1paulo na timotheo, vachumishi wa KRisto Yesu. kwa valee valiothengwa kachika Kristo wanavoishi wafilipi pamoya na vaangalidhi na mashemasi. 2Neema na ive kwenyu na amani ithokao kwa mungu Baba na Bwana wechu Yesu Kristo.3Nanshukuru Mungu angu kila ninavowakumbuka inyi. 4Mara dhothe kachika kila ombi langu kwa ajili enyu inyi vothe kua nafurahi nnapovaombea. 5Anashukurani nyingi kwasababu ushirika wenyu kachika injili changu siku akwandha mpaka eo. 6Nina hakika kuva iye aliandhisha kadhi njema ndani enyu athaendelea kukamilisha mpaka siku ya Bwana Yesu Kristo.7Ni sawa kwangu kusikia hia iyu enyu inyi vothe kwasababu ndhavaveka moyoni mwangu. Maana inyi mndhakuva washirika wendha kachika neema kachika kifungu changu na kachika uchechedhi na usibithishaji wangu wa injili. 8Mungu ni shahidi wangu jinsi nilivo na shauku iyu enyu vothe kachika undani wa pendho la Kristo Yesu.9Na ninaomba kwamba upendho wenyu uongetheke dhaidi na dhaidi. kachika maharifa na ufahqamu wothe. 10Ninaomba kwa ajili ya hili ili muvena uwedho wa kupima na kuthauwa mambo ali vo bora sana. Pia ninavaombea mue bora safi pasipo kuva na hathia yoyothe kachika siku ya Kristo. 11Na pia ili muyadhe na chunda la haki lipachikanalo kachika Yesu Kristo, kwa uthukufu na sifa ya mungu.12Sasa nduthangu nathaka muive kua mambo yaliothokea kwangu wandhafanya injili iendelee sana. 13Ndio maana dhifungo dhangu kachika Kristo, lindhaivikana kwa valindhi ikulu ote kwa kila nchu. 14vengi vandugu vana imanizaidi kachika Bwana, kwa sababu ya minyororo angu, navo vanaujasiri kuvanena ineno la Mungu bila uwoga.15Baadhi kweli hatha kuchangatha Kristo. kwa fithina na ugomvi na pia vangine. 16valee vanavo nchangatha Kristo kwa upendho wanavoivakua nthavekwa hapa kwa ajili ya uchechedhi wa injili. 17Bali vangine vanachangadha Kristo kwa ubinafsi na kwania mbovu. Hudhani kuva vanasababisha machachidho kwangu kachika minyororo angu.18Kwahio usijali aidha ndhia ikiva ni kwa hila au kwakweli, Kristo anachangadhwa na kachika hili chunafurahika kwa kuchangadhwa! Ndivo, ninafurahia. 19Kwakuva naiva yakuva ili lithaecha kufunguliwa kwangu. Yambo hili lithathokea kwa sababu yamaombi enyu na msaadha wa roho wa Yesu Kristo.20kuling'ana na matharajio angu ya uhakika na ukweli ni kwamba sithavona aibu. badala akekwa ujasiri othe kama ambavo siku dhothe na sasa natharajia kuva Kristo athanyuliwa kachika mwili ikiva kachika udhima ao kachika kifo. 21Kwa maana kwangu imi kuishi na Kristo na kufa ni faida.22Lakini kama kachika mwili kudhaa chunda kachika kadhi angu, kwahivo siisi lakuthaua? siisi . 23Maana ndhasukumwa sana na mavadho haa ya mwili na kua pamoya na Kristo, kichu ambacho ni sawa sanabora dhaidi. 24Ingawa kubakia kachika mwili huu ni yambo lamuhimu sana kwa ajili enyu.25kwakuva unao uhakika wa iyuu ya hili,naiva ithabakia nakuendelea kua pamoya nanyi vote, kwaajili ya maendeleo na furaha na imani enyu. 26Na hii itaecha furaha enyu kuru kachika Kristo Yesu. Kwa sababu angu ithaongedheka, kwasababu ya uwepo wangu tena pamoya nanyi. 27Unathakiwa kuishi maisha enyu kachika mwenendo ndhuri. Ipasavo injili ya Kristo. fanyeni hia ila nikia kuvavona ao nisipokuya nikie kuva mudhasimama imara kachika roho moya nathamani kusikia kuva mna roho moya, mkishindania imani ya injili kwa pamoya.28Na musichishwe na kichu chochothe kinachofanywa n maadui venyu, hii kwavo niishara ya uharibifu. Bali kwenyu niishara ya uokovu kuthoka kwa Mungu. 29Kwa maana inyi mndhapewa bure kwa ajili ya Kristo sikuamini thu, bali nakucheswa pia kachika iye. 30Kwa maana kuna mgogoro ule ule kama mlovona kwangu mnaskia kwamba.
1Ikiva kuna kuchiwa moyo kachika Kristo, kama kuna furaha kachika pendho lake, ikiva kuna ushirikiano wa roho, ikiva kuna rehema na huruma. 2Ikamilisheni furaha angu kwa nia moya ukiva na upedho mmoya, mukiva wa moya kachika roho nakuva nakusudi moya.3Musifanye na ubinafsi na majivuno. isipokuva kwa unyenyekevu mukivavona vangine kuva bora zaidi enyu. 4Kila mmoya wenyu asiangalie thu maithaji ake binafsi bali pia ajali maitaji yavengine.5Muve na nia kama alivonao Yesu Kristo. 6ikaawaje iye ni sawa na Mungu lakini hakujali kufa sawa na Mungu kichu cha kushikimana nacho. 7Badala ake aliishusha mwenewe, alithukua umbo la mthumishi akaidhokedha kachika mfano wa vanadamu. alivonekana kama mwanadhamu 8Iye alinyenyekea nakuva ndhii hadi kifo, kifo cha msalaba9Hiya basi Mungu alinthukudha sana alimpa ina ikuru lipichalo kila ina. 10Alifanya hiya ili kwamba kachika ina la Yesu kila ondo sheti linyame magochi ya walivo mbinguni n walivo iyuu na iti ya ardhi. 11Na alifanya hiya ili kwamba kila ulimi sharti ukiri kwamba Yesu ni Bwana kwa uthukufu wa Mungu Baba.12Kwaivo basi wapendhwa vangu kama mnaothii siku dhote si thuu kachika uwepo wangu kakini sasa ni dhaidi sana hata pasipo uwepo wangu. Hatha wajibikeni uwokovu wenyu wenyewe kwa hofu nakuchechemeka. 13kwakuva n Mungu anaechenda kadhi ndani enyu, ili kuwawedhesha na nia yakuchenda mambo yalee yampendhedhao iye.14Fanyeni mambo ote bila malalamiko na mabishano 15Fanyeni ivo ili kwamba musilaumike na kua vana va Mungu vaaminifu vasivo na lawama. Fanyenu ivo ili kwamba muwe na nuru aduniani kachika kidhadhi cha uasi 16Shikeni sana neno la udhima ili kwamba live la sababu yakutukua siku yakristo. kisha mufahamu kwamba sikubika mbio bure17Hatha kama ninamiminiwa kama sadaka iyuu ya dhabihu na huduma ya imani ndhafurahi ina ndhafurahi pamoya nanyi vote. 18Vile vile nanyi pia ninafurahi, munafurahika pamoya nanyi,19Lakimi nathumaini kachika Bwana Yesu kunchuma Timotheo kwenyu hiya nda huu, ili kwamba uwedhe kuchiwa moyo nthakapo kuiva mambo enyu. 20Kwakuva sina ngine alie na nchadhamo kama wake mwenye ukweli kwaajili enyu. 21Vangine vote ambavo ningevachuma kwenyu vathaandha thafudha mambo avo binafsi thuu.n mambo ya Yesu ,22Lakini mnaiva thamani ake kwa sababu kama mwana anavomhudumia Baba ake ndivyo ilivyo chumikaa pamoya nami kachika injili. 23Kwahiyo nathumaini kunchuma haraka pindi thuu ntakapo fahamu nini kithathokea kwangu. 24Lakiini nna hiyo thumaini kunchuma haraka pindi thuu nthakapo fahamu nini kithathikea kwangu lakini nina hakika kachika Bwana kwamba imi mwenyewe ntakuya hia nda huu.25Lakini nafikiri nimuhimu kumrudisha kwenyu Epafradito.Iye ni nduangu na nchenda kadhi mwendhangu na askari mwendhangu, mjumbe na nchumisi wenyu kwaajili ya mahithaji angu. 26Kwasababa alikuva na hofu na alithamani kuva pamoya nanyi vote, kwakuva ndhasikia kwamba alikuva ngonjwa. 27Maana hakika alikuva ngonjwa sana kiasi cha kufa.lakini Mungu alimhurumia na wema huo haukuva iyuu ake thuu, lakini pia alikuva iyuu angu ili kwamba nisive na huzuni iyuu ya huzuni.28Kwaivo nnarudisha kwenu haraka iwedhakanavo, ili kwamba ntakapo muona thena mpache kufurahi nanyi nntakuva mndhaondolewa wasiwasi. 29Mkaribisheni Epafradito kachika Bwana kwa furaha dhothe vaheshimuni vachu kama iye . 30Kwakuva ilikuva kwaajili ya kadhi ya Kristo kwamba alikaribia kufa.Alihathahatarisha maisha ake ili kuniokoa imi na athafanya kile ambacho hamukuedha kufanya kachika kunhudhumia imikwan mko mbali.
1Hatimae, duthangu furahini kachika Bwana. sivon, usumbufu kuwaandikia tena maneno ale ale haya mambo yatavapa usalama 2ihadharini. na ibwa. ihaadharini na wachenda kazi waovu , ihadharini na vale wajikachao miili vako. 3kwa kuva isi ndio twahara isi ndio huva twahara isi ndio huva chwamuabudu mungu kwa msaadha wa roho. chuivunioa kachika kristo Yesu, na ambavo hachuna ujasiri kachika mwili.4Hata hivyo , kama kungekuva na nchu vakunitumaini. mwili huu, imi ningewedha kufanya hia thaidi. 5kwani, nilitahiriwa siku ya nane, nilidhaliwa kachika kabila la waiziraili. nivakabila va binjameni kutimidha haki ya sheria ya musa, nilikuva Frarisayo.6Kwa juhudi, dhangu nililichesa kanisa langu kwa kuithi ya sheria, sikuva na lawama kisheria. 7lakini kachika mambo ote nilio yavona kua afaidha kwangu imi. niliyehesabu kuva kama chakachaka kwa sababu ya kumuidha Kristo,.8kwa kweli, na hisabu mambo ote kuva hasara, kutokana na ubora kwa kumuiva Kirsto Yesu Bwana wangu na yahesabu kama chakachaka ili nimpache kristo 9nivonekane ndani ake. sina haki angu binafsi kutoka kachika sheria, bali ninao haki ile ipachikanao kwa imani, kachika kristo itokao kwa mungu, yenye msingi kachika imani, 10kwa hia sasa nathaka kumuiva iye na ya ufufuo wake na ushirika wa macheso ake. nathaka kubadilishwa na kristo kachika mfano wa chake 11angalau kuva na matumaini kachika ufufuo wa wafu12Sio kweli kwamba tayari ndhapacha mambo hao. au kwamba ndhakuva kachika hao.bali naithahidi niwethe kupacha kile kilicho pachikana na kristo yesu, 13nduthangu sidhani , kwamba ndhskwisha kupacha mambo haa; bali nafanya yambo moya na sahau yanima nayaenga ya mbe. 14naitahidi kufika lengo kusudi ili nipache chudho ya iyu mwicho wa Mungu kachika kristo yesu15Vote chulivo kukulia uokovu, chunapaswa kuvudha namna hii, na ikiva ingine atafikiria kuva namna iliyotafauti kuhusu yambo lolote, Mungu pia talifunyia hilo kwenyu. 16hatha hia, hathua tuliosikilia na chwenende ndhidho huu,17Nduthangu thabeni imi vaengini kwa makini vale vanavokwenda kwa mfano ; ulio wajinsi echu. 18vangi vanavoishi valee ambavo mara nyingi ndharaambia, na sasa ndhaavambia kwa mathodhi vengi vanaoishi kama maadui wa nsalaba wa kristo. 19mwisho wavo ni uharibifu kwa kuva Mungu avo ni ichumbo na kiburi chao ilo kachika aibu yavo. wanafikiria mambo ya kidunia,20Bali uraia wechu uko mbiguni ambavo ninatarajia mwokozi wechu kristo . 21atabadilisha mwili dhaifu kuva kama mwili wake wautukufu kwa uwedho ule ule unaomuedhesha kuvithibiti vichu
1Kwaiva vapendhwa vangu, ambavo nawathamini, ambavo ni furaha na thaji langu. simameni imara kachika Bwana inyi marafiki wapendhwa chunakusihi uwe. Eudia 2nakusihi uwe Sintike mregeshe mahusiano ya amani kachi yenyu , kwa sababu inyi vote vavili na Bwana 3kwakweli niwasihi inyi wachenda kazi wenzdhangu ,muvasaaidie hava vanawake kwa kuva vachumishi vangine vya Bwana ambavo maina avo yandhaandhikwa kachika kitabu cha uzima4furahini kachika Bwana siku dhote tena furahini, kachika Bwana tena mthanena furahini 5upole wenyu na ujulikane kwa watu ote. Bwana yuko karibu. 6usiisumbue kwa yambo lolote. badala yake, fanyeni mambo yenu ote kwa ndhia ya kusali na kuomba na kushukuru. na mahitaji enu yajulikane kwa Mungu. 7basi amani ya Bwana iliyo kuru kuliko ufahamu ote thalinda mioyo na mawadho enyu kwamsaada wa Kristo Yesu ,8Hatimae nduthangu, yatakafarini .mambo ote enyu ukweli. heshima, haki, usafi, upendho, na alee enyu busara pamoya na alee anao hitaji kusifiwa. 9athekeledhini mambo alee mulioifudha, muliopokea mulivoaskia n yalee muliovona nae Baba echu waamani atakuva nanyi.10NInao furaha kuru sana iyuu enyu kachika Bwana nakuva inyi ntavaonesha thena nia yakuiuhusishwa kwenyu . iyuu ya maithali angu kwakweli, hapo awali hapukupacha fursa yakunisaidia. 11sineni hiya ili kuipachia kichu kwaajili ya mathitaji angu kwani ndhaifundha kuridhika kachika hali dhote. 12nafahamu kuishi kachika hali yakupungukia na pia kachika hali dhakuva na dhingi siri ya namna kula vakathi wa shibe na jinsi ya kula wakati wa ndaa. yani! dhingi nakuva muithaji, 13ninawedha kufanya haa kwakuedheshwa nae anchiao nguvu,14hatha hiya mulifanya dhema kushiriki nami kachika dhiki nguvu, 15inyi wafilipi munafahamu mwandhi wa injili nilipoondoka makendonia, hakuna kanisa lilio niwedhesha kachika mambo yanayohusu uthowaji na kupokea isipokuva inyi peke enyu 16hathia nilipokuva Thesalonike, inyi mulichumia msaada dhaidi ya mara moya kwaajili yamathitaji angu. 17simanishi kwamba natafudha msaada.bali hunena ila mpache machunda yalichao faidha kwenyu.18andapokea vichu dhote, na sasa nimeya na vichu dhingi. ndapokea dhichu venyu kutoka kwa Epafradito. ni dhichu dhidhuri dhenye kunukia mithiri ya mnyukacho, dhenye kukubalika ambao dhote ni sadaka inaompendetha Mungu . 19kwa ajili hiyo, mungu angu yathwajezeni maithtaji enyu kwa uthajiri wa utukufu wake kachika yesu kristo. 20sasa kwa mungu na baba echu uve uthukufu milele,. na milele amin.21salamu dhangu ndhinifikie kila muumini kachika Kristo Yesu , vapendhwa nilivo navo hapa wanisalimu. 22pia vaumini vote hapa vanawasalimieni , hususan vale va familia taisari. 23na sasa neema ya Bwana wechu Yesu Kristo iwe na Roho.
