
18Wana wa Kohathi walikuwa Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
19Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Hawa walikuwa koo za Walawi kwa familia za baba zao.
20Uzao wa Gerishomu ulianza na mwanae Libini. Mwana wa Libini alikuwa Jahathi. Mwanae alikuwa Zima.
21Mwanae alikuwa Yoa. Mwanae alikuwa alikuwa Ido. Mwanae alikuwa Zera. Mwanae alikuwa Yeatherai.
22Uzao wa Kohathi ulianza na mwanae Aminadabu. Mwanae alikuwa Kora. Mwanae alikuwa Asiri.
23Mwanae alikuwa Elikana. Mwanae alikuwa Ebiasa. Mwanae alikuwa Asiri.
24Mwanae alikuwa Tahathi. Mwanae alikuwa Urieli. Mwanae alikuwa uzia. Mwanae alikuwa Shauli.
25Wana wa Elikana walikuwa Amasai, Ahimothi
26Elikana mwanawe, Zofai mwanae, Nahathi mwanawe,
27Eliabu mwanawe, Yehoramu mwanawe na Elikana mwanawe.
28Wana wa Samwali walikuwa mzaliwa wa kwanza, Yoeli, na Abija, wa pili.
29Mwana wa Merari alikuwa Mahili. Mwanae alikuwa Libini.
30Mwanae alikuwa Shimei. Mwanae alikuwa Uza. Mwanae alikuwa Shimea. Mwanae alikuwa Hagia. Mwana alikuwa Asaia.

31Haya ndio majina ya wanaume ambao Daudi waliwaeka kusimamia muziki katika nyumba ya Yahweh, baada ya sanduku kuja hapo.32Walitumika kwa kuimba mbele ya hema, hema la kukutania, mpaka Sulemani alipo jenga nyumba ya Yahweh ndani ya Yerusalemu. Walikamilisha wajibu wao kwa kadiri ya maelekezo waliopewa.

33Hawa walitumika pamoja na wana wao. Katika makabila ya Wakohathi alitoka Hemani mwana muziki. Babu zake walikuwa hawa, kurudi nyuma ya wakati: Hemani alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Samweli.
34Samweli alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yerohamu. Yerohamu alikuwa mwana wa Elieli. Elieli alikuwa mwana wa Toa.
35Toa alikuwa mwana wa Zufi. Zufi alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Mahathi. Mahathi alikuwa mwana wa Amasai. Amasai alikuwa mwana wa Elikana.
36Amasai alikuwa mwana wa Elikana. Elikana alikuwa mwana wa Yoeli. Yoeli alikuwa mwana wa Azaria. Azaria alikuwa mwana wa Zefania.
37Zefania alikuwa mwana wa Tahathi. Tahathi alikuwa mwana wa Asiri. Asiri alikuwa mwana wa Ebiasa. Ebiasa alikuwa mwana wa Kora.
38Kora alikuwa mwana wa Izhari. Izhari alikuwa mwana wa Kohathi. Kohathi alikuwa mwana wa Lawi. Lawi alikuwa mwana wa Israeli.
39Mfanyakazi mwenzake Hemani alikuwa Asafu, aliye simama mkono wake wa kuume. Asafu alikuwa mwana Berekia. Berekia alikuwa mwana wa Shimea.
40Shimea alikuwa mwana Mikaeli. Mikaeli alikuwa mwana wa Baaseia. Baaseia alikuwa mwana wa Malikiya.
41Malikiya alikuwa mwana wa Ethini. Ethini alikuwa mwana wa Zera. Zera alikuwa mwana wa Adaia.
42Adaia alikuwa mwana wa Ethani. Ethani alikuwa mwana wa Zima. Zima alikuwa mwana wa Shimei.
43Shimei alikuwa mwana wa Yahathi. Yahathi alikuwa mwana wa Gerishomu. Gerishomu alikuwa mwana wa Lawi.
44Upande wa mkono wa kushoto wa Hemani walikuwa wafanyi kazi wa wana wa Merari. Alikuwa Ethani mwana wa Kishi. Kishi alikuwa mwana wa Abdi. Abdi alikuwa mwana wa Maluki.
45Maluki alikuwa mwana wa Hashabia. Hashabia alikuwa mwana wa Amazia. Amazia alikuwa mwana wa Hilikia.
46Hilikia alikuwa mwana wa Amzi. Amzi alikuwa mwana wa Bani. Bani alikuwa mwana wa Shemeri.
47Shemeri alikuwa mwana wa Mahili. Mahili alikuwa mwana wa Mushi. Mushi alikuwa mwana wa Merari. Merari alikuwa mwana wa Lawi.

48Washirika wao, Walawi, walipewa kazi yote ya hema, nyumba ya Mungu.

49Aruni na wana wake walitoa sadaka katika madhabahu kwa ajili ya sadaka za kuteketeza; na sadaka katika madhabahu ya uvumba kwa kazi zote katika pa patakatifu. Hizi sadaka zilifanya maombezi kwa ajili ya Waisraeli, kwa kadiri ya yote ambayo Musa mtumishi wa Mungu aliwaamuru.
50Uzao wa Aruni una kumbukwa kama ifuatavyo: Mwana wa Aruni alikuwa Eleazari. Mwana Eleazari alikuwa Finehasi. Mwana wa Finehasi alikuwa Abishua.
51Mwana wa Abishua alikuwa Buki. Mwana wa Buki alikuwa Uzi. Mwana wa Buki alikuwa Zerahia.
52Mwana wa Zerahia alikuwa Meraiothi. Mwana wa Meraiothi alikuwa Amaria. Mwana wa Amaria alikuwa Ahitubi.
53Mwana wa Ahitubi alikuwa Zadoki. Mwana wa Zadoki alikuwa Ahimazi.

54Hizi ni sehemu ambazo wazao wa Aruni walipangiwa kuishi, wazao wa Aruni ambao walitoka katika koo za Wakohathi (maeneo ya kwanza yalikuwa yao).55Walipewa Hebroni katika nchi ya Yuda na nchi ya malisho,56lakini maeneo ya mji na vijiji alipewa Kalebu mwana wa Yefune.57Kwa wazao wa Aruni waliwapa: Hebroni (mji wa makimblio), na Libina pamoja na nchi ya malisho, Yatiri, Eshitemoa pamoja na nchi ya malisho,58Hileni pamoja na nchi ya malisho, na Debiri pamoja na nchi ya malisho.59Na Ashani pamoja na nchi ya malisho na Bethi Shemeshi pamoja na nchi ya malisho;60na kutoka katika kabila la Benjamini walipewa Geba pamoja na nchi ya malisho, Alemethi pamoja na nchi ya malisho, na Anothothi na nchi ya malisho. Jumla ya miji yao ilikuwa kumi na tatu.

61Kwa mwengine wa Kohathi waliwapa kwa sehemu miji kumi kutoka kwa kabila la Manase.

62Kwa uzao wa Gerishomu kwa koo zao tofauti walipewa miji kumi na tatu kutoka kwa makabila ya Isakari, Asheri, Naftali, na nusu ya kabila la Manase huko Bashani.

63Kwa uzao wa Merari walipewa miji kumi, kulingana na koo zao, kutoka kwa makabila ya Rubeni, Gadi, na Zebuluni.

64Hivyo watu wa Israeli walitoa hii miji pamoja na nchi za malisho kwa Walawi.65Waligawa kwa kura miji iliyo tajwa kwa majina kutoka katika kabila za wana wa Yuda, Simeoni, na Benjamini.

66Kwa baadhi ya koo za Wakohathi walitoa miji kutoka kwa kabila la Efraimu.67Waliwapa: Shekemu (mji wa makimbilio) pamoja na nchi ya malisho katika milima ya Efraimu, Gezeri na nchi ya malisho,68Jokimeamu pamoja na nchi ya malisho, Bethi Horoni pamoja na nchi ya malisho,69Aiyaloni pamoja na nchi ya malisho, na Gathi Rimoni pamoja na nchi ya malisho.70Nusu ya kabila la Manase waliwapa Wakohathi: Aneri pamoja na nchi ya malisho na Bileamu pamoja na nchi ya malisho. Hizi zikawa mali za koo za Wakohathi.

71Kwa uzao wa Gerishomu kutoka koo za nusu ya kabila la Manase, waliwapa: Golani huko Baashani na nchi ya malisho na Ashitarothi pamoja na nchi ya malisho.
72Kabila la Isakari liliwapa uzao wa Gerishomu: Kedeshi pamoja na nchi ya malisho, Dabera pamoja na nchi ya malisho,
73Ramothi pamoja na nchi ya malisho, na Anemu pamoja na nchi ya malisho.
74Isakari alipokea kutoka kwa kabila la Asheri: Mashali pamoja na nchi ya malisho, Abdoni pamoja na nchi ya malisho,
75Hukoki pamoja na nchi ya malisho, na Rehobu pamoja na nchi ya malisho.
76Walipokea kutoka kabila la Naftali: Kedeshi iliyo Galileya pamoja na nchi ya malisho, Hamoni pamoja na nchi ya malisho, na Kiriathaimu pamoja na nchi ya malisho.
77Wazao wengine wa Merari walipokea kutoka Kwa kabila la Zebuluni: Yokineamu, Karita na Rimono pamoja na nchi ya malisho na Tabori pamoja na nchi ya malisho;
78na kutoka kabila la Rubeni upande wa pili wa Yordani upande wa mashariki wa Yeriko, walipokuwa Bezeri katika jangwa, Yahza,
79Kedemothi pamoja na nchi ya malisho, na Mefathi pamoja na nchi ya malisho
80Walawi walipokea kutoka kabila la Gadi: Ramothi ya Gileadi pamoja na nchi ya malisho, Mahanaimu pamoja na nchi ya malisho,
81Heshiboni pamoja na nchi ya malisho, na Yazeri pamoja na nchi ya malisho.

7

1Wana wanne wa Isakari walikuwa Tola, Pua, Yashubi, na Shimironi.

2Wana wa Tola walikuwa Uzi, Refaia, Yerie, Yamai, Ibisami, Samueli. Walikua vichwa katika nyumba za koo zao, toka uzao wa Tola na waliorodheshwa kama mashujaa hodari miongoni mwa kizazi chao. Katika siku za Daudi walikua na idadi ya 22,600.
3Mwana wa Uzi alikua Izrahia. Mwana wake walikua Michaeli, Obadia, Yoeli, na Ishia, wote watano walikua viongozi wa ukoo
4Pamoja nao walikua na jeshi la watu elfu thelathini na sita wa mapambano, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao, kwa kuwa walikuwa na wake wengi pamoja na wana wa kiume.
5Ndugu zao kutoka koo zote za Isakari, walikua na mashujaa hodari themanini na saba, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
6Wana watatu wa Benjamini walikuwa Bela, Beka, na Yediaeli.
7Wana watano wa Bela walikuwa Ezibono, Uzi, Uzieli, Yerimoti, na Iri. Walikua ni viongozi wa koo na mashujaa hodari. Walikuwa na idadi 22,034, kwa mujibu wa orodha zilizomilikiwa na koo za mababu zao.
8Wana wa Beka walikuwa Zemira, Yoashi, Elieza, Elionai, Omri, Yeremoti, Abiya, Anatoti, na Alemeti. Wote hawa walikuwa wana wake.
9Orodha ya koo zao ilikua na idadi ya 20,200 viongozi wa koo zao mashujaa hodari.
10Mwana wa Yediaeli alikuwa Bilhani. Wana wa Bilhani walikuwa Yeushi, Benjamini, Ehudi, Kenaana, Zetani, Tarishishi, na Ahishahari.
11Wote hawa waikuwa wana wa Yediaeli. Waliorodheshwa katika ukoo orodha ilikuwa 17,200 viongozi wa nyumba na mashujaa hodari waliofa kwa huduma ya kijeshi.
12Shupimu na Hupimu walikuwa waza wa Iri, na Hushimu walikuwa wazao wa Aheri.
13Wana wa Naftali walikuwa Yazieli, Guni, Yezeri, na Shilemu, wazao wa Bilhahi.
14Wazao wa Manasse walikua Asrieli, liyekuwa uzao wake kupitia suria wake wa Kiaramia. (Pia alimzaa Makiri, baba wa Gileadi.
15Kisha Makiri alimchukua mke wake kutoka kwa Hupimu na Shupimu na jinala dada yake lilikuwa Maaka.) Jina la wa pili ilikuwa Zelofehadi, ambaye alikuwa na mabinti pekee.
16Kisha Maaka, mke wa Makiri, alimzaa mwana wa kiume na alimuita Pereshi, na jina la Kaka yake lilikua Shereshi, na wana wake walikuwa Ulamu na Rakemu.
17Mwana wa Ulami alikuwa Bedani. Hawa walikuwa uzao wa Gileadi mwana wa Makiri mwana wa Manase.
18Dada wa Gileadi Hamoleketi alimzaa Ishihodi, Abiezeri, na Mahila.
19Wana wa Shemida walikuwa Ahiana, Shekemu, Liki, na Aniamu.
20Uzao wa Efraimu ulikuwa kama ifuatavyo: Efraimu mwana wa Shutela. Shutela mwana wa Beredi. Beredi mwana wa Tahati.
21Tahati mwana wa Eleada. Eleada mwana wa Shutela. Eza na Eleadi waliuawa na wanaume wa Gati, wenyeji wa nchi, walipoenda kuiba mifugo yao.
22Efraimu baba yao aliomboleza kwa siku nyingi, na kaka zake walikuja kumfariji.
23Alilala na mkewe. Akapata mimba akamzaa mwana. Efraimu akamuita Beria, kwa sababu maafa yalishakuja nyumbani mwake.
24Binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga miji juu na chini Beth Horon na Uzzen Sheerah.
25Mwana wake alikuwa Rafa. Mwana wa Rafa alikuwa Reshefi. Mwana wa Reshafi alikuwa Tela. Mwana wa Tela alikuwa Tahani.
26Mwana wa Tahani alikuwa Ladani. Mwana wa Ladani alikuwa Amihudi. Mwana wa Amihudi alikuwa Elishama.
27Mwana wa Elishama alikuwa Nuni. Mwana wa Nuni alikuwa Joshua.

28Mali zao na makazi yao yalikuwa Betheli na yalizungukwa na vijiji. Waliongeza upande wa mashariki hadi Naarani na upande wa magharibi hadi Gezeri na vijiji vyake, na Shekemu na vijiji vyake hadi Aya na vijiji vyake.
29Katika mipaka pamoja na Manasse kulikuwa na Beti shani na vijiji vyake, Taanaki na vijiji vyake, Megido na vijiji vyake, na Dori na vijiji vyake. Katika huu mji waliishi uzao wa Josefu mwana wa Israeli.
30Wana wa Asha walikuwa Imna, Ishiva, Ishivi, na Beria. Sera alikuwa dada yao.
31Wana wa Beria walikuwa Heberi na Malchieli, Ambaye alikuwa baba wa Birzaiti.
32Wana wa Heberi walikuwa Yafeti, Shomer, na Hotamu. Dada yao alikuwa Shua.
33Wana wa Yafeti walikuwa Pasaki, Bimhali, na Ashivati. Hawa walikuwa watoto wa yafeti.
34Shoma, kaka wa Yafeti alikuwa na wana hawa: Roga, Huba, na Aramu
35Kaka yake Shema, Helemu, alikuwa na wana hawa: Zofa, Imna, Sheleshi na Amali.
36Wana wa Zofa walikuwa Sua, Harinefa, Shua, Beri, Imra
37Beza, Hodi, Shamma, Shilsha, Ithrani, na Beera.
38Wana wa Yeta walikuwa Yefune, Pispa, na Ara.
39Wana wa Ulla walikwa Ara, Hannieli, na Rizia.

40Hawa wote walikuwa uzao wa Asha. Walikuwaviongozi wa koo, wanaume mashuhuri, mashujaa hodari, na wakuu kati ya viongozi. Kulikuwa na wanaume elfu ishirini na sita walioorodheshwa waliofaa kwa utumishi ya kijeshi, kwa mujibu wa idadi iliyo orodheshwa.

8

1Wana watano wa Benjamini walikuwa Bela mwana wake wa kwanza, Asibeli, Ahara,2Noha, na Rafa.

3Wana wa Bela walikuwa Adari, Gera, Abihudi,
4Abishau, Naamani, Ahoa,5Gera, Shefufani, na Huramu.
6Hawa walikuwa uzao wa Ehudi ambao walikuwa vichwa vya koo kwa wakazi wa Geba, ambao walihimizwa kuhamia Manahati:
7Naamani, Ahijahi, na Gera. Wa mwishi, Gera, aliwaongoza katika kuhama. Alikuwa baba wa Uza na Ahihudi.
8Shaharaimu akawa baba wa watoto katika ardhi ya Moabu, baada ya kuwatariki wake zake Hushimu na Baara.
9Kwa mke wake Hodeshi, Shaharaimu akawa baba wa Yobabu, Zibia, Mesha, Malkamu,10Yeuzi, Shachia, na Mirima. Hawa walikuwa wana wake, viongozi katika koo zao.11Alikwisha kuwa baba wa Abitubi, na Elipaali kwa Hushimu.
12Wana wa Elipaali walikuwa Eba, Mishamu, na Shemedi (ambao walijenga Ono na Lodi pamoja na vijiji vilivyozunguka.)
13Pia walikuwako Beria na Shema. Walikuwa vichwa vya nyumba za baba zao wa walioishi Aijaloni, ambao waliwaondoa wakazi wa Gati.
14Beria alikuwa na wana watatu: Ahio, Shashaki, Yeremothi,
15Zebadia, Aradi, Eda,16Mikaeli, Ishipa, na Joha
17walikuwa wa na wa Beria Zebadia, Meshulamu, Hiziki, Heba,
18Ishimerai, Izilia, na Yobabu walikuwa wana wa Elipaali.
19Yokimu, Zikri, Zabdi,
20Elienai, Zilletai, Elieli,21Adaia, Beraia, na Shimrati walikuwa wana wa Shimei.
22Ishipani, Eba, Elieli,
23Abdoni, Zikri, Hanani,24Hanania, Elamu, Antothiya,25Ifdeia, na Penueli walikuwa wana wa Shashaki.
26Shamsherai, Sheharia, Athalia,
27Yaareshia, Eliya, na Zikri walikuwa wana wa Yerohamu.

28Hawa walikuwa vichwa vya koo- kwa mujibu wa kumbukumbu za koo zao walikuwa vichwa. Walikuwa wanaume wakuu walioishi Yerusalemu.
29Baba wa Gibeoni, Jeieli, ambaye mke wake aliitwa Maaka, aliishi ndani ya Gibeoni.
30Mzaliwa wake wa kwanza wa kiume alikuwa Abdoni, akafuatiwa na Zuri, Kishi, Baali, Nadabu31Gedori, Ahio, na Zekari.
32Mwana mwingine wa Yeieli alikuwa Mikloti, ambaye akaja kuwa baba wa Shimea. Pia wanaishi karibu na ndugu zao Yerusalemu.
33Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, Malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
34Mwana wa Yonathani alikuwa Meribu Baali. Meribu Baali alikuwa baba wa Mika.
35Wana wa Mika walikuwa Pithoni, Meleki, Tarea, and Ahazi.
36Ahazi akawa baba wa Yehoada. Yehoada alikuwa baba wa Amelethi, Azimavethi, na Zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
37Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Rafa. Rafa alikuwa baba wa Eleasa. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
38Azeli alikuwa na wana sita: Azrikamu, Bokeru, Ishimaeli, Obadia, na Hanani. Wote hawa walikuwa wana wa Azeli.
39Wana wa Esheki, kaka yake, walikuwa Ulamu mzaliwa wake wa kwanza, Yeushi wa pili, na Elifeleti wa tatu.
40Wana wa Ulamu walikuwa wanaume wa mapambano na warusha mishale wa zuri. Walikuwa na wana wengi na wajukuu, jumla ya 150. Wote hawa walikuwa uzao wa Benjamini.

9

1Kwa hivyo watu wote wa Israeli walinakiliwa ki uzao. Walinakiliwa katika vitabu vya kifalme vya Israeli. Yuda, walipelekwa matekani Babylon kwasababu ya dhambi zao.2Wakwanza kurudi kuishi katika miiji yao walikuwa Waisraeli, Makuhani, Walawi, na Watumishi wa hekalu.

3Baadhi ya uzao wa Yuda, Benjamin, Efraimu, na Manase waliishi Yerusalemu.
4Wahamiaji walijumusha Uthai mwana wa Ammihudi mwana wa Omri mwana wa Bani, moja ya uzao wa Perezi mwana wa Yuda.
5Kati ya Washilani kulikuwa na Asaia mtoto wa kwanza na wana wake.
6Kati ya uzao wa Zera alikuwa Yeuli. Uzao wao ulikuwa na namba 690.
7Katika uzao Benjamini walikuwa Salu mwana wa Meshulamu mwana wa hodavia mwana wa Hssenua.
8Pia walikuwa Ibneia mwana wa Yerohamu; Ela mwana wa Uzzi mwana wa Mikri; na Meshullam mwana wa Shefatia mwana waReuli mwana wa Ibnija.
9Ndugu zao waliandika kwenye orodha ya namba 956 ya vizazi vyao. Wanaume wote hawa walikuwa viongozi wa koo za mababu zao.

10Makuhani walikuwa Yedaia, Yehoiarib, na Yokini.
11Walikuwa pia Azaria mwana wa Hilkia mwana wa Meshullamu mwana wa Zadoki mwana wa Meraioti mwana wa Ahitubi, aliyekuwa na mamlaka katika nyumba ya Mungu.
12Kulikuwa na Adaia mwana wa Yerohamu mwana wa Pashuri mwana wa Malkija. Pia kulikuwa na Maasai mwanawa Adieli mwana wa Yazera mwana wa Meshulamu mwana wa Meshilemiti mwana wa Imma.
13Ndugu zao, ambao walikuwa viongozi katika koo za mababu zao, idadi ya 1,760. Walikuwa ni wanaume wenye uwezo sana wa kufanya kazi katika nyumba ya Mungu.
14Kati ya Walawii, kulikuwa na Shemaia mwana wa Hashubu mwana wa Azrikam mwana wa Hashabia, kati ya uzao wa Merari.
15Walikuwako pia Bakbakari, Hereshi, Galali, na Mattania mwana wa Mika mwana wa Zikri mwana wa Asafu.
16Walikuwako pia Obadia mwana wa Shemaia mwana wa Galali mwana wa Yedutuni; na Berekia mwana wa Asa mwana wa Elkana, aliyeishikatika vijiji vya Wanetophathi.
17Walinzi wa lango walikuwa Shalumu, Akubi, Talimoni, Ahimani, na uzao wao. Shalumu alikuwa kiongozi wao.
18Awali walisimama kulinda katika geti la mfalme upande wa mashariki wa kambi ya uzao wa Walawi.
19Shalumu mwana wa Kore mwana wa Ebiasafu, ambaye kama mwana wa Kora, na ndugu zake kutoka nyumba ya baba yake, Korahite, alikuwa na mamlaka kwa kazi ya huduma, Walilinda mlango wa hema, kama mababu zao walivyolinda kambi ya Yawehi, na pia walilinda lango la kuingilia.
20Finehasi mwana wa Eleaza aliwaongoza kipindi cha nyuma, na Yahwehi alikuwa pamoja nae.
21Zekaria mwana wa Meshelemia alikua mlinzi katika mlango wa kuingilia hekalu, “eneo la kukutania.”

22Hawa wote walichaguliwa kana walinzi wa mageti ya kuingilia kwa idadi ya 212. Majina yao yaliandikwa kwenye kumbukumbu za watu katika vijiji vyao. Mtabiri aliwaweka Daudi na Samueli katika nafasi ya uaminifu.23Kwa hivyo wao na watoto wao walilinda mageti katika nyumba ya Yaweh, hema la kuabudia.24Walinzi wa mageti waliwekwa katika pande zote nne, upande wa mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini.25Kaka zao, walioishi kwenye vijiji vyao, walikuja kuwasaidia baada ya mzunguko wa siku saba.26Lakini viongozi wanne wa walinzi, ambao walikwa walawi, walipangiwa kulinda vyumba na vyumba vya kuhifadhi katika nyumba ya Mungu.27Walitumia usiku wao sehemu walizowekwa kuzunguka nyumba ya Mungu, kwao ilikuwa ni wajibu wao kulinda. Na walifungua geti kila asubuhi.

28Baadhi yao waliwajibika katika hekalu la vifaa; walihesabu makala zilizo ingizwa ndani na zilizo tolewa nje.29Baadhi yao pia waliwekwa kutunza vitu vitakatifu, vifaa, na vitu, kujuisha unga safi, mvinyo, mafuta, manukato, na uvumba.30Baadhi ya wana wa makuhani walichanganya uvumba.31Matithia, mmoja wa walawi, ambaye alikuwa mtoto wa kwanza wa Shalumu wa Wakorahi, alikuwa na wajibu wa kuandaa mikate kwa ajili ya sadaka.32Baadhi ya kaka zao, uzao wa kohathite, waliwajibika kwa mikate ya uwepo, kuandaa kila Sabato.

33Waimbaji na viongozi wa familia ya Walawi waliishi ndani ya vyumba katika mahali takatifu walipo kuwa hawafanyi kazi, kwa sababu wapiswa kufanya kazi walio pangiwa usiku na mchana.

34Hawa walikuwa viongozi wa familia miongoni mwa Walawi, kama ilivyo orodheshwa katika kumbukumbu za uzao wao. Waliishi Yerusalemu.
35Baba wa Gibeoni, Yeiel, ambaye mkewe aliitwa Maaka, aliishi Gibeoni.
36Mtoto wake wa kwanza alikuwa Abdoni, alafu wana wake Zuri, Kishi, Baali, Neri, Nadabu,
37Gedori, Ahio, Zekaria, na Mikloti.
38Mikloti alikuwa baba wa Shimeamu. Pia waliishi karibu na kaka yao huko Yerusalemu.
39Neri alikuwa baba wa Kishi. Kishi alikuwa baba wa Sauli. Sauli alikuwa baba wa Yonathani, malkishua, Abinadabu, na Ishbaali.
40Mwana wa Jonathani alikuwa Merib baali. Merib baali alikuwa baba wa Mika.
41Mwana wa Mika walikuwa pithoni, Meleki, Tahrea, na ahazi.
42Ahazi alikuwa baba wa Jara. Jara alikuwa baba wa Alemeti, Azmaveti, na zimri. Zimri alikuwa baba wa Moza.
43Moza alikuwa baba wa Binea. Binea alikuwa baba wa Refaia. Refaia alikuwa baba wa Eleas. Eleasa alikuwa baba wa Azeli.
44Wana sita wa Azeli walikuwa Azrikamu, Bochera, Ishmaeli, shearia, Obdia, na Hanani. Hawa walikuwa wana wa

10

1Wafilisti wakapigana dhidi ya Israeli. Kila mwanaume wa Israeli alikimbia Wafilisti na kuanguka na kufa katika Mlima Giliboa.2Wafilisti waliwakimbiza Sauli na mwanae. Waflisti walimuua Yonathani, Abinadabu, na Malikishua, wana wake.3Pambano lilikuwa zito kwa Sauli, na wapiga mishale wakamshambulia na kumjeruhi.

4Kisha Sauli akasema kwa mbeba ngao wake, “Vuta upanga wako na unichome nao. Lasihivyo, hawa wasio tahiriwa watukuja na kunitesa.” Lakini mbeba ngao wake hakutaka, kwa kuwa aliogopa sana. Kwa hiyo Sauli akachukuwa upanga wake na kuuangukia.

5Mbeba ngao alivyoona kuwa Sauli amekufa, naye akaangukia upanga wake na kufa.6Kwaiyo Sauli akafa, na wana wake watatu, wote wa nyumba yake wakafa pamoja.

7Kila mwanaume wa Israeli katika bonde alivyoona kuwa wamekimbia, na Sauli na wana wake wamekufa, walitelekeza miji yao na kukimbia. Kisha Wafilisti wakaja na kuishi humo.

8Ikawa siku inayofuata, Wafilisti walipo kuja kukagua wafu, walimkuta Sauli na wana wake wameanguka katika Mlima Giliboa.9Wakamvua nguo zote na kuchukuwa kichwa chake na ngao yake. Wakatuma wajumbe wapeleke habari Filistia yote kwa miungu yao na watu wote.10Ngao yake wakaeka ndani ya hekalu la miungu yao, na kichwa chake waka kining'iniza katika hekalu la Dagoni.

11Wakati Yabeshi Gileadi yote ilipo sikia Wafilisti waliyo mtendea Sauli,12wanaume wote wa vita wakaenda na kuchukuwa mwili wa Sauli na hiyo ya wanae, na kuirejesha Yabeshi. Walizika mifupa yao chini ya mti huko Yabeshi na wakafunga siku saba.

13Hivyo Sauli akafa kwa kuwa hakuwa mwaminifu kwa Yahweh. Hakutii maelekezo ya Yahweh, lakini akauliza ushauri kwa mtu anaye ongea na wafu.14Hakutafuta mwongozo kwa Yahweh, hivyo Yahweh akamua na kupindua ufalme kwa Daudi mwana wa Yese.

11

1Kisha Waisraeli wote walikuja Hebroni kwa Daudi na kusema, “Angalia, sisi ni nyama na mifupa yako.2Katika wakati uliopita, Sauli alipoo kuwa mfalme juu yetu, ni wewe uliye ongoza jeshi la Israeli. Yahweh Mungu wako alisema kwako, ‘utawachunga watu wangu wa Isaraeli, na utakuwa mtawala wa watu wangu wa Israeli.’”

3Kwaiyo wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni, na Daudi akafanya agano nao mbele ya Yahweh. Wakampaka mafuta Daudi kuwa mfalme wa Israeli. Kwa namna hii, neno la Yahweh lilo nenwa na Samweli likawa kweli.

4Daudi na Israeli yote wakaenda Yerusalemu (yani, Yebusi). Sasa Wayebusi, wakazi wa nchi, walikuwa pale.5Wakazi wa yebusi wakamwabia Daudi, “Hautakuja humu.” Lakini Daudi alichukuwa ngome ya Sayuni, mji wa Daudi.

6Daudi alikuwa amesema, “Yeyote atakaye washambulia Wayebusi akiwa wa kwanza atakuwa mkuu na komanda wa jeshi.” Kwaiyo Yoabu mwana wa Zeruia akashambulia wa kwanza, hivyo akafanywa mkuu wa jeshi.

7Kisha Daudi akaanza kuishi katika ngome. Kwaiyo wakaiita mji wa Daudi.8Akaimarisha mji kutoka Milo na hadi mpaka ukuta unao zunguka. Yoabu akaimairisha mji wote uliyo baki.9Daudi akawa mkuu na mkuu kwa sababu Yahweh wa Majeshi alikuwa naye.

10Hawa walikuwa viongozi Daudi aliyo kuwa nao, waliyo jionyesha imara katika ufalme wake, pamoja na Israeli, kumfanya mfalme, kutii neno la Yahweh kuhusu Israeli.11Hii ni orodha ya wanajeshi shupavu wa Daudi. Yashobeami, mwana wa Mhakimoni, alikuwa mkuu wa kikosi cha thelathini. Aliwaua wanaume mia tatu na mkuki wake katika sehemu moja.

12Baada ya yeye alikuwa Eleazari mwana wa Dodo, Mahohi, aliyekuwa mmoja wa wanaume watatu hodari.13Alikuwa na Daudi huko Pasidamimu, na pale Wafilisti wakakusanyika pamoja kwa mapambano, ambapo palikuwa na uwanja wa ngano na jeshi liliwakimbia Wafilisti.14Walisimama katikati ya uwanja. Wakautetea na kuwakata Wafilisti na Yahweh akawaokoa na ushindi mkubwa.

15Kisha watatu wa viongozi thelathini wakashuka chini kwenye mwamba wa Daudi, katika pango la Adulamu. Jeshi la Wafilisti walieka kambi katika bonde la Refaim.16Kwa wakati huo Daudi alikuwa katika ngome yake, pangoni, Wafilisti walikita kambi yao Bethilehemu.17Daudi alikuwa na kiu ya maji na akasema, “Laiti mtu akanipatia maji ya kunywa kutoka kisima kilicho Bethilehemu, kisima kilicho pembeni mwa lango!”18Hawa wanaume hodari watatu wakatoboa kupita jeshi la Wafilisti na kuchota maji kwenye kisima cha Bethilehemu, kisima pembeni mwa lango. Wakachukuwa maji na kumletea Daudi, lakini alikataa kunywa. Badala yake, akamwaga chini kwa Yahweh.19Kisha akasema, “Iwe mbali mbele ya Mungu kwamba nifanye hivi Je ninywe damu ya wanaume hawa walio hatarisha maisha yao?” Kwa sababu waliyaweka maisha ya hatarini, Daudi akakataa kuyanywa. Haya ni matendo ya wale mashujaa

20Abishai kaka wa Yoabu, alikuwa kiongozi wa wale watatu. Aliwahi kutumia mkuki wake dhidi ya watu mia tatu na kuwaua. Ametajwa pamoja na wale watatu.21Kati ya wale watatu, yeye alipewa heshima mara mbili na akawa kiongozi wao, ijapo hakuwa mmoja wa miongoni mwao.

22Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa shujaa jasiri kutoka Kabizeli, aliye fanya matendo makuu. Aliua wana wawili wakiume wa Arieli wa Moabu. Pia alishuka chini ya shimo na kumuua simba wakati theluji ilikuwa ikianguka.23Hata alimuua Mmisri, mwanaume mwenye mita mbili na theluthi moja. Mmisri alikuwa na mkuki kama gongo la mshonaji, lakini alimfuata chini na fimbo tu. Akakamata mkuki katika mkono wa Mmisri na kumuua na mkuki wake.24Benaia mwana wa Yehoiada alifanya haya matukio, na akatajwa miongoni mwa wale wanaume hodari watatu.25Alisifika zaidi ya wale wanajeshi thelathini kwa ujumla, lakini hakuwa pewa hadhi ya wale wanajeshi watatu hodari. Lakini Daudi alimweka juu ya walinzi wake.
26Mashujaa hodari walikuwa Asaheli kaka wa Yoabu, Elhanani mwana wa Dodo wa Bethilehemu,
27Shamothi Mherori, Helezi Mpeloni,
28Ira mwana wa Ikeshi Mtekoi, Abieza Manathothi,
29Sibekai Mhushathite, Ilai Mahohi,
30Maharai Mnetofathi, Heledi mwana wa Baana Mnetofathite,
31Itai mwana wa Ribai wa Gibea uzao wa Benjamini, Benaia Mpirathoni,
32Hurai wa mabonde ya Gaashi, Abieli Marbathi,
33Azmavethi Mbaharumi, Eliaba Mshaalboni,
34wana wa Hashemu Mgizoni, Yonathani mwana wa Shagee Mharari,
35Ahiamu mwana wa Sakari Mharari, Elifali mwana wa Uri,
36Hefa Mmekarathi, Ahija Mpeloni,
37Hezro Mkarimeli, Naarai mwana wa Ezibai,
38Yoeli kaka wa Nathani, Mibhari mwana wa Hagiri,
39Zeleki Mamoni, Naharai Mberothi (mbeba ngao ya Yoabu mwana wa Zeruia),
40Ira Mithire, Garebu Mithire,
41Uria Mhiti, Zabadi mwana wa Ahlai,
42Adina mwana wa Shiza Mreubeni (kiongozi wa Wareubeni) na thelathini pamoja naye,
43Hanani mwana wa Maaka, na Yoshafati Mmithini,
44Uzia Mashiterathi, Shama na Yeieli wana wa Hothamu Waaroeri,
45Jediaeli mwana wa Shimri, Joha (kaka yake Mtize),
46Elieli Mmahavi, Yeribai na Yoshavia wana wa Elnaamu, Ithima Mmoabi,
47Elieli, Obedi, na Yaasieli mmezobai.

12

1Hawa walikuwa wanaume walio kuja kwa Daudi huko Zikilagi, wakati akiwa bado amefukuzwa katika uwepo wa Sauli mwana wa Kishi. Walikuwa miongoni mwa wanajeshi, wasaidizi wake katika mapambano.2Walikuwa wana upinde na waliweza kutumia mkono wa kuume na wakushoto kurusha mawe na manati na kupiga mishale kutoka kwenye upinde. Walikuwa Wabenjamini, jamaa wa Sauli.

3Kiongozi alikuwa Ahi Eza, halafu Yoashi, Wana wote wa Shemaa Mgibeathi. Kulikuwa na Yezieli na Peleti, wana wa Azimavethi. Kulikuwa pia na Beraka, Yehu Waanathothi,
4Ishimaia Mgibeoni, mwanajeshi kati ya wale thelathini (na kiongozi wa wale thelathini); Yeremia, Yahazieli, Yohanani, Yozabadi Mgederathi
5Eluzai, Yerimothi, Bealia, Shemaria, Shefatia Mharufi,
6Wakorahi ni Elkana, Ishia, Azareli, Yoeza, Yashobeamu, na
7Yoela na Zebadia, wana wa Yeroham wa Gedori.

8Baadhi ya Wagadi walijiunga na Daudi katika ngome iliyo nyikani. Walikuwa mashujaa hodari, wanaume wa vita, tayari kwa vita, walioweza kumudu ngao na mkuki; ambao nyuso zao zilikuwa kali kama za simba. Walikuwa wepesikama swala juu ya milima.
9Kulikuwa na Eza kiongozi, Obadia wapili, Eliabu watatu,
10Mishimana wanne, Yeremia watano,
11Atai wasita, Elieli wasaba,
12Yohanani wanane, Elizabadi watisa,
13Yeremia wakumi, Makibanai wakumi na moja.

14Wana wa Gadi walikuwa viongozi wa jeshi. Wamwisho aliongoza mia moja, na mkubwa aliongoza elfu moja.15Walivuka Yordani mwezi wa kwanza, ilipofurika kingo zake, na kuwafanya wote wanaoishi katika mabonde kukimbia, kuelekea mashariki na kuelekea magharibi.

16Baadhi ya wanaume wa Benjamini na Yuda walikuja kwenye ngome kwa Daudi.17Daudi alienda nje kuwasalimu na kuwahutubia: “kama mmekuja kwa amani kunisaidia, moyo wangu utaungana nanyi Lakini kama mmekuja kunisaliti kwa maadui zangu, Mungu wa mababu zetu awaone na kuwakemea, kwa kuwa sijakosa.”

18Kisha roho ikaja juu ya Amasai, ambaye alikuwa kiongozi wa wale thelathini. Amasai alisema, “Sisi ni wako, Daudi. Sisi tupo upande wako, mwana wa Yesse. Na amani iwe juu ya yeyote atakaye kusaidia. Amani na iwe wanaokusaidia, kwa kuwa Mungu wako anakusaidia.” Kisha Daudi akawapokea na kuwafanya wakuu wa watu wake.

19Baadhi kutoka kwa Manase pia wakamwendea Daudi alipokuja na Wafilisti dhidi ya Sauli katika pambano. Lakini hawakuwasaidia Wafilisti kwasababu mabwana wa Wafilisti walishauriana na wakamfukuza Daudi. Walisema, “Atamwendea Bwana wake Sauli na kuhatarisha maisha yetu.”20Alipokwenda kwa Zikilagi, wanaume wa Manase walioungana nae walikuwa Adina, Yozabadi, Yediaeli, Yozabadi, Elihu, na Zilethai, viongozi wa maelfu wa Manase.21Walimsaidia Daudi kupigana na kikundi cha wezi, maana walikuwa wanaume wa mapambano. Baadae walikuwa wakuu katika jeshi.22Siku hadi siku, wanaume walikuja kwa Daudi kumsaidia, mpaka wakawa jeshi kubwa, kama jeshi la Mungu.

23Hii ni kumbukumbu ya wanajeshi wa vita, walio kuja kwa Daudi Hebroni, kuupindua ufalme wa Sauli kwake, ilikutimiza neno la Yahweh.
24Waanume wa Yuda walio beba ngao na mkuki ni 6,800, tayari kwa vita.
25Kutoka kwa Wasimeoni walikuwa 7,100 mashujaa hodari waliofunzwa vita.
26Kutoka kwa Walawi kulikuwa na wanaume wa mapambano 4,600.
27Yehoiada alikuwa kiongozi wa uzao wa Aruni, na kwa yeye walikuwa 3,700.
28Pamoja na Zadok, kijana mmoja, shujaa wa vita, walikuwa viongozi ishirini na mbili kutoka ukoo wake
29Kutoka kwa Benjamini, jamaa ya Sauli, walikuwa elfu tatu. Wengi wao walikuwa wameilinda nyumba ya Sauli mpaka wakati huu.
30Kutoka kwa Waefraimu palikuwa na mashujaa wa vita 20,800, wanaume maarufu kwenye koo zao.
31Kutoka kabila nusu la Manase palikuwa na wanaume elfu kumi na nane maarufu walio kuja kufanya Daudi mfalme.
32Kutoka kwa Isakari, palikuwa na viongozi mia mbili waliokuwa na ufahamu wa nyakati na walijua kile ambacho Israeli walipaswa kufanya. Ndugu zao wote walikuwa chini ya amri yao.
33Kutoka Zebuloni palikuwa na wanaume elfu hamsini wa mapambano, tayari kwa vita, na silaha zote za vita, na tayari kutoa uwaminifu usiogawanyika.
34Kutoka kwa Naftali palikuwa na askari elfu moja, na pamoja nao wanaume elfu thelathini na saba wenye ngao na mikuki.
35Kutoka kwa Wadani palikuwa na wanaume 28,600 wameandaliwa kwa ajili ya pambano.
36Kutoka kwa Asheri palikuwa na wanaume elfu arobaini wameandaliwa kwa pambano.
37Kutoka upande wa pili wa Yordani, kutoka kwa Warubeni, Wagadi, na nusu kabila la Manase, palikuwa na wanaume 120,000 wameandaliwa na silaha za kila namna kwa ajili ya pambano.

38Hawa wanajeshi wote, waliandaliwa kwa pambano, walikuja Hebroni na moyo wote ili kumfanya Daudi awe mfalme juu ya Israeli yote. Waisraeli wote waliosalia walikubali kumfanya Daudi mfalme pia.39Walikuwa pale na Daudi siku tatu, wakila na kunywa, kwa kuwa jamaa zao waliwapa mahitaji ya kwenda nayo.40Kwa kuongezea, wao walio kuwa karibu nao, kwa umbali wa Isakari na Zebuloni na Naftali, walileta mkate kwa punda, ngamia, nyumbu na fahali, na keki za tini, mvinyo, vishada vya zabibu kavu, divai, mafuta, ng'ombe na kondoo, kwa maana kulikwa na furaha katika Israeli.

13

1Daudi akashuriana na wakuu wa jeshi la maelfu na mamia, na kila kiongozi.2Daudi akasema kwa kusanyiko la Isaraeli, “Kama itakuwa vyema, na kama hii inatoka kwa Yahweh Mungu wetu, na tutume wajumbe kila sehemu kwa ndugu zetu walio baki maeneo yote ya Israeli, na kwa makuhani na Walawi walio kwenye miji yao. Waambiwe wakunje wajiunge nasi.3Na tulirudishe kwetu wenyewe sanduku la Mungu wetu; kwa maana hatukutafuta mapenzi yake katika siku za utawala Sauli.”4Kusanyiko lote liliafiki kufanya haya yote, kwa kuwa yalionekana sawa machoni pa watu wote.

5Kwaiyo Daudi akakusanya Israeli yote, kutoka mto Shihori ulio Misri hadi Lebo Hamathi, kuleta sandaku la Mungu kutoka Kiriathi Yearimu.6Daudi na Israeli yote walienda mpaka Baala, ambayo ni, Kiriathi Yearimu, ambao ni ya Yuda, kuleta sanduku la Mungu, ambalo linaitwa kwa jina la Yahweh, Yahweh, aketiye juu ya makerubi.

7Kwa hiyo wakaliweka sanduku la Mungu juu ya mkokoteni mpya. Wakalilitoa nje ya nyumba ya Abinadabu. Uza na Ahio walikuwa wakiongoza mkokoteni.8Daudi na Israeli yote walikuwa wakishangilia mbele za Mungu kwa nguvu zao zote. Walikuwa wakiimba kwa vinubi, na vinanda, matari, upatu, na tarumbeta.

9Walipo kuja eneo la kupepeta mazao huko Kidoni, Uza alinyoosha mkono wake ili kukamata sanduku kwa sababu ng'ombe walijikwa.10Hasira ya Yahweh ikawaka juu ya Uza, na Yahweh akamua kwa sababu Uza alishika na mkono wake sanduku. Akafa pale mbele za Mungu.

11Daudi alipatwa na hasira kwa kuwa Yahweh alimshambulia Uza. Hiyo sehemu inaitwa Perezi Uza hadi leo.

12Daudi alimuogopa Mungu hiyo siku. Akasema, “Nawezaje kuleta sanduku la Mungu nyumbani mwangu?”13Kwa hiyo Daudi hakuleta sanduku kwenye mji wa Daudi, lakini aliweka pembeni mwa nyumba ya Obedi Edomu Mgiti.14Sanduku la Mungu lilibaki nyumbani mwa Obedi Edomu kwa miezi mitatu. Kwaiyo Yahweh akabariki nyumba yake na yote aliyo miliki.

14

1Kisha Hiramu mfalme wa Tire alituma wajumbe kwa Daudi, na miti ya mierezi, maseremala, na wajenzi. Walijenga nyumba kwa ajili yake.2Daudi alijua kuwa Yahweh alimfanya kuwa mfalme juu ya Waisraeli, na hivyo ufalme wake ulitukuzwa juu sana kwa ajili ya watu wa Israeli.

3Ndani ya Yerusalemu, Daudi aliongeza wake, na akawa baba wa wana wengi na mabinti.4Haya yalikuwa majina ya watoto waliozaliwa nae huko yerusalemu: Shammua, Shobabu, Nathani, Suleimani,5Ibhari, Elishua, Elipeleti,6Noga, Nefegi, Yafia,7Elishama, Beliada, na Elifeleti.

8Sasa wakati Wafilisti waliposikia Daudi amepakwa mafuta kama mfalme juu ya Waisraeli yote, wote walitoka nje kwenda kumtafuta. Lakini Daudi alisikia kuhusu hilo naye akaenda nje kinyume nao.9Sasa wafilisti walikuja na kufanya shambulio katika bonde la Refaimu.10Kisha Daudi akaomba msaada kwa Mungu. Akasema, “Je niwashambulie Wafilisti? Utanipa ushindi juu yao?” Yahweh akamwambia, “Shambulia, kwa uhakika nitawakabidhi kwako.”

11Kwa hivyo wakaja Baali Perazimu na akawashinda. Akasema, “Yahweh kapasua maadui zangu kwa mkono wangu kama vile mpasuko wa mafuriko ya maji.” Hivyo jina la sehemu ile likawa Baali Perazimu.12Wafilisti walitelekeza miungu yao pale, na Daudi akatoa amri wateketezwe kwa moto.

13Kisha Wafilisti wakavamia kwa mara nyingine tena.14Hivyo Daudi akaomba msaada kwa Mungu tena. Mungu akamwambia, “Usiwashambulie kwa mbele, lakini wazunguke kwa nyuma yao na uwajie kupitia misitu ya balisamu.15Utakaposikia sauti ya wanajeshi wanatembea kwenye upepo uvumao kutoka juu ya miti ya balisamu, kisha shambulia kwa nguvu. Fanya hivyo kwasababu Mungu atakutangulia kwenda kuwashambulia majeshi ya wafilisti.”16Hivyo Daudi alifanya kama Mungu alivyo muamuru. Aliwashinda jeshi la Wafilisti kutoka Gibeoni mpaka Gezeri.

17Kisha umaarufu wa Daudi ukaenda katika nchi zote, na Yahweh akasababisha mataifa yote kumuhofia.

15

1Daudi akajingea nyumba zake katika mji wa Daudi. Akaanda sehemu kwa ajili ya sanduku la Mungu na hema lake.2Kisha Daudi akasema, “Walawi pekee ndio watabeba sanduku la Mungu, kwa kuwa walichaguliwa na Yahweh kubeba sanduku la Yahweh, na kumtumikia milele.”

3Kisha Daudi akakusanya Israeli yote Yerusalemu, kuleta sanduku la Yahweh sehemu aliyo iandaa.4Daudi akakusanya uzao wa Aruni na Walawi pamoja.5Kutoka uzao wa Kohathi, palikuwa na Urieli kiongozi na ndugu zake, wanaume 120.
6Kutoka uzao wa Merari, palikuwa na Asaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 220.
7Kutoka uzao wa Gerishomu, palikuwa na Yoeli kiongozi na ndugu zake, wanaume 130.
8Kutoka uzao wa Elizafani, palikuwa na Shemaia kiongozi na ndugu zake, wanaume 200.
9Kutoka uzao wa Hebroni, palikuwa na Elieli kiongozi na ndugu zake, wanaume themanini.
10Kutoka uzao wa Uzieli, palikuwa na Aminadabu kiongozi na ndugu zake, wanaume 112.

11Daudi akaagiza Zadoki kuitwa na Abiathari kuhuani, na Walawi Urieli, Asaia, Yoeli, Shemaia, Elieli, na Aminadabu.12Akasema, “Nyinyi ni viongozi wa familia za Kilawi. Jiwekeni wakfu, nyie na ndugu zenu, ilikwamba mlete sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli, kwenye sehemu niliyo iandaa.13Mara ya kwanza hamkubeba. Ndio maana Yahweh Mungu wetu akawa na hasira kwetu, kwa kuwa hatuku mtafuta wala kutii amri yake.”

14Hivyo makuhani na Walawi waka jiweka wakfu iliwaweze kuleta sanduku la Yahweh, Mungu wa Israeli.15Hivyo Walawi wakabeba sanduku la Mungu katika mabega yao na nguzo, kama Musa alivyo amuru-kwa kufuata sheria zilizo tolewa na Yahweh.

16Daudi akazungumza na viongozi wa Walawi kuwapangia ndugu zao kuwa wana muziki wenye vyombo vya muziki, vyombo vya uzi, vinubi na upatu, kwa kupiga kwa sauti na furaha wakipaza sauti zao.

17Hivyo Walawi wakamchagua Hemani mwana wa Yoeli na mmoja wa kaka zake, Asafu mwana wa Berekia. Pia walimchagua ndugu wa uzao wa Merari na Ethani mwana wa Kushaia.18Pamoja nao walikuwa ndugu wa daraja la pili: Zekarai, Yaazieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Benaia, Maasaeia, Matithia, Elifelehu, Mikineaia, Obedi Edomu, na Yeieli, mlinzi wa lango.

19Wanamuziki Hemani, Asafu, na Ethani walichaguliwa kupiga upatu wa shaba.20Zekaria, Azieli, Shemiramothi, Yehieli, Uni, Eliabu, Maaseia, na Benaia walicheza vinanda, vilivyowekwa kwa Alamothi21Matithia, Elifelehu, Mikineia, Obedi Edomu, Yeieli, na Azazia walitangulia kwa vinubi vilivyowekwa kwa Sheminithi.22Kenania, kiongozi wa Walawi, aliongoza uimbaji sababu alikuwa mwalimu wa muziki.

23Berekia na Elikana walikuwa walinzi wa sanduku.24Shebania, Yoshafati, Nethanieli, Amasai, Zekaria, Benaia, na Eliezeri, makuhani, walikuwa wa kupuliza matarumbeta mbele ya sanduku la Mungu. Obedi Edomu na Yehia walikuwa walinzi wa sanduku.

25Hivyo Daudi, wazee wa Israeli, na wakuu wa maelfu wakaenda kuchukua sanduku la agano la Yahweh kutoka nyumba ya Obedi Edomu kwa shangwe.26Wakati Mungu aliwasaidia Walawi waliolichukua sanduku la agano la Yahweh, walitoa dhabihu fahali saba na kondoo waume saba27Daudi alivishwa joho la kitani nzuri, kama vile Walawi walio beba sanduku, waimbaji, na Kenania, kiongozi wa nyimbo na waimbaji. Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.28Hivyo Israeli yote wakaleta sanduku la agano la Yahweh kwa kelele za furaha, na sauti za pembe na tarumbeta, kwa upatu, na kwa vinanda na vinubi.

29Lakini sanduku la agano la Yahweh lilipoingia mji wa Daudi, Mikali binti wa Sauli, alichungulia dirishani. Akamuona Mfalme Daudi akicheza na kusherehekea. Kisha akamdharau moyoni mwake.

16

1Wakaleta ndani Sanduku la Mungu na kuweka katikati ya hema ambalo Daudi aliandaa. Kisha wakatoa sadaka ya kuteketeza na sadaka ya ushirika mbele ya Mungu.2Daudi alipo maliza kutoa dhabiu ya kuteketeza na sadaka za ushirika, aliwabariki watu kwa jina la Yahweh.3Alisambaza kwa kila Misraeli, mwanaume na mwanamke, kipande cha mkate, na kipande cha nyama, na keki ya mzabibu.

4Daudi aliewapangia baadhi ya Walawi kutumika mbele ya sanduku la Yahweh, na kusheherekea, kushukuru na kumsifu Yahweh, Mungu wa Israeli.5Hawa Walawi walikuwa Asafu kiongozi, wa pili kutoka kwake Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaia, Obedi Edomu, na Yeieli. Hawa walikuwa wacheze vinanda na vinubi. Asafu alikuwa apige upatu, kwa kelele.6Benaia na Yahazieli walikuwa wakupiga tarumbeta kila mara, mbele sanduku la agano la Mungu.

7Kisha katika hiyo siku Daudi akawachagua Asafu na kaka zake kuimba hii nyimbo ya shukurani kwa Yahweh.
8Mpeni shukurani Yahweh, liitieni jina lake; fahamisheni mataifa matendo yake.
9Mwiimbieni, imbeni sifa kwake; semeni matendo yake ya ajabu.
10Jisifuni katika jina lake takatifu; acha mioyo ya wanao mtafuta Yahweh ishangilie.
11Mtafute Yahweh na nguvu zake; tafuteni uwepo wake siku zote.
12Kumbukeni matendo aliyo ya fanya kwenu, miujiza yake na amri za kinywa chake,
13enyi uzao wa Israeli mtumishi wake, enyi watu wa Yakobo, wateule wake.
14Yeye ni Yahweh, Mungu wetu. Amri zake zipo duniani kote.
15Tunzeni agano lake akilini mwenu milele, neno alilo liamuru kwa vizazi elfu moja.
16Anakumbuka agano alilo lifanya na Ibrahimu, na nadhiri yake kwake Isaka.
17Hili ndilo alilo lithibitisha kwa Yakobo kama amri maalumu, na kwa Israeli kama agano la milele.
18Alisema, “Nitakupa nchi ya Kanani kama sehemu ya urithi wako.”
19Walipokuwa wachache kwa idadi, wachache sana, kuwa wageni katika nchi,
20walitangatanga kutoka taifa hadi taifa, kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
21Hakumruhusu yeyote awatese; aliwahadhibu wafalme kwa ajili yao.
22Alisema, “Msiwaguse wapakwa mafuta wangu, na msiwadhuru manabii wangu.”
23Imbeni kwa Yahweh, dunia yote; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
24Tangazeni utukufu wake kwa mataifa, matendo yake makuu kwa mataifa yote.
25Kwa kuwa Yahweh ni mkuu na ni wakusifiwa sana, na ni wakuogopewa kuliko miungu yote.
26Kwa kuwa miungu ya mataifa ni sanamu, lakini ni Yahweh aliyeziumba mbingu.
27Fahari na ukuu zipo uweponi mwake. Nguvu na furaha zipo mahali pake.
28Mpeni sifa Yahweh, enyi koo za watu, mpeni Yahweh utukufu na nguvu;
29Mpeni Yahweh utukufu upasao jina lake. Leta sadaka na mje kwake. Muinamieni Yahweh katika fahari ya utakatifu
30Tetemeka mbele zake, dunia yote. Dunia imeimarishwa; haiwezi kutikisika.
31Mbingu nazifurahi, na dunia ishangilie; na wasema kati ya mataifa, “Yahweh anatawala.”
32Bahari na ingurume, na inayo ijaza ipige kelele kwa furaha. Mashamba yawe na furaha tele, na vyote vilivyomo ndani yake.
33Na miti iliyopo misituni ipige kelele kwa Yahweh, kwa kuwa anakuja kuhukumu dunia.
34Toeni shukurani kwa Yahweh, kwa kuwa ni mwema, kwa maana uaminifu wa agano lake hudumu milele.
35Kisha sema, “Tuokoe, Mungu wa wokovu wetu. Tukusanye pamoja na utuokoe kutoka kwa mataifa mengine, ilikwamba tutoe shukurani kwa jina lako takatifu na tufurahi katika sifa zako.”
36Na Yahweh, Mungu wa Israeli, asifiwe kutoka milele na milele. Watu wote wakasema, “Amina” na wakamsifu Yahweh.
37Hivyo Daudi akamwacha Asafu na kaka zake pale mbele ya sanduku la Yahweh, kutumika daima mbele ya sanduku, kama kazi za kila siku zilivyo itaji. Obedi Edomu pamoja na ndugu sitini na nane walijumuishwa.38Obedi Edomu mwana wa Yeduthuni, pamoja na Hosa, walikuwa wawe walinzi wa lango.

39Zadoki kuhani na makuhani wenzake walikuwa watumike mbele ya hema la Yahweh katika mahali pa juu huko Gibeoni.40Walikuwa watoe sadaka za kuteketeza kwa Yahweh kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketeza daima asubui na jioni, kwa mujibu wa yote yalio andikwa katika amri za Yahweh, aliyo wapa Waisraeli kama sheria.41Hemani na Yeduthuni walikuwa nao, pamoja na walio chaguliwa kwa jina, kumpa shukurani Yahweh, kwa sababu uaminifu wa agano lake la dumu hatamilele42Hemani na Yeduthuni walikuwa viongozi wa wao waliopiga tarumbeta, upatu, na vyombo vingine kwa muziki wa kumuabudu Mungu. Wana wa Yeduthuni walilinda lango.

43Kisha watu wote walirudi nyumbani, na Daudi akarudi kuwabariki watu wa nyumbani mwake.

17

1Ikawa kwamba baada ya Daudi kukaa nyumba mwake, alimwambia Nathani yule nabii, “Angalia, nina ishi katika nyumba iliyo jengwa na mierezi, lakini sanduku la agano la Yahweh lipo kwenye chini ya hema.”

2Kisha Nathani akasema kwa Daudi, “Nenda, fanya yalio moyoni mwako, kwa kuwa Mungu yupo nawe.”

3Lakini usiku huo neno la Mungu lilimjia Nathani, nakusema,4“Nenda umwambie Daudi mtumishi wangu, ‘Hivi ndivyo Yahweh asemavyo: Hautanijengea nyumba ya kuishi.5Kwa kuwa sijaishi katika nyumba toka ile siku niliyo ileta Israeli hadi leo. Badala yake, nimeishi ndani ya hema, hema la kukusanyikia, sehemu mbalimbali.6Katika sehemu zote nilizo enda na Israeli, niliwai kusema lolote kwa viongozi wa Israeli niliyo wachagua kuwa chunga watu wangu, kwa kusema, “Kwa nini haujanijengea mimi nyumba ya mierezi?”7“Kisha sasa, mwambie mtumishi wangu Daudi, ‘Hili ndilo Yahweh wa majeshi anasema: Nilikuchugua kutoka malishoni, kufuata kondoo, ilikwamba uwe mtawala wa watu wangu Waisraeli.8Nimekuwa nawe pote ulipo enda na nimewakata maadui zako wote, na na nitakufanyia jina, kama jina la wakuu wa dunia.9Nitateua mahali pa watu wangu Israeli na nitawapanda hapo, iliwaishi sehemu yao na wasisumbuliwe tena. Watu wa ovu hawata watesa tena, kama walivyo fanya hapo awali,10kama walivyo kuwa wakifanya toka siku zile nilipo waamuru waamuzi kuwa juu ya watu wangu Waisraeli. Kisha nitawatiisha maadui zako wote. Zaidi sana nina kwambia kwamba mimi, Yahweh, nitakujengea nyumba.11Itakuwa siku zako zitakapotimia za wewe kwenda kwa baba zako, nitainua uzao wako baada yako, na mmoja wa uzao wako nitaimarisha ufalme wake.12Yeye atanijengea nyumba, na nitaimarisha kiti chake cha enzi milele.13Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana wangu. Sitaondoa uwaminifu wa Agano langu kwake, kama nilivyo ondoa kwa Sauli, aliye tawala kabla yako.14Nitamweka juu ya nyumba yangu na katika ufalme wangu milele, na kiti chake cha enzi kitaimarishwa milele.”

15Nathani akanena haya kwa Daudi na kumtaarifu, na akamwambia kuhusu maono yote.

16Kisha Daudi mfalme akaenda ndani na kuketi mbele za Yahweh; akasema, “Mimi ni nani, Yahweh Mungu, na familia yangu ni nini, hadi unilete umbali huu?17Hili lilikuwa jambo dogo machoni pako, Mungu. Umezungumzia familia ya mtumishi wako kwa muda mrefu ujao, na umenionyesha vizazi vijavyo, Yahweh Mungu.18Nini zaidi mimi, Daudi, niseme? Umemheshimu mtumishi wako. Umempa mtumishi waki heshima ya kipekee.19Yahweh, kwa ajili ya mtumishi wako, na kutimiza kusudi lako, umefanya hili ilikudhihirisha matendo yako yote makuu.20Yahweh, hakuna aliye kama wewe, na hakuna Mungu zaidi yako, kama tulivyo sikia mara zote.21Maana ni taifa gani duniani lililo kama watu wako Israeli, ambao wewe, Mungu, ulikomboa kutoka Misri kuwa watu kwa ajili yako, ili ujifanyie jina kwa matendo makuu na ya kutisha? Uliondoa mataifa mbele za watu wako, ulio wakomboa kutoka Misri.22Ulifanya Israeli watu wako milele, na wewe, Yahweh, ukawa Mungu wao.23Hivyo sasa, Yahweh, ile ahadi uliyo iweka kuhusu mtumishi wako na nyumba yake lithibitishwe milele. Fanya kama ulivyo nena.24Jina lako na litukuzwe milele na kuwa kuu, ili watu waseme, ‘Yahweh wa majeshi ni Mungu wa Israeli,’ na nyumba yangu, mimi Daudi, mtumishi wako ikiwa imeimarishwa mbele zako.25Kwa kuwa wewe, Mungu wangu, umedhihirisha kwa mtumishi wako utamjengea nyumba. Hiyo ndio sababu, mimi mtumishi wako, nimepata ujasiri wa kuomba kwako.26Sasa, Yahweh, wewe ni Mungu, na umefanya hii ahadi nzuri kwa mtumishi wako:27Sasa imekupendeza kubariki nyumba ya mtumishi wako, iliiendelee milele mbele zako. Wewe, Yahweh, umeibariki, na itabarikiwa milele.”

18

1Baada ya haya Daudi akawashambulia Wafilisti na kuwashinda. Alichukuwa Gathi na vijiji vyake katika utawala wa Wafilisti.

2Kisha akamshinda Moabu, na Wamoabu wakawa watumishi wa Daudi na wakamlipa ushuru maalumu.

3Daudi kisha akamshinda Hadadezeri, mfalme wa Zoba huko Hamathi, wakati Hadadezeri alipo kuwa akisafiri kuimarisha utawala wake kwa Mto wa Frati.4Daudi akateka magari ya farasi elfu, wanaume wa farasi elfu saba, na wanajeshi wa miguu elfu ishirini. Daudi aliwajeruhi farasi wote wagari, lakini akahifadhi baadhi kwa ajili ya magari ya farasi mia moja.

5Wakati Waaramia wa Damasko walipo kuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Zoba, Daudi aliua wanaume elfu ishirini na mbili wa Kiaramia.6Kisha Daudi akaweka vikosi huko Aramu ya Damasko, na Waaramia wakawa watumishi wake na wakamletea ushuru maalaumu. Yahweh alimpatia Daudi ushindi popote alipoenda.

7Daudi alichukua ngao za dhahabu zilizo kuwa kwa watumishi wa Hadadezeri na kuleta Yerusalemu.8Kutoka Teba na Kuni, miji ya Hadadezeri, Daudi alichukuwa shaba nyingi sana. Ilikuwa shaba hii ambayo baadae Sulemani alifanya beseni ya shaba, iitwayo “bahari,” nguzo na vifaa vya shaba.

9Wakati Toi, mfalme wa Hamathi, aliposikia kuwa Daudi ameshinda majeshi yote ya Hadadezeri mfalme wa Zoba,10Toi akamtuma Hadoramu mwanae kwa Mfalme Daudi kumsalimia na kumbariki. Alifanya hili kwa sababu Daudi alipigana na Hadadezeri na kumshinda, na kwa sababu mara nyingi Toi alikuwa kwenye vita naHadadezeri. Toi pia alimtumia Daudi vyombo vya aina mbalimbali dhahabu, na fedha, na shaba.

11Mfalme Daudi alivitenga vitu hivi kwa Yahweh, pamoja na fedha na dhahabu aliyo ibeba kutoka kwa mataifa yote: Edomu, Moabu, watu wa Amoni, Wafilisti, na Waamaleki.

12Abishai mwana wa Zeruia akawaua Waedomi elfu kumi na nane katika Bonde la Chumvi.13Alieka vikosi huko Edomu, na Waedomi wote wakawa watumishi wa Daudi. Yahweh alimpa Daudi ushindi pote alipoenda.

14Daudi alitawala Israeli yote, na alitoa haki na uadilifu kwa watu wote.15Yoabu mwana wa Zeruia alikuwa mkuu wa jeshi, na Yehoshafati mwana wa Ahiludi alikuwa mtunza kumbukumbu.16Zadoki mwana wa Ahitubi na Ahimeleki mwana wa Abiathari walikuwa makuhani, na Shavisha alikuwa mwandishi.17Benaia mwana wa Yehoiada alikuwa kiongozi wa Wakerethi na Wapelethi, na wana wa Daudi walikuwa maofisa wakuu mkononi mwa mfalme.

19

1Ilikuja baadaye kwamba Nahashi, mfalme wa watu wa Amoni, akafa, na mwanae akawa mfalme baada yake.2Daudi akasema, “Nitaonyesha ukarimu kwa Hanuni mwana wa Nahashi, kwa sababu baba yake alionyesha ukarimu kwangu.” Hivyo Daudi akatuma wajumbe kumfariji kuhusu baba yake. Watumishi wa Daudi wakaingia nchi ya Waamoni na wakaenda kwa Hanuni, ilikumfariji.3Lakini wakuu wa Waamoni wakamwambia Hanuni, “Unadhani Daudi anamheshimu baba yako sababu ametuma watu kukufaraji? Watumishi wake hawaji kwako ili kuipeleleza na kuichunguza nchi ili waipindue?

4Hivyo Hanuni akawakamata watumishi wa Daudi, akawanyoa, akakata nguo zao katikati kwenye matako na kuwafukuza.

5Walipo eleza haya kwa Daudi, alienda kukutana nao, kwa maana watu hao waliona aibu sana. Mfalme akasema, “Bakini Yeriko hadi ndevu zenu ziote tena, kisha mrudi.”

6Wakati Waamoni waliona wamekuwa uvundo kwa Daudi, Hanuni na Waamoni walituma talanta elfu moja za fedha kukodisha magari ya farasi kwa Waaremei na wanaume wa farasi kutoka Naharaimu, Maka, na Zoba.7Waliwakodishia magari ya farasi elfu thelathini na mbili pamoja na mfalme wa Maka na jeshi lake, walio kuja na kueka kambi mbele ya Medeba. Kisha Waamoni wakajikusanya pamoja kutoka miji yao, na wakaja kwa vita.

8Wakati Daudi aliposikia, alimtuma Yoabu na jeshi lake lote la mashujaa.9Watu wa Amoni walikuja na kupanga mstari kwa ajili ya pambano katika lango la mji, nao wafalme waliokuja walikuwa peke yao katika shamba.

10Wakati Yoabu alipoona mistari ya pambano imemzunguka mbele na nyuma, alichagua wapiganaji bora wa Israeli na kuwapanga dhidi ya Waaremi.11Na jeshi lingine aliliweka chini ya Abishai kaka yake, akawapanga kwa mstari ya pambano dhidi jeshi la Amoni.12Yoabu akasema, “Kama Waaremi wananguvu kunishinda, basi wewe, Abishai, lazima uniokoe. Lakini kama jeshi la Waamoni lina nguvu kukuzidi, basi nitakuja kukuokoa.13Kuwa hodari na tujionyeshe kuwa hodari kwa ajili ya watu wetu na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu, kwa kuwa Yahweh atafanya lililo jema machoni mwake.”

14Hivyo Yoabu na askari wa jeshi lake wakasogea kwenye pambano dhidi ya Waaremi, walio lazimika kukimbia mbele ya jeshi la Waisraeli.15Wakati jeshi la Waamoni lilipoona kuwa Waaremi wamekimbia, nao pia wakamkimbia Abishai, ye Yoabu, na wakakurudi mjini. Kisha Yoabu akarudi kutoka kwa watu wa Amoni na kurudi Yerusalemu.

16Waaremi walipoona kwamba wameshindwa na Waisraeli, wakatuma wajumbe na kuwarudisha Waaremi kutoka ng'ambo ya Mto Frati, na Shofaki mkuu wajeshi la Hadadezeri.

17Daudi alipo ambiwa haya, akakusanya Israeli yote, akuvuka Yordani, na kuja juu yao. Alipanga jeshi kwa ajili ya pambano dhidi ya Waaremi, na wakapigana nao.18Waaremi waliwakimbia Waisraeli, na Daudi akaua waendesha magari ya farasi ya Waaremi elfu saba na wanajeshi wa miguu elfu arobaini. Pia alimuua Shopaki, mkuu wa jeshi.

19Wafalme wote walio kuwa watumishi wa Hadadezeri walipoona kuwa wameshindwa na Israeli, walifanya amani na Daudi na kumtumikia. Hivyo watu wa Aramu hawakuwa tayari kuwasaidia Waamoni.

20

1Ikaja kuwa wakati wa mvua, kipindi wafalme huenda vitani, Yoabu akaongaza jeshi kwenda kupambana na kuiharibu nchi ya Waamoni. Alienda na kuteka Raba. Daudi alibaki Yerusalemu. Yoabu alishambulia Raba na kuiharibu kabisa.2Daudi alichukuwa taji la mfalme wao kichwani mwake, na akagundua linauzito wa talanta moja ya dhahabu, na ndani yake kulikuwa na mawe ya thamani. Taji liliwekwa kichwani mwa Daudi, na akaleta mali nyingi za mji.3Aliwaleta watu walio kuwa ndani ya mji na kuwalazimisha wafanye kazi kwa msumeno na suluji za chuma na shoka. Daudi aliwataka watu wote wa mji kufanya kazi hii. Kisha Daudi na watu wote wakarudi Yerusalemu.

4Ilikuwa baada ya haya kukawa na pambano huko Gezeri na Wafilisti. Sibekai Mhushathi akamua Sipai, mmoja wa uzao wa Refaimu, na wa Filisti wakazidiwa.

5Ikawa tena katika pambano na Wafilisti huko Gobu, kwamba Elhanani mwana wa Yari Mbethilehemu akamua Lami kaka wa Goliathi Mgiti, ambaye mkuki wake ulikuwa kama gongo la mshonaji.

6Ikaja kuwa tena katika pambano lingine huko Gathi kwamba mwanaume mmoja aliye mrefu sana mwenye vidole sita kila mkono na vidole sita mguuni. Naye alikuwa pia wa uzao wa Refaimu.7Alipo dhihaki jeshi la Israeli, Yehonadabu mwana wa Shimea, kaka wa Daudi, akamuua.

8Hawa walikuwa uzao wa Refaimu wa Gathi, na waliuawa na mkono wa Daudi na mkono wa watumishi wake.

21

1Adui akainuka dhidi ya Israeli na kumchochea Daudi kuhesabu Israeli.

2Daudi akamwabia Yoabu na kwa wakuu wa Jeshi, “Nenda, wahesabu watu wa Israeli kutoka Beerisheba mpaka Dani na mniletee taarifa, ilinijue idadi yao.”

3Yoabu akasema, “Yahweh na afanya jeshi lake mara mia zaidi ya lilivyo. Lakini bwana wangu mfalme, je! Wote hawamtumikii bwana wangu? Kwa nini bwana wangu anataka hili? Kwa nini ulete hatia kwa Israeli?”

4Lakini neno la mfalme lilitimizwa juu ya Yoabu. Hivyo Yoabu akaondoka na kwenda Israeli yote. Kisha akarudi Yerusalemu.5Yoabu akatoa taarifa ya idadi ya jumla ya wanaume wa mapambano kwa Daudi. Kulikuwa ndani ya Israeli wanaume 1,100,000 walio beba upanga. Yuda peke yake kulikuwa na wanajeshi 470,000.6Lakini Law na Benjamini hawakuhesabiwa miongoni mwao, kwa kuwa amri ya mfalme ilichukiza Yoabu.

7Mungu alikwazika na hili tendo, hivyo akashambulia Israeli.8Daudi akamwambia Mungu, “Nimetenda dhambi kubwa kwa kufanya hili. Sasa chukua hatia ya mtumishi wako, maana nimefanya upumbavu sana.”

9Yahweh akamwambia Gadi, nabii wa Daudi,10“Nenda useme kwa Daudi, “Hili ndilo Yahweh anasema: Ninakupa maamuzi matatu. Chagua moja wapo.”

11Hivyo Gadi akaenda kwa Daudi na kusema, “Yahweh anasema hivi, ‘Chagua moja ya haya:12kati ya miaka mitatu ya ukame, miezi mitatu unakimbizwa na adui zako na kupatwa na upanga wao, au siku tatu za upanga wa Yahweh, yani, pigo katika nchi, malaika wa Yahweh akiharibu nchi yote ya Israeli.’ Hivyo sasa, amua jibu gani ni mpelekee yeye aliye nituma.”

13Kisha Daudi akamwambia Gadi, “Niko kwenye dhiki kubwa. Acha nianguke katika mikono ya Yahweh kuliko kuangukia mikono ya mwanadamu, sababu matendo yake ya rehema ni makubwa mno.”

14Hivyo Yahweh akatuma pigo Israeli, na watu elfu sabini wakafa.15Mungu akatuma malaika Yerusalemu kuiharibu. Alipokuwa anakaribia kuiharibu, Yahweh akatazama na kubadili nia yake kuhusu shambulio. Akasema kwa malaika wa uharibifu, “Imetosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Yahweh alikua amesimama eneo la kupeta la Orinani Myebusi.

16Daudi akatazama juu na kuona malaika wa Yahweh amesimama kati ya nchi na mbingu, akiwa na upanga mkonono mwake akiuelekeza Yerusalemu. Kisha Daudi na wazee, wakiwa wamevaa magunia, wakalala chini uso ukiwa kwenye ardhi.

17Daudi akamwambia Mungu, “Si ni mimi niliye amuru jeshi kuhesabiwa? Nilifanya hichi kitu kiovu. Lakini hawa kondoo, wamefanya nini? Yahweh Mungu wangu! Acha mkono wako unipige mimi na ukoo wangu, lakini usiache pigo iliendelee kubaki kwa watu wako.”

18Hivyo malaika wa Yahweh akamuamuru Gadi kusema kwa Daudi, kwamba Daudi aende juu na kujenga madhabahu ya Yahweh katika eneo la kupeta la Arauna Myebusi.19Daudi akaenda kama Gadi alivyo muelekeza cha kufanya kwa jina la Yahweh.

20Wakati Orinani akipepeta ngano, aligeuka na kumuona malaika. Yeye na wanawe wanne wakajificha.21Wakati Daudi alipo kuja kwa Orinani, Orinani akatazama na kumuona Daudi. Aliacha eneo la kupeta na akamuinamia Daudi uso wake ukiwa kwenye ardhi.

22Kisha Daudi akasema kwa Orinani, “Niuzie hili eneo la kupeta, iliniweze kumjenga Yahweh madhabahu. Nitalipa gharama yote, ili pigo liondolewe kwa watu.”

23Orinani wakwambia Daudi, “Chukuwa kama lako, bwana wangu mfalme. Fanya nalo linalo kupendeza. Tazama, nitakupa ng'ombe kwa sadaka ya kuteketeza, vifaa vya kupeta kwa ajili ya mbao, na ngano kwa sadaka ya mbegu; nitakupa yote wewe.”

24Mfalme Daudi akamwambia Orinani, “Hapana, nina sisitiza kununua kwa bei yote. Sitachukua kilicho chako na kutoa kama sadaka ya kuteketeza kwa Yahweh kama haitanighramu chochote.”

25Hivyo Daudi akalipa shekeli mia sita ya dhahabu kwa hilo eneo.26Daudi akajenga madhabahu ya Yahweh pale na kutoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za ushirika. Akamuita Yahweh, aliye mjibu kwa moto kutoka mbinguni kwenye madhabahu ya sadaka za kuteketezwa.

27Kisha Yahweh akampa agizo malaika, na malaika akarudisha upanga kwenye mfuko wake.28Daudi alipo ona kuwa Yahweh amemjibu kwenye eneo la kupeta la Orinani Myebusi, alitoa dhabihu pale pale kwa wakati huo.29Sasa kwa wakati huo, hema la kuabudia la Yahweh, ambalo Musa alilitengeneza nyikani, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa, zilikuwa sehemu ya juu huko Gibeoni.30Walakini, Daudi hakuweza kwenda huko kumuliza Mungu muelekeo, kwa kuwa alikuwa anaogopa upanga wa malaika wa Yahweh.

22

1Kisha Daudi akasema, “Hapo ndipo nyumba ya Yahweh Mungu itakuwepo, na madhabahu ya sadaka za kuteketezwa za Israeli.”

2Hivyo Daudi akaagiza watumishi wake wawakusanye pamoja wageni wote wanao ishi katika nchi ya Israeli. Aliwapangia kuwa wachonga mawe, kuchonga matofali ya mawe, ilikuweza kujenga nyumba ya Mungu.3Daudi alisambaza idadi kubwa ya chuma kwa ajili ya misumari na vitasa vya kuweka kwenye malango. Pia alitoa shaba zaidi kushinda kipimo,4na miti ya mierezi zaidi ya kipimo. (Wasidoni na Watiria walileta magogo mengi sana ya mierezi kwa Daudi asiweze kuhesabu

5Daudi akasema, “Mwanangu Sulemani ni mdogo na hana uzoefu, na nyumba itayo jengwa kwa Yahweh lazima iwe maridadi, ilikwamba iwe maarufu na ya utukufu kwa nchi zingine zote. Hivyo nitaanda ujenzi wake.” Hivyo Daudi akafanya maandalizi ya kina kabla ya mauti yake.

6Kisha akamwita Sulemani mwanae na kumuamuru ajenge nyumba ya Yahweh, Mungu wa Israeli.7Daudi akasema kwa Sulemani, “Mwanangu, ilikuwa dhamira yangu kujenga nyumba mwenyewe, kwa ajili ya jina la Yahweh Mungu wangu.8Lakini Yahweh alikuja kwangu na kusema, ‘Wewe umemwaga damu nyingi na umepigana mapambono mengi. Hautajenga nyumba kwa jina langu, kwa sababu umemwaga damu nyingi kwenye ardhi machoni pangu.9Walakini, utapata mwana ambaye atakuwa mtu wa amani. Nitampa kupumzika na maadui zake kwa kila upande. Kwa kuwa jina lake litaitwa Sulemani, na nitatoa amani na utulivu kwa Israeli katika siku zake.10Ata jenga nyumba kwa jina langu. Ata kuwa mwana wangu, na nitakuwa baba yake. Nitaimarisha kiti cha ufalme wake juu ya Israeli milele.

11Sasa, mwanangu, Yahweh awe nawe na kukuwezesha kufanikiwa. Uweze kujenga nyumba ya Yahweh Mungu wako, kama alivyo sema utajenga.12Yahweh tu akupe uwelewa na ufahamu, ili utii sheria ya Yahweh Mungu wako, ata kapokuweka kiongozi juu ya Israeli.13Kisha utafanikiwa, kama tu ukitii maagizo na amri Yahweh alizo mpa Musa kuhusu Israeli. Kuwa hodari na jasiri. Usiogope wala usikate tamaa

14Sasa, ona, kwa bidii kubwa nimeandaa kwa ajili ya nyumba ya Yahweh talanta 100,000 za dhahabu, talanta milioni moja za fedha, na shaba na chuma katika idadi kubwa. Pia nimetoa mbao na mawe. Lazima uongeze zaidi katika haya.15Una wafanya kazi wengi: wachonga mawe, waashi, maseremala, na mafundi stadi bila idadi wa kila aina,16wenyeuwezo wa kufanya kazi na dhahabu, fedha, shaba, na chuma. Inuka na uanze kazi, na Yahweh awe nawe.

17Daudi akawaagiza viongozi wote Waisraeli wamsaidie Sulemani mwanae, akisema,18“Yahweh Mungu wenu yupo nanyi na amewapa amani kila pande. Amewakabidhi mikononi mwangu wenyeji wote mkoa. Mkoa umetiishwa mbele za Yahweh na watu wake.19Sasa mtafuteni Yahweh Mungu wenu kwa moyo wenu wote na nafsi. Simameni na mjenge sehemu takatifu ya Yahweh Mungu. Kisha mwaweza kuleta sanduku la agano la Yahweh na vitu vya Mungu ndani ya nyumba iliyo jengwa kwa ajili ya jina la Yahweh.

23

1Daudi alipokuwa mzee na kukaribia mwisho wa maisha yake, alimfanya Sulemani mwanae mfalme juu ya Israeli.

2Aliwakusanya pamoja viongozi wote wa Israeli, na makuhani na Walawi.3Walawi walio kuwa miaka thelathini na zaidi walihesabiwa, na idadi yao ikawa elfu thelathini na nane.4Kwa hawa, elfu ishirini na nne walikuwa kusimamia kazi ya nyumba ya Yahweh, na elfu sita walikuwa maaskari na waamuzi.5Elfu nne walikuwa walinzi wa lango, na elfu nne walikuwa wamsifu Yahweh na vyombo nilivyo vitengeneza vya kusifu.” Daudi akasema.

6Akawatenganisha kwenye vikundi kulingana na wana wa Lawi: Gerishoni, Kohathi, na Merari.7Kwa koo za uzao wa Gerishoni, kulilkuwa na Ladani na Shimei.
8Palikuwa na watatu wa wana wa Ladani: Yehieli kiongozi, Zethami, na Yoeli.
9Palikuwa na watatu wa wana wa Shimei: Shelomothi, Hazieli, na Harani. Hawa walikuwa viongozi wa koo ya Ladani.
10Palikuwa na wanne wa wana wa Shimei: Yahathi, Ziza, Yeushi, na Beria.
11Yahathi alikuwa mkubwa, Ziza wapili, lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi, hivyo walihesabiwa kama ukoo mmoja na kupangiwa kazi sawa.
12Palikuwa na wanne wa wana wa Kohathi: Amramu, Izhari, Hebroni, na Uzieli.
13Hawa walina wa Amramu: Aruni na Musa. Aruni alichaguliwa kuandaa vitu vitakatifu, yeye na uzao wake watatoa uvumba kwa Yahweh, kumtumikia na kumpa baraka kwa jina lake.
14Lakini kwa Musa mtu wa Mungu, wana wake walihesabiwa kuwa Walawi.
15Wana wa Musa walikuwa Gerishomu na Eliezeri.
16Uzao wa Gerishomu ulikuwa Shebueli mkubwa.
17Uzao wa Eliezeri alikuwa Rehabia. Eliezeri hakuwa na wana wengine, lakini Rehabia alikuwa na uzao mkubwa.
18Mwana wa Izihari alikuwa Shelomithi kiongonzi.
19Uzao wa Hebroni ulikuwa Yeria, mkubwa, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
20Wana wa Uzieli walikuwa Mika mkubwa, na Ishia wapili.
21Wana wa Merari walikuwa Mahili na Mushi. Wana wa Mahili walikuwa Eleazari na Kishi.
22Eleazari alikufa bila mtoto wa kiume. Alikuwa na mabinti tu. Wana wa Kishi waliwaoa.
23Wana wa Mushi watatu walikuwa Mahili, Ederi, na Yeremothi.

24Hawa walikuwa uzao wa Lawi kulingana na koo zao. Walikuwa viongozi, wamehesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, kuanzia koo zilizo fanya kazi katika nyumba ya Yahweh, kutoka miaka ishirini na zaidi.25Kwa kuwa Daudi alisema, “Yahweh, Mungu wa Israeli, amewapa pumziko watu wake. Anafanya makao yake Yerusalemu milele.26Walawi hawatahitaji kubeba hema la kuabuadia na vifaa vyake vinavyo tumika kwenye utumishi wake.”27Kwa maneno ya Daudi ya mwisho Walawi walihesabiwa, miaka ishirini na kuendelea.

28Wajibu wao ulikuwa kuwasaidia wazao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh. Walikuwa washughulikie nyuani, vyumbani, utakasaji wa vitu vyote vya Yahweh, na kazi zingine katika utumishi wa nyumba ya Mungu.29Pia walishughulikia mkate wa uwepo, unga safi wa mbegu za sadaka, mikate kaki isiotiwa chachu, sadaka zilizookwa, sadaka ziliochanganywa na mafuta, na vipimo vyote vya kiasi na ukubwa wa vitu.30Pia walisimama kila asubui kumshukuru na kumsifu Yahweh. Pia walifanya hivi jioni31na kila wakati sadaka ya kuteketezwa ilipo tolewa kwa Yahweh, siku ya Sabato na sherehe za mwezi mpya na siku za maakuli. Idadi maalumu, iliyo tolewa kwa amri, siku zote ilibidi iwepo mbele ya Yahweh.

32Walikuwa viongozi wa hema la kukutania, patakatifu, na kuwasaidia jamaa zao wa uzao wa Aruni katika utumishi wa nyumba ya Yahweh.

24

1Makundi vya kazi kulingana na uzao wa Aroni yalikuwa haya: Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.

2Nadabu na Abihu walikufa kabla ya baba yao kufa. Walikuwa hawana watoto, kwa hiyo Eleazari na Ithamari walitumika kama makuhani.3Daudi pamoja na, uzao wa Eleazari, na Zadoki wa Ithamari, waliwagawanya katika makundi ya kazi yao kama makuhani.4Kulikuwa na wanaume viongozi zaidi kati ya uzao wa Eleazari kuliko kati ya uzao wa Ithamari, kwahiyo waligawanya uzao wa Eleazari katika makundi kumi na sita. Walifanya hivyo na viongozi wa ukoo na uzao wa Ithamari. Magawanyo haya yalikuwa nane kwa idadi, sambamba na koo zao.5Waliwagawanya bila upendeleo kwa kura, kwa kuwa walikuwa waamuzi watakatifu na waamuzi wa Mungu, kutoka pande zote uzao wa Eleazari na uzao wa Ithamari.

6Shemaia mwana wa Nethaneli mwandishi, Mlawi, aliandika majina yao mbele ya mfalme, muamuzi, kuhani Zadoki, Ahimeleki mwana wa Abiathari, na viongozi wa makuhani na familia za Walawi. Ukoo mmoja ulichaguliwa kwa kura kutoka uzao wa Eleazari, na kisha uliofata utachaguliwa kutoka uzao wa Ithhamari.
7Kura ya kwanza ilienda kwa Yehoiaribu, ya pili kwa Yedaia,
8ya tatu kwa Harimu, ya nne kwa Seorimu,
9ya tano kwa Malikija, ya sita kwa Mijamini,
10ya saba kwa Hakozi, ya nane kwa Abija,
11ya tisa kwa Yeshua, ya kumi kwa Shekania,
12ya kumi na moja kwa Eliashibu, ya kumi na mbili kwa Yakimu,
13ya kumi na tatu kwa Hupa, ya kumi na nne kwa Yesheheabu,
14ya kumi na tano kwa Biliga, ya kumi na sita kwa Imma,
15ya kumi na saba kwa Heziri, ya kumi na nane kwa Hapizezi,
16ya kumi na tisa kwa Pethaia, ya ishirini kwa Yehezikeli,
17ya ishirini na moja kwa Yakini, ya ishirini na mbili kwa Gamuli,
18ya ishirini na tatu kwa Delaia, na ya ishirini na nne kwa Maazia.

19Hii ilikuwa taratibu ya utumishi wao, walipo kuja kwenye nyumba ya Yahweh, wakifuata utaratibu waliopewa na Aruni babu yao, kama Yahweh, Mungu wa Israeli, alivyo waagiza.20Hawa walikuwa Walawi waliobakia: Wana wa Amiramu, Shebueli; wana wa Shebaeli, Yedeia.
21Wana wa Rehabia: wana wa Rehabia, Ishia kiongozi.
22Wa Waizari, Shelomothi; mwana wa Shelomothi, Yahathi.
23Wana wa Hebroni: Yeria kiongozi, Amaria wapili, Yahazieli watatu, na Yekameamu wanne.
24Wana wa uzao wa Uzieli ulimjumuisha Mika. Uzao wa Mika ulimjumuisha Shamiri.
25Kaka wa Mika alikuwa Ishia. Wana wa Ishia akijumuishwa Zakaria.
26Wana na Merari: Mahli na Mushi. Mwana wa Yaazia, Beno.
27Wana wa Merari: Yaazia, Beno, Shohamu, Zakuri, na Ibrri.
28Wana wa Mahili: eleazari, ambaye alikuwa hana wana.
29Wana wa Kishi: Yerameli
30wana wa Mushi: Mahli, Eda, na Yerimothi. Walikuwa Walawi, walio orodheshwa na familia zao.
31Wanaume hawa ambao walikuwa vichwa wa kila koona kila kaka zao wadogo zao, walipiga kura katika uwepo wa Mfalme Daudi, na Zadoki na Ahimeleki, pamoja na viongozi wa familia wa makuhani na Walawi. Walirusha kura kama uzao wa Aroni walivyofanya.

25

1Daudi na viongozi wa jeshi walichagua baadhi ya wana wa Asafu, Hemani, na Yeduthuni kutabiri kwa vinanda na vinubi, na kwa upatu. Hii ni orodha ya wanaume walioifanya hii kazi:2Kutoka wana wa Asafu: Zakuri, Yosefu, Nethania, na Asharela, wana wa Asafu, chini ya mwongozo wa Asafu, ambaye alitabiri chini ya uwangalizi wa mfalme.3Kutoka wana wa Yeduthuni: Gedalia, Zeri, Yeshaia, Shimei, Hashabia, na Matithia, sita kwa ujumla, chini ya mwongozo wa baba yao Yeduthuni, ambaye alitabiri, akipiga kinubi kwa kutoa shukurani na kumsifu Yahweh.

4Kutoka wana wa Hemani: Bukia, Matania, Uzieli, Shebueli, na Yerimothi, Hanania, Hanani, Eliatha, Gidalti, Romamti Ezeri, Yoshibekasha, Mallothi, Hothiri, na Mahaziothi.
5Hawa wote walikuwa wana wa Hemani, nabii wa mfalme. Mungu alimpa Hemani wana kumi na nne na mabinti watatu kuinua pembe yake.

6Hawa wote walikuwa chini ya mwongozo wa baba zao. Walikuwa ni waimbaji katika nyumba ya Yahweh kwa upatu, vinanda, na vyombo vya uzi, wakihudumu katika nyumba ya Mungu. Asafu, Yeduthuni, na Hemani walikuwa chini ya uwangalizi wa mfalme.7Wao na kaka zao waliokuwa na ujuzi na mafundisho ya kufanya muziki kwa Yahweh walikuwa na idadi ya 288.8Wapiga kura kwa ajili ya kazi zao, wote sawa, sawa vivyo hivyo kwa vijana na kwa wazee, kwa mwalimu na kwa mwanafunzi.
9Sasa kuhusu wana wa Asafu: kura ya kwanza iliangukia katika familia ya Yusufu; ya pili iliangukia katika familia ya Gedalia, idadi ya watu kumi na mbili;
10ya tatu iliangukia kwa Zakuri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;11ya nne iliangukia kwa Izri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;12ya tano iliangukia kwa Nethania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
13ya sita iliangukia kwa Bukia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
14ya saba iliangukia kwa Yesharela, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;15ya nane iliangukia kwa Yeshaia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;16ya tisa iliangukia kwa Matania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
17ya kumi iliangukia kwa Shimei, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
18ya kumi na moja iliangukia kwa Azareli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;19ya kumi na mbili iliangukia kwa Hashabia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;20ya kumi na tatu iliangukia kwa Shubaeli, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
21ya kumi na nne iliangukia kwa Matithia, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
22ya kumi na tano iliangukia kwa Yeromothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;23ya kumi na sita iliangukia kwa Hanania, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;24ya kumi na saba iliangukia kwa Yoshibekasha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
25ya kumi na nane iliangukia kwa Hanani, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
26ya kumi na tisa iliangukia kwa Malothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;27ya ishirini iliangukia kwa Eliatha, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;28ya ishirini na moja iliangukia kwa Hothiri, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
29ya ishirini na mbili iliangukia kwa Gidalti, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;
30ya ishirini na tatu iliangukia kwa Mahaziothi, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili;31ya ishirini na nne iliangukia kwa Romamti Eza, wana wake na ndugu zake, idadi ya watu kumi na mbili.

26

1Haya ndiyo makundi yawalinzi wa lango: Kutoka kwa Wakora, Meshelemia mwana wa Kore, wa uzao wa Asafu.

2Meshelemia alikuwa na wana wa kiume: Zekaria mzaliwa wa kwanza, Yediaeli wapili, Zebadia watatu, Yathinieli wanne,
3Elamu watano, Yehohanani wasita, Eliehoenai wasaba.
4Obedi alikuwa na wana wa kiume: Shemaia wa kwanza, Yehozabadi wapili, Yoa watatu, na Sakari wanne, na Nethanieli watano,
5Amieli wasita, Isakari wasaba, Peulethai wanane, kwa kuwa Mungu alimbariki Obedi Edomu.
6Kwa Shemaia mwanaye walizawa wana walio tawala koo zao; walikuwa wanaume wenye uwezo mkuu.
7Wana wa Shemaia walikuwa Othini, Refaeli, Obedi, na Elizabadi. Jamaa zake Elihu na Semakia walikuwa wanaume wenye uwezo mbali mbali.
8Hawa wote walikuwa uzao wa Obedi Edomu. Wao na wanao na jamaa zao walikuwa wanaume wenye uwezo wa kufanya wajibu wao katika huduma ya hema la kuabudia. Palikuwa na sitini na mbili walio kuwa na undugu na Obedi Edomu.
9Meshelemia alikuwa na wana na jamaa, wanaume wenye uwezo, jumla ya kumi na nane.
10Hosa, mzao wa Merari, alikuwa na wana: Shimiri kiongozi (ijapo hakuwa mzaliwa wa kwanza, baba yake alimfanya kiongozi),
11Hilikia wapili, Tebalia watatu, Zekaria wanne. Wote wa wana wa Hosa na jamaa walikuwa kumi na tatu kwa idadi.

12Haya makundi ya walinzi wa lango, sambamb a na viongozi, yalikuwa na majukumu, kama jamaa zao, kutumika katika nyumba ya Yahweh.13Walipiga kura, wadogo kwa wakubwa, kulingana na koo zao, kwa kila lango.14Kura ilipo pigwa kwa lango la mashariki, ilimuangukia Shelemia. Kisha wakapiga kura kwa Zekaria mwanaye, mshauri mwenye busara, na kura yake ikatokea kwa lango la kaskazini.
15Kwa Obedi Edomu alipangiwa lango la kusini, na wanawe walipangiwa nyumba za ghala.
16Shufimu na Hosa walipangiwa lango la magharibi pamoja na lango la Shalekethi, kwenye barabara ya juu. Walinzi walikuwa karibu sana.17Kwa mashariki walikuwa Walawi sita, kaskazini wanne kwa siku moja, kusini wanne kwa siku moja, na nyumba za ghala jozi mbili.18Kwenye nguzo upande wmagharibi wanne kulikuwa na wanne waliosimama kwenye barabara na wawili kwenye nguzo.

19Haya yalikuwa makundi ya walinzi wa lango waliokuwa uzao wa Kora na Merari.

20Miongoni mwa Walawi, Ahija alikuwa kiongozi wa hazina ya nyumba ya Mungu, na hazina ya vitu vya Yahweh.21Wazao wa Ladani, walitoka kwa Gerishoni kupitia kwake na walio kuwa viongozi wa familia za Ladani Mgerishoni, walikuwa Yehieli22na wanae Yehieli: Zethamu na Yoeli kaka yake. Walikuwa wamesimamia hazina za nyumba ya Yahweh.

23Kutoka koo za Amramu, koo za Izhari, koo za Hebroni, na koo za Uzieli:
24Shebueli uzao wa Gerishomu mwana wa Musa, alikuwa msimamizi wa hazina.
25Jamaa zake wa ukoo wa Eliezeri walikuwa Rehabia mwanawe, mwana wa Rehabia Yeshaia, mwana wa Yeshaia Yoramu, mwana wa Yoramu Zikiri, na mwana wa Zikiri Shelomothi.26Shelomothi na jamaa zake walikuwa wasimamizi wa hazina zote za ghala zinazo hifadhi vitu vyote vya Yahweh, ambavyo Daudi mfalme, viongozi wa familia, wakuu wa maelfu na mamia, na wakuu wa jeshi walivyo vitenga.27Walitenga vitu walivyo vichukuwa kwenye mapambano kwa ajili ya kutunza nyumba ya Yahweh.28Pia walikuwa wahusika wa kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh na Samweli nabii, Sauli mwana wa Kishi, Abneri mwana wa Neri, na Yoabu mwana wa Zeruia. Kila kitu kilicho tengwa kwa ajili ya Yahweh kilikuwa chini ya ulinzi wa shelomothi na jamaa zake.
29Wa uzao wa Izhari, Kenania na wana wake walikuwa wahusika wa mambo ya ndani ya Israeli. Walikuwa maafisa na waamuzi.
30Wa uzao wa Hebroni, Hashabia na kaka zake, wanaume wenye uwezo 1,700, walikuwa wahusika wa kazi ya Yahweh na kazi ya mfalme. Walikuwa upande wa mgharibi mwa Yordani.
31Kutoka uzao wa Hebroni, Yeriya alikuwa kiongozi wa koo, kulingana na orodha za familia zao. Katika mwaka wa arobaini wa utawala wa Daudi walitathimini kumbukumbu na kugundua miongoni mwao wanaume wa uwezo mkubwa katika Yazeri ya Gileadi.32Yerija alikuwa na ndugu 2,700, walio kuwa viongozi wenye uwezo katika familia. Daudi aliwafanya waangalizi wa makabila ya Rubeni na Gadi, na nusu kabila la Manase, kwa kila jambo linalo muhusu Mungu, na kwa mambo ya mfalme.

27

1Hii ni orodha ya familia za viongozi wa Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, pamoja na maafisa wa jeshi walio mtumikia mfalme kwa namna tofauti. Kila kikosi cha jeshi kilitumika mwenzi hadi mwezi kwa mwaka mzima. Kila kikosi kilikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.

2Juu ya kikosi kwa mwezi wa kwanzaalikuwa Yashobeamu mwana wa Zabdieli. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
3Alikuwa miongoni mwa uzao wa Perezi na msimamizi wa maafisa wa jeshi kwa mwezi wa kwanza.
4Juu ya kikosi kwa mwezi wa pili alikuwa Dodai, wa ukoo wa uliotoka kwa Ahoa. Mikilothi alikuwa wa pili kwa cheo. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
5Mkuu wa jeshi wa mwezi wa tatu alikuwa Benaia mwana wa Yehoiada, kuhani na kiongozi. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
6Huyu ni Benaia aliye kuwa kiongozi wa wale thelathini na juu ya wale thelathini. Amizabadi mwanae alikuwa katika kikosi chake.
7Mkuu kwa mwezi wa nne alikuwa Asaheli kaka wa Yoabu. Zebadia mwanae akawa mkuu baada yake. Katika kikosi chake kulikuwa na wanaume elfu ishirini na nne.
8Mkuu kwa mwezi wa tano alikuwa Shamihuthi, mzao wa Izra. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
9Mkuu kwa mwezi wa sita alikuwa Ira mwana wa Ikeshi, kutoka Tekoa. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
10Mkuu kwa mwezi wa saba alikuwa Helezi Mpeloni, kutoka watu wa Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
11Mkuu kwa mwezi wa nane alikuwa Sibekai Mhushathi, kutoka ukoo ulitoka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
12Mkuu kwa mwezi wa tisa alikuwa Abi Ezeri Manathothi, kutoka kwa kabila la Benjamini. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
13Mkuu kwa mwezi wa kumi alikuwa Maharai kutoka mji wa Netofa, kutoka ukoo ulio toka kwa Zera. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
14Mkuu kwa mwezi wa kumi na moja alikuwa Benaia kutoka mji wa Pirathoni, kutoka kabila la Efraimu. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.
15Mkuu kwa mwezi wa kumi na mbili alikuwa Helidai kutoka mji wa Netopafa, kutoka ukoo uliotoka kwa Othinieli. Katika kikosi chake walikuwa wanaume elfu ishirini na nne.

16Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli: Kwa kabila la Rubeni, Eliezeri mwana wa Zikri alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Simeoni, Shefatia mwana wa Maka alikuwa kiongozi.
17Kwa kabila la Lawi, Hashinia mwana wa Kemueli alikuwa kiongozi, na Zadoki aliongoza uzao wa Aruni.
18Kwa kabila la Yuda, Elihu, mmoja wa kaka zake Daudi, alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Isakari, Omri mwana wa Mikaeli alikuwa kiongozi.
19Kwa kabila la Zebuluni, Ishimaia mwana wa Obadia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Naftali, Yeremothi mwana wa Azirieli alikuwa kiongozi.
20Kwa kabila la Efraimu, Hoshea mwana wa Azazia alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Manase, Yoeli mwana wa Pedaia alikuwa kiongozi.
21Kwa nusu kabila la Manase lililo Gileadi, Ido mwana wa Zekaria alikuwa kiongozi. Kwa kabila la Benjamini, Yaasieli mwana wa Abneri alikuwa kiongozi.
22Kwa kabila la Dani, Azareli mwana wa Yerohamu alikuwa kiongozi. Hawa walikuwa viongozi wa makabila ya Israeli.

23Daudi hakuwa hesabu wenye umri wa miaka ishirini au chini zaidi, kwasababu Yahweh alihaidi kuongeza Israeli kama nyota za mbinguni.24Yoabu mwana wa Zeruia alianza kuhesabu wanaume, lakini hakumaliza. Gadhabu iliangukia Israeli kwa hili. Hii idadi haikuandikwa kwenye nyakati za mfalme Daudi.
25Azimavethi mwana wa Adieli alikuwa mhusika wa hazina za mfalme. Yonathani mwana wa Uzia alikuwa juu ya nyumba za ghala katika mashamba, kwenye miji, na vijijini, na kwenye minara iliyo imarishwa.
26Ezri mwana wa Kelubi alikuwa juu ya mashamba, hao walio lima ardhi.27Shimei kutoka Rama alikuwa juu ya mashamba ya mizabibu, na Zabdi Mshefamu alikuwa juu ya zabibu na pishi za mvinyo.
28Mwangalizi wa miti mizeituni na miti ya mikuyu iliyo kuwa bondeni alikuwa Baali Hanani kutoka Gederi, na juu ya nyumba za ghala za mafuta alikuwa Yoashi.
29Juu ya mifugo iliyo kuwa inalishwa huko Sharoni alikuwa Shitrai kutoka Sharoni, na juu ya mifugo iliyo kuwa mabondeni alikuwa Shafati mwana wa Adlai.
30Msimamizi wa ngamia alikuwa Obili Mishimaeli, na juu ya punda wakike alikuwa Yehideia kutoka Meronothi. Juu ya mifugo alikuwa Yazizi Mhagri.
31Hawa maafisa wote walikuwa wasimamizi wa mali za Mfalme Daudi.
32Yonathani, mjomba wake Daudi alikuwa mshauri, sababu alikuwa na busara na mwandishi. Yehieli mwana wa Hakimoni aliwajali wana wa mfalme.
33Ahithofeli alikuwa mshauri wa mfalme, na Hushai kutoka watu wa Mwarki aliyekuwa rafiki yake mfalme.34Nafasi ya Ahithofeli ilichukuliwa na Yehoiada mwana wa Benaia, na Abiathari. Yoabu alikuwa mkuu wa jeshi la mfalme.

28

1Daudi akakusanya maafisa wote wa Israeli Yerusalemu: maafisa wa makabila, maafisa wa vitengo walio mtumikia mfalme katika kazi walizo pangiwa, wakuu wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali zote za mfalme na wanawe, na maafisa na wanaume wa mapambano, ukijumuisha wale wenye ujuzi sana.

2Kisha Daudi mfalme akainuka kwa miguu yake na kusema, “Sikilizeni mimi, kaka zangu na watu wangu. Ilikuwa dhumuni langu kujenga hekalu kwa ajili ya sanduku la agano la Yahweh; stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu, na nimefanya maandalizi kuijenga.3Lakini Mungu akaniambia, ‘Hautajenga hekalu kwa ajili ya jina la langu, kwasababu wewe ni mwanaume wa vita na umemwaga damu.’

4Bado Yahweh, Mungu wa Israeli, alinichagua kutoka katika familia ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Amechagua kabila la Yuda kama kiongozi. Katika kabila la Yuda, na nyumba ya baba yangu, kutoka kwa wana wa baba yangu, amenichagua kuwa mfalme wa Israeli.5Kutoka kwa wana wengi ambao Yahweh amenipa, amemchagua Sulemani, mwanangu, kuketi katika kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli.6Aliniambia, ‘Sulemani mwanae atanijengea nyumba yangu na nyuani mwangu, kwa kuwa nimemchagua kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake.7Nitaimarisha ufalme wake, akidumu kutii sheria na amri zangu, kama ulivyo siku ya leo.’

8Kisha sasa, katika macho ya Waisraeli wote, hili kusanyiko la yahweh, na katika uwepo wa Mungu wetu, nyinyi nyote lazima mshike na kufanya amri zote za Yahweh Mungu wenu. Fanyeni hivi ili mmiliki nchi hii nzuri na kuiacha kama urithi kwa uzao wenu baada yenu milele.

9Kwako wewe, Sulemani mwanangu, mtii Mungu wa baba yako, mtumikie kwa moyo wako wote na roho ya utayari. Fanya hivi kwa sababu yahweh anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu. Ukimtafuta, ataonekana nawe, lakini ukimtelekeza, atakukataa milele.10Elewa kuwa Yahweh amekuchagua kulijenga hekalu hili kama patakatifu pake. Uwe hodari na uifanye.”

11Kisha Daudi akamkabidhi Sulemani mwanae mipango ya ukumbi wa hekalu, majengo ya hekalu, vyumba vya hifadhi, vyumba vya juu, vyumba vya ndani, na chumba chenye kifuniko cha upatanisho.12Alimpatia mipango aliyo chora ya nyuani kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vyumba vyote vilivyo zunguka, vyumba vya hifadhi katika nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vya Yahweh.13Alimpatia masharti kwa vitengo vya makuhani na Walawi, kwa majukumu walio pangiwa kwa utumishi wa nyumba ya Yahweh, na kwa vyombo vyote vinavyo tumika katika nyumba ya Yahweh.14Aliamua uzito wa vifaa vyote vya dhahabu kwa kila huduma, uzito wa vifaa vya fedha kwa kila huduma,15uzito wa dhahabu wa vifaa vyote vya dhahabu, kuwavinara vya taa na taa za dhahabu, uzito wa dhahabu kwa kila kinara cha taa, uzito wa fedha kwa kila kinara cha fedha, kulingana na matumizi ya kila kinara cha taakatika huduma.16Alitoa uzito wa dhahabu kwa ajili ya meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha.17Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa uma za nyama, beseni, na vikombe. Alitoa uzito kwa kila bakuli ya dhahabu, na uzito kwa kila bakuli ya fedha.18Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa ajili ya madhabahu ya uvumba, na za dhahabu kwa muundo wa gari, makerubi waliye tanda mabawa yao na kufunika sanduku la agano la Yahweh.

19Daudi akasema, “Nimeweka haya katika maandishi kama Yahweh alivyonielekeza na kunipa kuelewa kuhusu mchoro.”

20Daudi akasema kwa Sulemani mwanae, “Kuwa hodari na mjasiri. Fanya kazi. Usiogope au kufadhai, kwa kuwa Yahweh Mungu, Mungu wangu, yupo nawe. Hatakuacha wala kukutelekeza mpaka kazi ya huduma ya hekalu la Yahweh imekamilika.21Ona, hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi kwa huduma katika hekalu la Mungu. Watakuwa nawe, pamoja na wanaume walio tayari na wenye ujuzi, kukusaidia katika kazi na kutenda huduma. Maafisa na watu wote wako tayari kufuata amri zako.”

29

1Mfalme Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sulemani mwanangu, ambaye mwenyewe Mungu amemchagua, bado ni mdogo na hana uzoefu, na jukumu ni kubwa. Maana hekalu sio kwa ajili ya watu bali la Mungu.2Hivyo nimefanya kwa ubora wangu kutoa kwa ajili ya hekalu la Mungu. Nina toa dhahabu kwa vitu vitakavyotengenezwa na dhahabu, fedha kwa vitu vitu vitakavyotengenezwa na fedha, shaba kwa vitu vitakavyotengenezwa na shaba, nishati kwa vitu vitakavyotengenezwa na nishati, na mbao kwa vitu vitakavyotengenezwa na mbao. Pia nina toa mawe ya shohamu, mawe ya kupangwa, mawe ya upambaji wandani ya rangi mbali mbali - kila haina ya mawe ya thamani - na marimari kwa wingi.3Sasa, kwa sababu ya mapenzi yangu kwa nyumba ya Mungu, ninatoa hazina yangu binafsi ya dhahabu na fedha. Ninafanya hivi kwa nyongeza kwa yote niliyofanya katika hekalu takatifu:4talanta za dhahabu elfu tatu kutoka Ofiri, na talanta elfu saba za fedha zilizotakasika, ili kufunika kuta za majengo.5Ninachangia dhahabu kwa vitu vya kutengenezwa na dhahabu, na fedha kwa vitu vya kutengenezwa na fedha, na vitu vya kazi zote zinazotakiwa kufanywa na mafundi. Nani mwingine anataka kuchangia kwa Yahweh leo na kujitoa kwake?”

6Kisha sadaka za hiari zilitolewa na viongozi wa mababu wa familia zao, viongozi wa makabila ya Israeli, wakuu wa maelfu na mamia, na waamuzi walio juu ya kazi ya mfalme.7Walitoa kwa ajili ya huduma ya nyumba ya Mungu talanta elfu tano na darkoni elfu kumi za dhahabu, talanta elfu kumi za fedha, talanta elfu kumi na nane za shaba, na talanta za chuma 100,000.8Hao walio na mawe ya thamani waliyatoa katika Hazina ya nyumba Yahweh, chini ya usimamizi wa Yehieli, mzao wa Gerishoni.9Watu walifurahi kwa ajili ya hizi sadaka za hiari, kwa sababu walitoa kwa moyo wao wote kwa Yahweh. Mfalme Daudi pia alifurahi sana.

10Daudi alimbariki Yahweh mbele ya kusanyiko lote. Alisema, “Na uabudiwe, Yahweh, Mungu wa Israeli babu wetu, milele na milele.
11Kwako, Yahweh, kuna ukuu, nguvu, utukufu, ushindi, na enzi. Kwa kuwa yote yalio mbinguni na duniani ni yako. Kwako ni ufalme, Yahweh, na umetukuzwa kama mtawala juu ya vyote.
12Utajiri na heshima hutoka kwako, na unatawala juu ya watu wote. Mkononi mwako kuna nguvu na uwezo. Unao uweza na nguvu ya kuwafanya watu kuwa mkuu na kumpa uweza yeyote.
13Kisha sasa, Mungu wetu, tunakushukuru na kusifu jina lako tukufu.

14Lakini mimi ni nani, na watu wangu ni nani, hata tuwe na uwezo wa kutoa vitu hivi kwa hiari hivi? Hakika kila kitu kimetoka kwako, na tumerundisha kilicho chako
15Kwa maana sisi tu wageni na wapanganji mbele yako, kama babu zetu wote walivyokuwa. Siku zetu katika dunia ni kama kivuli, na hakuna tumaini la kubaki duniani.
16Yahweh Mungu wetu, utajiri huu wote tulio kusanya ili kujenga hekalu kwa kuheshimu jina lako - watoka kwako na ni wako.
17Nijua pia, Mungu wangu, ya kuwa wewe wauchunguza moyo na kuufurahia unyofu. Kwangu mimi, kwa unyofu wa moyo wangu nimetoa kwa hiari vitu hivi vyote, na sasa natazama kwa furaha watu wako waliopo hapa wakitoa zawadi kwa hiari kwako.
18Yahweh, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Israeli - mababu zetu - hifadhi hili katika fikra za watu wako. Elekeza mioyo yao kwako.
19Mjalie Sulemani mwanangu moyo mkamilifu ili azishike amri zako, na amri zako za maagano, na sheria zako, na atekeleze mipango hii yote ya kuijenga jumba hili ya kifalme niliyoiandaa.”

20Daudi akasema kwa kusanyiko lote, “Sasa mbariki Yahweh Mungu wenu.” Kusanyiko lote likambariki Yahweh, Munug wa mababu zao, wakainamisha vichwa vyao na kumuabudu Yahweh na kusujudu mbele za mfalme.

21Kwa siku iliyo fuata, wakatoa dhabiu kwa Yahweh na kumtolea sadaka ya kuteketeza. Walitoa sadaka ya fahali elfu moja, kondoo dume elfu moja, na wana-kondoo elfu moja, pamoja na sadaka zao za vinywaji na dhabihu tele kwa Israeli yote.22Siku ile, walikula na kunywa mbele za Yahweh kwa furaha kubwa. Walimfanya Sulemani, mwana wa Daudi, mfalme mara ya pili, na kum mafuta kwa mamlaka ya Yahweh kuwa mtawala. Pia walimpaka mafuta Zadoki kuwa kuhani.23Kisha Sulemani akaketi kwenye kiti cha enzi cha Yahweh kama mfalme mahali pa Daudi baba yake. Alifanikiwa, na Israeli yote ikamtii.24Viongozi wote, wanajeshi, na wana wa Mfalme Daudi wakatoa utii kwa Mfalme Sulemani.

25Yahweh alimheshimu sana Sulemani na akampa ukuu wa kifalme kuliko mfalme yeyote aliyetangulia kabla yake Israeli.

26Daudi mwana wa Yese alitawala juu ya Israeli yote.27Daudi alikuwa mfalme wa Israeli kwa miaka arobaini. Alitawala kwa miaka saba Hebroni na miaka thelathini na tatu Yerusalemu.28Alikufa katika uzee mwema, baada ya kufurahia maisha marefu, mali na heshima. Sulemani mwanawe alitawala baada yake.

29Mafanikio ya mfalme Daudi yameandikwa katika historia ya Samweli nabii, katika historia ya Nathani nabii, na katika historia ya Gadi nabii.30Yaliyo andikwa hapo ni matendo ya utawala wake, nguvu zake na matukio yaliyompata yeye, israelI, na falme zote za nchi nyingine.

2 Mambo ya nyakati

1

1Sulemani mwana wa Daudi, aliimarishwa katika utawala wake, na Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye na alimpa nguvu nyingi sana.

2Sulemani akasema kwa Israleli wote, na maakida wa maelfu na wa mamia, na kwa waamuzi, na kwa kila mfalme kiongozi katika Israeli yote, wakuu wa kaya.3Hivyo Sulemani na kusanyiko lote wakaenda pamoja naye sehemu ya juu iliyokuwa Gibeoni, maana ndipo palikuwepo hema ya kukutania ya Mungu, ambayo Musa mtumishi wa Yahwe, alikuwa ameitengeneza jangwani.4Lakini Daudi alikuwa ameleta pale sanduku la Mungu kutoka Kiriath yeriam hadi sehemu ambayo alikuwa ametayarisha, maana alikuwa ameliandalia hema huko Yerusalemu.5Zaidi ya hayo, madhabahu ya shaba iliyotengenezwa na Bezaleli mwana wa uri mwana wa Huri ilikuwepo huko kabla ya mbele ya madhabahu ya Yahwe; Sulemani na kusanyiko wakaenda ilikokuwa.6Sulemani akaenda huko kwenye madhabahu ya shaba mbele za Yahwe, ambayo ilikuwepo mahali pa hema ya kukutania, na akatoa sadaka elfu za kuteketezwa juu yake.

7Mungu akamtokea Sulemani usiku huo na akasema kwake, “Omba! Nikupe nini?”

8Sulemani akasema kwa Mungu, “Umeonyesha agano la uaminifu mkuu kwa Daudi baba yangu, na umenifanya mfalme katika nafasi yaye.9Sasa, Yahwe Mungu, ahadi yako kwa Daudi baba yangu itimie, maana umenifanya mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya dunia.10Sasa nipe hekima na maarifa, ili niweze kuwaongoza watu hawa, maana ni nani anayeweza kuwaamua watu wako, ambao ni wengi sana kwa idadi?”

11Mungu akasema kwa Sulemani, “Kwa kuwa hili lilikuwa kwenye moyo wako, na kwa kuwa hujaomba mali, utajiri, au heshima, wala maisha ya wale wanaokuchukia, wala maisha marefu kwa jili yako binafsi, lakini umeomba hekima na maarifa kwa ajili yako, ili uwatawale watu wangu, ambao juu yao nimekufanya mfalme, na hivi ndivyo nitafanya.12Sasa nitakupa hekima na maarifa, pia nitakupa mali na utajiri, na heshima, kuliko wafalme wote waliokuwepo kabla yako walivyokuwa, na baada yako hakuna yeyote atakayekuwa navyo.”13Kwa hiyo Sulemani akaenda Yerusalemu kutoka sehemu ya juu iliyokuwepo Gibeoni, kutoka mbele ya hema ya kukutania; akatawala juu ya Israeli.

14Sulemani akakusanya magari na wanaume waendesha farasi, naye alikuwa na magari 1,400 na waendesha farasi kumi na mbili elfu ambao aliwaweka katika miji ya magari, pamoja naye, mfalme katika Yerusalemu.15Mfalme akatengeneza fedha na dhahabu kuwa vitu vya kawaida kama mawe katika Yerusalemu, na mbao za mierezi kuwa kama miti ya mikuyu iliyomo katika nyanda za chini.16Sulemani katika uagizaji wa farasi kutoka Misiri, wafanya biashara wake walinunua farasi kutoka Misiri kwa bei stahiki.17Waliagiza gari kutoka Misiri kwa shekeli mia sita za fedha, na farasi mmoja kwa shekeli 150. Pia walinunua kutoka kwa wafalme wa Wahiti na wafalme wa Washamu.

2

1Sasa Sulemani akaamuru kulijenga nyumba kwa jina la Yahwe na nyumba kwa ajili ya ikulu ya ufalme wake.2Sulemeni akateua wanaume elfu sabini wabebe mizigo, na wanaume elfu themanini wa kukata mbao katika mlima, na wanaume 3,600 kwa ajili ya kusimamia.

3Sulemani akatuma ujumbe kwa Hiramu, mfalme wa Tiro, ukisema, “Kama ulivyofanya na Daudi baba yangu, ulivyomtumia magogo ya mierezi ili ajenge nyumba ya kuishi, fanya hivyo hivyo na mimi.4Tazama, niko karibu kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe Mungu wangu, kuiweka wakifu kwake, kwa ajili ya kumtolea sadaka za kuteketezwa zenye viungo vitamu mbele zake, kwa ajili ya mkate wa uwepo, na kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa asubuhi na jioni, katika siku za Sabato na za mwezi mpya, na katika sikukuu zilizoteuliwa kwa ajili ya Yahwe Mungu wetu. Hii itakuwa milele, kwa Israeli.5Nyumba nitakayoijenga itakuwa kubwa sana, maana Mungu wetu ni mkuu kuliko miungu mingine yote.6Lakini ni nani anayeweza kumjengea Mungu nyumba, kama dunia yote na hata mbingu yenyewe haviwezi kumtosha? Mimi ni nani hata nimjengee nyumba, isipokuwa kufukiza sadaka mbele zake?7Kwa hiyo nitumie mtu mwenye ujuzi wa kazi katika kazi ya dhahabu, fedha, shaba, na chuma, na ya dhambarau, na nyekundu, na sufu ya samawati, mtu anayejua kutengeza aina zote za mapambo ya mbao. Atakuwa na watu wenye ustadi waliopamoja nami katika Yuda na Yerusalemu, ambao Daudi baba yangu aliwaweka.8Nitumieni pia mierezi, miberoshi, na miti ya msandali kutoka Lebanoni, maana najua ya kuwa watumishi wako wanajua jinsi ya kukata mbao katika Lebanoni. Angalia, watumishi wangu watakuwa na watumishi wako,9ili kwamba watayarishe mbao nyingi kwa ajili yangu, maana nyumba ninayotaka kuijenga itakuwa kubwa na ya ajabu.10Angalia, nitawapa watumishi wako, watu watakaozikata mbao, kori ishirini elfu za ngano ya aridhini, kori ishirini elfu za shayiri, bathi ishirini elfu za mvinyo, na bathi ishirini elfu za mafuta.” 1

11Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akajibu kwa maandishi, ambayo alimtumia Sulemani: “Kwa kuwa Yahwe anawapenda watu wake, amekufanya kuwa mfalme juu yao.”12Zaidi ya hayo, Hiramu akasema, “Abarikiwe Yahwe, Mungu wa Israeli, aliyeziumba mbingu na dunia, amempa Daudi mwana mwenye hekima, mwenye karama ya busara na uelewa, ambaye atajenga nyumba kwa aajili ya Yahwe, na nyumba kwa ajili ya ufalme wake.13Sasa nimemtuma mtu mwenye ujuzi, mwenye karama ya uelewa, Hiramu, mtaalamu wangu.14Ni mwana wa mwanamke wa binti za Dani. Baba yake alikuwa mtu kutoka Tiro. Ana ujuzi katika kazi za dhahabu, fedha, shaba, chuma, mawe, na katika mbao, na katika dhambarau, samawati, na sufu yenkundu, na kitani safi. Pia ana ujuzi katika kutengeneza michoro ya aina yoyote na katika kubuni kitu chochote. Apatiwe nafasi miongoni mwa watumishi wako wenye ujuzi, na pamoja na wale wa bwana wangu, Daudi, baba yako.15Sasa, ngano na shayiri, mafuta na mvinyo, ambayo bwana wangu alisema, na apeleke sasa vitu hivi kwa watumishi wake.16Tutakata mbao kutoka Lebanoni, mbao nyingi kadri unavyohitaji. Tutazileta kwako kama mitumbwi kupitia bahari kwenda Yafa, na utazibeba hadi Yerusalemu.”

17Sulemani akawahesabu watu wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli, kwa kutumia njia ya Daudi, baba yake, aliyoitumia kuwahesabu. Waliwakuta kuwa 153,600.18Miongoni mwao aliwateua sabini elfu ili wabebe mizigo, themanini elfu kuwa wakataji wa mbao katika milima, na 3,600 kuwa wasimamizi wa kuwasimamia watu wafanye kazi.


1Maandishi ya kale yanasema: “kori ishirini elfu za ngano kama chakula.”

3

1Kisha Sulemani akaanza kuijenga nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu juu ya Mlima Moria, ambako Yahwe alimtokea Daudi baba yake. Aliandaa sehemu ambayo Daudi aliikusudia, katika sakafu ya kupuria ya Arauna Myebusi.2Alianza kujenga siku ya pili ya mwezi wa pili, katika mwaka wa nne wa utawala wake.

3Sasa hivi ndinyo vipimo vya ule msingi ambao Sulemani alijenga kwa ajili ya nyumba ya Mungu. Akitumia mtindo wa vipimo vya zamani, urefu ulikuwa mikono sitini, na upana ulikuwa mikono ishirini.4Urefu wa ukumbi mbele ya nyumba ulikuwa mikono ishirini, ukilingana na upana wa nyumba, urefu wake kwenda juu pia ulikuwa mikono ishirini, na Sulemani akaifunika sehemu ya ndani kwa dhahabu halisi.

5Akalitengeneza paa la ukumbi mkuu kwa miti ya miberoshi, ambayo aliifunika kwa dhahabu halisi, na ambayo aliifunika kwa miti ya mitende na minyororo.6Akaipamba nyumba kwa vito vya thamani; dhahabu ilikuwa dhahabu kutoka Parvaimu.

7Pia akazifunika boriti zake, vizingiti, kuta, na milango kwa dhahabu; akachonga makerubi juu ya kuta zake.8Akaijenga sehemu ya patakatifu pa patakatifu. Urefu wake ulilingana na upana wa nyumba, mikono ishirini, na upana wake pia ulikuwa mikono ishirini. Aliifunika kwa dhahabu halisi, thamani yake ilikuwa talanta mia sita.9Uzito wa misumari ulikuwa shekeli hamsini za dhahabu. Alizifunika sehemu za juu kwa dhahabu.

10Akachonga makerubi wawili kwa ajili ya sehemu zapatakatifu pa patakatifu, wahunzi wakayafunika kwa dhahabu. 111Mabawa ya makerubi yalikuwa na urefu wa mikono ishirini yote kwa pamoja; bawa la kerubi mmoja lilikuwa na urefu wa mikono mitano, lilifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa jingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano pia.12Bawa la kerubi mwingine lilikuwa mikono mitano, likifikia kwenye ukuta wa chumba; bawa lake jingine lilikuwa mikono mitano pia, likigusana na bawa la kerubi wa kwanza.

13Mabawa ya makerubi hawa yalienea jumla ya mikono ishirini. Makerubi yalisimama kwa miguu yake, na nyuso zao zikiuelekea ukumbi mkuu.

14Akatengeneza pazia la samawati, dhambarau, na sufu nyekundu, na kitani safi, na akachora makerubi juu yake.15SulemaniPia akatengeneza nguzo mbili, kila moja ikiwa na urefu wa mikono thelathini na tano kwenda juu, kwa maana mbele ya nyumba; taji ambazo zilikuwa juu ya nguzo zilikuwa na urefu wa mikono mitano kwenda juu.16Akatengeneza minyororo kwa ajili ya nguzo na akaiweka juu yake, pia akatengeneza makomamanga mia moja na akayaunganisha kwenye minyororo.17Akazisimamisha nguzo mbele ya hekalu, mkono wa kulia, na nyingine mkono wa kushoto; akaiita nguzo ya kulia Yakini, na nguzo ya kushoto akaiita Boazi.


1Maandishi ya kale yanasema: makerubi wawili waliochongwa kwenye mbao.

4

1Vilevile akatengeneza madhabahu ya shaba; urefu wake ulikuwa mikono ishirini, na upana wake ulikuwa mikono ishirini.2Pia akatengeneza bahari ya mduara ya chuma cha kuyeyushwa, mikono kumi kutoka ukingo hadi ukingo. Urefu wake kwenda juu ulikuwa mikono mitano, na bahari ilikuwa na mzunguko wa mikono thelatinini.3Chini ya kingo kuzunguka bahari kulikuwapo ng'ombe dume, kumi kila mkono,

4Bahari ilisimama juu ya ng'ombe wa kulima kumi na wawili, watatu wakiangalia kaskazini, watatu wakiangalia magharibi, na watatu wakiangalia kusini, na watatu wakiangalia mashariki. Bahari iliwekwa juu yao, na robo ya sehemu zao za nyuma zote zilikuwa ndani.5Bahari ilikuwa nene kama upana wa mkono, na ukingo wake ulikuwa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi. Bahari ilikuwa na mabafu elfu tatu ya maji.

6Pia akatengeneza birika kumi kwa ajili ya kuoshea vitu; tano akaziweka mkono wa kulia, na tano akaziweka kushoto; vifaa vilivyotumika katika kufanyia sadaka za kuteketezwa zilipaswa kuoshwa ndani ya hizo birika. Bahari, vilevile ilikuwa kwa ajili ya makuhan kuoga humo.

7Akatengeza vinara vya taa kumi vya dhahabu ambavyo vilitengenezwa kutokana na maelekezo ya jinsi vilivyopaswa kuwa; akaviweka hekaluni, vitanao mkno wa kulia, na vitano mkono wa kushoto.

8Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Akatengeneza birika mia moja za dhahabu.

9Zaidi ya hayo akatengeneza mahakama ya makuhani na mahakama kuu, na milangu kwa ajili ya mahakama, akaifunika milango yake kwa shaba.10Akaiweka bahari upande wa kulia wa nyumba, masharika, ikielekea upande wa kusini.

11Huramu akayatengeza masufuria, majembe, na mabakuli ya kunyunyizia. Hivyo Huramu akamaliza kazi aliyofanya kwa ajili ya mfalme Sulemani katika nyumba ya Mungu:12zile nguzo mbili, taji mfano wa upinde zilizo kuwa juu ya zile nguzo mbili, na nyavu mbili za mapambo zilizofunika zile taji mbili mfano wa upinde zilizokuwa juu ya zile nguzo.
13Alikuwa ametengeneza makomamanga mia nne kwa ajili ya zile nyavu za mapambo: safu mbili za makomamanga kwa kila wavu ili kufunika vimbe mbili zilizo kuwa juu ya nguzo.
14Pia akavitengeneza vitako na mabirika juu ya kitako,
15bahari moja na wale ng'ombe kumi na wawili chini yake,
16pia masufuria, majembe, nyuma za nyama, na vyombo vingine vyote. Huramu mtaalamu akavifanya kwa ajili ya Mfalme Sulemani, kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vya shaba iliyong'arishwa.
17Mfalme alikuwa amevisubu katika uwanda wa Yordani, katika udongo wa mfinyanzi kati kati ya Sukothi na Sereda.18Hivyo ndivyo Sulemani alivyovitengeneza vyombo vyote kwa wingi; kwa kweli, uzito wa shaba haukuweza kujulikana.

19Sulemani akazitengeza samani zote ambazo zilikuwa kwenye nyumba ya Mungu, pia madhabahu ya dhahabu, na meza ambazo juu yake mkate wa uwepo ulipaswa kuwekwa;
20vinara pamoja na taa zake, ambazo zilitengezwa ili kumulika mbele ya chumba cha ndani—hivi vilitengenezwa kwa dhahabu halisi;
21na maua, taa, na makoleo, ya dhahabu, dhahabu safi.
22Pia mikasi ya taa, na mabakuli, vijiko, na vikaango vya sadaka za kuteketezwa vyote vilitengenezwa kwa dhahabu safi. Kuhusu mlango wa kuingilia kwenye nyumba, milango yake ya ndani kwenye patakatifu pa patakatifu na milango ya nyumba, ambayo ni, ya hekalu, ilitengenezwa kwa dhahabu.

5

1Wakati ilipomalizika kazi aliyofanya Sulemani kwa ajili ya Yahwe, Sulemani akapeleka vitu ndani, ambavyo Daudi, baba yake, aliviweka wakfu kwa kusudi hilo, pamoja na zile fedha, dhahabu, na vyombo vyote akavileta ndani ya hazina ya nyumba ya Mungu.

2Kisha Sulemani akawakusanya wazee wa Israeli, wakuu wa makabila yote, na viongozi wa familia za watu wa Israeli, katika Yerusalemu, ili walilete sanduku la agano la Yahwe kutoka mji wa Daudi, ambao ni Sayuni.3Wanaume wote wa Israeli wakakusanyika mbele za mfalme katika sikukuu, ambayo ilikuwa katika mwezi wa saba.

4Wazee wote wa Israeli wakaja, na Walawiwakalichukua sanduku.5Wakalileta sanduku, hema ya kukutania, na vyombo vitakatifu vyote ambavyo vilikuwa ndani ya hema. Makuhani waliokuwa wa kabila la Lawi wakavileta vitu hivyo.6Mfalme Sulemani na kusanyiko lote la Israeli wakaja pamoja, mbele ya sanduku, wakitoa sadaka za kondoo na ng'ombe ambao hawakuweza kuhesabika.

7Makuhani wakalileta sanduku la angano laYahwe ndani mahali pake, katika chumba cha ndani cha nyumba, kwenye patakatifu pa patakatifu, chini ya mabawa ya makerubi.8Kwa kuwa makerubi walitandaza mabawa yao juu ya mahali pa sanduku, na walilifunika sanduku na miti yake ya kulibebea.9Miti ilikuwa mirefu sana kwamba ncha zake zilionekana kutoka ile sehemu takatifu mbele ya chumba cha ndani, lakini hazikuweza kuonekana kutoka nje. Zipo hapo hadi leo.10Hapakuwa na kitu katika sanduku isipokuwa zile meza mbili ambazo Musa aliziweka humo huko Horebu, wakati Mungu alipofanya agano na watu wa Israeli, walipotoka nje ya Misri.

11Ilikuwa makuhani walipotoka nje ya sehemu takatifu. Makuhani wote waliokuwepo wakajiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe, bila kujiamuru wenyewe kulingana na sehemu zao.12Pia makuhani waliokuwa waimbaji, wote kwa ujumla wao, pamoja na Asafu, Hemani, Yeduthuni, na wana wao na ndugu zao, wakiwa wamevalia kitani safi na wakipiga matoazi, vinanda, na vinubi, wakasimama upande wa Mashariki wa mwisho wa madhabahu. Pamoja nao palikuwa na makuhani 120 wakipuliza tarumbeta.13Ikawa kwamba wapuruza tarumbeta na waimbaji wakafanya mziki pamoja, wakifanya sauti moja isikike kwa ajili ya kumsifu na kumshukuru Yahwe. Walipaza sauti zao kwa tarumbeta, toazi na vyombo vingine, na wakamsifu Yahwe. Wakaimba, “Kwa maana Yeye ni mwema, kwa kuwa uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Kisha nyumba, ile nyumba ya Yahwe, ikajawa na wingu.14Makuhani hawakuweza kusimama ili wahudumu kwa sababu ya lile wingu, kwa maana utukufu wa Yahwe uliijaza nyumba yake.

6

1Kisha Sulemani akasema, “Yahwe alisema kwamba ataishi katika giza nene,2lakini nimekujengea makao makuu, sehemu kwa ajili yako ya kuishi milele.”

3Kisha mfalme akageuka nyuma na kuwabariki kusanyiko lote la Israeli, wakati kusanyiko lote la Israeli walikuwa wamesimama4Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, usifiwe, uliyesema na Daudi baba yangu, na ametimiza kwa mikono yake mwenyewe, akisema.5‘Tangu siku nilipowaleta watu wanagu nje ya nchi ya Misiri, sikuchagua mji wowote nje ya makabila yote ya Israeli ambamo nyumba ingejengwa, ili jina langu liwe humo. Wala sikuchagua mtu yeyote kuwamfalme juu ya watu wangu Israeli.6Aidha, nimechagua Yeruselemu, ili kwamba jina langu liwe humo, na nimemchagua Daudi kuwa juu ya watu wanangu Israeli.’7Sasa ilikuwa ndani ya moyo wa Daudi baba yangu, kujenga nyumba kwa ajili ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.8Lakini Yahwe alisema kwa Daudi Baba yangu. ‘Kwamba ilikuwa ndani ya moyo wako kujenga nyumba kwa ajili ya jina langu, ulifanya vizuri kwa hili kuliweka moyoni mwako.9Aidha, hutaijenga ile nyumba, badala yake, mwanao, mmoja atakayetoka kwenye viuno vyako, ataijenga nyumba kwa ajili ya jina langu.’10Yahwe ameyatimiza maneno aliyokuwa amesema, kwa maana nimeiinua sehemu ya Daudi baba yangu, na nitakaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, kama alivyoahidi Yahwe. Nimeijenga nyumba kwa ajii ya jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.11Nimeliweka humo sanduku, ambamo kuna agano la Yahwe, alilofanya na watu wa Israeli.”

12Sulemani akasimama mbele ya madhabahu ya Yahwe mbele za kusanyiko lote la Israeli, na akanyosha mikono yake.13Kwa maana alikuwa ametengeneza jukwaa la shaba, lenye urefu wa mikono mitano, upana wa mikono mitano, urefu wake kwenda juu mikono mitatu. Alikuwa ameliweka katikati ya uwanja. Akasimama juu yake na kupiga magoti mbele ya kusanyiko la Israeli, kisha akanyosha mikono yake kuzielekea mbingu.14Akasema, “Yahwe, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe katika mbingu, au juu ya dunia, ambaye anatunza agano na upendo imara na watumishi wako ambao hutembea mbele zako kwa moyo wao wote;15wewe uliyemtimizia Daudi baba yangu, uliyokuwa umemwahidi. Ndiyo, ulisema kwa kinywa chako na umetimiza kwa mkono wako, kama ilivyo leo.16Sasa, Yahwe, Mungu wa Israeli, tunza ahadi uliyoahidi kwa mtumishi wako Daudi baba yangu, uliposema, ‘Hautashindwa kupata mtu mbele yangu wa kukaa juu ya kiti cha enzi cha Israeli, ikiwa tu uzao wako ni waangalifu kutembea katika sheria zangu, kama wewe ulivyotembea mbele zangu.17Sasa, Mungu wa Israeli, ninaomba kwamba ahadi uliyofanya kwa mtumishi wako Daudi itakuwa kweli.18Lakini kweli Mungu ataishi na wanadamu juu ya dunia? Angalia, dunia yote na mbingu yenyewe haviwezi kukubeba -sembuse na hekalu hili nililojenga!19Nakusihi yaheshimu maombi haya ya mtumishi wako na ombi lake. Yahwe Mungu wangu; sikia kilio na maombi ambayo mtumishi wako anaomba mbele zako.20Fumbua macho yako kuelekea hekalu hili usiku na mchana, sehemu ambayo uliahidi kuliweka jina lako. Nakuomba usikie maombi atakayoomba mtumishi wako kuelekea sehemu hii.21Hivyo sikia maombi ya mtumishi na watu wako Israeli tunapoomba kuelekea sehemu hii. Ndiyo, sikia kutoka mahali unapoishi, kutoka mbinguni; na unaposikia, samehe.22Kama mtu atamtenda dhambi jirani yake na ikampasa kuapa kiapo, na ikiwa atakuja na kuapa kiapo mbele ya madhabahu yako katika nyumba hii,23basi sikia kutoka mbinguni kutenda. Ukawahukumu watumishi wako, ukamlipizie mwovu, ili kuyaleta matendo yake juu ya kichwa chake. Ukamtangaze mwenye haki kuwa hana hatia, ili kumlipa thawabu kwa ajili ya uaminifu wake.24Watu wako watakaposhindwa na adui kwa sababu wamekutenda dhambi, kama watageuka nyuma kwako, wakilikiri jina lako, wakisali na kuomba msamaha mbele zako hekaluni—25basi tafadhali sikia kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watu wako Israeli; uwarudishe katika nchi uliyoitoa kwa ajili yao na baba zao.26Wakati mbingu zimefungwa na hakuna mvua kwa sababu watu wamekutenda dhambi—ikiwa wataomba kuelekea sehemu hii, wakilikiri jina lako, na kuziacha dhambi zao utakapokuwa umewaadhibu—27basi sikia kutoka mbinguni na usamehe dhambi za watumishi wako na watu wako Israeli, utakapowaelekeza kwenye njia njema iwapasayo kutembea. Tuma mvua juu ya nchi yako, ambayo umewapa watu wako kama urithi.28Kama kuna njaa katika nchi, au kama kuna ugonjwa, tauni au ukungu, nzige au viwavijeshi, au kama adui wake wameyavamia malango ya mji katika nchi yao, au kwamba kuna pigo lolote au ugonjwa—29na ikiwa sala na maombi yamefanywa na mtu au watu wako wote Israeli—kila mmoja akilijua pigo na huzuni katika moyo wake akinyosha mikono yake kuelekea hekalu hili.30Basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi; samehe, na umlipe kila mtu kwa njia zake zote; unaujua moyo wake, kwa sababu wewe pekee unaijua mioyo ya wanadamu.31Fanya hivyo ili kwamba wakuogope wewe, ili waweze kutembea katika njia zako siku zote ambazo wataishi katika nchi uliyowapa baba zetu.32Kwa mgeni ambaye siyo sehemu ya watu wako Israeli, lakini ambaye- kwa sababu ya ukuu wa jina lako, mkono wako wenye nguvu, na mkono wako ulionyoshwa- akija na kuomba kuelekea sehemu nyumba hii,33basi sikiliza mbinguni, sehemu ambayo unaishi, na fanya yote ambayo mgeni atakuomba, ili kwamba watu wote wa dunia walijue jina lako na kukuogopa wewe, kama wafanyavyo watu wako Israeli, na kwamba waweze kujua kwamba nyumba hii niliyoijenga inaitwa kwa jina lako.34Ikiwa kwamba watu wako wakaenda nje kupigana dhidi ya adui zao, kwa njia yoyote ambayo unaweza kuwatuma, na ikiwa kwamba wakaomba kwako kuelekea mji huu ambao umeuchagua, na kuelekea nyumba ambayo nimeijenga kwa ajili ya jina lako.35Basi sikiliza maombi yao mbinguni, ombi lao, na uwasaidie.36Kama wametenda dhambi dhidi yako—kwa kuwa hakuna asiye tenda dhambi—na ikiwa una hasira nao na kuwakabidhi kwa adui zao, ili kwamba adui wakawabeba na kuwachukua kama mateka katika nchi zao, iwe mbali au karibu.37Kisha wakatambua kuwa wako katika nchi ambako wamewekwa utumwani, na ikiwa watatubu na kutafuta msaada kwako katika utumwa wao. Ikiwa watasema, ‘Tumetenda kinyume na kutenda dhambi. Tumetenda kwa uovu,’38ikiwa watarudi kwako kwa mioyo yao yote na kwa nia yao yote katika nchi ya utumwa wao, ambako walichukuliwa kama mateka, naikiwa wataomba kukabili nchi yao, uliyowapa baba zao, na kukabili mji ambao uliuchagua na kukabili nyumba ambayo niliijenga kwa ajili ya jina lako.39Basi sika kutoka mbinguni, mahali unapoishi, sikia kuomba kwao na maombi na wayaombayo, na uwasaidie shida zao. Wasamehe watu wako, ambao wamekutenda dhambi.40Sasa, Mungu wangu, ninakusihi, uyafungue macho yako, na masikio yako yasikie maombi yatakayofanywa katika sehemu hii.
41Sasa basi, amka, Yahwe Mungu, kwenye mahali pako pa kupumzikia, Wewe na sanduku la nguvu zako. Makuhani wako, Yahwe Mungu, wavikwe wokovu, na watakatifu wako wafurahi katika wema.
42Yahwe Mungu, usiugeuze nyuma uso wa masihi wako. Yakumbuke matendo yako katika agano lako la ufalme kwa ajili ya Daudi, mtumishi wako.

7

1Sasa Sulemani alipokuwa amemaliza kuomba, moto ukaja kutoka mbinguni na kuiteketeza sadaka ya kuteketezwa na dhabihu, na utukufu wa Yahwe ukaijaza nyumba.2Makuhani hawakuweza kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, kwa sababu utukufu wake uliijaza nyumba yake.3Watu wote wa Israeli wakaangalia juu moto uliposhuka chini na utukufu wa Yahwe ulikuwa juu ya nyumba. Wakalala kwa nyuso zao juu ya sakafu ya mawe, wakaabudu, na kutoa shukrani kwa Yahwe. Wakasema, “Kwa maana yeye ni mwema, kwa maana agano lake la kifalme ladumu milele.”4Kwa hiyo mfalme na watu wote wakamtolea Yahwe sadaka Yahwe.5Mfalme Sulemani akatoa sadaka ya ng'ombe ishirini na mbili elfu na kondoo 120,000 na mbuzi. Kwa hiyo mfalme na watu wote wakaiweka wakfu nyumba ya Mungu.6Makuhani wakasimama, kila mmoja akasimama mahali pake pa kuhudumu; Walawi pia pamoja na vyombo vya muziki vya Yahwe, ambavyo mfalme Daudi alivitengeza kwa ajili ya kumpa shukrani Yahwe katika nyimbo, “Kwa maana uaminifu wa agano lake wadumu milele.” Makuhani wote wakapiga matarumbeta mbele yao, na Israeli wote wakasimama.

7Sulemani akaitakasa sehemu ya katikati ya kiwanja cha mfalme mbele ya nyumba ya Yahwe. Humo akatoa sadaka za kuteketezwa na mafuta ya sadaka za amani, kwa sababu madhabahu ya shaba ambayo alikuwa ametengeza haikuweza kuzibeba sadaka, sadaka za nafaka, na za mafuta.

8Kwa hiyo Sulemani akaitisha sikukuu wakati huo kwa siku saba, na Israeli wote pamoja naye, kusanyiko kubwa, kutoka Lebo Hamathi mpaka kijito cha Misiri.9Siku ya nane wakaitisha kusanyiko la makini, kwa maana kwa siku saba walishika kuwekwa wakfu kwa ile madhabahu.10Katika siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa saba, Sulemani akawatanya watu kwenda kwenye nyumba zao kwa furaha na mioyo ya shangwe kwa sababu ya wema aliokuwaameuonyesha Yahwe kwa Daudi, Sulemani, Israeli, na watu wake.

11Hivyo Sulemani akaimaliza nyumba ya Yahwe na nyumba yake mwenyewe. Kila kitu kilichokuja katika moyo wa Sulemani kwa ajili ya kukitengeneza katika nyumba ya Yahwe na katika nyumba yake mwenyewe, alikitimiza kwa mafanikio.12Yahwe akamtokea Sulemani usiku na kusema kwake, “Nimesikia maombi yako, na nimeichagua sehemu hii kwa ajili yangu mwenyewe kama nyumba ya dhabihu.13Kama nitazifunga mbingu ili kwamba kusiwepo mvua, au kama nitaamuru nzige waimeze nchi, au kama nitatuma magonjwa kati kati ya watu wangu,14kisha watu wangu, ambao wameitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, kuomba, kuutafuta uso wangu, na kuziacha njia zao mbaya, nitasikia kutoka mbinguni, kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.15Sasa macho yangu yatakuwa wazi na masikio yangu yatasikiliza maombi yanayofanywa katika sehemu hii.16Kwa maana sasa nimeichagua na kuitakasa nyumba hii ilikwamba jina langu lipate kuwa humo milele. Masikio yangu na moyo wangu vitakuwako kila siku.17Kwako wewe, kama utatembea mbele zangu kama baba yako Daudi alivyotembea, ukitii yote niliyokuamuru na kuzishika sheria zangu na maagizo yangu,18basi nitakithibitisha kiti cha enzi cha ufalme wako, kama nilivyosema katika agano na Daudi baba yako, niliposema, ‘Mzaliwa wako hatashindwa kamwe kuwa mtawala katika Israeli.’19Lakini ukigeuka, na kuzisahau sheria zangu na amri ambazo nimeweka mbele yenu, na kama utaenda kuabudu miungu wengine na kuwasujudia,20basi nitawang'oa kutoka kwenye nchi yangu ambayo nimewapa. Nyumba hii ambayo nimeitakasa kwa ajili ya jina langu, nitaitupilia mbali kutoka mbele zangu, na nitaifanya kuwa methali na utani miongoni mwa watu wote.21Ingawa hekalu hili zuri sana kwa sasa, kila mtu apitaye karibu yake atashangazwa na ataguna. Watauliza, ‘Kwa nini Yahwe ameifanyia hivi nchi hii na nyumba hii.’22Wengine watajibu, ‘Kwa sababu walimsahau Yahwe, Mungu wao, ambaye alikuwa amewatoa babu zao nje ya nchi ya Misiri, na wakashikamana na miungu wengine na kuwainamia chini na kuwaabudu. Hii ndiyo maana Yahwe ameleta majanga haya yote juu yao.”

8

1Ikawa karibu ya mwisho wa miaka ishirini, kipindi ambacho Sulemani alikuwa ameijenga nyumba ya Yahwe na ya kwake mwenye,2kwamba Sulemani akaiajenga miji ambayo Hiramu alikuwa amempa, na ndani yake akawaweka watu wa Israeli.3Sulemani akauvamia Hamathzoba, akaushinda.4Akaijenga Tadmori katika nyika, na miji yote ya hazina, ambayo aliijenga katika Hamathi.5Pia akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, mijiiliyozungushiwa kwa ukuta, malango, na makomeo.6Akaujenga Baalathi na miji yote ya hazina aliyoimiliki, na miji yote kwa ajili ya magari yake na miji kwa ajili ya wapanda farasi wake, na chochote alichotamani kujenga kwa ajili ya starehe zake katika Yerusalemu, katika Lebanoni, na katika nchi zote zilizokuwa chini ya utawala wake.

7Kuhusu watu wengine wote ambao walikuwa wamesalia wa Wahiti, Waamori, Waperizi, Wahivi, Wayebusi, ambao hawakuwa wa Israeli,8watoto wao ambao waliachwa baada yao katika nchi, ambao watu wa Israeli hawakuwaangamiza—Sulemani akawafanyisha kazi kwa nguvu, ndivyo walivyo hata leo.9Vile vile, Sulemani hakuwafanyisha kazi kwa nguvu watu wa Israeli. Badala yake, wakawa wanajeshi wake, maakida wake, wakuu wake, na maakida wa magari ya majeshi yake na wapanda farasi wake.10Pia hawa walikuwa wakuu wa wakuu wakisimamia wasimamizi waliokuwa wa mfalme Sulemani, walikuwa 250, waliowasimamia watu walioifanya kazi.

11Sulemani akamleta binti Farao nje ya mji wa Daudi kwenye nyumba aaliyokuwa amemjengea, kwa maana alisema, “Mke wangu lazima asiishi katika nyumba ya Daudi mfalme wa Israeli, kwa sababu kila linapokuja sanduku la Yahwe ni pakatifu.”

12Kisha Sulemani akatoa sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe juu ya madhabahu yake ambayo alikuwa ametengeza mbele ya ukumbi.13Akatoa sadaka kama ilivyohitaka ratiba ya kila siku; akazitoa, kwa kufuata maelekezo yaliyokuwa katika amri ya Musa, katika siku za Sabato, miezi mipya, na katika siku zilizopangwa mara tatu kila mwaka: Sikukuu ya mikate isiyochachwa, sikukuu ya majuma, na sikuku ya vibanda.14Katika kuyatunza maagizo ya baba yake Daudi, Sulemani akayapanga makundi ya makuhani kwenye kazi yao, na Walawi kwenye nafasi zao, ili kumsifu Mungu na kuhudumu mbele za makuhani, kama ilivyotakiwa katika ratiba ya kila siku. Pia akawateua walinda lango kwa zamu zao kwa kila lango, kwa maana Daudi, mtu wa Mungu, alikuwa ameagiza hivyo pia.15Watu hawa hawakupotea kutoka kwenye amri ya mfalme kwa makuhani na Walawi kuhusu jambo lolote, au kuhusu vyumba vya hazina.

16Kazi yote aliyoagizwa na Sulemani ikakamilika, kutoka siku msingi wa nyumba ya Yahwe ulipowekwa hadi ilipokamilika. Nyumba ya Yahwe ikamalizika.

17Kisha Sulemani akaenda Esion geberi, na Elothi, juu ya pwani katika nchi ya Edomu.18Hiramu akatuma meli zake kupitia watumishi wake ambao walikuwa wana maji wenye uzoefu. Wakasafiri nawatumishi wa Sulemani hadi Ofiri. Wakachukua kutoka huko talanta 450 za dhahabu ambazo walimletea Sulemani.

9

1Malkia wa Sheba aliposikia kuhusu umaarufu wa Sulemani, akaja Yerusalemu kumjaribu kwa maswali magumu. Akaja pamoja na msafara mkubwa sana, pamoja na ngamia waliosheheni manukato, dhahabu nyingi, na vito vingi vya thamani. Alipofika kwa2Sulemani, akamwambia yaliyokuwa moyoni mwake. Sulemani akamjibu maswali yake yote; hakuna kitu kilichokuwa kigumu sana kwa Sulemani; hakuna swali ambalo hakulijibu.

3Malkia wa Sheba alipoiona hekima ya Sulemani na ikulu aliyokuwa amejenga,4chakula mezani kwake, mahali pa kukaa watumishi wake, kazi ya watumishi wake na mavazi yao, pia wabebakikombe na mavazi yao, na namna alivyotoa sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe, hapakuwa na roho zaidi ndani yake.

5Akasema kwa mfalme, “Ni kweli, taarifa nilioisikia katika nchi yangu kuhusu maneno yako na hekima yako.6Sikuamini nilichokisikia mpaka nilipokuja hapa, na sasa macho yangu yamekiona. Sikuambiwa nusu kuhusu hekima yako na utajiri wako! Umeuzidi umaarufu niliokuwa nimesikia kuhusu wewe.7Wamebarikiwa watu wako, na watumishi wako ambao husimama mbele yako, kwa sababu wanaisikia hekima yako. 18Amebarikiwa Yahwe Mungu wako, ambaye amepata raha ndani yako, aliyekuweka juu ya kiti chake cha enzi, ili uwe mfalme kwa ajili ya Yahwe Mungu wako. Kwa sababu Mungu wako anaipenda Israeli, ili kuwathibisha milele, amekufanya kuwa mfalme juu yao, ili ufanye hukumu na haki.

9Akampa mfalme talanta 120 za dhahabu na kiasi kikubwa manukato na vitu vya thamani. Sulemani hakupewa tena kiasi kikubwa cha manukato kama hiki ambacho alipewa na malkia wa Sheba.

10Watumishi wa Hiramu na mfalme Sulemani, ambaye alileta dhahabu kutoka Ofiri, miti ya msandali, na vito vya thamani.11Kwa miti hiyo ya msandali, mfalme Sulemani akatengeneza madari ya nyumba ya Yahwe na nyumba yake, na vinubi na vinanda kwa ajili ya wanamziki. Hapajaonekana tena mbao kama hiyo katika nchi ya Yuda.12Mfalme Sulemani akampa malkia wa Sheba kila kitu alichotaka, chochote alichoomba, zaidi ya vile alivyoleta kwa mfalme Sulemani. Kwa hiyo akaondoka na kurudi kwenye nchi yake, yeye na watumishi wake.

13Sasa uzito wa dhahabu ambayo ililetwa kwa Sulemani ndani ya mwaka mmoja ulikuwa talanta 666 za dhahabu,14nje na dhahabu ambayo waliileta wachukuzi na wafanya biashara. Wafalme wote wa Arabuni na maliwali katika nchi pia wakamletea Sulemani dhahabu na fedha.

15Mfalme Sulemani akatengeneza ngao kubwa mia mbili za dhahabu iliyofuliwa. Shekeli mia sita za dhahabu zikatumika kwa kila ngao.16Pia akatengeneza ngao mia tatu za dhahabu iliyopigwa. Mia tatu za dhahabu zikaenda kwa kila ngao; mfalme akaziweka kwenye ikulu ya Msitu wa Lebanoni.

17Kisha mfalme atengeneza kiti cha enzi kikubwa cha pembe na kufunika kwa dhahabu safi.18Kulikuwa na ngazi sita kwenda kwenye kiti cha enzi, na sehemu ya juu ya kiticha enzi ilikuwa duara. Kulikuwa na mikono kila upande wa kiti, na simba wawili wamesimama pembeni na hiyo mikono.19Simba kumi na wawili walisimama juu ya zile ngazi, mmoja kila upande wa ngazi sita.20Hapakuwa na kiti cha enzi kama hicho katika ufalme wowote mwingine. Vikombe vyote vya kunywea vya Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vikombe vyote vya mfalme katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu halisi. Hakuna hata kimoja kilichokuwa cha fedha kwa sababu fedha haikuchuliwa kuwa ya thamani katika siku za Sulemani.21Mfalme alikuwa na meli zilizosafiri baharini, pamoja na meli za Hiramu. Mara moja kwa mwaka meli zilileta dhahabu, fedha, na pembe, na manukato, na pia nyani na tausi.

22Kwa hiyo Mfalme Sulemani aliwazidi utajiri na hekima wafalme wote wa dunia.23Dunia yote waliutafuta uwepo wa Sulemani ili kusikia hekima yake, ambayo Mungu alikuwa ameiweka katika moyo wake.24Waliomtembelea walileta kodi, vyombo vya shaba na dhahabu, nguo, silaha, na manukato, na farasi na nyumbu, mwaka baada ya mwaka.

25Sulemani alikuwa na mazizi elfu nne kwa ajili ya farasi na magari, na wapanda farasi kumi na mbili elfu, ambao waliwaweka katika miji ya magari na pamoja naye katika Yerusalemu.26Akatawala juu ya wafalme wote kutoka mto Efrati hadi nchi ya Wafilisti, na hadi mpaka wa Misiri.27Mfalme alikuwa na fedha katika Yerusalemu, nyingi kama mawe juu ya ardhi. Akazifanya mbao za mierezi kuwa nyingi kama miti ya mikuyu ambayo iko nyanda za chini.28Wakaleta farasi kutoka Misri na kutoka nchi zote kwa ajili ya Sulemani.

29Kwa mambo mengine kuhusu Sulemani, mwanzo na mwisho, hayajaandikwa katika Historia ya Nathani Nabii, katika unabii wa Abiya Mshinoni, na katika Maono ya Ido mwonaji wa mambo ya Yeroboamu mwana wa Nabati?30Sulemani akatawala katika Yerusalemu juu ya Israeli yote kwa miaka arobaini.31Akalala na baba zake na watu wakamzika katika mji wa Daudi baba yake. Rehoboamu, mwanaye, akawa mfalme katika sehemu yake.


1Baadhi ya maandiko yanasema, “Wambarikiwa wake zako,” ikidhaniwa kwamba kifungu hicho kinapaswa kusomeka kama ilivyo katika Wafalme 10:8.

10

1Rehoboamu akaenda Shekemu, kwa maana Israeli wote walikuwa wanakuja Shekemu kwa ajili ya kumfanya yeye mfalme.2Ikatokea kwamba Yeroboamu mwana wa Nebati akasikia haya (kwa maana alikuwa katika Misiri, ambako alikuwa amekimbilia kutoka kwenye uwepo wa Mfalme Sulemani, lakini Yeroboamu akarudi kutoka Misiri).3Kwa hiyo wakatuma na kumuita yeye, na Yeroboamu na Israeli wote wakaja; wakamwambia Rehoboamu na kusema,4“Baba yako aliifanya nira yetu ngumu. Kwa hiyo sasa, ifanye kazi ngumu ya baba yako kuwa rahisi, na ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu, na sisi tutakutumikiawewe.”

5Rehoboamu akawaambia, “Njoni kwangu tena baada ya siku tatu.” Kwa hiyo watu wakaondoka.

6Mfalme Rehoboamu akaomba ushauri kwa wazee ambao walikuwa wamesimama mbele ya Sulemani baba yake wakati alipokuwa hai; akasema, Mnanishauri niwape jibu gani watu hawa?”

7Wakasema kwake, Ikiwa wewe ni mwema kwa watu hawa na uwapendeze, na usema maneno mazuri kwao, basi siku zote watakuwa watumishi wako.”

8Lakini Rehoboamu akapuuza ushauri wa wazee ambao walimpa, na akashauriana na wanaume vijana ambao walikuwa wa rika lake, ambao walisimama mbele yake.9Akawaambia, “Mnanipa ushauri gani, ili kwamba niwajibu watu waliozungumza kwangu na kusema, “Ifanye nyepesi nira yako ambayo baba yako aliiweka juu yetu’?”

10Wanaume vijana ambao walikuwa rika la Yeroboamu wakasema kwake, wakisema, “Hivi ndivyo utakavyosema kwa watu waliokuambia kwamba baba yako Sulemani aliifanya nira yao nzito, lakini kwamba lazima uifanye nyepesi. Hivi ndivyo utakavyosema kwao, ‘Kidole changu kidogo ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu.11Kwa hiyo sasa, ingawa baba yangu aliwatwika nira nzito, nitaiongeza nira yenu. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini nitawaadhibu kwa nge.”

12Kwa hiyo Yeroboamu na watu wote wakaja kwa Rehoboamu katika siku ya tatu, kama alivyosema mfalme, “Rudini kwangu katika siku ya tatu,”13Yeroboamu akasema kwao kwa ukatili, akiupuuza ushauri wa wazee.14Akasema kwao akiufuata ushauri wa wanaume vijana, akisema, “Baba yangu aliifanya nira yenu nzito, lakini mimi nitaiongeza. Baba yangu aliwaadhibu kwa mijeredi, lakini mimi nitawaadhibu kwa nge.”15Kwa hiyo mfalme hakuwasikiliza watu, kwa kuwa ilikuwa tukio lililoletwa na Mungu, kwamba Yahwe aweze kulitimiza neno lake ambalo Ahiya Mshiloni alikuwa amemwambia Yeroboamu mwana wa Nebati.

16Israeli wote, walipoona kwamba mfalme hakuwasikiliza, watu wakamjibu na kusema, “Tuna sehemu gani katika Daudi? Hatuna urithi katika wana wa Yese! Kila mmoja wenu anapaswa kwenda katika hema yake, Israeli. Sasa kila mtu aone nyumba yake, Daudi.” Kwa hiyo Israeli wote wakarudi kwenye hema zao.

17Lakini kwa watu wa Yuda walioishi katika miji ya Yuda, Yeroboamu akatawala juu yao.

18Kisha mfalme Rehoboamu akamtuma Adoramu, ambaye alikuwa msimamizi wa wafanya kazi, lakini watu wa Israeli walimuua kwa kumpiga mawe. Mfalme Rehoboamu akaingia haraka ndani ya gari lake kwenda Yerusalemu.19Kwa hiyo Israeli wakawa waasi dhidi ya nyumba ya Mungu hadi leo.

11

1Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akawakusanya nyumba ya Yuda na Benjamini, wanaume 180,000 waliochaguliwa ambao walikuwa wanajeshi, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Israeli, ili kuurudisha ufalme kwa Rehoboamu.

2Lakini neno la Yahwe likamjia Shemaya mtu wa Mungu, likisema,3“Sema kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na kwa Israeli katika Yuda na Benjamini,4Yahwe anasema hivi, “Msivamie wala kufanya vita dhidi ya ndugu zako. Kila mmoja lazima arudi kwenye nyumba yake, kwa maana nimesababisha jambo hili kutokea.” Kwa hiyo wakayatii maneno ya Yahwe na kuacha kumvamia Yeroboamu.

5Yeroboamu akaishi katika Yerusalemu na kujenga miji katika Yuda kwa ajili ya kujilinda.6Akaijenga Bethlehemu, Etamu Tekoa,7Bethsusi, Soko, Adulamu,8Gathi, Maresha, Zifu,9Adoraimu, Lakishi, Azeka,10Sora, Aiyaloni, na Hebroni. Hii ni miji yenye ngome katika Yuda na Benjamini.11Akaziimarisha ngome na kuweka maamri jeshi ndani yake, pamoja na hazina ya chakula, mafuta, na divai.12Akaweka ngao na mikuki katika miji yote na kuifanya imara sana. Kwa hiyo Yuda na Benjamini zikawa zake.

13Makuhani na Walawi waliokuwa katika Israeli yote wakaenda kwake kutoka ndani ya mipaka yao.14Kwa kuwa Walawi waliacha nchi za malisho yao na mali zao ili kuja Yuda na Yerusalemu, kwa maana15Yeroboamu na wanawe walikuwa wamewafukuza, ili kwamba wasifanye majukumu yao ya kikuhani kwa ajili ya sehemu za juu na mbuzi na sanamu za ndama alizokuwa ametengeneza.16Watu kutoka kabila zote za Israeli wakaja nyuma yao, wale waliokuwa wameielekeza mioyo yao kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli; wakaja Yerusalemu kwa ajili ya kumtolea dhabihu Yahwe. Mungu wa baba zao.17Kwa hiyo wakauimarisha ufalme wa Yuda na kumfanya imara Rehoboamu mwana wa Sulemani kwa miaka mitatu, na wakatembea kwa miaka mitatu katika njia ya Daudi na Sulemani.

18Rehoboamu akajitwalia mke: Mahalathi, binti wa Yerimothi, mwana wa Daudi na wa Abihaili, binti wa Eliabu, mwana wa Yese.19Akamzalia wana: Yeushi, Shemaraia, na Zahamu.20Baada ya Mahalathi, Rehoboamu akamchukua Maaka, binti wa Absalomu; akamzalia Abiya, Atai, Ziza, na Shelomithi.21Rehoboamu akampenda Maaka, binti Absalomu, zaidi kuliko wake zake wengine wote na masuria (alichukua wake kumi na nane na masuria sitini, na akawa baba wa wana ishirini na nane na mabinti sitini).

22Rehoboamu akamteua Abiya mwana wa Maaka kuwa mkuu, kiongozi miongoni mwa ndugu zake alikuwa na wazo la kumfanya mfalme.23Rehoboamu akatawala kwa hekima; akawatawanya wanaye katika nchi yote ya Yuda na Benjamini katika kila mji imara. Pia akawapa chakula kwa wingi na akatafuta wake wengi kwa ajili yao.

12

1Ikawa kwamba, Rehoboamu alipokuwa ameimarishwa na mwenye nguvu, kwamba akaikataa sheria ya Yahwe--na Waisraeli wote pamoja naye.2Ilitokea katika mwaka wa tano wa Mfalme Rehoboamu, kwamba, Shishaki, mfalme wa Israeli, akaja kinyume na Yerusalemu, kwa sababu watu walikuwa wameacha kuwa waaminifu kwa Yahwe.3Akaja na magari elfu moja na mia mbili pamoja naye na wapanda farasi elfu sitini. Askari wasio hesabika wakaja pamoja naye kutoka Misri: Walubi, Wasukii, na Waethiopia.4Akaiteka miji yenye ngome ya Yuda na akaja Yerusalemu.

5Sasa Shemaya nabii akaja kwa Rehoboamu na kwa viongozi wa Yuda ambao walikuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu kwa sababu ya Shishaki. Shemaya akasema kwao, “Hivi ndivyo anavyosema Yahwe: Mmenisahau, kwa hiyo pia nimewaweka katika mkono wa Shishaki.”

6Kisha wakuu wa Israeli na mfalme wakajinyenyekesha na kusema, “Yahwe ni mtakatifu.”

7Yahwe alipoona kuwa wamejinyenyekeza, neno la Yahwe likamjia Shemaya, likisema, “Wamejinyenyekesha. Sitawaadhibu; nitawaokoa kwa hatua fulani, na hasira yangu haitamiminwa juu ya Yerusalemu kwa mkono wa Shishaki.8Vile vile, watakuwa watumishi wake, ili kwamba wajue nini maana ya kunitumikia mimi na kuwatumikia watawala wa nchi zingine.”

9Kwa hiyo Shishaki, mfalme wa Misiri akaja Yerusalemu akazichukua hazina katika nyumba ya Yahwe, na hazina katika nyumba ya mfalme. Akachukua kila kitu; pia akazichukua ngao za dhahabu alizokuwa amezitengeneza Sulemani. Mfalme10Rehoboamu akatengeneza ngao za shaba katika nafasi zake na kuzikabidhi mikononi mwa maamri jeshi wa walinzi, ambao waliilinda milango ya kuelekea kwenye nyumba ya mfalme.11Ikawa kwamba mfalme kila alipoingia katika nyumba ya Yahwe, walinzi wakazibeba; kisha wakazirudisha katika nyumba ya ulinzi.

12Rehoboamu alipojinyenyekeza mwenyewe, ghadhabu ya Yahwe ikampisha mbali, kwa hiyo hakumwangamiza kabisa; pembeni, bado kulikuwa na baadhi ya wema wa kupatikana katika Yuda.

13Hivyo mfalme Rehoboamu akafanya ufalme wake imara katika Yerusalemu, na kwa hiyo akatawala. Rehoboamu alikuwa na umri wa miaka arobaini na moja alipoanza kutawala, na akatawala kwa muda wa miaka kumi na saba katika Yerusalemu, mji ambao Yahwe alikuwa ameuchagua kutoka kwa makabila ya Israeli ili kwamba aliweke jina lake humo. Jina la mamake aliitwa Naama, Mwamoni.14Akafanya yaliyokuwa maovu, kwa sababu hakuuelekeza moyo wake kumtafuta Yahwe.

15Kwa mambo mengine kuhusu Rehoboamu, mwanzo na mwisho, hayajaandikwa katika maandishi ya Shemaya nabii na ya Ido mwonaji, ambayo pia yana kumbukumbu ya vizazi na vita kati ya Rehoboamu na Yeroboamu?16Rehoboamu akalala pamoja na baba zake na alizikwa katika mji wa Daudi; Abiya mwanawe akawa mfalme katika nafasi yake.

13

1Katika mwaka wa kumi na nane wa Mfalme Yeroboamu, Abiya akaanza kutawala juu ya Yuda.2Akatawala kwa miaka mitatu katika Yerusalemu; jina la mama yake aliitwa Maaka, binti wa Urieli wa Gibea. Kulikuwa na vita kati ya Abiya na Yeroboamu.3Abiya akaingia vitani na jeshi la askari, wenye nguvu, hodari, 400,000 wanaume waliochaguliwa. Yeroboamu akapanga mistari ya vita dhidi yake yenye 800,000 wanaume askari waliochaguliwa, wenye nguvu, hodari.

4Abiya akasimama juu ya mlima Semaraimu, uliopo katika kilima cha nchi ya Efraimu, na akasema, “Nisikilizeni, Yeroboamu na Israeli wote!5Hamjui kwamba Yahwe, Mungu wa Israeli, alitoa sheria juu ya Israeli kwa Daudi milele, kwake na kwa wanawe kwa agano rasmi?6Bado Yeroboamu mwana wa Nebati, mtumishi wa Sulemani mwana wa Daudi, akainuka na kuasi dhidi ya bwana wake.7Watu wabaya, washirika wa karibu, wakamkusanyikia, wakamjia kinyume Rehoboamu mwana wa Sulemani, wakati Rehoboamu alipokuwa mdogo na asiye na uzoefu na hakuweza kuwamudu.

8Sasa mnasema kwamba mnaweza kuuzuia utawala wa Yahwe wenye nguvu katika mkono wa uzao wa Daudi. Ninyi ni jeshi kubwa, na pamoja nanyi kuna ndama wa dhahabu ambao Yeroboamu alitengeneza kama miungu kwa ajili yenu.9Hamkuwafukuza nje makuhani wa Yahwe, uzao wa Haruni, na Walawi? Hamkujifanyia makuhani katika namna ya watu wa nchi zingine? Yeyote ajaye kujitakasa mwenyewe na ngo'mbe dume kijana, na kondoo dume saba anaweza kuwa kuhani wa kile ambacho siyo miungu.

10Lakini kwetu, Yahwe ni Mungu wetu, na hatujamsahau. Tuna makuhani, uzao wa Haruni, wakimtumikia Yahwe, na Walawi, ambao wako katika kazi yao.11Kila asubuhi na jioni humtolea Yahwe sadaka za kuteketezwa na uvumba mtamu. Pia hupanga mkate wa uwepo juu ya meza takatifu; pia huweka kinara cha dhahabu pamoja na taa zake, ili watoe sadaka kila jioni. Sisi huzishika sheria za Yahwe, Mungu wetu, Lakini ninyi mmemsahau.12Ona, Mungu yuko pamoja nasi katika vichwa vyetu, na makuhani wake wako hapa na tarumbeta kwa ajili ya kutoa sauti dhidi yenu. Watu wa Israeli, msipigane na Yahwe, Mungu wa babu zenu, kwa maana hamtafanikiwa.”

13Lakini Yeroboamu akaandaa mavamizi nyuma yao; jeshi lake lilikuwa mbele ya Yuda, na wavamizi nyuma yao.14Yuda walipoangalia nyuma, tazama, mapigano yalikuwa pote mbele na nyuma yao. Wakamlilia Yahwe kwa sauti, na makuhani wakayapuliza matarumbeta.15Kisha wanaume wa Yuda wakapiga kelele; walipopiga kelele, ikawa kwamba Mungu akampiga Yeroboamu na Israeli wote mbele ya Abiya na Yuda.16Watu wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda, na akawatia kwenye mkono wa Yuda.17Abiya na jeshi lake wakawaua kwa mauaji makuu; 500,000 watu wanaume waliochaguliwa wa Israeliwakaanguka wamekufa.

18Katika namna hii hii, watu wa Israeli wakatiishwa chini wakati huo, watu wa Yuda wakashinda kwa sababu walimtegemea Yahwe, Mungu wa baba zao.

19Abiya akamshawishi Yeroboamu; akachukua miji kutoka kwake; Betheli pamoja na vijiji vyake, Yeshana pamoja na vijiji vyake, na Efroni pamoja na vijiji vyake.20Yeroboamu hakupata nguvu tena katika siku za Abiya; Yahwe akampiga, na akafa.

21Lakini Abiya akawa na nguvu sana; akachukua wanawake kumi na wanne kwa ajili yake na akawa baba wa wana ishirini na mbili na mabinti kumi na sita.

22Matendo ya Abiya yaliyosalia, tabia yake na maneno yake yameandikwa katika kamusi ya nabii Ido.

14

1Abiya akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Asa, mwanawe, akawa mfalme katika nafasi yake. Katika siku yake nchi ilikuwa tulivu miaka kumi.

2Asa alifanya yaliyomema na sahihi katika macho ya Yahwe Mungu wake,3kwa maana aliziondosha mbali madhabahu za kigeni na sehemu za juu. Akaziangusha chini nguzo za mawe na kuzikata nguzo za Maashera.4Akawaamuru Yuda kumtafuta Yahwe, Mungu wa baba zao, na kuzishika sheria na amri.5Pia akaziondosha mbali sehemu za juu na madhabahu za kufukiza kutoka miji yote ya Yuda. Ufalme ulikuwa na pumziko chini yake.6Akajenga miji ya ngome katika Yuda, kwa maana nchi ilikuwa tulivu, na hakukuwa na vita katika miaka hiyo, kwa sababu Yahwe alikuwa amempa amani.

7Kwa maana Asa aliwaambia Yuda, “Tuijenge miji hii na kuizungushia kuta, na minara, mageti, na makomeo; nchi bado yetu kwa sababu tumemtafuta Yahwe Mungu wetu. Tumemtafuta yeye, na ametupa amani katika kila upande.” Kwa hiyo walijenga na wakafanikiwa.

8Asa alikuwa na jeshi ambalo lilibeba ngao na mikuki; kutoka Yuda alikuwa na wanaume 300,000, na kutoka Benjamini, wanaume 280,000 waliobeba ngao na kuvuta pinde.

9Zera Mwethiopia akaja juu yao na jeshi la wanajeshi milioni moja na magari mia tatu; akaja Maresha.10Kisha Asa akatoka nje kukutana naye, na wakapanga mistari ya vita ya mapigano katika bonde la Sefatha huko Maresha.

11Asa akamlilia Yahwe, Mungu wake, na akasema, “Yahwe, hakuna aliye kama wewe lakini ni wewe wa kumsaidia mtu asiye na nguvu anapokutana na mengi. Tusaidie, Yahwe, Mungu wetu, kwa maana tunakutegemea wewe, na katika jina lako tumekuja kupambana na idadi hii kubwa ya adui. Yahwe, wewe ni Mungu wetu; usimuache mtu akushinde.”

12Kwa hiyo Yahwe akawapiga Waethiopia mbele za Asa na Yuda; Waethiopia wakakimbia.13Asa pamoja na wanajeshi waliokuwa pamoja naye wakawafukuza hadi Gerari. Kwa hiyo Waethiopia wengi wakajeruhiwakiasi kwamba hawakuweza kupona, kwa maana waliangamizwa kabisa mbele za Yahwe na jeshi lake. Jeshi likachukua mateka wengi sana.14Jeshi likaviangamiza vijiji vyote jirani karibu na Garari, kwa kuwa hofu ya Yahwe ilikuwa imekuja juu ya wakaaji. Jeshi likateka vijiji vyote, na vilikuwa na hazina nyingi sana ndani yake.15Jeshi pia likaipiga hema ya makazi ya wachungaji; wakabeba kondoo kwa wingi, ngamia vile vile, na kisha wakarudi Yerusalemu.

15

1Roho wa Mungu akaja juu ya Azaria mwana wa Odedi.2Akaenda nje kukutana na Asa na akamwambia, “Nisikilize, Asa, na Yuda wote na Benyamini: Yahwe yuko pamoja nanyi, pale mnapokuwa naye. Kama mtamtafuta, mtampata; lakini kama mtamsahau, atawasahau ninyi.3Sasa kwa muda mrefu, Israeli hawakuwa na Mungu wa kweli, bila kuhani wa kufundisha, na bila sheria.4Lakini katika dhiki yao wakamrudia Yahwe, Mungu wa Israeli, na wakamtafuta, wakampata.5Katika nyakati hizo hapakuwa na amani kwake aliyesafiri kwenda mbali, wala kwake aliyesafiri kuja hapa; badala yake shida kubwa zilikuwa juu ya wenyeji wote wa wanchi.6Waligawanyika vikundi vikundi, taifa dhidi ya taifa, na mji dhidi ya mji, kwa maana Mungu aliwapa shida za kila aina ya mateso.7Lakini muwe hodari, na msiuache mkono wenu kuwa dhaifu, kwa maana kazi yenu itapewa thawabu.”

8Asa aliposikia maneno haya, unabii wa odedi nabii, akajipa ujasiri na kuviondosha mbali vitu vya kuchukiza kutoka nchi yote ya Yuda na Benyamini, na kutoka miji yote aliyokuwa ameiteka kuanzia kilima cha nchi ya Efraimu, na akaijenga tena madhabahu ya Yahwe, ambayo ilikuwa mbele ya ukumbi wa nyumba ya Yahwe.9Akawakusanya Yuda wote na Benjamini, na wale waliokaa pamoja nao—watu wa kutoka Efraimu na Manase, na kutoka Simeoni. Kwa maana walikuja kwake katika hesabu kubwa kutoka Israeli, walipoona kwamba Yahwe Mungu wake alikuwa pamoja naye.

10Kwa hiyo wakakusanyika katika Yerusalemu katika mwezi wa tatu, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Asa.11Katika siku hiyo walimtolea Yahwe dhabihu baadhi ya nyara ambazo walikuwa wameleta; ng'ombe wa kulima mia saba na kondoo na mbuzi elfu saba.12Wakaingia katika agano kwa ajili ya kumtafuta Yahwe, Mungu wa babu zao, kwa moyo wao wote na roho yao yote.13Wakakubaliana kwamba yeyote atakayepuuza kumtafuta Yahwe, Mungu wa Israeli, atapaswa kuuawa, awe mdogo ama mkubwa, awe mwanaume ama mwanamke.14Wakaapa kwa Yahwe kwa sauti kubwa, kwa kelele, na kwa sauti za tarumbeta na baragumu.15Yuda wote wakakifurahia kile kiapo. Kwa maana walikuwa wameapa kwa moyo wao wote, na walimtafuta Mungu kwa nia yao yote, na walimuona. Yahwe akawapa amani pande zote.

16Pia Mfalme Asa akamwondoa Maaka, asiwe malkia, kwa sababu alikuwa amefanya sanamu ya kuchukiza ya Maashera. Asa akaivunja vunja sanamu ya kuchukiza, akaiweka kwenye mavumbi akaichoma moto huko kijitoni Kidroni.17Lakini sehemu za juu hazikuwa zimeondolewa nje ya Israeli. Vile vile, Moyo wa Asa ulijitoa kikamilifu siku zake zote.18Akaleta kwenye nyumba ya Mungu vitu vya baba yake na vitu vyake mwenyewe vilivyokuwa vya Yahwe: vitu vya fedha na dhahabu.

19Hapakuwa na vita zaidi hadi miaka thelathini na mitano ya utawala wa Asa.

16

1Katika mwaka wa thelathini na sita wa utawala wa Asa, Baasha, mfalme wa Israeli, akatenda kwa ukatili dhidi ya Yuda na akaujenga Rama, ili kwamba asimruhusu mtu yeyote kutoka wala kuingia katika nchi ya Asa, mfalme wa Yuda.

2Kisha Asa akaitoa fedha na dhahabu nje ya vyumba vya kuhifadhia katika nyumba ya Yahwe na nje ya nyumba ya mfalme, na akaituma kwa Ben Hadadi mfalme wa Aramu, ambaye aliishi Dameski. Akasema, pawe na agano kati yako na mimi, kama palivyokuwa na agano kati ya baba yangu na baba yako. Angalia, nimekutumia fedha na dhahabu.3Livunje agano lako na Baasha, mfalme wa Israeli, ili kwamba aniache.”

4Ben Hadadi akamsikiliza mfalme Asa na kutuma maakida wa majeshsi dhidi ya miji ya Israeli. Wakavamia Iyoni, Dani, Abelimaimu, na miji yoye ya kuhifadhia ya Naftali.5Ikawa kwamba Baasha aliposikia hili, akaacha kuujenga Rama, na akaistisha kazi yake.6Kisha Asa mfalme akawachukua Yuda wote pamoja naye. Wakayabeba mawe na mbao za Rama ambazo Baasha alikuwa anajengea ule mji. Kisha Mfalme Asa alitumia vifaa hivyo vya ujenzi kwa ajili ya kuijenga Gaba na Mispa.

7Wakati huo Hanani mwonaji akaenda kwa Asa, mfalme wa Yuda, na akamwambia, “Kwa sababu umemtegemea mfalme wa Aramu, na hukumtegemea Yahwe Mungu wako, jeshi la mfalme wa Aramu limetoroka nje ya mikono yako.8Waethiopia na Walubi hawakuwa jesi kubwa, wenye magari mengi na wapanda farasi wengi? Na bado, kwa sababau ulimtegemea Yahwe, alikupa ushindi juu yao.9Kwa maana macho ya Yahwe hukimbia kila mahali katika dunia yote, ili kwamba ajioneshe mwenyewe shujaa kwa niaba ya wale amabao mioyo yao ni mikamilifu kumwelekea yeye. Lakini umetenda kipumbavu katika jambo hili. Kwa maana tangu sasa na kuendelea, utakuwa na vita.” Kisha Asa akamkasirikia mwonaji, akamuweka gerezani, kwa maana alikuwa na hasira naye juu ya jambao10hili. Wakati huo huo, aliwagandamiza baadhi ya watu

11Tazma, matendo ya Asa, kutoka mwanzo hadi mwisho, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.12Katika mwaka wa thelathini na tisa wa utawala wake, Asa alipata ugonjwa kwenye miguu yake; ugonjwa wake ulikuwa mkali sana. Hata hivyo, hakutafuta msaada kutoka kwa Yahwe, lakini kutoka kwa waganga tu.13Asa akalala pamoja na babu zake; alikufa katika mwaka wa arobaiani na moja wa utawala wake. Wakamzika katika kaburi lake, ambalo alilichimba mwenyewe katika mji wa Daudi.14Walimlaza juu ya kitanda kilichokuwa kimewekewa manukato na aina mbali mbali ya dawa zilizotayarishwa na wale mafundi wa manukato. KIsha wakatengeneza moto kwa heshima yake.

17

1Yehoshafati mwana wa Asa akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoshafati akajiimarisha dhidi ya Israeli.2Akaweka majeshi katika miji yote Yuda yenye ngome, na akaweka magereza katika nchi ya Yuda na katika miji ya Efraimu, ambayo Asa baba yake alikuwa ameiteka.

3Yahwe alikuwa pamoja na Yehoshafati kwa sababu alitembea katika njia za kwanza za baba yake Daudi, na hakuwatafuta Mabaali. 14Badala yake, alimtegemea Mungu wa baba yake, na alitembea katika amri zake, siyo katika tabia ya Israeli.5Kwa hiyo Yahwe akaimarisha sheria katika mkono wake; Yuda wote wakaleta kodi kwa Yehoshafati. Alikuwa na utajiri na heshima kubwa.6Moyo wake ulikuwa umejikita katika njia za Yahwe. Pia aliziondoa sehemu za juu na Maashera mbali na Yuda.

7Katika mwaka wa tatu wa utawala wake aliwatuma wakuu wake Ben-haili, Obadia, Zekaria, Nethania, na Mikaya, ili wafundishe katika miji ya Yuda.8Pamoja nao walikuwepo Walawi: Shemaya, Nethanieli, Zebadia, Asaheli, Shemiramothi, Yehonathani, Adoniya, Tobia, na Tob-adonia, pamoja nao walikuwepo makuhani Elishama na Yehoramu.9Walifundisha katika Yuda, wakiwa na kitabau cha sheria ya Yahwe. Wakaenda karibu miji yote ya Yuda na kufundisha miongoni mwa watu.

10Hofu ya Yahwe ikashuka juu ya falme zote za nchi, zilizouzunguka Yuda, kwa hiyo hazikufanya vita dhidi ya Yehoshafati.11Baadhi ya Wafilisti wakamletea Yehoshafati zawadi, fedha kama kodi. Waarabu pia wakamletea makundi, 7,700 kondoo waume, na mbuzi 7,770.

12Yehoshafati akawa na nguvu sana.13Akajenga ngome na miji ya maghala katika Yuda. Alikuwa na kazi nyingi katika miji ya Yuda, na wanajeshsi—imara, wanaume hodari—katika Yerusalemu.14Hapa ni rodha yao, wamepangwa kwa majina ya nyumba za baba zo: Kutoka Yuda, maakida wa maelfu; Adna yule jemedari, na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 300,000;
15akifuatiwa na Yehonani jemedari, na pamoja naye wanaume 280, 00;
16akifuatiwa na Amasia mwana wa Zikri, ambaye kwa hiari alijitoa kumtumikia Yahwe; na pamoja naye wanaume wa kwenda vitani 200,000.
17Kutoka Benyamini: Eliada mtu jasiri, na pamoja naye watu 200,000 waliovaa upinde na ngao;
18akifutiwa na Yehozabadi, na pamoja naye askari 180,000 waliotayari kwa vita.
19Hawa walikuwa ni wale ambao walimtumikia mfalme, miongoni mwao ambao mfalme aliwaweka katika miji ya ngome katika Yuda yote.


1Baadhi ya mandiko ya kale hayana “Daudi,” na baadhi ya matoleo ya kisasa yameacha hili jina “Daudi.”

18

1Sasa Yehoshafati alikuwa na utajiri mwingi na heshima kubwa; alifanya undugu na Ahabu mmoja wa watu wa familia yake akamuoa binti yake.2Baada ya miaka kadhaa, akashuka chini kwa Ahabu huko Samaria. Ahabu akachinja kondoo na ngo'mbe wengi kwa ajili ya yake na watu waliokuwa pamoja naye. Ahabu pia akamshawishi kuivamia Ramothi-gileadi pamoja naye.3Ahabu, mfalme wa Israeli, akamwambia Yehoshafati, mfalme wa Yuda, “Utakwenda Ramothi-gileadi pamoja nami?” Yehoshafati akamjibu, “Mimi ni kama wewe, na watu wangu ni kama watu wako; tutakuwa pamoja nawe katika vita.”4Yehoshafati akamwambia mfalme wa Israeli, Tafadhali litafute neno la Yahwe kwanza kwa ajili ya jibu lako”

5Kisha mfalme wa Israeli akawakusanya manabii pamoja, wanauame mia nne, na akasema kwao, Tutaenda vitani Ramothi-gileadi, au nisiende?” Wakasema, “Vamia, kwa maana Mungu ataitia mkononi mwa mfalme.”

6Lakini Yehoshafati akasema, “Hakuna nabii mwingine hapa wa Yahwe ambaye kwake tunapaswa kutafuta ushauri?”

7Mfale wa Israeli akamwambia Yehoshafati, Bado kuna mtu mmoja amabaye kwake lazima tuutafute ushauri wa Yahwe, Mikaya mwana wa Imla, lakini namchukia kwa sababu yeye huwa hatabiri mema kamwe kunihusu, kila mara maovu,” Lakini Yehoshafati akasema, “Mfalme hapaswi kusema hivyo.”

8Kisha mfalme wa Israeli akamwita akida na kusema, Haraka mlete Mikaya mwana wa Imla.”

9Sasa Ahabu mfalme wa Israeli na Yehoshafati mfalme wa Yuda walikuwa wamekaa kila mmoja katika kiti cha enzi, wamevalia kanzu zao, katika sehemu ya uwazi katika maingilio ya lango la Samaria, na manabii wote walikuwa wakitabiri mbele zao.

10Zedekia mwana wa Kenaani akajitengenezea pembe za chuma na kusema, Yahwe anasema hivi: Kwa kutumia hizi pembe mtawasukuma Waaramu hadi waangamie.”11Manabii wote wakatabiri kitu kile kile, wakisema, “Vamia Raamothi-gleadi na shinda. Kwa maana Yahwe ameutia kwenye mkono wa mfalme.”

12Mjumbe aliyeenda kumuita Mikaya akasema kwake, akisema, “Sasa angalia, maneno ya manabii yanatangaza mambo mema kwa ajili ya mfalme kwa kinywa kimoja. Tafadhali maneno yako yawe kama maneno ya mmoja wao na sema mambo mema.”

13Mikaya akajibu, “Kama Yahwe aishivyo, mimi nitasema kile ambacho Mungu anasema.”

14Alipokuja kwamfalme, mfamle akamwambaia, “Mikaya, tutaenda Ramothi -gileadi kwa ajili ya vita, au la?” Mikaya akamjibu, “Vamia na utashinda! Kwa maana utakuwa na ushindi mkuu.”

15Kisha mfalme akasema kwake, “Ni mara ngapi ninapaswa kukuapisha ili usiniambie kitu chochote isipokuwa kweli katika jina la Yahwe?

16Kwa hiyo Mikaya akasema, “Niliwaoana Israeli wametawanyika katika mlima, kama kondoo wasio na mchungaji, na Yahwe akasema, hawa hawana mchungaji. Ebu kila mtu arudi nyumbani kwake kwa amani.”

17Kwa hiyo mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Sikukuambia kwamba asingeweza kutabiri mema juu yangu, bali majanga tu?

18Kisha Mikaya akasema, “Kwa hiyo ninyi nyote mnapashwa kulisikia neno la Yahwe: Nilimuona Yahwe amekaa juu ya kiti chake cha enzi, na majeshi yote ya mbinguni yalikuwa yamekaa mkono wake wa kulia na mkono wake wa kushoto.19Yahwe akasema, Ni nani atakayemrubuni Ahabu, mfalme wa Israeli, ili kwamba aende na kuanguka huko Ramothi-gileadi?’ Mmoja alisema hivi na mwingine hivi.

20Kisha roho ikaja moja kwa moja na kusimama mbele ya Yahwe na kusema, ‘Nitamrubuni.’ Yahwe akamwambia, ‘Kivipi?’

21Roho ikajibu, “nitatoka nje na nitakuwa roho ya uongo katika vinywa vya manabii wake wote.’ Yahwe akajibu, ‘utamrubuni, na pia utafanikiwa. Nenda sasa na fanya hivyo.’

22Sasa ona, Yahwe ameweka roho ya uongo katika midomo ya manabii wako hawa, na Yahwe ametangaza majanga kwa ajili yako.”

23Kisha Zedekia mwana wa Kenaana, akaja, akampiga kofi mika juu ya shavu, na kusema, “Kwa njia gani Roho wa Yahwe alitoka kwangu ili aseme nawe?”

24Mika akasema, Angalia, utalijua hilo katika siku hiyo, mtakapokimbia katika baadhi ya vyumba vya ndani kwa ajili ya kujificha.”

25Mfalme wa Israeli akasema kwa baadhi ya watumishi, “Enyi watu mkamateni Mikaya na mmpeleke hadi Amoni, mkuu wa mji na, na kwa Yoashi, mwanangu.26Nanyi mtamwambia, ‘Mfalme anasema: Muweke gerezani huyu mtu na umlishe kwa mkate kidogo tu na maji kidogo tu, mpaka nitakaporudi salama.”

27Kisha Mikaya akasema, “Kama utarudi salama, Yahwe hajasema nami.” Kisha akaongeza, “Sikiliza haya, enyi watu wote.”

28Kwa hiyo Ahabu, mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, mfalme wa Yuda, wakaenda juu ya Ramothi-giledi.29Mfalme wa Israeli akamwambia Yehoshafati, “Nitajibadilisha mwenyewe na kwenda vitani, lakini wewe vaa mavazi yako ya kifalme.” Kwa hiyo mfalame wa Israeli akajibadilisha, na wakaenda vitani.

30Sasa mfalme wa Aramu alikuwa amewaamuru maakida wa magari yake, akisema, Msiwavamie wanajeshi wasio wa muhimu wala wanajeshi muhimu. Badala yake, mvamieni mfalme wa Israeli pekee,”31Ikawa kwamba maakida wa magari walipomuona Yehoshafati wakasema, “Yule ni mfalme wa Israeli.” Wakageuka kumzunguka wamvamie, lakini Yehoshafati akalia, na Yahwe akamsaidia. Mungu akawageuza nyuma kutoka kwake.32Ikawa kwamba maakida wa magari walipoona ya kuwa hakuwa mfalme wa Israeli, wakarudi nyuma wasimfukuze.

33Lakini mtu mmoja akauvuta upinde wake kwa kubahatisha na kumpiga mfalme wa Israeli katikati ya maungio ya mavazi yake. Kisha Ahabu akamwambia dereva wa gari lake, “Geuza nyuma na nitoe nje ya mapigano, kwa maana nimejeruhiwa vibaya sana.”34Mapigano yakazidi kuwa makali siku hiyo, na mfalme wa israeli akashikiliwa katika gari lake kuwaelekea Waaramu hadi jioni. Muda jua lilipokaribia kwenda chini, akafa.

19

1Yehoshafati mfalme wa Yuda akarudi salama nyumbani kwake Yerusalemu.2Kisha Yehu mwana wa Hanani, mwonaji, akatoka kukutana naye na akasema kwa mfalme Yehoshafati, “Unapaswa kuwa unawasaidia waovu? Unapaswa kuwapenda wanaomchukia Yahwe? Kwa ajili ya tendo hili, ghadhabu toka kwa Yahwe iko juu yako.3Aidha, kuna baadhi ya mema ya kuonekana ndani yako, kwamba umeziondosha Maashera nje ya nchi, na umeukaza moyo wako kumtafuta Mungu.”

4Yehoshafati akaishi katika Yerusalemu; na akaenda nje tena miongoni mwa watu wa Beer- sheba hadi nchi ya kilima ya Efraimu na akawarudisha kwa Yahwe, Mungu wa baba zao.5Akaweka waamuzi katika nchi katika miji yote ya Yuda yenye ngome, mji kwa mji.6Akawaambia waamuzi, “Zingatieni mnachopaswa kufanya, kwa sababu hamuamui kwa ajili ya mwanadamu, bali kwa ajili ya Yahwe; yuko pamoja nanyi katika kazi ya kuamua,7Basi sasa iacheni hofu ya Mungu iwe juu yenu. Iweni waangalifu mnapoamua, kwa maana hakuna uovu wa Yahwe Mungu wetu, wala hakuna upendeleo wala hongo.”

8Vile vile, katika Yerusalemu Yehoshafati akateua baadhi ya Walawi na makuhani, na baahdhi ya viongozi wa nyumba za mababu wa Israeli, kwa ajili ya kufanya hukumu kwa ajili ya Yahwe, na kwa ajili ya migogoro. Wakaishi katika Yerusalemu.9Akawaelekeza, akisema, “Lazima mtumike kwa heshima kwa ajili ya Yahwe, kwa uaminifu, na kwa moyo wenu wote.10Kila mgogoro wowote utakapokuja kwenu kutoka kwa ndugu zenu wanaoishi katika miji yao, iwe inahusu mauji, iwe inahusu torati na amri, lazima muwaonye, ili kwamba wasiwe na hatia mbele za Yahwe, la sivyo ghadhabu itakuja juu yenu na juu ya ndugu zenu. Mnapaswa kufanya hivyo na hamtakuwa na hatia

11Ona, Amaria kuhani mkuu yuko juu yenu katika mambo yote ya Yahwe. Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa nyumba ya Yuda, ni kiongozi katika yote katika mambo yote ya mfalme. Pia, Walawi watakuwa wasimamizi wakiwatumikia ninyi. Muwe hodari na tiini maelekezo yenu, na Yahwe awe moja nao walio wema.”

20

1Ikawa baada ya hayo, kwamba watu wa Moabu na Amoni, na pamoja na baadhi ya Wameuni wakaja juu ya Yehoshafati ili kupigana vita. 1

2Kisha baadhi ya watu wakaja wakamwambia Yehoshafati, wakisema, “Umati mkubwa wanakuja juu yako ng'ambo ya Bahari iliyokufa, kutoka Edomu. Ona, wako Hason- tamari,” ambayo ndiyo En-gedi. 23Yehoshafati akaogopa na akajipanga kumtafuta Yahwe. Akatangaza haraka katika Yuda yote.4Yuda wakakusanyika pamoja kwa ajili ya kumtafuta Yahwe; wakaja kutoka miji yote ya Yuda kwa ajili ya kumtafauta Yahwe.

5Yehoshafati akasimama katika kusanyiko la Yuda na Yerusalemu, kwenye nyumba ya Yahwe, mbele ya kibaraza kipya.6Akasema, “Yahwe, Mungu wa baba zetu, hauko mbinguni? Wewe siyo mtawala juu ya falme zote za mataifa? Nguvu na uweza viko mkononi mwako, kwa hiyo hakuna anayeweza akukupinga wewe.7Mungu wetu, hukuwafukuza nje wakaaji wa nchi hii mbele ya watu wako Israeli, na kuitoa milele kwa ajili ya uzao wa Abrahamu?8Wakaishi ndani yake na kujenga sehemu takatifu kwa ajili ya jina lako, wakisema,9‘Ikiwa janga litakuja juu yetu —upanga, hukumu, au ugonjwa, au njaa—tutasimama mbele ya nyumba hii, na mbele zako (kwa maana jina lako limo ndani ya nyumba hii), na tutakulilia wewe katika mateso yetu, na utatusikia na kutuokoa.’ 310Tazama sasa, hapa kuna watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri ambao hukuwaacha Israeli wawapige walipotoka nchi ya Misri; badala yake, Israeli waliwageukia mbali na hawakuwaangamiza.11Ona jinsi wanavyotuzawadia; wanakuja kututoa nje ya nchi yako ambayo umetupa kuirithi.12Mungu wetu, hutawahukumu? Kwa maana hatuna nguvu dhidi ya hili jeshi kubwa ambalo linakuja juu yetu. Hatujui cha kufanya, lakini macho yetu yako kwako.

13Yuda wote wakasimama mbele ya Yahwe, pamoja na wadogo wao, wake, na watoto.

14Kisha kati kati ya kusanyiko, roho ya Yahwe ikaja juu ya Yahazieli, mwana wa Zekaria, mwana wa Benaya, mwana wa Yeieli, mwana wa Matania, mwana, Mlawi, mmoja wa wana wa Asafu.15Yahazieli akasema, “Sikilizeni, Yuda wote na ninyi wakaaji wa Yerusalemu, na Mfalme Yehoshafati. Hivi ndivyo Yahwe asemavyao kwenu, ‘Msiogope: msivunjike moyo kwa sababu ya hili jeshi kubwa, kwa maana vita siyo yenu, bali ni ya Mungu.16Lazima mwende chini juu yao kesho, Ona, wanakuja wakipanda kupita njia ya Sisi. Mtawakuta mwisho wa bonde, mbele ya jangwa la Yerueli.17Hamtahitaji kupigana katika vita hii. Simameni katika nafasi zenu, simameni wima, na muone wokovu wa Yahwe pamoja nanyi, Yuda na Yerusalemu. Msiogope wala kukata tamaa. Tokeni nje juu yao kesho, kwa maana yuko pamoja nanyi.”

18Yehoshafati akainamisha kichwa chake pamoja na uso wake chini. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakaanguka chini mbele za Yahwe, wakimwabudu yeye.19Walawi, wale wa uzao wa Wakohathi na wa uzao wa Wakorahi, wakasimama juu kumsifu Yahwe, Mungu wa Israeli, kwa sauti kubwa sana.

20Asubuhi mapema wakasimama na kwenda nje kwenye bonde la Tekoa. Walipokuwa wakienda nje, Yehoshafati akasimama na kusema, “Nisikilizeni, Yuda, na ninyi wakaaji wa Yerusalemu! Aminini katika Yahwe Mungu wenu, na mtasaidiwa. Aminini katika manabii zake, na mtafanikiwa.21Alipokuwa ameshauriana na watu, akawachagua wale ambao wangemwimbia Yahwe na kumpa sifa kwa ajili ya utukufu wake mtakatifu, walipokuwa wakienda wakilitangulia jeshi, na kusema, “Mshukuruni Yahwe, kwa maana uaminifu wa agano lake unadumu milele.”

22Walipoanza kuimba na kusifu, Yahwe akapanga wanaume katika mavamizi juu ya watu wa Amoni, Moabu, na wa Mlima Seiri, ambao walikuwa wanakuja dhidi ya Yuda. Walishindwa.23Kwa maana watu wa Aamoni na Moabu walisimama kupigana na wakaaji wa Mlima Seiri, ili kuwaua kabisa na kuwangamiza. Waliapokuwa wamemaliza kuwaangamiza wakaaji wa Mlima Seiri, wote wakasaidiana kuangamizana kila mmoja.

24Yuda walipokuwa katika sehemu hiyo wakiangalia jangwani, waliangalia nje juu ya jeshi. Tazama, walikuwa wamekufa, wameanguka chini; hakuna aliyekuwa amepona.

25Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara kutoka kwa hao watu, walikuta miongoni mwao bidhaa nyingi, nguo, na johari za thamani, ambazo walizichukua kwa ajili yao wenyewe, nyingi kuliko uwezo wao wa kubeba. Iliwachukua siku tatu kusomba nyara hizo, zilikuwa nyingi sana. 426Katika siku ya nne wakakusanyika katika bonde la Baraka, huko wakamsifu Yahwe, kwa hiyo jina la sehemu hiyo hata leo ni “Bonde la Baraka.”

27Kisha, wakarudi, kila mtu wa Yuda na Yerusalemu, na Yehoshafati katika uongozi wao, kwenda tena Yerusalemu kwa furaha, kwa maana Yahwe alikuwa amewafanya wafurahie juu ya adui zao.28Wakaja Yerusalemu na kwenye nyumba ya Yahwe kwa vinanda, vinubi matarumbeta.

29Hofu ya Yahwe ikawa juu ya falme zote za mataifa waliposikia kwamba Yahwe amepigana dhidi ya adui wa Israeli.30Kwa hiyo ufalme wa Yehoshafati ulikuwa mtiivu, kwa maana Mungu wake alimpa amani kuzunguuka pande zake zote.

31Yehoshafati akatawala juu ya Yuda: Alikuwa na umri wa miaka thelathini na mitano alipoanza kutawala. Jina la mama yake aliitwa Azubahi, binti wa Shilhi.32Akatembea katika njia za Asa, baba yake; hakugeuka popote kuziacha; akafanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe.33Vile vile, sehemu za juu hazikuwa zimeondoshwa mbali. Watu walikuwa bado hawajaelekeza mioyo yao kwa Mungu wa babu zao.

34Kwa mambo mengine kuhusu Yehoshafati, mwanzo na mwisho, tazama, yameandikwa katika historia ya kitabu cha wafalme wa Israeli.

35Baada ya hayo, Yehoshafati, mfalme wa Yuda, akapatana na Ahazia, mfalme wa Israeli, ambaye alitenda uovu mwingi.36Akapatana naye kujenga meli za kwenda Tarshishi; Wakazijenga meli hizo huko Esion-geberi.37Kisha Eliezeli, mwana wa Dadavahu wa Maresha, akatoa unabii juu ya Yehoshafati; akasema, “kwa sababu umepatana na Ahazia, Yahwe ameiharibu miradi yako.” Meli zilivunjika ili kwamba zisiweze kusafiri.


1Maandishi, “baadhi ya Wameuni,” yanatoa masahihisho kwa ajili ya maandishi ya Kiebrania, ambayo yanasomeka, “baadhi ya Waamoni.” Inadhaniwa kwamba “Wameuni” ndilo neno la asili, na wenye kunukuu walilibadili kuwa “baadhi ya Waamoni.” Lakaini jina hili la mwisho halileti maana, kwa sababu Waamoni tayari wamekwisha tajwa katika mstari huu. Vile vile, matoleo tofauti tofauti yanajihusha na tatizo hili katika namna mbali mbali.
2Badala ya “Edomu” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasomeka, “Aramu.”
3Badala ya “hukumu” baadhi ya maandiko ya zamani yanasema “mafuriko.”
4Badala ya “miongoni mwao,” baadhi ya maandishi ya zamani na ya kisasa yanasema, “ng'ombe.” badala ya “nguo” baadhi ya maandiko ya kale na ya kisasa yanasema, “miili iliyokufa.”

21

1Yehoshafati akalala pamoja na babu zake na kuzikwa pamoja nao katika mji wa Daudi;2Yehoramu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake. Yehoramu alikuwa na ndugu, wana wa Yehoshafati: Azaria, Yerieli, Zekaria, Azaria, Mikaeli, na Shefatia. Wote hawa walikuwa wana wa Yehoshafati, mfalme wa Israeli.3Baba yao alikuwa amewapa zawadi kubwa ya fedha, dhahabu, na vitu vingine vya thamani, na miji yenye ngome katika Yuda, lakini kiti cha enzi alimpa Yehoramu, kwa sababu alikuwa mzaliwa wake wa kwanza.

4Sasa Yehoramu alipokuwa ameinuka katika ufalme wa baba yake na kujiimarisha mwenyewe kama mfalme, akawaua ndugu zake wote kwa upanga, na pia viongozi wengine mbali mbali wa Israeli.5Yehoramu alikuwa na umri wa miaka thelathini na mbili alipoanza kutawala, na akatawala kwa miaka minane katika Yerusalemu.6Akatembea katika njia za wafalme wa Israeli, kama nyumba ya Ahabu ilivyokuwa ikifanya, kwa maana alikuwa na binti Ahabu kama mke wake, na akafanya yaliyo maovu katika macho ya Yahwe.7Vile vile, Yahwe hakutaka kuiangamiza nyumba ya Daudi, kwa sababu ya agano ambalo alikuwa amefanya na Daudi; alikuwa ameahidi kwamba siku zote angetoa uzima kwa ajili yake na kwa ajili ya vizazi vyake.

8Katika siku za Yehoramu, Edomu wakaasi wasiwe chini ya Yuda, na wakajisimamishia mfalme juu yao.9Kisha Yeroboamu akavuka ng'ambo pamoja na maakida na magari yake yote. Ilikuwa usiku aliposimama na kupigana dhidi ya Waedomu ambao walikuwa wamemzunguka na maakida wa magari yake.10Kwa hiyo Edomu iliasi kutoka kuwa chini ya Yuda mpaka leo. Libna piaaliasi wakati ule ule wasiwe chini yake. Kwa sababu Yehoramu alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa baba zake.

11Zaidi ya hayo, Yehoramu pia alikuwa amezijenga sehemu zake za juu katika milima ya Yuda na akawafanya wakaaji wa Yuda kuishi kama makahaba, na akawaongoza Yuda katika upotevu.

12Barua kutoka kwa nabii Eliya ikaja kwa Yerohamu. Ilisema, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi, babu yako, anasema: Kwa sababu hujatembea katika njia za Yehoshafafati, baba yako, wala katika njia za Asa, mfalme wa Yuda,13bali umetembea katika njia za wafalme wa Israeli, na umewafanya Yuda na wakaaji wa Yerusalemu kuenenda kama kahaba, kama nyumba ya Ahabu walivyofanya—na kwa sababu pia umewaua ndugu zako katika familia ya baba yako kwa upanga, watu waliokuwa bora kuliko wewe mwenyewe—14ona, Yahwe atawapiga watu wako na pigo kubwa, watoto wako, wake zako, na mali zako zote.15Wewe mwenyewe utakuwa na ugonjwa mwingi kwa sababu ya ugonjwa katika utumbo wako, mpaka utumbo wako uanguke nje kwa sababu ya ugonjwa, siku baada ya siku.

16Yahwe akaichochea roho ya Wafilisiti dhidi ya Yuda na ya Waarabu waliokuwa karibu na Waethiopia.17Wakaivamia Yuda, wakavamia katika nyumba ya mfalme. Pia wakawachukua wanaye na wake zake. Hakuna mwana aliyebakizwa kwa ajili yake ispokuwa, Yehoshafati, mwanaye mdogo.

18Baada ya haya yote, Yahwe akampiga katika utumbo wake kwa ugonjwa usiopona.19Ikawa wakati ulipofika, katika mwisho wa miaka miwili, kwamba utumbo wake ukaaanguka nje kwa sababu ya ugonjwa wake, na kwamba akafa kwa ugonjwa mkali. Watu wake hawakutengeneza moto kwa ajili ya heshima yake kama walivyokuwa wamefanyia baba zake.

20Alikuwa ameanza kutawala alipokuwa na umri wa miaka thelathini na mbili; akatawala katika Israeli kwa miaka minane, na alikufa bila kuombolezwa. Wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya kifalme.

22

1Wakaaji wa Yerusalemu wakamfanya Ahazia, mwana mdogo wa Yehoramu, mfalme katika nafasi yake, kwa maana kundi la watu ambalo lilikuja na Waarabu katika ngome lilikuwa limewauwa wanaye wakubwa wote. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akawa mfalme.

2Ahazia alikuwa na umri wa miaka arobaini na mbili alipoanza kutawala; alitawala kwa mwaka mmoja katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Athalia; alikuwa binti Omri.

3Pia Ahazia alitembea katika njia za nyumba ya Ahabu kwa maana mama yake alikuwa mshauri katika kufanya mambo maovu.4Ahazia alifanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama nyumba ya Ahabu walivyokuwa wakifanya, kwa maana walikuwawashauri wake baada ya kifo cha baba yake, hadi kuangamia kwake.5Pia aliufuata ushauri wao; akaenda pamoja na Yoramu mwana wa Ahabu, mfalme wa Israeli, kwa ajili ya kupigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu, huko Ramothi-gileadi. Waaramu wakamjeruhi Yoramu.

6Yoramu akarudi Yezreeli kwa ajili ya kuponywa majeraha ambayo walipata huko Rama, alipopigana dhidi ya Hazaeli, mfalme wa Aramu. Kwa hiyo Ahazia mwana wa Yehoramu, mfalme wa Yuda, akaenda chini Yezreeli ili kumuona Yoramu mwana wa Ahabu, kwa sababu Yoramu alikuwa amejeruhiwa.

7Sasa uharibifu wa Ahazia ulikuwa umeletwa na Mungu kupitia kutembelewa na Yoramu. Alipokuwa amewasili, alienda pamoja na Yeharamu ili kumvamia Yehu mwana wa Nimshi, ambaye Yahwe alikuwa amemchagua kwa ajili ya kuiangamiza nyumba ya Ahabu.8Ikawa kwamba, Yehu alikuwa akichukua hukumu ya Mungu juu ya nyumba ya Ahabu, kwamba aliwakuta viongozi wa Yuda na wana wa ndugu zake Ahazia wakimtumikia Ahazia. Yehu akawauwa.9Yehu akamtafuta Ahazia; Wakamkamata akiwa amejificha katika Samaria, wakamleta kwa Yehu, na wakamuua. Kisha wakamzika, kwa maana walisema, “Ni mwana wa Yehoshafati, ambaye alimtafuta Yahwe kwa moyo wake wote.” Kwa hiyo nyumba ya Ahazia haikuwa na nguvu zaidi kwa ajili ya kuutawala ule ufalme.

10Sasa Athalia, mama wa Ahazia, akaona kwamba mwanaye alikuwa amekufa, akainuka na kuwaua watoto wote wa kifalme katika nyumba ya Yehu.11Lakini Yehoshaba, binti wa mfalme, akamchukua Yoashi, mwana wa Ahazia, na akamvutia mbali kutoka miongoni mwa wana wa mfalme ambao waliuawa. Akamuweka yeye na mlezi wake katika chumba cha kulala. Kwa hiyo Yehoshaba, binti wa mfalme Yehoramu, mke wa Yehoiada kuhani (kwa maana alikuwa dada yake Ahazia), akamficha asimuone Athalia, kwa hiyo Athalia hakumuua.12Alikuwa pamoja nao, wakiwa wamejificha katika nyumba ya Mungu kwa miaka sita, Athalia alipotawala juu ya Yuda.

23

1Katika mwaka wa saba, Yehoyada alionesha nguvu zake na akaingia katika agano na maakida wa mamia, Azaria mwana wa Yerohamu, Ishmaeli mwana wa Yehohanani, Azaria mwana wa Obedi, Maaseya mwana wa Adaya, na Elishafati mwana wa Zikri.2Wakaenda katika Yuda na kuwakusanya Walawi kutoka miji yote ya Yuda, vile vile na wakuu wa nyumba za mababu wa Israeli, na wakaja hadi Yerusalemu.3Kusanyiko lote wakafanya aganao na mfalme katika nyumba ya Mungu. Yehoyada akawaambia, “Ona, mwana wa mfalme atatawala, kama Yahwe alivyosema kuhusu uzao wa Daudi.

4Hivi ndivyo mtakavyo fanya: theluthi yenu makuhani na Walawi ambao huja kuhudumu siku ya Sabato, mtakuwa walinzi katika milango.5Theluthi nyingine mtakuwa katika nyumba ya mfalme, na theluthi nyingine mtakuwa katika Msingi wa Lango. Watu wote watakuwa katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.6Msimruhusu yeyote kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, isipokuwa makuhani na Walawi wanaotumika. Wanao weza kuingia kwa sababu inawahusu.7Lakini watu wengine wote lazima mtii amri ya Yahwe. Walawi lazima wamzunguuke mfalme pande zote, kila mtu na silaha zake mkononi mwake. Yeyote atakayeingia katika nyumba, atauawa. Kaeni na mfalme aingiapo ndani na atokapo nje.”

8Kwa hiyo Walawi na Yuda wote walitumika kwa kila njia kama katika namna ambayo Yehoyada kuhani aliwaamuru. Kila mmoja alichukua watu wake, wale waliotakiwa kuja ndani kuhudumu katika Sabato, na wale watakaoondoka siku ya Sabato, kwa maana9Yehoyada, kuhani, hakuwa amezuilia mojawapo ya zamu zao. Kisha Yeliyadaya, kuhani, akaleta kwa maakida mikuki na ngao ndogo na kubwa zilizokuwa za mfalme Daudi ambazo zilikuwa katika nyumba ya Mungu.10Yehoyada akawaleta wanajeshi wote, kila mtu na mkuki wake katika mkono wake, upande wa kulia wa hekalu hadi upande wa kushoto wa hekalu, pembeni mwa madhabahu na hekalu, wakimzunguka mfalme.

11Kisha wakamleta nje mwana wa mfalme, wakaiweka taji juu yake, na kumpa agano la sheria. Kisha wakamfanya mfalme, na Yehoyda na wanaye wakampaka mafuta. Kisha wakasema, “Aishi maisha marefu mfalme.”

12Athalia aliposikia kelele za watu wakikimbia na kumsifu mfalme, akatoka ili awaone watu katika nyumba ya Yahwe.13Na akaangalia, na, tazama, mfamle alikuwa amesimama karibu na nguzo yake katika lango la, kuingilia na maakida na wapuliza tarumbeta walikuwa karibu na mfame. Watu wote wa nchi walikuwa wakifurahia na kupuliza tarumbeta na waimbaji walikuwa wakipiga vyombo vya muziki na kuongoza nyimbo za kusifu. Kisha Athalia akayararua mavazi yake na kupiga kelele. “Fitina! Fitina!”

14Kisha Yehoyada, kuhani, akawaleta nje maakida wa mamia waliokuwa juu ya jeshi na kusema, “Mleteni nje kati ya safu, yeyote atakayemfuata, auwawe kwa upanga.” Kwa maana kuhani alikwishasema, “Msimuue katika nyumba ya Yahwe.”15Kwa hiyo wakafanya njia kw ajili yake, na akaenda kwenye nyumba ya mfalme kupita njia ya Lango la Farasi, na huko wakamuuwa.16Kisha Yehoyada alifanya agano kati yake mwenyewe, watu wote, na mfalme, kwamba watakuwa watu wa Yahwe.17Kwa hiyo watu wote wakaenda kwenye nyumba ya Baali na kuiangusha chini. Wakazivunja vipande vipande madhabahu za Baali na sanamu zake, na wakamuua Matani, kuhani wa Baali, mbele ya madhabahu hizo.

18Yehoyada akateua wakuu kwa ajili ya nyumba ya Yahwe chini ya mkono wa makuhani, ambao walikuwa Walawi, ambao Daudi alikuwa amewapanga kwenye nyumba ya Yahwe, ili wamtolee Yahwe sadaka za kuteketezwa, kama ilivyoandikwa katika sheria ya Musa, pamoja na kushangilia na kuimba, kama alivyotoa maelekezo Daudi.19Yehoyada akaweka walinzi katikamalango ya nyumba ya Yahwe, ili kwamba kwa namna yoyote ile asiingie mtu asiyesafi.

20Yehoyada akachukua pamoja naye maakida wa mamia, watu wakubwa, watawala wa watu, na watu wote wa nchi. Akamleta chini mfalme kutoka kwenye nyumba ya Yahwe; watu wakaja kwenye nyumba ya mfalme kupitia Lango la juu na kumkalisha mfalme juu ya kiti cha enzi cha ufalme. 121Kwa hiyo watu wote wa nchi wakafurahia, na mji wote ulikuwa kimya. Kuhusu Asa walikuwa wamemuua kwa upanga.


1Baadhi ya maandiko ya kisasa yanasema, “wakamshusha chini mfalme.”

24

1Yoashi alikuwa na umri wa miaka saba alipoanza kutawala; akatawala kwa miaka arobaini katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba.2Yoashi alifanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe siku zote za Yehoyada, yule kuhani.3Yehoyada akajichukulia wake wawili kwa ajili yake, na akawa baba wa wana na mabinti.

4Ikawa baada ya haya, kwamba Yoashi aliamua kuitengeneza nyumba ya Yahwe.5Akawakusanya pamoja makuhani na Walawi, na kusema kwao, “Nendeni nje kila mwaka kwenye miji ya Yuda na kukusanya fedha kutoka Israeli yote kwa ajili ya kuikarabati nyumba ya Mungu wenu. Hakikisheni kwamba mnaanza haraka.” Walawi hawakufanya kitu kwanza.

6Kwa hiyo mfalme akamuita Yehoyada, yule kuhani, na kumwambia, “Kwa nini hukuwaagiza Walawi kuleta kutoka Yuda na Yerusalemu kodi iliyoagizwa na Musa mtumishi wa Yahwe na kusanyiko la Israeli, kwa ajili ya amri za hema ya agano?”

7Kwa maana wana wa Athalia, yule mwanamke muovu, walikuwa wameivunja nyumba ya Mungu na kuwapa Mabaali vitu vyote vitakatifu vya nyumba ya Yahwe.

8Kwa hiyo mfalme aliamuru, na wakatengeneza kasha na kulileta nje kwenye lango kwenye nyumba ya Yahwe.9Kisha wakafanya tangazo katika Yuda na Yerusalemu, kwa ajili ya watu kuleta kwa Yahwe kodi aliyoiagiza Musa mtumishi wa Mungu juu ya Israeli jangwani.10Viongozi wote na watu wote wakafurahia na wakaleta fedha na kuiweka kwenye kasha hadi walipomaliza kulijaza.11Ikatokea kwamba kila lilipoletwa kasha kwa mikono ya Walawi kwa wakuu wa mfalme, na kila walipoona kwamba kulikuwa na fedha nyingi sana ndani yake, waandishi wa mfalme na mkuu wa kuhani mkuu walikuja, kulihamishia fedha kasha, na kulirudisha sehemu yake. Walifanya hivyo siku baada siku, wakikusanya kiasi kikubwa cha fedha.12Mfalme na Yehoyada akawapa zile fedha wale waliofanya kazi ya kuhudumu katika nyumba ya Yahwe, Watu hawa waliwaajiri waashi na maseremala ili waijenge nyumba ya Yahwe, na pia wale waliofanya kazi katika chuma na shaba.

13Kwa hiyo wafanya kaziwakafanya kazi, na kazi ya kukarabati ikasonga mbele mikononi mwao; wakaisimamisha nyumba ya Mungu katika hali yake halisi na kuiimarisha.14Walipomaliza, wakaleta fedha zilizobaki kwa mfalme na Yehoyada. Fedha hizo zilitumika kutengenezea samani kwa ajili ya nyumba ya Yahwe, vyombo vya huduma na kutolea dhabihu—vijiko na vyombo vya dhahabu na fedha. Wakatoa sadaka za kuteketezwa bila kukoma katika nyumba ya Yahwe kwa siku zote za Yehoyada.

15Yehoyada akazeeka na alikuwa amejaa siku, na kisha akafa; alikuwa na umri wa mika 130 alipokufa.16Wakamzika katika mji wa Daudi miongoni mwa wafalme, kwa sababu alikuwa amefanya mema katika Israeli, kwa Mungu, na kwa ajili ya nyumba ya Mungu,

17Sasa baada ya kifo cha Yehoyada, kiongozi wa Yuda akaja na kutoa heshima kwa mfalme. Kisha mfalme akawasikiliza.18Wakaiacha nyumba ya Yahwe, Mungu wa baba zao, na kuwaabudu miungu na maashera na sanamu. Ghadhabu ya Mungu ikaja juu ya Yuda na Yerusalemu kwa sababau ya hili kosa lao.19Bado akatuma manabii kwao ili kuwaleta tena kwake, Yahwe, manabii wakatangaza juu ya watu, lakini walipuuza kusikiliza.

20Roho wa Mungu akaja juu ya Zekaria mwana wa Yehoyada, yule kuhani; Zekaria akasimama juu ya watu na kusema kwao, “Mungu anasema hivi: Kwa nini mnazivunja amri za Yahwe, ili kwamba msifanikiwe? Kwa kuwa mmemsahau Yahwe, pia amewasahau ninyi.”

21Lakini wakapanga njama dhidi yake; kwa amri ya mfalme, wakampiga kwa mawe katika uwanja wa nyumba ya Yahwe.22Katika namna hii hii, Yoashi, yule mfalme, akapuuza ukarimu ambao Yehoyada, baba yake Zekaria, alikuwa amemfanyia.

23Ikawa karibu mwisho wa mwaka, kwamba jeshi la Aramu wakaja juu yake Yoashi. Wakaja Yuda na Yerusalemu; wakawaua viongozi wote wa watu na kupeleka nyara zote kutoka kwao kwa mfalme wa Dameski.24Jeshi la Waaramu walikuwa wamekuja na jeshi dogo, lakini Yahwe akawapa ushindi juu ya jeshi kubwa, kwa sababu Yuda alikuwa amemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao. Katika namna hii Waaramu wakaleta hukumu juu ya Yoashi.25Katika muda ambao Waaramu walikuwa wameondoka, Yoashi alikuwa amejeruhiwa vikali. Watumishi wake wakapanga njama dhidi yake kwa sababu ya mauaji ya wana wa Yehoyada, yule kuhani. Wakamuua katika kitanda chake, na akafa; wakamzika katika mji wa Daudi, lakini siyo katika makaburi ya wafalme.

26Hawa walikuwa watu waliopanga njama dhidi yake: Zabadi mwana wa Shimeathi, Mwamoni; na Yehozabadi mwana wa Shimrithi, Mwanamke Mmoabu.27Sasa matukio kuhusu wanaye, unabii muhimu uliokuwa umesemwa kumhusu yeye, na kujengwa tena kwa nyumba ya Mungu, ona, yameandikwa katika Kamusi ya kitabu cha wafalme. Amazia mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

25

1Amaza alikuwa na umri wa miaka ishirini na na tano alipoanza kutawala; alitawala miaka ishirini na tisa katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yehoadani, wa Yerusalemu.2Alifanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, lakini siyo kwa moyo uliojitoa kikamilifu.3Ikawa kwamba mapema utawala wake ulipokuwa umeimarika, aliwaua watumishi ambao walikuwa wamemuua baba yake, mfalme.4Lakini hakuwaua watoto wa wale wauaji, bali alitenda kama kama ilivyo andikwa katika sheria, katika kitabu cha Musa, kama Yahwe alivyokuwa ameamuru. “Baba hatajuta kwa ajili ya watoto, wala watoto hawatakufa kwa ajili ya baba zao. Badala yake, kila mtu lazima afe kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe.”

5Aidha, Amazia aliwakusanya Yuda pamoja, na akawaandikisha kwa kufuata nyumba za baba zao, chini ya maakida wa maelfu na maakida wa mamia --wote wa Yuda na wa Benjamini. Akawahesabu kuanzia wa mika ishirini na kuendelea, na akawaona wako 300,000 wanaume waliochaguliwa, wawezao kwenda vitani, walioweza kushika mkuki na ngao.6Pia alikodi wanaume wa kupigana 100,000 kutoka Israeli kwa fedha mia moja.

7Lakini mtu wa Mungu alikuja kwake na kusema, “Mfalme, usiliache jeshi la Israeli kwenda nawe, kwa maana Yahwe hayupo pamoja na Israeli -wala na mtu Yeyote wa Efraimu.8Lakini hata kama mtaenda na mkiwa wenye ushupavu na imara katika vita, Mungu atawatupa chini mbele ya adui, kwa maana Mungu ana nguvu za kusaidia, na nguvu za kurusha chini.”

9Amazia akasema kwa mtu wa Mungu, “Lakini tutafanyaje kuhusu talanta mia moja nilizowapa jeshi la Israeli? Mtu wa Mungu akajibu, Yahwe ana uwezo wa kukupa vingi zaidi kuliko hivyo.”

10Kwa hiyo Amazia akalitenganisha jeshi lilokuja kwake kutoka Efraimu; akawarudisha nyumbani tena. Hivyo hasira yao iliwaka sana dhidi ya Yuda, na walirudi nyumbani kwa hasira kali.

11Amazia akajipa ujasiri na kuwaongoza watu wake kwenda nje kwenye bonde la chumvi, huko akawashinda wanaume elfu kumi wa Seiri.12Jeshi la Yuda likawachukua elfu kumi wengine wakiwa hai. Wakawapeleka juu ya mwamba na kuwarusha chini kutoka huko, hivyo wote wakavunjika vunjika katika vipande.

13Lakini watu wa jeshi ambalo Amazia alilirudisha, ili kwamba wasiende naye vitani, wakauvamia mji waYuda kuanzia Somaria hadi Beth- horoni. Wakawapiga watu elfu tatu na kuwateka wengi sana.

14Sasa ikawa kwamba baada ya Amazia kurudi kutoka kuwachinja Waedomu, akaileta miungu ya watu wa Seiri, na kuisimamisha iwe miungu yake. Akainama chini mbele ya hiyo miungu na kuitolea sadaka za uvumba.15Hivyo hasira ya Yahwe ikawaka dhidi ya Amazia. Akamtuma nabii kwake, ambaye alisema, “Kwa nini umeitafuta miungu ya watu ambayo haikuwaokoa hata watu wake yenyewe dhidi ya mkono wako?”

16Ikawa kwamba yule nabii alipokuwa anaongea naye, mfalme akamwambia, “Je, wewe tumekufanya kuwa mshauri wa mfalme? Acha! Kwa nini ujitakie kuuawa?” Kisha nabii akaacha na kusema, ninajua kwamba Mungu ameamua kukuangamiza kwa sababu umefanya tendo hili na hujasikiliza ushauri wangu.”

17Kisha Amazia akashauriana na washauri na kutuma wajumbe kwa Yehoashi mwana wa Yehoahazi mwana wa Yehu, mfalme wa Israel. Akisema, “Njoni, tukutane uso kwa uso katika vita.”

18Lakini Yehoashi mfalme wa Israeli akatuma wajumbe kwa Amazia mfalme wa Yuda, akisema, Mbaruti uliokuwa Lebanoni ulituma ujumbe kwa mwerezi ulioko Lebanoni, ukisema, Mtoe binti yako kwa mwanangu awe mke wake; lakini akapita hayawani katika Lebanoni akatembea na kuukanyaga chini mbaruti.19Umesema, ‘Ona, nimeipiga Edomu,’ na moyo wako umekuinua juu. Jipe fahari katika ushindi wako, lakini ukae nyumbani, kwa maana ni kwa nini ujisababishie matatizo mwenyewe na kuanguka, wote wewe na Yuda pamoja nawe?’

20Lakini Amazia hakusikiliza, kwa sababu tukio hili lilikuwa limetoka kwa Mungu, ili awatie Waisraeli katika mkono wa adui zao, kwa sababu walikuwa wametafuta ushauri kutoka kwa miungu ya Edomu.21Kwa hiyo, Yehoashsi, mfalme wa Israeli, akavamia; yeye na Amazia, mfalme wa Yuda, wakakutana uso kwa uso huko Beth -shemishi, ulioko Yuda.22Yuda akashindwa mbele za Israeli, na kila mtu akarudi nyumbani.23Yehoashi, mfalme wa Israeli, akamkamata Amazia mwana wa Yehoashi mwana wa Ahazia, mfalme wa Yuda, huko Beth - shemeshi. Akamleta Yerusalemu na kuuangusha chini ukuta wa Yerusalemu kuanzia Lango la Efraimu hadi kona ya Lango, umbali wa mikono mia nne.24Akachukua dhahabu na fedha zote, vitu vyote vilivyoonekana akatika nyumba aya Mungu kwa Obedi Edomu, na vitu vya thamani katika nyumba ya mfalme, na mateka pia, na akarudi Samaria.

25Amazia mwana wa Yoashi, mfalme wa Yuda, aliishi miaka kumi na tano baada ya kifo cha Yehoashi, mwana wa Yehoahazi, mfalme wa Israeli.26Kwa mambo mengine kuhusu Amzia, mwanzo na mwisho, tazama, je, hayajaandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli?27Sasa kutoka wakati ambao Amazia aligeukia mbali asimfuate Yahwe, walianza kupanga njamadhidi yake katika Yerusalemu. Akakimbilia Lachishi, lakini wakatuma watu nyuma yake wamfuate Lachishsi na walimuua huko.28Wakamleta juu ya farasi na wakamzika pamoja na baba zake katika Mji wa Yuda.

26

1Watu wote wa Yuda wakamchukua Uzia, ambaye alikuwa na umri wa miaka kumi na sita, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake Amazia.2Ndiye aliyeijenga tena Elathi nakuirejesha kwa Yuda. Baada ya hapo mfalme akalala pamoja na baba zake.

3Uzia alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala. Akatawala miaka ishirini na mbili katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yekolia; alikuwa wa Yerusalemu.4Akafanya yaliyokuwa sahihi katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, katika kila jamabo.5Alijitoa kumtafuta Mungu katiaka siku za Zekaria, ambaye alimpa maelekezo kwa ajili ya kumtii Mungu. Kadri alivyomtafuta Yahwe, Mungu alimfanikisha.

6Uzia akaenda na kupigana dhidi ya Wafilisti. Akaubomoa ukuta wa mji wa Gathi, Yabne, na Ashdodi; akajenga miji katika nchi ya Ashdodi na miongoni mwa Wafilisti.7Mungu akaamsaidia dhidi ya Wafilisti, dhidi ya Waarabu waliokuwa wakiishi Gur - baali, na dhidi ya Wameuni.8Waamoni wakalipa kodi kwa Uzia, na umaarufu wake ukaenea, hata kufika maingilio ya Misiri, kwa sababu alikuwa ameanza kuwa maarufu.

9Zaidi ya hayo, Uzia akajenga minara katika Yerusalemu katika kona ya Lango, kwenye Lango la Bonde, na kwenye kona ya ukuta, na akavizungushia ngome.10Akajenga minara ya ulinzi katika nyika na akachimba mabwawa, kwa maana alikuwa na ng'ombe wengi, katika visiwa vya chini na katika nchi tambarare. Alikuwa na wakulima na wapandaji wa zabibu katika mwinuko wa nchi na katika mashamba yenye rutuba, kwa maana alipenda kulima.

11Zaidi ya hayo, Uzia alikuwa na jeshi la wanaume wa kupigana vita ambao walienda vitani katika makundi ambayo idadi yake ilikuwa imehesabiwa na Yeieli, mwandishi. Na Maaseya, afisa, chini ya mamlaka ya Hanania, mmoja wa maamri jeshi wa mfalme.12Jumla ya wakuu wa nyumba za mababu, watu wa kupigana vita, walikuwa 2,600.13Chini ya mkono wao kulikuwa na jeshi la watu 307,500 ambao walifanya vita kwa nguvu ili kumsaidia mfalme idi ya maadui.14Uzia akaandaa kwa ajili yao—kwa ajili ya jeshi lote — ngao, mikuki, chapeo, deraya za majini, nyuta, na mawe ya kurusha.15Katka Yerusalemu alijenga mitambo, iliyobuniwa na watu wenye ujuzi, ili iwe juu ya minara na juu ya buruji, kwa ajili ya kurushia mishale na mawe makubwa. Umaarufu wake ukaenea hadi nchi za mbali, kwa maana alisaidiwa sana hadi alipokuwa na nguvu sana.

16Lakini Uzia alipokuwa amekuwa na nguvu nyingi, moyo wake ulijiinua akatenda kwa uovu; akafanya makosa zidi ya Yahwe, Mungu wake, kwa maana alienda kwenye nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kufukiza uvumba juu ya madhabahu ya kufukizia.17Azaria, kuhani, akamfuata, na pamoja naye makuhani themanini wa Yahwe, ambao walikuwa watu wenye ujasiri.18Walimzuia Uzia, mfalme, na wakasema kwake, “Siyo jukumu lako, Uzia, kumtolea Yahwe uvumba, bali ni kazi ya makuhani, wana wa Haruni, amabao wametengwa kwa ajili ya kutoa sadaka za uvumba. Toka nje ya sehemu takatifu, kwa maana huna uaminifu na hautaheshimiwa na Yahwe Mungu.”

19Kisha Uzia akakasirika. Alikuwa ameshikilia chetezo mkononi kwa ajili ya kufukiza uvumba. Wakati alipowaghadhabikia makuhani, ukoma ukatokea juu ya uso wake mbele ya makuhani katika nyumba ya Yahwe, pembeni mwa madhabahu ya uvumba.20Azaria kuhani mkuu na makuhani wote wakamwangalia, na, tazama, alikuwa amepatwa na ukoma juu ya uso wake. Walimwondoa pale haraka. Kwa hakika, aliharakisha kwenda nje, kwa maana Yahwe alikuwa amempiga.

21Uzia, mfalme, alikuwa mwenye ukoma hadi siku ya kufa kwake na aliishi katika nyumba ya kutengwa tangu alipokuwa mwenye ukoma, kwa maana alitengwa na nyumba ya Yahwe. Yothamu, mwanaye, alikuwa mkuu wa nyumba ya mfalme na aliwatawala watu wa nchi.

22Mambo mengine kuhusu Uzia, mwanzo na mwisho, yako katika kile ambacho Isaya, mwana wa Amozi, nabii, aliandika.23Kwa hiyo Uzia akalala pamoja na baba zake; walimzika pamoja na baba zake katika uwanja wa maziko wa Mfalme, kwa maana walisema, “Ni mwenye ukoma.” Yothamu, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

27

1Yothamu alikuwa na umri wa mika ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Jina la mama yake lilikuwa Yerusha; alikuwa binti Sadoki.2Akafanya yaliyo mema katika macho ya Yahwe, akiufuata mfano wa baba yake, Uzia, katika mambo yote. Pia alijiepusha kuingia katika hekalu la Yahwe. Lakini watu bado walikuwa wanaenda katika njia za uovu.

3Akalijenga tena lango la juu la nyumba ya Yahwe, na juu ya kilima cha Ofeli akajenga sana.4Vile vile alijenga miji katika kilima cha Yuda, na katika msitu alijenga ngome na minara.

5Pia alipigana na mfalme wa watu wa Amoni na akawashinda. Katika mwaka huo huo, watu wa Amoni walimpa talanta mia moja za fedha, kori elfu kumi za ngano, kori elfu kumi za shayiri. Watu wa Amoni wakampa hivyo hivyo katika mwaka wa pili na wa tatu.

6Kwa hiyo Yothamu akawa na nguvu sana kwa sababu alitembea imara mbele za Yahwe Mungu wake.

7Kwa mambo mengine kuhusu Yothamu, vita vyake vyote, na njia zake zote, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Israeli na Yuda.8Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; alitawala kwa miaka kumi na sita katika Yerusalemu.9Yothamu akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji wa Daudi. Ahazi, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

28

1Ahazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu. Hakufanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi babu yake alivyokuwa amefanya.2Badala yake, alitembea katika njia za wafalme wa Israeli; pia alitengeneza sanamu za kusubu kwa ajila ya Mabaali.3Zaidi ya hayo, akafukiza uvumba katika bonde la Beni Hinomu na akawaweka watoto wake ndani ya moto, kwa mjibu wa desturi za uzinzi za watu ambao Yahwe aliwafukuza nje ya nchi zao mbele za watu wa Israeli.4Akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika sehemu za juu na juu ya vilima na chini ya kila mti wenye majani mabichi.

5Kwa hiyo Yahwe Mungu wa Ahazi, akamweka katika mikono ya mfalme wa Shamu. Waaramu wakamshinda na kuchukua kutoka kwake kundi kubwa la mateka, wakawapeleka Damesiki. Ahazi pia aliwekwa katika mikono ya mfalme wa Israeli ambaye alimshinda kwa mauji makuu.6Kwa maana Peka mwana wa Remalia, aliwaua katika Yuda wanajeshi 120, 00 kwa siku moja, wote walikuwa wanaume hodari, kwa maana walikuwa wamemsahau Yahwe, Mungu wa babu zao.7Zikri, mtu mwenye nguvu kutoka Efraimu, akawaua Maaseya mwana wa mfalme, Azrikamu, mwangalizi mkuu wa ikulu, na Elkana, ambaye alikuwa karibu na mfalme.8Jeshi la Israeli likachukua mateka kutoka kwa ndugu zao 200,000 wake, wana, na mabinti. Pia wakachukua nyara nyingi, ambazo walipeleka Samaria.

9Lakini nabii wa Yahwe alikuwapo huko, jina lake aliitwa Odedi. Alikwenda nje kukutana na jeshi likiingia Samaria. Akawaambia, “Kwa sababu Yahwe, Mungu wa baba zenu, alikuwa na hasiri na Yuda, akawatia katika mikono yenu. Lakini mmewaua katika hasira inayofika juu mbinguni.10Sasa ninyi badala ya kuwahifadhi wanaume na wanawake wa Yuda na Yerusalemu kama watumwa wenu. Lakini je hamko na hatia ya dhambi zenu dhidi ya Yahwe Mungu wenu?11Sasa basi, nisikilizeni: warudisheni wafungwa, ambao mmewachukua wa ndugu zenu, kwa maana ghadhabu ya Yahwe iko juu yenu.”

12Kisha baadhi ya viongozi wa watu wa Efraimu--Azaria mwana wa Yohanani, Berekia mwana wa Meshiremothi, na Yehizikia mwana wa Shalumu, na Amasa mwana wa Hadlai, wakasimama kinyume na wale waliorudi kutoka vitani.13Wakasema kwao, “Lazima msiwalete wafungwa hapa, kwa kuwa mlikusudia jambo ambalo litaleta juu yetu dhambi dhidi ya Yahwe, kuongeza dhambi juu yetu na makosa yetu, kwa maana makosa yetu ni makubwa, na kuna hasira kali dhidi ya Israeli.”

14Hivyo watu wenye silaha wakawaacha wafungwa na mateka mbele ya viongozi wa Israeli na kusanyiko lote15Watu ambao walipangwa kwa majina wakanyanyuka na kuwachukua wafungwa, na kuwavika wote waliokuwa uchi miongoni mwa mateka. Wakawavika na kuwapa viatu. Wakawapa chakula wale na kunywa. Wakawahudumia majeraha yao na kuwaweka waliodhaifu juu ya punda. Wakawarudisha kwenye familia zao katika Yeriko, (Ulioitwa mji wa mitende). Kisha wakarudi Samaria.

16Wakati huo Mfalme Ahazi akatuma wajumbe kwa wafalme waAshuru kuwaomba wamsaidie.17Kwa maana Waedomu walikuwa wamekuja tena na kuvamia Yuda, wakachukua wafungwa.18Wafilisti pia wakavamia miji ya nchi ya chini na ya Negebu ya Yuda. Waliichukua Beth-shemeshi, Ayaloni, Giderothi, SoKo pamoja na vijiji vyake, Timna pamoja na vijiji vyake. Wakaenda kuishi katika sehemu hizo.19Kwa kuwa Yahwe aliishusha chini Yuda kwa sababu ya Ahazi, mfalme wa Israeli; kwa maana alikuwa ametenda maovu katika Yuda na alikuwa ametenda dhambi nzito sana dhidi ya Yahwe.20Tiglath-pileseri, mfalme wa Ashuru, akaja kwake na akampa taabu badala ya kumpa nguvu.21Kwa kuwa Ahazi aliteka nyara nyumba ya Yahwe na nyumba ya mfalme na viongozi, kwa ajili ya kuvitoa vitu vya thamani kwa mfalme wa Ashuru. Lakini kufanya hivyo hakukumfaidisha yeye.

22Mfalme Ahazi akatenda dhambi hata zaidi dhidi ya Yahwe katika muda wa mateso yake.23Kwa maana aliwatolea dhabihu miungu wa Dameski, miungu ambao walimshinda. Akasema, “Kwa sababu miungu wa mfalme wa Aramu waliwasaidia, nitawatolea sadaka ili wanisaidie.” Lakini walikuwa watesi wake na Israeli yote.

24Ahazi akazikusanya pamoja samani za nyumba ya Mungu na kuzikata vipande vipande. Akaifunga milango ya nyumba ya Yahwe na kuzitengeneza madhabahu kwa ajili yake mwenyewe katika kila kona ya Yerusalemu.25Katika kila mji wa Yuda akafanya sehemu za juu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa kwa miungu wengine. Akamfanya Yahwe, Mungu wa babu zake, akasirike.

26Sasa matendo yake yaliyobaki, na njia zake zote, mwanzo na mwisho, ona, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.27Ahazi akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mji, katika Yerusalemu, lakini hawakumleta kwenye makaburi ya wafalme wa Israeli. Hezekia, mwanaye, akawa mfamle katika nafasi yake.

29

1Hezekia alianza kutawala alipokuwa na umri wa miaka ishirini na mitano; alitawala miaka ishirini na nane katika Yerusalemu. Jina la mama yake aliitwa Abiya; alikuwa binti wa Zekaria.2Alifanya yaliyoadili katika macho ya Yahwe, kama Daudi baba yake alivyofanya.

3Katika mwaka wa kwanza wa utawala wake, katika mwezi wa kwanza, Hezekia aliifungua milango ya nyumba ya Yahwe na kuikarabati.4Akawaleta ndani makuhani na Walawi, na akawakusanya pamoja katika uwanda upande wa mashariki.5Akawaambia, “Nisikilizeni, ninyi Walawi! Jitakaseni wenyewe, na itakaseni nyumba ya Yahwe, Mungu wa babu zenu, na uondoeni mbali uchafu kutoka kwenye sehemu takatifu.6Kwa kuwa baba zetu walikosea na kufanya kilichokuwa uovu katika macho ya Yahwe Mungu wetu; walimsahau, wakageuzia mbali nyuso zao kutokasehemu ambapo Yahwe anaishi, na kuigeuzia migongo yao.7Pia waliifunga milango ya ukumbi nakuziweka nje taa; hawakufukiza uvumba au kutoa sadaka za kuteketezwa katika sehemu takatifu kwa Mungu wa Israeli.8Kwa hiyo hasira ya Yahwe ilikuwa imeshuka juu ya Yuda na Yerusalemu, na amewafanya kuwa kitu cha wasiwasi, cha hofu, na cha kudharauliwa, kama mnavyoona kwa macho yenu.9Hii ndiyo maana mababa zetu wameanguka kwa upanga, na wana wetu, binti zetu, na wake zetu wako katika utumwa kwa sababu ya hili.10Sasa ni katika moyo wangu kufanya agano na Yahwe, Mungu wa Israeli, ili kwamba hasira yake kali iweze kugeukia mbali nasi.11Wanangu, msiwe wavivu sasa, kwa kuwa Yahwe amewachagua kwa ajili ya kusimama mbele yake, kwa ajili ya kumwabudu yeye, na kwamba muwe watumishi wake na kufukiza uvumba.”

12Basi Walawi wakainuka; Mahathi mwana wa Amasai, na Yoeli mwana wa Azaria, wa watu wa Kohathi; na wa watu wa Merari, Kishi mwana wa Abdi, na Azaria mwana wa Yehaleleli; na wa Wargeshoni, Yoa mwana wa Zimna, na Edeni mwana wa Yoa;
13wa wana wa Elisafani, Shimri na Yeueli; wa wana wa Asafu, Zekaria na Matania;
14wa wana wa Hemani, Yehueli na Shimei; na wa wana Yeduthuni, Shemaya na Uzieli.

15Wakawakusanya ndugu zao, wakajitakasa wenyewe, na wakaenda ndani, kama alivyoamuru mfalme, wakifuata maneno ya Yahwe, kwa ajili ya kuisafisha nyumba ya Yahwe.16Makuhani wakaenda kwenye sehemu za ndani ya nyumba ya Yahwe kwa ajili ya kuisafisha; wakaleta nje uchafu wote walioukuta ndani ya hekalu la Yahwe katika uwanja wa nyumba. Walawi wakauchukua kuubeba nje ya hadi kwenye kijito cha Kidroni.17Sasa wakaanza utakaso katika siku ya kwanza ya mwezi. Katika siku ya nane ya mwezi wakaufikia ukumbi wa Yahwe. Kisha siku nane zaidi wakaitakasa nyumba ya Yahwe. Katika siku ya kumi na sita ya mwezi wa kwanza wakamaliza.

18Kisha wakaenda kwa Hezekia, mfalme, ndani ya ikulu na kusema, “Tumeisafisha nyumba yote ya Yahwe, madhabahu kwa ajili ya kutolea sadaka za kuteketezwa pamoja na vifaa vyake vyote, na meza ya mkate wa uwepo, pamoja na vifaa vyake vyote.19Kwa hiyo tumejiandaa na tumevitakasa vitu vyote ambavyo Mfalme Ahazi aliviondoa wakati alipoenda kwa ukengeufu katika kipindi cha utawala wake, ona, viko mbele ya madhabahu ya Yahwe.”

20Kisha Hezekia mfalme akaamka mapema asubuhi na kuwakusanya viongozi wa miji; akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.21Wakaleta ng'ombe waume saba, kondoo waume saba, wanakondoo saba, mbuzi waume saba kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya mfalme, kwa ajili ya patakatifu, kwa ajili ya Yuda. Akawaamuru makuhani, wana wa Haruni, kuwatoa sadaka juu ya madhabahu ya Yahwe.22Kwa hiyo wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu na kuinyunyiza juu ya madhabahu. Wakawachinja kondoo dume, na kunyunyiza damu juu ya madhabahu; Pia wakawachinja wanakondoo na kuinyunyiza damu juu ya madhabahu.23Wakawaleta mbuzi kwa ajili ya sadaka ya dhambi mbele ya mfalme na kusanyiko; wakaweka mikono yao juu ya hao mbuzi.24Makuhani wakawachinja, na wakafanya sadaka ya dhambi kwa damu yao juu ya madhabahu ili kufanya upatanisho kwa ajili ya Israeli wote, kwa maana mfalme alikuwa ameamuru kuwa sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya dhambi lazima zifanywe kwa ajili ya Israeli wote.

25Hezekia akawaweka Walawi katika nyumba ya Yahwe wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, akiwapanga kwa amri ya Daaudi, Gadi, mwonaji wa mfalme, na Nathani, nabii, kwa maana amri ilitoka kwa Yahwe kupitia manabii wake.26Walawi wakasimama na vyombo vya Daudi, na makauhani wakasimama na matarumbeta.

27Hezekia akawaamuru kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu. Sadaka zilipoanza, wimbo wa Yahwe ukaanza pia, kwa matarumbeta, pamoja na vyombo vya Daudi, mfalme wa Israeli.28Kusanyiko lote wakaabudu, waimbaji wakaimba, na wapiga matarumbeta wakapiga; yote hayo yakaendelea hadi sadaka za kuteketezwa zilizipokwisha.

29Walipomaliza kutoa sadaka, mfalme na watu waliokuwepo pamoja naye wakainama, na kusujudu.30Vile vile, Hezekia, mfalme, na viongozi wakawaamuru Walawi kuimba ili kumsifu Yahwe kwa maneno ya Daudi na ya Asafu, mwonaji. Wakaimba sifa kwa furaha, wakainama chini wakasujudu.

31Kisha Hezekia akasema, “Sasa mmejiweka wakfu wenyewe kwa Yahwe. Njoni hapa na mlete sadaka na dhabihu za shukrani katika nyumba ya Yahwe.” Kusanyiko wakaleta sadaka na dhabihu za shukrani, na wote waliokuwa na moyo wa kuhiyarika wakaleta sadaka za kuteketezwa.

32Hesabu ya sadaka za kuteketezwa ambazo kusanyiko walileta ilikuwa ng'ombe sabini, kondoo waume mia moja, na wanakondo waume mia mbili. Wote hao walikuwa kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa Yahwe.33Sadaka za kuwekwa wakfu zilikuwa ng'ombe mia sita na kondoo elfu tatu.34Lakini makuhani walikuwa wachache sana kuchuna sadaka zote za kuteketezwa, kwa hiyo ndugu zao, Walawi, wakawasaidia hadi kazi ilipoisha, na hadi makuhani walipoweza kujitakasa wenyewe, kwa maana Walawi walikuwa makini sana kujitakasa wenyewe kuliko makuhani.

35Zaidi ya hayo, palikuwa na sadaka za kuteketezwa nyingi sana; zilitolewa pamoja na sadaka za mafuta za amani, na kulikuwa na sadaka za vinywaji kwa kila sadaka ya kuteketezwa. Kwa hiyo huduma ya nyumba ya Yahwe ikawekwa katika utaratibu.36Hezekia akafurahia, na watu pia, kwa sababu ya kile ambacho Mungu alikuwa ameandaa kwa ajili ya watu, kwa maana kazi ilikuwa imekamilika haraka.

30

1Hezekia akatuma wajumbe kwa Israeli wote na Yuda, na pia akawaandikia barua Efraimu naManase, kwamba waje kwenye nyumba ya Yahwe katika Yerusalemu, kusherehekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli.2Kwa maana mfalme, viongozi wake, na kusanyiko lote katika Yerusalemu walikuwa wameshauriana pamoja, wakakubaliana kusherehekea Pasaka katika mwezi wa pili.3Hawakuweza kuisherehekea mapema kabla ya hapo, kwa sababu hapakuwa na makuhani wa kutosha waliojitakasa wenyewe, wala watu hawakuwa wamekusanyika pamoja Yerusalemu.4Pendekezo hili likaonekana sahihi katika macho ya mfalme na ya kusanyiko lote.5Kwa hiyo wakakubaliana kufanya tangazo katika Israeli yote, kuanzia Beer-sheba hadi Dani, kwamba watu lazima waje kusherehekea Pasaka ya Yahwe, Mungu wa Israeli, huko Yerusalemu. Kwa maana walikuwa hawakuwa wameisherehekea kwa hesabu kubwa ya watu, kwa mujibu wa jinsi ilivyokuwa imeandikwa.

6Hivyo matarishi wakaenda na barua kutoka kwa mfalme na viongozi wake katika Israeli na Yuda yote, kwa agizo la mfalme. Wakasema, “Ninyi watu wa Israeli, rudini kwa Yahwe, Mungu wa Abrahamu, Isaka na Israeli, ili kwamba aweze kuwarudia masalia wenu ninyi mlipona kutoka kwenye mkono wa wafalme wa Ashuru.7Msiwe kama baba zenu au ndugu zenu, ambao walimuasi Yahwe, Mungu wa mababa zao, hivyo akawaweka katika kuangamia, kama mnavyoona.8Sasa msiwe wasumbufu, kama babu zenu walivyokuwa; badala yake, jitoeni wenyewe kwa Yahwe na njooni kwenye sehemu yake takatifu, ambayo ameitakasa milele, na mwabuduni Yahwe Mungu wenu, ili kwamba uso wake wenye hasira uwageukie mbali.9Kwa maana ikiwa mtageuka nyuma kwa Yahwe, ndugu zenu na watoto wenu watapata huruma mbele ya hao wanaowaongoza kama wafungwa, na watarudi katika nchi hii. Kwa maana Yahwe Mungu wenu, ni mkarimu na mwenye huruma, na hatawageuzia mbali uso wake, kama mtarudi kwake.”

10Kwa hiyo matarishi wakapita mji kwa mji katika majimbo ya Efraimu na Manase, njia yote hadi Zabuloni, lakini watu waliwacheka na kuwazomea.11Lakini, watu wengine wa Asheri na Manase na Zabuloni walijinyenyekesha wenyewe na wakaja Yerusalemu.12Mkono wa Mungu pia ukaja juu ya Yuda, kuwapa moyo mmoja, ili kulikubali agizo la mfalme na viongozi kwa neno la Yahwe.

13Watu wengi, kusanyiko kubwa, likakusanyika Yerusalemu kusherehekea Sikukuu ya Mikate Isiyochacha katika mwezi wa pili.14Waliinuka na kuchukua madhabahu zilizokuwa Yerusalemu, madhabahu zote kwa ajili ya sadaka za kufukiza; wakazirusha katika kijito Kidroni.

15Kisha wakamuua mwanakondoo wa Paska katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa pili. Makuhani na Walawi wakaona aibu, kwa hiyo wakajitakasa wenyewe na kuleta sadaka za kuteketezwa katika nyumba ya Yahwe.

16Wakasimama katika sehemu zao katika makaundi yao, wakifuata maelekezo yaliyotolewa na sheria ya Musa, mtu wa Mungu. Makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi.17Kwa maana walikuwepo wengi katikakusanyiko ambao hawakuwa wamejitakasa wenyewe. Kwa hiyo Makuhani wakamchinja mwanakondoo wa Pasaka kwa ajili ya kila mmoja ambaye hakuwa amejisafisha na hakuweza kuzitakasa sadaka zake kwa Yahwe.18Kwa kuwa wingi wa watu, wengi wao kutoka Efraimu na Manase, Asakari na Zabuloni, hawakuwa wamejitakasa wenyewe, bado waliula mlo wa Pasaka, kinyume na maelekezo yaliyoandikwa. Kwa kuwa Hezekia alikuwa amewaombea, akisema, “Mungu Yahwe amsamehe kila mmoja19ambaye anauelekeza moyo wake kumtafuta Mungu, Yahwe, Mungu wa baba zake, hata kama hajasafiswa kwa utakaso wa viwango vya patakatifu.” 20Kwa hiyo Yahwe akamsikiliza Hezekia na akawaponya watu.

21Watu wa Israeli waliokuwepo Yerusalemu wakaitunza Sikukuu ya Mikaate Isiyochachwa na furaha kubwa kwa siku saba. Walawi na makuhani wakamsifu Yahwe siku baada ya siku, wakiimwimbia Yahwe kwa vyombo vya sauti kuu.

22Hezekia akazungumza kwa kuwatia moyo Walawi wote walioielewa ibada ya Yahwe, Kwa hiyo wakala kwa kipindi cha siku saba, wakitoa sadaka za amani, na kufanya toba kwa Yahwe, Mungu wa babu zao.

23Kusanyiko lote kisha likaamua kusherehekea kwa siku zingine saba, na wakafanya hivyo kwa furaha.24Kwa kuwa Hezekia mfalme wa Yuda aliwapa kusanyiko ng'ombe dume elfu moja, na kondoo elfu saba kama sadaka; na viongozi wakawapa kusanyiko ng'ombe dume elfu moja na kondoo na mbuzi elfu kumi. Idadi kubwa ya makuhani wakajitakasa wenyewe.25Kusanyiko lote la Yuda, pamoja na makuhani na Walawi na watu wote walikuja pamoja kutoka nchi ya Israeli na wale walioishi Yuda--wote wakafurahia.26Hivyo kulikuwa na furaha kuu katika Yerusalemu, kwa kuwa tangu wakati wa Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli, hapakuwa na kitu kama hicho katika Yerusalemu.27Kisha makuhani, Walawi, wakainuka na kuwabariki watu. Sauti zao zilisikika na maombi yao yakaenda juu mbinguni, sehemu takatifu ambapo Mungu anaishi.

31

1Sasa wakati haya yote yalipokwisha, watu wote wa Israeli waliokuwepo pale wakaenda huko kwenye mji wa Yuda na wakazivunja vipande vipande nguzo za mawe na wakazikata nchi za maashera, na wakazibomoa sehemu za juu na madhabahu katika Yuda yote na Benjamini, na katika Efraimu na Manase, hadi walipoziharibu zote. Kisha watu wote wa Israeli wakarudi, kila mtu kwenye mali zake na kwenye mji wake.

2Hezekia akayapanga makundi ya makuhani na Walawi wakajipanga kwa makundi yao, kila mtu akapangwa katika kazi yake, wote makuhani na Walawi. Aliwapanga wafanye sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani, kuhudumu, kutoa shukrani, na kusifu katika malango ya hekalu la Yahwe.3Pia akawapanga katika sehemu ya mfalme kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kutoka katika mali zake, hiyo ni kwa ajili ya, sadaka za kuteketezwa za asubuhi na jioni, na sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya siku za Sabato, mwezi mpya, na siku kuu zisizobadilika, kama ilivyokuwa imeandikwa katika sheria ya Yahwe.4Vilevile, akawaamuru watu walioishi Yerusalemu kutoa fungu kwa ajili ya makuhani na Walawi, ili kwamba wawe makini katika kuitii sheria ya Yahwe.5Mapema mara baada ya amri kutolewa, watu wa Israeli kwa ukarimu wakatoa malimbuko ya nafaka, divai mpya, mafuta. Asali, na kila kitu kutoka kwenye mavuno ya shamba. Wakaleta ndani fungu la kumi la kila kitu; ambavyo vilikuwa kiasi kikubwa sana.6Watu wa Israeli na Yuda ambao waliishi katika mji wa Yuda pia wakaleta zaka za ng'ombe na kondoo, na zaka za vitu vitakatifu amabavyo vilikuwa vimewekwa wakfu kwa Yahwe Mungu wao, na wakavifunga katika marundo.7Ilikuwa mwezi wa tatu wakati walipoanza kufunga michango yao katika marundo, na wakamaliza mwezi wa saba.8Hezekia na viongozi walipokuja na kuyaona marundo, wakambariki Yahwe na watu wake Israeli.

9Kisha Hezekia akawauliza makuhani na Walawi kuhusu marundo.10Azaria, kuhani mkuu, wa nyumba ya Zadoki, akamjibu na akasema, “Tangu watu walipoanza kuleta matoleo katika nyumba ya Yahwe, tumekula na tulikuwa navyo vya kutosha, tulibakiza vingi, kwa maana Yahwe amewabariki watu wake. Kilichokuwa kimebaki ni kiasi kikubwa hiki hapa.”

11Kisha Hezekia akaagiza vyumba vya kuhifadhia viandaliwe katika nyumba ya Yahwe, na wakaviandaa.12Kisha kwa uaminifu wakayaleta ndani matoleo, zaka, na vitu ambavyo ni vya Yahwe. Konania, Mlawi, alikuwa meneja mkuu wa hivyo vitu, na Shimei, ndu yake, alikuwa wa pili kwake.13Yehieli, Azaria, Nahathi, Asaheli, na Yerimothi, Yazabadi, Elieli, Ismakia, Mahathi, na Benania walikuwa wasimamizi chini ya mkono wa Konania na Shimei ndu yake, kwa uteuzi wa Hezekia, mfalme, na Azaria mwangalizi mkuu wa nyumba ya Mungu.

14Kore mwana wa Imna Mlawi, bawabu katika mlango wa mashariki, alikuwa juu ya sadaka za hiari za Mungu, msimamizi wa kugawa sadaka kwa Yahwe na sadaka takatifu kuliko zote.15Chini yake walikuwepo Edeni, Miniamini, Yoshua, Shemai, Amaaria, na Shekania, katika miji ya makuhani. Wakazijaza ofisi za uaminifu, ili kutoa sadaka hizi kwa ndugu zao fungu kwa fungu, kwa wote walio muhimu na wasio muhimu.

16Pia wakatoa kwa wale wanaume wenye umri wa miaka mitatu na kuendelea, amabao walikuwa wameandikwa katika kitabu cha baba zao walioiingia nyumba ya Yahwe, kwa mujibu wa ratiba ya kila siku, kuifanya kazi katika ofisi zao na zamu zao. 117Waliwaganya makuhani kwa mujibu wa kumbu kumbu za baba zao, na hivyo hivyo kwa Walawi wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, kwa mujibu wa ofisi zao na zamuzao.18Waliwajumuisha watoto wao wadogo wote, wake zao, wana wao, na binti zao, katika jamii yote, kwa maana walikuwa waaminifu katika kujitunza wenye watakatifu.

19Kwa maana makuhani, uzao wa Haruni, amabao walikuwa katika mashamba ya vijiji wakimilikiwa na miji yao, au katika kila mji, palikuwa na watu walioteuliwa kwa majina kutoa mafungu kwa ajili ya wanaume miongoni mwa makuhani, na kwa wote waliokuwa wameorodheshwa katika kumbukumbu za baba zao kuwa miongoni mwa Walawi.

20Hezekia alifanya haya katika Yuda yote. Akakamilisha kilichokuwa chema, haki, na uaminifu mbele za Yahwe Mungu wake.21Katika kila jambo ambalo alianzisha katika ibada ya nyumba ya Mungu, sheria, na zile amri, kumtafuta Mungu, alikifanya kwa moyo wake wote, na alifanikiwa.


1Mandishi ya kale yanasema hivi: “badala ya wanaume wa umri wa miaka mitatu na kuendelea,” wanaume wa mika thelathini na kuendelea.”

32

1Baada ya mambo haya na matendo haya ya uaminifu, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, akaja na kuingia Yuda. Alipiga kambi kwa ajili ya kuivamia miji yenye ngome, ambayo alikusudia kuiteka kwa ajili yake.2Sedekia alipoona kwamba Senakeribu amekuja na kwamba amedhamiria kupigana dhidi ya Yerusalemu,3aliwashirikisha viongozi wake na watu wake wenye nguvu kuyazuia maji ya chemichemi yaliyokuwa nje ya mji; waalimsaidia kufanya hivyo.4Kwa hiyo watu wengi wakakusanyika na kuyazuia maji ya chemichemi zote na mikondo yote amabayo ilikuwa inatiririka katikati ya nchi. Wakasema, “Kwa nini mfalme wa Ashuru aje na kupata maji mengi?”5Hezekia akijipa ujasiri na kuujenga ukuta wote uliokuwa umeangushwa chini. Akaijenga minara mirefu, na pia ukuta mwingine nje. Pia akaiimarisha Milo katika mji wa Daudi, na akafanya kiasi kikubwa cha silaha na ngao. 1

6Akaweka maamri jeshi juu wa watu. Akawakusanya pamoja kwake katika sehemu pana kwenye lango la mji na akasema kwao kwa ujasiri. Akasema,7“Muwe imara na wenye ujasiri mzuri. Msiogope wala kukata tamaa kwa sababu ya mfalme wa Ashuru na jeshi lote ambalo liko naye, kwa maana kuna mtu yuko pamoja nasi ambaye ni mkuu kuliko8walio naye mfalme wa Ashuru. Walionaye ni jeshi la mwili tu, lakini aliye nasi ni Yahwe, Mungu wetu, kwa ajili ya kutusaidia, na kupigana vita vyetu.” Kisha watu wakajifariji wenyewe kwa maneno ya Hezekia, mfalme wa Yuda.

9Baada ya hayo, Senakeribu, mfalme wa Ashuru, aliwatuma watumishi wake kwenda Yerusalemu (sasa alikuwa mbele ya Lakishi, na jeshi lake lote lilikuwa pamoja naye), kwa Hezekia, mfaalme wa Yuda, na watu wote wa Yuda walikuwa Yerusalemu. Akasema,10“Hivindivyo Senakeribu, mfalme wa Ashuru, anasema: Ni kitu gani mnategemea kwa ajili ya kuhimili uvamizi katika Yerusalemu?11Je, Hezekia hawapotoshi ninyi, ili kwamba awatoe kufa kwa njaa na kiu, anapowaambia, “Yahwe Mungu wetu atatuokoa na mkono wa mfalme wa Ashuru?12Je, siyo Hezekia yule yule ambaye amezipeleka juu sehemu zake na madhabahu zake na kuwaamuru Yuda na Yerusalemu, juu ya madhabahu moja lazima muabudu, na juu yake lazima mchome sadaka zenu?13Je, hamjui mimi na baba zangu tulifanya nini kwa makundi ya wote wa nchi zingine? Je, miungu ya watu wa hizo nchi iliweza kwa njia yoyote kuziokoa nchi zao dhidi ya nguvu zangu?14Miongoni mwa miungu yote ya mataifa hayo ambayo baba zangu walitekeza, je, kulikuwa na mungu yeyote aliyeweza kuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu? Itakuwaje Mungu wenu aweze kuwakoa ninyi dhidi ya nguvu zangu?15Sasa msimruhusu Hezekia awadanganye au kuwashawishi katika njia hii. Msimwamini, kwa maana hakuna mungu wa taifa lolote au ufalme amewahi kuwaokoa watu wake nje ya mkono wangu, au nje ya mkono wa baba zangu. Sembuse na Mungu wenu kwa namna gani atawaokoa na mkono wangu?

16Watumishi wa Senakeribu hata walinena mabaya zaidi juu ya Yahwe Mungu na juu ya mtumishi wake Hezekia.17Senakeribu pia akaandika barua ili kumdhihaki Yahwe, Mungu wa Israeli, na kunena kinyume naye. Alisema, “Kama ambavyo miungu ya mataifa haikuwaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu, hivyo hivyo na Mungu wa Hezekia hatawaokoa watu wake kutoka kwenye mkono wangu.”18Wakawalilia kwa lugha ya Wayahudi watu wa Yerusalemu waliokuwa juu ya ukuta, ili kuwaogopesha na kuwasumbua, ili kwamba waweze kuuteka mji.19Wakamnenea Mungu wa Yerusalemu kama walivyowanenea miungu ya Dunia, ambao ni kazi ya mikono ya wanadamu tu.

20Hezekia, mfalme, na Isaya mwana wa Amozi, nabii, wakaomba kwa sababu ya jambo hili na wakalia hadi mbinguni.21Yahwe akatuma malaika, ambaye aliwaua wanaume wa kupigana vita, majemedari, na maakida wa mfalme katika kambi. Kwa hiyo Senakeribu akarudi katika nchi yake akiwa na uso wa aibu. Alipokuwa ameenda katika nyumba ya mungu wake, baadhi ya watoto wake wakamuua huko kwa upanga.

22Katika namna hii, Yahwe akamwokoa Hezekia na wakaaji wa Yerusalemu kutoka kwenye mkono wa Senakeribu, mfalme wa Ashuru, na kutoka kwenye mikono ya wengine, na akawapa pumzika juu ya kila upande. 223Wengi walikuwa wakileta sadaka kwa Yahwe katika Yarusalemu, na zawadi za thamani kwa Hezekia mfalme wa Yuda, kwa hiyo aliinuliwa mbele za macho ya mataifa yote toka wakati huo na kuendelea.

24Katika siku hizo Hezekia akaugua hadi hatua ya kufa. Akaomba kwa Yahwe, ambaye alisema kwake na kumpaishara kwamba angeponywa.25Lakini Hezekia hakumlipa Yahwe kwa ajili ya msaada uliotolewa kwake, kwa maana moyo wake uliinuliwa juu.26Kwa hiyo hasira ikaja juu yake, na juu ya Yuda na Yerusalemu. Hata hivyo, baadaye Hezekia alijinyenyekesha mwenyewe kwa ajili ya kiburi cha moyo wake, wote Yeye na wakaaji wa Yerusalemu, hivyo hasira ya Yahwe haikuja juu yao wakati wa siku za Hezekia.

27Hezekia alikuwa na utajiri mwingi sana na heshima kubwa. Alijipatia mwenyewe vyumba vya kuhifadhia kwa ajili ya fedha, dhahabu, vito vya thamani, na kwa ajili ya manukato, na kwa ajili ya ngao na na vyombo vyote vya thamani pia.28Pia alikuwa na nyumba za maghala kwa ajili ya mavuno ya nafaka, divai mpya, na mafuta, na malisho kwa ajili ya aina zote za wanyama.29Pia alikuwa na makundi katika mazizi. Zaidi ya hayo, alijipatia mwenyewe miji na makundi ya na ng'ombe kwa wingi, kwa maana Mungu alikuwa amempa afya tele. 3

30Alikuwa ni Hezekia ambaye alisimamisha chemi chemi ya juu ya maji ya Gihoni, na aliyeileta moja kwa moja chini upande wa magharibi mwa mji wa Daudi. Hezekia alifanikiwa katika miradi yake yote.31Hata hivyo, katika jambo la mabalozi wa wakuu wa Babeli, waliotumwa kwake kuwauliza waliofahamu, kuhusu ishara za miujiza iliyokuwa imefanywa katika nchi, Mungu alimwachia mwenyewe, ili kumjaribu, na kujua yote yaliyokuwa katika moyo wake.

32Kwa mambo mengine kuhusu Hezekia, pamoja na matendo yake ya uaminifu wa agano, unaweza kuona kwamba yameandikwa katika Maono ya Nabii Isaya Mwana wa Amozi, na katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.33Hezekia akalala pamoja na baba zake, na wakamzika katika mlima wa makaburi ya vizazi vya Daudi. Yuda wote na wakaaji wa Yerusalemu wakamheshimu katika kifo chake. Manase mwanaye akawa mfalme katika nafasi yake.


1Maandishi ya kale yanasema hivi: “Badala ya, “akajenga minara mirefu,” baadhi ya matoleo ya zamani na kisasa yanasema, “akajenga minara mirefu juu yake,” Hii ni juu ya ukuta.
2Maandishi ya kale yanasema hivi: badala ya “akawapa pumziko juu ya kila pande,” baadhi ya matoleo ya zamani na ya kisasa yanasema, “akawaongoza juu ya kila pande.”
3Maandishi ya kale yanasema hivi: Badala ya “miji” baadhi ya matoleo ya kisasa yanasema “punda,” na baadhi mengine ya kisasa yanaacha neno nzima.

33

1Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala, alitawala miaka hamsini na tano katika Yerusalemu.2Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama yalivyo mambo ya machukizo ya mataifa ambao Yahwe alikuwa amewafukuza mbele ya watu wa Israeli.3Kwa maana alizijenga tena sehemu za juu ambazo baba yake Hezekia alikuwa amezibomoa, na akajenga madhabahu kwa ajili ya mabaali, akatengeneza sanamu za Maashera, na akaziinamia chini nyota zote za mbinguni na kuziabudu.4Manase akajenga madhabahu za kipagani katika nyumba ya Yahwe, ingawa Yahwe alikuwa ameamuru, “Ni katikaYerusalemu ambapo jina langu litawekwa milele.”5Alijenga madhabahu kwa ajili ya nyota zote za mbinguni katika vile viwanja viwili vya nyumba ya Yahwe.6Katika bonde la Beni Hinomu akawaweka wanawe katika moto. Akafanya misemo ya ubashiri, na uchawi, akasoma utabiri; akashauriana na wale waliozungumza na wafu na pepo. Akafanya maovu mengi katika macho ya Yahwe na alimfanya Mungu akasirike.

7Ile sanamu ya Maashera aliyokuwa amefanya, akaiweka katika nyumba ya Mungu. Ni kuhusu nyumba hii ambayo Mungu alikuwa amesema kwa Daudi na Sulemani mwanaye; alikuwa amesema, “Ni katika nyumba hii na katika Yerusalemu, ambao nimeuchagua kutoka makabila yote ya Israeli, kwamba nitaliweka jina langu milele.8Sitawaondoa tena watu wa Israeli katika nchi hii ambayo niliitoa kwa baba zao, ikiwa tu watakuwa makini katika kuyashika yote niliyowaamuru, kuzishika sheria zangu, amri zangu, na sheria zangu nilizowapa kupitia Musa.”9Manase akawaongoza Yuda na wakaaji wa Yerusalemu hata kufanya uovu zaidi kuliko hata watu wa mataifa ambao Yahwe alikuwa amewateketeza mbele za Israeli.

10Yahwe akasema kwa Manase, na kwa watu wake wote, lakini hawakumsikiliza.11Kwa hivyo Yahwe akaleta juu yao maamri wa jeshi la Ashuru, ambao walimchukua Manase katika minyonyoro, wakamfunga kwa pingu, na wakampeleka Babeli.12Manase alipokuwa katika dhiki, alimuomba Yahwe, Mungu wake, na akajinyenyekesha sana mbele za Mungu wa baba zake.13Akaomba kwake; na Mungu akamsikiliza, na Mungu akasikia kuomba kwake na akamrudisha Yerusalemu, katika ufalme wake. Kisha Manase akafahamu kwamba Yahwe alikuwa Mungu.

14Baada ya hayo, Manase akajenga ukuta wa nje ya mji wa Daudi, upande wa magharibi wa Gihoni, katika bonde, hadi kwenye lango la Samaki. Akauzungushia mlima wa Ofeli na akaupandisha ukuta hadi usawa mrefu sana. Akaweka maamri jeshi jasiri katika ngome zote za miji ya Yuda.15Akaipeleka mbali miungu yote ya kigeni, akaondoa sanamu zote kwenye nyumba ya Yahwe, na madhabahu zote ambazo alikuwa amejenga juu ya mlima wa nyumba ya Yahwe na katika Yerusalemu, na kuvitupa nje ya mji.16Akaijenga tena madhabahu ya Yahwe na juu yake akatoa sadaka za amani na sadaka za shukrani; akamwamuru Yuda amtumikie Yahwe, Mungu wa Israeli.17Hata hivyo watu bado walitoa sadaka mahali pa sehemu za juu, lakini kwa Yahwe, Mungu wao peke yake

18Katika mambo mengine kuhusu Manase, maombi yake kwa Mungu wake, na maneno ya waonaji ambao walisema kwake katika jina la Yahwe, Mungu wa Israeli, tazama, yameandikwa miongoni mwa matendo ya wafalme wa Israeli.19Katika matukio hayo kuna historia ya maombi yake, na jinsi Mungu alivyoguswa na maombi hayo. Pia kuna kumbu kumbu ya dhambi zake zote na makosa yake, na sehemu ambako alikuwa amejenga sehemu za juu na kuzisimamisha Maashera na sanamu za kuchonga, kabla ya kujinyenyekeshamwenyewe -- na imeandikwa kuhusu hayo katika tarehe ya waonaji. 120Kwa hiyo Manase akalala na baba zake, na wakamzika katika nyumba yake mwenyewe. Amoni, mwaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

21Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; alitawala miaka miwili katika Yerusalemu.22Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe, kama Manase, baba yake, alivyofanya. Amoni alitoa sadaka kwa sanamu zote za kuchonga ambazo alitengeneza Manase baba yake, na aliziabudu.23Hakujinyenyekesha mbele za Yahwe, kama baba yake Manase alivyokuwa amefanya. Badala yake, Amoni alifanya makosa zaidi na zaidi.

24Watumishi wake wakapanga njama dhid yake na wakamuua katika nyumba yake mwenyewe.25Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya njama dhidi ya Mfalme Amoni, na wakamfanya Yosia, mwanaye, mfalme katika nafasi yake.


1Maandishi ya kale yanasema hivi, “tarehe ya Hozai,” ambayo ni maandishi ya kifungu asili. Lakini matoleo mengi ya kisasa yamesahihisha na kusomeka “tarehe ya waonaji. Pia, matoleo machache ya kisasa yanasema “tarehe ya waonaji.”

34

1Yosia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miaka thelathini na moja katika Yerusalemu.2Alifanya yaliyo haki katika macho ya Yahwe, na alitembea katika njia za Daudi baba yake, na hakugeuka mbali iwe kulia au kushoto.

3Kwa maana ndani ya miaka minane ya ya utawala wake, alipokuwa bado kijana, alianza kumtafuta Mungu wa Daudi, babu yake. Katika miaka ishirini, alianza kuisafisha Yuda na Yerusalemu kutoka sehemu za juu, vituo vya Maashera, na sanamu za kuchonga na sanamu za chuma ya kuyeyushwa.4Watu wakazivunja madhabahu za Baali katika uwepo wake; akazibomoa nguzo za Maashera na na zile sanamu za kuchonga, na sanamu za chuma ya kuyeyushwa katika vipande hadi zikawa mavumbi. Akayasambaza mavumbi juu ya makaburi ya wale ambao walizitolea sadaka.5Akaichoma mifupa ya makuhani wao juu ya madhabahu zao. Katika namna hii, akaisafisha Yuda na Yerusalemu.6Alifanya hivyo hivyo katika miji ya Manase, Efraimu, na Simeoni, sehemu zote hadi Neftali, na katika maeneo yaliyoizunguka.7Alizivunja madhabahu, akayapiga Maashera, na sanamu za kuchonga kuwa unga, na kuzisambaratisha madhabahu zote za uvumba katika nchi yote ya Israeli; kisha akarudi Yerusalemu.

8Sasa katika kipindi cha miaka ishirini ya utawala wake, baada ya Yosia kuisafisha nchi na hekalu, alimtuma Shafani mwana wa Azali, Manaseya, akida wa mji, na Yoa mwana wa Yoahazi katibu, kuikarabati nyumba ya Yahwe Mungu wake.

9Wakaenda kwa Hilkia, kuhani mkuu, nawakakabidhi kwake fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Mungu, ambazo Walawi, walinzi wa milingo, walikuwa wamekusanya kutoka Manase na Efraimu, kutoka kwa masalia wote wa Israeli, kutoka Yuda yote na Benjamini, na kutoka kwa wakaaji wa Yerusalemu.

10Wakaikabidhi zile fedha kwa watu waliosimamia kazi ya hekalu ya Yahwe. Watu wale wakawalipa watendakazi waliokarabati na kulijenga tena hekalu.11Wakawalipa maseremala na wajenzi kwa ajili ya kununua mawe ya kuchonga na mbao kwa ajili ya kuungia, na kutengeneza boriti za nyumba ambazo baadhi ya wafalme wa Yuda waliziacha zikachakaa.

12Watu walifanya kazi kwa uaminifu. Wasimamizi wao Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, kutoka kwa wana wa Wakohathi. Walawi wengine, wote kati ya wale waliokuwa wana mziki wazuri sana, kwa ukaribu waliwaelekeza watendakazi.13Walawi hawa walikuwa viongozi wa wale waliobeba vifaa vya ujenzi na watu wengine wote waliofanya kazi kwa namna yoyote ile. Pia palikuwa na Walawi ambao walikuwa makatibu, watawala na walinda lango.

14Walipozileta fedha ambazo zilikuwa zimeletwa kwenye nyumba ya Yahwe, Hilikia yule kuhani alikipata kitabu cha sheria ya Yahwe ambacho kilikuwa kimetolewa kupitia Musa.15Hilikia akamwambia Shafani yule mwandishi, “Nimekipata kitabu cha sheria katika nyumba ya Yahwe.” Hilikia akakileta kitabu kwa Shefani.

16Shefani akakipeleka kitabu kwa mfalme, na pia akatoa taarifa kwake, akisema, “Watumishi wako wanafanya kila kitu walichokabidhiwa.17Walizitoa fedha zote ambazo zilipatikana katika nyumba ya Yahwe, na walizikabidhi katika mikono ya wasimamizi na watendakazi.”18Shefani mwandishi akamwambia mfalme.” Hilikia kuhani amenipa kitabu.” Kisha Shefani akamsomea mfalme katika hicho kitabu.

19Ikawa kwamba mfalme alipokuwa ameyasikia maneno ya sheria, aliyararua mavazi yake.20Mfalme akamwamuru Hilikia, Ahikamu mwana wa Shafani, Abdoni mwana wa Mika, Shafani mwandishi, na Asaya, mtumishi wake, akisema,21“Nendeni mkaulize mapenzi ya Yahwe kwa ajili yangu, na kwa wale waliobaki katika Israeli na Yuda, kwa sababu ya maneno ya kitabu ambacho kimeokotwa. Kwa maana ni kuu, ghadhabu zake Yahwe zilizomiminwa kwetu kwa sababu baba zetu hawakuyasikiliza maneno ya kitabu hiki ili kuyatii yote yaliyokuwa yameandikwa ndani yake.” 1

22Kwa hiyo Hilkia, na wale ambao mfalme alikuwa amewaamuru, wakaenda kwa Hulda nabii wa kike, mke wa Shalumu mwana wa Tohathi mwana wa Hasra, mtunza mavazi (aliishi katika Yerusalemu katika wilaya ya pili), na walizungumza naye katika namna hii.

23Akasema kwao, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Israeli, anasema: Mwambie mtu aliyewatuma kwangu,24Hivi ndivyo Yahwe anasema: Ona, niko karibu kuleta maafa juu ya sehemu hii na wakaaji wake, laana zote zilizoandikwa katika kitabu walichokisoma mbele ya mfalme wa Yuda.25Kwa sababu wamenisahau na wametoa sadaka za uvumba kwa miungu mingine, ili kwamba waniweke katika hasira kwa matendo yote waliyofanya -- kwa hiyo hasira yangu itamiminwa juu ya hii sehemu, na haitazimwa. (Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu,” baadhi ya matoleo yana “amabyo yamemlikwa dhid yetu.”)26Lakini kwa mfalme wa Yuda, aliyewatuma kumuuliza Yahwe alichopaswa kufanya, hivi ndivyo mtakavyosema kwake, ‘Yahwe, Mungu wa Israeli anasema hivi: Kuhusu maneno uliyosikia,27kwa sababu moyo wako ulipondeka, na ulijinyenyekeza mbele zangu ulipoyasikia maneno yake dhidi ya sehemu hii na wakaaji wake, na kwa sababu umejinyenyekeza mwenyewe mbele zangu, na umeyararua mavazi yako na kulia mbele zangu, nami pia nimekusikiliza —hili ni azimio la Yahwe28Ona nitakukusanya kwa mababa zako. Utakusanywa katika kaburi lako kwa amani, na macho yako hayataona maafa yoyote nitakayoleta juu ya sehemu hii na wakaaji wake.” Wale watu wakarudisha ujumbe huu kwa mfalme.29Mfalme akatuma wajumbe na kuwakusanya wazee wote wa Yuda na Yerusalemu.30Kisha mfalme akaenda kwenye nyumba ya Yahwe, na watu wote wa Yuda wakaaji wa Yerusalemu, na makuhani, Walawi, na watu wote, kuanzia wakubwa hadi wadogo. Kisha akasoma mbele zao maneno yote ya kitabu cha Agano kilichokuwa kimepatikana katika nyumba ya Yahwe.

31Mfalme akasimama katika sehemu yake na kufanya agano mbele za Yahwe, kutembea mbele za Yahwe, na kuzishika amri zake, taratibu zake, na sheria zake, kwa moyo wake wote na roho yake yote, kuyatii maneno ya agano yaliyokuwa yameandikwa katika kitabu hiki.

32Aliwasababisha wote walioonekana katika Yerusalemu na Benjamini kusimama kwa agano. Wakaaji wa Yerusalemu wakatembea kwa agano la Mungu, Mungu wa baba zao.

33Yosia akapeleka mbali mambo yote ya machukizo kutoka kwenye nchi iliyomilikiwa na watu wa Israeli. Akamfanya kila mtu katika Israeli amwabudu Yahwe, Mungu wao. Kwa maisha ya siku zake zote, hawakugeuka mbali kwa kutomfuata Yahwe, Mungu wa mababa zao.


1Badala ya “ambayo yamemiminwa juu yetu,” baadhi ya matoleo yanasema, “ambayo yamemulikwa dhidi yetu.”

35

1Yosia alisherehekea Pasaka kwa ajili ya Yahwe katika Yerusalemu, na wakachinja wanakondoo katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza.2Akawaweka makuhan katika nafasi zao na akawatia moyo katika huduma za nyumba ya Yahwe.3Akasema kwa Walawi waliowafundisha Israeli wote na waliokuwa wamewekwa wakfu kwa Yahwe, “Liwekeni sanduku takatifu katika nyumba ambayo Sulemani mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli aliijenga. Hamtakuwa na mzigo tena mabegani mwenu. Sasa mwabuduni Yahwe Mungu wenu, na watumikieni watu wake Israeli.4Jikusanyeni wenyewe kwa majina ya nyumba za baba zenu na zamu zenu, mkifuata maelekezo ya Daudi, mfalme wa Israeli, na yale ya Sulemani, mwanaye.

5Simameni katika sehemu takatifu, mkichukua nafasi zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababa wa ndugu zenu, uzao wa watu, na mchukue sehemu zenu kwa zamu zenu ndani ya nyumba za mababu wa Walawi.6Chinjeni wana kondoo wa Pasaka, jitakaseni wenyewe, andaeni wana kondoo kwa ajili ya ndugu zenu, kufanya sawa sawa na neno la Yahwe ambalo lilitolewa kwa mkono wa Musa.”

7Yosia akawapa watu wote wana kondoo elfu thelathini na wana mbuzi kutoka katika makundi kwa ajili ya sadaka za Pasaka kwa wote waliokuwepo, na akatoa ng'ombe dume elfu tatu; hawa walikuwa kutoka katika mali ya mfalme.

8Viongozi wake wakatoa sadaka za hiari kwa watu, makuhani, na Walawi. Hilikia, Zekaria, na Yeieli, viongozi wasimamizi wa nyumba ya Mungu, wakawapa makuhani ndama 2,600 na ng'ombe mia tatu kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.9Pia Konania, Shemaya na Nethaneli, ndugu zake, na Hashabia, Yeieli, na Yazabadi, mkuu wa Walawi, akawapa Walawi wana-kondoo elfu tano na fahali mia tano kwa ajili ya matoleo ya Pasaka.

10Kwa hiyo huduma iliandaliwa, na makuhani wakasimama katika sehemu zao, pamoja na Walawi kwa zamu zao, kwa mujibu wa agizo la mfalme.11Wakawachinja wana kondoo wa Pasaka, na makuhani wakainyunyiza damu waliyoipokea kutoka kwenye mikono ya Walawi, na Walawi wakawachuna wana kondoo.12Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, ili kuzisambaza katika makundi ya nyumba za mababa wa watu, ili wamtolee Yahwe, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Musa. Wakafanya vile vile kwa wale ng'ombe dume.13Wakawaoka kwa moto wanakondoo wa Pasaka wakifuata maelekezo, kuhusu sadaka takatifu, walizichemsha kwenye vyungu, masufuria na makaangoni, na haraka wakayapeleka kwa watu.14Baadaye waliandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, kwa sababu makuhani, uzao wa Haruni, walikuwa wametengwa katika kazi ya kutoa sadaka za kuteketezwa na za mafuta hadi usiku ulipoingia, kwa hiyo Walawi wakaandaa sadaka kwa ajili yao wenyewe na kwa ajili ya makuhani, wana wa Haruni.

15Waimbaji, wana wa Asafu, walikuwa katika nafasi zao, kama ilivyoagizwa na Daudi, Asafu, Hemani, na Yeduthuni, mwonaji wa mfalme, na walinzi walikuwa katika kila lango. Hawakutakiwa kuziacha huduma zao, kwa sababu ndugu zao Walawi walifanya maandalizikwa ajili yao.

16Kwa hiyo, wakati huo huduma yote ya Yahwe ilifanyika kwa ajili ya kusherehekea Pasaka na kutoa sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Yahwe, Kama alivyoamuru mfalme Yosia.17Watu wa Israeli ambao walikuwepo wakaifanya Pasaka wakati huo, na kisha Sikukuu ya Mikate isiyochachwa kwa siku saba.18Pasaka kama hiyo haijafanyika tena katikaIsraeli tangu siku za nabii Samweli, wala hakuna mfalme yeyote miongoni mwa wafalme wa Israeli ambaye amewahi kusherekea Pasaka kama Yosia alivyofanya, pamoja na makuhani, Walawi, na watu wote wa Yuda na Israeli waliokuwepo, na wakaaji wote wa Yerusalemu.19Pasaka hii ilitunzwa ndani ya miaka kumi na minane ya utawala wa Yosia.

20Baada ya haya yote, baada ya Yosia kuliweka hekalu katika utaratibu, Neko, mfalme wa Misiri, akaenda juu kupigana dhidi ya Karkemist karibu na mto Frati, na Yosia akaenda kupigana juu yake.21Lakini Niko akatuma wajumbe kwake, akisema, “Nikufanye nini, mfalme wa Yuda? Leo siji kinyume nawe, lakini dhidi ya nyumba ambayo nafanya vita nayo. Mungu ameniamuru kuharakisha, kwa hivyo acha kumwingilia Mungu, ambaye yuko pamoja nami, la sivyo atakuangamiza.”

22Hata hivyo, Yosia alipuuza kurudi nyuma. Akajibadilisha ili apigane naye. Hakusikiliza maneno ya Neko ambayo yalikuja kutoka kwenye kinywa cha Mungu; hivyo akaenda kupigana katika bonde la Megido.

23Wapiga upinde wakampiga Mfalme Yosia, na mfalme akawaambia watumishi wake, “Niondoeni hapa, kwa maana nimejeruhiwa vibaya.”24Kwa hiyo watumishi wake wakamtoa nje ya gari, na kumuweka katika gari lake la tahadhari. Wakampeleka Yerusalemu, ambako alikufa. Alizikwa katika makaburi ya baba zake. Yuda wote na Yerusalemu wakamwomboleza.

25Yeremia akamwomboleza Yosia; waimbaji wote wa kiume na wa kike wakaomboleza kuhusu Yosia hata leo. Nyimbo hizi zikawa desturi katika Israeli; tazama, zimeandikwa katika nyimbo za maombolezo.

26Kwa mambo mengine kuhusu Yosia, na matendo yake mema aliyoyafanya katika kuti kile kilichoandikwa katika sheria ya Yahwe—27na matendo yake, kutoka mwanzo hadi mwisho, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli.

36

1Kisha watu wa nchi wakamchukua Yehoazi mwana wa Yosia, na wakamfanya mfalme katika nafasi ya baba yake katika Yerusalemu.

2Yehoazi alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitatu alipoanza kutawala, na akatawala miezi mitatu katita Yerusalemu.3Mfalme wa Misiri akamwondoa katika Yerusalemu, na akamlazimisha kutoa faini kwa nchi ya talanta za fedha mia moja na talanta moja ya dhahabu.4Mfalme wa Misiri akamfanya Eliakimu, ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu, na akambadilisha jina lake kuwa Yehoakimu. Kisha Neko akamchukua ndugu yake Eliakimu - Yeahazi na kumpeleka Misiri.

5Yehoakimu alikuwa na umri wa miaka ishirini na tano alipoanza kutawala, na akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe Mungu wake.6KishaNebukadreza, mfalme wa Babeli, akamvamia na kumfunga katika minyororo kumuongoza kwenda mbali Babeli.7Nebukadreza pia akabeba baadhi ya vitu katika nyumba ya Yahwe kwenda Babeli, na akaviweka katika ikulu yake huko Babeli.

8Kwa mambo mengine kuhusu Yehoyakimu, mambo mabaya aliyofanya, na yaliyopatikana dhidi yake, tazama, yameandikwa katika kitabu cha wafalme wa Yuda na Israeli. Basi Yekonia, mwanaye, akawa mfalme katika nafasi yake.

9Yekonia alikuwa na umri wa miaka minane alipoanza kutawala; alitawala miezi mitatu na siku kumi katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu katika macho ya Yahwe.10Katika kipindi cha mwisho cha mwaka, mfalme Nebukadreza akatuma watu na wakampeleka Babeli, pamoja vitu vya thamani kutoka katika nyumba ya Yahwe, na kumfanya Sedekia ndugu yake, mfalme juu ya Yuda na Yerusalemu.

11Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na moja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na moja katika Yerusalemu. Akafanya yaliyokuwa maovu machoni mwa Yahwe Mungu wake.12Hakujinyenyekesha mwenyewe mbele za Yeremia nabii, ambaye alisema kutoka kinywani mwa Yahwe.13Sedekia pia akaasi dhidi ya Mfalme Nebukadreza, ambaye alikuwa amemfanya aape uaminifu kwake kupitia Mungu. Lakini Sedekia aliishupaza shingo yake na kuufanya moyo wake mgumu usigeuke kwa Yahwe, Mungu wa Israeli.14Vilevile, viongozi wote wa makuhani na watu hawakuwa waaminifu, na waliufuata uovu wa mataiafa. Wakainajisi nyumba ya Yahwe ambayo alikuwa ameitakasa katika Yerusalemu.

15Yahwe, Mungu wa baba zao, akatuma maneno kwao tena na tena kupitia wajumbe wake, kwa sababu alikuwa na huruma juu ya watu wake na juu ya sehemu anayoishi.16Lakini waliwadhihaki wajumbe wa Mungu, wakayadharau maneno yake, na kuwacheka manabii wake, hadi hasira ya Yahwe ilipoinuka dhidi ya watu wake, hadi pasiwepo na msaada.17Hivyo Mungu aliwapeleka juu yao mfalme wa Wakaldayo, ambaye aliwaua vijana wao kwa upanga nyumbani patakatifu, na hakuwa na huruma juu ya vijana au mabikra, watu wazee au wenye mvi. Mungu akawatoa wote mikononi mwake.18Vyombo vyote vya nyumba ya Mungu, vikubwa na vidogo, hazina za nyumba ya Yahwe, na hazina za mfalme na watumishi wake—vyote hivi akavipeleka Babeli.19Wakaichoma moto nyumba ya Mungu, wakauangusha chini ukuta wa Yerusalemu, wakachoma ikulu zake zote, na wakaviaribu vitu vizuri vyote ndani yake.

20Mfalme akawapeleka mbali Babeli wale waliokuwa wameoka na upanga. Wakawa watumishi wake pamoja na wanawe hadi utawala wa Waajemi.21Hili lilitokea ili kulitimiza neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia, hadi nchi itakapokuwa imefurahia mapumziko ya Sabato yake. Iliishika Sabato kwa muda mrefu hadi kukataliwa kwake, ili miaka sabini itimie katika namna hii.

22Sasa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalme wa Uajemi, ili kwamba neno la Yahwe kwa kinywa cha Yeremia liweze kutimizwa, Yahwe akaipa hamasa roho yaKoreshi, mfalme wa Uajemi, kwamba akafanya tangazo katika ufalme wake wote, na akaliweka pia katika maandishi. Akasema,

23“Hivi ndivyo Koreshi, mfalme wa Uajemi, anasema: Yahwe, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia. Ameniagiza nijenge nyumba kwa ajili yake katika Yerusalemu, ambayo ipo Yuda. Yeyote aliye miongoni mwenu kutoka katika watu wake wote, Yahwe Mungu wenu, awe naye. Akwee kwenye ile nchi.”

Ezra

Nehemiah

Esther

Job

Psalms

Proverbs

Mhubiri

1

1Haya ni maneno ya Mwalimu, mwana wa Daudi na mfalme katika Yerusalemu.

2Mwalimu asema hivi, “Kama mvuke wa ukungu, kama upepo mwanana katika upepo, kila kitu hutoweka na kuacha maswali mengi.
3Ni faida gani wanadamu huipata kutoka katika kazi zote wazifanyazo chini ya jua?
4Kizazi kimoja huenda, na kizazi kingine huja, lakini dunia yabaki milele.
5Jua huchomoza na jua huzama na kwenda kwa haraka, na kurudi mahali linapochomozea tena.
6Upepo huvuma kusini na huzunguka kaskazini, na mara zote huzunguka katika njia yake na kurudi tena.
7Mito yote hutiririka maji yake i baharini, lakini bahari haijai. Mahali mito inakoenda, ndiko inakoenda tena.
8Kila kitu huwa uchovu, na hakuna yeyote awezae kukielezea. Jicho halishibi na kile linachokiona, wala sikio haliridhiki na kile linachosikia.
9Chochote kilichopo ndicho kitakachokuwepo, kila kilichofanyika ndicho kitakachofanyika. Hakuna jipya chini jua.
10Je kuna jambo lolote ambalo watu wanaweza kusema, ‘Tazama, hili ni jipya’? Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo muda mwingi, wakati uliokuwepo kabla yetu.
11Hakuna anayeonekana kukumbuka kilichotokea nyakati za zamani. Na mambo yaliyo tokea siku zilizo pita na yale yatakayo tokea siku za mbele nayo hayatakumbukwa.”

12Mimi ni mwalimu, na nimekuwa mfalme juu ya Isareli katika Yerusalemu.13Nilitia akili yangu katika kusoma na kutafuta kwa hekima kila kitu kinachofanywa chini ya mbingu. Hili nalo ni jukumu zito ambalo Mungu amewapa wanadamu kujishughulisha nalo.14Nimeona matendo yote ambayo yanafanyika chini ya dunia, na tazama yote ni mvuke ni kujaribu kuuchunga upepo.
15Palipopinda hapawezi kunyoshwa! Kisicho kuwepo hakiwezi kuhesabiwa!

16Nimeuambia moyo wangu nikisema, “Tazama, nimepata hekima kubwa kuliko walioishi Yerusalemu kabla yangu. Akili yangu imeona hekima kubwa na ufahamu.”17Nilitia moyo wangu kujua hekima na upumbuvu na ujinga. Nikagundua kuwa hili nalo pia lilikuwa ni kujaribu kuuchunga upepo.18Kwa kuwa katika wingi wa hekima kuna masumbufu mengi, naye aongezae ujuzi, aongeza masikitiko.

2

1Nikauambia moyo wangu, “Njoo, na nitakujaribu kwa furaha. Kwa hiyo furahia.” Lakini tazama, huu nao ulikuwa ni upepo wa muda.2Nikasema juu ya kicheko, “Ni wazimu,” na kuhusu furaha, “Yafaa nini?”3Nikajipeleleza moyoni mwangu katika jinsi ya kutimiza hamu yangu kwa mvinyo. Nikaruhusu akili yangu iongozwe na hekima ingawa bado nilikuwa nikishikilia ujinga. Nilitaka kutafuta jambo lililo jema kwa wanadamu kufanya chini ya mbingu wakati wa siku za maisha yao.4Nilitimiza mambo makubwa. Nilijenga nyumba kwa ajili yangu na kupanda miti ya mizabibu.5Nilitengeneza bustani na viwanja; nikapanda aina zote za matunda ndani yake.6Nikatengeneza mabwawa ya maji ili kumwagilia msitu mahali miti ilikuwa imepandwa.7Nilinunua watumwa wa kiume na wa kiume; nilikuwa na watumwa waliozaliwa katika ikulu yangu. Pia nikawa na makundi makubwa na wanyama wa kufugwa, zaidi ya mfalme yeyote aliyetawala kabla yangu katika Yerusalemu.8Pia nilijikusanyia fedha na dhahabu, hazina ya wafalme na majimbo. Nikapata waimbaji wanaume na wanawake kwa ajili yangu, na kufurahia kutoka kwa wana wa wanadamu, masulia na wanawake.9Hivyo nikawa mkuu na tajiri kuliko wote waliokuwa Yerusalemu kabla yangu, na hekima yangu ilikuwa ndani yangu.

10Lolote ambalo macho yangu yalikitamani sikuyazuia. Sikuuzuia moyo wangu katika furaha yeyote, kwa sababu moyo wangu ulifurahi katika katka kazi yangu zote na furaha ilikuwa ni tunu kwa kazi zangu zote.
11Kisha nikatazama matendo yote ambayo mikono yangu iliyokwisha kuyatimiliza na juu ya kazi niliyokuwa nimeifanya, lakini tena, kila kitu kilikuwa ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo. Hakukuwa na faida chini ya jua.
12Kisha nikageuka kuitafakari hekima, na upumbavu na ujinga. Kwa maana ni kitu gani mfalme anayekuja baada yangu afanye, ambacho hakijafanyika?
13Kisha nikaanza kuelewa kwamba hekima ina faida kuliko upumbavu, kama nuru ilivyo bora kuliko giza.
14Mwenye hekima hutumia macho yake katika kichwa chake kuona mahali anakoenda, lakini mpumbavu hutembea katika giza, ingawa ninafahamu kuwa mwisho wa aina moja umetunzwa kwa kila mmoja.

15Kisha nikasema moyoni mwangu, “Kinachotokea kwa mpumbavu, ndicho kitachotokea na kwangu. Hivyo kuna utofauti gani kama mimi ni mwenye hekima sana?” Nikahitimisha moyoni mwangu, “Huu pia ni mvuke tu.”
16Kwa kuwa mwenye hekima, kama mpumbavu, hakumbukwi kwa muda mrefu. Katika siku zijazo, kila kitu kitakuwa kimesahauliwa. Mwenye hekima hufa kama navyokufa mpumbavu.

17Hivyo nikauchukia uhai kwa sababu kazi zote zilizofanyika chini ya jua zilikuwa mbaya kwangu. Hii ni kwa sababu kila kitu ni mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.

18Nikachukia yote niliyoyatimiza, ambayo nilikuwa nimekwisha yafanya chini ya jua kwa sababu ni lazima niyaache kwa mtu anaye kuja baada yangu.19Na ni nani ajuaye kama atakuwa mwenye hekima au mpumbavu? Ila atakuwa mtawala juu ya kila kitu chini ya jua ambayo kazi yangu na hekima yangu imeyajenga. Huu pia ni mvuke.20Kwa hiyo moyo wangu ukaanza kukata tamaa juu ya kazi zote nilizozifanya chini ya jua.21Kwa kuwa kunaweza kuwa na mtu anayefanya kazi kwa hekima, ufahamu, naumahili, lakini ataacha kila kitu alichonacho kwa mtu ambaye hajafanya chochote. Huu nao ni mvuke na hatari kubwa.22Kwa maana ni faida gani mtu hupata ambaye hufanya kazi kwa juhudi na kujaribu moyoni mwake kutimiza kazi zake chini ya jua?23Kila siku kazi yake ni maumivu na masikitiko, hivyo wakati wa usiku roho yake haipumziki. Huu pia ni mvuke.

24Hakuna jambo jema kwa mtu yeyote zaidi ya kula na kunywa na kuridhika na kile kilichochema katika kazi yake. Nikaona kwamba ukweli huu unatoka kutoka mkononi mwa Mungu.25Kwa kuwa ni nani anaweza kula au anaweza kupata furaha yoyote tofauti na Mungu?26Kwa kuwa kwa kila anayemfurahisha yeye, Mungu humpa hekimana ufahamu ba furaha. Ingawa, kwa mwenye dhambi humpa kazi ya kukusanya na kutunza ili kwamba ampe mtu anayempendeza Mungu. Huu pia ni sawa na mvuke na kujaribu kuuchunga upepo.

3

1Kwa kuwa kila kitu na wakati wake, na majira kwa kila kusudi chini ya mbingu.

2Kuna wakati wa kuzaliwa na wakati wa kufa, wakati wa kupanda na wakati wa kung'oa yaliyopandwa,
3Wakati wa kuua na wakati wa kuponya, wakati wa kubomoa na wakati wa kujenga.
4Kuna wakati wa kulia na wakati wa kucheka, wakati wa kuomboleza na wakati kucheza,
5Wakati wa kutupa mawe na wakati wa kukusanya mawe, wakati wa kukumbatia watu wengine wakati wa kutokumbatia.
6Kuna wakati wa kutafuta vitu na wakati wa kutotafuta, wakati wa kutunza vitu na wakati wa kuvitupa,
7Wakati wa kuchana mavazi na wakati wa kuyashona, wakati wa kunyamaza na wakati wa kuzungumza.
8Kuna wakati wa kupenda na wakati wa kuchukia, wakati wa vita na wakati wa amani.

9Ni faida gani mfanyakazi aipatayo katika kazi yake?10Nimeona kazi ambayo Mungu amewapa wanadamu kuitimiza.11Mungu amefanya kila kitu kuwa kizuri kwa wakati wake. Pia ameweka umilele ndani ya mioyo yao. Lakini mwanadamu hawezi kuelewa matendo ambayo Mungu ameyafanya, tangu mwanzo wao hadi mwisho.12Ninajua kuwa hakuna kilicho bora kwa mtu yeyote kuliko kufurahi na kutenda mema maadamu anaishi-13Na kwamba kila mmoja anapaswa ale na kunywa na anapaswa kuelewa jinsi ya kufurahia mazuri ambayo yanatoka katika kazi zake zote. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.14Ninajua kwamba chochote afanyacho Mungu kinadumu milele. Hakuna kinaweza kuongezwa au kuondolea, kwa sababu Mungu ndiye aliyekifanya, ili kwamba watu wamsogelee kwa heshima.
15Chochote kilichopo kimekwisha kuwepo; chochote kitakachokuwepo kimekwisha kuwepo. Mungu huwafanya wanadamu kutafuta vitu vilivyjificha.

16Na nimeona kwamba chini ya jua ubaya upo mahali palipopaswa kuwa na haki, na sehemu ya haki mara nyingi ina ubaya.

17Nikajiambia moyoni mwangu, “Mungu atahukumu mwenye haki na mbaya kwa wakati muafaka kwa kila jambo na kila tendo.

18Nikasema moyoni mwangu, “Mungu huwajaribu wanadamu kuwaonyesha kwamba wao ni kama wanyama.”19Kwa kuwa mwisho watoto wa wanadamu na mwisho wa wanyama ni sawa. Kifo cha mmoja ni sawa na kifo cha mwingine. Wote wana pumzi sawa. Hakuna faida kwa mwanadamu zaidi ya wanyama. Kwa kuwa hakuna kila kitu isipokuwa pumzi?20Kila kitu kinaenda sehemu moja. Kila kitu kinatoka mavumbini, na kila kitu kinarudi katika mavumbini.21Ni nani ajuaye kama roho ya mwanadamu inaenda juu na roho ya wanyama inaenda chini?

22Kwa hiyo tena nikatambua kwamba hakuna lililo jema kwa yeyote zaidi ya kufurahia kazi yake, kwa kuwa hilo ndilo jukumu lake. Ni nani awezaye kumleta tena kuona kinachotokea baada yake?

4

1Kisha tena nikafikiri kuhusu mateso yote yaliyo chii ya jua. Tazama machozi ya watu walioteswa. Hakuna anaye mfariji kwa ajili yao. Nguvu iko katika mikononi mwa watesaji, lakini wateswaji hawana mfariji.

2Hivyo nikawapongeza watu walio kufa, wale ambao tayari wamekufa, sio wanaoishi, wale ambao wako hai.
3Ingawa, bahati zaidi kuliko wote wawili ni yule ambaye hajaishi, yeye ambaye hajaona matendo yoyote mabaya ambayo yanafanyika chini ya jua.

4Kisha, nikaona kwamba kila tendo la kazi na kila kazi ya ujuzi wa mtu ni wivu wa jirani. Huu pia ni ubatili na mvuke na kujaribu kuushika upepo.
5Mpumbavu hukunja mikono yake na hafanyi kazi, hivyo chakula chake ni mwili wake.
6Lakini afadhali konzi ya faida pamoja na kazi ya haraka kuliko konzi mbili pamoja na kazi ambayo hujaribu kuushika upepo.

7Kisha nikarudi nikafikiria tena kuhusu ubatili chini ya jua:
8Kuna aina ya mtu ambaye yuko peke yake. Hana mtu, hana mwana, wala ndugu. Hakuna mwisho wa kazi zake zote, na macho yake hayaridhiki kwa kupata utajiri. Anashangaa, “Nina jihangaisha na kuharibu furaha yangu kwa ajili ya nani?” Huu pia ni ubatili na hali mbaya.
9Watu wawili wanafanya vizuri zaidi ya mmoja; kwa pamoja wanaweza kupata malipo mazuri kwa ajili ya kazi yao.
10Kwa kuwa kama mmoja akianguka, mwingine anaweza kumwinua rafiki yake. Ingawa, huzuni humfuata yeye aliye peke yake anapoanguka kama hakuna mtu wa kumwinua.
11Na kama wawili wakilala pamoja, wanaweza kupata joto, lakini mtu mmoja anawezaje kupata joto akiwa mwenyewe?
12Mtu akiwa peke yake anaweza kushindwa nguvu, lakini wawili wanaweza kusimama katika shambulio Na kamba ya nyuzi tatu haikatika upesi.

13Ni bora kuwa kijana masikini kuliko kuwa mfalme mzee na mpumbavu ambaye hajui jinsi ya kusikiliza maonyo.14Hii ni kweli hata kama mtu mdogo anapokuwa mfalme kutoka gerezani, au hata kama alizaliwa maskini katika ufalme wake.15Ingawa, niliona kila mmoja aliye kuwa hai na kuzunguka chini ya jua: aliyekua na kijana wa pili aliyejiinua kama mfalme. Aliyejiinua16Hakuna mwisho kwa watu wote wanaotaka kumtii mfalme mpya, lakini wengi wao hawatamsifu yeye. Hakika hali hii ni ubatili na kujaribu kuushika upepo.

5

1Linda mwenendo wako unapoenda kwenye nyumba ya Mungu. Nenda kule usikilize. Kusikiliza ni bora kuliko wapumbavu wanapotoa dhabihu wakati hawajui kuwa wanachofanya katika maisha ni kibaya.

2Usiwe mwepesi wa kuongea kwa mdomo wako, na usiufanye moyo wako kuleta jambo lolote kwa haraka mbele za Mungu. Mungu yuko mbinguni, lakini uko duniani, kwa hiyo maneno yako yawe machache.
3Kama una mambo mengi ya kufanya na kuhangaika, pengine utapata ndoto mbaya. Na pengine utaongea maneno mengi ya upumbavu.

4Ukiweka nadhiri kwa Mungu, usichelewe kuifanya, kwa kuwa Mungu hafurahii upumbavu. Fanya kile ulichoapa utakifanya.5Ni bora kutokuweka nadhiri kuliko kuweka nadhiri ambayo usiyoiondoa.6Usiuruhusu mdomo wako kusababisha mwili wako kutenda dhambi. Usiseme kwa mtumwa wa kuhani, “Kile kiapo kilikuwa kwa makosa.” Kwani nini kumfanya Mungu akasirike kwa kuapa kwa uongo, kumchochea Mungu aharibu kazi ya mikono yako?7Kwa kuwa katika ndoto nyingi, kama ilivyo katika maneno mengi, kuna ubatili. Hivyo mwogope Mungu.

8Unapomwona maskini akiteswa na kunyang'anywa haki na kutendewa vibaya katika jimbo lako, usishangae kama kwamba hakuna anaye fahamu, kwa sababu kuna watu katika mamlaka ambao hutazama, kuna hata walio juu yao.9Kwa nyongeza uzalishaji wa ardhi ni kwa kila mmoja, na mfalme mwenyewe huchukua uzalishaji kutoka mashambani.
10Yeyote apendaye fedha hatatosheka na fedha, na yeyote apendaye utajiri mara zote hutaka zaidi. Huu pia ni ubatili.
11Kadri mafanikio yanapoongezeka, ndivyo wanavyoongezeka watu wanaotumia. Kuna faida gani katika utajiri kwa mmiliki isipokuwa kuutazama kwa macho yake?
12Usingizi wa mfanyakazi ni mtamu, kama anakula kidogo au sana, lakini utajiri wa mtu tajiri haumuruhusu yeye kulala vizuri.

13Kuna jambo baya zaidi ambalo nimeliona chini ya jua: mali iliyowekwa akiba na mwenye nayo, inamsababishia taabu mwenyewe.
14Wakati tajiri anapopoteza utajiri wake kwa bahati mbaya, mwana wake, ambaye amemzaa, habakiziwi chochote mikononi mwake.
15Kama mtu azaliwavyo uchi kutoka tumboni mwa mamaye, vivyo hivyo ataondoka katika maisha haya akiwa uchi. Hachukui chochote kutoka katika kazi yake.

16Jambo jingine baya kabisa, kama mtu alivyo kuja ni lazima aende vivyo hivyo. Hivyo ni faida gani mtu yeyote aipatayo katika kufanya kwa ajili ya upepo?
17Wakati wa siku zake anakula gizani na anafedheheshwa sana na magonjwa na hasira.

18Tazama, kile nilichokiona kuwa kizuri na kufaa ni kula na knywa na kufurahia faida kutoka katika kazi zetu zote, tuzifanyazo chini ya jua wakati wa siku za maisha haya ambayo Mungu ametupa. Kwa kuwa huu ni wajibu wa mtu.19Yeyote ambaye Mungu amempa vitu na pesa na uwezo wa kupokea sehemu yake na kufurahi katika kazi yake hii ni zawadi kutoka kwa Mungu.20Kwa kuwa mara kadhaa hakumbuki siku za maisha yake, kwa sababu Mungu anamfanya kuhangaika na mambo ambayo anafurahia kuyafanya.

6

1Kuna ubaya ambao nimeuona chini ya jua, na ni mbaya kwa watu.2Mungu anaweza kumpa mtu mali na utajiri na heshima kwa kiasi kwamba hakosi chochote anachokitamani mwenyewe, lakini kisha hampi uwezo wa kukifurahia. Badala yake mtu mwingine hutumia vitu vyake. Huu ni ubatili, teso baya.

3Kama mtu akizaa watoto mia moja na kuishi miaka mingi, ili kwamba siku za miaka yake ni nyingi, lakini kama moyo wake hautosheki kwa mema na hazikwi kwa heshima, kisha ninasema kwamba, mtoto aliyezaliwa akiwa amekufa ni bora kuliko alivyo.4Hata mtoto huyo amezaliwa bila faida na anapita katika njia mbaya, na jina lake halitambuliki.5Ingawa mtoto huyu haoni jua au kujua kitu chochote, ana pumziko ingawa mtu huyo hakupumzika.6Hata kama mtu akiishi miaka elfu mbili lakini hajifunzi kufuraia vitu vizuri, aenda sehemu moja kama mtu yeyote yule.
7Ingawa kazi yote ya mtu ni kujaza mdomo wake, ila hamu yake haishibi.
8Hakika ni faida gani aliyo nayo mwenye hekima kuliko mpumbavu? Ni faida gani aliyo nayo maskini hata kama anajua jinsi ya kutenda mbele ya watu?
9Ni bora kuridhika na kile ambacho macho hukiona kuliko kutamani kile ambacho hamu isiyo tulia inatamani, ambayo pia ni ubatili na kujaribu kuushika upepo.
10Chochote ambacho kimekuwepo, tayari kimekwisha kupewa jina lake, na vile mtu alivyo ni kama tayari amekwisha fahamika. Hivyo imekuwa haifai kugombana na yule ambaye ni muhukumu mkuu wa wote.
11Maneno mengi ambayo yanaongelewa, ndivyo yasiyo na maana yanaongezeka, kwa hiyo ni faida gani iliyopo kwa mwanadamu?

12Kwa kuwa ni nani ajuaye nini kilicho kizuri kwa mtu katika maisha yake wakati wa ubatili wake, siku zilizo hesabika ambazo kwa hizo anapita kama kivuli? Ni nina anayeweza kumwambia mtu kile kitakacho kuja chini ya jua baada ya kupita?

7

1Jina zuri ni bora kuliko manukato ya gharama, na siku ya kufa ni bora kuliko siku ya kuzaliwa.

2Ni bora kwenda kwenye nyumba ya maombolezo kuliko nyumba ya karamu, kwa kuwa maombolezo huja kwa watu wote wakati wa mwisho wa uhai, kwa hiyo watu wanaoishi ni lazima waweke hili moyoni.
3Huzuni ni bora kuliko kicheko, kwa kuwa baada ya uso wa huzuni huja furaha ya moyo.
4Moyo wa mwenye hekima uko katika nyumba ya maombolezo, lakini moyo wa wapumbavu uko katika nyumba ya karamu.
5Ni bora kusikiliza maonyo ya mtu mwenye hekima kuliko kusikiliza wimbo wa wapumbavu.
6Kwa kuwa kama mlio wa miiba chini ya chungu, ndivyo kilivyo kicheko cha wapumbavu. Huu pia ni mvuke.
7Kweli jeuri humfanya mtu mwenye hekima kuwa mpumbavu, na rushwa huharibu moyo.
8Ni heri mwisho wa jambo kuliko mwanzo; na watu wenye uvumilivu ni bora kuliko wenye majivuno rohoni.
9Usikasirike haraka rohoni mwako, kwa sababu hasira hukaa katika mioyo ya wapumbavu.
10Usiseme, “Kwa nini siku za zamani zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa kuwa sio kwa sababu ya hekima kwamba unauliza swali hili.
11Hekima ni njema kama vitu vya thamani tunavyorithi kutoka kwa wazazi wetu. Inatoa faida kwa wale wanaoliona jua.
12Kwa kuwa hekima hutoa ulinzi kama vile fedha inavyoweza kutoa ulinzi, lakini faida ya maarifa ni kwamba hekima humpa uhai kwa yeyote aliye nayo.

13Tafakaria matendo ya Mungu: Ni nani awezaye kuimarisha chochote alichokipindisha?
14Wakati nyakati vinakuwa njema, ishi kwa furaha katika hali hiyo, lakini wakati unapokuwa mbaya, tafakari hili: Mungu ameruhusu hali zote ziwepo, Kwa sababu hii, hakuna mwanadamu yeyote atakaye fahamu chochote kinacho kuja baada yake.

15Nimeona mambo mengi katika siku zangu za ubatili. Kuna watu wenye haki ambao wanaangamia licha ya kwamba wana haki, na kuna watu waovu wanaoishi maisha marefu licha ya kwamba ni waovu.
16Usiwe mwenye haki katika macho yako mwenyewe. Kwa nini kujiharibu mwenyewe?
17Usiwe mwovu sana au mpumbavu. Kwa nini ufe kabla ya wakati wako?
18Ni vyema kwamba ushike hekima hii, na kwamba usiache haki iende zake. Kwa kuwa mtu amchae Mungu atatimiza ahadi zake zote.
19Hekima ina nguvu ndani ya mwenye hekima, zaidi ya watawala kumi katika mji.
20Hakuna mtu mwenye haki juu ya nchi anayefanya mema na hatendi dhambi.
21Usisikilize kila neno linaongelewa, kwa sababu unaweza kusikiamtumishi wako anakulaani.
22Vivyo hivyo unafahamu mwenyewe ndani ya moyo wako umewalaani wengine mara kadhaa.

23Haya yote nimeyathibitisha kwa hekima. Nikasema, “nitakuwa mwenye hekima,” lakini zaidi ambavyo ningekuwa.
24Hekima i mbali na kina sana. Ni nani awezaye kuipata?
25Nikageuza moyo wangu kujifunza kuchunguza na kutafuta hekima na ufafanuzi wa ukweli, na kufahamu kwamba ubaya ni ujinga na kwamba upumbavu ni wazimu.
26Nikapata kufahamu kwamba uchungu kuliko kifo, ndivo alivyo mwanamke yeyote ambaye moyo wake umejaa mitego, na nyavu, na ambaye mikono yake ni minyororo. Yeyote ampendezaye Mungu ataponyoka kutoka kwake, lakini mwenye dhambi atachukuliwa naye.

27“Tafakari kile nilichovumbua,” asema Mwalimu. “Nimekuwa nikiongeza uvumbuzi mmoja hadi mwingine ili kwamba nipate ufafanuzi wa ukweli.28Hii ndiyo bado natafuta, lakini bado sijapata. Sikupata mwanamme mmoja mwenye haki miongoni mwa elfu, lakini sikupata mwanamke miongoni mwa wale wote.29Nimegundua hili: kwamba Mungu alimuumba binadamu akiwa mnyoofu, lakini wametoka katika hali ya unyofu wakitafuta magumu mengi.

8

1Ni mtu gani mwenye hekima? Ambaye anafahamu matukio yana maana gani katika maisha? Hekima ndani ya mtu husababisha uso wake kung'ara, na ugumu wa uso wake hubadilika.

2Ninakushauri kuitii amri ya mfalme kwa sababu ya kiapo cha Mungu cha kumlinda yeye.3Usiharakishe kuondoka mbele ya uwepo wake, na usisimame kuunga mkono jambo lisilofaa, kwa kuwa mfalme anafanya chochote anacho tamani.4Neno la mfalme hutawala, kwa hiyo ni nani atakaye mwambia, ‘Unafanya nini?
5Yeyote ashikaye amri za mfalme hukwepa madhara. Moyo wa mwenye hekima hutambua mwelekeo muafaka na muda wa kuenda.
6Kwa kuwa kila jambo lina jibu sahihi, na wakati wa kujibu, kwa sababu taabu ya mtu ni kubwa.
7Hakuna anaye fahamu kinacho fuata. Ni nani awezaye kumwambia nini kinacho kuja?
8Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; wala hakuna kuruhusiwa katika vita vile; wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.

9Mambo hayo yote nimeyaona, nikatia moyo wangu katika kila kazi iliyofanyika chini ya jua. Kuna wakati ambapo mtu mmoja anayo mamlaka juu ya mwenziwe kwa hasira yake.10Hivyo niliwaona wabaya wakizikwa hadharani. Waliondolewa mahali patakatifu na kuzikwa mahali waliposifiwa na watu katika mji walipokuwa wamefanya matendo maovu. Hii nayo haifai.

11Wakati hukumu dhidi ya tendo ovu haihukumiwi haraka, hushawishi mioyo ya wanadamu kutenda ubaya.12Hata kama mwenye dhambi afanye uovu mara mia moja na bado aishi kwa muda mrefu, bado ninafahamu itakuwa vyema kwa wale wanao muheshimu Mungu, wanaouheshimu uwepo wake walio nao.13Lakini haitakuwa vyema kwa mtu mwovu; mkewe hatacheleweshwa. Siku zake kama kizuri kitowekacho upesi, kwa sababu hamuheshimu Mungu.

14Kuna ubatili mwingine usio faa, jambo jingine linaofanyika juu ya dunia. Mambo hutokea kwa watu wenye haki kama yatokeavyo kwa watu waovu, na mambo hutokea kwa wenye haki kama yatokeavyo kwa waovu. Ninasema hili pia ni ubatili usiofaa.15Kwa hiyo nikapendekeza furaha, kwa sababu mtu hana jambo bora chini ya jua zaidi ya kula na kunywa na kuwa na furaha. Furaha ndiyo itamfuata katika kazi zake kwa siku zote za maisha yake ambayo Mungu amempa chini ya jua.

16Nikauweka moyo wangu kufamu hekima na kufahamu kazi inayofanyika juu ya nchi, kazi ambayo inafanyika mara nyingi pasipo kufumba macho usiku au mchana.17Kisha nika tafakari matendo yote ya Mungu, na kwamba mtu hawezi kuelewa kazi inayofanyika chini ya jua. Bila kujali mtu anafanya kupata majibu, hatayapata. Ingawa mwenye hekima anaweza kuamini anajua, kitu kweli hajui.

9

1Kwa kuwa nilifikiri haya yote katika akili zangu kufahamu kuhusu watu wenye haki na wenye hekima na matendo yao. Wote wako katika mikono ya Mungu. Hakuna anayefahamu kama upendo au chuki itakuja kwa mtu.

2Kila mmoja ana mwisho sawa. Mwisho sawa una subiria watu wenye haki na waovu, wema, walio safi na wasio safi, yeye atoaye dhabibu na yule asiye dhabihu. Kama vile watu wema watakufa wenye dhambi nao watakufa vivyo hivyo. Kama vile yule anayeapa atakavyo kufa, vivyo hivyo mtu yule aogopaye kuweka kiapo naye atakufa.

3Kuna mwisho mwovu kwa kila kitu kinachofanyika chini ya jua, na mwisho kwa kila mtu. Moyo wa mwanadamu umejaa uovu, na wazimu uko katika mioyo yao wakati wanaishi. Hivyo baada ya hilo wanaenda kwa wafu.4Kwa kuwa yeyote anayeungana na wote walio hai kuna tumaini, kama vile mbwa aliye hai ni bora kuliko simba aliye kufa.
5Kwa kuwa watu walio hai, lakini walio kufa hawajui chochote. Hawana tena tuzo yeyote kwa sababu kumbukumbu yao imesahaulika.
6Upendo wao, chuki na wivu vimekatiliwa mbali muda mwingi. Hawatapata sehemu katika kitu chochote kinachofanyika chini ya jua.

7Nenda zako, kula mkate wako kwa furaha, na kunywa mvinyo wako na moyo wa furaha, kwa kuwa Mungu huruhusu kusherehekea kazi njema.8Nguo zako ziwe nyeupe siku zote, na kichwa chako kipake mafuta.9Ishi kwa furaha na mwanamke umpendaye siku zako zote za maisha yako ya ubatili, siku ambazo Mungu amekupatia chini ya jua wakati wa siku zako za ubatili. Hiyo ni thawabu kwa ajili yakazi yako chini ya jua.10Chochote mkono wako unakifanya, kifanye kwa nguvu zako kwa sababu hakuna kazi, au ufafanuzi au ujuzi au hekima katika kaburi, unapoenda.

11Nimeona baadhi ya vitu vyakuvutia chini ya jua: Mashindano hayatokani na watu wenye mbio. Vita havitokani na watu imara. Mkate hautokani na watu wenye busara. Mali hazitokani na watu wenye ufahamu. Kibali hakitokani na watu wenye ujuzi. Badala yake muda na bahati huwaathiri wao wote.

12Kwa kuwa hakuna anaye fahamu wakati wake wa kufa, kama vile samaki wanaswavyo katika nyavu ya kifo, au kama vile ndege akamatwavyo katika mtego. Kama wanyama wanadamu wamefungwa katika nyakati mbaya ambazo ghafla huwaangukia.

13Pia nimeona hekima chini ya jua kwa namna ambayo kwangu ilionekana kubwa.14Kulikuwa na mji mdogo na watu wachache ndani yake, na mfalme mkuu akaja kinyume na mji huo na akauzingira na akajenga mahandaki kwa ajili ya kuushambulia.15Na katika mji kulikuwa na maskini, mtu mwenye hekima, ambaye kwa hekima yake aliuokoa mji. Ila baadaye hakuna aliye mkumbuka yule maskini.16Hivyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu, lakini hekima ya mtu maskini hudharauliwa, na maneno yake hayasikilizwi.”
17Maneno ya watu wenye hekima yaliongewa polepole yanasikiwa vizuri kuliko makelele ya mtawala yeyote miongoni mwa wapumbavu.
18Hekima ni bora kuliko silaha za vita, lakini mwenye dhambi mmoja anaweza kuharibu mazuri mengi.

10

1Kama nzi walio kufa husababisha manukato kutoa harufu ya uozo, hivyo hivyo upumbavu kidogo hushinda hekima na heshima.

2Moyo wa mtu mwenye hekima huelekea kulia, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.
3Wakati mpumbavu anapotembea barabarani, fikira zake zina upungufu, ikithibitisha kwa kila mtu kwamba ni mpumbavu.
4Kama jaziba za mtawala zikiinuka kinyume na wewe, usiache kazi yako. Utulivu unaweza kutuliza ukatili mkubwa.
5Kuna uovu niliouona chini ya jua, aina ya kosa ambalo huja kutoka kwa mtawala:
6Wapumbavu wanapewa nafasi za uongozi, wakati watu walio faulu wanapewa nafasi za chini.
7Nimewaona watumwa wakipanda farasi, na watu walio faulu wakitembea kama watumwa juu ya ardhi.
8Yeyote anayechimba shimo anaweza kutumbukia ndani yake, na popote mtu anayevunja ukuta, nyoka anaweza kumuuma.
9Yeyote achongaye mawe, anaweza kuumizwa nayo. Na mtu achongaye mbao, anaweza kujihatarisha kwa hiyo.
10Kama chuma butu kisicho na makali, na mtu hainoi, kisha ni lazima atumie nguvu nyingi, lakini hekima hutoa faida kwa ufaulu.
11Kama nyoka akiuma kabla hajafurahi, hivyo hakuna faida kwa mfurahishaji.
12Maneno ya kinywa chamtu mwenye hekima yana huruma. Lakini midomo ya mpumbavu humumeza mwenyewe.
13Kama maneno yanavyo anza kutiririka mdomoni mwa mpumbavu, ujinga hutoka, na mwisho mdomo wake hutiririka wazimu mbaya.
14Mpumbavu huongeza maneno, lakini hakuna ajuaye kinachokuja. Ni nani ajuaye baada yake?
15Jasho la wapumbavu huwavaa wao, hivyo hawajui hata barabara ya kwenda mjini.
16Ole wako ardhi kama mfalme wako ni kijana mdogo, na kama viongozi wako huanza karamu asubuhi!
17Lakini umebarikiwa ardhi kama mfalme wako ni mwana wa waungwana, na kama vingozi wako hula wakati muafaka, kwa nguvu, na sio kwa ulevi.
18Kwa sababu ya uvivu paa huanguka. Na kwa sababu isiyo fanya kazi nyumba hupata ufa.
19Watu huandaa chakula kwa kicheko, divai huleta furaha maishani, na fedha hutimiza hitaji kwa kila kitu.
20Usimlaani mfalme, hata katika akili, na usiwalaani wenye mali katika chumba chako cha kulala. Kwa kuwa ndege wa angani inaweza kuchukua maneno yako. Chochote kilicho na mabawa kinaweza kusambaza jambo.

11

1Tawanya mkate wako juu ya maji mengi, kwa kuwa utaupata tena baada ya siku nyingi.

2Shiriki mkate na watu saba, hata wanane kwa kuwa haujui ni majanga gani yanayo kuja juu ya nchi.
3Kama mawingu yamejaa mvua, yanajivua yenyewe chini ya nchi. Na kama mti ukianguka kuelekea kusini au kuelekea kaskazini, popote mti unapoangukia papo hapo utabakia.
4Yeyote autazamaye upepo yawezekana asipande, na yeyote atazamaye mawingu yawezekana asivune.
5Kama usivyo jua njia ya upepo, wala vile ambavyo mtoto akuavyo tumboni, vivyo hivyo huwezi kuielewa kazi ya Mungu, aliye umba kila kitu.
6Asubuhi panda mbegu yako; hadi jioni, fanya kazi kwa mikono yako kama inavyo hitajika kwa kuwa haujui ni ipi itafanikiwa, jioni au asubuhi, au hii au ile au zote zitakuwa nzuri.
7Kweli nuru ni tamu, na ni kitu cha kufurahisha kwa ajili ya macho kuona jua.
8Kama mtu akiishi miaka mingi, na aifurahie yote, lakini na afikiri juu ya siku zijazo za giza, kwa kuwa zitakuwa nyingi. Kila kitu kijacho ni ubatili unaoteketea.
9Furahia kijana, katika ujana wako, na moyo wako ufurahie siku za ujana wako. Fuatilia yale mema ya moyo wako, chochote kilicho mbele ya macho yako. Ingawa, fahamu kwamba Mungu atakuleta hukumuni kwa ajili ya vitu hivi vyote.
10Ondoa hasira kutoka moyoni mwako, na usijali maumivu yoyote katika mwili wako, kwa sababu ujana na nguvu zake ni ubatili.

12

1Pia mkumbuke Muumba wako katika siku za za ujana, kabla ya siku za ugumu hazijaja, na kabla ya miaka haijafika utakapo sema, “Mimi sina furaha katika hizo,”

2fanya hivi kabla ya nuru ya jua na mwezi na nyota havijawa giza, na mawingu kurudi baada ya mvua.
3Huo utakuwa wakati ambapo mlinzi wa ikulu atatetemeka, na wanaume imara wameinama, na wanawake wanao saga kukoma, kwa sababu ni wachache, na wale wanao chungulia dirishani hawaoni vizuri tena.
4Huo utakuwa wakati ambao milango imefungwa katika mtaa, na mlio wa kusaga kukoma, wakati wanaume watasitushwa kwa mlio wa ndege, na wimbo wa sauti ya wasichana kukoma.
5Utakuwa wakati ambapo watu wataogopa vilivyoinuka na hatari iliyoko barabarani, na wakati ambapo mlozi utachanua maua, na wakati panzi watakapokokotana wenyewe, na wakati ambapo hamu za asili zitakaposhindwa. Kisha mtu aenda katika nyumba yake ya milele na waombolezaji wateremka mitaani.
6Mkumbuke Muumba wako kabla ya kamba ya fedha kukatwa, au bakuli ya dhahabu kupasuka, au gudulia kuvunjwa kwenye chemichemi, au torori la maji kuvunjika kisimani,
7Kabla mavumbi kurudia mahali yalipotoka, na roho kurudi kwa Mungu aliyeitoa.
8Kama ukungu wa mvuke,” asema mwalimu, kila kitu ni mvuke upoteao.

9Mwalimu alikuwa na hekima na aliwafundisha watu maarifa. Alisoma na kuazimu na kutunga mithali nyingi katika mpangilio.10Mwalimu alitafuta kuandika kwa kutumia vithibitisho dhahiri, maneno ya kweli yaliyo wima.

11Maneno ya watu wenye hekima ni kama mchokoo. Kama misumari iliyogongomewa ndani, ndivyo yalivyo maneno ya mabwana katika mkusanyiko wa mithali zao, ambazo zimefundishwa na mchungaji mmoja.12Mwanangu kuwa makini na kitu zaidi, utengenezaji wa vitabu vingi, ambavyo havina mwisho, na kusoma kwingi huleta uchovu mwilini.
13Mwisho wa jambo baada ya kila kitu umeshafika, kwamba ni lazima umche Mungu na kushika amri zake, kwa kuwa hili ndilo jukumu lote la mwanadamu.
14Kwa kuwa Mungu ataleta kila tendo hukumuni, pamoja na kila kitu kilichofichika, kizuri au kibaya.

Wimbo wa sulemani

1

1Wimbo ulio Bora, ambao ni wa Sulemani. Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake

2O, laiti angenibusu na mabasu ya mdomo wake, kwa kuwa upendo wake ni bora kuliko mvinyo.
3Mafuta yako ya upako yana manukato mazuri; jina lako ni kama marashi yaeleayo, hivyo wanawake wadogo wanakupenda.
4Nichukuwe kwako, na tutakimbia. Mwanamke akizungumza mwenyewe Mfalme amenipeleka vyumbani mwake. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake; nina furahi kuhusu wewe; acha ni shereheke upendo wako; ni bora kuliko mvinyo. Ni halisi kwa wanawake wengine kupenda. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
5Mimi ni mweusi lakini ni mzuri, enyi mabinti wa wanaume wa Yerusalemu - mweusi kama hema za Kedari, mzuri kama mapazia ya Sulemani.
6Usinishangae kwa sababu ni mweusi, kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mama yangu walikuwa na hasira juu yangu; walinifanya mtunzaji wa mashamba ya mizabibu, lakini shamba langu la mizabibu sijalitunza. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
7Niambie, wewe ambaye moyo wangu wakupenda, wapi unalishia mifugo yako? Wapi unapumzisha mifugo yako mchana? Kwa nini niwe kama mtu anaye hakangaika miongoni mwa mifugo ya marafiki zako? Mpenzi wake anamjibu
8Kama haujui, uliye mzuri miongoni mwa wanawake, fuata nyayo za mifugo yangu, na ulishe watoto wako wa mbuzi karibu na hema za wachungaji.
9Nina kulinganisha, mpenzi wangu, na farasi mzuri wa kike miongoni mwa farasi wa magari ya Farao.
10Mashavu yako ni mazuri kwa mapambo, shingo yako na mikufu ya madini.
11Nitakufanyia mapambo ya dhahabu yaliochanganywa na fedha. Mwanamke akiongea mwenyewe.
12Wakati mfalme akiwa amelala kitandani mwake, marashi yangu yakasambaza harufu.
13Mpenzi wangu kwangu ni kama mkebe wa marashi unaolala usiku kati ya maziwa yangu.
14Mpenzi wangu kwangu ni kama kifurushi cha maua ya hena katika mashamba ya mizabibu ya Eni Gedi. Mpenzi wake anazungumza naye.
15Sikiliza, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; ona, wewe ni mzuri; macho yako ni kama ya hua. Mwanamke anazungumza na mpenzi wake.
16Sikiliza, wewe ni mtanashati, mpenzi wangu, jinsi gani ulivyo mtanashati.
17Nguzo za nyumba yetu ni za matawi ya mierezi, na dari letu ni la matawi ya miberoshi.

2

1Mimi ni ua katika tambarare, nyinyoro katika bonde. Mwanaume akizungumza naye

2Kama nyinyoro miongoni mwa mimba, ndivyo wewe, mpenzi wangu, miongoni mwa mabinti wengine wote. Mwanamke akizungumza mwenyewe
3Kama mti wa mpera ulivyo miongoni mwa miti ya misituni, ndivyo mpenzi wangu alivyo miongoni mwa wanaume. Nina kaa chini ya kivuli chake kwa furaha sana, na tunda lake ni tamu kwa ladha yangu.
4Amenileta kwenye ukumbi wa maakuli, na bendera yake juu yangu ilikuwa upendo. Mwanamke akizungumza na mpenzi wake.
5Nihuishe kwa keki za mizabibu na kuniburudisha kwa mapera, kwa kuwa nimedhohofika na mapenzi. Mwanamke akizungumza mwenyewe
6Mkono wake wa kushuto upo chini ya kichwa changu, na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akizungumza na wanawake wengine.
7Ninawataka muape, mabinti wa Yerusalemu, kwa swala na paa wa porini, kwamba hamtaamsha au kuchochea mapenzi yetu hadi yatakapoisha yenyewe. Mwanamke akizungumza mwenyewe.
8Sauti ya mpenzi wangu hiyo! O, huyu yuwaja, akiruka ruka juu ya milima, akiruka vilimani.
9Mpenzi wangu ni kama swala au mtoto mdogo wa paa; angalia, amesimama nyuma ya ukuta wetu, akishangaa kupitia dirishani, akichungulia wavuni.
10Mpenzi wangu alizungumza na mimi na kusema, “Amka, mpenzi wangu; Mzuri wangu, twende pamoja nami.
11Angalia, baridi imepita; mvua imeisha na kutoweka.
12Maua yametokeza juu ya nchi; wakati wa kupunguza matawi na kuimba kwa ndege umekuja, na sauti za hua zimesikika nchini kwetu.
13Mti wa tini umepevusha tini zake za kijani, na mizabibu imechanua; yatoa marashi yake. Inuka, mpenzi wangu, mzuri wangu, na uje nami.
14Hua wangu, katika miamba ya mawe, katika miamba ya siri ya mipasuko ya milima, acha nione uso wako. Acha nisikie sauti yako, kwa kuwa sauti ni tamu, na uso wako ni mzuri.” Mwanamke akiongea mwenyewe.
15Wakamate mbweha kwa ajili yetu, mbweha wadogo wanao haribu mashamba ya mizabibu, kwa kuwa shamba letu la mizabibu limechanua.
16Mpenzi wangu ni wangu, na mimi ni wake; anakula penye nyinyoro kwa raha. Mwanamke anaongea na mpenzi wake
17Enenda zako, mpenzi wangu, kabla pepo za jioni hazija vuma na vivuli kutoweka. Nenda zako; kuwa kama ayala au mtoto mdogo wa paa katika milima ya mawe mengi.

3

1Usiku katika kitanda changu nilikuwa na shauku ya yeye nimpendaye; nilimtafuta, lakini sikumpata.

2Nilisema binafsi, “Nitainuka na kwenda kupitia mji, kupitia mitaa na sokoni; nitamtafuta yule moyo wangu umpendaye.” Nilimtafuta, lakini sikumpata.
3Walinzi walinipata walipokuwa doria katika mji. Nikawauliza, “Mmemuona wa moyo wangu yule nimpendaye?”
4Ni baada ya muda mfupi nilipokuwa nimewapita nikampata wa moyo nimpendaye. Nilimshika na sikumuacha hadi nilipomleta nyumbani mwa mama yangu, katika chumba cha yeye aliyenichukua mimba. Mwanamke akiongea na wanawake wengine.
5Ninataka muape, mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kwa ayala na paa wa porini, kuwa hamtachochea wala kuwasha mapenzi yetu hadi yatakapoisha yenyewe. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
6Nini hiyo inayo toka nyikani kama nguzo za moshi, umefukizwa manemane na ubani, pamoja na unga wote wa manukato unaouzwa na wafanya biashara?
7Angalia, nikitanda cha Sulemani; mashujaa sitini wamekizunguka, wakuu wa vita wa Israeli
8Wao ni wazoefu wa upanga na wanaujuzi wa vita. Kila mwanaume ana upanga wake pembeni yake, akijizatiti na maasi ya usiku.
9Mfalme Sulemani akajijengea kiti cha kifalme cha kubebwa na mbao za Lebanoni.
10Nguzo zake zilijengwa kwa fedha; nyuma kuliwekwa dhahabu, na kiti kwa kitambaa cha zambarau. Ndani mwake kulipambwa na upendo na mabinti wa wanaume wa Yerusalemu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa Yerusalemu
11Nenda nje, mabinti wa wanaume wa Sayuni, na mtazame mfalme Sulemani, akivikwa taji ambalo mamaye alimvika siku ya arusi yake, katika siku ya furaha ya maisha yake.

4

1O, wewe ni mzuri, mpenzi wangu; wewe ni mzuri. Macho yako ni ya hua nyuma ya kilemba chako cha uso. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka Mlima Gileadi.

2Meno yako ni kama kondoo walionyolewa, wakitoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja ana pacha, na hamna hata mmoja miongoni mwao aliyefiwa.
3Mdomo wako ni kama uzi mwekendu; mdomo wako wapendeza. Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kilemba chako cha uso.
4Shingo yako ni kama mnara wa Daudi ukiwa umejengwa kwa mistari ya mawe, na ngao elfu moja ikining'nia juu yake, ngao zote za wanajeshi.
5Maziwa yako mawili ni kama swala wawili, mapacha wa ayala, wakila miongoni mwa nyinyoro.
6Kabla jioni ifike na vivuli vitoweke, nitaenda kwenye mlima wa manemane na vilima vya ubani.
7Wewe ni mzuri kwa kila namna, mpenzi wangu na hakuna lawama ndani yako.
8Njoo nami kutoka Lebanoni, bibi harusi wangu. Njoo nami kutoka Lebanoni; njoo kutoka juu ya kilele cha Amana, kutoka juu ya vilele vya Seneri na Herimoni, kutoka shimoni mwa simba, Kutoka mashimo ya milima ya chui.
9Umeuiba moyo wangu, dada yangu, bibi harusi wangu; umeuiba moyo wangu, kwa mtazamo wako tu mmoja kwangu, ukiwa na mkufu wako mmoja wa shingo yako.
10Jinsi gani upendo wako ulivyo mzuri, dada yangu, bibi arusi wangu! Jinsi gani zaidi upendo wako ulivyo bora kuliko mvinyo, na harufu ya marashi yako kuliko manukato yeyote.
11Midomo yako, bibi harusi wangu, yatiririka asali; asali na maziwa viko chini ya ulimi wako; harufu ya mavazi yako ni kama marashi ya Lebanoni.
12Dada yangu, bibi harusi wangu ni bustani ilio fungwa, bustani iliyo fungwa, chemchemi iliyowekewa muhuri.
13Matawi yako ni kichaka cha miti ya komamanga yenye matunda tofauti, na ya mimea ya hina na nardo,
14Nardo na Zafarani, mchai na mdalasini pamoja na aina zote za uvumba, manemane na udi na aina bora za manukato.
15Wewe ni bustani ya chemchemi, kisima cha maji safi, mifereji inayoshuka kutoka Lebanoni. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
16Amka, upepo wa kaskazini; njoo, upepo wa kusini; vuma katika bustani yangu ili manukato yake yatoe marashi. Mpenzi wangu na aje katika bustani yake na kula matunda ya chaguo lake.

5

1Nimekuja katika bustani yangu, dada yangu, bibi arusi wangu; Nimekusanya udi wangu na manukato yangu. Nimekula sega langu la asali na asali yangu; Nimekunywa mvinyo wangu pamoja na maziwa yangu. Marafiki wanazungumza na wapenzi Kuleni, marafiki; kunyweni na mlewe na mapenzi. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe

2Nilikuwa nimelala, lakini moyo wangu ulikuwa macho katika ndoto. Sauti ya mpenzi wangu yabisha na kusema, “Nifungulie, dada yangu, mpenzi wangu, hua wangu, usiye na dosari, kwa kuwa kichwa changu kimelowa na matone, nywele zangu kwa unyevu wa usiku.”
3“Nimevua joho langu; je, azima nilivae tena? Nimeosha miguu yangu; je, lazima niichafue tena?”
4Mpenzi wangu kwa mkono wake kupitia kwenye kitasa cha mlango akanigusa, na moyo wangu ukawa umewaka kwa ajili yake.
5Nimeamka kumfungulia mlango mpenzi wangu; mikono yangu ikawa yamiminika na manemane, vidole vyangu na unyevu wa manemane, katika komeo la mlango.
6Nimemfungulia mlango mpenzi wangu, lakini mpenzi wangu alikuwa aligeuka na kuondoka. Moyo wangu ukadidimia aliponena; nikakosa tumaini. Nikamtafuta, lakini sikumpata; nikamuita, lakini hakunijibu.
7Walinzi waliokuwa wakizunguka mjini walinipata mimi; walinipiga chini na kunijeruhi; askari katika ukuta walichukua nguo yangu ya juu. Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
8Ninawataka muape, mabinti wa Yerusalemu, kwamba mkimuona mpenzi wangu, ni kitu gani mtamjulisha? Mwambie nimenyong'onyea sababu ya upendo wangu kwake. Wanawake wa mji wakizungumza na mwanamke mdogo
9Mpenzi wako ana ubora gani kuliko mwanaume mwengine, wewe uliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwanini mpenzi wako bora kuliko mpenzi mwengine, hadi utuulize tuweke nadhiri kama hii? Mwanamke mdogo akizungumza na wanawake wa mji
10Mpenzi wangu amenawiri na anang'aa, Kati ya wanaume elfu kumi.
11Kichwa chake ni dhahabu safi; nywele zake ni laini na nyeusi kama kunguru.
12Macho yake ni kama ya hua pembezoni mwa vijito vya maji, yameoshwa na maziwa, yameundwa kama mikufu.
13Mashavu yake ni kama vitanda vya manukato, vinavyotoa harufu ya marashi. Midomo yake ni nyinyoro, inayotiririka manemane.
14Mikono yake ni ya mianzi ya dhahabu iliyo zungushiwa mikufu; tumbo lake ni pembe lililofunikwa yakuti ya samawati.
15Miguu yake ni nguzo za marimari, iliyowekwa juu ya dhahabu safi; muonekano wake ni kama Lebanoni, mizuri kama mierezi.
16Mdomo wake ni mtamu kuliko; ni mzuri sana wa kupendeza. Huyu ni mpenzi wangu, na huyu ni rafiki yangu, mabinti wa Yerusalemu.

6

1Mpenzi wako ameenda wapi, aliye mzuri miongoni mwa wanawake? Kwa uelekeo gani mpenzi wako ameenda, ili tumtafute nawe? Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe

2Mpenzi wangu ameenda katika bustani yake, kwenye vitanda vya manukato, kwenda kula katika bustani na kukusanya nyinyoro.
3Mimi ni wa mpenzi wangu, na mpenzi wangu ni wangu; hula miongoni mwa nyinyoro kwa raha. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye
4Wewe ni mzuri kama Tirza, mpenzi wangu, wapendeza kama Yerusalemu, wahamasisha kwa utusho kama jeshi lenye bendera mbele.
5Geuza macho yako mbali na mimi, kwa kuwa yananizidi ukali. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi likishuka chini kutoka miteremko ya Mlima Gileadi.
6Meno yako ni kama kundi la kondoo likishuka kutoka sehemu ya kuoshwa. Kila mmoja anapacha, na hamna ata mmoja kati yao aliyefiwa.
7Mashavu yako ni kama majani ya komamanga nyuma ya kilemba chako cha uso. Mpenzi wa mwanamke akizungumza peke yake
8Kuna malikia sitini, masuria themanini, na wanawake wachanga bila idadi.
9Hua wangu, wangu asiye na dosari, ni yeye pekee; ni binti pekee wa mama yake; ndiye kipenzi cha mwanamke aliye mzaa. Mabinti wa wenzengu wamemuona na kumuita mbarikiwa; wanawake-malikia na masuria walimuona pia, na wakamsifia: Kile walicho sema wanawake-malikia na masuria
10“Ni nani huyo anaye jitokeza kama kukicha, mzuri kama mwezi, anayeng'aa kama jua, uamasisha-kwa utisho kama bendera ya jeshi?” Mpenzi wa mwanamke akizungumza mwenyewe
11Nilienda kwenye kichaka cha miti ya milozi kuona mimea midogo ikikua bondeni, kuona kama mizabibu ilikuwa imechipua, na kama mikomamanga imestawi.
12Sikujua ni lini nafsi yangu ilinikalisha juu ya gari la farasi la mfalme wangu waungwana. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
13Geuka nyuma, geuka nyuma, wewe mwanamke mshunami; geuka nyuma, geuka nyuma ili niweze kukutizama kwa mshangao! Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake Kwanini wanishangaa, mwanamke mkamilifu, kana kwamba nina cheza katikati ya mistari miwili ya wachezaji?

7

1Jinsi gani miguu yako ilivyo yaonekana mizuri kwenye viatu, binti wa mfalme! Mapaja yako ni kama mikufu, kama kazi ya mjenzi.

2Kitovu chako ni kama duara la bakuli; kamwe kisikose mchanganyiko wa mvinyo. Tumbo lako ni kama ngano iliyoumuka na kuzungushiwa nyinyoro.
3Maziwa yako mawili ni kama watoto wawili wa ayala, mapacha wa ayala.
4Shingo lako ni kama mnara wa pembe; macho yako ni kama maziwa ya Heshiboni kwenye lango la Bathi Rabimu. Pua yako ni kama mnara wa Lebanoni ambao watazama kuelekea Damasko.
5Kichwa chako ni kama Karmeli; nywele kichwani mwako ni za zambarau nyeusi. Mfalme amestaajabishwa na vifundo vyake vya nywele.
6Jinsi gani ulivyo mzuri na wakupendeza, mpenzi, na mazuri yako.
7Urefu wako ni wa kama mti wa mtende, na maziwa yako kama vifungu vya matunda.
8Nilisema, “Ninataka kuupanda huo mti wa mtende; nitashika matawi yake.” Maziwa yako nayawe kama vifungu vya mizabibu, na harufu ya pua yako iwe kama mapera.
9Mdomo wako na uwe kama mvinyo bora, ukishuka taratibu kwa mpenzi wangu, ukiteleza kwenye midomo yetu na meno. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
10Mimi ni wa mpenzi wangu, na ananitamani.
11Njoo, mpenzi wangu, twende nje ya mji; tulale usiku kwenye vijiji.
12Tuamke mapema twende kwenye mashamba ya mizabibu; tuone kama mizabibu imeweka machipukizi, kama maua yake yamechanua, na kama mikomamanga imetoa mau. Pale nitakupa penzi langu.
13Mitunguja ya toa harufu yake; katika mlango wa tunapoishi kuna kila aina ya matunda, mpya na ya kale, niliyokuhifadhia, mpenzi wangu.

8

1Ninatamani ungekua kama kaka yangu, aliyenyonya ziwa la mama yangu. Ila kila nilipokutana nawe nje ningekubusu pasipo mtu kunidharau.

2Ningekuongoza na kukuleta kwenye nyumba ya mama yangu, yeye aliyenifundisha. Ningekupa mvinyo uliochachwa unywe na baadhi ya jwisi ya komamanga. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
3Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu na mkono wake wa kulia wanikumbatia. Mwanamke akiongea na wanawake wengine
4Ninataka muape; mabinti wa wanaume wa Yerusalemu, kuwa hamsha au kuchochea mapenzi yetu hadi yatakapo isha yenyewe. Wanawake wa Yerusalemu wakizungumza.
5Ni nani huyu ambaye anakuja kutoka nyikani, akimuegemea mpenzi wake? Mwanamke mdogo akizungumza na mpenzi wake nimekuamsha chini ya mti wa mpera; pale mama yako alichukua mimba; pale alikuzaa, alijifungua wewe.
6Niweke kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako, kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti. Mapenzi mazito hayana kurudi kama kwenda kuzimu; miale yake yalipuka; ni miale ya moto inayo waka, miale yenye joto kuliko moto wowote.
7Maji yaliyozuka hayawezi kuzimisha upendo, wala mafuriko hayawezi kuuondoa. Mwanaume akitoa mali zake zote kwa ajili ya upendo, ukarimu wake utadharauliwa. Kaka zake mwanamke mdogo wakizungumza wenyewe
8Tuna dada mdogo, na matiti yake bado hayajakua. Tutamfanyia nini dada yetu siku hatakayoahidiwa kuolewa?
9Kama yeye ni ukuta, tutamjengea juu yake mnara wa fedha. Kama yeye ni mlango, tutampamba kwa mbao za mierezi. Mwanamke mdogo akizungumza peke yake
10Nilikuwa ukuta, lakini matiti yangu sasa ni kama nguzo imara; hivyo nimekomaa machoni pake mleta amani. Mwanamke mdogo akizungumza mwenyewe
11Sulemani alikuwa na shamba la mizabibu huko Baali Hamoni. Aliwakodishia wao ambao wangelitunza. Kila mmoja alipaswa kuleta shekeli elfu moja za fedha kwa matunda yake.
12Shamba langu la mzabibu ni langu hasa, li mbele yangu; shekeli elfu moja ni za kwako, Sulemani mpenzi, na shekeli mia mbili ni za wale wanaotunza matunda yake. Mpenzi wa mwanamke akizungumza naye.
13Wewe unayeishi katika bustani, marafiki zangu wanasikiliza sauti yako; acha na mimi niwezekuisikia pia. Mwanamke mdogo akiongea na mpenzi wake
14Harakisha, mpenzi wangu, na uwe kama paa au mtoto wa paa kwenye milima ya manukato.

Isaya

1

1Maono ya Isaya mwana wa Amozi ambayo aliyaona kuhusu Yuda na Yerusalemu katika vipindi vya utawala wa Uzia, Yothamu, Ahazi, na Hezekia, wafalme wa Yuda.

2Sikia enyi mbingu, tega sikio ewe nchi; kwa kuwa Yahwe amesema: “Nimewatunza na kuwalea watoto, lakini wamenigeuka.
3Ng'ombe anamjua anayemmiliki na punda anajua sehemu anapowekewa chakula, lakini Israeli hawajui, wala hawafahamu.”
4Ole! Taifa, wenye dhambi, mtu muovu, watoto wa wenye zambi, watoto wanaoenda kinyume, Wamemtelekeza Yahwe, wamedharau aliye Mtakatifu wa Israeli, wamejitenga wenyewe kutoka kwake.
5Kwa nini ulikuwa unaendelea kupigwa? Kwa nini unazidi kuasi zaidi na zaidi? Kichwa chote kinauma, moyo wote ni dhaifu.
6Kutoka kwenye unyayo wa mguu mpaka kichwani kila sehemu ina maumivu; ni madonda na majeraha mabichi yaliyoachwa wazi, ambayo hayajafungwa, kuasifishwa, kuwafunga vidonda vyao, wala kuwaponya kwa mafuta.
7Nchi yenu imeharibiwa; miji yenu imechomwa moto; mashamba yenu- mbele, wageni wamehiaribu- wamepatelekeza katika uharibifu, ulioangushwa na wageni
8Binti Sayuni ameacha kama kibanda katika shamba la mzabibu, kama kivuli kitika shamba la matango, kama mji unaomba.
9Kama Yahwe wa majeshi hakutuasha kwa mda mfupi tungekuwa kama Sodoma, tungekuwa kama Gomora.
10Sikiliza neno la Yahwe, enyi viongozi wa Sodomu; sikilizeni sheria ya Mungu wetu, enyi watu wa Gomora:
11“Sadaka zenu ni nyingi kiasi gani kwangu?” asema Yahwe. “Nimesikia vya kutosha kuhusu sadaka yenu ya mwana kondoo, na mnyama alionona; na damu ya ng'ombe, ndama, au mbuzi si vifurahii.
12Ulipokuja kuonekana mbele yangu, Ni nani aliyehitaji hili juu yako, kukanyaga katika mahama yangu?
13Msilete tena sadaka zisizo na maana; maana zinaniongezea uchafu mmekusanyika katika siku yenu mpya ya mwenzi na sabato-Mimi siwezi vumlia mikusanyiko hii ya waovu.
14Ninaichukia sherehe yenu mpya ya mwenzi na sherehe zilizoteuliwa; ni mzigo kwangu; nimechoka kuubeba.
15Hivyo basi mnapotawanya mikono yenu kitkika maombi, sitawangalia hata kama mkiomba sana, sitawasikiliza; mikono yenu imejaa damu.
16Jiosheni, jitakaseni wenyewe; ondoeni matendo maovu mbele ya macho yangu; acheni kutenda dhambi;
17jifunze kutenda mema; tafuta ukweli; msiwanyanyase, wapeni haki yatima, walindeni wajane.”
18Njooni sasa, njooni tusemezane, asema Yahwe, japokuwa dhambi zenu ni nyekundu kama bendera zitakuwa nyeupe kama theluji; japokuwa ni myekundu kama damu zitakuwa kama sufi.
19Kama utakubali na kutii, utakula mema ya nchi,
20lakini ukikataa na kugeuka, upanga utakuangamiza, maama Yahwe amesema.
21Ni kwa jinsi gani mji ulioaminika umekuwa kahaba! Ulikuwa ni mij wenye usawa na haki, lakini sasa mji umejaa mauwaji.
22Fedha zenu zimechafuka, na mvinyo wenu umechanganjwa na maji.
23Viongozi wenu wamemgeuka Mungu wamekuwa marafiki wa wezi; yeyote anayopenda rushwa na kuikimbilia. Hawawajali yatima, wala wajane wanaokuja kuwanyenyekea mbele yao.
24Hivyo basi hili ndilo tamko la Bwana, Yahwe wa majeshi, Shujaa wa Israeli: Ole wao! Nitachukua hatua kwa wale walio kinyume na mimi na niwaadhibu wale wanaonipinga;
25Nitaugeuza mkono wangu juu yako, nitatakasa chuma kilicho chakaa na kuondoa kutu yote.
26Nitailinda hukumu yako kama ilivyokuwa mwanzo, na washauri wako kama ilivyokuwa hapo mwanzo; baada ya hapo mtaitwa mji wa haki, mji wa imani.”
27Sayuni itakombolewa kwa haki, na wanaotubu kwa haki.
28Waasi na wenye dhambi wataangamizwa pamoja, na wale wataenda kinyume na Yahwe watauliwa.
29Kwa kuwa utaona aibu juu ya miti ya mialoni uliyoitamani, na utakuwa na hofu juu ya bustani uliyoichagua.
30Kwa kuwa utakuwa kama mualoni ambao majani yake yamenyauka, na kama bustani isiyokuwa na maji.
31Mtu mwenye nguvu atakuwa kama kitu kikavu, na kazi yake itakuwa kama cheche; zitawaka moto kwa pamoja, na hakuna hata mmoja ataweza kuuzima.”

2

1Vitu ambavyo Isaya mwana wa Amozi alivijua katika maono, kuhusu Yuda na Yerusalemu.

2Na itakuwa katika siku za mwisho, ule mlima wa nyumba ya Yahwe itaanzishwa kama mlima mrefu zaidi, na utanyanyuliwa juu ya vilima, na mataifa yote yatakusanyika pale.

3Watu wengi watakuja na kusema, “Njooni, twendeni juu ya mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo, kwa hiyo anaweza kutufundisha baadhi ya njia zake na tunaweza kutembea katika njia zake.” Nje ya Sayuni itaenda sheria na neno la Yahwe litatoka Yerualemu.
4Atahukumu kati ya mataifa na atatoa maamuzi kwa watu wote; watayapiga nyungo mapanga yao kuwa majembe, na mikiku yao kama ya kukatia ndoano; taifa halitanyanyua upanga juu ya taifa lingine, na wala hawata jiandaa kwa vita tena.
5Nyumba ya Yakobo, njooni, na tutembee katika mwanga wa Yahwe.
6Kwa maana mmewatekeleza watu wenu, nyumba ya Yakobo, wamejazwa na desturi kutoka mashariki na dalili kutokea kama mfilisti, na watasalimiana kwa mikono na wana wa wageni.
7Nchi yao imejaa fedha na dhahabu, na hakuna mipaka katika utajiri wao; nchi yao pia imejaa farasi, wala hakuna mipika ya magari.
8Nchi yao pia imejaa sanamu; wanaabu utengenezaji wa mikono yao wenyewe, vitu aambavyo vidole vyao vimetengeneza.
9Watu watainama chini, na kila mmoja atanguka chini; hivyo basi msiwanyanyue juu.
10Nendeni maeneo yenye miamba na mjifiche kwenye aridhi kwa hofu ya Yahwe na kwa utukufu wa enzi yake.
11Mtu anaye tazama kwa kujivuna atashushw chini, na kiburi cha watu kitashushwa chini, na Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
12Maana kutakuwa na siku ya Yahwe wa majeshi juu ya yeyote anayejigamba na kujiinua juu, na dhidi ya yeyote mwenye kiburi na atashushwa chini-
13na dhidi ya mierezi ya Lebanoni iliyo juu na kupandishwa juu, na dhidi ya mialoni ya Bashani.
14Siku hiyo ya Yahwe wa majeshi itakuwa dhidi ya milima yote mirefu, na dhidi ya vilima vyote vilivyonyanyuliwa juu,
15na dhidi ya minara mirefu, na dhidi ya kila ukuta unaojitokeza,
16na dhidi ya merikebu zote za Tarshishi, na dhidi ya vyombo vizuri vya meli.
17Kiburi cha kitashushwa chini, na kiburi cha wanaume kitaanguka; Yahwe mwenyewe atainuliwa siku hiyo.
18Sanamu zote zitaondolewa.
19Wanaume wataingia kwenye mapango ya miamba na mashimo ya aridhi, kwa hofu ya Yahwe, na kwa utukufu wa enzi yake, atakapo nyanyuka na kuitisha nchi.
20Siku hiyo watu watatupa sanamu zao za fedha na dhahabu ambazo wametengeneza wenyewe kwa ajili ya kuabudia - watazitupa mbali kwa fuko na popo.
21Watu wataingia kwenye miamba kupitia mwanya itakuwa miamba chakavu, kwa hofu ya Yahwe na utukufu wa enzi yake,
22usimwaminia mtu, ambae pumzi yake inatokea katika pua yake, ni kwa kiasi gan?

3

1Ona, Bwana, Yahwe wa majeshi, anakaribia kuwachukua kutoka Yerusalema na Yuda wasaidizi na wafanyakazi: wasambazaji wote wa mikate, wasambazaji wote wa maji;

2mtu mwenye nguvu, shuja, hakimu, nabii, dalili za msomaji, na mzee;
3naodha wa hamsini, raia husika, mshauri, fundi mtarajiwa, na mchawi stadi.
4Nitamuweka kijana tu kama kiongozi wenu, kijana atawaongoza wao.
5Watu watanyanyasika, kila mmoja mmoja na kila mmoja na jirani yake; watoto watawatusi wazee, na mivutano itawapa changamoto waheshimiwa.
6Mwanaume atamshikilia ndugu yake katika nyumba ya baba yake na kusema, ‘Unayo kanzu; uwe kiongozi wetu, na uharibifu huu uwe mikononi mwako.
7‘Siku hiyo atapaza sauti na kusema, ‘hautakuwa mganga; sina mkate wala mavazi. Hatanifanya kuwa kiongozi wa watu.
8Kwa maana Yerusalemu kuna mashaka, na Yuda imeanguka, kwa sababu mazungumzo yao na matendo yao yako kinyume na Yahwe, wanayapinga macho ya utukufu wake.
9Angalia nyuso zao zinashudia kinyume nao; na watasema dhambi zao kama Sodoma; hawatazificha, Ole wao! Maana wanakamilisha janga lao wenyewe.
10Mwambie mtu mwenye haki kwamba itakuwa vizuri, maana watakula matunda ya matendo yao.
11Ole kwa wakosaji! Itakuwa vibaya kwa yeye, maana malipo ya mikono yake yatafanyika kwake pia.
12Watu wangu-watoto wangu wanawakandamiza, na wanawake wanawaongoza wao. Watu wangu, wale wanaowaongoza wanawaongoza vibaya na kuchanganya muelekeo wa nja yenu.
13Yahwe simama juu ya mashitaka; yeye amesimama kuwashtaki watu.
14Yahwe atakuja na hukumu juu ya wazee na watu wao na viongozi wao: “Umeharibu shamba; nyara kutoka kwa masikni ziko kwenye nyumba zako.
15Kwa nini unaponda watu wangu na kusaga nyuso za masikini?” Hili ni tamko Bwana, Yahwe wa majeshi.

16Yahwe anasema hivyo kwa sababu mabinti wa Sayuni wanajigamba, wanatembea pekee yao vichwa vyao vikiwa juu, na kutaniana kwa macho yao, na kutakata kokote waendako na kuamua upatu kwa miguu yao,
17Kwa hiyo Bwana atafanya magonjwa ya mapele kwenye kichwa cha mabinti wa Sayuni, na Yahwe atawafanya upaa.

18Siku hiyo Bwana ataondoa mapambo mazuri yaliyoko kwenye kifundo cha miguu, bendi za kichwa chao, kaya zao; bangili za masikio,19bangili za miguu na taji zao;20kitambaa cha kichwa, chaini za miguu, mafurungu na maboksi ya marashi na na haiba ya bahati.21Atatoa bangili na kipini kwenye pua;22sherehe za mavazi, mapazia na mabegi ya mkononi;23vioo vya mkononi, sanda nzuri, vilemba vya kichwa na taji.
24Badala ya manukato mazuri kutakuwa na arufu mbaya; na badala ya ukunda, kamba, kufunika kwa vazi la gunia; kitia alama mwilini kwa moto badala ya uzuri. Wanaume wao wataanguka kwa upanga,
25na wanaume wenye nguvu wataanguka kwenye vita.
26Lango la Yerusalemu litaomboleza na kuomboleza; na atakuwa peke yake amekaa chini ya ardhi.

4

1Siku hiyo wanawake saba watamchukua mwanaume mmoja na kusema, “Tutakula chakula chetu wenyewe, tutavaa nguo zetu wenyewe. Lakini tunahitaji kuchukua jina lako ili tuondoe aibu zetu.”2Na siku hiyo tawi zuri la Yahwe na utukufu, na matunda yatakuwa na ladha nzuri na kupendeza kwa wale wanaoishi Israeli.3Itatokea kwa yule aliyeachwa Sayuni na wale waliobakia Yerusalemu wataitwa watakatifu, yeyeto aliyeandikwa chini anaishi Yerusalemu.4Hii itatokea pale ambapo Bwana atasafisha uchafu wa mabinti wa Sayuni, na atasafisha madoa ya damu kutoka kati ya Yerusalemu, kwa namna ya roho ya hukumu na roho ya kuungua na moto.5Tena juu ya mlima wote wa Sayuni na mahali pakukusanyikia, Yahwe atafanya wingu na moshi kwa wakati wa mchana na moto unaong'a wakati wa usiku; na itakuwa dari juu ya utukufu wote.6Kutakuwa na kivuli kwenye makazi wakati mchana kuzuia jua, na kimbilio na mfuniko kutoka kwenye mawimbi na mvua.

5

1Acha niimbe kwa mpendwa wangu mzuri, wimbo wa mpendwa wangu kuhusu shamba la mzabibu. Mpendwa wangu ana shamba kwenye mlima wenye rutuba.

2Analilima, anaondoa mawe, na anaotesha aina ya mizabibu iliyo bora. Na hujenga mnara katikati ya shamba akichimba shinikizo ndani yake. Anasubiria mzabibu uzae matunda lakini unazaa zabibu mwitu.
3Kwa hiyo sasa, wakazi wa Yerusalemu na watu wa Yuda, toa hukumu kati yangu na shamba la mzabibu.
4Je ni kitu gani cha ziada unaweza ukakifanya kwenye shamba langu la mizabibu, ambacho sijakifanya? Ninapoitazamia izae matunda, kwa nini inazaa matunda mwitu?
5Sasa nitawambia kitu nitakacho kifanya kwenye shamba langu la mzabibu: nitaondoa uzio, nitaligeuza kuwa malisho, Nitavunja ukuta wake chini. Na itakanyagwa chini.
6Nami nitaliharibu wala halitapaliliwa wala kulimwa, bali litatoa mbigiri na miba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshee mvua juu yake.
7Maana shamba la mzabibu la Yahwe Bwana wa majeshi ni nyumba ya Israeli, na mtu wa Yuda ndio mazao yake ya kupendeza; anaisubiria haki lakini badala ya yaki kuna mauwaji; maana haki, lakini badala yake ni kelele zikihitaji msaada.
8Ole wao wanaoungana nyumba kwa nyumba, shamba kwa shamba, mpaka wanamaliza, na umebaki mwenyewe kwenye shamba!

9Yahwe wa majeshi ameniambia mimi, nyumba nyingi zitakuwa wazi, hata kubwa na zinazovutia, hakuna mwenyeji yeyote.
10Maana mashamba ya mizabibu la nira kumi lilitoa bathi moja tu, na homeri ya mbegu itatoa efa tu.
11Ole wao wanaoamka asubuhi na mapema kutafuta pombe kali, wale wanaokaa usiku wa manane mpaka pombe inawaka moto.
12Wanasherekea kwa kinubi, kinanda, kigoma, filimbi, na mvinyo, lakini hawazitambui kazi za Yahwe, wala hawaziangalii kazi za mikono yake.
13Kwa hiyo watu wangu wameenda kifungoni kwa kukosa uelewa; viongozi wao wakuheshimiwa wanashinda na njaa, na watu wao hana kitu cha kunjwa.
14Hivyo basi kuzimu kumeongeza ladha yake na imefungua kinywa chake kwa kiasi kikubwa; wasomi wao, viongozi wao, manabii na wenye furaha miongoni mwao, watashuka kuzimu.
15Mtu atalazimishwa kuinama chini, na watu watakuwa wayenyekevu; na macho yao ya kujivuna yatatupwa chini,
16Yahwe wa majeshi atainuliwa katika haki yake, na Mungu mtakatifu atajidhirisha kuwa mtakatifu kwa haki yake.
17Ndipo kondoo watalishwa kama wako kwenye malisho yao wenyewe, na katika uharibifu, kondoo watachungwa kama wageni.
18Ole wao wanaovuta pamoja na waovu kwa kamba isiyo na maana na wanaovuta pamoja na dhambi kwa kamba za gari.
19Ole kwa wale wasemao, “Basi na Mungu afanye haraka, basi afanya upesi, ili tuweze kuona kinachotokea; na tuache mipango ya Mtakatifu wa Israeli ije, ili tuifahamu.”
20Ole wao waitao uovu wema, na wema ni uovu; inayowakilisha giza kama mwanga, na mwanga kama giza; inayowakilisha kitu kichungu kama kitamu, na kitamu kama kichungu!
21Ole kwa wale wenye busara machoni mwao, na buasra kwa uelewa wao!
22Ole wao ambao ni washindi kwa kunjwa mvinyo, na wazoefu wa kuchanganya pombe kali;
23ambao wako huru kumpa haki mtenda maovu, na kuwanyima haki wenye haki!
24Hivyo basi kama ndimi za moto zinazokula mabua, kama majani makavu yanavyochomwa na moto, hivyo basi mizizi yake itaoza na maua yake yataperuka kama mavumbi. Hii itatokea kwa sababu wameikataa sheria ya Yahwe wa majeshi, na kwa sababu wamedharau neno la Mtakatifu wa Israeli.
25Hivyo basi hasira ya Yahwe imewaka juu ya watu wake. Ameunyoosha mkono wake juu yao na kuwaadhibu wao. Milima inatikisika, na maiti ni kama takata mitaani. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake, ameunyoosha mkono wake nje.
26Atapandisha bendera ya ishara mabali na mataifa na atapuliza filimbi kwa wale walio mwisho wa nchi. Tazama watakuja wakikimbia mara moja.
27Hakuna tairi wala mashaka miongoni mwao; hakuna asinzae wala kulala usingizi. Au kama mkanda uliolegea, wala kamba za viatu kukatika.
28Mishale yao ni mikali na upinde wao umejikunja; kwato za farasi wao’ ni kama jiwe, na gari lao magurudumu yake ni kama miba.
29Mngurumo wao utakuwa kama wa simba, watanguruma kama mwana wa simba. Watanguruma na kukamata mawindo na kuvuta mbali, na hakuna atakayeokolewa.
30Siku hiyo atanguruma juu ya mawindo kama vile bahari kwa kishindo. Yeyote atakayeangalia nchi, ataona giza na mateso; hata mwanga hutafanjwa kuwa mweusi kwa mawingu.

6

1Nyakati zile za kifo cha mfalme Uzzia, nilimuona Bwana akiketi katika kiti cha cha enzi; alikuw juu na mahali palipo inuka, na pindo la vazi lake limejaa hekaluni.2Juu yake kuna maserafi; kila moja lina mabwa sita; mawili yamefunika uso wake, na mawili yamefunika miguu yake, na mawili ya kurukia.3Kila mmoja anaitana na mwenzake nakusema, “Mtakakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu. Ni Yahwe wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.”4Misingi ya vizingiti imeshtuka kwa sauti ya mtu aliye nje, na njumba imejaa moshi.

5Ndipo nikasema, “Ole wangu" ninastahili adhabu maan mimi ni mtu mwenye midomo michafu, na ninaishi na watu wenye midomo michafu, maana macho yangu yamemuona Mfalme, Yahwe, Yahwe wa majeshi.”

6Ndipo mmoja wa maserafi akaruka juu yangu; mkononi mwake akiwa amebeba makaa ya mawe yanayong'aa, ameyachukuwa kwa koleo mathebauni.7Akaugusa mdomo wangu kwa makaa ya mawe na akasema, “Ona, makaa ya mawe yameshika midomo yako; maovu yako yameondolewa, na dhambi zako zimelipiwa kwa hili.”

8Nilisikia sauti ya Bwana ikisema, “Nimtume nani; nani ataenda kwa niaba yetu?” Ndipo nikasema, “Niko hapa; nitume mimi.”

9Akasema, “nenda na uwambie watu, ‘mnasikiliza lakini hamelewi; anaona lakini hamuangalii.’
10Nenda ufanye mioyo ya watu hawa kuwa migumu, na masikio yao kuwa mazito, na macho yao kuwa vipofu. Hivyo basi wanaweza kuona kwa macho yao, kusikia kwa masikioa yao, na kuelewa kwa mioyo yao wakageuka na kuponywa.

11Ndipo nikasema, “Bwana, mda gani?” Akanijibu, mpaka mji itakapopata ajali na kuharibiwa na pasipo wakazi, na nyumba hazina watu, na nchi imeanguka katika ukiwa mtupu,
12na mpaka pale Yahwe atakapo wapeleka watu mbali, na upweke wa nchi ni mkubwa.
13Hata kama makumi ya watu watabaki kwenye nchi, itaharibiwa kwa mara nyingine kama mwaloni uliokatwa chini na shina lake likabaki, mbegu takatifu kwenye kisiki chake.”

7

1Siku zile wakati Ahazi mwana wa Yothani mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Rezeni mfalme wa Amramu, na Peka mwana wa Remaelia, mfalme wa Israeli, walienda Yerusalemu kupigana vita nao, lakini hawakuweza kushinda vita.

2Ilitaarifiwa kwa nyumba ya Daudi kwamba Amramu amejiunga na Efraimu. Moyo wake na moyo watu wake ukatetemeka, kama vile miti ya misitu inavyopepea kwa upepo.

3Ndipo Yahwe akamwambia Isaya, “Nenda nje na kijana wako, Sheari Jashubu ukaonane na Ahazi mwisho wa mfereji wa birika la juu, katika njia kuu ya uwanja Dobi.4Mwambie, ‘awe makini, awe mtulivu, asiogope au vitisho kwa sababu ya mikia hii miwili ya vingi hivi vitokavyo moshi, kwa sababu ya hasira kubwa ya Resini na Amramu, na mwana wa Remalia.5Amramu, Ephraimu, na mwana wa Remaeli wamepanga mabaya juu yako; wamesema,” njooni tuwavamie Yuda na kuwaogopesha,6njooni tujipange na tumueweke mfalme wetu ndani ya Yuda, mwana wa Tabaeli.”7Bwana Yahwe asema, “haitatokea; haitaonekana,
8maana kichwa cha Amramu ni Dameski, na kishwa cha Dameski ni Rezini. Ndani ya miaka sitini na tano, ndoto za Ephraimu zitasambaratishwa na hapatakuwa na watu.
9Efraimu ni kichwa Samaria, na kishwa cha Samaria ni mwana wa Remaria. Na kama hamtasimama imara katika imani yenu, hakika hamtakuwa salama.”

10Bwana akaongea tena na Ahazi,11“Omba ishara ya Yahwe Mungu wako; omba juu ya hilo kwa kina au kwa kiwango cha juu.”

12Lakini Ahazi anasema, sitaomba wala kumjaribu Yahwe.”

13Hivyo Isaya akajibu, “sikilizen, nyumba ya Daudi. Je haijatosha kwa watu kuujaribu uvumilivu wa watu? Je ni lazima kuujaribu uvumilivu wa Mungu?14Hivyo basi Mungu mwenyewe atawapa yeye mwenywe ishara: ona, mwanamke bikira atapata mimba na kumzaa mwana, na atamwita Emanueli.15Atakula siagi na asali na wakati anapojua kuyakataa maovu na kuchagua mema.16Maana kabla mwana ajajua kuyakataa maovu na kuchagua mema, nchi ambayo wewe unawachukia wafalme itakuwa ukiwa.17Yahwe ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako siku hazijatimmia tangu Efraimu alipompokea Yuda- atamleta mfalme wa Asiria.”

18Mda huo Yahwe atapuliza filimbikwa ajili ya kupaa kutoka mkondo wa umbali wa Misri, na maana nyuki kutoka nchi ya Asiria.19Zitakuja na kukaa chini ya korongo, ndani ya mapango ya miamba, kwenye vichaka vya miba, na kwenye malisho.20Katika mda huo Bwana atamnyoa kichwani kichwani na nywele za miguuni kwa wembe ulioazimwa mto Efrarate- mfalme wa Asiria - na vilevile utasafisha ndevu zote.21Siku hiyo, mtu atahifadhi ndama na na kondoo wawili,22na kwa sababu ya maziwa yatakayo patikana ni mengi, atakula siagi, maana kila atakaye bakia kwenye nchi atakula siagi na asali.23Mda huo, kutakuwa na maelfu ya mizabibu na thamani elfu za shekeli, hakutakuwa na kitu zaidi ya kuzalisha mbigiri na miiba.24Watu wataenda pale kuwinda kwa upinde, kwa sababu nchi yote itazalisha mbigiri na miiba.25Watakaa mbali na vilima vitalimwa kwa jembe, kwa sababu ya hofu ya mbigiri na miiba, lakini hapo patakuwa mahali pa kuchungia ngo'mbe na kondoo.

8

1Yahwe ameniambia mimi, “chukua meza kubwa na uandike juu yake, ‘Maheri Shalal Hash Baz.’2Nitachagua mashahidi waaminifu wanishuhudie mimi, kuhani Uria, Zakaria mototo wa Yeberekia.”

3Nilienda kwa huyo nabii mwanamke alipata mimba na kumzaa mwana. Halafu Yahwe akaniambia, “Muite jina lake Shalal Hash Baz;4Maana kabla mwana ajajua kulia, ‘Baba yangu, ‘Mama yangu; utajiri wa Dameski, na mateka wa Samaria watachukuliwa na mfalme wa Asiria.

5Yahwe aliongea na mimi tena,
6Kwa sababu watu hawa wameyakataa maji ya Shiloa na ni furaha kwa Rezeni na mwana wa Remalia,
7Hivyo basi Bwana anakairbia kuwaletea maji maji ya mto, yenye nguvu na mengi, mfalme Asiria na utukufu wake utakuja juu na kupita juu ya mifereji yake atafurika juu ya kingo zote.
8Mto utafurika kuelekea Yuda, utafurika mpaka kufika kwenye shingo yako. Mabawa yake yaliyonyooshwa utajaza upana wa nchi, Emanueli.”
9Nyie watu mtavunjika vipande vipande, Sikilizeni, nyote muishio nchi zilizo mbali; jiandaeni wenyewe na mtavunyika vipande vipande.
10Utatengeneza mpango, lakini haufanyiwa kazi; maana Mungu yuko pamoja nasi.

11Yahwe ameiniambia mimi, kwa mkono wake imara juu yangu, na amenikataza nisitembee katika njia za watu hawa. Nisiseme,
12Ni fitina habari ya mambo ambayo watu hawatasema, ni fitina msihofu wala msiogope.
13Yahwe wa majeshi ambaye mtakaye muheshimu kama mtakatifu; yeye ndie mtakayemuogopa na yeye ndiye mtakayemuhofia.
14Mtakatifu; lakini atakuwa kama jiwe la kikwazo na mwamba wa kujikwaza kwa nyumba zote za Israeli. Na atakuwa mtego na mtego kwa watu wake Yerusalemu.
15Wengi watajikwaa juu yao na kuanguka na kuvunjika, na kutekwa na kukamata mateka.
16Ufunge huo ushuhuda, tia muhuri, na uwape wafuasi wangu,
17Nitamsubiri Yahwe, afichaye uso wake kutoka nyumba ya Yakobo; Nitamsubiri yeye.
18Ona, Mimi na watoto ambaye Yahwe amenipa mimi ni ishara na maajabu tu katika Israeli kutoka kwa Yahwe wa Majeshi yeye aishiye mlima wa Sayuni.

19Watakuambia wewe, “tafuta habari kwa watu wenye pepo na wachawi,” walio kama ndege na kunong'ona dua. Lakini hawataacha kutafuta habari kwa Mungu wao? Je waenende kwa watu waliokufa badala ya walio hai?20Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatayasema mambo hayo ni kwa sababu hakuna mwanga wa alfajiri.21Nawatapita katikati ya nchi kwa shida kubwa na njaa. Walipokuwa na njaa, walipatwa na hasira na kumlaani mfalme wao na Mungu wao, na wakajeuza macho yao juu.22Wataiangalia nchi na kuona dhiki, giza, na ukandamizaji wa viza. Watapelekwa kwenye nchi ya giza.

9

1Giza itaondolewa kwa yeyote ambaye yuko kwenye dhiki. Katika kipindi cha awali aliifedhehesha nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, lakini kipindi cha baadaye ataifanya itukuke, njia ya kuelekea baharini, mbele ya Yordani na mataifa ya Galilaya.

2Watu wanao tembea katika giza wameona mwanga mkubwa; wale waishio katika nchi ya uvuli wa mauti, mwanga umewaka juu yao.
3Umeliongeza taifa; umeongeza furaha yao. Wamefurahia mbele yako kama furaha ya kipindi cha mavuno, kama watu wanavyofurahi kugawanya nyara.
4Maana nira ya mzigo wake, boriti katika mabega yake, fimbo ya mkandamizaji, umesambaratisha ndoto kama siku ya Midiamu.
5Kila buti likanyagalo gasia na vazi limekwisha kwenye damu itachomwa, mafuta kwa moto.
6Kwetu mwana amezaliwa, kwetu mwana ametoka; na mtawala atakuwa kwenye mabega yake; na jina lake ataitwa mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa Amani.
7Enzi yake na amani yake haitakuwa na mwisho, maana anatawala katika kiti cha enzi cha Daudi, na juu ya ufalme wake, ataanzisha hukumu ya haki, tangu sasa na hata milele. Bidii ya Yahwe wa majeshi itafanya haya.
8Bwana alituma neno juu ya Yakobo, na ikaanguka juu ya Israeli,
9Watu wote watajua, Hata Samaria na wakazi wote wa Samaria, wanaongea kwa kiburi na moyo wenye kiburi,
10Matofali yameanguka, lakini tutajenga tena kwa jiwe la patasi; mkuyu umekatwa chini, lakini tutaotesha mierezi katika eneo lao.
11Hivyo basi Yahwe atamwinua juu yao Rezini, adui zake, atawakoroga adui zake,
12Waaramea upande wa mashariki, na wafilisti upande wa magharibi. Nao watamla Israeli kwa mdomo uliowazi. Katika mambo yote haya hasira yake haijapungua; badala yake ameunyosha mkono wake nje.
13Lakini hawatageuka kwa yule anayewapiga wao, wala kumtafuta Yahwe wa majeshi.
14Hivyo basi yao atakata kichwa nakiwiwili cha Israeli, kuti na nyasi, katika siku moja.
15Viongozi na watu wenye vyeo na manabii wanaofundisha kuwa uongo ni mkia.
16Wale wanaowaongoza watu hawa wanawaongoza vibaya, na wale wanaongozwa wameangamia.
17Hivyo basi Bwana atafurahia juu ya vijana wadogo wala hatakuwa na huruma kwa yatima na wajane, maana kila mmoja hana Mungu na ni watenda dhambi, na kila mdomo unazungumza matendo mabaya. Mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake umenyooka hata sasa.
18Matendo mabaya yataungua kama moto, moto hulao mbigili na miiba; itachoma hata vichaka vya mwitu, na safu ya moshi mkubwa upaa.
19Japo hasira ya Yahwe wa majeshi imeunguza, na watu ni kama mafuta kwenye moto. Hakuna mtu aliyemuacha ndugu yake.
20Watanyakuwa chakula katika mkono kulia lakini bado watasikia njaa; watakula chakula kwa mkono wa kushoto lakini hawataridhika. Kila mmoja atakula nyama ya mkono wake mwenyewe.
21Manase; kwa pamoja watavamia Yuda. Mambo yote haya, hasira yake haitapungua; badala yake, amenyoosha mkono wake hata sasa.

10

1Ole wao watimizao sheria zisizo za haki na waandikao sheria zisizo na haki.

2Wanawanyima wahitaji haki yao, wanawaibia watu wangu walio masikini haki zao, wajane mateka wao, na kuwafanya waliofiwa na baba zao mawindo yao!
3Hutafanya nini siku ya hukumu pale siku ya uaribifu itakapokuja kutoka mbali, utakimbilia msaada kwa nani? Na utauacha utajiri wako wapi?
4Hakuna kitakachobaki, utaota miongoni mwa wafungwa au kuanguka miongoni mwa wauwaji. Katika mambo yote haya, hasira yake haijapungua; badala yake mkono wake ameunyoosha hata sasa.
5Ole kwa watu wa Asiria klabu ya asira yangu, fimbo ya asira yangu!
6Nimemtuma juu ya taifa lenye kiburi na juu ya watu waliobeba uwingi wa hasira. Ninaamuru chukua nyara, chukua mawindo, na kuwakanyaga wao kama matope mitaani.
7Lakini hichi sicho alichomaanisha, wala sivyo afikiriavyo. Maana katika moyo wake ni kuharibu na kuondoa mataifa.
8Maana amesema, “wakuu wote sio wafalme?
9Je, Kalno si kama Karkemish? Je, Hamathi si kama Arpadi? Je, Samaria si kama Demeski?
10Kama mikono yangu imeshinda falme za ibada ya sanamu, ikiwa sanamu zao za kuchonga ni bora kuliko sanamu za Yerusalemu,
11na Kama nilivyofanya kule Samaria na sanamu zake zisizo na maana, je sitaweza kufanya hivyo Yerusalemu na sanamu zake?”

12Pindi ambapo Bwana alipoimaliza kazi kwenye mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu maneno ya moyo wenye kiburi ya mfalme wa Asiria na majivuno yake.
13Maana asema, “Kwa nguvu zangu za mkono wangu nimetenda jambo hili, na kwa hekima yangu maana nina akili tena niemiondoa mipaka ya kabila za watu na kuzipora hazina zao wenyenji kama mtu shujaa.
14Na mkono wangu umezitoa mali za mataifa kama vile mtu ayakusanyavyo mayai, kama nilivyokusanya dunia yote. Hakuna atakayepeperusha mabawa yake au kufungua midomo yake au kulia.”
15Je shoka lijisifu lenyewe juu ya mtu anayelitumia? Je, msumeno ujitukuse juu yake auvutaye? Au fimbo ingemuinua yeye ambaye si mti.
16Hivyo basi Yahwe wa majeshi atatuma wadhaifu miongoni mwa wasomi wa kijeshi; na chini ya utukufu na kuteketea kama kuteketea kwa moto.
17Mwanga wa Israeli utakuwa moto, na Mtakatifu wake atakuwa ni moto unaoteketeza na kula mbigiri siku moja.
18Yahwe atauteketeza utukufu wa msitu wake na shamba lake linalo stawi, vyote nafsi na mwili; itakuwa kama vile mgonjwa apotezae maisha yake.
19Mabaka ya miti ya misitu itakuwa michache sana, ambayo mwana anaweza kuyahesabu.
20Siku hiyo, mabaki ya Israeli, familia ya Yakobo ambayo imekimbia, hawatategemea kushindwa, lakini watamtegemea Yahwe, Mtakatifu wa Israeli.
21Mabaki ya Yakobo yatarudi kwa Mungu mwenye nguvu.
22Kwa kupitia watu wako, Israeli ni kama mchanga kama pwani ya bahari, Mabaki yao tu ndio yatakayorudi. Uharibifu wa amri, na mahitaji ya wingi wa haki.
23Maana Bwana wa majeshi, anakaribia kuleta uharibifu utachukua nafasi kubwa katika nchi.

24Hivyo basi Bwana Yahwe wa majeshi anasema, “watu wangu muishio Sayuni, msiwaogope watu wa Asiria. Atawangamiza nyie kwa fimbo na atawanyua wafanyakazi juu yenu, kama ilivyotokea kwa Wamisri.
25Msimuogope, kwa mda mfupi hasira yangu itakwisha juu yenu, na hasira yangu italeta uharibifu.”
26Hivyo Yahwe wa majeshi atapiga mjeledi juu yenu kama vile alivyoishinda Midiani karibu na mwamba Orebu. Na atanyanyua fimbo yake juu ya bahari kama alivyofanya kule Misri.
27Siku hiyo mzigo wake utanyanyuliwa kwenye mabega yako na nira katika shingo yako, nayo nira itaharibiwa kwa sababu ya kutiwa mafuta.
28Adui amekuja Aiathi na amepitia Migroni; katika Michmashi ameyahifadhi mahitaji yake.
29Wamevuka juu ya njia na wamepumzika huko Geba. Rama inatetemeka na Gibea ya Sauli imekimbia.
30Lia kwa sauti, ewe binti wa Galimu! Sikiliza, ee Laisha maskini Anathothi!
31Madmena ni mkimbizi na mkazi wa Gebuni wamejikusanya wanakimbia kutafuta msaada.
32Siku hizi za leo atasimulia huko Nobi na atatingisha mlima wa binti Sayuni, mlima wa Yerusalemu.
33Tazama, Bwana Yahwe wa majeshi atapunguza matawi kwa nguvu za kutisha; miti mirefu itakatwa chini, wanaojivuna wataangushwa.
34Atang'oa vichaka vya msitu kwa shoka, Lebanoni na utukufu wake utaanguka.

11

1Miti itachipukia katika mizizi ya Yese, na matawi yanayotokana na mizizi yatazaa matunda.

2Na roho wa Bwana atashuka juu yake, roho wa hekima na maelewano, roho ya maelekezo na ukuu, roho ya maarifa na hofu ya Yahwe.
3Furaha yake itakuwa hofu ya Bwana; hatatoa hukumu kwa kile anachokiona, wala atatoa maamuzi kwa kile anachokisikia.
4Badala yake atawahukumu masikini kwa haki na atafanya maamuzi kwa usawa na unyenyekevu. Ataamurisha mgomo wa dunia kwa fimbo ya mdomo wake, na punzi ya midomo yake, atawauwa waovu.
5Haki itakuwa mkanda wa viuno kiuno chake kuzunguka mapaja yake.
6Mbwa mwitu atakaa pamoja na kondoo, na chui watalala chini pamoja na mwana wa mbuzi, ndama, mwana wa simba na ndama pamoja na ndama aliyenona. Mwana mdogo atawaongoza wao.
7Ng'ombe na dubu watachungwa pamoja. Na watoto wao watalala pamoja. Simba atakula majani kama ng'ombe.
8Mwana atacheza juu ya shimo la nyoka, na mwana aliyeachwa ataweka mkono wake katika pango la nyoka.
9Hawataumizwa wala kuharibiwa kwenye mlima mtakatifu; kwa maana dunia itakuwa imejaa maarifa ya Yahwe, kama maji yajaavyo kwenye bahari.

10Siku hiyo mzizi wa Yese utasimama kama bendera ya watu. Taifa litamtafuta yeye nje, na mahali pake pakupumzikia patatukuka.
11Siku hiyo, Bwana ataunyoosha mkono wake tena kuokoa mabaki ya watu wake yaliyosalia huko Asiria, Misri, Pathrosi, Kushi, Shinari, Hamathi, na kisiwa cha bahari.
12Ataweka bendera kwa kwa mataifa na atakusanya Waisreli waliotupwa na watu wa Juda waliotawanyika kitika pembe nne za dunia.
13Ataugeuza wivu wa Efraimu, na ukatili wa Yuda utakomeshwa. Efraimu atamuonea wivu Yuda, Yuda hatakuwa adui wa Efraimu tena.
14Badala yake, watashuka chini kwenye mlima wa Wafilisti upande wa magharibi, na pamoja watateka watu mashariki. Watavamia Edomu na Moabu, na watu wa Amoni watawatii wao.
15Yahwe atauharibu kabisa ghuba ya bahari ya Misri. Kwa mawimbi makali ambayo yanavuma juu ya mwana Efurate na itagawanyika katika mifereji saba, hivyo unaweza ukapita juu kwa viatu.
16Kutakuwa na njia kuu kwa ajili ya mabaki ya watu kurudi kutoka Asiria, maana kuna Waisraeli wanaokuja kutoka nchi ya Misri.

12

1Siku hiyo utasema, “Nitakushukuru wewe, Yahwe. Japo ulikuwa na hasira na mimi, laana yako imeondoka mbali, na umenifariji mimi,

2Ona Bwana ni wokovu wangu; nitamwamini na sitakuwa na hofu, kwa Yahwe, ndio, Yahwe ni nguvu yangu na wimbo wangu. Amekuwa wokovu wangu.”
3Kwa furaha utachota maji kwenye kisima cha wokovu.

4Siku hiyo utasema, “Mshukuru Yahwe na ita jina lake; tangaza matendo yake miongoni mwa watu, tangaza jina lake limeinuliwa.
5Mwiimbie Yahwe, maana ametenda matendo yaliotukuka; acha hili lijulikane dunia nzima.
6Lia kwa nguvu na piga kelele kwa furaha, enyi wakazi wa Sayuni, maana katikati yenu ni mtakatifu wa Israeli.

13

1Tamko kuhusu Babeli, ambalo Isaya mwana wa Amozi alipokea:

2Kwenye mlima wa wazi imewekwa bendera ya ishara, lia kwa sauti kwao, wapungie mikono waende kwenye lango la wenye vyeo.
3Nimewamuru watakatifu wangu, ndio, nimewaita watu wangu wenye nguvu kutekele za hasira yangu, na hata watu wangu wanojigamba na kujiinua wenyewe.
4Kelele za umati wa watu kwenye milima, za watu wengi! Kelele za ghasia za ufalme kama mataifa mengi yamekusanyika pamoja! Yahwe wa majeshi anapanga jeshi kwa vita.
5Wametoka katika nchi ya mbali, kutoka juu ya upeo wa macho. Ni Yahwe na silaha zake za hukumu, kuhiharibu nchi yetu.
6Omboleza maana siku ya Yahwe imekaribia; itakuja na uharibifu kutoka kwa Mwenyenzi.
7Hivyo basi mikono ining'inizwe kama kiwete, na kila moyo ulioyeyuka.
8Itawatisha; maumivu na uchungu atawapa wao, kama mwanamke ambaye anajifungua. Watangalia kwa kushangaa kwa kila mmoja mmoja; nyuso zao zitakuwa kama moto.
9Tazama, siku za Yahwe zinakuja na laana kali wingi wa hasira, kuifanya nchi yenye ukiwa na kuharibu wenye dhambi katika nchi.
10Nyota ya mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake. Jua litakuwa giza na hata mwenzi hautaangaza.
11Nitaiadhibu nchi kwa maovu yake na makosa ya uovu wao. Nitamaliza kiburi cha majivuno na nitawashusha wenye kiburi wasiwe makali.
12Nitawafanya watu kuwa nadra zaidi ya dhahabu nzuri na watu kuwa vigumu kupatikana zaidi ya dhahabu safi ya Ofiri.
13Hivyo basi nitazifanya mbingu kutingishika, na dunia itayumba kutoka sehemu iliyoko, Kwa hasira ya Yahwe wa majeshi, na siku ya hasira yake.
14Kama Paa anayewindwa au kama kondoo wasio na mchungaji, kila mtu atageukia watu wake na kukimbia kwenye nchi yake.
15Kwa yeyote atakayeonekana atauliwa, na yeyote atakaye kamatwa atauliwa kwa upanga.
16Watoto wao watakatwa vipandevipande mbele ya macho yao. Nyumba zao zitavamiwa na wake zao watabakwa.
17Tazama, ninakaribia kuwakoroga Wamede ili wawavamie wao, ambao hawaoni maana ya fedha wala furaha ya dhahabu.
18Mishale yao itawachoma vijana wadogo. Hakutakuwa na shimo kwa watoto wao na hawatawacha watoto wao.
19Na Babali ufalme unaovutia zaidi, fahari ya mapambo ya wakaldyo, itaangamizwa na Mungu kama Sodoma na Gomora.
20Hapatakuwa na wenyeji wala wakazi kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine. Mwarabu atapiga hema lake uko wala wachungaji hawatalaza mifugo yao pale.
21Lakini wanyama pori wa jangwani watalala pale. Nyumba zao zitajaa bundi; na mbuni watakaa huko na mbuzi pori wataruka pale.
22Fisi watalia kwenye ngome yao, na mbweha katika maeneo yao mazuri. Mda wao umekaribia, na siku zao hazitachelewa.

14

1Yahwe atakuwa na huruma juu ya Yakobo; atamchagua tena Israeli na kumrudisha tena kwenye nchi yake. Wageni wataungana nao na wataambatana wenyewe na nyumba ya Yakobo.2Mataifa yataletwa katika maeneo yao wenyewe. Ndipo nyumba ya Israeli itawachukwa katika nchi ya Yahwe kwa watumishi wa kiume na wakike. Watachukuwa wafungwa wale waliokamatwa, na watawaongoza wale waliokuwa wanawanyanyasa.

3Siku hiyo Yahwe atatoa pumziko kutoka kwenye mateso na maumivu, na kutoka kwenye kazi ngumu ambayo waliitajika kuzifanya,4mtaimba hii kauli wimbo juu ya mfalme wa Babeli, “Ni kwa jinsi gani wayanyasaji wamefika mwisho, kiburi cha hasira kimekwisha!
5Yahwe amevunja wafanyakazi waovu, fimbo ya hao viongozi,
6inayowapeleka watu kwenye laana na mapigo yasiyopimika, wanaoongoza taifa kwa hasira,
7yote iko katika pumziko na utulivu; wameanza kusherekea kwa kuimba.
8Hata mti wa mseprasi inafurahia pamoja na mierezi ya Lebanoni; inasema, Tangu ulipoweka chini, hakuna mkata kuni aliyekuja kutuangusha sisi,
9Kuzimu haina hamu kwa ajili yako unaye enda pale. Watafufuka waliokufa kwa ajili yako, wafalme wote wa dunia, wafanyeje watoke katika viti vyao vya enzi, wafalme wote wa mataifa.
10Watazungumza na kukuambia wewe, ‘umekuwa dhaifu kama sisi!
11Kiburi chako kimeshushwa hata kuzimu na sauti ya vinanda vyako; Funza wameongezeka chini yako na vijidudu vinakufunika wewe.’
12Kwa jinsi gani ulivyoanguka kutoka mbinguni! Nyota ya siku, jua la asubuhi! Ni kwa jinsi gani mlivyoshushwa chini, umeyashinda mataifa!
13Unasema katika moyo wako, ‘Nitapaa kutoka juu mbinguni, nitanyanyua enzi yangu juu ya nyota za Mungu, na nitakaa kwenye mlima wa kukusanyikia, kwa mbali kufika kaskazini.
14Nitapaa juu umbali wa mawingu; Nitalifanya mimi mwenyewe kama Mungu aliye juu zaidi.’
15Lakini kwa sasa umeshushwa chini kuzimu, kwenye kina cha shimo.
16Wale wanaokuona watakuangalia wewe, watakuangalia sana. Watasema, Je, ni huyu mtu aliyefanya dunia itetemeke, nani aliyetingisha falme,
17ni nani aliyefanya dunia kama jangwa, ni nani aliyeharibu miji yake, na hataki kuwachia wafungwa waende nyumbani?’
18Wafalme wote wamataifa, wote kwa pamoja wamelala chini kwa heshima, kila mtu kwa kaburi lake.
19Lakini umetupwa nje ya kaburi lako kama tawi lilivyotupwa mbali. Maiti imekufunika kama vazi, na wale wanaochomwa kwa upanga, nani wale washukao mpaka misingi ya shimo.
20Hautaunganishwa pamoja katika mazishi, kwa sababu umeiharibu nchi yako na kuuwa watu wako. Watoto wa watenda maovu hawatatajwa tena.”
21Anda machinjio kwa ajili ya watoto wake, kwa sababu ya uovu wa mababu zao, hivyo basi hawatanyanyuka juu na na kuimiliki aridhi ya nchi iliyojaa miji ya dunia yote.”
22Nitapanda juu yao"- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi. Nitang'oa jina katika Babeli, uzao, na ukoo"- hili ndilo tamko la Yahwe.
23Tena nitaifanya nchi hiyo kuwa makao ya bundi, dimbwi la maji, nanitawafagia kwa mfagio wa uharibifu"- hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.

24Yahwe wa majeshi ameapa, “Hakika, kama nilivyodhamiria, itakuwa kama ilivyo; na kama nilivyo kusudia itakuwa:
25Nitawavunja Waasiria kwa mikono yangu, na kukanyaga milima kwa miguu yangu mwenyewe. Hivyo nira yake itanyanyuliwa juu yao na mzigo juu ya mabega yao.”
26Huu ni mpango uliokusudiwa katika nchi yote, na huu ndio mkono ulionyanyuliwa juu ya mataifa.
27Kwa maana Yahwe wa majeshi amepanga hivi; ni nani atakayemzia yeye? Mkono wake umenyanyuliwa juu, ni nani atakajemrudisha nyuma?

28Katika miaka ambayo mfalme Ahazi alipokufa, hili ndio tamko lilokuja:
29Msishangilie, enyi wafilisti wote, kwamba fimbo ya kukupigia wewe imevunjika. Maana katika njia ya nyoka atatoka fira, na watoto wake watakuwa moto nyoka wanaopaa.
30Na mwana wa kwanza wa maskini watachunga kondoo wao kwenye malisho yangu, na wahitaji watalala chini salama. Nitaiuwa mizizi yenu kwa njaa ambayo atawauwa wakazi wenu wote.
31Omboleza, ewe lango, lia, ewe mji; ninyi nyote mtayeyukia mbali, Ufilisti. Maana kutoka kaskazini limetoka wingu la moshi, na hakuna hata mmoja atakaye odoka kwenye nafasi yake.
32Ni kivipi mtu mmoja atamjibu mjumbe wa taifa? Kwamba Yahwe ameipata Sayuni, na ndani yake walionewa watatafuta kimbilio.

15

1Tamko kuhusu Moabu, Kweli, kwa usiku mmoja Ari ya Moabu imeharibiwa kabisa na kuangamizwa; kweli, kwa usiku mmoja Kiri ya Moabu itaharibiwa na kuangamizwa.

2Wamenda juu hekaluni, watu wa Diboni wamenda juu kuomboleza; Moabu wanaomboleza juu ya Nebo na juu ya madeba. Vichwa vyao vimenyolewa viko wazi na na ndevu zao zimenyolewa.
3Wamevaa nguo za magunia katka mitaa yao; juu ya dari zao na kila kona ya mitaa yao, kuyeyuka kwa kumwaga machozi.
4Hishiboni na Elealehi wanalia wakihitaji msaada; Sauti zao zinasikika mpaka Jahazi. Hivyo basi vijana wa vita wa Moabu wanalia wakihitaji msaada; wanatetemeka wao wenyewe.
5Moyo wangu unalia juu ya Moabu; watuhumiwa wamekimbilia Zoari na Elgathi Shelishiyahi. Wanapaa juu ya Luhithi wakilia; katika barabara ya kwenda Horonaimu wanapiga kelele ole juu ya uharibifu.
6Maji ya Nimrimu yamekauka; majani yamepooza na majani yanyochikia yanakufa; hakuna ukijani hata kidogo.
7Hivyo basi vitu vingi vimekuwa na hifadhi wameipeleka juu ya kijito maarufu.
8Kilio kimezunguka katika himaya ya Moabu; malalamiko yamefika hata Eglaimu na Beer-Elimu.
9Maana maji ya Dimoni imejaa damu; Simba atawavamia wale waliokimbia kutoka Moabu pia na walbakia katika nchi.

16

1Mpeleke mwana kondoo kuongoza nchi kutoka Sela huko jangwani, kwenye mlima wa binti Sayuni.

2Kama ndege wazururao, viota vimetapakaa, hivyo basi wanawake wa Moabu watavuka kwenye mto Arnoni.
3Toa maelekezo, tekeleza haki; toa kivuli kama usiku wakati wa mchana; wahifadhi watuhumiwa; msiwahini watuhumiwa.
4Waache waishi miongoni mwenu, wakimbizi kutoka Moabu; muwe mahali pakujifichia wao wasiangamizwe.” Maana mateso yatakwisha, na uharibifu utapungua utakuwa na kikomo, wale wanotetemeka watapotea katika nchi.
5Kiti cha enzi kitaanzishwa katika agano la uaminifu; na mmoja katika hema la Daudi atakaa pale kwa uaminifu. Atahukumu kwa kufuata haki na atatenda haki.
6Tumesikia kiburi cha Moabu, kiburi chake, majivuno yake, na hasira yake. Lakini majivuno yake ni maneno tu.
7Hivyo basi Moabu atalia juu ya Moabu-wote watalia! Wataomboleza, nyie mlioharibiwa kabisa, mikate ya Kiri Haresethi.
8Shamba la Heshboni limekauka kabisa pamoja na mizabibu ya Sibma. Kiongozi wa mataifa amekanyaga mizabibu iliyochaguliwa na kuelekea Jazeri na kuelekea jangwani. Mizizi yake nje ya nchi; imenda juu ya bahari.
9Kweli nitalia pamoja Jazeri kwasababu ya shamba la mizabibu la Sibma. Nitakuloanisha kwa machozi yangu, Heshboni, na Eleale. Maana katika mashamba yenu kipindi cha majira ya joto matunda na mazao nitaishia kwa kupiga kelele za furaha.
10Furaha na shangwe zimezimwa na matunda ya miti ya shambani; na hakuna nyimbo wala kelele katika mashamba ya mizabibu, maana nimeweka mwisho wa kupiga kelele kwa yeyote anayetembea.
11Hivyo, moyo wangu unalia kama kinubi, na ndani yangu maana kwa ajili ya Kiri Hareseth.
12Pindi ambapo Moabu wamejivika mahali pa juu, na kuingia katika hekalu kuomba, maombi yake hayatatimiza chochote.

13Haya ndio maneno aliyoyazungumza Yahwe kuhusu Moabu iliyopita.14Tena Yahwe amesema, “Ndani ya miaka mitatu utukufuwa Moabu utatoweka; japo watu wake wengi, watakao bakia ni wachache, na wasionafaida.

17

1Tamko kuhusu Dameski.

2Miji ya Aroera itaharibiwa. Patakuwa na nafasi kwa ajili ya kutunzia mifugo, na hakuna atakayeizuia.
3Miji ilioachwa itatoweka kutoka Efraimu, ufalme katoka Dameski, na walobaki Aramu-watakuwa kama utukufu wa watu wa Israeli-Hili ni tamko la Yahwe wa majeshi.
4Itakuwa siku hiyo utukufu wa Yakobo utapungua, utakuwa mwembamba na kunona kwa mwili wake utapungua.
5Itakuwa kama mvuna ikusanyavyo mavuno, na mkono wake huvuna maganda ya mazao. Itakuwa kama mtu atoae maganda ya mavuno katika bonde la Refaimu.
6Masalia yataachwa, hata hivyo, mti wa mzabibu utatingishwa: Mizeituni miwili au mitatu iliyo juu sana matawi yake yako juu, manne au matano katka tawi la juu katika mti unaozaa-hili ni tamko la Yahwe, Mungu wa Israeli.
7Siku hiyo watu watawangalia Muumba wake, na macho yatamuangalia Mtakatifu wa Israeli.
8Hawatangalia madhabahu, kazi za mikono yao, wala hataangalia kile kinachofanywa na vidole vyao, nguzo za Ashera na picha ya jua.

9Siku hiyo miji yenye nguvu itakuwa kama msitu uliotelekezwa na juu ya kilele cha mlima, na palipo achwa kwa sababu ya wana wa Israeli patakuwa ukiwa.
10Maana mmemsahau Mungu wa wakovu wenu, na umeudharau mwamba wa nguvu zako. Hivyo basi umeotesha miti mizuri, na mizabibu mizuri iliyotoka ugenini,
11siku hiyo uliootesha na fensi na kulima. Mbegu zako zitaota mapema na kukua, lakini mavuno yatashindikana siku hiyo itakuwa huzuni na kukata tamaa.
12Ole! Watu wenye ghasia, kishindo chake ni kama mngurumo wa bahari, na kasi ya mataifa, wananguruma kama ngurumo ya maji mengi!
13Mataifa yatanguruma kama maji mengi yaendao kasi, lakini Mungu atawakemea.
14Watakimbia mbali sana na watafukuzwa kama pumba kwenye mlima mbele ya upepo, kama mavumbi yazungukayo kwenye dhoruba. Wakati wa usiku, ona, hofu! Na kabla ya alfajiri watakwenda; hili ndilo eneo la wale waliotupora, na wale wanaotunyang'anya mali zetu.

18

1Ole kwa nchi ya wezi wa mabawa, iliyoko mbali kupitia mito ya Ethiopia;

2wanowatuma mabalozi wao kwa kupitia bahari, na vyombo vya majani juu ya maji. Nendeni enyi wajumbe wepesi, kwa watu warefu na laini waishio kwenye nchi, kwa watu wanaoogopewa mbali na karibu, taifa lenye nguvu, wakanyagao watu, ambao mito imegawanya nchi yao.
3Watu wote wakaao duniani nao wakaao katika nchi, pale ishara itakaponyanyuliwa juu ya milima, angalia; na sikilizeni mbiu itakapopulizwa.
4Yahwe asema hivi, “nitachunguza kimyakimya kutoka nyumbani kwangu, kama kupika joto kwenye jua, na kama ukungu kwenye joto la mavuno.5Kabla ya mavuno, pale kipindi cha maua kinapoisha, na maua yako tayari kuwa zabibu. Atakata matawi kwa kupogoa ndoano, na atakatiwa chini na kuchukua matawi yaliyotawanyika.
6Wataachwa kwa pamoja maana ndege wa milimani na wanyama wa duniani. Ndege watatua kwao majira ya joto, na wanyama wote watakuwa kwao kipindi cha baridi.”

7Kwa mda huo kodi italetwa kwa Yahwe wa majeshi kwa watu warefu na laini, kwa watu wanaohofiwa kwa umbali na karibu, taifa imara na kukanyagwa chini, ambayo nchi yao imegawanywa na mito, kwa sehemu ya jina la Yahwe wa majeshi, mpaka mlima Sayuni.

19

1Tamko kuhusu Misri. Ona, Yahwe atasafiri katika mawimbi mepesi na anakuja Misri; Sanamu za Misri zitatemeka mbele yake, na mioyo ya Wamisri itayeyuka ndani yao wenyewe.

2Nitawachanganya Wamisri juu dhidi ya Wamisiri: Mtu atapigana dhidi ya ndugu yake, mji dhidi ya miji, na ufalme dhidi ya ufalme.
3Roho ya Misri itadhohofishwa kutoka ndani. Nitauharibu ushauri wake, japo wanafikiria ushauri wa sanamu, roho za watu waliokufa, na mizimu, na
4Nitawacha Wamisiri kwenye mikono ya viongozi wakatili, kiongozi imara atawaongoza wao- Hili ni tamko la Yahwe Bwana wa majehi.”
5Maji ya bahari yatakauka juu, na mto utakauka na kuwa mtupu.
6Mito itakuwa michafu; mikondo ya Misri itakuwa dhii na kukauka; mwanzi na bendera zake zitapeperushwa mbali.
7Mianzi ya Nile, kwa mdomo wa mto Nile, na mbegu zote zitakazo katika mashamba ya Nile zitakauka zote, zitageuka kuwa mavumbi, na kupeperukia mbali.
8Wavuvi watalia na kuomboleza, na wale watakao shusha neti kwenye maji watauzunika
9Wafanyakazi ya kuchana kitani watafaidika na hao washonao nguo nyeupe watageuka kuwa washonaji.
10Washona nguo wa Misri wataangamizwa; na wote walioajiriwa watahuzunika nafsini mwao.
11Wakuu wa Zoana ni wajinga kabisa. Washauri wenye busara wa Farao ni wapumbavu. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mwana wa watu wenye busara,
12“Wako wapi hao watu wenye busara? Mwana wa mfalme wa zamani? Waache wakuambie? Na ijulikane kitu ambacho Yahwe wa majeshi amekipanga kuhusiana na Misri.
13Wakuu wa Zoani wamekuwa wajinga, wakuu wa Memphisi wamegawanyika; wameifanya Misri iende kinyume, na mawe ya pembeni ya makabila yao.
14Yahwe amechanganya roho wa kuvurugwa katika yao, na wamefanya Wamisri kwenda kinyume kwa yote wanoyafanya, kama mlevi anavyoyumbayumba uku akitapika.
15Hakuna kitu ambacho mtu yeyote anaweza kukifanya kwa ajili ya Misri, kama kichwa au mkia, tawi au mwanzi

16Siku hiyo, Wamisri watakuwa kama wanawake; watatetemeka na kuogopa mkono wa Yahwe wa majeshi ulioinuliwa juu yao.17Nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri. Yeyote atakao wakumbusha wao kuhusu yeye, wataogopa sana, kwa sababu ya mpango wa Yahwe, anaoukusudia juu yao.

18Siku hiyo kutakuwa na miji mitano katika nchi ya Misri wanaozungumza lugha ya Kanaani na kuapa kumtii Yahwe wa majeshi. Moja kati ya miji hii itaitwa mji wa ulioharibiwa.

19Siku hiyo kutakuwa madhabahu kwa ajili ya Yahwe katika ya nchi ya Misri, na jiwe la chumvi karibu na Yahwe.20Itakuwa kama ishara na ushahidi kwa Yahwe wa majeshi katika nchi ya Misri. Atawatumia mkombozi na mlinzi, na atawokoa wao.21Yahwe atajulikana Misri, na Wamisri watamkubali Yahwe siku hiyo. Watamuabudu kwa sadaka na matoleo, na wataweka agano na kulitimiza.22Yahwe ataipiga Misri, ataipiga na kuiponya. Halafu watamrudia Yahwe; atasikiliza maombi yao na kuwaponya.

23Siku hiyo kutakuwa na njia kuu kutoka Misri kwenda Asiria, na Waasira watakuja Misri, na Wamisri watakwenda Asira; na Wamisri wataabudu pamoja na Waasiria.24Siku hiyo, Israeli itakuwa ya tatu pamoja na Misri na Asiria, baraka katikati ya nchi;25Yahwe wa majeshi atawabariki na kusema, “wabarikiwe Wamisri, watu wangu; Wasiria, kazi ya mikono yangu; na Israeli urithi wangu.

20

1Katika mwaka ambao Tartani alipofika kwa Ashdodi, alipotumwa na Sarjoni mfalme wa Asiria, nae akapigana na Ashdodi na akauchukua.2Mda huo Yahwe alizungumza na Isaya mwana wa Amozi, “Nenda ukaondoe nguo za magunia katika kiuno chako, na ondoeni viatu vyenu kwenye miguu.” Naye alifanya hivyo, akatembea uchi na miguu wazi.

3Yahwe asema, “Kama ilivyokuwa kwa mtumishi wangu Isaya alivyotembea uchi na pasipo kuvaa viatu kwa miaka mitatu, ni ishara na dalili kuhusu Misri na kuhusu Ethiopia-4katika njia hii mfalme wa Asiria atawaongoza mateka wa Misri, na walioko uhamishoni Ethiopia, watoto kwa wazee, waliouchi na wasio na viatu, na ambao hawajajisitiri kuiweka Misri katika aibu.5Watafadhaika na kuona aibu, kwa sababu ya Ethiopia ni matumaini yao na Misri ni utukufu wao.6Wenyeji wa pwani watasema siku hiyo, ‘Kweli, hichi ndicho chanzo chetu cha matumaini, tulipokimbilia kuhitaji msaada kutoka kwa mfalme wa Asiria, je ni kwa jinsi gani tunaweza kupona?”

21

1Tamko kuhusu jangwa pembezoni mwa bahari. Kama dhuruba yenye upepo inayotokea kupita Negevi kuelekea jangwani, kutoka kwenye aridhi ya kutisha.

2Nimepewa maono ya kusikitisha: Wasaliti wamepanga hila, na waharibifu kuharibu. Nenda juu na uvamie, Elamu; zingira Media; Mimi nitasimamisha maumivu yao yote.
3Hivyo basi simba wangu wamejawa na maumivu; ni kama mwanamke anayejifungua kwa uchungu yamenipata mimi; Nimeinama chini kwa kile nilichokisikia; nimesumbuliwa kwa kile nilichokiona.
4Moyo wangu unajinga, nimetitishika kwa hofu. Mapema jioni, mda wangu mzuri kwa siku, imeniletea hofu.
5Wameandaa meza, wametawanya vitambaa, na wanakula na kunywa; tokea, mkuu, pakeni ngao yenu kwa mafuta.

6Hili ndilo Bwana aliloniambia, “Nenda, baada ya mlinzi; lazima atoe taarifa kwa kile atakacho kiona.
7Kama ataona gari, jozi ya farasi, farasi juu ya punda na farasi juu ya ngamia, hivyo basi anatakiwa kuwa makini na kuwa macho.”

8Mlinzi analia nje, “Bwana, ninasimama juu ya mnara siku zote, kila siku, na kwa nguzo yangu nitasimama usiku wote.”
9Tazama gari linakuja na wakiwa wawili wawili. Anaita, “Babeli umeanguka, umeanguka, na sanamu za kuchonga za miungu yao zimevunjika chini.”
10Watu wangu niliwapururu na kuwapepeta, watoto niliyowatoa kwenye sakafu yangu mwenyewe. Nilichokisikia kutoka kwa Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, Nimekutangazia wewe.

11Tamko kuhusu Duma. Mtu mmoja ameniita mimi kutoka Seiri, “Mlinzi, ni kitu gani kilichobakizwa usiku?
12Mlinzi akasema, “Asubuhi itafika na vilevile usiku. Ikiwa unataka kuuliza basi uliza; na urudi tena.”

13Tamko kuhusu Arabia. Katika jangwa la Arabia mmeutumia usiku, enyi misafara ya Wadedani.
14Leteni maji kwa wenye kiu; wenyeji wa nchi ya Tema, waoneni watuhumiwa kwa mikate.
15Maana wameukimbia upanga, kutoka upanga unaotolewa, kutoka kwenye upinde ulopinda, na kutokana na uzito wa vita.

16Maana hili ndilo Bwana alichosema na mimi, “Ndani ya mwaka mmoja, kama mtu aliyeajiriwa kwa mwaka ataona, utukufu wa Kedari utakwisha.
17Ni baadhi ya ya wavuta upinde, mashujaa wa Kedari watabakia,” maana Bwana, Mungu wa Israeli, amesema.

22

1Tamko kuhusu bonde la maono: Kwa sababu gani mmepanda kwenye paa za nyumba zenu?

2Ili kuuskia Mji wenye kelele, mji umejaa maovu? Wafu hawajauwawa kwa upanga, na hawakuuwawa kwenye vita.
3Viongozi wenu wamekimbia pamoja, lakini wamekamatwa pasipo na upinde, wote kwa pamoja wamekamatwa na wamekamatwa pamoja; walikimbia kutoka mbali.
4Hivyo basi, Msiniangalie mimi, nitalia kwa uchungu; msijaribu kunifariji kuhusiana na kuharibika kwa binti ya watu wangu.
5Maana kuna siku za ghasia, akanyagaye chini, na fujo za Bwana, Yahwe wa majeshi, katika bonge la maono, kuanguka chini kwa ukuta, na watu wanalia juu ya milima.
6Elamu wakalichukua podo juu, pamoja na magari ya watu na wapanda farasi, na Kiri aliifunua ngao wazi.
7Siku hiyo ambapo mabonde ulioyachagua yatajaa magari, na farasi watachukua nafasi zao katika lango.
8Atauondolea mbali ulinzi wa Yuda; na utaona siku hiyo utaona silaha katika jumba la msitu.
9Umeona matawi ya mji wa Daudi, jinsi mlivyowengi, na kukusanya maji katika birika la chini.
10Umehesabu nyumba za Yerusalemu, na umerarua nyumba chini kuuimarisha ukuta.
11Na umefanya hifadhi katikati ya kuta mbili maana maji ya birika la zamani; maana haukuwahusisha walioujenga mji, walioupanga mji kutoka zamani.
12Bwana, Yahwe wa majeshi amewaita siku hiyo watu waje kuomboleza na kulia, wanyoe vichwa vyao na kuvaa nguo za magunia.
13Lakini angalia, badala yake sherehe na furaha, kuuwa ng'ombe na kuchinga kondoo, njooni tule na kunywa mvinyo maana kesho tutakufa.

14Hili limebanika kwenye masikio yangu na Yahwe wa majeshi: Hakika maovu haya hayatasamehewa, hata utakapokufa, “Amesema Bwana wa majeshi.

15Bwana, Yahwe wa majeshi, asema hivi, “Nenda kwa huyu kiongozi, kwa Shebana, aliye juu ya nyumba, na umwambie,
16Ni nani aliyekuruhusu kuchimba kaburi lako mwenyewe, kukata juu ya kaburi na juu ya urefu katika mahali pa kupumzikia ndani ya mwamba?”
17Yahwe anakaribia kukutupa chini; mtu mwenye nguvu, anakaribia kukutupa chini; atakuzongazonga.
18Atahakikisha anatuzungusha zungusha, na kutupa msukosuko kama mpira kwenye nchi kubwa. Pale utakapokufa, na pale gari lako tukufu litakapo kuwa; utakuwa aibu ya nyumba ya bwana wako!
19“Nami nitakuondoa katika ofisi yako na katika kituo chako. Na utavutwa chini.

20Na itakuwa hivi kuhusu siku hiyo nitamchukua Eliakimu mwana wa Hilkia mtumishi wangu.21Nitamvisha yeye kwa kanzu yenu na kumvika mkanda wenu, na nitahamisha mamlaka yenu kwenye mikono yake. Atakuwa baba wa wenyeji wa Yerusalemu na katika nyumba ya Yuda.22Nitaziweka funguo za nyumba ya Daudi kwenye mabega yake; Atafungua, na hakuna atakayefunga; na atafunga na hakuna atakayefungua.23Nami nitamuimarisha yeye, kigingi katika mahali salama, na atakuwa kiti cha utukufu katika nyumba ya baba yake.24Nao wataangukia juu yake utukufu wote wa baba nyumba ya baba yake, watoto wake na uzao wake na kila chombo kidogo kutoka vikombe mpaka majagi yote.

25Siku hiyo- hili ndilo tamko la Yahwe wa majeshi- kigingi kilichowekwa katika mazingira imara kitatoa njia, utavunjika, na kuanguka, na uzito ulionao utaondolewa- maana Yahwe amesema.

23

1Tamko kuhusu Tiro, Ombolezeni, enyi kondoo wa Tarishishi;

2maana hakuna nyumba wala bandari; kutoka katika nchi ya Kyprusi wamefunuliwa hilo.
3Na juu ya maji mengi ni nafaka za shiho, mazao ya Nile, na uzalishaji wao; mlikuwa wafanya biashara wa kimataifa.
4Kuwa na aibu, Sidoni; maana bahari imenena, mkuu wa bahari. Amesema, “Sijafanya kazi wala kuzaa wala kukuza vijana wadogo wala kuwalea mabinti.
5“Pale taarifa iitakapofika Misri, watahuzunika kuhusu Tiro.
6Piteni mpaka Tarishishi; Ole wenu, enyi wakazi wa pwani.
7Je, hili limeshawahi kuwatokea, mji wenye furaha, ambao kwa asili yake umetoka katika kipindi cha kale. Ambapo miguu yake imempeleka mbali kuishi kwenye maeneo ya ugenini?
8Ni nani aliyepanga haya dhidi ya Tiro, mtoa mataji, ambao wafanyabiashara wake ni wakuu, ambao wafanyabiashara ni watu wa kuheshimika duniani?
9Yahwe wa majeshi amepanga kuharibu kiburi chake na utukufu wake, na kuwahaibisha waheshimiwa wote wa dunia.
10Lima katika shamba lako, kama mtu alimavyo Nile, ewe binti Tarishishi. Maana hakuna tena eneo la soko huko Tite.
11Yahwe amenyoosha mkono wake juu ya bahari, na ametingisha falme; na amepewa amri juu ya Fonensia, kuziharibu ngome.
12Amesema, “Hamta furahia tena, binti bikira wa Sidoni uliyenyanyasika; nyanyuka, pitia Kyprusi; lakini wala hapatakuwa na pumziko.”
13Tazama nchi ya Wakaldayo. Hawa watu wamesitisha kuishi pale; Waasiria wamelifanya jangwa la wanyama pori. Wameizingira minara; wameliharibu eneo lao; wamelifanya kuwa chungu cha uharibifu.
14Omboleza ewe kondoo wa Tarishishi; maana kimbilio lako limeharibiwa.

15Katika siku hiyo, Tiro itasahaulika kwa miaka sabini, kama siku za mfalme. Baada ya miaka sabini kuisha huko Tiro kutatokea kitu kama wimbo wa malaya.
16Chukua kinubi, nenda zunguka mji, mmewasahau malaya; cheza kinubi vizuri, imba nyimbo nyingi, ili uweze kukumbuka.

17Itatokea baada ya miaka sabini, Yahwe ataisaidia Tiro, na wataanza kututafuta pesa tena kwa kufanya kazi ya umalaya, na atafanya utumishi wake katika falme za dunia.
18Faida yake na mapato yake yatatengwa kwa ajili ya Yahwe. Hayatahifadhiwa wala hayatakuwa na hazina, maana faida yao watapewa wale wanoishi madhabahuni mwa Yahwe na yatatumika kuwasambazia chakula cha kutosha na kupata mavazi yenye viwango bora.

24

1Angalia Yahwe anakaribia kuifanya dunia kuwa utupu, kuiharibu, kuharibu uso wake, na kuwatawanya wenyeji wake.

2Itakuwa kama ilivyo kwa watu itakuwa hivyo hivyo kwa kuhani; na kwa watumishi na kwa bwana wake, na kwa mfanyakazi wa ndani itakuwa hivyo na kwa tajiri yake, ndivyo itakavyokuwa kwa anayeuza na anayenunua; ndivyo itakavyokwa kwa wenye kupata faida na wenye madeni, na wale wenye kupokea faida itakuwa hivyo hivyo kwa wale wenye kutoa faida.
3Dunia itaharibiwa kabisa na kufanjwa ukiwa; maana Yahwe amenena maneno hayo. Dunia imekauka kabisa na kunyauka,
4Dunia inazimia n kudhohofika. Watu maarufu wa duniani watapotezwa.
5Dunia inavutwa na watu wakao ndani yake kwa sababu wamepindisha sheria, wameibadili amri na wamevunja agano la milele.
6Hivyo basi laana inaitafuna nchi, na wenyeji wake wamekutwa na makosa. Wakaao duniani wanateketea, na watu wachache wameachwa.
7Divai mpya imekauka, mizabibu imenyauka, na mioyo yote iliyochangamka inaugua.
8Sauti ya furha ya kigoma inasimama, na kelele za wenye furaha zimekwisha, na furaha ya kinubi imesitishwa.
9Hawatakunywa mvinyo tena na kuimba, bia chungu kwa wale wanokunywa.
10Mji uliochafuka umeangushwa chini; kila nyumba imefungwa na hakuna kitu.
11Kuna kilio mtaani kwa sababu ya mvinyo; furaha yote imetiwa giza, furaha ya nchi imetoweka.
12Ndani ya mji kumebaki ukiwa, na lango limebolewa kwa uharibifu.
13Hivi ndivyo itakavyofanyika kwa dunia yote mwiongoni mwa mataifa, pale mti wa mzabibu utakapopigwa, na waokotapo zabibu baada mavuno yake kuwa tayari.
14Watanyanyua sauti zao na kupiga kelele kwa Yahwe mwenye enzi, na utapaza sauti kutoka kwenye bahari.
15Hivyo basi mashariki mtukuze Yahwe, na katika kisiwa cha bahari tukuzeni jina la Yahwe, Mungu wa Israeli.
16Kutoka umbali wa sehemu ya dunia tumesika nyimbo, “Utukufu kwa watu wenye haki! Lakini nikasema, “Nimepita mbali, Ole wangu! Wasaliti walishuhulika na wenye hila; ndio, wasaliti walishuhulika na wenye hila.”
17Hofu, shimo, na mtego yako juu yako, wenyeji wa dunia.
18Amekimbia maana sauti ya hofu itaanguka kwenye shimo, na anayekuja juu katikati ya shimo atanaswa na mtego. Madirisha ya mbinguni yatafunguliwa, na misingi ya dunia itatikisika.
19Dunia itangamizwa kabisa, dunia itapasukia mbali; dunia itatatikisika vikali.
20Dunia itajikongoja kama mlevi na itachezacheza kurudi nyuma na mbele kama kibanda. Dhambi zao zitakuwa nzito juu yao na zitaanguka na hazitasimama tena.
21Itakuwa siku hiyo ambayo Yahwe ataliadhibu jeshi la aliye juu mahali pa juu, na falme za dunia katika dunia.
22Watakusanyika pamoja, wafungwa katika shimo, na watafungwa gerezani; na baada ya siku nying watadhibiwa.
23Halafu Mwenzi utatiwa aibu na jua pia litatiwa aibu, maana Yahwe wa majeshi atatawala katika mlima Sayuni na Yerusalemu, kabla ya wazee wake katika utukufu.

25

1Yahwe wewe ni Mungu wangu; nitakutukuza wewe, nitalisifu jina lako; maana umetenda matendo ya ajabu, mambo uliyoyapanga toka zamaini, kwa uaminifu na ukamilifu.

2Maana umeufanya mji kuwa chungu, ngome ya mji, uharibifu na ngome ya wageni kuwa si mji.
3Hivyo basi watu wenye nguvu watakutukuza wewe; na mji waishio watu wasio na ukatili watakuogopa wewe.
4Maana umekuwa katika eneo salama kwa aliye masikini, makazi kwa mhitaji ambaye yuko kwenye dhiki- makazi kwa aliyeko kwenye dhoruba na kivuli kwa aliyeko kwenye jua. Pale punzi ya watu wakatili imekuwa kama dhoruba dhidi ya ukuta,
5na jua kwenye aridhi kavu, na watazuia kelele za wageni, kama vile jua linavyozuiliwa na kivuli cha mawingu, hivyo basi nyimbo wasio na makosa zimejibiwa.
6Katika mlima huu Yahwe wa majeshi atafanya kwa watu sikukuu ya ya vitu vilivyonona, na mvinyo uliochaguliwa, zabuni ya nyama na sikuku juu ya sira.
7Na katika mlima huu atauharibu mfuniko uliowekwa juu watu wote, na mtandao wa kusuka juu ya mataifa.
8Atameza kifo daima, na Bwana Yahwe atayafuta machozi katika nyuso zetu; na aibu ya watu wake itatupwa mbali kutoka duniani kote, maana Yahwe amesema hivyo.

9Yatazungumzwa katika siku hiyo, “Huyu ni Mungu wetu; na tunayemngoja, na atatuokoa. Huyu ni Yahwe; tuliyemngoja, tutafurahia na kushangilia wokovu wake.”
10Maana katika mlima huu mkono wa Bwana utashuka; na Moabu atakanyagwakangwa chini kwenye eneo lake, na hata majani yatakanyagwakanyagwa chini katika shimo lililojaa mbolea.
11Wataitawanya mikono yao katikati yao, kama vile mpiga mbizi atawanyavyo mikono yake wakati akipiga mbizi. Lakini Bwana atashusha kiburi chao chini japo kuwa na ujuzi katika mikono yao.
12Na ataiangusha chini kwenye aridhi kuta za ngome, kwenye mavumbi.

26

1Siku hiyo wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda: Tuna mji imara; Mungu amefanya wokovu katika kuta na ngome zake.

2Fungua lango, ili mataifa yenye haki yaweze na yenye kutunza imani yaweze kuingia ndani.
3Akili mlionayo, mtamuhifadhi yeye katika amani kamili, maana anawamini ninyi.
4Mwamini Yahwe daima; maana, Yahwe, ni mwamba wa milele.
5Maana atawashusha wale wote wenye kiburi; mji ulio juu atushushwa chini, ataushusha chini kwenye aridhi; na ataulinganisha na mavumbi.
6Utakanyagwakanyagwa chini na miguu ya walio masikini na wahitaji.
7Mapito ya mwenye haki yamenyooka, wewe uliye mnyoofu wainyoosha mapito ya wenye haki.
8Ndio, katika mapito ya hukumu yako, Yahwe, tunakusubiri wewe; jina lako na sifa zako ni matamanio yetu.
9Nimekutamani wewe wakati wa usiku; ndio, roho iliyo ndani yangu ina kutafuta kwa bidii. Pindi hukumu yako itakapokuja duniani, wenyeji wa duniani watajua kuhusu haki.
10Na tuonyeshe upendeleo kwa waovu, lakini hawatajifunza haki. Katika nchi ya wanyofu anatenda maovu na haoni ukuu wa Yahwe.
11Yahwe, mkono wako umenyanyuliwa juu, lakini hawapati hizo taarifa. Lakini wataona bidii kwa watu na wataona aibu, kwa sababu idadi ya maadui watawatafuna.
12Yahwe, utaleta amani kwetu, maana kweli, umekamilisha kazi zetu zote.
13Yahwe Mungu wetu, viongozi wengine badala yako wametutawala sisi; Lakini tunalitukuza jina lako.
14Wamekufa, hawataishi tena; ni maremu hao, hawatafufuka tena. Kweli, umekuja kuwahukumu na kuwaharibu wao, na umefanya kila kumbukumbu kutoweka.
15Umeliongeza taifa, Yahwe, umeliongeza taifa; umeheshimiwa; umeinuliwa katika mipaka yote ya nchi.
16Yahwe, katika mateso yao walikuangalia wewe; walipatwa na wasiwasi katika maombi yao maana adhabu yako ilikuwa juu yao.
17Kama mwanamke mjamzito anayekaribia kujifungua, hupatwa na uchungu na hulia kwa uchungu, hivyo ndivyo tulivyokuwa kabla, Bwana.
18Tulikuwa wajawazito, tumekuwa katika mateso, lakini ni kama tumeshajifungua katika akili zetu. Hatujauleta wokovu duniani, na wakazi wa duniani hawakuanguka.
19Wafu wenu wataishi; watu wenu walio kufa watafufuka. Amka na uimbe kwa furaha, nyie muishio mavumbini; maana umande wenu ni umande wa mwanga, na dunia itawaleta mbele wafu wake.
20Enendeni, watu wangu, ingieni katika vyumba vyenu na mfunge mlango nyuma yenu; jificheni kwa mda mfupi, mpaka hasira itakapopita.
21Maana, angalia, Yahwe anakaribia kutoka katika eneo lake kuwaadhibu watu waishio duniani kwa ajili ya makosa yao; dunia itaachia umwagaji wa damu, na hawatawaficha tena waliokufa.

27

1Katika siku hiyo Yahwe kwa upanga wake ulio mgumu, mkubwa na mkali, atamuadhibu Leviathani na nyoka yule anayetambaa kwa kupenya, na atamuua mnyama anayeishi baharini.

2Siku hiyo: Shamba la zabibu, litawaimbia.
3“Mimi Yahwe ni mlinzi wake; Ninalimwagia maji kila wakati; hivyo hakuna anayelimiza, Ninalilinda usiku na mchana.
4Sina hasira, Oh, kama mbigiri na miiba! Katika vita nitatembea dhidi yao; Nitawachoma wote kwa pamoja;
5labda wafahamu ulinzi wangu na wafanye amani na mimi, waache wafanye amani na mimi.
6Kwa siku inayokuja, Yakobo atachukua mzizi; Israeli itatoa maua na kuchipua; na itaijaza aridhi yote kwa matunda.”
7Je, Yahwe alimshambulia Yakobo na Israeli na hayo mataifa yaliyomshambulia? Je, Yakobo na Israeli waliuliwa na wao kama mliowachinja katika mataifa mliowauwa wao?
8Kitika kipimo halisi cha kuridhisha, watume Yakobo na Israeli mbali; aliwaondosha mbali kwa upepo mkali, katika siku ya upepo wa mashariki.
9Hivyo kwa njia hii, maovu ya Yakobo yatalipiwa, maana hii itakuwa matunda yote yakuondolewa dhambi zake: pale atakapofanya madhabahu ya mawe kama chokaa na kuviangamiza katika vipande vipande, na hakuna nguzo za Ashera au madhabahu itakayoachwa imesimama.
10Maana mji imara umeharibiwa, makao yake na faragha yake yameachwa kama jangwa. Kuna ndama wanachungwa, na huko ndiko atakapo lala na kuyala matawi yake.
11Matawi yake yatakaponyauka yatanguka. Wanawake watakuja na kuyatumia kuyateketeza moto, maana hawa sio watu waelewa. Hivyo basi Muumba wao hatakuwa na huruma juu yao, na yeye aliyewaumba hatakuwa na huruma juu yao.

12Na siku hiyo itakuwa kwamba Yahwe atapururua kutoka mto Efrate mpaka Wadi ya Misri na njie, watu wa Israeli, tutakusanyika mahali pamoja mmoja mmoja.13Siku hiyo tarumbeta kubwa litapulizwa; na watu waliopotea katika nchi ya Asiria watakuja, na waliotupwa katika nchi ya Misri, watamuabudu Yahwe katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.

28

1Ole kwa taji la kiburi ambalo huvaliwa na kila mlevi wa Efraimu, na ua linalofifia la utukufu wa uzuri wake, ua lililowekwa kichwani mwa bonde linalostawi na hao wanaoshindwa na mvinyo!

2Tazama Bwana anamtuma aliye hodari na nguvu; kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo mkali unaoharibu, na atatupa kila taji la ua chini kwenye aridhi.
3Taji ya kiburi ya walevi wa Efraimu lililoko chini ya paa.
4Ua lililofifia la utukufu wa uzuri wake, juu ya kichwa cha bonde la utajiri, itakuwa kama tunda lililoiva mtini kabla ya maji yake, kwamba, wakati mtu anapoliona tunda, wakati likiwa bado mikononi mwake, analigugumia chini.
5Katika siku hiyo Yahwe wa majeshi atakuwa taji nzuri na taji ya uzuri kwa watu wake waliobakia,
6roho ya haki kwa yeye aliyekaa katika hukumu, nguvu kwa wale waliobadilisha adui zao katika malango yao.
7Lakini wale wanaoyumbayumba kwa ajili ya mvinyo, na wanaojikongoja kwa ajili ya pombe kali. Kuhani na nabii watayumbayuma kwa ajili ya pombe kali, na watamezwa na mvinyo. Watajikongoja kwa ajili ya pombe kali, Kujikongoja katika maono na kuyumbayuma katika maamuzi.
8Hakika, meza zote zimejaa matapishi. Hivyo basi hakuna sehemu iliyosafi.
9Ni nani atakaye tufundisha maarifa, na nani atayetuelezea ujumbe? Kwa walioachishwa maziwa au kwa wanaonyonya?
10Maana ni amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na hapa kidogo na pale kidogo.
11Kweli, kwa mdomo wa dharau na lugha za kigeni atazungumza na watu wake.
12Wakati uliopita aliwambia, ‘“Hawa ni wengine, wape punziko walio choka; maana huku ni kujifurahisha,” lakini hawakusikiliza.
13Hivyo basi neno la Yahwe litakuwa kwao amri juu ya amri, amri juu ya amri, utawala juu ya utawala; na kidogo hapa na kidogo pale, ili waende na kuanguka nyuma, na kuvunjwa, kutegwa, na kukamatwa.
14Hivyo basi sikiliza neno la Yahwe, yeyote afaanyae maskhara, wewe unaowaongoza watu hawa ambao wako Yerusalemu.
15Hii itatokea kwa sababu umesema, “Tumefanya magano na kifo; maana kuzimu wameyafikia makubaliano. Hivyo basi hukumu itakapopitishwa kwa wingi, haitatufika sisi, maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, na uongo kuwa makazi yetu.

16Hivyo basi Bwana Yahwe asema hivi, “Ona: Nitaiwekea Sayuni msingi wa mawe, jiwe la kujaribu, jiwe la pembeni lenye samani, msingi wa uhakika. Na yeyote atayeuamini hataaibika kamwe.
17Nitafanya haki kuwa fimbo ya usawa, na kuwa haki pima maji. Atasafishia mbali kimbilio la waongo, na mafuriko yatajaa balaa katika mahali pa siri.
18Agano lako na kifo litafutwa, na makubaliano yako na kuzimu hayatasimama. Pindi mafuriko makali yatapta, yatawazomba nyie.
19Maana pindi yatakopita, yatawazomba nyie yatapita asubuhi na asubuhi, na yatapita tena mchana na usiku utafika. Pale ujumbe utakapofika utasababisha hofu.
20Maana kitanda ni kifupi kwa mtu kunyoosha mkono wake nje, na blangeti ni jembamba kwa yeye kujizungushia ndani”
21Yahwe atanyanyuka kama mlima Perazimu; Atawahimiza yeye mwenye kufanya kazi yake katika bonde la Gibeoni, kazi ya ajabu, na kufanya matendo ya ajabu.
22Hivyo sasa msifanye maskhara, dhamana yako itakazwa, Nimesikia kutoka kwa Bwana, Yahwe wa majeshi, amri ya kuiharibu nchi.
23Kuwa tayari na sikiliza sauti yangu; kuwa makini na sikiliza maneno yangu.
24Je, mkulima anayelima siku zote kwa ajili ya kupanda, analima tu kwenye aridhi? Je, anaendelea kulima shamba lake pasipo kupanda?
25Pindi anapoliandaa shamba lake, Je, hatawanyi jira ya mbegu, anapanda jira, anaweka ngano katika mstari, shayiri katika mahali pake, na yameandikwa sehemu mbili?
26Mungu wake amemuelekeza; anamfundisha yeye kwa busara.
27Zaidi ya hayo, jira zile hazipuruliwi kwa chombo kikali; wala gurudumu la kukatia linalozunguka juu ya jira; lakini jira linapigwa kwa fimbo, na jira kwa fimbo.
28Nafaka ni mwanzo mkate lakini ni laini sana, japo gurudumu la gari lake na farasi wamezitawanya, na farasi wake hawajaiponda ponda.
29Haya yanatoka kwa Yahwe wa majeshi, yeye aliye mshauri wa ajabu na na mwenye ubara wa hekima.

29

1Ole kwa Arieli, Arieli, mji ambao Daudi ameweka kambi! Mwaka hadi mwaka unaongezeka; basi tamasha linakaribia kuja.

2Lakini nitauzingira Arieli, na watalia na kuomboleza; na watakuwa kwangu kama Arieli.
3Nitaweka kambi dhidi yako katika mzunguko, nitakuzingira kwa kuweka uzio dhidi yako.
4Utaletwa chini na utazungumza kutoka chini kwenye aridhi; maongezi yako yatashushwa kutoka mavumbini. Sauti yako itakuwa kama ya pepo kwenye ardhi, na maneno yako yatakuwa dhaifu kutoka mavumbini.
5Jeshi la maadui wako watakuwa kama vumbi ndogo, na wingi wa wasiotisha utakuwa kama makapi yanayopita. Itatokea mara moja, papo hapo.
6Yahwe wa majeshi atakuja kwenu kwa radi, tetemeko la aridhi, sauti kubwa, na upepo mkali na dhoruba kali, na mwali wa moto uteketezao.
7Itakuwa kama ndoto, maono ya usiku: Jeshi la mataifa yote yatapigana dhidi ya Arieli na ngome zake. Watawavamia yeye na ngome zinazowanyanyasa wao.
8Itakuwa kama mtu mwenye njaa anayeota anakula, lakini pindi anapoamka tumbo halina kitu. Itakuwa kama mtu mwenye kiu anayeota anakunywa maji, lakini anapoamka, anazirai, kwa sababu ya kiu na sio kuizima. Ndio, itakavyokuwa idadi kubwa ya wapiganaji dhidi ya Mlima Sayuni.
9Shangaeni wenyewe na mjishangae; jifanye kipofu na uwe kipofu! Uwe mlevi lakini sio wa mvinyo; yumbayumba lakini sio kwa bia.
10Maana Yahwe ameachila roho wake katika usingizi wa kina, Ameyafunga macho yako, manabii, na amefunika kichwa chako, waonaji.

11Ufunuo wote umekuja kwako kama maneno ya kitabu kilichotiwa muhuri, ambacho watu wanaweza kumpa mtu anayejifunza, na kusema hivi, “Soma hiki.” Na atasema, “Siwezi maana imetiwa muhuri.”12Kama kitabu kitapewa kwa mtu asiyeweza kusoma, na kumwambia, ‘“Soma hiki,” na anasema, “Siwezi kusoma.”

13Bwana asema, “Watu hawa wananikaribia mimi na kuniheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na mimi. Heshima yao kwangu ni kwa sababu tu ya amri waliofundishwa.
14Hivyo basi, tazama, Nitaendelea kufanya mambo ya ajabu mwiongoni mwa watu hawa, maajabu baada ya maajabu. Hekima ya wenye busara itatoweka, na uelewa wa watu wenye busara utatokomea.”
15Ole wao wale wanaoficha mipango yao kwa Yahwe, na wale ambao matendo yao ni ya giza. Wanasema, “Nani anayetuona sisi, na ni nani anayetutambua sisi?
16Nyie mnaebadilisha vitu juu chini! Je, mfinyanzi anaweza kufikiriwa kama udongo, hivyo basi vitu vinavyotengeneza vitasema kuhusu aliyevitengeneza, “Hajanitengeneza mimi, “au vitu vinavyotengenezwa viseme kuhusu aliyevitengeneza, Hajaelewa”?
17Katika mda mdogo uliobakia, Lebanoni itageuzwa kuwa shamba, na shamba litakuwa msitu.
18Siku hiyo viziwi watasikia maneno ya kitabu, na macho ya vipofu yataona katika giza nene.
19Waliodhulumiwa watafurahia pamoja na Yahwe, na masikini miongoni mwa watu watafurahia kwa Mtakatifu wa Israeli.
20Maana watu wasio katili watakwisha, na wenye dharau watatoweka. Wale wote wanopenda kutenda maovu wataondolewa,
21nani na kwa neno linamfanya mtu kuwa mkosaji. Watamuekea mtego kwa yeye anayeitafuta haki katika geti na kuweka haki chini kwa uongo usio na kitu.

22Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu nyumba ya Yakobo- Yahwe aliyemkomboa Ibrahimu, “Yakobo hataaibika tena, wala uso wake hautabadilika rangi yake.
23Lakini anapowaona watoto wake, kazi ya mikono yangu, watalitakasa jina langu, Watalitakasa jina langu Mtakatifu wa Yakobo, na watasimama katika hofu ya Mungu wa Israeli.
24Wale watakaopotea kiroho watapata uelewa na walalamikaji watajifunza maarifa.”

30

1Ole wa watoto waasi, “Hili ni tamko la Yahwe. “Wataweka mipango, lakini haitatoka kwangu; wataungana na mataifa mengine, lakini hawakuongozwa na Roho wangu, hivyo wanongeza dhambi baada ya dhambi.

2Wanapanga kushuka chini Misri, lakini hawajaniomba niwaelekeze. Wanatafuta ulinzi kutoka kwa Farao kuchukua kimbilio katika kivuli cha Misri.
3Hivyo basi ulinzi wa Farao utakuwa aibu yenu, na kimbilio lenu katika kivuli cha Misri, kitakuwa udhalilishaji wenu,
4japo wakuu wako Sayuni, na wajumbe wao wamekuja Hanesi.
5Wataaibika kwa sababu ya watu ambao hawawezi kuwasaidia, wala kuwa na faida, lakini ni aibu, na fedheha.

6Tamko kuhusu mnyama wa Negevi: kupitia kwenye mlango wa mateso na hatari, wa simba jike na simba dume, nyoka na nyoka wa moto aneyepaa, wamebeba utajiri wao kwenye mgongo wa punda, na hazina yao katika mabega ya ngamia, kwa watu ambao hawana msaada kwao.
7Maana msaada Misri hauna maana; hivyo basi nimemwita Rahabu, aliyekaa bado.
8Sasa nenda, andika hili mbele yao juu ya meza, na uyaandike katika kitabu, ili yahifadhiwe kwa mda mrefu kama ushuhuda.
9Maana ni watu waasi, watoto waongo, watoto ambao hawaskilizi maelekezo ya Yahwe.
10Wanawambia waonaji, “msiangalie; na kwa manabii, “msitabiri yaliyo ya kweli kwetu; zungumza maneno ya kupendeza kwetu, tabiri udanganyifu. Geukeni katika njia,
11ondokeni kwenye njia; maana Mtakatifu wa Israeli amesitisha kuongea mbele ya uso wetu.

12Hivyo basi mtakatifu wa Israeli asema, “Kwa sababu umekataa maneno haya na kujifunza ukandamizaji na udanganyifu,
13hivyo dhambi hii itakuwa kwenu kama kitu kilichovunjika tayari kwa kuanguka, kama kitu katika ukuta mrefu ambao anguko lake linakaribia, papo kwa hapo.”
14Atavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, hivyo basi hakitabaki kitu, hivyo hakuna vipande vyovyote vya kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, kuchota maji kisimani.

15Maana Bwana Yahwe, Mtakatifu wa Israeli asema hivi, “Kwa kurudi na kwa kupumzika mtaokolewa; katika utulivu na imani itakuwa ni nguvu zako, Lakini hamkuwa tayari.
16Amesema, ‘Hapana, maana kukimbia kwa farasi; hivyo tutakimbia; tutakimbia kwa kutumia farasi mwepesi; hivyo basi watakaojiingiza watakuwa wepesi.
17Watu eflu moja watakimbia kwa kumuhofia mtu mmoja; kwa vitisho vya watu watano mtakimbia mpaka mtakuwa kama nguzu ya bendera iliyoko juu ya mlima, au kama bendera kwenye kilima.”
18Lakini Bwana anawasubiri ili awape neema yake, Hivyo basi yuko tayari kuwaonyesha huruma. Maana Yahwe na Mungu wa haki; Huwabarikiwe wale wanaomsubiri yeye.

19Maana watu wataishi Sayuni, na Yerusalemu na hawatalia tena. Hakika atakuwa neema kwenu kwa sauti ya kilio chenu. Atakaposikia tu, atawajibu ninyi.20Kupitia Yahwe tunapata mkate wa shida na maji ya mateso, hata sasa, mwalimu wako hatajificha mwenyewe tena, lakini utamuona mwalimu wako kwa macho yako mwenyewe.21Masikio yako yatasikia maneno yanayosemwa nyuma, Hii ndio njia, pitia hii, “utakapogeuka upande wa kulia au utakageuka upande wa kushoto.22Mtakinajisi kifuniko chenu mlichokiweka juu ya pesa na dhahabu na kukitupa. Mtakitupa mbali kama hedhi kali, ‘“utawambia wao, “Ondokeni hapa.”

23Naye atatoa mvua kwenye mbegu zenu mtakapopanda kwenye aridhi, na mkate utakuwa kwa wingi kutoka kwenye aridhi na mazao yatazaa kwa wingi. Katika siku hizo ng'ombe zako zitachungwa katika eneo kubwa.24Ng'ombe na punda, wanaolima kwenye aridhi, watakula chakula cha majira kilicho tawanywa kwa koleo na uma.25Juu ya mlima mrefu na juu ya kilima kirefu, kutapitasha vijito na mifereji ya maji, katika siku siku ya machinjio makuu pale minara yote itakapoanguka.26Mwanga wa mwenzi utakuwa kama mwanga wa jua, na mwanga wa jua utang'aa mara saba, kama mwanga wa siku saba. Yahwe atakapofunga kuvunjwa kwa watu wake na kuyaponya majeraha waliyoyapata.
27Jina la Yahwe limekuja kutoka sehemu ya mbali, Linawaka kwa hasira yake na katika moshi mnene. Midomo yake imejaa hasira, na lugha yake nia kama moto unaoangamiza.
28Pumzi yake ni kama maji yaliyojaa yanayofika mpaka katikati ya shingo, kwa ajili kuchuja mataifa kwa kuhamasisha uharibifu. Pumzi yake ni mzabuni katika taya za watu wanowasababisha kutangatanga mbali.
29Utakuwa na wimbo kama usiku pale sherehe takatifu itakapofanyika, na moyo wenye furaha, pindi mmoja atakopo kwenda na katika mlima wa Yahwe, katika mwamba wa Israeli.
30Yahwe atafanya mapambo ya sauti yake inayosikika na atawaonyesha jinsi mkono wake ushukavyo na dhoruba ya hasira yake na moto uwakao, pamoja na upepo mkubwa, mvua kubwa, na mvua ya mawe.
31Maana kwa sauti ya Yahwe, Asiria itanyamazishwa; ataiharibu kwa fimbo.
32Na kila adhabu iliyochaguliwa amechagua fimbo ambayo Yahwe ataiweka juu yao na wakisidikizwa na mziki wa kigoma na kinubi kama wataanzisha vita na kupigana nao.
33Maana sehemu ya kuchoma iliandaliwa toka zamani. Kweli, imeandaliwa kwa mfalme, na Mungu amelifanya kuwa na kina na upana. Rundo liko tayari kwa moto na kuni za kutosha. Punzi ya Yahwe, ni kama mkondo kiberiti, na utawasha moto.

31

1Ole wao washukao Misri kuomba msaada na kutegemea farasi, kuweka imani katika magari (maana wako wengi) na (maana faras haziesabiki). Lakini hawausiani na Mtakatifu wa Israeli, wala hawamtafuti Yahwe!

2Lakini ni mwenye busara, na ataleta maafa na atakanusha maneno yake. Na atakuja juu ya nyumba zitendazo maovu, na dhidi ya wale wanaowasaidia kuteda dhambi.
3Misri ni mtu na sio Mungu, ni farasi wa mwili na sio wa roho. Yahwe atakapota nje kwa mkono wake, wote waliowasaidia watakuwa na mashaka, na yeyote atakayesidia atanguka; wote kwa pamoja watatoweka.

4Hivi ndivyo Yahwe alivyosema na mimi, “kama simba, na hata mwana wa simba, hunguruma juu ya mawindo yake, pale makundi ya wachungaji yanapoita dhidi yake, lakini hatatemeka kwa sauti zao, wala hatakwenda kwa sababu ya kelele zao, hivyo Yahwe wa majeshi atashuka kupigana kwenye mlima Sayuni, katika kilima hicho.
5Kama ndege apaavyo, hivyo Yahwe wa majeshi atailinda Yerusalemu; atailinda na kuiokoa kama apitavyo juu na kuilinda.

6Mrudieni yeye kutoka huyo mliyemgeukia, watu wa Israeli.7Maana katika siku hiyo kila mmoja ataondoa miungu ya fedha na miungu ya dhahabu iliyotegenezwa kwa mikono yenu yenye dhambi.
8Asiria atangamizwa kwa upanga; na upanga usioshikiwa na mtu utumaliza yeye. Ataukimbia upanga, na vijana wake wadogo watafanyishwa kazi ngumu.
9Na watashindwa kujiani kwa sababu ya hofu, na mkuu wao ataogopa mbele ya bendera ya jeshi la Yahwe.”- Hili ni tamko la Yahwe, ambao moto uko Sayuni na ambayo sufuria ya moto iko Yerusalemu.

32

1Tazama, mfalme atatawala kwa haki, wakuu wataongoza kwa haki.

2Kila mmoja atakuwa kama makazi kutoka kwenye upepo na kimbilio kutoka kwenye dhoruba, kama mifereji kwenye sehemu kavu, kama kivuli kwenye mwamba mkubwa katika nchi iliyochoka.
3Halafu macho ya wale wanaoona hayataona giza, na masikio ya wale wanosikia yatasikia vizuri.
4Wenye upele watafikiria kwa makini kwa uelewa wao, na wenye kigugumizi watazungumza dhahiri na kwa urahisi.
5Mjinga hataitwa tena muheshimiwa, wala muongo hataitwa mkuu.
6Maana mjinga anazungumza ujinga, na moyo wake unapanga maovu na matendo ya wasiomcha Mungu, na anaongea mambo mabaya kuhusu Yahwe. Na anawafanya wenye njaa kuwa tupu na wenye kiu kukosa maji
7Njia ya muongo ni maovu. Anajua kubuni mipango mibaya ya kuwalagai masikini kwa uongo, na hata kama masikini atazungumza ukweli.
8Lakini watu wa heshima wanapanga mipango ya kuheshimika; na kwa sababu ya matendo ya wenye heshima tutasimama.
9Nyanyukeni juu, enyi wanawake mlio wepesi, na sikilizeni sauti yangu; enyi mabinti msiowangalifu, nisikilizeni mimi.
10Maana kwa mda mfupi zaidi ya mwaka ujasiri wenu utavunjika, nyie wanawake msiojali, maana mavuno ya zabibu yatakwama, mavuno hayatakuwepo.
11Tetemekeni, enyi wanawake, mliowadhaifu; taabikeni enyi msiokuwa wangalifu; ondoeni nguo zenu nzuri mbaki wazi;
12Vaeni nguo za magunia katika viuno vyenu. Ole watakaojichukulia mashamba mazuri, kwa mzabibu ulio zaa sana.
13Kwenye aridhi ya watu wangu kutamea miiba na mbigiri, hata juu ya nyumba za furaha na mji ulio na shangwe.
14Maana jumba litaachwa, mji uliosongamana utakuwa faragha; kilima na mnara vitakuwa mapango daima, furaha ya punda, malisho ya mifugo;
15mpaka roho itushukie sisi kutoka juu, na jangwa litakuwa shamba linalozaa, na shamba linalozaa litachukuliwa kama msitu.
16Wenye haki wataishi jangwani; na wenye haki wataishi katika shamba linalozaa matunda.
17Kazi ya mwenye haki itakuwa ni ya amani; na matokeo ya wenye haki, ni utulivu na kujiamini daima.
18Watu wangu wataishi katika makao ya amani, na katika nyumba salama na mahali tulivu pa kupumzikia.
19Lakini hata kama ni mvua ya mawe na msitu umeharibiwa, na mji umeteketezwa,
20yule ambae anaye panda pembezoni mwa mifereji atabarikiwa, na yule atakaye wapeleka ng'ombe na punda kuchunga.

33

1Ole wenu, waharibifu ambao hamjaharibiwa! Ole wao wasaliti ambao hamjaslitiwa! Pindi mtakapoacha uharibifu, nanyi mtaharibiwa. Pindi mtakapoacha usaliti, nayi mtasalitiwa.

2Yahwe, tuhurumie sisi; tumekusubiri wewe; umekuwa mkono wetu kila asubuhi, na wokovu wetu katika kipindi cha mateso.
3Watu wamekimbia kwa kusikia sauti kubwa; uliponyanyuka, mataifa yametawanyika,
4Mateka wako wamejikusanya kama mkasanyiko wa nzige; kama nzige warukavyo, watu wataruka juu yake.
5Yahwe ameinuliwa. Anaishi mahali pa juu. Ataijaza Sayuni kwa haki na usawa.
6Atakuwa imara katika kipidi chenu, wingi wa wokovu, busara, na maarifa; hofu ya Yahwe iko katika hazina yake.
7Tazama, mashujaa wanalia mtaani; wajumbe wa Amani wanallia kwa uchungu.
8Barabara kuu imeachwa faragha; hakuna wasafiri tena. Maagano yamevujika, mashahidi wanadharaulika, na utu wa mtu hauheshimiki.
9Nchi imeomboleza na kunyaukia mbali; Lebanoni inaibisha na kunyaukia mbali; Sharoni imekuwa kama jangwa wazi; Bashani na Kermeli zimepuputisha majani yake.
10“Sasa nitanyanyuka,” asema Yahwe; “sasa nitanyanyuliwa juu; sasa nitainuliwa.
11Utashika mimba ya makapi na utazaa mabua; na punzi yako ni moto ambao utakuunguza wewe.
12Watu watachomwa na kuwa kama chokaa, kama miiba ya porini inavyokatwa na kuchomwa.
13Enyi mlio mbali sana, sikiliza nilicho kifanya; na enyi mlio karibu, kirini ukuu wangu.”
14Watenda dhambi wa Sayuni wanogopa; tetemeko limewakuta wasio na Mungu. Ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto mkali? Na ni nani miongoni mwetu anayeweza kukaa kwenye moto wa milele?
15Nyie mnaotembe katika haki na kuongea kwa uaminifu; yeye anayedharau mapato ya ukandamizaji, yeye anayekataa kuchuka rushwa, ambaye hausiki kwenye kupanga vurugu za kihalifu, na ambaye haangali maovu-
16Ataiweka nyumba yake juu; sehemu yake ya ulinzi itakuwa ni ngome ya mwamba; chakula na maji yake hayataisha.
17Macho yako yatamuona mfalme katika uzuri wake; watatazama nchi kubwa.
18Moyo wako utakumbuka hofu; yuko wapi mwandishi, yuko wapi yule aliye pima pesa? Na yuko wapi yeye ahesabuye minara?
19Hautawaona watu wanaopinga, watu wenye lugha ya ajabu ambayo hautaweza kuielewa.
20Itazame Sayuni, mji wa sikukuu yetu; macho yako yataiona Yerusalemu kama makao tulivu, hema ambalo halitatolewa, vigingi vyake havitatolewa wala kamba zake hazitakatika.
21Badala yake Yahwe katika ukuu wake atakuwa pamoja na sisi, katika eneo la maji mengi na mifereji mingi. Hakuna manuari na mpiga makasia watakayepita hapo, na hakuna mashua itakayopita uko.
22Maana Yahwe ni hakimu wetu, Yahwe ni mwanasheria wetu, Yahwe ni mfalme wetu; atatukomboa sisi.
23Kamba zako zimelegea; haziwezi kushika mlingoti katika eneo lake; haziwezi kuzunguka meli; pindi mateka wanavyogawanyika, hata vilema watawatoa nje kama mateka.
24Na wenyeji watasema, “Ninaumwa;” watu wanaoishi pale watasamehewa maovu yao.

34

1Njooni karibu enyi mataifa, sikilizeni na muwe makini, enyi watu! Dunia na vyote vijazavyo vinatakiwa kusikiliza, dunia na vyote vitokavyo,

2Maana Yahwe ana hasira na mataifa yote, ana hasira dhidi ya majeshi yao; amewaangamiza wao kabisa, ameawakabidhi kwa wachinjaji.
3Miili ya watu wao waliokufa itatupwa nje. Harufu ya miili iliyokufa itakuwa kila mahali; na mlilima italowekwa kwa damu yao.
4Nyota zote angani zitafifia, na anga litakunjwa kama kitabu; na nyota zake zitafifia mbali, kama tawi linavyonyauka kwenye mzabibu, kama tunda lilokomaa kwenye mti.
5Maana pale upanga wangu utakapokunywa na kushiba mbinguni; tazama, maana sasa utakuja chini huko Edomu, kwa watu ambao nimewaweka mbali na adhabu.
6Upanga wa Yahwe unadondosha matone ya damu na kufunikwa kwa mafuta, matone ya damu ya kondoo na mbuzi, yamefunikwa kwa figo za kondoo. Maana Yahwe ametoa sadaka katika Bozra na mauwaji katika nchi ya Edomu.
7Ng'ombe wa porini watachinjwa pamoja na wao, fahali wakubwa na fahali wadogo. Nchi yao italewa kwa damu, na mavumbi yake yatafanjwa kuwa mafuta na mafuta yaliyonona.
8Maana itakuwa ni siku ya kisasi kwa Yahwe na mwaka ambao anawalipa kwa sababu ya Sayuni.
9Mifereji ya Edomu itageuka kuwa lami, na mavumbi yake yatakuwa kiberiti na nchi itakuwa kama lami inayoungua.
10Itaungua usiku na mchana; moshi wake utatoka daima; na patakuwa nyika kizazi hata kizazi; na hakuna hata mmoja atakayepita hapo milele na milele.
11Lakini ndege na wanyama porini wataishi pale; bundi na kunguru watatengeneza viota vyao pale. Atanyoosha juu yake futi kamba ya uharibifu na kupima maji ya uharibifu.
12Wenye vyeo hawatakuwa na kitu kilichobakia kuita ufalme, na wakuu wote watakuwa si kitu.
13Miiba itaota katika maeneo yao, viwavi na mbigiri vitakuwa katika ngome zao. Yatakuwa makao ya mbweha, makazi ya mbuni.
14Wanyama wa porini na fisi watakusanyika pale, na mbuzi wa porini watalia wao kwa wao. Nyakati za usiku wanyama watakaa pale na watajitafutia wenyewe mahali pa kupumzikia.
15Bundi watatengeneza viota vyao, na kutotolea mayai yao, kila mmoja na mwenzake.

16Kutafuta kupitia kitabu cha Yahwe; hakuna hata kimoja ambacho hakitakuwepo. Hakuna kitakacho kosa mwenzake; maana mdoma wake umeamuru hivyo, roho yake imewakusanya wao.
17Atapiga kura katika eneo lao, na mkono wake umewapima kwa kamba. Wataimiliki daima; kutoka kizazi hata kizazi wataishi pale.

35

1Jangwa na Arabu watafurahia; na jangwa litafurahia na kuchanua. Kama waridi,

2Yatachanua kwa wingi na yatashangilia kwa furaha na nyimbo; litapewa utukufu wa Lebanoni, mapambo ya Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Yahwe, mapambo ya Mungu wetu.
3Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, na badala ya magoti yanayotingishika.
4Waambie wenye moyo wa uwoga, “Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.”
5Halafu macho ya vipofu yataona, na masikio ya viziwi yatasikia.
6Halafu kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wa bubu utaimba, maana maji yatabubujika Araba, na mifereji jangwani.
7Mchanga ulioungua utakuwa kisima, na aridhi iliyo na kiu itakua chemchem; katika makazi mbweha, pale waliopokuwa wanaishi, kutakuwa na nyasi pamoja na mianzi.
8Barabara kuu itaitwa Njia takatifu. Wasio safi hawatasifiri kwa kutumia njia hiyo. Lakini itakuwa kwa ajili ya mtu yeyote anayetembea juu yake. Hakuna mjinga atakayeipitia.
9Hakuna simba pale, wala mnyama mkali katika barabara hiyo; hawatakuwepo kabisa pale, lakini waliokombolewa watapita pale.
10Fidia ya Yahwe itarudi na itakuja kwa wimbo wa Sayuni, na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao; furaha na shangwe vitawazidi wao; huzuni na magonjwa yataondoshwa mbali.

36

1Katika mwaka wa kumi na nne wa mfalme Hezekia, Senacherebi, mfalme wa Asiria, alivamia miji yote ya Yuda na kuwakamata.2Halafu mfalme wa Asiria akamtuma kamanda mkuu na jeshi kubwa kutoka Lachishi mpaka Yerusalemu kwa mfalme Hezekia. Alipofika kwenye mfereji katika kisima cha juu, katika njia kuu na katika shamba la dobi na akasimama pale.3Maofisa wa Israeli waliotumwa kuzungumza nao walikuwa ni Eliakimu mwana wa Hilkia, kiongozi wa jumba, Shebna katibu wa mfalme, na Joa mwana wa Asapha, anayeandika makubaliano ya serekali.

4Kamanda mkuu wa jeshi akawaambia wao, “Mwambieni Hezekia kwamba mfalme mkuu, mfalme Asiria, asema, ‘Nini chanzo cha ujasiri wako?5Unaongea maneno yasiyo na maana tu, nasema kama kuna shauri na nguvu za vita. Sasa ni nani unayemuamini? Na ni nani aliyekupa ujasiri wa kuniasi mimi.6Tazama, umeweka imani yako Misri, maana banzi la mwanzi unalolitumia kama fimbo ya kutembelea, ikiwa mtu ataiegemea na kuishika kwenye mkono wake itamchoma. Hivyo ndovyo jinsi Farao mfalme wa Misri alivyo kwa yeyote anayemuamini.7Lakini ikiwa utasema nami, “Tunamwamini Yahwe Mungu wetu,” Je sio yeye ambaye Hezekia ameondosha mahali palipoinuka na madhabahu, asema kwa Yuda na Yerusalemu, “Lazima tuabudu mbele ya madhabahu hii katika Yerusalemu”?

8Hivyo sasa, nataka kukufanya wewe kuwa zawadi nzuri kwa Bwana mfalme Asiria. Nitakupa farasi elfu mbili, kama utaweza kuwatafutia dereva.9Ni kwa jinsi gani unaweza kumpinga moja kati ya nahodha aliye mdogo katika watumishi wa Bwana wangu? Mmeweka imani yenu Misri katika gari na farasi!10Halafu sasa, Je nimewezaje kusafiri mpaka hapa pasipo Yahwe kupigana dhidi ya nchi hii na kuhiaribu? Yahwe asema nami, Vamia nchi hii na uiharibu.

11Halafu Eliakimu mwana wa Hilkia, na Shebna na Joa asema kwa kamanda mkuu, Tafadhali zungumza na watu wako kwa lugha ya kiashuru, maana kiashuru tunakielewa. Usiongee na sisi kwa lugha kiyahudi katika masikio ya watu ambao wako ukutani.”

12Lakini kamanda mkuu akasema, “Je, bwana wenu ametuma kwa bwana wako na kuzungumza haya maneno? Je hajanituma kwa watu walio kaa kwenye ukuta, ili wale kinyesi chao mwenyewe na kunywa mkojo wao mwenyewe?

13Halafu kamanda mkuu akasimama na kupiga kelele kwa sauti kubwa kwa lugha ya kiyahudi, na akisema,14“Mfalme asema, ‘Msimruhusu Hezekia awadanganye ninyi, maana hataweza kuwaokoa ninyi.15Msimruhusu Hezekia awafanye mumuamini Yahwe, Nawambieni Hakika Yahwe atatukomboa sisi; mjii huu hautachukuliwa na mfalme wa Asiria.”

16Msimsikilize Hezekia, maana hivi ndivyo mfalme wa Asiria anavyosema: ‘Fanyeni amani na mimi na mje kwangu. Halafu kila mmoja wenu atakula kwenye mzabibu wake mwenyewe na tunda la mti wake mwenyewe, na kunjwa maji ya kisima chake mwenyewe.17Mtafanya hivi mpaka nije kuwachukua na kuwapeleka kwenye nchi kama ya kwenu. Nchi ya mavuno na mvinyo mpya, nchi ya mkate na shamba.

18Msimruhusu Hezekia awapotoshe nyie, akisema, Yahwe atatuokoa nyie; Je, kuna miungu ya aina yeyote ya watu iliyowakomboa kutoka mikononi mwa mfalme wa Asiria?19Wako wapi miungu wa Hamathi na Arpadi? Iko wapi miungu ya Sefarvaimu? Je, wameikomboa Samaria kutoka kwenye nguvu zangu?20Miongoni mwa miungu yote ya nchi hii, Je kuna miungu ya aina yeyote iliyoikomboa nchi yao kutoka kwenye nguvu yangu, ni kama Yahwe anaweza kuawokoa Yerusalemu kutoka kwenye nguvu yangu?”

21Lakini watu wanabaki kimya na hawataki kujibu, maana amri ya mfalme ilikuwa, “Msimjibu.”

22Halafu Eliakimu mwana wa Hilkia, yeye aliye juu ya kaya, Shebna mwandishi, na Joa mwana wa Asafu, na mtunza kumbukumbu, walikuja kwa Hezekia na nguo zilizotoboka na wakapeleka maneno ya kamanda mkuu.

37

1Ikawa siku hiyo mfalme Hezekia aliposika taarifa zao, alichana mavazi yake, na kujifunika nguo za magunia, na akaenda kwenye nyumba ya Yahwe.2Na alimtuma Eliakimu, ambae ni kiongozi wa kaya na Shebna mwandishi, na wazee wa makuhani, wote walijifunika nguo za magunia, kwa Isaya mwana wa Amozi, nabii.3Wakamwambia yeye, Hezekia akasema hivi, ‘Siku hii ni siku ya dhiki, kukemewa, na aibu, ni kama mwana aliye tayari kuzaliwa lakini mama yake hana nguvu za kumsukuma mwana.4Itakuwa Yahwe Mungu wenu atasikia maneno ya kamanda mkuu, ambao mfalme wa Asira Bwana wake alimtuma kumpinga Mungu anayeishi, na atakemea maneno ambayo Yahwe Mungu wenu ameyasikia. Sasa inueni maombi yenu juu mabaki yaliyoobakia hapa.”

5Sasa watumishi wa mfalme Hezekia walikuja kwa Isaya,6na Isaya akawambia, “Mwambieni Bwana wenu: ‘Yahwe amesma, “Msiogope kwa maneno mliyoyasikia, maneno ambayo mfalme wa Asiria amenitusi mimi.7Tazama nitaiweka roho yangu ndani yake na atasikiliiza taarifa fulani na atarudi kwenye nchi yake mwenyewe. Na nitamfanya anguke kwa upanga katika nchi yake mwenyewe.”

8Basi kamanda mkuu alirudi na kumkuta mfalme wa Asira anapigana dhidi ya Libna, Maana aliskia kwamba mfalme amekwenda mbali kutoka Lachishi.

9Halafu Sennacheribi alisikia kwamba Tirkhaka mfalme wa Ethiopia na Misri wamehamasishana kupigana dhidi yake. Hivyo akamtuma mjumbe mara nyingine kwa Hezekia apeleke ujumbe:

10“Mwambie Hezekia, mfalme wa Yuda, ‘Usimruhusu Mungu unayemwamini akudanganye, “Yerusalemu haitatiwa mikononi mwa mfalme wa Asiria.”11Umesikia kitu ambacho mfalme wa Asiria alichokifanya kwa nchi yote kwa kuiangamiza kabisa. Je, utawaokoa?12Je, miungu ya mataifa imewakomboa? Taifa ambalo baba yangu aliliangamiza: Gozani, Harani, Rezefi na watu wa Edeni katika Telassari?13Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, mfalme wa miji ya Sefarvaimi, wa Hema na Ivva?”

14Hezekia alipokea barua hii kutoka mikononi mwa mjumbe na kisoma. Halafu akaenda juu kwenye nyumba ya Yahwe na kuusoma mbele yake.15Hezekia alimuomba Mungu:16Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, wewe ambae uko juu ya makerubi, wewe ni Mungu mwenywe juu falme zote za dunia. Umezifanya mbingu na nchi.17Geuza masikio yako, Yahwe, na sikiliza. Fungua macho yako, Ee Yahwe na uone, na usikilize maneno ya Sanacheribi, ambayo ameyatuma kumfanyia mzadha Mungu anayeishi.

18Ni kweli Yahwe, mfalme wa Asiria ameangamiza mataifa yote na aridhi yao.19Wameiweka miungu yao katika moto, maana haikuwa miungu lakini kazi ya mikono ya wanadamu, ni kuni na jiwe tu.20Hivyo Waasiria wamewaangamiza wao. Hivyo saa Yahwe Mungu wetu, tuokoe kwa nguvu zako, ili falme zote za duniani zijue kwamba wewe ni Yahwe peke yako.”

21Basi Isaya mwana wa Amozi alituma ujumbe kwa Hezekia, na kusema, Yahwe Mungu wa Israeli amesema, Kwa sababu umeomba kwangu kuhusu Sannacheribi mfalme wa Asiria,22Haya ndiyo maneno ambayo Yahwe amezungumza kuhusu yeye, “Binti bikira wa Sayuni wanakudharau na kukucheka kwa dharau; mabinti wa Yerusalemu wanatingisha vichwa vyao kwa ajili yako.
23Ni nani unayempinga na kumtusi? Na dhidi ya nani unayenyanyua sauti yako na kunyanyua macho yako kwa kiburi? Dhidi ya mtakatifu wa Israeli.
24Kwa kupitia watumishi wako umempinga Bwana na amesema, ‘Kwa wingi wa gari nimepanda juu kwenye kilele cha milima, katika kilele cha mwuinuko wa Lebanoni. Nitaikata mierezi yake na kuchagua miti ya miseprasi pale, ni msitu uzao sana.
25Nimechimba kisima na kunywa maji; nimechimba mito yote ya Misri chini ya nyayo za miguu yangu.’
26Je, haujasikia jinsi nilivyoamua toka siku nyingi na nimelifanyia kazi toka kipindi cha kale? Ninayaleta sasa ili yaweze kutimia. Mko hapa kuhiaribu miji imara na yenye ulinzi wa kutosha na kuwa chungu cha uharibifu.
27Wakazi wake, waliowadhaifu, waliokata tamaa na wenye aibu. Wanaotesha shambani, majani mabichi, majani juu paa au kwenye shamba kabla ya upepo wa mashariki.
28Lakini najua kukaa kwenu chini, kutoka kwenu nje, mnapoingia ndani, na mnapokuwa wakali dhidi yangu.
29Kwa sababu mnakuwa wakali dhidi yangu, maana kiburi chenu kimeyafikia masikio yangu, Nitaweka ndoano katika pua zenu, na sauti katika midomo yenu; Nitawageuza nyuma kwenye njia mliyokuja nayo.

30Hii itakuwa wimbo kwenu: mwaka huu mtakula kinachoota porini na mwaka pili mtakula kinachoota hapo hapo. Lakini mwaka wa tatu lazima mpande na mvune, pandeni mizabibu na mle matunda yake.
31Mabaki ya nyumba ya Yuda ambao wanaishi watachukua mzizi tena na kuzalisha matunda.
32Maana katika Yerusalemu waliobaki watatoka; Kutoka kwenye mlima Sayuni waliobaki watakuja. Bidii ya Yahwe wa majeshi itafanikisha hili.”

33Hivyo basi Yahwe asema hivi kuhusu Asiria: “Atakuja katika miji, wala kurusha mkuki hapa. Wala atakuja hapa mbele kwa ngao au kujenga uzio njia panda dhidi yao.
34Njia atakayojia itakuwa njia hiyo hiyo atakayorudia; ataingia katika mji huu. Hili ni Tamko ya Yahwe.
35Maana nitaulinda huu mji na kuuokoa, kwa niaba yangu mimi mwenyewe na kwa niaba Daudi mtumishi wangu.”

36Halafu malaika wa Yahwe alienda nje na kuvamia kambi ya Waasiria, na kuwauwa askari 185,000. Watu walipoamka asubuhi na mapema, miili iliyokufa imelala kila mahali.37Hivyo Sennacheribi mfalme wa Asiria aliiacha Israeli na kwenda nyumbani na akakaa Ninawi.

38Baadaye, na alipokuwa anabudu katika nyumba ya Nisrochi mungu wake, mwana wake Adramaleki na Shareza alimuua kwa upanga. Halafu wakakimbilia kwenye nchi ya Ararati. Halafu Esarhadoni mwana wake akatawala katika sehemu ya baba yake.

38

1Siku zile Hezekia alikuwa anaumwa karibia na kufa. Hivyo Isaya mwana wa Amozi, nabii alikuja kwake na kumwambia, “Yahwe amesema, ‘panga mambo yako maana utakufa, hautaishi.’

2‘Halafu Hezekia akaugeukia ukuta na akamuomba Yahwe.3Na akasema, “samahani Yahwe, kumbuka jinsi nilivyoenenda kwa uaminifu mbele zako kwa moyo wangu wote, na jinsi nilivyofanya matendo mema katika macho yako.” Na Hezekia akalia kwa sauti.

4Basi neno la Yawe likamjia Isaya, na kusema,5“Nenda ukamwambie Hezekia, kiongozi wa watu wangu, “Hivi ndivyo Yahwe, Mungu wa Daudi babu yenu, amesema: Nimeyasikiliza maombi yako, na nimeyaona machozi yako. Ona ninakaribia kuongeza miaka kumi na tano katika maisha yako.6Na nitakukomboa wewe pamoja mji huu kutoka kwenye mkono wamfalme wa Asiria, na nitaulinda huu mji.

7Na hii itakuwa alama kwako kutoka kwangu, Yahwe, kwamba nitafanya nilichokisema.8Angalia, nitasababisha kimvuli katika nyumba ya Ahazi kwenda nyuma hautua kumi.” Hivvyo basi kivuli kilirudi nyuma hatua kumi juu ya nyumba iliyopanda juu.

9Haya ndiyo maandishi ya maombi ya Hezekia mfalme wa Yuda, alipokuwa anaumwa halafu akapona:
10“Nimesema kwamba nusu ya maisha yangu nitapita katika mlango wa kuzimu; Nilitumwa pale miaka yangu yote.
11Nikasema sitamuona tena Yahwe, Yahwe kaika nchi ninayoishi; sitaangalia watu tena au wenyeji wa dunia hii.
12Maisha yangu yameondolea na kupelekwa mbali na mimi kama hema la mchungaji; Niliyakunja maisha yangu juu kama mfumaji; ameniondoa katika kifungo; kati ya mchana na usiku ameyakomesha maisha yangu.
13Nililia mpaka asubuhi; kama simba anaivunja mifupa yangu. Kati ya usiku na mchana ameyakomesha maisha yangu.
14Kama mbayuwayu ndivyo nilivyolia; nililia kama njiwa; macho yangu yalichoka kuangalia juu. Bwana ninateseka; nisaidie mimi.
15Niseme nini? Wote wameongea na mimi na amefanya hivyo; Nitatembea taratibu miaka yangu yote maana ninayashinda kwa huzuni.
16Bwana, mateso uliyoyatuma ni mazuri kwangu; ikiwezekana nirudishiwe tena maisha yangu; umeyahifadhi maisha maisha yangu na afya yangu.
17Ni kwa faida yangu kwamba nimepitia huzuni kama hii. Umenikomboa kutoka kwenye shimo la uharibifu; maana umetupa dhambi zangu nyuma yako.
18Maana kuzimu hapata kushukuru wewe; kifo hakikusifu wewe; wale wote waendao ndani ya shimo hawana matumaini ya uaminifu wako.
19Mtu anayeishi, mtu anayeishi, ndiye anayekushukuru wewe, kama ninavyofanya leo; baba atawjulisha watoto uaminifu wako.
20Yahwe anakarbia kunikomboa mimi, na tutasherekea kwa mziki siku zote za maisha yetu katika nyumba ya Yahwe.”

21Sasa Isaya alisema, “Waacheni wachukue donge mitini na kuliweka kweye jipu naye atapona.

22“Hezekia pia alisema, “Je, ni ishara gani ya kwamba nitapanda niingie nyumbani mwa Yahwe?”

39

1Katika mda ule Merodaki mwana wa Baladani, mfalme wa Babeli, alituma zawadi na barua kwa Hezekia; maana alisikia Hezekia alikuwa anaumwa na amepona.2Hezekia alifurahishwa na hivi vitu; alimuonyesha mjumbe nyumba ya ghala la vitu vya thamani- vitu kama fedha, dhahabu, viungo, na mafuta ya thamani, ghala la kuwekea silaha zake, na vitu vyote vilivyopatikana kwenye stoo yake. Hapakuwa na kitu katika nyumba yake, wala ufalme wake wote, Hezekia hakuwaonyesha wao.

3Basi Isaya nabii alikuja kwa mfalme Hezekia na kumuuliza, “Je watu hawa wamekuambia nini? Wametoka wapi?” “Wamekuja kwangu kutoka mbali nchi ya Babeli.”

4Isaya akamuuliza je ni vitu gani walivyoviona katika nyumba yako? Hezekia akajibu, “Wameona kila kitu katika nyumba nyangu. Hakuna kitu miongoni mwa vitu vyangu vya thamani ambavyo sijawaonyesha.”

5Basi Isaya akamwambia Hezekia, “Sikiliza neno la Yahwe wa majeshi:6‘Tazama siku inakaribia kuja pale kila kitu katika nyumba yako, vitu ambavyo mababu zako wamevihifadhi mbali mpaka mda huu wa sasa Vitapelekwa Babeli. Hakuna kitakachobakizwa, asema Yahwe.7Na watoto watazaliwa kutoka kwako, ambao wewe mwenyewe utawazaa- watachukuliwa mbali, na watakuwa matoashi katika jumba la mfalme wa Babeli.”

8Basi Hezekia akamwambia Isaya, “Neno la Yahwe alilolizunumza ni zuri.” Maana alifikiria, “Patakuwa na amani na utulivu katika siku zangu.”

40

1“Faraja, faraja watu wangu,” amesema Mungu.

2“Ongea kwa upole kwa Yerusalemu; na tangaza vita vimeisha, maana maovu yao yamesamehewa, maana alipokea mara mbili kutoka kwa mkono wa Yahwe kwa dhambi zao.”
3Sauti inalia nje, “Katika jangwa tengeneza njia ya Yahwe; njoosha njia ya Araba katika njia kuu ya Mungu.”
4Kila bonde litanyanyuliwa juu, kila mlima na kilima kitasawazishwa; na aridhi ya mwinuko itasawazishwa, mahali palipokwaruzwa patakuwa na usawa;
5na utukufu wa Mungu utafunuliwa, na watu wote wataona kwa pamoja; maana mdomo wa Yahwe umezungumza.
6Sauti inasema, “Lia.” Jibu lingine, “Kwa nini nilie?” “Mwili wote ni nyasi na maagano yaliyoaminika ni kama ua kwenye shamba.
7Nyasi zinanyauka na maua yanaperuka pale Yehwe atakapo puliza punzi yake juu yake; hakika ubinadamu ni nyasi.
8Nyasi hunyauka, maua hupepea, lakini neno la Yahwe litasimama daima.”
9Nenda juu ya mlima mrefu, Sayuni, mbeba taarifa njema. Waambie miji ya Yuda, “Hapa ni Mungu wako!”
10Angalia, Bwana Yahwe anakuja kama mpiganaji shujaa na jeshi imara linatawa juu yake. Ona, zawadi yako iko kwake, na wale walikombolewa wataenda mbele yake.
11Atalilisha kundi lake kama mchungaji, Atawakusanya kondoo katika jeshi lake, na kulichukua karibu na moyo wake, kwa upole atawongoza wake kuwauuguza watoto wao.
12Ni nani aliyepima maji ya mashimo kwa mkono wake, anayepima anga kwa urefu wa mkono wake, na kuweka vumbi za nchi katika kikapu, kupima milima kwa mizani, au vilima kwa usawa?
13Ni nani aliyeelewa akili za Yahwe, au kumuelekeza yeye kama mshauri?
14Ni kutka kwa nani alipokea maelekezo milele? Nani alikufundisha njia sahihi ya kufanya vitu, kumfundisha yeye maarifa, au kumuonyesha njia ya ufahamu?
15Tazama, Mataifa ni kama tone katika ndoo, na kama mavumbi kwenye mizani; ona, na alipima kisiwa kama tundu.
16Lebanoni sio mafuta ya kutosha, wala wanyama pori wake hawatoshi kwa dhabihu ya kuteketezwa.
17Mataifa yote hayatochelezi mbele yake; wanachukuliwa na yeye kama hakuna kitu.
18Ni nanibasi utayemlingalisha na Mungu? Ni kwa sanamu ipi utakayomfananisha nayo?
19Sanamu! Ambayo fundi ameitupa: Mfua dhahabu ameka pamoja na mikufu bandi ya fedha.
20Kuafanya sadaka hii mtu atachagua kuni ambayo haiozi; anamtafuta fundi mwenye ujuzi wa kutengeneza sanamu ambayo haitaanguka.
21Je hamkujua? Je hamjasikia? Je hamkuambiwa tokea mwanzo? Je hamkuelewa toka misingi ya nchi?
22Yeye ndiye aketie juu ya upeo wa macho ya nchi? Na wenyeji wake ni kama panzi mbele yake. Akijinyoosha nje ya mbingu ni kama pazia na kutawnya nje kama hema la kuishi.
23Anawapunguza viongozi kuwa si kitu na amewafanya viongozi wa nchi kwa sio wenye umuhimu.
24Tazama wamekuwa wagumu kuotesha; tazama wamekuwa wagumu kupanda; imekuwa ni vigumu kuchukua mzizi katika nchi, kabla ajapuliza juu yao, na wakanyauka, na upepo unawaondosha mbali kama majani.
25Ni nani tena utakayemfananisha na mimi, ni nani ninayefanana naye?” amesema mtakatifu.
26Tazama juu kwenye anga! Nani aliyeziumba nyota hizi zote? Analileta nje jeshi na anawaita kwa majina yote. Kwa ukuu wa nguvu zake na kwa uimara wa nguvu zake, hakuna hata mmoja atakayekosa.
27Kwa nini unasema, Yakobo, na kutangaza, Israeli, “Njia yangu imefichwa Yahwe asione, na Mungu wangu hakuwekwa wazi kuhusiana na uthibitisho wangu”?
28Je hakufahamu? Mungu wa milele, Yahwe, Muumbaji wa miisho ya nchi, apatwi na uchovu wala hachoki; hakuna mipaka katika ufahamu wake.
29Anawapa nguvu waliochoka; na atawapa nguvu mpya waliowadhaifu.
30Hata vijana wadogo watapatwa na uchovu na kuchoka, vijana wadogo watapata mashaka na kuanguka:
31Lakini wale watakao mngojea Yahwe watapewa nguvu mpya; na watapaa kwa mabawa kama tai; watakimbia wala hawatachoka; watatembea wala hawatazimia.

41

1“Sikilizeni mbele yangu kwa ukimya, enyi mkao pwani; wacha mataifa yapate nguvu kwa upya; waache waje karibu na kuzungumza; na tusogee karibu tujadili mgogoro.

2Nani aliyechochea juu mmoja kutoka mashariki, anamuita katika haki yake kwenye huduma yake? Amemkabidhi mataifa juu yake ili amsaidie yeye kuwaangamiza wafalme. Aliwageuza kuwa mavumbi kwa neno lake, kama upepo unaovuma kwenye mabua kwa upinde wake.
3Aliwachukua wao na kuwapitisha salama, katika njia nyepesi ambayo miguu yake imegusa shida.
4Ni nani aliyeyafanya na kukamilisha matendo haya? Ni nanialiye chagua kizazi kutoka mwanzo? Mimi, Yahwe ni mwanzo na mwisho, mimi ndiye.
5Visiwa vimeona na kuogopa; miisho ya dunia yatetemeka; walikaribia n kuja.
6Kila mmoja amsaidie jirani yake, na kila mmoja asemezane na mwenzake, ‘Kuwa mfariji.’
7Hivyo basi seremala anamfariji mfua dhahabu, na yule anayefanya kazi kwa kutumia nyundo anamfariji anayefanya kazi kwa chuma, akisema kwa msemo wa kurehemu, “Ni mizuri; Naye ataupigilia kwa makini misumari ili isipinduke.
8Lakini wewe, Israeli mtumishi wangu, Yakobo niliyekuchagua, mwana wa Ibrahimu rafiki yangu,
9wewe ambaye ninakurudisha kutoka miisho ya nchi, na ambaye niliyekuita kutoka sehemu ya mbali, na kwako niliyekuambia, ‘Wewe ni mtumishi wangu;’ Nimekuchagua wewe na sijakukataa.
10Usiogope maana mimi niko pamoja na wewe. Usiwe na wasiwasi, maana mimi ni Mungu wako. Nitakutia nguvu, na nitakusaidia, wewe, na Nitakushika kwa mkono wa haki yangu.
11Tazama, watakuwa na aibu na hawataheshimiwa, wale wote waliokuwa na hasira na wewe; watakuwa si kitu na watatokomea, wale watakao kupinga wewe.
12Utawatafuta na wala hautawapata wale wanaopingana na wewe; wale wafanyao vita dhidi yako watakuwa kama si kitu, si kitu kabisa.
13Maana mimi Yahwe Mungu wako, nitawashika mkono wako wa kiume, nikikuambia wewe, ‘Usiogope; Nitakusaidia wewe.
14Usiogope, Yakobo wewe mdudu, na enyi watu wa Israeli; Nitawasaidia”- hili ni tamko la Yahwe, Mkombozi wako, Mtakatifu wa Israeli.
15Tazama, ninakufanya wewe kuwa chombo kikali cha kuparulia chenye makali pande mbili; utaparua milima na kuiponda; utafanya vilima kama makapi.
16Utawatawanya wao, na upepo utawabeba na kuwapeka mbali; upepo utawatanya wao. Utashanglia katika Yahwe, utashangiliakatika mtakatifu wa Israeli
17Waliodhulumiwa na masikini wanatafuta maji, lakini hakuna kitu, ndimi zao zimekauka kwa kiu; Mimi Yahwe, nitajibu maombi yao; Mimi Mungu wa Israeli, sitawacha wao.
18Nitatengeneza mikondo ya maji kushusha chini, na chemichem katikati ya mabonde; nitalifanya jangwa kuwa kisima cha maji, na aridhi kavu kuwa chemichem ya maji.
19Katika jangwa nitapanda mierezi, mshita, mhadisi, na mti wa mizeituni. Nitaotesha mberoshi katika uwazi wa jangwa, pamoja na mbono nitapanda mberoshi kitika jangwa lililo wazi.
20Nitayafanya haya ili waweze kuona, kutambua na kuelewa kwa pamoja, kwamba mkono wa Yahwe umetenda haya, kama Mtakatifu wa Israeli aliyeliumba.
21“Wakilisha keshi yako,” asema Yahwe; “wakilisha hoja zenu nzuri kwa sanamu yenu,” asema Mfalme wa Yakobo.
22Waache walete hoja zao wenyewe; waache waje mbele na watutangazie sisi nini kitakachotokea, ili tuweze kuelewa haya mambo vizuri. Tuwaache watupe tamko mapema, ili tuweze kulitafakari na tuweze kujua n kwa jinsi gani litatimia.
23Wajulishe kitu kuhusu baadaye, ili tujue kuwa ninyi ni miungu; fanya kitu kizuri au kibaya, ambacho kitatutisha na kutushangaza.
24Tazama sanamu zenu si kitu na matendo yenu si kitu; aliyewachagua ni machukizo.
25Nimemnyanyua mmoja kutoka kaskazini, naye amekuja kutoka mawio ya jua nimemchagua yeye alitajae jina langu, na atawakanyaga viongozi kama matope, kama mfinyanzi akanyagavyo udongo.
26Ni nani aliyetangaza hili tangu mwanzo, ili tuweze kujua? Na kabla ya mda, ili tuseme, “Yuko sawasawa”? Kweli hakuna hata mmoja aliyekiri hili, ndio hakuna hata mmoja aliyekusikia ukisema chochote.
27Kwanza nilizungumza na Sayuni, “Tazama hapo walipo;” Nimemtuma mhubiri Yerusalemu.
28Nilipoangalia, hakuna hata mmoja, hakuna hata miongoni mwao ambaye anaweza kutoa ushauri mzuri, nani, lini nimulize, awezaye kunijibu neno.
29Tazama, matendo yao si kitu; sanamu zao za chuma zilizotupwa ni upepo na utupu.

42

1Tazama, mtumishi wangu, niliyekushika; niliyekuchagua, kwake ninapata furaha. Nimeiweka roho yangu juu yake; ataleta haki kwa mataifa.

2Hatalia wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika mitaani.
3Mwanzi ulioangamizwa hatauvunja, na wala utambi unaowaka na kutoa mwanga hautaungua: atatekeleza haki kwa uaminifu.
4Wala hatazimia wala kukata tamaa mpaka atakapoanzisha haki katika nchi; na pwani inasubiria sheria yake.
5Mungu Yahwe asema hivi--yeye aliyeziumba mbingu na yeye zinyoosha nje, yeye aliyeiumba nchi na vitu vyote izalishavyo, yeye aliyewapa punzi watu na wale waishio juu:
6Mimi Yahwe nimekuita kwa haki yangu na nitakushika kwa mkono wangu. Nitakutunza wewe, na nitakuweka wewe kama agano kwa watu wangu, kama mwanga wa wayunani
7Kuyafungua macho ya vipofu, kuwatoa waliofungwa gerezani, kuwatoa wale walio gizani kutoka kwenye nyumba iliyofungiwa.
8Mimi ni Yahwe, Hilo ndilo jina langu; na utukufu wangu sitashiriana na mtu mwingine wala sifa zangu sitashirkiana na sanamu ya kuchonga.
9Tazama, mambo ya nyuma yamekuja na kupita, sasa ninakaribia kutangaza mambo mapya. Kabla hayajaanza kutokea nitawambia kuhusu wao.”
10Mwimbieni Yahwe wimbo mpya, na sifa zake kutoka mwisho wa nchi; wewe ushukae chini kwenye bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, waishio pwani na wale wanaoishi huko.
11Wacha jangwa na miji ilie, vijiji anavyoishi na Kaderi, lia kwa furaha! Waache wenyeji wa Sela waimbe; waache wapige kelele juu ya kilele cha mlima.
12Waache wamtukuze Yahwe na kutangaza sifa zake katika aridhi ya pwani.
13Yahwe atatoka nje kama shujaa; kama mtu wa vita ataichochea bidii yake. Atapiga kelele, ndio, atalia kwa kishindo katika vita yake; atawaonyesha adui zake nguvu zake.
14Nimenyamaza kimya kwa mda mrefu; bado nimendelea kujizuia mimi mwenyewe; Nitalia kama mwanamke anayetaka kuzaa; nitatweta na kuugua.
15Nitaiharibu milima na vilima na kukausha uoto wake wa asili; nitajeuza mito kuwa visiwa na nitakausha matindiga.
16Nitawaleta vipofu kwa njia wasioijua; katika njia wasiyoijua Nitawapitisha wao. Nitaligeuza giza kuwa mwanga mbele yao, na kupanyoosha mahali palipopotoka. Mambo yote haya nitayafanya, na sitaachana na wao
17Watageuka nyuma, wataaibishwa sana, wale wote wanaoiamini sanamu ya kuchonga, wanaosema na kuziambia sanamu za chuma, “Nyinyi ni miungu wetu.”
18Sikilizeni ewe kiziwi; tazama, ewe kipofu, ili uweze kuona.
19Aliye kipofu ila mtumishi wangu? Au kiziwi ni kama mjumbe niliyemtuma? Ni nani aliye kipofu kama mpenzi wangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe?
20Mmeona mambo mengi, lakini hamuelewi; masikio yamefunguka, lakini hakuna anayesikia.
21Itampendeza Yahwe kuisifu haki yake na kuitukuza sheria yake.
22Lakini watu hawa ni wale waliokamatwa na kutekwa; wote wamenaswa kwenye mashimo; wafungwa wote wamewekwa gerezani; wamekuwa mateka na hakuna hata mmoja wa kuwaokoa wao, hakuna asemaye, warudisheni.”
23Ni nani miongoni mwenu atalisikiliza hili? Nani atayasikia na ni nani atasikia wakati ujao?
24Ni nani aliyemtoa Yakobo kwa majambazi, na Israeli kwa wanyang'anyi? Je, hakuwa Yahwe, dhidi ya wale waliotenda dhambi, waliokataa kutembea katika njia zako na wale waliokataa kuiheshimu sheria yako.
25Hivyo basi humwaga asira yake kali nje dhidi yao, kwa uharibifu wa vita. Iliwaka kuwazunguka wao, hata hawakujua hilo, lakini hawakuyachukulia hayo moyoni mwao.

43

1Lakini sasa haya ndio Yahwe asemayo, yeye aliyekuumba ewe, Yakobo, na yeye aliyekuumba ewe, Israeli: “Usiogope, kwa maana nimekukomboa wewe; nmeikuita kwa jina lako, wewe ni wangu.

2Utakapopita katika maji, Nitakuwa pamoja na wewe; na katika mito, hayatakuzuru wewe. Utakapotembea katika moto hautaungua, na moto hautakuharibu wewe.
3Maana mimi Yahwe Mungu wako, Mtakatifu wa Israeli Mkombozi wenu. Nimewapa Misri kama fidia yenu, Ethiopia na Seba watabadilishana kwako.
4Kwa maana ulikuwa wa thamani na maalumu katika macho yangu, Ninakupenda; kwa sababu hiyo Nitatoa watu kwa ajili yako, na watu wengine kwa ajili ya maisha yako.
5Usiogope, maana Mimi niko pamoja na wewe; Nitawarudisha watoto wako kutoka mashariki, na kuwakusanya nyie kutoka magharibi.
6Nitasema na kaskazini, ‘Wakabidhini wao; na kwa kusini, Usiangalie ya nyuma; Leteni vijana wangu kutoka mbali na binti zangu kutoka vijiji vya mikoani katika nchi,
7yeyote aitwe kwa jina langu, niliyemuumba kwa utukufu wangu mwenyewe, Niliyemuumba, ndio, Mimi niliyemfanya.
8Waleteni nje watu ambao ni vipofu, hata kama wana macho, na viziwi, hata kama wana masikio.
9Mataifa yote yatakusanyika kwa pamoja na watu watakusanyika. Ni nani miongoni mwenu atakaye tamka na kutangaza kutumia mambo ya mwanzo? Waache walete mashahidi kuwashuhudia wao kama wako sahihi, waache wasikilize na kuthibitisha, ‘kama ni kweli.’
10Ninyi ni mashahidi wangu, ametangaza Yahwe, “na watumishi wangu niliowachagua, ili uweze kujua na kuniamini mimi, na kuelewa kwamba mimi ndiye. Kabla yangu hapana mungu mwingine aliyeumbwa, na wala hatatoke baada yangu.
11Mimi, naam Mimi ni Yahwe, na hakuna Mkombozi zaidi yangu.
12Nimetangaza, nimeokoa, na kutangaza, na hakuna Mungu mwingine miongoni mwenu, Ninyi ni mashahidi wangu asema Yahwe, “Mimi ni Mungu.
13Kuanzia leo na kuendelea mimi ndiye, na hakuna hata mmoja atakayewakomboa kwenye mkono wangu. Nitafanya, na nani awezaye kunizuia?”
14Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, yeye Mtakatifu wa Israeli: “Kwa niaba yenu nimemtuma mjumbe kwenda Babeli na kuwaongoza wao wote chini kama watuhumiwa, kubadilisha kelele za furaha za watu wa Babeli’ kuwa wimbo wa maombolezo.
15Mimi ni Yahwe, niliye Mtakatifu, Muumbaji wa Israeli, Mfalme wenu.
16Yahwe asema hivi, Ni nani aliyefungua njia katika bahari, na njia katika maji yenye nguvu,
17ni nani anayeongoza gari na farasi, majeshi na jeshi kuu. Walianguka chini kwa pamoja; hawakunyanyuka tena; wamezimwa, kama utambi unaoungua.
18Msifikirie hayo mambo yaliyopita, wala kuyafikiria mambo ya zamani.
19Tazama ninakaribia kufanya mambo mapya; sasa yanakaribia kutokea; Je humyajui haya? Nitafanya njia jangwani na na mikondo ya maji katika jangwa.
20Wanyama pori wa shambani wataniheshimu mimi, Mbweha na mbuni, kwa sababu ninatoa maji jangwani, na mito jangwani, ili watu wangu niliowachuga wapate kunywa,
21Watu hawa niliowaumba mwenyewe, kwamba wahesabu tena sifa zangu.
22Lakini hamjaniita mimi, Yakobo; umechoka na mimi, Israeli.
23Haujaniletea hata kondoo wako kama sadaka ya kuteketeza; na wala haujaniheshimu mimi kwa sadaka yako. Sijakutumisha wewe kwa sadaka ya mazao, wala sijawachosha kwa sadaka yenu ya ubani.
24Hamkuninunulia mimi manukato mazuri kwa fedha, hamkunimwagia mimi mafuta ya sadaka zenu; Lakini mnanichosha mimi na dhambi zenu na mnanichosha mimi kwa matendo yenu mabaya.
25Mimi, ndio, Mimi, ndiye niyafutaye maovu yenu kwa niaba yangu mimi mwenyewe; na Sitawaita na kuwakumbusha dhambi zenu tena.
26Nikumbusheni mimi kilichotokea. Njooni tusemezane pamoja; leta hoja zako, ili kusudi uthibitishe kuwa hauna hatia.
27Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, na viongozi wenu walitenda dhambi dhidi yangu.
28Hivyo basi Nitawatia unajisi viongozi watakatifu; Nitamkabidhi Yakobo kuwaharibu kabisa, na Israeli kulaani udhalilishaji.”

44

1Sasa, sikiliza, Yakobo mtumishi wangu, na Israeli, Niliyekuchagua:

2Yahwe asema hivi, yeye aliyekufanya na kukuumba wewe katika tumbo na yeye aliye kusadia wewe: Usiogope, Yakobo mtumishi wangu; na wewe Yeshuruni, niliyekuchagua.
3Maana nitashusha mvua kwenye aridhi yenye kiu, na mikondo ya maji kwenye ardhi kavu; Nitashusha roho yangu kwa watoto wako, na baraka zangu kwa watoto wako.
4Watakuwa miongoni mwa nyasi, kama mti pembeni ya mkondo wa maji.
5Mmoja atasema, ‘Mimi ni wa Yahwe; na mwingine ataita jina la Yakobo, na mwingine ataandika kwenye mkono wake ‘Mimi ni wa Yahwe, na kujiita mwenyewe kwa jina la Israeli.”
6Yahwe asema hivi--Mfalme wa Israeli na Mkombozi wake, Yahwe wa majeshi: “Mimi ni mwanzo na ni mwisho; na hakuna mungu ila mimi.
7Ni nani aliye kama mimi? Na atangaze na anielezee matukio yaliyotokea tangu nilipoanzisha watu wangu wa kale, na waache watangaze matukio yajayo.
8Usiogope wala usifadhaike. Je, si mimi niliyekutangazia toka zamani, na nikatangaza? Ninyi ni mashaidi wangu: Je kuna Mungu mwingine zaidi yangu? Hakuna Mwamba mwingine zaidi yangu; Ninajua hakuna.”
9Mitindo yote ya sanamu si kitu; vitu wanavyo vifurahia ndani havina maana; mashahidi wake hawawezi kuona au kujua chochote, na watapatwa katika aibu.
10Ni nani atengenezaye miungu au sanamu zisizo na maana?
11Tazama, washirika wote watapatwa na aibu; mafundi ni watu tu. Waache washikilie msimamo wao kwa pamoja; wataogopa na kuaibishwa.
12Mhunzi anafanya kazi kwa vyombo vyake, kutengeneza, kufanya kazi kwenye makaa ya mawe. Hurekebisha kwa kutumia nyundo na hufanya kazi kwa mkono wake wenye nguvu. Hupata njaa, na nguvu zake humuishia; Hajanywa maji na huzimia.
13Seremala hupima mbao kwa kamba na kuiweka alama kwa kitu kikali. Huichonga kwa vyombo vyake na kuweka alama kwa kutumia dira. Huichonga baada ya sanamu ya mtu, kama mtu anayevutia, ili iweze kukaa ndani ya nyumba.
14Huikata chini mierezi, huchagua miti ya miseprasi au miti ya mialoni. Huchukua mti yeye mwenyewe katika msitu. Huotesha mvinje na mvua huifanya ikue.
15Basi mtu hutumia kwa moto na kujipatia joto. Ndio, huwasha moto kuoka mkate. Halafu hutengeneza miungu ili ausujudie;
16Huchoma sehemu ya kuni kwa moto, na huchoma nyama yake juu yake. Hula na kushiba. Huota moto na kusema, “Ah, Nimepata joto, nimeouna moto.”
17Kwa kutumia mbao hutengeneza miungu, sanamu yake; huisujudu na kuiheshimu, huipa sifa na kusema, “njoo unikoe mimi, maana wewe ni mungu wangu.”
18Hawajui, wala hawaelewi, maana macho yao yamepofuka na hawaoni, na mioyo yao haiwezi kufahamu.
19Hakuna anayefikiria, wala kuelewa na kusema, “Nimechoma sehemu ya mbao kwenye moto; na pia nimeoka mkate kwa kutumia makaa yake. Nimechoma nyama kwa makaa yake nikala. Sasa Je, ninaweza kutengeneza kitu kinachochukiza kwa ajili ya kuabudia kwa sehemu ya mbao iliyobakia? Je ninaweza kusujudia sanamu ya mbao?”
20Ni kama anayejilisha majivu; moyo wake mdanganyifu unampoteza yeye. Huwezi kujiokoa mwenyewe, wala hawezi kusema, “Hiki kitu katika mkono wangu wa kulia sio mungu wa kweli.”
21Fikiria kuhusu vitu hivi, Yakobo na Israeli, maana wewe ni mtumishi wangu: Nimekuumba wewe; wewe ni mtumishi wangu.
22Nimeyafuta makosa yako, kama wingu zito, matendo yako mabaya, na wingu, ni kama dhambi zako; maana nimekukomboa wewe.
23Imba, enyi mbingu, maana Yahwe ameyafanya haya; piga kelele enyi mkaao katika nchi. Pazeni sauti enyi mlima milima, enyi misitu yenye miti ndani yake, ewe mlima, ewe msitu wenye kila aina ya mti ndani yak; Maana Yahwe amemkomboa Yakobo, na nitakuonyesha utukufu wake katika Israeli.
24Yahwe asema hivi, Mkombozi wako, yeye aliyekuumba wewe kutoka tumboni: “Mimi ni Yahwe, niliyefanya kila kitu, mimi mwenyewe nizinyooshaye mbingu, mimi peke niitengenezaye nchi.
25Mimi niliyezikata dalili za waongo na kuwaabisha wanaosoma dalili zake; Mimi niliyezigeuza busara za wenye hekima na kugeuza ushauri wao kuwa ujinga.
26Mimi, Yahwe, niliyethibitisha maneno ya mtumishi wake na kuutimiza utabiri wa mjumbe wake. Aliyezungumza kuhusu Yerusalemu, ‘Atakuwa mwenyeji; na katika mji wa Yuda, ‘Watatengeneza tena, na nitapatengeneza palipoharibika;
27awezae kusema kwa bahari kubwa, ‘Kauka,’ na yanakauka mda huo.’
28Yahwe ndiye amwambiye Koreshi, ‘Ni mchungaji wangu, atafanya kila nilitakalo; atatoa amri kuhusu Yerusalemu, ‘Utajengwa kwa upya, ‘na kuhusu Hekalu, ‘Basi na msingi wake uanzwe kuwekwa.”

45

1Yahwe asema hivi kwa mpakwa mafuta, kwa Koreshi, niliyemshika kwa mkono wa kuume, illi niweze kuangamiza mataifa mbele yake, kuwalinda wafalme, kufunguo milango mbele yao, ili lango liwe wazi:

2“Nitakwenda mbele yako na kusawazisha milima; nitavunjavunja vipandevipande milango ya shaba na kukuta vipandevipande nguzo za chuma,
3Nitakupa hazina iliyo gizani na utajiri uliofichwa mbali, ili ujue kwamba ni mimi Yahwe, niliyekuita kwa jina lako, Mimi, Mungu wa Israeli.
4Kwa niaba ya Jakobo mtumishi wangu, na Israeli chaguo langu, Nimekuita wewe kwa jina lako: nimekupa heshima iliyotukuka, jabo hakunijua mimi.
5Mimi ni Yahwe na hapana mwingine; hakuna Mungu ila mimi. Nitakuimarisha katika vita, japo hamkunifamu mimi;
6kwamba watu wajue kutoka mapambazuko ya jua, na kutoka magharibi, kwamba hakuna mungu mwngine ila mimi: Mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
7Nimefanya mwanga na nimeumba giza; Ninaleta amani na ninaumba majanga; Mimi Yahwe, nifanyaye haya yote.
8Enyi mbingu, nyesha kutoka juu! Acha anga lishushe chini haki, na acha nchi inyonje haki, ili wokovu uweze kuchipukia juu, na haki kutawanyika kwa pamoja. Mimi Yahwe nimewaumba wote kwa pamoja.
9Ole kwa yeyote anayesema kwa yule aliyemfanya yeye, kwake yeye ni kama chungu cha udongo miongoni mwa vyingu vya udongo katika aridhi! Je, udongo umwambia mfinyanzi, ‘Unatengeneza nini? Au’ Kazi yako haina kitu cha kushika?
10Ole wake asemaye kwa baba, ‘Unanizaa nini? Au kwa mwanamke, ‘unanizaa mimi nini?’
11Yahwe asema hivi, yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, muumbaji wake: ‘Kwa nini unauliza swali kuhusu nini nitakacho kifanya kwa watoto wangu? Je, unaweza kuniambia kuuhusiana na kazi ya mikono yangu?
12Nimeifanya nchi na kuumba mtu juu yake. Ni mkono yangu mimi nilioinyoosha ju ya mbingu, na nikazimuru nyota zote kutokea.
13Nimemuinua Keroshi juu katika haki yangu, na nitalainisha njia zake zote. Ataujenga mji wangu kwa upya; atawachia walioko uhamishoni kurudi nyumbani kwao, na so kwa pesa wala kwa rushwa,” asema Yahwe wa majeshi.

14Yahwe asema hivi, mapato ya Misri na bidhaa ya Ethiopia pamoja na Waseba jamii ya watu werefu, ninawaleta kwenu. Watakuwa wa kwenu. Watafuata baada yenu, watakuja na minyororo. Watakuinamia chini na kukuomba huku wakisema, ‘Hakika Mungu yuko pamoja na wewe na hakuna mwingine ila yeye.”
15Hakika mna Mungu aliyejifisha ndani yenu, Mungu wa Israeli, Mkombozi.
16Wote wataabishwa na kuzaraliwa kwa pamoja; wale wachongao sanamu watatembea katika udhalilishaji.
17Lakini Israeli itakombolewa na Yahwe kawa wokovu wa milele; na wala hautaabika tena au kudhalilishwa.
18Yahwe asem hivi, nani aliyeziumba mbingu, Mungu wa kweli ndiye aliyeiumbwa nchi na kuifaya, ndiye aliyeianzisha nchi. Aliiumba yeye, sio kama taka, aliimba ili pawe na wenyeji: “mimi ni Yahwe, na hakuna mwingine.
19Sijaongea katika siri, katika maeneo ya siri; Sijauambia ukoo wa Daudi, ‘Nitafute bure! Mimi ni Yahwe ninayezungumza ukweli; Ninatangaza vitu vilivyo vya kweli.
20Jikusanyeni wenyewe na mje! Kusanyikeni kwa pamoja, enyi wakimbizi kutoka miongoni mwa mataifa! Hawana maarifa, wale wanaobeba sanamu ya kuchonga na kuiomba miungu asiyewasidia.
21Sogeeni karibu na mnitangazie mimi, leteni ushahidi! Waache walete mashauri kwa pamoja. Ni nani aliyewaonyesha haya kutoka zamani? Ni nani aliyetangaza? Je sikuwa mimi, Yahwe? Na hakuna Mungu mwingine ila mimi, Mungu mwenye haki; na mkombozi; hakuna mwingine zaidi yake.
22Nijeukieni mimi, na mkaokolewe, miisho yote ya nchi; Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine. Mimi mwenyewe ninaapa, ninaongea katika haki yangu, na sitarudi nyuma:
23‘kwangu kila goti litapigwa, na kila ulimi utakiri.
24Wataniambia mimi, Ni katika Yahwe peke yake kuna wokovu na nguvu.” Wataaibika wale wote wenye hasira na Mungu.
25Katika Yahwe makabila yote ya Israeli yatahalalishwa; watachukua kiburi katika yeye.

46

1Beli huanguka chini, Nebo husujudu; miungu yao imebebwa na wanyama na mzigo wa mnyama. Sanamu hizi mlizobeba ni mzigo mzito kwa wanyama kuchoka.

2Kwa pamoja wanashuka chini; hawawezi kuziokoa sanamu zao, na wao wenyewe wameenda uhamishoni.
3Nisikilizeni mimi, nyumba ya Yakobo, wote mliobaki kwenye nyumba ya Israeli mliochukuliwa na mimi kutoka kabla amjazaliwa, mlichukuliwa mkiwa tumboni.
4Hata kwa uzee wenu Mimi ndiye, mpaka mmeshapata mvi nitawachukua. Nimewaumba ninyi na nitawabeba ninyi; Nitawachukua nyie na nitawakomboa nyie.
5Je, utanifananisha mimi na nani? Na mimi nimefanana na nani, ili utulinganishe?
6Watu humwaga dhahabu kutoka kwenye mabegi yao na uzito wa fedha kwenye uzani. Humuajiri mfua dhahabu, na hutengeneza kuwa dhahabu; na huinama chini na kuzisujudu.
7Wanazinyanyua juu ya mabega yao na kuzibeba; wanaziweka katika sehemu yake, na itasimama katika eneo lake na alitasongea kutoka pale, huililia, lakini haiwezi kujibu wala kumuokoa yeyote kwenye matatizo.
8Tafakari kuhusu hivi vitu; katu usivipuuzie, enyi waasi!
9Tafakari kuhusu vitu vya awali, nyakati zile zilizopita, Maana mimi ni Mungu, na hakuna mwingine, Mimi ni Mungu na hakuna kama mimi.
10Mimi ninatangaza mwisho kutoka mwanzo, na kabla ya kitu ambacho hakijatokea; Ninasema, “Mpango wangu utatokea na nitafanya kama ninavyotamani.”
11Nitamuita ndege wa mawindo kutoka mashariki, Mtu ambaye ni chaguo langu kutoka nchi ya mbali; Ndio nimesema; na pia nitayatimiza haya, nimekusudia, na pia nitafanya hivyo.
12Nisikilize mimi, enyi watu makaidi, ambao mko mbali na kutenda mema.
13Ninaileta haki yangu karibu; na wala sio mbali, na wokovu wangu hausubiri; na nitatoa wokovu wangu kwa Sayuni na uzuri wangu kwa Israeli.

47

1Njoo chini na ukae kwenye mavumbi, binti bikira wa Babeli; kaa juu ya aridhi pasipo enzi, ewe binti wa Wakaldayo. Hautaitwa tena mpenda anasa na maisha ya anasa.

2Chukua jiwe la kusagia na usage unga; ondoa pazia lako, ondoa mavazi yako, ondoa viatu miguuni, na vuka mkondo wa maji.
3Uchi wako utafunuliwa, ndio, na aibu yako itaonekana; Nitachukua kizazi na sitamuacha mtu,
4Mkombozi, Yahwe wa majeshi ndilo jina lake, Mtakatifu wa Israeli.
5Kaa kimya na nenda katika giza, ewe binti wa Wakaldoyo; maana hautaitwa tena malikia wa falme.
6Nilikuwa na hasira na watu wangu; Nimeunajisi urithi wangu na kuwakabidhi nyie katika mkono wenu, lakini hamkuomyesha huruma; umeweka nira kubwa kwa wazee.
7Umesema, “Nitaongoza daima kama malikia huru.” Haukuvichukua vitu hivi katika moyo, wala hakutafakari jinsi hivi vitu vitakavyojeuka.
8Hivyo sasa sikiliza hili, Ewe upendae anasa na kukaa salama; ewe usemae katika moyo wako, ‘Ninaishi, na hakuna mwingine kama mimi; Sitakaa kama mjane wala sitazoea kufiwa na watoto.
9“Lakini vitu hivi vitakuja kwako siku moja katika kipindi cha siku moja; kwa nguvu za kutosha yatakuja kwako, japo uchawi wako na dua zako na hirizi.
10Umeweka imani katika mapungufu yako; na kusema, “Hakuna anayeniona mimi;” hekima na maarifa yako yanakupoteza, lakini unasema katika moyo wako, “Nipo na hakuna hata mmoja kama mimi.”
11Maafa yatakuzidi wewe; hautaweza kuyaondoa kwa dua zako mwenyewe. Uharibifu utakuwa juu yako; hautaweza kuukata. Maafa yatakuangamiza ghafla, kabla haujajua kitu.
12Endeleni kutoa uganga wako na wachawi wengi ambao mlioaminishwa kusoma toka utotoni mwao; labda utafanikiwa, labda utayashinda maafa.
13Umejaribu sana kwa kushauriwa sana; waache hao watu wasimame na kukuokoa wewe- wale wanaoangalia mbingu na wanoangalia nyota, wale wanotangaza mwenzi mpya- waache wawaokoe nyie kutoka kwenye yaliyowapata.
14Tazama, watakuwa kama mabua. Moto utayachoma juu. Hayataweza kujisaidia yenyewe kutoka kwenye mkono wa moto. Hakuna makaa kuwapa joto wao na hakuna moto uliowekwa pembeni kwa ajili yao!
15Hivi ndio wamekuwa kwako, wale unaofanya nao kazi, na unauza na kununua na wao toka ulipo kuwa mdogo, na wale wanaendelea kufanya mambo yao ya kijinga; na unapolia kuhitaji msaada, hakuna hata mmjoa ambaye atakukomboa wewe.”

48

1Sikiliza hili, nyumba ya Jakobo, mlioitwa kwa jina la Israeli, na mmetoka katika mbegu ya Yuda; yeye akiriye kwa jina la Yahwe na kumuhusisha Mungu wa Israeli, lakini sio kweli wala kwa namna ya haki.

2Maana wanajiita wenyewe watu wa mji mtakatifu na kumuamini Mungu wa Israeli; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
3“Nimetangaza mambo ya kwanza tangu mwanzo; yalitoka katika kinywa changu, na nikawafanya wajulikane; halafu ghafla nimewafanyia, na yakatimia.
4Kwa sababu nilijua kwamba wewe ni mkaiidi, misuli ya shingo yako ni kama ya chuma, na paji la uso ni kama shaba,
5Hivyo basi nilitangaza vitu hivi kabla havijatokeo hivyo, nilikujulisha wewe, ‘Sanamu yangu imefanya haya au sanamu yangu ya kuchonga na sanamu yangu ya kuyeyusha, yamekwishisha vitu.
6Umesikia kuhusu mambo haya; angalia ushahidi wote; na wewe, Je hautakubali kwamba ninacho kisema ni cha kweli? Kuanzia sasa na kuendelea Nitawaonyesha vitu vipya, mambo yaliyofichika ambayo hamkuyajua.
7Sasa, na sio yaliyopita, yamekuwa sasa, na kabla ya leo hamkusikia kuhusu wao, hivyo hautaweza kusema, ‘Ndio, nilijua kuhusu wao.’
8Haukusikia; haukuelewa; haya mambo hayakufuniliwa katika masikio kabla ya. Maana nilijua kwamba umekuwa mdanganyifu, na kwamba umekuwa muasi kutoka kuzaliwa.
9Kwa niaba ya jina langu nitahairisha asira yangu, na kwa heshima yangu nitajizuia kutokumuharibu yeye.
10Tazama, Mimi niliwaandaa ninyi, lakini sio kama fedha; Nimekusafisha wewe katika tanuru la mateso.
11Kwa niaba yangu, kwa niaba yangu nitafanya; maana ni kwa jinsi gani niruhusu jina langu lisiheshimike? Sitampa utukufu wangu mtu yeyote.
12Nisikilize mimi, Yakobo, na Israeli niliyekuita: Mimi ndiye; Mimi ni wa kwanza, na pia wa mwisho.
13Ndio, mkono wangu umeweka msingi wa nchi, na mkono wangu wa kuume ulizitawanya mbingu, zimesimama juu kwa pamoja.
14Jikusanyeni wenyewe, nyinyi nyote, na sikilizeni; ni nani miongoni mwenu atangazaye mambo haya? Yahwe atakamilisha lengo lake dhidi ya Babeli. Atachukua mapenzi ya Yahwe dhidi ya wa Wakaldayo.
15Mimi, nimezungumza, ndio, nimemchagua yeye, nimemleta yeye, na yeye atafanikiwa.

16Sogea karibu na mimi, sikiliza hili; kutoka mwanzo sikuzungumza katika siri; lakini ilipotokea, Mimi niko hapa; na sasa Bwana Mungu amenituma mimi, na Roho wake.”
17Yahwe asema hivi, Mkombozi wenu, Mtakatifu wa Israeli anasema, “Mimi ni Yahwe Mungu wenu, ninayewafundisha juu ya kufanikiwa, ninayewaonyesha njia mtakayoiptia.
18Ikiwa kama mtaheshimu amri zangu! Hivyo amani na maendeleo yatatiririka kama mto, na wokovu wenu ni kama mawimbi kwenye bahari.
19Watoto wako watakuwa wengi kama mchanga, na watoto kutoka kwenye tombo zenu watakuwa wengi kama nafaka kwenye mchanga; majina yao hayataondolewa wala kufutwa mbele yangu.
20Tokeni nje ya Babeli! Wakimbieni Wakaldayo! Kwa sauti ya kupiga kelele tangaza kwamba! Hakikisha hili linajulikana, hakikisha hili linafika mpaka miisho ya nchi! Sema ‘Yahwe amemkomboa Yakobo mtumishi wake.
21Hawakupatwa na kiu alipowaongoza katika jangwa, alifanya maji kutokea kwenye mwamba kwa ajili yao; aliugawa na kufungua mwamba, na maji yakatoka nje.
22Hakuna amani kwa watenda makosa- amesema Yahwe.”

49

1Nisikilize mimi, enyi mkao pwani! Na kuwa makini, enyi watu mkao mbali. Yahwe amenita mimi kutoka kuzaliwa kwa jina, mama yangu aliponileta duniani.

2Amefanya mdomo wangu kuwa kama upanga mkali; amenificha mimi katika kivuli cha mkono wake; amenifanya mimi kuwa mshale unaong'aa; katika podo yake amenificha mimi.
3Amesema na mimi, “Wewe ni mtumishi wangu, Israeli, kupitia yeye nitaonyesha utukufu wangu.”
4Lakini nilimjibu, “Japo nilifikiria nilifanya kazi bure, nimetumia nguvu zangu bure, ikiwa haki yangu iko pamoja na Yahwe, na zawadi yangu iko kwa Mungu wangu.
5Na sasa Yahwe asema hivi, yeye aliyeniumba mimi toka kuzaliwa na kuwa mtumishi wake, kumrejesha Yakobo tena kwake mwenyewe, na Israeli wakusanyike kwake. Mimi ninaheshimika katika macho ya Yahwe, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu.
6Asema hivi, “Ni kitu kidogo sana kwa wewe kuwa mtumishi wangu ili kuanzisha ukoo wa Yakobo, na kuwarejesha wanaoishi Israeli. Nitakufanya wewe kuwa mwanga kwa Wayunani, ili uwe wokovu wangu katika mipaka ya nchi.
7Yahwe asema hivi, Mkombozi wa Israeli, Mtatakatifu wao, kwa yeye ambaye maisha yake yamedharauliwa, kuchukiwa na mataifa, na mtumwa wa viongozi, “Mfalme atakuona wewe na nyanyuka, na wakuu watakuona wewe na inama chini, kwa sababu ya Yahwe ambaye ni mwaminifu, hata mtakatifu wa Israeli, aliyewachagua ninyi.”

8Yahwe asema hivi, “Kwa mda huu nimeamua kuwaonyesha neema yangu na nitawajibu ninyi, na siku ya wokovu nitawasaidi ninyi; Nitakulinda wewe; na nitawapa kama agano kwa watu, kuitengeneza tena nchi, kuwarithisha urithi uliokuwa na ukiwa.
9Utasema kwa wafungwa, ‘Tokeni nje; kwa wale mlio katika giza gerezani, ‘Jionyeshe mwenyewe. ‘Watachunga pembeni ya barabara, na juu ya miteremko ya wazi yatakuwa malisho yake.
10Hawatasikia njaa wala kiu; wala joto au jua halitawaunguza, kwa yeye mwenye huruma juu yao atawaongoza wao; atawaongoza wao kwenye mikondo ya maji.
11Na nitafanya milima yote kuwa barabara, na kufanya njia za juu kuwa sawa.”
12Tazama, haya yatatoka kutoka mbali, baadhi kutoka kaskazini na magharibi; na wengine kutoka nchi ya Sinimi.
13Imba, ewe mbingu, na uwe na furaha, ewe nchi pazeni sauti ya kuimba enyi milima! Maana Yahwe anawafariji watu wake, na watakuwa na huruma kwa wale wanaoteseka.
14Lakin Sayuni asema, Yahwe ameniacha mimi, na Bwana amenisahau mimi.”
15“Je mwanamke anaweza kumsahau mwana wake, anayemnyonyesha, hivyo hana huruma na mwana aliye mzaa? Ndio, hawa waweza kusahau, lakini siwezi kukusahau wewe.
16Tazama, nimeliandika jina lako kwenye kiganja cha mkono wangu; Kuta zako zinaendelea kuwa mbele yangu.
17Watoto wangu wamerudi haraka, wakati wale wanaowaangamiza nyie wameenda mbali.
18Tazama karibu na uone, wote wamekusanyika na wanakuja kwako. Nitahakikisha kama niishivyo- hili ni tamko la Yahwe- hakika mtavivaaa kama kijiti; utajifungia kama bibi harusi.
19Japo umeharibiwa na kuwa na ukiwa, nchi iliyoharibiwa, sasa itakuwa ndogo sana kwa wenyeji, na wale nao waliokumeza watakuwa mbali,
20Watoto watakaozaliwa katika kipindi cha msiba watasema mkiwa mnawasikiliza, ‘Sehemu hii ni duni kwetu, tengeneza chumba kwa ajili yetu, ili tuweze kuishi hapa.
21Halafu utajiuliza mwenyewe, ni nani aliyewazaa watu hawa kwangu? Mimi nilifiwa na ni tasa, niliyefungwa na kupewa talaka. Ni nani aliyewalea hawa watoto? Tazama, niliachiwa yote mimi mwenyewe; Je haya yametoka wapi?”

22Yahwe asema hivi, “Tazama, nitanyanyua mkono wangu juu ya mataifa; Nitanyanyua bendera yangu ya ishara kwa watu. Watawaleta watoto wako kwenye mikono yao na watawabeba binti zako juu ya mabega yao.
23Wafalme watakuwa baba zako wa kambo, na malikia watakuwa wafanyakazi wa ndani; watakuinamia chini wewe kwa uso wao kwa nchi na kukung'uta mavumbi ya miguu yenu; wale wanonisubiri mimi hawataabika.”
24Je mateka wanaweza kuchukuliwa kwa shujaa, au wafungwa kukombolewa kutoka kwa mkali?

25Lakini Yahwe asema hivi, “Wafungwa watachukuliwa kutoka kwa shujaa, na mateka watakombolewa; maana utampinga adui yako na kuwakomboa watoto wako.
26Na nitawalisha wanaowaonea kwa mwili wao wenyewe; na watalewa kwa damu yao wenyewe, kama iliyo mvinyo; na watu wote watajua kwamba Mimi Yahwe, ni Mokozi wenu na Mkombozi wenu, yeye aliyemkuu wa Isareli.

50

1Yahwe asema hivi, “Kiko wapi cheti cha talaka ambacho nimempa talaka mama yako? Na kwa nani niliwauza mimi? Tazama, umewauza kwa sababu ya dhambi zako, na kwa sababu ya uasi wako, na mama yako amepelekwa mbali.

2Mbona nilipokuja hapakuwa na mtu pale? Kwa nini nimeita lakini hakuna aliyejibu? Je mkono wangu ni mfupi kukufidia wewe? Je hakuna nguvu katika ukombozi wangu kwako? Tazama, kwa maonyo yangu, nimeikausha bahari; nimeufanya mto kuwa jangwa; samaki wake wamekufa na kuoza kwa kukosa maji.
3Nimelivisha mbingu weusi, na kufanya nguo ya magunia kuwa kifuniko chao.”
4Bwana Yahwe amenipa mimi lugha kama wale wanayofundishwa, ili kwamba nizungumze maneno ya kudumisha kwa yeye aliyechoka; huniamsha mimi asubuhi kwa asubuhi; huyaamsha masikio yangu kama wale wanofundisha.
5Bwana Yahwe amefungua sikio langu, na sikuaasi, wala kurudi nyuma.
6Niliwapa mgongo wangu wale wanaonipiga mimi, na shavu langu kwa wale wanaopokonya nje ndevu zangu; Sitouficha uso wangu kutokana na matendo ya aibu na kutema mate.
7Maana Bwana Yahwe atanisaidia mimi; hivyo basi sitapatwa na aibu; hivyo nimeufanya uso wangu kama jiwe, maana ninajua kwamba sitaaibishwa.
8Yeye aliye nitakasa mimi yu karibu. Ni nani atakayenipinga mimi? Basi na tusimame tufarijiane mmoja mmoja. Nani aliye mshitaki? Muache aje karibu na mimi.
9Tazama, Bwana Yahwe atanisaidia mimi. Nani atakayetangaza kuwa mimi ni mwenye hatia? Tazama, watavaa nje kama vazi; mdomo utawala wao juu.
10Ni nani miongoni mwenu anayemuogopa Yahwe? Ni nani anayeiheshimu sauti ya Yahwe? Ni nani atakayetembea kwenye giza nene pasipo mwanga?
11Tazama, ninyi nyote mnaowasha, ni nani aliyewapa wenyewe kwa tochi: tembeeni katika mwanga wa moto wenu na katika moto mliouwasha. Hili ndilo mlilopokea kutoka kwangu: utalala chini katika mahali pachungu.

51

1Nisikilizeni mimi, enyi mtendao haki, enyi mtafutaye Yahwe: Tazama mwamba mliochongwa, shimo ambalo mlichimbwa.

2Mtazameni Ibrahimu, baba yenu, na Sara, aliyewazaa ninyi; maana alipokuwa na upweke yeye mwenyewe, Nilimuita yeye. Nikambariki yeye na kumfanya yeye kuwa wengi.
3Ndio, Yahwe ataifariji Sayuni; Ataifariji miji yake yote iliyo na ukiwa; jangwa lake atalifanya kama Edeni, na jangwa lililo wazi pembeni ya bonde la mto Yordani kama bustani ya Yahwe; Furaha na shangwe vitakuwa kwake, shukrani, na sauti ya kuimba.
4“Kuwa makini kwangu, watu wangu; na nisikilizeni mimi, watu wangu! Maana nitatoa amri, na nitaifanya haki yangu kuwa sheria ya mataifa.
5Haki yangu ipo karibu; wokovu wangu utaenda nje, na mikono yangu itahihukumu mataifa; Pwani itanisubiri mimi; maana wanashauku ya kuhusubiria mkono wangu.
6Nyanyueni macho yanu juu angani, na tazama nchi chini, maana mbingu zitatoweka mbali kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, na wenyeji wake watakufa kama inzi. Lakini wokovu wangu utaendelea daima, na haki yangu haitaacha kutenda kazi.
7Nisikizeni mimi, enyi mnaotambua ukweli, enyi watu wangu mliobeba sheria yangu katika mioyo yenu: Msiogope matusi ya watu, wala kukatishwa tamaa na unyanyasaji wao.
8Maana Nondo watawala wao kama vazi, na minyoo itawala wao kama sufu; lakini haki yangu itakuwa daima, na wokovu wangu katika vizazi vyote.”
9Amka, amka, jivishe wewe mwenyewe kwa nguvu, mkono wa Yahwe. Amka kama siku za zamani, kizazi cha nyakati za kale, Je, sio wewe uliyeangamiza mnyama wa baharini, na uliyemchoma joka?
10Je, haukukausha bahari, maji ya kina kirefu, na kufanya kina cha bahari kuwa nija ya ukombozi kupita?
11Fidia ya Yahwe itarudi na kwenda Sayuni kwa kilio cha furaha na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao, na huzuni na kuomboleza vitatoweka mbali.
12“Mimi, mimi ndiye niwapae faraja. Kwa nini uwaogope watu, ambao wanakufa, watoto wa wanadamu, waliofanywa kama majani?
13Kwa nini umemsahau Yahwe Muumba, yeye azinyooshaye mbingu na kuweka misingi ya nchi? Nyie ambao mna hofu za mara kwa mara kila siku kwa sababu ya hasira ya moto ya wanyanyasaji anapo fanya maamuzi ya kuangamiza. Iko wapi hasira ya wanyanyasaji?
14Yeye aliyeinama chini, Yahwe atafanya haraka kumuachia; hatakufa wala kwenda chini katika shimo, wala hatakosa mkate.
15Maana Yahwe Mungu wenu, anaye ifanya bahari itembee, hivyo mawimbi yake yavume kwa kishindo- Yahwe wa majeshi ndilo jina lake.
16Niweka maneno yangu mdomoni mwako, na nimekufunika wewe kwa kivuli cha mkono wangu, ili niweze kupanda mbingu, kuweka misingi ya nchi, na kutamkia Sayuni, ‘ninyi ni watu wangu.”
17Amka, amka, simama juu, Yerusalemu, ewe unyweae katika kikombe cha hasira ya Yahwe kutoka mkononi mwako; umekunywa katika kikombe, kikombe cha mateso, na umekunywa na kumaliza.
18Hakuna hata mmoja miongoni mwa watoto aliyewazaa wa kumuongoza yeye; hakuna hata mmoja miongoni mwa wote aliyewalea wa kumshika mkono wake.
19Shida hizi mbili ziliwatokea ninyi- ni nani atahuzunika pamoja nanyi? - Ukiwa na uharibifu, na njaa na upanga. Ni nani atakayekufariji wewe?
20Watoto wako walizimia; walilala kila kona ya mtaa, kama swala kwenye mtego; Wamejawa na hasira ya Yahwe, Laana ya Mungu wako.
21Lakini sasa sikiliza hili, ewe uliodhulumiwa na kulewa, lakini sio kwa mvinyo:
22Bwana wenu Yahwe Mungu, anayewasihi watu wake, asema hivi, “Tazama, Nimechukua kikombe cha ukubwa mkononi mwako- ukubwa wa kikombe cha hasira yangu - ili usiweze kunywa tena.
23Nitakuweka kwenye mikono ya watesaji, wale waliokuambia wewe, Lala chini, ili tutembee juu yako;’ wameufanya mgongo wako kama nchi na kama njia ya watu wapitao huko.”

52

1Amka, amka, vaa nguvu zako, Sayuni; vaa vazi lako zuri, mji mtakatifu; maana hakuna tena asiyetahiriwa wala wasio safi kuingia kwako.

2Jikung'ute mwenyewe kutoka mavumbini; nyanyuka na ukae, ewe Yerusalemu; ondoa shanga katika shingo yako, wafungwa, binti ya Sayuni.

3Maana Yahwe asema hivi, umeuzwa bure, na utakombolewa pasipo pesa.”

4Maana Bwana Yahwe asema hivi, “Hapo mwanzo watu wangu walishuka chini Misri kuishi kwa muda mfupi; Waasiria waliwanyanyasa wao hivi karibuni.

5Sasa ni kitu gani nilicho nacho hapa- Hili ni tamko Yahwe- aonae kwamba watu wake wanachukuliwa bure tu? Wale wanaowaongoza wao, wanafanya mzaha-Hili ni tamko la Yahwe- jina langu linakashifiwa mchana kutwa.
6Hivyo basi watu wangu watalijua jina langu; watajua kwamba siku hiyo mimi ndiye ninayesema “Ndiyo, Ni Mimi!”
7Ni kwa uzuri gani juu milimani miguu ya mjumbe aliyeleta habari njema, atangazaye amani, aliyebeba uzuri wa ukuu, aliyetangaza wokovu, anayesema kwa Sayuni, “Mungu wako anatawala!”
8Sikiliza enyi walinzi nyanyueni sauti zenu, kwa pamoja pigeni kelele kwa furaha, maana mtamuona, kwa kila jicho lenu, kurejea kwa Yahwe Sayuni.
9Pazeni sauti kwa kuimba kwa furaha, enyi mateka wa Yerusalemu; maana Yahwe amefariji watu wake; ameikomboa Yerusalemu.
10Yahwe amewaonyesha kwamba mkono wake mtakatifu katika macho ya mataifa yote; nchi yote itauona wokovu wa Mungu wetu.
11Ondokeni, ondokeni, enendeni mbali na hapa; msiguse kitu chochote ambacho ni najisi; au kuishi katikati yake; jitakase mwenyewe, enyi mliobeba vyombo vya Yahwe.
12Maana hautakwenda nje kwa kukimbia, wala hautaondoka kwa hofu; Maana Yahwe atakuwa mbele yako; na Mungu wa Israeli atakuwa mlinzi wako nyuma.
13Tazameni, mtumishi wangu atafanya hekima; atakuwa juu na atanyanyuliwa juu, na atapandishwa juu.
14Na wengi watamstajabia yeye- muonekano wake umekunjamana nje ya muonekano wa mwanadamu, hivyo basi upande wake ulikuwa mbali na kitu chochote ambacho ni binadamu-
15Na hivyo, mtumishi wangu atanyunyizia mataifa mengi na wafalme watafunga midomo yao kwa sababu yake. Kana kwamba hawajawahi kuambiwa, wataona, kana kwamba hawakusikia, wataelewa.

53

1Ni nani aliyesadiki habari zetu? Na mkono wa Yahwe umedhihirishwa kwa nani?

2Maana amekuwa mbele za Yahwe kama sampuli, na kama chipukizi katika aridhi kavu; hakuna maajabu yalionekana au mapambo; tulipo muona yeye, hapakuwa na uzuri kutuvutia sisi.
3Alidharauliwa na kukataliwa na watu; mtu wa huzuni, na mwenye maumivu. Kama mmoja aliyetoka kwa watu wafichao nyuso zao, alidharauliwa; na kujifikiria kuwa asiye na faida.
4Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhani kuwa aliadhibiwa na Mungu, amepigwa na Mungu, na kutaabishwa.
5Lakini alichomwa kwa sababu ya uaasi wa matendo yetu; aliangamizwa kwa sababu ya dhambi zetu. Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa majeraha yake sisi tumepona.
6Sisi ni kama kondoo tumepotoka; kila mmoja amegeuka katika njia yake, na Yahwe amemueka juu yake maovu kwetu sisi sote.
7Aliteswa; lakini alinyenyekea mwenyewe, hakufungua mdomo wake; kama kondoo aendaye kuchinjwa, na kama kondoo mbele ya mtu anayemkata manyoya yake taratibu, hivyo hakufungua mdomo wake.
8Alitolewa kutoka gerezani na hukumu, na ni nani atakayetangaza kizazi chake? Maana alikatiliwa mbali nan chi ya walio hai; kwa sababu ya makosa ya watu wangu adhabu ilikuwa juu yake.
9Wameliweka kaburi lake pamoja nawahalifu, kwa utajiri wa mtu katika kifo chake ingawa hakuwa na vurugu wala udanganyifu wowote katika mdomo wake.
10Lakini yalikuwa ni mapenzi ya Yahwe kumponda yeye na kumfanya yeye apone. Alipoyafanya maisha yake kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi, ataona watoto wake, ataongeza siku zao, na mapenzi ya Yahwe yatatimizwa kupitia yeye.
11Baada ya mateso ya maisha yake, ataona mwanga na ataridhika kwa maarifa yake.
12Hivyo basi, nitaweza kumpa yeye sehemu yake miongoni mwa wakuu, naye atagawanya mateka pamoja nao walio hodari; kwa sabubu aliimwaga nafsi yake hata kufa, amehesabiwa pamoja na wahalifu. Alichukua dhambi za watu wengi na kufanya maombezi kwa wahalifu.

54

1“Imba, ewe mwanamke tasa, ewe ambaye haujazaa; imba wimbo kwa furaha na lia kwa nguvu ewe ambaye hujapata uchungu wa kuzaa. Maana watoto walio katika ukiwa ni wengi kuliko watoto wa wanawake waliolewa,” asema Yahwe.

2Fanya hema lako kuwa kubwa na tawanya mapazia mbali, sio kidogo; nyoosha kamba zako na imarisha vigingi vyako.
3Maana utaenea katika mkono wa kulia na wa kushoto, na ukoo wako utashinda mataifa na kuwapatia miji iliyo na ukiwa.
4Usiogope maana hautaaibika, wala kukatishwa tamaa maana hautapatwa na aibu; utasahau aibu ya ujana wako na aibu ya kutelekezwa.
5Maana Muumba ni mume wako; Yahwe wa majeshi ndilo jina lake. Mtakatifu wa Israeli yeye ni mkombozi wenu; anaitwa Mungu wa nchi yote.
6Yahwe anakuita wewe urudi kama mwanamke aliyetelekezwa na mwenye roho ya huzuni, kama mwanamke mdogo aliyeolewa na kukataliwa, asema Mungu.
7“Kwa kipindi kifupi nimewatelekeza ninyi, lakini kwa huruma kubwa nitawakusanya ninyi.
8Katika gharikia ya hasira nimeuficha uso wangu kwa muda. Lakini kwa agano la milele la kuaminika nitakuwa na huruma na ninyi- amesema Yahwe, aliyewakomboa ninyi.
9Maana haya ni kama Nuhu kwangu: kama nilivyoapa maji ya Nuhu hayatapita tena katika nchi, Hivyo nimeapa kwama sitapatwa na hasira na ninyi wala kuwakemea ninyi.
10Japo milima yaweza kuanguka na vilima vyaweza kutikiswa, japo uimara wa pendo langu hautageuka nyuma kutoka kwenu, wala agano langu la amani kutikiswa- asema Yahwe, Yeye mwenye huruma juu yenu.
11Wanaotaabika, wanaopitia dhoruba na wasio na faraja, tazama, nitaweka lami kwa rangi nzuri, na kuweka misingi kwa yakuti.
12Nitaufanya mnara wa akiki na lango yake ya almasi na kuta zake za nje ni za mawe mazuri
13Na watoto wako wote watafundishwa na Yahwe; na amani ya watoto wako itakuwa kubwa.
14Katika haki nitakuanzisha tena. Hautaona dhiki tena, maana hautaogopa, na hakuna kitu cha kutisha kitakachokuja karibu yako.
15Tazama, ikiwa yeyote atakaye koroga matatizo, hayatoka kwangu; yeyote atakaye changanya matatizo pamaoja na wewe ataanguka kwa kishindo.
16Tazama, nimemuumba fundi, anayepuliza makaa yanayoungua na kuandaa silaha kama kazi yake, na nimemuumba mharibifu ili awaharibu.
17Hakuna silaha iliyotengenezwa dhidi yako itafanikiwa; na utamlaani kila mmjoa anayekutusi wewe. Huu ndio urithi wa watumishi wa Yahwe, na uthibitisho wake kutoka kwangu- Hili ndilo tamko la Yahwe.”

55

1“Njooni, kila aliye na kiu, njooni kwenye maji! Na ewe usio na pesa, njoo, ununua na ule! Njoo, nunua mvinyo na maziwa pasipo pesa na pasipo gharama.

2Kwa nini tunapima fedha kwa kitu ambacho sio mkate? Na kufanya kazi isiyoridhisha? Nisikilizeni mimi kwa makini na ule kilicho kizuri, na kujifurahisha mwenyewe kwa unono.
3Geuzeni masikio yenu, na mje kwangu! Sikiliza, iliuweze kuishi! Nitafanya agano ya milele na ninyi; pendo langu la kuaminika nililomuhaidi Daudi.
4Tazama, nimwemuweka yeye kama shahidi kwa mataifa, kama kiongozi na kamanda wa watu.
5Tazama, utaliita taifa ambalo haulijui; na taifa ambalo halikujui wewe litakukimbilia wewe kwa sababu wewe ni Yahwe Mungu wao, Mtakatifu wa Israeli, yeye aliyekutukuza wewe.
6Mtafuteni Yahwe maana anapatikana; muiteni yeye maana yu karibu.
7Tuwaache waovu waziache njia zao, na mtu mwenye dhambi mawazo yake. Muache yeye arudi kwa Yahwe, na atamuhurumia yeye, na kwa Mungu wetu, yeye ambaye atamsamehe huyo kwa wingi.
8Maana mawazo yangu sio mawazo yenu, wala njia zangu sio njia zenu- Hili ni tamko la Yahwe-
9maana kama vile mbingu zilivyo juu kuliko nchi, hivyo ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.
10Maana kama mvua na theluji zishukavyo chini kutoka mbinguni na hazirudi tena pale isipokuwa kueneza nchi na kufanya uzalishaji na chipukizi na kutoa mbegu kwa wakulima waliopanda na mkate kwa walaji,
11hivyo neno langu litakuwa linalotoka kwenye mdomo wangu: halitanirudia tena mimi bure, Lakini itatimiza lile nililokusudia, na litatimiza lile nililolituma.
12Maana utakwenda nje katika furaha na utaongozwa kwa amani; Milima na vilima vitapaza sauti kwa furaha mbele yako, na miti yote shambani itapiga makofi.
13Badala ya miiba ya porini, misonobari itakuwa; na badala ya mbigiri, mihadasi inaota, na itakuwa kwa Yahwe, maana jina lake, ni kama alama ya milele ambayo haiwezi kuondolewa.”

56

1Yahwe asema hivi, “Fanyeni yaliyo sahihi, fanyeni yaliyo ya haki; maana wakovu wangu u karibu, na haki yangu inakaribia kujidhihirisha.

2Abarikiwe mtu yule ataendaye haya, anayeyashika sana. Anaifuata sabato, na haitii unajisi, azuiaye mkono wake usitende maovu.”
3Usimuache mgeni yeyote aliyekuwa mfuasi wa Yahwe aseme, “Yahwe atahakikisha ananiondoa kwa watu wake.” Toashi ataweza kusema, “tazama, mimi ni mti mkavu.”
4Yahwe asema hivi, kwa matoashi wanaoitimiza sabato yangu huchagua mambo yanayonipendeza mimi, na hushika kwanza agano langu,
5kwao nitaiweka nyumba yangu na ndani ya kuta zangu kumbukumbu ambayo ni kubwa kuliko kuwa na vijana na mabinti. Nitawapa kumbumbu ya milele ambalo halitaondolewa.
6Pia wageni ambao wataungana wenyewe kwa Yahwe- kwa ajili ya kumtumikia yeye, na yeye alipendaye jina la Yahwe, kumuabudu yeye, na kila anayeheshimu sabato na wale wanoitunza isitiwe najisi, na wale walishikao agano langu-
7nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu na kuwafaya muwe na furaha katika nyumba yangu ya maombi; matoleo na sadaka zenu zitakubalika katika madhabahu yangu. Maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi kwa mataifa yote.
8Hili ni tamko la Yahwe, anayewakusanya watu wenye ukiwa katika Israeli- nitaendelea kuwakusanya wengine ili kuwaongeza wao.”
9Enyi nyote wanyama pori mlioko porini, njooni na mle, enyi wanyama mlioko msituni, Walinzi wao wote ni vipofu, hawaelewi.
10Wote ni mbwa wapole ambao hawawezi kubweka. Wanaota, na wanalala chini maana wanapenda kulala.
11Mbwa wanahamu kubwa; hawajawahi kuridhika; wachungaji wao hawawatambui; wamegeuka katika njia zao wenyewe, kila mmoja ana tamaa kupata faida isiyo yaa haki.
12“Njooni, “Tunywe mvinyo na pombe. Kesho itakuwa kama leo, siku kubwa zaidi ya kipimo.”

57

1Wenye haki watatoweka, lakini hakuna mtu atakayelitia maanani, na watu wa agano la kuaminika wamekusanyika mbali, lakini hakuna mtu anayefahamu kuwa wenye haki wamekusanyika mbali na maovu.

2Wameingia katika amani; wamepumzika katika vitanda vyao, wale wanaotembea katika haki.
3Lakini njooni hapa, enyi watoto wa wachawi, watoto wa wazinifu na mwanamke anayefanya ukahaba.
4Ni nani mnayemfanyia mzaha? Dhidi ya wale wanaofungua midomo yao na kutoa nje ndimi zao? Je, ninyi sio watoto wa uaasi, watoto wa uongo?
5Enyi mnaowasha tamaa wenyewe kwa kulala pamoja chini ya mualoni, kila chini ya mti mbichi, ewe unaeua watoto wako katika mabonde yaliyokauka, chini ya miamba inayoning'inia.
6Miongoni mwa vitu vilaini katika bonde la mto ni mambo uliyopewa uyafanyie kazi. Ni vitu vya ibada yako. Umemwaga nje kinywaji chako kwao na kutoa sadaka ya mazao. Katika haya mambo Je, ninaweza kuwa radhi na mambo haya?
7Umeandaa kitanda chako juu ya mlima mrefu; pia umeenda pale juu kutoa sadaka.
8Nyuma ya milango na mihimili ya milango umeweka ishara zako; kwa maana umejifunua kwa wale wasio Mimi, nawe umekwea kwao; umekifanya kitanda chako kuwa kikubwa. Umefanya agano na wao; ulipenda vitanda vyao; uliona sehemu zao za siri.
9Ulienda kwa Moleki pamoja na mafuta; umeongeza marashi. Ulimtuma balozi wako mbali sana; Alikwenda chini kuzimu.
10Ulichoka kwa safari yako ndefu, lakini haukusema, “Haina matumaini.” Umeyatafuta maisha katika mkono wako; Hivyo basi haukudhoofika.
11Ni nani uliyemuogopa? Ni nani uliye muhofia zaidi ambaye aliyekufanya wewe kutenda udanganyifu, kwa wingi namna hiyo ambapo hauwezi kunikumbuka mimi au kufikiria kuhusu mimi? Maana nilikuwa kimya kwa mda mrefu, hauniogopi mimi tena.
12Nitatangaza matendo na haki yako na nitawaambia kila kitu ulichokifanya, lakini hawatakusaidia.
13Utakapolia nje, wacha sanamu ulizozikusnya zikusaidie wewe. Badala yake upepo utavipeperusha vyote, punzi itavipeperusha mbali. Lakini yeye anayenikimbilia mimi atairithi aridhi na atachukua umiliki katika mlima wangu mtakatifu.

14Atasema, ‘Jenga, jenga! Safisha njia! Ondoeni vizuizi vyote katika njia ya watu wangu!”
15Maana yeye aliye juu palipoinuka, anayeishi katika uzima wa milele, ambaye jina lake ni mtakatifu, asema hivi, “Ninaishi mahali pa juu na mahali patakatifu pamoja na yeye pia aliyemnyenyekevu na moyo uliopondeka, ili kuzifufua roho za wanyenyekevu na kufufua mioyo ya wanaojutia.
16Maana sitawahukumu milele, wala sitakuwa na hasira milele, Kisha roho ya mtu itazimia mbele yangu, maisha niliyowafanyia.
17Kwa sababu ya dhambi ya mapato ya vurugu zake, Nilipatwa na hasira, na nikamuadhibu yeye; niliuficha uso wangu, nilikuwa na hasira, lakini alirudi nyuma katika njia za moyo wake mwenyewe.
18Nimeziona njia zake, lakini nitamponya yeye. Nitamuongoza yeye na kumfariji na kuwashauri wale wanaomliliia yeye,
19na natengeneza tunda la midomo. Amani, amani, kwa wale walio mbali sana na wale walio karibu-asema Yahwe nitawaponya ninyi.
20Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka, haiwezi kutulia, na maji yake yametanda juu ya matope.
21Hakuna amani kwa wakosaji, asema Mungu.”

58

1“Lia kwa sauti; usinyamaze. Paza sauti yako juu kama mbiu. Kabiliana na watu wangu wenye uasi, na nyumba ya Yakobo na dhambi zao.

2Bali wananitafuta mimi kila siku na kufurahia katika maarifa ya njia zangu, kama taifa linalotenda haki na hawakuiacha sheria ya Mungu wao. Wananiuliza mimi kuhusu hukumu ya haki; wamepata furaha katika mawazo yao ya kwa kumkaribia Mungu.
3Kwa nini tulifunga; walisema, ‘Lakini hamkuona hilo? Kwa nini tulijinyenyekeza wenywe, lakini hakutambua?’ Tazama, siku ya kufunga kwenu mnatatafuta furaha yenu mwenyewe na kuwanyanyasa wafanyakazi wenu wote.
4Tazama, ninyi mnafunga ili muwe wepesi wa kugombana na kupigana, na kupiga kwa ngumi ya uovu wako; haujafunga leo kuifanya sauti yako isikike juu.
5Kwa uhalisi aina ya mfungo huu ndio ambao ninauhitaji: Siku ambayo kila mtu hunyenyekea mwenyewe, huinamisha kichwa chake chini kama mwanzi, na hutawanya mavazi ya magunia na majivu chini yake? Je, kweli unauita huu ni mfungo, siku ya kumfurahisha Yahwe?
6Hii sio mfungo ambao niliuchagua mimi: kufungua vifungo vya waovu, kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioangamizwa, na kuharibu kila nira?
7Sio kwamba kula mkate na wenye njaa na kuwaleta masikini na kuwaleta wasio na makazi katika nyuma yako?” Unapomuana mtu yuko uchi, unatakiwa umvishe mavazi; na usijifiche mwenyewe na ndugu zako.
8Halafu mwanga wako utafunguliwa kama jua, na uponyaji wako utachipukia juu kwa haraka; haki yako itaenda mbele zake, na utukufu wa Yahwe utakuwa nyuma kukulinda.
9Halafu utamuita, na Yahwe atakuitikia; utalia ukihitaji msaada, na atasema, “Nipo hapa.” Ikiwa utaitoa nira isiwepo miongoni mwako, kidole kinachoshtaki, maongezi ya waovu,
10Ikiwa wewe mwenyewe utawapa wenye njaa na kuwaridhisha wahitaji katika shida, na giza lako litakuwa kama mchana.
11Halafu Yahwe ataendelea kuwaongoza ninyi na kuwaridhisha ninyi katika mikoa ambayo hakuna maji, Ataimarisha mifupa yenu. Mtakuwa kama bustani iliyonyeshewa maji, na kama mkondo wa maji, ambapo maji yake hayapungui.
12Baadhi yenu mtajenga tena sehumu za kale zilizoharibiwa; mtatengeneza sehemu zilizoharibiwa na vizazi vingi; na mtaitwa “Mrekebishaji wa ukuta,” kuwarejesha katika mtaa ya kuishi.”
13Tuseme kwamba ukigeuza nyuma miguu yenu kutoka safarini katika siku ya sabato, kufanya anasa siku yangu takatifu, Tuseme kwamba umeiita sabato siku ya furaha, na umeiita siku ya Bwana Yahwe mtakatifu na yenye kuheshimiwa. Tuseme kwamba unaiheshimu sabato kwa kuacha biashara zako, na hautafuti anasa zako mwenyewe na huzungumzi maneno yako mwenyewe.
14“Halafu utapata furaha kwa Yahwe; na nitaifanya safari yako juu ya urefu wa nchi; Nitakulisha wewe kwenye urithi wa Yakobo baba yenu- maana mdomo wa Yahwe umezungumza.”

59

1Tazama, mkono wa Yahwe sio mfupi ambao hautaweza kukuokoa wewe; wala sikio lake sio zito, ambalo haliwezi kusikia.

2Matendo yako ya dhambi, hata hivyo, zimekutenga wewe na Mungu, na dhambi zenu zimemfanya aufiche uso wake msimuone wala kumsikia yeye.
3Maana mikono yenu ina madoa ya damu na vidole vyenu vimejaa dhambi. Midomo yenu inazungumza uongo na ulimi wenu unazungumza kwa nia mbaya.
4Hakuna hata mmoja aitae haki, na hakuna anayewasihi kesi yake katika haki. Wanayamini maneno yasiyo ya haki, maneno ya uongo; wanashika matatizo na kuzaa dhambi.
5Wametoa mayai ya nyoka wenye sumu na hufuma mtandao wa buibui. Yeyote alaye mayai yake atakufa, na ikiwa yai litavunjika, litatotoa nyoka mwenye sumu.
6Mitando yao haitatumika kama mavazi, wala hawawezi kujifukia wenyewe kwa kazi yao. Kazi zao ni kazi za dhambi, na matendo ya vurugu yako mikononi mwao.
7Miguu yao inakimbilia uovu, na wanakimbilia kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo ya dhambi; vurugu na uharibifu ndio njia yao.
8Njia ya amani hawaijui, na hakuna haki katika njia zao. Wametengeneza njia zlizopotoka; yeyote atakaye safiri kupitia njia hizi hazijui amani.
9Hivyo basi haki iko mbali na sisi, wala haki haijatufikia sisi. Tunasubiri mwanga tunaona giza; tunatafuta mwangaza, lakini tunatembea gizani. Tunapapasa kwenye ukuta kama kipofu, kama wale wasiona,
10Tuna mashaka mchana kweupe kama kwenye mwanga unaofifia; miongoni mwa wenye nguvu tuko kama watu waliokufa.
11Sisi tunaunguruma kama dubu na kuomboleza kama njiwa; tunasubiria haki, lakini hakuna kitu; kwa ukombozi, lakini uko mbali na sisi.
12Maana makosa yetu mengi yako mbele zako, na dhambi zetu zinatushuhudia sisi; maana makosa yako pamoja na sisi.
13Tumeaasi, kumkana Yahwe na kuacha kumfuata Mungu. Tulizungumzia ulafi kugeuka nyuma, na kuanza kulalamika kutoka moyoni na maneno ya uongo.
14Haki imerudishwa nyuma, wenye haki wamesimama mbali sana; maana ukweli uko mashakani katika mraba wa umma, haki haiwezi kuja.
15Waaminifu wamenda zao, na yeyote anayegeuka mbali na maovu anajiathiri mwenyewe. Yahwe aliliona hilo na hakupendezwa maana hakuna haki.
16Aliona kwamba hakuna mtu, na akastaajabu kwamba hakuna mtu wa kuomba. Hivyo basi mkono wake uliletao wakovu kwake, na haki yake unamtosheleza yeye.
17Huivaa haki kama ngao kifuani na kofia ya chuma ya wokovu kichwani mwake. Anajivika mwenyewe kwa mavazi ya kisasi na kuvaa vazi la bidii.
18Analipa tena kwa kilichotokea, hukumu ya hasira kwa adui zake na kwa adui atairidisha adhabu ya kisiwa kama zawadi yao.
19Hivyo wataliogopa jina la Yahwe kutoka magharibi na utukufu wake kutoka mashariki; maana atakuja kama mkondo wa mto, inaendeshwa na pumzi ya Yahwe.
20Mkombozi atakuja Sayuni na wale watakaogeuka kutoka matendo yao ya uasi katika nyumba ya Yakobo- Hili ni tamko la Yahwe.

21Na kama mimi, hili ni agano langu pamoja nao- asema Yahwe- Roho yangu iliyo juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka kinywani mwenu, hayataondoka midomo mwenu au kuondoka mbali na midomo ya wajukuu wenu, au kwenda mbali asema Yahwe- kuanziia sasa na hata milele.”

60

1Nyanyuka, uangaze; maana mwanga wako umekuja, na utukufu wa Yahwe umekuja kwako.

2Japokuwa giza litatanda katika nchi, na giza nene katika mataifa; Lakini Yahwe atakuja juu yenu, na utukufu wake utaonekana kwenu.
3Mataifa yatakuja kwenye mwanga wako, na wafalme katika mwanga wako mkali uliokuja.
4Tazama na angalia pande zote. Wamekusanyika wao wenyewe kwa pamoja na wanakuja kwako. Watoto wako watatoka mbali, na binti zao watabebwa katika mikono yenu.
5Halafu wataangalia na kwa furaha, na moyo wako utafurahia na kufurika, maana wingi wa maji utamwagwa juu yenu, utajiri wa mataifa utakuja kwenu.
6Msafara wa ngamia utawafunika ninyi, na ngamia wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na ubani, wataimba sifa kwa Yahwe.
7Makundi yote ya Kedari yatakusanika kwa pamoja kwako, kondoo wa Nebaioti watabeba mahitaji yako; watakubalika kutolewa sadaka katika madhabahu yangu; na nitaitukuza nyumba yangu takatifu.
8Ni nani hawa wanaopaa wenyewe kama mawingu, na kama njiwa kwenye makazi yao?
9Pwani itanitafuta mimi, na meli ya Tarshishi huwaongoza, huwaleta watoto wenu kutoka mbali, pamoja na fedha zao na dhahabu zao, maana jina la Yahwe Mungu wenu, na Mtakatifu wa Israeli, maana amekuheshimu wewe.
10Watoto wa wageni watajenga tena kuta zenu, na wafalme wao watawatumikia ninyi; japo katika laana yangu nimewaadhibu ninyi, lakini kwa neema yangu nitawahurumia ninyi.
11Milango yenu itaendelea kuwa wazi; haitafungwa mchana au usiku, hivyo utajiri wa mataifa ili uweze kuletwa, pamoja na viongozi wanowaongoza.
12Kweli, mataifa na falme ambayo hayatakutumikia wewe yatatoweka; mataifa hayo yataangamizwa kabisa.
13Utukufu wa Lebanoni utakuja kwako, mti wa msonobari, mtidhari, pamoja na msonobari ili kupamba madhabahu yangu; na Nitalitukuza eneo la miguu yangu.
14Watakuja kwako kukusujudia wewe, watoto wa wale wanaokunyenyekea wewe; wataisujudia miguu yako; watakuita wewe mji wa Yahwe, Sayuni ya Mtakatifu wa Israeli.
15Badala yake uwepo wenu umetelekezwa na kuchukiwa, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayepita ndani yenu, nitawafanya kuwa kitu cha kiburi milele, furaha kutoka kizazi hata kizazi.
16Pia utakunywa maziwa ya mataifa, utatunzwa katika kifua cha wafalme; utajua kwamba Mimi Yahwe, Mimi ni mwokozi na mkombozi wenu, aliye Mkuu wa Israeli.
17Badala ya shaba Nitaleta dhahabu, badala ya chuma nitaleta fedha; badala ya mbao, shabana badala ya jiwe, chuma. Nitachagua amani kwa kiongozi wenu, na haki kiongozi wenu.
18Vurugu hazitasikika katika aridhi yenu, uharibifu wala uvunjaji katika mipaka yenu; lakini mtaita kuta zenu wokovu, na malango yenu mtayaita sifa.
19Jua halitakuwa mwanga wenu wakati wa mchana, wala mwanga wa mwenzi wakati wa usiku hautawawakia ninyi; Lakini Yahwe atakuwa mwanga wenu wa milele, na Mungu wenu na utukufu wenu.
20Jua lenu halitakuwepo wala mwezi utaondoshwa na kutoweka; maana Yahwe atakuwa mwanga wenu daima, na siku za maombolezo zitakwisha.
21Watu wako wote watakuwa wenye haki; watachukuwa urithi wa nchi kwa mda wote, tawi la mazao yangu, kazi ya mikono yangu, ili niweze kuitukuza.
22Mwana atakuwa maelfu, na mdogo atakuwa taifa la wenye nguvu; Mimi Yahwe Nitayatimiza hayo mda utakapowadia.

61

1Roho ya Bwana Yahwe i juu yangu, maana Yahwe amenipaka mafuta mimi kuhiubiri habari njema kwa wenye taabu. Amenituma mimi kuwaponya waliopondeka mioyo, kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kufungua gereza ili waliofungwa waweze kutoka.

2Amenituma mimi kuutangaza mwaka wa Yahwe uliokubalika, siku ya kisasi cha Mungu wetu, na kuwafariji wale wote wanaomboleza.
3Amenituma mimi - kuwapa wale waoombolezao katika Sayuni -kuwapa wao kilemba cha majivu, mafuta ya furaha badala ya kuomboleza, vazi la kusifu katika eneo la roho ya ubutu, kuwaita mialoni ya haki, iliyooteshwa na Yahwe, ili aweze kutukuzwa.
4Wataijenga tena mahali pa kale palipoharibiwa; wataparejesha mahali palipokuwa na ukiwa. Watairejesha miji iliyoharibiwa, Mahali penye ukiwa kutoka vizazi vingi vilivyopita.
5Wageni watasimama na kulisha makundi yako, na watoto wa wageni watafanya kazi kwenye mashamba yako na mizabu.
6Mtaitwa makuhani wa Yahwe; watawaita watumishi wa Mungu wetu. Mtakula utajiri wa mataifa, na utajivunia katika utajiri wake.
7Badala yake aibu yenu itaongezeka; na badala ya fedheha walifurahia juu ya sehemu yao. Hivyo basi sehemu yao itaongezeka mara mbili katika nchi na furaha ya milele itakuwa yao.
8Maana Mimi, Yahwe, ninapenda haki, na ninachukia wizi na vurugu zisizo za haki. Nitawalipa wao katika haki na Nitafanya agano la milele na wao.
9Uzao wao utajulikana miongoni mwa mataifa, na watoto wao miongoni mwa watu. Wote watakaowaona watawakubali wao, kwamba ni watu wangu ambao Yahwe amewabariki.
10Nitafurahia sana katika Yahwe; Katika Mungu nitafurahia. Maana amenivika mimi kwa vazi la wokovu; amenivika mimi kwa vazi la haki, kama bwana harusi aliyejipamba mwenywe kwa kilemba, na kama bibi harusi aliyejipamba kwa vito.
11Maana kama nchi inavyozalisha miti inayochipukia na kama bustani inavyofanya miti yake ikuie, hivyo Bwana atasasbabisha haki na sifa kuchipukia mbele ya mataifa yote.

62

1Kwa niaba ya Sayuni sitatulia, na kwa naiba ya Yerusalemu sitanyamaza kimya, mpaka haki yake itakapotokea, na wokovu wake kama tochi.

2Mataifa yataona haki yako, na wafalme wote wataona utukufu wako. Utaitwa kwa jina jipya ambalo Yahwe atalichagua.
3Pia utakuwa taji zuri katika mkono wa Yahwe, na kilemba cha ufalme katika mkono wa Mungu wako.
4Hautaambiwa tena, “Umetelekezwa;” wala kwa nchi yako hautasema tena, “Ukiwa.” Kweli, itaitwa “Neema yangu iko kwake,” na nchi yao “ndoa” mana furaha ya Yahwe ndani yenu, na nchi yenu itaolewa.
5Hakika, kama kijana mdogo akimuoa mwanamke mdogo, hivyo watoto wako watawaoa ninyi, na kama bwana harusi anavyofurahia juu ya bibi harusi, Mungu wenu atafuhai juu yenu.
6Nimemuweka mlinzi katika kuta zenu, Yerusalemu; hawatatulia mchana wala usiku. Utabaki kuwa Yahwe, usitulie.
7Usimuache apumzike mpaka aiimarishe tena Yerusalemu na kumfanya asifiwe duniani.
8Yahwe ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wa nguvu zake, “Hakika sitawapa tena nafaka kama chakula cha maadui zenu. Wageni hawatakunywa mvinyo wenu uliompya maana mlifanya kazi.
9Kwa wale watakao vuna nafaka watazila na kumsifu Yahwe, na wale wanaochuma zabibu watakunywa mvinyo katika mahakama ya madhabahu yangu takatifu.”
10Njooni pitieni, pitieni katika lango! Tengenezeni mapito ya watu! Itengenezeni, Tengeneza njia kuu! Kusanyeni mawe! Nyanyueni juu ishara ya bendera kwa mataifa!
11Tazama, Yahwe ametangaza mwisho wa nchi, “Waambie binti Sayuni: Tazama, Mkombozi wenu anakuja! Angalia, amebeba zawadi zake, na malipo yake yapo mbele yake.”
12Watakuita wewe, “Mtu mtakatifu; Uliokombolewa na Yahwe,” nawe utaitwa “Uliyetafutwa, Mji usiotelekezwa.”

63

1Ni nani ajaye kutoka Edomu, aliyevaa mavazi ya rangi nyekundu kutoka Bozra? Ni nani aliye katika mavazi ya kifahari, anayetembea kwa kujiamini kwa sababu ya ukuu wa nguvu zake? Ndiye mimi, nizungumzaye haki na uwezo mkubwa wa kuokoa.

2Kwa nini umevaa mavazi ya rangi nyekundu, na kwa nini wanaonekana kama akanyagae mizabibu katika vyombo vyake.
3Nimekanyaga zabibu lililoko katika vyombo vyenyewe, na hakuna hata mmoja kutoka mataifa aliyeungana na mimi. Niliwakanyaga kwa hasira yangu na niliwakanyaga wao kwa hasira yangu. Damu zao zimeruka katika nguo zangu na kuweka madoa nguo zangu zote.
4Maana niliangalia mbele katika siku ya kisasi, na mwaka wa ukombozi ulikwisha wadia.
5Mimi nilitazama, na hapo hapakuwa na mtu mmoja hata wa kutoa msaada, lakini mkono wangu mwenywe uliniletea ushindi mimi, na hasira yangu kubwa iliniongoza mimi.
6Niliwakanyaga watu wangu chini kwa hasira yangu na kuwafanya wao wanywe laana yangu, na nilimwaga damu zao juu ya nchi.
7Nitakusimulia matendo ya agano la Yahwe lenye kuaminika, matendo ya kusifu ya Yahwe. Nitawasimulia yote ambayo Yahwe ametutendea sisi, na ukuu wa uzuri wake katika nyumba ya Israeli. Huruma hii aliyetuonyesha sisi kwa sababu ya rehema zake na matendo ya agano lake la kuaminika.
8Maana alisema, “Baadhi yao ni watu wangu, watoto ambao sio waaminifu.” Amekuwa mwokozi wao.
9Kupitia mateso yao yote, aliteseka pia, na malaika kutoka mbele yake aliwaokoa wao. Katika upendo wake na rehema aliwakomboa wao, na aliwanyanyua juu na aliwabeba wote katika kipindi chote cha kale.
10Lakini walimuasi na kumuhuzunisha roho mtakatifu. Hivyo basi akawa adui wao na kupigana dhidi yao.
11Watu wake walifikiri kuhushu nyakati za kale za Musa. Walisema, “Yuko wapi Mungu, aliyewaleta juu nje ya bahari pamoja na mchungaji wa kundi lake? Yuko wapi Mungu, ambaye aliyeweka roho mtakatifu mwiongoni mwenu?
12Yuko wapi Mungu, aliyeufanya wingi wa utukufu wake kwenda katika mkono wa kuume wa Musa, na ukagawanya maji mbele yao, kulifanya jina lake milele yeye mwenyewe?
13Yuko wapi Mungu, aliyewaongoza katika maji mengi? Kama farasi anayekimbia kwenye aridhi ambayo ni tambarare, hawakua na mashaka.
14Kama ng'ombe anayeshuka chini kwenye bonde, Roho ya Yahwe imewapa punziko. Hivyo umewaongoza watu wako, kufanya wewe mwenyewe jina la kusifu.
15Tazama chini kutoka mbinguni na pata taarifa kutoka kwenye makao ya utukufu wako. Iko wapi bidii yenu na matendo makuu? Matendo yako ya huruma yamezuiliwaa kutoka kwetu.
16Maana wewe ni baba yetu, Japokuwa Ibrahimu hatujui sisi, na Israeli haitutambui sisi, wewe, Yahwe, wewe ni baba yetu. Mkombozi wetu limekuwa jina lako kutoka nyakati za kale.
17Yahwe, kwa nini unatufanya tutangetange na kuifanya mioyo yetu kuwa migumu, hivyo hatukukuheshimu wewe? Rudi kwa niaba ya watumishi wako, kabila la urithi wako.
18Watu wako walirithi mahali patakatifu kwa mda mfupi, halafu maadui zetu waliwakanyaga.
19Tumekuwa kama juu ya wale ambao hawajawai kuongoza, kama wale ambao hawajaitwa kwa jina lako.

64

1“Oh, ikiwa umeigawa kwa kuifungua mbingu na kushuka chini! Milima imetikisika mbele yako,

2ni kama vile moto uunguzao vichaka, moto uchemshao maji. Oh, jina lako lingejulikana kwa maadui wako, na ya kwamba mataifa yangetetemeka mbele yako!
3Awali, ulipofanya mambo ya ajabu ambayo hatukuyategemea, ulishuka chini, milima ikatetemeka mbele zako.
4Tangu nyakati za kale hakuna hata mmoja aliyesikia au kujua, wala jicho kuona Mungu yeyote karibu yake, ni nani afanyae mambo haya kwake anayemsubiri yeye.
5Umekuja kuwasidia wale wanaofurahia kutenda yaliyo ya haki, wale wanaowaita kuwakumbusha njia zake na kumheshimu yeye. Ulipatwa na hasira tulipotenda dhambi. Katika njia zako daima tutakombolewa.
6Maana sote tumekuwa kama mmoja aliye na unajisi, na matendo yetu ya haki yamekuwa kama hedhi kali. Sote tumenyauka kama majani; maovu yetu, ni kama upepo, unaotupeperusha sisi mbali.
7Hakuna hata mmoja anayeita jina lako, hakuna anayefanya jitihada za kukushika wewe; maana umeuficha uso wako mbali na sisi na kutufanya sisi kuwa takataka katika mkono wa maovu yetu.
8Na lakini, Yahwe, wewe ni baba yetu; sisi ni udongo. Wewe ni mfinyanzi wetu; sisi ni kazi ya mkono wako.
9Usiwe na hasira kubwa, Yahwe, wala daima usikumbuke maovu dhidi yetu, tafadhali sisi sote, watu wako.
10Miji yenu mitakatifu imekuwa jangwa; Sayuni imekuwa jangwa, Yerusalemu imekuwa ukiwa.
11Hekalu letu takatifu na zuri. Mahali ambapo baba zetu walikusifu wewe, limeangamizwa kwa moto, na kila kilichokuwa karibu kiliharibiwa.
12Je unawezaje kuendelea kumshika, Yahwe? Unawezaje kutulia kimya na kuendelea kutufedhehesha sisi?”

65

1Nilikuwa tayari kuchaguliwa na wale ambao hawakuniomba; Nilikuwa tayari kupatikana kwa wale ambao hawakunitafuta. Nilisema, “Niko hapa!’ kwa taifa ambalo halikuita jina langu.

2Nimetawanya mikono yangu siku zote kuwasumbua watu wangu, wanao tembea katika njia isiyopasa, wanaotembea kwa kufuata mawazo yao wenyewe na mipango yao.
3Kuna watu wanoendelea kunipinga mimi, wanatoa sadaka zao katika bustani, na kuchoma ubani juu ya matofali.
4Wamekaa miongoni mwa makaburi na kuangalia usiku kucha, na hula nyama ya nguruwe na mchuzi mchafu wa nyama katika vyombo vyao.
5Wanasema, ‘Simama mbali, usisogee karibu na mimi, maana mimi ni mtakatifu zaidi yako.’ Vitu hivi ni moshi katika pua zangu, moto uwakao mchana kutwa.
6Tazama, imeandikwa mbele yangu: Sitanyamaza, Maana nitawalipa wao tena; nitafanya malipo yao katika miguu yao,
7kwa sababu ya dhambi zao na dhambi za baba zao kwa pamoja.” Asema Yahwe. “Nitawajibu wao kwa kuchoma ubani juu ya milima na kunifanyia mimi juu ya vilima. Hivyo basi nitapima juu ya matendo yao ya kale katika miguu yao.”

8Yahwe asema hivi, “Ikiwa divai mpya itapatikana katika nguzo ya zabibu, wakati mmoja ataposema, ‘Usihiaribu hiyo, maa kuna uzuri ndani yake; hichi ndicho nitakachokifanya kwa niaba ya watumishi wangu: Sitawaribu wao wote.
9Nitazileta koo kutoka kwa Yakobo, na kutoka Yuda wao ambao watairithi milima yangu. Niliowachagua watairithi ardhi, na watumishi wangu wataishi pale.
10Sharoni itakuwa malisho ya makundi, na bonde la Akori itakuwa sehemu ya kupumzikia ya makundi yangu, kwa watu wangu wanaonitafuta mimi.
11Lakini yeye aliyeachana na Yahwe, anayeusahau mlima wangu mtakatifu, anayeandaa meza kwa bahati ya mungu, na kujaza kikombe cha mvinyo uliochanganywa na miungu inayoitwa Hatama.
12Nitaufikisha mwisho wenu kwa upanga, na wato mtainama chini kwa kuchinjwa, Kwa sababu nilipokuita wewe, haukuitikia; nilipozungumza haukunisikiliza. Lakini mlifanya yaliyo mabaya katika macho yangu na kuchagua kufanya yasiyo nipendeza mimi.”
13Bwana Yahwe asema hivi, “Tazama, mtumishi atakula, lakini atashikwa na njaa; tazama mtumishi wangu atakunywa lakini atakuwa na kiu; tazama mtumishi wangu atashangilia, lakini atatiwa katika aibu.
14Tazama, mtumishi wangu atapiga kelele za furaha kwa sababu ya furaha ya moyo, lakini utalia kwa sababu ya maumivu ya moyo, na mtapiga kelele kwa sababu ya kusagwa kwa roho zenu.
151 Nanyi mtaliacha jina lenu nyuma kama laana kwa watu niliowachagua wazungumze; Mimi Bwana Yahwe, Nitakuwa wewe; Nitawaita watumishi wangu kwa jina lingine.
16Yeyote atakaye tamka baraka juu ya nchi atabarikiwa na mimi, Mungu wa kweli. Yeyote achukuaye kiapo juu ya nchi anaapa na mimi, Mungu wa kweli, kwa sababu matatizo ya nyuma yatasaulika, maana yatafichwa machoni pangu.
17Maana tazama, Ninakaribia kuumba mbingu mpya na nchi mpya; na mambo ya kale hayatakumbukwa tena wala kufikiriwa katika akili.
18Lakini mtakuwa na furaha na kushangilia daima kwa nitakachokiumba. Tazama, Ninakaribia kuumba Yerusalemu mpya kama furaha na watu wake wenye furaha.
19Nitafurahia juu ya Yerusalemu watu wangu; kuomboleza na kilio cha dhiki hakitasikika tena ndani yake.
20Hakuna tena mwana atakayeishi pale japo kwa siku chache; wala mzee kufa kabla ya mda wake. Yule atakayekufa katika umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama mtu mdogo. Yeyote ambaye atashindwa kufikia umri wa miaka mia moja atachukuliwa kama laana.
21Watazijenga nyumba na kukaa huko, na watapanda mizabibu na kula matunda yake.
22Hawatajenga nyumba na wengine waishi humo; hawatapanda, na wengine wale; maana kama siku za miti zitakuwa siku za watu wangu. Watu wangu wataishi kikamilifu kwa kazi ya mikono yao.
23Hawatafanya kazi bure, wala kuzaa kwa kusikitishwa. Maana ni watoto wa waliobarikiwa na Yahwe, pamoja na koo zao.
24Kabla hawajaita, nitaitika; na wakati wanaendele kuzungumza, nitasikia. Mbwa mwitu na kondoo watachungwa pamoja, na simba atakula majani kama ng'ombe; lakini udongo utakuwa chakula cha nyoka.
25Hawataumiza tena wala kuharibu juu ya mlima wangu mtakatifu,” asema Yahwe.

66

1Yahwe asema hivi, “Mbinguni ni makao yangu, na nchi ni miguu yangu. Iko wapi nyumba uliyonitengenezea mimi? Iko wapi sehemu amabayo ninaweza kupumzika?

2Mkono wangu umeyafanya haya yote; hivi ndivyo jinsi ambavyo vitu vitatokeavyo---hili ndilo tamko la Yahwe. Mtu niliyempitisha, mwenye roho iliyopondeka na mwenye kujutia roho, na atetemekaye kwa ajili ya neno langu.
3Yeyote achinjaye ng'ombe humuua mtu pia; yeye anayetoa sadaka ya kondoo huvunja shingo ya mbwa pia; yeye anayetoa sadaka ya mavuno anatoa sadaka ya damu yangurue; yeye anayetoa kumbukumbu la vumba huwabariki wakosaji pia. Wamechagua njia zao wenyewe wanachukua radhi kwa uchafu wao wenyewe.
4Katika njia hiyo hiyo nitachagua adhabu yao wenyewe; Nitaleta juu yao kitu wanachokiogopa, maana nilipowaita, hakuna aliyeitika; nilipozungumza hakuna aliyenisikiliza mimi. Walifanya yaliyo maovu mbele yangu, na kuchagua yasiyo nipendeza mimi.”
5Sikiliza neno la Yahwe, ewe utetemekaye kwa neno lake, “Kaka zako wanaonichukia na kukutenga wewe kwa ajili ya jina langu walisema, ‘Na atukuzwe Yahwe, halafu tutaiona furaha yenu; lakini mtatiwa katika aibu.
6Sauti ya vita vya ghasi vinakuja katika mji, sauti kutoka hekaluni, sauti ya Yahwe anawarudia maadui zake.
7Kabla hajaenda katika chumba, hujifungua; kabla ya uchungu kumtoka hujifungua mwana wa kiume.
8Ni nani asikiaye mambo haya? Ni nani aonaye mambo haya? Je taifa linaweza kuanzishwa kwa wakati mmoja? Lakini kwa haraka Sayuni inapokwenda katika chumba, hujifungua watoto wake.
9Ninawezaje kumleta mwana azaliwe na nisimruhusu mwana azaliwe? Yahwe auliza? -- Au Je ninamleta mwana wakati tu wa kujifungua na halafu nimshikilie tena - anauliza Yahwe.”
10Furahia na Yerusalemu na fuhahia kwa ajili yake, ninyi nyote mnaopenda yeye; furahia pamoja na yeye, ninyi mnaomboleza juu yake!
11Maana utamuuguza na ataridhika, katika maziwa yake atakufariji; utakunywa mpaka ushibe na kufurahia kwa wingi wa utukufu wake.

12Yahwe asema hivi, “Ninakaribia kutawanya mafanikio juu katika mto, na utajiri wa mataifa kama wingi wa mkondo wa maji. Utamuuguza kwa upande wake, na kubebwa katika mikono yake, mtabebwa juu ya magoti yake.
13Kama vile mama anavyomfariji mwana wake, hivyo basi nami nitawafariji ninyi, na mtapata faraja katika Yerusalemu.”
14Utayaona haya, na moyo wako utafurahia, na mifupa yako itachipukia kama zabuni ya nyasi. Aridhi ya Yahwe itajulikana kwa watumishi wake, lakini atawaonyesha hasira yake dhidi ya maadui zake.
15Kwa kutazama, Yahwe anakuja kwa moto, na gari lake linakuja kama upepo wa dhoruba kuleta joto katika hasira yake na kukemea kwake ni kama moto uwakao.
16Maana Yahwe ametekeleza hukumu juu ya watu kwa moto na kwa upanga wake. Wale watakaouliwa na Yahwe watakuwa wengi.

17Watajiweka wakfu wenyewe na kujisafisha wenywe, ili waweze kuingia katika bustani, kumfuata aliyeko katikati ya wale walao nyama ya nguruwe na vitu haramu kama panya. “Watafika mwisho - hili ni tamko la Yahwe.

18Maana ninayajua matendo yao na mawazo yao. Wakati utafika nitakapoyakusanya mataifa yote na lugha zote. Watakuja na kuona utukufu wangu.

19Nitaweka ishara ya ukuu wangu miongoni mwao. Halafu nitawatuma wakazi kutoka miongoni mwao kwa mataifa. Kwa Tarshishi, Puti, na Ludi, upinde wale wanaochukua upinde wao, kwa Tubali, Javani, na umbali kuelekea katika pwani kule ambapo hawajasikia chochote kuhusu mimi wala kuona utukufu wangu. Watatangaza utukufu wangu miongoni mwa mataifa.20Watawaleta kaka zako wote nje ya mataifa yote, kama sadaka kwa Yahwe. Watakuja kwa farasi na kwa gari, na kwa gari, juu ya nyumbu na juu ya ngamia, kuelekea mlima wangu mtakatifu Yerusalemu - asema Yahwe. Maana watu wangu wa Israeli wataleta sadaka ya mavuno kwenye vyombo visafi katika nyumba ya Yahwe.21Baadhi ya vitu hivi nitavichagua kama makuhani na walawi -- asema Yahwe.

22Maana itakuwa mbingu mpya na nchi mpya ambayo nitakayoifanya ibaki mbele zangu-- Hili ndilo tamko la Yahwe-- Hivyo ndivyo ukoo wenu utakavyobakia, na jina lenu litabaki.23Kutoka mwenzi mmoja mpaka mwingine, na kutoka sabato moja mpaka nyingine, watu wote watakuja kukuinamia chini--- asema Yahwe.24Watakwenda nje na kuona miili ya wafu ya watu walioniasi mimi, maana wadudu wawalao wao hawatakufa, na moto uwaunguzao hautazimika; na itakuwa ni chuki kwa wale wote wenye mwili.’

Yeremia

1

1Hili ndilo neno la Yeremia mwana wa Hilikia; yeye alikuwa mmoja wa makuhani kule Anatothi katika nchi ya Benjamini.2Neno la BWANA lilimjia katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na tatu wa utawala wake.3Lakini pia lilimjia katika wakati wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, mpaka mwezi wa tano wa mwaka wa kumi na moja wa Zedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, wakati watu wa Yerusalemu walipochukuliwa kuwa watumwa.4Neno la BWANA lilinijia, likisema,

5“Kabla sijakuumba tumboni, Nilikuchagua; kabla hujazailiwa toka tumboni Nilikutenga; Nilikufanya kuwa nabii kwa mataifa.”

6“Ahaa, BWANA!” Nilisema, “mimi sijui kusema, kwa kuwa mimi ni mtoto.”7Lakini BWANA akaniambia, “Usiseme, ‘mimi ni mtoto.’ Utaenda kila mahali ninapokutuma, na utasema kila kitu ninachokuamuru!8Usiwaogope hao, kwa kuwa Mimi niko pamoja na wewe kukuokoa -BWANA asema.”9Kisha BWANA akanyosha mkono wake, akagusa kinywa changu, na akaniambia, “Nimeweka maneno yangu kinywani mwako.10Nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya wafalme, ili kung'oa na kuvunja, kuharibu na kutupa, kujenga na kupanda.”11Neno la BWANA lilinijia, likisema, “Yeremia, unaona nini?” Nikasema, “Ninaona tawi la mlozi.”

12BWANA akaniambia, “umeona vyema, kwa kuwa ninaliangalia neno langu ili nilitimize.”13Neno la BWANA lilinijia mara ya pili likisema, “Unaona nini? “Nikasema, “Ninaona chungu kikichemuka, ambacho mdomo wake unaelekea toka upande wa kaskazini,”

14BWANA akaniambia, “Janga litatokea kaskazini juu ya wote wanaoishi katika nchi hii.
15Kwa kuwa ninayaita makabila yote ya falme za kaskazini, asema BWANA. Yatakuja, na kila mmoja ataweka enzi yake katika malango ya Yerusalemu, dhidi ya kuta zote zinazoizunguka, na dhidi ya miji ya Yuda.
16Nitatamka hukumu dhidi yao juu ya uovu wao wa kuniacha, kwa kufukiza uvumba kwa miungu mingine, na kwa kuabudu kile walichotengeneza kwa mikono yao.

17Jiandae! Simama ukawaambie kila kitu ninachokuamuru. Usifadhaike mbele zao nisije nikakufadhaisha wewe mbele zao!18Tazama! Leo nimekufanya kuwa mji ulio na ngome, kuwa ngome ya chuma, na ukuta wa shaba dhidi ya nchi yote - dhidi ya wafalme wa Yuda, na juu ya wakuu wake, na juu ya makuhani wake, na juu ya watu wote wa nchi.19Watapigana na wewe, lakini hawatakushinda, kwa kuwa nitakuwa pamoja na wewe ili kukuokoa- asema BWANA.”

2

1Neno la BWANA lilinijia likisema,2“Nenda ukanene katika masikio ya Yerusalemu. Useme; BWANA asema hivi: Ninakumbuka agano la uaminifu la ujana wako, upendo wako wakati tulipokuwa tumechumbiana, ulipokuwa ukinihitaji kule jangwani, katika ile nchi iliyokuwa haijapandwa.

3Israeli alikuwa ametengwa kwa BWANA, malimbuko yake ya mavuno yake! Wote waliokula malimbuko yake walikuwa na hatia! Majanga yaliwajia--asema BWANA.’”
4Sikilizeni neno la BWANA, enyi nyumba ya Yakobo na kila familia katika nyumba ya Israeli.

5BWANA anasema hivi, “Ni makosa gani ambayo baba zenu waliyaona kwangu, hata wakatae kunifuata mimi? Hata wazifuate sanamu ambazo hazina chochote na wao kuwa si kitu?
6Wala hawakusema, BWANA yuko wapi, ambaye alitutoa katika nchi ya Misri? BWANA yuko wapi, ambaye alituongoza katika jangwa, katika nchi ya Araba na mashimo, katika nchi ya ukame na giza nene, katika nchi ambayo hakuna mtu apitaye wala hakuna mtu anayeishi humo?
7Lakini niliwaleta katika nchi ya Kameli, ili mle matunda yake na vitu vingine vyema! Lakini mlipokuja, mliitia unajisi nchi yangu, mliufanya urithi wangu kuwa chukizo!
8Hata makuhani hawakusema, ‘BWANA yuko wapi?’ na watalamu wa sheria hawakunijali mimi! Wachungaji wametenda dhambi dhidi yangu. Manabii wamemtolea Baali unabii na kuvitafuta vitu ambavyo havina faida.
9Kwa hiyo nitaendelea kuwashitaki - hili ni neno la BWANA - na nitawashitaki watoto wa watoto wenu.
10Kwa kuvuka kwenda hadi pwani ya Kitimu na kutazama. Tuma wajumbe kwenda Kedari na tafuta uone kama iliwahi kutokea hapo awali vitu kama hivi.
11Je, taifa limebadilisha miungu, hata kama haikuwa miungu? Lakini watu wangu wameubadili utukufu wao kwa kitu ambacho hakiwezi kuwasaidia.
12Sitaajabuni, enyi mbingu kwa sababu ya hili! Tetemekeni na kuogopa -asema BWANA.
13Kwa kuwa watu wangu wametenda maovu mawili dhidi yangu: Wameziacha chemichemi za maji ya uhai kwa kuchimba mabirika kwa ajili yao, mabirika yanayovuja yasiyoweza kutunza maji!
14Je, Israeli ni mtumwa? Kwani hakuzaliwa nyumbani? Kwa nini sasa amekuwa nyara?
15Wanasimba wameunguruma dhidi yake. Wamepiga kelele sana na kuifanya kuwa ukiwa. Miji yake imeharibiwa na kubaki bila watu.
16Pia watu wa Nufu na Tahapanesi watakinyoa kichwa chako.
17Je, hamkufanya haya kwa ajili yenu mlipomwacha BWANA, wakati Mungu wenu, alipokuwa akiwaongoza njiani?
18Kwa hiyo, kwa nini kutafuta msaada Misri na kunywa maji ya Shihori? Kwa nini kutafuta msaada Ashuru na kunywa maji ya Mto Frati?
19Uovu wako unakukemea, na maasi yako yatakuadhibu. Kwa hiyo yafikiri hayo; tambua kuwa ni uovu na uchungu kwenu ninyi kuniacha mimi, BWANA Mungu wako, na kutokuwa na hofu yangu - asema BWANA wa majeshi.
20Kwa kuwa niliivunja nira yenu mliyokuwa nayo wakati wa kale; Nilivichana vifungo vyako kutoka kwako. Lakini bado ulisema, ‘Sitamtumikia!’ tangu ulipopiga magoti katika kila kilima kuusogelea kila mti wenye majani mabichi, enyi makahaba.
21Lakini mimi mwenyewe niliwapanda kama mzabibu niliouchagua, mbegu iliyokamilika. Lakini tazama jinsi ulivyobadilika mbele yangu, na kuwa mzabibu usiofaa na mzabibu pori!
22Kwa kuwa hata kama utajisafisha mwenyewe mtoni na kuoga kwa sabuni kali, bado dhambi yako ni madoa mbele yangu - asema BWANA Mungu.
23Wawezaje kusema, ‘Mimi sijanajisika! Mimi sijaenda kwa Mabaali?’ Tazama tabia zako zilivyokuwa bondeni! Tambua kile ulichofanya kule bondeni, wewe ngamia mwepesi! Akimbiaye katika njia yake!
24Wewe ni punda wa mwitu, aliyeizoelea nyika, avutaye pumzi za upepo usiofaa katika tamaa ya kuishi! Ni nani awezaye kumgeuza anapotafuta dume la kumpanda? Na punda ndume amtafutaye hajichoshi mwenyewe. Huenda kwake wakati wa mwezi wa kupandwa.
25Lazima uizuie miguu yako isikose kiatu na koo lako kuwa na kiu! Lakini umesema, ‘Hakuna matumaini! Hapana! Nawapenda wageni nami huwatafuta!’
26Kama aibu ya mwizi ilivyo anapokuwa amekamatwa, ndivyo aibu ya Israeli itakavyokuwa - wao, wafalme wao, malikia wao, makuhani na manabii wao!
27Hawa ndio wale waiambiayo miti, ‘Ninyi ndio baba zangu,’ na mawe, ‘Ninyi ndio mlinizaa.’ Kwa kuwa migongo yao hunitazama na siyo nyuso zao. Hata hivyo, wakati wa shida husema, ‘Amka utuokoe!’
28Lakini iko wapi ile miungu mliyojitengenezea? Acha hao wainuke kama wanaweza kuwaokoa wakati wa shida, kwa kuwa hizo sanamu zenu zina idadi sawa na miji yenu, katika Yuda.
29Kwa hiyo kwa nini kunituhumu kwa kufanya makosa? Ninyi nyote mmeniasi - asema BWANA wa majeshi.
30Nimewaadhibu watu wenu bure. Wala hawakutaka kurudiwa. Upanga wako umewaangamiza manabii wenu kama simba aangamizaye!

31Enyi watu wa kizazi hiki! Sikilizeni neno langu, neno la BWANA! Je, nimekuwa jangwa kwa Israeli? Au nchi yenye giza nene? Kwa nini watu wangu husema, ‘Acha tuzunguke zunguke, hatutakuja kwako tena’?
32Je, mwanamwali anaweza kusahau mapambo yake, na bibi arusi mavazi yake? Lakini watu wangu wamenisahau mimi kwa siku nyingi!
33Jinsi mlivyotengeneza njia zenu vizuri ili kutafuta mapenzi. Hata mmewafundisha njia zenu wanawake waovu.
34Damu ambayo ilikuwa ndio uhai wa watu wasio na hatia, imeonekana katika mavazi yenu. Hawa watu hawajawahi kuonekana katika matendo maovu.
35Pamoja na mambo haya yote, wewe unaendelea kusema kuwa hauna hatia. Kwa hakika hasira ya BWANA itageuka kutoka kwangu. ‘Lakini tazama! Utahukumiwa kwa sababu, ‘Sikutenda dhambi.’
36Kwa nini mnatangatanga kwa urahisi katika njia zenu? Pia Misri itawahuzunisha sana, kama ilivyokuwa kwa Ashuru.
37Mtaondoka hapo mkiwa mmehuzunika sana, mkiwa mmeweka mikono vichwani mwenu, kwa kuwa BWANA amemkuta yule mliyemtumainia, kwa hiyo hamtapata msaada toka kwao.”

3

1Wanasema, ‘Mwanamume akimfukuza mke wake, naye akaondoka kwake na kuwa mke wa mwanamume mwingine. Je, anaweza kumrudia tena? Je huyo si najisi kabisa?’ Huyo mwanamke ndiyo hii nchi! Mmetenda kama Kahaba aliye na wapenzi wengi, na sasa mnapenda kurudi kwangu tena? - Asema BWANA wa majeshi.

2Inua macho yako uvitazame vielele tasa! Je kuna mahali ambapo hukufanya ukahaba? Pembeni mwa barabara ulikaa ukisubiri wapenzi wako, kama vile Mwarabu jangwani. Umeiharibu nchi kwa ukahaba na uovu wako.
3Kwa hiyo chemichemi za mvua zilizuiliwa na mvua za vuli hazikunyesha. Lakini uso wako una kiburi, kama uso wa mwanamke kahaba. Unakataa kuona aibu.
4Na sasa hutaniita mimi: ‘Baba yangu, hata marafiki zangu wa tangu ujanani! Je, atakuwa na hasira dhidi yangu milele?
5Je, utaendelea kuwa na hasira zako?’ Tazama! Umesema kuwa utatenda maovu, na kweli umetenda hivyo. Kwa hiyo endelea kufanya hivyo!”

6Kisha BWANA akanena nami katika siku za mfalme Yosia, “Je, unaona jinsi Israeli alivyoniasi? Yeye anaenda kwenye kila kilima na katika kila mti wenye majani mabichi, na kule anafanya kama mwanamke kahaba.7Nikisema, ‘Baada ya kuwa amefanya mambo haya yote, atanirudia,’ lakini hakurudi. Kisha dada yake Yuda ambaye ni mwasi pia aliona alichokifanya.8Kwa hiyo nami nikaona kuwa kwa sababu amefanya uzinzi huu wote. Huyo Israeli aliyeasi! Nilimfukuza na kumpatia talaka ya ndoa. Lakini dada yake Yuda mwenye hana hakuwa na hofu, na yeye akaenda kufanya kama mwanamke kahaba!9Na kwa kuwa yeye aliona kuwa ukahaba ni jambo ndogo sana kwake, ameinajisi nchi, na kufanya ukahaba kwa kutengeneza sanamu za miti na za mawe.10Kisha baada ya haya yote, wala Yuda dada yake muasi hakurudi kwangu na moyo wake wote, bali alikuja na uongo! -Asema BWANA wa majeshi,”

11Kisha BWANA akanena na mimi, “Israeli muasi amekuwa mwenye haki zaidi kuliko Yuda muasi!12Nenda ukaseme maneno haya huko kaskazini. Uwaambie, ‘Rudi wewe Israeli uliyeasi! - Asema BWANA - sitakuwa na hasira dhidi yako kila wakati. Kwa kuwa mimi ni mwaminifu - asema BWANA - sitakuwa na hasira milele.
13Kiri uovu wako, kwa kuwa umefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wako; umemshirikisha njia zako geni chini ya kila mti wenye majani mabichi! Wala hukuisikiliza sauti yangu! - Asema BWANA.
14Rudini, enyi watu waasi! - Asema BWANA - kwa kuwa mimi nimekuoa wewe! Nitakurudisha wewe, mmoja katika mji, wawili katika ukoo mmoja, na nitawarudisha Sayuni!
15Nitawapa wachungaji niwapendao, na watawachunga kwa maarifa na ufahamu.
16Ndipo itakapotokea kuwa utaongezeka na kuzaa matunda katika nchi hiyo siku hizo-asema BWANA. Hawataweza kusema kuwa, “Sanduku la agano la BWANA! Jambo hili hawatalikumbuka tena katika mioyo yao, kwa kuwa hawataliwaza tena wala kulijali tena. Usemi huu hawatau sema tena.’
17Katika wakati huo watasema juu ya Yerusalemu, ‘Hii ndiyo enzi ya BWANA,’ na mataifa mengine yote yatakusanyika Yerusalemu katika jina la BWANA. Hawataishi katika taabu ya uovu wa mioyo yao.
18Katika siku hizo, nyumba ya Yuda itaishi na nyumba ya Israeli. Watarudi pamoja kutoka katika nchi ya kaskazini katika nchi niliyowapa mababu wao kuwa urithi.

19Lakini mimi, Nilisema, ‘Jinsi nipendavyo kukuheshimu kama mwanangu na kukupa nchi ipendezayo, kuwa urithi mzuri kuliko ulio katika taifa lolote!’ Nami nikasema, “mtaniita baba yangu.” ‘Nami nitasema kwamba hamtageuka na kuacha kunifuata.
20Lakini kama mwanamke aliyemwasi mume wake, mmenisaliti, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA.”
21Sauti ilisikika juu ya nyanda, kilio na kusihi kwa watu wa Israeli! Kwa kuwa wamezibadili njia; wamemsahau BWANA, Mungu wao.
22“Rudini enyi watu mlioasi! Nami nitawaponya na uasi wenu!” “Tazama! Tutakuja kwako, kwa kuwa wewe ni BWANA, Mungu wetu!
23Hakika Uongo hutoka kwenye vilima, kutoka kwenye milima mingi. Kwa hakika wokovu wa Israeli unapatikana kwa BWANA, Mungu wetu.
24Lakini miungu ya aibu imeangamiza kazi ambayo mababu zetu waliifanya - makundi yao ya kondoo na ng'ombe, wana wao na binti zao!
25Na tulale chini kwa aibu. Aibu yetu na itufunike, kwa kuwa tumefanya dhambi dhidi ya BWANA, Mungu wetu! Sisi wenyewe na mababu zetu, kutoka wakati wa ujana wetu hadi leo, hatujaisikiliza sauti ya BWANA, Mungu wetu!”

4

1“Kama utarudi, Israeli- asema BWANA - ikawa kwangu kwamba umerudi. Kama utaondoa hayo mambo yachukizayo mbele yangu na ukaacha kunikimbia mimi tena,

2na ukaapa hivi, ‘kama BWANA aishivyo katika kweli, na haki, na katika hukumu.’ Mataifa yataniomba baraka, na yatanisifu mimi.

3Kwa kuwa BWANA asema hivi kwa kila mmoja katika Yuda na Yerusalemu; ‘Limeni shamba zenu na msipande katika miiba.
4Mtahiriwe kwa BWANA na kuondoa govi za mioyo yenu, ninyi wanaume wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu, vinginevyo hasira yangu itawaka kama moto na kuteketeza, na hakutakuwa na mtu wa kuizima, hii itatokea kwa sababu ya uovu wa matendo yenu.
5Waambie Yuda na Yerusalemu isikie. Waambie, “pigeni baragumu katika nchi.” Tangazeni, “Kusanyeni pamoja. Twendeni kwenye miji ya Maboma.”
6Inueni ishara za bendera na zielekezeni Sayuni, na kimbilieni usalama! Msibaki, kwa kuwa ninaleta majanga kutokea kaskazini na anguko kubwa.
7Simba anakuja kutokea kwenye kichaka chake na yeye atakayeyaharibu mataifa ameanza kuja. Anaondoka kwenye eneo lake ili aache hofu katika nchi yenu, kuibadili miji yenu kwa uharibifu, ambapo hakuna hata mmoja atakayeishi. Kwa sababu hii vaeni magunia, lieni na kuomboleza.

8Kwa kuwa nguvu ya hasira ya BWANA haijaondoka kwetu.
9Ndipo itakapotokea katika siku hiyo - asema BWANA - mioyo ya mfalme na wakuu itakufa. Makuhani watastaajabu na manabii watashangaa.’”

10Kwa hiyo nikasema, “Ahaa! Bwana Mungu. Kwa hakika umewadanganya watu hawa na Yerusalemu kwa kuwaambia, ‘Kutakuwa na amani kwenu.’ Wakati upanga unawaangukia dhidi ya maisha yao.”

11Wakati huo itasemwa juu ya mji huu na Yerusalemu kuwa, “Upepo uwakao kutoka katika nyanda za jangwani utachukua njia yake kuelekea kwa binti wa watu wangu. Hautapepetwa wala kuwatakasa.
12Upepo ulio na nguvu sana utakuja kwa amri yangu, na sasa nitapitisha hukumu dhidi yao.
13Tazama anavamia kama wingu, na magari yake ni kama dhoruba. Farasi wake wana mbio kuliko tai. Ole wetu kwa kuwa tutaharibiwa!
14Itakaseni mioyo yenu kutoka uovu wenu, Yerusalemu, ili kwamba muokolewe. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako mpaka lini?
15Kwa kuwa kuna sauti iletayo habari kutoka Dani, na janga lijalo linasikika kutoka vilele vya milima ya Efraimu.
16Yafanyeni mataifa kulifikiria hili: Tazama, na uwatangazie Yerusalemu kuwa wale watekaji wanakuja kutoka katika nchi ya mbali ili kupiga kelele za vita juu ya miji ya Yuda.
17Watakuwa kama walinzi wa shamba lililolimwa dhidi yake pande zote, kwa kuwa amekuwa mpinzani wangu - asema BWANA -
18tabia na matendo yako yamesababisha haya yatokee kwako. Hii itakuwa adhabu yako. Jinsi itakavyokuwa vibaya kwako! Itakupiga moyo wako.
19Moyo wangu! Moyo wangu! Niko katika maumivu ya moyo. Moyo wangu umefadhaika ndani yangu. Siwezi kunyamaza kwa kuwa nasikia sauti za pembe, sauti za vita.
20Anguko baada ya anguko limetangazwa, kwa kuwa nchi yote imeharibika. Wanaharibu masikani yangu na hema yangu ghafla.
21Vita hivi vitaendelea mpaka lini? Ni mpaka lini nitasikiliza sauti za pembe?
22Kwa kuwa upumbavu wa watu wangu - hawanijui mimi. Ni watu wajinga wasio na ufahamu. Wanaufahamu wa mambo maovu, tena hawajui kutenda mema.
23Niliiona nchi, na kuiona! Ilikuwa ukiwa na utupu. Kwa kuwa hapakuwa na taa za mbinguni.
24Nilitazama katika milima. Tazama, ilikuwa inatetemeka, na vilima vyote vilikuwa vinatikisika.
25Nilitazama. Tazama, hapakuwa na mtu, na ndege wote wa angani walikuwa wamekimbia.
26Nikaangalia. Tazama, mashamba yalikuwa jangwa na miji imeangushwa mbele za BWANA, mbele ya hasira yake.”

27Hiki ndicho BWANA asemacho, “Nchi yote itakuwa uharibifu, lakini sitaiharibu yote kabisa.
28Kwa sababu hii, nchi itaomboleza, na mbingu juu zitatiwa giza. Kwa kuwa nimesema haya na kuyakusudia; sitarudi nyuma; Sitaacha kuyatekeleza.
29Kila mji utakimbia kutoka katika kelele za wapandafarasi na wenye pinde; Watakimbilia msituni, Kila mji utapanda hadi mahali pa miamba. Miji itatelekezwa, kwa kuwa hakutakuwa na mtu wa kuishi katika miji hiyo.
30Sasa umeharibiwa, utafanya nini? Japokuwa unavaa mavazi mekundu, unajipamba na mapambo ya dhahabu, na kuyafanya macho yako yaonekane makubwa na kupakwa wanja, wajirembesha bure. Wale wanaume waliokutamani sasa wanakukataa. Badala yake wanajaribu kukuua.
31Kwa hiyo nasikia sauti ya maumivu, yenye uchungu kama ya mwanamke azaaye mtoto wake wa kwanza, sauti ya binti wa Sayuni. Atwetaye kupata pumzi. Ananyosha mikono yake na kusema, ‘Ole wangu mimi! Ninazimia kwa sababu ya wauaji hawa.’”

5

1Kimbieni mkapite katika mitaa ya Yerusalemu, Tafuteni katika viwanja vyake. Tazama na ufikiri kuhusu hili: Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja anayetenda kwa haki na kufanya kwa uaminifu, basi nitaisamehe Yerusalemu.

2Hata kama wanasema, ‘Kama BWANA aishivyo,’ wanaapa uongo.”
3BWANA, macho yako hayatazami uaminifu? Unawapiga watu, lakini hawasikii maumivu. Umewaangamiza kabisa, lakini bado wanakataa kuwa waadilifu. Wanafanya nyuso zao kuwa ngumu kama mwamba, kwa kuwa wanakataa kutubu.
4Kwa hiyo nilisema, “Hakika hawa ni watu masikini. Ni wapumbavu, kwa kuwa hawazijui njia za BWANA, wala maagizo ya Mungu wao.
5Nitaenda kwa watu wa muhimu na kutangaza ujumbe wa Mungu kwao, kwa kuwa angalau wanazijua njia za BWANA, maagizo ya Mungu wao. Lakini wote wanavunja nira yao pamoja; wote wanaivunja ile minyororo inayowafunga kwa ajili ya Mungu.
6Kwa hiyo simba kutoka mwituni atawavamia. Mbweha kutoka Arabaha atawaangamiza. Chui ataivunja miji yao. Mtu yeyota anayeenda nje ya mji wake atavunjwavunjwa. Kwa kuwa maovu yao yameongezeka. Matendo yao ya uasi hayana kikomo.
7Kwa nini niwasamehe hawa watu? Wana wenu wameniacha na wamefanya viapo na wale ambao si miungu. Niliwalisha vya kutosha, lakini wamefanya uasherati na kuchukua alama za nyumba ya uzinzi.
8Walikuwa farasi wanaotafuta kupandwa. Walitembea huku na huku wakitafuta kupandwa. Kila mwanaume alimkaribia mke wa jirani yake.
9Kwa hiyo kwa nini nisiwaadhibu - asema BWANA - na kwa nini nisijilipizie kisasi juu ya taifa kama hili?
10Nenda hadi kwenye kuta za shamba lake la mizabibu na ziharibuni. Lakini wao msiwaharibu kabisa. Ondoeni matawi kwa sababu hayatoki kwa Bwana.
11Kwa sababu nyumba ya Yuda na Israeli wamenisaliti kabisa - asema BWANA -
12Wamenena uongo juu ya Mungu wanasema, “Yeye si halisi. Maovu hayawezi kutupata, wala hatutaona upanga wala njaa.
13Kwa kuwa manabii wamekuwa kama upepo, neno haliko ndani yao, vitisho vyao na vijie wao wenyewe.”’

14Kwa hiyo BWANA, Mungu wa majeshi asema hivi, tazama nataka kuweka maneno yangu katika kinywa chako. Yatakuwa kama moto na watu hawa watakuwa kama kuni! Kwa kuwa utawaramba.
15Tazama nataka kuleta taifa dhidi yenu kutoka mbali, enyi nyumba ya Israeli - asema BWANA - ni taifa linalodumu, taifa la kale! Ni taifa ambalo lugha yake hamuijui, wala hamtaelewa wasemacho.
16Podo lao ni kaburi wazi. Wote ni wanajeshi.
17Kwa hiyo mavuno yako yataliwa, wana wako na binti zako pia, na chakula chako. Watakula kondoo wako na ng'ombe wako, watakula matunda ya zabibu zako na ya mitini. Wataiangusha chini miji yenu na boma zake ambazo mnazitumainia.

18Lakini hata katika siku hizo - asema Bwana - Sikusudii kuwaharibu kabisa.
19Itatokea kwenu, ninyi Yuda na Israeli, mkisema, ‘Kwa nini Bwana Mungu wetu ametufanyia haya yote?’ kwamba wewe Yeremia, utawaambia, ‘Kama vile mlivyomwacha Bwana na kuabudu miungu mingine katika nchi yenu, vivyo hivyo mtawatumikia wageni katika nchi ambayo si yenu.’
20Waambia haya watu wa nyumba ya Yakobo na yasikike katika Yuda. Waambie,
21‘Sikilizeni hili, enyi watu wapumbavu! Sanamu hazina matakwa; zina masikio lakini haziwezi kusikia.
22Je, hamnihofu mimi - asema Bwana - au kutetemeka mbele ya uso wangu? Nimeweka mpaka wa mchanga kwenye bahari, ambao ni agizo la kudumu ambalo halibomoki - hata kama bahari ina kupwa na kujaa, bado hauwezi kubomoka. Hata kama mawimbi yake yanaunguruma, hayawezi kuvuka.
23Lakini hawa watu wana mioyo ya usumbufu. Hugeuka kuwa wapinzani na kuondoka.
24Kwa kuwa hawasemi mioyoni mwao, “basi na tumche Bwana, Mungu wetu, yeye aletaye mvua za awali na mvua za vuli - kwa wakati wake, ambaye hutunza majuma ya mavuno kwa ajili yetu.”
25Uovu wako umezuia haya yasitokee. Dhambi zako zimeyazuia mambo mema yasitokee.
26Kwa kuwa watu waovu wamo kati ya watu wangu. Wanatazama kama mtu anayenyatia ili kukamata ndege; wanaweka mitego na kukamata watu;
27Kama tundu la mtego lijaavyo ndege, nyumba zao zimejaa uongo. Kwa hiyo wanakua na kutajirika.
28Wamenenepa; wanang'aa na kupendeza. Wamepitiliza hata mipaka ya maovu. Wala hawajali sababu ya kuwepo kwa watu na wala uwepo wa yatima. Wanafanikiwa hata kama hawatoi hukumu ya haki kwa yatima.
29Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya haya - asema Bwana - sitajilipizia kisasi juu ya taifa la namna hii?
30Jambo la ajabu na la kuchukiza limetokea katika nchi hii.
31Manabii wanatabiri kwa uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao. Watu wangu wanapenda mambo ya hivyo, lakini mwisho kitatokea nini?

6

1Tafuteni mahali salama, enyi watu wa Benjamini, kwa kuondoka Yerusalemu. Pigeni tarumbeta za Tekoa. Simamisheni ishara juu ya Beth- Hakeremu, kwa uovu unaonekana ukitokea kaskazini; pigo kubwa linakuja.

2Binti za Sayuni, mrembo na mwororo, wataangamizwa.
3Wachungaji na kondoo wao watawaendea; wataweka hema zao zikiwazunguka pande zote; kila mtu atachunga kwa mkono wake.
4Jitakaseni wenyewe kwa miungu kwa ajili ya vita. Inuka, twendeni tukamvamie wakati wa adhuhuri. Ole wetu! Mchana unatoweka na vivuli vya jioni vinakuja.
5Lakini tumvamieni usiku na na tuharibu ngome zake.

6Kwa kuwa Bwana Mungu wa majeshi asema hivi: Kateni miti yake, na tengenezeni vifusi vya kuitekea Yerusalemu. Huu ndio mji sahihi kuteka, kwa sababu umejaa ukandamizaji.
7Kama vile kisima kitoavyo maji, vivyo hivyo mji huu uzaavyo uovu. Uharibifu na jeuri vimesikika kwake. Mateso na tauni viko mbele yangu daima.
8Uadhibishwe, ee Yerusalemu, vingenevyo nitaondoka kwako na kukufanya ukiwa, na nchi isiyokaliwa na watu.

9Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, “Hakika wataokota mabaki ya Israeli waliobaki kama zabibu. Nyosha mkono wako ili uchume zabibu.
10Nitamwambia nani na kumwonya nani ili wasikilize? Tazama! Masikio yao hayakutahiriwa; hayawezi kutilia maanani! Tazama! Neno la Bwana limekuja kuwarudi, lakini hawalitaki.”
11Lakini nimejazwa na hasira za Bwana. Nimechoka kuizuia. Aliniambia, “Imwage mbele ya watoto mitaani na katika makundi ya vijana. Kwa kuwa kila mume atachukuliwa pamoja na mke wake; na kila mzee mwenye miaka mingi.
12Nyumba zao watapewa watu wengine. Kwa kuwa nitawavamia wakazi wa nchi kwa mkono wangu - asema Bwana Mungu wa majeshi.
13Bwana amesema hayo kutoka kwa mdogo hadi kwa mkubwa, kila mmoja anatamani mapato ya udanganyifu. Kuanzia kuhani hadi nabii, kila mmoja anafanya hila.
14Lakini wameponya vidonda vya watu wangu kwa juu juu tu. Wanasema, ‘Amani! Amani! Na kumbe amani haipo.
15Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hasha, hawakuona aibu! Hawakuwa na aibu. Kwa hiyo wataanguka pamoja na wale watakaoanguka wakati nitakapowaadhibu. Wataangushwa chini,” asema Bwana.

16Bwana asema hivi, “Simama kwenye njia panda utazame; uliza zile njia za zamani, ‘Je, hii tabia njema iko wapi?’ Kisha endelea nayo na tafuta mahali pa kupumzika. Lakini watu wanasema, ‘Hatutaenda.’
17Niliweka walinzi juu yenu ili wasikilize tarumbeta. Lakini walisema, ‘Hatutasikiliza.’
18Kwa hiyo, sikilizeni, enyi mataifa! Tazameni, enyi mashahidi, muone kile kitakacho wapata.
19Sikia, wewe dunia! Tazama, niko tayari kuleta janga kwa watu hawa - matunda ya fikra zao. Hawakusikiliza neno langu wala sheria zangu, badala yake walizikataa.
20Huu ubani kutoka sheba unaopanda una maana gani kwangu? Au huu udi kutoka nchi ya mbali? Sadaka zenu za kuteketezwa hazikubaliki kwangu wala dhabihu zenu.

21Kwa hiyo Bwana asema hivi, ‘Tazama, ‘Niko tayari kuweka kikwazo dhidi ya watu hawa. Watajikwaa juu yake - baba na watoto wao kwa pamoja watajikwaa. Wakazi na jirani zao pia watapotea.’

22Bwana asema hivi, ‘Tazama watu wanakuja toka nchi ya kaskazini. Kwa kuwa taifa kubwa limechochewa kutoka nchi ya mbali.
23Watachukua pinde na mishale yao. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mungurumo wa bahari, na wapanda farasi katika mfumo wa wanaume wa vita, enyi binti wa Sayuni,”’
24Tumesikia habari zao. Mikono yetu inalegea kwa dhiki. Na maumivu yametukamata kama utungu wa mwanamke anayezaa.
25Usiende nje mashambani, na usitembee barabarani, kwa kuwa upanga wa adui na hofu vimekaribia.
26Binti wa watu wangu, jivikeni magunia na kugaagaa kwenye majivu ya maombolezo ya mwana pekee. Ombolezeni kwa huzuni kuu, kwa kuwa anaye waangamiza anakuja kwetu ghafula juu yetu.

27“Nimekufanya wewe, Yeremia, kuwajaribu watu wangu kama mtu anayepima fedha, kwa hiyo utachunguza na kupima njia zao.
28Wao ni watu wasumbufu miongoni mwa watu, wanaoenda huko na kule wakisingizia wengine. Wote ni shaba na chuma, wakitenda kwa dhuluma.
29Mifuo inafukuta kwa moto unaoziunguza; risasi inaunguzwa na moto. Risasi tu ndiyo inayotoka kati yake, lakini haifai kitu kwa sababu uovu haujaondolewa.
30Wataitwa taka za fedha, kwa sababu BWANA amewakataa.

7

1Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Yeremia,2Simama katika lango la nyumba ya Bwana na utangaze ujumbe huu! Sikiilizeni neno la Bwana, ninyi nyote watu wa Yuda, ninyi mnaoingia katika malango haya kumwabudu Bwana.3Bwana Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Tengenezeni njia zenu na kufanya mema, nami nitawaacha muishi hapa.4Msitumainie maneno ya uongo mkisema, “Hekalu la Bwana! Hekalu la Bwana! Hekalu la Bwana!”5Bali kama mtazitengeneza njia zenu na kufanya mema; kama mtatoa hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake6kama hamtakandamiza anayekaa katika nchi, yatima, mjane, na kama hamtamwaga damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa, na kama hamtaenda kwa miungu mingine kwa ajili ya maumivu yenu7ndipo nitakapo waacha mkae mahali hapa, katika nchi ambayo niliwaapia mababu zenu toka zamani na hata milele.

8Tazama! Mnatumainia maneno ya uongo ambayo hayawasaidii.9Je, mnaiba. Mnaua, mnafanya uzinzi? Na mnaapa kwa uongo na kufukiza uvumba kwa Baali na kwenda kwa miungu mingine ambao hamkuwajua?10Je, mnakuja na kusimama mbele yangu katika nyumba hii ambapo jina langu linatangazwa na kusema, “Tumeokoka.” Hivyo mnaweza kufanya machukizo yote haya?11Je, hii ndiyo nyumba inayobeba jina langu, pango la wanyang'anyi mbele ya macho yenu? Lakini tazama, Nimeiona - asema Bwana.’

12Kwa hiyo uende mahali pangu kule Shiloh, Kule ambako mwanzoni niliruhusu jina langu kukaa, na tazama kile nilichofanya pale kwa sababu ya maovu ya watu wangu wa Israeli.13Kwa hiyo sasa, kwa sababu ya matendo yako haya yote - asema Bwana - Nilikuambia mara kadhaa, lakini hukusikiliza. Nilikuita, lakini hukuitika.14Kwa hiyo kile nilichofanya Shilo, ndicho ambacho pia nitakachofanya kwa nyumba yangu hii inayoitwa kwa jina langu, nyumba ambayo ninyi mmeitumainia, mahali hapa ambapo niliwapa ninyi na mababu zenu.15Kwa kuwa nitawafukuza mtoke kwangu kama vile nilivyowafukuza ndugu zenu wote, uzao wote wa Efraimu.’

16Na wewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa, na usiinue maombolezo ya kilio au kuomba sala kwa niaba yao, na usinisihi, kwa kuwa sitakusikiliza.17Kwani huoni kile wanachofanya katika miji ya Yuda na katika mitaa ya Yerusalemu?18Watoto wanakusanya kuni na baba zao huwasha moto! Wanawake hukanda unga ili kuoka mikate kwa ajili ya malkia wa mbinguni na kumimina sadaka ya vinywaji kwa miungu mingine ili kunikasirisha mimi.19Ni kweli wananikasirisha mimi? - Asema Bwana - Je, si wao wanaojikasirisha, ili kwamba aibu iwe juu yao?20Kwa hiyo Bwana Mungu asema hivi, ‘Tazama, hasira na gadhabu yangu zitamwagwa juu ya mahali hapa, kwa watu wote na wanyama, juu ya miti katika mashamba na mazao ya ardhi, Itawaka nayo haitazimishwa.

21Bwana Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Jiongezeeni sadaka za kuteketezwa katika dhabihu zenu na mle nyama zake.22Kwani wakati nilipowatoa mababu zenu kutoka nchi ya Misri, Sikuhitaji chochote kutoka kwao. Sikuwapa amri juu ya maswala ya sadaka za kuteketezwa na dhabihu.23Niliwapa amri hii tu, “Sikilizeni sauti yangu, nami nitakuwa Mungu wenu nanyi mtakuwa watu wangu. Kwa hiyo muishi katika njia ambazo ninawaamuru, ili mambo yenu yawe mazuri.”24Lakini hawakunisikiliza wala kuzingatia. Waliishi kwa kufuata mipango yao ya uasi ya mioyo ya maovu, kwa hiyo walirudi nyuma badala ya kuendelea mbele.25Tangu siku ambayo mababu zenu walitoka katika nchi ya Misri mpaka leo, Nimetuma watumishi wangu, manabii wangu, kwenu. Niliendelea kuwatuma.26Lakini hawakuwasikiliza. Hawakuzingatia. Badala yake walishupaza shingo zao. Walikuwa waovu zaidi ya mababu zao.

27Kwa hiyo yatangaze maneno haya yote kwao, japo hawatakusikiliza. Yatangaze mambo haya kwao, lakini hawatakujibu.28Waambie kuwa hili ni taifa ambalo halisikilizi sauti ya Bwana Mungu wake na lisilopokea mafundisho. Ukweli umeharibiwa na kukatwa kutoka kwenye vinywa vyao.
29Zikate nywele zako na kujinyoa, na kuzitupa. Imba wimbo wa maombolezo katika maeneo yaliyo wazi. Kwa kuwa Bwana amekikataa na kukitupa kizazi hiki cha hasira yake.
30Kwa kuwa wana wa Yuda wamefanya maovu mbele ya macho yangu - asema Bwana - wameweka machukizo yao katika nyumba ambayo jina langu hunenwa, ili kulinajisi.31Kisha wamejenga mahali palipoinuka pa Tofethi ambapo pako kwenye bonde la Ben Hinomu. Walifanya hivi ili kuwachoma wana na binti zao kwenye moto - kitu ambacho mimi sikuamuru, wala kuweka jambo hilo katika akili zangu.32Kwa hiyo, tazama siku zinakuja - asema Bwana - ambapo hapataitwa tena Tofethi au bonde la Ben Hinomu. Litakuwa bonde la machinjio; watazika maiti hapo Tofethi mpaka eneo lote lienee.33Mizoga ya watu hawa itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa duniani, na hakutakuwa na mtu wa kuwafukuza.34Nitazikomesha katika miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalaemu sauti za kuinuliwa na vicheko, Sauti ya bwana arusi na ya bibi arusi; kwa kuwa nchi hiyo itakuwa ukiwa.”

8

1Wakati huo - Bwana asema - wataleta kutoka makaburini mifupa ya wafalme wa Yuda na wakuu wake, mifupa ya makuhani na ya manabii na mifupa ya wakazi wa Yerusalemu.2Kisha wataitandaza nje mchana kweupe na mbalamwezi na nyota zote za angani; hivi vitu katika anga vimenifuata na kunitumikia, na kwamba vimetembea na kutafuta, na kwamba vimeniabudu. Mifupa haitakusanywa na kuzikwa tena. Itakuwa kama mavi juu ya uso wa dunia.3Na katika kila eneo lililobaki ambalo nimewafukuza, Watachagua mauti badala ya uzima kwa ajili yao, wote ambao watasalia kutokana na taifa hili ovu - asema Bwana wa majeshi.