1Paulo, mchuma wa Kristo Yesu kwa mapendhi a Mungu, na Timotheo nduechu. 2kwa vaumini vachu vachakachifu wa Mungu na ndugu vaaminifu kachika Kristo walioko Kolosai. Neema ive kwenu na amani kuthoka kwa Mungu Baba echu. 3Chunathoa shukrani kwa Mungu, Baba wa Bwana wechu Yesu Kristo na chunavaombea kila mara kwa mara.4Chumeskia imani enyu kachika Yesu Kristo na upendho mlionao kwa valee vachu vote valiothengwa kwa ajili ya wachakachifu wa Mungu. 5Kwa sababu ya daraja la uhakika lililohifadhiwa mbinguni kwa ajili enu, mdhasikia kuhusu daraja hio kwa uhakika kachika ineno la ukweli, inijili 6ambao idhakuya kwenyu. Na kwa ndhia hio hio, injili hii hudhaa chunda na inaenea ulimwenguni kothe. Indhakuva ikifanya ndani enyu changu siku mliposikia na kufahamu neema a Mungu hachika kweli.7Hii ndio injili kama mlivoifunza kuthoka kwa Epafra, nchumishi mwendhechu ambae ni mchumishi mwaminifu wa Kristo kwa ajili echu. 8Epafra adhaufanya uyulikane kwechu upendho wenyu kachika roho.9Kw sababu a upendho huu, changu siku chuliposikia hia hachuyakoma kuwaombea.Chumekuva chukiomba kwamba mthayazwa na maarifa a mapenzi ake kachika hekima ote na ufahamuu wa kiroho. 10Chumekua chukiomba kwamba mthadhembea kwa ustahimilivu wa Bwana kachika ndhia thimpendethatho Bwana. Chundhakua chukiomba mthadhaa chunda kachika kila chendo njema na kwamba mthakua kachika maarifa a Mungu.11Chunaomba muwedhe kutiwa nguvu kachika kila uwedho kulingana na nguvu dha udhukufu wake kachika uvumilivu na ustahimilivu wothe. 12Chunaomba kwamba kwa furaha mthathoa shukurani kwa Baba adhaowafanya inyi muwedhe kua na pahala kachika urithi va vaumini kachika nuru.13Andhakuokoa kuthoka kachika uthawala wa gidha na kuchuhamisha, akachuhamishia kachika ufalme wa Mwana wake mpendhwa. 14Kachika Mwanae chuna ukombothi na msamaha wa dhambi.15mwana ni mfano wa Mungu asievonekana, mdhawa wa kwandha wa uumbaji wothe. 16Kwa kuva kwa iye dhichu dhote dhiliumbwa, dhile dhilidhoko mbinguni na dhilidhoko duniani, dhichu dhinadhovoonekana na dhisidhovoonekana. Ikiva na dheadhi au mamlaka au uthawala au wenye nguvu, dhichu dhothe dhiliumbwa na iye kwa ajili ake. 17Iye andhakuwapo kabla a dhichu dhothe na kachika iye dhichu dhothe dhindhashikamana pamoya.18Na iye ndie kithwa cha mvili yani Kanisa. Iye ni mwandho na mdhaliwa wakwadha kuthoka miongoni mwa waafu, hivo ananafasi a kwandha miongoni mwa dhichu dhothe. 19kwa kuva Mungu alipendhedhwa kwamba uthimlifu wake wothe uishi ndani ake. 20Na kuoachanisha dhichu dhothe kwa ndhia a mwanae Mungu andhafanya amani kupichia damu a msalaba wake. Akapachanisha dhichu dhothe mwenewe, ikiwa ni dhichu dha duniani au dhichu dha mbinguni.21Inyi pia kwa vakathi mmoya, mlikuwa mdhathengwa na Mungu na mlikuwa maadhui ake kachika akili na machendo maovu. 22Lakini sasa andhavapachanisha inyi kwa mvili wake kupichia kifo. Andhafanya hia ili kuaecha inyi vathakathifu, vasio na lawama bila dosari mbee ake. 23Kama mkiendelea kachika imani, mndhaoimarisha na kuva thabithi pasipo kuondoswa kuthoka kwenye daraja la ujasiri la injili mdhaosikia. Hii ndio injili ambao indhahubiriwa kwa kila kiumbe thini a mbingu. Hii ndio injili ambao kua imi, Paulo, ndhakuva nchumishi.24Sasa naafurahia macheso angu kwa ajili enu. Nami nathimidha kachika mvili wangu kinachopugua kwa macheso a Kristo kwa ajili a mvili wake, ambao ni kanisa. 25Imi ni mchumishi va kanisa hili, savasava na vajibu nliopewa kuthoka kwa Mungu kwa ajili enyu, chulithimitha ineno la Mungu. 26Huu ni ukweli wa siri iliokuva indhasithwa kwa miaki mingi na kwa vothe vaaminio kachika iye. 27Ni kwa vale ambao Mungu alithaka kufungua ulivo uthajiri wa uthukufu wa siri wa ukweli miongoni mwa mathaifa. Ni kwamba Kristo umo ndani enu, ujasiri wa uthukufu uyao.28Huu ndie chunaemchangatha. Chunamkanya kila nchu na kumfudhisha kila nchu kwa hekima ote ili kwamba chumueche kila nchu mkamilifu kachika Kristo. 29Kwa ajili hii, imi naibidhilisha na kuithahidi kulingana na nguvu ake ifanyao kadhi ndani angu kachika uendha.
1Kwa kuva nataka mfahamu namna ambavo nimekuva na taabu ningi kwa ajili enu, kwa ote valioko Laodikia, na kwa ote ambavo hawayauvona uso angu kachika mwili. 2Nafanya kadhi ili nyoyo thao dhifarijiwe, kwa kuechwa pamoya kachika upendho na kachika utajiri ote wa wingi wa uhakika kamili na maarifa. Kachika kuiiva siri ya kweli ya Mungu ambavo ni Kristo. 3Kachika iye hadhina thote tha hekima na maarifa dhimesitwa.4Nanena hia ili kwamba mchu wowote asie kuwahadhaa kwa hutuba yenye ushawishi. 5Na ingawa sipo pamoya nainyi kachika mvili lakini nipo na inni kachika roho. Ninafurahia kuvona utaratibu wenyu mdhuri wene nguvu na imani yenye kachika Kristo.6Kama mlivompokea Kristo Bwana, tebeeni kachika iye muve na midhidhi ndani ake, mjenge kachika iye. 7Mwimarishwe kachika imani kama tu mlivyofundishwa, na kufungwa kachika shukurani ikuru.8Engani ya kuva mchu wowote asiwashike kwa falsafa na maneno machupu ya kuvahadaa kulingana mapokethi ya vanadamu, kulingana na kanuni tha kidunia, na thio kulingana na kristo. 9Kwa kuva kachika iye ukamilifu ote wa Mungu unaishi kachika mvili.10Nainyi mmdayathwa kachika iye. Iye ni kitwa cha kila uwetha na mamlaka. 11Kachika iye pia mundatahiriwa wa twahara ithio fanywa na vanadamu kachika kuodolewa mvili wa nama, lakini ni kachika twahara ya Kristo. 12Mlidhikwa pamoya na iye kachika ubajizo. Na kwa ndia ya imani kachika iye mdafufuliwa kwa uwetho wa Mun gu aliye mfufua kutoka kwa wafu.13Mlipokuva wafu kachika makosa enyu kutotahiriwa mvili enyu, andawafanya hai pamoya na iye na kuchusamehe makosa yechu ote. 14Alifucha kumbukumbu dha madeni iliyoandikwa na taratibu thilithokuva kinyume naisi. Aliondoa ote kugongolea msalabani. 15Alithiondoa nguvu na wene mamlaka. Andayaweka wathi na kuyafanya kuva sherehe ya ushindi kwa ndia ya msalaba ake.16Kwa hiya mchu eote athiwahukumu inyi kachika kula au kachika kunuwa, au kuhusu siku a sikukuu au mwethi mpia au thiku tha sabato. 17Hithi ni thivuli tha mambo yayao, lakini kiini ni Kristo.18Mchu aaye ote athinyang'anywe chutho ake kwa kutamani unyenyekevu na kuabudu malaika. Mchu wa jinsi hio huingia kachika mambo alioyavona na kushawishiwa na mavadho ake a kimwili. 19Iye hakishikilii kitwa. Nikutoka kachika kitwa kwamba mvili ake na mifupa huungwa na kushikamanishwa kwa pamoya na hakukuva kwa ukuaji utolewavo na Mungu.20Ikiva mlikufa pamoya na Kristo kwa tabia dha dunia mbona mnaishi kama mnavajibika kwa dunia. 21Msishike wala kuondha wala kugusa? 22Haa ote yameamuriwa kwa ajili a uharibifu uyao na machumidhi, sawasawa na maagidho na mafundisho a vanadamu. 23Sheria hidhi dhin a hekima a dini dhilidhochengenedhwa kwa ubinafsi na unyenyekevu na macheso a mvili. Lakini hadhina thamani dhidi atamaa dha mvili.
1Ikiwa basi Mungu amefuafufua pamoya na Kristo, yatefteni mamba ya yuu ambako Kristo anaketi mkono wa kuume wa Mungu. 2Fikirini kuhusu mambo haa yuu, sio kuhusu mambo ya duniani. 3Kwa maana mlikufa na maisha enyu yamesitwa pamoya na Kristo ndani a Mungu. 4Vakati Kristo atakapoonekana, ambae ni maisha enyu, ndipo ini pia mtakapo onekana naye kachika utukufu.5Kwa hiyo yasiteni mambo yalio kachika nchi yaani, uwasharati, uchafu, shauka mbaya, nia mbovu, na tamaa ambavo ni iba ya sanamu. 6Ni kwa ajili ya mambo haa ghadhabu ya Mungu iyao iyu ya vana vasio tii. 7Ni kwa ajili ya mambo haa ini pia mlikwenda kwavo mlipoishi kachi yao. 8Lakini sasa ni ladhima mwandoe mambo haa ote. Yaani, ghadhabu, hasira, nia mbovu, machusi na maneno machafu atokao midomo mwenyu.9Msihadane inyi kwa inyi kwa kuva mndhauvua uchu wenyu wakale na machendo yake. 10Mndha vaa uchu mpia, unofanywa lipia kachika maarifa sawasawa na mfano wa ule aouvumba. 11Kachika maarifa haa hakuna mionani wala miahudi kiutahiriwa wala kutotahiriwa msomi, asie msomi, mtumwa, mchuhuru, bali Kristo ni mambo yote kachika yote.12Kama vacheule wa Mungu, vachakachifu na vapendwao, jivikeni uchu wema, ukarimu, unyenyekevu, upole, na uvumilivu. 13Tukulianeni inyi kwa inyi. Hurumianeni kila mchu analalamiko dhidi ya n'ngine amsamehe kwa jinsi ile ile ambavo bwana alivo wasamehe inyi. 14Dhaidi ya mambo haya yote, muu na upendo ambao ndlo kigedho cha ukamilifu.15AmanI ya Kristo itawale nyoyoni mweni ili kuva nikwa amani hii mlichiwa kachika mwili mmoya iveni na shukurani. 16Na neno la Kristo liketi ndini enyu kwa wingi. Kwa hekima yote, fundishaneni na kushauriana inyi kwa inyi kwa dhaburi kachika hekima yote. Chuki mukimuimbia saburi ntendhi dha rohoni imbeni kwa a nyimbo, na shukurani nyoyoni mwenyu kwa Mungu. 17Na chochote afanyacho kachika maneno au kachika machendo, fanyani ote kachika jina la bwana Yesu. Mpeni shukurani Mungu baba kupichia iye.18Vanavake, vanyenyekeeni vaume dhenu, kama ipendedhavo kachika Bwana. 19Nanyi vana vavuli vapendeni vake dhenyu na msiwe vakali dhidi yavo. 20Vana vatwiini vadhadhi venyu kachika mambo ote, maana ndivo impendedhavo Bwana. 21Akina baba msivachokodhe vana venyu ili kwamba vasievakakacha tamaa.22Vachumwa, vatiini mabwana dhenyu kachika nvili kwa mambo ote, sio kwa huduma amato kama wapende dhavo vachu tu. Bali kwa moyo wa weli. Nchemi Mungu. 23Chochote mfunyacho, fanyeni kuto nafusini mwenyuBwana nasi kama vanadamu. 24Mnayua ya kwamba mtapokea ujira wa urithi kutoka kwa Bwana. Kristo Bwana mnae mchumikia. 25Kwa sababu ote achendae asio haki atapokea hukumu kwa machendo asio haki alio afanya. Na hakuna upendeleo.