4Kwa hiyo uwaambie, ‘Bwana asema hivi: Je, kuna mtu anayeanguka na hasimami? Je, kuna mtu anayepotea na hawezi kujaribu kurudi?
5Kwa nini hawa watu, Yerusalemu, wamegeukia uasi daima? Wanashikilia uongo na wanakataa kutubu.
6Nilikaa kwa uangalifu na nikasikiliza, lakini hawakuongea kilicho sahihi; hakuna aliyetubia uovu wake, hakuna asemaye, “Nimefanya nini?” Kila mmoja wao huenda kule anakotaka, kama farasi aendaye kasi vitani.
7Hata koikoi angani hujua wakati sahihi; na njiwa, na mbayuwayu, na korongo. Huhama kwa wakati sahihi, lakini watu wangu hawayajui maagizo ya Bwana.
8Mtasemaje, “Sisi tuna hekima! Na sheria ya Bwana tunayo?” Hakika, tazama! Kalamu yenye uongo ya mwandishi imefanya uongo.
9Wenye hekima wataaibishwa. Wameyeyuka na kunaswa. Tazama! Wanakataa neno la Bwana, kwa hiyo hekima yao ni kwa ajili ya matumizi gani?
10Kwa wake zao nitawapa wengine, na mashamba yao kwa wale watakao wamiliki, kwa kuwa kuanzia kijana hadi mkuu, kwa pamoja wanatamaa ya mali isiyohalali! Kuanzia nabii hadi kuhani, wote wanasema uongo.
11Kwa kuwa wametibu jeraha ya binti za watu wangu kwa juu juu. Walijisemea, “Amani, Amani,” na kumbe hapakuwa na amani.
12Je, waliona aibu walipofanya machukizo? Hawakuaibika. Hawakuwa na utu. Kwa hiyo wataanguka wakati wa adhabu, pamoja na wale walioanguka. Watatupwa chini, asema Bwana.
13Nitawaondoa kabisa - asema Bwana - hapatakuwa na zabibu kwenye mizabibu yao, wala tini katika mitini yao, kwa kuwa jani litanyauka, na kile nilichowapatia kitaisha.
14Kwa nini tunakaa hapa? Njoni pamoja; twendeni kwenye hiyo miji yenye maboma, na tutakaa kimya kule katika kifo. Kwa kuwa BWANA, Mungu wetu atatunyamazisha. Atatufanya tunywe sumu, kwa kuwa tumemtenda dhambi.
15Tunatumainia amani, lakini hakutakuwa na jema. Tunatumainia wakati wa uponyaji, lakini tazama kutakuwa na hofu.
16Mkoromo wa farasi wake umesikika kutoka Dani. Dunia nzima inatikisika kwa sababu ya sauti ya kukaribia kwa farasi wake wenye nguvu. Kwa kuwa watakuja kuiangamiza nchi na utajiri wake, mji na wote wakaao ndani yake.
17Hebu tazama, ninawatuma nyoka kati yenu, fira ambao hawawezi kuzuiliwa kwa uganga. Watawauma - asema Bwana.”
18Huzuni yangu haina kikomo, na moyo wangu unaugua.
19Tazama! Sauti ya maumivu ya binti wa watu wangu kutoka mbali! Je, Bwana hayumo Sayuni? Je, mfalme wake hayumo ndani yake? Kwa nini sasa wananichukiza kwa vitu vya kuchongwa na sanamu za kigeni zilizo batili?
20Mavuno yamepita, wakati wa hari umekwisha. Lakini sisi hatujaokoka.
21Nimeumia kwa sababu ya maumivu ya binti wa watu wangu. Ninaomboleza kwa sababu ya mambo ya kushangaza ambayo yametokea kwake; Nimeyeyuka.
22Je, kule Gileadi hakuna dawa? Je, huko hayuko mponyaji? Kwa nini uponyaji wa binti wa watu wangu hautokei?

9

1Kama kichwa changu kingetoa maji, na macho yangu kuwa chemichemi ya machozi! Kwa kuwa natamani kulia usiku na mchana kwa ajili yao waliokuwa binti za watu wangu ambao wameuawa.

2Kama mtu angenipatia mahali pa wasafiri nyikani ili nikae, mahali ambapo ningeenda kuwatelekeza watu wangu. Kama ningewaacha, kwa kuwa wote ni wazinzi, kundi la wenye hiana!
3“Huupinda ulimi wao kana kwamba ni upinde ili wapate kuongea uongo, lakini si kwa uamiinifu wao kwamba wanapata nguvu duniani. Wanatoka uovu mmoja hadi mwingine. Hawanijui mimi.” Asema Bwana.
4Kila mmoja wenu, awe mlinzi wa jirani yake na usimwamini hata ndugu yako yeyote. Kwa kuwa kila ndugu ni mwongo.
5Kila jirani anatembea akilaghai. Kila mwanaume anakejeli jirani yake na haongei ukweli. Ndimi zao hufundisha vitu vya uongo. Hujidhoofisha ili kusema uongo.
6Makazi yenu yako kati ya udanganyifu; kwa uongo wao wanakataa kunitambua mimi. Asema Bwana.”
7Kwa hiyo Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, “Tazama, Niko tayari kuwajaribu. Nitawajaribu nione. Jinsi gani niwezavyo kufanya kwa binti za watu wangu?
8Ndimi zao ni mishale iliyochongoka; huongea vitu vya uasi. Kwa midomo yao wanatangaza amani pamoja na jirani zao, lakini katika mioyo yao wanadanganya wakati wa kusubiri.
9Kwa nini nisiwaadhibu kwa sababu ya mambo haya - asema Bwana na kwa nini nisijilipizie kisasi kwa taifa ambalo liko kama hili?
10Nitaimba wimbo wa kuomboleza na kulia kwa ajili ya milima, na wimbo wa mazishi utaimbwa nyikani. Kwa kuwa wameteketezwa kwa hiyo hakuna anayeweza kupita kati kati yao. Hawatasikia sauti ya ng'ombe yeyote. Ndege wa angani na wanyama wote wamekimbia.
11Kwa hiyo nitaigeuza Yerusalemu kuwa vifusi vya ukiwa, maficho ya mbweha. Nitaifanya miji ya Yuda kuwa miji iliyoharibiwa isiyokaliwa na watu.
12Ni nani mwenye hekima anayeyaelewa haya? Je, kinywa cha Bwana kinatangaza nini kwake ili aweze kuyasema? Kwa nini nchi imepotea? Imeharibiwa kama jangwa, ambapo hakuna apitaye kati kati yake.

13Bwana asema, “Ni kwa sababu wameziacha sheria zangu ambazo niliwatengenezea, kwa sababu hawaisikilizi sauti yangu au kuishi kwa kuifuata.14Ni kwa sababu wameishi kwa ushupavu wa mioyo yao na wamewafuata Mabaali kama baba zao walivyowafundisha kufanya.15Kwa hiyo Bwana Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Tazama, Ninataka kuwafanya hawa watu wale pakanga na kunywa maji ya sumu.16Ndipo nitakapo wa sambaza kati ya mataifa ambayo hawajayajua, wao wala mababu zao. Nitatuma upanga kwa ajili yao mpaka nimewaangamiza wote kabisa.’
17Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, “Yafikirini haya: Waiteni waliaji; waje. Tumeni wanawake wenye taaluma ya kuomboleza, waje.
18Waje haraka waimbe wimbo wa maombolezo juu yetu, ili macho yetu yatokwe na machozi na kope zetu zibubujikwe na maji.
19Kwa kuwa sauti ya kilio imesikika Sayuni, ‘Jinsi tulivyoharibiwa. Tumeaibishwa sana, kwa kuwa tumeitelekeza nchi tangu walipoangusha nyumba zetu.’
20Kwa hiyo ninyi wanawake, sikieni neno la Bwana; zingatieni ujumbe unaokuja toka kinywani mwake. Kisha wafundisheni binti zenu wimbo wa maombolezo, na kila mwanamke wa jirani wimbo wa kilio.
21Kwa kuwa vifo vimekuja kupitia dirishani; vinaelekea mahali petu. Vinawaharibu watoto kutoka nje na vijana kwenye viwanja vya miji.
22Uyatangaze haya, ‘Asema Bwana- mizoga ya wanaume itaanguka kama mavi kwenye mashamba na kama mabua baada ya mvunaji, na hapatakuwa na mtu wa kuyakusanya.’
23Bwana asema hivi, “Usimwache mtu mwenye busara ajivune kwa ajili ya hekima yake, au shujaa kwa sababu ya uwezo wake. Usimwache mtu tajiri ajivunie utajiri wake.
24Kwa kuwa kama mtu atajivunia chochote kile, acha iwe hivi, yeye awe na busara na kunijua mimi. Kwa kuwa mimi ni Bwana, atendaye katika agano la wema, haki, na hukumu duniani. Ni katika hili kwamba ninafurahia- asema Bwana.

25Tazama, siku zaja - asema Bwana wakati nitakapo waadhibu wote ambao wametahiriwa miili tu.26Nitaiadhibu Misri na Yuda, Edomu, watu wa Amoni, Moabu, na watu wote wanaonyoa denge. Kwani mataifa yote haya hayajatahiriwa, na nyumba yote ya Israeli ina moyo ambao haujatahiriwa.”

10

1“Sikilizeni neno ambalo Bwana anawaambieni, enyi nyumba ya Israeli.

2Bwana asema hivi, ‘msijifunze njia za mataifa, na msishangazwe na ishara za mbinguni, kwa kuwa mataifa hushangazwa na haya.
3Kwa kuwa desturi za watu ni ubatili. Kwa kuwa mtu mmoja hukata mti msituni; kazi ya mikono ya mtu na shoka.
4Kisha huzipamba kwa fedha na dhahabu. Huikaza kwa misumari na nyundo ili isitikisike.
5Sanamu hizi ni mfano wa sanamu za kutishia ndege katika shamba la matango, kwa kuwa haziwezi kusema chochote, hubebwa, kwa kuwa haziwezi hata kusogea hatua moja. Usiwaogope, Kwani hawawezi kutenda maovu wala mema.”
6Hakuna aliye kama wewe, BWANA. Wewe ni mkuu, na jina lako lina nguvu.
7Ni nani asiyekuwa na hofu juu yako, wafalme wa mataifa? Kwa kuwa hiki ndicho unachostahili, kwa kuwa hakuna wa kuwa kama wewe kati ya wote wenye hekima katika mataifa yote au katika hali yao ya enzi.
8Wote wako sawa, ni kama wanyama na wapumbavu, wanafunzi wa sanamu ambazo si chochote isipokuwa miti tu.
9Wanaleta fedha iliyofuliwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi iliyotengenezwa na sonara, ni kazi ya ustadi. Mavazi yao ni ya rangi ya samawati na urujuani. Watu wao stadi waliyafanya haya yote.
10Lakini Bwana ndiye Mungu wa kweli. Yeye ni Mungu aliye hai na mfalme wa milele. Matetemeko yako katika hasira yake, na mataifa hayawezi kuvumilia hasira yake.

11Utawaambia hivi, “Miungu ambayo haikuumba mbingu na nchi itaangamia katika dunia hii na chini ya mbingu.”
12Aliyeiumba dunia kwa nguvu zake aliumba nchi kavu kwa hekima zake na kuzitandaza mbingu kwa fahamu zake.
13Sauti yake ndiyo itengenezayo mungurumo wa maji mbinguni, naye huzileta mbingu katika mwisho wa dunia. Hutengeneza radi kwa ajili ya mvua na kutuma upepo kutoka katika hazina yake.
14Kila mtu amekuwa mjinga, hawana maarifa. Kila mfua chuma ameaibishwa kwa sanamu zake. Maana sanamu yake ya kuyeyushwa ni uongo; hakuna pumzi ndani yake.
15Ni ubatili tu, ni kazi ya udanganyifu; zitapotea wakati wa hukumu.
16Lakini Mungu ni fungu la Yakobo, si kama hawa, kwa kuwa yeye ndiye aliyeviumba vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; Bwana Mungu wa majeshi ndiye jina lake.
17Kusanya vitu vyako na uiache nchi, wewe ambaye umekuwa ukiishi katika mazingirwa haya.
18Kwa kuwa Bwana asema hivi, “Tazama, Ni tayari kuwatupa wakazi wa nchi nje wakati huu. Nitawasababishia huzuni, na itakuwa hivyo.”
19Ole wangu! Kwa sababu ya mifupa yangu iliyovunjika, Jeraha zangu zimeumia. Kwa hiyo nilisema. “Hakika haya ni maumivu, lakini lazima nivumilie.”
20Hema yangu imeharibiwa, na kamba za hema yangu zote zimekatwa. Wamewachukua watoto wangu wote, Kwa hiyo hawaishi tena. Hakuna tena mtu wa kuitandaza hema yangu au wa kuziinua pazia za hema yangu.
21Kwa kuwa wachungaji wamekuwa wapumbavu. Hawamtafuti Bwana; Kwa hiyo hawana mafanikio; Kondoo wao wote wamesambaa.
22Taarifa imewadia, “Tazama! Inakuja, tetemeko kubwa linakuja kutoka katika nchi ya kaskazini kuifanya miji ya Yuda kuwa ukiwa, na maficho ya mbweha.
23Ninajua, Bwana, kwamba njia ya mtu haiji kutoka kwake. Wala hakuna mtu atembeaye anayeongoza hatua zake mwenyewe.
24Ee Bwana, unirudi, kwa hukumu za haki, si kwa hasira zako vinginevyo utaniangamiza.
25Mwaga hasira zako kwa mataifa ambazo hazikujui na katika familia ambazo hawakuiti kwa jina lako. Kwa kuwa wamemla Yakobo na kumwangamiza kabisa na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.

11

1Hili ndilo neno lililojia Yeremia kutoka kwa Bwana, akasema,2“Sikiliza maneno ya agano hili, uwaambie kila mtu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.3Uwaambie, ‘Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: na alaaniwe yeyote asiyesikiliza maneno ya agano hili.4Hili ndilo agano nililowaamuru baba zenu walishike siku nilipowatoa kutoka katika nchi ya Misri, kutoka tanuru ya chuma. Nikawaambia, “Sikilizeni sauti yangu na mfanye mambo yote kama nilivyowaamuru, kwa kuwa mtakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wenu.”5Nisikilizeni ili nipate kukitimiza kiapo nilichoapa kwa baba zenu, kiapo kwamba nitawapa nchi iliyojaa maziwa na asali kama ilivyo leo.’” Kisha mimi Yeremia nikajibu na kusema, “Ndio, Bwana!”

6Bwana akaniambia, “Hubiri habari hizi zote katika miji ya Yuda, na katika njia za Yerusalemu. Sema, “Sikilizeni maneno ya agano hili na mkayafanye.7Kwa maana nimewaagiza wazee wenu tangu siku ile niliyowaleta kutoka nchi ya Misri hadi wakati huu wa sasa, nimewaonya mara kwa mara na kusema, “Sikilizeni sauti yangu.’”8Lakini hawakusikiliza au wala kutega masikio yao. Kila mtu amekuwa akitembea katika ukaidi wa moyo wake mbaya. Kwa hiyo nilileta laana zote katika agano hili nililoamuru kuja juu yao. Lakini watu bado hawakuitii.”

9Kisha Bwana akaniambia, “Njama imeonekana kati ya watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu.10Wameugeukia uovu wa mababu zao wa mwanzo, ambao walikataa kusikiliza neno langu, ambao badala yake walifuata miungu mingine ili kuabudu. Waisraeli na nyumba ya Yuda walivunja agano langu nililoweka na baba zao.11Kwa hiyo Bwana asema hivi, ‘Tazameni, nitawaletea majanga juu yao, majanga ambayo hawataweza kuyaepuka. Ndipo wataniita, lakini sitawasikiliza.12Miji ya Yuda na wenyeji wa Yerusalemu watakwenda na kuiita miungu ambayo walitoa sadaka, lakini hakika hawatawaokoa wakati wa majanga yao.13Kwa kuwa idadi ya miungu yako ewe Yuda imeongezeka sawa na idadi ya miji yako. Na umefanya idadi ya madhabahu ya aibu huko Yerusalemu, madhabahu ya kufukiza uvumba kwa Baali, sawa na idadi ya njia zake.

14Kwa hiyo wewe mwenyewe, Yeremia, usiwaombee watu hawa. Lazima usiomboleze au kuomba kwa niaba yao. Kwa maana siwezi kusikiliza wakati wananiita katika majanga yao.

15Mpendwa wangu anafanya nini nyumbani kwangu, ikiwa amekuwa na nia mbaya? Nyama za sadaka yako hazitakusaidia. Unafurahi kwa sababu ya matendo yako mabaya.
16Katika siku za nyuma Bwana alikuita mti wa mzeituni wenye majani, mzuri wenye matunda mazuri. Lakini atawasha moto juu yake ambayo itaonekana kama sauti ya dhoruba; matawi yake yatavunjika.
17Kwa maana Bwana Mungu wa majeshi, aliyekupanda, aliyekua amekusudia maafa juu yako, kwa sababu ya matendo mabaya ambayo nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda wamefanya-wamenikasirisha kwa kumtolea Baali sadaka.’

18Bwana alinijulisha mambo haya, kwa hiyo nikayajua. Wewe, Bwana, umenifanya nione matendo yao.19Nilikuwa kama kondoo mpole unayeongozwa na mchinjaji. Sikujua kwamba walikuwa wameunda mipango dhidi yangu, “Hebu tuangamize mti na matunda yake! Hebu tumkatilie mbali na nchi ya walio hai ili jina lake lisikumbukwe tena.
20Lakini Bwana Mungu wa majeshi ndiye mwamuzi mwenye haki ambaye huchunguza moyo na akili. Mimi nitashuhudia kisasi chako dhidi yao, kwa kuwa nimekuletea kesi yangu kwako.

21Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya watu wa Anathothi, wanaotafuta uhai wako, “wanasema, ‘Usifanye unabii kwa jina la Bwana, usije ukafa kwa mkono wetu.’22Kwa hiyo Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, ‘Tazameni, nitawaadhibu. Vijana wao wenye nguvu watakufa kwa upanga. Wana wao na binti zao watakufa kwa njaa.23Hakuna hata mmoja atakayeachwa, kwa maana nitaleta maafa dhidi ya watu wa Anathothi, mwaka wa adhabu yao.’”

12

1Wewe ni mwenye haki, Bwana, wakati wowote ninapoleta mashtaka kwako. Lazima nikuambie sababu yangu ya kulalamika: Kwa nini njia za waovu hufanikiwa? Watu wote wasiokuwa na imani wanafanikiwa.

2Wewe uliwapanda nao wakawa na mizizi. Wanaendelea kuzaa matunda. Wewe upo karibu nao katika vinywa vyao, lakini mbali na mioyo yao.
3Lakini wewe mwenyewe unanijua, Bwana. Umeniona mimi na kuchunguza moyo wangu. Waondoe kama kondoo wa kuchinjwa. Ukawaweke tayari kwa siku ya kuchinjwa.
4Je! Nchi itakauka kwa muda gani, na mimea katika kila shamba itaota? Kwa sababu ya uovu wa wenyeji wake wanyama na ndege wameondolewa. Hakika, watu wanasema, “Mungu hajui nini kitatokea kwetu.”

5Bwana akasema, “Kweli, wewe, Yeremia, ikiwa umeshindana na askari wa miguu na wakakushinda, unawezaje kushindana dhidi ya farasi? Ikiwa unashuka chini ya nchi iliyo salama, utafanyaje katika misitu karibu na Yordani?
6Kwa maana hata ndugu zako na familia ya baba yako wamekudharau na kukukemea kwa sauti kubwa. Usiwaamini, hata kama wanasema mambo mazuri kwako.
7Nimeiacha nyumba yangu; Nimeacha urithi wangu. Nimewatia watu wangu wapendwa mikononi mwa adui zake.
8Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba katika tundu; yeye hujiweka juu yangu kwa sauti yake mwenyewe, hivyo nimemchukia.
9Malipo yangu ya thamani haijakuwa ndege wenye madoadoa karibu na kichwa chake? Nenda, ukakusanye viumbe vyote vilivyomo katika mashamba, na uwalete ili wale.
10Wachungaji wengi wameharibu shamba langu la mizabibu. Wameipoteza sehemu yangu yote ya ardhi; Waligeuza sehemu yangu nzuri kuwa jangwa, ukiwa.
11Wamemfanya kuwa ukiwa. Ninaomboleza kwa ajili yake; yeye ni ukiwa. Nchi yote imefanywa kuwa ukiwa, kwa maana hakuna mtu aliyeweka haya moyoni mwake.
12Waangamizi wamekuja juu ya maeneo yote yaliyo wazi jangwani, kwa maana upanga wa Bwana unakula kutoka upande mmoja wa nchi hadi mwingine. Hakuna usalama katika nchi kwa kiumbe chochote kilicho hai.
13Walipanda ngano lakini mavuno ya miiba. Wao wamechoka kutokana na kazi lakini hawajapata chochote. Basi muaibike kwa faida yenu kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana.”

14Bwana asema hivi dhidi ya majirani zangu wote, waovu wanaopiga milki niliyowarithisha watu wangu Israeli, “Tazama, mimi ndimi ambaye nitawafukuza kutoka nchi yao wenyewe, nami nitaifuta nyumba ya Yuda kutoka kati yao.15Ndipo baada ya kuangamiza mataifa hayo, itatokea kwamba nitakuwa na huruma juu yao na kuwaleta tena; Nitawarudi-kila mtu kwa urithi wake na nchi yake.16Kisha itakuwa ikiwa mataifa hayo yatajifunza kwa makini njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu ‘Kama Bwana aishivyo!’ vile vile kama walivyofundishwa watu wangu kuapa kwa Baali, basi watajengwa katikati ya watu wangu.17Lakini kama hakuna yeyote anayesikiliza, basi nitaling'oa taifa hilo. Kwa hakika litang'olewa na kuharibiwa-hili ndilo tamko la Bwana.”

13

1Bwana aliniambia hivi, “Nenda ukape nguo ya kitani na kuiweka karibu na kiuno chako, lakini usiiweke kwenye maji kwanza.”2Kwa hiyo nilinunua vazi kama vile Bwana alivyoagiza, na nikafunga karibu na kiuno changu.

3Ndipo neno la Bwana likanijia mara ya pili, kusema,4“Twaa vazi lako ulilolinunua lililo karibu na kiuno chako, uinuke, ukasafiri mpaka Frati. Ukaifiche huko katika mwamba wa jabali.5Basi nikaenda na kuificha katika Frati kama vile Bwana alivyoniamuru.

6Baada ya siku nyingi, Bwana akaniambia, “Simama, urudi Frati. Ukaichukue nguo ambayo nilikuambia ufiche.”7Kwa hiyo nikarudi Frati na kuchimba na kuchukua nguo mahali pale nilipoificha. Lakini tazama! Nguo hiyo ilikuwa imeharibika; haikuwa nzuri kabisa.

8Ndipo neno la Bwana likanijia tena, kusema,9“Bwana asema hivi, Nitakiangamiza kiburi cha Yuda na Yerusalemu.10Watu hawa waovu wanaokataa kusikia neno langu, ambao huenda katika ugumu wa mioyo yao, ambao hufuata miungu mingine ili kuabudu na kuinama-watakuwa kama hii nguo isiyofaa kwa lolote.11Kwa maana kama vile vazi lililofungwa kwenye viuno vya mtu, ndivyo nimeifanya nyumba yote ya Israeli na nyumba yote ya Yuda zimefungwa kwangu- hili ndilo tamko la Bwana-wawe watu wangu, ili kunifanya jina, sifa, na heshima. Lakini hawakunisikiliza.

12Basi uwaambie neno hili, ‘Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi Kila kiriba itajazwa divai.’ Watakuambia, ‘Je, hatujui kwamba kila chupa itajazwa divai?’13Basi uwaambie,’ Bwana asema hivi: Tazama, nitawajaza kila mkaaji wa nchi hii ulevi, na wafalme wanaokaa kiti cha Daudi, na makuhani, na manabii, na wenyeji wote wa Yerusalemu.14Ndipo nitawagonganisha kila mtu na mwenzake baba na watoto wao pamoja; hili ndilo tamko la Bwana-sitawahurumia au kuwa na huruma, wala sitawa rehemu kutoka kwenye uharibifu.
15Sikilizeni kwa makini. Msiwe na kiburi, kwa kuwa Bwana amenena.
16Mtukuze Bwana, Mungu wako, kabla hajaleta giza, na kabla ya kuifanya miguu yako kuwa na mashaka juu ya milima wakati wa jioni. Kwa maana unatarajia mwanga, lakini ataugeuza kuwa mahali pa giza, na kuwa giza nene.
17Kwa hiyo ikiwa husikilizi, nitaomboleza peke yangu kwa sababu ya kiburi chako. Hakika macho yangu yatalia na kutoa machozi, kwa sababu kundi la Bwana limechukuliwa mateka.
18“Mwambieni mfalme na mama wa malkia ‘Jinyenyekezeni! Kaeni chini! Kwa maana taji juu ya kichwa chako, kiburi chako na utukufu wako, umeanguka.’
19Miji ya Negebu itafungwa, bila mtu wa kufungua. Yuda watachukuliwa mateka, wote uhamishoni.
20Inua macho yako na angalia wale wanaokuja kutoka kaskazini. Je, ni kundi gani alilokupa, kundi ambalo lilikuwa zuri sana kwako?
21Je, unasema nini wakati Mungu anawaweka wale ambao uliwafundisha kuwa marafiki? Je, huu si mwanzo wa maumivu ya utungu ambayo yatakuchukua kama mwanamke aliye katika utungu wa kuzaa?
22Kisha unaweza kusema moyoni mwako, ‘Kwa nini mambo haya yanatokea kwangu?’ Itakuwa kwa uovu wa maovu yako ambapo marinda yako yamefunuliwa na umeumizwa.
23Je, watu wa Kushi hubadilisha rangi yao ya ngozi, au chui hubadilisha madoa yake? Ikiwa ndivyo, basi wewe mwenyewe, ingawa unazoea uovu, utaweza kufanya mema.
24Wa hiyo nitawaangamiza kama makapi ambayo yanaangamia katika upepo wa jangwa.
25Hii ndiyo niliyokupa, sehemu ambayo nimekuagiza kwako-hili ndilo tamko la Bwana - kwa sababu umenisahau na kuamini katika udanganyifu.
26Kwa hiyo mimi mwenyewe nitaondoa nguo zako, na sehemu zako za siri zitaonekana.
27Uzinzi na ubembe wako, aibu ya tabia yako ya usherati kwenye milima na katika mashamba! Nitayafanya yaonekane, mambo haya ya machukizo! Ole wako, Yerusalemu! Hutaki kuwa safi. Je! Hili litaendelea kwa muda gani?”

14

1Neno la Bwana lililomjia Yeremia kuhusu ukame,

2“Wayahudi waomboleze; basi milango yake ianguke. Wao wanaomboleza kwa ajili ya ardhi; Kilio chao kwa Yerusalemu kimepaa juu.
3Wenye nguvu huwatuma watumishi wao kwa ajili ya maji. Wanapoingia kwenye visima, hawawezi kupata maji. Wote wanarudi hawajafanikiwa; Wao hufunika vichwa vyao na aibu.
4Kwa sababu hii ardhi imepasuka, kwa maana hakuna mvua katika nchi. Wakulima huwa na aibu na kufunika vichwa vyao.
5Kwa maana hata kunguru huwaacha wanawe katika mashamba, kwa maana hakuna nyasi.
6Punda mwitu husimama kwenye mabonde yaliyo wazi na hupiga upepo kama mbweha. Macho yao yanashindwa kufanya kazi, kwa maana hakuna mimea.
7Hata ingawa maovu yetu yanatushuhudia, Bwana, tenda kwa ajili ya jina lako. Kwa sababu matendo yetu yasiyo na imani yamezidi; tumekutenda dhambi.
8Matumaini ya Israeli, yule anayemwokoa wakati wa dhiki, kwa nini utakuwa kama mgeni katika nchi, kama mtu akaaye nchi ya kigeni ambaye hujinyoosha na hutumia usiku mmoja tu?
9Kwa nini utakuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, kama shujaa ambaye hawezi kuokoa mtu yeyote? Kwa maana wewe u katikati yetu, Bwana! Jina lako limetangazwa juu yetu. Usiondoke

10Bwana awaambia hivi watu hawa “Kwa kuwa wanapenda kutanga tanga, hawakuzuia miguu yao kufanya hivyo.” Bwana hafurahi nao. Sasa anawakumbusha uovu wao na ameadhibu dhambi zao.

11Bwana akaniambia, Usiombe kwa ajili ya watu hawa.12Maana ikiwa wanafunga, sitasikiliza kulia kwao; na wanapotoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za unga, sitawafurahia. Kwa maana nitawaangamiza kwa upanga, njaa, na tauni.

13Ndipo nikasema, “Ee, Bwana Mungu! Angalia! Manabii wanawaambia watu, ‘Huwezi kuona upanga; hakutakuwa na njaa kwako, kwa kuwa nitakupa usalama wa kweli mahali hapa.’

14Bwana akaniambia, ‘manabii wanatabiri uongo kwa jina langu. Sikuwafukuza, wala sikuwapa amri au kusema nao. Lakini maono ya udanganyifu na ya maana, uchawi wa udanganyifu unaotokana na akili zao ndicho wanachowatabiria.”15Kwa hiyo Bwana asema hivi, “Kwa habari ya manabii wakihubiri kwa jina langu, ambao mimi sikuwatuma; wale wanaosema kuwa hakutakuwa na upanga wala njaa katika nchi hii manabii hawa wataangamia kwa upanga na njaa.16Na watu waliopewa utabiri watafukuzwa nje ya barabara za Yerusalemu kwa sababu ya njaa na upanga; kwa kuwa hakuna mtu wa kuwazika, na wake zao, na wana wao, wala binti zao; kwa maana nitamwaga uovu wao wenyewe juu yao.

17Sema neno hili kwao ‘Acha macho yangu yatokwe na machozi, usiku na mchana. Wala yasikome, kwa kuwa kutakuwa na kuanguka kwa bikira, binti ya watu wangu - jeraha kubwa lisilotibika.
18Ikiwa nitatoka kwenye shamba basi angalia! Kuna wale waliouawa kwa upanga. Na kama nitakuja mjini, basi, tazama! Kuna wale walio na ugonjwa wa njaa. Hata nabii na kuhani wote wanatembea juu ya nchi bila maarifa.’

19Je! Umemkataa kabisa Yuda? Je, unaichukia Sayuni? Kwa nini umetupiga wakati hakuna uponyaji kwetu? Tulitumaini amani, lakini hapakuwa na kitu kizuri-na kwa wakati wa uponyaji, lakini tazama, kuna hofu tu.
20Tunakubali, Bwana, makosa yetu, uovu wa babu zetu, kwa kuwa tumekukosea.
21Usitukatae! Kwa ajili ya jina lako, usikifedheheshe kiti chako cha enzi cha utukufu. Kumbuka na usivunje agano lako na sisi.
22Je, kuna miongoni mwa sanamu za mataifa yeyote zinazoweza kuifanya mbingu kutoa mvua? Je, si wewe, Bwana Mungu wetu, ambaye hufanya jambo hili? Tunatumaini kwako, kwa kuwa umefanya mambo haya yote.

15

1Kisha Bwana akaniambia, “Hata kama Musa au Samweli walisimama mbele yangu, bado sitawafikiria watu hawa. Watoe mbele yangu, ili waweze kuondoka.2Ikiwa watakuambia, ‘Tunapaswa kwenda wapi?’ Kisha uwaambie, ‘Bwana asema hivi Wale wanaotakiwa kufa wanapaswa kufa; wale waliotayarishwa kwa upanga wanapaswa kwenda kwa upanga. Wale waliopelekwa kwa njaa wanapaswa kwenda kwa njaa; na wale walio pelekwa uhamisho wanapaswa kuhamishwa.’

3Kwa kuwa nitawapa kwa makundi manne-hili ndilo tamko la Bwana-upanga wa kuua wengine, mbwa wararue, ndege wa angani na mnyama mkali wale na kuangamiza.4Nitawafanyia jambo lenye kutisha kwa falme zote za dunia, kwa sababu Manase mwana wa Hezekia, mfalme wa Yuda, alifanya huko Yerusalemu.
5Kwa maana ni nani atakayewahurumia, Yerusalemu?
6Umeniacha-hili ndilo tamko la Bwana-umerudi nyuma. Kwa hiyo nitawapiga kwa mkono wangu na kukuangamiza. Nimechoka kuwahurumia.
7Kwa hiyo nitawapepeta kwa kipepeo katika milango ya nchi. Nitawafukuza. Nitawaangamiza watu wangu kwani hawakurudi na kuziacha njia zao.
8Nitawafanya wajane wao kuwa zaidi ya mchanga wa bahari. Dhidi ya mama wa vijana nitamtuma mwangamizi mchana. Nitafanya mshtuko na hofu ghafla kuanguka juu yao.
9Mama aliyezaa watoto saba atazimia. Atapumua pumzi lake la mwisho. Jua lake limekuchwa wakati bado ni mchana. Yeye atakuwa na aibu na kufedheheka, kwa kuwa nitawatoa wale waliosalia kwa upanga mbele ya maadui zao-hili ndilo tamko la Bwana.”

10Ole wangu, mama yangu! Kwa maana umenizaa, mimi ambaye ni mtu wa kushindana na hoja katika nchi yote. Sijakopesha, wala hakuna mtu aliyenikopesha, lakini wote wananilaani.

11Bwana akasema: “Je sitakuokoa kwa manufaa? Kwa hakika nitawafanya maadui wako waombe msaada wakati wa msiba na dhiki.
12Je, mtu anaweza kusaga chuma? Hasa chuma kutoka kaskazini iliyochanganywa na shaba?
13Nitawapa adui zako utajiri wako na hazina yako kama nyara za bure. Nitafanya hili kwa sababu ya dhambi zako zote zilizofanywa ndani ya mipaka yako yote.
14Ndipo nitakufanya utumikie adui zako katika nchi ambayo huijui, maana moto utawaka, ukawaka katika ghadhabu yangu juu yako.”
15Wewe mwenyewe wajua, Bwana! Unikumbuke na kunisaidia. Ukanilipie kisasi kwa ajili ya wanaonifuata. Katika uvumilivu wako usiniondoe. Utambue kwamba nimekuwa na aibu kwa ajili yako. Maneno yako yamepatikana, na nikayala.
16Maneno yako yalikuwa furaha kwangu, furaha yangu kwa moyo wangu; kwa maana jina lako linatangazwa juu yangu, Bwana, Mungu wa majeshi.
17Sikuketi katika mkutano wa wale waliosherehekea au waliofurahi. Nimeketi kwa faragha kwa sababu ya mkono wako wenye nguvu, kwa maana umenijaza na hasira.
18Kwa nini maumivu yangu yanaendelea na jeraha langu halitibiki, linakataa kuponywa? Je, utakuwa kama maji ya udanganyifu kwangu, maji yanayokauka?

19Kwa hiyo Bwana asema hivi, “Yeremia, Ikiwa utatubu, nitakurejesha, nawe utasimama mbele yangu na kunitumikia. Kwa maana ukitenganisha mambo ya kipumbavu kwa vitu vya thamani, utakuwa kama kinywa changu. Watu watakuja kwako, lakini wewe mwenyewe usirudi kwao.
20Nitakufanya kama ukuta wa shaba usioweza kuingilika kwa watu hawa, nao watapigana vita dhidi yako. Lakini hawatakushinda, kwa kuwa mimi ni pamoja nawe ili kuokoa na kukuponya-hili ndilo tamko la Bwana-
21kwa maana nitakuokoa mikononi mwa waovu na kukukomboa katika mkono wa mshindani.”

16

1Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,2“Usiwe na mke, wala usiwe na wana au binti hapa.3Kwa kuwa Bwana asema hivi kwa wana na binti ambao wamezaliwa hapa, kwa mama waliowabeba, na kwa baba waliowafanya wazaliwe katika nchi hii,4‘Watakufa vifo vya magonjwa. Hawataombolezewa wala kuzikwa. Watakuwa kama samadi juu ya nchi. Kwa maana wataangamizwa kwa upanga na njaa, na miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.’

5Maana Bwana asema hivi, ‘Usiingie nyumba yoyote yenye kuomboleza. Usiende kuwaombolezea, wala usihuzunike kwa ajili ya watu hawa. Kwa maana nimeondoa amani yangu, uaminifu wa agano, na huruma, kutoka kwa watu hawa! Ndivyo asemavyo Bwana;6kwa hiyo wakuu na wadogo watakufa katika nchi hii. Wala hawatazikwa, wala hakuna yeyote atakaye omboleza kwa ajili yao. Hakuna mtu atakayejikata-kata au kunyoa vichwa vyao kwa ajili yao.7Hakuna mtu anayepaswa kugawa chakula chochote wakati wa kuomboleza ili kuwafariji kwa sababu ya vifo, na hawatawapa kikombe cha faraja kwa baba yake au mama yake ili kuwafariji.

8Usiende kwenye nyumba ya karamu ili ukae pamoja nao ili kula au kunywa.9Kwa maana Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Tazama, mbele yako, siku zako na mahali hapa, nitakomesha sauti ya furaha na sherehe, sauti ya bwana na bibi arusi.’

10Kisha itatokea kwamba utawaambia watu hawa maneno haya yote, na watakuambia, ‘Mbona Bwana amesema maafa yote haya juu yetu? Uovu wetu ni uovu gani na dhambi yetu tuliyomtendea Bwana, Mungu wetu?’

11Basi uwaambie, ‘hii ndiyo ahadi ya Bwana; Kwa sababu baba zenu waliniacha, nao wakafuata miungu mingine, wakaiabudu na kuisujudia. Waliniacha na hawakuishika sheria yangu.12Lakini ninyi wenyewe mmeleta uovu zaidi kuliko baba zenu, kwa maana, kila mtu anaenda kwa ukaidi wa moyo wake mbaya; hakuna mtu anayenisikiliza.13Kwa hiyo nitawafukuza kutoka nchi hii mpaka nchi msiyoijua, wewe wala baba zako, nanyi mtaiabudu miungu mingine huko mchana na usiku, kwa maana mimi sitawapa fadhili zangu.’

14Kwa hiyo tazama! Siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo haitasemwa tena, ‘Kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.’15Kwa maana, kama Bwana aishivyo, yeye aliyewaleta wana wa Israeli kutoka nchi ya kaskazini, na kutoka nchi aliyowaangamiza, nitawarudisha katika nchi niliyowapa baba zao.

16Angalia! Hili ni tamko la Bwana-Nitatuma wavuvi wengi-kwa hiyo watawavua watu. Baada ya hayo nitatuma wawindaji wengi ili waweze kuwinda kati ya milima na vilima vyote, na katika nyufa za miamba.17Kwa kuwa macho yangu yapo juu ya njia zao zote; hawawezi kujificha mbele yangu. Uovu wao hauwezi kufichika mbele ya macho yangu.18Nami kwanza nitawalipa mara mbili uovu na dhambi zao kwa kuwa wameichafua nchi yangu sanamu za machukizo, na kwa kujaza urithi wangu na sanamu zao za machukizo.
19Ee Bwana, wewe ndiwe ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama wangu siku ya shida. Mataifa yatakujia kwako kutoka mwisho wa dunia na kusema, ‘Hakika baba zetu walirithi udanganyifu. Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao. Je!
20Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe? Lakini wao sio miungu.
21Kwa hiyo tazama! Nitawafanya wajue wakati huu, nitawafanya watambue mkono wangu na nguvu zangu, kwa hiyo watajua kwamba Yahweh ni jina langu.”

17

1“Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma yenye ncha ya almasi. Imechongwa kwenye kibao cha mioyo yao na kwenye pembe za madhabahu zako.

2Watoto wao wanakumbuka madhabahu zao na miti yao ya Ashera kwa miti ya majani kwenye milima mirefu.
3Mlima wangu katika nchi ya wazi na mali yako yote pamoja na hazina zako zote, nitakupa kama nyara kwa wengine. Hiyo ndiyo thamani ya maeneo yako ya juu na dhambi iliyo katika maeneo yako yote.
4Utapoteza urithi niliokupa. Nitakutumikisha kwa adui zako katika nchi ambayo hujui, kwa maana umewasha moto katika ghadhabu yangu, ambao utawaka milele.”

5Bwana asema, “Mtu anayemtegemea mwanadamu amelaaniwa; amfanyaye mwanadamu kuwa nguvu yake na kugeuza moyo wake mbali na Bwana.
6Kwa maana atakuwa kama msitu mdogo katika Araba na hawezi kuona kitu kizuri kikija. Atakaa katika maeneo ya mawe jangwani, nchi isiyokuwa na wakazi.
7Lakini mtu anayemtegemea Bwana amebarikiwa, kwa kuwa Bwana ndiye tumaini lake.
8Kwa maana atakuwa kama mti uliopandwa karibu na maji kando ya mto; mizizi yake itaenea. Hawezi kuona joto likija, kwa kuwa majani yake yatakuwa mabichi. Kisha mwaka wa ukame hawezi kuwa na wasiwasi, wala hautaacha kuzalisha matunda.
9Moyo ni mdanganyifu zaidi kuliko kitu kingine chochote. Ni mgonjwa; ni nani anayeweza kuelewa?
10Mimi ni Bwana, ninayechunguza akili, ambaye hujaribu viuno. Ninampa kila mtu kulingana na njia zake, kulingana na matunda ya matendo yake.
11Kama Kware akusanyaye mayai asiyotaga. Mtu anaweza kuwa tajiri kwa udhalimu, lakini wakati nusu ya siku zake zikipita, utajiri huo utamuacha, na mwishowe atakuwa mpumbavu.”
12“Mahali pa hekalu letu ni kiti cha enzi cha utukufu, kilichoinuliwa tangu mwanzo.
13Bwana ni tumaini la Israeli. Wote ambao wanakuacha watakuwa na aibu. Wale walio katika nchi ambao wanageuka kutoka kwako watauliwa. Kwa maana wamemwacha Bwana, chemchemi ya maji yaliyo hai.
14Niponye, Bwana, na mimi nitaponywa! Niokoe mimi, nami nitaokolewa. Kwa maana wewe ndio wimbo wangu wa sifa.
15Tazama, wananiambia, ‘Neno la Bwana liko wapi? Hebu lije!’
16Mimi sikuwahi kuacha kuwa mchungaji nyuma yako. Sikuitamani siku ya maafa. Unajua yaliyotoka mdomoni mwangu. Yalifanyika mbele ya uwepo wako.
17Usiwe sababu ya hofu kwangu. Wewe ni kimbilio langu siku ya msiba.
18Waaibike watu wanaoniudhi, lakini nisiaibike mimi. Wataogopa, lakini usiache nifadhaike. Tuma siku ya maafa dhidi yao na kuwaangamiza maradufu.”

19Bwana akaniambia hivi: “Nenda ukasimame katika lango la watu ambako wafalme wa Yuda wanaingia na kutoka, basi katika malango mengine yote ya Yerusalemu.20Uwaambie, ‘Sikieni neno la Bwana, wafalme wa Yuda, na ninyi watu wote wa Yuda, na kila mtu wa Yerusalemu atakayeingia kwa njia ya malango haya.21Bwana asema hivi: “Jihadharini kwa ajili ya maisha yenu na msichukue mzigo siku ya sabato ili muilete katika malango ya Yerusalemu.22Wala msilete mzigo nje ya nyumba zenu siku ya sabato. Msifanye kazi yoyote, lakini muitenge siku ya Sabato, kama nilivyowaagiza wazee wako kufanya.’”23Hawakusikiliza wala kutega masikio yao, lakini walifanya shingo zao kuwa ngumu ili wasinisikilize wala kukubali maonyo.24Itatokea kwamba ikiwa mtanisikiliza kweli-hili ndilo tamko la Bwana-na msilete mzigo kwenye malango ya jiji hili siku ya sabato lakini badala yake mkatenga siku ya sabato kwa Bwana na msifanye kazi yoyote juu yake -25basi wafalme, wakuu, na wale wanaokaa kiti cha Daudi wataingia malango ya mji huu kwa magari na farasi, wao na viongozi wao, watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu. Na mji huu utakaa milele.26Watakuja kutoka miji ya Yuda na kutoka pande zote za Yerusalemu, kutoka nchi ya Benjamini na visiwa vya chini, kutoka milimani na kutoka kaskazini, wakileta sadaka za kuteketezwa, dhabihu, sadaka za nafaka na ubani, sadaka za shukrani kwenye nyumba ya Bwana.27Lakini ikiwa hamtasikiliza-kutakasa siku ya Sabato, kutochukua mizigo nzito, wala msiingie milango ya Yerusalemu siku ya sabato, nitawasha moto katika malango yake, nao utaangamiza majumba kuteketeza ngome za Yerusalemu, na hauwezi kuzimika.

18

1Neno la Bwana lilimjia Yeremia, kusema,2“Simama, uende kwa nyumba ya mfinyanzi; kwa maana nitakusikilizisha neno langu huko.3Basi, nikaenda nyumbani kwa mfinyanzi, na tazama! Mfinyanzi alikuwa akifanya kazi kwenye gurudumu la mfinyanzi.4Lakini chombo cha udongo ambacho alikuwa akikifinyanga kiliharibika mkononi mwake, kwa hiyo alibadili mawazo yake na akafanya kitu kingine ambacho kilionekana kuwa kizuri machoni pake.

5Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,6“Je, siwezi kuwa kama huyu mfinyanzi kwenu, nyumba ya Israeli? Angalia! Kama udongo katika mkono wa mfinyanzi-ndivyo ulivyo mkononi mwangu, nyumba ya Israeli.7Kwa wakati mmoja, ninaweza kutangaza jambo fulani juu ya taifa au ufalme, kwamba nitaufukuza, kuuvunja, au kuuharibu.8Lakini kama taifa ambalo nimefanya tamko hilo linageuka na kuacha maovu yake, basi nitaghairi nisitende maafa niliyokuwa nimepanga.9Wakati mwingine, ninaweza kutangaza jambo fulani kuhusu taifa au ufalme, kwamba nitaujenga au kuupanda.10Lakini ikiwa watafanya mabaya machoni pangu kwa kutosikiliza sauti yangu, basi nitaghairi mema ambayo nilikuwa nimewaambia nitawafanyia.

11Basi sasa, waambie watu wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu, ukisema, ‘Bwana asema hivi: Tazameni, nitawaangamiza. Mimi ni karibu kufinyanga mabaya dhidi yenu. Tubuni, kila mtu kutoka njia yake mbaya, hivyo njia zako na matendo yako yatakuletea mema.’

12Lakini watasema, ‘Hili halina maana. Tutafanya kulingana na mipango yetu wenyewe. Kila mmoja wetu atafanya mabaya kwa kuufuata ushubafu wa moyo wake.’

13Kwa hiyo Bwana asema hivi, ‘Uliza watu wa mataifa, ambao wamewahi kusikia habari kama hii? Bikira wa Israeli amefanya kitendo cha kutisha.
14Je, theluji ya Lebanoni imetoka milima yenye miamba juu ya pande zake? Je, mito ya mlima inayotoka mbali iliharibiwa, mito hiyo ya baridi?
15Hata hivyo watu wangu wamenisahau. Wamefanya sadaka kwa sanamu zisizo na maana na wamefanya mashaka katika njia zao; wameacha njia za kale za kutembea katika njia ndogo.
16Nchi yao itakuwa ya hofu, kitu cha kuzomewa milele. Kila mtu atakayepita karibu naye atashuhudia na kutingisha kichwa chake.
17Nitawaangamiza mbele ya adui zao kama upepo wa mashariki. Nitawageuzia kisogo, wala sio uso wangu, siku ya msiba wao.’

18Basi watu wakasema, “Njooni, tufanye njama dhidi ya Yeremia, maana sheria haitapotea kabisa kwa makuhani, wala ushauri kutoka kwa wenye hekima, au maneno ya manabii. Njoo, mshambulie kwa maneno yetu na tusisikilize tena chochote anachosema.”

19Sikiliza, Ee Bwana! Na kusikiliza sauti ya adui yangu.
20Je, maafa kutoka kwao itakuwa malipo yangu kwa kuwa mwema kwao? Kwa maana wamenichimbia shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele yako ili niseme mema kwa ajili yao na kugeuza ghadhabu yako isiwapate.
21Basi uwape watoto wao njaa, na uwatie mikononi mwa wale wanaotumia upanga. Basi, waache wanawake wao wafiwe na kuwa wajane, na watu wao watauawa, na vijana wao wauawe kwa upanga wa vita.
22Kelele ya kusikitisha isikiwe kutoka katika nyumba zao, kama utakapoleta washambuliaji ghafla juu yao. Kwa kuwa wamechimba shimo kunikamata na wameficha mitego katika miguu yangu.
23Lakini wewe, Bwana, unajua mipango yao yote dhidi yangu ya kuniua. Usisamehe uovu na dhambi zao. Usiondoe dhambi zao mbali nawe. Badala yake, waache waangamizwe mbele yako. Tenda juu yao wakati wa ghadhabu yako.

19

1Bwana akasema hivi, “Nenda ukanunue chupa ya udongo wakati ukiwa na wazee wa watu na makuhani.2Kisha uende mpaka bonde la Ben Hinomu wakati wa kuingia kwenye mlango uliovunjika wa mfinyanzi, na huko utatangaza maneno nitakayokuambia.3Ukisema, ‘Sikilizeni neno la Bwana, wafalme wa Yuda na wenyeji wa Yerusalemu! Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, “Tazameni, na nitaletea msiba juu ya mahali hapa, na masikio ya kila mtu anayesikia yatawaka.4Nitafanya hivyo kwa sababu wameniacha na kudharau mahali hapa. Katika mahali hapa wanatoa sadaka kwa miungu mingine ambayo hawakuijua. Wao, baba zao, na wafalme wa Yuda pia wamejaza mahali damu isiyo na hatia.5Walimjengea Baali mahali pa juu na kuwachoma watoto wao kwa moto kama sadaka za kuteketezwa kwake-kitu ambacho sijawaamuru au kutaja, wala haikuingia ndani ya akili yangu.6Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-ambapo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, bonde la Ben Hinomu, kwa kuwa litakuwa bonde la machinjo.7Katika mahali hapa nitatambua mipango ya Yuda na Yerusalemu. Nitawafanya wapate kuuawa kwa upanga mbele ya adui zao na kwa mkono wa wale wanaotafuta maisha yao. Ndipo nitawapa miili yao kuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama wa dunia.8Ndipo nitaufanya mji huu kuwa uharibifu na kitu cha kuzomewa, kila mtu anayepita atashangaa na kuzomea kwa sababu ya mateso yake yote.9Nitawafanya wale nyama ya wana wao na binti zao; kila mtu atakula mwili wa jirani yake katika dhiki na katika uchungu ambao umeletwa kwao na maadui zao na wale wanaotaka maisha yao.’

10Kisha utavunja chupa ya udongo mbele ya watu ambao walikwenda pamoja nawe.11Uwaambie,’ Bwana Mungu wa majeshi asema hivi: nitafanya jambo hili kwa watu hawa na mji huu- hii ndiyo ahadi ya Bwana, kama vile Yeremia alivyovunja chupa ya udongo ili isiweze kutengenezwa tena. Watu watazika wafu huko Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.12Hivyo ndivyo nitakavyofanya mahali hapa na wenyeji wake nitakapofanya jiji hili kama Tofethi, hili ndilo tamko la Bwana;13kwa hiyo nyumba za Yerusalemu na wafalme wa Yuda watakuwa kama Tofethi, nyumba zote zilizo juu ya watu waovu wanaoabudu nyota zote za mbinguni na kumwaga sadaka za kinywaji kwa miungu mingine.’

14Ndipo Yeremia akatoka Tofethi, ambako Bwana amemtuma ahubiri. Akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote,15“Bwana Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazameni, nitawaletea mji huu na miji yake yote maafa yote niliyonena dhidi yake, kwa kuwa walifanya shingo zao kuwa ngumu na kukataa kusikiliza maneno yangu.’”

20

1Pashuri, mwana wa Imeri, kuhani, alikuwa msimamizi mkuu, akamsikia Yeremia akihubiri maneno haya mbele ya nyumba ya Bwana.2Basi Pashuri akampiga nabii Yeremia, akamtia katika masanduku yaliyokuwa kwenye lango la juu la Benjamini ndani ya nyumba ya Bwana.3Ikawa siku ya pili Pashuri akamtoa Yeremia nje ya makabati. Yeremia akamwambia, “Bwana hakukuita Pashuri, lakini wewe ni Magor-Misabibu.4Kwa maana Bwana asema hivi, ‘Tazama, nitakufanya kuwa kitu cha kutisha, wewe na wapendwa wako wote; kwa maana wataanguka kwa upanga wa adui zao, na macho yako yataona. Nitawatia Yuda mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atawafanya kuwa mateka huko Babeli au kuwaangamiza kwa upanga.5Nitampa mali zote za jiji hili na utajiri wake wote, vitu vyote vya thamani na hazina zote za wafalme wa Yuda. Nitaweka vitu hivi mikononi mwa adui zako, nao watawakamata. Nao watawachukua na kuwaleta Babeli.6Lakini wewe Pashuri, na wenyeji wote wa nyumba yako watakwenda mateka. Utakwenda Babeli na kufa huko. Wewe na wapendwa wako wote ambao uliwatabiria maneno ya uongo mtazikwa huko.’”

7“Umenidanganya, Bwana. Kwa hakika nimedanganyika. Wewe ulinikamata na kunishinda. Nimekuwa kitu cha kuchekesha. Watu wananidharau kila siku, siku zote.
8Kwa maana wakati wowote nimenena, nimeita na kutangaza, ‘Vurugu na uharibifu.’ Na neno la Bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwangu kila siku.
9Nami nikisema, ‘Sitafikiria juu ya Bwana tena. Sitatangaza tena jina lake.’ Ni kama moto moyoni mwangu, uliofanyika ndani ya mifupa yangu. Kwa hiyo ninajitahidi kustahimili lakini siwezi.
10Nimesikia habari za ugaidi kutoka kwa watu wengi pande zote. ‘Mshitakini! Lazima tumshitaki’ Wale walio karibu nami kuangalia kama nitaanguka. ‘Labda anaweza kudanganywa. Ikiwa ndivyo, tunaweza kumshinda na kujilipiza kisasi kwake.’
11Lakini Bwana yu pamoja nami kama mpiganaji mwenye nguvu, hivyo wale wanaonifuata watajikwaa. Hawatanishinda. Watakuwa na aibu sana, kwa sababu hawatafanikiwa. Watakuwa na aibu ya kudumu, haitasahauliwa kamwe.
12Lakini wewe, Bwana Mungu wa majeshi, wewe unayemtazama mwenye haki na ambaye huona akili na moyo. Hebu nipate kuona kisasi chako juu yao kwa maana nimekuletea shitaka langu kwako.
13Mwimbieni Bwana! Msifuni Bwana! Kwa kuwa ameokoa maisha ya wale waliokandamizwa kutoka kwenye mikono ya waovu.
14Na ilaaniwe siku niliyozaliwa. Usiruhusu siku ambayo mama yangu alinizaa ibarikiwe.
15Na alaaniwe mtu aliyemwambia baba yangu akisema, ‘Amezaliwa mtoto wa kiume,’ na kusababisha furaha kubwa.
16Mtu huyo atakuwa kama miji ambayo Bwana aliiangamiza bila huruma. Na asikie wito wa msaada asubuhi na sauti ya vita wakati wa mchana.
17Hiyo itatokea, kwa kuwa Bwana hakuniua tumboni au kumfanya mama yangu kaburi langu, tumbo la ujauzito milele.
18Kwa nini nilitoka tumboni ili kuona matatizo na uchungu, ili siku zangu zijazwe na aibu?”

21

1Hili ndilo neno lililotoka kwa Bwana kwa Yeremia wakati mfalme Sedekia alimtuma Pashuri mwana wa Malkiya na Sefania mwana wa Maaseya, kuhani. Wakamwambia,2“Pata ushauri kutoka kwa Bwana kwa ajili yetu, kwa kuwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, analeta vita. Labda Bwana atafanya miujiza kwetu, kama ilivyokuwa zamani, na kumfanya aondoke kwetu.”

3Basi Yeremia akawaambia, “Hivi ndivyo mtakavyomwambia Sedekia4‘Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nageuza nyuma vyombo vya vita vilivyo mkononi mwenu, ambavyo mnapigana dhidi ya mfalme wa Babeli na Wakaldayo wanaokufunga kutoka nje ya kuta! Kwa maana nitawakusanya katikati ya jiji hili.5Nami nitapigana nanyi kwa mkono ulioinuka na mkono wenye nguvu, na ukali, ghadhabu, na hasira kubwa.6Kwa maana nitawaangamiza wenyeji wa mji huu, wanadamu na wanyama, watakufa kwa tauni kali.7Baada ya hayo- hii ndiyo ahadi ya Bwana-Sedekia mfalme wa Yuda, watumishi wake, watu, na kila mtu aishiye katika mji huu baada ya tauni, upanga na njaa, nitawatia wote mkononi mwa Nebukadneza mfalme wa Babeli, na mikononi mwa adui zao, na katika mkono wa wale wanaotaka uhai wao. Ndipo atawaua kwa makali ya upanga. Hatawahurumia, hatawaokoa, au kuwa na rehema.’

8Basi uwaambie watu hawa, ‘Bwana asema hivi Angalia, nitaweka mbele yako njia ya uzima na njia ya mauti.9Mtu yeyote anayeishi katika mji huu atakufa kwa upanga, njaa, na tauni; lakini mtu yeyote atakayetoka na kuanguka kwa magoti mbele ya Wakaldayo ambao wamefungwa dhidi yako ataishi. Yeye ataokoka na maisha yake.10Kwa maana nimeweka uso wangu juu ya mji huu ili kuleta maafa na sio kuleta mema-hili ndilo tamko la Bwana. Utatiwa mkononi mwa mfalme wa Babeli naye atauteketeza.’

11Kuhusu nyumba ya mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Bwana.12Nyumba ya Daudi, Bwana asema, “Hukumuni kwa haki asubuhi. Umuokoe yule aliyeibiwa kwa mkono wa mwenye kuonea, au ghadhabu yangu itatoka kama moto na kuchoma, na hakuna mtu anayeweza kuizima, kwa sababu ya matendo yako mabaya.
13Angalia, mwenyeji wa bonde na mwamba wa nchi ya wazi! Mimi niko juu yako, - hili ndilo tamko la Bwana- Mimi ni juu ya mtu yeyote anayesema, ‘Ni nani atashuka kutupiga?’ au ‘Ni nani atakayeingia kwenye nyumba zetu?’
14Nitawaadhibu kutokana na matunda ya matendo yako-hili ndilo tamko la Bwana- na nitawasha moto katika misitu, na utateketeza kila kitu.’

22

1Bwana asema hivi, “Nenda kwenye nyumba ya mfalme wa Yuda, utangaze neno hili huko.2Ukaseme, ‘Ewe Mfalme wa Yuda, wewe aliyeketi kiti cha Daudi, usikilize neno la Bwana. Nisikilizeni, enyi watumishi wake, na ninyi, watu wake mnaokuja kwa malango haya.3Bwana asema hivi, “Fanya haki na uadilifu, na mtu yeyote ambaye ameibiwa-muokoeni kutoka mkononi mwa mshindani. Usimtendee mabaya mgeni yeyote katika nchi yako, au yatima au mjane. Usifanye vurugu au kumwaga damu isiyo na hatia mahali hapa.4Kwa kuwa mkifanya mambo hayo, basi wafalme wanaoketi kiti cha Daudi wataingia milango ya nyumba hii wakiendesha gari na farasi, yeye, watumishi wake, na watu wake!5Lakini ikiwa hamsikilizi maneno haya kutoka kwangu ambayo nimeyasema-hili ndilo tamko la Bwana - basi nyumba hii ya kifalme itaharibiwa.’

6Kwa maana Bwana asema hivi juu ya nyumba ya mfalme wa Yuda, “Wewe uko kama Gileadi, au kama kilele cha Lebanoni kwangu. Hata hivyo nitakugeuza kuwa jangwa, katika miji isiyo na wenyeji.
7Kwa kuwa nimewaagiza waharibifu kuja juu yenu! Watu wenye silaha zao watakata mierezi yako iliyo bora na kuiacha kuanguka kwenye moto.

8Kisha mataifa mengi yatapita kwenye mji huu. Kila mtu atamwambia yule anayefuata, “Mbona Bwana amefanya hivi kwa jiji hili kuu?”9Na mwingine atajibu, “Kwa sababu waliiacha agano la Bwana, Mungu wao, wakainama kwa miungu mingine, wakaiabudu.”
10Usilie kwa ajili ya aliyekufa. Usiomboleze kwa ajili yake. Lakini mlilie mtu yeyote anayeingia kifungoni, kwa maana hatarudi tena kuiona nchi aliyozaliwa.’
11Maana Bwana asema hivi juu ya Yehoahazi, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, aliyekuwa mfalme badala ya Yosia babaye, ‘ametoka mahali hapa, wala hatarudi.12Atakufa huko mahali ambapo walimchukua mateka, na hataiona tena nchi hii.’
13Ole mtu yeyote anayejenga nyumba yake kwa uovu na vyumba vyake vya juu katika udhalimu; ambao wengine hufanya kazi, lakini hawalipwi.
14Ole mtu yeyote atakayesema, ‘Nitajenga nyumba ndefu na vyumba vya juu vipana, na hujenga madirisha mapana, na kuta zenye mwerezi, na huipaka rangi nyekundu.’
15Je, hii ndiyo inakufanya uwe mfalme mzuri, kwamba unataka kuwa na mbao za mwerezi? Je baba yako hakula na kunywa, lakini alifanya hukumu na haki? Kisha mambo yakawa mazuri kwa ajili yake.
16Alihukumu maneno ya masikini na mhitaji. Ilikuwa vizuri. Je, huku siko kunijua mimi? - Hili ni tamko la Bwana.
17Lakini hakuna kitu machoni na moyoni mwako isipokuwa wasiwasi kwa faida yako isiyo ya haki na kwa kumwaga damu isiyo na hatia, kwa ukandamizaji kuwatendea jeuri wengine.

18Kwa hiyo Bwana asema hivi juu ya Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Hawata mwomboleza wakisema ‘ole, ndugu yangu! Au ‘Ole, dada yangu!’ Hawata omboleza kwa kusema ‘Ole, bwana!’ au ‘ole, utukufu!’
19Atazikwa maziko ya punda, ataburuzwa mbali na kutupwa nje ya milango ya Yerusalemu.
20Panda milima ya Lebanoni piga kelele. Paza sauti yako Bashani. Piga kelele kutoka kwenye milima ya Abarimu, kwa maana marafiki zako wote wataharibiwa.
21Nilinena nawe wakati ulioko salama, lakini ukasema, ‘Sitasikia.’ Hii ilikuwa desturi yako tangu ujana wako, kwani hukusikiliza sauti yangu.
22Upepo utawalisha wachungaji wako wote, na marafiki zako watakwenda kufungwa. Hakika wewe utakuwa na aibu na kufadhaika kwa matendo yako yote mabaya.
23Wewe mfalme, wewe ambaye huishi katika Nyumba ya Msitu wa Lebanoni, wewe aliyefanya kiota kati ya mierezi, utakuwa na hali ya kuhurumiwa utakapopata utungu kama wakati wa kuzaa.”

24“Kama mimi niishivyo-hili ndilo tamko la Bwana-hata kama wewe, Konia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, ulikuwa alama ya mkono wangu wa kulia, ningekuangusha.25Kwa kuwa nimewatia mikono ya wale wanaotaka uhai wenu na kwenye mkono wa wale ambao mnawaogopa, hata mkononi mwa Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Wakaldayo.26Nitawatupa wewe na mama yako aliyekuzaa katika nchi nyingine, nchi ambayo hujazaliwa, na huko utakufa.27Na kuhusu eneo hili ambalo watataka kurudi, hawatarudi hapa.
28Je! Hiki ni chombo kilichodharauliwa na kilichopasuka? Je, Konia ni chombo kilichodharauliwa? Kwanini wamemtupa yeye na wazao wake, kumpeleka katika nchi wasiyoijua?
29Ee Ardhi, Ardhi, Ardhi! Sikieni neno la Bwana!
30Bwana asema hivi, ‘Andika juu ya mtu huyu Konia Yeye hatakuwa na mtoto. Hatafanikiwa wakati wa siku zake, wala hakuna hata mmoja kati ya uzao wake atakayefanikiwa au kuketi tena kwenye kiti cha Daudi na kutawala juu ya Yuda.’

23

1“Ole wao wachungaji ambao huangamiza na kuwatawanya kondoo wa malisho yangu-hii ndiyo ahadi ya Bwana.”2Kwa hiyo, Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi juu ya wachungaji ambao wanawachunga watu wake, “Ninyi mnawatawanya kundi langu na kuwafukuza. Hamuwajali hata kidogo. Tambueni hili! Mimi nitawalipiza uovu wa matendo yenu-hili ni tamko la Bwana.3Mimi mwenyewe nitakusanya mabaki ya kondoo wangu kutoka nchi zote nilizowafukuza, nami nitawarejesha kwenye eneo la malisho, ambako watazaa na kuongezeka.4Ndipo nitawainua wachungaji juu yao ambao watawachunga hivyo hawataogopa tena au kupotezwa. Hakuna hata mmoja atakayepotea-hili ni tamko la Bwana.

5Angalia, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-nitakapomuinulia Daudi tawi la haki. Atatawala kama mfalme; atatenda kwa busara na kusababisha hukumu na haki katika nchi.
6Katika siku zake Yuda ataokolewa, na Israeli wataishi kwa usalama. Na jina lake atakayeitwa Bwana ni haki yetu.

7Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja-hili ndilo tamko la Bwana-hawatasema tena, ‘Kama Bwana aishivyo, aliyewatoa wana wa Israeli kutoka nchi ya Misri.’8Badala yake watasema, ‘Kama Bwana aishivyo, ambaye aliwaleta na ambaye aliwaongoza wana wa nyumba ya Israeli kutoka nchi ya kaskazini na nchi zote walizofukuzwa.’ Nao watakaa katika nchi yao wenyewe.”

9Kuhusu manabii, moyo wangu umevunjika ndani yangu, na mifupa yangu yote imetetemeka. Nimekuwa kama mlevi, kama mtu ambaye ameshindwa na divai, kwa sababu ya Bwana na maneno yake matakatifu.
10Kwa maana nchi imejaa wazinzi. Kwa sababu ya hayo nchi inaomboleza. Milima katika jangwa imekauka. Njia hizi za manabii ni mbaya; nguvu zao hazitumiwi kwa namna sahihi.
11Kwa maana manabii na makuhani wote wamekufuru. Nimeona uovu wao ndani ya nyumba yangu! - Hili ndilo tamko la Bwana;
12kwa hiyo njia yao itakuwa kama mahali pa kupumzika katika giza. Watasukumwa chini. Wao wataanguka ndani yake. Kwa maana nitatuma mabaya juu yao katika mwaka wa adhabu yao; hili ndilo tamko la Bwana.
13Kwa maana nimeona uchungu kati ya manabii huko Samaria. Walitabiri kwa Baali na wakawaongoza watu wangu Israeli kwenye njia sahihi.
14Na miongoni mwa manabii huko Yerusalemu nimeona mambo ya kutisha: wanafanya uzinzi na huenda kwa udanganyifu. Wanaimarisha mikono ya waovu; hakuna mtu anarejea na kuacha uovu wake. Wote wamekuwa kama Sodoma kwangu na wenyeji wake kama Gomora!”

15Kwa hiyo, Bwana Mungu wa majeshi asema hivi juu ya manabii, “Tazameni, nitawafanya wale magugu na kunywa maji yenye sumu, kwa maana kufuru imetoka kwa manabii wa Yerusalemu na kuingia katika nchi yote.”

16Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, “Usisikilize maneno ya manabii wanaokuhubiri. Wamekudanganya! Wanatangaza maono kutoka kwenye mawazo yao wenyewe, si kwa kinywa cha Bwana.
17Wanasema daima kwa wale wanaonidharau mimi, ‘Bwana asema kutakuwa na amani kwako.’ Na kila mtu anayetembea katika ukaidi wa moyo wake anasema, ‘mabaya hayatakuja kwenu.’
18Lakini nani amesimama katika mkutano wa baraza la Bwana? Ni nani anayeona na kusikia neno lake? Ni nani anayezingatia maneno yake na kusikiliza?
19Tazama, kuna dhoruba inayotoka kwa Bwana! Hasira yake inatoka, na dhoruba inazunguka. Inazunguka vichwa vya waovu.
20Hasira ya Bwana haitarejea mpaka itakapotimiza nia ya moyo wake. Katika siku za mwisho, utaelewa.
21Sikuwatuma manabii hawa. Wao tu walionekana. Sikuwahubiria jambo lolote kwao, lakini bado wanatabiri.
22Kwa kuwa kama walisimama katika mkutano wangu wa baraza, wangeweza kuwasababisha watu wangu kusikia neno langu; wangewafanya wapate kuacha maneno yao mabaya na mazoea mabaya.
23Mimi ni Mungu aliye karibu-hili ni tamko la Bwana-mimi sio Mungu aliye mbali?
24Je, kuna mtu yeyote anayejificha mahali penye siri ili nisiweze kumwona? -Hili ndilo tamko la Bwana-Je mbingu na nchi hazikujawa nami? -Hili Ndilo tamko la Bwana.

25Nimesikia yale waliyosema manabii, wale waliokuwa wanatabiri uongo kwa jina langu. Wakisema, ‘Nilikuwa na ndoto!26Nilikuwa na ndoto!’ Je, hii itaendelea mpaka lini, manabii wanaotabiri uongo kutoka kwa akili zao, na wanasema nini kutokana na udanganyifu mioyoni mwao?27Wana mpango wa kuwafanya watu wangu kusahau jina langu kwa ndoto ambazo wanazoambiana, kila mmoja kwa jirani yake, kama vile babu zao walivyosahau jina langu kwa ajili ya jina la Baali.28Nabii aliye na ndoto, aseme ndoto hiyo. Lakini yule ambaye nimemwambia kitu fulani, basi aseme neno langu kwa kweli. Je, majani yanahusiana na nafaka? - Hili ni tamko la Bwana-29Na neno langu si kama moto? -Hili ni tamko la Bwana-na kama mwamba wenye kupiga nyundo?

30Tazameni, ninapingana na nabii-hii ndiyo ahadi ya Bwana-yeyote anayeiba maneno kutoka kwa mtu mwingine na anasema yanatoka kwangu.31Tazama, ninapingana na manabii-hili ndilo tamko la Bwana-ambao hutumia lugha zao kutabiri maneno.32Tazameni, ninapingana na manabii wanaoota ndoto-hii ndiyo ahadi ya Bwana-na kisha kuwahubiri na kwa njia hii kuwadanganya watu wangu kwa udanganyifu wao na kujivunia. Mimi ni juu yao, kwa kuwa sikuwatuma wala kuwapa amri. Kwa hivyo hawatawasaidia watu hawa - hili ndilo tamko la Bwana.

33Watu hawa au nabii au kuhani wakakuuliza, ‘Je, ni nini tamko la Bwana?’ basi lazima uwaambie, ‘Ni tamko gani? Kwa maana nimekuacha wewe-hili ndilo tamko la Bwana.34Kwa habari ya manabii, makuhani, na watu wanaosema, ‘Hili ndilo tamko la Bwana,’ nitamuadhibu mtu huyo na nyumba yake.35Endelea kusema, kila mtu kwa jirani yake na kila mtu kwa ndugu yake, ‘Bwana alijibu nini?’ na ‘Bwana alitangaza nini?’36Lakini usizungumze tena juu ya tamko la Bwana, kwa kuwa kila tamko kutoka kwa kila mtu limekuwa ujumbe wake mwenyewe, na umepotosha maneno ya Mungu aliye hai, Bwana wa majeshi, Mungu wetu.37Utamuuliza nabii hivi, ‘Bwana alikujibu nini? Je, Bwana alisema nini? Kisha unasema tamko kutoka kwa Bwana;38lakini Bwana asema hivi, Sema hivi, “Hili ni tamko la Bwana” ingawa nimekuagiza na kusema, “Usiseme: Hili ni tamko kutoka kwa Bwana.”
39Kwa hiyo, angalia, nitawachukua na kukutupa mbali na mimi, pamoja na jiji ambalo nilikupa wewe na baba zako.
40Ndipo nitaweka aibu ya milele na fedheha juu yenu ambayo haitasahauliwa.’

24

1Bwana alinionyesha kitu. Tazama, vikapu viwili vya tini viliwekwa mbele ya hekalu la Bwana. (Maono haya yalitokea baada ya Nebukadneza, mfalme wa Babeli, kumchukua mateka Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, maofisa wa Yuda, mafundi na wafua vyuma kutoka Yerusalemu na kuwapeleka Babeli.)2Kikapu kimoja cha tini kilikuwa kizuri sana, kama tini za kwanza zilizoiva, lakini kikapu kingine cha tini zilizokuwa mbaya sana zisizoweza kuliwa.

3Bwana akaniambia, “Unaona nini Yeremia?” Nikasema, “Tini. Tini ambazo ni nzuri sana na tini ambazo ni mbaya sana haziwezi kuliwa.”

4Ndipo neno la Bwana likanijia, kusema,5“Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi: nitawaangalia mateka wa Yuda kwa manufaa yao, kama vile tini hizi nzuri, nilipowatoa mateka kutoka hapa mpaka nchi ya Wakaldayo.6Nitaweka macho yangu kwao wapate mema na kuwarejeshea nchi hii. Nitawajenga, wala sitawaangamiza.7Nitawapanda, wala sitawang'oa. Ndipo nitawapa moyo wa kunijua; kwa kuwa mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu na mimi nitakuwa Mungu wao, hivyo watanirudia kwa mioyo yao yote.

8Lakini kama vile tini mbaya ambazo ni hazifai kuliwa - asema Bwana - nitatenda hivi kwa Sedekia, mfalme wa Yuda, pamoja na viongozi wake, na pamoja na wengine wa Yerusalemu ambao wanabaki katika nchi hii au kwenda kukaa katika nchi ya Misri.9Nitawafanya kuwa kitu cha kutisha, wapate maafa, mbele ya falme zote duniani, aibu na somo kwa mithali, matusi, na laana mahali pote nitakapowafukuza.10Nitatuma upanga, njaa, na tauni dhidi yao watapotelea mbali kutoka kwenye nchi niliyowapa wao na baba zao.”

25

1Hili ndilo neno ambalo lilimjia Yeremia juu ya watu wote wa Yuda. Ikawa mwaka wa nne wa Yehoyakimu, mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda. Huo ndio mwaka wa kwanza wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli.2Yeremia nabii aliwahubiria watu wote wa Yuda na wenyeji wote wa Yerusalemu.3Akasema, “Kwa miaka ishirini na mitatu, tangu mwaka wa kumi na tatu wa Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda mpaka leo, maneno ya Bwana yamekuja kwangu. Nimewahubiria ninyi. Nilikuwa na nia ya kutangaza, lakini hamkunisikiliza.

4Bwana akawapeleka watumishi wake wote manabii kwako. Walikuwa na nia ya kwenda, lakini hukusikiliza wala kutega masikio.5Manabaii hawa walisema, ‘Kila mtu auache uovu wake na udhalimu wa matendo yake na kurudi kwenye nchi ambayo Yahweh aliitoa wakati wa zamani kwa ajili ya babu zenu na ninyi, kama zawadi ya kudumu.6Kwa hiyo msiifuate miungu mingine ili kuiabudu au kuiinamia chini, na msimkasirishe kwa kazi ya mikono yenu ili kwamba awaumize.

7Lakini hamkunisikiliza-hili ndilo tamko la Bwana-kwa hiyo umenikasirisha kwa kazi ya mikono yako ili kujidhuru nafsi zenu.

8Basi, Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, ‘Kwa kuwa hukusikiliza maneno yangu,9tazama, nitaagiza amri ya kukusanya watu wote wa kaskazini- asema Bwana- na Nebukadneza, mtumishi wangu, mfalme wa Babeli, na kuwaleta juu ya nchi hii na wenyeji wake, na juu ya mataifa yote yaliyo karibu nawe. Kwa maana nitawaangamiza. Nitawageuza kuwa na hofu, kuwa kitu cha kuzomewa na ukiwa wa daima.10Sauti ya furaha na sherehe-sauti ya bwana arusi na bibi arusi, sauti ya mawe ya kusagia na mwanga wa taa-nitafanya mambo yote haya kutoweka kutoka kwa mataifa haya.11Ndipo nchi hii yote itakuwa ukiwa na hofu, na mataifa haya watamtumikia mfalme wa Babeli kwa miaka sabini.

12Kisha miaka sabini itakapokamilika, nitamuadhibu mfalme wa Babeli na taifa hilo, nchi ya Wakaldayo-hili ndilo tamko la Bwana-kwa uovu wao na kuifanya kuwa ukiwa milele.13Nami nitaleta juu ya nchi hiyo maneno yote niliyosema, na kila kitu kilichoandikwa katika kitabu hiki ambacho Yeremia ametabiri juu ya mataifa yote.14Kwa maana pia mataifa mengi na wafalme wakuu watapata watumwa kutoka mataifa haya. Nitawalipa kwa matendo yao na kazi za mikono yao.’

15Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, “Chukua kikombe hiki cha divai ya ghadhabu kutoka mkononi mwangu, ukawanyweshe mataifa yote niliyokutuma.16Kwa maana watakunywa na kisha watalewa na kufanya wazimu mbele ya upanga ambao nitaupeleka kati yao.”

17Basi, nikakichukua kikombe mkononi mwa Bwana, nikawanywesha mataifa yote ambayo Bwana alinituma:18Yerusalemu, miji ya Yuda, na wafalme wake, na wakuu wake, na kuwafanya kuwa ukiwa na kitu cha kutisha, na kuwa kitu cha kuzomewa na laana, kama ilivyo hata leo.19Mataifa mengine pia walipaswa kunywa: Farao mfalme wa Misri na watumishi wake; maafisa wake na watu wake wote;20watu wote wa urithi wa mchanganyiko na wafalme wote wa nchi ya Uzi; na wafalme wote wa nchi ya Wafilisti, na Ashkeloni, na Gaza, na Ekroni, na mabaki ya Ashdodi;21Edomu na Moabu na wana wa Amoni.22Wafalme wa Tiro na Sidoni, wafalme wa pwani ng'ambo ya pili ya bahari,23Dedani, Tema, na Busi pamoja na wale wanyoao nywele zao upande wa pili wa vichwa vyao, pia walipaswa kuinywa.24Watu hawa pia walitakiwa kuinywa; wafalme wote wa Uarabuni na wafalme wote wa watu wa asili mchanganyiko wanaoishi nyikani;25wafalme wote wa Zimri, wafalme wote wa Elamu, na wafalme wote wa Wamedi;26wafalme wote wa kaskazini, wale wa karibu na wale wa mbali—kila mmoja na ndugu zake na falme zote za ulimwengu ambazo ziko chini ya uso wa dunia. Hatimaye mfalme wa Babeli atakunywa baada yao wote.

27Bwana akaniambia, “Basi, uwaambie, ‘Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi kunywa na kulewa, kisha tapika, uanguke, wala usisimame mbele ya upanga nitakaoutuma kati yenu.’28Kisha itatokea kwamba ikiwa wanakataa kuchukua kikombe mkononi mwako ili kunywa, utawaambia, ‘Bwana Mungu wa majeshi asema hii lazima mnywe.29Kwa maana, tazama, nitaleta janga juu ya mji ulioitwa kwa jina langu, je ninyi mtaachiliwa msiadhibiwe? Hutakuwa huru, kwa maana nitaita upanga juu ya wenyeji wote wa nchi! - Hili ndilo tamko la Bwana Mungu wa majeshi.’

30Basi wewe mwenyewe, Yeremia, tabiri kwao maneno haya yote. Uwaambie, ‘Bwana atanguruma kutoka juu, naye atapaza sauti yake toka makao yake matakatifu, na radi kutoka mahali pake patakatifu; naye atapiga kelele kama wale wakanyagao zabibu dhidi ya wote wanaoishi duniani.
31Kelele huja mpaka mwisho wa nchi, kwa sababu mgogoro kutoka kwa Bwana utaleta mashtaka dhidi ya mataifa. Ataleta haki kwa wote wenye mwili. Yeye atawatia waovu katika upanga-hili ndi'o tamko la Bwana.’

32Bwana Mungu wa majeshi asema hivi, ‘Tazameni, taabu itatokea toka kwa taifa hadi taifa, na dhoruba kubwa itatokea toka pande za mwisho za dunia.
33Kisha wale waliouawa na Bwana watakuja kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine; hawataomboleza, kukusanyika, au kuzikwa. Watakuwa kama samadi chini.
34Pigeni Yowe, wachungaji, na pigeni kelele ya kuomba msaada! Gaagaa katika ardhi, enyi mlio hodari katika kundi. Kwa kuwa siku yako ya kuuawa na kutawanywa imekuja. Utaanguka kama kondoo waliochaguliwa.
35Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia. Hakuna kutoroka kwa watu walio hodari katika kundi.
36Kuna mlio wa wasiwasi wa wachungaji na milio ya kulalama kwa watu walio hodari katika kundi, kwa kuwa Yahweh anayaharibu malisho yao.
37Kwa hiyo, malisho ya amani yataharibiwa kwa sababu ya hasira ya Bwana.
38Kama simba, ameacha shimo lake, kwa kuwa ardhi yao itakuwa kitu cha kushangaza kwa sababu ya hasira ya muonevu, kwa sababu ya ghadhabu yake kali.’

26

1Mwanzoni mwa utawala wake Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa yuda, neno likaja kutoka kwa Yahweh, likisema,2“Yahweh anasema hivi: Simama katika uwanja wa nyumba yangu na sema kuhusu miji yote ya Yuda ambao huja kuabudu katika nyumba yangu. Tangaza maneno yote niliyokuamuru kuyasema kwao. Usipunguze neno lolote!3Labda watasikiliza, kwamba kila mtu ataziacha njia zake mbaya, ili nighairi majanga ninayokusudia kuyaleta juu yao kwa sababu ya uovu wa matendo yao.4Kwa hiyo lazima useme kwao, ‘Yahweh anasema hivi: Kama hamtanisikiliza ili mtembee katika sheria yangu ambayo nimeiweka mbele yenu—5kama hamsikilizi maneno ya watumishi wangu manabii ambao naendelea kuwatuma kwenu—lakini hamjasikiliza! —6Basi nitaifanya nyumba hii kuwa kama Shilo; nitaifanya nyumba hii kuwa laana katika macho ya mataifa yote ya dunia.

7Makuhani, manabii, na watu wote wakamsikia Yeremia akitangaza maneno haya katika nyumba ya Yahweh.8Kwa hiyo ikatokea kwamba Yeremia alipomaliza kutangaza yale Yahweh amemwamuru kuyasema kwa watu wote, makuhani, manabii, na watu wote wakamsimamisha na kusema, “Hakika utakufa!9Kwa nini umetabiri katika jina la Yahweh na kusema kwamba nyumba hii itakuwa kama Shilo na mji huu utakuwa ukiwa, pasipo wakaaji?” Kwa maana watu wote wameunda kundi dhidi ya Yeremia katika nyumba ya Yahweh.

10Kisha wakuu wa Yuda wakasikia maneno haya na wakapanda kutoka nyumba ya mfalme kwenda kwenye nyumba ya Yahweh. Wakakaa katika njia ya lango katika Lango Jipya la nyumba ya Yahweh.11Makuhani na manabii wakasema kwa wakuu wa Yuda na kwa watu wote. Wakasema, “Ni haki kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametabiri juu ya mji huu, kama mlivyosikia kwa masikio yenu!”

12Kwa hiyo Yeremia akasema kwa wakuu wote na watu wote, “Yahweh amenituma kutabiri juu ya nyumba hii na mji wake, kusema maneno yote ambayo mmeyasikia.13Kwa hiyo sasa, imarisheni njia zenu na matendo yenu, na sikieni sauti ya Yahweh Mungu wenu kwamba ataghairi kuhusu janga ambalo ametangaza dhidi yenu.14Mimi mwenyewe—niangalieni! —Niko mikononi mwenu. Nitendeeni yaliyo mema na sahihi katika macho yenu.15Lakini kwa hakika lazima mjue kwamba kama mtaniua mimi, basi mnaiweka damu isiyo na hatia juu yenu wenyewe na juu ya mji huu na wakaaji wake, kwa maana Yahweh amenituma kweli kwenu ili nitangaze maneno yote kwa ajili ya masikio yenu.”

16Kisha wakuu na watu wote wakasema kwa makuhani na manabii, “Si vyema kwa mtu huyu kufa, kwa maana ametangaza mambo haya kwetu katika jina la Yahweh Mungu wetu.”

17Kisha watu kutoka wazee wa nchi wakasimama na kusema kwa kusanyiko lote la watu.18Wakasema, “Mikaya Mmorashi alikuwa akitabiri katika siku za Hezekia mfalme wa Yuda. Alinena kwa watu wote wa Yuda na kusema, ‘Yahweh wa majeshi anasema hivi: Sayuni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa lundo la magofu, na mlima wa hekalu utakuwa kilima kilicho cha kichaka.’ Hezekia mfalme wa Yuda na Yuda wote walimuua?19Hakumwogopa Yahweh na kuutaka radhi uso wa Yahweh ili kwamba Yahweh angeghairi kuhusu janga ambalo alilitangaza kwao? Kwa hiyo tutafanya maovu makubwa zaidi juu ya maisha yetu sisi wenyewe?”

20Wakati huo huo palikuwa na mtu mwingine ambaye alitabiri katika jina la Yahweh—Uria mwana wa Shemaya kutoka Kiriath Yearimu—pia alitabiri juu ya mji na nchi hii, akikubaliana na maneno yote ya Yeremia.21Lakini Mfalme Yohoyakimu na wanajeshi wake wote na watumishi wake wote waliposikia maneno yake, kisha mfalme alijaribu kumuua, lakini Uria alisikia na kuogopa, kwa hiyo alikimbia na akaenda Misiri22Kisha mfalme Yehoyakimu alituma watu kwenda Misiri—Elnathani mwana wa Achbori na watu kwenda Misiri kumfuata Uria.23Wakamtoa Uria nje kutoka Misiri na kumleta kwa Mfalme Yehoyakimu. Kisha Yehoyakimu akamuua kwa upanga na kumpeleka nje kwenye makaburi ya watu wa kawaida.24Lakini mkono wa Ahikamu mwana wa Shapni alikuwa pamoja na Yeremia, hivyo hakutiwa mikononi mwa watu ili auawe.

27

1Katika mwanzo wa utawala wa Sedekia mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, neno hili lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahweh. 12Hiki ndicho Yahweh alisema kwangu, “Tengeneza vifungo na nira kwa ajili yako mwenyewe. Ziweke shingoni mwako.3Kisha akawatuma kwenda kwa mfalme wa Edomu, mfalme wa Moabu, mfalme wa watu wa amoni, mfalme wa Tiro, na kwa mfalme wa Sidoni. Watume kwa mkono wa wajumbe hao wa wafalme ambao walikuja Yerusalemu kwa Sedekia mfalme wa Yuda.4Toa amri kwao kwa ajili ya mabwana zao na sema, ‘Yahweh wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Hivyo ndivyo mtakavyosema kwa mabwana zenu,5Mimi mwenyewe niliiumba dunia kwa nguvu zangu kuu na mkono wangu ulioinuka. Pia niliwaumba watu na wanyama juu ya dunia, na nimewatoa kwa yeyote aliyesahihi katika macho yangu.6Kwa hiyo sasa, Mimi mwenyewe naziweka nchi hizi zote kwenye mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu. Pia, ninavikabidhi kwake viumbe hai vyote katika mashamba ili vimtumikie.7Kwa maana mataifa yote watamtumikia yeye, wanaye, na wajukuu zake hadi muda wa nchi yake ufike. Kisha mataifa mengi na wafalme wengi watamtiisha.

8Kwa hiyo taifa na ufalme ambo haumtumikii Nebukadneza, mfalme wa Babeli, na ule usioweka shingo yake chini ya nira ya Nebukadneza mfalme wa Babeli—nitaliadhibu taifa hilo kwa upanga, njaa, na pigo—hili ni tangazo la Yahweh—hadi nitakapokuwa nimewateketeza kwa mkono wake.9Kwa hiyo msiwasikilize manabii wenu, wabashiri wenu, waonaji wenu, ndoto zenu, watambuzi wenu, ambao wamekuwa wakisema kwenu na kusema, ‘Msimtumikie mfalme wa Babeli.’10Kwa maana wanatabiri uongo kwenu ili kuwapeleka mbali na nchi zenu, kwa maana nitawapeleka mbali, na mtakufa.11Lakini taifa ambalo wataweka shingo zao chini ya nira ya mfalme wa Babeli na kumtumikia, nitawaruhusu kupumzika katika nchi yao—hili ni tangazo la Yahweh—na watailima na kufanya nyumba zao humo.”

12Kwa hiyo nilisema kwa Sedekia mfalme wa Yuda na kumpa ujumbe huu, “Ziwekeni shingo zenu chini ya nira ya mfalme wa Babeli na mtumikieni yeye na watu wake, na mtaishi.13Kwa nini mfe—wewe na watu wako—kwa upanga, njaa, na pigo, kama vile nilivyotangaza kuhusu taifa ambalo watapuuza kumtumikia mfalme wa Babeli?14Msisikilize maneno ya manabii wanaozungumza kwenu na kusema, ‘Msimtumikie mfalme wa Babeli,’ kwa maana wanatabiri uongo kwenu.15‘Kwa maana mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahweh—kwa maana wanatabiri uongo katika jina langu ili kwamba niwafukeze inje na muangamie, ninyi nyote na manabii wanaotabiri kwenu.”

16Nilitangaza hili kwa makuhani na watu wote na kusema, “Yahweh anasema hivi: Msisikilize maneno ya manabii wanaotabiri kwenu na kusema, ‘Angalia! Vyombo vya nyumba ya Yahweh vinarudishwa kutoka Babeli sasa hivi!’ Wanatabiri uongo kwenu.17Msiwasikilize. Mtamtumikia mfalme wa Babeli na mtaishi. Kwa nini mji huu uangamizwe?18Kama ni manabii, na kama neno la Mungu limekuja kwao kweli, basi wamuombe Yahweh wa majeshi asivipeleke Babeli vyombo vilivyosalia katika nyumba, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu.19Yahweh wa majeshi anasema hivi kuhusu zile nguzo, bahari, na kitako, na vyombo vyote vilivyosalia katika mji huu—20vyombo ambavyo Nebukadreza mfalme wa Babeli hakuvichukua wakati alipomchukua Yekonia mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, katika utumwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli pamoja na wakuu wote wa Yuda na Yerusalemu.21Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu vyombo vilivyosalia katika nyumba ya Yahweh, nyumba ya mfalme wa Yuda, na Yerusalemu,22‘Vitaletwa Babeli, na vitabaki huko hadi siku niyovipangia kutimia—hili ni tangazo la Yahweh—kisha nitavileta na kuvirudisha kataika sehemu hii.”


1Ingawa nakala nyingi za Kiebrania zinasema “Yehoyakimu, matoleo mengi ya kisasa yanasema “Sedekia,” kwa sababu tukio katika sura hii lilitokea katika kipindi cha utawala wake.

28

1Ilitokea katika mwaka ule, mwanzoni mwa utawala wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne na mwezi wa tano, Hanania mwana wa Azuri nabii, alikuwa wa Gibeoni, alisema kwangu katika nyumba ya Yahweh mbele za makuhani na watu wote. Alisema,2“Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeivunja nira iliyowekwa na mfalme wa Babeli.3Ndani ya miaka miwili nitavirudisha katika sehemu hii vyombo vyote vya nyumba ya Yahweh ambavyo Nebukadneza mfalme wa Babeli alivichukua kutoka sehemu hii na kuvisafirisha hadi Babeli.4Kisha nitawarudisha katika sehemu hii Yekonia mwana wa Yehotakimu, mfalme wa Yuda, na mateka wote wa Yuda ambao walipelekwa Babeli—hili ni tangazo la Yahweh—kwa maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.”

5Kwa hiyo Yeremia nabii akasema kwa Hanania nabii mbele ya makuhani na kwa watu wote waliosimama katika nyumba ya Yahweh.6Yeremia nabii akasema, “na iwe hivyo! Yahweh ayathibitishe maneno ambayo ulitabiri na kuvirudisha katika sehemu hii vyombo vya nyumba ya Yahweh, na mateka wote kutoka Babeli.7Vile vile, sikilizeni neno ambalo ninalitangaza katika masikio yenu na katika masikio ya watu wote.8Manabii ambao walikuwepo mbele yangu na na mbele yenu muda mrefu uliopita pia walitabiri kuhusu mataifa mengi na juu ya falme kuu, kuhusu vita, njaa, na mapigo.9Kwa hiyo nabii anayetabiri kwamba kutakuwa na amani—kama neno lake litatimia, basi itajulikana kwamba yeye ni nabii kweli aliyetumwa na Yahweh.”

10Lakini Hanania nabii akaichukua nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia na kuivunja.11Kisha Hanania akanena mbele ya watu wote na kusema, “Yahweh anasema hivi: Kama hivi tu, ndani ya miaka miwili nitaivunja nira iliyowekwa na Nebukadneza mfalme wa Babeli kutoka kwenye shingo ya kila taifa.” Kisha Yeremia nabii akaenda njia yake.

12Baada ya Hanania nabii kuivunja nira kutoka kwenye shingo ya Yeremia nabii, neno la Yahweh likamjia Yeremia. Likisema,13Nenda ukamwambie Hanania, Yahweh anasema hivi: Uliivunja nira ya mbao, lakini badala yake nitafanya nira ya chuma.’14Kwa maana Yahweh wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nimeweka nira ya chuma shingoni mwa mataifa haya yote ili wamtumikie Nebukadreza mfalme wa Babeli, na watamtumikia. Pia nimempa wanyama wa mashambani awatawale.”

15Kisha nabii Yeremia akamwambia Hanania nabii, “Sikiliza Hanania! Yahweh hajakutuma, bali wewe mwenyewe umewasababisha watu hawa kuamini uongo.16Kwa hiyo Yahweh anasema hivi: Angalia, niko karibu kukuondoa duniani. Mwaka huu utakufa, kwa sababu umetangaza uasi dhidi ya Bwana.”

17Katika mwezi wa saba wa mwaka ule ule, Hanania nabii akafa.

29

1Haya ni maneno katika waraka ambao Yeremia nabii alituma kutoka Yerusalemu kwa wazee waliosalia miongoni mwa mateka na makuhani, manabii, na watu wote ambao Nebukadneza aliwapeleka utumwani kutoka Yerusalemu hadi Babeli.2Hii ilikuwa baada ya Yekonia mfalme, mama yake mfalme, na watumishi wakuu, viongozi wa Yuda na Yerusalemu, na wahunzi walikuwa wamepelekwa mbali na Yerusalemu.3Aliutuma waraka huu kwa mkono wa Elasa mwana wa Shafani, Gemaria mwana wa Hilkia, ambaye Sedekia, mfalme wa Yuda, alikuwa amemtuma kwa Nebukadreza mfalme wa Babeli

4Waraka ulisema, Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kwa mateka ambao niliwasababisha kuwa mateka kutoka Yerusalemu hadi Babeli,5‘Jengeni nyumba na muishi ndani yake. Pandeni bustani na mle matunda yake.6Chukueni wake na mzae wana na mabinti. Kisha chukueni wake kwa ajili ya wana wenu, na wapatieni waume binti zenu. Wazae wana na mabinti na waongezeke ili msiwe wachache sana.7Itafuteni amani ya mji ambako nimewafanya kuwa watumwa, na mkauombee kwangu kwa niaba yake kwa kuwa kutakuwa na amani kwenu kama mji uko katika amani.’

8Kwa maana Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, ‘Msiwaache manabii ambao wako katikati yenu na wabashiri wenu kuwadanganya, na msizisikilize ndoto ambazo ninyi wenyewe mnaota.9Kwa maana wanatabiri uongo kwenu katika jina langu. Mimi sikuwatuma—hili ni tangazo la Yahweh.’

10Kwa maana Yahweh anasema hivi, ‘Babeli atakapokuwa amewatawala kwa muda wa miaka sabini, nitawasaidia ninyi na kulitimiza neno langu jema kwa ajili yenu ili kuwarudisha ninyi katika sehemu hii.11Kwa maana mimi mwenyewe naijua mipango niliyonayo kwa ajili yenu—hili ni tangazo la Yahweh—mipango ya amani na siyo mabaya, ili kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.12Kisha mtaniita, na kwenda na kuniomba mimi, na nitawasikiliza.13Kwa maana mtanitafuta na kunipata, kwa kuwa mtanitafuta kwa moyo wenu wote.14Kisha nitapatikana kwenu—hili ni tangazo la Yahweh—na nitawarudisha watu wenu waliofungwa; nitawakusanya kutoka mataifa yote na sehemu zote ambako nimewatawanya—hili ni tangazo la Yahweh—kwa maana nitawarudisha kutoka sehemu ambako niliwasababisha kuwa mateka.

15Tangu mliposema kwamba Yahweh ameinua manabii kwa ajili yetu katika Babeli,16Yahweh asema hivi kwa mfalme aliyeketi katika kiti cha enzi cha Daudi na watu wote wakaao katika mji huo, ndugu zenu ambao hawakwenda pamoja nanyi utumwani—17Yahweh Mungu wa majeshi anasema hivi, “Ona, niko karibu kutuma upanga, njaa, na ugonjwa juu yao. Kwa maana nitawafanya kuwa kama tini mbovu ambazo ni mbaya sana hazifai kuliwa.18Kisha nitawafuata kwa upanga, njaa, na tauni na kuwafanya kuwa kitu cha kushangaza kwa falme zote juu ya dunia—kitu cha kuogofya, kitu cha kulaaniwa na kuzomewa, na kitu cha aibu miongoni mwa mataifa yote ambako nilimtawanya.19Hii ni kwa sababu hawakulisikiliza neno langu—hili ni tangazo la Yahweh—ambalo nililituma kwao kupitia watumishi wangu manabii. Niliwatuma tena na tena, lakini hamkusikiliza—hili ni tangazo la Yahweh.’

20Kwa hiyo ninyi wenyewe sikilizeni neno la Yahweh, ninyi mateka wote ambao amewatuma kutoka Yerusalemu hadi Babeli,21‘Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi kuhusu Ahabu mwana wa Kolaya na Sedekia mwana wa Maaseya, watabirio uongo kwenu katika jina langu: Ona, niko karibu kuwaweka katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli. Atawaua mbele ya macho yenu.22Kisha laana itatamkwa na wafungwa wote wa Yuda katika Babeli kuhusu watu hawa. Laana itasema: Yahweh awafanye kuwa kama Sedekia na Ahabu, ambao mfalme wa Babeli aliwaoka kwenye moto.23Hili litatokea kwa sababu ya mambo ya aibu waliyofanya katika Israeli walipofanya uzinzi na wake za majirani zao na kutangaza maneno ya uongo katika jina langu, mambo ambayo sikuwaamuru wayaseme. Kwa maana mimi ndiye nijuaye; mimi ni shahidi—hili ni tangazo la Yahweh.”

24Kuhusu Shemaya Mnehelami, sema hivi:25‘Yahweh wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Kwa sababu ulituma barua kwa jina lako kwa watu wote katika Yerusalemu, kwa Sefania mwana wa Maaseya kuhani, na kwa makuhani wote, na ulisema,

26“Yahweh aliwafanya ninyi kuwa makuhani badala ya Yehoyada kuhani, ili muwe wasimamizi wa nyumba ya Yahweh. Ninyi ni viongozi wa watu wote wajitiao wazimu na kujifanya wenyewe manabii. Mtawaweka katika mkatale na minyororo.27Kwa hiyo sasa, kwa nini hamkumkemea Yeremia wa Anathothi, ambaye hujifanya mwenyewe nabii juu yenu?28Kwa maana ametutumia sisi katika Babeli, ‘Itakuwa muda mrefu. Jengeni nyumba na muishi ndani yake, na pandeni busitani na mule matunda yake.”

29Sefania kuhani akaisoma barua hii mbele ya Yeremia nabii.30Kisha neno la Yahweh likaja kwa Yeremia, likisema,31“tuma neno kwa mateka wote na sema, ‘Yahweh anasema hivi kuhusu Shemaya Mnehelami: Kwa sababu Shemaya amewatabiria ninyi wakati mimi sikumtuma, na amewaongoza kuamini uongo,32kwa hiyo Yahweh anasema hivi: Angalia, niko karibu kumwadhibu Shemaya Mnehelami na uzao wake. Hapatakuwa na mtu wa kukaa miongoni mwa watu hawa kwa ajili yake. Hataona mema nitakayofanya kwa ajili ya watu wangu—hili ni tangazo la Yahweh—kwa maana ametangaza uasi dhidi ya Yahweh.”

30

1Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yahweh likisema,2“Hivi ndivyo Yahweh, Mungu wa Israeli, anasema, ‘Andika kwa kitabu maneno yote niliyonena kwako.3Maana tazama, siku zaja—hili ni tangazo la Yahweh—nitakapowarudisha mateka wa watu wangu Israeli na Yuda. Mimi, Yahweh, nimesema hili. Kwa maana nitawarudisha kwenye nchi ambayo niliwapa babu zao, na wataimiliki.”

4Haya ni maneno ambayo Yahweh anatangaza kuhusu Israeli na Yuda,5“Kwa maana Yahweh anasema hivi, ‘Tumesikia sauti ya kutetemesha ya hofu na wala siyo ya amani.
6Ulizeni na muone kama mwanaume kujifungua mtoto. Mbona ninamwona kila mwanaume kijana ameshika mikono yake juu ya kiuno chake kama mwanamke anayejifungua mtoto? Kwa nini nyuso zao wote zimegeuka rangi?
7Ole! Kwa maana siku hiyo itakuwa kuu, isiyofanana na yoyote. Utakuwa wakati wa huzuni kwa Yakobo, lakini ataokolewa.
8Kwa maana itakuwa katika siku hiyo—hili ni tangazo la Yahweh Mungu wa majeshi—kwamba nitaivunja nira ya shingo zenu, na nitaisambaza minyororo yenu, kwa hiyo wageni hawatawafanya watumwa tena.
9Bali watamwabudu Yahweh Mungu wao na kumtumikia Daudi mfalme wao, ambaye nitamfanya mfalme juu yao.
10Kwa hiyo wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope—hili ni tangazo la Yahweh—na usifadhaike, ee Israeli. Maana ona, niko karibu kukuokoa kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya utumwa. Yakobo atarudi na kuwa katika amani; na usalama, na hapatakuwa na hofu zaidi.
11Kwa maana niko pamoja nawe—hili ni tangazo la Yahweh—ili kukuokoa. Kisha nitaleta mwisho kamili kwa mataifa yote ambako nimewatawanya. Bali sitaweka mwisho kwako, ingawa ninakuadhibu kwa haki na kwa hakika sitakuacha bila kukuadhibu.’

12Kwa maana Yahweh anasema hivi, ‘Jeraha lako si la kupona; kidonda chako kimeenea.
13Hakuna mtu wa kukutetea kesi yako; hakuna utetezi kwa ajili ya kidonda chako ili upone.
14Wapenzi wako wote wamekusahau. Hawatakutafuta, kwa maana nimekujeruhi kwa jeraha la adui na nidhamu ya bwana mkatili kwa sababu ya uovu wako mwingi na dhambi zako zisizohesabika.
15Kwa nini unaita msaada kwa ajili ya jeraha lako? Maumivu yako hayaponyeki. Kwa sababu ya uovu wako mwingi, dhambi zako zisizohesabika, nimefanya mambo haya kwako.
16Kila mtu akulaye ataliwa, na adui zako wote wataenda utumwani. Kwa maana kila aliyekuteka nyara atatekwa, na nitawafanya wote wanaokuwinda kuwa mawindo.
17Kwa maana nitaleta uponyaji juu yako; nitakuponya majeraha yako—hili ni tangazo la Yahweh—nitafanya hivyo kwa sababu walikuita: Mwenyekutupwa. Hakuna anayejali Sayuni.”

18Yahweh anasema hivi, “Ona, niko karibu kuwarudisha mateka wa hema za Yakobo na kuwa na huruma juu ya nyumba zake. Kisha mji utajengwa juu ya lundo la magofu, na jumba litakuwepo tena kama ilivyokuwa kawaida.
19Kisha wimbo wa kusifu na sauti ya shangwe itasikika kutoka kwao, kwa maana nitawaongeza na wala sitawapunguza; nitawaheshimu ili kwamba wasifanywe wanyonge.
20Kisha watu watakuwa kama ilivyokuwa mwanzo, na kusanyiko lao litaanzishwa mbele yangu wakati nitakapowaadhibu wote wanaowatesa kwa sasa.
21Kiongozi wao atatoka miongoni mwao. Atatokeza kutoka kati yao nitakapomleta karibu na atakaponikaribia mimi. Kama sitafanya hivyo, ni nani atakayethubutu kunisongelea? —Hili ni tangazo la Yahweh.
22Kisha mtakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wenu.
23Ona, tufani ya Yahweh, ghadhabu yake, imekwenda nje. Ni tufani isiyokoma. Itazunguka juu ya vichwa vya watu waovu.
24Hasira ya Yahweh haitarudi mpaka itoke na kutimiza makusudi ya moyo wake. Katika siku za mwisho mtalielewa hili.”

31

1“Katika wakati huo—hili ni tangazo la Yahweh—Nitakuwa Mungu wa koo zote za Israel, na watakuwa watu wangu.”

2Yahweh anasema hivi, “Watu ambao wamenusurika na upanga wamepata kibali katika nyika; nitatoka nje kuwapa pumziko Israeli.”

3Yahweh alinitokea zamani na kusema, “Nimekupenda wewe, Israeli, kwa upendo wa milele. Kwa hiyo nimekuvuta kwangu kwa agano la uaminifu.
4Nitakujenga tena kwa hiyo utakuwa umejengwa, bikra wa Israeli. Utachukua tena matari zako na kwenda nje kwa ngoma za furaha.
5Utapanda mizabibu tena juu ya milima Samaria; wakulima watapanda na kuweka matunda kwa ajili ya matumizi mazuri.
6Kwa maana siku itakuja wakati walinzi watakapotangaza katika milima ya Efraimu, ‘Inuka, twendeni juu kwenye mlima wa Yahweh Mungu wetu.’

7Kwa maana Yahweh anasema hivi, Piga kelele za shangwe juu ya Yakobo! Pigeni kelele za furaha kwa ajili ya watu wakuu wa mataifa! Sifa zisikike. Sema, “Yahweh amewaokoa watu wake, masalia wa Israeli.’
8Ona, niko karibu kuwaleta kutoka nchi za kaskazini. Nitawakusanya kutoka sehemu za mbali za dunia. Vipofu na wenye ulemavu watakuwa katikati yao; wanawake wajawazito na wale waliokaribu kujifungua watakuwa pamoja nao. Kusanyiko kubwa litarudi hapa.
9Watakuja kwa kuomboleza; nitawaongoza huku wakifanya maombi yao. Nitawafanya wasafiri katika mikondo ya maji katika bara bara ilinyoka. Hawatajikwaa juu yake, kwa maana nitakuwa baba kwa Israeli, na Efraimu atakuwa mzaliwa wangu wa kwanza
10Sikia neno la Yahweh, mataifa. Litangazeni pembezoni mwa visiwa mbali. Enyi mataifa lazima museme, ‘Yule aliyemtawanya Israeli anamkusanya tena na kuwalinda kama mchungaji alindavyo kondoo.’
11Kwa maana Yahweh amemfidia Yakobo na kumkomboa kutoka mkono ambao ulikuwa na nguvu sana kwake.
12Kisha watakuja na kufurahia katika vilele vya Sayuni. Nyuso zao zitameremeta kwa sababu ya wema wa Yahweh, juu ya nafaka na divai mpya, juu ya mafuta na malimbuko ya kwanza ya makundi na ng'ombe. Kwa maana maisha yao yatakuwa kama bustani iliyomwagiliwa, na hatajisikilia huzuni tena.
13Kisha wanawali watafurahia kwa kucheza, na vijana na wanaume wazee watakuwa pamoja. Kwa maana nitayageuza maombolezo yao kuwa sherehe. Nitakuwa na huruma juu yao na kuwafanya kufurahi badala ya kuhuzunika.
14Kisha nitayaeneza sana maisha ya makuhani. Watu wangu watajijaza wenyewe kwa wema—hili ni tangazo la Yahweh.”

15Yahweh anasema hivi: “Sauti imesikika katika Rama, kilio na maombolezo mengi. Ni Raheli akiomboleza kwa ajili watoto wake. Hataki kufarijiwa tena juu yao, kwa maana hawako hai tena.”

16Yahweh anasema hivi, “Zuia sauti yako usilie na macho yako yasitoe machozi; kwa maana kuna fidia kwa ajili ya mateso yako—hili ni tangazo la Yahweh—watoto wako watarudi kutoka nchi ya adui.
17Kuna matumaini kwa ajili ya siku zenu za baadaye—hili ni tangazo la Yahweh—uzao wako watarudi ndani ya mipaka yao.”
18Kwa hakika nimemsikia Efraimu akilia, ‘Uliniadhibu, nami nimeadhibika kama ndama asiye na mafunzo. Nirudishe nami nitarudi, kwa maana wewe ni Yahweh Mungu wangu.
19Kwa maana baada ya kurudi kwako, nilikuwa na huzuni; baada ya kufundishwa, nilijipiga kofi shavu langu. Niliaibika na kudharirika, kwa maana nilizaliwa na hatia ya ujana wangu.’
20Efraimu siyo mwanangu wa thamani? Yeye si mpendwa wangu, mwanangu anipendezaye? Kwa maana kila ninaponena juu yake, bado nina mwita kipenzi cha akili yangu. Kwa namna hii moyo wangu unamtamani. Kwa hakika nitakuwa na huruma juu yake—hili ni tangazo la Yahweh.”
21Jiwekee alama za bara bara kwa ajili yako mwenyewe. Weka matangazo ya maelekezo kwa ajili yako mwenyewe. Iweke akili yako juu ya njia sahihi, njia unayopaswa kufuata. Rudi, bikra Israeli! Rudi kwenye hii miji yako.
22Utatangatanga hadi lini, binti usiye mwaminifu? Kwa maana Yahweh ameumba kitu fulani kipya juu ya dunia—mwanamke anamzunguka mwanaume.

23Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, ‘“Nitakapowarudisha watu katika nchi yao, watasema hivi katika nchi ya Yuda na miji yake, “Yahweh akubariki, wewe sehemu takatifu ambapo anaishi, ewe mlima mtakatifu.’24Kwa maana Yuda na miji yake yote wataishi pamoja humo, kama vile watakavyoishi wakulima na wachungaji pamoja na makundi yao.25Kwa maana nitawapa maji ya kunywa waliochoka, na nitamjaza kila anayeteseka na kiu.”

26Baada ya haya niliamka, na nikagundua kwamba usingizi wangu ulikuwa unaburudisha.

27Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahweh—nitakapoipanda nyumba ya Israeli na Yuda pamoja na wazawa wa wanadamu na wanyama.28Zamani, niliwaweka katika uangalizi ili kuwang'oa na kuwabomoa, kuwaangusha, kuwaharibu, na kuwaletea madhara. Lakini katika siku zijazo, nitawaangalia, ili niwajenge na kuwapanda—hili ni tangazo la Yahweh.29Katika siku hizo hakuna atakayesema tena, “Baba za watu wamekula zabibu kali, bali meno ya watoto ni butu.’30Kwa maana kila mtu atakuwa katika uovu wake mwenyewe; kila alaye zabibu kali, meno yake yatakuwa butu.31Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahweh—nitakapoanzisha agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.32Halitakuwa kama agano ambalo nilianzisha na baba zao nilipowatoa kwa mkono wao nje ya nchi ya Misiri. Hizo zilikuwa siku ambapo walilivunja agano langu, ingawa nilikuwa mume kwao—hili ni tangazo la Yahweh.33Lakini hili ni agano nitakaloanzisha na nyumba ya Israeli baada ya siku hizi—hili ni tangazo la Yahweh: Nitaiweka sheria yangu ndani yao na nitaiandika juu ya mioyo yao, kwa maana nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.34Kisha kila mtu hatamfundisha jirani yake, wala mtu hatamfundisha ndugu yake akisema, ‘Mjue Yahweh!’ Kwa maana wao wote, kuanzia mdogo wao hata mkubwa, watanijua—hili ni tangazo la Yahweh—kwa maana nitawasamehe uovu wao na sitazikumbuka tena dhambi zao.”’

35Yahweh anasema hivi—Yahweh, yeye afanyaye jua kuangaza mchana na kuzipanga mwezi na nyota kuangaza usiku. Yeye ndiye aiwekaye bahari katika mwendo ili mawimbi yake yangurume. Yahweh Mungu wa majeshi katika jina lake.
36“Ikiwa tu mambo haya yakudumu yakitoweka machoni pangu—hili ni agizo la Yahweh—uzao wa Israeli hawatasimama mbali nami wasiwe taifa.”

37Yahweh anasema hivi, “Kama tu urefu wa mbingu unaweza kupimwa, na kama tu misingi ya dunia chini inaweza kugunduliwa, nitawakataa uzao wote wa Israeli kwa sababu ya yote waliyofanya—hili ni tangazo la Yahweh.”

38“Angalia, siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahweh—ambapo mji utajengwa tena kwa ajili yangu, kutoka Mnara wa Hananeli hadi kwenye Lango la Pembeni.39Kisha mistari ya kupimia itaenda nje hadi mbali, hadi kwenye kilima cha Garebu na kuzunguka Goa.40Bonde lote la miili iliyokufa na majivu, na shamba lenye matuta linalofika hadi Bonde la Kidroni mbali hadi kwenye kona ya Lango la Farasi upande wa mashariki, litateuliwa kwa ajili ya Yahweh. Mji hautang'olewa wala kupinduliwa tena, milele.”

32

1Neno likaja kwa Yeremia kutoka kwa Yahweh katika mwaka wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadreza.2Katika wakati huo, jeshi la mfalme wa Babeli lilikuwa limezunguka Yerusalemu, na Jeremia nabii alikuwa amefungwa katika uwanja wa walinzi katika nyumba ya mfalme wa Yuda.3Sedekia mfalme wa Yuda alikuwa amemfunga na kusema, “Kwa nini unatabiri na kusema, ‘Yahweh anasema hivi: Angalia, niko karibu kuweka mji huu katika mikono ya mfalme wa Babeli, na atauteka.4Sedekia mfalme wa Yuda hatapona kutoka kwenye mikono ya Wakaldayo, kwa maana hakika atatiwa katika mkono wa mfalme wa Babeli. Mdomo wake utazungumza kwenye mdomo wa mfalme, na macho yake yatayaona macho ya mfalme.5Atampeleka Sedekia Babeli, na atabaki huko hadi nimuadhibu—hili ni tangazo la Yahweh. Ingawa unapigana dhidi ya Wakaldayo, hautafanikiwa.”

6Yeremia akasema, “Neno la Yahweh lilinijia, likisema, Angalia, Hanameli mwana wa Shalumu mjomba wako anakuja kwako na atasema,7“Linunue shamba langu ambalo liko katika Anathothi kwa ajili yako, kwa maana haki ya kununua ni yako.”

8Kisha, kama Yahweh alivyotangaza, Hanameli, mwana wa mjomba wangu, akaja kwangu katika uwanja wa walinzi, na akasema kwangu, ‘Linunue shamba langu kwa ajili yako ambalo liko Anathothi katika nchi ya Benjamini, kwa maana haki ya urithi ni ya kwako, na haki ya kulinunua ni yako. Linunue kwa ajili yako.’ Kisha nilijua kuwa hili lilikuwa neno la Yahweh.

9Kwa hiyo nililinua shamba katika Anathothi kutoka kwa Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na nilipima fedha kwa ajili yake, shekeli kumi na saba katika uzito.10Kisha niliandika katika barua na kuitia muhuri, na kulikuwa na mashahidi wakaishuhudia. Kisha nikampa fedha katika mizani.11Kisha nikaichukua hati ya manunuzi ambayo ilikuwa imepigwa muhuri, kwa kuifuata amri na taratibu, na kama ilivyo ada.12Ile barua nikampa Baruku mwana wa Neria wa Maaseya mbele ya Hanameli, mwana wa mjomba wangu, na mashahidi waliotia sahihi kwenye barua iliyopigwa muhuri, na mbele ya Wayahudi wote waliokaa katika uwanja wa walinzi.

13Kwa hiyo nikampa amri Baruku mbele yao. Nilisema,14Yahweh, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Chukua nyaraka hizi, vyote hati hii ya manunuzi iliyopigwa muhuri na nakala zisizopigwa muhuri za manunuzi, na uziweke katika chungu cha udongo ili vidumu kwa muda mrefu.15Kwa maana Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nyumba, mashamba, na mashamba ya mizabibu vitanunuliwa tena katika nchi hii.

16Baada ya kumpa Baruki mwana wa Neria ile hati ya manunuzi, nikaomba kwa Yahwe nikasema,17Ole, Bwana Yahweh! Angalia! Wewe peke yako umezitengeneza mbingu na dunia kwa nguvu zako kuu na kwa mkono wako ulioinuka. Hakuna kitu ambacho ukisema kwako ni kigumu sana kukifanya.18Wewe huonesha agano la uaminifu kwa maelfu na kumimina makosa ya wanadamu katika mapaja ya watoto wao baada yao. Wewe ni Mungu mkuu na mwenye nguvu.19Wewe ni mkuu katika hekima na una nguvu katika matendo, kwa maana macho yako yanaona njia zote za watu, ili kumlipa kila mtu stahiki ya matendo yake.20Ulifanya ishara na maajabu katika nchi ya Misiri. Hata leo hapa Israeli na kati ya wanadamu wengine wote, umelifanya jina lako kuwa maarufu.21Kwa maana uliwanunua watu wako Israeli kwa ishara na maajabu, kwa mkono hodari, kwa mkono ulioinuka, na kwa hofu kuu.22Kisha uliwapa nchi hii—ambayo uliapa kwa babu zao kwamba utawapa—nchi itiririkayo maziwa na asali.23Hivyo waliingia na kuimiliki. Lakini hawakuitii sauti yako wala kuishi kwa kuitii sheria yako. Hawakufanya chochote ulichowaamuru kufanya, kwa hiyo umeleta juu yao majanga haya yote.

24Angalia! Urefu wa maboma haya umefika hadi kwenye mji ili kuuteka. Kwa sababu ya upanga, njaa, na tauni, mji umetiwa kwenye mikono ya Wakaldayo wanaopigana dhidi yake. Kwa maana ulichosema kitatokea sasa kinatokea, na ona, unatazama.25Kisha wewe mwenyewe uliniambia, “Nunua shamba kwa fedha kwa ajili yako na mashahidi wameshuhudia, ingawa mji huu unatiwa mikononi mwa Wakaldayo.”

26Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,27“Angalia! Mimi ni Yahweh, Mungu wa wanadamu wote. Kuna kitu cho chote kigumu sana kwangu kukifanya?28Kwa hiyo Yahweh anasema hivi, ‘Ona, niko karibu kuutia mji huu kwenye mikono ya Wakaldayo na Nebukadneza, mfalme wa Babeli. Atauteka.29Wakaldayo wanaopigana dhidi ya mji huu watakuja na kuwasha moto kwenye mji huu na kuunguza, pamoja na nyumba juu ya paa la watu waliomwabudu Baali na kumimina dhabihu kwa miungu wengine ili kunikasirisha.

30Kwa maana watu wa Israeli na Yuda hakika wamekuwa watu wanaofanya maovu mbele ya macho yangu tangu ujana wao. Watu wa Israeli hakika wameniudhi kwa matendo ya mikono yao—hili ni tangazo la Yahweh.31Yahweh anatangaza kwamba mji huu umekuwa sababu ya hasira yangu na ghadhabu yangu tangu siku walipoujenga. Umekuwa hivyo hata leo. Kwa hiyo nitauondoa mbele ya uso wangu32kwa sababu ya uovu wote wa watu wa Israeli na Yuda, mambo waliyofanya ili kunichukiza—wao, wafalme wao, wana wa wafalme, makuhani, manabii, na kila mtu katika Yuda na wakaaji wa Yerusalemu.33Wamenigeuzia migongo yao badala ya nyuso zao, ingawa nilijitahidi kuwafundisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyenisikiliza ili kupokea marekebisho.34Walisimamisha sanamu zao za ajabu katika nyumba inayoitwa kwa jina langu, ili kunitia unajisi.35Wakazijenga sehemu za juu katika Bonde la Beni Hinomu ili kuwatia katika moto wana wao na binti zao kwa ajili ya Moleki. Mimi sikuwaagiza. Sikuweka akilini mwangu kamwe kwamba watafanya mambo maovu na kwa hiyo kuwasababisha Yuda watende dhambi.

36Kwa hiyo sasa, Mimi, Yahweh, Mungu wa Israeli, kuhusu mji huu ninasema hivi, ‘mji ambao mnasema, ‘Umetiwa mikononi mwa mfalme wa Babeli kwa upanga, njaa, na pigo.’37Ona, niko karibu kuwakusanya kutoka kila nchi nilikowapeleka katika hasira yangu, ghadhabu, na hasira kuu. Niko karibu kuwarudisha kwenye sehemu hii na kuwawezesha kuishi katika usalama.38Kisha watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao.39Nitawapa moyo mmoja na njia moja ya kuniheshimu kila siku ili kwamba yawepo mema kwa ajili yao na uzao wao baada yao.40Kisha nitafanya pamoja nao agano la milele, ili nisiache kufanya mema kwa ajili yao. Nitajiwekea heshima katika mioyo yao, ili kwamba wasiniache.41Kisha nitajifurahisha katika kufanya mema kwao. Kwa uaminifu nitawapanda katika nchi hii kwa moyo wangu wote na maisha yangu yote.

42Kwa maana Yahweh anasema hivi, ‘Kama tu nilivyoyaleta majanga haya makubwa yote juu ya watu hawa, vivyo hivyo nitaleta juu yao mambo mema niliyosema kwamba nitafanya kwa ajili yao.43Basi mashamba yatanunuliwa katika nchi hii, ambayo mnaisema, “Hii ni nchi iliyoharibiwa, isiyo na mwanadamu wala mnyama. Imetiwa mikononi mwa Wakaldayo”44Watanunua mashamba kwa fedha na kuandika katika barua zilizopigwa muhuri. Watawakusanya mashahidi katika nchi ya Benjamini, wote kuzunguka Yerusalemu na miji ya Yuda katika miji ya nchi yenye vilima, na katika nchi tambarare, na katika miji ya Negebu. Kwa maana nitawarejesha wafungwa wao—hili ni tangazo la Yahweh.”

33

1Kisha neno la Yahweh likaja kwa Yeremia mara ya pili, alipokuwa bado amefungwa ndani ya uwanja wa walinzi, likisema,2Yahwe muumbaji, anasema hivi—Yahweh, aumbaye ili athibitishe—Yahweh ndilo jina lake,3‘Niite, na nitakuitika, nitakuelezea mambo makuu, siri ambazo huzielewi.’4Kwa maana Yahweh, Mungu wa Israel, anasema hivi kuhusu nyumba zilizo katika mji huu na nyumba za wafalme wa Yuda zilizobomolewa kwa sababu ya maboma na upanga,5Wakaldayo wanakuja kupigana na kuzijaza nyumba kwa hizi kwa majeshi ya watu ambao wataua katika hasira yangu na ghadhabu yangu, nitakapouficha mji huu uso wangu kwa sababu ya uovu wao wote.

6Lakini ona, niko karibu kuleta uponyaji na tiba, kwa maana nitawaponya na nitawapa wingi wa, amani na uaminifu.7Kwa maana nitawarudisha wafungwa wao wa Yuda na Israeli; nitawajenga tena kama ilivyokuwa mwanzo.8Kisha nitawatakasa uovu wote walioufanya dhidi yangu. Nitasamehe makosa yote waliyonitenda, na njia zote walizo asi dhidi yangu.9Kwa maana mji huu kwa ajili yangu utakuwa chombo cha furaha, nyimbo, sifa na heshima kwa mataifa yote ya dunia ambao watasikia mambo yote mema ninayokwenda kufanya kwa ajili ya huu mji. Kisha wataogopa na kutetemeka kwa sababu ya mambo yote mema na amani nitakayoupa mji huu.’

10Yahweh anasema hivi, ‘Katika sehemu hii ambayo sasa mnaisema, “Imetengwa, sehemu isiyo na mwanadamu wala mnyama,” katika mji huu wa Yuda, na katika mitaa ya Yerusalemu ambayo imetengwa bila mwanadamu wala mnyama, zitasikika tena11sauti za furaha na sauti za shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti za wale wasemao, wanapoleta shukrani katika nyumba ya Yahweh, “Mshukuruni Yahweh Mungu wa majeshi, kwa maana Yahweh ni mwema, na upendo wake usioshindwa wadumu milele!” Kwa maana nitawafanya tena wafungwa wa nchi kuwa walivyokuwa mwanzo,’ asema Yahweh.

12Yahweh Mungu wa majeshi asema hivi: Katika sehemu hii ya ukiwa, ambamo sasa hakuna mwanadamu wala mnyama—katika miji yake yote kutakuwepo tena malisho ambapo wachungaji wataweza kupumzisha makundi yao.13Katika miji hii katika nchi ya vilima, nchi tambarare, na Negevu katika nchi ya Benjamini na kuzunguka Yerusalemu yote, na katika miji ya Yuda, makundi yatapata njia chini ya mkono wa yule anayewahesabu,’ asema Yahweh.

14Angalia! Siku zinakuja—hili ni tangazo la Yahweh—ambapo nitafanya niliyoahidi kwa nyumba ya Israeli na nyumba ya Yuda.
15Katika siku hizo na katika wakati huo nitachipua shina la haki kwa ajili ya Daudi, na atafanya hukumu na haki katika nchi.
16Katika siku hizo Yuda wataokolewa, na Yerusalemu utaishi katika usalama, kwa maana hivi ndivyo atakavyoitwa, “Yahweh ni haki yetu.”
17Kwa maana Yahweh anasema hivi: ‘Mwana kutoka ukoo wa Daudi hatakosa kuketi katika kiti cha nyumba ya Israeli,18wala mtu kutoka ukuhani wa Kilawi hatakosa kutoa sadaka za kuteketezwa mbele zangu, kutoa sadaka za chakula, na kutoa sadaka za nafaka wakati wote.”

19Neno la Yahweh likaja kwa Yeremia, likisema,20“Yahweh anasema hivi: ‘Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana na usiku ili kwamba siku isikawie wala usiku usikawie kuja kwa wakati wake,21basi mtaweza kulivunja agano langu na Daudi mtumishi wangu, ili kwamba asipate mwana wa kuketi juu ya kiti chake cha enzi, na agano langu na makuhuni wa Kilawi, watumishi wangu.22Kama vile majeshi ya mbinguni yasivyoweza kuhesabika, na kama vile mchanga wa ufukwe wa bahari usivyoweza kupimwa, ndivyo nitakavyouongeza uzao wa Daudi mtumishi wangu na Walawi watumikao mbele zangu.”

23Neno la Mungu likaja kwa Yeremia, likisema,24Hamkuzingatia walichotangaza watu hawa waliposema, ‘Zile Familia mbili ambazo Yahweh alizichagua, sasa amezikataa’? Kwa jinsi hii waliwapuuza watu wangu, wakisema kwamba si taifa tena katika macho yao.25Mimi, Yahweh, nasema hivi, ‘Kama sijalithibitisha agano la mchana na usiku, na kama sijaziweka sheria za mbingu na dunia,26basi nitawakataa uzao wa Yakobo na Daudi mtumishi wangu, na nisilete mtu kutoka kati yao wa kutawala juu ya uzao wa Abrahamu, Isaka, na Yakobo. Kwa maana nitawarudisha wafungwa wao na kuonesha huruma kwao.”

34

1Neno lililomjia Yeremia kutoka kwa Yahweh, wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli, majeshi yake yote, pamoja na falme zote za dunia, maeneo yote yaliyo chini ya mamlaka yake, na watu wake wote walikuwa wanapigana vita dhidi ya Yerusalemu na miji yake yote, kusema:2‘Yahweh, Mungu wa Israeli, anasema hivi: Nenda na uzungumze kwa Sedekia mfalme wa Yuda na useme kwake, ‘Yahweh asema hivi: Angalia, niko karibu kuutia mji huu mkononi mwa mfalme wa Babeli. Atauchoma moto.3Hautapona kutoka mkono wake, kwa maana kwa hakika utakamatwa na kutiwa mkononi mwake. Macho yako yatayaangalia macho ya mfalme wa Babeli; atazungumza kwako moja kwa moja ukiwa unaenda Babeli.’

4Sedekia mfalme wa Yuda, sikiliza neno la Yahweh! Yahweh anasema hivi kuhusu wewe, ‘Hautakufa kwa upanga.5Utakufa katika amani. Kama kwenye mafukizo ya babu zako, wafalme waliokuwepo kabla yako, watauchoma mwili wako. Watasema, ‘Ole, bwana!” Watakuomboleza. Sasa nimesema—hili ni tangazo la Yahweh.”

6Kwa hiyo Yeremia nabii akatangaza kwa Sedekia mfalme wa Yuda maneno haya yote katika Yerusalemu.7Jeshi la mfalme wa Babeli likafanya dhidi ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda iliyobaki: Lakishi, na Azeka. Miji hii ya yuda ilisalia kama miji yenye ngome.

8Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Yahweh baada ya mfalme Sedekia kufanya agano na watu wote katika Yerusalemu, ili kuwatangazia uhuru9ya kwamba kila mtu lazima amwachie huru mtumwa wake wa Kiebrania, wote wa kiume na wa kike, kwa hiyo mtu alipaswa kutomtumikisha Myahudi, ambaye alikuwa ndugu yake.10Kwa hiyo watu wote na viongozi wakaingia katika agano kwamba kila mtu amwachie huru mtumwa wake wa kiume na wakike ili asiwe mtumwa tena. Walitii na kuwaweka huru.11Lakini baada ya hapo walibadili mawazo yao. Wakawarudisha watumwa ambao walikuwa wamewaachia huru. Wakawalazimisha kuwa watumwa tena.

12Kwa hiyo neno la Yahweh likaja kwa Yeremia, likisema,13“Yahweh, Mungu wa Israeli, anasema hivi, ‘Mimi mwenyewe nilifanya agano na babu zenu katika siku ambayo niliwatoa nje ya nchi ya Misiri, nje ya nyumba ya utumwa. Hapo ndipo niliposema,14Katika mwisho wa mwaka wa saba, kila mtu lazima amwachie ndugu yake, Mwebrania mwenzake aliyejiuza mwenyewe kwako ili kukutumikia kwa miaka sita. Mwagize aende kwa uhuru.” Lakini babu zenu hawakunisikiliza wala kutega masikio yao kwangu.15Sasa ninyi wenyewe mlitubu na kuanza yaliyo mema katika macho yangu. Mlitangaza uhuru, kila mtu kwa jirani yake, na mlifanya agano mbele zangu kwenye nyumba iitwayo kwa jina langu.16Lakini tena mmegeuka na kulichafua jina langu; mmemsababisha kila mtu kumleta tena mtumwa wake wa kiume na wa kike, wale mliowaachia kwenda walikotaka. Mmewalazimisha kuwa watumwa tena.’

17Kwa hiyo Yahweh asema hivi, ‘Ninyi wenyewe hamkunisikiliza. Mlipaswa kuwa mmetangaza uhuru, kila mmoja wenu, kwa ndugu zenu na Waisraeli wenzenu. Kwa hiyo angalia! Niko karibu kutangaza uhuru kwenu—hili ni tangazo la Yahweh—uhuru wa upanga, tauni, na njaa, kwa maana naenda kuwafanya kitu cha ajabu katika macho ya kila ufalme juu ya dunia.18Kisha nitashughulika na watu waliolivuja agano langu, ambao hawakuyashika maneno ya agano ambalo walilithibitisha mbele zangu walipomkata ng'ombe dume katika vipande viwili na kutembea katika vipande vyake,19na kisha viongozi wa Yuda na Yerusalemu, matowashi na makuhani, na watu wote wa nchi wakatembea katika vipande vya yule ng'ombe dume.20Nitawatia katika mikono ya adui zao na katika mikono ya hao wanaoutafuta uhai wao. Miili yao itakuwa chakula cha ndege wa angani na wanyama juu ya dunia.

21Kwa hiyo nitawatia Sedekia mfalme wa Yuda na viongozi wake kwenye mikono ya adui zao na kwenye mikono ya wale wanaoutafuta uhai wao na katika mikono ya majeshi ya mfalme wa Babeli ambayo yameinuka dhidi yenu.22Angalia, niko karibu kutoa amri—hili ni tangazo la Yahweh—na nitawaleta tena kwenye mji huu ili wapigane dhidi yake, na kuunguza kwa moto. Kwa maana nitaigeuza miji ya Yuda kuwa sehemu za ukiwa ambamo hapatakuwa na wakaaji.”

35

1Neno kutoka kwa Yahweh likamjia Yeremia katika siku za Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda, kusema,2“Nenda kwenye familia ya Warekabi na zungumza nao. Kisha uwalete kwenye nyumba yangu, mle ndani ya mojawapo ya vyumba, na uwape divai wanywe.”

3Hivyo nilimchukua Yaazania mwana wa Yeremia mwana wa Habasinia na ndugu zake, wanawe wote, na familia yote ya Warekabi.4Nikawapeleka wote kwenye nyumba ya Yahweh, katika vyumba vya wana wa Hanani mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu. Vyumba hivi vilikuwa karibu na chumba cha viongozi, ambacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya mwana wa Shalumu, mtunza lango.

5Kisha nikaleta mabakuli na vikombe vilivyojaa divai mbele ya Warekabi na kusema kwao, ‘Kunyweni divai.”6Lakini walisema, “hatutakunywa divai yoyote, kwa maana babu yetu, Yonadabu mwana wa Rekabu, alituamuru, Msinywe divai yoyote, ninyi wala uzao wenu, milele.7Pia, msijenge nyumba yoyote, kupanda mbegu zozote, wala kupanda shamba lolote la mizabibu; hivi siyo kwa ajili yenu. Kwa maana lazima muishi katika hema maisha yenu yote, ili kwamba muweze kuishi siku nyingi katika nchi mnayoishi kama wageni.’8Tumeitii sauti ya Yonadabu mwana wa Rekabu, babu yetu, katika yote aliyotuamuru, kutokunywa divai maisha yetu yote, sisi, wake zetu, wana wetu, na binti zetu.9Hatutajenga nyumba kwa ajili ya kuishi ndani, na hatutakuwa na shamba la mizabu, konde, wala mbegu ya kumiliki sisi.10Tumeishi katika hema na tumetii na kufanya yote aliyotuamuru Yonadabu babu yetu.11Lakini Nebukadneza mfalme wa Babeli alipoivamia nchi, tulisema, ‘Njoo, lazima twende Yerusalemu ili tupone na mkono wa Wakaldayo na majeshi ya Waaramu. ‘Kwa hiyo tunaishi Yerusalemu.”

12Kisha neno la Yahweh likaja kwa Yeremia, likisema,13“Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, anasema hivi, ‘Nenda na useme kwa wanaume wa Yuda na wakaazi wa Yeruslemu, ‘Hamtapokea maelekezo na kulisikiliza neno langu? —Hili ni tangazo la Yahweh.14Maneno ya Yonadabu mwana wa Rekabu aliyowapa wanawe kama amri, wasinywe divai yoyote, yameheshimiwa hadi leo. Wameitii amri ya babu yao. Lakini mimi, nimekuwa nikifanya matangazo kwenu bila kukoma, lakini hamnisikilizi.15Niliwatuma kwenu watumishi wangu wote, manabii, nilikuwa nawatuma bila kukoma ili waseme, ‘Kila mtu auache uovu wake na kutenda matendo mema; asiwepo mtu wa kuifuata miungu mingine tena na badala yake, rudini kwenye nchi niliyowapa ninyi na babu zenu,’ bado hamtanisikiliza wala kutega maskio yenu kwangu.16Kwa maana uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu wamezishika amri za babu yao alizowapa, lakini watu hawa hupuuza kunisikiliza.”

17Kwa hiyo Yahweh, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Angalia, Ninaleta juu ya Yuda na juu ya kila mtu anayeishi Yerusalemu, majanga yote niliyotamka dhidi yao kwa sababu niliwaambia, lakini hawakusikiliza; niliwaita, lakini hawakuitika.”

18Yeremia akasema kwa familia ya Warekabi, “Yahweh wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi: mmezisikiliza amri za Yonadabu babu yenu na kuzishika zote—mmeyatii yote aliyowaamuru kufanya—19kwa hiyo Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, ‘Siku zote kutakuwa na mtu kutoka uzao wa Yonadabu mwana wa Rekabu kwa ajili ya kunitumikia.”

36

1Ilikuja tokea katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosiah mfalme wa Yuda, kwamba neno hili lilikuja kwa Yeremiah kutoka kwa Yahweh, na alisema,2“Chukua kitabu kwa ajili yako na uandike juu yake maneno yote ambayo nimekwisha kukuambia kuhusiana na Israeli na Yuda, na kila taifa. Fanya hivi kwa kila kitu nilichokuambia tokea siku za Yosia mpaka siku ile.3Huenda watu wa Yuda watasikiliza majanga yote ambayo ninakusudia kuleta juu yao. Huenda kila mmoja ataacha njia zake mbaya, ili kwamba niweze kuwasamehe maovu yao na dhambi zao.”

4Kisha Yeremia alimwita Baruku mwana wa Neria, na Baruku aliandika kwenye kitabu, kwa imla ya Yeremia, maneno yote ya Yahweh yalizunguzwa kwake.5Kisha Yeremia alitoa amri kwa Baruku. Alisema, “Niko gerezani na siwezi kwenda kwenye nyumba ya Yahweh.6Kwa hiyo unapaswa uende na kusoma kutoka kwenye kitabu ulichoandika kwa imla yangu. Kwa siku ya kufunga, unapaswa usome maneno ya Yahweh kwenye masikio ya watu katika nyumba yake, na pia kwenye masikio ya Yuda yote waliokuja kutoka katika miji yao. Tangaza maneno haya kwao.7Huenda maombi yao ya rehema yatakuja mbele ya Yahweh. Huenda kila mtu ataacha njia mbaya, kwani gathabu na hasira ya Yahweh imetangazwa dhidi ya watu kwa ukali.”

8Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alifanya kila kitu ambacho Yeremia nabii alimwamuru yeye kufanya. Alisoma kwa sauti maneno ya Yahweh ndani mwa nyumba ya Yahweh.9Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahweh.10Baruku alisoma kwa sauti maneno ya Yeremia katika nyumba ya Yahweh, kutoka kwenye chumba cha Gamaria mwana wa Shafani mwandishi, katika ua wa juu, kwa mlango wa kuingilia wa nyumba ya Yahweh. Alifanya hivi kwa masikio ya watu wote.

11Basi Mikaya mwana wa Gemaria alisikia maneno yote ya Yahweh kwenye kitabu.12Alienda chini kwenye nyumba ya mfalme, kwenye chumba cha katibu. Tazama, maafisa wote walikuwa wamekaa hapo: Elishama mwandishi, Delaiah mwana wa Shemaiah, Elnathan mwana wa Akbori, Gemaria mwana wa Shefani, na Sedekia mwana wa Hananiah, na maafisa wote.13Kisha Mikaya alitoa taarifa ya maneno yote kwao ambayo alikuwa amesikia ambayo Baruku alisoma kwa sauti kwenye masikio ya watu.14Kwa hiyo maafisa wote walimtuma Jehudi mwana wa Nethania mwana wa Shelemia mwana wa Kushi, kwa Baruku. Jehudi alisema kwa Baruku, “Chukua kitabu katika mkono wako, kitabu ambacho ulikuwa unakisoma kwa masikio ya watu na uje.” Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alichukua kitabu katika mkono wake na alienda kwa maafisa.15Kisha walisema naye, “Kaa chini na usome haya katika masikio yetu.” Kwa hiyo Baruku akasoma kitabu.

16Ilitokea wakati waliposikia haya maneno yote, kila mtu alipatwa na hofu kwa mtu aliye karibu naye na kusema kwa Baruku, “Kwa hakika tunapaswa kutoa taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.”17Kisha walimuuliza Baruku, “Tuambie, ulipataje kuandika maneno yote haya kwa imla ya Yeremia?”

18Baruku aliwaambia, “Alitoa imla ya maneno haya yote kwangu, na nikayaandika kwa wino kwenye kitabu hiki.”

19Kisha maafisa walisema kwa Baruku, “Nenda, jifiche mwenyewe, na Yeremiah, pia. Usipatikane mtu yeyote kujua uliko.”

20Kisha walienda kwa uwanja wa mfalme na wakatoa taarifa ya maneno haya kwake. Lakini kwanza walikihifadhi kitabu kwenye chumba cha katibu Elishama.

21Basi mfalme alimtuma Yehudi kuchukua kitabu. Yehudi alikichukua toka chumba cha Elishama katibu. Kisha alikisoma kwa sauti kwa mfalme na wote maafisa walikuwa wamesimama karibu naye.22Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake.23Ilitokea wakati Yehudi aliposoma kurasa tatu au nne, mfalme angeweza kuikata kwa kisu na kuitupa kwenye moto katika mkaa mpaka kitabu chote kiliteketea.24Lakini wala mfalme wala yeyote wa mjakazi wake aliyesikia haya maneno yote aliogopa, wala hawakuchana nguo zao.25Elinathani, Delaya, na Gemaria walikuwa wamemuomba mfalme asikichome kitabu, lakini hakuwasikiliza.26Basi mfalme alimwamuru Yerameeli, ndugu, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kumfunga Baruku mwandishi na Yeremia nabii, lakini Yahweh alikuwa amewaficha.

27Kisha neno la Yahweh lilikuja kwa Yeremia baada ya mfalme kuwa amechoma kitabu na maneno ya Baruku yaliyokuwa yameandikwa kwa imla ya Yeremia, na alisema,28“Rudi, chukua kitabu kingine kwa ajili yako, na uandike maneno haya yote ambayo yalikuwa kwenye kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikichoma.29Kisha unapaswa kusema hivi kwa mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: ‘Ulichoma hicho kitabu! Na ulisema: Kwanini umeandika juu yake, “Mfalme wa Babeli hakika atakuja na kuharibu nchi hii, kwa kuwa atawaangamiza wanaume wote na wanyama ndani yake?”30Kwa hiyo Yahweh anasema hivi kuhusu wewe, Yehoyakimu mfalme wa Yuda: “Hakuna mzao wako atawahi kukaa kwenye kiti cha Daudi. Kama wewe, maiti yako itatupwa kwenye siku ya joto na usiku wa baridi.31Kwa kuwa nitakuadhibu, wazao wako, na wajakazi wako kwa maovu yenu yote. Nitaleta kwenu, kwa wakazi wote wa Yerusalemu, na kwa kila mtu Yuda majanga ambayo nimewatishia ninyi, lakini hamkuwa makini.”

32Kwa hiyo Yeremia alichukua kitabu kingine na akampa Baruku mwana wa Neria mwandishi. Baruku aliandika juu yake kwa imla ya Yeremia maneno yote ambayo yalikuwa katika kitabu kilichochomwa moto na mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda. Zaidi, maneno mengi ya kufanana yaliongezwa kwenye kitabu hiki.

37

1Sasa Sedekia mwana wa Yosia alitawala kama mfalme badala ya Yehoyakini mwana wa Yehoyakimu. Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa amemfanya Sedekia mfalme juu ya nchi ya Yuda.2Lakini Sedekia, wajakazi wake, na watu wa nchi hawakusikiliza maneno ya Yahweh ambayo alitangaza kwa mkono wa Yeremia nabii.

3Kwa hiyo Mfalme Sedekia, Yehukali mwana wa Shelemia, na Zefania mwana wa Maaseya kuhani alituma ujumbe kwa Yeremia nabii. Walisema, “Omba kwa niaba yetu kwa Yahweh Mungu wetu.”

4Sasa Yeremia alikuwa anakuja na kwenda miongoni mwa watu, kwa kuwa alikuwa bado hajawekwa ndani ya gereza.

5Jeshi la Farao lilitoka Misri, na Wakaldayo waliozingira Yerusalemu walisikia habari kuhusu wao na kuondoka Yerusalemu.

6Kisha neno la Yahweh lilikuja kwa Yeremia nabii na kusema,7“Yahweh, Mungu wa Israeli, asema hivi: Hiki ndicho utakachosema kwa mfalme wa Yuda, kwa sababu amekutuma wewe kutafuta ushauri toka kwangu, ‘Ona, jeshi la Farao, ambalo lilikuja kukusaidia, liko tayari kurudi Misri, kwenye nchi yao.8Wakaldayo watarudi. Watapigana dhidi ya mji huu, kuuteka, na kuuchoma.’

9Yahweh asema hivi: Msidaganyane kwa kusema, “Hakika Wakaldayo wanatuacha sisi,’ kwa kuwa hawatatuacha.10Hata kama mmelishinda jeshi la Wakaldayo lote ambalo linapigana nanyi ili kwamba wanaume waliojeruhiwa walibakizwa katika mahema yao, wangeweza kunyanyuka na kuchoma mji huu.”

11Basi ilikuwa wakati jeshi la Wakaldayo lilipoondoka Yerusalemu wakati jeshi la Farao lilikuwa linakuja,12kisha Yeremia alienda toka Yerusalemu kwenda nchi ya Benjamini. Alitaka kumiliki njia ya nchi huko miongoni mwa watu wake.13Kama alivyokuwa katika mlango wa Benjamini, mlinzi mkuu aliyekuwa hapo. Jina lake lilikuwa Iriya mwana wa Shelemia mwana wa Hanania. Alimshika kwa kumnyakua Yeremia nabii na kusema, “Mnatoka jangwani kwa Wakaldayo.”

14Lakini Yeremia alisema, “Hiyo si kweli. Siendi jangwani kwa Wakaldayo.” Lakini Iriya hakumsikiliza. Alimchukua Yeremia na kumleta kwa maafisa.15Maafisa walikuwa wamemkasirikia Yeremia. Walimpiga na kumweka gerezani, ambayo ilikuwa nyumba ya Yonathani mwandishi, kwa kuwa waliigeuza kuwa gereza.

16Kwa hiyo Yeremia alikuwa amewekwa kwenye kifungo cha chini, ambako alikuwa huko kwa siku nyingi.17Kisha mfalme Sedekia alimtuma mtu mmoja aliyemleta kwenye ikulu. Kwenye nyumba yake, mfalme alimuuliza binafsi, “Kuna neno: Utatiwa kwenye mkono wa mfalme wa Babeli.”

18Kisha Yeremia alisema kwa mfalme Sedekia, “Kwa namna gani nime kutenda dhambi, mjakazi wako, au watu hawa kwamba umeniweka mimi kwenye gereza?19Wako wapi nabii wako, wale waliotabiri kwa ajili yako na kusema mfalme wa Babeli hatakuja dhidi yako au dhidi ya nchi hii?20Lakini sasa sikiliza, bwana wangu mfalme! Acha ombi langu liwe mbele yako. Usinirudishe mimi kwenye nyumba ya Yonathani mwandishi, au nitakufa huko.”

21Kwa hiyo mfalme Sedekia alitoa amri. Wajakazi wake walimwekea mipaka Yeremia katika uwanja wa walinzi. Alipewa mkate kila siku kutoka mtaa wa waokaji mkate, mpaka mkate wote mjini uliisha. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa walinzi.

38

1Shefatia mwana wa Matani, Gedalia mwana wa Pashuri, na Pashuri mwana wa Malkiya alisikia maneno ambayo Yeremia alikuwa akitangaza kwa watu wote. Alikuwa akisema,2“Yahweh asema hivi: Yeyote anayeishi kwenye mji huu atauwawa kwa upanga, njaa, na pigo. Lakini yeyote ambaye aendae kwa Wakaldayo ataishi. Atatoroka pamoja na maisha yake mwenyewe, na kuishi.3Yahweh asema hivi: Huu mji utapeanwa kwa mkono wa jeshi la mfalme wa Babeli, na ataukamata.”

4Kwa hiyo maafisa walisema kwa mfalme, “Acha mtu huyu afe, kwa kuwa kwa njia hii anadhoofisha mikono ya wanaume wapiganaji waliobaki kwenye mji huu, na mikono ya watu wote. Anatangaza maneno haya, kwa kuwa huyu mtu hafanyi kwa usalama wa watu hawa, lakini kwa majanga.”

5Basi mfalme Sedekia alisema, “Tazama, yuko mkononi mwako kwa kuwa hakuna mfalme awezaye kumpinga.”

6Kisha walimchukua Yeremia na kumtupa kwenye kisima cha Malkiya, mwana wa mfalme. Kisima kilikuwa kwenye uwanja wa mlinzi. Walimshusha Yeremia chini kwa kamba. Hapakuwa na maji kwenye kisima, lakini kulikuwa na matope, na alizama chini ya matope.

7Sasa Ebed Meleki Mkushi alikuwa mmoja wa watowashi katika nyumba ya mfalme. Alisikia kwamba walikuwa wamemuweka Yeremia kwenye kisima. Sasa mfalme alikuwa ameketi kwa mlango wa Benjamini.8Basi Ebed Meleki alienda toka nyumba ya mfalme na kuzungumza na mfalme. Alisema9“Bwana wangu mfalme, hawa wanaume wamefanya uovu kwa namna walivyomtendea Yeremia nabii. Walimtupa kwenye kisima kwa ajili ya kufa kutokana na njaa, tangu hakuna chakula zaidi katika mji.”

10Kisha mfalme alitoa amri kwa Ebed Meleki Mkushi. Alisema, “Chukua amri ya watu thelathini kutoka hapa na mmtoe Yeremia nabii nje ya kisima kabla hajafa.”

11Basi Ebed Meleki alichukua amri ya watu hao na akaenda nyumba ya mfalme, kwenye ghala la nguo chini ya nyumba. Toka hapo alichukua vitambaa na nguo zilizochanika na kuyashusha chini kwa kamba kwa Yeremia ndani ya kisima.12Ebed Meleki Mkushi alisema kwa Yeremia, “Weka matambara na nguo zilizoraruka chini ya mikono yako na juu ya kamba.” Basi Yeremia alifanya hivyo.13Kisha walimvuta Yeremia kwa kamba. Kwa njia hii walimtoa kutoka kisimani. Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi.

14Kisha Mfalme Sedekia alituma neno na kumleta Yeremia nabii kwake, kwenye lango la tatu la nyumba ya Yahweh. Mfalme alisema kwa Yeremia, “Nataka nikuulize kitu. Usinizuilie jibu mimi.”

15Yeremia alisema kwa Sedekia, “Kama nakujibu, hautaniua kwa hakika? Na kama nakupa ushauri, hautanisikiliza mimi.”

16Lakini Mfalme Sedekia aliapa kwa Yeremia kwa siri na kusema, “Kama Yahweh aishivyo, yeye aliyetufanya sisi, Sitakuua au kukuweka kwenye mkono wa watu wale wanaotafuta maisha yako.”

17Kwa hiyo Yeremia alisema kwa Sedekia, “Yahweh, Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama kwa kweli utatoka kwenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli basi utaishi, na mji huu hautachomwa. Wewe na familia yako mtaishi.18Lakini kama hautaenda kwa maafisa wa mfalme wa Babeli, basi mji huu utachukuliwa kwa mkono wa Wakaldayo. Watauchoma, na hautakwepa kutoka mkono wao.”

19Mfalme Sedekia alisema kwa Yeremia, “Lakini ninaogopa watu wa Yuda waliotoka jangwani kwenda kwa Wakaldayo, kwa sababu nitapewa katika mkono wao, kwa kunifanyia vibaya.”

20Yeremia alisema, “Hawatakutoa kwao. Tii ujumbe toka kwa Yahweh ambao ninakuambia, ili kusudi mambo yataenda vizuri kwako, na ili kusudi utaishi.21Lakini kama unakataa kutoka, hivi ndivyo Yahweh amenionesha mimi.22Tazama! Wanawake wote walioachwa kwenye nyumba yako, mfalme wa Yuda, ataletwa kwa maafisa wa mfalme wa Babeli. Hawa wanawake watasema kwako, “Umedaganywa na rafiki zako; wamekuharibu. Miguu yako sasa imezama kwenye matope, na rafiki zako watakimbia.’

23Kwa kuwa wake zenu wote na watoto wataletwa kwa Wakaldayo, na wewe mwenyewe hautatoroka nchi yao. Utashikwa na mkono wa mfalme wa Babeli, na mji huu utachomwa.”

24Kisha Sedekia alisema kwa Yeremia, “Usimjulishe yeyote kuhusu maneno haya, ili kwamba usije kufa.25Kama maafisa wanasikia kwamba nimeongea na wewe- kama wanakuja na kusema kwako, ‘Tuambie umezungumza nini pamoja na mfalme. Usitufiche, au tutakuua. Na tuambie nini mfalme amesema kwako’-26kisha unapaswa kusema nao, “Nilishawishiana pamoja na mfalme asirudi kwangu kwa nyumba ya Yonathani nitakufa humo.”

27Kisha maafisa wote walikuja kwa Yeremia na kumuuliza, basi aliwajibu kama mfalme alivyomwagiza. Basi waliacha kuongea pamoja naye, kwa sababu hawakusikia mazungumzo kati ya Yeremia na mfalme.

28Basi Yeremia alibaki kwenye uwanja wa mlinzi mpaka siku ile Yerusalemu ilipotekwa.

39

1Katika mwaka wa tisa na mwezi wa kumi wa Sedekia mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja pamoja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu na kuizingira.2Katika mwaka wa kumi na moja na mwezi wa nne wa Sedekia, siku ya tisa ya mwezi, mji uliharibiwa.3Kisha maafisa wote wa mfalme wa Babeli walikuja na kukaa kwenye lango la katikati: Nergali Sharezeri, Samgari Nebo, na Sasechimu, afisa muhimu. Nergal- Shareza alikuwa afisa mkuu na wote waliobaki maafisa wa mfalme wa Babeli.

4Ilitokea kwamba wakati Sedekia, mfalme wa Yuda, na wanaume wapiganaji wake wote walipowaona, walikimbia. Walitoka nje usiku toka kwenye mji kwa njia ya bustani ya mfalme, kupitia lango la kati la kuta mbili. Mfalme alitoka nje katika mwelekeo wa Arabah.

5Lakini jeshi la Wakaldayo walimfuatilia na kumpata Sedekia kwenye tambarare za mto Yordani karibu na Yeriko. Kisha walimshika na kumleta kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Riblah kwenye nchi ya Hamath, ambapo Nebukadneza alipitisha sentensi juu yake.6Mfalme wa Babeli aliwachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake huko Ribla. Pia aliwachinja wanaume wote wa heshima wa Yuda.7Kisha aling'oa macho ya Sedekia na kumfunga minyororo ya shaba ili kusudi kumpeleka Babeli.

8Kisha Wakaldayo walichoma nyumba ya mfalme na nyumba za watu. Pia walivunja kuta za Yerusalemu.9Nebukadneza, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliwachukua katika mateka watu wengine waliobaki katika mji. Hii ilijumuisha watu waliotoka jangwa kwenda Wakaldayo na watu wengine walioachwa katika mji.10Lakini Nebukadneza nahodha wa walinzi wa mfalme aliwaruhusu watu maskini ambayo hawakuwa na chochote wao kubaki katika chi ya Yuda. Aliwapa mashamba ya mizabibu na maeneo katika siku ile.

11Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa ametoa amri kuhusu Yeremia kwa Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme. Alikuwa amesema,12“Mchukue na umjali. Usimdhuru. Fanya kwa ajili yake chochote anachokuambia.”13Basi Nebuzaradani nahodha wa walinzi wa mfalme, Nebushazbani mkuu wa matoashi, Nergali Sharezeri afisa mkuu, na wote maafisa wa muhimu wa mfalme wa Babeli walituma watu nje.14Watu wao walimchukua Yeremia kutoka uwanja wa mlinzi na kumkabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikami mwana wa Shafani, kumchukua nyumbani, basi Yeremia alibaki miongoni mwa watu.

15Sasa neno la Yahweh lilikuwa limekuja kwa Yeremia wakati alipokuwa chini ya kifungo kwenye uwanja wa mlinzi, na alisema,16“Zungumza kwa Ebedi-Meleki Mkushi na sema, ‘Yahweh wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Ona, Nimekaribia kubeba maneno yangu dhidi ya mji huu kwa ajili ya janga na si kwa uzuri. Kwa kuwa yatakuwa kweli mbele yako katika siku hiyo.17Lakini nitakuokoa katika siku hiyo - hili ni tamko la Yahweh - na hautatiwa katika mkono wa wanaume ambao unawaogopa.18Kwa kuwa nitakuokoa hakika. Hautaanguka kwa upanga. Utatoroka pamoja na maisha yako, kwani unanitumaini - hili lilikuwa tamko la Yahweh.”

40

1Neno lilimjia Yeremia toka kwa Yahweh baada ya Nebuzaradani, kamanda wa walinzi wa mfalme, amemtuma mbali kutoka Ramah. Huko ndiko Yeremia alikuwa amechukuliwa, na huko alikuwa amefungwa kwa minyororo. Alikuwa miongoni mwa mateka wote ya Yerusalemu na Yuda ambayo walipaswa kuwa matekani Babeli.2Mlinzi mkuu alimchukua Yeremia na kusema kwake, “Yahweh Mungu wako aliamrisha maafa haya dhidi ya eneo hili.3Basi Yahweh aliileta. Alifanya kama alivyoamrisha, kwani ninyi watu mmefanya dhambi dhidi yake na hamkutii sauti yake. Hii ni sababu ya jambo hili limetokea kwenu. Lakini sasa tazama!4Nimekuacha huru leo toka kwenye minyororo iliyokuwa kwenye mikono yako. Kama ni vizuri katika macho yako kuja nami Babeli, njoo, na nitakujali. Lakini kama si vizuri katika macho yako kuja pamoja nami, basi usifanye hivyo. Tazama nchi yote mbele yako. Nenda ambapo ni pazuri na sawa katika macho yako kwenda.”5Wakati Yeremia hakujibu, Nebuzaradani alisema, “Nenda kwa Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafani, ambaye mfalme wa Babeli amemweka msimamizi wa miji ya Yuda. Baki pamoja naye miongoni mwa watu au nenda popote ni pazuri katika macho yako kwenda.” Amri wa walinzi wa mfalme alimpa chakula na zawadi, na kisha akamtuma mbali.

6Basi Yeremia alienda kwa Gedalia mwana wa Ahikam, huko Mizpah. Alibaki pamoja naye miongoni mwa watu ambao walibaki nyuma katika nchi.

7Sasa baadhi ya amri wa wanawajeshi wa Yuda ambao walikuwa bado katika uwanja- wao na watu wao - walisikia kuwa mfalme wa Babeli alimfanya Gedalia mwana wa Ahikam, liwali juu ya nchi. Pia walisikia kuwa amemweka kusimamia wanaume, wanawake, na watoto ambao walikuwa watu maskini katika nchi, wale ambao hawakuwa wamechukuliwa mateka Babeli.8Basi walienda kwa Gedalia huko Mizpa. Hawa watu walikuwa Ishmaeli mwana Nethania; Yohanani na Yonathani, wana wa Kareaa; Seraya mwana wa Tanhumethi; wana wa Efai Netofa; na Yezania mwana wa Mmaaka-wao na watu wao.9Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafan, alichukua kiapo kwao na kwa watu wao, na kusema kwao, “Usiogope kuwatumikia maafisa wa Wakaldayo. Ishi katika nchi na kumtumkia mfalme wa Babeli, na itakuwa vizuri kwenu.10Na tazama, Ninaishi Mizpa kukutana pamoja na Wakaldayo waliokuja kwetu. Basi vuna mvinyo, matunda ya kiangazi, na mafuta na viweke kwenye vyombo vyako. Uishi katika miji ambayo umechukua.”

11Kisha Wayahudi wote katika Moabu, miongoni mwa watu wa Ammoni, na katika Edomu, na katika kila nchi ilisikiwa kwamba mfalme wa Babuloni ameruhusu mabaki ya Yuda kubaki, kwamba alimteua Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani juu yao.12Basi Wayahudi wote walirudi toka kila eneo ambako walikuwa wametawanyika. Walirudi kwenye nchi ya Yuda, kwa Gedalia huko Mizpa. Walivuna mvinyo na matunda ya kiangazi kwa wingi.

13Yohanani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi katika uwanja walikuja kwa Gedalia huko Mizpa.14Walisema kwake, “Haujui kuwa Baali mfalme wa watu wa Ammoni amemtuma Ishmael mwana wa Nethania kukuua?” Lakini Gedalia mwana wa Ahikimu hakuwaamini.

15Basi Yohanani mwana wa Karea alizungumza kwa siri kwa Gedalia huko Mizpa na kusema, “Niruhusu niende kumuua Ishmael mwana wa Nethania. Hakuna atakaye nituhumu. Kwanini asikuue wewe? Kwanini kuruhusu Yuda yote ambayo imekusanywa kwako kutawanyishwa na mabaki ya Yuda kuharibiwa?”

16Lakini Gedalia mwana wa Ahikamu alisema kwa Yohanani mwana wa Karea, “Usifanye jambo hili, kwa kuwa unasema uongo kuhusu Ishmaeli.”

41

1Lakini ilitokea kwamba katika mwezi wa saba Ishmaeli mwana wa Nethania mwana wa Elishama, toka familia ya kifalme, na maafisa baadhi wa mfalme, walikuja - wanaume kumi walikuwa pamoja naye - kwa Gedalia mwana wa Ahikamu, huko Mizpa. Walikula chakula pamoja huko Mizpa.2Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania, na wanaume kumi ambao walikuwa pamoja naye waliinuka na kumvamia Gedalia mwana wa Ahikam mwana wa Shafan, kwa upanga. Ishmaeli alimuua Gedalia, ambaye mfalme wa Babeli alimweka kuwa msimamizi wa nchi.3Kisha Ishmaeli aliwauwa Wayahudi wote ambao walikuwa pamoja na Gedalia huko Mizpa na Wakaldayo wanaume wa kupigana kukutwa huko.

4Kisha ilikuwa siku ya pili baada ya kumuua Gedalia, lakini hakuna moja aliyejua.5Wanaume baadhi walikuja toka Shekemu, toka Shilo, na toka Samaria-wanaume themanini ambao walikuwa wamenyoa ndevu zao, walirarua nguo zao, na kujikata wenyewe- pamoja na chakula cha sadaka na ubani katika mikono yao kwenda kwa nyumba ya Yahweh.6Basi Ishmaeli mwana wa Nethania alienda toka Mizpa kukutana nao kama walivyoenda, wakitembea na kulia. Kisha ilitokea kwamba kama alivyokutana nao, alisema nao, “Njoo kwa Gedalia mwana wa Ahikamu!”

7Ilikuja kuwa kwamba wakati walipokuja katika mji, Ishmaeli mwana wa Nethania aliwauwa na kuwatupa kwenye shimo, yeye na wanaume ambao walikuwa pamoja naye.8Lakini palikuwa na wanaume kumi miongoni mwao ambao walisema kwa Ishmael, “Usituue, kwa kuwa kuna riziki zetu kwenye shamba: ngano na shayiri, mafuta na asali.” Kwa hiyo hakuwauwa pamoja na rafiki zao wengine.9Kisima ambacho Ishmaeli alitupa miili yote ya waliokufa ambaye yeye na Gedalia waliwapiga, kilikuwa ni kilekile ambacho mfalme Asa alichimba wakati alipokuwa akivamiwa na mfalme Baasha wa Israel. Ishmaeli mwana wa Nethania alilijaza wale ambao walikuwa wameuawa.

10Kisha Ishmaeli aliwashika watu wengine wote ambao walikuwa huko Mizpa, mabinti wa mfalme na watu wote ambao walikuwa wameachwa huko Mizpa ambayo Nebuzaradani mlinzi mkuu alikuwa amewakabidhi kwa Gedalia mwana wa Ahikamu. Basi Ishmaeli mwana wa Nethania aliwashika na kuvuka kwa watu wa Amoni.

11Lakini Yohanani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi pamoja naye walisikia madhara yote ambayo Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amefanya.12Basi waliwachukua wanaume wao na kwenda kupigana dhidi ya Ishmaeli mwana wa Nethania. Walipigana naye huko kwenye bwawa kuu la Gibeoni.13Kisha ilitokea kwamba wakati watu wote ambao walikuwa na Ishmaeli kuona Yohanani mwana wa Karea na amri wote wa jeshi ambao walikuwa pamoja naye, walikuwa na furaha.14Basi watu wote ambao Ishmael alikuwa amewashika huko Mizpa waligeuka na kwenda kwa Yohanani mwana wa Karea.15Lakini Ishmaeli mwana wa Nethania alitoroka na wanaume wanane toka kwa Yohanani. Alienda kwa watu wa Amoni.16Yohanani mwana wa Karea na amri jeshi pamoja naye walichukua toka Mizpa watu wote ambao walikuwa wameokolewa kutoka kwa Ishmaeli mwana wa Nethania. Hii ilikuwa baada ya Ishmaeli kuwa amemuuwa Gedalia mwana wa Ahikamu. Yohanani na rafiki zake walichukua wanaume shujaa, wanaume wapiganaji, wanawake na watoto, na mtoashi ambaye alikuwa ameokolewa huko Gibeoni.17Kisha walienda na kubaki kwa muda huko Geruthi Kimhamu, ambayo iko karibu Bethlehemu. Walikuwa wakienda Misri18kwa sababu ya Wakalidayo. Walikuwa wakiwaogopa kwani Ishmaeli mwana wa Nethania alikuwa amemua Gedalia mwana wa Ahikamu, ambaye mfalme wa Babeli amewekwa kwenye usimamizi wa nchi.

42

1Kisha amri wote wa jeshi na Yohanani mwana wa Karea, Jezania mwana wa Hoshaia, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa walimkaribia Yeremia nabii.2Walisema naye, “Acha maombi yetu yaje mbele yako. Omba kwa ajili yetu kwa Yahweh Mungu wako kwa ajili ya watu hawa ambao wanabaki kwani tuko wachache katika idadi, kama unavyoona.3Muulize Yahweh Mungu wako atuambia sisi njia yakuendea na nini tufanye.”

4Basi Yeremia nabii alisema nao, “Nimewasikia, Tazama, Nitaomba kwa Yahweh Mungu wenu kama mlivyoomba. Vyovyote Yahweh ananijibu, Nitawambia. Sitawaficha chochote ninyi.”

5Walisema na Yeremia, “Na Yahweh awe shahidi mkweli na mwaminifu dhidi yenu, kama hatutafanya kila kitu ambacho Yahwe Mungu wenu anatuambia kufanya.6Hata kama ni vizuri au vibaya, tutatii sauti ya Yahweh Mungu wetu, ambaye tunawatuma ninyi, ili kwamba iwe vizuri pamoja nasi wakati tunatii sauti ya Yahweh Mungu wetu.”

7Basi ilitokea kwamba baada ya siku kumi, neno la Yahweh lilikuja kwa Yeremia.8Kwa hiyo Yeremia alimwita Yohanani mwana wa Karea na amri wote jeshi pamoja naye, na watu wote kutoka mdogo kwa mkubwa.9Na alisema nao, “Yahweh, Mungu wa Israeli, ambaye umenituma mimi ili niweze kuweka maombi yako mbele zake. Yahwe asema hivi,10Kama mtarudi na kuishi katika nchi hii, basi nitawajenga na sitawararua chini; Nitapanda na sitawangoa, kwa kuwa nitageuza maafa ambayo nimeleta juu yako.11Msimuogope mfalme wa Babeli, ambaye mnamuogopa. Msimuogope-hili ni tamko la Yahweh kwani niko pamoja nanyi kuwahifadhi na kuwaokoa toka mkono wake.12Kwa kuwa nitawapa rehema. Nitakuwa na huruma juu yenu, na nitawarudisha kwenye nchi yenu.

13Lakini tudhani kusema kwamba, “Hatutakaa katika nchi hii”- kama hamtasikiliza sauti yangu, sauti ya Yahweh Mungu wenu.14Tudhani kwamba mnasema, “Hapana! Tutaenda kwenye nchi ya Misri, ambayo hatutaona vita yoyote, ambayo hatutasikia sauti ya tarumbeta, na hatutaona njaa ya chakula. Tutaishi huko.”15Sasa sikiliza neno hili la Yahweh, wewe mabaki ya Yuda. Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, ‘Kama kweli mtatoka kwenda Misri, kwenda na kuishi huko,16basi upanga ambao mnauogopa utawapita huko kwenye nchi ya Misri. Njaa ambayo mnawasi wasi nayo itawafatilia huko Misri. Na mtakufa huko.17Basi itatokea kwamba wanaume wote waliondoka kwenda Misri kuishi huko watakufa kwa upanga, njaa, au pigo. Hapatakuwa na mwathirika wao, hakuna atakayetoroka maafa ambayo nitaleta juu yao.

18Kwa kuwa Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Kama gadhabu yangu na hasira yangu imemwagwa juu ya wakazi wa Yerusalemu, kwa njia hiyo hasira yangu itamwagwa juu yenu kama mtaenda Misri. Mtakuwa sababu ya hasira na hofu, sababu la kuzungumza laana, na kitu kisichokuwa na heshima. Na hamtaona eneo hili tena.”

19Basi Yeremia alisema, “Yahweh amezungumza kuhusu ninyi - mabaki ya Yuda. Msiende Misri! Unajua kwa hakika kwamba nimekuwa shahidi dhidi yenu leo.20Kwa kuwa mmejidanganya vibaya wenyewe wakati mliponituma mimi kwenda kwa Yahweh Mungu wenu na kusema, ‘Omba kwa Yahweh Mungu wetu kwa ajili yetu. Kila kitu ambacho Yahweh Mungu wetu asema, tuambie, na tutaibeba.’21Kwa kuwa nimekwisha toa taarifa kwako leo, lakini hujasikiliza sauti ya Yahweh Mungu wenu au kwa chochote kuhusu ambacho alinituma mimi kwako.22Basi sasa, utajua kwa hakika kwamba utakufa kwa upanga, njaa, na pigo katika eneo ambalo ulitamani kwenda kuishi.”

43

1Ilitokea kwamba Yeremia alimaliza kuhubiri kwa watu wote maneno yote ya Yahweh Mungu wao kwamba Yahweh Mungu wao alimwambia kusema.2Azaria mwana wa Hoshaia, Yohanani mwana wa Karea, na watu wenye kiburi walisema kwa Yeremia, “Unasema uongo. Yahweh Mungu wetu hajakutuma wewe kusema, ‘Usiende Misri kuishi huko.’3Kwa kuwa Baruku mwana wa Neria anakuchochea dhidi yetu kututoa sisi kwenye mkono wa Wakaldayo, kwa kuwa wewe umesababisha kifo chetu na kutufanya sisi mateka huko Babeli.”

4Basi Yohanani mwana wa Karea, wakuu wa jeshi, na watu wote walikataa kusikiliza sauti ya Yahweh kuishi kwenye nchi ya Yuda.5Yohanani mwana wa Karea na amri jeshi wote waliwachukua mabaki wa Yuda ambao walikuwa wamerudi kutoka mataifa yote ambapo walikuwa wametawanyika kuishi katika nchi ya Yuda.6Waliwachukua wanaume na wanawake, watoto na mabinti wa mfalme, na kila mtu ambaye Nebuzaradani, nahodha wa walinzi wa mfalme, waliruhusu kubaki pamoja na Gedalia mwana wa Ahikamu mwana wa Shafani. Pia walimchukua Yeremia nabii na Baruku mwana wa Neria.7Walienda nchi ya Misri, kwa Tahpanhesi, kwa sababu hawakusikiliza sauti ya Yahweh.

8Basi neno la Yahweh lilikuja kwa Yeremia huko Tahpanhesi na kusema,9“Chukua mawe makubwa mkononi mwako, na, kwenye macho ya watu wa Yuda, yafiche kwenye chokaa kwenye njia ya kuingia katika nyumba ya Farao huko Tahpanhesi.10Kisha wakasema nao, “Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi, ‘Ona, nimekaribia kutuma wajumbe kumchukua Nebukadneza mfalme wa Babeli kama mtumwa wangu. Nitaweka kiti cha enzi juu ya mawe haya ambayo wewe, Yeremia, umeyazika. Nebukadneza ataweka banda lake juu yao.11Kwa kuwa atakuja na kuvamia nchi ya Misri. Yeyote aliyeandikiwa kufa atakufa. Yeyote aliyeandikiwa mateka atachukuliwa mateka. Na yeyote aliyeandikiwa kwa upanga atakufa kwa upanga.12Kisha nitawasha moto katika mahekalu ya miungu ya Misri. Nebukadneza atawachoma na kuwashika. Atasafisha nchi ya Misri kama wachungaji wanavyosafisha wanyama waharibio nguo zao. Ataenda nje kutoka eneo hilo kwa ushindi.13Atavunja nguzo za mawe huko Heliopolisi kwenye nchi ya Misri. Atachoma mahekalu ya miungu ya Misri.”

44

1Hili lilikuwa neno ambalo lilikuja kwa Yeremia kuhusu Wayahudi wote walioishi katika nchi ya Misri, wale wanaoishi Migidoli, Tahpanhesi, Memphisi, na katika nchi ya Patrosi.2“Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israel, asema hivi: Wewe mwenyewe umeyaona maafa yote niliyoleta juu ya Yerusalemu na miji yote ya Yuda. Ona, ni ukiwa leo. Hakuna yeyote anaishi mwao.3Hii ni kwa sababu ya mambo maovu waliyofanya kunikosea mimi kwa kwenda kuchoma ubani na kuabudu miungu mingine. Hawa walikuwa miungu ambao wala wao wenyewe, wala ninyi, wala mababu zenu walijua.4Basi nirudie kuwatuma watumwa wangu wote manabii kwao. Niliwatuma wao kusema, ‘Acha kufanya vitu hivi machukizo ambayo nachukia.5Lakini hawakunisikiliza. Walikataa kuwa makini au kuyaacha maovu kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine.6Basi hasira yangu na gadhabu yangu zilimwagwa na kuwasha moto kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Basi waliharibiwa na kuteketezwa, kama katika siku ya leo.”

7Basi sasa Yahweh, Mungu wa majeshi na Mungu wa Israeli, asema hivi, “Kwanini unafanya maovu makubwa dhidi yenu? Kwanini mnasababisha ninyi wenyewe kujitenga kutoka miongoni mwa Yuda - wanaume na wanawake, watoto na wanyonyao? Hakuna mabaki yenu yatabaki.8Kwa maovu yenu mmenikosea pamoja na matendo ya mikono yenu, kwa kuchoma ubani kwa miungu mingine kwenye nchi ya Misri, ambapo mmekwenda kuishi. Mmeenda huko ili kwamba mtaangamizwa, ili kwamba mtalaaniwa na mashutumu miongoni mwa mataifa yote ya duniani.9Mmesahau maovu yaliyofanywa na mababu zenu na maovu yaliyofanywa na wafalme wa Yuda na wake zao? Mmesahau uovu uliofanywa na ninyi na wake zenu katika nchi ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu?10Kwa siku hii, hawajanyenyekea bado. Hawaheshimu sheria yangu au maagizo niliyoweka mbele yao na mababu zao, wala hawatembei nazo.”

11Kwa hiyo sasa Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, “Ona, Nimekaribia kuweka uso wangu dhidi yenu kuleta maafa kwenu na kuiharibu Yuda yote.12Kwa kuwa nitachukua mabaki wa Yuda ambaye ameanza safari kwenda nchi ya Misri kuishi huko. Nitafanya hivi ili kwamba wataangamia wote katika nchi ya Misri. Wataanguka kwa upanga na njaa. Kutoka wadogo kwa wakubwa wataangamia kwa upanga na njaa. Watakufa na watakuwa sababu ya kuapa, kulaani, mashutumu, na kitu kibaya.13Kwa kuwa nitawaadhibu watu wakazi wa nchi ya Misri kama nilivyoadhibu Yerusalemu kwa upanga, njaa, na pigo.14Hakuna mkimbizi au mwathirika wa mabaki ya Yuda ambaye wataenda kuishi huko kwenye nchi ya Misri watarudi kwenye nchi ya Yuda, hata kama wanataka kurudi na kuishi huko. Hakuna kati yao atarudi, ijapokuwa wachache ambao watatoroka kutoka huko.”

15Kisha watu wote ambao walijua kwamba wake zao walikuwa wakichoma ubani kwa miungu mingine, na wanawake wote waliokuwa katika kusanyiko kuu, na watu wote ambao walikuwa wakiishi kwenye nchi ya Misri katika Pathrosi walimjibu Yeremia.16Walisema, “Kuhusu neno ambalo mmetuambia sisi kwa jina la Yahweh: Hatutakusikiliza.17Kwa hakika tutafanya mambo yote ambayo tulisema tungefanya: kuchoma ubani kwa malkia wa mbingu na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake kama sisi, mababu zetu, wafalme wetu, na viongozi wetu walivyofanya kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu. Kisha tutajazwa pamoja na chakula na tutafanikiwa, pasipo kupata maafa yoyote.18Wakati tunajiepusha kutofanya mambo haya, si kutoa sadaka ya ubani kwa Malkia wa mbinguni na si kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulikuwa wote tunaumwa umaskini na tulikuwa tunakufa kwa upanga na njaa.”

19Wanawake walisema, “Wakati tulipokuwa tunatengeneza ubani wa sadaka mbele ya Malkia wa Mbinguni na kumwaga kinywaji cha sadaka kwake, tulifanya hivi vitu pasipo waume wetu kujua.”

20Kisha Yeremia alisema kwa watu wote - kwa wanaume na wanawake, na watu wote waliomjibu yeye - alihubiri na kusema,21“Je Yahweh hakukumbuka ubani ambao mliuchoma kwenye miji ya Yuda na mitaa ya Yerusalemu - wewe na mababu zenu, wafalme wenu na viongozi, na watu wa nchi? Kwa kuwa Yahweh anakumbuka hili kwenye akili; inakuja kwenye mawazo yake.22Basi hawakuweza tena kuvumilia kwa sababu ya matendo yenu maovu, kwa sababu ya machukizo ambayo mlifanya. Basi nchi yenu imekuwa ukiwa, kutisha, na laana basi hapakuwa na mkazi tena kwa siku hii.23Kwa sababu mlichoma ubani na kufanya dhambi dhidi ya Yahweh, na kwa sababu msinge sikiliza sauti yake, sheria yake, amri zake, au maagizo ya agano lake, maafa haya dhidi yenu yemetokea kama kwa siku hii.

24Kisha Yeremia alisema kwa watu wote na wanawake wote, “Sikia neno la Yahweh, Yuda yote ambao wamo katika nchi ya Misri.25Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Wewe na wake zako wote mmesema kwa vinywa vyenu na kubeba kwa mikono yenu kile mlichosema, “Hakika tutabeba viapo ambavyo tulifanya kumwabudu Malkia wa Mbinguni, kumwaga kinywaji cha sadaka kwake.” Sasa timiza viapo vyenu, yafanyeni.”

26Basi, sikiliza neno la Yahweh, Yuda yote ambao mnaishi katika nchi ya Misri, ‘Ona, Nimeapa kwa jina langu kuu-asema Yahweh. Jina langu halitaitwa kwa vinywa vya wanaume wowote wa Yuda kwenye nchi ya Misri, wewe ambaye sasa unasema, “Kama Bwana Yahweh aishivyo.”27Ona, Ninakutazama juu yako kwa ajili ya maafa na si kwa uzuri. Kila mtu wa Yuda katika nchi ya Misri ataangamia kwa upanga na njaa mpaka wote wameishia.28Kisha waathirika wa upanga watarudi kutoka nchi ya Misri kwa nchi ya Yuda, peke idadi ndogo yao. Basi mabaki yote ya Yuda walioenda kwenye nchi ya Misri kuishi huko watajua ambao neno litakuwa kweli: yangu au yao.

29Hii itakuwa ishara kwa ajili yako - hili ni tamko la Yahweh - kwamba ninaweka dhidi yenu katika eneo hili, ili kwamba mtajua kwamba maneno yangu hakika yatawavamia pamoja na maafa.30Yahweh asema hivi, ‘Tazama, ninakaribia kumtoa Farao Hofra mfalme wa Misri kwenye mkono wa adui zake na kwenye mkono wa wale wanaotafuta kumuua. Itakuwa sawa kama wakati nilimpa Sedekia mfalme wa Yuda kwenye mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli, adui wake aliyetafuta maisha yake.

45

1Hili ni neno ambalo Yeremia nabii alimwambia Baruku mwana wa Neria. Hii ilitokea wakati alipoandika kwenye kitabu maneno haya kwa imla ya Yeremia - hii ilikuwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, na alisema,2“Yahweh, Mungu wa Israel, asema hivi kwako, Baruku:3Umesema, Ole mimi, kwa kuwa Yahwe ameongeza uchungu kwa maumivu yangu. Kuugua kwangu kumenichosha; sipati pumziko.’

4Hivi ndivyo unapaswa kusema kwake: “Yahweh asema hivi: Ona, nilichojenga, sasa ninararua chini. Nilichopanda, sasa ninang'oa. Hii ni kweli juu ya dunia.5Lakini unategemea mambo makubwa kwa ajili yako? Usitegemee hayo. Uone, maafa yanakuja kwa binadamu wote - hii ni tamko la Yahweh - lakini ninakupa maisha yangu kama nyara popote utakakoenda.”

46

1Hili ni neno la Yahweh lililomjia Yeremia nabii juu ya mataifa.

2Juu ya Misri; “Hili ni juu ya jeshi la Farao Neko, mfalme wa Misri aliyekuwako Karkemishi kando ya mto Frati. Hili ni jeshi alilolishinda Nebukadneza mfalme wa Babeli likishindwa katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda:
3Wekeni tayari ngao ndogo na kubwa, na msonge vitani.
4Watieni farasi lijamu na hatamu, na mpande juu yao, ninyi wapanda farasi. Jiwekeni mahali penu, mkiwa mmevaa kofia vichwani mwenu. Inoweni mishale yenu na kuvaa silaha zenu.
5Ninaona nini hapa? Wana uoga na wanakimbia, maana askari wao wameshindwa. Wanakimbia kwa usalama na hawaangalii nyuma. Kitisho kipo mahali pote - hili ni tamko la Yahweh -
6wepesi hawawezi kukimbia, na askari hawezi kukwepa. Wanajikwaa kaskazini na kuanguka kando ya mto Frati.
7Ni nani hawa wainukao kama mto Nili, ambao maji yao yanaruka juu na chini kama mito?
8Misri huinuka kama mto Nili, na maji yake yanaumuka juu na chini kama mito. Anasema, ‘nitapanda juu; nitaifunika nchi. Nitaiharibu miji na watu wake.
9Inukeni, farasi. Muwe na hasira, ninyi vibandawazi. Askari na waende, Kushi na Putu, watu walio na ujuzi wa ngao, na Ludimu, watu wenye ujuzi wa kupiga pinde zao.
10Siku hiyo itakuwa siku ya kisasi kwa Bwana Yahweh Mungu wa majeshi, naye atajilipizia kisasi juu ya adui zake. Upanga utararua na kujirishisha. Utakula na kujishibisha kwa damu yao. Kwa maana kutakuwa na sadaka kwa Bwana Yahweh Mungu wa majeshi katika nchi ya kaskazini kando ya mto Frati.
11Panda Gileadi ujipatie dawa, binti wa Misri uliye bikra. Haifai kwamba unaweka dawa nyingi juu yako. Hakuna uponyaji kwako.
12Mataifa wamesikia kuaibika kwako. Nchi imejawa na maombolezo yako, maana askari anajikwaa juu ya askari; na wote wawili huanguka pamoja.”

13Hili ndilo neno Yahweh alilomwambia nabii Yeremia wakati Nebukadneza mfalme wa Babeli alipokuja na kushambulia nchi ya Misri:
14Toa taarifa kwa Misri na isikiwe katika Migdoli na Memfisi. Wamesema katika Tapenesi, wekeni kituo na muwe imara, kwa maana upanga unakula wote kati yenu.
15Kwa nini Apisi mungu wenu amekimbia? Kwa nini ng'ombe dume mungu wenu hakuweza kusimama? Yahweh amemwangusha chini.
16Ameongeza idadi ya waliojikwaa. Kila askari anaanguka kinyume cha anayefuata. Wanasema, “Inuka. Haya twende nyumbani. Haya na turudi kwa watu wetu, katika nchi yetu ya asili. Na tuuache upanga huu unaotuuwa.”
17Walitangaza pale, “Farao mfalme wa Misri ni kelele tu, ameuacha wasaa wake mbali.”
18Kama niishivyo - hili ni tamko la mfalme - Yahweh Mungu wa majeshi kwa jina, kuna mtu atakuja aliye kama Mlima Tabori na Mlima Karmeli kando ya bahari.
19Wekeni masanduku yenu kuyachukua uhamishoni, binti muishio Misri. Kwani Memfisi haitafaa, magofu. Hakuna atakayeishi huko.
20Misri ni mtamba mzuri sana, lakini mdudu aumaye anakuja kutoka kaskazini. Anakuja.
21Askari wake wakukodiwa ni kama dume la ng'ombe lililonona kati yake. Lakini wao pia watageuka na kukimbia. Hawatasimama pamoja, kwani siku yao ya madhara inakuja kunyume chao, wakati wa kuadhibiwa kwao.
22Misri anatoa sauti kama ya nyoka na kuondoka kwa kutambaa, maana adui yake anajiandaa kinyume chake. Wanamkabili kama mkata miti aliye na shoka.
23Wataangusha misitu - japokuwa ni mingi sana - hili ni tamko la Yahweh. Kwa maana adui watakuwa wengi kuliko nzige, wasiohesabika.
24Binti Misri ataaibishwa. Atawekwa mkononi mwa watu kutoka kaskazini.”

25Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema, “Tazama, niko karibu kumwadhibu Amoni wa Thebesi, Farao, Misri na miungu yake, Farao mfalme wake, na wote wanaomtumaini.26Nitawaweka katika mkono wa wanaoyaona maisha yao, na katika mkono wa Nebukadneza mfalme wa Babeli na watumishi wake. Kisha baada ya haya Misri itakaliwa kama mwanzo - asema Yahweh.”
27Lakini, wewe Yakobo mtumishi wangu, usihofu. Usifadhaike, Israeli, maana tazama, nitakurudisha kutoka mbali, na uzao wako kutoka nchi ya mateka. Kisha Yakobo atarudi, tafuta amani, na kuwa salama, na hapata kuwa na wa kumwogovya.
28Wewe, mtumishi wangu Yakobo, usiogope - asema Yahweh - kwa maana nipo nawe, hivyo nitaleta maangamizi makamilifu dhidi ya mataifa yote nilikokupeleka. Lakini sitakuharibu kabisa. Hata hivyo nitakuadhibu kwa haki na hakika sitakuacha bila adhabu.”

47

1Hili ni neno la Yahweh lililokuja kwa Yeremia nabii juu ya Wafilisiti. Neno hili lilimjia kabla Farao hajaishambulia Gaza.

2“Yahweh asema hivi: Tazama, mafuriko ya maji yanainuka huko kaskazini. Yatakuwa kama mto uliofurika! Kisha yataigharikisha nchi na kila kitu ndani yake, miji yake na watu wakaao ndani yake! Kila mtu atapiga kelele ya kuomba msaada, na wakaaji wote wa nchi wataomboleza.
3Kwa sauti ya kukanyaga kwa kwato za farasi wao wenye nguvu, kwa mungurumo wa vibanda wazi vyao na kelele za magurudumu yao, wazazi hawatawasaidia watoto wao kwa sababu ya udhaifu wao.
4Kwa maana siku inakuja itakayowaacha ukiwa Wafilisiti wote, kumwondoa kila mtu aliyesalia anayetaka kuwasaidia. Kwa maana Yahweh anawaangamiza Wafilisiti, waliosalia katika kisiwa cha Kaftori.
5Maombolezo yatakuja juu ya Gaza. Hata kwa Ashikeloni, watu waliosalia bondeni watakuwa kimya. Ni kwa muda gani mtajiondoa katika maombolezo?
6Ole, upanga wa Yahweh! Itachukua muda gani hata unyamaze? Rudini alani mwenu! Acha na unyamaze.
7Wawezaje kuwa kimya, maana Yahweh amekuagiza. Amekuamuru kumpiga Ashikeloni na dhidi ya nchi ya pwani ya bahari.

48

1Juu ya Moabu, Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, “Ole kwa Nebo, kwani umekuwa ukiwa. Kiriathaimu umetekwa na kuaibishwa. Ngome zake zimeangushwa na kuaibishwa.

2Heshima ya Moabu haipo tena. Adui zake katika Heshboni walipanga njama za kumwangamiza. Walisema, ‘Njoni tumwangamize kama taifa. Madmena pia itaangamizwa - upanga utakutangulia.’
3Sikilizeni! Sauti ya mvumo inakuja kutoka Horonaimu.
4Moabu ameangamizwa. Vilio vya watoto wake vinasikika.
5Wanapanda kilima cha Luhithi wakilia, njia yote kuelekea Horonaimu, vilio vinasikika kutokana na maangamizi.
6Kimbieni! Okoeni maisha yenu kama kichaka cha mreteni katika nyika.
7Maana kwa sababu ya tumaini lenu katika matendo na utajiri wenu, ninyi pia mtatekwa. Kisha Kemoshi atachukuliwa matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
8Maana mharibu atafika kila mji; hakuna mji utakaookoka. Hivyo bonde litaangamia na tambarare itateketezwa, kama alivyosema Yahweh.
9Mpeni Moabu mabawa, maana ni lazima aruke mbali bila shaka. Miji yake itakuwa magofu, pasipo na mtu wa kuishi humo.
10Na alaaniwe kila aliye mvivu katika kufanya kazi ya Yahweh! Na alaaniwe kila auzuiaye upanga wake usimwage damu!
11Moabu amekuwa akijisikia salama tangu alipokuwa kijana. Yeye ni kama mvinyo wake ambao haujamiminwa kutoka mtungi kwenda mtungi mwingine. Hajaenda matekani. Hivyo radha yake ni njema kama mwanzo; radha yake haibadiliki.
12Hivyo tazama, siku zinakuja - asema Yahweh - nitakapompelekea watakao mchovya na kumwaga mitungi yake yote na kupasua mitungi yake.
13Kisha Moabu atamwaibikia Kemoshi kama ambavyo nyumba ya Israeli ilivyoiabikia Betheli, tumaini lao.
14Utawezaje kusema, ‘Tu askari, wapiganaji wenye nguvu’?
15Moabu itaangamizwa na miji yake kushambuliwa. Kwa maana vijana wake wazuri wameshuka katika eneo la machinjo. Hili ni tamko la mfalme! Yahweh Mungu wa majeshi ndilo jina lake.
16Maangazizo ya Moabu yanakaribia; maafa yanaharakisha.
17Ninyi nyote mlio karibu na Moabu, ombolezeni. Nanyi mjuao fahari yake, pigeni kelele hivi, ‘Ole, fimbo yenye nguvu, fimbo yenye heshima, imevunjwa.’
18Shukeni kutoka mahali penu pa heshima na kuketi katika nchi kavu, ewe binti uishie Diboni. Maana aiangamizaye Moabu anakushambulia, atakayeziharibu ngome zako.
19Simameni njiani na kuangalia, enyi muishio katika Aroeri. Waulizeni wanaokimbia na kutoroka. Sema, ‘Nini kimetokea?’
20Moabu ameaibika, maana amevujwa. Lieni kwa sauti na uchungu; pigeni yowe kuomba msaada. Wambieni watu waliokando ya Mto Arinoni kwamba Moabu ameangamizwa.
21Basi maangamizi yamefika katika nchi ya kilima, huko Holoni, Yakza, na Mefathi,
22huko Diboni, Nebo, na Bethi Diblathaimu,
23huko Kiriatahaimu, Beth Gamul, na Bethi Meoni,
24huko Keriothi na Bozra, na katika miji yote iliyomo katika nchi ya Moabu - miji iliyoko mbali na karibu.
25Nguvu za Moabu zimekwisha; mkono wake umevunjwa - asema Yahweh.
26Mnywesheni, maana alitenda kwa kiburi kinyume changu, Yahweh. Basi Moabu anapiga makofi kwa machukizo kwa matapiko yake mwenyewe, hivyo amekuwa pia kitu cha kuchekesha.
27Maana Israeli hakuwa kitu cha kuchekesha kwako? Alionekana miongoni mwa wezi, kwamba ulitikisa kichwa chako kwake mara ulipoongea juu yake?
28Jitengeni na miji na kuweka kambi katika minuko, enyi watu wa Moabu. Kuwa kama njiwa anayeatamia juu ya mlango wa tundu katika miamba.
29Tumesikia juu ya kiburi cha Moabu - majivuno yake, maringo, kiburi, utukufu binafsi na kujiinua moyoni.
30Hili ni tamko la Yahweh - mimi mwenyewe najua maneno yake ya ukaidi, yasiyosaidia chochote, kama matendo yake.
31Hivyo nitavumisha maombolezo kwa ajili ya Moabu, na nitapiga kelele katika huzuni kwa ajili ya Moabu. Nitaomboleza kwa ajili ya watu wa Kir Hereshi.
32Nitalia zaidi kwa ajili yenu kuliko nilivyofanya kwa Yazeri, mzabibu wa Sibma! Matawi yako yalipita katika Bahari ya Chumvi na kufika hata Yazeri. Mwaribu ameshambulia matunda yenu ya kiangazi na mzabibu wenu.
33Hivyo sherehe na furaha vimeondolewa kutoka miti ya matunda na nchi ya Moabu. Nimekomesha mvinyo kutoka mashinikizo yao. Hawatakanyanga kwa kelele za furaha. Kelele yoyote haitakuwa kelele ya furaha.
34Kutoka kelele huko Heshiboni hata kufika Eleale, sauti yao inasikika hata Yahazi, kutoka Soari hata Horonaimu na Eglathi Shelishiya, hata maji ya Nimrimu yamekauka.
35Maana nitamkomesha kila mtu katika Moabu atoaye sadaka mahali pa juu na kuteketeza uvumba kwa miungu yake - asema Yahweh.
36Hivyo moyo wangu unamwombolezea Moabu kama zumari. Moyo wangu unaomboleza kama zumari kwa ajili ya watu wa Kir Heresi. Utajiri walioupata umekwisha.
37Maana kila kichwa kina upara na kila kidevu kimenyolewa. Chale zipo katika kila mkono, na nguo za magunia katika viuno vyao.
38Maombolezo yapo kila mahali, juu ya kila paa la nyumba ya Moabu na katika masoko ya Moabu. Kwa maana nimeivunja Moabu kama chungu kisichotakiwa tena - asema Yahweh.
39Jinsi gani imeharibiwa! Jinsi wanavyopiga kelele katika maombolezo yao! Moabu ameigeuza kwa aibu! Hivyo Moabu atakuwa kitu cha kuchekwa na kitisho kwa wote wanaomzunguka.”

40Maana Yahweh asema hivi, “Tazama, adui atakuja akiruka kama tai, akieneza mabawa yake juu ya Moabu.
41Keriothi umetekwa, na ngome zake zimekamatwa. Maana siku hiyo moyo ya askari wa Moabu itakuwa kama mioyo ya wanawake katika uchungu wa kujifungua.
42Hivyo Moabu utaharibiwa kama watu, kwa kuwa walijivuna kinyume changu, Yahweh.
43Hofu na shimo, na mtego vinakujia, watu wa Moabu - asema Yahwe.
44Kila akimbiaye kwa sababu ya hofu ataanguka shimoni, na kila atokaye shimoni atanaswa na mtego, maana nitayaleta haya juu yao katika mwaka wa kisasi changu dhidi yao - asema Yahweh.
45Wakimbiao watasimama katika kivuli cha Heshboni bila nguvu, maana moto utatoka Heshboni, miale kutoka katikati ya Sihoni. Utateketeza paji la uso wa Moabu na juu ya vichwa vya watu wenye majivuno.
46Ole wako, Moabu! Watu wa Kemoshi wameangamizwa, Kwa maana wana wako wamechukuliwa kama mateka na binti zako matekani.
47Lakini nitazirejesha siku njema za Moabu katika siku zijazo - asema Yahweh.” Hukumu ya Moabu inaishia hapa.

49

1Juu ya watu wa Amoni, Yahweh asema hivi, “Je Israeli hana watoto? Je hakuna mtu wa kurithi chochote katika Israeli? Kwa nini Moleki aikalie Gadi, na watu wake kukaa katika miji yake?

2Hivyo tazama, siku zinakuja - asema Yahweh - nitakapo sikizisha ishara ya vita juu ya Raba miongoni mwa watu wa Amoni, hivyo itakuwa rundo lililoachwa na binti zake watawasha moto. Maana Israeli atawamiliki wanaommiliki,” asema Yahweh.
3Piga kelele kwa maombolezo, Heshboni, maana Ai utaangamizwa! Piga kelele, Binti za Raba! Vaeni nguo za magunia. Ombolezeni na kukimbia kwa kuchanganyikiwa, maana Moleki anakwenda matekani, pamoja na makuhani na viongozi wake.
4Kwa nini mnajivunia nguvu zenu? Nguvu zenu zitakwisha, binti wasioamini, ninyi mnaotumaini utajiri wenu. Mwasema, “Nani atakayekuja kinyume changu?’
5Tazama, nitaleta kitisho juu yenu - hili ni tamko la Yahweh, Bwana Mungu wa majeshi - kitisho hiki kitatoka kwao wote wanaowazunguka. Kila mmoja wenu atatawanyika mbele yake. Hakutakuwa na wa kuwakusanya wanaotawanyika.
6Lakini baada ya haya nitarejesha mema ya watu wa Amoni - hili ni tamko la Yahweh.”

7Juu ya Edomu, Yahweh wa majeshi asema hivi, Je hakuna tena hekima katika Temani? Je ushauri mwema umepotea kutoka kwa wenye ufahamu? Je hekima yao imeharibika?
8Kimbieni! Rudini nyuma! Bakini katika mashimo katika ardhi, wenyeji wa Dedani. Maana naleta maafa ya Esau juu yake wakati ninaomwadhibu.
9Ikiwa wavunaji wa zabibu walikuja kwako, je wasinge acha kidogo? Ikiwa wezi walikuja usiku, je wasingeiba kiasi walichotaka?
10Lakini nimempiga Esau kwa ukiwa. Nimefunua maficho yao. Hivyo hataweza kujificha mwenyewe. Watoto wake, ndugu zake, na jirani zake wameharibiwa, wamepotea.
11Acha nyuma yatima wako. Nitachukua uhai wao, na wajane wako wanaweza kuniamini.”

12Maana Yahweh asema hivi, “Tazama, wasiostahili ni lazima wanywe sehemu ya kikombe. Je mnadhani mtaachwa bila kuadhibiwa? Hapana, maana hakika mtakunywa.13Maana nimekwisha apa kwangu mimi mwenyewe - asema Yahweh - Hiyo Bozra itakuwa hofu, aibu, magofu, na kitu cha laana. Miji yake yote itakuwa magofu daima.

14Nimesikia habari kutoka kwa Yahweh, na mjumbe ametumwa katika mataifa, ‘Kusanyikeni na kumpiga. Jiandaeni kwa vita.’

15“Maana tazama, nimekufanya kuwa mdogo kulinganisha na mataifa mengine, yenye kudharauliwa na watu.
16Na kwa hofu yenu, kiburi cha moyo wako kimekudanganya, wakaaji wa maeneo ya mwinuko, ninyi mliomiliki vilele vya vilima ili mfanye viota vyenu kama tai. Nitawashusha kutoka huko - asema Yahweh.
17Edomu atakuwa kitisho kwa kila aipitaye. Kila mtu atatetemeka na kutoa sauti kwa sababu ya maafa yake.
18Kama maangamizi ya Sodoma na Gomora na jirani zake,” asema Yahweh, “hakuna atakayeishi pale; hakuna mtu atakayekaa huko.
19Tazama, nitapanda kama simba kutoka katika misitu ya Yordani hata eneo la malisho mabichi. Maana nitaharakisha kumfanya Edomu kumkimbia, nami nitamweka mwingine atakayekuwa amechaguliwa kwa usimamizi huo. Maana ni nani aliyekama mimi, ni nani atakayeniagiza kuja? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
20Hivyo sikiliza mipango ambayo Yahweh ameamua dhidi ya Edomu, mipango aliyoifanya kinyume cha wakaao Temani. Bila shaka wataondolewa, hata kundi ndogo kuliko yote. Nchi yao yenye malisho yao mabichi itageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
21Kwa kishindo cha kuanguka kwao nchi hutikisika. Sauti ya milio ya kukata tamaa inasikika katika Bahari ya Shamu.
22Tazama, mtu fulani atapiga kama tai, na kushuka chini kwa kasi na kueneza mabawa yake juu ya Bozra. Kisha katika siku hiyo, mioyo ya askari wa Edomu itakuwa kama moyo wa mwanamke katika kuzaa.”

23Juu ya Dameski: “Hamathi na Arpadi zitaaibika, maana wamesikia habari ya madhara. Wanayeyuka! Wamesumbuka kama bahari, isiyotulia.
24Dameski umekuwa dhaifu sana. Unageuka kukimbia; hofu imeushika, Mahangaiko na maumivu yameupata, kama uchungu wa mwanamke ajifunguaye.
25Watu wake wanasema, “Umekuwaje mji maarufu, mji ambao nimeufurahia, kabla haujaachwa?
26Kwa hiyo vijana wake wataanguka katika mitaa yake na askari wake wote watateketea siku hiyo - hili ni tamko la Yahweh Mungu wa majeshi.”
27“Maana nitawasha moto katika kuta za Dameski, nami nitazivunja ngome za Beni Hadadi.”

28Juu ya Kedari na falme za Hazori, Yahweh amwambia hivi Nebukadneza (Basi Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuwa akienda kuyashambulia maeneo haya): “Inuka na uipige Kedari na kuwaharibu wale watu wa mashariki.
29Jeshi lake litachukua hema zao na makundi yao, nguzo za hema yao, na vitu vyao vyote. Watachukua ngamia wao kutoka kwa watu wa Kedari na kuwaambia, ‘Hofu ipo pande zote!”
30Kimbia, Tangatanga mbali! Kaa katika mahandaki ardhini, mkaao Hazori - asema Yahweh - maana Nebukadneza mfalme wa Babeli amepanga mpango kinyume chenu. Kimbieni! Geukeni!
31Simama! Lishambulie taifa lililokatika amani, waishio salama,” asema Yahweh. Hawana malango wala nguzo ndani yao, na watu wake wanakaa wenyewe.
32Maana farasi wao watakuwa mateka, na wingi wa mali zao utakuwa mateka wa vita. Kisha nitawatawanya katika kila upepo wanaonyoa pembe za nywele zao, nami nitaleta madhara juu yao kutoka kila upande - hili ni tamko la Yahweh.
33Hazori utakuwa makao ya mbweha, nchi isiyofaa daima. Hakuna atakayeishi huko; hakuna mwanadamu atakayekaa huko.”

34Hili ni neno la Yahweh lililomjia Yeremia nabii kuhusu Elamu. Ilikuwa wakati wa mwanzo wa kutawala kwake Sedekia mfalme wa Yuda, naye akasema,

35“Yahweh Mungu wa majeshi asema hivi: Tazama, ninakaribia kumvunja mpiga upinde wa Elamu, sehemu kuu ya nguvu zao.
36Maana nitaleta pepo nne kutoka katika pande nne za mbingu, nami nitawatawanya watu wa Elamu katika pepo hizo zote. Hakutakuwa na taifa ambalo kwalo waliotawanywa kutoka Elamu hawatakwenda.
37Hivyo nitawavunjavunja Elamu mbele ya adui zao na mbele ya watafutao uhai wao. Maana nitaleta maangamizo dhidi yao, hasira ya gadhabu yangu - hili ni tamko la Yahweh - nami nitapeleka upanga nyuma yao hata nitakapowafuta wote.
38Kisha nitaweka kiti changu cha enzi huko Elamu na kumwangamiza mfalme na viongozi wao kutoka huko - asema Yahweh -
39na itakuwa siku zijazo kwamba nitarejesha mema ya Elamu - asema Yahweh.”

50

1Hili ni neno alilolisema Yahweh juu ya Babeli, nchi ya Wakaldayo, kwa mkono wa Yeremia nabii,

2“Wajulishe mataifa ili wasikie. Toa ishara ili wasikie. Usiiache. Sema, ‘Babeli imetwaliwa. Beli ameaibika. Merodaki amefadhaika. Sanamu zake zimeaibishwa; vinyago vyake vimefadhaika
3Taifa kutoka kaskazini litainuka kinyume chake, ili kuifanya nchi yake ukiwa. Hakuna hata mmoja, awe mtu au mnyama, atakayeishi ndani yake. Wataondoka.
4Katika siku hizo na wakati huo - hili ni tamko la Yahweh - watu wa Israeli na watu wa Yuda watakusanyika ili kwenda kwa kulia na kumtafuta Yahweh Mungu wao.
5Watauliza njia ya kwenda Sayuni nao watakwenda huko, wakisema, tutakwenda wenyewe ili kuungana na Yahweh katika agano la milele lisilosahaulikal
6Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea. Wachungaji wao wamewapoteza milimani; wamewageuza kutoka mlima hata mlima. Walikwenda, wakasahau mahali walipokuwa wanaishi.
7Kila awaendeaye anawararua. Washitaki wao walisema, ‘Hatuna hatia, kwa sababu walimtenda dhambi Yahwe, nyumbani kwao halisi - Yahweh, tumaini la mababu zao.’
8Tokeni kati ya Babeli; tokeni katika nchi ya Wakaldayo; iweni kama wafanyavyo mabeberu mbele ya kundi lote.
9Maana tazama, ninaelekea kupeleka na kuinua kinyume cha Babeli kundi la mataifa makubwa kutoka kaskazini. Yatajipanga yenyewe kinyume chake. Kutoka hapo Babeli utatekwa. Mishale yao ni kama shujaa mzoefu asiyerudi mikono tupu.
10Kaldayo itakuwa mateka. Wote waitekao wataridhika - asema Yahweh.
11Mnafurahi, mnasherehekea kuteka urithi wangu; mnarukaruka kama ndama anayekanyaga katika malisho yake; mnalia kama farasi mwenye nguvu.
12Hivyo mama yenu ataaibika sana; aliyewazaa atafadhaika. Tazama, atakuwa wa mwisho katika mataifa, nyika, nchi kame, na jangwa.
13Kwa sababu ya hasira ya Yahweh, Babeli haitakaliwa, lakini itakuwa ukiwa mtupu. Kila apitaye kando ataogopa kwa sababu ya Babeli na atatoa sauti kwa sababu ya majeraha yake.
14Jipangeni wenyewe kumzunguka Babeli kinyume chake. Kila apindaye upinde na ampige. Msizuie mshale wenu wowote, maana amemtenda dhambi Yahweh.
15Pigeni kelele za ushindi kinyume chake ninyi nyote mmzungukao. Amesalimu mamlaka yake; minara yake imeanguka. Kuta zake zimebomolewa, maana hiki ni kisasi cha Yahweh. Jilipizeni kisasi juu yake! Mtendeeni kama alivyoyatenda mataifa mengine.
16Waharibuni wote mkulima apandaye mbegu naye atumiaye mundu wakati wa mavuno katika Babeli. Haya kila mtu na arudi kwa watu wake kutoka upanga wa mtesaji; na wakimbilie katika nchi yao wenyewe.
17Israeli ni kondoo aliyetawanywa na kupelekwa na simba mbali. Kwanza mfalme wa Ashuru alimrarua; kisha baadaye, Nebukadneza mfalme wa Babeli akavunja mifupa yake.

18Kwa hiyo Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Tazama, nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake, kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.
19Nitamrudisha Israeli katika nchi yake; atajilisha katika Karmeli na Bashani. Kisha atajishibisha katika nchi ya kilima ya Efraimu na Gileadi.
20Siku hizo na wakati huo, asema Yahweh, uovu utatafutwa katika Israeli, lakini hautaonekana. Nitauliza kuhusu dhambi za Yuda, lakini hazitaonekana, maana nitawasamehe mabaki niliowaacha.”
21Inuka dhidi ya nchi ya Merathaimu, kinyume chake nao waishio Pekodi. Wapigeni kwa makali ya upanga na mwatenge kwa ajili ya maangamizo - asema Yahweh - fanyeni kila ninachowaamru.
22Sauti ya vita na maangamizi ya kustaajabisha yamo katika nchi.
23Jinsi gani nyundo ya mataifa yote imekatiliwa mbali na kuharibiwa. Jinsi Babeli amekuwa kitu cha kushangaza kati ya mataifa.
24Nimetega mtego dhidi yako. Umenaswa, Babeli, nawe haukutambua! Ulionekana na kukamatwa, tangu uliponidhihaki, Yahweh.
25Yahweh amefungua ghala lake la silaha na anachukua silaha kwa ajili ya kutekekeleza hasira yake. Kuna kazi kwa ajili ya Yahweh Mungu wa majeshi katika nchi ya Wakaldayo.
26Mshambulie kutokea mbali. Fungua maghala yake ya chakula na kumrundika kama marundo ya nafaka. Mtenge mbali na maangamizi. Usimbakizie masalia.
27Ua madume wake wote wa ng'ombe. Washushe sehemu ya machinjio. Ole wao, maana siku yao imefika - wakati wa kuadhibiwa kwao.
28Kuna sauti ya wale wanaokimbia, walionusurika, katika nchi ya Babeli. Hawa watatoa taarifa ya kisasi cha Yahweh Mungu wetu kwa Sayuni, kisasi kwa hekalu lake.”
29Ita wapiga pinde dhidi ya Babeli - wale wote wapindao pinde zao. Piga kambi kinyume chake, na msimwache yeyote kutoroka. Mlipeni kwa kile alichofanya. Mfanyieni kwa kipimo alichotumia. Maana amemdharau Yahweh, Mtakatifu wa Israeli.
30Hivyo vijana wake wataanguka katika viwanja vya mji, na wapiganaji wake wote wataangamizwa siku hiyo - hili ni tamko la Yahweh.”
31Tazama, mimi ni kunyume chako, mwenye majivuno - hili ni tamko la Bwana Yahweh Mungu wa majeshi - maana siku yako imefika, mwenye kiburi, wakati nitakapo kuadhibu.
32Hivyo wenye kiburi watajikwaa na kuanguka. Hakuna atakaye wainua. Nitawasha moto katika miji yao; utateketeza kila kitu kati yake.

33Yahweh Mungu wa majeshi asema hivi: watu wa Israeli wamenyanyaswa, pamoja na watu wa Yuda. Wote waliowateka bado wanawashikilia; wanakataa kuwaacha waondoke.
34Yeye awaokoaye ni mwenye nguvu. Yahweh Mungu wa majeshi ni jina lake. Kwa hakika atalitetea shitaka lao, ili kuleta pumziko katika nchi, na kuwapiga wakaao Babeli.
35Upanga u juu ya Wakalidayo - asema Yahweh - na juu ya wakaao Babeli, viongozi wake, na wenye hekima wake.
36Upanga unakuja juu ya waganga, ili wajione kuwa wajinga. Upanga utakuwa juu ya askari wake, hivyo watajaa hofu.
37Upanga utakuwa juu ya farasi wake, vibandawazi vyao na watu wote waliomo Babeli, hivyo watakuwa kama wanawake. Upanga utakuwa juu ya ghala zake, nazo zitatekwa.
38Ukame unakuja juu ya maji yake, hivyo yatakauka. Maana ni nchi ya miungu wasiofaa, na wanafanya kama watu waliofanywa punguani kwa miungu yao isiyosaidia.
39Hivyo wanyama wa jangwani wakaishi na mbwea wataishi huko, na watoto wa mbuni wataishi ndani yake. Kwa muda wote, hatakaliwa tena. Kutoka kizazi hata kizazi, hatakaliwa tena na watu.
40Kama vile Mungu alivyoziangamiza Sodoma na Gomora na majirani zake - asema Yahweh - hakuna atakayeishi huko; hakuna mtu atakayekaa ndani yake.”
41“Tazama, watu wanakuja kutoka kaskazini, maana taifa kubwa na wafalme wengi wamemtikisa kutokea mbali.
42Watachukua pinde na mishale. Ni wakatili na hawana huruma. Sauti yao ni kama mngurumo wa bahari, na wamepanda farasi katika mpangilio kama watu wapiganao, dhidi yako, binti Babeli.
43Mfalme wa Babeli amesikia habari yao na mikono yake imelegea kwa huzuni. Mashaka yamemshika kama mwanamke katika utungu.
44Tazama! Anakwenda juu kama simba atokaye katika miinuko ya Yordani kuelekea katika eneo la malisho ya uvumilivu. Maana kwa haraka nitawafanya wakimbie kutoka humo, nami nitamweka mtu aliyechaguliwa kwa uangalizi wake. Maana ni nani aliye kama mimi, na ni nani atakayeniagiza? Mchungaji gani awezaye kunizuia?
45Sikilizeni mipango ambayo Yahweh ameamua juu ya Babeli, mipango aliyonayo dhidi ya nchi ya Wakaldayo. Kwa hakika wataondolewa, hata kundi ndogo zaidi. Eneo lao la malisho litageuzwa kuwa sehemu zenye magofu.
46Kwa sauti ya kuangushwa kwa Babeli nchi inatikisika, na sauti ya mateso yao inasikiwa kati ya mataifa.”

51

1Yahweh asema hivi: Tazama, ninakwenda kuleta upepo wa maangamizi dhidi ya Babeli na dhidi yao waishio ndani ya Leb Kamai.

2Nitawatuma Babeli wageni. Watamtawanya na wataifanya ukiwa nchi yake, maana watakuja kinyume chake kutoka pote siku ya madhara.
3Msiwaache wapiga mishale wakapinda pinde zao; msiwache wakavaa silaha zao. Msiwahifadhi vijana wake wa kiume; litengeni jeshi lake lote kwa maangamizi.
4Maana watu waliojeruhiwa wataanguka katika nchi ya Wakaldayo; waliouawa wataanguka katika mitaa yake.
5Maana Israeli na Yuda hawajaachwa na Mungu wao, na Yahweh Mungu wa majeshi, japokuwa nchi yao imejaa na maasi yaliyotendwa kinyume cha Mmoja aliye Mtakatifu wa Israeli.
6Kimbieni kutoka Babeli; kila mtu na ajiokoe mwenyewe. Msiangamie katika maasi yake. Maana ni wakati wa kisasi cha Yahweh. Atamlipa kwa yote.
7Babeli alikuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa Yahweh kilichoinywesha nchi yote; mataifa walikunywa mvinyo wake wakawa wendawazimu.
8Babeli utaanguka ghafla na kuangamizwa. Mwombolezeeni! Mpeni dawa kwa maumivu yake; pengine aweza kupona.
9Tulinuia kumponya Babeli, lakini hajaponywa, haya na tumwache twende, katika nchi yetu. Maana hatia yake imefika juu mbinguni; imerundikwa kufika mawinguni.
10Yahweh ametamka kwamba sisi hatuna hatia. Njooni, teseme katika Sayuni matendo ya Yahweh Mungu wetu.’
11Noweni mishale na kuchukua ngao. Yahweh anaikoroga roho ya mfalme wa Wamedi katika mpango wa kuiangamiza Babeli. Hii ni kwa kisasi cha Yahweh, kisasi kwa maangamizi ya hekalu lake.
12Inueni bendera juu ya kuta za Babeli; wekeni walinzi. Wekeni waangalizi; wekeni askari waviziao ili kumkamata kila akimbiliaye mjini, maana Yahweh atafanya kile alichokipanga. Atafanya alichokisema juu ya wakaao Babeli.
13Enyi mwishio kati ya chemchemi nyingi za maji, ninyi mlio na wingi wa hazina, mwisho wenu umefika. Upindo wa maisha yenu umepunguzwa.
14Yahweh Mungu wa majeshi ameapa kwa maisha yake, ‘nitakujaza na watu, kama pigo la nzige; watainua kelele za vita juu yako.’
15Ameifanya dunia kwa nguvu zake; akaiweka dunia mahali kwa hekima yake. Kwa ufahamu wake alizitanda mbingu.
16Anapovuma, kunakuwa na mvumo wa maji mbinguni, maana huleta umande kutoka miisho ya dunia. Hufanya radi kwa ajili ya mvua na kuituma na kuutuma upepo kutoka katika maghala ya nyumba zake.
17Kila mtu anakuwa kama mnyama asiye na maarifa; kila mfua chuma ameaibishwa na sanamu zake. Maana mwonekano wake unadanganya; maana hakuna uzima ndani yake.
18Hazifai, kazi ya wafanya dhihaka; wataangamizwa wakati wa kuadhibiwa kwao.
19Lakini Mungu, urithi wa Yakobo, siyo kama hawa, maana yeye ndiye afanyaye vitu vyote. Israeli ni kabila ya urithi wake; Yahweh Mungu wa majeshi ni jina lake.
20Wewe ni nyundo ya vita yao, silaha ya vita yangu. Kwa wewe nitawaponda mataifa na kuharibu falme.
21Kwa wewe nitaponda farasi na wawapandao; kwa wewe nitaponda vibandawazi na madereva wake.
22Kwa wewe nitawafutilia mbali mwanaume na mwanamke; kwa wewe nitafutilia mbali mzee na kijana. Kwa wewe nitafutilia mbali kijana wa kiume na wasichana bikra.
23Kwa wewe nitafutilia mbali wachungaji na makundi yao; kwa wewe nitawafutilia mbali wakulima na jozi zao za kulimia. Kwa wewe nitawafutilia mbali watawala na maafisa.

24Maana mbele yako nitamlipa Babeli na wote wakaao Ukaldayo kwa maovu yote waliyoyafanya huko Sayuni - hili ni tamko la Yahweh.
25Tazama, mimi ni kinyume chako, ewe mlima, wewe unayewaharibu watu wengine - hili ni tamko la Yahweh - kuiharibu dunia yote. Nitakupiga na mikono yangu na kuvingirisha chini kutoka ukingo wa kilima. Kisha nitakufanya mlima ulioteketezwa kabisa kwa moto.
26Hivyo hawatachukua kwako jiwe lolote ili kujengea pembe ya nyumba au msingi; kwani utakuwa ukiwa wa milele - hili ni tamko la Yahweh.
27Inua bendera ya vita juu ya nchi. Piga tarumbeta katika mataifa. Yaite mataifa yamshambuliye: Ararati, Mini na Ashkenazi. Teua majemedari wa kumshambulia; leta farasi kama nzige warukao.
28Waandae mataifa kumshambulia: wafalme wa Wamedi na magavana wao, maafisa wake wote na nchi yake yote.
29Maana nchi itatikisika na kudhoofika, kwa kuwa mipango ya Yahweh inaendelea juu ya Babeli, kuifanya nchi ya Babeli kuwa nchi isiyofaa mahali pasipo na mtu.
30Maaskari wameacha kupigana huko Babeli; wamekaa katika ngome zao. Nguvu zao zimeshindwa; wamekuwa wanawake - nyumba zake zipo motoni, makomeo ya malango yake yamevunjika.
31Mjumbe hukimbia ili amwambie mjumbe mwingine, na mtoa habari humwambia mtoa habari mwingine ili amwambie mfalme wa Babeli kwamba mji wake umetwaliwa kutoka mwisho hata mwisho.
32Hivyo vivuko katika mito vimekamatwa; adui anaunguza mafunjo ya bwawa, na wapiganaji wa Babeli wamechanganyikiwa.

33Maana Yahweh Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Binti Babeli ni kama sakafu ya kupuria. Ni muda wa kumkanyaga. Ni kitambo kidogo wakati wa mavuno utakuja juu yake.
34Yerusalemu husema, ‘Nebukadneza mfalme wa Babeli amenirarua. Amenikausha na amenifanya kuwa mtungi mtupu. Amenimeza kama joka. Alijishibisha kwa chakula changu chema. Amenitupa mbali.’
35Wenyeji wa Sayuni watasema, ‘Gasia nilizofanyiwa na mwili wangu na ziwe kwa Babeli.’ Yerusalemu atasema, ‘Damu yangu na iwe juu ya wakaao Ukaldayo.’

36Kwa hiyo Yahweh asema hivi: Tazama, nikotayari kulitetea shitaka lako na kuleta kisasi kwa ajili yako. Maana nitayakausha maji ya Babeli na kufanya vyanzo vyake kukauka.
37Babeli utakuwa rundo la magofu, pango la mbweha, sehemu itishayo, kitu cha kutoa sauti ya nyoka, pasipo na watu.
38Wababeli wataunguruma kwa pamoja kama wanasimba. Watanguruma kama watoto wa simba.
39Wanapopashwa moto kwa hasira, nitawafanyia sherehe; nitawalewesha hata wafurahi, na kisha kulala usingizi usio na mwisho hata wasiamke - hili ni tamko la Yahweh -
40Nitawapeleka chini kama wanakondoo kwa mchinjaji, kama kondoo ndume pamoja na mbuzi majike.
41Jinsi Babeli ulivyotekwa! Hivyo fahari ya dunia yote imekamatwa. Jinsi Babeli ulivyofanyika sehemu yenye magofu kati ya mataifa.
42Bahari imekuja juu ya Babeli! Amefunikwa na mawimbi yavumayo.
43Miji yake imekuwa ukiwa, sehemu kame na nyika, nchi isiyo na watu, na hakuna mtu apitaye hapo.
44Hivyo nitamwadhibu Beli huko Babeli; nitakitoa kinywani mwake alichokimeza, na mataifa hawatamminikia tena pamoja na wazao wao. Kuta za Babeli zitaanguka.
45Tokeni kati yake, enyi watu wangu. Kila mmoja wenu aokowe maisha yake kutoka katika hasira ya gadhabu yangu.
46Msiache mioyo yenu ikaogopa au kuhofu habari iliyosikiwa nchini, maana habari itakuja siku moja. Baada yake mwaka unaofuata kutakuwa na habari, na ghasia zitakuwa nchini. Mtawala atakuwa kinyume cha mtawala.
47Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja nitakapo adhibu sanamu za Babeli. Nchi yake yote itaaibika, na wote waliochinjwa wataanguka ndani yake.
48Kisha mbingu na nchi, na vyote vilivyomo ndani yake vitafurahi juu ya Babeli. Maana mhalibifu atamjia kutoka kaskazini - hili ni tamko la Yahweh.
49“Kama Babeli alivyowafanya waliouawa wa Israeli kuanguka, hivyo waliouawa katika nchi yake wataanguka katika Babeli.
50Ondokeni!, Manusura wa vita, Msikawie. Mkumbukeni Yahweh tokea mbali; Yerusalemu na ikumbukwe.
51Tumeaibika, maana tumesikia matusi; dhihaka imefunika nyuso zetu, maana wageni wameingia mahali patakatifu pa nyumba ya Yahweh.
52Kwa hiyo, tazama, siku zinakuja - hivi ndivyo asemavyo Yahweh - nitakapoziadhibu sanamu zake, na waliojeruhiwa watanung'unika kwa maumivu katika nchi yake yote.
53Maana hata kama Babeli angepanda mbinguni au kujenga ngome zake ndefu, aharibuye kutoka kwangu angemwendea - hili ni tamko la Yahweh.
54Kelele ya maangamizi ilitoka Babeli, anguko kubwa kutoka nchi ya Wakaldayo.
55Maana Yahweh anaiharibu Babeli. Anaifanya kelele ya sauti yake kuisha. Adui zake wanaunguruma kama mawimbi ya maji mengi; kelele yao imekuwa na nguvu.
56Maana aharibuye amekuja kinyume chake - kinyume cha Babeli! - Na shujaa wake wametekwa. Pinde zao zimevunjwa, maana Yahweh ni Mungu wa kisasi; atatekeleza kisasi hiki.

57Maana nitawafanya wana wafalme wake, wenye hekima wake, maofisa wake, na maaskari wake kulewa, nao watalala usingizi kwa usingizi usioisha na bila kuamka - hili ni tamko la mfalme: Yahweh Mungu wa majeshi ndilo jina lake.

58Yahweh Mungu wa majeshi asema hivi: Ukuta mnene wa Babeli utaangushwa kabisa, na malango marefu yataunguzwa. Kisha watu wanaokuja kumsaidia watafanya kazi isiyofaa; kila mataifa wanachojaribu kukifanya kwa ajili yake kitateketezwa kwa moto.”

59Hili ndilo neno Yeremia nabii alilomwamuru Seraya mwana wa Neria mwana wa Makseya alipokwenda na Sedekia mfalme wa Yuda huko Babeli katika mwaka wa nne wa kutawala kwake. Basi Seraya alikuwa afisa mwandamizi.60Maana Yeremia alikuwa ameandika katika gombo kuhusu madhara yote yaliyokuwa yakienda kutendeka juu ya Babeli - maneno haya yote yaliyokuwa yameandikwa juu ya Babeli61Yeremia akamwambia Seraya, “Unapokwenda Babeli, hakikisha unayasoma maneno haya yote.62Nawe utasema, ‘Yahweh, wewe! - Wewe mwenyewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa. Hapatakuwa na wenyeji, watu au wanyama. Patakuwa nchi isiyofaa daima.’63Kisha mtakapomaliza kusoma gombo hili, funga jiwe kubwa juu yake na ulitupe katikati ya Frati.64Sema, ‘Babeli utazama kama hivi. Hautainuka kwa sababu ya mabaya ninayoyapeleka juu yake, nao wataanguka.” Maneno ya Yeremia yanaishia hapa.

52

1Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja huko Yerusalemu. Jina la mamaye lilikuwa Hamutali; alikuwa binti Yeremia wa Libna.2Akafanya maovu machoni pa Yahwe; akafanya kila alichokifanya Yehoyakimu.3Kwa hasira ya Yahweh, matukio haya yote yalitukia Yerusalemu na Yuda, hata alipowatoa mbele yake mwenyewe. Kisha Sedekia akaasi dhidi ya mfalme wa Babeli.4Ikawa katika mwaka wa tisa wa utawala wa mfalme Sedekia, katika mwezi wa kumi, na siku ya kumi ya mwezi huo, Nebukadneza, mfalme wa Babeli, alikuja na jeshi lake lote dhidi ya Yerusalemu. Wakapiga kambi kuukabili, nao wakajenga ukuta wa kuusuria kuuzunguka.5Hivyo mji ukausuriwa mpaka mwaka wa kumi na moja wa utawala wa mfalme Sedekia.

6Katika mwezi wa nne, siku ya tisa ya mwaka huo, njaa ikawa kali sana mjini hata hakukuwa na chakula kwa watu wa nchi.7Kisha mji ukatobolewa, na wapiganaji wote wakakimbia nje ya mji wakati wa usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya kuta mbili, kwa bustani ya mfalme, japokuwa Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji. Hivyo wakaenda kwa njia ya Araba.8Lakini jeshi la Wakaldayo likamfuatia mfalme na kumpata Sedekia katika tambarare za bonde la Mto Yordani karibu na Yeriko. Jeshi lote lilikuwa limetawanyika mbali naye.9Wakamkamata mfalme na kumleta hadi kwa mfalme wa Babeli huko Ribla katika nchi ya Hamathi, alipotoa hukumu juu yake.10Mfalme wa Babeli akawachinja wana wa Sedekia mbele ya macho yake, na huko Ribla akawachinja viongozi wote wa Yuda.11Kisha akayaondoa macho ya Sedekia, akamfunga katika vifungo vya shaba, na kumleta Babeli. Mfalme wa Babeli akamweka kifungoni hata siku ya kufa kwake.

12Basi mwezi wa tano, siku ya kumi ya mwezi, ambao ulikuwa mwaka wa kumi na tisa wa utawala wa mfalme Nebukadneza, mfalme wa Babeli, Nebuzaradani akaja Yerusalemu. Alikuwa jemedari wa walinzi wa mfalme na mtumishi wa mfalme wa Babeli.13Akaiteketeza nyumba ya Yahweh, kasiri, na nyumba zote za Yerusalemu; pia kila jengo mhimu mjini alilichoma.14Kama kwa kuta za kuuzunguka Yerusalemu, jeshi lote la Wababeli lililokuwa pamoja na jemedari wa mlinzi wakaviharibu.15Kama kwa watu maskini sana, watu waliosalia walioachwa katika mji, waliokuwa wamemwendea mfalme wa Babeli, na baadhi ya watu wenye ujuzi - Nebuzaradani, jemedari wa askari walinzi, akawachukua baadhi yao uhamishoni.16Lakini Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawaacha baadhi ya maskini sana wa nchi kuitunza mizabibu na mashamba.

17Lakini kwa nguzo za shaba zilizokuwa katika nyumba ya Yahwe, mishikio na bahari ya shaba iliyokuwa katika nyumba ya Yahweh, Wakaldayo wakaivunja vipande wakaondoka navyo kurudi Babeli.18Vyungu, makoleo, kinara cha taa, mabakuri, na vitu vyote vya shaba ambavyo makuhani walikuwa wakivitumia hekaluni - Wakaldayo wakavichukua vyote.19Makalai na chetezo cha uvumba, mabakuri, vyungu, kinara cha taa, vikaango, makalai zilizotengenezwa kwa dhahabu, na zilizotengenezwa kwa dhahabu - kapteni wa mlinzi wa mfalme akazichukua pia.

20Nguzo mbili, bahari, na ng'ombe kumi na wawili wa shaba waliokuwa chini yake, vitu Selemani alivyokuwa amevifanya kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vikiwa na shaba nyingi sana isiyoweza kupimwa.21Nguzo zilikuwa na urefu wa dhiraha kumi na nane kila moja, na mstari kuzunguka kila moja wenye urefu wa dhiraha kumi na mbili. Kila moja ilikuwa na unene wa vidole vinne na tundu.22Kichwa cha shaba kilikuwa juu yake. Kichwa kilikuwa dhiraha tano urefu wake, kazi ya waya zinazokingamana na makomamanga kukizunguka. Chote kilitengenezwa kwa shaba. Na nguzo nyingine ilikuwa na makomamanga yake vilikuwa kama ya kwanza.23Hivyo kulikuwa na makomamanga tisini na sita ubavuni mwa kila kichwa, na makomamanga mia moja juu ya nyaya zilizokingamana kukizunguka.

24Jemedari wa mlinzi akamchukua Seraya mfungwa, kuhani mkuu, pamoja na Sefania, kuhani wa pili, na wale walinda lango watatu.25Kutoka mjini akamchukua mfungwa afisa aliyekuwa juu ya askari, na watu saba wa wale waliomshauri mfalme, waliokuwa wamesalia mjini. Akamchukua mfungwa afisa wa jeshi la mfalme aliyekuwa na wajibu wa kuwaingiza watu katika jeshi, pamoja na watu mashuhuri sitini kutoka katika nchi waliokuwamo mjini.26Kisha Nebuzaradani, jemedari wa mlinzi, akawachukuwa na kuwaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.27Mfalme wa Babeli akawaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Kwa njia hii, Yuda akaondoka katika nchi yake na kwenda uhamishoni.28Hawa walikuwa watu Nebukadneza aliwahamisha: katika mwaka wa saba, Wayudea 3,023.29Katika mwaka wa kumi na nane wa Nebukadneza alichukuwa 832 kutoka Yerusalemu.30Katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, jemedari wa walinzi wa mfalme, aliwahamisha Wayudea 745. Jumla ya watu walioamishwa walikuwa 4,600.

31Ikawa baadaye katika mwaka wa thelathini na saba wa kufungwa kwake Yohoyakini, mfalme wa Yuda, katika mwezi wa kumi na mbili, siku ya ishirini na tano ya mwezi, Evili Merodaki, mfalme wa Babeli akamfungua Yehoyakini mfalme wa Yuda kutoka kifungoni. Ilikuwa mwaka ambao Evili Merodaki alianza kutawala.32Akaongea naye kwa ukarimu na akampa kiti cha heshima kuliko cha wafalme wengine aliokuwa pamoja nao huko Babeli.33Evili Merodaki akaondoa mavazi ya gerezani ya Yehoyakini, na Yehoyakini akala chakula cha daima katika meza ya mfalme siku zote zilizosalia za maisha yake.34Na alipewa posho ya chakula cha kila siku kwa maisha yake yote yaliyosalia mpaka siku ya kufa kwake.

Maombolezo

1

1Mji ambao mwanzo ulikuwa na watu wengi sasa umekaa peke yake. Umekuwa kama mjane, japo alikuwa taifa kubwa. Alikuwa mtoto wa mfalme miongoni mwa mataifa, lakini sasa amelazimishwa utumwani.

2Analia na kuomboleza usiku, na machozi yake yanafunika mashavu yake. Hamna hata mpenzi wake anaye mliwaza. Marafiki wake wote wamemsaliti. Wamekuwa maadui wake.
3Baada ya umaskini na mateso, Yuda ameenda matekani. Anaishi miongoni mwa mataifa na hapati pumziko lolote. Wanao wakimbiza wamewapata katika upweke wake.
4Barabara za Sayuni zinaomboleza kwasababu hakuna anaye kuja kwenye sherehe iliyo andaliwa. Malango yake yote ni ukiwa. Makuhani wake wote wana sononeka. Mabikra wake wana huzuni na yeye mwenyewe yupo katika ugumu.
5Maadui wake wamekuwa bwana zake; maadui wake wana fanikiwa. Yahweh amemuadhibu kwa dhambi zake nyingi. Watoto wake wadogo wanaenda matekani kwa maadui zake.
6Uzuri umemwacha binti wa Sayuni. Watoto wa mfalme wamekuwa kama ayala ambaye haoni malisho, na wanaenda bila uwezo kwa wanao wakimbiza.
7Katika siku za mateso yake na kutokuwa na nyumba, Yerusalemu itakumbuka hazina zake za thamani alizo kuwa nazo awali. Wakati watu wake walipo angukia mikononi mwa adui, hakuna aliye msaidia. Maadui waliwaona na kucheka maangamizo yake.
8Yerusalemu ili tenda dhambi sana, hivyo basi, amedalillika kama kitu kichafu. Wote walio mheshimu sasa wana mdharau kwa kuwa wameona uchi wake. Anasononeka na kujaribu kugeuka pembeni.
9Amekuwa mchafu chini ya sketi yake. Hakuwaza hatima yake. Anguko lake lilikuwa baya. Hakukuwa na wakumliwaza. Alilia, “Angalia mateso yangu, Yahweh, kwa kuwa adui amekuwa mkuu sana.”
10Adui ameeka mkono wake kwenye hazina zetu za thamani. Ameona mataifa yakiingia sehemu yake takatifu, japo uliamuru wasiingie katika sehemu yako ya kukusanyikia.
11Watu wote wana sononeka wanapo tafuta mkate. Wametoa hazina zao za thamani kwa ajili ya chakula cha kurejesha uhai wao. Tazama, Yahweh, ni kumbuke mimi, kwa kuwa nimekuwa sina faida.
12Sio kitu kwako, wote mnao pita? Angalia na uone kama kuna mtu mwenye huzuni kama huzuni ninao teswa nao, tangu Yahweh amenitesa mimi katika siku ya hasira yake kali.
13Ni kutoka juu ndipo alipo tuma moto kwenye mifupa yangu na umenishinda. Ametanda nyavu kwa miguu yangu na kunigeuza. Amenifanya ukiwa na dhahifu.
14Nira ya makosa yangu imefungwa na mikono yake. Zimesokotwa na kuwekwa shingoni mwangu. Amefanya uweza wangu kushindwa. Bwana amenikabidhi mikononi mwa, na siwezi kusimama.
15Bwana ametupa pembeni wanaume wangu hodari walio niokoa. Ameitisha kusanyiko dhidi yangu kuponda wanaume wangu imara. Bwana amewakanyaga binti bikra wa Yuda kwenye chombo cha kusagia mvinyo.
16Kwa vitu hivi ninalia. Macho yangu, maji yanashuka chini ya macho yangu tangu mfariji aliye paswa kurejesha maisha yangu yuko mbali na mimi. Watoto wangu wamekuwa ukiwa kwasababu adui yangu ameshinda.
17Sayuni ametandaza mikono yake; hakuna wakuwa mliwaza. Yahweh ameamuru hao karibu na Yakobo wawemaadui wake. Yerusalemu ni kitu kichafu kwao.
18Yahweh ni mwenye haki, kwa kuwa nimeasi dhidi ya amri zake. Sikia, ninyi watu, na muone huzuni yangu. Mabikra wangu na wanaume imara wameenda matekani.
19Niliita marafiki zangu, lakini walikuwa na hila kwangu. Makuhani wangu na wazee waliangamia kwenye mji, walipo kuwa wanatafuta chakula cha kurejesha uhai wao.
20Tazama, Yahweh, kwa kuwa nipo kwenye ugumu; tumbo langu lina nguruma, moyo wangu umetibuka ndani yangu, kwa kuwa nimekuwa muasi sana. Nnje, upanga umemaliza na, ndani ya nyumba kuna mauti tu.
21Wamesikia sononeko langu, lakini hakuna wakuni liwaza. Maadui zangu wote wamesikia shida zangu na wamefurahi umenifanyia hivi. Umeleta siku uliyo ahidi; sasa acha wawe kama mimi.
22Acha uovu wote uje mbele zako. Shughulika nao kama ulivyo shughulika na mimi kwasababu ya makosa yangu yote. Masononeko yangu ni mengi na moyo umezimia.

2

1Bwana amemfunika binti wa Sayuni chini ya wingu la hasira yake. Ametupa utukufu wa Israeli chini kutoka mbinguni hadi duniani. Hajakumba stuli yake ya miguu siku ya hasira yake.

2Bwana amemeza na hajawa na huruma kwa miji yote ya Yakobo. Siku za hasira zake ameangusha miji imara ya binti wa Yuda; kwa aibu ameshusha chini ufalme na watala wake.
3Kwa hasira kali amekata kila pembe ya Israeli. Ameurudisha mkono wake kutoka kwa adui. Amechoma Yakobo kama moto mkali unao teketeza kila kitu karibu yake.
4Kama adui amepindisha upinde wake kuelekea kwetu, na wakulia wake yupo tayari kushambulia. Amewachinja wote walio kuwa wanampendeza katika hema la binti wa Sayuni; Amemwaga gadhabu yake kama moto
5Bwana amekuwa kama adui. Amemeza Israeli. Amemeza majumba yake yote. Ameharibu ngome zake. Ameongeza kilio na maombolezo kati ya mabinti wa Yuda.
6Ameshambulia hema lake la kukutania kama kajumba ka bustani. Ameharibu sehemu ya kukusanyikia. Yahweh amesababisha kukusanyika na Sabato kusahaulika Sayuni, kwa kuwa amemdharau mfalme na kuhani katika ukali wa hasira yake.
7Bwana amekataa madhabahu yake na kukana sehemu yake takatifu. Ametoa kuta za majumba mikononi mwa adui. Wamepaza sauti nyumbani mwa Yahweh, kama siku ya sherehe.
8Yahweh aliamua kuharibu ukuta wa mji wa binti wa Sayuni. Amenyoosha kamba ya kipimo na hajauzuia mkono wake kutoharibu ukuta. Amefanya minara na ukuta kuomboleza; pamoja vilipotea.
9Malango yake yameanguka chini, ameharibu na kuvunja chuma za ukuta. Mfalme wake na watoto wa mfalme wapo miongoni mwa mataifa, sheria haipo tena na manabii wake hawapati maono kutoka kwa Yahweh.
10Wazee wa binti wa Sayuni wameketi chini na ukimya. Wamerusha vumbi kichwani mwao na kuvaa magunia. Mabikra wa Yerusalemu wameinamisha vichwa vyao chini.
11Macho yangu yamekaukiwa machozi yake; tumbo langu la nguruma; sehemu zangu za ndani zimemwagika chini kwasababu ya uharibifu wa binti wa watu wangu, watoto na wachanga wamezimia mitaani mwa mji.
12Wanasema kwa mama zao, “Mbegu ziko wapi na mvinyo?” kama wanavyo zimia kama mtu aliye jeruhiwa mitaani mwa mji, maisha yao yamemwagwa kwenye kifua cha mama zao.
13Nini naeza kusema kwako, binti wa Yerusalemu? Naweza kufananisha na nini, ili ni kufariji, binti bikra wa Sayuni? Jeraha lako ni kubwa kama bahari. Nani anaweza kukuponya?
14Manabii wako wameona uongo na maono batili kwa ajili yako. Hawaja weka wazi dhambi zako kurejesha mali zako, lakini kwako wametoa matamko ya uongo na ya kupotosha.
15Wote wanao pita pembeni mwa barabara wana piga makofi kwako. Wanaguna na kutikisa vichwa vyao dhidi ya binti wa Yerusalemu na kusema, “Huu ndio mji walio uita ‘Ukamilifu wa uzuri,’ ‘Furaha ya Dunia Yote’?”
16Maadui zako wote walifungua vinywa vyao na kukudhihaki. Walizomea na kusaga meno na kusema, “Tumemmeza yeye! Hii ni siku tulio subiri! Tumeishi kuweza kuiona!”
17Yahweh amefanya alivyo panga kufanya. Ametimiza neno lake. Amekupindua bila huruma, kwa kuwa amemruhusu adui kukusherehekea; amenyanyua pembe za maadui zako.
18Mioyo yao ikamlilia Bwana, kuta za binti wa Sayuni! Fanya machozi yako kutiririka chini kama mto usiku na mchana. Usijipatie hafueni, macho yako bila hafueni.
19Nyanyuka, lia usiku, mwanzo usiku wa manane! Mwaga moyo wako kama maji mbele za uso wa Bwana. Nyoosha juu mikono yako kwa ajili ya uzima wa watoto wako wanao zimia kwa njaa kwenye njia ya kila mtaa.
20Ona, Yahweh, na ukumbuke hao ulio watendea haya. Wanawake wale tunda la uzazi wao, watoto walio wajali? Makuhani na manabii wa chinjwe sehemu takatifu ya Bwana?
21Wote wadogo kwa wakubwa wana keti kwenye udongo wa mitaa. Wanawake wangu wadogo na wanaume wangu wadogo wameanguaka kwa upanga; umewachinja pasipo kuwa hurumia.
22Umeitisha, kama ungewaita watu katika siku ya maakuli, hofu yangu kila sehemu, katika siku ya hasira ya Yahweh hakuna aliye toroka; hao nilio wajali na kuwakuza, adui wangu amewaharibu.

3

1Mimi ni mwanaume nilyeona maangaiko chini ya gongo la hasira ya Yahweh.

2Amenifukuza na kunisababisha kutembea kwenye giza kuliko kwenye nuru.
3Hakika amenigeuzia mkono wake dhidi yangu tena na tena, siku yote.
4Amefanya mwili wangu na ngozi yangu kufifia; amevunja mifupa yangu.
5Amejenga vifusi vya udogo dhidi yangu, na kunizingira na uchungu na ugumu.
6Amefanya ni ishi sehemu za giza, kama hao walio kufa zamani.
7Amejenga ukuta kunizunguka na siwezi kutoroka. Amefanya minyororo yangu mizito
8na japo nina ita na kulilia msaada, anazima maombi yangu.
9Ameziba njia yangu kwa ukuta wa mawe ya kuchonga; amefanya njia yangu mbaya.
10Yeye ni kama dubu anasubiri kunishambulia, simba katika maficho;
11amegeuza pembeni njia zangu, amenifanya ukiwa.
12Amepindisha upinde wake na kunifanya mimi kama lengo la mshale wake.
13Ametoboa maini yangu kwa mishale ya mfuko wake.
14Nilikuwa kichekesho kwa watu wangu wote, kielelezo cha dhihaka yao siku nzima.
15Amenijaza kwa uchungu na kunilazimisha kunywa maji machungu.
16Alivunja meno yangu na kokoto; amenisukuma chini kwenye fumbi.
17Nafsi yangu imenyimwa amani; nimesahau furaha ni nini.
18Hivyo na sema, “Ustahimilivu wangu umeangamia na pia tumaini langu kwa Yahweh.”
19Kumbuka mateso yangu na kuangaika kwangu, maji machungu na uchungu.
20Ninaendelea kukumbuka na nimeinama ndani yangu.
21Lakini na vuta hili akilini mwangu na hivyo nina matumaini:
22Upendo dhabiti wa Yahweh haukomi na huruma zake haziishi,
23ni mpya kila asubui; uaminifu wako ni mkubwa.
24“Yahweh ni urithi wangu,” Nilisema, hivyo nitamtumainia.
25Yahweh ni mwema kwao wanao msubiri, kwa anaye mtafuta.
26Ni vizuri kusubiri taratibu kwa wokovu wa Yahweh.
27Ni vizuri kwa mtu kubeba nira katika ujana.
28Acha aketi peke yake katika utulivu, inapo kuwa imewekwa juu yake.
29Acha aeke mdomo wake kwenye vumbi - kunaweza bado kuwa na matumaini.
30Acha atoe shavu lake kwa yeye anaye mpiga, na ajazwe tele kwa aibu.
31Kwa kuwa Bwana hatatukataa milele,
32lakini japo anatia huzuni, ata kuwa na huruma kwa kadiri ya wingi wa upendo wake dhabiti.
33Kwa kuwa haadhibu kutoka moyoni mwake au kutesa watoto wa mwanadamu.
34Kukanyaga chini ya miguu wafungwa wote wa dunia,
35kumnyima haki mtu mbele ya uwepo wa Aliye Juu,
36Kumunyima haki mtu - Bwana hataidhinisha vitu kama hivyo!
37Ni nani aliye zungumza na ikatimia, kama sio Bwana kutamka?
38Sio kutoka mdomoni mwa Aliye Juu majanga na mazuri yanakuja?
39Mtu aliye hai anawezaje kulalamika? Mtu anawezaje kulalamika kwa adhabu ya dhambi zake?
40Natujichunguze njia zetu na kuzijaribu, na tumrudie Yahweh.
41Na tunyanyue mioyo yetu na mikono yetu kwa Yahweh mbinguni:
42“Tumekosea na kuasi, na haujasamehe.
43Umejifunika na hasira na kutukimbiza, umeua na haujanusuru.
44Umejifunika na wingu ili kwamba kusiwe na ombi linaloweza kupita.
45Umetufanya kama uchafu na taka miongoni mwa mataifa.
46Maadui wetu wote wametulaani,
47wasiwasi na shimo limetujia, maafa na uharibifu.
48Macho yangu yanatiririka na miferiji ya machozi kwasababu ya watu wangu.
49Macho yangu yatatoa machozi pasipo kikomo; pasipo hafueni,
50mpaka atakapo tazama chini na Yahweh ataona kutoka mbinguni.
51Macho yangu yana ni sababishia huzuni kwasababu ya mabinti wa mji wangu.
52Nimewindwa kama ndege hao walio kuwa maadui zangu; wameniwinda pasipo sababu.
53Wamenitupa kwenye shimo na wakanitupia jiwe,
54na maji yaka mwagika juu ya kichwa changu. Nilisema, “Nimekatwa mbali!”
55Nililiita jna lako, Yahweh, kutoka kina cha shimo.
56Ulisikia sauti yangu. Ulisikia sauti yangu nilipo sema, “Usifunge sikio lako kwa kilio changu cha msaada.”
57Ulikuja karibu siku niliyo kuiita; ulisema, “Usiogope”
58Bwana, ulitetea kesi yangu, uliokoa maisha yangu!
59Yahweh, umeona mabaya waliyo ni fanyia, hukumu kesi yangu.
60Umeona matusi yao, mipango yao yote dhidi yangu -
61Umesikia dhihaka yao, Yahweh, na mipango yao kunihusu.
62Midomo ya hao wanao inuka kinyume changu, na mashtaka yao, inakuja dhidi yangu siku nzima.
63Angalia jinsi wanavyo keti na kuinuka; wana nidhihaki na nyimbo zao.
64Walipize, Yahweh, kwa kadiri ya waliyo fanya.
65Hutaacha mioyo yao bila lawama! Hukumu yako iwe juu yao!
66Una wakimbiza kwa hasira na kuwaharibu chini ya mbingu, Yahweh!

4

1Dhahabu imechakaa; jinsi gani dhahabu safi imebadilika! Mawe matakatifu yamezagaa katika kila njia ya mtaa.

2Wana wa thamani wa Sayuni walikuwa na thamani ya uzito wa dhahabu safi, lakini sasa hawana dhamani zaidi ya majagi ya udogo, kazi ya mikono ya mfinyazi!
3Hata mbwa wa mitaani wanatoa maziwa yao kuwanyonyesha watoto wao, lakini binti wa watu wangu amekuwa katili, kama mbuni katika jangwa.
4Ulimi wa mtoto mchanga anaye nyonya unagota juu mdomo wake kwa kiu; watoto wanaomba chakula, lakini hakuna kwa ajili yao.
5Wao walizoea kula chakula cha gharama sasa wana shinda njaa mitaani; wao walio lelewa kwa kuvaa nguo za zambarau, sasa wamelala katika majalala.
6Hukumu ya binti wa watu wangu ni kubwa kuliko hiyo ya Sodoma, na ilipinduliwa kwa dakika na hakuna aliye yanyua mkono kumsaidia.
7Viongozi wake walikuwa wasafi kuliko theluji, weupe kuliko maziwa; miili yao ilikuwa imara kuliko jiwe, mwili wao ulikuwa kama yakuti samawi.
8Muonekano wao umekuwa mweusi kama giza; hawatambuliki mitaani. Ngozi zao zimesinya kwenye mifupa yao; imekuwa kavu kama kuni.
9Hao walio uawa kwa upanga walikuwa na furaha zaidi kuliko hao walio kufa kwa njaa, walio potea, wakatobolewa kwa ukosefu wa mavuno shambani.
10Mikono ya wanawake wenye huruma imewachemsha watoto wao; wamekuwa chakula chao wakati ambapo binti wa watu wangu alipo kuwa akiharibiwa.
11Yahweh alionyesha gadhabu yake yote; alimwaga hasira yake kali. Aliwasha moto Sayuni uliteketeza misingi yake.
12Wafalme wa dunia hawaku amini, wala wakazi wa dunia, kwamba maadui au wapinzani waliweza kuingia malango ya Yerusalemu.
13Haya yalitokea kwasababu ya dhambi za manabii na maasi ya makuhani walio mwaga damu ya wenye haki mbele zake.
14Walitanga tanga, kwa upofu, mitaani. Walikuwa wamejitia unajisi kwa damu hiyo ambapo hakuna aliye ruhusiwa kushika nguo zao.
15“Kaa mbali! Wewe mnajisi!” Watu waliwapazia sauti. “Kaa mbali! Kaa mbali! Usiguse!” Hivyo wakatanga; watu walisema miongoni mwa mataifa, “Hawawezi kukaa hapa tena.”
16Yahweh mwenyewe akawatawanyisha; hawatazami tena. Hawa waheshimu makuhani, na hawaonyeshi upendeleo kwa wazee.
17Macho yetu yalikwama, yakitazama bure kwa msaada; kutoka minara yetu ya ulinzi tulitazama taifa lisilo weza tuokoa.
18Walifuata hatua zetu, hatukuweza kutembea mitaani mwetu. Mwisho wetu ulikuwa karibu na siku zetu zilihesabiwa, mwisho wetu ulifika.
19Walio tukimbiza walikuwa wepesi kuliko tai wa aangani. Walitukimbiza kwenye milima na kutuwinda nyikani.
20Pumzi katika pua zetu - mpakwa mafuta wa Yahweh - ndiye aliye kamatwa katika shimo; ambaye ndiye aliye semewa, “Chini ya kivuli chake tutaishi miongoni mwa mataifa.”
21Shangilia na ufurahi, binti wa Edomu, wewe unaye ishi nchi ya Uzi. Lakini kwako pia kikombe kitapitishwa; utalewa na kuvua nguo.
22Binti wa Sayuni, hukumu yako itafika mwisho, hataongeza mateka yako lakini binti wa Edomu, ata muhadhibu; ata funua dhambi zako.

5

1Kumbuka, Yahweh, yaliyo tutokea na uone aibu yetu.

2Urithi wetu umegeuzwa kwa wageni; nyumba zetu kwa wageni.
3Tumekuwa yatima, bila baba, na mama zetu ni kama wajane.
4Lazima tulipe fedha kwa maji tunayo kunywa, na tulipe fedha kupata kuni zetu.
5Hao wanakuja kwetu wamekaribia nyuma yetu; tumechoka na hatuwezi pata mapumziko.
6Tumejitoa kwa Misri na kwa Assiria tupate chakula cha kutosha.
7Baba zetu walifanya dhambi, na hawapo tena, na tumebeba dhambi zao.
8Watumwa walitutawala, na hakuna wa kutuokoa na mikono yao.
9Tunapata mkate wetu pale tunapo hatarisha maisha, kwasababu ya upanga wa nyikani.
10Ngozi zetu zimekuwa na moto kama jiko kwasababu ya joto la njaa.
11Wanawake wanabakwa Sayuni, na mabikra katika mji wa Yuda.
12Watoto wa mfalme wamenyongwa na mikono yao, na hakuna heshima inayoonyeshwa kwa wazee.
13Wanaume vijana wanalizimishwa kusaga mbegu kwa jiwe la kusagia, na wavulana wanajikwa chini ya vifurushi vya kuni.
14Wazee wameacha lango la mji, na vijana wameacha miziki.
15Furaha ya moyo imekoma na kucheza kwetu kumegeuka kilio.
16Taji limeanguka kichwani mwetu; ole wetu, kwa kuwa tumetenda dhambi!
17Kwa kuwa moyo wetu umekuwa unaumwa, na machozi yetu ya fifia, kwa vitu hivi macho yetu yanafifia
18maana Mlima Sayuni umelala ukiwa, mbwa wa mitaani wanacheza juu yake.
19Lakini wewe, Yahweh, unatawala milele, na utaketi katika kiti chako cha enzi vizazi na vizazi. Kwanini unatusahau milele?
20Kwanini unatutelekeza kwa siku nyingi?
21Turejeshe kwako, Yahweh, na sisi tutarejea. Fanya upya siku zetu kama zilivyo kuwa hapo zamani -
22vinginevyo labda uwe umetukataa na una hasira kwetu kupita kiasi.

Ezekieli

1

1Katika mwaka wa thelathini, mwezi wa nne, na siku ya tano ya mwezi, ikawa kuhusu kwamba nilikuwa nikiishi miongoni mwa wafungwa karibu na Kebari Kanali. Mbingu zilifunguka, na kuona maono ya Mungu.2Katika siku ya tano katika mwezi huo-ilikuwa mwaka wa tano wa utumwani wa Mfalme Yehoyakini-3Neno la Yahwe likamjia Ezekieli mwana wa Buzi kuhani, katika nchi ya Wakaldayo karibu na Keberi Kanali, na mkono wa Yahwe ulikuwa juu yake hapo.

4Kisha nikaona, kulikuwa na upepo wa dhoruba unakuja kutoka kaskazini; wingu kubwa pamoja na moto wa nuru ndani yake na kung'aa ukizunguka ndani yake, na moto ulikuwa na rangi ya kaharabu ndani ya hilo wingu.5Katikati kulikuwa na viumbe vinne vinavyofanana. Mwonekano wao ulikuwa hivi: walikuwa wanamfanano wa mtu,6lakini walikuwa na sura nne kila mmoja, na kila mmoja alikuwa na mabawa manne.7Miguu yao ilikuwa imenyooka, lakini nyayo za miguu yao zilikuwa kama kwato za ndama zilizokuwa zinang'aa kama shaba iliyosuguliwa.8Bado walikuwa na mikono ya binadamu chini ya mabawa yao chini kwenye pande zote nne. Kwa wote wanne, nyuso zao na mabawa vilikuwa hivi:9mabawa yao yalikuwa yameungana na kiumbe kingine, na hawakurudi walipokuwa wameenda; badala yake, kila mmoja alienda mbele.

10Mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama uso wa mwanadamu. Wanne hao walikuwa na uso wa simba kwa upande wa kuume. Hao wanne pia walikuwa na uso wa tai.11Nyuso zao zilikuwa hivyo, na mabawa yao yalikuwa yametawanyika juu, hivyo basi kila kiumbe kilikuwa na jozi ya za mabawa yaliyokuwa yameshikamana na bawa la kiumbe kingine, na pia jozi za mabawa yaliyokuwa yamefunika miili yao.12Kila mmoja alienda mbele, hivyo basi popote Roho alipowaelekeza kwamba, walienda bila kurudi.13Kama kwa mfanano wa hao viumbe hai, mwonekano wao ulikuwa ni kama kuchoma kaa la moto, kama mwonekano wa nuru; mng'ao wa moto pia ulihama karibu na miongoni mwa viumbe, na kulikuwa na nuru za radi.14Hao viumbe hai walikuwa wakienda mbio mbele na nyuma, na walikuwa na mwonekano wa radi!

15Kisha nikawatazama wale viumbe hai; kulikuwa na gurudumu moja juu ya aridhi kando ya vile viumbe hai.16Huu ndio ulikuwa mwonekano na umbo wa hizo gurudumu: kila gurudumu lilikuwa kama zabarajadi, na manne hayo yalikuwa na mfano mmoja; mwonekano wao na umbo vilikuwa kama gurudumu lililoungana na jingine.17Wakati yale magurudumu yalipokuwa yakitembea, yalienda bila kurudi kwenye mwelekeo wowote viumbe vilipokuwa vimeelekea.18Katka habari za vivimbe vilikuwa virefu, vya kutisha nayo yote manne, yote manne vivimbe vyake vimejaa macho pande zote.

19Popote vile viumbe hai vilipokuwa vikielekea, yale magurudumu yalielekea karibu nao. Wakati vile viumbe hai vilipoinuka kutoka kwenye nchi, na yale magurudumu yaliinuka pia.20Popote Roho alipokwenda, walikwenda, na yale magurudumu yaliinuka karibu nao, roho wa kiumbe hai ilikuwa magurudumu.21Popote vile viumbe vilipoelekea, magurudumu pia yalielekea huko; na wakati wale viumbe viliposimama hata hivyo, magurudumu yalisimama bado; wakati viumbe viliposimama kutoka kwenye nchi, magurudumu yalisimama karibu nao, kwa sababu yule roho wa wale viumbe alikuwa kwenye magurudumu.

22Juu ya vichwa vya wale viumbe hai kulikuwa na mfanano wa anga la kutanuka; ilikuwa inang'aa kama mfano wa barafu juu ya vichwa vyao.23Chini ya anga, kila mabawa ya kiumbe kimoja yalinyooshwa mbele na kugusana kila mabawa na kiumbe kimoja. Pia kila kiumbe hai kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika vyenyewe; kila kimoja kilikuwa na jozi moja kwa ajili ya kujifunika mwili wake mwenyewe.24Kisha nikasikia sauti ya mabawa yao. Kama mlio wa maji mengi. Kama sauti ya mwenye enzi popote walipoelekea. Kama sauti ya jeshi. Popote pale waliposimama, walishusha mabawa yao.25Sauti ikaja kutoka juu ya anga juu ya vichwa vyao popote waliposimama na kushusha mabawa yao.

26Juu ya anga juu ya vichwa vyao kulikuwa na mfanao wa kiti cha enzi ambacho kilikuwa na mwonekano wa jiwe la samawati, na juu mfano wa kiti cha enzi kilifanana kama mwonekano wa mwanadamu.27Nikaona umbo lenye mwonekano wa chuma chenye kung'aa pamoja na moto ndani yake kutoka kwenye mwonekano wa juu ya nyonga zake juu; Nikaona kutoka kwenye mwonekano wa nyonga zake upande wa chini mwonekano wa moto na mung'ao umezunguka kote.28Kama mwonekano wa upinde wa mvua kwenye mawingu katika siku ya mvua ulikuwa na mwonekano wa taa iliyowaka imeizunguka. Kulikuwa na mwonekano unaofanana na utukufu wa Yahwe. Wakati nilipouona, nilihisi kwenye uso wangu, na nikasikia sauti ikiongea.

2

1Akaniambia, “Mwana wa adamu, simama kwa miguu yako; kisha nitaongea na wewe.”2Kisha, alipokuwa akiongea na mimi, Roho akaingia ndani yangu na ikaniweka kwenye miguu yangu, na nikamsikia akiongea na mimi.

3Akanambia, “Mwana wa adamu, nakutuma kwa watu wa Israeli, kwa mataifa yanayoasi ambayo yameasi dhidi yangu-wote wao na babu zao wameasi juu yangu hata hivi leo!4Vizazi vyao vina sura za kikaidi na mioyo migumu. Nakutuma wewe kwenda kwao, na utawaambia, ‘Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’5Labda watasikia au hawatasikia. Ni nyumba za uasi, lakini angalau watajua kwamba nabii alikuwa miongoni mwao.6Wewe, mwanadamu, usiwaogope au maneno yao. Usiogope, ingawa utakuwa pamoja na mitemba na miiba na ijapokuwa unaishi na nge. Usiogope maneno yao au kuvunjika moyo kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba zenye kuasi.7Lakini utawaambia maneno yangu, labda watasikia au hapana, kwa sababu ni waasi mno.8Lakini wewe, mwanadamu, silikiliza kile nisemacho kwako. Usiwe muasi kama nyumba za uasi. Fungua mdomo wako na ule kile ninachotaka kukupa!”

9Kisha nikaona, na mkono ulikuwa umenyooshwa kwangu; ndani yake kulikuwa na hati ya kukunja.10Akaikinjua mbele yangu; ilikuwa imeandikwa pande zote mbele na nyuma, na yalikuwa yameandikwa maombolezo kwenye hiyo hati ya kukunja, na huzuni, na ole.

3

1Akaniambia, “Mwanadamu, kile ulichokipata, kula. Kula hili gombo, kisha nenda kaongee na wana wa Israeli.”2Basi nikafungua kinywa changu, na akanilisha hilo gombo.

3Akanambia, “Mwana wa adamu, lisha tumbo lako na jaza tumbo lako kwa hili gombo ambalo nimekupa!” Basi nikalila, na lilikuwa tamu kama asali kwenye mdomo wangu.

4Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, nenda kwenye nyumba ya Israeli na ongea maneno yangu kwao.5Kwa kuwa hujatumwa kwa watu wenye maneno ya kushangaza au lugha ngumu, lakini kwa nyumba ya Israeli-6sio kwa taifa lenye nguvu ya maneno ya ajabu au lugha ngumu ambao maneno yao hutaweza kuyaelewa! Kama nikikutuma kwao, watakusikiliza.7Lakini nyumba ya Israeli haitakuwa tayari kukusikiliza, kwa kuwa hawako tayari kunisikiliza mimi. Hivyo nyumba yote ya Israeli ni paji gumu na moyo mgumu.8Kumbe nimeufanya uso wako kama kaidi kama nyuso zao na paji lako kuwa gumu kama mapaji yao.9Nimekufanya paji lako kama almasi, gumu kuliko jiwe la kiberiti! Usiwaogope wala kufadhaika kwa nyuso zao, kwa kuwa ni nyumba ya uasi.”

10Kisha akanambia, “Mwana wa adamu, maneno yote niliyokutangazia-yachukue kwenye moyo wako na wasikize kwa sikio lako!11Kisha nenda kwa watumwa, kwa watu wako, na uzungumze nao. Waambie, ‘Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo; iwapo watasikia au hapana.”

12Kisha Roho akaniinua juu, na nikasikia nyuma yangu sauti yenye tetemeko la aridhi: “Ubarikiwe utukufu wa Yahwe kutoka mahali pake!”13Ilikuwa sauti ya mabawa ya viumbe hai vilipokuwa vikigusana kila kimoja, na sauti ya magurudumu ambayo yalikuwa pamoja na hivyo viumbe, na sauti ya tetemeko kubwa arithi.14Roho akaniinua juu na kunichukua, Nikaenda kwa uchungu katika hasira kali rohoni mwangu, kwa kuwa mkono wa Yahwe ulikuwa na nguvu ukigandamiza juu yangu!15Hivyo nikaenda kwa watumwa huko Tel Abibu waliokuwa wakiishi karibu na Kebari Kanali, na niliishi miongoni mwao huko kwa mda wa miaka saba, kushinda kabisa katika mshangao.

16Kisha ikatokea baada ya siku saba kwamba neno la Yahwe likanijia, likisema,17“Mwana wa adamu, nimekufanya uwe mwangalizi kwa ajili ya nyumba ya Israeli, hivyo sikiliza neno kutoka kinywani mwangu, na uwapatie onyo langu.18Nitakaposema kwa waovu, ‘Utakufa hakika’ na usimuonye au kuzungumza onyo kwa waovu kuhusu matendo yao maovu hivyo anaweza kuishi-yule muovu atakufa kwa ajili ya dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.19Lakini kama ukimuonya muovo, na asiuache uovu wake au kutoka matendo yake maovu, kisha atakufa kwa dhambi yake, lakini utaokoa maisha yako mwenyewe.

20Kama mwenye haki ataicha haki yake na kutenda yasiyohaki, na nikaweka kizuizi mbele yake, atakufa. Kwasababu hukumuonya, atakufa katika dhambi yake, na sita kumbuka matendo ya haki aliyoyafanya, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako.21Lakini kama ukimuonya mwenye mtu mwenye haki kuacha kufanya dhambi halafu akaacha kutenda dhambi, ataishi hakika tangu alipo unywa; na utakuwa umeokoa maisha yako mwenyewe.”

22Hivyo mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu huko, akanambia, “Inuka! Nenda uwandani, na nitaongea na wewe huko!”23Nikainuka na kwenda uwandani, na huko utukufu wa Yahwe ulisimama, kama utukufu ambao niliokuwa nimeuona karibu na Kebari Kanali; hivyo nikaanguka kifudifudi.

24Roho akaja kwangu na kusimama juu ya miguu yangu; akaongea na mimi, na kunambia, “Nenda na jifungie mwenyewe kwenye nyumba yako,25kwa sasa, mwana wa adamu, wataweka kamba juu yako na kukufunga ili usiweze kutoka nje miongoni mwao.26Nitaufanya ulimi wako ugandamane na paa ya mdomo wako, ili kwamba uwe kimya, na hutaweza kuwakemea, kwa kuwa ni nyumba ya waasi.27Lakini nitakapozungumza na wewe, nitafungua mdomo wako hivyo utawaambia, ‘Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’ Yeye asikiaye na asikie; yeye asiyesikia na asisikie, kwa kuwa wao ni nyumba ya kuasi!”

4

1“Lakini wewe, mwana wa adamu, chukua tofali wewe mwenyewe na uliweke mbele yako. Kisha chonga mji wa Yerusalemu juu yake.2Kisha laza kuizunguka, ngome juu yake. Anza kushambulia juu yake na weka makambi kuizunguka. Weka shambulio la ghasia kuizunguka.3Kisha chukua kwa ajili yako mwenyewe sufuria ya chuma na itumie kama ukuta wa chuma kati yako mwenyewe na mji na weka uso wako dhidi yake. Kwa kuwa utazingirwa, na utaweka ukombozi juu yake. Hii itakuwa alama kwa nyumba ya Israeli.

4Kisha, lala juu upande wako wa kushoto na weka dhambi ya nyumba ya Israeli juu yake; utazibeba dhambi zao kwa hesabu za siku ambazo ulizolala juu ya nyumba ya Israeli.5Mimi mwenyewe nakuagiza kwako siku moja kuwakilisha kila mwaka wa adhabu yao: siku 390! Katika njia hii, utachukua dhambi ya nyumba ya Israeli.

6Wakati utakapomaliza hizi siku, kisha lala chini kwa mara ya pili kwa upande wako wa kulia, kwa kuwa utabeba dhambi ya nyumba ya Yuda kwa siku arobaini. Nakuteua wewe siku moja kwa kila mwaka.7Weka uso wako chini kuelekea Yerusalemu ambayo ni chini ya ngome, na kwa mkono wako funua unabii dhidi8yake. Tazama! Naweka vifungo juu yako hivyo hutarudi kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine hadi utakapoliza siku zako za kuzingirwa kwako.

9Chukua ngano kwa ajili yako, shayiri, dengu, mtama, kusemethi; viweke kwenye chombo kimoja na tengeneza mkate kwa ajili yako kulingana na hesabu ya siku ambazo utakazo lala katika upande wako. Kwa siku 390 utakazolala.10Chakula utakachokula kitapimwa, shekeli ishirini kwa siku, na utakila kwa mda uliopangwa kila siku.11Kisha utakunywa maji, kwa kuyapima sehemu ya sita ya hini, na utayanywa kwa mda uliopangwa.12Utakila kama keki za shayiri, lakini utaioka kwenye kinyesi kikavu cha mwanadamu mbele ya macho yao!”13Kwa kuwa Yahwe asema, “Hii inamaana kwamba ule mkate ambao watu wa Israeli watakula kitakuwa kinajisi, huko miongoni mwa mataifa ambapo nitakaowafukuza.”

14Lakini nikasema, “Ee, Bwana Yahwe! Sijawahi kuwa najisi! Sijawahi kula kitu chochote ambacho kimekufa au kitu chochote kilichouawa na wanyama, kutoka mdomoni mwangu hadi sasa, wala nyama ya kunuka haijawahi kuingia kinywani mwangu!”

15Ndivyo alivvyo niambia, “Tazama! Nimekupa mbolea ya ng'ombe badala ya kinyesi cha mwanadamu ili uweze kuandaa mkate wako juu ya hayo.”

16Pia akanambia, “Mwana wa adamu! Tazama! Nalivunja gongo la mkate katika Yerusalemu, na watakula mkate ukiwa umepimwa katika wasiwasi na kunywa maji kwa kuyapima katika hofu.17Kwa sabau watapungukiwa na mkate na maji, kila mtu atafadhaishwa na ndugu yake na kumpoteza kwa sababu ya udhalimu wao.”

5

1“Kisha wewe mwana wa adamu, chukua upanga mkali kama wembe wa kinyozi kwa ajili yako mwenyewe, na pitisha hayo makali juu ya kichwa chako na ndevu zako, kisha chukua mizani za kupimia uzito na uzigawanye nywele zako.2Choma theluthi ya tatu ya hiyo kwa moto katikati ya mji wakati siku za kuzingirwa zitakapokamilika, na chukua theluthi ya nywele na uipige kwa panga na kuuzunguka mji. Kisha tawanya theluthi yake kwenye upepo, na nitasogeza panga karibu ili kufukuza watu.3Lakini chukua kiasi kidogo cha nywele na zifunge kwenye pindo za nguo yako.4Kisha chukua tena zile nyewele na zitupe katikati ya moto; na zichome kwenye moto; kutoka hapo utatoka nje kwenda nyumba zote za Israeli.”

5Bwana Yahwe asema hivi, “Hii ndio Yerusalemu katikati ya mataifa, nilipomuweka, na ambapo nilipomzunguka kwa nchi zingine.6Lakini ana udhaifu wa kukataa amri zangu zaidi kuliko mataifa yalivyo, na sheria yangu zaidi kuliko mataifa ambayo yanayomzunguka. Watu wamezikataa humuku zangu na kuacha kutembea katika sheria zangu.”

7Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, “Kwa sababu mmekuwa kikwazo kuliko mataifa ambayo yanayowazunguka na kuacha kutembea kwenye amri zangu wala kutenda kulingana na amri zangu, wala hata kutenda kulingana na amri za mataifa yanayowazunguka,”8kwa hiyo Bwana asema hivi, “Tazama! Mimi mwenyewe nitatenda juu yenu. Nitatoa hukumu kati yenu ili mataifa waone.9Nitawafanyia yale ambayo sijawahi kuyafanya na kile ambacho sijakifanya tena, kwa sababu ya matendo yenu ya kuchukiza.10Kwa hiyo baba watawala watoto kati yenu, na watoto watawala baba zao, kwa kuwa nitafanya hukumu juu yenu na kuwatawanya kila mahali wote ninyi mliobaki.11Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hii ilikuwa kwa sababu umapanajisi patakatifu pangu kwa mambo ya machukizo yako yote na kwa matendo yako yote niyachukiayo, kwamba mimi mwenyewe nitakupunguza katika hesabu; jicho langu halitakuhurumia, na sitaacha kukuharibu.12Theluthi yenu mtakufa kwa tauni, na wataliwa na njaa katikati yenu. Theluthi wataanguka kwa upanga likiwazunguka. Kisha nitawatawanya theluthi katika mahali pote, na nitafuatisha upanga kuwafukuza pia.

13Hivi ndivyo ghadhabu yangu itavyokamilika, na nitasababisha ghadhabu yangu juu yao hata kulala. Nitajiridhisha, na watajua kwamba, mimi Yahwe, nimenena kwa ghadhabu yangu wakati nitakapo kamilisha ghadhabu yangu dhidi yao.

14Nitakufanya ukiwa kwa mataifa yanayokuzunguka kwenye uso wa kila mtu apitaye karibu.15Hivyo Yerusalemu itakuwa jambo kwa watu wengine kushutumu na kufanya mzaha, na chukizo kwa mataifa ambayo yanayowazunguka. Nitafanya hukumu dhidi yenu kwa ghadhabu na hasira, na kwa kukemea kwa hasira-Mimi, Yahwe nimesema hivi!16Nitatuma mishale mikali ya njaa juu yenu ambayo itakuwa na maana ya kwamba nitawaharibu. Kwa kuwa nitaongeza njaa juu yenu na kuvunja tegemeo lenu la mkate.17Nitaleta njaa na majanga dhidi yenu hivyo mtakuwa wagumba. Tauni na damu zitapita kati yako, na nitaleta upanga dhidi yenu-Mimi Yahwe, nimesema hivi.”

6

1Neno la Yahwe likanijia, likisema,2“Mwana wa adamu, weka uso wako dhidi ya milima ya Israeli na uwatabirie.3Sema, ‘Milima ya Israeli, silikilizeni neno la Bwana Yahwe! Bwana Yahwe asema hivi kwenye milima kwenye vilele, kwenye vijito na kwenye mabonde: Tazama! Naleta upanga dhidi yenu, na nitapaharibu pahali penu pa juu.4Kisha madhabahu zenu zitakuwa ukiwa na nguzo zenu zitaharibiwa, na nitatupa chini wafu wenu mbele ya sanamu zao.5Nitalaza miili iliyokufa kwa watu wa Israeli mbele ya sanamu zao, na kuitawanya mifupa yenu kuzizunguka madhabahu zenu.6Kila mahali utaishi, miji itaharibiwa na mahali pa juu kuangamia, hivyo basi madhabahu zenu zitaharibiwa na kufanywa ukiwa. Kisha zitavunjwa na kupotea, nguzo zenu zitaangushwa chini na kazi zenu zitafutwa mbali.7Waliokufa wataanguka chini kati yenu nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.

8Lakini nitahifadhi mabaki kwenu, na kutakuwa na wale watakao toroka upanga miongoni mwa mataifa,9Kisha wale watakao toroka watanikumbuka miongoni mwa mataifa amabapo watakapochukuliwa mateka, ndivyo nitakavoyowaponda mioyo yao ya kikahaba ambayo imeniacha, na kwa macho yao ya kikahaba kufuata sanamu zao. Kisha wataonyesha chuki kwenye nyuso zao kwa udhaifu walioufanya kwa machukizo yao yote.10Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe. Kulikuwa na sababu kwamba nimesema nitaleta huu uovu kwao.

11Bwana Yahwe asema hivi: Piga makofi na kanyaga kwa mguu wako! Sema! ‘Ole!’ kwa sababu ya uovu wote wa chukizo wa nyumba ya Israeli! Wataanguka kwa upanga, njaa, na tauni.12Yule aliye mbali sana atakufa kwa tauni, na yule aliyekaribu ataanguka kwa upanga. Wale watakaobaki na kuishi watakufa kwa upanga. Kwa njia hii ndivyo nitakavyo kamilisha madhabahu yangu dhidi yao.13Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati waliokufa watakapolala kati ya sanamu zao, kuzizunguka madhabahu, kwa kila mlima mrefu-juu ya vilele vya mlima, na chini ya mti wenye majani mabichi na mwalo mnene-sehemu wanapochomea ubani kwa sanamu zao zote.14Nitapiga kwa mkono wangu na kuifanya nchi ukiwa na isiyofaa, kutoka jangwa hata Dibla, kupita sehemu zote wanapoishi. Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe.”

7

1Neno la Yahwe likanijia, likisema,2Wewe, mwanadamu-Bwana Yahwe asema hivi kwa nchi ya Israeli.” ‘Mwisho! Mwisho umekuja kwenye mipaka minne ya nchi.3Sasa mwisho uko juu yako, kwa kuwa natuma ghadhabu yangu juu yako, nitakuhukumu kulingana na njia zako; nitaleta machukizo yako yote juu yako.4Kwa kuwa macho yangu hayatakuhurumia, na nitakuharibu. Badala yake, nitaleta njia zako zote juu yako, na machukizo yako yote yatakuwa katikati yako, hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe.

5Bwana Yahwe asema hivi: Msiba! Msiba wa pekee! Tazama, unakuja.6Mwisho unakuja hakika. Mwisho umeamsha dhidi yenu. Tazama! Unakuja!7Kifo chako kinakuja kwako ukaaye kwenye nchi. Mda umefika; siku ya uharibifu iko karibu, na milima haitakuwa na shangwe tena.8Sasa baada ya mda mfupi nitamwaga dhahabu yangu juu yako na kujaza hasira yangu juu yako wakati nitakapokuhukumu kulingana na njia zako na kuleta machukizo yako yote juu yako.9Kwa kuwa jicho langu halitaona huruma, nitakuharibu, kama ulivyofanya, nitafanya kwako; na machukizo yako yatakuwa katikati yako hivyo utajua kwamba ni mimi Yahwe, anayekuadhibu.

10Tazama, siku! Tazama, inakuja! Kifo kimetoka! Fimbo ya kuadhibia imechanua, kiburi kimechipua!11Udhalimu umekua kwenye fimbo ya udhaifu-hakuna kati yao, na hakuna katika kundi lao, hakuna katika utajiri wao, na hakuna wa muhimu wao atakaye baki!12Muda unakuja; siku imekaribia. Usimuache anayenunua shangwe, wala asihuzunike auzaye, kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kikundi kizima!13Kwa kuwa muuzaji hatarudia kile kilichouzwa, kadiri wanapoendelea kuishi, kwa kuwa maono yako juu yako kikundi kizima. Hawatarudi, kwa kuwa hakuna mtu anayeishi kwenye dhambi atakayejitia nguvu!14Wamepiga tarumbeta na kufanya kila kitu tayari, lakini hakuna mtu anayeenda kupigana; kwa kuwa hasira yangu iko juu ya kundi zima.

15Upanga uko nje, na tauni na njaa viko nje kwenye jengo. Wale walioko shambani watakufa kwa upanga, wakati njaa na tauni zitakapowala wale waliopo kwenye mji.16Lakini watakao salia watatoroka kutoka miongoni mwao, na watakwenda kwenye milima. Kama hua wa mabondeni, wote watalia-kila mtu kwa ajili ya uovu wake.17Kila mkono utasita na kila goti litakuwa dhaifu kama maji, na watavaa nguo za magunia, na hofu kuu itawafunika,18na aibu itakuwa juu ya kila uso, na upara juu ya vichwa vyao vyote.19Watatupa fedha yao kwenye mitaa na dhahabu yao itakuwa kama jalala. Fedha yao na dhahabu yao haitaweza kuwaokoa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe. Maisha yao hayataokolewa, na njaa yao haitashiba, kwa sababu uovu wao umekuwa kizuizi.20Kwenye fahari yao walichukua kito yake nzuri za mapambo, pamoja nao wakatengeza sanamu zao za vinyago, na vitu vyao vichukizavyo. Kwa hiyo, nayabadilisha haya kuwa kitu najisi kwao.21Kisha nitawapatia hivyo vitu kwenye mikono ya wageni kama mateka na kwa waovu wa dunia kama mateka, na watapanajisi.22Kisha nitaugeuza uso wangu mbali kutoka kwao watakapo najisi mahali pangu pa siri; maharamia wataingia humo na kupanajisi.

23Tengeneza mnyororo, kwa sababu nchi imejaa hukumu ya damu, na mji umejaa udhalimu.24Hivyo nitaleta waovu wengi wa mataifa, na watamilki nyumba zao, na nitaleta mwisho kwenye fahari ya uweza, kwenda mahali pao patakatifu patanajisiwa!25Hofu itakuja! Wataitafuta amani, lakini haitakuwepo.26Majanga juu ya majanga yatakuja juu yangu, na kutakuwa na tetesi juu ya tetesi. Kisha watatafuta ono moja kutoka kwa nabii, lakini sheria itawaangamiza kutoka kwa kuhani na shauri kutoka kwa wazee.27Mfalme ataomboleza na mwana wa mfalme atakata tamaa, wakati mikono ya watu wa nchi itatetemeka kwa hofu. Kulingana na njia zao wenyewe nitafanya hivi kwao! Nitawahukumu sawa sawa na wanavyostahili hadi watakapojua ya kwamba mimi ni Yahwe.’”

8

1Hivyo ikawa kuhusu katika mwaka wa sita na mwezi wa sita, katika siku ya tano ya mwezi, nilipokuwa nimeketi kwenye nyumba yangu na wazee wa Yuda waliketi mbele yangu, kwamba mkono wa Bwana Yahwe ukanijaza juu yangu huko.2Hivyo nikaona, na tazama, kulikuwa na mfano kama mwonekano wa mwanadamu. Kutoka kwenye mwonekano wake wa nyonga kwenda chini kulikuwa na moto. Na kutoka kwenye nyonga kwenda juu kulikuwa na mwonekano wa kitu kinachong'aa, kama mng'ao wa chuma.3Kisha akanyoosha kutoka kwenye mkono na kunichukua kwa nywele za kichwa changu; Roho akaniacha juu kati ya dunia na mbingu, na katika maono kutoka kwa Mungu, akaniletea hata Yerusalemu, kwenye mlango wa kuingia ndani ya lango la kaskazini, ambako sanamu ile iletayo wivu mkubwa ilipokuwa imesiamama.4Kisha tazama, utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa huko, kulingana na ono nililokuwa nimeliona kwenye uwanda.

5Kisha akanambia, “Mwanadamu, inua juu macho yako kwenda upande wa kaskazini.” Hivyo nikainua macho yangu kuelekea kaskazini, na kwenye lango la kaskazini kulekea kwenye madhabahu, huko kwenye lango la kuingilia, kulikuwa na sanamu ya wivu.

6Hivyo akanambia, “Mwanadamu, unaona wanayoyafanya? Haya ni machukizo makubwa ambayo nyumba ya Israeli wanayoyafanya hapa kunifanya niende mbali kutoka patakatifu pangu. Lakini utageuka na kuona machukizo makubwa zaidi.”

7Kisha akanileta hata kwenye mlango wa uzio, na nikatazama, kulikuwa na shimo kwenye ukuta.”8Akanambia, “Mwanadamu, chimba kwenye huu ukuta.” Basi nikachimba kwenye huo ukuta, na kulikuwa na mlango.

9Kisha akanambia, “Nenda na ukaone machukizo ya uovu ambayo wanayoyafanya hapa.”10Basi nilipokuwa nikienda ndani na nikaona, na tazama! Kulikuwa na kila umbo la vitu vikitembea polepole na mnyama achukizaye sana! Kila sanamu wa nyumba ya Israeli ilikuwa imechongwa kwenye ukuta pande zote.11Wazee sabini wa wa nyumba ya Israeli walikuwa huko, na Yaazania mwana wa Shafani alikuwa amesimama katikati yao. Walikuwa wamesimama mbele ya picha, na kila mtu alikuwa na chetezo kwenye mkono wake ili kwamba harufu ya ubani ingeweza kupanda juu.

12Akanambia, “mwanadamu, unaona kile ambacho wazee wa nyumba ya Israeli wanachokifanya kwenye giza? Kila mmoja hufanya hivi kwenye chumba cha sanamu yake, kwa kuwa husema, ‘Yahwe hatuoni! Yahwe ameitelekeza hii nchi.”’13Kisha akanambia, “Geuka tena na tazama machukizo makubwa ambayo wanayoyafanya.”

14Tena akanileta kwenye lango la kuingia la nyumba ya Yahwe lililokuwa upande waa kaskazini, na tazama! Wanawake walikuwa wameketi huko wakimlilia Tamuzi.15Hivyo akanambia, “Umeiona hii, mwanadamu? Geuka tena na uone machukizo makubwana zaidi kuliko hayo.”

16Akanileta hata kwenye uzio wa ndani wa nyumba ya Yahwe, na tazama! Huko kwenye lango la kuingia kwenye madhabahu, kulikuwa na takribani watu ishirini na tano waliokuwa wamelipa mgongo hekalu la Yahwe na nyuso zao kuelekea mashariki, na walikuwa wakiabudu jua.

17Akanambia, “Unaona hii, mwanadamu? Je ni kitu kidigo kwa ajili ya nyumba ya Yuda kufanya haya machukizo wanayoyafanya? Kwa kuwa wameijaza nchi kwa uovu na wamerudi tena ili kuniletea hasira, kuweka tawi kwenye pua zao.18Hivyo nitatenda miongoni mwao pia; jicho langu halitakuwa na huruma, sitaacha kuwaharibu. Hata watalia kwenye masikio yangu kwa sauti kubwa, sitawasikia.”

9

1Kisha akalia kwa sauti kubwa nikasikia kwenye masikio yangu, huku akisema, “Waache walinzi waje kwenye mji, kila mmoja na silaha yake ya uharibifu kwenye mkono wake.”2Kisha tazama! Watu wanne watakuja kutokea njia ya lango la juu linaloelekea kaskazini, kila mmoja na silaha yake ya kuchinjia kwenye mkono wake. Kulikuwa na mtu mmoja miongoni mwao alikuwa amevaa nguo ya kitani pamoja na kifaa cha uandishi ubavuni mwake. Hivyo waliingia na kusimama karibu na madhabahu ya shaba.

3Kisha utukufu wa Mungu wa Israeli ukapanda juu kutoka kwa kerubi ambapo ilikuwa kwenye kisingiti cha nyumba. Akamwita yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani na kifaa cha uandishi ubavuni mwake.4Yahwe akamwambia, “Pita kati ya mji-kati ya Yerusalemu-na weka alama katika vipaji vya uso vya wale waliolemewa na kuona kuhusu machukizo yote yanafanyika kati ya mji.”

5Kisha akaongea na wengine kupitia kusikia kwangu, “Pita kwenye mji baada ya yeye na kuua. Msiache macho yenu yawe na huruma, na msiogope kuharibu6iwe mzee, kijana, msichana, mtoto mdogo au wanawake. Waueni watu wote! Lakini msimkaribie mtu yeyote ambaye mwenye alama kwenye kichwa chake. Anzeni katika patakatifu pangu!” Hivyo wakaanza na wazee waliokuwa mbele ya nyumba.

7Akawaambia, “Najisi nyumba, na kujaza zio zake kwa waliokufa. Endeleeni!” Hivyo wakaenda na kuushambulia mji.8Walipokuwa wakiushambulia, nikajikuta mwenyewe na nikaangukia kwenye uso wangu na kulia kwa sauti na kusema, “Ee, Bwana Yahwe, utayaharibu mabaki yote ya Israeli wakati wa kumwaga ghadhabu yao juu ya Yerusalemu?”

9Akanambia, “Uovu wa nyumba ya Israeli na Yuda unaongezeka sana. Nchi imejaa damu na mji umejaa upotovu, tangu waliposema, ‘Yahwe ameisahau nchi; na Yahwe haoni!’10Hivyo kisha, macho yangu hataangalia kwa huruma, na sitaacha kuwaharibu. Badala yake nitaileta juu ya vichwa vyao.”

11Tazama! Yule mtu aliyekuwa amevaa nguo ya kitani aliyekuwa na kifaa cha uandishi kwa upande wa ubavuni mwake. Alitoa taarifa na kusema, “Nimemaliza yale yote uliyoniamuru.”

10

1Nilipokuwa nikingalia mbele ya anga ambalo lililokuwa juu ya vichwa vya kerubi; kitu kikawatokea juu yao kama rangi ya samawati mwonekano wake ulikuwa kama kiti cha enzi.2Kisha Yahwe akaongea na yule mtu alikuwa maevaa nguo za kitani na kusema, “Nenda kati ya magurudumu chini ya kerubi, na jaza mikono yako yote na watawanye juu ya mji.” Kisha yule mtu akaenda ndani nikiwa natazama.

3Kerubi a kasimama juu ya upande wa kulia wa nyumba wakati yule mtu alipoingia, na wingu likajaa ndani ya uzio.4Utukufu wa Yahwe ukainuka kutoka kwenye kerubi na kusimama kwenye kizingiti cha nyumba. Ukaijaza nyumaba kwa wingu, na uzio ulikuwa umejaa nuru ya utukufu wa Yahwe.5Sauti ya mabawa ya kerubi ikasikika kwa mbali nje ya uzio, kama sauti ya Mungu mwenyezi wakati akiwa anaongea.

6Ikawa kuhusu, Mungu alipoamwamuru yule mtu aliyekuwa amevaa nguo za kitani na kusema, “Chukua moto kutoka kwenye yule kerubi,” yule mtu akaenda na kusimama karibu na gurudumu.7Kerubi akaunyoosha mkono wake kwenye kerubi kwenye moto uliokuwa miongoni mwa kerubi, na kuiacha juu na kuiweka kwenye mikono ya yule mtu aliyekuwa amevaa vazi la kitani. Yule mtu akaichukua na kurudi.8Nikaona juu ya kerubi kitu kama mkono wa mtu juu ya mabawa yao.

9Hivyo nikaona, na tazama! Magurudumu manne yalikuwa karibu na kerubi-gurudumu moja karibu na kila kerubi-na mwonekano wa hayo magurudumu ulikuwa kama jiwe la zabarajadi.10Mwonekano wake ulikuwa unaofanana kama wa wote wanne, kama gurudumu lililokuwa kwenye gurudumu lingine.11Wakati walipokuwa wakitembea, walienda katika pande zote nne bila kugeuka katika kwenye njia nyingine. Badala yake, popote kichwa kilipoelekea, walilifuata. Hawakugeuka kwenye njia yeyote nyingine walipokuwa wakienda.12Mwili wao wote-pamoja na migongo yao, mikono yao, na mabawa yao-vilikuwa vimefunikwa kwa macho, na macho kufunika magurudumu manne kuzunguka pote pia.13Nilikuwa nasikia, magurudumu yalikuwa yakiita, “Kuzunguka.”14Walikuwa na nyuso nne kila moja; uso wa kwanza ulikuwa uso wa kerubi, uso wa pili ulikuwa uso wa mtu, uso wa tatu ulikuwa uso wa simba, na uso wa nne ulikuwa uso wa malaika.

15Kisha makerubi-hawa walikuwa viumbe hai nilivyokuwa nimeviona karibu na Keberi Kanali-wakainuka juu.16Popote makerubi walipoenda, magurudumu yalienda karibu nao, na popote makerubi walipoinua juu mabawa yao kupaa juu kutoka kwenye nchi, magurudumu hayakugeuka. Yaliendelea kuwa karibu nao.17Wakati makerubi waliposimama, magurudumu yalisimama pia, na wakati walipoinuka juu, magurudumu yaliinuka juu pamoja nao, kwa kuwa roho wa vile viumbe hai walikuwa kwenye magurudumu.

18Kisha utukufu wa Yahwe ukaja kutoka juu ya kizingiti cha nyumba na kusimama juu ya kerubi.19Yule kerubi akaacha juu mabawa na kuinuka kutoka kwenye jicho langu wakati walipotoka nje, na yale magurudumu yakafanya vivyo hivyo karibu nao. Wakasimama upande wa mashariki kuingia kwenye nyumba ya Yahwe, na utukufu wa Mungu wa Israeili ukaja juu yao kutoka juu.

20Hawa walikuwa viumbe hai ambao niliokuwa nimewaona chini ya Mungu wa Israeli karibu na Kebari Kanali, hivyo nilijua kwamba walikuwa makerubi!21Walikuwa na macho manne kila mmoja na mabawa manne, na mfanano wa nyuso zao zilikuwa na mfanano wa mikono ya mwanadamu chini ya mabawa yao,22na mfanano wa nyuso zao ulikuwa kama nyuso nilizokuwa nimeziona kwa maono huko Keberi Kanali, na kila mmoja wao alienda mbele.

11

1Kisha Roho akaniweka juu na kunileta kwenye lango la mashariki la nyumba ya Yahwe, kuelekea mashariki, na tazama, kwenye njia ya mlango wa lango kulikuwa na watu ishirini na tano. Nikamwona Yaazania mwana wa Azuri na Pelatia mwana wa Benaya, viongozi wa watu, miongoni mwao.2Mungu akanambia, “Mwana wa adamu, hawa ndio wale watu walioshauri udhalimu, na kuamua mipango miovu kwenye huu mji.3Wakisema, ‘Mda wa kujenga nyumba sio sasa; huu mji ni sufuria, na sisi ni nyama.’4Kwa hiyo tabiri juu yao. Tabiri, mwana wa adamu.”’

5Kisha Roho wa Yahwe akanijaza na akaniambia, “akisema: Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: kama usemavyo, nyumba ya Israeli; kwa kuwa najua kinachoendelea kwenye fikra zenu.6Mmewazidisha watu mliowaua kwenye huu mji na kuijaza mitaa kwa hao.

7Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Wale watu milowaua, ambao mmeilaza miili yao kati ya Yerusalemu, ni nyama, na huu mji ni sufuria. Lakini mnaenda kutolewa nje kutoka kati ya huu mji.8Mmeuogopa upanga, kwa hiyo nauleta huo upanga juu yenu-huu ndio usemi wa Bwana Yahwe.9Nitawatoa nje kutoka kati ya mji, na kuwaweka kwenye mikono ya wageni, kwa kuwa nitaleta hukumu dhidi yenu.10Mtaanguka kwa upanga. Nitawahukumu kati ya mipaka ya Israeli hivyo mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.11Huu mji hautakua sufuria yenu ya kupikia, wala hamtakuwa nyama ndani yake. Nitawahukumu kati ya mipaka ya Israeli.12Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe, yule ambaye hamuishi kwenye amri zake na ambaye hamkuzishika sheria zake. Badala yake, mmebeba hukumu za mataifa wanayowazunguka.”

13Ikawa kwamba nilipokuwa natabiri, Pelatia mwana wa Benaya, akafa. Hivyo nikaanguka kwenye uso wangu na kulia kwa sauti na kusema, “Ee, Bwana Yahwe

14Neno la Yahwe likanijia, likisema,15“Mwana wa adamu, ndugu zako! Ndugu zako! Watu wa ukoo wako na nyumba yote ya Israeli! Wote hao ndio hao ambao inasemekana wale wanaoishi Yerusalemu, ‘Wako mbali sana kutoka kwa Yahwe! Hii nchi tulipewa sisi kama milki yetu.’

16Kwa hiyo sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: kote nimewapitisha mbali kati ya mataifa, na kote nimewasambaza kati ya nchi, bado nimekuwa patakatifu kwa ajili yao kwa mda kidogo kwenye nchi ambazo walizoenda.’

17Kwa hiyo sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Nitawakusanya kutoka kwa watu, na kuwakutanisha kutoka kwenye nchi mlizokuwa mmetawanyika, na nitawapatia nchi ya Israeli.’

18Kisha wataenda huko na kuondoa kila kitu chenye karaha na kila chukizo kutoka hiyo sehemu.19Nitawapatia moyo mmoja, na nitaweka roho mpya kati yao. Nitaondoa moyo wa jiwe kutoka kwenye miili yao na kuwapatia moyo wa nyama,20ili kwamba waweze kutembea kwenye amri zangu, watayachukua maagizo yangu na kuyatenda. Kisha watakuwa watu wangu, na nitakuwa Mungu wao.21Lakini kwa wale watembeao kwa kujifanya kuendeleza mambo yao ya karaha na machukizo yao, nitaleta tabia yao kwenye vichwa vyao-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

22Makerubi wakainua mabawa yao na magurudumu yaliyokuwa karibu nao, na utukufu wa Mungu wa Israeli ulikuwa juu yao.23Kisha utukufu wa Yahwe ukaenda juu kutoka katikati ya mji na kusimama kwenye mlima hata mashariki mwa mji.24Roho akanichukua juu na kunileta hata Ukaldayo, hata uhamishoni, katika maono kutoka kwa Roho wa Mungu, na maono niliyokuwa nimeyaona yakaenda juu yakaniacha.25Kisha nikawaambia wale watumwa mambo yote ya Yahwe niliyokuwa nimeyaona. Je utayaharibu kabisa mabaki ya Israeli?”

12

1Neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwana wa adamu, unaishi kwenye nyumba ya uasi, wana macho ya kuona lakini hawaoni; na wana masikio ya kusikia lakini hawasikii, kwa sababu wao ni nyumba iliyoasi.

3Kwa hiyo wewe mwanadamu, andaa mambo yako kwa ajili ya uhamisho, na anza kuondoka mchana usoni kwao, kwa kuwa nitakuhamisha kwenye uso wao kutoka sehemu yao kwenda sehemu nyingine. Labda wataanza kuona, kuwa wao ni nyumba ya uasi.4Utatoa vitu vyako kwa ajili ya kuhamisha mchana katika macho yao; toka jioni kwenye macho yao kama ambavyo uendavyo kwenye uhamisho.5Chimba shimo ukutani kwenye uso wa macho yao, na ingia ndani yake.6Kwenye macho yao, chukua vitu vyako kwenye mabega yako, na uwalete kwenye giza. Funika uso wako kama ishara kwenye nyumba ya Israeli.”

7Hivyo nikafanya hivyo, kama nilivyokuwa nimeamriwa. Nikatoa vitu vya uhamisho wakati wa mchana, na katika jioni nikachimba shimo hata kwenye ukuta kwa mkono. Nikachukua vitu vyangu kwenye giza, na kuviweka juu kwenye bega langu katika macho yao.

8Kisha neno la Yahwe likanijia asubuhi, likisema,9Mwanadamu, je nyumba ya Israeli, ile ni nyumba ya uasi, hawakukwambia, ‘Unafanya nini?’

10Waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: hili tendo la kinabii linamhuusu mwana wa mfalme wa Yerusalemu, na nyumba yote ya Israeli walio kati yao.’11Sema, ‘Mimi ni ishara kwenu. Kama nilivyofanya, itafanyika kwao; watakwenda uhamishoni na kuwa wafungwa.12Yule mwana wa mfalme aliye miongoni mwao atavibeba vitu vyake kwenye bega lake katika giza, na ataenda zake kupitia kwenye ukuta. Watachimba kwenye ukuta na kutoa vitu vyao nje. Atafunika uso wake, hivyo hataona nchi kwa macho yake.13Nitausambaza wavu wangu juu yake naye atanaswa kwenye mtego wangu; kisha nitamleta Babeli, nchi ya Wakaldayo, lakini hataiona. Atafia huko.14Pia nitatawatawanya katika kila mwelekeo wale wote waliomzunguka wanaomsaidia na jeshi lake lote, na nitaufuata upanga nyuma yao.

15Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapo watawanya kwenye nchi zote.16Lakini nitaacha kuwaangamiza watu wachache kutoka miongoni mwao kutoka kwenye upanga, njaa, na tauni, hivyo wanaweza kukumbuka maovu yao yote katika nchi zao nilipowachukulia, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

17Neno la Yahwe likanijia, likisema,18“Mwanadamu, kula mkate wako kwa kutetemeka, na kunywa maji yako kwa mtetemo na hofu.19Kisha waambie watu wa nchi, ‘Bwana Yahwe asema hivi kuhusiana na wale wakaao Yerusalemu, na nchi ya Israeli: Watakula mikate yao kwa kutetemeka na kunywa maji yao wakiwa wanatetemeka, kwa kuwa nchi itaporwa vitu vyote viijazavyo kwa sababu ya kuwa kinyume na waishio huko.20Hivyo ile miji iliyokuwa wenyeji itachukuliwa, na nchi itakuwa ukiwa; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

21Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,22“Mwanadamu, je ni mithali gani hii mlio nayo katika nchi ya Israeli mliyoisema, ‘Siku zimerefushwa, na kila ono linaanguka’?23Kwa hiyo, waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Nitaweka mwisho wa hii mithali, na watu wa Israeli hawataitumia tena.’ Waambie, ‘Siku zi karibu wakati kila ono litatimizwa.24Kwa kuwa hakutakuwa na maono ya uongo yoyote wala upendeleo wa mgawanyiko kati ya nyumba ya Israeli.25Kwa kuwa mimi Yahwe! Nimesema, na nitayatimiza yale maneno nilyoyasema. Hakuna kitu kitakacho chelewesha. Kwa kuwa nitaongea hili neno katika siku zenu, nyumba ya uasi, na nitalitimiza! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’”

26Tena neno la Yahwe likanijia, likisema,27“Mwanadamu! Tazama, nyumba ya Israeli imesema, ‘Lile ono alionalo ni kwa siku nyingi kutoka sasa, na ametabiri kipindi kilicho mbali sana.’

28Kwa hiyo waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Neno langu halitacheleweshwa sana, lakini lile neno nililoliongea litatimizwa, hivi ndivyo Yahwe asemavyo.’”

13

1Tena, neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, tabiri dhidi ya manabii wanaotabiri katika Israeli, na uwaambie wale wanotabiri nje ya fikra zao wenyewe, ‘Lisikilizeni neno la Yahwe.3Bwana Yahwe asema hivi: Ole wao manbii wajinga ambao wanafuata roho zao wenyewe, lakini ni wale wasioona kitu!4Israeli, manabii zako wamekuwa kama mbweha kwenye ardhi iliyoharibiwa na vita.5Hamkwenda kwenye nyufa katika ukuta uliozunguka nyumba ya Israeli kwa ajili ya kuukarabati, ili kupigana katika vita katika siku ya Yahwe.6Watu wameona uongo na kufanya utabiri wa uongo, wale wasemao, “Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo.” Yahwe hajawatuma, lakini hata hivyo wamewafanya watu kutumaini kwamba ujumbe wao utakuwa kweli.7Je hamkusikia maono ya uongo na kufanya utabiri wa uongo, ninyi msemao, “Hivi na hivi ndivyo Yahwe asemavyo.” Wakati mimi mwenyewe sikuongea?’

8Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, ‘Kwa sababu mmesikia maono ya uongo na kuwaambia uongo-kwa hiyo hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo dhidi yenu:9Mkono wangu utakuwa juu yenu ninyi manabii mliodanganya maono na wale waliofanya unabii wa uongo. Hawatakuwepo kwenye kusanyiko la watu wangu, au kuandikishwa katika kumbukumbu ya nyumba ya Israeli; hawataenda kwenye nchi ya Israeli. Kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!

10Kwa sababu hiyo, na kwa sababu wamewaongoza watu wangu kuwapotosha na kusema, “Amani!” wakati hakuna amani, wanajenga ukuta ambao wataupaka rangi ya chokaa.’11Waambie wale wanaopaka chokaa ukuta, ‘Utaanguka chini; kutakuwa na mvua ya kufurika, na nitaleta mvua ya mawe kuufanya uanguke chini, na upepo wa dhoruba kupuliza hata kuuvunja chini.12Tazama, ukuta utaanguka chini. Je wengine hawakuwaambia, “Iko wapi chokaa mliyoipaka juu yake?”

13Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitaleta upepo wa dhoruba katika ghadhabu yangu, na kutakuwa na mafuriko ya mvua kwenye ghadhabu yangu! Mvua ya mawe katika ghadhabu yangu itauharibu kabisa.14Kwa kuwa nitaurarua chini ukuta ambao mlioufunika kwa chokaa, na nitaubomoa hata kwenye nchi na kuifunua misingi yake. Hivyo utaanguka, nanyi nyote mtaangamizwa katikati ya huo.15Ndivyo nitakavouangamiza kwa ghadhabu yangu ukuta na wale walioupaka chokaa. Nitawaambia, “Ukuta hautaonekana tena, wala watu wanaoupaka chokaa-16manabii wa Israeli wale waliotabiri kuhusu Yerusalemu na wale waliokuwa wameona amani kwa ajili yake. Lakini hakuna amani! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

17Hivyo wewe, mwanadamu, weka uso wako dhidi ya binti za watu wako wale wanaotabiri kwa akili zao wenyewe, na kutabiri dhidi yao.18Sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa wanawake washonao hiziri kwenye kila sehemu ya mkono wao na kutengeza vitambaa vya shela kwa ajili ya vichwa vyao kwa kila kipimo, ili kuwinda watu. Je mtawawinda watu wangu ila kuokoa maisha yenu wenyewe?19Ninyi mmenikufuru mbele ya watu wangu kwa ajili ya makonzi ya shayiri na vipande vya mkate, kuwaua watu ambao hawakutakiwa kufa, na kuyalinda maisha ya wale ambao hawatakiwi kuendelea kuishi, kwa sababu ya uongo wenu kwa watu wangu walio wasikiliza.

20Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Niko kinyume dhidi ya hirizi ambazo mlizozitumia kuyakamata kwa hila maisha ya watu kana kwamba wamekuwa ndege. Naam, nitazichana kutoka kwenye mikono yenu; na wale watu mlio watega kama ndege-nitawaacha waende huru.21Nitavichana mbali vitambaa vya shela na kuwaokoa watu wangu kutoka kwenye mikono yangu, kwa hiyo hawatategwa tena kwenye mikono yenu. Mtajua kwamba mimi ni Yahwe.22Kwa sababu mmeuvunja moyo wa mtu mwenye haki kwa uongo, ingawa hata mimi sikutamani kuvunjwa kwake moyo, na kwa sababu mmemtia moyo badala yake matendo ya mtu mwovu ili kwamba asiweze kurudi kutoka kwenye njia yake kuokoa maisha yake-23kwa hiyo hamtayaona tena maono ya uongo au kuendelea kufanya utabiri, kwa kuwa nitawaokoa watu wangu kutoka kwenye mkono wako. Nanyi mtajua kwamba mimi ni Yahwe.’”

14

1Baadhi ya viongozi wa Israeli wakaja kwangu na kuketi mbele yangu.2Ndipo neno la Yahwe likanijia, likisema,3“Mwanadamu, hawa watu wamchukua sanamu zao kwenye mioyo yao na kuweka pingamizi la uovu wao mbele ya nyuso zao wenyewe. Je naweza kuulizwa yote na wao?4Kwa hiyo watangazie hivi na waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Kila mtu wa nyumba ya Israeli achukuaye sanamu moyoni mwake, au awekeye pingamizi la uovu mbele ya uso wake, na kisha yule ajaye kwa nabii-Mimi, Yahwe, nitamjibu kulingana na sanamu zake.5Nitafanya hivi ili kwamba niweze kuirudisha nyumba ya Israeli katika mioyo yao ambayo ilikuwa mbali nami kwa ajili ya sanamu zao.’

6Kwa hiyo sema kwa nyumba ya Israeli, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tubuni na rudini kutoka kwenye sanamu zenu! Rudisheni nyuma nyuso zenu kutoka kwenye machukizo yenu yote.

7Kwa kuwa kila mmoja kutoka kwenye nyumba ya Israeli na kila mmoja wa wageni wanaoishi katika Israeli ajitengaye nami, achukuaye sanamu zake kwenye moyo wake na kuweka kwazo la uovu wake mbele ya uso wake mwenyewe, na kisha yule ajaye kwa nabii kunitafuta-mimi, Yahwe, nitamjibu mimi mwenyewe.8Hivyo nitauweka uso wangu juu ya huyo mtu na kumfanya ishara na mithali, kwa kuwa nitamkata kutoka kati ya watu wangu, na mtajua kuwa mimi ni Yahwe.

9Kama nabii atadanganywa na kuongea ujumbe, kisha Mimi Yahwe, nitamdanganya huyo nabii; Nitanyoosha mkono wangu na kumwangamiza toka kati ya watu wangu Israeli.10Watabeba uovu wao wenyewe; uwovu wa nabii utakua kama uovu wa yule aulizaye kutoka kwake.11Kwa sababu hiyo basi, nyumba ya Israeli haitaenda mbali kutoka kunifuata mimi wala kujinajisi wenyewe kupitia dhambi zao zote. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao-hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”’

12Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,13“Mwanadamu, wakati nchi itakapo asi dhidi yangu kwa kufanya dhambi ili kwamba ninyooshe mkono wangu dhidi yake na kuvunja tegemea la mkate wake, na kuleta njaa juu yake na kukata mnyama kutoka kwenye nchi;14kisha hata kama hawa watu watatu-Nuhu, Danieli, na Ayubu-walikuwa katikati ya nchi, wangeweza kuokoa maisha yao wenyewe kwa haki-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

15Kama nikileta wanyama waovu kwenye nchi na kuwafanya wasizae hivyo basi itakuwa hakuna mtu asiweze kupita kwa sababu ya hao wanyama,16kisha hata kama watu hawa hawa watatu ndani yake-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa hata watoto wao wala binti; isipokuwa maisha yao yataokoka, lakini nchi itakuwa ukiwa.

17Au nikileta upanga juu ya hiyo nchi na kusema, ‘Upanga, nenda kwenye nchi na wakate wote mtu na mnyama kutoka huo,’18kisha hata kama hawa watu watatu watakuwa katikatai ya nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuwaokoa japo watoto wao wala binti; ila tu maisha yao wenyewe yangeokolewa.

19Au kama nikipeleka tauni juu ya nchi na kumwaga dhahabu yangu juu yake kwa damu, ili kuwakata mtu na mnyama,20kisha hata kama Nuhu, Danieli, na Ayubu wangekuwa kwenye hiyo nchi-kama niishivyo, asema Bwana Yahwe-wasingeweza kuokoa hata watoto wao au binti; maisha yao pekee yangeokoka kwa haki.

21Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: hakika nitafanya mambo makali sana kwa kuleta adhabu zangu nne-njaa, upanga, wanyama wa porini, na tauni-juu ya Yerusalemu kuwakata wote mtu na mnyama kutoka kwake.22Kisha, tazama! Mabaki yatasalia kwake, watakaokoka wataenda pamoja na wana na binti. Tazama! Watawatokea, na mtaona njia zao na matendo yao yakiwafariji kuhusu adhabu niliyoipeleka Yerusalemu, na kuhusu kila kitu kingine ambacho nilichopeleka juu ya nchi.23Waliokoka watawafariji ninyi mtakapoona njia zao na matendo yao, hivyo mtayajua haya mambo niliyoyafanya juu yake, kwamba sijayafanya bure! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

15

1Kisha neno la Yahwe likanijia, liksema,2“Mwanadamu, je ni jinsi gani mzabibu ulivyo bora kuliko mti na matawi yaliyomo kwenye miti katika msitu?3Je watu huwa wanachukua mbao kutoka kwenye mzabibu kufanyia chochote? Au huwa wanatengenezea vitu kutokana na huo kuning'iniza chochote juu ya huo?4Tazama! Kama umetupwa kwenye moto kama kuni, na kama moto umezichoma ncha zake zote na katikati pia, je unafaa kwa chochote?5Tazama! Wakati ulipokuwa umekamilika, haukuweza kufanya chochote; kisha hakika, wakati moto ulipouchoma, lakini bado haukuweza kutengeneza kitu chochote kwa ajili ya matumizi yoyote.

6Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: haufanani na miti katika misitu, niliyoitoa mzabibu kama kuni kwa moto; nitatenda vivyo hivyo mbele ya wakaao Yerusalemu.7Kwa kuwa nitauweka uso wangu juu yao. Ingawa watatoka kutoka kwenye moto, bado moto utawala; hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakapoona uso wangu juu yenu.8Kisha nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamefanya dhambi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

16

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, mwambie Yerusalemu kuhusu machukizo yake,3na useme, ‘Bwana Yahwe asema hivi kwa Yerusalemu: Mwanzo wako na kuzaliwa kwako kulichukua nafasi katika nchi ya Kanaani; baba yako alikuwa Mwamori, na mama yako alikuwa Mhiti.4Katika siku ya kuzaliwa kwako, mama yako hakukata kitovu chako, wala hakukuosha kwenye maji usafishwe au kukuchua kwa chumvi, wala kukusitiri nguo.5Hakuna jicho lililokuhurumia kufanya haya mambo kwa ajili yako, kukuhurumia wewe. Katika siku uliyozaliwa, kwa kuchukiwa uhai wako, ulitupwa nje uwandani.

6Lakini nilipita karibu nawe, nalikuona ukijinyonga kwa damu yako mwenyewe, “kubaki hai!”7Nimekufanya ukue kama mmea katika shamba. Umeongezeka na kuwa mkubwa, na umekuwa mzuri wa wazuri. Maziwa yako yakawa thabiti, na nywele zako zikawa nyingi, ingawa ulikuwa uchi huna nguo.

8Nilipita karibu nawe tena, na nalikuona. Tazama! Wakati wa upendo umefika kwako, hivyo nikatandika joho langu juu yako na kufunika uchi wako. Kisha nikaapa kwako na kukuleta kwenye agano-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na ukawa wangu.

9Basi nilikuosha kwa maji na kukufuta damu yako, na kukupaka mafuta.10Nilikuvalisha nguo ya taraza na kukuwekea makuzi ya ngozi kwenye miguu yako. Nilikufungia kwa kitani kizuri na kukufunika kwa hariri.11Kisha nalikupamba kwa vito, na kukuvalisha vikuku kwenye mikono yako, na mkufu kwenye shingo yako.12Nalitia hazama katika pua yako na hereni katika masikio yako, na taji nzuri juu ya kichwa chako.13Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha, na ulivaa kitani safi, hariri, na ngu za taraza; ulikula unga mzuri, asali, na mafuta, na ulikuwa mzuri sana, na ukawa malkia.14Umaarufu wako ukaenda miongoni mwa mataifa kwa sababu ya uzuri wako, kwa kuwa ulikuwa mkamili katika ukuu niliokuwa nimekupa-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

15Lakini ulitumaini uzuri wako, na ukafanya kama kahaba kwa sababu ya umaarufu wako; umeyamwaga matendo yako ya kikahaba kwa kila aliyepita karibu, ili kwamba uzuri wako uwe wake.16Kisha ulichukua nguo zako na pamoja nao umepatengeneza mahali pa juu kwa ajili yako palipambwa kwa rangi tofauti tofauti, na hapo ulifanya kama kahaba. Haya hayatakuweko. Wala hayatatokea.17Umevichukua vito vizuri vya dhahabu na fedha nilizowapatia, na umejitengenezea sanamu za wanaume, na umefanya pamoja nao ukahaba afanyao.18Ulichukua nguo zako za tarizi na kuwafunika, na kuwawekea mafuta yangu na manukato mbele yao.19Mkate wangu niliokupatia-ulitengenezwa kwa unga mzuri, mafuta, na asali-umeviweka mbele yao kwa ajili ya kunukia harufu nzuri, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyotokea-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

20Kisha uliwachukua watoto wako ulionizalia, na kuwatoa sadaka kwa picha ili waliwe kama chakula. Je! Matendo yako ya kikahaba ni kitu kidogo?21Umewachinja watoto wangu na kuwatupia kwenye moto.22Katika machukizo yako yote na matendo yako ya kikahaba hukutafakari kuhusu siku za ujana wako, wakati ulipokuwa uchi na bila nguo kama kama umepigwa katika damu.

23Ole! Ole wako! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwahiyo, zaidi ya hapo kwa haya maovu yote,24umejijengea chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi.25Umepajenga mahali pako palipoinuka kwenye kichwa cha kila njia na kuunajisi uzuri wako, kwa kuwa umeutoa mwili wako kwa kila mtu apitaye karibu na umefanya matendo mengi zaidi ya ukahaba.26Umetenda kama kahaba pamoja na Wamisri, tamaa ya jirani zako, na umetenda matendo mengi zaidi ya kikahaba, ili kuchochea hasira yangu.27Tazama! Nitakunyooshea mkono wangu na kupunguza chakula chako. Nitauchukua uhai wako juu ya adui zako, binti za Wafilisti, ambao walikuwa na haya ya tabia yako ya uchafu.28Umetenda kama kahaba pamoja na Waashuru kwa sababu hukuweza kuridhika. Umetenda kama kahaba na bado hukuridhika.29Umefanya matendo mengi zaidi ya kikahaba katika nchi ya jamii ya wana maji wa Ukaldayo, na wala hukuridhika kwa hayo.

30Jinsi moyo wako ulivyo dhaifu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwamba utaweza kuyafanya haya mambo yote, matendo ya aibu ya kikahaba?31Mmepajenga mahali penu pa juu kwenye kichwa cha kila mtaa na kufanya chumba cha chini kwa chini katika kila sehemu ya watu wengi. Bado hukuwa kama kahaba kwa sababu ulikataa kulipwa ujira.

32Wewe mwanamke mzinifu, wewe upokeaye wageni badala ya mume wako.33Watu hulipa kwa kila kahaba, lakini wewe huwapa mshahara wako wapenzi wako wote na kuwapa rushwa ili waje kwako pande zote kwa matendo yako ya kikahaba.34Hivyo kuna tofauti kati yako na hao wanawake wengine, kwa kuwa hakuna hata mmoja ajaye kwako kukuuliza kulala pamoja nao. Badala yake, unawalipa. Hakuna akulipaye.

35Kwa hiyo, wewe kahaba, lisikilize neno la Yahwe.36Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umemwaga tamaa yako na kuonyesha sehemu zako za siri kupitia matendo yako ya ukahaba pamoja na wapenzi wako wote pamoja na sanamu zako za chukizo, na kwa sababu ya damu ya watoto wako uliyowapatia sanamu zako,37kwa hiyo, tazama! Nitawakusanya wapenzi wako wote uliokutana nao, wote ambao uliowapenda na wote uliowachukia, na nitawakusanya juu yako kila upande. Nitawaonyesha wazi sehemu zako za siri hivyo wanaweza kuona uchi wako wote.38Kwa kuwa nitakuadhibu kwa uasherati na kumwaga damu, na nitaleta juu yako damu ya hasira yangu na hasira kali.39Nitakutia kwenye mikono yao hivyo watakutupa chini kwenye chumba cha chini kwa chini na kupavunja mahali pako pa juu na watakuvua nguo zako na kuchukua vito vyako vyote. Watakuacha uchi bila nguo.40Kisha wataleta kundi la watu juu yako na kukupiga kwa mawe, na kukukata kwa panga zao.41Watachoma nyumba zako na kufanya matendo mengi ya adhabu juu yako kwenye uso wa wanawake wengi, kwa kuwa nitausimamisha ukahaba wako, na hutawalipa tena wapenzi wako.42Kisha nitatuliza ghadhabu yangu juu yako; hasira yangu itakuacha, kwa kuwa nitaridhika, na sitakuwa na hasira tena.

43Kwa sababu hukuzikumbuka siku za ujana wako na kunifanya nitetemeke kwa hasira kwa sababu ya haya mambo yote, kwa hiyo, tazama! Mimi mwenyewe nitashusha kwa kichwa chako mwenyewe adhabu kwa kile ulichokifanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Hutaongeza ukahaba kwa matendo yako yote ya machukizo?

44Tazama! Kila mtu azungumzaye Mithali kuhusu wewe atasema, “Kama alivyo, hivyo pia ni binti yake.”45Wewe ni binti wa mama yako, amchukiaye mume wake na mtoto wake, na wewe ni dada wa dada zako aliyewachukia waume zao na watoto wao. Mama yako alikuwa Mhiti, na baba yako alikuwa Mwamori.46Dada yako mkubwa alikuwa Samaria na binti zake walikuwa wale waliokuwa wakiishi kaskazini, wakati dada yako mdogo alikuwa ni yule aliyekuwa akiishi kusini mwako, ambaye ni, Sodoma na binti zake.47Hukuenenda katika njia zao na kuchukua tabia zao na matendo yao, lakini katika njia zako zote ulikuwa mbaya zaidi kuliko walivyokuwa wao.48Kama niishivyo- hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-dada yako Sodoma na binti zake, hawajafanya uovu mwingi kama wewe ulivyofanya na binti zako walivyofanya.

49Tazama! Hii ilikuwa dhambi ya dada yako Sodoma: Alikuwa na kiburi katika mafanikio yake, uzembe na kutojali kuhusu chochote. Hakuitia nguvu mikono ya maskini na watu wahitaji.50Alikuwa na kiburi na kufanya machukizo mbele yangu, hivyo niliwatoa kama nilivyoona.51Samaria hakufanya hata nusu ya dhambi zako; badala yake, umefanya machukizo mengi kuliko walivyofanya, na umewaonyesha hao dada zako walikuwa bora kuliko wewe kwa sababu ya machukizo yako uyafanyayo!52Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe; kwa njia hii umewaonyesha dada zako walikuwa bora kuliko wewe, kwa sababu ya dhambi ulizozifanya katika hayo machukizo yako yote. Dada zako sasa wanaonekana bora kuliko wewe. Hasa wewe, umeonyesha aibu yako mwenyewe, kwa njia hii umewaonyesha kwamba dada zako walikuwa bora kuliko wewe.

53Kwa kuwa nitarudisha masalia wao-masalia ya Sodoma na binti zake, na masalia ya Samaria na binti zake; lakini masalia yako yatakuwa miongoni mwao.54Kwa kufikiria haya mambo utaonyesha aibu yako; utakuwa mnyenyekevu kwa sababu ya kila kitu ulichokifanya, na kwa njia hii utakuwa faraja kwao.55Hivyo dada yako Sodoma na binti zake watarudishwa kwenye hali yao ya zamani, na Samaria na binti zake watarudishwa kwenye mashamba yao ya zamani. Kisha wewe na binti zako watarudishwa kwenye hali yako ya kawaida.56Sodoma dada yako hakutajwa hata kwa kinywa chako katika siku ulipojiinua,57kabla uovu wako haujafunuliwa. Lakini sasa wewe ni kitu cha dharau kwa binti za Edomu na binti wote wa Wafilisti waliomzunguka. Watu wote wanakudharau wewe.58Utaonyesha aibu yako na matendo yako ya machukizo! -Hivi ndivyo Yahwe asemavyo!

59Bwana Yahwe asema hivi: Nitashughulika na wewe kama unavyostahili, wewe uliyedharau kiapo chako kwa kulivunja agano.60Lakini mimi mwenyewe nitalikumbuka agano langu nililolifanya pamoja nawe katika siku za ujana wako, nitaliimarisha agano la milele pamoja na wewe.61Kisha utazikumbuka njia zako na kuona aibu utakapo wapokea dada zako wakubwa na dada zako wadogo. Nitakupatia wao kama binti zako, lakini kwa sababu ya agano lako.62Mimi nitaweka imara agano langou pamoja nawe, nawe utajua yakwamba mimi ni Yahwe.63Kwa sababu ya haya mambo, utakumbuka kila kitu na kuona aibu, hutafungua mdomo wako tena kuongea kwa sababu ya aibu yako, wakati nitakapokusamehe kwa yale yote uliyoyafanya-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

17

1Neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, tega kitendawili na sema fumbo kwa nyumba ya Israeli.3Sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tai mkubwa pamoja na mabawa makubwa, mwenye kujaa manyoya, na aliyekuwa na rangi nyingi alienda Lebanoni na kuchukua kilele cha mti wa mwerezi4Akakata ncha za matawi na kuzichukua hata nchi ya Kanaani; akaipanda katika mji wa wachuuzi.

5Pia akachukua mbegu ya nchi na kuipanda katika udongo wenye rutuba. Akaiweka kando ya maji mengi kama mti umeao karibu na maji.6Kisha ukachipusha na mzabibu wenye kusambaa chini kwenye ardhi. Matawi yake yakamwelekea yeye, na mizizi yake ikakua chini yake. Hivyo ukawa mzabibu na kuzaa matawi na kutoa matawi.

7Lakini kulikuwa na tai mwingine mkubwa wenye mabawa makubwa na manyoya mengi. Tazama! Huu mzabibu ukabadilisha mizizi yake kumwelekea tai, na ukasamabaza matawi yake kumwelekea tai kutoka mahali ulipokuwa umepandwa basi upate kumwagiliwa.8Ulikuwa umepandwa kwenye udongo mzuri kando ya maji mengi hivyo ungezaa matawi na kuanza kutoa matunda, ili kuwa mzabibu mzuri kabisa.’

9Waambie watu, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Je! Huo utafanikiwa? Je! Haitaing'oa mizizi yake na kuyakata matunda yake ili kwamba unyauke, na majani yake yote mabichi yanyauke? Hakuna jeshi imara au watu wengi watahitajika kuivuta kwa mizizi yake.10Basi tazama! Baada ya kuwa umepandwa, je utakua? Je hautanyauka wakati upepo wa mashariki utakapoupiga? Utanyauka kabisa katika kiwanja chake.”’

11Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,12“Waambie nyumba ya uasi, ‘Je! Hamjui maana ya mambo haya? Tazama! Mfalme wa Babeli amekuja Yerusalemu na kumchukua mfalme wake na wakuu wake na kuwaleta kwake mpaka Babebli.13Kisha akauchukua ukoo wa kifalme, akafanya agano pamoja naye, na kumleta chini ya kiapo. Akawachukua watu wa nchi wenye nguvu,14basi ufalme uwe duni na usijiinue wenyewe. Kwa kulitunza agano lake nchi itaokoka.15Lakini mfalme wa Yerusalemu ameasi juu yake kwa kupeleka mabalozi kwenda Misri ili kujipatia farasi na jeshi. Je! Atafanikiwa? Je! Yeye anayeyafanya haya mambo ataokoka?

16Kama niishivyo! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-atakufa hakika katika nchi ya mfalme aliyemfanya mfalme, yule mfalme ambaye aliyekidharau kiapo chake, na ambaye aliyevunja agano lake. Atakufa kati ya Babeli.17Farao na jeshi lake lenye nguvu na kusanyiko la watu wengi kwa ajili ya vita hawatamlinda katika vita, wakati jeshi la Wababeli watakapojenga tuta la ngome na kuta za ngome ili kuyaharibu maisha ya wengi.18Kwa kuwa mfalme amedharau kiapo chake kwa kulivunja agano. Tazama, ameunyoosha kwa mkono wake ili kufanya ahadi na bado ameyafanya haya mambo yote. Hataokoka.

19Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, Je! Hiki hakikuwa kiapo changu kwamba alidharau agano langu alilo livunja? Basi nitaleta nitamwadhibu juu ya kichwa chake!20Nitausambaza wavu wangu juu yake, na atanaswa katika wavu wangu wa kutegea. Kisha nitamleta hata Babeli na kuzitekeleza hukumu juu yake huko kwa ajili ya uhaini wake alioufanya amenisaliti!21Wakimbizi wake wote katika majeshi yake yataanguka kwa upanga, na wale watakaobakia watatawanyika kila mahali. Kisha utajua ya kwamba mimi ni Yahwe; nimesema hili litatokea.”

22Bwana Yahwe asema hivi, ‘Basi mimi mwenyewe nitaichukua sehemu ya juu ya mti wa mwerezi, na nitaupanda mbali na matawi yake laini. Nitaukata, na mimi mwenyewe nitaupanda juu ya mlima mrefu.23Nitaupanda juu ya milima ya Israeli hivyo utazaa matawi na kuzaa matunda, na utakuwa mwerezi wa fahari ili kwamba kila ndege arukaye ataishi chini ya huo. Watajenga viota chini ya kivuli cha matawi yake.24Kisha miti yote ya shambani itajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeishusha miti mirefu na nimeiinua juu miti mifupi. Naunyausha mti mbichi na kuufanya mti mkavu kuchanua. Mimi Yahwe, nimesema hivyo hii itatokea; nami nimelifanya hili.’”

18

1Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,2“Je mna maana gani, ninyi mliotumia hii mithali kuhusiana na nchi ya Israeli na kusema, ‘Wababa wamekula zabibu mbichi, na meno ya watoto imetiwa ganzi’?

3Kama nishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-bila shaka hakutakuwa na fursa yoyote tena kwa ajili yenu kuitumia hii mithali katika Israeli.4Tazama! Kila uhai ni mali yangu-uhai wa baba na uhai wa mwana pia, ni mali yangu! Roho itendayo dhambi ndiyo itakayo kufa!
5Itasemwaje kuhusu mtu mwenye haki na achukuaye yaliyo halali na haki-
6kama asipokula juu ya milima au kuinua macho yake kwa sananmu za nyumba ya Israeli, na hakumnajisi mke wa jirani yake, wala kumsemesha mwanamke katika kipindi chake cha mwezi, je! Yu mwenye haki?
7Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakumnyang'anya yeyote, na kumrudisha mdeni wake kwa kile kilichokuwa kimewekwa kwa ajili ya rehani, na hakuiba lakini kuwapatia chakula wenye njaa na kuwafunika uchi kwa nguo, je yu mwenye haki?
8Je! Itasemwaje kuhusu mtu ambaye hakuchukua faida kubwa kwa ile pesa aliyokopa, na hakuchukua faida kubwa kwa kile alichokiuza?
9Amesemwa kwamba amechukua yaliyo halali na kuimarisha uaminifu kati ya watu. Kama huyo mtu akitembea katika sheria zangu na kuzishika hukumu zangu kufanya kwa uaminifu, kisha ahadi kwa ajili ya mtu mwenye haki ni hii: Ataishi hakika! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

10Lakini akizaa mwana mnyang'anyi, mmwaga damu na kufanya mengi katika haya mambo kama yalivyotajwa hapa,
11hata kama baba yake hakufanya mojawapo katika haya mambo, lakini akala juu ya milima na akamnajisi mke wa jirani yake, Je! Itasemwaje juu yake?
12Huyu mtu huwadhulumu maskini na wahitaji, na huwakamata na kuwanyang'anya, na hawarudishii dhamana, na huyainua macho yake kwa sanamu na kufanya matendo maovu,
13na hukopesha pesa kwa faida ya juu sana na kufanya faida kubwa juu ya anachokiuza, Je! Huyo mtu ataishi? Hakika hataishi! Atakufa hakika na damu yake itakuwa juu yake kwa sababu amefanya haya mambo ya chuki.

14Lakini Tazama! Tuseme kuna mtu aliyezaa mwana, na mwana wake huona dhambi zote za baba yake alizozifanya, na kupitia kuziona, hakuyafanya hayo mambo.
15Huyo mwana hakula juu ya milima, na hakuinua macho yake kwa sanamu za nyumba ya Israeli, na hakumtia unajisi mke wa jirani yake, Je! Itasemwaje juu yake?
16Yule mwana hakumdhulumu yeyote, au kutwaa dhamana, au kupoteza vitu, lakini badala yake kutoa chakula chake kwa wenye njaa na kuwafunika wenye uchi kwa nguo.
17Huyo mwana hakumkandamiza yeyote au au kuchukua faida ambayo ni ya juu sana au kufanya manufaa kwa ajili ya mkopo, lakini ameyashika maagizo yangu na kuenenda sawa sawa na sheria zangu; huyo mwana hatakufa kwa ajili ya dhambi za baba yake: Ataishi hakika!
18Baba yake, kwa kuwa aliwakandamiza wengine kwa nguvu nyingi na kumnyang'anya ndugu yake, na kufanya yasiyo mema miongoni mwa watu wake-tazama, atakufa katika uovu wake.

19Lakini ninyi husema, ‘Kwa nini mwana asibebe uovu wa baba yake?’ Kwa sababu mwana hubeba yaliyo halali na haki na kuzitunza amri zangu; huzifanya. Ataishi hakika!20Yule atendaye dhambi, ndiye ambaye atakufa. Mwana hatabeba uovu wa baba yake, na baba hatabeba uovu wa mwana wake. Haki ya yule atendaye haki itakuwa juu yake mwenyewe, na uovu wa mwenye uovu utakuwa juu yake mwenyewe.

21Lakini kama mwovu ageukapo kutoka dhambi zake zote alizofanya, na kuzitunza sheria zangu zote na kufanya yaliyo halali na haki, kisha hakika ataishi na hatakufa.22Makosa yote aliyoyafanya hayatakumbukwa juu yake. Ataishi kwa hiyo haki aliyoitenda.23Je! Nitafurahia juu ya kifo cha mwovu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na sio katika kugeuka kwake kutoka njia yake ili kwamba aweze kuishi?

24Lakini kama mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki yake na kufanya maovu na kutenda machukizo kama machukizo yote ambayo mtu mwovu afanyayo, basi ataishi? Haki yake yote aliyoifanya haitakumbukwa wakati atakaponisaliti katika uhaini wake. Hivyo atakufa katika dhambi alizofanya.

25Lakini ninyi husema, ‘Njia ya Bwana si sawa!’ sikilizeni, nyumba ya Israeli! Je njia zangu haziko sawa? Je si njia zenu ambazo haziko sawa?26Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye makosa yake, na kufanya maovu na kufa kwa sababu ya hayo, kisha atakufa katika uovu ambao alioufanya.27Lakini wakati mtu mwovu ageukapo kutoka uovu wake alioufanya na kufanya yaliyo halali na haki, kisha ataulinda uhai wake.28Kwa kuwa ameona na kugeuka kutokana na makosa yake yote ambayo aliyoyafanya. Hakika ataishi, na hatakufa.29Lakini nyumba ya Israeli husema, ‘Njia ya Bwana haiko sawa!’ Ni namna gani njia zangu si sawa, nyumba ya Israeli? Ni njia zenu ndizo si sawa.

30Kwa hiyo nitamuhukumu kila mtu miongoni mwenu kulingana na njia zake, nyumba ya Israeli! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo. Tubuni na rudini kutoka kwenye makosa yenu yote ili kwamba yasiwe kikwazo cha uovu dhidi yenu. Asemavyo-hivyo tubuni na muishi!”31Tupilia mbali makosa yenu yote mliyoyafanya; jifanyieni moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, nyumba ya Israeli?32Kwa kuwa sifurahii kifo cha yule afaye-hivi ndivyo Bwana Yahwe.

19

1“Tena wewe, chukua maombolezo juu ya viongozi wa Israeli2na sema, ‘Mama yako alikuwa nani? Simba jike mmoja, aliishi na mtoto wa simba dume; katikati ya simba wadogo, aliwalisha watoto wake.

3Alimlea mmoja wa wale watoto kurarua wanyama wengine, na kisha alijifunza jinsi ya kuwinda watu na kuwala.
4Kisha mataifa wakasikia kuhusu yeye. Akakamatwa kwenye mtego wao, na wakamleta kwa kulabu hata nchi ya Misri.
5Kisha alipoona kwamba ingawa alikuwa akimsubiri arudi, matumaini yake sasa yalienda, hivyo alimchukua mtoto wake wengine katika watoto wake na kumlea hata kuwa mwana simba.
6Huyu mwana simba alitembea huku na huku katikati ya simba. Akawa mwana simba na kujifunza kuwinda mawindo; akala watu.
7Akawakamata wajane na kuiharibu miji. Nchi na viijazavyo vilitelekezwa kwa sababu ya sauti ya kunguruma kwake.
8Lakini mataifa yakaja juu yake kutoka mikoa yote; wakatengeneza nyavu juu yake. Akakamatwa kwenye mtego wao.
9Kwa kulabu wakamuweka kwenye tundu na kisha wakamleta hata kwa mfalme wa Babeli. Wakamleta hata kwenye ngome imara ili kwamba sauti yake isiweze kusikika juu ya milima ya Israeli.
10Mama yako alikuwa kama mzabibu uliopandwa kwenye damu yako karibu na maji. Ulizaa matunda na kujaa matawi kwa sababu ya wingi wa maji.
11Ulikuwa na matawi imara yaliyokuwa yakitumika kwa ajili ya fimbo ya utawala, na kipimo chake kiliinuka juu ya matawi, na urefu wake ulionekana kwa ukubwa wa majani yake.
12Lakini mzabibu uling'olewa kwa ghadhabu na kutupwa chini hata aridhini, na upepo wa mashariki uliuvunja na kunyauka na moto ukavila.
13Hivyo sasa, umepandwa jangwani, kwenye nchi ya ukame na kavu.
14Kwa kuwa moto ulitoka kwenye matawi makubwa na kuyala matunda yake. Hakuna tawi imara juu yake, hakuna fimbo ya kifalme kutawala.’ Haya ni maombolezo na yataimbwa kama maombolezo.”

20

1Ikawa ikaja katika mwaka wa saba, siku ya kumi ya mwezi wa tano, wazee wa Israeli wakaja kumuuliza Yahwe na kuketi mbele yangu.

2Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,3“mwanadamu, tangaza kwa wazee wa Israeli na uwaambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Je! Mmekuja kuniuliza swali? Kama niishivyo, sitaulizwa swali na ninyi! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’

4Je! Utawahukumu? Utamuhukumu, mwanadamu? Wajulishe kuhusu machukizo ya baba zao.5Waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyoichagua Israeli na kuinua mkono wangu kuapa kiapo kwa uzao wa nyumba ya Yakobo, na kufanya kujulikana mimi mwenyewe kwao katika nchi ya Misri, wakati nilipoinua mkono wangu kuapa kiapo kwao. Nalisema, “Mimi ni Yahwe Mungu wenu”-6siku hiyo niliinua mkono wangu kuapa kiapo kwa ajili yao kwamba nitawatoa kutoka nchi ya Misri kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimeichagua kwa umakini kwa ajili yao. Ilikuwa ikitiririka maziwa na asali; ilikuwa nzuri sana utukufu miongoni mwa nchi mbali mbali.7Nikawaambia, “Kila mtu atupilie mbali mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake na sanamu za Misri. Msijitie unajisi; mimi ni Yahwe Mungu wenu.”

8Lakini wameasi juu yangu hawakuwa tayari kunisikiliza. Kila mtu hakutupilia mbali mambo ya machukizo kutoka mbele ya macho yake wala kwa ajili ya sanamu za Misri, hivyo nikaona nimwage ghadhabu yangu juu yao kukamilisha hasira yangu miongoni mwao katikati ya nchi ya Misri.9Nilifanya kwa ajili ya jina langu ili lisinajisiwe katika macho ya mataifa ambao walikaa pamoja nao. Nilijifanya mwenyewe kujulikana kwao, katika macho yao, kwa kuwatoa katika nchi ya Misri.10Basi nikawatoa katika nchi ya Misri na kuwaleta kwenye jangwa.11Kisha nikawapa amri zangu na kufanya maagizo yangu kujulikana kwao, kwa kila mwanadamu atakayezishika ataishi.12Pia nikawapatia Sabato zangu kama ishara kati yangu na wao, ili wajue kwamba mimi ni Yahwe niwafanyao wawe watakatifu.

13Lakini nyumba ya Israeli imeasi dhidi yangu jangwani. Hawakuenenda katika amri zangu; badala yake, wameyakataa maagizo yangu, ambayo mwanadamu ataishi kama akiyatii. Wamezinajisi Sabato zangu sana, basi nikasema nitamwaga hasira yangu juu yao jangwani ili kuwamalliza.14Lakini nilifanya kwa ajili ya jina langu hivyo lisinajisiwe katika macho ya mataifa, ambao niliwatoa mbele ya macho yao kutoka Misri.15Basi mimi mwenyewe pia nimeinua mkono wangu kuapa kiapo kwao jangwani sitawarudisha kwenye nchi ile niliyokuwa naenda kuwapatia, nchi inayotiririkayo maziwa na asali, ambayo ilikuwa nzuri sana ambayo ni nzuri kati ya nchi zote.16Nimeapa hivi kwa sababu walikataa maagizo yangu na kutotembea katika amri zangu, na wazikufuru Sabato zangu.17Lakini jicho langu likawahurumia kutokana na uharibifu na sikuwaangamiza jangwani.18Nikawaambia watoto wao jangwani, “Msitembee kutokana na amri za wazazi wenu; msiweke maagizo yao au kujinajisi wenyewe kwa sanamu.19Mimi ni Yahwe Mungu wenu, tembeeni katika amri zangu; tunzeni maagizo yangu na kuyatii.20Zitunzeni Sabato zangu takatifu ili kwamba zitakuwa ishara kati yangu na ninyi, hivyo basi mtajua ya kwamba mimi ni Yahwe Mungu wenu.”

21Lakini watoto wao waliniasi. Hawakutembea kwenye sheria zangu au kushika maagizo yangu, ambazo mwanadamu ataishi kama akizitii. Wamezinajisi Sabato zangu, hivyo nimeamua kumwaga ghadhabu yangu juu yao kutimiza ghadhabu yangu dhidi yao katika jangwa.22Lakini niliurudisha mkono wangu na kutenda kwa ajili ya jina langu, hivyo lisitiwe unajisi katika macho ya mataifa ambao mbele ya macho yao niliwatoa Waisraeli.23Mimi mwenyewe pia nimeuinua mkono wangu kuapa juu yao jangwani, kwamba nitawatawanya kati ya maifa na kuwatawanya miongoni mwa nchi mabali mbali.24Nimeamua kufanya hivi kwa kuwa hawakuzitii amri zangu, na tangu walipo zikataa sheria zangu na kuzinajisi Sabato zangu. Macho yao yalizitamani sanamu za baba zao.25Kisha niliwapa amri ambazo hazikuwa nzuri, na maagizo ambayo hawakuweza kuishi kwayo.26Nikawafanya unajisi kwa zawadi zao wakati walipofanya dhabihu za kila limbuko la tumbo la uzazi na kutupa kwenye moto. Nalifanya hivi ili kuwaogofya hivyo wangeweza kujua kwamba mimi ni Yahwe!’

27Kwa hiyo, mwanadamu, waambie nyumba ya Israeli na waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Katika hili pia baba zenu walinikufuru wakati walipokuwa sio waaminifu kwangu.28Wakati nilipowaleta kwenye nchi ambayo niliyokuwa nimewaapia kuwapatia, na kisha popote walipoona jiwe lolote refu na mti wenye majani, walitoa sadaka zao, walinikasirisha kwa sadaka zao, na huko pia walichoma ubani wao wa kunukia na kumwaga sadaka zao za kinywaji.29Kisha nikawaambia, “Nini maana ya mahali palipoinuka ambapo mmeleta sadaka huko?” Hivyo jina lake linaitwa Bama hata leo.’

30Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Je! Kwa nini unajinajisi mwenyewe kwa njia za baba zako? Kwahiyo kwa nini unatenda kama makahaba, kutafuta kwa ajili ya mambo ya machukizo?31Kwa kuwa wakati mtoapo zawadi zenu na kuwaweka watoto wenu kwenye moto, siku hii mnajitia unajisi pamoja na sanamu zenu zote. Kwa hiyo kwa nini niwaache mniulize mimi, nyumba ya Israeli? Kama niishivyo-Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Sitawaacha mniulize swali.

32Mawazo yanayoumbika kwenye moyo wako hayatatokea kamwe. Mmesema, “Ngoja tuwe kama mataifa mengine, kama koo za nchi nyingine waabuduo miti na mawe.”33Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-Nitatawala hakika juu yenu kwa mkono wenye nguvu, mkono ulionyooshwa, na ghadhabu itakayomwagwa juu yenu.34Nitawatoa kutoka kwa watu wengine na kuwakusanya kutoka kwenye nchi mlizotawanyika ndani mwao. Nitafanya hivi kwa mkono hodari na kwa ghadhabu iliyomwagika.35Kisha nitawaleta kwenye jangwa la watu, na huko nitawahukumu uso kwa uso.36Kama nilivyo wahukumu baba zenu katika jangwa la nchi ya Misri, hivyo pia nitawahukumu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.37Nitawafanya mpite chini ya fimbo yangu, na nitawafanya kutii maagizo yangu ya agano.38Nitawasafisha kutoka miongoni mwenu maasi na wale ambao walionichukiza. Nitawatoa kutoka nchi ambayo wanayoishi kama wageni, lakini hawataingia kwenye nchi ya Israeli. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.

39Basi kwenu, nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Kila mmoja wenu ataenda kwa sanamu zake mwenyewe. Muziabudu kama mtakataa kunisikiliza, lakini hamtalikufuru tena jina langu takatifu kwa zawadi zenu na sanamu zenu.40Kwa kuwa juu ya mlima wangu mtakatifu, juu ya kilele cha mlima wa Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-wote wa nyumba ya Israeli mtaniabudu huko katika nchi. Nitabarikiwa kwa kutaka sadaka zenu huko, na pia malimbuko yenu ya shukrani pamoja na vitu vyenu vyote vitakatifu.41Nitawapokea kama harufu nzuri ya ubani wakati nitakapowatoa kutoka wale watu na kuwakusanya toka nchi ambazo mlizotawanyika. Nitajifunua mimi mwenyewe kama mtakatifu ndani yenu kwa ajili ya mataifa waone.42Kisha, wakati nitakapowaleta katika nchi ya Israeli, kwenye nchi ambayo niliuinulia mkono wangu kuapa kuwapatia baba zenu, mtajua ya kwamba mimi ni Yahwe.43Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya huko, na matendo yenu yote machafu mliyoyafanya wenyewe, na mtajichukia wenyewe katika macho yenu kwa matendo yenu yote maovu mliyoyafanya.44Hivyo mtajua kwamba mimi ni Yahwe nifanyapo haya kwenu kwa ajili ya jina langu, sio kwa njia zenu mbaya au matendo yenu mabovu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

45Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,46“Mwanadamu, weka uso wako kuelekea nchi za kusini, na kuongea juu ya kusini; tabiri juu ya msitu wa Negebu.47Uuambie msitu wa Negebu, ‘Hivi ndivyo Yahwe asemavyo-Bwana Yahwe asema hivi: Tazama, nitaweka moto ndani yako. Utakula kila mti mbichi na kila mti mkavu ndani yako. Miali ya moto haitazimika; na kila uso utokao kusini hata kaskazini utateketezwa kwa moto.48Kisha watu wote wenye mwili watajua ya kwamba mimi ni Yahwe nimeuwasha moto, na hautazimika.”’

49Kisha nimesema, Ee! Bwana Yahwe, Wananisema mimi, ‘Je! Yeye sio mwenye kusema mafumbo?”’

21

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, weka uso wako kuelekea Yerusalemu, na neno juu ya patakatifu; tabiri juu ya nchi ya Israeli.3Sema juu ya nchi ya Israeli, ‘Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako! Nitautoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake na kuwakatilia mbali wote yaani mtu mwenye haki na mtu mwovu kutoka kwako!4Ili niwakatilie mbali wote, mwenye haki na mwovu kutoka kwako, upanga wangu utatoka kwenye ala yake juu ya wote wenye mwili kutoka kusini hata kaskazini.5Kisha wote wenye mwili watajua yakwamba mimi, Yahwe, nimeutoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake. Hautarudi tena!’

6Kwa hiyo, mwanadamu, gumia kama kuvunjika kwa viuno vyako! Katika uchungu gumia mbele ya macho yao!7Kisha itatokea kwamba watakuuliza, ‘Kwa sababu gani unalia?’ Kisha utasema, ‘Kwa sababu ya habari inayokuja, kwa kuwa kila moyo utakuwa dhaifu, na kila mkono utasita! Kila roho itazimia, na kila goti litatiririrka kama maji. Tazama! Inakuja na itakuwa kama hivi! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

8Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,9“Mwanadamu, tabiri na sema, ‘Bwana asema hivi: sema: Upanga! Upanga! Utachongwa na kusuguliwa!
10Utanolewa ili kushiriki katika machinjio makubwa! Utasuguliwa ili uwe kama mng'ao wa radi! Je! Tufanye furaha katika fimbo ya mwana wa mfalme? Upanga ujao huchukia kila hiyo fimbo!
11Hivyo upanga utatolewa kwa ajili ya kusuguliwa, na kisha kushikika kwa mkono! Upanga umechongwa na umesuguliwa na utatolewa kwenye mkono wa yule auaye!’
12Ita msaada na omboleza, mwanadamu! Kwa kuwa upanga umekuja juu ya watu wangu! Uko juu ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa dhidi ya upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo, piga paja lako!
13Kwa kuwa kuna kujaribiwa, lakini itakuwaje kama fimbo ya kifalme haitakuwepo tena? -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
14Basi wewe, mwanadamu, tabiri, na piga makofi, kwa kuwa upanga utakushambulia hata mara tatu! Upanga kwa wale watakaochinjwa! Utakuwa upanga kwa ajili ya kuchinjia, ukiwatoboa pande zote!
15Ili kuyeyusha mioyo yao na kuongeza kuanguka kwao, nimeweka machinjio ya upanga juu ya malango! Ole! Umeundwa kama mng'ao wa radi, umetengwa kwa ajili ya kuua!
16Wewe, upanga! Nyooka upande wa kuume! Nyooka upande wa kushoto! Nenda popote ulipoelekeza uso wako.
17Kwa kuwa pia nitapiga mikono yangu miwili kwa pamoja (makofi), na kisha nitaleta ghadhabu yangu kwa waliobakia! Mimi, Yahwe, nimesema hivi!”

18Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,19“Sasa wewe, mwanadamu, teua njia mbili kwa ajili ya upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja. Njia hizo mbili zitaanza katika nchi moja, na kibao cha barabarani kitamwonyesha mmoja wao kama kuuelekea mji.20Onyesha njia moja kwa ajili ya jeshi la Wababeli kuja Raba, mji wa Waamoni. Onyesha nyingine kuelekea jeshi la Yuda na mji wa Yerusalemu, ambayo imeimarishwa.21Kwa kuwa mfalme wa Babeli atasimama kwenye makutano ya barabara, kwenye njia panda, ili kufanya uganga. Alitingisha mishale na kuuliza mwelekeo kutoka kwa sanamu na atalichunguza ini.22Katika mkono wake wa kuume kutakuwa na dalili kuhusu Yerusalemu, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya hiyo, kufungua kinywa chake kupanga kuchinja, kutoa sauti ya vita, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya malango, kujenga ngazi, na kusimamisha wima minara ya boma.23Itaonekana kuwa ishara isiyofaa katika macho ya wale walio katika Yerusalemu, wale walioapa kiapo kwa Wababeli! Lakini mfalme atawashtaki kwa kuvunja sheria ya mkataba ili kuwabariki!

24Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umeuleta uovu wako kwenye kumbukumbu zangu, makosa yenu yatafunuliwa! Dhambi zenu zitaonekana katika matendo yenu yote! Kwa sababu hii utamkumbusha kila mtu mtakamatwa kwa mkono wa adui yenu!

25Kama wewe, mchafu na mtawala mwovu wa Israeli, ambaye siku ya hukumu imekuja, na ambaye mda wa kufanya uovu umekoma,26Bwana Yahwe asema hivi kwako: Toa kilemba na vua taji! Mambo hayatakuwa tena kama yalivyokuwa! Kiinue kilicho chini na kiinue kilichoinuka!27Uharibifu! Uharibifu! Nitaiharibu! Haitakuwa tena hadi atakapokuja yeye ambaye ameteuliwa kutekeleza hukumu.

28Basi wewe, mwanadamu, tabiri na sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi hawa ni watu wa Amoni kuhusiana na ujio wa aibu yao: Upanga, upanga umefutwa! Umenolewa kwa ajili ya kuchinja, hivyo utakuwa kama kimuli muli cha radi!
29Wakati manabii wameona maono ya uongo juu yako, wakati watakapofanya matambiko kuuijia kwa uongo juu yako, huu upanga utaanguka chini juu ya shingo za mwovu ambao wako karibu kuuawa, ambao siku ya ghadhabu imekuja na ambao mda wa uovu unakaribia kuisha.
30Rudisha upanga kwenye ala yake. Katika mahali ulipoumbwa, katika nchi ya chimbuko lako, nitakuhukumu!
31Nitamwaga hasira yangu juu yako! Nitapuliza upepo wa moto wa ghadhabu juu yako na kukuweka kwenye mkono wa watu wakatili, watu wajuao kuangamiza!
32Utakuwa kuni kwa ajili ya moto! Damu yako itakuwa kati ya nchi. Hutakumbukwa tena, kwa kuwa mimi, Yahwe nimesema hivi!”’

22

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Sasa wewe, mwanadamu, Je! Utanihukumu? Utauhukumu mji kwa damu? Mfanye ajue machukizo yake yote.3Utasema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Huu ndiyo mji umbao umwagao damu kati yake ili kwamba muda wake ufike; mji ufanyao sanamu ili ujitie unajisi.4Umekuwa na hatia kwa damu uliyoimwaga, na kufanya unajisi kwa sanamu ulizozitengeneza. Kwa kuwa umezileta karibu siku zako na kuzikaribia siku zako za mwisho. Kwa hiyo nitakufanya lawama kwa mataifa na kejeli katika uso wa kila nchi.5Wote walio karibu na wale walio mbali nawe watakudhihaki, wewe mji mchafu, ujulikanao kila mahali kwa sifa mbaya kama kujaa machafuko.

6Tazama! Wakuu wa Israeli, kila mmoja kwa nguvu yake, wamekuja kwako kumwaga damu.7Wamefanya udanganyifu kwa baba na mama ndani yako, na wametenda yaliyo kinyume juu ya wageni kati yako. Wamewatenda vibaya yatima na wajane ndani mwako.8Umevidharau vitu vyangu vitakatifu na kuinajisi Sabato yangu.9Watu wasingiziaji wamekuja kati yako ili kumwaga damu, na hula juu ya milima. Hufanya uovu kati yako.10Uchi wa baba umefunuliwa ndani yako. Wamemtukana mwanamke mchafu ndani yako wakati wa uchafu wake.11Watu waliofanya machukizo pamoja na wake za majirani zao, na watu wafanyao uchafu wa aibu kwa mke wa mwanao mwenyewe; watu wawatukanao dada zao wenyewe-binti za baba zao wenyewe-haya yote yapo miongoni mwanu.12Hawa watu huchukua rushwa kati yenu ili kumwaga damu. Umechukua faida na kuongeza riba nyingi sana, na umenisahau-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

13Tazama! Kwa mkono wangu nimeipiga faida ambayo uliyoitengeneza kwa njia isiyo halali, na damu iliyo kati yako.14Je! Moyo wako utasimama, mikono yako itakuwa hodari katika siku wakati mimi mwenyewe nitakapo kushughulikia? Mimi, Yahwe, nasema hivi, na nitalifanya.15Hivyo nitakutawanya kati ya mataifa na kukutawanya kati ya nchi mbali mbali. Katika njia hii, nitausafisha uchafu kutoka kwako.16Hivyo utakuwa mchafu machoni mwa mataifa. Kisha utajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

17Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,18“Mwanadamu, nyumba ya Israeli imekuwa takataka kwangu. Wote wamekuwa masazo ya shaba na bati, na chuma na risasi kati yenu. Watakuwa kama takataka ya fedha katika tanuu.19Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, ‘Kwa sababu mmekuwa kama takataka, kwa hiyo, tazama! Nataka kuwakusanya katikakati ya mji wa Yerusalemu.20Kama kukusanya fedha na shaba, chuma, risasi na chuma kati ya tanuu ili kuvifukutia moto na kuviyeyusha juu yake, nitawayeyusha. Hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu. Nitawaweka hapo na kufukutisha moto juu yake ili kuiyeyusha; hivyo nitawakusanya katika hasira yangu na ghadhabu yangu, na nitawaweka hapo na kuwayeyusha.21Basi nitawakusanya na kuwafukutia kwa moto wa hasira yangu juu yenu hivyo basi mtamwagwa kati yake.22Kama kuyeyusha fedha kati ya tanuu, mtayeyushwa chini kati yake, na mtajua yakwamba mimi, Yahwe, nimemwaga ghdhabu yangu juu yenu!”’

23Neno la Yahwe likanijia, kusema,24“Mwanadamu, mwambie, ‘Wewe ni nchi ambayo haijasafishwa. Hakuna mvua siku ya hasira!25Kuna njama ya manabii wake kati yake, kama simba angurumaye akirarua mawindo. Wamekula uhai na kuchukua utajiri wa thamani; wamewafanya wajane wengi ndani yake!26Makuhani wake hufanya kinyume na sheria yangu, na wamevinajisi vitu vyangu vitakatifu. Hawawezi kutofautisha kati ya vitu vitakatifu na vitu vya najisi. Wanaficha macho yao kutoka Sabato zangu hivyo basi nimetiwa unajisi kati yao.27Wakuu wake ndani mwake wamekuwa kama mbwa mwitu wakirarua mawindo yao. Wamemwaga damu na kuharibu maisha, ili kupata faida kwa njia ya udanganyifu.28Manabii wake wamepakwa chokaa; wanaona maono ya uongo na kutabiri uongo kwao. Wanasema “Bwana Yahwe asema hivi”’ wakati Yahwe hajanena.29Watu wa nchi wamewakandamiza kwa kutaka kwa nguvu na kuwanyang'anya kwa nguvu, na wamewatesa maskini na wahitaji, na kuwakandamiza wageni bila haki.

30Nami nikatafuta mtu miongoni mwao atakayelitengeneza boma na kusimama mbele zangu mahali palipo bomoka kwa ajili nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.31Hivyo nitaimwaga ghadhabu yangu juu yao. Nitawamaliza kwa moto wa ghadhabu yangu na kuweka njia yao juu ya vichwa vyao wenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

23

1Neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, Kulikuwa na wanawake wawili, binti za mama mmoja.3Walifanya ukahaba katika Misri katika kipindi cha ujana wao. Walitenda kama makahaba huko. Maziwa yao yalikuwa yamebana na ubikira wa chuchu zao zilipapaswa huko.4Majina yao yalikuwa Ohola-dada mkubwa-na Oholiba-dada yake mdogo. Kisha wakawa wangu na kuzaa wana na binti. Majina yao yalikuwa yakimaanisha hivi: Ohola maana yake Samaria, na Oholiba maana yake Yerusalemu.

5Lakini Ohola alifanya kama kahaba hata alipokuwa wangu; aliwatamani wapenzi wake, kwa kuwa Waashuri Jirani zake6liwali aliyekuwa amevaa urijuana, na kwa ajili ya maafisa wake, waliokuwa hodari na wanaume wa kuvutia, wote walikuwa waendesha farasi.7Hivyo akajitoa yeye mwenyewe kama kahaba kwao, kwa watu bora wa Ashuru, na alijitia mwenyewe uchafu pamoja na kila mmoja aliyekuwa amemtamani-pamoja na sanamu zake zote.8Kwa kuwa hakuacha tabia zake za kikahaba nyuma katika Misri, wakati walipolala naye wakati alipokuwa msichana mdogo, wakati walipoanza kwanza kupapasa ubikira wa maziwa yake, wakati walipoanza kummwagia tabia ya uzinzi wao juu yake.

9Kwa hiyo nilimtia kwenye mkono wa wapenzi wake kwenye mkono wa Waashuru kwa kuwa aliwatamani.10Wakamfunua uchi wake. Wakawachukua wana wake na binti, na wakamuua kwa upanga, na akawa aibu kwa wanawake wengine, hivyo wakapitisha hukumu juu yake.

11Dada yake Oholiba akaliona hili, lakini aliyatamani zaidi na kufanya kama kahaba hata zaidi kuliko dada yake.12Aliwatamanai Waashuru, mabosi na watawala waliokuwa wamevaa ngua za ushawishi, walikuwa watu waendesha farasi. Wote walikuwa hodari, wote vijana wa kuvutia.13Nikaona kwamba alikuwa amefanya uchafu mwenyewe. Ilikuwa kama kwa wadada wote.

14Kisha akaongeza ukahaba wake tena zaidi. Aliona watu waume waliokuwa wamechorwa juu ya kuta, michoro ya Wakaldayo iliyochorwa kwa rangi nyekundu,15waliovaa mikanda kuzunguka viuno vyao, na vilemba virefu juu ya vichwa vyao. Wote walikuwa na mwonekano wa maafisa wa jeshi la waendesha farasi, mfano wa wana wa Wababeli, ambao asili ya nchi ni Ukaldayo.16Na mara macho yake yalipowaona, aliwatamani, hivyo akawatuma wajumbe wake kwao katika Ukaldayo.17Kisha Wababeli wakaja katika kitanda chake cha tamaa, na walimfanya unajisi kwa uzinzi wao. Kwa kile alichokuwa amekifanya alifanya unajisi, basi akageuka mwenyewe kutoka kwao katika karaha.18Alionyesha matendo yake ya ukahaba na alionyesha uchi wake, hivyo roho yangu ikageuka kutoka kwake, kama roho yangu ilivyogeuka kutoka kwa dada yake.19Kisha alifanya matendo mengi zaidi ya ukahaba, akakumbuka na kutafakari siku za ujana wake, wakati alipotenda kama kahaba katika nchi ya Misri.20Basi akawatamani wapenzi wake, ambao sehemu zao za siri zilikuwa kama zile za punda, na kile kizaliwacho hutoka kilikuwa kama wale farasi.21Hivi ndivyo ulivyofanya matendo ya aibu ya ujana wako, wakati Wamisri walipopapasa chuchu zako kuyaminya maziwa ya ujana wako.

22Kwa hiyo, Oholiba, Bwana Yahwe asema hivi, ‘Tazama! Nitawarudisha wapenzi wako dhidi yako. Wale ambao uliowarudisha, nitawaleta juu yako kutoka kila upande.23Wababeli na Wakaldayo wote, Pekodi, Shoa, na Koa, na Waashuru wote pamoja nao, hodari, vijana wa kutamanika, magavana na maamiri jeshi, wote ni maafisa na watu wote wenye sifa, wote wenye kuendesha farasi.24Watakuja juu yako kwa silaha, na kwa magari ya farasi na mikokoteni, na kundi kubwa la watu. Watapanga ngao kubwa, ngao ndogo, na kofia za chuma juu yako pande zote. Nitawapatia nafasi kukuadhibu, na watakuadhibu kwa matendo yao.25Kwa kuwa nitaweka hasira yangu ya wivu juu yako, na watashughulika na wewe kwa hasira. Watakukatilia mbali pua zako na masikio yako, na masalia yako wataanguka kwa upanga. Watawachukua wana wako na binti zako, na masalia yako watateketea kwa moto.26Watakuvua nguo zako na kuchukua mapambo yako ya vito.27Hivyo nitaiondoa tabia yako ya aibu kutoka kwako na matendo yako ya kikahaba kutoka nchi ya Misri. Hutainua macho yako kuwaelekea kwa shauku, na hutaikumbuka Misri tena.’

28Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi, ‘Tazama! Nitakutia katika mkono wa wale uwachukiao, kukurudisha kwenye mkono wa wale ambao uliokuwa umewarudisha.29Watashughulika pamoja nawe kwa chuki; watachukua milki zako zote na kukutelekeza uchi na kukuweka wazi. Uchi wa aibu ya ukahaba wako utafunuliwa, tabia yako ya aibu na uzinzi wako.30Haya mambo yatafanyika kwako kwa kuwa umetenda kama kahaba, tamaa za mataifa kwazo umetiwa unajisi kwa sanamu zao.31Umetembea katika njia za dada yako, hivyo nitaweka kikombe chake cha adhabu kwenye mkono wako.’

32Bwana Yahwe asema hivi, ‘Utakinywea kikombe cha dada yako ambacho ni kirefu na kikubwa. Utakuwa dhihaka na kutawaliwa na dharau-hiki kikombe kimejaa kiasi kikubwa.
33Utajazwa kwa ulevi na huzuni, kikombe cha ushangao na uharibifu; kikombe cha dada yako Samaria.
34Utakinywea na kubakia kitupu; kisha utakivunja vunja na kuyararua maziwa yako kuwa vipande vipande. Kwa kuwa nimesema hivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’

35Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi, ‘Kwa sababu umenisahau na kunitupa mbali nyumba ya mgongo wako, basi pia utachukua matokeo ya tabia zako za aibu na matendo ya uasherati.”’

36Yahwe akanambia, “Mwanadamu, Je! Utamhukumu Ohola na Oholiba? Basi waambie matendo yao ya machukizo,37kwa kuwa wamefanya uzinzi, na kwa kuwa kuna damu juu ya vichwa vyao. Wamefanya uzinzi na sanamu zao, na wamewaweka hata wana wao kwenye moto, kama chakula cha sanamu zao.38Kisha waliendelea kufanya hivi kwa ajili yangu: Wamepafanya patakatifu pangu unajisi, na katika siku hiyo hiyo wakainajisi Sabato zangu.39Kwa kuwa walipokuwa wamewachinjia watoto wao kwa ajili ya sanamu zao, kisha wakaja hata patakatifu pangu siku hiyo hiyo kupanajisi! Hivyo tazama! Hivi ndivyo walivyofanya kati ya nyumba yangu.

40Mmewatuma watu kutoka mbali, ambao wajumbe waliwatuma-sasa tazama. Wakaja kweli, ambao uliojiosha kwa ajili yao, uliweka rangi macho yako, na kujipamba kwa mapambo ya vito.41Huko ulikaa kwenye kitanda kizuri na kwenye meza iliyokuwa imepangwa mbele yake ulikuwa umeweka ubani na mafuta yangu.

42Hivyo sauti za watu zilikuwa zimemzunguka; pamoja na watu wa kila aina, hata walevi waliletwa kutoka jangwani, na wakawavalisha vikuku mikononi mwao na mataji mazuri juu ya vichwa vyao.43Kisha nikasema juu yake aliyekuwa ameonywa kwa uzinzi, ‘Sasa watazini pamoja naye, na yeye pamoja nao.’44Wakamwingilia na kulala naye kama watu wamwingiliavyo kahaba. Katika njia hii walilala Ohola na Oholiba, waliokuwa wanawake wazinzi.45Lakini watu wenye haki watapitisha hukumu na kuwaadhibu kama wazinzi, na watawaadhibu kwa hukumu kwa wale wamwagao damu, kwa sababu wao ni wazinzi na damu iko mikononi mwao.

46Hivyo Bwana Yahwe asema hivi: Nitainua kundi la watu juu yao na kuwatoa kuwa kitisho na kuteka nyara.47Kisha hilo kundi la watu litawapiga kwa mawe na kuwakatilia chini kwa panga zao. Watawaua wana wao na binti na kuzichoma nyumba zao.

48Kwa kuwa nitaondoa tabia ya aibu kutoka kwenye nchi na wanawake wote wafundishwe kutokutenda kama makahaba.49Hivyo wataweka tabia yenu ya aibu juu yenu. Mtachukua hatia ya dhambi zenu pamoja na sanamu zenu, na kwa njia hii mtajua yakuwa mimi ni Bwana Yahwe.”

24

1Neno la Yahwe likanijia katika mwaka wa nane mwezi wa kumi na siku ya kumi ya mwezi, kusema,2“Mwanadamu, andika kwa ajili yako jina la hii siku, siku hii sahihi mfalme wa Babeli ameizingira Yerusalimu.3Basi nena mithali juu ya hii nyumba ya kuasi, fumbo moja. Waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: weka sufuria ya kupikia. Iweke na weka maji kwenye hiyo sufuria

4Vikusanye vipande vya chakula ndani yake, kila kipande kizuri-paja na bega-na ijaze kwa mifupa bora.
5Chukua kundi bora na jaza mifupa chini yake. Ilete kuchemsha na ipike mifupa ndani yake.
6Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa mji wa damu. Nitakiongeza chungu cha mbao. Weka kuni nyingi na washa moto. Pika nyama vizuri na changanya katika viungo na iacha mifupa iteketee.
7Kwa kuwa damu iko kati yake. Ameiweka juu ya jiwe laini; hakuimwaga juu ya nchi kuifunika kwa mavumbi,
8hivyo inaleta hasira ya kulipa kisasi. Nimeweka damu yake juu ya jiwe laini ili isifunikwe.
9Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Ole kwa mji wa damu. Nitakiongeza chungu
10Weka kuni nyingi na washa moto. Pika nyama vizuri na changanya katika viungo na acha mifupa iteketee.
11Kisha weka chungu kitupu juu ya mkaa, ili kuchemsha na kuchoma shaba yake, hivyo uchafu wake ndani yake utayeyushwa, kutu yake iteketee.’
12Amechoka kwa sababu ya kazi ya taabu, lakini kutu yake haitoki kwake kwa moto.

13Tabia yako ya aibu iko ndani ya uchafu wako, kwa sababu nimekusafisha, lakini bado hutaweza kuwa msafi. Bado hutakuwa huru kutoka uchafu wako hadi hasira yako itakapotulia kutoka kwako.

14Mimi, Yahwe, nimesema hili, na nitalifanya. Sitatulia wala kupumzika kwa ajili ya hili. Kama njia zako zilivyokuwa, na kama matendo yako, yatakuhukumu! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

15Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,16“mwanadamu! Tazama, nitakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako, walakini hautaomboleza wala kulia wala yasichuruzike machozi yako.17Utagugumia bila kusikika. Usiendeshe mazishi kwa ajili ya aliyekufa. Funga kilemba chako juu yako na vaa viatu miguuni pako, lakini usivalishe shela nywele zako au kula mkate wa watu waombolezao kwa ajili ya kuwapoteza wake zao.”

18Hivyo nimeongea na watu asubuhi, na mke wangu amekufa asubuhi. Asubuhi nimefanya kile nilichokuwa nimeambiwa kukifanya.

19Watu wameniuliza, “Je! Hautatuambia haya mambo yana maana gani, mambo ambayo unayoyafanya?”

20Hivyo nimewaambia, “Neno la Yahwe likanijia, kusema,21‘Waambie nyumba ya Israeli, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitapanajisi patakatifu pangu-fahari ya nguvu yenu, mahali panapopendeza macho yenu, na panapotamaniwa na roho zenu, na wana wenu na binti zenu ambao mliowaacha nyuma wataanguka kwa upanga.22Kisha mtafanya hasa kama nilivyofanya: hutafunika nywele za sehemu ya chini za uso, wala kula mkate wa watu wanaoomboleza!23Badala yake, vilemba vyenu vitakuwa juu ya vichwa, na viatu vyenu miguuni mwenu; hutaomboleza wala kulia, kwa kuwa mtayeyuka katika maovu yenu, na kila mtu atagugumia kwa ya ajili ya ndugu yake.24Hivyo Ezekieli atakuwa ishara kwenu, kama kila kitu ambacho alichokifanya mtafanya wakati hili litakapokuja. Kisha mtajua yakwamba mimi ni Bwana Yahwe!”’

25“Lakini wewe, mwanadamu, siku ambayo nitachukua hekalu lao, ambalo ni furaha yao, kiburi chao, na kile waonacho na kutamaniwa wakati nikiwachukua wana wao na binti-26siku hiyo, mgeni atakuja kwako kukupatia habari!27Siku hiyo kinywa chako kitafunguliwa kwa huyo mgeni na utaongea-hutakuwa bubu tena. Utakuwa ishara kwao hivyo basi watajua kwamba mimi ni Yahwe.

25

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, weka uso wako juu ya watu wa Amoni na tabiri juu yao.3Waambie watu wa Amoni, ‘Sikiliza neno la Bwana Yahwe. Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Kwa sababu umesema, “Aha!” juu ya patakatifu pangu wakati palipotiwa unajisi, na juu ya nchi ya Israeli wakati ilipokuwa ukiwa, na juu ya nyumba ya Yuda wakati walipoenda utumwani,4kwa hiyo, tazama, nitakupatia kwa watu katika mashariki kama milki yao. Watafanya kambi juu yako na kuweka mahema miongoni mwako. Watakula matunda yako na watakunywa maziwa yako.5Nitamfanya Raba malisho ya ngamia na watu wa Amoni shamba la mifugo. Kisha utajua yakwamba mimi ni Yahwe.6Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Umepigia makofi mikono yako na kupiga chapa miguu yako, na kufurahi pamoja na dharau ndani yako dhidi ya nchi ya Israeli.7Kwa hiyo, tazama! Nitanyoosha mkono wangu na kukupatia kama mateka kwa mataifa. Nitakukatilia mbali kutoka watu na kukuangamiza kutoka miongoni mwa nchi! Nitakuharibu, na utajua yakwamba mimi ni Yahwe.’

8Bwana Yahwe asema hivi, ‘Kwa sababu Moabu na Seiri husema “Tazama! Nyumba ya Yuda ni kama kila taifa jingine.”9Kwa hiyo, tazama! Ntafungua miteremko ya Moabu, kuanzia kwenye miji yake juu ya mpaka-uzuri wa Beth Yeshimothi, Baal Meoni, na Kiriathaimu-10kwa watu wa mashariki waliokuwa juu ya watu wa Amoni. Nitawapatia kama milki ili kwamba watu wa Amoni hawatakumbukwa miongoni mwa mataifa.11Hivyo nitafanya hukumu juu ya Moabu, na watajua yakwamba mimi ni Yahwe.’

12Bwana Yahwe asema hivi, Edomu amelipiza kisasi juu ya nyumba ya Yuda na amefanya makosa katika kufanya hivyo.13Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Nitaunyoosha mkono wangu juu ya Edomu na kumharibu kila mtu na wanyama huko. Nitawaharibu, sehemu ya ukiwa, kutoka Temani hata Dedani. Wataanguka kwa upanga.14Nitaweka kisasi changu juu ya Edomu kwa mkono wa watu wangu Israeli, na watafanya kwa Edomu kulingana na hasira yangu na ghadhabu yangu, na wakitajua kisasi changu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’

15Bwana Yahwe asema hivi, ‘Wafilisti wamelipiza kisasi pamoja na uovu na kutoka ndani yao wamejaribu kuiharibu Yuda tena na tena.16Basi hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Tazam! Nitanyoosha mkono wangu dhidi ya Wafilisti, na nitakatilia mbali Wakerethi na kuwaharibu mabaki yaliyobaki karibu na pwani.17Kwa kuwa nitalipiza kisasi kikubwa dhidi yao pamoja na matendo ya ghadhabu kubwa ya adhabu, hivyo watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, nitakapolipiza kisasi juu yao.”’

26

1Hivyo ilikuwa katika mwaka wa kumi na moja, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, kwa sababu Tiro amesema juu ya Yerusalemuu, ‘Aha! Malango ya watu waliovunjika! Amenigeukia; Nitajazwa kwa sababu ameharibika.’3Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, ‘Tazama! Niko juu yako, Tiro, na nitayainua mataifa mengi juu yako kama bahari iiunuavyo mawimbi yake.4Wataziharibu kuta za Tiro na kuiangusha chini minara yao. Nitafagia mavumbi yake mbali na kumfanya kama jiwe tupu.5Atakuwa sehemu ya kuwekea nyavu kati ya bahari, kwa kuwa nimesema hilo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-na atakuwa mateka kwa ajili ya mataifa.6Binti zake walioko mashambani watachinjwa kwa panga, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.’

7Kwa kuwa hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo: Tazama, kutoka kaskazini namleta Nebukadreza mfalme wa Babeli, mfalme wa wafalme, dhidi ya Tiro, pamoja na farasi na magari ya farasi, na pamoja na waendesha farasi na watu wengi.8Atawaua binti zako katika shamba. Ataweka kazi ya boma na kujenga ulaghai dhidi ya kuta zako na kuziinua ngao dhidi yao.9Ataweka vyombo vya kubomolea dhidi ya kuta zako, na vyombo vyake vitaanguka chini ya minara yako.10Farasi zake zitakuwa nyingi kwamba mavumbi yao yatawafunika. Kuta zako zitatikisika kwa mlio wa waendesha farasi, magurudumu, na magari ya farasi. Wakati atakapoingia malango yako, ataingia kama watu waingiavyo kwenye mji ambao kuta zimebomolewa.11Kwato za farasi zake zitaikanyaga mitaa yako yote. Atawaua watu wako kwa upanga na nguzo za uweza wako zitaanguka chini.12Watauteka nyara utajiri wako na bidhaa iliyoporwa. Watabomoa kuta zako na kuziharibu nyumba zako za kifahari. Mawe yako, mbao zako, na kokoto watazitupa kwenye maji.13Nitaikomesha sauti ya nyimbo zako. Sauti ya vinubi haitasikika tena.14Nitakufanya jiwe tupu, utakuwa mahali ambapo nyavu zitasambazwa kuzikausha. Hutajengwa tena, kwa kuwa mimi, Bwana Yahwe nimesema-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

15Bwana Yahwe amwambia hivi Tiro, ‘Je visiwa havitatetemeka kwa mlio wa kuanguka kwako, na pamoja na watakaogumia kwa jeraha wakati machinjio mabaya yatakapokuwa kati yako?16Kisha wakuu wote wa bahari watakaposhuka kutoka kwenye viti vyao vya enzi na kuvua mavazi yao rasmi na kutupa mavazi yaliyonakshiwa. Watavaa wenyewe kwa kutetemeka, wataketi chini na kutetemeka kila wakati, na wataogopa kwa sababu yako.17Watainua maombolezo juu yako na kukwambia, umekuwaje, uliyekuwa umekaliwa na manahodha wa meli, umeharibika. Mji mashuhuri ulikuwa imara sana-sasa umetoka kwenye bahari. Wale wanaoishi ndani yake wanaotia hofu kuhusu wenyewe juu ya kila mmoja aliyeishi karibu nao.
18Sasa fukwe zitatetemeka katika siku ya kuanguka kwako. Visiwa katika bahari vimeogofya, kwa sababu umekufa.’

19Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: wakati nitakapokufanya wewe mji kuwa ukiwa, kama miji mingine ambayo haikaliwi, wakati nitakapoviinua vilindi dhidi yako, na wakati maji makuu yatakapokufunika,20kisha nitakushusha chini kwenda kwa watu wa nyakati za zamani, kama wengingine walioenda chini kwenye shimo; kwa kuwa nitakufanya uishi katika falme za chini za dunia kama uharibifu wa nyakati za zamani. Kwa sababu hii hutarudi na kusimama katika nchi ya walio hai.21Nitaweka janga juu yako, na hutakuwepo tena milele. Kisha utatafutwa, lakini hutapatikana milele tena-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

27

1Tena neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Sasa wewe, mwanadamu, anza kuomboleza kuhusiana na Tiro,3na mwambie Tiro, aishiye kwenye malango ya bahari, manahodha wa watu hata visiwa vingi, Bwana Yahwe asema hivi kwako: Tiro, umesema, mimi ni ukamilifu katika uzuri.’

4Mipaka yako iko kwenye moyo wa bahari; majengo yako yamekamilisha uzuri wako.
5Wametengeneza mbao nene na pana kwa mvinje kutoka Mlima Hermoni; wamechukua mwerezi kutoka Lebanoni kuufanya mlingoti.
6Wametengeneza makasia yako kutoka kwenye mialo ya Bashani; wametengeza sitaha zako kwa mbao za mvinje kutoka Kitimu, na wametengeneza kwa pembe.
7Tanga zako zilikuwa za rangi za kitani kutoka Misri ambazo zilikuwa kama beramu!
8Wale waliokuwa wakiishi Sidoni na Arvadi walikuwa wavuta makasia wako; wenye busara wa Tiro walikuwa ndani yenu; walikuwa marubani wako.
9Mafundi stadi wenye uzoefu wa hali ya juu kutoka Gabeli walijaza mishono; meli zote za bahari na mabaharia wao miongoni mwenu walikuwa wakiwabeba manahodha kwa ajili ya biashara.
10Uajemi, Ludi, na Putu walikuwa katika jeshi lako, watu wako wa vita. Walining'iniza ngao na chapeo ndani yako; walionyesha uzuri wako.
11Watu wa Arvadi na Heleki katika jeshi lako walikuwa juu ya kuta zako wamekuzunguka, na watu wa Gamadi walikuwa kwenye minara yako. Walinin'giniza juu ngao zao juu ya kuta zako zote zilizokuzunguka! Wakaukamilisha uzuri wako.

12Tarshishi alikuwa mdau wa biashara pamoja nawe kwa sababu ya wingi wa utajiri wako wa kuuza mizigo: fedha, chuma, bati, na risasi. Walinunua na kuuza bidhaa za biashara!

13Yavani, Tubali, na Mesheki-waliwauza watumwa na katika vitu kutengeneza shaba. Walibeba bidhaa zako.

14Beth Togarma waliandaa farasi, farasi dume, na nyumbu kama kama bidhaa zako.

15Watu wa Dedani walikuwa wafanya biashara wako kwenye pwani nyingi. Bidhaa zilikuwa mkononi mwako; walikutumia pembe, pembe za ndovu, na mpingo kama ushuru!

16Shamu alikuwa mchuuzi katika bidhaa zako nyingi; waliandaa zumaridi, zambarau, nguo zenye rangi mbali mbali, kitambaa kizuri, lulu, na kito chekundu cha thamani kama bidhaa zako.

17Yuda na nchi ya Israeli walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe. Waliandaa ngano kutoka Minithi, keki, asali, mafuta, na lihamu kama bidhaa zako.

18Dameski alikuwa mfanya biashara wa bidhaa zako zote, za utajiri mkubwa mno, na ya divai ya Helboni na sufu ya Zahari.

19Dani na Yavani kutoka Uzali walikwandalia bidhaa ya chuma kilichofuliwa, na mdalasini, na mchai. Hivi vikawa bidhaa yako.

20Dedani alikuwa mchuuzi katika nguo nzuri za kutandika.

21Arabuni na wakuu wote wa Kedari walikuwa wafanyabiashara pamoja nawe; walikuandalia wanakondoo, kondoo dume na mbuzi.

22Wafanya biashara wa Sheba na Raama walikuja kukuuzia kila aina ya viungo vizuri katika vito vyote vya thamani; waliuza dhahabu kwa ajili ya bidhaa.

23Harani, Kane, na Adina walikuwa wafanya biashara pamoja nawe, karibu na Sheba, Ashuru, na Kilmadi.24Hawa walikuwa wachuuzi wako mapambo ya joho ya nguo za urujuani pamoja na rangi zilibuniwa, na nguo zilizo sanifiwa vizuri katika sehemu zako za soko.
25Merikebu za Tarshishi zilikuwa misafara ya bidhaa yako! Hivyo ulijaa, shehena nzito katika moyo wa bahari!
26Wapiga makasia wako walikuleta kwenye bahari kuu mno; upepo wa mashariki umekuvunja kati yao.
27Utajiri wako, bidhaa, na mizigo ya biashara; wapiga makasia wako na marubani, na waunzi wa meli; wafanya biashara wako wa bidhaa na watu wote wa vita walio ndani yako, na jeshi lako-watazama kwenye kina cha bahari siku ya kuangamia kwako.
28Miji iliyopo kwenye bahari sauti itatetemeka kulia kwa rubani zako;
29Wote wavutao kasia watashuka chini kutoka kwenye meli zao; wanamaji na marubani wote juu ya bahari watasimama juu ya nchi.
30Kisha watakufanya kusikiliza sauti yao na kulia kwa uchungu; watarusha vumbi juu ya vichwa vyao. Watabingirika katika majivu.
31Watanyoa vichwa vyao upara kwa ajili yako na kujifunga wenyewe kwa nguo za magunia, na watalia kwa sauti.
32Watakuinulia maombolezo ya kuomboleza kwa ajili yako na kuimba nyimbo za maombolezo juu yako, ni nani aliye kama Tiro, ambaye sasa ameletwa kunyamazishwa kati ya bahari?
33Wakati bidhaa yako ilipoenda ufukweni kutoka kwenye bahari, imewarithisha watu wengi; uliwatajirisha wafalme wa dunia kwa wingi wa utajiri wako mkubwa na bidhaa!
34Lakini wakati ulipo vunjwavunjwa kwa bahari, kwa vilindi vya maji, bidhaa yako na wafanya kazi wako wote kuzama!
35Wote wakaao pwani walikuogopa, na wafalme wao kuvunjwa vunjwa katika kitisho! Nyuso zao zimetetemeka!
36Wafanya biashara wa meli wa watu wakuzomea; umekuwa tishio, na hutakuwepo tena milele.”

28

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, waambie watawala wa Tiro, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Moyo wako unakiburi! Umesema, “mimi ni mungu! Nitakaa kwenye kiti cha miungu katika moyo wa bahari!” Ingawa wewe ni mtu na sio mungu, unaufanya moyo wako kama moyo wa mungu,

3unafikiri kwamba unahekima kuliko Danieli, na kwamba hakuna siri ikushangazayo!
4Umejitajirisha mwenyewe pamoja na hekima na ujuzi, na kujipatia dhahabu na fedha katika hazina yako!
5Kwa hekima kubwa na kwa biashara yako, umeongeza utajiri wako, hivyo moyo wako una kiburi kwa sababu ya utajiri yako.

6Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umetengeza moyo wako kama moyo wa mungu,
7kwa hiyo nitaleta wageni juu yako, watu wa kuogofya kutoka mataifa mengine. Wataleta panga zao juu hekima ya uzuri wako, na watauchafua uzuri wako.
8Watakupeleka chini hata kwenye shimo, na utakufa kifo cha waliokufa katika Bahari.
9Je! Kweli utasema, “Mimi ni mungu” mbele ya uso wa yule akuuaye? Wewe ni mwanadamu na sio Mungu, na utakuwa kwenye mkono wa yule akutiae jeraha.
10Utakufa kifo cha asiyetahiriwa kwa mkono wa wageni kwa kuwa nimesema hili-asema Bwana Yahwe.

11Neno la Yahwe likanijia, kusema,12“Mwanadamu, inua maombolezo kwa ajili ya mfalme wa Tiro na umwambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Uliumbwa mkamilifu, umejaa hekima na ukamilifu wa hekima.
13Ulikuwa katika Edeni, bustani ya Mungu. Kila jiwe la thamani lilikufunika: akiki, yakuti manjano, almasi, zabarajadi, shohamu, yaspi, yakuti samawi, zumaridi, baharamani, na dhahabu. Ilikuwa siku uliyokuwa umeiumba ambayo walikuwa wameiandaa.
14Nimekuweka juu ya mlima mtakatifu wa Mungu kama kerubi nimekutia mafuta kwa ajili ya kumlinda mwanadamu. Ulikuwa kati ya mawe ya moto ulipozunguka.
15Ulikuwa mwadilifu kwenye njia zako kutoka siku ulipoumbwa hadi uovu ulipoonekana ndani yako.
16Kupitia biashara yako kubwa uliyokuwa umeijaza kwa udhalimu, hivyo umetenda dhambi. Hivyo nimekutupilia mbali ya mlima wa Mungu, kama mmoja wao wa aliyekuwa ameninajisi, na nimekuharibu, kerubi mlinzi, na kukutoa miongoni mwa mawe ya moto.
17Moyo wako ulikuwa na kiburi kwa uzuri wako; umeiharibu hekima yako kwa sababu ya fahari yako. Nimekupeleka chini kwenye dunia. Nimekuweka mbele ya wafalme ili waweze kukuona.
18Kwa sababu ya wingi wa dhambi zako na biashara za udanganyifu, umepanajisi mahali pako patakatifu. Basi nimetengeneza moto kutoka ndani yako; utakula wewe. Nitakugeuza kwenye majivu juu ya dunia katika macho ya wote wakutazamao.
19Wale wote waliokujua miongoni mwa watu watakustajabia; utakuwa kitu cha kutisha, na hutakuwepo tena milele.”’

20Kisha neno la Bwana Yahwe likanijia, kusema,21“Mwanadamu, elekeza uso wako Sidoni na toa utabiri juu yake.22Sema, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu yako, Sidoni! Kwa kuwa nitatukuzwa kati yako hivyo watu wako watajua kwamba mimi ni Yahwe wakati nitakapokuwa nimezitekeleza hukumu ndani yako. Nitaonyesha utakatifu ndani yako.
23Nitapeleka tauni juu yako na tazama mitaa yako, na walioua wataanguka kati yako. Wakati upanga utakapokuja juu yao kutoka pande zote, kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe.

24Kisha hakutakuwa na mwiba uchomao na maumivu ya miba kwa ajili ya nyumba ya Israeli kutoka wale wote waliomzunguka wanaowadharau watu wake, hivyo watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe!’

25Bwana Yahwe asema hivi, Nitakapowakusanya nyumba ya Israeli kutoka miongni mwa watu waliokuwa wamekusanyika, na wakati nilipokuwa nimewatenga miongoni mwao, hivyo mataifa wanaweza kuona, kisha watafanya nyumba zao katika nchi nitakayo mpatia mtumishi wangu Yakobo.26Kisha wataishi salama ndani yake na kujenga nyumba, kulima mizabibu, na kuishi salama wakati nitakapo zitekeleza hukumu juu ya wote wale ambao sasa wanawadharau kutoka sehemu zote; basi watajua ya kwamba mimi ni Yahwe Mungu wao!”’

29

1Katika siku ya kumi, katika mwezi wa kumi siku ya kumi na moja ya mwezi, neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, weka uso wako juu ya Farao, mfalme wa Misri; toa unabii juu yake na juu ya Israeli yote.3Nena na sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Farao, mfalme wa Misri. Wewe joka kubwa ambaye ujifichaye kati ya mto, husema, “Mto wangu ni wangu mwenyewe. Nimeufanya kwa ajili yangu mwenyewe.”

4Kwa kuwa nitaweka kulabu katika taya zako, na samaki za mto wako zitashikamana na magamba yako; nitakuinua juu kutoka kati ya mto wako karibu na samaki zote za mto walioshikamana na maganda yako.
5Nitakutupa chini kwenye jangwa, wewe pamoja na samaki wako wote kutoka kwenye mto wako. Utaanguka kwenye shamba la wazi; hutakusanya wala kuinua. Nimekutoa uwe chakula kwa viumbe hai vya dunia na kwenye ndege wa angani.
6Kisha wote wakaao Misri watajua kwamba mimi Yahwe, kwa sababu wamekuwa mwanzi wa kutegemewa hata kwenye nyumba ya Israeli.7Wakati watakapokushika kwa mkono wao, ulivunjika na kurarua wazi mabega yao; na watakapojifunza juu yako, ulivunjika, na kusababisha miguu yao kutokuwa imara.

8Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitaleta upanga juu yako. Nitawakatilia mbali wote mwanadamu na mnyama mbali nawe.9Hivyo nchi ya Misri itakuwa ukiwa na jangwa. Ndipo watakapojua kwamba mimi ni Yahwe, kwa sababu amesema, “Huu mto ni wangu, kwa kuwa nimeufanya mimi.”10Kwa hiyo, tazama! Ni juu yako na juu ya mto wako, hivyo nitaitoa nchi ya Misri juu ya ukiwa na jangwa, na utakuwa nchi yenye jangwa kutoka Migdoli hata Sewene na mipaka ya Kushi.11Hakutakuwa na mguu wa mtu kupitia, na hakuna mguu wa wanyaa pori watakao upitia. Haitakuwa makao kwa miaka arobaini.12Kwa kuwa nitaifanya nchi ya Misri kuwa ukiwa kati ya nchi zilizoharibiwa, na miji yake kati ya miji isiyotumika itakuwa ukiwa kwa miaka arobaini; kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa, nitawatapanya kati ya nchi mbali mbali.

13Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Mwisho wa miaka arobaini nitaikusanya Misri kutoka kwa watu miongoni mwao wale waliokuwa wametawanyika.14Nitawarudisha wageni wa Misri na kuwarudisha hata mkoa wa Pathrosi, hata kwenye nchi ya asili yao. Kisha huko watakuwa ufalme wa chini.15Utakuwa chini ya falme, na hautajiinua tena juu ya mataifa. Nitawapunguza hivyo hawatatawala tena juu ya mataifa.16Wamisri hawatakuwa sababu kwa ajili ya imani kwa ajili ya nyumba ya Israeli. Badala yake, watakuwa kumbusho la uovu ambao Israeli umeufanya walipogeukia Misri kwa ajili ya msaada. Kisha watajua kwamba mimi ni Bwana Yahwe.”’

17Kisha ikawa katika mwaka wa ishirini na saba siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,18“Mwanadamu, Nebukadreza mfalme wa Babeli amelinda jeshi lake kufanya kazi ngumu juu ya Tiro. Kila kichwa kilitiwa upara, na kila bega liliambuliwa ngozi. Kisha yeye na jeshi lake hawakupokea malipo kutoka Tiro kwa kazi ngumu aliyokuwa ameimaliza dhidi yake.19Kwa hiyo Bwana Mungu asema hivi, ‘Tazama! Ninawapatia Nebukadreza nchi ya Misri mfalme wa Babeli, na atachukua utajiri wake, kuziteka nyara milki zake, na kuchukua yote atakayoyakuta huko; nayo yatakuwa mshahara wa jeshi lake.20Nimempatia nchi ya Misri kama mshahara kwa ajili ya kazi waliyonifanyia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

21Siku hiyo nitachipusha pembe kwa ajili ya nyumba ya Israeli, na nitakufanya uzungumze kati yao, ili kwamba wajue yakwamba mimi ni Yahwe.”’

30

1Neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, toa unabii na sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Maombolezo. “Ole unakuja siku hiyo.”

3Siku ikaribu. Siku ikaribu kwa ajili ya Yahwe. Itakuwa siku ya mawingu, mda wa hukumu kwa ajili ya mataifa.
4Kisha upanga utakuja dhidi ya Misri, na huko kutakuwa na maumivu makali katika Kushi wakati wauaji wa watu watakapoanguka katika Misri-wakati watakapochukua utajiri, na wakati misingi yake itakapoharibiwa.

5Kushi, Putu, na Ludi, na wageni wote, pamoja na watu wa nyumba ya agano-wote wataanguka chini kwa upanga.

6Yahwe asema hivi: Basi wale wanaoisaidia Misri wataanguka, na kiburi cha uweza wake kitashuka chini. Kutoka Migdoli hata Sewene maaskari wao wataanguka kwa upanga-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.7Wataogofya kati ya nchi zilizotupwa, na miji yao itakuwa miongoni mwa miji yote iliharibika.
8Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapouweka moto katika Misri, na wakati wasaidizi wake wote watakapoharibiwa.

9Katika siku hiyo wajumbe watatoka mbele yangu katika meli ili kuitia hofu Kushi iliyo salama, na kutakuwa na maumivu makali miongoni mwao katika siku ya kuangamizwa Misri. Kwa kuwa tazama! Inakuja.

10Bwana Yahwe asema hivi: Nitaufanya mwisho wa watu wa Misri kwa mkono wa Nebukadreza, mfalme wa Babeli.
11Yeye na jeshi lake pamoja naye, hofu ya mataifa, italetwa kuiharibu nchi; watafuta panga zao juu ya Misri na kuijaza nchi pamoja na watu waliokufa.
12Nitaifanya mito kuwa nchi kavu, na nitaiuza nchi kwenye mkono wa watu waovu. Nitaifanya nchi na viijazavyo ukiwa kwa mkono wa wageni-mimi, Yahwe, nimesema.

13Bwana Yahwe asema hivi: Nitaziharibu sanamu, na nitaleta mwisho wa sanamu za ubatili za Nofu. Hakutakuwa na mkuu katika Misri, na nitaweka hofu katika nchi ya Misri.
14Kisha nitaifanya Pathrosi ukiwa na kuweka moto katika Soani, nitatekeleza matendo ya hukumu katika No.
15Kwa kuwa nitamwaga ghadhabu yangu juu Sini, ngome ya Misri, na kuwakatilia mbali watu wa mataifa.
16Kisha nitaweka moto katika Misri; Sini itakuwa katika dhiki kuu, No itavunjika, na Nofu itakabiliana na maadui kila siku.
17Vijana katika Oni na Pi-besethi wataanguka kwa upanga, na miji yao itaenda utumwani.
18Huko Tapanesi, siku itabadilika kuwa usiku nitakapo ivunja nira ya Misri huko, na kiburi cha uwezo wake kitaisha. Kutakuwa na wingu likimfunika, na binti zake wataenda utumwani.
19Nitatekeleza matendo ya hukumu katika Misri, hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

20Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa kwanza, katika siku ya saba ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,21“Mwanadamu, nimeuvunja mkono wa Farao, mfalme wa Misri. Tazama! Haukufungwa, au kufungwa kwa kitambaa cha bendeji ili upone, hivyo basi uweze kuwa imara kushika upanga.22Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi, ‘Tazama, mimi niko juu ya Farao, mfalme wa Misri. Kwa kuwa nitauvunja mkono wake, wote yule aliye hodari na yule aliyevunjika, nitaufanya upanga wangu kuanguka kutoka kwenye mkono wake.23Kisha nitaitawanya Misri miongoni mwa mataifa na kuwatawanya katika nchi mbali mbali.24Nitaunyoosha mkono kwa mfalme wa Babeli na kuweka upanga wangu katika mkono wake ili kwamba niweze kuiharibu mikono ya Farao. Atagugumia mbele ya mfalme wa Babeli kwa mgugumio wa mtu anayekufa.25Kwa kuwa nitainyoosha mikono ya mfalme wa Babeli, wakati mkono wa Farao utakapoanguka. Kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, nitakapoweka upanga wangu kwenye mkono wa mfalme wa Babeli; kwa kuwa ataishambulia nchi ya Misri kwa huo.26Hivyo nitaitawanya miongoni mwa mataifa na kuyatawanya kwenye nchi tofauti tofauti. Kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe.”’

31

1Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na moja, katika mwezi wa tatu, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, mwambie Farao, mfalme wa Misri, na watu wake wanaomzunguka, ‘Katika ukuu wako, je! Wewe ni kama nani?

3Tazama! Ashuru ilikuwa mwerezi katika Lebanoni pamoja na matawi mazuri, yakitoa kivuli kwenye msitu, na mirefu katika kimo, na matawi yalitengeneza kilele cha mti wake.
4Maji mengi yaliufanya kuwa mrefu; maji ya chini yaliufanya kuwa mkubwa. Mito ilitiririka sehemu zake zote, kwa kuwa mifereji yake ilitoa kuelekea kwenye miti yote katika shamba.
5Kimo chake kikubwa kilikuwa zaidi kuliko miti mingine yote katika shamba, na matawi yake yakawa mengi; matawi yake yalikuwa marefu kwa sababu ya maji mengi yalipokuwa yakikua.
6Kila ndege wa mbinguni alitengeza kiota kwenye matawi yake, wakati kila kiumbe hai cha shamba kilizaa mtoto chini ya tawi. Mataifa mengi yote yaliishi chini ya kivuli chake.
7Kwa kuwa ulikuwa uzuri katika ukuu wake na kimo cha matawi yake, kwa kuwa mizizi yake ilikuwa katika maji mengi.
8Mierezi katika bustani ya Mungu haikuweza kuwa sawa nayo. Hakuna miongoni mwa miti ya mivinje iliyofanana matawi yake, na miti ya miamori haikuweza kuwa sawa na majani yake. Hapakuwa na mti mwingine katika bustani ya Mungu ulikuwa kama huo katika uzuri wake.
9Nimeufanya kuwa mzuri pamoja na matawi yake mengi na miti yote ya Edeni iliyokuwa katika bustani ya Mungu ilimwonea wivu.

10Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ilikuwa mirefu kwa kina, na imekiweka kilele chake kati ya matawi yake, moyo wake umeinua kwa sababu ya urefu wake.11Nimeuweka kwenye mikono ya yeye mwenye uweza wa mataifa, kuishughulikia kulingana na yale maovu anayostahili. Nimeufukuza.12Wageni waliokuwa wakiogofya wa mataifa yote wameikatilia mbali kuiacha ife. Matawi yake yameanguka kwenye milima na mabonde yote, na matawi yake yameanguka katika mito yote ya nchi. Kisha mataifa yote juu ya nchi wakatoka nje kutoka chini ya kivuli na kwenda zao wakamwacha.13Ndege wa agani watapumzika kwenye shina la mti ulioanguka, na kila mnyama wa shambani atakuja kwenye matawi yake.14Hii ilitokea ili kwamba pasiwe na miti mingine itakayopandwa karibu na maji yatang'oa majani yake hata kwenye kina cha miti mirefu, na kwamba hakuna miti mingine itakayomea karibu na maji itakayofikia kwenye hicho kina. Wote wametolewa kufa, chini ya nchi, miongoni mwa watoto wa binadamu, pamoja na wale washukao chini.

15Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku wakati mwerezi uliposhuka chini nilileta maombolezo kwenye dunia. Niliyafunika maji ya chini juu yake, nikayarudisha maji ya bahari. Nilizuia maji makuu, nikaleta maombolezo hata Lebanoni kwa ajili yake. Hivyo miti yote ya shambani ikaomboleza kwa sababu yake.16Nimeleta tetemeko kwa mataifa wa sauti ya kuanguka kwake, wakati nitakapomtupa chini mpaka kuzimu pamoja na wale walioenda chini kwenye shimo. Hivyo niliitia moyo miti ya Edeni yote katika pande zote za nchi. Hii ilikuwa imechaguliwa na miti iliyokuwa bora ya Lenanoni; miti iliyokunywa maji.17Kwa kuwa walikwenda chini pia pamoja nayo hata kuzimu, kwa wale waliokuwa wameuawa kwa upanga. Kulikuwa na jeshi lake imara, yale mataifa yalikuwa yakiishi kati kivuli chake.

18Umefanana na nani hivi katika utukufu na ukuu kati ya mti wa Edeni? Kwa kuwa utashushwa chini pamoja na miti ya Edeni hata pande zote nne za dunia miongoni mwa wasiotahiriwa; utaishi pamoja na watu wake wote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

32

1Kisha ikawa katika mwezi wa kumi na mbili wa mwaka wa kumi na mbili, siku ya kwanza ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, inua maombolezo kuhusu Farao mfalme wa Misri; mwambie, ‘Wewe ni kama simba mdogo juu ya mataifa, lakini kama jitu la kutisha, unatoka kwenye maji, unayachafua maji kwa miguu yako na kuyachafua maji yao.

3Bwana Yahwe asema hivi: Basi nitautandaza wavu wangu juu yako katika kusanyiko la watu wengi, na watawainua juu katika wavu wangu.
4Nitakuacha katika nchi. Nitakutupa kwenye shamba na kufanya ndege wote wa angani watue juu yako; njaa ya wanyama wote waishio juu ya nchi watashibishwa na wewe.
5Kwa kuwa nitaiweka nyama yako juu ya milima, na nitayajaza mabonde kwa funza wako waliokufa.
6Kisha nitamwaga damu yako juu ya milima, na vitanda vya kijito vitajazwa kwa damu yako.
7Kisha wakati nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu na kuzitia giza nyota zake; nitalifunika jua kwa mawingu, na mwezi hautatoa nuru yake usiku.
8Mianga ya mbinguni nitaiweka giza juu yako, na nitaweka giza juu ya nchi-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
9Hivyo nitaitisha mioyo ya watu wengi katika nchi ambao huwajui, wakati nitakapoleta kuhusu uvunjifu miongoni mwa mataifa, miongoni mwa nchi ambazo hukuzijua.
10Nitawashangaza watu wengi kuhusiana na wewe; wafalme wao watatetemeka kwa hofu kuhusiana na wewe nitakapoutikisa upanga wangu mbele yao. Kila wakati kila mmoja atatetemeka kwa sababu yako, katika siku ya kuanguka kwako.

11Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Upanga wa mfalme wa Babeli utakuja juu yako.
12Nitawafanya watu wako kuanguka kwa panga za mashujaa-kila shujaa ni tishio la mataifa. Hawa mashujaa watateketeza kiburi cha Misri na kuangamiza watu wake wote.
13Kwa kuwa nitaiharibu mifugo yote kutoka karibu na maji mengi; na mguu wa mtu hautayatibua tena, wala kwato za wanyama hazitayatibua.
14Kisha nitayafanya maji yao kuwa matulivu na kufanya mito yao kukimbia kama mafuta-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
15Wakati nitakapoifanya nchi ya Misri sehemu iliyojitenga, wakati nchi iliyopungukiwa na vitu viijazavyo, wakati nitakapo washambulia wakaao ndani yake, watajua ya kwamba mimi ni Yahwe.

16Kutakuwa na maombolezo; binti za mataifa wataomboleza juu yake; wataomboleza juu ya Misri, juu ya watu wake wote wataomboleza-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

17Kisha ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya kumi na tano ya mwezi, lile neno la Yahwe likanijia, kusema,

18“Mwanadamu, omboleza kwa ajili watu wa misri na walete chini-yeye na binti za mataifa mashuhuri-hata chini ya dunia pamoja na wale walioshuka chini kwenye shimo.19‘Je! Wewe ni mzuri zaidi kuliko mtu mwingine yeyote? Nenda chini na lala chini pamoja na wasiotahiriwa.’20Wataanguka miongoni mwao waliokuwa wameuawa kwa upanga. Upanga ulikuwa umewekwa! Alikuwa amepatiwa upanga; watamkamata na watu wake.21Hodari wa wapiganaji katika Sheoli atasema kuhusu Misri na rafiki zake, ‘Wameshuka chini hapa! Watalala pamoja na wasiotahiriwa, pamoja na wale waliokuwa wameuawa kwa upanga.’

22Ashuru yupo huko pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yamemzunguka; wote waliuawa kwa upanga.23Wale ambao makaburi yao yamewekwa katika maficho ya mashimo yaliyo huko, pamoja na kusanyiko lake. Makaburi yake yakiwazunguka wote waliokuwa wameuawa, walioanguka kwa upanga, wale walioleta hofu juu ya nchi ya walio hai.

24Elamu yupo huko pamoja na watu wake wote. Makaburi yake yamemzunguka; wote walikuwa wameuawa. Wale walioawa kwa upanga, walioshuka chini wasiotahiriwa hata sehemu ya chini kabisa ya dunia, waliowatia hofu juu ya nchi ya walio hai na wale waliobeba aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao chini kwenye shimo.

25Wamemuwekea kitanda kwa ajili ya Elamu na watu wake wote kati ya wachinjaji; kaburi lake limemzunguka. Wote hawajatahiriwa, kukatwa vipande kwa upanga, kwa sababu waliwaleta mashujaa wao juu ya nchi ya walio hai. Hivyo wamechukua aibu yao wenyewe, pamoja na wale washukao kwenye shimo miongoni mwa wote waliouawa, wale washukao kwenda shimoni. Elamu yu miongoni mwa wale waliokuwa wameuawa.

26Mesheki, Tubali, na watu wake wote wako huko! Makaburi yao yamewazunguka. Wote hawajatahiriwa, wameuawa kwa upanga, kwa sababu walileta utiisho wao juu ya nchi ya walio hai.27Wasilale pamoja mashujaa walioanguka wa wasiotahiriwa walioshuka chini kwa Sheoli pamoja na silaha zao zote za vita, na pamoja na panga zao zote walizoziweka chini ya vichwa vyao na maovu yao juu ya mifupa yao. Kwa kuwa walikuwa tishio kwa mashujaa katika nchi ya walio hai.

28Basi wewe, Misri, utavunjika kati yao wasiotahiriwa! Utalala karibu nao waliokuwa wamekatwa vipande vipande kwa upanga.

29Edomu yuko huko na wafalme na viongozi wake wote. Walikuwa wamehifadhiwa katika uwezo wao pamoja na wale walioawa kwa upanga. Pamoja na wasiotahiriwa wamelala, pamoja na wale walioshuka kwenye shimo.

30Wakuu wa kaskazini wako huko-wote na Wasidoni wote walioshuka chini pamoja na hao waliokuwa wamekatwa vipande vipande. Walikuwa na nguvu na kuwafanya wengine kuogopa, lakini sasa wako huko kwa aibu, wasiotahiriwa pamoja na wale waliokatwa vipande vipande kwa upanga. Wamebeba aibu yao wenyewe, pamoja nao waendao kwenye shimo.

31Farao ataona na kupata faraja kuhusu kundi lake waliokatwa vipande vipande kwa upanga -Farao na jeshi lake lote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.32Nitamuweka kama utiisho wangu katika nchi ya walio hai, lakini atakuwa amelazwa chini katikati yao wasiotahiriwa, miongoni mwa wale walio katwa vipande kwa upanga, Farao na makundi yake yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

33

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, sema hivi kwa watu wako; waambie, ‘Nitakapoleta upanga juu ya nchi, kisha watu wa hiyo nchi wakamchukua mtu mmoja kutoka mingoni mwao na kumfanya awe mlinzi wao.3Atazamapo kwa upanga kama unakuja juu ya nchi, na apige tarumbeta kuwaonya watu!4Kama watu wakisikia sauti ya tarumbeta lakini bila kuchukua hatua, na kama upanga ukija na kuwaua, kisha damu ya kila mmoja iko juu ya kichwa chake mwenyewe.5Kama mtu akisikia sauti ya tarumbeta na hakuonywa, damu yake iko juu yake; lakini kama akisikia, ataokoa maisha yake mwenyewe.

6Bali, kama mlinzi akiona upanga unakuja, lakini kama asipopiga tarumbeta, pamoja na matokeo kwamba watu hawajaonywa, na kama upanga ukija na kuchukua uhai wa mtu yeyote, kisha yule mtu akafa kwenye dhambi yake mwenyewe, lakini nitaitaka damu yake kutoka mlinzi.’

7Sasa wewe mwenyewe, mwanadamu! Nimekufanya kuwa mlinzi kwa ajili ya nyumba ya Israeli; utasikia maneno kutoka kinywani mwangu na uwaonye badala yangu.8Kama nikimwambia mtu mwovu, ‘Mwovu, hakika utakufa!’ lakini kama hutangazi hivi ili kwa ajili ya kumuonya mtu mwovu kuhusu hii njia, kisha huyo mtu mwovu atakufa katika dhambi yake, lakini nitaitaka damu yake kutoka kwenye mkono wako!9Lakini wewe, kama ukimwonya mwovu kuhusu hii njia, hivyo basi anaweza kurudi kutoka hiyo, na kama kama asipogeuka kutoka njia yake, kisha atakufa katika dhambi yake, lakini wewe mwenyewe utakuwa umeokoa maisha yako.

10Basi wewe, mwanadamu, sema kwa nyumba ya Israeli, ‘Mnasema hivi, Makosa yetu na dhambi zetu zi juu yetu, na tunadhoofika kwa ajili yao! Je! Tutaishije?”’11Waambie, ‘Kama niishivyo-asema Bwana Yahwe-sifurahii kifo cha mwovu, kwa kuwa kama mwovu akitubu kutoka njia yake, kisha ataishi! Tubu! Tubu kutoka njia zako mbaya! Kwa nini mnataka kufa, nyumba ya Israeli?’

12Hivyo basi wewe, mwanadamu, waambie watu wako, ‘Haki ya mwenye haki haitamwokoa kama akikosa! Uovu wa mtu mwovu hautamfanya kuangamia kama akitubu dhambi zake! Kwa kuwa mtu mwenye haki hataweza kuishi kwa sababu ya haki yake kama akikosa.13Kama nikisema kwa mwenye haki, “Hakika ataisha!” na kama akiamini katika haki yake na kisha akafanya udhalimu, sitokumbuka haki yake yoyote. Atakufa kwa ajili ya uovu alioufanya.14Hivyo kama nikisema kwa mwovu, “Utakufa hakika,” lakini kama akitubu kutoka kwenye dhambi zake na kufanya yaliyo halali na haki-15kama akirudisha dhamana ambayo aliyomnyang'anya, au kama akirudisha alichokipoteza, na kama akitembea katika amri zitoazo uhai na bila kufanya dhambi-kisha ataishi hakika. Hatakufa.16Dhambi alizozifanya hazitakumbukwa kwa ajili yake. Ametenda halali na haki, na hivyo, ataishi hakika!

17Lakini watu wako husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” lakini ni njia zako ndizo haziko sawa!18Wakati mtu mwenye haki ageukapo kutoka kwenye haki na kufanya dhambi, kisha atakufa katika hiyo!19Wakati mtu mbaya ageukapo kutoka kwenye ubaya wake na kufanya iliyo halali na haki, ataishi kwa sababu ya hayo mambo!20Lakini ninyi watu husema, “Njia ya Bwana haiko sawa!” Nitawahukumu kila mmoja wenu kulingana na njia yake, nyumba ya Israeli!”’

21Ikawa katika mwaka wa kumi na mbili, siku ya tano ya mwezi wa kumi ya uhamisho wetu, mtu mmoja akatoroka kutoka Yerusalemuna kusema, “Mji umetekwa!”22Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu jioni kabla yule mtoro hajaja, na mdomo wangu ulikuwa wazi muda huo alikuja kwangu wakati wa mapambazuko. Hivyo mdomo wangu ulikuwa wazi; sikuwa bubu tena!

23Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,24“Mwanadamu, wale waishio mahali palipoharibika katika nchi ya Israeli huongea na kusema, ‘Ibrahimu alikuwa mtu pekee, na alirithi nchi, lakini sisi tukowengi! Tumepewa nchi kama wamiliki.”25Kwa hiyo waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Mnakula damu, na mmeziinulia macho yenu sanamu, kisha mnazimwagia damu za watu. Je! Mna uhakika wa kuimiliki hii nchi?26Mnategemea upanga wenu na mmetenda mambo maovu; kila mtu amemnajisi mke wa jirani yake. Je! Kweli mtaimiliki nchi?’

27Utawaambia hivi, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Kama niishivyo, hakika wale walio katika uharibifu wataanguka kwa upanga, na nitawapatia wale walio katika mashamba viumbe hai kama chakula, na wale walio katika ngome na mapango watakufa kwa tauni.28Kisha nitairudisha nchi kwenye ukiwa na tishio, na kiburi cha uwezo wake kitakoma, kwa kuwa milima ya Israeli itakuwa jangwa, na hakutakuwa na mtu yeyote atakayewapitia.’29Hivyo watajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapoifanya nchi ukiwa na tishio kwa sababu ya machukizo yote waliyoyafanya.

30Hivyo basi wewe, mwanadamu-watu wako wanasema mambo yako karibu na kuta na malango ya nyumba, na kila mmoja anaambizana na mwenzake-kila mtu na ndugu yake, ‘Twende na tukasikilize neno la nabii lililotoka kwa Yahwe!31Hivyo watu wangu watakuja kwako, kama wafanyavyo mara nyingi, na nitaketi mbele yako na kusikiliza maneno yako, lakini mioyo yao inafuata udhalimu kwa faida yao.32Kwa kuwa umekuwa kama wimbo mzuri kwao, sauti nzuri awezaye kucheza kinanda vizuri, hivyo watasikia maneno yako, lakini hakuna atakaye yatii.

33Hivyo wakati haya yote yatakapotokea-tazama! Itatokea! -Watajua yakwamba nabii alikuwa miongoni mwao.”

34

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, tabiri dhidi ya wachungaji wa Israeli. Toa unabii na waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi kwa wachungaji: Ole kwa wachungaji wa Israeli wanaojilisha wenyewe. Je! Wachungaji hawapaswi kulilinda kundi?3Mnakula mafungu yaliyonona na mnavaa sufu. Mnawachinja walionona. Hamkuwalisha siku zote.4Hamkuwatia nguvu wagonjwa, wala hamkuwaponya wenye maradhi. Hamkuwafunga wale waliovunjika, hamkuwarudisha waliofukuzwa au kuwatafuta waliopotea. Badala yake, mmetawala juu yao kwa nguvu na vurugu.5Kisha walikuwa wametawanyika bila mchungaji, na wakawa chakula kwa wanyama wote waishio katika mashamba, walipokuwa wametawanyika.6Kundi langu limetawanyika juu ya milima yote na juu ya kilima kirefu, na limetawanyika juu ya uso wote wa dunia. Wala hakuna anayewatafua.

7Kwa hiyo, wachungaji, sikilizeni neno la Yahwe:8Kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-kwa sababu kundi langu limekuwa mateka na chakula kwa ajili ya wanyama katika mashamba, kwa sababu hapakuwa na mchungaji yeyote, lakini wachungaji walijilisha wenyewe na hawakulisha kundi langu.9Kwa hiyo, wachungaji, lisikilizeni neno la Yahwe:10Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Niko juu ya wachungaji, na nitalitaka kundi langu kutoka mkononi mwenu. Kisha nitawaachisha kutoka kulichunga kundi; wala wachungaji hawatajilisha wenyewe tena kwa kuwa nitaliondoa kundi langu kutoka midomoni mwao, ili kwamba kundi langu lisiwe chakula kwa ajili yao tena.

11Kwa kuwa Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Mimi mwenyewe nitawatafuta kondoo wangu na kuwaulizia,12kama mchungaji atafutaye kundi lake juu ya siku hiyo yupo ndani ya kundi lake lililotawanyika. Hivyo nitalitafuta kundi langu, na nitalichunga kutoka sehemu lilipokuwa limetawanyika siku ya mawingu na giza.13Kisha nitalileta kutoka miongoni mwa watu; nitalikusanya kutoka nchi mbali mbali na kulileta kwenye nchi yao. Nitaliweka kwenye malisho juu ya pande za milima ya Israeli, karibu na vijito, na katika kila makazi katika nchi.14Nitawaweka kwenye malisho mema; juu ya milima ya Israeli itakuwa sehemu za malisho yao. Watalala chini huko katika sehemu nzuri kwa ajili ya malisho, katika malisho mengi, na watalisha juu ya milima ya Israeli.15Mimi mwenyewe nitachunga kondoo wangu, na mimi mwenyewe nitawalaza chini-hivi ndivyo Bwana Yahwe16asemavyo-Nitawatafuta waliopotea nitawarudisha waliofukuzwa. Nitawafunga waliovunjika na kuwaponya kondoo waliougua lakini wanene na wenye nguvu nitawaharibu. Nitawalisha kwa haki.

17Hivyo sasa ninyi, kundi langu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-tazama, nitakuwa hakimu kati ya kondoo na kondoo na kati ya kondoo dume na mbuzi dume.18Je! Haitoshi kulisha juu ya malisho mazuri, ambayo mtayakanyaga chini kwa miguu yenu kile kilichobakia kwenye malisho; na kunywa kutoka maji masafi, ambayo hakuna budi kuikanyaga mito kwa miguu yenu?19Kondoo zangu zitakula kile mlichokanyaga kwa miguu yenu, na kunywa maji yale mliyoyakanyaga kwa miguu yenu?

20Kwa hiyo Bwana Yahwe anawaambia hivi; Tazama! Mimi mwenyewe nitahukumu kati ya wanene na waliokonda,21Kwa kuwa mmewasukuma kwa ubavu wenu na mabega, na kuwapiga kwa pembe wadhaifu wote kwa pembe zenu hadi mtakapowatawanya mbali kutoka kwenye nchi.22Nitaliokoa kundi langu na hawatakuwa mateka tena, na nitahukumu kati ya kondoo mmoja na mwingine!23Nitaweka juu yao mchungaji mmoja, mtumishi wangu Daudi. Atawachunga, atawalisha, na atakuwa mchungaji wao.24Kwa kuwa mimi, Yahwe, nitakuwa Mungu wao, na mtumishi wangu Daudi atakuwa mkuu kati yao-mimi, Yahwe, nimesema hivi.

25Kisha nitafanya agano la amani pamoja nao na kuwaondoa wanyama waovu kutoka kwenye nchi, ili kwamba waishi salama katika jangwa na walale salama katika misitu.26Pia nitaleta baraka juu yao na juu ya maeneo yazungukao kilima changu, kwa kuwa nitaleta manyunyu kwa wakati wake. Haya yatakuwa manyunyu ya baraka.27Kisha miti ya shambani itazaa matunda yake, na dunia itashindwa kuzaa matunda yake. Kondoo wangu watakuwa salama katika nchi yao; kisha watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, wakati nitakazipovunja fito za kongwa zao, na wakati nitakapowalinda kutoka kwenye mkono wa wale walio watumikisha.28Hawatakuwa mateka tena kwa mataifa, na wanyama pori juu ya dunia hawatawameza tena. Kwa kuwa wataishi salama na wala hakuna mtu atakayewatia hofu.29Kwa kuwa nitatengeneza sehemu ya kulimia nzuri kwa ajili yao hivyo hawataangamia kwa njaa katika nchi, na mataifa hayataleta matukano juu ya yao.30Kisha watajua kwamba mimi, Yahwe Mungu wao, niko pamoja nao. Ni watu wangu, nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.31Kwa kuwa ninyi ni kondoo wangu, kundi la malisho yangu, na watu wangu, na mimi ni Mungu wenu-hivi ndivyo Bwana Mungu asemavyo.”

35

1Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,2“Mwanadamu, weka uso wako juu ya Mlima Seiri na tabiri dhidi yake.3Uiambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Mlima Seiri, nitakupiga kwa mkono wangu na kukufanya ukiwa na tishio.4Nitaiharibu miji yenu, na wewe mwenyewe utakuwa ukiwa; kisha utajua kuwa mimi ni Yahwe.

5Kwa sababu umekuwa adui kwa watu wangu Israeli siku zote, na kwa sababu umewatoa kwenye mikono ya upanga wakati wa mateso yao, wakati adhabu yao itakapokuwa katika ukubwa wake.6Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-nitaandaa kwa ajili ya damu, na damu na kukufuatilia! Kwa kuwa hukuchukia damu, damu itakufuatilia.7Nitaufanya Mlima Seiri mkamilifu na ukiwa wakati nitakapoukatilia mbali kutoka huo yeyote apitaye na arudiye tena.8Kisha nitaijaza milima kwa watu wao waliokufa. Milima yako na mabonde na mifereji-wale walioawa kwa upanga wataanguka kati yao.9Nitakufanya mkiwa daima. Miji yako haitakaliwa na watu, lakini mtajua kwamba mimi ni Yahwe.

10Umesema, “Haya mataifa mawili na hizi nchi mbili zitakuwa zangu, na tutazimiliki,” hata wakati Yahwe alipokuwa pamoja nao.11Kwa hiyo, kama niishivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-hivyo nitafanya kulingana na hasira yako na kulingana na wivu wako ambao uliousikia katika chuki yako ya Israeli, na nitajidhihirisha kwao nitakapokuhukumu.12Hivyo utajua kwamba mimi ni Yahwe. Nimeyasikia matukano yako yote uliyasema dhidi ya milima ya Israeli, uliposema, “Wameharibiwa; wametolewa kwetu tuwale.13“Nanyi mmejitukuza juu yangu kwa kile mlichokisema, na mmeongeza maneno juu yangu; na kuyasikia yote.14Bwana Yahwe asema hivi: Nitakufanya ukiwa, wakati dunia nzima itakapofurahi.15Kama vile unavyofurahi juu ya urithi wa watu wa Israeli kwa sababu ukiwa ya wake, ndivyo nitakavyokutenda wewe. Utakuwa ukiwa, Mlima Seiri, na Edomu yote! Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

36

1“Na wewe, mwanadamu, itabirie milima ya Israeli na useme, ‘Milima ya Israeli, lisikilizeni neno la Yahwe.2Bwana Yahwe asema hivi: Adui amesema kuhusu ninyi, “Aha!” na “Mahala pa juu pa zamani pamekuwa milki yetu.”’3Kwa hiyo tabiri na sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu ya ukiwa wenu na kwa sababu yaomashambulizi yaliyokuja juu yenu kutoka pande zote, mmekuwa milki ya mataifa mengine; mmeambiwa kwa midomo yao waongeao, na kwa masingizio ya watu.4Kwa hiyo, milima ya Israeli, sikilizeni neno la Bwana Yahwe: Bwana Yahwe asema hivi kwa milima na vilima, mifereji ya maji na mabonde, mahali palipoharibika kuwa ukiwa na miji iliyoachwa ambayo imetekwa nyara na kutokuwa huru kwa kutaniwa na mataifa yaliyowazunguka-5kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Hakika nimeongea katika moto wa hasira yangu juu ya mataifa meningine, juu ya Edomu na wote waliochukua nchi yangu kwa ajili yao wenyewe kama milki, dhidi ya wale walikuwa na furaha yote katika mioyo yao na dharau katika roho zao, kama walivyoitwaa nchi yangu kwamba wangeweza kudai nchi za malisho kwa ajili yao.6Kwa hiyo, tabiri kwa nchi ya Israeli na sema kwa milima na vilima, hata kwenye mifereji na mabonde, Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Katika ghadhabu yangu na hasira yangu nasema hivi kwa sababu mmechukua fedheha za mataifa.7Kwa hiyo, Bwana Yahwe asema hivi: Mimi mwenyewe nitainua mkono wangu kuapa kwamba mataifa yanayowazunguka yamkini yatawabebea aibu yao wenyewe.

8Lakini ninyi, milima ya Israeli, mtachipuza matawi na kuzaa matunda kwa ajili ya watu wangu Israeli, kwa kuwa watarudi kwenu.9Maana tazama, nipo kwa ajili yenu, na kuwachukulia kwa fadhili; mtalimwa na kupandwa mbegu.10Hivyo nitawaongeza juu ya milima yenu watu katika nyumba ya Israeli, yote. Miji itakaa na palipoharibiwa kujengwa.11Nitaongeza mtu na wanyama juu yenu milima ili kwamba itaongezeka na kuzaa. Kisha nitawafanya kuishi kama mlivyokuwa, na nitawafanya kustawi zaidi kuliko mlivyokuwa zamani, kwa kuwa mtajua yakwamba mimi ni Yahwe.12Nitawaleta watu, watu wangu Israeli, kutembea juu yenu. Watakumiliki, na utakuwa urithi wao, na hutasababisha tena watoto wao kufa.

13Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu wanakwambia, “Wewe unakula watu, na watoto wa nchi yako wamekufa,”14kwa hiyo hautawala watu wangu tena, na hutalifanya tena taifa lako kuomboleza vifo vyao. Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.15Wala sintokuruhusu kusikiliza fedheha za mataifa tena; hautachukua tena aibu ya watu au kufanya taifa lako kuanguka-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

16Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,17“Mwanadamu, wakati nyumba ya Israeli walipoikalia nchi yao, waliinajisi kwa njia zao na matendo yao. Njia zao zilikuwa kama uchafu wa hedhi ya mwanamke mbele yangu.18Hivyo nilimwaga ghadhabu yangu juu yao kwa ajili ya damu ambayo waliyoimwaga juu ya nchi na kwa ajili ya uchafu wa hiyo kwa sanamu zao.19Nimewatawanya miongoni mwa mataifa; walitawanyika katika nchi nyingi. Nimewahukumu kulingana na njia zao na matendo yao.20Kisha wakaenda kati ya mataifa, na popote walipoenda, walilitukana jina langu takatifu wakati watu waliwasema, ‘Je! Hawa kweli ni watu wa Yahwe? Kwa kuwa wamefukuzwa nje ya nchi yake.21Lakini nilikuwa na huruma kwa ajili ya jina langu takatifu ambalo nyumba ya Israeli walilinajisi miongoni mwa mataifa, walipoenda huko.

22Kwa hiyo waambie nyumba ya Israeli, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Sifanyi haya kwa ajili yenu, nyumba ya Israeli, lakini jina langu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa kila sehemu mlipoenda.23Kwa kuwa nitalifanya jina langu kuu kuwa takatifu, mlilolitukana miongoni mwa mataifa-katikati ya mataifa, mmelitukana. Kisha mataifa watajua kwamba mimi ni Yahwe-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe-asemavyo-wakati mtakapoona kwamba mimi ni mtakatifu.

24Nitawachukua kutoka mataifa na kuwakusanya kutoka kila nchi, na nitawaleta hata nchi yenu.25Kisha nitanyunyiza maji masafi juu yenu ili muwe wasafi kutoka kwenye uchafu wote, na nitawasafisha kutoka sanamu zenu zenu.26Nitawapatia moyo mpya na roho mpya sehemu zenu za ndani, na nitautoa moyo wa jiwe kutoka kwenye nyama zenu. Kwa kuwa nitawapatia moyo wa nyama.27Nitaiweka Roho yangu ndani yenu na kuwawezesha kutembea katika sheria zangu na kuziweka hukumu zangu, hivyo mtazitenda.28Kisha mtakaa katika nchi niliyowapa babu zenu; mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu.29Kwa kuwa nitawaokoa kutokana na uchafu wenu wote. Nitaita ngano na kuiongeza. Sitaweka tena njaa juu yenu.30Nitaongeza tunda la mti na kuzalisha kwenye mashamba ili kwamba msichukue tena aibu ya njaa juu ya mataifa.31Kisha mtazikumbuka njia zenu mbaya na matendo yenu ambayo hayakuwa mazuri, na mtaonyesha chuki kwenye nyuso zenu kwa sababu ya dhambi zenu na matendo yenu maovu.32Sifanyi hili kwa ajili yenu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ijulikane kwenu. Hivyo tahayarikeni na kufadhaika kwa sababu ya njia zenu, nyumba ya Israeli.

33Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku niliyowatakasa kutoka kwenye uovu wenu wote, nitaifanya miji ikaliwe na kuzijenga sehemu zilizoharibiwa.34Kwa kuwa mtailima nchi iliyoharibiwa hadi itakapoonekana haijaaharibika mbele za macho ya wote wapitao karibu.35Kisha watasema, “Hii nchi ilikuwa ukiwa, lakini imekuwa kama bustani ya Edeni; miji ya ukiwa na isiyo na wakaaji iliyo magofu ambayo ilibomolewa sasa inakaliwa.36Kisha mataifa mengine waliowazunguka watajua ya kwamba mimi ni Yahwe, kwamba nimejenga palipokuwa pameharibiwa na kuipanda mbegu sehemu iliyokuwa ukiwa.

37Bwana Yahwe asema hivi: Tena nitaulizwa na nyumba ya Israeli kufanya hivi kwa ajili yao, kuwaongeza kama kundi la watu.38Kama kundi lililotengwa kwa ajili ya sadaka, kama kundi katika Yerusalimu katika sikukuu yake iliyoteuliwa, hivyo miji itaharibiwa kwa kujazwa na makundi ya watu na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

37

1Mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu, na akanitoa kwa Roho wa Bwana Yahwe na kuniweka chini katikati ya bonde; lilikuwa limejaa mifupa.2Kisha akanifanya kupita kati yao kuizunguka pande zote. Tazama! Mingi yao mikubwa ilikuwa katika bonde! Ilikuwa mikavu sana.3Akaniambia, “Mwanadamu, Je! Hii mifupa inaweza kuishi?” Hivyo nikasema, “Bwana Yahwe, wajua wewe pekee.”

4Kisha akaniambia, “Tabiri juu ya hii mifupa na iambie, ‘Mifupa mikavu. Lisikilizeni neno la Yahwe.5Bwana Yahwe asema hivi kwenye hii mifupa: Tazama! Nitatia pumzi juu yenu, nanyi mtaishi.6Nitaweka mishipa juu yenu na kuleta nyama juu yenu. Nitawafunika kwa ngozi na kuweka pumzi ndani yenu hivyo mtaishi. Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe.”’

7Hivyo nikatoa unabii kama nilivyokuwa nimeamriwa, tazama palikuwa na mshindo mkuu, na tetemeko la nchi. Kisha mifupa ikasogeleana pamoja-mfupa juu ya mfupa.8Nikatazama na, kumbe, mishipa ilikuwa juu sasa, na nyama ikatoka juu na ngozi ikazifunika. Lakini hapakuwa na pumzi juu yao.

9Kisha Yahwe akanambia, “utabirie upepo tabiri, mwanadamu, na ukaumbie upepo, ‘Bwana Yahwe asema hivi: njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, kutoka pande za pepo nne ukawapilizie hawa waliouawa, hivyo wapate kuishi.”’10Hivyo nikatabiri kama nilivyokuwa nimeamriwa; pumzi ikawajilia na wakaishi. Kisha wakasimama kwa miguu yao, jeshi moja kubwa sana.

11Kisha Yahwe akanambia, “Mwanadamu, mifupa hii yote ni ya nyumba ya Israeli. Tazama! Wanasema, ‘Mifupa yetu imekauka, na tumaini letu limepotea. Tumekatwa.’12Kwa hiyo tabiri na waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nitayafunua makabiri yenu na kuwapandisha kutoka kwayo, watu wangu. Nitakurudisha hata katika nchi ya Israeli.13Kisha mtajua kwamba mimi ni Yahwe, nitakapo yafunua makaburi yenu na kuwatoa kutoka kwao, watu wangu.14Nitaweka Roho wangu ndani yenu hivyo mtaishi, na nitawafanya kupumzika katika nchi yenu mtakapojua yakwamba mimi ni Yahwe. Nasema na nitayafanya hayo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”’

15Kisha neno la Yahwe likanijia, likisema,16“Sasa wewe, mwanadamu, chukua fimbo moja kwa ajili yako na andika juu yake, ‘Kwa ajili Yuda na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake,’ Kisha fimbo nyingine andika juu yake, ‘Kwa kuwa Yusufu, tawi la Efraimu, na kwa ajili ya watu wa Israeli, wenzake.17Walete wote pamoja kwenye fimbo moja, ili wawe kitu kimoja katika mkono wako.

18Wakati watu wako watakapokwambia na kusema, ‘Je! Hutatuambia haya mambo yako yana maana gani?’19kisha waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nalichukua tawi la Yusufu ambalo lipo kwenye mkono wa Efraimu na kabila za Israeli wenzake na kuungana nalo hata kwenye tawi la Yuda, ili kwamba wawe tawi moja, na watakuwa kitu kimoja katika mikono yangu.’20Shika kwenye mkono wako na matawi uliyoandika mbele ya macho yao.21Waambie, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Nakaribia kuwachukua watu wa Israeli kutoka miongoni mwa mataifa walipoenda. Nitawakusanya kutoka nchi zilizozunguka na nitawaleta kwenye nchi yao.22Nitawafanya kuwa taifa moja katika nchi, juu ya milima ya Israeli, na kutakuwa na mfalme mmoja kama mfalme juu yao wote, na hawatakuwa mataifa mawili tena. Hawatagawanyika kwenye falme mbili tena.23Kisha hawatajitia unajisi tena kwa sanamu zao, mambo yao yachukizao, au dhambi zao nyingine. Kwa kuwa nitawaokoa kutoka matendo yao ya uongo ambayo wamefanya dhambi, na nitawatakasa, hivyo watakuwa watu wangu nami nitakuwa Mungu wao.

24Daudi mtumishi wangu atakuwa mfalme juu yao. Hivyo kutakuwa na mchungaji mmoja juu yao wote, na wataishi kulingana na sheria zangu na watazitunza amri zangu na kuzitii.25Wataishi katika nchi niliyowapatia watumishi wangu Yakobo, ambapo baba zenu walipoishi. Wataishi humo milele-wao, watoto wao, na wajukuu zao, kwa Daudi mtumishi wangu atakuwa mkuu wao milele.26Nitaweka agano la amani pamoja nao. Litakuwa agano la milele pamoja nao. Nitawaweka na kuwazidisha na kupaweka mahali patakatifu pangu katikati yao milele.27Maskani yangu yatakuwa pamoja nao; Nitakuwa Mungu wao, na watakuwa watu wangu.28Kisha mataifa watajua yakwamba mimi ni Yahwe niliyewatenga Israeli, wakati mahali pangu patakatifu patakapokuwa katikati yao milele.”

38

1Neno la Yahwe likanijia, likisema,2“Mwanadamu, weka uso wako kumwelekea Gogu, nchi ya Magogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali; na kutabiri dhidi yake.3Sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako, Gogu, kiongozi mkuu wa Mesheki na Tubali.4Hivyo nitakugeuza na kuweka kulabu kwenye taya yako; nitakupeleka nje pamoja na jeshi lako lote, farasi, na waendesha farasi, wote wakiwa wamevaa silaha, kusanyiko kubwa pamoja na ngao ndogo na ngao kubwa, wote wakishikilia panga!5Persia, Kushi, Uajemi wapo pamoja nao, wote pamoja na ngao na chapeo!6Gomeri na jeshi lake lote, na Beth-Togarma, kutoka sehemu za mbali ya kaskazini, na jeshi lake lote! Watu wengi wako pamoja nawe!

7Kuwa tayari! Ndio, jiandae na jeshi lako waliokusanyika pamoja na wewe, na amiri wao mkuu.8Utaitwa baada ya siku nyingi, na baada ya miaka michache utaenda kwenye nchi iliyofunikwa kutoka upanga na ambayo iliyokusanywa kutoka watu wengi, iliyowkusanya kuwarudisha milima ya Israeli ambayo imeendelea kuangamizwa. Lakini watu wa nchi watatolewa na kabila za watu, na wataishi salama, wote!9Hivyo utapanda juu kama tufani iendavyo; utakuwa kama wingu lililofunika nchi, wewe na jeshi lako lote, maaskari wako wote pamoja na wewe.

10Bwana Yahwe asema hivi: Itakuwa siku hiyo hayo mawazo yataingia moyoni mwako, na utatunga njama mbaya.’11Kisha utasema, ‘nitapanda hata nchi iliyowazi; nitaenda hata kwa watu wapole waishio salama, wote wakiishi mahali ambapo hakuna kuta wala makomeo, na mahali ambapo hakuna malango ya mji.12Nitanyakua mateka na kuiba mateka, ili nilete mkono wangu juu kuwaangamiza wale wakazi wapya, na juu ya watu waliokusanyika kutoka mataifa, watu wale waongezao wanyama na mali, na wale waishio katikati ya dunia.’13Sheba na Dedani, na wafanya biashara wa Tarshishi pamoja na mahodari wake wote watakwambia, ‘Je, umekuja kuteka nyara? Je, umewakusanya majeshi yako kuchukua mateka, kuchukua fedha na dhahabu, kuchukua mifugo yao na mali na kuwakokota mateka wengi sana?’

14Kwa hiyo tabiri, mwanadamu, na mwambie Gogu, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Katika siku hiyo, wakati watu wangu Israeli watakapoishi salama, je, hutajifunza kuhusu wao?15Utakuja kutoka mahali pangu mbali katika kaskazini pamoja na jeshi kubwa, wote wakiendesha farasi, kusanyiko kubwa, jeshi kubwa.16Utawashambulia watu wangu Israeli kama wingu lifunikavyo nchi. Katika siku za baadaye nitakuleta juu ya nchi yangu, ili mataifa wanijue nitakapojifunua mwenyewe kupitia wewe, Gogu, kuwa mtakatifu mbele ya macho yao.

17Bwana Yahwe asema hivi: Je, wewe siye yule ambaye niliyeongea naye katika siku za zamani kwa mkono wa watumishi wangu, manabii wa Israeli, waliotabiri katika mda wao wenyewe kwa miaka niliyowaleta juu yao?18Basi itakuwa katika siku hiyo wakati Gogu atakapo ishambulia nchi ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-ghadhabu yangu itapanda katika hasira yangu.19Katika wivu wangu katika hasira ya moto wangu, ninasema kwamba katika siku hiyo kutakuwa na tetemeko kubwa la nchi katika nchi ya Israeli.20Watatetemeka mbele yangu-samaki wa baharini na ndege wa angani, wanyama wa mashambani, na viumbe watambaao juu ya nchi, na kila mtu aliyeko juu ya uso wa nchi. Milima itaangushwa chini majabali yataanguka, hadi kila ukuta utaanguka kwenye nchi.21Nitaita upanga dhidi yake juu ya milima yangu yote-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-upanga wa kila mtu utakuwa kinyume na ndugu yake.22Kisha nitamuhukumu kwa tauni na damu; na kufurika mvua na mvua ya mawe na kuchoma kiberiti nitainyeshea chini juu yake na jeshi lake na mataifa mengi yaliyo pamoja naye.23Kwa kuwa nitaonyesha ukuu wangu na utakatifu wangu na nitafanya kujulikana mimi mwenyewe katika macho ya mataifa mengi, na watajua kwamba mimi ni Yahwe.”

39

1“Kisha wewe, mwanadamu, tabiri dhidi ya Gogu na sema, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Tazama! Ni kinyume nawe, Gogu, mkuu wa Mesheki na Tubali.2Nitakugeuza na kukuongoza; nitakupandisha juu kutoka mbali kaskazini na kukuleta hata milima ya Israeli.3Kisha nitaufunga upinde wako utoke katika mkono wako wa kushoto na kuifanya mishale kuanguka kutoka kwenye mkono wako wa kuume.4Utaanguka juu ya milima ya Israeli-wewe na jeshi lako lote na maaskari walio pamoja nawe. Nitawapatia ndege na wanyama pori wa mashambani kwa ajili ya chakula.5Utaanguka juu ya uso wa shamba, kwa kuwa mimi mwenyewe nimesema hivyo-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.6Kisha nitapeleka moto juu ya Magogu na kwa wale waishio salama juu ya pwani, na watajua ya kwamba mimi ni Yahwe.

7Kwa kuwa nitalifanya jina langu takatifu lijulikane kati ya watu wangu Israeli, na sitaruhusu tena jina langu takatifu litukanwe; mataifa watajua kwamba mimi ni Yahwe, Mtakatifu katika Israeli.8Tazama! Siku inakuja, na itachukua nafasi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

9Hao wakaao katika miji ya Israeli watatoka nje na watatumia silaha kuwasha moto na kutengeneza moto na kuwachoma-ngao ndogo, ngao kubwa, pinde, mishale, rungu, na mikuki; watatengeneza mioto pamoja nao kwa muda wa siku saba.10Hawatakusanya kuni kutoka mashambani wala kukata miti kutoka kwenye misitu, kwa kuwa watazichoma hizo silaha; watawateka nyara wale watakaotaka kuwateka nyara-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

11Kisha itakuwa katika hiyo siku ambayo nitaifanya sehemu huko kwa ajili ya Gogu-kaburi la Israeli, bonde kwa ajili ya wale wanaosafiri hata mashariki ya bahari. Litawazuia wale wanaotegemea kupita. Huko watamzika Gogu pamoja na kundi lake lote. Watapaita bonde la Hamon-Gogu.

12Kwa muda wa siku saba nyumba ya Israeli itawazika ili kuitakasa nchi.13Kwa kuwa watu wa nchi watawazika; itakuwa siku ya kukumbukwa kwao wakati nitakapo tukuzwa-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

14Kisha watawateua watu kuendelea kwenda kwenye nchi, kuwatafuta wale waliokuwa wakisafiri, lakini waliokufa na miili yao kubaki juu ya uso wa nchi, ili kwamba waweze kuwazika, kwa ajili ya kusafisha nchi. Katika siku ya mwisho ya mwezi wa saba wataanza kutafuta.15Kama hawa watu wapitao kwenye nchi, watakapoona mfupa wowote wa binadamu, wataweka alama kwa huo, hadi wachimba kaburi watakapokuja na kuizika katika bonde la Hamoni Gogu.16Kutakuwa na mji huko unaitwa Hamona. Wataitakasa nchi kwa njia hii.

17Kwako wewe, mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Waambie ndege wote wenye mabawa na wanyama wote wa porini katika mashamba, ‘Kusanyikeni pamoja na mje. Kusanyikeni kutoka pande zote kwenda kwenye dhabihu yote ambayo mimi mwenyewe ninayoifanya kwa ajili yako, dhabihu kubwa juu ya milima ya Israeli, ili kwamba mle nyama na kunywa damu.18Mtakula nyama ya walio hodari na kunywa damu ya wakuu wa dunia; watakuwa kondoo waume, wana kondoo, mbuzi, na ng'ombe, wote walikuwa wanene katika Basheni.19Kisha mtakula mafuta hata kuridhika kwenu; mtakunywa damu hadi kulewa; hii itakuwa dhabihu nitakayoichinja kwa ajili yenu.20Mtatosheka kwenye meza yangu pamoja na farasi, magari ya farasi, shujaa, na kila mtu wa vita-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.’

21Nitauweka utukufu wangu kati ya mataifa, na mataifa yote yataona hukumu yangu ninayo ionyesha na mkono wangu nimeuweka juu yao.22Nyumba ya Israeli itajua yakwamba mimi ni Yahwe Mungu wao kutoka hiyo siku na kuendelea.23Mataifa yatajua kwamba nyumba ya Israeli wameenda uhamishoni kwa sababu ya udhalimu wao kwa kunisaliti, hivyo naficha uso wangu kwao na kuwaweka kwenye mkono wa maadui zao ili kwamba wote waanguke kwa upanga.24Nimewafanyia kutokana na uchafu wao na dhambi zao, nitakapokuwa nimeuficha uso wangu kwao.

25Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Sasa nitawarudisha watu wa Yakobo, na kuwa na huruma juu ya nyumba yote ya Israeli, wakati nitakapoona wivu kwa ajili ya jina langu.26Kisha watabeba aibu yao na uhaini mkubwa walio nihaini. Watayasahau haya yote watakapopumzika katika nchi yao katika usalama, wala hakuna mtu atakaye waogofya.27Wakati nitakapokuwa nimewarudisha kutoka kwa watu na kuwakusanya kutoka kwenye nchi za maadui zao, nitajionyesha mimi mwenyewe kuwa mtakatifu kwenye uso wa mataifa mengi.28Kisha watajua kwamba mimi ni Yahwe Mungu wao, kwa kuwa nimewapeleka utumwani kati ya mataifa, lakini kisha nitawakusanya kuwarudisha hata nchi yao. Sitamuacha hata mmoja wao kati ya mataifa.29Sitawaficha uso wangu kwao wakati nitakapomwaga Roho wangu katika nyumba ya Israeli-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

40

1Katika mwaka wa ishirini na tano wa kuhamishwa kwetu mwanzoni mwa mwaka siku ya kumi ya mwezi, katika mwaka wa kumi na nne baada ya mji kuchukuliwa-katika siku hiyo hiyo, mkono wa Yahwe ulikuwa juu yangu na alinichukua huko.2Katika maono ya Mungu akanileta hata nchi ya Israeli. Akanileta kupumzika juu ya kila mlima mrefu sana; upande wa kusini kulikuwa na monekano kana kwamba majengo ya mji.3Kisha akanileta huko. Tazama, kulikuwa na mtu! Mwonekano wake ulikuwa kama mwonekano wa shaba. Alikuwa na uzi wa kitani na mwanzi wa kupimia mkononi mwake, na alisimama katika lango la mji.4Huyo mtu akanambia, “Mwanadamu, tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako, na elekeza moyo wako juu ya yote ninayokufunulia, kwa kuwa ulinileta hapa ili niweze kukufunulia haya wewe. Toa taarifa ya kila kitu utakachokiona kwa nyumba ya Israeli.

5Kulikuwa ukuta uliokuwa umezunguka eneo la hekalu. Urefu wa kipimo cha mwanzi katika mkono wa mtu ulikuwa dhiraa sita urefu, kila urefu wa dhiraa ulikuwa dhiraa moja na kipimo cha kiganja cha mkono urefu. Aliupima ukuta; ulikuwa kipimo cha mwanzi mmoja na ufito mmoja urefu.

6Kisha akaenda hata kwenye lango la hekalu lililokuwa limeelekea mashariki. Akapanda ngazi na kuipima kizingiti cha lango-mwanzi mmoja upana.7Vyumba vya ulinzi vilikuwa kila mwanzi mmoja urefu na mwanzi mmoja upana; kulikuwa na dhiraa tano katika kila vyumba viwili, na kizingiti cha lango la hekalu karibu na tawa la hekalu kilikuwa mwanzi mmoja urefu.

8Akapima tawa la lango; ulikuwa mwanzi mmoja urefu.9Akapima tawa la lango. Ilikuwa mwanzi mmoja kwenda chini. Mihimili ilikuwa dhiraa mbili upana. Hili lilikuwa tawa la lango kuelekea hekalu.10Kulikuwa na vyumba vitatu vya ulinzi pande zote za lango la mashariki, na yote yalikuwa na kipimo kile kile, na kuta zilizokuwa zimezigawanya zilikuwa na kipimo kile kile.

11Kisha yule mtu akapima upana wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi; na akapima urefu wa njia ya lango la kuingia-dhiraa kumi na tatu.12Akaupima ukuta uliokuwa mpaka mbele ya vyumba-dhiraa moja urefu. Vyumba vilipimwa dhiraa sita kila upande.13Kisha akapima lango la njia kutoka kwenye paa ya chumba kimoja kuelekea chumba kingine-dhiraa ishirini na tano, kutoka lango la kuingia chumba cha kwanza kuelekea kile cha pili.14Kisha akapima ukuta uliokuwa umeenda kati ya vyumba vya ulinzi-dhiraa sitini urefu; alipima kwa mbali na tawa la lango.15Lango la kuingia kutoka lango la mbele kuelekea lango jingine la tawa la mwisho lilikuwa dhiraa hamsini.16Kulikuwa na madirisha yaliyokuwa yamefungwa kuelekea vyumba na kuelekea nguzo zake kati ya malango kuzunguka kote; na vivyo hivyo kwa mabaraza. Kulikuwa na madirisha pande zote za ndani, na kila mhimili ulikuwa umepambwa kwa mitende.

17Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa nje mwa hekalu. Tazama, kulikuwa na vyumba, na kulikuwa na sakafu katika ua, pamoja na vyumba thelathini baada ya sakafu.18Sakafu ilienda juu hata upande wa malango, na upana wake ulikuwa sawsawa na urefu wa malango. Hii ilikuwa sakafu ya chini.19Kisha huyo mtu akapima umbali kutoka mebele ya lango la chini hata mbele ya lango la ndani; ilikuwa dhiraa mia moja upande wa mashariki, na sawasawa na upande wa kaskazini.

20Kisha akapima urefu na upana wa lango lililokuwa upande wa kaskazini mwa ua wa nje.21Kulikuwa na vyumba vitatu pande zote za lango, na lango na matawa yake yalipimwa sawa na lango kubwa-dhiraa hamsini upana wote na dhiraa ishirini na tano upana.22Madirisha yake, tawa, vyumba, na mitende yake vilikabiliana na lango ambalo linaloelekea mashariki. Ngazi saba kuupandia juu hata kwenye tawa lake.23Kulikuwa na lango kwenye ua wa ndani mbele kuelekea mashariki; huyo mtu alipima kutoka lango moja hadi lango lingine-dhiraa mia moja umbali.

24Kisha huyo mtu akanileta hata kwenye lango la kuingia la kusini, na kuta zake na tawa vilipimwa sawa kama malango mengine ya nje.25Kulikuwa na madirisha yaliyofungwa katika lango la njia na tawa lake kama lile lango. Lango la kusini na tawa lake vilipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.26Kulikuwa na ngazi saba hadi kwenye lango na matawa yake, na kulikuwa na mitende iliyochongoka juu ya kuta pande zote.27Kulikuwa na lango la ua wa ndani upande wa kusini, na yule mtu akapima kutoka hilo lango hata lango la kuingia upande wa kusini-dhiraa mia moja umbali.

28Kisha huyo mtu akanileta hata ua wa ndani karibu na lango lake la kusini, ambalo lilikuwa na vipimo vile vile kama malango mengine.29Vyumba vyake, kuta, na matao vilipimwa sawa kama malango mengine; kulikuwa na madirisha kuzunguka matao yote. Lango la ndani na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.30Pia kulikuwa na matao pande zote za kuta za ndani; haya yalikuwa dhiraa ishirini na tano urefu na dhiraa tano upana.31Hili tawa lilielekea ua wa nje pamoja na mitende iliyochongwa juu ya kuta zake na ngazi nane kuupandia.

32Kisha yule mtu akanileta hata kwenye ua wa ndani karibu na njia ya kaskazini na kulipima lango, ambalo lilikuwa na vipimo sawa kama malango mengine.33Vyumba vyake, kuta, na matawa yalikuwa na kipima sawa kama cha malango, na kulikuwa na madirisha pande zote. Lango la ndani na matawa yake yalikuwa dhiraa hamsini urefu na dhiraa ishirini na tano upana.34Matawa yake yalielekea nje ya ua; ilikuwa na mitende pande zote za hiyo na ngazi nane za kuupandia.

35Kisha huyo mtu akanileta hata lango la kaskazini na kulipima; likapimwa vivyo hivyo kama malango mengine.36Vyumba vyake, kuta, na ukumbi vilipimwa sawa na malango mengine, na kulikuwa na madirisha pande zote. Njia ya lango na matao yake yalipimwa dhiraa hamsini urefu na upana dhiraa ishirini na tano.37Tatawa lake lilielekea ua wa nje; ilikuwa na mitende pande zote za huo na ngazi nane kuupandia.

38Kulikuwa na chumba pamoja na mlango karibu na kila lango la ndani. Hapa ndipo ambako walipo oshea sadaka za kutekezwa.39Kulikuwa na meza mbili kila upande wa kila ukumbi, ambako sadaka ya kuteketezwa ilipochinjiwa, na pia sadaka ya dhambi na sadaka ya hatia.40Karibu na ukuta wa ua, kuelekea juu kwenye lango kuelekea kaskazini, kulikuwa na meza mbili. Pia kwa upande mwingine kulikuwa na meza mbili kwenye lango la ukumbi.41Kulikuwa na meza nne pande zote karibu na lango; wakachinja wanyama juu ya meza nane.42Kulikuwa na meza nne za mawe yaliyochongwa kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, dhiraa moja na nusu urefu, dhiraa moja na nusu upana, na kimo dhiraa moja. Juu yake waliweka vyombo pamoja ambavyo walivichinjia sadaka za kuteketezwa kwa ajili ya sadaka.43Kulabu mbili ujazo wa kiganja urefu uliokuwa umeunganishwa katika ua pande zote, na nyama ya matoleo ilikuwa imewekwa juu ya meza.

44Karibu na lango la ndani, katika ua wa ndani, kulikuwa na vyumba vya waimbaji. Moja ya hivi vyumba kilikuwa upande wa kaskazini, na kingine kusini.45Kisha yule mtu akaniambia, “Hiki chumba kinachoelekea kusini ni kwa ajili ya makuhani walio zamu katika hekalu.46Chumba kilichoelekea kaskazini kilikuwa kwa ajili ya makuhani waliokuwa zamu kwenye madhabahu. Hawa ni wana wa Sadoki ambaye huja humkaribia Yahwe kumtumikia; ambao ni miongoni mwa wana wa Lawi.”

47Kisha akaupima ule ua-dhiraa mia moja urefu na dhiraa mia moja upana mraba, pamoja na madhabahu mbele ya nyumba.

48Kisha yule mtu akanileta hata kwenye varanda ya nyumba na kupima mwimo wa milango yake-ilikuwa dhiraa tano unene upande huu. Njia ya kuingilia yenyewe ilikuwa dhiraa kumi na nne, na kuta pande zote za huo zilikuwa dhraa tatu upana.49Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake ulikuwa dhiraa kumi na moja. Kulikuwa na ngazi zilizokuwa zimepanda juu na nguzo zilizokuwa zimesimama pande zote za huo.

41

1Kisha yule mtu akanileta mahali patakatifu pa hekalu na mihimili-dhiraa sita upana pande zote.2Upana wa maingilio ulikuwa dhiraa kumi; ukuta kila upande dhiraa tano urefu kila upande. Kisha yule mtu akapima ukubwa wa mahali patakatifu-dhiraa arobaini upana urefu na dhiraa ishirini upana.

3Kisha yule mtu akaenda hata mahali patakatifu sana na kuipima mihimili ya matokeo-dhiraa mbili-kuta pande zote zilikuwa dhiraa saba upana.4Kisha akapima urefu wa vyumba-dhiraa ishirini. Upana wake-dhiraa ishirini hata mbele kwenye ukumbi wa hekalu. Kisha akanambia, “Hapa ndipo mahali patakatifu sana.”

5Kisha yule akapima kuta za nyumba-zilikuwa dhiraa sita unene. Upana wa kila upande wa chumba kuzunguka nyumba dhiraa nne upana.6Kulikuwa na pande tatu za vyumba, chumba kimoja juu ya kingine, vyumba thelathini, kulikuwa na kibao kitokezacho ukutani kuzunguka ukuta wa nyumba, kusaidia pande zote za vyumba, kwa kuwa hapakuwa na msaada uliokuwa umewekwa kwenye ukuta wa nyumba.7Hivyo mbavu za nyumba zilipanuka na kuzunguka kwenda juu, kwa kuwa nyumba ilizunguka kwenda juu, na ngazi kuelekea juu hata sehemu ya juu, kupitia sehemu ya katikati.

8Kisha nikaona sehemu iliyoinuka kuzunguka nyumba, msingi kwa ajili ya pande za vyumba; ikapimwa fimbo nzima urefu-dhiraa sita.9Upana wa ukuta wa vyumba vya pembeni kwa upande wa nje ulikuwa dhiraa tano. Kulikuwa na sehemu ya wazi kwa upande wa nje wa hivi vyumba katika patakatifu.10Kwa upande mwingine wa hii sehemu ya wazi kulikuwa na vyumba vya makuhani upande wa nje; hii sehemu ilikuwa na dhiraa ishirini upana kupazunguka patakatifu.11Kulikuwa na milango kwenye vyumba vya pembeni kutoka sehemu ya wazi nyingine-njia ya mlango moja uliokuwa upande wa kaskazini, na mwingine upande wa kusini. Upana wa hili eneo la wazi ulikuwa na dhiraa tano kupazunguka.

12Lile jengo lililokuwa limeelekea kwenye ua upande wa magaribi dhiraa sabini upana. Ukuta wake ulipimwa dhiraa tano pande zote, na ilikuwa dhiraa tisini urefu.

13Kisha yule mtu akapapima patakatifu-dhiraa mia moja urefu. Jengo lililokuwa limetengeka, kuta zake, na kwenye ua pia palipimwa dhiraa mia moja urefu.14Upana wa mbele kwenye ua mbele ya patakatifu pia kulikuwa dhiraa mia moja.

15Kisha yule mtu akapima urefu wa jengo karibu na patakatifu, kwa upande wake wa magharibi, na juu ya baraza pande zote-dhiraa mia moja. Mahali patakatifu na varanda,16kuta za ndani na madirisha, pamoja na madirisha madogo, na baraza za pande zote kwenye pande tatu, zilikuwa zimefungwa kwa mbao.17Juu ya lango la kuingilia hata patakatifu pa ndani na kuwekwa karibu na kuta kulikuwa na pazia lililokuwa limepimwa.18Palikuwa pamepambwa na makerubi mitende; pamoja na mitende kati ya kerubi na kerubi, na kila kerubi lilikuwa na nyuso mbili:19uso wa mtu aliyekuwa ameelekea mtende mmoja, na uso wa mwana simba ulitazama kuelekea mtende kwa upande mwingine. Vilifunikwa kuzunguka malango ya kuingia yote ya nyumba.20Kutoka chini hata juu kwenye njia ya mlango, makerubi na mtende vilifunikwa na ukuta wa nje ya nyumba.

21Mihimili ya lango la mahali patakatifu lilikuwa mraba. Umbo lao lilikuwa kama umbo la22kwanza madhabahu ya mbao mbele ya mahali patakatifu, ambapo kulikuwa na dhiraa tatu kwenda juu na dhiraa urefu kwa kila upande. Pembe zake mihimili, kitako, na kiunzi kilitengenezwa kwa mbao. Kisha yule mtu akaniambia, “Hii ni meza ambayo itakuwa kwa ajili ya Yahwe.”23Kulikuwa na milango miwili kwa ajili ya mahali patakatifu na mahali patakatifu sana.24Hii milango ilikuwa na bawaba mbili kila mlango paneli, paneli mbili kwa ajili ya mlango mmoja na paneli mbili kwa ajili ya mwingine.25Ilifunikwa-juu ya milango ya mahali patakatifu ambapo makerubi na mti wa mtende kama kuta ilipambwa, kulikuwa na paa ya mbao juu ya varanda kwa mbele.26Kulikuwa na madirisha madogo ya miti ya mitende kwenye varanda pande zote. Hivyo vilikuwa vyumba vya pembeni ya nyumba, na pia ilizielekea dari.

42

1Kisha yule mtu akanituma kwenda ua wa nje upande wa kaskazini, akanileta kwenye vyumba mbele ya ua wa nje na ukuta wa nje kaskazini.2Hivyo vyumba vilikuwa dhiraa mia moja karibu na mbele yake na dhiraa hamsini upana.3Baadhi ya hivyo vyumba vilielekea ua wa ndani na vilikuwa na dhiraa ishirini kutoka patakatifu. Kulikuwa na vyumba vitatu vinavyolingana, na kingine juu kilichokuwa kimetazama chini kuelekea kingine vilikuwa vimefunguliwa, vilikuwa na pakutokea. Baadhi ya vyumba vilielekea nje kwenye ua wa nje.4Njia dhiraa kumi upana dhiraa mia moja urefu kueleikea mbele ya vyumba. Milango ya vyumba ilikuwa mbele kaskazini.5Lakini kumbi za juu zilikuwa ndogo, kwa ajili ya njia za kutembea zilichukua kutoka kwazo sehemu kubwa kulikuwa walivyofanya kwenye vyumba vya chini na katikati usawa wa jengo.6Kwa kuwa orofa tatu hapakuwa na mihimili, kama zile nyua, ambazo zilikuwa na mihimili. Hivyo usawa wa vyumba vya juu vilikuwa sawa sawa katika kipimo cha kulinganisha na vyumba vya chini na usawa wa katikakati.7Ukuta wa nje karibu na vyumba mbele ya ua wa nje, ua uliokuwa mbele ya vyumba. Huo ukuta ulikuwa dhiraa hamsini urefu.8Urefu wa vyumba vya ua wa nje ulikuwa dhiraa hamsini, na vyumba vilivyokuwa vimeelekea patakatifu vilikuwa dhiraa mia moja urefu.9Kulikuwa na mahali pa kuingilia kwenye vyumba vidogo zaidi kutoka upande mashariki, kuingia kutoka ua wa nje.

10Karibu na ukuta wa ua wa nje juu ya upande wa mgaribi pa ua wa ndani, mbele ya patakatifu pa ua wa nje, pia kulikuwa na vyumba na njia ya mbele yao.11Zilikuwa kama umbo la vyumba kwa upande wa kaskazini. Zilikuwa urefu ule ule na upana na matokeo yale yale na mipangilio na madirisha.12Kwa upande wa kusini kulikuwa na madirisha kwenye vyumba ambavyo vilikuwa kama yale yaliyokuwa upande wa kaskazini. Ndani ilikuwa na mlango kwenye kichwa chake, na njia ilifunguliwa kwenye vyumba tafauti. Upande mashariki kulikuwa na malango wa njia kwenye njia mwishoni.

13Kisha yule mtu akaniambia, “Vyumba vya kaskazini na vyumba vya kusini vilivyokuwa mbele ya ua wa nje ni vyumba vitakatifu ambapo makuhani wafanyao kazi karibu sana na Yahwe waweze kula chakula kitakatifu sana. Wataweka vitu vitakatifu sana-sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia-kwa kuwa hapa ni mahali patakatifu.14Wakati makuhani watakapoingia hapo, wasitoke nje ya mahali patakatifu kwa ua wa nje, bila kuweka mavazi karibu mahali wahudumupo, kwa kuwa hapa ni patakatifu. Hivyo watavalia mahali pengine nguo kabla ya kwenda karibu na watu.”

15Yule mtu akamaliza kupima ndani ya nyumba na kisha akanichukua nje ya lango lililokuwa limeelekea magharibi na kuzipima sehemu zote zilizokuwa zimepazunguka hapo.16Akaupima upande wa mashariki na fimbo ya kupimia-dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia.17Akaupima upande wa kaskazini-dhiraa mia tano na fimbo ya kupimia.18Pia akaupima upande wa kusini dhraa mia tano na fimbo ya kupimia.19Pia akageuka na kuupima upande wa magharibi dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia,20Akaipima pande nne. Ilikuwa na ukuta umeizunguka ilikuwa dhiraa mia tano urefu, na dhiraa mia tano upana, kulitenganisha umbo takatifu kutoka ambapo ni pa kawaida.

43

1Yule mtu kisha akanileta hata kwenye lango lililokuwa linaelekea mashariki.2Tazama! Utukufu wa Mungu wa Israeli ukaja kutoka mashariki; sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi, na nchi iling'aa kwa utukufu wake.3Yalikuwa yanalingana na sura ya ono nililolona, kulingana na ono nililokuwa nimeliona wakati alipokuja kuuteketeza mji, na maono yalikuwa kama maono ambayo niliyokuwa nimeyaona Keberi Kanali nikaanguka kifudi fudi.4Hivyo utukufu wa Yahwe ukaja kwenye nyumba ya karibu na njia ya lango lililokuwa wazi kwa upande wa magharibi.5Kisha Roho akanichukua na kunileta kwenye ua wa ndani. Tazama! Utukufu wa Yahwe ulikuwa umeijaza nyumba.

6Mtu alisimama karibu na mimi, na nikamsikia mtu mwingine akizungumza na mimi kutoka kwenye nyumba.7Akaniambia, “Mwanadamu, hapa ndipo mahali pangu pa enzi na mahali kwa ajili ya ya miguu yangu, ambapo nitaishi kati ya watu wa Israeli milele. Nyumba ya Israeli haitalikufuru tena jina langu takatifu-wao au wafalme wao katika mahali patakatifu pao.8Hawatalikufuru tena jina langu takatifu kwa kuweka kizingiti chao karibu na kizingiti changu, na nguzo yao ya lango karibu na nguzo yangu ya lango, bila kitu lakini ukuta kati yangu na wao. Wamelikufuru jina langu kwa matendo yao machafu, hivyo nimewala kwa hasira yangu.9Sasa waache waondoe udanganyifu wao na maiti za wafalme wao kutoka kwangu, na nitaishi katikati yao milele.

10Mwanadamu, wewe mwenyewe utaiambia nyumba ya Israeli kuhusu nyumba hii hivyo watajiskia aibu ya uovu wao. Wanaweza kutafakari kuhusu haya maelezo.11Kwa kuwa wameaibika kwa yote waliyoyafanya, kisha waonyeshe mchoro wa nyumba, maelezo yake, matokeo yake, maingio yake, na mchoro wake, sheria zake zote na kanuni. Kisha andika hivi chini mbele ya macho yao ili waweze kutunza michoro yote na kanuni zake zote, hivyo kama wazitiivo.

12Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba: Kutoka kwenye kilele cha mlima hata mpaka wote unaoizunguka, patakuwa patakatifu sana. Tazama! Hii ndiyo sheria kwa ajili ya nyumba.

13Hivi vitakuwa vipimo vya madhabahu katika dhiraa-hiyo dhiraa kuwa dhiraa ya kawaida na urefu wa kiganja. Hivyo mfereji ulio uzunguka madhabahu utakuwa dhiraa moja chini, na upana wake pia utakuwa dhiraa moja. Mpaka wa karibu uizungukayo machinjio shubiri moja. Hii itakuwa kitako cha madhabahu.14Usawa wa kutoka kwenye mferji hadi kwenye machinjio ya chini ya madhabahu itakuwa dhiraa mbili, na hiyo machinjio yenyewe itakuwa dhiraa moja upana. Kisha kutoka machinjio madogo hadi kwenye machinjio makubwa ya madhabahu, itakuwa dhiraa nne, na machinjio makubwa yatakuwa dhraa moja upana.15Meko juu ya madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa ni dhiraa nne juu, na kuna pembe nne zilizoelekea juu kwenye meku.16Meku ina dhiraa kumi na moja urefu na dhiraa kumi na mbili upana, za mraba.17Mpaka wake ni dhiraa kumi na nne urefu na dhiraa kumi na nne upana pande zake zote nne, na ukingo wake ni nusu dhiraa upana. Mfereji ni dhiraa moja upana kuzuka kote pamoja na ngazi zielekeazo mashariki.”

18Kisha akanambia, “Mwanadamu, Bwana Yahwe asema hivi: Hizi ndizo sheria kwa ajili ya madhabahu katika siku watakayoitengeza, kwa ajili kutoa sadaka ya kuteketezwa kwenye hiyo, na kwa jili ya kunyunyiza damu juu yake.19Utatoa ng'ombe kutoka kwenye kundi kama sadaka ya dhambi kwa ajili ya Walawi makuhani ambao ni uzao wa Zadoki, wale wajao karibu nami kunitumikia-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.20Kisha utachukua baadhi ya damu yake na kuiweka juu pembe nne za madhabahu na pande nne za machinjio na kuuzunguka ukingo; utaitakasa na kufanya upatanisho kwa ajili yake.21Kisha chukua ng'ombe kama sadaka ya dhambi na iteketezwe katika eneneo lililotengwa la nje ya patakatifu.

22Kisha katika siku ya pili utatoa mbuzi dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini kama sadaka ya dhambi; makuhani wataisafisha madhabahu kama walivyoisafisha kwa ng'ombe.23Utakapomaliza kusafisha, toa ng'ombe asiyekuwa na dosari kutoka kwenye mifugo na kondoo dume asiyekuwa na dosari kutoka kundini.24Watoe mbele ya Yahwe; makuhani watanyunyiza chumvi juu yao na kuwainua juu kama sadaka ya kutekezwa kwa Yahwe.

25Utaandaa mbuzi dume kama sadaka ya dhambi kila siku kwa mda wa siku saba, na makuhani pia wataandaa ng'ombe asiye na dosari kutoka kwenye kundi na kondoo dume kutoka kwenye kundi.26Wataipatanisha madhabahu kwa siku saba na kuitakasa, wataitakasa kwa njia hii.27Watamaliza hizi siku saba, na katika siku ya nane na kuendelea itakuwa kwamba makuhani wataandaa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani kwenye madhabahu, ndipo nitakapowakubali-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

44

1Kisha yule mtu akanirudisha hata lango la nje la patakatifu linaloelekea mashariki; lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.2Yahwe akanambia, “Hili lango litakuwa limefungwa; halitafunguliwa. Hakuna mtu atakaye pitia hapo, kwa kuwa Yahwe, Mungu wa Israeli ameingia kwa hilo, hivyo lilikuwa limefungwa kwa kukazwa.3Mtawala wa Israeli atakaa katika hilo kula chakula mbele ya Yahwe. Ataingia kwa njia ya varanda na kutoka kwa njia hiyo hiyo.”

4Kisha akaniletea kwa njia ya lango la kaskazini linaloelekea kwenye nyumba. Hivyo nikaona na kutazama, utukufu wa Yahwe umejaa kwenye nyumba ya Yahwe, nikaanguka kifudifudi.

5Kisha Yahwe akanambia, “Mwanadamu, andaa moyo wako na tazama kwa macho yako na sikiliza kwa masikio yako kwa yote yale nikuambiayo, kwa amri zote za nyumba ya Yahwe na maagizo yote. Fikiri kuhusu malango ya nyumba na na matokeo ya malango.6Kisha waambie wale walioasi, nyumba ya Israeli, ‘Bwana Yahwe asema hivi: Acheni matendo yenu maovu kwenu, nyumba ya Israeli-7ambayo mmewaleta wageni pamoja na wasiotahiriwa mioyo na wasiotahiriwa mwili kuwa katika patakatifu pangu, kuikufuru nyumba yangu, wakati mlipokuwa mnanitolea chakula, mafuta na damu-mmevunja agano langu kwa matendo yenu maovu.8Hamkumaliza kazi zenu zinazohusiana na vitu vitakatifu, lakini mmewateua wengine kuchukua kazi zenu, na mmewatuma kupaangalia mahali patakatifu pangu.9Bwana Yahe asema hivi: hakuna mgeni, ambaye hajatahiriwa kwenye moyo wake na mwili, kutoka yeyote wa hao waishio miongoni mwa watu wa Israeli, awezaye kuingia patakatifu pangu.

10Kisha Walawi wakaenda mbali nami-wakapotea mbali nami, kwenda kwenye sanamu zao-lakini watalipa kwa ajili ya dhambi yao.11Wao ni watumishi katika patakatifu pangu, waangalizi wa malango ya nyumba na kutumika kwenye nyumba na kuchinja sadaka za kuteketezwa na dhabihu za watu, na watasimama mbele za watu na kuwatumikia.12Lakini kwa sababu wamefanya dhabihu mbele ya sanamu zao, wamekuwa kikwazo kwa dhambi ya nyumba ya Israeli. Kwa hiyo nitainua mkono wangu kuapa kiapo dhidi yao-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo-watabeba adhabu yao.13Hawatakuja karibu nami kufanya kama makuhani au kukaribia kila vitu vyangu vitakatifu, vitu vitakatifu sana. Badala yake, watabeba lawama zao na hatia zao kwa ajili ya matendo yao ya karaha waliyoyafanya.14Lakini nitawaweka kama watunzaji wa kazi katika nyumba, kwa kazi zote na kila kitu kitakachofanyika ndani yake.

15Kisha makuhani walawi, hao wana wa Zadoki ambao waliokamilisha kazi ya patakatifu pangu wakati wana wa Israeli walipotea mbali nami-watakuja karibu nami kuniambudu. Watasimama mbele yangu kunitolea mafuta na damu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.16Watakuja hata patakatifu pangu; wataikaribia meza yangu kuniabudu na kukamilisha kazi zao kwangu.

17Hivyo itakuwa kwamba watakapokuja kwenye malango ya ua wa ndani, watatakiwa kuvaa mavazi ya kitani, kwa kuwa hawatakuja na sufu ndani ya lango la ua wa ndani na nyumba yake.18Kutakuwa na vilemba juu ya vichwa vyao na kitani ndani ya viuno vyao. Ndani wasivae nguo ambayo itawafanya watoke jasho.19Wakati watakapotoka nje ya ua wa nje, hata kwenye ua wa ndani ili kwenda kwa watu, watavua nguo zao walizokuwa wamezivaa kisha wakatumika; watazivua na kuziweka chini katika chumba kitakatifu, hivyo wasiwafanye wengine watakatifu kwa kugusana na nguo zao maalumu.

20Hawatanyoa vichwa vyao wala kuruhusu nywele zao kuwa ndefu, watapunguza nywele za vichwa vyao.21Hakuna kuhani atakaye ruhusiwa kunywa mvinyo wakati atakapoingia kwenye uwa wa ndani,22hakuna kuchukua mjane au mwanamke aliyetalikiwa kama mke kwa ajili yake, lakini mwali kutoka safu ya nyumba ya Israeli au mjane aliyekuwa ameolewa na kuhani aliyepita.23Kwa kuwa watawafundisha watu wangu tofauti kati ya utakatifu na kukufuru; watawafanya kujua uchafu kutoka usafi.

24Katika kubishana watasimama kwenye hukumu pamoja na amri yangu; watakuwa waadilifu. Watashika sheria yangu na amri zangu katika sikukuu, na watasherekea siku yangu ya Sabato.

25Hawataenda kwa mtu aliyekufa ili wasiwe najisi, vinginevyo awe ni baba au mama yao, mwana wa kiume au binti, kaka au dada ambaye hajawahi kulala na mtu; vinginevyo, watakuwa najisi.26Baada ya kuhani kuwa najisi, watahesabu mda wa siku saba kwa ajili yake.27Katika siku atakayoingia mahali patakatifu, ndani kwenye uzio kutumika katika mahali patakatifu, ataleta sadaka ya dhambi kwa ajili yake mwenyewe-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.

28Hapatakuwa urithi wao: Mimi ndiyo urithi wao, na usiwapatie mali katika Israeli; nitakuwa mali yao!29Watakula chakula cha sadaka, sadaka za dhambi, sadaka za hatia, na kila kitakachotolewa kwa ajili ya Yahwe katika Israeli, vitakuwa vyao.30Malimbuko ya kwanza ya vitu na kila sadaka, kila kitu kitokanacho na sadaka zenu vitakuwa mali ya makuhani, mtatoa sadaka ya chakula kizuri kwa makuhani ili kwamba baraka iweze kukaa katika nyumba zenu.31Makuhani hawatakula mzoga au mnyama aliyeraruliwa, iwe ni ndege au mnyama.

45

1Wakati mtakapogawanya nchi kama urithi, mtafanya sadaka kwa kwa Yahwe; sadaka hiyo itakuwa sehemu takatifu ya nchi, dhiraa elfu ishirini na tano urefu, na dhiraa elfu kumi upana. Patakuwa patakatifu, ndani ya mipaka yake yote.2Kutoka hapa kutakuwa na dhiraa mia tano kwa dhiraa mia tano za mraba kuzunguka mahali patakatifu, kwa kuuzunguka mpaka dhiraa hamsini upana.3Kutoka hili eneo utapima fungu ambalo ni dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana; patakuwa patakatifu; mahali patakatifu palipo tukuka.4Patakuwa patakatifu katika nchi kwa ajili ya makuhani wanaomtumikia Yahwe, ajaye kwa Yahwe kumtumikia. Patakuwa mahali kwa ajili ya nyumba na eneo takatifu kwa ajili mahali patakatifu.5Hivyo itakuwa dhiraa elfu ishirini na tano urefu na elfu kumi upana, patakuwa kwa ajili ya miji ya Walawi wanaotumika kwenye nyumba.

6Mtadhihirisha eneo moja kwa ajili ya mji, dhiraa elfu tano na urefu ishirini na tano, hapo patakuwa kando kando ya eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu; huu mji utakuwa wa mali ya nyumba yote ya Israeli.

7Nchi ya mwana mfalme itakuwa kwa pande zote za eneo lililohifadhiwa kwa ajili ya mahali patakatifu na mji. Patakuwa kwa upande wao wa magharibi na upande wa mashariki. Urefu utalingana na urefu wa moja ya hayo mafungu, kutoka magaribi hata mashariki.8Hii nchi itakuwa mali ya mwana mfalme katika Israeli. Wana wafalme hawatawakandamiza watu wangu; badala yake, watawapatia nchi kwa nyumba ya Israeli, kwa ajili ya makabila yao.

9Bwana Yahwe asema hivi: Inatosha kwa ajili yenu, mwana mfalme wa Israeli! Ondoa dhuluma na mgogoro; fanya hukumu na haki! Usiwafukuze wapangaji wa watu wangu! -Hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.10Mtakuwa na mzani sahihi, efa sahihi, na bathi sahihi!11Efa na bathi zitakuwa kiasi kile kile, ili kwamba bathi iwe zaka ya homeri; efa itakuwa zaka ya hamori moja. Vipimo vyao vitakuwa vinafanana na homeri.12Shekeli zitakuwa gera ishirini, shekeli sita zitakuwa mane yenu.

13Hili ndilo toleo mtakalotoa: efa sita kwa kila homeri ya ngano, na mtatoa efa sita kwa kila homeri ya shayiri.14Sadaka ya kawaida ya mafuta itakuwa zaka ya bathi kwa kila kori (ambazo ni bathi), au kwa kila hamori, kwa kuwa hamori moja ni bathi kumi pia.15Kondoo mmoja au mbuzi kutoka mifugo kwa kila wanyama mia mbili kutoka malisho ya maji ya mikoa ya Israeli yatatumika kwa sadaka ya kuteketezwa yoyote au sadaka ya amani kufanya upatanisho kwa ajili ya watu-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.16Watu wote wa nchi watatoa hii sadaka kwa mwana mfalme wa Israeli.17Utakuwa wajibu wa mwana mfalme kutoa wanyama kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, sadaka ya unga, sadaka ya kinywaji, katika siku za sikukuu na sherehe za mwezi mpya, na katika siku za Sabato-sikukuu zote za kudumu za nyumba ya Israeli. Ataandaa kwa ajili ya sadaka za dhambi, sadaka za unga, sadaka za kuteketezwa, na sadaka za amani kwa ajili ya upatanisho badala ya nyumba ya Israeli.

18Bwana Yahwe asema hivi: Katika mwezi wa kwanza, siku ya kwanza ya mwezi, utachukua ng'ombe mmoja asiyekuwa na dosari kutoka kwenye kundi na kufanya sadaka ya dhambi kwa ajili ya patakatifu.19Kuhani atachukua baadhi ya damu ya sadaka ya dhambi na kuiweka juu ya miimo ya mlango na kwenye pembe nne za mpaka wa madhabahu, na miimo ya lango la uzio wa ndani.20Utafanya hivyo siku ya saba ya mwezi kwa dhambi ya kila mtu kwa ajili ya ujinga; katika njia hii mtaipatanisha hekalu.

21Katika siku ya mwezi siku ya kumi na nne ya mwezi, mtakuwa na sikukuu, sikukuu ya siku saba. Matakula mkate usiotiwa chachu.22Siku hiyo, mwana mfalme ataandaa ng'ombe kwa ajili yake na kwa ajili ya watu wote wa nchi kama sadaka ya dhambi.23Kwa siku saba za sikukuu, mwana wa mfalme ataandaa sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya Yahwe: ng'ombe saba na kondoo dume saba zisizokuwa na dosari kila siku kwa mda wa siku saba, na mbuzi dume kila siku kama sadaka ya dhambi.24Kisha mwana mfalme atatengeneza sadaka ya chakula ya efa moja kwa kila ng'ombe na efa moja kwa kila kondoo dume pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.

25Katika siku ya saba ya mwezi siku ya kumi na tano ya mwezi, katika sikukuu, mwana wa mfalme atafanya matoleo katika siku hizi saba: sadaka za dhambi, sadaka za kuteketezwa, sadaka za chakula, na sadaka za mafuta.

46

1Bwana Yahwe asema hivi: Lango la uzio wa ndani, linaloelekea mashariki, litafungwa kwa mda wa siku sita za kazi, lakini katika siku za Sabato litakuwa wazi, na katika siku ya mwezi mpya litafunguliwa.2Mwana wa mfalme ataingia kwa kutumia lango la njia ya nyuma ya varanda upande wa nje, na atasimama mbele ya muhimili wa mwimo wa lango la ndani wakati makuhani wakiwa wakitengeza sadaka ya kuteketezwa na sadaka ya amani. Kisha ataabudu kwenye kizingiti cha lango la ndani na kutoka nje, lakini lango halitakuwa linafungwa hadi jioni.3Watu wa nchi pia wataabudu mbele ya Yahwe kwenye hili lango la kuingilia katika siku ya Sabato na siku mpya za mwezi.4Sadaka ya kuteketezwa ambayo mwana wa mfalme aitoayo kwa Yahwe katika siku ya Sabato itakuwa wanakondoo sita wasiokuwa na dosari na kondoo dume asiyekuwa na dosari.5Sadaka ya unga pamoja na kondoo dume itakuwa efa moja, na sadaka ya unga pamoja na wanakondoo kiasi awezacho kutoa, na hini moja ya mafuta pamoja na kila efa ya unga.6Katika siku ya mwezi mpya atatoa ng'ombe mchanga asiyekuwa na dosari kutoka kuchungwa, wanakondoo sita, na kondoo asyekuwa na dosari.7Atatengeneza sadaka ya unga ya efa moja kwa ajili ya ng'ombe na efa moja kwa ajili ya kondoo, na kwa kiasi awezacho kukitoa kwa ajili ya wanakondoo, na hini ya mafuta kwa kila efa ya unga.8Wakati mwana wa mfalme atakapokuwa anaingia kwa njia ya lango lenye varanda, ataondoka kwa njia hiyo hiyo.

9Lakini wakati watu wa nchi watakaokuja kwa Yahwe katika sikukuu zilizoteuliwa, kila mmoja kuingia kupitia kwenye lango la kaskazini kuabudu ataondoka kupitia lango la kusini; na kila atakayeingillia kupitia lango la kusini atatoka kupitia lango la kaskazini. Hakuna atakayerudia kwa lile lango aliloingilia, kwa kuwa atatoka nje moja kwa moja.10Mwana wa mfalme atakuwa kati yao; watakapoingia, ataingia ndani, na watakapoondoka, atatoka nao.

11Kwenye sikukuu hizo, sadaka ya unga itakuwa efa moja ya unga kwa ng'ombe mmoja na efa moja kwa kondoo dume, na chochote atakacho kitoa pamoja na wanakondoo, na hini moja ya mafuta kwa kila efa.12Wakati mwana wa mfalme atakapotoa sadaka atakayojisikia kutoa, labda sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani kwa Yahwe, lango la kuelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka ya amani kama afanyavyo siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, na baada ya kutoka lango litafungwa.

13Kwa kuongeza, utatoa mwanakondoo asiyekuwa na dosari mwenye umri wa mwaka mmoja kama sadaka ya kuteketezwa kwa Yahwe kila siku; utafanya hivi kila asubuhi.14Utatoa sadaka ya unga pamoja nayo kila asubuhi, efa sita na sehemu ya tatu ya hini ya mafuta kuchanganya na sadaka ya unga kwa ajili ya Yahwe, kulingana na sheria ilivyo.15Watandaa mwanakondoo, sadaka ya kuteketezwa, na mafuta kila asubuhi, sadaka ya kuteketezwa ya kudumu.

16Bwana Yahwe asema hivi: Kama mwana wa mfalme akitoa zawadi kwa mmoja wa watoto wake, imekuwa urithi wake. Itakuwa mali ya mtoto wake, imekuwa urithi.17Lakini kama akimpatia zawadi kutoka urithi wake kwa mmoja wa watumishi wake, kisha itakuwa ya huyo mtumishi mpaka mwaka wa uhuru, na kisha itarudi kwa mwana wa mfalme. Urithi wake yamkini ukawa kwa ajili ya watoto wake.18Mwana wa mfalme hatawaondolea urithi wa watu kutoka kwenye mali zao wenyewe; ataandaa kwa ajili ya watoto wake mali ili kwamba watu wangu wasitawanyike, kila mtu mbali na milki yake mwenyewe.”

19Kisha yule mtu akanileta kwenye lango la kutokea hata kwenye vyumba vitakatifu kwa ajili ya makuhani, vilivyokuwa vimeelekea kaskazini na tazama! Kulikuwa na sehemu mbele magharibi.20Akanambia, “Hii ndio sehemu ambayo makuhani watakapo chemshia sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na walipookea sadaka ya unga. Wasilete sadaka nje ya uzio, kwa kuwa watu watatakaswa.”

21Kisha akanileta kwenye uzio wa nje akaniongoza kuzunguka pembe nne za uzio, nikaona kwamba katika kila pembe ya uzio kulikuwa na uwanja.22Katika hizo pembe nne za nje ya uzio kulikuwa na uzio nne ndogo, dhiraa arobaini urefu na thelathini upana. Ukubwa ule ule kwa uzio zote nne.23Kulikuwa na safu zilizokuwa zimetengenezwa kwa mawe kuzizunguka zote nne, na meko ya kupikia ilikuwa chini ya safu ya jiwe.24Yule mtu akanambia, “Hizi ndizo sehemu ambazo watumishi watachemshia dhabihu za watu.”

47

1Kisha yule mtu akanirudisha nyuma kwenye lango la kuingia la hekalu, na kulikuwa na maji yakitiririka nje kutoka chini ya hekalu kizingiti cha nyumba kuelekea masharikii-kwa mbele ya hekalu kulekea mashariki-na maji yalikuwa yakitiririka chini upande wa kusini mwa hekalu, kuelekea upande wa kuume wa madhabahu.2Hivyo akanileta kwenye lango la kaskazini na kuniongoza kuzunguka lango kuelekea mashariki, na hapo maji yalikuwa yakitiririka kutoka lango hili kwa upande wa kusini yake.

3Yule mtu alipokuwa akienda mashariki, kulikuwa na kamba ya kupimia kwenye mkono wake; akapima dhiraa elfu moja akanivusha kwenye maji hata maji yakafika kwenye magoti.4Kisha akapima dhiraa elfu moja tena akanivusha kwenye yale maji yaliyofika kwenye magoti; akapima dhiraa elfu kumi nyingine na kunivusha maji yakafika hata kwenye nyonga.5Tena akapima dhiraa elfu moja nyingine, lakini ulikuwa mto ambao sikuweza kuuvuka kwa sababu maji yalizidi na yalijaa maji ya kuogelea ndani-yalikuwa mto usiovukika6Yule mtu akaniambia, “Mwanadamu, unaona hii?” akanipeleka na kunirudisha karibu na ukingo wa mto.

7Nilipokuwa nikirudi, hapo kwenye ukingo wa mto kulikuwa na miti mingi katika huu upande na upande mwingine pia.8Yule mtu akaniambia, “Haya maji yanatoka kwenda pande za nchi ya mashariki na chini hata Araba; haya maji hutiririka kwenye Bahari ya Chumvi itaifanya kuwa mpya.9Itakuwa kwamba kila kiumbe hai kisongamanacho kitaishi mahali maji yanapoelekea; kutakuwa na samaki wengi, kwenye hayo maji yatiririkayo huko. Itafanya maji ya chumvi kuwa mapya. Kila kitu kitaishi popote mto utakapoelekea.10Kisha itatokea kwamba wavuvi wa Engedi watasimama karibu na maji, na kutakuwa na sehemu ya kutandazia nyavu za samaki karibu na Englaimu. Kutakuwa na samaki nyingi za aina tofauti tofauti katika Bahari ya Chumvi, kama samaki kwenye Bahari Kuu kwa wingi wao.11Lakini Bahari ya Chumvi ikajaa maji na matope hayataachwa mapya; yataachwa yawe kwa ajili ya kutengeneza chumvi.12Karibu na huo mto juu ya ukingo wake, pande zote, aina zote za miti utazaa chakula. Majani yake hayatanyauka na matunda yake hayataacha kukua. Kila mwezi miti itazaa matunda, kwa sababu maji kutoka patakatifu yatatirirka kwenda kwenye hiyo miti. Matunda yake yatakuwa kwa ajili ya chakula, na majani yake yatakuwa kwa ajili ya dawa.

13Bwana Yahwe asema hivi: Hii itakuwa njia ambayo mtaigawanya nchi kwa ajili ya kabila kumi na mbili za Israeli: Yusufu atakuwa na mafungu mawili.14Mtaigawa kila mtu sawa sawa ambayo niliinua mkono wangu na kuapa kuwapa baba zenu. Hii nchi itakuja kuwa urithi kwenu.

15Huu utakuwa mpaka wa nchi upande wa kaskazini kutoka Bahari Kubwa kwa njia ya Hethloni, na kisha kuelekea Zedada.
16Kisha mpaka utaenda hata Berotha, hadi Sibraimu, iliyopo kati ya Dameski na Hamathi, na kisha hata Hazer-hatikoni, iliyopo karibu na mpaka wa Haurani.
17Hivyo mpaka utaenda kutoka kwenye bahari hadi Hazar-enoni kwenye mpaka wa Dameski na Hamathi hata kaskazini. Huu utakuwa upande wa kaskazini.
18Kwa upande wa mashariki, kati ya Haurani na Damaskasi na kati ya Geliadi na nchi ya Israeli kutakuwa na mto Yordani. Mtapima kutoka kwenye mpaka hata kwenye bahari ya mashariki; huo wote utakuwa mpaka wa mashariki.
19Kisha upande wa kusini: kusini mwa Tamari hadi kwenye maji ya Meriba Kadeshi, kijito cha Misri hata Bahari Kuu, na upande wa kusini kuelekea kusini.
20Kisha mpaka wa magharibi utakuwa Bahari Kuu utaelekea hata nyuma ya Hamathi. Huu utakuwa upande wa mgharibi.

21Kwa njia hii mtaigawanya hii nchi kwa ajili yenu wenyewe, kwa kabila za Israeli.22Hivyo mtagawana urithi kwa ajili yenu wenyewe na kwa ajili ya wageni walio kati yenu, wale watakaozaa watoto kati yenu na waliokuwa, kati yenu, kama wazaliwa wa watu wa Israeli. Mtapewa urithi miongoni mwa makabila ya Israeli.23Kisha itatokea kwamba wageni watakuwa pamoja na kabila miongoni mwa yule anayeishi. Mtapatia urithi-hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”

48

1Haya ndiyo majina ya makabila. Kabila la Dani litapokea sehemu moja ya nchi; mipaka yake itakuwa karibu na upande wa mashariki mpaka wa Israeli karibu na njia ya Hethloni na Lebo Hamathi. Mpaka wake utaenda hata karibu na Hazari Enani na karibu na mpaka wa Dameski hata upande wa kaskazini na kisha karibu na Hamathi. Mpaka wa Dani utaenda kutoka mashariki moja kwa moja hata Bahari Kubwa.

2Kupakana na mpaka wa Dani, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, Asheri itakuwa na fungu moja.

3Kupakana na mpaka wa Asheri kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Naftali atakuwa na fungu moja.

4Kupakana na mpaka wa Naftali kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Manase atakuwa na fungu moja.

5Kupakana na mpaka wa Manase kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Efraimu atakuwa na fungu moja.

6Kupakana na mapaka wa Efraimu kutoka mashariki hata magharibi, Rubeni atakuwa na fungu moja.

7Kupakana na mpaka wa Rubeni kutoka mashariki hata magharibi, Yuda atakuwa na fungu moja.

8Sadaka ya nchi ambayo mtaifanya itakuwa karibu na mpaka wa Yuda na hapohapo kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano upana. Urefu unakaribiana na fungu la kabila moja kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, na hekalu litakuwa katikati yake.

9Huu mji mtakao utoa sadaka kwa ajili ya Yahwe utakuwa na ridhaa elfu ishirini na tano urefu wake na ridhaa elfu kumi upana.10Haya yatakuwa matoleo ya hili fungu takatifu la nchi: makuhani watakuwa na nchi watakayopewa kipimo chake ridhaa elfu ishirini na tano urefu kwa upande kaskazini; ridhaa elfu kumi upana upande wa magharibi; urefu wa ridhaa elfu kumi upande wa magharibi; na urefu dhiraa elfu ishirini na tano upande wa kusini, pamoja na mahali patakatifu pa Yahwe katikati yake.11Hii itakuwa wakfu na makuhani wa safu ya Sadoki, aliyenitumikia kwa uaminifu na ambaye hakwenda nje ya mstari wakati watu wa Israeli walipoeenda nje ya mstari, kama Walawi walivyofanya.12Sadaka yao itakuwa fungu la hiyo nchi takatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi.

13Nchi ya Walawi karibu na mpaka wa nchi ya makuhani itakuwa Dhiraa elfu ishirini na tano urefu na dhiraa elfu kumi upana. Urefu wote wa eneo la nchi utakuwa dhiraa elfu ishirini na tano urefu na dhiraa elfu ishirini upana.14Hawataiuza au kuibadilisha; hakuna malimbuko ya hiyo nchi ya Israeli itakayogawanywa kutoka haya maeneo, kwa kuwa yote ni matakatifu kwa ajili ya Yahwe.

15Nchi iliyobaki, irdhiraa elfu kumi na tano upana na dhiraa elfu ishirini na tano urefu, itakuwa kwa wote wanayoitumia hiyo nchi, nyumba, na sehemu ya malisho; huo mji utakuwa katikati yake.16Hivi ndivyo vitakuwa vipimo vya mji: upande wa kaskazini utakuwa dhiraa 4,500 urefu; upande wa kusini utakuwa dhiraa 4,500 urefu; upande wa magharibi utakuwa ridhaa 4,500 urefu; na magharibi itakuwa dhiraa 4,500 urefu.17Kutakuwa na malisho ya mji kuelekea kaskazini, dhiraa 250 kwenda chini; hata kusini, dhiraa 250 kwenda chini; kuelekea mashariki, ridhaa 250 kwenda chini, na kuelekea magharibi dhiraa 250 kwenda chini.18Eneo lililobaki la matoleo matakatifu litanyooshwa dhiraa elfu kumi hata mashariki na dhiraa elfu kumi kuelekea magharibi. Litanyooshwa karibu na mpaka wa matoleo matakatifu, na mazao yake yatakuwa chakula kwa ajili ya wale wanaofanya kazi katika nchi.19Wale wafanyao kazi katika mji, watu wote wa kabila za Israeli, watailima hiyo nchi.20Matoleo yote ya nchi yatapimwa dhiraa elfu ishirini na moja kwa dhiraa elfu ishirini na tano. Kwa njia hii mtatengeneza matoleo matakatifu ya nchi, pamoja na nchi kwa ajili mji.

21Mabaki ya nchi mojawapo upande wa matoleo matakatifu na eneo la mji litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme. Eneo la nchi ya mwana wa mfalme kuelekea mashariki litanyooshwa kwa dhiraa elfu ishirini na tano kutoka kwenye mpaka wa matoleo matakatifu hata mpaka wa mashariki-na eneo lake kuelekea mpaka wa magharibi. Katikati kutakuwa matolea matakatifu, na mahali patakatifu pa hekalu patakuwa katikati yake.22Nchi imenyooka kutoka mali ya Walawi na eneo la mji katikati yake litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme; itakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benjamini-hiyo nchi itakuwa kwa ajili ya mwana wa mfame.

23Kwa kabila zitakazobaki, mafungu yao yataunganishwa kutoka upande wa mashariki. Benjamini atapokea fungu moja.

24Kupakana na mpaka wa Benjamini kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Simioni atakuwa na fungu moja.

25Kupakana na mpaka wa Isakari kutakuwa na fungu moja.

26Kupakana na mpaka wa Isakari kutoka mashariki hata magharibi, Zebuloni atakuwa na fungu moja.

27Hata kusini mwa mpaka wa Zebuloni, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magahribi, kutakuwa na nchi ya Gadi-fungu moja.

28Mpaka wa kusini mwa Gadi kutanyooshwa kutoka Tamari hata kwenye maji ya Meriba Kadeshi, mbele hadi kijito cha Misri, na kisha hata Bahari kuu.

29Hii ndiyo nchi ambayo mtakazo gawana; kutakuwa na urithi wa makabila ya Israeli. Haya yatakuwa mafungu yao. Hivi ndivy Bwana Yahwe asemavyo.

30Hawa ndio watakaoishi kutoka kwenye nchi: upande wa kaskazini, ambapo patapimwa dhiraa 4,500 kwa urefu,31kutakuwa na malango matatu, yaitwayo kwa ajili ya Israeli: lango moja kwa ajili ya Rubeni, lango moja kwa ajili ya Yuda, na lango moja kwa ajili ya Walawi.

32Kwa upande wa mashariki, ambapo patapimwa dhiraa 4,500 kwa urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Yusufu, lango moja kwa ajili ya Benjamini, na lango moja kwa ajili ya Dani.

33Kwa upande wa mashariki, kutakuwa na kipimo cha dhiraa 4,500 urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Simioni, lango moja kwa ajili ya Isakari, na moja kwa ajili ya Zebuloni.

34Kwa upande wa magharibi, ambao kipimo chake kitakuwa dhiraa 4,500, kutakuwa ba malango matatu: lango moja kwa ajili ya Gadi, lango moja kwa ajili ya Asheri, na lango moja kwa ajili ya Naftali.

35Umbali kuuzunguka mji utakuwa dhiraa elfu kumi na nane; kutoka hiyo siku, jina la huo mji litakuwa “Yahwe yupo hapo.”

Danieli

1

1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, Nebukadneza mfalme wa Babeli alikuja Yerusalemu na kuuzunguka mji ili kuzuia mahitaji yake yote.2Bwana alimpa Nebukadneza ushindi dhidi ya Yehoyakimu mfalme wa Yuda, na alimpatia vitu vitakatifu kutoka nyumba ya Mungu. Alivipeleka vitu hivyo mpaka katika nchi ya Babeli, kwa nyumba ya mungu wake, na aliviweka vitu vitakatifu katika hazina ya mungu wake.

3Mfalme akamwambia Ashipenazi, afisa wake mkuu, awalete baadhi ya watu wa Israeli, wa familia ya kifalme na za kiungwana -4vijana wasio na hila, wenye mwonekano wa kuvutia, wenye ujuzi katika hekima yote, wenye kujawa na ufahamu na weledi, na wenye sifa za kutumika katika ikulu ya mfalme. Alitakiwa kuwafundisha maandiko na lugha ya Babeli.5Mfalme aliwatengea kwa ajili yao fungu kutoka katika chakula chake kizuri kwa kila siku na katika divai aliyokunywa. Vijana hawa walitakiwa kufunzwa kwa miaka mitatu, na baada ya hapo, wangeweza kumtumikia mfalme.

6Miongoni mwao walikuwa ni Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria, baadhi ya watu wa Yuda.7Afisa mkuu aliwapa majina: Danieli alimwita Belteshaza, Hanania alimwita Shadraka, Mishaeli alimwita Meshaki, na Azaria alimwita Abedinego.

8Lakini Danieli alinuia katika akili yake kuwa asingejitia ujanisi mwenyewe kwa chakula kizuri cha mfalme wala kwa divai ambayo alikunywa.9Basi, aliomba ruhusa kutoka kwa afisa mkuu ili kwamba asije akajitia uchafu yeye mwenyewe. Hivyo, Mungu alimpa Danieli kibali na huruma kupitia katika heshima ambayo afisa mkuu alikuwa nayo kwake.10Afisa mkuu alimwambia Danieli, “Ninamwogopa bwana wangu mfalme. Ameagiza aina ya chakula na vinywaji mnavyotakiwa kutumia. Kwa nini awaone ninyi mkiwa mnaonekana vibaya kuliko vijana wengine wa umri wenu? Mfalme aweza kukitwaa kichwa changu kwa sababu yenu.

11Kisha Daniel akamwambia msimamizi ambaye afisa mkuu alikuwa amemweka juu ya Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria.12Alisema, “Tafadhari tujaribuni, sisi watumishi wako kwa siku kumi. Tupatieni tu mboga za kula na maji ya kunywa.13Kisha ulinganishe mwonekano wetu na mwonekano wa vijana wanaokula vyakula vya mfalme, na mtutendee, sisi watu wako kulingana na kile unachokiona.”14Hivyo msimamizi alikubaliana naye kufanya hivi, na aliwajaribu kwa siku kumi.

15Katika mwisho wa siku kumi mwonekano wao ulikuwa ni wenye afya nzuri kuliko wa wale vijana waliokula vyakula vya kifalme.16Basi, msimamizi aliliondoa fungu lao la chakula na vivywaji vyao na walipewa mboga tu.

17Na kuhusu vijana hawa nne Mungu aliwapa uelewa na ufahamu katika maandiko yote na hekima, na Danieli aliweza kupambanua aina zote za maono na ndoto.

18Katika mwisho wa muda uliokuwa umepangwa na mfalme kuwaleta ndani, afisa mkuu aliwaleta mbele ya Nebukadneza.19Mfalme aliongea nao, na miongoni mwa kundi lote hapo hapakuwa na wa kuwalinganisha na akina Danieli, Hanania, Mishaeli, na Azaria. Walisimama mbele ya mfalme, wakiwa tayari kumtumikia.20Katika kila swali la hekima na ufahamu ambalo mfalme aliwauliza, aliwakuta wakiwa na uwezo mara kumi kuliko waganga wote na wale waliojidai kusema na wafu, waliokuwa katika ufalme wake wote.

21Danieli alikuwa hapo mpaka mwaka wa kwanza wa Mfalme Koreshi.

2

1Katika mwaka wa pili wa utawala wa Nebukadneza, alikuwa na ndoto. Akili yake ilisumbuka, na hakuweza kulala.2Ndipo mfalme alipowaita waganga na wale wenye kuongea na wafu. Lakini pia aliwaita wachawi na watu wenye hekima. Aliwataka wamwambie juu ya ndoto zake. Basi walikuja na kusimama mbele za mfalme.3Mfalme akawambia, “Nilikuwa na ndoto, na akili yangu ina mashaka nataka kujua ndoto hiyo nini maana yake.”

4Kisha watu wenye hekima wakamwambia mfalme katika Kiaramu, “Mfalme, aishi milele! Twambie sisi ndoto, watumishi wako, nasi tutaifunua maana yake.”

5Mfalme akawajibu watu wenye hekima, “Jambo hili limeshamalizika. Kama hamtaweza kuiweka wazi ndoto kwangu na kuitafsiri, miili yenu itakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vichuguu vya uchafu.6Lakini kama mtaniambia ndoto na maana yake, mtapokea zawadi kutoka kwangu, thawabu, na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto na maana yake.”

7Wakamjibu tena na kusema, “Mfalme na atuambie, watumishi wake, ndoto nasi tukwambia maana yake.”

8Mfalme akawajibu, “Ninajua kwa hakika mnahitaji muda zaidi kwa sababu mmeona maamuzi yangu ni magumu kuhusu jambo hili.9Lakini kama hamtaweza kuniambia ndoto, kuna sentensi moja tu kwa ajili yenu. Mmeamua kuandaa uongo na maneno ya kudanganya ambayo mmekubaliana kwa pamoja kuniambia mpaka pale nitakapobadili akili zangu. Basi, niambieni ndoto, na kisha nitajua kuwa mnaweza kuitafsiri kwa ajili yangu.”

10Watu wenye hekima wakamjibu mfalme, “Hakuna mtu katika dunia anayeweza kutimiza matakwa ya mfalme. Hakuna mfalme yoyote mkuu na mwenye nguvu ambaye alishataka jambo kama hilo kutoka kwa wachawi, wala wenye kuongea na wafu, wala mwenye hekima.11Kile anachokitaka mfalme ni kigumu, na hakuna yeyote awezaye kumwambia mfalme isipokuwa miungu, ambayo haishi miongoni mwa watu.”

12Jambo hili lilimfanya mfalme akasirike na kughadhabika sana, na alitoa amri kuwaangamiza wale wote waliojulikana kuwa ni wenye hekima zao katika Babeli.13Hivyo, amri ilitoka kwamba wale wote waliojulikana kwa hekima yao ni lazima wauawe. Na kwa sababu ya amri hii, walimtafuta Daniel na rafiki zake ili kwamba wauawe.

14Ndipo Daniel alipomjibu kwa busara na umakini, Arioki, kamanda wa walinzi wa mfalme, ambaye alikuwa amekuja kuwaua wale wote waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.15Danieli alimwuliza kamanda wa mfalme, “Kwanini amri ya mfalme ni ya haraka hivyo?” Hivyo, Arioki akamwambia Danieli kile kilichotokea.16Ndipo Danieli aliingia ndani na akaomba ahadi ya muda wa kuonana na mfalme ili kwamba aweze kuwasilisha tafsiri kwa mfalme.

17Kisha Danieli aliingia ndani ya nyumba na aliwaelezea Hanania, Mishaeli, na Azaria, kile kilichotokea.18Aliwasihi kutafuta rehema kutoka kwa Mungu wa mbinguni kuhusiana na siri hii ili kwamba yeye na wao wasije wakauawa pamoja na watu wengine waliosalia waliojulikana kuwa na hekima katika Babeli.19Usiku ule siri ilifunuliwa kwa Danieli katika maono. Kisha Danieli akamtukuza Mungu wa mbinguni20na kusema, “Litukuzwe jina la Mungu milele na milele; kwa kuwa hekima na nguvu ni zake.
21Anabadili wakati na majira; anaondoa wafalme na kuweka wafalme katika viti vyao vya enzi. Anawapa hekima wenye hekima na ufahamu kwa wenye weledi.
22Hufunua vitu vya chini na vilifichika kwa sababu anajua kile kilicho gizani, naye anaishi pamoja na mwanga.
23Mungu wa baba zetu, ninakushukuru na kukutukuza wewe kwa ajili ya hekima na nguvu uliyonipa. Sasa umeyafanya yawe wazi kwetu yale tuliyokuomba; umetujulisha mambo yamhusuyo mfalme.”

24Ndipo Danieli alienda kumwona Arioki (yule ambaye mfalme alimchagua kuua kila mtu aliyekuwa na hekima katika Babeli). Alimwendea na kumwambia, “Usiwauwe watu wenye hekima katika Babeli. Nipeleke kwa mfalme na nitamwonesha mfalme tafsiri ya ndoto yake.”

25Kisha Arioki kwa haraka alimleta Danieli mbele za mfalme na kusema, “Nimempata miongoni wa watu wa mateka wa Yuda mtu ambaye atafunua maana ya ndoto ya mfalme.”

26Mfalme akamwambia Danieli (ambaye alikuwa akiitwa Beliteshaza), “Je unaweza kuniambia ndoto niliyoiona na maana yake?”

27Danieli alimjibu mfalme na kusema, “Siri ambayo mfalme ameiomba haiwezi kufunuliwa na watu wenye hekima, wala wale wenye kuongea na wafu, wala wachawi, na wala wataalamu wa nyota.28Isipokuwa kuna Mungu ambaye anaishi mbinguni, ambaye hufunua siri, na amekwisha kukujulisha wewe, mfalme Nebukadneza, kile kitakachotokea katika siku zijazo. Hizi ndizo Ndoto na maono ya akili zako uliyoyaona wakati ulipokuwa umelala kitandani mwako.

29Na kwako Wewe, mfalme, mawazo yako kitandani mwako yalikuwa ni juu ya mambo yajayo, na yule afichuaye siri ameifanya ijulikane kwako kuhusu kile kilicho karibu kutokea.30Na kuhusu mimi, siri hii haikufunuliwa kwangu kwa sababu ya hekima yoyote niliyo nayo zaidi ya mtu yoyote anayeishi. Siri hii imefunliwa kwangu ili kwamba wewe, mfalme, uweze kufahamu maana, na ili kwamba ujue mawazo yaliyo ndani mwako.

31Mfalme, uliangalia juu na ukaona sanamu kubwa. Sanamu hii ambayo ilikuwa yenye nguvu na yenye kung'aa, ilisimama mbele yako. Mng'ao wake ulikuwa unatisha.32Kichwa cha sanamu kilikuwa kimetengenezwa kwa dhahabu safi. Kifua chake na mikono ilikuwa ya fedha. Sehemu ya katikati na mapaja yake yalikuwa yametengenezwa kwa shaba,33na miguu yake ilikuwa imetengenezwa kwa chuma. Miguu yake ilikuwa ilitengenezwa kwa sehemu chuma na sehemu kwa udongo.34Ulitazama juu, na jiwe lilikuwa limechongwa, ingawa si kwa mikono ya wanadamu, na liliipiga sanamu katika miguu yake ya chuma na udongo, na kuiponda ponda.35Kisha chuma, udongo, fedha, na dhahabu zilivunjwa katika vipande vipande kwa wakati mmoja na yakawa kama makapi yaliyo katika sakafu za kupuria kipindi cha kiangazi. Upepo ukavipeperushia mbali na hakuna alama inayoachwa. Lakini jiwe lililoipiga sanammu likawa mlima mkubwa na kuijaza dunia yote.

36Hii ndiyo ilikuwa ndoto yako. Na sasa tutamwambia mfalme maana yake.37Wewe, mfalme, ni mfalme wa wafalme kwa wale ambao Mungu wa mbinguni amekupa ufalme, nguvu, uweza na heshima.38Amevitia mkononi mwako sehemu ambazo binadamu huishi. Amekupa wanyama wa mwituni na ndege wa angani katika mkono wako, na amekufanya wewe utawale juu yao wote. Wewe u kichwa cha dhahabu cha sanamu.

39Baada yako, ufalme mwingine utainuka ambao ni mdogo kwako, na hata ufalme wa tatu wa shaba utatawala juu ya dunia yote.40Kutakuwa na ufalme wa tatu, wenye nguvu kama chuma, kwa kuwa chuma huvunja vipande vipande vitu vingine na kupondaponda kila kitu. Itaviharibu vitu hivi vyote na kuvisaga.41Kama vile ulivyoona, miguu na vidole vilikuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo na kwa sehemu vimefanywa kwa chuma, hivyo utakuwa ni ufalme uliogawanyika; baadhi ya nguvu za chuma zitakuwa ndani yake, kama tu ulivyoona kuwa chuma kimechanganyikana na udongo laini.42Kama vile vidole vya miguuni vilivyokuwa kwa sehemu vimetengenezwa kwa chuma na kwa sehemu vimetengenezwa kwa udongo, ndivyo ufalme utakuwa kwa sehemu una nguvu na kwa sehemu utakuwa dhaifu.43Kama ulivyoona chuma kimechanganywa na udongo laini, na hivyo na watu watakuwa wamechanganyikana; hawakai kwa pamoja, kama vile chuma isivyoweza kushikamana na udongo

44Katika siku za wafalme hao, Mungu wa mbinguni ataanzisha ufalme ambao hautaweza kuangushwa, wala kushindwa na watu wengine. Utazivunja falme zingine vipande vipande na kuzikomesha zote, nao utadumu milele.45Kama tu ulivyoona, jiwe lilichongwa kutoka katika mlima, lakini si kwa mikono ya wanadamu. Lilivunjavunja chuma, shaba, udongo, fedha, na dhahabu katika vipande vipande. Mungu mkuu amekujulisha wewe, mfalme, kile kitakachotokea baada ya haya. Ndoto ni ya kweli na tafsiri yake ni ya kuaminika.

46Mfalme Nebukadneza alianguka kifudifudi mbele ya Daniel na alimheshimu; aliamuru kwamba sadaka zitolewe na manukato yatolewe kwake.47Mfalme alimwambia Danieli, “Hakika Mungu wako ni Mungu wa miungu, Bwana wa wafalme, na ambaye hufunua mafumbo, kwa kuwa umekuwa ukiweza kufumbua mafumbo haya.”

48Ndipo mfalme alimfanya Danieli kuwa wa kuheshimiwa sana na alimpa zawadi nyingi nzuri. Alimfanya kuwa mtawala juu ya jimbo lote la Babeli. Danieli akawa liwali mkuu juu ya watu wenye hekima wa Babeli.49Danieli alipeleka ombi kwa mfalme, na mfalme aliwateua Shadraka, Meshaki na Abedinego kuwa watawala juu ya jimbo la Babeli. Lakini Danieli alisalia katika ikulu ya mfalme.

3

1Mfalme Nebukadneza alitengeneza sanamu ya dhahabu ambayo ilikuwa na urefu wa dhiraa sitini na upana dhiraa sita. Aliiweka katika uwanda wa Dura katika jimbo la Babeli.2Kisha Nebukadneza alituma ujumbe wa kuwaita pamoja magavana wote wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na na washauiri, wa hazina, waamuzi, mahakimu, na maafisa wengine wakuu wa majimbo ili waje kwa ajili ya uzinduzi wa sanamu aliyokuwa ameiweka.3Ndipo magavana wa majimbo, magavana wa mikoa, na magavana wa vijiji, pamoja na washauri, wahasibu, waamuzi, mahakimu, na maafisa wa juu wa majimbo walikusanyika kwa pamoja katika uzinduzi wa sanamu ambayo Nebukadneza aliyokuwa ameiweka. Walisimama mbele yake.

4Kisha mtangazaji alipiga kelele, “Enyi watu, mataifa, na lugha mmeamriwa5kwamba mtakaposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, ni sharti kuanguka na kuisujudia ninyi wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza alikuwa ameiweka.6Na yeyote asiyeanguka na kuiabudu, kwa wakati huo huo atatupwa katika tanuru la moto.”

7Basi watu walilposikia sauti za pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari na aina zote za muziki, watu wote, mataifa na lugha walianguka na kuisujudia wao wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo Nebukadneza mfalme alikuwa ameiweka.

8Wakati huu baadhi ya Walkadayo walikuja na kuleta mashitaka kinyume na Wayahudi.9Walimwambia mfalme Nebukadneza, “mfalme aishi milele!10Ewe mfalme, umeweka amri kwamba kila mtu aisikiye sauti ya pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinubi na zumari, na aina zote za muziki, lazima kuanguka na kuisujudia sanamu ya dhahabu.11Mtu yeyote asiyeanguka na kuiabudu sharti atupwe katika tanuru inayowaka moto.12Sasa kuna baadhi ya Wayahudi ambao umewaweka juu masuala ya jimbo la Babeli; majina yao ni Shadraka, Meshaki, na Abednego. Mfalme, hawa watu hawakutii wewe. Hawataiabudu, kuitumikia wala kuisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu ambayo umeiweka.”

13Ndipo Nebukadneza alijawa na hasira na ghadhabu, aliagiza kwamba Shadraka, Meshaki na Abednego waletwe kwake. Hivyo, waliwaleta hawa watu mbele ya mfalme.14Nebukadneza aliwaambia, “Je mmejipanga katika akili zenu, enyi Shadraka, Meshaki na Abedinego, kwamba hamtaiabudu miungu yangu wala kuisujudia wenyewe sanamu ile ya dhahabu ambayo nimeiweka?15Basi sasa kama mko tayari - mtakaposikia sauti pembe, filimbi, ala za muziki, zeze, vinumbi na zumari, aina zote za muziki - kuanguka chini na kuisujudia wenyewe sanamu ile ambayo nimeitengeneza, mambo yote yatakuwa mazuri. Lakini kama hamtaiabudu, mtatupwa mara hiyo katika tanuru la moto. Ni mungu gani atakayeweza kuwaokoa katika mikono yangu?”

16Shadraka, Meshaki, na Abednego wakamjibu mfalme, “Nebukadneza, hatuhitaji kukujibu wewe katika jambo hili.17Kama kuna jibu, ni kwamba Mungu wetu ambaye tunamtumikia anaweza kutuhifadhi sisi salama katika tanuru la moto, na atatuokoa sisi katika mkono wako, mfalme.18Kama sivyo, na ijulikane kwako, wewe mfalme, kwamba hatutaiabudu miungu yako, na wala hatutaisujudia wenyewe sanamu ya dhahabu uliyoiweka.

19Ndipo Nebukadneza alijawa na ghadhabu; mwonekano wa uso wake ulibadilika kinyume na Shadraka, Meshaki na Abedinego. Aliagiza kuwa tanuru lichochewe ukali mara saba zaidi kuliko lilivyokuwa kawaida.20Kisha aliwaamuru baadhi ya watu wenye nguvu katika jeshi lake kuwafunga Shadraka, Meshaki na Abednego na kuwatupa katika tanuru liwakalo moto.21Walifungwa akali wakiwa wamevaa nguo zao, kanzu, kilemba, na mavazi mengine, na walitupa katika tanuru liwakalo moto.22Kwa sababu ya agizo la mfalme lilifuatwa na tanuru lilikuwa na joto sana, miali ya moto iliwaua watu waliowatupa Shadraka, Meshaki, na Abedinego.23Hawa wanaume watatu, Shadraka, Meshaki, na Abednego, waliangukia katika tanuru liwakalo moto wakali wamefungwa.

24Kisha Nebukadneza mfalme alishangazwa na alisimama haraka. Aliwauliza washauri wake, “Je, hatukutupa watu watatu wakiwa wamefungwa katika moto?” Nao walimjibu mfalme, “Hakika mfalme.”

25Alisema, “Lakini ninaona watu wanne ambao hawajafungwa wakizunguka katika moto, na hawajaumizwa. Mng'ao wa mtu wa nne ni kama mwana wa miungu.”

26Ndipo Nebukadneza aliposongea karibu na mlango wa tanuru liwakalo moto na akaaita, “Shadraka, Meshaki na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni nje! Njooni hapa! Ndipo Shadraka, Meshaki na Abednego walitoka nje ya moto.

27Magavana wa majimbo, magavana wengine, na washauri wa mfalme waliokuwa wamekusanyika kwa pamoja waliwaona watu hawa. Moto haukuunguza miili yao; nywele katika vichwa vyao hazikuungua; mavazi yao yalikuwa hayajaharibiwa; na hawakuwa na harufu ya moto.

28Nebukadneza alisema, “Na tumsifu Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego, ambaye amemtuma mjumbe wake na amewapa ujumbe watumishi wake. Walimtumaini yeye wakati walipoikana amri yangu, na waliitoa miili yao badala ya kuabudu au kusujudia mungu mwingine isipokuwa Mungu wao.29Hivyo basi ninaagiza kwamba watu wote, taifa au lugha ambayo itazungumza kitu chochote kinyume na Mungu wa Shadraka, Meshaki na Abedinego lazima wakatwe vipande, na ya kwamba nyumba zao lazima zifanywe kuwa vichuguu vya uchafu kwa sababu hakuna mungu mwingine anayeweza kuokoa kama hivi.”

30Ndipo mfalme aliwapandisha cheo Shadraka, Meshaki na Abednego katika jimbo la Babeli.

4

1Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi: “Na amani yenu na iongezeke.2Imeonekana vizuri kwangu kuwaambia juu ya ishara na maajabu ambayo Mungu Mkuu Aliye juu amenifanyia.

3Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi.”
4Mimi, Nebukadneza, nilikuwa ninaishi kwa furaha katika nyumba yangu, na nilikuwa nikifurahia mafanikio katika ikulu yangu.5Lakini ndoto niliyoiota ilifanya niogope. Nilipokuwa nimejilaza pale, taswira niliyoiona na maono katika akili yangu yalinitaabisha.6Basi nilitoa agizo la kuwaleta mbele yangu watu wote wa Babeli waliokuwa na hekima ili kwamba waweze kunitafsiria ndoto.7Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria.8Bali mwishoni Danieli aliingia ndani - yeye ambaye huitwa Belteshaza jina la mungu wangu, na ambaye ndani yake kuna roho ya miungu mitakatifu - na nilimwambia juu ya ndoto.9“Belteshaza, mkuu wa wachawi, ninajua kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako na ya kwamba hakuna siri iliyo ngumu kwako. Niambie kile nilichokiona katika ndoto yangu na nini maana yake.10Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana.11Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote.12Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliishi katika matawi yake. Viumbe vyote hai viliishi katika mti huo.13Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni.14Alipiga kelele na kusema, ‘Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake.15Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na pingu ya chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini.16Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.17Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.’18Mimi, Mfalme Nebukadneza nilipata ndoto hii. Sasa, wewe Belteshaza, niambie tafsiri yake, kwa sababu hakuna mtu mwenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunitafsiria. Lakini wewe unaweza kufanya hivyo, kwa kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako.”19Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, “Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake.” Belteshaza akajibu, “Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.20Mti ule uliouona - uliokua na ukawa na wenye nguvu, na ambao sehemu yake ya juu ilifika hata mbinguni, na ambao waweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote -21ambao majani yake ni mazuri, na matunda yake yalikuwa ni mengi, ili kwamba ndani yake kulikuwa na chakula cha wote, na chini yake wanyama wa mwituni walipata kivuli, na ndani yake ndege wa angani waliishi -22huu mti ni wewe, mfalme, wewe uliyekua na kuwa na nguvu. Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia.23Ewe mfalme, ulimwona mjumbe akishuka kutoka mbinguni na akisema, “Ukateni mti na uteketezeni, lakini kiacheni kisiki cha mizizi yake katika nchi, kifungeni kwa ukanda wa chuma na shaba, katikati ya mche mororo katika shamba. Na kilowanishwe na umande kutoka mbinguni. Kiache kiishi katika wanyama wa mwituni katika mashamba mpaka ipite miaka saba.’24Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme.25Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu, na utaishi pamoja na wanyama wa mwituni huko mashambani. Utafanywa uwe unakula majani kama ng'ombe, na utalowanishwa na umande wa kutoka mbinguni, miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba yeye humpa falme hizo mtu yeyote amtakaye.26Kama ilivyoamriwa kwamba kukiacha kisiki cha mizizi ya mti, kwa njia hii ufalme wako utarudishiwa katika kipindi ambacho utajifunza kwamba mbingu inatawala.27Hivyo basi, mfalme, ushauri wangu na ukubalike kwako. Acha kutenda dhambi na utende haki. Geuka uache uovu wako wa kuonesha huruma kwa walionewa, na itakuwa kwamba mafanikio yako yataongezwa.”28Vitu hivi vyote vilitokea kwa mfalme Nebukadneza.29Baada ya miezi kumi na miwili alipokuwa akitembea juu ya dari la ikulu ya kifalme katika Babeli,30na alisema, “Je, hii si Babeli kuu, ambayo nimeijenga kwa ajili ya makao yangu ya kifalme, kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?”31Wakati maneno yakali katika midomo ya mfalme, sauti ilisikika kutoka mbinguni: “Mfalme Nebukadneza, imetangazwa kwako kwamba ufalme huu umeondolewa kutoka kwako.32Utafukuziwa mbali kutoka miongoni mwa watu, na makao yako yatakuwa pamoja na wanyama wa mwitu katika mashamba. Utafanywa kula majani kama ng'ombe. Miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na humpa falme mtu yeyote amtakaye.”33Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.34Na katika mwisho wa siku, mimi, Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, utimamu wa akili nilirudishiwa. “Nilimsifu Mungu Aliye Juu sana, na nilimheshimu na kumtukuza yeye aishiye milele. Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.
35Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure; hufanya lolote limpendezalo miongoni mwa jeshi la mbinguni na wakazi wa dunia. Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia au kumpa changamoto. Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, “Mbona umefanya hivi?”
36Kwa wakati ule ule utimamu wa akili zangu uliponirudia, utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na watu wenye heshima walitafuta msaada wangu. Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi.37Sasa basi, mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za adili. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.

5

1Mfalme Belshaza alifanya sherehe kubwa kwa kwa ajili ya wakuu wake wa kuheshimiwa wapatao elfu moja, na alikunywa divai mbele yao wote watu elfu moja.2Wakati Belshaza alipokuwa akionja divai, alitoa agizo la kuleta vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu au kwa fedha ambavyo Nebukadneza baba yake alikuwa amevichukua kutoka katika hekalu huko Yerusalemu, ambavyo yeye, na wakuu wake, na wake zake, na masuria waliweza kuvinywea.3Watumishi walivileta vyombo ya dhahabu vilivyokuwa vimechukulia katika hekalu, nyumba ya Mungu huko Yerusalemu. Mfalme na wakuu wake, na wake zake na masuria walivinywea.4Walikunywa divai na kuzisifu sanamu zao zilizotengenezwa kwa dhahabu na fedha, shaba, chuma, mbao na mawe.

5Kwa wakati huo huo vidole vya mkono wa mtu vilionekana mbele ya kinara cha taa na kuandika katika ukuta uliopigwa chokaa katika ikulu ya mfalme. Mfalme aliweza kuona sehemu ya mkono ulipokuwa unaandika.6Ndipo uso wa mfalme ulibadilika na mawazo yake yalimwogopesha; miguu yake haikuweza kumfanya asimame, na magoti yake yalikuwa yakigongana kwa pamoja.

7Mfalme alitoa agizo kwa kupiga kelele, waletwe ndani wale ambao hudai wanaweza kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wataalamu wa nyota. Mfalme akawaambia wale waliojulikana kwa hekima katika Babeli, “Yeyote atakayeyaeleza maandishi haya na maana yake atavikwa nguo za zambarau na atavikwa na mkufu wa dhahabu shingoni mwake. Naye atakuwa mtawala wa tatu wa juu kwa mamlaka katika ufalme.”

8Ndipo watu wote wa mfalme walikuwa wakijulikana kwa hekima yao waliingia ndani, lakini hawakuweza kuyasoma maandishi wala kueleza maana yake kwa mfalme.9Kisha mfalme Belshaza alishitushwa sana na mwonekano wa uso wake ulibadilika. Wakuu wake nao walishangazwa sana.

10Ndipo sasa malkia alikuja katika nyumba ya sherehe kwa sababu ya kile ambacho mfalme na wakuu wake walikuwa wamekisema. Malkia akasema, “Mfalme na aishi milele! Usiache mawazo yako yakakusumbua. Usiruhusu mwonekano wa uso wako ubadilike.11Kuna mtu katika ufalme wako ambaye ana roho ya miungu watakatifu dani yake. Katika siku za baba yako, mwanga na weledi na hekima ya miungu ilipatikana ndani yake. Mfalme Nebukadneza, baba yako mfalme, alimfanya kuwa mkuu wa waganga, pamoja na mkuu wa wale wanazungumza na wafu, na wa wenye hekima, na wa wataalamu wa nyota.12Roho bora, ufahamu, weledi, kutafsiri ndoto, kufafanua mafumbo na kutatua matatizo - hizi ni sifa zilizopatikana kwa mtu huyu Danieli, ambaye mfalme alimwita Belteshaza. Sasa mwiteni Danieli naye atawaambia maana ya kile kilichoandikwa.”

13Ndipo Danieli alipoletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamwambia, “Wewe ni yule Danieli, mmoja kati ya watu wa mateka wa Yuda, ambao baba yangu mfalme aliwaleta kutoka Yuda.14Nimesikia habari kukuhusu wewe, kwamba roho ya miungu iko ndani yako, na ya kwamba mwanga na ufahamu na hekima bora inapatikana ndani yako.15Na sasa watu wanaojulikana kwa hekima na wale wanaozungumza na wafu, wamekwisha kuletwa mbele yangu, ili kusoma maandishi haya na kunijulisha maana ya tafsiri yake, lakini hawakuweza kunijulisha tafsiri yake.16Nimesikia kwamba unaweza kutoa tafsiri na kutatua matatizo. Sasa kama utaweza kusoma maandishi na kuniambia maana yake, utavikwa nguo za zambarau na kuwa na kuvalishwa mkufu wa dhahabu shingoni mwako, na utakuwa mtawala wa tatu mwenye mamlaka katika ufalme.”

17Kisha Danieli akajibu mbele ya mfalme, “Zawadi yako na iwe kwa ajili yako mwenyewe, na thawabu yako na umpe mtu mwingine. Hata hivyo, mfalme, nitakusomea maandishi na nitakwaambia maana.

18Na juu yako, Ewe mfalme, Mungu Aliye juu sana alimpa Nebukadneza baba yako ufalme, ukuu, heshima na enzi.19Na kwa sababu ya ukuu huo, Mungu alimpa watu wote, mataifa, na lugha walimtetemekea na kumwogopa. Aliwauwa wale aliotaka wafe na aliwaacha hai wale aliotaka waishi. Aliwainua wale aliowataka, na aliwashusha wale aliowataka.20Lakini wakati moyo ulipokuwa na kiburi na roho yake ilifanywa kuwa mgumu na kwa sababu hiyo alitenda kwa kiburi, alishushwa kutoka kiti chake cha enzi cha kifalme, na waliiondoa enzi yake.21Aliondolewa katika ubinadamu, alikuwa na akili za mnyama, na aliishi na punda wa mwituni. Alikula majani kama ng'ombe. Mwili wake ulilowanishwa kwa umande wa kutoka mbinguni mpaka pale alipojifunza kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na ya kwamba humweka mtu yeyote amtakaye juu yake.

22Wewe mwana wake, Belshaza, haujaunyenyekeza moyo wako, ingawa uliyajua haya yote.23Umejiinua mwenyewe kinyume cha Bwana wa mbinguni. Katika nyumba yake walikuletea vyombo ambavyo wewe, wakuu wako, wake zako na masuria wako walivinywea, na kisha ukaisifia sana sanamu zilizotengenezwa kwa fedha na dhahabu, shaba, chuma, mbao, na mawe - sanamu ambazo haziwezi kuona, kusikia wa kujua kitu chochote. Haujamheshimu Mungu ambaye anaishikilia pumzi yako katika mkono wake na ambaye anazijua njia zako zote.24Ndipo Mungu aliutuma mkono kutoka katika makao yake na maandishi haya yaliandikwa.

25Haya ndiyo maandishi ambayo yaliandikwa: ‘Mene, Mene, Tekeli na Peresi.’

26Maana yake ni: ‘Mene,’ ‘Mungu ameuhesabu ufalme wako na ameukomesha.’
27‘Tekeli’ ‘umepimwa katika mizani na umeonekana umepungua.’
28‘Peresi’ ‘ufalme wako umegawanyika na wamepewa Wamedi na Waajemi.’”

29Ndipo Belshaza alitoa agizo, na walimvalisha Danieli mavazi ya zambarau. Mkufu wa dhahabu walimvisha shingoni, na mfalme alitoa tamko juu ya Danieli kuwa atakuwa mtawala mwenye mamlaka ya nafasi ya tatu katika ufalme.

30Usiku ule Belshaza, mfalme wa Babeli aliuawa,31na Dario Mwajemi aliuchukua ufalme alipokuwa na miaka ipatayo sitini na miwili.

6

1Ilimpendeza Dario kuchagua juu ya ufalme magavana wa majimbo 120 ambao wangetawala juu ya ufalme wote.2Juu yao kulikuwa na watawala wakuu watatu, na Daniel alikuwa mmoja wao. Hawa watawala waliwekwa ili waweze kuwasimamia magavana wa majimbo, ili kwamba mfalme asipate hasara.3Danieli alipata sifa juu ya watawala wakuu na juu ya magavana wa majimbo kwa sababu alikuwa na roho isiyo ya kawaida. Mfalme alikuwa akipanga kumweka juu ya ufalme wote.4Basi watawala wakuu wengine na magavana wa majimbo walitafuta makosa katika kazi ambazo Danieli alizifanya kwa ufalme, lakini hawakuweza kuona ufisadi au kushindwa katika majukumu yake kwa sababu alikuwa mwaminifu. Hakuna kosa au uzembe uliopatikana ndani yake.5Kisha watu hawa wakasema, “Hatukuweza kupata sababu yoyote ya kumshitaki huyu Danieli isipokuwa tukitafuta kitu fulani dhidi yake kuhusiana na sheria za Mungu wake.’”

6Ndipo watawala hawa na magavana walileta mpango mbele ya mfalme. Walimwambia, “Mfalme Dario, uishi milele!7Watawala wote wakuu wa ufalme, magavana wa mikoa, na magavana wa majimbo, washauri, na magavana wameshauriana kwa pamoja na kuamua kuwa wewe, mfalme, unapaswa kupitisha amri na kuitekeleza, ili kwamba mtu yeyote anayefanya dua kwa mungu yeyote au mtu kwa siku thelathini, isipokuwa wewe mfalme, mtu huyo lazima atupwe katika tundu la simba.8Sasa mfalme, litoe agizo na utie saini nyaraka ili kwamba isije ikabadilika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi, hivyo haiwezi ikabatilishwa.9Basi, mfalme Dario alitia saini nyaraka kwa kuifanya amri kuwa sheria.

10Danieli alipojua kuwa nyaraka imekwisha kutiwa sahihi kuwa sheria, alienda ndani ya nyumba yake (madirisha yake katika chumba cha juu yalikuwa wazi kuelekea Yerusalemu), na alipiga magoti yake, kama alivyokuwa akifanya mara tatu kwa siku, na aliomba na kushukuru mbele ya Mungu wake, kama alivyofanya hapo kabla.11Kisha watu hawa walikuwa wameunda hila kwa pamoja walimwona Danieli akiomba na kutafuta msaada kutoka kwa Mungu.12Ndipo walipomwendea mfalme na kuongea naye kuhusiana na amri yake, “Je, haukuweka amri kwamba mtu yeyote atakayefanya maombi kwa mungu mwingine au kwa binadamu ndani ya siku thelathini zijazo, isipokuwa kwako wewe, mfalme, lazima mtu huyo atupwe katika tundu la simba? Mfalme akajibu, “Jambo hili ni la hakika, kama ilivyoelekezwa katika sheria za Wamedi na Waajemi; ambazo haziwezi zikabatilishwa.”

13Kisha wakamjibu mfalme, “Mtu yule Daniel, ambaye ni mmoja wa watu wa mateka kutoka Yuda, hakutii wewe, mfalme wala maagizo yako uliyo tia sahihi. Yeye humwomba Mungu wake mara tatu kwa siku.”14Mfalme aliposikia haya, alisikitishwa sana, alitumia akili jinsi ya kumwokoa kutoka katika utawala huu. Alisumbuka sana mpaka wakati wa kuzama kwa jua akijaribu kumwokoa Danieli.

15Kisha watu hawa waliokuwa wamepanga njama walikusanyika kwa pamoja na mfalme, na wakamwambia, “Ujue mfalme kwamba ni sheria ya Wamedi na Waajemi kwamba hakuna amri au sanamu ambayo mfalme anaipitisha yaweza kubadilishwa.”

16Ndipo mfalme alitoa agizo, na walimleta ndani Danieli, na kisha wakamtupa katika tundu la simba. Mfalme akamwambia Danieli, “Mungu wako, ambaye unamtumikia daima, na akuokoe.”

17Jiwe lililetwa katika mlango wa tundu, na mfalme alilitia muhuri wa pete yake mwenyewe na pamoja na muhuri wa wakuu wake ili kwamba chochote kisiweze kubadilishwa kuhusiana na Danieli.18Basi mfalme alienda kwenye ikulu yake na usiku ule alikuwa na mfungo. Hakuna starehe yoyote iliyoletwa mbele yake, nao usingizi ulimkimbia.

19Kisha katika mapambazuko mfalme aliamka na kwa haraka alienda kwenye tundu la simba.20Na alipokaribia kwenye tundu, alimwita Danieli kwa sauti ya huzuni, akimwambia Danieli, “Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je Mungu wako ambaye anamtumkia daima ameweza kukuokoa kutoka katika simba?

21Ndipo Danieli akamwambia mfalme, “Mfalme, uishi milele!22Mungu wangu amemtuma mjumbe na amevifunga vinywa vya simba, na hawajaweza kunidhuru. Kwa kuwa sikuwa na hatia yoyote mbele yake na pia mbele yako, ewe mfalme, na sijakufanyia jambo lolote la kukudhuru.”

23Basi mfalme alikuwa na furaha sana. Alitoa agizo kwamba wanatakiwa wamtoe Danieli nje ya tundu. Hivyo Danieli aliondolewa kutoka katika tundu. Hakuna dhara lolote lililoonekana kwake, kwa kuwa alikuwa amemtumainia Mungu wake.

24Mfalme alitoa agizo, waletwe wale watu waliomshitaki Danieli na kisha akawatupa wao katika tundu la simba - wao, na watoto wao, na wake zao. Kabla hawajafika sakafuni, simba waliwararua na kuvunjavunja mifupa yao vipande vipande.

25Kisha mfalme Dario aliandika ujumbe kwa watu wote, mataifa na lugha ambazo ziliishi katika dunia yote: “Amani na iongezeke kwenu.26Ninaagiza kwamba katika utawala wote wa ufalme wangu watu watetemeka na kumcha mbele ya Mungu wa Danieli, kwa kuwa ni Mungu aliye hai na huishi milele, na ufalme wake hauwezi kuharibiwa; utawala wake utakuwepo hadi mwisho.
27Yeye anatuhifadhi salama na kutuokoa, na anafanya ishara na maajabu mbinguni na duniani; amemhifadhi Danieli salama dhidi ya uwezo wa simba.”

28Na hivyo basi, Danieli alifanikiwa katika utawala wa Dario na katika utawala wa Koreshi.

7

1Katika mwaka wa kwanza wa Belshaza mfalme wa Babelli, Danieli alikuwa na ndoto na maono katika akili zake wakati alipokuwa amelala kitandani kwake. Kisha akayaandika yale aliyoyaona katika ndoto. Aliandika matukio ya muhimu sana:

2Danieli alieleza, “Usiku katika ndoto zangu niliona pepo nne za mbinguni zilikuwa zinaitikisa bahari kuu.3Wanyama wakubwa wanne, kila mmoja alikuwa tofauti na mwenzake, walitoka katika bahari.

4Mnyama wa kwanza alikuwa kama simba, lakini alikuwa na mabawa ya tai. Nilipokuwa natazama, mabawa yake yalikuwa yamepasuka na alikuwa ameinuliwa katika ardhi na alikuwa amesimama kwa miguu miwili kama mtu. Na alipewa akili za kibinadamu.

5Na kulikuwa na mnyama wa pili, alikuwa kama dubu, na alikuwa ameinama, alikuwa na mbavu tatu katikati ya meno yake katika mdomo wake. Aliambiwa, ‘Inuka na umeze watu wangi.’

6Baada ya hili, niliangalia tena. Kulikuwa na mnyama mwingine ambaye alionekana kama chui. Mgongoni mwake alikuwa na mabawa manne kama mabawa ya ndege, na alikuwa na vichwa vinne. Alipewa mamlaka ya kutawala.

7Baada haya, niliona usiku katika ndoto yangu mnyama wa nne, mwenye kuogofya, na kutisha na mwenye nguvu. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; alikula, na kuvunjavunja katika vipande, na kusagasaga katika miguuni pake kile kilichosalia. Alikuwa ni wa tofauti na wanyama wengine, na alikuwa na pembe kumi.

8Na wakati nilipokuwa natafakari juu ya pembe, nilitazama na niliona pembe nyingine ndogo ilichipuka katikati ya pembe zingine. Mizizi ya pembe tatu kati ya pembe za mwanzo iling'olewa. Niliona katika pembe hii macho kama macho ya mtu na mdomo ambao ulikuwa ukijivuna kwa mambo makubwa.

9Na nilipotazama, viti vya enzi vilikuwa vimewekwa, na Mtu wa siku za kale alikaa sehemu yake. Mavazi yake yalikuwa meupe kama theruji, na nywele zake katika kichwa chake zilikuwa safi kama sufu. Kiti chake cha enzi kilikuwa na miali ya moto, na magurudumu yake yalikuwa yanawaka moto.
10Mto wa moto ulitiririka kutoka mbele yake, na maelfu elfu ya watu walimtumikia, na wengine elfu kumi mara elfu walikuwa wamesimama mbele yake. Na mahakama iliitishwa, na vitabu vilifunguliwa.

11Niliendelea kuangalia kwa sababu ya maneno ya kiburi yaliyosemwa na pembe. Nilitazama wakati mnyama anauliwa, na mwili wake uliharibiwa, na ulitolewa kwa ajili ya kuchomwa moto.12Na kwa wale wanyama wanne waliosalia, mamlaka yao yalitwaliwa mbali, lakini maisha yao yaliendelezwa kwa kipindi fulani cha muda.

13Katika maono yangu usiku ule, nilimwona mtu mmoja anakuja katika mawingu ya mbinguni alikuwa kama mwana wa mtu; alikuja kwa Mzee wa Siku na aliletwa mbele zake.14Naye alipewa mamlaka ya kiutawala na utukufu na mamlaka ya kifalme ili kwamba watu wote, na mataifa na lugha ziweze kumtumikia yeye. Mamlaka yake ya kutawala ni mamlaka ya milele ambayo hayatapita, na ufalme wake ni ule ambao hautaangamizwa.

15Na kwangu mimi, Danieli, roho yangu ilihuzunishwa ndani yangu, na maono niliyoyaona katika akili zangu yalinisumbua.16Nilimsongelea mmoja wa hawa walikuwa wamesimama hapo na nikamwomba anioneshe maana ya mambo haya.

17Hawa wanyama nne wakubwa ni wafalme wanne ambao watakoatokea katika nchi.18Lakini watu watakatifu wa Mungu aliyejuu wataupokea ufalme na wataumiliki milele na milele.’

19Ndipo nilipotaka kujua zaidi juu ya mnyama wa nne, ambaye alikuwa tofauti sana na wengine na alikuwa wa kutisha pamoja na meno yake ya chuma na makucha ya shaba; alimeza, na alivunja vipande vipande, na alisagasaga kwa miguu yake kile kilichokuwa kimesalia.20Nilitaka kujua juu ya pembe kumi katika kichwa chake, na kuhusu pembe nyingine iliyochomoza, na ambayo mbele yake pembe zingine tatu zilianguka chini. Nilitaka kujua kuhusu pembe yenye macho na kuhusu mdomo uliokuwa unajisifu kwa mambo makubwa na ambayo ilionekana kuwa ni kubwa kuliko zingine.21Na nilipotazama, pembe hii iliinua vita dhidi ya watu watakatifu na ilikuwa inawashinda mpaka pale22Mzee wa Siku alipokuja, na watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu Sana. Ndipo wakati ulipowadia ambapo watu watakatifu waliupokea ufalme.

23Hiki ndicho mtu yule alichokisema, ‘Kwa habari ya mnyama wanne, utakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia ambao utakuwa tofauti na falme zingine zote. Utaimeza dunia yote, na utaikanyaga yote chini na kuivunjavunja vipande vipande.24Na kuhusu pembe kumi, kutoka katika ufalme huu, wafalme kumi watainuka, na mwingine atainuka baada yao. Atakuwa wa tofauti na wale waliomtangulia, na atawashinda wale wafalme watatu.25Atazungumza maneno kinyume cha Yeye Aliye Juu sana na atawatesa watu watakatifu wa Mungu Aliye Juu. Atajaribu kuzibadili sikukuu na sheria. Mambo haya atapewa mikononi mwake kwa mwaka mmoja, miaka miwili na nusu mwaka.

26Lakini kikao cha mahakama kitaitishwa, na watazichukua nguvu zake za kifalme ili mwisho aweza kuharibiwa na kuteketezwa.27Ufalme na utawala, ukubwa wa falme chini ya mbingu yote, watapewa watu walio wa watu watakatifu wa Yeye Aliye juu Sana. Ufalme wake ni ufalme wa milele, na falme zingine zote zitamtumikia na kumtii yeye.’

28Na huu ndio mwisho wa mambo. Na kuhusu mimi, Danieli, mawazo yangu yanihuzunisha sana mimi na mwonekano wa uso wangu ulibadilika. Lakini mambo haya niliyahifadhi mimi mwenyewe.”

8

1Katika mwaka wa tatu wa utawala wa mfalme Belshaza, mimi Danieli niliona maono (baada ya maono ya awali yaliyonipata).2Nilipokuwa nikiangalia katika ndoto, niliona kwamba nilikuwa katika mji wa Shushani wenye ngome katika jimbo la Elamu. Niliona katika ndoto kuwa nilikuwa karibu na mfereji wa Ulai.3Nilitazama juu na nikaona mbele yangu kondoo dume lenye mapembe mawili, limesimama pembeni mwa mfereji. Pembe moja lilikuwa refu kuliko jingine, lakini pembe ndefu ilikuwa inakua pole pole kuliko ile fupi na pembe fupi ilirefuka na kuizidi nyingine.4Niliona kondoo mme akiishambulia magharibi, kisha kaskazini, na baadaye kusini; hakuna mnyama mwingine aliyeweza kusimama mbele yake. Hakuna yeyote aliyeweza kumwokoa yeyote katika mkono wake. Alifanya chochote kile alichokitaka, na alikuwa mtu mkubwa sana.

5Na nilipokuwa natafakari juu ya haya, niliona beberu akitoka magharibi, na kuvuka katika uso wa dunia yote, akikimbia kwa kasi kana kwamba hakuonekana kama aligusa ardhini. Mbuzi huyo alikuwa na pembe kubwa katikati ya macho yake.6Alienda mpaka kwa kondoo aliyekuwa na pembe mbili, nilikuwa nimemwona kondoo dume amesimama katika ukingo wa mfereji na mbuzi alikimbia kumwelekea kondoo dume kwa hasira kali.7Niliiona mbuzi ikija karibu na kondoo. Mbuzi alikuwa na hasira na kondoo, alimpiga kondoo na alizivunja pembe zake mbili. Kondoo hakuwa na nguvu za kusimama mbele zake. Mbuzi alimgonga kondoo akaanguka chini na akamkanyaga. Hapakuwa na yeyote wa kumwokoa kutoka katika nguvu zake.8Ndipo mbuzi alikua akawa mkubwa, lakini alipokuwa na nguvu, pembe kubwa ilivunjwa, na katika sehemu yake zilichipuka na kukua pembe nne kubwa zilizochomoza kuelekea pepo nne za mbingu.

9Kutoka katika pembe moja ilichipuka pembe nyingine, ilikuwa ndogo hapo awali, lakini baadaye ilikuwa pembe kubwa upande wa kusini, na mashariki, na katika nchi ya uzuri.10Pembe ilikuwa kubwa na matokeo yake iliinua vita dhidi ya jeshi la mbinguni. Baadhi ya jeshi na nyota kadhaa zilitupwa chini duniani, na zilikanyagwa.11Alizidi kuwa mkubwa, mkubwa kama kamanda wa jeshi la kimungu. Sadaka za kuteketezwa za kila siku ziliondolewa mbali na yeye, na sehemu yake takatifu zilitiwa unajisi.12Kwa sababu ya uasi, pembe ya mbuzi ilipewa jeshi, na sadaka za kuteketezwa zitasitishwa. Pembe itautupa ukweli chini ardhini, na itafanikiwa katika kila jambo ilifanyalo.

13Kisha nilimsikia mtakatifu mmoja akiongea na mtakatifu mwingine akamjibu, “Mambo haya yatadumu kwa muda gani, maono haya ya sadaka ya kuteketezwa, dhambi ile iletayo uharibifu, kukanyagisha patakatifu na jeshi?

14Aliniambia, “Itadumu kwa jioni na asubuhi zipatazo 2,300. Baada ya hapo, mahali patakatifu patawekwa sawa.”

15Wakati mimi Danieli, nilipoona maono, nilijaribu kuyaelewa. Na hapo mbele yangu alisimama yule aliyeoneakana kama mtu.16Niliisikia sauti ya mtu ikiita katikati ya kingo za mfereji wa Ulai. Alisema, “Gabrieli, msaidie mtu huyu kuelewa maono.”

17Basi alikuja karibu na mahali niliposimama. Na alipokuja, niliogopa na nilisujudia hadi chini. Aliniambia, “Fahamu, mwana wa mtu, kwamba maono ni kwa ajili ya wakati wa mwisho.”

18Alipokuwa anaongea na mimi, nilipata usiingizi mzito nikiwa nimelala kifudifudi. Kisha alinishika na kunisimamisha.

19Akaniambia, “Tazama, nitakuonyesha kile kitachotokea baadaye katika kipindi cha ghadhabu, kwa sababu maono haya yanahusu wakati wa mwisho uliopangwa.20Na kuhusu kondoo mme uliyemwona, yule mwenye pembe mbili - ni wafalme wawili wa Umedi na Uajemi.21Mbuzi dume ni mfalme wa Ugiriki. Pembe kubwa katikati ya macho yake ni mfalme wa kwanza.22Na kuhusu pembe iliyovunjika, ambayo katika nafasi yake pembe zingine nne zilichipuka - hizi ni falme nne zitakazoinuka kutoka katika taifa lake, lakini hazitakuwa na nguvu kubwa.

23Katika siku zijazo za falme hizo, wakati ambapo wahalifu watakuwa wamefikia kikomo chao, mfalme mwenye uso katili, na yeye mwenye akili sana, atainuka.24Nguvu zake zitakuwa kubwa, lakini si kwa nguvu zake mwenyewe. Atakuwa wa kustaajabisha kwa kile atakachokuwa anakiharibu; atafanya na kufanikiwa. Atawaangamiza watu wenye nguvu, watu miongoni wa watakatifu.25Ataufanya udanganyifu usitawi chini ya mkono wake kwa sababu ya ujanja wake. Atawaangamiza watu wengi bila kutegemea. Atainuka pia hata kinyume cha Mfalme wa wafalme, na atavunjwa, lakini si kwa mkono wowote wa binadamu.

26Maono kuhusu jioni na asubuhi ulizoambiwa ni ya kweli. Lakini uyafunge maono haya, kwa kuwa yanahusu siku nyingi za wakati ujao.

27Ndipo mimi, Danieli nilichoka sana na nikalala nikiwa dhaifu kwa siku kadhaa. Kisha nikainuka na nikaenda kufanya kazi za mfalme. Lakini nilikuwa nimetishwa sana na maono, na hapakuwa na mtu yeyote aliyeweza kuyaelewa.

9

1Dario mwana wa Ahasuero, wa uzao wa Wamedi. Alikuwa na Ahasuero ambaye alifanywa mfalme juu ya ufalme wa watu wa Babeli.2Sasa katika mwaka wa kwanza wa utawala wa Dario, mimi Danieli, nilikuwa najisomea vitabu vilivyo na neno la Yahweh, neno ambalo lilikuwa limemjia Yeremia nabii. Niligundua kwamba kungekuwa na miaka sabini hadi mwisho wa kuachwa kwa Yerusalemu ungefika.3Niliugeuza uso wangu kumwelekea Bwana Mungu, ili kumtafuta yeye kwa sala na maombi, kwa kufunga, na kuvaa nguo za magunia na kukaa katika majivu.

4Nilimwomba Yahweh Mungu wangu, na niliungama dhambi zetu. Nilisema, “Tafadhali, Bwana, wewe ni Mungu mkuu na mwenye kuheshimiwa, wewe hutunza maagano na uliye mwaminifu katika kuwapenda wale wanaokupenda wewe na kuzishika amri zako.5Tumetenda dhambi na tumefanya yaliyo mabaya. Tumeenenda kwa uovu na tumeasi, tumegeuka upande kinyume na amri na maagizo yako.6Hatukuwasikiliza watumishi wako manabii waliozungumza na wafalme wetu, viongozi wetu, baba zetu, na kwa watu wote wa nchi kwa jina lako.7Kwako Bwana, kuna uadilifu. Hata hivyo, kwetu kuna aibu katika nyuso zetu, kwa watu wa Yuda na wale wanaoishi Yerusalem, na kwa Israeli yote. Hii ni pamoja na wale walio karibu na wale walio mbali katika nchi zote ambazo kwazo uliwatawanya. Hii ni kwa sababu ya udanganyifu mkubwa tulioufanya kinyume chako.8Kwetu sisi, Yahweh, kuna fedheha katika nyuso, na kwa wafalme wetu, na kwa viongozi wetu, na kwa baba zetu, kwa sababu tumekutenda dhambi wewe.9Kwa Bwana Mungu wetu kuna huruma na msamaha, kwa kuwa tumemuasi yeye.10Hatujaitii sauti ya Yahweh Mungu wetu kwa kutembea katika sheria zake alizotupatia kupitia watumishi wake manabii.11Israeli wote wameiasi sheria yako na kugeukia upande, kwa kukataa kuitii sauti yako. Laana na viapo vilivyoandikwa katika sheria ya Musa, mtumishi wa Mungu, zimemwagwa juu yetu kwa kuwa tumetenda dhambi.12Yahweh ameyathibitisha maneno ambayo aliyasema kinyume na sisi na kinyume na viongozi wetu juu yetu, kwa kuleta juu yetu janga kubwa. Kwa kuwa chini ya mbingu yote haijawahi kufanyika kitu chochote ambacho kinaweza kulinganishwa na kile kilichofanyika huko Yerusalemu.13Kama ilivyoandikwa kwenye sheria ya Musa, baa hili lote limetupata, ingawa bado hatujaomba rehema kutoka kwa Yahweh Mungu wetu kwa kugeuka na kuacha maovu yetu na kuufuata ukweli wako.14Hivyo basi, Yahweh ameyaweka tayari maafa na ameyaleta juu yetu, kwa kuwa Yahweh Mungu wetu ni mwenye haki katika matendo yote anayoyafanya, ingawa bado hatujaitii sauti yake.15Basi sasa, Bwana Mungu wetu, uliwatoa watu wako katika nchi ya Misri kwa mkono wenye nguvu, na umejifanyia jina maarufu kwa ajli yako mwenyewe, hata siku hii ya leo. Lakini bado tumekutenda dhambi; tumefanya mambo ya hila. Kwa sababu ya matendo yako yote ya haki,16Bwana, iache hasira na ghadhabu yako iwe mbali na mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu. Hii ni kwasababu ya dhambi zetu, na kwasababu ya uovu wa baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamekuwa kitu cha kudharauliwa na wote wanaotuzunguka.17Basi sasa, Mungu wetu, sikiliza sala za mtumishi wako na maombi yake kwa ajili ya rehema; kwa ajili yako, Bwana ufanye uso wako ung'ae katika sehemu yako takatifu iliyoachwa ukiwa.18Mungu wangu, fungua masikio yako na usikie; fumbua macho yako na uone. Tumeharibiwa; utazame mji unaoitwa kwa jina lako. Hatukuombi msaada wako kwa sababu ya haki yetu, ila kwa sababu ya rehema zako kuu.19Bwana, sikiliza! Bwana, samehe! Bwana, tuangalie na ufanye jambo! Kwa ajili yako mwenyewe, usichelewe, Mungu wangu, kwa kuwa mji wako na watu wako wanaitwa kwa jina lako.”

20Nilipokuwa ninaongea kwa kuomba na kuungama dhambi yangu na dhambi ya watu wangu Israeli, na kuwasilisha maombi yangu mbele ya Yahweh Mungu wangu kwa niaba ya mlima mtakatifu wa Mungu.21Nilipokuwa ninaomba, mtu Gabrieli, ambaye nilikuwa nimemwona katika ndoto hapo awali, alipaa kwa kasi kushuka kuja nilipo, ilikuwa ni wakati wa sadaka ya jioni.22Alinipa ufahamu na aliniambia, “Danieli, nimekuja sasa ili nikupe utambuzi na ufahamu.23Ulipoanza kuomba rehema, amri ilitolewa na nimekuja kukueleza jibu, kwa kuwa unapendwa sana. Hivyo basi, tafakari neno hili na uufahamu ufunuo.

24Majuma sabini yameamriwa kwa ajili ya watu wako na mji wako mtakatifu kukomesha hatia na kumaliza dhambi, na kuleta haki ya milele, na kutimiza maono na unabii, na kupaweka wakfu mahali patakatifu sana.

25Ujue na kufahamu kuwa tangu kupitishwa kwa amri ya kurudi na kuijenga upya Yerusalemu mpaka ujio wa mpakwa mafuta (atakayekuwa kiongozi), kutakuwa na majuma saba na majuma sitini na mbili. Yerusalemu itajengwa pamoja na mitaa yake na handaki, licha ya kuwepo kwa nyakati za shida26Baada ya majuma sitini na mbili, mtiwa mafuta ataharibiwa na atakuwa hana kitu chochote. Jeshi la kiongozi ajaye litauangamiza mji na mahali patakatifu. Mwisho wake utatatokea kwa gharika, na kutakuwa na vita hata mwisho. Uharibifu umekwisha amriwa.27Atalithibitisha agano pamoja na watu wengi kwa muda wa juma moja; Lakini katikati ya juma atakomesha dhabihu na sadaka. Baada ya chukizo la uharibifu atatokea mtu atakayeleta ukiwa. Mwisho kamili na uharibifu umeamriwa kutokea kwa yeye aliyesababisha ukiwa.”

10

1Katika mwaka wa tatu wa Koreshi mfalme wa Uajemi, ujumbe ulifunuliwa kwa Danieli, aliyeitwa pia Belteshaza. Ujumbe huu ulikuwa ni wa kweli. Ulihusu vita kuu. Danieli aliufahamu ujumbe alipopata ufumbuzi kutoka katika maono.

2Katika siku hizo, mimi Danieli, nilikuwa katika maombolezo kwa wiki tatu.3Sikula chakula kizuri, sikula nyama, sikunywa divai, na sikujipaka mafuta mwenyewe mpaka ukamilifu wa wiki tatu nzima.

4Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kwanza, nilipokuwa niko karibu na mto mkubwa (ambao ni Tigrisi),5Nilitazama juu na nikamwona mtu aliyevaa kitani, akiwa na mkanda kiunoni mwake uliotengenezwa kwa dhahabu safi kutoka Ufazi.6Mwili wake ulikuwa kama kito, na sura yake ilikuwa kama radi. Macho yake yalikuwa kama miali ya tochi, na mikono yake na miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosafishwa. Sauti ya maneno yake ilikuwa kama sauti ya umati mkubwa wa watu.

7Mimi, Danieli peke yangu niliyaona maono, na watu niliokuwa na pamoja hawakuyaona maono. Lakini, jambo kuu la kuogofya liliwaijia juu yao, na walikimbia na kujificha wao wenyewe.8Hivyo niliachwa peke yangu na niliyaona maono haya ajabu. Hakuna nguvu iliyobakia ndani yangu; mwonekano wangu wa kung'aa ulibadilika na kuwa mwonekano wa uharibifu, na hazikubakia nguvu ndani yangu.9Kisha nikasikia maneno yake, na nilipoyasikia, nilianguka kifudifudi na kupata usingizi mzito.

10Mkono ulinigusa, na ilinifanya nitetemeke katika magoti yangu na viganja vya mikono yangu.11Malaika aliniambia, “Danieli, mtu aliyetunzwa sana, yafahamu maneno ninayokwambia wewe. Simama wima, kwa kuwa nimeshakutuma.” Na alipomaliza kuniambia ujumbe huu, nilisimama nikiwa natetemeka.

12Kisha aliniambia, “Usiogope, Danieli. Tangu siku ya kwanza ulipoiweka akili yako kutaka kufahamu na kujinyenyekeza mwenyewe mbele ya Mungu, maneno yako yalisikiwa, na nimekuja kwa sababu ya maneno yako.13Mwana wa mfalme wa ufalme wa Uajemi alinizuia, na niliwekwa huko na mfalme wa Uajemi kwa siku ishirini na moja. Lakini Mikaeli, mmoja kati ya wakuu alikuja kunisaidia.14Sasa nimekuja kukusaidia ili ufahamu kile kitakachotokea kwa watu wako katika siku za mwisho. Kwa kuwa maono ni kwa ajili siku ambazo hazijatokea bado.

15Na alipokuwa akali akiniambia maneno haya, niligeuza uso wangu na kuuelekeza chini na sikuwa na uwezo wa kuzungumza.16Yeye aliyekuwa kama wana wa mtu alinigusa mdomo wangu na nifumbua kinywa changu na nilimwambia huyo aliyekuwa amesimama mbele yangu: “Bwana wangu, niko katika masumbuko makali kwa sababu ya maono; sina nguvu ndani yangu iliyosalia.17Mimi ni mtumishi wako. Je, ninawezaje kuongea na Bwana wangu? Kwa kuwa sasa sina nguvu, na hakuna pumzi iliyosalia ndani yangu.”

18Tena yule mwenye mwonekano wa mtu alinigusa na kunitia nguvu.19Alisema, “Usiogope, mtu ulithaminiwa sana. Amani na iwe kwako! Uwe mwenye nguvu, uwe na nguvu!” Na alipokuwa anaongea na mimi, nilipata nguvu. Nilimwambia, “Bwana wangu na aseme, kwa kuwa umenitia nguvu.”

20Aliniambia, “Je unajua ni kwanini nimekuja kwako? Nitarudi hivi karibuni kupigana na mkuu wa Uajemi. Na nitakapoenda, mkuu wa Ugiriki atakuja.21Lakini nitakwambia kile kilichoandikwa katika Kitabu cha Ukweli. Hakuna yeyote anayejionesha kuwa na nguvu pamoja nami dhidi yao, isipokuwa Mikaeli mkuu wenu.”

11

1Katika mwaka wa kwanza wa Dario Mmedi, mimi mwenyewe nilikuja kumwezesha na kumlinda Mikaeli.

2Na sasa nitakufunulia ukweli. Wafalme watatu watainuka katika Uajemi, na mfalme wa nne atakuwa tajiri sana kuliko wengine wote. Na wakati atakapopata nguvu kupitia utajiri wake, atawachochea kila mtu kinyume na ufalme wa Ugiriki.

3Mfalme wenye nguvu atainuka ambaye atatawala ufalme mkubwa, na ataenenda kufuatana na matakwa yake mwenyewe.4Na atakapokuwa ameinuka, ufalme wake utavunjika na utagawanyika katika pepo nne za mbinguni, lakini hawatakuwa wazao wake mwenyewe, na si kwa nguvu zake kwa wakati alipokuwa akitawala. Kwa kuwa ufalme wake utang'olewa kwa ajili ya wengine tofauti na wazawa wake.5Mfalme wa Kusini atakuwa na nguvu, lakini mmoja kati ya maamiri jeshi wake atakuwa mwenye nguvu kuliko yeye na atautawala ufalme wake kwa nguvu kubwa.6Baada ya miaka michache, wakati muda utakapokuwa sawa, watafanya mwungano. Binti wa mfalme wa Kusini atakuja kwa mfalme wa Kaskazini kuyathibitisha makubaliano yao. Lakini hataweza kuzitunza nguvu za mkono wake, wala mfalme hatasimama wala mkono wake. Ataachwa na wale waliomleta, na baba yake, na yeye aliyemuunga mkono katika nyakati hizo.

7Lakini tawi kutoka katika mizizi yake litachipuka katika nafasi yake. Atalishambulia jeshi na kuingia ngome ya mfalme wa Kaskazini. Atapigana nao, na atawashinda.8Ataichukua miungu yao mpaka Misri pamoa na sanamu zao za chuma na vyombo vyao vya fedha na vya dhahabu vyenye thamani. Kwa miaka mingi atakaa mbali na mfalme wa Kaskazini.9Kisha mfalme wa Kaskazini atauvamia ufalme wa mfalme wa Kusini, lakini atajitoa na kwenda katika nchi yake mwenyewe.10Wana wake watajiweka tayari na kuunganisha jeshi kubwa. Litaendelea kukua na litagharikisha kila kitu, litapita katikati hadi kwenye ngome yake.

11Ndipo mfalme wa Kusini atakasirika, na ataenda na kupigana naye, mfalme wa Kaskazini. Mfalme wa Kaskazini atainua jeshi kubwa, bali jeshi litatiwa katika mkono wake.12Jeshi litachukuliwa, na moyo wa mfalme wa Kusini utainuliwa juu, na atawafanya makumi maelfu kuanguka, lakini hataweza kuwa mshindi.13Kisha mfalme wa Kaskazini atainua jeshi jingine, kubwa kuliko la kwanza. Baada ya miaka kadhaa, mfalme wa Kaskazini atakuja na jeshi kubwa likiwa na vifaa vingi.

14Katika siku hizo wengi watainuka kinyume na mfalmea wa Kusini. Wana wa vurugu miongoni mwa watu wake watasimama wao wenyewe ili kuyatimiliza maono, lakini watajikwaa.15Mfalme wa Kaskazini atakuja, kuizingira nchi kwa kuweka vilima, na kuuteka mji wenye ngome. Majeshi ya Kusini hayataweza kusimama, hata wanajeshi wake bora. Hawatakuwa na nguvu za kusimama.16Badala yake, yeye ajaye ataenenda kwa kufuata tamaa zake kinyume chake; hakuna yeyote atakayesimama katika njia yake. Atasimama katika nchi ya uzuri, na uharibifu utakuwa mkononi wake.17Mfalme wa Kaskazini atauelekeza uso wake ili kuja kwa nguvu za ufalme wake wote, na kutakuwa na makubaliano atakayoyafanya na mfalme wa Kusini. Atampatia katika ndoa binti wa wanawake ili kuuharibu ufalme wa Kusini. Lakini mpango huo hautafanikiwa wala kumsaidia.18Baada ya hayo, mfalme atafuatilia nchi za pwani na ataziteka nchi nyingi. Lakini amiri jeshi atakikomesha kiburi chake na atakisababisha kiburi chake kiishe.19Kisha atafuatilia miji yenye ngome katika nchi yake mwenyewe, lakini atajikwaa na kuanguka; na hatapatikana tena.

20Kisha mtu mwingine atainuka katika nafasi ambaye atamfanya mtoza ushuru apite kwa ajili ya ufahari wa ufalme. Lakini katika siku zijazo atakatiliwa mbali, lakini si kwa hasira wala si katika vita.

21Katika nafasi atainuka mtu wa kudharauliwa ambaye watu hawatampa heshima ya nguvu ya kifalme; atakuja bila kukusudiwa na atautwaa ufalme kwa ulaghai.22Mbele yake, kila jeshi litafutiliwa mbali kama gharika. Jeshi na kiongozi wa agano wataangamizwa wote kwa pamoja.23Tangu katika kipindi kile ambacho makubaliano yalifanywa pamoja naye, ataenenda kwa kwa hila; atakuwa mwenye nguvu akiwa na watu wachache tu.24Kwa ghafla ataingia katika sehemu tajiri sana za jimbo, na atafanya kile ambacho si baba yake wala baba wa baba yake alishakifanya. Atagawanya mateka, nyara, na mali zake miongoni mwa wafuasi wake. Atapanga mpango wa kuiangusha ngome, lakini ni kwa muda tu.

25Ataamsha nguvu zake na moyo wake kinyume na mfalme wa Kusini kwa jeshi kubwa. Mfalme wa Kusini atapigana vita akiwa na jeshi kubwa lenye nguvu, lakini hataweza kusimama kwa kuwa wengine watafanya njama dhidi yake.26Hata wale wanaokula chakula chake kizuri watajaribu kumwangamiza. Jeshi lake litakatiliwa mbali kama gharika, na wengi wao watauawa.27Wafalme wote hawa wawili, wakiwa na mioyo yao imejawa na uovu kinyume na mwenzake, watakaa katika meza moja na kudanganyana, lakini haitakuwa na maana yoyote. Kwa kuwa mwisho utatokea katika kipindi ambacho kimeshapangwa.28Kisha mfalme wa Kaskazini atarudi katika nchi yake akiwa na utajiri mkubwa, na moyo wake ukipinga vikali agano takatifu. Atatenda na kisha atarudi katika nchi yake mwenyewe.

29Katika muda uloamriwa atarudi na kuushambulia ufalme wa Kusini. Lakini katika kipindi hiki hakitakuwa kama awali.30Kwa kuwa meli kutoka Kitimu zitamshambulia, naye ataogopa na kurudi nyuma. Atakuwa mwenye hasira dhidi ya agano takatifu, na atawaonyesha mema wale watakaoliacha agano takatifu.31Majeshi yake yatainuka na kukufuru sehemu takatifu katika ngome. Wataziondoa sadaka za kawaida za kuteketezwa, na watasimamisha chukizo la uharibifu litakalosababisha ukiwa.

32Na kwa wale walioenenda kwa ouvu kinyume na agano, atawadanganya na kuwatia uovu. Bali watu wale wanaomjua Mungu wao watakuwa jasiri na watachukua hatua.33Watu wenye hekima miongoni mwa watu watawafanya watu waelewe. Lakini watajikwaa kwa upanga na kwa miali ya moto; watatiwa mateka na kunyang'anywa kwa siku.

34Katika siku za kujikwaa kwao, watasaidiwa kwa msaada kidogo. Watu wengi watajiunga nao wenyewe katika unafiki.35Baadhi ya watu wenye hekima watajikwaa ili kujisafisha kutokea kwao, na kujiosha, na kujitakasa, mpaka wakati wa mwisho. Kwa kuwa wakati ulioamriwa haujaja bado.

36Mfalme atafanya kutokana na matakwa yake. Atajiinua mwenyewe na kujifanya mkubwa kuliko kila mungu. Kinyume cha Mungu wa miungu, atasema vitu vibaya, kwa kuwa atafanikiwa mpaka pale ghadhabu itakapokuwa imekamilika. Kwa ajili kile kilichoamriwa kitakapokuwa kimefanyika.37Hatazijali miungu ya baba zake wala mungu anayependwa na wanawake. Wala hatamjali mungu mwingine yeyote. Kwa kuwa zaidi ya mtu yeyote atajifanya mwenyewe kuwa mkuu.38Atamheshimu mungu wa ngome badala ya haya. Ni mungu ambaye baba zake hawakumkubali ambaye atamheshimu kwa dhahabu na fedha, kwa mawe ya thamani na zawadi zenye kuthaminiwa.39Atazishambulia ngome imara sana kwa msaada wa mungu mgeni. Atampa heshima kubwa yeyote anayemkubali. Atawafanya kuwa watawala juu ya watu wengi, na ataigawanya nchi kwa rushwa.

40Kwa wakati wa mwisho mfalme wa Kusini atamshambulia. Mfalme wa Kaskazini atamvamia kwa ukali wa magari na wapanda farasi, na meli nyingi. Naye ataenda kinyume cha nchi, kuwagharikisha, na kupita katikati.41Naye ataingia katika nchi ya uzuri, makumi elfu ya Waisraeli wataanguka. Lakini watu hawa watatoroka kutoka katika mkono wake: Waedomu, Wamoabu, na mabaki ya watu wa Amoni.42Naye ataunyoosha mkono katika nchi; nchi ya Misri haitaokolewa.43Atakuwa na mamlaka juu ya hazina za dhahabu na za fedha, na juu ya utajiri wote wa Misri; watu wa Libya na Ethiopia watakuwa chini katika nyayo za miguu yake.44Lakini taarifa kutoka mashariki na kaskazini zitamwogopesha, naye atatoka akiwa mwenye hasira nyingi ili kuwaharibu kabisa na kuwahifadhi kwa ajli ya uharibifu.45Naye ataisimamisha hema ya makao yake ya kifalme kati ya bahari na milima ya uzuri wa utakatifu. Ataufikia mwisho wake, na hapatakuwa na msaidizi wa kumsadia.

12

1Katika kipindi hicho, Mikaeli, jemedari mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwa na wakati wa mateso ambao haujawahi kutokea tangu mwanzo wa taifa lolote mpaka kipindi hicho. Katika muda huo watu wako wataokolewa, yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu.2Na wengi wa wale waliolala katika mavumbi ya dunia watainuka. Baadhi kwa uzima wa milele na baadhi kwa ajili ya fedheha na kudharauliwa milele.3Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele.4Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya; ukakitie muhuri kitabu mpaka nyakati za mwisho. Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.

5Kisha mimi, Danieli, nilitazama, na kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama. Mmoja alisimama katika upande huu wa ukingo wa mto, na mwingine alisimama katika ukingo wa upande mwingine wa mto.6Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani, yeye aliyekuwa juu ya mkondo wa mto, “Je, itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?”

7Nilimsikia mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu katika mkondo wa mto, aliinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni na kuapa kwa yeye aishiye milele kwamba itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati. Na wakati nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimeshaharibiwa, mambo haya yote yatakuwa yamemalizika.

8Nilisikia, lakini sikufahamu. Basi nikamwuliza, “Bwana wangu, mambo haya yote yatakuwa na matokeo gani?”

9Alisema, “Nenda zako Danieli, kwa kuwa maneno yamefungwa, na kutiwa muhuri mpaka wakati wa mwisho.10Watu wengi watakuwa wametakaswa, wameoshwa, na kusafishwa, lakini waovu wataenenda katika uovu.11Katika muda ule ambapo sadaka ya kawaida ya kuteketezwa itakapokuwa imeondolewa na chukizo la uharibifu liliosababisha ukiwa limesimamishwa, kutakuwa na siku zipatazo 1,290.12Ana heri mtu yule anayengojea mpaka mwisho wa siku 1,335.

13Unapaswa uondoke uende njia yako hata mwisho, na kisha utapumzika. Utainuka katika sehemu uliyopewa, mwishoni mwa siku.”

Hosea

1

1Hili ni neno la Bwana lililofika kwa Hosea mwana wa Beeri siku za Uzia, Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda, na katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi, mfalme wa Israeli.

2Wakati Bwana alipozungumza kwanza kupitia Hosea, akamwambia, “Nenda ukajitwalie mke ambaye ni kahaba. Atakuwa na watoto ambao ni matokeo ya ukahaba wake. Kwa maana nchi inafanya uzinzi mkubwa kwa kumwacha Bwana.”3Basi Hosea akaenda akamwoa Gomeri binti Diblaimu, naye akachukua mimba, akazaa mtoto mwanamume.

4Bwana akamwambia Hosea, “Mwite jina lake Yezreeli. Kwa maana kwa muda mfupi nitaiadhibu nyumba ya Yehu kwa sababu ya kumwaga damu huko Yezreeli; nami nitamaliza ufalme wa nyumba ya Israeli.5Itatokea siku ile nitakapovunja upinde wa Israeli katika bonde la Yezreeli.”

6Gomeri akachukua mimba tena akamzaa binti. Ndipo Bwana akamwambia Hosea, “Mwite jina lake Lo Ruhama; kwa maana sitawahurumia tena nyumba ya Israeli, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.7Hata hivyo nitawahurumia nyumba ya Yuda, nami nitawaokoa mwenyewe, Bwana, Mungu wao. Sitawaokoa kwa upinde, upanga, vita, farasi, au wapanda farasi.”

8Baada ya Gomeri kumwachisha Lo Ruhama, alipata mimba na kuzaa mtoto mwingine mwanamume.9Ndipo Bwana akasema, “Mwite jina la Lo Ami; kwa kuwa ninyi si watu wangu, wala mimi si Mungu wenu.”

10Hata hivyo idadi ya watu wa Israeli itakuwa kama mchanga wa bahari, ambayo haiwezi kupimwa au kuhesabiwa. Itakuwa pale ambapo waliambiwa, “Ninyi si watu wangu,” wataambiwa, “Ninyi ni watu wa Mungu aliye hai.”11Watu wa Yuda na watu wa Israeli watakusanyika pamoja. Wao wataweka kiongozi mmoja wao wenyewe, na watatoka kutoka nchi, kwa maana itakuwa siku ya Yezreeli kuu.

2

1Waambie ndugu zenu wanaume, ‘Watu wangu!’ na kwa dada zako, ‘umeonyeshwa huruma.’”

2Leteni mashtaka dhidi ya mama yenu, leteni mashtaka, kwa kuwa yeye si mke wangu, wala mimi si mumewe. Na auondoe uzinzi wake mbele yake, na matendo yake ya uzinzi kati ya matiti yake.
3Ikiwa sio, nitamvua nguo na kumuonyesha uchi wake kama siku aliyozaliwa. Nami nitamfanya kama jangwa, kama nchi iliyoharibika, nami nitamfanya afe kutokana na kiu.
4Sitakuwa na rehema kwa watoto wake, kwa maana wao ni watoto wa ukahaba.
5Maana mama yao amekuwa kahaba, na yeye aliye mimba amefanya mambo ya aibu. Alisema, Nitawafuata wapenzi wangu, kwa maana wananipa mkate wangu na maji, sufu yangu na kitani, mafuta yangu na kinywaji.”
6Kwa hiyo nitajenga ua wa kuzuia njia yake kwa miiba. Nitajenga ukuta dhidi yake ili asiweze kupata njia. Yeye atawafuatilia wapenzi wake, lakini yeye hatawafikia.
7Yeye atawatafuta, lakini hatawapata. Kisha atasema, “Nitarejea kwa mume wangu wa kwanza, kwa maana ilikuwa ni bora kwangu zamani kuliko sasa.”
8Kwa maana hakujua kwamba mimi ndimi niliyempa nafaka, divai mpya na mafuta, na ambaye nilimwongezea fedha na dhahabu, ambazo walizitumia kwa Baali.
9Kwa hiyo nitachukua nafaka yake wakati wa mavuno, na divai yangu mpya katika msimu wake. Nitachukua sufu yangu na kitambaa kilichotumiwa kufunika uchi wake.
10Ndipo nitamvua nguo machoni pa wapenzi wake, wala hakuna mtu atakayemwokoa mkononi mwangu.
11Nitasitisha furaha yake yote- sikukuu zake, mwandamo wa mwezi, sabato zake na sikukuu zake zote zilizowekwa.
12Nitaharibu mizabibu yake na mtini wake, ambayo alisema, ‘Hii ni mishahara ambayo wapenzi wangu walinipa.’ Nitawafanya kuwa msitu, na wanyama wa shambani watakula.
13Nami nitamuadhibu kwa ajili ya Sikukuu ya Baali, alipowafukizia uvumba, akijipamba kwa pete zake na mavazi yake, naye akafuata wapenzi wake, akanisahau.” Hili ndilo tamko la Bwana.
14Kwa hiyo nitaenda kumshawishi. Nitamleta jangwani na kumwambia kwa huruma.
15Nami nitamrudishia mizabibu yake, na bonde la Akori kama mlango wa tumaini. Yeye atanijibu huko kama alivyofanya katika siku za ujana wake, kama katika siku ambazo alitoka katika nchi ya Misri.
16“Itakuwa katika siku hiyo”-hili ndilo tamko la Bwana-“kwamba utaniita, ‘Mume wangu,’ na hutaniita tena mimi, ‘Baali wangu.’
17Kwa maana nitaondoa majina ya Baali kinywani mwake; majina yao hayatakumbukwa tena.”
18“Siku hiyo nitafanya agano pamoja na wanyama katika mashamba kwa ajili yao, na ndege wa angani, na vitu vya kutambaa chini. Nitaondoa upinde, upanga, na vita katika nchi, nami nitakufanya ulale kwa usalama.
19Nitakuwa mume wako milele. Nitakuwa mume wako katika haki, hukumu, uaminifu wa agano, na huruma.
20Nitakuwa mume wako kwa uaminifu. Nawe utanijua mimi, Bwana.
21Na siku ile, nitajibu”-hili ndilo tamko la Bwana. “Nitazijibu mbingu, nao watajibu dunia.
22Dunia itashughulikia nafaka, divai mpya na mafuta, na watajibu Yezreeli.
23Nitampanda mwenyewe katika nchi kwa ajili yangu, na nitamhurumia Lo Ruhama. Nami nitamwambia Lo Ami, ‘Wewe ni Ami Ata,’ nao wataniambia, ‘Wewe ni Mungu wangu.’”

3

1Bwana akaniambia, “Nenda tena, mpendeni mwanamke, aliyependwa na mumewe; lakini ni mzinzi. Mpende kama mimi, Bwana, ninavyowapenda watu wa Israeli, ingawa wanaigeukia miungu mingine na kupenda mikate ya zabibu.”

2Kwa hiyo nimemnunua mwenyewe kwa vipande kumi na tano vya fedha na homeri na letheki ya shayiri.3Nilimwambia, “Lazima uishi pamoja nami siku nyingi. Huwezi kuwa kahaba au kuwa na mtu mwingine yeyote. Kwa njia hiyo hiyo, nitakuwa pamoja nanyi.”

4Kwa maana wana wa Israeli wataishi kwa siku nyingi bila mfalme, mtu mkuu, dhabihu, nguzo ya mawe, efodi au sanamu za nyumbani.5Baadaye watu wa Israeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Na katika siku za mwisho, watakuja wakitetemeka mbele za Bwana na wema wake.

4

1Sikilizeni neno la Bwana, enyi watu wa Israeli. Bwana ana mashtaka dhidi ya wenyeji wa nchi, kwa sababu hakuna ukweli au uaminifu wa agano, hakuna ujuzi wa Mungu katika nchi.

2Kuna laana, uongo, mauaji, wizi na uzinzi. Watu wamevunja mipaka yote, na damu inakuja baada ya damu.
3Kwa hiyo nchi inakauka, na kila mtu aliyeishi ndani yake anaangamia; wanyama katika mashamba na ndege angani, hata samaki katika bahari, wanaondolewa.
4Lakini usiruhusu mtu yeyote kuleta mashtaka; msiruhusu mtu yeyote ahukumu mtu mwingine. Kwa maana ninyi ndio makuhani, ninaowashtaki.
5Ninyi makuhani mtajikwaa wakati wa mchana; manabii pia watajikwaa pamoja nanyi usiku, nami nitamwangamiza mama yako.
6Watu wangu wanaharibiwa kwa sababu ya ukosefu wa maarifa. Kwa sababu makuhani wamekataa maarifa, nami nitawakataa msiwe makuhani kwangu. Kwa sababu umesahau sheria yangu, ingawa mimi ni Mungu wako, nami pia nitasahau watoto wako.
7Makuhani wengi waliongezeka, zaidi walifanya dhambi dhidi yangu. Walibadilisha heshima zao kwa aibu.
8Wanajilisha dhambi ya watu wangu; wao ni wenye tamaa zaidi ya uovu wao.
9Itakuwa sawa kwa watu kama kwa makuhani: nitawaadhibu wote kwa matendo yao; Nitawalipa kwa matendo yao.
10Watakula lakini hawatashiba; watafanya uzinzi lakini hawataongezeka, kwa sababu wamekwenda mbali na Bwana.
11Wanapenda uasherati, divai, na divai mpya, ambayo imechukua ufahamu wao.
12Watu wangu hutaka shauri kwa sanamu zao za mbao, na fimbo zao za kutembelea huwapa unabii. Kwa maana mawazo ya uasherati yamewadanganya, na wamefanya kama makahaba badala ya kuwa waminifu kwa Mungu wao.
13Wanatoa sadaka juu ya milima na kuteketeza uvumba kwenye milima, chini ya mialoni, milibua na miela, kwa sababu kivuli ni kizuri. Basi binti zenu hufanya uasherati, na binti zenu wanazini.
14Mimi siwaadhibu binti zako wakati wanachagua kutenda uasherati, wala binti zako wakati wazini. Kwa maana wanaume pia wanajitoa kwa makahaba, na hutoa dhabihu ili waweze kufanya vitendo vya uasherati na makahaba. Hivyo watu wasiofahamu wataangamizwa.
15Ingawa wewe, Israeli, umefanya uzinzi, lakini Yuda asiwe na hatia. Ninyi msiende Gilgali; msiende hadi Beth Aveni. Wala msiape, “Aishivyo Bwana.”
16Kwa maana Israeli amefanya ukaidi, kama ndama mkaidi. Je! Bwana anaweza kuwaleta kwenye malisho kama kondoo mahali penye nafasi?
17Efraimu alijiunga na sanamu; mwache peke yake.
18Hata wakati kileo chao kimeondoka wakaendelea kufanya uzinzi; watawala wake hupenda sana aibu yao.19Upepo utamfunga kwa mabawa yake; nao wataona aibu kwa sababu ya dhabihu zao.

5

1Sikilizeni haya, makuhani! Kuweni makini, nyumba ya Israeli! Sikilizeni, nyumba ya mfalme! Kwa maana hukumu itakuja juu yenu nyote. Mmekuwa mtego huko Mizpa na wavu uliosambazwa juu ya Tabori.2Waasi husimama sana katika mauaji, lakini nitawaadhibu wote.

3Najua Efraimu, na Israeli hajajificha kwangu. Efraimu, sasa umekuwa kama kahaba; Israeli ni unajisi.
4Matendo yao hayatawaruhusu kumgeukia Mungu, maana mawazo ya uzinzi yako ndani yao, na hawatamjua Bwana.
5Kiburi cha Israeli kinawashuhudia; Kwa hiyo Israeli na Efraimu watajikwaa kwa hatia zao; na Yuda pia wataanguka pamoja nao.
6Watakwenda pamoja na kondoo zao na ng'ombe zao kumtafuta Bwana, lakini hawatamuona, kwa kuwa amejiondoa kutoka kwao.
7Walikuwa wasio waaminifu kwa Bwana, kwa kuwa wamezaa watoto haramu. Sasa sherehe mpya za mwezi zitawaangamiza na mashamba yao.
8Piga tarumbeta huko Gibea, na tarumbeta huko Rama. Sauti ya kilio cha vita huko Beth Aveni ‘Tutakufuata, Benyamini!’
9Efraimu itakuwa ukiwa siku ya adhabu. Miongoni mwa makabila ya Israeli nimetangaza habari itakayotokea.
10Viongozi wa Yuda ni kama wale waondoao jiwe la mipaka. Nami nitamwaga ghadhabu yangu juu yao kama maji.
11Efraimu ameangamizwa; ameangamizwa kwa hukumu, kwa sababu ametembea kwa hiari kufuata sanamu.
12Kwa hiyo nitakuwa kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa nyumba ya Yuda.
13Efraimu alipoona ugonjwa wake, Yuda akaona jeraha lake; Efraimu akaenda Ashuru; Yuda akatuma wajumbe kwa mfalme mkuu. Lakini hakuweza kuwaponya watu au kuponya jeraha lako.
14Kwa hiyo nitakuwa kama simba kwa Efraimu, na kama simba kwa nyumba ya Yuda. Mimi, naam mimi, nitapotea na kwenda mbali; Nitawachukua, na hakutakuwa na mtu wa kuwaokoa.
15Nitakwenda na kurudi mahali pangu, mpaka watambue hatia yao na kutafuta uso wangu, hata wakanitafute kwa bidii katika dhiki yao.

6

1“Njooni, turudi kwa Bwana. Kwa maana ametuvunja vipande vipande, lakini atatuponya; ametujeruhi, lakini atatufunga majeraha yetu.

2Baada ya siku mbili atatufufua; siku ya tatu atatuinua, na tutaishi mbele yake.
3Nasi tumjue Bwana; tukaendelee kumjua Bwana. Kuja kwake ni hakika kama asubuhi; atakuja kwetu kama mvua, kama mvua ya vuli ambayo huinyeshea ardhi.”
4Efraimu, nikufanyie nini? Yuda, nikufanyie nini? Uaminifu wako ni kama wingu la asubuhi, kama umande unaoondoka mapema.
5Kwa hiyo nimewavunja vipande vipande kwa vinywa vya manabii, nimewaua kwa maneno ya kinywa changu. Maagizo yako ni kama nuru inayoangaza.
6Kwa maana natamani uaminifu wala si dhabihu, na kumjua Mungu kuliko sadaka za kuteketezwa.
7Kama Adamu, wamevunja agano; hawakuwa waaminifu kwangu.
8Gileadi ni jiji la wahalifu wenye miguu ya damu.
9Kama makundi ya wanyang'anyi wanaomngojea mtu, hivyo makuhani hujiunga pamoja kufanya mauaji kwa njia ya Shekemu; wamefanya uhalifu wa aibu.
10Katika nyumba ya Israeli nimeona jambo baya; Uzinzi wa Efraimu uko pale, na Israeli ametiwa unajisi.
11Kwa maana wewe, Yuda, mavuno yameteuliwa, nitakaporudisha urithi wa watu wangu.

7

1Wakati wowote ninapotaka kuponya Israeli, dhambi ya Efraimu inafunuliwa, pamoja na matendo maovu ya Samaria, kwa sababu wanafanya udanganyifu; mwizi huingia, na kundi la wanyang'anyi hushambulia mitaani.

2Hawatambui mioyoni mwao kwamba ninakumbuka matendo yao mabaya. Sasa matendo yao huwazunguka; yapo mbele ya uso wangu.
3Kwa sababu ya uovu wao wamemfanya mfalme awe na furaha, na maofisa wao kwa uongo wao.
4Wote ni wazinzi, kama tanuru iliyochomwa na mwokaji, ambaye huacha kuuchochea moto tangu kukanda unga mpaka kuwa chachu.
5Siku ya mfalme wetu, viongozi walijifanya wagonjwa na ukali wa divai. Alinyoosha mkono wake kwa wale waliokuwa wakidhihaki.
6Kwa mioyo kama tanuri, wao hupanga mipango yao ya udanganyifu. Hasira zao hulala usiku wote; asubuhi huwaka juu kama moto.
7Wote wamepata moto kama tanuru, na huwaangamiza wale wanaowatawala. Wafalme wao wote wameanguka; hakuna hata mmoja wao ananiita.
8Efraimu anajichanganya mwenyewe kati ya watu. Efraimu ni mkate ambao haujawahi kugeuzwa.
9Wageni wamekula nguvu zake, lakini hajui. Nywele za mvi hunyunyiza juu yake, lakini hajui.
10Kiburi cha Israeli kinawashuhudia; hata hivyo, hawajarudi kwa Bwana, Mungu wao, wala hawakumtafuta licha ya hayo yote.
11Efraimu ni kama njiwa, baradhuli na asiye na busara, humwita kwenda Misri, kisha huruka kwenda Ashuru.
12Wakienda, nitasambaza wavu wangu juu yao, nami nitawaangusha kama ndege wa angani. Nitawaadhibu katika kusonga kwao pamoja.
13Ole wao! Kwa maana wamepotea kutoka kwangu. Uharibifu unawajia! Wao wameasi dhidi yangu! Napenda kuwaokoa, lakini waliongea uongo dhidi yangu.
14Wala hawakunililia kwa moyo wao wote, lakini wanaomboleza kwenye vitanda vyao. Wanakusanyika kwa ajili ya nafaka na divai mpya, nao wananiasi mimi.
15Ingawa niliwafundisha na kuimarisha mikono yao, sasa wanapanga mabaya dhidi yangu.
16Wanarudi, lakini hawarudi kwangu, Niliye Juu. Wao ni kama upinde usiotumainika. Maofisa wao wataanguka kwa upanga kwa sababu ya udhalimu wa vinywa. Hii itakuwa ni aibu yao katika nchi ya Misri.

8

1“Weka tarumbeta katika midomo yako! Tai anakuja juu ya nyumba ya Bwana kwa sababu watu wamevunja agano langu na waliasi dhidi ya sheria yangu.

2Wananililia, ‘Mungu wangu, sisi katika Israeli tunakujua.’
3Lakini Israeli amekataa mema, na adui atamfuata.
4Wameweka wafalme, lakini sio kwa shauri langu. Wamewafanya wakuu, lakini sikuwa na habari. Kwa fedha zao na dhahabu wamejifanyia sanamu wenyewe, ili wakatiliwe mbali.”
5“Ndama wako amekataliwa, Samaria. Hasira yangu inawaka juu ya watu hawa. Kwa muda gani watakuwa na hatia?
6Kwa maana sanamu hii ilitoka Israeli; fundi aliifanya; si Mungu! Ndama ya Samaria itavunjwa vipande vipande.
7Kwa maana watu hupanda upepo na kuvuna kimbunga. Mbegu zilizosimama hazina vichwa; haitoi unga. Ikiwa itakomaa, wageni watakula.
8Israeli imemezwa; sasa wanalala kati ya mataifa kama kitu kisicho na maana.
9Kwa maana walikwenda Ashuru kama punda wa mwitu pekee. Efraimu ameajiri wapenzi kwa ajili yake mwenyewe.
10Hata ingawa wameajiri wapenzi kati ya mataifa, sasa nitawakusanya pamoja. Wao wataanza kupotea kwa sababu ya unyanyasaji wa mfalme wa wakuu.
11Kwa maana Efraimu ameongeza madhabahu kwa sadaka za dhambi, lakini zimekuwa madhabahu kwa kufanya dhambi.
12Niliweza kuandika sheria yangu kwao mara elfu kumi, lakini wangeiona kama kitu cha ajabu kwao.
13Kwa ajili ya dhabihu za sadaka zangu, hutoa nyama na kuila, lakini mimi, Bwana, siwakubali. Sasa nitafikiri juu ya uovu wao na kuadhibu dhambi zao. Watarudi Misri.
14Israeli imenisahau mimi, Muumba wake, na amejenga majumba. Yuda imeimarisha miji mingi, lakini nitatuma moto juu ya miji yake; itaharibu ngome zake.

9

1Usifurahi, Israeli, kwa furaha kama watu wengine. Kwa maana haukuwa mwaminifu, umemuacha Mungu wako. Unapenda kulipa mshahara kwa kahaba kwenye sakafu zote za nafaka.

2Lakini sakafu na divai hazitawalisha; divai mpya itampungukia.
3Hawawezi kuendelea kuishi katika nchi ya Bwana; badala yake, Efraimu atarudi Misri, na siku moja watakula chakula kichafu katika Ashuru.
4Hawatamtolea Bwana sadaka za divai, wala hawatamfurahisha. Dhabihu zao zitakuwa kwao kama chakula cha matanga wote wanaolila watakuwa wamejisikia. Maana chakula chao kitakuwa chao pekee; hakitaingia nyumbani mwa Bwana.
5Utafanya nini siku ya sikukuu iliyowekwa rasmi, siku ya sikukuu ya Yahweh?
6Kwa maana, angalia, wamekimbia uharibifu, Misri itawakusanya, na Nofu itawazika. Maana hazina zao za pesa za fedha zitakuwa nao, na miiba itajaza hema zao.
7Siku za adhabu zinakuja; siku za kulipiza kisasi zinakuja. Waisraeli wote wajue mambo haya. Nabii ni mpumbavu, na mtu aliyevuviwa ni mwendawazimu, kwa sababu ya uovu wako mkubwa na uadui mkubwa.
8Nabii ndiye mlinzi wa Mungu wangu juu ya Efraimu. Lakini mtego wa ndege ni juu ya njia zake zote, na uadui umo katika nyumba ya Mungu wake.
9Wamejiharibu wenyewe kama siku za Gibea. Mungu atawakumbusha uovu wao, naye atawaadhibu dhambi zao.
10Bwana asema, “Nilipoikuta Israeli, ilikuwa kama kutafuta zabibu jangwani. Kama matunda ya kwanza ya msimu kwenye mtini, nimewaona baba zenu. Lakini wakaenda Baal Peori, nao wakajitoa kwenye sanamu ya aibu. Walikuwa chukizo kama sanamu waliyoipenda.
11Na kwa ajili ya Efraimu, utukufu wao utatoka kama ndege. Hakutakuwa na kuzaa, hakuna mimba, wala achukuaye mimba.
12Ingawa wameleta watoto, nitawachukua ili asibaki hata mmoja. Ole wao nikiwaacha!
13Nimeiona Efraimu, kama vile Tiro, alipandwa katika mlima, lakini Efraimu atatoa watoto wake kwa mtu atakayewaua.
14Wape, Bwana-utawapa nini? Wape tumbo lenye kuharibu mimba na matiti ambayo hayatoi maziwa.
15‘Kwa sababu ya uovu wao wote huko Gilgali, ndivyo nilipowachukia. Kwa sababu ya matendo yao ya dhambi, nitawafukuza nje ya nyumba yangu. Sitawapenda tena; maofisa wao wote ni waasi.
16Efraimu ni mgonjwa, na mizizi yao imekauka; hawazai matunda. Hata ikiwa wana watoto, nitawaua watoto wao wapendwa.
17Mungu wangu atawakataa kwa sababu hawakumtii. Watakuwa watu wa kutangatanga kati ya mataifa.

10

1Israeli ni mzabibu mzuri ambao huzaa matunda yake; kwa kadiri matunda yake yanavyoongezeka vivyo hivyo anajenga madhabahu nyingi. Kwa kuwa nchi yake ilizalishwa zaidi, aliboresha nguzo zake.

2Moyo wao ni udanganyifu; sasa wanapaswa kubeba hatia yao. Bwana ataharibu madhabahu zao; ataharibu nguzo zao.
3Kwa maana watasema, “Hatuna mfalme, kwa maana hatukumcha Bwana. Na mfalme-angeweza kutufanyia nini?”
4Wanasema maneno tupu na kufanya maagano kwa kuapa uongo. Kwa hivyo haki inakuja kama magugu yenye sumu katika mito ya shamba.
5Wakazi wa Samaria wataogopa kwa sababu ya ndama za Beth Aveni. Watu wake waliomboleza juu yao, kama walivyofanya wale makuhani wa sanamu ambao walikuwa wamefurahi juu yao na utukufu wao, lakini hawako tena.
6Wao watachukuliwa kwenda Ashuru kama sadaka kwa mfalme mkuu. Efraimu atakuwa na aibu, na Israeli itakuwa na aibu kwa sanamu yake.
7Mfalme wa Samaria ataangamizwa, kama chipu cha kuni juu ya uso wa maji.
8Sehemu za juu za uovu zitaharibiwa. Hii ndiyo dhambi ya Israeli! Miti na vichaka vitakua juu ya madhabahu zao. Watu wataiambia milima, “Tufunike sisi!” na kwa vilima, “Tuangukieni!”
9Ee Israeli, umetenda dhambi tangu siku za Gibea; huko umebaki. Je, vita vitawapata wana wa uovu huko Gibea?
10Nitakapotaka, nitawaadhibu. Mataifa wataungana pamoja nao na kuwaweka katika vifungo kwa uovu wao mara mbili.
11Efraimu ni ndama mwenye mafunzo ambaye anapenda kupura nafaka, hivyo nitaweka jozi juu ya shingo yake nzuri. Efraimu nitauweka jozi; Yuda ataimea; Yakobo atauvuta pigo kwa nafsi yake.
12Jifanyieni haki, vuneni matunda ya uaminifu wa agano. Chimbueni ardhi yenu isiyopandwa, kwa maana ni wakati wa kumtafuta Bwana, mpaka atakapokuja na kuinua haki juu yenu.
13Mmelima uovu; mmevuna udhalimu. Mmekula matunda ya udanganyifu kwa sababu uliamini katika mipango yako na katika askari wako wengi.
14Kwa hiyo mlipuko wa vita utafufuka kati ya watu wako, na miji yako yote yenye ngome itaharibiwa. Itakuwa kama Shalmani aliharibu Beth Arbeli siku ya vita, wakati mama alivunjika vipande vipande na watoto wake.
15Kwa hiyo itakuwa kwako, Betheli, kwa sababu ya uovu wako mkubwa. Wakati wa mchana mfalme wa Israeli atakatwa kabisa.

11

1“Wakati Israeli alikuwa kijana nilimpenda, na nikamwita mtoto wangu kutoka Misri.

2Kwa kadiri waliyoitwa, ndivyo walivyoondoka kwangu. Wakawafanyia dhabihu Baali, wakatafuta uvumba kwa sanamu.
3Lakini mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea. Ndiye niliyewainua kwa silaha zao, lakini hawakujua kwamba niliwajali.
4Niliwaongoza kwa kamba za ubinadamu, na mafungo ya upendo. Mimi nilikuwa kama mtu aliyepunguza jozi juu ya taya zao, na nikainama na kuwalisha.
5Je, hawatarudi nchi ya Misri? Je, Ashuru haitatawala juu yao kwa sababu wanakataa kurudi kwangu?
6Upanga utaanguka juu ya miji yao na kuharibu makomeo ya milango yao; itawaangamiza kwa sababu ya mipango yao wenyewe.
7Watu wangu wameamua kuniacha. Ingawa wanaita kwa Aliye Juu, hakuna mtu atawasaidia.
8Ninawezaje kukuacha, Efraimu? Ninawezaje kukupeleka, Israeli? Ninawezaje kukufanya kama Adma? Ninawezaje kukufanya kama Seboimu? Moyo wangu umebadilika ndani yangu; huruma zangu zote zimeongezeka.
9Sitafanya hasira yangu kali; Mimi sitawaangamiza Efraimu tena. Kwa maana mimi ni Mungu, wala si mtu; Mimi ni Mtakatifu kati yenu, nami sitakuja katika ghadhabu.
10Watanifuata, Bwana. Nitanguruma kama simba. Nami nitaomboleza, na watu watakuja wakitetemeka kutoka magharibi.
11Watakuja wakitetemeka kama ndege kutoka Misri, kama njiwa kutoka nchi ya Ashuru. Nitawafanya wapate kuishi katika nyumba zao.” Hii ndiyo tamko la Bwana.
12Efraimu ananizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu. Lakini Yuda bado anaendelea nami, Mungu, na ni mwaminifu kwangu, Mtakatifu.

12

1Efraimu hujilisha upepo na kufuata upepo wa mashariki. Yeye daima huzidisha uongo na unyanyasaji. Wanafanya agano na Ashuru na huchukua mafuta ya Misri.

2Bwana pia ana mashtaka dhidi ya Yuda na ataadhibu Yakobo kwa yale aliyoyatenda; atamlipa kwa matendo yake.
3Katika tumbo Yakobo akamshika ndugu yake kisigino, na katika ubinadamu wake alijitahidi kwa Mungu.
4Alishindana na malaika akashinda. Alilia na kuomba kwa neema yake. Alikutana na Mungu huko Betheli; huko Mungu aliongea naye.
5Huyu ndiye Bwana, Mungu wa majeshi; “Yahweh” ndilo jina lake.
6Basi tembea na mungu wako. Shika uaminifu na uhuru wa agano, na umsubiri Mungu wako daima.
7Wafanyabiashara wana mizani ya uongo mikononi mwao; wanapenda kudanganya.
8Efraimu akasema, “Kwa hakika mimi ni tajiri sana; Nimepata utajiri kwa nafsi yangu. Katika kazi yangu yote hawataona uovu wowote ndani yangu, chochote ambacho kitakuwa dhambi.”
9Mimi ndimi Bwana, Mungu wako, tangu ulipotoka nchi ya Misri. Nitakufanya uishi tena katika hema, kama siku za karamu iliyowekwa.
10Niliwaambia manabii, na nimewapa maono mengi kwa ajili yenu. Kwa mkono wa manabii nilitoa mifano.
11Ikiwa kuna uovu huko Gileadi, hakika watu hawafai. Gilgali wanachinja ng'ombe; madhabahu zao zitakuwa kama miundo ya jiwe katika miamba ya mashamba.
12Yakobo akakimbia mpaka nchi ya Aramu; Israeli alifanya kazi ili kupata mke; naye akachunga kundi la kondoo ili kupata mke.
13Bwana akawaleta Israeli kutoka Misri kwa kutumia nabii, naye akawatunza kwa nabii.
14Efraimu amemkasirisha sana Bwana. Basi Bwana wake ataachia damu yake, naye atamrudishia aibu yake.

13

1Efraimu alipozungumza, kulikuwa na tetemeko. Alijikuza katika Israeli, lakini akawa na hatia kwa sababu ya ibada ya Baali, naye akafa.

2Sasa wanafanya dhambi zaidi na zaidi. Wanatengeneza sanamu za chuma kutoka kwenye fedha zao, sanamu kwa kadiri ya ufanisi wao, zote ni kazi ya mafundi. Watu wanasema juu yao, ‘Watu hawa watoao dhabihu na kumbusu ndama.’
3Kwa hiyo watakuwa kama mawingu ya asubuhi, kama umande unaoondoka mapema, kama makapi yanayotokana na upepo kutoka kwenye sakafu, na kama moshi utokao kwenye bomba.
4Lakini mimi ndimi Bwana, Mungu wako, tangu nchi ya Misri. Hutamjua Mungu mwingine bali mimi; wala zaidi yangu, hakuna mkombozi mwingine.
5Nilikujua jangwani, katika nchi yenye kame.
6Wakati ulipokuwa na malisho, ulishiba; na wakati uliposhiba, moyo wako ukainuliwa. Kwa sababu hiyo umenisahau.
7Nitakuwa kama simba; kama chui nitaangalia kando ya njia.
8Nitawaangamiza kama dubu aliyenyang'anywa watoto wake. Nami nitararua vifua vyao, na huko nitawaangamiza kama simba, kama vile mnyama wa mwitu atakayerarua vipande vipande.
9Nitawaangamiza, Israeli; nani atakayekusaidia?
10Mfalme wako yuko wapi, ili akuokoe katika miji yako yote? Wako wapi wakuu, ambao kwao umeniambia hivi, ‘Nipe mfalme na wakuu’?
11Nimekupa mfalme kwa hasira yangu, nikamchukua kwa ghadhabu yangu.
12Uovu wa Efraimu umehifadhiwa; hatia yake imehifadhiwa.
13Atakuwa na uchungu wa kujifungua, lakini ni mwana mjinga, kwa maana wakati wa kuzaliwa, hatatoka tumboni.
14Je, nitawaokoa na mkono wa kaburi? Je, nitawaokoa na kifo? Ewe Mauti yako wapi mapigo yako? Ewe kaburi kuko wapi kuharibu kwako? Huruma itafichwa na macho yangu.
15Ingawa Efraimu anafanikiwa kati ya ndugu zake, upepo wa mashariki utakuja; upepo wa Bwana utapiga kutoka jangwani. Kijito cha maji cha Efraimu kitakauka, na kisima chake hakitakuwa na maji. Adui yake atapora ghala lake la kila kitu cha thamani.
16Samaria itakuwa na hatia, kwa sababu amemuasi dhidi ya Mungu wake. Wataanguka kwa upanga; watoto wao wadogo watavunjwa, na wanawake wao wajawazito watatambuliwa wazi.

14

1Israeli, rudi kwa Bwana, Mungu wako, kwa kuwa umeanguka kwa sababu ya uovu wako.

2Chukueni maneno pamoja nanyi na mrudieni Yahweh. Mwambieni, “Ondoa uovu wetu wote, uyakubali mema, ili tuweze kukupa matunda ya midomo yetu.
3Ashuru haitatuokoa; hatutapanda farasi kwenda vitani. Hatuwezi tena kuiambia kazi ya mikono yetu, ‘ninyi ni miungu yetu,’ kwa maana kwako mtu asiye na baba hupata huruma.”
4‘Nitawaponya kugeuka kwao; Nami nitawapenda kwa moyo, kwa maana hasira yangu itaondoka kwake.
5Nitakuwa kama umande kwa Israeli; atachanua kama maua na kuchukua mizizi kama mwerezi nchini Lebanoni.
6Matawi yake yataenea; Uzuri wake utakuwa kama mizeituni, na harufu yake kama mierezi ya Lebanoni.
7Watu wanaoishi katika kivuli chake watarejea; watafufuliwa kama nafaka na maua kama mizabibu. Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni.
8Efraimu, nifanye nini tena na sanamu? Mimi nitamjibu na kumtunza. Mimi ni kama mberoshi majani yake ni ya kijani daima; kutoka kwangu huja matunda yako.”
9Nani mwenye busara ili aelewe mambo haya? Nani anaelewa mambo haya ili ayatambue? Kwa kuwa njia za Bwana ni sawa, na wenye haki watatembea ndani yao, lakini waasi wataanguka ndani yake.

Joeli

1

1Neno la Bwana lililomjia Yoeli mwana wa Pethueli.

2Sikieni haya, ninyi wazee, tegeni masikio, ninyi wenyeji wote wa nchi. Je! Jambo kama hili limetokea katika siku zenu, au hata katika siku za baba zenu?
3Waambieni watoto habari hii, na watoto wenu wawaambie watoto wao, na watoto kuwaambia wao kizazi kingine.
4Yale yaliyosazwa na tunutu yameliwa na nzige wakubwa; yale yaliyosazwa na nzige, panzi wameyala; na yaliyosazwa na panzi yameliwa na madumadu
5Amkeni, enyi walevi, lieni! Omboleza, ninyi nyote mnywao divai, kwa sababu divai nzuri imekatwa kutoka kwenu.
6Kwa maana taifa limekuja juu ya nchi yangu, lenye nguvu, lisilo na hesabu; Meno yake ni meno ya simba, Na ng'ambo za simba mkali.
7Ameharibu mzabibu wangu, ameharibu mtini wangu; Ameivua na kuitupa mbali; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
8Omboleza kama bikira aliyevaa magunia kwa kifo cha mumewe mdogo.
9Sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimekatiliwa mbali na nyumba ya Bwana. Makuhani, watumishi wa Bwana, huomboleza.
10Shamba limeharibika, na nchi inaomboleza; Kwa maana nafaka imeharibika, divai mpya imekauka, na mafuta yamepungua.
11Oneni aibu, enyi wakulima, pigeni yowe, enyi watunza mzabibu, kwa ajili ya ngano na shayiri. Kwa sababu mavuno ya shambani yameharibika.
12Mzabibu umekauka na mitini umenyauka; miti ya mkomamanga, pia mitende, na miti ya epo - miti yote ya shambani imenyauka. Hakika furaha imekauka kwa kwa wanadamu.
13Jifungeni viuno, mkaomboleze, enyi makuhani! Pigeni yowe, enyi watumishi wa madhabahu. Njoni, mlale usiku wote mlale katika magunia, enyi watumishi wa Mungu wangu. Maana sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiliwa nyumbani mwa Mungu wenu.
14Takaseni saumu, iteni kusanyiko takatifu. Wakusanyeni wazee na wenyeji wote wa nchi wafike nyumbani kwa Bwana Mungu wenu, mkamlilie Bwana.
15Ole kwa siku Kwa maana siku ya Bwana imekaribia. Nayo itakuja kama uharibifu kutoka kwa Mwenyezi.
16Je, chakula hakikukatiliwa mbali mbele ya macho yetu, na furaha na kicheko kutoka nyumbani mwa Mungu wetu?
17Mbegu zinaoza chini ya udongo wake, ghala zimekuwa ukiwa, na mabanda yamevunjika, kwa maana nafaka imekauka.
18Jinsi wanyama wanavyougua! Makundi ya Ng'ombe wanateseka kwa sababu hawana malisho. Pia, makundi ya kondoo yanateseka.
19Bwana, nakulilia wewe. Kwa maana moto umekula malisho ya jangwani, na moto umeteketeza miti yote ya mashamba.
20Hata wanyama wa kondeni wanakulilia, kwa maana mito ya maji imekauka, na moto umeteketeza malisho ya jangwani.

2

1Piga tarumbeta katika Sayuni, na piga kelele juu ya mlima wangu mtakatifu! Wakazi wote wa nchi watetemeke kwa hofu; maana siku ya Bwana inakuja; Hakika iko karibu.

2Ni siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza nene. Kama asubuhi inayoenea kwenye milima, jeshi kubwa na la nguvu linakaribia. Hakujawahi kuwako jeshi kama hilo, na hakutakuwa tena, hata baada ya vizazi vingi.
3Moto unakula mbele yako, na nyuma yao miali ya moto inawaka. Nayo nchi hiyo ni kama bustani ya Edeni mbele yao, lakini nyuma yao kuna jangwa tupu Hakika hakuna chochote kitakachowaepuka
4Kuonekana kwao ni kama kuonekana kwa farasi; Na kama farasi wepesi, ndivyo wanavyokimbiaa.
5Kwa kelele kama magari ya vita huruka juu ya vilele vya milima, Kama sauti ya mwali wa moto utekekezao mabua makavu, Kama jeshi la nguvu lililo tayari kwa vita.
6Mbele yao watu wanahangaika katika uchungu na nyuso zao zimegeuka kua nyeupe kwa hofu.
7Wanakimbia kama wapiganaji wenye nguvu; wanapanda kuta kama askari; wanasonga, kila mmoja kwa hatua, na hawavunji safu zao.
8Wala hakuna mmoja anayemsukuma mwingine kando; wanasonga, kila mmoja katika safu yake; hujifanyizia njia kwa nguvu kati ya silaha wala hawaachi kuifuata njia yao.
9Wanakimbilia jiji, wanakimbia kwenye ukuta, wanapanda ndani ya nyumba, na hupita kupitia madirisha kama wezi.
10Nchi hutikisika mbele yao, mbingu hutetemeka, jua na mwezi hutiwa giza, na nyota zinaacha kuangaza.
11Bwana huinua sauti yake mbele ya jeshi lake; maana wapiganaji wake ni wengi sana; kwa maana wao ni wenye nguvu, wale wanaofanya amri zake. Kwa maana siku ya Bwana ni kubwa na ya kutisha sana. Nani anayeweza kuiistahimili?

12“Lakini hata sasa,” asema Bwana, “Nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza.”
13Basi rarueni mioyo yenu, wala si mavazi yenu, Mruienina Mungu wenu. Kwa maana ni mwenye neema, amejaa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema; na Yeye hughairi kufanya ubaya.
14Nani anajuaye kwamba atageuka na kughairi, na kuacha baraka nyuma yake, sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji kwa Bwana, Mungu wenu?
15Pigeni tarumbeta katika Sayuni, Tkaseni saumu, iteni kusanyiko takatifu.
16Kusanyeni watu, litakaseni kusanyiko, Kusanyeni wazee, kusanyeni watoto na wanyonyao; Bwana arusi na atoke chumbani mwake, na bibi arusi katika hema yake.
17Basi makuhani, watumishi wa Bwana, na waliae kati ya patakatifu na madhabahu; na waseme “uwaachilie watu wako, Ee Bwana, wala usiutoe urithi wako upate aibu, ili mataifa watawale juu yao. Kwa nini waseme kusema kati ya mataifa, “Yuko wapi Mungu wao?” Ndipo Bwana atakuwa na wivu kwa ajili yanchi yake, na kuwahurumia watu wake.
18Ndipo Bwana atakuwa na wivu kwa ajili ya nchi yake, na kuwahurumia watu wake.

19Bwana atajibu na kuwaambia watu wake, Tazamani, nitawaletea nafaka, divai, na mafuta, nanyi mtashimba kwa vitu hivyo; ala sitawafanya kuwa aibu kati ya mataifa.
20Lakini jeshi lilotoka kazkazini nitaliondolea mbali nanyi nami nitalifukuza mpaka nchi ya ukame na ukiwa, uso wake ukielekea bahari ya mashariki, na mgongo wake kuelekea bahari ya magharibi; Uvundo wake utapanda juu, na harufu yake mbaya itapanda kwa sababu amefanya mambo ya kuchukiza sana.
21Ee nchi, usiogope, shangilieni na kufurahi, kwa kuwa Bwana amefanya mambo makuu.
22Msiogope enyi wanyama wa porini, kwa kuwa malisho yajangwani yanachipukana mti unazaa matunda yake, na mMtini na mzabibu hutoa nguvu zake.
23Furahini basi, enyi watu wa Sayuni, mkamfurahie Bwana, Mungu wenu. Kwa maana amewapa ninyi mvua ya masika kwa uaminifu, naye atawanyeshea mvu, mvua ya masika, na mvua ya vuli katika mwezi wa kwanza.
24Sakafu za kupepetea zitajaa ngano, na mashinikizo yatafurika kwa divai mpya na mafuta.
25“Nimi nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, Parare, na madumadu, na tunutu, - jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.
26Mtakula chakula tele na kushiba, na kulitukuza jina la Bwana, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawataaibishwa kamwe.
27Nanyi mtajua ya kwamba mimi niko kati ya Israeli, na kwamba mimi ni Bwana, Mungu wenu, wala hakuna mwingine. Watu wangu hawataaibishwa kamwe.
28Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina Roho yangu juu ya wote wenye mwili, na wana wenu na binti zenu watatabiri. Wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono.
29Tena juu ya watumishi wangu na wajakazi wangu nitamimina Roho yangu siku zile.
30Nami nitaonyesha maajabu mbinguni na duniani; damu, moto na nguzo za moshi.
31Jua litageuzwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja ile siku ya Bwana iliyo kuu na ya kutisha.
32Na itakuwa kwamba kila mtu anayeliitia jina la Bwana ataokolewa. Kwa maana juu ya Mlima Sayuni na Yerusalemu kutakuwapo wokovu, kama Bwana alivyosema; Miongoni mwa mabaki ambao Bwana atawaita.

3

1Tazama, katika siku hizo na wakati huo, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,

2Nami nitakusanya mataifa yote, na kuwaleta mpaka bonde la Yehoshafati. Nami nitawahukumu huko, kwa sababu ya watu wangu, na urithi wangu Israeli, ambao wamewatawanya kati ya mataifa, na kwa sababu wamegawanya nchi yangu.
3Wamewapigia kura watu wangu, wametoa mtoto wa kiume kama malipo ya kahaba, na kumuuza msichana kwa divai ili wapate kunywa.

4Hakika, mna nini nami, enyi Tiro, Sidoni na mikoa yote ya Wafilisti? Je! Mtanirudishia malipo? Hata kama mtanilipa, mara moja nitawarudishia malipo yenu juu ya vichwa vyenu wenyewe.5Kwa maana mmechukua fedha yangu na dhahabu yangu, nanyi mkavichukua hazina zangu za thamani na kuzileta katika hekalu zenu.6Mmewauza watu wa Yuda na wenyenji wa Yerusalemu kwa Wayunani, ili kuwaondoa mbali na maeneo yao.

7Tazama, nitawaamsha, watoke mahali ambako mliwauza, na nitawarudishia malipo juu ya vichwa vyenu wenyewe.8Nitawauza wana wenu na binti zenu, kwa mkono wa watu wa Yuda. Wao watawauza Sheba, kwa taifa mbali. Kwa maana Bwana amesema.
9Tangazeni haya kati ya mataifa, ‘Jitayarisheni wenyewe kwa ajili ya vita, waamsheni mashujaa, waacheni wakaribie, mashujaa wote wa vita wapande juu.
10Yafueni majembe yenu kuwa panga na visu vyenu vya kuchongea kuwa mikuki. Basi wadhaifu waseme, ‘Nina nguvu.’
11Haraka na mje, mataifa yote ya karibu, jikusanyeni pamoja huko. Ee Bwana, washushe mashujaa wako.
12Naam, mataifa yajihimize yenyewe kuja hadi bonde la Yehoshafati. Kwa maana nitaketi huko kuhukumu mataifa yote ya jirani.
13Wekamundu, kwa maana mavuno yameiva. Njoo, mponde zabibu, kwa ajiri shinikizo limejaa. Mashinikizo yanafurika, kwa sababu uovu wao ni mkubwa sana.
14Umati wa watu, makutano katika bonde la uamuzi! Kwa maana siku ya Bwana i karibu katika bonde la hukumu.
15Jua na mwezi vitatiwa giza, nyota zitapunguza mwanga wake.
16Bwana naye ataunguruma kutoka Sayuni, na atatoa sautiyake toka Yerusalemu. Mbingu na nchi zitatikisika; Bali BWANA atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli.
17Nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, ninayekaa katika Sayuni, mlima wangu mtakatifu. Ndipo Yerusalemu utakuwa mtakatifu, na hakuna mgeni atakayepita tena ndani yake kamwe.
18Na itakuwa Katika siku hiyo ya kwamba milima itadondosha divai mpya, vilima vitatiririka maziwa, na vijito vya Yuda vitafurika maji, na chemchemi itatoka katika nyumba ya BWANA na kumwagilia maji bonde la Shitimu.
19Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya udhalimu juu ya watu wa Yuda, kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao.
20Bali Yuda atakaa milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi.
21Maana nitawaondolea hatia ya umwagaji wa damu, ambao sikuwaondolea kuwa na hatia; kwa maana Bwana anakaa katika Sayuni.

Amosi

1

1Haya ni mambo yanayoihusu Israeli ambayo Amosi, mmoja wa wachungaji katika Tekoa, aliyapokea katika ufunuo. Alipokea haya mambo katika siku za Uzia mfalme wa Yuda, na pia katika siku za Yeroboamu mwana wa Yoashi mfalme wa Israeli, miaka miwili kabla ya tetemeko la aridhi.

2Alisema, “Yahwe atanguruma kutoka Sayuni; atainua sauti yake kutoka Yerusalemu. Malisho ya wachungaji yanaomboleza; Na kilele cha Karmeli kitanyauka.

3Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu ya Dameski, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wameipura Gileadi kwa vyombo vya chuma.
4Lakini nitapeleka moto kwenye nyumba ya Hazaeli, utakaoteketeza majumba ya Ben-Hadadi.
5Nitalivunja komeo la Dameski na kuwakatilia mbali wakaaji katika bonde la Aveni, na pia yule mtu ashikaye fimbo ya kifalme katika Beth-Edeni. Na watu wa shamu watakwenda utumwani hata Kiri,” asema Yahwe.

6Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Gaza, hata manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu waliwachukua mateka watu wote, kuwaweka juu ya mkono wa Edomu.
7Lakini nitatuma moto kwenye kuta za Gaza, na kuziteketeza majumba yake zake.
8Nami nitamkatilia mbali ya mwenyeji katika Ashdodi na mtu ashikaye fimbo ya kifalme kutoka Ashkeloni. Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni, na mabaki ya Wafilisti wataangamia,” asema Bwana Yahwe.

9Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Tiro, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu waliwapelekea watu wote kwa Edomu, na wamevunja agano lao la undugu.
10Nitapeleka moto kwenye kuta za Tiro, nao utaziteketeza ngome zake.”

11Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Kwa makosa matatu za Edomu, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu alimfuatilia ndugu yake kwa upanga na kutupilia mbali huruma zote. Hasira yake ikaendelea kuwa kali, na ghadhabu yake ikabaki milele.
12Nitapeleka moto juu ya Temani, na utaziteketeza nyumba za kifalme za Bozra.”

13Hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Kwa makosa matatu za watu wa Amoni, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake, kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili waweze kupanua mipaka yao.
14Nitawasha moto katika kuta za Raba, nao utaziteketeza nyumba za kifalme, pamoja na kupiga kelele katika siku ya vita, pamoja na dhoruba katika siku ya kimbunga.
15Mfalme wao ataenda utumwani, yeye na maafisa wake pamoja,” asema Yahwe.

2

1Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Moabu, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu amechoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hadi kuwa chokaa.

2Nitatuma moto juu ya Moabu, na utaangamiza majumba ya Keriothi. Moabu atakufa katika ghasia, pamoja na kelele na sauti ya tarumbeta.
3Nami nitamkatilia mbali mwamuzi kati yake, na nitawaua wakuu wake wote pamoja na yeye,” asema Yahwe.

4Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Yuda, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu wameikataa sheria ya Yahwe na hawakuzishika amri zake. Uongo wao umewapotosha, ambao baba zao pia waliufuata.
5Nitatuma moto juu ya Yuda, na utaimeza majumba ya Yerusalemu.”

6Hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Kwa makosa matatu za Israeli, hata kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate, kwa sababu wamewauza wasio na hatia kwa fedha na maskini kwa jozi moja ya viatu.
7Nao hupeperusha mavumbi ya nchi yaliyo kichwani mwa maskini, na kuipotosha njia ya wanyenyekevu. Mtu na baba yake wanalala na msichana mmoja na hivyo kulitia unajisi jina langu takatifu.
8Nao hulala chini karibu na kila madhabahu kwenye nguo zilizowekwa dhamana, na katika nyumba ya Mungu wao hunywa divai ya wale ambao walitozwa faini.
9Bado nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi; alikuwa na nguvu kama mialoni. Kisha nikaharibu matunda yake juu na mizizi yake chini.
10Pia, niliwapandisha kutoka nchi ya Misri na kuwaongoza miaka arobaini nyikani ili mmiliki nchi ya Wamori.
11Nimewainua manabii kutoka miongoni mwa watoto wenu wawe Wanadhiri kutoka vijana wenu. Je sio hivyo, watu wa Israeli? -Hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
12Lakini mmewashawishi Wanadhiri kunywa mvinyo na kuwaamuru manabii wasifanye unabii.
13Tazama, nitawakanyaga kama mkokoteni uliojaa miganda inayoweza kumkanyaga mtu.
14Mtu akimbiaye hatapata kimbilio; mwenye nguvu hataongeza nguvu zake mwenyewe; wala shujaa kujiokoa mwenyewe.
15Apindaye upinde hatasimama; mkimbiaji sana hatakimbia; mwendesha farasi hatajiokoa mwenyewe.
16Hata wapiganaji shujaa watakimbia uchi katika siku hiyo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.”

3

1Sikieni neno la Yahwe aliloongea juu yenu, enyi wana wa Israeli, juu ya familia nzima ambayo niliwatoa kutoka nchi ya Misri, nikisema,

2“Nimewachagua ninyi tu kutoka familia zote za dunia. Kwa hiyo nitawaadhibu kwa dhambi zenu zote.”
3Je wawili wanaweza kutembea pamoja isipokuwa wamekubaliana?
4Je, simba huunguruma msituni wakati hakuna mawindo? Je, mwana simba ataunguruma kutoka pangoni mwake kama hajakamata kitu?
5Je, ndege ataanguka kwenye mtego ardhini wakati hakuna chambo kimewekwa kwa ajili yake? Je, mtego utafyatuka juu ardhini wakati hakuna kitu cha kukamata?
6Je, tarumbeta itapigwa mjini na watu wasitetemeke? Je, janga laweza kuja mjini bila kuletwa na Yahwe?
7Hakika Bwana Yahwe hatafanya kitu isipokuwa awafunulie mpango watumishi wake manabii.
8Simba ameshaunguruma! Nani hataogopa? Bwana Yahwe amekwisha ongea; nani asiyeweza kutabiri?
9Tangazeni hii katika majumba ya Ashidodi, na katika majumba ya nchi ya Misri; mkaseme, “Kusanyikeni juu ya milima ya Samaria; tazama machafuko makubwa kati yake, na waliokandamizwa ndani yake.
10Kwa kuwa hawajui jinsi ya kufanya haki -asema Yahwe - hao wawekao akiba ya jeuri na unyang'anyi katika majumba yao.”

11Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, “Adui ataizunguka nchi pande zote. Ataziondoa nguvu zako kutoka kwako, na majumba yako yatatekwa nyara.”

12Hivi ndivyo Yahwe asemavyo,” Kama mchungaji aokoavyo katika kinywa cha simba miguu miwili tu au kipande cha sikio, ndivyo wana wa Israeli watakavyookolewa wale waishio katika Samaria, penye pembe ya kitanda. Kwenye ukingo wa kochi.”

13Sikieni na kushuhudia juu ya nyumba ya Yakobo -hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi,
14“Kwa kuwa katika siku ambayo nimeadhibu dhambi za Israeli, pia nitaziadhibu madhabahu za Betheli. Pembe za madhabahu zitakatwa na kuanguka chini.
15Nitaiharibu nyumba ya wakati baridi pamoja na nyumba ya wakati wa hari. Nyumba za pembe zitaangamia, na nyumba kubwa zitakuwa na mwisho,” - hivi ndivyo Yahwe asemavyo.

4

1Lisikilizeni neno hili, ninyi ng'ombe wa Bashani, ninyi mliomo katika mlima wa Samaria, ninyi mnaowakandamiza maskini, ninyi mnaowaponda wahitaji, ninyi mnaowaambia waume zenu, “Leteni divai tunywe.”

2Bwana Yahwe ameapa kwa utakatifu wake, “Tazama, siku zitakuja kwenu atakapowaondoa kwa ndoana, na wazao wenu kwa ndoana.
3Mtatoka kupitia mahali palipo bomolewa kwenye kuta za mji, kila mwanamke moja kwa moja mbele yake, nanyi mtatupwa katika Harmoni” -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
4“Nendeni Betheli na mtende uovu, hata Gilgali mkaongeza dhambi, leteni dhabihu zenu kila asubuhi, na zaka zenu kila baada ya siku tatu.
5Toeni dhabihu za shukurani ya kitu kilichotiwa chachue; mkatangaze sadaka mtoazo kwa hiari; na kuzihubiri habari zake kwa kuwa hii ndiyo iwapendezayo, ninyi watu wa Israeli -hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe.
6Niliwapeni usafi wa meno katika miji yenu yote, na kupungukiwa na mkate katika sehemu zenu zote. Lakini hamkunirudia mimi -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
7Pia nikaizuia mvua ilipokuwa imebaki miezi mitatu kabla ya mavuno. Nikaifanya inyeshe juu ya mji mmoja na kuifanya isinyeshe katika mji mwingine. Kipande kimoja cha nchi ilinyesha, lakini kipande kingine cha nchi ambapo haikunyesha palikuwa pakavu.
8Basi miji miwili mitatu ikatangatanga kwenda kwenda mji mwingine ili kunywa maji, lakini hawakutosheka. Bado hamkunirudia mimi -asema Yahwe.
9Nimewapiga kwa maradhi yanayosababisha kuvu. Wingi wa bustani na mashamba yenu ya mizabibu, na mitini yenu, na mizaituni yenu, na nzige iliwala. Bado hamkunirudia mimi, hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
10Nami nalituma kati yenu tauni kama tauni ya Misri. Nimewaua vijana wenu kwa upanga, farasi wenu nimewachukulia mbali; nami nimeupandisha uvundo wa kambi zenu nakuiingiza katika mianzi y pua zenu. Bado hamkunirudia mimi -hivi ndivyo asemavyo Yahwe.
11Naliwaangamiza baadhi yenu, kama wakati Mungu alipoiangamiza Sodoma na Gomora. Mlikuwa kama kijinga kilichonyakuliwa kutoka kwenye moto. Bado hamkunirudia mimi- asema Yahwe.
12Kwa hiyo nitafanya jambo baya kwako, Israeli; na kwa sababu nitafanya jambo baya kwako, jiandae kukutana na Mungu, Israeli!
13Kwa kuwa, tazama, yeye atengenezaye milima pia ndiye aumbaye upepo, humfunulia mawazo yake mwanadamu, hufanya asubuhi kuwa giza, na kupakanyaga mahala pa juu ya dunia. Yahwe, Mungu wa majeshi, ndilo jina lake.”

5

1Sikilizeni hili neno ambalo nisemalo kama maombelezo juu yenu, nyumba ya Israeli.

2Bikira wa Israeli ameanguka; hatainuka tena; ameachwa katika ardhi yake, hakuna mtu wa kumwinua.

3Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo: “Mji ule utokao nje kwa elfu watabaki watu mia, na mji utokao nje kwa mia watabaki watu kumi kwa nyumba ya Israeli.”

4Kwa kuwa hivi ndivyo Yahwe asemavyo kwa nyumba ya Israeli: “Nitafuteni na mtaishi!
5Bali msitafute Betheli; wala msiiingie Gilgali; wala msisafiri kwenda Berisheba. Kwa kuwa Gilgali hakika itachukuliwa mateka, na Betheli itakua ubatili.
6Mtafuteni Yahwe nanyi mtaishi, asinje akawaka kama moto kwenye nyumba ya Yusufu. Nao utateketeza, na hakutakuwa na mtu hata mmoja kuuzima katika Betheli-
7Ninyi manaogeuza haki kuwa uchungu na kuiangusha haki chini!”
8Alizifanya Kilimia na Orioni; Hugeuza uvuli wa mauti kuwa asubuhi; na kuufanya mchana kuwa giza kama usiku; na huyaita maji ya bahari na kuyamwaga juu ya uso wa nchi. Yahwe ndilo jina lake!
9Huwanyeshea wenye nguvu uharibifu wa ghafla hata uharibifu uje juu ya ngome.
10Wanamchukia yyeye akemeaye langoni, nao humchukia yeye anenaye kwa unyofu.
11Basi kwa kuwa mnamkanyaga maskini, na kumtoza ngano - injapokuwa mmejenga nyumba za mawe yaliyochongwa, hamtaishi kwenye nyumba hizo. Mmependezwa na mashamba ya mizabibu, lakini hamtakunywa divai yake.
12Kwa kuwa najua ni jinsi gani mlivyo na makosa mengi na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa- ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji kwenye langoni wasipate haki yao.
13Kwa hiyo kila mtu mwenye busara atanyamaza kimya kwenye wakati kama huo, kwa kuwa ni wakati wa uovu.
14Tafuteni mazuri na sio mabaya, ili kwamba mpate kuishi. Hivyo Yahwe, Mungu wa majeshi, atakuwa na ninyi, kama msemavyo.
15Chukieni mabaya, yapendeni mema; mkaithibitishe haki langoni. Huenda Yahwe, Mungu wa majeshi, atawafadhili mabaki ya Yusufu.

16Kwa hiyo, hivi ndivyo Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, Bwana, “Kutakuwa na maombolezo kwenye njia kuu zote, na watasema kwenye mitaa yote, ‘Ole! Ole!’ Watawaita wakulima kuomboleza na waombolezao stadi waomboleze.
17Katika mashamba yote ya mizabibu kutakuwa na kilio, kwa kuwa nitapita katikati yako,” asema Yahwe.
18Ole wenu ninyi mnaoitamani siku ya Yahwe! Kwa nini mnaitamani? Itakuwa giza na sio nuru,
19kama wakati mtu anamkimbia simba na kukutana na dubu, au aliingia katika nyumba na kuweka mkono wake kwenye ukuta na kung'atwa na nyoka.
20Je, siku ya Yahwe sia giza, wala si nuru? Je, si giza sana, na hakuna mwangaza ndani yake?
21“Nazichukia, nazidharau sikukuu zenu, wala siyapendezwi na makusanyiko yenu matakatifu.
22Hata kama mnanitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka za unga, sitazipokea, wala kuzitazama sadaka za amani na za wanyama walionona.
23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu; kwa maana sitaisikia sauti za vinanda vyenu.
24Badala yake, acheni hukumu itelwmke kama maji, na haki kama maji makuu.
25Je, mmeniletea dhabihu na sadaka za kuteketeza jangwani kwa mda wa miaka arobaini, enyi nyumba ya israeli?
26Tena mlimchukua li Sikuthi kama mfalme wenu, na Kiuni, sanamu zenu, nyota ya miungu yenu, mliyojifanyia wenyewe.
27Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni nje ya Dameski,” asema Yahwe, ambaye jina lake ni Mungu wa majeshi.