1Vavuli thoeni kwa vachumwa mambo alio haki na adili.Mnaiva pia kwamba mnae Bwana Mbinguni.2
1Paulo,Silivano na Timothy kwa kanisa la wathesolonike kachika Mungu Baba na Bwana Yesu Kristo.Neema na amani ive na inyi.2chunathoa shukrani kwa Mungu kila Mara kwa ajili enu nothe vakathi chuvachaapo kachika Maombi echu. 3Chunaikumbuka bila kukoma mbee a Baba echu kadhi enu a imani,upedho, na uvumilivu wene ujasiri kachika Bwana Yesu Kristo.4Wapendhi wa Mungu ,ivan vitu venu. 5Hu injili echu iavo kwenu si ineno thu, ila pia kwa nguvu ,kwa roho nthakathifu, na uhaki ka kwa hia mwaiva isi ni uachu na aina gani iu enu.6Mdhachuthaba isi na Bwana ,kama ndholipakea kwa furaha ineno ia roho mthakathifu. 7Na matokea ake akava mfano kwa makendonia na akaiya ambavo walikuva valiamini.8Kwa kuva ineno a Mungu limeenea koto,sikwa makendonia wa akaiya ote valiamini imani yenyu imeenda kwa kila mahali na matokea ya kumuamini Bwana hatuhitaji kunena chochothe. 9Avo veneve vanaambidhana ujio wechu uvie namna ipi kachi enu,Huambathana uilee mulivomdhunguka Mungu kuadhia sanamu na kunchumikia Mungu wa kweli. 10Valothoa chechesi kuva hungojea Mwana wake kuthoka mavinguni,andhofufuliwa kuthoka wafu.Huu ni Yesu,anaechuveka huru kuthoka kwenu ghadhabu iyao.
1Kwa kuva ini veneve mnaiva,mwenechu kuva kuiwa kwechu kwenyu haukuvu vabure. 2Mnaiva kwamba mwandoni chulichekesekana valichu chenda kwa aibu kulee filipi,kama uivavo chulikuva na ijasiri kachika Mungu kunena injili a Mungu hata kama taabu ningi3Kwa maana mausia echu haatokana na uwovu wala kachika uchafu,wala kachika hila. 4Badala ake kama yavulee chulivokubalika na Mungu na kuaminiwa injili,ndivo tunavo chunanena,sikwa kuafurahisha vachu,lakini kumfurahisha Mungu ,iye pwekee ndieachungu dhae nyoyo dhechu.5Kwa maana hachukuchuma maneno a kuipendekedha wakatote kama muivavo,wala hachukuchumia maneno kama kasingidhio kwa tamaa ,Mungu ni shahidi wechu. 6walahachukutafudha utukufu kwa wechu wala kutoka kwenyu au kwa vangine tungewedha kudai kupendelewa kama michume kama Kriso.7Badala ake chukuliva vapole kachi enyu kama avafarijio vana vake veneve. 8Kwani ndia hii chulikuva na upendo kwenyu chulikuva radhi kuvashiri kisha situu injili a Mungu bali pia namaisha echu weneve kwa kuva mlikuva vapendwa vechu. 9Kwa kuva venechu mnakumbuka kadhi na taabu echu usikunantana tulikuva chukifanya kadhi kusudi chusie chukamuemea oyote kachika iyoo chulivahubiria injili a Mungu.10Ini nimashahidi na Mungu pia nikwa uchakachifu wa namna gani waki nabila lawama tulivoenda veneve mbee enyu mnavoamini. 11Hivo unaiva ni kwa namna gani kwa kila mmoya wenyu kama Baba alivo kwa vanaye. 12Chulivo wahimidhanakuvachi a moyo chulishuhudia yakuva mulipaswa kuenenda kamaulivo mwicho wenyu wake.13Kwa sababu hiyo chwamshukuru Mungu pia kili wakati ,kwa kuva wakati mlipo pokea kutoka kwechu ujumbe wa Mungu mlivousikia mlivopokea sikama ineno la vanadamu,Badala ake mlipokea kama kweli alivo ineno la Mungu ni ineno hili ambalo linalo fanya kadhi enyu kachi enyo mnavaamini.14Kwa hio ini mwenechu ,muve vafuasi va makanisa a Mungu yalioko kachika Kristo Yesu kwa kuvaini pia mlicheseka kachika mambo ale ale kutoka kwa vachu venyu kama ilivokuva kutoka kwa vayahudi. 15Vayahui ni vayahudi valivo mvua Yesu Kristo valikuva havampendi Mungu namaadui hata kwa vanadamu. 16Valichudhuia chusinene ma mataifa ili vapache kuokolewa matokea ake ni vanaendea kuchenda dhamb dhavo mwisho gadhabu indakuya iyu avo.1718Kwa kuva chulitaka kuya kwenyu,imi paulo kwa mara moya nahata ingine,Lakini shetani alichudhuia. 19Kwa kuva kiiamini kinechu nini aufuraha .au taji kujivunia mbee dhabwana wechu Yesu wakati wa kuya kwake,Je si ini dhaidi kama valivo vengine. 20Kwa kuva ini ni utukufu na furaha echu.
1Kwa hiyon thulipo kuva hathuwezi kuvumilia zaidi, tulifikiri kuwa ilikuva vema kubaki kule Athene peke yetu. 2Tulimtuma Timotheo, nduetu na mchumishi wa Mungu kachika injili a Kristo, kuwaimalisha na kuvafariji kuhusiana na imani enu. 3Tulifanya haya ili kusudi asiwepo eote wa kuteteleka kuthokana na macheso haya. kwa kuva venyewe mnajua kwamba tumekwisha teuliwa kwa ajili ya hili.4Kwa kweli, vakati tulipokuwa pamoja nanyi, tulitanguliza kuwaeleza ya kuwa thulikuwa karibu kupacha macheso ma haya yalitokea kama mjuavyo. 5Kwa sababu hii, nilipo kuwa siwedhi vumilia tena, nilituma ilikusudi nipate kudhua juu ya imani enu. Huenda mjaribu angalau amewajaribu na kadhi etu ikawa ni bure.6Lakini timotheo alikuja kwetu kuthokea kwenu na akathulethea habari ndhuri juu ya imani na upendo enu. Alitwambia ya kuwa mnayo kumbukumbu nzuri juu etu na kuwa mnatadhamani kutuona kama ambavyo nasi twadhamani kuwaona inyi. 7Kwa sababu hii ndugu tulifaarijika sana na inyi kwa sababu ya imani enu kachika taabu na macheso etu ote.8Kwa sasa thunaishi, kama mkidhimama imara kwa Bwana, 9Kwani ni shukurani zii tumpe Mungu kwa ajili enu, kwa furaha ote dhuliyonayo mbele za Mungu juu enu? 10Tunaomba sana uthiku na mchana ili thuweze kudhiona nyuso zenu na kuvaongezea kunachopungua kachika imani enu.11Mungu echu na Baba mwenyewe, na Bwana wetu Yesu atuongoze njia etu chufike kwenu. 12Na Bwana awafanye muongezeke na kuzidi kachika upendho, mkipendhana na kuwapendha vachu vote, kama tunavyowafanyia inyi. 13na afanye hivi ili kuiimarisha mioyo enu iwe bila lawama kachika uchakachifu mbele za Mungu wechu na Baba yetu kachika ujio wa Bwana Yesu pamoja na wachakachifu ake vote.
1Hatimae ndugu, twawachia moyo na kuwasihi kwa Yesu Kristo. Kama mlivyopokea maeleketho kutoka kwechu namna ivapasavo kuenenda na kumpendetha Mungu, kwa ndia hiyo pia mwenede na kuchenda thaidi. 2Kwakuva mwaiva ni maeleketho gani chulio yapa kupichia Bwana Yesu.3Kwa kuva haa ndio mapendi a Mungu, uchakasu wenyu, kwamba muepuke thinaa, 4Kwamba kila mmoya wenyu anaiva namna a kumiliki nke ake mwenewe kachika uchakachifu na heshima. 5Kwa ajili a tamaa tha mvili (kama matata yasio muiva Mungu). 6Asiweko mchu eote atakae vuka mipaka na kumkosea ndue kwa ajili ya yambo hili. Kwa kuva Bwana ndie mwenewe kulipa kisasi kwa mambo ote haa, kama chulivo changulia kuvavonya na kushuhudia.7Kwa kuva Bwana hakuchuicha kwa uchafu bali kwa uchakachifu. 8Kwa hiyo anae likachaa hili hawalikachai wachu, bali anamkacha Mungu, anae vapa Roho ake Mchakachifu.9Kuhusu upendo wa ndugu, hakuna haja a mchu eote kuvandikia, kwa kuva mdafundishwa na Mungu kupendana inni kwa inni. 10Hakika, mlifanya haa ote kwa ndugu valivoko makedonia ote, lakini chwavasihi, ndugu, mfanye hata na dhaidi. 11Chwavasihi mtamani kuishi maisha ya utulivu, kujali shughuli thenyu, na kufanya kathi na mikono enyu, kama chulivo amuru. 12Fanya haa ili uwethe kuenenda uthuri na kwa heshima kwa hao vyalio nde a imani, ili msipungukiwe na hitaji lolote.13Hatutaki mkose kuiva, enyi nduangu iyu ya hao walio yala, ili msie mkahudhunika kama vangine wasivo na uhai kuhusu wakati weyao. 14Ivapo chunaamini kuva Yesu alikufa na akafufuka tena, hivo hivo Mungu atavaecha pamoya na Yesu havo walioyala mauti kachika ieye. 15Kwa ajili a hao chwavambia inyi kwa ineno la Bwana, kwa isi chulivo hai, chutakuvepo wakati wa kuya kwake Bwana, hakika hatutachakuli valee valio yala mauti.171816Bwana mwenewe atashuka kutoka mavingo pamoya na malaika mkuu na parapanda ya Mungu na vale wafu na valioko hai sute chutatangama kumpokea Bwana kutoka mavingu. Na vale valio kufa kachika Kristo watafufuka kwanda.
1Sasa, kwa habari amuda na nyakati, ndugu, hamna haja kuvaadhikia. 2Kwa kuva ninyi veneve mwayua ya kuva siku a Bwana inakuya kama mwizi ayapo usiku. 3Pale vanenapo kuna "amani na usalama", ndipo uharibifu huwailia ghafla. Ni kama utungu mama mwene mimba. Havatuepuka kwa ndhia oote.4Lakini inyi, ndugu ampo kwene gidha hata ile siku ivaie kama mwidhi. 5Kwa maana inyi note ivana va nuru navana va ntama, isi sivo vana va usiku au a gidha. 6Hiyo basi, tusi yale kama vengine valivo. Bali chukeshe na kuvamakini. 7Kwa kuva anaoyala huiyala usiku na vanavo leva huleva usiku.108Kwa kuva sisi ni vana va mtama, tuvemakini. Tuvae ngao a imani na upendo, na, kofia ambayo ni uhakika awokovu wa vakati uyao. 9Kwa kuva Mungu hakuchutauwa mwandho alie chufia ili kwamba, chukiwa mato au chume lala chuta ishi pamoya nae. 11Kwa hio farijameni na kujijenga ini kwa ini kamba ambavo tayari mnafanya.12Ndugu, chwavaomba muvachambue valee vanavochumi ka miongoni mwenyu valivo yuu yenu kachi ka Bwana na vale vanavo vashauri. 13Pia mvachambue na kuvapa heshima kachika upendo kwa sababu a kadhi avo. Muve na amani miongoni mwenyu ini veneve. 14Chwavaishi, ndugu muvaonyeshe vasio kwenda kwa taratibu vachieni moyo valivokacha tamaa, vasaidieni valivo vanyonge na mvevavumilivu kwa ote.15Angalien asivepo mchu eote anaelipa baya kwa baya kwa mchu eote. Badala ake fanyeni aliomema kwa kila mmoya venyu na kwakuva vachi vote. 16Furahini siku dhote. 17Ombeni bila kukoma. 18Mshukuni Mungu kwa kila yambo, kwa sababu hao ndio mapendhi a Mungu kwenyu kachika Yesu Kristo.19Msimdhishie Roho. 20Msiudharau unabii. 21Yajaribuni mambo ote mlishike lilojema. 22Epukeni kila muonekano va uovu.23Mungu va amani avakamilishie uchakachifu. Roho, nafsi na mvili vichundhwe pasipo mawaa kachika kuya kwake bwa vechu Yesu Kristo. 24Iye alievaicha ni mwanifu, nae ndie mwene kuchenda.25Ndugu, chuombeni pia. 26Vaalimni ndugu vote kwa ibusu chakachifu. 27Navahisi kachika Bwana kwamba barua hii isomwe kwa ndugu ote. 28Neema a Bana vetu Yesu Kristo ive pamoya nani.