6

1Ole wenu ninyi mnaostarehe katika Sayuni, mnaotumainia mlima wa Samaria, watu mashuhuri katika taifa kuu, ambao nyumba ya Israeli huwaendea!

2“Vukeni hata Kalne, mkaone; na kutoka huko nendeni hadi Hamathi, mji mkuu; kisha shuka mpaka Gathi ya Wafilisti. Je! Weweni wabora kuliko falme hizi? Au je, eneo lao ni kubwa kuliko eneo lenu?”
3Ole wenu ninyi mnaoweka mbali siku ya adhabu, mnaoleta karibumakao ya jeuri.
4Ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe na kujinyoosha juu ya viti vyenu. Mnaokula wana kondoo kutoka kwenye kundi na ndama kutoka kwenye zizi.
5Ninyi mnaoimba nyimbo za kijinga pamoja na sauti ya vinanda; na kujifanyizia vinanda vya namna nyingi kama vile Daudi.
6Ninyi mnaokunywa divai katika mabakuli na kujipaka marahamu ilyo nzuri, lakini hawahuzuniki juu ya mateso ya Yusufu.
7Kwa hiyo sasa watachukuliwa mateka, kama wafungwa wa kwanza, na hao waketio katika karamu wataondolewa.

8“Mimi Bwana Yahwe, nimeapa kwa nafsi yangu -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo, Mungu wa majeshi, naizira fahari ya Yakobo; nachukia boma zake. Kwa hiyo nitautoa huo mji pamoja vyote vilivyomo humo.”

9Kisha itakuwa, watu kumi wakikaa katika nyumba moja, watakufa.10Na mtu wa jamaa ya wafu, pamoja na mtu atakayezichoma moto, atakapoichukua mizoga na kuitoa nje ya nyumba, atamwambia aliye ndani ya nyumba, “Je! Kuna zaidi na wewe?” Kisha mtu atasema, “Hapana” Naye atasema, nyamaza ulimi wako, kwa maana hatuthubutu kulitaja jina la Bwana.
11Tazama, Yahwe atatoa amri, na nyumba kubwa itapigwa kuwa vipande vipande, na nyumba ndogo kuwa na nyufa.
12Je, farasi watakimbia juu ya mteremko wa miamba? Je, mtu atalima huko na ng'ombe? Bado mmegeuza haki kuwa sumu na tunda la haki kuwa uchungu.
13Ninyi mnaofurahia Lo Debari, msemao, “Je! Hatukujitwalia Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
14“Lakini tazama, nitainua juu yenu taifa, enyi nyumba ya Israeli,” hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe, Mungu wa majeshi. “Watawatesa ninyi kuanzia maingilio ya Hamathi mpaka kijito cha Araba.”

7

1Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha. Tazama, aliumba kundi kubwa la nzige wakati wa kuchipuka kwa mmea, na, tazama, ulikuwa ni mmea wa mwisho baada ya mavuno ya mfalme.2Wakati walipomaliza kula mbogamboga za nchi, kisha nikasema, “Bwana Yahwe, tafadhali nisamehe; Je, Yakobo ataishije? Kwa kuwa yeye ni mdogo sana.”

3Yahwe akapunguza hasira kuhusu hili. “Haitatokea,” akasema.

4Hivi ndivyo ambavyo Bwana Yahwe alivyonionyesha: Tazama, Bwana Yahwe aliita juu ya moto kuhukumu. Nao ukakausha sana, kilindi chini ya dunia na kutaka kuitekeza nchi, pia.5Lakini nikasema, “Bwana Yahwe, acha tafadhali; Yakobo ataishije? Kwa kuwa yeye ni mdogo sana.”

6Yahwe akagairi kuhusiana na hili, “Hili halitajitokeza pia,” asema Bwana Yahwe.

7Hivi ndivyo ambavyo Yahwe alivyo nionyesha: Tazama, Bwana amesimama karibu na ukuta, pamoja na uzi wa timazi kwenye mkono wake.8Yahwe akanambia, “Amosi, unaona nini?” nikasema, “Uzi wa timazi.” Kisha Bwana akasema, “Tazama, nitaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli. Sitawapita tena.
9Mahala pa juu pa Isaka pataharibiwa, patakatifu pa Israeli pataangamia, na nitainuka juu ya nyumba ya Yeroboamu kwa upanga”

10Kisha Amazia, yule kuhani wa Betheli, akatuma ujumbe kwa Yeroboamu, mfalme wa Israeli: “Amosi amefanya njama dhidi yako katikati ya nyumba ya Israeli. Nchi haiwezi kubeba maneno yote haya.11Kwa kuwa hivi ndivyo asemavyo Amosi, ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga, na hakika Israeli itakwenda utumwani kutoka nchi yake.”

12Amazia akamwambia Amosi, “Mwonaji, nenda, kimbia irudie nchi ya Yuda, na hapo ule mkate na kutabiri.13Lakini usitabiri tena hapa katika Betheli, kwa kuwa ni patakatifu pa mfalme na nyumba ya kifalme.”

14Kisha Amosi akamwambia Amazia, “Mimi sio nabii wala mwana wa nabii. Mimi ni mchungaji wa mifugo, na mtunza mikuyu.15Lakini Yahwe akanichukua kutoka kuchunga mifugo na kunambia, ‘Nenda, katabiri kwa watu wangu Israeli.’
16Sasa sikia neno la Yahwe. Wewe usemaye, ‘Usitabiri juu ya Israeli, na usiongee juu ya nyumba ya Isaka.

17Kwa hiyo hivi ndivyo Yahwe asemavyo, ‘Mke wako atakuwa kahaba katika mji; wana wako waume na binti zako wataanguka kwa upanga; nchi yako itapimwa na kugawanywa; utakufia katika nchi najisi, na Israeli hakika itakwenda utumwani kutoka nchi yake.”’

8

1Hiki ndicho ambacho bwana Yahwe amenionyesha. Tazama, kikapu cha matunda ya hari!2Akasema, “Unaona nini, Amosi?” Nikasema, “Kikapu cha matunda ya hari.” Kisha Yahwe akaniambia, “Mwisho umefika kwa watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe.

3Nyimbo za kwenye hekalu zitakuwa vilio. Katika siku hiyo-hivi ndivyo asemavyo Bwana Yahwe. Mizoga itakuwa mingi, katika kila sehemu wataitupa katika ukimya!”
4Sikieni haya, ninyi mnaowameza wahitaji na kuwakomesha maskini.

5Wakisema, “Mwezi mpya utaondoka lini, hivyo tunaweza kuuza nafaka tena? Na Sabato, ili tufanye biashara yangano? Kuifanya efa kuwa ndogo, na shekeli kuwa kubwa, na kuipotosha mizani kwa hila.
6Hivi ndivyo ambavyo tunaweza kuuza ngano mbaya, kununua fukara kwa fedha, na masikini kwa jozi moja ya viatu.”

7Yahwe ameapa kwa fahari ya Yakobo, “Hakika sitasahau kamwe kazi zao hata moja.”
8Je, nchi haitatetemeka kwa ajili ya hayo, na kuomboleza kila mtu akaaye ndani yake? Yote hayo yatainuka kama Mto Naili, nayo itataabika juu na kupwa tena, kama mto wa Misri.

9“Itakuja siku ambayo -huu ndio usemi wa Bwana Yahwe- kwamba nitafanya jua litue wakati wa mchana, na nitaiweka giza dunia wakati wa mchana.
10Nitazigeuza sikukuu zenu kuwa maombolezo, na nyimbo zenu zote kuwa maombolezoo. Nitaleta nguo za magunia juu ya viuno vyote, na kila kichwa kitakua na kipara. Nitayafanya kuwa kama maombolezo yamwana wa pekee, na mwisho wake kama siku ya uchungu.
11Tazama, siku zinakuja -asema Bwana Yahwe- wakati nitakapoleta njaa katika nchi, sio njaa ya mkate, wala kiu ya maji, bali ya kuyasikia maneno ya Yahwe.
12Nao watatangatanga toka bahari hata bahari; toka upande wa kaskazini hata mashariki; wataenda mbio huko na huko, wakilitafuta neno la Yahwe, lakini hawataliona.

13Katika siku hiyo wanawali wazuri na wavulana watazimia kutokana na kiu.
14Wale waapao kwa dhambi ya Samaria na kusema, “kama aishivyo Mungu wako, Ee Dani, na kama iishivyo njia ya Beeri-Sheba!’, wataanguka na hawatainuka tena.”

9

1Nikamwona Bwana amesimama karibu na madhabahu, akasema, “Vipige vichwa vya nguzo ili kwamba misingi itikisike. Vivunje vipande vipande juu ya vichwa vyao vyote, nami nitawaua wa mwisho wao kwa upanga. Hakuna mmoja wao atakaye kimbiawala atakayeokoka.

2Hata kama watachimba kwenye Sheoli, kuna mkono wangu utawachukua. Hata kama watapanda juu kwenda mbinguni, huko nitawaleta chini.
3Hata kama watajificha juu ya Karmeli, nitawatafuta huko na kuwachukua. Hata kama watajificha kwenye vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka, na atawauma.
4Hata kama wataenda kwenye utumwa, watabanwa na maadui zao mbele yao, nitauagiza upanga huko, na utawaua. Nitaelekeza macho yangu juu yao kwa ubaya sio kwa uzuri.”
5Bwana, Mungu wa majeshi, yeye aigusaye nchi nayo ikayeyuka; na wote wakaao humo wanaomboleza; yote yatafurika kama Mto, na kupungua kama mto wa Misri.
6Yeye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi yake katika nchi. Yeye ndiye anayeyaita maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa dunia, Yahwe ndilo jina lake.
7“Je, ninyi si kama wana wa Kushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli? - Hivi ndivyo Yahwe asemavyo. “Je! Sikuwapandisha Israeli kutoka nchi ya misri, Wafilisti kutoka Kaftori, na Washami kutoka Kiri?
8Tazama, macho ya Bwana Yahwe yanauelekea ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia, lakini sitaiharibu nyumba ya Yakobo kabisa, -hivi ndivyo Yahwe asemavyo.
9Maana hakik nitaamuru, na nitaipepeta nyumba ya Israeli kati ya mataifa yote, kama vile nafaka inavyopepetwa katikaungo, walakini punje ndogo haitaanguka chini.
10Wenye dhambi wote wa watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, ‘Msiba hautatupata wala kutukabili.’
11Katika siku hiyo nitaiinua hema ya Daudi, iliyoanguka, na kutengeneza mahali palipobomoka. Nitayainua magofu yake, na kuijenga tena kama katika siku za kale,
12ili wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote walioitwa kwa jina langu -hivi ndivyo Yahwe asemavyo-afanyaye jambo hili haya.

13Tazama, siku zinakuja-hivi ndivyo Yahwe asemavyo-ambaye alimaye atamfikilia avunaye na akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu. Milima itadondosha divai tamu, na vilima vyote vitatiririka.
14Nami nitawarudisha kutoka utumwani watu wangu Israeli. Wataijenga miji iliyoharibiwa na kukaa ndani yake. Watapanda bustani za mizabibu na kunywa divai yake, nao watatengeneza bustani na kula matunda yake.
15Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena kutoka katika nchi niliyowapa,” asema Yahwe Mungu wako.

Obadia

1

1Maono ya Obadia. Bwana Mungu asema hivi juu ya Edomu Tumesikia habari kutoka kwa Bwana, na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, akisema, Inukeni! Tuinuke dhidi yake kwa vita!”

2Tazama, nitawafanya wadogo kati ya mataifa, mutadharauliwa sana.
3Kiburi cha moyo wako kimekudanganya wewe, wewe ambaye unaishi katika makaburi ya miamba, katika nyumba yako ya juu; asemaye moyoni mwako, ‘Ni nani atakayenishusha mimi chini?’
4Ingawa unasimama juu kama tai na ingawa kiota chako huwekwa kati ya nyota, nitakushusha chini kutoka huko, asema Yahweh.
5Kama wezi walikuja kwako, ikiwa wanyang'anyi wangekujilia usiku (jinsi ungekatiliwa mbali wasingeweza), kuiba vya kuwatosha? Ikiwa wakusanya zabibu wangekujilia, wasingeacha mavuno?
6Jinsi Esau amekwisha kupigwa, na hazina zake zilizofichwa zimewekwa nje!
7Watu wote wa ushirikiano wako watakupeleka katika njia hadi mpakani. Watu waliokuwa na amani pamoja nawe wamekudanganya, na kukushinda. Wale wanaokula mkate wako wameweka mtego chini yako. Hakuna uelewa ndani yake.
8Je! Sikuweza siku hiyo, asema Bwana, kuwaangamiza watu wenye hekima kutoka Edomu na kuelewa kutoka mlima wa Esau?
9Mashujaa wako watafadhaika, Temani, ili kila mtu akatiliwe mbali kutoka mlima wa Esau kwa kuuawa.
10Kwa sababu ya ukatili uliofanywa kwa ndugu yako Yakobo, utafunikwa na aibu, nawe utakatiliwa mbali milele.
11Siku ile ulikuwa umesimama, siku wageni walichukua mali zake, na waliokuwa wageni katika malango yake, na kupiga kura kwa Yerusalemu, wewe ulikuwa kama mmoja wao.
12Lakini usifurahi siku ya ndugu yako, siku ya msiba wake, wala usifurahi juu ya watu wa Yuda siku ya uharibifu wao; msijisifu siku ya dhiki yao.
13Usiingie mlango wa watu wangu siku ya msiba wao; usifurahi juu ya taabu yao siku ya msiba wao, wala msipotee utajiri wao siku ya uharibifu wao.
14Usisimame kwenye njia panda, ili kuwakatilia mbali wakimbizi wake na usiwatoe waathirika wake katika siku ya dhiki.
15Kwa maana siku ya Bwana iko karibu na mataifa yote. Kama ulivyofanya, itafanyika kwako; matendo yako yatarudi juu ya kichwa chako mwenyewe.
16Kwa vile mlivyokunywa katika mlima wangu mtakatifu, ndivyo mataifa yote yatakavyo kunywa daima. Watakunywa na kumeza na itakuwa kana kwamba hawakuwepo kabisa.
17Lakini katika Mlima Sayuni kutakuwa na wale waliookoka na watakuwa watakatifu; na nyumba ya Yakobo watamiliki miliki zao.
18Nyumba ya Yakobo itakuwa moto, na nyumba ya Yusufu ni mwali wa moto, na nyumba ya Esau itakuwa mabua makavu, nao watawaunguza, na kuwateketeza. Hakutakuwa na waathirika kwa nyumba ya Esau, kwa kuwa Bwana amesema.
19Wote kutoka Negebu watamiliki mlima wa Esau na wale wa Shepela watamiliki nchi ya Wafilisti. Wao wataimiliki nchi ya Efraimu na nchi ya Samaria; na Benyamini atamiliki Gileadi.
20Wahamiaji wa jeshi hili la watu wa Israeli watamiliki ardhi ya Kanaani mpaka Sarepta. Wahamiaji wa Yerusalemu, waliopo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.
21Waokoaji watakwenda hadi juu ya Mlima Sayuni kutawala nchi ya vilima ya Esau, na ufalme utakuwa wa Bwana

Yona

1

1Ndipo neno la Bwana lilimjia Yona mwana wa Amittai, kusema,2“Simama uende Ninawi, mji kuu, na ukapaze sauti dhidi yake, kwa sababu uovu wao umeinuka mbele yangu.”3Lakini Yona akaondoka kukimbia kutoka mbele ya Bwana na kwenda Tarshishi. Akatelemka mpaka Yafa na akaona melikebu inayokwenda Tarshishi. Kwa hiyo alilipa nauli na akapanda melikebu kwenda nayo Tarishishi, mbali na uwepo wa Yahweh.

4Lakini Bwana akatuma upepo mkubwa juu ya bahari, ikawa tufani juu ya bahari. Hivi karibuni ikaonekana kwamba meli ilikuwa inataka kuzama.5Wale baharia waliogopa sana na kila mtu alilia kwa mungu wake mwenyewe. Wakatupa mizigo bahari iliyokuwa merikebuni ili kuifungua. Yona alikuwa ameshuka hapa pande za ndani ya melikebu, naye alikuwa amelala huko usingizi.

6Basi nahoza akamwendea akamwambia, “kwa nini unalala? Amka! Ukamwombe mungu wako! Labda mungu wako atatutambua na hatutapotea.”

7Wote wakaambiana, ‘Njoni, tupige kura, ili tujue ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata.’ Basi wakapiga kura, na kura ikaangukia kwa Yona.

8Kisha wakamwambia Yona, “Tafadhali tuambie ni nani ndiye sababu ya mabaya haya yanayotupata. Unafanya kazi gani, na umetoka wapi? Nchi yako ni ipi, na kutoka kwa watu wa kabila gani?”9Yona akawaambia, Mimi ni Mhebrania; Nami namuogopa Bwana, Mungu wa mbinguni, aliyeifanya bahari na nchi kavu.10Ndipo watu hao waliogopa zaidi, wakamwambia Yona, Ni jambo gani hili ulilolifanya? Kwa maana hao watu walijua kwamba alikuwa akikimbia mbele ya Bwana, kwa sababu alikuwa amewaambia.

11Ndipo wakamwambia Yona, Tukufanyie nini ili bahari iweze kutulia? Kwa maana bahari ilikuwa imechafuka zaidi na zaidi.12Yona akawaambia, “Nikamateni na nitupeni baharini. Kisha bahari itatulia kwa ajili yenu, kwa maana najua kwamba ni kwa sababu yangu kwamba tufani hii kubwa iwapate.”

13Hata hivyo, watu hao wavuta makasia kwa bidii ili kurudi nchi kavu, lakini hawakuweza kufanya hivyo kwa sababu bahari ilikuwa imechafuka zaidi dhidi yao.

14Basi wakamwomba Bwana, wakasema, Tunakuomba, Bwana, tunakuomba, usiache tuangamie kwa sababu ya maisha ya mtu huyu; wala usituwekee hatia ya kufa kwake, kwa kuwa wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda.15Basi wakamchukua Yona wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka.16Ndipo watu wale wakamuogopa Bwana sana. Wakamtolea dhabihu Bwana na kuweka nadhiri.

17Bwana alikuwa ameandaa samaki mkubwa kummeza Yona, na Yona alikuwa ndani ya tumbo lasamaki siku tatu na usiku wa tatu.

2

1Kisha Yona akamwomba Bwana Mungu wake kutoka katika tumbo la samaki.2Akasema, Nimemwita Bwana juu ya shida yangu naye akanijibu; kutoka tumbo la Kuzimu nililia kwa msaada! Uliisikia sauti yangu.3Ulikuwa umenitupa ndani ya kina, ndani ya moyo wa bahari, na maji yaliyonizunguka; mawimbi yako yote na gharika yalipita juu yangu.4Nikasema, ‘Nimefukuzwa mbele ya macho yako; lakini nitaangalia tena juu ya hekalu lako takatifu.’5Maji yalifunika kunizunguka karibu na shingo yangu; kina kilinizunguka; mwani ukakizinga kichwa changu.6Nilikwenda chini ya milima; nchi na baa zake zimefungwa juu yangu milele. Lakini wewe umeinua uhai wangu shimoni, Bwana, Mungu wangu!7Wakati nafsi yangu ilipozimia ndani yangu, nikamwita Bwana; basi sala yangu ilikujia, katika hekalu lako takatifu.8Wote ambao huzingatia miungu isiyofaa hukataa uaminifu wako wao wenyewe.9Lakini mimi, nitakuchinjia kwa sauti ya shukrani; Nitayatimiza yale niliyoapa. Wokovu hutoka kwa Bwana!

10Kisha Bwana akanena na samaki, akamtapika Yona juu ya nchi kavu.

3

1Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, akisema,2“Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, na uhubiri ujumbe ule ambao nitakuagiza.”

3Basi Yona akaondoka akaenda Niniawi kwa kutii neno la Bwana. Sasa Ninawi ilikuwa mji mkubwa sana, ilikuwa safari ya siku tatu.4Yona akaanza kuingia ndani ya mji, na baada ya safari ya siku, akapaza sauti, akasema, “Katika siku arobaini Ninawi itaangamizwa.”

5Watu wa Ninawi walimwamini Mungu na wakatangaza kufunga. Wote wakavaa nguo za magunia, kutoka aliyemkubwa hata mdogo.

6Mapema habari zilimfikia mfalme wa Ninawi. Akasimama kutoka kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika magunia, akaketi katika majivu.7Alitoa tangazo ambalo llsem, “katika mji wa Ninawi, kwa mamlaka ya mfalme na wakuu wake, msiruhusu mtu wala mnyama, ng'ombe wala kundi, asionje kitu chochote. Wao wasile wala kunywe maji.8Lakini watu na wanyama wawe wamefunikwa kwa magunia na walie kwa sauti kubwa kwa Mungu. Kila mtu ageuke na kuacha njia yake mbaya na kutoka katika udhalimu uliyopo mikononi mwake.9Nani anajua? Mungu anaweza kurejea na kubadili mawazo yake na kuacha ghadhabu yake kali ili tusiangamie.”

10Mungu akaona yale waliyoyafanya, wakaziacha njia zao mbaya. Kwa hiyo Mungu alibadili mawazo yake juu ya adhabu aliyowaambia angewafanyia, nae hakufanya hivyo.

4

1Lakini hili lilimchukiza Yona naye akakasirika.2Basi Yona akamwomba Bwana akasema, “Ee, Bwana, hiya sio yale niliyosema wakati niliporudi katika nchi yangu? Ndiyo maana nilifanya haraka na kujaribu kukimbia Tarshishi-kwa sababu nilijua kuwa wewe ni Mungu mwenye neema, mwenye huruma, si meingi wa hasira, mwingi kwa uaminifu, na hughairi maafa.3Kwa hiyo sasa, Bwana, nakuomba, uniondoe uhai wangu, kwa maana ni bora kwangu kufa kuliko kuishi.”

4Bwana akasema, Je, ni vema kwamba umekasirika?”

5Kisha Yona akaondoka mjini akaketi upande wa mashariki wa jiji. Huko alifanya makao na akaketi chini yake katika kivuli ili aweze kuona mji utakuwaje.6Bwana Mungu aliandaa mmea na kuukuza juu ya Yona ili uwe kivuli juu ya kichwa chake ili kupunguza dhiki yake. Yona alikuwa na furaha kubwa kwa sababu ya mmea.7Lakini Mungu aliandaa mdudu kulipopambazuka asubuhi iliyofuata. Alishambulia mmea na mmea ukapooza.8Ikawa wakati jua lilipochomoza asubuhi, Mungu aliandaa upepo mkali wa mashariki. Pia, jua lilipiga kichwa cha Yona na akaanguka. Kisha Yona alitamani kufa. Akajiambia, “Ni bora kwangu kufa kuliko kuishi.”

9Kisha Mungu akamwambia Yona, “Je, ni vema wewe kuwa na hasira juu ya mmea?” Yona akasema, Ni vyema kuwa nimekasirika hata kufa.

10Bwana akasema, Umeuhurumia mmea, ambao haukuufanyia kazi wala haukukua. Uliomea katika usiku na kufa usiku.11Kwa hiyo mimi, haikunipassa kuuhurumia Ninawi, mji mkuu, ambalo kuna watu zaidi ya mia na ishirini elfu ambao hawajui tofauti kati ya mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto, na pia ng'ombe wengi?

Mika

1

1Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Mika Mmorashti katika siku za Yotahamu, Ahazi, na Hezekeia, mfalme wa Yuda, lile neno aliloliona kuhusiana na Samaria na Yerusalemu.

2Sikilizeni, ninyi watu wote. Sikilizeni, dunia, na vyote vilivyomo kwenye dunia. Acheni Yahwe ashuhudiwe dhidi yenu, Bwana kutoka kwenye hekalu lake takatifu.
3Tazama, Yahwe anakuja kutoka mahali pake; atashuka chini na kupakanyaga mahali pa juu katika dunia.
4Milima itayeyuka chini yake; mabonde yatapasuka vipande vipande kama mshumaa mbele ya moto, kama maji ambayo yamemwagika chini ya mteremko mkali.
5Haya yote ni kwa sababu ya uasi wa Yakobo, na kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli. Je sababu ilikuwa nini kwa uasi wa Yakobo? Je ilikuwa Samaria? Je sababu ilikuwa nini kwa mahali pa juu pa Yuda? Je haiukuwa Yerusalemu?
6“Nitaifanya Samaria rundo la uharibifu katika shamba, kama eneo la kupandia mizabibu. Nitayavuta mawe ya jengo lake kwenda kwenye bonde; Nitaifunua misingi yake.
7Sanamu zake zote za kuchonga zitapondwa vipande vipande; na zawadi zake zote zitachomwa moto. Kwa kuwa zawadi zake za ukahaba amezikusanya, na kama malipo ya ukahaba yatarudi.”
8Kwa sababu hii nitalia na kuomboleza; nitaenda peku peku na uchi; Nitaomboleza kama mbweha na kuomboleza kama bundi.
9Kwa kuwa jeraha lake haliponi, kwa kuwa imefika kwa Yuda. Imefikia lango la watu wangu, hadi Yerusalemu.
10Msiache kuwambia kuhusu katika Gathi; msilie tena. Katika Bethi Leafra najiviriingisha mwenyewe kwenye mavumbi.
11Piteni karibu na, makao ya Shafiri, katika uchi na aibu. Makazi ya Zaanani hayatatoka nje. Maombolezo ya Beth Ezeli, kwa ajili ya ulinzi yamechukuliwa.
12Kwa kuwa wakaaji wa Marothi hungoja habari njema, kwa sababu hofu, kwa sababu msiba umetoka kwa Yahwe hadi kwenye malango ya Yerusalemu.
13Wafungueni lijamu farasi wakokote gari la farasi, makazi ya Lakishi. Wewe Lakishi, ulikuwa mwanzo wa dhambi kwa binti Sayuni, kwa kuwa makosa ya Israeli yalionekana kwako.
14Hivyo utaipa zawadi ya kuagia Moreshethi Gathi; mji wa Akzibu utawavunja moyo wafalme wa Israeli.
15Tena nitaleta ushindi kwako, makazi ya Maresha; uzuri wa Israeli utakuja Adulamu.
16Kata kipara chako na kata nywele zako kwa ajili ya watoto ambao unaowafurahisha. Fanya kipara chako mwenyewe kama tai, kwa ajili ya watoto wako watakao kwenda utumwani kutoka kwako.

2

1Ole wao wale wanao wanaokusudia mabaya, kwa wale wanaokusudia kwenye vitanda vyao kufanya maovu. Katika asubuhi wanayafanya kwa sababu wana nguvu.

2Wanatamani mashamba na kuyapunguza; wanazitamani nyumba na kuzichukua. Wanadhulumu mtu na nyumba yake, mtu na urithi wake.

3Kwa hiyo Yahwe asema hivi, “Tazama, nakaribia kuleta janga dhidi ya huu ukoo, ambalo hamtazitoa shingo zenu. Hamtatembea kwa kiburi, kwa kuwa itakuwa wakati wa uovu.
4Katika siku hiyo maadui zako wataimba wimbo kuhusu wewe, na kuomboleza kwa maombolezo ya huzuni. Wataimba, ‘Sisi Waisraeli tumeangamizwa kabisa; Yahwe hubadilisha eneo la watu wangu. Je ataliondoaje kutoka kwangu? Huwagawia mshamba yetu kusaliti.’
5Kwa hiyo, ninyi watu matajiri hamtakuwa uzao kugawanya eneo kwa kupiga kura katika mkutano wa Yahwe.
6“Msitabiri,” wanasema. “Hawatayatabiri haya mambo; lawama hazitakuja.”
7Je litasemwa kweli, nyumba ya Yakobo, “je Roho ya Yahwe? Je haya ni matendo yake kweli?” Maneno yangu hayafai kwa kila mmoja atembeaye kwa unyoofu?
8Hivi karibuni watu wangu wameinuka kama adui. Mmelivua joho, nguo, kutoka wale wapitao wasioshutumiwa, kama maaskari kurudi kutoka kwenye vita kwa kile wakifikiriacho ni salama.
9Mnawaendesha wanawake wangu kwa watu wangu kutoka kwenye nyumba nzuri; mnachukua baraka kutoka kwa watoto wao wadogo daima.
10Inukeni na muondoke, kwa kuwa hii sio sehemu ambayo mnaweza kuishi, kwa sababu ya unajisi wake; imeangamizwa kwa maangamizo kabisa.
11Kama mtu akija kwenu katika roho ya uongo na kudanganya na kusema, “Nitatabiri kwenu kuhusu mvinyo na kilevi kikali,” angeweza kufikiriwa kuwa nabii kwa ajili ya hawa watu.
12Nitawaleta pamoja wote hakika, Yakobo. Hakika nitawakusanya mabaki ya Israeli. Nitawaleta pamoja kama kondoo katika zizi, kama kundi la wanyama katika malisho. Kutakuwa na kelele kwa sababu ya wingi wa watu.
13Mtu avunjaye hufungua njia zao kwa ajili yao kwenda mbele yao. Wamebomoa kupitia lango na kutoka nje; mfalme wao atapita mbele yao. Yahwe atakuwa mbele yao.

3

1Nimesema, “Sasa sikilizeni, ninyi viongozi wa Yakobo na kutawala nyumba ya Israeli: Je siyo sahihi kwenu kuielewa haki?

2Ninyi manaochukia mazuri na kupenda uovu, ninyi mnaoambua ngozi yao, miili yao kutoka kwenye mifupa yao-
3ninyi mnaokula pia miili ya watu wangu, na kuambua ngozi yao, kuvunja mifupa yao, na kuwakatakata katika vipande vipande, kama nyama kwenye chungu, kama nyama kwenye sufuria kubwa.
4Kisha ninyi watawala mtalia kwa Yahwe, lakini hatawajibu. Atauficha uso wake kutoka kwenu kipindi hicho, kwa sababu mmefanya matendo maovu.”

5Yahwe asema hivi kuhusu manabii ambao wawafanyao watu wangu kushindwa, “Kwa wale wawalishao wanatangaza, ‘Kutakuwa na ustawi.’ Lakini kwa wale wasioweka kitu kwenye vinywa vyao, wanaanzisha vita dhidi yake.
6Kwa hiyo, itakuwa usiku kwenu usiokuwa na maono juu yenu; itakuwa giza ili kwamba msiweze kubashiri. Jua litakwenda chini juu ya manabii, na siku itakuwa giza juu yao.
7Waonaji watawekwa kwenye aibu, waaguzi wa watachanganyikiwa. Wote watafunga midomo yao, kwa kuwa hakuna jibu kutoka kwangu.”
8Lakini kwangu, nimejazwa nguvu kutoka kwa Roho wa Yahwe, na nimejaa haki na uweza, kumwambia Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake.
9Sasa sikieni hii, ninyi viongozi wa nyumba ya Yakobo, na watawala wa nyumba ya Israeli, ninyi ambao mnaochukia haki, na kupotosha kila haki.
10Mnaijenga Sayuni kwa damu na Yerusalemu kwa uovu.
11Viongozi wenu huhukumu kwa rushwa, makuhani wenu hufundisha kwa hijara, na manabii wenu hufanya utabiri kwa ajili ya pesa. Hata hivyo bado mtamtegemea Yahwe na kusema, “Je hayupo Yahwe pamoja nasi? Hakuna uovu utakaokuja juu yetu.”
12Kwa hiyo, kwa sababu yenu, Sayuni italimwa kama shamba, Yerusalemu itakuwa rundo la kifusi, na mwinuko wa hekalu utakuwa kama mwinuko wa msituni.

4

1Lakini katika siku za mwisho itakuja kuhusu kwamba mlima wa nyumba ya Yahwe utawekwa imara juu ya milima mingine. Utainuliwa juu ya milima, na watu watautakabisha.

2Mataifa mengi yataenda na kusema, “Njoni, twendeni juu kwenye mlima wa Yahwe, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, na tutembea katika njia zake.” Kwa kuwa kutoka Sayuni sheria itatoka, na neno la Yahwe kutoka Yerusalemu.
3Atahukumu miongoni mwa watu na kuamua kuhusiana na mataifa mengi ya mbali. Watafua mapanga yao kuwa plau na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa, wala kutawala kwa vita tena.
4Badala yake, wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake. Hakuna mtu atakayewafanya waogope, kwa kuwa mdomo wa Yahwe wa majeshi umesema.
5Kwa kuwa watu wote wataenenda, kila mmoja, katika jina la mungu wake. Lakini sisi tutaenenda katika jina la Yahwe Mungu wetu milele na milele.

6“Katika siku hiyo,” aseme Yahwe, “Nitamkusanya achechemeaye na kumkusanya aliyefukuzwa, wale ambao nimewatesa.
7Nitamrudisha aliyechechemea kwenye mabaki, na yeye aliyetupwa kwenye taifa imara, na mimi, Yahwe, nitatawala juu yao katika Milima Sayuni, sasa na milelev.
8Kama kwako, mnara wa saa kwa ajili ya kundi, mlima wa binti wa Sayuni utakuja kwenu, utawala wenu wa zamani utarudishwa, ufalme ambao unaomilikiwa na binti wa Yerusalemu.
9Sasa, kwa nini unapiga kelele kwa sauti kuu? Je hakuna mfalme miongoni mwenu? Je mshauri wako amekufa? Kwa nini uchungu umekushika kama yule mwanamke akiwa anazaa?
10Kuwa katika uchungu wa kuzaa ili uzae, binti Sayuni, kama mwanamke mwenye uchungu. Kwa sasa utatoka nje ya mji, kuishi kwenye shamba, na kwenda Babeli. Huko utaokolewa. Huko Yahwe atakuokoa kutoka kwenye mikono ya maadui.
11Sasa mataifa mengi yamekusanyika juu yako; wakisema; ‘Atiwe unajisi; macho yenu yaangalie Sayuni.”
12Nabii asema, “Hawayajui mawazo ya Yahwe, wala hawaelewi mpango wake, kwa kuwa wamewakusanaya kama miganda kupura sakafuni.”
13Yahwe asema, “simama na upure, binti Sayuni, kwa kuwa nitaifanya pembe yako kuwa chuma, na nitazifanya kwato zako kuwa shaba. Utaponda watu wengi. Nitaweka wakfu udhalimu wao kwangu mwenyewe, Yahwe, miliki zao kwangu, Bwana wa dunia nzima.

5

1Sasa njoni pamoja katika safu ya kupigana, binti wa maaskari; maaskari wameuzingira mji, kwa ufito watampiga mwamuzi wa Israeli kwenye shavu.

2Lakini wewe, Bethlehemu Efrata, hata kama uko mdogo miongoni mwa koo za Yuda, kutoka kweko mmoja atakuja kwangu kutawala Israeli, ambaye mwanzo wake ni kutoka nyakati za kale, toka milele.
3Kwa hiyo Mungu atawapa, hata mda wa yeye aliye katika uchungu kuzaa mtoto, na mabaki ya ndugu zake yatawarudia wana wa Israeli.
4Atasimama na kuchunga kundi lake kwa nguvu za Yahwe, kwa ukuu wa enzi ya jina la Yahwe Mungu wake. Watabaki, kwa kuwa atakuwa mashuhuri hata mwisho wa dunia.
5Atakuwa amani yetu. Wakati Waashuru watakapokuja kwenye nchi yetu, wakati wakitembea dhidi ya boma yetu, kisha tutainuka juu yao wachungaji saba na viongozi nane juu ya watu.
6Watachunga nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake. Atatuokoa kutoka kwa Waashuru, watakapokuja kwenye nchi yetu, watakapoingia kwenye mipaka yetu.
7Mabaki ya Yakobo yatakuwa katika kabila za watu wengi, kama umande utokao kwa Yahwe, kama manyunyu kwenye majani, ambayo hayamsubiri mtu, na hayawasubiri watoto wa mwanadamu.
8Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa, miongoni mwa watu wengi, kama simba katikati ya kundi la kondoo. Wakati akipita katikati yao, atawakanyaga juu yao na kuwachachana kuwa vipande vipande, na hakutakuwa na mtu wa kuwaokoa.
9Mkono wako utainuliwa dhidi ya maadui zako, na utawaharibu.

10“Itatokea siku hiyo,” asema Yahwe, “kwamba nitawaharibu farasi wako kutoka miongoni mwenu na nitayavunja magari yako ya farasi.
11Nitaiharibu miji katika nchi yako na kuziangusha ngome zako zote.
12Nitauharibu uchawi kwenye mkono wako, na hakutakuwa na waaguzi tena.
13Nitaziharibu sanamu zako za pango na nguzo za mawe kutoka miongoni mwako. Hautaabudu tena ustadi wa mikono yako.
14Nitazin'goa nguzo zako za Ashera kutoka miongoni mwenu, na nitaiharibu miji yenu.
15Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu juu ya mataifa ambayo hayakusikiliza.”

6

1Sasa sikilizeni kile ambacho Yahwe asemacho, “Inuka na ueleze kesi yako mbele ya milima; acha milima isikie sauti yako.

2Sikilizeni madai ya Yahwe, enyi milima, na ninyi misingi mivumilivu ya dunia. Kwa kuwa Yahwe anavumilia pamoja na watu wake, na atapigana katika mahakama juu ya Israeli.”
3Watu wangu, nimefanya nini kwenu? Nimewachosha mara ngapi? Shuhudieni dhidi yangu!
4Kwa kuwa niliwaleta kutoka nchi ya Misri na kuwaokoa kutoka kwenye nyumba ya utumwa. Nawatuma Musa, Aruni, na Mariamu kwako.
5Watu wangu, kumbukeni ambavyo Balaki mfalme wa Moabu alivyotunga, na vile ambavyo Balamu mwana wa Beori alivyomjibu kama ulipokuwa ukienda kutoka kwa Gilgali, hivyo mnaweza kujua matendo ya haki ya Yahwe.”
6Je nilete nini kwa Yahwe, ninapoenda kumwinamia Mungu aliye juu? Je ninaweza kuja kwake na sadaka za kuteketeza, pamoja na ndama wenye mwaka mmoja?
7Je Yahwe atapendezwa na maelfu ya kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe?
8Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.
9Sauti ya Yahwe inatangaza kwenye mji hata sasa hekima hukukiri jina lako: “Kaa tayari kwa ajili ya fimbo, na kwa yule aliyeiweka.
10Kuna utajiri katika nyumba za waovu, na kipimo cha uongo hilo ni chukizo mno.
11Ningeweza kumfikiria mtu kuwa hana hatia kama anatumia kipimo cha ulaghai, pamoja na mfuko wa kipimo wa udanganyifu?
12Matajiri wamejaa uharibifu, makazi yao yamesema uongo, na ulimi wao katika midomo yao unaudanganyifu.
13Kwa hiyo nimekupiga kwa pigo linaloumiza, nimekufanya gofu kwa sababu ya dhambi zako.
14Utakula lakini hutatosheka; utupu wako utabakia ndani yako. Utatunza mizigo mbali lakini hutahifadhi, na kile unachokihifadhi nitakitoa kwa upanga.
15Utapanda lakini hutavuna; utazikusanya zaituni lakini hutajipaka mafuta; utasindika zabibu lakini hutakunywa divai.
16Kanuni zilizotengenezwa na Omri zimetunzwa, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu. Mnatembea kwa ushauri wao. Hivyo nitakufanya wewe, mji, gofu, na makazi yako jambo la zomeo, na matabeba dharau kama watu wangu.”

7

1Ole wangu! Kwangu mimi ni kama msimu wa mavuno ulipokwisha, na pia makombo ya mavuno ya zabibu kwenye shamba la mizabibu: Hakuna tena kishamba cha matunda kinachoonekana, hakuna matini ya malimbuka ambayo ninayoyatamani.

2Watu waaminifu wamepotelea kutoka kwenye nchi, hakuna mtu mwadilifu katika wanadamu wote. Wote hudanganya katika kusubiri kumwaga damu; kila mtu humuwinda ndugu yake mwenyewe kwa wavu.
3Mikono yao ni mizuri mno kwa kufanya madhara. Watawala huuliza pesa, hakimu yuko tayari kwa rushwa, na mtu mwenye nguvu anawaambia wengine kile anachokitaka kujipatia. Hivyo ndivyo waundavyo kwa pamoja.
4Mtu bora kwao ni kama mitemba, mwadilifu sana ni kama mche wa miba. Imefika siku iliyosemwa nyuma na walinzi wako, siku ya hukumu. Sasa ni mda wa machafuko.
5Msimwamini kila jirani; msimuweke kiongozi katika rafiki yeyote. Kuweni makini kuhusiana na kile msemacho hata kwa mwanamke ambaye adanganyaye kwenye mikono yenu.
6Kwa kuwa mwana humfedhehesha baba yake, binti huinuka kushindana na mama yake, na mke wa mwana wa kiume hushindana na mama mkwe wake. Adui wa watu ni watu wa nyumba yake mwenyewe.
7Lakini kama kwangu mimi, nitamtazama Yahwe. Nitamsubiri Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu ataniskia.
8Usifurahi juu yangu, adui yangu. Niangukapo, nitainuka. Wakati nitakapokuwa nimekaa katika giza, Yahwe atakuwa mwanga kwangu.
9Kwa sababu nimetenda dhambi dhidi ya Yahwe, nitachukua ghadhabu yake hata aniteteapo kosa langu, na kutekeleza hukumu kwa ajili yangu. Atanileta kwenye nuru, na nitamwona akiniokoa kwenye haki yake.
10Kisha adui yangu atakapoliona hilo, na aibu itamfunika yule aliyeniambia, “Yahwe Mungu wako yuko wapi?” macho yangu yatamtazama; atakanyagwa chini kama tope kwenye mitaa.
11Siku ya kujenga kuta zako zitafika; siku hiyo mipaka itasogezwa mbali sana.
12Siku hiyo watu watakuja kwako, kutoka Ashuru na miji katika Misri, kutoka Misri hata mto mkubwa, kutoka bahari kwenda bahari, na kutoka mlima kwenda mlima.
13Hizo nchi zitakuwa zimejitenga kwa sababu ya watu ambao wanaishi huko sasa, kwa sababu ya tunda la matendo yao.
14Chunga watu wako kwa fimbo yako, kundi la urithi wako. Wanaishi wenyewe kwenye msitu, katikati ya msitu. Wachunge katika Bashani na Gileadi kama siku za zamani.

15Kama katika siku wakati mlipotoka nje ya nchi ya Misri, nitawaonyesha maajabu.
16Mataifa yataona na kuwa na aibu ya nguvu zao zote. Wataweka mikono yao kwenye midomo yao; masikio yao yatakuwa kiziwi.
17Watalamba vumbi kama nyoka, kama viumbe vitaambavyo juu ya nchi. Watatoka nje kwenye maficho kwa hofu; watakuja kwako kwa hofu, Yahwe Mungu wetu, na wataogopa kwa sababu yako.
18Ni nani aliye Mungu kama wewe, wewe uchukuaye dhambi, wewe upitaye juu ya kosa la mabaki ya mrithi wako? Hutunzi hasira yako milele, kwa sababu unapenda kutuonyesha agano lako la aminifu.
19Tena utakuwa na huruma juu yetu; utayakanyaga maovu chini ya miguu yako. Utazitupa dhambi zetu zote kwenye vilindi vya bahari.
20Utampatia ukweli Yakobo na agano aminifu kwa Abrahamu, ulipoapa kwa babu zetu katika siku za kale.

Nahumu

1

1Tamko kuhusu Ninawi. Kitabu cha maono ya Nahumu, Mwelkoshi.

2Yehova ni Mungu mwenye wivu na mlipiza kisasi; Yehova hulipiza kisasi na amejaa ghadhabu; Yehova ni Mungu hulipiza kisasi kwa adui zake, na huiendeleza hasira yake kwa adui zake.
3Yehova si mwepesi wa hasira na ni mwenye nguvu; hatawahesabia haki watu waovu. Yehova hufanya njia yake kwenye upepo wa kisulisuli na dhoruba, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.
4Huikemea bahari na kuifanya ikauke; hukausha mito yote. Bashani ni dhaifu, na Karmeli pia; maua ya Lebanoni imekuwa dhaifu.
5Milima hutetemeka uweponi mwake, na vilima huyeyuka; nchi huanguka mbele zake, kweli, dunia na watu wote wanaoishi ndani yake.
6Nani anaweza simama mbele ya ghadhabu yake? Nani anaweza zuia ukali wa hasira yake? Ghadhabu yake imemwagwa kama moto, na miamba ameipasua.
7Yehova ni mwema, boma katika siku ya taabu; na yeye huwatambua wale wanaomkimbilia.
8Lakini atafanya mwisho wa adui zake kwa mafuriko ya kutisha; atawawinda kwenye giza.
9Watu wanapanga nini dhidi ya Yehova? Yeye atakomesha; taabu haitainuka mara ya pili.
10Kama michongoma na kama mvinyo wa walewao, wataharibiwa kama mabua makavu.
11Kutoka kwako, Ninawi, amejitokeza mmoja ambaye alipanga uovu dhidi ya Yehova, mshauri muovu.
12Hivi ndivyo anavyosema Yehova, “Hata kama wana nguvu zao timilifu na idadi timilifu, hata hivyo wataondolewa; watu wao hawatakuwepo tena. Lakini wewe, Yuda: Ingawa nimekutesa, sitakutesa tena.
13Sasa nitaivunja ile nira ya watu kutoka kwako; nitaikata minyororo yako.”
14Yehova ametoa amri juu yako, Ninawi: “Hakutakuwa na uzao tena utakaoendeleza jina lako. Nitaharibu sanamu zilizochongwa na kuziondoa sanamu za chuma kutoka kwenye nyumba za miungu yenu. Nitaandaa kaburi lako, kwa kuwa umedharauliwa.”
15Tazama, juu ya milima kuna miguu ya mtu aletaye habari njema, anayetangaza amani! Sherehekeeni sikukuu zenu, Yuda, na timizeni nadhiri zenu, kwa maana yule mwovu hatawavamia tena; ameondolewa kabisa.

2

1Yule ambaye atakutawanya anakuja dhidi yako. Linda kuta za mji, linda barabara, imarisha viuno vyako, kusanya nguvu zako zote.2Maana Yehova anarejesha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli, ingawa wateka nyara waliwaharibu na kuharibu matawi ya zabibu zao.3Ngao za mashujaa wake ni nyekundu, na askari wamevaa nguo nyekundu; magari ya vita yanang'ara na vyuma vyake katika siku ambayo yaliandaliwa, na mikuki ya mivinje inarushwa hewani.

4Magari ya vita yanapita kasi kwenye mitaa; yanakimbia nyuma na mbele kwenye mitaa mipana. Yapo kama mienge, na yanakimbia kama umeme.
5Huwakumbuka mashujaa wake; wanajikwaa kila mmoja kwa mwingine katika kutembea kwao; wanaharakisha kuushambulia ukuta wa mji. Ngao kubwa imetayarishwa kuwakinga hawa washambuliaji.
6Malango kwenye mito yamelazimishwa kufunguka, na jumba la mfalme limeanguka.
7Huzabu amevuliwa mavazi yake na amachukuliwa; watumishi wake wa kike wanaomboleza kama njiwa, wakipiga vifua vyao.
8Ninawi ni kama bwawa la maji linalovuja, huku watu wake wakikimbia kama maji yanayotiririka. Wengine wanasema, “Simama, simama,” lakini hakuna anayegeuka nyuma.
9Chukua nyara ya fedha, chukua nyara ya dhahabu, maana hakuna mwisho wa hazina, kwa fahari ya vitu vyote vizuri vya Ninawi.
10Ninawi ipo tupu; tupu na imeharibiwa. Moyo wa kila mtu unayeyuka, magoti ya kila mmoja yanagongana pamoja, na uchungu upo kwa viuno vya kila mmoja; sura zao wote zimepauka.
11Sasa liko wapi pango la simba, sehemu ambapo wana-simba wadogo hula chakula, sehemu ambapo simba dume na simba jike walitembea, na wana-simba, ambapo hawakuogopa kitu chochote?
12Simba alirarua mawindo yake vipande vipande kwa ajili ya watoto wake; aliwanyonga mawindo wake kwa ajili ya wake zake, na kulijaza pango lake mawindo, tundu lake kwa mizoga iliyoraruliwa.
13“Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi. Nitayachoma magari yenu ya vita katika moshi, na upanga utameza wana-simba wenu. Nitakatilia nyara zenu kutoka kwenye nchi yenu, na sauti za wajumbe wenu hazitasikika tena.”

3

1Ole kwa mji uliojaa damu! Wote umejaa uongo na mali za wizi; waadhiriwa wapo kwake daima.2Lakini sasa kuna kelele za mijeledi na sauti za magurudumu yanayozunguka, farasi wanaokimbia, na magari ya vita yanao rukaruka.3Wapanda farasi wanashambulia, panga zinameremeta na mikuki inang'aa, marundo ya maiti, idadi kubwa ya miili isiyohesabika- washambuliaji wanajikwaa juu yake.4Hii inatokea kwa sababu ya matendo ya tamaa ya kahaba mrembo, mtaalam wa uchawi, mwenye kuuza mataifa kupitia kwa ukahaba wake, na watu kupitia matendo yake ya kichawi.

5“Tazama, mimi nipo kinyume na wewe --- hili ni neno la Yehova wa majeshi-- sketi yako nitaiinua juu ya uso wako na kuzionyesha sehemu zako za siri kwa mataifa, aibu yako kwa falme.
6Nitarusha uchafu wa kuchukiza kwako na kukufanya uwe mbaya sana; nitakufanya uwe mtu wa kutazamwa na kila mmoja.
7Itakuwa kwamba kila mmoja anayekutazama atakukimbia na kusema, ‘Ninawi ameharibika; ni nani ataomboleza kwa ajili yake?’ Ni wapi nitampata mtu anayeweza kukufariji?”
8Ninawi, je wewe ni bora kuliko No-amoni, uliojengwa juu ya Mto Naili, uliokuwa umezungukwa na maji, ambao ulinzi wake ilikuwa bahari, na bahari ilikuwa ukuta wake?
9Ethiopia na Misri walikuwa nguvu zake, na mwisho wake haukuwepo; Putu na Libya walikuwa rafiki zake.
10Lakini No-amoni alichukuliwa; alikwenda kwenye mateka; watoto wake wadogo walivunjwa vipande vipande katika kila makao makuu ya mtaa; adui zake walipiga kura kwa watu wake wenye heshima, na wakuu wake wote walifungwa minyororo.
11Wewe pia utalewa; utajaribu kujificha, na utatafuta kimbilio kutoka kwa adui yako.
12Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva mapema: kama zikitikiswa, zitaangukia ndani ya kinywa cha mlaji.
13Tazama, watu miongoni mwenu ni wanawake; malango ya nchi yako yamefunguliwa wazi kwa adui zako; moto umeharibu bawaba zake.
14Nenda ukachote maji kwa ajili ya kuzingirwa; ziimarishe ngome zako; nenda kwenye udongo na kandamiza matope; finyanga kwa ajili ya matofali.
15Moto utakuteketeza pale, na upanga utakuangamiza. Utateketezwa kama nzige wachanga wanavyoteketeza kila kitu. Ninyi wenyewe mjitengeneze kuwa wengi kama nzige wachanga, na wengi kama nzinge waliopevuka.
16Umezidisha wafanyabiashara wako zaidi kuliko nyota mbinguni; lakini wapo kama nzige wachanga; wanapora nchi na kisha kuruka kwenda zake.
17Wafalme wenu wapo kama kundi la nzige, na wakuu wenu wa majeshi ni kama nzige watuao kwenye ukuta wakati wa siku ya baridi. Lakini jua linapowaka wanaruka kwenda zao; na mahali waendapo hakuna anayepajua.
18Mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala; watawala wako wamejilaza chini kupumzika. Watu wako wametawanyika juu ya milima, na hakuna hata mmoja wa kuwakusanya.
19Hakuna uponyaji unaowezekana kwa ajili ya vidonda vyako. Vidonda vyako ni vikubwa. Kila anayesikia habari zako atapiga makofi kwa furaha juu yako. Ni nani ambaye hajaguswa na uovu wako wa daima?

Habakuki

1

1Ujumbe ambao habakuki nabii aliona.

2“Yahwe, kwa muda gani nitalilia msaada, na hutasikia? Nakulilia wewe kwasababu ya, ‘vurugu!’ lakini hutaokoa.
3Kwa nini unanifanya nione maovu na kuangalia matendo mabaya? Uharibifu na vurugu viko mbele yangu; kuna mapambano, na ushindani unainuka.
4Kwa hivyo sheria ni dhaifu, na haki haidumu kwa wakati wowote. Kwa kuwa waovu wanawazunguka wenye haki; kwa hivyo haki iliyobadilishwa inatoweka.”
5“Angalia mataifa na uwachunguze; ukastajaabu na ushangae! Kwa maana hakika niko karibu kufanya jambo katika siku zako ambalo hutaamini utakapoambiwa.
6Kwa maana angalia! Nakaribia kuwainua Wakaldayo _taifa katili na lenye haraka _wanapita katika upana wa nchi kuteka makao yasiyo yao.
7Wanatisha na kuogofya; hukumu yao na ukuu wao hutoka kwao wenyewe.
8Farasi wao pia wanambio sana kuliko chui, wakali kuliko mbwa mwitu wa jioni. Farasi wao huwaseta, na wapanda farasi wao huja kutoka mbali _ wanapaa kama tai anayewahi kula.
9Wote huja kwa vurugu; makundi yao yanakwenda kama upepo wa jangwani, na wanakusanya mateka kama mchanga.
10Wanawadhihaki wafalme, na watawala ni dhihaka kwao. Huicheka kila ngome, maana huibomoa kama udongo na kuukamata.
11Ndipo kama upepo atapita; ataendelea kupita _watu wenye hatia, ambao nguvu zao ni mungu wao.”
12“Wewe si wa tangu milele, Yahwe Mungu wangu, uliye Mtakatifu wangu? Hatutakufa. Yahwe aliwatenga kwa ajili ya hukumu, nawe, Mwamba, umewaimarisha kwa ajili ya kusahihisha.
13Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuangalia maovu kwa fadhila; kwa nini basi umeangalia kwa upendeleo ambao wanasaliti? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wenye haki kuliko wao wenyewe?
14Unawafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe vitambaavyo bila mtawala.
15Huwaleta wote kwa ndoana; anawakokota watu kutoka kwenye nyavu za samaki na kuwakusanya kwenye wavu wao; kwa hiyo anashangilia na kufurahi.
16Kwa hiyo anatoa sadaka kwa wavu wake na kuchoma ubani kwa juya lake, kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, nachakula chake ni aina tajiri zaidi.
17Kwa hiyo ataendelea kumwaga wavu wake, na kuendelea kuyachinja mataifa bila huruma?”

2

1Nitasimama kwenye nguzo ya ulinzi na kujiweka juu ya mnara, na nitazame nione atakaloniambia na nione vile nitakavyotoka katika lalamiko langu.

2Yahwe alinijibu na alisema, “Rekodi maono haya, na uandike dhahiri juu ya kibao ili kwamba anayesoma anaweza kusoma.
3Sababu maono haya bado ni kwa wakati ulioamriwa na yatashuhudia na hayatakosea. Ingawa yanakawia, yasubiri. Sababu kwa hakika itatimia na haitachelewa.
4Tazama! Yule ambaye hamu zake si haki ndani yake ni mwenye majivuno. Lakini mwenye haki ataishi kwa imani.
5Kwa kweli, kama vile mvinyo ni mdanganyifu, hata hivyo mtu mwenye kiburi hakai nyumbani. Amefanya koo lake lipanuke kama kuzimu; na kama kifo, hatosheki. Ameyakusanya pamoja mataifa, na kujiwekea watu wote kwake.
6Hawatachukua hawa wote methali na dhihaka, mafumbo kumhusu, wakisema,’ wake yule aongezaye visivyo vya kwake! Ni kwa muda gani utaongeza uzito wa dhamana uliyochukua?’
7Je hao wanaokuuma hawatainuka ghafla na hao wanaokutisha kuamka? Utakuwa mwathirika kwa ajili yao.
8Kwa sababu umeteka nyara watu wengi, mabaki yote ya watu yatakuteka nyarawewe. Sababu umemwaga damu ya binadamu na umeitendeanchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa ndani yake.
9Ole kwa yule anayepata mapato maovu kwa ajili ya nyumba yake, hivyo apate kukiweka kiota chake juu ili apate kujiepusha na mkono wa uovu.’
10Umebuni aibu kwa nyumba yako kwa kukatilia mbali watu wengi, na umefanya dhambi dhidi ya maisha yako mwenyewe
11Sababu mawe yatapasa sauti kutoka ukutani, na pao la mbao litawajibu,
12‘Ole wake yule ajengaye mji kwa damu, na anayeimarisha mji kwa uovu.
13Haikutoka kwa Bwana wa majeshi kwamba watu wafanye kazi kwa ajili ya moto na mataifa yanajichosha yenyewe bure?
14Bado nchi itajazwa maarifa ya utukufu wa Bwana kama maji yaifunikavyo bahari.
15‘Ole wake yule anayelazimisha majirani wake kulewa _unaonyesha hasira yako na kuwafanya walewe ili uweze kutazama uchi wao.’
16Utajazwa na aibu badala ya utukufu. Sasa ni zamu yako! Kunywa, na utafichua govi lako ambalo halijatahiriwa! Kikombe cha mkono wa kuume wa Bwana kinakujia, na aibu itafunika utukufu wako.
17Udhalimu uliotendewa Lebanoni utakufunikiza na uharibifu wa wanyama utakuogopesha. Sababu umemwaga damu ya mtu na umei tendea nchi udhalimu, miji, na wote wanaokaa humo.
18Ni faida gani iliyoko kwa sanamu ya kuchongwa? Sababu yule aliyeichonga hiyo! Au kinyago cha kuyeyuka, mwalimu wa uongo? Sababu aliyetengeneza hutumaini kile ametengeneza anapozifanya sanamu zisizo na faida
19‘Ole kwa yule auambiaye ubao, Amka! Au kwa jiwe lisilo na uhai, Inuka!’ Vitu hivi vinafundisha? Angalia, hiki juu kimefunikwa kwa dhahabu na fedha, lakini ndani yake hakina pumzi kabisa.
20Lakini Bwana yumo katika hekalu lake takatifu! Nchi yote iwe kimya mbele zake.

3

1Maombi ya Habakuki nabii:2Yahwe, nimesikia habari zako, na mimi naogopa. Yahwe, fufua kazi yako katikati ya nyakati hizi; katikati ya miaka hii fanya ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako.

3Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. Sela Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa sifa zake.
4Na mng'ao wake kama mwanga, mionzi miwili ilimulika kutoka mkononi mwake; ambapo uweza wake ulifichwa.
5Ugonjwa wa kufisha ulitangulia mbele yake, na tauni ilitoka miguuni pake.
6Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na akayatikisa mataifa. Hata milima ya milele ikatawanyika, na vilima vya kale vikainama. Njia yake ni ya kale.
7Niliona hema za Wakushi katika mateso, na vitambaa vya hema za nchi ya Midiani vinatetemeka
8Yahwe alikasirikia pale mitoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasina magari yako ya ushindi
9Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! Sela Uliigawa nchi na mito.
10Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa uchungu. Gharika ya maji ikapita juu yao; vilindi vikapaza sauti. Vikainua juu mikono yake
11Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako ilipopaa, kwa mwanga wa mkuki wako umeremetao
12Umetembea juu ya nchi kwa hasira. Katika ghadhabu umewapura mataifa.
13Ulikwenda nje kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajil ya wokovu wa mteule wako. Wewe huponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi kutoka kwa msingi mpaka kwa shingo. Sela
14Umekichoma kichwa cha mashujaa wake kwa mishale yake mwenyewe sababu walikuja kama mawimbi kututawanya wivu wao ulikuwa kama mtu anayemwangamiza maskini mafichoni.
15Umekanyaga juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyarundika maji makuu.
16Nilisikia, viungo vyangu ndani vilitetemeka! Midomo yangu ilitetemeka kwa sauti ile. Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu natetemeka nikisubiri kwa kimya siku ya dhiki iwajilie watu waliotushambulia
17Ingawa mtini hautachanua na hakuna mazao kutoka kwa mizabibu; ingawaje matunda wa mti wa mzaituni inakatisha tamaa na mashamba hayatoi chakula; iwapo kundi la mifugo limekatwa kutoka kwa kibanda na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya.
18Bado, nitafurahia katika Bwana. Nitashangilia kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu.
19Bwana Yahwe ni nguvu yangu na huifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya niende mbele mahali pangu pa juu. - Kwa mwelekezi wa muziki, kwa vyombo vyangu vya nyuzi.

Sefania

1

1Hili ni neno la Yahwe ambalo lilikuja kwa Sefania mwana wa Kushi mwana wa Gedalia mwana wa Amaria mwana wa Hezekia, katika siku za Yosia mwana wa Amoni, mfalme wa Yuda.”

2Nitaangamiza kabisa kila kitu kutoka usoni mwa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
3Nitamwangamiza mtu na mnyama; Nitawaangamiza ndege wa mbinguni na samaki wa baharini, uharibifu pamoja na waovu. Hivyo nitamfutilia mbali mtu kutoka uso wa dunia - hili ni tamko la Bwana mwenyewe.
4Nitafika kwa mkono wangu juu ya Yuda na wote wenyeji wa Yerusalemu. Nitafutilia mbali kila mabaki ya Baali kutoka sehemu hii na majina ya watu waabuduo sanamu miongoni mwa makuhani,
5watu ambao juu ya nyumba huabudu miili ya mbinguni, na watu ambao huabudu na kuapa kwa Yahwe bali ambao pia huapa kwa mfalme wao.
6Nitawafutilia mbali pia wale ambao wamegeuka nyuma kutoka kumfuata Yahwe, wale ambao pia humtafuta Yahwe pasipo kuuliza ulinzi wake.
7Uwe kimya mbele ya Bwana Yahwe! Kwa kuwa siku ya Yahwe ni karibu, Yahwe ameandaa dhabihu na amewatenga wageni wake.
8“Itakuja katika siku ya dhabihu ya Bwana, hivyo nitawapiga wakuu na wana wa mfalme, na kila mmoja aliyevikwa mavazi ya kigeni.
9Katika siku hiyo nitawapiga wote wale ambao huruka juu ya kizingiti, wale ambao hujaza nyumba ya bwana wao kwa vurugu na udanganyifu.
10Itakuwa katika siku ile - hili ni tangazo la Yahwe - kwamba kilio cha huzuni kitakuja kutoka kwenye mlango wa samaki, ikipiga yowe kutoka Wilaya ya Pili, na sauti ya kishindo kikuu kutoka vilimani.
11Pigeni yowe, wenyeji wa Soko la Wilaya, kwa wote wafanyabiashara watakuwa wameharibiwa, wote wale ambao hupima fedha watakuwa wamefutiliwa mbali.
12Itakuwa katika siku ile nitaitafuta Yerusalemu kwa taa na kuwapiga wanaume ambao watakuwa wamekaa kwenye mvinyo wao na kusema mioyoni mwao, ‘Yahwe hatafanya chochote, ama kizuri au kiovu.’
13Mali zao zitakuja kuporwa, na nyumba zao zitakuwa zimetelekezwa kwa maangamizi! Watajenga nyumba lakini hawataishi humo, na kupanda mizabibu lakini hawatakunywa mvinyo wake.
14Siku kubwa ya Yahwe i karibu, karibu na inaharakisha upesi! Sauti ya siku ya Yahwe itakuwa ya kilio cha uchungu wa kishujaa!
15Siku hiyo itakuwa siku ya ghadhabu, siku ya huzuni na uchungu, siku ya dhoruba na maangamizi, siku ya giza na utusitusi, siku ya mawingu na giza nene.
16Itakuwa siku ya parapanda na kengele dhidi ya ngome mijini.
17Hivyo nitaleta dhiki juu ya wanadamu, kwa hiyo watatembea karibu kama wanaume vipofu tangu walipofanya dhambi dhidi ya Yahwe. Damu yao itamwagwa kama vumbi, na sehemu zao za ndani kama kinyesi.
18Wala fedha zao wala dhahabu zao hazitaweza kuwaokoa juu ya ghadhabu ya Yahwe. Ndani ya moto wa wivu wake dunia yote itateketezwa, hivyo ataleta ukamilifu, mwisho wa kutisha kwa wote wakaao duniani.”

2

1Kusanyikeni pamoja ninyi wenyewe mkutano wa hadhara na kusanyikeni, taifa lisilokuwa na aibu -

2kabla amri kuchukua madhara na siku hiyo kupita kama makapi, kabla hasira kali ya ghadhabu ya Yahwe kuja juu yenu, kabla siku ya ghadhabu ya Bwana kuja juu yenu.
3Mtafuteni Yahwe, ninyi watu wote wanyenyekevu duniani mnaozitii amri zake! Tafuteni haki yake. Tafuteni unyenyekevu, na labda mtalindwa katika siku ya ghadhabu ya Yahwe.
4Hivyo Gaza utatelekezwa, na Ashkeloni utageuka kuwa uharibifu. Watauondoshea mbali Ashdodi wakati wa mchana, na wataung'oa Ekroni!
5Ole kwa wanaokaa kando ya bahari, taifa la Wakerethi! Yahwe amesema dhidi yenu, Kanaani, nchi ya Wafilisiti. Nitawaangamiza hakuna mkazi atakayebakia.
6Hiyo nchi ya kando ya bahari itakuwa malisho kwa wachungaji na kwa mazizi ya kondoo.
7Nchi ya kando ya bahari itakuwa mali ya mabaki ya watu wa nyumba ya Yuda, watakaochungia makundi yao huko. Watu wao watalala jioni katika nyumba ya Ashikeloni, kwa kuwa Yahwe Mungu wao atawatunza na kurejesha wafungwa wao.

8Nilizisikia dhihaka za Moabu na wakiwatukana watu wa Amoni wakati walipowadhihaki watu wangu na kujitukuza mipakani mwao.
9Kwa hiyo, kama ninavyoishi - hili ni tamko la Yahwe wa majeshi, Mungu wa Israeli, -‘Moabu itakuja kuwa kama Sodoma, na watu wa Amoni kama Gomora; mahali pachafu na shimo la chumvi, jangwa la daima. Lakini watu wangu waliosalia watawateka mateka, na watu wa taifa langu waliobaki watachukua umiliki wao.’
10Hili litatokea kwa Moabu na Amoni kwa sababu ya kiburi chao, tangu walipowadhihaki na kuwatukana watu wa Yahwe wa majeshi.
11Ndipo watamwogopa Yahwe, kwa kuwa ataidhihaki miungu yote ya dunia. Kila mmoja atamwabudu yeye, kila mmoja kutoka mahali pake, kutoka kila upande wa pwani.
12Ninyi Wakushi pia mtakufa kwa upanga wangu,
13na mkono wa Mungu utaishambulia kaskazini na kuiangamiza Ashuru, Kwa hiyo Ninawi utatelekezwa kwa kuteketezwa, kuwa pakavu kama jangwa.
14Ndipo makundi ya wanyama yatalala pale, kila mnyama wa mataifa, wote kirukanjia na nungunungu watapumzika juu ya safu zao. Sauti itasikika kutoka madirishani; kifusi kitakuwa milangoni; nakshi za mwerezi wao mihimili itakuwa imeifunua.
15Huu ni mji wa kushangiliwa ambao umekaa pasipo hofu, ambaye husema moyoni mwake, “Mimi niko, na hakuna mwingine wa kufanana na Mimi.” Kwa namna ulivyokuwa wa kutisha, mahali pa kulala wanyama ndani yake. Kila mmoja ambaye hupitia kwake huuhisia na kutingisha mikono yake.

3

1Ole kwa mji ulioasi! Mji wenye vurugu umenajisiwa.

2Haukuisikiliza sauti ya Mungu, wala haukupokea masahihisho kutoka kwa Yahwe. Hakumtumaini Yahwe na hatamkaribia Mungu wake.
3Wafalme wao ni simba wanaounguruma miongoni mwao. Waamuzi wao ni mbwa mwitu wa jioni wasiobakiza kitu ambacho kitakuwa kimemung'unywa asubuhi yake.
4Manabii wake wanakiburi na wanaume wasaliti. Makuhani wake wamepanajisi mahali patakatifu na wameifanyia vurugu sheria.
5Yahwe ni mwenye haki miongoni mwao. Hawezi kufanya makosa. Kila asubuhi husimamia haki yake! Haitafichika nuruni, hata hivyo watu wasio wenye haki hawajui kuona aibu.

6Nimeyaharibu mataifa; ngome zao zimeharibiwa. Nimeifanya mitaa yao magofu, hivyo hakuna hata mmoja anayepitia kwake. Miji yao imeharibiwa kwa hiyo hakuna mtu anayeikaa.
7Nikasema, ‘Hakika mtaniogopa mimi. Pokeeni masahihisho na msikatiliwe mbali kutoka kwenye miji yenu kwa yote yale niliyokuwa nimeyapanga kuyafanya kwenu.’ Lakini walikuwa na shauku kuanza kila siku kwa kuharibu matendo yao yote.
8Kwa hiyo ningojeni - hili ni tamko la Yahwe - mpaka siku ambayo nitainuka kwa ajili ya waathirika. Uaamuzi wangu nikuwakusanya mataifa, kuzikusanya falme, na kumwaga juu yao hasira yangu, uchungu wangu wote mkali, hivyo nchi yote itamezwa kwa moto wa hasira yangu.
9Ndipo nitawapa midomo safi watu, kuwaita wote kwa jina la Bwana kunitumikia wakisimama bega kwa bega.
10Kutoka ng'ambo ya mto Ethiopia waniabuduo - watu wangu waliotawanyika - wataleta dhabihu kwa sababu yangu.
11Katika siku hiyo hamtawekwa kwenye woga kwa matendo yenu yote ambayo mmeyafanya dhidi yangu, tangu wakati ule nitaondoa kutoka kwenu wale waliosherehekea fahari yenu, na kwa sababu hamtakuwa na muda mrefu kufanya majivuno juu ya mlima wangu mtakatifu.
12Lakini nitawaacha kama wa chini zaidi na watu masikini, na mtapata kimbilio katika jina la Yahwe.
13Mkazi wa Israeli si muda mrefu hatafanya udhalimu au kusema uongo, na hakuna ulimi wa udanganyifu utakaoonekana mdomoni mwao; hivyo watalisha na kulala chini, na hakuna hata mmoja atakayewafanya kuogopa.”
14Imba, binti Sayuni! Piga kelele, Israeli. Ufurahi na kushangilia kwa moyo wako wote, binti wa Yerusalemu.
15Yahwe ameiondoa hukumu yako; amewafukuzia mbali adui zako! Yahwe ni mfalme wa Israeli miongoni mwenu. Kamwe hamtamwogopa tena mwovu!
16Katika siku hizo watasema kwa Yerusalemu, “Usiogope, Sayuni. Usiiache mikono yako ilegee.
17Yahwe Mungu wako yuko katikati yenu, mwenye nguvu wa kuwaokoa. Atasherehekea juu yenu na kwa furaha atakuwa kimya juu yenu kwa upendo wake. Atakuwa na furaha juu yenu na atashangilia kwa furaha,
18katika siku maalumu ya sherehe. Nitaondoa maafa kutoka kwenu; si muda mrefu hamtabeba aibu kwa ajili yake.
19Tazama, niko tayari kuwashughulikia watesi wenu wote. Katika wakati ule, nitawaokoa waliolemaa na kuwakusanya waliotupiliwa mbali. Nitawafanya kuwa sifa, na nitaibadilisha aibu yao iwe sifa katika dunia yote.
20Katika wakati ule nitawaongoza; katika wakati ule nitawakusanya pamoja. Nitawafanya mataifa yote ya dunia kuwaheshimu na kuwasifu, wakati mtakapoona hivyo, nitakuwa nimewarudisha,” asema Yahwe.

Hagai

1

1Katika mwaka wa pili wa mfalme Dario, katika mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kupitia kwa nabii Hagai kwenda kwa gavana wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, kusema,

2Bwana wa Majeshi asema: “Hawa watu husema, si wakati wetu kuja au kujenga nyumba ya Jehova.”

3Tena neno la Bwana lilikuja kwa mkono wa nabii Hagai kusema,4“Je ni wakati kwenu wenyewe kuishi katika nyumba zilizokamilika, na wakati nyumba hii inaharibika?5Kwa hivyo sasa Bwana wa Majeshi asema hivi: ‘zitafakarini njia zenu!6Mmepanda mbegu nyingi, lakini mkaleta mavuno kidogo; mnakula lakini hamshibi, mnakunywa lakini hamutosheki na vinywaji. Mnavaa nguo lakini hampati joto wenyewe, na mtu wa mshahara hupata pesa na kuziweka kwenye mfuko uliotoboka!’

7Bwana wa Majeshi asema haya:8‘Zitafakarini njia zenu! Pandeni milimani, mkalete mbao, na mjenge nyumba yangu; ndipo nitaifurahia na nitatukuzwa!’ Asema Bwana.9‘Mmetazamia kupata vingi, lakini tazama! Mmeleta nyumbani vichache, kwa kuwa nilivipeperusha mbali! Kwa nini?’- Hivi ndivyo asemavyo Bwana wa Majeshi! Kwa sababu nyumba yangu inakaa kwenye uharibifu, lakini kila mtu yuko radhi kwenye nyumba yake.10Kwa sababu ya hii mbingu zimeshikiliwa zisitoe umande kwako, na ardhi imeshikilia mazao yake.11Nimeagiza ukame juu ya ardhi na juu ya milima, juu ya nafaka na juu ya divai mpya, juu ya mafuta na juu ya mavuno ya ardhi, juu ya watu na juu ya wanyama, na juu ya kazi zote za mikono yenu.

12Kisha Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kuhani mkuu Yoshua mwana wa Yehozadaki, pamoja na mabaki ya watu, wakatii sauti ya Bwana Mungu wao, na maneno ya nabii Hagai, kwa sababu Bwana Mungu wao alikuwa amemtuma na watu wakaogopa uso wa Bwana.

13Ndipo Hagai, mjumbe wa Bwana, akaongea ujumbe wa Bwana kwa watu na kusema, “‘Niko pamoja nanyi!’- Hivi ndivyo asema Bwana!”14Bwana alitibua roho ya mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na roho ya kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki, na roho ya masalia ya watu, kwa kiasi kwamba wakaenda kufanya kazi katika nyumba ya Bwana Mungu wa Majeshi, Mungu wao.15Katika siku ya ishirini na Mwezi wa sita, katika mwaka wa pili wa utawala wa Mfalme Dario.

2

1Katika Mwezi wa saba siku ya ishirini na moja ya mwezi, neno la Bwana lilikuja kupitia kwa nabii Hagai, na kusema,2“Ongea na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli mwana wa Shealitieli, na kwa kuhani mkuu Yehozadaki; na kwa masalia ya watu. Sema,3Ni nani aliyebaki kati yenu aliyeuona utukufu wa nyumba hii iliyokuwa ya kwanza? Na mnaionaje kwa sasa? Je sio kama si chochote machoni penu?4Sasa, muwe hodari, Zerubabeli’ -hivi ndivyo asema Bwana - na uwe hodari, kuhani mkuu Joshua mwana wa Yehozadaki; muwe hodari, enyi watu wa nchi! - Hivi ndivyo asema Bwana - na mfanye kazi, kwa kuwa mimi ni pamoja nanyi! Hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi.5Na hii ndiyo agano niliyoiweka na nyinyi mlipokuwa mukitoka Misri, na Roho wangu anadumu katikati yenu. Msiogope6kwa kuwa Bwana wa majeshi anasema haya: “kitambo kidogo kwa mara nyingine nitatikisa mbingu na dunia, bahari na nchi kavu!7Na nitalitikisa kila taifa, na kila taifa litaleta vitu vyao vya thamani kwangu, na nitaijaza nyumba hii na utukufu!’ asema Bwana wa Majeshi.8Dhahabu na fedha ni yangu! - Hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi.9Utukufu wa nyumba hii utakuwa mkubwa siku zijazo kuliko utukufu wa nyumba ya kwanza,’ asema Bwana wa majeshi, ‘na nitawapa amani mahali hapa! - Hivi ndivyo asema Bwana wa majeshi.”

10Katika siku ya ishirini na nne mwezi wa tisa, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Bwana lilimjia nabii Hagai na kusema,11“Bwana wa Majeshi asema hivi: Muulizeni kuhani kuhusu sheria, na useme:12Kama mtu atabeba nyama iliyotolewa kwa Bwana katika pindo la vazi lake, kama upindo utagusa mkate au mchuzi, mvinyo au mafuta, au chakula kingine, je chakula hicho kinafanyika kitakatifu?” Kuhani alijibu akasema, “Hapana”

13Halafu Hagai akasema. “Kama mtu ni najisi kwa ajili ya kumgusa maiti na kugusa vitu hivi, vyote vinaweza kuwa najisi?” Kuhani akajibu na kusema, “Ndiyo, vitakuwa najisi.”

14Kwa hiyo Hagai akajibu nakusema, “Ni pamoja na hawa watu na pamoja na taifa liliko mbele yangu! - Haya anayasema Bwana- na pia kila kitu kimekwisha kwa mkono wake: walichotoa hakikuwa kisafi kilikuwa kichafu.

15Kwa hiyo sasa, tafakarini hayo kuanzia leo na kuendelea, kabla jiwe halijawekwa juu ya jiwe lingine katika hekalu la Bwana,16Ilikuwaje basi? Kila mtu alipokuja kwenye vipimo ishirini vya nafaka, kumbe kulikuwa na vipimo kumi tu, na aliyekuja kuchota divai ya vipimo hamsini, kumbe kuliwa na vipimo ishirini tu.17Niliwataabisha ninyi na kazi za mikono yenu kwa ukame na ukungu na mvua ya mawe lakini hamkunirudia’- asema Bwana.

18Tafakari siku hii ya leo na kuendelea, kutoka siku ya ishirini na nne katika mwezi wa tisa, toka siku ile msingi wa hekalu la Bwana uliwekwa. Tafakarini hilo!19Je, bado kuna mbegu katika ghala? Mzabibu, mti wa mtini, komamanga, na mti wa mzeituni havikuzaa matunda! Lakini kutoka siku hii ya leo nitawabariki!”

20Tena neno la Bwana likaja kwa mara ya pili kwa Hagai siku ya ishiri na nne katika mwezi kusema,21“Sema na mkuu wa mkoa wa Yuda, Zerubabeli umwambie, ‘Nitatikisa mbingu na dunia.22Kwa hiyo nitaangusha viti vya falme na kuharibu nguvu za falme za mataifa! Nitaangusha magari na wapandao; farasi na wapanda farasi wataanguka, kila mmoja kwa sababu ya upanga wa ndugu yake.

23Siku hiyo'-hivi ndivyo asema Bwana wa Majeshi- ‘Nitakuchukua wewe Zerubabeli mwana wa Shealitieli, kama mtumishi wangu! Hivi ndivyo Bwana anavyosema. “Nitakutumia kama pete ya muhuri wangu, kwa sababu mimi nimekuchagua!- asema Bwana wa Majeshi!”

Zekaria

1

1Katika mwezi wa nane mwaka wa pili wa kutawala kwake Dario, neno la Yahwe lilimjia nabii Zekaria, mwana wa Berekia mwana wa Ido, kusema,

2“Yahwe” alikuwa na hasira sana juu ya baba zenu!3Waambie, ‘Yahwe wa majeshi asema hivi: Nirudieni! - Nami nitawarudia ninyi, asema Yahwe wa majeshi.4Msiwe kama baba zenu ambao hapo zamani manabii waliwaambia, wakisema, “Yahwe wa majeshi asema hivi: Geukeni kutoka katika njia zenu mbaya na matendo yenu mabaya!” Lakini hawakuweza kusikia wala kunijali - asema Yahwe.’5Wako wapi baba zenu? Na manabii, je wapo hapa daima?6Lakini maneno yangu na maagizo niliyowaamru watumishi wangu manabii, je hayakuwapata baba zenu? Hivyo walitubu na kusema, ‘Kama vile Yahwe wa majeshi alivyokusudia kututenda kwa kadili zinavyostahili njia na matendo yetu, ndivyo alivyotutenda.”

7Katika siku ya ishirini na nne ya mwezi wa kumi na moja, ndiyo mwezi wa Shebati, mwaka wa pili wa utawala wa Dario, neno la Yahwe lilimjia nabii Zekaria mwana wa Berekia mwana wa Ido, akasema,8“niliona wakati wa usiku, na tazama! Mtu alikuwa amepanda farasi mwekundu, naye alikuwa kati ya miti ya mihadasi iliyoko bondeni; na nyuma yake kulikuwa na farasi mwekundu, farasi wa kijivu, na farasi mweupe.”

9Nikauliza, “Bwana, hivi ni vitu gani?” Malaika aliyesema nami akaniambia, “Nitakueleza vitu hivi ni nini.”

10Kisha mtu aliyesimama kati ya miti ya mihadasi akajibu na kusema, “Hawa ndiyo Yahwe aliowatuma kuzunguka katika dunia yote.”

11Wakamjibu malaika wa Yahwe aliyekuwa amesimama kati ya miti ya mihadasi na kumwambia, “Tumekuwa tukizunguka duniani pote; tazama, dunia yote imekaa na kutulia.”

12Ndipo malaika wa Yahwe alipojibu na kusema, “Yahwe wa majeshi, hata lini usiuhurumie Yerusalemu na miji ya Yuda ambayo imeteswa na kudhulumiwa miaka hii sabini?”13Yahwe akamjibu malaika aliyekuwa amesema nami, kwa maneno mazuri, maneno ya faraja.

14Hivyo malaika aliyekuwa anaongea nami akaniambia, “Ita kwa sauti na useme ‘Yahwe wa majeshi asema: Nina wivu kwa ajili ya Yerusalemu yaani Sayuni kwa uchungu mkubwa!15Nami nina hasira juu ya mataifa yaliyo na utulivu. Kwa maana nilikasirika kidogo tu, lakini wao wakasababisha madhara mabaya.16Kwa hiyo Yahwe wa majeshi asema hivi: Nimeirudia Yerusalema kwa huruma. Hivyo nyumba yangu itajengwa ndani yake - asema Yahwe wa majeshi. Kipimo kitanyoshwa juu ya Yerusalemu!17Ita tena, ukisema, ‘Yahwe wa majeshi asema hivi: Miji yangu kwa mara nyingine itajawa na uzuri, na Yahwe ataifariji tena Sayuni, na kuichagua Yerusalemu kwa mara nyingine tena.”

18Kisha nikainua macho na kuona pembe nne!19Nikaongea na malaika aliyesema nami, “Hivi ni vitu gani? Akanijibu “hizi ni pembe zilisosababisha kutawanyika kwa Yuda, Israeli, na Yerusalemu.”

20Kisha Yahwe akanionyesha mafundi stadi wanne.21Nikasema, “Watu hawa wanakuja kufanya nini?” Akajibu na kusema, “Hizi ni pembe zililoitawanya Yuda na hakuna mtu angeweza kuinua kichwa chake. Lakini watu hawa wanakuja kuziondoa, kutupa chini pembe za mataifa yaliyoinua nguvu zao kinyume cha nchi ya Yuda na kuisambaza.”

2

1Kisha nikainua macho yangu na kuona mtu akiwa na timanzi mkononi mwake.2Nikamwuliza, “Unakwenda wapi?” Akaniambia, “Ninakwenda kuipima Yerusalemu ili kujua upana na urefu wake.”

3Ndipo malaika aliyekuwa anaongea nami akaondoka na malaika mwingine akaenda kukutana naye.4Malaika wa pili akamwambia, “Nenda uongee na yule kijana umwambie, ‘Yerusalemu utakuwa bila kuta kwa sababu ya wingi wa watu na wanyama ndani yake.5Kwa maana Yahwe asema, Nitakuwa mlinzi wake, na nitakuwa utukufu katikati yake.

6Kimbieni! Kimbieni! Kimbieni kutoka nchi ya kaskazini - asema Yahwe - kwa maana nimewatawanya kama pepo nne za anga! - Asema Yahwe.

7Kimbilieni Sayuni haraka! Ninyi mnaokaa na binti Babeli!” Asema Yahwe.8Kwa maana baada ya Yahwe wa majeshi kuniheshimu aliniweka kinyume na mataifa yaliyowateka - kwani awagusaye, agusa mboni ya jicho la Mungu! - Baada ya Yahwe kutenda hivi, alisema,9“Mimi mwenyewe nitatikisa mkono wangu juu yao, nao watakuwa mateka kwa watumwa wao.” Ndipo mtakapojua kwamba Yahwe wa majeshi amenituma.

10“Imba kwa furaha, binti Sayuni, kwa maana mimi mwenyewe nitakaa nawe! - Asema Yahwe

11Mataifa makubwa yataungana na Yahwe siku hiyo. “Nanyi mtakuwa watu wangu; kwa kuwa nitakaa kati yenu,” nanyi mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.12Kwa maana Yahwe ataimiliki Yuda kama miliki yake halali katika nchi takatifu, na kwa mara nyingine tena atauchagua Yerusalemu kwa ajili yake mwenyewe.13Nyamazeni, mbele za Yahwe, ninyi wote wenye mwili, maana ameinuka kutoka mahali patakatifu pake!

3

1Kisha Yahwe akanionesha Yoshua kuhani mkuu amesimama mbele za malaika wa Yahwe na Shetani amesimama mkono wake wa kushoto kumshitaki kwa ajili ya dhambi.2Malaika wa Yahwe akamwambia Shetani, “Yahwe na akukemee, Yahwe, aliyeuchagua Yerusalemu, akukemee! Je hiki si kinga kilichotolewa motoni”

3Yoshua alikuwa na mavazi machafu aliposimama mbele ya malaika.4Malaika akawaambia waliosimama mbele yake, “Mvueni hayo mavazi machafu.” Kisha akamwambia Yoshua, “Tazama! Nimeuondoa uovu wako na nitakuvika mavazi safi.”

5Haya wamvike kilemba safi kichwani!” Hivyo wakaweka kilemba safi kichwani pa Yoshua na wakamvika mavazi safi wakati malaika wa Yahwe amesimama kando.

6Kisha malaika wa Yahwe akamwagiza Yoshua na kusema,7Yahwe wa majeshi asema hivi: “Ikiwa utatembea katika njia zangu, na kutunza amri zangu, ndipo utakapoisimamia nyumba yangu na kulinda sheria zangu, kwa maana nitakuruhusu kwenda na kutoka kati ya wasimamao mbele zangu.

8WeweYoshua kuhani mkuu na wenzako wanaoishi nawe! Sikilizeni. Watu hawa ni ishara, kwa kuwa mimi mwenyewe nitamwinua mtumishi wangu aitwaye Tawi.9Tazameni jiwe nililoliweka mbele ya Yoshua. Kuna macho saba juu ya jiwe hili moja, nami nitaandika maneno juu yake - asema Yahwe wa majeshi - nami nitaondoa dhambi katika nchi hii kwa siku moja.

10Katika siku hiyo kila mtu atamwalika jirani yake kukaa chini ya mzabibu na mtini wake.” Asema Yahwe wa majeshi.

4

1Ndipo malaika aliyekuwa akiongea nami akageuka na kuniamsha kama mtu aamshwavyo usingizini.2Akaniuliza, “Unaona nini?” Nikasema, “Ninaona kinara cha taa kimetengenezwa kwa dhahabu tupu, na bakuli juu yake. Kina taa saba juu yake na mirija mmoja kwa kila taa.3Kando yake kuna mizeituni miwili, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.”

4Kisha nikamuuliza tena na malaika aliyeongea nami. “Mambo haya yana maana gani, Bwana wangu?”

5Naye akanijibu na kusema, Haujui mambo haya yanamaanisha nini?” Nikasema, “ndiyo sijui Bwana wangu.”

6Hivyo akaniambia, “Hili ni neno la Yahwe kwa Zerubabeli: lisemalo siyo kwa uwezo wala kwa nguvu, lakini ni kwa Roho wangu, asema Yahwe wa majeshi.7U nini wewe, mlima mrefu? Mbele ya Zerubabeli utakuwa tambarare, naye ataondoa jiwe la juu kwa kelele ya ‘Neema! Kwake!”

8Neno la Yahwe likanijia kusema,9“Mikono ya Zerubabeli imeweka misingi ya nyumba hii nayo itaimaliza. Ndipo mtakapojua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu.

10Ni nani aliyedharau siku ya mambo madogo? Watu hawa wataona jiwe la kupimia mkononi mwa Zerubabeli, nao watafurahi. (Taa saba ni macho ya Yahwe yanayozunguka duniani mwote.)”11Ndipo nilipomuuliza malaika, Mizeituni hii miwili isimamayo upande wa kushoto na kulia wa kinara cha taa ni nini?”12Nikauliza kwa mara nyingine tena, “Haya matawi mawili ya mizeituni kando ya mirija miwili ya dhahabu iliyo na mafuta ya dhahabu yanatiririka kutoka ndani yake?

13Naye akaniambia, “Hauvijui vitu hivi” nini?” Nami nikasema, “Hapana, Bwana wangu.”

14Akasema, “Hawa ni wawili waliopakwa mafuta wasimamao mbele ya Bwana wa dunia yote.”

5

1Kisha nikageuka na kuinua macho yangu, nami nikaona, tazama, gombo lirukalo!

2Malaika akaniuliza, “Unaona nini?” Nikajibu, “Ninaona gombo lirukalo, urefu wake dhiraa ishirini na upana wake dhiraa kumi.”

3Ndipo aliponiambia, “Hii ni laana iendayo juu ya uso wa nchi yote, kwani tangu sasa kila mwivi ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mmoja, wakati kila aapaye kiapo cha uongo ataondolewa kulingana na lisemavyo upande mwingine, kwa kadili ya maneno yake.4“Nitalituma - asema Yahwe wa majeshi - hivyo litaingia nyumbani mwa mwivi na nyumbani mwa aapaye kwa uongo kwa jina langu. Litasalia nyumbani mwake na kuteketeza mbao na mawe yake.”

5Ndipo malaika aliyekuwa akisema nami alipoenda nje na kuniambia, “Inua macho yako uone kinachokuja!”

6Nikasema, “Ni nini hiki?” Akasema, “Hiki ni kikapu kilicho na efa ijayo. Huu ni uovu wao katika nchi yote.”

7Kisha mfuniko wa risasi ukainuliwa kutoka ndani ya kikapu na kulikuwa na mwanamke chini yake amekaa ndani yake!8Malaika akasema, “Huu ni uovu!” na akamtupa tena kikapuni, na kurusha mfuniko wa risasi mlango pake.

9Nilipoinua macho nikaona wanawake wawili wakija kwangu, na upepo ulikuwa ndani ya mabawa yao - walikuwa na mabawa kama mabawa ya korongo. Wakainua kikapu kati ya mbingu na nchi.

10Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, “Wanapeleka wapi kikapu?”

11Akaniambia, “Wanakwenda kujengea hekalu katika nchi ya Shinari kwa ajili yake, hekalu litakapokuwa tayari, kikapu kitawekwa kwenye msingi ulioandaliwa kwa ajili yake.”

6

1Kisha nikageuka na kuinua macho na nikaona vibandawazi vinne vya farasi vikija kutoka kati ya milima miwili; na milima hiyo ilikuwa imetengenezwa kwa shaba.2Kibandawazi cha kwanza kilikuwa na farasi wekundu, kibandawazi cha pili kilikuwa na farasi weusi,3kibandawazi cha tatu kilikuwa na farasi weupe, na kibandawazi cha nne kilikuwa na farasi wa kijivu.4Hivyo nikamwuliza malaika aliyesema nami, “Ni vitu gani hivi bwana wangu?”

5Malaika akajibu na kuniambia, “Hizi ni pepo nne za mbinguni zisimamazo mbele ya Bwana wa dunia yote.6Lenye farasi weusi linakwenda nchi ya kaskazini; farasi weupe wanakwenda nchi ya magharibi; na farasi wa kijivu wanakwenda nchi ya kusini.”

7Farasi hawa wenye nguvu walitoka na wanatafuta kwenda na kuzunguka juu ya nchi, hivyo malaika akasema, “Nendeni na mzunguke juu ya nchi!” nao wakaenda juu ya dunia yote.

8Kisha akaniita na kuniambia, “Tazama wale wanaokwenda nchi ya kaskazini, wataituliza roho yangu juu nchi hiyo.”

9Hivyo neno la Yahwe likanijia kusema,10“Chukua sadaka kutoka kwa waliohamishwa - kutoka kwa Helidai, Tobiya na Yedaya - leo hii uende na kuipeleka katika nyumba ya Yosia mwana wa Zefania, aliyetoka Babeli.11Kisha uchukue fedha na dhahabu, ufanye taji na uivike katika kichwa cha Yoshua mwana wa Yehosadaki kuhani mkuu.12Ongea naye na useme, Yahwe wa majeshi asema hivi: Mtu huyu, jina lake Tawi! Naye atakuwa alipo na kisha atajenga hekalu la Yahwe!13Ndiye atakayejenga hekalu la Yahwe naye atauinua utukufu wake; kisha ataketi na kutawala katika kiti chake cha enzi. Atakuwa kuhani juu ya kiti cha enzi na ufahamu wa amani utakuwa kati ya vyote viwili.14Taji itawekwa hekaluni mwa Yahwe kwa heshima ya Heldai, Tobiya na Yedaya na kama kumbukumbu ya ukarimu wa mwana wa Zefania.15Ndipo walio mbali watakapokuja na kulijenga hekalu la Yahwe, hivyo mtajua kuwa Yahwe wa majeshi amenituma kwenu; kwani ikiwa kweli mnaisikiliza sauti ya Yahwe Mungu wenu hili litatendeka!”

7

1Mwaka wa nnwa utawala mfalme Dario, siku ya nne ya mwezi wa Kisleu (ambao ni mwezi wa tisa), neno la Yahwe lilimjia Zekaria kusema.2Watu wa Betheli wamemtuma Shareza, Regemu Meleki na watu wao kuomba mbele ya uso wa Yahwe.3Wakaongea na makuhani waliokuwa katika nyumba ya Yahwe wa majeshi na kwa manabii; wakasema, “Je niomboleze katika mwezi wa tano kwa njia ya kufunga, kama nilivyofanya miaka mingi hii?”

4Ndipo neno la Yahwe wa majeshi liliponijia kusema,5“Ongea na watu wote wa nchi na makuhani uwaambie, “Mlipofunga na kuomboleza katika mwezi wa tano na wa saba katika hii miaka sabini, je kweli mlifunga kwa ajili yangu?6Na mlipokula na kunywa, hamkula na kunywa kwa ajili yenu wenyewe?7Je hayo siyo maneno aliyosema Yahwe kwa vinywa vya manabii wa zamani, mlipokuwa bado mnaishi Yerusalemu na miji ya kandokando yenye mafanikio na iliyokaa Negebu, na upande wa magharibi chini ya vilima?”

8Neno la Yahwe likamjia Zekaria kusema,9“Yahwe wa majeshi asema hivi, ‘Hukumuni kwa haki, uaminifu wa agano, na rehema. Kila mtu na amtendee hivyo ndugu yake.10Juu ya mjane na yatima, mgeni, na masikini - usiwanyanyase, na asiwepo miongoni mwenu anayepanga madhara yoyote dhidi ya mwingine mioyoni mwenu.

11Lakini waliyashupaza mabega yao na hawakujali. Waliziba masikio yao ili wasisikie.12Waliifanya mioyo yao kuwa migumu kama mwamba ili wasiisikie sheria au neno la Yahwe wa majeshi. Alipeleka ujumbe kwa watu nyakati za zamani kwa Roho wake, kwa vinywa vya manabii. Lakini watu hawakusikia, hivyo Yahwe wa majeshi aliwakasirikia sana.

13Hata ikawa alipoita hawakusikia. Vilevile,” asema Yahwe wa majeshi, “wataniita, lakini sitasikiliza.14Kwa maana nitawatawanya kwa upepo wa kisurisuri katika mataifa yote ambayo hawajawai kuyaona, na baada yao nchi itakuwa wazi. Kwa kuwa hakuna hata mmoja atakayepita au kukaa katika hiyo nchi kwa kuwa wameigeuza nchi yao yenye kupendeza kuwa isiyofaa.

8

1Neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,2“Yahwe wa majeshi asema hivi: Nina huzuni kwa ajili ya Sayuni kwa wivu mkuu na ninamaumivu kwa hasira nyingi!

3Yahwe wa majeshi asema hivi: Nitairudia Sayuni nami nitakaa kati ya Yerusalemu, kwa kuwa Yerusalemu itaitwa mji wa kweli na mlima wa Yahwe wa majeshi utaitwa Mlima Mtakatifu!

4Yahwe wa majeshi asema hivi: Kwa mara nyingine tena kutakuwa na vikongwe katika mitaa ya Yerusalemu, na kila mtu atahitaji mkongojo mkononi mwake kwa vile alivyo mzee.5Pia mitaa ya mji itajazwa na vijana wa kiume na kike wachezao.

6Yahwe wa majeshi asema hivi: ikiwa jambo hili laonekana haliwezekani katika macho ya masalia ya watu hawa katika siku hizo, je haliwezekani pia machoni pangu? - Asema Yahwe.

7Yahwe wa majeshi asema hivi: Tazama, nipo tayari kuwaokoa watu wangu kutoka nchi ya mawio na ya machweo ya jua!8Kwa maana nitawarudisha tena, nao wataishi ndani ya Yerusalemu, hivyo watakuwa watu wangu tena, nami nitakuwa Mungu wao katika kweli na utakatifu!

9Yahwe wa majeshi asema hivi: Ninyi mnaoendelea kusikia maneno yaleyale yaliyotoka katika vinywa vya manabii msingi wa nyumba yangu ulipowekwa - hii nyumba yangu, Yahwe wa majeshi: Itieni nguvu mikono yenu ili hekalu lijengwe.10Kwani kabla ya siku hizo hakuna mazao yaliyokusanywa na yeyote ndani yake, hakukuwa na faida siyo kwa mtu hata mnyama, na hakukuwa na amani kutoka kwa adui kwa kila aliyekwenda au kuja. Nilimfanya kila mtu kuwa kinyume cha mwenzake.11Lakini sasa haitakuwa kama mwanzo, nitakuwa pamoja na masalia ya watu hawa - asema Yahwe wa majeshi.

12Kwani mbegu za amani zitapandwa; mzabibu unaokua utatoa mande, kwa maana nitawapa masalia ya watu hawa kumilki haya yote.13Ulikuwa mfano wa laana kwa mataifa mengine, enyi nyumba ya Yuda na nyumba ya Israeli. Hivyo nitawaokoa nanyi mtakuwa baraka. Msiogope; haya mikono yenu iwe na nguvu!

14Kwa maana Yahwe wa majeshi asema hivi: Kama nilivyopanga kuwatenda mabaya baba zenu walipochokoza hasira yangu - asema Yahwe wa majeshi - na wala sikujuta,15ndivyo nitakavyoazimia kuutenda mema tena Yerusalemu na nyumba ya Yuda katika siku hizi! Msiogope!16Haya ndiyo mambo mnayopaswa kufanya: Kasemeni kweli, kila mtu na jirani yake. Hukumuni kwa haki, usawa na amani katika malango yenu.17Na asiwepo miongoni mwenu anayefikri uovu moyoni mwake dhidi ya jirani yake, wala kuvutwa na viapo vya uongo; kwani haya yote ndiyo mambo ninayoyachukia! - Asema Yahwe.”

18Kisha neno la Yahwe wa majeshi likanijia kusema,19“Yahwe wa majeshi asema hivi: Mifungo ya mwezi wa nne, mwezi wa tano, mwezi wa saba na mwezi wa kumi itakuwa nyakati za furaha ya kila aina, kwa nyumba ya Yuda! Kwa hiyo pendeni kweli na amani!

20Yahwe wa majeshi asema hivi: Watu watakuja tena, hata wanaoishi miji mingine.21Watu wa mji mmoja watakwenda mji mwingine na kusema, “Haya twendeni haraka mbele ya Yahwe tukaombe na kumtafuta Yahwe wa majeshi! Sisi wenyewe tunakwenda pia.22Watu wengi na mataifa yenye nguvu yatakuja kumtafuta Yahwe wa majeshi huko Yerusalemu na kuomba upendeleo kwa Yahwe!

23Yahwe wa majeshi asema hivi: Katika siku hizo watu kumi kutoka katika kila lugha na taifa watashika upindo wa kanzu zenu, na kusema, “Haya sisi nasi tutakwenda pamoja nanyi, kwani tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.

9

1Hili ni tamko la neno la Yahwe kuhusu nchi ya Hadiraki na Damesiki. Kwa maana jicho la Yahwe liko juu ya wanadamu wote, na juu ya kabila zote za Israeli pia.2Azimio hili pia linaihusu Hamathi, inayopakana na Damesiki, na linahusu Tiro na Sidoni, japokuwa ni werevu sana.3Tiro amejijengea ngome na kurundika fedha kama mavumbi na dhahabu safi kama matope mitaani.4Tazama! Bwana atamnyang'anya na kuharibu nguvu zake juu ya bahari, kwa hiyo atateketezwa kwa moto.5Ashikeloni ataona na kuogopa! Gaza pia atatetemeka sana! Ekironi, tumaini lake litatikiswa! Mfalme ataangamizwa kuanzia Gaza, na Ashikeloni haitakuwa na watu tena!6Wageni watafanya makao yao katika Ashidodi, nami nitakiondoa kiburi cha Wafilisiti.7Kwani nitaondoa damu yao katika vinywa vyao na machukizo yao kutoka kati ya meno yao. Ndipo watakapokuwa masalia kwa Mungu wetu kama ukoo katika Yuda, na Ekironi atakuwa kama Wayebusi.8Nitaweka kambi kuzunguka nchi yangu kinyume cha majeshi ya adui hata hakuna atakayeweza kupita ndani yake tena, kwani hakuna mtesaji atakayeipita tena. Kwa kuwa sasa nitaangalia nchi yangu kwa macho yangu mwenyewe!9Pigakelele kwa furaha, ewe binti Sayuni! Piga kelele kwa shangwe, ewe binti Yerusalemu! Tazama! Mfalme wako anakuja kwako pamoja na uadilifu na anakuokoa. Ni mnyenyekevu, amepanda punda, mwanapunda.10Ndipo nitakapoondoa kibandawazi kutoka Efraimu na farasi kutoka Yerusalemu, na upinde utaondolewa katika vita; kwani atasema amani kwa mataifa, na utawala wake utakuwa kutoka bahari hata bahari, na kutoka katika mto hadi miisho ya dunia!11Lakini kwenu, kwa sababu ya damu ya agano langu nanyi, nitawaweka wafungwa wenu huru kutoka shimoni pasipo na maji.12Rudini ngomeni, wafungwa wa matumaini! Hata leo natamka kwamba nitawarudishia mara mbili, kwani nimempinda Yuda kama upinde wangu.13Hata nimelijaza podo langu pamoja na Efraimu. Nimewainua wana wenu, Sayuni, kinyume cha wana wenu, Ugiriki, na amekufanya wewe, Sayuni, kama upanga wa shujaa!14Yahwe atawatokea, na mishale yake itapiga kama radi! Kwa maana Yahwe Bwana wangu atapiga tarumbeta naye ataendelea pamoja na dhoruba kutoka Temani.15Yahwe wa majeshi atawatetea, nao watawararua na kuyashinda mawe ya kombeo. Ndipo watakapo kunywa na kupiga kelele kama mtu aliyelewa kwa mvunyo, nao watajazwa na mvinyo kama mabakuri, kama pembe za madhabahu.16Hivyo Yahwe Mungu wao atawaokoa siku hiyo; watakuwa kama kundi la kondoo lililo na watu wake, kwani watakuwa mapambo ya taji, yaliyoinuliwa juu ya nchi yake.17Jinsi gani watakavyokuwa wazuri na warembo! Vijana watastawi juu ya nafaka na bikira juu ya divai tamu!

10

1Mwombeni Yahwe mvua nyakati za kipupwe - Yahwe afanyaye mvua ya radi - naye hufanya mvua inyeshe kwa kila mmoja na uoto kondeni.2Kwani sanamu za wenye nyumba husema uongo; waganga hunena uongo; wanasema ndoto za udanganyifu na hutoa faraja tupu, hivyo wapotea kama kondoo na wanaumia kwa sababu hakuna mchungaji.3Gadhabu yangu inawaka dhidi ya wachungaji; ni mabeberu - viongozi - nitakao waadhibu. Yahwe wa majeshi atalihudumia pia kundi la kondoo wake, nyumba ya Yuda, na kuwafanya kama farasi wake wa vita!4Kutoka kwao litatoka jiwe kuu la pembeni; kutoka kwao kitatoka kigingi cha hema; kutoka kwao utatoka upinde wa vita; kutoka kwao watakuja viongozi wote kwa pamoja.5Watakuwa kama mashujaa wawakanyagao adui zao katika matope ya mitaani vitani; watafanya vita, kwa maana Yahwe yu pamoja nao, nao watawaabisha wapanda farasi wa vita.6Nitaitia nguvu nyumba ya Yuda na kuiokoa nyumba ya Yusufu; kwani nitawarejesha na kuwahurumia. Watakuwa kama nilikuwa sijawaondoa, kwani mimi ni Yahwe Mungu wao, nami nitawaitikia.7Ndipo Efraimu atakapokuwa kama shujaa, na mioyo yao itafurahi kama kwa mvinyo; wana wao wataona na kufurahi. Mioyo yao itanifurahia!8Nitawanong'oneza na kuwakusanya, kwani nitawaokoa, nao watakuwa wakuu kama walivyokuwa mwanzo!9Niliwapanda kati ya watu, lakini watanikumbuka katika nchi ya mbali, hivyo wao na wana wao wataishi na kurejea.10Kwa maana nitawarejesha kutoka nchi ya Misri na kuwakusanya kutoka Ashuru. Nitawaleta katika nchi ya Gileadi na Lebanoni mpaka kutakapokuwa hakuna nafasi tena kwa ajili yao.11Nitapita katika bahari ya mateso yao; nitayapiga mawimbi ya bahari hiyo na nitavikausha vilindi vyote vya Mto. Utukufu wa Ashuru utashushwa chini, na fimbo ya Misri itakwenda mbali kutoka kwa Wamisri.12Nitawatia nguvu mimi mwenyewe, nao watatembea katika jina langu, asema Yahwe.

11

1Fungua milango yako, ee Lebanoni, ili moto uteketeze mielezi yako!2Omboleza, enyi miti ya misonobari, kwani mierezi imeanguka! Kilichokuwa cha fahari kimeteketezwa! Ombolezeni, enyi mialoni ya Bashani, kwani msitu wenye nguvu umeshushwa.3Wachungaji wanapiga yowe, kwa kuwa utukufu wao umeharibiwa! Sauti ya mungurumo wa wana simba, kwa kuwa kiburi cha Mto Yordani kimeharibiwa!

4Hivi ndivyo asemavyo Yahwe Mungu wangu, “Lichungeni kundi la kondoo lililo tayari kuchinjwa!5(Wanaowanunua wanawachinja bila kuhadhibiwa, nao wawauzao husema, ‘Atukuzwe Yahwe! Nimetajirika! Kwa maana wachungaji wafanyao kazi kwa wenye kondoo hawawahurumii.)6Kwa maana hiyo sitawahurumia tena wenyeji wa nchi! - Hivi ndivyo asemavyo Yahwe. Tazama! Mimi mwenyewe nipo tayari kumwelekeza kila mtu katika mkono wa jirani yake na katika mkono wa mfalme wake, nao wataiharibu nchi na hakuna hata mmoja wao nitakayemwokoa kutoka katika mkono wao.”

7Hivyo nikawa mchungaji wa kondoo walioamriwa kuchinjwa, kwa wanaowashughulikia kondoo. Nilichukua fimbo mbili; fimbo moja nikaiita “Neema” na nyingine nikaiita “Umoja.” Kwa njia hii niliwachunga kondoo.8Ndani ya mwezi mmoja niliwaangamiza wachungaji watatu, kwa maana sikuwavumilia tena, wao pia walinichukia.

9Ndipo nilipowaambia wamiliki, “Sitafanya kazi kama mchungaji wenu tena. Kondoo wafao - na wafe; kondoo wanaoangamizwa - na waangamizwe. Na kondoo wasaliao kila mmoja ale nyama ya jirani yake.”

10Hivyo nikaichukua fimbo yangu “Neema” na nikaivunja kuvunja agano nililokuwa nimelifanya na kabila zangu zote.11Katika siku hiyo agano lilivunjwa, na wale wanaoshughulika na kondoo na waliokuwa wakiniangalia walifahamu kwamba Yahwe amesema.

12Nikawaambia, “Ikiwa itawapendeza, nilipeni ujira wangu. Kama sivyo, msifanye hivyo.” Hivyo wakapima ujira wangu - vipande thelathini vya fedha.

13Kisha Yahwe akaniambia, “Weka fedha katika hazina, thamani nzuri zaidi ambayo walikupa!” Hivyo nikachukua vipande thelathini vya fedha na kuviweka katika hazina ndani ya nyumba ya Yahwe.

14Kisha nikavunja fimbo yangu ya pili, “Umoja,” kuvunja undugu kati ya Yuda na Israeli.

15Yahwe akaniambia, “Tena, chukua chombo cha mchungaji mpumbavu kwa ajili yako mwenyewe,16kwa maana tazama, niko tayari kumuweka mahali mchungaji katika nchi. Hataangalia kondoo wanaoangamia. Hatatafuta kondoo wapoteao, wala kuwaponya kondoo wachechemeao. Hatawalisha kondoo wenye afya, lakini atakula nyama ya kondoo walionona naye atapasua kwato zao.17Ole kwa wachungaji wasiofaa wanaoliacha kundi la kondoo! Upanga na uje dhidi ya mkono wake na jicho lake la kulia! Mkono wake na ukauke na jicho lake la kulia lipofuke!

12

1Hili ni tamko la neno la Yahwe kwa Israeli - Bwana asema, azitandaye mbingu na kuweka msingi wa dunia, aiumbaye roho ya mtu ndani yake,2“Tazama, nitaifanya Yerusalemu kuwa kikombe kiwafadhaishacho watu wote wamzungukao. Itakuwa hivyo hivyo pia kwa Yuda wakati wa kuhusuriwa kwa Yerusalemu.3Katika siku hiyo, nitaifanya Yerusalemu kuwa jiwe zito kwa watu wa jamaa zote. Kila atakayejaribu kuliinua jiwe hilo atajiumiza sana, na mataifa yote ya dunia yatakusanyika kinyume cha mji huo.4Katika siku hiyo asema Yahwe - nitampiga kila farasi kwa ushangao na kila mpanda farasi kwa wenda wazimu. Nitaiangalia nyumba ya Yuda kwa upendeleo nami nitawapiga kwa upofu farasi wa majeshi.5Ndipo watawala wa Yuda watakapojisemea mioyoni mwao, ‘Wakaao Yerusalemu ndio nguvu yetu kwa sababu ya Yahwe wa majeshi, Mungu wao.’

6Katika siku hiyo nitawafanya watawala wa Yuda kuwa kama mitungi ya moto katika miti na kama miali ya moto kati ya nafaka isimamayo, kwani utateketeza watu wote walio karibu upande wao wa kulia na kushoto. Yerusalemu atakaa mahali pake tena.

7Yahwe ataziokoa hema za Yuda kwanza, ili kwamba utukufu wa nyumba ya Daudi na utukufu wa wale waishio Yerusalemu hautazidi sehemu iliyosalia ya Yuda.8Katika siku hiyo Yahwe atakuwa mtetezi wa wakao Yerusalemu, na siku hiyo waliodhaifu miongoni mwao watakuwa kama Daudi, wakati nyumba ya Daudi watakuwa kama Mungu, kama malaika wa Yahwe mbele yao.9“Itakuwa kwamba katika siku hiyo nitaanza kuyaharibu mataifa yote yajayo kinyume cha Yerusalemu.

10Lakini nitamwaga roho ya huruma na kuiombea nyumba ya Daudi na wakaao Yerusalemu, hivyo wataniangalia mimi, waliomchoma kwa mkuki. Wataniombolezea, kama amuombolezeaye mwana wa pekee; watamuombolezea kwa uchungu sana kama aombolezaye kifo cha mzaliwa wa kwanza.11Katika siku hiyo maombolezo huko Yerusalemu yatakuwa kama maombolezo ya Hadadi Rimoni katika tambarare za Megido.12Nchi itaomboleza, kila ukoo peke yao. Ukoo wa nyumba ya Daudi utakuwa peke yake na wake zao watakuwa peke yao mbali na wanaume. Ukoo wa nyumba ya Nathani utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume.13Ukoo wa nyumba ya Lawi utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume. Ukoo wa Washimei utakuwa peke yao na wake zao watakuwa peke yao mbali na waume.14Kila ukoo uliosalia - kila mmoja utakuwa peke yake na wake watakuwa pekee mbali na waume.

13

1Katika siku hiyo kijito kitafunguliwa kwa ajili ya nyumba ya Daudi na wenyeji wa Yerusalemu, kwa ajili ya dhambi na uchafu wao.

2Katika siku hiyo - asema Yahwe wa majeshi - kwamba nitaondoa majina ya sanamu katika nchi ili kwamba yasikumbukwe tena. Nitawaondoa pia katika nchi manabii wa uongo na roho wao mchafu3Ikiwa mtu yeyote ataendelea kutoa unabii, baba yake na mama yake waliomzaa watamwambia, ‘Hautaishi, kwa kuwa umenena uongo kwa jina la Yahwe! Ndipo baba na mama waliomzaa watakapomchoma wakati akitabiri.

4Katika siku hiyo kila nabii ataonea aibu maono yake aendapo kutoa unabii. Manabii hawa hawatavaa tena vazi la singa, ili kuwadanganya watu.5Kwa maana kila mmoja atasema, ‘Mimi siyo nabii! Mimi ni mkulima, kwa maana ardhi ndiyo kazi yangu tangu ujana wangu!6Lakini mtu mwingine atamwambia, ‘Majeraha haya kati ya mikono yako ni ya nini?’ naye atajibu, nilijeruhiwa na waliokuwa katika nyumba ya rafiki zangu.”

7Upanga! Inuka mwenyewe dhidi ya mchungaji wangu, mtu asimamaye karibu nami - hivi ndivyo asemavyo Yahwe wa majeshi. Mpige mchungaji, na kondoo watatawanyika! Kwa maana nitageuza mkono wangu dhidi ya wadogo.8Kisha itakuwa kwamba katika nchi yote - hivi ndivyo asemavyo Yahwe - kwamba theluthi mbili yake itaondolewa! Watu hao wataangamia; theluthi moja tu ndiyo itakayosalia.9Nitaipitisha hiyo ya tatu motoni na kuwasafisha kama fedha isafishwavyo; nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo. Wataliitia jina langu nami nitawajibu na kusema, ‘Hawa ni watu wangu!’ nao watasema, Yahwe ndiye Mungu wangu!”

14

1Tazama! Siku ya Yahwe inakuja wakati mateka wenu watakapogawanywa katikati yenu.

2Kwa maana nitayakusanya mataifa yote kinyume cha Yerusalemu kwa vita na mji utatekwa. Nyumba zitatekwa na wanawake watabakwa. Nusu ya mji itapelekwa matekani, lakini kumbukumbu ya watu haitaondolewa mjini.

3Lakini Yahwe ataondoka na kufanya vita dhidi ya mataifa kama apigavyo vita katika siku ya vita.4Siku hiyo miguu yake itasimama juu ya Mlima wa Mizeituni, uliopo kando ya Yerusalemu upande wa mashariki. Mlima wa Mizeituni utagawanyika katikati kati ya mashariki na magharibi kwa bonde kubwa sana na nusu ya mlima itarudi nyuma kuelekea kaskazini na nusu kuelekea kusini.5Ndipo mtakapokimbia katika bonde kati ya milima ya Yahwe, kwa kuwa bonde kati ya hiyo milima litafika hata Azali. Mtakimbia kama siku mliyokimbia tetemeko la nchi siku za Uzia, mfalme wa Yuda. Ndipo Yahwe Mungu wangu atakapokuja na watakatifu wake wote.

6Hakutakuwa na nuru katika siku hiyo, lakini hakuna baridi wala barafu.7Siku hiyo, siku aijuaye Yahwe peke yake, hakutakuwa tena na mchana wala usiku, kwani jioni itakuwa wakati wa nuru.

8Siku hiyo maji yaliyo hai yatatiririka kutoka Yerusalemu. Nusu yake yatatiririka kuelekea bahari ya mashariki na nusu bahari ya magharibi, wakati wa masika na wakati wa kiangazi.

9Yahwe atakuwa mfalme juu ya dunia yote. Katika siku hiyo kutakuwa na Yahwe, Mungu mmoja, na jina lake pekee.

10Nchi yote itakuwa kama Araba, kuanzia Geba hadi Rimoni kusini mwa Yerusalemu. Na Yerusalemu itaendelea kuwa juu. Ataishi mahali pake mwenyewe, kutoka lango la Benjamini hata mahali lilipokuwa lango la kwanza, hata Lango la Pembeni, na kutoka Mnara wa Hananeli hata shinikizo la mfalme.11Watu watakaa Yerusalemu na hakutakuwa na maangamizi kamili tena kutoka kwa Mungu dhidi yao. Yerusalemu itakuwa salama.

12Hii itakuwa tauni ambayo kwayo Yahwe atawapiga jamaa zote za watu wapigao vita juu ya Yerusalemu: miili yao itaoza hata wakiwa wamesimama kwa miguu yao. Macho yao yataoza katika matundu yake na ndimi zao zitaoza katika vinywa vyao.13Siku hiyo ile hofu kuu kutoka kwa Yahwe itakuwa miongoni mwao. Kila mmoja ataushika mkono wa mwingine, na mkono wa mwingine utainuliwa kinyume cha mkono wa mwenzake.14Yuda pia atapigana na Yerusalemu. Watakusanya utajiri wa mataifa yote yanayowazunguka - dhahabu, fedha, na wingi wa nguo safi.15Tauni itakuwa pia juu ya farasi na nyumbu, ngamia na punda, na kila mnyama katika kambi hizo atapigwa kwa hilo pigo.

16Kisha itakuwa wote watakaosalia katika mataifa yaliyo kinyume na Yerusalemu watakwenda mwaka kwa mwaka kumwabudu mfalme, Yahwe wa majeshi, na kutunza Sikukuu ya Vibanda.17Na itakuwa kwamba ikiwa mtu yeyote kutoka katika mataifa yote ya dunia haendi Yerusalemu kumwabudu mfalme, Yahwe wa majeshi, ndipo Yahwe hataleta mvua juu yao.18Na ikiwa nchi ya Misri hawatakwenda, ndipo hawatapata mvua. Tauni kutoka kwa Yahwe itayashambulia mataifa yote yasiyokwea kutunza Sikukuu ya Vibanda.19Hii itakuwa ni adhabu kwa Misri na adhabu kwa kila taifa lisilopanda kutunza Sikukuu ya Vibanda.

20Lakini katika siku hiyo, kengele za farasi zitasema, “Jitengeni kwa ajili ya Yahwe,” na makarai katika nyumba ya Yahwe yatakuwa kama mabakuri mbele ya madhabahu.21Kwa kuwa kila chungu katika Yerusalemu na Yuda kitatengwa kwa ajili ya Yahwe wa majeshi na kila mmoja aletaye sadaka atakula ndani yake na kuyachemshia. Hakutakuwa na wafanya biashara tena katika nyumba ya Yahwe wa majeshi siku hiyo.

Malaki

1

1Tamko la neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki.

2“Nilikupenda, “asema Bwana. Lakini unasema, “kwa jinsi gani ulinipenda?” Esau siyo ndugu yake Yakobo?” asema Bwana. “Na bado nampenda Yakobo,3lakini nimemchukia Esau. Nimeifanya milima yake kuwa ukiwa, na nimepafanya urithi wake kuwa makao ya mbweha wa jangwani.”

4Kama Edomu husema, “Tumepigwa, lakini tutarudi na kujenga palipoharibiwa; “Bwana wa Majeshi asama hivi, “Watajenga lakini nitaiangusha chini; na wanaume watawaita ‘Nchi ya uovu,’ na ‘Watu ambao Mungu ana hasira nao milele.”5Kwa macho yenu mtaona hili, na mtasema, “Bwana ni mkuu mbele ya mipaka ya Israel.”

6Mtoto amtii baba yake, na mtumwa amtii bwana wake. Ikiwa mimi, ni baba, iko wapi heshima yangu? Na kama mimi ni bwana, iko wapi heshima yangu? Bwana wa majeshi asema hivi kwenu, makuhani, mnaodharau jina langu. Lakini mnasema, ‘tumeridharauje jina lako?7Kwa kutoa mikate iliyonajisi madhabahuni kwangu. Na mnasema kuwa, ‘Tumekudharau kwa namna gani?’ Kwa kusema hivyo meza ya Bwana imedharauliwa.8Mkitoa sadaka ya wanyama vipofu, hiyo siyo dhambi? Na kama mkitoa vilema na wagonjwa, hiyo siyo dhambi? Pelekeni hili kwa liwali; atawakubali au atainua nyuso zetu?” asema Bwana wa Majeshi.

9Na sasa, mnajaribu kutafuta neema ya Mungu, ili kwamba awe mwema kwetu. “Na aina gani ya sadaka kwa sehemu yenu, ataziinua nyuso zenu? Asema Bwana wa Majeshi.

10Kama kungekuwa na mtu ambaye angefunga lango la Hekalu, ili kwamba kusiwepo na moto madhabahuni bure! Lakini sina radhi na ninyi, “asema Bwana wa majeshi, “na sitaikubali sadaka yeyote kutoka katika mikono yenu.11Kutoka mawio ya jua mpaka machweo jina langu litakuwa kuu katikati ya mataifa; katika kila sehemu uvumba utatolewa katika jina langu, na pia sadaka safi. Kwa sababu jina langu litakuwa kuu sana katikati ya mataifa,” asema Bwana wa majeshi.

12“Lakini ninyi mnachafua mnaposema meza ya Bwana mnainajisi, na matunda yake, na chakula chake kudharaurika.”13Na ninyi pia mwasema, “jambo hili limetuchosha, nanyi mnalidharau,” asema Bwana wa majeshi. “Mmerudisha kilichokuwa kimechukuliwa na wanyama wa mwitu au vilema au walio wagonjwa; na ndicho mnaleta kuwa sadaka zenu! Je naweza kuikubali hii mikononi mwenu?” asema Bwana.

14Alaaniwe aliye mdanganyifu, ambaye anaye mnyama dume katika kundi lake na akaahidi kunitolea, lakini bado anatoa kwangu, mimi Bwana, ambayo ni kiujanja ujanja; kwa kuwa mimi ni mfalme mkuu,” asema Bwana wa Majeshi, “na jina langu litaogopwa katika mataifa.”

2

1“Sasa, ninyi makuhani, amri hii ni kwa ajili yenu.2Kama hamtasikiliza, na kama hamtalichukua hili mioyoni mwenu na kunipa utukufu kwa jina langu,” asema Bwana wa Majeshi, Kisha nitatuma laana kwenu, na nitalaani baraka zenu. Kiukweli, nilishawalaani tayari, kwa sababu hujaweka sheria zangu moyoni.3Tazama, nitakikemea kizazi chako, na nitapaka mavi juu ya uso wako, mavi ya dhabihu zenu, na mtachukuliwa pamoja nayo.

4Na mtajua kwamba nimetuma hii sheria kwenu, kwamba agano langu litakuwa ni juu yangu na Lawi,” asema Bwana wa Majeshi.5Agano langu na yeye lilikuwa agano la uhai na amani, na nilimpa vitu hivi kama njia ya kuniheshimu. Aliniheshima na alisimama akawa na hofu kwa jina langu.6Mafundisho ya kweli yalikuwa kwenye kinywa chake, na uovu haukupatikana kinywani mwake. Alitembea na mimi kwa amani na unyofu, na aliwarudisha wengi kutoka dhambini.

7Kwa sababu midomo ya makuhani huhifadhi maarifa, na watu watatafuta maagizo kutoka kwenye kichwa chake, kwa sababu ni mjumbe wa Bwana wa Majeshi.

8Lakini umepita mbali na njia ya kweli. Umesababisha wengi kuwa na mashaka ya kutii sheria. Umeliharibu agano la Lawi,” asema Bwana wa Majeshi.9Kwa hiyo nimewafanya ninyi nanyi kudharauliwa mbele ya watu, kwa sababu hamkutunza njia zangu, lakini badala yake mnapendelea katika maagizo yenu.

10Sisi sote hatuna baba mmoja? Siyo Mungu yule mmoja aliyetuumba sote? Kwa nini tunafanyiana hila kila mtu na ndugu yake, mnaliharibu agano la baba zetu?

11Yuda amefanya hila na ameona kinyaa kwa vitu vilivyowekwa katika Israeli na Yerusalem. Yuda amenajisi mahali patakatifu pa Bwana ambapo anapapenda, na ameoa binti wa miungu migeni.12Mungu akukatilie mbali kutoka kwenye hema ya Yakobo na uzao wa mtu aliyefanya haya, hata yule anayeleta sadaka kwa Bwana wa Majeshi.

13Na wewe pia fanya hivyo. Unafunika madhabahu ya Bwana kwa machozi, kwa kilio na kuugua, kwa sababu hatakubali sadaka na kuzipokea kutoka mikononi mwako.14Lakini wasema, ni kwa sababu gani?” Kwa sababu Bwana amekuwa shahidi kati yako wewe na mke wako wa ujana wako, kinyume chake umekuwa si mwaminifu, ingawa yeye ni mwenzako na mke wa agano lako.

15Je yeye hakuwafanya kuwa mmoja, hata kwa sehemu ya roho yake? Sasa ni kwa nini aliwafanya ninyi kuwa mmoja? Kwa sababu alikuwa anategemea kupata watoto wacha Mungu. Kwa hiyo jiepushe mwenyewe ndani ya moyo wako, na asiwepo mtu asiye mwaminifu kwa mke wa ujana wake.

16“Nakuchukia kuachana,” asema Bwana, Mungu wa Israel, “afunikizaye nguo yake kwa udhalimu,” asema Bwana wa Majeshi. “Kwa hiyo jilinde ewe mwenyewe ndani ya roho yako na usiwe mtu asiye mwaminifu.”

17Mmemchosha Bwana na maneno. Lakini mwasema, “Tumekuchoshaje?” Kwa kusema Kila mmoja aliyefanya uovu ni mzuri kwa upande wa Bwana, na anafuraha nao;” au “Yuko wapi Mungu wa Haki?”

3

1Tazama, namtuma mjumbe wangu, atakaye andaa njia mbele yangu. Na Bwana, ambaye mnamtafuta, atakuja ghafla katika hekalu lake; na mjumbe wa agano, ambaye katika yeye mnafurahi, tazama anakuja.” Asema.” Bwana wa Majeshi.

2Nani nani atakeye vumilia siku ya kuja kwake? Ni nani atasimama akishatokea? Yeye ni kama mtu asafishaye kwa moto na kama sabuni ya kufulia.3Atakaa na kutawala kama msafishaji wa fedha, na atawasafisha wana wa Lawi. Na atawafanya wawe safi kama dhahabu na fedha, na wataleta sadaka za haki kwa Bwana.4Na sadaka ya Yuda na Yerusalem itampendeza Bwana, kama siku za kale, na miaka ya zamani.

5Kisha nitapita karibu na ninyi kuwahukumu. Na nitakuwa shahidi mwepesi dhidi ya wachawi, wazinzi, mashahidi wa uongo, na kinyume cha wale wanao onea wafanya kazi katika mizigo yake, wanao onea wajane na yatima, na anayemfukuza mgeni kutoka kwenye haki yake, na kwa wale wasionitii mimi,” asema Bwana wa majeshi.6Mimi Bwana, sibadiliki; pia ninyi, watu wa Yakobo, hamkutumia.7Toka siku za baba zenu mmegeukia mbali na amri zangu na hamkuzitunza. Nigeukieni, nami nitawarudia ninyi,”,” asema Bwana wa majeshi. Lakini mwasema, tutakurudiaje?8Mwanadamu anaweza kumwibia Mungu? Mnaniibia mimi, lakini mwasema, ‘Tumekuibiaje?’‘ kwa zaka na sadaka.9Mmelaaniwa kwa laana, kwa kuniibia mimi, taifa lote hili.10Leteni zaka kamili katika ghalani, ili kwamba kiwemo chakula katika nyumba yangu. Na mnijaribu kwa hili,” asema Bwana wa Majeshi. “Kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni na kuwamwagia baraka juu yenu, ili kwamba hakutakuwa na sehemu ya kutosha kuzipokea.11Nitamkemea mharibifu kwako, kwamba asiharibu mavuno yenu ya nchi yenu; mizazibu yenu katika shamba haitapukutisha kabla ya wakati wake,”,” asema Bwana wa Majeshi.12Mataifa yote watakuita mbarikiwa; kwa ajili yako itakuwa ni nchi ya furaha,” asema Bwana wa Majeshi.13“Maneno yenu yamekuwa magumu kinyume changu,” asema Bwana. “Lakini mwasema, ‘Tumesema nini kinyume chako?’

14Mmesema, ‘Hakuna maana kumtumikia Mungu. Kuna faida ya namna gani kutunza maagizo yake au kutembea huku mkiomboleza mbele za Bwana wa Majeshi?15Na sasa tunamwita mwenye kiburi mbarikiwa. Wahalifu si kufanikiwa tu, bali kumjaribu Mungu na kumuepuka.”

16Kisha wale wanao muheshimu Bwana walisemezana mmoja baada ya mwingine; Bwana yuko makini kutusikiliza, na kitabu cha kumbukumbu kiliandikwa mbele zake kwa ajili ya wale walio mwogopa Bwana na kuliheshimu jina lake.

17“Watakuwa wangu,” asema Bwana wa majeshi,” hazina zangu, katika siku nitakayotenda; nitawapenda, kama mtu anavyompenda mwanawe anayemhudumia.18Kisha zaidi sana nitatofautisha kati ya wenye haki na waovu, kati ya anayemwabudu Mungu na asiyemwabudu yeye.

4

1Tazama, siku inakuja, inawaka kama tanuru, ambayo wote wenye kiburi na wahalifu watakuwa mabua. Siku inakuja itawachoma,” asema Bwana wa Majeshi, “siku hiyo itaondoa mzizi au shina.2Lakini kwenu mnaoliogopa jina langu, jua la haki litawaangazia na uponyaji katika mbawa zake. Mtarukaruka kama ndama zizini.3Na waovu wote mtawakanyaga chini, watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu siku hiyo nitatenda,” asema Bwana wa Majeshi.

4Kumbukeni kutii sheria za mtumishi wangu Musa, amri na sheria nilizomwamuru huko Horebu, kwa Israeli wote.

5Tazama, nitamtuma Eliya nabii mbele yenu kabla ya siku kuu na yenye kutisha ya kuja kwa Bwana.6Atarudisha moyo wa baba kwa watoto, na mioyo ya watoto kwa baba zao; ili kwamba nisije nikaiangamiza nchi kwa uharibifu wote.”

Mathayo

1

1Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu.2Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake.3Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.4Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni.5Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese,6Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.7Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa.8Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.9Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia.10Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia.11Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.

12Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli.13Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori.14Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.15Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo.16Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo.

17Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.

18Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.19Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.20Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,” Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.21Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.”22Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema,23“Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli”-- maana yake, “Mungu pamoja nasi.”24Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe.25Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.

2

1Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, wataalamu wa nyota kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema,2“Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu.”

3Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.4Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, “Kristo atazaliwa wapi?”5Wakamwabia, “Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii,6Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli.”

7Hivyo Herode aliwaita wale watalaamu wa nyota kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana.8Akawatuma Bethelehem, akisema, “Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu.”

9Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa.10Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.11Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane.12Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.

13Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, “Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize.14Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri.15Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, “Kutoka Misri nimemwita mwanangu.”16Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watalaamu wa nyota, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watalaamu wa nyota.17Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia,
18“Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena.”

19Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema,20“Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa.”21Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.

22Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya23na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.

3

1Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema,2“Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu.”3Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, “Sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; ‘wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake.”’

4Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.5Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake.6Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.

7Lakini alipowaona wengi wa Mafarisayo na Masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, “Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?8Zaeni matunda yaipasayo toba.9Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, ‘Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.’ Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.10Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto.

11Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.12Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.

13Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana.14Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, “Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?”15Yesu akajibu akasema, “Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.” Kisha Yohana akamruhusu.

16Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake.17Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ninaye pendezwa sana naye.”

4

1Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.2Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa.3Mjaribu akaja na akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate.”4Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.’”5Kisha Ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu,6na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, ‘Ataamuru malaika wake waje wakudake,’ na, ‘watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe.’”7Yesu akamwambia, “Tena imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”

8Kisha, Ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote.9Akamwambia, “Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu.”10Kisha Yesu akamwambia, “Nenda zako Shetani! Kwa maana imeandikwa, ‘Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.’”11Kisha Ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.

12Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya.13Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.14Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya,
15“Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa!
16Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.”

17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, “Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.”

18Alipokuwa akitembea kandokando ya bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki.19Yesu akawaambia, “Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.”20Mara moja waliziacha nyavu zao na kumfuata.

21Na Yesu alipokwenda mbele kidogo, aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita,22na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.

23Yesu alikuwa akizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri injili ya ufalme, na akiponya kila aina ya maradhi na magonjwa miongoni mwa watu.24Habari zake zilienea Siria yote, na watu wakawaleta kwake wale wote waliokuwa wakiugua, wakiwa na maradhi mbalimbali na maumivu, waliokuwa na mapepo, na wenye kifafa na waliopooza. Yesu aliwaponya.25Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani.

5

1Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.2Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,

3“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5Heri wenye upole, maana watairithi nchi.
6Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.
7Heri wenye rehema maana hao watapata rehema.
8Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.
9Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.
12Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

13Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.14Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.15Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.16Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.

17Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza.18Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.19Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.20Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

21Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, ‘Usiue’ na ‘Yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.’22Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, ‘Wewe ni mtu usiyefaa!’ atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, ‘Wewe mjinga!’ atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.23Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako,24iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.25Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.26Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.

27Mmesikia imenenwa kuwa, ‘Usizini.’28Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.29Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.30Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa Jehanamu.

31Imenenwa pia, ‘Yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.’32Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.

33Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, ‘Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.’34Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu;35wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Yerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.

36Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.37Bali maneno yenu yawe, ‘Ndiyo, ndiyo, hapana, hapana.’ Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

38Mmesikia imenenwa kuwa, ‘Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.’39Lakini mimi namwambia, msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.40Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia.41Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.42Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.

43Mmesikia imenenwa, ‘Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.’44Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,45Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.46Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?47Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je, watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?48Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

6

1Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni.2Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.3Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia,4ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.

5Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao.6Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.7Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.8Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake.9Hivyo basi omba hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako.
10Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.
11Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku.
12Utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu.
13Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.’

14Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi.15Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

16Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.17Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako.18Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.

19Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba.20Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba.21Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.

22Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru.23Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani!

24Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.

25Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi?26Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?27Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake?

28Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha.29Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.30Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo?31Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, ‘Je tutakula nini?’ au ‘Je tutakunywa nini?’ au ‘Je tutavaa nguo gani?’32Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo.33Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako.34Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.

7

1Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa.2Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.3Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako?4Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako?5Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.

6Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.

7Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa.8Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa.

9Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake akimwomba kipande cha mkate atampa jiwe?10Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?11Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye?

12Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.

13Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo.14Njia ni jembamba, njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.

15Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbwa mwitu wakali.16Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti?17Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.18Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri.19Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto.20Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.

21Si kila mtu aniambiaye mimi, ‘Bwana, Bwana,’ ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.22Watu wengi wataniambia siku hiyo, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?’23Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!’

24Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba.25Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.26Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga.27Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika.”

28Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake,29kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.

8

1Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata.2Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, “Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi.”

3Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, “Niko tayari. Uwe msafi.” Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.4Yesu akamwambia, “Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao.”

5Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, jemedari akaja kwake akamuuliza6akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha.”

7Yesu akamwambia, “Nitakuja na kumponya.”

8Jemedari akajibu na kumwambia, “Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa.9Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu ‘Nenda,’ na huenda, na kwa mwingine ‘Njoo,’ na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, ‘Fanya hivi,’ na yeye anafanya hivyo.”

10Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, “Kweli ninawaambia, sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.11Ninawaambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahamu, Isaka, na Yakobo, katika ufalme wa mbinguni.12Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno.”13Yesu akamwambia jemedari, “Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako.” Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.

14Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa.15Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. Kisha akaamka akaanza kumhudumia.

16Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya.17Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, “Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu.”

18Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa bahari ya Galilaya.19Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda.”

20Yesu akamwambia, “Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake.”

21Mwanafunzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu.”

22Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao.”

23Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini.24Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala.25Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!”

26Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?” Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu,27wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, “Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?”

28Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile.29Tazama, walipaza sauti na kusema, “Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?”30Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa,31pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. “Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe.”

32Yesu akawaambia, “Nendeni!” Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.33Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo.34Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.

9

1Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi.2Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. Alipoiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, “Mwanangu, uwe na furaha, dhambi zako zimesamehewa.”

3Tazama, baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, “Huyu mtu anakufuru.”4Yesu akatambua mawazo yao na kusema, “Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu?5Kipi kilicho rahisi kusema, ‘Dhambi zako zimesamehewa’ au kusema, ‘Simama na utembee?’6Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi.” Aliyasema haya kwa yule aliyepooza, “Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako.”7Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake.8Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu.

9Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, “Nifuate mimi.” Naye akasimama na kumfuata.10Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake.

11Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi, “Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?”

12Yesu aliposikia hayo, naye alisema, “Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa.13Inawapasa muende mkajifunze maana yake, ‘Ninapenda rehema na siyo dhabihu,’ kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.”

14Ndipo wanafunzi wa Yohana wakaja kwake na kusema, “Kwa nini sisi na mafarisayo tunafunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?”

15Yesu akawaambia, “Je, wasindikizaji wa arusi wanaweza kuwa na huzuni pindi Bwana arusi anapokuwa pamoja nao? Lakini siku zinakuja ambapo Bwana arusi atachukuliwa kutoka kwao, na ndipo watakapofunga.

16Hakuna mtu anayeweka kipande cha nguo mpya kwenye nguo ya zamani, kiraka kitaipasua nguo na mpasuko mkubwa utatokea.17Hakuna watu wanaoweka mvinyo mpya katika chombo cha mvinyo wa zamani, ikiwa watafanya, ngozi itachanika, mvinyo utatoweka na ngozi itaharibika. Badala yake, huweka mvinyo mpya katika ngozi mpya na vyote vitakuwa salama.”

18Wakati Yesu alipokuwa akiwaambia mambo hayo, tazama, afisa akaja akasujudu mbele yake, naye akasema, “Binti yangu amefariki punde, lakini njoo na uweke mkono wako juu yake na yeye ataishi tena.”19Ndipo Yesu akasimama na kumfuata na wanafunzi wake pia.20Tazama, mwanamke ambaye alikuwa anatokwa damu kwa muda wa miaka kumi na miwili, akaja karibu na Yesu na akagusa sehemu ya pindo la vazi lake.

21Kwa kuwa alisema, “Endapo nitagusa vazi lake, nami nitapata uponyaji.”

22Yesu akageuka na kumtazama na kumwambia. “Binti, jipe moyo, imani yako imekufanya upone.” Na muda huo huo mwanamke akapata uponyaji.

23Na Yesu alipofika kwenye nyumba ya afisa, naye aliwaona wapiga tarumbeta na umati wa watu ulikuwa ukipiga kelele.24Naye akasema, “Tokeni hapa, kwa kuwa binti hajafa, bali amelala.” Lakini wao walicheka na kumkebehi.25Na wale watu walipotolewa nje, naye akaingia chumbani na kumshika mkono na msichana akaamka.26Na habari hizi zikaenea katika mji mzima.

27Ndipo Yesu alipokuwa akipita kutoka pale, wanaume wawili vipofu wakamfuata. Waliendelea kupaza sauti wakisema, “Tunaomba uturehemu, Mwana wa Daudi.”28Pindi Yesu apokuwa amefika kwenye nyumba, wale vipofu wakaja kwake. Yesu akawaambia, “Mnaamini kwamba ninaweza kutenda?” Nao wakamwambia “Ndiyo, Bwana.”

29Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Na ifanyike hivyo kwenu kama imani yenu ilivyo.”30Na macho yao yakafumbuka. Ndipo Yesu akasisitiza akawaamuru na kusema, “Angalieni mtu yeyote asifahamu kuhusu jambo hili.”31Lakini watu hawa wawili wakaondoka na kutangaza habari hizi sehemu zote za mji.

32Ndipo wale wanaume wawili walipokuwa wakienda zao, tazama, mtu mmoja bubu aliyepagawa na pepo akaletwa kwa Yesu.33Na pepo walipomtoka, yule mtu bubu akaanza kuongea. Umati ukashangazwa na kusema, “Hii haijawahi kutokea katika Israel.”

34Lakini Mafarisayo walikuwa wakisema, “Kwa wakuu wa pepo, anawafukuza mapepo.”

35Yesu akaenda kwenye miji yote na vijiji. Naye akaendelea kufundisha katika masinagogi, akihubiri injili ya ufalme, na kuponya magonjwa ya kila aina na udhaifu wa aina zote.36Wakati alipotazama umati, naye aliwaonea huruma, kwa sababu walisumbuka na kuvunjika moyo. Walikuwa kama kondoo wasio na mchungaji.37Naye akawaambia wanafunzi wake. “Mavuno ni mengi, lakini wafanya kazi ni wachache.38Hivyo basi upesi mwombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume wafanya kazi katika mavuno yake.”

10

1Yesu akawaita wanafunzi wake kumi na wawili pamoja na kuwapa mamlaka juu ya pepo wachafu, kuwakemea na kuwafukuza na kuponya aina zote za maradhi na aina zote za magonjwa.2Majina ya mitume kumi na wawili ni haya. La kwanza, Simeoni (ambaye pia anaitwa Petro), na Andrea kaka yake, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake:3Filipo, na Bartelemayo, Thomaso, na Mathayo mtoza ushuru, Yakobo mwana wa Alfayo, na Tadeo,4Simoni mkananayo, na Yuda Iskariote, ambaye alimsaliti.

5Hawa kumi na wawili Yesu aliwatuma. Naye aliwaelekeza akisema, “Msiende sehemu wanakoishi wamataifa na msiingie kwenye miji ya Wasamaria.6Badala yake, mwende kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israel.7Na mnapokwenda, hubirini na kusema, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’8Ponyeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma na fukuzeni pepo. Mmepokea bure, toeni bure.9Msichukue dhahabu, almasi au shaba kwenye pochi zenu.10Usichukue mkoba katika safari yenu, au nguo za ziada, viatu au fimbo, kwa kuwa mfanyakazi anastahili chakula chake.11Mji wowote au kijiji mtakachoingia, tafuteni ambaye anastahili na mkae pale mpaka mtakapoondoka.12Mtakapoingia katika nyumba salimieni.13Endapo nyumba inastahili, amani yenu ibaki pale, lakini kama nyumba haistahili, amani yenu iondoke pamoja nanyi.14Na kwa wale wasiowapokea ninyi au kusikiliza maneno yenu, wakati mnaondoka kwenye nyumba au mji huo, kung'uta mavumbi ya nyayo zenu mahali hapo.15Kweli ninawaambia, itakuwa ya kustahimili zaidi miji ya Sodoma na Gomorah siku ya hukumu kuliko mji huo.

16Angalia, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu, kwa hiyo iweni na werevu kama nyoka na wapole kama njiwa.17Muwe waangalifu na watu, watawapeleka kwenye mabaraza, na watawapiga kwenye masinagogi.18Na mtaletwa mbele ya wakuu na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao na kwa mataifa.19Pindi watakapowashutumu, msiwe na wasiwasi jinsi gani au nini cha kuongea, kwa kuwa kitu cha kusema mtapewa kwa wakati huo.20Kwa kuwa sio ninyi mtakaoongea, lakini Roho wa Baba yenu ataongea ndani yenu.21Ndugu atamwinukia ndugu yake kumwua, na baba kwa mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi, na kuwasababishia kifo.22Nanyi mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini yeyote atakayevumilia mpaka mwisho mtu huyo ataokolewa.23Pindi wanapowatesa katika mji huu, kimbilieni mji unaofuata, kwa kweli ninawaambia, hamtakuwa mmekwenda kwenye miji yote ya Israeli kabla ya Mwana wa Adam hajarudi.

24Mwanafunzi si mkuu kuliko mwalimu wake, wala mtumwa aliye juu ya Bwana wake.25Inatosha kwa mwanafunzi kwamba awe kama mwalimu wake, na mtumishi kama Bwana wake. Ikiwa wamemwita Bwana wa nyumba Belzabuli, ni kwa kiasi gani zaidi watawakashifu wa nyumba yake!

26Hivyo basi msiwahofu wao, kwa kuwa hakuna jambo ambalo halitafunuliwa, na hakuna lililofichika ambalo halitajulikana.27Kile ninachowaambia gizani, mkiseme nuruni, na mnachokisikia kwa ulaini masikioni mwenu, mkitangaze mkiwa juu ya nyumba.28Msiwaogope wale ambao wanaua mwili lakini hawana uwezo wa kuua roho. Badala yake, mwogopeni yule ambaye awezaye kuangamiza mwili na roho kule kuzimu.29Je kasuku wawili hawauzwi kwa senti ndogo? Hata hivyo hakuna anayeweza kuanguka chini bila Baba yenu kufahamu.30Lakini hata idadi ya nywele zenu zimehesabiwa.31Msiwe na hofu, kwa kuwa mnathamani zaidi kuliko kasuku wengi.32Hivyo basi kila mmoja atakaye nikiri mbele za watu, nami pia nitamkiri mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.33Lakini yeye atakaye nikana mbele za watu, nami pia nitamkana mbele ya Baba yangu aliye mbinguni.

34Msifikiri kwamba nimekuja kuleta amani duniani. Sikuja kuleta amani, lakini upanga.35Kwa kuwa nilikuja kumweka mtu apingane na baba yake, na binti dhidi ya mama yake, na mkwe dhidi ya mama mkwe wake.36Adui wa mtu watakuwa wale wa nyumbani mwake.37Yeye ambaye anampenda baba au mama zaidi kuliko mimi huyo hanistahili. Na yeye anayempenda kijana au binti zaidi kuliko mimi huyo hanistahili.38Yeye ambaye hatabeba msalaba na kunifuata mimi hanistahili.39Yeye atakayetafuta maisha atayapoteza. Lakini yeye atakayepoteza maisha kwa ajili yangu atayapata.

40Yeye atakayewakaribisha amenikaribisha mimi, na yeye atakayenikaribisha mimi amemkaribisha yeye aliyenituma mimi.41Na yeye atakayemkaribisha nabii kwa sababu ni nabii atapokea thawabu ya nabii. Na yeye atakayemkaribisha mwenye haki kwa sababu ni mtu wa haki atapokea thawabu ya mtu wa haki.42Yeyote atakayempatia mmoja wa wadogo hawa, hata kikombe cha maji ya kunywa ya baridi, kwa sababu yeye ni mwanafunzi, kweli ninawaambia, yeye hawezi kukosa kwa njia yeyote thawabu yake.”

11

1Ikawa baada ya Yesu kumaliza kuwaelekeza wanafunzi wake kumi na wawili aliondoka pale kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao.

2Na Yohana akiwa gerezani aliposikia habari juu ya matendo ya Kristo, alituma ujumbe kupitia wanafunzi wake,3na wakamuuliza, “Wewe ni yule ajaye, au kuna mwingine tunapaswa kumtazamia?”

4Yesu akajibu na kusema kwao “Nendeni mkamwambie Yohana yale mnayoyaona na yale mnayoyasikia.5Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wakoma wanatakaswa, viziwi wanasikia tena, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa habari njema.6Na amebarikiwa yule asiyeona shaka juu yangu.

7Wakati watu hawa walipoondoka, Yesu alianza kusema na umati juu ya Yohana, “Ni nini mlikwenda kuona katika jangwa, matete likitikiswa na upepo?8Lakini nini mlikwenda kuona huko, mtu aliyevaa mavazi mororo? Hakika, wale wavaao mavazi mororo hukaa katika nyumba za wafalme.9Lakini mliondoka kuona nini - Nabii? Ndiyo, nawaambia, na zaidi ya Nabii.10Huyu ndiye aliyeandikiwa, ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, ambaye ataandaa njia yako mbele yako.’

11Mimi nawaambia kweli, kati ya waliozaliwa na wanawake hakuna aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji. Lakini aliye mdogo katika ufalme wa mbinguni ni mkubwa kuliko yeye.12Toka siku za Yohana Mbatizaji mpaka sasa, ufalme wa Mbinguni ni wa nguvu, na watu wenye nguvu, huuchukua kwa nguvu.13Kwa kuwa manabii na sheria, walikuwa wakitabiri mpaka kwa Yohana.14Na kama mko tayari kukubali, huyu ni Eliya, yule ajaye.15Aliye na masikio ya kusikia na asikie.

16Nikifananishe na nini kizazi hiki? Ni mfano wa watoto wanaocheza maeneo ya sokoni, wanaokaa na kuitana17na kusema, ‘Tuliwapigia filimbi na hamkucheza. Tuliomboleza, na hamukulia.’18Kwa kuwa Yohana alikuja bila kula mkate au kunywa mvinyo, na wakawa wanasema, ‘Ana pepo.’19Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa na wakasema, ‘Angalia, ni mtu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!’ Lakini hekima inadhihirishwa kwa matendo yake.”

20Yesu alianza kuikemea miji ambamo baadhi ya matendo yake ya ajabu yalitendeka, kwa sababu walikuwa hawajatubu,21Ole wako, Kolazini, Ole wako Bethsaida! Kama matendo makuu yaliyofanyika kwenu yangefanyika Tiro na Sidoni, wangekuwa wametubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.22Lakini nawaambia itakuwa rahisi zaidi kwa Tiro na Sidoni kustahimili siku ya hukumu kuliko ninyi.23Wewe, Kapernaumu, unadhani utainuliwa hadi mbinguni? Hapana, utashushwa hadi chini kuzimu. Kama kwa Sodoma kungefanyika matendo makuu, kama yalifanyika kwako, ingekuwepo hadi leo.24Bali nasema kwako kwamba itakuwa rahisi kwa nchi ya Sodoma kusimama siku ya hukumu kuliko wewe.

25Katika muda huo Yesu alisema, “Nakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu uliwaficha mambo haya wenye hekima na ufahamu, na kuyaweka wazi kwa wasio na elimu, kama watoto wadogo.26Baba, kwa kuwa ilikupendeza hivyo machoni pako.

27Mambo yote yamekabidhiwa kwangu kutoka kwa Baba. Na hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba, na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana, na yeyote ambaye Mwana ana hamu ya kumfunulia.28Njooni kwangu, ninyi nyote mnaosumbuka na mnaolemewa na mzigo mzito, nami nitawapumzisha.29Jitieni nira yangu na mjifunze kutoka kwangu, kwa kuwa mimi ni mnyenyekevu na mpole wa moyo na mtapata pumziko la nafsi zenu.30Kwa kuwa nira yangu ni laini na mzigo wangu ni mwepesi.”

12

1Wakati huo Yesu alienda siku ya sabato kupitia mashambani. Wanafunzi wake walikuwa na njaa na wakaanza kuyavunja masuke na kuyala.2Lakini Mafarisayo walipoona hayo, wakamwambia Yesu, “Angalia wanafunzi wako wanavunja sheria wanatenda yasiyo ruhusiwa siku ya Sabato.”

3Lakini Yesu akawaambia, “Hamjasoma jinsi Daudi aliyoyafanya, wakati alipokuwa na njaa, pamoja na watu aliokuwa nao?4Namna alivyoingia ndani ya nyumba ya Mungu na kula mikate iliyowekwa wakfu, ambayo ilikuwa siyo halali kwake kuila na wale aliokuwa nao, ila halali kwa makuhani?5Bado hamjasoma katika sheria, kwamba katika siku ya Sabato makuhani ndani ya hekalu huiharibu Sabato, lakini hawana hatia?6Lakini nasema kwenu kuwa aliye mkuu kuliko hekalu yuko hapa.7Kama mngelifahamu hii ina maanisha nini, ‘Nataka rehema na siyo dhabihu,’ msingaliwahukumu wasio na hatia.8Kwa kuwa Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato.”

9Kisha Yesu akatoka pale akaenda katika sinagogi lao.10Tazama kulikuwa na mtu aliyepooza mkono. Mafarisayo wakamuuliza Yesu, wakisema. “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?” ili kwamba waweze kumshitaki kwa kutenda dhambi.

11Yesu akawaambia, “Nani kati yenu, ambaye ikiwa ana kondoo mmoja, na huyu kondoo akaanguka ndani ya shimo siku ya sabato, hatamshika na kumtoa kwa nguvu ndani ya shimo?12Je, ni kipi chenye thamani zaidi, kwani mtu si zaidi ya kondoo? Kwa hivyo ni halali kutenda mema siku ya Sabato.”13Kisha Yesu akamwambia yule mtu,” Nyosha mkono wako.” Akaunyosha, na ukapata afya, kama ule mwingine.14Lakini Mafarisayo wakatoka nje na wakapanga jinsi ya kumwangamiza, walienda nje kupanga kinyume chake. Walikuwa wakitafuta jinsi ya kumuua.

15Yesu alipojua hili aliondoka hapo. Watu wengi walimfuata, na akawaponya wote.16Aliwaagiza wasije wakamfanya ajulikane kwa wengine.17Kwamba itimie ile kweli, iliyokuwa imesemwa na nabii Isaya, akisema,
18“Tazama, mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, katika yeye nafsi yangu imependezwa. Nitaweka Roho yangu juu yake, na atatangaza hukumu kwa mataifa.
19Hatahangaika wala kulia kwa nguvu; wala awaye yote kusikia sauti yake mitaani.
20Hatalivunja tete lililochubuliwa; hatazima utambi wowote utoao moshi, mpaka atakapoleta hukumu ikashinda.
21Na mataifa watakuwa na ujasiri katika jina lake.”

22Mtu fulani kipofu na bubu, aliyepagawa na pepo aliletwa mbele ya Yesu. Akamponya, pamoja na matokeo ya kwamba mtu bubu alisema na kuona.23Umati wote walishangaa na kusema, “Yaweza mtu huyu kuwa mwana wa Daudi?”

24Lakini wakati Mafarisayo waliposikia muujiza huu, walisema, “Huyu mtu hatoi pepo kwa nguvu zake mwenyewe isipokuwa kwa nguvu za Belzebuli, mkuu wa pepo.”

25Lakini Yesu alijua fikra zao na kuwaambia, “Kila ufalme uliogawanyika wenyewe huharibika, na kila mji au nyumba inayogawanyika yenyewe haitasimama.26Ikiwa Shetani, atamwondoa Shetani, basi anajipinga katika nafsi yake mwenyewe.27Ni namna gani ufalme wake utasimama? Na kama natoa pepo kwa nguvu za Belizabuli, wafuasi wenu watatoa kwa nija ya nani? Kwa ajili ya hili watakuwa mahakimu wenu.28Na kama natoa pepo kwa nguvu za Roho wa Mungu, basi ufalme wa Mungu umekjua kwenu.

29Na mtu atawezaje kuingia ndani ya nyumba ya mwenye nguvu na kuiba, bila kumfunga mwenye nguvu kwanza? Ndipo atakapoiba mali yake kutoka ndani ya nyumba.

30Yeyote asiye kuwa pamoja nami yuko kinyume changu, naye asiye kusanya pamoja nami huyo hutawanya.

31Kwa hiyo nasema kwenu, kila dhambi na kufuru watu watasamehewa, ila kumkufuru Roho Mtakatifu hawatasamehewa.32Na yeyote asemaye neno kinyume cha Mwana wa Adamu, huyo atasamehewa. Lakini yeyote asemaye kinyume na Roho Mtakatifu, huyo hatasamehewa, katika ulimwengu huu, na wala ule ujao.

33Ama ufanye mti kuwa mzuri na tunda lake zuri, au uuharibu mti na tunda lake, kwa kuwa mti hutambulika kwa tunda lake.34Enyi kizazi cha nyoka, nyie ni waovu, mnawezaje kusema mambo mazuri? Kwa kuwa kinywa husema kutoka katika akiba ya yaliyomo moyoni.35Mtu mwema katika akiba njema ya moyo wake hutoka mema, na mtu mwovu katika akiba ovu ya moyo wake, hutoa kilicho kiovu.36Nasema kuwa katika siku ya hukumu watu watatoa hesabu ya kila neno lisilo na maana walilosema.37Kwa kuwa kwa maneno yako utahesabiwa haki na kwa maneno yako utahukumiwa.”

38Kisha baadhi ya waandishi na Mafarisayo walimjibu Yesu wakisema, “Mwalimu, tungependa kuona ishara kutoka kwako.”

39Lakini Yesu alijibu na kusema, “Kizazi kiovu na cha zinaa kinatafuta ishara. Lakini hakuna ishara itakayotolewa kwao isipokuwa ile ishara ya Yona nabii.40Kama vile nabii Yona alivyokuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu mchana na usiku, hivyo ndivyo Mwana wa Adam atakavyo kuwa ndani ya moyo wa nchi kwa siku tatu mchana na usiku.41Watu wa Ninawi watasimama mbele ya hukumu pamoja na kizazi cha watu hawa na watakihukumu. Kwa kuwa walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, mtu huyu mkuu kuliko Yona yuko hapa.42Malkia wa kusini atainuka kwenye hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki na kukihukumu. Alikuja toka miisho ya dunia kuja kusikia hekima ya Selemani, na tazama, mtu huyu mkuu kuliko Selemani yupo hapa.

43Wakati pepo mchafu amtokapo mtu, hupita mahali pasipo na maji akitafuta kupumzika, lakini hapaoni44Kisha husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu niliyotoka.’ Arudipo hukuta ile nyumba imesafishwa na iko tayari.45Kisha huenda na kuwaleta wengine roho wachafu saba walio wabaya zaidi kuliko yeye, huja kuishi wote pale. Na hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza. Hivyo ndivyo itakavyo kuwa kwa kizazi hiki kiovu.”

46Wakati Yesu alipokuwa akizungumza na umati tazama, mama yake na ndugu zake walisimama nje, wakitafuta kuongea naye.47Mtu mmoja akamwambia, “Tazama mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanatafuta kuongea nawe.”

48Lakini Yesu alijibu na kumwambia aliyemjulisha, “Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani?”49Naye alinyoosha mkono wake kwa wanafunzi na kusema, “Tazama, hawa ni mama na ndugu zangu!50Kwa kuwa yeyote afanyae mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, mtu huyo ndiye ndugu yangu, dada yangu na mama yangu.”

13

1Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.2Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama pembeni ya bahari.3Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano. Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda.4Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.5Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.6Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.7Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini.9Aliye na masikio na asikie.

10Wanafunzi walikuja na kumwambia Yesu, “Kwa nini unazungumza na umati kwa mifano?”

11Yesu alijibu kusema, “Mmepewa upendeleo wa kujua siri za ufalme wa mbinguni, bali kwao hawajapewa.12Lakini yeyote aliyenacho, kwake yeye ataongezewa zaidi, na atapata faida kubwa. Ila asiye nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa.13Hivyo naongea nao kwa mifano kwa sababu ingawa wanaona, wasione kweli. Na ingawa wanasikia wasisikie wala kujua.14Unabii wa Isaya umetimia kwao, ule usemao, ‘Msikiapo msikie, lakini kwa namna yoyote hamtaelewa; wakati mwonapo mwaweza kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue.

15Na mioyo ya watu hawa imekuwa giza, ni vigumu kusikia, na wamefumba macho yao, ili wasiweze kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao, au kufahamu kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena, na ningewaponya.’

16Bali macho yenu yamebarikiwa, kwa kuwa yanaona, na masikio yenu kwa kuwa yanasikia.17Hakika nawaambia manabii wengi na watu wenye haki walikuwa na hamu ya kuyaona mambo yale myaonayo, na hawakuweza kuyaona. Walitamani kusikia mambo yale mnayosikia, hawakuyasikia.

18Sasa sikilizeni mfano wa mpanzi.19Wakati wowote asikiapo neno la ufalme na asilielewe, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kuwekwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.20Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.21Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.22Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.23Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.”

24Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, “Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake.25Lakini watu walipolala, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake.26Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia.27Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, ‘Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu?’

28Akawaambia, ‘Adui ametenda hili.’ Watumishi walimwambia, ‘Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?’

29Mwenye shamba akasema, ‘Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano.30Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, ‘Kwanza yang'oeni magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.’”

31Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake.32Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”

33Akawaambia mfano mwingine tena. “Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke.”

34Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao.35Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, “Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu.”

36Kisha Yesu aliwaacha umati na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.”

37Yesu alijibu na kusema, “Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.38Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni Ibilisi.39Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.40Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu.41Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi.42Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.43Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na asikie.

44Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba.

45Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani.46Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.

47Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina.48Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali.49Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki.50Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno.

51Mmefahamu mambo yote haya?” Wanafunzi walimjibu, “Ndiyo.”

52Kisha Yesu akawaambia, “Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

53IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo.54Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, “Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?55Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda?56Na dada zake tunao hapa kwetu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?”

57Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, “Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao.”58Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.

14

1Kwa wakati huo, Herode alisikia habari juu ya Yesu.2Akawaambia watumishi wake, “Huyu ni Yohana Mbatizaji amefufuka kutoka katika wafu. Kwa hiyo nguvu hizi zipo juu yake.”

3Kwa kuwa Herode alikuwa amemkamata Yohana akamfunga na kumtupa gerezani kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo kaka yake.4Kwa kuwa Yohana alimwambia, “Si halali kumchukua yeye kuwa mke wake.”5Herode angemwua lakini aliwaogopa watu kwa sababu walimwona Yohana kuwa nabii.

6Lakini wakati siku ya kuzaliwa Herode ilipofika binti wa Herodia alicheza katikati ya watu na kumpendeza Herode.7Katika kujibu aliahidi kwa kiapo kwamba atampa chochote atakachoomba.8Baada ya kushauriwa na mama yake, alisema, “Nipe mimi hapa katika kombe kichwa cha Yohana Mbatizaji.”9Mfalme alikuwa na sikitiko kwa maombi ya binti, lakini kwa ajili ya kiapo chake, kwa sababu ya wote waliokuwa chakulani pamoja naye aliamuru kwamba inapaswa ifanyike.10Alituma Yohana aletwe kutoka gerezani11ili akatwe kichwa chake na kikaletwa juu ya sinia na akapewa binti na akakipeleka kwa mama yake.12Kisha wanafunzi wake wakaja kuuchukua ule mwili na kuuzika, baada ya hili walienda kumwambia Yesu.13Naye Yesu aliposika haya, akijatenga kutoka mahali pale akapanda ndani ya mashuka akaenda sehemu iliyotengwa. Wakati umati ulipo fahamu alikokuwa, walimfuata kwa miguu kutoka mijini.14Kisha Yesu alikuja mbele yao akauona umati mkubwa. Akawaonea huruma na kuponya magonjwa yao.

15Jioni ilifika, wanafunzi wakaja kwake na kusema, “Hii ni sehemu ya jangwa, na siku tayari imepita. Watawanyishe makutano ili waende vijijini wakanunue chakula kwa ajili yao.

16Lakini Yesu akawaambia, “Hawana haja ya kwenda zao. Wapeni ninyi chakula”

17Wakamwambia, “Hapa tunayo mikate mitano na samaki wawili tu.”

18Yesu akasema, “Ileteni kwangu.”19Kisha Yesu akauamuru umati kukaa chini kwenye nyasi. Akachukuwa mikate mitano na samaki wawili. Akatazama juu mbinguni, akabariki na kumega mikate akawapa wanafunzi. Wanafunzi wakaupatia umati.20Wakala wote na kushiba. Kisha wakavikusanya vipande vyote vya chakula na kujaza vikapu kumi na mbili.21Wale waliokula walikadiriwa kuwa wanaume elfu tano bila ya kusehabu wanawake na watoto.

22Mara moja aliwaamuru wanafunzi waingie ndani ya mashua, wakati huo yeye akawaaga umati waende zao.23Baada ya kuwaaga umati kwenda zao, akapanda juu mlimani kuomba pekee yake. Wakati ilipokuwa jioni alikuwa huko pekee yake.24Lakini sasa mashua ilipokuwa katikati ya bahari ukiyumbayumba kwa sababu ya mawimbi, kwani upepo ulikuwa wa mbisho.25Katika usiku wa zamu ya nne Yesu aliwakaribia, akitembea juu ya maji.26Wakati wanafunzi wake walipomwona akiitembea juu ya bahari, walihofu na kusema, “Ni mzuka,” na kupaza sauti katika hali ya uoga.27Yesu akawaambia mara moja, akisema, “Jipeni moyo! Ni mimi! Msiogope.”

28Petro alimjibu kwa kusema, “Bwana, kama ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.”

29Yesu akasema, “Njoo.” Hivyo Petro akatoka ndani ya mashua na akatembea juu ya maji kwenda kwa Yesu.30Lakini Petro alipoona mawimbi, aliogopa, na kuanza kuzama, chini, akaita sauti na kusema, “Bwana, niokoe!”

31Haraka Yesu akanyoosha mkono wake akamnyanyua Petro, na kumwambia, “Wewe mwenye imani ndogo, kwa nini ulikuwa na mashaka?”32Ndipo Yesu na Petro walipoingia katika mashua, upepo ulitulia kuvuma.

33Wanafunzi mashuani wakamwabudu Yesu na kusema, “Kweli wewe ni Mwana wa Mungu.”

34Na walipokwisha kuvuka, walifika katika nchi ya Genesareti.35Na watu katika eneo lile walipomtambua Yesu, walituma ujumbe kila sehemu za kando, na kuleta kila aliyekuwa mgonjwa.

36Walimsihi kwamba waweze kugusa pindo la vazi lake, na wengi walioligusa waliponywa.

15

1Ndipo Mafarisayo na waadishi walikuja kwa Yesu kutoka Yerusalemu. Na kusema,2“Kwa nini wanafunzi wanayaharibu mapokeo ya wazee? Kwa kuwa hawanawi mikono yao wanapokuwa wanakula chakula.”

3Yesu akawajibu na kusema, “Nanyi, kwa nini mnaiharibu sheria ya Bwana kwa ajili ya mapokeo yenu?4Kwa kuwa Mungu alisema, ‘Mheshimu baba yako na mama yako;’ na ‘Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.’

5Lakini ninyi husema, ‘Kila amwambiaye baba yake na mama yake, ‘Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kwa Mungu,”6Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitoa neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.7Enyi wanafiki, ni vema kama Isaya alivyo tabiri juu yenu aliposema,8‘Watu hawa wananiheshimu mimi kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali nami.9Wananiabudu bure, kwa sababu wanafundisha mafundisho yaliyo maagizo ya wanadamu.”’

10Ndipo akawaita umati na kuwaambia, “Sikilizeni na muelewe.11Hakuna kitu kiingiacho mdomoni mwa mtu na kumfanya najisi. Bali, kile kitokacho kinywani, hiki ndicho kimfanyacho mtu kuwa najisi.”

12Ndipo wanafunzi wakamfuata na kusema na Yesu, “Je! Unafahamu Mafarisayo walipolisikia lile neno walikwazika?”13Yesu aliwajibu na kusema, “Kila mmea ambao Baba yangu wa mbinguni hajaupanda utang'olewa.14Waacheni pekee, wao ni viongozi vipofu. Kama mtu kipofu atamuongoza kipofu mwenzake, wote wawili wataanguka shimoni.”

15Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Tuelezee mfano huu kwetu.”

16Yesu akajibu, “Nanyi pia bado hamuelewi?17Ninyi hamuoni kuwa kila kiendacho mdomoni hupitia tumboni na kwenda chooni?18Lakini vitu vyote vitokavyo mdomoni hutoka ndani ya moyo. Ndivyo vitu vimtiavyo mtu unajisi.19Kwa kuwa katika moyo hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati, wizi, ushuhuda wa uongo, na matusi.20Haya ndiyo mambo yamtiayo mtu unajisi. Lakini kula bila kunawa mikono hakumfanyi mtu kuwa najisi.”

21Ndipo Yesu akatoka mahali pale na akajitenga kuelekea pande za miji ya Tiro na Sidoni.22Tazama akaja mwanamke Mkanani kutoka pande hizo. Akapaza sauti akisema, “Nihurumie, Bwana, Mwana wa Daudi; binti yangu anateswa sana na pepo.”

23Lakini Yesu hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakaja wakimsisitiza, wakisema, “Muondoe aende zake, maana anatupigia kelele.”

24Yesu aliwajibu na kusema, “Sikutumwa kwa mtu yeyoye isipokuwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.”

25Lakini alikuja na kuinama mbele yake, akisema, “Bwana nisaidie.”

26Alimjibu na kusema, “Siyo vema kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

27Akasema, “Ndiyo, Bwana, hata hivyo mbwa wadogo hula chakula kiagukacho mezani mwa Bwana wao.”

28Ndipo Yesu akajibu na akisema, “Mwanamke, imani yako ni kubwa. Na ifanyike kwako kama utakavyo.” Na binti yake alikuwa ameponywa katika wakati huo.

29Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko.30Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya.31Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.

32Yesu akawaita wanafunzi wake na kusema, “Nimewaonea huruma umati, kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu bila kula kitu chochote. Sitawaaga waende kwao bila kula, wasije wakazimia njiani.”

33Wanafunzi wake wakamwambia, “Ni wapi tunaweza kupata mikate ya kutosha hapa nyikani kushibisha umati mkubwa hivi?”34Yesu akawaambia, “Mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba, na samaki wadogo wachache.”

35Yesu akawaamuru umati uketi chini.36Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati.37Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba.38Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto.

39Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.

16

1Mafarisayo na Masadukayo walimjia na kumjaribu Yesu awaonyeshe ishara inayotoka angani.

2Lakini Yesu aliwajibu na kuwaambia kuwa “Ikiwa ni jioni mnasema kuwa hali ya hewa ni nzuri, kwa kuwa anga ni jekundu.3Na asubuhi mnasema ‘Hali ya hewa leo si nzuri kwa kuwa anga ni jekundu na mawingu yameifunika anga yote.’ Mnajua kufafanua mwonekano wa anga, lakini hamwezi kufafanua ishara za nyakati.4Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakuna ishara yoyote kitakachopewa, isipokuwa ile ya Yona.” Kisha Yesu akawaacha na akaenda zake.

5Wanafunzi wakaja upande wa pili, lakini walikuwa wamesahau kuchukua mikate.6Yesu akawaambia “Jitahadharini na iweni makini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”

7Wanafunzi wakahojiana miongoni mwao na kusema. “Ni kwa sababu hatukuchukua mikate.”

8Yesu alitambua hilo na kusema, “Enyi wenye imani ndogo, kwa nini mmewaza na kusemezana miongoni mwenu na kusema kuwa ni kwa sababu hamkuchukua mikate?9Je bado hamtambui wala hamkumbuki ile mikate mitano kwa watu elfu tano, na vikapu vingapi mlivyokusanya?10Au mikate saba kwa watu elfu nne, na ni vikapu vingapi mlichukua?11Imekuwaje kuwa hata hamuelewi ya kuwa nilikuwa sizungumzi nanyi juu ya mikate? Jitunzeni na jihadharini na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”12Kisha wakatambua kuwa alikuwa hawaambii juu ya kujihadhari na mikate iliyo na chachu, bali kujihadhari na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

13Wakati Yesu alipofika sehemu za Kaisaria ya Filipi, akawauliza wanafunzi wake, akisema, “Watu wanasema kuwa Mwana wa Adamu ni nani?”

14Wakasema, “Wengine husema kuwa ni Yohana Mbatizaji; wengine, Eliya; na wengine, Yeremia, au mojawapo wa manabii.”

15Akawaambia, “Ninyi mwasema mimi ni nani?”

16Kwa akijibu, Simoni Petro akasema, “Wewe ni Kristo Mwana wa Mungu aliye hai.”

17Yesu akamjibu na kumwambia, “Umebarikiwa wewe, Simoni Bar Yona, kwa kuwa damu na nyama havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.18Nami pia ninakwambia kuwa wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu. Milango ya kuzimu haitalishinda.19Nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni. Chochote utakachokifunga duniani kitakuwa kimefungwa mbinguni, na chochote utakachokifungua duniani kitafunguliwa na mbinguni.”20Kisha Yesu akawaamuru wanafunzi wasimwambie mtu yeyote kuwa yeye alikuwa ni Kristo.

21Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu.22Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, na kusema, “Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako.”

23Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu Shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu.”

24Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kama mtu yeyote akitaka kunifuata mimi, ni lazima ajikane yeye mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.25Kwa kuwa anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na kwa yeyote anayepoteza maisha yake kwa ajili yangu atayaokoa.26Je! Ni faida gani atakayopata mtu akipata dunia yote lakini akapoteza maisha yake? Je! Ni kitu gani atakachotoa mtu katika kubadilishana na maisha yake?27Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake na malaika wake. Naye atamlipa kila mtu kulingana na matendo yake.28Kweli nawaambieni kuna baadhi yenu mliosimama hapa ambao hawataonja mauti mpaka watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.”

17

1Siku sita baadaye Yesu aliwachukua pamoja naye Petro, na Yakobo, na Yohana nduguye, na akawachukua mpaka juu ya mlima mrefu wao wenyewe.2Alibadilishwa mbele yao. Uso wake ukang'aa kama jua, na nguo zake zilionekana zenye kung'aa kama nuru.3Tazama, pale walitokea Musa na Eliya wakiongea naye.4Petro akajibu na kumwambia Yesu, “Bwana, ni vema kwetu sisi kuwepo mahali hapa. Kama ukitamani, nitajenga hapa vibanda vitatu - kimoja chako, na kimoja kwa ajili ya Musa, na kimoja kwa ajili ya Eliya.”

5Wakati anaongea, tazama wingu jeupe likawatia kivuli, na tazama, ikatokea sauti toka kwenye wingu, ikisema, “Huyu ni Mwanangu mpendwa ninayependezwa naye. Msikilizeni.”6Wanafunzi waliposikia hayo, wakaanguka kifudifudi na wakaogopa sana.

7Kisha Yesu akaja akawagusa na kusema, “Inukeni wala msiogope.”8Nao wakainua nyuso zao juu lakini hawakumwona mtu isipokuwa Yesu pekee.

9Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akasema, “Msitoe habari ya maono hayo mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka katika wafu.”

10Wanafunzi wake wakamwuliza, wakisema, “Ni kwa nini waandishi wanasema kuwa Eliya atakuja kwanza?”

11Yesu akawajibu na kusema, “Eliya atakuja kweli na atarudisha mambo yote.12Lakini naawaambieni ninyi, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua. Badala yake, walimfanyia mambo watakayo wao. Na hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyoteswa katika mikono yao.”13Ndipo wanafunzi wakatambua kuwa alikuwa akiongea habari za Yohana Mbatizaji.

14Walipofika katika umati, mtu mmoja alimwendea, akapiga magoti mbele zake, na kumwambia,15“Bwana, umhurumie mwanangu, maana amekuwa na kifafa na kuteseka sana. Kwa kuwa mara nyingi huanguka motoni au kwenye maji.16Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini hawakuweza kumponya.”

17Yesu akajibu akisema, “Enyi Kizazi kisichoamini na kilichoharibika, nitakaa pamoja nanyi mpaka lini? Nitavumiliana nanyi hata lini? Mlete hapa kwangu.”18Yesu alimkemea, na pepo akamtoka. Kijana aliponywa tangu saa ile.

19Kisha wanafunzi wakamjia Yesu kwa siri na kumwuliza, “Kwa nini hatukuweza kumfukuza?”

20Yesu akawaambia, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Kweli nawaambieni, kama mtakuwa na imani hata ndogo kama punje ya mbegu ya haradali, mtaweza kuuambia mlima huu, hama kutoka hapa uende kule, nao utahama na hakutakuwa na kitu chochote cha kushindikana kwenu.211

22Wakati wakiwa bado Galilaya, Yesu akawaambia Wanafunzi wake, “Mwana wa Adamu atatiwa mikononi mwa watu.23Na watamwua, na siku ya tatu atafufuka.” Wanafunzi walihuzunika sana.

24Nao walipofika Kapenaumu, watu wakusanyao kodi ya nusu shekeli wakamwendea Petro na kusema, “Je mwalimu wenu hulipa kodi ya nusu shekeli?”25Akasema, “Ndiyo” Lakini Petro alipoingia ndani ya nyumba, Yesu akaongea na Petro kwanza na kusema, “Unafikiria nini Simoni? Wafalme wa dunia, hupokea kodi au ushuru kutoka nani? Kwa wale wanaowatawala au kutoka kwa wageni?

26Na wakati Petro aliposema, “Kutoka kwa wageni” Yesu akamwambia, hivyo watawaliwa wameondolewa katika ulipaji.27Lakini tusije tukawafanya watoza ushuru wakatenda dhambi, nenda baharini, tupa ndoano, na umtwae yule samaki ajaye kwanza. Baada ya kuufungua mdomo wake, utakuta mle shekeli moja. Ichukue na uwape watoza ushuru kwa ajili yangu na wewe.


1Zingatia: Maneno ya msitari wa 21 “Lakini, aina hii ya pepo haiwezekani kutoka, ila kwa maombi na Kufunga” hayaonekani katika nakala bora za kale.

18

1Muda huo huo wanafunzi wakaja kwa Yesu na kumwambia, “Ni nani aliye mkubwa katika ufalme wa mbinguni?”

2Yesu akamwita mtoto mdogo, akamweka katikati yao,3na kusema, “Kweli nawaambieni, msipotubu na kuwa kama watoto wadogo hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.4Hivyo yeyote ajishushaye kama mtoto mdogo, mtu kama huyo ni mkuu katika ufalme wa mbinguni.5Na yeyote ampokeaye mtoto mdogo kwa jina langu anipokea mimi.

6Lakini yeyote asababishaye mmoja kati ya wadogo hawa wanaoniamini kuasi, itakuwa vizuri kwa mtu huyo jiwe kuu la kusagia likafungwa shingoni mwake, na kuzamishwa kilindini mwa bahari.7Ole kwa dunia kwa sababu ya wakati wa kukwazwa! Kwa kuwa haina budi kwa nyakati hizo kuja, lakini ole kwake kwa mtu yule nyakati hizo zitakuja kwa ajili yake!8Kama mkono wako au mguu wako ukikusababishia kukwazika, ukate na uutupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe kuingia kwenye uzima ukiwa bila mkono au kilema, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na mikono yote au miguu yote.9Kama jicho lako likikukwaza, uling`oe na ulitupe mbali na wewe. Ni vizuri zaidi kwako wewe uingie kwenye uzima na jicho moja, kuliko kutupwa kwenye moto wa milele ukiwa na macho yote.

10Tazameni kwamba msije mkamdharau mmoja wa wadogo hawa. Kwa maana nawambieni kuwa mbinguni kuna malaika wao siku zote wakiutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni.11112Mnafikiri nini? Ikiwa mtu ana kondoo mia moja, na mmoja wao akapotea, je hatawaacha tisini na tisa mlimani na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea?13Na akisha kumpata, kweli nawaambieni, anamfurahia kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.14Vivyo hivyo, siyo mapenzi ya Baba yenu wa mbinguni kuwa mmoja wa wadogo hawa aangamie.

15Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako.16Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa.17Na kama akipuuza kuwasikiliza, liambie kanisa jambo hilo, kama akipuuza vilevile kulisikiliza kanisa, basi na awe kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.18Kweli nawaambieni, chochote kile mtakachokifunga duniani na mbinguni kitafungwa. Na chochote mtakachokifungua duniani na mbinguni kitafunguliwa.19Tena nawaambieni kwamba kama watu wawili kati yenu wakikubaliana juu ya jambo lolote duniani waliombalo, hilo Baba yangu wa mbinguni atalifanya.20Kwa kuwa wawili au watatu wakikusanyika pamoja kwa jina langu, Mimi niko katikati yao.

21Tena Petro akaja na kumwambia Yesu, “Bwana, ni mara ngapi ndugu yangu akinikosea nami nimsamehe? Hata mara saba?”

22Yesu akamwambia, “Sikuambii mara saba, lakini hata sabini mara saba.23Kwa sababu hiyo ufalme wa mbinguni ni sawa na mfalme fulani aliyetaka kusahihisha hesabu kutoka kwa watumwa wake.24Alipoanza kusahihisha hesabu, mtumwa moja akaletwa kwake ambaye alikuwa anamdai talanta elfu kumi.25Kwa kuwa hakuwa na njia ya kulipa, bwana wake aliagiza auzwe, mke wake pamoja na watoto wake na kila kitu alichokuwa nacho, na malipo yafanyike.26Hivyo mtumwa alianguka, akapiga magoti mbele yake, akisema, ‘Bwana, uwe na uvumilivu pamoja nami, na nitakulipa kila kitu.’27Hivyo bwana wa yule mtumwa, kwa kuwa alisukumwa sana na huruma, alimwachilia na kumsamehe deni hilo28Lakini mtumwa yule alitoka na kumpata mmoja kati ya watumwa wenzake, aliyekuwa anamdai denari mia. Alimvuta, akamkaba kooni, na kumwambia, ‘Nilipe kile ninachokudai.’

29Lakini yule mtumwa mwenzake alianguka na kumsihi sana, akisema, ‘Uwe na uvumilivu nami, na nitakulipa.’30Lakini mtumwa yule wa kwanza alikataa. Badala yake, alienda na kumtupa gerezani, mpaka atakapo mlipa kile anachomdai.31Na walipoona watumwa wenzake kile kilichotokea. Walisikitishwa sana. Walikuja na kumwambia bwana wao kila kitu kilichotokea.

32Ndipo yule bwana wa mtumwa yule alimwita, na kumwambia, ‘Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni langu lote kwa sababu ulinisihi sana.33Je! Haukutakiwa kuwa na huruma kwa mtumwa mwenzio, kama mimi nilivyokuhurumia wewe?34Bwana wake alikasirika na kumkabidhi kwa wale watesaji mpaka atakapolipa kiasi chote alichokuwa anadaiwa.35Hivyo ndivyo Baba yangu wa Mbinguni atakavyowafanyia, kama kila mmoja wenu hatamsamehe ndugu yake kutoka moyoni mwenu.”


1Zingatia: Maneno yanayoonekana kama ya msitari wa 11, “Kwa kuwa Mwana wa Adamu alikuja kuokoa kile kilichokuwa kimepotea” hayakuonekana katika nakala bora za kale.

19

1Ilitokea wakati Yesu alipomaliza maneno hayo, akaondoka Galilaya, na akaenda mpakani mwa Yudea mbele ya mto Jordani.2Umati mkubwa ukamfuata, na akawaponya huko.

3Mafarisayo wakamjia, wakamjaribu, wakamwambia, “Je ni halali kwa mtu kumwacha mke wake kwa sababu yoyote?”

4Yesu akajibu na kusema, “Hamkusoma, kwamba yeye aliyewaumba mwanzo aliwaumba mume na mke?5Na tena akasema, ‘Kwa sababu hiyo mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuungana na mke wake, nao wawili watakuwa mwili mmoja?’6Hivyo siyo wawili tena, bali mwili mmoja. Basi, kile alichokiunganisha Mungu, mtu yeyote asikitenganishe.”

7Wakamwambia, “Sasa kwa nini Musa alituamuru kutoa hati ya talaka na kumwacha?”

8Akawaambia, “Kwa ugumu wenu wa mioyo Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu, lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.9Nawaambieni, kwamba yeyote atakayemwacha mke wake, isipokuwa kwa sababu ya uzinzi, na akamwoa mwingine, amezini. Na mwanaume atakayemwoa mke aliyeachwa amezini.”

10Wanafunzi wakamwambia Yesu, “Kama ndivyo ilivyo kwa mume na mkewe, siyo vizuri kuoa.”

11Lakini Yesu akawaambia, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya, bali ni kwa wale tu walioruhusiwa kupokea.12Kwa vile wapo matowashi waliozaliwa tokea tumboni mwa mama zao. Na vile vile kuna matowashi waliofanywa na watu. Na kuna matowashi waliojifanya matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kupokea mafundisho haya na ayapokee.”

13Kisha akaletewa baadhi ya watoto wadogo ili awawekee mikono juu yao na kuomba, lakini wanafunzi wake wakawakemea.14Bali Yesu akasema, “Waruhusu watoto wadogo, wala msiwakataze kuja kwangu, kwa maana ufalme wa mbinguni ni wa watu kama wao.15Naye akaweka mikono yake juu yao, na kisha akaondoka pale.

16Tazama mtu mmoja akaja kwa Yesu na kusema, “Mwalimu, ni kitu gani kizuri ninachotakiwa kufanya ili nipate kuwa na uzima wa milele?”

17Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniuliza ni kitu gani kizuri? Kuna mmoja tu aliye mwema, lakini kama ukitaka kupata uzima, shika sheria za Mungu.”

18Yule mtu akamwuliza, “Ni sheria zipi?” Yesu akasema, “Usiue, usizini, usiibe, usishuhudie uongo,19waheshimu baba yako na mama yako, na mpende jirani yako kama nafsi yako.”

20Mtu yule akamwambia, “Mambo yote hayo nimeyatii. Bado ninahitaji nini?

21“Yesu akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze ulivyo navyo, na uwape maskini, na utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo unifuate.”22Lakini kijana yule aliposikia yale Yesu aliyomwambia, akaondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa amemiliki mali nyingi.

23Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kweli nawaambieni, ni vigumu kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni.24Tena nawaambieni, ni rahisi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”

25Wanafunzi waliposikia hivyo, wakashangaa sana na kusema, “Ni yupi basi atakayeokoka?”

26Yesu akawatazama na kusema, “Kwa wanadamu hilo haliwezekani, lakini kwa Mungu yote yanawezekana.”

27Kisha Petro akamjibu na kumwambia, “Tazama, tumeacha vyote na kukufuata wewe. Ni kitu gani tutakachopata?”

28Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, yeye aliyenifuata mimi, katika uzao mpya wakati Mwana wa Adam atakapoketi katika kiti cha enzi cha utukufu wake, ninyi pia mtaketi juu ya viti kumi na viwili vya enzi, kuwahukumu makabila kumi na mawili ya Israeli.29Kila mmoja wenu aliyeacha nyumba, kaka, dada, baba, mama, watoto, au shamba kwa ajili ya jina langu, atapokea mara mia na kuurithi uzima wa milele.

30Lakini wengi walio wa kwanza sasa, watakuwa wa mwisho, na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.

20

1Kwa maana ufalme wa mbinguni unafanana na mmliki wa shamba, aliyeamka asubuhi na mapema ili kuajiri wafanyakazi katika shamba lake la mizabibu.2Baada ya kuwa amekubaliana na wafanyakazi dinari moja kwa kutwa, aliwatuma kwenda katika shamba lake la mizabibu.3Alienda tena baada ya masaa matatu hivi na aliona wafanyakazi wengine wakiwa wamesimama bila kazi katika eneo la soko.4Akawaambia, ‘Ninyi pia, nendeni katika shamba la mizabibu, na chochote kilicho halali nitawapa.’ Hivyo wakaenda kufanya kazi.5Akaenda tena baada ya masaa sita na tena katika saa ya tisa, na alifanya hivyo hivyo.6Mara nyingine tena mnamo saa kumi na moja, alienda na kuwakuta watu wengine wamesimama bila kazi. Aliwaambia, ‘kwa nini mmesimama hapa bila kazi yoyote kwa siku nzima?

7Wakamwambia, kwasababu hakuna mtu yeyote aliyetuajiri. Akawaambia, ‘Nanyi pia nendeni katika shamba la mizabibu.’

8Wakati wa jioni ulipofika, mwenye shamba la mizabibu alimwambia msimamizi wake, ‘Waite wafanyakazi na uwalipe mishahara, kwa kuanza na wa mwisho hadi wa kwanza.’9Walipokuja wale walioajiriwa saa kumi na moja, kila mmoja wao alipokea dinari.10Walipokuja wafanyakazi wa kwanza, walifikiri kuwa watapokea zaidi, lakini walipokea pia kila mmoja dinari moja kila mtu.11Baada ya kupokea malipo yao, walimlalamikia mmiliki wa shamba.

12Wakasema, ‘Hawa wafanyakazi wa mwisho wametumia saa moja tu katika kufanya kazi, lakini umewalinganisha na sisi, sisi tumebeba mzigo kwa siku nzima na kuungua na joto.’

13Lakini mwenye shamba akajibu na kusema kwa mmoja wao, ‘Rafiki, sikutenda jambo baya. Je! Hatukukubaliana na mimi kwa dinari moja?14Pokea kile kilicho halali yako na uende zako. Ni furaha yangu kuwapa hawa wafanyakazi walioajiriwa mwisho sawa sawa na wewe.

15Je! Si haki kwangu kufanya kile ninachotaka na mali zangu? Au jicho lako ni ovu kwa sababu mimi ni mwema?16Hivyo wa mwisho atakuwa wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho”

17Yesu alipokuwa akipanda kwenda Yerusalem, aliwachukuwa wanafunzi wake kumi na mbili pembeni, na njiani akawaambia,18“Tazama tunaelekea Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atatiwa katika mikono ya wakuu wa makuhani na waandishi. Watamhukumu kifo19na watamtoa kwa watu wa mataifa ili kumdhihaki, kumchapa na kumsulubisha. Lakini katika siku ya tatu atafufuka.”

20Kisha mama wa wana wa Zebedayo alikuja kwa Yesu na wana wake. Alipiga magoti mbele yake na kumwomba kitu kutoka kwake.21Yesu akamwambia, “Unataka nini?” Akamwambia, “Amuru kuwa hawa wanangu wawili wakae, mmoja mkono wako wa kulia na mmoja mkono wako wa kushoto katika ufalme wako.”

22Lakini Yesu akajibu na kusema, “Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?” Wakamwambia, “Tunaweza.”

23Akawaambia, “Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu.”

24Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.25Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, “Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao.26Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.27Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu.28Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi.”

29Wakati wakitoka Yeriko, umati mkubwa ulimfuata.30Na waliwaona vipofu wawili wameketi kando ya barabara. Waliposikia kuwa Yesu alikuwa anapita, walipaza sauti na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”31Lakini umati ukawakemea, na kuwaambia nyamazeni. Hata hivyo, wao wakapaza sauti zaidi na kusema, “Bwana, Mwana wa Daudi, utuhurumie.”

32Kisha Yesu alisimama na aliwaita na kuwauliza, “Mnataka niwafanyie nini?”33Wakamwambia, “Bwana kwamba macho yetu yafumbuliwe.”34Basi Yesu, akiwa amevutwa na huruma, akayagusa macho yao, mara hiyo, wakapokea uwezo wa kuona na wakamfuata.

21

1Yesu na wanafunzi wake wakafika karibu na Jerusalemu na wakaenda mpaka Bethania, katika mlima mizeituni, kisha Yesu akawatuma wanafunzi wawili,2akiwaambia, “Nendeni katika kijiji kinachofuata, na mara moja mtamkuta punda amefungwa pale, na mwanapunda pamoja naye. Wafungueni na kuwaleta kwangu.3Ikiwa mtu yeyote akiwaambia chochote kuhusu hilo, mtasema, ‘Bwana anawahitaji,’ na mtu huyo mara moja atawaruhusu mje pamoja nao.”

4Jambo hili lilitokea ni lile lililosemwa kupitia kwa nabii lazima litimizwe. Akawaambia,5‘Waambie binti Sayuni, tazama, mfalme wako anakuja kwenu, mnyenyekevu na akiwa amempanda punda, na mwana punda mme.’

6Kisha wanafunzi waliondoka na kufanya kama Yesu alivyowaagiza.7Wakamleta punda na mwanapunda, na kuweka nguo zao juu yao, naye Yesu akakaa pale.8Wengi katika mkusanyiko walitandaza nguo zao njiani, na wengine walikata matawi kutoka kwenye miti na kutandaza barabarani.9Umati uliomtangulia Yesu na wale waliomfuata walipaza sauti, wakisema, “Hosana kwa mwana wa Daudi! Ni mbarikiwa ajaye kwa jina la Bwana. Hosana juu zaidi!”

10Yesu alipofika Yerusalemu, mji mzima ulishtuka na kusema, “Huyu ni nani?

11“Umati ulijibu, “Huyu ni Yesu Nabii, kutoka Nazareti ya Galilaya.”

12Kisha Yesu akaingia katika hekalu la Mungu. Akawafukuza nje wote waliokuwa wakinunua na kuuza hekaluni. Pia alipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wauza njiwa.13Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya maombi,’ lakini ninyi mmeifanya pango la wanyang'anyi.”

14Kisha vipofu na vilema wakamjia hekaluni, naye akawaponya.

15Lakini wakati wakuu wa makuhani na waandishi walipoona maajabu aliyoyatenda, na waliposikia watoto wakipiga kelele hekaluni na kusema, “Hosana kwa Mwana wa Daudi,” walishikwa na hasira.

16Wakamwambia, “Umesikia kile kinachosemwa na hawa watu?” Yesu akawaambia, “Ndiyo! Lakini hamjawahi kusoma, ‘Kutoka kwa midomo ya watoto na watoto wachanga wanyonyao mna sifa kamili?”

17Kisha Yesu akawaacha na kwenda nje ya mji katika Bethania na kulala huko.

18Asubuhi alipokuwa anarudi mjini, alikuwa na njaa.19Aliona mtini kandokando ya barabara. Akauendea, lakini hakupata kitu juu yake isipokuwa majani. Aliuambia, “Kusiwe na matunda kwako daima tena.” Na mara hiyo mtini ule ukanyauka.

20Wanafunzi walipoona, wakastaajabu na kusema, “Imekuwaje mtini umenyauka mara moja?”

21Yesu akajibu na kuwaambia, “Kweli nawaambieni, kama mkiwa na imani na bila wasiwasi, hamtafanya kile kilichofanyika kwa huo mtini tu, lakini mtauambia hata huo mlima, ‘Uchukuliwe na ukatupwe baharini,’ na itafanyika.22Chochote mtakachoomba kwa sala, huku mkiamini, mtapokea.”

23Yesu alipofika hekaluni, wakuu wa makuhani na wazee wa watu wakamjia wakati alipokuwa akifundisha na kumwuliza, “Ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Na ni nani aliyekupa mamlaka haya?”

24Yesu akajibu na kuwaambia, “Nami tena nitawauliza swali moja. Kama mkiniambia, nami vile vile nitawaambia ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.25Ubatizo wa Yohana- ulitoka wapi, mbinguni au kwa wanadamu?” Wakahojiana wenyewe, wakisema, “Tukisema, ulitoka mbinguni, atatuambia, ‘Kwa nini hamkumwamini?’26Lakini tukisema, ‘Ulitoka kwa wanadamu,’ tunawaogopa makutano, kwa sababu wote wanamwona Yohana kama nabii.”27Kisha wakamjibu Yesu na kusema, “Hatujui” Akawaambia pia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nafanya mambo haya.

28Lakini mnafikiri nini? Mtu mwenye wana wawili. Akaenda kwa moja na kumwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi katika shamba la mizabibu29leo.’ ‘Mwana akajibu na kusema, ‘sitakwenda.’ Lakini baadaye akabadilisha mawazo yake na akaenda.

30Na mtu yule akaenda kwa mwana wa pili na kusema kitu kile kile. Mwana huyu akajibu na kusema, ‘Nitakwenda, bwana.’ Lakini hakwenda.31Yupi kati ya wana wawili aliyefanya matakwa ya baba yake? Wakasema, “Mwana wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, wakusanya ushuru na makahaba wataingia kwenye ufalme wa Mungu kabla yenu kuingia.32Kwa maana Yohana alikuja kwenu kwa njia iliyo nyoofu, lakini hamkumwamini, wakati wakusanya ushuru na makahaba walimwamini. Na ninyi, mlipoona hilo likitendeka, hamkuweza kutubu ili baadaye mumwamini.

33Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye eneo kubwa la ardhi. Alipanda mizabibu, akaiwekea uzio, akatengeneza na chombo cha kukamulia divai, akajenga na mnara wa walinzi, na akalikodisha kwa watunza zabibu. Kisha akaenda katika nchi nyingine.34Wakati wa mavuno ya mizabibu ulipokaribia, aliwatuma baadhi ya watumishi kwa wakulima wa mizabibu kuchukua mizabibu yake.35Lakini wakulima wa zabibu wakawachukua watumishi wake, wakampiga mmoja, wakamwua mwingine, na wakampiga mmoja kwa mawe.36Kwa mara nyingine, mmiliki aliwatuma watumishi wengine, wengi zaidi ya wale wa kwanza, lakini wakulima wa mizabibu waliwatendea vile vile.37Baada ya hapo bwana yule akamtuma kwao mwana wake, akisema, ‘Watamheshimu mwanangu.’

38Lakini wakulima wa mizabibu walipomwona kijana yule, wakaambiana, ‘Huyu ni mrithi. Njooni tumuue na tumiliki urithi.’39Hivyo wakamchukua, wakamtupa nje ya shamba la mizabibu na kumwua.40Je mmliki wa shamba la mizabibu atakapokuja, atawafanya nini wakulima wa mizabibu?”

41Wakamwambia, “Atawaharibu hao watu waovu katika njia ya ukali zaidi, na kisha atalikodisha shamba la mizabibu kwa wakulima wengine wa mizabibu, watu ambao watalipa kwa ajili ya mizabibu itakapoiva.”

42Yesu akawaambia, “Hamkusoma katika maandiko, ‘Jiwe walilolikataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi. Hili lilitoka kwa Bwana, na inashangaza machoni petu?’

43Hivyo nawaambieni, Ufalme wa Mungu utatwaliwa kutoka kwenu na kupewa taifa linalojali matunda yake.44Yeyote atakayeanguka juu ya jiwe hilo atavunjwa vipandevipande. Lakini kwa yeyote litakayemwangukia, litamsaga.”

45Wakuu wa makuhani na mafarisayo waliposikia mifano yake, wakaona kuwa anawazungumzia wao.46Lakini kila walipotaka kunyosha mikono juu yake, waliogopa makutano, kwa sababu watu walimtazama kama nabii.

22

1Yesu alisema nao tena katika mifano, akisema,2“Ufalme wa mbinguni unafanana na mfalme aliyeandaa sherehe ya harusi ya mwanawe.3Akawatuma watumishi wake kuwakaribisha waliokuwa wamealikwa kuja katika sherehe ya harusi, lakini hawakufika.4Mfalme aliwatuma tena watumishi wengine, akisema. “Waambieni wote walioalikwa, ‘Angalieni, nimeandaa chakula. Fahali na ndama wangu wanono wamechinjwa, na mambo yote yako tayari. Njoni katika sherehe ya harusi.”5Lakini watu hao hawakuzingatia kwa dhati mwaliko wake. Baadhi walirejea katika mashamba yao, na wengine walirudi katika sehemu zao za biashara.6Wengine waliwainukia watumishi wa mfalme na kuwadhalilisha na kuwaua.7Lakini mfalme alikasirika. Alituma jeshi lake, akawaua wale wauaji na kuuteketeza mji wao kwa moto.8Kisha aliwaambia watumishi wake, ‘Harusi iko tayari, lakini walioalikwa hawakustahili.9Kwa hiyo nendeni kwenye makutano ya njia kuu, waalikeni watu wengi kadri iwezekanavyo waje kwenye sherehe ya harusi.’10Watumishi walienda njia kuu na kuwakaribisha watu wowote waliowaona, wema na wabaya. Hivyo ukumbi wa harusi ulijaa wageni.11Lakini mfalme alipoingia kuwatazama wageni, alimuona mtu mmoja ambaye hakuvaa vazi rasmi la harusi!12Mfalme alimwuliza, ‘Rafiki, ulipataje kufika hapa ndani bila vazi la harusi?’ Na mtu huyo hakujibu chochote.13Ndipo mfalme alipowaambia watumishi wake, ‘Mfungeni mtu huyu mikono na miguu na mtupeni nje katika giza, huko ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.14Kwa kuwa watu wengi wanaitwa, lakini wateule ni wachache.’”

15Ndipo Mafarisayo waliondoka na kupanga jinsi ya kumkamata Yesu katika maneno yake mwenyewe.16Ndipo walipowatuma wanafunzi wao pamoja na Maherode. Na walimwambia Yesu, “Mwalimu, tunajua kuwa wewe ni mtu wa kweli, na kwamba unafundisha matakwa ya Mungu katika ukweli. Haujali maoni ya mtu mwingine na hauoneshi upendeleo kwa watu.17Kwa hiyo tuambie, unafikiri nini? Je, ni sahihi kisheria kulipa kodi kwa Kaisari au hapana?”

18Yesu alifahamu uovu wao na akasema, “Kwa nini mnanijaribu, enyi wanafiki?19Nionesheni pesa itumikayo kulipia kodi.” Ndipo wakamletea dinari.20Yesu akawauliza, “Sura na jina hili ni vya nani?”

21Wakamjibu, “Vya Kaisari.” Ndipo Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu.”22Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.

23Siku hiyo baadhi ya Masadukayo walikuja kwa Yesu, wale wasemao kuwa hakuna ufufuo wa wafu. Wakamwuliza,24wakisema, “Mwalimu, Musa alisema, ikiwa mtu amefariki bila kuzaa watoto, ndugu yake na amrithi huyo mwanamke na ampatie mtoto kwa ajili ya ndugu yake.25Walikuwapo ndugu saba. Wa kwanza alioa na kisha akafariki bila kuzaa watoto. Akamwachia mke nduguye.26Kisha ndugu yake wa pili naye akafanya vivyo hivyo, kisha yule wa tatu, ikawa hivyo hadi kwa yule wa saba.27Baada ya kufanya hivyo wote, yule mwanamke naye alifariki.28Sasa katika ufufuo huyo mwanamke atakuwa mke wa nani katika ndugu hao saba? Kwa sababu wote walimuoa.”

29Lakina Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Mnakosea, kwa sababu hamjui Maandiko wala nguvu za Mungu.30Kwa kuwa katika ufufuo, watu hawaoi wala kuolewa. Badala yake watu huwa kama malaika huko mbinguni.31Lakini kuhusu ufufuo wa walio kufa, hamjawahi kusoma kile ambacho Mungu alikisema kwenu, akisema,32“Mimi ni Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa waliokufa, bali ni Mungu wa walio hai.”

33Wakati umati waliposikia hili, waliyashangaa mafundisho yake.

34Lakini Mafarisayo waliposikia kuwa Yesu amewanyamazisha Masadukayo, walijikusanya wao wenyewe kwa pamoja.35Mmoja wao, akiwa mwana sheria, alimwuliza swali kwa kumjaribu.36“Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu kuliko zote katika sheria?”

37Yesu akamjibu, “Lazima umpende Bwana kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.38Hii ndiyo amri iliyo kuu na ya kwanza.39Na ya pili inafanana na hiyo. Ni lazima kumpenda jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.40Sheria zote na Manabii hutegemea amri hizi mbili.”

41Na Mafarisayo walipokuwa bado wamejikusanya pamoja, Yesu aliwauliza swali.42Akisema, “Je, mwafikiri nini juu ya Kristo? Yeye ni Mwana wa nani?” Nao wakamjibu, “Ni mwana wa Daudi.”

43Yesu akawajibu, “Ni kwa namna gani Daudi katika Roho anamwita Bwana, akisema,44‘Bwana alimwambia Bwana wangu, ‘Kaa mkono wangu wa kuume, hadi nitakapowafanya maadui zako wawekwe chini ya miguu yako.”45Kama Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ jinsi gani atakuwa mtoto wake?”46Hakuna aliyeweza kumjibu neno tena, na hakuna aliyethubutu tena kumwuliza maswali zaidi tangu siku hiyo na kuendelea.

23

1Baadaye aliongea na umati na wanafunzi wake. Akasema,2“Waandishi na Mafarisayo wanakalia kiti cha Musa.3Kwa hiyo chochote wanacho waamuru kufanya, fanyeni huku mkiwachunguza. Lakini msije mkaiga matendo yao, kwa sababu wao hutamka mambo wasiyoyafanya.4Kweli, wao hufunga mizigo mizito ambayo ni vigumu kuibeba, na kisha huwabebesha watu mabegani mwao. Lakini wao wenyewe hawasogezi hata kidole kuibeba.5Matendo yao yote, huyafanya ili watazamwe na watu. Kwa sababu wao hupanua masanduku yao na huongeza ukubwa wa mapindo ya mavazi yao.6Wao hupendelea kukaa maeneo ya kifahari katika sherehe na katika viti vya heshima ndani ya masinagogi,7na kusalimiwa kwa heshima maeneo ya sokoni, na kuitwa ‘Walimu’ na watu.8Lakini ninyi hampaswi kuitwa “Walimu,” Kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja, na ninyi wote ni ndugu.9Msimuite mtu yeyote hapa duniani kuwa baba yenu, kwa kuwa mnaye Baba mmoja tu, naye yuko mbinguni.10Wala msije kuitwa ‘walimu,’ kwa kuwa mnaye Mwalimu mmoja tu, yaani Kristo.11Bali aliye mkubwa miongoni mwenu atakuwa mtumishi wenu.12Yeyote ajiinuae atashushwa. Na yeyote anaye jishusha atainuliwa.

13Lakini ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnawafungia watu ufalme wa mbinguni. Nanyi hamwezi kuuingia, na hamwaruhusu wanaoingia kufanya hivyo.141

15Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Mnavuka ng'ambo ya bahari na kufika kumfanya mtu mmoja aamini yale mnayoyafundisha, na anapokuwa kama ninyi, mnamfanya mara mbili mwana wa jehanamu kama ninyi wenyewe mlivyo.

16Ole wenu viongozi vipofu, ninyi msemao, ‘Yeyote aapaye kwa hekalu, si kitu. Lakini anayeapa kwa dhahabu ya hekalu, amefungwa na kiapo chake.’17Enyi vipofu wapumbavu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, dhahabu au hekalu ambalo limeweka wakfu dhahabu kwa Mungu?18Na, yeyote aapaye kwa madhabahu, si kitu. Bali anayeapa kwa sadaka iliyo juu yake, amefungwa na kiapo chake.19Enyi watu vipofu, kipi ni kikubwa kuliko kingine, sadaka au madhabahu ambayo huweka wakfu sadaka zinazotolewa kwa Mungu?20Kwa hiyo, yeye aapaye kwa madhabahu huapa kwa hiyo na kwa vitu vyote vilivyo juu yake.21Naye aapaye kwa hekalu, huapa kwa hilo na kwa yeye akaaye ndani yake.22Na yeye aapaye kwa mbingu, huapa kwa kiti cha enzi cha Mungu na kwa yeye aketie juu yake.

23Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnalipa zaka kwa bizali, mnaanaa na mchicha, lakini mnaacha mambo mazito ya sheria- haki, rehema, na imani. Lakini haya mnapaswa kuwa mmeyafanya, na siyo kuacha mengine bila kuyatekeleza.24Enyi viongozi vipofu, ninyi ambao mnachuja mdudu mdogo lakini mnameza ngamia!

25Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya vikombe na nje ya sahani, lakini ndani pamejaa dhuluma na kutokuwa na kiasi.26Enyi Mafarisayo vipofu, safisheni kwanza ndani ya kikombe na ndani ya sahani, ili upande wa nje nao pia uwe safi.

27Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnafanana na makaburi yaliyopakwa chokaa, ambayo kwa nje huonekana mazuri, lakini kwa ndani yamejaa mifupa ya waliokufa na kila kitu kilicho kichafu.28Vivyo hivyo, nanyi kwa nje mwaonekana wenye haki mbele ya watu, lakini kwa ndani mmejaa unafiki na udhalimu.

29Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki.30Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii.31Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.32Pia ninyi mnakamilisha kujaza sehemu inayostahili dhambi ya baba zenu.33Enyi nyoka, wana wa majoka, kwa namna gani mtaikwepa hukumu ya jehanamu?34Kwahiyo, tazama, nawatuma kwenu manabii, watu wenye hekima, na waandishi. Baadhi yao mtawaua na kuwasulubisha. Na baadhi yao mtawachapa ndani ya masinagogi yenu na kuwafukuza kutoka mji mmoja hadi mwingine.35Matokeo ni kwamba juu yenu patatokea damu zote za wenye haki zilizomwagwa duniani, kuanzia damu ya Habili mwenye haki hadi kwa damu ya Zakaria mwana wa Barakia, mliye muua kati ya patakatifu na madhabahu.36Kweli, nawaambieni, mambo haya yote yatakipata kizazi hiki.

37Yerusalemu, Yerusalemu, wewe unayewaua manabii na kuwapiga mawe wale ambao wanatumwa kwako! Mara ngapi nimewakusanya watoto wako pamoja kama vile kuku awakusanyavyo vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini haukukubali!38Tazama, nyumba yako imebaki ukiwa.39Nami nakuambia, kuanzia sasa na kuendelea hautaniona, hadi utakaposema, ‘Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana.”’


1Zingatia: Msitari wa 14 hauonekani katika nakala bora za kale. Baadhi ya nakala huongeza msitari huu baada ya msitari wa 12. Msitari wa 14 ‘Ole wenu wandishi na Mafarisayo wanafiki! Kwa kuwa mnawameza wajane.’

24

1Yesu alitoka hekaluni na kwenda zake. Wanafunzi wake walimwendea na kumuonesha majengo ya hekalu.2Lakini aliwajibu na kusema, “Je, hamuyaoni mambo haya yote? Kweli nawaambia, hakuna jiwe litalobaki juu ya lingine bila kubomolewa.”

3Na alipokaa katika lima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, “Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?”

4Yesu aliwajibu na kuwaambia, “Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha.5Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, ‘Mimi ndiye Kristo,’ na watawapotosha wengi.6Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado.7Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali.8Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua.

9Ndipo watawatoa kwa ajili ya mateso na kuwaua. Mtachukiwa na mataifa yote kwa sababu ya jina langu.10Ndipo wengi watajikwaa na kusalitiana na watachukiana wenyewe kwa wenyewe.11Manabii wengi wa uongo watatokea na kuwadanganya wengi.12Kwa sababu uovu utaongezeka, upendo wa wengi utapungua.13Lakini atakaye vumilia mpaka mwisho, ataokolewa.14Hii Injili ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu mzima kama ushuhuda kwa mataifa yote. Na ndipo ule mwisho utafika.

15Kwa hiyo, mtakapoona chukizo la uharibifu, lililosemwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu),16ndipo walioko Yuda wakimbilie milimani.17Na yule aliyeko juu ya paa la nyumba asiweze kuteremka chini kuchukua kitu chochote kutoka ndani ya nyumba yake,18naye aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.19Lakini ole wao ambao wana mtoto na wale ambao wananyonyesha katika siku hizo!20Ombeni kwamba kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.21Kwa kuwa kutakuwa na dhiki kuu, ambayo haijawahi kuwapo tangu kuumbwa kwa ulimwengu hadi sasa, na wala haitakuwapo tena.22Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna ambaye angeokoka. Lakini kwa sababu ya wateule, siku hizo zitafupishwa.

23Kisha ikiwa mtu yeyote atawaambia ‘Tazama, Kristo yuko hapa! Au, ‘Kristo yuko kule’ msiamini maneno hayo.24Kwa kuwa Makristo wa uongo na manabii wa uongo watakuja na kuonesha ishara kubwa na maajabu, kwa kusudi la kupotosha, kama ingewezekana hata na wateule.25Tazameni, nimewatahadharisha kabla ya mambo hayo kutokea.26Kwa hiyo, ikiwa watawaambia, “Kristo yuko jangwani,’ msiende huko jangwani. Au, ‘Tazameni, yuko ndani ya nyumba,’ msiamini maneno hayo.27Kama vile radi inavyomulika kutokea mashariki na kuangaza hadi magharibi, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.28Popote ulipo mzoga, huko ndiko tai wakusanyikapo.

29Lakini mara baada ya dhiki kuu ya siku zile, Jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake, nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbinguni zitatikisika.30Ndipo ishara ya Mwana wa Adamu itaonekana angani, na makabila yote ya dunia wataomboleza. Watamwona Mwana wa Adamu akija katika mawingu ya angani kwa nguvu na utukufu mkuu.31Atawatuma malaika wake kwa sauti kuu ya tarumbeta, nao watawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande nne za dunia, kutoka mwisho mmoja wa mbingu hadi mwingine.

32Jifunzeni somo kutokana na mti mtini. Mara tu tawi linapochipuka na kutoa majani, mnajua kwamba kiangazi kinakaribia.33Hivyo pia, mtakapoona mambo haya yote, mnapaswa kujua kwamba amekaribia, karibu na malango.34Kweli nawaambia, kizazi hiki hakitapita, hadi mambo yote haya yatakuwa yametokea.35Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

36Lakini kuhusu siku ile na saa hakuna mtu ajuaye, hata malaika wa mbinguni, wala Mwana, bali Baba peke yake.37Kama vile ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.38Kwa kuwa katika siku hizo kabla ya gharika watu walikuwa wakila na kunywa, wakioa na kuolewa hadi siku ile ambayo Nuhu aliingia katika safina,39na hawakujua kitu chochote hadi gharika ilipokuja na kuwasomba wote - ndivyo itakavyokuwa kuja kwa Mwana wa Adamu.40Ndipo watu wawili watakuwa shambani- mmoja atachukuliwa, na mmoja ataachwa nyuma.41Wanawake wawili watakuwa wanasaga pamoja - mmoja atachukuliwa, na mmoja atabaki.42Kwa hiyo, kuweni macho kwa sababu hamjui ni siku gani ambayo atakuja Bwana wenu.43Lakini mjue kwamba, ikiwa bwana mwenye nyumba angejua ni saa ipi ambayo mwizi angekuja, angekesha na asingeruhusu nyumba yake kuvamiwa.44Kwa hiyo, pia mnapaswa kuwa tayari, kwa kuwa Mwana wa Adamu atakuja katika saa msiyoitarajia.

45Hivyo ni nani aliye mwaminifu, mtumwa mwenye akili, ambaye bwana wake amempa madaraka juu ya walio katika nyumba yake, ili awape chakula kwa wakati unaofaa?46Amebarikiwa mtumishi huyo, ambaye bwana wake atamkuta akifanya hivyo wakati ajapo.47Kweli nawaambia kwamba bwana atamweka juu ya kila kitu kilicho chake.48Lakini kama mtumwa mwovu akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu amekawia,’49na akaanza kuwapiga watumishi wake, na akala na kulewa vileo,50Bwana wa mtumwa huyo atakuja katika siku ambayo haitarajii, na katika saa ambayo haijui.51Bwana wake atamkata vipande viwili na kumweka katika nafasi moja sawa na wanafiki, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.

25

1Ndipo ufalme wa mbinguni utafananishwa na wanawali kumi waliochukua taa zao na kuondoka kwenda kumpokea bwana harusi.2Watano miongoni mwao walikuwa wapumbavu na watano wengine walikuwa werevu.3Wanawali wapumbavu walipochukua taa zao, hawakuchukua mafuta yoyote.4Bali wanawali welevu walichukua vyombo vyenye mafuta pamoja na taa zao.5Sasa wakati bwana harusi amechelewa kufika, wote walishikwa usingizi na wakalala.

6Lakini wakati wa usiku wa manane kulikuwa na yowe, ‘Tazama, bwana harusi! Tokeni nje mkampokee.’7Ndipo hao wanawali waliamka wote na kuwasha taa zao.

8Wale wapumbavu waliwaambia wale werevu, ‘Mtupatie sehemu ya mafuta yenu kwa sababu taa zetu zinazimika.’9Lakini wale werevu waliwajibu na kuwaambia, ‘Kwa kuwa hayatatutosha sisi na ninyi, badala yake nendeni kwa wanaouza mjinunulie kiasi kwa ajili yenu.’10Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa.

11Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, ‘Bwana, bwana, tufungulie.’12Lakini alijibu na kusema, ‘Kweli nawaambia, Mimi siwajui.’

13Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.

14Kwa kuwa ni sawa na mtu alipotaka kusafiri kwenda nchi nyingine. Aliwaita watumwa wake na kuwakabidhi utajiri wake.15Mmoja wao alimpatia talanta tano, mwingine alimpa mbili, na yule mwingine alimpa talanta moja. Kila mmoja alipokea kiasi kulingana na uwezo wake, na yule mtu alisafari kwenda zake.16Mapema yule aliyepokea talanta tano alienda kuziwekeza, na kuzalisha talanta zingine tano.17Vile vile yule aliyepokea talanta mbili, alizalisha zingine mbili.18Lakini mtumwa aliyepokea talanta moja, alienda zake, akachimba shimo ardhini, na kuificha fedha ya bwana wake.

19Na baada ya muda mrefu, bwana wa watumwa hao alirudi na kutengeneza mahesabu nao.20Yule mtumwa aliyepokea talanta tano alikuja na kuleta talanta zingine tano, akasema, ‘Bwana, ulinipa talanta tano. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine tano.’

21Bwana wake akamwambia, ‘Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vidogo. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.’

22Mtumwa aliyepokea talanta mbili alikuja na kusema, ‘Bwana, ulinipa talanta mbili. Tazama, nimepata faida ya talanta zingine mbili,’

23Bwana wake akamwambia, ‘Hongera, mtumwa mzuri na mwaminifu! Umekuwa mwaminifu kwa vitu vichache. Nitakupa madaraka juu ya vitu vingi. Ingia katika furaha ya bwana wako.’

24Baadaye mtumwa aliyepokea talanta moja alikuja na kusema, ‘Bwana, najua kuwa wewe ni mtu mkali. Unachuma mahali ambapo hukupanda, na unavuna mahali ambapo hukusia.25Mimi niliogopa, nikaenda zangu na kuificha talanta yako katika udongo. Tazama, unayo hapa ile iliyo yako.’

26Lakini bwana wake alijibu na kusema, ‘Wewe mtumwa mwovu na mzembe, ulijua kwamba ninachuma mahali ambapo sijapanda na kuvuna mahali ambapo sikusia.27Kwahiyo ulipaswa kuwapa fedha yangu watu wa benki, na wakati wa kurudi kwangu ningeipokea ile yangu pamoja na faida.28Kwa hiyo mnyang'anyeni hiyo talanta na mpeni yule mtumwa aliye na talanta kumi.29Kila mtu aliye nacho, ataongezewa zaidi-hata kwa kuzidishiwa sana. Lakini kwa yeyote asiye na kitu, hata alicho nacho atanyang'anywa.30Mtupeni nje gizani huyo mtumwa asiyefaa, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.’

31Wakati Mwana wa Adamu atakapokuja katika utukufu wake, na malaika wote pamoja naye, ndipo atakapokaa juu ya kiti chake cha utukufu.32Mataifa yote yatakusanyika mbele zake, naye atawatenganisha watu, kama vile mchungaji anavyowatenganisha kondoo na mbuzi.33Atawaweka kondoo mkono wake wa kuume, bali mbuzi atawaweka mkono wa kushoto.

34Kisha mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kulia, ‘Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme ulioandaliwa kwa ajili yenu tangu kuwekwa msingi wa ulimwengu.35Kwa kuwa nilikuwa na njaa na mlinipa chakula; Nilikuwa mgeni na mlinikaribisha;36Nilikuwa uchi, na mlinivika nguo; Nilikuwa mgonjwa na mkanitunza; Nilikuwa kifungoni na mkaniijia.’

37Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, ‘Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji?38Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo?39Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia?

40Na mfalme atawajibu na kuwaambia, ‘Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’

41Ndipo atawaambia hao walio mkono wake wa kushoto, ‘Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, nendeni katika moto wa milele ulioandaliwa kwa ajili ya shetani na malaika zake,42kwa sababu nilikuwa na njaa lakini hamkunipa chakula; Nilikuwa na kiu lakini hamkunipa maji;43Nilikuwa mgeni lakini hamkunikaribisha; nikiwa uchi lakini hamkunipa mavazi; nikiwa mgonjwa na nikiwa kifungoni, lakini hamkunitunza.’

44Ndipo wao pia watamjibu na kusema, ‘Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, au una kiu, au u mgeni, au ukiwa uchi, au ukiwa mgonjwa, au ukiwa mfungwa, na hatukukuhudumia?

45Kisha atawajibu na kusema, ‘Kweli nawaambia, kile ambacho hamkutenda kwa mmoja wa hawa wadogo, hamkunitendea mimi.’

46Hawa watakwenda katika adhabu ya milele bali wenye haki katika uzima wa milele.”

26

1Wakati Yesu alipomaliza kusema maneno yote hayo, aliwaambia wanafunzi wake,2“Mnajua kwamba baada ya siku mbili kutakuwa na sikukuu ya pasaka, na mwana wa Adamu atatolewa ili asulibiwe.”

3Baadaye wakuu wa makuhani na wazee wa watu walikutana pamoja katika makao ya Kuhani Mkuu, aliye kuwa anaitwa Kayafa.4Kwa pamoja walipanga njama ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.5Kwa kuwa walisema, “Isifanyike wakati wa sikukuu, kusudi isije ikazuka ghasia miongoni mwa watu.”

6Wakati Yesu alipokuwa Bethania katika nyumba ya Simoni mkoma,7alipokuwa amejinyoosha mezani, mwanamke mmoja alikuja kwake akiwa amebeba mkebe wa alabasta iliyokuwa na mafuta yenye thamani kubwa, na aliyamimina juu ya kichwa chake.8Lakini wanafunzi wake walipoona jambo hilo, walichukia na kusema, “Nini sababu ya hasara hii?9Haya yangeweza kuuzwa kwa kiasi kikubwa na kupewa maskini.”

10Lakini Yesu, akiwa anajua hili, akawaambia, “Kwa nini mnamsumbua mwanamke huyu? Kwa kuwa amefanya kitu kizuri kwangu.11Masikini mnao siku zote, lakini hamtakuwa pamoja nami daima.12Kwa sababu alipomimina mafuta haya juu ya mwili wangu, alifanya hivyo kwa ajili ya maziko yangu.13Kweli nawaambieni, popote Injili hii itakapohubiriwa katika ulimwengu mzima, kitendo alichofanya huyu mwanamke, pia kitakuwa kinasemwa kwa ajili ya kumkumbuka.”

14Ndipo mmoja wa wale Kumi na wawili, aliyeitwa Yuda Iskariote, alienda kwa wakuu wa makuhani15na kusema, “Mtanipatia nini nikimsaliti?” Wakampimia Yuda vipande thelathini vya fedha.16Tangu muda huo alitafuta nafasi ya kumsaliti.

17Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, “Wapi unataka tukuandalie ule chakula cha Pasaka?”

18Akawaambia, “Nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni, Mwalimu anasema, ‘Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako.’”19Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza, na waliandaa chakula cha Pasaka.

20Ilipofika jioni, aliketi kula chakula pamoja na wale wanafunzi kumi na wawili.21Walipokuwa wanakula chakula, alisema, “Kweli nawaambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”

22Walihuzunika sana, na kila mmoja alianza kumuuliza, “Je, hakika siyo mimi, Bwana?”

23Akawajibu, “Yule ambaye anachovya mkono wake pamoja nami katika bakuli ndiye atakaye nisaliti.24Mwana wa Adamu ataondoka, kama alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu ambaye atamsaliti Mwana wa Adamu! Ingekuwa vizuri kwa mtu huyo kama asingezaliwa.”25Yuda, ambaye angemsaliti alisema, “Je, ni mimi Rabi?” Yesu akamwambia, “Umesema jambo hilo wewe mwenyewe.”

26Walipokuwa wakila chakula, Yesu aliutwaa mkate, akaubariki, na kuumega. Akawapa wanafunzi wake akisema, “Chukueni, mle. Huu ni mwili wangu.”27Akatwaa kikombe na kushukuru, akawapa na kusema, “Kunyweni wote katika hiki.28Kwa kuwa hii ni damu ya agano langu, inayomwagwa kwa ajili ya wengi kwa msamaha wa dhambi.29Lakini nawaambieni, sitakunywa tena matunda ya mzabibu huu, hadi siku ile nitakapokunywa mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”

30Walipokuwa wamemaliza kuimba wimbo, walitoka kwenda Mlima wa Mizeituni.

31Kisha Yesu akawaambia, “Usiku huu ninyi nyote mtajikwaa kwa sababu yangu, kwa kuwa imeandikwa, Nitampiga mchungaji na kondoo wa kundi watatawanyika.32Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”

33Lakini Petro alimwambia, “Hata kama wote watakukataa kwa sababu ya mambo yatakayokupata, mimi sitakukataa.”

34Yesu akamjibu, “Kweli nakuambia, usiku huu kabla jogoo hajawika, utanikana mara tatu.”

35Petro akamwambia, “Hata kama ingenipasa kufa na wewe, sitakukana.” Na wanafunzi wengine wote wakasema vivyo hivyo.

36Baadaye Yesu alienda nao mahali panapoitwa Gethsemane na aliwaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati nikienda huko na kuomba.”37Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo na akaanza kuhuzunika na kusononeka.38Kisha akawaambia, “Roho yangu ina huzuni kubwa sana, hata kiasi cha kufa. Bakini hapa na mkeshe pamoja nami.”39Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, na kuomba. Akasema, “Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniepuke. Isiwe kama ninavyotaka mimi, bali kama utakavyo wewe.”40Akawaendea wanafunzi na akawakuta wamelala usingizi, na akamwambia Petro, “Kwa nini hamkuweza kukesha nami kwa saa moja?41Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”

42Akaenda zake mara ya pili na kuomba, akasema, “Baba yangu, kama jambo hili haliwezi kuepukika na ni lazima nikinywee kikombe hiki, mapenzi yako yatimizwe.”

43Akarudi tena na kuwakuta wamelala usingizi, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito.44Kisha akawaacha tena akaenda zake. Akaomba mara ya tatu akisema maneno yaleyale.45Baadaye Yesu aliwaendea wanafunzi wake na kuwaambia, “Bado mmelala tu na kujipumzisha? Tazameni, saa imekaribia, na Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.46Amkeni, tuondoke. Tazama, yule anaye nisaliti amekaribia.”

47Wakati alipokuwa bado anaongea, Yuda mmoja wa wale kumi na wawili, akafika. Kundi kubwa lilifika pamoja naye likitokea kwa wakuu wa Makuhani na wazee wa watu. Walikuja na mapanga na marungu.48Tena mtu aliyekusudia kumsaliti Yesu alikuwa amewapa ishara, akisema, “Yule nitakayembusu, ndiye yeye. Mkamateni.”49Mara hiyo alikuja kwa Yesu na kusema, “Salamu, Mwalimu!” Na akambusu.

50Yesu akamwambia, “Rafiki, lifanye lile ambalo limekuleta.” Ndipo wakaja, na kumnyoshea mikono Yesu, na kumkamata.51Tazama, mtu mmoja wa wale waliokuwa pamoja na Yesu, alinyosha mkono wake, akachomoa upanga wake, na akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, na kumkata sikio lake.52Ndipo Yesu akamwambia, rudisha upanga wako pale ulipoutoa, kwa kuwa wote watumiao upanga wataangamizwa kwa upanga.53Mnadhani kuwa siwezi kumwita Baba yangu, naye akanitumia makundi ya majeshi zaidi ya kumi na mawili ya malaika?54Lakini basi jinsi gani maandiko yangeweza kutimizwa, hivi ndivyo inapasa kutokea?”

55Wakati huo Yesu akauambia umati, “Je! Mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kama mnyang'anyi? Kila siku nilikaa hekaluni nikifundisha, na hamkunishika!56Lakini yote haya yametendeka ili Maandiko ya manabii yatimie.” Ndipo wanafunzi wake wakamwacha na kukimbia.

57Wale waliomkamata Yesu walimpeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, mahali ambapo waandishi na wazee walikuwa wamekusanyika pamoja.58Lakini Petro alimfuata nyuma kwa mbali hadi katika ukumbi wa Kuhani Mkuu. Aliingia ndani na kukaa pamoja na walinzi aone kitakachotokea.

59Basi wakuu wa makuhani na Baraza lote walikuwa wakitafuta ushahidi wa uongo dhidi ya Yesu, kusudi wapate kumuua.60Ingawa walijitokeza mashahidi wengi, lakini hawakupata sababu yoyote. Baadaye mashahidi wawili walijitokeza mbele61na kusema, “Mtu huyu alisema, “Naweza kulivunja hekalu la Mungu na kulijenga tena kwa siku tatu.”

62Kuhani Mkuu alisimama na kumwuliza, “Hauwezi kujibu? Hawa wanakushuhudia nini dhidi yako?”63Lakini Yesu alikaa kimya. Kuhani Mkuu akamwambia, “Kama Mungu aishivyo, nakuamuru utwambie, kama wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu.”

64Yesu akamjibu, “Wewe mwenyewe umesema jambo hilo. Lakini nakuambia, toka sasa na kuendelea utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wenye nguvu, na akija katika mawingu ya mbinguni.”

65Ndipo Kuhani Mkuu alirarua mavazi yake na kusema, “Amekufuru! Je, twahitaji tena ushahidi wa nini? Angalia, tayari mmesikia akikufuru.66Je! Mnawaza nini? Wakajibu na kusema, “Anastahili kifo.”67Kisha walimtemea mate usoni na kumpiga ngumi, na kumchapa makofi kwa mikono yao,68na kusema, “Tutabirie, wewe Kristo. Ni nani amekuchapa?”

69Wakati huo Petro alikuwa amekaa nje katika ukumbi, na mtumishi wa kike alimwendea na kusema, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Yesu wa Galilaya.”

70Lakini alikana mbele yao wote, akisema, “Sijui kitu unachosema.”

71Alipoenda nje ya lango, mtumishi mwingine wa kike alimwona na kuwaambia waliokuwepo hapo, “Mtu huyu pia alikuwa pamoja na Yesu wa Nazareti.”

72Akakana tena kwa kiapo, “Mimi simjui mtu huyu.”

73Muda mfupi baadaye, wale waliokuwa wamesimama karibu, walimwendea na kusema na Petro, “Kwa hakika wewe pia ni mmoja wao, kwa kuwa hata lafudhi yako inaonesha.”

74Ndipo alianza kulaani na kuapa, “Mimi simfahamu mtu huyu,” na mara hiyo jogoo akawika.

75Petro alikumbuka maneno aliyoambiwa na Yesu, “Kabla jogoo hajawika utanikana mara tatu.”

27

1Muda wa asubuhi ulipofika, wakuu wote wa makuhani na wazee wa watu walikula njama dhidi ya Yesu wapate kumuua.2Walimfunga, walimwongoza, na kumfikisha kwa Liwali Pilato.

3Kisha wakati Yuda, ambaye alikuwa amemsaliti, aliona kwamba Yesu amekwisha kuhukumiwa, alijuta na kurudisha vipande thelathini vya fedha kwa mkuu wa makuhani na wazee,4na akasema, “Nimefanya dhambi kwa kuisaliti damu isiyo na hatia.” Lakini wakajibu, “Inatuhusu nini sisi? Yaangalie hayo mwenyewe.”5Kisha alivirusha chini vile vipande vya fedha katika hekalu, na kuondoka zake na kujinyonga mwenyewe.

6Mkuu wa makuhani alivichukua vile vipande vya fedha na kusema, “Si halali kuiweka fedha hii katika hazina, kwa sababu ni gharama ya damu.”7Walijadiliana kwa pamoja na fedha ikatumika kununulia shamba la mfinyazi la kuzika wageni.8Kwa sababu hii shamba hilo limekuwa likiitwa, “Shamba la damu” hadi leo hii.

9Kisha lile neno lililokuwa limenenwa na nabii Yeremia lilitimia, kusema, “Walitwaa vipande thelathini vya fedha, gharama iliyopangwa na watu wa Israel kwa ajili yake,10na waliitumia kwa shamba la mfinyanzi, kama Bwana alivyokuwa amenielekeza.”

11Sasa Yesu alisimama mbele ya Liwali, na Liwali akamwuliza, “Je! Wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu alimjibu, “Wewe wasema hivyo.”

12Lakini wakati aliposhitakiwa na wakuu wa makuhani na wazee, hakujibu chochote.

13Kisha Pilato akamwambia, “Hujayasikia haya mashitaka yote dhidi yako?”14Lakini hakumjibu hata neno moja, hivyo Liwali alijawa na mshangao.

15Sasa katika sikukuu ilikuwa desturi ya Liwali kumfungua mfungwa mmoja anayechaguliwa na umati.16Wakati huo walikuwa na mfungwa sugu jina lake Baraba.

17Hivyo wakati walipokuwa wamekusanyika pamoja, Pilato aliwauliza, “Ni nani mnataka tumfungue kwa ajili yenu?” Baraba au Yesu anayeitwa Kristo?”18Kwa sababu alijua kwamba wamekwisha kumkamata kwa sababu ya chuki.

19Wakati alipokuwa akiketi kwenye kiti chake cha hukumu, mke wake alimtumia neno na kusema, “Usitende jambo lolote kwa mtu huyo asiye na hatia. Kwani nimeteswa mno hata leo katika ndoto kwa sababu yake.”

20Ndipo wakuu wa makuhani na wazee waliwashawishi makutano wamwombe Baraba, na Yesu auawe.21Liwali aliwauliza, “Ni yupi kati ya wawili mnataka mimi nimwachie kwenu?” Walisema, “Baraba.”

22Pilato akawaambia, “Nimtendee nini Yesu anayeitwa Kristo?” Wote wakajibu, “Msulibishe”23Naye akasema, “Kwa nini, ni kosa gani ametenda?” Lakini walizidi kupaza sauti hata juu mno, “Msulibishe.”

24Hivyo wakati Pilato alipoona hawezi kufanya lolote, lakini badala yake vurugu zilikuwa zimeanza, alitwaa maji akanawa mikono yake mbele ya umati, na kusema, “Mimi sina hatia juu ya damu ya mtu huyu asiye na hatia. Yaangalieni haya wenyewe.”

25Watu wote wakasema, “Damu yake iwe juu yetu na watoto wetu.”26Kisha akamfungulia Baraba kwao, lakini alimpiga mijeredi Yesu na kumkabidhi kwao kwenda kusulibiwa.

27Kisha askari wa Liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakakusanyishwa.28Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu.29Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeli, wakisema, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi?”30Na walimtemea mate, na walitwaa mwanzi na kumpiga kichwani.31Wakati walipokuwa wakimkejeli, walimvua ile kanzu na kumvika nguo zake, na kumwongoza kwenda kumsulibisha.

32Walipotoka nje, walimwona mtu kutoka Krene jina lake Simeoni, ambaye walimlazimisha kwenda nao ili apate kuubeba msalaba wake.33Walipofika mahali paitwapo Galigotha, maana yake, ‘Eneo la fuvu la Kichwa.’34Walimpa siki iliyochanganywa na nyongo anywe. Lakini alipoionja, hakuweza kuinywa.35Wakati walipokuwa wamemsulubisha, waligawana mavazi yake kwa kupiga kura.36Na waliketi na kumwangalia.37Juu ya kichwa chake waliweka mashitaka dhidi yake yakisomeka, “Huyu ni Yesu, mfalme wa Wayahudi.”38Wanyang'anyi wawili walisulubiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto.39Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao40na kusema, “Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!”

41Katika hali ile ile wakuu wa makuhani walikuwa wakimkashifu, pamoja na waandishi na wazee, na kusema,42“Aliokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe. Yeye ni Mfalme wa Wayahudi. Na ashuke chini toka msalabani, ndipo tutakapomwamini.43Alimtumaini Mungu. Acha Mungu amwokoe sasa kama anataka, kwa sababu alisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu.’”44Na wale wanyang'anyi waliokuwa wamesulubiwa pamoja naye pia walisema maneno ya kumdhihaki.

45Sasa kutoka saa sita kulikuwa na giza katika nchi yote hadi saa tisa.46Ilipofika saa tisa, Yesu akalia kwa sauti kuu, “Eloi, Eloi, lama thabakithan?” akimaanisha, “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”47Wakati huo baadhi yao waliokuwa wamesimama pale walisikia, wakasema, “Anamwita Eliya.”48Mara moja mmoja wao alikimbia kuchukua sifongo na kuijaza kinywaji kichungu, akaiweka juu ya mti na kumpa apate kunywa.

49Nao waliosalia wakasema, “Mwacheni peke yake, acheni tuone kama Eliya atakuja kumwokoa.”50Kisha Yesu akalia tena kwa sauti kuu na akaitoa roho yake.51Tazama, Pazia la hekalu lilipasuka sehemu mbili kutokea juu hadi chini. Na ardhi ikatetemeka na miamba ikapasuka vipande.52Makaburi yalifunguka, na miili ya watakatifu wengi waliokuwa wamelala usingizi walifufuliwa.53Walitoka kwenye makaburi baada ya ufufuo wake, waliingia mji mtakatifu, na wakaonekana na wengi.

54Basi yule akida na wale ambao walikuwa wakimtazama Yesu waliona tetemeko na mambo yaliyokuwa yakitokea, walijawa na woga sana na kusema, “Kweli huyu alikuwa Mwana wa Mungu.”

55Wanawake wengi waliokuwa wakimfuata Yesu kutoka Galilaya ili kumhudumia walikuwa pale wakitazama kutoka kwa mbali.56Miongini mwao walikuwa Mariamu Magdarena, Mariamu mama yake Yakobo na Joseph, na mama wa watoto wa Zebedayo

57Ilipofika jioni, alikuja mtu tajiri kutoka Arimathayo, aliyeitwa Yusufu, ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa Yesu.58Alimwendea Pilato na kuuomba mwili wa Yesu. Kisha Pilato aliagiza apate kupewa.59Yusufu aliuchukua mwili akaufunga na sanda ya sufi safi,60na akaulaza katika kaburi jipya lake alilokuwa amelichonga mwambani. Kisha akavingirisha jiwe kubwa likafunika mlango wa kaburi na akaenda zake.61Mariamu Magdalena na Mariamu mwingine walikuwa pale, wamekaa kuelekea kaburi.

62Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato.63Wakamwambia, “Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, ‘Baada ya siku tatu atafufuka tena.’64Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, ‘Amefufuka kutoka kwa wafu.’ Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza.”

65Pilato akawaambia, “Chukueni walinzi. Nendeni mkafanye hali ya usalama kama muwezavyo.”66Hivyo walikwenda na kufanya kaburi kuwa salama, jiwe liligongwa mhuri na kuweka walinzi.

28

1Baadaye jioni siku ya Sabato, jua lilipokuwa likichwa kuelekea siku ya kwanza ya juma, Mariamu magadalena, na yule Mariam mwingine walikuja kuliona kaburi.2Tazama kulikuwa na tetemeko kubwa, kwa sababu malaika wa Bwana alishuka na kulivingirisha lile jiwe, kisha akalikalia.3Sura yake ilikuwa kama ya umeme, na mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji.4Wale walinzi walijawa na hofu na kuwa kama wafu.

5Yule malaika akawafafanulia wale wanawake akisema, “Msiogope kwa maana najua kuwa mnamtafuta Yesu, aliyesulubiwa.6Hayupo hapa, lakini amefufuka kama alivyowaambia. Njooni muone mahali ambapo Bwana alilala.

7Nendeni haraka mkawaambie wanafunzi wake, ‘Amefufuka toka wafu, tazama amewatangulia Galilaya. Huko ndiko mtamwona.’ Tazama mimi nimewaambia.”

8Wale wanawake waliondoka pale kaburini haraka wakiwa na hofu na furaha kubwa, na wakakimbia kuwaambia wanafunzi wake.9Tazama Yesu akakutana nao na kusema, “Salamu.” Wale wanawake walikuja na kushika miguu yake, na kisha wakamwabudu.10Kisha Yesu akawaambia, “Msiogope, nendeni mkawaambie ndugu zangu watangulie Galilaya. Huko wataniona.”

11Wakati wale wanawake walipokuwa wakienda, tazama baadhi ya walinzi walienda mjini na kuwaambia wakuu wa makuhani mambo yote yaliyokuwa yametokea.12Nao makuhani walipokuwa wamekutana na wazee na kulijadili jambo hilo pamoja nao, walitoa kiasi kikubwa cha pesa kwa wale askari13na kuwaambia, “Waambieni wengine kuwa, ‘Wanafunzi wa Yesu walikuja usiku wakauiba mwili wa Yesu wakati sisi tulipokuwa tumelala.’14Kama taarifa hii itamfikia Liwali, sisi tutamshawishi na kuwaondoleeni ninyi mashaka yote.”15Kwa hiyo wale askari wakazichukua zile pesa na kufanya kama walivyokuwa wameelekezwa. Habari hii ikaenea sana kwa Wayahudi na imekuwa hivyo hadi leo.

16Lakini wale mitume kumi na mmoja walienda Galilaya, kwenye ule mlima aliokuwa amewaelekeza.17Nao walipomwona, walimwabudu. Lakini baadhi yao waliona shaka.18Yesu akaja kwao akawambia akisema, “Nimepewa mamlaka yote duniani na mbinguni.19Kwa hiyo enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Wabatizeni katika jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtatkatifu.20Wafundisheni kuyatii mambo yote niliyowaagiza, na tazama, mimi niko pamoja nanyi daima, hata mpaka mwisho wa dunia.

Marko

1

1Huu ndio mwanzo wa injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.2Kama ilivyoandikwa na nabii Isaya, “Tazama, ninamtuma mjumbe wangu mbele yako, mmoja atakayetayarisha njia yako.

3Sauti ya mtu aliaye nyikani, “Ikamilisheni njia ya Bwana; zinyosheni njia zake.”

4Yohana alikuja, akibatiza nyikani na kuhubiri ubatizo wa toba iletayo msamaha wa dhambi.5Nchi yote ya Yudea na watu wote wa Yerusalemu walikwenda kwake. Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yordani, wakiungama dhambi zao.6Yohana alikuwa anavaa vazi la singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake, na alikuwa anakula nzige na asali ya porini.7Alihubiri na kusema, “Yupo mmoja anakuja baada yangu mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, na sina hadhi hata ya kuinama chini na kufungua kamba za viatu vyake.8Mimi niliwabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu.”

9Ilitokea katika siku hizo kwamba Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, na alibatizwa na Yohana katika mto Yordani.10Naye Yesu alipoinuka kutoka kwenye maji, aliona mbingu zimefunguka wazi na Roho akishuka juu yake kama mfano wa njiwa.11Na sauti ilitoka mbinguni, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”12Kisha mara moja Roho akamwongoza kwenda nyikani.13Alikuwako nyikani siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika walimhudumia.

14Sasa baada ya Yohana kukamatwa, Yesu alikuja Galilaya akitangaza injili ya Mungu,15akisema, “Muda umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuamini katika injili.”

16Na alipokuwa anapita kando ya bahari ya Galilaya, alimwona Simoni na Andrea ndugu wa Simoni wakitupa nyavu zao katika bahari, kwa kuwa walikuwa wavuvi.17Yesu aliwaambia, “Njooni, nifuateni, na nitawafanya wavuvi wa watu.”18Na mara moja waliacha nyavu na wakamfuata.19Wakati Yesu alipotembea umbali kidogo, alimwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana ndugu yake; walikuwa kwenye mtumbwi wakitengeneza nyavu.20Mara aliwaita na wao walimwacha baba yao Zebedayo ndani ya mtumbwi na watumishi waliokodiwa, wakamfuata.

21Na walipofika Kaperinaumu, siku ya Sabato, Yesu aliingia kwenye sinagogi na kufundisha.22Walilishangaa mafundisho yake, kwa vile alikuwa akiwafundisha kama mtu ambaye ana mamlaka na siyo kama waandishi.23Wakati huo huo kulikuwa na mtu katika sinagogi lao aliyekuwa na roho mchafu, na alipiga kelele,24akisema, “Tuna nini cha kufanya na wewe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Nakujua u nani. Wewe ni Mtakatifu wa Mungu!”

25Yesu alimkemea pepo na kusema, “Nyamaza na utoke ndani yake!”26Na roho mchafu alimwangusha chini na akatoka kwake akilia kwa sauti ya juu.

27Na watu wote walishangaa, hivyo wakaulizana kila mmoja, “Hii ni nini Ni mafundisho mapya yenye mamlaka? Hata huamuru pepo wachafu nao wanamtii!”28Na habari kuhusu yeye mara moja zikasambaa kila mahali ndani ya mkoa wote wa Galilaya.

29Na mara moja baada ya kutoka nje ya sinagogi, waliingia nyumbani mwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.30Mama mkwe wa Simoni alikuwa amelala mgonjwa wa homa, na mara moja walimwambia Yesu habari zake.31Hivyo alikuja, alimshika kwa mkono, na kumwinua juu; homa ikaondoka kwake, na akaanza kuwahudumia.

32Jioni hiyo wakati jua limekwisha zama, walimletea kwake wote waliokuwa wagonjwa, na waliopagawa na mapepo.33Mji wote walikusanyika pamoja nje ya mlango.34Aliwaponya wengi waliokuwa wagonjwa wa magonjwa mbalimbali na kutoa mapepo mengi, bali hakuruhusu mapepo kuongea kwa sababu walimjua.

35Aliamka asubuhi na mapema, wakati kulikuwa bado giza; aliondoka na kwenda mahali pa faragha na aliomba huko.36Simoni na wote waliokuwa pamoja naye walimtafuta.37Walimpata na wakamwambia, “Kila mmoja anakutafuta”

38Aliwaambia, “Tunapaswa kwenda mahali pengine, nje katika miji inayozunguka, ili niweze kuhubiri huko pia. Ndiyo sababu nilikuja hapa.”39Alikwenda akipita Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kukemea mapepo.

40Mwenye ukoma mmoja alikuja kwake. Alikuwa akimwomba; alipiga magoti na alimwambia, “Kama unataka, waweza kunifanya niwe safi.”

41Yesu alimwonea huruma, alinyosha mkono wake na kumgusa, akimwambia, “Ninataka, uwe msafi.”42Mara moja ukoma ukamtoka, na alifanywa kuwa msafi.43Yesu akamwonya vikali na akamwambia aende mara moja,44Alimwambia, “Hakikisha hausemi neno kwa yeyote, lakini nenda, ujionyeshe kwa kuhani, na utoe dhabihu kwa ajili ya utakaso ambayo Musa aliagiza, kama ushuhuda kwao.”45Lakini alikwenda na kuanza kumwambia kila mmoja na kueneza neno zaidi hata Yesu hakuweza tena kuingia mjini kwa uhuru. Hivyo alikaa mahali pa faragha na watu walikuja kwake kutoka kila mahali.

2

1Yesu aliporudi Kapernaumu baada ya siku chache walisikia kwamba yupo nyumbani.2Watu wengi sana walikusanyika pale na haikuwepo nafasi tena, hata ile ya mlangoni, na Yesu alisema neno kwao.3Kisha baadhi ya watu walikuja kwake waliomleta mtu aliyekuwa amepooza; watu wanne walikuwa wamembeba.4Wakati waliposhindwa kumpitisha kwa sababu ya umati wa watu, waliondoa paa juu mahali pale alipokuwa Yesu. Na walipokuwa wamekwishatoboa tundu, walishusha kitanda ambacho mtu aliyepooza alikuwa amelala.5Alipoiona imani yao, Yesu alimwambia mtu aliyepooza, “mwanangu, dhambi zako zimesamehewa.”

6Lakini baadhi ya waandishi wale waliokuwa wamekaa pale walijihoji mioyoni mwao,7“Mtu huyu anawezaje kusema hivi? Anakufuru! Nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?”

8Mara Yesu alijua rohoni mwake walichokuwa wakifikiri miongoni mwao wenyewe. Aliwaambia, “Kwa nini mnafikiri hivi mioyoni mwenu?9Lipi ni jepesi zaidi kusema kwa mtu aliyepooza, ‘Dhambi zako zimesamehewa’ au kusema ‘Simama, chukua kitanda chakomkeka wako, na utembee?’10Lakini ili wapate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka ya kusamehe dhambi katika dunia, alimwambia yule aliyepooza,11“Inuka, chukua mkeka wako, na uende nyumbani kwako.”

12Alisimama na mara moja akachukua mkeka wake, na alienda nje ya nyumba mbele ya kila mtu, hivyo wote wakashangaa na wakampa Mungu utukufu, nakusema “Kamwe, hatujawahi kuona jambo kama hili.”

13Alienda tena kando ya ziwa, na umati wote wa watu walikuja kwake, na akawafundisha.14Alipokuwa akipita alimwona Lawi mwana wa Alfayo ameketi kwenye sehemu ya kukusanyia kodi na akamwambia, “Nifuate.” Alisimama na kumfuata.

15Na wakati Yesu alipokuwa akipata chakula katika nyumba ya Lawi, wakusanya kodi wengi na watu wenye dhambi walikuwa wakila na Yesu na wanafunzi wake, kwa kuwa walikuwa wengi nao walimfuata.16Wakati waandishi, ambao walikuwa Mafarisayo, walipoona kwamba Yesu alikuwa akila na watu wenye dhambi na wakusanya kodi, waliwaambia wanafunzi wake, “Kwa nini anakula na wakusanya kodi na watu wenye dhambi?”

17Wakati Yesu aliposikia hivi aliwaambia, “Watu walio na afya katika mwili hawamhitaji tabibu; ni watu wagonjwa pekee ndio wanamhitaji. Sikuja kuwaita watu wenye haki, lakini watu wenye dhambi.”

18Wanafunzi wa Yohana na Mafarisayo walikuwa wakifunga. Na baadhi ya watu walikuja kwake na kumwambia, “Kwa nini wanafunzi wa Yohana na mafarisayo hufunga, lakini wanafunzi wako hawafungi?

19Yesu aliwaambia, “Je waliohudhuria harusi wanaweza kufunga wakati bwana harusi bado akiwa pamoja nao? Kwa vyovyote bwana harusi akiwa bado yuko pamoja nao hawawezi kufunga.”20Lakini siku zitakuja wakati bwana harusi atakapoondolewa kwao, na katika siku hizo wao watafunga.

21Hakuna mtu ashonaye kipande kipya cha nguo kwenye vazi kuukuu, vinginevyo kiraka kitararuka kutoka katika hilo, kipya kitararuka kutoka katika kikuukuu, nayo itachanika zaidi.22Hakuna mtu atiaye divai mpya kwenye viriba vikuukuu, vinginevyo divai itavipasua viriba na vyote viwili divai na viriba vitapotea. Badala yake, weka divai mpya katika viriba vipya.”

23Katika siku ya Sabato Yesu alipita kwenye baadhi ya mashamba, na wanafunzi wake walianza kuchukua baadhi ya masuke ya ngano.24Na Mafarisayo walimwambia, “Tazama, kwa nini wanafanya kitu ambacho ni kinyume cha sheria katika siku ya Sabato?”

25Aliwaambia, “Hamkusoma kile alichofanya Daudi alipokuwa katika uhitaji na njaa—yeye pamoja na watu waliokuwa pamoja naye?26Jinsi alivyoenda katika nyumba ya Mungu wakati Abiathari alipokuwa kuhani mkuu na akala mkate uliowekwa mbele—ambao ilikuwa kinyume cha sheria kwa mtu yeyote kula isipokuwa makuhani— tu. Na aliwapa hata baadhi ya wale waliokuwa pamoja naye?”27Yesu alisema, “Sabato ilifanywa kwa ajili ya mwanadamu, siyo mwanadamu kwa ajili ya Sabato.28Kwa hiyo, Mwana wa Adamu ni Bwana, wa Sabato.”

3

1Tena Yesu aliingia ndani ya sinagogi na palikuwa na mtu mwenye mkono uliopooza.2Baadhi ya watu walikuwa wakimfuatilia kwa ukaribu kuona kama atamponya siku ya Sabato ili wamshitaki.3Yesu alimwambia mtu mwenye mkono uliopooza, “Inuka simama katikati ya umati huu.”4Kisha akawaambia wale watu, “Je ni halali kutenda tendo jema siku ya Sabato au kutenda yasiyo haki; kuokoa maisha, au kuua?” Lakini hawakujibu walibaki kimya.5Akawatazama kwa hasira, akihuzunika kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao, na akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha na Yesu akamponya mkono wake.6Mafarisayo wakaenda nje wakafanya njama pamoja na Maherodi dhidi yake ili kumuua.

7Kisha Yesu, pamoja na wanafunzi wake, walienda baharini, na umati mkubwa wa watu uliwafuata ukitokea Galilaya na Uyahudi 8na kutoka Yerusalemu na Idumaya na mbele ya Yordani na jirani ya Tiro na Sidoni, umati mkubwa, uliposikia kila kitu alichokuwa anakifanya, walikuja kwake.9Na aliwaambia wanafunzi wake kuandaa mtumbwi mdogo kwa ajili yake kwa sababu ya umati, ili kwamba wasije wakamsonga.10Kwa kuwa aliwaponya wengi, kila mtu aliyekuwa na mateso alikuwa na shauku ya kumfikia ili amguse apone.11Popote roho wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kulia, na walisema, “Wewe ni Mwana wa Mungu.”12Aliwakemea kwa msisitizo wasimfanye akajulikana.

13Alipanda juu ya mlima, na akawaita aliowataka, na wakamwendea.14Akawachagua kumi na wawili (aliowaita mitume), ili kwamba wawe pamoja naye na akawatuma kuhubiri,15na kuwapa mamlaka ya kutoa mapepo.16Na akawachagua kumi na wawili: Simoni, aliyempa jina la Petro,17Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake Yakobo, aliyepewa jina la Bonagesi, hao ni, wana wa ngurumo,18na Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,19na Yuda Iskariote, ambaye atamsaliti.

20Kisha alienda nyumbani, na umati wa watu wakimfuata kwa pamoja, tena, hata wasiweze kula hata mkate.21Familia yake waliposikia habari hiyo, walienda kumkamata, kwani walisema, “Amerukwa na akili.”

22Waandishi waliokuja kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli,” na, “KwaNi mtawala wa mapepo na anatoa mapepo.”

23Yesu aliwaita kwake na kusema nao kwa mifano, “Jinsi gani Shetani aweza kumtoa Shetani?24Kama ufalme ukigawanyika wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.25Kama nyumba ikigawanyika yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.26Kama Shetani atainuka kinyume chake mwenyewe na kugawanyika, hawezi kusimama, na atakuwa amefika mwisho wake.27Lakini hakuna hata mmoja awezaye kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake bila kumfunga kwanza, na kisha kukusanya vilivyomo nyumbani.28Kweli nawambieni, dhambi zote za wana wa watu zitasamehewa, pamoja na kufuru ambazo wanatamka,29lakini yeyote atakaye mkufuru Roho Mtakatifu hatasamehewa kamwe, bali ana hatia ya dhambi ya milele.”

30Yesu alilisema hili kwa sababu walikuwa wakisema, “Ana roho mchafu.”

31Kisha mama yake na ndugu zake walikuja na kusimama nje. Wakatuma mtu, kumwita.32Na umati wa watu uliokuwa umekaa umeketi karibu naye wakamwambia, “mama yako na ndugu zako wako nje, na wanakutafuta wewe.”

33Aliwajibu, “Ni nani mama yangu na ndugu zangu?”34Aliwatazama waliokuwa wamekaa wamemzunguka, na akasema, “Tazama, hawa ni mama zangu na ndugu zangu!35Yeyote afanyaye mapenzi ya Mungu, mtu huyo ni ndugu yangu, na dada yangu, na mama yangu.”

4

1Tena alianza kufundisha kando ya bahari, na umati mkubwa ulikusanyika ukamzunguka. Akaingia ndani ya mtumbwi baharini, na kuketi ndani ya mtumbwi. Umati wote ulikuwa pembeni mwa bahari ufukweni.2Na akawafundisha mambo mengi kwa mafumbo, na akawaambia katika mafundisho yake.3“Sikilizeni, mpanzi alienda kupanda mbegu.4Alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu zilianguka njiani, na ndege wakaja wakazila.5Mbegu zingine zilianguka kwenye mwamba, ambako hapakuwa na udongo mwingi. Maramoja zikaibuka, kwa sababu haikua na udongo ya kutosha.6Lakini jua lilipochomoza, mimea zilinyauka, kwa sababu hayakua na mizizi, zilikauka.7Mbegu ziingine zilianguka katikati ya miiba. Miiba ilikua na ikazisonga, na hazikuzaa matunda yoyote.8Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na zikazaa matunda wakati zikikua na kuongezeka na kuzaa mara thelathini zaidi, sitini, na pia mara mia moja.”9Na akasema, “Yeyote mwenye masikio ya kusikia, na asikie!”

10Yesu alipokuwa peke yake, wale waliokuwa karibu naye na wale kumi na wawili walimuuliza kuhusu mafumbo.11Akawaambia, “Kwenu ninyi Mungu amewafunulia siri za ufalme wake. Lakini kwa walio nje kila kitu ni kwa mafumbo,
12ili wakitazama, ndiyo watazame, lakini wasione, na wakisikia, ndiyo watasikia, lakini wasielewe, ama sivyo wakageuka na Mungu atawasamehe.”

13Yesu akawaambia, “Je hamuelewi mfumbo huu? Sasa mtawezaje kuelewa mifano mingine?”14Mpanzi alipanda neno.15Hawa ndio wale walio kando ya njia, mahali neno lilipopandwa. Walipolisikia, maramoja Shetani akaja na kulichukua neno ambalo lilipandwa ndani yao.16Na baadhi ni mbegu zilizopandwa juu ya mwamba; ambao, wanapolisikia neno wanalipokea mara moja kwa furaha.17Lakini hawana mizizi yoyote ndani yao, lakini huvumilia kwa muda. Baadaye wakati dhiki na mateso yanapokuja kwa sababu ya neno, mara moja huacha imani.18Na wengine ni wale waliopandwa katika miiba. Wale ambao hulisikia neno,19lakini masumbuko ya dunia na udanganyifu wa mali na tamaa za mambo mengine huja na kulisonga neno, na haina tija.20Wale ambao walipandwa kwa udongo mzuri ni wale wanaoskia neno, kulipokea na huzaa matunda, thelathini, sitini, na mara mia moja zaidi.

21Yesu akawaambia, “Je huwa unaleta taa ndani ya nyumba na kuiweka chini ya kikapu au chini ya kitanda? Huileta ndani na kuiweka juu ya kinara.22Kwa kuwa hakuna chochote kilichojificha ambacho hakitajulikana, na hakuna siri ambayo haitakua wazi.23Yule aliye na masikio ya kusikia, na asikie!”

24Akawaambia, “Muwe makini kwa kile mnachosikia, kwa kuwa kipimo mtatumia ndicho mtakachopimiwa, na zaidi yataongezwa kwenu.25Kwa sababu yeye aliye nacho, ataongezewa zaidi, na yule asiye nacho, kwake kitachukuliwa hata kile alicho nacho.”

26Akasema, “Ufalme wa Mungu ni kama mtu aliyepanda mbegu katika udongo.27Anayelala usiku na kuamka asubuhi, na kukuta mbegu zimechipuka na kukua, ingawa hajui zilivyo chipuka.28Aridhi huzaa nafaka yenyewe: kwanza majani, halafu maua, halafu nafaka iliyo komaa.29Wakati mazao yameiva, yeye hutuma mara moja hupeleka mundu kwa maana mavuno yamefika.”

30Na tena akasema, “ni nini tunaweza kulinganisha na ufalme wa Mungu, au ni mfumbo mgani tunaweza tumia kuieleza?31Ni kama mbegu ya haradali, ambayo, inapopandwa, ni ndogo zaidi kuliko mbegu zote duniani.32Hata, wakati imepandwa, hukua kubwa zaidi ya mimea yote ya bustani, na huunda matawi makubwa, kwahivyo ndege wa angani wanaweza kutengeneza viota kwa kivuli chake.”

33Mafumbo mengi kama hii, yesu alinena nao neno, kwa kadri walivyoweza kuelewa,34na hakusema nao bila mafumbo. Lakini alipokuwa peke yake, aliwaelewesha wanafunzi wake.

35Siku hiyo, wakati wa jioni ulipofika, akawaambia, “Twendeni ng'ambo ile ingine.”36Hivyo wakauacha umati wa watu, wakamchukua Yesu, vile alivyokua, ndani ya mtumbwi. Kulikua na mitumbwi mingine yaliyoambatana naye.37Dhoruba ya upepo mkali ikatokea, na mawimbi yalikuwa yakiingia ndani ya mashua hata mashua karibu kujaa maji.38Lakini Yesu mwenyewe alikuwa numa ya meli, amelala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamuamsha wakamwambia, “Mwalimu, hujali kwamba tuko karibu kuangamia?”

39Akaamka, akaukemea ule upepo, na akaiambia bahari, “Amani! Tulia” Ule upepo ukakoma, na kukawa na utulivu mkubwa.40Akasema nao, “Mbona mnaogopa? Bado hamna Imani?”

41Walijawa na hofu kubwa ndani yao na wakaambiana, “Huyu ni nani, hata upepo na bahari vinamtii?”

5

1Walikuja mpaka ng'ambo ya bahari, katika mkoa wa Gerasi.2Wakati Yesu alipokua akitoka kwa mtumbwi, mwanaume mwenye pepochafu alikuja kwake kutoka makaburini.3Mtu huyu aliishi makaburini. Hakuna aliyeweza kumzuia kamwe, hata kwa kumfunga minyororo.4Alikuwa amefungwa mara kadhaa kwa pingu na minyororo. Alikata minyororo na pingu zake zikavunjika. Hakuna hata mmoja aliyekuwa na nguvu za kumshinda.5Usiku na mchana akiwa makaburini na milimani, alilia na kujikata mwenyewe kwa mawe makali.6Alipomwona Yesu kwa umbali, alimkimbilia na kuinama mbele yake.7Akalia kwa sauti kubwa, “Nina shughuli gani na wewe, Yesu, Mwana wa Mungu aliye Juu? Nakuomba kwa jina la Mungu mwenyewe, usinitese.”8Kwa kuwa Yesu alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe roho mchafu.”

9Yesu akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Naye alimjibu, “Jina langu ni Jeshi, kwa kuwa tuko wengi.”10Alimsihi tena na tena asiwapeleke nje ya mkoa.11Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe walikua wakilisha mlimani,12nao walimsihi, wakisema, “Utupeleke ndani ya nguruwe; tuingie ndani yao.”13Hivyo aliwaruhusu; roho wachafu walimtoka na kuingia ndani ya nguruwe, nao nguruwe walikimbia chini ya kilima mwinuko mpaka baharini, na angalau nguruwe elfu mbili walizama baharini.

14Na wale waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia nakwenda kutoa taarifa ya yaliyotendeka katika mji na mashambani, na watu wengi walitoka kwenda kuona kilichotokea.15Walikuja kwa Yesu na kumuona mtu aliyepagawa na pepo, aliyekuwa amepagawa na Jeshi la mapepo, amekaa hapo, amevishwa na katika akili yake sawa na wakaogopa.16Wale waliokuwa wameshudia kilichotendeka kwa mtu aliyekuwa amepagawa na mapepo waliwaambia kilichotokea kwa undani, na pia kuhusu nguruwe.17Nao walianza kumsihi Yesu aondoke katika mkoa wao.

18Alipokuwa akiingia ndani ya mtumbwi, yule aliyekuwa amepagawa na mapepo alimsihi kwamba aende pamoja naye.

19Lakini Yesu hakumruhusu, lakini akamwambia, “Nenda nyumbani kwako na kwa watu wako na uwaambie alichokufanyia Bwana, na huruma aliyokuonyesha.”20Hivyo alienda na kuanza kutangaza mambo makuu ambayo Yesu amefanya kwake katika maeneo yote ya Dekapoli, na kila mtu alistaajabu.

21Na wakati Yesu alipovuka tena upande mwingine ndani ya mtumbwi, umati mkubwa ulikusanyika karibu naye, alipokuwa kando ya bahari.22Mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo alikuja, na alipomwona, alianguka miguuni pake.23Akamsihi zaidi na zaidi, akisema, “Binti yangu mdogo anakaribia kufa. Ninakusihi, njoo na uweke mikono yako juu yake ili aweze kupata afya na kuishi.”24Hivyo alienda pamoja naye, na umati mkubwa watu ulimfuata nao walisonga karibu wakimzunguka.

25Kulikuwa na mwanamke kati yao ambaye damu yake ilikuwa inamtoka kwa miaka kumi na miwili.26Aliteseka vya kutosha chini ya matabibu wengi na alitumia kila kitu alichokuwa nacho, lakini badala kuendelea vizuri hali yake iliendelea kuwa mbaya.27Aliposikia habari kuhusu Yesu, alikuja nyuma yake katikati ya umati na akagusa vazi lake.28Kwa kuwa alisema, “Kama nitayagusa mavazi yake, nitapona.”29Alipomgusa, kutokwa damu kulikoma, na alijisikia katika mwili wake kwamba ameponywa kutoka mateso yake.

30Na ghafla Yesu aligundua ndani yake mwenyewe kwamba nguvu zimemtoka. Akageuka katika ya umati ya watu na kuuliza, “Ni nani aliyeligusa vazi langu?”

31Wanafunzi wake walimwambia, “Unaona umati huu umekusonga nawe wauliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’”32Lakini Yesu alitazama pande zote kuona ambaye aliye mgusa.

33Mwanamke huyo, akijua kilichomtendekea, aliogopa na kutetemeka. Alikuja na alianguka chini mbele yake na kumwambia ukweli wote.34Yesu akamwambia, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa amani na uponywe kutoka kwenye mateso yako.”

35Yesu alipokuwa akizungumza, baadhi ya watu walikuja kutoka kwa kiongozi wa Sinagogi, wakisema, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua mwalimu?”

36Lakini Yesu aliposikia ambacho walikisema, alimwambia kiongozi wa Sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”37Hakumruhusu yeyote kuongozana naye, isipokuwa Petro, Yakobo, na Yohana, ndugu yake Yakobo.38Walikuja nyumbani kwa kiongozi wa Sinagogi naye aliona vurugu; za kulia kwingi na kuomboleza kwa nguvu.39Alipoingia nyumbani, aliwaambia, “Kwa nini mnahuzunika na kwa nini mnalia? Mtoto hajafa bali amelala.”40Walianza kumkejeli. Lakini aliwatoa wote nje na kumchukua baba ya mtoto na mama na wale waliokuwa naye, na akaingia mahali alipokuwa mtoto.41Aliuchukua mkono wa mtoto na kumwambia, “Talitha koum!” ambayo ni kusema, “Binti mdogo, nakuambia, amka.”42Ghafla mtoto akaamka na kutembea (kwa kuwa alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili). Na ghafla walishikwa na mshangao mkubwa.43Aliwaamuru kwa ukali kwamba mtu yeyote asijue kuhusu hili. Kisha akawaambia wampe binti chakula.

6

1Na akaondoka hapo na kwenda mjini kwao Nazareti, na wanafunzi wake wakamfuata.2Sabato ilipofika, alianza kufundisha katika Sinagogi. Watu wengi walimsikiliza na wakashangazwa. Wakasema, “Amepata wapi mafundisho haya?” “Ni hekima ya namna gani hii aliyo ipata?” “Huyu Yesu anatendaje miujiza hii kwa mikono yake?”3“Je huyu si yule mtoto wa seremala, mwana wa Mariamu na ndugu yao ambao ni Yakobo, Yose, Yuda na Simioni? Je dada zake si tunaishi nao hapa pamoja nasi?” Watu wa nazareti hawakufurahishwa na mafundisho ya Yesu.

4Yesu akawaambia, “Nabii hapati heshima, katika mji wake hata kwa ndugu zake wa nyumbani mwake.”

5Hakuweza kutenda miujiza, ila aliwawekea mikono wagonjwa wachache akawaponya.6Alishangazwa sana kwa sababu ya kutokuamini kwao. Kisha alivitembelea vijiji vya jirani akifundisha.

7Aliwaita wale wanafunzi kumi na wawili akaanza kuwatuma wawili wawili. Aliwapa mamlaka juu ya pepo wachafu,8na kuwaamuru wasichukue chochote wanapokwenda isipokuwa fimbo tu. Wasichukue chakula, wala mkoba, wala fedha kibindoni;9lakini wavae viatu, na siyo kanzu mbili.10Na akawaambia, “Nyumba yoyote mtakayoingia, kaeni hapo mpaka mtakapoondoka.11Na mji wowote usipowapokea wala kuwasikiliza, ondokeni kwao, kung'uteni mavumbi ya miguu yenu, iwe ushuhuda kwao.”12Nao wakaenda wakiwaambia watu watubu na kuacha dhambi zao.13Wanafunzi walipo kwenda waliyafukuza mapepo wengi, na waliwapaka mafuta wagonjwa na wakaponywa.

14Mfalme Herode aliposikia kuhusu, habari za Yesu jinsi anavyo ponya na kufukuza mapepo, na kutambulika kwa watu. Baadhi ya watu walisema, “Itakuwa Yohana mbatizaji amefufuka na kwa sababu hiyo, hii nguvu ya miujiza inafanya kazi ndani yake.”15Baadhi watu wakasema, “Huyu ni Eliya,” Ambaye Mungu aliahidi kwamba atarudi, wengine wakasema, “Huyu ni nabii, kama mmoja wa wale manabii wa zamani.”

16Lakini Herode aliposikia haya akasema, “Yohana, niliye agiza askari wamkate kichwa amefufuka.”

17Maana Herode mwenyewe alituma askari Yohana akamatwe na alimfunga gerezani kwa sababu ya Herodia (mke wa kaka yake ambaye ni Filipo) kwa sababu Herode alikuwa amemuoa.18Kwa maana Yohana alimwambia Herode, “Si halali kumuoa mke wa kaka yako.”19Lakini Herodia alianza kumchukia na alikuwa akitaka kumuuaYohana, lakini hakuweza, Hivyo alitafuta njia ya kumuua20maana Herode alimwogopa Yohana; alijua kwamba ni mwenye haki mtu mtakatifu, na alimwacha salama. Na alipoendelea kumsikiliza Yohana alihuzunika sana, lakini alifurahia mazungumzo yake kuyasikiliza.

21Hata ulipofika wakati mwafaka ikawa imekaribia siku ya kuzaliwa Herode akawaandalia maofisa wake sherehe, na makamanda, na viongozi wa Galilaya.22Ndipo binti yake Herodia akaingia na kucheza mbele yao, akamfurahisha mfalme Herode na wageni walioketi wakati wa chakula cha jioni. Ndipo mfalme akamwambia binti, “Niombe chochote unachotaka nami nitakupa.”23Akamwekea kiapo na kusema, chochote utakachoniomba, nitakupa, hata nusu ya ufalme wangu ninao miliki.”

24Binti akatoka nje ya chumba cha sherehe akamuuliza mama yake, “Niombe nini?” Mama Akasema omba, “Kichwa cha Yohana Mbatizaji.”

25Kwa haraka sana akaingia kwa mfalme akaanza kusema, “Nataka unipatie juu ya sahani, kichwa cha Yohana Mbatizaji.”26Mfalme alisikitishwa sana na ombi la binti, lakini kwa sababu ya kiapo chake na kwa ajili ya wageni, hakuweza kumkatalia ombi lake.27Hivyo, mfalme akatuma askari kati ya walinzi wake na kuwaagiza kwenda kumletea binti kichwa cha Yohana. Mlinzi alikwenda kumkata kichwa Yohana akiwa kifungoni.28Akakileta kichwa chake kwenye sahani na kumpatia binti, na binti akampa mama yake.29Na wanafunzi wa Yohana waliposikia hayo, walikwenda kuuchukua mwili wake wakaenda kuuzika kaburini.

30Na mitume, waliporudi kutoka kuhubiri walikusanyika pamoja mbele ya Yesu, wakamweleza yote waliyofanya na waliyoyafundisha.31Naye akawaambia, “Njooni ninyi wanafunzi wangu mahali pa faragha na tupumzike kwa muda.” Watu wengi walikuwa wanakuja kwa mitume na kuondoka, hata hawakupata muda wa kula chakula.32Hivyo wakapanda mashua wakaenda mahali pa faragha pasipokuwa na watu.33Lakini watu waliwaona Yesu na wanafunzi wake wakiondoka na wengi wakawatambua, kwa pamoja walikimbia kwa kupitia njia ya miguu kutoka miji yote, nao wakafika pwani kabla yao.34Yesu na wanafunzi wake Walipofika pwani, aliona umati mkubwa na akawahurumia, kwa sababu walikuwa kama kondoo wasiokuwa na mchungaji. Na akaanza kuwafundisha mambo mengi.

35Muda uliendelea sana ilikuwa ni jioni, wanafunzi wakamjia wakamwambia, “Hapa ni mahali pa faragha hakuna makazi ya watu, na muda umeendelea sana.36Uwaage watu waende miji ya jirani na vijiji ili wakajinunulie chakula.”

37Lakini akawajibu akisema, “Wapeni ninyi chakula.” Wakamwambia, “Tunaweza kwenda na kununua mikate yenye thamani ya dinari mia mbili na kuwapa wale?”

38Akawauliza,” Mna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Walipotazama wakamwambia, “Mikate mitano na samaki wawili.”39Akawaamuru watu waketi katika makundi makundi, juu ya majani mabichi.40Wakawaketisha katika makundi; makundi ya mamia kwa hamsini.41Kisha akachukua mikate mitano na samaki wawili, na kutazama mbinguni, akamshukuru, Mungu, kisha akawapa wanafunzi waweke, ili wawape makutano. Wakaiweka mbele ya umati. Na kisha aligawa samaki wawili na kuwapa watu wote.42Watu wote walikula hadi wakatosheka.43Walikusanya vipande vya mikate iliyobaki, Vikajaa vikapu kumi na viwili, na pia vipande vya samaki.44Na walikuwa wanaume elfu tano waliokula mikate. Na samaki. Lakini wanawake na watoto hawakuhesabiwa.

45Kisha akawaambia wanafunzi wake, wapande kwenye mashua waende sehemu nyingine, hadi Bethsaida, wakati Yeye akiwaaga makutano.46Watu walipokwisha kuondoka, Yesu akaenda mlimani kuomba.47Ilipofika jioni, na mashua yao ilikuwa katikati ya bahari, naye Yesu alikuwa peke yake pwani.48Na aliwaona wakitaabika kupiga makasia kwa sababu upepo uliwazuia. Ilipokaribia asubuhi akawaendea, akitembea juu ya maji, na alitaka kuwapita.49Lakini walipomwona Yesu anatembea juu ya maji, wakaingiwa na wasiwasi wakidhani ni mzimu wakapiga kelele.50Kwa sababu walimwona wakajawa na hofu. Mara Yesu akasema nao akawaambia, “Muwe na ujasiri! Ni mimi! Msiwe na hofu.”51Akaingia ndani ya mashua, na upepo ukaacha kuvuma, nao wakamshangaa sana.52Hivyo hawakuwa wameelewa maana ya ile mikate. Maana akili zao zilikuwa zimeshindwa kuelewa.

53Nao walipovuka ng'ambo, walifika nchi ya Genesareti mashua ikatia nanga.54Walipotoka nje ya mashua, watu wakamtambua, Yesu na wanafunzi wake.55Wakakimbia kutangaza katika mkoa mzima na wakaanza kuwaleta watu wagonjwa kwa machela, kila waliposikia amekuja.56Popote alipoingia katika vijiji, au mjini, au katika nchi, watu waliwaweka wagonjwa mahali pa soko, na watu wakamwomba awaruhusu wagonjwa kugusa pindo la vazi lake. Na wote waliomgusa waliponywa.

7

1Mafarisayo na baadhi ya waandishi ambao walikuwa wametokea Yerusalemu walikusanyika. Wakimzunguka Yesu.2Na mafarisayo wandishi waliona kuwa baadhi ya wanafunzi wake walikula mkate kwa mikono najisi, hiyo haijaoshwa.3(Kwa sababu Mafarisayo na Wayahudi wote hawali mpaka wameosha mikono yao vizuri; wanashikilia utamaduni wa wazee.4Mafarisayo wanaporudi kutoka mahali pa soko, hawali mpaka wameoga kwanza. Na kuna sheria zingine ambazo wanazifuata kabisa, ikiwa ni pamoja na kuosha vikombe, masufuria, vyombo vya shaba, na hata viti vinavyotumika wakati wa chakula.)

5Mafarisayo na waandishi walimuuliza Yesu, “Kwa nini wanafunzi wako hawatii na kufuata utamaduni wa wazee wetu, wanakula chakula pasipo kunawa mikono?”

6Lakini yeye aliwaambia, “Isaya alitabiri vizuri kuhusu ninyi mafarisayo na wandishi wanafiki, aliandika, ‘Watu hawa wananiheshimu kwa midomo yao, lakini mioyo yao iko mbali na mimi.
7Wananifanyia ibaada zisizo na maana, wakifundisha sheria za wanadamu kama mapokeo yao.’

8Mmeiacha sheria ya Mungu na kushikilia kwa tamaduni za wazee wenu.”9Yesu kawaambia, “Mmezikataa amri za Mungu kwa kwamba mtunze tamaduni zenu!10Kwa kuwa Musa alisema, ‘mheshimu baba yako na mama yako,’ na ‘Yeye aamtukanaye baba yake au mama yake hakika atakufa.’11Lakini mnasema, ‘kama mtu akisema kitu cha kumwahidi baba yake au mama, cha “Msaada wowote ambao mngepokea kutoka kwangu ni hazina ya Hekalu,”’ (hiyo ni kusema kwamba, ‘nimeutoa kwa Mungu’)12hivyo haumruhusu mtoto kufanya jambo lolote kwa ajili ya baba au mama yake.13Mnazifanya amri za Mungu kuwa bure kwa kuleta tamaduni zenu. Mnafanya mengi ya jinsi hiyo yanayofanana.”

14Yesu aliwaita makutano tena na kuwaambia, “Mnisikilize mimi, ninyi nyote, na mpate kunielewa.15Hakuna chakula chochote kitokacho nje ya mtu ambacho chaweza kumchafua mtu kiingiapo ndani yake. Bali ni kile asemacho mtu ndicho kimchafuacho.16“Kama mtu yeyote ana masikio ya kusikia na asikie jambo hili, na aelewe.”

17Yesu alipowaacha umati wa watu kuingia nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza kuhusu mfano huo.18Yesu akasema, “Na ninyi pia bado hamjaelewa? Hamuoni kwamba chakula chochote kimuingiacho mtu hakiwezi kumchafua,19kwa sababu hakiwezi kwenda kwenye moyo wake, lakini kinaingia katika tumbo lake na kisha kinapita kwenda chooni.” Kwa maelezo haya Yesu alivifanya vyakula vyote kuwa safi.20Yesu alisema, “kile ambacho kinamtoka mtu ndani ndicho kimchafuacho.21Kwa kuwa hutoka ndani ya mtu, ndani ya moyo, hutoka mawazo maovu, usherati, wizi, mauaji,22uzinzi, tamaa mbaya, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, majivuno, ujinga.23Maovu haya yote yanatoka ndani, na ndiyo yale yamchafuayo mtu.”

24Yesu aliamka kutoka pale alipokuwa ameketi na kuondoka kwenda katika mkoa wa Tiro na Sidoni. Aliingia ndani na hakutaka mtu yeyote ajue kuwa alikuwa hapo, lakini haikuwezekana kumficha.25Lakini ghafla mwanamke alikuja kwa Yesu, ambaye mtoto wake mdogo alikuwa na roho mchafu, alisikia habari zake, akaja, na kupiga magoti miguuni pake Yesu.26Mwanamke huyo alikuwa Myunani, wa kabila la Kifoenike. Alimsihi yesu amfukuze pepo atoke kwa binti yake.27Yesu akamwambia mwanamke, “Waache watoto walishwe kwanza, chakula, kwa kuwa sio sawa kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

28Lakini yule mwanamke akamjibu na kusema, “Ndiyo Bwana, hata mbwa chini ya meza hula mabaki ya chakula cha watoto.”

29Yesu akamwambia, “Kwa kuwa unaamini hivi, uko huru kwenda. Pepo amemtoka binti yako.”30Mwanamke alirudi nyumbani kwake na akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo alikuwa amemtoka.

31Yesu alitoka tena nje ya mkoa wa Tiro na kupitia Sidoni kuelekea Bahari ya Galilaya mpaka kanda ya Dekapoli.32Na wakamletea mtu aliyekuwa kiziwi na alikuwa hawezi kuzungumza vizuri, walimsihi Yesu aweke mikono juu yake.33Yesu alimtoa mtu huyu nje ya kusanyiko kwa siri, na akaweka vidole vyake kwenye masikio yake, na baada ya kutema mate, aligusa ulimi wakewa yule mtu.34Yesu alitazama juu mbinguni, akahema na kumwambia, “Efatha,” hiyo ni kusema “funguka!”35Na muda ule ule masikio yakafunguka, na kilichokuwa kimezuia ulimi kiliharibiwa na akaweza kuongea vizuri.

36Na aliwaamuru wasimwambie mtu yeyote. Lakini kadri alivyowaamuru, ndivyo walivyotangaza habari hizo kwa wingi.37Hakika walishangazwa, na kusema, “Amefanya kila kitu vizuri. Hata amewafanya viziwi kusikia na mabubu kuongea.”

8

1Katika siku hizo, kulikuwa tena na umati mkubwa, na hawakuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake na akawaambia,2Ninauhurumia umati huu, kwa sababu wameendelea kuwa nami kwa muda wa siku tatu na hawana chakula.3Nikiwaaga warudi majumbani mwao bila kula wanaweza wakazimia njiani kwa njaa. Na baadhi yao wametoka mbali sana.”

4Wanafunzi wake wakamjibu, “Tutaweza kupata wapi mikate ya kutosha katika sehemu kama hii isiyo na watu ili kuwashibisha watu hawa?”

5Akawauliza, “mna mikate mingapi?” Wakasema, “Saba.”

6Akauamuru umati ukae chini. Akachukua mikate saba, akamshukuru Mungu, na kuivunja. Akawapa wanafunzi wake waiweke mbele yao, nao wakaiweka mbele ya umati.7Pia walikuwa na samaki wadogo wachache, na baada ya kushukuru, aliwaamuru wanafunzi wake wawagawie hivi pia.8Walikula na wakatosheka. Na walikusanya vipande vilivyo baki, vikapu vikubwa saba.9Kulikuwa na watu kama elfu nne. Kisha aliwaacha waende.10Mara akapanda mashua pamoja na wanafunzi wake, na wakaenda katika ukanda wa Dalmanutha.

11Kisha Mafarisayo wakatoka na kuanza kubishana naye. Walitaka awape ishara kutoka mbinguni, ili kumjaribu.12Akahuzunika moyoni mwake akasema, “Kwa nini kizazi hiki kinatafuta ishara? Nawaambia ninyi kweli, hakuna ishara itakayotolewa kwa kizazi hiki.”13Kisha akawaacha, akaingia ndani ya mashua tena, akaondoka kuelekea upande mwingine.14Wakati huo wanafunzi walikuwa wamesahau kuchukua mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu ndani ya mashua.15Yesu akawaonya akisema, “Muwe macho na mjilinde dhidi ya chachu ya Mafarisayo na chachu ya Herode.

16Wanafunzi walikuwa wakibishana wao kwa wao juu ya kutokuwa na mikate

17Yesu alipotambua hayo, akawauliza, “Mbona mnabishana kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamuoni au hamuelewi? Mna mioyo migumu?18Mna macho, hamuoni? Mna masikio, hamsikii? Hamkumbuki?19Nilipoimega mikate mitano kwa watu elfu tano, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?” Wakamjibu, “kumi na mbili.”

20“Na nilipoimega mikate saba kati ya watu elfu nne, mlichukua vikapu vingapi vilivyo jaa vipande vya mikate?” Wakasema, “Saba.”21Akawaambia, “Bado hamuelewi?”

22Wakafika Bethsaida. Watu pale wakamleta kipofu mmoja kwa Yesu na kumsihi Yesu amguse.23Yesu akamshika mkono yule kipofu, na kumwongoza nje ya kijiji. Alipomtemea mate machoni na kumwekea mikono, alimuuliza, “Unaona chochote?”

24Alitazama juu na kusema, “Naona watu wanaonekana kama miti inatembea.”25Kisha akaweka tena mikono juu ya macho yake, na mtu yule akafungua macho yake, uwezo wake wa kuona ukarejea, naye aliona vitu vyote waziwazi.

26Yesu akamwachilia aende nyumbani kwake na akamwambia, “Usiingie kijijini.”

27Yesu aliondoka na wanafunzi wake kwenda vijiji vya Kaisaria ya Filipi. Wakiwa njiani aliwauliza wanafunzi wake, “Watu wanasema mimi ni nani?”28Wakamjibu wakasema, “Yohana mbatizaji. Wengine wanasema, ‘Eliya’ na wengine, ‘Mmoja wa Manabii.”

29Akawauliza, “Lakini ninyi mnasema mimi ni nani?” Petro akamwambia, “Wewe ni Kristo.”

30Yesu akawaonya wasimwabie mtu yeyote kumuhusu Yeye.

31Na akaanza kuwafundisha ya kuwa Mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi, na atakataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na atauawa, na baada ya siku tatu atafufuka.32Aliongea ujumbe huo waziwazi. Kisha Petro akamchukua pembeni kando na akaanza kumkemea.33Lakini Yesu aligeuka na kuwatazama wanafunzi wake na kisha akamkemea Petro na kusema, “Nenda nyuma yangu, Shetani! Huyawazi mambo ya Mungu, bali ya wanadamu.”

34Kisha akauita umati na wanafunzi wake pamoja, na kuwaambia, “mtu yeyote akitaka kunifuata, ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, na anifuate.35Kwa kuwa yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, na yeyote atakayepoteza maisha yake kwa ajili yangu na kwa ajili ya injili, atayaokoa.36Inamfaidia nini mtu, kuupata ulimwengu wote, na kisha kuyapoteza maisha yake?37Mtu anaweza kutoa nini badala ya maisha yake?38Yeyote anayenionea haya mimi na maneno yangu katika kizazi hiki cha uzinzi na dhambi, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo atakapokuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika watakatifu.

9

1Akawaambia, “Amini nawaambia, wako baadhi yenu wasimamao hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”

2Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye juu ya mlima, peke yao. Kisha akageuka sura mbele yao.3Mavazi yake yakang'aa sana, meupe kuliko ambavyo mtu yeyote duniani angeweza kuyang'arisha.4Kisha Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu.5Petro alijibu akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya.”6(Kwa maana hakujua la kusema, maana waliogopa sana.)

7Wingu likaja na kuwafunika. Kisha sauti ikatoka katika lile wingu,” Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.”8Ghafla, walipotazama huku na huko, hawakumuona tena mtu yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu.

9Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, akawaamuru wasimwambie mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.10Kwa hiyo wakaweka jambo hilo ndani ya mioyo yao wenyewe, lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake “kufufuka kutoka kwa wafu”

11Walimwuliza Yesu, “Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?”

12Akawaambia, “Eliya anakuja kwanza kurejesha mambo yote, Kwa nini basi imeandikwa kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi kudharauliwa?13Lakini nawaambia ya kwamba Eliya amekwisha kuja, na wakamfanyia walivyotaka, kama ilivyoandikwa juu yake.”

14Na walipofika kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na waandishi walikuwa wanabishana nao.15Na mara walipomwona Yesu, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia.16Aliwauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao juu ya nini?”

17Mtu katika umati alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu inayomfanya asiweze kuongea,18Humkamata na kumwangusha chini, naye anatoa povu mdomoni na kusaga meno na kuwa mgumu. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo pepo, lakini hawakuweza.

19Akawajibu, “Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi hadi lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kwangu.”20Wakamleta yule mvulana kwake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.21Yesu alimwuliza baba yake, “Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?” Baba alisema, “Tangu utoto.22Mara nyingine humwangusha katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie.”

23Yesu alimwambia, “Kama unaweza’? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.”

24Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”

25Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, “wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru toka kwake, usimwiiingie tena.”

26Akalia na kumhangaisha mvulana kwa nguvu nakisha akamtoka. Mvulana alionekana kama amekufa, Ndipo wengi wakasema, “Amekufa,”27Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mvulana akasimama.

28Wakati Yesu alipoingia ndani ya nyumba, wanafunzi wake walimwuliza kwa faragha, “Kwa nini hatukuweza kuitoa?”

29Akawaambia, “Aina hii haitoki isipokuwa kwa maombi.”

30Wakatoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,31kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, “Mwana wa Adamu atapeanwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.”32Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumuuliza.

33Ndipo walifika Kapernaumu. Baada ya kuingia ndani ya nyumba akawauliza, “Mlikuwa mnajadili nini njiani”?34Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.35Alipoketi chini akawaita kumi na wawili pamoja, na akawambia, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”36Akamchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake na akawambia,37“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”

38Yohana akamwambia, “Mwalimu, tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.”

39Lakini Yesu akasema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo kisha baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.40Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.41Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa jina langu wewe ni wa Kristo, Amin nawaambia, hatapoteza thawabu yake.

42Yeyote anayewakosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio mimi kujikwaa, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.43Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kuzimu ukiwa na mikono yote, katika moto “usiozimika.”44“Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika.” 145Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa kuzimu na miguu miwili.46[“Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika.”]47Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu.48Mahali ambapo funza wao hawafi, na moto usiozimika.

49Kwa maana kila mtu atatiwa chumvi kwa moto.50Chumvi ni nzuri, lakini kama chumvi ikipoteza ladha yake, unawezaje kuifanya iwe chumvi tena? Muwe na chumvi ninyi kwa ninyi na muwe na Amani kila mmoja na mwingine.”


1haumo katika nakala za kale.

10

1Yesu akaondoka eneo hilo na akaenda katika mkoa wa Yudea na eneo ng'ambo ya Mto Yorodani, na makutano walimfuata tena. Aliwafundisha tena, kama ilivyokuwa kawaida yake kufanya.2Na Mafarisayo walikuja kumjaribu na wakamuuliza, “Ni halali kwa bwana kumpa talaka mkewe?”

3Yesu akawajibu, “Musa aliwaamuru nini?”

4Wakasema, “Musa aliruhusu kuandika cheti cha talaka na kisha kumwacha mkewe.”

5“Ni kwa sababu ya mioyo yenu migumu ndiyo maana aliwaandikia sheria hii,” Yesu aliwaambia.6“Lakini kutoka mwanzo wa uumbaji, ‘Mungu aliwaumba mwanamume na mwanamke.7‘Kwa sababu hii mwanamume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake,8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; Kwa kuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.9Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.”

10Walipokuwa ndani ya nyumba, wanafunzi wake wakamwuliza tena kuhusu hili.11Akawaambia, “Yeyote anayemtaliki mke wake na kuoa mke mwingine, anafanya uzinzi dhidi yake.12Mwanamke naye akimwacha mme wake na kuolewa na mwanamme mwingine, anafanya uzinzi.”

13Kisha walimletea watoto wao wadogo ili awaguse, lakini wanafunzi wakawakemea.14Lakini Yesu alipotambua hilo, alikasirika na akawaambia, “Waruhusuni watoto wadogo waje kwangu, na msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa walio kama15Ukweli nawaambia, yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hakika hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.16Kisha akawachukua watoto mikononi mwake na akawabariki akiwawekea mikono yake juu yao.

17Na alipoanza safari yake mtu mmoja alimkimbilia na akapiga magoti mbele yake, akamwuliza, “Mwalimu Mwema, nifanye nini ili niweze kurithi uzima wa milele?”

18Na Yesu akasema, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna aliye mwema, isipokuwa Mungu peke yake.19Unazijua amri: ‘Usiue, usizini, usiibe, usishuhudieusitoe ushhidi wa uongo, usidanganyeusilaghai, mheshimu baba na mama yako.’”

20Mtu yule akasema, “Mwalimu, haya yote nimeyatii tangu nikiwa kijana.”

21Yesu alimwangalia na kumpenda. Akawambia, “Unapungukiwa kitu kimoja. Unapaswa kuuza vyote ulivyo navyo na uwape masikini, na utakuwa na hazina mbinguni. NdipoKisha uje unifuate.”22Lakini alikata tamaa kwa sababu ya maelezo haya; aliondokakauli hii alionekana mwenye huzuni na akaenda zake akiwa mwenyena huzuni, kwa kuwa alikuwa na mali nyingi.23Yesu akatazama pande zote na kuwaambia wanafunzi wake, “Ni vigumu jinsi gani ilivyo vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu!24Wanafunzi walishangazwa kwa maneno haya. Lakini Yesu akawaambia tena, “Watoto, ni vigumu jinsi gani kuingia katika ufalme wa Mungu!25Ni rahisi kwa ngamia kupita kwenye tundu la sindano, kuliko mtu tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.”

26Walishangazwa sana na wakasemezana, “Hivyo nani ataokoka”

27Yesu akawaangalia na kusema, “Kwa binadamu haiwezekani, lakini sio kwa Mungu. Kwa kuwa katika Mungu yote yanawezekana.”

28“Petro akaanza kuzungumza naye, “Angalia tumeacha vyote na tumekufuata.”

29Yesu akasema, “Ukweli nawaambia ninyi, hakuna aliyeacha nyumba, au kaka, au dada, au mama, au baba, au watoto, au ardhi, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Injili,30ambaye hatapokea mara mia zaidi ya sasa hapa duniani katika zama hizi: nyumba, kaka, dada, mama, watoto, na ardhi, kwa pamoja na mateso, na ulimwengu ujao, uzima wa milele.31Lakini wengi walio wa kwanza watakuwa wa mwisho na walio wa mwisho watakuwa wa kwanza.”

32Walipokuwa njiani, kwenda Yerusalemu, Yesu alikuwa amewatangulia mbele yao. Wanafunzi walishangaa, na wale waliokuwa wanafuata nyuma waliogopa. Ndipo Yesu akawatoa akawachukua pembeni tena wale kumi na wawili na akaanza kuwaeleza ambacho kitamtokea kwake hivi karibuni:33“Tazama, tunakwenda mpaka Yerusalemu, na Mwana wa Adamu atafikishwa kwa makuhani wakuu na waandishi. Watamhukumu afe na watamtoa kwa watu wa Mataifa.34Watamdhihaki, watamtemea mate, watampiga fimbo watamchapa mijeledi, na watamwua. Lakini baada ya siku tatu atafufuka.”

35Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, walikuja kwake na kusema, “Mwalimu, tunakuhitaji tunataka utufanyie chochote tukuombacho.”

36Aliwaambia, “Mnataka niwatendee nini?”

37Wakasema, “Turuhusu tukae nawe katika utukufu wako, mmoja katika mkono wako wa kuume na mwingine mkono wako wa kushoto.”

38Lakini Yesu aliwajibu, “Hamjui mnachoomba. Mnaweza kukinywea kikombe ambacho nitakiyweanitakinywea au kustahimili ubatizo ambao nitabatizwa?”

39Wakamwambia, “Tunaweza” Yesu akawaambia, “Kikombe nitakachokinywea, mtakinywea. Na ubatizo ambao kwao nimebatizwa, mtaustahimili.40Lakini atakayekaa mkono wangu wa kuume au mkono wangu wa kushoto sio mimi wa kutoa, lakini ni kwa wale ambao kwao imekwisha andaliwa.”

41Wale wanafunzi wengine kumi waliposikia haya, wakaanza kuwakasirikia sana Yakobo na Yohana.42Yesu akawaita kwake na kusema, “Mnajua kuwa wale wanaodhaniwa hao wanaochukuliwa kuwa watawala wa watu wa Mataifa huwatawala na maofisa wao mashuhuri hutekeleza mamlaka juu yao.”43Lakini haipaswi kuwa hivi kati yenu. Yeyote atakaye kuwa mkubwa kati yenu lazima awatumikie,44na yeyote atakaye kuwa wa kwanza kati yenu ni lazima awe mtumwa wa wote.45Kwa kuwa Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa bali kutumika, na kuyatoa maisha yakekutoa uhai wake kuwa fidia kwaya wengi.”

46Wakaja Yeriko. Alipokuwa akiondoka Yeriko na wanafunzi wake na kundi kubwa, mwana wa Timayo, Batimayo, kipofu mwombaji, alikaa kando ya barabara.47Aliposikia kuwa ni Yesu Mnazareti, alianzaakaanza kupiga kelele na kusema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”48Wengi walimkemea yule kipofu, wakimwambia anyamaze. Lakini alilia kwa sauti zaidi, “Mwana wa Daudi, nihurumie!”

49Yesu alisimama na kuamuru aitwe. Walimwita yule kipofu, wakisema, “Kuwa shujaa! Inuka! Yesu anakuita.”50Akalitupa pembeni koti lake, akaruka juu, na kuja kwa Yesu.

51Yesu akamjibu na kusema, “Unataka nikufanyie nini?” Yule mwanaume kipofu akamjibu, “Mwalimu, ninataka kuona.”

52Yesu akamwambia, “Nenda. Imani yako imekuponya.” Hapo hapo macho yake yakaona mara akaweza kuona tena; na akamfuata Yesu barabarani.

11

1Sasa walipokuwa wakifika Yerusalemu, walikuwa karibu na Bethfage na Bethania, kwenye Mlima wa Mizeituni, Yesu akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake2na akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mkabala wenu. Mara mtakapoingia humo, mtamkuta mwanapunda ambaye hajapandwa. Mfungueni na mmlete kwangu.3Na kama yeyote akiwaambia, ‘Kwa nini mnafanya hivi?’ mnapaswa kusema, ‘Bwana anamhitaji na mara atamrudisha hapa.’”

4Wakaenda, wakamkuta mwana-punda amefungwa nje mlangoni nje ya njia kuu nao wakamfungua.5Na baadhi ya watu waliokuwa wamesimama pale wakawaambia, “Mnafanya nini, kumfungua mwana-punda huyo?”6Wakawaambia kama Yesu alivyowaambia, na watu wakawaacha waende.

7Wakamleta mwana-punda kwa Yesu na wakatandika nguo zao, naye akaketi.8Watu wengi wakatandaza mavazi yao barabarani, na wengine wakatandaza matawi waliyoyakata mashambani.9Wale waliotangulia mbele yake na wale waliomfuata walipiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa anayekuja kwa jina la Bwana.10Umebarikiwa ufalme ujao wa baba yetu Daudi! Hosana juu mbinguni”

11Kisha Yesu kaingia Yerusalemu, akaingia hekaluni akatazama kila kitu. Sasa, wakati ulikuwa umeenda, alitoka kwenda Bethania pamoja nao kumi na wawili.

12Kesho yake walipokuwa wakitoka Bethania, aliona njaa.13Na akaona kwa mbali mtini wenye majani, akaenda ili aone kama angeweza kupata matunda juu yake, alipofika akakuta majani tu, kwa kuwa haikuwa majira ya tini.14Akauambia, “Hakuna yeyote atakayekula tunda kutoka kwako tena.” Na wanafunzi wake wakasikia.

15Wakafika Yerusalemu, naye akaingia hekaluni na kuanza kuwatoa nje wauzaji na wanunuzi ndani ya hekalu. Akazipindua meza za wabadilishaji wa fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.16Hakumruhusu yeyote kubeba chochote hekaluni kilichoweza kuuzwa.17Akawafundisha na kusema, “Je haikuandikwa, ‘nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote’? Lakini mmeifanya pango la wanyang'anyi.”18Makuhani wakuu na waandishi walisikia alivyokuwa amesema, nao walitafuta njia ya kumwangamiza. Hata hivyo walimwogopa kwa sababu umati ulishangazwa na mafundisho yake.19Na jioni ilipofika, waliondoka mjini.

20Walipokuwa wakitembea asubuhi, waliuona mti wa mtini umekauka mpaka kwenye mizizi yake.21Petro akakumbuka na kusema, “Rabi! Tazama, mti wa mtini ulioulaani umekauka.”

22Yesu akawajibu, “Muwe na imani katika Mungu.23Amini nawaambia kwamba kila auambiaye mlima huu, ‘Ondoka, na ukajitupe mwenyewe baharini, ‘na kama hana mashaka moyoni mwake lakini anaamini kwamba alichokisema kitatokea, hivyo ndivyo Mungu atakavyofanya.24Kwa hiyo ninawaambia: yoyote myaombayo, aminini kwamba mmeyapokea, nayo yatakuwa yenu.25Msimamapo na kuomba, mnapaswa kusamehe chochote mlichonacho dhidi ya yeyote, ili kwamba Baba yenu aliye mbinguni awasamehe pia ninyi makosa yenu.26[“Lakini msiposamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatasamehe dhambi zenu.”]

27Wakarudi Yerusalemu tena. Na Yesu alipokuwa akitembea hekaluni, makuhani wakuu, waandishi na wazee walikuja kwake.28Na wakamwambia, “Kwa mamlaka gani unafanya mambo haya?” Na ni nani aliyekupa mamlaka kuyafanya haya?”

29Yesu akawaambia, “Nitawauliza swali moja. Niambieni na mimi nitawaambia kwa mamlaka gani ninayafanya mambo haya.30Je, ubatizo wa Yohana ulitoka mbinguni au ulitoka kwa wanadamu? Nijibuni.”

31Wakajadiliana miongoni mwao na kushindana na kusema, “Kama tukisema, ‘Kutoka mbinguni,’ atasema, ‘Kwa nini basi hamkumwamini?’32Lakini kama tukisema, ‘Kutoka kwa wanadamu,’...” Waliwaogopa watu, kwa kuwa wote walishawishika kwamba Yohana alikuwa Nabii.33Ndipo walimjibu Yesu na kusema, “Hatujui.” Ndipo Yesu akawaambia, “Wala mimi sitawaambia ni kwa mamlaka gani nayafanya mambo haya.

12

1Kisha Yesu alianza kuwafundisha kwa mafumbo. Akasema, “Mtu alipanda shamba la mizabibu, akalizungushia uzio, na akachimba shimo la shinikizo la divai. Akajenga mnara na kisha akalipangisha shamba la mizabibu kwa wakulima wa mizabibu. Kisha alisafiri safari ya mbali.2Wakati ulipofika, alimtuma mtumishi kwa wakulima wa mizabibu kupokea kutoka kwao baadhi ya matunda ya shamba la mizabibu.3Lakini walimkamata, wakampiga, na wakamfukuza bila chochote.4Tena akatuma kwao mtumishi mwingine, na wakamjeruhi kichwani na kumtendea aibu.5Bado akamtuma mwingine, na huyu wakamwua. Waliwatendea wengine wengi mambo kama hayo hayo, wakiwapiga wengine na kuwaua wengine.6Alikuwa bado na mtu mmoja zaidi wa kutuma, mwana mpendwa. Naye akawa wa mwisho aliyetumwa kwao. Akisema, “Watamheshimu mwanangu.”7Lakini wale wakulima wa mizabibu wakaambiana “Huyu ndiye mrithi. Njooni, tumuue yeye, na urithi utakuwa wetu.”8Walimvamia, wakamuua na kumtupa nje ya shamba la mizabibu.9Kwa hiyo, Je! Atafanya nini mmiliki wa shamba la mizabibu? Atakuja na kuwaangamiza wakulima wa mizabibu na atalikabidhi shamba la mizabibu kwa wengine.10Hamjapata kusoma andiko hili? “Jiwe ambalo wajenzi walilikataa, limekuwa jiwe la pembeni.11Hili lilitoka kwa Bwana, na ni la ajabu machoni petu.”

12Baada ya haya, viongozi wa kiyahudi walitafuta njia ya kumkamata Yesu, kwani walifahamu yakuwa alinena mfano huo juu yao. Lakini waliogopa umati wa watu. Hivyo walimwacha na wakaenda zao.

13Kisha wakawatuma baadhi ya mafarisayo na maherodia kwake ili kumtega kwa maneno.14Walipofika, wakamwambia, “Mwalimu, tunajua wewe ni wa kweli na huyumbishwi na mtu yeyote, kwa kuwa huna upendeleo. Unafundisha njia ya Mungu katika ukweli. Je! Ni haki kulipa kodi kwa Kaisari au la? Je! Twaweza kulipa au la?

15Lakini Yesu alijua unafiki wao na kuwaambia, “Kwa nini mnanijaribu? Nipeni dinari niweze kuitazama.”16Wakaleta moja kwa Yesu. Akawaambia, “Je! Ni sura na maandishi ya nani yaliyo hapa? Wakasema, “Ya Kaisari.”

17Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vitu vya Kaisari na Mungu vitu vya Mungu.” Wakamstaajabia.

18Kisha Masadukayo, wasemao hakuna ufufuo, walimwendea. Wakamuwuliza, wakisema,19“Mwalimu, Musa alituandikia kuwa, ‘Ikiwa ndugu ya mtu akifa na kumwacha mke nyuma yake, lakini hakuacha mtoto, mtu atamchukua mke wa ndugu yake, na kujipatia watoto kwa ajili ya ndugu yake.’20Kulikuwa na ndugu saba, wa kwanza alitwaa mke na kisha akafa, hakuacha watoto.21Kisha wa pili alimchukua naye akafa, hakuacha watoto. Na wa tatu hali kadhalika. Hawakuacha watoto.22Na wote saba hawakuacha watoto! Mwishowe na mwanamke pia akafa.23Wakati wa ufufuo, watakapofufuka tena, Je! Atakuwa mke wa nani? Kwa maana ndugu wote saba walikuwa wamemwoa.”

24Yesu aliwaambia, “Je! Hii sio sababu yenu kukosea, kwa sababu hamjui maandiko wala nguvu za Mungu?”25Maana watakapofufuka kutoka kwa wafu, hawaoi wala hawaolewi, bali ni kama malaika mbinguni.26Lakini, kuhusu wafu ambao wanafufuliwa, Je! Hamjasoma katika kitabu cha Musa, katika habari za kichaka, jinsi Mungu alivyosema naye na kumwambia, ‘Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo?’27Yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai. Mmekosea kabisa.”

28Mmoja wa waandishi akaja na kuyasikia mazungumzo yao; aliona kwamba Yesu aliwajibu vema. Alimwuliza, “Je! Ni amri ipi iliyo ya muhimu zaidi kuliko zote?”

29Yesu alimjibu, “Iliyo ya muhimu ni hii, “Sikia, Israeli, Bwana Mungu wetu, Bwana ni mmoja.30Lazima umpende Bwana Mungu wako, kwa moyo wako wote, kwa nafsi yako yote, kwa akili yako yote, na kwa nguvu zako zote.’31Amri ya pili ni hii, ‘Lazima umpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe.’ Hakuna amri nyingine kuu zaidi ya hizi.”

32Mwandishi akasema, “Vema, Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja, na kwamba hakuna mwingine zaidi yake.33Kumpenda yeye kwa moyo wote, na kwa ufahamu wote na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani kama mtu anavyojipenda mwenyewe, ni zaidi ya sadaka zote za kuteketezwa na dhabihu.”

34Wakati Yesu alipoona ametoa jibu la busara, akamwambia, “Wewe hauko mbali na ufalme wa Mungu.” Baada ya hapo hakuna hata mmoja aliye thubutu kumwuliza Yesu maswali yoyote.

35Na Yesu alipokuwa akifundisha hekaluni, alisema, “Je! Imekuwaje waandishi husemaje kuwa Kristo ni mwana wa Daudi?36Daudi mwenyewe katika Roho Mtakatifu, alisema, ‘Bwana alisema kwa Bwana wangu, keti katika mkono wangu wa kuume, mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.’37Daudi mwenyewe humwita ‘Bwana’ Je! Kristo anaweza kuwa mwana wa Daudi kwa jinsi gani?” Na kusanyiko kuu la watu walimsikiliza kwa furaha.

38Katika mafundisho yake Yesu akasema, “Jihadharini na waandishi, wanaotamani kutembea na kanzu ndefu na kusalimiwa kwenye masoko39na kuketi kwenye viti vya wakuu katika. Masinagogi na mahali pa heshima shereheni.40Pia wanakula nyumba za wajane na wanaomba maombi marefu ili watu wawaone. Hawa watu watapokea hukumu iliyo kuu.”

41Kisha Yesu akaketi chini karibu na sanduku la sadaka ndani ya eneo la hekalu; alikuwa akitazama watu waliokuwa wakitia pesa zao ndani ya sanduku. Watu wengi matajiri waliweka kiasi kikubwa cha pesa.42Kisha mwanamke mjane maskini alikuja na kutia sarafu mbili za thamani ya senti moja.43Akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Amini nawaambia, mwanamke huyu mjane maskini ametia kiasi kikubwa zaidi ya wote ambao wameshatoa katika sanduku la sadaka.44Kwani wote wametoa kutokana na wingi wa mapato yao. Lakini mwanamke mjane huyu, kutoka katika umaskini wake, katia pesa yote ambayo alipaswa kuitumia kwa maisha yake.” Na kuketi kwenye viti vya wakuu katika masinagogi na mahali pa heshima shereheni.

13

1Yesu alipokuwa akitembea kutoka hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake akamwuliza, “Mwalimu, tazama mawe haya na majengo yakushangaza!”,2Yesu akamwambia, “Unaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalo salia juu ya jingine ambalo halitaangushwa chini.”

3Na alipokuwa amekaa juu ya Mlima wa Mizeituni kinyume na hekalu, Petro, Yakobo, Yohana na Andrea wakamwuliza kwa siri,4“Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Ni nini dalili ya mambo haya kutokea?”

5Yesu akaanza kuwaambia, “jihadharini mtu asiwapotoshe.6Wengi watakuja kwa jina langu wakisema, ‘Mimi ndiye,’ na watawapotosha wengi.7Mtakaposikia habari za vita na fununu za vita, msiogope; mambo haya lazima yatatokea, lakini mwisho bado.8Kwa maana taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Patakuwa na matetemeko ya ardhi sehemu mbalimbali, na njaa. Hayo ni mwanzo wa utungu.

9Jihadharini. Watawapeleka hadi mabarazani, na mtapigwa katika masinagogi. Mtasimamishwa mbele ya watawala na wafalme kwa ajili yangu, kama ushuhuda kwao.10Lakini injili lazima kwanza ihubiriwe kwa mataifa yote.11Watakapo wakamata na kuwakabidhi, msiogope kuhusu kile mtakachosema. Kwa maana katika muda huo, mtapewa kile mtakachokisema; haitakuwa nyinyi mnaosema, bali Roho Mtakatifu.12Ndugu atamsaliti ndugu auawe, baba atamsaliti mtoto wake. Watoto watainuka dhidi ya wazazi wao na kuwafanya wauwawe.13Mtachukiwa na kila mtu kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho, mtu huyo ataokoka.

14Mtakapoliona chukizo la uharibifu limesimama mahali ambapo halipaswi kusimama (asomaye na afahamu), ndipo walioko ndani ya Yudea wakimbilie milimani,15naye aliyeko juu ya paa asishuke ndani ya nyumba, wala kuchukua kitu ndani yake,16na aliyeko shambani asirudi kuchukua vazi lake.17Lakini ole wao wanawake wenye mimba na wanyonyeshao katika siku hizo!18Ombeni kwamba isitokee wakati wa baridi.19Kwa maana hizo zitakua siku za dhiki kuu, ambayo, hajatokea namna yake tangu Mungu alipoumba ulimwengu, hata sasa, wala haitakuwapo tena.20Kama Bwana asingalifupisha siku hizo, hakuna mtu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule, aliowachagua alifupisha siku hizo.21Wakati huo kama mtu yeyote atawaambia, “Tazama, Kristo yuko hapa!’ au ‘Tazama, yuko pale!’ msiamini.22Kwani makristo wa uongo na manabii wa uongo watatokea na watatoa ishara na maajabu, ili kwamba, wawadanganye, yamkini hata wateule.23Jihadharini. Nimekwisha wambia haya yote kabla ya wakati.

24Lakini baada ya dhiki ya siku hizo, jua litatiwa giza, mwezi hautatoa mwanga wake,
25nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu zilizoko mbinguni zitatikisika.
26Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni kwa nguvu kubwa na utukufu.27Ndipo atatuma malaika zake na atawakusanya pamoja wateule wake kutoka pande kuu nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.

28Jifunzeni kutoka kwa mtini. Mara tu tawi linapoanza kuwa laini na kuchipua majani yake, mnajua majira ya kiangazi yamekaribia.29Vivyo hivyo, mwonapo mambo hayo yakitendeka, tambueni ya kuwa yeye yu karibu na malango.30Kweli, nawambieni, kizazi hiki hakitapita mpaka mambo haya yote yatukie.31Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.32Lakini kuhusu siku hiyo au saa, hakuna ajuaye, hata malaika mbinguni, wala Mwana, ila Baba.33Kuweni wangalifu, Kesheni, kwa sababu hamjui ni muda gani yatatokea.34Ni kama mtu anayesafiri, anaacha nyumba yake, na kuweka watumishi wake kuwa watawala wa nyumba, kila mmoja na kazi yake, Na kumwamuru mlinzi kukaa macho.35Kwa hiyo iweni macho! Kwani hamjui ni lini bwana wa nyumba atakaporudi nyumbani, yawezekana ni jioni, usiku wa manane, wakati jogoo atakapowika, au asubuhi.36Kama akija ghafla, asikute umelala.37Ninachowaambia nawaambia kila mtu: Kesheni!”

14

1Ilikuwa siku mbili tu kabla ya sikukuu ya Pasaka na ya Mikate isiyotiwa Chachu. Makuhani wakuu na waandishi walikuwa wakitafuta namna ya kumkamata Yesu kwa siri na kumuua.2Maana walikua wanasema, “Sio wakati wa sikukuu, watu wasije wakafanya ghasia.”

3Wakati Yesu alipokuwa Bethania nyumbani kwa Simoni mkoma, na alipokuwa akiegemea mezani, mwanamke mmoja akaja kwake akiwa na chupa ya alabasta yenye manukato ya thamani kubwa, ambayo ni nardo safi. Akaivunja ile chupa na kumwaga ile nardo kichwani mwake.4Lakini kulikuwa na baadhi yao waliokasirika. Wakazungumza wao kwa wao na kusema, “Ni nini sababu ya upotevu wa manukato haya?5Manukato haya yangeweza kuuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na wakapewa maskini.” Kisha wakamkemea.

6Lakini Yesu akasema, “Mwacheni. Kwa nini mnamsumbua? Amefanya jambo zuri kwangu.7Siku zote mnao maskini pamoja nanyi, na wakati wowote mnapotamani mnaweza kufanya mazuri kwao, lakini hamtakuwa nami wakati wote.8Amefanya kile anachoweza: ameupaka mwili wangu mafuta kwa ajili ya maziko.9Kweli nawaambia, kila mahali injili inapohubiriwa katika ulimwengu wote, kile alichofanya mwanamke huyu kitazungumzwa kwa ukumbusho wake.

10Kisha Yudas Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili, alikwenda kwa makuhani wakuu ili kwamba apate kumkabidhi kwao.11Wakati makuhani wakuu walisikia hivyo, walifurahi na wakaahidi kumpa fedha. Alianza kutafuta nafasi ya kumkabidhi kwao.

12Siku ya kwanza ya mkate usiotiwa chachu, wakati walipotoa mwanakondoo wa pasaka, wanafunzi wake walimwambia, “Unataka twende wapi tukaandae ili upate kula mlo wa Pasaka?”

13Akawatuma wawili wa wanafuzi wake na kuwaambia, “Nendeni mjini, na mwanamume amebeba mtungi wa maji atakutana nanyi. Mfuateni.14Nyumba atakayoingia, mfuateni na mumwambie mwenye nyumba hiyo, ‘Mwalimu asema, “Kiko wapi chumba cha wageni mahali nitakapokula Pasaka na wanafunzi wangu?”15Atawaonesha chumba kikubwa cha juu kilicho na samani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi kwa ajili yetu pale.”16Wanafunzi waliondoka wakaenda mjini. Walikuta kila kitu kama alivyokuwa amewaambia, na wakaandaa mlo wa Pasaka.17Wakati ilipokuwa jioni, alikuja na wale Kumi na wawili.

18Na walipokuwa wakiikaribia meza na kula, Yesu alisema, “Kweli nawaambia, mmoja kati yenu anayekula pamoja nami atanisaliti.”

19Wote walisikitika, na mmoja baada ya mwingine walimwambia, “Hakika siyo mimi?”

20Yesu alijibu na kuwaambia, “Ni mmoja wa Kumi na wawili kati yenu, mmoja ambaye sasa anachovya tonge katika bakuli pamoja nami.21Kwa kuwa Mwana wa Adamu atakwenda kama vile maandiko yasemavyo juu yake. Lakini ole wake mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu atasalitiwa! Ingekuwa vizuri zaidi kwake kama mtu yule asingezaliwa.”

22Na walipokuwa wakila, Yesu akachukua mkate, akaubariki, na kuumega. Aliwapa akisema, “Chukueni. Huu ni mwili wangu.”23Akachukua kikombe, akashukuru, na akawapatia, na wote wakakinywea.24Akawaambia, “Hii ni damu yangu ya agano, damu imwagikayo kwa ajili ya wengi.25Kweli nawaambia, sitakunywa tena katika zao hili la mzabibu mpaka siku ile nitakapokunywa mpya katika ufalme wa Mungu.”26Walipokwisha kuimba wimbo, walikwenda nje katika Mlima wa Mizeituni.

27Yesu akawaaambia, “Ninyi nyote mtajitenga mbali nami, kwa kuwa imeandikwa, ‘Nitampiga mchungaji na kondoo watatawanyika.’28Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia mbele yenu Galilaya.”

29Petro alimwambia, “Hata kama wote watakuacha, mimi sitakuacha.”

30Yesu akamwambia, “Kweli nakuambia, leo-naam, usiku huu huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, utakuwa umenikana mara tatu.”

31Lakini Petro akasema kwa msisitizo, “ikiwa ni lazima nife nawe, sitakukana.” Wote walitoa ahadi ile ile.

32Wakafika mahali paitwapo Gethsemane, na Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa wakati nasali.”33Akawachukua Petro, Yakobo, na Yohana pamoja naye, akaanza kuhuzunika na kutaabika sana.34Aliwaambia, “Nafsi yangu ina huzuni sana, hata kufa. Bakini hapa na mkeshe.”35Yesu akaenda mbele kidogo, akaanguka chini, akaomba, kama ingewezekana, kwamba saa hii ingemwepuka.36Alisema, “Aba, Baba, Mambo yote yanawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini siyo mapenzi yangu, bali mapenzi yako.”37Akarudi na kuwakuta wamelala, na akamwambia Petro, “Simoni, je umelala? Hukuweza kukesha hata saa moja?38Kesheni na muombe kwamba msije mkaingia katika majaribu. Hakika roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.”39Akaenda tena na kuomba, na alitumia maneno yaleyale.40Aliporudi tena, akawakuta wamelala, kwa kuwa macho yao yalikuwa mazito. Hawakujua nini cha kumwambia.41Akarudi mara ya tatu na kuwaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Yatosha! Saa imefika. Tazama! Mwana wa Adamu anasalitiwa mikononi mwa wenye dhambi.42Amkeni, twendeni. Tazama, yule anayenisaliti yuko karibu.”

43Alipokuwa bado anaongea, Yudas, mmoja wa wale kumi na wawili, akafika, na kundi kubwa pamoja naye wenye mapanga na marungu, kutoka kwamakuhani wakuu, waandishi na wazee.44Wakati huo msaliti wake alikuwa amewapa ishara, akisema, Yule nitakayembusu, ndiye. Mkamateni na kumpeleka chini ya ulinzi.”45Wakati Yuda alipofika, moja kwa moja alienda kwa Yesu na kusema, “Mwalimu!” Na akambusu.46Kisha wakamtia chini ya ulinzi na kumkamata.47Lakini mmoja kati yao aliyesimama karibu naye akachomoa upanga wake akampiga mtumishi wa kuhani mkuu na kumkata sikio.

48Yesu akawaambia, “Mmekuja kunikamata kwa mapanga na marungu kama mnyang'anyi?49Wakati kila siku nilikuwa nanyi na nikifundisha hekaluni, hamkunikamata. Lakini hili limefanyika ili maandiko yatimie.

50Na wale wote waliokuwa na Yesu walimwacha na kukimbia.51Kijana mmoja, aliyekuwa amevaa vazi la kitani pekee alilokuwa amejizungushia, alikua anamfuata Yesu. Wale watu walipomkamata,52aliiacha ile nguo ya kitani na kukimbia uchi.

53Walimwongoza Yesu kwa kuhani mkuu. Pale walikusanyika pamoja naye wakuu wa makuhani wote, wazee, na waandishi.54Sasa Petro akamfuata kwa mbali, kuelekea kwenye ua wa kuhani mkuu. Aliketi pamoja na maafisa, akiota moto ili kupata joto.55Wakati huo makuhani wakuu wote na Baraza zima la wayahudi walikuwa wakitafuta ushahidi dhidi ya Yesu ili wapate kumwua. Lakini hawakuupata.56Kwa kuwa watu wengi walileta ushuhuda wa uongo dhidi yake, lakini hata ushahidi wao haukufanana.57Baadhi walisimama na kuleta ushahidi wa uongo dhidi yake; wakisema,58“Tulimsikia akisema, ‘Nitaliharibu hekalu hili lililotengenezwa kwa mikono, na ndani ya siku tatu nitajenga lingine lisilotengenezwa kwa mikono.’”59Lakini hata ushahidi wao haukufanana.

60Kuhani mkuu akasimama katikati yao na akamwuliza Yesu, “Je, huna jibu? Watu hawa wanashuhudia nini dhidi yako?”61Lakini alikaa kimya na hakujibu chochote. Mara tena Kuhani mkuu akamhoji na kusema, “Je wewe ni Kristo, mwana wa Mungu aliye, barikiwa?”

62Yesu alisema, “Mimi ndiye. Na utamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kulia wa nguvu na akija na mawingu ya mbinguni.”

63Kuhani mkuu akararua mavazi yake na kusema, “Je, bado tunahitaji mashahidi?64Mmesikia kufuru. Uamuzi wenu ni upi?” Na wote walimhukumu kama mmoja aliyestahili kifo.

65Baadhi wakaanza kumtemea mate na kumfunika uso na kumpiga kwa ngumi zao na kumwambia, “Tabiri!” Maafisa walimchukua na kumpiga.

66Huku Petro alipokuwa yuko chini uani, mtumishi mmoja wa watumishi wa kike wa kuhani mkuu akaja kwake.67Alimwona Petro alipokuwa amesimama akiota moto, na akamtazama kwa karibu na kusema, “Nawe pia ulikuwa na Mnazareti, Yesu.”

68Lakini alikanusha, akisema, “Sijui wala sielewi unachoongea!” Kisha akatoka mpaka langonii Na jogoo akawika.

69Lakini mtumishi wa kike, alimwona na alianza kuwaambia tena wale ambao walikuwa wamesimama pale, “Mtu huyu ni mmoja wao!”

70Lakini alikana tena. Baadaye kidogo wale waliokuwa wamesimama pale walikuwa wakimwambia Petro, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya.”

71Lakini alianza kujiweka mwenyewe chini ya laana na kuapa, “Simjui huyu mtu mnayemzungumzia.”

72Mara jogoo aliwika mara ya pili. Kisha Petro akakumbuka maneno ambayo Yesu aliyokuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Na aliangua kilio.

15

1Asubuhi na mapema wakuu wa makuhani, na wazee na waandishi na baraza zima la wayahudi wakashauriana pamoja. Kisha wakamfunga Yesu na kumuongoza na wakampeleka kwa Pilato.2Pilato akamwuliza, “wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” “Akamjibu, “Wewe umesema hivyo.”3Wakuu wa makuhani wakaeleza mashitaka mengi juu ya Yesu.4Pilato akamwuliza tena, “Hujibu chochote? Huoni jinsi wanavyokushtaki kwa mambo mengi?5Lakini Yesu hakumjibu Pilato, na hiyo ilimshangaza.

6Kwa kawaida wakati wa sikukuu Pilato humfungulia mfungwa mmoja, mfungwa waliyemwomba.7Palikua na mtu aitwaye Baraba gerezani, amefungwa pamoja na waasi walioua wakati wa uasi.8Umati ukaja kwa Pilato, na kumwomba kuwafanyia kama alivyofanya hapo awali.9Pilato akawajibu na kusema, “Mnataka niwaachilie Mfalme wa Wayahudi?”10Kwa kuwa alijua ni kwa sababu ya wivu wakuu wa makuhani walimkamata Yesu na kumleta kwake.11Lakini wakuu wa makuhani walichochea umati kupiga kelele kwa sauti kwamba Baraba aachiliwe badala yake.12Pilato akawajibu tena na kusema, “Nimfanye nini Mfalme wa Wayahudi?

13Wakapiga kelele tena, “Msulibishe!”

14Pilato akawaambia, “Amefanya jambo gani baya?” Lakini wakazidi kupiga kelele zaidi na zaidi “Msulibishe.”15Pilato akitaka kuwaridhisha umati, akawafungulia Baraba. Akampiga Yesu mijeledi kisha akamtoa ili asulibiwe.

16Askari walimwongoza hadi ndani ya ua (ulio makao makuu ya serikali) na wakakusanya kikosi kizima cha askari.17Wakamvika Yesu kanzu ya rangi ya zambarau, na wakasokota taji ya miiba wakamvika.18Wakaanza kumdhihaki na kusema, “Salam, Mfalme wa Wayahudi!”19Walikua wakimpiga kichwani kwa fimbo ya mwanzi na kumtemea mate. Wakapiga magoti mbele yake kwa kumheshimu.20Hata wakiisha kumdhihaki, wakamvua ile kanzu ya rangi ya zambarau na kumvika mavazi yake, na wakamtoa nje kwenda kumsulubisha.

21Mtu fulani, Simoni Mkirene, aliyekuwa anaingia mjini kutoka shambani (baba yake Aleksanda na Rufo) na wakamlazimisha kubeba mslaba wa Yesu.22Askari wakampeleka Yesu mahali paitwapo Goligotha (maana ya tafsiri hii ni, Sehemu ya Fuvu la kichwa).23Wakampa mvinyo iliyochanganywa na manemane, lakini hakunywa.24Wakamsulibisha na wakagawana mavazi yake, wakayapigia kura kuamua kipande atakachopata kila askari.

25Yapata saa tatu asubuhi walipomsulibisha.26Wakaweka juu yake ubao ulioandikwa shitaka, “Mfalme wa Wayahudi.”27Walimsulubisha pamoja na majambazi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine kushoto kwake.28“Na maandiko yakatimia yaliyonena kwamba alihesabiwa pamoja na waasi.29Nao waliokuwa wakipita walimtukana, wakitikisa vichwa vyao wakisema, “Aha! Wewe utakayevunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu,30jiokoe mwenyewe na ushuke chini toka msalabani!”

31Kwa namna ile ile wakuu wa makuhani walimdhihaki wakisemezana, pamoja na waandishi na kusema, “Aliwaokoa wengine, lakini hawezi kujiokoa mwenyewe.32Mwache Kristo, Mfalme wa Israel, shuka chini sasa toka msalabani, ili tuweze kuona na kuamini. “Na wale waliosulubiwa pamoja naye pia wakamtukana.

33Ilipofika saa sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa tisa.34Wakati wa saa tisa, Yesu alipiga kelele kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lama sabaktani?” ikiwa na maana “Mungu wangu, Mungu wangu, kwa nini umeniacha?”

35Baadhi ya hao waliosimama waliposikia wakasema, “Tazama, anamwita Eliya.”

36Mtu mmoja akakimbia, aweka divai ya siki katika sponji na kuiweka juu ya mti wa mwanzi, akampa ili anywe. Mtu mmoja akasema, “Ngoja tuone kama Eliya atakuja kumshusha chini.”37Kisha Yesu akalia kwa sauti kubwa na akafa.38Pazia la hekalu likagawanyika vipande viwili toka juu mpaka chini.

39Wakati jemadari mmoja aliyekuwa amesimama akimwelekea Yesu, alipoona amekufa kwa jinsi ile, akasema, “Kweli huyu mtu alikuwa Mwana wa Mungu.”40Walikuwepo pia wanawake waliokuwa wakitazama kwa mbali. Miongoni mwao alikuwepo Mariamu Magdalena, Mariamu (mama yake Yakobo mdogo wa Yose), na Salome.41Wakati alipokuwa Galilaya walimfuata na kumtumikia. Na wanawake wengine wengi pia waliambatana naye hadi Yerusalemu.

42Kulipokuwa jioni, na kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio, siku kabla ya Sabato,43Yusufu wa Arimathaya alikuja pale. Alikuwa ni mjumbe wa Baraza anayeheshimiwa mtu anayeutarajia Ufalme wa Mungu. Kwa ujasiri akaenda kwa Pilato, na kuuomba mwili wa Yesu.44Pilato akashangazwa kwamba Yesu tayari amekufa; akamwita yule jemedari akamwuliza kama Yesu amekufa.45Alipopata uhakika kwa jemadari kwamba amekufa, alimruhusu Yusufu kuuchukua mwili.46Yusufu alikuwa amenunua sanda. Akamshusha toka msalabani, akamfunga kwa sanda, na kumweka ndani ya kaburi lililochimbwa katika mwamba. Kisha akalivingirisha jiwe mlangoni mwa kaburi.47Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yose waliona sehemu alipozikwa Yesu.

16

1Wakati sabato ilipokwisha, Mariamu Magdalena na Mariamu mama yake Yakobo, na Salome, walinunua manukato mazuri, ili waweze kuja na kuupaka mafuta mwili wa Yesu.2Asubuhi na mapema siku ya kwanza ya juma, walienda kwenye kaburi wakati jua lilipochomoza.3Wakisemezana wao kwa wao, “Nani atavingirisha jiwe kwa ajili yetu ili tuingie kaburini?”4Wakati walipotazama, waliona ya kuwa jiwe limekwisha kuvingirishwa, nalo lilikuwa kubwa sana.

5Wakaingia kwenye kaburi na wakamwona kijana amevaa joho jeupe, ameketi upande wa kulia, na wakashangazwa.6Akawaambia, “Msiogope. Mnamtafuta Yesu, Mnazareti, aliyesulibiwa. Amefufuka! Hayupo hapa. Tazama mahali pale walipokuwa wamemweka.7Lakini nendeni, mkawaambie wanafunzi wake na Petro ya kuwa amewatangulia kuelekea Galilaya. Huko mtamwona, kama alivyokua amewaambia.”8Wakaondoka na kukimbia kutoka kwenye kaburi; wakitetemeka na kushangaa. Hawakusema chochote kwa mtu yeyote sababu waliogopa sana.

9Mapema katika siku ya kwanza ya juma, baada ya kufufuka, alimtokea kwanza Mariamu Magdalena, ambaye kutoka kwake alimtoa mapepo saba.10Aliondoka na kuwaambia wale ambao walikuwa pamoja naye, wakati walipokuwa wakiomboleza na kulia.11Wakasikia kwamba yu hai na ameonekana naye, lakini hawakumwamini.12Baada ya mambo haya, alionekana katika sura tofauti na wawili wao walipokuwa wakienda mashambani.13Wakarudi na kuwaambia wanafunzi wengine waliobaki, lakini hawakuwaamini.14Yesu baadaye akajitokeza kwa wale kumi na mmoja walipokuwa wakila mezani, na akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo, kwa sababu hawakuwaamini wale waliomwona baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.

15Akawaambia, “Enendeni ulimwenguni mwote, na kuhubiri injili kwa viumbe vyote.16Yeyote aaminiye na kubatizwa ataokolewa, na yule asiyeamini atahukumiwa.17Ishara hizi zitaambatana na wote waaminio. Kwa jina langu watatoa pepo. Watasema kwa lugha mpya.18Watashika nyoka kwa mikono yao, na hata wakinywa kitu chochote cha kuuwa hakitawadhuru. Wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.”

19Baada ya Bwana Yesu kusema nao, akachukuliwa juu mbinguni na ameketi mkono wa kuume wa Mungu.20Wanafunzi wakaondoka, wakahubiri kila mahali, naye Bwana akitenda kazi pamoja nao na kulithibitisha lile neno kwa ishara zilizoambatana nao.]

Luke

1

1Wengi wamejitahidi kuweka katika mpangilio simulizi kuhusu masuala ambayo yametimizwa kati yetu,2kama walivyotupatia sisi, ambao tangu mwanzo ni mashahidi wa macho na watumishi wa ujumbe.3Hivyo nami pia, baada ya kuchuguza kwa uangalifu chanzo cha mambo haya yote tokea mwanzo - nimeona ni vema kwangu pia kukuandikia katika mpangilio wake - mheshimiwa sana Theofilo.4Ili kwamba uweze kujua ukweli wa mambo uliyofundishwa.

5Katika siku za Herode, mfalme wa Yudea, palikuwa na kuhani fulani aliyeitwa Zekaria, wa ukoo wa Abiya. Mke wake alitoka kwa binti za Haruni, na jina lake aliitwa Elizabeti.6Wote walikuwa wenye haki mbele za Mungu; walitembea bila lawama katika amri zote na maagizo ya Bwana.7Lakini hawakuwa na mtoto, kwa sababu Elizabethi alikuwa tasa, na kwa wakati huu wote wawili walikuwa wazee sana.

8Sasa ilitokea kwamba Zakaria alikuwa katika uwepo wa Mungu, akiendelea na wajibu wa kikuhani katika utaratibu wa zamu yake.9Kulingana na desturi ya kuchagua ni kuhani yupi atakayehudumu, alikuwa amechaguliwa kwa kura kuingia katika hekalu la Bwana na hivyo angefukiza uvumba.10Kundi lote la watu lilikuwa likiomba nje wakati wa kufukizwa kwa ufumba.11Sasa malaika wa Bwana alimtokea na kasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia.12Zakaria alitishika alipomuona; hofu ikamwangukia.13Lakini malaika akamwambia, “Usiogope Zakaria, kwa sababu maombi yako yamesikika. Mke wako Elizabeth atakuzalia mwana. Jina lake utamwita Yohana.14Utakuwa na furaha na uchangamfu, na wengi watafurahia kuzaliwa kwake.15Kwa kuwa atakuwa mkuu mbele ya macho ya Bwana. Hatakunywa divai au kinywaji kikali, na atakuwa amejazwa na Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake.16Na watu wengi wa Israel watageuzwa kwa Bwana Mungu wao.17Atakwenda mbele za uso wa Bwana katika roho na nguvu ya Eliya. Atafanya hivi ili kurejesha mioyo ya baba kwa watoto, ili kwamba wasiotii wataenenda katika hekima ya wenye haki. Atafanya hivi kuweka tayari kwa Bwana watu ambao wameandaliwa kwa ajili yake.”

18Zakaria akamwambia malaika, “Nitawezaje kujua hili? Kwa sababu mimi ni mzee na mke wangu miaka yake imekuwa mingi sana.”

19Malaika akajibu na kumwambia, “Mimi ni Gabrieli, ambaye husimama mbele za Mungu. Nilitumwa kukwambia, kukuletea habari hii njema.20Na tazama, hutaongea, utakuwa kimya, hutaweza kuongea mpaka siku ile mambo haya yatakapotokea. Hii ni kwa sababu ulishindwa kuamini maneno yangu ambayo yatatimizwa kwa wakati mwafaka.”

21Sasa watu walikuwa wakimsubiri Zakaria. Walishangazwa kwa kutumia muda mwingi hekaluni.22Lakini alipotoka nje, hakuweza kuongea nao. Wakatambua kwamba alikuwa amepata maono alipokuwa hekaluni. Aliendelea kuonesha ishara na alibaki kimya.

23Ikatokea kwamba siku za huduma yake zilipokwisha aliondoka kurudi nyumbani kwake.

24Baada ya Zakaria kurudi nyumbani kutoka kwenye huduma yake hekaluni, mke wake akawa mjamzito. Naye hakutoka nyumbani mwake kwa muda wa miezi mitano. Akasema,25“Hili ndilo ambalo Bwana amefanya kwangu aliponitazama kwa upendeleo ili kuiondoa aibu yangu mbele za watu.”

26Sasa, katika mwezi wa sita wa mimba ya Elizabeti, Mungu alimwambia malaika Gabrieli kwenda kwenye mji wa Galilaya uitwao Nazareti,27kwa bikra aliyekuwa ameposwa na mwanaume ambaye jina lake Yusufu. Yeye alikuwa wa ukoo wa Daudi, na jina la bikra huyo lilikuwa Mariamu.28Akaingia nyumbani kwake akasema, “Salaam, wewe uliyepokea neema kuu! Bwana amependezwa nawe.”29Lakini maneno ya malaika yalimchanganya na hakuelewa kwa nini malaika alisema salaam hii ya ajabu kwake.30Malaika akamwambia, “Usiogope, Mariamu, maana umepata neema kutoka kwa Mungu.31Na tazama, utabeba mimba katika tumbo lako na utazaa mwana. Nawe utamwita jina lake ‘Yesu.’32Atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Sana. Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi baba yake.33Atatawala juu ya ukoo wa Yakobo milele na ufalme wake hautakuwa na mwisho.

34Mariamu akamwambia malaika, “Hili litatokea kwa namna gani, maana sijawahi kulala na mwanaume yeyote?”35Malaika akajibu na akamwambia, “Roho Mtakatifu atakujia juu yako, na nguvu ya Aliye Juu Sana itakuja juu yako. Kwa hiyo, mtakatifu atakayezaliwa ataitwa Mwana wa Mungu.36Na tazama, ndugu yako Elizabeti anaujauzito wa mwana kwenye umri wake wa uzee. Huu ni mwezi wa sita kwake, ambaye alikuwa anaitwa mgumba.37Maana hakuna lisilowezekana kwa Mungu.”

38Mariamu akasema, “Tazama, mimi ni mtumishi wa kike wa Bwana. Acha iwe hivyo kwangu sawa sawa na ujumbe wako.” Kisha malaika akamwacha.

39Ndipo katika siku hizo Mariamu aliondoka na kwa haraka alikwenda katika nchi ya vilima, kwenye mji katika nchi ya Yudea.40Alikwenda nyumbani kwa Zakaria na akamsalimia Elizabeti.41Ikawa, Elizabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake. Elizabeti akajazwa na Roho Mtakatifu.42Akapaza sauti yake na kusema kwa sauti kuu, “Umebarikiwa wewe zaidi miongoni mwa wanawake, na mtoto aliyemo tumboni mwako amebarikiwa.43Na imekuwaje kwangu kwamba, mama wa Bwana wangu anijilie mimi?44Maana, iliposikika sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa furaha.45Na amebarikiwe mwanamke yule ambaye aliamini ya kwamba ungetokea ukamilifu wa mambo yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana.”

46Mariamu akasema, “Nafsi yangu inamsifu Bwana,
47na roho yangu imefurahi katika Mungu Mwokozi wangu.
48Kwa maana ameiangalia hali ya chini ya mtumishi wake wa kike. Tazama, tangu sasa katika vizazi vyote wataniita mbarikiwa.
49Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.
50Na rehema yake inadumu toka kizazi hata kizazi kwa wale wanao mtii yeye.
51Amefanya nguvu kwa mkono wake; amewatawanya wale ambao walijivuna juu ya mawazo ya mioyo yao.
52Amewashusha chini wana wa wafalme toka katika viti vyao vya enzi na kuwainua juu walio na hali ya chini.
53Aliwashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu.
54Ametoa msaada kwa Israeli mtumishi wake, ili kukumbuka kuonesha rehema
55(kama alivyosema kwa baba zetu) kwa Abrahamu na uzao wake milele.”

56Mariamu alikaa na Elizabeti yapata miezi mitatu hivi ndipo akarudi nyumbani kwake.

57Sasa wakati ulikuwa umewadia kwa Elizabeti kujifungua mtoto wake na akajifungua mtoto wa kiume.58Jirani zake na ndugu zake walisikia jinsi Bwana alivyoikuza rehema kwake, na wakafurahi pamoja naye.59Sasa ilitokea siku ya nane kwamba walikuja kumtahiri mtoto. Ingewapasa kumwita jina lake, “Zakaria,” kwa kuzingatia jina la baba yake,60Lakini mama yake akajibu na kusema, “Hapana; ataitwa Yohana.”61Wakamwambia, “Hakuna hata mmoja katika ndugu zako anayeitwa kwa jina hili.”62Wakamfanyia ishara baba yake kuashiria yeye alitaka jina aitwe nani.63Baba yake akahitaji kibao cha kuandikia, na akaandika, “Jina lake ni Yohana.” Wote wakashangazwa na hili.64Ghafla mdomo wake ukafunguliwa na ulimi wake ukawa huru. Akaongea na kumsifu Mungu.65Hofu ikawajia wote walioishi karibu nao. Mambo haya yakaenea katika nchi yote ya vilima vya Yudea.66Na wote walioyasikia wakayatunza mioyoni mwao, wakisema, “Mtoto huyu kuwa wa namna gani?” Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye.67Baba yake Zakaria alijazwa na Roho Mtakatifu na akatoa unabii, akisema,
68“Asifiwe Bwana, Mungu wa Israeli, kwa sababu amesaidia na alishughulikia wokovu kwa watu wake.
69Ametuinulia pembe ya wokovu katika nyumba ya mtumishi wake Daudi, kutoka miongoi mwa ukoo wa mtumishi wake Daudi,
70kama alivyosema kwa kinywa cha manabii wake waliokuweko katika nyakati za kale.
71Atatuokoa kutoka kwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia.
72Atafanya hivi kuonesha rehema kwa baba zetu, na kukumbuka agano lake takatifu,
73kiapo alichokisema kwa Abrahamu baba yetu.
74Aliapa kuthibitha kwamba ingewezekana kumtumikia Yeye bila hofu, baada ya kuokolewa kutoka katika mikononi ya adui zetu,
75katika utakatifu na haki mbele zake siku zetu zote.

76Ndiyo, na wewe mtoto, utaitwa nabii wa Aliye Juu Sana, kwa kuwa utaenenda mbele za uso wa Bwana ili kumwandalia njia, kuwaandaa watu kwa ajili ya ujio wake,
77kuwafahamisha watu wake kwamba, wataokolewa kwa njia ya kusamehewa dhambi zao.
78Hili litatokea kwa sababu ya huruma ya Mungu wetu, sababu ambayo jua tokea juu litatujia,
79kuangaza kwao wakaao gizani na katika uvuli wa mauti. Atafanya hivi kuiongoza miguu yetu kwenye njia ya amani.”

80Sasa, yule mtoto akakua na kuwa mwenye nguvu rohoni na alikaa nyikani mpaka siku ya kujitokeza kwake kwa Israeli.

2

1Sasa katika siku hizo, ikatokea kwamba Kaisari Agusto alitoa agizo akielekeza kwamba ichukuliwe sensa ya watu wote wanaoishi duniani.2Hii ilikuwa ni sensa ya kwanza iliyofanyika wakati Krenio akiwa gavana wa Siria.3Hivyo kila mmoja akaenda mjini kwake kuandikishwa sensa.4Naye Yusufu aliondoka pia katika mji wa Nazareti huko Galilaya na akasafiri Yudea katika mji wa Bethlehemu, ujulikanao kama mji wa Daudi, kwa sababu alitokea katika ukoo wa Daudi.5Alikwenda huko kujiandikisha pamoja na Mariamu, ambaye alikuwa amemposa na alikuwa akitazamia mtoto.6Sasa ilitokea kwamba, wakiwa kule wakati wake wa kujifungua mtoto ukawadia.7Akajifungua mtoto wa kiume, mzaliwa wake wa kwanza, akamzungushia nguo mwilini kumkinga na baridi mtoto. Ndipo akamweka kwenye kihori cha kulishia wanyama, kwa sababu haikuwepo nafasi kwenye nyumba za wageni.

8Katika eneo hilo, walikuwapo wachungaji walioishi mashambani wakilinda makundi ya Kondoo wao usiku.9Ghafla, malaika wa Bwana akawatokea, na utukufu wa Bwana ukang'aa kuwazunguka, na wakawa na hofu sana.10Ndipo malaika akwaambia, “Msiogope, kwa sababu nawaletea habari njema ambayo italeta furaha kuu kwa watu wote.11Leo Mwokozi kazaliwa kwa ajili yenu mjini mwa Daudi! Yeye ndiye Kristo Bwana!12Hii ndiyo ishara ambayo mtapewa, mtamkuta mtoto amefungwa nguo na amelala kwenye hori la kulishia wanyama.”

13Ghafla kukawa na jeshi kubwa la mbinguni likaungana na malaika huyo wakamsifu Mungu, wakisema,
14“Utukufu kwa Mungu aliye juu sana, na amani iwe duniani kwa wote ambao anapendezwa nao.”

15Ikawa kwamba malaika walipokwisha kuondoka kwenda mbinguni, wachungaji wakasemezena wao kwa wao, “Twendeni sasa kule Bethlehemu, na tukaone hiki kitu ambacho kimetokea, ambacho Bwana ametufahamisha.”16Wakaharakisha kule, na wakamkuta Mariamu na Yusufu, na wakamuona mtoto amelala kwenye hori la kulishia wanyama.17Na walipoona hivi, wakawajulisha watu kile walichokuwa wameambiwa kumhusu mtoto.18Wote waliosikia habari hii wakashangazwa na kile kilichosemwa na wachungaji.19Lakini Mariamu akaendelea kufikiri kuhusu yote aliyokwisha kuyasikia, akiyatunza moyoni mwake.20Wachungaji wakarudi wakimtukuza na kumsifu Mungu kwa ajili ya kila kitu walichokwisha sikia na kuona, kama tu ilivyokuwa imenenwa kwao.

21Ilipofika siku ya nane na ilikuwa ni wakati wa kumtahiri mtoto, wakamwita jina Yesu, jina alilokwishapewa na yule malaika kabla mimba haijatungwa tumboni.

22Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kulingana na sheria ya Musa, Yusufu na Mariamu wakampeleka hekaluni kule Yerusalemu kumweka mbele za Bwana.23Kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, “Kila mwanaume anayefungua tumbo ataitwa aliyetolewa wakfu kwa Bwana.”24Wao vilevile walikuja kutoa sadaka kulingana na kile kinachosemwa katika sheria ya Bwana, “Jozi ya njiwa au makinda mawili ya njiwa.”

25Tazama, palikuwa na mtu katika Yerusalemu ambaye jina lake alikuwa akiitwa Simeoni. Mtu huyu alikuwa mwenye haki na mcha Mungu. Yeye alikuwa akisubiri kwa ajili ya mfariji wa Israeli, na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake.26Ilikuwa imekwisha funuliwa kwake kupitia Roho Mtakatifu kwamba yeye hangelikufa kabla ya kuwomwona Kristo wa Bwana.27Siku moja alikuja ndani ya hekalu, akiongozwa na Roho Mtakatifu. Ambapo wazazi walimleta mtoto, Yesu, kumfanyia yale yaliyopasa kawaida ya sheria,28ndipo Simeoni alimpokea mikononi mwake, na akamsifu Mungu na kusema,
29“Sasa ruhusu mtumishi wako aende kwa amani Bwana, kulingana na Neno lako.
30Kwa kuwa macho yangu yameuona wakovu wako,
31ambao umeonekana kwa macho ya watu wote.
32Yeye ni nuru kwa ajili ya ufunuo wa mataifa na utukufu wa watu Israeli.”

33Baba na mama wa mtoto walishangazwa kwa mambo ambayo yalizungumzwa juu yake.34Ndipo Simeoni akawabariki na akasema kwa Mariamu mama yake, “Sikiliza kwa makini! Mtoto huyu atakuwa sababu ya kuanguka na kuinuka kwa watu wengi katika Israeli na ni ishara ambayo watu wengi wataipinga.35Pia ni upanga utakaochoma nafsi yako mwenyewe, ili kwamba mawazo ya mioyo ya wengi yadhihirike.”

36Nabii mwanamke aliyeitwa Ana pia alikuwako hekaluni. Yeye alikuwa binti wa Fanueli kutoka kabila la Asheri. Alikuwa na miaka mingi sana. Naye aliishi na mume wake kwa miaka saba baada ya kuoana,37na ndipo akawa mjane kwa miaka themanini na minne. Naye hakuwahi kuondoka hekaluni na alikuwa akiendelea kumwabudu Mungu pamoja na kufunga na kuomba, usiku na mchana.38Na kwa wakati huo, alikuja pale walipo akaanza kumshukuru Mungu. Aliongea kumhusu mtoto kwa kila mtu ambaye alikuwa akisubiri ukombozi wa Yerusalemu.

39Walipomaliza kila kitu walichotakiwa kufanya kuligana na sheria ya Bwana, walirudi Galilaya, mjini kwao, Nazareti.40Mtoto alikua, na akawa na nguvu, akiongezeka katika hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake.

41Wazazi wake kila mwaka walikwenda Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pasaka.42Alipokuwa na umri wa miaka kumi na miwili, walikwenda tena wakati mwafaka kidesturi kwa ajili ya sikukuu.43Baada ya kubaki siku zote kwa ajili ya sikukuu, walianza kurudi nyumbani. Lakini mvulana Yesu alibaki nyuma mle Yerusalemu na wazazi wake hawakujua hili.44Walidhani kwamba yumo kwenye kundi walilokuwa wakisafiri nalo, hivyo walisafiri safari ya siku. Ndipo wakaanza kumtafuta miongoni wa ndugu na marafiki zao.45Waliposhindwa kumpata, walirudi Yerusalemu na wakaanza kumtafuta humo.46Ikatokea kwamba baada ya siku tatu, wakampata hekaluni, akiwa ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.47Wote waliomsikia walishangazwa na ufahamu wake na majibu yake.48Walipomwona, walistaajabu. Mama yake akamwambia, “Mwanangu, kwa nini umetutendea hivi? Sikiliza, baba yako na mimi tumekuwa tukikutafuta kwa wasiwasi mkubwa.”49Akawaambia, “Kwa nini mmekuwa mkinitafuta? Hamkujua kwamba lazima niwe kwenye nyumba ya Baba yangu?”50Lakini hawakuelewa nini alichomaanisha kwa maneno hayo.51Ndipo akaenda pamoja nao mpaka nyumbani Nazareti na alikuwa mtii kwao. Mama yake alihifadhi mambo yote moyoni mwake.

52Lakini Yesu aliendelea kukua katika hekima na kimo, na akazidi kupendwa na Mungu na watu.

3

1Sasa, katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberia, wakati Pontio Pilato alikuwa gavana wa Uyahudi, Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo ndugu yake alikuwa mkuu wa mkoa wa Iturea na Trakoniti, na Lisania alikuwa mkuu wa mkoa wa Abilene,2na wakati wa ukuhani mkuu wa Anasi na Kayafa, Neno la Mungu lilimjia Yohana mwana wa Zakaria, jangwani.3Alisafiri katika mkoa wote kuzunguka mto Yordani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi4Kama ilivyoandikwa katika kitabu cha maneno ya Isaya nabii, ‘Sauti ya mtu aliaye nyikani: Itengenezeni tayari njia ya Bwana, yatengenezeni mapito yake yaliyoonyoka.

5Kila bonde litajazwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa, barabara zilizopinda zitanyoshwa, na njia zilizoparaza zitalainishwa.
6Watu wote watauona wokovu wa Mungu.’

7Hivyo, Yohana akawaambia makutano makubwa ya watu waliomjia wapate kubatizwa na yeye, “Ninyi uzao wa nyoka wenye sumu, nani aliwaonya kuikimbia gadhabu inayokuja?8Zaeni matunda yanayoedana na toba, na msianze kusema ndani yenu, “Tunaye Ibarahimu ambaye ni baba yetu,” kwa sababu nawaambia ya kwamba, Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutokana na mawe haya.9Tayari shoka limeshawekwa kwenye mzizi wa miti. Hivyo, kila mti usiozaa matunda mema, hukatwa na kutupwa motoni.

10Kisha watu katika makutano walimuuliza wakisema, “Sasa tunatakiwa tufanyeje?”

11Alijibu na kuwaambia, “Kama mtu ana kanzu mbili anatakiwa atoe kanzu moja kwa mwingine ambaye hana kabisa, na ambaye ana chakula na afanye vivyo hivyo.”

12Kisha baadhi ya watoza ushuru walikuja pia kubatizwa, na wakamwambia, “Mwalimu, tunatakiwa kufanya nini?

13Akawaambia, “Msikusanye fedha zaidi kuliko mnachotakiwa kukusanya.”

14Baadhi ya maaskari pia wakamuuliza wakisema, “Na sisi je? Tunatakiwa tufanye nini?” Akawaambia, “Msichukue fedha kwa mtu yeyote kwa nguvu, na msimtuhumu mtu yeyote kwa uongo. Ridhikeni na mishahara yenu.”15Sasa, kwa kuwa watu walikuwa na shauku ya kumngojea Kristo atakaye kuja, kila mmoja alikuwa anawaza moyoni mwake kuhusu Yohana kama yeye ndiye Kristo.16Yohana akajibu kwa kuwaambia wote, “Mimi nawabatiza ninyi kwa maji, lakini kuna mmoja ajaye ambaye ana nguvu kuliko mimi, na sisitahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Atawabatiza ninyi kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.17Pepeto lake liko mkononi mwake ili kusafisha vizuri uwanda wake wa kupepetea ngano na kuikusanya ngano ghalani mwake. Lakini, atayateketeza makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.”

18Kwa maonyo mengine mengi pia, alihubiri habari njema kwa watu.19Yohana alimkemea pia Herode mkuu wa mkoa kwa kumuoa Herodia, mke wa ndugu yake na kwa maovu mengine mengi ambayo Herode alikuwa ameyatenda.20Lakini baadaye Herode alifanya uovu mwingine mbaya sana. Alimfunga Yohana gerezani.21Kisha ilitokea kwamba, wakati watu wote walipokuwa wakibatizwa na Yohana, naye Yesu alibatizwa pia. Wakati alipokuwa akiomba, mbingu zikafunguka.22Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama njiwa, wakati huo huo sauti ikaja kutoka mbinguni ikisema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa. Ninapendezwa sana na wewe.”23Sasa Yesu mwenyewe, alipoanza kufundisha, alikuwa na umri upatao miaka thelathini. Alikuwa ni mwana (kama ilivyodhaniwa) wa Yusufu, mwana wa Eli,24mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yana, mwana wa Yusufu,25mwana wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Esli, mwana wa Nagai,26mwana wa Maati, mwana wa Matathia, mwana wa Semeini, mwana wa Yusufu, mwana wa Yuda,27mwana wa Yoanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa Neri,28mwana wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,29mwana wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Matathi, mwana wa Lawi,30mwana wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yusufu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliyakimu,31mwana wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,32mwana wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,33mwana wa Abinadabu, mwana wa Aramu, mwana wa Hesroni, mwana wa Peresi, mwana wa Yuda,34mwana wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Ibrahimu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,35mwana wa Seruig, mwana wa Ragau, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala.36Mwana wa Kenani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Nuhu, mwana wa Lameki,37mwana wa Methusela, mwana wa Henoko, mwana wa Yaredi, mwana Mahalalei, mwana wa Kenani,38mwana wa Enoshi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, mwana wa Mungu.

4

1Kisha, Yesu akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka mto Jordani, na aliongozwa na Roho jangwani2kwa siku arobaini, na huko alijaribiwa na Ibilisi. Wakati huo hakula chochote, na mwisho wa wakati huo alihisi njaa.3Ibilisi akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, liamru jiwe hili kuwa mkate.”

4Yesu akamjibu, “Imeandikwa; ‘Mtu hataishi kwa mkate pekee.’”

5Kisha Ibilisi alimwongoza juu kwenye kilele cha mlima, na akamwonyesha falme zote za dunia kwa muda mfupi.6Ibilisi akamwambia, “Nitakupa mamlaka ya kutawala falme hizi zote pamoja na fahari zake. Naweza kufanya hivyo kwa sababu vyote vimekabidhiwa kwangu nivitawale, na ninaweza kumpa yeyote nitakaye kumpa.7Kwa hiyo, kama utaniinamia na kuniabudu, vitu hivi vyote vitakuwa vyako.”

8Lakini Yesu alijibu na kumwambia, “Imeandikwa, ‘lazima umwabudu Bwana Mungu wako, na lazima umtumikie Yeye peke yake.’”

9Baadaye Ibilisi alimwongoza Yesu hadi Yerusalemu na kumweka sehemu ya juu kabisa ya jengo la hekalu na kumwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini kutoka hapa.10Kwa sababu imeandikwa, ‘Atawaagiza malaika zake wakutunze na kukulinda,11na watakuinua juu mikononi mwao ili kwamba usiumize miguu yako juu ya jiwe.’”

12Yesu akijibu alimwambia, “Imenenwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’”

13Ibilisi alipomaliza kumjaribu Yesu, alienda zake na kumwacha hadi wakati mwingine.

14Kisha Yesu alirudi Galilaya kwa nguvu za Roho, na habari kumhusu yeye zikaenea na kusambaa katika mikoa jirani yote.15Alifundisha katika masinagogi yao, na kila mmoja alimsifu.

16Siku moja alikwenda Nazareti, mji ambao alilelewa na kukulia. Kama ilivyokuwa desturi yake aliingia kwenye sinagogi siku ya sabato, na alisimama kusoma maandiko.17Alikabidhiwa kitabu cha nabii Isaya, hivyo, alikifungua kitabu na akatafuta sehemu iliyoandikwa,
18‘Roho wa Bwana yuu juu yangu, kwa sababu alinitia mafuta kuhubiri habari njema kwa maskini. Amenituma kutangaza uhuru kwa wafungwa, na kuwafanya wasioona waweze kuona tena. Kuwaweka huru wale wanaogandamizwa,
19kuutangaza mwaka ambao Bwana ataonesha wema wake.’

20Kisha akalifunga gombo, akamrudishia kiongozi wa sinagogi, na akaketi chini. Macho ya watu wote waliokuwa katika sinagogi yalimwangalia yeye.21Alianza kuzungumza nao akisema, “Leo andiko hili limetimizwa masikioni mwenu.”

22Kila mmoja pale alishuhudia kile alichokisema Yesu, na wengi miongoni mwao walishangazwa na maneno ya hekima yaliyokuwa yakitoka katika kinywa chake. Walikuwa wakisema, “Huyu ni kijana tu wa Yusufu, siyo hivyo?”

23Yesu akawaambia, “Hakika mtasema methali hii kwangu, ‘Tabibu, jiponye mwenyewe. Chochote tulichosikia ukifanya Kapernaumu, kifanye hapa pia kijijini kwako.’”24Pia alisema, “Hakika nawaambia ninyi, hakuna nabii anayekubalika katika nchi yake.25Lakini nawaambia ninyi kweli kwamba kulikuwa na wajane wengi Israel katika kipindi cha Eliya, wakati mbingu ilipofungwa kusiwe na mvua kwa miaka mitatu na nusu, wakati kulipokuwa na njaa kubwa katika nchi yote.26Lakini Eliya hakutumwa kwa yeyote mmoja wao, lakini kwa mjane mmoja tu aliyeishi Sarepta karibu na mji wa Sidoni.27Pia, kulikuwa na wakoma wengi Israel katika kipindi cha Elisha nabii, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeponywa isipokuwa Naamani mtu wa Siria.”28Watu wote ndani ya sinagogi walijawa na hasira walipoyasikia haya yote.29Walisimama na kumsukumizia nje ya mji, na kumwongoza mpaka kwenye ukingo wa mlima ambapo mji wao ulijengwa juu yake, ili waweze kumtupa chini.30Lakini alipita salama katikati yao na akaenda zake.

31Kisha alitelemkia Kapernaumu, katika mji wa Galilaya. Sabato moja alikuwa akifundisha watu ndani ya sinagogi.32Walishangazwa na mafundisho yake, kwa sababu alifundisha kwa mamlaka.33Sasa siku hiyo ndani ya sinagogi, kulikuwa na mtu aliyekuwa na roho ya pepo mchafu, na alilia kwa sauti ya juu,34“Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Umekuja kutuangamiza? Ninajua wewe ni nani! Wewe ni mtakatifu wa Mungu!”

35Yesu alimkemea pepo akisema, “Nyamaza kimya, na umtoke mtu huyu!” Pepo yule alipomtupa mtu yule chini katikati yao, alimtoka yule mtu bila ya kumsababishia maumivu yoyote.

36Watu wote walishangaa, na waliendelea kuzungumzia jambo hilo kila mmoja na mwenzake. Wakasema, “Ni maneno ya aina gani haya?” Anawaamuru roho wachafu kwa mamlaka na nguvu na wanatoka.”37Hivyo, habari juu ya Yesu zilienea kila sehemu katika maeneo yanayozunguka mkoa huo.

38Kisha Yesu aliondoka katika mji huo na akaingia katika nyumba ya Simoni. Sasa, mama mkwe wake na Simoni alikuwa anaumwa homa kali, na wakamsihi kwa niaba yake.39Hivyo, Yesu alimsogelea, akaikemea ile homa na ikamwachia. Ghafla alisimama na akaanza kuwatumikia.

40Jua lilipokuwa likizama, watu walimletea Yesu kila mmoja aliyekuwa mgonjwa wa maradhi ya aina mbalimbali. Aliweka mikono yake juu ya kila mgonjwa na akawaponya wote.41Mapepo pia yaliwatoka wengi wao yakilia kwa sauti na kusema, “Wewe ni mwana wa Mungu!” Yesu aliwakemea mapepo na hakuwaruhusu waongee, kwa sababu walijua kwamba yeye alikuwa ni Kristo.

42Hata kulipokucha, alienda eneo lisilokuwa na watu. Makutano ya watu walikuwa wakimtafuta na wakaja katika eneo alilokuwapo. Walijaribu kumzuia asiende mbali na wao.43Lakini akawaambia, “Lazima pia nihubiri habari njema za ufalme wa Mungu katika miji mingine mingi, kwa kuwa hii ndiyo sababu nilitumwa hapa.”44Kisha aliendelea kuhubiri ndani ya masinagogi katika uyahudi wote.

5

1Ikawa makutano walipomsonga Yesu na kusikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti.2Akaona mashua mbili zimetia nanga pembeni mwa ziwa. Wavuvi walikuwa wametoka na walikuwa wakiosha nyavu zao.3Yesu akaingia katika mojawapo ya zile mashua, ambayo ilikuwa ya Simoni na kumwomba aipeleke majini mbali kidogo na nchi kavu. Kisha akakaa na kufundisha kutokea kwenye mashua.4Kuongea, akamwambia Simoni, “Ipeleke mashua yako mpaka kwenye kina kirefu cha maji nakushusha nyavu zako ili kuvua samaki.”

5Simon akajibu na kusema, “Bwana, tumefanya kazi usiku wote, na hatukupata chochote, lakini kwa neno lako, nitazishusha nyavu.”6Walipofanya hivyo walikusanya kiasi kikubwa cha samaki na nyavu zao zikaanza kukatika.7Hivyo wakawaashiria washirika wao kwenye mashua nyingine ili waje na kuwasaidia. Walikuja wakazijaza mashua zote, kiasi kwamba zikaanza kuzama.8Lakini Simoni Petro, alipoona hivyo, alianguka magotini pa Yesu akisema, “Ondoka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi Bwana.”9Kwa sababu alishangazwa, na wote waliokuwa pamoja naye, kwa uvuvi wa samaki waliokuwa wameufanya.10Hili liliwajumuisha Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo, ambao walikuwa washirika wa Simoni. Na Yesu akamwambia Simoni, “Usiogope, kwa sababu kuanzia sasa na kuendelea utavua watu.”11Walipokwishazileta mashua zao nchi kavu, waliacha kila kitu na kumfuata yeye.

12Ikawa alipokuwa katika mji mmojawapo, mtu aliyekuwa amejaa ukoma alikuwa huko. Wakati alipomuona Yesu, alianguka akiinamisha uso kwake mpaka chini na kumuomba, akisema, “Bwana, ikiwa unataka, waweza kunitakasa.”

13Kisha Yesu alinyoosha mkono wake na kumgusa, akisema, “Nataka. Takasika.” Na saa ileile ukoma ukamwacha.14Alimwagiza asimwambie mtu yeyote, lakini alimwambia, “Nenda zako, na ukajionyeshe kwa makuhani na utoe sadaka ya utakaso wako, sawasawa na kile Musa alichokiamuru, kwa ushuhuda kwao.”15Lakini habari kumuhusu yeye zikaenea mbali zaidi, na umati mkubwa wa watu ukaja pamoja kumsikiliza akifundisha na kuponywa magonjwa yao.16Lakini mara kwa mara alijitenga faraghani na kuomba.

17Ikawa moja kati ya hizo siku alikuwa akifundisha, na walikuwapo Mafarisayo na waalimu wa sheria wamekaa hapo ambao walikuja wakitokea vijiji vingi tofauti katika mkoa wa Galilaya na Yudea, na pia kutokea katika mji wa Yerusalemu. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kuponya.18Watu kadhaa walikuja, wamembeba kwenye mkeka mtu aliyepooza, na wakatafuta njia ya kumwingiza ndani ili kumlaza chini mbele ya Yesu.19Hawakupata njia ya kumwingiza ndani kwa sababu ya umati, hivyo walipanda juu ya paa la nyumba na kumshusha yule mtu chini kupitia kwenye vigae, juu mkeka wake katikati ya watu, mbele kabisa ya Yesu.20Akiangalia imani yao, Yesu alisema, “Rafiki, dhambi zako umesamehewa.”

21Waandishi na Mafarisayo waliaanza kuhoji hilo, wakisema, “Ni nani huyu asemaye maneno ya kukufuru? Ni nani anaweza kusamehe dhambi ila Mungu pekee yake?”

22Lakini Yesu, akitambua nini walichokuwa wakifikiri, aliwajibu na kuwaambia, “Kwa nini mnaulizana hili mioyoni mwenu?23Kipi ni rahisi kusema, ‘Dhambi zako zimesamehewa’ au kusema ‘Simama utembee?’24Lakini mjue ya kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi, nakwambia wewe, ‘Amka, chukua mkeka wako na uende nyumbani kwako.’”25Wakati huo huo akaamka mbele yao na akachukua mkeka wake aliokuwa ameulalia. Kisha akarudi nyumbani kwake akimtukuza Mungu.

26Kila mmoja alishangazwa na wakamtukuza Mungu. Walijawa na hofu, wakisema, “Tumeona mambo yasiyo ya kawaida leo.”

27Baada ya mambo haya kutokea, Yesu alitoka huko na akamwona mtoza ushuru aliyeitwa Lawi amekaa eneo la kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate.”28Hivyo Lawi akanyanyuka na kumfuata, akiacha kila kitu nyuma.

29Kisha Lawi akaandaa nyumbani kwake sherehe kubwa kwa ajili ya Yesu. Walikuwapo watozaushuru wengi kule na watu wengi walioketi mezani wakila pamoja nao.30Lakini Mafarisayo na waandishi wao walikuwa wakiwanung'unikia wanafunzi, wakisema, “Kwa nini mnakula na kunywa na watoza ushuru pamoja na watu wengine wenye dhambi?”

31Yesu akawajibu, “Watu walio katika afya njema hawahitaji tabibu, ni wale tu wanaoumwa ndiyo watakao mhitaji mmoja.32Sikuja kuwaita watu wenye haki wapate kutubu, bali kuwaita wenye dhambi wapate kutubu.”

33Wakamwambia, “Wanafunzi wa Yohana mara nyingi hufunga na kuomba, na wanafunzi wa Mafarisayo nao hufanya vivyo hivyo. Lakini wanafunzi wako hula na kunywa.”

34Yesu akawaambia, “Inawezekana mtu yeyote akawafanya waliohudhuria harusi ya Bwana Arusi kufunga wakati Bwana Arusi bado yu pamoja nao?35Lakini siku zitakuja wakati Bwana Arusi atakapoondolewa kwao, ndipo katika siku hizo watafunga.”

36Kisha Yesu aliongea pia kwao kwa mfano. “Hakuna anayechana kipande cha nguo kutoka kwenye vazi jipya na kukitumia kurekebisha vazi la zamani. Kama akifanya hivyo, ataichana nguo mpya, na kipande cha nguo kutoka vazi jipya kisengefaa kutumika na nguo ya vazi la zamani.37Pia, hakuna mtu ambaye huweka divai mpya kwenye viriba vikuukuu. Kama akifanya hivyo, divai mpya ingepasua kile chombo, na divai ingemwagika, na viriba vingeharibika.38Lakini divai mpya lazima iwekwe kwenye viriba vipya.

39Na hakuna mtu baada ya kunywa divai ya zamani, hutaka mpya, kwa sababu husema, ‘Ya zamani ni bora.”’

6

1Ikawa siku ya sabato moja Yesu alikuwa akipita katika shamba la nafaka na wanafunzi wake walikuwa wakichuma mbegu, wakayasuguasugua kati ya mikono yao wakala nafaka.2Lakini baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Kwa nini mnafanya kitu ambacho si halali kisheria kukifanya siku ya sabato?”

3Yesu, akawajibu, akisema, “Hamkuwahi kusoma kile Daudi alifanya alipokuwa na njaa, yeye na wanaume waliokuwa pamoja naye?4Alikwenda katika nyumba ya Mungu, na akachukuwa mikate mitakatifu na kuila baadhi, na kuitoa baadhi kwa watu aliokuwa nao kuila, hata kama ilikuwa halali kwa makuhani kuila.”5Kisha akawaambia, “Mwana wa Adamu ni Bwana wa Sabato.”

6Ilitokea katika Sabato nyingine kwamba alikwenda ndani ya sinagogi na kuwafundisha watu huko. Palikuwa na mtu ambaye mkono wake wa kulia ulikuwa umepooza.7Waandishi na Mafarisayo walikuwa wanamwangalia kwa makini kuona kama angemponya mtu siku ya Sabato, ili waweze kupata sababu ya kumshtaki kwa kufanya kosa.8Lakini alijua nini walikuwa wanafikiri na akasema kwa mtu aliyekuwa amepooza mkono, “Amka, simama hapa katikati ya kila mmoja.” Hivyo huyo mtu akanyanyuka na kusimama pale.9Yesu akasema kwao, “Nawauliza ninyi, ni halali siku ya Sabato kufanya mema au kufanya madhara, kuokoa maisha au kuyaharibu?” Kisha aliwaangalia wote na kumwambia yule mtu,10“Nyoosha mkono wako.” Akafanya hivyo, na mkono wake ulikuwa umeponywa.11Lakini walijawa na hasira, wakaongeleshana wao kwa wao kuhusu nini wanapaswa wafanye kwa Yesu.

12Ikawa siku zile aliondoka kwenda mlimani kuomba. Aliendelea usiku mzima akimwomba Mungu.13Ilipokuwa asubuhi, aliwaita wanafunzi wake kwake, na akawachagua kumi na wawili kati yao, ambao pia aliwaita “Mitume.”14Majina ya wale mitume yalikuwa Simoni (ambaye pia alimwita Petro) na Andrea ndugu yake, Yakobo, Yohana, Filipo, Bartolomayo,15Mathayo, Tomaso na Yakobo mwana wa Alfayo, Simoni, ambaye aliitwa Zelote,16Yuda mwana Yakobo na Yuda Iskariote, ambaye alikuwa msaliti.

17Kisha Yesu alitelemka pamoja nao toka mlimani na kusimama mahali tambarare. Idadi kubwa ya wanafunzi wake walikuwa huko, pamoja na idadi kubwa ya watu kutoka Uyahudi na Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.18Walikuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Watu waliokuwa wakisumbuliwa na pepo wachafu waliponywa pia.19Kila mmoja kwenye hilo kusanyiko alijaribu kumgusa kwa sababu nguvu za uponyaji zilikuwa zikitokea ndani yake, na aliwaponya wote.20Kisha akawaangalia wanafunzi wake, na kusema, “Mmebarikiwa ninyi mlio maskini, kwa maana ufalme wa Mungu ni wenu.21Mmebarikiwa ninyi mlio na njaa sasa, kwa maana mtashibishwa. Mmebarikiwa ninyi mliao sasa, kwa maana mtacheka.

22Mmebarikiwa ninyi ambao watu watakapowachukia na kuwatenga na kuwashutumu ninyi kwamba ni waovu, kwa ajili ya Mwana Adamu.23Furahini katika siku hiyo na kurukaruka kwa furaha, kwa sababu hakika mtakuwa na thawabu kubwa mbinguni, kwa maana baba zao waliwatendea vivyohivyo manabii.

24Lakini ole wenu mlio matajiri! Kwa maana mmekwisha pata faraja yenu.25Ole wenu mlio shiba sasa! Kwa maana mtaona njaa baadaye. Ole wenu mnaocheka sasa! Kwa maana mtaomboleza na kulia baadaye.26Ole wenu, mtakaposifiwa na watu wote! Kwa maana baba zao waliwatendea manabii wa uongo vivyohivyo.

27Lakini nasema kwenu ninyi mnaonisikiliza, wapendeni adui zenu na kufanya mema kwa wanao wachukieni.28Wabarikini wale wanao walaani ninyi na waombeeni wale wanaowaonea.29Kwake yeye akupigaye shavu moja, mgeuzie na la pili. Kama mtu akikunyang'anya joho lako usimzuilie na kanzu.30Mpe kila akuombaye. Kama mtu akikunyang'anya kitu ambacho ni mali yako, usimuombe akurudishie.31Kama mpendavyo watu wawatendee, nanyi watendeeni vivyo hivyo.

32Kama mkiwapenda watu wawapendao ninyi tu, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.33Kama mkiwatendea mema wale wanaowatendea ninyi mema, hiyo ni thawabu gani kwenu? Kwa maana hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.34Kama mkikopesha vitu kwa watu ambao mnategemea watawarudishia, hiyo ni thawabu gani kwenu? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, na hutegemea kupokea kiasi hicho hicho tena.35Lakini wapendeni adui zenu na watendeeni mema. Wakopesheni na msihofu kuhusu kurudishiwa, na thawabu yenu itakuwa kubwa. Mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa sababu yeye mwenyewe ni mwema kwa watu wasio na shukurani na waovu.36Iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.

37Msihukumu, nanyi hamta hukumiwa. Msilaani, nanyi hamtalaaniwa. Sameheni wengine, nanyi mtasamehewa.38Wapeni wengine, nanyi mtapewa. Kiasi cha ukarimu - kilichoshindiliwa, kusukwasukwa na kumwagika - kitamwagika magotini penu. Kwa sababu kwa kipimo chochote mnachotumia kupimia, kipimo hicho hicho kitatumika kuwapimia ninyi.”

39Kisha akawaambia mfano pia. “Je mtu aliye kipofu aweza kumwongoza mtu mwingine kipofu? Kama alifanya hivyo, basi wote wangalitumbukia shimoni, je wasingetumbukia?40Mwanafunzi hawi mkubwa kuliko mwalimu wake, lakini kila mtu akiisha kufundishwa kwa ukamilifu atakuwa kama mwalimu wake.

41Na kwa nini basi wakitazama kijiti kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na kigogo kilicho ndani ya jicho lako hukiangalii?42Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, naomba nikitoe kijiti kilicho ndani ya jicho lako,’ nawe huangalii kigogo kilicho katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Kwanza kitoe kigogo katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaona vizuri kutoa kijiti katika jicho la ndugu yako.

43Kwa sababu hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala hakuna mti mbaya uzaao matunda mazuri.44Kwa sababu kila mti hutambulika kwa matunda yake. Kwa sababu watu hawachumi tini kutoka kwenye miba, wala hawachumi zabibu kutoka kwenye michongoma.45Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu. Kwa sababu kinywa chake husema yale yaujazayo moyo wake.

46Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ na bado hamyatendi yale nisemayo?47Kila mtu ajaye kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatendea kazi, nitawaonyesha jinsi alivyo.48Anafanana na mtu ajengae nyumba yake, ambaye huchimba chini sana, na kujenga msingi wa nyumba juu ya mwamba imara. Mafuriko yalipokuja, maporomoko ya maji yaliipiga nyumba, lakini hayakuweza kuitikisa, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri.49Lakini yeyote asikiaye neno langu na hakulitii; mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi, mto ulipoishukia kwa nguvu, nyumba ile iliharibika kabisa.”

7

1Baada ya Yesu kumaliza kila kitu alichokuwa anasema kwa watu waliomsikiliza, akaingia Kapernaumu.2Mtumwa fulani wa akida, aliyekuwa wa thamani sana kwake, alikuwa mgonjwa sana na alikuwa karibu ya kufa.3Lakini akiwa amesikia kuhusu Yesu, yule akida alimtuma kiongozi wa kiyahudi, kumwomba aje kumwokoa mtumwa wake ili asife.4Walipofika karibu na Yesu, walimsihi kwa bidii na kusema, “Anastahili kwamba unapaswa kufanya hivi kwa ajili yake,5kwa sababu analipenda taifa letu, na ndiye aliyejenga sinagogi kwa ajili yetu.”

6Yesu akaendelea na safari yake pamoja nao. Lakini kabla hajaenda mbali na nyumba, afisa mmoja aliwatuma marafiki zake kuzungumza naye. “Bwana, usijichoshe mwenyewe kwa sababu mimi sistahili wewe kuingia kwenye dari yangu.7Kwa sababu hii sikufikiria hata mimi mwenyewe kuwa ninafaa kuja kwako, lakini sema neno tu na mtumishi wangu atapona.8Kwani mimi pia ni mtu niliyewekwa kwenye mamlaka na nina askari chini yangu. Husema kwa huyu ‘Nenda’ na huenda, na kwa mwingine, ‘Njoo’ naye huja, na kwa mtumishi wangu ‘Fanya hiki,’ na yeye hufanya.”

9Yesu aliposikia haya alishangaa, na kuwageukia makutano waliokuwa wanamfuata na kusema. “Nawaambia, hata katika Israeli, sijawahi kuona mtu mwenye imani kuu kama huyu.”10Kisha wale waliokuwa wametumwa walirudi nyumbani na kumkuta mtumishi akiwa mzima.

11Baada ya haya, Yesu alikwenda mji ulioitwa Naini. Wanafunzi wake wakaenda pamoja naye wakiambatana na umati wa watu.12Alipokaribia lango la mji, tazama, mtu aliyekufa alikuwa amebebwa, na ni mtoto wa pekee kwa mama yake aliyekuwa mjane, na watu wengi kutoka kwenye mji walikuwa pamoja naye.13Alipomwona, Bwana akamsogelea kwa huruma kubwa sana juu yake na akamwambia, “Usilie.”14Kisha akasogea mbele akaligusa jeneza ambalo walibebea mwili, na wale waliobeba wakasimama akasema “Kijana nasema amka.”15Mfu akainuka na kukaa chini na akaanza kuongea. Kisha Yesu akamkabidhi kwa mama yake.

16Kisha hofu ikawajaa wote, wakaendelea kumtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ameinuliwa miongoni mwetu na Mungu amewaangalia watu wake.”17Hizi habari njema za Yesu zilienea Yudea yote na kwa mikoa yote ya jirani.

18Wanafunzi wa Yohana walimwamwambia mambo haya yote.19Ndipo Yohana akawaita wawili wa wanafunzi wake na kuwatuma kwa Bwana kusema “Wewe ndiye yule ajaye, au kuna mtu mwingine tumtazamie?”

20Walipofika karibu na Yesu hawa wakasema, “Yohana mbatizaji ametutuma kwako kusema, ‘Wewe ni yule ajaye au kuna mtu mwingine tumtazamie?’”

21Kwa wakati huo aliowaponya watu wengi kutoka katika magonjwa na mateso, kutoka kwa roho wachafu, na kwa watu wenye upofu aliwapa kuona.22Yesu akajibu na kusema kwao. “Baada ya kuwa mmekwenda mlikotoka mtamjulisha Yohana mlichokiona na kukisikia. Wenye upofu wanapokea kuona na viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na kuwa hai tena, masikini wanaambiwa habari njema.23Na mtu ambaye hataacha kuniamini mimi kwa sababu ya matendo yangu amebarikiwa.”

24Baada ya wale waliotumwa na Yohana kurudi walikotoka, Yesu akaanza kusema kwa makutano juu ya Yohana, “Mlikwenda nje kuona nini, mwanzi ukiwa unatikiswa na upepo?25Lakini mlikwenda nje kuona nini, mtu aliyevaa vizuri? Tazama watu wale wanaovaa mavazi ya kifalme na kuishi maisha ya starehe wako kwenye nafasi za wafalme.26Lakini mnakwenda nje kuona nini, Nabii? Ndiyo, ninasema kwenu na zaidi sana kuliko nabii.27Huyu ndiye aliyeandikiwa, ‘Tazama, namtuma mjumbe wangu mbele ya macho yenu, atakeyeandaa njia kwa ajili yangu.’

28Nasema kwenu, kati ya wale waliozaliwa na mwanamke, hakuna mkuu kama Yohana, lakini mtu asiye muhimu sana atakayeishi na Mungu mahali alipo yeye, atakuwa mkuu kuliko Yohana.”

29Na watu wote waliposikia haya pamoja na watoza ushuru, walitangaza kuwa Mungu ni mwenye haki. Walikuwepo kati yao wale waliobatizwa kwa ubatizo wa Yohana.30Lakini mafarisayo na wataalamu wa sheria za kiyahudi, ambao hawakubatizwa na yeye walikataa hekima za Mungu kwa ajili yao wenyewe.

31Tena naweza kuwalinganisha na nini watu wa kizazi hiki? Wakoje hasa?32Wanafanana na watoto wanaocheza kwenye eneo la soko, wanaokaa na kuitana mmoja baada wa mwingine wakisema, “Tumepuliza filimbi kwa ajili yenu, na hamkucheza. Tumeomboleza na hamkulia.”33Yohana mbatizaji alikuja hakula mkate wala hakunywa divai, na mkasema, “Ana pepo.”34Mwana wa Mtu amekuja amekula na kunywa na mkasema, “Angali ni mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi!”35Lakini hekima imetambulika kuwa ina haki kwa watoto wake wote.

36Mmoja wa mafarisayo alimwomba Yesu aende kula pamoja naye. Baada ya Yesu kuingia kwenye nyumba ya farisayo, aliegemea kwenye meza ili ale.37Tazama kulikuwa na mwanamke mmoja katika jiji hilo aliyekuwa na dhambi. Akagundua kuwa alikuwa amekaa kwa Farisayo, akaleta chupa ya manukato.38Alisimama nyuma yake karibu na miguu yake huku akilia. Tena alianza kulowanisha miguu yake kwa machozi, na kuifuta kwa nywele za kichwa chake, akiibusu miguu yake na kuipaka manukato.39Na yule farisayo aliyekuwa amemwalika Yesu alipoona hivyo, akawaza mwenyewe akisema, “Kama huyu mtu angekuwa nabii, angejua huyu ni nani na ni aina gani ya mwanamke anayemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.”

40Yesu akajibu na kumwambia, “Simoni nina kitu cha kukuambia.” Akasema, “Kiseme tu mwalimu!”41Yesu akasema, “Kulikuwa na wadaiwa wawili kwa mkopeshaji mmoja. Mmoja alikuwa anadaiwa dinari mia tano na wa pili alidaiwa dinari hamsini.42Na walipokuwa hawana pesa ya kumlipa aliwasamehe wote. Sasa ni nani atampenda zaidi?”

43Simoni akamjibu na kusema, “Nadhani aliyesamehewa zaidi.” Yesu akamwambia, “Umehukumu kwa usahihi.”44Yesu akamgeukia mwanamke na kusema kwa Simoni, “Unamwona huyu mwanamke. Nimeingia kwenye Nyumba yako. Hukunipa maji kwa ajili ya miguu yangu, lakini huyu, kwa machozi yake, alilowanisha miguu yangu na kuifuta kwa nywele zake.45Hukunibusu, lakini yeye, tangu alipoingia humu hakuacha kunibusu miguu yangu.46Hukuipaka miguu yangu kwa mafuta, lakini ameipaka miguu yangu kwa manukato.47Kwa jambo hili, nakwambia kwamba alikuwa na dhambi nyingi na amesamehewa zaidi, na pia alipenda zaidi. Lakini aliyesamehewa kidogo, hupenda kidogo tu.”48Baadaye akamwambia mwanamke, “Dhambi zako zimesamehewa.”

49Wale waliokaa mezani pamoja naye wakaanza kusemezana wao kwa wao, “Huyu ni nani mpaka anasamehe dhambi?”

50Na Yesu akamwambia mwanamke, “Imani yako imekuokoa. Enenda kwa amani.”

8

1Ikawa baada ya hayo Yesu alianza kusafiri katika miji na vijiji mbalimbali, akihubiri na kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu. Na wale kumi wawili walikwenda pamoja naye,2vilevile wanawake fulani waliokuwa wameponywa kutoka kwa roho wachafu na magonjwa mbalimbali. Walikuwa ni Mariamu aliyeitwa Magdalena ambaye alikuwa ametolewa pepo saba.3Yoana mke wa Kuza na meneja wa Herode, Susana, na wanawake wengine wengi, waliotoa mali vyao kwa ajili yao wenyewe.

4Na baada ya umati wa watu kukusanyika pamoja, wakiwemo na watu waliokuja kwake kutoka miji mbalimbali, akazungumza nao kwa kutumia mifano.5“Mpandaji alienda kupanda mbegu, alipokuwa akipanda, baadhi ya mbegu hizo ziliangukia kando ya njia zikakanyagwa chini ya miguu, na ndege wa angani wakazila.6Mbegu zingine zilianguka juu ya udongo wa miamba na zilipoota na kuwa miche zilipooza kwa sababu hakukuwa na unyevunyevu.7Mbegu zingine ziliangukia kwenye miti ya miiba, nayo hiyo miti ya miiba ikakua pamoja na zile mbegu na zikasongwa.8Lakini mbegu zingine ziliangukia kwenye udongo unaofaa na zikazaa mazao mara mia zaidi.” Baada ya Yesu kusema mambo haya, alipaza sauti, “Yeyote aliye na masikio ya kusikia na asikie.”

9Tena wanafunzi wake wakamuuliza maana ya mfano huo,10Yesu akawaambia, “Mmepewa upendeleo wa kujua siri ya ufalme wa Mungu, lakini watu wengine watafundishwa tu kwa mifano, ili kwamba ‘wakiona wasione na wakisikia wasielewe.’

11Na hii ndiyo maana ya mfano huu. Mbegu ni neno la Mungu.12Mbegu zile zilizoanguka kando kando ya njia ndiyo wale watu wanaolisikia neno, na baadaye mwovu shetani hulichukua mbali kutoka moyoni, ili kwamba wasiamini na kuokolewa.13Kisha na zile zilizoangukia kwenye mwamba ni watu wale wanaosikia neno na kulipokea kwa furaha lakini hawana mizizi yeyote, wanaamini tu kwa muda mfupi, na wakati wa majaribu huanguka.14Na mbegu zile zilizoangukia kwenye miiba ni watu wanaosikia neno, lakini wanapoendelea kukua husongwa na shughuli na utajiri na anasa za maisha haya na hawazai matunda.15Lakini zile mbegu zilizoangukia kwenye udongo mzuri ni wale watu, ambao ni wanyeyekevu na mioyo mizuri, baada ya kulisikia neno hulishikilia na likawa salama na kuazaa matunda ya uvumilivu.

16Sasa, hakuna hata mmoja, anayewasha taa na kuifunika kwa bakuli au kuiweka chini ya kitanda. Badala ya kuiweka taa juu ili kwamba kila mmoja anayeingia apate kuiona.17Kwa kuwa hakuna kitakachojificha ambacho hakitajulikana, au chochote kilicho sirini ambacho hakitajulikana kikiwa kwenye mwanga.18Kwa hiyo kuwa makini unapokuwa unasikiliza. Kwa sababu aliye nacho, kwake ataongezewa zaidi, lakini asiye nacho hata kile kidogo alicho nacho kitachukuliwa.”

19Baadaye mama yake Yesu na ndugu zake wakaja kwake hawakukaribia kwa sababu ya umati wa watu.20Na akataarifiwa, “Mama yako na ndugu zako wako pale nje wanahitaji kukuona wewe.

21Lakini, Yesu akajibu akasema, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wanaolisikia neno la Mungu na kulitii.”

22Ikawa siku mojawapo kati ya siku zile Yesu na wanafunzi wake walipanda kwenye mtumbwi, na akawaambia, “Na tuvuke ng'ambo ya pili ya ziwa.” Wakaandaa mashua yao.23Lakini walipoanza kuondoka, Yesu akalala usingizi, na dhoruba kali yenye upepo, na mashua yao ikaanza kujaa maji na walikuwa kwenye hatari kubwa sana.

24Baadaye wanafunzi wake wakaja kwake na kumwamsha, wakisema, “Bwana mkubwa! Bwana mkubwa! Tuko karibu kufa!” Akaamka na akaukemea upepo na mawimbi ya maji vikatulia na kukawa na utulivu.

25Tena akawaambia, “Imani yenu iko wapi?” Wakaogopa, walishangaa, wakasemezana kia mmoja na mwenzake, “Huyu ni nani, kiasi kwamba anaamuru hata upepo, na maji na humtii?”

26Wakafika kwenye mji wa Gerasini iliyo upande wa nyuma ya Galilaya.27Yesu aliposhuka na kukanya kwenye ardhi, mtu fulani kutoka mjini, akakutana naye, na huyu mtu alikuwa na nguvu za giza. Kwa muda mrefu alikuwa havai nguo, na alikuwa haishi kwenye Nyumba, lakini aliishi kwenye makaburi.

28Alipomwona Yesu akalia kwa sauti, na akaanguka chini mbele yake, kwa sauti kubwa akisema, “Nimefanya nini kwako, Yesu mwana wa Mungu aliye juu? Nakusihi, usiniadhibu mimi.”29Yesu akaamuru roho mchafu imtoke mtu yule, kwa kuwa amepagawa naye mara nyingi. Hata kama alikuwa amefungwa minyororo na kubanwa na kuwekwa chini ya ulinzi, alivunja vifungo na kuendeshwa na mapepo mpaka jangwani.

30Yesu akamwuliza, “Jina lako nani?” Akajibu akisema, “Legioni.” Kwa maana mapepo mengi yameingia kwake.31Wakaendelea kumsihi usituamuru twende kwenye shimo.32Kundi la Nguruwe lilikuwa likichunga juu ya kilima, wakamsihi awaruhusu wakaingie kwa hao nguruwe. Na akawaruhusu kufanya hivyo.33Kwa hiyo wale mapepo wakamtoka mtu yule na kuingia kwa wale nguruwe, na lile kundi likakimbia kwenye mwinuko wa mlima mpaka ziwani na wakazama humo.

34Wale watu waliokuwa wanachunga wale nguruwe walipoona kilichotokea, wakakimbia na wakatoa taarifa pale mjini na nje katika miji iliyowazunguka.35Watu waliposikia hayo walienda kuona kilichotokea, na wakaja kwa Yesu na wakamwona mtu ambaye mapepo yalikuwa yamemtoka, alikuwa amevaa vizuri na mwenye akili timamu, amekaa kwenye miguu ya Yesu, na waliogopa.36Ndipo mmoja wao aliyeona kilichotokea alianza kuwasimlia wengine jinsi huyu mtu aliyekuwa anaongozwa na mapepo alivyoponywa.37Watu wote wa mkoa wa Wagerasi na maeneo yaliyozunguka walimwomba Yesu aondoke kwao kwa sababu walikuwa na hofu kuu. Na aliingia kwenye mtumbwi ili arudi.38Mtu yule aliyetokwa na pepo alimsihi Yesu kwenda naye, lakini Yesu alimwambia aende na kusema,39“Rudi kwenye nyumba yako na uhesabu yale yote ambayo Mungu amekutendea.” Huyu mtu aliondoka, akitangaza pote katika mji wote yale yote ambayo Yesu aliyofanya kwa ajili yake.

40Na Yesu akarudi, makutano wakamkaribisha, kwa sababu wote walikuwa wanamngoja.41Tazama akaja mtu mmoja anaitwa Yairo ni mmoja kati ya viongozi katika sinagogi. Yairo akaanguka miguuni pa Yesu na kumsihi aende nyumbani kwake,42kwa sababu alikuwa na mtoto msichana mmoja tu, mwenye umri wa miaka kumi na miwili, na alikuwa katika hali ya kufa. Na alipokuwa akienda, makutano walikuwa wakimsonga.43Mwanamke mwenye kutokwa damu kwa miaka kumi na miwili alikuwa pale na alitumia pesa zote kwa waganga, lakini hakuna aliyemponya hata mmoja,44alikuja nyuma ya yesu na kugusa pindo la vazi lake, na ghafla kutokwa damu kukakoma.45Yesu akasema, “Nani ambaye kanigusa?” Walipokataa wote, Petro akasema, “Bwana Mkubwa, umati wa watu wanakusukuma na wanakusonga.”

46Lakini Yesu akasema, “Mtu mmoja alinigusa, maana nilijua nguvu zimetoka kwangu.”47Mwanamke alipoona ya kuwa hawezi kuficha alichokifanya, akaanza kutetemeka, akaanguka chini mbele za Yesu alitangaza mbele ya watu wote sababu zilizofanya amguse na vile alivyoponywa gafla.48Kisha akasema kwake, “Binti, imani yako imekufanya uwe mzima. Enenda kwa Amani.”

49Alipokuwa akiendelea kusema, mtu mmoja akaja kutoka kwenye nyumba ya kiongozi wa sinagogi, akisema, “Binti yako amefariki. Usimsumbue mwalimu.”

50Lakini Yesu aliposikia hivyo, alimjibu, “Usiogope. Amini tu, naye ataponywa.”51Kisha alipoingia kwenye hiyo nyumba, hakuruhusu mtu yeyote kuingia pamoja naye, isipokuwa Petro, Yohana na Yakobo, baba yake binti, na mama yake.52Sasa watu wote walikuwa wanaomboleza na kutoa sauti kwa ajili yake, lakini akasema, “Msipige kelele, hajafa, lakini amelala tu.”53Lakini wakamcheka kwa dharau, wakijua kuwa amekufa.54Lakini Yeye, akimshika binti mkono, akaita kwa sauti, akisema, “Mtoto, inuka,”55roho yake ikamrudia, na akainuka wakati huohuo. Akaamrisha kwamba, apewe kitu furani ili ale.56Wazazi wake wakashangaa, lakini aliwaamuru wasimwambie mtu kilichokuwa kimetokea.

9

1Akawaita wale kumi na wawili pamoja, akawapa uwezo na mamlaka juu ya mapepo yote na kuponya magonjwa.2Akawatuma waende kuhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.3Akawaambia, “Msichukue chochote kwa ajili ya safari yenu wala fimbo, wala mkoba, wala chakula, wala pesa wala msichukue kanzu mbili.4Na nyumba yoyote mtakayo iingia, kaeni humo mpaka mtakapo ondoka mahali hapo.5Na kwa wale wasio wapokea, mtakapo ondoka mji huo, jikung'uteni vumbi katika miguu yenu kwa ushuhuda juu yao.”6Wakaondoka na kwenda kupitia vijijini, wakitangaza habari njema na kuponya watu kila mahali.

7Sasa Herode, mtawala, alisikia yote yaliyo kuwa yakitokea alitaabika sana, kwa sababu ilisemekana na baadhi kwamba Yohana mbatizaji amefufuka kutoka wafu,8na baathi kwamba Elia amekwisha tokea, na kwa wengine kwamba mmoja wa manabii wa zamani amefufuka katika wafu tena.9Herode alisema, “Nilimchinja Yohana, lakini huyu ni nani ninae sikia habari zake?” Na Herode alitafuta njia ya kumwona Yesu.

10Wakati waliporudi wale waliotumwa, wakamwambia kila kitu walicho fanya. Akawachukua pamoja naye, akaenda peke yake katika mji uitwao Bethsadia.11Lakini makutano wakasikia kuhusu hili wakamfuata, na aliwakaribisha, na akaongea nao kuhusu ufalme wa Mungu, na aliwaponya wale waliohitaji uponyaji.

12Siku ikaanza kuisha, na wale kumi na wawili wakaenda kwake na kusema, “Watawanye makutano kwamba waende katika vijiji vya karibu na mijini wakatafute mapumziko na chakula, kwa sababu tupo eneo la nyikani.”

13Lakini akawaambia, “Nyie wapeni kitu cha kula.” Wakasema, “Hatuna zaidi ya vipande vitano vya mikate na samaki wawili, isipokuwa tungeenda na kununua chakula kwa ajili ya kusanyiko hili la watu.”

14Kulikua na wanaume wapatao elfu tano pale. Akawambia wanafunzi wake. “Wakalisheni chini katika makundi ya watu wapatao hamsini kwa kila kundi.”15Kwa hiyo wakafanya hivyo na watu wa wakaketi chini.16Akachukua mikate mitano na samaki wawili na akatazama mbinguni, akavibariki, na kuvimega katika vipande, akawapa wanafunzi wake ili waviweke mbele ya makutano.17Wote wakala na wakashiba, na vipande vya chakula vilivyo baki viliokotwa na kujaza vikapu kumi na viwili.

18Nayo ikawa kwamba, alipokuwa akiomba peke yake, wanafunzi wake walikuwa pamoja naye, na akawauliza akisema, “Watu husema mimi ni nani?”

19Wakijibu, wakasema, “Yohana mbatizaji, lakini wengine husema Eliya, na wengine husema mmoja wa manabii wa nyakati za zamani amefufuka tena.”

20Akawaambia, “Lakini ninyi mwasema mimi ni nani?” Akijibu Petro akasema, “Kristo kutoka kwa Mungu.”

21Lakini kwa kuwaonya, Yesu akawaelekeza kutomwambia yeyote juu ya hili,22akasema kwamba mwana wa Adamu lazima ateseke kwa mambo mengi na kukataliwa na wazee na Makuhani wakuu na waandishi, na atauawa, na siku ya tatu atafufuka.

23Akawaambia wote, “Kama mtu yeyote akitaka kunifuata, lazima ajikane mwenyewe, achukue msalaba wake kila siku, na anifuate.24Yeyote ajaribuye kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote apotezae maisha yake kwa faida yangu, atayaokoa.25Je itamfaidi nini mwanadamu, kama akiupata ulimwengu wote, lakini akapoteza au akapata hasara ya nafsi yake?26Yeyote atakaye nionea aibu mimi na maneno yangu, kwake yeye Mwana wa Adam atamuonea aibu atakapo kuwa katika utukufu wake, na utukufu wa Baba na malaika watakatifu.27Lakini ninawaambia ukweli, kuna baadhi yenu wasimamao hapa, hawata onja umauti mpaka wauone ufalme wa Mungu.”

28Baada ya maneno hayo yapata siku nane, akawachukua Petro, Yohana na, Yakobo, wakapanda mlimani kuomba.29Na alipokuwa katika kuomba, muonekano wa uso wake ulibadilika, na mavazi yake yakawa meupe na ya kung'aa.30Na tazama, walikuwepo wanaume wawili wakiongea naye! Walikuwa Musa na Elia,31walionekana katika utukufu. Waliongea kuhusu kuondoka kwake, jambo ambalo alikaribia kulitimiza Yerusalem.32Sasa Petro na wale waliokua pamoja naye walikuwa katika usingizi mzito. Lakini walipokuamka, waliuona utukufu wake na wanaume wawili waliokuwa wamesimama pamoja nae.33Ikatokea kwamba, walipokuwa wakiondoka kwa Yesu, Petro akamwambia, “Bwana, ni vizuri kwetu kukaa hapa na inatupasa tutengeneze makazi ya watu watatu. Tutengeneze moja kwa ajili yako, moja kwa ajili ya Musa, na moja kwa ajili ya Eliya.” Hakuelewa alichokuwa akiongelea.34Alipokuwa akisema hayo, likaja wingu na likawafunika; na waliogopa walipoona wamezunguwa na wamezungukwa na wingu.

35Sauti ikatoka kwenye wingu ikasema, “Huyu ni Mwanangu mteule. Msikilizeni yeye.”36Sauti iliponyamaza, Yesu alikuwa peke yake. Walikaa kimya, na katika siku hizo hawakumwambia yeyote lolote miongoni mwa waliyoyaona.

37Siku iliyofuata, baada ya kutoka mlimani, kusanyiko kubwa la watu lilikutana naye.38Tazama, mwanaume kutoka kwenye kusanyiko alilia kwa sauti, akisema, “Mwalimu ninakuomba umtazame mwanangu, kwa kuwa ni mwanangu wa pekee.39Unaona roho chafu humshika, na mara hupiga kelele, na pia humfanya achanganyikiwe na kutokwa povu kinywani. Nayo humtoka kwa shida, ikimsababshia maumivu makali.40Niliwasihi wanafunzi wako wamtoe, lakini hawakuweza.”

41Yesu akajibu akasema, “Enyi kizazi kisichoamini na kilichopotoka, mpaka lini nitakaa nanyi na kuchukuliana nanyi? Mlete mwanao hapa.”42Kijana alipokuwa anakuja, pepo akamuangusha chini na kumtikisa kwa kifafa. Lakini Yesu aliikemea ile roho chafu, alimponya mvulana, na kamkabidhi kwa baba yake.43Wote walishangazwa na ukuu wa Mungu. Lakini walipokuwa wakistaajabu wote kwa mambo yote aliyo yaliyotedeka, akasema kwa wanafunzi wake,44“Maneno yawakae masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu atatolewa mikononi mwa wanadamu.”45Lakini hawakuelewa maana ya maneno hayo, na yalifichwa machoni pao, ili wasije wakalielewa. Waliogopa kumuuliza kuhusu neno hilo.

46Wakaanza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao.47Lakini Yesu alipotambua walichokuwa wakihojiana mioyoni mwao, alimchukua mtoto mdogo, na kumuweka upande wake,48na akasema, “Kama mtu yeyote akimpokea mtoto mdogo kama huyu kwa jina langu, anipokea mimi pia, na yeyote akinipokea mimi, ampokea pia aliyenituma, kwa kuwa aliye mdogo kati yenu wote ndiye alie mkuu.”

49Yohana akajibu akasema, “Bwana, tulimuona mtu akifukuza pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu haambatani na sisi.”

50Lakini Yesu akamwambia, “Msimzuie, kwa kuwa asiye kinyume na ninyi ni wa kwenu.”

51Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye alielekeza uso wake Yerusalemu.52Akatuma wajumbe mbele yake, nao wakaenda na kuingia katika kijiji cha Wasamaria ili wamtayarishie mahali.53Lakini watu huko hawakumpokea, kwa sababu alikua ameelekeza uso wake Yerusalemu.54Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipo liona hili, wakasema, “Bwana unahitaji tuamuru moto ushuke chini kutoka mbinguni uwateketeze?”55Lakini aliwageukia akawakemea.56Kisha walikwenda kijiji kingine.

57Walipokuwa wakienda katika njia yao, mtu mmoja akamwambia, “Nitakufuata popote uendapo.”

58Yesu akamwambia, “Mbweha wanamashimo, ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana pakulaza kichwa chake.”59Ndipo akamwambia mtu mwingine, “Nifuate.” Lakini yeye akasema, “Bwana, niruhusu kwanza niende nikamzika baba yangu,”

60Lakini yeye akamwambia, “Waache wafu wawazike wafu wao, lakini wewe nenda ukautangaze ufalme wa Mungu kila mahali.”

61Pia mtu mwingine akasema. “Nitakufuata, Bwana, lakini niruhusu kwanza nikawaage walio katika nyumba yangu.”

62Lakini Yesu akamwambia, “Hakuna mtu, atiaye mkono wake kulima na kuangalia nyuma atakayefaa kwa ufalme wa Mungu.”

10

1Baada ya mambo hayo, Bwana akachagua sabini wengine, na kuwatuma wawili wawili wamtangulie katika kila mji na eneo alilotarajia kwenda.2Akawaambia, “Mavuno ni mengi, lakini wafanyakazi ni wachache. Hivyo basi muombeni Bwana wa mavuno, ili kwamba atume haraka wafanyakazi katika mavuno yake.3Enendeni katika miji. Angalieni, ninawatuma kama kondoo katikati ya mbwa mwitu.4Msibebe mfuko wa pesa, wala mikoba ya wasafiri, wala viatu, wala msimsalimie yeyote njiani.5Katika nyumba yeyote mtakayo ingia, kwanza semeni, ‘Amani iwe katika nyumba hii.’6Kama mtu wa amani yupo pale, amani yenu itabaki juu yake, lakini kama sivyo, itarudi kwenu.7Bakini katika nyumba hiyo, kuleni na mnywe watakachokitoa, kwa maana mfanyakazi anastahili mshahara wake. Msihame kutoka nyumba hii kwenda nyingine.8Mji wowote muuingiao, na wakawapokea, kuleni chochote kitakachowekwa mbele yenu,9na ponyeni wagonjwa waliomo humo. Semeni kwao, ‘Ufalme wa Mungu umewakaribia.’10Lakini katika mji wowote mtakaoingia, na wasiwapokee, nendeni nje katika barabara na semeni,11‘Hata vumbi katika mji wenu lililonata miguu mwetu tunalikung'uta dhidi yenu! Lakini tambueni hili, Ufalme wa Mungu umekaribia.’12Ninawambieni kwamba siku ya hukumu itakuwa ni usitahimilivu zaidi kwa Sodoma kuliko mji huo.

13Ole kwako Korazini, Ole kwako Bethsaida! Kama kazi kuu zilizo fanyika ndani yako ingalifanyika Tiro na Sidoni, wangelitubu zamani sana, wakikaa ndani ya nguo za gunia na majivu.14Lakini itakuwa usitahimilivu zaidi siku ya hukumu kwa Tiro na Sidoni zaidi yenu.15Wewe Kapernaumu, unafikiri utainuliwa mpaka Mbinguni? Hapana, utashushwa chini mpaka kuzimu.

16Atakaye wasikiliza ninyi anisikiliza mimi, na yeyote atakaye wakataa anikataa mimi, na yeyote anikataaye mimi amtakaa aliyenituma.”

17Wale sabini walirud i kwa furaha, wakisema, “Bwana, hata mapepo wanatutii katika jina lako.”18Yesu akawaambia, “Nilimwona Shetani akianguka kutoka mbinguni kama radi.19Tazama, nimewapa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za adui, na hapana chochote kwa njia yoyote kitakachowadhuru.20Hata hivyo msifurahi tu katika hili, kwamba roho zinawatii, lakini furahini zaidi kwamba majina yenu yameandikwa mbinguni.”

21Katika mda uleule alifurahi sana katika Roho Mtakatifu, na kusema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbingu na dunia, kwa sababu umeyaficha mambo haya kutoka kwa wenye hekima na akili, na kuyafunua kwa wasio fundishwa, kama watoto wadogo. Ndio, Baba, kwa kuwa ilipendeza katika machoni pako.”22“Kila kitu kimekabidhiwa kwangu na Baba yangu, na hakuna afahamuye Mwana ni nani ila Baba, na hakuna afahamuye Baba ni nani ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana hutamani kujifunua kwake.”

23Akawageukia wanafunzi, akasema faraghani, “Wamebarikiwa wayaonayo haya ambayo ninyi mnayaona.24Ninawaambia ninyi, kwamba manabii wengi na wafalme walitamani kuona mambo myaonayo, na hawakuyaona, na kusikia kusikia mnayoyaikia, na hawakuyasikia.”

25Tazama, mwalimu fulani wa sheria ya Kiyahudi alisimama na kumjaribu, akisema, “Mwalimu, nifanye nini niurithi uzima wa milele?”

26Yesu akamwambia, “Kimeandikwa nini katika sheria? Unaisoma je?”

27Akajibu akasema, “Utampenda Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho yako yote, kwa nguvu zako zote, na kwa akili zako zote, na jirani yako kama nafsi yako mwenyewe.”

28Yesu akasema, “Umejibu kwa usahihi. Fanya hivi na utaishi.”

29Lakini mwalimu, akitamani kujihesabia haki mwenyewe, akamwambia Yesu, “Na jirani yangu ni nani?”

30Yesu akijibu akasema, “Mtu fulani alikuwa akitelemka kutoka Yerusalem kwenda Yeriko. Akaangukia kati ya wanyang'anyi, waliomnyang'anya mali yake, na kumpiga na kumuacha karibu ya kufa.31Kwa bahati kuhani fulani alikuwa akishuka katika njia hiyo, alipo muona alipita upande mwingine.32Vivyo hivyo Mlawi pia, alipofika mahali pale na kumuona, akapita upande mwingine.33Lakini Msamaria mmoja, alipokuwa akisafiri, alipita pale alipokuwa mtu huyo. Alipomuona, alisukumwa kwa huruma.34Alimkaribia na kumfunga vidonda vyake, akimwiga mafuta na divai juu yake. Alimpandisha juu ya mnyama wake, na kumpeleka katika nyumba ya wageni na kumhudumia.35Siku ilyofuata alichukua dinari mbili, na akampatia mmiliki wa nyumba ya wageni na kumwambia, ‘Muhudumie na chochote cha ziada utakacho tumia, nitakulipa nitakaporudi.’36Ni yupi kati ya hawa watatu, unafikiri, alikuwa ni jirani kwake yeye aliyeangukia kati ya wanyang'anyi?”

37Mwalimu alisema, “Ni yule aliyeonesha huruma kwake.” Yesu akamwambia, “Nenda na ukafanye vivyo hivyo”

38Ikawa walipokuwa wakisafiri, waliingia katika kijiji fulani, na mwanamke mmoja jina lake Martha alimkaribisha nyumbani kwake.39Alikuwa na dada aliyeitwa Mariamu, aliekaa miguuni pa Bwana na kusikiliza neno lake.40Lakini Martha alijipa shughuli nyingi za kuandaa mlo. Alikwenda kwa Yesu, na kusema, “Bwana, haujali kwamba dada yangu ameniacha nihudumu peke yangu? Hivyo basi mwambie anisaidie.”

41Lakini Bwana alimjibu na kumwambia, “Martha, Martha, una sumbuka juu ya mambo mengi,42lakini ni kitu kimoja tu cha muhimu. Mariamu amechagua kilicho chema, ambacho hakitaondolewa kutoka kwake.”

11

1Ilitokea wakati Yesu alipokuwa anaomba mahali fulani, mmoja wa mwanafunzi wake alimwambia, “Bwana, tufundishe sisi kuomba kama Yohana alivyo wafundisha wanafunzi wake.”

2Yesu akawaambia, Msalipo, semeni, “Baba, Jina lako litakazwe. Ufalme wako uje.3Utupe mkate wetu wa kila siku.4Utusamehe makosa yetu, kama nasi tunavyowasamehe wote waliotukosea. Usituongoze katika majaribu.”

5Yesu akawaambia, “Ni nani kwenu atakuwa na rafiki, ambaye atamuendea usiku, na kumwambia, ‘Rafiki niazime mikate mitatu.6Kwa sababu rafiki yangu amenijia sasa hivi kutoka safarini, nami sina cha kumuandalia.’

7Na yule aliyeko ndani akamjibu, ‘Usinitaabishe, mlango umekwisha kufungwa, na watoto wangu, pamoja nami tumekwisha kulala kitandani. Siwezi kuamka na kukupa wewe mikate.’8Nawaambia, japo kuwa haamki na kukupatia mikate kama rafiki yake, kwa sababu ya kuendelea kumgongea bila aibu, ataamka na kukupatia vipande vingi vya mikate kulingana na mahitaji yako.9Nami pia nawaambieni, ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtapata, pigeni hodi nanyi mtafunguliwa.10Kwa kuwa kila mtu aombaye atapokea, na kila mtu atafutaye atapata, na kila mtu apigaye hodi, mlango utafunguliwa kwake.11Ni baba yupi miongoni mwenu, mwanaye akimuomba samaki atampa nyoka badala yake?12Au akimuomba yai atampa nge?13Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajuwa kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, je si zaidi sana Baba yenu wa mbinguni kwamba atawapa Roho Mtakatifu hao wamuombao?”

14Baadaye, Yesu akawa anakemea pepo, na mtu mwenye pepo alikuwa bubu. Ikawa pepo lilipomtoka, mtu huyo aliweza kuongea. Umati wakastaajabu sana.15Lakini watu wengine wakasema, huyu anatoa mapepo kwa Beelzebul, mkuu wa mapepo.16Wengine walimjaribu na kumtaka awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.

17Lakini Yesu aliyatambua mawazo yao na kuwaambia, “Kila ufalme utakaogawanyika itakuwa ukiwa, na nyumba iliyo gawanyika itaanguka.18Kama Shetani atakuwa amegawanyika, ufalme wake utasimamaje? Kwa sababu mwasema natoa mapepo kwa Belzebuli19Kama mimi natoa mapepo kwa Belzebuli, je wenzenu wanatoa mapepo kwa njia gani? Kwa sababu hii, wao watawahukumu ninyi.20Lakini, kama natoa mapepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umewajia.

21Mtu mwenye nguvu aliye na silaha akilinda nyumba yake, vitu vyake vitakaa salama.22Lakini akivamiwa na mtu mwenye nguvu zaidi, Yule mtu mwenye nguvu atamnyang'anya silaha zake, na kuzichukua mali zake zote.23Yeye asiye pamoja nami yuko kinyume nami, na yeye asiyekusanya pamoja nami hutapanya.

24Pepo mchafu amtokapo mtu, huenda na kutafuta mahali pasipo na maji ili ajipumzishe. Atakapokuwa amekosa, husema, ‘Nitarudi nilipotoka.’25Akirudi na kukuta nyumba imefagiliwa na imekaa vizuri.26Hivyo huenda na kutafuta mapepo saba walio waovu kuliko yeye mwenyewe na kuwaleta waje wakae mahali pale. Na hali ya mtu huyo huwa mbaya kuliko ilivyokuwa mara ya kwanza.”

27Ilitokea kwamba alipokuwa akisema maneno hayo, mwanamke fulani alipaza sauti yake zaidi ya wote kwenye mkutano wa watu na kusema “Limebarikiwa tumbo lililo kuzaa na matiti uliyoyanyonya.”28Lakini yeye akasema, “Wamebarikiwa wale wasikio neno la Mungu na kulitunza.”

29Wakati umati wa watu wanakusanyika na kuongezeka, Yesu akaanza kusema, “Kizazi hiki ni kizazi cha uovu. Hutafuta ishara, na hakuna ishara watayopewa zaidi ya ile ishara ya Yona.30Maana kama Yona alivyokuwa ishara kwa watu wa Ninawi, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa ishara kwa kizazi hiki31Malkia wa Kusini atasimama siku ya hukumu na watu wa kizazi hiki na kuwahukumu wao, kwani yeye alitoka katika mwisho wa nchi ili aje asikilize hekima za Solomoni, na hapa yuko aliye mkuu kuliko Solomoni.32Watu wa Ninawi watasimama katika hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki siku ya hukumu watakihukumu, kwani wao walitubu kwa mahubiri ya Yona, na tazama, hapa yuko aliye mkuu kuliko Yona.

33Hakuna Mtu yeyote, awashaye taa na kuiweka sehemu ya chini yenye giza isiyoonekana au chini ya kikapu, ila huwasha na kuweka juu ya kitu ili kila mtu aingiaye aweze kuona mwanga.34Jicho lako ni taa ya mwili. Jicho lako likiwa zuri basi mwili wako wote utakuwa kwenye mwanga. Lakini jicho lako likiwa baya basi mwili wako wote utakuwa kwenye giza.35Kwa hiyo, mjihadhari ili mwanga ulio ndani yenu usitiwe giza.36Hivyo basi, kama mwili wako wote uko kwenye mwanga, na hakuna sehemu iliyo katika giza, basi mwili wako utakuwa sawa na taa iwakayo na kutoa mwanga kwenu.”

37Alipomaliza kuongea, Farisayo alimwalika akale chakula nyumbani kwake, naye Yesu akaingia ndani na kuwa pamoja nao.38Na Mafarisayo wakashangaa kwa jinsi ambavyo hakunawa kwanza kabla ya chakula cha jioni.39Lakini Bwana akawaambia, “Ninyi Mafarisayo mnaosha nje ya vikombe na bakuli, lakini ndani yenu mmejaa tamaa na uovu.40Ninyi watu msio na ufahamu, Je yeye aliyeumba nje hakuumba na ndani pia?41Wapeni masikini yaliyo ndani, na mambo yote yatakuwa safi kwenu.

42Lakini ole wenu Mafarisayo, kwani mnatoa zaka ya mnanaa na mchicha na kila aina ya mboga ya bustani. Lakini mmeacha mambo ya haki na kumpenda Mungu. Ni muhimu zaidi kufanya yaliyo ya haki na kumpenda Mungu, bila kuacha kufanya na hayo mengine pia.43Ole wenu Mafarisayo, kwa kuwa mnapenda kukaa katika viti vya mbele kwenye masinagogi na kuamkiwa kwa salamu za heshima sokoni.44Ole wenu, kwani mnafanana na makaburi yasiyo na alama ambayo watu hutembea juu yake pasipokujua.”

45Mwalimu mmoja wa sheria za Kiyahudi akamjibu na kumwambia, “Mwalimu, unachokisema kinatuudhi pia sisi.”

46Yesu akasema, “Ole wenu, waalimu wa sheria! Kwani mnawapa watu mizigo mikubwa wasiyoweza kuibeba, walakini ninyi hamgusi mizigo hiyo hata kwa moja ya vidole vyenu.47Ole wenu, kwa sababu mnajenga na kuweka kumbukumbu kwenye makaburi ya manabii’ ambao waliuwawa na mababu zenu.48Hivyo ninyi mwashuhudia na kukubaliana na kazi walizozifanya mababu zenu, kwa sababu hakika waliwauwa manabii ambao mnajenga kumbukumbu katika makaburi yao.49Kwa sababu hiyo pia, hekima ya Mungu inasema, ‘Nitawatumia manabii na mitume nao watawatesa na kuwaua baadhi yao.50Kizazi hiki kitawajibika kwa damu ya manabii waliouawa tangu kuanza kwa dunia,51Kutoka damu ya Abeli hadi damu ya Zakaria, aliyeuawa katikati ya madhabahu na patakatifu. Ndiyo, nawaambia ninyi, kizazi hiki kitawajibika.52Ole wenu waalimu wa sheria za Kiyahudi, kwa sababu mmechukua funguo za ufahamu; nyie wenyewe hamuingii, na wale wanaotaka kuingia mnawazuia.”

53Baada ya Yesu kuondoka pale, waandishi na mafarisayo walimpinga na kubishana naye juu ya mambo mengi,54wakimvizia, ili wapate neno litokalo kinywani mwake.

12

1Kwa wakati huo, maelfu mengi ya watu walikusanyika pamoja, kiasi cha kuanza kukanyagana, akaanza kusema na wanafunzi wake kwanza, “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo ambayo ni unafiki.2Na hapatakuwepo na siri iliyofichika ambayo haitafunuliwa, wala jambo lililofichwa ambalo halitajulikana.3Na lolote mlilolisema katika giza, litasikiwa katika mwanga. Na yoyote mliyoyasema kwenye sikio ndani ya vyumba vyenu vya ndani vilivyofungwa yatatangazwa juu ya paa la nyumba.

4Nawaambieni rafiki zangu, msiwaogope wale wauao mwili na kisha hawana kitu kingine cha kufanya,5Lakini nitawaonya mtakaye mwogopa. Mwogopeni yule ambaye baada ya kuwa ameua, ana mamlaka ya kutupa jehanamu. Ndiyo, nawaambiani ninyi, mwogopeni huyo.6Je shomoro watano hawauzwi kwa sarafu mbili? Hata hivyo hakuna hata mmoja wao atakayesahaulika mbele za Mungu.7Lakini mjue kuwa, nywele za vichwa vyenu vimehesabiwa. Msiogope. Ninyi ni wa thamani kubwa kuliko shomoro wengi.

8Ninawaambia, yeyote atakayenikiri Mimi mbele za watu, Mwana wa Adamu atamkiri mbele za malaika wa Mungu.9Lakini yeyeyote atakayenikana mbele za watu naye atakanwa mbele ya Malaika wa Mungu.10Yeyote atakayesema neno baya juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, lakini yeyote atakayemkufuru Roho Mtakatifu, hatasamehewa.11Watakapowapeleka mbele za wakuu wa masinagogi, watawala, na wenye mamlaka, msiogope juu na namna ya kuongea katika kujitetea au nini mtakachosema,12kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha namna mtakavyosema kwa wakati huo.”

13Mtu mmoja katika kusanyiko akamwambia, “Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie sehemu ya uruthi wangu.”

14Yesu akamjibu, “Ni nani aliye niweka kuwa mwamuzi na mpatanishi kati yenu?”15Ndipo akawaambia, “Jihadharini na kila namna ya tamaa, kwa sababu uzima wa mtu hauko katika wingi wa vitu alivyo navyo.”

16Yesu akawaambia mfano, akisema, “Shamba la mtu mmoja tajiri lilizaa sana,17na akajiuliza ndani yake, akisema, ‘Nitafanyaje kwani sina mahali pa kuhifadhi mazao yangu?’18Akasema, ‘Nitafanya hivi. Nitavunja ghala zangu ndogo na kujenga iliyo kubwa, na kuyahifadhi mazao yangu yote na vitu vingine.19Nitaiambia nafsi yangu, ‘Nafsi, umejiwekea akiba ya vitu vingi kwa miaka mingi. Pumzika, ule, unywe na kustarehe.”

20Lakini Mungu akamwambia, ‘Ewe mtu mpumbavu, usiku wa leo wanahitaji roho kutoka kwako, na vitu vyote ulivyoviandaa vitakuwa vya nini?’

21Ndivyo itakavyokuwa kwa kila mtu anayejiwekea mali na si kujitajirisha kwa ajili ya Bwana.”

22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa hiyo nawaambia msihofu juu ya maisha yenu__ya kuwa mtakula nini au juu ya miili yenu __ya kuwa mtavaa nini23Kwa kuwa maisha ni zaidi ya chakula, na mwili ni zaidi ya mavazi.24Angalieni ndege wa angani, hawalimi wala hawavuni. Hawana chumba wala ghala ya kuhifadhia, lakini Baba yenu huwalisha. Ninyi si bora zaidi kuliko ndege!25Ni yupi kati yenu ambaye akijisumbua ataweza kuongeza dhiraa moja katika maisha yake?26Ikiwa basi hamuwezi kufanya hicho kitu kidogo kilicho rahisi kwa nini basi kusumbukia hayo mengine?27Tafakarini jinsi maua yanavyomea. Hayafanyi kazi wala hayasokoti. Lakini nawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya,28Kama Mungu huyavika vizuri majani ya kondeni, ambayo leo yapo, na kesho hutupwa kwenye moto. Je si zaidi atawavika ninyi? Enyi wa imani haba!29Msisumbukie juu ya kuwa mtakula nini au mtakunywa nini, wala msiwe na hofu.30Kwa kuwa Mataifa yote ya dunia husumbukia mambao yao. Na Baba yenu anajua ya kuwa mnahitaji hayo.31Lakini tafuteni ufalme wake kwanza, na hayo mengine mtazidishiwa,32msiogope, enyi kundi dogo, kwa sababu Baba yenu anafurahia kuwapa ninyi huo ufalme.33Uzeni mali zenu na mkawape maskini, mjifanyie mifuko isiyoishiwa, hazina ya mbinguni isiyokoma, sehemu ambapo wezi hawatakaribia wala nondo haitaweza kuharibu.34Kwa kuwa palipo na hazina yako, ndipo na roho yako itakapokuwepo.

35Nguo zenu ndefu ziwe zimefungwa kwa mkanda, na taa zenu zihakikishwe kuwa zinaendelee kuwaka,36na muwe kama watu wanaomtazamia Bwana wao kutoka kwenye sherehe ya harusi, ili kwamba akija na kupiga hodi, wataweze kumfungulia mlango kwa haraka.37Wamebarikiwa wale watumishi, ambao Bwana atawakuta wako macho. Hakika atafunga nguo yake ndefu kwa mkanda, kisha atawaketisha chini kwa chakula, na kisha kuwahudumia.38Kama Bwana atakuja kwa zamu ya pili ya ulinzi ya usiku, au hata zamu ya tatu ya ulinzi, na kuwakuta wakiwa tayari, itakuwa ni heri kwa hao watumishi.39Lakini fahamuni neno hili, kama bwana mwenye nyumba angelijua saa ambayo mwivi anakuja, asingeliruhusu nyumba yake ifunjwe.40Iweni tayari pia kwani hamjui ni wakati gani mwana wa Adamu atarudi.

41Petro akasema, “Bwana, watuambia sisi wenyewe hii mifano, au unamwambia kila mtu?”

42Bwana akawaambia, “Ni nani mtumwa mwaminifu au mwenye hekima ambaye bwana wake atamweka juu ya watumishi wengine, ili awagawie chakula chao kwa wakati mwafaka?43Amebarikiwa mtumishi yule, ambaye bwana wake akija atamkuta akifanya yale aliyoagizwa.44Hakika nawaambia ninyi ya kuwa atamweka juu ya mali yake yote.45Lakini Mtumishi yule akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anachelewa kurudi;’ hivyo akaanza kuwapiga wale watumishi wa kiume na wa kike, kisha akaanza kula, kunywa na kulewa,46bwana wake yule mtumwa atakuja katika siku asiyotegemea na saa asiyoijua, naye atamkata vipande vipande na kumuweka katika sehemu pamoja na wasiokuwawaaminifu.47Mtumishi, anayejua mapenzi ya bwana wake, naye hakujiandaaa wala hakufanya sawa sawa na mapenzi yake, atapigwa viboko vingi.48Lakini mtumishi asiyejua mapenzi ya bwana wake, lakini akafanya yanayostahili adhabu, atapigwa viboko vichache. Kwa kuwa yeye aliyepewa vingi, vingi hudaiwa kutoka kwake, na yeye aliyeaminiwa kwa vingi, kwake vitadaiwa vingi zaidi.

49Nimekuja kuwasha moto duniani, na natamani iwe umekwishawaka.50Lakini nina ubatizo ambao nitabatizwa, na nina huzuni mpaka utakapokamilika!51Je mnafikiri kuwa nimekuja kuleta amani duniani? Hapana, nawaambieni, badala yake nimeleta mgawanyiko.52Tangu sasa na kuendelea kutakuwa na watu watano katika nyumba moja wamegawanyika, na watatu watakuwa kinyume na wawili, na wawili watakuwa kinyume na watatu.53Watagawanyika, baba atakuwa kinyume na mwanae, na mwanae atakuwa kinyume na babaye, mama atakuwa kinyume na binti yake, na binti atakuwa kinyume na mama yake, Mama mkwe atakuwa kinyume na mkwe wake naye mkwe atakuwa kinyume na mama mkwe wake.”

54Yesu akawa anawaambia makutano pia, “Mara muonapo mawingu yakitokea magharibi, mnasema, ‘Nyakati za mvua zimewadia,’ na ndivyo inavyo kuwa,55Na upepo wa kusini ukivuma, mnasema, ‘Patakuwepo na joto kali,’ na ndivyo inavyokuwa.56Enyi wanafiki, mnaweza kutafsiri mwonekano wa nchi na anga, lakini inakuwaje hamuwezi kuutafsiri wakati uliopo?

57Ni kwa nini kila mmoja wenu asipambanue lililo sahihi kwake kulifanya wakati ambapo angali na nafasi ya kufanya hivyo?58Maana mkienda na mshitaki wako mbele ya hakimu, jitahidi kupatana na mshitaki wako mungali bado mko njiani asije akakupeleka kwa hakimu, na hakimu akupeleka kwa ofisa, na ofisa akakutupa gerezani.59Nakuambia, hutatoka huko hadi umelipa mpaka senti ya mwisho.”

13

1Wakati huo huo, kulikuwa na baadhi watu waliomtaarifu juu ya Wagalilaya ambao Pilato aliwaua na kuchanganya damu yao na sadaka zao.2Yesu akajibu na kuwaambia, “Je mwadhani kuwa Wagalilaya hao walikuwa na dhambi kuliko Wagalilaya wengine wote ndiyo maana wamepatwa na mabaya hayo?3Hapana, nawaambia, lakini msipotubu, nanyi mtaangamia vivyo hivyo.4Au wale watu kumi na nane katika Siloamu ambao mnara ulianguka na kuwaua, mnafikiri wao walikuwa wenye dhambi zaidi kuliko watu wengine katika Yerusalemu?5Hapana, mimi nasema, lakini kama msipotubu, ninyi nyote pia mtaangamia.

6Yesu aliwaambia mfano huu, “Mtu mmoja alikuwa na mtini umepandwa katika shamba lake na alikwenda kutafuta matunda juu yake lakini hakupata.7Akamwambia mtunza bustani, ‘Tazama, kwa miaka mitatu nimekuja na kujaribu kutafuta matunda kwenye mtini huu lakini sikupata. Uukate. Kwani unaleta uharibifu wa ardhi?’

8Mtunza bustani akajibu na kusema, ‘Uache mwaka huu ili niupalilie na kuweka mbolea juu yake.9Kama ukizaa matunda mwaka ujao, ni vema; lakini kama hautazaa, uukate!”’

10Sasa Yesu alikuwa akifundisha katika mojawapo ya Masinagogi wakati wa Sabato11Tazama, alikuwepo mama mmoja ambaye kwa miaka kumi na minane alikuwa na roho mchafu wa udhaifu, na yeye alikuwa amepinda na hana uwezo kabisa wa kusimama.12Yesu alipomwona, alimwita, akamwambia, “Mama, umewekwa huru kutoka kwenye udhaifu wako.”13Akaweka mikono yake juu yake, na mara mwili wake akajinyoosha na akamtukuza Mungu.

14Lakini mkuu wa sinagogi alikasirika kwa sababu Yesu alikuwa amemponya siku ya Sabato. Hivyo mtawala akajibu akawambia makutano, “Kuna siku sita ambazo ni lazima kufanya kazi. Njoni kuponywa basi, si katika siku ya Sabato.”

15Bwana akamjibu na akasema, “Wanafiki! Hakuna kila mmoja wenu kufungua punda wako au ng'ombe kutoka zizini na kuwaongoza kumpeleka kunywa siku ya Sabato?16Hivyo pia binti wa Abrahamu, ambaye Shetani amemfunga kwa miaka kumi na minane, je haikumpasa kifungo chake kisifunguliwe siku ya sabato?”17Alipokuwa akisema maneno hayo, wale wote waliompinga waliona aibu, bali makutano wote wa wengine walishangilia kwa ajili ya mambo ya ajabu aliyotenda.

18Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na nini, na naweza kuulinganisha na nini?19Ni kama mbegu ya haradari aliyoitwaa mtu mmoja na kuipanda shambani mwake, na ikamea ikawa mti mkubwa, na ndege wa mbinguni wakajenga viota vyao katika matawi yake.

20Tena akasema, “Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?21Ni kama chachu ambayo mwanamke aliichukua na kuchanganya kwenye vipimo vitatu vya unga hata ukaumuka.”

22Yesu alitembelea kila mji na kijiji njiani akielekea Yerusalemu na kuwafundisha.23Mtu mmoja akauliza, “Bwana, ni watu wachache tu watakaookolewa?” Hivyo akawaambia,24“Jitahidi kuingia kwa kupitia mlango mwembamba, kwa sababu wengi watajaribu na hawataweza kuingia.25Mara baada ya mmiliki wa nyumba kusimama na kufunga mlango, basi mtasimama nje na kupiga hodi mlangoni na kusema, ‘Bwana, Bwana, tufungulie,’ yeye atajibu na kuwaambia, ‘Siwajui ninyi wala mtokako.’

26Ndipo mtasema, ‘Tulikula na kunywa mbele yako na wewe ulifundisha katika mitaa yetu.’

27Lakini yeye atawajibu, ‘Nawaambia, siwajui mtokako, ondokeni kwangu, ninyi watenda maovu!’28Kutakuwa na kilio na kusaga meno wakati mtakapowaona Abrahamu, Isaka, Yakobo na manabii wote katika ufalme wa Mungu, lakini ninyi wenyewe mmetupwa nje.29Watafika kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, na kupumzika katika meza ya chakula cha jioni katika ufalme wa Mungu.30Na tambua hili, wa mwisho ni wa kwanza na wa kwanza atakuwa wa mwisho.”

31Muda mfupi baadaye, baadhi ya Mafarisayo walikuja na kumwambia, “Nenda na ondoka hapa kwa sababu Herode anataka kukuua.”

32Yesu akasema, “Nendeni mkamwambie yule mbweha, ‘Tazama, ninawafukuza pepo na kufanya uponyaji leo na kesho, na siku ya tatu nitatimiza lengo langu.33Katika hali yoyote, ni muhimu kwa ajili yangu kuendelea leo, kesho, na siku iliyofuata, kwa vile haikubaliki kumuua nabii mbali na Yerusalemu.

34Yerusalemu, Yerusalemu, nani anawaua manabii na kuwapiga mawe wale waliotumwa kwenu. Mara ngapi nimetaka kuwakusanya watoto wenu kama vile kuku anavyokusanya vifaranga vyake chini ya mbawa zake, lakini humkulitaka hili.35Tazama, nyumba yako imetelekezwa. Nami nawaambia, hamuwezi kuniona hata mtakaposema ‘Amebarikiwa huyo ajaye kwa jina la Bwana.’”

14

1Ilitokea siku ya Sabato, alipokua akienda nyumbani kwa mmoja wa viongozi wa Mafarisayo kula mkate, nao walikuwa wakimchunguza kwa karibu.2Tazama, pale mbele yake alikuwa mtu ambaye anasumbuliwa na uvimbe.3Yesu aliuliza wataalam katika sheria ya Wayahudi na Mafarisayo, “Je, ni halali kumponya siku ya Sabato, au sivyo?”4Lakini wao walikuwa kimya, kwa hiyo Yesu akamshika, akamponya na kumruhusu aende zake.5Naye akawaambia, “Ni nani kati yenu ambaye ana mtoto au ng'ombe ametumbukia kisimani siku ya Sabato hata mvuta nje mara moja?”6Wao hawakuwa na uwezo wa kutoa jibu kwa mambo haya.

7Wakati Yesu alipogundua jinsi wale walioalikwa kwamba wamechagua viti vya heshima, akawaambia mfano, akiwaambia,8“Wakati mnapoalikwa na mtu harusini, usiketia nafasi za heshima, kwa sababu inawezekana amealikwa mtu ambaye ni wakuheshimiwa zaidi kuliko wewe.9Wakati mtu aliyewaalika ninyi wawili akifika, atakuambia wewe, “Mpishe mtu huyu nafasi yako,” na kisha kwa aibu utaanza kuchukua nafasi ya mwisho.10Lakini wewe ukialikwa, nenda ukakae mahali pa mwisho, ili wakati yule aliyekualika akija, aweze kukuambia wewe, ‘Rafiki, nenda mbele zaidi.’ Ndipo utakuwa umeheshimika mbele ya wote walioketi pamoja nawe mezani.11Kwa maana kila ajikwezaye atashushwa, na yeye ajishushae atakwezwa.”

12Yesu pia alimwambia mtu aliyemwalika, “Unapotoa chakula cha mchana au cha jioni, usiwaalike rafiki zako au ndugu zako au jamaa zako au majirani zako matajiri, ili kwamba wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo.13Badala yake, unapofanya sherehe, waalike maskini, vilema, viwete na vipofu,14na wewe utabarikiwa, kwa sababu hawawezi kukulipa. Kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.”

15Wakati mmoja wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu aliposikia hayo, naye akamwaambia, “Amebarikiwe yule atakayekula mkate katika Ufalme wa Mungu!”

16Lakini Yesu akamwaambia, “Mtu mmoja aliandaa sherehe kubwa, akaalika watu wengi.17Wakati sherehe ilipokuwa tayari, alimtuma mtumishi wake kuwaambia wale walioalikwa, ‘Njooni, kwa sababu vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari.’

18Wote, wakaanza kuomba radhi. Wa kwanza akamwambia mtumishi, ‘Nimenunua shamba, lazima niende kuliona. Tafadhali unisamehe.’

19Na mwingine akasema, ‘Nimenunua jozi tano za ng'ombe, na mimi naenda kuwajaribu. Tafadhali uniwie radhi.’

20Na mtu mwingine akasema, ‘Nimeoa mke, kwa hiyo siwezi kuja.’

21Mtumishi akarudi na kumwambia bwana wake mambo hayo. Yule mwenye nyumba alikasirika akamwambia mtumishi wake, ‘Nenda upesi mitaani na katika vichochoro vya mji ukawalete hapa maskini, vilema, vipofu na walemavu.’

22Mtumishi akasema, ‘Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, na hata sasa bado kuna nafasi.’

23Bwana akamwambia mtumishi, ‘Nenda katika njia kuu na vichochoro na uwashurutishe watu waingie, ili nyumba yangu ijae.’24Kwa maana nawaambia, katika wale walioalikwa wa kwanza hapana atakayeonja sherehe yangu.”

25Sasa umati mkubwa walikuwa wanakwenda pamoja naye, naye akageuka na akawaambia,26“Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, mama yake, mke wake, watoto wake, ndugu zake waume na wanawake- ndio, na hata maisha yake pia -hawezi kuwa mwanafunzi wangu.27Mtu asipochukua msalaba wake na kuja nyuma yangu hawezi kuwa mwanafunzi wangu.28Maana ni nani kati yenu, ambaye anatamani kujenga mnara hataketi kwanza akadirie gharama kwa mahesabu kama ana kile anachohitaji ili kukamilisha hilo?29Vinginevyo, baada ya kuweka msingi na kushindwa kumaliza, wote walioona wataanza kumdhihaki,30wakisema, ‘Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza.’

31Au mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine katika vita, ambae hatakaa chini kwanza na kuchukua ushauri kuhusu kama ataweza, pamoja na watu elfu kumi kupigana na mfalme mwingine anayekuja juu yake na watu elfu ishirini?32Na kama sivyo, wakati jeshi la wengine bado liko mbali, hutuma balozi kutaka masharti ya amani.33Kwa hiyo basi, yeyote kati yenu ambaye hataacha vyote alivyo navyo, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

34Chumvi ni nzuri, lakini ikiwa Chumvi imepoteza ladha yake, jinsi gani inaweza kuwa chumvi tena?35Haina matumizi kwa udongo au hata kwa mbolea. Hutupwa mbali. Yeye aliye na masikio ya kusikia, na asikie.”

15

1Basi watoza ushuru wote na wengine wenye dhambi walikuja kwa Yesu na kumsikiliza.2Mafarisayo wote na waandishi wakanung'unika wakisema, “Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi na hata hula nao.”

3Yesu akasema mfano huu kwao, akisema4“Nani kwenu, kama ana kondoo mia moja na akipotelewa na mmoja wao, hatawaacha wale tisini na tisa nyikani, na aende akamtafute yule aliyepotea hadi amwone?5Naye akisha kumpata humweka mabegani pake na kufurahia.6Afikapo kwenye nyumba, huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia ‘Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimempata kondoo wangu aliyepotea.’7Nawaambia vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, zaidi ya wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.

8Au kuna mwanamke gani mwenye sarafu kumi za fedha, akipotewa na sarafua moja, hata washa taa na kufagia nyumba na kutafuta kwa bidii hadi atakapoipata?9Na akiisha kuiona huwaita rafiki zake na jirani zake akawaambia ‘Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena sarafu yangu niliyokua nimeipoteza.’10Hata hivyo nawaambia kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.”

11Na Yesu akasema, “Mtu mmoja alikua na wana wawili12yule mdogo akamwambia babaye, ‘Baba nipe sehemu ya mali inayonistali kuirithi.’ Hivyo akagawanya mali zake kati yao.13Siku si nyingi yule mdogo akakusanya vyote anavyomiliki akaenda nchi ya mbali, na huko akatapanya hela zake, kwa kununua vitu asivyo vihitaji, na kutapanya fedha zake kwa anasa.14Nae alipokua amekwisha tumia vyote njaa kuu iliingia nchi ile naye akaanza kuwa katika uhitaji.15Akaenda na kujiajiri mwenyewe kwa mmoja wa raia wa nchi ile, naye alimpeleka shambani kwake kulisha nguruwe.16Na akawa akitamani kujishibisha kwa maganda waliyokula nguruwe kwa sababu hakuna mtu aliempa kitu chochote apate kula.17Ila yule mwana mdogo alipozingatia moyoni mwake, alisema ‘Ni watumishi wangapi wa baba yangu wanachakula kingi cha kutosha na mimi niko hapa, ninakufa na njaa!18Nitaondoka na kwenda kwa baba yangu, na kumwambia, ‘Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako.19Sistahili kuitwa mwana wako tena; nifanye kama mmoja wa watumishi wako.”20Ndipo akaondoka akaenda kwa baba yake. Alipokua angali mbali baba yake alimuona akamwonea huruma akaenda mbio na kumkumbatia na kumbusu.21Yule mwana akamwambia, ‘Baba nimekosa juu ya mbingu na mbele ya macho yako sistahili kuitwa mwana wako.’

22Yule baba aliwaambia watumishi wake, ‘Lileteni upesi vazi lililo bora, mkamvike mtieni na pete kidoleni na viatu miguuni.23Kisha mleteni ndama yule alienona mkamchinje tule na kufurai.24Kwa kuwa mwanangu alikua amekufa naye yu hai. Alikua amepotea nae ameonekana,’ wakaanza kushangilia.

25Basi yule mwanae mkubwa alikuwako shamba. Alipokuwa akija na kuikaribia nyumba alisikia sauti ya nyimbo na michezo.26Akaita mtumishi mmoja akamuuliza, ‘Mambo haya maana yake nini?’27Mtumishi akamwambia, ‘Mdogo wako amekuja na baba yako amemchinjia ndama aliyenona kwa sababu amerudi salama.’

28Mwana mkubwa akakasirika akakataa kuingia ndani na babaye alitoka nje kumsihi.29Ila akamjibu baba yake akisema, ‘Tazama mimi nimekutumikia miaka mingi, wala sijakosa amri yako, lakini hujanipa mwana mbuzi, ili niweze kusherehekea na rafiki zangu.30Lakini alipokuja huyu mwana wako aliyetapanya mali yako yote pamoja na makahaba umemchinjia ndama alienona.’

31Baba akamwambia, ‘Mwanangu, wewe u pamoja nami siku zote na vyote nilivyo navyo ni vyako.32Ila ilikua vyema kwetu kufanya sherehe na kufurahi, huyu ndugu yako alikua amekufa, na sasa yu hai; alikua amepotea naye ameonekana.’”

16

1Yesu aliwaambia tena wanafunzi wake, “Palikuwa na mtu mmoja tajiri aliyekuwa na meneja, na alitaarifiwa ya kwamba meneja huyu anatapanya mali zake.2Hivyo tajiri akamwita, akamwambia, ‘Ni nini hii ninayo isikia juu yako? Toa hesabu ya umeneja wako, kwa kuwa huwezi kuwa meneja tena.’

3Yule meneja akasema moyoni mwake, ‘Nifanye nini, maana bwana wangu ananiondolea kazi yangu ya umeneja? Sina nguvu za kulima, na kuomba naona haya.4Najua nitakalotenda ili nitakapotolewa katika kazi yangu ya uwakili watu wanikaribishe nyumbani mwao.’5Hivyo wakili akawaita wadeni wa bwana wake kila mmoja akamwambia wa kwanza, ‘Unadaiwa kiasi gani na bwana wangu?’

6Akasema ‘Vipimo mia moja vya mafuta,’ akamwambia, ‘Chukua hati yako keti upesi andika hamsini.’

7Kisha akamwambia mwingine, ‘Na wewe unadaiwa kiasi gani?’ akasema, ‘Vipimo mia moja vya unga vya ngano.’ Akamwambia, ‘Twaa hati yako andika themanini.’8Yule bwana akamsifu meneja dhalimu kwa vile alivyotenda kwa werevu. Kwakua watoto wa ulimwengu huu ni werevu na hushughulika kwa ujanja na watu wa upande wao kuliko walivyo watoto wa nuru.9Nami nawaambia jifanyieni marafiki kwa mali ya udhalimu ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele.10Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia. Na aliye dhalimu katika lililo dogo huwa dhalimu katika lililo kubwa pia.11Kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu ni nani atakayewaamini katika mali ya kweli?12Na kama hamkuwa waaminifu katika kutumia mali ya mtu mwingine ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe?13Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili, kwa maana atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.”

14Basi Mafarisayo, ambao walikuwa wanapenda fedha waliyasikia haya yote na wakamdhihaki.15Na akawaambia, “Ninyi ndiyo mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu.

16Sheria na manabii vilikuwapo mpaka Yohana alivyokuja. Tangu wakati huo, habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujaribu kujiingiza kwa nguvu.17Lakini ni rahisi kwa mbingu na nchi vitoweke kuliko hata herufi moja ya sheria ikosekane.

18Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini, naye amwooaye yeye aliyeachwa na mumewe azini.

19Palikua na mtu mmoja tajiri aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi na alikua akifurahia kila siku utajiri wake mkubwa.20Na maskini mmoja jina lake Lazaro aliwekwa getini pake, na ana vidonda.21Naye alikua akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri hata mbwa wakaja wakamlamba vidonda vyake.22Ikawa yule maskini alikufa na akachukuliwa na Malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa akazikwa.23Na kule kuzimu alipokua katika mateso aliyainua macho yake akamuona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro kifuani mwake.24Akalia akasema, ‘Baba Ibrahimu, nihurumue umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.

25Lakini Ibrahimu akasema, ‘Mwanangu kumbuka ya kwamba katika maisha yako uliyapokea mambo yako mema, na Lazaro vivyo alipata mabaya. Ila sasa yupo hapa anafarijiwa na wewe unaumizwa.26Na zaidi ya hayo, kumewekwa shimo kubwa na refu kati yetu, ili wale wanaotaka kutoka huku kwenda kwenu wasiweze wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu.’

27Yule tajiri akasema, ‘Nakuomba Baba Ibrahimu, kwamba umtume nyumbani kwa baba yangu28kwa kuwa ninao ndugu watano ili awaonye, kwa hofu kwamba wao pia watakuja mahali hapa pa mateso.’

29Lakini Ibrahimu akasema, ‘Wanao Musa na manabii. Waache wawasikilize wao.’

30Yule tajiri akasema, ‘Hapana, Baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu watatubu.’

31Lakini Ibrahimu akamwambia, ‘Wasipowasikia Musa na manabii hawatashawishiwa hata mtu akifufuka katika wafu.’”

17

1Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mambo yasababishayo watu watende dhambi hayana budi kutokea, lakini ole wake mtu anayeyasababisha!2Ingekua ni heri kama mtu huyo angefungiwa jiwe zito la kusagia shingoni na kutubwa baharini, kuliko kumfanya mmoja wa hawa wadogo atende dhambi.3Jilindeni. Kama ndugu yako akikukosea mwonye, naye akitubu msamehe.4Kama akikukosea mara saba kwa siku moja na mara saba kwa siku moja akaja kwako akisema, ‘Ninatubu,’ msamehe!”

5Mitume wake wakamwambia Bwana, “Tuongezee imani yetu.”

6Bwana akasema, “Kama mgekuwa na imani kama punje ya haradarii, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘N'goka na ukaote baharini,’ nao ungewatii.

7Lakini nani miongoni mwenu, ambaye ana mtumishi anayelima shamba au anayechunga kondoo, atamwambia arudipo shambani, ‘Njoo haraka na keti ule chakula?’8Je hatamwambia, ‘Niandalie chakula nile, na jifunge mkanda na unitumikie mpaka nitakapo maliza kula na kunywa. Baada ya hapo uta kula na kunywa?’9Hata mshukuru mtumishi huyo kwa sababu katimiza yale aliyoamriwa?10Vivyo hivyo nanyi mkiisha kufanya mliyoagizwa semeni, ‘Sisi tu watumishi tusiostahili. Tumefanya tu yale tuliyopaswa kufanya.’”

11Ilitokea kwamba alivyokua akisafiri kwenda Yerusalemu, alipita mpakani mwa Samaria na Galilaya.12Alipokua akiingia kwenye kijiji kimoja, huko alikutana na watu kumi waliokuwa na ukoma. Wakasimama mbali13wakapaza sauti wakasema “Yesu, Bwana tuhurumie.”

14Alipowaona akawaambia, “Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani.” Nao walipokua wakienda wakatakasika.15Mmoja wao alipoona kwamba amepona, akarudi kwa sauti kuu akimsifu Mungu.16Akapiga magoti miguuni mwa Yesu akamshukuru. Yeye alikua msamaria.17Yesu akajibu, akasema, “Je hawakutakasika wote kumi? Wako wapi wale wengine tisa?18Hakuna hata mmoja aliyeonekana kurudi ili kumtukuza Mungu, isipokuwa huyu mgeni?”19Akamwambia, “Inuka na uende zako imani yako imekuponya.”

20Alipoulizwa na mafarisayo ufalme wa Mungu utakuja lini, Yesu akawajibu akisema, “Ufalme wa Mungu sio kitu ambacho kinaweza kuonekana.21Wala watu hawatasema, ‘Angalia hapa!’ au, ‘Angalia kule!’ kwa maana ufalme wa Mungu umo ndani yenu.”

22Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Wakati utafika ambapo mtatamani kuiona moja ya siku ya Mwana wa Adamu, lakini hamtaiona.23Watawaambia, ‘Angalia, kule! Angalia, hapa!’ Lakini msiende kuangalia, wala kuwafuata,24kama umeme wa radi umulikao katika anga kuanzia upande mmoja hadi mwingine. Hivyo hata Mwana wa Adamu atakuwa ivyo katika siku yake.25Lakini kwanza itampasa kuteseka katika mambo mengi na kukataliwa na kizazi hiki.26Kama ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo itakavyokua katika siku ya Mwana wa Adamu.27Walikula, walikunywa, wakioa na kuolewa mpaka siku ile ambayo Nuhu alipoingia katika safina na gharika ikaja na kuwaangamiza wote.28Ndivyo ilivyokua katika siku za Lutu, walikula, kunywa, wakinunua na kuuza, kulima na walijenga.29Lakini siku ile Lutu alipoondoka Sodoma, ikanyesha mvua ya moto na kiberiti kutoka mbinguni ikawaangamiza wote.30Hivyo ndivyo itakavyo kuwa siku ile ya Mwana wa Adamu atakapofunuliwa.31Siku hiyo, usimruhusu aliye kwenye dari ya nyumba ashuke kuchukue bidhaa zake ndani ya nyumba. Na usimruhusu aliyeko shambani kurudi nyumbani.32Mkumbuke mke wa Lutu.33Ye yote anaejaribu kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini ye yote atakayeyapoteza maisha yake atayaokoa.34Nakwambia, usiku huo kutakua na watu wawili katika kitanda kimoja. Mmoja atachukuliwa, na mwingine ataachwa.35Kutakua na wanawake wawili wanasaga nafaka pamoja, mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa.”

37Wakamwuliza, “Wapi, Mungu?” Akawaambia, “Pale ulipo mzoga, ndipo tai hukusanyika kwa pamoja.”

18

1Kisha akawaambia mfano wa namna wanavyopaswa kuomba daima, na wasikate tamaa.2Akaisema, “Kulikuwa na hakimu katika mji fulani, ambaye hakuwa anamwogopa Mungu na hakuwaheshimu watu.3Kulikuwa na mjane katika jiji hilo, naye alimwendea mara nyingi, akisema, ‘Nisaidie kupata haki dhidi ya mpinzani wangu.’

4Kwa muda mrefu hakuwa tayari kumsaidia, lakini baada ya muda akasema moyoni mwake, ‘Ingawa mimi simwogopi Mungu au kuheshimu mtu,5lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua nitamsaidia kupata haki yake, ili asije akanichosha kwa kunijia mara kwa mara.’”6Kisha Bwana akasema, “Sikiliza alivyosema huyo hakimu dhalimu.7Je Mungu pia hataleta haki kwa wateule wake ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, yeye hatakuwa mvumilivu kwao?8Nawaambia kwamba ataleta haki kwao upesi. Lakini wakati Mwana wa Adamu atakapokuja, je, atakuta imani duniani?”

9Ndipo akawaambia mfano huu kwa baadhi ya watu ambao wanajiona wenyewe kuwa wenye haki na kuwadharau watu wengine,10“Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: mmoja Mfarisayo mwingine mtoza ushuru.11Farisayo akasimama akaomba mambo haya juu yake mwenyewe, ‘Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine ambao ni wanyang'anyi, watu wasio waadilifu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru.12Nafunga mara mbili kila wiki. Natoa zaka katika mapato yote ninayopata.’

13Lakini yule mtoza ushuru, alisimama mbali, bila hakuweza hata kuinua macho yake mbinguni, akagonga kifua chake akisema, ‘Mungu, nirehemu mimi mwenye dhambi.’14Nawaambia, mtu huyu alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki kuliko yule mwingine, kwa sababu kila ajikwezaye atashushwa, lakini kila mtu anayejinyenyekeza atainuliwa.”

15Watu walimletea watoto wao wachanga, ili aweze kuwagusa, lakini wanafunzi wake walipoona hayo, wakawazuia.16Lakini Yesu akawaita kwake akisema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie. Maana ufalme wa Mungu ni wa watu kama hao.17Amini, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto ni dhahiri hatauingia.”

18Mtawala mmoja akamwuliza, akisema, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele?”

19Yesu akamwambia, “Kwa nini unaniita mwema? Hakuna mtu aliye mwema, ila Mungu peke yake.

20Unazijua amri- usizini, usiue, Usiibe, usishuhudie uongo, waheshimu baba yako na mama yako.”

21Yule mtawala akasema, “Mambo haya yote nimeyashika tangu nilipokuwa kijana.”

22Yesu alipoyasikia hayo akamwambia, ‘“Umepungukiwa jambo moja. Lazima uuze vyote ulivyonavyo na uwagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni -kisha njoo, unifuate.”23Lakini tajiri aliposikia hayo, alihuzunika sana, kwa sababu alikuwa tajiri sana.24Kisha Yesu, akamwona alivyohuzunika sana akasema, “Jinsi gani itakavyokuwa vigumu kwa matajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu!25Maana ni rahisi sana kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko kwa tajiri kuingia katika Ufalme wa Mungu.”

26Wale waliosikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeweza kuokolewa?”

27Yesu akajibu, “Mambo yasiyowezekana kwa mwanadamu kwa Mungu yanawezekana.”

28Petro akasema, “Naam, sisi tumeacha kila kitu na tumekufuata wewe.”

29Kisha Yesu akawaambia, “Amini, nawaambia kwamba hakuna mtu aliyeacha nyumba, au mke, au ndugu, au wazazi au watoto, kwa ajili ya Ufalme wa Mungu,30ambaye hatapokea mengi zaidi katika ulimwengu huu, na katika ulimwengu ujao, uzima wa milele.”

31Baada ya kuwakusanya wale kumi na wawili, akawaambia, “Tazama, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote ambayo yameandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Adamu yatakamilishwa.32Kwa maana atatiwa mikononi mwa watu wa Mataifa na atatendewa dhihaka na jeuri, na kutemewa mate.33Baada ya kumchapa viboko watamwua na siku ya tatu atafufuka.”34Hawakuelewa mambo haya, na neno hili lilikuwa limefichwa kwao, na hawakuelewa mambo yaliyosemwa.

35Ikawa Yesu ulipokaribia Yeriko, mtu mmoja kipofu alikuwa ameketi kando ya barabara akiomba msaada,36aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza nini kinatokea.

37Wakamwambia kwamba Yesu wa Nazareti anapita.

38Hivyo yule kipofu akalia kwa sauti, akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, unirehemu.”39Wale waliokuwa wakitembea walimkemea huyo kipofu, wakamwambia anyamaze. Lakini yeye akazidi kulia kwa sauti, “Mwana wa Daudi, unirehemu.”

40Yesu akasimama akaamuru mtu yule aletwe kwake. Kisha yule kipofu alipomkaribia, Yesu akamwuliza,41“Unataka nikufanyie nini.” Akasema, “Bwana, nataka kuona.”

42Yesu akamwambia, “Upate kuona. Imani yako imekuponya.”43Mara hiyo akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Walipoona hili, watu wote wakamsifu Mungu.

19

1Yesu aliingia na kupita katikati ya Yeriko.2Na hapo palikuwa na mtu mmoja aitwaye Zakayo. Ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.3Alikuwa anajaribu kumwona Yesu ni mtu wa namna gani, lakini hakuweza kuona kwa sababu ya umati wa watu, kwa kuwa alikuwa mfupi wa kimo.4Hivyo, alitangulia mbio mbele za watu, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona, kwa sababu Yesu alikaribia kupita njia hiyo.5Wakati Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, “Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako.”6Akafanya haraka, akashuka na kumkaribisha kwa furaha.7Watu wote walipoona hayo, wakalalamika, wakisema, “Amekwenda kumtembelea mtu mwenye dhambi.”

8Zakayo akasimama akamwambia Bwana, “Tazama Bwana nusu ya mali yangu nawapa maskini, na ikiwa nimemnyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”

9Yesu akamwambia, “Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa sababu yeye pia ni mwana wa Ibrahimu.10Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa watu waliopotea.”

11Waliposikia hayo, aliendelea kuongea na alitoa mfano, kwa sababu alikuwa karibu na Yerusalemu, na wao walidhani ya kuwa ufalme wa Mungu ulikuwa karibu kuonekana mara moja.12Hivyo akawaambia, “Ofisa mmoja alikwenda nchi ya mbali ili apokee ufalme na kisha aurudi.13Aliwaita watumishi wake kumi, akawapa mafungu kumi, akawaambia, ‘Fanyeni biashara mpaka nitakaporudi.’

14Lakini wananchi wake walimchukia na hivyo wakatuma wajumbe waende kumfuata na kusema, ‘Hatutaki mtu huyu atutawale.’15Ikawa aliporudi nyumbani baada ya kufanywa mfalme, akaamuru wale watumishi aliokuwa amewaachia fedha waitwe kwake, apate kujua faida gani waliyoipata kwa kufanya biashara.

16Wa kwanza akaja, akasema, ‘Bwana, fungu lako limefanya mafungu kumi zaidi.’

17Huyo Ofisa akamwambia, ‘Vema, mtumishi mwema. Kwa sababu ulikuwa mwaminifu katika jambo dogo, utakuwa na madaraka juu ya miji kumi.’

18Wa pili akaja, akasema, ‘Bwana, fungu lako limefanya mafungu matano.’

19Huyo Afisa akamwambia, ‘Chukua mamlaka juu ya miji mitano.’

20Na mwingine akaja, akasema, ‘Bwana hii hapa fedha yako, ambayo niliihifadhi salama katika kitambaa,21kwa maana niliogopa kwa sababu wewe ni mtu mkali. Unaondoa kile usichokiweka na kuvuna usichopanda.’

22Huyo Ofisa akamwambia, ‘Kwa maneno yako mwenyewe, nitakuhukumu, ewe mtumishi mbaya. Ulijua kwamba mimi ni mtu mkali, nachukua nisichokiweka na kuvuna ambacho sikupanda.23Basi, mbona hukuweka fedha yangu katika benki, ili nikirudi niichukue pamoja na faida?’24Ofisa akawaambia watu waliokuwa wamesimama hapo, ‘Mnyang'anyeni hilo fungu na kumpa yule mwenye mafungu kumi.’

25Wakamwambia, ‘Bwana, yeye ana mafungu kumi.’

26‘Nawaambia, kila mtu ambaye anacho atapewa zaidi, lakini ambaye hana, hata kile alicho nacho kitachukuliwa.27Lakini hawa maadui zangu, ambao hawakutaka niwe Mfalme wao, waleteni hapa na kuwaua mbele yangu.’”

28Baada ya kusema hayo, aliendelea mbele akipanda kwenda Yerusalemu.29Ikawa alipokaribia Bethfage na Bethania, karibu na mlima wa Mizeituni, aliwatuma wanafunzi wake wawili,30akisema: “Nendeni katika kijiji cha jirani. Mkiingia, mtakuta mwana-punda hajapandwa bado. Mfungueni, mkamlete kwangu.31Kama mtu akiwauliza, ‘Mbona mnamfungua?’ Semeni, ‘Bwana anamhitaji.’”32Wale waliotumwa wakaenda wakamwona mwana-punda kama Yesu alivyokuwa amewaambia.

33Walipokuwa wanamfungua mwana punda wamiliki wakawaambia, “Kwa nini mnamfungua mwana punda huyu?”

34Wakasema, “Bwana anamhitaji.”35Basi, wakampelekea Yesu, wakatandika nguo zao juu ya mwana punda na wakampandisha Yesu juu yake.36Alipokuwa akienda watu wakatandaza mavazi yao barabarani.

37Alipokuwa anateremka mlima wa Mizeituni, jumuiya yote ya wanafunzi wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa, kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona,38wakisema, “Ndiye mbarikiwa Mfalme ajaye kwa jina la Bwana! Amani mbinguni, na utukufu juu!”

39Baadhi ya Mafarisayo katika mkutano wakamwambia, “Mwalimu, wanyamazishe wanafunzi wako.”

40Yesu akajibu, akasema, “Nawaambieni, kama hawa wakinyamaza, mawe yatapaza sauti.”

41Yesu alipoukaribia mji aliulilia,42akisema, “Laiti ungelijua hata wewe, katika siku hii mambo ambayo yanayokuletea amani! Lakini sasa yamefichika machoni pako.43Kwa kuwa siku zinakuja ambapo adui zako watajenga boma karibu na wewe, na kukuzunguka na kukukandamiza kutoka kila upande.44Watakuangusha chini wewe na watoto wako. Hawatakuachia hata jiwe moja juu ya jingine, kwa sababu haukutambua wakati Mungu alipokuwa anajaribu kukuokoa.”

45Yesu aliingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza wale waliokuwa wakiuza,46akiwaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang'anyi.”

47Kwa hiyo, Yesu alikuwa akifundisha kila siku hekaluni. Makuhani wakuu na walimu wa Sheria na viongozi wa watu walitaka kumuua,48lakini hawakuweza kupata njia ya kufanya hivyo, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsikiliza kwa makini.

20

1Ikawa siku moja, Yesu alipokuwa akiwafundisha watu hekaluni na kuhubiri injili, makuhani wakuu na walimu wa sheria walimwendea pamoja na wazee.2Walizungumza, wakimwambia, “Tuambie ni kwa mamlaka gani unafanya mambo haya? Au ni nani huyo ambaye amekupa mamlaka haya?”

3Naye akajibu, akawaambia, “Nami pia nitawauliza swali. Niambieni4ubatizo wa Yohana. Je, ulitoka mbinguni ama kwa watu?”

5Lakini wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Tukisema ilitoka mbinguni, atatuuliza, ‘Basi, mbona hamkumwamini?’

6Na tukisema; ‘Ilitoka kwa wanadamu;’ watu wote hapa watatupiga mawe, maana wote wanaamini kwamba Yohana alikuwa nabii.”7Basi, wakamjibu ya kwamba hawakujua ilikotoka.

8Yesu akawaambia, ‘“Wala mimi siwaambii ninyi ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.”

9Aliwaambia watu mfano huu, “Mtu mmoja alipanda shamba la mizabibu, akalikodisha kwa wakulima wa mizabibu, na akaenda nchi nyingine kwa muda mrefu.10Kwa muda uliopangwa, alimtuma mtumishi kwa wakulima mizabibu, kwamba wampe sehemu ya matunda ya shamba la mizabibu. Lakini wakulima wa mzabibu wakampiga, wakamrudisha mikono- mitupu.11Kisha akamtuma tena mtumishi mwingine na nao wakampiga, kumtendea vibaya, na wakamrudisha mikono- mitupu.12Alimtuma tena wa tatu na nao wakamjeruhi na kumtupa nje.13Hivyo bwana wa shamba akasema, ‘Nitafanya nini? Nitamtuma mwanangu mpendwa. Labda watamheshimu.’

14Lakini wakulima wa mzabibu walipomwona, walijadili wao kwa wao wakisema, ‘Huyu ndiye mrithi. Tumuue, ili urithi wake uwe wetu.’15Wakamtoa nje ya shamba la mizabibu na kumuua. Je bwana shamba atawafanya nini?16Atakuja kuwaangamiza wakulima wa mzabibu, na atawapa shamba hilo wengine.” Nao waliposikia hayo, wakasema, “Mungu amekataa.”

17Lakini Yesu akawatazama, akasema, “Je andiko hili lina maana gani? ‘Jiwe walilolikataa wajenzi, limekuwa jiwe la pembeni?

18Kila mtu aangukaye juu ya jiwe hilo, atavunjika vipande vipande. Lakini yule ambaye litamwangukia, litamponda.’”

19Hivyo waandishi na wakuu wa makuhani walitafuta njia ya kumkamata wakati huohuo, walijua kwamba alikuwa amesema mfano huu dhidi yao. Lakini waliwaogopa watu.20Walimuangalia kwa makini, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wapate kupata kosa kwa hotuba yake, ili kumpelekakwa watawala na wenye mamlaka.21Nao wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, tunajua kwamba unasema na kufundisha mambo ya kweli na si kushawishiwa na mtu yeyote, lakini wewe hufundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu.22Je, ni halali kwetu kulipa kodi kwa Kaisari, au la?”

23Lakini Yesu alitambua mtego wao, akawaambia,24“Nionyesheni dinari. Sura na chapa ya nani ipo juu yake?” Walisema, “Ya Kaisari.”

25Naye akawaambia, “Basi, mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari, na Mungu yaliyo yake Mungu.”26Waandishi na wakuu wa makuhani hawakuwa na uwezo wa kukosoa kile alichosema mbele ya watu. Wakastaajabia majibu yake na hawakusema chochote.

27Baadhi ya Masadukayo wakamwendea, wale ambao wanasema kwamba hakuna ufufuo,28wakamwuliza, wakisema, “Mwalimu, Musa alituandikia kwamba kama mtu akifiwa na ndugu mwenye mke ambaye hana mtoto basi anapaswa kumchukuna mke wa ndugu yake na kuzaa nae kwa ajili ya kaka yake.29Kulikuwa na ndugu saba Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto,30na wa pili pia.31Wa tatu akamchukua vilevile, vivyo hivyo wa saba hakuacha watoto na akafa.32Baadaye yule mwanamke pia akafa.33Katika ufufuo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba walikuwa wamemwoa.”

34Yesu akawaambia, “Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa.35Lakini wale wanastaohili kupokea ufufuo wa wafu na kuingia uzima wa milele hawaoi wala hawaolewi.36Wala hawawezi kufa tena, kwa sababu huwa sawasawa na malaika na ni watoto wa Mungu, wana wa ufufuo.37Lakini hiyo wafu wanafufuliwa, hata Musa alionyesha mahali katika habari za kichaka, pale alimwita Bwana kama Mungu wa Ibrahimu na Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.38Sasa, yeye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai, kwa sababu wote huishi kwake.”

39Baadhi ya walimu wa Sheria wakamjibu, “Mwalimu, umejibu vema.”40Hawakuthubutu kumwuliza maswali mengine zaidi.

41Yesu akawaambia, “Kivipi watu wanasema kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?42Maana Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti mkono wa kulia,
43mpaka niwaweke adui zako chini ya miguu yako.’

44Daudi anamwita Kristo ‘Bwana,’ basi atakuwaje mwana wa Daudi?”

45Watu wote walipokuwa wakimsikiliza akawaambia wanafunzi wake,46“Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na wapenda salamu maalum sokoni na viti vya heshima katika masinagogi, na maeneo ya heshima karamuni.47Wao pia hula nyumba za wajane, na wanajifanya wanasali sala ndefu. Hawa watapokea hukumu kubwa zaidi.”

21

1Yesu alitazama akawaona wanaume matajiri waliokuwa wanaweka zawadi zao kwenye hazina.2Akamuona mjane mmoja masikini akiweka senti zake mbili.3Hivyo akasema, “Kweli nawaambieni, huyu mjane maskini ameweka nyingi kuliko wengine wote.4Hawa wote wametoa hizi zawadi kutoka katika vingi walivyonavyo. Lakini huyu mjane, katika umaskini wake, ametoa fedha zote alizokuwa nazo kwa ajili ya kuishi kwake.”

5Wakati wengine walipokuwa wakisema juu ya hekalu, namna lilivyokuwa limepambwa na mawe mazuri na matoleo, alisema,6“Kwa habari ya mambo haya mnayoyaona, siku zitakuja ambazo hakuna jiwe moja ambalo litaachwa juu ya jiwe jingine ambalo halitabomolewa.”

7Hivyo wakamuuliza, wakasema, “Mwalimu, mambo haya yatatokea lini? Na nini ni itakuwa ishara kwamba haya mambo yako karibu kutokea?”

8Yesu akajibu, “Muwe waangalifu kwamba msidanganywe. Kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakisema, ‘Mimi ndiye,’ na ‘Muda umekaribia.’ Msiwafuate.9Mkisikia vita na vuruguvurugu msiogope, kwa sababu haya mambo lazima yatokee kwanza, lakini mwisho hautatokea upesi.”

10Kisha akawaambia, “Taifa litainuka kupigana na taifa jingine, na ufalme juu ya ufalme mwingine.11Kutakuwa na matetemeko makubwa, na njaa na tauni katika maeneo mbalimbali. Kutakuwa na matukio ya kutisha na ishara za kutisha kutoka mbinguni.12Lakini kabla ya mambo haya yote, wataweka mikono yao juu yenu na kuwatesa, kuwapeleka kwenye masinagogi na magereza, kuwaleta mbele za wafalme na wenye mamlaka kwa sababu ya jina langu.13Hii itawafungulia fursa kwa ushuhuda wenu.14Kwa hiyo amueni mioyoni mwenu kutoandaa utetezi wenu mapema,15kwa sababu nitawapa maneno na hekima, ambayo adui zenu wote hawataweza kuipinga au kuikana.16Lakini mtakataliwa pia na wazazi wenu, ndugu zenu, jamaa zenu na rafiki zenu, na watawaua baadhi yenu.17Mtachukiwa na kila mmoja kwa sababu ya jina langu.18Lakini hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.19Katika kuvumilia mtaziponya nafsi zenu.

20Mtakapoona Yerusalemu imezungukwa na majeshi, basi jueni kwamba uharibifu wake umekaribia.21Hapo wale walioko Yudea wakimbilie milimani, na wale walioko katikati ya jiji waondoke, na msiwaache walioko vijijini kuingia.22Maana hizi ni siku za kisasi, ili kwamba mambo yote yaliyoandikwa yapate kutimilika.23Ole ni kwa wale walio na mimba na kwa wale wanyonyeshao katika siku hizo! Kwa maana kutakuwa na adha kuu juu ya nchi, na ghadhabu kwa watu hawa.24Na wataanguka kwa ncha ya upanga na watachukuliwa mateka kwa mataifa yote, na Yerusalem itakanyagwa na watu wa mataifa, mpaka wakati wa watu wa mataifa utakapotimilika.

25Kutakuwa na ishara katika jua, mwezi na nyota. Na katika nchi kutakuwa na dhiki ya mataifa, katika kukata tamaa kutokana na mlio wa bahari na mawimbi.26Kutakuwa na watu wakizimia kwa hofu na katika kutarajia mambo yatakoyo tokea juu ya dunia. Kwa maana nguvu za mbingu zitatikiswa.27Kisha watamwona Mwana wa Adamu akija mawinguni katika nguvu na utukufu mkuu.28Lakini mambo haya yatakapoanza kutokea, simameni, inueni vichwa vyenu, kwa sababu ukombozi wenu umesogea karibu.”

29Yesu akawaambia kwa mfano, “Uangalieni mtini, na miti yote.30Inapotoa machipukizi, mnajionea wenyewe na kutambua kwamba kiangazi tayari kiko karibu.31Vivyo hivyo, mnapoona mambo haya yanatokea, ninyi tambueni ya kwamba ufalme wa Mungu umekaribia.32Kweli, nawaambieni, kizazi hiki hakitapita, mpaka mambo haya yote yatakapotokea.33Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.

34Lakini jiangalieni wenyewe, ili kwamba mioyo yenu isije ikalemewa na ufisadi, ulevi, na mahangaiko ya maisha haya. Kwa sababu ile siku itawajia ghafla35kama mtego. Kwa sababu itakuwa juu ya kila mmoja aishiye katika uso wa dunia nzima.36Lakini mwe tayari wakati wote, mwombe kwamba mtakuwa imara vya kutosha kuyaepuka haya yote yatakayotokea, na kusimama mbele za Mwana wa Adamu.”

37Hivyo wakati wa mchana alikuwa akifundisha hekaluni na usiku alitoka nje, na kwenda kukesha katika mlima unaoitwa wa Mzeituni.38Watu wote walimjia asubuhi na mapema ili kumsikiliza ndani ya hekalu.

22

1Basi sikukuu ya mkate usiyotiwa chachu ilikuwa imekaribia, ambayo inaitwa pasaka.2Makuhani wakuu na waandishi wakajadiliana namna ya kumuua Yesu, kwa sababu waliwaogopa watu.

3Shetani akaingia ndani ya Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na mbili.4Yuda akaenda kujadiliana na wakuu wa makuhani na wakuu namna ambavyo atamkabidhi Yesu kwao.5Walifurahi, na kukubaliana kumpa fedha.6Yeye aliridhia, na alitafuta fursa ya kumkabidhi Yesu kwao mbali na kundi la watu.

7Siku ya mikate isiyotiwa chachu ikafika, ambapo kondoo wa Pasaka lazima atolewe.8Yesu akawatuma Petro na Yohana, akasema, “Nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka ili tuje tukile.”

9Wakamuuliza, “Wapi unataka tuyafanyie hayo maandalizi?”

10Akawajibu, “Sikilizeni, mtakapokuwa mmeingia mjini, mwanamume ambaye amebeba mtungi wa maji atakutana na ninyi. Mfuateni kwenye nyumba ambayo ataingia.11Kisha mwambieni bwana wa nyumba, “Mwalimu anakwambia, ‘Kiko wapi chumba cha wageni, mahali ambapo nitakula Pasaka na wanafunzi wangu?’”12Atawaonyesha chumba cha ghorofani ambacho kiko tayari. Fanyeni maandalizi humo.”13Hivyo wakaenda, na wakakuta kila kitu kama alivyowaambia. Kisha wakaandaa chakula cha Pasaka.

14Muda ulipofika alikaa na wale mitume.15Kisha akawaambia, “Nina shauku kubwa ya kula sikukuu hii ya Pasaka na ninyi kabla ya kuteswa kwangu.16Kwa maana nawaambieni, sitakula tena mpaka itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu.”17Kisha Yesu akachukua kikombe, na alipokwisha kushukuru, akasema, “Chukueni hiki, na mgawane ninyi kwa ninyi.18Kwa maana nawaambia, sitakunywa tena mzao wa mzabibu, mpaka ufalme wa Mungu utakapokuja.”19Kisha akachukua mkate, na alipokwisha kushukuru, akaumega, na kuwapa, akisema, “Huu ni mwili wangu ambao umetolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.”20Akachukua kikombe vivyo hivyo baada ya chakula cha usiku akisema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, ambayo imemwagika kwa ajili yenu.”21Lakini angalieni. Yule anisalitie yuko pamoja nami mezani.22Kwa maana Mwana wa Adamu kwa kweli aenda zake kama ilivyokwisha amuliwa. Lakini ole kwa mtu yule ambaye kupitia yeye Mwana wa Adamu asalitiwa!”

23Wakaanza kuulizana wao kwa wao, nani miongoni mwao ambaye angefanya jambo hili.

24Kisha yakatokea mabishano katikati yao kwamba ni nani anaye dhaniwa kuwa mkuu kuliko wote.

25Akawaambia, “Wafalme wa watu wa mataifa wana ubwana juu yao, na wale mwenye mamlaka juu yao wanaitwa waheshimiwa watawala.26Lakini haitakiwi kabisa kuwa hivi kwenu ninyi. Badala yake, acha yule ambaye ni mkubwa kati yenu awe kama mdogo. Na yule ambaye ni wa muhimu sana awe kama atumikaye.27Kwa sababu yupi mkubwa, yule akaaye mezani au yule anayetumika? Je si yule aketie mezani? Na mimi bado ni kati yenu kama atumikaye.

28Lakini ninyi ndio ambao mmeendelea kuwa nami katika majaribu yangu.29Nawapa ninyi ufalme, kama vile Baba alivyonipa mimi ufalme,30kwamba mpate kula na kunywa mezani kwangu kwenye ufalme wangu. Na mtakaa kwenye viti vya enzi mkizihukumu kabila kumi na mbili za Israel.

31Simoni, Simoni, fahamu kwamba, Shetani ameomba awapate ili awapepete kama ngano.32Lakini nimekuombea, kwamba imani yako isishindwe. Baada ya kuwa umerudi tena, waimarishe ndugu zako.”

33Petro akamwambia, “Bwana, niko tayari kwenda na wewe gerezani na hata katika mauti.”

34Yesu akajibu, “Nakwambia, Petro, Jogoo hatawika leo, kabla hujanikana mara tatu kwamba unanijua.”

35Kisha Yesu akawaambia, “Nilipowapeleka ninyi bila mfuko, kikapu cha vyakula, ua viatu, je mlipungukiwa na kitu?” Wakajibu “Hakuna.”

36Kisha akawaambia, “Lakini sasa, kila mwenye mfuko, na auchukue pamoja na kikapu cha vyakula. Yule ambaye hana upanga imempasa auze joho lake anunue mmoja.37Kwa sababu nawaambia, yote ambayo yameandikwa kwa ajili yangu lazima yatimilike, ‘Na alichukuliwa kama mtu ambaye anavunja torati.’ Kwa sababu kile kilichotabiriwa kwa ajili yangu kinatimizwa.”

38Kisha wakasema, “Bwana, tazama! Hizi hapa panga mbili.” Na akawaambia, “Yatosha.”

39Baada ya chakula cha usiku, Yesu aliondoka, kama ambavyo amekuwa akifanya mara kwa mara, akaenda mlima wa Mzeituni, na wanafunzi wakamfuata.40Walipofika, aliwaambia, “Ombeni kwamba msiingie majaribuni.”41Akaenda mbali na wao kama mrusho wa jiwe, akapiga magoti akaomba,42akisema, “Baba, kama unataka, niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nitakavyo mimi, lakini mapenzi yako yafanyike.”43Kisha malaika kutoka mbinguni akamtokea, akamtia nguvu.44Akiwa katika kuugua, akaomba kwa dhati zaidi, na jasho lake likawa kama matone makubwa ya damu yakidondoka chini.45Wakati alipoamka kutoka katika maombi yake, alikuja kwa wanafunzi, na akawakuta wamelala kwa sababu ya huzuni yao,46na akawauliza, “Kwa nini mnalala? Amkeni muombe, kwamba msiingie majaribuni.”

47Wakati alipokuwa bado akiongea, tazama, kundi kubwa la watu likatokea, na Yuda, mmoja wa mitume kumi na wawili akiwaongoza. Akaja karibu na Yesu ili ambusu,48lakini Yesu akamwambia, “Yuda, je unamsaliti Mwana wa Adamu kwa busu?”

49Wakati wale waliokuwa karibu na Yesu walipoona hayo yanayotokea, wakasema, “Bwana, je tuwapige kwa upanga?”50Kisha mmoja wao akampiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio lake la kulia.

51Yesu akasema, “Hii inatosha.” Na akagusa sikio lake, akamponya.52Yesu akasema kwa kuhani mkuu, na kwa wakuu wa hekalu, na kwa wazee waliokuja kinyume chake, “Je mnakuja kana kwamba mnakuja kupambana na mnyang'anyi, na marungu na mapanga?53Nilipokuwa pamoja nanyi siku zote kwenye hekalu, hamkuweka mikono yenu juu yangu. Lakini hii ni saa yako, na mamlaka ya giza.”

54Wakamkamata, wakamuongoza, wakamleta nyumbani mwa kuhani mkuu. Lakini Petro akamfuatilia kwa mbali.55Baada ya kuwa wamewasha moto katika ule uwanda wa ndani na walipokwisha kukaa chini pamoja, Petro akakaa katikati yao.56Mtumishi mmoja wa kike akamuona Petro alipokuwa amekaa katika mwanga utokanao na moto, akamtazama akamwambia, “Huyu mtu pia alikuwa pamoja naye.”

57Lakini Petro akakana, akasema, “Mwanamke, mimi simjui.”

58Baada ya muda kidogo, mtu mwingine akamuona akasema “Wewe pia ni mmoja wao.” Lakini Petro akajibu, “Mwanaume, mimi siyo.”

59Baada ya kama saa moja hivi, mwanaume mmoja akasisitiza akasema, “Kweli kabisa huyu mtu pia alikuwa pamoja naye, maana ni Mgalilaya.”

60Lakini Petro akasema, “Mwanaume, sijui usemalo.” Na mara, wakati akiongea, jogoo akawika.

61Akageuka, Bwana akamtazama Petro. Na Petro akalikumbuka neno la Bwana, pale alipomwambia, “Kabla ya jogoo kuwika leo, utanikana mimi mara tatu.”62Akienda nje, Petro akalia kwa uchungu mwingi.

63Kisha wale wanaume waliokuwa wakimlinda Yesu, wakamdhihaki na kumpiga.64Baada ya kumfunika macho, wakamuuliza, wakisema, “Tabiri! Ni nani aliyekupiga?”65Wakaongea mambo mengine mengi kinyume cha Yesu na kumkufuru yeye.

66Mara ilipokuwa asubuhi, wazee wa watu walikusanyika pamoja, wakuu wa makuhani na waandishi. Wakampeleka kwenye Baraza,67wakisema, “Kama wewe ni Kristo, tuambie.” Lakini yeye akawaambia, “Kama nikiwaambia, hamtaniamini,68na kama nikiwauliza hamtanijibu.”69Lakini kuanzia sasa na kuendelea, Mwana wa Adamu atakuwa amekaa mkono wa kuume wa nguvu ya Mungu.”

70Wote wakasema, “Kwa hiyo wewe ni Mwana wa Mungu?” Na Yesu akawaambia, “Ninyi mmesema mimi ndiye.”71Wakasema, “Kwa nini bado tunahitaji tena ushahidi? Kwa sababu sisi wenyewe tumesikia kutoka katika kinywa chake mwenyewe.”

23

1Mkutano wote wakasimama, wakampeleka Yesu mbele ya Pilato.2Wakaanza kumshutumu, wakisema, “Tumemkuta mtu huyu akipotosha taifa letu, kwa kukataza tusitoe kodi kwa Kaisari, na akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, Mfalme.”

3Pilato akamuuliza, akisema, “Je wewe ni Mfalme wa Wayahudi?” Na Yesu akamjibu akisema, “Wewe wasema hivyo.”

4Pilato akamuambia kuhani mkuu na makutano, “Sioni kosa kwa mtu huyu.”

5Lakini wao wakasisitiza, wakisema, “Amekuwa akiwachochea watu, akifundisha katika Uyahudi yote, kuanzia Galilaya na sasa yuko hapa.”

6Pilato aliposikia haya, akaulizia kama mtu huyo ni wa Galilaya?7Alipotambua kuwa alikuwa chini ya utawala wa Herode, akampeleka Yesu kwa Herode, ambaye naye alikuwa Yerusalemu kwa siku hizo.8Herode alipomuona Yesu, alifurahi sana kwa sababu alitaka kumuona kwa siku nyingi. Alisikia habari zake na alitamani kuona moja ya miujiza ikifanywa na yeye.9Herode alimhoji Yesu kwa maneno mengi, lakini Yesu hakumjibu chochote.10Makuhani wakuu pamoja na waandishi walisimama kwa ukali wakimshitaki.11Herode pamoja na maaskari wake, walimtukana na kumdhihaki, na kumvika mavazi mazuri, kisha akamrudisha Yesu kwa Pilato.12Herode na Pilato wakawa marafiki kuanzia siku hiyo, (kabla ya hapo walikuwa maadui).

13Pilato akawaita pomoja makuhani wakuu na watawala na umati wa watu,14Akawaambia, “Mmeniletea mtu huyu kama mtu anaye waongoza watu wafanye mabaya, na tazama, baada ya kuwa nimemhoji mbele yenu, sikuona kosa kwa mtu huyu kuhusu mambo yote ambayo ninyi mnamshitaki yeye.15Hapana, wala Herode, kwa maana amemrudisha kwetu, na tazama hakuna chochote alichokifanya kinachostahili adhabu ya kifo.16Kwa hiyo basi nitamuadhibu na kumuachilia.17[Sasa, Pilato anawajibika kumuachilia mfungwa mmoja kwa wayahudi wakati wa sikukuu.]

18Lakini wote wakapiga kelele pamoja, wakisema, “Mwondoe huyo, na tufungulie Baraba!”19Baraba alikuwa ni mtu ambaye amewekwa gerezani kwa sababu ya uasi fulani katika jiji na kwa kuua.20Pilato akawaambia tena, akitamani kumwachilia Yesu.

21Lakini wao wakapiga kelele, wakisema, “Msulibishe, msulibishe.”22Akawauliza kwa mara ya tatu, “Kwa nini, huyu mtu amefanya maovu gani? Sikupata kosa linalostahili adhabu ya kifo kwake. Kwa hiyo nitakapo maliza kumuadhibu nitamuachilia.”23Lakini wakasisitiza kwa sauti ya juu, wakitaka asulubiwe. Na sauti zao zikamshawishi Pilato.24Hivyo Pilato akaamua kuwapatia matakwa yao.25Akamuachilia yule waliyemtaka ambaye alifungwa kwa kusababisha ghasia na kuua. Lakini akamtoa Yesu kwa matakwa yao.

26Walipokuwa wakimpeleka, walimkamata mtu mmoja aitwaye Simoni wa Ukirene, akitokea katika nchi, wakamtwika msalaba ili abebe, akimfuata Yesu.27Umati mkubwa wa watu, na wanawake ambao walihuzunika na kuomboleza kwa ajili yake, walikuwa wakimfuata.28Lakini akawageukia, Yesu akawaambia, ‘Mabinti wa Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni ninyi wenyewe na kwa ya ajili watoto wenu.29Tazama, siku zinakuja ambazo watasema, “Wamebarikiwa walio tasa na matumbo yasiyozaa, na matiti ambayo hayakunyonyesha.30Ndipo watakapo anza kuiambia milima, ‘Tuangukieni,’ na vilima, ‘Mtufunike.’31Maana kama wakifanya mambo haya ikiwa mti mbichi, itakuwaje ukiwa mkavu?”

32Wanaume wengine, wahalifu wawili, walipelekwa pamoja naye ili wauwawe.33Walipofika mahali paitwapo Fuvu la kichwa, ndipo wakamsulubisha pamoja na wale wahalifu, mmoja upande wa kulia na mwingine upande wa kushoto.34Yesu alisema, “Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. “Nao wakapiga kura, kugawa mavazi yake.35Watu walikuwa wamesimama wakiangalia huku watawala wakimdhihaki, wakisema, “Aliwaokoa wengine. Sasa ajiokoe mwenyewe, kama yeye ni Kristo wa Mungu, mteule,”

36Askari pia walimdharau, walimkaribia yeye na wakumpa siki,37wakisema, “Kama wewe ni Mfalme wa Wayahudi jiokoe mwenyewe”38Kulikuwa pia na alama juu yake iliyoandikwa “HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI.”

39Mmoja wa wahalifu aliyesulubishwa alimtukana akisema, “Wewe si Kristo? Jiokoe mwenyewe na sisi”

40Lakini yule mwingine akajibu, akimkemea na akisema, “Je wewe humuogopi Mungu, nawe uko katika hukumu hiyo hiyo?41Sisi tupo hapa kwa haki, kwa maana sisi tunapokea kile tunachostahili kwa matendo yetu. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya.”42Na aliongeza, “Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako.”

43Yesu akamwambia, “Amini nakuambia, leo hii utakuwa pamoja nami Paradiso.”

44Hapo ilikuwa karibu saa ya sita, giza likaja juu ya nchi yote hadi saa ya tisa,45Mwanga wa jua ulizimika. Kisha pazia la hekalu likagawanyika katikati kuanzia juu.46Akilia kwa sauti kuu, Yesu alisema, “Baba mikononi mwako naiweka roho yangu,” baada ya kusema haya, akafa.

47Wakati Akida alipoona yaliyotendeka alimtukuza Mungu akisema, “Hakika huyu alikuwa mtu mwenye haki.”48Wakati umati wa watu waliokuja pamoja kushuhudia walipoona mambo yaliyofanyika, walirudi huku wakipiga vifua vyao.49Lakini marafiki zake, na wanawake waliomfuata toka Galilaya, walisimama kwa mbali wakiangalia hayo mambo.

50Tazama, palikuwepo na mtu aitwaye Yusufu, ambaye ni mmoja wa baraza, mtu mzuri na mwenye haki,51(alikuwa hajakubaliana na maamuzi au matendo yao), kutoka Armathaya, mji wa Kiyahudi, ambao ulikua ukisubiria ufalme wa Mungu.52Mtu huyu, alimkaribia Pilato, akaomba apewe mwili wa Yesu.53Alimshusha, na akauzungushia sanda, na akaumweka katika kaburi lililokuwa limechongwa katika jiwe, ambalo hakuna aliyewahi kuzikwa.54Ilikuwa ni siku ya maandalizi, na Sabato inakaribia.55Wanawake, waliokuja nao kutoka Galilaya, walimfuata, na wakaona kaburi na jinsi mwili wake ulivyolazwa.56Walirudi na kuanza kuandaa manukato na marashi. Kisha siku ya sabato walipumzika kwa mujibu wa sheria.

24

1Mapema sana siku ya kwanza ya juma, walikuja kaburini, wakileta manukato ambayo walikuwa wameyaandaa.2Wakakuta jiwe limevingirishwa mbali na kaburi.3Wakaingia ndani, lakini hawakuukuta mwili wa Bwana Yesu.4Ilitokea kwamba, wakati wamechanganyikiwa kuhusu hili, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi ya kung'aa.5Wanawake wakiwa wamejaa hofu na wakiinamisha nyuso zao chini, wakawaambia wanawake, “Kwa nini mnamtafuta aliye hai miongoni mwa wafu?6Hayupo hapa, ila amefufuka! Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa angali Galilaya,7akisema kwamba Mwana wa Adamu lazima atolewe kwenye mikono ya watu wenye dhambi na asulubishwe, na siku ya tatu, afufuke tena.”8Wale wanawake wakakumbuka maneno yake,9na wakarudi kutoka kaburini na wakawaambia mambo haya yote wale kumi na moja na wengine wote.10Basi Maria Magdalena, Joana, Maria mama wa Yakobo, na wanawake wengine pamoja nao wakatoa taarifa hizi kwa mitume.11Lakini ujumbe huu ukaonekana kama mzaha tu kwa mitume, na hawakuwaamini wale wanawake.12Hata hivyo Petro aliamka, na akakimbia kuelekea kaburini, na akichungulia na kuangalia ndani, aliona sanda peke yake. Petro kisha akaondoka akaenda nyumbani kwake, akistaajabu nini ambacho kimetokea.

13Na tazama, wawili miongoni mwao walikuwa wakienda siku hiyo hiyo katika kijiji kimoja kiitwacho Emmau, ambacho kilikuwa maili sitini kutoka Yerusalemu.14Wakajadiliana wao kwa wao kuhusu mambo yote yaliyotokea.15Ikatokea kwamba, wakati walipokuwa wakijadiliana na kuulizana maswali, Yesu akasogea karibu akaambatana nao.16Lakini macho yao yalizuiliwa katika kumtambua yeye.17Yesu akawaambia, “Nini ambacho ninyi wawili mnakiongelea wakati mnatembea?” Wakasimama pale wakionekana na huzuni.

18Mmoja wao, jina lake Cleopa, akamjibu, “Je wewe ni mtu pekee hapa Yerusalemu ambaye hajui mambo yaliyotokea huko siku hizi?”

19Yesu akawaambia, “Mambo gani?” Wakamjibu, “Mambo kuhusu Yesu Mnazareti, ambaye alikuwa nabii, muweza katika matendo na maneno mbele za Mungu na watu wote.20Na kwa jinsi ambayo wakuu wa makuhani na viongozi wetu walivyomtoa kuhukumiwa kifo na kumsulubisha.21Lakini tulitumaini kwamba yeye ndiye atakaye waweka huru Israeli. Ndiyo, mbali na haya yote, sasa ni siku ya tatu tangu mambo haya yatokee.22Lakini pia, baadhi ya wanawake kutoka katika kundi letu walitushangaza, baada ya kuwapo kaburini asubuhi na mapema.23Walipoukosa mwili wake, wakaja, wakisema kwamba waliona pia maono ya malaika waliosema kwamba yu hai.24Baadhi ya wanaume ambao walikuwa pamoja nasi walienda kaburini, na kukuta ni kama vile wanawake walivyosema. Lakini hawakumuona yeye.”

25Yesu akawaambia, “Ninyi watu wajinga na wenye mioyo mizito ya kuamini yote ambayo manabii wamesema!26Je haikuwa lazima Yesu kuteseka kwa mambo haya, na kuingia katika utukufu wake?”27Kisha kuanzia kutoka kwa Musa na manabii wote, Yesu akawatafsiria mambo yanayomuhusu yeye katika maandiko yote.

28Walipokaribia kile kijiji, huko walikokuwa wakienda, Yesu akafanya kana kwamba anaendelea mbele.29Lakini walimlazimisha, wakisema, “Kaa pamoja nasi, maana inaelekea jioni na siku ni kama imeisha.” Hivyo Yesu akaingia kwenda kukaa nao.30Ilitokea kwamba, wakati amekaa nao kula, alichukua mkate, akaubariki, na kuuvunja, akawapa.31Kisha macho yao yakafunguliwa, wakamjua, na akatoweka ghafla mbele ya macho yao.32Wakasemezana wao kwa wao, “Hivi mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, wakati alipoongea nasi njiani, wakati alipotufungulia maandiko?”33Wakanyanyuka saa hiyo hiyo, na kurudi Yerusalemu. Wakawakuta wale kumi na mmoja wamekusanyika pamoja, na wale waliokuwa pamoja nao,34wakisema, “Bwana amefufuka kwelikweli, na amemtokea Simoni.”35Hivyo wakawaambia mambo yaliyotokea njiani, na namna Yesu alivyodhihirishwa kwao katika kuumega mkate.

36Wakati wakiongea mambo hayo, Yesu mwenyewe alisimama katikati yao, na akawaambia, “Amani iwe kwenu.”37Lakini waliogopa na kujawa na hofu, na wakafikiri kwamba waliona roho.38Yesu akawaambia, Kwa nini mnafadhaika? Kwa nini maswali yanainuka mioyoni mwenu?39Angalieni mikono yangu na miguu yangu, kwamba ni mimi mwenyewe. Niguseni na muone. Kwa maana roho haina nyama na mifupa, kama mnionavyo mimi kuwa navyo.”40Alipokwisha kusema hivi, akawaonyesha mikono yake na miguu yake.41Walipokuwa bado na furaha iliyochanganyikana na kutokuamini, na kustaajabu, Yesu akawaambia, “Je mna kitu chochote cha kula?”42Wakampa kipande cha samaki aliyechomwa.43Yesu akakichukua, na kukila mbele yao.

44Akawaambia, “Nilipokuwa nanyi, niliwaambia kwamba yote yalioandikwa kwenye sheria ya Musa na manabii na Zaburi lazima yatimilike.”45Kisha akafungua akili zao, kwamba waweze kuyaelewa maandiko.46Akawaambia, “Kwamba imeandikwa, Kristo lazima ateseke, na kufufuka tena kutoka katika wafu siku ya tatu.47Na toba na msamaha wa dhambi lazima ihubiriwe kwa jina lake kwa mataifa yote, kuanzia kutokea Yerusalemu.48Ninyi ni mashahidi wa mambo haya.49Angalia, nawapelekea ahadi ya Baba yangu juu yenu. Lakini subirini hapa jijini, mpaka mtakapovishwa nguvu kutoka juu.

50Kisha Yesu akawaongoza nje mpaka walipokaribia Bethania. Akainua mikono yake juu, na akawabariki.51Ikatokea kwamba, wakati alipokuwa akiwabariki, aliwaacha na akabebwa juu kuelekea mbinguni.52Basi wakamwabudu, na kurudi Yerusalemu na furaha kuu.53Waliendelea kuwepo hekaluni, wakimsifu Mungu.

Yohana

1

1Hapo mwanzo kulikuwako Neno, na Neno alikuwa pamoja na Mungu, na Neno alikuwa Mungu.2Huyu, Neno, Mwanzoni alikuwa pamoja na Mungu.3Vitu vyote vilifanyika kupitia yeye, na pasipo yeye hakuna hata kitu kimoja kilichokuwa kimefanyika.4Ndani yake kulikuwa uzima, na huo uzima ulikuwa nuru ya wanadamu wote.5Nuru yang'aa gizani, wala giza haikuishinda.

6Palikuwa na mtu aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.7Alikuja kama shahidi kushuhudia kuhusu ile nuru, ili kwamba wote waweze kuamini kupitia yeye.8Yohana hakuwa ile nuru, bali alikuja ili ashuhudie kuhusu ile nuru.9Huyo iliye nuru ya kweli na ambaye huwapa wanadamu wote nuru alikuwa yuaja duniani.

10Alikuwa katika dunia, na dunia iliumbwa kupitia yeye, ilhali dunia haikumjua.11Alikuja kwa watu wake, na watu wake hawakumpokea.12Bali kwa wale wote waliompokea, walioamini katika jina lake, aliwapa kibali cha kuwa wana wa Mungu.13Hawa walizaliwa, sio kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili, wala kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu mwenyewe.

14Neno alifanyika mwili na akaishi miongoni mwetu. Tumeuona utukufu wake, utukufu kama wa yule aliyekuja kutoka kwa Baba, akiwa amejaa neema na kweli.

15Yohana alishuhudia kumhusu, na akapaza sauti akisema, “Huyu ndiye niliye sema habari zake; ‘Ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa amekuwako kabla yangu.’16Kwa kuwa kutoka katika utimilifu wake, sisi sote tumepokea neema baada ya neema.17Kwa kuwa sheria ililetwa kupitia Musa. Neema na kweli vilikuja kupitia Yesu Kristo.18Hamna mwanadamu yeyote aliyewahi kumwona Mungu wakati wowote. Mungu mwana pekee, aliye katika upande wa Baba, amemfanya yeye ajulikane.”

19Na huu ndio ushuhuda wa Yohana wakati Makuhani na Walawi waliotumwa kwake na Wayahudi kumwuliza, “Wewe ni nani?”20Alikiri na hakukana, bali aliungama, “Mimi sio Kristo.”21Hivyo wakamuuliza, “Kwa hiyo wewe ni nani sasa? Wewe ni Eliya?” Akasema, “Mimi siye.” Wakasema, “Wewe ni nabii?” Akajibu, “Hapana.”22Kisha wakamwambia, “Wewe ni nani, ili kwamba tuwape jibu waliotutuma? Wajishuhudiaje wewe mwenyewe?”23Akasema, “Mimi ni sauti yake aliaye nyikani; ‘Inyosheni njia ya Bwana,’ kama nabii Isaya alivyosema.”

24Basi kulikuwa na watu wametumwa pale kutoka kwa Mafarisayo. Wakamuuliza na kusema,25“Kwa nini unabatiza basi kama wewe sio Kristo wala Eliya wala nabii?”26Yohana aliwajibu akisema, “Ninabatiza kwa maji. Hata hivyo, miongoni mwenu anasimama mtu msiyemtambua.27Huyu ndiye ajaye baada yangu. Mimi sistahili kulegeza kamba za viatu vyake.”

28Mambo haya yalitendeka huko Bethania, ng'ambo ya Yordani, mahali ambapo Yohana alikuwa akibatiza.

29Siku iliyofuata Yohana alimwona Yesu akija kwake akasema, “Tazama mwanakondoo wa Mungu aichukuae dhambi ya ulimwengu!30Huyu ndiye niliyesema habari zake nikisema, ‘Yeye ajaye nyuma yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’31Sikumtambua yeye, lakini ilifanyika hivyo ili kwamba afunuliwe katika Israeli, ndipo nikaja nikibatiza kwa maji.”

32Yohana alishuhudia, “Niliona Roho akishuka kutoka mbinguni mfano wa njiwa, na ilibaki juu yake.33Mimi sikumtambua lakini yeye aliyenituma ili nibatize kwa maji aliniambia, ‘Yule ambaye utaona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyo ndiye abatizaye kwa Roho Mtakatifu.’34Nimeona na nimeshuhudia kwamba huyu ni Mwana wa Mungu.”

35Tena siku iliyofuata Yohana alikuwa amesimama pamoja na wanafunzi wake wawili,36walimwona Yesu akitembea na Yohana akasema, “Tazama, Mwana kondoo wa Mungu!”37Wanafunzi wawili wakamsikia Yohana akisema haya wakamfuata Yesu.38Hapo Yesu aligeuka na kuwaona wanafunzi wale wakimfuata, na akawauliza, “Mnataka nini?” Wakajibu, “Rabbi, (maana yake ‘mwalimu,’ unaishi wapi?”39Akawaambia, “Njooni muone.” Kisha walikwenda na kuona mahali alipokuwa akiishi. Walikaa pamoja naye siku hiyo, kwa kuwa ilikuwa yapata kama saa kumi hivi.

40Mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana akiongea na kisha kumfuata Yesu alikuwa ni Andrea, ndugu yake Simoni Petro.41Akamwona ndugu yake Simoni na akamwambia, “Tumempata Masihi” (ambayo inatafsiriwa Kristo).42Akamleta kwa Yesu. Yesu akamtazama na akasema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana, utaitwa Kefa,” (maana yake ‘Petro’).

43Siku iliyofuata wakati Yesu alipotaka kuondoka kwenda Galilaya, alimpata Filipo na akamwambia, “Nifuate mimi.”44Filipo alikuwa ni mwenyeji wa Bethsaida, mji wa Andrea na Petro.45Filipo alimpata Nathanaeli na kumwambia, “Tumempata yule ambaye Musa aliandika habari zake katika sheria na Manabii. Yesu mwana wa Yusufu, kutoka Nazareti.”46Nathanaeli akamwambia, “Je kitu chema chaweza kutokea Nazareti?” Filipo akamwambia, Njoo na uone.”47Yesu akamwona Nathanaeli akija kwake na akasema, “Tazama, Mwisraeli kweli kweli asiye na udanganyifu ndani yake!”48Nathanaeli akamwambia, “Wanifahamuje mimi?” Yesu akajibu na akamwambia, “Kabla Filipo hajakuita ulipokuwa chini ya mtini, nilikuona.”49Nathanaeli akajibu, “Rabi wewe u Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”50Yesu akajibu akamwambia, “Kwa sababu nilikuambia ‘Nilikuona chini ya mtini,’ je waamini? Utaona matendo makubwa kuliko haya.”51Yesu akasema, “Amini, amini nawambieni. Mtaziona mbingu zikifunguka, na kuwaona malaika wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”

2

1Baada ya siku tatu, kulikuwa na arusi huko Kana ya Galilaya na mama yake Yesu alikuwa huko.2Yesu na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa katika arusi.3Wakati walipoishiwa na divai, mama yake Yesu akamwambia, “Hawana divai.”4Yesu akajibu, “Mwanamke kwa nini wanijia mimi? Muda wangu mimi bado haujatimia.”5Mama yake akawambia watumishi, “Chochote atakachowambia fanyeni.”6Basi kulikuwa na mitungi sita ya mawe pale iliyowekwa kwa ajili ya kunawa katika sikukuu za Wayahudi, kila moja lilikuwa na ujazo wa nzio mbili tatu.7Yesu akawaambia, “Ijazeni maji mitungi ya mawe.” Wakajaza hadi juu.8Kisha akawambia wale watumishi, “Chukueni kiasi sasa na mpeleke kwa muhudumu mkuu wa meza.” Wakafanya kama walivyoagizwa.9Mhudumu mkuu aliyaonja yale maji yaliyokuwa yamebadilika na kuwa divai, ila hakujua yalikotoka (lakini watumishi waliochota maji walijua yalikotoka). Kisha akamwita bwana harusi na10kumwambia, “Kila mmoja huanza kuwahudumia watu divai nzuri na wakiishalewa huwapa divai isiyo nzuri. Lakini wewe umeitunza divai nzuri hadi sasa”11Ishara hii ya Kana ya Galilaya, ilikuwa ndiyo mwanzo wa ishara za miujiza aliyoifanya Yesu, akifunua utukufu wake, hivyo wanafunzi wake wakamwamini.”

12Baada ya hii, Yesu, mama yake, ndugu zake na wanafunzi wake walienda katika mji wa Kapernaum na wakaa huko kwa siku chache.

13Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia, hivyo Yesu akaenda Yerusalemu.14Akawakuta wauzaji wa ng'ombe, kondoo, na njiwa ndani ya Hekalu. Pia na wabadilisha fedha walikuwa wameketi ndani ya Hekalu.15Yesu akatengeneza mjeledi wenye vifundo, akawatoa wote waliokuwemo katika hekalu, ikijumuisha ng'ombe na kondoo. Akamwaga fedha za wabadili fedha na kuzipindua meza zao.16Kwa wauzaji wa njiwa akawambia, “Toeni vitu hivi mbali na mahali hapa. Acheni kuifanya nyumba ya Baba yangu kuwa mahali pa soko.”17Wanafunzi wake wakakumbuka kuwa ilikuwa imeandikwa, ‘Wivu wa nyumba yako utanila.’

18Wakuu wa Kiyahudi wakajibu, wakamwambia, “Ni ishara ipi utakayoionyesha kwa sababu unayafanya mambo haya?”19Yesu akawajibu, “Libomoeni hekalu hili nami nitalijenga baada ya siku tatu.”20Kisha wakuu wa Wayahudi wakasema, “Ilichukua miaka arobaini na sita kujenga hekalu hili nawe unasema utalijenga kwa siku tatu?”21Ingawa, yeye aliongea hekalu akimaanisha mwili wake.22Hivyo baadaye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu, wanafunzi wake wakakumbuka kuwa alisema hivyo, wakaamini maandiko na kauli hii ambayo Yesu alikuwa amekwisha kuisema.

23Basi alipokuwa Yerusalemu wakati wa sikukuu ya Pasaka, watu wengi waliamini jina lake, walipoona ishara ya miujiza aliyoifanya.24Lakini Yesu hakuwa na imani nao kwa sababu aliwajua wanadamu wote.25Hakuhitaji mtu yeyote kumwambia kuhusu walivyo wanadamu kwa sababu alijua kilichokuwamo ndani yao.

3

1Basi palikuwa na Farisayo mmoja jina lake Nikodemo, na kiongazi wa Kiyahudi.2Alimjia Yesu usiku na kumwambia, “Rabi, twajua wewe ni mwalimu atokaye kwa Mungu, maana hamna mtu yeyote awezaye kufanya ishara hizi uzifanyazo asipokuwa Mungu yu pamoja naye.”3Yesu akamjibu, “Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”4Nikodemo akasema,” Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?”5Yesu akajibu, “Amini, amini mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.6Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.7Usishangae kwa sababu nilikuwambia, ‘ni lazima kuzaliwa mara ya pili.’8Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho.9Nikodemo akajibu, kwa kusema, “Mambo haya yawezekanaje?”10Yesu akamjibu, “Wewe u mwalimu wa Israeli, hata hauyajui mambo haya?11Amini, amini, nakuambia, twanena kile tunachokifahamu na twakishuhudia kile tulichokiona. Bali hampokei ushuhuda wetu.12Kama nimewambia mambo ya hapa duniani na hamuamini, mtawezaje kuamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni?13Maana hakuna aliyepanda kwenda juu mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka kutoka nbinguni, Mwana wa Adamu.14Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe,15ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele.

16Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele.17Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.18Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ashahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.19Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu.20Kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi.21Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu kwa Mungu.

22Baada ya haya, Yesu pamoja na wanafunzi walienda katika nchi ya Yudea. Huko alitumia muda pamoja nao na alikuwa akibatiza.

23Sasa Yohana pia alikuwa akibatiza huko Ainea karibu na Salim maana kulikuwa na maji mengi pale. Watu walikuwa wakija kwake na kubatizwa,24kwa kuwa Yohana alikuwa hajatupwa gerezani.25Kisha palitokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi kuhusu shughuli za utakaso.26Wakaenda kwa Yohana wakamwambia, “Rabi, yeye uliyekuwa naye ng'ambo ya mto Yorodani, yeye uliyeshuhudia habari zake, tazama, anabatiza na wote wanaenda wanamfuata.”27Yohana akajibu “Mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa kama amepewa kutoka mbinguni.28Ninyi wenyewe mwashuhudia kuwa nilisema kuwa, ‘Mimi sio Kristo,’ badala yake nilisema, ‘Nimetumwa mbele yake.’29Bibi arusi ni wa bwana arusi. Sasa rafiki wa bwana arusi, asimamaye na kusikiliza hufurahia sana kwa sababu ya sauti ya bwana arusi. Hii sasa ni furaha yangu iliyotimilika.30Anapaswa kuzidi, nami napaswa kupungua.

31Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote.32Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake.33Yeye aliye pokea ushuhuda wake amehakikisha kuwa Mungu ni mkweli.34Kwa maana yeye aliyetumwa na Mungu huongea maneno ya Mungu. Kwa kuwa Mungu hampi Roho kwa kipimo.35Baba humpenda Mwana na amempa vitu vyote mikononi mwake.36Yeye amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini kwa yeye asiye mtii Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hukaa juu yake.”

4

1Basi Yesu alipofahamu kuwa Mafarisayo wamesikia kuwa alikuwa anafuasa na kuwabatiza zaidi ya Yohana,2(ingawa Yesu mwenyewe alikuwa habatizi ila wanafunzi wake),3alitoka Judea na akaenda Galilaya.4Hivyo ilikuwa muhimu kupitia Samaria.5Na akafika kwenye mji wa Samaria, unaoitwa Sikari, karibu na eneo ambalo Yakobo alimpa mwanae Yusufu.6Na kisima cha Yakobo kilikuwa hapo. Yesu alikuwa amechoka kwa ajili ya safari na akakaa karibu na kisima. Ilikuwa muda wa saa sita mchana.7Mwanamke Msamaria alikuja kuteka maji, na Yesu akamwambia, “Nipe maji ninywe.”8Kwa sababu wanafunzi wake walikuwa wameenda zao mjini kununua chakula.9Yule mwanamke Msamaria akamwambia, “Inakuaje wewe Myahudi, kuniomba mimi mwanamke Msamaria, kitu cha kunywa?” Kwa sababu Wayahudi hawatangamani na Wasamaria.10Yesu akamjibu, “Kama ungelijua karama ya Mungu, na yule anayekuambia ‘Nipe maji,’ ungelimwomba, na angelikupa maji ya uzima.”11Mwanamke akajibu, “Bwana hauna ndoo ya kuchotea, na kisima ni kirefu. Utayapata wapi Maji ya Uzima?12Je wewe ni mkuu, kuliko baba yetu Yakobo, ambaye alitupa kisima hiki, na yeye mwenyewe na watoto wake pamoja na mifugo yake wakanywa maji ya kisima hiki?”13Yesu akajibu, “Yeyote anywae maji haya atapata kiu tena,14lakini yeye atakaye kunywa maji nitakayompa hatapata kiu tena. Badala yake maji nitakayompa yatakuwa chemchemi inayobubujika hata uzima milele.”15Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, nayaomba maji hayo ili nisipate kiu, na nisihangaike kuja hapa kuchota maji.”

16Yesu akamwambia, “Nenda kamwite mumeo, kisha urudi.”17Yule mwanamke akamwambia, “Sina mume.” Yesu akajibu, “Umesema vyema, ‘Sina mume,’18kwa maana ushakuwa na wanaume watano, na hata ambaye unaye sasa sio mume wako. Ambalo umelisema kweli!”

19Mwanamke akamwambia, “Bwana naona yakuwa wewe ni nabii.20Baba zetu waliabudu katika mlima huu. Lakini ninyi mwasema ya kuwa Yerusalemu ndiyo sehemu ambayo watu wanapaswa kuabudu.”21Yesu akamjibu, “Mwanamke, niamini, wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu wala Yerusalemu.22Ninyi watu mwaabudu kile msichokijua, lakini sisi twaabudu tunachokijua, kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi.23Hata hivyo, wakati waja, na sasa upo hapa, wakati waabuduo kweli watamwabudu Baba katika Roho na kweli, kwa sababu Baba anawatafuta watu wa namna hiyo kuwa watu wake wanao mwabudu.24Mungu ni Roho, na wale wanaomwabudu wanapaswa kumwabudu kwa Roho na kweli.”25Mwanamke akamwambia, “Ninajua kuwa Masihi anakuja, (aitwaye Kristo). Huyo atakapokuja atatwelezea mambo yote.”26Yesu akamwambia, “Mimi unayesema nami ndiye.”

27Wakati huo huo wanafunzi wake wakarudi. Nao walishangaa kwa nini alikuwa akizungumza na mwanamke, lakini hakuna aliyethubutu kumuuliza, “Unataka nini?” au “Kwa nini unazungumza naye?”

28Hivyo mwanamke akauacha mtungi wake wa maji na akaenda mjini na akawaambia watu,29“Njooni mwone mtu aliyeniambia mambo yangu yote niliyoyatenda, je yawezekana akawa ndiye Kristo?”30Wakatoka mjini wakaja kwa Yesu.

31Wakati huohuo, wanafunzi wake walimsihi wakisema, “Rabi kula chakula.”32Lakini yeye aliwambia, “Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi.”33Wanafunzi wakaambiana, hakuna aliyemletea kitu chochote kula. Je walileta?”34Yesu akawaambia, “Chakula changu ni kufanya mapenzi yake yeye aliyenituma na kutimiza kazi yake.35Je, hamsemi, ‘Bado miezi minne na mavuno yatakuwa tayari?’ Ninawaambieni, tazameni mashamba yalivyo tayari kwa mavuno!36Yeye avunaye hupokea mishahara na kukusanya matunda kwa ajili ya uzima wa milele, ili kwamba yeye apandaye naye avunaye wafurahi pamoja.37Kwa kuwa msemo huu ni wa kweli, ‘Mmoja apanda na mwingine avuna.’38Niliwatuma kuvuna ambacho hamkukihangaikia. Wengine wamefanya kazi na ninyi mmeingia katika furaha ya kazi yao.”

39Wasamaria wengi katika mji ule walimwamini kwa sababu ya taarifa ya yule mwanamke aliyekuwa akishuhudia, “Aliyeniambia mambo yote niliyoyafanya.”40Hivyo Wasamaria walipokuja walimsihi akae pamoja nao na akakaa kwao kwa siku mbili.41Na wengi zaidi wakamwamini kwa sababu ya neno lake.42Wakamwambia yule mwanamke, “Tunaamini sio tu kwa maneno yako, kwa sababu sisi wenyewe tumesikia, na sasa twafahamu kuwa hakika huyu ndiye mwokozi wa ulimwengu.”

43Baada ya siku hizo mbili, Yesu akaondoka na kuelekea Galilaya.44Kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa ametangaza kuwa nabii hana heshima katika nchi yake mwenyewe.45Alipokuja katika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha. Walikuwa wameona mambo yote aliyoyafanya Yerusalemu kwenye sikukuu, kwa sababu na wao pia walikuwa wamehudhuria kwenye sikukuu.46Alikuja tena Kana ya Galilaya huko alikoyabadilisha maji kuwa divai. Palikuwa na ofisa ambaye mwanaye alikuwa ni mgonjwa huko Kapernaumu.47Aliposikia kuwa Yesu alitoka Judea na kwenda Galilaya, alienda kwa Yesu na kumsihi ateremke amponye mwanawe, ambaye alikuwa karibu kufa.48Ndipo Yesu akamwambia, “Ninyi msipoona ishara na maajabu hamwezi kuamini.49Kiongozi akasema, “Bwana shuka chini kabla mwanangu hajafa.”50Yesu akamwambia, “Nenda, mwanao aishi.” Yule mtu akaamini neno alilolisema Yesu na akaenda zake.51Alipokuwa akishuka, watumishi wake walimpokea na kumwambia mwanaye alikuwa mzima.52Hivyo akawauliza ni muda gani alipata nafuu. Wakajibu, “Jana muda wa saa saba homa ilipomwacha.”53Ndipo baba yake akatambua kuwa ni muda ule ule Yesu aliosema, “Mwana wako ni mzima.” Hivyo yeye na familia yake wakaamini.

54Hii ilikuwa ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu alipotoka Yudea kwenda Galilaya.

5

1Baada ya hapo kulikuwa na sikukuu ya Wayahudi, na Yesu alipanda kwenda Yerusalemu.2Na kule Yerusalemu palikuwa na birika kwenye mlango wa kondoo, lililokuwa likiitwa kwa lugha ya Kiaramu Bethzatha, nalo lina matao matano.3Idadi kubwa ya wagonjwa ilikuwemo, vipofu, viwete, au waliopooza walikuwa wamelala katika matao hayo. 1 Kwa hakikia wakati fulani malaika alishuka ndani ya Bwana na kuyatibua maji.4Hivi kwamba, yule ambaye alikuwa wa kwanza kuingia ndani baada ya maji kutibuliwa alifanywa mzima kutokana na chochote kilichokuwa kimemshika kwa wakati huo.5Palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa ameugua kwa muda wa miaka thelathini na minane ndani ya matao.6Yesu alipomwona amelala ndani ya matao na baada ya kutambua kuwa amelala pale kwa muda mrefu, Yesu alimwambia, “Je unataka kuwa mzima?”7Yule mgonjwa akamjibu, “Bwana sina mtu, wa kuniweka katika birika wakati maji yanapotibuliwa. Wakati ninapokuja kuingia mtu mwingine hunitangulia.”8Yesu akamwambia, “Inuka na uchukue godoro lako na uende.”9Mara yule mtu akaponywa, akachukua kintanda chake na akaenda. Na siku hiyo ilikuwa siku ya Sabato.10Hivyo Wayahudi wakamwambia yule mtu aliyeponywa, “Leo ni siku ya Sabato, na hauruhusiwi kubeba godoro lako.”11Akajibu, yeye aliyeniponya ndiye aliyeniambia, “Chukua godoro lako na uende.”12Wakauliza, “Ni nani aliyekuambia, ‘Chukua godoro lako na uende?’”13Hata hivyo, yule aliyeponywa hakumjua, kwa sababu Yesu alikuwa ameondoka kwa siri. Kwa kuwa kulikuwa na umati katika sehemu hiyo.

14Baada ya hapo Yesu alimkuta yule mtu hekaluni na akamwambia, “Tazama, umepona! Usitende dhambi tena usije ukapatwa na jambo baya zaidi.”15Yule mtu akaenda na kuwataarifu Wayahudi kuwa Yesu ndiye aliyemponya.16Hivyo, kwa sababu ya mambo hayo Wayahudi walimtesa Yesu, kwa sababu alifanya mambo haya siku ya Sabato.17Yesu akawaambia, “Baba yangu anafanya kazi hata sasa nami nafanya kazi.”18Kwa sababu hiyo Wayahudi walizidi kumtafuta ili wamuue sio tu kwa sababu ya kuivunja Sabato, bali kwa kumwita Mungu Baba yake, akijifanya kuwa sawa na Mungu.

19Yesu akawajibu, “Amini, amini, Mwana hawezi kufanya kitu chochote isipokuwa kile ambacho amemwona Baba yake anakifanya, kwa kuwa chochote Baba akifanyacho ndicho na Mwana atakachofanya.20Kwa kuwa Baba ampenda Mwana, na amwonyesha kila kitu anachokifanya na atamwonyesha mambo makubwa kuliko haya ili kwamba mzidi kushangaa.”21Kwa kuwa kama vile ambavyo Baba awafufuavyo wafu na kuwapa uzima, halikadhalika Mwana pia humpa uzima yeyote apendaye.22Kwa kuwa Baba hamhukumu yeyote, bali amempa Mwana hukumu yote23ili kwamba wote wamuheshimu Mwana kama vile Mwana anavyomuheshimu Baba. Yeye asiyemuheshimu Mwana hamuheshimu Baba aliyemtuma.24Amini, amini, yeye asikiaye neno langu na kumwamini yeye aliyenituma anao uzima wa milele na hatahukumiwa. Badala yake, amepita kutoka mautini na kuingia uzimani.

25Amini, amini, nawaambia wakati unakuja na sasa upo ambao wafu watasikia sauti ya Mwana wa Mungu, na wote watakao sikia wataishi.26Kwa kuwa kama vile Baba alivyo na uzima ndani yake mwenyewe,27kadhalika amempa Mwana kuwa na uzima ndani yake, na Baba amempa Mwana mamlaka ili kwamba ahukumu kwa kuwa ni Mwana wa Adamu.28Msishangazwe na hili, kwa kuwa wakati unakuja ambao wafu wote waliomo makaburini wataisikia sauti yake29nao watatoka nje: waliotenda mema kwa ufufuo wa uzima, na walio tenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu.30Siwezi kufanya kitu chochote kutoka kwangu mwenyewe. Kama nisikiavyo, ndivyo ninavyo hukumu na hukumu yangu ni ya haki kwa kuwa sitafuti mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.

31Kama nikijishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu usingelikuwa wa kweli.32Kuna mwingine anayenishuhudia na ninajua kwa hakika ushuhuda anaonishuhudia ni wa kweli.33Mlituma watu kwa Yohana naye ameishuhudia kweli.34Hatahivyo, ushuhuda ninaoupokea hautoki kwa mwanadamu. Ninayasema haya ili kwamba mweze kuokolewa.35Yohana alikuwa ni taa iliyokuwa ikiwaka na kung'ara, na mlikuwa tayari kuifurahia kwa muda kitambo nuru yake.36Bali ushuhuda nilionao ni mkuu kuliko ule wa Yohana, kwa kuwa kazi ambazo Baba amenipa kuzikamilisha, hizo kazi nizifanyazo zashuhudia kuwa Baba amenituma.37Baba aliyenituma yeye mwenyewe ameshuhudia kuhusu mimi. Hamjawahi kusikia sauti yake wala kuona umbo lake wakati wowote.38Hamna neno lake linalokaa ndani yenu kwa kuwa hamumwamini yeye aliyetumwa.39Mnayachunguza maandiko mkidhani ndani yake mna uzima wa milele, na hayo maandiko yanashuhudia habari zangu na40wala hamtaki kuja kwangu ili mpate uzima wa milele.

41Sipokei sifa kutoka kwa watu,42lakini ninajua kuwa hamna upendo wa Mungu ndani yenu ninyi wenyewe.43Nimekuja kwa jina la Baba yangu, hamukuweza kunipokea. Kama mwingine akija kwa jina lake mngempokea.44Je mnawezaje kuamini ninyi ambao mnapokea sifa wenyewe kwa wenyewe lakini hamtafuti sifa itokayo kwa Mungu wa pekee?

45Msidhani mimi nitawashitaki mbele za Baba. Anayewashitaki ninyi ni Musa, ambaye ninyi mmeweka matumaini yenu kwake.46Kama mngekuwa mnamwamini Musa, mngeniamini mimi kwa sababu aliandika kuhusu mimi.47Kama hamuamini maandiko yake, mtawezaje kuamini maneno yangu?


1Zingatia: Maneno ya mstari wa 3 hayaonekani katika nakala nzuri za kale. “Wakisubiri maji kutibuliwa.”

6

1Baada ya mambo haya, Yesu alienda upande wa pili wa bahari ya Galilaya, pia huitwa bahari ya Tiberia.2Umati mkubwa ulikuwa ukimfuata kwa sababu waliona ishara alizozifanya kwa waliokuwa wagonjwa.3Yesu alikwea juu ya mlima na akakaa huko na wanafunzi wake.4(Na Pasaka, sikukuu ya Wayahudi ilikuwa imekaribia).5Yesu alipoinua macho yake juu na kuona umati mkubwa unakuja kwake, akamwambia Filipo, “Tutakwenda wapi kununua mikate ili hawa waweze kula?”6(Lakini Yesu aliyasema haya kwa Filipo kwa kumjaribu kwa kuwa yeye mwenyewe alijua atakachofanya).7Filipo akamjibu, “Hata mikate ya thamani ya dinari mia mbili isingelitosha hata kila mmoja kupata hata kipande kidogo.”8Andrea, mmoja wa wanafunzi wake ndugu yake Simoni Petro akamwambia9Yesu, “Kuna mvulana hapa ana mikate mitano ya shayiri na samaki wawili, lakini hii yafaa nini kwa watu wengi namna hii?”10Yesu akawaambia, “Waketisheni watu chini” (kulikuwa na nyasi nyingi mahali pale). Hivyo wanaume wapata elfu tano wakakaa chini.11Kisha Yesu akachukua ile mikate mitano akashukuru akawagawia wale waliokuwa wamekaa. Vivyo hivyo akawagawia samaki kwa kadiri ya vile wavyohitaji.12Watu waliposhiba, aliwambia wanafunzi wake, “Vikusanyeni vipande vya mabaki, vilivyobaki ili kwamba kisipotee chochote.”13Basi wakakusanya na kujaza vikapu kumi na viwili, vipande vya mikate mitano ya shayiri- vipande vilivyosazwa na wale waliokula.

14Kisha watu walipoona ishara hii aliyoifanya walisema, “Kweli huyu ndiye yule nabii ajaye ulimwenguni.”15Yesu alipotambua kuwa walikuwa wanataka kumkamata ili wamfanye kuwa mfalme wao kwa nguvu, alijitenga, na akaenda mlimani yeye peke yake.

16Ilipokuwa jioni, wanafunzi wake walishuka kwenda ziwani.17Wakapanda kwenye mtumbwi na walikuwa wakivuka kuelekea Kapernaumu. (Giza lilikuwa limeingia na Yesu alikuwa bado hajaja kwao).18Wakati huo upepo mkali ulikuwa ukivuma, na bahari ilikuwa ikiendelea kuchafuka.19Tena wanafunzi wake walipokuwa wamepiga makasia kama ishirini na matano au thelathini, wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari kuukaribia mtumbwi, na wakaogopa.20Lakini akawambia, “Ni mimi! Msiogope.”21Tena walikuwa tayari kumbeba kwenye mtumbwi, na mara mtumbwi ulifika kwenye nchi mahali walipokuwa wakienda.

22Siku iliyofuata, mkutano uliokuwa umesimama upande wa bahari waliona kuwa hakuna mtumbwi mwingine isipokuwa ule ambao Yesu na wanafunzi wake walikuwa hawajaupanda lakini wanafunzi wake walikuwa wameenda zao wenyewe.23(Ingawa, kulikuwa na baadhi ya mitumbwi iliyotoka Tiberia karibu na mahali walipokula mikate baada ya Bwana kutoa shukrani).24Wakati makutano walipotambua kuwa sio Yesu wala wanafunzi wake walikuwa kule, wao wenyewe walipanda ndani ya mitumbwi wakaenda Kapernaumu wakimtafuta Yesu.

25Baada ya kumpata upande mwingine wa ziwa wakamuuliza, “Rabi ulikuja lini huku?”26Yesu akawajibu, akawambia, “Amini, amini, mnanitafuta mimi, sio kwa sababu mliziona ishara, bali kwa sababu mlikula mikate na kushiba.27Acheni kukifanyia kazi chakula chenye kuharibika, bali mkifanyie kazi chakula kidumucho hata milele kile ambacho mwana wa Adamu atawapa, kwa kuwa Mungu Baba ameweka muhuri juu yake.”

28Kisha wakamwambia, “Ni nini tunapaswa kufanya ili kuzifanya kazi za Mungu?”29Yesu akajibu, “Hii ndiyo kazi ya Mungu: kwamba mmwamini yeye aliyemtuma.”30Basi wakamwambia, “Ni ishara zipi utakazofanya, kwamba tunaweza kuziona na kukuamini? Utafanya nini?31Baba zetu walikula manna jangwani, kama ilivyo andikwa, “Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.”

32Kisha Yesu akawajibu, “Amini, amini, sio Musa aliyewapa mkate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye awapaye mkate wa kweli kutoka mbinguni.33Kwa kuwa mkate wa Mungu ni ule ushukao kutoka mbinguni na kuupatia uzima ulimwengu.

34Basi wakamwambia, “Bwana tupatie huu mkate wakati wote.”35Yesu akawaambia, “Mimi ndiye mkate wa uzima, yeye ajaye kwangu hatapata njaa na yeye aniaminiye hatahisi kiu kamwe.”36Ingawa niliwaambia kwamba, mmeniona, na bado hamuamini.37Wote ambao Baba anaonipa watakuja kwangu, na yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.38Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni, sio kwa ajili ya kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenituma.39Na haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali nitawafufua siku ya mwisho.40Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Baba yangu, kwamba yeyote amtazamaye Mwana na kumwamini apate uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho.

41Kisha Wayahudi wakamnung'unikia kwa sababu alisema, “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.”42Wakasema, “Huyu siyo Yesu mwana wa Yusufu, ambaye baba yake na mama yake tunamfahamu? Imekuwaje sasa anasema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni?’”43Yesu akajibu, akawaambia, “Msinung'unikiane miongoni mwenu wenyewe.44Hakuna mtu ajaye kwangu asipovutwa na Baba yangu aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.45Kwa kuwa imeandikwa katika manabii, ‘Watafundishwa na Mungu.’ Kila aliyesikia na amejifunza kutoka kwa Baba, huja kwangu.46Sio kwamba kuna mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu- amemwona Baba.47Amini, amini yeye aaminiye anao uzima wa milele.48Mimi ni mkate wa uzima.49Mababa zenu walikula manna jangwani, na wakafa.50Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, ili kwamba mtu aule sehemu yake ili asife.51Mimi ni mkate uishio ambao umeshuka kutoka mbinguni. Kama mtu yeyote akila sehemu ya mkate huu, ataishi milele. Mkate nitakao utoa ni mwili wangu kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”

52Wayahudi wakakasirika wenyewe kwa wenyewe na wakaanza kubishana wakisema, “Mtu huyu anawezaje kutupa mwili wake tuule?”53Kisha Yesu akawaambia, “Amini, amini, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamta kuwa na uzima ndani yenu.54Yeyote aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.55Kwa kuwa mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.56Yeye aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami ndani yake.57Kama Baba mwenye uzima alivyonituma, na kama niishivyo kwa sababu ya Baba, vivyo hivyo yeye alae mwili wangu ataishi kwa sababu yangu.58Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, sio kama vile mababa walivyo kula wakafa. Yeye aulaye mkate huu ataishi milele.59Yesu aliyasema mambo haya ndani ya sinagogi alipokuwa akifundisha huko Kapernaumu.

60Ndipo wengi wa wanafunzi wake waliposikia haya, wakasema, “Hili ni fundisho gumu ni nani awezaye kulipokea?”61Yesu kwa sababu alijua ya kuwa wanafunzi wake walikuwa wakilinung'unikia jambo hili, akawambia, ‘Je, jambo hili linawakwaza?62Basi itakuaje mtakapomwona mwana wa Adamu akipaa kurudi alikokuwa kabla?63Ni Roho ndiye atoaye uzima. Mwili haufaidii kitu chochote. Maneno niliyoyasema kwenu ni Roho na ni uzima.64Bado kuna watu kati yenu wasioamini.” Kwa sababu Yesu alijua tangu mwanzo yule ambaye asiyeweza kuamini na yeye ambaye angemsaliti.

65Akawaambia, “Ni kwa sababu hii niliwambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amekubaliwa na Baba.”

66Baada ya haya wanafunzi wake wengi walirudi nyuma na hawakuambatana naye tena.67Yesu akawaambia wale kumi na wawili, “Je na ninyi mnataka kuondoka?”68Simoni Petro akamjibu, “Bwana twende kwa nani kwani wewe unayo maneno ya uzima wa milele,69na tumeamini na kujua kuwa wewe ni Mtakatifu wa Mungu.”70Yesu akawaambia, “Je mimi sikuwachagua ninyi, na mmoja wenu ni Ibilisi?”71Sasa alikuwa akiongea kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote, kwa kuwa alikuwa ni yeye akiwa mmoja wa wale kumi na wawili, ambaye ndiye angemsaliti Yesu.

7

1Na baada ya mambo haya Yesu alisafiri hivi katika Galilaya, kwa sababu hakupenda kwenda Uyahudi kwa sababu hakupenda kuingia Yudea maana Wayahudi walikuwa wakifanya mipango ya kumwua.2Sasa sikukuu ya Wayahudi, sikukuu ya Vibanda, ilikuwa karibu.3Ndipo ndugu zake walipomwambia, “Ondoka mahali hapa uende Uyahudi, ili kwamba wanafunzi wako vile vile wayaone matendo ufanyayo.4Hakuna afanyaye lolote kwa siri iwapo yeye mwenyewe anataka kujulikana wazi. Iwapo unafanya mambo haya, jionyeshe mwenyewe kwa ulimwengu.”5Maana ndugu zake pia hawakumwamini.6Ndipo Yesu alipowaambia, “Wakati wangu haujafika bado, lakini wakati wenu kila mara uko tayari.7Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, bali unanichukia mimi kwa sababu ninaushuhudia kuwa matendo yake ni maovu.8Pandeni kwenda katika sikukuu; mimi siendi katika sikukuu hii kwa sababu muda wangu haujatimilika bado.”9Baada ya kusema mambo hayo kwao, alibaki Galilaya.

10Hata hivyo, ndugu zake walipokuwa wamekwenda katika sikukuu, ndipo naye alienda, siyo kwa wazi bali kwa siri.11Wayahudi walikuwa wakimtafuta katika sikukuu na kusema, “Yuko wapi?”12Kulikuwa na majadiliano mengi miongoni mwa makutano juu yake. Wengine walisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walisema, “Hapana, huwapotosha makutano.”13Hata hivyo hakuna aliyezungumza wazi juu yake kwa kuwaogopa Wayahudi.

14Wakati sikukuu ilipofika katikati, Yesu alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.15Wayahudi wakawa wakishangaa na kusema, “Kwa jinsi gani mtu huyu anajua mambo mengi? Hajasoma kamwe.”16Yesu akawajibu na kuwaambia, “Mafundisho yangu siyo yangu, bali ni yake yeye aliyenituma.17Iwapo yeyote atapenda kufanya mapenzi yake yeye, atajua kuhusu mafundisho haya, kama yanatoka kwa Mungu, au kama ninazungumza kutoka kwangu mwenyewe.18Kila anayezungumza yatokayo kwake mwenywe hutafuta utukufu wake, bali kila atafutaye utukufu wake yeye aliyemtuma, mtu huyo ni wa kweli, na ndani yake hakuna kutotenda haki.19Musa hakuwapa nyinyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja kati yenu atendaye sheria. Kwa nini mnataka kuniua?

20Makutano wakajibu, “Una pepo. Nani anataka kukuua?”21Yesu akajibu na akawaambia, “Nimetenda kazi moja, nanyi nyote mmeshangazwa kwa sababu yake.22Musa aliwapa tohara (siyo kwamba inatoka kwa Musa, bali ile inatoka kwa mababa), na katika Sabato mnamtahiri mtu.23Iwapo mtu atapokea tohara katika siku ya Sabato ili kwamba sheria ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia mimi kwa sababu nimemfanya mtu kuwa mzima kabisa katika Sabato?24Msihukumu kulingana na mwonekano, bali hukumuni kwa hak

25Baadhi yao kutoka Yerusalemu wakasema, “Siye huyu wanayemtafuta kumwua?26Na tazama, anaongea wazi wazi, na hawasemi chochote juu yake. Haiwezi ikawa kwamba viongozi wanajua kweli kuwa huyu ni Kristo, inaweza kuwa?27Tunajua huyu mtu anatokea wapi. Kristo atakapokuja, hata hivyo, hakuna atakayejua wapi anakotoka.”

28Yesu akapaza sauti yake hekaluni, akifundisha na kusema, “Ninyi nyote mnanijua mimi na mnajua nitokako. Sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye aliyenituma ni wa kweli, na hamumjui yeye.29Ninamjua yeye kwa sababu nimetoka kwake na alinituma.”

30Walikuwa wanajaribu kumkamata, lakini hakuna hata mmoja aliyeinua mkono wake juu yake kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.31Hata hivyo, wengi katika makutano walimwamini. Walisema, “Kristo atakapokuja, atafanya ishara nyingi kuliko alizofanya mtu huyu?”32Mafarisayo waliwasikia makutano wakinong'onezana mambo haya kuhusu Yesu, na wakuu wa makuhani na Mafarisayo wakatuma maafisa ili kumkamata.

33Ndipo Yesu aliposema, “Bado kuna muda kitambo niko pamoja nanyi, na baadaye nitakwenda kwake yeye aliyenituma.34Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako, hamtaweza kuja.”35Kwa hiyo Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu atakwenda wapi kwamba tusiweze kumuona? Ataenda kwa waliotawanyika kati ya Wayunani na kuwafundisha Wayunani?36Ni neno gani hili alilolisema, ‘Mtanitafuta wala hamtaniona; kule niendako hamtamweza kuja’?”

37Sasa katika siku ya mwisho, siku kubwa ya sikukuu, Yesu alisimama akapaza sauti, akisema, “Ikiwa yeyote ana kiu, na aje kwangu anywe.38Yeye aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyosema, kutoka ndani yake itatiririka mito ya maji ya uzima.”39Lakini aliyasema haya kuhusu Roho, ambaye wao wamwaminio watampokea; Roho alikuwa bado hajatolewa kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa bado.

40Baadhi ya makutano, waliposikia maneno haya, walisema, “Kweli huyu ni nabii.”41Wengine walisema, “Huyu ni Kristo.” Lakini wengine walisema, “Lini, Kristo aweza kutoka Galilaya?42Maandiko hayajasema kuwa Kristo atatokea katika ukoo wa Daudi na kutoka Bethlehemu, kijiji ambacho Daudi alikuwa?43Hivyo, pale ukainuka mgawanyiko katikati ya makutano kwa ajili yake.44Wengine kati yao wangelimkamata, lakini hakuna aliyenyosha mikono yake juu yake.

45Ndipo wale maofisa wakarudi kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, nao wakawaambia, “Kwa nini hamjamleta?”46Maofisa wakajibu, “Hakuna mtu aliyewahi kuzungumza kama huyu kabla.”47Ndipo Mafarisayo walipowajibu, “Na nyinyi pia mmepotoshwa?48Kuna yeyote kati ya watawala anayemwamini, au yeyote wa Mafarisayo?49Bali hawa makutano wasiojua sheria - wamelaaniwa.”

50Nikodemo akawaambia (yeye aliyemwendea Yesu zamani, akiwa mmoja wa Mafarisayo),51“Je sheria yetu inamhukumu mtu isipokuwa amesikilizwa kwanza na kujua anachokifanya?”52Walijibu na kumwambia, “Na wewe pia unatokea Galilaya? Tafuta na uone kwamba hakuna nabii aliyetokea Galilaya.”

531 Kisha kila mtu alienda nyumbani kwake.


1Zingatia: Baadhi ya maneno ya Yohana 7:53 - 8:11 hayamo katika nakala bora za kale.

8

11 Yesu alienda mlima wa Mizeituni.2Mapema asubuhi akaja tena hekaluni, na watu wote wakamwendea; akakaa na kuwafundisha.3Waandishi na Mafarisayo wakamletea mwanamke aliyekamatwa katika kitendo cha kuzini. Wakamweka katikati.42 Ndipo wakamwambia Yesu, “Mwalimu, mwanamke huyu amekamatwa katika tendo uzinzi kabisa.5Sasa, katika sheria, Musa ametuamuru kuwapiga mawe watu kama hawa, unasemaje juu yake?6Walisema haya ili kumnasa ili kwamba wapate jambo la kumshitaki, lakini Yesu akainama chini akaandika katika ardhi kwa kidole chake.73 Walipoendelea kumwuliza maswali, alisimama na kuwaambia, “Yeye asiyekuwa na dhambi miongoni mwenu, awe wa kwanza kumpiga mawe.”8Akainama tena chini, akaandika katika ardhi kwa kidole chake.94 Waliposikia hayo, waliondoka mmoja mmoja, kuanzia aliye mzee. Mwishowe Yesu aliachwa peke yake, pamoja na mwanamke aliyekuwa katikati yao.10Yesu alisimama na kumwambia, “Mwanamke, waliokushitaki wako wapi? Hakuna hata mmoja aliyekuhukumu?”11Akasema, “Hakuna hata mmoja Bwana.” Yesu akasema, “Hata mimi sikuhukumu. Enenda. Kuanzia sasa na kuendelea usitende dhambi tena.”

12Tena Yesu akazungumza na watu akisema, “Mimi ni nuru ya ulimwengu; yeyote anifuataye hatatembea gizani bali atakuwa na nuru ya uzima.”13Mafarisayo wakamwambia, “Wajishuhudia mwenyewe; ushuhuda wako siyo wa kweli.”14Yesu alijibu akawaambia, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli. Ninajua mahali nilikotoka na kule ninakoenda, lakini ninyi hamjui mahali ninapotoka au kule ninakoenda.15Nyinyi mnahukumu kimwili; mimi simhukumu yeyote.16Mimi hata nikihukumu, hukumu yangu ni kweli kwa sababu siko peke yangu, bali niko pamoja na baba aliyenituma.17Ndiyo, na katika sheria yenu imeandikwa kwamba ushuhuda wa watu wawili ni kweli.18Mimi ndiye ninayejishuhudia, na Baba aliyenituma ananishuhudia.”

19Wakamwambia, “Baba yako yuko wapi?” Yesu akajibu, “Mimi hamnijui wala Baba yangu hammjui. Mngelikuwa mnanijua mimi, mngemjua na Baba yangu pia.”20Alisema maneno haya akiwa karibu na hazina alipokuwa akifundisha hekaluni, na hakuna hata mmoja aliyemkamata kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijafika.

21Basi akawaambia tena, “Ninaenda zangu; mtanitafuta na mtakufa katika dhambi zenu. Kule niendako, hamuwezi kuja.”22Wayahudi wakasema, “Atajiua mwenyewe, maana anasema, ‘Kule niendako hamuwezi kuja?’”23Yesu akawaambia, “Mnatoka chini; mimi natoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu.24Kwa hiyo, niliwaambieni kuwa mtakufa katika dhambi zenu. Vinginevyo muamini kuwa MIMI NDIYE, mtakufa katika dhambi zenu.”

25Kwa hiyo wakamwambia, “Wewe ni nani?” Yesu akawaambia, “Yale niliyowaambia tangu mwanzo.26Ninayo mambo mengi ya kuzungumza na kuhukumu juu yenu. Hata hivyo, yeye aliyenituma ni wa kweli; na mambo niliyoyasikia kutoka kwake, mambo haya nayasema kwa ulimwengu.”

27Hawakumuelewa kwamba alikuwa akiongea nao kuhusu Baba.28Yesu akasema, “Mtakapomwinua juu Mwana wa Mtu, ndipo mtakapojua kuwa MIMI NDIYE, na kwamba sifanyi lolote kwa nafsi yangu. Kama Baba alivyonifundisha, ninazungumza mambo haya.29Yeye aliyenituma yuko pamoja nami, na yeye hajaniacha peke yangu, kwani kila mara nafanya yale yanayompendeza.”30Wakati Yesu akisema mambo haya, wengi wakamwamini.

31Yesu akasema kwa wale Wayahudi waliomwamini, “Ikiwa mtakaa katika neno langu, ndipo mtakuwa wanafunzi wangu kweli,32nanyi mtaijua kweli, na kweli itawaweka huru.”33Walimjibu, “Sisi ni uzao wa Ibrahimu na kamwe hatujawahi kuwa chini ya utumwa wa yeyote; utasemaje, “Tutawekwa huru?”34Yesu aliwajibu, “Amini, amini, nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.35Mtumwa hakai nyumbani wakati wote; mwana hudumu siku zote.36Kwa hiyo, ikiwa Mwana atawaweka huru, mtakuwa huru kweli.”37Ninajua kwamba ninyi ni uzao wa Ibrahimu; mnatafuta kuniua kwa sababu neno langu halina nafasi ndani yenu.38Ninasema mambo ambayo nimeyaona pamoja na Baba yangu, na ninyi vile vile mnafanya mambo ambayo mliyasikia kutoka kwa baba yenu.”

39Walijibu na kumwambia, “Baba yetu ni Ibrahimu.” Yesu akawaambia, “Kama mngelikuwa watoto wa Ibrahimu, mngefanya kazi za Ibrahimu.40Hata sasa mnatafuta kuniua, mtu aliyewaambia ukweli kwamba nilisikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya hivi.41Mnafanya kazi za baba yenu.” Wakamwambia, “Hatukuzaliwa katika uzinzi, tunaye Baba mmoja, Mungu.”42Yesu akawaambia, “Ikiwa Mungu ni Baba yenu, mngenipenda mimi, kwa maana nimetoka kwa Mungu; wala sikuja kwa nafsi yangu, bali yeye alinituma.43Kwa nini hamyaelewi maneno yangu? Kwa sababu hamuwezi kuvumilia kuyasikia maneno yangu.44Ninyi ni wa baba yenu, shetani, na mnataka kuzitenda tamaa za baba yenu. Alikuwa mwuaji tangu mwanzo na hawezi kusimama katika kweli kwa sababu kweli haimo ndani yake. Anapoongea uongo, anaongea kutoka kwenye asili yake kwa sababu ni mwongo na baba wa uongo.45Hata sasa, kwa sababu ninasema iliyo kweli, hamniamini.46Ni nani kati yenu anayenishuhudia kuwa nina dhambi? Ikiwa ninasema iliyo kweli, kwa nini hamniamini?47Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu; ninyi hamyasikii kwa sababu ninyi si wa Mungu.”

48Wayahudi wakamjibu na kumwambia, hatujasema kweli kuwa wewe ni Msamaria na una pepo?”49Yesu akajibu, sina pepo; lakini namheshimu Baba yangu, nanyi hamniheshimu.50Sitafuti utukufu wangu; kuna mmoja atafutaye na kuhukumu.51Amini, amini, nawaambia, iwapo yeyote atalishika neno langu, hataona mauti kamwe.”

52Wayahudi wakamwambia, “Sasa tumejua kuwa una pepo. Ibrahimu na nabii walikufa; lakini unasema, ‘Ikiwa mtu atalishika neno langu, hataonja mauti.’53Wewe si mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu aliyekufa, sivyo? Manabii pia walikufa. Wewe wajifanya kuwa nani?”54Yesu akajibu, “Ikiwa nitajitukuza mwenyewe, utukufu wangu ni bure; ni Baba yangu anayenitukuza - yule mnayemsema kuwa ni Mungu wenu.55Ninyi hamjamjua yeye, lakini mimi namjua yeye. Ikiwa nitasema, ‘Simjui,’ nitakuwa kama nyinyi, muongo. Hata hivyo, ninamjua na maneno yake nimeyashika.56Baba yenu Abrahamu alishangilia alivyoiona siku yangu; aliiona na alifurahi.

57Wayahudi wakamwambia, “Haujafikisha umri wa miaka hamsini bado, nawe umemuona Ibrahimu?”58Yesu akawaambia, “Amini, amini, nawaambia, kabla Ibrahimu hajazaliwa, MIMI NIKO.”59Ndipo walichukua mawe wapate kumpiga, lakini Yesu alijificha na akatoka nje ya hekalu.


1Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7:53 - 8:11 hapo juu.
2Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7:53 - 8:11 hapo juu.
3Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7:53 - 8:11 hapo juu.
4Zingatia: Angalia ufafanuzi wa Yohana 7:53 - 8:11 hapo juu.

9

1Hata Yesu alipokuwa akipita, alimwona mtu kipofu tangu kuzaliwa kwake.2Wanafunzi wake wakamwuliza, “Rabi, nani aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu?”3Yesu akawajibu, “Siyo huyu mtu wala wazazi wake waliotenda dhambi, bali kazi za Mungu zipate kufunuliwa kupitia kwake.4Tunapaswa kufanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana. Usiku waja wakati ambapo hakuna atakayeweza kufanya kazi.5Wakati niwapo ulimwenguni, mimi ndimi nuru ya ulimwengu.”

6Baada ya Yesu kusema maneno haya, alitema mate kwenye ardhi, alifanya tope, na akampaka yule mtu lile tope machoni.7Akamwambia, nenda kaoge katika kisima cha Siloam (Inayotafsiriwa kama ‘aliyetumwa’).” Kwa hiyo huyo mtu alienda, akanawa, na akarudi, anaona.8Majirani wa yule mtu na wale waliomuona mwanzo kama mwombaji wakawa wanasema, Je! Huyu siye yule mtu aliyekuwa akikaa na kuomba?” Wengine walisema, “Ni yeye.”9Na wengine walisema, “Hapana, bali anafanana naye.” Lakini alikuwa akisema, “Ni mimi.”10Wakamwambia, “Basi macho yako yalifunguliwaje?”11Alijibu, “Mtu aitwaye Yesu alifanya tope na kupaka macho yangu na kuniambia, ‘Nenda Siloam ukanawe.’ Kwa hiyo nilienda, na nikanawa, na nikapata kuona tena.”12Wakamwambia, “Yuko wapi?” Alijibu, “Sijui.”

13Wakampeleka yule mtu aliyewahi kuwa kipofu kwa Mafarisayo.14Nayo ilikuwa siku ya Sabato wakati Yesu alipotengeneza tope na kuyafumbua macho yake.15Ndipo tena Mafarisayo wakamwuliza alipataje kuona. Aliwaambia, “Aliweka tope katika macho yangu, nikanawa, na sasa naweza kuona.”16Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Mtu huyu hajatoka kwa Mungu kwa sababu haishiki Sabato.” Wengine walisema, “Inawezekanaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo?” Kwa hiyo kukawa na mgawanyiko kati yao.17Ndipo wakamwuliza yule kipofu tena, “Unasemaje juu yake kwa sababu aliyafungua macho yako?” Kipofu akasema, “Ni nabii.”

18Hata wakati huu Wayahudi hawakumwamini kwamba alikuwa kipofu naye amepata kuona mpaka walipowaita wazazi wake yeye aliyepata kuona.19Waliwauliza wazazi, “Je, huyu ni mtoto wenu mnayesema alizaliwa kipofu? Amewezaje sasa kuona?”20Hivyo wazazi wake wakamjibu, “Tunajua kuwa huyu ni mtoto wetu na kwamba alizaliwa kipofu.21Jinsi gani sasa anaona, hatujui, na yeye aliyemfumbua macho yake, hatumjui. Mwulizeni yeye. Ni mtu mzima. Anaweza kujieleza mwenyewe.”22Wazazi wake walisema mambo haya, kwa sababu waliwaogopa Wayahudi. Kwa maana Wayahudi walikuwa wamekubaliana tayari kuwa, ikiwa yeyote atakiri kuwa Yesu ni Kristo, atatengwa na sinagogi.23Kwa sababu hii, wazazi wake walisema, “Ni mtu mzima, mwulizeni yeye.”

24Kwa hiyo kwa mara ya pili, walimwita yule mtu aliyewahi kuwa kipofu na kumwambia, “Mpe Mungu utukufu. Tunajua kwamba mtu huyu ni mwenye dhambi.”25Ndipo yule mtu alijibu, “Awe ni mwenye dhambi, mimi sijui. Kitu kimoja ninachokijua: nilikuwa kipofu, na sasa ninaona.”26Ndipo walipomwambia, “Amekufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?”27Alijibu, “Nimekwishawaambia tayari, na ninyi hamkusikiliza! Kwa nini mnataka kusikia tena? Nanyi hamtaki kuwa wanafunzi wake pia, sivyo?28Walimtukana na kusema, “Wewe ni mwanafunzi wake, lakini sisi ni wanafunzi wa Musa.29Tunajua kwamba Mungu alinena na Musa, lakini kwa huyu mtu, hatujui kule atokako.”30Yule mtu akajibu na kuwaambia, “Kwa nini, hili ni jambo la kushangaza, kwamba hamjui anakotoka, na bado ameyafumbua macho yangu.31Tunajua kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini ikiwa mtu yeyote anamwabudu Mungu na hufanya mapenzi yake, Mungu humsikiliza.32Tangu kuanza kwa ulimwengu haijawahi kamwe kusikiwa kwamba yeyote ameyafumbua macho ya mtu aliyezaliwa kipofu.33Ikiwa mtu huyu hakutoka kwa Mungu, asingelifanya chochote.”34Walijibu na kumwambia, “Ulizaliwa katika dhambi kabisa, na wewe unatufundisha sisi?” Ndipo walipomfukuza kutoka katika sinagogi.

35Yesu alisikia kwamba wamemwondoa kwenye sinagogi. Alimpata na kumwambia, “Unamwamini Mwana wa Mtu?”36Alijibu na kusema, “Ni nani, Bwana, ili nami nipate kumwamini?”37Yesu akamwambia, “Umeshamuona, naye unayezungumza naye ndiye.”38Yule mtu akasema, “Bwana, Naamini.” Ndipo akamsujudia.

39Yesu akasema, “Kwa hukumu nimekuja katika ulimwengu huu ili kwamba wale wasioona wapate kuona na wale wanaoona wawe vipofu.”40Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pamoja naye wakasikia maneno hayo na kumwuliza, “Na sisi pia ni vipofu?”41Yesu akawaambia, “Kama mngelikuwa vipofu, msingelikuwa na dhambi. Hata hivyo, sasa mnasema, ‘Tunaona,’ dhambi yenu inakaa.”

10

1Amini, amini nawaambieni, yule asiyeingia kwa kupitia mlango wa zizi la kondoo, lakini anapanda kwa njia nyingine, mtu huyo ni mwizi na mnyang'anyi.2Yeye aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo.3Kwake mlinzi wa mlango humfungulia. Kondoo waisikia sauti yake na huwaita kondoo zake kwa majina yao na kuwaongoza nje.4Atakapowatoa nje hao walio wake, huwatangulia, na kondoo humfuata, kwa sababu wanaijua sauti yake.5Hawatamfuata mgeni lakini badala yake watamuepuka, kwa sababu hawaijui sauti ya wageni.”

6Yesu alisema mfano huu kwao, lakini hawakuyaelewa mambo haya ambayo alikuwa akisema kwao.7Yesu akasema nao tena, “Amini, amini, nawaambia, Mimi ni mlango wa kondoo.8Wote walionitangulia ni wezi na wanyang'anyi, lakini kondoo hawakuwasikiliza.9Mimi ni mlango. Yeyote aingiaye kupitia kwangu, ataokolewa; ataingia ndani na kutoka, naye atajipatia malisho.10Mwizi haji isipokuwa kuiba, kuua, na kuangamiza. Nimekuja ili kwamba wapate uzima na wawe nao tele.

11Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.12Mtumishi aliyeajiriwa, na siyo mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, huwaona mbwa mwitu wakija huwaacha na kuwakimbia kondoo.13Na mbwa mwitu huwakamata na kuwatawanya. Hukimbia kwa sababu ni mtumishi wa kuajiriwa na hawajali kondoo.14Mimi ndimi mchungaji mwema, na ninawajua kondoo walio wangu, nao kondoo walio wangu wananijua mimi.15Baba ananijua, nami namjua Baba, nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.16Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Hao pia, yanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu ili kwamba pawepo na kundi moja na mchungaji mmoja.17Hii ndiyo sababu Baba ananipenda: Niutoe uhai wangu halafu niutwae tena.18Hakuna auchukuaye kutoka kwangu, lakini mimi nautoa mwenyewe. Ninayo mamlaka ya kuutoa, na ninayo mamlaka ya kuutwaa pia. Nimelipokea agizo hili kutoka kwa Baba.”

19Mgawanyiko tena ukatokea kati ya Wayahudi kwa sababu ya maneno haya.20Wengi wao wakasema, “Ana pepo na ni kichaa. Kwa nini mnamsikiliza?”21Wengine wakasema, “Haya siyo maneno ya mtu aliyepagawa na mapepo. Pepo linaweza kufungua macho ya kipofu?”

22Ndipo ikaja sikukuu ya Kuwekwa Wakfu Yerusalemu.23Ulikuwa wakati wa baridi, na Yesu alikuwa akitembea hekaluni katika ukumbi wa Selemani.24Ndipo Wayahudi walipomzunguka na kumwambia, “Mpaka lini utatuweka katika mashaka? Kama wewe ni Kristo, tuambie wazi.25Yesu akawajibu, “Nimekwisha waambia lakini hamuamini. Kazi nizifanyazo kwa jina la Baba yangu, hizo zinashuhudia juu yangu.26Hata hivyo hamuamini kwa sababu ninyi si kondoo wangu.27Kondoo wangu waisikia sauti yangu; Nawajua, nao wanifuata mimi.28Ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, na hakuna hata mmoja atakayewanyakuwa kutoka mkononi mwangu.29Baba yangu, aliyenipa hao, ni mkuu kuliko wengine wote, na hakuna hata mmoja awezaye kuwanyakua kutoka mkononi mwa Baba.30Mimi na Baba tu mmoja.”

31Wakabeba mawe ili wampige tena.32Yesu akawajibu, “Nimeshawaonesha kazi nyingi nzuri kutoka kwa Baba. Kwa kazi zipi kati ya hizo mnataka kunipiga mawe?”33Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa kazi yoyote iliyo nzuri, lakini kwa kukufuru, kwa sababu wewe, uliye mtu, unajifanya kuwa Mungu.”34Yesu akawajibu, “Haikuandikwa katika sheria yenu, ‘Nilisema, ninyi ni miungu?’35Ikiwa aliwaita miungu, kwa wale ambao Neno la Mungu liliwajilia (na Maandiko hayawezi kuvunjwa),36mnasema juu ya yule ambaye Baba alimtoa na kumtuma katika ulimwengu, ‘Unakufuru,’ kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu’?37“Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, msiniamini.38Hata hivyo, ikiwa ninazifanya, hata kama hamniamini, ziaminini kazi ili kwamba muweze kujua na kufahamu kwamba Baba yuko ndani yangu na mimi niko ndani ya Baba.”

39Wakajaribu tena kumkamata Yesu, lakini alienda zake kutoka mikononi mwao.

40Yesu akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani sehemu ambayo Yohana alikuwa akibatiza kwanza, na akakaa huko.41Watu wengi wakaja kwa Yesu huku wakisema, “Yohana kweli hakufanya ishara yoyote, lakini mambo yote aliyoyasema Yohana juu ya huyu mtu ni ya kweli.”42Watu wengi wakamwamini Yesu hapo.

11

1Basi mtu mmoja jina lake Lazaro alikuwa mgonjwa. Alitokea Bethania, kijiji cha Mariamu na dada yake Martha.2Alikuwa ni Mariamu yule yule aliyempaka Bwana marhamu na kumfuta miguu yake kwa nywele zake, ambaye ndugu yake Lazaro alikuwa ni mgonjwa.3Ndipo dada hawa walituma ujumbe kwa Yesu na kusema, “Bwana, angalia yule umpendaye ni mgonjwa.”4Yesu aliposikia alisema, “Ugonjwa huu si wa mauti, lakini, badala yake ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu ili kwamba Mwana wa Mungu apate kutukuzwa katika huo ugonjwa.”5Ikawa Yesu alimpenda Martha na dada yake na Lazaro.6Aliposikia kuwa Lazaro ni mgonjwa, Yesu alikaa siku mbili zaidi mahali alipokuwa.

7Ndipo baada ya hili aliwaambia wanafunzi wake, “Twendeni Yudea tena.”8Wanafunzi wakamwambia, “Rabi, Wayahudi walikuwa wakijaribu kukupiga mawe, na wewe unataka kurudi huko tena?”9Yesu akawajibu, “Saa za mchana si kumi na mbili? Mtu anapotembea mchana hawezi kujikwaa, kwa sababu anaona kwa mwanga wa ulimwengu huu.10Hata hivyo, ikiwa atatembea usiku, atajikwaa kwa sababu nuru haiko ndani yake.”

11Yesu akasema mambo haya, na baada ya mambo haya, akawaambia, “Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini ninakwenda ili kwamba nipate kumuamsha kutoka usingizini.”12Ndipo wanafunzi wakamwambia, “Bwana, kama amelala, ataamka.13Wakati huu Yesu alikuwa akizungumza habari za kifo cha Lazaro, lakini wao walidhani anazungumza juu ya kulala usingizi.14Ndipo Yesu akazungumza nao wazi wazi, “Lazaro amekufa.15Nina furaha kwa ajili yenu, kwamba sikuwepo kule ili kwamba mpate kuamini. Twendeni kwake.”16Basi Tomaso, aliyeitwa Pacha, aliwaambia wanafunzi wenzake, “Nasi twendeni pia tukafe pamoja na Yesu.”

17Wakati Yesu alipokuja, alikuta kwamba Lazaro tayari amekwishakuwa kaburini siku nne.18Nayo Bethania ilikuwa karibu na Yerusalemu kama kilomita mbili hivi.19Wengi kati ya Wayahudi wakaja kwa Martha na Mariamu kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.20Ndipo Martha aliposikia kuwa Yesu anakuja, alienda kukutana naye, lakini Mariamu aliendelea kukaa nyumbani.21Ndipo Martha akamwambia Yesu, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, kaka yangu asingelikufa.22Hata sasa, najua ya kuwa lolote utakaloomba kutoka kwa Mungu, atakupatia.”23Yesu akamwambia, kaka yako atafufuka tena.”24Martha akamwambia, najua kwamba atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.”25Yesu akamwambia, “Mimi ndimi ufufuo na uzima; yeye aniaminiye, ingawa atakufa, hata hivyo atakuwa anaishi;26na yeye aishiye na kuniamini mimi hatakufa. Unaamini hili?”27Akamwambia, “Ndiyo, Bwana naamini kwamba wewe ni Kristo, Mwana wa Mungu, yeye ajaye katika ulimwengu.”

28Alipokwisha kusema hili, alienda zake na kumwita dada yake Mariamu faraghani. Akasema, “Mwalimu yuko hapa na anakuita.”29Mariamu aliposikia haya, aliinuka kwa haraka na kwenda kwa Yesu.30Naye Yesu alikuwa hajaja bado ndani ya kijiji, bali alikuwa bado mahali alipokutana na Martha.31Ndipo Wayahudi waliokuwa na Mariamu katika nyumba na wale waliokuwa wakimfariji, walipomuona akiinuka haraka na kutoka nje, walimfuata; walidhani kuwa anaenda kaburini ili akalie huko.

32Wakati Mariamu, alipofika pale Yesu alipokuwa alimuona na, akaanguka chini ya miguu yake na kumwambia, “Bwana, kama ungelikuwa hapa, ndugu yangu asingelikufa.”33Yesu alipomuona analia, na Wayahudi waliokuja pamoja naye walikuwa wakilia pia, aliomboleza katika roho na kufadhaika;34akasema, “Mmemlaza wapi?” Wakamwambia, “Bwana, njoo utazame.”35Yesu akalia.36Ndipo Wayahudi wakasema, “Angalia alivyompenda Lazaro!”37Lakini wengine kati yao wakasema, “Siyo huyu, mtu aliyeyafumbua macho ya yule aliyekuwa kipofu, hakuweza kumfanya huyu mtu asife?”

38Ndipo Yesu, huku akiomboleza nafsini mwake tena, alienda kwenye kaburi. Sasa lilikuwa pango, na jiwe limewekwa juu yake.39Yesu akasema, “Liondoweni jiwe.” Martha, dada yake na Lazaro, yeye aliyekufa, akamwambia Yesu, “Bwana, kwa muda huu, mwili utakuwa umeoza, kwa sababu amekwishakuwa maiti kwa siku nne.”40Yesu akamwambia, “Mimi sikuwaambia ya kwamba, kama ukiamini, utauona utukufu wa Mungu?”

41Basi wakaliondoa jiwe. Yesu akainua macho yake juu na kusema, “Baba, nakushukuru kwa kuwa unanisikiliza.42Nilijua kwamba unanisikia mara zote, lakini ni kwa sababu ya kusanyiko ambalo limesimama kunizunguka kwamba nimesema haya, ili kwamba wapate kuamini kuwa wewe umenituma.”43Baada ya kusema haya, alilia kwa sauti kubwa, “Lazaro, toka nje!”44Mfu alitoka nje amefungwa mikono na miguu kwa sanda za kuzikia, na uso wake ulifungwa na kitambaa.” Yesu akawaambia, “Mfungueni mkamwache aende.”

45Ndipo Wayahudi wengi waliokuja kwa Mariamu na kuona Yesu alichofanya, walimwamini;46lakini baadhi yao walienda kwa Mafarisayo na kuwaambia mambo aliyoyafanya Yesu.47Ndipo wakuu wa Makuhani na Mafarisayo wakakusanyika pamoja katika baraza na kusema, “Tutafanya nini? Mtu huyu anafanya ishara nyingi.48Ikiwa tutamwacha hivi peke yake, wote watamwamini; Warumi watakuja na kuchukua vyote mahali petu na taifa letu.”

49Hata hivyo, mtu mmoja kati yao, Kayafa, aliyekuwa kuhani mkuu mwaka huo, akawaambia, “Hamjui chochote kabisa.50Hamfikirii kwamba yafaa kwa ajili yenu kwamba mtu mmoja yapasa kufa kwa ajili ya watu kuliko taifa lote kuangamia.”51Haya hakuyasema yakitoka kwake mwenyewe, badala yake, kwa kuwa alikuwa kuhani mkuu mwaka ule, alitabiri kwamba Yesu atakufa kwa ajili ya taifa;52na si kwa taifa peke yake, bali Yesu apate vile vile kuwakusanya watoto wa Mungu ambao wametawanyika sehemu mbali mbali.53Kwa hiyo kuanzia siku hiyo na kuendelea wakapanga namna ya kumwua Yesu.

54Yesu hakutembea tena wazi wazi kati ya Wayahudi, bali aliondoka hapo na kwenda nchi iliyo karibu na jangwa katika mji uitwao Efraimu. Hapo alikaa na wanafunzi.

55Basi Pasaka ya Wayahudi ilikuwa karibu, na wengi wakapanda kwenda Yerusalemu nje ya mji kabla ya Pasaka ili wapate kujitakasa wenyewe.56Walikuwa wakimtafuta Yesu, huku kuzungumza mmoja kwa mwingine walipokuwa wamesimama hekaluni, “Mnafikiri nini? Kwamba hatakuja katika sikukuu?”57Wakati huu wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikuwa wametoa amri kwamba ikiwa mmoja atajua Yesu alipo, anapaswa kutoa taarifa ili kwamba wapate kumkamata.

12

1Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu.2Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi mezani pamoja na Yesu.3Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.

4Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi wake, ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,5“Kwanini manukato haya yasingeuzwa kwa dinari mia tatu na wakapewa maskini?”6Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.7Yesu alisema, “Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.8Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote.”

9Basi umati mkubwa wa Wayahudi walipata kujua ya kuwa Yesu yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila wamwone na Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka katika wafu.10Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri ili wamue Lazaro;11maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walienda zao na wakamwamini Yesu.

12Na siku iliyofuata umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,13walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli.”14Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,
15“Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.”

16Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.

17Basi lile kundi la watu waliokuwepo pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, wakashuhudia kwa wengine.18Na ilikuwa kwa sababu hii pia kwamba kundi la watu walikwenda kumlaki kwasababu walisikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.19Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, “Tazama, sasa hamwezi kufanya lolote; tazama, ulimwengu umekwenda kwake.”

20Sasa baadhi ya Wayunani walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakienda kuabudu kwenye sikukuu.21Hawa walimwendea Filipo, ambaye alitoka Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, “Bwana, sisi tunatamani kumwona Yesu.”22Filipo akaenda akamwambia Andrea; Andrea na Filipo wakaenda na kumwambia Yesu.23Yesu akawajibu akasema, “Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.24Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa mazao mengi.25Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele.26Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.

27Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? ‘Baba, uniokoe katika saa hii’? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii.28Baba, ulitukuze jina lako.” Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, “Nimelitukuza nami nitalitukuza tena.”29Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, “Malaika amesema naye.”30Yesu akajibu na kusema, “Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.31Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje.32Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.”33Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.

34Mkutano wakamjibu, “Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, ‘Mwana Adamu lazima ainuliwe juu?’ Huyu Mwana wa Mtu ni nani?”35Basi Yesu akawaambia, “Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Tembeeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendeaye gizani hajui aendako.36Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.37Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini38ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: “Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”39Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,40“Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya.”

41Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.

42Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakafurushwa kutoka kwa sinagogi.43Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.

44Yesu akapaza sauti na kusema, “Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi,45naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma.46Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.

47Ikiwa mtu yeyote atayasikia maneno yangu lakini asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.48Yeye anikataye mimi na asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.49Maana mimi sikunena kwa nafsi yangu tu. Bali ni Baba aliyenituma, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.50Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi - kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao.”

13

1Sasa kabla ya sikukuu ya pasaka, kwa sababu Yesu alifahamu kuwa saa yake imefika ambayo atatoka katika dunia hii kwenda kwa baba, akiwa amewapenda watu wake ambao walikuwa duniani, aliwapenda mpaka mwisho.2Ikawa tayari Ibilisi alikuwa amewaka katika moyo wa Yuda Isikariote, mwana wa simoni, kumsaliti Yesu.3Yesu alifahamu kuwa baba ameweka vitu vyote katika mikono yake na kwamba ametoka kwa Mungu na alikuwa anakwenda tena kwa Mungu.4Aliamka chakulani na akatandika chini vazi lake la nje. Kisha alichukua taulo na akajifunga mwenyewe.5Kisha akatia maji katika bakuli na akaanza kuwaosha miguu wanafunzi wake na kuwafuta na taulo ambayo alijifunga yeye mwenyewe.

6Akaja kwa Simoni Petro, na Petro akamwambia, “Bwana, unataka kuniosha miguu yangu?”7Yesu akajibu na kumwambia, “Nifanyalo hulijui sasa, lakini utaelewa baadaye.”8Petro akamwambia, “Hutaniosha miguu yangu kamwe.” Yesu akamjibu, “Ikiwa sitakuosha, hutakuwa na sehemu pamoja nami.”9Simoni Petro akamwambia, “Bwana, usinioshe miguu yangu tuu, bali pia na mikono na kichwa changu.”10Yesu akamwambia, “Yeyote ambaye amekwisha kuoga haitaji kuoga isipokuwa miguu yake, na amekuwa safi mwili wake wote; ninyi mmekuwa safi, lakini si nyote.”11Kwa kuwa Yesu alijua yule atakaye msaliti; hii ndiyo sababu alisema, si nyote mmekuwa safi.”

12Wakati Yesu alipokuwa amewaosha miguu yao na akiisha chukua vazi lake na kukaa tena, aliwaambia, “Je mnaelewa kile ambacho nimewafanyia?13Mnaniita mimi “Mwalimu” na “Bwana,” hii mnasema kweli, maana ndivyo nilivyo.14Ikiwa mimi Bwana na mwalimu, nimewaosha miguu yenu, ninyi pia imewapasa kuwaosha wenzenu miguu.15Kwa kuwa nimewapa mfano ili kwamba ninyi pia mfanye kama mimi nilivyo fanya kwenu.16Amini, Amini, nawambia, mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala yule ambaye ametumwa si mkuu kuliko yule aliye mtuma.17Ikiwa unafahamu mambo haya, umebarikiwa ukiyatenda.18Sisemi kuhusu ninyi nyote, kwa kuwa nawajua wale ambao nimewachagua - bali nasema haya ili kwamba maandiko yaweze kutimilizwa: ‘Yeye alaye mkate wangu ameniinulia kisigino chake.’

19Ninawambia hili sasa kabla halijatokea ili kwamba litakapotokea, muweze kuamini kuwa mimi NDIYE.20“Amini, amini, nawambia, anipokeaye mimi humpokea ambaye nina mtuma, na yule anipokeaye mimi humpokea yule aliye nituma mimi.”

21Wakati Yesu aliposema haya, alisumbuka rohoni, alishuhudia na kusema, “Amini, amini, nawambia kwamba mmoja wenu atanisaliti.”22Wanafunzi wake wakatazamana, wakishangaa ni kwa ajili ya nani alizungumza.23Kulikuwa katika meza, mmoja wa wanafunzi wake ameegama kifuani mwa Yesu yule ambaye Yesu alimpenda.24Simoni Petro alimuuliza mwanafunzi huyu na kusema, “Twambie ni yupi ambaye kwake anazungumza.”25Mwanafunzi yule aliye egama kifuani mwa Yesu na akamwambia, “Bwana, ni nani?”26Kisha Yesu alijibu, “Ni kwake yule nitakaye chovya kipande cha mkate na kumpatia.” Hivyo alipo kuwa amechovya mkate, alimpatia Yuda mwana wa Simon Iskariote.27Na baada ya mkate, Shetani alimuingia. Kisha Yesu akamwambia, “Kile ambacho unataka kukifanya ukifanye haraka.”28Sasa hakuna mtu katika meza alijua sababu ya Yesu kusema jambo hili kwake.29Baadhi yao walidhani kwamba, kwa sababu Yuda alishika mfuko wa fedha, Yesu alimwambia, “Nunua vitu tunavyohitaji kwa ajili ya sikukuu,” au kwamba anapaswa kutoa kitu kwa masikini.30Baada ya Yuda kupokea mkate, alitoka nje haraka; na ilikuwa usiku.

31Wakati Yuda alipokuwa ameondoka, Yesu alisema, “Sasa mwana wa Adam ametukuzwa, na Mungu ametukuzwa katika yeye.32Mungu atamtukuza katika yeye mwenyewe, na atamtukuza mara moja.

33Watoto wadogo, niko pamoja nanyi kitambo kidogo. Mtanitafuta, na kama nilivyowambia Wayahudi, ‘Niendako, hamuwezi kuja.’ Sasa nawambia ninyi, pia.34Ninawapa amri mpya, kwamba mpendane; kama mimi nilivyo wapenda ninyi, vivyo hivyo nanyi pia imewapasa kupendana ninyi kwa ninyi.35Kwa ajili ya hili watu watatambua kuwa ninyi ni wanafunzi wangu, ikiwa mna upendo kwa kila mmoja na mwingine.”

36Simoni Petro alimwambia, “Bwana, unakwenda wapi?” Yesu akajibu, “Mahali ninapokwenda kwa sasa hutaweza kunifuata, lakini utanifuata baadaye.”37Petro akamwambia, “Bwana, kwa nini nisikufuate hata sasa? Mimi nitayatoa maisha yangu kwa ajili yako.”38Yesu akajibu, “Je utayatoa maisha yako kwa ajili yangu? Amini amini nakwambia, jogoo hatawika kabla hujanikana mara tatu.”

14

1“Usiruhusu moyo wako kuwa katika mahangaiko. Unamwamini Mungu niamini pia na mimi.2Katika nyumba ya Baba yangu kuna makazi mengi; kama isingekuwa hivyo, ningekuwa nimekuambia, kwa vile ninakwenda kukuandalia mahali kwa ajili yako.3Kama nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena kuwakaribisha kwangu, ili mahali nilipo pia nanyi muwepo.4Mnajua njia mahali ninakoenda.”

5Tomaso alimwambia Yesu, “Bwana, hatujui mahali unakoenda; Je! Tunawezaje kuijua njia?6Yesu alimwambia, “Mimi ndiye njia, kweli, na uzima; hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwangu.7Kama mngeli nijua mimi, mngalikuwa mnamjua na Baba yangu pia; kuanzia sasa na kuendelea mnamjua na mmeshamuona yeye.”

8Filipo alimwambia Yesu, “Bwana, tuonyeshe Baba, na hivyo itakuwa imetutosha.”9Yesu akamwambia, “Sijakuwa pamoja nanyi kwa muda mrefu, na bado hunijui mimi, Filipo? Yeyote aliyeniona mimi amemwona Baba; Jinsi gani unasema, ‘Tuonyeshe Baba?’10Hamuamini kuwa mimi ni ndani ya Baba, na Baba yu ndani yangu? Maneno ninayoyasema kwenu sisemi kwa kusudi langu mwenyewe; badala yake, ni Baba anayeishi ndani yangu anayetenda kazi yake.11Niamini mimi, kwamba niko ndani ya Baba, na Baba yuko ndani yangu; kadhalika niamini mimi kwa sababu ya kazi zangu hasa.12Amini, amini, nawaambia, yeye aniaminiye, mimi kazi zile nizifanyazo, atazifanya kazi hizi pia; na atafanya hata kazi kubwa kwasababu ninakwenda kwa Baba.13Chochote mkiomba katika jina langu, nitafanya ili kwamba Baba aweze kutukuzwa katika Mwana.14Nanyi mkiomba kitu chochote katika jina langu, hilo nitafanya.

15Kama mkinipenda, mtazishika amri zangu.16Na nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine ili kwamba aweze kuwa pamoja nanyi milele,17Roho wa kweli. Ulimwengu hauwezi kumpokea yeye kwa sababu haumuoni, au kumjuwa yeye. Hata hivyo ninyi, mnamjua yeye, kwani anakaa pamoja nayi na atakuwa ndani yenu.18Sitawaacha kama yatima, nitarudi kwenu.19Kwa muda kidogo, ulimwengu hautaniona tena, lakini ninyi mwaniona. Kwa sababu ninaishi, nanyi mtaishi pia.20Katika siku hiyo mtajua kwamba mimi niko ndani ya Baba, na kwamba ninyi mko ndani yangu, na kwamba mimi niko ndani yenu.21Yeyote azishikaye amri zangu na kuzitenda, ndiye ambaye anipenda mimi; na ambaye anipenda mimi atapendwa na Baba yangu, na nitampenda na nitajionyesha mimi mwenyewe kwake.”

22Yuda (siyo Iskariote) akamwambia Yesu, “Bwana, Je! Ni nini kinatokea kwamba utajionyesha mwenyewe kwetu na siyo kwa ulimwengu?23Yesu alijibu akamwambia, “Kama yeyote akinipenda, atalishika neno langu. Baba yangu atampenda, na tutakuja kwake na tutafanya makao yetu pamoja naye.24Yeyote ambaye hanipendi mimi, hashiki maneno yangu. Neno ambalo mnasikia siyo langu bali la Baba ambaye alinituma.25Nimeyasema mambo haya kwenu, wakati bado ninaishi miongoni mwenu.26Hata hivyo, Mfariji, Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha mambo yote na atawafanya mkumbuke yote ambayo niliyasema kwenu.27Amani nawapa amani yangu ninyi. Siwapi hii kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyo yenu wala msiwe na woga.

28Mlisikia vile nilivyowaambia, ‘Ninaenda zangu, na nitarudi kwenu.’ Kama mngelinipenda mimi, mngekuwa na furaha kwa sababu ninakwenda kwa Baba, kwa kuwa Baba ni mkuu kuliko mimi.29Sasa nimekwisha kuwaambia kabla haijatokea ili kwamba, wakati ikitokea, mweze kuamini.30Sitaongea nanyi maneno mengi, kwa kuwa mkuu wa dunia hii anakuja. Yeye hana nguvu juu yangu,31lakini ili kwamba ulimwengu upate kujua kwamba nampenda Baba, nafanya ambacho Baba ananiagiza mimi, kama vile alivyonipa amri. Inukeni, na tutoke mahali hapa.

15

1Mimi ni mzabibu wa kweli, na baba yangu ndiye mkulima.2Kila tawi ndani yangu ambalo halizai tunda, huliondoa na husafisha kila tawi ambalo huzaa ili kwamba liweze kuzaa matunda zaidi.3Ninyi tayari mmekuwa safi kwa sababu ya ujumbe ambao nimekwisha waambia.4Mkae ndani yangu, na mimi ndani yenu. Kama tawi lisivyoweza kuzaa peke yake lisipo kuwa katika mzabibu, vivyo hivyo nayi, msipo kaa ndani yangu.

5Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi. Yeyote anayedumuye ndani yangu na mimi ndani yake, yeye huzaa matunda mengi, kwa kuwa pasipo mimi hamuwezi kufanya jambo lolote.6Ikiwa mtu yeyote hatasalia ndani yangu, hutupwa kama tawi na kukauka; watu hukusanya matawi na kuyatupa katika moto, na kuteketea.7Ikiwa mtadumu ndani yangu, na kama maneno yangu yakidumu ndani yenu, ombeni lolote mtakalo, nanyi mtafanyiwa.8Katika hili baba yangu ametukuzwa, kwamba mnazaa matunda mengi na kwa hili mnadhihirisha kwamba ni wanafunzi wangu.

9Kama baba yangu alivyonipenda mimi, mimi pia nimewapenda ninyi; dumuni katika pendo langu.10Ikiwa mtashika amri zangu, mtadumu katika pendo langu kama nilivyo shika amri za baba yangu na kudumu katika pendo lake.11Nimesema mambo haya kwenu ili kwamba furaha yangu iwe ndani yenu na ili kwamba furaha yenu ifanyike kuwa timilifu.12Hii ndiyo amri yangu, kwamba mpendane ninyi kwa ninyi kama nilivyo wapenda ninyi.13Hakuna mtu aliye na upendo mkuu kuliko huu, kwamba ayatoe maisha yake kwa ajiliya rafiki zake.14Ninyi ni rafiki zangu ikiwa mtafanya yale niwaagizayo.15Siwaiti watumwa, kwa kuwa mtumwa hajui kile afanyacho bwana wake. Nimewaita ninyi marafiki, kwa kuwa nimewajulisheni mambo yote ambayo nimeyasikia kutoka kwa Baba.16Hamkunichagua mimi, bali mimi niliwachagua ninyi na kuwaweka mwende mzae matunda, na tunda lenu lipate kukaa. Hili liko hivi ili kwamba chochote muombacho kwa Baba kwa jina langu, atawapeni.17Mambo haya ninawaagiza, kwamba mpendane kila mtu na mwenzake.

18Kama ulimwengu utawachukia, mjuwe kwamba ulinichukia mimi kabla haujawachukia ninyi.19Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda kama wa kwao. Lakini kwa sababau ninyi sio wa ulimwengu na kwa sababu niliwachagua kutoka katika ulimwengu, ni kwa ajili hii ulimwengu huwachukia.20Kumbukeni neno ambalo niliwaambia, ‘Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake.’ Ikiwa walinitesa mimi, watawateseni ninyi pia; Kama walishika neno langu, watalishika la kwenu pia.21Watawatenda mambo haya yote kwa ajili ya jina langu kwa sababu hawamjui yule aliyenituma.22Kama nisingekuja na kuwaambia, wasingalikuwa na dhambi; lakini sasa hawana udhuru kwa dhambi yao.23Anichukiaye mimi humchukia Baba pia.24Ikiwa sijafanya kazi miongoni mwao ambayo hapana mmoja aliyeifanya, wangelikuwa hawana dhambi; lakini sasa wamefanya yote mawili wameona na wamenichukia mimi na Baba yangu.25Hili linatokea ili kwamba neno litimie ambalo limeandikwa katika sheria yao: ‘Wananichukia mimi bila sababu.’

26Wakati mfariji amekuja, ambaye nitamtuma kwenu kutoka kwa Baba, huyu ndiye, Roho wa kweli, ambaye anatokea kwa Baba, atanishuhudia.27Ninyi pia mnanishuhudia kwa sababu mmekuwa pamoja nami tangu mwanzo.

16

1Nimewaambia mambo haya ili msiweze kukwazwa.2Watawatoa nje ya masinagogi; hakika saa inakuja ambayo kila atakayewaua atafikiri kuwa anafanya kazi njema kwa ajili ya Mungu.3Watawatendea mambo haya kwa sababu hawamfahamu Baba wala mimi.4Nimewaambia mambo haya ili kwamba wakati wa haya kutokea ukifika, mtakumbuka jinsi nilivyowaambia. Sikuwaambia kuhusu mambo haya tangu mwanzo kwa sababu nilikuwa pamoja nanyi.

5Sasa naenda kwa yule aliyenituma; lakini hakuna kati yenu anayeniuliza, “Unaenda wapi?”6Kwa sababu nimesema maneno haya kwenu, huzuni imejaa mioyoni mwenu.7Hata hivyo, nawaambia ukweli: ni vyema kwenu nikiondoka; kwa maana nisipoondoka, mfariji hatakuja kwenu; lakini nikienda ntamtuma kwenu.8Atakapokuja, mfariji atauthibitishia ulimwengu dhambi, utauwa na hukumu.9Kuhusiana na dhambi, kwa sababu hawakuniamini,10kuhusiana na utauwa, kwa maana naenda kwa baba,11na kuhusiana na hukumu kwa sababu mkuu wa dunia hii ashahukumiwa.

12Ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamtayaelewa sasa.13Lakini, yeye, Roho wa kweli, akija, atawaongoza katika kweli yote; kwa kuwa hataongea kwa ajili yake mwenyewe; lakini yoyote atakayoyasikia, atayasema mambo hayo; na atawajulisha juu ya mambo yatakayokuja.14Yeye atanitukuza mimi, kwa sababu atayachukua mambo yangu na atayatangaza kwenu.15Vitu vyote alivyonavyo Baba ni vyangu; kwa hiyo, nimesema kwamba Roho atachukua mambo yangu na atayadhihirisha kwenu.

16Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi tena, mtaniona.”17Baadhi ya wanafunzi wake wakaambiana, “Ni nini anachotuambia, “Muda mfupi, na hamtaniona tena,’ na, kisha, mda mfupi mtaniona,’ na, ‘Kwa sababu naenda kwa Baba?”18Kwa hiyo wakasema, “Ni kitu gani anachosema, ‘Bado mda mfupi?’ Hatujui asemavyo.”

19Yesu aliona kuwa walitamani kumuuliza, naye akawaambia, “Mnajiuliza wenyewe kuhusu hili, nilivyosema, ‘Bado muda mfupi, hamtaniona tena; na baada ya muda mfupi mtaniona?’20Amini, amini, nawaambia, mtalia na kuomboleza, lakini ulimwengu utashangilia, mtakuwa na huzuni lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha.21Mwanamke anakuwa na huzuni wakati anapokuwa na uchungu kwa sababu wakati wa kujifungua umefika; lakini anapojifungua mtoto, hakumbuki tena maumivu kwa sababu ya furaha yake kwamba mtoto amezaliwa duniani.22Ninyi pia mna huzuni sasa, lakini nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi na hakuna atakayeweza kuiondoa furaha yenu.23Siku hiyo hamtaniuliza maswali. Amini, Amini, nawaambia, mkiomba lolote kwa Baba, atawapa kwa jina langu.24Mpaka sasa hamjaomba lolote kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapokea ili kwamba furaha yenu itimilike.

25Nimezungumza na ninyi kwa lugha isiyoeleweka, lakini saa inakuja ambapo sitazungumza kwa lugha isiyoeleweka lakini badala yake nitawaambia waziwazi kuhusu Baba.26Siku hiyo mtaomba kwa jina langu, na siwaambii kwamba nitaomba kwa Baba kwa ajili yenu;27Kwa kuwa Baba mwenyewe anawapenda kwa sababu mmenipenda mimi na kwa sababu mmeniamini kuwa nimetoka kwa Baba.28Nilitoka kwa Baba na nimekuja ulimwenguni; tena, naondoka ulimwenguni na ninaenda kwa Baba.”

29Wanafunzi wake wakamwambia, “Unaona, sasa unaongea wazi wazi na hautumii mafumbo.30Sasa, tunajua kwamba unajua mambo yote, na hauhitaji mtu yoyote akuulize maswali. Kwa sababu hii tunaamini kuwa unatoka kwa Mungu.

31Yesu akawajibu, “Sasa mmeamini?”32Tazama, saa inakuja, ndiyo na hakika imefika, ambapo mtatawanyika kila mmoja na kwao mtaniacha mwenyewe. Lakini siko peke yangu kwa sababu Baba yupo nami.33Nawaambia mambo haya ili kwamba ndani yangu muwe na amani. Duniani mna matatizo, lakini jipeni moyo, nimeushinda ulimwengu.

17

1Yesu aliyasema mambo haya; kisha akainua macho yake kuelelea mbinguni na akasema, “Baba, saa imewadia; mtukuze mwanao ili na mwana naye akutukuze wewe -2kama vile ulivyompatia mamlaka juu ya vyote vyenye mwili ili awape uzima wa milele wale wote uliompatia.3Huu ndio uzima wa milele: kwamba wakujue wewe, Mungu wa kweli na wa pekee, na yeye uliyemtuma, Yesu Kristo.4Nimekutukuza hapa duniani, na kuikamilisha kazi uliyonipa niifanye.5Sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja na wewe mwenyewe kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ya ulimwengu kuumbwa.

6Nililifunua jina lako kwa watu ulionipa hapa duniani. Walikuwa watu wako; lakini ulinikabidhi mimi. Nao wamelishika neno lako.7Sasa wanajua kuwa kila kitu ulichonipa mimi kinatoka kwako,8kwa kuwa nimewapa maneno yale yote uliyonipatia mimi. Waliyapokea na kweli wakajua ya kuwa mimi nimetoka kwako, na wakaamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.9Ninawaombea wao. Siuombei ulimwaengu bali wale ulionipa kwa kuwa wao ni wako.10Vitu vyote ambavyo ni vyangu ni vyako, na vile ulivyonavyo wewe ni vyangu; nami ninatukuzwa katika hivyo.11Mimi simo tena ulimwenguni, bali wao wamo ulimwenguni, nami sasa naja kwako. Baba Mtakatifu, watunze kwa jina lako lile ulilonipa mimi ili wao nao wawe kitu kimoja, kama vile mimi na wewe tu kitu kimoja.12Nilipokuwa nao, niliwalinda kwa jina ulilonipa; Niliwalinda, na hakuna hata mmoja wao aliyepotea isipokuwa mwana wa upotevu, ili kwamba maandiko yatimie.

13Sasa ninakuja kwako; lakini ninasema haya ulimwenguni ili kwamba furaha yangu ikamilishwe ndani yao wenyewe.14Nimewapa neno lako; dunia imewachukia kwa sababu wao si wa ulimwengu, kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwengu15Siwaombei kwamba uwatoe ulimwenguni bali uwalinde na yule mwovu.16Wao si wa dunia kama vile mimi nisivyokuwa wa ulimwenguni.17Uwaweke wakfu kwako mwenyewe katika kweli; neno lako ndiyo kweli.18Jinsi ulivyonituma ulimwenguni, nami nimewatuma ulimwenguni.19Kwa ajili yao mimi mwenyewe ninajitoa kwako ili kwamba na wao wajitoe kwako kwa ile kweli.

20Si hawa tu ninaowaombea, bali na wale watakaoamini kupitia neno lao21ili kwamba wao nao wawe kitu kimoja, kama vila wewe Baba, ulivyo ndani yangu nami ndani yako. Nawaombea ili kwamba wao pia waweze kuwa ndani yetu ili ulimwengu uweze kuamini kuwa wewe ndiye uliyenituma.22Utukufu ule ulionipa mimi - nimewapa wao, ili kwamba waweze kuwa kitu kimoja, kama vile sisi tulivyo kitu kimoja -23Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili waweze kukamilishwa katika umoja; ili ulimwengu ujue kuwa hakika wewe ndiye uliyenituma, na kuwapenda, kama vile wewe ulivyonipenda, mimi.

24Baba, kile ulichonipa mimi - natamani kwamba wao pia waweze kuwa pamoja nami mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu, ule ulionipa: kwa kuwa wewe ulinipenda mimi kabla ya kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.

25Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua wewe, lakini mimi nakujua wewe; na hawa wanajua kwamba ulinituma.26Nililifanya jina lako lijulikane kwao, na nitalifanya lijulikane ili kwamba lile pendo ambalo kwalo ulinipenda mimi liweze kuwa ndani yao, na mimi niweze kuwa ndani yao.”

18

1Baada ya Yesu kusema maneno haya, aliondoka na wanafunzi wake kuelekea upande wa pili wa kijito cha Kidron, ambako kulikuwa na bustani, ambayo yeye na wanafunzi wake wakaingia ndani yake.

2Sasa yule Yuda, aliyetaka kumsaliti, naye alilijua eneo hilo, kwani Yesu alikuwa akikutana na wanafunzi wake mara kwa mara.3Naye Yudasi, baada ya kuwa amepata kundi la maaskari na maofisa toka kwa wakuu wa makuhani, wakaja wakiwa na taa, kurunzi na silaha.4Naye Yesu, haku akijua kila kitu kilichokuwa kikifanyika dhidi yake, alijitokeza mbele na akawauliza, “Ni nani mnayemtafuta?”5Nao wakamjibu, “Yesu Mnazareth.” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Naye Yudasi aliyemsaliti, alikuwa amesimama pamoja na wale askari.6Kwa hiyo alipowaambia, “Mimi ndiye,” walirudi kinyume na kuanguka chini.7Halafu akawauliza tena, “Ni nani mnayemtafuta? Nao wakamjibu tena “Yesu mnazareth.”8Yesu akawajibu, “Nimekwisha kuwaambia kuwa Mimi ndiye; kwa hiyo kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa wengine waende.”9Haya yalikuwa hivyo ili lile neno litimilike; pale aliposema; “Katika wale ulionipa, sikumpoteza hata mmoja.”

10Ndipo Simon Petro, aliyekuwa na upanga, akaufuta na kumkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani mkuu. Na jina lake mtumishi yule lilikuwa Malko.11Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako kwenye ala yake. Kwa nini nisikinywee kikombe kile alichonipa Baba?”

12Basi lile kundi la askari na jemedari, na watumishi wa Wayahudi, walimkamata Yesu na kumfunga.13Nao wakamwongoza kwanza mpaka kwa Anasi, kwani yeye alikuwa mkwe wa Kayafa, ambaye ndiye aliyekuwa Kuhani mkuu kwa mwaka huo.14Sasa Kayafa ndiye aliyekuwa amewapa ushauri Wayahudi ya kwamba ilimpasa mtu mmoja afe kwa ajili ya watu.

15Simon Petro alimfuata Yesu, na vivyo hivyo mwanafunzi mwingine. Na yule mwanafunzi alikuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, naye akaingia pamoja na Yesu katika behewa ya Kuhani mkuu;16lakini Petro alikuwa amesimama nje ya mlango. Basi yule mwanafunzi aliyekuwa akifahamika kwa kuhani mkuu, alitoka nje akaenda kuongea na yule mlinda mlango na kumwingiza Petro ndani.17Basi yule kijakazi aliyekuwa akilinda mlango, alimwambia Petro, “Je wewe si mmoja wa wafuasi wa huyu mtu?” Naye akasema, “Mimi siye.”18Na wale watumishi na wakuu walikuwa wamesimama mahali pale; wamekoka moto wa makaa kwa maana, kulikuwa na baridi, na hivyo walikuwa wakiota moto ili kupata joto. Naye Petro alikuwa nao, akiota moto akiwa amesimama.

19Kuhani mkuu alimhoji Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.20Yesu akamjbu, “Nimeuambia waziwazi ulimwengu. Mimi nilifundisha wakati wote kwenye masinagogi na hekaluni mahali ambapo wayahudi hukusanyika. Nami sikusema lolote katika siri.21Kwa nini mliniuliza? Waulizeni walionisikiliza juu ya kile nilichosema. Hawa watu wanajua mambo yale niliyosema.22Yesu alipokwisha sema hivyo, mmoja wa maofisa aliyekuwa amesimama akampiga kofi na kisha akasema, “Je, hivyo ndivyo inavyokupasa kumjibu kuhani mkuu?”23Naye Yesu akamjibu, “Kama nimesema jambo lolote baya basi uwe shahidi kwa ajili ya uovu, na kama nimemjibu vyema kwa nini kunipiga?24Ndipo Anasi alipompeleka Yesu kwa Kayafa kuhani mkuu akiwa amefungwa.

25Sasa Simoni Petro alikuwa amesimama akijipasha joto mwenyewe. Halafu wale watu wakamwambia. “Je, wewe pia si mmoja wa wanaafunzi wake?” Akakana akisema “Mimi siye.”26Mmoja wa watumishi wa kuhani mkuu, ambaye alikuwa ndugu wa yule mwanaume ambaye Petro alimkata sikio, alisema, “Je si wewe niliyekuona naye kule bustanini?”27Petro akakana tena, na mara Jogoo akawika.

28Kisha wakamchukua Yesu toka kwa Kayafa mpaka kwenye Praitorio. Ilikwa asubuhi na mapema. Wao wenyewe hawakuiingia ile Praitorio ili wasije wakanajisika bali waweze kuila pasaka.29Kwa hiyo Pilato akawaendea akisema. “Ni shitaka gani mnalolileta kuhusu huyu mtu?”30Wakamjibu na kumwambia, “Kama huyu mtu asingekuwa mtenda maovu, tusingemleta kwako.”31Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kulingana na sheria zenu.” Nao Wayahudi wakamwambia, “Sheria haituruhusu sisi kumwua mtu yeyote.”32Walisema haya ili neno la Yesu litimilike, neno ambalo alikuwa amekwisha sema juu ya aina ya kifo chake.

33Basi Pilato akaingia tena Praitorio akumwita Yesu; akamwambia, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?”34Yesu akamjibu, “Je, wewe waniuliza swali hili kwa sababu wataka kujua au kwa sababu wengine wamekutuma ili uniulize mimi?”35Naye Pilato akamjibu, “Mimi si Myahudi, au sivyo?” Taifa lako na kuhani mkuu ndio waliokuleta kwangu; wewe umefanya nini?36Yesu akajibu; “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu, kama ufalme wangu ungekuwa na sehemu katika ulimwengu huu watumwa wangu wangenipigania ili nisitolewe kwa Wayahudi. Kwa kweli ufalme wangu hautoki hapa.” Basi37Pilato akamwambia, “Je, wewe basi u mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe ndivyo unanvyosema kuwa mimi ni mfalme, kwa sababu hii mimi nilizaliwa na kwa sababu hii mimi nimekuja ulimwenguni ili niwe shahidi wa ile kweli. Yeyote aliye wa hiyo kweli huisikiliza sauti yangu.38Pilato akamwambia, “Kweli ni nini?” Naye alipokwisha sema haya akaenda kwa Wayahudi na kuwaambia “Sioni kosa lolote katika mtu huyu.39Walakini, ninyi mna utamaduni unaonifanya nimfunfungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Je mnataka nimfungulie mfalme wa Wayahudi.”40Kisha walipiga kelele wakisema, “Siyo huyu, tufungulie Baraba.” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.

19

1Basi Pilato alimchukua Yesu na kuamuru apigwe mijeredi.2Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.3Wakamjia na kusema, “Wewe mfalme wa Wayahudi!” na kisha kumpiga kwa mikono yao.

4Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, “Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake.”5Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, “Tazameni mtu huyu hapa!”

6Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe, msulubishe.” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake.”7Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.”

8Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,9akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.10Kisha Pilato akamwambia, “Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?”
11Yesu akamjibu, “Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa.”

12Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, “Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cha Kaisari.”

13Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.

14Ilikuwa siku ya maandalizi ya Pasaka panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!”

15Wakapiga kelele, “Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!” Pilato akawaambia, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Naye Kuhani mkuu akajibu, “Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari.”

16Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulubiwe.

17Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.18Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao.

19Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI.20Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.

21Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, “Usiandike, ‘Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi.”

22Naye Pilato akawajibu, “Niliyoandika nimeandika.”

23Baada ya askari kumsulubisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo. Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.24Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.”

25Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.26Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!”
27Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.

28Baada ya hilo, huku Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.”29Chombo kilichokuwa kimejaa siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.30Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.

31Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale waliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.32Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.33Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.34Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu.35Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini.

36Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata mfupa wake mmoja utakaovunjwa.”37Tena andiko lingine husema, “Watamtazama yeye waliyemchoma”

38Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.39Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja.40Kwa hiyo waukauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya Wayahudi wakati wa kuzika.41Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo.42Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.

20

1Mapema siku ya kwanza ya juma, kungali bado giza, Mariamu Magdalena alikuja kaburini; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.2Kwa hiyo akakimbia mbio kwenda kwa Simon Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, kisha akawaambia, “Wamemchukua Bwana kaburini, nasi hatujui kule walikomlaza.”

3Kisha Petro na yule mwanafunzi mwingine wakatoka, kuelekea kaburini.4Wote walipiga mbio kwa pamoja; yule mwanafunzi mwingine alikimbia kwa kasi zaidi ya Petro na kufika kaburini wa kwanza.5Akasimama na kisha kuangalia kaburini; akaiona ile sanda ya kitani imelala, lakini hakuingia ndani.

6Kisha Simon Petro naye akafika akaingia ndani ya kaburi. Akaiona ile sanda ya kitani imelala pale7na ile leso iliyokuwa kichwani pake haikuwa imelala pamoja na zile sanda za kitani bali ilikuwa imelala pembeni peke yake.8Ndipo yule mwanafunzi mwingine naye alipoingia ndani ya kaburi; akaona na kuamini.9Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajayajua maandiko kwamba ilimlazimu Yesu afufuke tena katika wafu.

10Kisha wanafunzi wakaenda tena nyumbani kwao.11Hata hivyo, Mariamu alikuwa amesimama kaburini akilia, alivyokuwa akiendelea kulia aliinama kisha akatazama kaburini.12Akaona malaika wawili waliovalia mavazi meupe wamekaa mmoja kichwani na mwingine miguuni mahali ambapo Yesu alikuwa amelala.

13Nao wakamwambia, “Mwanamke, kwa nini unalia?” Naye akawaambia, “Ni kwa sababu wamemchukua Bwana wangu, nami sijui walikomweka.”14Alipokwisha sema hayo, aligeuka na kumwona Yesu akiwa amesimama. Lakini hakutambua kama huyo alikuwa Yesu.
15Naye Yesu akamwambia, “Mama, kwa nini unalia? Unamtafuta nani?” Naye huku akidhani kuwa ni mtunza bustani akamwambia, “Bwana, kama ni wewe uliyemchukua, niambie ulikomweka, nami nitamchukua.”

16Yesu akamwambia, “Mariamu.” Naye akageuka mwenyewe na kumwambia kwa Kiaramu, “Raboni,” yaani hii ni kusema, “Mwalimu.”
17Yesu akamwambia, “Usiniguse, kwani bado sijapaa kwenda kwa baba; bali uende kwa ndugu zangu ukawaambie kuwa nitapaa kwenda kwa Baba yangu ambaye pia ni Baba yenu, Mungu wangu na Mungu wenu.”
18Mariamu Magdalena akaja kuwaambia wanafunzi, “Nimemwona Bwana,” na kwamba amemwambia mambo haya.

19Na ilipokuwa jioni, siku hiyo, siku ya kwanza ya juma, na milango ikiwa imefungwa mahali wanafunzi walipokuwapo kwa kuwahofia Wayahudi, Yesu alikuja na kusimama katikati yao na kuwaambia, “Amani iwe kwenu.”20Alipokwisha sema haya akawaonesha mikono yake na ubavu wake. Nao wanafunzi walipomwona Bwana walifurahi.

21Kisha Yesu akawaambia tena, “Amani iwe nanyi. Kama vile Baba alivyonituma mimi, vivyo hivyo nami nawatuma ninyi.”22Yesu alipokwisha sema hayo, akawavuvia akawaambia, “Pokeeni Roho Mtakatifu.23Yeyote mmsameheye dhambi, amesamehewa; na wale mtakaowafungia watafungiwa.”

24Thomaso, mmoja wa wale kumi na wawili, aliyeitwa Didimas, hakuwa na wanafunzi wenzake Yesu alipokuja.25Wale wanafunzi wengine waka mwambia baadaye, “Tumemwona Bwana.” Naye akawaambia, “Kama sitaona alama za misumari katika mikono yake, na kuweka vidole vyangu kwenye hizo alama, na pia kuweka mkono wangu kwenye ubavu wake sitaamini.”

26Baada ya siku nane wanafunzi walikuwa chumbani tena, naye Thomaso alikuwa pamoja nao. Wakati milango ilipokuwa imefungwa Yesu alisimama katikati yao. Na akasema, “Amani na iwe nanyi.”
27Kisha akamwambia Thomaso, leta kidole chako na uone mikono yangu; leta hapa mikono yako na uweke kwenye ubavu wangu; wala usiwe asiyeamini bali aaminiye.”
28Naye Thomaso akajibu na kumwambia, “Bwana wangu na Mungu wangu.”
29Yesu akamwambia, Kwa kuwa umeniona, umeamini. Wamebarikiwa wao wanaoamini, pasipokuona.”

30Kisha Yesu alifanya ishara nyingi mbele ya wanafunzi, ambazo hazijawahi kuandikwa katika kitabu hiki;31bali hizi zimeandikwa ili kwamba muweze kuamini kwamba Yesu ndiye Kristo, mwana wa Mungu, na kwamba muaminipo muwe na uzima katika jina lake.

21

1Baada ya mambo hayo Yesu alijidhihirisha tena kwa wanafunzi katika bahari ya Tiberia; hivi ndivyo alivyojidhihirisha mwenyewe:2Simon Petro alikuwa pamoja na Thomaso aitwaye Didimas, Nathanaeli wa Kana ya Galilaya, wana wa Zebedayo na wanafunzi wengine wawili wa Yesu.3Simon Petro akawaambia, “Mimi naenda kuvua samaki.” Nao wakamwambia, “Sisi, pia tutaenda nawe.” Wakaenda wakaingia kwenye mashua, lakini usiku huo wote hawakupata chochote.

4Na asubuhi kulipokucha, Yesu alisimama ufukweni, nao wanafunzi hawakutambua kuwa alikuwa Yesu.
5Kisha Yesu akawaambia, “Vijana, mna chochote cha kula?” Nao wakamjibu, “Hapana.”
6Akawaambia, “Shusheni wavu upande wa kuume wa mashua, nanyi mtapata kiasi.” Kwa hiyo wakashusha wavu nao hawakuweza kulivuta tena kwa sababu ya wingi wa samaki.
7Basi yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akamwambia Petro, “Ni Bwana.” Naye Simon Petro aliposikia kuwa ni Bwana, akajifunga vazi lake (maana hakuwa amelivaa vizuri), kisha akajitupa baharini.8Wale wanafunzi wengine wakaja kwenye mashua (kwani hawakuwa mbali na pwani, yapata mita mia moja kutoka ufukweni), nao walikuwa wakivuta zile nyavu zilizokuwa zimejaa samaki.9Walipofika ufukweni, waliona moto wa mkaa pale na juu yake kulikuwa na samaki pamoja na mkate.

10Yesu akawambia, “Leteni baadhi ya samaki mliovua sasa hivi.”11Basi Simon Petro akapanda na kuukokota ule wavu uliokuwa umejaa samaki wakubwa, kiasi cha samaki 153; japo walikuwa wengi, ule wavu haukuchanika.

12Yesu akawaambia, “Njooni mpate kifungua kinywa.” Hakuna hata mmoja wa wanfunzi aliyethubutu kumwuliza, “Wewe ni nani?” Walijua kuwa alikuwa ni Bwana.13Yesu akaja, akachukua ule mkate, kisha akawapa, akafanya vivyo hivyo na kwa wale samaki.14Hii ilikuwa mara ya tatu kwa Yesu kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka toka wafu.

15Baada ya kuwa wamefungua kinywa, Yesu akamwambia Simon Petro, “Simon mwana wa Yohana je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Petro akajibu, “Ndiyo, Bwana; “Wewe wajua kuwa mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Lisha wanakondoo wangu.”

16Akamwambia mara ya pili, “Simon mwana wa Yona, je, wanipenda?” Petro akamwambia, “Ndiyo, Bwana; wewe wajua kuwa nakupenda. “Yesu akamwambia, “Chunga kondoo wangu.”

17Akamwambia tena mara ya tatu, “Simon, mwana wa Yohana, Je wanipenda?” Naye Petro alihuzunika kwa vile alivyomwambia mara ya tatu, “Je Wewe wanipenda?” Naye akamwambia, “Bwana, unajua yote; unajua kuwa nakupenda.” Yesu akamwambia, Lisha kondoo wangu.

18Amini, amini, nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kuvaa nguo mwenyewe na kwenda kokote ulikotaka; lakini utakapokuwa mzee, utanyosha mikono yako, na mwingine atakuvalisha nguo na kukupeleka usikotaka kwenda.”19Yesu alisema haya ili kuonesha ni aina gani ya kifo ambacho Petro angemtukuza Mungu. Baada ya kuwa amesema haya, akamwambia Petro, “Nifuate.”

20Petro aligeuka na kumwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda akawafuata- Huyu ndiye aliyekuwa amajiegemeza kwenye kifua cha Yesu wakati wa chakula cha jioni na kumwuliza, “Bwana, ni nani atakayekusaliti?”21Petro alimwona na kisha akamwuliza Yesu, “Bwana, Huyu mtu atafanya nini?”

22Yesu akamjibu, “Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, hilo linakuhusu nini?” Nifuate.”23Kwa hiyo habari hii ikaenea miongoni mwa wale ndugu, kwamba mwanafunzi huyo hatakufa. Lakini Yesu hakumwambia Petro kuwa, mwanafunzi huyo hafi, “Kama nataka yeye abaki mpaka nitakapokuja yakuhusu nini?”

24Huyu ndiye mwanafunzi atoaye ushuhuda wa mambo haya, na ndiye aliye andika mambo haya, na tunajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli.

25Kuna mambo mengine mengi ambayo Yesu aliyafanya. Kama kila moja lingeandikwa, nadhani kwamba ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa.

Matendo ya mitume

1

1Katika kitabu cha kwanza, ewe ndugu Theofilo, nilikiandika nikisema yote Yesu aliyoanza kufanya na kufundisha,2mpaka siku ambayo Yeye alipokelewa juu. Hii ilikuwa baada ya kutoa amri kupitia Roho Mtakatifu kwa mitume aliokuwa amewachagua.3Baada ya mateso yake, Yeye alionekana kwao akiwa hai pia na vithibitisho vingi vikishuhudia. Kwa siku arobaini alijidhihirisha kwao, na alizungumza kuhusu ufalme wa Mungu.

4Alipokuwa akikutana pamoja nao, aliwaamuru wasiondoke Yerusalemu, lakini wasubiri kwa ajili ya ahadi ya Baba, ambayo, alisema, “Mlisikia kutoka kwangu5kwamba Yohana alibatiza kabisa kwa maji, lakini mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu kwa siku hizi chache.”

6Na walipokuwa wamekutanika pamoja walimuuliza, “Bwana, je, huu ndio muda utakaowarudishia Israeli ufalme?”7Yeye akawaambia, “Siyo sawa kwenu kujua wakati au majira ambayo Baba amekusudia kwa mamlaka yake mwenyewe.”8Lakini mtapokea nguvu, wakati Roho Mtakatifu atakapokuja juu yenu, na ninyi mtakuwa mashahidi wangu kote katika Yerusalemu na Yudea yote na Samaria mpaka mwisho wa dunia.”9Bwana Yesu alipokwisha yasema haya, wakiwa wanatazama juu, Yeye aliinuliwa juu, na wingu likamfunika wasimwone kwa macho yao.

10Wakati wanatazama mbinguni kwa makini akienda, ghafla, watu wawili walisimama katikati yao wamevaa mavazi meupe.11Walisema, “Enyi watu wa Galilaya, kwa nini mnasimama hapa mkitazama mbinguni? Huyu Yesu aliyepaa juu mbinguni atarudi kwa namna ile ile kama mlivyomuona akienda mbinguni.”

12Ndipo wakarudi Yerusalemu kutoka kwenye mlima wa mizeituni, ambao uko karibu na Yerusalemu, kiasi cha umbali wa kutembea mwendo wa Sabato.13Walipofika walikwenda ghorofani walikokuwa wakikaa. Nao ni Petro, Yohana, Yakobo, Andrea, Filipo, Thomaso, Batholomayo, Mathayo, Yakobo Mwana wa Alfayo, Simoni Zelote na Yuda Mwana wa Yakobo.14Wote walikuwa wamejitolea kwa nia moja kuomba, miongoni mwao walikuwemo wanawake, Mariamu Mama yake Yesu, na kaka zake.

15Katika siku zile Petro alisimama katikati ya ndugu, kama watu 120, akasema,16“Ndugu, ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe, ambapo zamani Roho Mtakatifu alisema kwa kinywa cha Daudi kuhusiana na Yuda, ambaye aliwaelekeza wale waliomkamata Yesu.17Kwa kuwa yeye alikuwa mmoja wetu na alipokea fungu lake la faida katika huduma hii.”

18(Sasa mtu huyu alinunua eneo kwa kile alichokipokea kwa uovu wake na hapo alianguka akitanguliza kichwa, mwili ukapasuka na matumbo yake yote yakamwagika.19Wote walioishi Yerusalemu walisikia kuhusu hili, hivyo eneo hilo wakaliita kwa lugha yao “Akeldama,” kwamba ni “Shamba la Damu.”)

20Kwenye kitabu cha Zaburi imeandikwa, ‘Ngoja eneo lake liwe mahame na asiruhusiwe hata mtu mmoja kuishi pale;’ ‘Acha mtu mwingine achukue nafasi yake ya uongozi.’

21Ni muhimu, kwa hiyo, kwamba mmoja wetu ambaye aliambatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipotoka na kuingia kati yetu,22kuanzia kwenye ubatizo wa Yohana mpaka siku ile alipotwaliwa juu, awe shahidi wa ufufuo pamoja nasi.”

23Wakaweka mbele wanaume wawili, Yusufu aitwaye Barsaba, ambaye pia aliitwa Yusto, na Mathia.24Wao waliomba wakisema, “Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, hivyo weka wazi yupi kati ya wawili hawa ambaye umemchagua25kuchukua nafasi katika huduma na utume, ambapo Yuda alitenda uovu na kwenda mahali pake.”26Wakapiga kura kwa ajili yao, na kura ikamwangukia Mathia ambaye alihesabiwa pamoja na wale mitume kumi na moja.

2

1Ilipofika siku ya Pentekoste, wote walikuwa pamoja mahali pamoja.2Ghafla ikatokea sauti ya mgurumo kama mvumo wa upepo mkali kutoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi.3Hapo zikawatokea ndimi kama za moto zimegawanyika, zikatua juu ya kila mmoja wao.4Wao wote wakajazwa na Roho Mtakatifu na wakaanza kusema kwa lugha zingine, kama vile Roho alivyowawezesha.

5Sasa walikuwapo Wayahudi waliokuwa wanaishi Yerusalemu, wacha Mungu, kutoka kila taifa chini ya mbingu.6Sauti hizi ziliposikika, kundi la watu likaja pamoja wakiwa na wasiwasi kwa sababu kila mtu aliwasikia wakiongea kwa lugha yake mwenyewe.7Waliduwaa na kushangazwa; wao wakasema, “Kweli, hawa wote wanaoongea siyo Wagalilaya?8Kwa nini sisi tunawasikia, kila mmoja kwa lugha tulizozaliwa nazo?9Waparthia na Wamedi na Waelamu, na hao waishio Mesopotamia, Uyahudi, na Kapadokia, na katika Ponto na Asia,10katika Frigia, Pamfilia, katika Misri, na sehemu ya Libya hata Kirene, na wageni kutoka Rumi,11Wayahudi na Waongofu, Wakrete na Waarabu, tunawasikia wakizungumza katika lugha zetu kuhusu kazi za uweza wa Mungu.”12Wote walikuwa wameduwaa na kutatanishwa; walisemezana wao kwa wao, “Hii ina maana gani?”13Lakini wengine walidhihaki wakisema, “Hawa wamejazwa kwa mvinyo mpya.”

14Lakini Petro akasimama pamoja na wale kumi na mmoja, akapaza sauti, akawaambia, “Watu wa Yudea na wote mnaoishi hapa Yerusalemu, hili lijulikane kwenu, sikilizeni kwa makini maneno yangu.15Watu hawa hawajalewa kama mnavyodhani, sababu saa hizi ni asubuhi saa tatu.16Lakini hili lilikuwa limesemwa kupitia kwa nabii Yoeli:

17‘Itakuwa katika siku za mwisho; Mungu asema, nitamwaga Roho wangu kwa watu wote. Wana wenu na binti zenu watatoa unabii, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.18Vilevile juu ya watumishi wangu na watumishi wangu wa kike katika siku hizo, nitamwaga Roho wangu, nao watatabiri.19Nitaonesha maajabu juu angani na ishara chini duniani, damu, moto, na mafusho ya moshi.20Na jua litabadilishwa kuwa giza na mwezi kuwa damu, kabla haijaja siku kuu na ya ajabu ya Bwana.21Itakuwa ya kwamba kila mmoja ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.’

22Watu wa Israeli, sikieni maneno haya: Yesu wa Nazareti, mwanadamu aliyethibitishwa na Mungu kwenu kwa matendo ya uweza na maajabu, na ishara ambazo Mungu kupitia Yeye katikati yenu, kama ninyi wenyewe mnavyojua.23Kwa sababu ya mpango uliokusudiwa tangu mwanzo, na maarifa ya Mungu, alitolewa na ninyi, kwa mikono ya watu wahalifu, mlimsulubisha na kumuua24ambaye Mungu alimwinua, akauondoa uchungu wa mauti kwake, kwa sababu haikuwezekana kwake kumilikiwa na huo.

25Hivyo Daudi anasema kuhusu yeye, ‘Nilimwona Bwana daima mbele ya uso wangu, yeye yuko mkono wangu wa kulia hivyo basi sitasogezwa.26Kwa hiyo moyo wangu ulikuwa na furaha na ulimi wangu ulifurahishwa. Pia mwili wangu utaishi katika tumaini.27Kwa kuwa hutaiacha nafsi yangu iende kuzimu wala hutaruhusu Mtakatifu wako kuona uozo.28Wewe umenijulisha njia za uzima; utanifanya nijae furaha mbele ya uso wako.’

29Ndugu, ninaweza kuzungumza kwenu kwa ujasiri kuhusu baba yetu Daudi, yeye alikufa na akazikwa, na kaburi lake liko pamoja nasi hata hivi leo.30Hivyo, alikuwa nabii na alijua kuwa Mungu alishaapa kwa kiapo, kwamba ataweka mmoja katika uzao wake kwenye kiti chake cha enzi.31Aliona yale yangetendeka baadaye kuhusu ufufuo wa Kristo, yakuwa hakuachwa kuzimu, wala mwili wake haukuoza.

32Huyu Yesu, Mungu alimfufua, ambaye sisi wote ni mashahidi.33Kwa hiyo, akiwa ameinuliwa katika mkono wa kuume wa Mungu, na akiwa amepokea ahadi ya Roho Mtakatifu kutoka kwa Baba, yeye amemimina hii ahadi ambayo ninyi mnaona na kusikia.34Kwa kuwa Daudi hakupaa kwenda mbinguni, lakini asema, ‘BWANA alisema kwa Bwana wangu, keti mkono wangu wa kulia,35mpaka nitakapowafanya adui zako kigoda kwa ajili ya miguu yako.’

36Kwa hiyo nyumba yote ya Israeli na ijue kwa hakika kwamba Mungu amemfanya Yeye kuwa Bwana na Kristo, huyu Yesu ambaye mlimsulibisha.”

37Sasa waliposikia hayo, wakachomwa katika mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, “Ndugu, tufanyeje?”

38Na Petro akawaambia, “Tubuni na mbatizwe, kila mmoja wenu, katika jina la Yesu Kristo kwa ajili ya msamaha wa dhambi zenu, na mtapokea zawadi ya Roho Mtakatifu.39Kwa kuwa ahadi ni kwenu na kwa watoto wenu na kwa wale wote walioko mbali, watu wengi kwa kadri Bwana Mungu wetu atakavyowaita.”40Kwa maneno mengine mengi aliwashuhudia na kuwasihi, “Jiokoeni mtoke katika kizazi hiki kiovu.”

41Ndipo wakayapokea maneno yake na wakabatizwa, hapo wakaongezeka katika siku hiyo kama nafsi elfu tatu.42Wakaendelea katika mafundisho ya mitume na ushirikiano, katika kuumega mkate na katika maombi.

43Hofu ikaja juu ya kila nafsi, na maajabu mengi na ishara zikafanyika kupitia mitume.44Wote walioamini walikuwa pamoja na kuwa na vitu vyao kwa pamoja,45na waliuza vitu na milki zao na kugawanya kwa wote kulingana na hitaji la kila mmoja.46Hivyo siku baada ya siku waliendelea wakiwa na lengo moja katika hekalu. Pia walimega mkate kwenye kaya, na walishiriki chakula kwa furaha na ukarimu wa mioyo,47wakimsifu Mungu na kuwa na kibali na watu wote. Bwana aliwaongeza siku kwa siku ambao walikuwa wakiokolewa.

3

1Sasa Petro na Yohana walikuwa wanaelekea katika hekalu wakati wa maombi, saa tisa.2Ikawa mtu fulani, kiwete tangu kuzaliwa, alikuwa akibebwa kila siku na alikuwa akilazwa katika mlango wa hekalu uitwao Mzuri, ili aweze kuomba sadaka kutoka kwa watu waliokuwa wakielekea hekaluni.

3Alipowaona Petro na Yohana wanakaribia kuingia hekaluni, aliomba sadaka.4Petro, akimkazia macho, pamoja na Yohana, alisema, “Tutazame sisi.”5Mtu yule kiwete akawatazama, akitazamia kupokea kitu fulani kutoka kwao.6Lakini Petro akasema, “Fedha na dhahabu mimi sina, lakini kile nilichonacho nitakupa. Katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth, tembea.”7Petro akamchukua kwa mkono wake wa kulia, na akamwinua juu. Mara moja miguu yake na vifundo vya mifupa yake vikapata nguvu.8Akiruka juu yule kiwete alisimama na akaanza kutembea; na akaingia hekaluni pamoja na Petro na Yohana, akitembea, akirukaruka, na kumsifu Mungu.

9Watu wote walimwona akitembea na akimsifu Mungu.10Wakatambua kwamba alikuwa ni yule mtu ambaye alikuwa akiomba sadaka kwenye mlango Mzuri wa hekalu; walijawa na mshangao na kustaajabu kwa sababu ya kile kilichotokea kwake.11AKiwa amewashikilia Petro na Yohana, watu wote kwa pamoja wakakimbilia kwenye ukumbi uitwao wa Sulemani, wakishangaa sana.

12Petro alipoliona hili, yeye akawajibu watu, “Enyi watu wa Israel, kwa nini mnashangaa? Kwa nini mnayaelekeza macho yenu kwetu, kana kwamba tumemfanya huyu atembee kwa nguvu zetu wenyewe au uchaji wetu?13Mungu wa Ibrahimu, na wa Isaka, na wa Yakobo, Mungu wa Baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu. Huyu ndiye ambaye ninyi mlimkabidhi na kumkataa mbele ya uso wa Pilato, japo yeye alikuwa ameamua kumwachia huru.14Mlimkataa Mtakatifu na Mwenye Haki, na badala yake mkataka muuaji aachwe huru.15Ninyi mlimuua Mwanzilishi wa uzima, ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, sisi ni mashahidi wa hili.16Sasa kwa imani katika jina lake, mtu huyu, ambaye mnamwona na kumjua, alifanywa kuwa na nguvu. Imani ambayo nikupitia kwa Yesu imempa yeye afya hii kamilifu, mbele ya uwepo wenu ninyi nyote.

17Sasa, ndugu, najua kwamba mlitenda katika ujinga, ndivyo pia walivyofanya watawala wenu.18Lakini mambo ambayo Mungu aliwaambia mapema kupitia vinywa vya manabii wote, kwamba huyu Kristo atateseka, sasa ameyatimiza.19Kwa hiyo, tubuni na mgeuke, ili kwamba dhambi zenu ziweze kuondolewa kabisa, kusudi zije nyakati za kuburudika kutokana na uwepo wa Bwana;20kusudi aweze kumtuma Kristo ambaye ameshateuliwa kwa ajili yenu, Yesu.21Yeye ndiye ambaye lazima mbingu zimpokee mpaka wakati wa kurejeshwa kwa vitu vyote, ambavyo Mungu alizungumzia zamani za kale kupitia kwa vinywa vya manabii watakatifu.22Hakika Musa alisema, ‘Bwana Mungu atainua nabii kama mimi kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Lazima mtasikiliza kila kitu ambacho atawaambia ninyi.23Itatokea kwamba kila mtu ambaye hasikilizi kwa nabii huyo ataangamizwa kabisa atoke kati ya watu.’24Ndiyo, na manabii wote tokea Samweli na wale waliofuata baada yake, walizungumza na kutangaza siku hizi.25Ninyi ni wana wa manabii na wa agano ambalo Mungu alilifanya pamoja na mababu, kama alivyosema kwa Abrahamu, ‘Katika mbegu yako familia zote za dunia zitabarikiwa.’26Baada ya Mungu kumwinua mtumishi wake, alimtuma kwenu kwanza, ili awabariki ninyi kwa kugeuka kutoka katika uovu wenu.”

4

1Wakati Petro na Yohana walipokuwa wakizungumza na watu, makuhani na mkuu wa hekalu na Masadukayo waliwaendea.2Walikuwa wameudhika sana kwa sababu Petro na Yohana walikuwa wanafundisha watu kuhusu Yesu na kutangaza kufufuka kwake kutoka kwa wafu.3Waliwakamata na kuwaweka gerezani hadi asubuhi iliyofuata, kwani tayari ilikuwa jioni.4Lakini watu wengi waliokuwa wamesikia ujumbe waliamini; na idadi ya wanaume waliokuwa wameamini walikadiliwa kuwa elfu tano.

5Hata ilipofika asubuhi siku iliyofuata, kwamba wakuu wao, wazee na waandishi, kwa pamoja walikusanyika Yerusalemu.6Anasi kuhani mkuu alikuwepo, na Kayafa, na Yohana, na Iskanda, na wote waliokuwa ni ndugu wa kuhani mkuu.7Walipokuwa wamewaweka Petro na Yohana katikati yao, waliwauliza, “Kwa uwezo gani, au kwa jina gani mmefanya hili?”

8Kisha, Petro, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, akawaambia, “Ninyi watawala wa watu, na wazee,9kama sisi siku ya leo tunahojiwa kuhusu tendo jema lililofanywa kwa mtu huyu mgonjwa na kwa namna gani mtu huyu aliponywa,10hebu lijulikane hilo kwenu na kwa watu wote katika Israel kwamba huyu mtu ambaye anasimama mbele yenu akiwa mwenye afya kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye mlimsulubisha, na ambaye Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, ni kwa jina lake huyu mtu anasimama hapa mbele yenu akiwa mwenye afya.

11Yesu Kristo ni jiwe ambalo ninyi wajenzi mlilikataa lakini ambalo limefanywa kuwa jiwe kuu la pembeni.12Hakuna wokovu katika mtu mwingine yeyote yule, kwa maana hakuna jina jingine chini ya mbingu walilopewa watu, ambalo kwa hilo tunaweza kuokolewa.”

13Sasa walipoona ujasiri wa Petro na Yohana na wakagundua kwamba walikuwa ni watu wa kawaida, wasio na elimu, walishangaa, wakafahamu kwamba Petro na Yohana wamekuwa pamoja na Yesu.14Kwa sababu walimwona yule mtu aliyeponywa amesimama pamoja nao, hawakuwa na kitu cha kusema dhidi ya hili.

15Lakini walipokuwa wakwisha kuwaamuru mitume waondoke mbele ya mkutano wa baraza, walizungumza wao kwa wao.16Walisema, “Tuwafanyeje watu hawa? Ni kweli kwamba muujiza wa ajabu umefanyika kupitia wao na unajulikana na kila mmoja anayeishi Yerusalemu, na hatuwezi kulikataa hilo.17Lakini, ili kwamba jambo hili lisienee miongoni mwa watu, hebu tuwaonye wasinene tena kwa mtu yeyote kwa jina hili.”18Waliwaita Petro na Yohana ndani na kuwaamuru kamwe wasinene wala kufundisha kwa jina la Yesu.

19Lakini Petro na Yohana walijibu na kuwaambia, “Kama ni sahihi machoni pa Mungu kuwatii ninyi kuliko Mungu, hukumuni wenyewe.20Maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo ambayo tumeyaona na kuyasikia.”

21Baada ya kuwaonya sana Petro na Yohana, waliwaacha waende. Hawakuweza kupata sababu yoyote ya kuwaadhibu, kwa sababu watu wote walikuwa wakimsifu Mungu kwa kile kilichokuwa kimetendeka.22Yule mtu aliyekuwa amepokea muujiza wa uponyaji alipata kuwa na umri zaidi ya miaka arobaini.

23Baada ya kuwaacha huru, Petro na Yohana walikuja kwa watu wao na wakawapasha habari yote ambayo makuhani wakuu na wazee walikuwa wamewaambia.24Walipoyasikia, walipaza sauti zao kwa pamoja kwa Mungu na kusema, “Bwana, wewe uliyeumba mbingu na dunia na bahari na kila kitu ndani yake,25wewe ambaye kwa Roho Mtakatifu kupitia kwa kinywa cha mtumishi wako, baba yetu Daudi, ulisema, ‘Kwanini watu wa mataifa wamefanya ghasia, na watu wametafakari mambo yasiyofaa?’
26Ulisema, ‘Wafalme wa dunia wamejipanga pamoja, na watawala wamekusanyika kwa pamoja dhidi ya Bwana, na dhidi ya Masihi wake.’

27Ni hakika, wote Herode na Pontio Pilato, pamoja na watu wa mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika kwa pamoja katika mji huu dhidi ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, ambaye ulimpaka mafuta.28Walikusanyika kwa pamoja kufanya yote ambayo mkono na mpango wako uliamua tangu awali, yangefanyika.

29Sasa, Bwana, yaangalie matisho yao, na ukawajalie watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri wote.30Sasa, Bwana, yaangalie matisho yao, na ukawajalie watumishi wako kulinena neno lako kwa ujasiri wote.

31Walipomaliza kuomba, eneo walilokuwa wamekusanyika pamoja likatikiswa, na wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, na kunena neno la Mungu kwa ujasiri.

32Idadi kubwa ya wale walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja. Hakuna hata mmoja wao aliyesema kwamba chochote alichomiliki kilikuwa cha kwake mwenyewe, badala yake walikuwa na vitu vyote shirika.33Kwa nguvu kubwa mitume walikuwa wakiutangaza ushuhuda wao kuhusu ufufuo wa Bwana Yesu, na neema kubwa ilikuwa juu yao wote.34Hapakuwa na mtu yeyote miongoni mwao aliyepungukiwa na chochote, kwa sababu watu wote waliokuwa na hati za viwanja au nyumba, waliviuza na kuleta pesa ya vitu waliyokuwa wameuza35na kuviweka chini ya miguu ya mitume, na viligawanywa kwa kila muumini kulingana na hitaji lake.

36Yusufu, Mlawii, mtu kutoka Kipro, alipewa jina la Barnaba na mitume (hiyo ikitafsiriwa, ni mwana wa kutia moyo).37Aliliuza shamba lake, na akaleta fedha, akaziweka chini ya miguu ya mitume.

5

1Sasa mtu mmoja aliyeitwa Anania, na Safira mkewe, waliuza sehemu ya mali,2na akaficha sehemu ya fedha waliyouza (mke wake pia alilijua hili), na akaleta sehemu iliyobakia na kuiweka kwenye miguu ya mitume.

3Lakini Petro akasema, “Anania, kwa nini Shetani ameujaza moyo wako kumdanganya Roho Mtakatifu na kuficha sehemu ya mali ya shamba?4Wakati lilipokuwa halijauzwa, halikuwa ni mali yako, na baada ya kuuzwa, halikuwa chini ya mamlaka yako? Ilikuwaje uwaze jambo hili moyoni mwako? Hujawadanganya wanadamu, bali umemdanganya Mungu.”5Kwa kusikia maneno haya, Anania alidondoka chini na akakata roho, na hofu kubwa iliwajia wote waliolisikia hili.6Vijana wakaja mbele na wakamfunga sanda, na kumpeleka nje na kumzika.