21Paulo,Silawano,na Timotheo,kwa kanisa la wathesalonike kuchika Mungu baba echu na Bwana Yesu Kristo.
1Sasa kuhusa,kuya kwa Bwana wechu Kristo na kukusa nywa pamoja ilichuve naei chunavaomba ini ndugu dhechu. 2Kwamba musisumbuliwe wala kutaabishwa kwa urahisi,kwa roho,au kwa ujumbe au kwabarua inayo onekana kuva imetokakwechu,ikinena yakura siku tayari imekuya.3Nchu nasivandanganye kwa nanna yeyote ,kwa kuva haitakuya mpaka lileanguko litokeledhe kwanda na nchu wauasi afunuliwe ,utee mwana wauharibifu. 4Huyu ndie apingae huinyua mwenewe akimpingu Mungu na chochote kinacho abudiwa,namatokeo ake huketi kenehekalu la Mungu nakuvonesha ie kuva kama Mungu.5Je hamukumbuki kuva nilipokuva nani nilivaambia iyu ya mambo haa? 6Sasa mnaiva kile kinacho mdhuia ili kwamba awedhe kufunuliwa kwa wakati wasahihi utakapowadia. 7kwakuva siri ya ule nchu mwene kuasi inafanya kadhi mpaka sasa ,ila tu kuna anaendhivia sasa mpaka atakapotowa njiani.8Ndipo ule mwene kuasi atakapo funuliwa,atamuua ya kwa pundhi ya ndomo wake Bwana wake .Bwana kuvasi chochote kwaufunuo wa uyio wake, 9Uyio waulee mwenekuasi atakuva kwa sababu ya kadhi ashetani kwa nguvu dhote ishara na maajabu a uwongo 10Na uongo wote wenu udhalimu mambo haa atakuvepo kwa vale vanavopotea kwa sababu havakupokea upendo wakwe kwa ajili yakuokolewa kwavo.11Kwa sababu hiyo Mungu atavaachumia kadhi ene uwovu ilivaamini uwongo. 12Matokeo ake nikwamba vote vitahukumiwa vale ambavo huvakuamini ukweli bali wao huifurahisha kachika udhalimu.13Lakini inachupasa chumshukuru Mungu kila mara kwa ajili enyu ndugu mupendwavo na Bwana.Kwa sababu alivatuaini kama malibu ya uokovu kwauchakaso waroho na imani kachika ile kweli. 14Hiki ndicho alichovaiitia ini,kwamba kupichia injili mwawedha kuupacha utukufu wa Bwana wechu Yesu Kristo. 15Kwahio,ndugu,simameni imara,uelewe uleutamanduni mliofundishwa kwa neneno au kwa barua Yechu.16Sasa,Bwana wechu Yesu Kristo mwenewe na Mungu Baba yechu aliechupenda nakuchupa faraja a milele na ujasiri mwema kwa ajili ya amaisha yayavo kupichia neema. 17Awafariji na kuifanya imara nyoyo dhenu kathika kilaneno nikadhi njema.
1Na sasa ,ndugu,chumbeeni,kwamba ineno la Bwana liwedhe kuenea na na kuthuzua kama alivo pia kwenyu, 2Ombeni kwamba chuedhe kuokolewa kuthoka kachika uovu na vachu vaovu kwa kuva sivothe vanaimani. 3Lakini Bwana nimuaminifu ,ambaye athavaimarisha inyi na kuvalinda kuthoka kwa ulee muovu.4
1Paulo mtume wa Yesu Kristo kwa mapendhi a Mungu, sawa na ahadi a udhima luio ndani a Kristo Yesu. 2kwa Timotheo, mwenechu mpendwa: neema ive kwako, rehema na imani hutoka ka Mungu Baba na Kristo Yesu Bwana wechu.3Ninamshukuru Mungu, iye ninamchumikia kwa nia njema kama valifofana baba dhangu, nikumbukapo dunia kachika maombi angu usiku na ntana 4natamani kumuona, ili akwamba niave na furaha , nakumbuka machozi ako. 5Huva nakumbuka kuhusu imani ako halisi, ambavo hapo kwandha aliketi kwa nke vako Loisi na mama vako Yunisi. Nayiva imani hio huketi ndani ako pia.6Hiya ndio sabau nakukumbusa kutotea karama a Mungu iliomo ndani ako kwa ndhia a kuvekeva mikono angu. 7Kwa kuva Mungu hakuchupa roho a kucha, bali a nguvu na upendo na moyo na nidhamu.8Kwa hiya usivone haya ushuhuda kuhusu Bwana wechu, wala vangu imi Paulo mfungwa vake. Bali ushirik macheso kwa ajili a injili, savasava na uwedho wa Mungu. 9Ni Mungu aliechuokoa kwa mwicho mchakachifu. Hakufanya hia kulingana na kadhi dhechu ila kulingana na neema a pamoya vake veneve. Alichupa mambo haa kachika Kristo yesu kabla a nyakati kuandha. 10Kuva sasa vokovu va Mungu umekwisha funuliva kwa kuya kwa mwokodhi wechu Kristo yesu, ni Kristo alieikomesha mauti na kulecha udhima usiosia kwa nuru a injili. 11Kwa hiya nilitauliwa kuwa mhubiri, mchume na mwalimu.12Kwa hiya nacheseka pia lakini sioni haya kwa ruva namuiva iye niliekwisha kumuamini, naamini kuva iye anawedha kukichundha kilee nilichokikabidhi kwake hata siku ile. 13Ukimbuke nfano wa ujumbe va uaminifu uhusikao kutoka kwangu pamoya na imani na upendo ulio ndani a Kristo Yesu. 14Achundhe mambo madhuri aliokukabidhi Mungu kupichia roho mchakachifu iashie ndani echu.15Waiyua a kuva ote vaisio kachika asia volinivata kwene kundi hili vamo Figelo na Hemogene. 16Bwana arehemu numba a Onesiforo kwa kuva mara ningi aliniburudisha na hakuivonea haya minyororo angu. 17Badala ake alipokuva Roma alinitafuta kwa bidii na akanivona. 18Mungu amjaalie kupacha rehema kutoka kwake siku ile. Kamaalivonisaidia nilipokuva Efeso, uwe waiwa vyema.
1Hia eve mwanangu, uve na neema ndani a Kristo Yesu. 2Na dhichu kwa mashahidi vangi, uvape vachu muhimu ambavo vathavafundisha vangine pia.3Shiriki macheso pamoya na imi, kama askari ndhuri wa Yesu Kristo. 4Hakuna askari achumukiae na thena afanye kadhi thingine tha maisha haa, ili apendhedhe mkuru ake. 5Na nchu nshindani kama mkimbiaji, hapachi thaji asipothifacha sharia.6Nkulima wa kwanda ni haki apache madhao wa kwandha. 7Thafakari ninenacho, maana Bwana athachupa ueleva kachika mambo othe.8Uive Yesu Kristo, changu udhao wa Daudi andhofufuliwa kuthoka vafu. Hii indhalingana na maeledho angu a injili, 9ambava kwa hao ninacheswa na kuchachilwa kamba kama nkosefu. Nchenda maovu, ila ineno la halifungwi kwa kamba. 10Hia navumilia ote kwa ajili o vatheute, nauvo vaupache okovu kachika Kristo Yesu pamoya na uthukufu va milele.11Uneni huu ni vakuaminika: "Kama chundhakifu pamoya nae, chuthaishi pamoya nae pia, 12Chukivumilia, chuthaongotha pamoa nae pia, chunkana iye, nae achathukana isi. 13Chusipokuwa vaaminifu, iye athabaki mwaminifu, maana hawedhi kuikana mwenewe."14Usiuthe kuvakumbusa iyu a mambo haa, vokanye mbee a Mungu, vaathe kuchecha kuhusu ineno.Hia hakuna faida kachika iyambo hili. Hia kuthakuva na upochoshaji kwa valee vasikilidhavo. 15Ivonesheni kwa Mungu kama vachenda kadhi vasio laumika. Lichumieni ineno la kweli kwa usasi16Iepusheni na majadiliano a kidunia ambao si a dini. 17Maneno ao athasambaa kama idonda ndugu. Kachi ao ni Himenayo na Fileto. 18Hava ni vachu vandhaukosa ukweli. Hunena kuva ufufuo undhakwishafanyika, hupindua imani a baadhi a vachu.19Hatha hia nthingi dhabithi undhasimam, wene chapa hii, "Bwana avaiva valio vake, na alichayae ina la Bwana ni ladhima aithenge a udhalimu." 20Ndani a numba a kithajiri, sio kuva sivo dhombo dha dhahabu na shaba thu. Pia dhombo dha michi na uvongo. Baadhi ake ni kwa machumidhi a adabu na dhengine ni kwa machumidhi asio a adabu. 21Nchu achakasadhao kutho machumidhi asio a adabu, iye ni chombo ha kuheshimika. Andathengwe maalum, ana manufaa kwa Bwana na andhachiliva kila kadhi ndhuri.22Dhikimbie dhamaa dha ujanani, ukifuacha haki, imani, upendho pamoya na valee vamwichao Bwana kwa roho safi. 23Ila uidhe upumbavu na maswali a kipuudhi maana hudhaa dhicha.24Nchumishi wa Bwana hafai ave kuva mpendha dhicha, ila ave ,mpole kwa vachu vothe.Awedhao kufundhisha uvumilivu. 25Ladhima avaelimishe valee vampingao. Mwishoe Mungu awedhe kuvapachia thoba kwa kuiva kweli. 26Vapoche kuiva thena kuepuka nchego wa shethani. Baada a kuva vandhachekwa na iye kwa mapendhi ake.
1Chufahamuni neno hili, kachika siku tha mwsiho kutakuva na nyakati ngumu. 2Kwa sababu vachu watakufa vene kuipenda venewe, vene kupenda sinti vene kuithifu, vene majivuno, vene dhihaka, vasiotii wathathi vao, vasiokuva na shukurani na waovu. 3Vasio na upendo asili,vasiotaka kuishi kwa amani eote, vachonganishi vasingithiaje, vasiowetha kuidhuia, wene kuecha thicha, vasiopenda madhuri. 4Vatakuva vasaliti vakaidi wene kuipenda wenewe na wapenda anasa kuliko kumpenda Mungu.5Kwa inde sura thao huvonesha kuva vao nivacha Mungu lakini vataiacha nguvu ake. Iepusheni na vachu havo. 6Kwa kuva baadhi yavo ni vanaume wanavoingia familia tha vyachu na kuvashawishi vanavake wainga. Hava vanavake vandajaliwa na dhambi na ni venye kuongothwa na tamaa tha kila aina. 7Vanavake hava huifunda siku thote lakini hawawethi kusikilia ule ufahamu wa ukweli.8Kama yaule Yane na Yambre valivo simama kinume na Musa, kwa sababu hini vaalimu hava vyaurong husimama kinume cha ukweli. Ni vachu valioharibiwa mawatho yavo na vasio kubalika kuhusiana na imani. 9Lakin havataendelea mbali, kwa upumbavu wao utavekwa wathi kwa vachu ote, kama undavo kua kwa valee vachu.10Lakini uwe undayafuacha mafundisho, uvumilivu, upendo na ustahimilivu angu, 11macheso na maumivu valionipacha kule Antiokia, ikonia na Listra. Nindayavumilia macheso. Bwana andavoniokoa kachika macheso ote. 12Vote wanavotaka kuishi kachika maisha hakumcha Mungu kachika Kristo Yesu watacheswa. 13Vachu aovu na vadanganyifu natadhidi kuva vaovu dhaidi. Watavopochosha vengine, vao venewe vamepochoswa.14Lakin uwe dumu kachika mambo uliyo jifunda na kuyamini kwaudhabiti kwa kuva univya umejifunda kwa nani. 15Nachambuwa kuva thangu vidodi ako uliyajua maadhiko machakachifu. Haa yanaweza kukuhedhimisha kwa ajilo a uokovu kwa ndhia a imani kachika Kristo Yesu.16Kila andiko limethiwa pumzi na Mungu. Linafaa kwa mafundhisho venye faida, ushawishi, kurekebisha makotha na kufundhisha kachika haki. 17Hii ni kwamba nchu a Mungu ave kamili akiwa amepewa nyendho ote kwa ajili a kuchenda kila kadhi ndhuri.
1Ndakuagidha mbee dha Mungu na Kiristo Yesu, atakaye vahukumu valivo vai na vafu, na kwa kufunuliwa kwenyu na ufalme wake. 2Hubiri ineno, uwe tayari kwa wakati ufaao na usiofaa. Aambie vatu dhambi dhao, kemea, himiza, kwa uvumilivu vote na mafundhisho.3Kwa maana vakati udhakuja vakati ambao vachu havatachukuliana na mafundhisho a kweli. Badala ake, wadhajidhafutia valimu va kufundisha kulingana na tamaa dhao. Kwa ndhia hii masikio yao vatakuwa vametekenywa. 4Vataacha kudhikiliza mafundhisho a kweli na kugeukia hadithi. 5Lakini ewe uwe mwaminifu hachika mambo ote, vumilia magumu, fanya kadhi ya mwinjilisti; dhimiza huduma ako.6Kwa maana imi tayari nimekwisha kudhiminwa. Mudha wa kuondhoka kwangu umewadia. 7Nimeshindhana kachika haki, Mwendho nimeumalidha, Imani nimelindha. 8Taji ya haki imewekwa kwa ajili angu, ambayo Bwana, anayehukumu kwa haki adhanipa thiku ile. Na siyo kwangu tu bali pia va ote vanavongojea kwa shauku kuvonekana kwake.9Jidhahidi kuya angu haraka. 10Kwa kuva dema ameniacha. Anaupendha ulimwengu wa sasa na amekwenda Thesalonike, Kreseni alikwenda Galatia na Tito alikwenda Dalmatia.11Luka tu ndiye yuko pamoya nami. Umchukue Marko uye nae kwani eye ni muhimu kwangu kachika huduma. 12Nimemthuma Tikiko Efeso. 13lile joho ambalo niliacha Troa kwa Karpo, utakapokuja lilete, pamoya na vile vidhabu hasa vile vya ngozi.14Alekizenda mfua chuma alinithendea maovu mengi. Bwana atamlipa kulingana na machendo ake. 15Nawe pia jihadhari naye, kwani alidhapinga sana ineno echu. 16Kachika utetezi angu wa kwanza, hakuna nchu eote aliesimama pamoya nami, badala ake, kila mmoya aliniacha. Mungu asiwahesabie hatia.17Lakini Bwana alisima pamoya nami, akanichia nguvu ilikuva kupichia kwangu neno linenwe kwa ukamilifu na mataifa vapache kusikia nikiokolewa kachika kanwa la simba. 18Bwana ataniepusha na machendo ote maovu na kuniokowa kwa ajili aa ufalme wa mbinguni utukufu uwe kwake milele na milele. Amina.19Msalimiya Priska, Akila na numba a Onesiforo. 20Erasto alibaki huko Korito lakini Trifimo nilimudha Mileto akiwa mngojwa. 21Fana hima uye kabla kipindi cha baridi. Eubulo anakusalimiya, pia Pude, Lino, Claudia na ndugu dhake vote, 22Mungu ave pamoya na roho ako,Neema naiwe pamoya nawe.
1Paulo nchumishi wa Mungu na ntume wa Yesu Kristo kwa ajili a imani na vatheule wa Mungu na maarifa a kweli lechao utauwa. 2vapo kachika thumaini la uzima wa milele ambao Mungu asiewedha kunena urongo,uliahidi changu dhamani kabla ya edhi dhothe dha vakathi. 3Kwa vakathi ulofaa alilifunua ineno lake kachika ujumbe ulionipa imi kuhubiri ilinipasa kufanya hia kwa andri a Mungu mwokodhi wechu4Kwa Tito mwana wa kweli kachika imani yechu chushirikiao suthe.Neema na amani kuthoka kwa Mungu Baba na Yesu Kristo Muokodhi weche. 5Kwa sababu hiri nalikuatha krete ili apache kupanga mambo ambao bado hayajakamilika na kuveka wakfu vathe vakanisa kwa kila mui kama nguagidhevo.6Mdhee vakanisa ladhima asive nalawawia mvuli wa nke mmoya ,alie na vana vaaminifu vasioshuhudiwa na maovu au wasiotusi. 7Ni muhimu kwa muangalithi,kama msimamithi wa nyumba a Mungu ,asive na lawama,asive nchu mwenye kiburi hakadhiriki haraka ,si mraibu wa chembo si baa na asive mwenye thamaa.8Baada ake ave nchu nkarinu apendhae vema,mwenye busara,mnyoofu ,mchakachifu na anaejidhibithi. 9Awedhae kushika sana ujumbe va kuaminika afundishweo,ili awedhe kuwachia moyo vangine kwa mafuundisho a ukweli na kuvareke bisha valee vampingao.10Kwa kuva kuna vaasi vengine vanenao machupu na vahandaavo,hasa valee na tohara maneno ao ni aupudhi vanahandaa na kuvaongodha vachu kachika upochofu. 11Ni ladhima kuvadhiwa vachu kama hao vanafundisha alee asiopaswa kwa faida dha aibu na kuharibu familia dhote.12Mmoya va manabii vao vamenena wakrete daima nivarongo ,vanyama vabaya,vadavadhi,vadhivu. 13Ushuhuda huu ni ukweli kwa hio verekebishe kwa nguvu ,ila kwa vavedhe kunena ukweli kachika imani.14Bila kudhingathia hekaa dhakiahudi au anri dha vachu valadhao kweli.uwe usijihusishe na hadithi dhisidho dha kweli dha kiahudi au anri dha vachu ambavo hurudisha nyuma ukweli.15Kwa vothe valio safii ,dhichu dhothe ni dhisafi bali kwalioharibika na wasioamini,hakuna kilicho kisafi,lakini dhao,na dhamiri dhao dhimeharibika. 16vanakiri kumuiva Mungu lakini kwa machendo ao vanamkana wao ni muthukidho,vasiodhii,na vasiofaa kichu kwa kadhi yoyothe njema.
1Nena yake vanayo ambachana na mafundisho a kweli. 2Vafundishe vadhe vanaume kuva na kiasi, vene hishima, vene busara na timamu kachika upendo na uvumilivu.3Vifundisha vanavake vadhee kuwa na tabia aheshima, sivasingiaji , visiwe vachumwa wa divai nyingi vawewalimu wa ale aliomema. 4nakufundisha vanavake vadogo kuvapenda vaume dhavo na vachocho vavo. 5Kuva na busara,vasafi , vatundaji vadhuri vanyumba dhavo na kuvatii vaume dhavo veneve ili neno la Mungu lisinenwe kuva maovu.6Vachie moyo vdhijana vakiume vawe na busara. 7Kachika nd'ia dhote ivonyeshe mwanewe kama nfano vamachendo mema, kachika mafundisho yako vonesha udilifu, heshima. 8Vanene naujumbe vakweli ili kwamba vovote vakupivo vaaaibishwe kwa sababu hawana ubaya vakunena iuyechu.9Vachumwa navavatii mabwana dhavo kachika kila kichu, vavafurahishe na sio kubishana navo. 10Vasivaibie. Bali vavaoneshe nia njema yote ili kwa ndia dhote vaieche sifa mafundisho kumuhusu Mungu muokodhi wetu.11Kwakuva neema a Mungu imevonekana kwa ajili ya uokovu wa vachu vote. 12Inachufundisha kukachaa, mambo yasiyo ya Mungu na tamaa dha kidunia, na kuishi maisha akiasi, uadilifu, na utaua kachika dhama hidhi. 13Hukuki chuki cha dhamia kupokea tumaini lechu lenye baraka kuvonekana kwa utukufu wa Mungu wechu mkuru na mokodhi wechu Yesu Kristo.14Yesu aliitoa nafsi kwa ji echu ili achukomboe na maasi ote na kuji chakasia vachu maalum valivo na hamu akufanya machendo mema.15Anene mambo haa, vachie vachu moyo kuya timidha na utoe marekebisho kwa mamlako ote. Usikubali nchu oote akupuudhe.
1Vakumbushe kunyenyekea kwa watawala na wene mamlaka, kuwatii na kuva tayari kwa kila kadhi njema. 2Wasichukane yeyote, waepuke madibithano, wave wapole na kuvonesha unyenyekevu kwa vachu vote.3Kwa kuva hapo awali isi pia chulikuva na mawadho pochovu na wasio tiichulipochosha na kufanywa wachumwa wa tamaa na anasa mbalimbali. Chuliishi kwa ouvu n chuki. Chulikua wasi na kuchukiana.4Ila vakati ukarimu wa Mungu muokodhi wechu na upendo na upendo ake kwa wanadamu ulipovonekana. 5Haikuva kwa machendo yechu ya haki chulivochenda, bali andachuokoa kwa neema ake alichuokoa kwa kudhaliwa upiya na kufanya upia kwa roho nchakachifu.6Mungu alimwaya roho mchakachifu kwa wingi iyu echu kupichia muokodhi wechu Yesu Kristo. 7Andafanya hiya ili kwamba chukisha kuhesabiwa kwa neema ake, chupache kuva waridhi wenye tumaini la uthima wa milele.8Huu ni ujumbe wa kuaminika. Nataka niyanene mambo haa, ili walee wanao muamini Mungu vawe vaangalifu kachika kuchenda mema. Mambo haa ni madhuri nahufaa kila nchu.9Ila jiepushe na mijadala ya kiupumbavu na nasaba, mashindano na migongano kuhusu sheria. Mambo haa hayana faida na hayafai. 10Mkachaeni wowote asababishae migawanyiko kadhi enyu. Baada ya onyo moya ama mawili. 11Ivan kwambu nchu ya jinsia hiyo andaata ndia iliyo sawa huchenda dhambi na kuihukumu mwenewe.12Nitakapo mchuma kwako Artema au Tikiko, harakisha vye kwangu huku Nikopoli, ambapo nitoamua kuketi vakati wa ubaridi. 13Fanya kila uwedhalo kuwa chuma zenu mwanasheria na Apolo, pasipo kupungukiwa na kichu.14Wachu wechu ladhima vaifundishe kuishuhulisha kachika kadhi ndhuri ambatho thinatimitha mahitaji muhimu ili kwamba wasie wakawa wasiozaa machunda.15Vyote walio pamoya naimi wanakusalimia. Wasalimieni walee watupendao kachika imani. Neema na ive nainyi nyute.
1Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu,na ndugu timotheo kwa Filemoni,mpendhwa rafiki yechu na mchenda kathi pamoya nasi, 2na kwa afia dadaechu na Arkipas Askari mwendaniwechu, na kwa kanisa lile linalokuchana numbani kwako 3Neema ive kwenyu na amani itokao kwa Mungu Baba yechu Yesu kristo.4vakati ote namsukuru Mungu wangu, hukuchaya kachika maombi angu. 5Kwa sababu ndhasikia kuhusu Imani ulionao kachika Bwana Yesu upendho ulionao kwa vathakathifu ote. 6ndhaomba kwamba ushirika wa Imani enyu iwe na ufanisi kachika ujudhi wa kila yambo dhuri lilioko kachi yechu kachika kristo. 7kwa kuva na furaha na faraja kwa sababu y upendho vako, kwa sababu nyoyo wathakathifu ote imekuva ikichudwa nawe.8Kwa hivo , ingava nina ujasiri ote kachika kristo kukuamuru uwe kufanya kile unachowedha kufanya, 9ime Paulo niliyendhee, n nda huu ni mfungwa kwa ajili ya Yesu kristo.10Nakusihi kuhusu mwanangu Onesmo, niliyemdha kachika dhifungo dhangu. 11kwa kuva mwandhoni hakukufaa, lakini ndha huu anatufaa vyote , uwe na imi . 12imi ndhamchuma akurudie uwe, aliye moyo wangu haswa. 13Nataraji angeendelea kubaki pamoya na imi ile anichumkea badala ako, vakati niko kifungoni kwa ajli ya Injili.14Lakini sikuthaka kufanya yambo lolote bila ruhusa ako. nilifanya hiya ile kwamba yambo lolote dhuri lisifanyike kwa sababu ndakulazimisha bali kwa sababu ndapenda mwenewe kulichenda . 15labuda ni sababu alitengwa kwa mda ilikuva hivyo ili uwe pamoya naye dhaima. 16ili kwamba asive tena mchumwa,bali bora dhaidi ya nchumwa kama nduangu mpendwa iye ni mpendwa haswa kwangu na dhaidi sana kwako kachika mwili na kachika Bwana.17Na hivyo kama wanitukulia imi nshirika , mpokee kama ambavo undhanipokea imi. 18lakini kama undakosea yambo lolote, au unamdai kichu chochote, kidai hicho kutoka kwangu. 19imi Paulo , ndaandika kwa mkono wangu mwenewe. imi nitakulipa pasipo na kukuambia yakua ninakudai uwe binafsi uhai haswa. 20naamu nduangu ata nipache faida kuthako kwako kachika Bwana ; kuiburudisha nafsi angu kachika kristo .21Nikiva na imani kuhusu utii vako, nakuandikia nikiiva kwamba utafanya hata dhaidi ya vile nikuombavo, 22vakati hoo, hoo andaa chumba cha vageni kwa ajili angu, kwa kuva ninatumaini kupichia maombi ako nitarudishwa kwenyu .23Epafra, mfungwa mwendani wangu kachika Kristo Yesu anakusalimu, 24na kama afanyavo Marko, Aristarko, Dema Luka Wachenda kazi pamoya nami. 25Neema ya bwana wechu Yesu Kristo iwe pamoya n roho ako.