7Baada ya masaa matatu hivi, mke wake aliingia ndani, asijue ni nini kilichokuwa kimetokea.8Petro akamwambia, “Niambie, kama mliuza shamba kwa thamani hiyo.” Akasema, “Ndiyo, kwa thamani hiyo.”9Kisha Petro akamwambia, “Inakuwaje kwamba mmepatana kwa pamoja kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu ya wale waliomzika mme wako iko mlangoni, na watakubeba na kukupeleka nje.”10Ghafla akaanguka miguuni pa Petro, akakata roho, na wale vijana wakaja ndani wakamkuta ameshakufa. Wakambeba kumpeleka nje, na kumzika karibu na mmewe.

11Hofu kubwa ikaja juu ya kanisa zima, na juu ya wote walioyasikia mambo haya.

12Ishara nyingi na maajabu zilikuwa zinatokea miongoni mwa watu kupitia mikono ya mitume. Walikuwa pamoja katika ukumbi wa Sulemani.13Lakini, hakuna mtu mwingine tofauti aliyekuwa na ujasiri wa kujiunga nao; hata hivyo, walipewa heshima ya juu na watu.14Na pia, waamini wengi walikuwa wakiongezeka kwa Bwana, umati mkubwa wa wanaume na wanawake,15kiasi kwamba hata waliwabeba wagonjwa mitaani, na kuwalaza vitandani na kwenye makochi, ili kwamba Petro akiwa anapita, kivuli chake kiweze kushuka juu ya baadhi yao.16Hapo pia, idadi kubwa ya watu walikuja pamoja kutoka miji iliyozunguka Yerusalem, wakiwaleta wagonjwa na wote waliopagawa na roho wachafu, na wote waliponywa.

17Lakini kuhani mkuu aliinuka, na wote waliokuwa pamoja naye (ambao ni wa dhehebu la Masadukayo); na walijawa na wivu18na wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume na kuwaweka ndani ya gereza la jumla.19Hata hivyo wakati wa usiku malaika wa Bwana akaifungua milango ya gereza na kuwaongoza nje na kusema,20“Nendeni, mkasimame hekaluni na kuwaambia watu maneno yote ya uzima huu.”21Waliposikia hili, waliingia hekaluni wakati wa kupambazuka na kufundisha. Lakini, kuhani mkuu alikuja na wote waliokuwa naye, na kuitisha baraza lote kwa pamoja, na wazee wote wa watu wa Israeli, na kuwatuma gerezani ili kuwaleta mitume.22Lakini watumishi waliokwenda, hawakuwakuta gerezani, walirudi na kutoa taarifa,23“Tumekuta gereza limefungwa vizuri salama, na walinzi wamesimama langoni, lakini tulipolifungua, hatukuona mtu ndani.”24Sasa wakati mkuu wa hekalu na makuhani wakuu waliposikia maneno haya, waliingiwa na wasiwasi mkubwa kuhusu nini kingeliwatokea kutokana na hilo.

25Ndipo mtu mmoja akaja na kuwaambia, “Watu mliowaweka gerezani wamesimama hekaluni na wanafundisha watu.”26Hivyo jemedari alienda pamoja na watumishi, na wakawaleta, lakini bila ya kufanya vurugu, kwa sababu waliogopa kwamba watu wangeweza kuwapiga kwa mawe.

27Walipokwisha kuwaleta, waliwaweka mbele ya baraza. Kuhani mkuu aliwahoji28akisema, “Tuliwaamuru msifundishe kwa jina hili, na bado mmeijaza Yerusalemu kwa fundisho lenu, na kutamani kuleta damu ya mtu huyu juu yetu.”29Lakini Petro na mitume wakajibu, “Lazima tumtii Mungu kuliko watu.30Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, mliyemuua kwa kumtundika juu ya mti.31Mungu alimtukuza katika mkono wake wa kuume, na kumfanya kuwa Mkuu na Mwokozi, kutoa toba kwa Israeli, na msamaha wa dhambi.32Sisi ni mashahidi wa mambo haya, na Roho Mtakatifu, ambaye Mungu amemtoa kwa wale wanaomtii.”33Wajumbe wa baraza waliposikia hivi, walishikwa na hasira wakataka kuwaua mitume.

34Lakini Farisayo aliyeitwa Gamalieli, mwalimu wa sheria, aliyeheshimiwa na watu wote, alisimama na kuwaamuru mitume watolewe nje kwa muda mfupi.35Kisha akawaambia, “Wanaume wa Israeli, iweni makini sana na kile mnachopendekeza kuwafanyia watu hawa.36Kwa sababu, zamani zilizopita, Theuda aliinuka na kujidai kuwa mtu mkuu, na idadi ya watu, wapata mia nne walijiunga naye. Aliuawa, na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika na kuwa si kitu.37Baada ya mtu huyu, Yuda mgalilaya, aliinuka siku zile za kuandikwa sensa, akavuta watu wengi nyuma yake. Naye pia aliangamia na wote waliokuwa wakimtii walitawanyika.38Sasa nawaambia, jiepusheni na watu hawa na muwaache wenyewe, kwa sababu, kama mpango huu au kazi hii ni ya wanadamu, itatupwa.39Lakini kama ni ya Mungu, hamtaweza kuwazuia; mnaweza mkajikuta hata mnashindana na Mungu.” Hivyo, walishawishikana maneno yake.40Kisha, waliwaita mitume ndani na kuwachapa na kuwaamuru wasinene kwa jina la Yesu, na wakawaacha waende zao.

41Waliondoka mbele ya baraza wakifurahi kwa sababu wamehesabiwa kuwa wamestahili kuteseka na kutoheshimiwa kwa ajili ya Jina hilo.42Kwa hiyo, kila siku, ndani ya hekalu na kutoka nyumba hadi nyumba waliendelea kufundisha na kutangaza habari njema kwamba Kristo ni Yesu.

6

1Sasa katika siku hizi, wakati idadi ya wanafunzi ilipokuwa inaongezeka, lalamiko la Wayahudi wa Kiyunani lilianza dhidi ya Waebrania, kwa sababu wajane wao walikuwa wanasahaulika katika mgao wa kila siku wa msaada wa chakula.

2Mitume kumi na wawili waliwaita kusanyiko lote la wanafunzi na kusema, “Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu na kuhudumia mezani.3Kwa hiyo, ndugu, inawapasa mchague, wanaume saba, kutoka miongoni mwenu, watu wema, waliojaa Roho na hekima, ambao tunaweza kuwakabidhi huduma hii.4Na sisi, tutaendelea daima katika kuomba na katika huduma ya neno.”

5Hotuba yao ikaupendeza mkutano wote. Hivyo, wakamchagua Stefano, mtu aliyejaa imani na Roho Mtakatifu, na Filipo, Prokoro, Nikanori, Timoni, Parmena, na Nikolao, mwongofu kutoka Antiokia.6Waumini waliwaleta watu hawa mbele ya mitume, ambao walioomba na badaye wakawawekea mikono yao.

7Hivyo, neno la Mungu liliendelea kuenea; na idadi ya wanafunzi ilizidi kuongezeka huko Yerusalem; na idadi kubwa ya makuhani wakawa watii wa imani.

8Na Stefano, aliyejaa neema na nguvu, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa miongoni mwa watu.9Lakini hapo wakainuka baadhi ya watu wafuasi wa sinagogi liitwalo Sinagogi la Mahuru, la Wakirene na la Waeskanderia, na baadhi kutoka Kilikia na Asia. Watu hawa walikuwa wakihojiana na Stefano.10Lakini, hawakuweza kushindana na hekima na Roho ambayo Stefano alikuwa akitumia katika kuzungumza.

11Kisha waliwahonga baadhi ya watu kwa siri kusema, “Tumesikia Stefano akizungumza maneno ya kufuru dhidi ya Musa na dhidi ya Mungu.”12Waliwachochea watu, wazee, na waandishi, na kumwendea Stefano, wakamkamata, na kumleta mbele ya baraza.13Waliwaleta mashahidi wa uongo, waliosema, “Mtu huyu haachi kunena maneno mabaya dhidi ya eneo hili takatifu na sheria.14Kwani tumemsikia akisema kwamba huyu Yesu wa Nazareti atapaharibu mahali hapa na kuzibadili desturi tulizokabidhiwa na Musa.”

15Kila mmoja aliyekuwa katika baraza, akaelekeza macho yake kumwangalia Stefano, nao wakauona uso wake ulikuwa kama uso wa malaika.

7

1Kuhani mkuu akasema, “Mambo haya ni ya kweli?”

2Stefano akasema, “Ndugu na mababa zangu, nisikilizeni mimi: Mungu wa utukufu alimtokea baba yetu Abrahamu wakati alipokuwa Mesopotamia, kabla hajaishi Harani,3akamwambia, ‘Ondoka katika nchi yako na jamaa zako na uende katika nchi nitakayokuonyesha.’

4Kisha akaondoka katika nchi ya Ukaldayo akaishi Harani, kutoka hapo, baada ya baba yake kufa, Mungu akamleta kwenye nchi hii, mnayoishi sasa.5Hakumpa chochote kama urithi wake, hapakuwa na sehemu hata ya kuweka mguu. Lakini Abrahamu aliahidiwa hata kabla hajapata mtoto kuwa atapewa nchi kama miliki yake na uzao wake.6Mungu alinena naye hivi, ya kwamba wazao wake wangeishi kwa muda katika nchi ya ugeni, na kwamba wenyeji wa huko watawafanya kuwa watumwa na kuwanyanyasa kwa miaka mia nne.7Na Mungu akasema, ‘Nitalihukumu taifa ambalo litawafanya watumwa, na baada ya hapo watatoka na kuniabudu katika mahali hapa.’8Basi Mungu akampa Abrahamu agano la tohara, hivyo Abrahamu akawa baba wa Isaka akamtahiri siku ya nane; Isaka akawa baba wa Yakobo, na Yakobo akawa baba wa mababa zetu kumi na wawili.

9Mababa zetu wakamwonea wivu Yusufu wakamuuza katika nchi ya Misri, na Mungu alikuwa pamoja naye,10na akamwokoa katika dhiki yake yote, na akampa fadhili na hekima mbele ya Farao mfalme wa Misri. Farao akamfanya awe mtawala juu ya Misri na juu ya nyumba yake yote.

11Basi kukawa na njaa na dhiki kuu katika nchi ya Misri na Kanani, na baba zetu hawakupata chakula.12Lakini Yakobo aliposikia kwamba kuna nafaka Misri, aliwatuma baba zetu kwa mara ya kwanza.13Katika safari ya pili Yusufu akajionyesha kwa ndugu zake, na familia ya Yusufu ikajulikana kwa Farao.14Yusufu akawatuma ndugu zake kwenda kumwambia Yakobo baba yao aje Misri, pamoja na jamaa yake yote, jumla ya watu wote ni sabini na watano.15Hivyo Yakobo akashuka Misri; kisha akafa yeye pamoja na baba zetu.16Wakachukuliwa hata Shekemu wakazikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alilinunua kwa vipande vya fedha kutoka kwa wana wa Hamori huko Shekemu.

17Wakati wa ile ahadi ambayo Mungu alimwahidi Abrahamu ulipokaribia, watu wakiwa wameongezeka huko Misri,18wakati huo aliinuka mfalme mwingine juu ya Misri, mfalme ambaye hakujua kuhusu Yusufu.19Huyo mfalme mwingine akawadanganya watu wetu na kuwatenda mabaya baba zetu, kuwatupa watoto wao wachanga ili wasiishi.

20Katika kipindi kile Musa alizaliwa; alikuwa mzuri mbele za Mungu na kwa miezi mitatu alikuwa akilelewa kwenye nyumba ya baba yake.21Wakati alipotupwa binti wa Farao alimchukua akamlea kama mwanawe.22Musa alifudishwa katika hekima yote ya Kimisri. Alikuwa mwenye nguvu kwa maneno na matendo yake.

23Lakini baada ya kutimiza miaka arobaini, ikamjia katika moyo wake kuwatembelea ndugu zake, wana wa Israeli.24Alipomwona Mwisraeli akitendewa mabaya, Musa alimtetea na kulipiza kisasi aliyekuwa akimwonea kwa kumpiga Mmisiri:25akifikiri kuwa ndugu zake watafahamu kwamba Mungu anawaokoa kwa mkono wake lakini hawakuelewa.26Siku iliyofuata akaenda kwa baadhi ya Waisraeli waliokuwa wanagombana akajaribu kuwapatanisha akisema, ‘Mabwana ninyi ni ndugu; kwanini mnakoseana ninyi kwa ninyi?27Lakini aliyekuwa amemkosea jirani yake akamsukumia mbali, na kusema, “Nani kakuteua kuwa mtawala na hakimu juu yetu?28Wewe unataka kuniua, kama ulivyomuua Mmisri jana?”29Musa akakimbia baada ya kusikia hivyo; akawa mgeni katika nchi ya Midiani, ambapo akawa baba wa wana wawili.

30Baada ya miaka arobaini kupita, malaika akamtokea katika jangwa la mlima Sinai, katika mwali wa moto ndani ya kichaka.31Wakati Musa alipoona moto, alishangaa na kustaajabia kile alichokiona, na alipojaribu kukisogelea ili kukitazama, sauti ya Bwana ikamjia ikisema,32‘Mimi ni Mungu wa baba zako, Mungu wa Abrahamu, na wa Isaka, na wa Yakobo.’ Musa alitetemeka na hakuthubutu kuangalia.33Bwana akamwambia, ‘Vua viatu vyako, sehemu uliposimama ni mahali patakatifu.34Hakika nimeona mateso ya watu wangu walioko Misri; Nimesikia kuugua kwao, nami nimeshuka ili niwaokoe; sasa njoo, nitakutuma wewe Misri.’

35Huyo Musa ambaye walimkataa, wakati waliposema, ‘Nani kakuteua kuwa mtawala na mwamuzi wetu?’ alikuwa ndiye ambaye Mungu alimtuma awe mtawala na mkombozi. Mungu alimtuma kwa mkono wa malaika ambaye alimtokea Musa kichakani.36Musa aliwaongoza kutoka Misri baada ya kufanya miujiza na ishara katika Misri na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa kwa kipindi cha miaka arobaini.37Ni Musa yule yule aliyewaambia watu wa Isiraeli kuwa, ‘Mungu atawainulieni nabii kutoka miongoni mwa ndugu zenu, nabii kama mimi.’38Huyu ni mtu ambaye alikuwa katika mkutano jangwani na malaika ambaye aliongea naye katika mlima Sinai. Huyu ndiye mtu ambaye alikuwa na baba zetu, huyu ni mtu ambaye alipokea neno lililo hai na kutupatia sisi.

39Lakini baba zetu walikataa kumtii; walimsukumia mbali nao, na katika mioyo yao waligeuka kurudi Misri.40Katika kipindi hicho walimwambia Haruni, ‘Tutengenezee miungu itakayotuongoza. Kwakua huyu Musa, aliyekuwa akituongoza kutoka katika nchi ya Misri, hatujui kilichompata.’41Hivyo wakatengeneza ndama kwa siku hizo na wakatoa sadaka kwa hiyo sanamu na wakafurahi kwa sababu ya kazi ya mikono yao.42Lakini Mungu aliwageuka na kuwaacha waabudu nyota wa angani, kama ilivyoandikwa kwenye kitabu cha manabii, ‘Je mmenitolea mimi sadaka za wanyama mliowachinja jangwani kwa muda wa miaka arobaini, nyumba ya Israeli?43Mmekubali hema ya kukutania ya Moleki na nyota ya mungu refani, na sanamu mlizozitengeneza kuziabudu: na nitawapeleka mbali zaidi ya Babeli.’

44Baba zetu walikuwa na hema ya kukutania ya ushuhuda jangwani, kama Mungu alivyoamuru alipoongea na Musa, kwamba ilimpasa aitengeneze mfano wa muundo ule aliouona.45Hili ni hema ambalo baba zetu, kwa wakati wao waliletwa katika nchi na Joshua. Hii ilitokea wakati walipoingia kumiliki taifa ambalo Mungu aliwafukuza kabla ya uwepo wa baba zetu. Hii ilikuwa hivi hadi siku za Daudi,46ambaye alipata kibali machoni pa Mungu, na akaomba kutafuta makao kwa Mungu wa Yakobo.47Lakini ni Suleimani aliyejenga nyumba ya Mungu.

48Hata hivyo aliye juu sana haishi kwenye nyumba zilizojengwa kwa mikono; kama nabii alivyosema,
49‘Mbingu ni kiti changu cha enzi, na dunia ni sehemu ya kuwekea miguu yangu. Nyumba ya aina gani mtanijengea? Asema Bwana: au ni wapi sehemu yangu ya kupumzikia?
50Mkono wangu haukufanya hivi vyote?’

51Enyi watu wenye shingo ngumu msiotahiriwa mioyo na masikio, kila mara mnampinga Roho Mtakatifu, mnatenda kama baba zenu walivyotenda.52Ni nabii yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumtesa? Waliwaua manabii wote waliotokea kabla ya ujio wa yule mwenye Haki, na sasa mmekuwa wasaliti na wauaji wake pia.53Enyi watu mliopokea sheria ile iliyoagizwa na malaika lakini hamkuishika.”

54Kisha wajumbe wa baraza waliposikia mambo haya, walighadhabika sana mioyoni mwao, na wakamsagia meno Stefano.

55Lakini yeye, akiwa amejaa Roho Mtakatifu, alitazama mbinguni kwa makini na akauona utukufu wa Mungu, na kumwona Yesu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.56Stefano akasema, “Angalia, ninaona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adam amesimama mkono wa kuume wa Mungu.”

57Kwa hili wajumbe wa baraza waliziba masikio yao na kupiga kelele kwa sauti ya juu na kumvamia kwa kusudi moja.58Kwa nguvu wakamtupa nje ya mji na wakampiga mawe: na mashahidi wakavua nguo zao za nje na kuweka chini karibu na miguu ya kijana aliyeitwa Sauli.59Walipokuwa wakimpiga mawe Stefano, aliendelea kumwita Bwana na kusema, “Bwana Yesu, pokea roho yangu.”

60Akapiga magoti na kuita kwa sauti kubwa, “Bwana, usiwahesabie dhambi hii.” Aliposema haya, akakata roho.

8

1Sauli alikuwa kwenye makubaliano ya kifo chake. Ndipo siku hiyo yakaanza mateso makuu kinyume cha kanisa lililokuwa Yerusalemu; na waaminio wote walitawanyika katika majimbo ya Yudea na Samaria, isipokuwa mitume.2Watu wachamungu walimzika Stefano na kufanya maombolezo makubwa juu yake.3Lakini Sauli alilidhuru sana kanisa. Alikwenda nyumba kwa nyumba na kuwavuruta nje wanawake na waume, na kuwatupa gerezani.

4Waaminio ambao walikuwa wametawanyika bado walienda wakilihubiri neno.5Filipo akashuka katika mji wa Samaria na akamtangaza Kristo huko.6Baada ya makutano kusikia na nakuziona ishara alizofanya Filipo; wakaweka umakini juu ya kile alichokisema.7Kutoka hapo watu wengi waliokuwa na pepo wachafu waliwatoka, huku wakilia kwa sauti kuu na wengi waliokuwa wamepooza na kulemaa waliponywa.8Na kulikuwa na furaha kubwa katika mji.

9Lakini palikuwepo na mtu mmoja katika mji ule akiitwa Simoni, ambaye hapo awali alikuwa akifanya uchawi; ambao aliutumia kuwashangaza watu wa mji wa Samaria, wakati akisema kuwa yeye ni mtu wa muhimu.10Wasamaria wote tangu mdogo hadi mkubwa, wakamakinika kwake huku wakisema; ‘Mtu huyu ni ile nguvu ya Mungu ambayo ni kuu.’11Wakamsikiliza kwa sababu alikuwa kwa uchawi wake amewashangaza kwa muda mrefu.12Lakini wakati walipoamini Filipo alipokuwa akitangaza juu ya ufalme wa Mungu na juu ya jina la Yesu Kristo, walibatizwa, wanaume kwa wanawake.13Hata Simoni mwenyewe aliamini na baada ya kubatizwa, aliendelea kuwa na Filipo na alipoona ishara na miujiza iliyokuwa ikitendeka, alishangaa.

14Wakati mitume wa Yerusalemu waliposikia kuwa sasa Samaria imepokea neno la Mungu, wakawatuma kwao Petro na Yohana.15Wakati walipokuwa washashuka waliwaombea, kwamba wampokee Roho Mtakatifu.16Kwani mpaka wakati huo Roho Mtakatifu alikuwa hajawashukia hata mmoja wao; walikuwa tu wamebatizwa kwa jina la Bwana Yesu.17Ndipo Petro na Yohana wakawawekea mikono, nao wakampokea Roho Mtakatifu.

18Wakati Simoni alipoona kwamba Roho Mtakatifu ametolewa kupitia kuwekewa mikono na mitume; akataka kuwapa pesa,19akasema, “Nipeni haya mamlaka, ili kila nitakayemwekea mikono apokee Roho Mtakatifu.”

20Lakini Petro akamwambia; “Pesa yako na iangamie pamoja nawe, kwa sababu umefikiri kuwa karama ya Mungu inapatikana kwa pesa.21Hauna sehemu katika jambo hili, kwa sababu moyo wako si mnyoofu mbele za Mungu.22Hivyo basi, tubu uovu wako huu na kumwomba Bwana anaweza labda kukusamehe nia ya moyo wako.23Kwa maana naona uko katika sumu ya uchungu na kifungo cha dhambi.”

24Simoni akajibu na kusema, “Mwombeni Bwana kwa ajili yangu, kwa kuwa mambo yote mliyozungumza yaweza kunitokea.”

25Wakati Petro na Yohana walipokuwa wameshuhudia na kuhubiri neno la Bwana, walirudi Yerusalemu; wakihubiri injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.

26Basi malaika wa Bwana akanena na Filipo na kusema, “Inuka na uende kusini katika njia iendayo chini ya kutoka Yerusalemu kuelekea Gaza.” (Njia hii iko katika jangwa).27Akainuka na kwenda. Tazama, kulikuwa na mtu wa Ethiopia, towashi mwenye mamlaka kuu chini ya Kandasa; malkia wa Ethiopia. Ndiye aliyekuwa msimamizi wa hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu.28Alikuwa akirejea ameketi garini mwake akisoma kitabu cha nabii Isaya.

29Roho akasema na Filipo, “Sogea karibu na gari hili ukashikamane nalo.”

30Hivyo Filipo akamkimbilia, akamsikia akisoma katika kitabu cha nabii Isaya; akasema, “Je, unafahamu unachokisoma?”

31Ndipo Muethiopia akasema, “Nitawezaje mtu asiponiongoza?” Akamsihi Filipo apande garini na kuketi pamoja naye.

32Sasa fungu la maandiko alilokuwa akisoma Muethiopia ni hili; ‘Aliongozwa kama kondoo kwenda machinjioni kuchinjwa, na kama kondoo alinyamaza kimya, hakufungua kinywa chake:
33Kwa kuhuzunishwa kwake hukumu yake iliondolewa: Nani ataeleza kizazi chake? Maisha yake yameondolewa katika nchi.’

34Hivyo towashi akamwuliza Filipo, na kusema, “Nakuomba, ni nabii yupi ambaye anaongelewa habari zake, ni kuhusu yeye, au za mtu mwingine?”35Filipo alianza kuzungumza, na kuanzia andiko hili la Isaya alimtangazia injili kuhusu Yesu.

36Wakiwa njiani, wakafika mahali penye maji, towashi akasema, “Tazama, pana maji hapa. Nini kinazuia nisibatizwe?”37Filipo akamwambia, “Ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Hivyo Muethiopia akajibu, “Naamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”38Ndipo Muethiopia akaamuru gari lisimame. Walikwenda ndani ya maji, Filipo pamoja na towashi, na Filipo akambatiza.39Wakati walipotoka kwenye maji, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo mbali; towashi hakumwona tena, akaenda njia yake akifurahia.

40Lakini Filipo akatokea Azoto. Alipita katika mkoa ule na kuhubiri injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.

9

1Lakini Sauli, bado akiendelea kuongea vitisho hata vya kifo kwa wanafunzi wa Bwana, alikwenda kwa kuhani mkuu2na kumwomba barua kwa ajili ya masinagogi huko Dameski, ili kwamba akimpata mtu aliye katika njia ile, awe mwanaume au mwanamke, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.

3Hata alipokuwa akisafiri, ilitokea kwamba alipokaribia Dameski, ghafla ikamwangaza kotekote nuru kutoka mbinguni,4naye akaanguka chini na akasikia sauti ikimwambia, “Sauli, Sauli, mbona wanitesa mimi?”5Sauli akajibu, “U nani wewe Bwana?” Bwana akasema, “Mimi ndiye Yesu ambaye unamtesa:6Lakini inuka, ingia mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda.”7Wale watu waliosafiri pamoja na Sauli wakasimama kimya, wakisikiliza sauti, wasione mtu.8Sauli akainuka kutoka ardhini, na alipofungua macho yake, hakuweza kuona kitu, hivyo wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski.9Kwa siku tatu alikuwa haoni, naye hakula, wala kunywa.

10Basi palikuwapo mwanafunzi Dameski jina lake Anania. Bwana alisema naye katika maono, “Anania!” Naye akajibu akasema, “Nipo hapa, Bwana.”11Bwana akamwambia, “Inuka uende zako katika mtaa uitwao Nyoofu, na katika nyumba ya Yuda na ukaulize mtu kutoka Tarso aitwaye Sauli; maana angali anaomba.12Ameona katika maono mtu jina lake Anania akiingia na kumwekea mikono juu yake ili apate kuona tena.”

13Lakini Anania akajibu, “Bwana, nimesikia kutoka kwa watu wengi kuhusu mtu huyu, kwa kiasi gani amewafanyia mabaya watu wako watakatifu walioko Yerusalemu.14Anayo mamlaka kutoka kwa kuhani mkuu kuweka katika vifungo kila mtu anayeliitia jina lako.”

15Lakini Bwana akamwambia, “Nenda, kwa maana yeye ni chombo teule kwangu, kulibeba jina langu mbele ya watu wa mataifa na wafalme na wana wa Israeli.16Kwa maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya jina langu.”

17Hivyo Anania akaondoka, akaingia mle nyumbani; akaweka mikono yake juu yake, akasema, “Ndugu Sauli, Bwana Yesu, aliyekutokea katika njia ulipokuwa unakuja, amenituma ili upate kuona tena na ujazwe Roho Mtakatifu.”18Mara vitu kama magamba vilianguka kutoka kwa macho ya Sauli, naye akapata kuona, akasimama, na kubatizwa;19akala chakula na kupata nguvu. Akakaa pamoja na wanafunzi huko Dameski kwa siku kadhaa.

20Wakati huo huo akamtangaza Yesu katika masinagogi, akisema kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.21Na wote waliosikia walishangaa na kusema, “Siyo mtu huyu aliyewaharibu wote walioita jina hili huko Yerusalemu? Na hapa amekuja kwa kusudi la kuwafunga na kuwapeleka kwa makuhani.”22Lakini Sauli aliwezeshwa kuhubiri kwa nguvu zaidi na zaidi, naye alikuwa akisababisha dhiki miongoni mwa Wayahudi waliokaa Dameski, akithibitisha ya kuwa Yesu ndiye Kristo.

23Baada ya siku nyingi, Wayahudi walipanga shauri pamoja kumuua.24Lakini mpango wao ukajulikana na Sauli. Wakamvizia mlangoni mchana na usiku wapate kumuua.25Lakini wanafunzi wake wakamchukua usiku na kumteremsha kupitia ukutani wakitumia kikapu.

26Wakati Sauli alipofika Yerusalemu, alijaribu kujiunga na wanafunzi lakini walikuwa wakimuogopa, wasisadiki kuwa yeye ni mwanafunzi.27Lakini Barnaba akamchukua na kumpeleka kwa mitume, na akawaeleza jinsi Sauli alivyomuona Bwana njiani na Bwana alivyozungumza naye, na jinsi Sauli alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Yesu huko Dameski.28Alikuwa pamoja nao walipoingia na kutoka Yerusalemu. Akanena kwa ujasiri kwa jina la Bwana Yesu,29huku akijadiliana na Wayahudi wa Kiyunani lakini walizidi kujaribu mara kwa mara kumuua.30Wakati ndugu walipojua jambo hilo, wakamleta Kaisaria, na kumpeleka Tarso.

31Basi kanisa lote katika Uyahudi, Galilaya na Samaria, lilikuwa na amani, na likajengwa, na likatembea katika hofu ya Bwana na faraja ya Roho Mtakatifu, kanisa likakua kwa kuongezeka idadi.

32Kisha ilitokea Petro alipokuwa akizungukazunguka pande zote za mkoa, alishuka pia kwa watu watakatifu wa Mungu waishio katika mji wa Lida.33Akamuona huko mtu mmoja jina lake Ainea, aliyekuwa kitandani kwa miaka minane; maana alikuwa amepooza.34Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo akuponye; inuka na utandike kitanda chako.” Mara akainuka35na watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona mtu huyo, wakamgeukia Bwana.

36Sasa palikuwa na mwanafunzi Yafa aitwaye Tabitha (ikitafsiriwa “Dorcas”). Huyu mwanamke alijaa kazi njema na matendo ya huruma aliyowatendea maskini.37Ilitokea katika siku hizo aliugua na akafa; walipomsafisha, walimpandisha chumba cha juu na kumlaza.

38Kwa vile Lida ilikuwa karibu na Yafa, na wanafunzi walisikia kwamba Petro alikuwa huko, waliwatuma watu wawili kwake, wakimsihi, “Njoo kwetu bila kuchelewa.”39Petro akaamka na akaondoka pamoja nao. Alipofika, walimleta katika chumba cha juu. Na wajane wote walisimama karibu naye wakilia, wakimwonyesha kanzu na nguo ambazo Dorcas aliwashonea wakati alikuwa pamoja nao.40Petro akawatoa wote nje ya chumba, akapiga magoti akaomba, kisha akaugekia mwili, akasema, “Tabitha, inuka.” Hapo akafungua macho yake na alipomwona Petro akakaa chini.41Kisha Petro akampa mkono wake akamwinua, na alipowaita watu watakatifu wa Mungu na wajane, akawakabidhi kwao akiwa hai.42Jambo hili likajulikana Yafa yote, na watu wengi wakamwamini Bwana.43Ilitokea Petro akakaa siku nyingi huko Yafa na mtu mmoja jina lake Simoni, mtengeneza ngozi.

10

1Sasa palikuwa na mtu fulani katika mji wa kaisaria, jina lake aliitwa Kornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha askari wa Kiitaliano.2Alikuwa mtu mcha Mungu, na aliyemwabudu Mungu pamoja na nyumba yake yote; alitoa sadaka nyingi kwa watu na kumwomba Mungu siku zote.

3Muda wa saa tisa za mchana, aliona wazi katika maono Malaika wa Mungu akija kwake. Malaika akamwambia “Kornelio!”

4Kornelio akatazama malaika na akaogopa sana akasema, “Kuna nini bwana?” Malaika akamwambia “Maombi yako na zawadi zako kwa masikini zimepanda juu kama kumbukumbu kwenye uwepo wa Mungu.5Sasa tuma watu kwenda mji wa Yafa kumleta mtu anayeitwa Simoni ambaye pia huitwa Petro.6Anakaa na mtengenezaji wa Ngozi aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”7Baada ya Malaika aliyekuwa akisema naye kuondoka, Kornelio akawaita wawili wa watumishi wa nyumbani kwake, na askari mcha Mungu kutoka miongoni mwao waliokuwa wanamtumikia.8Kornelio aliwaambia yote yaliyotokea na akawatuma Yafa.

9Sasa siku iliyofuata muda wa saa sita wakiwa katika safari yao, huku wakiukaribia mji, Petro alipanda juu darini kuomba.10Yeye basi akawa na njaa na alihitaji kitu cha kula, lakini wakati watu walipokuwa wanapika chakula, akaonyeshwa maono,11akaona anga limefunguka na chombo kinashuka na, kitu fulani kama shuka kubwa ikishuka chini duniani kikishikiliwa, kwa pembe zake zote nne.12Ndani yake kulikuwa na aina zote za wanyama wenye miguu minne na watambaao juu ya ardhi, na ndege wa angani.13Tena sauti ikasema kwake “Amka, Petro chinja na ule.”

14Lakini Petro akasema “Siyo hivyo, Bwana kwa sababu sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu.”

15Lakini sauti ikaja kwake tena kwa mara ya pili. “Alichokitakasa Mungu usikiite najisi wala kichafu.”16Hii ilitokea mara tatu, na kile chombo kikawa kimechukuliwa tena angani.

17Na wakati Petro akiwa katika hali ya kuchanganyikiwa juu ya maono hayo aliyokuwa ameyaona yanamaanisha nini, tazama, watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakasimama mbele ya lango, wakiuliza njia ya kwenda kwenye nyumba.18Waliita na kuuliza kama Simoni ambaye pia aliitwa Petro alikuwa anakaa pale.

19Wakati huo Petro alipokuwa akiwaza juu ya hayo maono, Roho akasema naye, “Tazama watu watatu wanakutafuta.20Amka na ushuke chini na uende nao. Usisite kwenda nao, kwa sababu nimewatuma.”

21Petro akashuka chini kwao na kusema “Mimi ndiye yule mnayemtafuta. Kwa nini mmekuja?”

22Wakasema, “Akida mmoja jina lake Kornelio, mtu mwenye haki na anayemcha Mungu, na watu humsema vyema katika taifa lote la kiyahudi, aliagizwa na malaika mtakatifu wa Mungu kukutumania ili kwenda kwenye nyumba yake, ili asikie ujumbe kutoka kwako.”23Petro akawakaribisha kuingia ndani na kukaa pamoja naye. Asubuhi iliyofuata akaamka akaenda pamoja nao, na ndugu wachache kutoka Yafa wakaambatana naye.

24Siku iliyofuata wakafika Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwasubiri; na alikuwa amewaita pamoja ndugu zake na marafiki zake wa karibu.25Ikawa kwamba wakati Petro aliingia ndani, Kornelio akamlaki na kuanguka chini miguuni pake ili kumwabudu.26Lakini Petro akamwinua na kusema “Simama! Mimi mwenyewe pia ni mwanadamu.”

27Wakati Petro akiwa anaongea naye, alienda ndani akakuta watu wengi wamekusanyika pamoja.28Akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua kuwa si halali kwa Myahudi kushirikiana na au kumtembelea mgeni asiye wa taifa letu. Lakini Mungu amenionyesha mimi kuwa sipaswi kumwita mtu yeyote najisi au mchafu.29Na ndiyo maana nimekuja bila kubishana nilipotumwa hapa. Hivyo nauliza wewe kwa nini umeniita.”

30Kornelio akasema, “Siku nne zilizopita, wakati kama huu, nilikuwa naomba muda wa saa tisa mchana ndani ya nyumba yangu; Na tazama, mtu alisimama mbele yangu mavazi yenye kung'aa.31Akasema ‘Kornelio maombi yako yamesikiwa na Mungu, na zawadi zako kwa masikini zimemkumbusha Mungu juu yako.32Hivyo tuma mtu Yafa na akamwite mtu mmoja anayeitwa Simoni aje kwako, ambaye pia huitwa Petro. Ambaye anayeishi kwa mtengenezaji wa Ngozi mmoja aitwaye Simoni ambaye nyumba yake iko pembeni mwa bahari.’33Kwa hiyo mara moja nilikutumania. Wewe ni mwema umekuja. Sasa basi, sisi sote tupo hapa mbele za Mungu kusikia kila kitu ambacho umeagizwa na Bwana kusema.”

34Ndipo Petro akafungua mdomo wake na kusema “Kweli, nimeelewa kuwa Mungu hawezi kuwa na upendeleo.35Badala yake, katika kila taifa mtu yeyote anayemwogopa na kufanya matendo ya haki anakubalika kwake.36Unajua ujumbe alioutoa kwa watu wa Israel, alipokuwa akitangaza habari njema ya amani kupitia Yesu Kristo ambaye ni Bwana wa wote-37ninyi wenyewe mnajua tukio lililotokea, ambalo limetokea Yudea yote, kuanzia Galilaya, baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza.38Tukio lililokuwa linamhusu Yesu Kristo wa Nazareti jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu. Alienda akifanya mema na kuponya wote walioteswa na Ibilisi, kwa kuwa Mungu alikuwa pamoja naye.

39Sisi ni mashahidi wa mambo yote Yesu aliyoyafanya katika nchi za Uyahudi na katika Yerusalemu. Walimuua kwa kumtundika juu ya mti.40Lakini Mungu alimfufua siku ya tatu na kumfanya aonekane,41si kwa watu wote, lakini kwa mashahidi waliochaguliwa kabla na Mungu. Sisi wenyewe, tulio kula naye na kunywa naye baada ya kufufuka kutoka kwa wafu.42Ametuagiza kuhubiri kwa watu na kushuhudia kuwa huyu ndiye ambaye amechaguliwa na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na waliokufa.43Katika yeye manabii wote washuhudia, ili kwamba kila anayeamini katika yeye hupokea msamaha wa dhambi kupitia jina lake.”

44Wakati Petro akiendelea kusema haya, Roho Mtakatifu akawajaza wote waliokuwa wakisikiliza ujumbe wake.45Watu waliokuwa kwa kundi la tohara la waumini - wale wote waliokuja na Petro- walishangazwa, kwa sababu ya karama ya Roho Mtakatifu aliyemwagwa pia kwa watu wa mataifa.46Kwa kuwa walisikia hawa watu wa mataifa wakizungumza kwa lugha zingine na kumtukuza Mungu. Kisha Petro akajibu,47“Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi?”48Ndipo akawaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Baadaye wakamwomba akae nao kwa siku kadhaa.

11

1Sasa mitume na ndugu wale waliokuwa huko Yudea walisikia kuwa watu wa mataifa wamelipokea neno la Mungu.2Petro alipokuwa amepanda kwenda huko Yerusalemu, lile kundi la watu waliotahiriwa wakaanza kumkosoa;3Walisema “Umeshikamana na watu wasiotahiriwa na kula nao!”

4Lakini Petro alianza kuwaeleza tukio kwa kina; akisema,5“Nilikuwa naomba katika mji wa Yafa, na nikaona maono ya chombo kikishuka chini kama shuka kubwa ikishuka kutoka mbinguni katika pembe zake zote nne. Kikashuka kwangu.6Nilikitazama na kufikiri juu yake. Nikaona wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, na wanyama wa porini na wanyama watambaao na ndege wa angani.7Kisha nikasikia sauti ikisema nami, ‘Amka, Petro, chinja na ule!’

8Nikasema, ‘Siyo hivyo, Bwana, kwa maana mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu au kichafu.’

9Lakini sauti ikajibu tena kutoka Mbinguni, ‘Kile ambacho Mungu amekitakasa, usikiite najisi.’10Hii ilitokea mara tatu, na kisha kila kitu kikachukuliwa mbinguni tena.

11Tazama, wakati huo watu watatu walikuwa wamesimama mbele ya nyumba ile tulimokuwa; walikuwa wametumwa kutoka Kaisaria kuja kwangu.12Roho akaniamuru niende pamoja nao, na nisitofautiane nao. Hawa ndugu sita wakaenda pamoja na mimi na tuliende kwenye nyumba ya mtu yule.13Alituambia vile alivyomwona malaika amesimama ndani ya nyumba yake akisema, ‘Watume watu Yafa wakamlete Simoni ambaye jina lake lingine ni Petro.14Atasema ujumbe kwako katika huo utaokoka wewe na nyumba yako yote.’15Nilipoanza kusema nao, Roho Mtakatifu akaja juu yao kama alivyokuja kwetu mwanzoni.16Nikakumbuka maneno ya Bwana, alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji; lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’17Basi ikiwa Mungu aliwapa karama ile ile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi nilikuwa nani, kwamba ningeweza kumpinga Mungu?”

18Waliposikia mambo haya, hawakujibu chochote, bali walimtukuza Mungu na kusema, “Basi Mungu ametoa toba ya uzima kwa watu wa mataifa pia.”

19Basi waamini ambao walitawanyika kwa mateso yaliyoanzia kwenye kifo cha Stefano, walitawanyika kutoka Yerusalem wakaenea hadi mpaka Foinike, Kipro na Antiokia, wakilihubiri neno ila kwa Wayahudi peke yao.20Lakini baadhi yao, watu kutoka Kipro na Krene, walikuja Antiokia na kusema na Wayunani na kuwahubiria injili kuhusu Bwana Yesu.21Na mkono wa Bwana ulikuwa pamoja nao, na idadi kubwa ya watu waliamini na kumgeukia Bwana.

22Habari kuwahusu zikafikia masikioni mwa kanisa la Yerusalemu: na wakamtuma Barnaba aende mpaka Antiokia.23Alipokuja na kuona neema ya Mungu alifurahi na aliwatia moyo wote kubaki na Bwana katika kusudi la moyo.24Kwa sababu alikuwa mtu mwema na amejazwa na Roho Mtakatifu na imani na watu wengi wakaongezeka kwa Bwana.

25Baadaye Barnaba alienda Tarso kumtafuta kwa makini Sauli.26Alipompata, akamleta Antiokia. Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa kwanza Wakristo huko Antiokia.

27Sasa katika siku hizi manabii wakashuka kutoka Yerusalemu mpaka Antiokia.28Mmoja wao, ni Agabo kwa jina, akasimama na kuonyeshwa na Roho kuwa njaa kubwa ingetokea duniani kote. Hii ilitokea wakati wa siku za Klaudio.29Kwa hiyo, wanafunzi, kila mmoja alivyo fanikiwa, waliamua kupeleka misaada kwa ndugu walioko Uyahudi.30Walifanya hivi; Walituma pesa kwa mkono wa Barnaba na Sauli.

12

1Wakati huo mfalme Herode alinyosha mkono wake kwa baadhi ya watu wa kanisa ili apate kuwatesa.2Akamwua Yakobo nduguye Yohana kwa upanga.3Baada ya kuona kwamba hili liliwapendeza Wayahudi, alimkamata Petro. Hii ilikuwa wakati wa siku za mikate isiyotiwa chachu.4Alipomkamata, akamweka gerezani na akamweka chini ya vikosi vinne vya askari ili kumlinda, alikuwa akitarajia kumpeleka kwa hadhara baada ya Pasaka.

5Petro akawekwa gerezani, lakini maombi yalifanywa kwa bidii na kanisa kwa ajili yake kwa Mungu.6Usiku huo kabla Herode hajaenda kumtoa kwa ajili ya kesi, Petro alikuwa amelala katikati ya maaskari wawili, akiwa amefungwa na minyororo miwili, huku walinzi wakiwa mbele ya mlango wakilinda gereza.7Tazama, Malaika wa Bwana ghafla akamtokea na nuru ikang'aa ndani ya gereza. Akampiga Petro ubavuni na kumwamsha akisema, “Amka haraka,” na minyororo aliyokuwa amefungwa ikaanguka kutoka mikononi mwake.8Malaika akamwambia, “Vaa nguo zako na vaa viatu vyako.” Petro akafanya hivyo. Malaika akamwambia, “Vaa koti lako na unifuate.”9Hivyo Petro akamfuata Malaika na akatoka nje. Hakujua kama kilichofanywa na malaika ni cha kweli. Alidhani anaona maono.10Baada ya kupita lindo la kwanza na la pili, wakafika kwenye lango la chuma la kuingilia kwenda mjini, likafunguka lenyewe kwa ajili yao. Wakatoka nje na wakashuka kwenye mtaa, mara Malaika akamwacha.11Petro alipojitambua, akasema, “Sasa nimeamini kwa kweli Bwana alimtuma Malaika wake ili kunitoa katika mkono wa Herode, na kwa matarajio ya watu wote wa Uyahudi.”

12Baada ya kujua haya, akaja kwenye nyumba ya Mariamu mama yake Yohana ambaye pia huitwa Marko; ambako Wakristo wengi walikuwa wamekusanyika wakiomba.13Alipobisha kwenye mlango wa lango, mtumishi mmoja msichana anayeitwa Roda akaja kufungua.14Alipotambua ni sauti ya Petro, kwa furaha akashindwa kuufungua mlango; badala yake, akakimbia ndani ya chumba; na kuwajulisha kuwa Petro amesimama mbele ya mlango.15Hivyo, wakasema kwake, “Wewe ni mwendawazimu,” lakini alikazia kuwa kwa kweli ni yeye. Wakasema, “Huyo ni malaika wake.”16Lakini Petro aliendelea kubisha, na walipofungua mlango, wakamwona na wakashangaa sana. Petro akawaashiria kwa mkono wakae kimya na akawaambia jinsi Bwana alivyomtoa kutoka gerezani. Akasema,17“Wajulishe haya mambo Yakobo na ndugu zake.” Kisha akaondoka akaenda sehemu nyingine.

18Sasa kulipokuwa mchana, kukawa na vurugu si kidogo kati ya askari, kuhusiana na kilichotokea kwa Petro.19Baada ya Herode kumtafuta na kutompata akawauliza walinzi na akaamuru wauawe. Akaenda kutoka Uyahudi mpaka Kaisaria na kukaa huko.

20Ikawa Herode alikuwa na hasira juu ya watu wa Tiro na Sidoni. Wakaenda kwake kwa nia moja na baada ya kumshawishi Blasto, aliyekuwa msaidizi wa mfalme Herode kuwa urafiki nao, waliomba awasaidie. Waliomba amani kwa sababu nchi yao ilipokea chakula kutoka nchi ya mfalme.21Siku iliyokusudiwa Herode alivaa mavazi ya kifalme na kukaa kwenye kiti chake cha kifalme, na akawahutubia.22Watu wakapasa sauti, “Hii ni sauti ya mungu wala si sauti ya mwanadamu!”23Mara hiyo hiyo malaika akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na chango na akafa.

24Lakini neno la Mungu likakua na kusambaa.

25Basi ikawa Barnaba na Sauli walipokamilisha huduma yao pale wakarejea Yerusalemu huku wakimchukua pamoja nao Yohana aitwaye Marko.

13

1Sasa katika kanisa la Antiokia, palikuwa na baadhi ya manabii na walimu. Walikua Barnaba, Simeoni (aliyeitwa Nigeri). Lukio wa Kirene, Manaeni (ndugu asiye wa damu wa Herode kiongozi wa mkoa), na Sauli.2Walipokuwa wakimwabudu Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu alisema, “Nitengeeni pembeni Barnaba na Sauli, waifanye kazi niliyo waitia.”3Baada ya Kanisa kufunga, kuomba, na kuweka mikono yao juu ya watu hawa, wakawaacha waende.

4Kwa hiyo Barnaba na Sauli walimtii Roho Mtakatifu na waliteremka kuelekea Seleukia. Kutoka huko walisafiri baharini kuelekea kisiwa cha Kipro.5Walipokuwa katika mji wa Salami, walilitangaza neno la Mungu katika masinagogi ya Wayahudi. Pia walikuwa pamoja na Yohana Marko kama msaidizi wao.

6Walipokuwa wamekipitia kisiwa chote mpaka Pafo, walimpata mchawi fulani, Myahudi nabii wa uongo, ambaye jina lake lilikuwa Bar Yesu.7Mchawi huyu alishirikiana na Liwali Sergio Paulo, aliyekuwa mtu mwerewa. Mtu huyu aliwaalika Barnaba na Sauli, kwa sababu alihitaji kusikia neno la Mungu.8Lakini Elima ‘yule mchawi’ (hivyo ndivyo jina lake lilivyo tafsiriwa) aliwapinga; alijaribu kumgeuza yule liwali atoke kwenye imani.9Lakini Sauli aliyeitwa Paulo, alikuwa amejazwa na Roho Mtakatikfu, akamkazia macho10na akasema “Ewe mwana wa Ibilisi, umejawa na aina zote za udanganyifu na uovu. Wewe ni adui wa kila aina ya haki. Hautakoma kuzigeuza njia za Bwana, zilizonyooka, je utaweza?11Sasa tazama, mkono wa Bwana upo juu yako, na utakuwa kipofu. Hautaliona jua kwa muda.” Mara moja ukungu na giza vilianguka juu ya Elima; alianza kuzunguka pale akiomba watu wamwongoze kwa kumshika mkono.12Baada ya liwali kuona kilichotokea, aliamini, kwa sababu alishangazwa kwa mafundisho kuhusu Bwana.

13Sasa Paulo na rafiki zake walisafiri majini kutoka Pafo na wakafika Perge katika Pamfilia. Lakini Yohana aliwaacha na kurudi Yerusalemu.14Paulo na rafiki yake walisafiri kutoka Perge na wakafika Antiokia ya Pisidia. Huko walikwenda katika sinagogi siku ya Sabato na kukaa chini.15Baada ya kusoma sheria na manabii, viongozi wa sinagogi aliwatumia ujumbe wakisema, “Ndugu, kama mnao ujumbe wa kutia moyo watu hapa, semeni.”

16Kwa hiyo Paulo alisimama na kuwapungia mkono; alisema, “Wanaume wa Israeli na enyi mnao mtii Mungu, sikilizeni.17Mungu wa hawa watu wa Israeli aliwachagua baba zetu na kuwafanya watu wengi walipokaa katika nchi ya Misri, na kwa mkono wake ulioinuliwa aliwaongoza nje yake.18Kwa miaka arobaini aliwavumilia katika jangwa.19Baada ya kuyaharibu mataifa saba katika nchi ya Kaanani, aliwapa watu wetu nchi yao iwe urithi.20Matukio haya yote yalitokea zaidi ya miaka mia nne na hamsini. Baada ya vitu hivi vyote, Mungu aliwapa waamuzi mpaka Samweli Nabii.21Baada ya haya, watu waliomba mfalme, hivyo Mungu aliwapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila la Benjamini, kuwa mfalme kwa miaka arobaini.22Kisha baada ya Mungu kumuondoa katika ufalme, alimwinua Daudi kuwa mfalme wao. Ilikuwa ni kuhusu Daudi kwamba Mungu alishuhudia na kusema, ‘Nimempata Daudi mwana wa Yese kuwa mtu apendezwaye na moyo wangu; ambaye atafanya kila kitu nipendacho.’

23Kutoka kwenye ukoo wa mtu huyu Mungu ameiletea Israeli mkombozi, Yesu, kama alivyoahidi kufanya.24Kabla ya Yesu kuja, Yohana kwanza alitangaza ubatizo wa toba kwa watu wote wa Israeli.25Naye Yohana alipokuwa akimalizia kazi yake, alisema, ‘Mwanifikiri mimi kua ni nani? Mimi si yule. Lakini sikilizeni, ajaye nyuma yangu, sisitahili kulegeza kamba za viatu vya miguu yake.’

26Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu, ni kwa ajili yetu kwamba ujumbe huu wa ukombozi umetumwa.27Kwa wale waishio Yerusalemu, na watawala wao, hawakumtambua kwa uhalisia, na wala hawakuutambua ujumbe wa manabii ambao husomwa kila Sabato; kwa hiyo walitimiliza ujumbe wa manabii kwa kumhukumu kifo Yesu.28Ijapokuwa hawakupata sababu nzuri za adhabu ya kifo juu yake, walimwomba Pilato amuue.29Walipokua wamekamilisha mambo yote yaliyoandikwa kuhusu yeye, walimshusha kutoka mtini na kumlaza kaburini.30Lakini Mungu alimfufua kutoka wafu.31Alionekana kwa siku nyingi kwa wale waliokwenda pamoja naye kutoka Galilaya kuelekea Yerusalemu. Watu hawa sasa ni mashahidi wa watu.32Hivyo tunawaletea habari njema kuhusu ahadi walizopewa mababu zetu.33Mungu ametimiza ahadi hizi kwetu, watoto wao, kwa kumfufua Yesu na kumrudisha tena katika uhai. Kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili: ‘Wewe ni Mwanangu, leo nimekuwa Baba yako.’

34Nayo kuhusu kumfufua kutoka kwa wafu ili kwamba mwili wake usione uozo; amesema hivi: ‘Nitakupa baraka halisi na takatifu za Daudi.’35Hii ndiyo sababu amesema pia katika zaburi nyingine, ‘Hautaruhusu mtakatifu wako kuuona uozo.’36Kwa kuwa baada ya Daudi kutumikia mapenzi ya Mungu katika kizazi chake, alilala, alilazwa pamoja na baba zake, na mwili wake uliona uaharibifu,37Lakini aliyefufuliwa na Mungu hakuuona uharibifu.

38Hivyo na ifahamike kwenu, ndugu, kupitia mtu huyu, msamaha wa dhambi umehubiriwa.39Kwa yeye kila aaminiye anahesabiwa haki na mambo yote ambayo sheria ya Musa isingewafanya wenye haki.40Hivyo basi kuweni waangalifu kwamba kitu walichokiongelea manabii kisitokee kwenu:
41‘Tazama, enyi mnaodharau, na mkashangae na mkaangamie; kwa vile nafanya kazi katika siku zenu, kazi ambayo hamwezi kuiamini, hata kama mtu atawaeleza.’”

42Wakati Paulo na Barnaba wakiondoka, watu wakawaomba waongee maneno haya siku ya Sabato iliyofuata.43Wakati mkutano wa sinagogi ulipokwisha, Wayahudi wengi na waongofu thabiti waliwafuata Paulo na Barnaba, ambao waliongea nao na waliwahimiza waendelee katika neema ya Mungu.

44Sabato iliyofuata, karibu mji mzima ulikusanyika kusikia neno la Mungu.45Wayahudi walipoona makutano, walijawa na wivu na kuongea maneno yaliyopinga vitu vilivyosemwa na Paulo na walimtukana.46Lakini Paulo na Barnaba waliongea kwa ujasiri na kusema, “Ilikuwa ni muhimu kwamba neno la Mungu linenwe kwanza kwenu. Tunapowaona mnalisukumia mbali kutoka kwenu nakujiona kuwa hamkusitahili uzima wa milele, angalieni tutawageukia mataifa.47Kama ambavyo Bwana ametuamuru, akisema, ‘Nimewaweka ninyi kama nuru kwa watu wa mataifa, kwamba mlete wokovu kwa pande zote za dunia.’”

48Mataifa waliposikia hili, walifurahi na kulitukuza neno la Bwana. Wengi waliochaguliwa kwa uzima wa milele waliamini.49Neno la Bwana lilienea nchi ile yote.

50Lakini Wayahudi waliwachochea waliojitoa na wanawake muhimu, pia na viongozi wa mji. Haya yalichochea mateso dhidi ya Paulo na Barnaba na waliwatupa nje ya mipaka ya mji.51Lakini Paulo na Barnaba walikung'utia vumbi ya miguu yao. Kisha walienda kwenye mji wa Ikonia.52Na wanafunzi walijawa na furaha pamoja na Roho mtakatifu.

14

1Ikatokea ndani ya Ikonio kwamba Paulo na Barnaba waliingia pamoja ndani ya sinagogi la Wayahudi na kuongea namna ambavyo kundi kubwa la watu Wayahudi na Wayunani waliamini.2Lakini Wayahudi wasiotii waliwachochea akili wamataifa na kuwafanya kuwa wabaya dhidi ya ndugu.3Kwa hiyo walikaa huko kwa muda mrefu, wakiongea kwa ujasiri kwa nguvu ya Bwana, huku wakitoa ushahidi kuhusu ujumbe wa neema yake. Alifanya hivi kwa kutoa ishara na majaabu vifanywe kwa mikono ya Paulo na Barnaba.

4Lakini watu wa mji waligawanyika: baadhi walikuwa pamoja na Wayahudi, na baadhi pamoja na mitume.5Wakati watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na viongozi wao walipojaribu kuwatendea mabaya na kuwapiga kwa mawe, Paulo na Barnaba,6walipotambua hilo wakakimbilia katika miji ya Likaonia, Listra na Derbe, na maeneo yanayozunguka pale,7ambako waliendelea kutangaza injili.

8Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja aliyekaa, hakuwa na nguvu miguuni mwake, kilema kutoka tumboni mwa mama yake, hajawahi kutembea.9Mtu huyu alimsikia Paulo akiongea. Paulo alimkazia macho na akaona kwamba alikuwa na imani ya kuponywa.10Hivyo alisema kwake kwa sauti ya juu, “Simama kwa miguu yako.” Na yule mtu alisimama juu na kuanza kutembea.

11Umati ulipoona alichokifanya Paulo, waliinua sauti zao, wakisema katika lahaja ya Kilikaonio, “Miungu imetushukia kwa namna ya binadamu.”12Walimwita Barnaba “Zeu,” na Paulo “Herme” kwa sababu alikuwa msemaji mkuu.13Kuhani wa Zeu, ambaye hekalu lake lilikuwa nje ya mji, alileta fahari la ng'ombe na mtungo wa maua mpaka kwenye lango la mji. Yeye na umati walitaka kutoa sadaka.

14Lakini mitume, Barnaba na Paulo, walipolisikia hili, walirarua mavazi yao na kwa haraka wakaenda nje kwenye umati, wakilia15na kusema, “Enyi watu, kwanini mnafanya mambo haya? Na sisi pia ni binadamu wenye hisia kama za kwenu. Tunawaletea habari njema, kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu hivi visivyofaa na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu, dunia na bahari na kila kitu kilichomo.16Katika nyakati zilizopita, aliwaruhusu mataifa kutembea katika njia zao wenyewe.17Lakini bado, hakuacha kama hana shahidi, katika hilo alifanya vizuri na akawapatia mvua kutoka mbinguni na nyakati za mazao, akiwajaza mioyo yenu kwa vyakula na furaha.”18Hata kwa maneno haya, Paulo na Barnaba kwa shida waliuzuia umati kuwatolea sadaka.

19Lakini baadhi ya Wayahudi kutoka Antiokia na Ikonio walikuja kuushawishi umati. Wakampiga mawe Paulo na kumburura hadi nje ya mji, wakidhani alikuwa amekufa.20Hata hivyo wanafunzi walikuwa wamesimama karibu naye, aliamka, wakaingia mjini. Siku ya pili, walienda Derbe na Barnaba.21Baada ya kutangaza injili katika mji ule na kuwafanya wanafunzi wengi, walirudi Listra, hadi Ikoniamu, na hadi Antiokia.22Waliendelea kuimarisha nafsi za wanafunzi na kuwatia moyo kuendelea katika imani, akasema, “Lazima tuingie katika ufalme wa Mungu kwa kupitia mateso mengi.”23Walipo wateua wazee kwa kila kusanyiko la waaminio, na wakiwa wameomba na kufunga, waliwakabidhi kwa Bwana, ambaye wao walimwamini.

24Kisha walipita katika Pisidia, walifika Pamfilia.25Wakati walipoongea maneno katika Perga, waliteremka kwenda Atalia.26Kutoka huko walipanda meli hadi Antiokia ambako walikuwa wamejitoa kwa neema ya Mungu kwa ajili ya kazi ambayo sasa walikuwa wameikamilisha.27Walipofika huko Antiokia, na kulikusanya kanisa pamoja, wakatoa taarifa ya mambo ambayo Mungu amefanya kwao, na jinsi alivyowafungulia mlango wa imani kwa watu wa Mataifa.28Walikaa kwa muda mrefu na wanafunzi.

15

1Watu fulani walishuka kutoka Uyahudi na kuwafundisha ndugu, wakisema, “Msipotahiriwa kama desturi ya Musa, hamwezi kuokolewa.”2Hili lilileta mzozo na mdahalo mkubwa kati ya Paulo na Barnaba pamoja nao ndugu waliamua kwamba Paulo, Barnaba, na wengine kadhaa waende Yerusalem kwa mitume na wazee kwa ajili ya swali hili.

3Kwa hiyo, kwa kutumwa kwao na kanisa, walipitia Foinike na Samaria wakitangaza kugeuzwa nia kwa wamataifa. Walileta furaha kuu kwa ndugu wote.4Walipokuja Yerusalem, walikaribishwa na Kanisa na mitume na wazee, na waliwasilisha taarifa ya mambo yote ambayo Mungu amefanya pamoja nao.

5Lakini watu fulani walioamini, waliokuwa katika kundi la Mafarisayo, walisimama nakusema, “Ni muhimu kuwatahiri na kuwaamuru waishike sheria ya Musa.”

6Hivyo mitume na wazee walisimama pamoja kulifikiria hili swala.7Baada ya majadiliano marefu, Petro alisimama na kusema kwao, “Ndugu mwatambua kwamba kitambo kizuri kilichopita Mungu alifanya chaguo kati yenu, kwamba kwa mdomo wangu mataifa wasikie neno la injili, na kuamini.8Mungu, anayefahamu mioyo, anashuhudia kwao, anawapa Roho mtakatifu, kama alivyofanya kwetu;9na hakutengeneza utofauti kati yetu na wao, akiifanya mioyo yao safi kwa imani.10Kwa hiyo, kwa nini mnamjaribu Mungu kwamba muweke nira juu ya shingo za wanafunzi ambayo hata baba zetu wala sisi hatukuweza kustahimili?11Lakini twaamini kwamba tutaokolewa kwa neema ya Bwana Yesu, kama vile naowalivyo.”

12Kusanyiko lote lilinyamaza walipokua wakimsikiliza Barnaba na Paulo walipokuwa wakitoa taarifa ya ishara na maajabu ambayo Mungu alifanya pamoja nao kati ya watu wa mataifa.

13Walipoacha kuongea, Yakobo alijibu akisema, “Ndugu nisikilizeni.14Simoni ameelezea jinsi kwanza Mungu kwa neema aliwasaidia mataifa ili kwamba ajipatie kutoka kwao watu kwa ajili ya jina lake.15Maneno ya manabii yanakubaliana na hili kama lilivyoandikwa.
16‘Baada ya mambo haya nitarudi na kuijenga tena hema ya Daudi, iliyoanguka chini; nitainua na kuhuisha uhararibifu wake,
17ili kwamba watu waliobaki wamtafute Bwana, pamoja na watu wa mataifa walioitwa kwa jina langu.’18Hivi ndivyo asemavyo Bwana aliyefanya mambo haya yajulikanayo tangu enzi za zamani.

19Hivyo basi, ushauri wangu ni kwamba, tusiwapatie shida watu wa mataifa wamgeukiao Mungu;20lakini tuandike kwao kwamba wajiepushe mbali na uharibifu wa sanamu, tamaa za uasherati, na vilivyonyongwa, na damu.21Kutoka vizazi vya wazee kuna watu katika kila mji wahubirio na kumsoma Musa katika masinagogi kila Sabato.”

22Kwa hiyo ikaonekana kuwa imewapendeza mitume na wazee, pamoja na kanisa lote, kumchagua Yuda aliyeitwa Barsaba, na Silas, waliokuwa viongozi wa kanisa, na kuwatuma Antiokia pamoja na Paulo na Barnaba.23Waliandika hivi, “Mitume na wazee, kwa ndugu wa mataifa walioko Antiokia, Shamu na Kilikia, salamu.24Tulisika kwamba watu fulani ambao hatukuwapatia amri hiyo, walitoka kwetu na wamewataabisha kwa mafundisho yaletayo shida nafsini mwenu.25Kwa hiyo imeonekana vyema kwetu sote kuchagua watu na kuwatuma kwenu pamoja na wapendwa wetu Barnaba na Paulo,26watu walio hatarisha maisha yao kwa ajili ya jina la Bwana Yesu Kristo.27Kwa hiyo tumemtuma Yuda na Sila, watawaambia mambo yayo hayo.28Kwa kuwa ilionekana vyema kwa Roho Mtakatifu na kwetu, kutoweka juu yenu mzigo mkubwa kuliko mambo haya yaliyo ya lazima:
29kwamba mgeuke kutoka kwenye vitu vitolewavyo kwa sanamu, damu, vitu vya kunyongwa, na uasherati. Kama mtajiweka mbali na hivi, itakuwa vyema kwenu. Kwa herini.”

30Hivyo basi, walivyotawanyishwa, waliteremkia Antiokia; baada ya kukusanya kusanyiko pamoja, waliwasilisha barua.31Walipokua wameisoma, walifurahi kwa sababu ya kutiwa moyo.32Yuda na Sila, na manabii, waliwatia moyo ndugu kwa maneno mengi na kuwatia nguvu.

33Baada ya kukaa muda fulani huko, walitawanyishwa kwa amani kutoka kwa ndugu kwa wale waliowatuma.34[ Lakini ilionekana vyema Sila kubaki huko. ]35Lakini Paulo na wengine walikaa Antiokia pamoja na wengine wengi, ambapo walifundisha na kuhubiri neno la Bwana.

36Baada ya siku kadhaa Paulo alisema kwa Barnaba, “Na turudi sasa na kuwatembelea ndugu katika kila mji tulipohubiri neno la Bwana, na kuwaona walivyo.”37Barnaba alihitaji pia kumchukua pamoja nao Yohana aliyeitwa Marko.38Lakini Paulo alifikiria haikuwa vizuri kumchukua Marko, aliyewaacha huko Pamfilia na hakuendelea nao katika kazi.39Kisha hapo kukatokea mabishano makubwa kwa hiyo walitengana, na Barnaba alimchukua Marko na kusafiri kwa meli mpaka Kipro,40Lakini Paulo alimchagua Sila na kuondoka, baada ya kukabidhiwa na ndugu katika neema ya Bwana.41Na alienda kupitia Shamu na Kilikia, akiimarisha makanisa.

16

1Paulo pia alikuja Derbe na Lystra; na tazama, pale palikuwepo na mwanafunzi aitwaye Timotheo, ni kijana aliyezaliwa na mama wa Kiyahudi ambaye ni muumini lakini baba yake ni Mgiriki.2Watu wa Listra na Ikonia walimshudia vizuri.3Paulo alimtaka ili asafiri naye, hivyo akamchukua na kumtahiri kwa sababu ya Wayahudi waliokuwako huko kwani wote walimjua kuwa baba yake ni Mgiriki.

4Walipokuwa wakienda walipita kwenye miji na kutoa maagizo kwa makanisa ili kuyatii maagizo hayo yaliandikwa na mitume na wazee huko Yerusalemu.

5Hivyo makanisa yakaimarishwa katika imani na walioamini wakaongezeka kwa idadi kila siku.

6Paulo na wenzake wakaenda Firigia na Galatia, kwani Roho wa Mungu aliwakanya kuhubiri neno huko kwenye jimbo la Asia.7Walipokaribia Misia, walijaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu akawakataza.8Kwa hiyo wakapita Misia wakaja mpaka mji wa Troa.9Maono yalimtokea Paulo usiku, kulikuwa na mtu wa Makedonia amesimama, akimwita na kusema “Njoni mtusaidie huku Makedonia.”10Paulo alipoona maono, mara tukajiandaa kwenda Makedonia, akijua kwamba Mungu alituita kwenda kuwahubiria injili.

11Hivyo tukaondoka kutoka Troa, tukaenda moja kwa moja Samothrake, na siku iliyofuata tukafika mji wa Neapoli.12Kutoka hapo tukaenda Filipi ambao ni moja ya mji wa Makedonia, mji muhimu katika wilaya na utawala wa Kirumi na tukakaa siku kadhaa.

13Siku ya Sabato, tulikwenda nje ya lango kwa njia ya mto, sehemu ambayo tulidhania kutakuwa na mahali pa kufanyia maombi. Tulikaa chini na kuongea na akinamama waliokuja pamoja.14Mwanamke mmoja aitwaye Lidia, muuzaji wa zambarau, kutoka katika mji wa Tiatira, mwenye kumwabudu Mungu, alitusikiliza. Bwana alimfungua moyo wake na kuweka maanani maneno yaliyosemwa na Paulo.15Baada ya kubatizwa, yeye na nyumba yake yote, alitusihi akisema, “Kama mmeniona kuwa mimi ni mwaminifu katika Bwana, basi njooni muingie na kukaa kwangu.” Akatushawishi sana.

16Ikawa kwamba, tulipokuwa tunaenda mahali pa kuomba, msichana mmoja aliyekuwa na pepo la utambuzi akakutana nasi. Alimletea bwana wake faida nyingi kwa kubashiri.17Mwanamke huyu alimfuata Paulo pamoja na sisi, akipiga kelele na kusema “Hawa wanaume ni watumishi wa Mungu aliye Mkuu, wanaowatangazia ninyi habari ya wokovu.”

18Alifanya hivyo kwa siku nyingi, lakini Paulo akiwa amekasirishwa na tendo hilo, aligeuka nyuma na kumwambia pepo, “Nakuamuru kwa Jina la Yesu umtoke ndani yake.” Naye akatoka na kumwacha mara moja.19Mabwana zake walipoona ya kuwa tumaini la faida yao limeondoka, waliwakamata Paulo na Sila na kuwaburuza sokoni mbele ya wenye mamlaka.20Walipowafikisha kwa mahakimu, walisema, “Hawa wanaume ni Wayahudi na wanasababisha ghasia kubwa katika mji wetu.21Wanafundisha mambo ambayo siyo sheria sisi kuyapokea wala kuyafuata kama Warumi.”22Umati ukawainukia kinyume Paulo na Sila, mahakimu wakararua nguo zao na kuwavua na kuamuru wachapwe viboko23Baada ya kuwachapa viboko vingi, waliwatupa gerezani na kumuamuru askari wa gereza kuwalinda vyema.24Baada ya kupokea amri hiyo, askari wa gereza aliwatupa katika chumba cha ndani ya gereza na kuwafunga miguu yao kwenye sehemu alipowahifadhi.

25Wakati wa usiku wa manane, Paulo na Sila wakawa wakiomba na kuimba nyimbo za kumsifu Mungu, huku wafungwa wengine wakiwasikiliza,26Ghafla kukatokea tetemeko kuu na misingi ya gereza ikatikiswa, milango ya gereza ikafunguka, na minyororo ya wafungwa wote ikalegezwa.27Mlinzi wa Gereza aliamka kutoka usingizini na akaona milango yote ya gereza imefunguliwa; hivyo akachukua upanga wake maana alitaka kujiua kwa sababu alifikiri wafungwa wote walikwishatoroka.28Lakini, Paulo akapiga kelele kwa sauti kuu, akisema, “Usijidhuru kwa sababu wote tuko mahali hapa.”29Mlinzi wa gereza aliomba taa ziletwe na akaingia ndani ya gereza kwa haraka, akitetemeka na kuogopa, akawaangukia Paulo na Sila,30na kuwatoa nje ya gereza na kusema, “Waheshimiwa, nifanye nini ili nipate kuokoka?”31Nao wakamwambia, “Mwamini Bwana Yesu nawe utaokoka pamoja na nyumba yako.”

32Walinena neno la Bwana kwake, pamoja na watu wote wa nyumbani kwake,33Mlinzi wa gereza aliwachukua usiku ule na kuwaosha sehemu walizoumia, yeye pamoja na watu wa nyumbani mwake wakabatizwa mara.34Akawaleta Paulo na Sila nyumbani kwake na kuwatengea chakula. Naye akawa na furaha kuu pamoja na watu wa nyumbani mwake kwa sababu walimwamini Mungu.

35Ilipokuwa mchana, mahakimu walituma ujumbe kwa yule mlinzi wa gereza wakisema, “Waruhusu wale watu waende.”

36Mlinzi wa gereza akamjulisha Paulo juu ya maneno hayo ya kuwa, “Mahakimu walituma ujumbe niruhusu mwondoke: hivyo tokeni nje na mwende kwa amani.”

37Lakini Paulo akawaambia, “Walitupiga hadharani, watu ambao ni Warumi bila kutuhukumu na waliamua kututupa gerezani; halafu sasa wanataka kututoa kwa siri? Hapana, haitawezekana, wao wenyewe waje kututoa mahali hapa.”38Walinzi wakawajulisha mahakimu juu ya maneno hayo, mahakimu wakaogopa sana pale walipojua kuwa Paulo na Sila ni Warumi.39Mahakimu wakaja na kuwasihi watoke, na walipowatoa nje ya gereza, waliwaomba Paulo na Sila watoke nje ya mji wao.40Kwa hiyo Paulo na Sila wakatoka nje ya gereza wakaja nyumbani kwa Lidia. Paulo na Sila walipowaona ndugu, waliwatia moyo na kisha kuondoka katika mji huo.

17

1Na walipopita katika miji ya Amfipoli na Apolonia, walikuja mpaka mji wa Thesalonike ambao kulikuwa na sinagogi la Wayahudi.2Kama ilivyo kawaida ya Paulo, alienda kwao, na kwa muda wa siku tatu za Sabato alijadiliana nao juu ya maandiko.3Alikuwa akiwafungulia maandiko na kuwaeleza kuwa, ilimpasa Kristo ateseke na kisha kufufuka tena kutoka kwa wafu. Aliwaambia, “Huyu Yesu ninayewaambia habari zake ndiye Kristo.”4Baadhi ya Wayahudi walishawishika na kuungana na Paulo na Sila, pamoja na Wagiriki wachamungu, akinamama wengi waongofu na kundi kubwa la watu.

5Lakini baadhi ya Wayahudi wasioamini, waliojawa na wivu, walienda sokoni na kuwachukuwa baadhi ya watu waovu, wakakusanya umati wa watu pamoja, na kusababisha ghasia mjini, kisha wakaivamia nyumba ya Yasoni, wakitaka kuwakamata Paulo na Sila ilikuwaleta mbele za watu.6Lakini walipowakosa, walimkamata Yasoni na baadhi ya ndugu wengine na kuwapeleka mbele ya maofisa wa mji, wakipiga kelele, “Hawa wanaume walioupindua ulimwengu wamefika mpaka huku pia.7Wanaume hawa waliokaribishwa na Yasoni wanaihalifu sheria ya Kaisari, wanasema kuna mfalme mwingine anayeitwa Yesu.”8Umati na maofisa wa mji waliposikia mambo hayo, walipatwa na wasiwasi.9Baada ya kuwa wamekwisha kuchukua fedha ya thamani ya ulinzi kutoka kwa Yason na wengine, waliwaachia waende.

10Usiku ule ndugu walimtuma Paulo na Sila Beroya. Na walipofika kule walikwenda katika sinagogi la Wayahudi.11Watu wale walikuwa wenye werevu mkubwa kuliko wale watu wa Thesalonike, kwa sababu walikuwa na utayari wa kulipokea neno kwa akili zao, na kuchunguza maandiko kila siku ili kuona kama maneno yaliyonenwa ndivyo yalivyo.12Kwa hiyo wengi wao waliamini, wakiwemo wanawake wenye ushawishi mkubwa wa Kigiriki na wanaume wengi.

13Lakini Wayahudi wa Thesalonike walipogundua kwamba Paulo anatangaza neno la Mungu huko Beroya, walienda huko na kuchochea na kisha kuanzisha ghasia kwa watu.14Kwa haraka, ndugu wakampeleka Paulo kwa njia ya ziwa, lakini Sila na Timotheo wakabaki pale.15Wale ndugu waliompeleka Paulo walienda naye hadi Athene, walipomwacha Paulo huko, walipokea maagizo kutoka kwake kuwa, Sila na Timotheo waje kwake kwa haraka iwezekanavyo.

16Na wakati akiwasubiri huko Athene, roho yake ilikasirishwa ndani yake kwa jinsi alivyouona mji ulivyojaa sanamu nyingi.17Hivyo akajadiliana katika sinagogi na wayahudi wale waliomcha Mungu na kwa wale wote aliokutana nao kila siku sokoni.

18Lakini baathi ya Wanafalsafa wa Waepikureo na Wastoiko wakamkabili. Na wengine wakasema, “Ni nini anachokisema huyu mwongeaji mchanga?” Wengine wakasema, “Inaonekana anahubiri habari ya mungu mgeni,” kwa sababu anahubiri habari ya Yesu na ufufuo.

19Wakamchukua Paulo na kumleta Areopago, wakisema, “Twaweza kujua haya mafundisho mapya unayoyaongea?20Kwa sababu unaleta mambo mapya katika masikio yetu. Kwa hivyo tunataka kujua haya mambo yana maana gani?”21(Na watu wote wa Athene pamoja na wageni waliopo kwao, hutumia muda wao aidha katika kuongea na kusikiliza juu ya jambo jipya.)

22Kwa hiyo Paulo akasimama katikati ya watu wa Areopago na kusema, “Enyi watu wa Athene, naona kuwa ninyi ni watu wa dini kwa kila namna,23Kwani katika kupita kwangu na kuangalia vitu vyenu vya kuabudu, nimeona maneno yalioandikwa kwenye moja ya madhabahu yenu, ikisema “KWA MUNGU ASIYEJULIKANA.” Hivyo basi, huyo mnayemwabudu pasipokujua, ndiye ninayewajulisha ninyi.

24Mungu aliyeumba dunia na kila kitu kilichoko ndani, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na nchi, hawezi kukaa katika mahekalu yaliyotengenezwa na mikono.25Na pia hatumikiwi na mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu kwao, kwani yeye mwenyewe huwapa watu uzima na pumzi na vitu vingine vyote.

26Kupitia mtu mmoja, alifanya mataifa yote ya watu waishio juu ya uso wa dunia, na akawawekea nyakati na mipaka katika maeneo wanaoishi.27Kwa hiyo, wanatakiwa kumtafuta Mungu, na yamkini wamfikie na kumpata, na kwa uhakika hayupo mbali na kila mmoja wetu.28Kwake tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu, kama vile mtunzi wenu mmoja wa shairi aliposema, ‘Tu wazaliwa wake.’

29Kwa hiyo, ikiwa sisi ni wazaliwa wa Mungu, hatupaswi kufikiri kuwa uungu ni kama dhahabu, au shaba, au mawe, sanamu iliyochongwa kwa ustadi na mawazo ya watu.30Kwa hiyo, Mungu alinyamazia nyakati zile za ujinga, lakini sasa anaamuru watu wote kila mahali wapate kutubu.31Hii ni kwa sababu ameweka siku atakayo ihukumu dunia kwa haki kwa mtu ambaye alimchagua. Mungu alitoa uhakika wa mtu huyu kwa kila mtu pale alipomfufua kutoka kwa wafu.”

32Na watu wa Athene waliposikia habari ya kufufuliwa kwa wafu, baadhi yao wakamdhihaki Paulo, ila wengine wakasema, “Tutakusikiliza tena kwa habari ya jambo hili.”33Baada ya hapo, Paulo akawaacha.34Lakini baadhi ya watu waliungana naye wakaamini, akiwemo Dionisio Mwareopago, na Mwanamke anaitwa Damari na wengine pamoja nao.

18

1Baada ya mambo hayo, Paulo aliondoka Athene kwenda Korintho.2Huko akampata Myahudi aitwaye Akwila mzaliwa wa Ponto, yeye na mke wake aitwaye Prisila walikuja kutoka huko Italia, kwa sababu Klaudia aliamuru Wayahudi wote waondoke Roma; Paulo akaja kwao;3Paulo akaishi na kufanya kazi nao kwani yeye anafanya kazi inayofanana na yao. Wao walikuwa ni watengeneza mahema.4Paulo akajadiliana nao katika sinagogi kila siku ya Sabato. Aliwashawishi Wayahudi pamoja na Wagiriki.

5Lakini Sila na Timotheo walipokuja kutoka Makedonia, Paulo alisukumwa na Roho kuwashuhudia Wayahudi kuwa Yesu ndiye Kristo.6Wakati Wayahudi walipompinga na kumdhihaki, hivyo Paulo akakung'uta vazi lake mbele yao, na kuwaambia, “Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu wenyewe; Mimi sina hatia. Kutoka sasa na kuendelea, nawaendea mataifa.”7Hivyo akaondoka kutoka pale akaenda kwenye nyumba ya Tito Yusto, mtu anayemwabudu Mungu. Nyumba yake iko karibu na sinagogi.8Krispo, kiongozi wa sinagogi pamoja na watu wa nyumbani mwake wakamwamini Bwana. Watu wengi wa Korintho waliomsikia Paulo akiongea waliamini na kubatizwa.

9Bwana akamwambia Paulo usiku kwa njia ya maono, “Usiogope, lakini ongea na usinyamaze.10Kwani mimi niko pamoja nawe, na hakuna atakayejaribu kukudhuru, maana nina watu wengi katika mji huu.”11Paulo akakaa huko kwa muda wa mwaka mmoja na miezi sita akifundisha neno la Mungu miongoni mwao.

12Lakini Galio alipofanywa mtawala wa Akaya, Wayahudi walisimama pamoja kinyume na Paulo na kumpeleka mbele ya kiti cha hukumu,13wakisema, “Mtu huyu huwashawishi watu wamwabudu Mungu kinyume cha sheria.”

14Wakati Paulo alipokuwa akitaka kusema, Galio akawaambia Wayahudi, “Ninyi Wayahudi, kama ingelikuwa ni kosa au uhalifu, ingekuwa halali kuwashughulikia.15Lakini kwa sababu ni maswali, yanayohusu maneno na majina, na sheria zenu, basi hukumuni ninyi wenyewe. Mimi sitamani kuwa hakimu kwa habari ya mambo hayo.”16Galio akawaamuru waondoke mbele ya kiti cha hukumu.17Hivyo, wakamkamata Sosthene, kiongozi wa sinagogi, wakampiga mbele ya kiti cha hukumu. Lakini Galio hakujali walichokifanya.

18Paulo, baada ya kukaa pale kwa muda mrefu, aliwaacha ndugu na kwenda kwa meli Shamu pamoja na Prisila na Akwila. Kabla ya kuondoka bandarini, alinyoa nywele zake kwani alikuwa ameapa kuwa Mnadhiri.19Walipofika Efeso, Paulo alimwacha Prisila na Akwila pale, lakini yeye mwenyewe akaingia kwenye sinagogi na kujadiliana na Wayahudi.20Walipomwambia Paulo akae nao kwa muda mrefu, yeye alikataa.21Lakini akaondoka kwao, akawaambia, “Nitarudi tena kwenu, ikiwa ni mapenzi ya Mungu.” Baada ya hapo, akaondoka kwa meli kutoka Efeso.

22Paulo alipotua Kaisaria, alipanda kwenda kusalimia Kanisa la Yerusalemu, kisha akashuka kwenda kwa kanisa la Antiokia.

23Baada ya kukaa kwa muda pale, Paulo aliondoka kupitia maeneo ya Galatia na Frigia huku akiwatia moyo wanafunzi wote.

24Myahudi mmoja aitwaye Apolo, mzaliwa wa Alexandria, alikuja Efeso. Alikuwa na ufasaha katika kuongea na hodari katika Maandiko.25Apollo alikuwa ameelekezwa katika mafundisho ya Bwana. Kwa jinsi alivyokuwa na bidii katika roho, aliongea na kufundisha kwa usahihi mambo yanayomuhusu Yesu, ila alijua tu ubatizo wa Yohana.26Apolo akaanza kuzungumza kwa ujasiri katika hekalu. Lakini Prisila na Akwila walipomsikia, walifanya urafiki naye na wakamwelezea juu ya njia za Mungu kwa usahihi.

27Alipotamani kuondoka kwenda Akaya, ndugu walimtia moyo na kuwaandikia barua wanafunzi walioko Akaya ili wapate kumpokea. Alipowasili, kwa neema aliwasaidia sana wale waliomini.28Kwa nguvu zake na maarifa, Apolo aliwazidi Wayahudi hadharani akionesha kupitia maandiko ya kuwa Yesu ndiye Kristo.

19

1Ikawa kwamba Apolo alipokuwa Korintho, Paulo akapita nyanda za juu na kufika katika mji wa Efeso, na akakuta wanafunzi kadhaa huko.2Paulo akawaambia, “Je, mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” Wakamwambia, “Hapana, hatukuweza hata kusikia kuhusu Roho Mtakatifu.”

3Paul alisema, “Sasa ninyi mlibatizwaje?” Wakasema, “Katika ubatizo wa Yohana.”

4Basi Paulo akajibu, “Yohana alibatiza kwa ubatizo wa toba. Akawaambia wale watu kwamba wanapaswa kumwamini yule ambaye angekuja baada yake, yaani, Yesu.”5Watu waliposikia habari hii, wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu.6Na ikawa Paulo alipoweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao na wakaanza kunena kwa lugha na kutabiri.7Jumla yao walikuwa wanaume wapatao kumi na wawili.

8Paulo alienda katika sinagogi akanena kwa ujasiri kwa muda wa miezi mitatu. Alikuwa akiongoza majadiliano na kuwashawishi watu kuhusu mambo yanayohusu ufalme wa Mungu.9Lakini Wayahudi wengine waliokuwa wakaidi na wasiotii, walianza kusema mabaya kuhusu njia ya Kristo mbele ya umati. Basi Paulo aliachana nao na akawatenga waaminio mbali nao. Naye alianza kuongea kila siku katika ukumbi wa Tirano.10Hii iliendelea kwa miaka miwili, kwa hiyo wote waliokuwa wanaishi katika Asia walisikia neno la Bwana, wote Wayahudi na Wayunani.

11Mungu alikuwa akifanya matendo makuu kwa mikono ya Paulo,12kwamba hata wagonjwa waliponywa, na roho chafu waliwatoka, wakati walipochukua vitambaa na nguo zilizokuwa zimeguza mwilini wa Paulo.

13Lakini palikuwapo Wayahudi wapunga pepo wakisafiri kupitia eneo hilo, wakilitumia jina la Yesu ili wawe na nguvu juu ya pepo wabaya. Wakiwaambia wale walikuwa na pepo wachafu; Wakisema, “Ninawaamuru mtoke kwa jina la Yesu ambaye Paulo anamhubiri.”14Waliofanya haya walikuwa wana saba wa kuhani Mkuu wa Kiyahudi, aliyeitwa Skeva.

15Roho mchafu akawajibu, “Yesu namjua, na Paulo namjua; lakini ninyi ni nani?”16Yule roho mchafu ndani ya mtu akawarukia wapunga pepo na akawashinda nguvu na kuwapiga. Ndipo wakakimbia kutoka ile nyumba wakiwa uchi na kujeruhiwa.17Jambo hili likajulikana kwa wote, Wayahudi na Wayunani, ambao waliishi huko Efeso. Wakawa na hofu sana, na jina la Bwana likazidi kuheshimiwa.

18Pia, wengi wa waumini walikuja na wakaungama na wakidhihirisha matendo mabaya waliyoyafanya.19Wengi waliokuwa wakifanya uganga wakakusanya vitabu vyao, wakavichoma mbele ya kila mtu. Wakati wao walipohesabu thamani ya vitu hivyo, ilikuwa vipande hamsini elfu vya fedha.

20Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana na katika nguvu.

21Sasa baada ya Paulo kukamilisha huduma yake kule Efeso, Paulo akaamua kwa mwongozo wa Roho kwenda Yerusalemu kupitia Makedonia na Akaya; Akasema, “Baada ya kuwako huko, yanipasa kuiona Rumi pia.”22Paul akawatuma Makedonia wanafunzi wake wawili, Timotheo na Erasto, ambao walikuwa wamemsaidia. Lakini yeye mwenyewe akabaki Asia kwa muda.

23Wakati huo kulitokea ghasia kubwa huko Efeso kuhusu ile Njia. 24Sonara mmoja jina lake Demetrio, ambaye aliyetengeneza visanamu vya fedha vya mungu Diana, alileta biashara kubwa kwa mafundi.

25Hivyo akawakusanya mafundi wa kazi hiyo na kusema, “Waheshimiwa, mnajua kwamba katika biashara hii sisi tunaingiza pesa nyingi.26Mnaona na kusikia kwamba, si tu hapa Efeso, bali karibia Asia yote, huyu Paulo amewashawishi na kuwageuza watu wengi. Anasema kwamba hakuna miungu ambayo imefanywa kwa mikono.27Na si tu iko hatari kwamba biashara yetu itakuwa haihitajiki tena, lakini pia na hekalu la mungu mke aliye mkuu Diana anaweza kuchukuliwa kuwa hana maana. Tena angeweza hata kupoteza ukuu wake, yeye ambaye Asia na dunia humwabudu.”

28Waliposikia haya, walijawa na hasira na wakapiga kelele, wakisema, “Diana wa Waefeso ni mkuu.”29Mji wote ukajaa ghasia, na watu wakakimbia pamoja ndani ya ukumbi wa michezo. Wakawakamata wasafiri wenzake na Paulo, Gayo na Aristariko, waliotoka Makedonia.30Paulo alitaka kuingia katika umati wa watu, lakini wanafunzi walimzuia.31Pia, baadhi ya maafisa wa mkoa wa Asia ambao walikuwa marafiki zake wakampelekea ujumbe kwa nguvu kumwomba asiingie katika ukumbi wa michezo.

32Baadhi ya watu walikuwa wakisema kitu hiki na wengine jambo lile, kwa sababu umati wa watu ulikuwa umechanganyikiwa. Wengi wao hawakuweza hata kujua kwa nini walikuja pamoja.33Wayahudi wakamleta Iskanda nje ya umati wa watu na kumuweka juu mbele ya watu. Iskanda akatoa ishara kwa mkono wake kutoa maelezo kwa watu.34Lakini walipotambua kuwa yeye ni Myahudi, wote wakapiga kelele kwa sauti moja kwa muda wa saa mbili, “Diana ni mkuu wa Wafeso.”

35Baada ya karani wa mji kuunyamazisha umati, alisema, ‘Enyi watu wa Efeso, ni nani asiyejua kwamba mji huu wa Efeso ni mtunzaji wa hekalu la Diana mkuu na ile sanamu iliyoanguka kutoka mbinguni?36Kuona basi kwamba mambo haya hayapingiki, tunapaswa kuwa na utulivu na msifanye chochote kwa haraka.37Kwa maana mmewaita watu hawa hapa mahakamani ambao si wezi wa hekalu wala si wenye kumkufuru mungu wetu mke.38Kwa hiyo, kama Demetrio na mafundi waliopamoja naye wana mashtaka dhidi ya mtu yeyote, mahakama ziko wazi na maliwali wapo. Na waletwe mbele ya shauri.39Lakini kama wewe ukitafuta chochote kuhusu mambo mengine, yatashughurikiwa katika kikao halali.40Kwa kuwa tuko katika hatari ya kutuhumiwa kuhusu ghasia siku hii. Hakuna sababu ya machafuko haya, na hatutakuwa na uwezo wa kuyaeleza.41Baada ya kusema haya, aliwatawanya makutano.

20

1Baada ya ghasia kumalizika, Paulo aliwatumania wanafunzi na baada ya kuwatia moyo aliwaaga akaondoka na kwenda Makedonia.2Naye akiishakupita mikoa hiyo na kwa maneno mengi ya kuwatia moyo waamuni, akaingia Uyunani.3Baada ya yeye kuwa pale kwa muda wa miezi mitatu, njama ziliundwa dhidi yake na Wayahudi alipokuwa akikaribia kusafiri kwa njia ya bahari kuelekea Shamu, hivyo aliamua kurudi kupitia Makedonia.4Walioandamana naye hadi Asia walikuwa Sopatro, mwana wa Pirho kutoka Berea; Aristariko na Sekundo, wote kutoka waamini wa Wathesalonike; Gayo wa Derbe; Timotheo; Tikiko na Trofimo kutoka Asia.5Lakini watu hawa wamekwisha tangulia na walikuwa wanatungojea kule Troa.6Kwa njia ya Bahari kutoka Filipi baada ya siku za mikate isiyotiwa chachu, na katika siku tano tukawafikia huko Troa. Tulikaa huko kwa siku saba.

7Hata siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekusanyika pamoja ili kuumega mkate, Paulo alizungumza na Waamini. Alikuwa akipanga kuondoka kesho yake, hivyo akaendelea kuongea hadi usiku wa manane.8Kulikuwa na taa nyingi katika chumba cha juu ambapo tulikuwa tumekusanyika pamoja.9Katika dirisha alikuwa amekaa kijana mmoja jina lake Utiko, ambaye alilemewa na usingizi mzito. Hata Paulo alipokuwa akihutubu kwa muda mrefu, kijana huyu, akiwa amelala, akaanguka chini kutoka ghorofa ya tatu na aliokotwa akiwa amekufa.10Lakini Paulo alishuka chini, alijinyoosha yeye mwenyewe juu yake, akamkumbatia. Kisha akasema, “Msikate tamaa, kwa kuwa yu hai.”11Kisha akapanda tena ghorofani na akaumega mkate, akala. Baada ya kuzungumza nao kwa muda mrefu hadi alfajiri, akaondoka.12Wakamleta yule kijana akiwa hai wakafarijika sana.

13Sisi wenyewe tulitangulia mbele ya Paulo kwa meli na tukaelekea Aso, ambapo sisi tulipanga kumchukua Paulo huko. Hiki ndicho yeye mwenyewe alitaka kufanya, kwa sababu alipanga kwenda kupitia nchi kavu.14Alipotufikia huko Aso, tukampakia kwenye Meli tukaenda Mitilene.15Kisha sisi tukatoka kutoka huko na siku ya pili tulifika upande wa pili wa kisiwa cha Kio. Siku iliyofuata, tukawasili kisiwa cha Samo, na kesho yake tukafika mji wa Mileto.16Kwa sababu Paulo alikuwa ameamua kusafiri kupitia Efeso, ili kwamba asitumie muda wowote katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka ya kuwahi Yerusalemu kwa ajili ya sikukuu ya Pentekoste, kama ingeliwezekana yeye kufanya hivyo.

17Kutoka Mileto akatuma watu hadi Efeso na akawaita wazee wa Kanisa.

18Walipofika kwake, akawaambia, “Ninyi wenyewe mwajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu muda wote.19Nimemtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi, na mateso yaliyonipata mimi kwa hila za Wayahudi.20Mwajua jinsi ambavyo sikujizuia kutangaza kwenu kitu chochote ambacho kilikuwa muhimu, na jinsi mimi nilivyowafundisha wazi wazi na pia kwenda nyumba kwa nyumba.21Mnajua jinsi mimi nilivyoendelea kuwaonya Wayahudi na Wayunani juu ya toba kwa Mungu na imani katika Bwana wetu Yesu.

22Na sasa, angalieni, mimi, nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko,23ila kwa kuwa Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi katika kila mji na anasema kwamba minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea.24Lakini mimi si kufikiria kwamba maisha yangu ni kwa njia yoyote ya thamani kwangu, ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu, kuishuhudia injili ya neema ya Mungu.25Na sasa, tazama, najua kwamba wote, miongoni mwa wale nilioenda kuwahubiria Ufalme, hamtaniona uso tena.26Kwa hiyo nawashuhudia leo hii, kwamba sina hatia kwa damu ya mtu yeyote.27Kwa maana sikujizuia kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.28Kwa hiyo iweni waangalifu juu yenu ninyi wenyewe, na juu ya kundi lolote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi. Iweni waangalifu kulichunga kusanyiko la Bwana, ambalo alilinunua kwa damu yake mwenyewe.29Najua kwamba baada ya kuondoka kwangu, mbwa mwitu wakali wataingia kwenu, na wasilihurumie kundi.30Najua kwamba hata miongoni mwenu wenyewe baadhi ya watu watakuja na kusema mambo mapotovu, ili kuwavuta wanafunzi wawafuate wao.31Kwa hiyo muwe macho. Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuweza kuacha kuwafundisha kila mmoja wenu kwa machozi usiku na mchana.

32Na sasa mimi nawakabidhi kwa Mungu, na kwa neno la neema yake, ambalo laweza kuwajenga na kuwapa urithi pamoja nao wote waliowekwa wakfu kwa Mungu.

33Sikutamani fedha, dhahabu, au mavazi.34Mnajua ninyi wenyewe kwamba mikono hii imenipatia mahitaji yangu mwenyewe na mahitaji ya wale waliokuwa pamoja nami.35Katika mambo yote niliwapa mfano wa jinsi inavyopasa kuwasaidia wanyonge kwa kufanya kazi, na jinsi mnavyopaswa kukumbuka maneno ya Bwana Yesu, maneno ambayo yeye mwenyewe alisema: “Ni heri kutoa kuliko kupokea.”

36Baada ya kusema namna hii, alipiga magoti akaomba pamoja nao.37Wote wakalia sana na kumwangukia Paulo shingoni na kumbusu.38Walihuzunika zaidi ya yote kwa sababu ya kile ambacho alikuwa amesema, kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Kisha wakamsindikiza merikebuni.

21

1Wakati tulipokua tumeachana nao, na tunasafiri baharini, tukafika moja kwa moja kwenye mji wa Kosi, na kesho yake tukafika mji wa Rodo, na kutoka huko tukafika mji wa Patara.2Tulipopata meli inayovuka kwenda Foinike, tulipanda tukasafiri.3Tulipofika mbele ya kisiwa cha Kipro, tukaiacha upande wa kushoto, tukasafiri hadi Siria, tukaweka nanga katika mji wa Tiro, kwa sababu huko ndiko meli ilikuwa ipakuliwe shehena yake.

4Baada ya kuwaona wanafunzi, tukakaa huko siku saba. Wanafunzi hawa wakamwambia Paulo kupitia kwa Roho kwamba yeye asikanyange Yerusalemu.5Hata tulipotimiza siku zile, sisi tukaondoka tukaenda zetu. Wote pamoja, na wanawake zao na watoto wao, walitusindikiza katika njia zetu hadi tulipotoka nje ya mji. Kisha tukapiga magoti pwani, tukaomba, tukaagana kila mmoja.6Tukapanda meli, huku nao wakarudi nyumbani kwao tena.

7Hata tulipomaliza safari yetu kutoka Tiro, tukafika Tolemai. Pale tulisalimia ndugu, na kukakaa nao kwa siku moja.8Kesho yake tuliondoka tukaenda Kaisaria. Sisi tukaingia nyumbani mwa Filipo, mhubiri wa injili, aliyekuwa mmoja wa wale saba, nasi tukakaa pamoja naye.9Mtu huyu alikuwa na mabinti wanne mabikira ambao walitabiri.

10Baada ya kukaa huko kwa siku kadhaa, akashuka kutoka Uyahudi nabii mmoja aitwaye Agabo.11Yeye alikuja kwetu na akautwaa mkanda wa Paulo. Kwa huo alijifunga miguu na mikono yake mwenyewe na kusema, “Roho Mtakatifu asema hivi, Wayahudi wa Yerusalemu watamfunga mtu anayemiliki mkanda huu, nao watamkabidhi mikononi mwa watu wa mataifa.”

12Tuliposikia mambo hayo, sisi na watu waliokuwa wakiishi mahali pale tulimsihi Paulo asipande kwende Yerusalemu.

13Ndipo Paulo alijibu, “Mnafanya nini, mnalia na kunivunja moyo wangu? Kwa maana niko tayari, siyo tu kufungwa, lakini pia kufia huko Yerusalemu kwa ajili ya jina la Bwana Yesu.”

14Kwa vile Paulo hakutaka kushawishiwa, tuliacha na kusema, “Basi mapenzi ya Bwana yafanyike.”

15Baada ya siku hizi, tulichukua mifuko yetu na tukapanda Yerusalemu.16Baadhi ya wanafunzi kutoka Kaisaria pia walifuatana nasi. Wakamleta mtu mmoja aitwaye Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani, ambaye tulikaa naye.

17Tulipofika Yerusalemu, ndugu walitukaribisha kwa furaha.18Kesho yake Paulo alienda pamoja nasi kwa Yakobo, na wazee wote walikuwepo.19Baada ya kuwasalimu, aliwapa taarifa moja baada ya nyingine ya mambo ambayo Mungu aliyotenda miongoni mwa mataifa kwa kupitia huduma yake.20Wakati waliposikia hayo, wakamsifu Mungu, na wakamwambia, “Unaona, ndugu, kuna maelfu wangapi wameamini miongoni mwa Wayahudi. Wao wote wana nia ya kushika sheria.21Wameambiwa kuhusu wewe, kwamba unafundisha Wayahudi wanaoishi kati ya mataifa kuachana na Musa, na kwamba unawaambia wasiwatahiri watoto wao, na wasifuate desturi za zamani.22Tunapaswa tufanye nini? Bila shaka watasikia kwamba wewe umekuja.23Hivyo fanya kile sisi tunachokuambia sasa: tunao watu wanne ambao wameweka nadhiri.24Wachukue watu hawa na ujitakase mwenyewe pamoja nao, na uwalipie gharama zao, ili waweze kunyoa vichwa vyao. Hivyo kila mmoja apate kujua kwamba mambo waliyoambiwa kuhusu wewe ni ya uongo. Watajifunza kwamba wewe pia unafuata sheria.25Lakini kwa habari za mataifa ambao wamekuwa waumini, tuliandika na kutoa maagizo kwamba wanapaswa kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu, na damu, kutokana na kile kilichonyongwa, na wajiepushe na uasherati.”26Ndipo, Paulo aliwatwaa wale wanaume, na siku ya pili, akajitakasa mwenyewe pamoja nao, akaingia Hekaluni, kutangaza kipindi cha siku za kujitakasa, hadi sadaka itolewa kwa ajili ya kila mmoja wao.

27Siku hizo saba zilipokaribia kumalizika, baadhi ya Wayahudi kutoka Asia wakamuona Paulo hekaluni, wakachochea makutano, na wakamnyoshea mikono.28Walikuwa wanapiga kelele, “Watu wa Israeli, tusaidieni. Huyu ni yule mtu anayewafundisha watu kila mahali mambo ambayo ni kinyume na watu, sheria, na mahali hapa. Pia amewaleta Wayunani katika hekalu na kupanajisi mahali hapa patakatifu.”29Kwa kuwa mwanzoni walikuwa wamemwona Trofimo Muefeso akiwa pamoja naye mjini, nao walidhani kwamba Paulo alimleta hekaluni.30Mji wote ulikuwa na taharuki, na watu wakakimbia pamoja na kumkamata Paulo. Wakamtoa nje ya hekalu, na milango mara ikafungwa.

31Walipokuwa wakijaribu kumuua, habari zilimfikia mkuu wa jeshi la walinzi kuwa Yerusalemu yote ilikuwa imejaa ghasia.32Mara hiyo akawachukua askari na jemadari akaukimbilia umati. Wakati watu walipomwona mkuu wa jeshi na askari, wakaacha kumpiga Paulo.

33Kisha mkuu wa jeshi alimkaribia na akamshika Paulo, na akaamuru afungwe minyororo miwili. Akamuuliza yeye ni nani na amefanya nini.34Baadhi ya watu kwenye umati walikuwa wanapayuka kitu hiki na wengine kingine. Kwa kuwa jemadari hakuweza kutambua chochote kwa sababu ya zile kelele, akaamuru Paulo aletwe ndani ya ngome.35Basi alipofika kwenye ngazi, akachukuliwa na askari kwa sababu ya ghasia za umati.36Maana umati wa watu walimfuata na waliendelea kupiga kelele, “Mwondoeni huyu!”

37Paulo alipokuwa analetwa ndani ya ngome, alimwambia mkuu wa jeshi, “Naweza kukwambia kitu?” Yule mkuu wa jeshi akasema, “Je unaongea Kiyunani?38Je, wewe si yule Mmisri ambaye awali aliongoza uasi na alichukua magaidi elfu nne nyikani?”

39Paulo akasema, “Mimi ni Myahudi, kutoka mji wa Tarso ya Kilikia. Mimi ni raia wa mji maarufu. Nawaomba, mniruhusu nizungumze na watu.”40Wakati jemadari alipompa ruhusa, Paulo akasimama penye ngazi na akatoa ishara kwa watu kwa mkono wake. Wakati kulipokuwa na ukimya sana, akaongea nao kwa Kihebrania. Akasema,

22

1“Ndugu na baba zangu, sikilizeni utetezi wangu nitakaofanya kwenu sasa.”2Makutano walipo sikia Paulo akiongea nao kwa kiebrania, wakanyamaza. Akasema,3“Mimi ni myahudi, nimezaliwa mji wa Tarso eneo la Kilikia, ila nilipata elimu katika mji huu, miguuni pa Gamalieli. Nilifundishwa kulingana na njia sahihi za sheria za baba zetu. Mimi ninabidii ya Mungu, kama ninyi nyote mlivyo leo.4Niliwatesa kwa njia hii hadi kufa; nikawafunga wanaume na wanawake na kuwatupa gerezani.5Hata kuhani mkuu na wazee wote wanaweza kutoa ushahidi kwamba nilipokea barua kutoka kwao kwa ajili ya ndugu walio Dameski, kwangu mimi kusafiri kwenda huko. Ilikuwa niwalete watu Yerusalemu wa njia ile ili wafungwe na kuadhibiwa.

6Ilitokea kwamba pale nilipokua nikisafiri nakaribia Dameski, majira ya mchana ghafla nuru kuu ikatokea mbinguni ikaanza kuniangaza kotekote.7Nikaanguka chini na kusikia sauti ikiniambia, ‘Sauli, Sauli kwanini unanitesa?’

8Nikajibu, ‘Wewe ni nani, Bwana?’ Akaniambia, ‘Mini ni Yesu Mnazareti, ambaye wewe unanitesa.’

9Wale waliokuwa na mimi waliiona nuru, ila hawakusikia sauti ya yule alieongea na mimi.10Nikasema, ‘Nifanye nini, Bwana?’ Bwana akaniambia, ‘Simama na uingie Dameski; huko utaambiwa kila kitu unachopaswa kufanya.’11Sikuweza kuona kwa sababu ya muangaza wa nuru ile, ndipo nikaenda Dameski kwa kuongozwa na mikono ya wale waliokuwa na mimi.12Huko nikakutana na mtu aitwaye Anania, alikuwa mtu aliyeshika sheria na mwenye kuheshimika mbele ya Wayahudi wote walioishi huko.13Akaja kwangu, akasimama mbele yangu, na kusema, ‘Ndugu yangu Sauli, upate kuona. ‘Kwa muda ule ule nikamuona.14Akasema, ‘Mungu wa baba zetu amekuchagua wewe upate kujua mapenzi yake, kumuona yule mwenye haki, na kusikia sauti itokayo kwenye kinywa chake.15Kwa sababu utakuwa shahidi wake kwa watu wote juu ya uliyoyaona na kusikia.16Basi sasa kwa nini unasubiri? Amka, ubatizwe, ukaoshe dhambi zako, ukiliitia jina lake.’

17Baada ya kurejea Yerusalemu, na nilipokuwa nikisali ndani ya hekalu, ikatokea kwamba nikapewa maono.18Nikamuona akiniambia, ‘Hima na utoke Yerusalemu haraka, kwa sababu hawatakubali ushuhuda wako kuhusu mimi.’19Nikasema, ‘Bwana, wao wenyewe wanajua niliwafunga gerezani na kuwapiga wale waliokuamini katika kila sinagogi20Na damu ya Stefano shahidi wako ilipomwagwa, mimi pia nilikuwa nimesimama karibu na kukubali na nilikuwa nalinda nguo za wale waliomwua.’21Lakini aliniambia, ‘Enenda, kwa sababu mimi nitakutuma uende mbali kwa watu wa mataifa.”’

22Watu wakamsikiza mpaka alipotamka maneno hayo. Hapo walipaza sauti na kusema, “Mwondoe mtu huyu katika nchi: kwa sababu sio sahihi aishi.”

23Walipokuwa wakipaza sauti, na kutupa mavazi yao na kutupa mavumbi juu,24jemedari mkuu akaamuru Paulo aletwe ngomeni. Akaamuru aulizwe huku anapigwa mijeledi, ili yeye mwenyewe ajue kwa nini walikuwa wanampigia kelele namna ile.

25Hata walipokuwa wamemfunga kwa kamba, Paulo akamwambia yule akida aliye simama karibu naye, “Je! Ni haki kwenu kumpiga mtu aliye Mrumi na bado hajahukumiwa?”

26Yule akida aliposikia maneno haya, akaenda kwa jemedari mkuu na kumwambia, akisema, “Unataka kufanya nini? Kwa maana mtu huyu ni Mrumi.”

27Jemedari mkuu akaja na kumwambia, “Niambie, je wewe ni raia wa Rumi?” Paulo akasema, “Ndiyo.”

28Jemedari akamjibu, “Ni kupitia kiasi kikubwa cha pesa ndipo nilipata uraia.” Lakini Paulo akamwambia, “Mimi ni Mrumi wa kuzaliwa.”29Basi wale waliokuwa tayari kwenda kumhoji wakaondoka na kumwacha wakati huo huo. Na jemedari naye akaogopa, alipojua kuwa Paulo ni Mrumi, na kwa sababu amemfunga.

30Siku iliyofuata, jemedari mkuu alitaka kujua ukweli kuhusu mashtaka ya Wayahudi dhidi ya Paulo. Hivyo akamfungua vifungo vyake akaamuru wakuu wa makuhani na baraza lote wakutane. Akamleta Paulo chini, na kumweka katikati yao.

23

1Paulo akawaangalia moja kwa moja watu wa baraza na kusema, “Ndugu zangu, nimeishi mbele za Mungu kwa dhamira nzuri hadi hivi leo.”2Kuhani mkuu Anania akawaamuru wale waliosimama karibu naye wampige kinywa chake.

3Ndipo Paulo akamwambia, “Mungu atakupiga wewe, ukuta uliopakwa chokaa. Umekaa ukinihukumu kwa sheria, nawe unaamuru nipigwe kinyume cha sheria?”

4Wale waliokuwa wamesimama karibu naye wakasema, “Hivi ndivyo unavyomtukana kuhani mkuu wa Mungu?”

5Paulo akasema, “Ndugu zangu, mimi sikujua kwamba huyu ni kuhani mkuu. Kwa kuwa imeandikwa, ‘Hutazungumza vibaya juu ya mtawala wa watu wako.’”

6Paulo alipoona ya kwamba upande mmoja wa baraza ni Masadukayo na wengine Mafarisayo, akapaza sauti na kusema, “Ndugu zangu, mimi ni Mfarisayo, mwana wa Mfarisayo. Ni kwa sababu hii nategemea kwa ujasiri ufufuo wa wafu ninao hukumiwa nao.”7Alipoyasema haya, marumbano makubwa yakatokea baina ya Mafarisayo na Masadukayo, na mkutano ukagawanyika.8Kwani Masadukayo husema hakuna ufufuo, malaika wala hakuna roho, ila Mafarisayo husema haya yote yapo.

9Ghasia kubwa ikatokea na baadhi ya waandishi waliokuwa upande wa Mafarisayo wakasimama na kujadili, wakisema, “Hatujaona chochote kibaya dhidi ya mtu huyu. Vipi kama roho au malaika ameongea na yeye?”10Wakati kulitokea hoja kubwa, mkuu wa majeshi aliogopa kwamba Paulo angeraruliwa vipande vipande na wao, hivyo akaamuru wanajeshi washuke chini na kumchukua kwa nguvu kutoka kwa wajumbe wa baraza, na kumleta katika ngome.

11Usiku uliofuata bwana alisimama karibu naye na kusema, “Usiogope, kwa kuwa umenishuhudia katika Yerusalemu, hivyo utatoa ushahidi pia katika Roma.”

12Kulipokucha, baadhi ya Wayahudi walifanya agano na kuita laana juu yao wenyewe: walisema ya kwamba hawatakula wala kunywa chochote mpaka watakapomuua Paulo.13Kulikuwa na watu zaidi ya arobaini ambao walifanya njama hii.14Wakaenda kwa wakuu wa makuhani na wazee na kusema, “Tumejiweka wenyewe kwenye laana kuu, tusile chochote hadi tutakapomwua Paulo.15Hivyo sasa, baraza limwambie jemadari mkuu amlete kwenu, kana kwamba mnaamua kesi yake kwa usahihi. Kwetu sisi tuko tayari kumwua kabla hajaja hapa.”

16Lakini mtoto wa dada yake na Paulo akasikia kwamba kulikuwa na njama, akaenda akaingia ndani ya ngome na kumwambia Paulo.17Paulo akamwita akida mmoja akasema, “Mchukue kijana huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwambia.”18Basi akida akamchukua yule kijana akampeleka kwa jemedari mkuu akamwambia, “Paulo yule mfungwa aliniita akataka nikuletee kijana huyu kwako. Ana neno la kukuambia.”19Yule jemadari mkuu akamshika kwa mkono akajitenga naye kando, na akamwuliza, “Ni kitu gani unachotaka kuniambia?”20Kijana yule akasema, “Wayahudi wamepatana kukuomba umlete Paulo kesho kwenye baraza kana kwamba wanataka kupata habari zake kwa usahihi zaidi.21Basi wewe usikubali kwa maana watu zaidi ya arobaini wanamvizia. Wamejifunga kwa laana, wasile wala wasinywe hata watakapomwua. Hata sasa wako tayari, wakisubiria kibali toka kwako.”22Basi yule jemadari mkuu akamwacha kijana aende zake, baada ya kumwagiza, “Usimwambie mtu yeyote ya kwamba umeniarifu haya.”

23Akawaita maakida wawili akasema watayarisheni askari mia mbili kwenda Kaisaria na askari wapanda farasi sabini, na wenye mikuki mia mbili, mtaondoka zamu ya tatu ya usiku.24Akawaambia kuweka wanyama tayari ambaye Paulo atamtumia na kumchukua salama kwa Feliki Gavana.25Akaandika barua kwa namna hii,26“Klaudio Lisia kwa Liwali mtukufu Feliki, salamu.27Mtu huyu alikamatwa na wayahudi wakawa karibu kumwua, ndipo nikaenda pamoja na kikosi cha askari nikamwokoa, nilipopata habari ya kuwa yeye ni raia wa kirumi.28Nilitaka kujua kwa nini wamemshtaki, hivyo nikampeleka kwenye baraza.29Nikaona kwamba alikuwa ameshitakiwa kwa ajili ya maswali ya sheria yao, wala hakushitakiwa neno lolote la kustahili kuuawa wala kufungwa.30Kisha ikajulikana kwangu kwamba kuna njama dhidi yake, hivyo kwa haraka nikamtuma kwako, na kuwaagiza wanaomshitaki pia walete mashitaka dhidi yake mbele yako. Kwaheri.”

31Basi wale askari wakatii amri: wakamchukua Paulo wakampeleka hata Antipatri usiku.32Siku iliyofuata, maaskari wengi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja naye, nao wakarudi zao ngomeni.33Na wapanda farasi walipofika Kaisaria, na kumpa liwali ile barua, wakamweka Paulo mikononi mwake.

34Naye liwali alipoisoma barua, alimuuliza Paulo alitokea jimbo gani; alipojua ya kwamba ni mtu wa Kilikia,35akasema, “Nitakusikia wewe watakapo kuja wale waliokushitaki,” akaamuru awekwe katika ikulu ya Herode.

24

1Baada ya siku tano, Anania kuhani mkuu, baadhi ya wazee na msemaji mmoja aitwaye Tertulo, wakaenda pale. Watu hawa wameleta mashtaka dhidi ya Paulo kwa gavana.2Paulo alipo simama mbele ya gavana, Tertulo akaanza kumshitaki na kusema kwa gavana, “Kwa sababu yako tuna amani kuu; na kwa maono yako yanaleta mageuzi mazuri katika taifa letu;3basi kwa shukurani yote tunapokea kila kitu ukifanyacho, mtukufu mheshimiwa Feliki.4Lakini nisikuchoshe zaidi, nakusihi unisikilize maneno machache kwa fadhili zako.5Kwa maana tumempata mtu huyu mkorofi, na anasababisha Wayahudi wote duniani kuasi. Tena ni kiongozi wa madhehebu ya Wanazarayo. 16Na tena alijaribu kulitia hekalu unajisi hivyo tukamkamata. 27Lisiasi, afisa, alikuja na akamchukua kwa nguvu mikononi mwetu. 38Ukimwuliza Paulo kuhusu mambo haya, hata utaweza kujifunza ni kitu gani tumemshtakia.9Wayahudi nao wakamshtaki Paulo, wakisema kwamba haya mambo yalikuwa kweli.

10Liwali alipompungia mkono ili Paulo aongee, Paulo alijibu, “Ninajua ya kwamba kwa miaka mingi umekua mwamuzi wa taifa hili, na nina furaha kujieleza mwenyewe kwako.11Waweza kuhakikisha kuwa hazijapita siku zaidi ya kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda kuabudu Yerusalemu.12Na waliponikuta katika hekalu, sikubishana na mtu yeyote, na sikufanya fujo katika mkutano, wala katika masinagogi wala ndani ya mji;13na wala hawawezi kuhakikisha kwako mashitaka wanayoyashitaki dhidi yangu.14Ila nakiri hili kwako, ya kwamba kwa njia ile ambayo wanaiita dhehebu, kwa njia hiyo hiyo ninamtumikia Mungu wa baba zetu. Mimi ni mwaminifu kwa yote yaliyoko kwenye sheria na maandiko ya manabii.15Nina ujasiri ule ule kwa Mungu ambao hata hao nao wanaungojea, kuja kwa ufufuo wa wafu, kwa wote wenye haki na wasio na haki pia;16na kwa hili, ninang'ang'ana ili niwe na dhamira isiyo na hatia mbele za Mungu na mbele ya watu kupitia mambo yote.17Sasa baada ya miaka mingi nimekuja kuleta msaada kwa taifa langu na zawadi ya fedha.18Nilipofanya hivi, Wayahudi fulani wa Asia wakanikuta ndani ya sherehe ya utakaso ndani ya hekalu, bila kundi la watu wala ghasia.19Watu hawa ambao imewapasa kuwapo mbele yako sasa hivi na waseme kile walichonacho juu yangu kama wana neno lo lote.20Au watu hawa wenyewe na waseme ni kosa gani waliloliona kwangu niliposimama mbele za baraza la Kiyahudi;21isipokuwa kwa ajili ya kitu kimoja nilichokisema kwa sauti niliposimama katikati yao, ‘Ni kwa sababu ya ufufuo wa wafu nimeshtakiwa mbele yako leo.”’

22Baadaye Feliki ambaye alikuwa ametaarifiwa vizuri kuihusu Njia, akauahirisha mkutano. Akasema, “Lisia jemedari atakaposhuka kutoka Yerusalemu nitatoa maamuzi dhidi ya mashitaka yenu.”23Ndipo akamwamuru akida amlinde Paulo, ila awe na uhuru na hata asiwepo mtu wakuwakataza marafiki zake wasimsaidie wala wasimtembelee.

24Baada ya siku kadhaa, Feliki akarudi na Drusila mkewe aliyekuwa Myahudi, akatuma kumwita Paulo na akasikiliza toka kwake habari za imani ndani ya Kristo Yesu.25Ila Paulo alipokuwa akijadiliana naye kuhusu haki, kuwa na kiasi na hukumu itakayokuja, Feliki akapata hofu akajibu, “Nenda mbali kwa sasa, ila nikipata muda tena, nitakuita.”26Muda huo huo, alitegemea kwamba Paulo atampa fedha kwa hiyo alimwita mara nyingi akaongea naye.

27Ila miaka miwili ilipopita, Porkio Festo akawa Liwali baada ya Feliki, ila Feliki alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, hivyo akamwacha Paulo chini ya uangalizi.


1Zingatia: Sehemu ya maneno ya mstari huu 24:6
2Zingatia: Mstari huu haumo kwenye nakala bora za kale
3haumo kwenye nakala bora za maandiko ya kale.

25

1Ndipo Festo alipoingia katika jimbo hilo na baada ya siku tatu alienda toka Kaisaria hadi Yerusalemu.2Kuhani mkuu na Wayahudi mashuhuri walileta shutuma dhidi ya Paulo kwa Festo, na walizungumza kwa nguvu kwa Festo.3Na walimwomba Festo fadhili juu ya habari za Paulo apate kumwita Yerusalemu ili waweze kumwua njiani.4Lakini Festo alijibu kwamba Paulo alikuwa mfungwa katika Kaisaria, na kwamba yeye mwenyewe atarudi huko haraka.5Alisema “Kwa hiyo, wale ambao wanaweza, wanaweza kwenda huko na sisi. Kama kuna kitu kibaya kwa mtu huyu, mnapaswa kumshtaki.”

6Baada ya kukaa siku nane au kumi zaidi, akarudi Kaisaria. Na siku iliyofuata akakaa katika kiti cha hukumu na kuamuru Paulo aletwe kwake.7Alipofika, Wayahudi kutoka Yerusalemu wakasimama karibu, Wakatoa mashtaka mengi mazito ambayo hawakuweza kuyathibitisha.

8Paulo alijitetea na kusema, ‘Si dhidi ya jina la Wayahudi, si juu ya hekalu, na si juu ya Kaisari, nimefanya mabaya.’

9Lakini Festo alitaka kujipendekeza kwa Wayahudi, na hivyo akamjibu Paulo kwa kusema, ‘Je, unataka kwenda Yerusalemu na kuhukumiwa na mimi kuhusu mambo haya huko?’

10Paulo alisema, ‘Ninasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Kaisari ambapo napaswa kuhukumiwa. Sijawakosea Wayahudi, kama wewe ujuavyo vema.11Ikiwa nimekosa na kama nimefanya kinachostahili kifo, sikatai kufa. Lakini kama shutuma zao si kitu, hakuna mtu anaweza kunikabidhi kwao. Natoa rufaa kwa Kaisari.”

12Baada ya Festo kuongea na baraza akajibu, “Umeomba rufaa kwa Kaisari; utaenda kwa Kaisari.”

13Baada ya siku kadhaa, mfalme Agripa na Bernike walifika Kaisaria kufanya ziara rasmi kwa Festo.14Baada ya kukaa hapo kwa siku nyingi, Festo aliwasilisha kesi ya Paulo kwa mfalme; Akasema, “Mtu mmoja aliachwa hapa na Feliki kama mfungwa.15Nilipokuwa Yerusalemu makuhani wakuu na wazee wa Wayahudi walileta mashtaka juu ya mtu huyu kwangu, nao waliuliza juu ya hukumu dhidi yake.16Kwa hili mimi niliwajibu kwamba si desturi ya Waroma kumtoa mtu kwa upendeleo, badala yake, mtuhumiwa anapaswa kuwa na nafasi ya kuwakabili washitaki wake na kujitetea dhidi ya tuhuma hizo.17Kwa hiyo, walipokuja pamoja hapa, sikuweza kusubiri, lakini siku iliyofuata niliketi katika kiti cha hukumu na kuamuru mtu huyo aletwe ndani.18Wakati washitaki waliposimama na kumshtaki, nilifikiri kwamba hakuna mashtaka makubwa yaliyoletwa dhidi yake.19Badala yake, walikuwa na mabishano fulani pamoja naye kuhusu dini yao na kuhusu Yesu ambaye alikuwa amekufa, lakini Paulo anadai kuwa yu hai.20Nilikuwa nimefumbwa jinsi ya kuchunguza suala hili, na nikamwuliza kama angeenda Yerusalemu kuhukumiwa kuhusu mambo haya.21Lakini Paulo alipoitwa awekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uamuzi wa Mfalme, niliamuru awekwe hata nitakapompeleka kwa Kaisari.”22Agripa alizungumza na Festo, “Ningependa pia kumsikiliza mtu huyu.” Festo, akasema, “Kesho utamsikiliza.”

23Hivyo kesho yake, Agripa na Bernike walifika na sherehe nyingi; walifika katika ukumbi na maafisa wa kijeshi, na watu mashuhuri wa mji. Na Festo alipotoa amri, Paulo aliletwa kwao.24Festo akasema, “Mfalme Agripa, na watu wote ambao wapo hapa pamoja nasi, mnamwona mtu huyu; jumuiya yote ya Wayahudi huko Yerusalemu na hapa pia wametaka niwashauri, na wao wakapiga kelele kwangu kwamba asiishi.25Naliona kwamba hakufanya lolote linalostahili kifo; lakini kwa sababu amemwita Mfalme, niliamua kumpeleka kwake.26Lakini sina kitu dhahiri cha kuandika kwa Mfalme. Kwa sababu hii, nimemleta kwako, hasa kwako wewe, Mfalme Agripa, ili nipate kuwa na kitu cha kuandika kuhusu kesi.27Kwa kuwa naona haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili.

26

1Hivyo, Agripa akamwambia Paulo, “Unaruhusiwa kujitetea.” Ndipo Paulo akanyoosha mkono wake akajitetea hivi.2“Najiona mwenye furaha, Mfalme Agripa, ili kufanya kesi yangu mbele yako leo dhidi ya mashtaka yote ya Wayahudi.3Hasa, kwa sababu wewe ni mtaalamu wa desturi za Wayahudi na maswali. Hivyo naomba unisikilize kwa uvumilivu.

4Kweli, Wayahudi wote wanajua jinsi nilivyoishi tangu ujana wangu katika taifa langu huko Yerusalemu.5Wananijua tangu mwanzo na wanapaswa kukubali kwamba niliishi kama Mfarisayo, dhehebu lenye msimamo mkali kwenye dini yetu.

6Sasa nimesimama hapa nihukumiwe kwa sababu mimi naliangalia ahadi ambayo Mungu aliifanya na baba zetu.7Hii ni ahadi ambayo makabila yetu kumi na mbili yanatumaini kupokea kama wakimwabudu Mungu kwa bidii usiku na mchana. Ni kwa ajili ya tumaini hili, mfalme Agripa, kwamba Wayahudi wananishitaki.8Kwa nini yeyote kati yenu anafikiri ni ajabu kwamba Mungu hufufua wafu?

9Wakati mmoja nilifikiria mwenyewe kwamba ningefanya mambo mengi dhidi ya jina la Yesu wa Nazareti.10Nilifanya haya katika Yerusalemu; Niliwafunga waamini wengi gerezani, na nilikuwa na mamlaka kutoka kwa wakuu wa makuhani kufanya hivyo; na wakati wanauawa, nilipiga kura dhidi yao.11Mara nyingi niliwaadhibu katika masinagogi yote na nilijaribu kuwafanya waikane imani yao. Nilikuwa na hasira sana juu yao na niliwafukuza hata katika miji ya ugenini.

12Wakati nilipokuwa nikifanya haya, nilienda Dameski, nikiwa na mamlaka na maagizo kutoka kwa makuhani wakuu;13nilipokuwa njiani wakati wa mchana, Mfalme, niliona mwanga kutoka mbinguni uliokuwa mkali kuliko jua na uling'aa kutuzunguka mimi na watu waliokuwa wakisafiri pamoja nami.14Sisi sote tulipoanguka chini, nilisikia sauti ikizungumza na mimi ikisema katika lugha ya Kiebrania: ‘Sauli, Sauli! Kwa nini unanitesa? Ni vigumu kwako kuupiga teke mchokoo.’

15Ndipo nikasema, ‘Wewe ni nani, Bwana?’ Bwana akajibu, ‘Mimi ni Yesu ambaye unanitesa.16Sasa inuka usimame kwa miguu yako; sababu kwa kusudi hili mimi nimeonekana kwako, nimekuteua kuwa mtumishi na shahidi juu ya mambo ambayo unajua kuhusu mimi sasa na mambo nitakayokuonyesha baadaye;17na nitakuokoa kutoka kwa watu na watu wa mataifa ambapo ninakutuma,18kufungua macho yao na kuwatoa gizani kwenda kwenye mwanga na kutoka kwenye nguvu za shetani wamgeukie Mungu; ili wapate kuupokea kutoka kwa Mungu msamaha wa dhambi na urithi ambao nimewapa wale niliowatenga kwa imani iliyo kwangu.

19Hivyo, mfalme Agripa, sikuweza kuasi maono ya mbinguni,20lakini, kwa wale walio katika Dameski kwanza, na kisha Yerusalemu na nchi yote ya Yudea, na pia kwa watu wa mataifa mengine, nilihubiri kwamba watubu na kumgeukia Mungu, wafanye matendo yanayostahili toba.

21Kwa sababu hiyo Wayahudi walinikamata hekaluni, wakajaribu kuniua.22Mungu amenisaidia mpaka sasa, hivyo nasimama na kushuhudia kwa watu wa kawaida na kwa wale wakubwa juu ya yale ambayo manabii na Musa walisema yatatokea na si vingine;23kwamba Kristo lazima atateseka na atakuwa wa kwanza kufufuka kutoka kwa wafu na kutangaza mwanga kwa Wayahudi na watu wa mataifa.”

24Paulo alipomaliza kujitetea, Festo alisema kwa sauti kubwa, “Paulo, wewe ni mwendawazimu! Masomo yako yamekufanya uwe mwendawazimu.”25Lakini Paulo akasema, “Mimi si mwendawazimu, mheshimiwa Festo; lakini kwa ujasiri nasema maneno ya ukweli mtupu.26Kwa kuwa mfalme anajua kuhusu mambo haya; na hivyo, ninaongea kwa uhuru kwake, kwa maana nina hakika kwamba hakuna lolote lililofichwa kwake; kwa kuwa hili halijafanywa pembeni.27Je, unaamini manabii, Mfalme Agripa? Najua kwamba unaamini.”28Agripa akamwambia Paulo, “Kwa muda mfupi unaweza kunishawishi mimi na kunifanya Mkristo?”

29Paulo akasema, “Namwomba Mungu kwamba, kwa muda mfupi au mrefu, si wewe tu, bali pia wote wanaonisikia leo, wawe kama mimi, lakini bila hii minyororo ya gerezani.”30Ndipo mfalme alisimama, na liwali, na Bernike pia, na wale waliokuwa wamekaa pamoja nao,31walipoondoka ukumbini, walizungumziana wao kwa wao na kusema, “Mtu huyu hastahili kifo wala kifungo.”

32Agripa akamwambia Festo, “Mtu huyu angeweza kuwekwa huru kama asingekata rufani kwa Kaisari.”

27

1Ilipoamuliwa kwamba tunatakiwa tusafiri kwa maji kwenda Italia, walimkabidhi Paulo na wafungwa wengine kwa afisa mmoja wa jeshi la Kiroma aliyeitwa Julio, wa kikosi cha Agustani.2Tukapanda meli kutoka Adramitamu, ambayo ilikuwa isafiri kandokando ya pwani ya Asia. Hivyo tukaingia baharini. Aristaka kutoka Thesolanike ya Makedonia akaenda pamoja nasi.3Siku iliyofuata tukatua nanga katika mji wa Sidoni, ambapo Julio alimtendea Paulo kwa ukarimu na akamruhusu kwenda kwa rafiki zake kupokea ukarimu wao.4Kutoka hapo tukaenda baharini tukasafiri kuzunguka kisiwa cha Kipro ambacho kilikuwa kimeukinga upepo, kwa sababu upepo ulikuwa ukitukabili.5Baada ya kuwa tumesafiri katika maji yaliyo karibu na Kilikia na Pamfilia, tukaja Mira, mji wa Lisia.6Pale yule afisa wa jeshi la Kiroma, akaikuta meli kutoka Alexandria ambayo ilikuwa isafiri kuelekea Italia. Akatupandisha ndani yake.7Baada ya kuwa tumesafiri polepole kwa siku nyingi na hatimaye tukawa tumefika kwa taabu karibu na Nido, upepo haukuturuhusu tena kuelekea njia hiyo, hivyo tukasafiri kandokando ya kivuli cha Krete tukiukinga upepo, mkabala na Salmone.8Tukasafiri kandokando ya pwani kwa ugumu, mpaka tukafika mahali palipoitwa Badari Nzuri ambayo iko karibu na mji wa Lasi.

9Tulikuwa tumechukua muda mwingi sana, na muda wa mfungo wa Kiyahudi ulikuwa umepita pia, na sasa ilikuwa ni hatari kuendelea kusafiri. Hivyo Paulo akatuonya,10na kusema, “Mabwana, naona safari ambayo tunataka tuichukue itakuwa na madhara na hasara nyingi, siyo tu ya mizigo na meli, lakini pia ya maisha yetu.”11Lakini afisa wa jeshi la Kiroma akamsikiliza zaidi bwana wake na mmiliki wa meli, kuliko mambo yale ambayo yalizungumzwa na Paulo.12Kwa sababu bandari haikuwa sehemu rahisi kukaa wakati wa baridi, mabaharia wengi wakashauri tusafiri kutoka pale, ili kwa namna yoyote tukiweza kuufikia mji wa Foinike, tukae pale wakati wa baridi. Foinike ni bandari huko Krete, na inatazama kaskazini mashariki na kusini mashariki.13Upepo wa kusini ulipoanza kuvuma polepole, mabaharia wakafikiri wamepata kile ambacho walikuwa wanakihitaji. Wakang'oa nanga na kusafiri kandokando ya Krete karibu na pwani.14Lakini baada ya muda mfupi upepo mkali, ulioitwa wa kaskazini mashariki, ukaanza kutupiga kutoka ng'ambo ya kisiwa.15Wakati meli ilipolemewa na kushindwa kuukabili upepo, tukakubaliana na hali hiyo, tukasafirishwa nao.16Tukakimbia kupitia ule upande uliokuwa unaukinga upepo wa kisiwa kiitwacho Kauda; na kwa taabu sana tulifanikiwa kuuokoa mtumbwi.17Baada ya kuwa wameivuta, walitumia kamba kuifunga meli. Waliogopa kwamba tungeweza kwenda kwenye eneo la mchanga mwingi la Syiti, hivyo wakashusha nanga na waliendeshwa kandokando.18Tulipigwa kwa nguvu sana na dhoruba, hivyo siku iliyofuata mabaharia wakaanza kutupa mizigo kutoka melini.19Siku ya tatu, mabaharia wakaanza kuyatoa maji kwa mikono yao wenyewe.20Wakati ambapo jua na nyota hazikutuangazia kwa siku nyingi, bado dhoruba kubwa ilitupiga, na matumaini kwamba tungeokolewa yalitoweka.

21Baada ya kuwa wameenda muda mrefu bila chakula, hapo Paulo akasimama katikati ya mabaharia akasema, “Enyi watu, mlipaswa mnisikilize, na tusingengo'a nanga kutoka Krete, ili kupata haya madhara na hasara.22Na sasa nawafariji mjitie moyo, kwa sababu hakutakuwa upotevu maisha kati yenu, isipokuwa hasara ya meli tu.23Kwa sababu usiku uliopita malaika wa Mungu, ambaye mimi ni wake, na ambaye ninamwabudu pia - malaika wake alisimama pembeni mwangu24na kusema, ‘Usiogope Paulo. Lazima usimame mbele ya Kaisari, na tazama, Mungu katika wema wake amekupa hawa wote ambao wanasafiri pamoja nawe.’25Hivyo, enyi watu, jipeni moyo, kwa sababu namwamini Mungu, kwamba itakuwa kama nilivyoambiwa.26Lakini lazima meli yetu itakwama katika kisiwa fulani.”

27Ulipofika usiku wa kumi na nne, tulipokuwa tukiendeshwa huko na huko kwenye bahari ya Adria, kama usiku wa manane hivi, mabaharia walifikiri kwamba wamekaribia nchi kavu.28Walitumia milio kupima kina cha maji na wakapata mita thelathini na sita, baada ya muda mfupi wakapima tena wakapata mita ishirini na saba.29Waliogopa kwanza tunaweza kugonga miamba, hivyo wakashusha nanga nne kutoka katika sehemu ya kuwekea nanga na wakaomba kwamba asubuhi ingekuja haraka.30Wale mabaharia walikuwa wanatafuta namna ya kuitelekeza ile meli na walizishusha majini mashua ndogo ndogo za kuokolea maisha, na wakajifanya kwamba wanatupa nanga kutoka sehemu ya mbele ya mashua.31Lakini Paulo akamwambia yule askari wa jeshi la Kiroma na wale askari, “Hamuwezi kuokoka isipokuwa hawa watu wanabaki kwenye meli.”32Kisha wale askari wakakata kamba za ile mashua na ikaachwa ichukuliwe na maji.

33Wakati mwanga wa asubuhi ulipokuwa unajitokeza, Paulo akawasihi wote angalau wale kidogo. Akasema, “Hii ni siku ya kumi na nne mnasuburi bila kula, hamjala kitu.34Hivyo nawasihi mchukue chakula kidogo, kwa sababu hii ni kwa ajili ya kuishi kwenu; na hakuna hata unywele mmoja wa vichwa vyenu utakaopotea.35Alipokwisha kusema hayo, akachukua mkate akamshukuru Mungu mbele ya macho ya kila mtu. Kisha akaumega mkate akaanza kula.36Kisha wote wakatiwa moyo na wao wakachukua chakula.37Tulikuwa watu 276 ndani ya meli.38Walipokwisha kula vya kutosha, waliifanya meli nyepesi kwa kutupa ngano ndani ya bahari.

39Ilipokuwa mchana, hawakuitambua nchi ile, lakini wakaona sehemu ya nchi kavu iliyoingia majini iliyokuwa na mchanga mwingi. Wakajadiliana kama wanaweza kuiendesha meli kuelekea hapo.40Hivyo wakazilegeza nanga wakaziacha baharini. Katika muda huo huo wakazilegeza kamba za nanga na wakaiinua sehemu ya mbele kuelekea kwenye upepo, hivyo wakaelekea kwenye hiyo sehemu ya mchanga mwingi.41Lakini wakaja mahali ambapo mikondo miwili ya maji inakutana, na meli ikaelekea mchangani. Na ile sehemu ya mbele ya meli ikakwama pale na haikuweza kutoka, lakini sehemu ya mbele ya meli ikaanza kuvunjika kwa sababu ya ukali wa mawimbi.

42Mpango wa wale askari ulikuwa ni kuwaua wafungwa, ili kwamba pasiwe na mtu ambaye angeogelea na kutoroka.43Lakini yule askari wa jeshi la Kiroma alitaka kumwokoa Paulo, hivyo akausimamisha mpango wao; na akawaamuru wale ambao wanaweza kuogelea, waruke kutoka melini kwanza na waende nchi kavu.44Kisha wale wengine watafuata, wengine juu ya vipande vya mbao na wengine juu ya vitu vingine kutoka kwenye meli. Kwa njia hii ikatokea kwamba wote tukafika salama nchi kavu.

28

1Tulipofikishwa salama, tulitambua kwamba kisiwa kinaitwa Malta.2Watu wenyeji wa pale si tu kwamba walitupa ukarimu wa kawaida, bali waliwasha moto na kutukaribisha sote, kwa sababu ya mvua na baridi iliyokuwa ikiendelea.3Lakini Paulo alipokuwa amekusanya mzigo wa kuni na kuuweka motoni, nyoka mwenye sumu akatoka kwenye zile kuni kwa sababu ya lile joto, na akajizungusha kwenye mkono wake.4Wakati wenyeji wa pale walipoona mnyama ananing'inia kutoka kwenye mkono wake, wakasemezana wao kwa wao, “Mtu huyu hakika ni muuaji ambaye ametoroka baharini, lakini haki haimuruhusu kuishi.”5Lakini yeye akamtikisia huyo nyoka katika moto na hakupata madhara yoyote.6Wao walimngojea avimbe kwa homa au aanguke ghafla na kufa. Lakini baada ya kumwangalia kwa muda mrefu na kuona kwamba hakuna jambo ambalo si la kawaida kwake, walibadilisha mawazo yao na kusema alikuwa mungu.

7Basi mahali pale karibu palikuwa na ardhi ambayo ilikuwa mali ya mkuu wa kisiwa, mtu aliyeitwa Pablio. Alitukaribisha na kutukarimu kwa siku tatu.8Ilitokea kwamba baba wa Pablio alishikwa na homa na ugonjwa wa kuhara. Na Paulo alipomwendea, aliomba, akaweka mikono juu yake, na kumponya.9Baada ya hili kutokea, watu wengine pale kisiwani waliokuwa wanaumwa pia walikwenda na waliponywa.10Watu wakatuheshimu kwa heshima nyingi. Tulipokuwa tunajiandaa kusafiri, walitupa vile tulivyovihitaji.

11Baada ya miezi mitatu, tulisafiri ndani ya meli ya Iskanda iitwayo miuungu pacha ambayo ilikuwa imetia nanga hapo kisiwani wakati wote wa baridi.12Baada ya kuwa tumetua katika mji wa Sirakusa, tulikaa pale siku tatu.13Kutokea pale tulisafiri tukafika katika mji wa Regio. Baada ya siku moja upepo wa kusini ulitokea ghafla, na baada ya siku mbili tukafika katika mji wa Putoli.14Huko tuliwakuta baadhi ya ndugu na tulikaribishwa kukaa nao kwa siku saba. Kwa njia hii tukaja Rumi.

15Kutoka huko wale ndugu, baada ya kuwa wamesikia habari zetu, walikuja kutupokea huko soko la Apia na Mikahawa Mitatu. Paulo alipowaona wale ndugu alimshukuru Mungu akajitia ujasiri.16Tulipoingia Roma, Paulo aliruhusiwa kuishi peke yake pamoja na yule askari aliyekuwa akimlinda.

17Basi ilikuwa baada ya siku tatu Paulo aliwaita pamoja wale watu waliokuwa viongozi kati ya Wayahudi. Walipokuja pamoja, alisema kwao, “Ndugu, pamoja na kwamba sijafanya kosa lolote kwa watu hawa au kufanya kinyume na taratibu za mababa zetu waliotutangulia, nilitolewa kama mfungwa kutoka Yerusalemu hadi kwenye mikono ya Warumi.18Baada ya kunihoji, walitamani kuniacha huru, kwa sababu kulikuwa hakuna sababu kwangu mimi ya kustahili adhabu ya kifo.19Lakini wale Wayahudi walipoongea kinyume cha shauku yao, nililazimika kukata rufaa kwa Kaisaria, japokuwa haikuwa kana kwamba naleta mashtaka juu ya taifa langu.20Kwa sababu ya kukata kwangu rufaa, hivyo, niliomba kuwaona na kuongea nanyi. Ni kwa sababu ya kile ambacho Israel anaujasiri kwacho, nimefungwa na kifungo hiki.”

21Kisha wakamwambia, “Hatujawahi kupokea barua kutoka Yudea kukuhusu wewe, wala hakuna ndugu aliyekuja na kutoa taarifa au kusema neno lolote mbaya kuhusu wewe.22Lakini tunataka kusikia kutoka kwako unafikiri nini kuhusu hili kundi la watu hawa, kwa sababu inajulikana kwetu kwamba linaongea kinyume kila mahali.”

23Walipokuwa wametenga siku kwa ajili yake, watu wengi zaidi walimjia mahali alipokuwa anaishi. Alisema lile jambo kwao na kushuhudia kuhusu ufalme wa Mungu. Alijaribu kuwashawishi kuhusu Yesu, kwa namna zote mbili kutoka katika sheria za Musa na kutoka kwa manabii, kuanzia asubuhi hadi jioni.24Baadhi yao walishawishika kuhusu mambo yale yaliyosemwa, wakati wengine hawakuamini.25Waliposhindwa kukubaliana wao kwa wao, waliondoka baada ya Paulo kulisema jambo hili moja, “Roho Mtakatifu alisema vyema kupitia Isaya nabii kwa baba zenu.
26Alisema, ‘Nenda kwa watu hawa useme, ‘Kwa masikio yenu mtasikia, lakini hamtaelewa; Na kwa macho yenu mtaona lakini hamtatambua.
27Kwa ajili ya mioyo ya watu hawa imekuwa dhaifu, masikio yao yamesikia kwa taabu, wamefumba macho yao; ili kwamba wasijekutambua kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kuelewa kwa mioyo yao, na kugeuka tena, na ningeliwaponya.’

28Kwa hiyo, mnapaswa kujua kwamba huu wokovu wa Mungu umepelekwa kwa watu wa mataifa, na watasikiliza.”291

30Paulo alikaa katika nyumba yake ya kupanga kwa miaka yote miwili, na aliwakaribisha wote waliokuja kwake.31Alikuwa akihubiri ufalme wa Mungu na alikuwa akifundisha mambo juu ya Bwana Yesu Kristo kwa ujasiri wote. Hakuna aliyemzuia.


1Zingatia: Mstari huu “Wakati alipokuwa amesema mambo haya, Wayahudi waliondoka, wakiwa na mashindano makubwa kati yao.” haumo kwenye nakala bora za kale.

Warumi

1

1Paulo, mtumishi wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kutengwa kwa ajili ya Injili ya Mungu.2Hii ndio ile Injili aliyoiahidi zamani kupitia manabii wake katika maandiko matakatifu.3Ni kuhusu Mwana wake, aliyezaliwa kutoka ukoo wa Daudi kwa jinsi ya mwili.4Yeye alitangazwa kuwa Mwana wa Mungu kwa nguvu ya Roho mtakatifu kwa ufufuo wa wafu, Yesu Kristo Bwana wetu.5Kupitia yeye tumepokea neema na utume kwa utii wa imani kati ya mataifa yote, kwa ajili ya jina lake.6Kati ya mataifa haya, ninyi pia mmeitwa kuwa wa Yesu Kristo.7Barua hii ni kwa wote walioko Rumi, wapendwao na Mungu, walioitwa kuwa watu watakatifu. Neema na iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

8Kwanza, namshukuru Mungu wangu katika Yesu Kristo kwa ajili yenu nyote, kwa sababu imani yenu inahubiriwa katika dunia nzima.9Kwa maana Mungu ni shahidi wangu, ambaye ninamtumikia kwa roho yangu katika injili ya Mwana wake, jinsi niwatajavyo bila kukoma.10Daima naomba katika sala zangu kwamba kwa njia yoyote nipate mwishowe kuwa na mafanikio sasa kwa mapenzi ya Mungu katika kuja kwenu.11Maana natamani kuwaona, ili nipate kuwapa ninyi baadhi ya karama za rohoni, nipate kuwaimarisha.12Yaani, natazamia kutiwa moyo pamoja nanyi, kwa njia ya imani ya kila mmoja wetu, yenu na yangu.13Sasa ndugu, sitaki mkose kufahamu kwamba, mara nyingi nimekusudia kuja kwenu (lakini nimezuiliwa mpaka sasa). Nilitaka hivi ili kuwa na matunda kwenu kama ilivyo pia miongoni mwa watu wa mataifa.14Nadaiwa na Wayunani na wageni pia, werevu na wajinga.15Kwa hiyo, kwa upande wangu, mimi niko tayari kutangaza injili kwenu pia ninyi mlio huko Roma.

16Kwa maana siionei haya injili, kwa kuwa ni uweza wa Mungu uletao wokovu kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza na kwa Myunani pia.17Kwa maana haki ya Mungu imedhihirishwa kutoka imani hata imani, kama ilivyo andikwa, “Mwenye haki ataishi kwa imani.”

18Maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni dhidi ya uasi na uovu wote wa watu, ambao kwa njia ya udhalimu huificha kweli.

19Hii ni kwa sababu, yote yanayoweza kujulikana juu ya Mungu ni wazi kwao. Maana Mungu amewafahamisha.20Maana mambo yake yasioonekana vizuri yamekuwa wazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu. Yanaeleweka kupitia vitu vilivyoumbwa. Mambo haya ni uwezo wake wa milele na asili ya uungu. Matokeo yake, watu hawa hawana udhuru.21Hii ni kwa sababu, ingawa walijua kuhusu Mungu, hawakumtukuza yeye kama Mungu, wala hawakumpa shukrani. Badala yake, wamekuwa wapumbavu katika mawazo yao, na mioyo yao yenye ujinga ilitiwa giza.22Walijiita kuwa ni werevu, lakini wakawa wajinga.23Waliubadili utukufu wa Mungu asie na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, ya wanyama wenye miguu minne, na ya viumbe vitambaavyo.

24Kwa hiyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa za mioyo yao kwa uchafu, kwa miili yao kufedheheshwa baina yao.25Ni wao walioibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, na ambao waliabudu na kutumikia viumbe badala ya Muumbaji, ambaye anasifiwa milele. Amina.

26Kwa sababu hii, Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, kwa kuwa wanawake wao walibadilisha matumizi yao ya asili kwa kile kilicho kinyume na asili.27Hali kadhalika, wanaume pia wakaacha matumizi yao ya asili kwa wanawake na kuwakwa na tamaa dhidi yao wenyewe. Hawa walikuwa wanaume ambao walifanya na wanaume wenzao yasiyo wapasa, na ambao walipokea adhabu iliyostahili upotovu wao.

28Kwa sababu walikataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wafanye mambo yale yasiyofaa.29Wamejawa na udhalimu wote, uovu, tamaa na ubaya. Wamejawa na wivu, uuaji, ugomvi, udanganyifu, na nia mbaya.30Wao pia ni wasengenyaji, wasingiziaji, na wenye kumchukia Mungu. Wenye vurugu, kiburi, na majivuno. Wao ni watunga mabaya, na wasiotii wazazi wao.31Wao hawana ufahamu; wasioaminika, hawana mapenzi ya asili, na wasio na huruma.32Wanaelewa kanuni za Mungu, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo wanastahili kifo. Lakini si tu wanafanya mambo hayo, wao pia wanakubaliana na wale wanaofanya mambo hayo.

2

1Kwa hiyo hauna udhuru, wewe uhukumuye, kwa maana katika yale uhukumuyo mwingine wajitia hatiani mwenyewe. Kwa maana wewe uhukumuye unafanya mambo yale yale.2Lakini twajua kwamba hukumu ya Mungu ni ya kweli juu yao wafanyao mambo kama hayo.3Lakini wewe tafakari hili, wewe ambaye unahukumu wale wanaotenda mambo hayo ingawa nawe unafanya mambo yayo hayo. Je utaepuka hukumu ya Mungu?4Au unafikiri kidogo sana juu ya wingi wa wema wake, kuchelewa kwa adhabu yake, na uvumilivu wake? Je, hujui kwamba wema wake unapaswa kukuelekeza katika toba?5Bali kwa kadiri ya ugumu wako na kwa moyo wako usio na toba wajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu kwa siku ile ya ghadhabu, yaani, siku ile ya ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu.

6Yeye atamlipa kila mtu kipimo sawa na matendo yake:7kwa wale ambao kwa uthabiti wa matendo mema wametafuta sifa, heshima na kutokuharibika, atawapa uzima wa milele.8Lakini kwa wale ambao ni wabinafsi, wasioitii kweli bali hutii dhuluma, ghadhabu na hasira kali itakuja.9Mungu ataleta dhiki na shida juu ya kila nafsi ya binadamu aliyefanya uovu, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.10Lakini sifa, heshima na amani itakuja kwa kila mtu atendaye mema, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia.11Kwa maana hakuna upendeleo kwa Mungu.

12Kwa maana kama vile wengi waliokosa pasipo sheria watapotea pasipo sheria, na kama vile wengi waliokosa kulingana na sheria watahukumiwa kwa sheria.13Maana si wasikiaji wa sheria walio wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale waitendao sheria watakaohesabiwa haki.14Kwa maana watu wa Mataifa, ambao hawana sheria, wanafanya kwa asili mambo ya sheria, wao, wamekuwa sheria kwa nafsi zao, ingawa wao hawana sheria.15Kwa hili wanaonesha kwamba matendo yanayohitajika kwa mujibu wa sheria yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia zinawashuhudia wao, na mawazo yao wenyewe ama huwashitaki au huwalinda wao wenyewe.16Haya yatatokea katika siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu wote, sawasawa na injili yangu, kwa njia ya Yesu Kristo.

17Tuseme kwamba unajiita mwenyewe Myahudi, aliyekaa katika sheria, shangilia kwa kujisifu katika Mungu,18yajue mapenzi yake, na kupima mambo ambayo yanatofautiana nayo, baada ya kuagizwa na sheria.19Na tuseme kwamba una ujasiri kwamba wewe mwenyewe ni kiongozi wa kipofu, mwanga kwa wale walio gizani,20msahihishaji wa wajinga, mwalimu wa watoto, na kwamba unayo katika sheria jinsi ya elimu na kweli.21Wewe basi, uhubiriye mwingine, je, hujifundishi mwenyewe? Wewe uhubiriye kutokuiba, je wewe huiba?22Wewe usemae usizini, je unazini? Wewe uchukiaye sanamu, je unaiba hekaluni?23Wewe ujisifuye katika sheria, je haumfedheheshi Mungu katika kuvunja sheria?24Kwa maana “jina la Mungu linafedheheshwa kati ya watu wa mataifa kwa sababu yenu,” kama ilivyoandikwa.

25Kwa maana Kutahiriwa kweli kwafaa kama ukitii sheria, lakini kama wewe ni mkiukaji wa sheria, kutahiriwa kwako kunakuwa kutokutahiriwa.26Basi, ikiwa, mtu asiyetahiriwa anaendelea kushika matakwa ya sheria, je kutokutahiriwa kwake hakutachukuliwa kana kwamba ametahiriwa?27Na yeye asiyetahiriwa kwa asili hatakuhukumu kama akitimiza sheria? Hii ni kwa sababu una maandiko yaliyoandikwa na tohara pia lakini bado u mkiukaji wa sheria!28Kwa maana yeye si Myahudi aliye kwa hali ya nje; wala kutahiriwa si kule ambako ni kwa nje tu katika mwili.29Lakini yeye ni Myahudi aliye kwa ndani, na tohara ni ya moyo, katika roho, si katika andiko. Sifa ya mtu wa namna hiyo haitokani na watu bali yatoka kwa Mungu.

3

1Kisha ni faida gani aliyo nayo Myahudi? Na faida ya tohara ni nini?2Ni vyema sana kwa kila njia. Awali ya yote, Wayahudi walikabidhiwa ufunuo kutoka kwa Mungu.3Lakini, itakuwaje iwapo baadhi ya Wayahudi hawakuwa na imani? Je, kutokuamini kwao kutafanya uaminifu wa Mungu kuwa batili?4La hasha. Badala yake, acha Mungu aonekane kuwa kweli, hata kama kila mtu ni mwongo. Kama ilivyokuwa imeandikwa, “Ya kwamba uweze kuonekana kuwa mwenye haki katika maneno yako, na uweze kushinda uingiapo katika hukumu.”

5Lakini ikiwa uovu wetu unaonesha haki ya Mungu, tuseme nini? Mungu si dhalimu atoapo ghadhabu yake, je yupo hivyo? (Naongea kutokana na mantiki ya kibinadamu.)6La hasha! Ni jinsi gani basi Mungu atauhukumu ulimwengu?7Lakini ikiwa kweli ya Mungu kupitia uongo wangu hutoa sifa tele kwa ajili yake, kwa nini ningali bado nahukumiwa kama mwenye dhambi?8Kwa nini tusiseme, kama tulivyosingiziwa na kama wengine wanavyothibitisha kwamba tunasema, “Tufanye uovu, ili mema yaje”? Hukumu juu yao ni ya haki.

9Ni nini basi? Tunajitetea wenyewe? Hapana kabisa. Kwa kuwa sisi tayari tumewatuhumu Wayahudi na Wayunani wote pamoja, ya kuwa wapo chini ya dhambi.10Hii ni kama ilivyoandikwa: “Hakuna mwenye haki, hata mmoja.11Hakuna mtu ambaye anaelewa. Hakuna mtu ambaye anamtafuta Mungu.

12Wote wamegeuka. Wao kwa pamoja wamekuwa hawana maana. Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja.
13“Makoo yao ni kaburi lililo wazi. Ndimi zao zimedanganya. Sumu ya nyoka ipo chini ya midomo yao.
14“Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu.”
15“Miguu yao ina mbio kumwaga damu.
16Uharibifu na mateso yapo katika njia zao.
17Watu hawa hawajajua njia ya amani.
18“Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yao.”

19Sasa tunajua kwamba chochote sheria isemacho, husema na wale walio chini ya sheria. Hii ni ili kwamba kila kinywa kifungwe, na hivyo kwamba ulimwengu wote uweze kuwajibika kwa Mungu.20Hii ni kwa sababu hakuna mwili utakaohesabiwa haki kwa matendo ya sheria mbele za macho yake. Kwa kuwa kupitia Sheria huja ufahamu wa dhambi.

21Lakini sasa pasipo sheria, haki ya Mungu imejulikana. Ilishuhudiwa kwa sheria na Manabii,22hiyo ni, haki ya Mungu kupitia imani katika Yesu Kristo kwa wale wote wanaoamini. Maana hakuna tofauti.23Kwa kuwa wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.24Wamehesabiwa haki bure kwa neema yake kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.25Kwa maana Mungu alimtoa Kristo Yesu awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Alimtoa Kristo kama ushahidi wa haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizopita26katika uvumilivu wake. Haya yote yalitokea ili kuonesha haki yake wakati huu wa sasa. Hii ilikuwa ili aweze kujithibitisha mwenyewe kuwa haki, na kuonesha kwamba humhesabia haki mtu yeyote kwa sababu ya imani katika Yesu.

27Kuwapi basi kujisifu? Kumetengwa. Kwa misingi ipi? Misingi ya matendo? Hapana, lakini kwa misingi ya imani.28Hivyo tunahitimisha kwamba mtu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.29Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia.30Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani. 29 Au Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Je yeye si Mungu wa watu wa Mataifa pia? Ndiyo, wa mataifa pia. Ikiwa kwa kweli Mungu ni mmoja, atawahesabia haki walio wa tohara kwa imani, na wasiotahiriwa kwa njia ya imani.31Je sisi twaibatilisha sheria kwa imani? La hasha! Kinyume cha hayo, sisi twaithibitisha sheria.

4

1Tutasema nini tena kwamba Abrahamu, baba yetu kwa jinsi ya mwili, amepatikana?2Kwa maana ikiwa Abrahamu alihesabiwa haki kwa matendo, angekuwa na sababu ya kujisifu, lakini si mbele za Mungu.3Kwani maandiko yanasemaje? “Abrahamu alimwamini Mungu, na ikahesabiwa kwake kuwa haki.”4Sasa kwa mtu afanyaye kazi, malipo yake hayahesabiwi kuwa ni neema, bali kuwa ni deni.5Lakini kwa mtu asiyefanya kazi bali anamwamini yeye ambaye amhesabia haki asiyekuwa mtaua, imani yake mtu huyo imehesabiwa kuwa haki.6Daudi pia hunena baraka juu ya mtu ambaye Mungu amhesabia haki pasipo matendo.

7Alisema, “Wamebarikiwa wale ambao maovu yao yamesamehewa na ambao dhambi zao zimefunikwa.
8Amebarikiwa mtu yule ambaye Bwana hamhesabii dhambi.

9“Basi je baraka hizi ni kwa wale waliotahiriwa tu, au pia kwa wale wasiotahiriwa? Kwa maana twasema, “kwa Abrahamu imani yake ilihesabiwa kuwa ni haki.”10Hivyo ilihesabiwaje basi? Wakati Abrahamu alikuwa katika tohara, au kabla hajatahiriwa? Haikuwa katika kutahiriwa, bali katika kutotahiriwa.11Abrahamu alipokea alama ya kutahiriwa. Huu ulikuwa muhuri wa ile haki ya imani aliyokuwa nayo tayari kabla hajatahiriwa. Matokeo ya ishara hii ni kwamba alifanyika kuwa baba wa wote waaminio, hata kama wapo katika kutotahiriwa. Hii ina maana kwamba haki itahesabiwa kwao.12Hii pia ilimaanisha kuwa Abrahamu alifanyika baba wa tohara si tu kwa wale wanaotokana na tohara, bali pia wale wanaozifuata nyayo za baba yetu Abrahamu. Na hii ndiyo imani aliyokuwa nayo kwa wasiotahiriwa.

13Kwa maana haikuwa kwa sheria kwamba ahadi ilitolewa kwa Abrahamu na uzao wake, ahadi hii ya kwamba watakuwa warithi wa dunia. Isipokuwa, ilikuwa kupitia haki ya imani.14Kwa maana kama wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika.15Kwa sababu sheria huleta ghadhabu, lakini pale ambapo hakuna sheria, pia hakuna kutotii.16Kwa sababu hii hili hutokea kwa imani, ili iwe kwa neema. Matokeo yake, ahadi ni dhahiri kwa uzao wote. Na wazawa hawa si tu wale wanaojua sheria, bali pia wale ambao ni wa imani ya Abrahamu. Kwa maana yeye ni baba yetu sisi sote,17kama ilivyoandikwa, “Nimekufanya wewe kuwa baba wa mataifa mengi.” Abrahamu alikuwa katika uwepo wa yule aliyemwamini, yaani, Mungu ambaye huwapa wafu uzima na kuyaita mambo ambayo hayapo ili yaweze kuwepo.18Licha ya hali zote za nje, Abrahamu kwa ujasiri alimuamini Mungu kwa siku zijazo. Hivyo akawa baba wa mataifa mengi, kulingana na kile kilichonenwa,”... Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.”19Yeye hakuwa dhaifu katika imani. Abrahamu alikiri kwamba mwili wake mwenyewe ulikwisha kufa - alikuwa na umri wa karibu miaka mia moja. Pia alikubaliana na hali ya kufa ya tumbo la Sara.20Lakini kwa sababu ya ahadi ya Mungu, Abrahamu hakusita katika kutokuamini. Bali, alitiwa nguvu katika imani na alimsifu Mungu.21Alikuwa akijua hakika ya kuwa kile ambacho Mungu ameahidi, alikuwa na uwezo wa kukikamilisha.22Kwa hiyo hii, “ilihesabiwa kwake kuwa ni haki.”

23Sasa haikuandikwa tu kwa faida yake, kwamba, “ilihesabiwa kwake.”24Iliandikwa kwa ajili yetu pia, kwa waliowekewa kuhesabiwa, sisi ambao tunaamini katika yeye aliyemfufua Bwana wetu Yesu kutoka wafu.25Huyu ni yule ambaye alitolewa kwa ajili ya makosa yetu na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.

5

1Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.2Kupitia yeye sisi pia tuna fursa kwa njia ya imani katika neema hii ambayo ndani yake tunasimama. Tunafurahi katika ujasiri atupao Mungu kwa ajili ya baadaye, ujasiri ambao tutashiriki katika utukufu wa Mungu.3Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu.4Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye.5Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.

6Kwa tulipokuwa tungali tu dhaifu, kwa wakati muafaka Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.7Kwa kuwa itakuwa vigumu mmoja kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki. Hii ni kwamba, pengine mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.8Lakini Mungu amehakikisha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.9Kisha zaidi ya yote, sasa kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa kwa hiyo kutoka katika gadhabu ya Mungu.10Kwa kuwa, ikiwa wakati tulipokuwa maadui, tulipatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumekwisha patanishwa, tutaokolewa kwa maisha yake.11Siyo hivi tu, bali pia tunafurahi katika Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo, kupitia yeye ambaye sasa tumepokea upatanisho huu.

12Kwa hiyo basi, kama kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani, kwa njia hii kifo kiliingia kwa njia ya dhambi. Na kifo kikasambaa kwa watu wote, kwa sababu wote walifanya dhambi.13Kwa kuwa hadi sheria, dhambi ilikuwa duniani, lakini dhambi haihesabiki wakati hakuna sheria.14Hata hivyo, kifo kilitawala kutoka Adamu hadi Musa, hata juu ya wale ambao hawakufanya dhambi kama kutotii kwa Adamu, ambaye ni mfano wa yeye ambaye angekuja.15Lakini hata hivyo, zawadi ya bure si kama kosa. Kwa kuwa ikiwa kwa kosa la mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na zawadi kwa neema ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imezidi kuongezeka kwa wengi!16Kwa kuwa zawadi si kama matokeo ya yule ambaye alifanya dhambi. Kwa kuwa kwa upande mwingine, hukumu ya adhabu ilikuja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Lakini kwa upande mwingine, kipawa cha bure kinachotoka katika kuhesabiwa haki kilikuja baada ya makosa mengi.17Kwa maana, ikiwa kwa kosa la mmoja, kifo kilitawala kupitia mmoja, zaidi sana wale ambao watapokea neema nyingi pamoja na kipawa cha haki watatawala kupitia maisha ya mmoja, Yesu Kristo.

18Hivyo basi, kama kupitia kosa moja watu wote walikuja kwenye hukumu, ingawa kupitia tendo moja la haki kulikuja kuhesabiwa haki ya maisha kwa watu wote.19Kwa kuwa kama kupitia kutotii kwa mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, hivyo kupitia utii wa mmoja wengi watafanywa wenye haki.20Lakini sheria iliingia pamoja, ili kwamba kosa liweze kuenea. Lakini mahali ambapo dhambi ilizidi kuwa nyingi, neema iliongezeka hata zaidi.21Hii ilitokea ili kwamba, kama dhambi ilivyotawala katika kifo, ndivyo hata neema inaweza kutawala kupitia haki kwa ajili ya maisha ya milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu.

6

1Tuseme nini basi? Tuendelee katika dhambi ili neema iongezeke?2La hasha. Sisi tuliokufa katika dhambi, tunawezaje tena kuishi katika hiyo?3Je hamjui ya kuwa wale waliobatizwa katika Kristo walibatizwa katika mauti yake?4Tulikuwa tumezikwa pamoja naye kupitia ubatizo katika kifo. Hii ilifanyika ili kwamba kama vile Kristo alivyoinuliwa kutoka mauti kupitia utukufu wa Baba, ili kwamba nasi tuweze kutembea katika upya wa maisha.5Maana ikiwa tumeunganishwa pamoja naye katika mfano wa kifo chake, pia tutaunganishwa katika ufufuo wake.6Sisi tunajua hivi, utu wetu wa zamani ulisulubiwa pamoja naye, ili kwamba mwili wa dhambi uharibiwe. Hii ilitokea ili kwamba tusiendelee kuwa watumwa wa dhambi.7Yeye aliyekufa amefanywa mwenye haki kulingana na dhambi.8Lakini kama tumekufa pamoja na Kristo, tunaamini kwamba tutaishi pamoja naye pia.9Tunajua kwamba Kristo amefufuliwa kutoka katika wafu, na kwamba si mfu tena. Kifo hakimtawali tena.10Maana kwa habari ya kifo alichokufa kwa dhambi, alikufa mara moja kwa ajili ya wote. Hata hivyo, maisha anayoishi, anaishi kwa ajili ya Mungu.11Kwa njia iyo hiyo, nanyi pia mnapaswa kujihesabu kuwa wafu katika dhambi, bali hai kwa Mungu katika Kristo Yesu.12Kwa sababu hiyo usiruhusu dhambi itawale mwili wako ili kusudi uweze kuzitii tamaa zake.13Usitoe sehemu za mwili wako katika dhambi kama vyombo visivyo na haki, bali jitoeni wenyewe kwa Mungu, kama walio hai kutoka mautini. Na zitoeni sehemu za miili yenu kama vyombo vya haki kwa Mungu.14Msiiruhusu dhambi iwatawale. Kwa kuwa hamko chini ya sheria, bali chini ya neema.

15Nini basi? Tutende dhambi kwa kuwa hatupo chini ya sheria, bali chini ya neema? La hasha.16Hamjui ya kuwa kwake yeye ambaye mnajitoa wenyewe kama watumishi ndiye ambaye ninyi mnakuwa watumishi wake, yeye mnayepaswa kumtii? Hii ni kweli hata kama ninyi ni watumwa katika dhambi ambayo inapelekea mauti, au watumwa wa utii unaopelekea haki.17Lakini ashukuriwe Mungu! Kwa kuwa mlikuwa watumwa wa dhambi, lakini mmetii kutoka moyoni ile namna ya fundisho mliopewa.18Mmefanywa huru kutoka kwenye dhambi, na mmefanywa watumwa wa haki.19Ninazungumza kama mtu kwa sababu ya madhaifu ya miili yenu. Kwa maana kama vile mlivyotoa viungo vya miili yenu kuwa watumwa kwa uchafu na uovu, kwa jinsi iyo hiyo, sasa toeni viungo vya miili yenu kuwa watumwa wa haki kwa utakaso.20Kwa kuwa mlipokuwa watumwa wa dhambi, mlikuwa huru mbali na haki.21Kwa wakati huo, mlikuwa na tunda lipi kwa mambo ambayo kwa sasa mnaona aibu kwayo? Kwa kuwa matokeo ya mambo hayo ni kifo.22Lakini kwa kuwa sasa mmefanywa huru mbali na dhambi na mmefanyika watumwa kwa Mungu, mna tunda kwa ajili ya utakaso. Tokeo ni uzima wa milele.23Kwa kuwa mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.

7

1Au hamjui, ndugu zangu (kwa kuwa naongea na watu wanaoijua sheria), kwamba sheria humtawala mtu anapokuwa hai?2Kwa maana mwanamke aliyeolewa amefungwa na sheria kwa yule mme wake anapokuwa hai, lakini ikiwa mme wake atakufa, atakuwa amewekwa huru kutoka sheria ya ndoa.3Hivyo basi, wakati mme wake angali akiishi, ikiwa anaishi na mwanamme mwingine, ataitwa mzinzi. Lakini ikiwa mme wake akifa, yuko huru dhidi ya sheria, hivyo hatakuwa mzinzi ikiwa anaishi na mwanamme mwingine.4Kwa hiyo, ndugu zangu, ninyi pia mlifanywa wafu kwa sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Imekuwa hivi ili mpate kuunganishwa na mwingine, kwake yeye ambaye alifufuliwa kutoka wafu ili tuweze kumzalia Mungu matunda.5Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi ziliamshwa katika viungo vyetu kwa njia ya sheria na kuizalia mauti matunda.6Lakini sasa tumefunguliwa kutoka katika sheria. Tumeifia ile hali iliyotupinga. Ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya Roho, na si katika hali ya zamani ya andiko.

7Tusemeje basi? Sheria ni dhambi? La hasha. Hata hivyo, nisingelitambua dhambi, isingelikuwa kwa njia ya sheria. Kwa kuwa nisingelijua kutamani kama sheria isingelisema, “Usitamani.”8Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikaleta ndani yangu kila aina ya kutamani. Kwa maana dhambi pasipo sheria imekufa.9Nami nilikuwa hai hapo kwanza bila sheria, lakini ilipokuja ile amri, dhambi ilipata uhai, nami nikafa.10Ile amri na ambayo ingelileta uzima iligeuka kuwa mauti kwangu.11Kwa maana dhambi ilipata nafasi kwa ile amri na ikanidanganya. Kupitia ile amri, iliniua.12Hivyo sheria ni takatifu, na ile amri ni takatifu, ya yaki, na njema.

13Hivyo basi ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Isiwe hivyo kamwe. Lakini dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa kupitia ile njema, ilileta mauti ndani yangu. Hii ilikuwa ili kwamba kupitia ile amri, dhambi izidi kuwa mbaya mno.

14Kwa maana twajua ya kuwa sheria asili yake ni ya rohoni, lakini mimi ni mtu wa mwilini. Nimeuzwa chini ya utumwa wa dhambi.15Maana nifanyalo, silielewi dhahiri. Kwa kuwa lile nilipendalo kutenda, silitendi, na lile nilichukialo, ndilo ninalolitenda.16Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, nakubaliana na sheria ya kuwa sheria ni njema.17Lakini sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.18Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani ndani ya mwili wangu, halikai jambo jema. Kwa kuwa tamaa ya lililo jema imo ndani yangu, lakini silitendi.19Kwa maana lile jema nilipendalo silitendi, bali lile ovu nisilolipenda ndilo nilitendalo.20Sasa kama natenda lile nisilolipenda, si mimi binafsi nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.21Nimefahamu, tena, imo kanuni ndani yangu ya kutaka kutenda lililo jema, lakini uovu hakika umo ndani yangu.22Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani.23Lakini naona kanuni iliyo tofauti katika viungo vya mwili wangu. Inapiga vita dhidi ya kanuni mpya katika akili zangu. Inanifanya mimi mateka kwa kanuni ya dhambi iliyo katika viungo vya mwili wangu.24Mimi ni mtu wa huzuni! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?25Lakini shukrani kwa Mungu kwa Yesu Kristo Bwana wetu! Hivyo basi. Mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu. Bali, kwa mwili naitumikia kanuni ya dhambi.

8

1Kwa hiyo basi hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu.2Kwa kuwa kanuni ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imenifanya mimi kuwa huru mbali na kanuni ya dhambi na mauti.3Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya. Alimtuma Mwana wake wa pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi awe sadaka ya dhambi, na akaihukumu dhambi katika mwili.4Alifanya hivi ili maagizo ya sheria yatimilizwe ndani yetu, sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali kwa kufuata mambo ya Roho.5Wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili, lakini wale waifuatao Roho huyafikiri mambo ya Roho.6Kwa kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya Roho ni uzima na amani.7Hii ni kwa sababu ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.8Wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.9Hata hivyo, hampo katika mwili bali katika Roho, kama ni kweli kwamba Roho wa Mungu huishi ndani yenu. Lakini kama mtu hana Roho wa Kristo, yeye si wake.10Kama Kristo yumo ndani yenu, mwili umekufa kwa mambo ya dhambi, bali roho ni hai kwa mambo ya haki.11Ikiwa Roho wa yule aliyemfufua Yesu kutoka wafu huishi ndani yenu, yeye yule aliyemfufua Kristo kutoka katika wafu ataipa pia miili yenu ya mauti uhai kwa njia ya Roho wake, aishie ndani yenu.

12Hivyo basi, ndugu zangu, sisi tu wadeni, lakini si kwa mwili kwamba tuishi kwa jinsi ya mwili.13Maana ikiwa mnaishi kwa jinsi ya mwili, mpo karibu kufa, lakini ikiwa kwa Roho mnayafisha matendo ya mwili, nanyi mtaishi.

14Maana kama ambavyo wengi wanaongozwa na Roho wa Mungu, hawa ni wana wa Mungu.15Kwa kuwa hamkupokea roho wa utumwa tena hata muogope. Badala yake, mlipokea roho ya kufanywa kuwa wana, ambayo kwayo tunalia, “Abba, Baba!”16Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu ya kuwa tu watoto wa Mungu.17Ikiwa tu watoto, basi tu warithi pia, warithi wa Mungu. Na sisi tu warithi pamoja na Kristo, ikiwa kwa kweli tunateseka na yeye ili tupate kutukuzwa pamoja naye.

18Kwa kuwa nayahesabu mateso ya wakati huu kuwa si kitu nikilinganisha na utukufu utakaofunuliwa kwetu.19Kwa maana viumbe vyote pia vinatazamia kwa shauku nyingi kufunuliwa kwa wana wa Mungu.20Kwa maana uumbaji pia ulitiishwa chini ya ubatili, si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye aliyevitiisha. Ni katika tumaini21kwamba uumbaji wenyewe nao utawekwa huru na kutolewa katika utumwa wa uharibifu, na kuingizwa katika uhuru wa utukufu wa watoto wa Mungu.22Kwa maana twajua ya kuwa uumbaji nao pia unaugua na kuteseka kwa uchungu pamoja hata sasa.23Si hivyo tu, ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho - sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukisubiri kufanywa wana, yaani ukombozi wa miili yetu.24Kwa maana ni kwa taraja hili tuliokolewa. Lakini kitu kilichotarajiwa kikionekana hakuna taraja tena, kwa maana ni nani anayekitarajia kile akionacho?25Bali tukikitarajia kitu tusichokiona, twakingojea kwa saburi.

26Kwa jinsi iyo hiyo, Roho naye hutusaidia katika udhaifu wetu. Kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.27Na yeye aichunguzaye mioyo huijua akili ya Roho, kwa sababu huomba kwa niaba yao walioamini kulingana na mapenzi ya Mungu.

28Nasi twajua ya kuwa kwa wote wampendao Mungu, yeye hufanya mambo yote pamoja kwa wema, kwa wale wote walioitwa kwa kusudi lake.29Kwa sababu wale wote aliowajua tangu asili, pia aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.30Na wale aliowachagua tangu asili, hao aliwaita pia. Na wale aliowaita, hao aliwahesabia haki. Na wale aliowahesabia haki, hao pia akawatukuza.

31Tuseme nini basi juu ya mambo haya? Mungu akiwa upande wetu, ni nani aliye juu yetu?32Yeye asiyemwachilia mwana wake mwenyewe bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?33Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.34Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa kwa ajili yetu, na zaidi ya hayo, naye alifufuka. Naye anatawala pamoja na Mungu mahali pa heshima, na tena ndiye anayetuombea sisi.35Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Dhiki, au shida, au mateso, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?36Kama ilivyoandikwa, “Kwa faida yako tunauawa mchana kutwa. Tulihesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa.”37Katika mambo haya yote sisi tu zaidi ya washindi katika yeye aliyetupenda.38Kwa maana nimekwisha kushawishika kwamba wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala mamlaka, wala vitu vilivyopo, wala vitu vijavyo, wala nguvu,39wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote, hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu, ambaye ni Kristo Yesu Bwana wetu.

9

1Nasema ukweli katika Kristo. Sisemi uongo, na dhamira yangu hushuhudia pamoja nami katika Roho Mtakatifu,2kwamba kuna huzuni kubwa na maumivu yasiyo koma ndani ya moyo wangu.3Kwamba ningetamani mimi mwenyewe kulaaniwa na kutengwa mbali na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, wale wa jamii yangu katika mwili.4Wao ni Waisraeli. Walio na hali ya kufanyika watoto, wa utukufu, wa maagano, na zawadi ya sheria, kumwabudu Mungu, na ahadi.5Wao ni watangulizi ambako Kristo amekuja kwa heshima kuvaa mwili huu - ambaye yeye ni Mungu wa vyote. Naye asifiwe milele. Amina.

6Lakini si kwamba ahadi za Mungu zimeshindwa kutimia. Maana si kila mtu aliye Israeli ni Mwiisraeli halisi.7Sivyo hata kwa uzao wa Abrahamu kuwa ni watoto wake halisi. Lakini, “ni kupitia Isaka uzao wako utaitwa.”8Hii ni kwamba, watoto wa mwili si watoto wa Mungu. Lakini watoto wa ahadi wanatazamwa kuwa kama uzao.9Maana hili ndilo neno la ahadi: “Katika majira haya nitakuja, na Sara atapewa mtoto.”10Si hili tu, lakini baada ya Rebeka kupata mimba kwa mtu mmoja, Isaka baba yetu-11kwamba watoto walikuwa bado hawajazaliwa na alikuwa hajafanya jambo lolote zuri au baya, ili kwamba kusudi la Mungu kulingana na uchaguzi lisimame, wala si kwa matendo, lakini ni kwa sababu ya yule aitae.12Ilinenwa kwake, “Mkubwa atamtumikia mdogo.”13Kama ilivyo kwisha andikwa: “Yakobo nilimpenda, lakini Esau nilimchukia.”

14Basi tena tutasema nini? Je kuna udhalimu kwa Mungu? La hasha.15Kwa kuwa anasema kwa Musa, “nitakuwa na rehema kwa yule nitakayemrehemu, na nitakuwa na huruma kwa yule nitakayemhurumia.”16Kwa hiyo basi, si kwa sababu ya yeye atakaye, wala si kwa sababu ya yeye ambaye hukimbia, lakini kwa sababu ya Mungu, ambaye huonesha rehema.17Kwa kuwa maandiko husema kwa Farao, “Kwa kusudi hili maalumu nilikuinua, ili kwamba nioneshe nguvu zangu katika wewe, na ili kwamba jina langu litangazwe katika nchi yote.”18Hivyo basi, Mungu huwa na rehema kwa yeyote ampendaye, na kwa ambaye humpenda, humfanya kuwa mkaidi.

19Kisha utasema kwangu, “Kwa nini bado anaona kosa? Ni yupi ambaye alikwisha kustahimili matakwa yake?”20Kinyume chake, mwanadamu, wewe ni nani ujibue kinyume na Mungu? Kuna uwezekano wowote wa kilichofinyangwa kusema kwa mfinyanzi, “Kwanini ulinifanya hivi mimi?”21Je mfinyazi huwa hana haki juu ya udongo kutengeneza chombo kwa matumizi maalumu kutokana na bonge lile lile, na chombo kingine kwa matumizi ya kila siku?22Vipi kama Mungu, ambaye ana utayari wa kuonesha gadhabu yake na kufanya nguvu yake kujulikana, alistahimili kwa uvumilivu wa kutosha vyombo vya gadhabu vilivyoandaliwa kwa kuangamiza?23Vipi kama alifanya hivi ili kwamba aoneshe wingi wa utukufu wake juu ya vyombo vya rehema, ambavyo alikwisha kuviandaa kwa ajili ya utukufu?24Vipi kama alifanya hii pia kwetu, ambaye pia alituita, si tu kutoka kwa Wayahudi, lakini pia kutoka kwa watu wa Mataifa?25Kama asemavyo pia katika Hosea: “Nitawaita watu wangu ambao hawakuwa watu wangu, na mpendwa wake ambaye hakupendwa.

26Na itakuwa kwamba pale iliposemwa kwao, ‘Ninyi si watu wangu,’ pale wataitwa ‘wana wa Mungu aliye hai.”

27Isaya analia kuhusiana na Israeli, “Kama hesabu ya wana wa Israeli ingekuwa kama mchanga wa bahari, itakuwa ni masalia ambao wataokolewa.28Kwa kuwa Bwana atalichukua neno lake juu ya nchi, mapema na kwa utimilifu.

29Na kama jinsi Isaya alivyosema awali, “Kama Bwana wa majeshi hakutuachia nyuma uzao kwa ajili yetu, tungekuwa kama Sodoma, na tungefanywa kama Gomora.

30Tutasema nini basi? Kwamba watu wa Mataifa ambao walikuwa hawatafuti haki, walipata haki, haki kwa imani.31Lakini Israeli, ambaye alitafuta sheria ya haki, hakuifikia.32Kwanini si hivyo? Kwa sababu hawakuitafuta kwa imani, bali kwa matendo. Walijikwaa juu ya jiwe la kujikwaa,33kama ilivyo kwisha andikwa, “Tazama, nimelaza jiwe la kujikwaa katika Sayuni na mwamba wa kukosa. Yeye ambaye huamini katika hili hataaibika.”

10

1Ndugu, nia ya moyo wangu na ombi langu kwa Mungu ni kwa ajili yao, kwa ajili ya wokovu wao.2Kwa kuwa nawashuhudia kwamba wanajuhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si kwa ajili ya ufahamu.3Kwa kuwa hawajui haki ya Mungu, na wanatafuta kujenga haki yao wenyewe. Hawakuwa watiifu kwa haki ya Mungu.4Kwa kuwa Kristo ndiye utimilifu wa sheria kwa ajili ya haki ya kila mtu aaminiye.

5Kwa kuwa Musa anaandika kuhusu haki ambayo huja kutokana na sheria: “Mtu ambaye hutenda haki ya sheria ataishi kwa haki hii.”6Lakini haki ambayo inatokana na imani husema hivi, “Usiseme moyoni mwako, ‘Nani atapaa kwenda mbinguni?’ (Hii ni kumleta Kristo chini).7Na usiseme, ‘Nani atashuka katika shimo?”’ (Hii ni, kumleta Kristo juu kutoka kwa wafu).8Lakini inasema nini? “Neno liko karibu na wewe, katika kinywa chako na katika moyo wako.” Hilo ni neno la imani, ambalo tunatangaza.9Kwa kuwa kama kwa kinywa chako unamkiri Yesu ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako kwamba Mungu alimfufua kutoka kwa wafu, utaokoka.10Kwa kuwa kwa moyo mtu huamini na kupata haki, na kwa kinywa hukiri na kupata wokovu.11Kwa kuwa andiko lasema, “Kila amwaminiye hata aibika.”12Kwa kuwa hakuna tofauti kati ya Myahudi na Myunani. Kwa kuwa Bwana yule yule ni Bwana wa wote, na ni tajiri kwa wote wamwitao.13Kwa kuwa kila mtu ambaye huliitia jina la Bwana ataokoka.

14Kwa jinsi gani wanaweza kumwita yeye ambaye hawajamwamini? Na jinsi gani wanaweza kuamini katika yeye ambaye hawajamsikia? Na watasikiaje pasipo muhubiri?15Na jinsi gani wanaweza kuhubiri, isipokuwa wametumwa? - Kama ilivyoandikwa, “Jinsi gani ni mizuri miguu ya wale ambao wanatangaza habari njema!”16Lakini wote hawakusikiliza injili. Kwa kuwa Isaya hunena, “Bwana, ni nani aliyesikia ujumbe wetu?”17Hivyo imani huja kutokana na kusikia, na kusikia kwa neno la Kristo.

18Lakini nasema, “Je hawakusikia?” Ndiyo, kwa hakika sana. “Sauti yao imekwisha toka nje katika nchi yote, na maneno yao kwenda miisho ya dunia.”

19Zaidi ya yote, Ninasema, “Je Israel hakujua?” Kwanza Musa hunena, “Nitawachokoza kuwatia wivu kwa watu ambao si taifa. Kwa njia ya taifa lisilo na uelewa, nitawachochea hadi mkasirike.”

20Na Isaya ni jasiri sana na husema, “Nilipatikana na wale ambao hawakunitafuta. Nilionekana kwa wale ambao hawakunihitaji.”

21Lakini kwa Israel husema, “Siku zote nilinyoosha mikono yangu kwa wasiotii na kwa watu wagumu.”

11

1Basi nasema, je, Mungu aliwakataa watu wake? Hata kidogo. Kwa kuwa mimi pia ni Mwiisraeli, wa ukoo wa Abrahamu, wa kabila la Benyamini.2Mungu hakuwakataa watu wake, aliowajua tangu mwanzo. Je hamjui andiko linasema nini kuhusu Eliya, jinsi alivyomsihi Mungu juu ya Israeli?3“Bwana, wamewaua manabii wako, nao wamebomoa madhabahu zako. Mimi peke yangu nimesalia, nao wanatafuta uhai wangu.”4Lakini jibu la Mungu lasema nini kwako? “Nimetunza kwa ajili yangu watu elfu saba ambao hawampigii magoti Baali.”5Hata hivyo, wakati huu wa sasa pia kuna walio salia kwa sababu ya uchaguzi wa neema.6Lakini ikiwa ni kwa neema, si tena kwa matendo. Vinginevyo neema haitakuwa tena neema.

7Ni nini basi? Jambo ambalo Israeli alikuwa akitafuta, hakukipata, bali wateule walikipata, na wengine walitiwa uzito.8Ni kama ilivyoandikwa: “Mungu amewapa roho ya ubutu, macho ili wasione, na masikio ili wasisikie, mpaka leo hii.”9Naye Daudi anasema, “Acha meza zao na ziwe wavu, mtego, sehemu ya kujikwaa, na kulipiza kisasi dhidi yao.
10Acha macho yao yatiwe giza ili wasiweze kuona. Ukawainamishe migongo yao daima.”

11Basi nasema, “Je, wamejikwaa hata kuanguka?” Isiwe hivyo kamwe. Badala yake, kwa kushindwa kwao, wokovu umefika kwa Mataifa, ili wao wenyewe watiwe wivu.12Sasa ikiwa kushindwa kwao ni utajiri wa ulimwengu, na kama hasara yao ni utajiri wa mataifa, ni kiasi gani zaidi itakuwa kukamilika kwao?

13Na sasa naongea nanyi watu wa Mataifa. Kwa kuwa nimekuwa mtume kwa watu wa Mataifa mengine, najivunia huduma yangu.14Labda nitawatia wivu walio mwili mmoja na mimi. Labda tutawaokoa baadhi yao.15Maana ikiwa kukataliwa kwao ni maridhiano ya dunia, kupokelewa kwao kutakuwaje ila uhai toka kwa wafu?16Kama matunda ya kwanza ni akiba, ndivyo ilivyo kwa donge la unga. Kama mzizi ni akiba, matawi nayo kadhalika.

17Lakini kama baadhi ya matawi yamekatwa, kama wewe, tawi pori la mzeituni, ulipandikizwa kati yao, na kama ulishiriki pamoja nao katika mizizi ya utajiri wa mzeituni,18usijisifu juu ya matawi. Lakini kama unajisifu, si wewe ambaye unaisaidia mizizi, bali mizizi inakusaidia wewe.19Basi utasema, “Matawi yalikatwa ili nipate kupandikizwa katika shina.”20Hiyo ni kweli. Kwa sababu ya kutoamini kwao walikatwa, lakini wewe ulisimama imara kwa sababu ya imani yako. Usijifikirie mwenyewe kwa hali ya juu sana, bali ogopa.21Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, hatakuhurumia wewe pia.

22Angalia, basi, matendo mema na ukali wa Mungu. Kwa upande mmoja, ukali ulikuja juu ya Wayahudi ambao walianguka. Lakini kwa upande mwingine, wema wa Mungu huja juu yako, kama utadumu katika wema wake. Vinginevyo wewe pia utakatiliwa mbali.23Na pia, kama hawataendelea katika kutoamini kwao, watapandikizwa tena. Maana Mungu anao uwezo wa kuwapandikiza tena.24Kwa maana ikiwa ninyi mlikatwa nje kwa ulio kwa asili mzeituni mwitu, na kinyume cha asili mlipandikizwa katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana hawa Wayahudi, ambao ni kama matawi ya asili kuweza kupandikizwa tena ndani ya mzeituni wao wenyewe?

25Kwa maana ndugu sitaki msijue, kuhusiana na siri hii, ili kwamba msiwe na hekima katika kufikiri kwenu wenyewe. Siri hii ni kwamba ugumu umetokea katika Israeli, hadi kukamilika kwa mataifa kutakapokuja.26Hivyo Israeli wote wataokoka, kama ilivyoandikwa: “Kutoka Sayuni atakuja Mkombozi. Atauondoa uovu kutoka kwa Yakobo.

27Na hili litakuwa agano langu pamoja nao, wakati nitakapoziondoa dhambi zao.”

28Kwa upande mmoja kuhusu injili, wanachukiwa kwa sababu yenu. Kwa upande mwingine kutokana na uchaguzi wa Mungu, wamependwa kwa sababu ya mababu.29Kwa kuwa zawadi na wito wa Mungu haubadiliki.30Kwa kuwa awali ninyi mlikuwa mmemwasi Mungu, lakini sasa mmeipokea rehema kwa sababu ya kuasi kwao.31Kwa njia iyo hiyo, sasa hawa Wayahudi wameasi. Matokeo yake ni kwamba kutokana na huruma mliyojaliwa ninyi wanaweza pia kupokea rehema.32Maana Mungu amewafunga watu wote katika uasi, ili aweze kuwahurumia wote.

33Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hazichunguziki hukumu zake, na njia zake hazigunduliki!34“Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani amekuwa mshauri wake?35Au ni nani kwanza aliyempa kitu Mungu, ili alipwe tena?”

36Kwa maana kutoka kwake, na kwa njia yake na kwake, vitu vyote vipo. Kwake uwe utukufu milele. Amina.

12

1Kwa hiyo nawasihi, ndugu, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, inayokubalika kwa Mungu. Hii ndiyo ibada yenu yenye maana.2Wala msiifuatishe namna ya dunia hii, bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu. Fanyeni hivi mpate kujua mapenzi ya Mungu yaliyo mema, yakumpendeza na kamilifu.

3Kwa maana nasema, kwa sababu ya neema niliyopewa, kwamba kila mtu ambaye yupo miongoni mwenu hapaswi kufikiri zaidi juu yake mwenyewe kuliko inavyompasa kufikiri. Bali, imempasa kufikiri kwa hekima, kama ambavyo Mungu amewapa kila mmoja kiasi fulani cha imani.4Kwa kuwa tuna viungo vingi katika mwili mmoja, lakini si viungo vyote vina kazi moja.5Vivyo hivyo, sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo kila mmoja kwa mwenzake.6Tuna karama zilizo mbalimbali kwa kadiri ya neema mliyopewa. Ikiwa karama ya mtu ni unabii, na itendeke kwa kadiri ya imani yake.7Ikiwa karama ya mtu ni huduma, na atumike. Ikiwa mwingine ana karama ya kufundisha, basi, afundishe.8Ikiwa karama ya mtu ni faraja, basi, afariji. Ikiwa karama ya mtu ni kutoa, afanye hivyo kwa ukarimu. Ikiwa karama ya mtu ni kuongoza, na litendeke kwa uangalifu. Ikiwa karama ya mtu ni katika kuonesha huruma, na litendeke kwa furaha.

9Pendo lisiwe na unafiki. Chukieni uovu; mshikilie yaliyo mema.10Kuhusu upendo wa ndugu, pendaneni ninyi kwa ninyi. Kuhusu heshima, heshimianeni ninyi kwa ninyi.11Kuhusu bidii, msiwe walegevu. Kuhusu roho, iweni na shauku. Kuhusu Bwana, mtumikieni.12Furahini katika ujasiri mlionao kuhusu siku zijazo. Muwe na subira katika matatizo yenu. Mdumu katika kuomba.13Mshiriki katika mahitaji ya waumini. Tafuteni njia nyingi za kuonesha ukarimu.14Watakieni baraka wote wanaowatesa ninyi; muwabariki na wala msiwalaani.15Furahini pamoja na wanaofurahi, lieni pamoja na wanaolia.16Muwe na nia moja ninyi kwa ninyi. Msifikiri kwa kujivuna, lakini wakubalini watu wa hali ya chini. Msiwe na hekima juu ya mawazo yenu wenyewe.17Msimlipe mtu yeyote ovu kwa ovu. Fanyeni mambo mema machoni pa watu wote.18Kama inawezekana, kama ilivyowekwa kwenu, muwe na amani na watu wote.

19Wapenzi, msijilipizie kisasi wenyewe, lakini ipisheni ghadhabu ya Mungu. Kwa maana imeandikwa, “‘kisasi ni changu; Mimi nitalipa,’ asema Bwana.”20“Lakini ikiwa adui yako ana njaa, mlishe. Akiwa na kiu, mnyweshe. Kwa maana ukifanya hivyo, utampalia makaa ya moto juu ya kichwa chake.”21Usishindwe na ubaya, bali ushinde ubaya kwa wema.

13

1Kila nafsi na iwe na utii kwa mamlaka ya juu, kwa kuwa hakuna mamlaka isipokuwa imetoka kwa Mungu. Na mamlaka zilizopo zimewekwa na Mungu.2Kwa hiyo ambaye anapinga mamlaka hiyo hupinga amri ya Mungu; na wale waipingao watapokea hukumu juu yao wenyewe.3Kwa kuwa watawala si tishio kwa watendao mema, bali kwa watendao maovu. Je unatamani kutoogopa mamlaka? Fanya yaliyo mema, na utasifiwa nayo.4Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Bali kama utatenda yaliyo maovu, ogopa; kwa kuwa habebi upanga bila sababu. Kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, mlipa kisasi kwa ghadhabu juu ya yule afanyaye uovu.5Kwa hiyo inakupasa utii, si tu kwa sababu ya gadhabu, bali pia kwa sababu ya dhamiri.6Kwa ajili hii pia unalipa kodi. Kwa kuwa wenye mamlaka ni watumishi wa Mungu, ambao wanaendelea kufanya jambo hili.7Mlipeni kila mmoja ambacho wanawadai: kodi kwa astahiliye kodi; ushuru kwa astahiliye ushuru; hofu kwa astahiliye hofu; heshima kwa astahiliye heshima.

8Msidaiwe na mtu kitu chochote, isipokuwa kupendana ninyi kwa ninyi. Kwa kuwa yeye ampendaye jirani yake ametimiliza sheria.9Kwa kuwa, “Hautazini, hautaua, hautaiba, hautatamani,” na kama kuna amri nyingine pia, imejumlishwa katika sentensi hii: “Utampenda jirani yako kama wewe mwenyewe.”10Upendo hamdhuru jirani wa mtu. Kwa hiyo, upendo ni ukamilifu wa sheria.

11Kwa sababu ya hili, mnajua wakati, kwamba tayari ni wakati wa kutoka katika usingizi. Kwa kuwa wokovu wetu umekaribia zaidi ya wakati ule tulio amini kwanza.12Usiku umeendelea, na mchana umekaribia. Na tuweke pembeni matendo ya giza, na tuvae silaha za nuru.13Na tuenende sawa sawa, kama katika nuru, si kwa sherehe za uovu au ulevi. Na tusienende katika zinaa au tamaa isiyoweza kudhibitiwa, na si katika fitina au wivu.14Bali tumvae Bwana Yesu Kristo, na tusiweke nafasi kwa ajili ya mwili, kwa tamaa zake.

14

1Mpokeeni yeyote ambaye ni dhaifu katika imani, bila kutoa hukumu kuhusu mawazo yake.2Mtu mmoja ana imani ya kula chochote, mwingine ambaye ni dhaifu anakula mboga tu.3Mtu ambaye anakula kila kitu asimdharau yeye asiyekula kila kitu. Na yeye ambaye hali kila kitu asimuhukumu mwingine ambaye hula kila kitu. Kwa kuwa Mungu amekwisha mpokea.4Wewe ni nani, wewe ambaye unamuhukumu mtumishi ambaye ni miliki ya mtu mwingine? Ni mbele ya Bwana wake kwamba husimama au huanguka. Lakini atainuliwa, kwa kuwa Bwana anaweza kumfanya asimame.

5Mtu mmoja huthamini siku moja kuliko nyingine. Mwingine huthamini kila siku sawa sawa. Hebu kila mtu na ashawishike katika akili yake mwenyewe.6Yeye ambaye anashika siku, anashika kwa ajili ya Bwana. Na kwa yeye alaye, hula kwa ajili ya Bwana, kwa kuwa anampa Mungu shukrani. Yeye ambaye hali, hujizuia kutokula kwa ajili ya Bwana. Yeye pia hutoa shukrani kwa Mungu.7Kwa kuwa hakuna aishie kwa nafsi yake, na hakuna afae kwa ajili yake mwenyewe.8Kwa kuwa ikiwa tunaishi, tunaishi kwa ajili ya Bwana. Na ikiwa tunakufa, tunakufa kwa ajili ya Bwana. Basi ikiwa tunaishi au tunakufa tu mali ya Bwana.9Kwa kuwa ni kwa kusudi hili Kristo alikufa na kuishi tena, kwamba awe Bwana wa wote wafu na waishio.

10Lakini wewe, kwa nini unamuhukumu ndugu yako? Na wewe, kwa nini unamdharau ndugu yako? Kwa kuwa sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.11Kwa kuwa imeandikwa, “Kama niishivyo,” asema Bwana, “Kwangu mimi kila goti litapigwa, na kila ulimi utatoa sifa kwa Mungu.”

12Hivyo basi, kila mmoja wetu atatoa hesabu yake mwenyewe kwa Mungu.

13Kwa hiyo, tusiendelee tena kuhukumiana, lakini badala yake amua hivi, kwamba hakuna atakaye weka kikwazo au mtego kwa ndugu yake.14Ninajua na nimeshawishika katika Bwana Yesu, kwamba hakuna kitu kilicho najisi chenyewe. Ni kwa yeye tu anayedhani kuwa chochote ni najisi, kwa kuwa kwake ni najisi.15Ikiwa kwa sababu ya chakula ndugu yako anahuzunika, hautembei tena katika upendo. Usimharibu kwa chakula chako mtu ambaye kwa ajili yake Kristo alikufa.16Hivyo msiruhusu matendo yenu mema yakasababisha watu kuwadhihaki.17Kwa kuwa ufalme wa Mungu si kwa ajili ya chakula na kinywaji, bali ni kwa ajili ya haki, amani, na furaha katika Roho Mtakatifu.18Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo kwa jinsi hii amekubalika kwa Mungu na amekubalika kwa watu.

19Kwa hiyo basi, na tufuate mambo ya amani na mambo ambayo humjenga mtu na mwingine20Usiharibu kazi ya Mungu kwa sababu ya chakula. Vitu vyote kwa kweli ni safi, lakini ni vibaya kwa mtu yule ambaye hula na kumsababisha yeye kujikwaa.21Ni vyema kutokula nyama, wala kunywa divai, wala chochote ambacho kwa hicho ndugu yako hukwazwa.22Hizi imani maalumu ulizo nazo, ziweke kati yako mwenyewe na Mungu. Amebalikiwa yule ambaye hajihukumu mwenyewe katika kile anachokikubali.23Aliye na mashaka amehukumiwa ikiwa anakula, kwa sababu haitokani na imani. Na chochote kisichotokana na imani ni dhambi.

15

1Sasa sisi tulio na nguvu tunapaswa kuuchukua udhaifu wa walio dhaifu, na hatupaswi kujipendeza wenyewe.2Kila mmoja wetu ampendeze jirani yake kwani ni jambo jema, kwa lengo la kumjenga.3Kwani hata Kristo hakujipendeza mwenyewe. Badala yake, ilikuwa kama ilivyoandikwa, “Matusi ya wale waliokutukana yamenipata mimi.”4Kwa chochote kilichotangulia kuandikwa, kiliandikwa kwa kutuelekeza, kwa kusudi kwamba kupitia uvumilivu na kupitia kutiwa moyo na maandiko tungekuwa na ujasiri.

5Sasa Mungu wa uvumilivu na wa kutia moyo awape kuwa na nia sawa kwa kila mmoja kulingana na Yesu Kristo.6Aweze kufanya hivi kwa nia moja muweze kumsifu kwa kinywa kimoja Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.

7Kwa hiyo mpokeeni kila mmoja, kama vile Kristo alivyowapokea, kwa utukufu wa Mungu.8Kwani nasema kwamba Kristo amefanywa mtumishi wa tohara kwa niaba ya ukweli wa Mungu. Alifanya hivi ili kwamba aweze kuthibitisha ahadi zilizotolewa kwa mababa,9na kwa mataifa kumtukuza Mungu kwa neema yake. Kama ambavyo imeandikwa, “Kwa hiyo nitatoa sifa kwako miongoni mwa mataifa na kuimba sifa katika jina lako.”10Tena inasema, “Furahini, ninyi watu wa mataifa, pamoja na watu wake.”11Na tena, “Msifuni Bwana, ninyi mataifa yote; acha watu wa mataifa yote wamsifu yeye.”12Tena Isaya asema, “Kutakuwa na shina la Yese, na mmoja atakayeinuka kutawala juu ya mataifa. Mataifa watakuwa na tumaini katika yeye.”

13Sasa Mungu wa tumaini awajaze na furaha yote na amani kwa kuamini, ili kwamba muweze kuzidi katika tumaini, kwa nguvu ya Roho Mtakatifu.

14Mimi mwenyewe pia nimeshawishiwa nanyi, ndugu zangu. Nimeshawishiwa kwamba pia ninyi wenyewe mmejazwa na wema, mmejazwa na maarifa yote. Ninashawishiwa kwamba, ninyi mwaweza pia kuhimizana kila mmoja na mwenzake.15Lakini ninaandika kwa ujasiri zaidi kwenu juu ya mambo fulani ili kuwakumbusha tena, sababu ya kipawa nilichopewa na Mungu.16Kipawa hiki kilikuwa kwamba niweze kuwa mtumishi wa Yesu Kristo aliyetumwa kwa mataifa, kujitoa kama kuhani wa injili ya Mungu. Ningeweza kufanya hivi ili kujitoa kwangu kwa mataifa kuwe kumekubaliwa, kumetengwa na Mungu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

17Hivyo furaha yangu iko katika Kristo Yesu na katika mambo ya Mungu.18Kwani sitaweza kuthubutu kunena lolote isipokuwa kwamba Kristo amekamilisha kupitia kwangu utii wa mataifa. Haya mambo yametimizwa kwa neno na tendo,19kwa nguvu za ishara na maajabu, na kwa nguvu za Roho Mtakatifu. Hii ilikuwa ili kwamba kutoka Yerusalem, na kuzungukia mbali kama Iliriko, niweze kuichukua nje kwa ukamilifu injili ya Kristo.20Kwa njia hii, nia yangu imekuwa kuitangaza injili, lakini si mahali Kristo anajulikana kwa jina, ili kwamba nisiweze kujenga juu ya msingi wa mtu mwingine.21Kama ilivyoandikwa: “Ambao kwa yeye hawana habari zake alikuja watamwona, na wale ambao hawakumsikia watamfahamu.”

22Kwahiyo nilikuwa pia nimezuiliwa mara nyingi kuja kwenu.23Lakini sasa, sina tena sehemu yoyote katika mikoa hii, na nimekuwa nikitamani kwa miaka mingi kuja kwenu.24Hivyo mara zote nikienda Hispania, ninatumaini kuwaona nikipita, na kuweza kupelekwa njia yangu na ninyi, baada ya kuwa nimefurahia ushirika na ninyi kwa muda.25Lakini sasa ninakwenda Yerusalemu kuwahudumia waumini.26Maana iliwapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo maalumu kwa masikini miongoni mwa waumini huko Yerusalemu.27Ndiyo, ilikuwa kwa upendo wao, na hakika, wamekuwa wadeni wao. Maana ikiwa mataifa wameshiriki katika mambo yao ya kiroho, wanadaiwa na wao pia kuwahudumia katika mahitaji ya vitu.28Kwahiyo, wakati nimekamilisha hivi na kuwa na utoshelevu wa tunda hili kwao, mimi nitakwenda njiani pamoja nanyi huko Hispania.29Najua kwamba, wakati nikija kwenu, nitakuja katika utimilifu wa baraka za Kristo.

30Sasa ninawasihi, ndugu, kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, kwamba mshiriki pamoja nami katika maombi yenu kwa Mungu kwa ajili yangu.31Ombeni kwamba niweze kuokolewa kutoka kwao wasio na utii katika Yudea, na kwamba huduma yangu huko Yerusalemu iweze kupokelewa na waumini.32Ombeni kwamba ninaweza kuja kwenu kwa furaha kupitia mapenzi ya Mungu, na kwamba niweze kuwa pamoja nanyi, kupata kupumzika.33Na Mungu wa amani awe pamoja nanyi nyote. Amina.

16

1Namkabidhi kwenu Fibi dada yetu, ambaye ni mtumishi wa kanisa ambalo liko Kenkrea,2ili kwamba mnaweza kumpokea katika Bwana. Fanyeni hivi katika kicho cha thamani cha waumini, na msimame pamoja naye katika jambo lolote atakalokuwa na uhitaji nalo. Maana yeye mwenyewe amekuwa mhudumu wa wengi, na kwa ajili yangu mwenyewe.

3Msalimu Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu,4ambao kwa maisha yangu waliyahatarisha maisha yao wenyewe. Ninatoa shukrani kwao, na siyo tu mimi, bali pia kwa makanisa yote ya mataifa.5Lisalimie kanisa ambalo liko nyumbani kwao. Msalimie Epanieto mpendwa wangu, ambaye ni mzaliwa wa kwanza wa Kristo katika Asia.6Msalimie Mariamu ambaye ametenda kazi kwa bidii kwa ajili yenu.7Msalimie Androniko na Yunia, jamaa zangu, na wafungwa pamoja nami. Ni wa muhimu miongoni mwa mitume, ambao pia walitangulia kumjua Kristo kabla yangu.8Msalimie Ampliato, mpendwa wangu katika Bwana.9Msalimie Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi mpendwa wangu.10Msalimie Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Wasalimie wote ambao walio katika nyumba ya Aristobulo.11Nisalimie Herodioni, jamaa yangu. Nisalimie wote walio katika nyumba ya Narkiso, ambao wako katika Bwana.12Nisalimie Trifaina na Trifosa, wanaotenda kazi kwa bidii katika Bwana. Msalimie Persisi mpendwa, ambaye ametenda kazi zaidi kwa Bwana,13Nisalimie Rufo, aliyechaguliwa katika Bwana na mama yake ambaye ni mama yangu pia.14Msalimie Asinkrito, Flegon, Herme, Patroba, Herma, na ndugu wote walio pamoja nao.15Nisalimie Filologo naYulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na waumini wote walio pamoja nao.16Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu. Makanisa yote katika Kristo yawasalimu.

17Sasa nawasihi, ndugu, kutafakari juu ya hao ambao wanasababisha mgawanyiko na vipingamizi. Wanakwenda kinyume na mafundisho ambayo mmekwisha kujifunza. Geukeni mtoke kwao.18Kwa maana watu kama hawa hawamtumikii Kristo Bwana, bali matumbo yao wenyewe. Kwa maneno yao laini na pongezi za uongo wanadanganya mioyo ya wasio na hatia.19Kwa mfano wa utii wenu mwamfikia kila mmoja. Kwa hiyo, nafurahi juu yenu, lakini nawataka ninyi mwe na busara katika hali ya wema, na kutokuwa na hatia mbele ya uovu.20Mungu wa amani hatakawia kumwangamiza shetani chini ya nyayo zenu. Neema ya Bwana Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

21Timotheo, mtendakazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, Yasoni na Sospeter, jamaa zangu.22Mimi, Tertio, niliyeuandika waraka huu, nawasalimu katika jina la Bwana.23Gayo, aliyenitunza na kwa kanisa lote, lawasalimu. Erasto, mtunza hazina wa mji, awasalimu, pamoja na Kwarto aliye ndugu.241

25Sasa kwake yeye aliye na uwezo kufanya msimame kulingana na injili na mafundisho ya Yesu Kristo, kulingana na ufunuo wa siri iliyofichwa kwa muda mrefu,26lakini sasa imekwisha funuliwa na kufanywa kujulikana na maandiko ya unabii kulingana na amri ya Mungu wa milele, kwa utii wa imani miongoni mwa mataifa yote?27Kwa Mungu pekee mwenye hekima, kupitia Yesu Kristo, kuwe na utukufu milele yote. Amina


1Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. Tazama Warumi 16: 20. “Neema ya Bwana Yesu Kristo ikae nanyi nyote. Amina.”

1 Wakorintho

1

1Paulo, aliyeitwa na Kristo kuwa mtume kwa mapenzi ya Mungu, na Sosthene ndugu yetu,2kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wale ambao wamewekwa wakfu katika Yesu Kristo, ambao wameitwa kuwa watu watakatifu. Tunawaandikia pia wale wote wanaolitii jina la Bwana wetu Yesu Kristo katika mahali pote, Bwana wao na wetu.

3Neema na amani iwe kwenu kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.

4Siku zote namshukru Mungu wangu kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema ya Mungu ambayo Kristo Yesu aliwapa.5Amewafanya kuwa matajiri katika kila njia, katika usemi na pamoja na maarifa yote.6Amewafanya matajiri, kama ushuhuda kuhusu Kristo ya kwamba amethibitishwa kuwa kweli miongoni mwenu.7Kwa hiyo hampungukiwi karama za kiroho, kama mlivyo na matumaini ya kusubiri ufunuo wa Bwana wetu Yesu Kristo.8Atawaimarisha ninyi pia hadi mwisho, ili msilaumiwe siku ya Bwana wetu Yesu Kristo.9Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita ninyi katika ushirika wa mwana wake, Yesu Kristo Bwana wetu.

10Sasa nawasihi kaka na dada zangu, kupitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba wote mkubali, na kwamba pasiwe na migawanyiko miongoni mwenu. Nawasihi kuwa muungane pamoja katika nia moja na katika kusudi moja.11Kwani watu wa nyumba ya Kloe wamenitaarifu kuwa kuna mgawanyiko unaoendelea miongoni mwenu12Nina maana hii: Kila mmoja wenu husema, “Mimi ni wa Paulo,” au “Mimi ni wa Apolo,” au “Mimi ni wa Kefa,” au “Mimi ni wa Kristo.”13Je! Kristo amegawanyika? Je! Paulo alisulubiwa kwa ajili yenu? Je! Mlibatizwa kwa jina la Paulo?14Namshukuru Mungu kwa kuwa sikumbatiza yeyote, isipokuwa Krispo na Gayo.15Hii ilikuwa kwamba hakuna yeyote angesema mlibatizwa kwa jina langu.16(Pia niliwabatiza wa nyumba ya Stephania. Zaidi ya hapo, sijui kama nilimbatiza mtu mwingine yeyote).17Kwa maana, Kristo hakunituma kubatiza bali kuhubiri injili. Hakunituma kuhubiri kwa maneno ya hekima ya kibinadamu, ili kwa nguvu ya msalaba wa Kristo isiondolewe.

18Kwa kuwa ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa wale wanaomuasi Mungu. Lakini kwa wale ambao Mungu anawaokoa, ni nguvu ya Mungu.19Kwa kuwa imeandikwa, “Nitaiharibu hekima ya wenye busara. Nitauharibu ufahamu wa wenye akili.”

20Yuko wapi mtu mwenye busara? Yuko wapi mwenye elimu? Yuko wapi msemaji mshawishi wa dunia hii? Je, Mungu hakuigeuza hekima ya dunia hii kuwa ujinga?21Tangu dunia imekuwa katika hekima yake haikumjua Mungu, ilimpendeza Mungu katika ujinga wao wa kuhubiri ili kuokoa wale wanaoamini.22Kwa Wayahudi huuliza ishara za miujiza na kwa Wayunani hutafuta hekima.23Lakini tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa, aliye kikwazo kwa Wayahudi na ni ujinga kwa Wayunani.24Lakini kwa wale ambao waliitwa na Mungu, Wayahudi na Wayunani, tunamhubiri Kristo kama nguvu na hekima ya Mungu.25Kwa kuwa ujinga wa Mungu una hekima kuliko ya wanadamu, na udhaifu wa Mungu una nguvu zaidi ya wanadamu.

26Angalia wito wa Mungu juu yenu, kaka na dada zangu. Si wengi wenu mlikuwa na hekima katika viwango vya kibinadamu. Si wengi wenu mlikuwa na nguvu. Si wengi wenu mlizaliwa katika ukuu.27Lakini Mungu alichagua vitu vijinga vya dunia ili kuviaibisha vyenye hekima. Mungu alichagua kilicho dhaifu katika dunia kukiaibisha chenye nguvu.28Mungu alichagua kile kilicho cha hali ya chini na kilichodharauliwa katika dunia. Alichagua hata vitu ambavyo havikuhesabiwa kuwa kitu, kwa kuvifanya si kitu vitu vilivyo na thamani.29Alifanya hivi ili asiwepo yeyote aliye na sababu ya kujivuna mbele zake.30Kwa sababu ya kile Mungu alichofanya, sasa mko ndani ya Kristo Yesu, ambaye amefanyika hekima kwa ajili yetu kutoka kwa Mungu. Alikuwa haki yetu, utakatifu na ukombozi.31Kama matokeo, kama andiko lisemavyo, “Anayejisifu, ajisifu katika Bwana.”

2

1Nilipokuja kwenu kaka na dada zangu, sikuja kwa maneno ya ushawishi na hekima kama nilivyohubiri kweli iliyofichika kuhusu Mungu.2Niliamua kutojua chochote nilipokuwa miongoni mwenu isipokuwa Yesu Kristo, na yeye aliyesulubiwa.3Na nilikuwa nanyi katika udhaifu, na katika hofu, na katika kutetemeka sana.4Na ujumbe wangu na kuhubiri kwangu hakukuwa katika maneno ya ushawishi na hekima. Badala yake, yalikuwa katika kudhihirisha dalili za Roho na za nguvu,5ili kwamba imani yenu isiwe katika hekima ya wanadadamu, bali katika nguvu ya Mungu.

6Sasa tunaizungumza hekima miongoni mwa watu wazima, lakini si hekima ya dunia hii, au ya watawala wa nyakati hizi, ambao wanaopita.7Badala yake, tunaizungumza hekima ya Mungu katika ukweli uliofichika, hekima iliyofichika ambayo Mungu aliichagua kabla ya nyakati za utukufu wetu.8Hakuna yeyote wa watawala wa nyakati hizi aliyeijua hekima hii, Kama wangeifahamu katika nyakati zile, wasingelimsulubisha Bwana wa utukufu.9Lakini kama ilivyoandikwa, “Mambo mbayo hakuna jicho limeyaona, hakuna sikio lililoyasikia, mawazo hayakufikiri, mambo ambayo Mungu ameyaandaa kwa ajili ya wale wampendao yeye.”

10Haya ni mambo ambayo Mungu ameyafunua kwetu kupitia Roho, Kwa kuwa Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu.11Kwa kuwa nani afahamuye mawazo ya mtu, isipokuwa roho ya mtu ndani yake? Hivyo pia, hakuna ajuaye mambo ya ndani ya Mungu, isipokuwa Roho wa Mungu.12Lakini sisi hatukupokea roho ya dunia, bali Roho ambaye anatoka kwa Mungu, ili tuweze kujua mambo tuliyopewa na Mungu kwa uhuru.13Tunasema mambo haya kwa maneno, ambayo hekima ya mtu haiwezi kufundisha, lakini ambayo Roho hutufundisha. Roho hutafasiri maneno ya kiroho kwa hekima ya kiroho.14Mtu asiye wa kiroho hapokei mambo ambayo ni ya Roho wa Mungu, kwa kuwa hayo ni upuuzi kwake. Hawezi kuyajua kwa sababu yanatambuliwa kiroho.15Kwa yule wa kiroho huhukumu mambo yote. Lakini huhukumiwa na wengine.16“Ni nani anaweza kuyajua mawazo ya Bwana, ambaye anaweza kumfundisha yeye?” Lakini tuna mawazo ya Kristo.

3

1Na mimi, kaka na dada zangu, sikusema nanyi kama watu kiroho, lakini kama na watu wa kimwili. Kama na watoto wadogo katika Kristo.2Niliwanywesha maziwa na si nyama, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa kula nyama. Na hata sasa hamjawa tayari.3Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?4Kwa kuwa mmoja husema, “Namfuata Paulo.” Mwingine husema “Namfuata Apolo,” hamuishi kama wanadamu?

5Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.6Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu akakuza.7Kwa hiyo, si aliye panda wala aliyetia maji ana chochote. Lakini ni Mungu anayekuza.8Sasa apandaye na atiaye maji wote ni sawa, na kila mmoja atapokea ujira wake kulingana na kazi yake.9Kwa kuwa sisi tu watendakazi wa Mungu, ninyi ni bustani ya Mungu, jengo la Mungu.

10Kutokana na neema ya Mungu niliyopewa kama mjenzi mkuu, niliuweka msingi, na mwingine anajenga juu yake. Lakini mtu awe makini jinsi ajengavyo juu yake.11Kwa kuwa hakuna mwingine awezaye kujenga msingi mwingine zaidi ya uliojengwa, ambao ni Yesu Kristo.12Sasa, kama mmoja wenu ajenga juu yake kwa dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, nyasi, au majani,13kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.14Kama chochote mtu alichojenga kitabaki, yeye atapokea zawadi.15Lakini kama kazi ya mtu ikiteketea kwa moto, atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama vile kuepuka katika moto.

16Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?17Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.

18Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima.19Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”20Na tena “Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili.”

21Hivyo mtu asijivunie wanadamu! Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu.22Kama ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au dunia, au maisha, au kifo, au vitu vilivyopo, au vitakavyokuwepo. Vyote ni vyenu,23na ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu.

4

1Kwa hiyo mtu atuhesabu sisi, kama watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za kweli za Mungu.2Katika hili, kinachotakiwa kwa mawakili ni kwamba wawe wa kutumainiwa.3Lakini, kwangu mimi ni kitu kidogo sana kuhukumiwa na ninyi, kwa hukumu ya kibinadamu. Kwa kuwa sijihukumu hata mimi mwenyewe.4Sijihukumu mimi mwenyewe, hii haina maana kuwa mimi ni mwenye haki. Ni Bwana anihukumuye.5Kwa hiyo, msitamke hukumu juu ya lolote kabla ya wakati, kabla ya kuja kwa Bwana. Atayaleta nuruni mambo yaliyofichika gizani na kufunua makusudi ya mioyo. Ndipo kila mmoja atapokea sifa yake kutoka kwa Mungu.

6Sasa, kaka na dada zangu, mimi mwenyewe na Apolo tumetumia kanuni hizi kwa ajili yenu. Ili kwamba kutoka kwetu mnaweza kujifunza maana ya usemi, “Usiende zaidi ya kilivyoandikwa.” Hii ni kwamba hakuna mmoja wenu ajivunaye juu ya mwingine.7Kwani ni nani aonaye tofauti kati yenu na mwingine? Ni kipi ulicho nacho hukukipokea bure? Kama umekwisha kupokea bure, kwa nini mnajivuna kama hamkufanya hivyo?

8Tayari mmeshapata vyote ambavyo mngetaka! Tayari mmekuwa na utajiri! Mmeanza kutawala; na kwamba mnamiliki zaidi yetu sisi! Kweli, nawatakia umililki mwema ili kwamba tumiliki pamoja nanyi.9Kwa hiyo ninadhani Mungu ametuweka sisi mitume kama kutuonyesha wa mwisho katika mustari wa maandamano na kama watu waliohukumiwa kuuawa. Tumekuwa kama tamasha kwa ulimwengu, kwa malaika na kwa wanadamu.10Sisi ni wajinga kwa ajili ya Kristo, lakini ninyi ni wenye hekima katika Kristo. Tu wanyonge, lakini ninyi mna nguvu. Mnaheshimiwa, lakini sisi tunadharauliwa.11Hata saa hii tuna njaa na kiu, hatuna nguo, tuna mapigo, na tena hatuna mahali pa kuishi.12Tunafanya kazi kwa bidii, kwa mikono yetu wenyewe. Tunapodharauliwa, tunabariki. Wakati tunapoteswa, twavumilia.13Tunapotukanwa, twarudisha kwa upole. Tumekuwa, na sisi bado tunahesabiwa kuwa kama kukataliwa na dunia na takataka kwa mambo yote.

14Siandiki mambo haya kuwaaibisha ninyi, lakini kuwarudi ninyi kama watoto wangu niwapendao.15Hata kama mna waalimu makumi elfu katika Kristo, hamna baba wengi. Kwa kuwa nimekuwa baba yenu katika Yesu Kristo kupitia injili.16Hivyo ninawasihi mniige mimi.17Hiyo ndiyo sababu nilimtuma kwenu Timotheo, mpendwa wangu na mtoto mwaminifu katika Bwana. Atawakumbusheni njia zangu katika Kristo, kama ninavyofundisha kila mahali na kila kanisa.

18Sasa baadhi yenu wanajisifu, wakitenda kana kwamba sitakuja kwenu.19Lakini nitakuja kwenu kitambo, kama Bwana akipenda. Ndipo nitajua si maneno yao tu wanaojisifu, lakini nitaona nguvu zao.20Kwa kuwa ufalme wa Mungu hauwi katika maneno bali katika nguvu.21Mnataka nini? Nije kwenu na fimbo au kwa upendo na katika roho ya upole?

5

1Tumesikia taarifa kuwa kuna zinaa miongoni mwenu, aina ya zinaa ambayo haipo hata katikati ya watu wa Mataifa. Tuna taarifa kwamba mmoja wenu analala na mke wa baba yake.2Nanyi mwajisifu! Badala ya kuhuzunika? Yule aliyefanya hivyo anapaswa kuondolewa miongoni mwenu.3Ingawa sipo pamoja nanyi kimwili lakini nipo nanyi kiroho, nimekwisha mhukumu yeye aliyefanya hivi, kama vile nilikuwepo.4Mnapokutanika pamoja katika jina la Bwana wetu Yesu, na roho yangu ipo pale kama kwa nguvu za Bwana wetu Yesu, nimekwisha mhukumu mtu huyu.5Nimekwisha kumkabidhi mtu huyu kwa Shetani ili kwamba mwili wake uharibiwe, ili roho yake iweze kuokolewa katika siku ya Bwana.

6Majivuno yenu si kitu kizuri. Hamjui chachu kidogo huharibu donge zima?7Jisafisheni ninyi wenyewe chachu ya kale, ili kwamba muwe donge jipya, ili kwamba mwe mkate usiochachuliwa. Kwa kuwa, Kristo, Mwana Kondoo wetu wa pasaka amekwisha kuchinjwa.8Kwa hiyo tusherekee karamu si kwa chachu ya kale, chachu ya tabia mbaya na uovu. Badala yake, tusherekee na mkate usiotiwa chachu wa unyenyekevu na kweli.

9Niliandika katika barua yangu kuwa msichangamane na wazinzi.10Sikua na maananisha wazinzi wa dunia hii, au na wenye tamaa au wanyang'anyi au waabudu sanamu, kwa kukaa mbali nao, basi ingewapasa mtoke duniani.11Lakini sasa nawaandikia kutojichanganya na yeyote anayeitwa kaka au dada katika Kristo, lakini anaishi katika uzinzi au ambaye ni mwenye kutamani, au mnyang'anyi, au mwabudu sanamu, au mtukanaji au mlevi. Wala msile naye mtu wa namna ile.12Kwa hiyo nitajihusishaje kuwahukumu walio nje ya Kanisa? Badala yake, ninyi hamkuwahukumu walio ndani ya kanisa?13Lakini Mungu anawahukumu walio nje. “Mwondoeni mtu mwovu miongoni mwenu.

6

1Mmoja wenu anapokuwa na tatizo na mwenzake, anathubutu kwenda kwa mahakama ya wasio haki kuliko mbele ya waumini?2Hamjui kuwa waumini watauhukumu ulimwengu? Na kama mtauhukumu ulimwengu, hamuwezi kuamua mambo yasiyo muhimu?3Hamjui kuwa tutawahukumu malaika? Kwa kiasi gani zaidi, tunaweza kuamua mambo ya maisha haya?4Kama tunaweza kuhukumu mambo ya maisha haya, kwa nini mnathubutu kupeleka mashitaka mbele ya wasiosimama kanisani?5Nasema haya kwa aibu yenu. Hakuna mwenye busara miongoni mwenu wa kutosha kuweka mambo sawa kati ya ndugu na ndugu?6Lakini kama ilivyo sasa, mwamini mmoja huenda mahakamani dhidi ya muumini mwingine, na mashitaka hayo huwekwa mbele ya hakimu asiyeamini!

7Ukweli ni kwamba kuna matatizo katikati ya Wakristo yaliyoleta tayari usumbufu kwenu. Kwanini msiteseke kwa mabaya? Kwanini mnakubali kudanganywa?8Lakini mmetenda uovu na kudanganya wengine, na hao ni kaka na dada zenu!

9Hamjui kwamba wasio haki hawataurithi ufalme wa Mungu? Msiamini uongo. Waasherati, waabudu sanamu, wazinzi, wafiraji, walawiti,10wevi, wachoyo, walevi, wanyang'anyi, watukanaji-hakuna miongoni mwao atakayeurithi ufalme wa Mungu.11Na hao walikuwa baadhi yao ni ninyi. Lakini mmekwisha kutakaswa, lakini mmekwisha kuoshwa, lakini mmekwisha kutengwa kwa Mungu, lakini mmefanywa haki mbele za Mungu katika jina la Bwana Yesu Kristo na kwa Roho wa Mungu wetu.

12“Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini si kila kitu kina faida. “Vitu vyote ni halali kwangu,” lakini sitatawaliwa na kimoja cha hivyo.13“Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu atavitowesha vyote. Mwili haujaumbwa kwa ajili ya ukahaba, badala yake, mwili ni kwa ajili ya Bwana, na Bwana atauhudumia mwili.14Mungu alimfufua Bwana na sisi pia atatufufua kwa nguvu zake.

15Hamjui kwamba miili yenu ina muunganiko na Kristo? Mwawezaje kuvitoa viungo vya Kristo na kwenda kuviunganisha na kahaba? Haiwezekani!16Hamjui kwamba anayeungana na kahaba amekuwa mwili mmoja naye? Kama andiko lisemavyo, “Wawili watakuwa mwili mmoja.”17Lakini anayeungana na Bwana anakuwa roho moja pamoja naye.

18Ikimbieni zinaa! Kila dhambi aifanyayo mtu ni nje na mwili wake. Lakini, mtu afanyaye zinaa hutenda dhambi dhidi ya mwili wake mwenyewe.19Hamjui kuwa miili yenu ni hekalu la Roho Mtakatifu, akaaye ndani yenu, yule ambaye mlipewa kutoka kwa Mungu? Hamjui kwamba si ninyi wenyewe?20Kwamba mlinunuliwa kwa thamani. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu kwa miili yenu.

7

1Kuhusu mambo mliyoniandikia; Ni vizuri mwanaume asimguse mwanamke.2Lakini kwa sababu ya majaribu mengi ya zinaa kila mwanaume awe na mkewe, na kila mwanamke awe na mmewe.3Mume anapaswa kumpa mke haki yake ya ndoa, na vile vile mke naye kwa mmewe.4Mke hana mamlaka juu ya mwili wake, bali mumewe. Na vile vile, mume hana mamlaka juu ya mwili wake bali mkewe.5Msinyimane mnapolala pamoja, isipokuwa mmekubaliana kwa muda maalum. Fanyeni hivyo ili kupata muda wa maombi. Kisha mnaweza kurudiana tena pamoja, Ili kwamba Shetani asije akawajaribu kwa kukosa kiasi.

6Lakini nasema haya mambo kwa hiari na si kama amri.7Natamani kila mmoja angekuwa kama mimi nilivyo. Lakini kila mmoja ana karama yake kutoka kwa Mungu. Huyu ana karama hii, na yule ana karama ile.

8Kwa wasioolewa na wajane ninasema kwamba, ni vizuri kwao kama wakibaki bila kuolewa, kama nilivyo mimi.9Lakini kama hawawezi kujizuia, wanapaswa kuolewa. Kwa kuwa ni heri kuolewa kuliko kuwaka tamaa ya mwili.

10Sasa kwa wale walioolewa nawapa amri, si mimi bali ni Bwana. “Mke asitengane na mume wake.”11Lakini kama akijitenga kutoka kwa mumewe, abaki hivyo bila kuolewa au vinginevyo apatane na mumewe. Na “Mume asimpe talaka mke wake.”

12Lakini kwa waliobaki, nasema- mimi, si Bwana- kwamba kama ndugu yeyote ana mke asiyeamini na anaridhika kuishi naye, hapaswi kumwacha.13Kama mwanamke ana mume asiyeamini, na kama anaridhika kuishi naye, asimwache.14Kwa mume asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya imani ya mkewe. Na mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa sababu ya mumewe aaminiye. Kama isingekua hivyo, watoto wenu wangekuwa si safi, lakini kwa kweli wametakaswa.

15Lakini mwenzi asiyeamini akiondoka, na aondoke. Kwa namna hiyo, kaka au dada hafungwi na viapo vyao. Mungu ametuita tuishi kwa amani.16Unajuaje kama wewe mwanamke, huenda utamwokoa mumeo? Au unajuaje kama wewe mwanaume, huenda utamwokoa mkeo?

17Kila mmoja tu aishi maisha kama Bwana alivyowagawia, kila mmoja kama Mungu alivyowaita wao. Huu ni mwongozo wangu kwa makanisa yote.18Yupo aliyekuwa ametahiriwa alipoitwa kuamini? Asijaribu kuondoa alama ya tohara yake. Yupo yeyote aliyeitwa katika imani hajatahiriwa? Hapaswi kutahiriwa.19Kwa hili aidha ametahiriwa wala asiye tahiriwa hakuna matatizo. Chenye matatizo ni kutii amri za Mungu.20Kila mmoja abaki katika wito alivyokuwa alipoitwa na Mungu kuamini.21Ulikuwa mtumwa wakati Mungu alipokuita? Usijali kuhusu hilo. Lakini kama unaweza kuwa huru, fanya hivyo.22Kwa mmoja aliyeitwa na Bwana kama mtumwa ni mtu huru katika Bwana. Kama vile, mmoja aliye huru alipoitwa kuamini ni mtumwa wa Kristo.23Mmekwisha nunuliwa kwa thamani, hivyo msiwe watumwa wa wanadamu.24Kaka na dada zangu, katika maisha yoyote kila mmoja wetu tulipoitwa kuamini, tubaki kama vile.

25Basi, kuhusu mabikira, sina amri kutoka kwa Bwana, bali nawapa ushauri wangu kama mtu ambaye kwa huruma za Bwana ni mwaminifu.26Kwa hiyo, ninafikiri hivyo kwa sababu ya usumbufu, ni vyema mwanaume abaki kama alivyo.27Umefungwa kwa mwanamke na kiapo cha ndoa? Usitake uhuru kutoka kwa hiyo. Una uhuru kutoka kwa mke au hujaolewa? Usitafute mke.28Lakini kama ukioa, hujafanya dhambi. Na kama mwanamke hajaolewa akiolewa, hajafanya dhambi. Bado wale wanaoana wanapata masumbufu ya aina mbalimbali. Nami nataka niwaepushe hayo.

29Lakini nasema hivi, kaka na dada zangu, muda ni mfupi. Tangu sasa na kuendelea, wale walio na wake waishi kama hawana.30Wote walio na huzuni wajifanye kama walikuwa hawana huzuni, na wote wanaofurahi, kama walikuwa hawafurahi, na wote wanaonunua kitu chochote, kama hawakumiliki chochote.31Na wote wanaoshughulika na ulimwengu, wawe kama hawakushughulika nao. Kwa kuwa mitindo ya dunia inafikia mwisho wake.

32Ninataka muwe huru kwa masumbufu yote. Mwanaume asiyeoa anajihusisha na vitu vinavyo mhusu Bwana, namna ya kumpendeza yeye.33Lakini mwanaume aliyeoa hujihusisha na mambo ya dunia, namna ya kumpendeza mkewe,34amegawanyika. Mwanawake asiyeolewa au bikira hujihusisha na vitu kuhusu Bwana, namna ya kujitenga katika mwili na katika roho. Lakini mwanamke aliyeolewa hujihusisha kuhusu vitu dunia, namna ya kumfurahisha mme wake.35Nasema hivi kwa faida yenu wenyewe, na siweki mtego kwenu. Nasema hivi kwa vile ni haki, ili kwamba mnaweza kujiweka wakfu kwa Bwana bila kikwazo chochote.

36Lakini kama mtu anafikiri hawezi kumtendea kwa heshima mwanawali wake, kwa sababu ya hisia zake zina nguvu sana, acha aoane naye kama apendavyo. Siyo dhambi.37Lakini kama amefanya maamuzi kutokuoa, na hakuna haja ya lazima, na kama anaweza kutawala hamu yake, atafanya vyema kama hatamwoa.38Hivyo, anayemwoa mwanamwali wake afanya vyema, na yeyote ambaye anachagua kutooa atafanya vyema zaidi.

39Mwanamke amefungwa na mmewe wakati yu hai. Lakini kama mmewe akifa, yuko huru kuolewa na yeyote ampendaye, lakini katika Bwana tu.40Bado katika maamuzi yangu, atakuwa na furaha zaidi kama akiishi kama alivyo. Na ninafikiri kuwa nami pia nina Roho wa Mungu.

8

1Sasa kuhusu vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua ya kwamba sisi sote tuna maarifa. Maarifa huleta majivuno, bali upendo hujenga.2Ikiwa mtu yeyote anadhani kwamba anajua jambo fulani, mtu huyo bado hajui kama impasavyo kujua.3Lakini ikiwa mmoja wapo akimpenda Mungu, mtu huyo anajulikana naye.

4Basi kuhusu kula vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu: twajua kuwa sanamu si kitu katika dunia hii, na ya kuwa hakuna Mungu ila mmoja tu.5Kwa maana kuna wengi waitwao miungu ikiwa ni mbinguni au duniani, kama vile walivyo miungu na mabwana wengi.6Ijapokuwa kwetu kuna Mungu mmoja tu ambaye ni Baba, vitu vyote vimetoka kwake, nasi tunaishi kwake, na Bwana mmoja Yesu Kristo, ambaye kwake vitu vyote vimekuwapo, na kwa yeye sisi tupo.

7Hata hivyo, ujuzi huu haupo ndani ya kila mmoja. Badala yake, wengine walishiriki ibada za sanamu hapo zamani, na hata sasa wanakula vyakula hivi kana kwamba ni kitu kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Dhamiri zao zimepotoshwa kwa kuwa ni dhaifu.8Lakini chakula hakitatuthibitisha sisi kwa Mungu. Sisi sio wabaya sana kama tusipo kula, wala wema sana ikiwa tutakula.9Lakini iweni makini ya kwamba uhuru wenu usiwe sababu ya kumkwaza aliye dhaifu katika imani.10Hebu fikiri kwamba mtu amekuona, wewe uliye na ujuzi, unakula chakula katika hekalu la sanamu. Dhamiri yake mtu huyo haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu?11Kwa hiyo kwa sababu ya ufahamu wako wa ukweli juu ya asili ya sanamu, kaka au dada yako aliye dhaifu, ambaye pia Kristo alikufa kwa ajili yake, anaangamizwa.12Hivyo, unapofanya dhambi dhidi ya kaka na dada zako na kuzijeruhi dhamiri zao zilizo dhaifu, mnatenda dhambi dhidi ya Kristo.13Kwa hiyo, ikiwa chakula kinasababisha kumkwaza kaka au dada, sitakula nyama kamwe, ili nisimsababishe kaka au dada yangu kuanguka.

9

1Je, Mimi si huru? Mimi si mtume? Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana?2Ikiwa mimi si mtume kwa wengine, angalau ni mtume kwenu ninyi. Kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana.

3Huu ndio utetezi wangu kwa wale wanaonichunguza mimi.4Je, hatuna haki ya kula na kunywa?5Hatuna haki kuchukua mke aliye amini kama wafanyavyo mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?6Au ni mimi peke yangu na Barnaba ambao tunapaswa kufanya kazi?7Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mzabibu na asile matunda yake? Au ni nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake?

8Je, ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu? Sheria nayo haisemi haya?9Kwa kuwa imeandikwa katika sheria ya Musa, “usimfunge ng'ombe kinywa apulapo nafaka.” Ni kweli kwamba hapa Mungu anajali ng'ombe?10Au je, hasemi hayo kwa ajili yetu? Imeandikwa kwa ajili yetu, kwa sababu yeye alimaye nafaka inampasa kulima kwa matumaini, naye avunaye inampasa avune kwa matarajio ya kushiriki katika mavuno.11Ikiwa tulipanda vitu vya rohoni miongoni mwenu, Je! Ni neno kubwa kwetu tukivuna vitu vya mwilini kutoka kwenu?12Ikiwa wengine walipata haki hii kutoka kwenu, Je! Sisi si zaidi? Hata hivyo, hatukuidai haki hii. Badala yake, tulivumilia mambo yote badala ya kuwa kikwazo cha injili ya Kristo.13Hamjui ya kuwa wote wafanyao kazi hekaluni hupata chakula chao kutoka hekaluni? Hamjui ya kuwa wote watendao kazi madhabahuni hupata sehemu ya kile kilichotolewa madhabahuni?14Kwa jinsi iyo hiyo, Bwana aliagiza ya kuwa wote wanaoitangaza injili sharti wapate kuishi kutokana na hiyo injili.

15Lakini sijawadai haki zote hizi. Na siandiki haya ili jambo lolote lifanyike kwa ajili yangu. Ni heri mimi nife kuliko mtu yeyote kubatilisha huku kujisifu kwangu.16Maana ikiwa naihubiri injili, sina sababu ya kujisifu, kwa sababu ni lazima nifanye hivi. Na ole wangu nisipoihubiri injili!17Kwa maana nikifanya hivi kwa hiari yangu, nina thawabu. Lakini ikiwa si kwa hiari, bado nina jukumu nililopewa kuwa wakili.18Basi thawabu yangu ni nini? Ya kuwa nihubiripo, nitaitoa injili pasipo gharama na bila kutumia kwa utimilifu wa haki yangu niliyonayo katika Injili.

19Maana japo nimekuwa huru kwa wote, nilifanyika mtumwa wa wote, ili kwamba niweze kuwapata wengi zaidi.20Kwa Wayahudi nilikuwa kama Myahudi, ili niwapate Wayahudi. Kwa wale walio chini ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao aliye chini ya sheria ili niwapate wale walio chini ya sheria. Nilifanya hivyo ingawa mimi binafsi sikuwa chini ya sheria.21Kwa wale walio nje ya sheria, nilikuwa kama mmoja wao nje ya sheria, ingawa mimi binafsi sikuwa nje ya sheria ya Mungu, bali chini ya sheria ya Kristo. Nilifanya hivyo ili niwapate wale walio nje ya sheria.22Kwa walio wanyonge nilikuwa mnyonge, ili niwapate walio wanyonge. Nimekuwa hali zote kwa watu wote, ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi.23Nami nafanya mambo yote kwa ajili ya injili, ili nipate kushiriki katika baraka.

24Hamjui ya kuwa katika mbio wote washindanao hupiga mbio, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Hivyo pigeni mbio ili mpate tuzo.25Mwana michezo hujizuia katika yote awapo katika mafunzo. Hao hufanya hivyo ili wapokee taji iharibikayo, lakini sisi tunakimbia ili tupate taji isiyoharibika.26Kwa hiyo mimi sikimbii bila sababu au napigana ngumi kama kupiga hewa.27Lakini nautesa mwili wangu na kuufanya kama mtumwa, ili kwamba nijapokwisha kuwahubiri wengine, mimi mwenyewe nisiwe wa kukataliwa.

10

1Nataka ninyi mjue kaka na dada zangu, ya kuwa baba zetu walikuwa chini ya wingu na wote walipita katika bahari.2Wote walibatizwa wawe wa Musa ndani ya wingu na ndani ya bahari,3na wote walikula chakula kile kile cha roho.4Wote walikunywa kinywaji kile kile cha roho. Maana walikunywa kutoka katika mwamba wa roho uliowafuata, na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.5Lakini Mungu hakupendezwa sana na wengi wao, na maiti zao zilisambazwa jangwani.

6Basi mambo haya yote yalikuwa mifano kwetu, ili sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya kama walivyofanya.7Msiwe waabudu sanamu, kama wengi wao walivyokuwa. Hii ni kama ilivyoandikwa, “Watu walikaa chini wakila na kunywa, na waliinuka kucheza kwa tamaa za mapenzi.”8Tusifanye uasherati kama wengi wao walivyofanya. Wakafa siku moja watu ishirini na tatu elfu kwa sababu hiyo.9Wala tusimjaribu Kristo, kama wengi wao walivyofanya na wakaharibiwa kwa nyoka.10Na pia msinung'unike, kama wengi wao walivyonung'unika na kuharibiwa na malaika wa mauti.

11Basi mambo hayo yalitendeka kama mifano kwetu. Yakaandikwa ili kutuonya sisi - tuliofikiliwa na miisho ya zamani.12Kwa hiyo kila ajionaye amesimama awe makini asije akaanguka.13Hakuna jaribu lililowapata ninyi lisilo kawaida ya wanadamu. Ila Mungu ni mwaminifu. Hatawaacha mjaribiwe kupita uwezo wenu. Pamoja na jaribu yeye atawapa mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili.

14Kwa hiyo, wapendwa wangu, ikimbieni ibada ya sanamu.15Nasema nanyi kama watu wenye akili, ili muamue juu ya ninalosema.16Kikombe cha baraka tubarikicho, si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo?17Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja. Sisi sote twapokea mkate mmoja kwa pamoja.

18Watazameni watu wa Israeli: Je! Wale wote walao dhabihu si washiriki katika madhabahu?19Nasema nini basi? Ya kuwa sanamu ni kitu? Au ya kuwa chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu?20Lakini nasema juu ya vitu vile wavitoavyo sadaka watu wapagani wa Mataifa, ya kuwa wanatoa vitu hivi kwa mapepo na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi kushirikiana na mapepo!21Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mapepo. Hamwezi kuwa na ushirika katika meza ya Bwana na katika meza ya mapepo.22Au twamtia Bwana wivu? Tuna nguvu zaidi yake?

23“Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote vifaavyo. “Vitu vyote ni halali,” lakini si vyote viwajengavyo watu.24Hakuna hata mmoja angetafuta mazuri yake tu. Badala yake, kila mmoja angetafuta mazuri ya mwenzake.25Mnaweza kula kila kitu kiuzwacho sokoni bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.26Maana “dunia ni mali ya Bwana, na vyote viijazavyo.”27Na mtu asiyeamini akiwaalika kula, na mnataka kwenda, kuleni chochote awapacho pasipo kuuliza maswali ya dhamiri.28Lakini mtu akiwaambia, “Chakula hiki kimetokana na sadaka ya wapagani,” msile. Hii ni kwa ajili yake aliyewaambia, na kwa ajili ya dhamiri.29Nami simaanishi dhamiri zenu, bali dhamiri ya yule mwingine. Maana kwanini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine?30Ikiwa mimi natumia chakula kwa shukrani, kwanini nitukanwe kwa kitu ambacho nimeshukuru kwacho?

31Kwa hiyo, chochote mnachokula au kunywa, au chochote mfanyacho, fanyeni yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu.32Msiwakoseshe Wayahudi au Wayunani, au kanisa la Mungu.33Jaribuni kama mimi ninavyojaribu kuwapendeza watu wote kwa mambo yote. Sitafuti faida yangu mwenyewe, bali ya wengi. Nami nafanya hivi ili wapate kuokolewa.

11

1Nifuateni mimi, kama na mimi ninavyomfuata Kristo.

2Sasa nawasifu kwasababu ya vile mnavyonikumbuka katika mambo yote. Nawasifu kwasababu mmeyashika mapokeo kama nilivyoyaleta kwenu.3Basi nataka mfahamu ya kuwa Kristo ni kichwa cha kila mwanaume, naye mwanaume ni kichwa cha mwanamke, na ya kuwa Mungu ni kichwa cha Kristo.4Kila mwanaume aombaye au atoae unabii akiwa amefunika kichwa anakiabisha kichwa chake.5Lakini kila mwanamke aombae au kutoa unabii hali kichwa chake kikiwa wazi anakiaibisha kichwa chake. Kwa maana ni sawa sawa na kama amenyolewa.6Ikiwa kama mwanamke hatafunika kichwa chake, na akatwe nywele zake ziwe fupi. Maana ikiwa ni aibu mwanamke kukata nywele zake au kunyolewa, basi afunike kichwa chake.7Kwani haimpasi mwanamume kufunika kichwa chake, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.8Maana mwanamume hakutokana na mwanamke. Bali mwanamke alitokana na mwanamume.9Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke. Bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume.10Hii ndio sababu mwanamke anapaswa kuwa na ishara ya mamlaka juu ya kichwa chake, kwa sababu ya malaika.

11Hata hivyo, katika Bwana, mwanamke hayupo peke yake pasipo mwanamume, au mwanamume pasipo mwanamke.12Maana kama vile mwanamke alitoka kwa mwanamume, vile vile mwanamume alitoka kwa mwanamke. Na vitu vyote hutoka kwa Mungu.13Hukumuni wenyewe: Je! Ni sahihi mwanamke amuombe Mungu hali kichwa chake kikiwa wazi?14Je hata asili peke yake haiwafundishi ya kwamba mwanamume akiwa na nywele ndefu ni aibu kwake?15Je, asili haiwafundishi ya kwamba mwanamke akiwa na nywele ndefu ni utukufu kwake? Maana amepewa zile nywele ndefu kama vazi lake.16Lakini ikiwa mtu yeyote anataka kubishana juu ya hili, sisi hatuna namna nyingine, wala makanisa ya Mungu.

17Katika maagizo yafuatayo, mimi siwasifu. Maana mnapokusanyika, sio kwa faida bali kwa hasara.18Maana kwanza, nasikia ya kuwa mkutanikapo kanisani, kuna migawanyiko kati yenu, na kwa sehemu ninaamini.19Kwa maana ni lazima iwepo misuguano kati yenu, ili wale waliokubaliwa wajulikane kwenu.20Kwa maana mkutanikapo, mnachokula sio chakula cha Bwana.21Mnapokula, kila mmoja hula chakula chake mwenyewe kabla wengine hawajala. Hata huyu ana njaa, na huyu amelewa.22Je hamna nyumba za kulia na kunywea? Je mnalidharau kanisa la Mungu na kuwafedhehesha wasio na Kitu? Niseme nini kwenu? Niwasifu? Sitawasifu katika hili!

23Maana nilipokea kutoka kwa Bwana kile ambacho nimewapa ninyi ya kuwa Bwana Yesu, usiku ule aliposalitiwa, alichukua mkate.24Baada ya kushukuru, aliuvunja na kusema, “Huu ndio mwili wangu, ulio kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa kunikumbuka mimi.”25Na vivi hivi akachukua kikombe baada ya kula, na kusema, “Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi mara nyingi kila mywapo, kwa kunikumbuka mimi.”26Kwa kila muda mlapo mkate huu na kukinywea kikombe, mwaitangaza mauti ya Bwana mpaka atakapokuja.

27Kwa hiyo, kila aulaye mkate au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana.28Mtu ajihoji mwenyewe kwanza, na hivyo aule mkate, na kukinywea kikombe.29Maana alaye na kunywa bila kuupambanua mwili, hula na kunywa hukumu yake mwenyewe.30Hii ndiyo sababu watu wengi kati yenu ni wagonjwa na dhaifu, na baadhi yenu wamekufa.31Lakini tukijichunguza wenyewe hatutahukumiwa.32Ila tunapohukumiwa na Bwana, twarudiwa, ili tusije tukahukumiwa pamoja na dunia.

33Kwa hiyo, kaka na dada zangu, mkutanikapo mpate kula, ngojeaneni.34Mtu akiwa na njaa, na ale nyumbani kwake, ili kwamba mkutanikapo pamoja isiwe kwa hukumu. Na kuhusu mambo mengine mliyoandika, nitawaelekeza nitakapokuja.

12

1Kuhusu karama za rohoni, kaka na dada zangu sitaki mkose kufahamu.2Mwajua ya kuwa mlipokuwa wapagani mliongozwa kufuata sanamu zisizoongea, kwa njia zozote mliongozwa nazo.3Kwa hiyo, nataka mfahamu kwamba hakuna yeyote anenaye kwa Roho wa Mungu akisema, “Yesu amelaaniwa.” Hakuna yeyote atakayesema, “Yesu ni Bwana,” isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

4Basi kuna karama tofauti tofauti, bali Roho ni yeye yule.5Na kuna huduma tofauti tofauti, bali Bwana ni yeye yule.6Na kuna aina mbalimbali za kazi, lakini Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote.

7Basi kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa faida ya wote.8Maana mtu mmoja amepewa na Roho neno la hekima, na mwingine neno la maarifa kwa Roho yule yule.9Kwa mwingine humpa imani kwa Roho yeye yule, na kwa mwingine karama ya uponyaji kwa Roho mmoja.10Kwa mwingine matendo ya nguvu, na mwingine unabii. Na kwa mwingine uwezo wa kupambanua roho, mwingine aina mbalimbali za lugha, na kwa mwingnine tafsiri za lugha.11Lakini Roho ni yule yule atendaye kazi hizi zote, kumpa kila mtu karama kwa kadiri ya uchaguzi wake mwenyewe.

12Kwa maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote ni vya mwili ule ule, vivyo hivyo na Kristo.13Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi au Wayunani, kwamba tu watumwa au huru, na wote tulinyweshwa Roho mmoja.

14Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.15Ikiwa mguu utasema, “kwa kuwa mimi si mkono, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo haiufanyi kutokuwa sehemu ya mwili.16Na ikiwa sikio litasema, “kwa kuwa mimi si jicho, mimi si sehemu ya mwili,” hiyo hailifanyi kutokuwa sehemu ya mwili.17Kama mwili wote utakuwa jicho, kungekuwa wapi kusikia? Kama mwili wote ukiwa sikio, kungekuwa wapi kunusa?18Lakini Mungu aliweka kila kiungo cha mwili mahali pake kama alivyopanga mwenyewe.19Na kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?20Hivyo sasa viungo ni vingi, lakini mwili ni mmoja.21Jicho haliwezi kuuambia mkono, “sina haja na wewe.” Wala kichwa hakiwezi kuiambia miguu, sina haja na ninyi.”22Lakini viungo vya mwili vinavyoonekana kuwa na heshima kidogo vyahitajika zaidi.23Na viungo vya mwili tunavyodhani vina heshima kidogo, twavipa heshima zaidi, na viungo vyetu visivyo na mvuto vina uzuri zaidi.24Na sasa viungo vyetu vilivyo na mvuto havina haja ya kupewa heshima, kwa kuwa tayari vina heshima. Lakini Mungu ameviunganisha viungo vyote pamoja, na amevipa heshima zaidi vile visivyo heshimiwa.25Alifanya hivyo ili pasiwepo mgawanyiko katika mwili, bali viungo vyote vitunzane kwa upendo wa mmoja.26Na wakati kiungo kimoja kikiumia, viungo vyote vyaumia kwa pamoja. Au wakati kiungo kimoja kikiheshimiwa, viungo vyote vifurahi kwa pamoja.

27Sasa ninyi ni mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake.28Na Mungu ameweka katika kanisa kwanza mitume, pili manabii, tatu waalimu, kisha wale wote watendao matendo makuu, kisha karama za uponyaji, wale wasaidiao, wale wafanyao kazi ya kuongoza, na wote walio na aina mbalimbali za lugha.29Je sisi sote ni mitume? Sisi sote ni manabii? Sisi sote ni waalimu? Je sisi sote tunafanya matendo ya miujiza?30Je, sisi sote tuna karama ya uponyaji? Sisi sote tunaongea kwa lugha? Sisi sote tunatafsiri lugha?31Tafuteni sana karama zilizo kuu. Nami nitawaonesha njia iliyo bora zaidi.

13

1Nijaposema kwa lugha za wanadamu na za malaika, lakini kama sina upendo, nimekuwa shaba iliayo au upatu uvumao.2Tena nijapokuwa nina karama ya unabii na ufahamu wa kweli zilizofichika na maarifa, na kwamba ninayo imani ya kuhamisha milima, lakini ikiwa sina upendo, mimi si kitu.3Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha masikini, tena nikiutoa mwili wangu nichomwe moto, lakini kama sina upendo, hainifaidii kitu.

4Upendo huvumilia na hufadhili. Upendo haujisifu au kujivuna. Hauna kiburi5au ukorofi. Hautafuti mambo yake, hauoni uchungu haraka, wala hauhesabu mabaya.6Haufurahii udhalimu. Badala yake, hufurahi katika kweli.7Upendo huvumilia mambo yote; huamini mambo yote, una ujasiri katika mambo yote, na hustahimili mambo yote.

8Upendo haukomi. Ikiwa kuna unabii, wote utapita. Ikiwa kuna lugha, zitakoma. Ikiwa kuna maarifa, yatapita.9Kwa kuwa tunajua kwa sehemu na tunafanya unabii kwa sehemu.10Lakini ijapo ile iliyo kamili, ile isiyo kamili itapita.11Nilipokuwa mtoto, nilisema kama mtoto, nilifikiri kama mtoto, niliamua kama mtoto. Nilipokuwa mtu mzima, niliweka mbali nami mambo ya kitoto.12Kwa kuwa sasa tunaona kama kwa kioo, kama sura gizani, lakini wakati ule tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kwa sehemu, lakini wakati ule nitajua sana kama na mimi ninavyojulikana sana.13Lakini sasa mambo haya matatu yanadumu: imani, tumaini lijalo, na upendo. Lakini lililo kuu zaidi ya haya ni upendo.

14

1Utafuteni upendo na kutamani sana karama za rohoni, zaidi sana mpate kutoa unabii.2Maana yeye anenaye kwa lugha hasemi na watu bali husema na Mungu. Maana hakuna aelewaye kwa sababu anena mambo yaliyofichika katika Roho.3Lakini yeye atoaye unabii, asema na watu na kuwajenga, kuwatia moyo, na kuwafariji.4Yeye anenaye kwa lugha hujijenga mwenyewe, lakini yeye atoaye unabii hulijenga kanisa.

5Sasa natamani kwamba ninyi nyote mnene kwa lugha. Lakini zaidi ya hayo, natamani ya kwamba mtoe unabii. Yeye atoaye unabii ni mkuu kuliko yeye anenaye kwa lugha (labda awepo wa kutafasiri), ili kwamba kanisa lipate kujengwa.

6Lakini sasa, kaka na dada zangu, nikija kwenu na kunena kwa lugha, nitawafaidia nini ninyi? Siwezi, isipokuwa nasema nanyi kwa njia ya ufunuo, au kwa njia ya maarifa, au unabii, au kwa njia ya fundisho.7Ikiwa vitu visivyo na uhai kama filimbi au kinubi visipotoa sauti zilizo na tofauti, itatambulikanaje ni chombo gani kinachezwa?8Kwa maana ikiwa baragumu itatoa sauti isiyojulikana, ni jinsi gani mtu atatambua ya kuwa ni muda wa kujiandaa kwa vita?9Vivyo hivyo na ninyi. Mkitoa kwa ulimi neno lisilo dhahiri, ni jinsi gani mtu ataelewa mnachosema? Mtakuwa mkiongea, na hakuna atakayewaelewa.10Hakuna shaka kwamba kuna lugha nyingi mbalimbali duniani, na hakuna hata moja isiyo na maana.11Lakini ikiwa sijui maana ya lugha, nitakuwa mgeni kwake yeye anenaye, naye anenaye atakuwa mgeni kwangu.12Vivyo hivyo na ninyi. Kwa kuwa mnatamani sana kuona uthihirisho wa Roho, takeni kwamba mzidi sana kulijenga kanisa.

13Hivyo, yeye anenaye kwa lugha na aombe apewe kutafasiri.14Kwa maana nikiomba kwa lugha, roho yangu huomba, lakini akili zangu hazina matunda.15Nifanye nini? Nitaomba kwa roho yangu, lakini pia nitaomba kwa akili zangu. Nitaimba kwa roho yangu, na nitaimba kwa akili zangu pia.16Vinginevyo, ukimsifu Mungu kwa roho, yeye aliye mgeni ataitikaje “Amina” utoapo shukurani, akiwa hayajui usemayo?17Maana ni kweli wewe washukuru vema, lakini yule mwingine hajengwi.18Namshukuru Mungu kwa kuwa nanena kwa lugha zaidi ya ninyi nyote.19Lakini katika kanisa ni heri ninene maneno matano kwa ufahamu wangu ili nipate kuwafundisha wengine, zaidi ya kunena maneno kumi elfu kwa lugha.

20Kaka na dada zangu, msiwe watoto katika kufikiri kwenu. Badala yake, kuhusiana na uovu, iweni kama watoto wachanga. Lakini katika kufikiri kwenu mkawe watu wazima.21Imeandikwa katika sheria, “Kwa watu wa lugha nyingine na kwa midomo ya wageni nitasema na watu hawa. Wala hata hivyo hawatanisikia,” asema Bwana.

22Hivyo, ndimi ni ishara, sio kwa walioamini, bali kwa wasioamini. Lakini kutoa unabii ni ishara, sio kwa wasioamini, bali kwa ajili yao waaminio.23Haya, ikiwa kanisa lote limekusanyika pamoja na wote wanene kwa lugha, na wageni na wasioamini wameingia, je hawawezi kusema kwamba mna wazimu?24Lakini ikiwa wote mnatoa unabii na asiyeamini au mgeni akaingia, atashawishiwa na yote asikiayo. Atahukumiwa na yote yasemwayo.25Siri za moyo wake zingefunuliwa. Matokeo yake, angeanguka kifudifudi na kumwabudu Mungu. Angekiri ya kwamba Mungu yu kati yenu.

26Nini kifuatacho basi, kaka na dada zangu? Mnapokutana pamoja, kila mmoja ana Zaburi, mafundisho, mafunuo, lugha au tafsiri. Fanyeni kila kitu ili kwamba mlijenge kanisa.27Kama yeyote ananena kwa lugha, wawepo wawili au watatu, na kila mmoja katika zamu. Na mtu lazima atafasiri kilichosemwa.28Lakini kama hakuna mtu wa kutafasiri, basi kila mmoja wao akae kimya ndani ya kanisa. Basi kila mmoja aongee peke yake na kwa Mungu.

29Na manabii wawili au watatu wanene, na wengine wasikilize kwa kupambanua kilichosemwa.30Lakini aliyeketi akifunuliwa jambo katika huduma, yule ambaye alikuwa ananena na anyamaze.31Kwa kuwa kila mmoja wenu anaweza kutoa unabii mmoja baada ya mwingine ili kwamba kila mmoja aweze kujifunza na wote waweze kutiwa moyo.32Kwa kuwa roho za manabii ziko chini ya uangalizi wa manabii.33Kwa kuwa Mungu si Mungu wa machafuko, bali wa amani. Kama ilivyo katika makanisa yote ya waumini,34imewapasa wanawake wakae kimya katika kanisa. Kwa kuwa hawaruhusiwi kuzungumza. Badala yake, wanapaswa kuwa katika unyenyekevu, kama pia sheria inavyosema.35Kama kuna chochote wanatamani kujifunza, basi wawaulize waume zao nyumbani. Kwa kuwa ni aibu kwa mwanamke kuongea katika kanisa.36Je neno la Mungu lilitoka kwenu? Je limewafikia ninyi tu?37Kama mtu akijiona kuwa ni nabii au wa rohoni, inampasa ayatambue mambo ninayowaandikia ya kwamba ni maagizo ya Bwana.38Lakini asipotambua haya, mwacheni asitambuliwe.

39Hivyo basi, kaka na dada zangu, takeni sana kutoa unabii, na msimzuie mtu yeyote kunena kwa lugha.40Lakini mambo yote yatendeke kwa uzuri na kwa utaratibu.

15

1Basi, ninawakumbusha, kaka na dada zangu, juu ya injili niliyowahubiria, ambayo mliipokea na kusimama kwayo.2Ni katika injili hii mmeokolewa, kama mkilishika imara neno nililowahubiri ninyi, isipokuwa mliamini bure.

3Kama kwanza nilivyo ipokea kwa umuhimu niliileta kwenu kama ilivyo: kwamba kutokana na maandiko, Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu,4kutokana na maandiko alizikwa, na kwamba alifufuka siku ya tatu.5Na kwamba alimtokea Kefa, kisha kwa wale kumi na wawili.6Kisha aliwatokea kwa wakati mmoja akina kaka na akina dada zaidi ya mia tano. Wengi wao bado wako hai, lakini baadhi yao wamelala usingizi.7Kisha alimtokea Yakobo, kisha mitume wote.8Mwisho wa yote, alinitokea mimi, kama vile kwa mtoto aliye zaliwa katika wakati usio sahihi.9Kwa kuwa mimi ni mdogo kati ya mitume. Sistahili kuitwa mtume, kwa sababu nililitesa kanisa la Mungu.10Lakini kwa neema ya Mungu nipo kama nilivyo, na neema yake kwangu haikuwa bure. Badala yake, nilifanya bidii kuliko wote. Lakini haikuwa mimi, bali neema ya Mungu iliyo ndani yangu.11Kwa hiyo kama ni mimi au wao, tuna hubiri hivyo na tunaamini hivyo.

12Sasa kama Kristo alihubiriwa kama aliyefufuka kwa wafu, iweje baadhi yenu mseme hakuna ufufuo wa wafu?13Lakini kama hakuna ufufuo wa wafu, basi hata Kristo pia hakufufuka.14Na kama Kristo hakufufuka, hivyo mahubiri yetu ni bure, na imani yenu ni bure.15Na tumepatikana kuwa mashahidi wa uongo kumuhusu Mungu, kwa sababu tulimshushuhudia Mungu kinyume, kusema alimfufua Kristo, wakati hakumfufua.16Kama ikiwa wafu hawafufuliwi, Yesu pia hakufufuliwa.17Na kama Kristo hakufufuliwa, imani yenu ni bure na bado mko kwenye dhambi zenu.18Na hapo wao nao waliokufa katika Kristo pia wameangamia.19Ikiwa kwa maisha haya peke yake tunaujasiri kwa wakati ujao ndani ya Kristo, watu wote, sisi niwakuhurumiwa zaidi ya watu wote.

20Lakini sasa Kristo amefufuka kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wale waliokufa.21Kwa maana kifo kilikuja kupitia mwanadamu, pia kupitia mwanadamu ufufuo wa wafu.22Kwa kuwa kama katika Adam wote wanakufa, hivyo pia katika Kristo wote watafanywa hai.23Lakini kila moja katika mpango wake: Kristo, matunda ya kwanza, na kisha wale walio wa Kristo watafanywa kuwa hai wakati wa kuja kwake.24Ndipo utakuwa mwisho, pale Kristo atakapo kabidhi ufalme kwa Mungu Baba. Hii ni pale atakapo komesha utawala wote na mamlaka yote na nguvu.25Kwa kuwa lazima atawale mpaka atakapoweka maadui zake wote chini ya nyayo zake.26Adui wa mwisho kuharibiwa ni kifo.27Kwa kuwa “ameweka kila kitu chini ya nyayo zake.” Lakini inaposema “ameweka kila kitu,” ni wazi kwamba hii haihusishi wale walioweka kila kitu chini yake mwenyewe.28Wakati vitu vyote vimewekwa chini yake, kisha Mwana mwenyewe atawekwa chini kwake Yeye ambaye aliviweka vitu vyote chini yake. Hii itatokea ili kwamba Mungu Baba awe yote katika vyote.

29Au pia watafanya nini wale waliobatizwa kwa ajili ya wafu? Kama wafu hawafufuliwi kabisa, kwa nini tena wanabatizwa kwa ajili yao?30Na kwa nini tuko katika hatari kila saa?31Kaka na dada zangu, kupitia kujisifu kwangu katika ninyi, ambayo ninayo katika Kristo Yesu Bwana wetu, natangaza hivi: nakufa kila siku.32Inanifaidia nini, katika mtazamo wa wanadamu, kama nilipigana na wanyama wakali huko Efeso, kama wafu hawafufuliwi? “Acha basi tule na kunywa, kwa kuwa kesho tunakufa.”33Msidanganywe: “Makundi mabaya hupotosha tabia njema.34“Muwe na kiasi! Muishi katika haki! Msiendelee kutenda dhambi. Kwa kuwa baadhi yenu hamna maarifa ya Mungu. Nasema hivi kwa aibu yenu.

35Lakini mtu mwingine atauliza, “Ni jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?”36Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa.37Na kile unachopanda sio mwili ambao utakuwa, bali ni mbegu iliyochipua. Inaweza kuwa ngano au kitu kingine.38Lakini Mungu ataipa mwili kama apendavyo, na katika kila mbengu mwili wake mwenyewe.39Miili yote haifanani. Isipokuwa, kuna mwili mmoja wa wanadamu, na mwili mwingine wa wanyama, na wili mwingine wa ndege, na mwingine kwa ajili ya samaki.40Pia kuna miili ya mbinguni na miili ya duniani. Lakini utukufu wa miili ya mbinguni ni aina moja na utukufu wa duniani ni mwingine.41Kuna utukufu mmoja wa jua, na utukufu mwingine wa mwezi, na utukufu mwingine wa nyota. Kwa kuwa nyota moja inatofautiana na nyota nyingine katika utukufu.

42Hivyo ndivyo ulivyo pia ufufuo wa wafu. Kinacho pandwa kinaharibika, na kinacho ota hakiharibiki.43Kimepandwa katika matumizi ya kawaida, kinaoteshwa katika utukufu. Kimepandwa katika udhaifu, kinaoteshwa katika nguvu.44Kimepandwa katika mwili wa asili, kinaoteshwa katika mwili wa kiroho. Kama kuna mwili wa asili, kuna mwili wa kiroho pia.

45Hivyo pia imeandikwa, “Mtu wa kwanza Adamu alifanyika roho inayo ishi.” Adamu wa mwisho alifanyika roho itoayo uhai.46Lakini wa kiroho hakuja kwanza bali wa asili, na kisha wa kiroho.47Mtu wa kwanza ni wa dunia, alitengenezwa kwa mavumbi. Mtu wa pili alitoka mbinguni.48Kama vile yule aliyetengenezwa kwa mavumbi, hivyo pia wale waliotengenezwa kwa mavumbi. Kama vile mtu wa mbinguni alivyo, hivyo pia wale wa mbinguni.49Kama ambavyo tumebeba mfano wa mtu wa mavumbi, tutabeba pia mfano wa mtu wa mbinguni.

50Sasa nawaambia, kaka na dada zangu, kwamba mwili na damu havitaweza kuurithi ufalme wa Mungu. Wala wakuharibika kurithi wakutoharibika.51Tazama! Nawaambia ninyi siri ya kweli: Hatutakufa sote, bali wote tutabadilishwa.52Tutabadilishwa katika wakati, katika kufumba na kufumbua kwa jicho, katika tarumbeta ya mwisho. Kwa kuwa tarumbeta italia, na wafu watafufuliwa na hali ya kutoharibika, na tutabadilishwa.53Kwani huu wa kuharibika lazima uvae wa kutoharibika, na huu wa kufa lazima uvae wa kutokufa.54Lakini wakati huu wa kuharibika ukivikwa wa kutokuharibika, na huu wa kufa ukivaa wa kutokufa, ndipo utakuja msemo ambao umeandikwa, “Kifo kimemezwa katika ushindi.”
55“Kifo, ushindi wako uko wapi? Kifo, uko wapi uchungu wako?”

56Uchungu wa kifo ni dhambi, na nguvu ya dhambi ni sheria.57Lakini shukurani kwa Mungu, atupaye sisi ushindi kupitia Bwana wetu Yesu Kristo!

58Kwa hiyo, wapendwa kaka na dada zangu, iweni imara na msitikisike. Daima itendeni kazi ya Bwana, kwa sababu mnajua kuwa kazi yenu katika Bwana siyo bure.

16

1Sasa, kuhusu michango kwa ajili ya waumini, kama nilivyo elekeza makanisa ya Galatia, vivyo hivyo mwapaswa kufanya.2Katika siku ya kwanza ya wiki, kila mmoja wenu aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, kama muwezavyo. Fanyeni hivyo ili kwamba kusiwe na michango wakati nikija.3Na nitakapofika, yeyote mtakayemchagua, nitamtuma pamoja na barua kutoa sadaka yenu huko Yerusalem.4Na kama ni sahihi kwa mimi kwenda pia, watakwenda pamoja nami.

5Lakini nitakuja kwenu, wakati ninapitia Makedonia. Kwa kuwa nitapitia Makedonia.6Labda naweza kukaa nanyi au hata kumaliza majira ya baridi, ili kwamba muweze kunisaidia katika safari yangu, popote niendako.7Kwa kuwa sitarajii kuwaona sasa kwa muda mfupi. Kwani ninatumaini kukaa nanyi kwa muda fulani, kama Bwana ataniruhusu.8Lakini nitakaa Efeso mpaka Pentekoste,9kwa kuwa mlango mpana umefunguliwa kwa ajili yangu, na kuna maadui wengi wanipingao.

10Sasa wakati Timotheo akija, muoneni kwamba yuko na ninyi pasipo kuogopa, anafanya kazi ya Bwana, kama ninavyofanya.11Mtu yeyote asimdharau. Mumsaidie katika njia yake kwa amani, ili kwamba aweze kuja kwangu. Kwa kuwa ninamtarajia aje pamoja na ndugu.

12Sasa kuhusiana na ndugu yetu Apolo. Nilimtia moyo sana kuwatembelea ninyi pamoja na ndugu. Lakini aliamua kutokuja kwa sasa. Hata hivyo, atakuja wakati ana nafasi.

13Muwe macho, simameni imara, mtende kama wanaume, muwe na nguvu.14Basi yote myafanyayo yafanyike katika upendo.

15Mnaijua kaya ya Stefana. Mnajua kwamba walikuwa waamini wa kwanza huko Akaya, na kwamba walijiweka wenyewe kwenye huduma ya waumini. Na sasa nawasihi, kaka na dada zangu,16kuweni wanyenyekevu kwa watu kama hao, na kwa kila mtu anayesaidia katika kazi na watenda kazi pamoja nasi.17Na ninafurahi kwa ujio wa Stefana, Fotunato, na Akiko. Wamesimama mahali ambapo ninyi mgepaswa kuwa.18Kwa kuwa wameifurahisha roho yangu na yenu. Kwa hiyo sasa, watambueni watu.

19Makanisa ya Asia wametuma salamu kwenu. Akila na Priska wanawasalimu katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko nyumbani kwao.20Kaka na dada zangu wote wanawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.

21Mimi, Paulo, naandika hivi kwa mkono wangu.22Kama yeyote hampendi Bwana, basi laana iwe juu yake. Bwana wetu, njoo!23Neema ya Bwana Yesu iwe nanyi.24Upendo wangu uwe pamoja nanyi katika Kristo Yesu.

2 Wakorintho

1

1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu, kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, na kwa watakatifu wote walioko katika mkoa wote wa Akaya.2Neema na iwe kwenu na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

3Na asifiwe Mungu na Baba wa Bwana Yesu Kristo. Yeye ni Baba wa rehema na Mungu wa faraja yote.4Anayetufariji sisi katika mateso yetu yote, ili kwamba tuweze kuwafariji wale walio katika mateso. Tunawafariji wengine kwa faraja ileile ambayo Mungu alitumia kutufariji na sisi.5Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo huongezeka kwa ajili yetu, vile vile faraja yetu huongezeka kupitia Kristo.6Lakini kama sisi tunataabishwa, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu. Na kama tunafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu. Faraja yenu inafanya kazi kikamilifu mnaposhiriki mateso kwa uvumilivu kama sisi pia tunavyoteseka.7Na ujasiri wetu juu yenu ni thabiti. Tunajua kwamba kama vile ambavyo mnashiriki mateso, vile vile mnashiriki faraja.

8Kwa kuwa hatutaki ninyi msijue, kuhusu matatizo tuliyokuwa nayo huko Asia. Tulizidiwa mno zaidi ya vile tuwezavyo kubeba, hata hatukuwa na tumaini la kuishi tena.9Kweli, tulikuwa na hukumu ya kifo juu yetu. Lakini hiyo ilikuwa ni kutufanya sisi tusiweke tumaini juu yetu wenyewe, badala yake tuweke tumaini katika Mungu, afufuaye wafu.10Alituokoa sisi kutoka hayo maafa ya mauti, na atatuokoa tena. Tumeweka ujasiri wetu katika yeye ya kwamba atatuokoa tena.11Atafanya hivi kama vile ninyi pia mtusaidiavyo kwa maombi yenu. Hivyo wengi watatoa shukurani kwa niaba yetu kwa ajili ya upendeleo wa neema tuliyopewa sisi kupitia maombi ya wengi.

12Tunajivunia hili: ushuhuda wa dhamiri yetu. Kwa kuwa ni katika nia safi na usafi wa Mungu kwamba tulienenda wenyewe katika dunia. Tumefanya hivi hasa na ninyi, na sio katika hekima ya ulimwengu, lakini badala yake ni katika neema ya Mungu.13Hatuwaandikii chochote ambacho hamwezi kukisoma au kuelewa. Ninaujasiri14kwamba kwa sehemu mumekwisha kutuelewa. Na ninaujasiri kwamba katika siku ya Bwana Yesu tutakuwa sababu yenu kwa ajili ya kiburi chenu, kama vile mtakavyokuwa kwetu.

15Kwa sababu nilikuwa na ujasiri kuhusu hili, nilitaka kuja kwenu kwanza, ili kwamba muweze kupokea faida ya kutembelewa mara mbili.16Nilikuwa napanga kuwatembelea ninyi wakati nikielekea Makedonia. Tena nilitaka kuwatembelea tena wakati nikirudi kutoka Makedonia, na kisha ninyi kunituma mimi wakati nikielekea Uyahudi.17Nilipokuwa nafikiria namna hii, je, nilikuwa nasitasita? Je, ninapanga mambo kulingana na viwango vya kibinadamu, ili kwamba niseme “Ndiyo, ndiyo” na “Hapana, hapana” kwa wakati mmoja?18Lakini kama vile Mungu alivyo mwaminifu, hatusemi vyote “Ndiyo” na “Hapana.”19Kwa kuwa mwana wa Mungu, Yesu Kristo, ambaye Silvano, Timotheo na mimi tulimtangaza miongoni mwenu, siyo “Ndiyo” na “Hapana.” Badala yake, yeye wakati wote ni “Ndiyo.”20Kwa kuwa ahadi zote za Mungu ni “Ndiyo” katika yeye. Hivyo pia kupitia yeye tunasema “Amina” kwa utukufu wa Mungu.21Sasa ni Mungu ambaye hututhibitisha sisi pamoja nanyi katika Kristo, na alitutuma sisi.22Aliweka muhuri juu yetu na alitupa Roho katika mioyo yetu kama dhamana ya kile ambacho angetupatia baadaye.

23Zaidi ya hayo namwita Mungu kuwa shahidi juu ya nafsi yangu ya kuwa ni kwa ajili ya kuwahurumia sikuja tena Korintho.24Hii sio kwamba twaitawala imani yenu, bali twafanya kazi pamoja nanyi kwa ajiliya furaha yenu, maana ni kwa imani mnasimama imara.

2

1Kwa hiyo niliamua kwa sehemu yangu mwenyewe kwamba nisingekuja tena kwenu katika hali ya uchungu.2Kama niliwasababishia ninyi maumivu, ni nani angenifurahisha mimi, lakini ni yule ambaye aliumizwa na mimi?3Niliandika kama nilivyofanya ili kwamba wakati nikija kwenu nisiweze kuumizwa na wale ambao wangekuwa wamenifanya nifurahi. Ninao ujasiri kuhusu ninyi nyote kwamba furaha yangu ni furaha ile ile mliyonayo ninyi nyote.4Kwa kuwa niliwaandikia ninyi kutokana na mateso makubwa, na dhiki ya moyo, na kwa machozi mengi. Sikutaka kuwasababishia ninyi maumivu. Badala yake, nilitaka mjue upendo wa kina nilionao kwa ajili yenu.

5Kama kuna yeyote amesababisha maumivu, hajasababisha tu kwangu, lakini kwa kiwango fulani - bila kuweka ukali zaidi - kwenu ninyi nyote.6Hii adhabu ya mtu huyo kwa wengi inatosha.7Kwa hiyo sasa badala ya adhabu, mnapaswa kumsamehe na kumfariji. Fanyeni hivi ili kwamba asiweze kushindwa na huzuni iliyozidi.

8Kwa hiyo ninawatia moyo kuthibitisha upendo wenu hadharani kwa ajili yake.9Hii ndiyo sababu niliandika, ili kwamba niweze kuwajaribu na kujua kuwa kama ni watii katika kila kitu.10Kama mkimsamehe yeyote, na mimi pia namsamehe mtu huyo. Kile nilicho kisamehe - kama nimesamehe chochote-kimesamehewa kwa faida yenu katika uwepo wa Kristo.11Hii ni kwamba Shetani asije akatufanyia madanganyo. Kwa kuwa sisi sio wajinga kwa mipango yake.

12Mlango ulifunguliwa kwangu na Bwana nilipokuja kwenye mji wa Troa kuhubiri injili ya Kristo pale.13Hata hivyo, sikuwa na amani ya moyo, kwa sababu sikumkuta ndugu yangu Tito pale. Hivyo niliwaacha na nikarudi Makedonia.14Lakini ashukuriwe Mungu, ambaye katika Kristo mara zote hutuongoza sisi katika ushindi. Kupitia sisi husambaza harufu nzuri ya maarifa yake mahala pote.15Kwa kuwa sisi kwa Mungu, ni harufu nzuri ya Kristo, wote kati ya wale waliookolewa na kati ya wale wanaoangamia.16Kwa watu ambao wanaangamia, ni harufu kutoka kifo hadi kifo. Kwa wale wanaookolewa, ni harufu nzuri kutoka uzima hadi uzima. Ni nani anayestahili vitu hivi?17Kwa maana sisi si kama watu wengi wanaouza neno la Mungu kwa faida. Badala yake, kwa usafi wa nia, tunanena katika Kristo kama tumetumwa na Mungu, mbele ya Mungu.

3

1Je, tumeanza kujisifia wenyewe tena? Hatuhitaji barua ya mapendekezo kwenu au kutoka kwenu, kama baadhi ya watu, je twahitaji?2Ninyi wenyewe ni barua yetu ya mapendekezo, iliyoandikwa kwenye mioyo yetu, inayojulikana na kusomwa na watu wote.3Na mnaonesha kwamba ninyi ni barua kutoka kwa Kristo, iliyotolewa na sisi. Iliandikwa siyo kwa wino bali kwa Roho wa Mungu aliye hai. Haikuandikwa juu ya vibao vya mawe, bali juu ya vibao vya mioyo ya wanadamu.

4Na huu ndiyo ujasiri tulio nao katika Mungu kupitia Kristo.5Hatujiamini wenyewe kwa kudai chochote kama kutoka kwetu. Badala yake, kujiamini kwetu kunatoka kwa Mungu.6Ni Mungu ambaye alitufanya tuweze kuwa watumishi wa agano jipya. Hili ni agano sio la barua bali ni la Roho. Kwa kuwa barua huua, lakini roho inatoa uhai.

7Sasa kazi ya kifo iliyokuwa imechongwa katika herufi juu ya mawe ilikuja kwa namna ya utukufu kwamba watu wa Israeli hawakuangalia moja kwa moja kwenye uso wa Musa. Hii ni kwa sababu ya utukufu wa uso wake, utukufu ambao ulikuwa unafifia.8Je, kazi ya Roho haitakuwa na utukufu zaidi?9Kwa kuwa kama huduma ya hukumu ilikuwa na utukufu, ni mara ngapi zaidi huduma ya haki huzidi sana katika utukufu!10Ni kweli kwamba, kile kilichofanywa utukufu kwanza hakina utukufu tena katika heshima hii, kwa sababu ya utukufu unaouzidi.11Kwa kuwa kama kile ambacho kilikuwa kinapita kilikuwa na utukufu, ni kwa kiasi gani zaidi kile ambacho ni cha kudumu kitakuwa na utukufu!

12Kwa kuwa tunajiamini hiyo, tunaujasiri sana.13Hatuko kama Musa, aliyeweka utaji juu ya uso wake, ili kwamba watu wa Israel wasiweze kuangalia moja kwa moja kwenye mwisho wa utukufu ambao ulikuwa unatoweka.14Lakini fahamu zao zilikuwa zimefungwa. Hata mpaka siku hii utaji uleule bado unabaki juu ya usomaji wa agano la kale. Haijawekwa wazi, kwa sababu ni katika Kristo pekee inaondolewa mbali.15Lakini hata leo, wakati wowote Musa asomwapo, utaji hukaa juu ya mioyo yao.16Lakini mtu anapogeuka kwa Bwana, utaji unaondolewa.17Sasa Bwana ni Roho. Palipo na Roho wa Bwana, kuna uhuru.18Sasa sisi sote, pamoja na nyuso zisizo wekewa utaji, huona utukufu wa Bwana. Tunabadilishwa ndani ya muonekano uleule wa utukufu kutoka shahada moja ya utukufu kwenda nyingine, kama ilivyo kutoka kwa Bwana, ambaye ni Roho.

4

1Kwa hiyo, kwa sababu tuna huduma hii, na kama ambavyo tumeipokea rehema, hatukati tamaa.2Badala yake, tumekataa njia zote za aibu na zilizofichika. Hatuishi kwa hila, na hatulitumii vibaya neno la Mungu. Kwa kuwasilisha iliyo kweli, tunajionyesha wenyewe kwa dhamiri ya kila mtu mbele ya Mungu.3Lakini kama injili yetu imefichika, imefichika kwa wale tu wanaoangamia.4Katika uchaguzi wao, mungu wa ulimwengu huu amewapofusha fahamu zao zisizoamini. Matokeo yake, hawawezi kuona nuru ya injili ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano wa Mungu.5Kwa kuwa hatujitangazi wenyewe, bali Kristo Yesu kama Bwana, na sisi wenyewe kama watumishi wenu kwa ajili ya Yesu.6Kwa kuwa Mungu ndiye ambaye aliyesema, “Mwanga utaangaza toka gizani.” Ameangaza katika mioyo yetu, kutoa mwanga wa maarifa ya utukufu wa Mungu katika uwepo wa Yesu Kristo.

7Lakini tuna hazina hii katika vyombo vya udongo, ili kwamba ieleweke kuwa nguvu kuu sana ni ya Mungu na sio yetu.8Tunataabika katika kila hali, lakini hatusongwi. Twaona shaka lakini hatujawi na kukata tamaa.9Tunateswa lakini hatujatelekezwa. Twatupwa chini lakini hatuangamizwi.10Siku zote tunabeba katika mwili wetu kifo cha Yesu, ili kwamba uzima wa Yesu uonekane pia katika miili yetu.11Sisi tulio hai siku zote tumetolewa kufa kwa ajili ya Yesu, ili kwamba uhai wa Yesu uonekane katika miili yetu ya kibinadamu.12Kwa sababu hii, kifo kinafanya kazi ndani yetu, bali uzima unafanya kazi ndani yenu.

13Lakini tuna roho ileile ya imani kulingana na kile kilicho andikwa: “Niliamini, na hivyo nilinena.” Sisi pia tunaamini, na hivyo pia tunanena.14Tunajua kuwa yule aliye mfufua Bwana Yesu pia atatufufua sisi pamoja naye. Tunajua kuwa atatuleta sisi pamoja nanyi katika uwepo wake.15Kila kitu ni kwa ajili yenu ili kwamba, kwa kadri neema inavyo enea kwa watu wengi, shukurani zizidi kuongezeka kwa utukufu wa Mungu.

16Hivyo hatukati tamaa. Japokuwa kwa nje tunachakaa, kwa ndani tunafanywa upya siku hadi siku.17Kwa kipindi hiki kifupi, mateso haya mepesi yanatuandaa sisi kwa ajili ya umilele mzito wa utukufu uzidio vipimo vyote.18Kwa kuwa hatutazami kwa ajili ya vitu ambavyo vinaonekana, bali kwa ajili ya vitu visivyoonekana. Vitu tunavyoweza kuviona ni vya muda tu, bali vitu ambayo havionekani ni vya milele.

5

1Tunajua kwamba kama maskani ya ulimwenguni ambayo tunaishi humo yanaharibiwa, tunalo jengo kutoka kwa Mungu. Ni nyumba isiyotengenezwa kwa mikono ya wanadamu, bali ni nyumba ya milele, katika mbingu.2Kwa kuwa katika hema hii tunaugua, tukitamani kuvikwa kwa maskani yetu mbinguni.3Tunatamani kwa ajili ya hii kwa sababu kwa kuivaa hatutaonekana kuwa tu uchi.

4Kwa hakika wakati tuko ndani ya hema hii, twaugua tukilemewa. Hatutaki kuvuliwa. Badala yake, tunataka kuvalishwa, ili kwamba kile kilicho kufa kiweze kumezwa na uzima.5Yule aliyetuandaa sisi kwa kitu hiki ni Mungu, ambaye alitupa sisi Roho kama ahadi ya kile kitakacho kuja.

6Kwa hiyo muwe na ujasiri siku zote. Muwe macho kwamba wakati tuko nyumbani katika mwili, tuko mbali na Bwana.7Kwa kuwa tunatembea kwa imani, sio kwa kuona. Kwa hiyo tunaujasiri.8Ni bora tuwe mbali kutoka kwenye mwili na nyumbani pamoja na Bwana.9Kwa hiyo tunaifanya kuwa lengo letu, kama tukiwa nyumbani au mbali, tumpendeze yeye.10Kwa kuwa lazima wote tuonekane mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kwamba kila mmoja aweze kupokea kile kinachostahili kwa mambo yaliyofanyika katika mwili, ikiwa ni kwa uzuri au kwa ubaya.

11Kwa hiyo, kwa kuijua hofu ya Bwana, tunawashawishi watu. Jinsi tulivyo, inaonekana wazi na Mungu. Ninatumaini kuwa inaeleweka pia kwenye dhamiri zenu.12Hatujaribu kuwashawishi ninyi tena kutuona sisi kama wakweli. Badala yake, tunawapa ninyi sababu ya kujivuna kwa ajili yetu, ili kwamba muweze kuwa na jibu kwa wale wanaojivunia kuhusu mwonekano lakini sio kile kilicho ndani ya moyo.13Kwa kuwa ikiwa kama tumerukwa na akili, ni kwa ajili ya Mungu. Na kama tuko kwenye akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu.14Kwa kuwa upendo wa Kristo watushurutisha, kwa sababu tuna uhakika na hili: kuwa mtu mmoja alikufa kwa ajili ya wote, na kwa hiyo wote wamekufa.15Na Kristo alikufa kwa ajili ya wote, ili kwamba wale wanaoishi wasiishi tena kwa ajili yao wenyewe. Badala yake, lazima waishi kwa ajili yake yeye ambaye alikufa na alifufuliwa.

16Kwa sababu hii, kuanzia sasa na kuendelea hatumuhukumu mtu kulingana na viwango vya wanadamu, ingawa hapo kwanza tulimtazama Kristo katika namna hii. Lakini sasa hatumuhukumu yeyote kwa namna hii tena.17Kwa hiyo, ikiwa mtu yeyote yuko ndani ya Kristo, yeye ni kiumbe kipya. Mambo ya kale yamepita. Tazama, yamekuwa mapya.18Vitu vyote hivi vyatoka kwa Mungu. Alitupatanisha sisi kwake mwenyewe kupitia Kristo, na ametupatia huduma ya upatanisho.19Hiyo ni kusema, katika Kristo, Mungu anaupatanisha ulimwengu kwake mwenyewe, sio kuhesabu makosa yao dhidi yao. Anawekeza kwetu ujumbe wa upatanisho.20Kwa hiyo tunateuliwa kama wawakilishi wa Kristo, kana kwamba Mungu alikuwa anafanya rufaa yake kupitia sisi. Tunawasihi ninyi kwa ajili ya Kristo: “Mpatanishwe kwa Mungu!”21Alimfanya Kristo kuwa sadaka kwa ajili ya dhambi zetu. Yeye ndiye ambaye hakutenda dhambi. Alifanya hivi ili tuweze kufanyika haki ya Mungu katika yeye.

6

1Na kwa hiyo, kufanya kazi pamoja, tunawasihi ninyi msiipokee neema ya Mungu bure.2Kwa kuwa anasema, “Wakati uliokubalika nilikuwa makini kwenu, na siku ya wokovu niliwasaidia.” Tazama, wakati uliokubalika ndio sasa, siku ya wokovu ndio sasa.

3Hatuwezi kuwa kizuizi mbele ya mtu yeyote, kwa kuwa hatuitaki huduma yetu ijulikane katika sifa mbaya.4Badala yake kwa kila njia twanjisifu wenyewe kuwa watumishi wa Mungu katika wingi wa ustahimilivu, katika mateso, katika dhiki, na katika ugumu wa maisha,5katika kupigwa, vifungo, ghasia, katika kazi ngumu, katika kukosa usingizi usiku, katika njaa,6katika usafi, maarifa, uvumilivu, wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo halisi,7katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu. Tuna silaha ya haki kwa ajili ya mkono wa kulia na wa kushoto.8Tunafanya kazi katika utukufu na aibu, katika kashfa na sifa, kama wadanganyifu na bado wakweli.9Tunafanya kazi kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Tunafanya kazi kama wanaokufa, na tazama! - Bado tunaishi, kana kwamba tunaadhibiwa kwa matendo yetu, lakini hatujauakwa.10Tunafanya kazi kama wenye masikitiko, lakini kila wakatituna furaha, kama maskini, lakini tunatajirisha wengi, kana kwamba hatuna kitu lakini tunamiliki vitu vyote.

11Tumezungumza ukweli wote kwenu, Wakorintho, na mioyo yetu imefunguka kwa upana.12Hamkuzuiliwal nasi, bali mnazuiliwa na mioyo yenu wenyewe.13Sasa katika kubadilishana kwa haki - ninaongea kama kwa watoto - jifungueni kwa upana pia.

14Msifungwe nira pamoja na wasioamini. Kwa kuwa kuna muungano gani kati ya haki na uasi? Na kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?15Ni makubaliano gani Kristo anaweza kuwa nayo na Beliali? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na asiyeamini?16Na kuna makubaliano gani yapo kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi ni hekalu la Mungu aliye hai, kama ambavyo Mungu alisema: “Nitakaa kati yao na kutembea kati yao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”

17Kwa hiyo, “Tokeni kati yao, na mkatengwe nao,” asema Bwana. “Msiguse kitu kichafu, na nitawakaribisha ninyi.18Nitakuwa Baba kwenu, nanyi mtakuwa wanangu wa kiume na wa kike,” asema Bwana Mwenyezi.

7

1Wapendwa, kwa kuwa tuna ahadi hizi, na tujitakase wenyewe kwa kila jambo ambalo linatufanya kuwa wachafu katika miili yetu na katika roho. Tuwe na utakatifu kamili katika kumcha Mungu.

2Fanyeni nafasi kwa ajili yetu! Hatujamkosea mtu yeyote. Hatukumdhuru mtu yeyote. Hatujajinufaisha kwa faida ya mtu yeyote.3Sio kuwahukumu kwamba nasema hivi. Kwa kuwa nimeshasema kwamba mmo mioyoni mwetu, kwetu sisi kufa pamoja na kuishi pamoja.4Nina imani kubwa ndani yenu, na fahari yangu ni kubwa juu yenu. Nimejawa na faraja. Nimefurika na furaha hata katikak dhiki zetu zote.

5Tulipokuja Makedonia, miili yetu haikupumzika. Badala yake, tulipata taabu kwa namna zote kwa kupigwa vita upande wa nje na hofu upande wa ndani.6Lakini Mungu, anayefariji wanyonge, alitufariji kwa kuwasili Tito.7Haikuwa kwa kuwasili kwake tu kwamba Mungu alitufariji. Ilikuwa pia faraja zile Tito alizopokea kutoka kwenu. Yeye alituambia upendo mkuu mlionao, huzuni yenu, na bidii yenu kwa ajili yangu. Hivyo nilifurahi zaidi.

8Hata ingawa waraka wangu uliwafanya kusikitika, mimi siujutii. Lakini nilijutia wakati nilipoona waraka huo uliwafanya ninyi kuwa na huzuni hata kama kwa muda mfupi.9Sasa nina furaha, si kwa sababu mlikuwa na huzuni, lakini kwa sababu huzuni yenu iliwaleta kwenye toba. Mlipatwa na huzuni ya kiungu, hamkupata hasara kwa sababu yetu.10Kwa kuwa huzuni ya kiungu huleta toba ambayo hukamilisha wokovu bila ya kuwa na majuto. Huzuni ya kidunia, hata hivyo, huleta mauti.11Tazama jinsi huzuni hii ya kiungu ilivyozaa bidii kubwa ndani yenu. Jinsi ulivyokuwa dhamira kubwa ndani yenu ya kuwazuia kuwa hamkuwa na hatia. Kwa jinsi gani uchungu wenu ulivyokuwa mkubwa, hofu yenu, matamanio yenu, bidii yenu, na shauku yenu kuona kwamba haki inapaswa kutendeka! Katika kila jambo mmethibitisha wenyewe kutokuwa na hatia.12Ingawa niliwaandikia ninyi, sikuandika kwa ajili ya mkosaji, wala si kwa mtu aliyeteswa na maovu. Nimeandika ili kwamba udhati wa mioyo yenu kwa ajili yetu ifanywe kujulikana kwenu mbele ya macho ya Mungu.13Ni kwa ajili ya hii kwamba tunafarijika. Katika nyongeza ya faraja yetu wenyewe, tunafurahi pia, hata zaidi kwa sababu ya furaha ya Tito, kwa kuwa roho yake iliburudishwa na ninyi nyote.14Kwa kuwa kama nilijivuna kwake kuhusiana na ninyi, sikuwa na aibu. Kinyume chake, kama tu kila neno tulilolisema kwenu lilikuwa kweli, majivuno yetu kuhusu ninyi kwa Tito yalithibitisha kuwa kweli.15Upendo wake kwa ajili yenu hata ni mkubwa zaidi, kama akumbukapo utii wenu nyote, jinsi mlivyomkaribisha yeye kwa hofu na kutetemeka.16Ninafurahi kwa sababu nina ujasiri kamili ndani yenu.

8

1Tunawataka ninyi mjue, kaka na dada, kuhusu neema ya Mungu ambayo imetolewa kwa makanisa ya Makedonia.2Wakati wa jaribu kubwa la mateso, wingi wa furaha yao na ongezeko la umaskini wao umezaa utajiri mkubwa wa ukarimu.3Kwa maana nashuhudia kwamba walitoa kwa kadiri ya walivyoweza, na hata zaidi ya uwezo wao.4Na kwa hiari yao wenyewe walitusihi kwa bidii nyingi ili tupatependeleo la kushiriki katika utumishi huu kwa watu watakatifu wa mungu.5Hii haikutokea kama tulivyokuwa tunatarajia. Badala yake, kwanza walijitoa wao wenyewe kwa Bwana, kisha wakajitoa wao wenyewe kwetu kwa mapenzi ya Mungu.6Hivyo tulimsihi Tito, aliyekuwa tayari ameanzisha kazi hii, ili kukamilisha kati yenu hili tendo la neema.7Lakini ninyi mna wingi katika kila kitu- katika imani, katika usemi, katika maarifa, katika bidii yote, na katika upendo wenu kwa ajili yetu. Hivyo hakikisheni kwamba ninyi mnakuwa na wingi pia katika hili tendo la neema.

8Nasema hili si kama amri, lakini ili kupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine.9Kwa maana mnajua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu akawa maskini ili kwamba kupitia umaskini wake muweze kuwa matajiri.10Katika jambo hili nitawapa ushauri ambao utawasaidia. Mwaka mmoja uliopita, hamkuanza tuu kufanya jambo, lakini mlitamani kulifanya.11Sasa likamilisheni. Kama tu kulivyokuwa na shauku na nia ya kulifanya, kisha, je, mngeweza pia kulileta katika ukamilifu, kwa kadri ya mnavyoweza.12Kwa maana mkitamani kufanya tendo hili, ni jambo zuri na linakubalika. Lazima lisimame juu ya kile alichonacho mtu, siyo juu ya asichokuwa nacho mtu.13Kwa maana hiii si kuleta kitulizo kwa wengine na dhiki kwenu, bali kwa ajili ya haki.14Wingi wenu wa wakati wa sasa utasaidia kwa kile wanachohitaji. Hii ni hivyo pia ili kwamba wingi wao uweze kusaidia mahitaji yenu, na kwamba kuwe na haki.15Hii ni kama ilivyoandikwa; “Yeye aliye na vingi hakuwa na kitu chochote kilichobaki na yeye aliyekuwa na kidogo hakuwa na uhitaji wowote.”

16Lakini ashukuriwe Mungu, aliyeweka ndani ya moyo wa Tito moyo uleule wa bidii ya kujali ambyo ninayo kwa ajili yenu.17Kwa kuwa si tu alipokea maombi yetu, bali pia alikuwa na bidii kuhusiana na maombi hayo. Alikuja kwenu kwa hiari yake mwenyewe.18Tumemtuma pamoja naye ndugu ambaye anasifiwa miongoni mwa makanisa kwa ajili ya kazi yake katika kutangaza injili.19Si hivi tu, lakini pia alichaguliwa na makanisa kusafiri nasisi katika kulibeba sehemu mbalimbali tendo hili la ukarimu. Hii ni kwa utukufu wa Bwana mwenyewe na kwa shauku yetu ya kusaidia.

20Tunaepuka uwezekano kwamba yeyote napaswa kulalamika kuhusiana na sisi kuhusiana na ukarimu huu ambao tunaubeba.21Tunachukua uangalifu kufanya kilicho cha heshima, sio tu mbele za Bwana, lakini pia mbele za watu.22Pia tunamtuma ndugu mwingine pamoja nao. Tumempima mara nyingi, na tumemwona ni mwenye shauku for ajili ya kazi nyingi. Hata sasa ana bidii zaidi kwa sababu ya ujasiri mkubwa alionao ndani yenu.23Kwa habari ya Tito, yeye ni mshirika mwenza wangu na mtendakazi mwenzangu kwa ajili yenu. Kama kwa ndugu zetu, wanatumwa na makanisa. Ni waheshima kwa Kristo.24Hivyo, waonesheni upendo wenu, na muoneshe kwa makanisa sababu ya majivuno yetu kwa ajili yenu.

9

1Kuhusiana na huduma kwa ajili ya waumini, ni bora zaidi kwangu kuwaandikia.2Ninajua kuhusu shauku yenu, ambayo nilijivunia kwa watu wa Makedonia. Niliwaambia kwamba Akaya imekuwa tayari tangu mwaka uliopita. Hamu yenu imewatia moyo wengi wao kutenda.3Sasa, nimewatuma ndugu ili kwamba majivuno yetu kuhusu ninyi yasiwe ya bure, na ili kwamba mngekuwa tayari, kama nilivyosema mngekuwa.4Vinginevyo, kama mtu yeyote wa Makedonia akija pamoja nami na kuwakuta hamjawa tayari, tungeona haya --- sisemi chochote kuhusu ninyi--kwa kuwa jasiri sana katika ninyi.5Hivyo niliona ilikuwa muhimu kuwasihi ndugu kuja kwenu na kufanya mipango mapema kwa ajili ya zawadi mlizoahidi. Hii ni hivyo ili kwamba ziwe tayari kama baraka, na si kama kitu kilichoamriwa.

6Wazo ni hili: mtu apandaye haba pia atavuna haba, na yeyote apandaye kwa lengo la baraka pia atavuna baraka.7Basi na kila mmoja atoe kama alivyopanga moyoni mwake. Basi naye asitoe kwa huzuni au kwa kulazimishwa. Kwa kuwa Mungu humpenda yule atoaye kwa furaha.8Na Mungu anaweza kuizidishia kila baraka kwa ajili yenu, ili kwamba, kila wakati, katika mambo yote, muweze kupata yote mnayohitaji. Hii itakuwa ili kwamba mueze kuzidisha kila tendo jema.9Ni kama ilivyoandikwa: “Ametapanya utajiri wake na kuutoa kwa maskini. Haki yake yadumu milele.”

10Naye atoaye mbegu kwa mpanzi na mkate kwa ajili ya chakula, pia atatoa na kuzidisha mbegu yenu kwa ajili ya kupanda. Yeye ataongeza mavuno ya haki yenu.11Mtatajirishwa kwa kila namna ili kwamba muweze kuwa wakarimu. Hii italeta shukrani kwa Mungu kupitia sisi.

12Kwa kufanya huduma hii sio tu inagusa mahitaji ya waumini. Pia huzidisha katika matendo mengi ya shukrani kwa Mungu.13Kwa sababu ya kupimwa kwenu na kuthibitishwa kwa huduma hii, pia mtamtukuza Mungu kwa utii kwa ukiri wenu wa injili ya Kristo. Pia mtamtukuza Mungu kwa ukarimu wa karama yenu kwao na kwa kila mmoja.14Wanawatamani, na wanaomba kwa ajili yenu. Wanafanya hivi kwa sababu ya neema kubwa ya Mungu iliyo juu yenu.15Shukrani ziwe kwa Mungu kwa karama yake isiyoelezeka!

10

1Mimi Paulo, mwenyewe nawasihi kwa unyenyekevu na upole wa Kristo. Mimi ni mpole wakati nikiwa mbele yenu, Lakini ninaujasiri kwenu wakati nikiwa mbali nanyi.2Nawaomba ninyi kwamba, wakati nikiwepo pamoja nanyi, sitahitaji kuwa jasiri na kujiamini kwangu mwenyewe. Lakini nafikiri nitahitaji kuwa jasiri wakati nikiwapinga wale wanaodhani kwamba tunaishi kwa jinsi ya mwili.3Kwa kuwa hata kama tunatembea katika mwili, hatupigani vita kwa jinsi ya mwili.4Kwa kuwa silaha tunazotumia kupigana si za kimwili. Badala yake, zina nguvu ya kiungu ya kuharibu ngome. Zinaondosha kabisa mijadara inayopotosha.5Pia, tunaharibu kila chenye mamlaka kijiinuacho dhidi ya maarifa ya Mungu. Tunalifanya mateka kila wazo katika utii kwa Kristo.6Na tunapata utayari wa kuadhibu kila matendo lisilo na utii, mara tu utii wenu unapokuwa kamili.

7Tazama kile kilichowazi mbele yenu. Kama yeyote anashawishika kwamba yeye ni wa Kristo, na hebu ajikumbushe yeye mwenyewe kwamba kama tu alivyo ni wa Kristo, hivyo ndiyo na sisi pia tuko hivyo.8Kwa kuwa hata nikijivuna kidogo zaidi kuhusu mamlaka yetu, ambayo Bwana aliyatoa kwa ajili yetu kuwajenga ninyi na siyo kuwaharibu, sitaona haya.9Sihitaji hili lionekane kwamba nawatisha ninyi kwa nyaraka zangu.10Kwa vile baadhi ya watu husema, “Nyaraka zake ni kali na zina nguvu, lakini kimwili yeye ni dhaifu. Maneno yake hayastahili kusikilizwa.”11Hebu watu wa jinsi hiyo waelewe kwamba kile tusemacho kwa waraka wakati tukiwa mbali, ni sawasawa na vile tutakavyotenda wakati tukiwa pale.

12Hatuendi mbali mno kama kujikusanya wenyewe au kujilinganisha wenyewe na wale ambao hujisifia wenyewe. Lakini wanapojipima wenyewe na kila mmoja wao, hawana akili.13Sisi, hata hivyo, hatutajivuna kupita mipaka. Badala yake, tutafanya hivyo tu ndani ya mipaka ambayo Mungu ametupimia sisi, mipaka inayofika umbali kama wenu ulivyo.14Kwa kuwa hatukujizidishia wenyewe tulipowafikia ninyi. Tulikuwa wa kwanza kufika kwa umbali kama wenu kwa injili ya Kristo.

15Hatujajivuna kupita mipaka kuhusu kazi za wengine. Badala yake, tunatumaini kama imani yenu ikuwavyo kwamba eneo letu la kazi litapanuliwa sana, na bado ni ndani ya mipaka sahihi.16Tunatumaini kwa hili, ili kwamba tuweze kuhubiri injili hata kwenye mikoa zaidi yenu. Hatutajivuna kuhusu kazi inayofanywa katika maeneo mengine.17“Lakini yeyote ajivunaye, ajivune katika Bwana.”

18Kwa maana siyo yule ajithibitishaye mwenyewe anathibitishwa. Isipokuwa, ni yule ambaye Bwana humthibitisha.

11

1Nahisi kwamba mngevumiliana na mimi katika baadhi ya upumbavu. Lakini kwa kweli mnavumiliana na mimi.2Kwa kuwa ni mwenye wivu kuhusu ninyi. Nina wivu wa Mungu kwa ajili yenu, tangu nilipowaahidi ninyi kwenye ndoa ya mume mmoja. Niliahidi kuwaleta ninyi kwa Kristo kama bikra safi.3Lakini ninaogopa kwamba kwa namna fulani, kama nyoka alivyomdanganya Eva kwa hila yake, mawazo yenu yanaweza kupotoshwa mbali kutoka kwenye ibada halisi na safi kwa Kristo.4Kwa kuwa kwa mfano kwamba mtu fulani akaja na kutangaza Yesu mwingine tofauti na yule tuliyewahubiri. Au kwa mfano kwamba mkapokea roho mwingine tofauti na yule mliyempokea. Au kwa mfano kwamba mkapokea injili nyingine tofauti na ile mliyoipokea. Mkavumilia mambo haya vema inatosha!5Kwa kuwa nadhani kwamba mimi si miongoni mwa walio duni kwa hao wanaoitwa mitume-bora.6Lakini hata kama mimi sijafundishwa katika kutoa hotuba, siko hivyo katika maarifa. Kwa kila namna na katika mambo yote tumelifanya hili kujulikana kwenu.

7Je, nilifanya dhambi kwa kujinyenyekeza mwenyewe ili ninyi muweze kuinuliwa? Kwa kuwa nilihubiri kwa uhuru injili ya Mungu kwenu.8Nilinyang'anya makanisa mengine kwa kupokea msaada kutoka kwao ili kwamba ningeweza kuwahudumia ninyi.9Wakati nilipokuwa nanyi na nilikuwa katika uhitaji, sikumlemea yeyote. Kwa kuwa mahitaji yangu yalitoshelezwa na ndugu waliokuja kutoka Makedonia. Katika kila kitu nimejizuia mwenyewe kutokuwa mzigo kwenu, na nitaendelea kufanya hivyo.10Kama kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, huku kujisifu kwangu, hakutanyamazishwa katika sehemu za Akaya.11Kwa nini? Kwa sababu siwapendi? Mungu anajua nawapenda.

12Lakini kile ninachokifanya, nitakifanya pia. Nitakifanya ili kwamba niweze kuzuia nafasi ya wale wanaotamani nafasi ya kuwa kama tulivyo katika kile kile wanachojivunia.13Kwa kuwa watu wale ni mitume wa uongo na watendakazi wadanganyifu. Wanajigeuza wenyewe kama mitume wa Kristo.14Na hii haishangazi, kwa kuwa hata Shetani hujigeuza mwenyewe kama malaika wa nuru.15Hii haina mshangao mkubwa kama watumishi wake pia kujigeuza wenyewe kama watumishi wa haki. Hatma yao itakuwa kama matendo yao yastahilivyo.

16Nasema tena: Basi na asiwepo mtu yeyote anayefikiri mimi ni mpumbavu. Lakini kama mkifanya, nipokeeni mimi kama mpumbavu ili niweze kujisifu kidogo.17Kile ninachosema kuhusu huku kujiamini kwa kujivuna hakuhukumiwi na Bwana, lakini nazungumza kama mpumbavu.18Kwa vile watu wengi hujivuna kwa jinsi ya mwili, nitajivuna pia.19Kwa kuwa mlichukuliana kwa furaha na wapumbavu, ninyi wenyewe mna busara!20Kwa kuwa mnachukuliana na mtu kama akikutia utumwani, kama husababisha mgawanyiko kati yenu, kama akiwatumia ninyi kwa faida yake, kama akijiweka juu hewani, au kama akiwapiga usoni.21Nitasema kwa aibu yetu kwamba sisi tulikua dhaifu sana kufanya hivyo. Lakini kama kuna mtu anaujasiri-- nazungumza kama mpumbavu-- mimi pia nitakuwa jasiri22Je, wao ni Wayahudi? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni Waisraeli? Na mimi ni hivyo. Je, wao ni uzao wa Abrahamu? Na mimi ni hivyo.23Je, wao ni watumishi wa Kristo? (Nanena kama nilirukwa na akili zangu.) Mimi ni zaidi: katika kazi ngumu, katika vifungo zaidi, katika kupigwa kupita kiasi, katika kukabili hatari nyingi za kifo.24Kutoka kwa Wayahudi nimepokea mara tano “mapigo arobaini kutoa moja.”25Mara tatu nilipigwa kwa fimbo. Mara moja nilipigwa mawe. Mara tatu nilinusurika melini. Nimetumia usiku na mchana katika bahari wazi.26Nimekuwa katika safari za mara kwa mara, katika hatari za mito, katika hatari za majambazi, katika hatari kutoka kwa watu wangu mwenyewe, katika hatari kutoka kwa watu wa mataifa, katika hatari ya mji, katika hatari ya jangwa, katika hatari ya bahari, katika hatari kutoka kwa ndugu waongo.27Nimekuwa katika kazi ngumu na katika maisha magumu, katika usiku mwingi wa kutolala, katika njaa na kiu, mara nyingi katika kufunga, katika baridi na uchi.28Mbali na kila kitu kingine, kuna msukumo wa kila siku juu yangu wa wasiwasi wangu kwa ajili ya makanisa.29Nani ni dhaifu, na mimi siyo dhaifu? Nani amesababisha mwingine kuanguka dhambini, na mimi siungui ndani?

30Kama ni lazima nijivune, nitajivunia kuhusu kile kinachoonyesha udhaifu wangu.31Mungu na Baba wa Bwana Yesu, yeye ambaye anatukuzwa milele, anajua kwamba mimi sidanganyi.

32Kule Dameski, mkuu wa mkoa chini ya mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Dameski ili kunikamata.33Lakini niliwekwa kikapuni, kupitia dirishani katika ukuta, na nikanusurika kutoka mikononi mwake.

12

1Ni lazima nijivune, lakini hakuna kinachoongezwa na hilo. Bali nitaendelea kwenye maono na mafunuo kutoka kwa Bwana.2Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita ambaye- ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua- alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu.3Na ninajua kwamba mtu huyu---ikiwa katika mwili, ama njenymwili, mimi sinjui, Mungu anajua- jinsi4alichukuliwa juu hadi paradiso na kusikia maneno yasiyoelezeka ambayo watu hawaruhusiwi kuyasema.5Kwa niaba ya mtu kama huyo nitajivuna. Lakini kwa niaba yangu mwenyewe sitajivuna. Isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.6Kama nikitaka kujivuna, nisingekuwa mpumbavu, kwa kuwa ningekuwa ninazungumza ukweli. Lakini sitajivuna, ili kwamba asiwepo yeyote atakayenifikiria zaidi ya hayo kuliko kinachoonekana ndani yangu au kusikika kutoka kwangu.7Ili nisijiinue mimi mwenyewe kwa sababu ya ufunuo upitao ukuu, mwiba uliwekwa ndani ya mwili wangu, mjumbe wa shetani kunishambulia mimi, ili nisiwe na majivuno.8Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili Yeye auondoe kutoka kwangu.9Lakini akaniambia, “Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu.” Hivyo, ningetamani kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu.10Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.

11Mimi nimekuwa mpumbavu! Ninyi mlinilazimisha kwa hili, kwa kuwa ningekuwa nimesifiwa na ninyi. Kwa kuwa sikuwa duni kabisa kwa hao waitwao mitume wakuu, hata kama mimi si kitu.12Ishara za kweli za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu, ishara na maajabu na matendo makuu.13Kwa namna gani mlikuwa wa muhimu wa chini kuliko makanisa yaliyobaki, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kwa kosa hili!

14Tazama! Mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto.15Nitafurahi zaidi kutumia na kutumiwa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama ninawapenda zaidi, natakiwa kupendwa kidogo?

16Lakini kama ilivyo, sikuwalemea ninyi kama mzigo. Lakini kwa kuwa mimi ni mwerevu sana, mimi ni yule aliyewashika ninyi kwa udanganyifu.17Je, nilichukua kwa kujifanyia faida kwa yeyote niliyemtuma kwenu?18Nilimsihi Tito kuja kwenu, na nilituma ndugu mwingine pamoja naye. Je, Tito aliwafanyia faida ninyi? Je, hatukutembea katika njia ile ile? Je, hatukutembea katika nyayo zile zile?

19Mnadhani kwa muda huu wote tumekuwa tukijitetea sisi wenyewe kwenu? Mbele za Mungu, na katika Kristo, tumekuwa tukisema kila kitu kwa ajili ya kuwaimarisha ninyi.20Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza nisiwapate ninyi kama ninavyotamani. Nina hofu kwamba mnaweza msinipate mimi kama mnavyotamani. Nahofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi.21Nina hofu kwamba nitakaporudi tena, Mungu wangu anaweza kuninyenyekeza mbele yenu. Nina hofu kwamba ninaweza kuhuzunishwa na wengi ambao wamefanya dhambi kabla ya sasa, na ambao hawakutubu uchafu, na uasherati na mambo ya tamaa wanayoyatenda.

13

1Hii ni mara ya tatu kwamba nakuja kwenu. “Kila shitaka lazima lijengwe na uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu.2Nimekwishasema kwa hao waliotenda dhambi kabla na kwa wengine wote wakati nilipokuwa huko mara ya pili, na ninasema tena: Nitakapokuja tena, sitawavumilia.3Nawaambia ninyi hili kwa sababu mnatafuta ushahidi kwamba Kristo ananena kupitia mimi. Yeye sio dhaifu kwenu, badala yake, yeye ni mwenye nguvu ndani yenu.4Kwa kuwa alisulibiwa katika udhaifu, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Kwa kuwa sisi pia tu dhaifu ndani yake, lakini tutaishi naye kwa nguvu za Mungu miongoni mwenu.

5Jichunguzeni wenyewe muone kama mko katika imani. Jipimeni wenyewe. Hamgundui kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Yeye yumo, vinginevyo kama hamjathibitishwa.6Na nina ujasiri kwamba ninyi mtagundua kwamba sisi hatukukataliwa.7Sasa tunaomba kwa Mungu kwamba msiweze kufanya chochote kibaya. Siombi kwamba sisi tuweze kuonekana tumeshinda jaribu. Badala yake, ninaomba kwamba muweze kufanya kilicho sahihi, ingawa tunaweza kuonekana kama tumeshindwa jaribu.8Kwa kuwa sisi hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, lakini ni kwa ajili ya kweli tu.9Kwa kuwa tunafurahi wakati tunapokuwa dhaifu nanyi mkiwa na nguvu. Tunaomba pia kwamba muweze kufanywa wakamilifu.10Nayaandika mambo haya wakati nikiwa mbali nanyi, ili kwamba wakati nikiwa pamoja nanyi sihitaji kuwaonesha ukali ninyi katika kutumia mamlaka yangu, ambayo Bwana aliyonipaa mimi niwajenge na siyo kuwaangusha.