1Petro, mchume wa Yesu Kristo, kwa vageni valivotavanyika, wateule, kachika Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. 2Kutokana na ufumu wa kimbele wa Mungu Baba kupichia kadhi a uchakoso aroko, kwa utiifu na kwa kunyinyidhiwa damu a Yesu Kristo. Neema ive nenyu na amani enyu iongedheke.3Na ahidimiwe Mungu na Baba wa Bwana wechu Yesu Kristo kachika ukuru wa rehema ake, alichupa kudhaliwa upia kwa ujasisi wa urithi kupichia ufufuo wa Yesu Kristo kuchoka kachika wafu. 4Kwaurithi usio angamia , hautakuva na uchafu wala kupungua. Umehifadhiwa kwaajili enyu. 5Kwa uwedho wa Mungu mnalindwa kupichia imani kwa uokovu ambavo upo tayari hufunuliwa kachika nyakati dha mwisho.6Frahini kachika hil ingava sasa ni ladhima kwenyu huisikia hudhuni kachika majaribu ya aina mbalimbali. 7Ili kwamba kwa imani enyu ambayo inathamani kuru kuliko dhahabu iharibikavo iyapo kuva hiyo na jaribiwa kwa mocho huvonekana kuva kwene sifa, utukufu na heshima kachika ufunuo wa Yesu Kristo.8Hamyavona iye lakini mwampenda. Hamvoni sasa lakini mndhaamini kachika iye namno mnafuraha isio wedha kuledheka kwa furaha ambavo imeyawa na utukufu. 9Sasa mnapokea matokeo ya imani, wokovu a nafsi dhenyu. 10Manabii walitafudha na kuulidha kwa umakini kuhusu wokovu huu kuhusu neema ambavo ingekuva enyu.11Walitafudha kuiva ni aina gani ya uokovu ambavo ungekuya . Walitafuddha pia kuiva ni mda gani roho a Kristo alie ndani avo alikuva ana dhungu mdha nini nao. Hii ilikuva indhatokea wakati alipokuva anawaambia mapema kuhusu macheso a Kristo na utukufu ambao ungemfuata. 12Indhafunuliwa kwa manabii kwamba walikuva wanayatumikia mambo haa na sikwa ajili yavo veneve bali kwa ajili enyu- masimulidhi ya mambo haa kupichia vale vanao echa injili kwenyu kwa ndhia a roho nchakachifu alie mchumwa kutoka mbinguni, mambo ambao hata na malaika vanatamani kufunuliwa kwake.13Kwa hio fungeni dhiuno dha akili dhenyu muve vachulivu kachika fikira dhenyu. Muve naujasiri kamilifu kachika neema ambavo itaechwa kwenyu wakati wa kufunuliwa kwa Yesu Kristo. 14Kama vana vatiifu msifungwe veneve na tamaa ambadho mudholidhifuacha wakati mlipokuva hamna ufahamu.15Lakin kama vile alivovaicha alivomchakachifu, nani pia muve vachakachifu kachika tabia enyu ote maishani. 16Kwakuva imeandhikwa, " Iveni vachakachifu kwa sababu imi ni mchakachifu." 17Nakama mkiita "Baba" ule ahukumiye kwa haki kulingana na kdhi ya kila mchu, chumia muda wa safari ako kachika unyenyekevu.18Mnafahamu kwamba haiva kwa fedhaao dhahabu dhichu dhinadhoharibika- ambadho mmekombolewa kutoka kwene tabia dhenyu dhaujinga ambadho muliifunda kutoka kwa baba dhenyu. 19Lakini mmekombolewa kwa damu a heshima a Kristo kama akondoo asie na hila wala doa.20Kristo alitauliwa kabila a msingi a dunia lakini sasa siku hidhi dhamwisho, amefunuliwa kwenyu. 21Mnamwamini Mungu kupichia iye ambae Mungu alimfufua kutoka kwa wafu na ambae alimpoutukufu ilikwamba imana enyu na ujasiri ue kachika Mungu.22Mmefanya nafsi dhenyu kuva safi na tii wa ilee kweli kwa dhumuni la upendo la kindugu lililo na unyofu hivo pendaneni kwa bidii toka moyoni. 23Mumekwisha dhaliwa mara apili si kwa mbeu iharibikao lakini kutoka kachika mbeu isioharibika kupichia udhima na neno la Mungu lililo salia.24Kwa maan "miili ote nikama mayani na utukufu ake ote nikama ua la yani, yani hunyauka na ua hudondoka. 25Lakini neno la Bwana hubaki milele."Huu ni ujumbe ambao ulichangadhwa kama injili kwenyu.
1Kwa hia vekeni pembeni uovu vothe, udanganyifu, unafiki, wivu na kashifa. 2Kama vadodo vachanga, mtamani maziwa safi a kiroho, ili kwamba mwedhe kukua ndani a wokovu, 3kama mmeonj kwamba Bwana ni mwema.4Njoni ake aliye jiwe hai linaloishi ambatho limekadhaliwa na vachu, lakini hilo limedhaguliwa na Mungu na ni la thamani kwake. 5Inni pia nikama mawe yaliyo hai yaliyojengwa juu kwa nyumba a kiroho, ili kuva ukuhani mchakachifu ambao hudhoa dhabihu va kiroho dhinadhokubaliwa kwa Mungu kupidhia Yesu Kristo.6Andiko husema hivi, "Tazama, nimeveka kachika Sayuni jiwe va pembeni, kuu na lililothaguliwa na la dhamani.Eote aaminiye kachika eye hadhaona aibu."7Hivo hedhima ni enyu kwenyu ini mnaoamini. Lakini, "Dhiwe lililokachaliwa na wajendhi limekuwa jiwe kuru dha vembeni"- 8na, "jiwe dha kujikwaa na mwamba a kujikwaa." Wao hujikwaa, wanaolikadhaa ineno, kwa lile ambalo pia valikuwa vameteuliwa kwalo.9Lakini inyi ni ukoo uliodhaguliwa, ukuhani wa kifalume, dhaifa dhakachifu, vachu va miliki ya Mungu, ili kwamba mweze kuthangaza machezo va ajabu a yule aliyevaita kuthoka gidhani kuya kwene nuru ake a ajabu. 10Inni kwanza hamkuwa vatu, lakini sasa inni ni vachu va Mungu. Ninyi hamkupokea rehema, lakini sasa mmepokea rehema.11Vapendwa, nimevaita kama vageni na wadhururaji kujinyima kuchoka kwene tamaa mbaya za dhambi, ambadho zinapigana vita na roho venu. 12Mnapathwa kuwa na thabia njema kachi ya mataifa, ili kwamba, kama watawasema kama kwamba mmechenda maovu, watadhiangalia kadhi zenyu njema na kumsifu Mungu kachika siku a kuya kwake.13Tii kila mamlaka a mwanadamu kwa ajili a Bwana, ikiva mfalme kama mkuru, 14ikiva vatavala valiotumwa kuvaadhibu vatenda mabaya nakuvasifu vale vanaotenda mema. 15Kwa kuva ni mapendhi a mungu kwamba kwa kuchenda mema mwanyamazisha mazungumdho a kipuuzi a wachu wapumbavu. 16Kama wachu huru, msiutumie uhuru venu kama kifuniko kwa maovu, bali muve kama vatumishi va Mungu. 17Vaheshimuni vachu vote. Vapendheni ndugu, mwogopeni Mungu. Mwedhimuni mfalme.18Vatumwa, vatiini bwana zenyu kwa heshima ote sio tu bwana valio vadhuri na vapole, lakini pia valio vaovu. 19Kwa kuva ni sifa kama eote adhavumilia maumivu vakachi anapodheseka pasipo haki va sababu a dhamiri ake kwa Mungu. 20Ni faida gani iliyopo kama vanadamu kuchenda dhambi kisha mwendelee kuadhibiwa? Lakini kama mmechenda mema na ndhipo mcheseke kwa kuhukumiwa, hii ni sifa njema kwa Mungu.21Kwa hii mlitwa, kwa sababu Kristo pia alicheswa kwa ajili enu, amevaachia mfano kwa ajili enu kufuata nyayo dhake. 22Eye hakuchenda dhambi, wala hakuvonekana udhanganyifu oote kinywani mwake. 23Vakati eye alipochukanwa, hakurudhisha machukano, alipocheseka, hakutisha bali alijitoa mwenewe kwake yesu ahukumiye kwa haki.24Eye mwenewe alidhibeba dhambi zetu kachika mvili vake kwene mti, ili kwamba tusiwe na sehemu tena kachika dhambi, na kwamba chuishi kwa ajili ya haki. Kwa kupigwa vake inni mmevona. 25Vote valiokuwa mkidhangadhanga kama kondoo aliyepodhea, lakini thatha mmerudhi va mchungaji na mlindhi wa roho venu.
1Kwa ndia hii, inni ambavo ni ake mnapaswa kuitoa kwa wavule thenyu wenewe ili hata kama baadhi ao hawayaliti neno, kupichia tabia thao vake thao wanawetha kuvuchwa pasipo neno, 2Kwa sababu wao wenewe vameivona tabia yenyu njema pamoya na heshima.3Hi ifanyike sivo kwa mapambo ya inde kusuka nee vicho vya dhahabu au mavathi ya michindo. 4Lakini badala ake uchu wa ndani a moyo na kudhidi kachika udhuri waunyenyekevu na uchulivu wa moyo ambavo nivathamani mbee tha Mungu.5kwa kuva vanavake vachakachifu waliipamba wenewe kwa ndia hii walikuva na imani kachika Mungu valivatii wavuli vyavo wenewe. 6Kwa ndia Sara alimtii Ibrahim na kumuicha iye "bwana" ake. Inni sasa ni vana vake kama mtafanya a lio madhuri na kama hamuchi maovu.7Kwa ndia hio hio inni wanawavuli munapaswa kuishi na wake thenyu mviiva kuva wao mwenzi wa kike dhaifu mukivachambua vao kama wapokeaji wenthenyu wa thawadi ya udhima, fanyani hia ili kwamba maombi yenyu yasidhuwiliwe.8Hatimae, inni vyote muve na nia moya, wene huruma, upendo kama ndugu wanyenyekevu na wapole. 9Msilipidhe ouvu kwa uovu au ichusi kwa ichusi kinime mwendele kubari kwa sababu muliichwa ili kwamba muwethe kurithi baraka.10Iye atakae kupenda maisha na kuvoa siku njema lathima adhuwie ulimwi ake kwa maovu na ndomo ae kunena hila. 11nageuke na kuata maovu nakufanya yalio madhuri atafudhe amani na kuifuacha. 12Mato ya Bwana humvona mwene haki na masikio ake huskia maombi. Lakini vuso wa Bwana uko kinume cha vale vachendavo uovu.13Nyani atakaewashuri inne ikiva mwatamani lililo dhuri? 14Lakini kama mukicheseka kwa haki mumebarikiwa musiche alee ambavo ivo yanayacha msivi na wasiwasi.15Badala ake mveke Kristo Bwana kachika mioyo enyu kama mchakachifu kila mara mvetayari kumjibu kila mchu anae wavulidhwa inni kwa inni munatumaini kachika Mungu. Fanyeni hia kwa upole na heshima. 16Mve na dhamiri njema ili kwamba wanao chukana maisha yenyu mema kachika Kristo wawedhe kuaibika kwa kuwa wananena kinume dhidi enyu kama kwa mulikuva wachenda maovu. 17Niudhuri thaidi ikiva Mungu anatamani kwamba mwacheseka kwa kufanya mema kuliko kufanya maovu .18Kristo pia alicheseka kwa ajili a dhambi iye mabae mwene haki alicheseka kwa ajili echu ambavo hachukuva vene haki, ili kwamba achucheche kwa Mungu. Alikufa kachika mwili lakini alifanywa mdhima kachika roho. 19Kachika roho alinenda na kudhihubiri roho ambadho sasa dhiko kifungoni. 20Hadhikua thiifu vakathi uvumilivu wa Mungu ulipokuva unangojea vakathi va Nuhu dhiku dha ujedhi wa safina na Mungu aliokoa vachu vachache- nafsi nane- kuthoka kachika mayi.21Hii ni alama ya ubachidho inaovaokoa inyi sasa si kama kuosa uchafu kuthoka mvilini lakini kama ombi la dhamiri njema kwa Mungu kupichia ufunuo wa Yesu Kristo. 22iye uko mkono wa kuume wa Mungu. Alinenda mbinguni , malaika, mamlaka na nguvu ladhima dhimthi iye.
1Kwa kuwa Kristo alichesela kachika mvili, ivikeni Kwa nia io hio. Kwa oote alicheseka kachika mvili vandha atana na dhambi. 2Mchu wa namna hio kwa wakati wake uliobaki kachika mvili haishi tena kachika tamaa dha vanadamu, bali anaishi kachikka mapendhi a Mungu.3Kwa muda uliopicha umetosa kuchenda mambo ambayo vamataifa vanataka kufanya ufisadi,nia mbaya, ulevi, ulafi, sherehe za kipagani na ibada dha sanamu dhenye machukidho. 4Vanafikiria ni ajabu mnapojiepusa kuchenda mambo haa pamoya nao, hiya wanu nena maovu iyu enu. 5Vatatoa hesabu kwake ahe tayari kuhukumu valio hai na wafu. 6Kwa kusudi hii injili indhahubiriwa kwavo avo valiokwisha kufa, kwamba ivapo kuva valikwisha hukimiwa kichika mvili avo kama vana damu, ili vaveze kishi kulingana na Mungu kachiko roho.7Mwisho a mambo ote waiva, kwa hia muve na ufahamu ulio sahii - na iveni na nia ndhuri kwa ajili a maombi enu. 8Iyu a mambo ote iveni na bidii kachika upendho kwa kila mmoya kwa kuva upendho hauthafudhi kufinua dhambi dha vengine. 9Vonesheni ukarimu kwa kila mmoya bila kuinung'unika10Kama ambavo kila mmoya venu alivopokea karama. Ichumieni kachika kuhudumiana kama vasimamidhi vema va karama, ningi dhilidhotholewa buree na Mungu. 11Kama nchu akinena, na ive kama mausia a Mungu na kama nchu akihudumu na ive kama uedho andhopewa na Mungu, ili kwamba kwa kila yambo Mungu apache kuthukudhwa kupicha Yesu Kristo. Uthukufu na uedho vina e milele na milele. Amina.12Vapendhwa msiheasabu jaribu ambalo huya kuvajaribu kama kichu kigeni, ingava kuna kichu kigeni kilicho kuva kinathokea kwenu. 13Lakini kwa kadri mnaodhidi kupicha udhoefu wa macheso a Kristo, furahini ili kwamba mfurahi pia na kushangilia kachika ufunuo va uchakachifu vake. 14Ivapo mndhachukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mndhabarikiwa, kwa sababu a roho kwa uthukufu wa Mungu hukaa iyu enu.15Lakin asiveko oote mwene kucheswa kama muuaji, mwidhi mchenda maovu au aishuhulishae na mambo a vengine. 16Ikiva nchu hucheswa kama Kristo, asivone aibu ila anthukuthe Mungu kachika ina hilo.17Kwa kuva vakathi andhafika kwa hukumu kuandhia kachika numba a Mungu. Na kama inaandhia kwechu ithakuae kwa vale vasio thii injili a Mungu? 18Kama mwene haki huokolewa kupichia Mungu ithakuae kwa nchu asiehaki na mwene dhambi? 19Kwa hio vote vachesekao kuthokana na mapendhi a Mungu vakabidhi nafsi dhao kwa muumba mwaminifu ili hali ilihali vakichenda mema.
1Nnawasihi vathee valiomo miongoni mwenyu, imi nilie nthe mwendani vao na shahidi wa machezo a Kristo, na ambavo hia hia ni mshirika kachika utukufu utakavo dhihirika. 2Kwa hiyo ninawachia mioyo inyi vathee lilindeni ikundi la Mungu lililo miongoni mwenyu. Liengeni, sivyo kwa sababu mnapaswa lakini kwa kuwa mnathamani hia kulingana na Mungu. Liengeni, sivo kwa kupenda sinto tha aibu lakini kwa kupenda. 3Msiifanye wavuli iyi a vachu valio iti a uangalithi wenyu, lakini mve mfano kachika ikundi. 4Mchungaji mkuru atakapodhihirishwa, mtaipokea taji a utukufu isiopotedha uthamani ake.5Naini vana thidodi nyenyekeeni kwa wakuru thenyu. Ini vote uvaeni unyenyekevu kuchumikiana inni kwa inni kwani Mungu humponda mwene kiburi na huvapa neema wanyenyekevu. 6Nyenyekeeni iti ya mkono wa Mungu uliyo hodari ili kuva avanyue kwa wakati ake. 7Mvekeeni fadhaa thenu iyu ake kwa sababu avajali.8Iveni na busara, ive wangalifu. Ule adui enu ibilisi, kama thimba angurumae ananyatia, akisaka mchu wa kumrarua. 9Thimameni kinime chake. Kuveni na nguvu kachika imani yenyu. Mkiiva kwamba nduthenyu valivoko ulimwenguni wanapichia macheso kama hao.10Baada ya kucheseka muda kichambo, Mungu wa neema ote, alievaicha kachika utukufu wa milele ndani ya Kristo, atavakamilisha atavaimarisha na kuwachia nguvu. 11Enthi ive kwake milele a milele. Amina.12Namthamani siliwano kama Ndugu muaminifu na ndawaandikia inni kwa ufupi kupichia kwake. Ndavatia moyo na ndashuhudia kwamba nilicho kiandika ni neema ya ukweli a Mungu hivo simameni ndani ake. 13Vaamini valivoko Babeli, walivotauliwa pamoja nanyi vanawasalimu na Marko mwanangu anawasalimu. 14Salimianeni kila mmoya kwa busu na imani ive kwenyu mlio ndani ya Kristo.
1Kilee chulichokivona changu mwandho-kilee chulichokisikia, chulichokivona kwa matho yechu, kilee chulichokienga na mikono yechu indhakishika- kuhusu ineno la udhima. 2Na ulee udhima un dhafanywa kuyulikana wadhi, na chundhauvona na kuushuhudia na kuwachangandhia udhima wa milele ambao udhakuako kwa Baba na undhafanywa kuivwa kwechu.3Kile chulichokivona na kukisikidha chwakichangadha kwenyu ili kuva muedhe kuthangamana nasi na ushirika vechu pamoya na Baba na Mwanave Yesu Kristo. 4Chunavaandikia mambo haa inyi ili kuva furaha echu ive kamilifu5Hunu ndio ujumbe chundhaosikia kuthoka kwake na kuvachangadhia ya kuwa Mungu ni nuru na ndani ake hakuna gidha. 6Chukinena kwamba chuna ushirika nae na chwanenda gidhani, chwahadaa na hachufanyi kweli. 7Chukinkurena kadhika nuru kama alivyo iye nuruni, Twashirikiana isi kwa isi na damu a Yesu Krsto, mwanawe yachuchakasa kuthoka dhambini.8Kama chukinena hachuna dhambi chwaihadaa enyewe na kwei haiko dani echu. 9Chukidhikiri dhambi dhech, iye ni muaminifu na haki kuchusamehe dhambi dhechu na kuchuchakosa na wovo wonthe. 10Chukinena kwamba hachuyachenda dhambi, chamfanya iye nrongo na indeno lake halimondanoi
1Vana vandu vapendwa, na vaandikia mambo haa kwenyu ili msichende dhambi, lakini kama mmoya wenyu akichenda dhambi chunae wakili aliepamoya na Baba, Yesu Kristo, ambae ni mwenehaki. 2Ienimpachanishi kwa dhambi dhechu, na si kwa dhambi dhechu pwekee, lakini kwa ulimwengu nndhima. 3Kwa hili chwaiva kwamba chwan'yiva ie kama chukidhichund'a amri dhake.4Ie anenae, "Namuiva Mungu, "lakini hamdhikishiki amri dhake, nimongo, nakweli haimo ndani ake. 5Lakini oote ashikae neno lake, kweli kachika mchu ulee upendo wamungu unda kamilishwa kachika hili chwaiva kwamba chuko ndani ake. 6Iye anenae anaishi ndani ya Mungu inampasa iye mwenewe pia kutembea kama vile Yesu Kristo alivo tembea.7Vapenzi, sivaandiki amri mpia, bali amri adhamani mumekwsisha kuva nao changu wand'o. Amri adhamani nineno ambalo mlilo lishika. 8Hata hivo nind'a vaandikia in amri mpia ambao ni kweli kachika Kristo na kwenyu, kwa sababu kidha kina picha, na nuru na ya kweli iko tayari inaangadha.9Ie anenae uko kwene nuru na hutukia ndue uko kachika kidha hata sasa. 10Ie ampendae nduake anaeshi katika nuru na hakuna yambo lolote liwedhalo kunkwadha. 11Lakini ie antukiae nduake ukokidhani anana anaenenda gidhani, ie haisi wapi aendapo kwa kuwa gidha limempofusha mato ake.12Navaandikia vana vapendwa kwa sababu mmesamehewa dhambi dhenyu kwa ajili ina lake. 13Navaandikia akina baba kwa sababu mnaiva ie alie changu mwando. Navaandikia dhijana kwa sababu mdha shinda ule m'ovu. Nimevaandikia vana vadodi kwa sababu mnamuiva baba. 14Nimevaandikia akinababa kwa sababu mna inamuiva ie aliechangu mwando, nimevaandikia vana kwa sababu na nguvu , na neno la Mungu lind'a keti ndani enyu na mmemshindaule muovu.15Msiipende dunia wala vichu ambadho dhimo kachiki dunia. Iwapo yule ataipenda dunia, upend'o wakumpenda baba haumo ndani ake. 16Kwani kila kichu kilichomo kachika dunia- tamaa a mwili, tamaa amato, na kiburi cha udhima hadhitokani na baba lakini dhina dunia. 17Dunia na tamaa dhake dhinapicha, ie afanyae mapendhi ya Mungu hoo hudumu milele.18Vana vadodi nivakati va mwisho ambavo mndiasikia kwamba mpinga Kristo weyao, hata sasa vapinga Kristo vameshakuya, kwa hali hii chunaiva ni wakati wamwisho. 19Valiondoka dhavo kutoka kwechu, kwani hava kuva vakwechu. Vange kuva va kwechu vangeendelea kuva pamoya nasi lakini wakati walipokwenda dhavo, hicho kilivonyesha havaku va wakwechu.20Lakini mmechiqwa mafuta kutoka kwa ulee nchakachifu, nani nyote mwaiva kweli. 21Sikuvaandikia ini kwa sababu hamuishukweli , bali kwasababu mnaiva na hakuna uongo waile kweli.22Nyani ni muongo bali ndie anae pinga kwamba Yesu ni Kristo?Huu nchu nipnga Kristo pale anapompinga Baba na Mwana. 23Hakuna anaempinga Mwana akava na Baba oote anaenkiri Mwana anae Baba.24Kama kwa ajili enyu, kile mulokisikia changu mwandho atha kiendelee kuva ndani enyu . Kilee mlichosikia changu mwandho kitaketi ndani enyu, pia mtaketi ndani a Mwana na Baba. 25NA hii ni ahadi alochupa isi: udhima wa milele. 26Nidhawaandikia haa inyi kuhusu valee ambavo vangevaongodha inyi kachika inyi kachika upothevu27Kwajili enyu ale mafucha mloyapokea kuthoka kwake huketi ndani enyu na hamtataka nchu wowote kuvafubdisha, ila kama mafucha ake huwafundisha kuhusu mambo ote na ni kweli na sio uongo hatakama yashawafundisha kethini ndani ake. 28Sasa vana vapendwa ketini ndani ake ili atakapotokeza, chuwedhe kua na ujasiri na sio kujiona aibu mbee ake na kachika kuya kwake. 29Kama mnaiva kuwe iye ni mwenye haki mnaiva kamba kila mmoya achendae haki andhazaliwa nae.
1Voneni ni pendo la nmana gani alochupa Baba kwamba chunaichwa vana va Mungu na hivo ndivo chulivo kwa sababu ulimwengu hauchumbui kwa kuva haukumchambua iye. 2Vapendwa isi ni vana va Mungu na harahiahidhirika bado jinsi chuthakavo kuva. Chwaiva kwamba Kristo athakapovonekana, chuthafana nae kwani chuthamuona kama alivo. 3Kila mmoya ambae ana ujasiri huu kuhusu vakathi vyao ulioelekedhwa kwake, huichakasa mwenewe kama iye alivo nchakachifu.4Kila nchu anaendelea kuchenda dhambi huvundha sheria kwa sababu dhambi ni uvundhaji wa sheria. 5Unaivo Kristo aliadhirishwa ili kudhiondoa dhambi kabisa na ndani yake hamna dhambi. 6Hakuna hatha mmoya akethio ndani ake na kuendelea kuchenda dhambi. Hakuna nchu hatha mmoya akethio kachika dhambi akiva amevonba na kuiva iye.7Vachocho vapendhwa msikubali kupochoshwa na nchu oote. Nchendae haki ni mwene haki,kama vile Kristo alivo mwene haki. 8Alichenda dhambi na wanaibilisi kwa sababu wao ni nchenda dhambi changu mwandho. Kwa sababu hii Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili awedhe kudhiharibu kadhi dha iblisi.9Oothe alie dhaliwa na Mungu hachendi dhambi kwa sababu mbeu a Mungu hukethi ndani ake. Haedhi kuendelea kuchenda dhambi kwa sababu amedhaliwa na Mungu. 10kachika hili vana va Mungu na va ibilisi vanaivikana. Oothe asiechenda kilicho cha haki si wamungu wala ulee ambae hawedhi kumpenda nduake.11Kwani huu ndio ujumbe muliousikia kuthoka musandho kwamba chunapaswa kupendhana isi kwa isi. 12Sivo kama Kaini ambae alikua muovu na alee a ndugu ake. Na kwanini alimuua?Kwa sababu machendo ake alikuva maovu na alee a ndugu ake alikuva a haki.13Ndugu dhangu msishangae endapo ulimwengu utharathukidha. 14Chwaiva chumekwisha kuthoka mauthini na kuingia udhimani kwa sababu chunavapendha ndugu. Oothe ambae hana upendho hudumu kachika mauthi. 15Nchu oote anaenthukia nduake ni muuaji na mnaiva kuva udhima wa milele haukethi ndani a muuaji.16Kachia hili chaliva pendho kwa sababu Kristo aliuthoa uha wake kwa ajili echu. Nasi yachupasa kuathoa maisha echu kwa ajili a ndugu. 17Lakini oote aliena dhichu na amuonae ndugu ake mwenye uhithaji , lakini huuzuia moyo ake wa huruma kwa ajili ake; Je, upendho wa Mungu unakaae ndani ake? 18Vana vangu vapendhi, chusipendhe kwa midoma wala kwa maneno machupu ila kachiki dhichendo na kweli.19Kachika hili chunaiva kwamba isi chuko kachika kweli, na moyo echu inadhibithika kachika iye. 20Ikiva kama mioyo echu achuhukumu, Mungu ni nkuru kuliko mioyo echu na iye huiva mambo ote. 21Vapendhi, kama mioyo echu haichuhukumu chunao ujasiri kwa Mungu. 22Chochote chuombacho chatakipokea kutoka kwake, kwa sababu chunadhishika amri dhake na chunafanya23Na hii ndio amri ake- akwamba achupasa kuamini kachika ina la mwanae Yesu Kristo na kupendana isi kwa isi- kama alivo chupachia amri ake. 24Anaedhitii amri dhake hudumu ndani ake, na kwa sababu hii chaiva kuva hukaa ndani echu kwa ule roho alie chupa.
1Vapendwa msiamini Kilaroho,lakini dhijariburi roho muvone kama dhinatokana na Mungu kwa sababu manabii vengi vauongo wametokea duniani, 2kwa hilo mtamuiva roho amungu kila roho itakaokiri kuva Yesu Kristo amekuya kachika mwili ni wakutoka kwa Mungu. 3Kilaroho isionkiri Yesu si ya Mungu bali niroho ya mpinga Yesu Kristo mulioisikia kuva inakuya na iko duniani.4Ini ni vana va vamungu na mmekwisha vashinda kwa sababu iye alie ndani yenyu ni mkuru kuliko aliye kachika ulimwengu. 5Vao nivaulimwengu kwa hiyo vanachokinena ni cha ulimwengu na unawasikidha. 6Isi ni vamungu.Iye amuyuvae Mungu huchusikidha na asie wamungu hawedhi kuchusikidha. Kachika hili chunaiva roho ya kweli na roho auongo.7Vyapendwa chupendane isi kwa isi,kwa vilee upendo kutoka kwa Mungu na Kila mmoya apendae amedhaliwa na Mungu na kumuiva Mungu. 8Mchu asie mpenda hamuisi Mungu kwa kuwa iye ni upendo. .9Kachika hili pendo la Mungu lilifunuliwa miyongoni mwechu kwamba alimchuma mwanawe ulimwenguni ili chuishi kupichia iye. 10Kachika hili pendo sikuva chulimpenda Mungi lakini iye alichupenda na akamchuma mwanawe ave fidia kwa ajili ya dhambi thechu.11Vapendwa ikiva Mungu alitupenda isi vilee chunapaswa kupendana isi kwa isi. 12Hakuna hata mmoya alie muvuona Mungu kama chukipenda isi kwa isi, Mungu anaketi ndani yechu na upendo ake undokamilika ndani yechu. 13Hachika hili chunaiva kuva chunaketi ndani ake na iye ndani echu kwa sababu amechupa roho ake. 14Tena isi chundavonana na kushudia kuva Baba amemchuma mwanawe kuva muokothi wa ulimwengu.15Kila anae kiri kwamba Yesu ni mwana wa Mungu nae anakaa ndani ake na iye ndani ya Mungu. 16Chumeiva na kuamini upendo alio nao Mungu kwa ajili yechu kwa kuwa Mungu ni upendo , anae keti ndani ya upendo anaketi ndani ya Mungu nae huketi ndani ake.17Kwa hili, upendo huu undakwisha kamilika kachikachi echu, ili chuve na ujasiri siku ya hukumu kwa sababu kma iye alivo, na isi ndivo chulivo kachika ulimwengu huu. 18Hakuna hofu ndani ya pendo kwa kuwa linaitupa hofu inde maana hofu huhusiana na hukumu. Iye achae hayakamilishwa kachika pendo.19Chunapenda kwasababu Mungu alichupenda kwanda. 20Ikiva mmoya atanena "Nampenda Mungu" lakini hawethi kumpenda ndue ni muongo kwa sababu asiempenda ndue anaemuvona hawedhi kumpenda Mungu ambae hamuvoni. 21Hii ndio amri chulio nao kutoka kwake:ote ampenda Mungu anapaswa kumpenda ndue pia.