11Hatimaye, ndugu, furahini! Fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, fikirieni sawasawa, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.12Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu. Watakatifu wote wa Mungu wanawasalimu.13Waumini wote wanawasalimu14Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja nanyi nyote.

Wagalatia

1

1Mimi ni Paulo mtume. Mimi si mtume kutoka kwa wanadamu wala kupitia kwa mwanadamu, lakini kupitia kwa Yesu Kristo na Mungu Baba aliyemfufua kutoka kwa wafu.2Pamoja na ndugu wote na mimi, ninayaandikia makanisa ya Galatia.3Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo,4aliyejitoa mwenyewe kwa ajili ya dhambi zetu ili kwamba atukomboe na nyakati hizi za uovu, kutokana na mapenzi ya Mungu wetu na Baba.5Kwake uwe utukufu milele na milele. Amina

6Ninashangaa kwamba mnageukia haraka kwenye injili nyingine. Ninashangaa kwamba mnageukia mbali kutoka kwake yeye aliyewaita kwa neema ya Kristo.7Hakuna injili nyingine, lakini kuna baadhi ya watu wanao wasababishia matatizo na kutaka kubadilisha injili ya Kristo.8Lakini hata kama ni sisi au malaika kutoka mbinguni atatangaza kwenu injili tofauti na ile tuliyoitangaza kwenu, na alaaniwe.9Kama tulivyo sema mwanzoni, na sasa nasema tena, “Kama kuna mtu atawatangazia kwenu injili tofauti na mliyoipokea, na alaaniwe.”10Kwani sasa hivi ninatafuta uthibitisho wa watu au Mungu? Ninatafuta kuwafurahisha wanadamu? Kama ninaendelea kujaribu kuwafurahisha wanadamu, mimi sio mtumishi wa Kristo.

11Ndugu, ninataka ninyi mjue kwamba injili niliyoitangaza haitokani na wanadamu.12Sikuipokea kutoka kwa mtu, wala sikufundishwa. Badala yake, ilikuwa ni kwa ufunuo wa Yesu Kristo kwangu.

13Mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya nyuma katika dini ya Kiyahudi, jinsi nilivyokuwa nikilitesa kwa ukali kanisa la Mungu zaidi ya kipimo na kuliteketeza.14Nilikuwa nimeendelea katika Dini ya Kiyahudi zaidi ya ndugu zangu wengi Wayahudi. Nilikuwa na bidii sana katika tamaduni za baba zangu.15Lakini Mungu alipendezwa kunichagua mimi kutoka tumboni mwa mama. Aliniita mimi kupitia neema yake16kumdhihirisha Mwanawe ndani yangu, ili kwamba nimtangaze yeye miongoni mwa watu wa mataifa. Wala sikutafuta ushauri wa mwili na damu17na sikupanda kwenda Yerusalem kwa wale waliokuwa mitume kabla yangu. Badala yake nilienda Uarabuni na baadae kurudi Damesiki.18Kisha baada ya miaka mitatu nilipanda kwenda Yerusalemu kumtembelea Kefa, nikakaa naye kwa siku kumi na tano.19Lakini sikuona mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake na Bwana.20Tazama mbele za Mungu kwamba sidanganyi kile niandikacho kwenu.21Kisha nilikwenda mikoa ya Shamu na Kilikia.22Sikuwa najulikana kwa macho kwa makanisa ya Uyahudi yale yaliyokuwa katika Kristo,23lakini walikuwa wakisikia tu, “Yeye aliyekuwa akitutesa sasa anatangaza imani aliyokuwa akiiharibu.”24Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.

2

1Baada ya miaka kumi na nne nilienda tena Yerusalemu pamoja na Barnaba. Pia nilimchukua Tito pamoja nami.2Nilienda kwa sababu Mungu alijidhihirisha kwangu kwamba nilipaswa kwenda. Niliweka mbele yao Injili ambayo niliitangaza kwa watu wa mataifa. (Lakini niliongea kwa siri kwa waliosemekana kuwa viongozi muhimu). Nilifanya hivi ili kuhakikisha kwamba nilikuwa sikimbii, au nilikimbia bure.3Lakini hata Tito, aliyekuwa pamoja nami, aliyekuwa Myunani, alilazimishwa kutahiriwa.4Jambo hili lilitokea kwa sababu ya ndugu wa uongo waliokuja kwa siri kupeleleza uhuru tuliokuwa nao katika Kristo Yesu. Walitamani kutufanya sisi kuwa watumwa wa sheria.5Hatukujitoa kuwatii hata kwa saa moja, ili kwamba injili ya kweli ibaki bila kubadilika kwenu.6Lakini wale waliosemwa kuwa walikuwa viongozi hawakuchangia chochote kwangu. Chochote walichokuwa wakikifanya hakikuwa na maana kwangu. Mungu hakubali upendeleo wa wanadamu.7Badala yake, waliniona kwamba nimeaminiwa kuitangaza injili kwa wale ambao hawakutahiriwa. Ilikuwa kama Petro atangaze injili kwa waliotahiriwa.8Kwa maana Mungu, aliyefanya kazi ndani ya Petro kwa ajili ya utume kwa wale waliotahiriwa, pia alifanya kazi ndani yangu kwa watu wa mataifa.9Wakati Yakobo, Kefa, na Yohana, waliotambulika kuwa waliojenga Kanisa, walifahamu neema niliyopewa mimi, walitupokea katika ushirika mimi na Barnaba. Walifanya hivi ili kwamba twende kwa watu wa mataifa, na ili kwamba waweze kwenda kwa wale waliotahiriwa.10Pia walitutaka sisi kuwakumbuka masikini. Mimi pia nilikuwa natamani kufanya jambo hili.

11Wakati Kefa alipokuja Antiokia, nilimpinga waziwazi kwa sababu alikuwa amekosea.12Kabla ya watu kadhaa kuja kutoka kwa Yakobo, Kefa alikuwa akila pamoja na watu wa mataifa. Lakini hawa watu walipokuja, aliacha na kuondoka kutoka kwa watu wa mataifa. Alikuwa anaogopa watu ambao walihitaji tohara.13Vilevile Wayahudi wengine waliungana na unafiki huu pamoja na Kefa. Matokeo yake yalikuwa kwamba hata Barnaba alichukuliwa na unafiki wao.14Lakini nilipoona kwamba walikuwa hawafuati injili ya kweli, nilimwambia Kefa mbele yao wote, “Kama ninyi ni Wayahudi lakini mnaishi tabia za watu wa mataifa badala ya tabia za Kiyahudi, kwa nini mnawalazimisha watu wa mataifa kuishi kama Wayahudi?”15Sisi ambao ni Wayahudi kwa kuzaliwa na siyo “Watu wa mataifa wenye dhambi”16fahamu kwamba hakuna anayehesabiwa haki kwa matendo ya sheria. Badala yake, wanahesabiwa haki kwa imani ndani ya Yesu Kristo. Tulikuja kwa imani ndani ya Kristo Yesu ili kwamba tunahesabiwa haki kwa imani ndani ya Kristo na siyo kwa matendo ya sheria. Kwa matendo ya sheria hakuna mwili utakao hesabiwa haki.17Lakini kama tunapomtafuta Mungu kwa kutuhesabia haki ndani ya Kristo, tunajikuta wenyewe pia kuwa wenye dhambi, je Kristo alifanywa mtumwa wa dhambi? Siyo hivyo!

18Maana kama nikijenga tegemeo langu juu ya kutunza sheria, tegemeo ambalo nilikwisha liondoa, najionesha mwenyewe kuwa mvunja sheria.19Kupitia sheria nilikufa kwa sheria, kwa hiyo napaswa kuishi kwa ajili ya Mungu.20Nimesulubiwa pamoja na Kristo. Si mimi tena ninayeishi, bali Kristo anaishi ndani yangu. Maisha ninayoishi katika mwili ninaishi kwa imani ndani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda na akajitoa kwa ajili yangu.21Siikani neema ya Mungu, maana kama haki ilikuwepo kupitia sheria, basi Kristo angekuwa amekufa bure.

3

1Wagalatia wajinga, ni nani aliyewaroga? Je Yesu Kristo hakuoneshwa kama msulubiwa mbele ya macho yenu?2Mimi nataka tu kufahamu hili kutoka kwenu. Je mlimpokea Roho kwa matendo ya sheria au kwa kuamini kile mlichosikia?3Je, ninyi ni wajinga kiasi hiki? Je mlianza katika Roho ili mmalize katika mwili?4Je mliteseka kwa mambo mengi bure, kama kweli yalikuwa ya bure?5Je yeye atoaye Roho kwenu na kutenda matendo ya nguvu kati yenu hufanya kwa matendo ya sheria au kwa kusikia pamoja na imani?

6Abrahamu “Alimwamini Mungu akahesabiwa kuwa mwenye haki.”7Kwa namna ile ile eleweni kwamba, wale ambao wanaamini ni watoto wa Abrahamu.8Andiko lilitabiri kwamba Mungu angewahesabia haki watu wa mataifa kwa njia ya imani. Injili ilihubiriwa kwanza kwa Abrahamu: “katika wewe mataifa yote yatabarikiwa.”9Ili baadaye wale ambao wana imani wabarikiwe pamoja na Abrahamu, ambaye alikuwa na imani.10Wale ambao wanategemea matendo ya sheria wako chini ya laana. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu ambaye hashikamani na mambo yote yaliyoandikwa katika kitabu cha sheria, kuyatenda yote.”11Sasa ni wazi kwamba Mungu hamhesabii haki hata mmoja kwa sheria, kwa kuwa “Mwenye haki ataishi kwa imani.”12Sheria haitokani na imani, lakini badala yake “Ambaye hufanya mambo haya katika sheria, ataishi kwa sheria.”

13Kristo alitukomboa sisi kutoka katika laana ya sheria wakati alipofanyika laana kwa ajili yetu. Kwa kuwa imeandikwa, “Amelaaniwa kila mtu aangikwaye juu ya mti.”14Lengo lilikuwa kwamba, baraka ambazo zilikuwa kwa Abrahamu zingekuja kwa watu wa mataifa katika Kristo Yesu, ili kwamba tuweze kupokea ahadi ya Roho kupitia imani.

15Ndugu, ninazungumza kwa namna ya kibinadamu. Hata wakati ambapo agano la kibinadamu limekwisha kuwekwa imara, hakuna awezaye kupuuza au kuongezea.16Sasa ahadi zilisemwa kwa Abrahamu na kwa kizazi chake. Haisemi, “kwa vizazi,” kumaanisha wengi, bali badala yake kwa mmoja pekee, “kwa kizazi chako,” ambaye ni Kristo.17Sasa nasema hivi, sheria ambayo ilikuja miaka 430 baadaye, haiondoi agano la nyuma lililowekwa na Mungu.18Kwa kuwa kama urithi ungelikuja kwa njia ya sheria, usingekuwa tena umekuja kwa njia ya ahadi. Lakini Mungu aliutoa bure kwa Abrahamu kwa njia ya ahadi.

19Kwa nini sasa sheria ilitolewa? Iliongezwa kwa sababu ya makosa, mpaka mzao wa Abrahamu aje kwa wale ambao kwao alikuwa ameahidiwa. Sheria iliwekwa katika shinikizo kupitia malaika kwa mkono wa mpatanishi.20Sasa mpatanishi humaanisha zaidi ya mtu mmoja, bali Mungu ni mmoja peke yake.

21Kwa hiyo je sheria iko kinyume na ahadi za Mungu? La hasha! Kwa kuwa kama sheria iliyokuwa imetolewa ilikuwa na uwezo wa kuleta uzima, haki ingepatikana kwa sheria.22Lakini badala yake, andiko limefunga mambo yote chini ya dhambi. Mungu alifanya hivi ili kwamba ahadi yake ya kutuokoa sisi kwa imani katika Yesu Kristo iweze kupatikana kwa wale wanao amini.23Lakini kabla ya imani katika Kristo haijaja, tulikuwa tumefungwa na kuwa chini ya sheria hadi uje ufunuo wa imani.24Kwa hiyo sheria ilituongoza hadi Kristo alipokuja, ili kwamba tuhesabiwe haki kwa imani.25Sasa kwa kuwa imani imekuja, hatuko tena chini ya mwangalizi.

26Kwa kuwa ninyi nyote ni watoto wa Mungu kupitia imani katika Kristo Yesu.27Wote ambao mlibatizwa katika Kristo mmejivika Kristo.28Hakuna Myahudi wala Myunani, mtumwa wala huru, mwanaume wala mwanamke, kwa kuwa ninyi nyote ni mmoja katika Kristo Yesu.29Kama ninyi ni wa Kristo, basi ni uzao wa Abrahamu, warithi kwa mujibu wa ahadi.

4

1Ninasema kwamba maadamu mrithi ni mtoto, hana tofauti na mtumwa, hata ingawa ni mmiliki wa mali yote.2Badala yake, yuko chini ya waangalizi na wadhamini mpaka wakati uliowekwa na baba yake.3Kadhalika pia na sisi, tulipokuwa watoto, tulishikiliwa katika utumwa wa kanuni za kwanza za ulimwengu.4Lakini wakati sahihi ulipofika, Mungu alimtuma mwanawe, mzaliwa wa mwanamke, mzaliwa chini ya sheria.5Alifanya hivi ili kuwakomboa wale waliokuwa chini ya sheria, ili kwamba tupokee hali ya kuwa kama wana.6Kwa sababu ninyi ni wana, Mungu alimtuma Roho wa mwanawe ndani ya mioyo yetu, Roho aitaye, “Abba, Baba.”7Kwa sababu hii wewe si mtumwa tena bali mwana. Kama ni mwana, basi wewe pia ni mrithi kupitia Mungu.

8Hata kabla, wakati hamkumjua Mungu, mlikuwa watumwa kwa wale ambao kwa asili si miungu kabisa.9Lakini sasa kwamba mnamjua Mungu, au kwamba mnajulikana na Mungu, kwa nini mnarudi tena kwenye kanuni dhaifu za kwanza na zisizo za thamani? Je mnataka kuwa watumwa tena?10Mnashika kwa uangalifu siku maalumu, miandamo ya miezi, majira, na miaka.11Ninaogopa kwamba kwa namna fulani nimejitaabisha bure.12Ninawasihi, ndugu, muwe kama nilivyo, kwa kuwa pia nimekuwa kama mlivyo. Hamkunikosea.

13Bali mnajua kwamba ilikuwa ni kwa sababu ya ugonjwa wa mwili kwamba nilihubiri injili kwenu kwa mara ya kwanza.14Ingawa hali yangu ya mwili iliwaweka katika jaribu, hamkunidharau au kunikataa. Badala yake mlinipokea kama malaika wa Mungu, kana kwamba nilikuwa Kristo Yesu mwenyewe.15Kwa hiyo, iko wapi sasa furaha yenu? Kwa kuwa ninashuhudia kwenu kwamba, ikiwezekana, mungelin'goa macho yenu na kunipa mimi.16Hivyo sasa, je nimekuwa adui yenu kwa sababu ninawaambia ukweli?17Wanawatafuta kwa shauku, bali si kwa mema. Wanataka kuwatenganisha ninyi na mimi ili muwafuate.18Ni vyema daima kuwa na shauku kwa sababu zilizo njema, na si tu wakati ninapokuwa pamoja nanyi.19Wanangu wadogo, ninaumwa uchungu kwa ajili yenu tena mpaka Kristo aumbike ndani yenu.20Ningependa kuwepo pale pamoja nanyi sasa na kugeuza sauti yangu, kwa sababu ninamashaka juu yenu.

21Niambieni, ninyi ambao mnatamani kuwa chini ya sheria, hamsikii sheria isemavyo?22Kwa kuwa imeandikwa kwamba Abrahamu alikuwa na wana wa kiume wawili, mmoja kwa yule mwanamke mtumwa na mwingine kwa mwanamke huru.23Hata hivyo, yule wa mtumwa alizaliwa kwa mwili tu, bali yule wa mwanamke huru alizaliwa kwa ahadi.24Mambo haya yanaweza kuelezwa kwa kutumia mfano, kwa kuwa wanawake hawa wanafanana na maagano mawili. Mojawapo kutoka katika mlima Sinai. Huzaa watoto ambao ni watumwa. Huyu ni Hajiri.25Sasa Hajiri ni mlima Sinai ulioko Arabuni. Hufananishwa na Yerusalem ya sasa, kwa kuwa ni mtumwa pamoja na watoto wake.26Bali Yerusalemu ambayo iko juu ni huru, na hii ndiyo mama yetu.27Kwa kuwa imeandikwa, “Furahi, wewe mwanamke uliye tasa, wewe usiye zaa. Paza sauti na upige kelele kwa furaha, wewe ambaye huna uzoefu wa kuzaa. Kwa maana wengi ni watoto wa aliye tasa, zaidi ya wale wa yule ambaye ana mume.”

28Sasa ndugu, kama Isaka, ninyi ni watoto wa ahadi.29Kwa wakati ule ambao mtu ambaye alizaliwa kwa mujibu wa mwili alimtesa yule aliyezaliwa kwa mujibu wa Roho. Kwa sasa ni vilevile.30Maandiko husemaje? “Muondoe mwanamke mtumwa pamoja na mwanawe wa kiume. Kwa kuwa mtoto wa mwanamke mtumwa hatarithi pamoja na mtoto wa mwanamke huru.”31Kwa hiyo, ndugu, sisi si watoto wa mwanamke mtumwa, bali ni wa mwanamke huru.

5

1Ni kwa sababu Kristo alitupa uhuru ili tuwe huru. Hivyo, simameni imara wala msinaswe tena katika kongwa la utumwa.2Tazama, Mimi Paulo, ninawaambia kwamba ikiwa mtatahiriwa, Kristo hatawafaidia kwa njia yoyote ile.3Tena, namshuhudia kila mwanaume aliyetahiriwa kwamba anapaswa kuwajibika kwa sheria yote.4Mmetengwa mbali na Kristo, wale wote “mnaohesabiwa haki” kwa sheria. Mmeanguka mbali na neema.5Maana kwa njia ya Roho, kwa imani tunasubiri ujasiri wa haki.6Katika Kristo Yesu kutahiriwa au kutokutahiriwa hakuna maana yoyote. Ni imani pekee inayofanya kazi kupitia upendo ndiyo humaanisha kitu.

7Mlikuwa mnapiga mbio vizuri. Nani aliwazuia kutokuitii kweli?8Ushawishi wa kufanya hivyo hautoki kwake yeye anayewaita ninyi.9Chachu kidogo huathiri donge zima.10Nina matumaini na ninyi katika Bwana kwamba hamtafikiri kwa njia nyingine yoyote. Yeyote yule atakayewapotosha atabeba hukumu yake yeye mwenyewe, yeyote yule.11Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwanini bado ninateswa? Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa.12Ni matakwa yangu kuwa wale wanaowaongoza vibaya watajiharibu wenyewe.

13Mungu amewaiteni ninyi, ndugu, kwenye uhuru. Ila msiutumie uhuru wenu kama fursa kwa mwili. Badala yake kwa upendo mhudumiane ninyi kwa ninyi.14Kwa kuwa sheria yote imekamilika katika amri moja; nayo ni “Ni lazima umpende jirani yako kama wewe mwenyewe.”15Lakini kama mkiumana na kulana, jiangalieni kwamba msijiharibu ninyi kwa ninyi.

16Nasema, tembeeni kwa roho, na wala hamtazitimiza tamaa za mwili.17Kwa kuwa mwili una tamaa kubwa dhidi ya Roho, na Roho ina tamaa kubwa dhidi ya mwili. Hizi zinapingana kila moja na nyingine. Matokeo ni kwamba hamfanyi vitu mnavyotamani kuvifanya.18Lakini kama Roho anawaongoza ninyi, hamko chini ya sheria.

19Sasa matendo ya mwili yanaonekana. Nayo ni uasherati, uchafu, ufisadi,20ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, husuda, kuwaka hasira, ushindani, faraka, mgawanyiko.21Wivu, ulevi, ulafi na mambo mengine kama haya. Nawaonya ninyi, kama nilivyowaonya mwanzoni, kwamba wale wanaofanya mambo kama hayo hawataurithi ufalme wa Mungu.22Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, ukarimu, utu wema, imani,23upole, na kiasi. Hakuna sheria dhidi ya mambo kama hayo.24Wale walio wa Kristo Yesu wameusulubisha mwili pamoja na shauku na tamaa zao mbaya.

25Kama tukiishi kwa Roho, pia tutembee kwa Roho.26Tusiwe wa kujivuna, tusichokozane kila mmoja na mwenzake, wala tusioneane wivu.

6

1Ndugu, ikiwa mtu amekamatwa katika uovu, ninyi mlio wa kiroho, mnawiwa kumrejesha huyo ndugu katika roho ya upole. Huku mkijiangalia wenyewe ili msijaribiwe.2Mchukuliane mizigo, na kwa hiyo mtaikamilisha sheria ya Kristo.3Ikiwa mtu yeyote anajiona ni bora wakati si kitu, anajidanganya mwenyewe.4Kila mmoja na aipime kazi yake. Kisha atakuwa na kitu mwenyewe peke yake cha kujisifu, bila kujilinganisha mwenyewe na mtu yeyote.5Maana kila mtu atachukua mzigo wake mwenyewe.

6Mtu aliyefundishwa neno lazima amshirikishe mazuri yote mwalimu wake.7Msidanganyike. Mungu hadhihakiwi. Kila apandacho mtu, ndicho atakachovuna pia.8Kila apandaye mbegu katika asili yake ya dhambi atavuna uharibifu, lakini yeye apandaye mbegu katika Roho, atavuna uzima wa milele kutoka kwa Roho.9Tusichoke katika kutenda mema, maana kwa wakati wake tutavuna ikiwa hatutakata tamaa.10Hivyo basi, wakati tutakapokuwa na nafasi, tutende mema kwa kila mmoja. Tutende mema zaidi hasa kwa walio ndani ya imani.

11Angalieni ukubwa wa barua nilizowaandikia kwa mkono wangu mwenyewe.12Wale wanaotaka kufanya mema kwa mtazamo wa mwili ndiyo wenye kuwalazimisha mtahiriwe. Wanafanya hivyo kwa sababu wasiingie kwenye mateso ya msalaba wa Kristo.13Maana hata hao waliotahiriwa wenyewe hawaishiki sheria. Badala yake wanataka ninyi mtahiriwe ili waweze kujivunia miili yenu.14Isitokee nikajivuna isipokuwa kwa msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Ni katika yeye ulimwengu umesulubiwa kwangu na mimi katika ulimwengu.15Kwa kuwa haijalishi kutahiriwa au kutokutahiriwa kuwa ni kitu. Badala yake uzao mpya ni muhimu.16Kwa wote wenye kuishi kwa kanuni hii, wawe na amani na rehema iwe juu yao wote, na juu ya Israel ya Mungu.

17Tangu sasa mtu yeyote asinitaabishe, maana nimebeba chapa za Yesu mwilini mwangu.

18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu, ndugu. Amina.

Waefeso

1

1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, kwa waliotengwa kwa ajili ya Mungu walioko Efeso na ambao ni waaminifu katika Kristo Yesu.2Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.

3Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo apewe sifa. Ni yeye aliyetubariki kwa kila baraka za kiroho, katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo.4Kabla ya kuumbwa ulimwengu, Mungu alituchagua sisi ambao tunaamini katika Kristo. Alituchagua sisi ili tuweze kuwa watakatifu na tusiolaumika mbele yake.5Katika pendo Mungu alituchagua mwanzo kwa kututwaa kama watoto wake kwa njia ya Yesu Kristo. Alifanya hivi kwa sababu alipendezwa kufanya kile alichotamani.6Matokeo yake ni kwamba Mungu anatukuzwa kwa neema ya utukufu wake. Hiki ndicho alichotupatia bure kwa njia ya mpendwa wake.

7Kwa kuwa katika mpendwa wake, tunaukombozi kupitia damu yake, msamaha wa dhambi. Tunalo hili kwa sababu ya utajiri wa neema yake.8Alifanya neema hii kuwa nyingi kwa ajili yetu katika hekima na ufahamu.9Mungu alifanya ijulikane kwetu ile kweli iliyofichika ya mpango, kutokana na hamu iliyodhihirishwa ndani ya Kristo.10Wakati nyakati zimetimia kwa utimilifu wa mpango wake, Mungu ataviweka pamoja kila kitu cha mbinguni na cha juu ya nchi ndani ya Kristo.11Katika Kristo tulikuwa tumechaguliwa na kukusudiwa kabla ya wakati. Hii ilikuwa ni kutokana na mpango wa anayefanya vitu vyote kwa kusudi la mapenzi yake.12Mungu alifanya hivyo ili kwamba tuweze kuwapo kwa sifa ya utukufu wake. Tulikuwa wa kwanza kuwa na ujasiri ndani ya Kristo.13Ilikuwa kwa njia ya Kristo kwamba mlisikia neno la kweli, injili ya wokovu wenu kwa njia ya Kristo. Ilikuwa katika yeye pia kwamba mmeamini na kutiwa mhuri na Roho Mtakatifu aliye ahidiwa.14Roho ndiyo dhamana ya urithi wetu mpaka umiliki utakapopatikana. Hii ilikuwa ni kwa sifa ya utukufu wake.

15Kwa sababu hii, tangu wakati niliposikia kuhusu imani yenu ndani ya Bwana Yesu na kuhusu pendo lenu kwa wale wote ambao wametengwa kwa ajili yake.16Sijaacha kumshukuru Mungu kwa ajili yenu na kuwataja katika maombi yangu.17Ninaomba kwamba Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, atawapeni roho ya hekima, mafunuo ya ufahamu wake.18Ninaomba kwamba macho yenu ya moyoni yatiwe nuru kwa ninyi kujua ni upi ujasiri wa kuitwa kwenu. Naomba kwamba mjue utajiri wa utukufu wa urithi wake miongoni mwa wale waliotengwa kwa ajili yake.19Naomba kwamba ujue ukuu uzidio wa nguvu yake ndani yetu ambao tunaamini. Huu ukuu ni kutokana na kufanya kazi katika nguvu zake.20Hii ni nguvu iliyofanya kazi ndani ya Kristo wakati Mungu alipomfufua kutoka kwa wafu na kumketisha katika mkono wake wa kuume katika mahali pa mbingu.21Alimketisha Kristo juu mbali na utawala, mamlaka, nguvu, enzi, na kila jina litajwalo. Alimketisha Yesu si tu kwa wakati huu lakini kwa wakati ujao pia.22Mungu amevitiisha vitu vyote chini ya miguu ya Kristo. Amemfanya yeye kichwa juu ya vitu vyote katika kanisa.23Ni kanisa kwamba ndilo mwili wake, ukamilifu wake ambaye hujaza vitu vyote katika njia zote.

2

1Kama vile mlivyo kuwa mmekufa katika makosa na dhambi zenu.2Ilikuwa katika hali kwamba kwanza mlienenda kulingana na nyakati za ulimwengu huu. Mlikuwa mkienenda kwa kufuata mtawala wa mamlaka ya anga. Hii ndiyo roho yake yule afanyaye kazi katika wana wa kuasi.3Sisi wote hapo mwanzo tulikuwa miongoni mwa hawa wasioamini. Tulikuwa tukitenda kwa tamaa mbaya za miili yetu. Tulikuwa tukifanya mapenzi ya mwili na ufahamu wetu. Tulikuwa kwa asili wana wa ghadhabu kama wengine.

4Lakini Mungu ni mwingi wa rehema kwa sababu ya pendo lake kubwa alilotupenda sisi.5Wakati tulipokuwa wafu katika makosa yetu, alituleta pamoja katika maisha mapya ndani ya Kristo. Ni kwa neema kwamba tumeokolewa.6Mungu alitufufua pamoja na kutufanya kukaa pamoja katika mahali pa mbingu ndani ya Kristo Yesu.7Alifanya hivi ili katika nyakati zijazo aweze kutuonesha utajiri mkuu wa neema yake. Hutuonesha sisi hili kwa njia ya wema wake ndani ya Kristo Yesu.

8Kwa neema mmeokolewa kwa njia ya imani. Na hii haikutoka kwetu. Ni zawadi ya Mungu.9Haitokani na matendo. Matokeo yake, asiwepo mmoja wapo wa kujisifu.10Kwa sababu sisi tu kazi ya Mungu, tumeumbwa katika Kristo Yesu kutenda matendo mema. Ni matendo haya ambayo Mungu aliyapanga tangu zamani za kale kwa ajili yetu, ili tutembee katika hayo.

11Kwa hiyo kumbukeni kwamba hapo zamani mlikuwa watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili. Mnaitwa “msio na tohara” kwa kile kinachoitwa tohara ya mwili inayofanywa kwa mikono ya binadamu.12Kwa wakati huo mlikuwa mmetengwa na Kristo. Mlikuwa wageni kwa watu wa Israel. Mlikuwa wageni kwa agano la ahadi. Hamkuwa na uhakika wa wakati ujao. Mlikuwa bila Mungu katika ulimwengiu.13Lakini sasa katika Kristo Yesu ninyi ambao hapo mwanzo mlikuwa mbali na Mungu mmeletwa karibu na Mungu kwa damu ya Kristo.

14Kwa maana yeye ndiye amani yetu. Alifanya wawili kuwa mmoja. Kwa mwili wake aliuharibu ukuta wa utengano ambao ulikuwa umetutenganisha, huo uadui.15Kwamba alikomesha sheria ya amri na kanuni ili kwamba aumbe mtu mmoja mpya ndani yake. Akafanya amani.16Alifanya hivi ili kuwapatanisha makundi mawili ya watu kuwa mwili mmoja kwa Mungu kupitia msalaba. Kwa njia ya msalaba aliufisha uadui.17Yesu alikuja na kutangaza amani kwenu ninyi mliokuwa mbali na amani muwe na wale waliokuwa karibu.18Kwa maana kwa njia ya Yesu sisi wote wawili tuna nafasi kwa yule Roho mmoja kuingia kwa Baba.

19Hivyo basi, ninyi watu wa mataifa si wasafiri na wageni tena. Bali ni wenyeji pamoja na wale watakatifu kwa ajili ya Mungu na wajumbe katika nyumba ya Mungu.20Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii. Kristo Yesu mwenyewe alikuwa jiwe kuu la pembeni.21Katika yeye jengo lote limeungamanishwa pamoja na kukua kama hekalu ndani ya Bwana.22Ni ndani yake ninyi nanyi mnajengwa pamoja kama mahali pa kuishi pa Mungu katika Roho Mtakatifu.

3

1Kwa sababu hiyo mimi, Paulo, ni mfungwa wa Yesu Kristo kwa ajili yenu Mataifa.2Naamini ya kwamba mmesikia juu ya kazi ya neema ya Mungu aliyo nipa kwa ajili yenu.3Nawaandikieni kutokana na jinsi ufunuo ulivyo funuliwa kwangu. Huu ni ukweli uliyofichika ambao niliandika kwa kifupi kwenye barua nyingine.4Usomapo kuhusu haya, utaweza kutambua busara yangu katika ukweli huu uliofichika kuhusu Kristo.5Kwa vizazi vingine ukweli huu haukufanywa utambulike kwa wana wa watu. Ila kwa sasa umewekwa wazi kwa Roho kwa Mitume waliotengwa na Manabii.6Ukweli huu uliofichika ni kwamba watu wa Mataifa ni washiriki wenzetu na wajumbe wenzetu wa mwili. Niwashiriki pamoja na ahadi ya Kristo Yesu kupitia injili.7Na kwa hili nimefanyika mtumishi kwa zawadi ya neema ya Mungu iliyotolewa kwangu kupitia utendaji wa nguvu yake.

8Mungu alitoa zawadi hii kwangu, japo kuwa mimi ni mtu mdogo wa wote kuliko wale waliotengwa kwa ajili ya Mungu. Zawadi hii ni kwamba inanipasa kuwatangazia mataifa injili yenye utajiri usiochunguzika wa Kristo.9Inanipasa kuwa tangazia watu wote juu ya nini ni mpango wa Mungu wa siri. Huu ni mpango ambao ulikuwa umefichwa kwa miaka mingi iliyopita, na Mungu ambaye aliviumba vitu vyote.10Hii ilikuwa kwamba, kupitia Kanisa, watawala na mamlaka katika sehemu za mbingu wapate kujua pande nyingi za asili ya hekima ya Mungu.11Haya yangetokea kupitia mpango wa milele ambao aliukamilisha ndani ya Kristo Yesu Bwana wetu.12Kwa kuwa katika Kristo tuna ujasiri na uwezo wa kuingia kwa ujasiri kwa sababu ya imani yetu kwake.13Kwa hiyo nawaomba msikate tamaa kwa sababu ya mateso yangu kwa ajili yenu. Haya ni utukufu wenu.

14Kwa sababu hii napiga magoti kwa Baba.15Ambaye kwake yeye kila familia mbinguni na juu ya nchi imeitwa jina.16Ninaomba kwamba apate kuwaneemesha, kutokana na utajiri wa utukufu wake, awafanye imara kwa nguvu kupitia Roho wake, ambaye yu ndani yenu.17Ninaomba kwamba Kristo aishi ndani ya mioyo yenu kupitia imani.18Ninaomba kwamba muwe na shina na msingi wa upendo wake. Muwe katika pendo lake ili muweze kuelewa, pamoja na wote waaminio, jinsi upana, na urefu na kimo na kina cha upendo wa Kristo.19Ninaomba Kwamba mjue ukuu wa upendo wa Kristo, ambao unazidi ufahamu. Mfanye haya ili mjazwe na ukamilifu wote wa Mungu.

20Na sasa kwake yeye awezaye kufanya kila jambo, zaidi ya yote tuyaombayo au tuyawazayo, kupitia nguvu yake itendayo kazi ndani yetu,21kwake yeye kuwe na utukufu ndani ya kanisa na katika Kristo Yesu kwa vizazi vyote milele na milele. Amina.

4

1Kwa hiyo, kama mfungwa kwa ajili ya Bwana, nawasihi mtembee sawasawa na wito ambao Mungu aliwaita.2Muishi kwa unyenyekevu mkuu na upole na uvumilivu. Mkichukuliana katika upendo.3Fanyeni bidii kuutunza umoja wa Roho katika kifungo cha amani.4Kuna mwili mmoja na Roho moja, kama ambavyo pia mlikuwa mmeitwa katika uhakika wa taraja moja la wito wenu.5Na kuna Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja,6na Mungu mmoja na Baba wa wote. Yeye yuko juu ya yote, na katika yote na ndani ya yote.

7Kwa kila mmoja wetu amepewa kipawa kulingana na kipimo cha kipawa cha Kristo.8Ni kama maandiko yasemavyo: “Alipopaa juu sana, aliteka mateka. Akawapa wanadamu vipawa.”

9Ni nini maana ya, “Alipaa,” isipokuwa kwamba alishuka pia pande za chini za dunia?10Yeye ambaye alishuka ni mtu yuleyule ambae pia alipaa mbali juu ya mbingu zote. Alifanya hivi ili uwepo wake uwe katika vitu vyote.11Kristo alitoa vipawa kama hivi: mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji, na waalimu.12Alifanya hivi kuwawezesha waumini kwa ajili ya kazi ya huduma, kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo.13Anafanya hivi hadi sisi sote tufikie umoja wa imani na maarifa ya mwana wa Mungu. Anafanya hivi hadi tuweze kukomaa kama wale waliofikia kimo kamili cha Kristo.14Hii ni ili kwamba tusiwe tena kama watoto, tusirushwerushwe huku na huko. Ili kwamba tusichukuliwe na kila aina ya upepo wa fundisho, kwa hila za watu katika ujanja wa udanganyifu uliopotoka.15Badala yake, tutaongea ukweli katika upendo na kukua zaidi katika njia zote ndani yake ambaye ndiye kichwa, Kristo.16Kristo ameunganisha, kwa pamoja, mwili wote wa waumini. Umeungamanishwa pamoja na kila kiungo ili kwamba mwili wote ukue na kujijenga wenyewe katika upendo.

17Kwa hiyo, nasema hili, na nawasihi katika Bwana: Msitembee tena kama watu wa mataifa wanavyotembea katika ubatili wa akili zao.18Wametiwa giza katika mawazo yao. Wamefukuzwa kutoka katika uzima wa Mungu kwa ujinga ulio ndani yao kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao.19Hawajisikii aibu. Wamejikabidhi wenyewe kwa ufisadi katika matendo machafu, katika kila aina ya uchoyo.

20Lakini, hivi sivyo mlivyojifunza kuhusu Kristo.21Nadhani kwamba mmesikia kuhusu yeye. Nadhani kwamba mmekuwa mkifundishwa katika yeye, kama tu ukweli ulivyo ndani ya Yesu.22Lazima mvue mambo yote yanayoendana na mwenendo wenu wa zamani, utu wa zamani. Ni utu wa zamani unaooza kwa sababu ya tamaa za udanganyifu.23Vueni utu wenu wa zamani ili kwamba mfanywe upya katika roho ya akili zenu.24Fanyeni hivi ili muweze kuvaa utu mpya, unaoendana na Mungu. Umeumbwa katika haki na utakatifu wa kweli.

25Kwa hiyo, weka mbali udanganyifu. “Ongeeni ukweli, kila mmoja na jirani yake,” kwa sababu tu washirika kwa kila mmoja kwa mwenzake.26Mwe na hasira, lakini msitende dhambi.” Jua lisizame mkiwa katika hasira zenu.27Msimpe Ibilisi nafasi.28Yeyote aibaye lazima asiibe tena. Badala yake ni lazima afanye kazi. Afanye kazi yenye manufaa kwa mikono yake, ili kwamba aweze kumhudumia mtu aliye na hitaji.29Kauli mbaya isitoke kinywani mwenu. Badala yake, maneno lazima yatoke katika vinywa vyenu yafaayo kwa mahitaji, kuwapa faida wale wanaosikiliza.30Na msimhuzunishe Roho Mtakatifu wa Mungu. Ni kwa Yeye kwamba mmewekewa muhuri kwa ajili ya siku ya ukombozi.31Lazima muweke mbali uchungu wote, ghadhabu, hasira, ugomvi, na matusi, pamoja na kila aina ya uovu. Iweni wema ninyi kwa ninyi.32Mwe na huruma. Msameheane ninyi kwa ninyi, kama vile Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.

5

1Kwa hiyo muwe watu wa kumfuata Mungu, kama watoto wake wapendwao.2Mtembee katika pendo, vilevile kama Kristo alivyotupenda sisi, alijitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Yeye alikuwa sadaka na dhabihu, kuwa harufu nzuri ya kumfurahisha Mungu.3Zinaa na uchafu wowote na tamaa mbaya visitajwe kati yenu, kama inavyotakiwa kwa waaminio,4wala machukizo yasitajwe kwenu na mazungumzo ya kipumbavu, au mizaha ya udhalilishaji, ambayo siyo sawa, badala yake iwepo shukrani.5Mnaweza kuwa na uhakika ya kwamba kuna zinaa, uchafu, wala atamaniye, huyo ni mwabudu sanamu, hana urithi wowote katika ufalme wa Kristo na Mungu.6Mtu yeyote asikudanganye kwa maneno matupu, kwa sababu ya mambo haya ya hasira ya Mungu inakuja juu ya wana wasiotii.

7Hivyo usishiriki pamoja nao.8Kwa kuwa ninyi mwanzo mlikuwa giza, lakini sasa mmekuwa nuru katika Bwana. Hivyo tembeeni kama watoto wa nuru.9Kwa kuwa matunda ya nuru yanajumuisha uzuri wote, haki na ukweli.10Tafuta kile kinacho furahisha Bwana.11Usiwepo ushiriki katika kazi za giza zisizo na matunda, badala yake ziweke wazi.12Kwa sababu mambo yanayofanywa na wao sirini ni aibu sana hata kuyaelezea.13Mambo yote, yanapofichuliwa na nuru, huwa wazi,14kwa kuwa Kila kitu kilichofichuliwa kinakuwa nuruni. Hivyo husema hivi, “Amka, wewe uliyelala, na inuka kutoka kwa wafu na Kristo atakuangazia.”

15Hivyo iweni makini jinsi mtembeavyo, siyo kama watu wasio werevu bali kama werevu.16Ukomboeni muda kwa kuwa siku ni za uovu.17Msiwe wajinga, badala yake, fahamuni nini mapenzi ya Bwana.

18Msilewe kwa mvinyo, huongoza kwenye uharibifu, badala yake mjazwe na Roho Mtakatifu.19Msemezane kila mmoja wenu kwa zaburi, na sifa, na tenzi za rohoni. Imbeni na sifuni kwa Bwana kwa moyo.20Daima toa shukrani kwa mambo yote katika jina la Kristo Yesu Bwana wetu kwa Mungu Baba.21Jitoeni wenyewe kila mmoja kwa mwingine kwa heshima ya Kristo.

22Wake, watiini waume zenu, kama kwa Bwana.23Kwa sababu mume ni kichwa cha mke, kama Kristo alivyo kichwa cha kanisa. Ni mwokozi wa mwili.24Lakini kama kanisa lilivyo chini ya Kristo, vilevile wake lazima wafanye hivyo kwa waume zao katika kila jambo.

25Waume, wapendeni wake zenu kama vile Kristo alivyolipenda kanisa na akajitoa mwenyewe kwa ajili yake.26Alifanya hivyo ili liwe takatifu. Alilitakasa kwa kuliosha na maji katika neno.27Alifanya hivi ili kwamba aweze kujiwasilishia mwenyewe kanisa tukufu, pasipo na doa wala mawaa au kitu kifananacho na haya, badala yake ni takatifu lisilo na kosa.28Kwa njia ile ile, waume wanatakiwa kuwapenda wake zao kama miili yao. Yule ampendae mke wake anajipenda mwenyewe.29Hakuna hata mmoja anayechukia mwili wake. Badala yake, huulisha na kuupenda, kama Kristo pia alivyolipenda kanisa.30Kwa kuwa sisi ni washiriki wa mwili wake.31“Kwa sababu hii, mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na ataungana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”

32Huu ukweli ulikuwa umefichika. Lakini ninasema kuhusu Kristo na kanisa.33Lakini, kila mmoja wenu lazima ampende mke wake kama mwenyewe, na mke lazima amheshimu mumewe.

6

1Watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa maana hii ni haki.2“Mheshimu baba yako na mama yako” (Maana hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi),3“ili iwe heri kwenu na muweze kuishi maisha marefu duniani.”

4Na ninyi akina baba, msiwakwaze watoto na kuwasababishia hasira, badala yake, waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.

5Enyi watumwa, iweni watiifu kwa mabwana zenu wa hapa duniani kwa heshima kubwa na kutetemeka kwa hofu itokayo mioyoni mwenu. Muwe watiifu kwao kama vile mnavyomtii Kristo.6Utii wenu usiwe tu pale mabwana zenu wanapowatazama ili kuwafurahisha. Badala yake, iweni watiifu kama watumwa wa Kristo. Fanyeni Mapenzi ya Mungu kutoka mioyoni mwenu,7watumikieni kwa mioyo yenu yote, kwa kuwa mnamtumikia Bwana na wala si wanadamu,8mnapaswa kujua kwamba katika kila tendo jema mtu analofanya, atapokea zawadi kutoka kwa Bwana, ikiwa ni mtumwa au mtu huru.

9Na Mabwana fanyeni vivyo hivyo kwa watumwa wenu. Msiwatishe mkijua kwamba yeye aliye Bwana wa wote ni yule aliye mbinguni. Mkijua kuwa hakuna upendeleo ndani yake.

10Hatimaye, iweni na nguvu katika Bwana na katika uwezo wa nguvu zake.11Vaeni silaha zote za Mungu, ili kwamba muweze kuzipinga hila za shetani.12Kwa kuwa vita vyetu si vya damu na nyama, bali ni dhidi ya falme na mamlaka ya roho na watawala wa ulimwengu wa uovu na giza, dhidi ya pepo katika ulimwengu wa roho.13Kwa hiyo, vaeni silaha zote za Mungu, ili mpate kusimama imara dhidi ya uovu katika kipindi hiki kiovu. Baada ya kumaliza kila kitu, mtasimama imara.

14Hatimaye simameni imara, Mkiwa mmefunga ukweli kiunoni, na kuvaa ya haki kifuani.15Fanyeni hivi mkiwa mmevaa utayari miguuni mwenu wa kutangaza injili ya amani.16Katika kila hali mkichukua ngao ya imani, ambayo itakuwezesha kuizima mishale yenye moto ya yule mwovu.17Vaeni kofia ya wokovu na upanga wa Roho, ambayo ni neno la Mungu.18Pamoja na maombi na sala. Ombeni kwa Roho kila wakati. Kwa mtazamo huu iweni waangalifu kila wakati kwa uvumilivu wote na maombi kwa ajili ya waamini wote.19Ombeni kwa ajili yangu, ili nipewe ujumbe ninapofungua mdomo wangu. Ombeni kwamba nieleweshe kwa ujasiri kweli iliyofichika ihusuyo injili.20Ni kwa ajili ya injili mimi ni balozi niliyefungwa minyororo, ili kwamba ndani mwao niseme kwa ujasiri kama ninavyopaswa kusema.

21Lakini ninyi pia mjue mambo yangu na jinsi ninavyoendelea, Tikiko ndugu yangu kipenzi na mtumishi mwaminifu katika Bwana, atawajulisha kila kitu.22Nimemtuma kwenu kwa kusudi hili maalumu, ili kwamba mjue mambo kuhusu sisi, aweze kuwafariji mioyo yenu.

23Amani na iwe kwa ndugu, na upendo pamoja na imani kutoka kwa Mungu baba na Bwana Yesu Kristo.24Neema na iwe pamoja na wote wampendao Bwana Yesu Kristo kwa pendo lile lisilo haribika.

Wafilipi

1

1Paulo na Timotheo, watumishi wa Kristo Yesu, Kwa wale walitengwa katika Kristo wanaoishi Filipi, pamoja na waangalizi na mashemasi.2Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na Bwana wetu Yesu Kristo.

3Namshukuru Mungu wangu kila ninapowakumbuka ninyi nyote.4Mara zote katika kila ombi langu kwa ajili yenu ninyi nyote, huwa na furahi ninapowaombea.5Nina shukrani nyingi kwa sababu ya ushirika wenu katika injili tangu siku ya kwanza mpaka leo.6Nina hakika kuwa yeye aliyeanzisha kazi njema ndani yenu ataendelea kuikamilisha mpaka siku ya Bwana Yesu Kristo.7Ni sawa kwangu kujisikia hivi juu yenu ninyi nyote kwa sababu nimewaweka moyoni mwangu. Maana ninyi mmekuwa washirika wenza katika neema, katika kifungo changu na katika utetezi na uthibitishaji wangu wa injili.8Mungu ni shahidi wangu, jinsi nilivyo na shauku juu yenu nyote katika undani wa pendo la Kristo Yesu.

9Na ninaomba kwamba: upendo wenu uongezeke zaidi na zaidi katika maarifa na ufahamu wote.10Ninaomba kwa ajili ya hili ili muwe na uwezo wa kupima na kuchagua mambo yaliyo bora sana. Pia ninawaombea ili muwe safi pasipokuwa na hatia yoyote katika siku ya Kristo.11Na pia ili mjazwe na tunda la haki lipatikanalo katika Yesu Kristo, kwa utukufu na sifa ya Mungu.

12Sasa ndugu zangu, nataka mjue kuwa, mambo yaliyotokea kwangu yameifanya injili iendelee sana.13Ndiyo maana vifungo vyangu katika Kristo, vimejulikana kwa walinzi wa ikulu yote na kwa kila mtu pia.14Na ndugu wengi katika Bwana, kwa sababu ya vifungo vyangu, wameshawishika na kuthubutu kulihubiri Neno pasipo hofu.

15Baadhi kweli hata humtangaza Kristo kwa fitina na ugomvi, na pia wengine kwa nia njema.16Wale wanaomtangaza Kristo kwa upendo wanajua kuwa nimewekwa hapa kwa ajili ya utetezi wa injili.17Bali wengine wanamtangaza Kristo kwa ubinafsi na nia mbaya. Hudhani kuwa wanasababisha matatizo kwangu katika minyororo yangu.18Kwa hiyo Sijali, aidha njia ikiwa ni kwa hila au kwa kweli, Kristo anatangazwa, na katika hili ninafurahia! Ndiyo, nitafurahia.

19Kwa kuwa ninajua ya kuwa hili litaleta kufunguliwa kwangu. Jambo hili litatokea kwa sababu ya maombi yenu na kwa msaada wa Roho wa Yesu Kristo.20Kulingana na matarajio yangu ya uhakika na kweli ni kwamba, sitaona aibu. Badala yake, kwa ujasiri wote, kama ambavyo siku zote na sasa, natarajia kuwa Kristo atainuliwa katika mwili wangu, ikiwa katika uzima au katika kifo.

21Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo na kufa ni faida.22Lakini, kama kuishi katika mwili huzaa tunda katika kazi yangu, kwa hiyo sijui ni lipi la kuchagua.23Maana ninasukumwa sana na mawazo haya mawili. Nina hamu ya kuuacha mwili na kuwa pamoja na Kristo, kitu ambacho ni bora zaidi.24Ingawa, kubaki katika mwili huu ni jambo la muhimu sana kwa ajili yenu.25Kwa kuwa nina uhakika juu ya hili, ninajua nitabaki na kuendelea kuwa pamoja nanyi nyote, kwa ajili ya maendeleo na furaha ya imani yenu.26Na hii italeta furaha yenu kubwa katika Kristo Yesu, kwa sababu yangu itaongezeka, kwa sababu ya uwepo wangu tena pamoja nanyi.

27Mnatakiwa kuishi maisha yenu katika mwenendo mzuri uipasayo injili ya Kristo. Fanyeni hivyo ili nikija kuwaona au nisipokuja, nisikie kuwa mmesimama imara katika roho moja. Natamani kusikia kuwa mna roho moja, mkiishindania imani ya injili kwa pamoja.28Na msitishwe na kitu chochote kinachofanywa na maadui zenu. Hii kwao ni ishara ya uharibifu. Bali kwenu ni ishara ya wokovu kutoka kwa Mungu.29Kwa maana ninyi mmepewa kwa ajili ya Kristo, si kumwamini tu, bali na kuteswa pia katika Yeye.30Kwa maana mna mgogoro uleule kama mliouona kwangu na mnasikia kwamba ninao hata sasa.

2

1Ikiwa kuna kutiwa moyo katika Kristo, Ikiwa kuna faraja kutoka katika pendo lake, Ikiwa kuna ushirika wa Roho, Ikiwa kuna rehema na huruma.2Ikamilisheni furaha yangu kwa nia moja mkiwa na upendo mmoja, mkiwa wamoja katika roho, na kuwa na kusudi moja.3Msifanye kwa ubinafsi na majivuno. Isipokuwa kwa unyenyekevu mkiwaona wengine kuwa bora zaidi yenu.4Kila mmoja wenu asiangalie tu mahitaji yake binafsi, bali pia ajali mahitaji ya wengine.

5Muwe na nia kama aliyonayo Kristo Yesu.
6Ingawaje yeye ni sawa na Mungu. Lakini hakujali kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho.
7Badala yake, alijishusha mwenyewe, Alichukua umbo la mtumishi. Akajitokeza katika mfano wa wanadamu. Alionekana kama mwanadamu.
8Yeye alijinyenyekeza na kuwa mtii hadi kifo, kifo cha msalaba.
9Hivyo basi Mungu alimtukuza sana. Alimpa jina kuu lipitalo kila jina.
10Alifanya hivyo ili kwamba katika jina la Yesu kila goti sharti liiname. Magoti ya walio mbinguni na walio juu ya ardhi na chini ya ardhi.
11Na alifanya hivyo ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu kristo ni Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

12Kwa hiyo basi, wapendwa wangu kama mnavyotii siku zote, si tu katika uwepo wangu lakini sasa ni zaidi sana hata pasipo uwepo wangu, uwajibikieni wokovu wenu wenyewe kwa hofu na kutetemeka.13Kwa kuwa ni Mungu anayetenda kazi ndani yenu, ili kuwawezesha kunia na kutenda mambo yale yampendezayo yeye.

14Fanyeni mambo yote bila malalamiko na mabishano.15Fanyeni hivyo ili kwamba msilaumike na kuwa watoto wa Mungu waaminifu wasiyo na lawama. Fanyeni hivyo ili kwamba muwe nuru ya dunia, katika kizazi cha uasi na uovu.16Shikeni sana neno la uzima ili kwamba niwe na sababu ya kutukuza siku ya Kristo. Kisha nitafahamu kwamba sikupiga mbio bure wala sikutaabika bure.

17Lakini hata kama ninamiminwa kama sadaka juu ya dhabidhu na huduma ya imani yenu, ninafurahi, na ninafurahi pamoja nanyi nyote.18Vilevile na ninyi pia mnafurahi, na mnafurahi pamoja nami.

19Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo kwenu hivi karibuni, ili kwamba niweze kutiwa moyo nitakapojua mambo yenu.20Kwa kuwa sina mwingine aliye na mtazamo kama wake, mwenye nia ya kweli kwa ajili yenu.21Wengine wote ambao ningewatuma kwenu wanatafuta mambo yao binafsi tu, na siyo mambo ya Yesu Kristo.22Lakini mnaijua thamani yake, kwa sababu kama mtoto anavyomhudumia baba yake, ndivyo alivyotumika pamoja nami katika injili.23Kwa hiyo ninatumaini kumtuma haraka pindi tu nitakapofahamu nini kitatokea kwangu.24Lakini nina hakika katika Bwana kwamba mimi mwenyewe pia nitakuja hivi karibuni.

25Lakini nafikiri ni muhimu kumrejesha kwenu Epafradito. Yeye ni ndugu yangu na mtenda kazi mwenzangu na askari mwenzangu, mjumbe na mtumishi wenu kwa ajili ya mahitaji yangu.26Kwa sababu alikuwa na hofu na alitamani kuwa pamoja nanyi nyote, kwa kuwa mlisikia kwamba alikuwa mgonjwa.27Maana hakika alikuwa mgonjwa sana kiasi cha kufa. Lakini Mungu alimhurumia, na wema huo haukuwa juu yake tu, lakini pia ulikuwa juu yangu, ili kwamba nisiwe na huzuni juu ya huzuni.28Kwa hiyo ninamrejesha kwenu haraka iwezekanavyo, Ili kwamba mtakapomwona tena mpate kufurahi na mimi nitakuwa nimeondolewa wasi wasi.29Mkaribisheni Epafradito katika Bwana kwa furaha zote. Waheshimuni watu kama yeye.30Kwa kuwa ilikuwa kwa ajili ya kazi ya Kristo kwamba alikaribia kufa. Alihatarisha maisha yake ili kuniokoa mimi na akafanya kile ambacho hamkuweza kufanya katika kunihudumia mimi kwani mko mbali nami.

3

1Hatimaye, ndugu zangu furahini katika Bwana. Sioni usumbufu kuwaandikia tena maneno yaleyale. Haya mambo yatawapa usalama.

2Jihadharini na mbwa. Jihadharini na watenda kazi wabaya. Jihadharini na wale wajikatao miili yao.3Kwa kuwa sisi ndiyo tohara. Sisi ndiyo huwa tumwabudu Mungu kwa msaada wa Roho. Tujivuniao katika Kristo Yesu, na ambao hatuna ujasiri katika mwili.4Hata hivyo, kama kungekuwa na mtu wa kuutumainia mwili huu, mimi ningeweza kufanya hivyo zaidi.

5Kwani nilitahiriwa siku ya nane, nilizaliwa katika kabila la Waisraeli. Ni wa kabila la Benjamini. Ni Mwebrania wa waebrani. Katika kuitimiza haki ya sheria ya Musa, nilikuwa, Farisayo.6Kwa juhudi zangu nililitesa Kanisa. Kwa kuitii haki ya sheria, sikuwa na lawama kisheria.

7Lakini katika mambo yote niliyoyaona kuwa ya faida kwangu mimi, niliyahesabu kama takataka kwa sababu ya kumfahamu Kristo.8Kwa kweli, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kutokana na ubora wa kumjua wa Kristo Yesu Bwana wangu. Kwa ajili yake nimeaacha mambo yote, nayahesabu kama takataka ili nimpate Kristo9na nionekane ndani yake. Sina haki yangu binafisi kutoka katika sheria, bali ninayo haki ile ipatikanayo kwa imani katika Kristo, itokayo kwa Mungu, yenye msingi katika imani.10Kwa hivyo sasa nataka kumfahamu yeye na nguvu ya ufufuo wake na ushirika wa mateso yake. Nataka kubadilishwa na Kristo katika mfano wa kifo chake,11angalau niweze kuwa na matumaini katika ufufuo wa wafu.

12Siyo kweli kwamba tayari nimeyapata mambo hayo, au kwamba nimekuwa mkamilifu katika hayo. Bali najitahidi ili niweze kupata kile nilichopatikana na Kristo Yesu.13Ndugu zangu, sidhani kwamba nimekwisha kupata mambo haya. Bali nafanya jambo moja: nasahau ya nyuma nayatazamia ya mbele.14Najitahidi kufikia lengo kusudi ili nipate tuzo ya juu ya wito wa Mungu katika Kristo Yesu.15Sote tulio ukulia wokovu, tunapaswa kuwaza namna hii. Na ikiwa mwingine atafikiri kwa namna iliyotofauti kuhusu jambo lo lote, Mungu pia atalifunua hilo kwenu.16Hata hivyo, hatua tuliyo ifikia na tuenende katika mtindo huo.

17Ndugu zangu, niigeni mimi. Waangalieni kwa makini wale wanaoenenda kwa mfano ulio wa jinsi yetu.18Wengi wanaoishi ni ni wale ambao mara nyingi nimewaambieni, na sasa nawaambia kwa machozi wengi wanaishi kama maadui wa msalaba wa Kristo.19Mwisho wao ni uharibifu Kwa kuwa Mungu wao ni tumbo, na kiburi chao kiko katika aibu yao. Wanafikiria mambo ya kidunia.20Bali uraia wetu uko mbinguni, ambako tunamtarajia mwokozi wetu Yesu Kristo.21Atabadilisha miili yetu dhaifu kuwa kama mwili wake wa utukufu; kwa uweza ule ule unaomwezesha kuvidhibiti vitu vyote.

4

1Kwa hiyo wapendwa wangu, ambao nawatamani, ambao ni furaha na taji yangu. Simameni imara katika Bwana, enyi rafiki wapendwa.

2Ninakusihi wewe Eudia, pia ninakusihi wewe Sintike, mrejeshe mahusiano ya amani kati yenu, kwa sababu ninyi, nyote wawili mliungana na Bwana.3Kwa kweli, niwasihi pia ninyi watenda kazi wenzangu, muwasaidie hawa wanawake kwa kuwa walitumika pamoja na mimi katika kueneza injili ya Bwana tukiwa na Kelementi pamoja na watumishi wengine wa Bwana, ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima.

4Furahini katika Bwana siku zote, tena nitasema, furahini.5Upole wenu na ujulikane kwa watu wote. Bwana yuko karibu.6Msijisumbue kwa jambo lolote. Badala yake, fanyeni mambo yenu yote kwa njia ya kusali na kuomba na kushukuru. Na mahitaji yenu yajulikane kwa Mungu.7Basi amani ya Bwana iliyo kuu kuliko ufahamu wote, italinda mioyo na mawazo yenu kwa msaada wa Kristo Yesu.

8Hatimaye, ndugu zangu; yatakafarini sana mambo yote yenye ukweli, heshima, haki, usafi, upendo, na yale yenye taarifa njema, yenye busara, pamoja na yale yanayohitaji kusifiwa.9Yatekelezeni mambo yale mliojifunza, mliyopokea mliyoyasikia na yale mliyoyaona kwangu naye Baba yetu wa amani atakuwa nanyi.

10Ninayo furaha kubwa sana juu yenu katika Bwana kwa kuwa ninyi mmeonyesha tena nia ya kujihusisha kwenu juu ya mahitaji yangu. Kwa kweli, hapo awali mlitamani kunijali kwa mahitaji yangu japo hamkupata fursa ya kunisaidia.11Sisemi hivyo ili kujipatia kitu kwa ajili ya mahitaji yangu. Kwani nimejifunza kuridhika katika hali zote.12Nafahamu kuishi katika hali ya kupungukiwa na pia katika hali ya kuwa na vingi. Katika mazingira yote haya mimi nimejifunza siri ya namna ya kula wakati wa shibe na jinsi ya kula wakati wa njaa, yaani vingi na kuwa mhitaji.13Ninaweza kufanya haya kwa kuwezeshwa na Yeye anitiaye nguvu.14Hata hivyo, mlifanya vyema kushiriki nami katika dhiki zangu.

15Ninyi Wafilipi mnafahamu kwamba mwanzo wa injili nilipoondoka Makedonia, hakuna Kanisa lililoniwezesha katika mambo yanayohusu utoaji na kupokea isipokuwa ninyi pekee yenu.16Hata nilipokuwa Thesalonike, ninyi mlinitumia msaada zaidi ya mara moja kwa ajili ya mahitaji yangu.17Simaanishi kwamba natafuta msaada. Bali nasema ili mpate matunda yaletayo faida kwenu.

18Nimepokea vitu vyote, na sasa nimejazwa na vitu vingi. Nimepokea vitu vyenu kutoka kwa Epafradito. Ni vitu vizuri vyenye kunukia mithiri ya manukato, vyenye kukubalika ambavyo vyote ni sadaka inayompendeza Mungu.19Kwa ajili hiyo, Mungu wangu atawajazeni mahitaji yenu kwa utajiri wa utukufu wake katikaYesu Kristo.20Sasa kwa Mungu na Baba yetu uwe utukufu milele na milele. Amina.

21Salamu zangu zimfikie kila muumini katika Kristo Yesu. Wapendwa nilio nao hapa wanawasalimieni.22Pia waumini wote hapa wanawasalimieni, hususani wale wa familia ya Kaisari.

23Na sasa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe na roho zenu.

Wakolosai

1

1Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu,2kwa watu watakatifu wa Mungu na ndugu waaminifu katika Kristo walioko Kolosai. Neema iwe kwenu, na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.

3Tunatoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, na tunawaombea kila mara.4Tumesikia imani yenu katika Yesu Kristo na upendo mlionao kwa watu wote watakatifu wa Mungu,5kwa sababu ya taraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili yenuMlisikia kuhusu taraja hiyo ya uhakika katika neno la ukweli, injili6ambayo imekuja kwenu. Na kwa njia hiyo hiyo, Injili hii inazaa tunda na inaenea ulimwenguni koteImekuwa ikifanya hivi ndani yenu tangu siku mlipoisikia na kufahamu neema ya Mungu katika kweli.7Hii ndiyo injili kama mlivyojifunza kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetuambaye ni mtumishi mwaminifu wa Kristo kwa ajili yetu.8Epafra ameufanya ujulikane kwetu upendo wenu katika Roho.

9Kwa sababu ya upendo huu, tangu siku tuliposikia hivi, hatujakoma kuwaombea. Tumekuwa tukiomba kwamba mtajazwa na maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa kiroho,10Tumekuwa tukiomba kwamba mtatembea kwa ustahimilivu wa bwana katika njia zipendezazo Bwana. Tumekua tukiomba mtazaa tunda katika kila tendo jema na kwamba mtakua katika maarifa ya Mungu.11Tunaomba muweze kutiwa nguvu katika kila uwezo kulingana na nguvu za utukufu wakekatika uvumilivu na ustahimilivu wote.12Tunaomba kwamba kwa furahamtatoa shukrani kwa Baba aliyewafanya ninyi mweze kuwa na sehemu katika urithi wa waumini katika nuru.

13Ametuokoa kutoka katika utawala wa giza, akatuhamishia katika ufalme wa Mwana wake mpendwa.14Katika mwanae tuna ukombozi na msamaha wa dhambi.15Mwana ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa uumbaji wote.16Kwa kuwa kwa yeye vitu vyote viliumbwa, vile vilivyoko mbinguni na vilivyoko duniani, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Ikiwa ni vya enzi au mamlaka au utawala au wenye nguvu, vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.17Yeye amekuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.18Na yeye ndiye kichwa cha mwili yaani kanisa, yeye ni mwanzo, na mzaliwa wa kwanza kutoka miongoni mwa wafu, hivyo, ana nafasi ya kwanza miongoni mwa vitu vyote.19Kwa kuwa Mungu alipendezwa kwamba utimilifu wake wote uishi ndani yake,20na kupatanisha vitu vyote kwake kwa njia ya Mwanawe. Mungu alifanya amani kupitia damu ya msalaba wake. Akapatanisha vitu vyote kwake mwenyewe, ikiwa ni vitu vya duniani au vitu vya mbinguni.

21Nanyi pia, kwa wakati mmoja, mlikuwa mmetengwa na Mungu na mlikua maadui katika akili na matendo maovu.22Lakini sasa amewapatanisha ninyi kwa mwili wake kupitia kifo. Alifanya hivi ili kuwaleta ninyi watakatifu, wasio na lawama na bila dosari mbele yake,23kama mkiendelea katika imani, mliyoimarishwa na kuwa thabiti, pasipo kuondoshwa kutoka kwenye taraja la ujasiri la injili mliyoisikia. Hii ndiyo injili ambayo ilihubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu. Hii ndiyo injili ambayo kwayo mimi, Paulo, nimekuwa mtumishi.

24Sasa nayafurahia mateso yangu kwa ajili yenu. Nami natimiliza katika mwili wangu kinachopungua kwa mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa.25Mimi ni mtumishi wa kanisa hili, sawasawa na wajibu niliopewa kutoka kwa Mungu kwa ajili yenu, kulitimiza neno la Mungu.26Huu ni ukweli wa siri iliyofichwa kwa miaka mingi na kwa vizazi. Lakini sasa imefunuliwa kwa wote waaminio katika yeye.27Ni kwa wale ambao Mungu alitaka kufunua ulivyo utajiri wa utukufu wa siri ya ukweli miongoni mwa Mataifa, Ni kwamba Kristo yumo ndani yenu, ujasiri wa utukufu ujao.28Huyu ndiye tunayemtangaza. Tunamwonya kila mtu, na kumfundisha kila mtukwa hekima yote, ili kwamba tumlete kila mtu mkamilifu katika Kristo.29Kwa ajili hii, mimi najibiidisha na kujitahidi kulingana na nguvu yake ifanyayo kazi ndani yangu katika uweza.

2

1Kwa kuwa nataka mfahamu jinsi ambavyo nimekuwa na taabu nyingi kwa ajili yenu, kwa wote walioko Laodikia, na kwa wote ambao hawajauona uso wangu katika mwili.2Nafanya kazi ili mioyo yao ifarijiwe, kwa kuletwa pamoja katika upendo na katika utajiri wote wa wingi wa uhakika kamili na maarifa, katika kuijua siri ya kweli ya Mungu, ambaye ni Kristo.3Katika Yeye hazina zote za hekima na maarifa zimefichwa.4Nasema hivi ili kwamba mtu yeyote asije akawadanganya kwa hotuba yeye ushawishi.5Na ingawa sipo pamoja nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Ninafurahi kuona utaratibu wenu mzuri na nguvu ya imani yenu katika Kristo.

6Kama mlivyompokea Kristo Bwana, tembeeni katika yeye.7Mwe na mzizi ndani yake, mjengwe katika yeye, mwimarishwe katika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa katika shukrani nyingi.

8Angalieni ya kwamba mtu yeyote asiwanase kwa falsafa na maneno matupu ya udanganyifu kulingana na mapokeo ya wanadamu, kulingana na kanuni za kidunia, na sio kulingana na Kristo.9Kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi katika mwili.10Nanyi mmejazwa katika yeye. Yeye ni kichwa cha kila uweza na mamlaka.11Katika yeye pia mlitahiriwa kwa tohara isiyofanywa na wanadamu katika kuondolewa mwili wa nyama, lakini ni katika tohara ya Kristo.12Mlizikwa pamoja naye katika ubatizo. Na kwa njia ya imani katika yeye mlifufuliwa kwa uweza wa Mungu, aliyemfufua kutoka kwa wafu.13Mlipokuwa wafu katika makosa yenu na kutokutahiriwa kwa miili yenu, aliwafanya hai pamoja naye na kutusamehe makosa yetu yote.14Alifuta kumbukumbu ya madeni iliyoandikwa, na taratibu zilizokuwa kinyume nasi. Aliiondoa yote na kuigongomea msalabani.15Aliziondoa nguvu na wenye mamlakaAliyaweka wazi na kuyafanya kuwa sherehe ya ushindi kwa njia ya msalaba wake.

16Kwa hiyo, mtu yeyote asiwahukumu ninyi katika kula au katika kunywa, au kuhusu siku ya sikukuu au mwezi mpya, au siku za Sabato.17Hivi ni vivuli vya mambo yajayo, lakini kiini ni Kristo.18Mtu awaye yeyote asinyang'anywe tuzo yake kwa kutamani unyenyekevu na kuabudu malaika. Mtu wa jinsi hiyo huingia katika mambo aliyoyaona na kushawishiwa na mawazo yake ya kimwili.19Yeye hakishikilii kichwa. Ni kutoka katika kichwa kwamba mwili wote kupitia viungo vyake na mifupa huungwa na kushikamanishwa kwa pamoja; na hukua kwa ukuaji utolewao na Mungu.

20Ikiwa mlikufa pamoja na Kristo kwa tabia za dunia, mbona mnaishi kama mnawajibika kwa dunia:21“Msishike, wala kuonja, wala kugusa?”22Haya yote yameamuriwa kwa ajili ya uharibifu ujao na matumizi, sawasawa na maagizo na mafundisho ya wanadamu.23Sheria hizi zina hekima ya dini zilizotengenezwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na mateso ya mwili. Lakini hazina thamani dhidi ya tamaa za mwili.

3

1Ikiwa basi Mungu amewafufua pamoja na Kristo, yatafuteni mambo ya juu ambako Kristo anakaa mkono wa kuume wa Mungu.2Fikirini kuhusu mambo ya juu, sio kuhusu mambo ya duniani.3Kwa maana mlikufa na maisha yenu yamefichwa pamoja na kristo ndani ya mungu.4Wakati kristo atakapoonekana, ambaye ni maisha yenu, ndipo nanyi pia mtakapoonekana, naye katika utukufu.

5Kwa hiyo yafisheni mambo yaliyo katika nchi yaani, uasherati, uchafu, shauku mbaya, nia mbaya, na tamaa, ambayo ni ibada ya sanamu.6Ni kwa ajili ya mambo haya ghadhabu ya Mungu inakuja juu ya wana wasio tii.7Ni kwa ajili ya mambo haya ninyi pia mlitembea kwayo mlipoishi kati yao.8Lakini sasa ni lazima myaondoe mambo haya yote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbaya, matusi, na maneno machafu yatokayo vinywani mwenu.9Msidanganyane ninyi kwa ninyi, kwa kuwa mmeuvua utu wenu wa kale na matendo yake.10Mmevaa utu upya, unaofanywa upya katika maarifa sawasawa na mfano wa yule aliyeuumba.11Katika maarifa haya, hakuna Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala kutokutahiriwa, msomi, asiye msomi, mtumwa, mtu huru, bali Kristo ni mambo yote katika yote.

12Kama wateule wa Mungu, watakatifu na wapendwao, jivikeni utu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole na uvumilivu.13Chukulianeni ninyi kwa ninyi. Hurumianeni kila mtu na mwenzake. Kama mtu analalamiko dhidi ya mwingine, amsamehe kwa jinsi ileile ambayo Bwana alivyo wasamehe ninyi.14Zaidi ya mambo haya yote, muwe na upendo, ambao ndio kigezo cha ukamilifu.

15Amani ya Kristo itawale mioyoni mwenu. Ilikuwa ni kwa ajili ya amani hii mliitiwa katika mwili mmoja. Iweni na shukrani.16Na Neno la Kristo likae ndani yenu kwa wingi. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana ninyi kwa ninyi kwa Zaburi katika hekima yote, mkimwimbia saburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni. Imbeni kwa shukrani mioyoni mwenu kwa Mungu.

17Na chochote mfanyacho katika maneno au katika matendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu. Mpeni shukrani Mungu baba kupitia Yeye.

18Wake, wanyenyekeeni waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana.19Nanyi waume, wapendeni wake zenu, na msiwe wakali dhidi yao.

20Watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote, maana ndivyo impendezavyo Bwana.21Akina baba msiwachokoze watoto wenu, ili kwamba wasije wakakata tamaa.

22Watumwa, watiini mabwana zenu katika mwili kwa mambo yote, sio kwa huduma ya macho kama wapendezao watu tu, bali kwa moyo wa kweli. Mcheni Mungu.23Chochote mfanyacho, fanyeni kutoka nafsini mwenu kama kwa Bwana na si kama kwa wanadamu.24Mnajua ya kwamba mtapokea ujira wa urithi kutoka kwa Bwana. Ni Kristo Bwana mnayemtumikia.25Kwa sababu yeyote atendaye yasiyo haki atapokea hukumu kwa matendo yasiyo haki aliyoyafanya, na hakuna upendeleo.

4

1Mabwana, toeni kwa watumwa mambo yaliyo haki na ya adili. Mnajua pia kwamba mnaye Bwana mbinguni.

2Endeleeni kuwa thabiti katika maombi. Kaeni macho katika hilo kwa shukrani.3Mkituombea pamoja pia, ili kwamba Mungu afungue mlango kwa ajili ya neno, kunena siri ya ukweli ya Kristo. Kwa sababu ya hili nimefungwa minyororo.4Ombeni kwamba niweze kulweka wazi kama inavyonipasa kusema.

5Enenda kwa hekima kwa wale walioko nje, na muukomboe wakati.6Maneno yenu na yawe na neema wakati wote, na yakolee chumvi majira yote, ili kwamba mweze kujua jinsi inavyowapasa kumjibu kila mtu.

7Kwa mambo yanayonihusu mimi, Tikiko atayafanya yajulikane kwenu. Yeye ni ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, na mtumwa mwenzetu katika Bwana.8Namtuma kwenu kwa ajili ya hili, kwamba mweze kujua mambo kuhusu sisi, na pia kwamba aweze kuwatia moyo.9Namtuma pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa mwaminifu, na mmoja wenu. Watawaambia kila kitu kilichotokea hapa.

10Aristarko, mfungwa mwenzangu, anawasalimu, pia na Marko binamu yake na Barnaba mliyepokea utaratibu kutoka kwake, “kama akija kwenu, mpokeeni,”11Na pia Yesu aitwaye Yusto. Hawa peke yao wa tohara ni watendakazi wenzangu kwa ajili ya ufalme wa Mungu. Wamekuwa ni faraja kwangu.12Epafra anawasalimu. Yeye ni mmoja wenu na mtumwa wa Kristo Yesu. Yeye hujitahidi siku zote katika maombi kwa ajili yenu ili kwamba mweze kusimama kwa ukamilifu na kuhakikishwa kikamilifu katika mapenzi yote ya Mungu.13Kwa kuwa ninamshuhudia, kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, kwa hao walioko Laodekia, na kwa hao walioko Hierapoli.14Luka yule tabibu mpendwa, na Dema wanawasalimu.

15Wasalimu ndugu zangu walioko Laodekia, na Nimfa, na kanisa lile lililoko nyumbani kwake.16Barua hii ikishasomwa kwenu, isomwe pia katika kanisa la walaodekia, nanyi pia hakikisheni mnaisoma ile barua kutoka Laodekia.17Sema kwa Arkipo, “Angalia ile huduma ambayo umeipokea katika Bwana, kwamba unapaswa kuitimiza.”

18Salamu hii ni kwa mkono wangu mwenyewe - Paulo. Ikuumbukeni minyororo yangu. Neema na iwe nanyi.

1 Wathesalonike

1

1Paulo, Silwano na Timotheo kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo. Neema na amani iwe nanyi

2Tunatoa shukrani kwa Mungu kila mara kwa ajili yenu nyote, wakati tunapowataja katika maombi yetu.3Tunaikumbuka bila kukoma mbele ya Mungu na baba yetu kazi yenu ya imani, juhudi ya upendo, na uvumilivu wenye ujasiri kwa ajili ya baadaye katika Bwana Yesu Kristo.4Ndugu Mnaopendwa na Mungu, tunajua wito wenu.5Na jinsi injili yetu ilivyokuja kwenu si kwa neno tu, bali pia katika nguvu, katika Roho Mtakatifu, na katika uhakika. Kwa namna hiyo, mnajua pia sisi tulikuwa watu wa namna gani miongoni mwenu kwa ajili yenu.6Mlikuwa watu wa kutuiga sisi na Bwana, kama mlivyopokea neno katika taabu kwa furaha itokayo kwa Roho Mtakatifu.7Na matokeo yake, mkawa mfano kwa wote katika Makedonia na Akaiya ambao wanaamini.8Kwa kuwa kutoka kwenu neno la Mungu limeenea kote, na si kwa Mekadonia na Akaiya peke yake. Badala yake, kwa kila mahali imani yenu katika Mungu imeenea kote. Na matokeo yake, hatuhitaji kusema chochote.9Kwa kuwa wao wenyewe wanaarifu ujio wetu ulikuwa wa namna gani kati yenu. Wanasimulia jinsi mulivyomgeukia Mungu kutoka katika sanamu na kumtumikia Mungu aliye hai na wa kweli.10Walitoa habari kuwa mnamsubiri Mwana wake kutoka mbinguni, aliyefufuliwa kutoka kwa wafu. Na huyu ni Yesu, anayetuweka huru kutoka kwenye ghadhabu ijayo.

2

1Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua, ndugu, kuwa ujio wetu kwenu haukuwa wa bure.2Mnajua kwamba mwanzoni tuliteseka na walitutenda kwa aibu kule Filipi, kama mujuavyo. Tulikuwa na ujasiri katika Mungu kunena injili ya Mungu hata katika taabu nyingi.3Kwa maana mahusia yetu hayatokani na ubaya, wala katika uchafu, wala katika hila.4Badala yake, kama vile tulivyokubalika na Mungu na kuaminiwa injili, ndivyo tunenavyo. Tunanena, si kwa kuwafurahisha watu, lakini kumfurahisha Mungu. Yeye pekee ndiye achunguzaye mioyo yetu.5Kwa maana hatukutumia maneno ya kujipendekeza wakati wote, kama mjuavyo, wala hatukutumia maneno kama kisingizio kwa tamaa, Mungu ni shahidi wetu.6Wala hatukutafuta utukufu kwa watu, wala kutoka kwenu au kwa wengine. Tungeweza kudai kupendelewa kama mitume wa Kristo.7Badala yake tulikuwa wapole kati yenu kama mama awafarijivyo watoto wake mwenyewe.8Kwa njia hii tulikuwa na upendo kwenu. Tulikuwa radhi kuwashirikisha si tu injili ya Mungu bali pia na maisha yetu wenyewe. Kwa kuwa mlikuwa wapendwa wetu.9Kwa kuwa ndugu, mnakumbuka kazi na taabu yetu. Usiku na mchana tulikuwa tukifanya kazi kusudi tusije tukamlemea yeyote. Wakati huo, tuliwahubiria injili ya Mungu.10Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, ni kwa utakatifu wa namna gani, haki, na bila lawama tulivyoenenda wenyewe mbele yenu mnaoamini.11Vivyo hivyo, mnajua ni kwa namna gani kwa kila mmoja wenu, kama baba alivyo kwa wanawe tulivyowahimiza na kuwatia moyo. Tulishuhudia12kwamba mlipaswa kuenenda kama ulivyo mwito wenu kwa Mungu, aliyewaita kwenye ufalme na utukufu wake.

13Kwa sababu hiyo twamshukuru Mungu pia kila wakati. Kwa kuwa wakati mlipo pokea kutoka kwetu ujumbe wa Mungu mliosikia, mlipokea si kama neno la wanadamu. Badala yake, mlipokea kama kweli ilivyo, neno la Mungu. Ni neno hili ambalo linalofanya kazi kati yenu mnaoamini.14Kwa hivyo ninyi, ndugu, muwe wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyoko katika Uyahudi katika Kristo Yesu. Kwa kuwa ninyi pia mliteseka katika mambo yale yale kutoka kwa watu wenu, kama ilivyo kuwa kutoka kwa wayahudi.15Walikuwa ni Wayahudi ndiyo waliomuua Bwana Yesu pamoja na manabii. Ni Wayahudi ambao walitufukuza tutoke nje. Hawampendezi Mungu na ni maadui kwa watu wote.16Walituzuia tusiseme na Mataifa ili wapate kuokolewa. Matokeo yake ni kwamba wanaendelea na dhambi zao. Mwisho ghadhabu imekuja juu yao.

17Sisi, ndugu, tulikuwa tumetengana nanyi kwa muda mfupi, kimwili, si katika roho. Tulifanya kwa uwezo wetu na kwa shauku kuu kuona nyuso zenu.18Kwa kuwa tulitaka kuja kwenu, mimi Paulo, kwa mara moja na mara nyingine, lakini shetani alituzuia.19Kwa kuwa kujiamini kwetu ni nini, au furaha, au taji ya kujivunia mbele za Bwana wetu Yesu wakati wa kuja kwake? Je si ninyi zaidi kama walivyo wengine?20Kwa kuwa ninyi ni utukufu na furaha yetu.

3

1Kwa hiyo, tulipo kuwa hatuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuwa vema kubaki kule Athene peke yetu.2Tulimtuma Timotheo, ndugu yetu na mtumishi wa Mungu katika injili ya Kristo, kuwaimalisha na kuwafariji kuhusiana na imani yenu.3Tulifanya haya ili kusudi asiwepo yeyote wa kuteteleka kutokana na mateso haya, kwa kuwa wenyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili.4Kwa kweli, wakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitangulia kuwaeleza ya kuwa tulikuwa karibu kupata mateso, na hayo yalitokea kama mjuavyo.5Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwezi kuvumilia tena, nilituma mtu ilikusudi nipate kujua juu ya imani yenu. Huenda mjaribu alikuwa angalau amewajaribu, na kazi yetu ikawa ni bure.

6Lakini Timotheo alikuja kwetu kutokea kwenu na akatuletea habari njema juu ya imani na upendo wenu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu yetu, na kuwa mnatamani kutuona kama ambavyo nasi twatamani kuwaona ninyi.7Kwa sababu hii, ndugu tulifarijika sana na ninyi kwa sababu ya imani yenu, katika taabu na mateso yetu yote.8Kwa sasa tunaishi, kama mkisimama imara kwa Bwana,9Kwani ni shukurani zipi tumpe Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha yote tuliyonayo mbele za Mungu juu yenu?10Tunaomba sana usiku na mchana ili tuweze kuziona nyuso zenu na kuwaongezea kinachopungua katika imani yenu.

11Mungu wetu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia yetu tufike kwenu.12Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi katika pendo, mkipendana na kuwapenda watu wote, kama tunavyowafanyia ninyi.13Na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo yenu iwe bila lawama katika utakatifu mbele za Mungu wetu na Baba yetu katika ujio wa Bwana Yesu pamoja na watakatifu wake wote.

4

1Hatimaye, ndugu, twawatia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maelekezo toka kwetu namna iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kwa njia hiyo pia muenende na kutenda zaidi.2Kwa kuwa mwajua ni maelekezo gani tuliyowapa kupitia Bwana Yesu.

3Kwa kuwa haya ndiyo mapenzi ya Mungu: utakaso wenu - kwamba muepuke zinaa,4Kwamba kila mmoja wenu anajua namna ya kumiliki mke wake mwenyewe katika utakatifu na heshima.5Usiwe na mke kwa ajili ya tamaa za mwili (kama Mataifa wasiomjua Mungu).6Asiwepo mtu yeyote atakaye vuka mipaka na kumkosea nduguye kwa ajili ya jambo hili. Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye kulipa kisasi kwa mambo yote haya, kama tulivyo tangulia kuwaonya na kushuhudia.7Kwa kuwa Bwana hakutuita kwa uchafu, bali kwa utakatifu.8Kwa hiyo anayelikataa hili hawakatai watu, bali anamkataa Mungu, anayewapa Roho wake Mtakatifu.

9Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja ya mtu yeyote kuwaandikia, kwa kuwa mmefundishwa na Mungu kupendana ninyi kwa ninyi.10Hakika, mlifanya haya yote kwa ndugu walioko Makedonia yote, lakini twawasihi, ndugu, mfanye hata na zaidi.11Twawasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu, kama tulivyowaamuru.12Fanya haya ili uweze kuenenda vizuri na kwa heshima kwa hao walio nje ya imani, ili msipungukiwe na hitaji lolote.

13Hatutaki mkose kujua, enyi ndugu, juu ya hao waliolala, ili msije mkahuzunika kama wengine wasio na uhakika kuhusu wakati ujao.14Iwapo tunaamini kuwa Yesu alikufa na akafufuka tena, vivyo hivyo Mungu atawaleta pamoja na Yesu hao waliolala mauti katika yeye.15Kwa ajili ya hayo twawaambia ninyi kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaokuwepo wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wale waliolala mauti.16Kwa kuwa Bwana mwenyewe atashuka toka mawinguni. Atakuja na sauti kuu, pamoja na sauti ya malaika mkuu, pamoja na parapanda ya Mungu, nao waliokufa katika Kristo watafufuka kwanza.17Kisha sisi tulio hai, tuliobaki, tutaungana katika mawingu pamoja nao kumlaki Bwana hewani. Kwa njia hii tutakuwa na Bwana milele.18Kwa hiyo, mfarijiane ninyi kwa ninyi kwa maneno haya.

5

1Sasa, kwa habari ya muda na nyakati, ndugu, hamna haja kuwaandikia.2Kwa kuwa ninyi wenyewe mwajua ya kuwa siku ya Bwana inakuja kama mwizi ajapo usiku.3Pale wasemapo kuna “Amani na usalama,” ndipo uharibifu huwajia ghafla. Ni kama utungu umjiavyo mama mwenye mimba. Hawataepuka kwa njia yeyote.4Lakini ninyi, ndugu hampo kwenye giza hata ile siku iwajie kama mwizi.5Kwa maana ninyi nyote ni wana wa nuru na wana wa mchana. Sisi siyo wana wa usiku au wa gizani.6Hivyo basi, tusilale kama wengine walalavyo. Bali tukeshe na kuwa makini.7Kwa kuwa wanaolala hulala usiku na wanao lewa hulewa usiku.8Kwa kuwa sisi ni wana wa mchana, tuwe makini. Tuvae ngao ya imani na upendo, na, kofia ya chuma, ambayo ni uhakika wa wokovu wa wakati ujao.

9Kwa kuwa Mungu hakutuchagua mwanzo kwa ajili ya gadhabu, bali kwa kupata wokovu kwa njia ya Bwana Yesu Kristo.10Yeye ndiye aliyetufia ili kwamba, tukiwa macho au tumelala, tutaishi pamoja naye.11Kwa hiyo, farijianeni na kujengana ninyi kwa ninyi, kama ambavyo tayari mnafanya.

12Ndugu, twawaomba muwatambue wale wanaotumika miongoni mwenu na wale walio juu yenu katika Bwana na wale wanao washauri.13Tunawaomba pia muwatambue na kuwapa heshima katika upendo kwa sababu ya kazi yao. Muwe na amani miongoni mwenu ninyi wenyewe.

14Twawasihi, ndugu: muwaonye wasio kwenda kwa utaratibu, watieni moyo walio kata tamaa, Wasaidieni walio wanyonge, na muwe wavumilivu kwa wote.15Angalieni asiwepo mtu yeyote anayelipa baya kwa baya kwa mtu yeyote. Badala yake, fanyeni yaliyo mema kwa kila mmoja wenu na kwa watu wote.

16Furahini siku zote.17Ombeni bila kukoma.18Mshukuruni Mungu kwa kila jambo, kwa sababu hayo ndiyo mapenzi ya Mungu kwenu katika Yesu Kristo.

19Msimzimishe Roho.20Msiudharau unabii.21Yajaribuni mambo yote. Mlishike lililo jema.22Epukeni kila mwonekano wa uovu.

23Mungu wa amani awakamilishe katika utakatifu. Roho, nafsi na mwili vitunzwe pasipo mawaa katika kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo.24Yeye aliyewaita ni mwaminifu, naye ndiye mwenye kutenda.

25Ndugu, tuombeeni pia.26Wasalimuni ndugu wote kwa busu takatifu.27Nawasihi katika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu wote.28Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi.

2 Wathesalonike

1

1Paulo, Silwano, na Timotheo, kwa kanisa la Wathesalonike katika Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.2Neema na iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

3Imetupasa sisi kumshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu, ndugu. Maana hivi ndivyo itupasavyo, kwa kuwa imani yenu inakua sana, na upendo wenu kwa kila mtu unazidi kuongezeka.4Hivyo sisi wenyewe tunaongea kwa fahari juu yenu katika makanisa ya Mungu. Tunazungumza habari ya saburi yenu na imani mliyo nayo katika mateso yote. Tunaongea kwa habari ya mateso mnayostahimili.

5Hii ndiyo ishara ya hukumu ya haki ya Mungu. Matokeo ya haya ni kuwa ninyi mhesabiwe kuwa mwastahili kuuingia ufalme wa Mungu ambao kwa ajili yake mnateswa.6Kwa kuwa ni haki kwa Mungu kuwalipa mateso wale wawatesao ninyi,7na kuwapa raha ninyi mteswao pamoja nasi. Atafanya hivi wakati wa kufunuliwa kwake Bwana Yesu kutoka mbinguni pamoja na malaika wa uweza wake.8Katika mwali wa moto atawalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu na wao wasioitii injili ya Bwana wetu Yesu.9Watateseka kwa maangamizi ya milele wakiwa wametengwa na uwepo wa Bwana na utukufu wa nguvu zake.10Atafanya wakati atakapokuja ili kutukuzwa na watu wake na kustaajabishwa na wote walioamini. Kwa sababu ushuhuda wetu kwenu ulisadikiwa kwenu.

11Kwa sababu hii twawaombea ninyi siku zote. Twaomba kwamba Mungu wetu awahesabu kuwa mlistahili kuitwa. Twaomba kwamba apate kutimiza kila haja ya wema na kila kazi ya imani kwa nguvu.12Tunaomba mambo haya ili mpate kulitukuza jina la Bwana Yesu. Tunaomba kwamba mpate kutukuzwa naye, kwa sababu ya neema ya Mungu na ya Bwana Yesu Kristo.

2

1Sasa kuhusu kuja kwa Bwana wetu Yesu Kristo na kukusanywa pamoja ili tuwe naye: tunawaomba ninyi ndugu zetu,2kwamba msisumbuliwe wala kutaabishwa kwa urahisi, kwa roho, au kwa ujumbe au kwa barua inayoonekana kuwa imetoka kwetu, ikisema ya kuwa siku ya Bwana tayari imekuja.3Mtu na asiwadanganye kwa namna yoyote. Kwa kuwa haitakuja mpaka lile anguko litokee kwanza na mtu wa uasi afunuliwe, yule mwana wa uharibifu.4Huyu ndiye apingaye naye hujiinua mwenyewe akimpinga Mungu na chochote kinachoabudiwa. Na matokeo yake, hukaa kwenye hekalu la Mungu na kujionyesha yeye kuwa kama Mungu.5Je, hamkumbuki kuwa nilipokuwa nanyi niliwaambia juu ya mambo haya?

6Sasa mnajua kile kinachomzuia, ili kwamba aweze kufunuliwa kwa wakati sahihi utakapowadia.7Kwa kuwa siri ya yule mtu mwenye kuasi inafanya kazi mpaka sasa, ila tu kuna anaye mzuia sasa mpaka atakapotolewa njiani.8Ndipo yule mwenye kuasi atakapofunuliwa, amabaye Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake. Bwana atamfanya kuwa si chochote kwa ufunuo wa ujio wake.

9Ujio wa yule mwenye kuasi utakuwa kwa sababu ya kazi ya shetani kwa nguvu zote, ishara na maajabu ya uongo,10na uongo wote wenye udhalimu. Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea, kwa sababu hawakuupokea upendo wa kweli kwa ajili ya kuokolewa kwao.11Kwa sababu hiyo Mungu anawatumia kazi yenye uovu ili waamini uongo.12Matokeo yake ni kwamba wote watahukumiwa, wale ambao hawakuamini ukweli bali wao hujifurahisha katika udhalimu.

13Lakini inatupasa tumshukuru Mungu kila mara kwa ajili yenu ndugu mpendwao na Bwana. Kwa sababu Bwana aliwachagua ninyi kama malimbuko ya wokovu kwa utakaso wa Roho na imani katika ile kweli.14Hiki ndicho alichowaitieni ninyi, kwamba kupitia injili muweza kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo.

15Kwa hiyo, ndugu, simameni imara. Ueleweni ule utamaduni mliofundishwa, kwa neno au kwa barua yetu.

16Sasa, Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu aliyetupenda na kutupa faraja ya milele na ujasiri mwema kwa ajili ya maisha yajayo kupitia neema,17awafariji na kuifanya imara mioyo yenu katika kila neno na kazi njema.

3

1Na sasa, ndugu, tuombeeni, kwamba neno la Bwana liweze kuenea na kutukuzwa, kama ilivyo pia kwenu.2Ombeni kwamba tuweze kuokolewa kutoka katika uovu na watu waasi, kwa kuwa si wote wana imani.

3Lakini Bwana ni mwaminifu, ambaye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutoka kwa yule mwovu.4Tunaujasiri katika Bwana kwa ajili yenu, kwamba mnatenda na mtaendelea kutenda mambo ambayo tunawaagiza.5Bwana aweze kuongoza mioyo yenu katika upendo na katika uvumilivu wa Kristo.

6Sasa tunawaagiza, ndugu, katika jina la Bwana Yesu Kristo, kwamba mwepuke kila ndugu ambaye anaishi maisha ya uvivu na siyo kwa kutokana na desturi ambazo mlipokea kutoka kwetu.7Kwa kuwa ninyi wenyewe mnajua ni sawa kwenu kutuiga sisi. Hatukuishi miongoni mwenu kama wale ambao hawakuwa na nidhamu.8Na hatukula chakula cha mtu yeyote bila kukilipia. Badala yake, tulifanya kazi usiku na mchana kwa kazi ngumu na kwa shida, ili tusiweze kuwa mzigo kwa yeyote katika ninyi.9Tulifanya hivi si kwa sababu hatuna mamlaka. Badala yake, tulifanya hivi ili tuwe mfano kwenu, ili kwamba mweze kutuiga sisi.10Wakati tulipokuwa pamoja nanyi tuliwaagiza, “Ikiwa mmoja wenu hataki kufanya kazi, na asile.”11Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi wanaenenda kwa uvivu miongoni mwenu. Hawafanyi kazi lakini badala yake ni watu wasio na utaratibu.

12Sasa hao nao tunaagiza na kuwaasa katika Bwana Yesu Kristo, kwamba lazima wafanye kazi kwa utulivu na kula chakula chao wenyewe.

13Lakini ninyi, ndugu, msizimie roho katika kufanya yaliyo sahihi.

14Ikiwa mtu yeyote hataki kutii neno letu katika waraka huu, muwe makini naye na msiwe na ushirika pamoja naye, ili kwamba aweze kuaibika.15Msimchukulie kama adui, lakini mwonyeni kama ndugu.

16Bwana wa amani mwenyewe awape amani wakati wowote katika njia zote. Bwana awe nanyi nyote.17Hizi ni salamu zangu, mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe, ambayo ni alama katika kila waraka. Hivi ndivyo niandikavyo.18Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iweze kuwa nanyi nyote.

1 Timotheo

1

1Paulo, Mtume wa Kristo Yesu, kulingana na amri ya Mungu na Mwokozi wetu Yesu Kristo aliye ujasiri wetu,2kwa Timotheo, mwanangu wa kweli katika imani: Neema, rehema na amani zitokazo kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.

3Kama nilivyokusihi nilipoondoka kwenda Makedonia, ubaki Efeso ili kwamba uweze kuwaamuru watu fulani wasifundishe mafundisho tofauti.4Pia wasisikilize hadithi na orodha za nasaba zisizo na mwisho. Haya husababisha mabishano zaidi kuliko kuwasaidia kuendeleza mpango wa Mungu wa imani.5Basi lengo la agizo hili ni upendo utokao katika moyo safi, katika dhamiri nzuri na katika imani ya kweli.6Baadhi ya watu wamelikosa lengo wakayaacha mafundisho haya na kugeukia mazungumzo ya kipumbavu.7Wanataka kuwa waalimu wa sheria, lakini hawafahamu wanachosema au wanachosisitiza.

8Lakini tunajua kwamba sheria ni njema kama mtu ataitumia kwa usahihi.9Tunajua kuwa, sheria haikutungwa kwa ajili ya mtu mwenye haki, bali kwa ajili ya wavunja sheria na waasi, watu wasio wataua na wenye dhambi, na ambao hawana Mungu na waovu. Imetungwa kwa ajili ya wauao baba na mama zao, kwa ajili ya wauaji wa watu,10kwa ajili ya waasherati, kwa ajili ya watu wazinzi, kwa ajili ya wale wanaoteka watu na kuwafanya watumwa, kwa ajili ya waongo, kwa ajili ya mashahidi wa uongo, na yeyote aliye kinyume na maelekezo ya uaminifu.11Maelekezo haya yanatokana na injili yenye utukufu wa Mungu mwenye kubarikiwa ambayo kwayo nimeaminiwa.

12Ninamshukuru Yesu Kristo Bwana wetu. Alinitia nguvu, kwa kuwa alinihesabu mimi kuwa mwaminifu, na akaniweka katika huduma.13Nilikuwa mtu wa kukufuru, mtesaji na mtu wa vurugu. Lakini nilipata rehema kwa sababu nilitenda kwa ujinga kwa kutoamini.14Lakini neema ya Mungu wetu imejaa imani na upendo ulio katika Kristo Yesu.

15Ujumbe huu ni wa kuaminika na unastahili kupokelewa na wote, ya kuwa Kristo Yesu alikuja duniani kuokoa wenye dhambi, ambao mimi ni mbaya zaidi ya wote.16Lakini kwa sababu hii mimi nilipata rehema ili kwamba ndani yangu mimi, niliyekuwa mwenye dhambi kuliko wote, Kristo Yesu adhihirishe uvumilivu usio na kikomo, ili niwe kielelezo kwa wote watakaomwamini na wapate uzima wa milele.

17Na sasa kwa Mfalme asiye na ukomo, asiyekufa, asiyeonekana, Mungu pekee, iwe heshima na utukufu milele na milele. Amina.18Ninaliweka agizo hili mbele yako Timotheo, mtoto wangu. Nafanya hivi kulingana na unabii uliotolewa hapo kwanza kukuhusu wewe, ili kwamba uhusike katika vita vyema.19Fanya hivyo ili kwamba uwe na imani na dhamiri njema. Baadhi ya watu wameyakataa haya wakaangamiza imani.20Kama vile Himeneyo na Alekizanda, ambao nimempa shetani ili wafundishwe wasikufuru.

2

1Kwa hiyo awali ya yote, nahitaji maombi, na dua, na maombezi, na shukrani vifanyike kwa ajili ya watu wote,2kwa ajili ya wafalme na wote ambao wako kwenye mamlaka, ili kwamba tuweze kuishi maisha ya amani na utulivu katika utauwa wote na heshima.3Hili ni jema na lenye kukubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu.4Yeye hutamani kuwa watu wote waokolewe na wapate kuijua kweli.5Kwa kuwa kuna Mungu mmoja, na kuna mpatanishi mmoja kati ya Mungu na mwanadamu ambaye ni Kristo Yesu.6Alijitoa mwenyewe kama fidia kwa wote, kama ushuhuda kwa wakati muafaka.7Kwa sababu hii, mimi mwenyewe nilifanywa kuwa mjumbe wa injili na mtume. (Nasema kweli. Sisemi uongo). Mimi ni mwalimu wa watu wa Mataifa katika imani na kweli.

8Kwa hiyo, nataka wanaume kila mahali waombe na kuinua mikono mitakatifu bila ghadhabu na mashaka.9Vivyo hivyo, nataka wanawake wajivike mavazi yanayokubalika, kwa heshima na kujizuia. Wasiwe na nywele zilizosukwa, au dhahabu, au Lulu, au mavazi ya gharama kubwa.10Pia nataka wavae mavazi yanayowastahili wanawake wanaokiri uchaji kwa kupitia matendo mema.11Mwanamke na ajifunze katika hali ya utulivu na kwa utii wote.12Simruhusu mwanamke kufundisha, au kuwa na mamlaka juu ya mwanaume bali aishi katika hali ya ukimya.13Kwa kuwa Adamu aliumbwa kwanza, kisha Eva.14Adamu hakudanganywa, lakini mwanamke alidanganywa kabisa katika uasi.15Hata hivyo, ataokolewa kwa kupitia kuzaa watoto, kama wataendelea katika imani na upendo na katika utakaso na akili njema.

3

1Usemi huu ni wakuaminika: Kama mtu anatamani kuwa Msimamizi, anatamani kazi njema.2Kwa hiyo msimamizi ni lazima asiwe na lawama. Ni lazima awe mume wa mke mmoja. Ni lazima awe na kiasi, busara, mwenye utaratibu, mkarimu. Ni lazima awe na uwezo wa kufundisha.3Asiwe anatumia mvinyo, asiwe mgomvi, bali mpole, mwenye amani. Ni lazima asiwe mwenye kupenda fedha.4Inampasa kuwasimamia vema watu wa nyumbani mwake mwenyewe, na watoto wake imewapasa kumtii kwa heshima zote.5Maana ikiwa mtu hajui kuwasimamia watu wa nyumbani mwake mwenyewe, atalileaje kanisa la Mungu?6Asiwe mwamini mpya, ili kwamba asije akajivuna na kuanguka katika hukumu kama yule mwovu.7Lazima pia awe na sifa njema kwa wote walioko nje, ili asije akaanguka kwenye aibu na mtego wa mwovu.

8Mashemasi, vilevile wanapaswa kuwa wenye kustahili heshima, wasiwe wenye kauli mbili. Wasitumie mvinyo kupita kiasi au kuwa na tamaa.9Waweze kuitunza kwa dhamiri safi ile kweli ya imani iliyofunuliwa.10Wawe pia wamethibitishwa kwanza, halafu waweze kuhudumu kwa sababu hawana lawama.11Wanawake vivyo hivyo wawe wenye heshima. Wasiwe wasingiziaji. Wawe na kiasi na waaminifu kwa mambo yote.12Mashemasi ni lazima wawe waume wa mke mmoja. Lazima waweze kuwasimamia vema watoto wao na wa nyumbani mwao.13Kwa kuwa wale wanaotumika vizuri hupata msimamo mzuri na ujasiri mkubwa katika imani iliyo katika Kristo Yesu.

14Ninaandika mambo haya kwako, na ninatumaini kuja kwako hivi karibuni.15Lakini ikiwa nitachelewa, ninaandika ili upate kujua namna ya kuenenda katika nyumba ya Mungu, ambalo ni kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msaada wa kweli.16Na haipingiki kwamba kweli ya Uungu uliyofunuliwa ni mkuu: “Alionekana katika mwili, akathibitishwa na Roho, akaonekana na malaika, akatangazwa miongoni mwa mataifa, akaaminiwa na ulimwengu, na akachukuliwa juu katika utukufu.”

4

1Sasa Roho anasema waziwazi kwamba katika nyakati zijazo baadhi ya watu wataiacha imani na kuwa makini kusikiliza roho zidanganyazo na mafundisho ya kipepo yatakayofundishwa2katika uongo na unafiki. Dhamiri zao zitabadilishwa.3Watawazuia kuoa na kupokea vyakula ambavyo Mungu aliviumba vitumiwe kwa shukrani miongoni mwao waaminio na wenye kuijua kweli.4Kwa sababu kila kitu ambacho Mungu amekiumba ni chema. Hakuna ambacho tunapokea kwa shukrani kinastahili kukataliwa.5Kwa sababu kinatakaswa kupitia neno la Mungu na kwa njia ya maombi.6Kama utayaweka mambo haya mbele ya ndugu, utakuwa mtumishi mzuri wa Yesu Kristo. Kwa sababu umestawishwa kwa maneno ya imani na kwa mafundisho mazuri ambayo umeyafuata.7Lakini zikatae hadithi za kidunia ambazo zinapendwa na wanawake wazee. Badala yake, jifunze mwenyewe katika utaua.8Kwa maana mazoezi ya mwili yafaa kidogo, bali utauwa wafaa sana kwa mambo yote. Hutunza ahadi kwa maisha ya sasa na yale yajayo.9Ujumbe huu ni wakuaminiwa na unastahili kukubaliwa kabisa.10Kwa kuwa ni kwa sababu hii tunataabika na kufanya kazi kwa bidii sana. Kwa kuwa tunao ujasiri katika Mungu aliye hai, ambaye ni Mwokozi wa watu wote, lakini hasa kwa waaminio.11Uyaseme na kuyafundisha mambo haya.

12Mtu yeyote asiudharau ujana wako. Badala yake, uwe mfano kwa wote waaminio, katika usemi, mwenendo, upendo, uaminifu, na usafi.13Mpaka nitakapokuja, dumu katika kusoma, katika kuonya, na katika kufundisha.14Usiipuuze karama iliyomo ndani yako, ambayo ulipewa kupitia unabii, kwa kuwekewa mikono na wazee.15Uyajali mambo haya. Ishi katika hayo ili kukua kwako kuwe dhahiri kwa watu wote. Zingatia sana mwenendo wako na mafundisho.

16Dumu katika mambo haya. Maana kwa kufanya hivyo utajiokoa mwenyewe na wale wanaokusikiliza.

5

1Usimkemee mwanamume mzee. Bali mtie moyo kama baba yako. Uwatiye moyo vijana wa kiume kana kwamba ni ndugu zako.2Uwatie moyo wanawake wazee kama mama zako, na wanawake vijana kama dada zako kwa usafi wote.

3Waheshimu wajane, wale walio wajane kweli kweli.4Lakini kama mjane ana watoto au wajukuu, waache kwanza wajifunze kuonesha heshima kwa watu wa nyumbani mwao wenyewe. Waache wawalipe wazazi wao mema, kwa kuwa hii inapendeza mbele za Mungu.5Lakini mjane kweli kweli ni yule aliyeachwa peke yake. Naye huweka tegemeo lake kwa Mungu. Siku zote hudumu katika sala na maombi usiku na mchana.6Hata hivyo, mwanamke yule aishiye kwa anasa amekufa, ingawaje yu hai.7Na uyahubiri haya mambo ili kwamba wasiwe na lawama.8Ila kama mtu asipowatunza ndugu zake, hususani wale walioko nyumbani mwake, ameikana imani na ni mbaya kuliko mtu asiye amini.

9Basi mwanamke aandikishwe kwenye orodha kama mjane akiwa na umri usiopungua miaka sitini, na ni mke wa mume mmoja.10Lazima awe amejulikana kwa matendo mema, ikiwa ni kwamba amewajali watoto, au ameshakuwa mkarimu kwa wageni, au ameosha miguu ya waaminio, au amewasaidia ambao wamekuwa wakiteswa, au alijitoa kwa kazi yeyote njema.11Lakini kwa wale wajane vijana, kataa kuwaandikisha kwenye orodha ya wajane. Kwa kuwa wakiingia kwenye matamanio ya kimwili yakizidi kule kujitoa kwao kwa Kristo, watataka kuolewa.12Kwa njia hii huingia kwenye hatia kwa kuwa huvunja kujitoa kwao kwa awali.13Na pia huingia kwenye mazoea ya uvivu. Wao huzunguka nyumba kwa nyumba. Si tu kwamba ni wavivu, bali pia huwa wasengenyaji na wenye kuingilia mambo ya wengine. Wao husema mambo wasiyopaswa kuyasema.14Kwa hiyo mimi nataka wanawake vijana waolewe, wazae watoto, wasimamie nyumba zao, ili kutokumpa adui nafasi ya kutushitaki kwa kufanya dhambi.15Kwa sababu baadhi yao wameshamgeukia Shetani.

16Kama mwanamke yeyote aaminiye ana wajane, basi na awasaidie, ili kanisa lisilemewe, ili liweze kuwasaidia wale walio wajane kweli kweli.

17Basi wazee wale watawalao vyema wahesabiwe kuwa wamestahili heshima maradufu, hasa wale wanaojishughulisha na kufundisha neno la Mungu.18Kwa kuwa maandiko yanasema, “Usimfumbe ng'ombe kinywa apurapo nafaka,” na “Mfanya kazi anastahili mshahara wake.”

19Usipokee mashitaka dhidi ya mzee isipokuwa kuna mashahidi wawili au watatu.20Waonye wakosaji mbele ya watu wote ili wengine waliobaki labda wataogopa.

21Nakuagiza kwa dhati mbele ya Mungu, na mbele ya Kristo Yesu, na malaika wateule, kwamba uyatunze maagizo haya bila ubaguzi wowote, na kwamba usifanye jambo lolote kwa upendeleo.

22Usimwekee mtu yeyote mikono haraka. Usishiriki dhambi ya mtu mwingine. Yakupasa kujitunza mwenyewe uwe msafi.23Haikupasi kunywa maji pekee. Badala yake, unywe mvinyo kidogo kwa ajili ya tumbo na magonjwa yako ya mara kwa mara.24Dhambi za baadhi ya watu hujulikana kwa uwazi, na huwatangulia hukumuni. Lakini baadhi ya dhambi hufuata baadaye.25Vivyo hivyo, baadhi ya kazi njema hujulikana kwa uwazi, lakini hata zingine hazitafichika.

6

1Acha wale wote walio chini ya nira kama watumwa wawachukulie mabwana zao kama wenye heshima zote. Wanatakiwa kufanya hivyo ili jina la Mungu na mafundisho yasitukanwe.

2Watumwa wenye mabwana waaminio wasiwadharau kwa sababu wao ni ndugu. Badala yake, wawatumikie zaidi. Kwa sababu mabwana wanaosaidiwa kazi zao ni waamini na wanapendwa. Fundisha na kuyatangaza mambo haya.

3Iwapo mtu fulani anafundisha kwa upotovu na hayapokei maelekezo yetu yenye kuaminika, ambayo ni maneno ya Bwana wetu Yesu Kristo, iwapo hawalikubali fundisho liongozalo kwenye utauwa.4Mtu huyo anajivuna na hajui chochote. Badala yake, ana vurugu na mabishano juu ya maneno. Maneno haya huzaa wivu, ugomvi, matukano, shuku mbaya,5na vurugu za mara kwa mara kati ya watu wenye akili zilizoharibika. Wanaiacha kweli. Wanafikiri kwamba utauwa ni njia ya kuwa matajiri”

6Sasa utauwa na kuridhika ni faida kubwa.7Kwa maana hatukuja na chochote duniani. Wala hatuwezi kuchukua chochote kutoka duniani.8Badala yake, tutosheke na chakula na mavazi.9Sasa hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu, katika mtego. Huanguka katika upumbavu mwingi na tamaa mbaya, na katika kitu chochote kinachowafanya watu wazame katika maangamizi na uharibifu.10Kwa kuwa kupenda fedha ni chanzo cha aina zote za uovu. Watu ambao hutamani hiyo, wamepotoshwa mbali na imani na wamejichoma wenyewe kwa huzuni nyingi.

11Lakini wewe mtu wa Mungu, yakimbie mambo hayo. Fuata haki, utauwa, uaminifu, upendo, ustahimilivu, na upole.12Piga vita vizuri vya imani. Shikilia uzima wa milele ulioitiwa. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba ulitoa ushuhuda mbele ya mashahidi wengi kwa kile kilicho chema.

13Nakupa amri hii mbele za Mungu, anayesababisha vitu vyote kuishi, na mbele ya Yesu Kristo, aliyenena iliyo kweli kwa Pontio Pilato:14itunze amri kwa ukamilifu, pasipo mashaka, hadi ujio wa Bwana wetu Yesu Kristo.15Mungu atadhihirisha ujio wake kwa wakati sahihi- Mungu, Mbarikiwa, nguvu pekee, Mfalme anayetawala, Bwana anayeongoza.16Peke yake anaishi milele na akaaye katika mwanga usiokaribiwa. Hakuna mtu awezaye kumwona wala awezaye kumtazama. Kwake iwe heshima na uweza wa milele. Amina.

17Waambie matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, na wasitumaini katika utajiri, ambao siyo wa uhakika. Badala yake, wanapaswa kumtumaini Mungu. Ambaye hutupatia utajiri wote wa kweli ili tufurahie.18Waambie watende mema, watajirike katika kazi njema, wawe wakarimu, na utayari wa kutoa.19Katika njia hiyo watajiwekea msingi mzuri kwa mambo yajayo, ili kwamba waweze kushika maisha halisi.

20Timotheo, linda kile ulichopewa. Jiepushe na majadiliano ya kipumbavu na mabishano yasiyo na maana ambayo kwa uongo huitwa maarifa.21Baadhi ya watu huyatangaza mambo haya, na hivyo wameikosa imani. Neema na iwe pamoja nawe.

2 Timotheo

1

1Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapenzi ya Mungu, sawasawa na ahadi ya uzima ulio ndani ya Kristo Yesu,2kwa Timotheo, mwanangu mpendwa. Neema iwe kwako, rehema na amani toka kwa Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wetu.

3Ninamshukuru Mungu, ambaye ninamtumikia kwa nia njema kama walivyofanya baba zangu, ninapokukumbuka daima katika maombi yangu, Usiku na mchana4ninatamani kukuona, ili kwamba nijawe na furaha, ninayakumbuka machozi yako.5Nimekuwa nikikumbuka kuhusu imani yako halisi, ambayo hapo kwanza ilikaa kwa bibi yako Loisi na mama yako Yunisi, na nina hakika ya kwamba imani hiyo inakaa ndani yako pia.

6Hii ndiyo sababu nakukumbusha kuchochea karama ya Mungu iliyomo ndani yako kwa njia ya kuwekewa mikono yangu.7Kwa kuwa Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na upendo na moyo wa kiasi.

8Kwa hiyo usiuonee haya ushuhuda kuhusu Bwana wetu, wala wangu mimi Paulo mfungwa wake, Bali ushiriki mateso kwa ajili ya Injili, sawasawa na uweza wa Mungu.9Ni Mungu aliyetuokoa na kutuita kwa wito mtakatifu. Hakufanya hivi kulingana na kazi zetu bali kulingana na neema na mpango wake mwenyewe, Alitupatia mambo haya katika Kristo Yesu kabla ya nyakati kuanza.10Lakini sasa wokovu wa Mungu umekwishafunuliwa kwa kuja kwa mwokozi wetu Kristo Yesu, Ni Kristo aliyeikomesha mauti na kuleta uzima usiokoma kwa nuru ya Injili.11Kwa sababu hiyo nilichaguliwa kuwa mhubiri, mtume na mwalimu.12Kwa sababu hii nateseka pia, lakini sioni haya kwa kuwa namjua yeye niliyekwisha kumuamini, nina hakika kuwa yeye anaweza kukitunza kile nilichokikabidhi kwake hata siku ile.

13Ukumbuke mfano wa ujumbe wa uaminifu uliousikia toka kwangu, pamoja na imani na upendo ulio ndani ya Kristo Yesu.14Yatunze Mambo mazuri aliyokukabidhi Mungu kupitia Roho Mtakatifu aishiye ndani yetu.

15Unajua ya kuwa, wote waishio katika Asia waliniacha, Kwenye kundi hili wamo Figelo na Hemogene.16Bwana airehemu nyumba ya Onesiforo kwa kuwa mara nyingi aliniburudisha na hakuionea aibu minyororo yangu.17Badala yake, alipokuwa Roma alinitafuta kwa bidii na akanipata.18Mungu amjalie kupata rehema kutoka kwake siku ile. Kama alivyonisaidia nilipokuwa Efeso, wewe wajua vyema.

2

1Kwa hiyo, wewe mwanangu, uwe hodari katika neema iliyo ndani ya Kristo Yesu.2Na mambo uliyoyasikia kwangu miongoni mwa mashahidi wengi, uyakabidhi kwa watu waaminifu ambao wataweza kuwafundisha wengine pia.

3Shiriki mateso pamoja nami, kama askari mwema wa Kristo Yesu.4Hakuna askari atumikae wakati huo huo akijihusisha na shughuli za kawaida za maisha haya, ili kwamba ampendeze ofisa wake mkuu.5Pia kama mtu akishindana kama mwanariadha, hatapewa taji asiposhindana kwa kufuata kanuni.6Ni Muhimu kwamba mkulima mwenye bidii awe wa kwanza kupokea mgao wa mazao yake.7Tafakari kuhusu nisemacho, kwa maana Bwana atakupa uelewa katika mambo yote.8Mkumbuke Yesu Kristo, kutoka uzao wa Daudi, ambaye alifufuliwa kutoka kwa wafu. Hii ni kulingana na ujumbe wangu wa Injili,9ambao kwa sababu ya huo ninateswa hata kufungwa minyororo kama mtenda mabaya; Lakini neno la Mungu halifungwi kwa minyororo.10Kwa hiyo, navumilia mambo yote kwa ajili ya wateule, ili kwamba nao pia waupate wokovu ulio katika Kristo Yesu pamoja na utukufu wa milele.11Usemi huu ni wakuaminika: “kama tumekufa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia,
12kama tukivumilia, tutatawala pamoja naye pia, kama tukimkana yeye, naye pia atatukana sisi.
13Kama hatutakuwa waaminifu, yeye atabaki kuwa mwaminifu, maana hawezi kujikana mwenyewe.”

14Endelea kuwakumbusha juu ya mambo haya, Waonye mbele za Mungu, waache kubishana kuhusu maneno. Kwa kuwa hakuna manufaa katika jambo hili. Kutokana na hili kuna uharibifu kwa wale wanaosikiliza.

15Jitahidi kujionesha kuwa umekubalika kwa Mungu kama mtenda kazi asiye na sababu ya kulaumiwa. Litumie neno la kweli kwa usahihi.

16Jiepushe na majadiliano ya kidunia, ambayo si ya dini.17Maneno yao yatasambaa kama donda ndugu. Miongoni mwao ni Himenayo na Fileto.18Hawa ni watu walioukosa ukweli, Wanasema ya kuwa ufufuo tayari umekwishatokea, Wanapindua imani ya baadhi ya watu.19Hata hivyo, msingi imara wa Mungu unasimama, wenye mhuri huu, “Bwana anawajua walio wake, na kila alitajaye jina la Bwana ni lazima ajitenge na udhalimu.”

20Kwenye nyumba ya kitajiri, siyo kwamba vimo vyombo vya dhahabu na shaba tu, Pia kuna vyombo vya miti na udongo. Baadhi ya hivi ni kwa ajili ya matumizi ya heshima na baadhi yake ni kwa matumizi yasiyo ya heshima.21Ikiwa mtu atajitakasa mwenyewe kutoka kwenye matumizi yasiyo ya heshima, yeye ni chombo chenye kuheshimika, ametengwa maalumu, mwenye manufaa kwa Bwana, na ameandaliwa kwa kila kazi njema.22Lakini zikimbie tamaa za ujanani, Ukifuata haki, imani, upendo na amani pamoja na wale wamwitao Bwana kwa moyo safi.

23Lakini ukatae upumbavu na maswali ya kipuuzi, Kwani ukijua ya kuwa huzaa ugomvi.24Mtumishi wa Bwana hapaswi kuwa mgomvi, badala yake inampasa kuwa mpole kwa watu wote, awezaye kufundisha, na mvumilivu.25Ni lazima awaelimishe kwa upole wale wampingao, Yamkini Mungu aweze kuwapatia toba kwa kuifahamu kweli.26Waweze kupata ufahamu tena na kuepuka mtego wa Shetani, baada ya kuwa wametekwa na yeye kwa ajili ya mapenzi yake.

3

1Lakini ufahamu neno hili: katika siku za mwisho kutakuwa na nyakati ngumu.2Kwa sababu watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye majivuno, wenye dhihaka, wasiotii wazazi wao, wasiokuwa na shukurani na waovu.3Wasio na upendo wa asili, wasiotaka kuishi kwa amani na yeyote, wachonganishi, wasingiziaji, wasioweza kujizuia, wenye vurugu, wasiopenda mema.4Watakuwa wasaliti, wakaidi, wenye kujipenda wenyewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.5Kwa nje watakuwa na sura ya ucha Mungu, lakini wakikana nguvu yake; Jiepushe na watu hao.6Kwa kuwa baadhi yao ni wanaume wanaoingia kwenye familia za watu na kushawishi wanawake wajinga, Hawa ni wanawake waliojawa dhambi na wenye kuongozwa na tamaa za kila aina.7Wakijifunza siku zote, lakini kamwe hawawezi kuufikia ufahamu wa ile kweli.8Kama vile ambavyo Yane na Yambre walivyopingana na Musa, Kwa njia hii walimu hawa wa uongo husimama kinyume na kweli; Ni watu walioharibiwa katika fikira zao, wasiokubalika kuhusiana na imani.9Lakini hawataendelea mbali; Kwa kuwa upumbavu wao utawekwa wazi kwa watu wote, kama ulivyokuwa wa wale watu.

10Lakini wewe umeyafuata mafundisho yangu, mwenendo wangu, makusudi yangu, imani yangu, uvumilivu wangu upendo wangu na ustahimilivu wangu,11mateso na maumivu yaliyonipata kule Antiokia, Ikonio na Listra, Bwana aliniokoa katika yote hayo.12Wote wanaotaka kuishi katika maisha ya kumcha Mungu katika Kristo Yesu watateswa.13Watu waovu na wadanganyifu watazidi kuwa waovu zaidi, Watawapotosha wengine. Wao wenyewe wamepotoshwa.14Lakini wewe, dumu katika mambo uliyojifunza na kuyaamini kwa uthabiti, Kwa kuwa unajua umejifunza kwa nani;15Unatambua ya kuwa tangu utotoni mwako uliyajua maandiko matakatifu. Haya yanaweza kukuhekimisha kwa ajili ya wokovu kwa njia ya imani iliyo katika kristo Yesu.16Kila andiko lenye pumzi ya Mungu, Lafaa kwa mafundisho, kwa kuonya watu, kwa kurekebisha makosa, na kwa kufundishia katika haki.17Hii ni kwamba mtu wa Mungu awe kamili, akiwa amepewa nyenzo zote kwa ajili ya kutenda kila kazi njema.

4

1Ninakuagiza mbele za Mungu na Kristo Yesu, atakaye wahukumu walio hai na wafu, na kwa sababu ya kufunuliwa kwake na Ufalme wake:2Lihubiri Neno, Uwe tayari, wakati ufaao na usiofaa. Waambie watu dhambi zao, kemea, onya kwa uvumilivu wote na mafundisho.3Kwa maana wakati utakuja ambao watu watakapoyakataa mafundisho ya kweli, badala yake, watajitafutia walimu wa kufundisha kulingana na tamaa zao.4Wataacha kusikiliza mafundisho ya kweli, na kugeukia hadithi za uongo.5Lakini wewe uwe mwaminifu katika mambo yote, vumilia magumu, fanya kazi ya mhubiri wa Injili; timiza huduma yako.

6Kwa maana mimi tayari nimekwisha kumiminwa, Muda wa kufariki kwangu umewadia.7Nimevipiga vita vilivyo vizuri, Mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.8Taji ya haki imewekwa kwa ajili yangu, ambayo Bwana, anayehukumu kwa haki, atanipa siku ile, na siyo kwangu tu bali pia kwa wote wanaongojea kwa shauku kuonekana kwake.9Jitahidi kuja kwangu haraka.10Kwa kuwa Dema ameniacha Ameupenda ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni amekwenda Galatia, na Tito amekwenda Dalmatia.11Luka tu ndiye yuko pamoja nami. Umchukue Marko, uje naye, kwani yeye ni muhimu kwangu katika huduma.12Nimemtuma Tikiko Efeso.13Lile joho ambalo nililiacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoja na vile vitabu hasa vile vya ngozi.

14Iskanda, mfua chuma alinitendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na matendo yake.15Nawe pia jihadhari naye, kwani aliyapinga sana maneno yetu.

16Katika utetezi wangu wa kwanza, hakuna mtu yeyote aliyesimama pamoja nami, badala yake, kila mmoja aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia.17Lakini Bwana alisimama pamoja nami, akanitia nguvu ili kwamba kupitia kwangu, neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa wapate kusikia. Niliokolewa katika kinywa cha Simba.18Bwana ataniepusha na matendo yote maovu na kuniokoa kwa ajili ya ufalme wake wa mbinguni. Utukufu uwe kwake milele na milele. Amina.

19Msalimie Priska na Akila na nyumba ya Onesiforo.20Erasto alibaki huko Korintho, lakini Trifimo nilimuacha Mileto akiwa mgonjwa.21Fanya hima uje kabla ya kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimu, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu wote.22Mungu awe pamoja na roho yako. Neema iwe pamoja nawe.

Tito

1

1Paulo, mtumishi wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo, kwa ajili ya imani ya wateule wa Mungu na maarifa ya kweli iletayo utauwa,2Wapo katika tumaini la uzima wa milele ambao Munguasiyeweza kusema uongo, aliuahidi tangu milelekabla ya enzi zote za wakati.3Kwa wakati uliofaa alilifunua neno lake katika ujumbe alionipa mimi kuhubirilinipasa kufanya hivi kwa amri ya Mungu mwokozi wetu.4Kwa Tito, mwana wa kweli katika imani yetu tunayoshiriki sote. Neema na amani kutoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo mwokozi wetu.5Kwa sababu hii nalikuacha Krete, ili upate kupanga mambo ambayo bado hayajakamilika na kuweka wakfu wazee wa kanisa kwa kila mji kama nilivyokuagiza.6Mzee wa kanisa lazima asiwe na lawama, mme wa mke mmoja, aliye na watoto waaminifu wasioshuhundiwa mabaya au wasiotii.7Ni muhimu kwa mwangalizi, kama msimamizi wa nyumba ya Mungu, asiwe na lawama. Asiwe mtu mwenye kiburi, hakasiriki haraka, si mraibu wa mvinyo, si mgomvi na asiwe mwenye tamaa.8Badala yake: awe mtu mkarimu, apendaye wema, mwenye busara, mnyoofu, mtakatifu na anayejidhibiti.9Awezaye kushika sana ujumbe wa kuaminika uliofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho ya ukweli na kuwarekebisha wale wanaompinga.

10Kwa kuwa kuna waasi wengi, wanenao matupu na wandanganyao, hasa wale wa tohara. Maneno yao ni ya upuuzi. Wanandanganya na kuwaongoza watu katika upotovu.11Ni lazima kuwazuiawatu kama haoWanafundisha yale wasiopaswa kwa faida za aibu na kuharibu familia zote.12Mmoja wa manabii wao amesema “Wakrete daima ni waongo, wanyama wabaya, walafi wavivu.”13Ushuhuda huu ni kweli. Kwa hiyo warekebishe kwa nguvu, ili kwamba waweze kusema kweli katika imani,14Wewe usijihusishe na hadithi zisizo za kweli za Kiyahudi au amri za watu, ambao hurudisha nyuma ukweli.15Kwa wote walio safi, vitu vyote ni visafi. Bali kwa walioharibika na wasioamini, hakuna kilicho kisafi, lakini akili zao na dhamiri zao zimeharibika.16Wanakiri kumjua Mungu, lakini kwa matendo yao wanamkana. Wao ni machukizo, wasiotii, na wasiofaa kitu kwa kazi yo yote njema.

2

1Lakini wewe, sema yale yanayo ambatana na mafundisho ya kweli.2Wafundishe wanaume wazee kuwa na kiasi, wenye heshima, wenye busara na timamu katika imani, katika upendo, na katika uvumilivu.3Vvyo hivyo, fundisha wanawake wazee kuwa na tabia ya heshima, si wasingiziaji, na wasiwe watumwa wa divai nyingi lakini wawe walimu wa yale yaliyo mema.4Na kufundisha wanawake wadogo kuwapenda waume zao na watoto wao,5kuwa na busara, wasafi, watunzaji wazuri wa nyumba zao, na kuwatii waume zao wenyewe, ili neno la Mungu lisisemwe kuwa mabaya.6Vivyo hivyo, watie moyo vijana wa kiume wawe na busara.7Katika njia zote jionyeshe mwenyewe kama mfano wa matendo mema. Katika mfundisho yako onyesha uadilifu, heshima,8na ujumbe wa ukweli usioweza kukosolewa, ili kwamba yeyote wakupingao waaibishwe kwa sababu hawana ubaya wa kusema juu yetu.9Watumwa na wawatii mabwana zao katika kila kitu, wawafurahishe na sio kubishana nao,10wasiwaibie, bali waonyeshe nia njema yote, ili kwa njia zote wailete sifa mafundisho kumhusu Mungu mwokozi wetu.

11Kwa kuwa neema ya Mungu imeonekana kwa ajili ya wokovu wa watu wote.12Inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia, na kuishi maisha ya kiasi, uadilifu, na utauwa katika zama hizi,13huku tukitazamia kupokea tumaini letu lenye baraka, kuonekana kwa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo.14Yesu alijitoa nafsi kwa ajili yetu ili atukomboe na maasi yote na kujitakasia watu maalum walio na hamu ya kufanya matendo mema.

15Yaseme mambo haya, watie watu moyo kuyatimiza na utoe marekembisho kwa mamlaka yote. Usikubali mtu yeyote akupuuze.

3

1Wakumbushe kunyenyekea kwa watawala na wenye mamlaka, kuwatii na kuwa tayari kwa kila kazi njema.2Wakumbushe kutomtendea mtu yeyoteubayawaepuke majibizano, wawape nafasi watu wengine katika kufanya maamuzi na kuonyesha unyenyekevu kwa watu wote.

3Kwa kuwa hapo awali sisi pia tulikuwa na mawazo potofu na wakaidiwaasi. Tulipotoshwa na kufanywa watumwa wa tamaa na anasa mbalimbali.4Lakini wakati ukarimu wa Mungu mwokozi wetu na upendo wake kwa wanadamu ulipoonekana,5haikuwa kwa matendo yetu ya haki tuliyoitenda, bali alituokoa kwa neema yake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa upya na kufanywa upya kwa Roho Mtakatifu.6Mungu alimwaga Roho Mtakatifu kwa wingi juu yetu kupitia mwokozi wetu Yesu Kristo.7Alifanya hivi ili kwamba, tukiisha kuhesabiwa haki kwa neema yake, tupate kuwa warithi wenye tumaini la uzima wa milele.

8Huu ni ujumbe wa kuaminika. Ninataka myanene mambo haya, ili wale wanaomwamini Mungu wawe waangalifu katika kutenda mema. Mambo haya ni mazuri na yanafaa kwa kila mtu.9Lakini jiepusheni na mijadala ya na nasaba, mashindano na migongano kuhusu sheria. Mambo hayo hayana faida na hayafai.10Mkataeni yeyote anayesababisha migawanyiko kati yenuBaada ya onyo moja ama mawili,11jueni kwamba mtu wa jinsi hiyo ameiacha njia iliyo sahihi na anatenda dhambi na kujihukumu mwenyewe.

12Nitakapomtuma kwako Artema au Tikiko, harakisha uje kwangu huku Nikopoli ambapo nimeamua kukaa kipindi cha baridi.13Fanya kila uwezalo kuwatuma Zena mwanasheria, na Apolo, pasipo kupungukiwa na kitu.14Watu wetu lazima wajifunze kujishughulisha katika kazi nzuri ambazo zinatimiza mahitaji muhimu ili kwamba wasije wakawa wasiozaa matunda.

15Wote walio pamoja nami wanakusalimu. Wasalimie wale wanaotupenda katika imani. Neema na iwe nanyi nyote.

Filemoni

1

1Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na ndugu Timotheo kwa Filemoni, mpendwa rafiki yetu na mtenda kazi pamoja nasi,2na kwa Afia dada yetu, na kwa Arkipas askari mwenzetu, na kwa kanisa lile linalokutana nyumbani kwako.3Neema iwe kwenu na amani itokayo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.

4Wakati wote namshukuru Mungu wangu, ninakutaja katika maombi yangu,5Kwa sababu nasikia kuhusu imani uliyonayo katika Bwana Yesu na upendo ulio nao kwa watakatifu wote.6Ninaomba kwamba ushirika wa imani yenu iwe na ufanisi katika ujuzi wa kila jambo jema lililoko kati yetu katika Kristo.7Kwa kuwa nimekuwa na furaha na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa sababu mioyo ya watakatifu wote imekuwa ikitulizwa nawe.

8Kwa hiyo, ingawa nina ujasiri wote katika Kristo kukuamuru wewe kufanya kile unachoweza kufanya,9lakini kwa sababu ya upendo, badala yake nakusihi - mimi, Paulo niliye mzee, na sasa ni mfungwa kwa ajili ya Kristo Yesu.10Ninakusihi kuhusu mwanangu Onesmo, niliyemzaa katika vifungo vyangu.11Kwa kuwa mwanzoni hakukufaa, lakini sasa anatufaa sote, wewe na mimi.

12Mimi nimemtuma akurudie wewe, aliye moyo wangu hasa.13Nataraji angeendelea kubaki pamoja nami, ili anitumikie badala yako, wakati niko kifungoni kwa ajili ya injili.14Lakini sikutaka kufanya jambo lolote bila ruhusa yako. Nilifanya hivi ili kwamba jambo lolote zuri lisifanyike kwa sababu nilikulazimisha, bali kwa sababu ulipenda mwenyewe kulitenda.15Labda ni sababu alitengwa nawe kwa muda, ilikuwa hivyo ili uwe pamoja naye milele.16Ili kwamba asiwe tena mtumwa, bali bora zaidi ya mtumwa, kama ndugu mpendwa. Yeye ni mpendwa hasa kwangu, na zaidi sana kwako, katika mwili na katika Bwana.

17Na hivyo kama wanichukulia mimi mshirika, mpokee kama ambavyo ungenipokea mimi.18Lakini kama amekukosea jambo lolote, au unamdai kitu chochote, kidai hicho kutoka kwangu.19Mimi Paulo, ninaandika kwa mkono wangu mwenyewe. Mimi nitakulipa pasipo na kukuambia yakua ninakudai wewe binafsi uhai hasa.

20Naamu ndugu, acha nipate faida kutoka kwako katika Bwana; uiburudishe nafsi wangu katika Kristo.

21Nikiwa na imani kuhusu utii wako, nakuandikia nikijua kwamba utafanya hata zaidi ya vile ninavyokuomba.

22Wakati huo huo, andaa chumba cha wageni kwa ajili yangu, kwa kuwa ninatumaini kupitia maombi yako nitarudishwa kwenu.

23Epafra, mfungwa mwenzangu katika Kristo Yesu anakusalimu,24na kama afanyavyo Marko, Aristarko, Dema, Luka, watendakazi pamoja nami.25Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja na roho yako. Amina.

Waebrania

1

1Nyakati zilizopita Mungu alizungumza na mababu zetu kupitia manabii mara nyingi na kwa njia nyingi.2Lakini katika siku hizi tulizonazo, Mungu ameongea nasi kupitia Mwana, ambaye alimweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia yeye pia aliumba ulimwengu.3Mwanawe ni nuru ya utukufu wake, tabia pekee ya asili yake, na anayeendeleza vitu vyote kwa neno la nguvu zake. Baada ya kukamilisha utakaso wa dhambi, aliketi chini mkono wa kulia wa enzi huko juu.

4Amekuwa bora kuliko malaika, kama vile jina alilolirithi lilivyo bora zaidi kuliko jina lao.5Kwa maana ni kwa malaika gani aliwahi kusema, “Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa baba yako?” Na tena, “Nitakuwa baba kwake, naye atakuwa mwana kwangu?”

6Tena, wakati Mungu alipomleta mzaliwa wa kwanza ulimwenguni, husema, “Malaika wote wa Mungu lazima wamwabudu.”

7Kuhusu malaika asema, “Yeye ambaye hufanya malaika zake kuwa roho, na watumishi wake kuwa ndimi za moto.”

8Lakini kuhusu Mwana husema, “Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele. Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya haki.
9Umependa haki na kuchukia uvunjaji wa sheria, kwa hiyo Mungu wako, amekupaka mafuta ya furaha kuliko wenzako.”

10Hapo mwanzo, Bwana, uliweka msingi wa dunia. Mbingu ni kazi za mikono yako.
11Zitatoweka, lakini wewe utaendelea. Zote zitachakaa kama vazi.
12Utazikunjakunja kama koti, nazo zitabadilika kama vazi. Lakini wewe ni yule yule, na miaka yako haitakoma.”

13Lakini ni kwa malaika yupi Mungu alisema wakati wowote, “Keti mkono wangu wa kulia mpaka nitakapowafanya adui zako kuwa kiti cha miguu yako”?

14Je, malaika wote siyo roho zilizotumwa kuwahudumia na kuwatunza wale watakaourithi wokovu

2

1Kwa hiyo ni lazima tuweke kipaumbele zaidi kwa yale tuliyosikia, ili kwamba tusije tukatengwa mbali nayo.2Kwa maana ikiwa ujumbe uliozungumzwa na malaika ni halali, na kila kosa na uasi hupokea adhabu tu,3tutapataje kuepuka kama tusipojali wokovu huu mkuu? —Wokuvu ambao kwanza ulitangazwa na Bwana na kuthibitishwa kwetu na wale waliousikia.4Mungu pia aliuthibitisha kwa ishara, maajabu, na kwa matendo makuu mbalimbali, na kwa zawadi za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake mwenyewe.

5Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika.6Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, “Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze?
7Mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. 1
8Umeweka kila kitu chini ya miguu yake.” Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake.
9Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu.

10Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake.11Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu.12Anasema, “Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko.”

13Tena asema, “Nitaamini katika yeye.” Na tena, “Tazama, hapa nipo na watoto ambao Mungu amenipa.”

14Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vile vile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni Ibilisi.15Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa.16Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abrahamu.17Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu.18Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.


1Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. “Na umemuweka juu ya kazi ya mikono yako.

3

1Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.2Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu.3Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.4Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.5Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao.6Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini.

7Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, kama utasikia sauti yake,8usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani.9Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu.

10Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, ‘Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu.

11Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu.”

12Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai.13Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.14Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.15Kuhusu hili imekwisha kusemwa, “Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi.”

16Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri?17Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani?18Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye?19Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.

4

1Kwa hiyo, tunapaswa kuwa makini ili kwamba kati yenu asiwepo hata mmoja atakayeonekana kushindwa kufikia ahadi endelevu ya kuingia katika pumzika la Mungu.2Kwani tumekuwa na habari njema kuhusu pumziko la Mungu lililotangazwa kwetu kama Waisrael walivyokuwa nayo, lakini ujumbe huo haukuwasaidia wale ambao waliusikia bila kuunganisha imani kwa hilo.3Kwa sisi, ambao tumekwisha amini-sisi ndio miongoni tutakaoingia katika lile pumuziko, Kama inavyosema, “Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia katika pumziko langu.” Alisema hili, ingawa kazi zote alizotengeneza zilikuwa zimekamilika tangu mwanzo wa ulimwengu.4Kwani ameshasema sehemu fulani kuhusu siku ya saba, “Mungu alipumzika siku ya saba katika yote aliyoyafanya.”

5Tena ameshasema, “Hawataingia kwenye pumziko langu.”

6Kwa sababu hiyo, tangu pumziko la Mungu bado ni akiba kwa ajili ya baadhi kuingia, na tangu Waisraeli wengi ambao walisikia habari njema kuhusu pumziko lake hawakuingia kwa sababu ya kutotii,7Mungu aliweka tena siku fulani, iitwayo “Leo.” Yeye aliiongeza siku hii alipozungumza kupitia Daudi, ambaye alisema kwa muda mrefu baada ya yaliyosemwa kwanza, “Leo kama mtasikia sauti yake, msifanye mioyo yenu kuwa migumu.”

8Kwani kama Yoshua aliwapatia pumziko, Mungu asingelisema juu ya siku nyingine.9Kwa hiyo bado kuna Sabato ya pumziko iliyotunzwa kwa ajili ya watu wa Mungu.10Kwani anayeingia katika pumziko la Mungu yeye mwenyewe pia amepumzika kutokana na matendo yake, kama Mungu alivyofanya katika yeye.

11Kwa hiyo tuweni na shauku ya kuingia katika lile pumziko, ili kwamba asiwepo atakayeanguka katika aina ya uasi waliofanya.12Kwa maana neno la Mungu li hai na lina nguvu na lina ukali kuliko upanga wowote wenye makali kuwili. Na huchoma hata kufikia kugawanya nafsi na roho, na viungo kutika ubongo. Na lenye kuweza kufahamu fikra za moyo na nia yake.13Hakuna kilichoumbwa kilichojificha katika uso wa Mungu. Badala yake, kila kitu ni dhahiri na wazi kwa macho ya mmoja ambaye ni lazima tutoe hesabu.

14Baadaye kuwa na kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu Mwana wa Mungu, kwa uimara tushikilie imani zetu.15Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kuhisi huruma kwa ajili udhaifu wetu, lakini yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi, isipokuwa yeye ambaye hakutenda dhambi.16Na tuje kwa ujasiri katika kiti cha enzi cha neema, ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.

5

1Kwani kila kuhani mkuu, aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa watu, amechaguliwa kusimama badala yao katika vitu vinavyohusiana na Mungu, ili aweze kutoa kwa pamoja zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi.2Anaweza kujishughulisha kwa upole na wajinga na wabishi kwa kuwa yeye mwenyewe pia amezungukwa na udhaifu.3Kwa sababu ya hili, ana wajibu wa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake kama afanyavyo kwa dhambi za watu.4Na hakuna mtu achukuaye heshima hii kwa ajili yake mwenyewe, lakini badala yake, lazima aitwe na Mungu, kama alivyokuwa Haruni.5Hata Kristo hakujipa heshima mwenyewe kwa kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Badala yake, Mungu alisema kwake, “Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako.”

6Ni kama asemavyo pia sehemu nyingine, “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.”

7Wakati wa kipindi chake katika mwili, aliomba na kuombea, alimwomba Mungu kwa machozi, kwa yeye awezaye kumwokoa kutoka kwenye kifo. Kwa sababu ya unyenyekevu wake kwa Mungu, alisikiwa.8Ijapokuwa alikua mwana, alijifunza kutii kwa mambo yaliyomtesa.9Alikamilishwa na kwa njia hii alifanyika kwa kila mtu amwaminiye kuwa sababu ya wokovu wa milele,10kwa kutengwa na Mungu kama kuhani Mkuu baada ya zamu ya Melkizedeki.

11Tuna mengi ya kusema kuhusu Yesu, lakini ni vigumu kuwaelezea kwa kuwa ninyi ni wavivu wa kusikia.12Ijapokuwa kwa kipindi hiki mlipaswa kuwa walimu, bado kuna umuhimu wa mtu kuwafundisha mafundisho ya awali ya kanuni za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa na si chakula kigumu.13Kwa kuwa yeyote anywaye maziwa tu hana uzoefu katika ujumbe wa haki, kwa kuwa bado ni mtoto.14Kwa upande mwingine, chakula kigumu ni cha watu wazima, wale ambao kwa sababu ya uzoefu wao katika kutofautisha haki na ubaya wamefundishwa kutambua jema na ovu.

6

1Kwa hiyo, tukiacha tulichojifunza kwanza kuhusu ujumbe wa Kristo, twapaswa kuwa na juhudi kuelekea kwenye ukomavu, tusiweke tena misingi ya toba kutoka katika kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu,2wala misingi ya mafundisho ya ubatizo, na kuwawekea mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele.3Na tutafanya hivi ikiwa Mungu ataruhusu.4Kwa kuwa haiwezekani kwa wale ambao waliipata nuru awali, ambao walionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu,5na ambao walionja uzuri wa neno la Mungu na kwa nguvu za wakati ujao,6na kisha wakaanguka - haiwezekani kuwarejesha tena katika toba. Hii ni kwa sababu wamemsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, wakimfanya kuwa chombo cha dhihaka hadharani.7Kwa kuwa ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake, na ikatoa mazao muhimu kwa hao waliofanya kazi katika ardhi, hupokea baraka kutoka kwa Mungu.8Lakini ikiwa huzaa miiba na magugu, haina tena thamani na ipo katika hatari ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuteketezwa.

9Ijapokuwa tunazungumza hivi, rafiki wapenzi, tunashawishiwa na mambo mazuri yawahusuyo ninyi na mambo yahusuyo wokovu.10Kwa kuwa Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na kwa upendo mliouonesha kwa ajili ya jina lake, katika hili mliwatumikia waamini na bado mngali mnawatumikia.11Na tunatamani sana kwamba kila mmoja wenu aweze kuonesha bidii ile ile mpaka mwisho kwa uhakika wa ujasiri.12Hatutaki muwe wavivu, lakini muwe wafuasi wa wale warithio ahadi kwa sababu ya imani na uvumilivu.

13Kwa maana Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa nafsi yake, kwa kuwa asingeliapa kwa mwingine yeyote aliye mkubwa kuliko yeye.14Alisema, “Hakika nitakubariki, na nitauongeza uzao wako zaidi.”15Kwa njia hii, Abrahamu alipokea kile alichoahidiwa baada ya kusubiria kwa uvumilivu.16Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, na kwao ukomo wa mashindano yote ni kiapo kwa kuyathibitisha.17Wakati Mungu alipoamua kuonesha kwa uwazi zaidi kwa warithi wa ahadi kusudi lake zuri lisilobadilika, alilithibitisha kwa kiapo.18Alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tulioikimbilia hifadhi tupate kutiwa moyo kushikilia kwa nguvu tumaini lililowekwa mbele yetu.19Tunao ujasiri huu kama nanga imara na ya kutegemea ya roho zetu, ujasiri ambao unaingia sehemu ya ndani nyuma ya pazia.20Yesu aliingia sehemu ile kama mtangulizi wetu, akisha kufanyika kuhani mkuu hata milele baada ya utaratibu wa Melkizedeki.

7

1Ilikuwa hivi Melkizedeki, mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Abrahamu akirudi kutoka kuwaua wafalme na akambariki.2Abrahamu alimpa moja ya kumi ya kila kitu alichokuwa amekiteka. Jina lake “Melkizedeki” maana yake “mfalme wa haki” na pia “mflame wa Salemu” ambayo ni “mfalme wa amani.”3Hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku wala mwisho wa maisha yake. Badala yake, anabakia kuhani milele, kama mwana wa Mungu.

4Sasa fikiria jinsi huyu mtu alivyokuwa mkuu. Mzazi wetu Abrahamu alimpa moja ya kumi ya vitu vizuri alivyovichukua vitani.5Na hakika, ukoo wa Walawi waliopokea ofisi za kikuhani walikuwa na amri kutoka kwenye sheria kukusanya moja ya kumi kutoka kwa watu, ambayo ni, kutoka kwa Waisraeli wenzao, pamoja na kwamba wao, pia, ni ukoo kutoka kwa Abrahamu.6Lakini Melkizedeki, ambaye hakuwa wa ukoo kutoka kwa Walawi, alipokea moja ya kumi kutoka kwa Abrahamu, na akambariki, yeye aliyekuwa na ahadi.7Hapo haikataliwi kwamba mtu mdogo hubarikiwa na mkubwa.8Kwa jambo hili mtu apokeaye moja ya kumi atakufa siku moja, lakini kwa jambo jingine mmoja aliyepokea moja ya kumi kwa Abrahamu ikaelezwa kama anayeishi.9Na kwa namna ya kuzungumza, Lawi aliyepokea moja ya kumi, pia alitoa moja ya kumi kwa Abrahamu,10kwa sababu Lawi alikuwa katika viuno vya baba yake Abrahamu wakati Melkizedeki alipokutana na Abrahamu.

11Sasa kama ukamilifu uliwezekana kupitia ukuhani wa Lawi, (hivyo chini yake watu hupokea sheria), kulikuwa na hitaji gani zaidi kwa kuhani mwingine kuinuka baada ya mfumo wa Melkizedeki, na siyo kuitwa baada ya mpangilio wa Haruni?12Kwa hiyo ukuhani ukibadilika, hapana budi sheria nayo kubadilika.13Kwa mmoja ambaye mambo haya yalisemwa kuhusu kabila jingine, kutoka kwake hakuna aliyehudumu madhabahuni.14Sasa ni wazi kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambalo Musa hakutaja kuhusu makuhani.15Na haya tusemayo ni wazi hasa ikiwa kuhani mwingine atatokea kwa mfano wa Melkizedeki.16Kuhani huyu mpya siyo mmoja ambaye amekuwa kuhani juu ya msingi wa sheria zinazohusiana na uzao wa mtu, lakini katika msingi wa nguvu ya maisha yasiyoweza kuharibika.17Hivyo maandiko yanashuhudia kuhusu yeye: “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.”

18Kwa kuwa amri iliyotangulia iliwekwa pembeni kwa sababu ilikuwa dhaifu na haifai.19Hivyo sheria haikufanya chochote kikamilifu. Isipokuwa, kulikuwa na ujasiri mzuri kwa hayo tunamsogelea Mungu.

20Na ujasiri huu mzuri haukutokea pasipo kuzungumzia kiapo, kwa hili makuhani wengine hawakuchukua kiapo chochote.21Lakini Mungu alichukua kiapo wakati aliposema kuhusu Yesu, “Bwana ameapa na hatabadilisha mawazo yake.’ Wewe ni kuhani milele.”

22Kwa hili Yesu pia amekuja kuwa dhamana ya agano bora.

23Kwa hakika, kifo huzuia makuhani kuhudumu milele. Hii ni kwa sababu walikuwapo makuhani wengi, mmoja baada ya mwingine.24Lakini kwa sababu Yesu anaishi milele, ukuhani wake haubadiliki.25Kwa hiyo yeye pia anaweza kwa ukamilifu kukamilisha kuwaokoa wanaomkaribia Mungu kupitia kwake, kwa kuwa yeye anaishi daima kwa kuomba kwa ajili yao.

26Kwa hiyo kuhani mkuu wa namna hii anastahili kwetu. Asiye na dhambi, hatia, msafi, aliyetengwa kutoka kwa wenye dhambi, na amekuwa juu kuliko mbingu.27Yeye hakuwa na uhitaji, mfano wa makuhani wakuu, kutoa dhabihu kila siku, kwanza kwa dhambi yake mwenyewe, na baadaye kwa dhambi za watu. Alifanya hivi mara moja kwa wote, alipojitoa yeye mwenyewe.28Kwa sheria huwateua watu dhaifu kuwa makuhani wakuu, lakini neno la kiapo, lililokuja baada ya sheria, alimteua Mwana, aliyefanywa kuwa mkamilifu milele.

8

1Sasa jambo ambalo tunasema ni hili: tunaye kuhani mkuu aliyekaa chini katika mkono wa kulia wa kiti cha enzi Mbinguni.2Yeye ni mtumishi katika mahali patakatifu, hema la kweli ambalo Bwana ameliweka, siyo mtu yeyote wa kufa.

3Kwa maana kila kuhani mkuu huwekwa kutoa zawadi na dhabihu; kwa hiyo ni muhimu kuwa na kitu cha kutoa.4Sasa kama Kristo alikuwa juu ya nchi, yeye asingekuwa kuhani zaidi ya hapo. Kwa kuwa walikuwa tayari wale waliotoa vipawa kulingana na sheria.5Walihudumu kitu ambacho kilikuwa nakala na kivuli cha vitu vya mbinguni, sawa kama Musa alipoonywa na Mungu wakati alipotaka kujenga hema. “Ona,” Mungu akasema, “kwamba tengeneza kila kitu kulingana na muundo ulioonyeshwa juu ya mlima.”6Lakini sasa Kristo amepokea huduma bora zaidi kwa sababu yeye pia ni mpatanishi wa agano zuri, ambalo limekwisha kuimarishwa kwa ahadi nzuri.

7Hivyo kama agano la kwanza lisingekuwa na makosa, ndipo hakungekuwa na haja kutafuta agano la pili.8Kwa kuwa wakati Mungu alipogundua makosa kwa watu alisema, “Tazama, siku zinakuja,’ asema Bwana, ‘wakati nitakapotengeneza agano jipya pamoja na nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda.
9Halitakuwa kama agano nililofanya pamoja na baba zao siku ambayo niliwachukua kwa mkono kuwaongoza kutoka nchi ya Misri. Kwa kuwa hawakuendelea katika agano langu, nami sikuwajali tena,’ asema Bwana.
10Kwa kuwa hili ndilo agano nitafanya kwa nyumba ya Israeli baada ya siku hizo,’ asema Bwana. ‘Nitaweka sheria zangu mawazoni mwao, na nitaziandika mioyoni mwao. Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
11Hawatafundishana kila mmoja na jirani yake, na kila mmoja na ndugu, yake, akisema, “Mjue Bwana,” hivyo wote watanijua mimi, kutoka mdogo hadi mkubwa wao.
12Hivyo nitaonyesha rehema kwa matendo yao yasiyo ya haki, na sizitazikumbuka dhambi zao tena.”

13Kwa kusema “Mpya,” amelifanya agano la kwanza kuwa kuukuu. Na hilo ambalo amelitangaza kuwa kuukuu liko tayari kutoweka.

9

1Sasa hata agano la kwanza lilikuwa na sehemu ya ibada hapa duniani na taratibu za ibada.2Kwani katika hema kulikuwa na chumba kimeandaliwa, chumba cha nje, paliitwa mahali patakatifu. Katika eneo hili palikuwa na kinara cha taa, meza na mikate ya wonyesho.3Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi.4Mlikuwemo madhabahu ya dhahabu kwa kuvukizia uvumba. Pia mlikuwemo sanduku la agano, ambalo lilikuwa limejengwa kwa dhahabu tupu. Ndani yake kulikuwa na bakuli la dhahabu lenye manna, fimbo ya Haruni iliyoota majani, na zile mbao za mawe za agano.5Juu ya sanduku la agano maumbo ya maserafi wa utukufu wafunika mabawa yao mbele ya kiti cha upatanisho, ambacho kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa kina.

6Baada ya vitu hivi kuwa vimekwisha andaliwa, Makuhani kawaida huingia chumba cha nje cha hema kutoa huduma zao.7Lakini kuhani mkuu huingia kile chumba cha pili pekee mara moja kila mwaka, na pasipo kuacha kutoa dhabihu kwa ajili yake binafsi, na kwa dhambi za watu walizozitenda pasipo kukusudia.8Roho Mtakatifu anashuhudia kwamba, njia ya mahali patakatifu zaidi bado haijafunuliwa kwa vile ile hema la kwanza bado linasimama.9Hili ni kielelezo cha muda huu wa sasa. Vyote zawadi na dhabihu ambavyo vinatolewa sasa haviwezi kukamilisha dhamiri ya anayeabudu.10Ni vyakula na vinywaji pekee vimeunganishwa katika namna ya taratibu za ibada ya kujiosha. Vyote hivi vilikuwa taratibu za kimwili vilivyokuwa vimeandaliwa hadi ije amri mpya itakayowekwa mahali pake.

11Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. Kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa.12Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele.13Kama kwa damu ya mbuzi na mafahari na kunyunyiziwa kwa majivu ya ndama katika hao wasiosafi walitengwa kwa Mungu na kufanya miili yao safi,14Je si zaidi sana damu ya Kristo ambaye kupitia Roho wa milele alijitoa mwenyewe bila mawaa kwa Mungu, kuosha dhamiri zetu kutoka matendo mafu kumtumikia Mungu aliye hai?

15Kwa sababu hiyo, Kristo ni mjumbe wa agano jipya. Hii ndiyo sababu mauti imewaacha huru wote walio wa agano la kwanza kutoka katika hatia ya dhambi zao, ili kwamba wote walioitwa na Mungu waweze kupokea ahadi ya urithi wao wa milele.16Kama kuna agano linadumu, ni lazima kuthibitishwa kwa kifo cha mtu yule aliyelifanya.17Kwani agano linakuwa na nguvu mahali kunatokea mauti, kwa sababu hakuna nguvu wakati mwenye kulifanya akiwa anaishi.18Hivyo hata si lile agano la kwanza lilikuwa limewekwa pasipo damu.19Wakati Musa alipokuwa ametoa kila agizo la sheria kwa watu wote, alichukua damu ya ng'ombe na mbuzi, pamoja na maji, kitambaa chekundu, na hisopo, na kuwanyunyizia gombo lenyewe na watu wote.20Kisha alisema, “Hii ni damu ya agano ambayo Mungu amewapa amri kwenu.”21Katika hali ileile, aliinyunyiza damu juu ya hema na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa huduma ya ukuhani.22Na kulingana na sheria, karibu kila kitu kinatakaswa kwa damu. Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha.

23Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba nakala za vitu vya mbinguni sharti visafishwe kwa hii dhabihu ya wanyama. Hata hivyo, vitu vya mbinguni vyenyewe vilipaswa kusafishwa kwa dhabihu iliyo bora zaidi.24Kwani Kristo hakuingia mahali patakatifu sana palipofanywa na mikono, ambayo ni nakala ya kitu halisi. Badala yake aliingia mbingu yenyewe, mahali ambapo sasa yuko mbele za uso wa Mungu kwa ajili yetu.25Hakuingia kule kwa ajili ya kujitoa sadaka kwa ajili yake mara kwa mara, kama afanyavyo kuhani mkuu, ambaye huingia mahali patakatifu zaidi mwaka baada ya mwaka pamoja na damu ya mwingine,26kama hiyo ilikuwa kweli, basi ingekuwa lazima kwake kuteswa mara nyingi zaidi tangu mwanzo wa ulimwengu. Lakini sasa ni mara moja hadi mwisho wa miaka aliyojifunua kuiondoa dhambi kwa dhabihu yake mwenyewe.27Kama ilivyo kwa kila mtu kufa mara moja, na baada ya hiyo huja hukumu,28ndivyo hivyo Kristo naye ambaye alitolewa mara moja kuziondoa dhambi za wengi, atatokea mara ya pili, si kwa kusudi la kushughulikia dhambi, bali kwa ukombozi kwa wale wamgojeao kwa saburi.

10

1Kwa vile sheria ni kivuli cha mambo mema yajayo, si yale yaliyo halisi. Sheria kamwe haiwezi kuwakamilisha wale ambao wanaomkaribia Mungu kwa njia ya dhabihu zilezile ambazo makuhani waliendelea kutoa mwaka baada ya mwaka.2Au vinginevyo dhabihu hizo zisingeweza kukoma kutolewa? Kwa kigezo hicho waabuduo, wakiwa wamesafishwa mara moja, wasingelikuwa na utambuzi zaidi wa dhambi.3Bali katika dhabihu hizo kuna ukumbusho wa dhambi zilizotendwa mwaka baada ya mwaka.4Kwa kuwa haiwezekani kwa damu ya mafahari na mbuzi kuziondoa dhambi.

5Wakati Kristo alipokuja duniani, alisema, “Hamkutamani matoleo au dhabihu, badala yake, mliandaa mwili kwa ajili yangu.
6Hamkuwa na thamani katika matoleo yote ya kuteketezwa au dhabihu kwa ajili ya dhambi.
7Kisha nilisema, “Ona, hapa ninayafanya mapenzi yako, Mungu, kama ilivyoandikwa kunihusu mimi katika gombo.”

8Alisema kama ilivyo semwa hapo juu: “Hamkutamani dhabihu, matoleo, au sadaka ya kuteketezwa kwa ajili ya dhambi, wala hukuona furaha ndani yake” dhabihu ambazo zinatolewa kulingana na sheria.9Kisha alisema, “Ona, niko hapa kufanya mapenzi yako.” Ameweka pembeni taratibu zilizo za awali ili kuimarisha zile za pili.10Katika taratibu za pili, tumekwisha tengwa kwa Mungu kwa mapenzi yake kupitia kujitoa kwa mwili wa Yesu Kristo mara moja kwa nyakati zote.

11Ni kweli, kila kuhani husimama kwa huduma siku kwa siku, akitoa dhabihu ile ile, ambayo, kwa vyovyote, kamwe isingeweza kuziondoa dhambi.12Lakini baada ya Kristo kutoa dhabihu mara moja kwa dhambi milele yote, aliketi mkono wa kuume wa Mungu,13akisubiri mpaka maadui zake watiwe chini na kufanywa kiti kwa ajili ya miguu yake.14Kwa kuwa kwa njia ya toleo moja amewakamilisha milele wale ambao wametengwa kwa Mungu.15Na Roho Mtakatifu pia ashuhudia kwetu. Kwa kuwa kwanza alisema,
16“Hili ni agano nitakalofanya pamoja nao baada ya siku hizo; asema Bwana: nitaweka sheria zangu ndani ya mioyo yao, na nitaziandika katika akili zao.”

17Kisha alisema, “Hawatazikumbuka tena dhambi na matendo yao mafu.”

18Sasa mahali palipo na msamaha kwa hawa, hakuna tena dhabihu yoyote kwa ajili ya dhambi.

19Kwa hiyo, ndugu, tunao ujasiri wa kuingia mahali patakatifu zaidi kwa damu ya Yesu.20Hiyo ni njia ambayo ameifungua kwa ajili yetu kwa njia ya mwili wake, mpya na hai inayopitia kwenye pazia.21Na kwa sababu tunaye kuhani mkuu juu ya nyumba ya Mungu,22na tumkaribie na moyo wa kweli katika utimilifu wa uhakika wa imani tukiwa na mioyo iliyonyunyiziwa safi kutoka uovu wa dhamiri na kuwa na miili yetu iliyooshwa kwa maji safi.23Basi na tushikilie kwa uthabiti katika ungamo la ujasiri wa tumaini letu, bila ya kugeuka, kwa sababu Mungu aliyeahidi ni mwaminifu.24Na tuzidi kutafakari namna ya kumtia moyo kila mmoja kupenda na matendo mema.25Na tusiache kukusanyika pamoja, kama wafanyavyo wengine. Badala yake, kutiana moyo kila mmoja zaidi na zaidi, kama muonavyo siku inakaribia.

26Kama tukifanya makusudi kuendelea kutenda dhambi baada ya kuwa tumepokea elimu ya ukweli, Dhabihu nyingine ya dhambi haisalii tena.27Badala yake, kuna tarajio pekee la hukumu ya kutisha, na ukali wa moto ambao utawateketeza maadui wa Mungu.28Yeyote ambaye ameikataa sheria ya Musa hufa bila rehema mbele ya ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.29Kiwango gani zaidi cha adhabu unafikiri kinamstahili kila mmoja ambaye amemdharau mwana wa Mungu, yeyote aliyeitendea damu ya agano kama kitu kisicho kitakatifu, damu ambayo kwayo aliiweka wakfu kwa Mungu - yeyote ambaye amemtukana Roho wa neema?30Kwa kuwa tunajua mmoja ambaye aliyesema, “Kisasi ni changu, nitalipa.” Na tena, “Bwana atawahukumu watu wake.”31Ni jambo la kuogofya mtu kuangukia katika mikono ya Mungu aliye hai!

32Lakini kumbuka siku zilizopita, baada ya kutiwa kwenu nuru, ni jinsi gani mliweza kuvumilia maumivu makali.33Mlikuwa mmewekwa wazi katika dhihaka ya matukano na mateso, na mlikuwa washiriki pamoja na wale waliopitia mateso kama hayo.34Kwa kuwa mlikuwa na moyo wa huruma kwa hao waliokuwa wafungwa, na mlipokea kwa furaha adhabu ya urithi wenu, mkijua kwamba ninyi wenyewe mlikuwa na urithi bora na wa kudumu milele.35Kwa hiyo msiutupe ujasiri wenu, ulio na zawadi kuu.36Kwa kuwa mnahitaji uvumilivu, ili kwamba mpate kupokea ambacho Mungu amekiahidi, baada ya kuwa mmekwisha yatenda mapenzi yake.37Kwa kuwa baada ya kitambo kidogo, mmoja anayekuja, atakuja hakika na hatakawia.
38Mwenye haki wangu ataishi kwa imani. Kama atarudi nyuma, sitapendezwa naye.”

39Lakini sisi si kama wale warudio nyuma kwa kuangamia. Badala yake, sisi ni baadhi ya wale tulio na imani ya kuzilinda roho zetu.

11

1Sasa imani ni hakika aliyo nayo mtu wakati atarajiapo kitu fulani kwa ujasiri. Ni hakika ya kitu ambacho bado hakijaonekana.2Kwa sababu hii mababu zetu walithibitika kwa imani yao.3Kwa imani tunafahamu kwamba ulimwengu uliumbwa kwa amri ya Mungu, ili kwamba kile kinachoonekana hakikutengenezwa kutokana na vitu ambavyo vilikuwa vinaonekana.

4Ilikuwa kwa sababu ya imani kwamba Habili alimtolea Mungu sadaka ya kufaa kuliko alivyofanya Kaini. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisifiwa kuwa mwenye haki. Mungu alimsifu kwa sababu ya zawadi alizoleta. Kwa sababu hiyo, Habili bado ananena, ingawa amekufa.

5Ilikuwa kwa imani kwamba Enoko alichukuliwa juu na hakuona mauti. “Hakuonekana, kwa sababu Mungu alimchukua” kwa vile ilinenwa juu yake kuwa alimpendeza Mungu kabla ya kuchukuliwa juu.6Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa kuwa ajaye kwa Mungu lazima aamini kwamba Mungu anaishi na kwamba huwapatia zawadi wale wamtafutao.

7Ilikuwa ni kwa imani kwamba Nuhu, akiwa ameonywa na Mungu kuhusiana na mambo ambayo hayakuwa yameonekana, kwa heshima ya ki Mungu alitengeneza safina kwa ajili ya kuiokoa familia yake. Kwa kufanya hivi, aliuhukumu ulimwengu na akawa mrithi wa haki ambayo huja kupitia imani.

8Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, alipoitwa alitii na kwenda mahali ambapo alipaswa kupokea kama urithi. Alitoka bila kujua mahali gani alikuwa anakwenda.9Ilikuwa ni kwa imani kwamba aliishi katika nchi ya ahadi kama mgeni. Aliishi katika mahema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi wenzake wa ahadi ile ile.10Hii ni kwa sababu alitarajia kuupata mji ambao mwenye kuubuni na mjenzi wake angelikuwa ni Mungu.11Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu, na Sara mwenyewe, walipokea nguvu ya kutunga mimba ingawa walikuwa wazee sana, kwa kuwa walimuona Mungu kuwa mwaminifu, ambaye aliwaahidia mtoto wa kiume.12Kwa hiyo pia kutoka kwa mtu huyu mmoja ambaye alikuwa amekaribia kufa wakazaliwa watoto wasiohesabika. Walikuwa wengi kama nyota za angani na wengi kama mchanga katika ufukwe wa bahari.

13Hawa wote walikufa katika imani pasipo kupokea ahadi. Isipokuwa, wakiwa wameziona na kuzikaribisha kwa mbali, walikiri kwamba walikuwa wageni na wapitaji juu ya nchi.14Kwa wale wasemao mambo kama haya wanaweka bayana kuwa wanatafuta nchi yao wenyewe.15Kwa kweli, kama wangekuwa wakiifikiria nchi ambayo kwayo walitoka, wangelikuwa na nafasi ya kurejea.16Lakini kama ilivyo, wanatamani nchi iliyo bora, ambayo, ni ya kimbingu. Kwa hiyo Mungu haoni aibu kuitwa Mungu wao, kwa kuwa ametayarisha mji kwa ajili yao.

17Ilikuwa ni kwa imani kwamba Ibrahimu baada ya kujaribiwa, alimtoa Isaka. Ndiyo, yeye ambaye alipokea kwa furaha ahadi, alimtoa mwanawe wa pekee,18ambaye juu yake ilinenwa, “Kutoka kwa Isaka uzao wako utaitwa.”19Ibrahimu alijua kwamba Mungu alikuwa na uwezo wa kumfufua Isaka kutoka katika wafu, na kwa kuzungumza kwa lugha ya mafumbo, alimpokea.

20Ilikuwa ni kwa imani kwamba Isaka alimbariki Yakobo na Esau kuhusu mambo yajayo.

21Ilikuwa ni kwa imani Yakobo alipokuwa katika hali ya kufa, alimbariki kila mmoja wa watoto wa Yusufu. Yakobo akaabudu, akiegemea juu ya fimbo yake.22Ilikuwa ni kwa imani Yusufu wakati wake wa mwisho ulipokaribia, alinena juu ya kutoka kwa wana wa Israel Misri na akawaagiza kuchukua pamoja nao mifupa yake.

23Ilikuwa ni kwa imani Musa, alipozaliwa, alifichwa kwa miezi mitatu na wazazi wake kwa sababu walimuona kuwa ni mtoto mchanga aliyekuwa mzuri, na hawakutishwa na amri ya mfalme.24Ilikuwa ni kwa imani Musa, alipokuwa mtu mzima, alikataa kuitwa mtoto wa binti Farao.25Badala yake, alichagua kushiriki mateso pamoja na watu wa Mungu badala ya kufurahia anasa za dhambi kwa kitambo.26Alifikiri aibu ya kumfuata Kristo kuwa ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri kwa kuwa alikaza macho yake katika zawadi ya wakati wake ujao.27Ilikuwa ni kwa imani Musa alitoka Misri. Hakuhofia hasira ya Mfalme, kwa kuwa alivumilia kwa kutazama kwa asiyeonekana.28Ilikuwa ni kwa imani aliishika pasaka na kunyunyiza damu, ili kwamba mharibu wa mzaliwa wa kwanza asiweze kuwagusa wazaliwa wa kwanza wa kiume wa waisrael.

29Ilikuwa ni kwa imani walipita katika bahari ya shamu kama katika nchi kavu. Wakati wamisri walipojaribu kupita, walimezwa.

30Ilikuwa ni kwa imani ukuta wa Yeriko ulianguka chini, baada ya kuuzunguka kwa siku saba.

31Ilikuwa ni kwa imani Rahabu yule kahaba hakuangamia pamoja na wale ambao hawakuwa watiifu, kwa sababu alikuwa amewapokea wapelelezi na kuwahifadhi salama.

32Na niseme nini zaidi? Maana muda hautoshi kusimulia ya Gideoni, Barak, Samsoni, Yeftha, Daudi, Samwel na za manabii,33ambao kupitia imani walizishinda falme, walitenda haki, na wakapokea ahadi. Walizuia vinywa vya simba,34walizima nguvu za moto, walikwepa ncha ya upanga, waliponywa kutoka katika magonjwa, walikuwa mashujaa vitani, na walisababisha majeshi wageni kukimbia.35Wanawake walipokea wafu wao kwa njia ya ufufuo. Wengine waliteswa, bila kukubali kuachwa huru ili kwamba waweze kupata uzoefu wa ufufuo ulio bora zaidi.36Wengine waliteswa kwa dhihaka na kwa vichapo, naam, hata kwa vifungo na kwa kutiwa gerezani.37Walipondwa mawe. Walikatwa vipande kwa misumeno. Waliuawa kwa upanga. Walikwenda kwa ngozi za kondoo na ngozi za mbuzi walikuwa wahitaji, wakiendelea katika maumivu na wakitendewa mabaya38(ambayo ulimwengu haukustahili kuwa nao), wakitangatanga nyikani, milimani, katika mapango na katika mashimo ya ardhini.

39Ingawa watu wote hawa walikubaliwa na Mungu kwa sababu ya imani yao, hawakupokea alichoahidi.40Mungu alitangulia kutupatia kitu kilichobora, ili kwamba bila sisi wasingeweza kukamilishwa.

12

1Kwa hiyo, kwa kuwa tumezungukwa na wingu kubwa la mashaidi, na tutupe kila kitu kinacho tulemea pamoja na dhambi ambayo inatuzingira kwa urahisi. Tupige mbio kwa saburi katika mashindano yaliyowekwa mbele yetu.2Tuyaelekeze macho yetu kwa Yesu, aliye mwanzilishi na mwenye kutimiliza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahmili msalaba, akiidharau aibu yake, na akakaa chini mkono wa kulia wa kiti cha enzi cha Mungu.

3Maana mtafakarini yeye aliye stahimili maneno ya chuki kutoka kwa wenye dhambi, dhidi yake mwenyewe ili kwamba msije mkachoka au kuzimia mioyo yenu.4Hamjataabika au kuteseka mkishindana na dhambi kiasi cha kutoa damu.5Tena mmesahau kule kutiwa moyo ambako kunawaelekeza kama watoto wa kiume: “Mwanangu, usiyachukuwe kwa wepesi marudia ya Bwana, wala usikate tamaa unapo rekebishwa na yeye.”
6Kwa kuwa Bwana humrudi yeyote ambaye anampenda, na humwadhibu kila mwana ambaye humpokea.

7Stahimili majaribu kama kurudiwa. Mungu hushughulika nanyi kama anavyoshughulika na watoto, maana ni mtoto yupi ambaye baba yake hawezi kumrudi?8Lakini kama hakuna kurudiwa, ambako sisi sote tunashiriki, basi ninyi ni haramu na si watoto wake.9Zaidi ya yote, tulikuwa na baba zetu kidunia wa kuturudi, na tuliwaheshimu. Je haitupasi hata zaidi kumtii Baba wa kiroho na kuishi?10Kwa hakika baba zetu walituadhibu kwa miaka michache kama ilivyoonekana sawa kwao, lakini Mungu hutuadhibu kwa faida yetu ili tushiriki utakatifu wake.11Hakuna adhabu inayofurahisha kwa wakati huo. Huwa na maumivu. Hata hivyo, baadaye huzaa tunda la amani ya utauwa kwa wale waliofundishwa nayo.

12Kwa hiyo inueni mikono yenu iliyolegea na kufanya magoti yenu yaliyo dhaifu kuwa yenye nguvu tena;13nyosheni mapito ya nyayo zenu, ili kwamba yeyote aliye mlemavu hataongozwa upotevuni lakini apate kuponywa.14Tafuteni amani na watu wote, na pia utakatifu ambao bila huo hakuna atakayemwona Bwana.15Muwe waangalifu ili kwamba asiwepo atakayetengwa mbali na neema ya Mungu, na kwamba lisije shina la uchungu litakalochipuka na kusababisha shida na kukengeusha wengi.16Angalieni kuwa hakuna zinaa au mtu asiye mtauwa kama vile Esau, ambaye kwa sababu ya mlo mmoja aliuza haki yake ya kuzaliwa.17Kwa kuwa mnajua kwamba baadaye, alipotamani kurithi baraka, alikataliwa, kwa sababu hakupata fursa ya kutubu pamoja na baba yake, hata ingawa alitafuta sana kwa machozi.

18Kwa kuwa hamkuja katika mlima ambao unaweza kuguswa, mlima unaowaka moto, giza, kukatisha tamaa na dhoruba.19Hamkuja kwa sauti za tarumbeta, au kwa maneno yatokanayo na sauti ambayo ilisababisha kila wasikiao wasiombe neno lolote kusemwa kwao.20Kwa kuwa hawakuweza kuvumilia kile kilichoamuliwa: “Ikiwa hata mnyama agusaye mlima, lazima apigwe kwa mawe.”21Ya kutisha zaidi aliyoyaona Musa alisema, “Nimeogopa sana kiasi cha kutetemeka.”22Badala yake, mmekuja mlima Sayuni na katika mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu ya mbinguni, na kwa malaika elfu kumi wanaosherehekea.23Mmekuja katika kusanyiko la wazaliwa wa kwanza wote waliosajiliwa mbinguni, kwa Mungu hakimu wa wote, na kwa roho za watakatifu ambao wamekamilishwa.24Mmekuja kwa Yesu mpatanishi wa agano jipya, na kwa damu iliyonyunyizwa ambayo hunena mema zaidi kuliko damu ya Habili.

25Angalia kuwa usije ukamkataa mmoja ambaye anenaye. Kwa kuwa kama hawakuepuka walipomkataa mmoja aliye waonya duniani, kwa hakika hatutaepuka ikiwa tutageuka mbali kutoka kwa yule atuonyaye kutoka mbinguni.26Kwa wakati huo sauti yake ilitikisa dunia. Lakini sasa ameahidi na kunena, “Bado mara nyingine tena sitatikisa dunia pekee, bali mbingu pia.”27Maneno haya, “Mara moja tena,” inaonyesha kutoweshwa kwa vitu vile vitetemeshwavyo, hivi ni, vitu vile ambavyo vimeumbwa, ili kwamba vile vitu visivyotetemeshwa vibakie.28Kwa hiyo, tupokee ufalme ambao hautetemeshwi, tufurahi katika hali ya kumwabudu Mungu kwa kukubali pamoja na kunyenyekea katika kicho,29kwa maana Mungu wetu ni moto ulao.

13

1Basi upendo wa ndugu na uendelee.2Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua.3Kumbuka wote waliomo gerezani, kana kwamba mulikuwa nao kule pamoja nao, na kama miili yenu ilitendewa kama wao.

4Basi ndoa na iheshimiwe na wote na basi kitanda cha ndoa kifanywe kuwa safi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.5Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanao ridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, “Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi.”

6Basi turidhike ili tusema kwa ujasiri, “Bwana ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?”

7Wafikirieni wale walio waongoza, wale waliongea neno la Mungu kwenu, na kumbukeni matokeo ya mienendo yao; igeni imani zao.8Yesu Kristo ni yeye jana, leo, na ata milele.9Usije ukaongozwa na mafundisho mbalimbali ya kigeni kwani ni vizuri kwamba moyo ujengwe kwa neema, na siyo kwa sheria kuhusu chakula hayo hayatawasaidia wale wanaoishi kwa hayo.

10Tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumika ndani ya hekalu hawana haki ya kula.11Kwa kuwa damu za wanyama, zilizotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi, ililetwa na kuhani mkuu ndani ya sehemu takatifu, lakini miili yao ilichomwa nje ya kambi.12Kwa hiyo Yesu naye aliteseka nje ya lango la mji, hili kwamba kuweka wakfu watu kwa Mungu kupitia damu yake.

13Na kwa hiyo twendeni kwake nje ya kambi, tukizibeba fedheha zake.14Kwani hatuna makao ya kudumu katika mji huu. Badala yake tutafute mji ambao unakuja.

15Kupitia Yesu mnapaswa mara kwa mara kujitoa sadaka ya kumtukuza Mungu, kumsifu kwamba tunda la midomo yetu likiri jina lake.

16Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana.

17Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia.

18Tuombeni, kwani tuna uhakika kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote.19Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni.

20Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele,21Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina.

22Sasa ninakutia moyo, ndugu, kuchukuliana na neno la kutia moyo ambalo kwa ufupi nililiandika kwenu.

23Fahamu kwamba ndugu yetu Timotheo ameshaachiwa huru, ambaye pamoja naye nitawaona kama atakuja hivi karibuni.

24Salimia viongozi wako wote na waumini wote. Wale wanaotoka Italia wanakusalimia.

25Na neema iwe nanyi nyote.

Waraka wa yakobo

1

1Yakobo, mtumwa wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mbili yaliyotawanyika, nawasalimu.

2Hesabuni kuwa ni furaha zaidi, ndugu zangu, mnapopita katika majaribu mbali mbali,3mkijua kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huwapa uvumilivu.4Basi acheni uvumilivu uikamilishe kazi yake, ili kwamba muweze kukomaa kikamilifu, bila kupungukiwa neno lolote.

5Lakini kama mtu kati yenu anahitaji hekima, aiombe kutoka kwa Mungu, ambaye hutoa kwa ukarimu na pasipo kukemea kwa wote wamwombao, na atawapa hekima.6Lakini aombe kwa imani, bila shaka, kwa kuwa mwenye kutia shaka ni kama mawimbi katikati ya bahari, huchukuliwa na upepo na kutupwa huku na huko.7Kwa hakika mtu huyu asifikirie kwamba atapokelewa ombi lake kutoka kwa Bwana;8mtu huyu ana nia mbili, hana msimamo katika njia zake zote.

9Ndugu aliye maskini anapaswa kujivuna katika kusimama kwake juu,10wakati huo huo ndugu aliye tajiri awe na unyenyekevu wake, kwa sababu atatoweka kama ua la kondeni katika shamba.11Jua huchomoza na joto la kuunguza na kukausha mimea, na maua huanguka na uzuri wake hupotea. Vivyo hivyo watu matajiri watachakaa katikati ya kazi zao.

12Amebarikiwa mtu yule anayevumilia majaribu, kwa kuwa baada ya kushinda jaribu hilo, atapokea taji ya uzima, ambayo imeahidiwa kwa wale wampendao Mungu.

13Mtu yeyote hapaswi kusema anapojaribiwa, “Kwamba jaribu hili latoka kwa Mungu,” kwa sababu Mungu hajaribiwi na uovu, na Mungu mwenyewe hamjaribu mtu yeyote.14Bali kila mtu hujaribiwa na tamaa zake mbaya za mambo maovu zinazomshawishi na kumvuta kwenda mbali na Mungu.15Ndipo baada ya tamaa ya dhambi kubeba mimba, dhambi huzaliwa. Dhambi ikiisha kukomaa sawasawa, huishia katika mauti.

16Ndugu zangu wapendwa, msidanganyike.17Kila zawadi iliyo nzuri na kila zawadi iliyokamilika hutoka juu, hushuka chini kutoka kwa Baba wa nuru. Yeye habadilika kama kivuli kibadilikavyo.18Mungu alichagua kutupa sisi uzima kwa Neno la kweli, ili kwamba tuweze kuwa kama uzao wa kwanza miongoni mwa viumbe vyake.

19Mnajua hili, ndugu zangu wapendwa. Kila mmoja anapaswa kuwa mwepesi wa kusikia, siyo mwepesi wa kuongea wala kukasirika,20kwa kuwa hasira ya mwanadamu haiwezi kutenda haki ya Mungu.

21Kwa hiyo wekeni mbali uchafu wa dhambi na ubaya wote ulio mahali popote, na kwa unyenyekevu lipokeeni neno lililopandwa ndani yenu, ambalo lina uwezo wa kuokoa roho zenu.22Litiini neno, msilisikie tu, mkijidanganya nafsi zenu wenyewe.23Kwa kuwa kama yeyote alisikiaye neno bila kulitendea kazi ni sawa na mtu ajiangaliaye uso wake kwenye kioo kama alivyo.24Hujitathimini uso wake, na huenda zake na baada ya muda mfupi husahau anavyofanana.25Bali mtu yule anayeiangalia kwa uangalifu sheria kamili, sheria ya uhuru, na kuendelea kuitii, si kwa sababu yeye ni msikilizaji tu anayesahau, huyu mtu atabarikiwa anapolitenda neno.

26Ikiwa mtu yeyote atafikiri moyoni mwake kuwa ni mtu wa dini, lakini hawezi kuudhibiti ulimi wake, huundanganya moyo wake na dini yake ni bure.27Dini iliyo safi na isiyoharibiwa mbele za Mungu wetu na Baba wa mbinguni ni hii: kuwasaidia yatima na wajane katika mateso yao, na kujilinda e na ufisadi wa dunia.

2

1Ndugu zangu, msiifuate imani ya Bwana Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, kwa kupendelea watu fulani.2Kama mtu fulani akiingia kwenye mikutano yenu amevaa pete za dhahabu na mavazi mazuri, pia akaingia masikini mwenye mavazi machafu,3na mkaonyesha kumjali zaidi yule mwenye mavazi mazuri na kusema, “Tafadhari wewe keti hapa mahali pazuri” lakini mkamwambia yule masikini, “Wewe simama pale,” au “Kaa chini ya miguu yangu.”4Je, hamuhukumiani ninyi wenyewe, na kuwa waamuzi wenye mawazo mabaya?5Sikilizeni, ndugu zangu wapendwa, je, Mungu hakuwachagua watu masikini wa dunia hii kuwa matajiri katika imani na kurithi ufalme wa Mungu aliowaahidia wampendao?6Lakini mmewadharau masikini! Je, sio matajiri wanaowatendea ninyi na sio wao wanaowaburuta ninyi mahakamani?7Je, si matajiri wanaolitukana jina lile zuri la Yesu kristo ambalo kwalo mnaitiwa?8Hivyo, basi kama mwaitimiza ile sheria ya kifalme kama ilivyoandikwa katika maandiko, “Utampenda kila mtu kama wewe mwenyewe unavyojipenda,” mwafanya vyema.9Lakini kama mkipendelea baadhi ya watu, matajiri na wenye vyeo mnatenda dhambi, mwahukumiwa na sheria kuwa ni wavunja sheria.

10Kwa kuwa yeyote anayetii sheria yote, na bado akajikwaa katika jambo moja tu, amekuwa na hatia ya kuvunja sheria yote!11Kwa kuwa Mungu aliyesema, “Usizini,” ndiye pia aliyesema, “Usiue.” Kama hauzini, lakini una uwa, umekwishavunja sheria ya Mungu.

12Kwa hiyo kutii kama wale ambao mko karibu kuhukumiwa na sheria ya uhuru wa kweli.13Kwa kuwa hukumu huja pasipo huruma kwa wale wasio na huruma. Huruma hujitukuza juu ya hukumu.

14Kuna uzuri gani, ndugu zangu, kama mtu anasema ninayo imani kwa Mungu, lakini hana matendo mema? Je, imani hiyo yaweza kumwokoa mtu huyo kutoka kwenye hukumu ya Mungu?15Kama ndugu wa kiume au wa kike ni muhitaji wa mavazi au chakula cha kila siku,16na mmoja wenu akawaambia, “Nendeni kwa amani, mkaote moto na mle vizuri,” lakini hamuwapi mahitaji muhimu ya mwili, hiyo yafaa nini?17Hali kadhalika, imani pekee, kama haina matendo mema, imekufa.

18Lakini mtu fulani anaweza kushindana kusema, “Una imani, na mimi ninayo matendo.” Nionyeshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonyesha imani yangu kwa matendo yangu.19Waamini kuwa kuna Mungu mmoja; uko sahihi. Hata mapepo nayo yanaamini hivyo na kutetemeka.20Je, unataka kujua, ewe mtu mpumbavu, namna ambavyo imani hiyo pasipo matendo mema isivyofaa?21Je, si baba yetu Abrahamualihesabiwa haki kwa matendo alipomtoa mwanawe Isaka juu ya madhabahu?22Mnaona kuwa imani yake ilifanya kazi na matendo yake mema, na kwa matendo yake, imani yake ilifikia kusudio lake.23Maandiko yalitimizwa yasemayo, “Abrahamu alimwamini Mungu, na akahesabiwa kuwa ni mwenye haki.” Hivyo Abrahamu aliitwa rafiki wa Mungu.24Mwaona kuwa kwa matendo mtu huhesabiwa haki, na si kwa imani tu.25Hali kadhalika, Rahabu yule kahaba alihesabiwa haki kwa matendo, alipowakaribisha wajumbe na kuwapeleka kwa barabara nyingine?

26Kwa kuwa kama vile mwili usipokuwa na roho umekufa, vivyo hivyo imani pasipo matendo imekufa.

3

1Ndugu zangu, siyo wengi wenu mnapaswa kuwa walimu, mkijua kwamba tutapokea hukumu kubwa zaidi.2Kwa kuwa wote tunakosea katika njia nyingi. Kama yeyote huwa hajikwai katika maneno yake, huyo ni mtu mkamilifu, aweza kudhibiti mwili wake wote pia.3Sasa kama tunaweka lijamu za farasi katika vinywa vyao wanatutii, na tunaweza kuigeuza miili yao yote.4Tambua pia kwamba meli, ingawa ni kubwa na husukumwa na upepo mkali, inaongozwa kwa usukani mdogo sana kwenda popote anakotaka nahodha.5Vivyo hivyo, ulimi ni kiungo kidogo cha mwili, lakini hujisifia makuu sana. Angalia msitu mkubwa unavyoweza kuwashwa kwa cheche ndogo ya moto!

6Ulimi ni kama moto, ni ulimwengu wa uovu, umewekwa miongoni mwa viungo vya mwili wetu, ambao hunajisi mwili wote na huiweka juu ya moto njia ya maisha, na wenyewe kuchomwa na moto wa kuzimu.7Kila aina ya mnyama wa porini, ndege, kitambaacho na kiumbe cha baharini kinadhibitiwa na wanadamu.8Lakini hakuna mwanadamu hata mmoja ambaye anaweza kudhibiti ulimi; ni uovu usiotulia, umejaa sumu ya kufisha.9Kwa ulimi twamtukuza Bwana na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu ambao wameumbwa kwa mfano wa Mungu.10Katika kinywa hichohicho husema maneno ya baraka na laana. Ndugu zangu mambo haya hayapaswi kuwa hivi.11Je, kisima kimoja huweza kutoa maji matamu na machungu?12Ndugu zangu, Je, mti wa mtini unaweza kuzaa matunda ya mzeituni, au mzabibu unazaa matunda ya mtini? Wala chemchemi ya maji chumvi haitoi maji yasio na chumvi.

13Ni nani miongoni mwenu aliye na hekima na ufahamu? Hebu mtu huyo na aoneshe matendo mema katika kazi zake kwa unyenyekevu utokanao na hekima.14Lakini kama mnao wivu mkali na nia ya ubinafsi mioyoni mwenu, msijivune na kusema uongo mkiupinga ukweli.15Hii siyo hekima ile ishukayo kutoka juu, lakini badala yake ni ya kidunia, si ya kiroho ni ya kipepo.16Kwa kuwa palipo na wivu na ubinafsi upo, kuna vurugu na kila matendo maovu17Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, kisha kupenda amani, upole na ukarimu, yenye kujaa rehema na matunda mema, bila kupendelea watu fulani, na kweli.18Na tunda la haki hupandwa katika amani kwa wale ambao wanatenda mambo ya amani.

4

1Ugomvi na migogoro miongoni mwenu vyatoka wapi? Je, haviinuki kutoka katika tamaa zenu mbaya zinazoleta vita ndani ya washirika wenu?2Mnatamani kile msichokuwa nacho. Mnauwa na mnafukuzia kile msichoweza kuwa nacho. Mnapigana na kugombana, na bado hampati kwa sababu hamumwombi Mungu.3Mnaomba na hampokei kwa sababu mnaomba kwa ajili ya mambo yenu mabaya, ili kwamba muweze kuvitumia kwa tamaa zenu mbaya.

4Enyi wazinzi! Hamjui kwamba urafiki na ulimwengu ni kuwa adui wa Mungu? Kwa hiyo, yeyote aamuaye kuwa rafiki wa ulimwengu hujifanya mwenyewe kuwa adui wa Mungu.5Au mnadhani maandiko hayana maana yasemapo kwamba Roho aliyoweka ndani yetu ana wivu sana kwa ajili yetu?6Lakini Mungu hutoa neema zaidi, ndiyo maana maandiko husema, “Mungu humpinga mwenye kiburi, lakini humpa neema mnyenyekevu.”

7Hivyo basi jitoeni kwa Mungu. Mpingeni ibilisi na yeye atakimbia kutoka kwenu.8Mkaribieni Mungu, na yeye atakaribia karibu nanyi. Safisheni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na takaseni mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.9Huzunikeni, ombolezeni, na kulia! Geuzeni kicheko chenu kuwa huzuni na furaha yenu kuwa maombolezo.10Jinyenyekezeni wenyewe mbele za Bwana, na atawainua juu.

11Msineneane kinyume ninyi kwa ninyi, ndugu. Mtu anenaye kinyume na ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, hunena kinyume na sheria na huihukumu sheria ya Mungu. Mkiihukumu sheria, hamuitii sheria, bali mnaihukumu.12Ni mmoja tu ambaye ni mtoa sheria na hakimu, Mungu, yeye aliye na uwezo wa kuokoa na kuangamiza. Wewe ni nani ambaye unamhukumu jirani yako?

13Sikilizeni, ninyi msemao, “Leo au kesho tutakwenda katika mji huu, na kukaa mwaka huko, na kufanya biashara, na kutengeneza faida.”14Ni nani ajuaye nini kitakachotokea kesho juu ya maisha yenu ninyi? Kwa kuwa mnafanana kama ukungu unaotokea kwa muda mfupi na kisha hupotea.15Badala yake mngepaswa kusema, “kama ni mapenzi ya Bwana, tutaishi na tutafanya hiki au kile.”16Lakini sasa mnajivuna juu ya mipango yenu. Majivuno yote hayo ni uovu.

17Kwahiyo, kwake yeye ajuaye kutenda mema lakini hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

5

1Njoni sasa, enyi mlio matajiri, lieni kwa sauti ya juu kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu.2Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu.3Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani, na uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu na kuangamiza miili yenu kama moto. Mmejiwekea hazina yenu katika siku za mwisho.4Tazameni, malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa mishahara kwa kazi ya kuvuna katika mashamba yenu- wanalia! Na kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimefika masikioni mwa Bwana wa Majeshi.5Mmeishi kwa anasa duniani na kujifurahisha ninyi wenyewe. Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo.6Mmemhukumu na kumuua mwenye haki asiyeweza kuwapinga.

7Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima ahusubiria mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha.8Pia ninyi muwe wavumilivu; kazeni mioyo yenu, kwa sababu kuja kwake Bwana ni karibu.9Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, kusudi msije mkahukumiwa. Tazama, hakimu anasimama mlangoni.10Kwa mfano, ndugu, angalieni mateso na uvumilivu wa manabii walionena katika jina la Bwana.11Tazama, twawaita wale wanaovumilia, “heri.” Mmesikia uvumilivu wa Ayubu, na mnalijua kusudi la Bwana kwa ajili ya Ayubu, ni kwa jinsi gani Bwana amejaa huruma na rehema.

12Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, aidha kwa mbingu ama kwa nchi, au kwa kiapo cha aina nyingine. Bali hebu “ndiyo” yenu na imaanishe “ndiyo” na “hapana” yenu na imaanishe “hapana,” ili kwamba msije kuangukia chini ya hukumu.

13Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Yampasa aombe. Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa.14Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao wazee wa kanisa waombe juu yake, wakimpaka mafuta katika jina la Bwana,15na maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama atakuwa ametenda dhambi, Mungu atamsamehe.16Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana kila mmoja na mwenzake, ili muweze kuponywa. Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa.17Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.18Na Eliya aliomba tena, na mbingu zilimwaga mvua juu ya nchi na nchi ikatoa mavuno.

19Ndugu zangu, kama yeyote miongoni mwenu amepotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha,20hebu na ajue kuwa yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.

1 Petro

1

1Petro, mtume wa Yesu Kristo, kwa wageni waliotawanyika, wateule, kote Ponto Galatia, Kapadokia, Asia, na Bithinia.2Hii ni kutokana na ufahamu wa kimbele wa Mungu Baba, kupitia kazi ya utakaso ya Roho, kwa utiifu na kwa kunyunyuziwa damu ya Yesu Kristo. Neema iwe kwenu, na amani yenu iongezeke.

3Na ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo. Katika ukuu wa rehema yake, alitupa kuzaliwa upya kwa ujasiri wa urithi kupitia ufufuo wa Yesu Kristo kutoka katika wafu,4kwa urithi usioangamia, hautakua na uchafu wala kupungua. Umehihifadhiwa mbinguni kwa ajili yenu.5Kwa uwezo wa Mungu mnalindwa kupitia imani kwa wokovu ambao upo tayari kufunuliwa katika nyakati za mwisho.6Furahini katika hili, ingawaje sasa ni lazima kwenu kujisikia huzuni katika majaribu ya aina mbali mbali.7Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu iharibikayo, ijapokua hiyo inajaribiwa kwa moto kuonekane kuwa kwenye sifa, utukufu, na heshima katika ufunuo wa Yesu Kristo.8Hamjamuona yeye, lakini mnampenda. Hamumuoni sasa, lakini mnaamini katika yeye na mna furaha isiyoweza kuelezeka kwa furaha ambayo imejawa na utukufu.9Sasa mnapokea wenyewe matokeo ya imani yenu, wokovu wa nafsi zenu.

10Manabii walitafuta na kuuliza kwa umakini kuhusu wokovu huu, kuhusu neema ambayo ingekuwa yenu.11Walitafuta kujua ni aina gani ya wokovu ambao ungekuja. Walitafuta pia kujua ni muda gani Roho wa Kristo aliye ndani yao alikuwa anazungumza nini nao. Hii ilikua inatokea wakati alipokuwa anawaambia mapema kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ambao ungemfuata.12Ilifunuliwa kwa manabii kwamba walikua wanayatumikia mambo haya, na si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili yenu - masimulizi ya mambo haya kupitia wale wanaoleta injili kwenu kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni, mambo ambayo hata malaika wanatamani kufunuliwa kwake.

13Kwa hiyo fungeni viuno vya akili zenu. Muwe watulivu katika fikra zenu. Muwe na ujasiri mkamilifu katika neema ambayo italetwa kwenu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo.14Kama watoto watiifu, msifungwe wenyewe na tamaa ambazo mlizifuata wakati mlipokua hamna ufahamu.15Lakini kama vile aliyewaita alivyo mtakatifu, nanyi, pia, muwe watakatifu katika tabia yenu yote maishani.16Kwa kuwa imeandkwa, “Iweni watakatifu, kwa sababu Mimi ni mtakatifu.”

17Na kama mkiita “Baba” yule ahukumuye kwa haki kulingana na kazi ya kila mtu, tumia muda wa safari yako katika unyenyekevu.18Mnafahamu kwamba haikuwa kwa fedha au dhahabu - vitu vinavyoharibika- ambavyo mmekombolewa kutoka kwenye tabia zenu za ujinga ambazo mlijifunza kutoka kwa baba zenu.19Lakini mmekombolewa kwa damu ya heshima ya Kristo, kama ya kondoo asiye na hila wala doa.20Kristo alichaguliwa kabla ya misingi ya dunia, lakini sasa siku hizi za mwisho, amefunuliwa kwenu.21Mnamwamini Mungu kupitia yeye, ambaye Mungu alimfufua toka kwa wafu na ambaye alimpa utukufu ili kwamba imani yenu na ujasiri uwe katika Mungu.

22Mmefanya nafsi zenu kuwa safi kwa utii wa ile kweli, kwa dhumuni la pendo la kidugu lililo na unyofu, hivyo pendaneni kwa bidii toka moyoni.23Mmekwisha zaliwa mara ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, lakini kutoka katika mbegu isiyoharibika, kupitia uzima na neno la Mungu lililosalia.24Kwa maana, “miili yote ni kama majani, na utukufu wake wote ni kama ua la jani. Jani hunyauka, na ua hudondoka,
25lakini neno la Bwana hubakia milele.” Huu ni ujumbe ambao ulitangazwa kama injili kwenu.

2

1Kwa hiyo wekeni pembeni uovu wote, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa.2Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwamba mweze kukua ndani ya wokovu,3kama mmeonja kwamba Bwana ni mwema.

4Njoni kwake aliye jiwe hai linaloishi ambalo limekataliwa na watu, lakini hilo limechaguliwa na Mungu na ni la thamani kwake.5Ninyi pia ni kama mawe yaliyo hai yanayojengwa juu kuwa nyumba ya kiroho, ili kuwa ukuhani mtakatifu ambao hutoa dhabihu za kiroho zinazokubaliwa kwa Mungu kupitia Yesu Kristo.6Andiko husema hivi, “Tazama, nimeweka katika Sayuni jiwe la pembeni, kuu na lililochaguliwa na la thamani. Yeyote aaminiye katika yeye hataona aibu.”

7Hivyo heshima ni yenu kwenu ninyi mnaoamini. Lakini, “jiwe lililokataliwa na wajenzi, hili limekuwa jiwe kuu la pembeni”8na, “jiwe la kujikwaa na mwamba wa kujikwaa.” Wao hujikwaa, wanaolikataa neno, kwa lile ambalo pia walikuwa wameteuliwa kwalo.

9Lakini ninyi ni ukoo uliochaguliwa, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kutangaza matendo ya ajabu ya yule aliyewaita kutoka gizani kuja kwenye nuru yake ya ajabu.10Ninyi kwanza hamkuwa watu, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Ninyi hamkupokea rehema, lakini sasa mmepokea rehema.

11Wapendwa, nimewasihi kama wageni na wasafiri kujinyima kutoka kwenye tamaa mbaya za dhambi, ambazo zinapigana vita na roho zenu.12Mnapaswa kuwa na tabia njema kati ya mataifa, ili kwamba, kama watawasema kama kwamba mmefanya mambo maovu, wataziangalia kazi zenu njema na kumsifu Mungu katika siku ya kuja kwake.

13Tii kila mamlaka ya mwanadamu kwa ajili ya Bwana, ikiwa mfalme kama mkuu,14ikiwa watawala waliotumwa kuwaadhibu watenda mabaya na kuwasifu wale wanaotenda mema.15Kwa kuwa ni mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kufanya mema mwanyamazisha mazungumzo ya kipuuzi ya watu wapumbavu.16Kama watu huru, msiutumie uhuru wenu kama kifuniko kwa maovu, bali muwe kama watumishi wa Mungu.17Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mwogopeni Mungu. Mweshimuni mfalme.

18Watumwa, watiini bwana zenu kwa heshima yote, siyo tu bwana walio wazuri na wapole, lakini pia walio waovu.19Kwa kuwa ni sifa kama yeyote atavumilia maumivu wakati anapoteseka pasipo haki kwa sababu ya dhamiri yake kwa Mungu.20Ni faida gani iliyopo kama mwadumu kutenda dhambi kisha mwendelee kuadhibiwa? Lakini kama mmefanya mema na ndipo mteseke kwa kuhukumiwa, hii ni sifa njema kwa Mungu.21Kwa hili mliitwa, kwa sababu Kristo pia aliteswa kwa ajili yenu, amewaachia mfano kwa ajili yenu kufuata nyayo zake.22Yeye hakufanya dhambi, wala haukuonekana udanganyifu wowote kinywani mwake.
23Wakati yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano, alipoteseka, hakutisha bali alijitoa mwenyewe kwake Yeye ahukumuye kwa haki.
24Yeye mwenyewe alizibeba dhambi zetu katika mwili wake kwenye mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena katika dhambi, na kwamba tuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa kwake ninyi mmepona.
25Wote mliokuwa mkitangatanga kama kondoo aliyepotea, lakini sasa mmerudi kwa mchungaji na mlinzi wa roho zenu.

3

1Kwa njia hii, ninyi ambao ni wake mnapaswa kujitoa kwa waume zenu wenyewe, ili, hata kama baadhi yao hawajalitii neno, kupitia tabia za wake zao wanaweza kuvutwa pasipo neno,2kwa sababu wao wenyewe watakuwa wameiona tabia yenu njema pamoja na heshima.3Hii ifanyike siyo kwa mapambo ya nje—kusuka nywele, vito vya dhahabu, au mavazi ya mtindo.4Lakini badala yake ifanyike kwa utu wa ndani wa moyo, na kuzidi katika uzuri wa unyenyekevu na utulivu wa moyo, ambao ni wa thamani mbele za Mungu.5Kwa kuwa wanawake watakatifu walijipamba wenyewe kwa njia hii. Walikuwa na imani katika Mungu na waliwatii waume zao wenyewe.6Kwa njia hii Sara alimtii Ibrahamu na kumwita yeye “bwana” wake. Ninyi sasa ni watoto wake kama mtafanya yaliyo mazuri na kama hamwogopi mabaya.

7Kwa njia hiyo hiyo, ninyi wanaume mnapaswa kuishi na wake zenu mkijua kuwa wao ni wenzi wa kike dhaifu, mkiwatambua wao kama wapokeaji wenzenu wa zawadi ya uzima. Fanyeni hivi ili kwamba maombi yenu yasizuiliwe.

8Hatimaye, ninyi nyote, muwe na nia moja, wenye huruma, upendo kama ndugu, wanyenyekevu, na wapole.9Msilipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi. Kinyume chake, mwendelee kubariki, kwa sababu hii mliitwa, ili kwamba muweze kurithi baraka.10“Yeye atakaye kupenda maisha na kuona siku njema lazima auzuie ulimi wake kwa mabaya na midomo yake kusema hila.
11Na ageuke na kuacha mabaya na kufanya yaliyo mazuri. Atafute amani na kuifuata.
12Macho ya Bwana humwona mwenye haki na masikio yake husikia maombi yake. Lakini uso wa Bwana uko kinyume cha wale watendao uovu.”

13Ni nani atakayewadhuru ninyi, ikiwa mwatamani lililo zuri?14Lakini kama mkiteseka kwa haki, mmebarikiwa. Msiogope yale ambayo wao wanayaogopa. Msiwe na wasiwasi.15Badala yake, mmuweke Kristo Bwana katika mioyo yenu kama mtakatifu. Kila mara muwe tayari kumjibu kila mtu anayewauliza ninyi kwa nini mna tumaini katika Mungu. Fanyeni hivi kwa upole na heshima.16Muwe na dhamiri njema ili kwamba watu wanaotukana maisha yenu mema katika Kristo waweze kuaibika kwa sababu wanaongea kinyume dhidi yenu kama kwamba mlikuwa watenda maovu.17Ni vizuri zaidi, ikiwa Mungu anatamani, kwamba mwateseka kwa kufanya mema kuliko kwa kufanya mabaya.18Kristo pia aliteseka mara moja kwa ajili ya dhambi. Yeye ambaye ni mwenye haki aliteseka kwa ajili yetu, ambao hatukuwa wenye haki, ili kwamba atulete sisi kwa Mungu. Alikufa katika mwili, lakini alifanywa mzima katika roho.19Katika roho, alikwenda na kuzihubiri roho ambazo sasa ziko kifungoni.20Hazikuwa tiifu wakati uvumilivu wa Mungu ulipokuwa unasubiri wakati wa Nuhu, siku za ujenzi wa safina, na Mungu aliokoa watu wachache—nafsi nane—kutoka katika maji.21Hii ni alama ya ubatizo unaowaokoa ninyi sasa, siyo kama kuosha uchafu kutoka mwilini, lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu, kupitia ufufuo wa Yesu Kristo.22Yeye yuko mkono wa kuume wa Mungu. Alikwenda mbinguni. Malaika, mamlaka, na nguvu lazima vimtii yeye.

4

1Kwa hiyo, kwa sababu Kristo aliteseka katika mwili, jivikeni kwa nia iyo hiyo. Kwa yeyote aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi.2Kwa hiyo, mtu wa namna hiyo, kwa wakati wake uliobaki katika mwili, haishi tena katika tamaa za wanadamu, bali anaishi katika mapenzi ya Mungu.3Kwa muda uliopita umetosha kutenda mambo ambayo wamataifa wanataka kufanya- ufisadi, nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada za sanamu zenye machukizo.4Wanafikiri ni ajabu mnapojiepusha kutenda mambo hayo pamoja nao, hivyo wananena maovu juu yenu.5Watatoa hesabu kwake aliye tayari kuhukumu walio hai na wafu.6Kwa kusudi hili injili ilihubiriwa kwao waliokwisha kufa, kwamba ijapokuwa walikwisha hukumiwa katika miili yao kama wanadamu, ili waweze kuishi kulingana na Mungu katika roho.7Mwisho wa mambo yote unakuja. Kwa hiyo, mwe na ufahamu ulio sahihi, na iweni na nia njema kwa ajili ya maombi yenu.8Kabla ya mambo yote, eweni na bidii katika upendo kwa kila mmoja, kwa kuwa upendo hautafuti kufunua dhambi za wengine.9Onyesheni ukarimu kwa kila mmoja bila kunung'unika.10Kama ambavyo kila mmoja wenu alivyopokea karama, itumieni katika kuhudumiana, kama wasimamizi wema wa karama nyingi zilizotolewa bure na Mungu.11Kama mtu akiongea, na iwe kama mausia ya Mungu, na kama mtu akihudumu, na iwe kama uwezo aliopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila jambo Mungu apate kutukuzwa kupitia Yesu Kristo. Utukufu na uweza vina Yeye milele na milele. Amina.12Wapendwa, msihesabu jaribu ambalo huja kuwajaribu kama kitu kigeni, ingawa kuna kitu kigeni kilichokuwa kinatukia kwenu.13Lakini kwa kadri mnavyozidi kupata uzoefu wa mateso ya Kristo, furahini, ili kwamba mfurahi pia na kushangilia katika ufunuo wa utukufu wake.14Iwapo mmetukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu ya Roho wa utukufu na Roho wa Mungu anakaa juu yenu.15Lakini asiwepo yeyote mwenye kuteswa kama muuaji, mwizi, mtenda maovu, au ajishughulishaye na mambo ya wengine.16Lakini ikiwa mtu anateswa kama Mkristo, asione aibu, bali amtukuze Mungu katika jina hilo.17Kwa kuwa wakati umefika kwa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Na kama inaanzia kwetu, itakuwaje kwa wale wasioitii injili ya Mungu?18Na kama “mwenye haki anaokolewa kupitia magumu, itakuwaje kwa mtu asiyehaki na mwenye dhambi?”

19Kwa hiyo wote wanaoteseka kutokana na mapenzi ya Mungu wakabidhi nafsi zao kwa Muumba mwaminifu ili hali wakitenda mema.

5

1Ninawasihi wazee waliomo miongoni mwenu, mimi, niliye mzee mwenzao na shahidi wa mateso ya Kristo, na ambaye vile vile ni mshirika katika utukufu utakaodhihirika.2Kwa hiyo, ninawatia moyo ninyi wazee, lichungeni kundi la Mungu lililo miongoni mwenu. Liangalieni, sio kwa sababu mnapaswa, lakini kwa sababu mnatamani hivyo, kulingana na Mungu. Liaangalieni, sio kwa kupenda pesa za aibu, lakini kwa kupenda.3Msijifanye mabwana juu ya watu waliyochini ya uangalizi wenu, lakini iweni mfano katika kundi.4Pale Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtaipokea taji ya utukufu isiyopoteza uthamani wake.

5Vilevile, nanyi vijana wadogo, nyenyekeni kwa wakubwa wenu. Ninyi nyote, uvaeni unyenyekevu na kuhudumiana ninyi kwa ninyi, kwani Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa neema wanyenyekevu.

6Kwa hiyo nyenyekeni chini ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kwamba awainue kwa wakati wake.7Mwekeeni fadhaa zenu juu yake, kwa sababu anawajali.

8Iweni na busara, iweni waangalifu. Yule adui yenu, ibilisi, kama simba aungurumaye ananyatia, akisaka mtu wa kumrarua.9Simameni kinyume chake. Kuweni na nguvu katika imani yenu. Mkijua kwamba ndugu zenu walioko ulimwenguni wanapitia mateso kama hayo.10Baada ya kuteseka kwa muda kitambo, Mungu wa neema yote, aliyewaita katika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atawakamilisha, atawaimarisha na kuwatia nguvu.11Enzi iwe kwake milele na milele. Amina.

12Namthamini Silwano kama ndugu mwaminifu, na nimewaandikia ninyi kwa ufupi kupitia kwake. Ninawatia moyo na ninashuhudia kwamba nilichokiandika ni neema ya kweli ya Mungu. Simameni ndani yake.

13Waamini waliloko Babeli, waliochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu, na Marko mwanangu, anawasalimu.14Salimianeni kila mmoja kwa busu la upendo. Na amani iwe kwenu mliondani ya Kristo.

2 Petro

1

1Simon Petro, Mtumwa na Mtume wa Yesu Kristo, Kwa wale walioipokea imani ile ile ya thamani kama tulivyoipokea sisi, imani iliyo ndani ya haki ya Mungu na mwokozi wetu Yesu Kristo.2Neema na amani iwe kwenu; iongezeke kupitia maarifa ya Mungu na Bwana wetu Yesu.

3Kupitia maarifa ya Mungu tumepata mambo yake yote kwa ajili ya uchaji wamaisha, toka kwa Mungu aliyetuita kwa ajili ya uzuri wa utukufu wake.4Kwa njia hii alitutumainishia ahadi kuu za thamani. Alifanya hili ili kutufanya warithi wa asili ya Mungu, kwa kadiri tunavyoendelea kuuacha uovu wa dunia hii.

5Kwa sababu hii, fanyeni bidii kuongeza uzuri wa maarifa kwa njia ya imani yenu.6Kupitia maarifa, kiasi, na kupitia kiasi saburi, na kupitia saburi, utauwa.7Kupitia utauwa upendo wa ndugu na kupitia upendo wa ndugu, upendo.8Kama mambo haya yamo ndani yenu, yakiendelea kukua ndani yenu, basi ninyi hamtakuwa watu msiozaa matunda katika maarifa ya Bwana wetu Yesu Kristo.9Lakini yeyote asiyekuwa na mambo haya, huyaona mambo ya karibu tu; yeye ni kipofu. Amesahau utakaso wa dhambi zake za kale.10Kwa hiyo, ndugu zangu, fanyeni juhudi ili kujihakikishia uteule na wito kwa ajili yenu. Kama mtayafanya haya, hamtajikwaa.11Hivyo mtajipatia nafasi ya kuingilia katika ufalme wa milele wa Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo.

12Kwa hiyo mimi nitakuwa tayari kuwakumbusha mambo haya kila mara, hata kama mnayafahamu, na sasa mmekuwa imara katika kweli.13Nafikiria kuwa niko sahihi kuwaamsha na kuwakumbusha juu ya mambo haya, nikiwa ningali katika mwili huu.14Kwa maana najua kuwa si muda mrefu nitatengwa na mwili wangu, kama Bwana Yesu Kristo alivyonionyesha.15Nitajitahidi kwa bidii kwa ajili yenu ili mkumbuke mambo haya baada ya mimi kuondoka.

16Kwa kuwa sisi hatukufuata hadithi zilizoingizwa kwa ustadi pale tulipowaeleza juu ya nguvu na kujidhihirisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, bali sisi tulikuwa mashahidi wa utukufu wake.17Yeye alipokea utukufu na heshima toka kwa Mungu baba pale sauti iliposikika toka katika utukufu mkuu ikisema, “Huyu ndiye mwanangu, mpendwa wangu ambaye nimependezwa naye.”18Tuliisikia sauti hii ikitokea mbinguni pale tulipokuwa naye kwenye ule mlima mtakatifu.19Tunalo hili neno la unabii lililothibitika, ambalo kwalo mwafanya vyema kulitekeleza. Ni kama taa ing'aayo gizani mpaka kuchapo na nyota za mawio zionekanazo katika mioyo yenu.20Tambueni haya ya kwamba, hakuna unabii unaoandikwa kwa fikra za nabii mwenyewe.21Kwa kuwa hakuna unabii uliokuja kwa mapenzi ya mwanadamu, isipokuwa wanadamu waliwezeshwa na Roho Mtakatifu aliyeongea toka kwa Mungu.

2

1Manabii wa uongo walijitokeza kwa Waisraeli, na walimu wa uongo watakuja pia kwenu. Kwa siri wataleta mafundisho ya uongo nao watamkana Bwana aliyewanunua. Wanajiletea uharibifu wa haraka juu yao wenyewe.2Wengi watafuata njia zao za aibu na kupitia wao wataikufuru njia ya ukweli.3Kwa uchoyo watawandanganya watu wakitumia maneno ya uongo, hukumu yao haitachelewa, uharibifu utawafuata.

4Maana Mungu hakuwaacha malaika waliokengeuka. Bali aliwatupa kuzimu ili wafungwe minyororo mpaka hukumu itakapowajilia.5Wala Mungu hakuuvumilia ulimwengu wa zamani. Bali, alimhifadhi Nuhu, mwenye wito wa haki, pamoja na wengine saba, wakati alipoachila gharika juu ya ulimwengu ulioasi.6Mungu aliihukumu miji ya Sodoma na Gomora kiasi cha kuwa majivu na uharibifu ili iwe mfano kwa ajili ya waovu katika siku za usoni7Lakini alipofanya hilo, alimwokoa Lutu mtu wa haki, aliyekuwa amehuzunishwa na tabia chafu za wasiofuata sheria za Mungu.8Kwa kuwa huyo mtu wa haki, aliyeishi nao siku kwa siku akiitesa nafsi yake kwa ajili ya yale aliyoyasikia na kuyaona.9Kwa hiyo Bwana anajua jinsi ya kuwaokoa watu wake wakati wa mateso na jinsi ya kuwavumilia waovu kwa ajili ya hukumu katika siku ya mwisho.10Kwa hakika huu ndio ukweli kwa wale wanoendelea kuishi katika tamaa za mwili huu na kuyadharau mamlaka. Watu wa jinsi hii wana ujasiri katika dhamiri zao, hawaogopi wenye mamlaka.11Ingawa malaika wana uwezo na nguvu kuliko wanadamu, lakini hawawezi kuleta hukumu dhidi yao kwa Bwana12Lakini hawa wanyama wasio na akili wametengenezwa kwa asili ya kukamatwa na kuangamizwa.13Wanaumizwa kwa ujira wa maovu yao. Mchana kutwa huishi kwa anasa. Wamejaa uchafu na maovu. Hufurahia anasa za udanganyifu wanaposherehekea na wewe.14Macho yao yamefunikwa na uzinzi; hawatosheki kutenda dhambi. Huwalaghai na kuwaangusha waumini wachanga katika dhambi. Wana mioyo iliyojaa tamaa, ni watoto waliolaaniwa.15Wameiacha njia ya kweli. Wamepotoka na wameifuata njia ya Balaam mwana wa Beori, aliyependa kupata malipo ya udhalimu.16Lakini alikemewa kwa ajili ya ukosaji wake. Punda aliyekuwa bubu akiongea katika sauti ya binadamu, alizuia wazimu wa nabii.

17Watu hawa ni kama chemichemi zisizo na maji. Ni kama mawingu yanayopeperushwa na upepo. Wingu zito limehifadhiwa kwa ajili yao.18Huongea kwa majivuno matupu. Huwaangusha watu kwa tamaa ya mwili. Huwalaghai watu wanaojaribu kuwakimbia wale waishio katika ukosaji.19Huwahidi watu uhuru wakati wao wenyewe ni watumwa wa dhambi ya ufisadi. Maana mwanadamu hufanywa kuwa mtumwa wa kile kinachomtawala.20Yeye ajiepushaye na uchafu wa ulimwengu kwa kutumia maarifa ya Bwana na mwokozi Yesu Kristo, na kisha akarudia uchafu huo tena, hali yake huwa mbaya kuliko ile ya mwanzo.21Ingefaa watu hao kama wasingeifahamu njia ya haki kuliko kuifahamu na kisha tena kuziacha amri takatifu walizopewa.22Mithali hii huwa na ukweli kwao. “Mbwa huyarudia matapishi yake. Na nguruwe aliyeoshwa hurudi tena kwenye matope.”

3

1Sasa, ninakuandikia wewe, mpendwa hii barua ya pili ili kukuamsha katika akili,2ili kwamba uweze kukumbuka maneno yaliyosemwa kabla na manabii watakatifu na kuhusu amri ya Bwana wetu na mwokozi kwa kutumia mitume.

3Ujue ili kwanza, kwamba wasaliti watakuja katika siku za mwisho kuwasaliti ninyi, wakienenda sawasawa na matakwa yao.4Na wakisema “Iko wapi ahadi ya kurudi? Baba zetu walikufa, Lakini vitu vyote vilikuwa hivyo tangu mwanzo wa uumbaji.5Wakajifanya kusahau kwamba nchi na mbingu vilianza kutokana na maji na kupitia maji zamani za kale, kwa neno la Mungu,6na kwamba kupitia neno lake na maji yakawa ulimwengu kwa kipindi hicho, ikiwa imejaa maji, iliharibiwa.7Lakini sasa mbingu na dunia zimetunzwa kwa neno hilo hilo kwa ajili ya moto. Vimehifadhiwa kwa ajili ya siku ya hukumu na maangamizi ya watu wasio wa Mungu8Wapendwa, kwamba siku moja kwa bwana ni kama miaka elfu moja. Na miaka elfu moja ni kama siku moja.9Si kwamba Bwana anafanya pole pole kutimiza ahadi, kama inavyofikiriwa kuwa, Lakini yeye ni mvumilivu kwa ajili yenu, yeye hatamani hata mmoja aangamie, Lakini hutamani kutoa muda ili wote wapate kutubu.10Ingawa, siku ya Bwana itakuja kama mwizi, mbingu itapita kwa kupaza kelele. Vitu vitateketezwa kwa moto. Nchi na vitu vyote vilivyomo vitafunuliwa wazi.

11Kwa kuwa vitu vyote vutateketezwa kwa njia hii. Je utakuwa mtu wa aina gani? Uishi kitakatifu na maisha ya kimungu.12Inakupasa kujua na kutambua haraka ujio wa siku ya Mungu. Siku hiyo mbingu itateketezwa kwa moto. Na vitu vitayeyushwa katika joto kali.13Lakini kutokana na ahadi yake, tunasubiri mbingu mpya na nchi mpya, ambapo wenye haki wataishi

14Hivyo wapendwa kwa kuwa tunatarajia vitu hivi, jitahidi kuwa makini na kutolaumika na kuwa na amani pamoja naye.15Na zingatia uvumilivu wa Bwana wetu katika wokovu, kama mpendwa kaka yetu Paulo, alivyowaandikia ninyi, kutokana na hekima ambayo alipewa.16Paulo anaongelea hayo yote katika barua zake, kuna vitu ambavyo ni vigumu kuvielewa. Watu wasio na adabu na uimara wameviharibu vitu hivyo, na kama wanavyofanya kwa maandiko. Kuelekea maangamizi yao.17Hivyo, wapendwa kwa kuwa mnayafahamu hayo. Jilindeni wenyewe ili kwamba msipotoshwe na udanganyifu wa walaghai na kupoteza uaminifu.18Lakini mkue katika neema na ufahamu wa Bwana na mwokozi Yesu Kristo. Na sasa utukufu una yeye sasa na milele. Amina.

1 Yohana

1

1Kile tulichokiona tangu mwanzo, kile tulichokisikia, kile tulichokiona kwa macho yetu, kile tulichokitazama, na mikono yetu imekishika kuhusu Neno la uzima.2Na ule uzima ulifanywa kujulikana wazi na tumeuona, na kuushuhudia, na kuwatangazia uzima wa milele, ambao ulikuwako kwa Baba na ulifanywa kujulikana kwetu.3Kile tulichokiona na kukisikia twakitangaza kwenu, ili kwamba muweze kujumuika pamoja nasi, na ushirika wetu pamoja na Baba na Mwanae Yesu Kristo.4Na tunawaandikia mambo haya ninyi ili kwamba furaha yetu iwe timilifu.

5Huu ndio ujumbe tuliousikia kutoka kwake na kuwatangazia ya kwamba Mungu ni nuru na ndani yake hakuna giza hata kidogo.6Kama tukisema kwamba tunaushirika naye na twatembea gizani, twadanganya na hatutendi kweli.7Lakini tukitembea katika nuru kama alivyo yeye nuruni, Twashirikiana sisi kwa sisi, na damu ya Yesu Kristo, mwanae yatutakasa kutoka dhambini.8Kama tukisema hatuna dhambi, twajidanganya wenyewe, na kweli haimo ndani yetu.9Lakini tukiziungama dhambi zetu, yeye ni mwaminifu na haki kutusamehe dhambi zetu na kututakasa na uovu wote.10Tukisema kwamba hatujatenda dhambi, twamfanya yeye kuwa muongo, na neno lake halimo ndani yetu.

2

1Watoto wangu wapendwa, nawaandikia mambo haya kwenu ili msitende dhambi. Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi, tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Yesu Kristo- ambaye ni mwenye haki.2Yeye ni mpatanishi kwa dhambi zetu, na si kwa dhambi zetu pekee, lakini pia kwa ulimwengu mzima.

3Kwa hili twajua kwamba twamjua yeye, kama tukizitunza amri zake.4Yeye asemaye, “Namjua Mungu,” lakini hazishiki amri zake, ni mwongo, na kweli haimo ndani yake.5Lakini yeyote ashikaye neno lake, kweli katika mtu yule upendo wa Mungu umekamilishwa. Katika hili twajua kwamba tuko ndani yake.6Yeye asemaye anaishi ndani ya Mungu inampasa yeye mwenyewe pia kutembea kama vile Yesu Kristo alivyotembea.

7Wapenzi, siwaandikii ninyi amri mpya, bali amri ya zamani ambayo mmekwisha kuwa nayo tangu mwanzo. Amri ya zamani ni neno ambalo mlilolisikia.8Hata hivyo ninawaandikia ninyi amri mpya, ambayo ni kweli katika Kristo na kwenu, kwa sababu giza linapita, na nuru ya kweli iko tayari inaangaza9Yeye asemeye yuko kwenye nuru na amchukia ndugu yake yuko katika giza hata sasa.10Yeye ampendaye ndugu yake anaishi katika nuru na hakuna jambo lolote liwezalo kumkwaza.11Lakini yeye amchukiaye ndugu yake yuko gizani na anatembea gizani; Yeye hajui wapi aendako, kwa sababu giza limeyapofusha macho yake.

12Nawaandikia ninyi, watoto wapendwa, kwa sababu mmesamehewa dhambi zenu kwa ajili ya jina lake.13Nawaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nawaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mmemshinda yule mwovu. Nimewaandikia ninyi, watoto wadogo, kwa sababu mnamjua Baba.14Nimewaandikia ninyi, akina baba, kwa sababu mnamjua yeye aliye tangu mwanzo. Nimewaandikia ninyi, vijana, kwa sababu mko na nguvu, na neno la Mungu linakaa ndani yenu, na mmemshinda yule mwovu.

15Msiipende dunia wala vitu ambavyo vimo katika dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upendo wa kumpenda Baba haumo ndani yake.16Kwani kila kitu kilichomo katika dunia- tamaa ya mwili, tamaa ya macho, na kiburi cha uzima- havitokani na Baba lakini vinatokana na dunia.17Dunia na tamaa zake zinapita. Bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu huyo adumu milele.

18Watoto wadogo, ni wakati wa mwisho. Kama ambavyo mmesikia kwamba mpinga kristo anakuja, hata sasa wapinga kristo wameshakuja, kwa hali hii tunajua kwamba ni wakati wa mwisho.19Waliondoka zao kutoka kwetu, kwani hawakuwa wa kwetu. Kama vile wangekuwa wa kwetu wangeendelea kuwa pamoja nasi. Lakini wakati walipo kwenda zao, hicho kilionyesha hawakuwa wa kwetu.20Lakini ninyi mmetiwa mafuta kutoka kwa yule Mtakatifu, nanyi nyote mnajua kweli.21Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamujui ukweli, bali kwa sababu mnaijua na kwa sababu hakuna uongo wa ile kweli22Nani ni mwongo bali ni yeye anayepinga kwamba Yesu ni Kristo? Huyu mtu ni mpinga kristo, pale anapo mpinga Baba na Mwana.23Hakuna anaye mpinga Mwana akawa na Baba. Yeyote anaye mkiri Mwana anaye Baba pia.24Kama kwa ajili yenu, kile mlichosikia toka mwanzo acha kiendelee kuwa ndani yenu. Kama kile mlichosikia toka mwanzo kitakaa ndani yenu, pia, mtakaa ndani ya Mwana na Baba.25Na hii ni ahadi aliyotupatia sisi: uzima wa milele.

26Nimewaandikia haya ninyi kuhusu wale ambao wangewaongoza ninyi katika upotevu.27Na kwa ajili yenu, yale mafuta mliyoyapokea kutoka kwake yanakaa ndani yenu, na hamtahitaji mtu yeyote kuwafundisha. Bali kama mafuta yake yanawafundisha kuhusu mambo yote na ni kweli na siyo uongo, na hata kama yameshawafundisha, kaeni ndani yake.

28Na sasa, watoto wapendwa, kaeni ndani yake, ili wakati atakapotokea, tuweze kuwa na ujasiri na siyo kujisikia aibu mbele yake katika kuja kwake.29Kama mnajua kuwa yeye ni mwenye haki, mnajua kwamba kila mmoja atendaye haki amezaliwa na yeye.

3

1Oneni ni pendo la namna gani ametupatia Baba, kwamba tunaitwa watoto wa Mungu, na hivi ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui kwa kuwa haukumtambua yeye.2Wapendwa sisi sasa ni watoto wa Mungu, na haijadhihirika bado jinsi tutakavyokuwa. Twajua kwamba Kristo atakapoonekana, tutafanana naye, kwani tutamuona kama alivyo.3Na kila mmoja ambaye ana ujasiri huu kuhusu wakati ujao ulioelekezwa kwake, hujitakasa mwenyewe kama yeye alivyo mtakatifu.4Kila mtu anayeendelea kutenda dhambi huvunja sheria. Kwa sababu dhambi ni uvunjaji sheria.5Mnajua Kristo alidhihilishwa ili kuziondoa dhambi kabisa. Na ndani yake hamna dhambi.6Hakuna hata mmoja akaae ndani yake na kuendelea kutenda dhambi. Hakuna mtu hata mmoja akaae katika dhambi ikiwa amemuona au kumfahamu yeye.7Watoto wapendwa, msikubali kupotoshwa na mtu yeyote. Atendaye haki ni mwenye haki, kama vile Kristo naye alivyo mwenye haki.8Atendaye dhambi ni wa ibilisi, kwa sababu ibilisi ni mtenda dhambi tangu mwanzo. Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihilishwa ili aweze kuziharibu kazi za ibilisi.9Yeyote aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu mbegu ya Mungu hukaa ndani yake. Hawezi kuendelea kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa na Mungu.10Katika hili watoto wa Mungu na watoto wa ibilisi wanafahamika. Yeyote asiyetenda kilicho cha haki, siyo wa Mungu, wala yule ambaye hawezi kumpenda ndugu yake.

11Kwani huu ndio ujumbe mliousikia kutoka mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi,12siyo kama Kaini ambaye alikuwa wa mwovu na alimuua ndugu yake. Na kwa nini alimuua? Kwa sababu matendo yake yalikuwa maovu, na yale ya ndugu yake yalikuwa ya haki.13Ndugu zangu, msishangae, endapo ulimwengu utawachukia.14Twajua tumekwisha toka mautini na kuingia uzimani, kwa sababu tunawapenda ndugu. Yeyote ambaye hana upendo hudumu katika mauti.15Mtu yeyote anaye mchukia ndugu yake ni muuaji. Na mnajua kuwa uzima wa milele haukai ndani ya muuaji.16Katika hili tunalijua pendo, kwa sababu kristo aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi yatupasa kuyatoa maisha yetu kwa ajili ya ndugu.17Lakini yeyote aliye na vitu, na anamuona ndugu yake mwenye uhitaji, lakini huuzuia moyo wake wa huruma kwa ajili yake; je, upendo wa Mungu unakaaje ndani yake?18Watoto wangu wapenzi, tusipende kwa midomo wala kwa maneno matupu bali katika vitendo na kweli.

19Katika hili tunajua kwamba sisi tuko katika kweli, na mioyo yetu inathibitika katika yeye.20Ikiwa kama mioyo yetu yatuhukumu, Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu, na yeye hujua mambo yote.21Wapenzi, kama mioyo yetu haituhukumu, tunao ujasiri kwa Mungu.22Na chochote tuombacho tutakipokea kutoka kwake, kwa sababu tunazishika amri zake na tunafanya mambo yanayopendeza mbele zake.23Na hii ndiyo amri yake ya kwamba yatupasa kuamini katika jina la Mwanaye Yesu Kristo na kupendana sisi kwa sisi kama alivyotupatia amri yake.24Anayezitii amri zake hudumu ndani yake, na Mungu hukaa ndani yake. Na kwa sababu hii twajua kuwa hukaa ndani yetu, Kwa yule Roho aliyetupa.

4

1Wapendwa, msiiamini kila roho, lakini zijaribuni roho muone kama zinatokana na Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea duniani.2Kwa hili mtamjua Roho wa Mungu - kila roho itakayokiri kuwa Yesu Kristo amekuja katika mwili ni wakutoka kwa Mungu,3na kila roho isiyomkiri Yesu si ya Mungu. Hii ni roho ya mpinga kristo, ambayo mliyoisikia kuwa inakuja, na sasa tayari iko duniani.

4Ninyi ni wa Mungu, watoto na mmekwisha washinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.5Wao ni wa ulimwengu, kwa hiyo wanachokisema ni cha ulimwengu, na ulimwengu unawasikiliza.6Sisi ni wa Mungu. Yeye amjuaye Mungu hutusikiliza sisi. Yeye asiye wa Mungu hawezi kutusikiliza. Katika hili tunajua roho wa kweli na roho wa uongo.

7Wapendwa, tupendane sisi kwa sisi, kwa vile upendo hutoka kwa Mungu, na kila mmoja apendaye amezaliwa na Mungu na kumjua Mungu.8Mtu asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni upendo.9Katika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miongoni mwetu, kwamba Mungu alimtuma Mwanae wa pekee ulimwenguni ili tuishi kupitia yeye.10Katika hili pendo, si kwamba tulimpenda Mungu, lakini yeye alitupenda, na akamtuma Mwanawe awe fidia kwa ajili ya dhambi zetu.11Wapendwa, ikiwa Mungu alitupenda sisi, vile vile tunapaswa kupendana sisi kwa sisi.

12Hakuna hata mmoja aliyemuona Mungu. Kama tukipendana sisi kwa sisi, Mungu anakaa ndani yetu na upendo wake umekamilika ndani yetu.13Katika hili tunajua kuwa tunakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa Roho wake.14Tena, sisi tumeonana na kushuhudia kuwa Baba amemtuma Mwana kuwa mwokozi wa ulimwengu.15Kila anayekiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu anakaa ndani yake na yeye ndani ya Mungu.16Tena tumejua na kuamini upendo alio nao Mungu kwa ajili yetu. Mungu ni pendo, na yeye anayekaa ndani ya upendo anakaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.17Kwa sababu hii, upendo huu umekwisha kukamilika katikati yetu, ili tuwe na ujasiri siku ya hukumu, kwa sababu kama yeye alivyo, na sisi ndivyo tulivyo katika ulimwenngu huu.18Hakuna hofu ndani ya pendo. Lakini pendo kamili huitupa hofu nje, kwa sababu hofu huhusiana na hukumu. Lakini yeye aogopaye hajakamilishwa katika pendo.19Tunapenda kwa sababu Mungu alitupenda kwanza.20Ikiwa mmoja atasema, “Nampenda Mungu” lakini hawezi kumpenda ndugu yake, ni mwongo. Kwa sababu asiyempenda ndugu yake, anayemuona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hajamuona.21Na hii ndiyo amri tuliyo nayo kutoka kwake: Yeyote ampendaye Mungu, anapaswa kumpenda ndugu yake pia.

5

1Yeyote anayeamini kuwa Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na yeyote ampendaye yeye ambaye ametoka kwa Baba pia huwapenda watoto wake.2Kwa hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu -- tunapompenda Mungu na kutii amri zake.3Hivi ndivyo tunavyompenda Mungu kwamba twazitii amri zake. Na amri zake ni nyepesi.4Kwa kuwa kila aliyezaliwa na Mungu huushinda ulimwengu. Na huu ndio ushindi wa kuushinda ulimwengu, hata imani yetu.5Ni nani aushindaye ulimwengu? Ni yule aaminiye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.

6Huyu ndiye aliyekuja kwa maji na damu- Yesu Kristo. Hakuja tu kwa maji bali kwa maji na damu.7Kwa kuwa kuna watatu washuhudiao:8Roho, maji na damu. Hawa watatu hukubaliana. 19Kama tunaupokea ushuhuda wa wanadamu ushuhuda wa Mungu ni mkuu kuliko huo. Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu ni huu- kwamba anao ushuhuda kuhusiana na Mwanawe.10Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu ana ushuhuda ndani yake mwenyewe. Na yeyote asiye mwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu ameuleta kuhusu Mwanawe.11Na ushuhuda ndio huu -- kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo ndani ya Mwanawe.12Aliye naye Mwana ana uzima. Asiye na Mwana wa Mungu hana uzima.

13Nimewaandikia haya mambo muweze kujua kwamba mnao uzima wa milele - ninyi mnaoamini katika jina la Mwana wa Mungu.14Na huu ndio ujasiri tulionao mbele zake, kwamba kama tukiomba kitu chochote sawa sawa na mapenzi yake, hutusikia.15Na kama tunajua kwamba hutusikia -- chochote tumwombacho tunajua kwamba tunacho hicho tulichomwomba.

16Kama mtu amwonaye ndugu yake anatenda dhambi isiyopelekea kifo, yampasa kuomba na Mungu atampa uzima. Ninasema kwa wale ambao dhambi yao ni ile isiyopelekea kifo. Kuna dhambi ipelekeayo kifo; sisemi kwamba anapaswa kuomba kwa ajilli ya dhambi hiyo.17Matendo yote yasiyo ya haki ni dhambi, lakini kuna dhambi isiyopelekea kifo.18Tunajua ya kuwa aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi. Bali aliyezaliwa na Mungu hutunzwa naye salama daima, na yule mwovu hawezi kumdhuru.19Tunajua kuwa sisi ni wa Mungu na tunajua kwamba ulimwengu wote uko chini ya utawala wa yule mwovu.20Lakini twajua kwamba Mwana wa Mungu amekuja na ametupatia ujuzi, kwamba tunamjua yeye aliye kweli na kwamba tumo ndani yake yeye aliye kweli, hata katika Mwanawe Yesu Kristo. Ni Mungu wa kweli na uzima wa milele.

21Watoto wapenzi, jiepusheni na sanamu.


1Zingatia: Maneno haya “Baba, Neno, na Roho Mtakatifu” hayaonekani katika nakala bora za kale.

2 Yohana

1

1Kutoka kwa mzee kwenda kwa mwanamke mteule na watoto wake, niwapendao katika kweli na si mimi tu, bali na wote wale wanao ifahamu kweli,2kwa sababu ya kweli iliyomo ndani yetu na itakayodumu pamoja nasi milele.3Neema, rehema, amani zitakuwa nasi kutoka kwa Mungu Baba na kutoka kwa Yesu Kristo, Mwana wa Baba, katika kweli na pendo.

4Ninafurahi sana kwamba nimegundua baadhi ya watoto wanaenenda katika kweli, kama vile tulivyoipokea amri hii kutoka kwa Baba.

5Na sasa nakusihi wewe, mwanamke, siyo kwamba nakuandikia amri mpya, bali ile tuliyokuwa nayo tokea mwanzo, kwamba tunapaswa kupendana sisi kwa sisi. Na huu ndiyo upendo, tunaopaswa kuenenda nayo, kulingana na amri yake.6Hii ndiyo ile amri, kama mlivyoisikia tokea mwanzo, kwamba mnapaswa kuenenda katika hiyo.

7Kwa kuwa wadanganyifu wengi wametawanyika katika ulimwengu, na hawakiri kwamba Yesu Kristo alikuja katika mwili. Huyu ndiye mdanganyifu na mpinga Kristo.8Jiangalieni wenyewe kwamba hampotezi mambo yale tuliyokwisha fanyia kazi, lakini ili kwamba mweze kuipokea tuzo kamili.9Yeyote aendeleae mbele na hadumu katika fundisho la Kristo, hana Mungu. Yeye adumuye katika fundisho anaye Baba na Mwana pia.10Kama mtu anakuja kwenu na haleti fundisho hili, msimkaribishe katika nyumba zenu na msimsalimie.11Kwa kuwa amsalimuye hushiriki katika matendo yake maovu.

12Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, na sikutaka kuyaandika kwa karatasi na wino. Lakini natumaini kuja kwenu na kuongea uso kwa uso, kwamba furaha yetu ipate kufanywa kamili.13Watoto wa dada yenu mteule wanawasalimia.

3 Yohana

1

1Mimi Yohana Mzee, nakuandikia Gayo mpenzi, ninayempenda katika kweli.2Mpendwa, nakuombea ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya njema, kama vile roho yako inavyofanikiwa.3Maana nilifurahi sana wakati nilipoambiwa na waumuni waliokuja na kutoa ushuhuda juu ya kweli yako, kama vile unavyoenenda katika kweli.4Sina furaha kubwa zaidi ya hii, kusikia kwamba watoto wangu wa kiroho wanatembea katika kweli.5Mpendwa, unaenenda kwa uaminifu kwa Mungu unapowahudumia ndugu na wageni,6wageni wametoa ushuhuda wa upendo wako mbele ya kanisa. Unafanya vizuri kuwasaidia kuwasafirisha katika safari zao kwa namna ambayo inampendeza Mungu.

7Kwa ajili ya Jina la Yesu, walienda bila kuchukua kitu chochote kutoka kwa watu wa Mataifa.8Hivyo, tunatakiwa kuwakaribisha watu kama hawa, ili tuwe watenda kazi tukishirikiana kwa ajili ya kutangaza kweli ya Mungu.

9Nimekuandikia wewe pamoja na kusanyiko jambo fulani, lakini Diotrofe, anayependa kujifanya kuwa kiongozi miongoni mwa waumini, hakubaliani na mimi Yohana na waumini wenzangu.10Hivyo, kama nikija nitayakumbuka matendo yake anayoyafanya, jinsi anavyosema maneno mabaya yakutushutumu kinyume nasi. Hajaridhika na matendo haya, yeye mwenyewe Diotrofe hawapokei waumini. Pia huwakataza wengine ambao wanatamani kuwakaribisha hao waumini na kuwafukuza watoke kwenye kusanyiko.

11Mpenzi, Gayo usiige kilicho kibaya, bali iga kilicho chema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu; na yeye atendaye mabaya hajamwamini Mungu.

12Demetrio ameshuhudiwa na wote na kweli yenyewe. Sisi pia ni mashahidi, na unajua kuwa ushahuhuda wetu ni wa kweli.

13Ninayo mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa kalamu na wino.14Bali ninatarajia kukuona hivi karibuni, na tutaongea nawe ana kwa ana. 15Amani iwe pamoja nawe. Marafiki nilionao hapa wanakusalimu. Pia nawasalimu marafiki kila mmoja kwa jina lake.

Yuda

1

1Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo, kwa wale ambao wameitwa, wapendwao katika Mungu Baba, na waliotunzwa kwa ajili ya Yesu Kristo:2rehema na amani na upendo viongezwe kwenu.

3Wapendwa wakati nilipokuwa nikifanya kila juhudi kuwaandikia ninyi kuhusu wokovu wetu sote, ilinilazimu kuwaandikia kwa ajili ya kuwashauri ili mshindanie kwa uaminifu imani ambayo ilikuwa imekabidhiwa mara moja tu kwa waamini.4Kwa sababu watu fulani wamejiingiza kwa siri kati yenu - watu ambao walitiwa alama kwa ajili ya hukumu - watu wasio wataua ambao hubadili neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, na kumkana Bwana wetu pekee na Bwana Yesu Kristo.

5Sasa napenda kuwakumbusha ninyi ingawa kuna wakati mlijua kwa ukamilifu kwamba Bwana aliwaokoa watu kutoka nchi ya Misri, lakini baadaye akawaangamiza wale ambao hawakuamini.6Pia malaika ambao hawakuilinda enzi yao wenyewe lakini wakaacha makao yao maalum Mungu amewaweka katika minyororo ya milele, ndani ya giza, kwa ajili ya hukumu ya siku ile kuu.7Vile vile Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka, ambayo pia ilijiingiza yenyewe katika uasherati na wakafuata tamaa isiyo ya asili. Walioneshwa kama mifano ya wale ambao huteseka katika hukumu ya moto wa milele.8Hali kadhalika, kwa njia ile ile waota ndoto hawa pia huchafua miili yao, na hukataa mamlaka, na wananena uongo dhidi ya viumbe takatifu

9Lakini hata Mikaeli malaika mkuu, wakati alipokuwa akishindana na ibilisi na kugombana kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kuleta hukumu ya uongo dhidi yake, lakini badala yake alisema, “Bwana akukemee!”10Lakini watu hawa huleta uongo dhidi ya chochote wasicho kifahamu. Na kile wasicho kifahamu- kile ambacho wanyama wasio na akili hujua kwa silika- haya ndiyo yaliyo waharibu.

11Ole wao! Kwa kuwa wametembea katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu. Wameangamia katika uasi wa Kora.12Hawa ni miamba katika sherehe zenu za upendo, wakisherehekea pas uoga wachungaji wanaojilisha wenyewe tu. Ni mawingu yasiyo na mvua, yanayobebwa na upepo, ni miti iliyopukutika isiyo na matunda iliyo kufa mara mbili, iliyong'olewa mizizi13Ni mawimbi ya bahari yenye kelele yakitoa aibu yao wenyewe, Ni nyota zinazorandaranda ambazo weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele.

14Enoko, wa saba kutoka kwa Adamu, alitabiri kuhusu wao, akisema, “Tazama! Bwana anakuja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,15ili afanye hukumu juu ya kila mtu, na kutia hatia wote wasiomcha Mungu juu ya matendo yao yote waliyokwishafanya katika njia zisizo za kitauwa, na kwa maneno yote ya ukali ambayo wasio watauwa wameyanena dhidi yake.”16Hawa ni wale wanung'unikao, walalamikao ambao hufuata tamaa zao za uovu, wajivunao mno, ambao kwa faida yao hudanganya wengi

17Lakini ninyi, wapendwa, kumbukeni maneno ambayo yalinenwa zamani na mitume wa Bwana Yesu Kristo.18Walisema kwenu, “Katika nyakatii za mwisho kutakuwa na watu wanaodhihaki ambao hufuata tamaa zao zisizo za kitauwa.”19Watu hawa ni watenganishaji, wanatawaliwa na tamaa za kidunia na hawana Roho.

20Lakini ninyi, wapendwa, jijengeni katika imani yenu takatifu sana na muombe katika Roho Mtakatifu,21jitunzeni katika upendo wa Mungu, na msubiri rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo huwapatia uzima wa milele.

22Onesheni rehema kwa wale walio na shaka.23Waokoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka katika moto. Kwa wengine onesheni huruma kwa hofu, mkichukia hata vazi lililotiwa doa na mwili.

24Sasa kwake awezaye kuwalinda msijikwae, na kuwasababisha msimame mbele ya utukufu wake, bila mawaa na kuwa na furaha kuu,25kwake Mungu pekee mwokozi kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu uwe kwake, ukuu, uwezo na nguvu kabla ya nyakati zote, na sasa na hata milele. Amina.

Ufunuo

1

1Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo ambao Mungu alimpa ili kuwaonesha watumishi wake mambo ambayo lazima yatokee karibuni. Aliyafanya yajulikane kwa kumtuma malaika wake kwa mtumishi wake Yohana.2Yohana alitoa ushuhuda wa kila kitu alichoona kuhusiana na neno la Mungu na kwa ushuhuda uliotolewa kuhusu Yesu Kristo.3Amebarikiwa yeye asomaye kwa sauti na wale wote wanaoyasikia maneno ya unabii huu na kutii kilichoandikwa humo, kwa sababu muda umekaribia.

4Yohana, kwa makanisa saba yaliyoko Asia: Neema iwe kwenu na amani kutoka kwake aliyepo, aliyekuwepo, na atakayekuja, na kutoka kwa Roho saba walio mbele ya kiti chake cha enzi,5na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mtawala wa wafalme wa dunia hii. Kwake yeye atupendaye na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake,6ametufanya kuwa ufalme, makuhani wa Mungu na Baba yake - kwake kuwa utukufu na nguvu milele daima. Amina.

7Tazama, anakuja na mawingu; kila jicho litamwona, pamoja na wote waliomchoma. Kabila zote za dunia wataomboleza kwa sababu yake.8“Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Yeye aliyepo, na aliyekuwepo, na ambaye anakuja, Mwenye nguvu.”

9Mimi, Yohana - ndugu yenu na mmoja anayeshiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu thabiti ulio katika Yesu; nilikuwa katika kisiwa kiitwacho Patimo kwa sababu ya neno la Mungu na ushuhuda kuhusu Yesu.10Nilikuwa katika Roho siku ya Bwana. Nilisikia nyuma yangu sauti ya juu kama ya tarumbeta,11ikisema, “Andika katika kitabu unayo yaona, na uyatume kwa makanisa saba, kwenda Efeso, kwenda Smirna, kwenda Pergamo, kwenda Thiatira, kwenda Sardi, kwenda Philadelphia, na kwenda Laodikia.”12Nikageuka kuona ni sauti ya nani aliyekuwa akiongea nami, na nilipogeuka niliona kinara cha dhahabu cha taa saba.13Katikati ya kinara cha taa alikuwemo mmoja kama Mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu iliyofika chini ya miguu yake, na mkanda wa dhababu kuzunguka kifua chake.14Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji, na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto.15Nyayo zake zilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama shaba ambayo imekwisha pitishwa katika moto, na sauti yake ilikuwa kama sauti ya maji mengi yanayotiririka kwa kasi.16Alikuwa ameshikilia nyota saba katika mkono wake wa kuume, na kutoka kinywani mwake kulikuwa na upanga mkali wenye makali kuwili. Uso wake ulikuwa uking'aa kama mwanga mkali wa jua.17Nilipomwona, nikaanguka miguuni pake kama mtu aliyekufa. Akaweka mkono wake wa kulia juu yangu na kusema, “Usiogope! Mimi ni wa Kwanza na wa Mwisho,18na ambaye ninaishi. Nilikuwa nimekufa, lakini tazama, ninaishi milele! Na ninazo funguo za mauti na kuzimu.19Kwa hiyo, yaandike uliyoyaona, yaliyopo sasa, na yale yatakayotokea baada ya haya.20Kuhusu siri ya nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kuume, na kile kinara cha dhahabu cha taa saba: Nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba, na kinara cha taa saba ni yale makanisa saba.

2

1Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika: ‘Haya ni maneno ya yule anayeshikilia zile nyota saba katika mkono wake wa kuume. Yeye atembeaye kati ya vinara vya dhahabu vya taa saba asema hivi,2‘Najua matendo na bidii yako ya kazi na uvumilivu wako thabiti, na kwamba huwezi kuhusiana nao walio waovu, bali, umewajaribu wote wanaojiita kuwa mitume na kumbe siyo, na wameonekana kuwa waongo.3Najua una subira na uvumilivu, na umepitia mengi kwa sababu ya jina langu, na haujachoka bado.4Lakini hili ndilo nililonalo dhidi yako, umeuacha upendo wako wa kwanza.5Kwa hiyo kumbuka ulipoanguka, ukatubu na kufanya matendo uliyofanya tangu mwanzo. Usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako kutoka mahali pake.6Lakini wewe una hili, unachukia yale ambayo Wanikolai wameyatenda, ambayo hata mimi nayachukia.7Na aliye na sikio asikie yale ambayo Roho anayaambia makanisa. Na kwa yeye ashindaye nitampa kibali cha kula kutoka katika mti wa uzima ulio katika paradiso ya Mungu.’

8Kwa malaika wa kanisa la Smirna andika: ‘Haya ni maneno ya yule ambaye ni mwanzo na mwisho ambaye alikufa na kuwa hai tena:9Nayajua mateso yako na umasikini wako (lakini wewe ni tajiri), na uongo wa wale wanaosema ni wayahudi (lakini siyo - wao ni sinagogi la Shetani).10Usiogope mateso yatakayowapata. Tazama! Ibilisi anataka kuwatupa baadhi yenu gerezani ili mpate kujaribiwa, na mtateseka kwa siku kumi. Iweni waaminifu hadi kufa, na nitawapa taji ya uzima.11Aliye na sikio, na asikie Roho anavyoyaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapata madhara ya mauti ya pili.’

12Kwa malaika wa kanisa la Pergamo andika: ‘Haya ndiyo anenayo yeye aliye nao huo upanga mkali, wenye makali kuwili.13Najua mahali unapoishi -mahali kilipo kiti cha enzi cha Shetani. Hata hivyo wewe walishika sana jina langu, na hukuikana imani yako iliyo kwangu, hata siku zile za Antipasi shahidi wangu, mwaminifu wangu, aliyeuawa miongoni mwenu, hapo ndipo Shetani anaishi.14Lakini nina mambo machache dhidi yako: unao huko watu washikao mafundisho ya Balaamu, yeye aliyemfundisha Balaki kuweka vikwazo mbele ya wana wa Israeli, ili wale vyakula vilivyotolewa sadaka kwa miungu ili wanajisike.15Katika hali hiyo hiyo, unao baadhi yao wanaoshika mafundisho ya Wanikolai.16Basi tubu! Na usipofanya hivyo, naja upesi, na nitafanya vita dhidi yao kwa upanga utokao katika kinywa changu.17Na aliye na sikio, asikie Roho anachowaambia makanisa. Kwa yeye ashindaye, nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, pia nitampa jiwe jeupe lililoandikwa jina jipya, jina ambalo hakuna alijuaye isipokuwa yeye alipokeaye.’

18Kwa malaika wa kanisa la Thiatira andika: ‘Haya ndiyo maneno ya Mwana wa Mungu, yeye aliye na macho yake kama mwali wa moto, na nyayo kama shaba iliyosuguliwa sana:19Najua matendo yako - upendo wako na imani na huduma na uvumilivu wako thabiti, na kwamba kile ulichofanya hivi karibuni ni zaidi ya kile ulichofanya mwanzo.20Lakini ninalo hili dhidi yako: unamvumilia mwanamke Yezebeli anayejiita nabii mke. Kwa mafundisho yake, anawapotosha watumishi wangu kuzini na kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu.21Nilimpa muda wa kutubu, lakini hayuko tayari kuutubia uovu wake.22Angalia! Nitamtupa kwenye kitanda cha maradhi, na wale watendao uasherati naye kwenye mateso makali, vinginevyo watubu matendo yake.23Nitawapiga wanawe wafe na makanisa yote watajua kwamba mimi ndiye niyachunguzaye mawazo na mioyo. Nitampa kila mmoja wenu kadiri ya matendo yake.24Lakini kwa baadhi yenu mliosalia katika Thiatira, kwa wale wote msioshika fundisho hili, na msiojua kile ambacho baadhi huita mafumbo ya Shetani, nasema kwenu, ‘Sitaweka juu yenu mzigo wowote.’25Kwa jambo lolote, lazima muwe imara mpaka nitakapokuja.26Yeyote ashindaye na kufanya kile nilichofanya hadi mwisho, kwake yeye nitampa mamlaka juu ya mataifa.27‘Atawatawala kwa fimbo ya chuma, kama mabakuli ya udongo, atawavunja vipande vipande.’28Kama nilivyopokea kutoka kwa Baba yangu, nitampa pia nyota ya asubuhi.29Aliye na sikio na asikilize kile ambacho Roho anayaambia makanisa.’

3

1Kwa malaika wa kanisa la Sardi andika: ‘Maneno ya yule anayeshikilia zile Roho saba za Mungu na nyota saba. “Najua matendo yako. Una sifa ya kuwa hai, lakini u-mfu.2Amka na kuimarisha yaliyosalia, lakini yako karibu kufa, kwa sababu sikuyaona matendo yako yamekamilika machoni pa Mungu wangu.3Kwa hiyo, kumbuka, yale uliyoyapokea na kusikia. Yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwizi, na hutajua saa ipi nitakayokuja juu yako.4Lakini kuna majina machache ya watu katika Sardi ambao hawakuchafua nguo zao. Watatembea pamoja nami, wakiwa wamevaa nguo nyeupe, kwa sababu wanastahili.5Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe, na kamwe sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, na nitalitaja jina lake mbele ya Baba yangu, na mbele ya malaika.6Na aliye na sikio, asikilize vile Roho ayaambiavyo makanisa.’

7Kwa malaika wa kanisa la Filadefia andika: ‘Maneno ya aliye mtakatifu na kweli - aliye na funguo za Daudi, hufungua na hakuna afungaye, hufunga na hakuna awezaye kufungua.8Najua ambacho umetenda. Tazama, nimekuwekea mbele yako mlango uliofunguliwa ambao hakuna awezaye kuufunga. Najua unazo nguvu kidogo, lakini umelitii neno langu na hujalikana jina langu.9Angalia! Wote walio wa sinagogi la Shetani, wale wasemao wao ni Wayahudi na kumbe siyo, badala yake wanadanganya. Nitawafanya waje na kusujudu mbele ya miguu yako, na watajua ya kuwa nakupenda.

10Kwa kuwa umetunza amri yangu kwa uvumilivu wa uthabiti, nitakulinda pia katika saa yako ya kujaribiwa ambayo inakuja katika ulimwengu wote, kuwajaribu wale wote wanaoishi katika nchi.11Naja upesi. Shikilia sana kile ulichonacho ili asiwepo mtu wa kuitwaa taji yako.12Nitamfanya yeye ashindaye kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka nje kamwe. Nitaliandika kwake jina la Mungu wangu, jina la mji wa Mungu wangu (Yerusalemu mpya, ushukao chini toka mbinguni kwa Mungu wangu), na jina langu jipya.13Yeye aliye na sikio, na asikie ambacho Roho anasema kwa makanisa.’

14Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika: ‘Maneno yake aliye Amina, wakutegemewa na shahidi mwaminifu, mtawala juu ya uumbaji wa Mungu.15Najua ambacho umefanya, na kwamba wewe si baridi wala moto, natamani kwamba ungekuwa wa baridi au moto!16Hivyo, kwa sababu wewe ni vuguvugu, si moto wala baridi, nitakutapika utoke kinywani mwangu.17Kwa kuwa unasema, ‘Mimi ni tajiri, nimekuwa na mali nyingi, na sihitaji chochote.’ Lakini hujui kwamba wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi.18Sikiliza ushauri kwangu: Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri, na nguo nyeupe za kumetameta ili ujivike mwenyewe na usioneshe aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka katika macho yako upate kuona.19Kila nimpendaye, namwelekeza na kuwafundisha namna iwapasavyo kuishi; kwa hiyo, kuwa mkweli na kutubu.20Tazama nasimama katika mlango na kubisha. Yeyote asikiaye sauti yangu na kufungua mlango, nitakuja na kuingia nyumbani kwake, na kula chakula naye na yeye pamoja nami.21Yeye ashindaye, nitampa haki ya kukaa chini pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na kukaa chini pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi.22Yeye aliye na sikio, na asikilize ambacho Roho ayaambia makanisa.’”

4

1Baada ya mambo haya nilitazama, nikaona kuwa mlango ulikuwa umefunguliwa mbinguni. Ile sauti ya kwanza, ikizungumza nami kama tarumbeta, ikisema, “Njoo hapa, nitakuonesha yatakayotokea baada ya mambo haya.”2Mara moja nilikuwa katika Roho, niliona kulikuwa na kiti cha enzi kimewekwa mbinguni, na mtu amekikalia.3Mmoja aliyekuwa amekikalia alionekana kama jiwe la yaspi na akiki. Kulikuwa na upinde wa mvua umekizunguka kiti cha enzi. Upinde wa mvua ulionekana kama zumaridi.4Kukizunguka kiti cha enzi kulikuwa na viti vya enzi vingine ishirini na vinne, na waliokaa kwenye viti vya enzi walikuwa wazee ishirini na wanne, wamevikwa mavazi meupe na taji za dhahabu vichwani mwao.5Kutoka katika kiti cha enzi kulitoka miale ya radi, muungurumo na radi. Taa saba zilikuwa zikiwaka mbele ya kiti cha enzi, taa ambazo ni Roho saba za Mungu.6Tena mbele ya kiti cha enzi kulikuwa na bahari, iliyowazi kama kioo. Katikati mwa kiti cha enzi kulikuwa na viumbe wenye uhai wanne, waliojaa macho mbele na nyuma.7Kiumbe wa kwanza mwenye uhai alikuwa kama simba, kiumbe wa pili mwenye uhai alikuwa kama ndama, kiumbe wa tatu mwenye uhai alikuwa na uso kama wa mwanadamu, na yule mwenye uhai wa nne alikuwa kama tai apaaye.8Viumbe wenye uhai wanne kila mmoja alikuwa na mabawa sita, wamejaa macho juu na chini yake. Usiku na mchana hawakomi kusema, “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu ni Bwana Mungu, mtawala juu ya wote, aliyekuwepo, na aliyepo na atakayekuja.”

9Kila wakati viumbe wenye uhai walipotoa utukufu, heshima, na kushukuru mbele za aliyekuwa ameketi kwenye hicho kiti cha enzi, yeye aishiye milele na daima,10wazee ishirini na wanne walisujudu wenyewe mbele yake aliyekikalia kiti cha enzi. Waliinama chini kwake aishiye milele na daima na kutupa chini taji zao mbele ya kiti cha enzi wakisema,
11“Wastahili wewe, Bwana wetu na Mungu wetu, kupokea utukufu na heshima na nguvu. Kwa kuwa uliviumba vitu vyote, na kwa mapenzi yako, vilikuwepo na viliumbwa.”

5

1Kisha nikaona katika mkono wa kulia wa yule aliyekuwa amekaa katika kiti cha enzi, gombo lililoandikwa mbele na nyuma, na lilikuwa limetiwa mihuri saba.2Nilimwona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kubwa, “Nani astahiliye kulifungua gombo na kuivunja mihuri yake?”3Hakuna mtu mbinguni au duniani au chini ya dunia aliyeweza kulifungua gombo au kulisoma.4Nililia kwa uchungu kwa kuwa hakupatikana yeyote aliyestahili kulifungua gombo au kulisoma.5Lakini mmoja wa wazee akaniambia, “Usilie. Tazama! Simba wa kabila ya Yuda, shina la Daudi, ameshinda, na anaweza kulifungua gombo na mihuri yake saba.”6Kati ya kiti cha enzi na wenye uhai wanne na miongoni mwa wazee, niliona mwanakondoo amesimama, akionekana kama aliye uawa. Alikuwa na pembe saba na macho saba - hizi ni roho saba za Mungu zilizotumwa duniani kote.7Akaenda akalichukua gombo kutoka katika mkono wa kuume wa yule aliye kaa katika kiti cha enzi.8Alipolichukua gombo, viumbe wenye uhai wanne na wazee ishirini na wanne wakainama hadi nchi mbele ya mwanakondoo. Kila mmoja alikuwa na kinubi na bakuli ya dhahabu iliyojaa uvumba ambayo ni maombi ya watakatifu wa Mungu.9Waliimba wimbo mpya: “Unastahili kulitwaa gombo na kuzifungua muhuri zake. Kwa kuwa ulichinjwa, na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu wa kila kabila, lugha, jamaa na taifa.

10Ukawafanya ufalme na makuhani kwa ajili ya kumtumikia Mungu wetu, nao watatawala juu ya nchi.”

11Kisha nilitazama na nikasikia sauti ya malaika wengi walio kizunguka kiti cha enzi na viumbe wenye uhai na wazee. Idadi yao ilikuwa kumi maelfu kwa kumi maelfu na maelfu kwa maelfu.12Wakasema kwa sauti kuu, “Astahili mwanakondoo ambaye amechinjwa kupokea uwezo, utajiri, hekima, nguvu, heshima, utukufu, na sifa.”

13Nikasikia kila kilichoumbwa kilichokuwa mbinguni na duniani na chini ya nchi na juu ya bahari, kila kitu ndani yake kikisema, “Kwake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi na kwa mwanakondoo, kuwe sifa, heshima, utukufu na nguvu ya kutawala milele na milele.”

14Wenye uhai wanne wakasema, “Amina!” na wazee wakainama chini na kuabudu.

6

1Nikatazama wakati mwanakondoo alipofungua moja ya zile muhuri saba, nikasikia mmoja wa wale wenye uhai wanne akisema kwa sauti iliyofanana na radi, “Njoo!”2Nikatazama na palikuwa na farasi mweupe! Aliyempanda alikuwa na bakuli, na akapewa taji. Alitokea kama mshindi ili aendelee kushinda.3Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri wa pili, nikasikia kiumbe mwenye uhai wa pili akisema, “Njoo!”4Kisha farasi mwingine akatokea - mwekundu kama moto. Aliye mpanda alipewa ruhusa ya kuondoa amani duniani, ili kwamba watu wachinjane. Huyu aliye mpanda alipewa upanga mkubwa.5Wakati mwanakondoo alipofungua ule muhuri wa tatu, nikasikia mwenye uhai wa tatu akisema, “Njoo!” Nikaona farasi mweusi, na aliyempanda ana mizani mkononi mwake.6Nikasikia sauti kuwa sauti miongoni mwa wale viumbe wenye uhai ikisema, “Kibaba cha ngano kwa dinari moja na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja. Lakini usiyadhuru mafuta na divai.”7Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya nne, nilisikia sauti ya kiumbe mwenye uhai wa nne ikisema, “Njoo!”8Kisha nikaona farasi wa kijivu. Aliye mpanda aliitwa jina lake mauti, na kuzimu ilikuwa ikimfuata. Walipewa mamlaka juu ya robo ya nchi, kuua kwa upanga, kwa njaa na kwa ugonjwa, na kwa wanyama wa mwitu katika nchi.

9Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya tano, niliona chini ya madhabahu roho za wale waliokuwa wameuawa kwa sababu ya neno la Mungu na kutokana na ushuhuda walioushika kwa uthabiti.10Wakalia kwa sauti kuu, “Mpaka lini, Mtawala wa vyote, mtakatifu na mkweli, utahukumu wakaao juu ya nchi, na kulipiza kisasi damu yetu?”11Kisha kila mmoja alipewa kanzu nyeupe na wakaambiwa kuwa wanapaswa kusubiri kidogo hata itakapotimia hesabu kamili ya watumishi wenzao na ndugu zao wa kike na wa kiume itakapotimia ambao watauawa, kama vile ambavyo wao waliuawa.

12Wakati mwanakondoo alipofungua muhuri ya sita, nilitazama na palikuwa na tetemeko kuu la ardhi. Jua likawa jeusi kama gunia la singa, na mwezi mzima ukawa kama damu.13Nyota za mbinguni zikaanguka katika nchi, kama mtini upukutishavyo matunda yake ya wakati wa baridi unapotikiswa na kimbunga.14Anga ilitoweka kama gombo lililoviringishwa. Kila mlima na kisiwa vilihamishwa mahali pake.15Kisha wafalme wa nchi na watu maarufu na majemadari, matajiri, wenye nguvu, na kila mmoja aliye mtumwa na huru, wakajificha katika mapango na katika miamba ya milima.16Wakaiambia milima na miamba, “Tuangukieni! Tuficheni dhidi ya uso wake aketiye kwenye kiti cha enzi na kutoka hasira ya mwanakondoo.”17Kwa kuwa siku kuu ya gadhabu yao imewadia, na ni nani awezaye kuistahimili?

7

1Baada ya haya niliona malaika wanne wamesimama kwenye kona nne za dunia, wamezuia pepo nne za nchi kwa nguvu ili kwamba pasiwe na upepo unaovuma katika nchi, juu ya bahari au dhidi ya mti wowote.2Nikaona malaika mwingine akija kutoka mashariki, aliyekuwa na muhuri wa Mungu aliye hai. Akalia kwa sauti kuu kwa malaika wanne ambao walipewa ruhusa ya kudhuru nchi na bahari:3“Msiidhuru nchi, bahari, au miti mpaka tutakapokuwa tumekwishaweka muhuri katika paji za vichwa vya watumishi wa Mungu wetu.”4Nikasikia idadi ya wale waliotiwa muhuri: 144,000, ambao walitiwa muhuri kutoka kila kabila ya watu wa Israel:512,000 kutoka katika kabila ya Yuda walitiwa muhuri, 12,000 kutoka katika kabila ya Rubeni, 12,000 kutoka katika kabila ya Gadi.612,000 kutoka katika kabila ya Asheri, 12,000 kutoka katika kabila ya Naftali, 12,000 kutoka katika kabila ya Manase.712,000 kutoka kabila ya Simioni, 12,000 kutoka kabila ya Lawi, 12,000 kutoka kabila ya Isakari,812,000 kutoka kabila ya Zebuloni, 12,000 kutoka kabila ya Yusufu, na 12,000 kutoka kabila ya Benyamini walitiwa muhuri.

9Baada ya mambo haya nilitazama, na kulikuwa na umati mkubwa ambao hapana mtu angeweza kuuhesabu - kutoka kila taifa, kabila, jamaa, na lugha - wamesimama mbele ya kiti cha enzi na mbele ya Mwanakondoo. Walikuwa wamevaa kanzu nyeupe na wana matawi ya mitende mikononi mwao,10na walikuwa wakiita kwa sauti ya juu: “Wokovu ni kwa Mungu ambaye ameketi katika kiti cha enzi, na kwa Mwanakondoo!”11Malaika wote waliokuwa wamesimama kuzunguka kiti cha enzi na kuwazunguka wale wazee pamoja na wenye uhai wanne, wakainama chini ardhini na wakaweka nyuso zao juu ya ardhi mbele ya kiti cha enzi na wakamwabudu Mungu,12wakisema, “Amina! Sifa, utukufu, hekima, shukurani, heshima, uwezo na nguvu viwe kwa Mungu wetu milele na milele! Amina!”

13Kisha mmoja wa wale wazee akaniuliza, “Hawa ni akina nani waliovaa kanzu nyeupe, na wametoka wapi?14Nikamwambia, “Bwana mkubwa, unajua wewe,” na akaniambia, “Hawa ni wale waliotoka katika dhiki kuu. Wamezifua kanzu zao na kuzifanya nyeupe kwa damu ya Mwanakondoo.15Kwa sababu hii, wako mbele ya kiti cha enzi cha Mungu, na wanamwabudu yeye usiku na mchana katika hekalu lake. Yeye aliye keti juu ya kiti cha enzi atasambaza hema yake juu yao.16Hawataona njaa tena, wala kiu tena. Jua halitawachoma, wala joto la kuunguza.17Kwa kuwa Mwanakondoo aliye katikati ya kiti cha enzi atakuwa mchungaji wao, na atawaongoza katika chemchemi ya maji ya uzima, na Mungu atafuta kila chozi katika macho yao.”

8

1Wakati Mwanakondoo alipofungua muhuri ya saba, kukawa na ukimya mbinguni takribani nusu saa.2Kisha nikaona malaika saba wasimamao mbele za Mungu, na wakapewa tarumbeta saba.3Malaika mwingine akaja, ameshikilia bakuli ya dhahabu yenye uvumba, amesimama madhabahuni. Akapewa uvumba mwingi ili kwamba autoe pamoja na maombi ya waamini wote katika madhabahu ya dhahabu mbele ya kiti cha enzi.4Moshi wa ule uvumba, pamoja na maombi ya waamini, ukapanda juu mbele za Mungu kutoka mkononi mwa malaika.5Malaika akatwaa bakuli la uvumba na akalijaza moto kutoka kwenye madhabahu. Kisha akalitupa chini juu ya nchi, na kukatokea sauti za radi, miale ya radi na tetemeko la ardhi.

6Wale malaika saba ambao walikuwa na tarumbeta saba wakawa tayari kuzipiga.7Malaika wa kwanza akaipiga tarumbeta yake, na kukatokea mvua ya mawe na moto uliochanganyikana na damu. Vikatupwa chini katika nchi ili kwamba theluthi yake iungue, theluthi ya miti ikaungua na nyasi zote za kijani zikaungua.8Malaika wa pili akaipiga tarumbeta yake, na kitu kama mlima mkubwa uliokuwa unaungua kwa moto ukatupwa baharini. Theluthi ya bahari ikawa damu,9theluthi ya viumbe hai katika bahari vikafa, na theluthi ya meli zikaharibiwa.10Malaika wa tatu akaipiga tarumbeta yake, na nyota kubwa ikaanguka kutoka mbinguni, ikimulika kama kurunzi, juu ya theluthi ya mito na chemichemi za maji.11Jina la nyota ni pakanga. Theluthi ya maji ikawa pakanga, na watu wengi wakafa kutokana na maji yaliyokuwa machungu.12Malaika wa nne alipiga tarumbeta yake, na theluthi ya jua ikapigwa, pamoja na theluthi ya mwezi na theluthi ya nyota. Kwa hiyo theluthi ya vyote ikageuka kuwa giza; theluthi ya mchana na theluthi ya usiku havikuwa na mwanga.

13Nilitazama, na nikasikia tai aliye kuwa anaruka katikati ya anga, akiita kwa sauti kuu, “Ole, ole, ole, kwa wale wakaao katika nchi, kwa sababu ya mlipuko wa tarumbeta iliyosalia ambayo imekaribia kupigwa na malaika watatu.”

9

1Kisha malaika wa tano alipiga tarumbeta yake. Niliona nyota kutoka mbinguni iliyokuwa imeanguka kwenye dunia. Nyota ilipewa ufunguo wa shimo linaloelekea kwenye shimo lisilo na mwisho.2Alifungua shimo lisilo na kikomo, na moshi ukapanda juu kwa safu kutoka ndani ya shimo kama moshi kutoka katika tanuru kubwa. Jua na anga vilibadilika vikawa giza kwa sababu ya moshi uliotoka shimoni.3Ndani ya moshi nzige walitoka kuja juu ya dunia, nao walipewa nguvu kama ile ya nge juu ya dunia.4Waliambiwa kutokudhuru majani katika nchi au mmea wowote wa kijani au mti, isipokuwa tu watu ambao hawakuwa na muhuri wa Mungu katika paji za nyuso zao.5Hawakupewa ruhusa ya kuwaua hao watu, bali kuwatesa tu kwa miezi mitano. Uchungu wao ulikuwa kama ule wa kuumwa na nge amwumapo mtu.6Katika siku hizo watu watatafuta kifo, lakini hawatakipata. Watatamani kufa, lakini kifo kitawakimbia.7Nzige walifanana na farasi walioandaliwa kwa vita. Kwenye vichwa vyao kulikuwa na kitu kama taji ya dhahabu na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.8Walikuwa na nywele kama za wanawake na meno yao yalikuwa kama ya simba.9Walikuwa na vifua kama vifua vya chuma na sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya magari mengi ya vita na farasi wakimbiao kwenda vitani.10Walikuwa na mikia inayouma kama nge; katika mikia yao walikuwa na nguvu ya kudhuru watu kwa miezi mitano.11Walikuwa naye kama mfalme juu yao malaika wa shimo lisilokuwa na mwisho. Jina lake katika Kiebrania ni Abadoni, na katika Kiyunani ana jina Apolioni.

12Ole ya kwanza imepita. Angalia! Baada ya hili kuna maafa mawili yajayo.

13Malaika wa sita alipiga tarumbeta yake, na nikasikia sauti ikitoka katika pembe ya madhabahu ya dhahabu ambayo iko mbele za Mungu.14Sauti ilimwambia malaika wa sita aliyekuwa na tarumbeta, “Waachie malaika wanne ambao wamefungwa katika mto mkubwa Efrata.”15Malaika wale wanne waliokuwa wameandaliwa kwa saa hiyo maalumu, siku hiyo, mwezi huo, na mwaka huo, waliachiwa wawaue theluthi ya wanadamu.16Idadi ya maaskari waliokuwa juu ya farasi ilikuwa 200,000,000. Nilisikia idadi yao.17Hivi ndivyo nilivyoona farasi katika maono yangu na wale waliopanda juu yao: Vifua vyao vilikuwa vyekundu kama moto, bluu iliyoiva na njano isiyoiva. Vichwa vya farasi vilifanana na vichwa vya simba, na midomoni mwao ulitoka moto, moshi na salfa.18Theluthi ya wanadamu waliuawa na haya mapigo matatu: moto, moshi, na salfa iliyotoka katika midomo yao.19Kwa kuwa nguvu ya farasi ilikuwa katika midomo yao na katika mikia yao—kwa kuwa mikia yao ilikuwa kama nyoka, na walikuwa na vichwa ambavyo walitumia kuwatia majeraha wanadamu.20Watu waliobaki, wale ambao walikuwa hawajauawa na mapigo haya, hawakutubia matendo yao waliyokuwa wamefanya, wala hawakuacha kuabudu mapepo na miungu ya dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti—vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia au kutembea.21Wala hawakutubia uuaji wao, uchawi wao, uasherati wao au njia zao za wizi.

10

1Kisha nikaona malaika mwingine mkuu akishuka chini kutoka mbinguni. Alikuwa amevalia wingu, na kulikuwa na upinde wa mvua juu ya kichwa chake. Uso wake ulikuwa kama jua na miguu yake ilikuwa kama nguzo za moto.2Alishikilia gombo dogo katika mkono wake lililokuwa limefunuliwa, naye aliweka mguu wake wa kulia juu ya bahari na mguu wake wa kushoto juu ya nchi kavu.3Kisha alipaza sauti ya juu kama simba aungurumapo, na wakati alipopaza sauti radi saba zilinguruma.4Wakati radi saba zilipounguruma, nilikuwa nakaribia kuandika, lakini nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Tunza iwe siri kile ambacho radi saba zimesema. Usiiandike.”5Kisha malaika niliyemwona amesimama juu ya bahari na nchi kavu, aliinua mkono wake juu mbinguni6na kuapa kwa yule aishiye milele na milele —aliyeumba mbingu na vyote vilivyomo, dunia na vyote vilivyomo, na bahari na vyote vilivyomo: “Hakutakuwepo kusubiri tena!”7Lakini katika siku ile, wakati malaika wa saba atakapokaribia kupiga tarumbeta yake, ndipo siri ya Mungu itakuwa imetimizwa, kama alivyotangaza kwa watumishi wake manabii.”

8Sauti niliyosikia kutoka mbinguni iliniambia tena: “Nenda, chukua gombo dogo lililofunuliwa ambalo kiko katika mkono wa malaika aliyesimama juu ya bahari na juu ya nchi kavu.”9Kisha nilikwenda kwa malaika na kumwambia anipe gombo dogo. Aliniambia, “Chukua gombo na ule. Litalifanya tumbo lako liwe na uchungu, lakini katika mdomo wako litakuwa tamu kama asali.”10Nilichukua gombo dogo kutoka mkononi mwa malaika na kulila. Lilikuwa tamu kama asali katika mdomo wangu, lakini baada ya kula, tumbo langu lilikuwa na uchungu.11Kisha baadhi ya sauti ziliniambia, “Unapaswa kutabiri tena kuhusu watu wengi, mataifa, lugha, na wafalme.”

11

1Nilipewa mwanzi wa kutumia kama fimbo ya kupimia. Niliambiwa, “Ondoka na ukapime hekalu la Mungu na madhabahu, na wale wanaoabudu ndani yake.2Lakini usipime eneo la ua wa nje ya hekalu, kwa kuwa wamepewa watu wa Mataifa. Wataukanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.3Nitawapa mashahidi wangu wawili mamlaka ya kutabiri kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa magunia.”4Hawa mashahidi ni miti miwili ya mizeituni na vinara viwili ambavyo vimesimama mbele ya Bwana wa dunia.5Kama mtu yeyote ataamua kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwadhuru adui zao. Yeyote anayetaka kuwadhuru lazima auawe kwa njia hii.6Hawa mashahidi wana uwezo wa kufunga anga ili kwamba mvua isinyeshe wakati wanatabiri. Wana nguvu ya kubadili maji kuwa damu na kuipiga nchi kwa kila aina ya pigo wakati wowote wakitaka.7Wakati watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama anayetoka kwenye shimo lisilo na mwisho atafanya vita dhidi yao. Atawashinda na kuwaua.8Miili yao italala katika mtaa wa mji mkuu (ambao kimfano unaitwa Sodoma na Misri) ambapo Bwana wao alisulubiwa.9Kwa siku tatu na nusu baadhi kutoka katika jamaa za watu, kabila, lugha na kila taifa watatazama miili yao na hawatatoa kibali kuwekwa katika kaburi.10Wale wanaoishi katika nchi watafurahi kwa ajili yao na kushangilia, hata kutumiana zawadi kwa sababu hao manabii wawili waliwatesa wale walioishi katika nchi.11Lakini baada ya siku tatu na nusu pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu itawaingia nao watasimama kwa miguu yao. Hofu kuu itawaangukia wale wanaowaona.12Kisha watasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njoni huku!” Nao watakwenda juu mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakitazama.13Katika saa hiyo kutakuwepo na tetemeko kuu la ardhi na moja ya kumi ya mji itaanguka. Watu elfu saba watauawa katika tetemeko na watakaobaki hai wataogopeshwa na kumpa utukufu Mungu wa mbinguni.

14Ole ya pili imepita. Angalia! Ole ya tatu inakuja upesi.

15Kisha malaika wa saba alipiga tarumbeta yake, na sauti kubwa zilinena mbinguni na kusema, “Ufalme wa dunia umeshakuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake. Atatawala milele na milele.”16Kisha wazee ishirini na wanne waliokuwa wameketi kwenye viti vya enzi mbele ya Mungu walianguka wenyewe chini kwenye ardhi, nyuso zao zimeinama chini, nao walimwabudu Mungu.17Walisema, “Twatoa shukrani zetu kwako, Bwana Mungu, mtawala juu ya vyote, ambaye upo na ambaye ulikuwepo, kwa sababu umetwaa nguvu yako kuu na kuanza kutawala.
18Mataifa walikasirika, lakini gadhabu yako imekuja. Wakati umefika kwa wafu kuhukumiwa na wewe kuwazawadia watumishi wako manabii, waamini na wale walio na hofu ya jina lako, wote wawili wasiofaa kitu na wenye nguvu. Na wakati wako umefika wa kuwaharibu wale ambao wamekuwa wakiiharibu dunia.”

19Kisha hekalu la Mungu mbinguni lilifunuliwa na sanduku la agano lake lilionekana ndani ya hekalu lake. Kulikuwa na miali ya mwanga, kelele, ngurumo za radi, tetemeko la ardhi na mawe ya mvua.

12

1Ishara kuu ilionekana mbinguni: mwanamke aliyefunikwa na jua, na akiwa na mwezi chini ya miguu yake; na taji ya nyota kumi na mbili ilikuwa juu ya kichwa chake.2Alikuwa na mimba na alikuwa analia kwa ajili ya maumivu ya kuzaa—katika uchungu wa kujifungua.3Na ishara nyingine ilionekana mbinguni: Tazama! Kulikuwa na joka mwekundu mkubwa ambaye alikuwa na vichwa saba na pembe kumi, na kulikuwa na taji saba kwenye vichwa vyake.4Mkia wake ulikokota theluthi moja ya nyota mbinguni na kuzitupa chini duniani. Joka alisimama mbele ya mwanamke aliyekuwa anakaribia kuzaa, ili kwamba wakati anazaa, apate kummeza mtoto wake.5Alimzaa mwana, mtoto wa kiume, ambaye atayatawala mataifa yote kwa fimbo ya chuma. Mtoto wake alinyakuliwa juu kwa Mungu na kwenye kiti chake cha enzi,6na mwanamke alikimbilia nyikani, mahali ambapo Mungu alikuwa ameandaa eneo kwa ajili yake, ili aweze kuhudumiwa kwa siku 1,260.

7Sasa kulikuwa na vita mbinguni. Mikaeli na malaika zake wakapigana na yule joka; naye joka mkubwa na malaika zake wakapigana nao.8Lakini joka hakuwa na nguvu za kutosha kushinda. Kwa hiyo haikuwepo tena nafasi mbinguni kwa ajili yake na malaika zake.9Joka mkubwa—yule nyoka wa zamani aitwaye Ibilisi au Shetani ambaye hudanganya - dunia nzima akatupwa chini katika dunia, na malaika wake wakatupwa chini pamoja naye.10Kisha nikasikia sauti kubwa kutoka mbinguni: “Sasa wokovu umekuja, nguvu—na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake. Kwa kuwa mshitaki wa ndugu zetu ametupwa chini—ambaye aliwashitaki mbele za Mungu wetu mchana na usiku.
11Walimshinda kwa damu ya Mwanakondoo na kwa neno la ushuhuda wao, kwa maana hawakupenda sana maisha yao, hata kufa.
12Kwa hiyo, shangilieni, ninyi mbingu, na wote mnaokaa ndani yake. Lakini ole wa nchi na bahari kwa sababu mwovu ameshuka kwenu. Amejawa na hasira kali, kwa sababu anajua kwamba ana muda mchache tu.

13Wakati joka alipotambua kuwa ametupwa chini kwenye nchi, alimfuata mwanamke ambaye alikuwa amezaa mtoto wa kiume.14Lakini mwanamke alipewa mabawa mawili ya tai mkubwa, ili kwamba aweze kuruka hadi kwenye eneo lililoandaliwa kwa ajili yake kule jangwani, eneo ambalo angeweza kutunzwa, kwa wakati, nyakati na nusu wakati-mahali asipoweza kupafikia huyo nyoka.15Nyoka alimwaga maji kutoka mdomoni mwake kama mto, ili afanye gharika ya kumgharikisha.16Lakini ardhi ilimsaidia mwanamke. Ilifunua kinywa chake na kuumeza mto alioutema joka kutoka kinywani mwake.17Kisha joka akamkasirikia mwanamke naye aliondoka na kufanya vita na uzao wake wote—wale wanaotii amri za Mungu na kushikilia ushuhuda kuhusu Yesu.18Kisha joka alisimama juu ya mchanga wa ufuo wa bahari.

13

1Kisha nikaona mnyama akitoka kwenye bahari. Alikuwa na pembe kumi na vichwa saba. Katika pembe zake kulikuwa na taji kumi, na katika kichwa chake kulikuwa na maneno ya kufuru kwa Mungu.2Huyu mnyama niliyemuona ni kama chui. Miguu yake ilikuwa kama ya dubu, na mdomo wake ulikuwa kama wa simba. Yule joka akampa nguvu, zake kiti chake cha enzi, na mamlaka yenye nguvu sana ya kutawala.3Kichwa cha mnyama mmojawapo kilionekana kuwa na jeraha kubwa ambalo lingesababisha mauti yake. Lakini jeraha lake likapona, na dunia yote ikashangazwa na ikamfuata mnyama.4Pia wakamwabudu joka, maana alimpa mamlaka yule mnyama. Wakamwabudu mnyama pia, na wakaendelea kusema, “Nani kama mnyama? Na “Nani atapigana naye?”5Mnyama akapewa mdomo ili azungumze maneno ya kujisifu na matusi. Aliruhusiwa kuwa na mamlaka kwa miezi arobaini na miwili.6Hivyo mnyama alifungua mdomo wake kuongea matusi dhidi ya Mungu, akalitukana jina lake, eneo alililokuwa akiishi na wale wanaoishi mbinguni.7Mnyama aliruhusiwa kufanya vita na waamini na kuwashinda. Pia, alipewa mamlaka juu ya kila kabila, watu, lugha na taifa.8Wote walioishi duniani watamwabudu yeye, kila mmoja ambaye jina lake halijaandikwa, toka uumbaji wa dunia, katika kitabu cha uzima, ambacho ni cha Mwana Kondoo, ambaye alichinjwa.9Ikiwa yeyote ana sikio, na asikilize.10Ikiwa mmojawapo amechukuliwa mateka, na kwenye mateka ataenda. Ikiwa mmojawapo ataua kwa upanga, kwa upanga atauawa. Huu ni mwito wa utulivu na uvumilivu na imani kwa hao walio watakatifu.

11Tena nikaona mnyama mwingine anakuja kutoka katika nchi. Alikuwa mwenye pembe mbili kama kondoo na akazungumza kama joka.12Alidhihirisha mamlaka yote ya mnyama yule wa kwanza katika uwepo wake, na kufanya katika dunia na wale walioishi wamuabudu yule mnyama wa kwanza, yule ambaye jeraha lake limepona.13Akafanya miujiza yenye nguvu, hata akafanya moto ushuke katika dunia kutoka mbinguni mbele ya watu,14na kwa ishara aliruhusiwa kufanya, akawadanganya hao wakaao katika dunia, akiwaambia kutengeneza sanamu kwa heshima ya mnyama ambaye alikuwa amejeruhiwa kwa upanga, lakini bado aliishi.15Aliruhusiwa kutoa pumzi katika ile sanamu ya mnyama ili sanamu iweze kusema na kusababisha wale wote waliokataa kumwabudu mnyama wauawe.16Pia akalazimisha kila mmoja, asiye na thamani na mwenye nguvu, tajiri na maskini, huru na mtumwa, kupokea alama katika mkono wa kuume au katika paji la uso.17Ilikuwa haiwezekani kwa kila mtu kuuza au kununua isipokuwa mwenye alama ya mnyama, na hii ni namba yenye kuwakilisha jina lake.18Hii inahitaji busara. Ikiwa yeyote ana ufahamu, mwache aweze kufanya hesabu ya namba ya mnyama. Maana ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666.

14

1Nilitazama na nikaona Mwana Kondoo amesimama mbele yangu juu ya Mlima Sayuni. Pamoja naye walikuwa 144,000 wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao.2Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisikika kama ngurumo za maji mengi na sauti kubwa ya radi. Sauti niliyoisikia ni kama wapiga vinubi wapigao vinubi vyao.3Wakiimba wimbo mpya mbele za kiti cha enzi na mbele za wenye uhai wanne na wazee. Hakuna hata mwenye uwezo wa kujifunza huo wimbo isipokuwa kwa 144,000 ambao wamekombolewa kutoka duniani.4Hawa ni wale ambao hawakujichafua wenyewe kwa wanawake, maana walijitunza wenyewe dhidi ya matendo ya zinaa. Ni hawa ambao walimfuata Mwana Kondoo popote alipoenda. Hawa walikombolewa kutoka kwa wanadamu wakiwa matunda ya kwanza kwa Mungu na kwa Mwana Kondoo.5Hakuna uongo uliopatikana katika vinywa vyao; hawalaumiwi.

6Nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, ambaye mwenye ujumbe wa mbinguni wa habari njema kwa kuwatangazia wenye kuishi duniani kwa kila taifa, kabila, lugha, na watu.7Akawaita kwa sauti kuu, “Mwogopeni Mungu na mpeni utukufu. Kwa maana muda wa hukumu umekaribia. Mwabuduni yeye, yeye aliyeumba mbingu, na dunia, na bahari, na chemchemi za maji.”8Malaika mwingine - malaika wa pili - akafuata akisema, “Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu, ambaye uliwanywesha mataifa divai ya ukahaba, divai ambayo ilileta ghadhabu juu yake.”9Malaika mwingine - malaika wa tatu - aliwafuata, akasema kwa sauti kuu, “Yeyote atakayemwabudu huyo mnyama na sanamu yake, na kupokea alama katika paji lake la uso au mkononi,10yeye pia atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu, divai ambayo imeandaliwa na kumwagwa bila kuchanganywa katika kikombe cha hasira yake. Mtu atakayekunywa atateswa kwa moto na moto wa kiberiti mbele za malaika zake watakatifu na mbele za Mwana Kondoo.11Na moshi wa maumivu yao ukaenda milele na milele, na hawakuwa na mapumziko mchana au usiku - hao waabuduo mnyama na sanamu yake, na kila mtu aliyepokea alama ya jina lake.12Huu ni wito wa subira na uvumilivu kwa waamini, wale ambao hutii amri za Mungu na imani katika Yesu.”13Nilisikia sauti kutoka mbinguni ikisema, “Andika haya: Heri wafu wafao katika Bwana.” “Ndiyo,” asema Roho, “Ili waweze kupumzika kutoka kwenye kazi zao, maana matendo yao yatawafuata.”

14Nilitazama na nikaona kulikuwa na wingu jeupe, na aliyeketi kwenye wingu ni mmoja aliyekuwa na mfano wa Mwana wa Mtu. Alikuwa na taji ya dhahabu katika kichwa chake na mundu mkali katika mkono wake.15Malaika mwingine tena alikuja kutoka kwenye hekalu na aliita kwa sauti kuu kwenda kwa yule aliyekaa katika wingu: “Chukua mundu wako na uanze kuvuna. Kwa kuwa muda wa mavuno umeshawadia, maana mavuno yaliyo katika dunia yameshaiva.”16Tena yule aliyekuwa kwenye wingu aliupitisha mundu wake juu ya dunia, na dunia ikavunwa.17Na malaika mwingine akaja kutoka kwenye hekalu la mbinguni; naye alikuwa na mundu mkali.18Na bado malaika mwingine akaja kutoka kwenye madhabahu, na malaika aliyekuwa na mamlaka juu ya moto. Akamwita kwa sauti kuu malaika ambaye alikuwa na mundu mkali, “Chukua mundu mkali na uyakusanye matawi ya mzabibu kutoka kwenye mzabibu wa nchi, kwa kuwa zabibu sasa zimeiva.”19Malaika alipeleka mundu wake katika dunia na alikusanya mavuno ya zabibu ya dunia na alirusha katika pipa kubwa la divai ya ghadhabu ya Mungu.20Chujio la divai lilipondwapondwa nje ya mji na damu ikamwagika kutoka katika hicho kimo cha hatamu ya farasi, kwa stadia 1,600.

15

1Tena nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na yenye kushangaza; Kulikuwa na malaika saba wenye mapigo saba, ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho (katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika).

2Niliona kile kilichotokea kuwa bahari ya bilauri iliyochanganywa na moto, na ikasimama pembeni mwa bahari ambapo wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake, na juu ya namba inayowakilisha jina lake. Walikuwa wameshikilia vinubi walivyopewa na Mungu.3Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo: “Matendo yako ni makubwa na yenye kushangaza, Bwana Mungu, utawalaye vyote. Mwaminifu na njia zako ni za kweli, Mfalme wa mataifa.
4Nani hatakuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu mbele zako kwa sababu u mwema na matendo yako yamejulikana.”

5Baada ya mambo hayo nilitazama, na sehemu takatifu sana, ambapo palikuwa na hema ya ushuhuda, iliyofungukia mbinguni.6Kutoka mahali patakatifu sana wakaja malaika saba wenye mapigo saba, wamevaa mavazi safi, kitani yenye kung'aa na mshipi wa dhahabu kuzunguka vifua vyao.7Mmoja wa wale wenye uhai wanne akatoa kwa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu mwenye kuishi milele na milele.8Mahali patakatifu sana kulijawa moshi kutoka kwenye utukufu wa Mungu na kutoka kwenye uwezo wake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika.

16

1Nikasikia sauti kubwa ikiita kutoka kwenye sehemu ya patakatifu na ikasema kwa wale malaika saba, “Nenda na ukamwage juu ya dunia mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu.”2Malaika wa kwanza alienda na kumwaga bakuli lake katika dunia; majeraha mabaya na yenye maumivu makali yalikuja kwa watu wenye alama ya mnyama, kwa wale ambao waliabudu sanamu yake.3Malaika wa pili alimwaga bakuli lake katika bahari; ikawa kama damu ya mtu aliyekufa, na kila kiumbe hai katika bahari kikafa.4Malaika wa tatu akamwaga bakuli lake katika mito na katika chemichemi za maji; zikawa damu.5Nikasikia malaika wa maji akisema, “Wewe ni mtakatifu uliyepo na uliyekuwako, Mtakatifu - kwa sababu umezileta hukumu hizi.6Kwa sababu walimwaga damu za waamini na manabii, umewapa wao kunywa damu; ndicho wanachostahili.”7Nikasikia madhabahu ikijibu, “Ndiyo! Bwana Mungu mwenye kutawala juu ya vyote, hukumu zako ni kweli na za haki.”8Malaika wa nne akamwaga kutoka kwenye bakuli lake juu ya jua, na likapewa ruhusa kuunguza watu kwa moto.9Waliunguzwa kwa joto lenye kutisha, na wakalikufuru neno la Mungu, mwenye nguvu juu ya mapigo yote. Hawakutubu wala kumpa yeye utukufu.

10Malaika wa tano akamwaga kutoka kwenye bakuli lake katika kiti cha enzi cha mnyama, na giza likaufunika ufalme wake. Walisaga meno katika maumivu makali.11Wakamtukana Mungu wa mbinguni kwa sababu ya maumivu yao na majeraha yao, na bado waliendelea kutokutubu kwa kile walichotenda.12Malaika wa sita alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika mto mkubwa, Frati, na maji yake yakakauka ili kuweza kuandaa njia kwa wafalme watakaokuja kutoka mashariki.13Nikaona roho tatu chafu zilizoonekana kama chura watokao nje ya mdomo wa yule joka, yule mnyama, na yule nabii wa uongo.14Ni roho za pepo zitendazo ishara na miujiza. Walikuwa wakienda kwa wafalme wa dunia yote ili kuweza kuwakusanya pamoja kwa vita katika siku kuu ya Mungu, mwenye nguvu zote.15(“Tazama! Ninakuja kama mwizi! Heri yule adumuye katika kukesha, atunzaye mavazi yake ili asiweze kwenda nje uchi na kuiona aibu yake.”)16Waliwaleta pamoja katika sehemu iliyoitwa katika kiebrania Amagedoni.

17Malaika wa saba alimwaga kutoka kwenye bakuli lake katika anga. Kisha sauti kuu ikasikika kutoka pakatifu na kutoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha!”18Kulikuwa na miale ya mwanga wa radi, ngurumo, vishindo vya radi, na tetemeko la kutisha - tetemeko kubwa la ardhi ambalo halijawahi kutokea duniani tangu wanadamu wamekuwepo duniani, hivyo ni tetemeko kubwa zaidi.19Mji mkuu uligawanyika katika sehemu tatu, na miji ya mataifa ikaanguka. Kisha Mungu akamkumbusha Babeli mkuu, na akaupa mji huo kikombe kilichokuwa kimejaa divai kutoka kwenye ghadhabu yake iliyo kali.20Kila kisiwa kikapotea na milima haikuonekana tena.21Mvua kubwa ya mawe, ikiwa na uzito wa talanta, ikashuka kutoka mbinguni juu ya watu, na wakamlaani Mungu kwa mapigo ya mvua ya mawe kwa sababu lile pigo lilikuwa baya sana.

17

1Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, “Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi,2ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa.”

3Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.4Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake.5Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI.”6Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu.

7Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).8Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja.9Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake.10Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.11Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na mwenyewe anaenda kwenye uharibifu wake.12Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama.13Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama.14Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na waliyo naye ni wale walioitwa, waliochaguliwa, na walio waaminifu.”15Malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.16Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto.17Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.18Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi.”

18

1Baada ya vitu hivi nilimwona malaika mwingine akishuka chini kutoka mbinguni. Yeye alikuwa na mamlaka kuu, na nchi iliangazwa kwa utukufu wake.2Alilia kwa sauti kuu, akisema, “Umeanguka, umeanguka, ule mji mkuu Babeli! Umekuwa sehemu yakaapo mapepo, na sehemu ikaapo kila roho chafu, na sehemu akaapo kila mchafu na ndege achukizaye.3Kwa kuwa mataifa yote yamekunywa mvinyo ya tamaa ya uasherati wake ambayo humletea ghadhabu. Wafalme wa nchi wamezini naye. Wafanyabiashara wa nchi wamekuwa matajiri kwa nguvu ya maisha yake ya anasa.”

4Kisha nilisikia sauti nyingine kutoka mbinguni iikisema, “Tokeni kwake watu wangu, ili msije mkashiriki katika dhambi zake, na ili msije mkapokea mapigo yake yoyote.5Dhambi zake zimerundikana juu kama mbingu, na Mungu ameyakumbuka matendo yake maovu.

6Mlipeni kama alivyowalipa wengine, na mkamlipe mara mbili kwa jinsi alivyotenda; katika kikombe alichokichanganya, mchanganyishieni mara mbili kwa ajili yake.7Kama alivyojitukuza yeye mwenyewe, na aliishi kwa anasa, mpeni mateso mengi na huzuni. Kwa kuwa husema moyoni mwake, ‘Nimekaa kama malkia; wala siyo mjane, na wala sitaona maombolezo.’8Kwa hiyo ndani ya siku moja mapigo yake yatamlemea: kifo, maombolezo, na njaa. Atateketezwa kwa moto, kwa kuwa Bwana Mungu ni mwenye nguvu, na ni mhukumu wake.”

9Wafalme wa nchi waliozini na kuchanganyikiwa pamoja naye watalia na kumwombolezea watakapouona moshi wa kuungua kwake.10Watasimama mbali naye, kwa hofu ya maumivu yake wakisema, “Ole, ole kwa mji mkuu, Babeli, mji wenye nguvu! Kwa saa moja hukumu yako imekuja.”11Wafanyabiashara wa nchi lieni na kuomboleza kwa ajili yake, kwa kuwa hakuna hata mmoja anunuaye bidhaa zake tena -12bidhaa za dhahabu, fedha, mawe ya thamani, lulu, kitani nzuri, zambarau, hariri, nyekundu, aina zote za miti ya harufu nzuri, kila chombo cha pembe za ndovu, kila chombo kilichotengenezwa kwa miti ya thamani, shaba, chuma, jiwe,13mdalasini, viungo, uvumba, manemane, ubani, mvinyo, mafuta, unga mzuri, ngano, ng'ombe na kondoo, farasi na magari, na watumwa, na roho za watu.14Matunda uliyoyatamani kwa nguvu zako yameondoka kutoka kwako. Anasa zako zote na mapambo yametoweka, hayatapatikana tena.15Wafanyabiashara wa vitu hivi waliopata utajiri kwa mapenzi yake watasimama mbali kutoka kwake kwa sababu ya hofu ya maumivu yake, wakilia na sauti ya maombolezo.16Wakisema, “Ole, ole mji ule mkuu uliovikwa kitani nzuri, zambarau, na nyekundu, na kupambwa kwa dhahabu, na vito vya thamani na lulu!”17Ndani ya saa moja utajiri wote huo ulitoweka. Kila nahodha wa meli, kila baharia, na wote wanamaji, na wote wafanyao kazi baharini, walisimama mbali.18Walilia walipouona moshi wa kuungua kwake. Walisema, “Ni mji gani unafanana na mji huu mkubwa?”19Walitupa mavumbi juu ya vichwa vyao, na walilia, wakitokwa machozi na kuomboleza, “Ole, ole mji mkubwa mahali wote waliokuwa na meli zao baharini walikuwa matajiri kutokana na mali zake. Ndani ya saa moja umeangamizwa.”

20“Furahini juu yake, mbingu, ninyi waumini, mitume, na manabii, kwa maana Mungu ameleta hukumu yenu juu yake!”

21Malaika mwenye nguvu aliinua jiwe kama jiwe kuu la kusagia na alilitupa baharini, akisema, “Kwa njia hii, Babeli, ule mji mkuu, utatupwa chini kwa ukatili na hautaonekana tena.22Sauti ya vinanda, wanamuziki, wacheza filimbi, na tarumbeta hawatasikika tena kwenu. Wala fundi wa aina yoyote hataonekana kwenu. Wala sauti ya kinu haitasikika tena kwenu.23Mwanga wa taa hautaangaza ndani yako. Sauti ya bwana harusi na bibi harusi hazitasikiwa tena ndani yako, maana wafanyabiashara wako walikuwa wakuu wa nchi, na wa mataifa, wamedanganywa kwa uchawi wako.24Ndani yake damu ya manabii na waamini ilionekana, na damu ya wote waliouawa juu ya nchi.”

19

1Baada ya mambo haya nilisikia sauti kama ya mlio mkubwa wa kundi kubwa la watu mbinguni ikisema, “Haleluya. Wokovu, utukufu, na nguvu ni vya Mungu wetu.

2Hukumu zake ni za kweli na za haki, kwa kuwa amemhukumu kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uzinzi wake. Amefanya kisasi kwa damu ya watumishi wake, ambayo aliimwaga yeye mwenyewe.”
3Kwa mara ya pili walisema, “Haleluya! Moshi hutoka kwake milele na milele.”
4Wale wazee ishirini na wanne na viumbe hai wanne wakasujudu na kumwabudu Mungu akaaye kwenye kiti cha enzi. Walikuwa wakisema, “Amina. Haleluya!”
5Ndipo sauti ilitoka kwenye kiti cha enzi, ikisema, “Msifuni Mungu wetu, enyi watumishi wake wote, ninyi mnaomcha yeye, wote wasio na umuhimu na wenye nguvu.”6Ndipo nilisikia sauti kama sauti ya kundi kubwa la watu, kama sauti ya ngurumo ya maji mengi, na kama ngurumo ya radi, ikisema, “Haleluya! Maana Bwanai Mungu wetu mwenye nguvu, ni mtawala juu ya wote, hutawala.
7Na tushangilie na kufurahi na kumpa utukufu kwa sababu harusi na sherehe ya Mwana Kondoo imekuja, na bibi harusi yuko tayari.”
8Aliruhusiwa kuvalishwa kitani safi na yenye kung'aa (kitani safi ni matendo ya haki ya waumini).

9Malaika akasema nami, “Yaandike haya: Wamebarikiwa walioalikwa kwenye sherehe ya harusi ya Mwana kondoo.” Vilevile akaniambia, “Haya ni maneno ya kweli ya Mungu.”10Nilisujudu mbele ya miguu yake nikamwabudu, lakini akaniambia, “Usifanye hivi! Mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako mwenye kuushika ushuhuda wa Yesu. Mwabudu Mungu, kwa kuwa ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.”

11Kisha niliona mbingu zimefunguka, na tazama kulikuwa na farasi mweupe! Na yule aliyekuwa amempanda anaitwa Mwaminifu na wa Kweli. Huhukumu kwa haki na kufanya vita.12Macho yake ni kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake ana taji nyingi. Ana jina lililoandikwa juu yake asilolifahamu mtu yeyote isipokuwa yeye mwenyewe.13Amevaa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aliitwa Neno la Mungu.14Majeshi ya mbinguni yalikuwa yakimfuata juu ya farasi weupe, walivalishwa kitani nzuri, nyeupe na safi.15Kinywani mwake hutoka upanga mkali ambao huyaangamiza mataifa, naye atawatawala kwa fimbo ya chuma. Naye hukanyaga vyombo vya mvinyo kwa hasira kali ya Mungu, hutawala juu ya wote.16Naye ameandikwa juu ya vazi lake na katika paja lake jina, MFALME WA WAFALME NA BWANA WA MABWANA.

17Niliona malaika amesimama kwenye jua. Aliwaita kwa sauti kuu ndege wote warukao juu, “Njoni, kusanyikeni pamoja kwenye chakula kikuu cha Mungu.18Njoni mle nyama ya wafalme, nyama ya majemedari, nyama ya watu wakubwa, nyama ya farasi na wapanda farasi, na nyama ya watu wote, walio huru na watumwa, wasio na umuhimu na wenye nguvu.”19Nilimwona mnyama na wafalme wa nchi pamoja na majeshi yao. Walikuwa wamejipanga kwa ajili ya kufanya vita na mmoja aliyepanda farasi na jeshi lake.20Mnyama alikamatwa na nabii wake wa uongo aliyezifanya ishara katika uwepo wake. Kwa ishara hizi aliwadanganya wale walioipokea chapa ya mnyama na walioisujudia sanamu yake. Wote wawili walitupwa wangali hai katika ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti.21Wale waliobaki waliuawa kwa upanga uliotoka kinywani mwa mmoja aliyepanda juu ya farasi. Ndege wote walikula mizoga ya miili yao.

20

1Kisha niliona malaika akishuka kutoka mbinguni, akiwa na ufunguo wa shimo lisilo na mwisho na mnyororo mkubwa mkononi mwake.2Alimshika yule joka, nyoka wa zamani, ambaye ni ibilisi au Shetani, na kumfunga miaka elfu.3Alimtupa kwenye shimo lisilo na mwisho, akalifunga na kulitia mhuri juu yake. Hii ilikuwa hivyo ili kwamba asiwadanganye mataifa tena mpaka miaka elfu itakapoisha. Baada ya hapo, ataachiwa huru kwa muda mchache.

4Kisha niliona viti vya enzi. Waliokuwa wamevikalia ni wale ambao walikuwa wamepewa mamlaka ya kuhukumu. Vilevile niliona nafsi za wale ambao walikuwa wamekatwa vichwa kwa ajili ya ushuhuda kuhusu Yesu na kwa neno la Mungu. Walikuwa hawajamwabudu mnyama au sanamu yake, na walikataa kupokea alama juu ya paji za nyuso zao au mkono. Walirudi uhai na wakatawala pamoja na Kristo kwa miaka elfu.5Wafu waliobaki hawakurudi uhai mpaka miaka elfu ilipokuwa imeisha. Huu ndio ufufuo wa kwanza.6Mbarikiwa na mtakatifu ni mtu yeyote ambaye atashiriki katika ufufuo wa kwanza! Mauti ya pili haina nguvu juu ya watu kama hawa. Watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo na watatawala na yeye kwa miaka elfu.

7Wakati miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa kutoka gerezani mwake.8Atakwenda kuwadanganya mataifa katika kona nne za dunia -Gogu na Magogu - kuwaleta pamoja kwa ajili ya vita. Watakuwa wengi kama mchanga wa bahari.9Walikwea juu kwenye tambarare ya nchi nao walizunguka kambi ya waumini, mji upendwao. Lakini moto ulishuka kutoka mbinguni na kuwaangamiza.10Shetani, ambaye aliwadanganya, alitupwa ndani ya ziwa liwakalo kiberiti, ambamo mnyama na nabii wa uongo walikuwa wameshatupwa. Watateswa mchana na usiku milele na milele.

11Kisha niliona kiti cha enzi kikubwa cheupe na yule ambaye alikaa juu yake. Dunia na mbingu zilikimbia mbali kutoka katika uwepo wake, lakini hapakuwako nafasi ya wao kutolokea.12Niliwaona waliokufa - hodari na wasio wa muhimu wamesimama mbele ya kiti cha enzi, na vitabu vilifunuliwa. Kisha kitabu kingine kilifunguliwa - Kitabu cha Uzima. Wafu walihukumiwa kwa kile kilichoandikwa ndani ya vitabu, matokeo ya kile walichokifanya.13Bahari iliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake. Kifo na kuzimu viliwatoa wafu ambao walikuwa ndani yake, na wafu walihukumiwa kulingana na matendo yao.14Kifo na kuzimu zilitupwa ndani ya ziwa la moto. Hii ni mauti ya pili - ziwa la moto.15Kama jina la yeyote halikupatikana limeandikwa ndani ya Kitabu cha Uzima, alitupwa ndani ya ziwa la moto.*

21

1Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimekwishapita na bahari haikuwepo tena.2Niliona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, uliyoshuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu, ulioandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.3Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao.4Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao na hapatakuwa na kifo tena au kuomboleza au kulia au maumivu. Mambo ya kale yameshapita.

5Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, “Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya.” Alisema, “Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli.”6Aliniambia, “Mambo haya yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aonaye kiu nitampatia kinywaji bila gharama kutoka katika chemchemi za maji ya uzima.7Yeye ashindaye atayarithi mambo haya, na nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.8Lakini kama ilivyo kwa waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao itakuwa katika ziwa la moto wa kiberiti uunguzao. Hiyo ndiyo mauti ya pili.”

9Mmoja wa malaika saba alikuja kwangu, yeye ambaye alikuwa na mabakuli saba yaliyojaa mapigo saba ya mwisho na alisema, “Njoo hapa. Nitakuonesha bibi harusi, mke wa mwana kondoo.”

10Kisha alinichukua mbali katika Roho kwenye mlima mkubwa na mrefu na alinionesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu.11Yerusalemu ulikuwa na utukufu wa Mungu, na uzuri wake ulikuwa kama kito cha thamani, kama jiwe la kioo safi la yaspi.12Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na miwili, pamoja na malaika kumi na wawili milangoni. Juu ya milango palikuwa pameandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli.13Upande wa mashariki palikuwa na milango mitatu, upande wa kusini milango mitatu, upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa magharibi milango mitatu.14Ukuta wa mji uilikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake palikuwa na majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo.

15Yeye aliyeongea nami alikuwa na kipimo cha fimbo iliyotengenezwa kwa dhahabu kwa ajili ya kupima mji, milango yake na ukuta wake.16Mji ulijengwa mraba; urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Alipima mji kwa kipimio cha fimbo, stadia 12,000 kwa urefu (urefu wake, upana, na kimo vilifanana).17Vilevile alipima ukuta wake, unene wake ulikuwa dhiraa 144 kwa vipimo vya kibinadamu (ambavyo pia ni vipimo vya malaika).

18Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi nao mji dhahabu safi, kama kioo safi.19Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa na kila aina ya jiwe la thamani. La kwanza lilikuwa yaspi, la pili lilikuwa yakuti samawi, la tatu lilikuwa kalkedon, la nne zumaridi,20la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolitho, la nane zabarajadi, la tisa yakuti ya manjano, la kumi krisopraso, la kumi na moja hiakintho, la kumi na mbili amethisto.21Ile milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili, kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja. Mitaa ya mji ilikuwa dhahabu safi, ikionekana kama kioo safi.

22Sikuona hekalu lolote ndani ya mji, kwa kuwa Bwana Mungu, ambaye anatawala juu ya vyote, na Mwana Kondoo ni hekalu lake.23Mji haukuhitaji jua au mwezi ili kungaza juu yake kwa sababu utukufu wa Mungu uliangaza juu yake, na taa yake ni Mwana Kondoo.24Mataifa watatembea kwa mwanga wa mji huo. Wafalme wa dunia wataleta fahari zao ndani yake.25Milango yake haitafungwa wakati wa mchana, na hapatakuwa na usiku pale.26Wataleta fahari na heshima ya mataifa ndani yake,27na hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake wala yeyote ambaye afanyaye jambo lolote linalochukiza au udanganyifu bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo.

22

1Kisha malaika akanionesha mto wa maji ya uzima, maji yalikuwa ya mng'ao kama wa bilauri. Yalikuwa yakitiririka kutoka katika kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo2yakipitia katikati ya mtaa wa mji. Katika kila upande wa mto palikuwa na mti wa uzima, unaozaa aina kumi na mbili za matunda, na huzaa matunda kila mwezi. Majani ya mti ni kwa ajili ya uponyaji wa mataifa.3Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana Kondoo kitakuwemo ndani ya mji, na watumishi wake watamtumikia.4Watamuona uso wake, na jina lake litakuwa juu ya vipaji vya nyuso zao.5Hapatakuwa na usiku tena; wala hapatakuwa na hitaji la mwanga wa taa au jua kwa sababu Bwana Mungu ataangaza juu yao. Nao watatawala milele na milele.

6Malaika akaniambia, “Maneno haya ni ya kuaminika na kweli. Bwana Mungu wa roho za manabii alimtuma malaika wake kuwaonesha watumishi wake kitakachotokea hivi karibuni.”7“Tazama! Ninakuja upesi! Amebarikiwa yeye anayeyatii maneno ya unabii wa kitabu hiki.”

8Mimi, Yohana, ndiye niliyesikia na kuona mambo haya. Nilipoyasikia na kuyaona, nilianguka chini mwenyewe mbele ya miguu ya malaika kumwabudu, malaika aliyenionesha mambo haya.9Akaniambia, “Usifanye hivyo! Mimi ni mtumishi mwenzako, pamoja na ndugu zako manabii, pamoja na wale wanaotii maneno ya kitabu hiki. Mwabudu Mungu!”10Kisha akaniambia, “Usiyatie muhuri maneno ya unabii wa kitabu hiki, maana wakati umekaribia.11Asiye mwenye haki, aendelee kutokuwa mwenye haki. Ambaye ni mchafu kimaadili, na aendelee kuwa mchafu kimaadili. Mwenye haki, na aendelee kuwa mwenye haki. Aliye mtakatifu, na aendelee kuwa mtakatifu.”

12“Tazama! Naja upesi. Ujira wangu uko pamoja nami, kumlipa kila mmoja kulingana na alichokifanya.13Mimi ndimi Alfa na Omega, wa Kwanza na wa Mwisho, Mwanzo na Mwisho.14Wamebarikiwa wale waoshao mavazi yao ili kwamba wapate haki ya kula kutoka katika mti wa uzima na kuuingia mji kupitia malangoni.15Nje kuna mbwa, wachawi, wazinzi, wauwaji, waabudu sanamu, na kila apendaye na ashuhudiaye ushahidi wa uongo.

16Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia kuhusu mambo haya kwa makanisa. Mimi ni mzizi wa uzao wa Daudi, Nyota ya Asubuhi ing'aayo.”

17Roho na Bibi harusi wasema, “Njoo!” Na yeye asikiaye aseme, “Njoo!” Yeyote aliye na kiu, na aje, na yeyote anayeyatamani, na ayapate maji ya uzima bure.

18Namshuhudia kila mtu asikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki: Kama yeyote ataongeza katika hayo, Mungu atamuongezea mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki.19Kama mtu yeyote atayaondoa maneno ya kitabu hiki cha unabii, Mungu ataondoa sehemu yake katika mti wa uzima na katika mji mtakatifu, ambayo habari zake zimeandikwa ndani ya kitabu hiki.

20Yeye ashuhudiaye mambo haya asema, “Ndiyo! Naja upesi.” Amina! Njoo, Bwana Yesu!

21Neema ya Bwana Yesu iwe na kila mtu. Amina.