1Wowote anaeamini kuva Yesu ni Kristo aliezaliwa na Mungu,na ampendhao iye ambae andhathoka kwa Baba pia huvapendha vanave. 2Kwa hili twaiva kwamba chwapendhana vana vamungu, chonapompendha Mungu na kuthii anri dhake 3Ndivo chunavompendha Mungu kwamba chwazitwi anri dhake ambatho ni nyepesi.4Kwa kuva Kila alodhaliwa na Mungu hushinda ulimwengu na huu ndio ushindi wakushinda ulimwengu, hatha Imani echu. 5Ni nani aushindae ulimwengu?ni ulee aminiae kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu.6Huu ndie aliekuya kwa mai na dani -Yesu Kristo.Hakuya thu kwa mayi bali kwa mayi na damu. 7Kwa kuva na vachu vashuhudiao. 8Ruru,mayi na damu. Hawa wachachu hukubaliana .9Kama chunaupokea ushuhuda wa vanadamu ushuhuda wa Mungu ni nkuru kuliko hoo Kwa kuwa ushuhuda wa Mungu nihuu-kwamba unao ushuhuda kuhusiana na mwanae. 10Iye amwaminie Mwana wa Mungu anaushuhuda ndani ake mwenewe na asie mwamini Mungu andhamfanya kuva muongo, Kwa kuva hakuamini ushuhuda ambao Mungu andhauecha kuhusu mwanae11Ushuhuda ndio huu- kwamba Mungu andhachupa udhima wa milele na uko ndani a mwanae. 12Alie nae Mwana wa Mungu ana udhima na asie nae hana undhima.13Nimevaandhika haa mambo muedhe kuiva kwamba mnao udhima wa milele- inyi mnao amini kachika ina la Mwana wa Mungu. 14Huu ndio ujasiri chulionao mbee dhake kwamba chukiomba kichu chochote sawasawa na mapendho ake huchusikia. 15Kama chunaiva kwamba huchusikia- chochote chumuombacho chunaiva kwamba chunacho hicho chulamuomba.16Nchu amvonae ndu ake anachenda dhambi isopelekea kifo yampasa kuomba na Mungu athampa udhima. Nadhungumudha kwa valee ambavo dhambi dhavo ni dhilee dhisiopelekea kifo.Kuna dhambi ipelekeao kifo;sineni kwamba anapaswa kuomba Kwa ajili a dhambi hio. 17Machendo othe asiokua na dhambi hila kuna dhambi isopelekea kifo.18Chwaiva kuva aliedhaliwa na Mungu hachendi dhambi bali huchudwa nae salama daima na ulee muovu haedhi kumdhuru. 19Chwaiva kuva isi ni va Mungu na chunaiva kwamba ulimwengu othe uko ithi a utawala wa ulee muovu20Chwaiva kwamba Mwana wa Mungu andhakuya na andhachupa ujuzi kwamba twamuiva iye alie kweli na chumo ndani ake, hata kama Mwanae Yesu Kristo ni Mungu wa kweli na udhima wa milele. 21Vana vapendhi jithengeni na sanamu.
1kuthoka kwa nthee kuvamwamke na mtheule na vake, nivapendhavo kachika kweli na si imi thuu, bali na vote vale vanao ifahamu kweli, 2Kwa sababu ya kweli ilioko ndani yechu na ithakao dumu pamoya nasi milele. 3Neema arehema,amanithithakua nasi kuthoka kwa mungu Baba nakuthoka kwa Yesu Kristo,Mwana wa Baba,kachika kweli na pendho.4ninafurahika sana kwamba ndhachambua baadhi ya vana vanaonende kachika kweli kama vile chulivo ipokea amri hii kuthoka kwa Baba. 5nNa sasa nakudhania uwe, mwanamke, sivo kwamba nakuandhikia amri mpia, ila ile chuliokua nao changu mwandho ,kwamba chunapaswa kupendhana isi kwa isi. 6na huu ndio upendho chunaopaswa kunenda nao, kulingana na amri ake. Hhii ndio ilee amri kama mlivo isikia thokea mwandho, kwamba mnafaa kuendelea kachika hio.7Kwa kuva vaongovengi vandhaenea kachika ulimwengu na havakiri kwamba Yesu Kristo alikuya kachika mwili huu ndie muongo na mpinga Kristo. 8iyangalieni venyeve kwamba hampothedhi mambo alee chuliokwisha kufanya kadhi,lakini kwamba muedhe kuipokea.9Yoyothe aendeleao mbee na huduma kachika fundisho la Kristo, hana Mungu. Iye adumuo kachika fundisho anae Baba na Mwana pia. 10Kama nchu uyao kwenyu haechi fundisho hili, musimkaribishe kachika numba enyu na msimsalimie. 11kwa kuva ansalimiao hushiriki kachika machendo ake maovu.12ninao mambo mangi yakukuandhikia, na sikuthaka kuyaandhika kwa karathasi na wino. Lakini nathumaini kuya kwenyu na kunena vuso kwa vuso. kwamba furaha echu ipache kufanywa kamili. 13vachocho vadada enyu ntheule.
1Kuthoka kwa ndhee hadi kwa Gayo mpendhi, ninayempendha kachika kweli. 2Mpendwa, nakuombea ufanikiwe kachika mambo ote na kuva na afiya njema, kama vile roho ako inavyofanikiwa. 3Maana nilifurahi sana vakati nilipoambiwa na vaumini valiokuya na kutoa ushuhuda iyu ya kweli wako kama vile unavokwenda kachika kweli. 4Sina furaha kuru dhaidi ya hii, kusikia kwamba vanavangu wa kiroho wanatembea kachika kwel.5Mpendhwa, unaenenda kwa uaminifu kwa Mungu unapovahudumia ndugu n vageni 6vametoa ushuhuda wa upendovako mbee ya kanisa. unafanya udhuri kuwaasaidia kuwasafirisha kachika safari dhavo kwa namna ambayo inampendetha Mungu. 7Kwa ajili ya jina la Yesu , walienenda bila kutukua kichu chochote, kwa vachu wa mataifa. 8Hivo tunatakiwa kuvakaribisha vachu kama hava,. mathaifa.ilichuve wafanya kadhi tukishirikiana kwa ajili ya kuchangaza kweli kwa mungu.9Ndhakuandikia uwe pamoya na kusanyiko yambo fulani, lakini Diotrofe ,apendae kuifanya kuva kiongodhi miongoni mwa vaumini vendhangu. 10Hivo , kama nikia nitakumbuka machendo ake anayofanya, jinsi anavonena maneno maovu ya kushutumu kinyime nasi. hayaridhika na machendo haa, iye mwenewe havapokie vaumini pia kuvakachadha vangine ambavo vanatamani kuvakaribisha havo vaumini na kuva kuwafukudha vatoke kwenye mkusanyiko.11Mpendhi Gayo usitabe kilicho kiovu, ila thaba kilicho chema. achendae mema ni wa Mungu ;na iye achendavo maovu hayamuamini Mungu . 12Demetrio andhashuhudiwa na vote na kweli venyewe . isi pia ni mashahidi, na waiva kuva ushuhuda wechu ni wa kweli.13Ninao mambo mangi ya kukuandhikia, lakini sipendhi kukuandhikia kwa kalamu na wino. 14Bali natarajikia kukuvona hiya karibuni, na chundhanena nawe vuso kwa vuso. 15Amani ive pamoya nawe, marafiki nilivonvo hapa vanakusalimia pia navasalimu marafiki kila moya kwa ina.
1Yuda, nchumwa wa Yesu Kristo, na nduake Yakobo, kwa valee ambao vandhaichwa, vapendhwao kachika Mungu baba, na valochudhwa kwa ajili ya Yesu Kristo. 2Rehema na amani na upendho uongedheke kwenyu.3Vapendhwa vakathi nilivokuva nikifanya kila juhudi kuvaanghikia inyi kuhusu uokovu wechu, iliniladhimu kuvaandhikia kwa ajili ya kuvashauri ili mshindanie kwa uaminifu, iman ambao ilikuva indhakabidhiwa mara moya thu kwa vaaminio. 4Kwa sababu vachu fulani vandhangia kwa siri kachi enyu vachu ambavo valichiwa alama kwa ajili yakuhukumu vachu vasio vathaua ambavo hubadili neema ya Mungu Wechu kuvaa ufisadi ,na kunkana Bwana Wechu Yesu Kristo.5Sasa napendha kuvakumbusha inyi ingava kuna vakati mlivaa kwa ukamilifu kwamba Bwana alivaokoa vachu kuthoka nchi ya misiri, lakini baadae akavaangamidha valee ambavo havakuvaamini. 6Na malaika ambavo havakuilinda enzi avo venyev lakini vakaatha makathi avo maalumu Mungu uvavesee kachika minyororo ya milele ndani ya kidha kwa ajili ya hukumu ,ya siku ile kuru.7Kama vilee Sodoma na Gomora na mii iliyodhunguka ambao pia iliichia enyewe kachika uwasharathi na vakaandhama thamaa isio ya asili. valivonesha kama mifano ya valee ambavo hucheseka kachika hukumu ya mocho wa milele. 8Hali kadhalika kwa ndhia ilee ilee waocha ndocho hava pia huchafua miili avo, na hukachaa mamlaka na hunena uongo dhidi ya vathukufu.9Lakini hatha mikaeli malaika nkuru, vakathi alivokuva akishindana na ibilisi na kuchecha kwa ajili ya mwili wa Musa hakuthubuthu kuecha hukumu auongo dhidi ake ,lakini badhala ake alinena, ''Bwana akukemee!'' 10Lakini vachu hava huecha uongo dhidi ya chochothe vasichokiiva. Na kilee vasichokiiva- kama vanyama vasivo na akili, haa ndio yalivovaharibu. 11Ole wavo! kwakuva vandhanenda kachika ndhia ya kaini, nakuliandhama kosa la balaamu.Vandhaangamia kachika uasi wa Kora.12Hava nimiamba kachika sherehe dhenyu dha upendho, vakisherehekea pasipo aibu, vathungaji valioilisha venyeva thu. Nimavingu asio na mvua athukuliwao na upepo, ni michi iliyopukusika isio na machunda ilio kufa mara mbili iliosumuliwa midhidhi. 13Ni madhimbi ya bahari enye kele yakithoa aibu avo venyene, ni nocha thinadho rangaranga ambatho weusi wa kidha umechudha kwa ajili avo.14Enoko, wa sabaa kuthoka kwa Adamu, alithabiri kuhusu ivo, akinena, ''Eng! Bwana uyaona maelfu na maelfu ya wathakathifu vake, 15Iliafanye hukumu iyu ya kila kichu nchu, na kuchia hathia ote wasomcha mungu iyu ya machendo avo otewalivokwisha kufanya kachika ndhia dhisidho kithavua, na kwamaneno ote ya ukali ambao wasivo wathavua wandhanena dhidi ake.'' 16Hava ni valee vanung'unikavo walalamikavo ambavo thamaa dhavo dha uovo, wajivunio mno, ambavo kwa faidadhavo kuhadaha vangi17Lakini inyi, wapendwao, kumbukeni maneno ambao yalinenwa dhamani na Michume ya Bwana Yesu Kristo. 18Valinena kwenyu, ''kachika nyakathi dhamwisho kuthakua na vachu wanaodhihaki ambao ambavo huandhama thamaa thavo thisitho dha kithauwa.'' 19vachu hava ni vathenganishaji, vanathavaliwa na thamaa dha kidunia na havana Roho.20lakini ndinyi, vapendwa, jijengeni kachika imani enyu thakathifusana na muombe kachika Roho Mthakathifu. 21Ithundheni kachika upendho wa mungu, na msubiri rehema ya bwana wechu Yesu Kristo ambao huwapachia udhima wa milele.22Onesheni rehema kwa valee valivo namashaka, 23Vaokoenivangine kwa kuvanyakua kuthoka kachika mocho. Kwa vangine vonesheni huruma kwa hofu, mkithukia lilichiwa doa na mwili.24Sasa kwake awedhae kuwalinda msijikwae, na kuwasabisha msimame mbee ya uthukufu wake biia mawaana nakuva na furaha kuru. 25kwake Mungu pekee mwokodhi kupichia Yesu KristoBwana Wechu, uthukufu uwe kwake, ukuru, uwedho na nguvu kabla ya nyakathi zothe, na sasa na hatha milele.